Upload
denniseudes
View
848
Download
4
Embed Size (px)
DESCRIPTION
Wanafunzi Wanaoomba Kudahiliwa Upya(Re-application for Admission)
Citation preview
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania- TCU
Yah: Wanafunzi Wanaoomba Kudahiliwa Upya (Re-application for Admission) Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania inapenda kuwaarifu wanafunzi waliokuwa wamedahiliwa miaka ya nyuma na kwa sababu moja au nyingine wakashindwa kuendelea na masomo yao wanatakiwa wafanye yafuatayo; 1. Kwa wale ambao walichaguliwa na hawakuripoti kwenye vyuo
walivyodahiliwa wanatakiwa waandike barua Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania wakitoa maelezo na sababu zilizopelekea wao kushindwa kuanza masomo yao na kwamba wanaomba kuruhusiwa kufanya maombi upya. Barua hizi zinatakiwa ziambatanishwe na taarifa ya uthibitisho wa kutokuripoti (confirmation letters) kutoka vyuo walivyokuwa wamedahiliwa
2. Kwa wale wanafunzi ambao walidahiliwa na kusajiliwa kwenye vyuo husika, wanatakiwa waandikie barua Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, wakieleza vyuo na programu walizokuwa wamedahiliwa pamoja na sababu zilizopelekea wao kushindwa kuendelea na masomo yao na kwamba wanaomba kuruhusiwa kuomba upya. Barua hizi zinatakiwa ziambatanishwe na taarifa ya kuacha masomo (clearance letters) kutoka vyuo walivyokuwa wamesajiliwa
NB: 1.Barua za waombaji wa aina zote mbili lazima ziwe na taarifa za msingi ikiwa ni pamoja na majina halisi ya mwombaji, Index namba ya Kidato cha Nne na
mwaka aliomaliza, barua pepe (email address) pamoja na namba ya simu ya mhusika ili kurahisisha mawasiliano 2. Majina ya waombaji yaliyokwishafanyiwa kazi na kupatiwa kibali cha kuruhusiwa kuomba upya yatatangazwa kwenye tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania. Pia watapata taarifa kupitia namba zao za simu na barua pepe. MUHIMU. Kusoma ama kupakua orodha ya walioruhusiwa kuomba upya udahili kwa mwaka wa masomo 2015/16 bonyeza hapa chini.
1. Batch One.