7
WIZARA ILIVYOJIPANGA KUONGEZA UBORA WA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII Na Erasto Ching’oro – Msemaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Katika jamii yoyote ile inayopenda maendeleo, ushirikishwaji wa wananchi wake ndilo jambo la msingi na la muhimu ili kuwa na maendeleo endelevu ya jamii hiyo na mabadiliko ya miundombinu yaliyo thabiti. Hali hii imekuwa ikionekana katika maeneo mengi hususan katika nchi zilizoendelea kiuchumi na zinazoendelea duniani. Kutokana na mtazamo huo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sehemu ya Maendeleo ya Jamii, imejipanga kuendelea kuboresha mafunzo ya taaluma ya maendeleo ya Jamii ili kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuchochea maendeleo ya wananchi nchini. Mbali na Vyuo 55 vya Maendeleo ya Wananchi vilivyopo, Wizara ina Vyuo tisa vya Maendeleo ya Jamii, amabavyo ni Tengeru, Buhare, Rungemba, Uyole, Mlale, Mabughai, Monduli, Missungwi na Ruaha, Vyuo hivi vinaoa umaarufu wa kihistoria katika maendeleo ya watu na Taifa. Inakumbukwa kuwa, mwaka 1960 serikali ya kikoloni ilianzisha Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, na baadaye vingine vikafuata. Vyuo hivi vimendelea kutekelezwa lengo lake la kuwajengea uwezo kwa kutoa elimu, ujuzi na mbinu zitakazowasaidia wataalam wa Maendeleo ya Jamii kutekeleza dhana ya maendeleo ya jamii kwa vitendo katika jamii kwa kuwawezesha watu kutambua uwezo walio nao wa kubaini matatizo na uwezo wao wa kutumia raslimali zilizopo ili kuongeza kipato na kupunguza umaskini wa watu ili kuboresha hali ya misha yao. baadhi ya Vyuo vilianzishwa kati ya miaka ya 1970 na 1980 kwa kurithi majengo ya taasisi mbalimbali yaliyojengwa kati ya mwaka 1950 hadi 1963. Kutokana na majengo haya kuwa makuu kuu, kwa sasa ni machakavu na hayaendani na mahitaji ya kutolea mafunzo katika mazingira yenye ushindani. Viongozi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii waliokutana kwa hivi karibuni kwa muda wa wiki moja mkoani Dodoma, wametoa rai kwa Serikali kutenga fedha ya kukarabati majengo ya vyuo hivi ili kumudu ushindani wa soko na kuwa na kuwa na majengo na miundombinu mipya na ya kisasa. Vyuo hivi vikisaidiwa kujengewa uwezo wa kukabilina na uhaba wa majengo, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, vyombo vya usafiri, na upungufu wa watumishi, udahili utaongezeka kutoka wanachuo 940 mwaka 2005/06 hadi kufikia wanachuo 3,634 (2014/15). Uwekezaji huu utakuwa na manufaa makubwa maana vyuo hivi vitaandaa wataalamu wengi wenye

€¦ · Web viewNa Erasto Ching’oro – Msemaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Katika jamii yoyote ile inayopenda maendeleo, ushirikishwaji wa wananchi wake

  • Upload
    lamtu

  • View
    320

  • Download
    8

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: €¦ · Web viewNa Erasto Ching’oro – Msemaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Katika jamii yoyote ile inayopenda maendeleo, ushirikishwaji wa wananchi wake

WIZARA ILIVYOJIPANGA KUONGEZA UBORA WA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII

Na Erasto Ching’oro – Msemaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Katika jamii yoyote ile inayopenda maendeleo, ushirikishwaji wa wananchi wake ndilo jambo la msingi na la muhimu ili kuwa na maendeleo endelevu ya jamii hiyo na mabadiliko ya miundombinu yaliyo thabiti.

Hali hii imekuwa ikionekana katika maeneo mengi hususan katika nchi zilizoendelea kiuchumi na zinazoendelea duniani. Kutokana na mtazamo huo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sehemu ya Maendeleo ya Jamii, imejipanga kuendelea kuboresha mafunzo ya taaluma ya maendeleo ya Jamii ili kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuchochea maendeleo ya wananchi nchini.

Mbali na Vyuo 55 vya Maendeleo ya Wananchi vilivyopo, Wizara ina Vyuo tisa vya Maendeleo ya Jamii, amabavyo ni Tengeru, Buhare, Rungemba, Uyole, Mlale, Mabughai, Monduli, Missungwi na Ruaha, Vyuo hivi vinaoa umaarufu wa kihistoria katika maendeleo ya watu na Taifa. Inakumbukwa kuwa, mwaka 1960 serikali ya kikoloni ilianzisha Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, na baadaye vingine vikafuata.

Vyuo hivi vimendelea kutekelezwa lengo lake la kuwajengea uwezo kwa kutoa elimu, ujuzi na mbinu zitakazowasaidia wataalam wa Maendeleo ya Jamii kutekeleza dhana ya maendeleo ya jamii kwa vitendo katika jamii kwa kuwawezesha watu kutambua uwezo walio nao wa kubaini matatizo na uwezo wao wa kutumia raslimali zilizopo ili kuongeza kipato na kupunguza umaskini wa watu ili kuboresha hali ya misha yao. baadhi ya Vyuo vilianzishwa kati ya miaka ya 1970 na 1980 kwa kurithi majengo ya taasisi mbalimbali yaliyojengwa kati ya mwaka 1950 hadi 1963. Kutokana na majengo haya kuwa makuu kuu, kwa sasa ni machakavu na hayaendani na mahitaji ya kutolea mafunzo katika mazingira yenye ushindani. Viongozi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii waliokutana kwa hivi karibuni kwa muda wa wiki moja mkoani Dodoma, wametoa rai kwa Serikali kutenga fedha ya kukarabati majengo ya vyuo hivi ili kumudu ushindani wa soko na kuwa na kuwa na majengo na miundombinu mipya na ya kisasa.

Vyuo hivi vikisaidiwa kujengewa uwezo wa kukabilina na uhaba wa majengo, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, vyombo vya usafiri, na upungufu wa watumishi, udahili utaongezeka kutoka wanachuo 940 mwaka 2005/06 hadi kufikia wanachuo 3,634 (2014/15). Uwekezaji huu utakuwa na manufaa makubwa maana vyuo hivi vitaandaa wataalamu wengi wenye ari ya kusimamia shughuli za maendeleo maeneo ya vijijini na mijini.

Watumishi hao wa taaluma ya maendeleo ya jamii watasaidia kuhimiza jamii zetu kubadili tabia zao kutoka katika uchumi wa kijungu jiko, na desturi za imani hasi na hivyo kuwa na fikra chanya zenye uchu uchu wa kupaa kimaendeleo. Kama nilivyoeleza awali kwamba ili kuwepo na maendeleo endelevu hapana budi wananchi wakashirikishwa na kuendelezwa katika kazi mbalimbali ili waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na maendeleo ya vitu na miundo mbinu yakaenda sambamba na utimamu wa kifkra.

Kutokana na umuhimu wa vyuo hivi, Uongozi wa Vyuo vya Maendeleo ya jamii vinatoa pendekezo nyenyekevu vikiomba Serikali kukarabati vyuo hivi, ili kuboresha mafunzo na kuongeza idadi ya wahamasishaji hawa wa maendeleo ya jamii katika halmashauri. Wataalamu hawa wakienda kwenye jamii zetu, wakaishi na watu huko walipo, wakajifunza kutoka kwao, watakuwa msaada mkubwa katika kushawishi jamii kuacha tabia hasi na kuwa utayari wa kupokea mabadiliko na hivyo taaifa letu kuwa na msukumo mpya katika kmaendeleo ya kweli.

Page 2: €¦ · Web viewNa Erasto Ching’oro – Msemaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Katika jamii yoyote ile inayopenda maendeleo, ushirikishwaji wa wananchi wake

Azma iliyooneshwa na Wizara hii, inalenga katika utekelezaji wa kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’, na kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya Tanzania tunayoitaka sasa, hata kabla ya mwaka 2030. Maboresho ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii yakifanyika, vitatoa mchango mkubwa katika kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii maana vyuo hivi vitaendelea kuwa vitivo vya elimu, utafiti, ushauri, mafunzo na maonesho maalum, na hivyo kuwa kichocheo cha maendeleo. Mbali na jukumu la msingi la kuandaa wataalamu, vinaweza kulea kijiji fulani cha mfano, na jamii ya pale ikashirikishwa kujadili na kutatua matatizo yao kwa kutumia fursa walizonazo katika maeneo yao, na pale inapowezekana, watasaidiwa na Serikali na wahisani wengine. Matokeo yatakayopatikana yatakuwa somo la kuigwa katika maeneo mengine. Jambo hili linawezekana.

Hii inaweza pia kufananishwa na mifano halisi ya nchi nyingine zilizoendelea kama nchi ya Korea Kusini. Mathalani, katika miaka ya 1970 nchi ya Korea kusini ilichukuwa hatua madhubuti za kuondokana na umaskini, nchi hiyo ilianzisha kampeni ya ‘Saemaul Undong’, kwa maana ya maendeleo endelevu ya jamii kwa kuzingatia mahitaji ya watu. Kampeni hii ilianzishwa na Serikali kwa imani kwamba itasaidia vijiji vya Korea kuweza kupaa kimaendeleo vikiwa na maendeleo yenye kuvifanya vijiji hivyo kuwa mahali penye maendeleo yenye mafanikio. Utekelezaji wa kampeni hiyo uliratibiwa kwa kushirikisha watu wenyewe kwa kupitia jumuia za mitaa.

Malengo mahususi ya kampeni hiyo ilikuwa ni kustawisha jamii kisasa yenye amani na maisha ubora, kuanzisha uwekezaji unaotoa ajira zenye staha kwa wafanyakazi wake, mahali ambapo ukuaji endelevu unafikiwa katika mazingira yenye huduma bora za afya, watu wake watafurahia ushirikishwaji katika mipango, kujenga taifa lenye mafanikio endelevu ambalo linakuza uzalendo wake na kila mtu anajivunia uraia na utaifa wake.

Kutokana na malengo hayo, kampeni iliwajenga wananchi waliitikia kufanya kazi kwa ari kubwa, walikuwa tayari kujitegemea, waliimarisha ushirikiano, matokeo yake waliboresha hali ya maisha na kukuza ushindani wa kimaendeleo katika jamii za taifa lao.

Kwa mfano huo, ni dhahiri kwamba dhamira ya kuwepo vyuo vya maendeleo ya jamii sanjari na vyuo vya maendeleo ya wananachi, haitofautiani sana na Kampeni ya ‘Saemaul undong’, kwani msingi wa vyuo hivyo ni kutoa ufahamu ambao wananchi huelimishwa ili kujiendeleza, na sehemu kubwa ya vyuo hivyo viko katika maeneo ya vijijini na hivyo uwepo wa maafisa maendeleo ya jamii huleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja, vikundi na jamii nzima kwa ujumla kama ambavyo dhana ya maendeleo ya jamii inavyoweka mkazo kuwa ‘maendeleo ya watu ni mchakato undelevu katika kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutawala na hivyo kuwezesha maisha ya watu kuwa bora kwa kuzingatia misingi ya ushirikishwaji, usawa, kuaminiana na kuheshimiana miongoni mwao.

Vilevile, dhana hii inazingatia kuwa wahusika wakuu katika mchakato wa kuleta mabadiliko yanayotarajiwa ni watu wenyewe, wakishirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine.

Hii inadhihirisha wazi kwamba, katika dhana ya maendeleo ya jamii ambayo inaeleza kwamba, ongezeko la ushiriki wa watu katika masuala ya kijamii na maendeleo kutoka kiwango kidogo cha ushiriki na kuwa watu wengi zaidi na wanaopenda wenyewe ndio nguvu ya jamii kwani jamii inakuwa na uwezo na nguvu za kuweza kujitegemea yenyewe na kuleta maendeleo katika sehemu husika na hivyo kunufaisha jamii na Taifa.

Katika makala hii hatumaanishi kunakiri mbinu zilizotumiwa na nchi ya Korea kusini katika kujiletea maendeleo yetu maana kunatofauti za kimazingira. Linalositizwa ni kuwa na mikakati thabiti inayotegemeana na kushabihiana katika programu ya kufikia maendeleo yanayokusudiwa. Tunatakiwa kuendelea kubaini mchango wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kuwa ni wa muhimu sana katika kuleta maendeleo ya jamii zetu na taifa kwa ujumla.

Tunaimani kubwa kwamba Serikali na wadau mbalimbali wataweza kuunga mkono juhudi za Wizara

Page 3: €¦ · Web viewNa Erasto Ching’oro – Msemaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Katika jamii yoyote ile inayopenda maendeleo, ushirikishwaji wa wananchi wake

ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto katika kufanya maboresho muhimu ya vyuo hivi kwa kuongeza ufadhili ili kuendeleza ukarabati wa miundombinu. Aidha nafarijika na juhudi za uongozi wa Wizara hii kufanya mapitio ya taratibu za uendeshaji wa mafunzo ili kuimarisha mazingira ya masomo na mitaala ya mafunzo zoezi ambalo limefanyika kwa umahiri mkubwa mapema, hapa mkoani Dodoma.

Mstari wa Mele katikati, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Deogratias Yinza akiwa na viongozi wa Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, waliohudhuria kikao kazi cha Uendeshaji wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Ukumbi wa Hazina, mkoani Dodoma. (15/7/2016).

Page 4: €¦ · Web viewNa Erasto Ching’oro – Msemaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Katika jamii yoyote ile inayopenda maendeleo, ushirikishwaji wa wananchi wake

Kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Deogratias Yinza, akifunga kikao cha Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, katikati ni Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Erasmus T. Rugarabamu, na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii, Enterberth Nyoni, wakifuatilia nasaha za Mgeni rasmi wakati wa kufunga kikao katika Ukumbi wa Hazina, mkoani Dodoma tarehe 15/7/2016.

Makamu wa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli, Arusha, Columba Maboko akitoa neno la shukrani kwa Mgeni rasmi (hayupo pichani) aliyefika kufunga kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vya

Page 5: €¦ · Web viewNa Erasto Ching’oro – Msemaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Katika jamii yoyote ile inayopenda maendeleo, ushirikishwaji wa wananchi wake

Maendeleo ya Jamii nchini kilichofanyika Ukumbi wa Hazina, mkoani Dodoma tarehe 15/7/2016.

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakidurusu mada zilizowasilishwa kuhusu uendeshaji na maboresho ya Vyuo hivyo nchini.

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Erasmus T. Rugarabamu, katika ukumbi wa Hazina, mkoani Dodoma, tarehe 15/7/2016.