13
The African e-Journals Project has digitized full text of articles of eleven social science and humanities journals. This item is from the digital archive maintained by Michigan State University Library. Find more at: http://digital.lib.msu.edu/projects/africanjournals/ Available through a partnership with Scroll down to read the article.

The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

The African e-Journals Project has digitized full text of articles of eleven social science and humanities journals.   This item is from the digital archive maintained by Michigan State University Library. Find more at: http://digital.lib.msu.edu/projects/africanjournals/

Available through a partnership with

Scroll down to read the article.

Page 2: The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

MWONGOZO WA SUALA LA KUTAFSIRI NCHINITANZANIA

A. S. NCHIMBI*

1. Kwa watu wengi, neno hili la TAFSIRI ni la kawaida katika mazungurnzoyao ya kila siku. Maana inayoeleweka na kukubalika na wengi wetu ya nenohili TAFSIRI-ni ile ya kutoa "maana" ya hahari fulani "Maana" hiyoinaweza ama kutolewa katika maneno ya lugha ile ile (L1) ya habari ambayoinatarajiwa kutafsiriwa: (t=m+a),l ama katika lugha tofauti (~) na ile (L1)ya habari yenyewe inayotarajiwa kutafsiriwa: (t-;"~ml+al)'

Wana-Isimu wa siku hizi wamekubaIiana kwamba hapana uwezekano wa"kuitafsiri habari fulani" iIiyoandikwa katika lugha L1 katika lugha K2 kwaasilimia 'mia moja taslim.' Maadam TAFSIRI inamhitaji anayetafsiri kufa-hamu barabara habari yenyewe inayotarajiwa kutafsiriwa, yaani Ll na piakuifahamu barabara miundo mbaIi mbaIi ya lugha ~ ambamo TAFSIRIhiyo itafanyika, ni dhahiri kwamba aina yo yote ya TAFSIRllazima ifanyikekatika lugha ambayo anayetafsiri awe amezaliwa nayo. Zaidi ya hayo, mamboambayo yanasaidia kuifanya TAFSIRI yo yote iwe sahihi zaidi ni elimu yamfasiri katika utamaduni, siasa na mazingira ya nehi ambamo lugha zinazotu-mika katika TAFSIRI hiyo zimekomazwa.8

2. Kwa nini TAFSIRI ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku? SwaIi hilini muhimu sana, kwani tusipofafanua umaarufu wa TAFSIRI katika maishayetu ya kila siku, basi ni halali pia kusahau suala la TAFSIRI. Lakini ukwelini kwamba maisha yetu daima hujitafsiri kufuatana na utamaduni wetu, siasayetu na mazingira yetu. Kwa hiyo, suala la TAFSIRI ni la faradhi katikamaisha ya binadamu. Kwa mfano, ni sisi Watanzania pekee tunaoweza kuhisijinsi gani siasa ya Ujamaa na Kujitegemea inavyoweza kutusukuma mbelekwa haraka kimaendeleo kutokana na utamaduni wetu, ujuzi wetu wa siasazingine mbaIi mbali, na mazingira ya nehi yetu yaIivyo. Kutokana na hisi zetukatika mambo hayo mbaIi mbali ambayo yanafanya sehemu muhimu yaubinadamu wetu, ndipo tutakapoweza kutoa TAFSIRI iliyo sahihi kabisa;kwani lugha pekee ndiyo inayoweza kueleza bisi hizo katika mambo hayombaIi mbaIi. Kwa biyo, ni dhahiri kwamba mfasiri anayetumia lugha mbiliambazo kwake yeye ni za kigeni tupu, aghaIabu hutoa TAFSIRI zilizo sahibi.

3. Ni matumaini yetu kwamba cho chote wanachofanya Watanzania hapamakwao au katika ncbi za ng'ambo, lazima kiwe kwa manufaa ya Watanzaniawenyewe; na hasa kwa manufaa ya wale waisbio nyumbani, Tanzania. Nitegemeo letu pia kwamba wafanyakazi wa kigeni hapa ncbini katika kutekeleza

•A. S. Nichimbi is an assistant lecturer in the Department of Languages and Linguistics,99 University of Oar es Salaam.

Page 3: The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

wajibu wa kazi zao, lazima uwe katika kulifikia lengo hilo hilo, yaani "kwa UTAFlTIajili ya manufaa ya Watanzania wenyewe."

4. Lugha itumiwayo na Watanzania wengi hapa nehini katika utatuzi wavikwazo mbali mbali vinavyowakabili katika maisha yao ya kila siku ni KISW A-HILI ambacho msamiati wake ni mchanganyiko wa maneno mbali mbali yavijilugha vyote vya hapa nchini vyenye asili ya Kibantu. Zaidi ya hapo, kunamaneno mengine pia yaliyojiingiza katika KISW AHILI yenye asili ya lughaza Watawala wetu wa Kikoloni; kama vile maneno yenye asili ya Kiarabu,Kireno, Kifaransa, Kijerumani, Kiingereza, n.k. Sarufi ya Kiswahili ni yakibantu kitupu. Kwa Watanzania, KISWAHILI ni lugha yao ya Taifa tangumwaka 1968. Ingawaje uamuzi huu ulichelewa kutamkwa rasmi na serikaIi,ukweli ni kwamba, kwa muda wa kame nyingi, KISW AHILI kimejidhihirishakwa Watanzania wengi, kwamba ndiyo lugha pekee ambayo wameitumiakatika mawasiliano tangu enzi hizo mpaka leo katika maisha yao ya kila siku.

5. Tangu mwanzo wa kame hii ya ishirini, Watanzania tumeonyesha ari yakutaka kujifunza lugha za kigeni; sio zile tu za waliokuwa Watawala wetuwa Kikoloni, kama vile Kiarabu, Kijerumani na Kiingereza, bali pia Kifaransa,Kireno, Kirusi, na nyingi nyinginezo. Kwa hivi sasa, lugha rasmi za kigeniambazo Watanzania tunajifunza kusema na kuandika kwa ufasaha ni Kiinge-reza na Kifaransa;nazo hufundishwa katika mashule yetu ya hapa nehinikwa idhini ya serikaIi ya Wananchi wenyewe. Si ajabu kwamba serikali yaWananchi huenda ikaamua kuongeza ufundishaji wa lugha zingine za kigenikatika mashule yetu hapa nchini hapo baadaye, kama vile Kireno, Kichina,Kijerumani n.k.

6. Mara nyingi, Watanzania wanapoamua jambo fulani kwa njia ya serikaIiyao huwa wana sababu mahsusi. Sababu ya uamuzi wa serikali ya Tanzaniawa kukifanya Kiswahili kuwa Lugha ya Taifa ni kwamba lugha hii, kamailivyosemwa hapo awali, ni lugha ya mawasiliano baina ya Watanzania; zaidiya hayo, KiswahiIi ni sehemu muhimu ya utu wa Mtanzania kwani ndiyolugha pekee anayoweza kuitumia kueleza kinaganaga utamaduni wake,siasa yake na mazingira ya nehi yake huyo Mtanzania. Hivi leo, Kiswahilikinatumika katika kufundishia masomo mbali mbali ya Pani na Sayansi katikashule nyingi na vyuo vingi nehini.

Kiingereza na Kifaransa hufundishwa kama lugha za kigeni hapa nchini.Moja wapo ya sababu muhimu zilizopendekezwa na wananchi katika kuamuaufundishaji wa lugha mbili hizi za kigeni hapa nehini, ni kwamba lugha mbilihizi hutumiwa na watu wengi hapa duniani ambao kimaisha wanatuhusu sana;kwa mfano, tunaendelea kujifunza Kiingereza kwa sababu Waingereza badotunahusiana nao. Tunajifunza Kifaransa kwa sababu kuna Waafrika watumiaolugha ya Kifaransa na ambao tunahusiana nao sio katika Uafrika tu, bali piakatika uendeshaji wa vita vyetu vya kulikomboa bara letu la Afrika kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni. Kiwe Kiswahili au Kiingereza, Kifaransa au Kireno,n.k. tunajifunza lugha hizi illpawepo na mawasiliano ya hall ya juu baina yetusisi Waswahili na hao wenzetu watumiao lugha zingine wakati tunapokabitiwa 100

Page 4: The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

UTAFITI na tatizo Iinalotuhusu wote katika jumuia yetu. Mataifa ambayo huhusianakatika usawa wa matatizo yao lakini ambayo yanatofautiana katika lugha,hayana budi kuanzisha madarasa ya kuwafundisha wananchi wake lughazinazowahusu. Kwa mfano, iwapo sisi Watanzania tuna uhusiano wa ainafulani na Wachina, uhusiano ambao utasababisha pande zote mbili hizi kuonanamara kwa mara katika jitihada zetu za kutatua tatizo fulani linalotukabili,basi hapana budi serikali ya Watanzania iamue kuanzisha madarasa ya kuru-ndishia wananchi wake lugha ya KICHINA. Hali kadhalika, serikali ya Wachinaitabidi iamue kuanzisha madarasa ya kufundishia wananchi wake lugha yaWatanzaoia, yaani KISWAHILI. Iwapo nadharia kama hii ingedhihirishwakimatendo tangu miaka mingi iliyopita kati yetu sisi Watanzania na Wachina,TAFSIRI ambayo ingetumika wakati wa mikutano mbali mbali ya Wakuuwa serikali za mataifa hayo mawili katika jitihada zao za kutafuta jawabu lasuala linalowakabili ingekuwa imechukua sura kama ifuatayo:l. Kwa upande wa Wachina:

KISW AHIL! ) KICHINA(Lugha ya kigeni) (Lugha ya kwao)(Mchina aliye hodari katika Kiswahili na aliyefuzu utaalamu wa kutafsiriatahitajika kumtafsiria katika Kichina Mkuu wa serikali yake yale yase-mwayo kwa Kiswahili na Mkuu wa serikali ya Watanzania katika mku-tano huo).

II. Kwa upande wa Watanzania:KICHINA--- -.--------.-~KISW AHIL!(Lugha ya kigeni) (Lugha ya kwetu)(Mtanzania aliye hodari katika Kichina na aliyefuzu utaalamu wa kutafsiriatahitajika kumtafsiria katika Kiswahili Mkuu wa serikali yetu yaleyasemwayo kwa Kichina na Mkuu wa serikali ya Wachina katika mkutanohuo).

7. Ni dhahiri kwamba kama pangekuwa na haja, Mwalimu-Mtaalamu waKichina wa kutafsiri Kiswahili katika Kichina angeweza kuajiriwa na serikaliya Watanzania ili nasi pia tuupate utaalamu wa kuitoa tafsiri iliyo sahihi zaidiyenye sura kama ifuatavyo:Ill. KISW AHIL! ) KICHINA

(Lugha ya kwetu) (Lugha ya kigeni)Hali kadhalika, Mwalimu Mtaalamu wa Kitanzania wa kutafsiri Kichina

katika Kiswahili angeweza kuajiriwa na serikali ya Wachina ili nao pia wapateutaalamu wa kuitoa tafsiri iliyo sahibi zaidi yenye sura kama ifuatavyo:IV. KICHINA+-- --+KISWAHIL!

(Lugha ya kwao) (Lugha ya kwetu)Ndiyo kusema kwamba katika nchi bizi mbili tuogeshuhudia kuwepo kwamadarasa yanayofundisha wanaochi wake tafsiri zenye sura mbili, kamazifuatazo:(a) Kwa sisi Wataozania, sura za TAFSIRI zetu ziogekuwa kamazifuatazo:

101 V. KICHINA+-- --+KlSWAHIL!

Page 5: The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

- .-

i j ~- S , r. !~ c

.~ ,~

Qc - t- >.. -- .I! - 0 >..

J! >.. ~.c ~:;2 , ..., -Q - ~- , ii j.~ >.. ~

J! .c ~;; ..t-,

..J

UTAFITI

Page 6: The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

UTAFITI (b) Kwa wenzetu Waehina, sura za TAFSIRI zao zingekuwa kama zifua-zo:

VI. KISWAHILI~ ~KICHINA8. Ni lazima ikumbukwe daima kwamba MTU BINAFSI ana namna yake

pekee ya kufafanua jambo fulani katika jitihada yake ya kulitafsiri jambo hilokwa uwezo wake wote; TAIF A nalo pia, lina msimamo wake katika ufafanuziwa jambo fulani ili kulitafsiri jambo hilo kwa usahihi wa hali ya juu liwezavyo;JUMillA NDOGO YA MATAIFA HURU, nayo pia, ina msimamo wakemahsusi ambao huenda ukawa tofauti na ule wa MTU BINAFSI au wa TAIFAfulani katika ufafanuzi wa jambo fulani iIi kulitafsiri jambo hilo kwa usahihiwa hali ya juu iwezavyo. IIi pawepo na uwezekano wa kufafanua jambo fulanikatika jitihada ya kulitafsiri jambo hilo kwa usahihi "a hali ya juu iwezeka-navyo, anayehusika na ufafanuzi huo wa hali ya juu na hatimaye kuifikia tafsirii/iyo sahihi kabisa, hana budi kutumia ujuzi wake wote wa (i) utamaduni waTaifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira ya nehi yake yote. Kwahiyo, katika kupeana mawazo juu ya tatizo fulani linalokabili MAT AIF Amawili ambayo yamepania kumaliza tatizo hilo, lazima kila TAIF A, kwaupande wake, litumie lugha ya Wananchi wake katika kujieleza bila wasi wasikifikra kuliko kuwa katika hali ya juu. Twaweza kufafanua zaidi haya yaliyo-semwa hapo juu. Twaweza kufafanua zaidi hayo yaliyosemwa juu kwa msaadawa mehoro ufuatao:

9. Mabwana zetu Waingereza (na hata baadhi ya Watanzania wenzetuwaliolewa kasumba ya kusema na kuandika lugha ya Kiingereza) wangependakuona kwamba habari zinazosemwa au zilizoandikwa katika lugha zinginezote zitafsiriwe katika lugha ya Mabwana zetu Waingereza-yaani Kiingereza.Kwa hiyo, sura za utumiaji wa lugha mbali mbali katika Tanzania wangependaziwe kama zifuatazo:(i) Katika mawasiliano ya aina yo yote kati ya Watanzania wenyewe kwa

wenyewe, sura ya utumiaji wa lugha ingekuwa kama ifuatayo:Kiswahili-----------------+Kiingereza

auKiingereza~ ~ Kiingereza

(ii) Katika mawasiliano kati ya Watanzania na watu wa mataifa mengine,sura ya utumiaji wa lugha mbali mbali katika Tanzania ingekuwa kamaifuatayo:

Kireno

103

Kihispaniola

Kijerumani

Kifaransa

Kiarabu

Kiingereza

Page 7: The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

--~---

:=1":"1~,i \"" \

\1-

\

\

\\

N \"N\.!! N;;. N

"N ~ "~ ~~ ;;2:i -0

i: 1

,-----

--

- --I

I/

//

/~

/

..~...."~

I....=g

Page 8: The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

UTAFITl n.k.Jibu linalotoka kwa Watanzania kwenda kwa mataifa hayo wangependaliwe kwa Kiingereza.

Lakini tukiehunguza sana mpango huu wa matumizi ya lugha hizi, tutaonakwamba kuna mushkeli mahali fulani. Kwa mfano:(a) Ni dhahiri kwamba Watanzania hawajui Kifaransa, lakini Waingereza

wengi wanajua Kifaransa. Iwapo tatizo lilikuwa linawahusu Watanzaniana Wafaransa, basi Taifa la Tanzania lingelazimika kuajiri Wataalamuwa Kiingereza wa kutafsiri Kifaransa katika Kiingereza. Na iwapotatizo hilo lingekuwa Ia kudumu, basi haja ya kuwaajiri Wataa-lamu-Waingereza ingekuwa ya kudumu pia. Ni dhahiri kwamba, hiini njia mojawapo ya sisi wanyonge kujiona tunalazimika kumpa kaziMwingereza. Na Waingereza, kwa upande wao, wangeweza kutumiambinu kadha wa kadha ili kuudumisha unyonge wetu huo wa kujionakwamba tunalazimika kumuajiri kila mara yeye tu katika kazi za aina hii.Kwa hiyo iwapo Watanzania walio wengi wangependa kuarifiwa mamboyaliyozungumzwa kati ya Wakuu wa serikali ya Wafaransa na Wakuuwa serikali yetu, Wakuu wa serikali yetu ingewabidi wapate TAFSIRIya habari iliyoandikwa au iliyosemwa kwa Kifaransa katika Kiingerezakwanza, halafu apatikane Mtaalamu mwingine wa kutafsiri tafsiri hii yaKiingereza katika Kiswahili, lugha ambayo sasa itumike kuwaarifuWatanzania wote kwa njia ya magazeti na taarifa za habari za Idhaa yaRedio, Tanzania. Twaweza kuionyesha sura ya mfano huu wa matumizi yaIugha hapa Tanzania kama hii ifuatayo:

(b) Mwanaehuo Mtanzania wa Chuo Kikuu eha Dar es Salaam anayeamuakuehukua tafsiri inayohusu lugha za Kiingereza na Kifaransa-{Kiingereza~Kifaransa) yu katika mkondo wa kuzishughulikia lugha mbilizilizo ngeni kwake kwa kila hali. KITA MA DUNI hapana Jugha hata mojakati ya hizo mbili inayoweza kueleza kinaganaga hisi zetu; KIJIOGRAFIA,Iugha zote mbili hizi zimetoka mbali sana na Tanzania-yaani, Uingerezana Ufaransa. Kwa hiyo, mazingira ambamo lugha mbili hizi zimekomaani mageni pia kwa Mwanaehuo-Mtanzania. Mtindo wa SIASA ya Wai-ngereza na Wafaransa ni tofauti na huu wetu sisi Watanzania: Kiingerezana Kifaransa ni Iugha zilizokomazwa, na zinaendeIea kukomazwa zaidi,katika SIASA ya kibepari. Mwanaehuo-Mtanzania anakomazwa katikaSIASA ya Ujamaa na Kujitegemea iliyofanana sana na mila za kabila lake.

Lakini kwa upande mwingine, tafsiri hii hii inayohusu Iugha za Kiingerezana Kifaransa-(Kiingereza+- ---+Kifaransa) si ngeni kwa hali yoyote kwa Mwanaehuo-Mwingereza au Mwanaehuo-Mfaransa kwa sababuambazo ni dhahiri. Kwa hiyo, ukweli ni kwamba Mwanaehuo-Mtanzaniawa Chuo Kikuu eha Dar es Salaam anapotahiniwa juu ya tafsiri ya habariinayohusu lugha ya Kiingereza na Kifaransa, itambidi ajitahidi mara dufuzaidi kuIiko Mwanaehuo-Mwingereza za wa Chuo Kikuu eha Landani au

105 Mwanachuo-Mfaransa wa Chuo Kikuu eha Parisi kama nao hao wange

Page 9: The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

tahimiwa juu ya tafsiri ya habari hiyo ili matokeo yao ya mwisho, baada ya UTAFmmasahihisho ya mitihani yao, yastahili, kama alama ya asili-mia arobaini(40%). Kwa Mwanachuo-Mwingereza au Mwanachuo-Mfaransa, tafsiri yaaina hii, yaani-Kiingereza~ -Kifaransa, ni ya kawaida kwake;kwani lugha mojawapo ya hizo mbili, kwake ni ya kuzaliwa nayo. Kwa hiyo,alikuwa amefanya mtihani wa kutafsiri lugha ya kigeni katika lugha ya kwake.Na apewapo alama ya asili-mia arobaini (40%) kwa kazi yake, walimwenguwake watamweka mahali pake katika kusifiwa; yaani, kama ni HODARIau HODARI WA WASTANI au HAFA! kwa kutafsiri. Kwa kawaida ya VyuoVikuu mbali mbali vya ulimwengu, alama ya asili-mia arobaini (4O%=C)inastahili sifa hii: HODARI WA WASTANI.

Mwanachuo- Mtanzania aliyepata alama ya asili-mia arobaini (40 %),atawekwa mahali gani kisifa na walimwengu wake? Akumbuke kwambamtahiniwa huyu ilimbidi ajifunze kwanza lugha mbili hizi, yaani Kiingerezana Kifaransa, kabla ya kujifunza isimu yake na hatimaye kuitumia elimu hiyokatika majaribio ya kiutalaamu, kama mitihani hii ya kutafsiri. Mtahiniwamwenzake Mwanachuo-Mwingereza au Mwanachuo-Mfaransa hakuwa nahaja ya kujifunza kwanza lugha yake hapo chuoni pake kwa sababu lugha hiyoamezaliwa nayo; yeye alianza kujifunza moja kwa moja isimu ya lugha yakena utaalamu wa kuitafsiri lugha yake katika lugha ya kigeni kwa mudawake wote alioishi hapo ehuoni pake. Mara nyingi Vyuo Vikuu mbalimbali vya ulimwengu vimetumia wembe ule ule-yaani a1ama ya asili-miaarobaini (4O%=C) istahili sifa ya: HODARI WA WASTANI, Uamuzi huu nisawa: lakini matokeo yake ni mabaya kwa upande wa Mwanachuo-Mtanzania.Ukweli ni kwamba kwa Mwanachuo-Mtanzania anayestahili alama ya asili-miaarobaini (4O%=C) ana aki/i zaidi kuliko Mwanachuo-Mwingereza au Mwana-ehuo-Mfaransa anayestahili alama ya asili-mia arobaini (40%=C) katikamtihani huo wa kutafsiri Kiingereza~Kifaransa. Yaani, Mwanaehuo-Mtanzania aliyestahili kupata alama ya asili-mia arobaini (40 %=C) ingebidialingane na Mwanachuo-Mwingereza au Mwanaehuo-Mfaransa aliyestahilikupata a1ama ya asili-mia, kama hamsini na tanG (55%=B). Hii ina maanakwambajuhudi ambazo tungetegemea Mwaoaehuo-Mtanzania (40%) kuzionye-sha katika utekelezaji wa wajibu wake wa kazi za Wizara au Shirika lililomwajiriingeliogana na i1ejuhudiya Mwanachuo-Mwingereza au Mwanachuo-Mfaransa(55%).

Lakini kwa sababu ya unyonge wetu, tunalazimika kumtukuza Mwanaehuo-Mwingereza (4O%=C) au Mwanachuo-Mfaransa (4O%=C) kwa kumtunukiasifa ya Mwanachuo-Mtanzania wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayestahilisifa ya a1ama ya asili-mia (55 %=), yaani, HODARI.

Unyonge huu wa TAIF A la Watanzania kujiona kwamba wanalazimikakumwajiri Mwingereza, eti kwa sababu ya ujuzi wa lugha yake ya Kiingerezana nyinginezo za huko Ulaya, kutufanyia kazi ya kutafsiri habari yo yoteitokapo papa hapa nchini au nehi za nje, waweza kupigwa vita, na. unyonp 106

Page 10: The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

UTAFITI wetu huo kutoweka kabisa katika TAIFA letu, iwapo tu, tukikubaliana kushiri-kiana katika utekelezaji wa mambo haya yafuatayo:I. Sisi Watanzania tukatae kuamini kwamba ni lugha ya Kiingereza tu

inayoweza kueleza utamaduni, siasa na mazingira ya binadamu koteulimwenguni na kwamba lugha zingine, lugha yetu tukufu ya Kiswahiliikiwa mojawapo haziwezi kufanya hivyo.

II. Sisi Watanzania tujenge imani kwamba lugha yo yote ya binadamu katikataifa lake imejikamilisha yenyewe katika kueleza vilivyo utamaduni, siasana mazingira ya binadamu wa taifa hilo kuliko lugha nyingine yo yoteya bandia.

III. TANU na vyombo vyake, vizidi kutoa uamuzi wa busara wa kimapinduzikatika jitihada yake ya kukomboa wananchi wake. Kwa mfano, izidikutoa uamuzi wa kutumia lugha ya Kiswahili katika ufundishaji wa masomoyote ya shule za hapa nchini, kufuatana na hali ilivyo katika shule hizo.

IV. Sisi Watanzania tusiwe chanzo cha kuwepo kwa hali ambayo inawezakusababisha uzorotaji katika kutekeleza jambo Namba III hapo juu.IIi uepukane na sifa mbaya kama hii, itakubidi, na hasa ukiwa kamaKiongozi wa wenzako hapo kazini au hapo uishipo, kuwahoji wenzakojuu ya njia mbali mbali ambazo zingesaidia kutatua vikwazo vya hapokazini au kijijini penu.

V. Sisi Watanzania tuwe macho kugundua hila zo zote za wageni za kutakakuunyonya utaalamu wetu katika utamaduni wetu, siasa na mazingirayetu.

VI. Kutokana na yale tunayoyashuhudia yanatokea mwaka hata mwaka katikataifa letu; sisi Watanzania tunaamini kwamba taifa letu linaendelea.Tunaposema kwamba taifa linaendelea, tunamaanisha kwamba binadamuwa taifa hili wanaendelea; na kuendelea kwa binadamu ni kuendeleakwa utamaduni wake, siasa yake na mazingira yake pamoja. Lugha pekeeya binadamu wa taifa 10 lote ndiyo itakayoweza kueleza maendeleo hayokatika daraja mbali mbali zilizotajwa hapo juu. Kwa sisi Watanzania,lugha iliyo na jukumu kama hili ni Kiswahili.

VII. Sisi Watanzania, tujenge moyo wa kutafutatafuta msamiati wa kitaalamukatika mambo mbali mbali yanayotuhusu. Tufundishane msamiati huoili tuutumie vilivyo katika mawasiliano yanayotuhusu.

10. Kwa kuwa KlSWAHILI ndiyo lugha ya Taifa la Watanzania wanaoende-lea mwaka hata mwaka kiutamaduni, kisiasa na kimazingira, ninapenda suraza matumizi ya lugha hapa nchini ziwe kama zifuatazo:(i) Katika mawasiliano kati ya Watanzania wenyewe kwa wenyewe:

Kiswahili +- -Kiswahili.(ii) Katika mawasiliano kati ya Taifa]a Watanzania na Mataifa mengine:

Hapana budi tukumbuke pia, kwamba iwapo Watanzania tutatilia mkazo107 zaidi katika TAFSIRI zinazohusu KISWAHILI na lugha yo yote yenye asili

Page 11: The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

UTAFITI

______________ -+_Kiswahili

______________ -_Kiswahili

_____________ -+_Kiswahili

_____________ -+_,Kiswahili

-=======================--,:,-,:,-,:,-,:,-':'-+_,Kiswahili

______________ -+._Kiswahili

______________ -+_Kiswahili

_____________ -+_Kiswahili

______________ -+_Kiswahili

___________ .__ -'>_Kiswahili

_____________ -+_Kiswahili

Lugha ya Kigeni +-

Kwa mfano:

(a) Kikemba +-

(b) Kiingereza +-

(c) Kiarabu +-

(d) Kilingala +-

(e) Kifaransa +-

(f) Kiwolofu +-

(g) Kiurdu +-

(h) Kihausa +-

(i) Kireno +-

U) Kichina +-

ya Mwafrika, tutakuwa tunauendeleza sio utaalamu wetu katika kutafsiri tu,bali pia utamaduni wa Mwafrika, siasa ya Mwafrika, mazingira ya Mwafrikana hasa lugha ya Mwafrika.

FOOTNOTESI. ambapo: (t, m, a, )=L12. (t, m',a', )L=23. Kutokana na yaliyomo katika kitabu kiitwa.cho: "Language- Teaching Abstracts",

Volume 7, No.3, July, 1974).4. Neno hili Mabwana (wengi) Bwana (mmoja), linaonyesha kwamba kati ya wale

wanaolitumia, mmoja wao ni mtwana. Siku hizi, Watanzania hutumia neno Ndugu.

t08

Page 12: The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

SUMMARY

THE RATIONALE OF TRANSLATION IN TANZANIA

This article is purely the author's point of view with regard to the useof languages in the day~to-day official duties of a Tanzanian residing in hishome country. Apart from Kiswahili, his national language, the Tanzanianofficial is faced with another problem: that of having to consult an expa-triate officer who does not know Kiswahili on matters of grea.t nationalin,terest. In this matter he has at least one alternaltive: the use of the Englishlanguage. But Tanzania has invited so many expatriate officers to carry outdifferent national projects. Not all of these expatriate officers are English-speaking; we have French, Germans, Scandinavians, Russians, Chinese, etc.,who would like to express their feelings to Tanzanian nationals in theirrespectilVe native languages.

Is ~t not true that the use of a native language by its native speakeris an indication of what this native speaker really intends to convey to thepublic concerned? On the other hand is it not true that the use of a nativelanguage by a non-native speaker may not be an indication of what thisnon-native speaker really wants to convey to his public? The non-Englishexpatriate officers and surely the Tanzanian nationals themselves, may bevictims of this second category. Every time Tanzanians have expressed theirfeelings about a certain problem by using the English language to Englishnationals, we have never been fully understood by the na,tive Englishspeakers. As a result, the necessary and immediate action that ought to havebeen taken thereafter as required by the Tanzanian nationals is often delayedfor years! The point has to be clarified again and again for the simple reasonthat the former wasn't clear enough!

This article suggests only one of the possible ways by which Tanzaniaand her friends can overcomethio; crucial problem of being misunderstoodby one or the other; the adoption of the "Rationa:1e of Translation in Tan-zania". This is based on the assumption that if two friendly nations speakdifferent native languages, it is the duty of both nations to learn the nativelanguage of the other, so that in times of common crisis, what one nationsays about it in its native language is clearly understood by the other friendlynation. This means getting down to translation work by both the nationsconcerned.

As stated earlier, the national language of Tanzania is Kiswahili. The"Rationale of Translation in Tanzania" should, therefore, be from a foreignlanguage into Kiswahili and vice versa, for instance: English ~ Kiswahili

109 French~Kiswahili; Chinese ~Kiswahili; Wolo~Kiswahili Hausa~Kiswahili

Page 13: The African e-Journals Project has digitized full text of articles ...archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti...Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira

etc. This type of translation should be encouraged in all our learning institu- UTAFITItions including our places of work. It would automatically mean implement-ing the TAND and Government decision on the use of Kiswahili in thecountry which was pronounced in 1968.

The type of translation whereby two foreign languages are involved is notadViisable in Tanzania for the purpose of large-scale nationaJ. interests. Ittrains nationals to think and reason entirely in foreign languages about ma1ltersof our own national cUl'ture. Not only is the information distorted andmisunderstood when using these foreign languages to describe our owncmture. but also practicaJly not one natiooal of present Tanzania would takeheed of the information stated in the foreign languages.

"Ensemble il nous mut cultiver Ie jardin mnza.nien! Le Kiswahiii estit la fois un prestige et une identire des indigenes du pays."

1.10