51
KITINI CHA HABARI NA MAPENDEKEZO YA KISERA WANYAMAPORI KWA WATANZANIA WOTE: KUSIMAMISHA UPOTEVU, KUENDELEZA RASLIMALI NA KUPANUA MAFAO Jumiko la Maliasili Tanzania Tanzania Natural Resource Forum Oktoba 2008 Kwa kushirikiana na

WANYAMAPORI KWA WATANZANIA WOTE: KUSIMAMISHA … · 2008. 10. 18. · KITINI CHA HABARI NA MAPENDEKEZO YA KISERA WANYAMAPORI KWA WATANZANIA WOTE: KUSIMAMISHA UPOTEVU, KUENDELEZA RASLIMALI

  • Upload
    others

  • View
    7

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

  • KITINI CHA HABARI NA MAPENDEKEZO YA KISERA

    WANYAMAPORI KWA WATANZANIA WOTE:

    KUSIMAMISHA UPOTEVU, KUENDELEZA RASLIMALI NA KUPANUA MAFAO

    Jumiko la Maliasili Tanzania

    Tanzania Natural Resource Forum

    Oktoba 2008Kwa kushirikiana na

  • HABARI JUU YA WANYAMAPORI KATIKA TANZANIA

    Wanyamapori kwa watanzania wote: Kusimamisha upotevu, kuendeleza raslimali na kupanua mafao

    Jumiko la Maliasili Tanzania

    Tanzania Natural Resource Forum

    Yaliyomo

    Kwa kushirikiana na

    © JMT 2008

    Kuhusu Machapisho Haya

    Muhtasari

    Chapisho Na. 1: Mwisho wa Wanyamapori? Kupungua na Kuharibiwa kwa Wanyamapori Tanzania

    Chapisho Na. 2: Sababu za Kupungua kwa Wanyamapori Tanzania

    Chapisho Na. 3: Kukuza Maduhuli kutokana na Matumizi Endelevu ya Wanyamapori

    Chapisho Na. 4: Usimamizi wa Wanyamapori na Kupunguza Umaskini

    Chapisho Na. 5: Kuwianisha Wanyamapori na Maslahi ya Jamii: Umuhimu wa Kushirikisha Sekta Mbalimbali

    Chapisho Na. 6: Desturi Nzuri za Usimamizi wa Wanyamapori - Kujifunza kutoka katika Kanda

    Chapisho Na. 7: Mapendekezo ya Kisera kwa Kuendeleza Wanyamapori Tanzania Rejea

    A-1

    M-1

    1-1

    2-1

    3-1

    4-1

    5-1

    6-1

    7-1

    R-1

  • HABARI JUU YA WANYAMAPORI KATIKA TANZANIA

    Wanyamapori kwa watanzania wote: Kusimamisha upotevu, kuendeleza raslimali na kupanua mafao

    Jumiko la Maliasili Tanzania

    Tanzania Natural Resource Forum

    KUHUSU MACHAPISHO HAYAKwanini wanyamapori?Wanyamapori ni moja ya maliasili muhimu Tanzania. Kwa kuweka msingi wa utalii nchini, wanyamapori wana umuhimu wa kiuchumi. Ingawa serikali imewekeza vya kutosha, wanyamapori wameendelea kupungua kwa nchi nzima kama zinavyoonesha takwimu. Kupungua kwa wanyamapori kutaendelea kujitokeza mahali mahali kwa vile idadi ya watu imeongezeka mara nne tangu wakati wa uhuru na hivyo ardhi zaidi inatakiwa kwa ajili ya kilimo na matumizi mengine. Hata hivyo watu wengi wanafikiria kupungua kwa wanyamapori kunahusishwa na mfumo uliopo wa usimamizi wa wanyamapori. Na mapungufu hayo yamesababisha kutofikia malengo ya kugawanya mafao ya kiuchumi kitaifa na katika jamii, kukosekana kwa uwekezaji katika wanyamapori, migogoro baina ya mahitaji ya jamii na sera za uhifadhi, na hatimaye kupungua kwa idadi ya wanyamapori.

    Machapisho haya ya kisera yanalenga kutoa mapendekezo ya kujenga juu ya jinsi uwekezaji unaovutia kwa serikali ya Tanzania na jamii katika uhifadhi wa wanyamapori uboreshwe ili kuwa endelevu, wenye haki na matokeo yenye manufaa. Ni kwa vipi wanyamapori wanaweza kuwa na faida kwa kila mtanzania hasa watanzania waishio vijijini ambako maisha ya wanyamapori yanategemea?

    Machapisho haya ni kwa ajili ya nani?Machapisho haya yameandaliwa kama vitini kwa ajili ya watunga sera na umma kwa ujumla ambao wanataka habari katika sekta ya wanyamapori. Machapisho

    haya yanatoa habari, takwimu, na uchambuzi yakinifu juu ya mwelekeo na idadi ya wanyamapori Tanzania, sababu za mwenendo huo na uhusiano wa ukuaji wa uchumi kitaifa, kupunguza umaskini, na usimamizi wa wanyamapori. Lengo la habari ni kuhimiza mjadala uliojuvywa juu ya sera na desturi zinazosimamia wanyamapori katika Tanzania.

    Je, machapisho haya yana uwiano sawa na ni yenye haki?Kila jitihada imefanyika ili kuanzisha uchambuzi wenye uwiano sawa juu ya masuala kwa kutegemea takwimu na habari zilizopo. Utalii wa uwindaji na ule wa picha, vyama hiari (mashirika ya kijamii, mashiriki yasiyo ya kiserikali nchini, na yale ya kimataifa), serikali (Idara ya Wanyamapori) na watalaam wa kujitegemea wote wamehusishwa katika uandaaji wa machapisho haya. Kila jitihada imefanyika ili kutokuhimiza matakwa ya mtu au kikundi binafsi dhidi ya wengine – kila mmoja ana nafasi katika usimamizi na kufaidika kutokana na wanyamapori Tanzania!

    Kuchimbua zaidi kutokana na machapisho haya Muhtasari wa mapitio mwanzoni mwa machapisho haya unatoa habari muhimu na mapendekezo ya kisera kwa ufupi. Baada ya hapo machapisho yamepangwa kwa mfuatano wa mada kwa maeneo makuu ya sekta ya wanyamapori. Orodha ya vyanzo vya habari na kujifunza zaidi vimewekwa.

    © JMT 2008

    Kwa kushirikiana na

  • HABARI JUU YA WANYAMAPORI KATIKA TANZANIA

    Wanyamapori kwa watanzania wote: Kusimamisha upotevu, kuendeleza raslimali na kupanua mafao

    Jumiko la Maliasili Tanzania

    Tanzania Natural Resource Forum

    MUHTASARI

    CHAPISHO NA. 1: MWISHO WA WANYAMApori? KUPUNGUA NA KUHARIBIWA KWA WANYAMAPORI TANZANIA

    Tanzania ina maeneo makubwa na wanyama wengi dunianiTanzania ina idadi kubwa ya wanyama wakubwa waliobaki kupita taifa lolote lile duniani. Tanzania ndiyo yenye idadi kubwa kabisa ya simba na nyati wengi zaidi. Na idadi ya tembo inayoongezeka inakaribia na ile ya Botswana ambayo ina idadi kubwa Barani Afrika. Makundi ya wanyamapori katika mifumo ya ikolojia ya Serengeti – zaidi ya pundamilia milioni mbili, nyumbu, jamii ya swala – ya mkini inawakilisha mkusanyiko mkubwa wa wanyamapori waliobaki katika sayari yetu. Tanzania imeanzisha moja ya mitandao mikubwa ya maeneo yaliyohifadhiwa kuliko nchi yoyote ile duniani, takribani asilimia 30 ya eneo la nchi limehifadhiwa kama Hifadhi za Taifa, Mapori

    ya Akiba na Misitu ya Hifadhi.

    Idadi ya wanyamapori Tanzania imetawanyika wakipatikana ndani ya hifadhi, mapori ya akiba na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa mahali ambako wanaishi na binadamu katika ardhi za vijiji na za watu binafsi. Wanyamapori ni msingi wa biashara ya utalii wa kupiga picha na ya uwindaji na hivyo, ni raslimali muhimu ya kiuchumi Tanzania.

    Tanzania inapoteza wanyamaporiLicha ya maeneo makubwa yaliyohifadhiwa na mengine yenye wanyamapori yanayochukua karibu asilimia 30 ya eneo la nchi, takwimu za kiutafiti za hivi karibuni zilizoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) mwishoni mwa miaka ya 1980 hadi mwanzoni mwa miaka 2000 na kuchapishwa katika majarida ya kimataifa ya kisayansi zinazonesha wazi kuwa aina, kiasi na mtawanyiko wa wanyamapori Tanzania unaendelea kupungua kwa kasi. Takwimu hizi bora za kisayansi zinaonesha kupungua kwa wanyamapori katika maeneo yote ya muhimu ya wanyama na mifumo ikolojia yakiwemo maeneo nyeti yaliyohifadhiwa kama vile Hifadhi za Taifa na Mapori ya Akiba. Spishi nyingi ukiondoa tu twiga na tembo zimepungua kwa kasi kwa idadi zao tangu katikati ya miaka ya 1980.

    Muhtasari huu ni dondoo muhimu zilizochambuliwa kutoka katika kila kitini kumwezesha msomaji apate uelewa wa haraka kuhusiana na masuala muhimu ndani ya Idara ya Wanyamapori. Wakati muhtasari huu ukitoa habari kwa ufupi, inapendekezwa kuwa kila kitini cha kisera kisomwe chote ili kupata uelewa mzuri wa masuala muhimu katika sekta ya wanyamapori kupitia takwimu na ushaidi uliotolewa.

    MASUALA MUHIMU:

    Takwimu bora na za kisasa zina-pendekeza kuwa wanyamapori wanapungua katika maeneo yote muhimu ya wanyamapori na mifumo ya uhifadhi Tanzania, ikiwa ni pamoja na maeneo makubwa yaliyohifadhiwa kama vile Hifadhi za Taifa na Mapori ya Akiba.

    © JMT 2008

    Kwa kushirikiana na

    M-1

  • CHAPISHO NA. 2: SABABU ZA KUPUNGUA KWA WANYAMAPORI TANZANIA

    Kwanini wanyamapori hupungua Tanzania? Leo hii Tanzania imetenga asilimia 30 ya ardhi yake kama maeneo yaliyohifadhiwa ambako watu wamezuiliwa kuishi. Mataifa machache duniani yameweza kufanya hivyo. Idadi ya Hifadhi za Taifa na Mapori ya Akiba yamepanuliwa mfufulizo tangu uhuru. Kwa hiyo, kwa nini wanyamapori hupungua?

    1. Maeneo yaliyohifadhiwa hayawezi kujitosheleza yenyeweSehemu ya kwanza muhimu ya maelezo ni kwamba katika maeneo mengi duniani hifadhi na mapori ya akiba siku zote havikidhi haja kwa uhifadhi wa wanyamapori katika eneo husika. Sababu ni kwamba maeneo hayo hayajitoshelezi. Wanyamapori huondokea nje ya mipaka ya maeneo yaliyohifadhiwa mara nyingi kwa sababu raslimali kama chakula na maji hupatikana nje ya maeneo hayo. Kama wanyamapori wangeweza kubaki ndani ya mipaka ya hifadhi na mapori ya akiba mathalani kwa kuweka uzio wa kuwazuia wanyama ndani, idadi ingepungua haraka. Hii ni kweli kwa wanyama wanaohama kama vile nyumbu na tembo. Kwa kawaida wanyamapori huhitaji maslahi ya kiikolojia kipindi fulani cha mwaka ambayo hupatikana nje ya mipaka ya hifadhi kama vile nyanda za malisho, maji, maeneo ya kupumzikia na maeneo ya kuzalia.

    2. Kisheria wanyamapori hawawanufaishi vya kutosha wanajamiiWanyamapori wanapotea katika maeneo ya vijiji kwa sababu tatu muhimu:

    Serikali humiliki wanyamapori lakini haina uwezo wa kuwalinda wanyama katika vijiji na ardhi binafsi nje ya maeneo ya hifadhi na mapori ya akiba.

    Jamii hubeba gharama za kuishi na wanyamapori lakini mara nyingi hawapati manufaa kisheria.

    Kama wanyamapori wana gharama zaidi kuliko faida kwa wanavijiji hivyo wanavijiji watafanya kila wawezalo kuwaondoa wanyamapori ili waweze kuboresha maisha yao na ustawi wa familia zao. Kwa mfano watapanua mashamba na kuharibu makazi ya wanyamapori kwa sababu kilimo kina faida na wanyamapori huleta hasara.

    Usimamizi wa sasa wa wanyamapori Tanzania hautoi mifumo yenye tija kwa kuwezesha jamii zifaidike kisheria kutokana na wanyamapori.

    MASUALA MUHIMU:

    Tanzania imeonesha dhamiri imara juu ya uhifadhi wa wanymaapori na bioanuai ikitenga kiasia cha asilimia 30 ya ardhi kama maeneo yaliyohifadhiwa ambako makazi ya binadamu yamezuiliwa.

    Hata hivyo hifadhi hizo na mapori ya akiba mara nyingi hayakidhi haja ya hifadhi ya wanyamapori katika maeneo husika. Spishi nyingi zinahitaji raslimali ambazo zinapatikana nje ya maeneo yaliyohifadhiwa katika misimu fulani kwa mwaka. Pia wanyama wengi wanaishi nje ya maeneo yaliyohifadhiwa wakati wote.

    Uhifadhi hutegemea wanyamapori waliohifadhiwa ndani ya mipaka ya hifadhi na mapori ya akiba na pia nje ya maeneo haya katika ardhi za vijiji na ardhi binafsi.

    Tanzania bado haijafanikiwa vizuri kuhifadhi wanyamapori walio nje ya maeneo yalioyohifadhiwa. Hii ni kwa sababu jamii na watu binafsi hawajaona motisha ya kuhifadhi wanyamapori. Kisheria maduhuli yaliyokusanywa huenda hazina na taasisi za serikali. Kiwango kidogo sana cha maduhuli hubakizwa au hurudishwa kwa jamii au watu binafsi.

    Idara ya Wanyamapori pia ina upungufu wa raslimali unaosabibishwa na mfumo huo wa kugawana mapato.

    Ili wanyamapori wahifadhiwe ni lazima kisheria kuwepo thamani ya kiuchumi kwa jamii ambayo ndiyo yenye maamuzi juu ya matumizi ya raslimali zilizo katika ardhi zao.

    Sekta binafsi na vyama huru ni budu kutoa mchango katika uandaaji wa viwango, matendo ya kiusimamizi na mifano ya biashara bunifu kwa uratibu na Idara ya Wanyamapori.

    M-2

  • CHAPISHO NA. 3: KUKUZA MADUHULI KUTOKANA NA MATUMIZI ENDELEVU YA WANYAMAPORI

    Wanyamapori wanaweza kuchangia zaidi katika ukuaji wa uchumi Idadi ya wanyamapori Tanzania ambayo ni kubwa kuliko nchi yoyote Afrika na duniani inathaminiwa na utalii wa picha na ule wa uwindaji. Kwa hiyo wanyamapori ni chanzo cha uchumi shindani wa Taifa. Hii ina maana kuwa Tanzania ina tabia za asili ambazo zinaifanya kuwa nzuri kuliko nchi nyingine

    katika kuendeleza wanyamapori na kuiuzia dunia kupitia uwindaji wa kitalii na utalii wa picha. Wakati Tanzania ikiwa na vyanzo muhimu vya maduhuli na biashara kama vile kahawa, maua na korosho, ni rahisi zaidi kwa nchi nyingine duniani kushindana na Tanzania katika biashara ya mazao haya.

    Kwa sasa wanyamapori ni moja ya raslimali nyeti Tanzania. Ni thamani kuu katika biashara ya kitalii inayokadiriwa kufikia dola za kimarekani milioni 862 (TZS trilioni 1.03) kwa mwaka 2006. Utalii umekuwa ni moja ya vichocheo vikuu vya ukuaji wa uchumi na urejeshwaji wa uchumi kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.

    Wanyamapori hutoa msingi wa utalii wa uwindaji Tanzania, ambayo na ni moja ya maeneo makubwa Afrika katika uwindaji (ya pili tu kutoka Afrika Kusini).

    Taratibu za Mikataba ya Vitalu vya Uwindaji Ni kanuni ya msingi ya kiuchumi kwamba ushindani wa wazi uwepo kati ya wanunuzi kwa kununua bidhaa kufuatia maamuzi ya soko kwa bei nzuri na sahihi ya bidhaa. Hii ndiyo maana, kwa mfano, wafugaji katika Tanzania hupeleka mifugo yao sokoni kuiuza kwa kila soko la wiki ili waweze kupata bei nzuri ya kuuza bidhaa zao katika soko shindani. Hii inaitwa sheria ya ‘ugavi na mahitaji.’

    Somo tunalojifunza kutokana na uzoefu huu ni kwamba tatizo la kuweka thamani ndogo ya maeneo ya uwindaji haliwezi kutawaliwa na utaratibu wa kuongeza ada ya maeneo ya uwindaji na nyara za wanyamapori. Si serikali wala makampuni ya uwindaji wanaelewa ‘bei sahihi’ iweje.

    Ni kupitia tu ushindani wa soko miongoni mwa makampuni kwa maeneo ya uwindaji itahakikisha Tanzania inaweza kukuza mapato kutokana na uwindaji wa wanyamapori. Ni soko tu linaloelewa bei halisi! Uwepo uhakiki wa kuwa soko linaendeshwa kwa haki na kwa tija na halijaghushiwa. Kwa kukosekana kwa uwazi na mifumo shindani ya kugawanya maeneo ya uwindaji siku zote kutatoa na kulea mianya ya ufisadi katika ugawanyaji wa vitalu vya uwindaji.

    Kuwianisha uwindaji wa kitalii na utalii wa pichaUwindaji wa kitalii na utalii wa picha ni njia mbili tofauti lakini zote ni muhimu kiuchumi na kifedha kwa kuzalisha maduhuli na uwekezaji dhidi ya

    MASUALA MUHIMU:

    Wanyamapori ni moja ya maliasili muhimu Tanzania na chanzo nyeti cha uchumi shindani katika Taifa.

    Ili kupata manufaa makubwa kutokana na wanyamapori ni muhimu kuhimiza soko shindani la uwazi kwa kuwa na uhakika wa kuwatumia wanyamapori kupitia shughuli za utalii wa uwindaji na ule wa picha.

    Tatizo la uwindaji usio na thamani haliwezi kutatuliwa na serikali kwa kupandisha bei za kulipia vitalu vya uwindaji na nyara. Si serikali wala makampuni ya uwindaji anayeelewa bei ingekuwaje. Ni kwa kupitia tu soko shindani la uwazi tunaweza kupata bei halisi.

    Utalii wa picha na ule wa uwindaji ni njia mbadala za kutumia wanyamapori. Uwindaji huleta maduhuli mengi kutoka kwa wageni lakini utalii wa picha unaweza kupanuka na kukua haraka kuliko ule wa uwindaji.

    Uwindaji wa kiutalii utaendelea kuwa ni muhimu hasa katika maeneo yale ambayo yana uwezekano mdogo wa utalii wa picha (utalii wa kuona wanyama) ambako hubakia ndiyo uchaguzi pekee wa kutumia wanyama.

    Katika maeneo ambayo utalii uko juu, kiuchumi inalipa zaidi kwa kuwatumia wanyamapori kwa kupitia utalii wa picha. Uwindaji wa kitalii unaweza kufanyika pamoja na utalii wa picha kama kuna mipango mizuri.

    Idara ya Wanyamapori inahitaji kufadhiliwa vizuri na kupewa raslimali ili kusimamia kwa tija wanyamapori kwa kushirikiana na sekta binafsi, jamii na mashirika ya hiari. Kwa sasa hakuna uwekezaji wa kutosha katika sekta ya wanyamapori nje ya maeneo yaliyohifadhiwa.

    M-3

  • wanyamapori. Uwindaji wa kitalii huleta ada kubwa kutoka kwa mgeni kuliko utalii wa picha. Hata hivyo, uwindaji unaweza tu kuchukua idadi ndogo ya wateja katika eneo husika kila mwaka kwa sababu wanyama wanaoweza kuwindwa kiutaratibu ni wachache na hivyo kundi moja tu la wateja laweza kuwinda eneo moja kwa wakati moja.

    Kiyume chake, utalii wa picha unaweza kupokea wateja wengi na zaidi ya maelfu ya watu wanaweza kuona na kupiga picha simba mmoja ndani ya Serengeti, wakati ni mwindaji mmoja anayeweza kupiga simba katika kitalu cha uwindaji ndani ya Selous. Utalii wa picha una bei ya chini lakini una mauzo makubwa kuliko uwindaji. Tofauti nyingine ni kwamba utalii wa picha huhitaji miundombinu zaidi - kama barabara, makambi, hoteli - wakati uwindaji wa kitalii huweza kufanyika mahala ambapo hakuna miundombinu ya kudumu. Utalii wa picha, kwa sababu huhusisha wageni wengi, huvutia uwekezaji, ajira na mapato kupitia huduma mbalimbali - hizi huitwa ‘matokeo zidisho.’

    Tofauti kati ya uwindaji wa kitalii na utalii wa picha kuna viashiria muhimu kwa jitihada za kukuza pato la Taifa kutokana na wanyamapori. Kwa ujumla, uwindaji wa kitalii ni njia muhimu ya kupata mapato kutokana na wanyamapori katika maeneo ya asili yasio na miundombinu, mandhari za kuvutia na idadi kubwa ya wanyamapori ambavyo ni vivutio vya utalii wa picha. Lakini pale utalii wa picha unapokomaa mapato kutokana na kuongezeka kwa utalii wa picha yanaweza kuzidi mapato yanayozalishwa na uwindaji wa kitalii.

    Uwekezaji duni katika usimamizi wa wanyamaporiKatika ngazi ya kijamii kumekuwa na urejeshwaji duni wa matumizi ya wanyamapori, mafao na haki za kusimamia na hizo ni sababu muhimu katika kupungua kwa idadi ya wanyamapori na hiyo inaweza kuonekana pia kama ni uwekezaji duni.

    Takwimu za serikali zinaonesha kuwa TANAPA ina uwezo wa kutumia takribani dola za kimarekani 1,130 kwa kila kilomita ya mraba kwa mwaka kwa ajili ya usimamizi wa wanyamapori, wakati Idara ya Wanyamapori inaweza tu kutumia kiasi kinachofikia dola za kimarekani 24 katika kilomita moja ya mraba kwa mwaka.

    Hata hivyo, mwaka 2007 Hifadhi za Taifa (TANAPA) walipata TShs bilioni 69.0 lakini ni asilimia 1.8 tu zilipelekwa kwa shughuli za ujirani mwema (TANAPA Annual General Report 2007). Kinyume chake, katika mwaka 2006 Idara ya Wanyamapori ilipata TShs bilioni 15.3 kutokana na matumizi endelevu ya wanyamapori, na ilikuwa na uwezo wa kurudisha asilimia 12.8 katika wilaya husika (Economic Survey 2006).Kwa nini ni mapato kidogo sana hurudishwa kwa jamii na usimamizi wa wanyamapori - hususan kwa TANAPA - wakati wanyama wanaendelea kupungua?

    Ni wajibu wa serikali kuwekeza katika wanyamapori kama raslimali ya umma. Kulingana na umuhimu wake kiuchumi haishauriwi kuendelea ‘kumkamua ng’ombe hadi akauke.’ Hii ni kuiomba Idara ya Wanyamapori, Serikali za Mitaa, Asasi zilizoidhinishwa na Jamii kukifikia kisichowezekana.

    Mchoro wa dhana kuonesha jinsi muundo wa mapato kutoka sekta ya wanyamapori ungepaswa kuwa. Hazina hukusanya tu kodi za ongezeko la thamani, zingine zinawekezwa katika usimamizi wa wanyamapori na maendeleo ya jamii.

    M-4

  • CHAPISHO NA. 4: USIMAMIZI WA WANYAMAPORI NA KUPUNGUZA UMASKINI

    Nafasi ya wanyamapori katika kupunguza umaskiniNi muhimu kuhakikisha kuwa wanyamapori wanatoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania (angalisa Chapisho Na. 3). Ni muhimu pia kuwa wanyamapori watoe mchango mkubwa katika kupunguza umaskini na kukuza utajiri katika ngazi ya kijamii. Umuhimu wa kuboresha uhusiano kati ya uchumi wa kitaifa na kupunguza umaskini ngazi ya jamii ndiyo mada kuu katika Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA). MKUKUTA unaahidi jitihada za kuhakikisha kuwa mafao ya ukuaji uchumi yanasambaa hadi vijijini kwa wanajamii na maskini.

    Kikwazo kikuu katika kufikia fursa hii ni kwamba tangu wakati wa ukoloni jamii zilizuiliwa kisheria kutumia wanyamapori na haki za kutumia wan-yamapori zilibakia na kuthibitiwa na serikali.

    MASUALA MUHIMU:

    Wanyamapori wangeweza kutoa mchango mkubwa kisheria katika kupunguza umaskini na kukuza uchumi wa jamii zinazoishi katika maeneo yenye wanyamapori.

    Kwa sasa wanyamapori wana thamani katika jamii zinazofaidika na biashara haramu ya wanyamapori.

    Maendeleo katika kuendeleza usimamizi wa kijamii wa wanyamapori kupitia maeneo ya hifadhi za jamii umekuwa wa utaratibu na aghali.

    Haki kamili za kusimamia na kufaidika kutokana na wanyamapori zinahitaji kurudishwa katika ngazi ya jamii mapema iwezekanavyo ili kutoa motisha chanya juu ya usimamizi endelevu wa wanyamapori miongoni mwa vijiji vinavyopatika kando ya wanyamapori.

    Kama wanyamapori hawataonesha nafasi katika kupunguza umaskini na kukuza uchumi wa jamii, hivyo shughuli zingine za kiuchumi zitachukua nafasi, na wanyama wataendelea kupungua na kutoweka. Na hii ni kwa sababu wananchi hawatakuwa na utetezi wa kiuchumi ili kuwasimamia wanyamapori kwa njia endelevu.

    Maeneo ya Hifadhi za Jamii (WMA)

    Sera ya Wanyamapori ya mwaka 1998 ilielekeza mabadiliko ya kisheria yatakayoruhusu uundwaji wa WMA mahali ambapo jamii wangekuwa wasimamizi kisheria na kufaidika na wanyamapori katika ardhi za vijiji.

    Katika mwaka 2002 serikali iliunda kanuni za kuongoza WMA, zilizorejewa mwaka 2005, chini ya Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 1974 ambayo inaruhusu uanzishwaji wa maeneo ya hifadhi za jamii katika ardhi za vijiji. Kuanzia Januari 2003 Waziri wa Maliasili ya Utalii amefanya kazi na jamii, Serikali za Wilaya na mashirika binafsi mbalimbali ili kuanzisha maeneo ya hifadhi za jamii yapatayo 16 kwa nchi nzima. Hadi Septemba 2008 maeneo kumi ya hayo yalitangazwa kama WMA, na baadhi ya hayo yalikuwa yameshaingia katika mikataba ya uwekezaji.

    Wakati jitihadi zimefanyika katika kuanzisha WMA, matatizo ya kimsingi yamekwamisha maendeleo:

    Awali, kanuni za uanzishwaji maeneo ya WMA ziko changamano na jamii zinahitaji msaada kutoka nje ili kutimiza masharti yote. Hii imehafifisha uanzishwaji wa WMA. Maeneo hayo kama yalivyoanzishwa ni aghali sana kuyaendeleza.

    Pili, maeneo ya WMA hayatoi mamlaka ya kutosha kuthibiti mafao ya kiuchumi kwa jamii kutokana na wanyamapori.

    Kufikiria aina mbadala juu ya usimamizi wa wanyamapori kijamiiZaidi ya WMA kuna njia zingine ambazo jamii zinaweza kupata manufaa ya kiuchumi kutokana na wanyamapori. WMA zimeanzishwa kutoa haki kwa jamii juu ya matumizi ya wanyamapori lakini pia utalii usio wa uvunaji waweza kufanyika katika ardhi za vijiji ambako WMA hazijaanzishwa, kwa vile utalii wa kupiga picha hauvuni wanyamapori.

    Kaskazini mwa Tanzania, vijiji vimeingia katika mikataba na wawekezaji ili kuendesha utalii ambao utaleta faida kwa jamii kutokana na wanyamapori.Mingi ya mikatabi hii vijiji na wawekezaji iko katika vijiji kuzunguka hifadhi za Serengeti and Tarangire, na imekuwepo zaida ya miaka 10 hadi 15 iliyopita. Kumekuwepo na mawakala mbalimbali wa serikali ambao wamesaidia kusukuma jitihada hizo.

    M-5

  • CHAPISHO NA. 5: MASLAHI YA JAMII: UMUHIMU WA KUSHIRIKISHA SEKTA MBALIMBALI

    Nafasi ya wanyama katika kupunguzu umaskiniUsimamizi ulioboreshwa wa wanyamapori ungeweza kutoa manufaa mengi kwa jamii. Lakini pia ingeweza kusimamiwa kusaidia mahitaji ya jamii katika njia ambayo ni pana zaidi. Kile ambacho kingeleta maana zaidi kwa jamii ni kuwa na ‘maeneo ya usimamizi maliasili kijamii’ ambako vyote raslimali, wanyamapori na misitu vinasimamiwa katika ngazi ya kijiji badala ya kutenganishwa kama maeneo ya WMA na misitu ya vijiji. Kupitia mazingira wezeshi ya kisera hii ingekuwa rahisi katika maeneo mengi ambayo yana vyote, WMA na misitu ya vijiji.

    CHAPISHO NA. 6: DESTURI NZURI KATIKA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI KUJIFUNZA KUTOKA KATIKA KANDA

    Kuendeleza mafanikio na kujumuisha uzoefu wa kandaNchi zingine katika kanda zina uzoefu na somo saidizi kwa Tanzania kuhusiana na desturi bora na njia bunifu za kukuza mapato ya matumizi ya wanyamapori - kiuchumi, kiikolojia na kijamii. Kwa ujumla, nchi kusini mwa Afika kama vile Namibia, Botswana, Zimbabwe, na Afrika Kusini zina uwezo wa kusimamia wanyamapori ili idadi ya wanyama wa spishi nyingi imekuwa sawa au kukua, na mafao kutokana na wanyamapori katika ngazi za jamii na Taifa yameongezeka sana. Mashariki mwa Afrika sera na desturi za wanyamapori zina mafanikio machache zaidi.

    MASUALA MUHIMU:

    Ili kuweza kukuza mchango chanya wa wanyamapori kwa maslahi ya jamii na shughuli za kiuchumi, ni muhimu kuchukua mtazamo wa kushirikisha sekta tofauti ili kuratibu usimamizi wa wanyamapori pamoja na sekta za ardhi, utalii, misitu na mifugo.

    Matendo ya usimamizi wa wanyamapori huweza kuleta migogoro na vijiji vyenye hati za ardhi hasa kupitia mwingiliano wa Mapori Tengefu na Ardhi za Vijiji.

    Usimamizi wa wanyamapori na hifadhi ya misitu ya jamii katika ngazi ya kijiji vinahitaji kuwianishwa ili kutoa manufaa ya kutosha vijijini, kwa sababu wanyamapori na misitu ni raslimali zinazoweza kupatikana kwa pamoja katika ardhi za pamoja za vijiji.

    Matendo na sera ya usimamizi wa wanyamapori vinatakiwa kuwianishwa na malengo ya ukuaji wa sekta ya utalii kitaifa, ili kuwanufaisha wananchi.

    Usimamizi wa wanyamapori ni budi uwe na uwiano wa sera ya sekta ya mifugo pamoja na malengo ya maendeleo kwa vile wanyamapori na mifugo vyote vinategemea nyanda za malisho na vyanzo vya maji katika maeneo mengi na husabibisha ushindani na wakulima.

    Mtazamo wa kuhusisha sera nyingi ni muhimu ili kuweka thamani kubwa kwa wanajamii waweze kufaidika kutokana na ardhi na raslimali zilizopo.

    MASUALA MUHIMU:

    Pote mashariki na kusini mwa Afrika wanyampori ni raslimali muhimu , lakini nchi zingine zimekuwa na desturi zenye usimamizi wenye tija kuliko nchi zingine.

    Nchini Kenya, wanyama wamepungua kwa asilimia 50 tangu katikati ya miaka ya 1970, kwa sababu katazo la uwindaji wa mwaka 1977 inapunguza chaguzi za kiuchumi kwa serikali, jamii na watu binafsi kutokana na wanyamapori. Ambako biashara imara za utalii wa picha zina msingi mzuri na kuzalisha mapato kwa wenye ardhi, wanyamapori Kenya wameongezeka au kuendelea sawa mathalani Kajiado na Laikipia.

    Namibia inayo mmoja ya mifumo yenye mafanikio mazuri ya usimamizi wa wanyamapori katika Afrika, ambako wanyamapori wanaongezeka, thamani ya wanyamapori kitaifa inaendelea kukua, na mapato zaidi ya jamii yanatokana na wanyamapori. Umuhimu wa mfumo wa Namibia ni kwamba wanajamii na wenye ardhi binafsi wana mamlaka ya kufaidika na asilimia 100 ya mapato ya wanyamapori katika ardhi zao.

    Somo la msingi kutoka kwa uzoefu na usimamizi wa wanyamapori wa kanda ni kwamba nchi zilizowezesha watu binafsi wa jamii na umoja wa wenye ardhi ili kufaidika na thamani kiuchumi ya wanyamapori, zinaweza kukuza idadi ya wanyamapori na kuongeza mapato kijamii na kitaifa kutokana na wanyamapori.

    M-6

  • CHAPISHO NA. 7: MAPENDEKEZO YA KISERA ILI KUENDELEZA WANYAMAPORI WA TANZANIA

    Wanyamapori huipatia Tanzania soko lenye ushindani katika ulimwengu wa leo wenye utanda wazi am-bapo hakuna raslimali nyingine inaweza kutoa. Wanyamapori ni raslimali endelevu. Ikiwa Tanzania itaandaa sera na matendo yenye usimamizi endelevu wa wanyamapori, shughuli za kiuchumi zinazotokana na wan-yamapori zitaendelea kukua na kupanuka kwa miongo mingi ijayo. Cha kusikitisha ni kwamba wanyamapori wa Tanzania wanapotea, na hivyo kupoteza ushindani katika soko la kikanda kama vile Namibia au Botwana ambako wana idadi ya wanyama inayoongezeka ama iliyotulia, na ambako pia kuna utalii wenye nguvu un-aokua hasa ule wa uwindaji na wa upigaji picha.

    Kipindi cha miaka ya 1990 Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania ilifanya tathmini ambayo ilihitimisha kwamba:

    “Ni muhimu kwa uhifadhi wa wanyamapori hapo baadaye kwa hapa Tanzania wananchi waishio pamoja na wanyamapori wapatiwe mafao ya moja kwa moja yatokanayo na wanyama.”

    Ili kuchangia katika jitihada za watunga sera, wadau wote wa kiserikali na wale wasiowa kiserikali na ili wanyamapori wawe na faida kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho, mapendekezo yafuatayo ya kisera yamewekwa na inafaa yasomwe kwa kina katika Chapisho Na 7.

    1. KUREKEBISHA SHERIA NA SERA YA WANYAMAPORI ILI KUKABILI CHANGAMOTO ZA SASA NA KUUNDA MFUMO WA KITAASISI KWA AJILI YA USIMAMIZI ENDELEVU WA WANYAMAPORI TANZANIA

    2. KUBORESHA NA KUFAFANUA KANUNI ZA UANZISHWAJI MAENEO YA HIFADHI ZA JAMII (WMA) KATIKA ARDHI ZA VIJIJI

    3. KUSAIDIA NJIA MBADALA ZA KUWANUFAISHA WANANCHI KUTOKANA NA WANYAMAPORI KUPITIA UTALII WA BIASHARA-UBIA ZA JAMII NA SEKTA BINAFSI

    4. KUKUZA THAMANI YA UCHUMI WA WANYAMAPORI KWA KUANZISHA MFUMO WA USHINDANI KATIKA UGAWAJI WA VITALU VYA UWINDAJI KAMA VILE ILIVYO KATIKA ZABUNI AU MINADA YA WAZI

    5. SERIKALI IONGEZE MAPATO YA HAZINA KUU KUTOKANA NA WANYAMAPORI IKITILIA MKAZO UKUSANYAJI WA MAPATO YA UPILI – HASA KODI ZILIZOPO, NA KUHAKIKISHA JAMII NA WAMILIKI WA ARDHI BINAFSI WAKIPATA MAPATO YA MOJA KWA MOJA KAMA VILE ADA ZA MAENEO YA UWINDAJI NA UTALII WA PICHA6. KUTATUA MIGOGORO BAINA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI NA HAKI ZA ARDHI YA JAMII

    Kisanduku Na. 1: Mambo muhimu katika kuboresha biashara ya uwindaji wa kitalii

    Kuboresha biashara ya uwindaji wa kitalii ili iweze kuakisi thamani halisi ya soko la wanyamapori katika Tanzania itahitaji maandalizi muhimu kwa upande wa serikali kwa kushirikiana na wawindaji, wataalam na mashirika ya hiari. Imependekezwa na watalaam kwamba mfumo wa zabuni za wazi ikiwa maombi na viwango yaweza kuwa ndiyo njia nzuri. Katika kubuni mfumo huo masuala yafuatayo yanahitaji kufikiriwa kwa uangalifu kwa maana ya namna ya kuyafikia yafuatayo:

    • Kuyavutia makampuni yenye rekodi nzuri ya usimamizi na utendaji; • Kuanzisha mfumo wa uwindaji wenye uwiano wa utendaji wa kiuchumi na ulinzi wa raslimali kwa

    kipindi sahihi na ushindani katika kuomba upya;• Kujenga ubia wa muda mrefu unaochochewa na utendaji kati ya serikali na sekta binafsi ikiwa na

    ufuatiliaji wa uwazi na tathmini kulingana na vigezo vilivyowekwa;• Kutoa vivutio vyenye nguvu kwa ulinzi wa wanyamapori na makazi na kuboresha maeneo ya

    wanyamapori yaliyoharibiwa ama kupungua kwa thamani ya nyara;• Kuvutia maslahi katika vitalu vizuri vya uwindaji na vitalu visivyo na mvuto vinavyohitaji kuboreshwa;• Kuwarekebisha wazabuni wakubwa ambao hawana rekodi nzuri ya kiusimamizi na matumizi ya vitalu

    vya uwindaji;• Kuhimiza makampuni ya kitanzania ili yaweze kuingia na kushindana na makampuni ya kutoka nje;• Kuiyapa makampuni uhuru ili kufikia utendaji wa juu.

    M-7

  • HABARI JUU YA WANYAMAPORI KATIKA TANZANIA

    Wanyamapori kwa watanzania wote: Kusimamisha upotevu, kuendeleza raslimali na kupanua mafao

    Jumiko la Maliasili Tanzania

    Tanzania Natural Resource Forum

    CHAPISHO NA. 1MWISHO WA WANYAMA? KUPUNGUA NA KUHARIBIWA KWA

    WANYAMAPORI TANZANIA

    MASUALA MUHIMU:

    Takwimu bora na za kisasa zinapendekeza kuwa wanyamapori wanapungua katika maeneo yote muhimu ya wanyamapori na mifumo ya uhifadhi Tanzania, ikiwa ni pamoja na maeneo makubwa yaliyohifadhiwa kama vile Hifadhi za Taifa na Mapori ya Akiba.

    © JMT 2008

    Kwa kushirikiana na

    1-1

  • milioni mbili, nyumbu, na jamii ya swala – yamkini inawakilisha mkusanyiko mkubwa wa wanyamapori waliobaki katika sayari yetu. Tanzania imeanzisha moja ya mitandao mikubwa ya maeneo yaliyohifadhiwa kuliko nchi yoyote ile duniani, takribani asilimia 30 ya eneo la nchi limehifadhiwa kama Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba na Misitu ya Hifadhi.

    Idadi ya wanyamapori Tanzania imetawanyika wakipatikana ndani ya hifadhi, mapori ya akiba na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa mahali ambako wanaishi na binadamu katika ardhi za vijiji na za watu binafsi. Wanyamapori ni msingi wa biashara ya utalii wa kupiga picha na ya uwindaji na hivyo, ni raslimali muhimu ya kiuchumi Tanzania.

    Maeneo ya wanyamaporiWanyamapori Tanzania husimamiwa chini ya mifumo ya kiasasi tofauti. Kila mfumo una malengo yake na changamoto za kiuhifadhi. Muhtasari unafuata chini:

    Tanzania ina maeneo makubwa na wanyama wengi dunianiTanzania ina idadi kubwa ya wanyama wakubwa waliobaki kupita taifa lolote lile duniani. Tanzania ndiyo yenye idadi kubwa kabisa ya simba na nyati wengi zaidi. Na idadi ya tembo inayoongezeka inakaribiana na ile ya Botswana ambayo ina idadi kubwa Barani Afrika. Makundi ya wanyamapori katika mifumo ya ikolojia ya Serengeti – zaidi ya pundamilia

    Uhamaji wa nyumbu Serengeti – tukio kubwa duniani

    Aina & Malengo Msimamizi Asilimia ya eneo la nchiHifadhi za Taifa

    Ulinzi na matumizi yasiyo ya uvunaji tuSerikali(Shirika la Umma)

    4.4%

    Mamlaka ya Hifadhi ya NgorongoroUlinzi pamoja na matumizi mseto ya ardhi bila uvunaji

    Serikali(Shirika la Umma)

    0.9%

    Mapori ya Akiba

    Ulinzi pamoja na uvunaji na matumizi yasiyo ya uvunaji ya wanyamapori (Uwindaji na kupiga picha)

    Serikali(Idara ya Wanyamapori) 13.0%

    Mapori TengefuUvunaji na matumizi yasiyo ya uvunaji ya wanyamapori

    (Uwindaji na kupiga picha)

    Serikali (Idara ya Wanyamapori pamoja na Halmashauri za Wilaya)(Mapori Tengefu mara nyingi hubebana na Ardhi za Vijiji)

    5.5%

    Maeneo ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Jamii (WMA)Uvunaji na matumizi yasiyo ya uvunaji ya wanyamapori

    (Uwindaji na kupiga picha)

    Asasi zilizoidhinishwa za WMA kwa niaba ya Halmashauri za Vijiji (kwa kushirikiana na vijiji wanachama, Serikali za Mitaa na Idara ya Wanyamapori)

    3.7%

    Misitu ya HifadhiUlinzi pamoja na matumizi ya uvunaji

    Idara ya Misitu na Nyuki na Halmashauri za Wilaya 16.2%

    Misitu ya VijijiUvunaji na matumizi yasiyo ya uvunaji wa mazao ya

    misitu na ya wanyamapori

    Serikali za vijiji kwa niaba ya Halmashauri za Vijiji 2.6%

    Muhimu: Misitu ya Vijiji imeongezewa katika takwimu hizi kwa kuwa Misitu ni muhimu kwa ajili ya wanyamapori hasa kwa kuz-

    ingatia bioanuai isiyopatikana kokote duniani. (Takwimu zimetolewa katika vyanzo tofauti na maeneo mengine yanaingiliana)1-2

  • Tanzania inapoteza wanyamaporiLicha ya maeneo makubwa yaliyohifadhiwa na mengine yenye wanyamapori yanayochukua karibu asilimia 40 ya eneo la nchi, takwimu za kiutafiti za hivi karibuni zilizoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) na kuchapishwa katika majarida ya kimataifa ya kisayansi zinaonesha wazi kuwa aina kiasi na mtawanyiko wa wanyamapori Tanzania unaendelea kupungua kwa kasi.

    Takwimu hizi zina msingi katika hesabu za wanyama

    Kielelezo Na. 1: Asilimia ya wanyamapori wanaopungua na asilimia ya wanyamapori wanaoongezeka katika maeneo tofauti ya kijiografia Tanzania kwa kufuata takwimu za hesabu za angani (kipindi cha masika) mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 2000.

    Muhimu: Kupungua kwa spishi kumeoneshwa kwa rangi nyekundu na spishi zilizoongezeka kwa rangi ya kijani. Kielelezo hiki kinaonesha tu kitakwimu kiasi muhimu na kilichopungua na kuongezeka. Na hiyo ndiyo sababu hesabu yake katika kielelezo haitimii asilimia 100.

    zilizofanywa toka angani katika maeneo muhimu ya wanyamapori Tanzania – ikiwa ni pamoja na maeneo yaliyohifadhiwa na maeneo ya vijiji yanayozunguka maeneo yaliyohifadhiwa. Na takwimu katika hesabu hizo zimekusanywa tangu mwishoni wa miaka ya 1980 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000. Hivyo takwimu zinaonesha ni kwa vipi na wapi wanyamapori wamepungua au kuongezeka kwa kipindi cha miaka kumi.

    Takwimu katika Kielelezo Na. 1 zinadhihirisha maeneo yote muhimu ya wanyamapori, aina ya wanyama wanapungua kwa uwingi kuliko kuongezeka.

    Na zaidi:

    Idadi ya wanyama wakati wa kiangazi katika mfumo ikolojia wa Ruaha Mkuu inaashiria kuwa karibu asilimia 73 ya spishi zimepungua sana. Na ni karibu asilimia 9 tu ya spishi ndiyo zimeongezeka kwa kiwango kizuri.

    Katika mfumo ikolojia wa Tarangire asilimia 46 ya spishi zimeonesha kupungua wakati wa hesebu za kiangazi kukiwa hakuna spishi iliyoongezeka. Wakati wa hesabu za masika asilimia 68 ya spishi zilipungua na asilimia 7 tu ya spishi ziliongezeka.

    Hesabu ya wanyama iliofanyika kwa ndege katika mfumo ikolojia wa Tarangire

    1-3

  • Mfumo ikolojia wa Tarangire (ukijumuisha Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Ardhi za Vijiji vinavyoizunguka) ni kitu muhimu katika utalii kaskazini mwa Tanzania, na Ruaha ni Hifadhi ya Taifa kubwa katika Afrika, ambayo inapatikana katika eneo la kusini linalokua kwa kasi kiutalii.

    Asilimia kubwa ya spishi zilipungua katika eneo lililohesabiwa la Burigi-Biharamulo, ambako asilimia 69 ya spishi zilipungua wakati wa hesabu za masika na asilimia 80 zilipungua wakati wa hesabu za kiangazi. Hakuna spishi iliongezeka katika misimu yote. Katika Burigi-Biharamulo, upungufu huu wa kutisha kwa muda unaweza kuhusishwa na wakimbizi katika eneo hilo kutokea Rwanda katikati ya miaka ya 1990 na waliovuna wanyamapori bila kudhibitiwa. Kielelezo Na. 2 kinaonesha spishi zilizochaguliwa ambazo zinapungua na kuongezeka katika kipindi cha kuidadi

    Kuendelea kupungua kwa idadi ya wanyamapori katika mifumo ikolojia muhimu nchini kutakuwa na athari kubwa za kiuchumi kitaifa.

    Kielelezo Na. 2: Asilimia ya maeneo yaliyohesabiwa ambako spishi za wanyama wakubwa zimepungua na kuongezeka mwishoni mwa miaka ya 1980 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000.

    Muhimu: Kupungua kwa spishi kumeoneshwa kwa rangi nyekundu na spishi zilizoongezeka kwa rangi ya kijani. Spishi zilizohesabiwa ni pundamilia, nyumbu, palahala weusi, palahala hudhurungi, korongo, twiga, tembo, pofu na mbogo.

    1-4

  • wanyamapori kwa miaka kumi. Kwa ujumla, kwa mujibu wa takwimu hizi, wanyama jamii ya swala na pundamilia walipungua.

    Mathalani:

    Pundamilia ambao ni spishi iliyo na wanyama wengi waliotawanyika na kusambaa katika mae-neo mengi Tanzania wamepungua katika asilimia 80 ya kanda zilizokaguliwa wakati wa masika na kiangazi. Hakukuwa na rekodi ya ongezeko la pun-damilia mahali popote. Hii inaonesha kuwa punda-milia wanapungua sana kote Tanzania.

    Spishi nyingine za jamii ya swala kama vile pal-ahala mweusi ni muhimu kwa uwindaji wa kiutalii. Spishi hizi nazo zinapungua. Takwimu zinaonesha kuwa palahala weusi wamepungua katika nusu ya maeneo yaliyokaguliwa na hakuna mahali wal-ipoongezeka. Palahala hudhurungi walipungua ka-tika hesabu za masika na kiangazi.

    Twiga wameonesha kutobadilika wakati tembo wameongezeka katika maeneo mengi yaliyokaguli-wa. Sababu za kuongezeka kwa tembo ni kwamba kuidadi kulipoanza mwisho mwa miaka ya 1980 tembo walikuwa katika zahama ya kuwindwa na majangili kwa ajili ya nyara zao. Kufuatia kuzuiwa kwa biashara ya meno ya tembo na uboreshwaji katika usimamizi wa sheria kuanzia 1989 na kuen-delea idadi ya tembo ikarejea.

    Chapisho Na. 2 huonesha mchanganuo wa kiini cha visababishi.

    Chapisho hili lina msingi katika muhtasari wa takwimu zilizochaguliwa kutoka: Stoner, C., T. Caro, S. Mduma, C. Mlingwa, G. Sabuni, M. Borner, and C. Schelten. 2007. Changes in large herbivore populations across large areas of Tanzania. African Journal of Ecology 45: 202-215.

    Si tu idadi ya wanyamapori inapungua katika maeneo muhimu ya wanyamapori lakini spishi nyingi za wanyama wakubwa zinapungua kwa uwingi.

    Takwimu bora za kisayansi zinaonesha kupungua kwa wanyamapori katika maeneo yote ya muhimu ya wanyama na mifumo ikolojia yakiwemo mae-neo nyeti yaliyohifadhiwa kama vile Hifadhi za Taifa na Mapori ya Akiba.

    Vilevile takwimu zinaonesha spishi nyingi ukion-doa tu twiga na tembo wamepungua kwa kasi kwa idadi zao tangu katikati ya miaka ya 1980.

    1-5

  • HABARI JUU YA WANYAMAPORI KATIKA TANZANIA

    Wanyamapori kwa watanzania wote: Kusimamisha upotevu, kuendeleza raslimali na kupanua mafao

    Jumiko la Maliasili Tanzania

    Tanzania Natural Resource Forum

    CHAPISHO NA. 2SABABU ZA KUPUNGUA KWA WANYAMAPORI TANZANIA

    MAMBO MUHIMU:

    Tanzania imeonesha dhamiri imara juu ya uhifadhi wa wanymaapori na bioanuai ikitenga kiasia cha asilimia 30 ya ardhi kama maeneo yaliyohifadhiwa ambako makazi ya binadamu yamezuiliwa.

    Hata hivyo hifadhi hizo na mapori ya akiba mara nyingi hayakidhi haja ya hifadhi ya wanyamapori katika maeneo husika. Spishi nyingi zinahitaji raslimali ambazo zinapatikana nje ya maeneo yaliyohifadhiwa katika misimu fulani kwa mwaka. Pia wanyama wengi wanaishi nje ya maeneo yaliyohifadhiwa wakati wote.

    Uhifadhi hutegemea wanyamapori waliohifadhiwa ndani ya mipaka ya hifadhi na mapori ya akiba na pia nje ya maeneo haya katika ardhi za vijiji na ardhi binafsi.

    Tanzania bado haijafanikiwa vizuri kuhifadhi wanyamapori walio nje ya maeneo yalioyohifadhiwa. Hii ni kwa sababu jamii na watu binafsi hawajaona motisha ya kuhifadhi wanyamapori. Kisheria maduhuli yaliyokusanywa huenda hazina na taasisi za serikali. Kiwango kidogo sana cha maduhuli hubakizwa au hurudishwa kwa jamii au watu binafsi.

    Idara ya Wanyamapori pia ina upungufu wa raslimali unaosabibishwa na mfumo huo wa kugawana mapato.

    Ili wanyamapori wahifadhiwe ni lazima kisheria kuwepo thamani ya kiuchumi kwa jamii ambayo ndiyo yenye maamuzi juu ya matumizi ya raslimali zilizo katika ardhi zao.

    Sekta binafsi na vyama huru ni budu kutoa mchango katika uandaaji wa viwango, matendo ya kiusimamizi na mifano ya biashara bunifu kwa uratibu na Idara ya Wanyamapori.

    © JMT 2008

    Kwa kushirikiana na

    4-1

  • yamepanuliwa mfufulizo tangu uhuru.Wanyamapori nje ya hifadhi na mapori ya akibaSehemu ya kwanza muhimu ya maelezo ni kwamba katika maeneo mengi duniani hifadhi na mapori ya akiba siku zote havikidhi haja kwa uhifadhi wa wanyamapori katika eneo husika. Sababu ni kwamba maeneo hayo hayajitoshelezi. Wanyamapori huondokea nje ya mipaka ya maeneo yaliyohifadhiwa mara nyingi kwa sababu raslimali kama chakula na maji hupatikana nje ya maeneo hayo. Kama wanyamapori wangeweza kubaki ndani ya mipaka ya hifadhi na mapori ya akiba mathalani kwa kuweka uzio wa kuwazuia wanyama ndani, idadi ingepungua haraka. Hii ni kweli kwa wanyama wanaohama kama vile nyumbu na tembo. Kwa kawaida wanyamapori huhitaji maslahi ya kiikolojia kipindi fulani cha mwaka ambayo hupatikana nje ya mipaka ya hifadhi kama

    vile nyanda za malisho, maji, maeneo ya kupumzikia na maeneo ya kuzalia.

    Kwa mfano:

    Hata kama Pori la Akiba la Selous ndiyo eneo kubwa lililohifadhiwa Afrika, karibu kilomita za mraba 50,000; miondoko ya tembo huenda nje ya eneo la hifadhi kwa pande zote ikifikia takribani kilomita za mraba 100,000.

    Kaskazini mwa Tanzania spishi kama nyumbu, pundamilia na jamii ya swala huhama maeneo makubwa kila mwaka kati ya maeneo yenye maji ya kudumu kipindi cha kiangazi na maeneo yenye malisho mazuri kipindi cha masika.

    Kwa mfano:

    Katika Hifadhi ya Taifa Tarangire wanyama huhama hifadhi kipindi cha masika na kutawanyika kwenda kaskazini, mashariki na kusini mwa hifadhi katika ardhi ndani ya mipaka ya vijiji mbalimbali Wilaya za Monduli, Simanjiro na Kiteto. Hifadhi ya Tarangire hutoa asilimia ndogo (chini ya asilimia 20) ya eneo lote la ardhi na makazi ambayo wanyamapori wanahitaji kwa kipindi cha mwaka.

    Hata Serengeti ambako Mapori ya Akiba matatu, Hifadhi moja ya Taifa, na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro hutoa kama kilomita za mraba 30,000 za ardhi iliyohifadhiwa, wanyamapori bado hutumia maeneo muhimu nje ya maeneo ya hifadhi katika Wilaya ya Ngorongoro (Tarafa ya Loliondo) na katika Wilaya za Serengeti na Tarime katika kipindi cha uhamaji wa nyumbu katika mwaka.

    Kwanini wanyamapori hupungua Tanzania? Inaweza kushangaza kuwa idadi ya wanyamapori Tanzania wanapungua wakati Tanzania imepata mafanikio makubwa katika uhifadhi wa wanyamapori. Tangu uhuru, miaka 47 iliyopita Tanzania imepanua maeneo ya ardhi iliyohifadhiwa kwa ajili ya wanyamapori, bioanuai na ulinzi wa mazingira. Na katika kipindi hichohicho idadi ya watanzania imeongezeka mara tano kutoka watu milioni 8 hadi watu milioni 38. Ongezeko la watu linamaanisha ardhi zaidi inahitajika kwa ajili ya kilimo, malisho na makazi na bado kuna ongezeko la mahitaji ya maliasili – ikiwemo mkaa, nyama za porini na mazao ya mbao. Changamoto zilizopo katika kuhimiza maslahi endelevu na kufikia usimamizi endelevu wa maliasili zimechangiwa na utendaji dhaifu katika upangaji wa matumizi bora ya ardhi.

    Leo hii Tanzania imetenga asilimia 30 ya ardhi

    yake kama maeneo yaliyohifadhiwa ambako watu wamezuiliwa kuishi. Mataifa machache duniani yameweza kufanya hivyo. Kama Kielelezo Na. 1 kinavyoonesha Hifadhi za Taifa na Mapori ya Akiba

    Kielelezo Na. 1: Upanuzi wa baadhi ya Hifadhi za Taifa na Mapori ya Akiba Tanzania, 1964-2004

    Chanzo: World Database of Protected Areas, World Conservation Monitoring Centre 2005

    Lakini leo hii wanyamapori wanapungua licha ya Tanzania kuwa imetenga asilimia kubwa ya ardhi yake kama maeneo yaliyohifadhiwa. Kwa hiyo tatizo ni nini?

    4-2

  • Kielelezo Na. 2: Njia za uhamaji wanyamapori na maeneo ya kutawanyika kwa wanyamapori kipindi cha masika nje ya mipaka ya maeneo yaliohifadhiwa katika mifumo ikolojia ya Serengeti na Tarangire

    Baadhi ya maeneo nje ya hifadhi na mapori ya akiba yametengwa kama Mapori Tengefu (GCA) lakini kinyume na Mapori ya Akiba na Hifadhi za Taifa, Mapori Tengefu hayatoi ulinzi wowote wenye maana (angalia Kisanduku Na. 1).

    Tathmini kubwa ya sekta ya wanyamapori ilifanyika mwaka 1995. Ingawa tathmini zilizofuata zimefanyika katika maeneo tofauti tofauti ndani ya sekta ya wanyamapori, tathmini ya mwaka 1995 ndiyo pekee iliyofanyika kwa kina. Changamoto za msingi zilitambuliwa katika tathmini hiyo na bado ni za msingi hata leo.

    Wanyamapori wanapotea katika maeneo ya vijiji kwa sababu tatu muhimu:

    Serikali humiliki wanyamapori lakini haina uwezo wa kuwalinda wanyama katika vijiji na ardhi binafsi nje ya maeneo ya hifadhi na mapori ya akiba.

    Jamii hubeba gharama za kuishi na wanyamapori lakini mara nyingi hawapati manufaa kisheria.

    Kutokana na wanyamapori kutumia maeneo makubwa, uhifadhi hutegemea wanyamapori waliohifadhiwa ndani ya hifadhi na mapori ya akiba na nje ya maeneo haya katika ardhi za vijiji na watu binafsi.

    Kisanduku Na. 1: Mapori Tengefu ni nini?

    Mapori Tengefu (GCA) wakati fulani hurejewa kama maeneo yaliyohifadhiwa lakini kuyaita Mapori Tengefu yamehifadhiwa inachanganya kwa sababu hayatoi ulinzi wowote kwa wanyamapori. Mapori Tengefu yalianzishwa wakati wa ukoloni kama maeneo yaliyotengwa ambako wanyama wasingewindwa bila leseni. Mapori Tengefu hayajawahi kudhibiti makazi au shughuli zingine za kibinadamu ndani ya mipaka na hivyo kutotoa ulinzi kwa makazi ya wanyamapori. Chini ya Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 1974 popote Tanzania hakuna wanyama wanaoweza kuwindwa bila leseni hivyo Mapori Tengefu hayana maana—hayatimizi kusudi lolote kwa vile wanyama popote pale Tanzania hawawezi kuwindwa bila leseni.

    Mapori ya Akiba yanatofautiana sana na Mapori Tengefu. Katika Mapori ya Akiba watu hawaruhusiwi kuishi wala kufanya shughuli za kiuchumi bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori. Vilevile katika Hifadhi za Taifa uvunaji wa maliasili umezuiliwa kabisa na uwindaji hauruhusiwi. Uwindaji unaruhusiwa katika Mapori ya Akiba kwa msingi wa kupewa kiasi cha wanyama na leseni kama ilivyo mahali popote pale nchini.

    Mapori Tengefu hayatoi ulinzi wa maana kwa makazi ya wanyamapori isipokuwa tu katazo la uwindaji wa wanyamapori ambao unazuiliwa mahali popote Tanzania. Katika tathmini ya sekta ya wanyamapori ya mwaka 1995 Mapori Tengefu hayakuonesha kuwa na tija yoyote kwa kuchangia uhifadhi wa wanyamapori. Sera ya Wanyamapori Tanzania ya mwaka 1998 ilipendekeza Mapori Tengefu ama yapandishwe kuwa Mapori ya Akiba au yabadilishwe kuwa maeneo ya hifadhi za jamii ambako haki ya kutumia wanyamapori ingetolewa na faida ya wanyamapori katika ardhi za vijiji ingeonekana.

    4-3

  • uvunaji wa nyama endelevu, mapato kutoka kwa biashara za wanyamapori kama vile upigaji picha na uwindaji, ajira ikiwemo uanzishaji wa ujasiriamali unaoendana na utalii wa wanyamapori.

    Wanyamapori wana faida na jamii ina fursa nyingi za kutafuta maslahi kutokana na wanyamapori ikiwa wanapata haki sawa za kusimamia wanyamapori na kupokea mapato.

    Kwa mfano: Utafiti wa serikali wa kiuchumi unaonesha kuwa matumizi ya wanyamapori (uwindaji, ukamataji wanyama hai na mapato mengine ya kiuvunaji) yalitoa mapato ya shilingi bilioni 15.3 (dola milioni 13) mwaka 2006, bila kuhesabu kiasi kikubwa cha mapato yaliyokusanywa kutoka kwa utalii wa kupiga picha Serengeti na Hifadhi zingine za Taifa.

    Mgao dhaifu wa matumizi, faida na haki za kusimamia wanyamapori kwa jamii ni sababu za msingi za kupungua kwa idadi ya wanyamapori. Bado wanajamii hawajaona motisha za kuhifadhi au kulinda wanyamapori nje ya maeneo ya hifadhi na mapori ya akiba.

    Kama wanyamapori wana gharama zaidi kuliko faida kwa wanavijiji hivyo wanavijiji watafanya kila wawezalo kuwaondoa wanyamapori ili waweze kuboresha maisha yao na ustawi wa familia zao. Kwa mfano watapanua mashamba na kuharibu makazi ya wanyamapori kwa sababu kilimo kina faida na wanyamapori huleta hasara.

    Usimamizi wa sasa wa wanyamapori Tanzania hautoi mifumo yenye tija kwa kuwezesha jamii zifaidike kisheria kutokana na wanyamapori.

    Kwa mfano:

    Kuna biashara kubwa inayokua ya nyama za porini katika maeneo mbalimbali nchini. Mfano, Mikoa ya Kigoma, Kagera na Mara ambako jamii wanafaidika kwa kiwango kikubwa ingawa sio kwa halali kutokana na wanyamapori. Kwa sababu uwindaji wa wanyamapori ni haramu lakini jamii haina motisha wa kudhibiti uvunaji wa wanyamapori na hakuna mifumo saidizi ya kuwezesha kutimiza azma hiyo. Matokeo yake uwindaji nyama za porini umekuwa na athari kubwa kwa idadi ya wanyamapori. (Chanzo: TRAFFIC, 2000 na 2007)

    Kwa hiyo, kama tathmini ya sekta ya wanyamapori ya mwaka 1995 na Sera ya Wanyamapori Tanzania ya mwaka 1998 (toleo lililorekebishwa 2007) vinatambua kuwa ili wanyama wadumu Tanzania lazima mwenendo wa sasa ubadilishwe, ni lazima wanyamapori wawe na thamani kwa jamii, na jamii inahitaji kuwa na uwezo wa kusimamia wanyamapori kama vile wanavyosimamia mifugo, kilimo, misitu, na maliasili nyingine katika ngazi ya kijiji. Hivyo mafao ambayo wananchi wanaweza kupata kutoka wanyamapori yanaweza kuwa kwa njia nyingi:

    Licha ya mwongozo sahihi wa tathmini ya sekta ya wanyamapori ya mwaka 1995 na Sera ya Wan-yamapori Tanzania (toleo lililorekebishwa mwaka 2007), usimamizi wa wanyamapori kijamii bado haujatekelezwa vizuri – ikiwa na madhara kwa wanyamapori nchini.

    Tembo (Loxodonta africana) katika mfumo ikolojia wa Tarangire4-4

  • HABARI JUU YA WANYAMAPORI KATIKA TANZANIA

    Wanyamapori kwa watanzania wote: Kusimamisha upotevu, kuendeleza raslimali na kupanua mafao

    Jumiko la Maliasili Tanzania

    Tanzania Natural Resource Forum

    CHAPISHO NA. 3

    KUKUZA MADUHULI KUTOKANA NA MATUMIZI ENDELEVU YA WANYAMAPORI

    MASUALA MUHIMU:

    Wanyamapori ni moja ya maliasili muhimu Tanzania na chanzo nyeti cha uchumi shindani kitaifa.

    Ili kupata manufaa makubwa kutokana na wanyamapori ni muhimu kuhimiza soko shindani la uwazi kwa kuwa na uhakika wa kuwatumia wanyamapori kupitia shughuli za utalii wa uwindaji na ule wa picha.

    Tatizo la uwindaji usio na thamani haliwezi kutatuliwa na serikali kwa kupandisha bei za kulipia vitalu vya uwindaji na nyara. Si serikali wala makampuni ya uwindaji anayeelewa bei ingekuwaje. Ni kwa kupitia tu soko shindani la uwazi tunaweza kupata bei halisi.

    Utalii wa picha na ule wa uwindaji ni njia mbadala za kutumia wanyamapori. Uwindaji huleta maduhuli mengi kutoka kwa wageni lakini utalii wa picha unaweza kupanuka na kukua haraka kuliko ule wa uwindaji.

    Uwindaji wa kiutalii utaendelea kuwa ni muhimu hasa katika maeneo yale ambayo yana uwezekano mdogo wa utalii wa picha (utalii wa kuona wanyama) ambako hubakia ndiyo uchaguzi pekee wa kutumia wanyamapori.

    Katika maeneo ambayo utalii uko juu, kiuchumi inalipa zaidi kwa kuwatumia wanyamapori kwa kupitia utalii wa picha. Uwindaji wa kitalii unaweza kufanyika pamoja na utalii wa picha kama kuna mipango mizuri.

    Idara ya Wanyamapori inahitaji kufadhiliwa vizuri na kupewa raslimali ili kusimamia kwa tija wanyamapori kwa kushirikiana na sekta binafsi, jamii na mashirika ya hiari. Kwa sasa hakuna uwekezaji wa kutosha katika sekta ya wanyamapori nje ya maeneo yaliyohifadhiwa.

    © JMT 2008

    Kwa kushirikiana na

    3-1

  • Wanyamapori na mandhari ya Tanzania ni samani za kipekee katika uliwengu wa leo. Hata hivyo raslimali haijasimamiwa kwa namna ambayo inatoa faida kwa Taifa. Chapisho hili linaangalia kwanini hali hiyo iko hivyo na nini kifanyike ili kukuza manufaa ya kitaifa kutokana na wanyamapori.

    Wanyamapori wanaweza kuchangia zaidi katika ukuaji wa uchumi Idadi ya wanyamapori Tanzania ambayo ni kubwa kuliko nchi yoyote Afrika na duniani inathaminiwa kuwa utalii wa picha na ule wa uwindaji. Kwa hiyo wanyamapori ni chanzo cha uchumi shindani wa Taifa. Hii ina maana kuwa Tanzania ina tabia za asili ambazo zinaifanya kuwa nzuri kuliko nchi nyingine katika kuendeleza wanyamapori na kuiuzia dunia kupitia uwindaji wa kitalii na utalii wa picha. Wakati Tanzania ikiwa na vyanzo muhimu vya maduhuli na biashara kama vile kahawa, maua na korosho, ni rahisi zaidi kwa nchi nyingine duniani kushindana na Tanzania katika biashara ya mazao haya.

    Kwa mfano:

    Nchi nyingine huzalisha kahawa au korosho katika hekta moja kuliko Tanzania kwa sababu ya tofauti ya hali ya hewa, magonjwa ya mazao na teknolojia za uzalishaji.

    Katika miaka ya 1990 biashara ya kahawa Tanzania ilishuka ghafla kwa sababu nchi nyingine ziliongeza uzalishaji katika maeneo mazuri ya kilimo yenye hali nzuri kwa kahawa.

    Kwa sasa wanyamapori ni moja ya raslimali nyeti Tanzania. Wana thamani kuu katika biashara ya kitalii inayokadiriwa kufikia dola za kimarekani milioni 862 (TZS trilioni 1.03) kwa mwaka 2006. Utalii umekuwa ni moja ya vichocheo vikuu vya ukuaji wa uchumi na urejeshwaji wa uchumi kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita (angalia Kielelezo Na. 1). Kupitia utalii wanyamapori wanaongoza kwa mchango wa ukuaji wa pato la Taifa kwa fedha za kigeni. Serikali ya Tanzania imeanza kuhimiza mapato kutoka utalii ikiwa ni pamoja na jitihada mpya ya kutangaza vivutio vya kitalii vya nchi. Kwa sekta nyingi za uchumi kama vile ndege hutegemea moja kwa

    moja sekta ya wanyamapori.

    Hakuna nchi duniani ambayo ina ushindani wa kiasili unapozungumzia wanyamapori kama Tanzania. Hakuna nchi inayoweza kuzalisha wanyama kama Tanzania kwa sababu Tanzania ina ushindani wa kiasili kwa kuzingatia utajiri wa kiikolojia. Kwa sababu Tanzania ina ushindani wa kiuchumi kuhusiana na wanyamapori, lengo la kimantiki la sera ya wanyamapori linatakiwa kuwa ni kukuza mapato ya kiuchumi kutokana samani hii ya kitaifa.

    Kielelezo Na. 1: Jumla ya mapato kutokana na utalii Tanzania, 1989-2006

    Chanzo: Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT), Economic Survey, 2006

    3-2

  • Wanyamapori hutoa msingi wa utalii wa uwindaji Tanzania, ambayo ni moja ya maeneo makubwa Afrika kwa uwindaji (ya pili tu kutoka Afrika Kusini) na ambayo huzalisha wastani wa dola za kimarekani milioni 30 (TZS bilioni 36) kwa jumla (kwa mwaka 2006), ukiwa na takribani dola za kimarekani milioni 11 (TZS bilioni 13.2) wastani wa mapato ya serikali (angalia Kielelezo Na. 2). Kama kilomita za mraba 250,000 zinatumika kwa uwindaji wa kitalii (angalia

    Kielelezo Na. 3) - karibu theluthi moja ya eneo la Tanzania ikijumuisha Mapori ya Akiba na maeneo mengi nje ya yale yaliyohifadhiwa. Vitalu vya uwindaji hutolewa kwa miaka mitano mitano na husimamiwa na Idara ya Wanyamapori; mikataba ya sasa muda wa kuisha ni mwaka 2009.

    Moja ya malengo muhimu ya sera Tanzania katika ngazi ya kitaifa ni kukuza maduhuli endelevu kutoka

    wanyamapori na mapato kiuchumi. Ili kufikia lengo hilo kuna masuala mawili ya kiusimamizi ambayo lazima yafikiriwe.

    1. Je, mikataba ya uwindaji imetolewa kwa njia ambayo italeta maduhuli zaidi kutokana na matumizi endelevu ya wanyamapori?

    2. Je, mfumo wa matumizi wa wanyamapori ikiwemo uwiano baina ya uwindaji wa kitalii na utalii wa picha unafikiriwa kwa namna ambayo utakuza mapato ya Taifa kiuchumi kutokana na wanyamapori?

    Kielelezo Na. 2: Kadirio la mapato ya uwindaji wa kitalii, 1988-2006

    Chanzo: MNRT Economic Survey, 2006; Baldus & Cauldwell 2004; Lindsey, et al 2007

    Kielelezo Na. 3: Maneneo yaliyohifadhiwa Tanzania, 2004 (Muhimu: Mapori yote ya Akiba yana vitalu vya uwindaji isipokuwa kaskazini mwa Selous)

    3-3

  • Kwa mfano:

    Ada ya pembe ya ndovu nchini Zimbabwe iliongezeka kutoka dola za kimarekani 1,200 (TZS 1.4) mwaka 1984 hadi dola za kimarekani 9,000 (TZS milioni 10.8) mwaka 1999 kama matokeo ya soko shindani na wazi ambalo lilichochea bei kupanda.

    Katika Tanzania, ada ya kitalu cha uwindaji kwa miaka mingi ilibakia kuwa dola za kimarekani 7,500 (TZS milioni 9), ambayo ilikuwa chini ya thamani ya soko ukilinganisha na nchi nyingine za SADC. Vilevile ada ya nyara kwa wanyamapori wa Tanzania ilipangwa katika madaraja ambayo yako chini kwa wanyama wale wale katika nchi zingine za kanda hii. Kwa kutambua hili lilikuwa ni tatizo Wizara ya Maliasili na Utalii ilipandisha ada za vitalu vya uwindaji katika mwaka 2007 kupitia kikao cha bajeti ya Bunge bila taarifa ya kimbele. Mabadiliko hayo yalisabibisha upinzani kutoka kwa wajumbe wa biashara ya uwindaji na hivyo ada zikashushwa tena.

    Somo tunalojifunza kutokana na uzoefu huu ni kwamba tatizo la kuweka thamani ndogo ya maeneo ya uwindaji haliwezi kutawaliwa na utaratibu wa kuongeza ada ya maeneo ya uwindaji na nyara za wanyamapori. Si serikali wala makampuni ya uwindaji wanaelewa ‘bei sahihi’ iweje.

    Ni kupitia tu ushindani wa soko miongoni mwa makampuni kwa maeneo ya uwindaji itahakikisha Tanzania inaweza kukuza mapato kutokana na

    Taratibu za Mikataba ya Vitalu vya Uwindaji Ni kanuni ya msingi ya kiuchumi kwamba ushindani wa wazi uwepo kati ya wanunuzi kwa kununua bidhaa kufuatia maamuzi ya soko kwa bei nzuri na sahihi ya bidhaa. Hii ndiyo maana, kwa mfano, wafugaji katika Tanzania hupeleka mifugo yao sokoni kuiuza kwa kila soko la wiki ili waweze kupata bei nzuri ya kuuza bidhaa zao katika soko shindani. Hii inaitwa ‘sheria ya ugavi na mahitaji ’.

    Tanzania ndiyo nchi pekee mashariki na kusini mwa Afrika ambayo haitumii kanuni ya soko shindani ili kuisaidia kupata mapato kutoka raslimali ya wanyamapori. Tanzania haitumii minada ya wazi ili kupanga maeneo ya uwindaji na badala yake hutumia utaratibu wa kutoa vitalu vya uwindaji vinavyosimamiwa na Idara ya Wanyamapori na wakisaidiwa na Kamati ya Ushauri. Mfumo wa Tanzania wa kutoa maeneo ya uwindaji una matokeo mawili yenye matatizo: wanyamapori kupewa thamani ndogo na kuendekeza ufisadi.

    Ushindani miongoni mwa makampuni ya uwindaji ili kupata vitalu vizuri ungepelekea kupanda kwa bei katika vitalu ambavyo ni bora zaidi. Na hii hufanyika katika nchi nyingine ambazo hutumia mifumo shindani kama minada ya wazi na mfumo wa zabuni - bei hupanda kutokana na ugavi na mahitaji.

    Kisanduku Na. 1: Mambo muhimu katika kuboresha biashara ya uwindaji wa kitalii

    Kuboresha biashara ya uwindaji wa kitalii ili iweze kuakisi thamani halisi ya soko la wanyamapori katika Tanzania itahitaji maandalizi muhimu kwa upande wa serikali kwa kushirikiana na wawindaji, wataalam na mashirika ya hiari. Imependekezwa na watalaam kwamba mfumo wa zabuni za wazi zikiwa na maombi na viwango yaweza kuwa ndiyo njia nzuri. Katika kubuni mfumo huo masuala yafuatayo yanahitaji kufikiriwa kwa uangalifu kwa lengo la kuyafikia yafuatayo:

    • Kuyavutia makampuni yenye rekodi nzuri ya usimamizi na utendaji; • Kuanzisha mfumo wa uwindaji wenye uwiano wa utendaji wa kiuchumi na ulinzi wa raslimali kwa

    kipindi sahihi na ushindani katika kuomba upya;• Kujenga ubia wa muda mrefu unaochochewa na utendaji kati ya serikali na sekta binafsi ikiwa na

    ufuatiliaji wa uwazi na tathmini kulingana na vigezo vilivyowekwa;• Kutoa vivutio vyenye nguvu kwa ulinzi wa wanyamapori na makazi na kuboresha maeneo ya

    wanyamapori yaliyoharibiwa ama kupungua kwa thamani ya nyara;• Kuvutia maslahi katika vitalu vizuri vya uwindaji na vitalu visivyo na mvuto vinavyohitaji kuboreshwa;• Kuwarekebisha wazabuni wakubwa ambao hawana rekodi nzuri ya kiusimamizi na matumizi ya vitalu

    vya uwindaji;• Kuhimiza makampuni ya kitanzania ili yaweze kuingia na kushindana na makampuni ya kutoka nje;• Kuyapa makampuni uhuru ili kufikia utendaji wa juu.

    3-4

  • uwindaji wa wanyamapori. Ni soko tu linaloelewa bei halisi! Uwepo uhakiki wa kuwa soko linaendeshwa kwa haki na kwa tija na halijaghushiwa (angalia Kisanduku Na. 1).

    Kwa kukosekana kwa uwazi na mifumo shindani ya kugawanya maeneo ya uwindaji siku zote kutatoa na kulea mianya ya ufisadi katika ugawanyaji wa vitalu vya uwindaji. Na hii ilikuwa hitimisho la taarifa ya uwindaji wa kitalii katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afika (SADC) na ilitolewa na taasisi ya ufuatiliaji ya kimataifa, TRAFFIC:

    ‘Kushindwa kufuata mchakato wenye uwazi na uwajibikaji katika kutoa maeneo ya uwindaji kwa serikali au kwa maeneo ya jamii kunaalika malalamiko ya ufisadi, ubadhilifu na usimamizi mbovu. Mchakato wa zabuni za maeneo ya uwindaji ni budi uwe na ushindani kwa makampuni na ubuniwe kukuza faida za kifedha kwa wamiliki wa ardhi ili kuzuia njama ambazo zitapelekea kuwanufaisha watu binafsi badala ya serikali na ama jamii na wadau.’

    Chanzo: Barnett & Patterson, 2006

    Ikumbukwe kuwa mwaka 1995 Wizara ya Maliasili na Utalii iliandaa ‘Mpango wa Usimamizi wa Uwindaji wa Kitalii’ ambao ulihitaji kufuata mfumo wa kisoko ulio wazi katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji, lakini mpango huo haukutekelezwa. Pia ikumbukwe kuwa katika Sheria ya Manunuzi ya Tanzania inasema raslimali za umma lazima zipatikane kwa mfumo wa uwazi na mfumo wa zabuni. Ajabu, raslimali ya wanyamapori imekuwa tofauti na sheria na hii ni hasara kwa uchumi wa nchi. Hii pia ina mkito hasi dhidi ya uwezo wa mamlaka zilizo na dhamana ya kusimamia wanyamapori.

    Matumizi ya raslimali ya wanyamapori hayajapewa thamani na hivyo sekta hii inachangia kidogo sana kitaifa kuliko ilivyotegemewa. Licha ya kuwepo uwezo wa kuzidisha mapato kutokana na wanyamapori kupitia misingi ya ushindani wa kiuchumi, hili halifanyiki. Hii inatoa fursa kwa ufisadi. Kawaida iliyopo katika usimamizi wa wanyamapori kwa sasa hairuhusu kukuza manufaa ya uchumi kitaifa kutokana raslimali wanyamapori.

    Kuwianisha uwindaji wa kitalii na utalii wa pichaUwindaji wa kitalii na utalii wa picha ni njia mbili tofauti lakini zote ni muhimu kiuchumi na kifedha kwa kuzalisha maduhuli na uwekezaji dhidi ya wanyamapori. Uwindaji wa kitalii huleta ada kubwa kutoka kwa mgeni; uwindaji wa wiki tatu wenye mteja mmoja au wawili tu unaweza kuuzwa kwa dola za kimarekani 50,000 (zaidi ya TZS milioni 55). Wakati utalii wa picha ambao hata ni ghali, wenye malazi katika makambi ya hadhi ya juu na hoteli hauwezi kuleta fedha zinazolingana na zile za uwindaji wa kitalii. Hata hivyo, uwindaji unaweza tu kuchukua idadi ndogo ya wateja katika eneo husika kila mwaka kwa sababu wanyama wanaoweza kuwindwa kiutaratibu ni wachache na hivyo kundi moja tu la wateja laweza kuwinda eneo moja kwa wakati moja.

    Kiyume chake, utalii wa picha unaweza kupokea wateja wengi na zaidi ya maelfu ya watu wanaweza kuona na kupiga picha simba mmoja ndani ya Serengeti, wakati ni mwindaji mmoja anayeweza kupiga simba katika kitalu cha uwindaji ndani ya Selous. Utalii wa picha una bei ya chini lakini una mauzo makubwa kuliko uwindaji. Tofauti nyingine ni kwamba utalii wa picha huhitaji miundombinu zaidi - kama barabara, makambi, hoteli - wakati uwindaji wa kitalii huweza kufanyika mahala ambapo hakuna miundombinu ya kudumu. Utalii wa picha, kwa sababu huhusisha wageni wengi, huvutia uwekezaji, ajira na mapato kupitia huduma mbalimbali - hivi huitwa ‘matokeo zidisho.’

    Tofauti kati ya uwindaji wa kitalii na utalii wa picha kuna viashiria muhimu kwa jitihada za kukuza pato la Taifa kutokana na wanyamapori. Kwa ujumla, uwindaji

    Mwindaji wa kitalii, mteja na wasaidizi wakiwa na nyara - pofu (mbunju) (Taurotragus oryx) katika Tanzania kati

    3-5

  • wa kitalii ni njia muhimu ya kupata mapato kutokana na wanyamapori katika maeneo ya mbali na asili yasiyo na miundombinu, mandhari za kuvutia na idadi kubwa ya wanyamapori ambavyo ni vivutio vya utalii wa picha. Lakini pale utalii wa picha unapokomaa mapato kutokana na kuongezeka kwa utalii wa picha yanaweza kuzidi mapato yanayozalishwa na uwindaji wa kitalii.

    Mapato ya wastani kutoka katika maeneo ya uwindaji wa kitalii kitaifa katika mwaka 2004 yalikadiriwa kufikia dola za kimarekani 40 kwa kilomita moja ya mraba (TZS 48,000 / km2); katika pori la Akiba la Selous kiwango ni dola za kimarekani 70 (TZS 84,000) kwa kilomita ya mraba (angalia Kielelezo Na. 3). Kwa msingi wa kielelezo hiki, Pori la Akiba la Selous lilizalisha dola za kimarekani milioni 3.3 (TZS bilioni 3.96) kwa mwaka 2003. Kwa bahati mbaya takwimu za hivi karibuni kutoka katika mapato ya kiuwindaji hazijatolewa kwa umma.

    Kinyume chake hifadhi ya Serengeti pekee ambayo ni hifadhi ya pili kimapato baada ya Kilimanjaro inataarifiwa kupata dola za kimarekani milioni 21 (TZS bilioni 25.2) kwa mwaka 2006, ambayo ni zaidi ya mapato yote ya serikali kutokana na biashara ya uwindaji wa kitalii. Kielelezo Na. 3 kinaonesha kuwa hifadhi za kaskazini mwa Tanzania hupata mapato zaidi kwa kila kilomita ya mraba kuliko maeneo ya uwindaji ndani ya Selous kusini.

    Ni muhimu kuelewa kuwa vielelezo hivi vya mapato na sababu zinazoandamana kwa sababu watunga sera na wasimamizi wa wanyamapori (Idara ya Wanyamapori na jamii), wanapaswa kuelewa manufaa na hasara za kutenga maeneo ya uwindaji au utalii wa picha.

    Mathalani:

    Kama Hifadhi za Taifa katika kanda ya kaskazini zingetumika kwa uwindaji wa kitalii badala ya utalii wa picha, hii ingekuwa na matokeo makubwa kimapato. Ingawa uwindaji huonesha tija ya uzalishaji mapato kutokana

    Utalii wa picha ni chanzo kikuu cha maduhuli katika maeneo nyeti ya wanyamapori Tanzania

    Kielelezo Na. 3: Mapato ya Taifa kwa eneo kutoka utalii wa picha katika Hifadhi za Serengeti, Tarangire, na Ruaha, na uwindaji wa kitalii katika Pori la Akiba la Selous

    Chanzo: 2006 takwimu toka WMU Economic Survey, 2006; 2003 takwimu toka Baldus & Cauldwell 2004

    Muhimu: Takwimu kutoka Hifadhi za Taifa tatu tangu mwaka 2006, wakati Selous ni kuanzia 2003.

    3-6

  • na wanyamapori katika maeneo mengi hususan magharibi na kusini mwa nchi (mf. Mikoa ya Tabora, Rukwa na Lindi) ambako idadi ya wageni wa utalii wa picha inakwamishwa kwa sasa. Lakini kadiri idadi ya wageni inavyoongezeka katika maeneo mengine kama vile Selous, inakuwa ni vizuri kiuchumi kufikiria kubadilisha maeneo ya uwindaji kuwa ya utalii wa kupiga picha. Na hii imekwisha kufanyika kwa sehemu katika pori la Selous na eneo lote lililotengwa kwa utalii wa picha kinyume na uwindaji wa kitalii linaweza kuongezeka siku za usoni. Mbadala wake ni kuunganisha uwindaji wa kitalii na utalii wa picha katika eneo moja kutegemea msimu na eneo.

    Masuala haya ya kiuchumi ni ya muhimu pia katika ardhi ya kijiji.

    Mathalani:

    Kijiji cha Emboreet, Wilayani Simanjiro hupata dola za kimarekani zaidi ya 40,000 (TZS milioni 48) kwa mwaka kutoka kwa wawekezaji wawili wa kitalii waliopanga katika eneo la kilomita za mraba 156 ndani ya ardhi ya kijiji kwa mapato ya dola za kimarekani 270 (TZS 324,000) kwa kilomita ya mraba. Maeneo yote ya uwindaji ndani ya Wilaya ya Simanjiro huipatia Idara ya Wanyamapori kiasi cha dola za kimarekani 250,000 (TZS milioni 300) katika eneo la kilomita za mraba 12,000 na huzalisha dola za kimarekani 20 (TZS 24,000) kwa kilomita ya mraba (Kibebe 2005; Sachedina 2006). Ni dhahiri katika ardhi za vijiji ambako kuna uwezo mkubwa wa kiutalii - kama vile vijiji kando kando ya Hifadhi za Taifa za Tarangire, Ziwa Manyara na Serengeti

    - huzalisha zaidi kiuchumi ikiwa maeneo haya yatatumiwa kwa utalii shirikishi wa wanavijiji na wawekezaji kuliko maeneo ya uwindaji wa kitalii. Uwezo wa kukua kwa uchumi kiutalii katika maeneo ya kaskazini mwa Tanzania sasa ni wa juu zaidi kuliko uwindaji wa kitalii kufuatia ukuaji wa biashara ya kitalii Tanzania kwa miongo miwili.

    Uwekezaji duni katika usimamizi wa wanyamaporiKatika ngazi ya kijamii kumekuwa na urejeshwaji duni wa matumizi ya wanyamapori, mafao na haki za kusimamia na hizo ni sababu muhimu katika kupungua kwa idadi ya wanyamapori na hiyo inaweza kuonekana pia kama ni uwekezaji duni.

    Vilevile, kiwango cha raslimali ambacho Idara ya Wanyamapori inapewa na hazina kinachangia uwekezaji duni katika usimamizi wa wanyamapori katika maeneo ya kilomita za mraba 250,000 ya maeneo yaliyohifadhiwa. Idara ya Wanyamapori ina upungufu wa uwezo wa raslimali watu, mifumo ya usimamizi an utaratibu wa usimamizi wenye tija katika maeneo hayo yaliyohifadhiwa. Pamoja na ushirikiano na msaada kutoka katika sekta binafsi jamii na mashirika ya hiari, utekelezaji bado unasuasua. Hali ya sasa ya vitendea kazi duni, upungufu wa watumishi na maslahi duni ni chachu ya kuendeleza ufisadi na utendaji mbovu.

    Linganisha hali ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na ile ya Idara ya Wanyamapori. Hifadhi za Taifa ni shirika la serikali lenye bodi, muundo na mifumo ya usimamizi na watumishi. TANAPA hulipa asilimia 20

    Takwimu za serikali zinaonesha kuwa:

    TANAPA ina uwezo wa kutumia takribani dola za kimarekani 1,130 kwa kila kilomita ya mraba kwa mwaka kwa ajili ya usimamizi wa wanyamapori,

    ...wakati...

    Idara ya Wanyamapori inaweza tu kutumia kiasi kinachofikia dola za kimarekani 24 katika kilomita moja ya mraba kwa mwaka

    Hata hivyo,

    Mwaka 2007 Hifadhi za Taifa (TANAPA) walipata TShs bilioni 69.0 lakini ni asilimia 1.8 tu zilipelekwa kwa shughuli za ujirani mwema (TANAPA Annual General Report 2007).

    Kinyume chake, katika mwaka 2006 Idara ya Wanyamapori ilipata TShs bilioni 15.3 kutokana na matumizi endelevu ya wanyamapori, na ilikuwa na uwezo wa kurudisha asilimia 12.8 katika Wilaya husika (Economic Survey 2006).

    Kwa nini ni mapato kidogo sana hurudishwa kwa jamii na usimamizi wa wanyamapori - hususan kwa TANAPA - wakati wanyama wanaendelea kupungua?

    3-7

  • ya ongezeko la thamani katika mapato yake na kiasi kinachobaki hutumika katika uendeshaji wa shirika. Kwa kulinganisha, Idara ya Wanyamapori hupokea asilimia 25 ya mapato yote yaliyokusanywa kutokana na matumizi ya wanyamapori nje ya Hifadhi za Taifa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na pia hupata zidio la asilimia 25 ambalo hupelekwa katika Mfuko wa Hifadhi za Wanyamapori Tanzania (TWPF). Mfuko huo hausimamiwi kwa uwazi na hesabu zake zilizokaguliwa haziko wazi kwa umma.

    Ni kwa vipi mapato ya sekta ya wanyamapori yanaweza kutumika kwa ufanisi kuendeleza wanyamapori?Serikali ya Tanzania iko chini ya shinikizo kubwa kuongeza makusanyo ya mapato ya maliasili ili kuweza kuongeza bajeti ya Taifa, ili kutoa huduma na kuendeleza miundombinu.

    Kwa vile ni dhahiri wanyamapori ni moja ya maliasili muhimu ambayo hutoa msingi wa biashara ya utalii nchini, fikra kubwa zinatakiwa zielekezwe katika kuboresha uwekezaji ambao ni duni katika usimamizi wa wanyamapori Tanzania. Wanyamapori wana matokeo mazuri ya kuzidisha shughuli za kiuchumi na hivyo kupanua uwigo wa kodi kwa nchi.

    Msingi wa raslimali ya wanyamapori unaweza kuwekezwa kwa kutumia njia mchanganyiko:

    Kuruhusu Idara ya Wanyamapori ibakize ada zote za matumizi ya wanyamapori na ada za

    maeneo ya uwindaji katika Mapori ya Akiba

    Kuruhusu jamii (asasi zilizoidhinishwa na serikali za vijiji) kubakiza ada za uwekezaji katika ardhi za vijiji

    Kuruhusu jamii (asasi zilizoidhinishwa na serikali za vijiji) kugawana ada za matumizi na Idara ya Wanyamapori moja kwa moja kutokana na kutumia wanyama katika ardhi za vijiji

    Hii itaongeza shughuli za uchumi na uzalishaji wa wanyamapori kupitia kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kodi ya mashirika na ushuru mwingine. Serikali za vijiji na asasi zilizoidhinishwa zinaweza pia kulipa ongezeko la thamani kwa vile ni taasisi zinazojitegemea kisheria.

    Kwa kubakiza fedha za kutosha katika Idara ya Wanyamapori na jamii kwa ajili ya kuwekeza katika usimamizi wa wanyamapori kwa kushirikiana na sekta binafsi kuna uwezekano mkubwa kuwa idadi ya wanyamapori itaboreshwa. Idadi nzuri ya wanyamapori itaongeza pato katika Idara ya Wanyamapori na jamii na pia kuongeza kodi kwenda hazina kupitia ongezeko la matokeo zidisho.

    Kielelezo Na. 4: Mchoro wa dhana kuonesha jinsi muundo wa mapato kutoka sekta ya wanyamapori ungepaswa kuwa. Hazina hukusanya tu kodi za ongezeko la thamani, zingine zinawekezwa katika usimamizi wa wanyamapori na maendeleo ya jamii.

    Ni wajibu wa serikali kuwekeza katika wanyamapori kama raslimali ya umma. Kulingana na umuhimu wake kiuchumi haishauriwi kuendelea ‘kumkamua ng’ombe hadi akauke.’ Hii ni kuiomba Idara ya Wanyamapori, Serikali za Mitaa, Asasi zilizoidhinishwa na Jamii kukifikia kisichowezekana.

    3-8

  • HABARI JUU YA WANYAMAPORI KATIKA TANZANIA

    Wanyamapori kwa watanzania wote: Kusimamisha upotevu, kuendeleza raslimali na kupanua mafao

    Jumiko la Maliasili Tanzania

    Tanzania Natural Resource Forum

    CHAPISHO NA. 4

    USIMAMIZI WA WANYAMAPORI NA KUPUNGUZA UMASIKINI

    MASUALA MUHIMU:

    Wanyamapori wangeweza kutoa mchango mkubwa kisheria katika kupunguza umaskini na kukuza uchumi wa jamii zinazoishi katika maeneo yenye wanyamapori.

    Kwa sasa wanyamapori wana thamani katika jamii zinazofaidika na biashara haramu ya wanyamapori.

    Maendeleo katika kuendeleza usimamizi wa kijamii wa wanyamapori kupitia maeneo ya hifadhi za jamii umekuwa wa polepole na aghali.

    Haki zote za kusimamia na kufaidika kutokana na wanyamapori zinahitaji kurudishwa katika ngazi ya jamii mapema iwezekanavyo ili kutoa motisha chanya juu ya usimamizi endelevu wa wanyamapori miongoni mwa vijiji vinavyopatika na kando ya wanyamapori.

    Kama wanyamapori hawataonesha nafasi katika kupunguza umaskini na kukuza uchumi wa jamii, hivyo shughuli zingine za kiuchumi zitachukua nafasi, na wanyama wataendelea kupungua na kutoweka. Na hii ni kwa sababu wananchi hawatakuwa na ari ya utetezi wa kiuchumi ili kuwasimamia wanyamapori kwa njia endelevu.

    © JMT 2008

    Kwa kushirikiana na

    4-1

  • na yasiyokaliwa nje ya maeneo yaliyohifadhiwa kwa wanajamii na sekta binafsi.”

    Sera ya Wanyamapori ya mwaka 2007 inaendelea kutambua ushirikishwaji wa jamii na utoaji wa haki ya kutumia raslimali. Hata hivyo, sera hii mpya iko mbali na uwazi wa kutambua umuhimu wa jamii kupokea mafao kutoka wanyamapori ili kupunguza umaskini na kuanzisha motisha kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori.

    Sera ya mwaka 2007 inafafanua maeneo ya hifadhi za jamii (WMA) kama mfumo wa kulinda makazi ya wanyamapori na kuepukana na uharibifu wa maeneo oevu. Sera inasema kuwa serikali itahakikisha mgawanyo wa haki wa hasara na mafao ambao unajali nafasi ya wadau kutegemeana na makundi ya ardhi na jitihada zilizowekezwa na taasisi katika uhifadhi.Kauli hii inaweza kulinganishwa na sera ya mwaka 1998 ambayo ilisema kwamba jamii watapewa “mamlaka yote” katika usimamizi wa wanyamapori katika maeneo ya hifadhi za jamii (WMA) yaliyo katika ardhi za vijiji.

    Nafasi ya wanyamapori katika kupunguza umaskiniNi muhimu kuhakikisha kuwa wanyamapori wanatoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania (angalia Chapisho Na. 3). Ni muhimu pia kuwa wanyamapori watoe mchango mkubwa katika kupunguza umaskini na kukuza utajiri katika ngazi ya kijamii. Umuhimu wa kuboresha uhusiano kati ya uchumi wa kitaifa na kupunguza umaskini ngazi ya jamii ndiyo mada kuu katika Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA). MKUKUTA unaahidi jitihada za kuhakikisha kuwa mafao ya ukuaji uchumi yanasambaa hadi vijijini kwa wanajamii na maskini.

    MKUKUTA pia unaelekeza mikakati mahususi ambayo itachangia “michango zaidi kutoka wanyamapori, misitu, na uvuvi na sama kuwaongezea mapato wananchi wa vijijini.”

    Sera ya Wanyamapori ya mwaka 1998 ilitambua umuhimu wa kuongeza mafao ya moja kwa moja kwa wanajamii kutokana na wanyamapori. Lengo la sera lilitamka

    “...jamii na watu binafsi watasimamia wanyamapori katika ardhi zao kwa manufaa yao” na “kurudisha majukumu ya usimamizi katika maeneo yanayokaliwa

    Kikwazo kikuu katika kufikia fursa hii ni kwamba tangu wakati wa ukoloni jamii zilizuiliwa kisheria kutumia wanyamapori na haki za kutumia wan-yamapori zilibakia na kuthibitiwa na serikali.

    Kielelezo Na. 1: Mabadiliko katika matumizi ya ardhi katika tambarare za Simanjiro. Je, uchaguzi sahihi wa kiuchumi na kiikolojia unafanyika? Nani anafanya? Nani anafaidika?

    4-2

  • Kama ilivyoelezwa katika Chapisho Na. 3, mwelekeo wa soko wa sasa wa kuongeza uwindaji wa kitalii na utalii wa picha vina uwezo wa kuanzisha fursa za kiuchumi kwa ajili ya wanajamii. Ukweli ni kwamba Tanzania kuna wanyama wengi ukilinganisha na nchi zingine za Afrika, lakini bado maisha ya vijijini (angalia Chapisho Na. 2) nje ya maeneo ya serikali yaliyohifadhiwa ina maana kuwa wanyamapori wana uwezo wa kuzalisha kipato cha moja kwa moja kwa wananchi.

    Maeneo ya Hifadhi za Jamii (WMA)

    Sera ya Wanyamapori ya mwaka 1998 ilielekeza mabadiliko ya kisheria yatakayoruhusu uundwaji wa WMA mahali ambapo jamii wangekuwa wasimamizi kisheria na kufaidika na wanyamapori katika ardhi za vijiji.

    Katika mwaka 2002 serikali iliunda kanuni za kuongoza WMA, zilizorejewa mwaka 2005, chini ya Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 1974 ambayo inaruhusu uanzishwaji wa maeneo ya hifadhi za jamii katika ardhi za vijiji. Kuanzia Januari 2003 Waziri wa Maliasili ya Utalii amefanya kazi na jamii, Serikali za Wilaya na mashirika binafsi mbalimbali ili kuanzisha maeneo ya hifadhi za jamii yapatayo 16 kwa nchi nzima. Hadi Septemba 2008 maeneo kumi ya hayo yalitangazwa kama WMA, na baadhi ya hayo yalikuwa yameshaingia katika mikataba ya uwekezaji.

    Wakati jitihadi zimefanyika katika kuanzisha WMA, matatizo ya kimsingi yamekwamisha maendeleo:

    Awali, kanuni za uanzishwaji maeneo ya WMA ziko changamano na jamii zinahitaji msaada kutoka nje ili kutimiza masharti yote. Hii imehafifisha uanzishwaji wa WMA. Maeneo hayo kama yalivyoanzishwa ni aghali sana kuyaendeleza.

    Pili, maeneo ya WMA hayatoi mamlaka ya kutosha kuthibiti mafao ya kiuchumi kwa jamii kutokana na wanyamapori.

    Kauli nyofu ya kisera inatakiwa kuwekwa kusaidia utoaji wa haki za kutumia, haki za kusimamia wanyamapori na kubakiza mafao ya kijamii katika ardhi za vijiji kama njia ya kupunguza umaskini, kuongeza utajiri na kuboresha matokeo ya uhifadhi.

    Kauli nyofu ya kisera inahitaji kuwekwa kuruhusu uwezekano wa ubunifu na taratibu za usimamizi mbadala kwa jamii ili kusimamia na kupata mafao yatokanayo na wanyamapori katika ardhi za vijiji, kwa mfano, kwa kushirikiana na sekta binafsi.

    Kauli nyofu ya kisera inahitaji kutamka uwezo na umuhimu wa jamii katika kusimamia pamoja na serikali maeneo yaliyohifadhiwa - kama ilivyo katika sera ya sekta ya misitu.

    Kupanga matumizi ya ardhi katika WMA ya Idodi-Pawaga - kukubaliana maeneo ya malisho na yale ya wanyamapori kwa njia shirikishi

    4-3

  • Mathalani: TANAPA wamesaidia kijiji cha Ololosokwan kando kando ya Hifadhi ya Serengeti kuanzisha makambi ya kiutalii ili wanajamii waweze kupata mafao ya ziada kutokana na utalii wa wanyamapori. Tangu mwishoni mwa miaka 1990 mapato ya kijiji cha Ololosokwan na vijiji vingine katika Tarafa ya Loliondo (Wilaya ya Ngorongoro) yameongezeka kufika zaidi ya dola za kimarekani 300,00 (TZS milioni 360) kila mwaka kutokana na biashara ya utalii.

    Mwenendo wa masoko umesaidia jamii nyingi, kama vile vijiji vya Loliondo kuongeza mapato kutokana na utalii, kwa vile idadi ya watalii wanaokuja Tanzania imeongezeka.

    Hata hivyo, jitihada hizi zimekabaliwa na changamoto nyingi. Shughuli za kiutalii katika maeneo haya zimesababisha migogoro na makampuni ya uwindaji yenye vitalu maeneo hayo hayo, hivyo kuweka mafao ya jamii katika hatari. Wawindaji adilifu wamehisi wamelazimishwa kubeba gharama za kuendesha vitalu vya na kwamba makampuni ya utalii wa kupiga picha wamefaidika isivyo halali kutonana na uwekezaji wao. Taratibu mpya zimeanza kuandaliwa kati ya waendeshaji wa makampuni ya uwindaji wa kiutalii na yale ya utalii wapicha, ili kuona namna ya kugawanya hasara na faida za uendeshaji maeneo hayo kwa haki. Na hivyo kuboresha mafao ya jamii. Hata hivyo,

    Kufikiria aina mbadala juu ya usimamizi wa wanyamapori kijamiiZaidi ya WMA kuna njia zingine ambazo jamii zinaweza kupata manufaa ya kiuchumi kutokana na wanyamapori. WMA zimeanzishwa kutoa haki kwa jamii juu ya matumizi ya wanyamapori lakini pia utalii usio wa uvunaji waweza kufanyika katika ardhi za vijiji ambako WMA hazijaanzishwa, kwa vile utalii wa kupiga picha hauvuni wanyamapori.

    Kaskazini mwa Tanzania, vijiji vimeingia katika mikataba na wawekezaji ili kuendesha utalii ambao utaleta faida kwa jamii kutokana na wanyamapori.Mingi ya mikatabi hii ya vijiji na wawekezaji iko katika vijiji kuzunguka hifadhi za Serengeti and Tarangire, na imekuwepo kwa zaidi ya miaka 10 hadi 15 iliyopita. Kumekuwepo na mawakala mbalimbali wa serikali ambao wamesaidia kusukuma jitihada hizo.

    Kielelezo Na. 2: Kuongeza mapato kutoka utalii usio wa uvunaji kwa vijiji saba Tarafa ya Loliondo na kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, 1996-2007.

    Moja ya changamoto kubwa ni kwamba kugawana mapato yaliyozalishwa katika maeneo ya WMA hakuko wazi; kanuni zinaeleza tu kuwa mgawanyo wa mafao utaamuliwa kutokana na maelekezo kupitia “nyaraka zitakazotolewa na serikali nyakati tofauti.” Kiasi cha maduhuli kutokana na wanyamapori katika WMA hakijawahi kufafanuliwa; Hii inafanya kuwa vigumu kwa jamii kuelewa kama uanzishwaji wa WMA utawaendeleza au la.

    Chanzo: Wawekezaji wa Loliondo

    4-4

  • kanuni za utumiaji wasio wa kuvuna wanyamapori zilizotolewa mwaka 2007 zinahitaji malipo makubwa kwenda Idara ya Wanyamapori kutoka makampuni ya kiutalii yanayofanya kazi ya utalii katika maeneo hayo. Malipo kama yalivyoelezwa katika kanuni, yatapunguza fedha kwa kiwango kikubwa ambazo makampuni ya kiutalii yanatakiwa kulipa vijijini. Hii itapunguza motisha kwa vijiji kutenga ardhi kwa ajili ya wanyamapori.

    Masuala haya ya kugawana mapato kwa sasa yanajadiliwa na wadau mbalimbali na Idara ya Wanyamapori kama yalivyojadiliwa katika Chapisho Na. 3.

    Wavulana wa kihadzabe wakikagua nyayo: Wanyamapori pia huwakilisha thamani ya kijamii na kiutamaduni isiyo na mbadala – baadhi yake zina zaidi ya miaka 40,000

    4-5

  • HABARI JUU YA WANYAMAPORI KATIKA TANZANIA

    Wanyamapori kwa watanzania wote: Kusimamisha upotevu, kuendeleza raslimali na kupanua mafao

    Jumiko la Maliasili Tanzania

    Tanzania Natural Resource Forum

    CHAPISHO NA. 5KUWIANISHA WANYAMAPORI NA MASLAHI YA JAMII:

    UMUHIMU WA KUSHIRIKISHA SEKTA MBALIMBALI

    MASUALA MUHIMU:

    Ili kuweza kukuza mchango chanya wa wanyamapori kwa maslahi ya jamii na shughuli za kiuchumi, ni muhimu kuchukua mtazamo wa kushirikisha sekta tofauti ili kuratibu usimamizi wa wanyamapori pamoja na sekta za ardhi, utalii, misitu na mifugo.

    Matendo ya usimamizi wa wanyamapori huweza kuleta migogoro na vijiji vyenye hati za ardhi hasa kupitia mwingiliano wa Mapori Tengefu na Ardhi za Vijiji.

    Usimamizi wa wanyamapori na hifadhi ya misitu ya jamii katika ngazi ya kijiji vinahitaji kuwianishwa ili kutoa manufaa ya kutosha vijijini, kwa sababu wanyamapori na misitu ni raslimali zinazoweza kupatikana kwa pamoja katika ardhi za pamoja za vijiji.

    Matendo na sera ya usimamizi wa wanyamapori vinatakiwa kuwianishwa na malengo ya ukuaji wa sekta ya utalii kitaifa, ili kuwanufaisha wananchi.

    Usimamizi wa wanyamapori ni budi uwe na uwiano wa sera ya sekta ya mifugo pamoja na malengo ya maendeleo kwa vile wanyamapori na mifugo vyote vinategemea nyanda za malisho na vyanzo vya maji katika maeneo mengi na husabibisha ushindani na wakulima.

    Mtazamo wa kuhusisha sera nyingi ni muhimu ili kuweka thamani kubwa kwa wanajamii waweze kufaidika kutokana na ardhi na raslimali zilizopo.

    © JMT 2008

    Kwa kushirikiana na

    5-1

  • yaliyotengwa kwa misingi ya sheria mbalimbali za kisekta, ikiwemo Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 1974. Ardhi ya Jumla inajumuisha ardhi nyingine yote isiyo Ardhi ya Kijiji au ardhi iliyohifadhiwa - mathalani ardhi ndani ya hatimiliki.

    Kama ilivyoelezwa katika Chapisho Na. 2, Mapori Tengefu (GCA) ni ardhi iliyohifadhiwa ambako matumizi yanatawaliwa na sheria - kilimo, mifugo na makazi vinaruhusiwa. Ni karibu maeneo yote Mapori Tengefu yalianzishwa katika maeneo ambayo yamekaliwa na watu.

    Mfano:

    Zaidi ya asilimia 90 ya ardhi Wilaya za Monduli, Simanjiro, na Longido zinaangukia ndani ya mipaka ya Mapori Tengefu. Lakini pia, maeneo haya yote yamewekwa mipaka kama ardhi za vijiji ambako wanajamii wana haki za kuishi kimila. Kwa hivyo hii hufanya maeneo haya kuwa ni ‘Ardhi za Vijiji’ na ‘Ardhi zilizohifadhiwa’ kulingana na tafsiri za Sheria ya Ardhi.

    Mgawanyo huu unaoingiliana husababisha migogoro juu ya nani mwenye mamlaka ya kusimamia ardhi hizo na anayeweza kupata hati za kumiliki kwa ardhi ambayo wananchi wanaishi katika Mapori Tengefu.

    Usimamizi ulioboreshwa wa wanyamapori ungeweza kutoa manufaa mengi kwa jamii (angalia Chapisho Na. 4). Lakini pia ingeweza kusimamiwa kusaidia mahitaji ya jamii katika njia ambayo ni pana zaidi. Hii ina maana kuwa usimamizi wa wanyamapori ni budi ufikiriwe kulingana na sekta zilizopo kama vile ardhi, misitu, utalii na mifugo, kwa vile raslimali hizi zote mara nyingi hupatikana pamoja katika ngazi ya kijiji.

    ArdhiKupata hati za ardhi ni moja ya misingi ya maendeleo ya kiuchumi. Moja ya malengo ya Sera ya Ardhi ya mwaka 1997 ni kuhakikisha haki za kimila za kumiliki ardhi zinatambuliwa na kutolewa kisheria.

    Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya mwaka 1999 zinatoa msingi wa kisheria wa kupata hati za ardhi kwa vijiji kulingana na malengo ya sera ya Taifa. Sheria hizo huunda makundi matatu ya ardhi:

    Ardhi ya Kijiji

    Ardhi iliyohifadhiwa

    Ardhi ya Jumla.

    Ardhi ya Kijiji inajumuisha ardhi yote iliyotumika kimila na jamii ndani ya mipaka ya kijiji kilichosajiliwa. Ardhi iliyohifadhiwa inajumuisha maeneo yote

    Wanajamii wakishirikiana raslimali na wanyamapori katika Mapori Tengefu

    5-2

  • MisituJamii nyingi zenye wanyamapori pia huwa na raslimali misitu katika ardhi zao. Ili kukuza uwezo wa kijamii kufaidika na maliasili, ni muhimu kwa jamii kuwa na uwezo wa kusimamia kwa uwiano misitu na wanyamapori kwa pamoja.

    Mara nyingi maeneo ya WMA na maeneo ya Misitu ya Hifadhi za Vijiji (VLFR) yamehamasishwa na kuanzishwa mahali pengi bila mwingiliano. Mahali pengine, misitu ya vijiji na maeneo ya WMA vimeanzishwa kwa kushabihiana.

    Hata hivyo, ili jamii iweze kupata mafao zaidi kutokana na raslimali, ingefaa waweze kutumia raslimali wanyamapori na misitu (mbao, asali, madawa, kuni na majengo) katika sehemu moja. Kwa maneno mengine ina maana ni kuanzisha maeneo ya WMA na misitu ya vijiji kwa pamoja. Changamoto katika hilo linakuja katika michakato tofauti ambayo inatakiwa katika kuanzisha WMA na misitu ya vijiji.

    Wakati njia za uanzishwaji wa maeneo ya WMA ni changamano na aghali, njia za uanzishwaji

    maeneo ya misitu ya vijiji ni rahisi. Pia, maeneo ya WMA yanasimamiwa na asasi za kijamii ambazo zinawakilisha vijiji vingi, wakati maeneo ya misitu ya vijiji yanasimamiwa na serikali za vijiji au na umoja wa serikali mbalimbali za vijiji.

    Hata hivyo, njia za kuanzisha maeneo ya WMA na misitu ya vijiji katika sehemu moja zingesaidia kuhakikishia wananchi wanakuza faida kutokana na raslimali kwa kuongeza njia tofauti za mapato wanayokusanya, kama vile uvunaji, na upiga picha wa wanyamapori, mbao na mazao misitu mengine yasiyo miti.

    Kile ambacho kingeleta maana zaidi kwa jamii ni kuwa na ‘maeneo ya usimamizi maliasili kijamii’ ambako vyote raslimali, wanyamapori na misitu vinasimamiwa katika ngazi ya kijiji badala ya kutenganishwa kama maeneo ya WMA na misitu ya vijiji. Kupitia mazingira wezeshi ya kisera hii ingekuwa rahisi katika maeneo mengi ambayo yana vyote, WMA na misitu ya vijiji.

    Nyika kubwa na misitu haijalindwa chini ya ‘Hifadhi za Misitu’ lakini badala yake zimeanza kusimamiwa na jamii

    5-3

  • Azma ya Sera ya Taifa ya Mifugo ya mwaka 2006 ni “Kuhakikisha raslimali mifugo inaendelezwa na kusimamiwa ili kukuza uchumi na kuboresha maslahi ya jamii.”

    MKUKUTA inasema sekta ya mifugo iongeze mchango wake katika pato la Taifa, kutoka asilimia 2.7 ya 2000/01 hadi asilimia 9 kwa mwaka 2010. Hata hivyo, kupanua sekta ya mifugo kutahitaji kufanyike kwa njia ambayo inakubaliana na malengo ya sekta zingine, kama vile wanyamapori na utalii ili kuhahikisha ukuaji wa sekta moja hauhafifishi ukuaji wa sekta nyingine.

    Njia moja ya kufanya hili ni kuwapatia hatimiliki jamii za kifugaji ili kusimamia manufaa kutokana na wanyamapori na kujibu matatizo yanayokabili maeneo ya WMA kama ilivyoelezwa katika Chapisho Na. 4. Jambo muhimu ni kusaidia uzalishwaji wa mifugo kupitia desturi za matumizi ya ardhi ya kifugaji na kutambua kuwa uanzishwaji wa ufugaji wa kibiashara katika ranchi zilizowekewa uzio kutasababisha kupungua kwa idadi ya wanyamapori na hivyo kupunguza uwezo wa kiutalii.

    Kuwianisha maboresho katika usimamizi wa wanyamapori, maendeleo ya utalii, uzalishaji wa mifugo unawezekana, lak