16

U T A N G U L I Z I

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: U T A N G U L I Z I
Page 2: U T A N G U L I Z I

1

Mwaka 2020 unatimiza maadhimisho ya miaka ishirinina mitano ya Kongamano la Nne Duniani la Wanawakena utumizi wa Azimio la Beijing na Jukwaa la Uamsho(1995). Kabla ya hapo, Mkutano wa 1 wa shirika laUmoja wa Mataifa (UN) Duniani kuhusu Wanawakeulifanyika huko Mexico mwaka wa 1975, katika kipindicha Mwaka wa Wanawake wa Umoja wa AfrikaKimataifa. Mkutano huu ulikuwa wa kwanza kwa asiliyake kulenga mahsusi masuala ya wanawake na uliwekaalama ya mageuzi katika utengenezaji wa sera.

Shirika la Umoja wa Afrika liliitangaza miaka ya 1976-1985 kuwa Mlongo wa Wanawake, ambao katika huoMkutano wa 2 Kimataifa uliohusu Wanawake ulifanyikahuko Copenhagen, Denmark mwaka wa 1980, naulijikita zaidi katika kuimarisha mitandao ya wanawake.Mkutano wa 3 ulifanyika mjini Nairobi, Kenya mwakawa 1985 na ulikamilisha Mlongo wa Umoja wa Arikakwa ajili ya Wanawake, na kutathmini maendeleoyaliyopatikana na utumizi wa “Mikakati ya KusongaMbele kwa ajili ya Maendeleo ya Wanawake”. Mkutanohuu ulikuwa msingi wa majadiliano ya Mkutano wa 4wa Kimataifa kuhusu Wanawake uliofanyika jijiniBeijing na kuacha mwongozo kuhusiana nauwezeshwaji wa wanawake na usawa wa jinsia.

2020 pia inatimiza maadhimisho ya miaka 20 ya Azimiola 1325 (S/RES/1325) juu ya wanawake, amani nausalama, lililothibitisha tena kwa mara nyingineumuhimu wa wanawake katika uzuizi wa migogoro nakusisitiza umuhimu wa ushiriki sawa na ujumuishwajikikamilifu katika jitihada zote za kudumisha na kukuzaamani na usalama.

Kwa bahati mbaya, licha ya hatua iliyofikiwa, hakunanchi iliyoweza kufikia usawa wa kijinsia. Kwakulizingatia hili, taasisi za jamii pamoja na Wanawakewa Umoja wa Afrika wamezindua kampeni ya: “Kizazicha Usawa: Utambuzi wa haki za wanawake kwa ajili yaUsawa siku za mbeleni”, iliyolenga kukutanisha vizazivya wanaharakati wa haki za wanawake kushughulikiasuala hili la uwezeshwaji wa wanawake ambalo badohalijakamilika.

UTANGULIZI

1

MADAI10

Page 3: U T A N G U L I Z I

Ndani ya ngazi ya bara la Afrika; katika Mkutano Usiowa Kawaida wa Mawaziri wa Jinsia na Masuala yaWanawake huko Maseru, Lesotho Desemba 2008,Shirika la Umoja wa Afrika (AU) Mawaziri wa Jinsia naMasuala ya Wanawake walilitaka Shirika la Umoja waAfrika kutangaza miaka ya 2010-2020 kuwa Mlongo waWanawake wa Afrika uliopitishwa na Mkutano waDesemba. 487 (XIX) chini ya Kichwa cha Mada: MbinuMsingi za Usawa wa Jinsia na Uwezeshwaji waWanawake.

Jitihada hii madhubuti imeingizwa katika azimio lamlongo mpya (2020-2030) wa Ujumuishwaji waWanawake katika Masuala ya Fedha na Uchumi,lililowekwa na viongozi wa Afrika mwezi Februarimwaka wa 2020. Azimio hili ni matokeo ya dhamira yaviongozi wa Afrika kuimarisha hatua za ujumuishwajiendelevu wa kijinsia katika maendeleo endelevu yangazi za kitaifa, kikanda na kibara. 2020 pia imetimizamaudhui ya mwaka ya Umoja wa Afrika ya“Unyamazishaji wa Bunduki: Utengenezaji wa MazingiraRafiki kwa ajili ya Maendeleo ya Afrika” yaliyoamuliwana Baraza la Watendaji kipindi cha Kilele chaUshirikiano wa Umoja wa Afrika huko Niamey, Niger,Julai 2019 na kutumika kipindi cha 33 cha Kilele chaUmoja wa Afrika, jijini Addis Ababa Februari 2020.

Katika kusheherekea hatua hizi, mifumo ya vijana nifunguo wa kuimarisha haki za vijana zinazojumuisha, ilazisizozuiwa tu katika, “Uwekezaji katika Vijana kwa ajiliya Kunufaika katika Mgao wa Idadi ya Watu”, maudhuiya mwaka 2017 ya Umoja wa Ulaya, Kampeni ya Vijanakatika Unyamazishaji wa Bunduki mwaka 2020, Mfumowa Vijana katika ngazi ya Bara, Amani na Usalama, naAzimio la Vijana wa Afrika katika KunyamazishaBunduki.

Uzinduzi wa kampeni hii umesababisha utengenezwajiwa Jukwaa la Kizazi cha Usawa (GEF) ambalolitaendesha mkutano wa kimataifa kwa ajili ya usawa wawanawake, utakaoitishwa na Wanawake wa Umoja waMataifa na kusimamiwa na Ufaransa pamoja na Mexico,kwa kushirikiana na asasi za kiraia. Kutokana na mlipukowa janga la COVID-19, GEF imehairishwa hadi 2021.Mfumo wa utekelezaji wa GEF uliahidi kujengwa katikamsingi wa kanuni za ujumuishaji, na mkakati wa kwanziachini kuelekea juu, ulioundwa katika msingi wakujumuisha nguvu kwa pamoja, katika ushirikiano wakimataifa, wenye wadau wengi, uliolenga kuhamasishaserikali, jamii, taasisi za kimataifa na sekta binafsi.

2

HATUPENDEKEZITUNADAI

Page 4: U T A N G U L I Z I

Makala ya 23 ya Katiba ya Vijana wa Afrika, inazungumzia mahsusi Wasichana na Mabinti, kwa kuitishaulinzi wa wasichana na mabinti dhidi ya unyonywaji wa kiuchumi na ufanyaji wa kazi hatarishi,zinazowaondoa kutoka mashuleni ama zinazoweza kudhuru afya yao ya kiakili na kimwili. Chapisho laSauti صوتي la Umoja wa Afrika limeelezea zaidi changamoto hizi kutoka kwenye nyanja za kiuchumi,kitamaduni na kisiasa hadi katika utengwaji wa mabinti katika sera za vijana na wanawake, sekta namifumo, unaopelekea changamoto zao mahsusi kutoshughulikiwa. Janga la sasa la COVID-19limezidisha changamoto hizi zinazowakumba mabinti; kwanzia kwenye suala la ugumu wa kiuchumihadi katika ukatishwaji wa shule na matumizi mabaya ya vipindi vya kujifungia ndani kamailivyoainishwa katika chapisho la sera ya Uongozi wa Vijana Afrika "Taarifa Halisi & Takwimu zaChangamoto za Uwakala wa Vijana wa Afrika na Mpango wa Urejeshi baada ya COVID-19".

Mchakato wa kutengeneza na kuhamasisha ilani hii umezingatia pia mapitio ya mabinti, jambolinalohakikisha kuwa ilani hii itaweza kumilikiwa na wigo mpana wa kikatiba. Hivyo mabinti huwezeshwakutumia sauti zao kuleta vijana wengi zaidi katika harakati hii. Washiriki wa kanda tano za majadilianowametokea nchi 45, ambazo ni Algeria, Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Kameruni, Chad, CôteD’Ivoire, Visiwa vya Komoro, Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Djibouti, Eswatini, Misri,Ethiopia, Eritrea, Ghana, Gambia, Kenya, Liberia, Libya, Lesotho, Malawi, Mozambique, Morocco,Mauritania, Madagaska, Mauritius, Namibia, Nigeria, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu yaSahrawi, Afrika Kusini, Sierra Leone, Senegal, Somalia, Sudani Kusini, Sudani, Tanzania, Tunisia, Togo,Uganda, Zimbabwe, na Zambia.

Hivyo, ilani hii hutoa jukwaa la madai ya pamoja ya kufikia usawa wa kijinsia pamoja na Ajenda ya 2063na Ajenda ya 2030. Huwezesha mabinti kueleza masuala yao na kulinda dhamira angavu na ya wazi,Jukwaa la Kizazi cha Usawa na Uongozi wa Utendaji wa pamoja, ambazo huweka alama katika serazilizopo, michakato ya kitaasisi, na mikakati na programu za ujumla. Madai haya yatahakikisha kwambawasichana na mabinti wanaweza kushiriki kiamilifu, kwa usawa na kwa ufanisi, kwenye ngazi zote zakijamii, kielimu, kisiasa, kitamaduni, maisha ya kiraia na uongozi pamoja na jitihada za kisayansi.

uongozi ujumuishao vizazimbalimbali, na mahojianomiongoni mwa wanawake,wadau wa Mashirika ya Umojawa Afika na Umoja wa Mataifa

mabinti katika kanda tofauti tofautikushirikisha mapendekezo yao nakushirikishwa katika ngazi za kijamii,kitaifa, kikanda na kibara

ilani hii ya Mabinti waAfrika yenye madai 10ya utendaji

KUZA WEZESHA HAMASISHA

3

Hivyo, ilani hii ya Mabinti wa Afrika ni nyaraka ya kisiasa inayoainisha masuala muhimu yahusuyomabinti wa Afrika na kuweka madai ya kushughulikia masuala hayo. Ilani hii ni matokeo ya Mabaraza 5ya Kikanda ya Mabinti wa Afrika Beijing+25 yaliyojumuisha zaidi ya washiriki 1500 na zaidi yawanachama 30 wenye malengo ya FEM:

Page 5: U T A N G U L I Z I

Imetosha!

Usawa katika kazi, ajira zinazoheshimika, kaziyenye ujira, mafunzo ya kazi yenye ujira namishahara sawa katika ujira wa lisaa, kwenye ajiraza nusu muda na ajira za muda kamili, katika halizinazofanana. Kwanini tulazimike kuweka juhudimara mbili ili tu kuonyesha kwamba tunaweza?Malipo pungufu kwa wanawake yanamaanishakuwa sisi tuna ‘thamani pungufu’

Utekelezaji wa haki na adhima kwa mabintiwaliopo ndani ya sekta nyeti kama vile kazi zakutoa huduma ya uangalizi, kazi za usafi, tasniaya utumishi na malezi, kazi za kihisia na kazi zandani

Utambuzi wa mchango wa mabinti katika ujumlawake, ndani ya sehemu ya kazi na ndani yautengenezaji wa sera, kulingana na ujuzi navipaji vyetu, na si kulingana na jinsia, umri auwadhifa wa ndoa. Tuna ustadi na tunawezakulingana na adili ya bidii zetu, ustahili, uerevuwa kihisia na uongozi wa wanawake

Uhakikisho wa haki za mabinti katika upewajiwa malipo ya likizo ya baada ya kujifungua, bilakubaguliwa, kuwekewa vikwazo au kufutwa kazi

Sisi, Mabinti wa Afrika, tunadai:

Hakuna tena kufanya kazi zisizo na malipona kutoa huduma bure

DAI LA HAKIYA KIUCHUMI

4

Ukadirifu muhimu wa athari ya makazi ya mudaau yasiyo salama, misaada ya kiserikali isiyotoshelevu ama yenye muenendo mbovu,kwenye uwezo wa mabinti wa kutafuta nakudumu katika kazi, pamoja na hatua madhubutiza kuhamasisha ajira zenye kipato kizuri nazinazoheshimika kwa mabinti.

KAZI YENYEMALIPO

Page 6: U T A N G U L I Z I

Imetosha!

■ Upigwaji marufuku wa janga la Ukatili wa Kijinsiakatika miundo yake yote hasa katika migogoro,kuhamishwa makazi na masuala ya ukatili wa binadamuyanayojumuisha uuwaji wa wanawake, ubakaji,mienendo ya uharibifu, ukeketwaji, ndoa za utotoni nandoa zisizo za hiari, udhia wa kingono, kutumiwa vibayakingono, matumizi mabaya kijamii na kiuchumi, uuzaji wabinadamu na miundo mingine yote ya ukatili.

■ Utekelezaji wa sera za ziada ili kuzuia ukatili wakingono na kijamii, pamoja na kuhakikisha kwamba kesiza unyanyasaji, ukatili na vitendo vibaya dhidi yawanawake zinatambuliwa, zinachunguzwa na wahalifukuhukumiwa.

■Utoaji wa msaada wa kisheria, kimwili na kisaikolojia,makazi na huduma za kitaalamu kwa mabinti waliopitiavitendo vibaya vya kijamii na miundo mingine ya ukatili

DAI LA KUPIGA MARUFUKUUKATILI WA KIJINSIA

■ Ugavi wa fedha za kusaidia utafiti na uvumbuzi wavijana kwa ajili ya kupambana na suala la Ukatili waKijinsia

Jamii lazima iwekwe huru dhidi ya Ukatili wa Kijinsia

Sisi, Mabinti wa Afrika, tunadai:

5

HAPANA! NDOA ZAKUSHURUTISHWA

Page 7: U T A N G U L I Z I

4

Imetosha!

■ Uanzishi wa mikakati ya kisheria inayoondoamiundo yote ya ubaguzi dhidi ya wasichana namabinti kwa msingi wa jinsia yao, hadhi ya ndoa, rangiya ngozi, uraia na urithi, au umri, ili kuhakikisha hakizao za kibinadamu na msingi wa uhuru

Sisi, Mabinti wa Afrika, tunadai:

■ Upatikanaji wa haki na unaoweza kumudiwa wabidhaa, huduma za umma na fursa kwa mabintiwaishio vijijini, mabinti wenye ulemavu, mabintiwanaotafuta hifadhi, mabinti wakimbizi na mabintiwahamiaji na wasio na makazi. Huduma hizizinajumuisha upatikanaji wa ulinzi wa kijamii, maji yakunywa, haki za urithi, chakula na lishe, makazi, uleziwa watoto, miongoni mwa haki na huduma nyingine

■ Uondoaji wa miundo yote ya ubaguzi dhidi yamabinti hasa ule unaoathiri mabinti maskini nawengine wote waliopo katika mazingira hatarishi,jambo linaloweza kusababisha kuondelewa kwaokatika ufanyaji maamuzi

■ Ufikivu sawa katika umiliki wa ardhi nakuhakikisha uhuru wa kiuchumi na uwezeshwajibinafsi. Mabinti wanaopigana dhidi ya sheria, mila namienendo inayowakandamiza wanawake, katikausimamizi wa urithi, na ile inayoingilia ufikivu sawawa wanawake kwenye umiliki wa ardhi na rasilimaliasilia

Lazima tukomeshe ubaguzi wa kijinsia

6

■ Utoaji wa mifumo endelevu ya kifedha kwamabinti wanaotafuta hifadhi na mabinti wakimbizi ilikuhakikisha riziki yao na ujumuishwaji mpya, pamojana usalama wao na ustawi

DAI LA KUKOMESHA UBAGUZI WA KIJINSIA

UFIKIVU WAHUDUMA

KWA MABINTIWENYE

ULEMAVU

Page 8: U T A N G U L I Z I

DAI LA UPATIKANAJIWA HAKI NA ULINZI

Imetosha!

■ Mapitio, marekebisho au maboresho ya sheriazinazowakandamiza mabinti ili kuhakikisha kwambakunakuwepo usawa katika uso wa sheria na ufikivusawa wa haki. Hili hujumuisha, ila si tu, ulinzi wa hakiza mabinti hasa katika vipindi vya mapiganoyatumiayo silaha, majanga ya kiasili na upotevu wamakazi. Ni wajibu wa jamii ya kimataifakushughulikia visababishi vikuu vya migogoro hiiinayoathiri sana mabinti waliopo kwenye mazingirahatarishi

■ Utoaji wa taarifa kuhusiana na haki za mabinti nawasichana katika namna inayoweza kufikika, yauwazi na iliyo katika miundo na lugha inayoeleweka,pamoja na michakato na zana angavu na fanisi zakudai haki hizo ili kuhakikisha kwamba zinatekelezwakikamilifu

Sisi, Mabinti wa Afrika, tunadai:

■ Utoaji wa elimu kupitia mafunzo, kampeni naprogramu za uamsho, kwa ajili ya wasichana nawavulana, familia, jamii na mfumo mzima wa uongoziwa kiserikali katika kulinda haki za mabinti nawasichana

■ Ugavi wa kifedha ili kuimarisha uwezo wa mabintikupitia ufikivu ulioboreshwa wa taarifa na usaidiziwa kisheria pasipo kujali hali na vizingiti vyao vyakijamii na uchumi

Usawa & Haki mbele ya Sheria

7

UFIKIVU WATAARIFA &

USAIDIZI WAKISHERIA

Page 9: U T A N G U L I Z I

Imetosha!

DAI LA HAKI ZA AFYA YAKIJINSIA NA UZAZI

■ Utambulishi na utekelezaji wa kozi na programufanisi za Elimu ya Kina ya Jinsia mashuleni ilikuelimisha mabinti juu ya afya zao na namnamaamuzi yao yanaweza kuathiri ustawi wao na wawatu wengine. Kama mabinti, tuna haki ya kuongozamiili yetu wenyewe, kufanya maamuzi kwa uhuru nakwa kuwajibika, kuhusiana na masualayanayohusiana na uhuru wetu wa kijinsia, ubaguzi naukatili

■ Upatikanaji wa haki na huduma muhimu zakimataifa za afya ya kijinsia na uzazi hasa kwa walewaliopo maeneo ya vijijini, ijumuishayo ushaurinasaha kwa mabinti kuhusiana na uhuru wao wakijinsia na uzazi. Afya yetu ya uzazi si jambo la aibu,usumbufu, au sababu ya kubaguliwa.

■ Uondoaji wa kodi katika bidhaa za hedhi,utekelezaji wa sera endelevu za vipindi vya hedhikwenye maeneo yote ya kazi, na utoaji wa pedi burena zana za usafi ndani ya shule zote. Ni jambolisilokubalika kabisa mwaka 2020 kwamba wasichanawaache shule au kupoteza ajira zao kwa sababu tu yahedhi zao

Sisi, Mabinti wa Afrika, tunadai:

■ Kutoa misaada ya kifedha kwa taasisi zinazotoamuongozo wa taarifa na programu za elimu ya kina yamasuala nyeti ya kijinsia, elimu ya afya ya jinsia nauzazi, na uwezeshaji wa ustawi wa mabinti

Miili Yetu, Chaguzi Zetu!

8

ELIMU YAJINSIA

Page 10: U T A N G U L I Z I

Imetosha!

Sisi, Mabinti ya Afrika, tunadai:

■ Utoaji wa huduma za afya ya akili zinazoelewaathari ya ubaguzi wa kijinsia, chuki na unyanyasajiunaosababisha changamoto kubwa zinazoathiri afyaya kiakili ya mabinti

■ Utengenezaji na utekelezaji wa sera, huduma namienendo inayoshughulikia changamoto za afya yakiakili, zilizotengenezwa kwa kuzingatia mapito halisiya mabinti na kufaa mahitaji yao binafsi

■ Utekelezaji wa mabadilisho ya kimfumo nauundwaji mpya wa mifumo ili kuboresha uwasilishwajiwa huduma inayohusiana na afya ya kiakili, ushaurinasaha, msaada wa kutatua mfadhaiko, kwa kutumiamkakati makini, unaozingatia jinsia, na kulenga vijana

■ Uondoaji wa vizingiti vyote vinavyoweza kuwa naathari mbaya katika ujumuishwaji mkamilifu wa vijanawenye changamoto za kiakili na kimwili ndani ya jamii,ikiwa ni pamoja na utoaji wa miundombinu na hudumasahihi za kuwezesha ujumuishwaji na upatikanaji sawawa fursa, bila kuwepo kwa ubaguzi wowote

Huduma ya afya ya kiakili shartiipatikane kote na kwa usalama

9

■ Fedha kwa ajili ya huduma endelevu na ya usawa yaafya ya kiakili. Matatizo ya kiakili yanachangia sehemukubwa na inayokua ya mzigo wa magonjwa wa barahili, hatahivyo bado hubaki kupewa kipaumbele kidogosana katika uwezeshwaji wa umma kifedha ndani yamifumo ya afya

DAI LA AFYA YAAKILI NA USTAWI

UGAVI WA FEDHA KATIKAAFYA YA AKILI

Page 11: U T A N G U L I Z I

Imetosha!

DAI LA ELIMU JUMUISHI, YENYEUSAWA NA YENYE UBORA

■ Uondolewaji wa vizingiti katika elimu ya mabintina wasichana, vinavyojumuisha umaskini, ada zashule, usafiri, umbali na usalama wa shule, ndoa zautotoni na ushurutishwaji wa ndoa, mimba zautotoni na zisizotarajiwa, ukosefu wa nyenzo zausafi na za uhifadhi wa hedhi, upendeleo wa kijinsiana dhana potofu kiujumla, nyenzo za kujifunzia namichakato ya elimu, uonevu, vitendo ovu na ukatilimashuleni, vyuo vya awali na vyuo vikuu

Sisi, Mabinti wa Afrika, tunadai:

■ Kuongezeka kwa mgao wa bajeti ya kitaifakwenye elimu (na kupunguza ile ya matumizi yakijeshi) ili kuchochea mifumo ya mafunzo yakieletroniki katika uwasilishaji wa elimu yenye ubora,jumuishi na itolewayo bure, ya awali, msingi,sekondari na elimu ya juu hasa kwa mabinti nawasichana waliopo maeneo ya mashambani

■ Taasisi zinazotoa elimu kwa wavulana kuhusukuwaheshimu wasichana na kuenenda nao kwausawa, huku wakielewa asili ya mfumo dume yenyemahusiano yasiyo na usawa katika uongozi, wajibuna dhana za kijinsia

■ Uhakikisho wa upatikanaji na ufikivu wa usawakatika uhitimu wa shule za ufundi, sekondari na elimuya juu, ili kutatua kwa ufanisi ukosefu wa usawauliopo baina ya vijana wa kiume na wa kike katikataaluma fulani

Elimu ni haki, si pendeleo

10

■ Uwezeshwaji wa mabinti wanaotoka kwenye jamiihatarishi na zilizotengwa, mazingira ya migogoro na yamisaada ya kibinadamu, na kuwapatia nafasi sawa zakujiunga na vyuo vikuu bora kupitia huduma yaufadhili hasa katika Sayansi, Teknolojia, Uhandisi naHisabati

ELIMU NI HAKISIO PENDELEO

Page 12: U T A N G U L I Z I

Imetosha!

DAI LA HAKI YA KIDIGITALISisi, Mabinti wa Afrika, tunadai:

■ Uongezaji wa kasi katika mageuzi ya kidigitali hasakwa mabinti waliopo vijijini na maeneo hatarishi, ikiwani pamoja na upatikanaji rahisi wa intaneti, inayowezakumudiwa na kutegemeka, pamoja na uwekezajikatika miundombinu na teknolojia zinazowezeshauchumi wa kidigitali na fursa mpya kwa mabinti

■ Upigwaji marufuku wa vizuizi vilivyopitiliza kiasikatika uhuru wa intaneti na kufungwa kwa intaneti

■ Demokrasia katika Nyanja ya kidigitali ili kuruhusuuchangizi na ushiriki sawa kwani mabinti wengihuachwa nyuma katika mageuzi ya kidigitali

■ Ulinzi dhidi ya udhalilishwaji wa kupitia mitandaoya intaneti, vitisho na lugha za ubaguzi wa kijinsiazinazojaribu kuwanyamazisha mabinti katika kuelezamaoni yao, na kuwanyima haki yao kamili yakustawisha utu wao wa kidigitali, na ushiriki waokatika mahojiano ya kijamii, kitamaduni na kisiasa

Heshimu utu wetu wa kidigitali.

11

UHURU WA

INTANETI

Page 13: U T A N G U L I Z I

Imetosha!

Sisi, Mabinti wa Afrika, tunadai:

■ Ulinzi wa haki za mabinti na uwajibishwaji katikavipindi vya mapigano yatumiayo silaha, uchukuajiwa maeneo, majanga ya kiasili na dharura zakibinadamu. Sisi, kama mabinti, hatuzalishi, kuuzawala kununua bunduki, sasa kwanini tunalazimikakulipa gharama ya wababe wa vita?

■ Ulinzi wa haki ya mabinti katika kushirikimaandamano ya amani, mikutano na uhuru wakujieleza pamoja na utekelezaji wa sera namichakato ya kuchunguza ukatili wa polisi namanyanyaso dhidi ya wanawake na haki nyinginezoza kibinadamu katika kipindi cha janga lililopo nasiku zote zijazo

■ Urasimishaji wa ushiriki wa mabinti katika jitihadana michakato ya kujenga amani, upatanishi namazungumzo, huku michango yao ikinakiliwa

■ Ugavi wa fedha na usaidizi kwa mabinti, taasisi,programu maalum za mabinti za ujenzi wa amanindani ya makutano ya ajenda za kati ya Vijana,Amani na Usalama, Wanawake Amani na Usalama

Afrika Tunayoitaka ni Ile Isiyo na Migogoro

DAI LA KUNYAMAZISHA

BUNDUKI

12

SITISHABUNDUKI!

Page 14: U T A N G U L I Z I

Imetosha!

■ Urasimishwaji wa uongozi kwa ajili yaushirikishwaji mkamilifu na fanisi wa mabinti, katikasiasa, na fursa sawa za uongozi katika ngazi zote zaufanyaji maamuzi ndani ya nyanja za kisiasa, kijamii,kitamaduni, kiuchumi na kiraia maishani, hukuzikiimarisha sauti za mabinti na kutengeneza rasilimalikwa ajili ya ajenda zao

Sisi, Mabinti wa Afrika, tunadai:

■ Utekelezaji wa upigaji kura wa mabinti ndani yakura za wanawake na vijana. Hatujui tuko wapi ndaniya mifumo ya sera, kura za vijana na takwimu zakijinsia hazijaweza bayana nafasi ya wanawake, hakina ushiriki wao

■ Uteuzi wa mabinti wataalamu na WashauriMaalum/Wajumbe na nafasi nyingine katika tasnia,taasisi na kila ngazi ya kitaifa, kikanda na uongozi zakimataifa

■ Utengenezaji wa jukwaa endelevu za majadilianokwa ajili ya kuimarisha mitandao ya Pan-African naujumuishwaji wa mabinti na wanawake katikamafunzo, ushirikishaji, ushauri, ushikamano nauwezeshaji

Ni muda wa kuongoza pamoja sasa

DAI LA UJUMUISHWAJI KATIKA UONGOZI WA PAMOJA

13

NI MUDAWA

KUONGOZAKWA

PAMOJASASA

Page 15: U T A N G U L I Z I

Imetengenezwa na

Imeungwa mkono na

Page 16: U T A N G U L I Z I