Upload
others
View
11
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
UCHANGANUZI WA MATUMIZI YA AGOTI MIONGONI MWA WAFUNGWA:
HALI YA MAGEREZA TEULE KATIKA JIMBO LA KISUMU, KENYA
NA
OGUTU PETER OKOTH
B.ED. ARTS (MOI UNIVERSITY)
TASNIFU ILIYOWASILISHWA ILI KUTIMIZA BAADHI YA MAHITAJI YA
SHAHADA YA UZAMILI KATIKA KISWAHILI, KATIKA KITIVO CHA SANAA
NA SAYANSI JAMII, IDARA YA LUGHA, ISIMU NA FASIHI, CHUO KIKUU
CHA KISII
NOVEMBA, 2018
ii
UNGAMO
Tasnifu hii ni kazi yangu mwenyewe na haijawahi kuhudhurishwa katika chuo kikuu
chochote kwa lengo la kufuzu shahada yoyote.
Mtahiniwa :
Ogutu Peter Okoth …. ………………………….. ……………………..
(MAS16/60013/14) (Sahihi) (Tarehe)
Tasnifu hii imewasilishwa kwa madhumuni ya kutahiniwa kwa idhini yetu kama
wasimamizi walioteuliwa na Chuo Kikuu cha Kisii.
Dkt. Opande Nilson Isaac, Ph.D.
Mhadhiri, Idara ya Lugha, Isumu na Fasihi
Chuo Kikuu cha Kisii …………………………… …………………………..
(Sahihi) (Tarehe)
Dkt. Stephen Oluoch, Ph.D.
Mhadhiri, Idara ya Lugha, Isimu na Fasihi
Chuo Kikuu cha Kisii ………………………………. …………………………..
(Sahihi) (Tarehe)
iii
UNGAMO LA KITAALUMA
UNGAMO LA MTAHINIWA
i) Ninaungama kuwa, nimesoma na kuelewa sheria na masharti yanayotawala
mitihani ya masomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Kisii pamoja na nakala
zingine zinazohusu utovu wa maadili ya kiakademia.
ii) Ninaelewa kuwa kutofahamu sheria na masharti haya si kigezo cha kukiuka
sheria hizi.
iii) Kama nina maswali au atiati, ninatambua kuwa ni jukumu langu kutafuta
majibu au usaidizi hadi nipate welewa wa kutosha.
iv) Ninaelewa kuwa sharti nifanye kazi yangu mwenyewe.
v) Pia ninaelewa kuwa kama nimepatikana na hatia ya utovu wa maadili ya
kiakademia kwa mfano, wizi wa kitaaluma, tasnifu yangu inaweza kuangushwa
kwa kupewa alama „F‟.
vi) Isitoshe, ninaelewa kuwa kusoma kwangu katika Chuo Kikuu cha Kisii
kunaweza kusimamishwa kwa muda au kusitishwa kabisa kutokana na kukiuka
maadili ya kiakademia.
Jina………………………………………………
Sahihi…………………………………….
Nambari ya usajili………………………………… Tarehe………………………………….
UNGAMO LA WATAHINI
i) Tunaungama kuwa tasnifu hii imewasilishwa katika idara ya uchunguzi wa wizi
wa kitaaluma.
ii) Tasnifu hii ina chini ya asilimia 20 ya kazi ambazo asili zao hazijatambulishwa.
iii) Hivyo basi, tunatoa kibali cha usahihishaji.
1. Jina …………………………………………
Sahihi…………………………………
Idara…………………………………........... Tarehe………………………………
2. Jina ………………………………………… Sahihi………………………………..
iv
UNGAMO LA IDADI YA MANENO
Jina la Mtahiniwa…………………………………………………………………………..
Nambari ya usajili ………………………………………………………………………….
Kitivo……………………………………………..Idara……………………………………
Mada :…………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..
Ninaungama kuwa urefu wa :
1) Tasnifu hii, pamoja na maandishi ya tiniwayo ni ………………… 2) na marejeleo ni
ni…………………… na kama inawezekana, 3) Pamoja na viambatisho ni…………......
Pia, ninaungama kuwa tasnifu iliyo kwenye mfumo wa kielektroniki ni sawa na nakala
yangu ya mwisho na tena ni sawa na ile ambayo watahini walipendekeza kwa ajili ya
shahada ya uzamili.
Sahihi………………………………………………. Tarehe………………………………
Ninaungama kuwa, tasnifu ambayo imewasilishwa na mwanafunzi mtajwa hapo juu
imeafiki urefu unaohitajika kwa misingi iliyowekwa na kitengo cha masomo ya juu pamoja
na tume inayoongoza masomo katika vyuo vikuu kwa ajili ya shahada ya uzamili.
Sahihi………….Baruapepe…………..………..Na. ya simu…….………..Tarehe………….
(Msimamizi 1)
Sahihi………….Baruapepe…………..………..Na. ya simu…….………..Tarehe………….
(Msimamizi 2)
v
HAKIMILIKI
Haki zote zimehifadhiwa. Sehemu yoyote ya tasnifu hii au kazi nzima hairuhusiwi kuigwa,
kunakiliwa, kupigwa chapa, kusambazwa kielektroniki au kwa njia yoyote ile bila ridhaa ya
awali ya mwandishi au ya Chuo Kikuu cha Kisii kwa niaba ya mwandishi.
© 2018, Ogutu Peter Okoth
vi
TABARUKU
Tasnifu hii naitabaruku kwa wazazi wangu mzee Eliakim Ogutu na mama Anjeline Ogutu
kwa kunilea katika misingi bora ya kidini na ya kijamii kwa jumla. Nina hakika kuwa kila
hatua ninayopiga mnajivunia kuona matunda ya kazi ngumu mliyofanya ya kunielimisha.
vii
SHUKURANI
Awali ya yote, shukurani za dhati zimwendee Mwenyezi Mungu ambaye kwa hakika ndiye
nahodha mkuu wa kazi hii. Namshukuru kwa kunipa nguvu na uwezo wa kuitimiza ndoto
yangu ya kupata shahada ya uzamili.
Shukrani zangu pia ziwaendee wasimamizi wangu Dkt. Opande na Dkt. Oluoch kwa
ushauri, mawaidha na mwongozo ili kutamatisha kazi hii. Kutokana na jitihada zenu,
jinamizi hili limeniondokea.
Ninamshukuru Msarifu Mwandamizi wa Shule ya St Mary‟s Yala Bwana Jacob Amunga
kwa ushauri wake hadi kukamilisha uandilizi wa tasnifu hii.
Ninamshukuru babangu Sajini Mwandamizi mstaafu wa Magereza, Eliakim Ogutu Owiti
pamoja na ndugu yangu Koplo wa Magereza, Elias Otieno Ogutu. Jitihada zenu na
kujitolea kwenu kuwarekebisha wafungwa kwa haki katika gereza kuu la Kibos kulinitia
moyo na kunichochea kufanya utafiti huu.
Kupitia kwa Idara ya Magereza ya Kenya natoa shukurani za dhati kwa watafitiwa wote
ambao walishiriki katika utafiti huu. Isitoshe, ninamshukuru Kamanda Mkuu wa Magereza
katika eneo la Nyanza, Bwana Amos K. Misik (DCP) kwa ushauri wake kuhusiana na
utafiti huu na katika ulimwengu wa kiakademia kwa ujumla.
Shukurani nyingi sana zimwendee Mrakibu wa Magereza (SP) Martin Okoko pamoja na
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza P.W. Ngara (SACP/A) kwa ushauri wao na
kwa kunisaidia kupata kibali cha kukusanya data katika magereza ya Kenya.
Shukran jaziilan!
viii
IKISIRI
Utafiti huu ulilenga kuchanganua matumizi ya agoti miongoni mwa wafungwa wa
magereza ya Kisumu. Utafiti huu utachangia tafiti katika taasisi na vyuo vikuu kwa sababu
uliibua muktadha wa matumizi ya lugha ambao haujatafitiwa nchini Kenya. Utafiti huu
ulikuwa na madhumuni matatu; kujadili vikoa maana katika agoti zinazotumiwa na
wafungwa wa magereza ya Kisumu. Pili, kufafanua mabadiliko ya kimaana yanayojitokeza
katika agoti zinazotumiwa na wafungwa wa magereza ya Kisumu. Tatu, kujadili mbinu za
uundaji wa agoti zinazotumiwa na wafungwa wa magereza ya Kisumu. Mtafiti alijikita
katika Nadharia ya Pragmatiki Leksika ambayo huchunguza jinsi maana ya neno kiisimu
hubadilika kimatumizi. Utafiti huu uliongozwa na muundo wa usoroveya elezi. Kupitia
kwayo mtafiti alifanikiwa kupata habari alizotaka kuhusu agoti za wafungwa. Data
ilikusanywa kwa kutumia kalamu na daftari. Utafiti wenyewe ulifanywa katika magereza
ya Kibos na Kodiaga mjini Kisumu. Uteuzi wa sampuli kusudio ulitumiwa kupata
watafitiwa mia moja themanini na watano ambao walishirikishwa katika utafiti. Jumla ya
agoti mia mbili sitini na tatu zilikusanywa na kutokana na idadi hii, mtafiti aliteua agoti mia
moja themanini na nane ambazo zilichanganuliwa. Agoti hizi ndizo zilizotimiza upeo na
mipaka ya utafiti huu. Usaili na mahojiano ya kimakundi yalitumiwa kama mbinu za
kukusanya data. Data ilichambuliwa kwa misingi ya nadharia iliyoteuliwa na kwa kutumia
mkabala wa kimaelezo. Utafiti huu ulifanikiwa kufafanua vikoa vitano vya maana ambavyo
agoti za wafungwa huweza kuanishwa kwayvyo. Mtafiti alidhihirisha kuwa baadhi ya
leksimu zenye maana kiisimu hubadili maana kimatumizi katika muktadha wa jela. Ubanaji
na upanuzi wa maana ulijitokeza kama mabadiliko makuu ya kimaana katika agoti za
wafungwa. Isitoshe, utafiti huu ulifanikiwa kujadili mbinu mbalimbali za uundaji wa agoti
zinazotumiwa na wafungwa wa magereza ya Kisumu. Utafiti huu ulifikia hitimisho kuwa
agoti za wafungwa ni hazina ya maana kutokana na jinsi wafungwa walivyoonyesha
ubunifu wa kuyapa maneno maana, kubadili maana ya maneno na kwa kubuni leksimu za
kuwasiliana miongoni mwao. Hatimaye utafiti huu ulitoa mapendekezo kwa watafiti wa
baadaye ambao wangependa kushughulikia eneo la lugha ya wafungwa.
ix
ABSTRACT
This study aimed at analysing the argot terms used by the inmates in Kisumu County,
Kenya. The study will contribute to research in the universities as it comes out with a
context of language usage which has not been researched in Kenya. The study had three
objectives; to discuss the sets of semantic fields in the argot terms used by the prisoners at
the Kisumu Prisons. To explain the changes in meaning in the argot terms used by the
prisoners at the Kisumu Prisons. Lastly, to discuss the techniques used in the formation of
argot terms used by the prisoners at the Kisumu Prisons. The researcher used the Lexical
Pragmatic Theory which explains how words change meaning in context. The argot terms
collected from the respondents were noted down in a book. The study was carried out at the
Kibos and Kodiaga maximum prisons in Kisumu County. Purposive sampling was used to
identify one hundred and eighty five prisoners who acted as the respondents. A total of two
hundred and sixty three argot terms were collected. Out of these, one hundred and eighty
eight terms were selected to be analysed in the study. These were the terms which met the
scope of the study. Interviews and guided group discussions were used to collect data. The
study found five semantic fileds under which different argot terms were discussed. Lexical
narrowing and lexical broadening were found to be the major lexical pragmatic processes
which caused shifts in the meaning of the argot terms. The study managed to discuss the
various techniques used in the formation of argot terms. It was found that the formation of
words in prisons was mostly accompanied by changes in meaning in the words formed.
This study reached a conclusion that prison argot is a rich resource of meaning going by the
creativity which was shown in the assigning of meaning to terms, shifting of meaning of
terms and in the creation of words used for communication in the prisons. After reaching its
objectives, the study gave out recommendations for further research in the field of prison
lingo.
x
YALIYOMO
UNGAMO……………………………………………………………………….………….ii
UNGAMO LA KITAALUMA ........................................................................................... iii
UNGAMO LA IDADI YA MANENO ............................................................................... iv
HAKIMILIKI ........................................................................................................................ v
TABARUKU ......................................................................................................................... vi
SHUKURANI ..................................................................................................................... vii
IKISIRI .............................................................................................................................. viii
ABSTRACT .......................................................................................................................... ix
YALIYOMO .......................................................................................................................... x
ORODHA YA MAJEDWALI .......................................................................................... xiv
ORODHA YA VIAMBATISHO ……………………………………………….………..xv
ORODHA YA VIFUPISHO ............................................................................................. xvi
UFAFANUZI WA ISTILAHI ......................................................................................... xvii
SURA YA KWANZA
MISINGI YA UTAFITI ....................................................................................................... 1
1.1 Usuli wa suala la utafiti ................................................................................................. 1
1.2 Suala la Utafiti ............................................................................................................... 3
1.3 Misingi ya uteuzi wa mada ........................................................................................... 4
1.4 Malengo ya utafiti ......................................................................................................... 5
1.5 Maswali ya utafiti .......................................................................................................... 6
xi
1.6 Umuhimu wa utafiti ...................................................................................................... 6
1.7 Upeo na mipaka ya utafiti ............................................................................................. 7
1.8 Changamoto za utafiti ................................................................................................... 8
SURA YA PILI
UHAKIKI WA MAANDISHI ............................................................................................ 10
2.1 Utangulizi .................................................................................................................... 10
2.2 Dhana ya agoti ............................................................................................................. 10
2.2.1 Agoti za wafungwa ............................................................................................... 13
2.3 Msingi wa kinadharia .................................................................................................. 15
2.3.1 Semantiki Kileksika .............................................................................................. 15
2.3.4 Michakato ya Pragmatiki Leksika ........................................................................ 16
2.3.4.1 Ubanaji wa kileksika ......................................................................................... 16
2.3.4.2 Upanuzi wa kileksika ........................................................................................ 17
2.3.4.3 Kisio la maana ................................................................................................... 20
2.4 Vikoa maana katika agoti za wafungwa ...................................................................... 21
2.4.1 Vitendo vya ngono na mapenzi ............................................................................ 22
2.4.2 Marufuku .............................................................................................................. 23
2.4.3 Michakato ya kitaasisi .......................................................................................... 24
2.5 Mabadiliko ya maana .................................................................................................. 25
2.6 Uundaji wa agoti za wafungwa ................................................................................... 28
2.6.1 Ukopaji na utohozi ............................................................................................... 29
2.6.2 Mbinu ya ukatizaji ................................................................................................ 29
2.6.3 Mbinu ya uambishaji ............................................................................................ 29
2.6.4 Mbinu ya ubadilishaji silabi ................................................................................. 30
2.6.5 Onomatopia: Tanakali za Sauti ............................................................................ 30
2.7 Pengo la utafiti ............................................................................................................ 30
2.8 Hitimisho ..................................................................................................................... 31
xii
SURA YA TATU
MBINU ZA UTAFITI ........................................................................................................ 32
3.1 Utangulizi .................................................................................................................... 32
3.2 Mbinu za utafiti ........................................................................................................... 32
3.3 Muundo wa utafiti ....................................................................................................... 33
3.4 Eneo la utafiti .............................................................................................................. 34
3.5 Sampuli na usampulishaji ........................................................................................... 35
3.5.1 Usampulishaji ....................................................................................................... 35
3.5.2 Sampuli lengwa .................................................................................................... 35
3.5.3 Sampuli iliyoteuliwa ............................................................................................. 36
3.6 Vifaa vya kukusanya data ........................................................................................... 37
3.7 Ukusanyaji wa data ..................................................................................................... 37
3.8 Uchanganuzi wa data .................................................................................................. 37
3.9 Majaribio ya vifaa vya utafiti ...................................................................................... 38
3.9.1 Uhalali .................................................................................................................. 39
3.9.2 Utumainifu ............................................................................................................ 39
3.10 Maadili ya utafiti ....................................................................................................... 40
3.10.1 Maadili ya utafiti yanayomhusu mtafiti ............................................................. 40
3.10.2 Maadili ya utafiti yanayohusu watafitiwa .......................................................... 40
3.10.3 Maadili ya utafiti yanayohusu mchakato wa utafiti ........................................... 41
3.11 Hitimisho ................................................................................................................... 41
SURA YA NNE
UWASILISHAJI NA UCHANGANUZI WA DATA ...................................................... 42
4.1 Utangulizi .................................................................................................................... 42
4.2 Vikoa maana katika agoti za wafungwa ...................................................................... 43
4.2.1 Kikoa cha mahusiano ya kimapenzi ..................................................................... 44
4.2.2 Kikoa cha marufuku na dawa za kulevya ............................................................. 47
4.2.3 Kikoa cha mambo na shughuli za jela .................................................................. 50
4.2.4 Kikoa cha wafungwa ............................................................................................ 55
xiii
4.2.5 Kikoa cha maafisa wa magereza .......................................................................... 58
4.2.6 Agoti zaidi ................................................................................................................ 61
4.3 Mabadiliko ya maana .................................................................................................. 63
4.3.1 Ubanaji wa kileksia .............................................................................................. 63
4.3.2 Upanuzi wa kileksia ............................................................................................. 69
4.3.3 Kisio la maana ...................................................................................................... 86
4.4 Uundaji wa agoti za wafungwa na ubunaji wa maana mpya ...................................... 88
4.4.1 Ukopaji wa maneno .............................................................................................. 89
4.4.2 Ubadilishaji silabi katika maneno ........................................................................ 90
4.4.3 Ubunifu wa leksimu ............................................................................................. 92
4.4.5 Kuchanganya msimbo .......................................................................................... 93
4.4.6 Ubadilishaji ........................................................................................................... 96
4.5 Hitimisho ..................................................................................................................... 97
SURA YA TANO
HITIMISHO NA MAPENDEKEZO ................................................................................ 99
5.1 Utangulizi .................................................................................................................... 99
5.2 Muhtasari wa utafiti .................................................................................................... 99
5.3 Matokeo ya utafiti ..................................................................................................... 101
5.4 Mchango wa utafiti ................................................................................................... 103
5.5 Hitimisho la utafiti .................................................................................................... 104
5.6 Mapendekezo ............................................................................................................ 105
MAREJELEO ................................................................................................................... 107
VIAMBATISHO ............................................................................................................... 120
xiv
ORODHA YA MAJEDWALI
Jedwali 4.01: Agoti zinazohusu mahusiano ……………………….……………….……..44
Jedwali 4.02: Agoti zinazohusu marufuku na dawa za kulevya……………………….… .47
Jedwali 4.03: Agoti zinazohusu mambo na shughuli za jela…………….………...……....50
Jedwali 4.04: Agoti zinazowarejelea wafungwa………………………..………………….55
Jedwali 4.05: Agoti zinazowarejelea maafisa wa magereza…………..……….……….….58
Jedwali 4.06: Agoti zaidi kutoka kwa wahojiwa……………………...…………….…..…61
Jedwali 4.07: Agoti zilizobanika kimaana…………………….…………...………………64
Jedwali 4.08: Agoti zilizopanuka kimaana…………………………………………..….…69
Jedwali 4.09: Agoti zilizopanuka kisitiari……………………………….…………..…..…75
Jedwali 4.10: Agoti zilizopanuka maana kichuku………………………..………..……….83
Jedwali 4.11: Agoti zilizopauka kikategoria…………………………..………………..….85
Jedwali 4.12: Agoti zilizopanuka kwa kukisia maana………………………………..……86
Jedwali 4.13: Agoti zilizokopwa……………………………………………………...……89
Jedwali 4.14: Mifano ya agoti zilizobadilisha silabi….……………………………...…….91
Jedwali 4.15: Agoti zilizobuniwa……………………………………………………..……92
Jedwali 4.16: Mifano ya uchanganyaji misimbo………………………………………...…94
Jedwali 4.17: Mifano ya agoti zilizobadilishana nafasi…………………...…………….…96
xv
ORODHA YA VIAMBATISHO
KIAMBATISHO I: MWONGOZO WA MAHOJIANO ……………….………………..120
KIAMBATISHO II: KIBALI CHA UTAFITI (KAUNTI YA KISUMU)…...…………. 121
KIAMBATISHO III: BARUA YA IDHINI (NACOSTI)………………………….…….122
KIAMBATISHO IV: CHETI CHA IDHINI (NACOSTI)…………………………….…123
KIAMBATISHO V: KIBALI CHA UTAFITI (MAGEREZA YA KENYA)……………124
KIAMBATISHO VI: KIBALI CHA KUHOJIWA………………………………...…….125
KIAMBATISHO VII: UCHAPISHAJI…………………………………………………..126
KIAMBATISHO VIII: RIPOTI YA UHALALI WA UTAFITI…………...…………….127
xvi
ORODHA YA VIFUPISHO
UKIMWI - Ukosefu wa Kinga Mwilini
Taz. - Tazama
N.k. - Na kadhalika
K.v. - Kama vile
N.w. - Na wenzake
xvii
UFAFANUZI WA ISTILAHI
Jagoni - Ni aina mojawapo ya lugha inayotumika katika taaluma fulani mahususi kama vile
fasihi, isimu, sheria, sayansi, uhandisi, biashara na kadhalika. Ni lugha
inayofahamika na wale tu walioko katika taaluma hiyo.
Misimu - Ni misemo isiyo rasmi ambayo huhusishwa na kikundi kidogo cha wanajamii na
ambayo aghalabu hupotea baada ya muda.
Agoti - Ni maneno au lugha itumiwayo na kundi fulani la wahalifu au watu ambao
wanaficha uovu wao usifahamike katika jamii wanamoishi.
Agoti ya wafungwa - Ni lugha au maneno ambayo ni ya kipekee miongoni mwa
wafungwa gerezani.
Kirai Nomino - Neno au fungu la maneno ambayo hukitwa kwenye Nomino au
Kiwakilishi kama neno kuu.
Kirai Kitenzi – Neno au fungu la maneno ambayo hukitwa kwenye Kitenzi kama neno
kuu.
Vikoa maana – Matapo ya maneno yenye maana yanayohusiana.
Mabadiliko ya manaa – Neno kupata maana tofauti na maana yake asilia.
Pragmatiki leksika – Nadharia ambayo inashughulikia maana za leksimu kimuktadha.
Semantiki kileksika – Semantiki inayoshughulikia maana za kileksika za maneno.
Michakato ya kileksika – Mikondo ambayo leksimu hupitia kuibua fahiwa au dhana mpya
(dhana inayowasilishwa kwenye tamko).
1
SURA YA KWANZA
MISINGI YA UTAFITI
1.1 Usuli wa suala la utafiti
Utafiti huu unahusu uchanganuzi wa matumizi ya agoti miongoni mwa wafungwa, hali ya
magereza teule katika jimbo la Kisumu. Ito na wenzake (1996) wanafafanua agoti kama jagoni
ambayo hubadili maana ya maneno ya lugha kwa njia maalumu na ambayo ni wazi tu kwa
watumiaji wa agoti hiyo. Ni lugha itumiwayo na kundi fulani la wahalifu au watu ambao
wanaficha uovu wao usifahamike katika jamii wanamoishi. Aghalabu lugha hii hutumiwa katika
mazingira yasiyo rasmi na kikundi cha watu kama vile madereva wa magari, watumiaji wa dawa
za kulevya, majambazi, vibaka na wahuni wa mtaani. Kwa mujibu wa Looser (2001) agoti ya
wafungwa ni lugha au maneno ambayo ni ya kipekee katika magereza na katika tamaduni
zingine za kihuni. Anaeleza kuwa, agoti ya wafungwa ni maneno yanayochipuka kutokana na
kutengwa kwa wafungwa na jamii pana. Anderson na Trudgil (1990) wanafafanua kuwa mahitaji
ya kimsingi ya lugha ya kundi fulani katika jamii huwasilishwa kupitia misimu. Agoti, ambayo
awali wanafafanua kama jagoni ya wezi na wafungwa, ni aina fulani ya msimu (Nielson na
Scarpitti, 1995). Kwa mujibu wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili- TUKI (1990) simo ni
mitindo ya lugha ambayo huzuka katika kipindi fulani na kutumiwa na kundi fulani la watu.
Ulimwenguni kote, Uingereza ndilo eneo lenye historia ndefu ya agoti za wafungwa (Coleman,
2004). Hata hivyo, taifa la Amerika ndilo taifa lenye maandishi na tafiti changamano kuhusu
lugha ya wafungwa. Hii inatokana na idadi kubwa ya wafungwa iliyokuwepo, inayozidi kukua,
na iliyofika kilele mwaka wa 2004 kwa kuwepo kwa zaidi ya wafungwa milioni mbili (Coleman,
2004). Kwa mujibu wa Szabo (2005), hadi kufikia miaka ya themanini, watu wengi waliiona
2
agoti kama lugha ya majambazi na tafiti kuhusu misimu na agoti kuonekana kama zisizo na
thamani. Hata hivyo, tangu karne ya ishirini wanaisimu wamechanganua misimu na agoti na
kuzikubali kama kitengo cha isimu. Kwa mujibu wa Mekacha (2011), imekubalika kuwa hivi
leo, ndani ya jamii-lugha moja kuna migawanyiko inayofuata sulubu maalumu na kwamba ndani
ya lugha moja kuna vilugha ambavyo pia vimegawanyika kufuata sulubu maalumu. Mekacha
(2011) anaeleza kuwa kazi za Labov (1972), Gumperz (1972) na Milroy (1980) ndizo vyanzo
vya mkabala wa utofauti ndani ya lugha katika isimu. Gal (1979) anaeleza kuwa kuwepo kwa
vilugha katika jamii ni jambo la kawaida.
Kwa mujibu wa Gohodzi (2013), tafiti nyingi kuhusu agoti za wafungwa zimefanywa ughaibuni.
Mfano wa kazi hizi ni utafiti wa Looser (2001). Katika utafiti huu, Looser (2001) anachukua
mwelekeo wa kihistoria ambamo anachanganua matumizi ya agoti za wafungwa katika taifa la
New Zealand iliyotumiwa kati ya miaka ya 1996-2000. Tofauti iliyopo kati ya utafiti huu na ule
wa Looser (2001) ni kuwa ulifanywa katika muktadha wa lugha na mazingira yaliyo tofauti.
Isitoshe, kazi ya Looser (2001) aliwashirikisha wafungwa wa jinsia zote. Utafiti huu ulichunguza
agoti za wafungwa wanaume tu.
Hapa Afrika, tafiti chache sana zimefanywa kuhusu lugha za wafungwa (Gohodzi, 2013).
Gohodzi alijaribu kujaza pengo hili kwa kuchanganua matumizi ya agoti katika gereza la
Whahwa nchini Zimbabwe. Gohodzi (2013) alitumia wafungwa ambao walikuwa
wamefunguliwa kupata data zake. Nchini Kenya, tafiti nyingi zimefanywa kuhusu matumizi ya
lugha katika miktadha mbalimbali (Mekacha, 2011). Hata hivyo, tafiti hizi zaidi zimefanywa
uraiani. Binyanya (2014) anaeleza kuwa, tafiti nyingi nchini Kenya kuhusu vilugha vya
Kiswahili zimefanywa zaidi katika miktadha ya maabadini, siasa na uchuuzi. Mugendi (2016)
alichunguza matumizi ya agoti ya Gatamanyana miongoni mwa wahudumu wa magari katika
3
mji wa Embu. Nyakundi (2010) naye alichunguza matumizi ya agoti ya Egesemba inayotumiwa
miongoni mwa wazungumzaji wanaume katika jamii ya Wakisii. Tafiti hizi ni muhimu lakini
zinahusu jumuiya lugha tofauti. Utafiti huu uliwachunguza wafungwa kama jumuiya lugha.
Pengine uchache wa tafiti kuhusu matumizi ya lugha katika eneo lenye hazina kubwa ya lugha
kama jela unatokana na mtazamo finyu wa baadhi ya wanaisimu kuhusu vilugha. Kwa mfano,
Ramani (2006) anaandika makala, „Leave Sheng to Matatu Touts and Musicians‟. Kobia (2006)
naye anaandika, „Sheng is not a language but a popular slang.‟
Magereza ya nchi ya Kenya yamejengwa katika misingi ya magereza ya Uingereza (Newbold,
1978). Katika kuingia kwenye taasisi jumuishi kama jela, wafungwa hupitia maingiliano ya
kitawi (Goffman, 1962). Maingiliano ya kitawi ni „Ubwiaji wa tamaduni na itikadi za „vijidunia‟
vya taasisi fulani‟ (Berger & Luckman, 1971). Jinsi upokeaji wa lugha ni jambo la lazima katika
usimilisho asilia, vivyo hivyo ujifunzaji wa lugha ni jambo la shuruti katika usimilisho huu wa
pili. Lugha anayojifundisha mfungwa gerezani si lugha ya kawaida kwani huwa na sifa za
kipekee. Hivyo basi katika utafiti huu, kulichanganuliwa agoti ambazo huwawezesha wafungwa
wa magereza ya Kisumu kuwasiliana.
1.2 Suala la Utafiti
Mawasiliano ni muhimu katika jamii. Wafungwa wanapojihusisha na mambo ya kisiri, wanaibua
na kujifundisha mitindo ya kisiri ya mawasiliano ili kukidhi mahitaji yao. Katika kufanya hivi,
wafungwa huibua lugha ya siri au agoti ambazo zinafahamika tu na kundi lao. Isitoshe,
wafungwa hubadili maana ya maneno ili kukidhi haja ya kuficha siri katika mawasiliano. Hali hii
husababisha neno kupata maana mpya ambayo huweza kutofautiana kwa kiasi fulani na maana
4
yeke asilia. Wafungwa pia hubuni maneno mapya ili kurejelea hali mbalimbali katika mazingira
ya jela.
Tafiti kuhusiana na matumizi ya agoti miongoni mwa wafungwa zimefanywa sana katika nchi za
kimagharibi. Matumizi ya lugha katika muktadha wa magereza ya Kenya hayajashughulikiwa na
watafiti. Tafiti nyingi kuhusu vilugha vya Kiswahili zimefanywa kuhusu msimbo wa Sheng.
Tafiti zingine zimechanganua viswahili vya manamba, wauzaji nguo, msimbo wa maafisa wa
polisi na hata lugha katika muktadha wa hoteli. Hapana lolote linalosemwa kuhusu lugha ya jela.
Utafiti huu hivyo basi ulichanganua maneno ambayo wafungwa wa magereza ya Kisumu
hutumia na kuibua muktadha mwingine wa matumizi ya lugha ambao haukuwa umetafitiwa
nchini Kenya.
1.3 Misingi ya uteuzi wa mada
Utafiti huu una mchango mkubwa kwa utafiti katika taasisi na vyuo vikuu. Kama ilivyodokezwa
na Gohodzi (2013) tafiti chache kuhusu matumizi ya agoti miongoni mwa wafungwa
zimefanywa barani Afrika. Binyanya (2014) alithibitisha kauli hii kwa kueleza kuwa tafiti nyingi
zilizofanywa kuhusu matumizi ya vilugha zimefanywa zaidi katika miktadha ya maabadini, siasa
na uchuuzi. Hivyo basi, utafiti huu umeweka msingi kwa wanafunzi na watafiti wanaonuia
kuchanganua matumizi ya agoti za wafungwa nchini Kenya. Utafiti huu umechukua mtazamo wa
kipragmatiki ila watafiti wengine wanaweza kutumia data ya utafiti huu na kuchanganua agoti
kihistoria au kuchukua mtazamo wa kisintaksia.
Mchango mwingine kwa utafiti katika taasisi na vyuo ni kuwa, utafiti huu umehifadhi kwa mara
ya kwanza leksimu zinazotumiwa na wafungwa katika magereza ya Kenya. Hii ni muhimu
5
kwani utafiti huu utakuwa kumbukumbu kwa watafiti wa baadaye ambao watapenda kutambua
jinsi lugha ya wafungwa itakavyokuwa imebadilika katika miaka ya baadaye.
Mchango kwa taaluma ni kuwa, waandishi mbalimbali katika taaluma ya Isiimujamii na
pragmatiki hawajashughulikia matumizi ya lugha gerezani. Kwa mfano, Mekacha (2011)
anaorodhesha maeneo mbalimbali ya matumizi ya lugha : nyumbani na miongoni mwa familia,
maeneo ya makazi, miongoni mwa majirani, shughuli za mila na desturi, sehemu za kazi,
michezo na burudani, masoko na biashara, usafiri wa umma, ibada na shughuli za dini, vyombo
vya habari, uandishi na usomaji wa kazi za fasihi, utawala na siasa, sheria na mahakama, elimu
na mafunzo, mawasiliano na biashara ya kimataifa. Hakuna lolote linalosemwa kuhusu
magereza. Utafiti huu hivyo basi umechangia kuwepo kwa muktadha mwingine wa matumizi ya
lugha ambao haujatafitiwa katika Kiswahili.
Mchango kwa sera ya lugha ni kuwa, kupitia kwa data ambayo ilipatikana, ilibainika ni kwa
kiwango gani wafungwa hujihusisha na lugha rasmi za nchi ya Kenya, Kiswahili na Kiingereza.
Ilidhihirika kuwa wafungwa wanatumia Kiswahili zaidi katika mawasiliano yao. Hii ilitokana na
ukweli kuwa, maneno mengi yanayotumiwa ni ya Kiswahili au yalikuwa na uhusiano na lugha
ya Kiswahili. Ngugi (1986) anaeleza kuwa watu huzibadili lugha sanifu na kuzitumia kwa
mahitaji yao. Mekacha (2011) anaeleza kuwa nchini Tanzania, lugha ya Kiswahili ndiyo ambayo
imeenea zaidi katika maeneo rasmi na yasiyo rasmi. Utafiti huu umefaidi katika kuhakikisha
ukweli wa kauli hii hapa Kenya. Isitoshe, utafiti huu umebainisha Kiswahili kama lugha ya dola,
lugha ya jamii na lugha ya vijijamii.
1.4 Malengo ya utafiti
Utafiti huu uliongozwa malengo yafuatayo :
6
i) Kujadili vikoa maana katika agoti zinazotumiwa na wafungwa wa magereza ya
Kisumu.
ii) Kufafanua mabadiliko ya kimaana yanayojitokeza katika agoti zinazotumiwa na
wafungwa wa magereza ya Kisumu.
iii) Kujadili mbinu za uundaji wa agoti zinazotumiwa na wafungwa wa magereza ya
Kisumu.
1.5 Maswali ya utafiti
Utafiti huu uliongozwa na maswali yafuatayo :
i) Je, agoti zinazotumiwa na wafungwa wa magereza ya Kisumu zinaweza kuanishwa
katika vikoa vipi vya maana ?
ii) Je, mabadiliko yapi ya kimaana hujitokeza katika agoti zinazotumiwa na wafungwa
wa magereza ya Kisumu ?
iii) Je, mbinu zipi hutumika katika uundaji wa agoti zinazotumiwa na wafungwa wa
magereza ya Kisumu ?
1.6 Umuhimu wa utafiti
Utafiti huu utawafaidi maafisa wanaoshughulikia ulinzi na urekebishaji wa wafungwa gerezani.
Urekebishaji wa mfungwa unategemea sana ufahamu wa tabia na imani za mfungwa husika. Ni
muhimu sana kwa mwelekezi kutambua lugha ya wale anaotagusana nao (Condon na Yousef,
1975). Kwa mujibu wa Cardzo-Freeman (1995), welewa wa agoti za mfungwa ni dira ya kujua
mielekeo ya kitamaduni ya jela husika pamoja na muundo wa kijamii wa jela hiyo.
7
Kwa kuwa siku hizi wafungwa huruhusiwa kusoma gerezani, utafiti huu utawafaidi pakubwa
walimu, hasa walimu wa lugha wanaofundisha gerezani. Kutegemea ukweli kuwa mawasiliano
ya maana ni muhimu kati ya mwalimu na mwanafunzi (Foster, 1986) walimu wa wanafunzi-
wafungwa sharti wawe na welewa wa lugha ya wafungwa ili kurahisisha mtagusano kati yao.
Kwa mujibu wa Mclntyre na Mack (1993), walimu wa wafungwa wasiokuwa na ufahamu wa
lugha ya wanafunzi wao wamo katika hatari ya kuchezewa shere na wafungwa au hata masomo
yao kutatizwa na wafungwa hao.
Utafiti huu utakuwa muhimu kwa wanaleksikografia ambao huunda kamusi za magereza. Hii ni
muhimu kwa sababu hapa Kenya hapana kamusi inayoeleza maana za leksimu zinazotumiwa
katika mazingira ya jela, tofauti na ilivyo katika mataifa yaliyoendelea. Kwa mfano, Knight
(2014) alitunga kamusi The Dictionary of Victorian Prison Slang ambayo inafafanua maneno
yanayotumiwa na wafungwa katika muktadha wa magereza ya taifa lake.
Utafiti huu pia unaendeleza na kuikuza lugha katika idara ya magereza. Hivyo basi, utafiti huu ni
wa faida hapa nchini na kwa mataifa mengine ya ulimwengu kwani utasaidia kueneza lugha ya
jela ya Kenya ulimwenguni. Kimsingi, utafiti huu utatumika kama daraja linalounganisha jamii
ya wafungwa wa Kenya na jamii za magereza mbalimbali. Hali hii itawasaidia watafiti wa lugha
na wasimamizi wa magereza kutambua hali za magereza ulimwenguni kote au hata kufanya tafiti
changamano kuhusu lugha za wafungwa katika mabara tofauti.
1.7 Upeo na mipaka ya utafiti
Utafiti huu ulihusu uchanganuzi wa matumizi ya agoti miongoni mwa wafungwa wa magereza
ya Kisumu. Kwa mujibu wa Looser (2001) watafiti wa awali wa lugha na utamuduni wa
magereza wametumia mielekeo minne. Mwelekeo wa kwanza ni mfungwa binafsi kufanya
8
utafiti wake anapokuwa gerezani. Pili, mtafiti kuchunguza lugha ya gereza moja. Mfano ni kazi
ya Lyons (1984). Aghalabu watu hawa huwa wameajiriwa na jela kufanya kazi hii. Mwelekeo
wa tatu ni kufanya utafiti wa kindani na wa muda mrefu wa jela fulani. Kwa mfano kazi
changamano ya Cardzo-Freeman katika gereza la Walla Walla, Washington katika mwaka wa
1984. Mwelekeo wa nne ni ule wa kutafiti lugha ya magereza mengi ya aina moja. Mfano mzuri
ni kazi ya Becker ya mwaka 1994 ambapo alitafiti magereza manne. Kwa misingi hii, utafiti huu
ulishikirikisha mwelekeo wa nne. Hii inatokana na ukweli kuwa mtafiti alichunguza magereza
mawili ya aina moja. Gereza la Kibos na Kodiaga yote ni magereza makuu katika jimbo la
Kisumu.
Utafiti huu ulijikita katika kutambua zile agoti ambazo hutumiwa katika magereza ya Kibos na
Kodiaga. Agoti hizo ziliweza kuainishwa katika vikoa maana mbalimbali. Agoti ambazo
zilizozingatiwa ni zile ambazo hubainika katika lugha ya mazungumzo tu. Matini za kimaandishi
hazikuchunguzwa. Pia mtafiti alijikita katika agoti za Kiswahili, za Sheng pamoja na zile
zilizoundwa kwa kuchanganya Kiswahili na misimbo mingine. Tulielekezwa na kauli ya
Mekacha (2011) kuwa, lugha ya Kiswahili ndiyo inatawala katika maeneo yote. Palipotokea hali
ya uchanganyaji misimbo, sababu zakuchanganywa kwa misimbo zilifafanuliwa.
1.8 Changamoto za utafiti
Mtafiti alifanikiwa kukusanya data kwa kiasi kikubwa kama alivyotarajia. Hata hivyo, kama
ilivyo ada, hakuna jambo linalokosa changamoto katika utekelezaji wake. Mtafiti kukusanya data
kutoka kwa wafungwa asiowafahamu hakukuwa rahisi. Ilimlazimu kuwatumia wafungwa na
maafisa wa magereza kuwateua wafungwa waaminifu ambao hawangeupotosha utafiti.
9
Jela huwa na sheria zake kali na mambo yote hufanywa kwa muda. Wakati mwingine mtafiti
aliwapata wahojiwa wakishughulikia kazi zao za jela na ikambidi kuwasubiri hadi wakamilishe
kazi zao. Hivyo basi, pana nyakati ambapo muda ulikuwa mfupi sana na wahojiwa wengine
kutoka kabla mahojiano hayajakamilishwa. Hali kama hii ilipotokea mtafiti aliendeleza
mahojiano siku iliyofuata.
Baadhi ya maafisa waliodumisha usalama walisonga karibu nasi sana kiasi cha kuwapa
wahojiwa wasiwasi kwamba yale ambayo wangesema yangetumiwa vibaya dhidi yao. Hata
hivyo, mtafiti aliwaomba maafisa kusimama mbali kidogo na sehemu ya mahojiano ili kuwapa
wahojiwa uhuru wa kuwasiliana.
10
SURA YA PILI
UHAKIKI WA MAANDISHI
2.1 Utangulizi
Sura ya kwanza ilitoa usuli na msingi ambamo utafiti huu umefanywa. Sura hii ya pili inatoa
uhakiki wa maandishi yaliyohusiana na utafiti huu na kubainisha mianya iliyopo. Kwa mujibu
wa Boswell na Cannon (2009) uhakiki wa maandishi ni kitendo cha kusoma, kuchanganua na
kuchunguza kwa urazini maandishi mbalimbali. Sehemu ya kwanza ya sura hii ni utangulizi.
Sehemu ya pili inafafanua dhana ya agoti na kutofautisha agoti na mitindo mingine ya lugha ya
mazungumzo. Kitengo hiki pia kimeangazia suala zima la agoti za wafungwa. Sehemu ya tatu
imeangazia msingi wa kinadharia. Sehemu ya nne imeangazia suala la vikoa maana. Katika
sehemu ya tano kazi mbalimbali kuhusu mabadiliko ya kimaana zimehakikiwa. Sehemu ya sita
imeshughulikia uundaji wa agoti. Sehemu ya saba imedhihirisha pengo ambalo utafiti huu
ulinuia kujaza. Sehemu ya nane ni hitimisho la sura hii.
2.2 Dhana ya agoti
Katika kufafanua dhana ya agoti ni muhimu kwanza kufafanua istilahi ambazo huwa na uhusiano
wa karibu na agoti, yaani, misimu na jagoni. Mijelezo iliyotolewa katika sura ya kwanza huenda
isitoshe mahitaji ya utafiti huu. Kwa mujibu wa Msanjila na wenzake (2009) misimu ni aina ya
misemo katika lugha ambayo huzuka na kutoweka. Sifa kuu ya misimu ni kwamba haidumu
muda mrefu na sio lugha sanifu, na watumiaji wa misimu huwa ni kikundi cha wazungumzaji wa
lugha katika jamii ambao kimsingi huishi katika eneo moja. Ngure (2003) anaonekeana
kukubaliana na Msanjila kwa kiasi ila yeye anaweka mkazo zaidi anapodai kuwa uzukaji wa
11
misimu ni wa ghafla na wakati fulani hufuatana na mambo au matukio maalumu ya wakati au
msimu huo. Kwa mujibu wa McArthur (1996), sharti tutofautishe misimu na mitindo mingine ya
lugha kama vile jagoni, agoti, maneno ya kilahaja na matusi.
Maelezo haya kuhusu misimu ni muhimu kwani yalisaidia kubainisha kuwa agoti za wafungwa
hutumiwa katika mazingira yasiyo rasmi na si kila agoti huzuka na kudumu kwa muda mfupi.
Utafiti huu ulipata kuwa, pana baadhi ya istilahi kama mruru, mende na kunguru ambazo
watafitiwa walizipata zikitumiwa gerezani, wakajifundisha na kuendelea kuzitumia. Hivyo basi
kurejelea agoti za wafungwa tu kama misimu ni kuzinyima hadhi zao.
Kwa mujibu wa Yule (2006) jagoni ni lugha inayotumiwa na kundi au wataalamu wa tasnia
fulani. Ni lugha ambayo ipo, ikimaanisha kuwa haiwezi kufa kama ilivyo katika mitindo mingine
ya lugha kama vile misimu. Ni matumizi ya istilahi katika taaluma fulani. Hujitofautisha
kimsamiati na lugha zingine. Yule (keshatajwa) anapendekeza njia tatu za kutambua jagoni;
istilahi, miundo ya kisarufi na nduni za kifonolojia. Jagoni ni utambulisho wa mtu katika jamii.
Yaani, kwamba ametoka katika tasnia au nyanja ipi? Kwa mfano taaluma ya uhandisi huwa na
jagoni zake.
Yule (1996) naye anadahili kuwa jagoni ni misamiati ya kitaaluma ambayo inahusihwa na kundi
fulani spesheli na husaidia katika mwingiliano wa wale wanaojiona kama watu wa kundi la
ndani. Kwa mujibu wa Burke na Porter (1995) jagoni ni istilahi iliyopatikana kutoka lugha ya
Kifaransa katika karne za kumi na mbili na kumi na tatu, na katika Kiingereza ikatokea baadaye
ikirejelea maneno yasiyo na maana. Kazi hizi ni muhimu kwani zilimsaidia mtafiti kutambua
kuwa jagoni hutumiwa kitaaluma. Ufungwa si taaluma. Ingawa hivyo, pana wataalamu
wanaosema kuwa agoti ni jagoni ya wezi (Nielson na Scrapitti, 1995).
12
Kwa upande mwingine, agoti ni maneno ambayo hutumiwa na makundi ambayo hufanya kazi
kinyume na sheria kama vile wezi, makahaba na watumiaji wa dawa za kulevya (Looser, 2001).
Watafiti wa awali walisisitiza dhana ya usiri katika agoti kama kipengele cha kuanisha agoti
lakini watafiti wa leo kama vile Partridge (1971) wamejaribu kuondoa sifa hii. Maelezo haya ni
muhimu kwani mtafiti alikusudia kuchanganua agoti zote zilizotumiwa katika muktadha wa jela,
za siri au zisizo za siri.
Maurer (1951) ambaye ni mtafiti mkuu katika mitindo ya lugha anaeleza kuwa agoti ni maneno
au lugha ambazo ni za kipekee na zinaashira maisha yanavyokuwa katika vikundi halifu. Ni
muhimu katika kutambua mielekeo, namna ya kufikiria hadi katika kueleza muundo wa kijamii
wa kundi hilo. Nielson na Scrapitti (1995) wanaeleza kuwa agoti ni jagoni ya wezi lakini pia
inaweza kutumiwa na makundi mengine katika jamii.
Ito na wenzake (1996) wanafafanua agoti kama jagoni ambayo hubadili lugha ya kawaida kwa
njia maalumu na kwa njia ambayo ni wazi tu kwa wale ambao wana welewa. Agoti huwa
misamiati ya kipekee ambayo hutumiwa na kundi ndogo la watu katika jamii ambalo aghalabu
huwa wana umoja na usiri fulani (Harris, 2012). Agoti huhusishwa zaidi na wahalifu japo watu
wa eneo fulani au tabaka fulani pia wanaweza kuitumia katika kuwasiliana (Age, 1990). Agoti
hutumiwa na kundi fulani shikamani na hivyo basi kuunda kundi la „sisi‟ na „wao.‟ Misamiati ya
agoti pia inaweza kutumiwa kuzungumza kuhusu mambo ya kiuhalifu bila woga wa kutambulika
(Harris, 2012). Kazi hizi ni muhimu kwani zinabainisha agoti kama lugha ya makundi, ifahamike
kuwa wafungwa ni kundi la jamii ambalo aghalabu huchukuliwa kuwa pambani.
Kwa mujibu wa Bullock (1996) kuna mifumo miwili ya agoti. Moja ni ya kileksia ambapo pana
ubadilishaji wa maana na ya pili inabadili sura ya neno kwa kubadili sauti au silabi katika neno
13
husika. Leslau (1998) anaelekea kukubaliana na maoni haya kwa kueleza kuwa sifa za kipekee
za agoti zipo katika uundaji wa mizizi na katika uwanja wa kisemantiki.
Kazi hizi mbili ni muhimu katika utafiti huu ambao ulinuia kuchambua mbinu za uundaji wa
agoti za wafungwa ambapo ubadilishaji silabi ni miongoni mwa mbinu zilizojitokeza na
hubainika ili kufanikisha ufumbaji wa maana.
2.2.1 Agoti za wafungwa
Mahitaji maalum ya lugha na kundi fulani hujitokeza kupitia misimu (Anderson na Trudgil,
1990). Agoti, ambayo ni lugha ya wafungwa ilielezwa awali kama lugha ya wezi, pia ni aina
fulani ya misimu (Nielson na Scrapitti, 1995). Imejadiliwa kuwa wafungwa huishi, hufikiri na
kufanya kazi ndani ya duara la agoti linalotumiwa gerezani, hivyo basi, agoti ya wafungwa
imesimikwa katika dhima inayotekeleza miongoni mwa wafungwa (Bondesson, 1989).
Agoti ya wafungwa ni lugha au maneno ya kipekee yanayotumiwa na wafungwa, na asili yake ni
neno la Kifaransa lenye maana ya „misimu‟ (Sykes, 1958). Lugha ya wafungwa ilizuka kama
njia fiche ya mawasiliano baina ya wafungwa na hunuiwa kuwatenga maafisa wa magereza
katika mawasiliano yanayohusu marufuku na matendo yao gerezani. Lugha ya wafungwa
hutofautiana kulingana na jinsia (Einat na Einat, 2000). Maelezo haya ni muhimu kwa sababu
utafiti huu ulikusudia kuchanganua matumizi ya agoti miongoni mwa wafungwa wa magereza ya
Kisumu. Kwa ambavyo lugha ya wafungwa hutofautiana kulingana na jinsia, utafiti huu ulijikita
katika kuchunguza agoti za wafungwa wanaume.
Usimbaji wa kitabia na maendeleo yake yamefanyiwa utafiti na kurekodiwa kwa upana (Irwin,
1985; Toch, 1992). Itikadi na thamani ya msimbo huunda msingi wa utamaduni wa wafungwa,
ikiwapa wafungwa njia isiyo rasmi ya kupata nguvu na hivyo basi kuendeleza hisia za kutengwa
14
na jamii na kufidia kutokuwepo kwa usalama na uhuru wa kujiamulia (Bondesson, 1989). Kwa
sababu hii, kwa mfungwa, matumizi ya agoti na usimbaji ni mchakato wa mwingiliano na
kuzoeana na maisha ya ndani ya jela. Imejadiliwa kuwa jamii ya kawaida, ishara zake,
viwakilishi vyake ni adui asilia ya mfungwa, hivyo uwepo wa agoti gerezani ni jambo la lazima
katika magereza yote ulimwenguni (Irwin, 1980). Misimbo hutazamwa kama njia ya kuingiliana
na kuzoea na mazingira ya magereza (Fisher, 1990). Maelezo haya ni muhimu kwani yalimsaidia
mtafiti kutambua kuwa agoti za wafungwa hazijitokezi katika ombwe tupu.
Lugha kama njia kuu ya mawasiliano ni msingi mkubwa katika mchakato mzima wa
mwingiliano wa kijamii na maendeleo ya tabia zao (Dean-Brown, 1992). Hivyo basi, vitengo
tofauti vya jamii huwa na sifa tofauti za lugha wanazotumia. Kimsingi, vitengo vya jamii
vitatofautishwa na lugha tofauti wanazotumia (Hudson, 1980). Lugha ya kundi fulani huweza
kuhusisha ishara mbalimbali ambazo hazimo katika lugha ya jamii pana, kwa yakini, ishara hizo
huenda zimekopwa na kupewa maana mpya (Alatis, 1992). Mahitaji ya kipekee ya kundi fulani
ndogo huwasilishwa kwa kutumia misimbo (Anderson na Tradgill, 1990). Imejadiliwa kuwa
mfungwa huishi, hufikiria na hutenda kazi ndani ya miktadha inayoamuliwa na agoti na hivyo
basi agoti ya wafungwa itasimikwa ndani ya dhima yake kwa mfungwa (Bondesson, 1989).
Tafiti kuhusu agoti za wafungwa zimefanywa zaidi katika mataifa ya Marekani, Australia
pamoja na Asia (Looser, 2001). Tafiti chache kuhusu agoti za wafungwa zimefanywa Afrika na
hasa katika nchi ya Kenya. Agoti za wafungwa katika magereza ya ughaibuni zimehifadhiwa
vitabuni na mitandaoni lakini taifa la Kenya linakosa uhifadhi na tafiti katika eneo hili muhimu.
Hivyo basi utafiti huu ulichanganua agoti za wafungwa wa magereza ya Kisumu na hivyo
kuweka msingi kwa tafiti za baadaye katika muktadha huu wa matumizi ya lugha.
15
2.3 Msingi wa kinadharia
Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Pragmatiki Leksika. Nadharia hii ilianzishwa na Blutner
mwaka wa 1990. Baadaye iliendelezwa na Wilson (2003) kwenye mihadhara yake katika Chuo
Kikuu cha Havard. Pia iliendelezwa na Wilson na Carston (2007) katika miaka ya baadaye.
Nadharia hii inajikita katika kuchanganua jinsi maana hubadilika katika muktadha, kwa hivyo
mtazamo huu ni faafau zaidi katika kuwakilisha dhana.
Mtazamo huu umejikita katika stadi za mabadiliko ya maana. Mtazamo wa Pragmatiki Leksika
unaelezea mwelekeo kwamba, faridi za kileksika za lugha zinachanganuliwa kiutaratibu na
kufasiriwa kulingana na muktadha mahususi.
Mchango wa semantiki katika ufasiri wa kijumla wa tamko umebanwa kuliko ilivyodhaniwa
mwanzoni. Pragmatiki Leksika inajaribu kuelezea fenomena za kipragmatiki ambazo
zimeunganika na semantiki hiyo chini ya umahususi wa faridi za kileksika.
Nadharia hii ina mihimili mingi ila tufafanua ile iliyokuwa na uhusiano na utafiti huu.
2.3.1 Semantiki Kileksika
Semantiki kileksika inajishughulisha na maana ya neno. Maneno huweza kuchukuliwa kuashiria
vitu katika ulimwengu au katika dhana kutegemea mtazamo mahususi wa semantiki kileksika.
Kwa mujibu wa Mmbwanga (2010) vitengo vya maana katika semantiki kileksika ni vitengo vya
kileksika ambavyo kwavyo msemaji huweza kuongezea kwa mfululizo maishani pamoja na
ujifunzaji wa maneno mapya na maana hayo.
Mhimili huu ulimsaidia mtafiti katika kuanisha agoti za wafungwa katika vikoa maana
mbalimbali. Maneno yaliyowekwa katika kikoa kimoja yalikuwa na uhusiano wa kimaana.
16
Kikoa maana kama dhana ya kisemantiki ilitumika katika kuweka faridi za kileksika katika
matapo mbalimbali ya kimaana. Katika utafiti huu, vikoa maana vilivyojadililiwa vilikuwa;
kikoa cha mahusiano ya kimapenzi, kikoa cha marufuku na dawa za kulevya, kikoa cha mambo
na shughuli za jela, agoti zilizowarejelea wafungwa na hatimaye, agoti zilizowarejelea maafisa
wa magereza.
2.3.4 Michakato ya Pragmatiki Leksika
Kulingana na Blutner (2011), mambo ya kimsingi yanayoshughulikiwa katika pragmatiki leksika
akiwarejelea Wilson (2003) na Cartson (2002), yanaweza kugawika katika mambo matatu ya
kimsingi ambayo tuliyatumia katika uchanganuzi.
i) Ubanaji wa kileksika
ii) Upanuzi wa kileksika
iii) Kukisia maana
2.3.4.1 Ubanaji wa kileksika
Kwa mujibu wa Kolaiti na Wilson (2012) ubanaji wa kileksika ni mchakato ambao unahusu
matumizi ya neno au kirai katika kuonesha dhana mahususi zaidi (ambayo ina maana finyu)
kuliko maana iliyosimbwa ya kiisimu. Mtafiti alikubalina na ufafanuzi huu na kushadidia kuwa,
maana pana ya neno ndiyo iliyosimbwa kiisimu. Wakati ambapo ubanaji unafanywa, tunapata
dhana ndogo katika muktadha wa uzungumzaji. Maana inayojitokeza huwa ni kisehemu cha
maana pana ambayo imesimbwa. Anusu (2015) anatoa mfano; Niko ndani ndani ya Jubliee.
Neno ndani katika Kiswahili limesimba dhana ya NDANI. Ili kuelewa maana ya ndani, sharti
msikilizaji afanye ufasiri kutegemea muktadha. Hii ni kwa sababu, maana ya ndani ndani ni pana
kwa kiwango fulani. Horn na Ward (2004) wanafafanua kuwa ubanaji kwa kiwango kikubwa ni
17
mchakato ambao unaweza kusawazishwa na hutegemea muktadha. Maana iliyosimbwa inaweza
kubanwa katika viwago tofauti kutegemea muktadha. Maana pana ni kuwa ndani, maana
mahususi ni kuwa ndani ya chama na hakuna kinachoweza kukutoa humo.
Mfano wa pili, Onyango ana kirusi. Neno kirusi limesimba dhana KIRUSI ambayo inajumuisha
aina nyingi za virusi vinavyoweza kusababisha magonjwa. Lakini katika muktadha huu, maana
ya kirusi imebanwa kumaanisha UKIMWI. Kwa mujibu wa Blutner (1998) ubanaji ni kutumia
faridi leksika kupitisha maana ambayo imebanwa zaidi kuliko ile ambayo imesimbwa
kisemantiki. Kisemantiki, kirusi kina maana ya kiini kisababishacho ugonjwa (Mdee n.w, 2011).
Katika muktadha wa mazungumzo, kirusi kina maana ya kirusi cha UKIMWI. Virusi vingine
vimetengwa katika muktadha huu (Anusu, 2015).
2.3.4.2 Upanuzi wa kileksika
Kwa mujibu wa Fromkin na Rodman (1978), upanuzi wa kileksika ni mchakato ambao kwao
maana ya neno hupanuka. Neno linamaanisha kila kitu kilichokuwa kikimaanishwa na kuzidisha
maana nyingine. Mtafiti alikubaliana na maelezo haya na kuongeza kuwa, neno linapopanuka
kimaana, neno hilo huwa limeongezewa vitajwa na kujumuisha vitajwa vingine. Kwa mfano,
neno mguu linaweza kutumiwa kutoa maana nyingi. Maana ya kileksika ya neno mguu ni kiungo
cha mwili wa binadamu, mnyama au mdudu kinachomwezesha kusimama au kwenda (TUKI,
2013). Hata hivyo, neno hili linaweza kutumiwa kumaanisha mwanamke anayetumiwa katika
mapenzi kisha baadaye anaachwa. Pia, linaweza kumaanisha sehemu ya siri ya mwanamke.
Hivyo basi neno hili linapata fahiwa nyingi zaidi ya maana yake ya kisemantiki. Ullmann (1970)
anafafanua kuwa maneno yanapewa maana moja bunifu au zaidi bila ya maana asilia kupotea. Ile
maana asilia na maana ya pili zinaishi upande upande bora tu kusiwepo na ukinzano (Anusu,
2015).
18
2.3.4.2.1 Upanuzi wa kisitiari
Simiyu (2016) anaeleza kuwa upanuzi wa kisitiari ni mchakato ambao kwao maana ya neno ipo
mbali na maana wazi. Yaani, maana ya neno fulani katika muktadha wa mazungumzo ni tofauti
kabisa na maana ya neno hilo kiisimu. Yaani, katika upanuzi wa kisitiari maana ya neno huwa
mbali na maana halisi kwa kuhamisha maana ya neno hilo toka kwa kiashiria kimoja hadi
kiashiria kingine. Anusu (2015) anatoa mfano wa sentensi Onyango ni mburukenge sana.
Mburukenge ni mnyama lakini Onyango ni binadamu. Hapa, Onyango anafananishwa na
mburekenge kwa sababu ya tabia zake (Aitchison, 2003). Leksimu mburukenge limesimba
dhana MBURUKENGE. Msikilizaji anatengeza dhana za dharura kama vile, mburukenge ni
mnyama asiye na akili timamu. Ukweli ni kuwa sicho anachomaanisha msemaji. Hivyo basi
msikilizaji anachukua kuwa Onyango ni mjinga. Aitchison (2003) anafafanua kuwa kwenye
sitiari ya sampuli ya kiasili, vitu ambavyo vinalinganishwa vina uwezekano wa kutofautiana,
yaani, vinatokana na vikoa maana tofauti, na kufanana. Zinalingana katika sifa chache za
kawaida.
2.3.4.2.2 Chuku
Wilson (2003) anasema kuwa hili ndilo badiliko ambalo linaonekana kuhusisha kiwango
kukubwa zaidi cha upanuzi wa maana na hivyo kunakuwepo na utengano mkubwa kutoka kwa
dhana ambayo imesimbwa. Mtafiti alikubaliana na maelezo haya na kuongeza kuwa, hili
badiliko linahusu upigaji chuku au kutia chumvi ila haimaanishi hivyo waziwazi tu. Mfano,
Onyango hatoboki.
Leksimu toboka katika lugha ya Kiswahili ina maana ya kitu kupata tundu na kuweza kupitisha
maji au hewa. Kitu kinapotoboka huvuja bila kujizuia. Tukisema Onyango hatobiki tunatilia
chumvi dhana ya kuwa Onyango hawezi kutoa pesa.
19
Kwa mujibu wa Bloomfield (1933) chuku ni badiliko linalotoka kwenye maana yenye nguvu
hadi maana ambayo ni legevu.
2.3.4.2.3 Upanuzi wa kategoria
Katika aina hii ya badiliko, jina la kitu ambacho kinajulikana zaidi katika jamii linapanuliwa na
kutumiwa katika jamii nzima ambamo kitu hicho hupatikana (Wilson, 2003). Mtafiti
alikubaliana na maelezo haya na kuongeza kuwa, hili jina linapotumiwa katika jamii nzima,
huwa linafanya maana inayopitishwa kujitenga zaidi toka kwenye maana iliyosimbwa na
leksimu hiyo.
Kwa mujibu wa Wilson na Carston (2007) majina ya kipekee na nomino za kawaida huwa
zinachangia katika badiliko hili. Glucksberg (2001) anatoa mifano ya majina Chomsky na
Shakespeare.
Mfano; Onyango ni Shakespeare wa Afrika. Shakespeare ni jina la kipekee. Kwa kuwa alikuwa
mwandishi shupavu na alitambulika ulimwenguni kote kwa uandishi wake, jina lake linatumika
na watu wanaopenda uandishi wake kurejelea watu wenye ufundi katika uandishi. Dhana
ambayo inawasilishwa katika muktadha huu inajitenga na dhana ambayo imesimbwa
inayoashiria Shakespeare aliyewahi kuishi. Jeffers na Lehiste (1979) wanafafanua kuwa upanuzi
wa maana huwa unatokana na kujumuisha hali mahususi hadi katika jamii ambayo ile hali
mahusisi inashiriki. Hii ni kwa sababu, majina ya pekee yanajitokeza kurejelea jamii ya kijumla
ya ile fenomena.
2.3.4.2.4 Ubunaji wa maana mpya na uundaji wa leksimu
Ubunaji wa maana ni mchakato wa kuzua maana mpya na maneno mapya kutoka kwa yale
maneno ambayo tayari yapo katika lugha fulani. Hivyo basi ubunaji wa maana mpya unaweza
20
kutokea kupitia mkondo wa uundaji wa kileksimu. Hii inaashiria kuwa tunapounda leksimu
mpya, leksimu hiyo huweza kupata maana mpya.
Kwa mfano; Onyango asilete ubeberu wake hapa. Neno hili ubeberu liliwahi kuundwa kutokana
na neno beberu lenye maana wazi ya mbuzi dume. Maana inayowasilishwa ni kuwa Onyango
asiwanyanyase wengine.
Kupitia kipengele hiki mtafiti aliweza kujadili uundaji wa agoti katika magereza ambayo
aghalabu huambatana na ubadilishaji wa maana. Kitengo hiki kimejadiliwa kwa kina katika
kitengo cha uundaji wa agoti (2.6).
2.3.4.3 Kisio la maana
Ni badiliko la maana ambalo kwalo leksimu iliyo na maana thabiti kiasi hupanuliwa ukingoni na
kujumuisha mawanda ya makundi ambayo kwa hakika yanapatikana nje ya maana yake kamili
ya kiisimu. Mifano mizuri kwa mujibu wa Wilson (2003) ni kama matumizi ya kilegevu ya
takwimu za kukadiria, misamiati ya kijiografia na misamiti ambayo inaelezwa kwa njia ya
kukanusha. Kimsingi, dhana ambazo zinapanuliwa ukingoni ndizo zinazowasilishwa na
wasemaji katika usemi huku dhana thabiti ya leksimu ikiwa ndiyo ambayo imesimbwa
kisemantiki na neno hilo.
Marisya (2017) anafafanua kuwa ni hali ambapo ufasiri wa neno ambalo lina maana finyu
hupanuka ili kuhusiana na maana ya kitu ambacho kinahusiana nacho ambacho kina maana
tofauti na maana halisi ya neno hilo kiisimu. Kwa mfano, neno karatasi hutumiwa kurejelea
ugonjwa wa ukimwi katika jamii ya Wanyore. Hii ni kwa sababu mtu ambaye anaugua ugonjwa
huu huwa amekonda na ni mwepesi kama karatasi (Anusu, 2015).
21
Katika badiliko hili, dhana ambayo inawasilishwa na neno fulani hujitenga zaidi kutoka kwa ile
dhana ambayo imesimbwa kama ambavyo ipo katika upanuzi wa kisitiari. Mfano; Chakula
kimeletwa mapema, leo saa saba imefika mapema.
Saa saba ni wakati thabiti ila hapa msemaji anachukulia kuwa wakati wowote ni saa saba mradi
tu chakula kiwe kiko tayari. Hivyo basi maana hii imejitenga sana na maana halisi ya saaa saba.
Saa saba inatumika kwa njia legevu.
Kwa muhtasari, michakato hii ya kipragmatiki leksika ilimwezesha mtafiti kuchanganua
mabadiliko ya kimaana katika agoti za wafungwa pamoja na kujadili uundaji wa agoti za
wafungwa.
2.4 Vikoa maana katika agoti za wafungwa
Kwa mujibu wa Kempson (1977) semantiki ni taaluma ambayo hujishughulisha na kufafanua
maana za maneno, maana za sentensi, pamoja na maana za matini za usemaji. Kama chombo cha
mawasiliano, lugha huhitaji tafsiri ya maana zilizobebwa pamoja na maumbo ya kisarufi ili
kutimiliza wajibu wake mkuu. Maana ni za aina mbili; kwanza maana inayorejelea muktadha wa
uzungumzi huchunguzwa katika pragmatiki. Hii hueleza alichokusudia msemaji katika
mawasiliano. Pili, ni maana kileksia ambayo husawiri maana ya kila neno katika lugha. Maana
hii huwakilishwa na vidahizo katika kamusi za lugha na ndiyo maana ya msingi na
isoyobadilika. Katika utafiti huu agoti zilifafanuliwa kwa kutegemea maana zao katika muktadha
wa jela.
Maneno yanapohusiana kwa njia mbalimbali huleta ukoa maana. Kwa mujibu wa Habwe na
Karanja (2004) ukoa maana ni mahusiano ya kimuundo ambapo kuna ufinyu au upana wa maana
22
za maneno. Katika utafiti huu, ukoa maana ulitumika kurejelea tapo la maneno yenye maana
yanayohusiana.
Mugambi (2007) anaainisha leksimu mbalimbali za Sheng katika vikoa maana. Aliibuka na
vikoa maana vya mapenzi, biashara, elimu, michezo na utawala. Kwa mfano, katika kikoa cha
elimu anaainisha na kufafanua maana ya leksimu bayo, kemu, ziki, pizo na swa. Maneno haya
yanahusiana kwani yanarejelea aina mbalimbali za masomo katika shule za upili. Katika kikoa
cha michezo anafafanua aina mbalimbali za michezo kama zinavyorejelewa katika Sheng, futa,
bake, kagutha na voli. Kazi hii ni muhimu kwetu kwani, japo ilishughulikia ukoa maana katika
msimbo wa Sheng, ulitupa mwelekeo wa kuziweka agoti za wafungwa katika vikoa maana
mbalimbali.
Maana zinazowasilishwa na agoti za wafungwa hutegemea muktadha na mazingira. Ellis (2005)
“Prison-House and Language: Modern American Prison Argot” anatoa vikoa mbali mbali
ambavyo kwavyo agoti za wafungwa huweza kupata maana;
2.4.1 Vitendo vya ngono na mapenzi
Ushoga katika magereza ya Marekani umeandikwa na kuhifadhiwa sana katika karne ya ishirini
(Hensley na wenzake, 2003) na maneno mengi na maana yanatokana na mapenzi na ngono.
Maneno yanaweza kuanishwa katika vitengo vya wenye nguvu na wale wanyenyekevu,
kuhusiana na dhima zinazotekelezwa na wafungwa tofauti tofauti. Kwa mfano pana neno punk
lenye maana ya mfungwa anayekuwa kama mwanamke (Cardzo-Freeman nw., 1984). Neno hili
punk linatumiwa hadi leo kule Marekani. Flipflop ni wale walio na uwezo wa kuwa kama
wanawake na pia kuwa kama wanaume (Bently nw., 1992). Neno fish anaeleza kuwa lina maana
ya wafungwa wageni (Encinas, 2001) lakini katika magereza ya leo ya Waafrika-Wazungu zaidi
23
huwa neno hili lina viashiria vya ushoga (Hensley nw., 2002). Kwa kutumia mwelekeo huu
mtafiti alitafuta istilahi ambazo zilihuhisiana kimaana na mahusiano ya kimapenzi.
2.4.2 Marufuku
Pana maneno mengi yanayoashiria marufuku, haswa yanayotumiwa katika shughuli zilizo
kinyume na matakwa ya magereza. Kuna vitengo viwili vya marufuku: vitu visiyo na madhara
yoyote, dawa za kulevya na silaha. Mfano bora zaidi ya marufuku isiyo na madhara ni donuts
ambayo inarejelea mafuta inayotumiwa kupika (Cardzo nw., 1984). Mifano mingine ni tat
inayorejelea hali ya kuchora miili ya mfungwa. Kategoria hiyo ina maana mbalimbali kama vile
tat gun, tat man na tat motor (Benltely, 1992). Agoti zinazorejelea uchoraji wa mwili
zimejadiliwa zaidi na Encinas (2001). Maneno yanayorejelea dawa za kulevya huwa ni ya siri
sana na hivyo huchukua mfumo wa misimu hivi kwamba yakitambuliwa na askari, hubadilishwa.
Kwa mfano bing kurejelea dawa nyingi zisizorejelewa kwa jina moja (Cardozo- Freeman, 1984)
au binky kumaanisha sindano. Ubunifu wa mfungwa huenea zaidi katika silaha na virejelewa
vyao kwa mfano Shivs na shanks ni maneno yanayotumiwa kurejelea visu vilivyotengezwa
gerezani (Encinas, 2001). Neno lingine ni zip gun, neno linalotumiwa kurejelea bunduki rejareja
zinazoundwa na wafungwa na kutumiwa ndani ya jela, na ili kuficha maana, zaidi huitwa „Z‟
(Bentley, 1992).
Kazi hizi ni muhimu katika kuainisha agoti. Katika utafiti huu hata hivyo tofauti na (Bentley,
1992) mtafiti alijikita katika lugha ya mazungumzo tu, pasi na kutafiti maneno yaliyoandikwa
mwilini au kwenye kuta za jela.
24
2.4.3 Michakato ya kitaasisi
Japo agoti kwenye kikoa hiki ndizo za kipekee toka gereza moja hadi lingine, ndizo
zinazobadilika zaidi kulingana na namna ambavyo mabadiliko ya masuala ya kisheria
yanavyoleta maneno mageni na tofauti. Maneno mahususi ya megereza ni kama oregon boots
yenye maana ya miguu ya chuma, ambayo ilipata jina hilo kutokana na gereza la kwanza
lilimotumika (Oregon). Sheria na masharti ya gereza fulani huweza pia kusababisha uundaji wa
neno fulani kurejelea hatua za kinidhamu. Kwa mfano pana maneno majors na minors kurejelea
viwango vya kosa alilofanya mfungwa. Aidha, pana maneno kama parakeet kurejelea askari
ambaye huwaiga kimzaha wakubwa wake (Jackson, 1967). Maneno mengine ni kama brown
shirt inayorejelea mavazi ya askari na tabia zao za kiukandamizi (Bentley, 1992).
Thamani ya tafiti hizi zilizofanywa kuhusiana na agoti ya wafungwa haiwezi kupuuziliwa mbali.
Hata hivyo, maneno haya yanahusiana na magereza ya ughaibuni. Afrika, na hasa nchini Kenya,
maneno macheche yanayojulikana kutumiwa gerezani yanatokana na filamu zilizoigizwa na
baadhi ya vitabu vilivyoandikwa na wafungwa waliofunguliwa. Katika miktadha hii, maneno
yanayotumiwa gerezani huwa kama maneno matano au kama zaidi maneno kumi. Na mengi yao
huwa si sahihi (Coleman, 2004). Hata hivyo kuna wengine ambao pia wamejaribu kuainisha
agoti za wafungwa kwa mfano Halliday (1978) na Clemmer (1940). Clemmer alipata maneno
1063 katika magereza yote ya Marekani na akayaweka katika vikoa vya; ngono na mapenzi,
sehemu za mwili, maelezo kuhusu wengine, pombe na dawa za kulevya, maneno yanayohusu
jela na matusi (vagabondage). Kupitia kwa maelezo haya utafiti huu ulichanganua agoti za
wafungwa na kuziweka katika vikoa maana mbalimbali.
25
2.5 Mabadiliko ya maana
Dhana ya mabadiliko ya maana yalizungumziwa mwanzo na Edward Sapir aliyeeleza kuwa kila
neno na kila elementi ya kiisimu hubadilika polepole (Sapir katika Ullman, 1977). Keith na
Shuttleworth (2000) wanaeleza kuwa, „Mabadiliko ni sehemu muhimu katika maisha; bila
mabadiliko, maisha yanakoma. Lugha pia lazima ibadilike ili iwe hai.‟ Mabadiliko ya maana
hujitokeza wakati neno linapotumiwa kuwasilisha maana ambayo haikuwa nayo awali (Lourens
nw, 1992).
Bloomfield (1930) anajadili aina mbalimbali za mabadiliko ya maana. Anataja upanuzi wa
kimaana, upanuzi wa kisitiari na chuku miongoni mwa mabadiliko mengine. Anadai kuwa kila
badiliko la kimaana litaathiri maneno mengine katika kikoa maana. Kutokana na kazi hiyo ya
Bloomfiled utafiti huu ulipata mwelekeo wa kujadili mabadiliko ya kimaana yanayojitokeza
katika agoti za wafungwa wa magereza ya Kisumu. Utafiti huu ulijikita katika aina mbalimbali
za mabadiliko ya kimaana ambapo upanuzi wa kileksika unajidhihirisha kwa njia anuwai.
Katika tasnifu yake ambayo haijachapishwa, Wambugu (2010) anaangazia mabadiliko ya
kimaana katika leksimu za Kikuyu kwa kutumia mtazamo wa kipragmatiki leksika. Anaendelea
na kufafanua maana za ziada ambazo leksimu hizi zimepokea. Anahusisha kazi yake na kazi ya
Muyuku (2009).
Ullmann (1957, 1962) anaibuka na uchanganuzi ambao unaenda juu zaidi ya ufafanuzi wa
leksimu mojamoja. Anaiga kazi ya Trier (1931) ambaye alisema kuwa badiliko la kimaana
litaathiri maneno mengine katika kikoa husika.
Blank (1998) ni mtafiti mwingine ambaye aliandika kuhusu mabadiliko ya kimaana kwa
kuangazia hali mbalimbali ambazo husababisha mabadiliko ya kimaana. Blank anasema kuwa
26
mabadiliko ya kimaana yanaweza kusababishwa na masuala ya kiisimu katika lugha husika.
Maneno yanaweza kutumika katika miktadha mbalimbali ili kuibua maana tofauti ambayo
msemaji ananuia kuwasilisha. Pia anafafanua hali za kisaikolojia ambazo huweza kuathiri namna
ambavyo watu huteua na kutumia maneno katika lugha kutegemea chukulizi zao kuhusu maneno
hayo. Msemaji anapoona kuwa neno fulani ni kinyume na maadili ya kijamii atatumia tasfida
katika kuwasilisha ujumbe wake.
Habwe (1999) alichunguza diskosi ya hotuba za kisiasa kwa kujikita katika Nadharia ya
Ushirikiano miongoni mwa nadharia nyingine. Alizamia katika kufafanua jinsi ambavyo
implikecha huundwa katika kufasiri ujumbe ambao umo kwenye matamko ya wanasiasa. Utafiti
huu ulimfaa mtafiti katika kuelewa implikecha za mazungumzo zinavyoundwa katika lugha ya
Kiswahili. Aidha, utafiti huu ulimfaa mtafiti katika kuelewa jinsi masuala ya kipragmatiki
huelezwa katika diskosi za Kiswahili. Utafiti huu ni tofauti na wa Habwe (keshtajwa) kwa
sababu ulishughulikia mabadiliko ya kimaana kwa kujikita katika Nadharia ya Pragmatiki
Leksika.
Carston (2002) alifafanua kwa kina mihimili mikuu ya Nadharia ya Pragmatiki Leksika.
Alifafanua namna msikilizaji anavyojenga dhana za dharura na pia kufafanua michakato ya
Pragmatiki Leksika kama vile upanuzi wa kileksika na ubanaji wa kileksika. Isitoshe,
amefafanua kwa undani upanuzi wa kisitiari kwa kuonyesha jinsi dhana zilivyosimbwa na sitiari
huweza kusimbuliwa na msikilizaji. Kazi hii ilitufaa katika kuelewa michakato ya Nadharia ya
Pragmatiki Leksika na kuitimia katika kujadili mabadiliko ya kimaana katika agoti za wafungwa.
Muyuku (2009) alitafiti jinsi uchanganyaji lugha hujitokeza katika matangazo ya benki ya
Commercial banks pamoja na Mobile Telecommunications kwa kujikita katika Nadharia ya
27
Pragmatiki Leksika. Alifafanua jinsi dhana zinavyosimbwa na kusimbuliwa ili kuwavutia na
kuwashawishi wateja. Ilibainika katika kazi hii kwamba Kiswahili ni kati ya lugha ambazo
zilitumiwa kwa wingi. Utafiti huu ulimfaa mtafiti kwa kumpa mwelekeo wa jinsi maneno ya
Kiswahili husimbwa na kusimbuliwa. Tofauti ni kuwa utafiti huu ulijikita katika agoti za
wafungwa na ilichunguza mabadiliko ya kimaana na wala si uchanganyaji lugha.
Njimu (2010) naye aliangazia matumizi ya leksimu kwenye magazeti ya michezo katika taifa la
Kenya kwa kujikita katika Nadharia ya Pragmatiki Leksika. Lengo lake lilikuwa ni kuonyesha
umuhimu wa muktadha katika kuzua zile dhana za dharura. Alijikita katika magazeti matatu; The
Nation, The Standard, na The Star. Mtafiti alinufaika na utafiti huu kwani ulimwezesha kuelewa
jinsi maana hubadilika katika muktadha.
Ochoki (2010) alitumia data toka kwenye mtandao na kutumia Nadharia ya Pragmatiki Leksika
kuchunguza jinsi maana zinavyosimbwa katika nyimbo za Hip hop za nchi ya Kenya. Alitumia
michakato ya upanuzi na ubanaji wa maana katika kufafanua usimbaji huu wa maana. Mtafiti
alifaidika na utafiti huu kwani ulimwezesha kuelewa jinsi dhana zinavyosimbwa na kusimbuliwa
katika Kiswahili.
Ochichi (2013) alijikita katika kuchunguza umaanisho na usimbaji wa maana kumazungumzo
katika lugha ya Kiswahili na Ekegusii. Kufanikisha kazi yake, alitumia Nadharia ya Pragmatiki
Leksika na kategoria za kimuktadha. Isitoshe, alichunguza uwazi na umaanisho wa kauli za
Ekegusii na Kiswahili. Utafiti huu ulimsaidia mtafiti katika kufahamu namna usimbaji hujitokeza
katika Kiswahili. Tofauti ni kuwa mtafiti alijikita katika agoti za wafungwa.
28
Kazi hizi ni muhimu kwani zinazungumzia mabadiliko ya kimaana. Ingawa hivyo, zinaangazia
mabadiliko ya kimaana katika jumuiya lugha iliyo tofauti na ya utafiti huu. Katika kazi hii,
mtafiti aliangazia mabadiliko ya kimaana katika katika agoti ambazo hutumiwa na wafungwa.
2.6 Uundaji wa agoti za wafungwa
Kama ilivyojadiliwa awali, uundaji wa maneno mapya pamoja na ubunaji wa maana mpya ni
kitengo cha upanuzi wa maana ambacho pia hushughulikiwa na Nadharia ya Pragmatiki Leksika
(Wilson, 2003). Hii hutoa data zaidi kwa nadharia hii na kutoa welewa wa mikakati ya kiakili na
hali za kimaumbile ambazo huhusika. Leksia huashiria umbo lenye maana msingi kama vile
vitenzi au nomino (Buliba, Njogu na Mwihaki, 2006). Utafiti huu ulichunguza namna agoti za
wafungwa huundwa.
Katika miaka ya sabini, Ohly (1977) alitoa baadhi ya ruwaza za kuanzisha misamiati mipya
katika Kiswahili. Kwanza, alifafanua ukopaji wa maneno kisha akaangazia uundaji wa maana
mpya ambao unaweza kuwa; uundaji wa maneno mpya kikamilifu, maneno yaliyokuwepo
kuidhinishiwa maana mpya au kupewa mawanda ya kisemantiki ya kipekee au kwa kutumia
makundi ya kisintaksia yenye kijalizo. Mtafiti alikubaliana na ufafanuzi huu kwani hadi nyakati
hizi pana leksimu ambazo zinaundwa au zinapata maana mpya au zinabadilishwa miundo
kimofolojia au kifonolojia na kwa njia hiyo kupata maana mpya.
Uundaji wa agoti miongoni mwa wafungwa ulikisiwa kuwa ni karibu sawa na uundaji wa
maneno katika jamii na hasa katika aina nyingine za misimbo. Kwa mujibu wa Jefwa (2010)
uundaji wa maneno ni uambatanishaji wa mofimu moja au zaidi kufikia kiwango cha mofimu
hiyo au hizo kuleta maana kileksika katika lugha yoyote ile. Kwa mujibu wa mtaalamu huyu,
mbinu za kimofolojia zitumikazo katika uundaji wa maneno katika lugha za ulimwengu ni
29
pamoja na: Unominishaji, ukopaji na utohozi, uhulutishaji, ukatizaji, akronimu, uambatanishaji
na uambishaji.
2.6.1 Ukopaji na utohozi
Ukopaji ni hali inayojumuisha uhamishaji wa kipashio fulani kutoka lugha moja na kukiingiza
katika lugha nyingine. Kwa hivyo, kuna lugha changizi na lugha pokezi (Jefwa, 2010). Hock na
Joseph (1996) wanasema kuwa ukopaji ni uhamishaji wa leksimu mahususi au seti ya leksimu au
faridi fulani kutoka lugha moja au lahaja moja hadi nyingine. Kuna aina mbili za ukopaji:
ukopaji sisisi na ukopaji tohozi. Ukopaji sisisi ni pale ambapo leksimu fulani inahamishwa
kutoka katika lugha changizi hadi lugha lengwa bila ya kufanyiwa marekebisho yoyote. Maneno
yanaweza kukopwa toka lugha ya Kiswahili au lugha ya Kiingereza. Kwa mfano neno wode
limekopwa toka neno la Kiingereza water.
2.6.2 Mbinu ya ukatizaji
Ukatizaji ni mbinu ya kuunda maneno kwa kuyafupisha. Katika mbinu hii vile vile, maneno
huundwa kwa kudondosha silabi moja au zaidi (Jefwa, 2010). Kwa mujibu wa TUKI (1990)
ukatizaji ni hatua ya kufupisha neno kwa kuondoa sehemu ya mwanzoni au mwishoni. Mbinu hii
ya uundaji wa maneno hutumika na lugha nyingi ulimwenguni. Lugha ya Kiingereza kwa mfano
imeunda maneno yafuatayo kutumia mbinu hii; bike inatokana na bicycle. Prof inatokana na
Professor.
2.6.3 Mbinu ya uambishaji
Kwa mujibu wa Jefwa (2010), uambishaji huwa utaratibu wa kuongezea viambishi katika mzizi
wa leksimu ili kuunda leksimu mpya. Mbinu hii hujumuisha viambishi awali na viambishi
tamati. Viambishi hivi huambishwa kwenye mzizi wa neno ili kuunda maneno mapya.
30
Matthews (1997) naye anaeleza ya kwamba uambishaji ni utaratibu wa kuongezea herufi, sauti
au makundi yao katika mzizi wa neno na kwamba nyongeza hiyo hubadilisha maana na uamilifu
wa neno hilo. Sheng kwa mfano huitumia mbinu hii ili kujiundia leksimu mpya. Hata hivyo
leksimu za Sheng zilizoundwa kwa mbinu hii huwa za mkopo. Kwa mfano msupa yenye maana
ya msichana imeundwa kwa uambishaji mofu (M+SUPA).
2.6.4 Mbinu ya ubadilishaji silabi
Ogechi (2005) anasema kwamba neno husika hukopwa kisha matamshi ya neno hilo
hurekebishwa kabla ya silabi za neno hilo kurekebishwa. Ubadilishaji silabi huu huwa utaratibu
wa kimakusudi ambao hutumiwa na Sheng kuundia leksimu zake. Kwa mfano bread kuwa dibre
na story kuwa risto.
2.6.5 Onomatopia: Tanakali za Sauti
Onomatopia pia hujulikana kama tanakali za sauti. Onomatopia ni ujenzi wa neno kwa kuiga
sauti au mlio wa kitu (TUKI, 2009). Mwangi na Mukhwana (2011) nao wanadai kwamba
onomatopea ni mbinu ya uundaji leksimu ambapo leksimu huundwa kutokana na sifa, uamilifu,
umbo, sauti au milio. Kuna madai mengine yanayosema kwamba onomatopia ni uundaji wa
maneno kutokana na sauti asilia. Kwa mfano neno kacha la Sheng linamaanisha pingu. Bling
bling nalo lina maana ya pambo ghali. Utafiti huu ulitaka kutambua ni mbinu zipi ambazo
hutumiwa katika kuunda agoti za wafungwa wa magereza ya Kisumu.
2.7 Pengo la utafiti
Kwa ujumla, lugha ya wafungwa ni moja kati ya maeneo ambayo yamefanyiwa utafiti katika
mataifa ya kimagharibi. Katika mataifa ya Afrika, tafiti kuhusu lugha za wafungwa ni chache
31
mno. Ilivyojitokeza, hakukuwa na ufafanuzi wowote wa kina uliowahi kutolewa kuhusu lugha
kama inavyotumika katika magereza ya mataifa ya Afrika Mashariki.
Hivyo, utafiti huu ulikusudia kuliziba pengo hili kwa kujadili vikoa maana katika agoti
zinazotumiwa miongoni mwa wafungwa wa magereza ya Kisumu, kujadili mabadiliko ya
kimaana katika agoti zinazotumiwa na wafungwa wa magereza ya Kisumu na hatimaye
kubainisha mbinu zinazotumiwa katika uundaji wa agoti za wafungwa wa magereza ya Kisumu.
2.8 Hitimisho
Katika sura hii mtafiti ameonyesha dhana muhimu katika utafiti huu na namna zilivyotumiwa na
watafiti wa awali. Amehakiki namna watafiti wa awali walivyoainisha vikoa maana vya agoti za
wafungwa wa mataifa yao, maana ya agoti hizo pamoja na michakato mbalimbali ya mabadiliko
ya kimaana. Pia, ameeleza mbinu mbalimbali za uundaji wa maneno kwa ujumla. Utafiti huu
ulichunguza namna hali hizi zinavyosadifu muktadha wa taifa la Kenya. Sura inayofuata
inajadili njia na mbinu za utafiti zilizotumiwa katika utafiti huu.
32
SURA YA TATU
MBINU ZA UTAFITI
3.1 Utangulizi
Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchanganua matumizi ya agoti miongoni mwa wafungwa
katika magereza teule ya jimbo la Kisumu, nchini Kenya. Kwa mujibu wa Mugenda na Mugenda
(2005), mbinu ya utafiti ni utaratibu makini wa kiuchunguzi unaotumia mbinu za kisayansi
zilizokubaliwa ili kutatua matatizo na kuibua ujuzi mpya. Sura hii imegawika katika sehemu
kumi na moja. Sehemu ya kwanza inatoa utangulizi wa sura, sehemu ya pili inafafanua mbinu za
utafiti. Sehemu ya tatu inaangazia eneo la utafiti na sehemu ya nne inaeleza kuhusu eneo la
utafiti. Katika sehemu ya tano, mtafiti anaangazia sampuli na usampulishaji. Sehemu ya sita
imeelezea vifaa vya utafiti. Sehemu ya saba imeshughulikia ukusanyaji wa data. Sehemu ya nane
imeelezea uchanganuzi wa data. Sehemu ya tisa mtafiti amefafanua jinsi vifaa vya utafiti
vilijaribiwa. Sehemu ya kumi inaeleza kuhusu maadili ya utafiti. Mwisho wa sura ni hitimisho.
3.2 Mbinu za utafiti
Kothari (2008) anaeleza kuwa mbinu za utafiti ni mwongozo uliopangwa kufuatwa katika
ukusanyaji na uchambuzi wa data ili kujibu maswali ya utafiti husika. Mtafiti alitumia
mahojiano katika utafiti huu. Kombo na Tromp (2006) wanaeleza kuwa mahojiano ni majibizano
ya ana kwa ana (au ya simu, barua, kidijiti/barua pepe) kati ya watu wawili au zaidi kwa lengo la
kukusanya taarifa au maoni kuhusu suala fulani la kiutafiti lililoainishwa. Utafiti huu ulitumia
mahojiano ya ana kwa ana. Kothari (2008) anasema kuwa, katika mahojiano ya ana kwa ana,
33
mtafiti huwauliza watafitiwa maswali na wakati mwingine watafitiwa nao huuliza maswali na
mtafiti huyajibu.
Mbinu hii iliteuliwa ili kupata uthabiti wa majibu ya watafitiwa pamoja na kupata uthabiti wa
mbinu za kukusanyia data. Pia, ilikuwa ni rahisi kwa mtafiti kuthibiti sampuli kwa usahihi zaidi.
Hii ilitokea kwa sababu mtafiti alikutana na wahojiwa ana kwa ana na kuwauliza maswali kisha
akarekodi majibu yao. Tatu, ni rahisi kwa mtafiti kukusanya taarifa nyingi kwa kina zaidi kwa
sababu watafitiwa wanaweza kuuliza maswali. Mtafiti pia huwa huru kuuliza maswali ya ziada
ambayo si rahisi kufanyika unapotumia mbinu nyingine kama hojaji au utazamaji nyanjani.
Mahojiano ya kimakundi pia yalitumiwa kupata data ya utafiti huu. Mahojiano ya kimakundi ni
njia ya kupata data inayohusisha maswali na majibu yanayofanywa kwa mazungumzo kati ya
mtafiti na kundi la watafitiwa (Kothari, 2008). Mbinu hii ilimsaidia mtafiti kupata taarifa za
msingi zilizohusiana na mada ya utafiti. Katika makundi hayo ilibainika kuwa wahojiwa
waliweza kuwarekebisha wenzao walipotoa maelezo ambayo hayakufaa. Kila awamu ya
mahojiano ya kimakundi ilihusisha watafitiwa kumi.
3.3 Muundo wa utafiti
Utafiti huu ulitumia muundo wa usoroveya elezi. Kwa mujibu wa Kombo na Tromp (2006)
muundo huu hutumiwa kupata data kuhusu mielekeo, maoni, mazoea na pia mambo muhimu
yanayohusu elimu na masuala ya jamii. Good (1972) ameeleza kuwa kwa kutumia muundo huu
wa usoroveya elezi, mtafiti anaweza kupata data ya kutathmini njia mbalimbali zinazotumiwa ili
kufikia uamuzi mwafaka. Kwa kutumia muundo huu, mtafiti alifanikiwa kupata habari kuhusu
agoti za wafungwa ikiwepo maana mbalimbali za agoti na maoni yao kuhusu lugha waliyotumia
katika muktadha wa jela.
34
Utafiti huu ulichukua mwelekeo wa utafiti nyanjani. Katika utafiti nyanjani, mtafiti huhusishwa,
hushirikishwa pamoja na kutangamana na watafitiwa. Lengo la kufanya hivi ni kudhihirisha hali
ilivyo na kutoa uamuzi kutegemea data iliyoshuhudiwa. Mkondo wa utafiti elezi ulichukuliwa
kwa kuwa utafiti elezi hunuia kueleza sababu, maoni, mitazamo na misukumo ya mambo
mbalimbali. Mugenda na Mugenda (2005) wanaeleza kuwa utafiti elezi ni uchunguzi wa vitu
katika hali zao asilia, na kujaribu kufasiri maana ambayo wanajamii huipa vitu hivyo.
3.4 Eneo la utafiti
Utafiti huu ulifanywa katika magereza makuu ya Kibos na Kodiaga. Gereza la Kibos lipo katika
jimbo la Kisumu takriban kilomita sita kutoka jiji la Kisumu (Owino, Omar na Akong‟a, 2015).
Mtafiti aliyachagua magereza haya kutokana na misukumo kadha. Kwanza, mtafiti aliishi katika
mazingira ya magereza haya kwa takriban miaka ishirini kwa jumla. Hivyo basi alikuwa katika
nafasi nzuri ya kuelewana na hata kuwasiliana na maafisa wa magereza hali iliyomrahisishia
ukusanyaji wa data. Pili, ni ukaribu. Ukaribu huu ulirahisisha utafiti wenyewe kwani ulimpa
muda mzuri wa kukusanya data. Eneo la Kibos lina magereza mawili lakini mtafiti alifanya
utafiti wake katika gereza kuu la Kibos. Kama ilivyotarajiwa, wengi wa wafungwa katika gereza
hili walikuwa wameishi gerezani kwa muda mrefu na hivyo kuwa wenye hazina kubwa ya
misamiati ya wafungwa gerezani.
Eneo la Kodiaga lina magereza matatu. Magereza mengine mawili hayakuteuliwa kuwa gereza
moja ni la wanawake. Mtafiti alikusudia kuchunguza agoti zilizotumiwa na wafungwa wanaume
tu. Gereza jingine ni gereza dogo. Wafungwa wa gereza hili hufungwa kwa miaka michache
hivyo basi walitarajiwa kutokuwa na umilisi wa lugha ya jela. Gereza kuu la Kodiaga liliteuliwa
35
kwa sababu huhifadhi wafungwa wanaohudumia miaka miaka mingi. Hawa walitarajiwa kuwa
na ujuzi mkubwa wa lugha ya jela.
3.5 Sampuli na usampulishaji
3.5.1 Usampulishaji
Sampuli iliyotumika katika utafiti huu ilitokana na makundi mawili ya kimsingi. Sampuli ya
watafitiwa na samupuli ya agoti zilizokusanywa kutoka kwa watafitiwa. Kwa mujibu wa Kothari
(2004), sampuli ni kundi dogo la kutafiti ambalo huchaguliwa kutoka katika kundi kubwa
ambalo kutoka kwalo mtafiti hupata data na kutoa mahitimisho yake. Sigh (2007) naye anaeleza
kuwa uteuzi wa sampuli ni mchakato wa kuteua kundi dogo kutoka kundi kubwa la watafitiwa ili
kulifanyia kundi lengwa makisio. Mugenda na Mugenda (2005) wanasema kuwa
kinachomwongoza mtafiti katika uteuzi wa sampuli yake ni sababu fulani maalumu aliyonayo.
Kwa mfano, anaweza kuteua kundi au sehemu fulani kwa sababu ni rahisi kwenda huko,
anapajua vizuri au mdhamini wake anapapendelea. Anateua wahojiwa kulingana na madhumuni
yake. Wahojiwa wanateuliwa kwa sababu wana taarifa au wana sifa anazohitaji mtafiti.
Katika utafiti huu mtafiti alitumia uteuzi wa sampuli kusudio kuteuwa watafiti na agoti za
kushirikishwa katika utafiti huu. Kwa mujibu wa Gall n.w. (1996) lengo la uteuzi wa sampuli
kusudio ni kuteua watafitiwa au vitu vya kutafiti ambavyo vina habari za kutosha katika
muktadha wa utafiti elezi.
3.5.2 Sampuli lengwa
Kwa mujibu wa Walliman (2011), sampuli au kundi lengwa ni jumla ya vitu vyote
vinavyohusika katika kufanyiwa utafiti, yaani taasisi, watu, vitu au matukio. Kimsingi, kundi
lengwa ni jumla ya walengwa wote wa utafiti ambapo sampuli inaweza kuchaguliwa. Sampuli
36
lengwa ya kwanza katika utafiti huu ni wafungwa wa magereza ya Kisumu. Kwa mujibu wa
ripoti ya Tume ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Kenya (KHRC, 2002), gereza la Kibos lina
wafungwa 647 ilhali gereza la Kodiaga lina wafungwa 1,206. Ni kutokana na sampuli hii lengwa
ambapo mtafiti aliteua sampuli ya kutafiti. Hili ndilo kundi ambalo yamkini ingeweza kutumia
agoti ambazo utafiti huu ulikuwa ukichunguza.
Sampuli ya pili ni jumla ya agoti ambazo mtafiti alikusanya kutoka kwa watafitiwa. Mtafiti
alikusanya jumla ya agoti 263. Kutokana na agoti hizi mtafiti aliteua agoti za kushirikishwa
katika utafiti.
3.5.3 Sampuli iliyoteuliwa
Gay na Diehl (1992) wanasema kuwa sampuli inayoteuliwa kutoka kwenye kundi lengwa
hutegemea aina ya utafiti. Katika utafiti elezi wanapendekeza kuwa sampuli iwe 10% ya kundi
lengwa. Kwa mwelekeo huu mtafiti aliteua wafungwa 185 kimakusudi ili kushiriki katika utafiti
huu. Yaliyozingatiwa ni: Sharti mtafitiwa angekuwa na miaka 18 au zaidi, sharti mtafitiwa
angekuwa amehudumia kufungo katika gereza hilo kwa zaidi ya miaka mitatu. Kigezo cha miaka
mitatu kilihakikisha kuwa mtafiti aliwahoji watatifitiwa wenye umilisi wa agoti za wafungwa.
Kati ya agoti 263 mtafiti aliteua agoti 188 zilizoshirikishwa katika utafiti huu. Agoti hizo 188
ziliteuliwa kimakusudi kwa sababu zilikuwa na sifa alizotaka mtafiti. Agoti hizo zilikuwa ni
leksimu za Kiswahili, Sheng au leksimu zilizoundwa kwa kuachanganya Kiswahili na lugha
nyingine. Agoti zingine 75 hazikushirikishwa katika utafiti kwa sababu zilikuwa aidha za
Kiingereza au lugha za kienyeji. Mtafiti alijikita katika virai nomino na virai vitenzi tu.
37
3.6 Vifaa vya kukusanya data
Vifaa alivyotumia mtafiti ni kalamu na daftari. Kila mara watafitiwa walipojibu swali mtafiti
alilinakili kwenye daftari. Japo kinasa-sauti kingefaa zaidi katika kunasa na kurekodi sauti na
hali zote za muktadha wa mahojiano baina ya mtafiti na watafitiwa, ilibainika kuwa sheria
hazikuruhusu vyombo kama hivyo kutumiwa gerezani. Hata hivyo, mtafiti aliweza kuvitumia
vifaa alivyokuwa navyo vizuri kwa kunakili kila hoja na ufafanuzi uliotolewa na watafitiwa.
3.7 Ukusanyaji wa data
Kabla ya kuanza utafiti rasmi, mtafiti alikuwa katika harakati za kukusanya agoti zilizokuwa
zikutumiwa na wafungwa kwani aliishi katika mazingira hayo ya jela. Alizikusanya data hizo za
awali alipowasikia wafungwa wakiwasiliana katika maeneo yao ya kazi. Hata hivyo, katika
ukusanyaji rasmi wa data, mtafiti alitumia jumla ya miezi miwili katika kukusanya data yake.
Kila alipokusanya data mtafiti alishirikiana na maafisa wa magereza kuwateua wahojiwa ambao
wangeshiriki katika usaili. Mwongozo ule ule wa usaili ndio uliotumiwa katika mahojiano ya
kimakundi. Kati ya sampuli ya watafitiwa 185, mtafiti atulitumia mahojiano ya ana kwa ana
kukusanya data kutoka kwa watafitiwa 105. Mahojiano ya kimakundi yalitumiwa kukusanya
data toka kwa watafitiwa 80. Mahojiano haya ya kimakundi katika kila gereza yaliwashirikisha
watafitiwa 10 katika kila awamu.
3.8 Uchanganuzi wa data
Kwa mujibu wa Kothari (2008), uchanganuzi wa data ni kitendo cha kufupisha na kupangilia
vizuri data ambayo imekusanywa kwa njia ambayo inasaidia kujibu maswali ya utafiti husika.
Hii ni hatua muhimu katika kupata majibu ya maswali ya utafiti (Bogdan na Biklen, 1992).
38
Utafiti huu ulitumia mkabala wa kimaelezo katika kuchanganua data. Enon (1998) anasema
kwamba mkabala huu ni mbinu ya kuchanganua data ambapo mtafiti huieleza data yake
kimaelezo. Kress (2008) kwa upande wake anafafanua mkabala huu kwa kusema kuwa unaeleza
vipi na ni kwa nini matukio yametokea. Mtafiti alitumia mkabala huu kwa sababu majibu
yalihitaji maelezo ya kina kuhusu agoti za wafungwa pamoja na maana yazo. Kimsingi, data
iliwasilishwa kwa kutumia majedwali kisha maelezo yakatolewa baadaye.
Aidha, data ilichanganuliwa kwa misingi ya Nadharia ya Pragmatiki Leksika. Kipengele cha
semantiki leksika kilitumiwa kutambua vikoa maana katika agoti za wafungwa na kuanisha agoti
hizo katika kila kikoa cha maana. Kipengele cha michakato ya kipragamtiki leksika kilitumiwa
kufafanua mabadiliko ya kimaana katika agoti za wafungwa. Hatimaye, kipengele cha ubunaji
mpya wa maana na uundaji wa leksimu kama aina ya upanuzi wa maana kilitumiwa kujadili
mbinu za uundaji wa agoti katika muktadha wa magereza. Data ilichanganuliwa kwa
kuiambatanisha na mifano mahususi ili kuithibitisha mada ya utafiti.
3.9 Majaribio ya vifaa vya utafiti
Wiersman (1985) anaeleza kuwa majaribio ya utafiti hubainisha udhaifu wa vifaa vya utafiti na
kurekebisha makosa yaliyomo kabla ya kuvitumia katika utafiti wenyewe. Majaribio hayo pia
hudhihirisha uhalali na utumainifu wa vifaa hivyo. Mtafiti aliifanyia mwongozo wa mahojiano
majaribio i1i kuhakiki uhalali na utumainifu wake. Mtafiti aliwatumia raia wanne aliowafahamu
ambao waliwahi kuhudumia vifungo vya jela. Kabla ya majaribio, mwongozo wa mahojiano
ulikuwa na sehemu iliyowauliza watafitiwa majukumu ya agoti. Baada ya majaribio, sehemu hii
iliondolewa kwa sababu haikusaidia katika kupata agoti kutoka kwa watafitiwa.
39
3.9.1 Uhalali
Kulingana na Orodho (2005), uhalali ni kiwango ambacho vifaa vya utafiti vinatumika
vinavyofaa.Vifaa hivi sharti vichunguzwe uhalali wao kabla ya kutumiwa katika utafiti kamili.
Swala kuu la kuzingatia ni uhalali wa vifaa hivyo katika mada husika. Majaribio yalifanyiwa
vifaa vya utafti kukadiria uhalali ili kuhakikisha maswali yalilenga mada. Uhalali pia ulitathmini
kiwango cha lugha katika hojaji. Jedwali sailifu lilitumiwa kuchunguza ufaafu wa maswali
yaliyokuwa katika hojaji. Wasimamizi wa mtafiti pia walichunguza uhalali wa maswali
yaliyokuwa katika hojaji. Baadaye mwongozo sahihi wa mahojiano ulitayarishwa ili kutumika
katika ukusanyaji wa data nyanjani.
3.9.2 Utumainifu
Utumainifu wa vifaa ni kiasi ambacho vifaa vya utafiti vinaweza kuleta matokeo yaleyale
vinapotumiwa mara kadha (Orodho, 2005). Kulingana na Mugenda na Mugenda (2003)
utumainifu ni kiwango ambacho vifaa vya utafiti vinazalisha matokeo yanayotegemewa kila
wakati vinapotumiwa. Mbinu ya majaribio ya kurudiwa hutumiwa kwa kundi husika kukiwa na
mpito wa wakati baina ya jaribio la kwanza na la pili. Kipimo cha Pearson kinaruhusu kiwango
kati ya 0.5 na 1, (Ingule na Gatumu, 1996). Katika kuhakikisha utumainifu, majaribio yalifanywa
kwa kurudiwa kwa wafungwa wanne waliokwisha funguliwa. Matokeo ya majaribio katika
kipimo cha uwiano yalionyesha kuwa mwongozo wa mahojiano ungeweza kutegemewa katika
kufanya utafiti.
40
3.10 Maadili ya utafiti
Ukusanyaji wa data kupitia mbinu yoyote ile huhitaji kuzingatia maadili kwa upande wa
watafitiwa, mtafiti na katika mchakato wa utafiti (Mulokozi, 2003). Utafiti huu ulizingatia
maadili kama yafuatavyo;
3.10.1 Maadili ya utafiti yanayomhusu mtafiti
Mtafiti aliandika barua ya kujitambulisha na kuomba kibali cha kukusanya data kutoka kwa
Halmashauri ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi. Halmashauri hii ilimpa barua na
cheti cha idhini ya kukusanya data gerezani (Taz. Kiambatisho III na IV). Kabla ya utafiti,
mtafiti aliwasiliana na kujitambulisha kwa mkuu wa jimbo la Kisumu. Mkuu wa jimbo alimpa
mtafiti idhini ya kukusanya data kata jimbo la Kisumu (Taz. Kiambatisho II). Hatimaye mtafiti
aliandika barua kwa mkuu wa magereza nchini ili kukusanya data kutoka kwa wafungwa. Idara
ya magereza nchini ilimpa mtafiti idhini ya kuingia katika magereza ya Kisumu na Kibos
kukusanya data.
Kabla ya kukusanya data mtafiti aliwatembelea wakuu wa magereza ya Kodiaga na Kibos na
kuwafafanulia sababu za kufanya utafiti pamoja na kuwaeleza kuhusu vifaa ambavyo angetumia
kukusanya data.
3.10.2 Maadili ya utafiti yanayohusu watafitiwa
Mtafiti alijitambulisha kwa watafitiwa kwa kuwaonyesha kitambulisho chake cha kitaifa na kwa
kuwaonyesha barua kutoka Halmashauri ya Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi iliyompa kibali
cha kufanya utafiti katika magereza ya Kisumu.
Kila siku kabla ya kuwahoji watafitiwa, mtafiti aliwaeleza watafitiwa sababu za kukusanya agoti
na kuwahakikishia kuwa utafiti ule ulikuwa wa kiakademia tu na wala majina yao
41
hayangechapishwa popote. Mtafiti hakuwalazimisha watafitiwa kushiriki katika utafiti (Taz.
Kiambatisho VI).
3.10.3 Maadili ya utafiti yanayohusu mchakato wa utafiti
Utafiti huu ulizingatia maadili ya utafiti kwa kunukuu kazi za kitaaluma zilizohusiana na mada
ya utafiti. Vilevile, utafiti huu uliweka wazi matokeo ya utafiti na kupendekeza sehemu ambazo
zingeweza kufanyiwa utafiti wa baadaye kuhusiana na mada ya utafiti.
3.11 Hitimisho
Kwenye sura hii ya tatu mtafiti ameelezea njia na mbinu mbalimbali za utafiti alizotumia katika
kukusanya data pamoja na vifaa vilivyotumiwa wakati wa kukusanya na kuchambua data. Mbinu
hizi ndizo zilizomwongoza mtafiti katika kukusanya na kuchanganua data. Katika sura
inayofuata, yaani sura ya nne, data iliyokusanywa kwa kutumia mbinu zilizojadiliwa katika sura
hii itachanganuliwa.
42
SURA YA NNE
UWASILISHAJI NA UCHANGANUZI WA DATA
4.1 Utangulizi
Lengo la sura hii ni kuwasilisha na kuchambua data iiliyokusanywa kuhusu agoti za wafungwa
katika magereza teule ya jimbo la Kisumu. Kwa mujibu wa Kombo na Tromp (2006) uchambuzi
wa data ni kuchunguza kwa undani data iliyopangwa na kuitolea mahitimisho. Wanasema kuwa
uwasilishaji wa data ni namna ya kupangilia data ili ieleweke vizuri. Data yote ambayo
ilikusanywa kwa njia ya mahojiano ya kimakundi na usaili imewasilishwa na kuchambuliwa kwa
kina katika sura hii.
Mtafiti alitumia data ya msingi. Vartanian (2011) anaeleza kuwa data ya msingi ni ile ambayo
mtafiti ameikusanya kwa kutumia mbinu kama hojaji, vikundi lengwa, uchunzaji au mbinu
nyinginezo. Hii ni data ambayo hutoka moja kwa moja kwa mtafiwa. Mtafiti aliwasilisha
matokeo yake kulingana na madhumuni mahususi ya utafiti huu pamoja na maswali
yaliyoambatana na madhumuni hayo. Mgawanyo huu ulimpa nafasi ya kuchanganua data kwa
urahisi. Baada ya kuwasilisha matokeo, mtafiti aliyajadili moja kwa moja. Sura hii ina sehemu
tano. Sehemu ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Sehemu ya pili inaangazia vikoa maana katika
agoti za wafungwa. Sehemu ya tatu inawasilisha na kuchambua data kuhusiana na mabadiliko ya
kimaana katika agoti za wafungwa. Katika sehemu ya nne mtafiti alishughulikia uundaji wa agoti
za wafungwa. Sehemu ya tano ya utafiti huu ni hitimisho la sura.
43
4.2 Vikoa maana katika agoti za wafungwa
Semantiki kileksika inajishughulisha na maana ya maneno. Maneno huweza kuchukuliwa
kuashiria vitu katika ulimwengu au katika dhana kutegemea mtazamo mahususi wa semantiki
kileksika. Kwa mujibu wa Mmbwanga (2010) vitengo vya maana katika semantiki kileksika ni
vitengo vya kileksika ambavyo kwavyo msemaji huweza kuongezea kwa mfululizo maishani
pamoja na ujifunzaji wa maneno mapya na maana hayo.
Semantiki kileksika kama kipengele cha Nadharia ya Pragmatiki Leksika ilimsaidia mtafiti
katika kuanisha agoti za wafungwa katika vikoa maana mbalimbali. Maneno yaliyowekwa
katika kikoa kimoja yalikuwa na uhusiano wa kimaana. Dhana ya kikoa maana ya semantiki
ilitumiwa kuweka maneno katika matapo mbalimbali lakini maana ya maneno yalifafanuliwa
kimuktadha.
Uchanganuzi wa data ulidhihirisha vikoa maana mbalimbali vya agoti za wafungwa wa
magereza ya Kisumu. Pallock (2006) anaeleza kuwa misimbo hutumiwa katika tamaduni za
wafungwa ulimwenguni kote na zinaweza kuainishwa katika vikoa mbalimbali tokea vyakula
hadi kwa maafisa wa magereza. Katika utafiti huu agoti za wafungwa zimepangwa katika vikoa
vya: mahusiano ya kimapenzi, marufuku na dawa za kulevya, mambo na shughuli za jela, agoti
zinazorejelea wafungwa, maafisa wa megereza na hatimaye tulichanganua agoti zaidi tulizopewa
na wahojiwa.
Katika utafiti huu ukoa wa maana ulitumika kurejelea mahusiano yanayotokana na seti yoyote ile
ya msamiati na hivyo basi kuwa katika kundi maalum la kimantiki.
44
4.2.1 Kikoa cha mahusiano ya kimapenzi
Baadhi ya wahojiwa walikiri kuwa palikuwepo na mahusiano ya kimapenzi katika magereza.
Mhojiwa mmoja alieleza kuwa, „Mahusiano hapa jela ni kitu cha kawaida kama vile kuna
marelationships pale nje‟. Yaani, mahusiano hapa gerezani ni jambo la kawaida jinsi yalivyo
mahusiano miongoni mwa raia. Mhojiwa mwingine alishadidia kwa kueleza kuwa „Hiyo ni
kawaida ya life. Hapa ndani mafeelings zetu hazijafungwa. Kwa hivyo mahusiano yapo‟. Yaani
„Hiyo ni kawaida ya maisha. Hapa gerezani hisia zetu hazijafungwa kwa hivyo mahusiano yapo.‟
Hata hivyo mhojiwa huyo alisisitiza kuwa mahusiano hayo ni ya viwango. Kulikuwa na urafiki
wa kawaida na uadui wa kawaida. Wafungwa wengine walihusiana kimapenzi japo ni kinyume
cha sheria za magereza.
Mhojiwa mwingine alisema kuwa, fikra kuhusu usenge unaoendelea gerezani wakati mwingine
hutiliwa chumvi kwa kuwa si kila mfungwa huwa na mahusiano ya kimapenzi. Kuhusiana na
maneno yanayotumiwa kurejelea mahusiano kwenye jela, wahojiwa walifafanua maneno
yafuatayo:
Jedwali 4.01: Agoti zinazohusu mahusiano
Agoti Maana
Mtoto/kijana/mwana/maua Mfungwa anayetekeleza majukumu ya
„mke‟ katika mahusiano ya kimapenzi
gerezani
Mende/ongosh
Mfungwa anayetekeleza majukumu ya
„mwanamume‟ katika mahusiano ya
kimapenzi gerezani
45
Gundu Kisirani anachokuwa nacho mfungwa baada
ya tendo la ngono
Kutiana Tendo la ngono. Kufirana.
Kukula biskuti Kupiga punyeto
Marufuku
Mfungwa ambaye amekuwa na mahusiano
mengi ya kimapenzi
Malaya Mfungwa anayetoa siri kwa maafisa wa
magereza
Kuchange quarter Watoto au maua wawili wanaposhiriki
katika ngono
Kunyemelea
Mfungwa kumshurutisha mfungwa
mwenzake kushiriki ngono. Ubakaji.
Jedwali 4.01 linaonyesha agoti zinazohusu mahusiano ya kimapenzi gerezani. Kwa sababu
maneno haya yanarejelea masuala ya kimapenzi mtafiti aliongozwa na kipengele cha Semantiki
Kileksika katika kuziweka katika kikoa kimoja cha maana. Maana kuu katika tapo hili ni
mahusiano ya kimapenzi. Chini ya dhana ya mahusiano ya kimapenzi mna leksimu ambazo
zinarejelea hali mbalimbali za mahusiano katika jela.
Neno mende au ongosh linarejelea basha. Mtoto/kijana/mwana/maua ni lekzimu zinazotumiwa
kurejelea yule mfungwa anayetekeleza majukumu ya mwanamke katika mahusiano ya kimapenzi
gerezani. Gundu ni kisirani anachokuwa nacho mfungwa baada ya tendo la ngono. Kuchange
quarter ni hali ambapo wafungwa wawili wanaume ambao hutekeleza majukumu ya kike katika
mahusiano ya kimapenzi wanaposhiriki ngono. Kukula biskuti nako ni kupiga punyeto.
46
Marufuku ni kama malaya katika Kiswahili sanifu. Agoti hizi zinahusiana kwa sababu zote
zinahusu mahusiano ya kimapenzi.
Leksimu hizi zilidhihirisha moja kati ya mambo mengi machungu katika jela, wafungwa
kunyimwa mahusiano ya kawaida ya kimapenzi. Data ilidhihirisha kuwa kunyimwa huku kwa
mahusiano ya kawaida ya kimapenzi huwaelekeza baadhi ya wafungwa kushiriki katika mapenzi
wenyewe kwa wenyewe ili kuziba pengo hilo. Leksimu nyingi zilipatikana kushadidia
mahusiano haya. Kutiana ni neno ambalo hutumiwa kurejelea hali ya kufirana.
Data ilidhihirisha kuwa kama ilivyo uraiani, mna umalaya gerezani. Mfungwa ambaye ana
mahusiano mengi ya kimapenzi anarejelewa kama marufuku. Mtafiti alipata kuwa hali hii
hutokea mfungwa huyo anapokuwa ni mnyonge sana au hana pesa na inambidi ajihusishe
kimapenzi ili apate baadhi ya mahitaji kama vile dawa za kulevya.
Istilahi hizi zinaelekea kufanana na tafiti zilizofanywa na wanaisimu mbalimbali katika mataifa
tofauti. Hensley n.w. (2003) walipata istilahi anuwai katika kikoa cha mapenzi na mahusiano.
Katika utafiti huu mfungwa mwanamume ambaye katika ushoga hutekeleza majukumu ya
mwanamume huitwa mende. Henseley n.w. (2003) walibaini kuwa huyu huitwa punk. Gohodzi
(2013) naye alipata kuwa mfungwa huyu huitwa Nqondo kule Zimbabwe. Kama katika utafiti
wa Gohodzi msenge hurejelewa kama mwana.
Hata hivyo, tofauti na tafiti za awali, utafiti huu ulipata maneno machache katika kikoa hiki cha
mahusiano na mapenzi. Pengine hali hii ilitokana na ukweli kuwa maafisa waliowalinda wale
wafungwa walisimama karibu sana wakati wa mahojiano na baadhi yao walitega masikio
kusikiza yale tuliyokuwa tukiyazungumzia. Hali hii pia huenda ilitokana na kutoshabikiwa kwa
tendo hili.
47
Uchache wa istilahi kwenye kikoa hiki unaingiliana na kazi ya Einat & Einat (2000) ambao
walipata kuwa maneno yanayohusiana na ngono ndiyo yaliyokuwa machache mno. Isitoshe,
kutumiwa kwa neno malaya kurejelea msaliti miongoni mwa wafungwa unaingiliana na kazi ya
Einat & Einat (2003) ambao walipata kuwa maneno ambayo awali yalitumika kurejelea ngono
katika muktadha wa jela siku hizi hutumiwa kukashifu baadhi ya matendo mabaya gerezani
kama usaliti wa kutoa siri kwa askari.
4.2.2 Kikoa cha marufuku na dawa za kulevya
Watafitiwa waliombwa kufafanua istilahi zilizohusiana na marufuku pamoja na dawa za kulevya.
Jedwali 4.02: Agoti zinazohusu marufuku na dawa za kulevya
Agoti Maana
Mzigo Marufuku
Charaza Wembe
Redio Simu
Gari/ndechu/waya/mongorio Simu
Ruara Dawa za kupiga chafya
Ndovu Dawa ya kulevya ambayo hutiwa ndani ya
mdomo wa chini
Unga Kokeni
Shetani mwekundu Dawa za wendawazimu ambazo wafungwa
hutumia ili kulewa
Bichi Pombe ambayo imetengezwa na chachu
Tei/wode Pombe
48
Stimu Kileo chochote
Waya/makuti Kifaa kinachotengezwa na mfungwa na
ambacho hutumiwa kuwasha sigara.
Gwara/ngwara/rwanga Chuma kinachonolewa na kutumiwa kukata
mfungwa mwingine wanapokosana
Boza/widi/godee/bata Bangi
Tinga Kifaa cha kuwasha sigara
Kochipo Bangi iliyochanganywa na kiraiko
Gife/kuku/nogwez Sigara
Buti/mtaro Shimo katikati ya makalio ambamo
marufuku hufichwa
Kinena Sehemu ya mbele ya tupu ya mwanamume
ambamo marufuku hufichwa
Kapiece/kapienga Kijisehemu cha chochote, hasa sigara au
bangi
Tigris Jiko lililotengezwa kistadi na wafungwa
ambalo hutumiwa kupikia ndani ya seli
kinyume na sheria
Jedwali 4.02 linaonyesha maneno katika kikoa cha marufuku. Maana ya jumla ya kikoa hiki ni
marufuku, yaani, vitu ambavyo usimamizi wa jela hauruhusu viwe katika mazingira ya jela.
Chini ya maana hii kuu kuliainishwa mitandao ya leksimu mbalimbali ambazo zilipigwa
49
marufuku na usimamizi wa magereza. Agoti katika kikoa hiki ni zile zinazorejelea dawa za
kulevya na silaha mbalimbali ambazo wafungwa hutumia katika muktadha wa jela.
Data ilishadidia kauli ya Bondesson (1989) kuwa dawa za kulevya ni uti wa mgongo wa
utamaduni wa jela. Wafungwa hutumia dawa za kulevya ili kupunguza uchungu na utamaushi
wao gerezani. Ilidhihirika kuwa ulimwengu wa jela ni wa dawa za kulevya kutokana na istilahi
nyingi za dawa za kulevya zilizofafanuliwa katika jedwali 4.02.
Data ilidhihirisha kuwa marufuku katika jela yanaweza kuwekwa katika vikoa zaidi vya maana.
Kwa mfano, majina ya dawa za kulevya boza, widi, godee, bata au kochipo ni maneno ambayo
hurejelea bangi. Tei ni pombe na ruara ni dawa za kupiga chafya. Bichi ni pombe ambayo
imetengezwa na chachu. Sigara hurejelewa kama kuku, fegi au gife. Pia pana kikoa cha silaha ;
Waya ni kifaa maalumu kinachotengezwa na mfungwa na ambacho hutumiwa kuwasha sigara.
Kifaa hiki pia huweza kurejelewa kama makuti. Gwara au ngwara ni chuma kinachonolewa na
kutumiwa kumkata mfungwa mwingine wanapokosana. Wembe hurejelewa kama charaza.
Agoti hizi zilizorejelea silaha zilidhihirisha kuwa jamii ya jela imesheheni vita au
mashambuliano ya mara kwa mara miongoni mwa wafungwa.
Uchanganuzi wa data pia ulibaini kuwa maneno yanayohusu dawa za kulevya zaidi yalikopwa
kutoka katika msimbo wa Sheng. Kwa mfano maneno steam, tei na ruara hutumika pia na
vijana katika mawasiliano yao. Hata hivyo, maneno yaliyohusu silaha yalipatikana kuwa
yalibuniwa au yalibadilishwa kwa mfano, neno charaza hutumiwa kurejelea wembe.
Umuhimu wa dawa za kulevya unajitokeza kutokana na istalahi zilizoteuliwa kutumiwa. Kwa
mfano, bangi inarejelewa kwa maneno matano, boza, godee, widi, bata na kochipo. Huenda
uraibu huu unashabikiwa sana kifungoni.
50
4.2.3 Kikoa cha mambo na shughuli za jela
Katika kikoa hiki wahojiwa walitupa istilahi zifuatazo pamoja na maelezo yaliyoandamanishwa.
Jedwali 4.03: Agoti zinazohusu mambo na shughuli za jela
Agoti (Nomino/Virai Nomino) Maana
Rotiko Korti
Mchwaa Mpesa
Baraza Mkutano wa wafungwa ambao mwenyekiti
wake huwa mfungwa msimamizi wa nyumba
Bukta Suruali ya kulalia
Kunguru Vazi la mfungwa linalovaliwa gerezani
Ugali/maharagwe/ mchele ya pan Chakula spesheli. Hukaangwa vizuri kwa
mafuta ya kutosha
Dondo Maharagwe
Sembe /mbese Ugali
Kibaba Kipimo kinachofanana na kifuniko cha chupa
ya soda ambacho hutumiwa kumpimia
mfungwa mafuta ya kutia kwenye chakula
Breki Viatu vinavyotengezwa kwa gurudumu la gari
na hutumiwa kufunga mlango kwa ndani ili
askari asiweze kuingia kwenye seli
Chepechepe/Chebechebe/mawetete
Chakula spesheli kilichoandaliwa vizuri
51
Kisuguu Mnara wa ulinzi
Baruti Pilipili inayotiwa kwenye chakula
Mtoto ya laini Mtoto wa askari
Nchi ingine Uraiani
Jela ya kazi Jela ndogo
Jela ya kupumzika Jela kubwa kama gereza la Kamiti, Kibos au
Kodiaga
Randa Kiboko
Neti/ngome/chimano/shamba ya mawe/ nchi
ya saba/Zimbabwe/
Jela
Shamba ng‟aa Shamba linalolimwa gerezani. Neno hili
hutumika tu katika gereza la Kibos
Njugu mawe Mahindi ambayo hayajaoza
Biskuti Mahindi ambayo yameoza
Mpesa Karatasi
Kiswahili Ujanja/uongo
Taukuz Ukuta
Mruru Mkebe ambamo mfungwa huwekewa chakula
Pengle/kipengele Kifuniko cha mruru
Bakuli Kijisahani cha kutia mboga
Dishi Chakula
Frayola Chakula kilichokaangwa
Kijiko Kifaa cha kupima chakula
52
Skanja Kifaa cha kushikilia chochote kilicho moto
Chedes/chapenda Pesa
Sheria za nyumba Zile sheria wanazozitunga wafungwa
kuwaongoza katika seli zao
Lota Mikebe wanayotumia wafungwa waislamu
kubeba maji wanapokwenda msalani
Ikulu Maeneo mazuri (kona nzuri) kwenye seli
ambamo wafungwa wenye ushawishi au wenye
nguvu hulala.
Dhochi Lugha isiyoeleweka
Bangili/chegere Pingu
Banda Sehemu katikati ya wadi mbili ambamo
wafungwa huota jua
Agoti (Vitenzi/Virai vitenzi) Maana
Kumaliziwa Ile hali ya korti ya mwisho kuhakikisha kifungo
hata baada ya kukata rufaa
Kukwachua Kupata pesa kotoka kwa raia kwa njia za
kilaghai / kutapeli
Kukaa na ndoo Kuketi tu bila kuwa na shughuli yoyote.
Kupitisha wakati
Kuonwa Kutembelewa na watu kutoka uraiani
Tero Wafungwa kufanyiwa upekuzi
Kibitiko Kupigwa kinyama
53
Kukata Kiswahili/kuongeza Kiswahili Kumsingizia mfungwa ili achapwe.
Kudanganya kwa kutumia ujanja
Kuunganisha propaganda Kumsingizia mfungwa ili achapwe
Kuweka mawe Kuomba msamaha au kufinyilia kitu kibaya
kisijulikane
Kukaba Kuchutama ukisubiri maelekezi
Kuingia block Askari kufanya upekuzi kwenye seli
Tuone ukae
Toa pesa au hongo ndipo uishi vizuri gerezani
kama mfungwa
Kutoboa Kumaliza kifungo
Kutoboa namba Kujifanya kuwa mgonjwa ndipo usifanye kazi
(jela ndogo)
Kuenda Kenya
Kuenda uraiani, kufunguliwa jela, kumaliza
kifungo
Kugenya Kufa
Kuuza mtu Kumtilia mtu ujanja ili apigwe na askari
Kunyeshewa na randa Kupigwa au kuchapwa na askari
Kusaidiwa hosii Kupewa ruhusa ya kuenda hospitalini
Kukula copper Kupigwa risasi
Kuingiza boot/buti Kuficha kitu kwenye njia ya choo
Kukaa kisuguu/kutower Mfungwa kuwachungulia askari ili wenzake
wanaofanya kitu kinyume na sheria za jela
wasipatikane
54
Semantiki kileksika inajuhusisha na maana ya maneno. Dhana kuu katika kikoa hiki ni shughuli
na mambo mbalimbali ambayo hupatikana katika jela. Leksimu katika kikoa hiki zinahusiana
kwani zinaonyesha jinsi mambo mbalimbali yanavyorejelewa katika jela.
Kikoa hiki kilitenganishwa katika viwango viwili. Kitengo cha kwanza ni Virai Nomino ambapo
mtafiti amefafanua namna vitu mbali mbali hurejelewa na wafungwa. Kikoa hiki kinaweza
kuainishwa katika vikoa zaidi. Palidhihirika maneno yaliyorejelea vyakula; dondo, ugali ya pan,
sembe, mbese, baruti, dishi, frayola. Maneno yaliyorejelea jela au sehemu za jela; kisuguu, jela
ya kazi, jela ya kupumzika, neti, ngome, chimano, shamba ya mawe, ikulu, banda n.k.
Katika kitengo cha pili mtafiti alifafanua virai vitenzi katika lugha ya wafungwa. Hapa alielezea
namna vitendo mbalimbali hurejelewa na wafungwa gerezani. Kwa mfano kukaa kisuguu ni
mfungwa kukaa chonjo akiwachungulia askari ili wenzake wanaofanya kitu kinyume na sheria
ya jela wasipatikane. Kunyeshewa randa humaanisha kupigwa au kuchapwa na askari.
Kusaidiwa hosii nako ni kusaidiwa ruhusa ya kuenda hospitali. Kukula copper ni kupigwa risasi.
Kutoboa ni kumaliza kifungo.
Katika utafiti huu, kikoa hiki ndicho kilichotokea kuwa na agoti nyingi. Hii ni tofauti na maelezo
ya Mulvey (2010) kuwa maeneo yenye istilahi nyingi katika lugha ya wafungwa ni kitengo cha
mahusiano na dawa za kulevya. Hata hivyo mtafiti alikubaliana na Looser (2001) kwamba kama
mfungwa anaponigiliana na mazingira yake mapya anakumbana na mazingira mapya pamoja na
michakato mipya. Lugha yake sharti iunde maneno mapya na kuyapa maana. Anaeleza kuwa
„mwingiliano wa kitawi huhitaji maneno ya kipekee‟. Maneno mengi ya kipekee yanayotumiwa
katika muktadha wa jela yalibainika.
55
4.2.4 Kikoa cha wafungwa
Wahojiwa waliulizwa kueleza na kufafanua maneno ambayo wao hutumia kuwarejelea
wafungwa wenzao. Istilahi zifuatazo zilipatikana:
Jedwali 4.04: Agoti zinazowarejelea wafungwa
Agoti Maana
Maisha Wafungwa wanaohudumia vifungo vya maisha
Roho geng/roho Wafungwa wanaofanya kazi kwenye maghala
ya jela
Wasanii/wadhii/wanaboma Wafungwa
Warogoti Wafungwa ambao hukusanya mabakuli
Mfungwa staff Mfungwa ambaye ana hadhi katika jela. Si
lazima awe ana cheo. Hadhi hii inaweza
kutokana na mfungwa huyo kuwa na fedha
nyingi
Mwewe Mfungwa mlafi, asiyeshiba. Hana uwezo wa
kununua chakula. Aghalabu umasikini huo
hutokana mfungwa husika kutotembelewa
Nyoka/kanyoz Mfungwa anayependa kutoa siri kwa askari.
Msudi Mfungwa anayependa kutoa siri kwa askari.
Anayepeleka kiswahili kwa wakubwa
Trekta Mfungwa mgeni. Ndiye hufanya kazi sana
Mashujaa Wafungwa ambao wameishi sana gerezani
56
Mijikumi/wazee wa nyumba Wafungwa ambao hawana cheo lakini wanapata
heshima kutokana na miaka yao. Hasa wa miaka
themanini au zaidi.
Mzee wa mtaa Ana hadhi sawa na ya mijikumi
Mzee wa boma Ni wafungwa ambao wamekaa sana kwenye jela
Kurutu
Mfungwa mpumbavu. Hajui mambo mengi
kwenye jela
Mabuluu / Nguo ya matress
Wafungwa wanaoaminiwa zaidi kwenye jela. Ni
cheo cha juu zaidi wanachopewa wafungwa
wasimamizi
Majani Wafungwa ambao huvaa beji la kijani kibichi.
Kiherehere Mfungwa anayeteuliwa na askari kufanya kazi
fulani ya kiusimamizi. Aghalabu husababisha
wafungwa wengine kuchapwa
Kairo Ni kundi la wafungwa wanaosafisha vyoo
gerezani
Kisuguu Mfungwa anayeketi kuwachunga wafungwa
wengine wasivuke mipaka/ukuta wa jela. Pia
humrejelea mfungwa anayechungulia ili askari
asiwapate wenzake wanaokikuka sheria
Mahuru/sugu Mfungwa mwenye kichwa kigumu ambaye
amezoea kufanya mambo kiyume na sheria za
magereza
57
Mahuru ya jela
Mfungwa ambaye hata baada ya kufunguliwa
hufungwa tena na tena
Wazuri/malaika Wafungwa wazuri wasioasi
Simu Mfungwa anayewaita wafungwa
wanapotembelewa na wageni kutoka uraiani
Geng‟ Kundi la wafungwa wanaofanya kazi pamoja
Maana kuu katika agoti zilizo kwenye Jedwali 4.04 ni majina ya wafungwa. Chini ya dhana hii
kuu mtafiti alianisha agoti mbalimbali ambazo wafungwa huwarejelea wafungwa wenzao katika
mazingira ya jela. Wafungwa wenyewe hujirejelea kama wasanii, wadhii au wanaboma.
Wafungwa wenye kichwa kigumu hurejelewa kama mahuru. Mahuru ya jela ni wale wafungwa
ambao hata baada ya kufunguliwa hukamatwa na kufungwa tena. Kisuguu ni yule mfungwa
ambaye huketi akiwachunga wafungwa wengine wasivuke mipaka ya jela au wasipatikane na
askari wanapofanya jambo lililo kinyume na sheria za jela. Malaika ni wale wafungwa wazuri
ambao wanachukuliwa kuwa hawafanyi makosa mle gerezani.
Data ilidhihirisha umuhimu wa uaminifu gerezani (Irwin, 1985). Kwa mfano, mfungwa ambaye
anapeleka udaku kwa maafisa hurejelewa kama msudi au nyoka. Inaashiria kuwa, watu kama hao
hawajakubalika miongoni mwa wafungwa wengine. Kikoa hiki pia kilidhihirisha usinonimu wa
hali ya juu ambapo maneno tofauti yanamaanisha kitu kimoja. Kwa mfano, wafungwa
hurejelewa kama wadhii, wasanii au wanaboma.
Wafungwa huwa na majukumu au kazi wanazofanya kwenye jela. Simu ni wafungwa ambao
hufanya kazi ya kuwaita wafungwa wenzao wanapotembelewa na wageni. Kairo ni wafungwa
58
ambao hufanya kazi ya kusafisha vyoo. Roho ni wafungwa ambao hufanya kazi kwenye maghala
ya jela kwa kubeba na kupanga magunia ya nafaka.
Katika jela, wafungwa huwa na hadhi tofauti kwani wafungwa wenye hadhi ya juu hurejelewa
kwa njia mahususi. Kwa mfano mashujaa ni wafungwa ambao wameishi sana gerezani. Mijikumi
huwa ni wafungwa ambao hawana cheo lakini wanapata heshima kutokana na miaka yao
maishani, hasa wale wa miaka themanini na zaidi. Mzee wa mtaa naye ana hadhi sawa na ya
mijikumi. Mfungwa staff ni yule mfungwa ambaye anafanya shughuli zake kama askari. Chakula
chake ni kizuri na pia mavazi yake ni safi, hapigi foleni ili kupokea chakula.
Ilibainika wazi kuwa pana wafungwa wenye hadhi ya chini na wana njia ya kipekee ambayo
wanarejelewa kwayo. Kwa mfano, trekta ni mfungwa mgeni na ndiye hufanya kazi sana. Kurutu
naye ni mfungwa mpumbavu ambaye hafahamu mambo mengi kwenye jela. Inaweza kufikiwa
hitimisho kuwa wafungwa wana njia zao za kujitambulisha. Wanaweza kujitambulisha kama mtu
binafsi au kama makundi ya wafungwa.
4.2.5 Kikoa cha maafisa wa magereza
Wahojiwa waliulizwa kutaja na kufafanua baadhi ya istilahi ambazo wao hutumia kuwarejelea
maafisa wa magereza. Kama katika agoti zinazorejelea wafungwa, maafisa wa magereza pia
hurejelewa kwa misimbo anuwai. Wahojiwa walifafanua maneno yafuatayo kama ambayo wao
hutumia kuwarejelea maafisa wa magereza.
Jedwali 4.05: Agoti zinazowarejelea maafisa wa magereza
Agoti Maana
Afande/gavaa/sirikali/kraoni/pai Askari wa jela
59
CPL / uzi mbili Koplo wa magereza
Uzi tatu Sajini wa magereza
Mawe mbili/stone mbee Spekta wa magereza
Mawe tatu/stone tatu Spekta mkuu wa magereza
Mastone Askari walio na vyeo vya juu (zaidi ya
sajini mkuu)
Simba Sajini kambi wa gereza/sajini
mwandamizi
Simba/bigi Askari mkuu msimamizi wa jela
Kurutu Askari ambao wameajiriwa majuzi
Kurutu Askari ambaye amempata mfungwa
kwenye jela fulani. Si lazima awe
ameajiriwa karibuni
Simba kabarasi Askari wanaoogopwa sana na wafungwa,
kutokana na ukali wao
Baba yao Askari wa cheo cha juu zaidi
Malilio Askari anayepokea malalamishi ya askari
na wafungwa.
Afande mwewe Askari mlafi ambaye hula chakula cha
wafungwa
Kwekwe Askari wanaowafanyia askari wenzao
upekuzi ili wasiingize marufuku gerezani
Mzazi Askari mzuri
60
Dhana kuu katika kikoa hiki ni maafisa wa magereza. Chini ya dhana hii kuu mtafiti alifafanua
agoti mbalimbali. Agoti hizi zilihusiana kimaana kwa sababu zote zilitumiwa kuwarejelea
maafisa wa magereza.
Mifano katika jedwali 4.05 inabainisha wazi kuwa maafisa hurejelewa kwa vyeo vyao kule
kwenye jela. Kulingana na mifano yetu, CPL/uzi mbili ni koplo wa magereza. Uzi tatu
humrejelea sajenti wa magereza. Mawe mbili hutumiwa kumrejelea spekta wa magereza. Mawe
tatu ambayo ni cheo kinachofuata kile cha spekta hutumiwa kumrejelea spekta mkuu wa
magereza.
Wafungwa pia hutumia majukumu ya askari kuwarejelea askari wao. Kwa mfano, askari ambaye
hushughulikia matatizo ya wafungwa yaani welfare officer hurejelewa kama malilio. Kwekwe
nao ni kundi la askari ambao huwafanyia askari wenzao upekuzi ili wasiingize marufuku
gerezani. Wanatafuta marufuku na kuyaondoa kama „kwekwe‟ inavyoondolewa shambani.
Askari hawa wanaogopwa sana na akari wenzao.
Kuna maneno ambayo hudhihirisha uhusiano mbaya uliopo baina ya askari na wafungwa au
mtazamo hasi wa wafungwa kwa askari. Afande mwewe huwa ni askari mlafi ambaye lazima
atue kwenye mali au chakula cha mfungwa. Askari kama hawa hawaheshimiwi na wafungwa.
Bondesson (1989) anaeleza kuwa kutokana na uhusiano mbaya kati ya askari na mfungwa,
wafungwa huunda istalahi ambazo huelekea kuwakejeli maafisa wa magereza. Hata hivyo kuna
wale wa hadhi ya juu kwa mfano baba yao ni askari mwenye cheo cha juu na huheshimiwa na
wafngwa. Simba kabarasi naye ni askari wanaoogopwa sana na wafungwa kutokana na ukali
wao. Maafisa wanaorejelewa hivi huwa wana hadhi kubwa katika jamii ya jela tofauti na wale
wanaorejelewa kama mwewe.
61
4.2.6 Agoti zaidi
Wahojiwa waliulizwa kufafanua agoti zaidi wanazozifahamu, istilahi zifuatazo zilitolewa.
Jedwali 4.06: Agoti zaidi kutoka kwa wahojiwa
Jina Maana
Matii Godoro
Kuchukua rada Kuchungulia
Mgondii Mfungwa mwizi
Mariam Lori la kuwasafirishia wafungwa
Chapenda Kutoa hongo ili kosa lako lisitolewe
nje/pesa
Kuangusha probox Askari au mfungwa kupatikana na marufuku
akiingiza ndani ya jela
Zimbabwe
Jela. Limepata jina hili kutokana na
kwamba bei ya bidhaa ni juu sana gerezani
Awuori Basi la kuwasafirisha wafungwa
Uchanganuzi wa data ulibaini kuwa istilahi kwenye jedwali 4.06 zingeweza kuwekwa katika
vikoa vile tulivyojadili awali. Kwa mfano, matii yenye maana ya godoro, Zimbabwe kumaanisha
jela, Awuori inayorejelea basi la kuwasafirishia wafungwa tungeziweka katika kikoa cha vifaa na
michakato ya jela. Istilahi mgondii ingewekwa katika kikoa kinachohusiana na maneno
yanayorejelea wafungwa.
62
Istilahi matii na mgondii ni maneno ambayo wafungwa hutumia gerezani lakini uchambuzi wetu
ulibaini kuwa ni maneno ambayo yamekopwa kutoka msimbo wa Sheng. Ni wazi kuwa katika
mazungumzo ya wafungwa, pana nyakati ambapo wanatumia maneno ambayo hutumiwa na
vijana katika mazungumzo yao. Neno mariam nalo limetolewa katika sajili ya dini. Maria ni
mamake Yesu, „mama wa ulimwengu wote‟. Wafungwa hulirejelea gari lao kama mariam kwa
sababu huwabeba wafungwa wengi mno. Husemwa kuwa gari hilo halijai. Wafungwa
hulazimishwa kujazana humo ndani wanaposafirishwa. Basi la jela lina jina la Awuori. Jina hili
lilitokana na jina la Makamu wa Rais katika serikali ya Kibaki baada ya Hayati Wamalwa. Yeye
ndiye alileta kwa mara ya kwanza matumizi ya mabasi kama mtindo wa usafirishaji wa
wafungwa tofauti na lori (Mariam) ambalo lilitumiwa awali.
Kwa muhtasari, uchanganuzi wa vikoa maana katika agoti za wafungwa ulidhihirisha mahusiano
ya kimaana ya maneno katika kila kikoa. Palikuwepo na dhana au maana kuu na chini ya maana
hiyo agoti mbalimbali ziliweza kuainishwa. Uchambuzi wa vikoa maana ulidhihirisha lugha ya
wafungwa kama kioo cha ulimwengu wa jela. Kikoa maana cha mahusiano ya kimapenzi
kilionyesha uchungu wanaopitia wafungwa kwa kutengwa na wapenzi wao wa jinsia ya kike.
Leksimu nyingi zilipatikana zililizodhihirisha kuwepo kwa ubasha gerezani. Kikoa maana cha
marufuku na dawa za kulevya kilidhihirisha jinsi baadhi wafungwa wanavyoshabikia dawa za
kulevya. Leksimu nyingi zililizojadiliwa katika kikoa hiki zilionyesha kuwepo kwa kiwango
fulani cha matumizi ya dawa za kulevya gerezani na thamani ya juu ya bangi ikilinganishwa na
sigara. Leksimu zilizotumiwa kurejelea silaha mbalimbali zilidhihirisha ulimwengu wa jela kama
ulimwengu uliojaa vita na mashambiliano ya mara kwa mara miongoni mwa wafungwa. Kikoa
maana cha wafungwa kilidhihirisha umuhimu wa uaminifu mingoni mwa wafungwa. Wafungwa
ambao si waaminifu kwa wafungwa wenzao walipewa majina ya kuwadunisha. Leksimu katika
63
kikoa hiki pia zilidhihirisha ngazi za kiutawala miongoni mwa wafungwa. Hatimaye, kikoa
maana cha maafisa wa magereza kilionyesha mahusiano kati ya wafungwa na askari.
Kulijadiliwa baadhi ya leksimu zilizoonyesha mahusiano mabaya yaliokuwepo kati ya wafungwa
na askari. Agoti zingine pia zilionyesha kuwa kulikuweko na askari ambao waliheshimiwa sana
na wafungwa.
4.3 Mabadiliko ya maana
Lengo la pili la utafiti huu lililikuwa kufafanua mabadiliko ya kimaana yanayojitokeza katika
agoti zinazotumiwa na wafungwa wa magereza ya Kisumu. Uchanganuzi wa data ulizingatia
Nadharia ya Pragmatiki Leksika iliyoasisiwa na Blutner katika miaka ya 1990. Blutner (2011)
akimrejelea Wilson (2003), anafafanua masuala ya kimsingi ambayo yanashughulikiwa katika
Nadharia ya Pragmatiki Leksika kama; kubanika kwa neno, kupanuka kwa neno na kukisia neno.
Utafiti huu ulitumia michakato hii ya kiprakmatiki leksika katika kufafanua mabadiliko ya
kimaana yaliyojitokeza katika agoti zilizotumiwa na wafungwa. Michakato hii ya kipragmatiki
leksika hutekeleza majukumu maalumu kwani kila mojawapo humwezesha msikilizaji kufasiri
semi kwa njia tofauti na ule ufasiri wa kisemantiki. Utafiti huu uljikita katika aina mbalimbali za
mabadiliko ya kimaana ambapo upanuzi wa kileksika hujidhihirisha kwa njia anuwai.
4.3.1 Ubanaji wa kileksia
Mchakato wa kwanza wa kipragmatiki leksika ni ubanaji wa kileksika. Kwa mujibu wa Wilson
(2003) hii ni hali ambapo neno linatumiwa kuonyesha fahiwa mahususi zaidi kuliko ile
iliyosimbwa. Husababisha kutokea kwa maana finyu zaidi ya ile ya kileksia. Uchanganuzi wa
matini ulibaini leksimu zifuatazo ambazo zilipitia mchakato huu wa ubanaji wa kimaana.
64
Jedwali 4.07: Agoti zilizobanika kimaana
Agoti Maana ya kisemantiki Maana mahusisi gerezani
Afande Jina la heshima ambalo askari
humwita mkubwa wake
Askari wa jela
Pai Polisi Askari wa jela
Kutia Fanya kitu kiwemo ndani ya
kingine
Kushiriki ngono
Marufuku Jambo lilokatazwa kufanyika Vitu vilivyokatazwa visiingizwe
gerezani
Kunyemelea Endea kitu kimya na polepole Kunajisi
Mzigo Kitu kizito kilichobebwa Marufuku
Unga Chochote kilichosagwa na
kuwa kama vumbivumbi
Kokeni
Kunguru Kitambaa chenye michoro ya
vyumba vyenye umbo la
mraba
Vazi la mfungwa
Baraza Mkusanyiko wa watu kwa
ajili ya mazungumzo
Mkutano unaoongozwa na mkuu
wa nyumba gerezani
Serikali Chombo chenye mamlaka ya
kuendesha utawala wa nchi
Askri au usimamizi wa jela
Kraoni Askari Askari wa jela
Tuone Tambua kitu kwa macho Kuona mfungwa ili utoe hongo
65
Kumaliziwa Kufikiwa na hatua ya mwisho Kuhakikishiwa kifungo na korti
Kuonwa Kutambuliwa kwa macho Kutembelewa gerezani
Kutoboa Kufanya kuwa tundu Kumaliza kifungo
Wadhii Watu Wafungwa
Warogoti Watu wanaookota Wanaokusanya bakuli
Jedwali 4.07 linaonyesha leksimu ambazo zimepitia mchakato wa ubaniji wa maana. Neno
afande limesimba dhana AFANDE ambayo imejumuisha aina mbalimbali za askari katika taifa
la Kenya. Kwenye diskosi hii, tunachukulia kuwa, anayesikiliza anaposikia neno afande, tayari
ana maarifa mapana kuhusiana na afande. Hivyo, inambidi msikilizaji kutafuta njia rahisi ya
kumfanya kuelewa dhana inayowasilishwa na neno afande. Kupitia maarifa yake kuhusu neno
afande, anafanya ubanaji na kufikia maana mahususi inayowasilishwa. Msikilizaji ana maarifa
kuwa afande anaweza kuwa polisi wa utawala, askari wa kulinda misitu au hata mwanajeshi.
Blutner (1998) anafafanua kuwa ubanaji una maana ya kutumia faridi leksika katika kupitisha
ufasiri uliobanwa zaidi ya ule uliosimbwa kisemantiki. Kisemantiki, afande ni jina la heshima la
kumrejelea askari yeyote aliye mkuu (TUKI, 2013). Mtafiti alichukulia kwamba, maana hii
ndiyo iliyosimbwa kisemantiki. Maana hii pana inajumuisha aina mbambali za askari. Katika
muktadha wa jela, neno afande linabanwa kumrejela askari wa jela tu.
Neno pai limekopwa toka msimbo wa Sheng na hurejelea polisi. Kisemantiki, polisi ni askari
mwenye dhamana ya kuona kuwa sheria na usalama wa nchi hauvunjwi (TUKI, 2013). Inambidi
msikilizaji kufanya ubanaji wa maana pana ya neno pai ili afikie ile dhana inayowasilishwa. Pai
kama ilivyo katika afande inaweza kutumiwa kumrejelea askari yeyote. Lakini katika muktadha
wa jela mfungwa akitumia neno pai atakuwa amelibana kurejelea askari wa jela tu na si kitengo
66
kingine cha askari. Mchakato huu ni sawa kwa ubanaji unaotokea katika leksimu kraoni kama
ilivyofafanuliwa kwenye jedwali.
Neno kutia kisemantiki ni kufanya kitu kiwemo ndani ya kingine (TUKI, 2013). Katika
muktadha wa jela, neno hili linabanwa kimaana ili kumaanisha ubasha au usenge. Kisemantiki,
kutia kunaweza kuwa kwingi; kutia nguo kwenye begi, kutia kalamu kwenye mfuko, kutia gari
kwenye mtaro n.k. lakini katika diskosi hii, kutia si kwingine bali ni kutia tupu katika njia ya
choo. Yaani, dhana ya kutia katika jela ni mahususi zaidi.
Leksimu marufuku kisemantiki inarejelea jambo ambalo limekatazwa kufanyika (TUKI, 2013).
Ni jambo au kitu chochote ambacho hakiruhusiwi kufanyika. Katika muktadha wa jela, inambidi
msikilizaji kufanya ubanaji wa maana pana ya neno marufuku ili kufikia dhana ambayo
inawasilishwa. Katika muktadha wa jela, marufuku haya ni yale mambo ambayo yamekatazwa tu
katika muktadha wa jela kama vile sigara au pombe. Marufuku katika muktadha wa jela ni ya
kipekee na hayajumuishi marufuku katika miktadha ya uraiani. Hivyo, maana ya marufuku
inabanwa ili kusawiri maana mahususi katika muktadha wa jela.
Maana ya kunyemelea katika kamusi ni kuendea kitu polepole na kimyakimya (TUKI, 2013).
Matumizi ya neno hili yanamhitaji msikilizaji katika muktadha wa jela afanye ubanaji wa maana
hii pana ya kunyemelea ili kufikia ukamilifu wa dhana inayopitishwa. Kunyemelea kwaweza
kuwa kwingi katika welewa wa kawaida wa neno hili. Kunyemelea ili kuona, kunyemelea kuua,
kunyemelea kushika, kunyemelea kuchunguza. Msikilizaji anaunda dhana za dharura kuhusu
njia na aina mbalimbali za kunyemelea. Anavuta maarifa yake kuhusu njia mbalimbali za
kunyemelea. Katika muktadha wa jela anafikia dhana mahususi zaidi ya kunajisi. Maana hii ni
finyu ikilinganishwa na maana pana ya kunyemelea.
67
Maana ya kawaida ya neno mzigo ni kitu kizito kilichobebwa (TUKI, 2013). Maana hii ni pana
kwani inajumlisha mizigo tofauti tofauti ambayo inaweza kuwepo. Mizigo katika kichwa, mizigo
katika gari, mizigo ya dhambi, mizigo ya shida katika maisha n.k. Katika muktadha wa jela,
maana ya mzigo inabanwa kurejelea marufuku. Yaani, mizigo ni yale mambo ambayo usimamizi
wa jela umekataa kuwa hayaruhusuwi kuingizwa gerezani kama vile pombe au sigara. Maana hii
inaelekea kuwa finyu zaidi ya ile maana ya kisemantiki ambayo inajumlisha mizigo yoyote ile.
Kisemantiki neno unga lina maana ya kitu kilichosagwa na kuwa vumbivumbi (Mdee, Njogu na
Shafi, 2011). Maana hii ni pana katika muktadha wa kawaida. Neno unga linajumlisha vitu vingi
vya ungaunga, unga wa mahindi, unga wa wimbi n.k. Katika diskosi hii, maana ya unga
inabanwa na kuwa kokeni, dawa ya kulevya ambayo ni ungaunga. Mfungwa anaposikia neno
unga, anaibana kupata maana yake katika muktadha wa jela na moja kwa moja anafahamu kuwa
ni kokeni wala si aina nyingine ya unga.
Neno baraza kawaida hurejelea kundi la watu kwa majukumu maalumu, mkusanyiko wa watu
wengi kwa ajili ya kuwa na mjadala fulani au mazungumzo ya kawaida, mahali ambapo kesi
husikilizwa au kitala (Mdee n.w., 2011). Maana hii ni pana sana. Katika muktadha wa jela
baraza hurejelea mkutano wa wafungwa unaoongozwa na mkuu wa nyumba ili kuzungumzia
masuala mbalimbali yanayowahusu wafungwa kwenye seli zao. Maana hii imebanwa
ikilinganishwa na maana pana ya leksimu hii katika miktadha iliyo nje ya magereza ya Kisumu.
Maana ya kisemantiki ya neno serikali ni chombo chenye mamlaka ya kuendesha utawala wa
nchi (TUKI, 2013). Maana hii ni pana kwani inarejelea chombo cha utawala wa taifa zima
ambalo aghalabu huongozwa na rais. Katika diskosi hii, maana ya neno serikali inabanwa
kumaanisha askari wa jela au usimamizi wa jela. Jela ni chombo cha serikali kinachotumiwa
68
katika kurekebisha tabia. Hivyo basi katika muktadha wa jela, askari au usimamizi wa jela
unaporejelewa kama serikali, maana hii itakuwa imebanwa katika kurejelea kitu kilicho finyu
zaidi ya hali yake ya kawaida.
Kisemantiki kuona ni kutazama kitu kwa kutumia macho, lola. Pia ni kupata fahamu ya kitu
kupitia hisi za mwili (Mdee n.w., 2011). Maana hii ni pana kwani ni kutumia macho kutazama
chochote kile. Katika muktadha wa jela, maana ya neno hili inabanwa na kusalia kumaanisha
kumwona mfungwa na kutoa hongo. Inatoka katika kutazama chochote kile hadi katika
kumwona mfungwa fulani na kutoa hongo pengine ili kitendo kiovu alichofanya mfungwa
kisiwafikie askari.
Kisemantiki, kumaliziwa huwa na maana ya kufikiwa kwa hatua ya mwisho. Yaani kuishiwa.
Maana hii ni pana zaidi kwani kunaweza kuwa kuishiwa na mali, kuishiwa na matumaini, au
kuishiwa na nguvu. Katika diskosi hii, mfungwa anapomwambia mwenzake amemaliziwa huwa
ana maana ya kuwa ameishiwa na hatua zote za kufanya ili aweze kutoka jela kwa njia za
kisheria. Ni korti ya rufaa kufikia uamuzi kuwa mfungwa atabaki kuwa gerezani. Maana hii
inajitokeza kuwa finyu zaidi ya maana ile pana.
Kuonwa ni kutambuliwa kwa macho (TUKI, 2013). Maana hii ni pana kwani inajumuisha
utazamaji wowote ule na mtazamaji yeyote yule. Hii ndiyo maana ya kisemantiki ambayo
hupatikana katika kamusi ya Kiswahili. Katika muktadha wa jela hata hivyo maana hii inajibana
katika kuonwa na mgeni kutoka uraiani. Mfungwa anapotembelewa na mgeni hurejelewa kuwa
ameonwa. Hivyo basi maana ya neno kuonwa inabanwa na kuwa mfungwa kuonwa na mgeni
katika chumba cha mazungumzo. Maana hii ni finyu kwani inafungia uonaji mwingine nje ya
maana hii mahususi.
69
Wadhii ni leksimu ambayo imekopwa kutoka msimbo wa Sheng. Neno hili hutumiwa kurejelea
watu. Maana hii ni pana kwani inarejelea mtu yeyote yule. Katika muktadha wa utafiti huu,
wadhii hutumiwa tu kurejelea wafungwa. Maana ya neno wadhii inabanwa na kusalia tu
kumaanisha watu ambao ni wafungwa na wala si kundi jingine lolote la watu. Maana hii ni finyu
zaidi ya maana halisi ya neno hili.
4.3.2 Upanuzi wa kileksia
Mchakato wa pili wa kileksika katika Nadharia ya Pragmatiki Leksika ni upanuzi wa kimaana.
Kwa mujibu wa Fromkin na Rodman (1993) upanuzi wa kileksika ni mchakato ambao kwao
maana ya neno hupanuka. Neno linamaanisha kila kitu kilichokuwa kikimaanishwa na kuzidisha
maana nyingine. Mtafiti aliongezea maelezo haya na kusema kuwa neno linapopanuka kimaana
huwa limeongezewa vitajwa na kujumuisha vitajwa vingine. Ullmann (1970) anafafanua kuwa
maneno yanapewa maana moja bunifu au zaidi bila ya maana asilia kupotea. Ile maana asilia na
maana ya pili zinaishi upande-upande bora tu kusiwepo na mkinzano. Uchambuzi wa data
ulibaini leksimu zifuatazo ambazo zilipitia upanuzi wa kimaana katika muktadha wa jela.
Jedwali 4.08: Agoti zilizopanuka kimaana
Agoti Maana ya kisemantiki Maana ya ziada
Mtoto Kiumbe anayezaliwa hasa na mtu au
mnyama
Anayetekeleza majukumu ya
mwanamke katika mahusiano ya
kimapenzi
Charaza Piga kwa mfululizo Wembe
Gari Chombo cha kusafiri kiendacho kwa
magurudumu
Bangi
70
Kuku Ndege anayefugwa na anafanana sana na
kware mkubwa
Sigara
Buti Sehemu maalumu ya kuweka mizigo
ambayo aghalabu iko upande wa nyuma
ya gari
Njia ya choo mwilini
Randa Kifaa cha seremala chenye kusawazisha
mbao
Kiboko
Njugu mawe Mmea wa jamii ya fiwi unaozaa punje
ngumu mviringo
Mahindi ambayo hayajaoza.
Mahindi magumu
Kiswahili Lugha ya kibantu yenye asili ya
mwambao wa pwani ya Afrika mashariki.
Ujanja au ukora
Kisuguu Asili yake ni kichuguu yenye maana ya
mwinuko wa ardhi
Mfungwa anayechungulia askari.
Pia ni mnara wa ulinzi
Bangili Pambo la mviringo lililotengenezwa kwa
madini
Pingu
Majani Sehemu ya mmea yenye rangi ya kijani
ambayo huota kwenye matawi
Wafungwa ambao huvaa beji la
kijani kibichi. Ni wafungwa
wasimamizi.
Kairo Mji mkuu wa Misri Wafungwa wanaosafisha vyoo
vya jela
Kurutu Askari mwanafunzi ambaye bado
hajahitimu
Askari mgeni katika jela. Pia
huwa na maana ya mfungwa
71
Jedwali hili linaonyesha upanuzi wa maana unavyojitokeza katika agoti za wafungwa wa
magereza ya Kisumu. Kama tulivyoeleza awali, kupanuka kwa neno ni mchakato wa kufasiri
ujumbe ambapo maana ya neno inapanuka zaidi ya inavyotumika katika hali ya kawaida. Maana
ya kileksika ya neno mtoto ni kiumbe anayezaliwa hasa na mtu au mnyama (TUKI, 2013).
Katika muktadha wa jela maana ya neno hili inapanuliwa kurejelea mfungwa basha
anayetekeleza majukumu ya mwanamke katika mahusiano ya kimapenzi. Hivyo basi, neno mtoto
limeongeza vitajwa vingine katika maelezo ya maana yake. Ullman (1970) anasema kuwa,
maneno huweza kupewa maana moja ya ziada bila kupoteza ile maana yake asilia.
Kitenzi charaza katika muktadha wa kawaida hurejelea kupiga kwa mfululizo. Katika muktadha
wa jela kitenzi hiki kinatumiwa kurejelea nomino, wembe. Maana ya neno hili imepanuka na
kuongeza maana ya ziada kimuktadha. Hali hii inajitokeza kwa sababu wakati mwingine wembe
mjinga.
Redio Chombo kinachopokea mawimbi ya sauti
k.v. ya mtangazaji, kupitia hewani na
kumwezesha mtu mwingine kusikia
kinachotangazwa
Simu
Ndovu Mnyama mkubwa wa nchi kavu mwenye
masikio makubwa na mapana, mkonga na
pembe mbili mdomoni
Dawa ya kulevya ambayo hutiwa
ndani ya mdomo wa chini
Kwekwe Mmea unaoota mahali usipotakiwa Askari wanaowafanyia askari
wenzao upekuzi ili wasiingize
marufuku gerezani
72
hutumika kama silaha. Ili kuficha maana yake ya kawaida, kitenzi charaza kinatumiwa ili askari
asiweze kufahamu mawasiliano baina ya wafungwa wanapozungumzia silaha.
Leksimu gari katika Kiswahili hurejelea chombo cha kusafiri kiendacho kwa magurudumu
(TUKI, 2013). Katika jela, maana ya neno hili inapanuliwa na kutumiwa kurejelea bangi.
Hapana uhusiano wa kisemantiki kati ya neno gari na bangi. Hata hivyo, kwa sababu gari
huchukuliwa kuwa chombo cha thamani kama ilivyo bangi katika jela maana ya neno hili
inapanuliwa kurejelea bangi ili kusimba dhana inayorejelewa.
Neno kuku katika muktadha wa kawaida hurejelea ndege anayefugwa na anafanana sana na
kware mkubwa (TUKI, 2013). Maana ya neno hili inapanuliwa kusimba dhana ya sigara. Kuku
hutumiwa kurejelea sigara kwa sababu ni marufuku isiyokuwa na thamani sana ikilinganishwa
na bangi ambayo hurejelewa kama bata. Kuku ni nyepesi kwa mizani na bei yake sokoni ni ya
chini ikilinganishwa na bata. Sigara pia bei yake iko chini ikilinganishwa na bangi katika „soko
la jela‟.
Upanuzi wa maana pia unadhihirika katika leksimu buti. Maana ya kileksika ya neno hili ni
sehemu maalumu ya kuweka mizigo ambayo aghalabu iko upande wa nyuma wa gari (Mdee
n.w., 2015). Katika muktadha wa jela maana ya neno hili inatanuliwa kurejelea njia ya choo
kwenye mwili wa mfungwa. Sehemu hii hurejelewa kama buti kwa sababu baadhi ya wafungwa
huficha marufuku kama vile bangi, sigara au hata pesa kwenye makalio yao. Kama ambavyo buti
ya gari hubeba mizigo ndivyo buti katika muktadha wa jela hutumiwa kubeba na kuficha
marufuku.
Katika mazungumzo ya kawaida, leksimu randa ni kifaa cha seremala ambacho hutumiwa
kusawazishia mbao (TUKI, 2013). Katika diskosi ya jela, maana ya randa inapanuliwa kurejelea
73
viboko. Upanuzi huu unatokea kwa sababu jinsi randa inavyosawazisha mbao ndivyo viboko
vinavyotumiwa kuwasawazisha wafungwa ambao wamekataa kufuata sheria na masharti ya
magereza. Hivyo basi, maana ya kwanza ya randa pamoja na maana hii ya pili hutumiwa katika
jela.
Maana ya kikamusi ya neno Kiswahili ni lugha ya kibantu yenye asili ya mwambao wa pwani ya
Afrika Mashariki TUKI (2013). Katika muktadha wa jela, neno hili linapitia mchakato wa
upanuzi wa kimaana na kutumiwa kurejelea ujanja. Mfungwa au askari ambaye ni mjanja au ana
ukora mwingi hurejelewa kama mswahili. Uswahili ni ujuaji. Hivyo basi, maana ya neno hili
ambalo hutumiwa kurejelea lugha ya Waswahili inatumiwa kurejelea ujanja, ukora au uongo
katika muktadha wa jela.
Leksimu kisuguu imekopwa toka neno la Kiswahili kichuguu. Baada ya neno hili kukopwa
linafanyiwa mabadiliko ya kimuundo na kisha kutumiwa katika muktadha wa jela. Maana
kileksia ya neno kichuguu ni mwinuko wa ardhi. Neno hili katika muktadha wa jela linapata
fahiwa mbili za ziada. Kwanza, kibanda kwenye jela ambamo askari huketi kuchunga wafungwa.
Pili, mfungwa anayeketi kuchungulia askari anapokuja ili wafungwa wenzake wasipatikane.
Bangili ni neno ambalo hutumiwa kawaida kurejelea pambo la mviringo lililotengenezwa kwa
madini na huvaliwa na wanawake mikononi (TUKI, 2013). Katika muktadha wa jela neno hili
hupata upanuzi wa maana na kutumiwa kurejelea pingu ambazo hutumiwa kuwafunga wafungwa
mikono.
Leksimu Kairo hutumiwa kawaida kurejelea mji mkuu wa Misri. Katika muktadha wa jela, neno
hili hutumiwa kurejelea wale wafungwa ambao jukumu lao gerezani ni kuosha na kusafisha
vyoo. Wafungwa hawa hurejelewa kama kairo au geng ya kairo. Hapana uhusiano wa
74
kisemantiki kati ya mji wa Misri na wafungwa wanaosafisha vyoo. Hii inatuelekeza katika
kufikia uamuzi kuwa neno hili limepata upanuzi wa maana na kupata fahiwa bunifu ya ziada
ambayo neno hili halikuwa nalo (katika muktadha wa kawaida).
Katika mazungumzo ya kawaida, kurutu ni askari mwanafunzi ambaye bado hajahitimu (TUKI,
2013). Katika muktadha wa jela, neno hili linapanuliwa na kutumiwa kurejelea askari yeyote
ambaye ni mgeni katika gereza husika. Neno hili pia wakati mwingine hutumiwa kimatusi
kumdhihaki mfungwa anayetenda jambo la kijinga. Hivyo basi, maana ya neno kurutu
imepanuliwa na kujumuisha maana ambazo awali haikuwa nayo.
Maana ya kileksia ya neno redio ni chombo kinachopokea mawimbi ya sauti k.v. ya mtangazaji,
kupitia hewani na kumwezesha mtu mwingine kusikia kinachotangazwa (TUKI, 2013). Hii
ndiyo maana ya kawaida inayojulikana na mtu yeyote yule. Katika muktadha wa jela, maana ya
neno hili inapanuliwa na kutumiwa pia kumaanisha simu. Upanuzi huu wa maana unajitokeza
kwa dhima ya kusababisha ufumbaji. Wafungwa hutaka kuzungumza mambo kuhusu simu bila
maafisa wa magereza kufahamu. Hivyo basi wanatanua maana ya kawaida ya redio na kuitumia
kurejelea simu.
Ndovu kileksia ni mnyama mkubwa wa nchi kavu mwenye masikio makubwa na mapana,
mkonga na pembe mbili mdomoni. Hii ndiyo maana kawaida inayojulikana na mjuzi wa lugha
ya Kiswahili. Hata hivyo, maana ya neno hili inatanuliwa katika muktadha wa jela na kurejelea
dawa ya kulevya ambayo hutiwa ndani ya mdomo wa chini.
Hatimaye upanuzi wa kisemantiki unajitokeza katika leksimu kwekwe. Maana ya kisemantiki ya
neno hili ni mmea unaoota mahali usipotakiwa (Mdee n.w., 2011). Katika muktadha wa jela,
maana ya neno hili inatanuliwa na kutumiwa kurejelea askari wanaowafanyia askari wenzao
75
upekuzi ili wasiingize marufuku gerezani. Kisemantiki, hapana uhusiano kati ya kwekwe, mmea,
na askari wa jela, binadamu. Hata hivyo, kwa sababu askari hawa hufanya kazi ya kutafuta
kwekwe ambayo huenda askari wengine wakaingiza ndani ya jela, neno hili linatumiwa
kuwarejelea maafisa hawa na hivyo leksimu hii kupata upanuzi wa maana yake.
4.3.2.1 Upanuzi wa kisitiari
Simiyu (2016) anaeleza kuwa upanuzi wa kisitiari ni mchakato ambao kwao maana ya neno ipo
mbali na maana wazi. Yaani, maana ya neno fulani katika muktadha wa mazungumzo ni tofauti
kabisa na maana ya neno hilo kiisimu. Mtafiti anaongeza na kusema kuwa katika upanuzi wa
kisitiari, maana ya neno huwa mbali na maana halisi kwa kuhamisha maana ya neno hilo toka
kwa kiashiria kimoja hadi kiashiria kingine. Uchambuzi wa data ulibaini leksimu zifuatazo
ambazo zilipitia upanuzi wa kisitiari
Jedwali 4.09: Agoti zilipanuka kisitiari
Agoti Maana ya kisemantiki Maana iliyopanuliwa
Mtoto Kiumbe anayezaliwa hasa na mtu au
mnyama
Shoga anayetekeleza majukumu
ya mwanamke katika mahusiano
ya kimapenzi
Mwana Kiumbe aliyezaliwa na binadamu au
mnyama
Shoga anayetekeleza majukumu
ya mwanamke katika mahusiano
ya kimapenzi
Maua Sehemu ya mmea inayochanua Shoga anayetekeleza majukumu
ya mwanamke katika mahusiano
ya kimapenzi
76
Mende Mdudu Shoga anayetekeleza majukumu
ya mume katika mahusiano ya
kimapenzi
Kijana Mtu ambaye si mzee wala si mtoto Shoga anayetekeleza majukumu
ya mwanamke katika mahusiano
ya kimapenzi
Malaya Mwanamke au mwanamume mwenye
tabia ya uzinzi
Mfungwa anayetoa siri za
wafunwa kwa askari
Kuku Ndege anayefugwa na anafanana sana na
kware mkubwa
Sigara
Bata Ndege wa porini au anayefugwa,
mkubwa kuliko kuku
Bangi
Baruti Unga wa kijivujivu unaolipuka Pilipili
Neti Kitambaa kinachoning‟inizwa kitandani
kukinga mbu
Jela
Roho Kitu kisichoonekana ambacho hufikiriwa
kuwa ni sehemu ya mwili ya kiumbe
ambayo hukiwezesha kuwa hai
Wafungwa wanaofanya kazi
ghalani
Nguo ya mattres Vazi la godoro Wafungwa wa cheo cha juu
zaidi.
Malaika Kiumbe asiyeonekana na ambaye
hudaiwa kuwa mtumishi wa Mungu
Wafungwa wazuri
Simba Mnyama mkubwa wa porini wa jamii ya Askari mkuu zaidi katika jela
77
paka mwenye manyoya ya rangi ya
majani makavu na ambaye hula nyama
Mtaro Mfereji mpana wa kupitisha bomba la
maji
Njia ya choo kwenye mwili wa
mfungwa
Mzazi Mama au baba mtu Askari wazuri
Mwewe Ndege mkubwa anayefanana na tai
ambaye hukamata vifaranga wa kuku
Mfungwa au askari mlafi
Nyoka Mnyama mrefu na mwembamba mwenye
magamba asiye na miguu, anayetambaa
na hutaga mayai
Mfungwa ambaye hutoa siri kwa
askari
Dhana iliyosimbwa na neno mtoto ni MTOTO. Msikilizaji anaposikia neno hili anaunda dhana
za dharura kama vile mtoto ni kitu kinachopachikwa kwenye kitu kingine, kiumbe anayezaliwa
hasa na mtu au mnyama au mtoto ni kidoa cheupe kinachomea ndani ya mboni ya jicho (TUKI,
2013). Katika muktadha wa jela, dhana hizi ni wazi na haziwezi kuwa ndizo zinazowasilishwa na
neno mtoto. Katika jela neno mtoto linatumiwa kurejelea mfungwa shoga ambaye hutekeleza
majukumu ya kike katika mahusiano ya kimapenzi. Dhana hii imejitenga kutoka kwa maana
wazi ya neno hili mtoto. Kwa mujibu wa Bloomfield (1933), upanuzi wa kisitiari hutumiwa ili
kuficha ujumbe unaowasilishwa. Kwa kuwa mtoto wa binadamu huwa dhaifu na huhitaji malezi
vivyo hivyo mfungwa shoga (anayekuwa kama kike) huhitaji malezi na ulinzi kutoka kwa
mpenzi wake wa kiume. Hivyo basi, sifa hii ya mtoto inahawilishwa hadi kwa mrejelewa
(mfungwa shoga anayetekeleza majukumu ya kike kimapenzi).
78
Maelezo kuhusu leksimu mwana ni sawa na yale ya mtoto. Maana ya kawaida ya mwana ni
kiumbe aliyezaliwa na binadamu au mnyama (TUKI, 2013). Maana hii ni tofauti kabisa na
maana ya leksimu hii katika muktadha wa jela. Katika jela mwana ni mfungwa shoga
anayetekeleza majukumu ya mwanamke katika mahusiano ya kimapenzi gerezani. Haya ni
mambo mawili tofauti. Hata hivyo, mwana ana sifa ambayo inamfanya kuhusishwa na mfungwa
shoga. Mwana huhitaji malezi kama alivyo mfungwa huyu shoga anayetekeleza majukumu ya
kike. Mtafiti anakubaliana na maelezo ya Aitchison (2003) kuwa kwenye sampuli ya kiasili, vitu
ambavyo vinafananishwa vinaweza kutofautiana, kwa mfano; kwa kutokana na vikoa vya
kisemantiki tofauti. Pia vinaweza kufanana hivi kwamba vinashiriki katika baadhi ya sifa za
kawaida.
Kisemantiki, maua ni sehemu ya mmea inayochanua (TUKI, 2001). Ni sehemu ambayo
hupendeza macho. Katika muktadha wa jela, maana hii inapanuliwa kurejelea mfungwa shoga
anayetekeleza majukumu ya kike kimapenzi. Hizi ni maana mbili tofauti kabisa. Upande mmoja
maua ni sehemu ya mmea, upande mwingine (katika muktadha) maua ni binadamu. Mfungwa
shoga anayetekeleza majukumu ya kike anarejelewa hivi kwa kuwa ana sifa fulani inayomfanya
kuwa mauamaua. Kwanza, kama maua, wengi wa wafungwa kama hawa huwa wana miili
myororo au laini kama ya wanawake na hivyo kutamanika na wafungwa wenzao. Pia, wana sifa
ya kimaua hivi kwamba wanaweza kunyauka. Mahusiano ya kimapenzi gerezani aghalabu
hayadumu kwa muda mrefu. Inategemea nani ana pesa zaidi au nani mwenye nguvu zaidi.
Leksimu malaya kwa maana ya kawaida ni mwanamke au mwanamume ambaye ana tabia ya
uzinzi (TUKI, 2013). Maana hii ni tofauti kabisa na maana ya neno hili katika muktadha wa jela.
Gerezani, malaya ni mfungwa ambaye ana tabia ya kutoboa siri za wafungwa wenzake kwa
maafisa wa magereza. Tabia ya malaya kawaida huonekana kama usaliti. Sifa hii ya usaliti wa
79
malaya ndio inayoelekeza upanuzi wa neno hili katika muktadha wa jela hadi kurejelea mfungwa
msaliti anayetoa siri kwa askari.
Kisemantiki, kuku ni ndege anayefugwa na anafanana sana na kware mkubwa (TUKI, 2013).
Katika muktadha wa jela kuku inapanuliwa kurejelea sigara. Upanuzi huu wa kisitiari unafanywa
ili kusimba dhana inayowasilishwa kwa kuwa sigara ni marufuku katika jela. Hivyo basi
wafungwa wanatumia leksimu kuku kusimba dhana ya SIGARA. Bei ya kuku sokoni huwa chini
ikilinganishwa na bei ya bata, vivyo hivyo sigara ni marufuku yenye thamani ya chini katika jela
ikilinganishwa na bangi inayorejelewa kama bata. Inambidi msikilizaji katika muktadha wa jela
kuhawilisha sifa hii ya thamani ya chini ya kuku hadi katika thamani ya chini ya sigara kama
kitu marufuku katika jela.
Kisemantiki, baruti hurejelea unga wa kijivujivu unaolipuka (TUKI, 2013). Katika muktadha wa
jela baruti hutumiwa kurejelea pilipili. Kileksia, baruti na pilipili ni maneno mawili yenye
maana tofauti kabisa. Hata hivyo, katika muktadha wa jela, neno baruti linatumiwa kufumba
neno pilipili kwani pilipili ni marufuku gerezani. Neno baruti linapanuliwa kimaana kurejelea
pilipili kwani baruti ina sifa sawa na pilipili. Pilipili huwasha na kulipuka kwenye mdomo jinsi
baruti hulipua vifaa mbambali kama vile mawe.
Neno neti limetoholewa toka kwenye lugha ya Kiingereza net. Katika mazungumzo ya kawaida,
neti ni kitambaa cha wavuwavu kinachoning‟inizwa kitandani kukinga mbu (Mdee n.w., 2011).
Jela pia lina maana ya kipekee kisemantiki, pahali wanapowekwa wahalifu wa sheria kuadhibiwa
ili wajirekebishe (TUKI, 2013). Leksimu hizi pamoja na maana zao ni tofauti kabisa kisemantiki.
Hata hivyo, neno neti lina sifa ya kuwa humfungia binadamu ili asiumwe na mbu. Hiyo sifa ya
neti ndiyo inafanya leksimu hii kupanuliwa na kumaanisha jela ambayo hutumiwa na serikali
80
kuwafungia wafungwa ili kuelekezwa na kurekebishwa. Ingawa hivyo, utafiti huu ulipata kuwa
maelezo ya kisemantiki kuhusu jela hayaingiliani na maana ya jela kama ilivyo sasa katika taifa
la Kenya. TUKI (2013) inasisitiza swala la kuadhibiwa kwa wafungwa ili kujirekebisha.
Magereza ya Kenya ya sasa hayaelekezwi katika kuadhibu bali katika kufundisha na kuelekeza
ili kuwepo kwa mabadiliko ya kitabia na wala si kama inavyofafanuliwa na TUKI (2013).
Leksimu roho ina maana ya kitu kisichoonekana ambacho hufikiriwa kuwa ni sehemu ya mwili
wa kiumbe ambayo hukiwezesha kuwa hai (TUKI, 2013). Hapana uhusiano wa moja kwa moja
katika ya neno hili roho na wafungwa. Roho inadaiwa kuwa sehemu ya mwili lakini wafungwa
ni wanadamu. Hata hivyo, pana dhehebu la ‘ROHO’ ambalo wafuasi wake huvalia mavazi
meupe pamoja na kofia. Wafungwa wanaofanya kazi katika maghala ya jela pia hujifunga kwa
vitambaa vyeupe mwilini na kuvaa kofia nyeupe ili kukinga uchafu unaotakana na magunia ya
mahindi na unga wanaobeba. Sifa hii ndiyo inayofanya leksimu roho kupanuliwa hadi kuashiria
wafungwa hawa wanaofanya kazi kwenye maghala ya jela.
Nguo kawaida hurejelea vazi analovaa mtu. Katika muktadha wa jela, nguo ya matress
hutumiwa kurejelea wale wafungwa wenye vyeo vya juu zaidi gerezani. Nguo ni vazi lakini
kirejelewa katika muktadha wa jela ni wanadamu. Hapana uhusiano wa moja kwa moja kati ya
nguo na mtu. Hata hivyo, baadhi ya magodoro hufunikwa kwa kiguo cha rangi ya buluu.
Wafungwa hawa wasimamizi pia huvalia mavazi ya rangi ya buluu. Kwa namna hii, nguo ya
matress inapanuliwa kurejelea wafungwa wasimamizi ambao huvalia nguo za rangi ya samawati.
Leksimu malaika kisemantiki humaanisha kiumbe asiyeonekana na ambaye hudaiwa kuwa
mtumishi wa Mungu (TUKI, 2013). Kiumbe huyu kawaida huchukuliwa kuwa mzuri na asiye na
doa. Hapana uhusiano wa kisemantiki ulio wa moja kwa moja kati ya malaika, ambaye ni
81
kiumbe wa kiroho asiyeoonekana, na mfungwa ambaye yumo gerezani. Hata hivyo, malaika
huwa wana sifa kuwa ni wazuri tena ni walinzi wa binadamu. Sifa hii ndiyo inayowafanya
wafungwa kupanua maana ya neno hili na kulitumia kuwarejelea wafungwa ambao ni wazuri
pale gerezani. Wazuri hapa ikiwa na maana ya kuwa hawakiuki sheria na kanuni za magereza na
pia hawana ujanja wa jela (Kiswahili ya jela).
Kisemantiki, simba ni mnyama mkubwa wa porini wa jamii ya paka mwenye manyoya ya rangi
ya majani (TUKI, 2013). Simba huchukuliwa katika mazungumzo ya kawaida kuwa ndiye
mfalme wa wanyama porini. Hapana uhusiano wa moja kwa moja kati ya simba, mnyama na
askari mkuu gerezani, yaani binadamu. Hata hivyo, kwa sababu simba huwa na sifa ya kuwa
ndiye mfalme wa wanyama wa porini, maana ya neno hili hupanuliwa katika muktadha wa jela
ili kurejelea askari mkuu wa gereza ambaye ndiye mtawala mkuu katika muktadha wa jela
husika (Officer in Charge).
Katika mazungumzo ya kawaida, mzazi ni leksimu ambayo hutumiwa kurejelea baba au mama
mtu (TUKI, 2013). Katika jela, wazazi wa wafungwa hawaruhusiwi kuishi na watoto wao mle
isipokuwa ikiwa wao nao ni wafungwa. Mzazi katika muktadha wa jela ni askari mzuri. Hapana
uhusiano wa kibayolojia na hivyo basi wa kisemantiki baina ya huyu mzazi katika jela na mzazi
halisi wa mfungwa kwani ni makundi mawili tofauti ya watu. Neno mzazi hupita upanuzi wa
kimaana na kurejelea askari mzuri kwa sababu huyu askari mzuri huwa na sifa za kiuzazi. Ni
askari anayewaelewa wafungwa, anawashauri, anawatia moyo, anawasaidia wanapokuwa na
mahitaji. Yaani, ni kama mzazi anavyowalea watoto wake nyumbani.
Kisemantiki, mwewe hurejelea ndege mkubwa anayefanana na tai ambaye huwakamata vifaranga
wa kuku (TUKI, 2013). Hakuna uhusiano wa kisemantiki kati ya mwewe na askari au mfungwa.
82
Mwewe ni ndege, na mfungwa au askari ni binadamau. Hata hivyo, mwewe ana sifa ya kunyakua
au kuiba vifaranga wa kuku. Gerezani pia mna wafungwa-mwewe wasioshiba ambao hata baada
ya kula hulazimika kurudi kwenye vyombo vya kupikia na kuvichokora ili kupata kitu cha
kuongeza matumboni. Pia pana afande-mwewe ambao wafungwa huwachukulia kuwa walafi.
Askari hawa hupapia na kuchukua vyakula vya wafungwa, hasa nyama. Tabia hii ya kuchukua
nyama kutoka kwenye bakuli ya mfungwa inahusishwa na tabia ya mwewe ya kuiba vifaranga
wa kuku. Hivyo basi, neno mwewe linapanuliwa kumaanisha askari mlafi au mfungwa mlafi.
Katika Kiswahili cha kawaida, nyoka ni mnyama mrefu na mwembamba mwenye magamba na
asiye na miguu, anayetambaa na hutaga mayai (TUKI, 2013). Nyoka huwa na sumu na
akimwuma binadamu bila kutibiwa, binadamu huyo huishia kufariki. Hapana uhusiano wa
kisemantiki kati ya nyoka na mfungwa. Nyoka ni mnyama lakini mfungwa ni binadamu. Ingawa
hivyo, nyoka huwa na sifa ya kuwa ana sumu kali ya kufisha. Baadhi ya wafungwa wenye kutoa
siri kwa maafisa wa magereza huweza kusababisha wafungwa wenzao kuadhibiwa au hata
kupata uhamisho. Sifa hii ya nyoka huifanya leksimu hii kupanuka kimaana katika muktadha wa
jela na kutumiwa kuwarejelea hawa wafungwa wasaliti.
4.3.2.2 Chuku
Wilson (2003) anasema kuwa hili ndilo badiliko ambalo linaonekana kuhusisha kiwango
kikubwa zaidi cha upanuzi wa maana na hivyo kunakuwepo na utengano mkubwa kutoka kwa
dhana ambayo imesimbwa. Mtafiti alikubaliana na maelezo haya na kuongeza kuwa hili
badiliko linahusu upigaji chuku au kutia chumvi.
83
4.10: Agoti zilizopanuka maana kichuku
Agoti Maana ya kawaida Maana kimuktadha
Kutoboa Fanya kuwa na tundu Kumaliza kifungo
Tero Mashambulizi ya kigaidi Wafungwa kufanyiwa upekuzi
Kunyeshewa randa Kuangukiwa na randa Kuchapwa
Kuuza mtu Kubadilisha mfungwa kwa
fedha
Kumfanya mfungwa
mwenzako achapwe
Kukula copper Kukula risasi Kupigwa risasi
Nchi ingine Taifa tofauti Uraiani
Nchi ya saba Taifa la saba Jela
Leksimu toboa katika lugha ya Kiswahili ina maana kufanya kitu kuwa tundu (TUKI, 2013). Ni
wazi kuwa kitu kikitoboka huwa kinawacha nafasi na kile kilicho ndani kupita. Hii ni maana ya
kawaida ya neno hili. Katika muktadha wa jela, maana ya neno hili ni mfungwa kumaliza
kifungo chake. Hali ya kutoboka kunalinganishwa na mfungwa kufunguliwa jela na kuwa huru.
Mskilizaji anapata ufasiri kuwa jinsi maji yanavyopita katika tundu la kifaa kama chupa, ndivyo
mfungwa anavyotoka katika kifungo. Ufasiri huu unaonekana kuwa masafa ya mbali zaidi na
maana ya kitu kuwa na tundu. Hivyo basi, maana neno hili imepanuliwa kwa kutiwa chumvi.
Tero ni neno ambalo limekopwa toka lugha ya Kiingereza terrorize yenye maana ya
kushambulia kigaidi. Inachukuliwa kuwa msikilizaji ana vitomeo vya maarifa ya ufahamu wa
namna mashambulizi ya kigaidi hufanywa. Kwa mfano, mashambulizi yanapofanywa huwa pana
mateso, kupigwa au hata umwagaji damu. Katika muktadha wa jela tero hutumiwa kurejelea
84
upekuzi wa dharura ambao hufanywa na maafisa wa magereza kwenye seli ya wafungwa.
Kutokana na maelezo ya wahojiwa kuwa mara nyingi upekuzi unapofanywa wafungwa huvuliwa
uchi upekuzi huu ambao ni mchakato wa kawaida wa jela unapanuliwa kwa namna ya
kuongezwa chumvi na kurejelewa kama mashambulizi ya kigaidi.
Katika maelezo ya kawaida, kunyeshewa randa ni kuangukiwa na kile chombo ambacho
hutumiwa kusawazisha mbao. Katika muktadha wa jela, kuchapwa kunarejelewa kama
kunyeshewa randa. Kunyeshewa randa ni kauli ambayo imetiliwa chumvi kudhihirisha uchungu
wa kichapo anachopata mfungwa mkononi mwa askari anapoadhibiwa. Wingi wa viboko
unahusishwa na mvua ya randa kunyesha.
Kuuza mtu, kawaida ni kule kumbadilisha na pesa. Hii ni maana ambayo imetiwa chumvi kutoa
ile dhana ya mfungwa kumfanya mwenzake kuchapwa. Maana ya kileksia ya kuuza ipo mbali
sana na maana ya kimuktadha ya neno hili ambayo ni kusaliti. Uchungu huo wa mfungwa
kumsaliti mwenzake kwa maafisa wa magereza hadi kufikia mfungwa husika kuchapwa
kunawafanya wafungwa katika muktadha huu kupanua maana ya neno hili kwa kutia chumvi ili
kurejelea hali ya kusaliti.
Kukula copper kisemantiki ni hali ya mtu kutia risasi mdomoni. Katika muktadha wa jela kukula
copper ni mtu kupigwa risasi. Kukula ni tofauti kabisa na kupigwa risasi katika muktadha wa
kawaida wa matumizi ya maneno haya. Hivyo basi, huku kukula copper kumepanuliwa maana
kwa kupigiwa chuku kumaanisha kupigwa risasi.
Maana ya kawaida ya nchi ya saba ni taifa la saba. Maneno haya yanatumiwa kurejelea jela.
Huku ni kutiwa chumvi kwani jela ni sehemu ya taifa wala si taifa tofauti. Hata hivyo, kutokana
na hali kuwa maisha ya jela ni magumu, bei ya bidhaa kuwa ghali ikilinganishwa na bei
85
miongoni mwa raia wa kawaida, maana ya neno jela inapanuliwa kwa kutiwa chumvi na
kurejelewa kama nchi ya saba. Maana hii iliyopanuliwa kisitiari inaonyesha tofauti kubwa
iliyopo katika maisha ya jela na maisha ya jamii ya kawaida.
4.3.2.3 Upanuzi wa kategoria
Katika aina hii ya badiliko, jina la kitu ambacho kinajulikana zaidi katika jamii linapanuliwa
kimaana na kutumiwa katika jamii nzima ambamo kitu hicho hupatikana (Wilson, 2003). Mtafiti
alikubaliana na maelezo haya na kuongeza kuwa, hili jina linapotumiwa katika jamii nzima huwa
linafanya maana inayopitishwa kujitenga zaidi toka kwenye maana iliyosimbwa na leksimu hiyo.
Kwa mujibu wa Wilson na Carston (2007) majina ya kipekee na nomino za kawaida huwa
zinachangia katika badiliko hili.
4.11: Agoti zilizopanuka kikategoria
Agoti Maana ya kawaida Maana kimuktadha
Mariam Maria ni mamake Yesu Lori la magereza
Awuori Aliyekuwa makamu wa rais Basi la magereza
Kutokana na jedwali 4.11, Maria ni jina la kipekee. Maria ni mamake Yesu katika muktadha wa
kawaida. Kwamba Wakristo wanaamini kuwa Yesu ni Mungu, Maria anachukuliwa na baadhi
madhehebu ya kikristo kama mama ambaye amebarikiwa. Kwa sababu Maria anachukuliwa
kama mama wa madhehebu ya kikristo, ambayo ni mengi, lori la magereza hurejelewa kama
Mariam kwani huweza kubeba watu wengi sana kwa safari moja. Wahojiwa walifafanua kuwa,
mariam huchukuliwa kuwa haiwezi kujaa, walivyo wengi Wakristo. Pia, mtu yeyote huweza
kubebwa na lori hili.
86
Awuori ni jina la kipekee. Alikuwa ni naibu wa raisi aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani
ya taifa. Alipokuwa waziri alianzisha rasmi matumizi ya mabasi kuwasafirisha wafungwa. Kwa
sababu ndiye aliyeanzisha matumizi haya ya mabasi, baadhi ya wafungwa hutumia jina lake
kurejelea mabasi ya magereza. Ni muhimu kutaja kuwa, Awuori ni binadamu wala si gari. Hata
hivyo, katika muktadha wa jela, jina lake linapanuliwa maana na kurejelea basi la jela. Mtafiti
alikubaliana na Jeffers na Lehiste (1979) kuwa upanuzi huu wa maana huwa unatokana na
kujumuisha hali mahususi hadi katika jamii ambayo ile hali mahusisi inashiriki. Hii ndiyo sababu
majina ya kipekee kama Awuori na Maria yanajitokeza kurejelea jamii ya kijumla ya ile
fenomena.
4.3.3 Kisio la maana
Katika Nadhria ya Pragmatiki Leksika, mchakato wa tatu wa kipragmatiki ni kisio la maana. Hili
ni badiliko ambalo kwalo leksimu iliyo na maana thabiti kiasi hupanuliwa ukingoni na
kujumuisha mawanda ya makundi ambayo kwa hakika yanapatikana nje ya maana yake kamili
ya kiisimu. Mifano mizuri kwa mujibu wa Wilson (2003) ni kama matumizi ya kilegevu ya
takwimu za kukadiria, misamiati ya kijiografia na misamiti ambayo inaelezwa kwa njia ya
kukanusha. Hapa, dhana ambayo inawasilishwa inajitenga zaidi na dhana ambayo imesimbwa.
4.12: Agoti zilizopanuka kwa kukisiwa kimaana
Agoti Maana ya kawaida Maana ya kimuktadha
Nchi ya saba Taifa la saba Jela
Kwenda Kenya Kwenda katika nchi ya Kenya Kwenda kuwa raia wa
kawaida
87
Katika jedwali 4.12, agoti nchi ya saba imesimba dhana ya NCHI YA SABA. Dhana hii ambayo
imesimbwa ni mbali sana na maana ya nchi ya saba katika lugha ya Kiswahili. Nchi ni leksimu
bayana ambayo ina maana ya sehemu ya ardhi katika ulimwengu iliyogawika kisiasa kwa
mipaka na kutambuliwa kwa taifa lake au ni sehemu ya ardhi isiyofunikwa na maji (TUKI,
2013). Si bayana nchi ya saba inayozungumziwa ni nchi ya saba gani? Ni nchi ya saba, nchi ya
kwanza ikiwa ipi? Ni katika muktadha wa jela ndipo nchi hii ya saba inaweza kukadiriwa kuwa
ni jela. Agoti hii inatumiwa kudhihirisha utengano au tofauti kati ya maisha ya jela na maisha ya
kawaida ya raia. Tofauti hii inaifanya jela kuonekana kama dunia tofauti. Nchi ya saba ni legevu
ila inatumiwa kurejelea jela.
Katika muktadha wa kawaida, kuenda Kenya ni kusafiri kuenda nchi ya Kenya. Maana hii ya
kipekee inapanuliwa na kuhusisha maana ambayo kwa hakika awali haikuwepo katika maneno
haya. Msikilizaji anabaki akijiuliza, mtu anaenda vipi Kenya iwapo tayari yupo katika taifa la
Kenya? Maneno haya yanatumiwa kwa njia legevu kudhihaki mazingira ya jela kuwa mabaya
na kuwa si sehemu ya taifa la Kenya. Inambidi msikilizaji kufanya ukadiriaji ili aweze kubaini
Kenya hii inayozungumziwa i wapi ikiwa tayari yupo katika taifa la Kenya. Mtafiti alikubaliana
na Carston (2002) kuwa katika upanuzi wa maana, ile maana ya kawaida inadondoshwa ili
kuweza kuzalika kwa maana iliyosimbwa.
Kwa muhtasari, mabadiliko ya kimaana katika agoti za wafungwa yalidhihirisha kuwa lugha ya
wafungwa ni hazina ya maana. Michakato yote ya kipragmatiki leksika ilijitokeza katika agoti za
wafungwa huku upanuzi na ubanaji wa kimaana ukijitokeza kwa upana zaidi. Mabadiliko ya
kimaana katika leksimu za wafungwa pia yalidhihirisha kuwa jamii ya wafungwa imeumbika
kinyume na jamii ya kawaida nje ya jela. Wafungwa wanakiuka matumizi ya kawaida ya
maneno katika Kiswahili na kuyabadilishia maneno hayo maana kwa manufaa yao. Kutokana na
88
hali hii, jamii ya wafungwa inaweza kurejelewa kama jamii yenye uasi kwa maana ya anti-
society. Isitoshe, mabadiliko ya kimaana yalidhihirisha usiri uliopo katika mawasiliano miongoni
mwa wafungwa. Utafiti huu ulibaini kuwa usiri ndio sababu kuu ya mabadiliko ya kimaana
kutokea katika lugha ya wafungwa. Wafungwa hubadili maana ya maneno ili kuficha siri zao
zisifahamike na askari au hata na wafungwa wengine.
4.4 Uundaji wa agoti za wafungwa na ubunaji wa maana mpya
Lengo la tatu la utafiti huu lilikuwa kujadili mbinu za uundaji wa agoti zinazotumiwa na
wafungwa wa magereza ya Kisumu. Uundaji wa maneno mapya pamoja na ubunaji wa maana
mpya ni kitengo ambacho pia hushughulikiwa na Nadharia ya Pragmatiki Leksika (Wilson,
2003). Hii husaidia katika kutoa data zaidi kwa nadharia hii na kupeana welewa wa mikakati ya
kiakili na hali za kimaumbile ambazo huhusika.
Ohly (1977) alitoa baadhi ya ruwaza za kuanzisha misamiati mipya katika Kiswahili. Kwanza
alizungumzia ukopaji wa maneno (Kutoka lugha ya Kingereza). Pili, uundaji wa maana mpya
ambayo inaweza kuwa; uundaji wa maneno mapya kikamilifu, maneno yaliyokuwepo
kuidhinishiwa maana mpya au kupewa mawanda ya kisemantiki ya kipekee au kwa kutumia
makundi ya kisintaksia yenye kijalizo. Mtafiti alikubaliana na mawazo haya kwani hadi nyakati
hizi pana leksimu ambazo zinaundwa au zinapata maana mpya au zinabadilishwa miundo
kimofolojia au kifonolojia na kwa njia hiyo kupata maana mpya.
Utafiti huu ulitumia kipengele hiki cha upanuzi wa maana katika kujadili mbinu mbalimbali za
uundaji wa agoti za wafungwa.
89
4.4.1 Ukopaji wa maneno
Agoti za wafungwa zinaundwa kwa ukopaji wa meneno. Ukopaji unahusu uhamishaji wa
kipashio fulani kutoka lugha moja na kukiingiza katika lugha tofauti. Yaani, kuna lugha pokezi
na lugha changizi (Jefwa, 2010). Hock na Joseph (1996) nao wanasema kuwa ukopaji ni
uhamishaji wa leksimu mahususi kutoka lugha moja au lahaja moja hadi nyingine. Huwepo aina
mbili za ukopaji: ukopaji sisisi na ukopaji tohozi. Ukopaji sisisi ni pale ambapo leksimu fulani
inahamishwa kutoka lugha changizi hadi lugha lengwa bila ya kufanyiwa marekebisho yoyote.
Jedwali 4.13: Mifano ya agoti zilizokopwa
Leksimu mkopo Leksimu asili Maana Lugha changizi
Karao/Krauni Crown Askari Kiingereza
Buti Boot Njia ya choo Kiingereza
Mablue Blue Mfungwa
msimamizi
Kiingereza
Geng’ Gang Kundi la wafungwa Kingereza
Wode Water Maji /pombe Kiingereza
Kurutu Recruit Asiyefahamu
mambo
Kiingereza
Wadhii Watu Wafungwa Kiswahili
Waya Wire Kifaa cha kuwasha
sigara
Kiingereza
Biskuti Biscuit Mahindi yaliyooza Kiingereza
Hoteli Hotel Jikoni Kiingereza
90
Neti Net Jela Kiingereza
Trekta Tractor Mfungwa mgeni Kiingereza
Ongosh Ongogo Mende Kijaluo
Redio Radio Simu Kiingereza
Katika mifano kwenye jedwali 4.13, si lazima neno lililokopwa liwe na maana ileile iliyopo
katika lugha changizi. Kwa mfano, neno neti lina maana ya jela katika muktadha wa jela. Maana
hii ni tofauti na maana ya neno hili katika lugha ya Kiswahili na pia katika lugha yenyewe
changizi. Neno hoteli pia linakopwa kutoka lugha ya Kiingereza hotel lakini linapewa maana
tofauti ili kurejelea jikoni. Hali hiyo pia ni sawa kwa neno trekta ambalo linatarajiwa
kumaanisha – chombo kinachofanana na gari na ambacho hutumiwa kukokota vitu. Linakopwa
toka neno la Kiingereza tractor lakini linapewa maana ya wafungwa wageni katika jela. Hivyo
basi, utohozi unaojitokeza katika lugha ya wafungwa ni wa viwango. Unahusu utohozi wa
kifonolojia na kimofolojia lakini si wa kisemantiki kwani maana inayotolewa baada ya kukopwa
ni tofauti.
4.4.2 Ubadilishaji silabi katika maneno
Ubadilishaji silabi ulibainika kama mbinu ya uundaji wa agoti za wafungwa. Katika ubadilishaji
silabi, neno kopwa huweza kutoholewa kwanza. Halafu, silabi za neno hilo toholewa
hupanguliwa. Upanguaji huu upya wa silabi za neno hilo husika hulipa neno hilo ujenzi au
muundo mpya wa kinyumenyume. Kama katika maelezo kuhusu utohozi, hapa pia maana ya
neno inaweza kubadilishwa.
91
Jedwali 4.14: Mifano ya agoti zilizobadilishiwa silabi
Leksimu changizi Agoti Lugha changizi
Fegi Gife Sheng
Card Dika Kiingereza
Gweno Nogwez Kijaluo
Mbwa Mbwauz Kiswahili
Ukuta Taukuz Kiswahili
Nyoka Kanyoz Kiswahili
Ngwara Rwanga -
Jedwali 4.14 linaonyesha baadhi ya istilahi zilizobadilishwa na wafungwa ili kuficha maana.
Neno fegi linabadilishwa na kuwa gife. Neno hili limekopwa kutoka msimbo wa Sheng. Card
ambalo ni neno la Kiingereza linatoholewa na kuwa kadi kisha linabadilishwa na kuwa dika.
Dika ina maana ya kitambulisho cha mfungwa. Neno gweno ambalo ni la Kijaluo linabadilishwa
na kuwa nogwez na kutumika katika mawasiliano ya Kiswahili. Nogwez yenye maana ya kuku
katika Kiswahili hutumiwa kurejelea bangi. Neno ukuta linabadilishwa na kuwa taukuz. Mageuzi
haya ya ukuta ni sawa na yale yanayotokea kwa nyoka ambayo inakuwa kanyoz. Neno ngwara
ambalo linatumika tu katika lugha ya wafungwa pia linabadilishiwa silabi na kuwa rwanga.
Kulingana na mifano hii, leksimu changizi ni maneno ambayo yanafahamika na wafungwa
pamoja maafisa wa magereza. Hata hivyo, wafungwa wanapotaka kuwapotosha askari,
wanazifanyia marekebisho leksimu zilizozoeleka ili kuwatenga askari husika. Tofauti na katika
92
Sheng ambapo hali hii pia hujitokeza, ubadilishaji silabi katika agoti za wafungwa aghalabu
huambatana na kubadilika kwa maana.
Ilibainika kuwa sifa hii ya lugha ya wafungwa huwafaidi zaidi wafungwa kwa sababu
inawawezesha kuficha siri zao ili maafisa wa magereza wasipate kuwaelewa moja kwa moja.
Ogechi (2005) anaeleza kwamba, neno husika hukopwa kisha matamshi ya neno hilo
kubadilishwa. Ubadilishaji silabi huu huwa ni utaratibu wa kimakusudi ambao hutumiwa na
wafungwa kuunda leksimu zao.
4.4.3 Ubunifu wa leksimu
Agoti za wafungwa zilidhihirisha ubunifu wa leksimu kama mbinu ya uundaji wa maneno. Kwa
mujibu wa Hartmann na Stork (1972) ubunifu ni mchakato wa kuunda leksimu mpya kimakusudi
kutokana na faridi za kimofolojia ambazo zipo. Katika jamii, hali fulani hujitokeza na kuwabidi
wanajamii husika kubuni msamiati wa kurejelea kifaa au hali ambayo ni geni kwao. Leksimu
hiyo huwa haihusishwi na ukopaji wala utohozi. Wafungwa wanapokumbana na vifaa vipya au
hali mpya katika mazingira ya jela, wao huzipa urejeleo. Leksimu katika lugha ya wafungwa
ambazo zinaonyesha hali hii ni:
Jedwali 4.15: Agoti zilizobuniwa
Leksimu zilizobuniwa gerezani Maana
Kibaba Kifaa cha kuwapimia wafungwa mafuta
Ngwara Silaha ya kukata wakati wa vita
Mruru Chombo kama mkebe cha kutia chakula
Mburga Jikoni
93
Chimano Jela
Kisuguu Mnara wa ulinzi
Jedwali hili linadhihirisha ubunifu wa kiwango kikubwa katika lugha ya wafungwa. Maneno
mapya yanabuniwa ili kurejelea hali mbalimbali au vitu vipya ambavyo vinapatikana katika
mazingira ya jela. Sehemu ya kupikia inavumbuliwa neno jipya mburga ambalo si neno la
kawaida katika Kiswahili sanifu. Jela pia linavumbuliwa neno jipya chimano.
Istilahi hizi zaelekea kusadifu maoni ya Irwin (1980) kuwa hali ngumu za magereza humpa
mfungwa ubunifu wa kiisimu na ule wa kufanya marekebisho (tazama pia Andersson na Trudgil,
1990)
Hivyo basi, lugha ya wafungwa wa magereza ya Kisumu ni „lugha pambani‟. Kwa mujibu wa
Looser (2001) sifa moja kati ya zile mbili za lugha pambani ni kuundwa kwa maneno mapya
kutokana na yale ambayo yapo. Maneno katika lugha ya kawaida yanabadilishwa na maneno
mapya ambayo yamebuniwa katika magereza na wafungwa. Katika data iliyopatikana, maneno
mengi yalichukua nafasi ya maneno ya Kiswahili sanifu. Nafasi ya neno jikoni ilichukuliwa na
neno jipya mburga. Nafasi ya neno jela ilichukuliwa na neno jipya chimano. Yaani, pana
uumbaji upya wa maneno (Halliday, 1978). Ingawa hivyo, ubunaji huu mpya wa maneno
kulingana na utafiti huu ni wa viwango kwani si kila neno katika Kiswahili sanifu limeumbiwa
neno jipya katika lugha ya wafungwa.
4.4.5 Kuchanganya msimbo
Uchambuzi wa data ulidhihirisha kuwa uchanganyaji msimbo kama mbinu ya uundaji wa
leksimu ni bayana. Kwa mujibu wa Fasold (1984) msimbo ni utaratibu wa mawasiliano
94
unaozingatia kanuni bayana za kisarufi na hasa uteuzi wa msamiati na maumbo ya sentensi.
Kuchanganya msimbo kunafafanuliwa na Richards na wenzake (1985) kama dhana ya
kuchopeka maneno au sehemu ya neno la lugha moja kwenye usemi wa lugha nyingine. Agoti
ambazo zilidhihirisha uchanganyaji msimbo ni:
Jedwali 4.16: Mifano ya uchanganyaji msimbo
Uchangayaji msimbo Maana
Ugali ya pan Ugali spesheli
Kuingiza boot Kuficha kwenye njia ya choo ili kisipatikane
na askari
Leta steam Leta pombe
Toa finger Toa pesa/hongo ili uishi vizuri
Kukula copper Kupigwa risasi
Mtu ordinary Anayeelewa hali na njia za jela
Mfungwa staff Mfungwa mwenye hadhi, hasa kutokana na
kuwa ana fedha nyingi
Kuchange quarter Wafungwa mashoga (ambao huwa kama
kike) wakishiriki ngono. Watoto wawili
wakishiriki ngono
Kutower Mfungwa mmoja kuchungulia ili askari
asiwapate wenzake wanaokiuka sheria
95
Jedwali 4.16 linaonyesha kuwa agoti za wafungwa zimesheheni uchanganyaji msimbo. Data
inaonyesha kuwa lugha zinazochanganywa zaidi katika uundaji wa agoti za wafungwa ni
Kiswahili na Kiingereza. Kwa mfano, kuingiza boot yenye maana ya kuficha kitu kwenye
makalio ili kisipatikane na askari kumeundwa kwa maneno kuingiza, ambalo ni neno la
Kiswahili pamoja na boot neno la Kiingereza. Ugali ya pan nayo ina neno la Kiingereza pan.
Hiki ni chakula kizuri kilichopikwa kwa mara ya pili; ugali uliokaangwa. Leta steam
imechanganya maneno leta ambalo ni Kitenzi katika Kiswahili na steam ambalo ni Nomino ya
Kiingereza. Kukula copper yenye maana ya kupigwa risasi imeundwa kwa kukula, neno la
Kiswahili na copper, neno la Kiingereza. Ni bayana kuwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili
ndizo zinachanganywa zaidi.
Tofauti na anavyosema Rayfields (1970) kuwa katika lugha ya kisasa, uchanganyaji msimbo
hutumiwa kusisitiza, utafiti huu ulibaini kuwa uchanganyaji msimbo hutumiwa na wafungwa
zaidi katika urejeleaji. Kwa mfano, mfungwa staff hurejelea mfungwa mwenye hadhi katika jela,
hutokana na hali kuwa mfungwa husika ana fedha nyingi, ana uwezo na anaheshimiwa. Ingawa
hivyo, sifa hii pia hujitokeza wakati ambapo mfungwa anatoa kauli au agizo. Kwa mfano,
mfungwa anapomwambia mwenzake „ingiza boot‟ anamwambia afiche vitu walivyonavyo. Toa
finger huambiwa mfungwa na mwenzake ili atoe hongo ili atetewe na wenzake gerezani.
Uchanganyaji msimbo pia unatokea katika mazingira ya jela ili kuficha siri. Kauli
zinazochanganyiwa lugha ni zile zinafahamika wazi katika Kiswahili cha kawaida. Kwa sababu
mfungwa hangetaka askari afahamu kile wanachozungumzia wanaingiza neno la Kiingereza ili
kumpotosha. Kutoa hongo linafumbwa katika maneno toa finger. Yaani, utoe kitu kidogo. Kula
copper, ni kukula risasi. Risasi ndiyo inafumbwa katika neno copper.
96
4.4.6 Ubadilishaji
De Klerk (1955) anafafanua kuwa ubadilishaji ni mchakato ambapo maneno yanabadilishana
kimaana. Data ilionyesha kuwa baadhi ya maneno katika lugha ya wafungwa yalibadilishana
nafasi.
Jedwali 4.17: mifano ya agoti zilizobadilishana nafasi
Agoti Asili
Redio Simu
Hoteli Jikoni
Neti Jela
Randa Kiboko
Kiswahili Ujanja
Kwekwe Askari mpekuzi
Jedwali 4.17 linadhihirisha hali ya ubadilishaji wa maneno. Redio ambayo ni chombo
kinachopokea mawimbi ya sauti k.v. ya mtangazaji kupitia hewani ili mtu mwingine asikie
kinachotangazwa, kinachukua nafasi ya neno simu ambayo ina maana tofauti. Mfungwa
hurejelea simu kama redio katika mawasiliano yao ili askari asipate kuwaelewa. Neno hoteli
linachukua nafasi ya neno jikoni katika mazungumzo ya wafungwa. Neno neti linatumiwa
kurejelea jela badala ya neno mwafaka, jela. Neno Randa ambalo lina maana tofauti na kiboko
linatumiwa kukirejelea kiboko. Kiswahili kinachukua nafasi ya neno ujanja. Ubadilishaji huu
hutokea ili kuficha siri za wafungwa zisifahamike na askari.
97
Uundaji wa agoti na ubunaji wa maana mpya ulidhihirisha ubunifu uliopo katika agoti za
wafungwa. Wafungwa walitumia mbinu mbalimbali kuunda agoti zilizotumika katika muktadha
wa jela. Hii ni kwa sababu uundaji wa agoti za wafungwa aghalabu uliandamana na ubadilishaji
wa maana au neno husika kuongezewa maana mpya. Hali ngumu za jela ziliibua ubunifu wa
kiisumu mingoni mwa wafungwa.
4.5 Hitimisho
Katika sura hii mtafiti amewasilisha na kuchanganua data aliyokusanya kupitia mahojiano ya
makundi na usaili. Uwasilishaji na uchambuzi huu wa data ulifanywa kwa kuzingatia
madhumuni mahususi ya utafiti huu na uliongozwa na mkabala wa kimaelezo. Aidha, Nadharia
Pragmatiki Leksika iliyotumika katika utafiti huu ulimsaidia mtafiti kupambanua misimbo katika
lugha ya wafungwa.
Utafiti huu ulifanikiwa kubainisha kuwepo kwa agoti zinazotumiwa na wafungwa. Mtafiti
aliziainisha agoti hizo katika vikoa maana mbalimbali. Uchambuzi wa mahusiano ya maneno
kimaana katika kila kikoa ulidhihirisha ulimwengu wa jela ulivyo. Uchambuzi wa mabadiliko ya
kimaana ulionyesha jinsi mabadiliko yote ya kimaana yalivyojitokeza katika agoti za wafungwa.
Mtafiti alifikia hitimisho kuwa agoti za wafungwa ni hazina ya maana. Michakato ya
kipragmatiki leksika pia ilionyesha jamii ya jela kama jamii yenye uasi kwa namna inavyobadili
matumizi ya kawaida ya maneno na kuyatumia katika jela kwa njia tofauti. Uasi huu
ulimwelekeza mtafiti kufikia hitimisho kuwa mabadiliko ya kimaana katika agoti za wafungwa
hutokea ili kukidhi haja ya kuficha siri katika mawasiliano miongoni mwa wafungwa. Hatimaye,
mtafiti alijadili uundaji wa agoti za wafungwa ambao ulisawiri lugha ya wafungwa kama iliyo na
98
kiwango cha juu cha ubunifu. Data kutoka kwa watafitiwa ilithibitisha madhumuni yote ya utafiti
huu.
99
SURA YA TANO
HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
5.1 Utangulizi
Sura hii inahitimisha utafiti uliohusu uchanganuzi wa matumizi ya agoti miongoni mwa
wafungwa wa magereza ya Kisumu. Sura hii imegawika katika sehemu sita. Sehemu ya kwanza
imetoa utangulizi wa sura. Sehemu ya pili inaeleza muhtasari wa utafiti. Sehemu ya tatu
inaangazia matokeo ya utafiti. Sehemu ya nne inafafanua mchango wa utafiti. Sehemu ya tano ni
hitimisho la utafiti. Sehemu ya sita inapendekeza maeneo yanayohitaji kufanyiwa utafiti zaidi.
5.2 Muhtasari wa utafiti
Utafiti huu uliochunguza matumizi ya agoti miongoni mwa wafungwa ulifanyika katika
magereza makuu ya Kibos na Kodiaga mjini Kisumu. Utafiti wenyewe ulikuwa na madhumuni
matatu. Kwanza, kujadili vikoa maana katika agoti zinazotumiwa na wafungwa wa magereza ya
Kisumu. Pili, kufafanua mabadiliko ya kimaana yanayojitokeza katika agoti zinazotumiwa na
wafungwa wa magereza ya Kisumu. Tatu, kujadili mbinu za uundaji wa agoti zinazotumiwa na
wafungwa wa magereza ya Kisumu. Mpangilio mzima wa kazi hii ulikuwa kama ufuatavyo:
Sura ya kwanza imebainisha taarifa zinazohusiana na mada ya utafiti. Sura hii imegawika katika
sehemu nane. Sehemu ya kwanza imetoa usuli wa utafiti. Sehemu ya pili imeangazia suala la
utafiti. Sehemu ya tatu imeeleza misingi ya uteuzi wa mada. Sehemu ya nne imezungumzia
lengo la utafiti. Katika kitengo cha tano mtafiti ameangazia maswali ya utafiti. Sehemu ya sita
imeelezea umuhimu wa utafiti. Kitengo cha saba kimefafanua upeo wa utafiti. Sehemu ya nane
imeangazia changamoto za utafiti.
100
Sura ya pili imechambua matini zinazohusiana na matumizi ya agoti miongoni mwa wafungwa.
Baada ya utangulizi mtafiti amepambanua matini kwa kujikita katika vipengele vinavyobainika
katika madhumuni ya utafiti. Sura hii pia imedhihirisha mwanya uliopo ambao utafiti huu
ulinuia kuziba.
Sura ya ya tatu ya utafiti huu unahusu njia na mbinu za utafiti. Sura hii imegawika katika sehemu
kumi. Baada ya utangulizi, sehemu ya pili inafafanua kuhusu mbinu za utafiti. Sehemu ya tatu
inaangazia muundo wa utafiti. Sehemu ya nne inaeleza kuhuu eneo la utafiti. Katika kitengo cha
tano, mtafiti ameangazia sampuli na usampulishaji. Sehemu ya sita imeelezea kuhusu vifaa vya
utafiti. Kitengo cha saba kimeshughulikia ukusanyaji wa data. Sehemu ya nane imeelezea
uchanganuzi wa data. Sehemu ya tisa imeangazia majaribio ya vifaa vya utafiti. Sehemu ya kumi
imefafanua kuhusu maadili ya utafiti.
Katika sura ya nne mtafiti ameshughulikia uwasilishaji na uchambuzi wa data. Sura hii ina
vitengo vitano. Sehemu ya pili inaangazia vikoa maana katika agoti za wafungwa. Sehemu ya
tatu inachambua na kujadili data iliyohusiana na mabadiliko ya kimaana katika agoti za
wafungwa wa magereza ya Kisumu. Katika sehemu ya nne, mtafiti amewasilisha na kuchambua
data kuhusu mbinu za uundaji wa agoti za wafungwa wa magereza ya Kisumu.
Katika sura ya mwisho, sura ya tano, mtafiti ametoa hitimisho na mapendekezo ya utafiti. Katika
sehemu ya pili pametolewa muhtasari wa kijumla wa utafiti. Katika sehemu ya tatu mtafiti
amefafanua matokeo ya utafiti huu. Kitengo cha nne kimeangazia mchango wa utafiti na sehemu
ya tano imetoa hitimisho la utafiti. Mwisho, sura hii imetoa mapendekezo kwa tafiti za baadaye.
101
5.3 Matokeo ya utafiti
Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchanganua matumizi ya agoti miongoni mwa wafungwa wa
magereza ya Kisumu. Matokeo ya utafiti huu yametolewa kulingana na madhumuni mahususi ya
utafiti.
Lengo la kwanza katika utafiti huu lilikuwa kujadili vikoa maana vya agoti zinazotumiwa na
wafungwa wa magereza ya Kisumu. Utafiti huu ulibainisha kuwa wafungwa wana agoti zao
ambazo huwawezesha kuwasiliana katika mazingira ya jela. Agoti zilizochambuliwa zilikuwa
katika lugha ya Kiswahili. Pahala ambapo palikuwepo na uchanganyaji wa msimbo sababu za
kuchanganya msimbo zilitolewa.
Palikuwepo na agoti zilizojumuishwa katika kikoa kipana cha mambo na shughuli za jela. Utafiti
huu ulibaini kuwa kitengo hiki ndicho chenye agoti nyingi zaidi. Agoti hizi zilihakikisha madai
kuwa wafungwa wanapoingia gerezani sharti wapitie maingiliano ya kitawi na kubuni na
kujifundisha lugha ya ulimwengu huu wa pili.
Palikuwepo pia na agoti zilizojitokeza katika kikoa maana cha wafungwa. Hizi zilikuwa leksimu
mbalimbali ambazo wafungwa hutumia kuwarejelea wafungwa wenzao katika muktadha wa jela.
Ufafanuzi wa agoti hizi ulibainisha kuwa pana wafungwa wa hadhi ya juu na wale wa hadhi ya
chini.
Kikoa maana kingine kilichochambuliwa ni kikoa cha maafisa wa magereza. Ni lesksimu
mbalimbali ambazo wafungwa hutumia kuwarejelea maafisa wa magereza. Ufafanuzi wa maana
za agoti hizi ulidhihirisha kuwepo kwa maafisa wa hadhi ya juu na wale wa hadhi ya chini kwa
mtazamo wa wafungwa. Agoti hizi pia zilidhihirisha uhusiano uliopo baina ya wafungwa na
102
maafisa wa magereza. Isitoshe, agoti hizi zilibainisha majukumu mbalimbali za maafisa wa
magereza kingazi.
Hivyo basi utafiti huu ulifanikiwa kuainisha agoti za wafungwa katika vikoa maana mbalimbali
kama ilivyodhamiriwa.
Lengo la pili la tafiti huu lilikuwa kufafanua mabadiliko ya kimaana yanayojitokeza katika agoti
zinazotumiwa na wafungwa wa magereza ya Kisumu. Mtafiti alipata kuwa agoti za wafungwa
zilipitia mabadiliko ya kimaana na kupata miktadha mipya kutokana na michakato mbalimbali ya
kipragmatiki leksika.
Aina zote za mabadiliko ya kimaana zilijitokeza katika agoti zinazotumiwa na wafungwa wa
magereza ya Kisumu na ziliweza kufafanuliwa kwa kujikita katika nadharia ya Pragmatiki
Leksika. Zile aina mbili kuu za mabadiliko ya kimaana, upanuzi wa maana na ubanaji wa maana
zilijitokeza. Kisio la maana lilijitokeza kwa leksimu chache sana likilinganishwa na mabadiliko
mengine ya maana. Upanuzi wa maana ulishirikisha aina zifuatazo za mabadiliko ya maana;
chuku, upanuzi wa kisitiari na upanuzi wa kategoria.
Utafiti huu ulibainisha kuwa agoti za wafungwa hazikupoteza maana zao za kileksika ila maana
hizi zilifanyiwa mageuzi kwa kujikita katika muktadha wa jela na zikapata fahiwa mpya.
Isitoshe, mtafiti alipata kuwa mabadiliko ya kimaana hujitokeza katika agoti za wafungwa ili
kukidhi haja ya wafungwa kufumba jumbe zao wanapowasiliana.
Lengo la tatu la utafiti huu lilikuwa kujadili mbinu za uundaji wa agoti zinazotumiwa na
wafungwa wa magereza ya Kisumu. Mtafiti alitumia kipengele cha ubunaji wa maana mpya na
uundaji wa leksimu kama aina ya upanuzi wa kimaana kujadili mbinu mbalimbali za uundaji wa
agoti za wafungwa.
103
Utafiti huu ulibainisha kuwa agoti za wafungwa huundwa kwa ukopaji wa maneno. Maneno
yalikopwa zaidi kutoka lugha ya Kiingereza. Ukopaji katika msimbo wa wafungwa ulipatikana
kuwa ni wa viwango kwa kuwa ulihusu utohozi wa kifonolojia na kimofolojia lakini si wa
kisemantiki. Maneno yaliyokopwa yalipewa maana tofauti na maana katika lugha changizi.
Baadhi ya agoti za wafungwa ziliundwa kwa kubadili silabi katika maneno. Neno lililozoeleka
au la kukopwa hupanguliwa kinyumenyume. Upanguaji huu upya hulipa neno husika muundo
tofauti. Ubadilishaji silabi hutumika zaidi katika kuficha siri. Mifano iliyofafanuliwa ilidhihirisha
kuwa neno lililopanguliwa upya liliweza kuongezewa silabi ili kulifumba zaidi.
Uchanganuzi wa data ulidhihirisha kuwa kulikuwepo na leksimu za wafungwa ambazo
ziliundwa kiubunifu katika mazingira ya jela. Mifano iliyotolewa ilibainisha kuwepo kwa
maneno mapya ambayo wafungwa hubuni ili kurejelea mambo mbalimbali katika mazingira ya
jela. Leksimu kama hizi mtafiti alipata kuwa hazikuhusishwa na ukopaji wala utohozi.
Uchanganyaji msimbo ulibainika kama mbinu ya uundaji wa agoti za wafungwa. Hapa, neno la
lugha ya kigeni linachopekwa katika maneno ya Kiswahili. Ilibainika kuwa wafungwa
huchanganya msimbo katika maneno ili kufumba maana za maneno, ili kurejelea mambo
mbalimbali, na kutoa agizo au kauli. Isitoshe, utafiti huu ulipata kuwa maneno katika lugha ya
wafungwa hubadilishana nafasi. Maneno mawili tofauti yaliweza kubadilishana maana. Neno
fulani lenye maana tofauti lilitumiwa kurejelea kitu kingine tofauti.
5.4 Mchango wa utafiti
Utafiti huu utachochea ari ya uundaji wa kamusi za agoti za wafungwa. Utafiti huu ulibainisha
kuwepo kwa agoti za wafungwa ambazo ziliainishwa katika vikoa maana mbalimbali. Kwa
104
kutumia agoti hizi na kuongezea zingine zinazotumiwa katika magereza mengine,
wanaleksikografia wataweza kutunga kamusi zenye kufafanua maana za istilahi mbalimbali
zinazotumiwa katika magereza. Kamusi zinazofafanua maneno katika muktadha wa jela
zimeweza kutungwa katika mataifa mengine, kwa mfano, Knight (2014) alitunga kamusi The
Dictionary of Victorian Prison Slang.
Utafiti huu umeibua muktadha mwingine wa matumizi ya lugha ambao haujatafitiwa katika
Kiswahili. Tafiti nyingi zilizochunguza miktadha ya matumizi ya Kiswahili zilifanywa
miongoni mwa raia. Utafiti huu hivyo basi utaibua ari ya watafiti kushughulikia lugha ya
wafungwa katika ngazi za Sintaksia, Semantiki, Pragmatiki na Isimujamii.
Nadharia ya Pragmatiki Leksika iliyotumiwa katika utafiti huu utakuwa ya manufaa katika
Kiswahili. Nadharia hii itawafaa watafiti wengine ambao watakuwa na haja ya kuitumia katika
kuchanganua na kuchunguza masuala ya kiisimu na kifasihi. Utafiti huu utakuwa kielelezo cha
kuonesha kuwa Nadharia ya Pragmatiki Leksika inafaa zaidi katika kuchanganua mabadiliko ya
kimaana katika lugha. Hii inatokana na ukweli kuwa nadharia hii ilifaulu kufafanua mabadiliko
ya kimaana katika muktadha wa jela.
Utafiti huu pia unachangia ukuzaji na uhifadhi wa agoti ambazo hutumiwa na wafungwa. Hii
itawasaidia watafiti wa baadaye kafanya urejeleaji na kufanya tafiti kuhusu mabadiliko ya
kimaana kiwakati.
5.5 Hitimisho la utafiti
Kwa kutimilika kwa malengo ya utafiti huu, ilidhihirika kuwa agoti za wafungwa ni hazina ya
maana. Leksimu mbalimbali zinazotumiwa na wafungwa ziliweza kufafanuliwa kimaana chini
105
ya kila kikoa maana. Michakato ya kipragmatiki leksika pia zilibainisha jinsi wafungwa hubadili
maana ya maneno katika muktadha wa jela ili kukidhi haja zao. Mtafiti pia alionyesha jinsi
wafungwa huunda maneno katika jela na kuyapa maana tofauti au kuyaongezea maana. Mtafiti
alifikia hitimisho kuwa lugha ya wafungwa ni hazina kuu ya isimu kutokana na jinsi wafungwa
walivyoonyesha ubunifu wa kiwango cha juu wa kuyapa maneno maana, kubadili maana ya
maneno na kubuni leksimu za kutumiwa kuwasiliana miongoni mwao.
5.6 Mapendekezo
Kwa kuwa utafiti huu ni wa kwanza kufanywa katika Kiswahili kuhusiana na lugha ya
wafungwa, na kwenye msingi wa ukweli kuwa tulibanwa kwenye upeo na mipaka yetu, pana
mambo mbalimbali ya kufanyiwa utafiti katika eneo hili la lugha ya wafungwa ambayo
hayakushughulikiwa katika utafiti huu. Hivyo basi mtafiti anapendekeza yafuatayo:
Kufanywe utafiti ambao utachunguza mabadiliko ya kidaikronia ambayo yanaweza kuwepo
katika agoti za wafungwa. Kwenye utafiti huu, mtafiti alijibana katika kujadili mabadiliko ya
kimaana katika agoti za wafungwa kwa kujikita katika muktadha wa matumizi. Hakuingia ndani
na kushughulikia etimolojia ya kale ya leksimu hizi ambayo ingempa msingi mzuri sana wa
mabadiliko ya kimaana kulingana na vipindi tofauti vya wakati.
Ni bayana kuwa utafiti huu ulijikita katika matini za kimazungumzo. Kwa kuwa sajili ya jela ni
kimuli cha msingi wa utangamano wa jamii, panahitajika utafiti zaidi ambao utashughulikia
matini andishi za jela. Watafiti wanaweza kuchunguza lugha katika hadithi mbalimbali
walizoziandika wafungwa, maandishi kwenye seli na vyoo vya wafungwa pamoja na maandishi
kwenye miili ya wafungwa.
106
Mwisho, utafiti huu ulichunguza matumizi ya lugha katika gereza la wafungwa wanaume. Ni
bayana kuwa wanawake na wanaume hutumia lugha kwa njia tofauti. Hivyo basi, mtafiti
anapendekeza kuwa kufanywe tafiti kuchunguza matumizi ya lugha katika gereza la wanawake
na ulinganisho wa kina ufanywe.
107
MAREJELEO
Aitchison, J. (2003). Words in the Mind: An Introduction to the Mental Lexicon. (Third Edition).
U.S. A: Blackwell Publishing Limited.
Alatias, J. (1992). Language Communication and Social Meaning. Washington, D.C: Gergetown
University Press.
Allan, K. & Burridge, K. (2009). Forbidden words: Taboo and Censoring of Language.
Cambridge: Cambridge University press.
Anderson, L., & Trudgil, P. (1990). Bad Language. Oxford, UK: Blackwell.
Anusu, A. (2015). Usawazishaji Leksimu katika Kiswahili: Utafiti wa Vihiga. Tasnifu ya uzamili
ambayo haijachapichwa, Chuo Kikuu cha Nairobi.
Bentley, William K. & James M. (1992). Prison Slang: Words and Expressions Depicting Life
Behind Bars. Jefferson: McFarland and Company.
Berger, P., & Luckman, T. (1971). The Social Construction of Reality: A Treatise in the
Sociology of Knowledge. Harmondsworth: Penguin University Books.
Binyanya, M. (2014). Sajili ya Maafisa wa Polisi: Tathmini ya Matumizi ya Lugha ya Kiswahili
katika Kituo cha Polisi cha Central, Nairobi. Tasnifu ya uzamifu ambayo
haijachapishwa, Chuo Kikuu cha Nairobi.
Blank, A. (1998). Historical Semantics and Cognition, Berlin and New York: Mouton.
Bloomfield, L. (1930). Language. New York: Holt, Reinhart and Winston.
108
Bloomfield, L. (1933). Language. London: Compton Printing ltd.
Blutner, R. (1998). Lexical Pragmatics. In A Journal of Semantics, Volume 15(2).
Blutner, R. (2011). Some Perspectives on Lexical Pragmatics, Pragmatics Reader: Routledge,
London.
Bogdad, R. & Biklen, S. (1992). Quantitative research for Education: An introduction to Theory
and Methods, (2nd
ed.), Boston, Allyn and Bacon.
Bondesson, U. (1989). Prisoners in the prison societies. New-Brunswick, NJ: Transaction.
Boswell, C. & Cannon, S. (2009). Introduction to nursing research: incorporating evidence-
based practice 2nd ed. UK: Jones & Bartlett Learning.
Buliba, A., Njogu, K. na Mwihaki, A. (2006). Isimujamii Kwa Wanafunzi wa Kiswahili.
Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
Bullock, B. (1996). Popular Derivation and Linguistic Inquiry; les Javanis. AATF.
Burke, P. & Porter, R. (Eds.) (1995). Languages and Jargons: Contributions to a Social History
of Language. Polity Press.
Cardozo-Freeman, I. (1995). The lingo of the Pintos. Bilingual Review, 20(1)
Carston, R. (2002) Thoughts and Utterances: The Pragmatics of Explicit Communication.
Oxford: Blackwell Publishing.
Carston, R. (2004) Thoughts and Utterances: The Pragmatics of Explicit Communication,
Oxford: Blackwell Publishers Limited.
109
Ciechanowska, N. (2015). Towards the functions of prison slang. Univeristy of Rzeszow.
Clemmer, D. (1940). The Prison Community. Newyork: Elsevier.
Coleman, J. (2004). A History of Cant and Slang Dictionaries. 2Vols. Oxford: Oxford UP.
Condon, J.C. & Yousef, F. (1975). An introduction to intercultural communication. New York:
Macmillan.
Dean-Brown, J. (1992). Social Meaning in Language, Curriculum and Through Language
Curriculum. In Alatias, J. (Ed) Language Communication and Social Meaning.
Washington, DC: Georgetown University Press.
Dirk, G. (2010). Theories of Lexical Semantics. Oxford University Press: New York
Einat, T., & Einat, H. (2000). Inmate argot as an expression of prison subculture: The Israeli
Case. The Prison Journal, 80(3), 309-325.
Einat, T., & Einat, H. (2003). The Evolving Nature of Prison Argot and Sexual Hierachies. The
Prison Journal, 83 (33), 289-300.
Ellis, P. (2005). The Prison-House and Language: Modern American Prison Argot, Toronto.
Encinas, G. (2001). Prison argot: A sociolinguistic and Lexicographic Study. Lanham,
Maryland; UP of America.
Enon, C. J. (1998). Education Research and Measurement, Department of Distance Education;
Makerere University; Uganda.
Fasold, R. (1984). The Sociolinguistics of Language. Oxford: Blackwell.
110
Fishman. J. A. (1972). The sociology of language: An interdisciplinary social science approach
to language in society. Rowley, M.A: Newbury House.
Fisher, S. (1990). On the Move: The Psychology of Change and Transition. Chichester, UK:
Wiley.
Foster, H. (1986). Ribbin', jivin', & playin' the dozens. Amherst, NY: Foster & Associates.
Fromkin, V. & Rodman, R. (1993). An Introduction to Language (5th
ed.). New York: Harcourt
Brace College Publishers.
Gal, S. (1979). Language Shift: Social determinants of linguistic change in bilingual Asustria.
New York: Academic Press.
Gall, M. et al. (1996) Educational Research: An Introduction. New Yorl: Longman.
Gay, L. & Diehl, P. (1992) Research Methods for Busines and Management. New York:
Mcmillan.
Glucksberg, S. (2001). Understanding Figurative Language: From Metaphors to Idioms.
Oxford: Oxford University Press.
Goffman, E. (1962). Asylums: Essays on the Social Situation of Mental Patients and Other
Inmates. Chicago: Aldine Publishing Company.
Good, C. (1972). Essentials of Education: Research Methodology and Design. New York:
Meredith Corporation.
111
Gohodzi, I. (2013). A critical Analysis of Prison as Discourse Communities; an Examination of
Whahwa Prison Complex. Unpublished Research Project, Midlands State
University.
Gumperz, J. (1982). Language and Social Identity. Cambridge: Cambridge University Press.
Habwe, J. (199). Discourse Analysis of Swahili Political Speeches. Chuo Kikuu cha Nairobi.
Tasnifu ya PhD. (Haijachapishwa).
Habwe, J. & Karanja P. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers
Limited.
Halliday, M. et al. (1964). The Linguistics Science and Language Teaching.London: Longman.
Halliday, M. (1994). An Introduction to functional grammar. 2nd edition. London: OUP
Halliday, M. (1978). Language as Social Semiotic: The Social Interpretation of Language and
Meaning. London: Edward Arnold.
Holloway, I & Wheeler, S. (2002) Qualitattive Research in Nursing. 2nd edition. Oxford:
Blackwell Publishing
Holloway, I. (1997). Basic Concepts in Qualitative Research. Oxford. Blackwell Science
Hartmann, R., & Stork, F. (1972). Dictionary of Language and Linguistics. London: Applied
Sciences.
Harris, B. (2012). What Is Argot? (n.d.). Retrieved November 20, 2017, from wise
GEEK:http://www.wisegeek.com/what-is-argot.htm. Conjecture Corporation.
112
Hensley, C. (Ed.). (2002). Prison sex: Practice and policy. Boulder, CO: Lynne
RiennerPublishers.sexual hiereches.
Hensley, C. et al (2003). The evolving nature of prison argot and sexual hirechies. The Prison
Journal 83.3.
Hock, H & Joseph, B. (1996) Trends in Linguistics Studies and Monographs 93: Language
History, Language Change and Language Relationship; An Introduction to
Historical and Comperative Linguistic. New York: Mouton DeGruter.
Horn, L. & Ward, G. (2004). The Handbook of Pragmatics, Oxford: Blackwell
Hudson, R.A. (1980). Sociolinguistics. Cambridge, UK: Cambridge University Press.
Ingule, F. & Gatumu, H. (1996). Esssentials of Educational Statistics. Nairobi. East African
Educational Publishers.
Irwin, J. (1980). Prisons in turmoil. Boston: Little, Brown.
Irwin, J. (1985). The jail. Berkeley: University of California Press.
Ito, J. Y. Kitagawa & A. Mester (1996). Prosodic Faithfulness and Correspondence: Evidence
from Japanese Argot. Lingua, 237-258.
Jackson, B. (1967). Prison Nicknames. Western Folklore 26.1: pg48-54.
Jeffers, J & Lehiste, I. (1979) Principles and Methods for Historical Linguistics. London: The
MIT Press-Cambridge, Massachusetts
Jefwa, G. (2010). Utangulizi wa Isimu. Nairobi: Kenya Literature Bureau.
113
Keith, G., & Shuttleworth, J. (2000). Living Language. London: Hodder and Stoughton.
Kempson, R. (1977). Semantic Theory. Cambridge University Press.
Kenya Human Rights Commission (2002). Improving Prison Conditions in Kenya: Propasals
and Recommendations
Kimani, N; Njogu, K. & Buliba, A., (2006). Isumujamii kwa wanafunzi wa Kiswahili. Nairobi:
Jomo Kenyatta Foundation.
Knight, J. (2014). A Dictionary of Victorian Prison Slang. Victoria: Australia.
Kobia, J. (2006). Sheng is not a Language but a Popular Slang. Sunday Nation, Nairobi,
February 2.
Kolaiti, P. & Wilson, D. (2012). Corpus Analysis and Lexical Pragmatics: An Overview.
http:www.phon.ucl.ac.uk? home/deride
Kress, T. (2008). Critical Praxis Research; Breathing New Life into Research Methods for
Teachers, United States of America; Springer.
Kombo, D. & Tromp, D. (2006). Proposal and Thesis Writing: An Introduction, Pauline‟s
Publications Africa, Nairobi.
Kothari, C. R. (1990). Research Methodology: Methods and Technique, Willey Eastern Limited,
New Delhi.
Kothari, C. R. (2004). Research Methodology; Methods and Techniques, 2nd Edition, New
Delhi; New Age International (P) Limited Publishers.
114
Kothari, C. R. (2008). Research Methodology; Methods and Technique. New Age International
(P) Limited, New Delhi.
Labov, W. (1972). Language in the inner city. Philadelphia: Pennyslavania University Press.
Lee, D. (1992). Competing Discourses: Perspective and Ideology in Language. New York:
Longman.
Leslau, W. (1988). Fifty Years of Research: Selection of articles on Semitic, Ethiopian Semitic
and Cushitic Languages. Harrasswitz: Wobaden.
Looser, D. (2001). Boobslang: A lexicographical study of the argot of New Zealand prison
inmates, in the period 1996-200. Unpublished PhD theses, University of Cantebury.
Lourens, L et al. (1992). Only Study Guide for SEMANO-Y (Revised Ed). Pretoria: UNISA.
Lyons, G. (1984). Inmates and Convicts: The Language of Inclusion and Exclusion. The SECOL
Review: Southeastern Conference on Linguistics 8 (3). Murfreesboro, Tenn.: The
Conference.
Mathews, P. (1997). The Concise Oxford Dictionary of Linguistics. Oxford-New York: Oxford
University Press.
Maurer, D. (1981). Language of the Underland. Lexington, KY: The University Press.
Mmbwanga, K. (2010). New Words and Meanings on Facebook: A LexicalPragmatics Analysis,
Unpublished M. A. Thesis: University of Nairobi.
115
McArthur, T. (1996) The Oxford Companion to The English Language. GB: Oxford University
Press
McCawley, J. (1978). Where you can shove infixes. Syllables and segments, ed. by Alan Bell &
Joan Hooper, 213-21. Amsterdam: North-Holland.
Mclntyre, T. & Mack, D. (1993). The streetsmart correc tional educator. Educating Adjudicated,
Incarcer ated & At-Risk Youth, 1, 35-43.
Mdee, J. na wenzake (2011). Kamusi ya Karne ya 21, Nairobi; Longhorn Publishers Limited.
Mekacha, D. (2011). Isimujamii: Nadharia na Muktadha wa Kiswahili. Dar es Salaam: TUKI
Milroy, L. (1980). Language and Social Networks: Oxford: Basil Blackwell.
Msanjila, Y. P na wenzake (2009). Isimujamii Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam.TUKI.
Msanjila, Y. P na wenzake (2011) Isimujamii: Sekondari na Vyuo. TUKI. Dar es Saalam.
Mugambi, A. (2007). Utohozi Maana Katika Maneno ya Sheng. Tasnifu ambayo
haijachapishwa, Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Mugenda, O., & Mugenda, A. (2005). Research Methods: Quantitative Approaches. Nairobi:
ACTS Press.
Mugendi, N. (2016). Morphology of the Gitamanya argot of the Matatu Crew of Embu Town;
Unpulished MA Thesis: Kenyatta University.
Mukhwana, A (2008). Language Attitudes in Urban Kenya: A Case Study of Nairobi, Kisumu
and Mombasa. Phd Theses (unpublished), University of Nairobi.
116
Mulokozi, M. (2003). Utafiti wa fasihi simulizi, katika makala ya semina ya Kimataifa ya
waandishi wa Kiswahili. TUKI. Dar es Salaam. Uk 18-26.
Mulvey, C. (2013). Prison Lingo: The Language of the Prison Community. Universuty of
Wnichester, Sparkford, Winchester.
Muyuku, A. (2009). Language Mixing in the Language of Advertising: A Case Study of
Commercial Banks and Mobile Telecommunications in Kenya, Unpublished M. A.
Thesis: University of Nairobi.
Mwangi, P. & Mukhwana, A. (2011) Isimujamii. Nairobi: Focus Publishers
Nyakundi, P. (2010). Motivation, Morpho-phonological Processes in Egesembesa Argot Among
Ekegusii-Speaking Males of Western Kenya; Unpublished MA Thesis: Kenyatta
University.
Newbold, G. (1989). The Maximum Security Prisons in New Zealand. Oxford University Press.
Ngugu, T. (1986). Decolonizing the mind: language of African politics, Heinemann: London.
Ngure, A. (2003). Fasihi Simulizi kwa Shule za Sekondari. Nairobi: Pheonix Publishers.
Nielson, A., & Scrapitti, T. (1995). Argot use in theraupitic community; Deviant Behavior,
16(3), 127-129.
Njimu, P. (2010). Lexical Adjustments of Sports Language in Three Kenyan Newspapers. Chuo
Kikuu cha Nairobi. Tasnifu ya M.A (Haijachapishwa).
117
Ochichi, A. (2013). Uwazi na Umaanisho: Usimbaji Maana Kimazungumzo Katika Ekegusii na
Kiswahili. Chuo Kikuu cha Nairobi. Tasnifu ya M,A (Haijachapishwa)
Ochoki, B. (2010). Pragmatics Interpretation Contraints in Kenyan Hip Hpo Lyrics. Chuo Kikuu
cha Nairobi. Tasnifu ya M.A (Haijachapishwa).
Ogechi, N.O. (2005). Lexocalization in Sheng. Nordic Journal of African Studies 14 (3), 334-33.
Ohly, R. (1977) Patterns of New-Coined Abstract Terms (Nominal forms) in Modern Swahili
katika Journal of the Institute of Kiswahili Research (Vol.47/1) Dar es Salaam:
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Orodho, J. (2005). Elements of Educational and Social Science Research Methods. Nairobi:
Masola Publishers.
Owino, B., Omar, B., & Akong‟a, J. (2015). Looking in the Mirror: Reflections in
implementation of the principles of penal systems in Kenya‟s prisons. In the
Journal of International Academic Research for Multidisciplinary VOL 1(3).
Pallock, J. (2006). Prisons today and tomorrow. Sundbry: Jones and Burtlett Publishers.
Partridge, E. (1970). Slang today and yesterday. London: Routledge, Kegan & Paul.
Rayfields, J. (1970). The Languages of a Bilingual Community.The Hague: Mouton.
Richards et al, (1985). Longman Dictionary of Applied Linguistics. U.K, Longman Group.
Ramani, K (2006). Leave Sheng to Matatu Touts and Mucisians. The Standard, September 29.
Sigh, K. (2007). Quantitative Social Reseach Methods, India; SAGE Publication.
118
Simiyu, C. (2016) The Portrayal of men and women in selected Bukusu Circumcision Songs: A
Lexical Pragmatic Approach. Chuo Kikuu cha Nairobi. Tasnifu ya M.A.
(Haijachapishwa)
Sykes, M. G. (1958). The Society of Captives. Princeton, NJ: Princeton University Press.
Sykes, M.G., & Messsinger, S.L (1960). The inmate social code and its functions: Social science
research council. 15, 401-405.
Szabo, E. (2005). Hungarian Prison Slang Today; From 1996-2005. (Phd Theses), Debrecen.
Ngugi, T. (1986). Decolonising the Mind: The Politics of Language in African Literature.
London: J. Currey Ltd
Trier, J. 1931. Der deutsche Wortschatz im Sinnbezirk des Verstandes. Heidelberg: Winter.
TUKI (1990). Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. Dar es Salaam: Education publishers and
Distribution LTD.
TUKI (2013). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press
Toch, H. (1992). Mosaic of Despair. Washington, DC: American Psychological Association.
Toch, H., & Johnson, R. (1982). The pains of imprisonment. Beverly Hills, CA: Sage.
Ullmann, S. (1957). The Principles of Semantics, Blackwell and Mott.
Ullmann, S. (1962). An Introduction to the Science of Meaning, Oxford: Blackwell.
Ullmann, S. (1970). Semantics: An Introduction to the Science of Meaning. Oxford: Basil
119
Ullman, S. (1977). Change of Meaning. In H. Hungerford et al., English Linguistics. Illinois:
Scott, Foresman and Company.
Vartanian, T. P (2011). Secondary Data Analysis, New York; Oxford University Press.
Yule, G. (1996). Pragmatics. Oxford: Oxford University Press.
Yule, G. (2006). The Study of Language: An Introduction .Cambridge: Cambridge University
Press.
Walliman, N. (2011). Research Methods; The BasicLondon & New York; Routledge Taylor&
Francis Group.
Wambugu, W. (2010). Semantic Shifts in Gikuyu Lexemes: A Lexical Pragmatic Approach.
Unpublished M.A. Thesis: University of Nairobi.
Wamitila, K. (2010). Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. Vide Muwa Publishers, Kenya.
Wilson, D. (2003). Relevance and Lexical Pragmatics, in Italian Journal of Linguistics, Italy.
Wilson, D. & Cartson, R. (2007). A Unitary Approach to Lexical Pragmatics: Relevance,
Inference and ad hoc Concepts.
120
KIAMBATISHO I: MWONGOZO WA MAHOJIANO
Ninaitwa Ogutu Peter. Mimi ni mwanafunzi wa somo la Isimu ya Kiswahili (uzamili) katika
Chuo Kikuu cha Kisii. Ninafanya utafiti kuhusu agoti ya wafungwa. Naomba uchukue muda
wako kujadiliana nami kuhususiana na masuala haya. Toa habari za kweli bila uoga wowote.
Jina lako halitachapishwa popote katika kazi hii. Habari zote zitashughulikiwa kama siri.
Sehemu A
1) Umri wako (age)
………………
2) Kiwango cha elimu
a) Elimu ya msingi …….b) Elimu ya sekondari…….c) Elimu ya chuo cha anuwai….d) Chuo
kikuu……….e) Nyingineyo (bainisha) ……..
Sehemu B
1) Kwa ujumla, je pana maneno ambayo mnayafahamu na lakini maafisa wenu hawawezi
kuyaelewa? Je, kuna maneno ambayo nyote mwaelewa?
2) Je pana mahusiano ya kimapenzi ndani ya magereza? Kama ndiyo maneno yepi yanatumia
kurejelea mahusiano haya? Wafungwa na vitendo vya ngono vinarejelewa vipi humu gerezani?
3) Pana marufuku, bidhaa na vifaa ambavyo haviruhusiwi kuingizwa gerezani? Maneno yapi
hutumiwa kurejelea vitu hivi?
4) Je, dawa za kulevya zinarejelewa kwa kutumia majina yapi? Nipe maana ya maneno haya
121
5) Kuna baadhi ya mambo na shughuli zinazofanywa hapa gerezani. Je mnazirejelea kwa majina
gani?
6) Mnatagusana na maafisa wa magereza katika maisha yenu humu? Maneno yapi mbalimbali
ambayo ninyi hutumia kuwarejelea
7) Kuna maneno mbalimbali ambayo ninyi hutumia kuwarejelea wafungwa wenzenu? Je maneno
haya ni yapi? Tafadhali nipe maana ya maneno haya?
8) Je, pana maneno fulani ambayo yanatumiwa na kundi fulani la wafungwa? Je maneno haya ni
yapi?
Sehemu C
13) Je una maoni yoyote kuhusu lugha ya mnayozungumza humu ambayo itasaidia utafiti huu ?
Tujadiliane.
14) Pana neno lolote linalotumiwa humu ambalo hatujajadiliana kulihusu? Tafadhali liandike
katika kijikaratasi ninayokupa na unipe maana.
122
KIAMBATISHO II: KIBALI CHA UTAFITI (KAUNTI YA KISUMU)
123
KIAMBATISHO III: BARUA YA IDHINI (NACOSTI)
124
KIAMBATISHO IV: CHETI CHA IDHINI (NACOSTI)
125
KIAMBATOSHO V: KIBALI CHA UTAFITI (MAGEREZA YA KENYA)
126
KIAMBATISHO VI : KIBALI CHA KUHOJIWA
127
KIAMBATISHO VII: UCHAPISHAJI
128
KIAMBATISHO VIII: RIPOTI YA UHALALI WA UTAFITI