16
Baada ya kuachiliwa Gwajima akitumia mimbari ya kanisani kwake Jumapili iliyofuatia (Feb- ruari 26) alijibu mapigo na kutoa madai mazito ambayo tayari yali- kuwa yameanza kuenea mitaani kuwa Makonda halikuwa jina la kuzaliwa la Mkuu wa Mkoa wa Dar na kuwa alikuwa anatumia jina la mtu mwingine. Mchungaji Gwajima alitoa ma- dai kuwa Paul Makonda alizaliwa Mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Mis- ungwi kwenye Kijiji cha Kolomije na kupewa jina la Daud Albert Bashite. Alisoma elimu ya msingi na sekondari akitumia majina yake ya kuzaliwa hadi alipofika sekondari na kuhitimu kidato cha nne. Kwa mujibu wa Gwajima ni baada ya kufeli elimu ya sekondari ndipo alipoamua kutumia cheti cha mtu mwingine. Gwajima katika madai yake amesema kuwa Makonda aliun- ganishwa na dada mmoja aitwaye ROS NOSTO ODIT LAN ULLA FACIN HENIM ..................................................................... 1 RAESEQCTET NIAM ......................................................................................................... 1 SCIEM INE VERIPIO NSULIN ............................................................................................ 1 ASTIUS PUBLIS ETRIDET .................................................................................................. 1 ACIDUISMODIO ...........................................................................................2 HENDION DUNT ............................................................................................................... 2 AT ATUE ........................................................................................................................... 2 GIAM VER......................................................................................................................... 2 TIO VERIUSC ILIQUAT ..................................................................................3 ENIM IUSTO OD DOLORE VELENT WIS ALIQUIS ............................................................... 3 RAESEQCTET NIAM ......................................................................................................... 3 RAESEQCTET NIAM ......................................................................................................... 3 CULLA REM TUS ..........................................................................................4 UNTERE EFFRE DIO SULTORUM ....................................................................................... 4 AXIMPL. DUCESCIEMUS................................................................................................... 4 TO VE, MORUDE ............................................................................................................... 4 UGAIT AUGUE TAT ........................................................................................................... 5 ALISMOD BLANDRE .....................................................................................6 LOR ILIQUIS ALIQUIPIT .................................................................................................... 6 HENDION DUNT ............................................................................................................... 6 ED DOLOBOR PERCILIS .................................................................................................... 6 AMCORPER UTAT .........................................................................................7 SIM DIT ACING ................................................................................................................ 7 VEL BLAM CONSENT ESTO .............................................................................................. 7 NITALATORUS PROX NUM ............................................................................................... 8 INT, CONSIMISQUAM FACTALABUS ................................................................................. 8 VIDIIS NONSULA RITAMPL .............................................................................................. 8 SUM ALISCIP ERCILLA .................................................................................9 EXER SUSCILIQUAT AD DOLORPE RATING EL ULLA FEUGUE ........................................... 9 LOREM ULLAOR ILIT EXERO ............................................................................................ 9 ALISMOD SECTE BLANDRE ......................................................................... 10 ET, CONSEQUIPIT NULLAM ALIS NUM IN UTAT .............................................................. 10 VEL DOLUPTAT . ............................................................................................................. 10 PUTE MOD EXMINIBH AUTEM ....................................................................................... 10 DO AUGAIT EUGAIT ................................................................................... 11 OSTO DOLORE VER IUSCI TAT VELIT AM NIT ................................................................... 11 FEU FACI ETUEROS NIM VOLOBOR ................................................................................ 11 ED ELIQUIP ISMODOL ................................................................................................... 12 LIT NIAM .................................................................................................. 13 SERATUAM IUS PRICA ................................................................................................... 13 SERES NORUM MED ECONSUS INAM ............................................................................. 13 TOLEO LA KILA WIKI ISNN: Toleo la MAJARIBIO 2 MACHI 13, 2017 BEI SH 800/- TU ZAMA MPYA! Gazeti la Utetezi wa Fikra Mpya! Unachokijali Ndicho Tunachokijali... RC MAKONDA AZIDI KUNG’ANG’ANIWA Askofu Gwajima aongoza mashambulizi Adai jina lake la asili ni Daud Albert Bashite MHARIRI: “Mabadiliko CCM Yamechelewa” Mkutano maalum utaonesha chama kinachojisahihisha au kilichopotea Chama cha Mapinduzi MAKAMPUNI YA UTALII YAMUUNGA MKONO RC SIMIYU Na. Mwandishi Wetu KAMPUNI za kitalii zilizo chini ya Friedkin Conservation Fund (FCF) Tanzania iliyowekeza katika pori la Makao wilayani Meatu na Maswa Mkoani Simiyu imechan- gia mifuko 3000 ya saruji na ma- bati na 1000 kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani humo. Misaada hiyo yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 70 imetolewa na kampuni hizo ikiwa ni kuunga mko- no mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli kuendeleza elimu ya hasa katika INDEX » Inaendelea UK. 6 » Inaendelea, UK. 2 SOFIA SIMBA ATIMULIWA CCM Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa MIJADALA NA HOJA Uk. 6 MAKALA YA MWANAKIJIJI - “Wasiokubaliana na Magufuli CCM Wajiondoe Wenyewe?” Uk. 9 MICHEZO: Cameron Yanyakua Ubingwa AFCON’17 Uk. 14 MIKOANI: Madaktari wa Korea Wato Tiba SengeremaUk. 3 ALIYEKUWA MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake wa Tanza- nia (UWT) ambayo ni mojawapo ya jumuiya za Chama cha Map- induzi Bi. Sofia Simba ambaye pia alikuwa ni Mbunge wa viti maalum amefukuzwa uanachama wa chama hicho. Taarifa za kufukuzwa kwake zime- tolewa siku ya Jumamosi kufuatia kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ambacho kilikaa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Rais John P. Magufuli. Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Bw. Humphrey Polepole ilisema tu kuwa waliopewa adhabu mbalim- bali walipewa adhabu hizo sababu ya kukiuka maadili kinyuma na Ka- tiba na Kanuni za chama cha map- induzi. Sofia Simba alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa CCM ambao walikuwa wazi katika kumuunga mkono aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa ambaye jina lake lilikatwa wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2015. Kikao cha Kamati Kuu ya CCM am- bacho kimefanyika Dodoma kime- kaa kama sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambao unaanza siku mbili zijazo na ambazo unatarajiwa ku- fanyia marekebisho makubwa ya Kikatiba ambayo yanadaiwa kuwa yanalengo la kukiimarisha chama zaidi. Sofia Simba ameondolewa pamo- ja na kundi la viongozi wengine mbalimbali na wa ngazi mbalim- bali za chama hicho ambao nao walikutwa na hatia katika makosa ya maadili dhidi yao. Viongozi wengine wa CCM am- bao wameondolewa, kushushwa vyeo au kufukuzwa uanachama ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar-es-Salaam Bw. Ra- madhan Rashid Madabida. We- nyeviti wengine wa mikoa ambao wamefukuzwa uanachama ni pamoja na Jesca Msambatavangu HABARI ZILIZOMO Na. Tizzo Chuma Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Sa- laam Bw. Paul Makonda (pichani) amejikuta aking’ang’aniwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii na nje ya mitandao hiyo akidaiwa kuwa katika safari yake ya elimu alikuwa ametumia vyeti ambavyo si vyake na kuwa jina analotumia si lake bali ni la mtu mwingine. Tuhuma dhidi ya Makonda zil- ianza taratibu kama minong’ono wiki chache zilizopita hasa baada ya yeye Makonda kusimama na kuanza kutaja majina ya watu ambao aliwatuhumu kuwa wa- najihusisha kwa namna moja au nyingine na biashara ya madawa ya kulevya Jijini Dar-es-Salaam. Mmoja wa watu aliowataja kwenye ile iliyoitwa orodha yake na kumtaka afike kituo cha polisi cha Mkoa Jijini Dar (Police Central) ni mchungaji maarufu jijini Dar Bw. Josephat Gwajima wa kanisa la Uzima. Gwajima (pichani juu) alifika polisi na kuhojiwa na polisi kwa muda wa zaidi ya masaa 24 pamoja na kupekuliwa nyumbani kwake. Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM kukata jina la Edward Lowassa mwaka 2015 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais » inaendelea, UK. 3 Na. Dotto Kwilasa MAKAO MAKUU, DODOMA » Inaendelea, UK. 7 Chama cha Mapinduzi kimeanza hatua za ku- jisafisha na kusimamia wanachama wake; kad- haa wafukuzwa! MAWASILIANO MATANGAZO OZ Media House Gazeti la Zama Mpya P. O. Box 90159 Dar es Salaam, Tanzania +255 746 202 000

Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

Baada ya kuachiliwa Gwajima akitumia mimbari ya kanisani kwake Jumapili iliyofuatia (Feb-ruari 26) alijibu mapigo na kutoa madai mazito ambayo tayari yali-kuwa yameanza kuenea mitaani kuwa Makonda halikuwa jina la kuzaliwa la Mkuu wa Mkoa wa Dar na kuwa alikuwa anatumia jina la mtu mwingine.

Mchungaji Gwajima alitoa ma-dai kuwa Paul Makonda alizaliwa Mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Mis-ungwi kwenye Kijiji cha Kolomije na kupewa jina la Daud Albert Bashite.

Alisoma elimu ya msingi na sekondari akitumia majina yake ya kuzaliwa hadi alipofika sekondari na kuhitimu kidato cha nne. Kwa mujibu wa Gwajima ni baada ya kufeli elimu ya sekondari ndipo alipoamua kutumia cheti cha mtu mwingine.

Gwajima katika madai yake amesema kuwa Makonda aliun-ganishwa na dada mmoja aitwaye

ROS NOSTO ODIT LAN ULLA FACIN HENIM .....................................................................1RAESEQCTET NIAM .........................................................................................................1SCIEM INE VERIPIO NSULIN ............................................................................................1ASTIUS PUBLIS ETRIDET ..................................................................................................1ACIDUISMODIO ...........................................................................................2HENDION DUNT ...............................................................................................................2AT ATUE ...........................................................................................................................2GIAM VER.........................................................................................................................2TIO VERIUSC ILIQUAT ..................................................................................3ENIM IUSTO OD DOLORE VELENT WIS ALIQUIS ...............................................................3RAESEQCTET NIAM .........................................................................................................3RAESEQCTET NIAM .........................................................................................................3CULLA REM TUS ..........................................................................................4UNTERE EFFRE DIO SULTORUM .......................................................................................4

AXIMPL. DUCESCIEMUS...................................................................................................4TO VE, MORUDE ...............................................................................................................4UGAIT AUGUE TAT ...........................................................................................................5ALISMOD BLANDRE .....................................................................................6LOR ILIQUIS ALIQUIPIT ....................................................................................................6HENDION DUNT ...............................................................................................................6ED DOLOBOR PERCILIS ....................................................................................................6AMCORPER UTAT .........................................................................................7SIM DIT ACING ................................................................................................................7VEL BLAM CONSENT ESTO ..............................................................................................7NITALATORUS PROX NUM ...............................................................................................8INT, CONSIMISQUAM FACTALABUS .................................................................................8VIDIIS NONSULA RITAMPL ..............................................................................................8SUM ALISCIP ERCILLA .................................................................................9

EXER SUSCILIQUAT AD DOLORPE RATING EL ULLA FEUGUE ...........................................9LOREM ULLAOR ILIT EXERO ............................................................................................9ALISMOD SECTE BLANDRE .........................................................................10ET, CONSEQUIPIT NULLAM ALIS NUM IN UTAT ..............................................................10VEL DOLUPTAT. .............................................................................................................10PUTE MOD EXMINIBH AUTEM .......................................................................................10DO AUGAIT EUGAIT ...................................................................................11OSTO DOLORE VER IUSCI TAT VELIT AM NIT ...................................................................11FEU FACI ETUEROS NIM VOLOBOR ................................................................................11ED ELIQUIP ISMODOL ...................................................................................................12LIT NIAM ..................................................................................................13SERATUAM IUS PRICA ...................................................................................................13SERES NORUM MED ECONSUS INAM .............................................................................13

TOLEO LA KILA WIKI ISNN: Toleo la MAJARIBIO 2 MACHI 13, 2017 BEI SH 800/- TU

ZAMAMPYA!Gazeti la Utetezi wa Fikra Mpya! Unachokijali Ndicho Tunachokijali...

RC MAKONDA AZIDI KUNG’ANG’ANIWA• Askofu Gwajima aongoza mashambulizi

• Adai jina lake la asili ni Daud Albert Bashite

MHARIRI: “Mabadiliko CCM Yamechelewa”Mkutano maalum utaonesha chama kinachojisahihisha au kilichopotea

Chama cha Mapinduzi

MAKAMPUNI YA UTALII

YAMUUNGA MKONO RC

SIMIYUNa. Mwandishi Wetu

KAMPUNI za kitalii zilizo chini ya Friedkin Conservation Fund (FCF) Tanzania iliyowekeza katika pori la Makao wilayani Meatu na Maswa Mkoani Simiyu imechan-gia mifuko 3000 ya saruji na ma-bati na 1000 kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani humo.

Misaada hiyo yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 70 imetolewa na kampuni hizo ikiwa ni kuunga mko-no mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli kuendeleza elimu ya hasa katika

INDEX

» Inaendelea UK. 6

» Inaendelea, UK. 2

SOFIA SIMBA ATIMULIWA CCM Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa

MIJADALA NA HOJA Uk. 6 MAKALA YA MWANAKIJIJI - “Wasiokubaliana na Magufuli CCM Wajiondoe Wenyewe?” Uk. 9

MICHEZO: Cameron Yanyakua Ubingwa AFCON’17 Uk. 14

MIKOANI: Madaktari wa Korea Wato Tiba SengeremaUk. 3

ALIYEKUWA MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake wa Tanza-nia (UWT) ambayo ni mojawapo ya jumuiya za Chama cha Map-induzi Bi. Sofia Simba ambaye pia alikuwa ni Mbunge wa viti maalum amefukuzwa uanachama wa chama hicho.

Taarifa za kufukuzwa kwake zime-tolewa siku ya Jumamosi kufuatia kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ambacho kilikaa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Rais John P. Magufuli.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Bw. Humphrey Polepole ilisema tu kuwa waliopewa adhabu mbalim-bali walipewa adhabu hizo sababu ya kukiuka maadili kinyuma na Ka-

tiba na Kanuni za chama cha map-induzi.

Sofia Simba alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa CCM ambao walikuwa wazi katika kumuunga mkono aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa ambaye jina lake lilikatwa wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2015.

Kikao cha Kamati Kuu ya CCM am-bacho kimefanyika Dodoma kime-kaa kama sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambao unaanza siku mbili zijazo na ambazo unatarajiwa ku-fanyia marekebisho makubwa ya Kikatiba ambayo yanadaiwa kuwa yanalengo la kukiimarisha chama zaidi.

Sofia Simba ameondolewa pamo-ja na kundi la viongozi wengine mbalimbali na wa ngazi mbalim-

bali za chama hicho ambao nao walikutwa na hatia katika makosa ya maadili dhidi yao.

Viongozi wengine wa CCM am-

bao wameondolewa, kushushwa vyeo au kufukuzwa uanachama ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar-es-Salaam Bw. Ra-madhan Rashid Madabida. We-

nyeviti wengine wa mikoa ambao wamefukuzwa uanachama ni pamoja na Jesca Msambatavangu

HABARI ZILIZOMO

Na. Tizzo Chuma

Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Sa-laam Bw. Paul Makonda (pichani)amejikuta aking’ang’aniwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii na nje ya mitandao hiyo akidaiwa kuwa katika safari yake ya elimu alikuwa ametumia vyeti ambavyo si vyake na kuwa jina analotumia si lake bali ni la mtu mwingine.

Tuhuma dhidi ya Makonda zil-ianza taratibu kama minong’ono wiki chache zilizopita hasa baada ya yeye Makonda kusimama na kuanza kutaja majina ya watu

ambao aliwatuhumu kuwa wa-najihusisha kwa namna moja au nyingine na biashara ya madawa ya kulevya Jijini Dar-es-Salaam.

Mmoja wa watu aliowataja kwenye ile iliyoitwa orodha yake na kumtaka afike kituo cha polisi cha Mkoa Jijini Dar (Police Central) ni mchungaji maarufu jijini Dar Bw. Josephat Gwajima wa kanisa la Uzima. Gwajima (pichani juu) alifika polisi na kuhojiwa na polisi kwa muda wa zaidi ya masaa 24 pamoja na kupekuliwa nyumbani kwake.

Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM kukata jina la Edward Lowassa mwaka 2015 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais

» inaendelea, UK. 3

Na. Dotto Kwilasa

MAKAO MAKUU, DODOMA

» Inaendelea, UK. 7

Chama cha Mapinduzi

kimeanza hatua za ku-

jisafisha na kusimamia

wanachama wake; kad-

haa wafukuzwa!

MAWASILIANO

MATANGAZO

OZ Media House

Gazeti la Zama Mpya

P. O. Box 90159

Dar es Salaam,

Tanzania

+255 746 202 000

Page 2: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

Na. Dotto Kwilasa

DODOMA - WAZIRI WA Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako (pichani juu) amewaa-giza wakuu wote wa vyuo nchini kuwat-ambua wanafunzi wanaojihusisha na matumizi ya dawa ya kulevya na kupeleka taarifa kwake .

Profesa Ndalichako ambaye pia ni mjumbe wa Tume ya Kuratibu uthibiti wa dawa za kulevya nchini, alitoa kauli mjini hapa jana wakati akifungua kikao cha kazi cha wakuu wa vyuo vya maendeleo ya Wananchi (FDCs) kilichofanyika katika ukumbi wa Veta mjini hapa.

“Vita hii ni ya kwetu sote hivyo hakiki-sheni taasisi zote zilizopo chini ya wizara ya Elimu mnashiriki katika mapambano hayo na kupinga vita matumizi madawa ya kulevya, kwani ni hatari sana kwa vi-jana ambao ndio wanaotegemewa katika taifa siku za usoni.

Alisema agizo hilo amelitoa kwa wakuu wa vyuo vyote nchini kuona kuwa wa-nakuwa makini kuhakikisha kuwa kwanza vyuo vyao havigeuzwi kuwa vijiwe vya watu wanaotumia madawa ya kulevya la-kini pili kuwatambua vijana wote wanao-soma katika vyuo vyao kama wanatumia madawa ya kulevya.

Mjumbe huyo alifafanua kuwa seri-kali imejiwekea malengo ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa kujenga viwanda na rasilimali kubwa wa-nayoitegemea ni vijana walioko mashule-ni, na kwamba kama juhudi za makusudi hazitafanyika katika kupambana na dawa ya kulevya malengo hayatafikiwa kamwe.

Waziri huyo alibainisha kuwa, vijana wengi waliopo vyuo vikuu wameharibiki-wa kutokana na madawa ya kulevya hivyo nguvu kubwa inahitajika katika mapam-bano hayo ili kulinusuru taifa kwa kuwa wizara hiyo ndiyo yenye dhamana kubwa ya kuhakikisha kuwa Tanzania ya viwanda inafikiwa.

Profesa Ndalichako, alisema katika mapambano hayo ni lazima kila mmoja ajitoe muhanga na kushiriki kikamilifu kwani vita hiyo sio lelemama.

Katika hatua nyingine Profesa Ndali-chako, aliuagiza uongozi wa vyuo vya maendeleo ya Wananchi kote nchini kuhakikisha vinajitangaza kwa jamii ili vi-onekane kuwa vipo kwani kwa sasa vyuo vingi havina wanafunzi wa kutosha.

“Kuna chuo kimoja kina mwanafuzni mmoja tu hiyo ni hatari kubwa, ili chuo chochote kitambulikane kuwa ni chuo ni

2 ZAMAMPYA Machi 13, 2017

DONDOO YA MABADILIKO YA

KATIBA YA CCM 2017 Mkutano Mkuu Maalum wa CCM umepitisha mabadiliko kadhaa katika Katiba ya CCM. Hii ni dondoo ya mabadiliko hayo.

Na. Mwandishi Wetu

DODOMA, Chama cha Mapinduzi katika Mkutano wake Maalum wa 2017 uliofanyika Dodoma siku ya Jumapili umepitisha mabadi-liko mbalimbali katika katiba yake. Baadhi ya mabadiliko hayo ambayo yatagusa viongozi wengi ndani ya chama ni haya. 1. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka mikoani watatoka kwenye mkoa badala ya kila wilaya ilivyo sasa. Kwa hiyo mkoa mmoja utakuwa na mjumbe mmoja wa NEC mmoja badala ya kila Wilaya. 2. Makatibu wa Fedha na Uchumi wamefutwa. 3. Makatibu Wasaidizi wamefutwa. 3. Wajumbe 2 wa kuchaguliwa kwenye Kamati za Siasa wameondolewa. 4. Shirikisho la Vyuo sasa litakuwa idara ya UVCCM. 5. Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi wamepungua hadi 24 kutoka 34. 6. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wamepungua hadi 163 kutoka 388. 7. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wamepungua hadi 1706 kutoka 2380. 8. Shina litakuwa na wanachama kuanzia 50 na tawi 250 hadi 1000 mjini na vijijini 150 hadi 1000. 9. Kura za maoni za wanaotaka kugombea Ubunge zitapigwa na Mkutano Mkuu wa Jimbo na kwa wale wanaotaka kugombea Udiwani zitapigwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kata na sio na wanachama wote kama awali na majina kabla ya kura za maoni yata-rudishwa na Kamati Kuu na baadae baada ya kura ya maoni NEC ndio itafanya uamuzi wa mwisho.

MAKONDA ANG’ANGANIWA TUHUMA ZA

KUFOJI VYETI

HABARI ZA KITAIFA

Christina ambaye alimtafutia vyeti vya kaka yake Paul Christian Muy-enge. Alichukua vyeti vya huyo bwana na kwenda kusomea Chuo cha Uvuvi Nyegezi. Gwajima alidai kuwa ana vyeti vyote vinavyoonesha kuwa Makonda alitumia vyeti vya mtu mwingine.

Hata hivyo, Makonda hadi gazeti hili linaenda mitamboni hajaweza kuanika wazi safari yake ya kielimu na kujibu tuhuma hizi ambazo zina-onekana kumshika vibaya.

Tangu kutolewa kwa tuhuma hizo Makonda ameendelea na kazi zake lakini pia kuzipuuzia mbali pamoja na kujitokeza mbele ya viongozi mbalimbali wa kidini ili wamuombee.

Hata hivyo Gwajima katika madai yake yale alionya kuwa suala la vyeti halali au vya kugushi haliwezi kuon-dolewa kwa kuombewa. “Vyeti feki huwa havisaliwi, huwezi kumwom-bea mtu mwenye cheti feki eti kiwe original. Maombi ya namna hiyo mimi sijawahi kuyaomba tangu kuza-liwa” alisema Mchungaji Gwajima.

Hata hivyo katika kuonesha kuwa jambo hili haliishi kirahisi rahisi siku ya Jumapili iliyopita Paul Makonda naye alienda tena kanisani ambapo pamoja na mengine alijaribu kue-lezea jinsi gani anapambana vita hivi na kuwa yote ni matokeo ya vita yake dhidi ya madawa ya kulevya.

Akizungumza katika Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Kimara Bw. Makonda amesema kuwa yote yanayotokea sasa hivi ni sehemu ya vita ambayo aliita ni ya “kiroho”. Makonda alizungumza kanisani hapo na kujaribu kutetea jitihada zake lakini bila kugusia wala kujibu tuhuma za kugushi vyeti zilizorushwa kwake na watu mbalim-bali akiwemo Mchungaji Gwajima.

Uchunguzi wa ZAMA MPYA una-onesha kuwa tatizo la watu kutumia vyeti vya watu wengine ama kwa ajili ya kupata elimu au kwa ajili ya kutafuta ajira nchini si tatizo dogo; ni tatizo kubwa na limedumu kwa muda mrefu na lina sura mbalimbali.

Tayari kwa miaka kadhaa sasa baadhi ya watu wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za kujipatia ajira kwa kutumia vyeti vya kufoji. Mifano ya hili iko mingi; huko Mara kwa mfano, mwaka 2014 wauguzi 6 walifukuzwa kazi baada ya kugundulika kuwa hawakuwa na elimu ya kidato cha nne bali walitumia vyeti vya kufoji kuonesha kuwa wamefikia elimu hiyo ilhali walikuwa wameishia da-rasa la saba tu.

Mwaka huo huo kwenye Chuo cha Polisi Moshi wanafunzi zaidi ya 200 waliachishwa mafunzo baada ya ku-gundulika kuwa walipata nafasi hizo kwa kutumia vyeti feki vya kidato cha nne.

Hadi hivi sasa Ikulu haijatoa neno lolote la kuonesha msimamo wake juu ya tuhuma zinazomkabili Paul Makonda. Siku ya Jumapili hiyo Makonda aliondoka kwenda Afrika ya kusini akiacha nyuma mwangwi mzito wa tuhuma dhidi yake.

lazima kiwe na idadi ya kutosha ya wana-funzi pamoja na idadi ya kutosha ya wana-funzi wanaochukua kozi husika sasa kama chuo kina mwananfunzi mmoja wewe mkuu wa chuo hapo una sifa gani za kuendelea kuitwa mkuu wa hicho chu, alisema Waziri na kumhoji mkuu wa chuo hicho ambacho hakukitaja jina.

Sambamba na hilo, alivitaka vyuo hivyo kujitangaza kwa jamii inayowazunguka na kutoa elimu kulingana na mahitaji ya jamii hizo kwa kuhamasisha maendeleo katika Nyanja mbalimbali za kilimo chenye tija, ufu-gaji na uvuvi ili kuhakikisha kuwa vyuo hivyo vinawanufaisha wananchi wenyewe.

“Wakuu hao wa vyuo kujadili katika kikao hicho mitaala ya mafunzo yanayotolewa ka-tika vyuo hivyo ambapo Wizara itayapokea mapendekezo na kuyafanyia kazi, lengo likiwa ni kuwawezesha hata vijana waliomal-iza elimu ya msingi kujiunga na vyuo hivyo tofauti na sasa ambapo wanaosoma ni watu wazima tuu,”alisema.

Awali, Kaimu mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, Mhandisi Thomas Katebalirwe aliiomba Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuwarudisha kazini wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Wananchi waliosimamishwa kazi ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kila siku.

“Kuna baadhi ya wakuu wao wa vyuo wali-simamishwa kazi kutokana na majungu tu kazini lakini walikuwa na malengo mazuri ya kuviendeleza vyuo walivyokuwa wanavisi-mamia hivyo aliomba mchakato wa kuwa-rudisha uharakishwe,”alisema.

Waziri huyo alieleza kuwa, vyuo vingi vya Maendeleo ya Wananchi vinakabiliwa na uchakavu wa miundombinu pamoja na vitendea kazi kwani vingi tangu vilipoanzish-wa mwaka 1975 havijawahi kufanyiwa ukarabati wala kuletewa vifaa vipya vya kujifunzia.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk.Leonard Akwilapo alivitaka vyuo hivyo kutoa elimu inayoendana na mahitaji ya dunia kwa sasa.

NDALICHAKO ATAKA VYUO KUTOA TAARIFA

ZA WANAFUNZI WANAOJIHUSISHA

NA MADAWA

Page 3: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

SOFIA SIMBA HABARI ZA TANZANIAMachi 13, 2017 ZAMAMPYA 3

(Iringa), Erasto Izengo Kwilasa (Shinyan-ga), na Christopher Sayna (mara).

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ambao wamepewa adhabu mbalim-bali ni pamoja na Ally Sumaye (Babati Mjini) - amefukuzwa uanachama, Mathias Manga (Arumeru) -amefukuzwa uana-chama, Ali Mchumo (Kilwa) -amepewa onyo kali, Ajili Kalolo (Tunduru) amevuli-wa uongozi, Hassan Mazala (Singida Mjini) -amevuliwa uongozi) na Valeria Buretta (Kibaha Vijijini) - amevuliwa uongozi.

Pamoja na hao wenyeviti wa CCM wa wila-ya mbalimbali nao wameadhibiwa kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Polepole. Vion-gozi waliovuliwa unachama ni pamoja na Omari Awadhi (Gairo), Ally Msuya (Babati Mjini), Makolo Laizer (Longido), Salum Madenge (Kinondoni), na Wilfred Mollel (Arusha Mjini).

Wailioondolewa kwenye uongozi wa wilaya ni pamjoa na Abeid Kiponza (Ir-inga Mjini), Assa Haroun (Ilala), na Hamisi Nguli (Singida Mjini. Muhaji Mushako wa Muleba amepewa onyo kali. Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kigoma Bi. Josephine Genzabuke amepewa onyo kali.

Mjumbe wa Kamati Kuu Bw. Emmanuel Nchimbi ambaye ni balozi wa Tanzania nchini Brazili amepewa onyo kali na am-etakiwa kuomba radhi. Nchini alikuwa ni miongoni mwa kundi la kina Sofia Simba ambalo lilikuwa limejiweka katika kambi ya Lowassa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Bw. Adam Kimbisa amesamehewa.

Taarifa hiyo ya Polepole hata hivyo haikue-lewa kila mmoja wa viongozi hao alikuwa anakabiliwa na tuhuma gani na ni juhudi gazi zilifanyika kuwapa nafasi ya kujitetea au kujieleza na kama yawezekana uamuzi wa kuwandoa ulichukuliwa bila ya kujali utetezi wao.

Wakati huo huo Wabunge watatu wa CCM walijikuta wakishikiliwa na polisi kwa muda mjini Dodoma katika kile amba-cho kilidaiwa na baadhi ya vyanzo kuwa walionekana kujipanga kuja na hoja am-bazo zingepingana na ajenda maalum za Mkutano Mkuu. Wabunge hao ni pamoja na Hussein Bashe (Nzega Mjini), Joseph Kasheku maarufu kama Msukuma (Geita Vijijini) na Adam Malima (Mkuranga).

Hata hivyo, wabunge hao waliachiliwa baada ya mahojiano na polisi kwa muda mfupi. Haijulikani kama ni kweli tuhuma dhidi yao zilikuwepo au walikamatwa kwa sababu nyingine.

Na. Dotto Kwillasa

DODOMA - JUMLA YA WATUMISHI 2059 wa serikali ya Muungano wameshahamia Makao Makuu ya Serikali mjini Dodoma hadi kufikia Ijumaa ya wiki iliyopita kutii agizo la Rais John Magufuli la kuhamishia serikali nzima Dodoma katika kutekeleza uamuzi wa zaidi ya miaka arobaini sasa wa kuhamishia makao makuu ya nchi mjini Dodoma.

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu Bw. Kassim Majaliwa siku ya IJumaa mjini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha mawaziri na manaibu waziri kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma chini ya uenyekiti wake.

Waziri Mkuu alitaka apewe taarifa na mawaziri wote juu ya utekelezaji wa agizo hilo la Rais na pia waeleze ofisi zao zipo wapi ili kwani amepanga kutembelea ofisi hizo siku za mbeleni.

Mawaziri wote walithibitisha kuwa wao wenyewe na viongozi wa juu wa wizara zao (wakiwemo Makatibu Wakuu) wame-shahamia Dodoma na kuwa watumishi wengine waliobakia watahamia mjini humo katika awamo nne zilizobakia kwa mujibu wa ratiba ya serikalil.

Kutekelezwa kwa sehemu tu ya agizo hilo ni mafanikio makubwa kwa serikali ya Ma-gufuli ambayo watu wengi hawakutarajia kuweza kufanyika hasa kwa vile kwa muda mrefu jambo hilo limeonekana ni kama mfupi uliomshinda fisi.

Katika ratiba ya kuhamia Dodoma ku-likuwa na hatua sita ambazo zilikuwa zimepangwa kutekelezwa hadi ifikapo Juni 2020 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano atatakiwa kuhama Dar-es-Salaam na kwenda Dodoma na hivyo ku-fanya Dodoma kuwa rasmi kama Makao Makuu ya nchi.

Katika hotuba yake ya kuahirisha Bunge kikao cha 4 cha Bunge la 11 Septemba 16 mwaka jana Waziri Mkuu Majaliwa alitan-gaza ratiba itakayofuatwa ili kuhakikisha kuwa serikali inahamia Dodoma katika utaratibu unaoeleweka na utakaotekelez-wa na watumishi wote wa umma.

Katika hatua ya kwanza, kati ya Sep-temba 1, 2016 na Februari 28, 2017 “Wa-ziri Mkuu na Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wote, Manaibu Makatibu Wakuu wote watahamia Dodoma katika Awamu ya Kwanza. Aidha, kila Wizara itatakiwa kuhamisha Watumishi wa Idara moja au mbili, na wakati huo huo kuendelea ku-weka utaratibu wa kupeleka Watumishi wa Idara nyingine kuhamia Dodoma”

Katika hatua ya pili ambayo itafanyika kati ya Machi 2017 na Augusti 2017 “Kip-indi hiki kitawapa fursa watendaji wa wiz-ara mbalimbali kuweka katika Bajeti zao za mwaka 2017/2018 gharama za kuen-delea kuhamisha watumishi wake kuja Dodoma.”

Hatua ya tatu ambayo itakuwa kati ya Septemba 2017 na Februari 2018 “Wizara zitaendelea na uhamishaji wa Watumishi wa Idara zilizo ndani ya Wizara.”

Katika hatua ya nne ambayo itakuwa ni kati ya Machi 18 na Augusti 2018 wizara zitaendelea kuhamishia watumishi wake mbalimbali Makao Makuu Dodoma.

Katika hatua ya tano ambayo itakuwa ni kati ya Septemba 2018 na Februari 2020 wizara zitaendelea kuhamishia wa-tumishi wake kwenda Dodoma.

Katika hatua ya mwisho Ofisi ya Rais ikiongozwa na Rais mwenyewe itaanza kuhamia Dodoma mwezi Machi 2020 na ifikapo Juni 2929 basi Ikulu ya Rais wa Tanzania itakuwa imehamia Dodoma na hivyo kukamilisha utaratibu wa serikali kuhamia Dodoma.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu Majali-wa aliwaataarifu waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa kikao hicho namna ambavyo Tume ya kuratibu udhibiti wa dawa za kulevya nchini inavyoendelea na utendaji wake wa kazi ambapo hadi ku-fikia siku hiyo ilikuwa imewatia mbaroni watuhumiwa 76 waliokutwa dawa za ku-levya aina ya heroin na cocaine.

Moja ya ajenda katika kikao hicho ili-kuwa ni mawaziri ambao ni wajumbe wa Tume hiyo kupokea taarifa ya kazi iliyok-wisha fanywa na katika kukabiliana na kukamata kwa dawa za kulevya tangu kuanza kazi kwa tume hiyo. Ajenda ny-ingine ni wizara zote kutoa taarifa na idadi ya watumishi waliohamia Dodoma kwa awamu ya kwanza kati ya watumishi wangapi waliopo kwenye Wizara na kue-leza wanadhani Wizara zao kwa mpango waliojiwekea watakamilisha lini kuhamia Dodoma na katika awamu ngapi kati ya awamu sita zilizopangwa.

Mbali na hayo aliitaja nyingine kuwa ni kupokea taarifa ya matumizi ya fedha na miradi ya maendeleo kwa mwezi Ju-

lai 2016 hadi Februari 2017 ajenda, ajenda mbayo haitajadiliwa kama mwanzo kwa kila wizara kutoa taarifa ya fedha iliyoingia na kazi zilizofanywa na badala yake watapata taarifa kutoka kwa Waziri wa Fedha na kila wizara itakwenda kufanya mapitio na kuji-weka vizuri.

Kuhusiana na vita dhidi ya madawa ya kulevya, Waziri mkuu ametoa taarifa ya mwenendo wa vita ya dawa za kulevya nchini, ambapo alisema Tume hiyo ilianza kazi Februari mwaka jana, na katika kipindi cha Julai 2016 hadi Januari 2017 jumla ya watuhumiwa 11503 wamekamatwa kwa ku-jihusisha na uzalishaji, uuzaji uzambazaji na utumiaji wa dawa hizo.

Majaliwa, alibainisha kuwa, kati ya watuhumiwa hao 11303, watuhumiwa 9811 walikutwa na kesi za kujibu huku 9174 wakitiwa hatiani baada ya kubaini kuhusika na makosa hayo. Wengine 238 hawakukutwa na hatia na hivyo kuachiliwa na mahakama huku wengine 478 upelelezi wa kesi zao uki-wa unaendelea.

Katika kikao hicho waziri mkuu aliwaagiza mawaziri wote ambao ni wajumbe wa baraza la tume ya kuratibu udhibiti wa dawa ya ku-levya nchini kushiriki kikamilifu katika vita hiyo huku akiwakabidhi namba ya kamishina wa dawa za kulevya aliyeteuliwa na Rais hivi karibuni Bw. Rogers Sianga ili waweze kump-atia taarifa mara wanapokutana na matukio yanayohusiana na dawa za kulevya.

“Taarifa hii imehusisha dawa za viwandani pekee bila kuhusisha bangi na mirungi huku akipongeza mapambano yanayofanywa ka-tika mikoa yote juu ya vita hiyo pamoja na kuwataka wananchi kuendelea kutoa ush-irikiano kwa mamlaka zote zinazohusika bila woga,”alisema.

Kuhusu pombe haramu na pombe zinazo-fungashwa kwenye vifungashio vya plastiki maarufu kama viroba waziri mkuu alisema, msako wa kuondoa bidhaa hizo ambazo zili-kuwa zikihatarisha ustawi wa taifa unaende-lea.

Alisema katika msako huo walibaini ku-wepo kwa kwa makampuni yanayozalisha pombe hizo bila vibali huku wengine waki-weka pombe haramu ya gongo kwenye vi-roba hivyo.

TUNDU LISSU AACHI-WA, AKAMATWA TENANa. Mwandishi Wetu

Mbunge wa Singida Mashariki Bw. Tundu Lissu kwa mara nyingine tena amejikuta akiwekwa mikononi mwa polisi kwa masaa machache mara tu baada ya kuachiwa na

» Inaendelea, UK. 5

WAZIRI MKUU: MAWAZIRI WAHAMIA DODOMA•Serikaliyapigamarufukuviroba

•Vitayamadawayakulevyayapambamoto

Page 4: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

4 ZAMAMPYA Machi 13, 2017

Waliomuua Mdogo wa Rais wa Korea Kaskazini Kupandishwa KizimbaniKim Jong Nam aliuawa kwa kugusishwa na sumu ya VX

Mwandishi Wetu

KUALA LUMPUR, (UPI) Maafisa wa usalama wa Malaysia wamesema kuwa mdogo wa rais wa Korea ya Kaskazini ambaye aliuawa Februari 13 kwa kushambuliwa na kina dada wawili ambao walikuwa wamejipaka sumu kali mikononi aliuawa akiwa na maumivu makali sana kutoka na sumu hiyo. Kim Jong Nam (45) ambaye ni mkubwa kwa Rais wa Korea ya Kaskini kwa mama mwingine alipakwa usoni na sumu ya VX (never agent) ambayo inashambulia ubongo wakati akijiandaa kuingia kwenye ndege kwenye uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur. Uchunguzi wa kitabibu wa mwili wake umeonesha kuwa sumu aliyopakwa nayo Kim ilichukua kati ya dakika 15-20 tangu ilipoanza kuingia mwilini kupitia ngozi hadi iliposababisha mauti. Kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa Malaysia Subramaniam Sathasivam hakuna kinga yeyote ambayo ingeweza kuondoa madhara ya sumu hiyo. Kina dada hao mmoja raia wa Singapore na mwingine wa Vietnam wamesema baada ya kukamatwa kuwa walikuwa wanaamini wanashiriki katika mcheto wa mzaha kwenye televisheni na walilipwa kama dola 80 kila mmoja ili kushiriki. Hata hivyo, polisi wanatilia mashaka maelezo hayo ya kina mama hao na wanaendelea kuwashirikia baadhi ya watu huku wengine wakiende-lea kutafutwa miongoni mwao akiwemo afisa wa ubalozi wa Korea ya Kaskani nchini Malaysia. Kina dada hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa mauaji ya Kim na kwa mujibu wa mwendesha mashtaka endapo watakutwa na hatia basi watahukumiwa kunyongwa. Sumu ya VX imepigwa marufuku duniani na ni miongoni mwa sumu zinachukuliwa kama silaha kikemia ambazo ni za maanga-mizi ya halaiki (weapons of mass destruc-tion) na nyingi zimepiga marufuku. Korea ya Kaskazini haijatia saini mkataba wa

kuzuia Silaha za Kikemikali (Chemical Weap-ons Convention) wa 1993.

Kina Obama Kulipwa Dola Milioni 60 Kuandika Kitabu

Kiasi kikubwa zaidi kwa mwandishi wa kitabu kulipwa

Mwandishi Wetu

RAIS MSTAAFU wa Marekani Bw. Barack Obama na mkewe Bi. Michelle Obama wame-ingia mkataba wa dola milioni 60 sawa na shilingi bilioni 134 hivi) ambapo wenza hao wataandika kitabu juu ya maisha yao katika miaka nane ambapo Obama alikuwa Rais wa Marekani.Kwa mujibu wa gazeti la New York Times la Marekani baada ya mashindano ya kumpata Obama kuandika kitabu makampuni kadhaa ya vitabu yalifikia kiasi hicho cha fedha ambapo kampuni ya Penguin Random House iliwashinda wapinzani wake. Ni kampuni hiyo hiyo ndiyo iliyochapisha vitabu vitatu vya zamani vya Obama na hivyo kuonekana kuwa na nafasi ya kushinda tenda hiyo.

Obama aliandika kitabu cha Dreams from my Father (Ndoto Kutoka kwa Baba Yangu) mwaka 2004 na baadaye akaandika kitabu cha The Audacity of Hope (Uthubutu wa Matumaini) mwaka 2006. Mwaka 2010 akiwa Rais wa Marekani aliandika kitabu cha watoto kiitwacho Of Thee I sing (Juu Yako Nakuimba). Vitabu vyote hivyo katika miaka 11 iliyopita vimemuingizia Obama dola milioni 15. Hata hivyo, mapato ya kitabu cha watoto alitoa

HABARI ZA KIMATAIFA136 Washirikiwa A.Kusini kwa Kuwapiga Wageni Makundi ya vijana yamekuwa kishambulia wahamiaji wa kigeni kutoka nchi za Kiafrika

Mwandishi Wetu

PRETORIA, AFRIKA YA KUSINI, (ZAMA-MPYA) Watu zaidi 136 wanashirikiwa nchini Afrika ya Kusini kufuatia kuibuka tena kwa wimbi la kuwapiga na kuwatesa wahamiaji wa kigeni kutoka nchi za Kiafrika ambako kumesababisha wengi wao kupigwa, kuharibiwa mali zao na maisha yao kuwa mashakakani. Kama ilivyotokea mwaka 2008 matukio ya mashambulizi dhidi ya wahamiaji wa kigeni kutoka nchi za Kiafri-ka yamejirudia wiki chache zilizopita na yameendelea katika miji mbalimbali iki-wemo Pretoria, Johannesburg, na Durban.

Matukio hayo yamekuwa yakifanywa na vijana wa Afrika ya Kusini ambao wanaona kuwa wahamiaji hao wanaotoka katika nchi mbalimbali za Kiafrika hasa Nigeria, Zimba-bwe, na Somalia wanachukua kazi ambazo zingeweza kufanywa na wananchi hao. Hali ya ajira nchini ya Afrika ya Kusini inaonesha kuwa zaidi ya asilimia 25 ya wananchi wake

hawana ajira na hilo limechangia hisia ya kuona kuwa wageni wanachukua kazi hizo.

Kwa upande wake serikali ya Afrika ya Kusini kupitia Waziri wake wa Mambo ya Ndani Bw. Malusi Gigaba imetoa maelekezo makali kwa waajiri mbalimbali kuhakikisha kuwa wanaajiri raia wa Afrika ya Kusini na kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya waa-jiri ambao wanaajiri wageni bila taratibu au vibali maalum.

Katika matukio ya 2008 wageni wapatao 60 waliuawa kufuatia mashambulizi dhidi ya wahamiaji wa kigeni. Matukio ya 2015 yaliacha wageni 6 wameuawa huko Durban kufuatia mashambulizi kama haya yanayo-endelea sasa.

Safari hii hata hivyo inaonekana masham-bulizi yamewalenga kwa namna ya pekee wahamiaji kutoka Nigeria kitu ambacho kinazidi kuongeza msuguano kati ya nchi hizo zenye nguvu zaidi ya kiuchumi katika Afrika. Wanigeria kwa upande wao – kama walivyo Waafrika wengine – wanaona kuwa Waafrika ya Kusini ni watu wasio na shukra-ni hasa kwa vile nchi nyingi ambazo raia wao wanalaumiwa kwa kuuza madawa na kuchukua kazi mbalimbali ndizo zilijitolea sana wakati wa kupigania haki za weusi.

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi la Nigeria (TCU) limetaka serikali ya nchi hiyo kufanya utaratibu wa kuwaondoa Wanige-ria wanaoteseka au kudhulumiwa kuon-doka Afrika ya Kusini. “Kinachoshangaza ni kuwa ni wazungu ambao ni asilimia 8 tu ya wananchi wa Afrika ya Kusini ambao wanamiliki asilimia 35 ya utajiri wa Afrika ya Kusini lakini ni hawa weusi wenzao ndio wanachukuliwa kama maadui wao” lime-sema tamko la shirikisho hilo.

Page 5: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

Machi 13, 2017 ZAMAMPYA 5

HABARI ZA TANZANIA« TAIFA: TUNDU LISSU AACHIWA, AKAMATWA TENA

mahakama katika kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa upinzani Bungeni (Minority whip) na mwa-nasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anakabiliwa na mlolongo wa mashtaka mbalimbali ambayo yanahusiana na harakati zake za kisiasa. Baa-dhi ya mashtaka hayo yanatokana na kauli zake mbalimbali ambazo vyombo vya dola vimekuwa vikidai ni za kichochezi.

Tangu kuingia kwa utawala wa Rais Magu-fuli kufuatia uchaguzi mkuu wa 2015 Tundu Lissu amejikuta miongoni mwa wanasiasa ambao wamekuwa wakipaza sauti za ukosoa-ji wa serikali ya awamu ya tano na hivyo mara kadhaa kujikuta kwenye matatizo.

Hata hivyo safari hii baada ya kuachiwa ku-kamatwa kwake kumehusishwa na baadhi ya wachambuzi wa kisiasa kuwa kunahusiana na nia yake ya kugombea kuongoza chama cha mawakili cha Tanganyika (Tanganyika Law Society) kitu ambacho serikali kupitia Waziri wa Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe imepin-ga vikali.

Baada ya Tundu Lissu kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo pamoja na Lawrence Masha ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mam-bo ya Ndani ya Nchi na baadaye kuhama CCM na kujiunga CHADEMA kuelekea uchaguzi wa 2015 kunaonekana kutokukubalika na vion-gozi serikalini.

Siku ya Jumamosi iliyopita uongozi wa TLS ukiongozwa na rais wa sasa wa chama hicho Bw. John Seka ulimtembelea Waziri Mwaky-embe huko Dodoma ili kupata ufafanuzi la-kini msimamo wa Mwakyembe ni kuwa TLS haitoachwa kutumiwa na wanasiasa.

Katikati ya mwezi wa pili mara tu baada ya Tundu Lissu kuchukua fomu za kugombea urais wa TLS Waziri Mwakyembe alitoa onyo kwa viongozi waliomtembelea Dar-es-Sa-laam wakati ule na kuwaambia kuwa “Ikiwa TLS sasa inajiona imekua kiasi cha kutosha na sasa inataka iingie kwenye majukumu ya ziada ya uanaharakati wa kisiasa, Serikali hai-tasita kuifuta sheria iliyoanzisha TLS ili chama hicho kijisajili chini ya Sheria ya Vyama kama NGOs zingine nchini au ikiwezekana chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa kama vyama vingine vya siasa nchini”

Hata hivyo, misimamo ya taasisi mbalimbali na wadau mbalimbali ni kuwa TLS ina haki ya kuchagua mtu anayekidhi vigezo vya uon-gozi bila kujali kama mtu huyo ana nafasi ny-ingine ya kisiasa. Uchaguzi wa TLS unafanyika wiki ijayo tarehe kumi na tatu na hadi hivi sasa tayari kampeni mbalimbali zimekuwa zikifanyika miongoni mwa wanasheria.

Ni wazi endapo Tundu Lissu atashinda kutakuwa na mgongano na serikali. Tayari Lissu mwenyewe amekuwa akiandika kwenye mitandao ya kijamii hofu yake kuwa inaweze-kana akaswekwa ndani kabla ya uchaguzi

huo ili kuzuia wajumbe kumpigia kura. Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo ndani ya TLS hakuna kanuni inayomtaka mtu anayegombea nafasi ya uongozi ndani ya chama hicho lazima awe ndani ya ukumbi wa kupigia kura ili aweze kuchaguliwa.

Wakati huo huo, Mbunge wa Arusha Mjini Bw. Godbless Lema ameruhusiwa kutoka rumande baada ya kukaa huko kwa takribani miezi minne baada ya maombi yake ya dhamana kukubaliwa na mahakama.

Lema anakabiliwa na kesi ya uchochezi ambayo inatokana na ndoto aliyoota. Mwaka jana Lema alidai kuoteshwa ndoto kuwa endapo Rais Magufuli “hatojirekebi-sha” basi hatofika 2020. Kauli hiyo ilim-letea matatizo na kusababisha awekwe ndani na kunyimwa dhamana.

Hata hivyo, kinyume na matarajio ya wengi badala ya kuachiliwa kwa dhamana kwa haraka Lema alijikuta akisota jela kwa karibu miezi hii minne wakati mawakili wake na wale wa serikali wakishindana juu ya upatikanaji wa dhamana.

Katika hotuba yake siku ya Ijumaa ikiwa ni ya kwanza tangu kutoka jela Lema ali-zungumzia zaidi hali ya wale aliowakuta gerezani na aliahidi kuendelea kutetea maslahi yao. Kesi Lema na kesi nyingine mbalimbali zinazowakabili wanasiasa (hasa wa upinzani) na zile zinazohusiana na haki ya maoni zinaendelea kusikilizwa katika mahakama mbalimbali nchini.

Page 6: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

6 ZAMAMPYA Machi 10, 2017

Na. Ebbie Mkandara

Toleo la leo latugusa sote katika kufanya tathimini juu ya Mustakabali wa taifa letu. Mengi sana yameandikwa na kusemwa kuhusiana na uongozi wa serikali hii ya Awamu ya tano. Lakini pamoja ya yote si-jasikia wala kusoma andiko linalowahusu wananchi ambao wao ndio waloyataka mabadiliko kumchagua rais Magufuli na Chama cha CCM kuwaongoza, leo tu-nashuhudia mabadiliko waloahidiwa ya-kitimizwa ghafla imekuwa kisebusebu na Kiroho papo. (Refusing and wanting at the same time)

Hakuna ukweli wowote kwamba mabadi-liko tuloyataka wala tuloahidiwa sio haya ikiwa tunaitumikia katiba ile ile na tume-kichagua chama kile kile kuunda serikali halafu tutegemee mabadiliko tofauti yato-kane na Uongozi wake ambao utawajibika ndani ya katiba tulikuwa nayo.

Laukama tungependa mabadiliko tofauti basi bila shaka CCM isingekuwepo madara-kani. Na maadam wananchi wengi waliich-agua CCM wakaamini mabadiliko yataletwa na rais huyu chini ya ilani ya CCM, kwa nini tunapinga mabadiliko tuloyavulia nguo leo tunaogopa hata kuyakoga!

Waswahili husema – Hila ya Kikwapa ku-nuka pasipo kidonda! Tanzania yetu kwa ujumla inanuka Rushwa, inanuka Ufisadi, inanuka Uadilifu, inanuka hadhi zote za kutokuwa na UTU na Uzalendo, na mchan-ganyiko wa harufu zote hizi nani atakaye weza kuzivumilia?

Haya mazoea yetu ya kunuka kwapa tu-napoambiwa tunanuka kwa nini tumeku-wa wepesi sana wa kuchukia. Maana kwa kawaida ya mtu mwenye kasoro ya kunuka kikwapa huwa hakuna njia nyepesi ya kum-taarifu. Jiulizeni, utaweza vipi kumwam-bia mtu ananuka kikwapa? Kama huwezi basi kinachobakia aidha kuvumiliana ama kutengana! Lipi jepesi kwenu?

Na amletaye Nyoka nyumbani akili zake hazimo kichwani. Maana haiwezekani wa-nanchi tumemchagua wenyewe Magufuli ambaye tulimjua wazi kabisa ni mtu wa aina gani, mwenye sifa na uwezo gani aje ku-pambana na watu wa aina gani halafu leo tumegeuka na kushangazwa wakati haya ndio tuloyaomba na Mwenyezi Mungu ka-sikia vilio na dua zetu tukapewa kiongozi wa aina hiyo na hakuna maajabu ya Mussa wala Firauni ya kujiridhisha ati Magufuli an-gekuwa kiongozi wa aina tofauti. Jamani Sharubu za Paka kazaliwa nazo!

Hakika kwa Mwendawazimu ameingia Mlevi, kwa maana ada yetu sisi wananchi imekuwa kuvumiliana hata kwa harufu za Ufisadi, kazi kulalamika na Serikali in-ayochukua hatua kali kupiga vita kundi la wananchi wanaonuka Ufisadi wakitumia silaha ya Utajiri (FEDHA) kuwa ndio msingi wa Maendeleo badala ya fedha kuwa ma-tokeo ya maendeleo. Yamkiniki wananchi asilimia kubwa masikini hawana mtaji wa fedha iweje wategemee maendeleo yato-kane na Utajiri? Ama kweli Fedha sabuni ya roho na mapenzi ya roho hugeuza harufu kuwa utuli wa kufukizwa.

Miaka ya nyuma kabla rais Magufuli ku-ingia Ikulu tuliomba na kulia na viongozi walopita kwa kutambua Urasimu na Ufisa-di mkubwa wa Serikali na Watumishi wa Umma, na sisi wenyewe tukipiga kelele na mayowe juu ya kukosekana kwa UADILIFU, UWAJIBIKAJI, UZALENDO na UWAZI maana haya ndio yalokuwa mapungufu makubwa tuloyaona sisi kwa ujumla. Tena tuliomba ikiwezekana tupate kiongozi Dikteta am-baye pekee ataweza kupambana na marad-hi haya yalohitaji Upasuaji tukiamini Ufisadi hauwezi kuondoka pasipo sharia na vita kali ya dhidi ya wadhalimu.

Yawezekana kabisa rais Magufuli ana ma-pungufu yake na mengi tu, yeye sii malaika ni binadamu na pengine serikali yake hu-fanya makosa ya Utekelezaji katika kupam-bana na Ufisadi (Uhalifu) kwa matumizi ya Amri za kimamlaka alopewa lakini haipen-dezi kama tunashindwa kupambanua ma-pungufu hayo, nini kifanyike, hatua gani zichukuliwe katika kuhakikisha Ufanisi un-apatikana kwa njia maridhawa zenye kutu-kuzwa. Kukosoana ndio Uungawana na sii matumizi ya siasa kutumia lugha za dharau na kejeri kana kwamba tuna mashindano ya ngojela na mipasho kugombania umas-kini, Haipendezi.

Hutuwezi kupambana na changamoto za ukombozi wa Mtanzania kiuchumi ikiwa kuna Uhasama baina yetu, Watanzania leo tumegawanyika kwa makundi ya kinafiki kwani kazi kubwa ya Ukoloni Mamboleo ni kutugawa wananchi wakundi tusielewane. Kupambana na Uchumi Tegemezi haitokani na rais wala Serikali pekee bali ni Mjumuiko wa sisi sote wananchi pamoja na Umoja wetu kwa ari ya kuyapata mageuzi hayo na sio ya Kisiasa kulishana ngada.

Na inapofikia kwamba sisi wananchi wa-tendaji ndio tumegeuzwa mateja wa ki-siasa tukasahau wajibu wetu, kuna hatari kubwa ya kupoteza hata UTU wetu. Hakuna Elevi mbaya kama kulishwa sana siasa za uongo, hugeuka Hila ya kwapa kunuka bila

Kidonda. Tunaweza kabisa kuvumiliana, kusahihishana pasipo matamshi ya kukata tamaa kama Taifa na maisha yakaendelea. Siasa za Ukinzani hufikia matusi na un-apomwambia mtu hata iwe kwa nia njema kabisa ananuka kikwapa, sii rahisi akakuba-li ana kasoro hiyo bali atachukulia kuwa ni dharau na matusi ya nguoni.

Imekuwa kama hatuna utamaduni wa ku-kosoana bali kudhalilishana kwa sababu imani na elimu yetu dhaifu. Hatuna uta-maduni wa kukemeana isipokuwa watoto wadogo maana mila na desturi zetu zinatu-funga katika kuamini mkubwa hakosei - Uzee ni hekima na busara na hizi ndio tunu zilotujenga ndani ya umaskini na utumwa wa fikra. Sasa Ifike mahala tujadili maswala kwa kutambua kwanza udhaifu wetu kama Taifa. Ni yapi yalotusibu hadi sasa nitaiweka bayana yale yalotufikia hapa tulipo na tu-mekosea wapi.

MAAZIMIO – DECLARATION

Yabidi tujiulize dhana kuu ya Uhuru wetu ilikuwa nini? Je, Tuliutaka Uhuru kwa sa-babu gani? Nini haswa malengo ya kuutaka Uhuru wetu ikiwa leo baada ya miaka 56 bado kuna wajanja wachache ndio wa-namiliki Uchumi wa nchi hii tena kwa njia zisizo halali?

Toka tupate Uhuru ni Mazimio gani tulowe-ka kufikia Uhuru kamili? Ni mabadiliko gani yalopatikana toka Uchumi wa Kutawaliwa hadi Uchumi unaomilikiwa na Wananchi ikiwa KUTOTAWALIWA KIUCHUMI ndio ad-hima ya Uhuru tuloutaka!.

Baada ya Utawala wa Mwalimu Nyerere na kubadilisha gia hewani, tumekuwa Taifa lisilokuwa na malengo, halina dira, halina Maazimio zaidi ya dhana na tunzi mufisili za kujikomboa Kiuchumi pasipo mwongozo wetu sisi wenyewe kulingana na uwezo na mazingira yetu - HATUNA.

Maana sikumbuki leo hii Watanzania wa-natumikia Azimio gani lilowekwa na ku-tungiwa sera za kisheria ili kufikia malengo yake kama tulivyounda Azimio la Arusha, La Musoma na kadhalika na yote yakapewa sharia na mwongozo Kitaifa. Leo hii hatuna mwongozo bali tunayo malengo ya Mille-nium tulopangiwa na wahisani - KOSA.

MIGOGORO YA KISIASA - POLITICAL INSTA-BILITY

Kabla taifa hatujajizatiti vizuri kwa misngi ya Kiuchumi tukafungashiwa ngada la De-mokrasia kuwa mbele ya ukombozi wetu KIUCHUMI. Bwawa limeingia Ruba, na kwa miaka 26 sasa ugomvi wetu mkubwa Kitai-

« MHARIRI: Mabadiliko CCM Yamechelewakinatarajiwa kuwa na mkutano wako Maalum wiki ijayo mjini Dodoma. Mkutano huo maalum wa Chama cha Mapinduzi unatarajiwa kufanyia mabadiliko makubwa katika Katiba ya chama hicho na hivyo kutoa mwelekeo mpya wa chama hicho chini ya uongozi wa mwenyekiti wake ambaye ni Rais wa Jamhuri y a Muungano Dkt. John Magufuli.

Kwa muda mrefu CCM kimekuwa kikiongozwa na Katiba ambayo bado inabeba masalia ya fikra za kisiasa za wakati wa mfumo wa chama kimoja na hivyo kujikuta kikiwa katika kiza cha kutoonesha mweleko mzuri wa kisiasa.

Matokao ya mfumo wake huo uliodumu

muda mrefu yalijitokeza sana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa 2015 ambapo tuliweza kuona jinsi gani kama chama hakikuwa bado na mifumo mizuri ya kuchuja wagombea wake, na kusimamia wanachama wake kiasi kwamba, tuhuma na shutma mbalimbali zilikuwa zinarushwa toka upande mmoja kwenda mwingine.

Kama chama tawala ni muhim,u kwa chama cha mapinduzi kujionesha kuwa ni chama ambacho kinaweza kujiangalia, kujitathmini, kujisahihisha na kujipa mwelekeo mpya wa kiuongozi.

Baadhi ya matatizo ambayo yalitajwa na Rais Magufuli mara baada ya kutangazwa

mshindi kufuatia uchaguzi mkuu wa 2015 pale makao makuu madogo ya chama Lumumba Jijini Dar-es-Salaam yangeweza kuepukika kabisa endapo katiba ya chama ingekuwa imetengenezwa kwa kuhakikisha kuwa mifumo mbalimbali ya chama inafanya kazi vizuri ya kusimamia nidhamu na taratibu vizuri.

Hata fukuza fukuza ambayo tumeiona ikitokea baadaye kufuatia tuhuma dhidi ya wanachama (viongozi na wasio viongozi) ingeweza kuepukika mapema kama chama kingekuwa kimebuni mifumo mizuri ya kusimamia kampeni za wagombea wake kuanzia wakati wa kura za maoni

EBBIE MKANDARA - HILA ZA KIKWAPA KUNUKA PASI YA KIDONDA

» Inaendelea, UK. 7

Page 7: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

Machi 10, 2017 ZAMAMPYA 7

vyake – na kusema kuwa “(Obama na Mkewe) kwa maneno na uongozi wao wamebadilisha dunia na sisi kila siku katika vitabu tunavyochapisha hapa Penguin Random House tunajitahidi kufanya vivyo hivyo”. Kampuni ya Penguin inatarajia kutoa mchango wa dola milioni moja kwa taasisi za misaada kwa niaba ya Rais Obama. Hata hivyo tarehe ya kuzinduliwa kwa vitabu hivyo bado haijawekwa. .

za ndani ya chama na hata katika ule mchakato wa kutafuta wadhamini.

Wengi tunakumbuka jinsi mfumo wa kutafuta wadhamini wa nafasi ya urais ulivyokuwa una mwamko wake lakini pia uliokuwa unaonesha ni jinsi gani mtu mmoja anaweza kuwa na nguvu ya kukitikisa chama lakini pia mtu huyo huyo kutokupewa nafasi ya kushinda kwa sababu mifumo ya chama haikuweza kumruhusu kwa hofu yeyote ambayo watu walikuwa nayo.

Ni wazi basi mkutano huu mkuu maalum ni lazima utumiwe kama nafasi ya chama kujisahishisha vinginevyo, nafasi hii inaweza kuwa ni nafasi ya mwisho kwa CCM kujichunguza na kujisahihisha kwani, hata mtu kukosea anaweza kukosoea kwa kiasi tu lakini mwisho wa siku watu watatambua kuwa mtu huyo hawezi kujisahihisha.

CCM inapaswa kuonesha uwezo wa kujisahihisha na hivyo kuwa somo kwa vyama vingine vya kisiasa nchini ambavyo navyo vina matatizo yao mbalimbali na havijachukua hatua makini za kujisahihisha.

.

KIMATAIFA: OBAMA

« MHARIRI: Kwa Hili CCM Ibebe Lawama Kubwa Zaidi

kwa shirika la hisani linalomilikiwa na Pen-guin Random House. Kina Obama wanaingia na kuweka rekodi ya kiasi kikubwa cha fedha ambacho mtu amewahi kulipwa kwa kuandika na ni kiasi cha juu kuliko marais wengine wote waliom-tangulia. Rais Bill Clinton alilipwa milioni 15 alipoandika kitabu cha My Life (Maisha Yangu) wakati mke wake Bi. Hillary Clinton alilipwa dola milioni 14 kwa kitabu chake cha Hard Choices (Maamuzi Magumu). Rais George W. Bush alilipwa dola milioni 10 kwa kitabu chake cha Decision Points (Nukta za Maamuzi). Afisa Mtendaji wa Penguin Random House Bw. Markus Dohle amethibitisha mkataba huo – bila kuingilia kwa undani vipengele

« MAKAMPUNI YA UTALII SIMIYU , kutoka Uk.1 maeneo ya wafugaji ambako kampuni hizo zinafanya shughuli za uwindaji wa kitalii.

Kampuni zilizokabidhi misaada hiyo juzi katika sherehe zilizofanyika mjini hapa ni pamoja na Mwiba Holdings na Tanzania Game Trackers ambazo kwa pamoja zimetoa saruji hiyo ye-nye thamani ya sh milioni 48 na ma-bati yakiwa na thamani ya sh milioni 25.

Vifaa hivyo vya ujenzi vitatumika ku-jenga vyumba vya madarasa na mabweni kwa ajili ya shule zitakazotumiwa na wato-to wa jamii za wafugaji zinazoishi jirani na maeneo ya shughuli za uwindaji wa kitalii wilayani Meatu katika mkoa wa Simiyu

Akizungumza kabla ya kumkabidhi mchango huo Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, wakati wa hafla iliyo-fanyikia katika viwanja vya stendi Mjini Mwanhnuzi, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Abdulkadir Mohamed alisema kuwa mchango huo unatokana na kuanzishwa kwa mfuko uwekezaji katika pori hilo.

‘’ Tunatoa msaada huo ikiwa ni kuun-ga mkono Serikali yetu ya awamu ya tano katika jitihada za kuimarisha sekta ya elimu nchini,na tumeanza kuwa-saidia wananchi tunaoshirikiana nao katika shughuli za uhifadhi na huu ndio mwanzo wa kuendeleza ushirikiano huu ikiwa ni sehemu ya mchango wetu kwa jamii,” alisisitiza Mkurugenzi huyo

Alisema kuwa pamoja na kuchan-gia misaada hiyo,kampuni yake ime-kuwa ikitoa misaada katika vijiji tisa vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi za Wanyama Pori Makao (WMA) na ranchi ya Mwiba hasa katika kusaidia ubore-shaji wa huduma za jamii na hasa elimu.

“ Mpaka sasa Kampuni kupitia makam-

puni yake matatu tayari wamechangia kiasi cha sh Milioni 3000 kwa vijiji tisa pamoja na vingine 15 vinavyopakana pori hilo, ambapo shule, zahanati, pamoja na vituo vya maende-leo vimejsengwa katika vijiji hivyo kwa kush-irikiana na halmashauri” Alisema Mohamed

Aidha, aliongeza kuwa mchango huo umechangiwa na mafanikio mazuri ya shu-ghuli za utalii zinazoendelea katika maeneo hayo na uwekezaji wa kampuni hiyo wilayani humo, huku akibainisha kuwa shughuli hizo zinazidi kupanda kila mwaka wilayani humo

Mkurugenzi huyo aliahidi kuwa kutokana na kuimarika kwa shughuli hizo na kuwepo kwa mazingira mazuri ya uwekezaji,hasa ushirikiano wanaoupata kutoka kwa wa-nanchi, hasa wavijiji vinavyopakana na pori hilo, wamepanga kuongeza uwekezaji wao kwa dola za kimarekani milioni 100.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalum Mkoa (CCM) Leah Komanya alipongeza mchango wa mwekezaji huyo, huku akiunga mkono kwa kuchangia mabati 50 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni shule ya sekondari Makao.

“ niwaombe hawa wawekezaji wetu wa-sichangie kwenye vijiji hivyo tisa peke yake, bali wachangie hata kwenye kata nyingine za wilaya yetu ambayo ipo chini sana kielimu ili kila mwananchi atambue mchango wao, na niwapongeze kwa kuun-ga mkono ujenzi wa shule hasa mabweni kwa watoto wa kike” Alisema Komanya

Mkuu wa mkoa wa Simiyu,akizungumza kabla ya kupokea msaada huo, alimtaka Mku-rugenzi huyo ambao alidai kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro ya kila mara kati ya wa-nanchi na kampuni hiyo ili kurejesha imani ya kuendelea kushirikiana na wawekezaji hao.

Mbali na hilo Mtaka alipongeza Kampuni hiyo kwa mchango wake, huku akielele-keza saruji hiyo pamoja na mabati vitumike kwa ajili ya kujenga mabweni katika shule za sekondari zinazopakana na pori hilo.

Mtaka aliwataka wawekezaji hao kuwa kari-bu na wananchi kwa kushirikiana na watend-aji wa halmashauri na alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo ku-wapatia kiwanja cha kujenga ofisi ili iweze kura-tibu kwa karibu ushirikiano huo na wananchi.

Page 8: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

8 ZAMAMPYA Machi 13, 2017

MAISHA NA JAMIIW/Mitaa Waidai Halmashauri Milioni 180 DodomaWatoa malalamiko mbele ya Mkuu wa Wilaya

Na. Mwandishi Wetu

DODOMA - Wenyeviti wa mitaa katika Hal-mashauri ya Manispaa ya Dodoma wame-toa malalamiko yao kwa mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mdeme kwa kutolipwa posho zao za miezi 8 na halmashauri hiyo wanayoidai jumla ya sh.milioni 180.

Hayo yalielezwa na Hellena Matonya ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Math-ias kata ya Miyuji Manispaa ya Dodoma kwaniaba ya wenyeviti .

Hellena alitoa malalamiko hayo katika kikao kilichoitishwa na Mkuu wa wilaya ya Dodoma,Christina Mdeme kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.

Akichangia mada katika mkutano huo Matonya alisema wenyeviti wa mitaa wana-fanya kazi kwa mazingira magumu sana licha ya serikali kutaka kuwatumia viongozi hao ndomana wengine wanapokea rushwa.

Wenyeviti tumekuwa tukipambana na waharifu ikiwemo kuwakamata watu ambao wanauza madawa ya kulevya lakini wanapo wapeleka polisi watuhumiwa hao wanaachi-wa huru.

Kwa upande wake mwenyeki-ti wa wenyeviti katika Manispaa ya Dodoma,Matwiga Kiyatya alisema kuwa anashangazwa na halmashauri kushindwa kulipa posho ya wenyeviti kwa muda wa miezi nane sasa.

“Pamoja na kuwa mkuu unatutaka tufanye kazi kwa ushirikiano lakini mpaka sasa wenyeviti wanadai posho yao ya sh.20,000 kila mwezi pamoja na pesa nyingine lakini hadi sasa miezi nane hawajalipwa”alisema Kyatya.

“Tumekuwa tukifuatilia kwa mkurugenzi lakini imekuwa ni bure kabisa jambo ambalo linawakatisha tamaa wenyeviti hao”alisema.

Akijibu malalamiko hayo mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mdeme,alisema kitendo cha halmashauri kutowalipa posho wenyeviti ni kutokuwatendea haki.

“Haiwezekani wenyeviti ambao wana-fanya kazi kubwa wanakaa muda wa miezi nane sasa bila kulipwa,lakini kwa sasa nim-ezungumza na Mkurugenzi wa Manispaa kasema mtalipwa ndani ya siku 30”alisema Mndeme.

Aidha alisema Pamoja na mambo men-gine anawataka wenyeviti ambao wanaji-husisha na kuwatetea wauzaji,watumiaji wa madawa ya kulevya kuacha mara moja kwani atapambana nao.

Tanzania Kudai Fidia ya Ukoloni toka Ujerumani

Wana Mazingira Wataka Ushirikiano Zaidi na Serikali Chama cha mazingira chataka ushirikiano zaidi

Na Dotto Kwilasa, Dodoma.

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itashirikiana bega kwa bega na wataalamu wa mazingira nchini ili kuhakikisha elimu ya mazingira inatolewa kwa jamii nzima ikiwa ni pamoja na kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji.

Hayo yamezungumzwa hivi karibuni mjini hapa wakati wa uzinduzi wa chama hicho chenye lengo la kulinda na kutetea taaluma ya mazingira hapa nchini ,taaluma inayotajwa kutopewa kipaumele na seri-kali.

Akiongea kwa niaba ya waziri wan chi ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira,Naibu katibu mkuu wa wizara hiyo Mgosi Mwihava alisema serikali ime-anza kufanya marekebesho Ya sera mpya

ya mazingira ili kuhakikisha kwamba maz-ingira yanalindwa.

Hatua hii imekuja baada ya Chama cha kitaaluma cha wataalam wa mazingira Nchini TEPA kuiomba serikali kurekebisha mfumo mzima wa sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 kwani mfumo huo umeonekana kuwa na mapungufu makubwa ambapo Chama hicho kimesema kuwa taangu sheria hiyo ianzishwe imech-elewa kuwatambua wataalam wa mazingira waliopo hapa nchini.

Akiongea kwa niaba ya wanachama wengine , mwenyekiti wa chama cha kita-aluma cha wataalam wa mazingira nchini TEPA Venance segere alisema wanamaz-ingira wanapata wakati mgumu kuto-kana na kutopewa ushirikiano na serikali amapo amesisitiza kuwa serikali haiwajali wanamazingira hali inayopelekea kutowa-pa kipaumbele cha ajira.

Mbali na hayo amesema, chama hicho kimesema bado kuna uelewa mdogo wa wananchi ambao wanaendelea na utara-tibu wa mazoea ya kutumia rasilimali za misitu bilakuzingatia matumizi endelevu ya utunzaji wa mazingira na hivyo ni jukumu la kila mwanajamii kuyaenzi mazingira.

Kwa upande wake kaimu mkuu wa chuo cha maendeleo ya mipango viji-jini ambae pia ni mdau wa mazingira Prof Hozen Mayaya alisema utunzaji wa maz-ingira unahitaji bajeti ya kutosha na hivyo kuiomba serikali na wadau mabalimbali wa mazingira kujitolea kusaidia utunzaji wa mazingira kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.

Uzinduzi wa chama cha kitaaluma cha wataalam wa mazingira umeenda sam-bamba na zoezi la upandaji miti katika chuo cha mpingo ya maendeleo vijijini kama ishara ya kuhamasisha jamii kushiriki katika kupanda miti ili kulinda mazingira.

na Uingereza Bunge laitaka Serikali kudai fidia kutoka Ujerumani

Mwandishi Wetu

BUNGENI, DODOMA - Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakusudia kuandaa mashtaka dhidi ya Ujerumani ili kulailazimi-sha Marekani kulipa fidia ya vitendo vya kika-tili vilivyofanywa na Ujerumani katika ardhi ya Tanganyika wakati ambao Ujerumani ilikuwa ni mtawala wa kikoloni.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussen Mwinyi, mpango huo upo ili kufanya kile ambacho kimefanywa pia na nchi nyingine za Kiafrika kama Kenya na Namibia ambazo zote zimedai fidia Uje-rumani.

Kwa upande wa Ujerumani serikali inakusu-dia kudai fidia kutoka na vitendo mbalimbali vilivyofanywa na Ujerumani wakati huo katika kuzima harakati za kukataa ukoloni wakati wa vita vya Majimaji.

Ujerumani iliikalia ardhi ya Tanganyika kuanzia 1890 hadi 1919. Vita vya Majimaji vilitokea kati ya 1905-1907 ambapo makabila mbalimbali ya Tanganyika yaliunganisha na kuanzisha uasi dhidi ya utawala wa Mdachi. Ili kuzima uasi huo Ujerumani nguvu kubwa ikiwemo kuwanyonga na kuwapiga risasi viongozi mbalimbali wa vita hivyo na katika tukio ambalo limebakia kama dola kuteketeza mazao yaliyokuwa shambani na kusababisha baa la njaa kutokea na kusababisha vifo vya maelfu ya watu na kulazimisha ushindi.

Januari mwaka huu Ujerumani ilitangaza kuwa imelipa fidia kwa Serikali ya Namibia kufuatia mauaji makubwa ya zaidi ya Wana-mibia 65,000 na kufanya tukio hilo kuchuku-liwa na wanahistoria wengi kuwa ni mauaji ya kwanza ya halaiki katika karne ya ishirini.

Uingereza nayo imelipa fidia ya zaidi ya

dola milioni 21 kwa Kenya mwaka 2013 kama sehemu ya kuwajibika kwake kwa vitendo vili-vyofanywa na serikali hiyo wakati wa utawala wa kikoloni.

Hata hivyo utaratibu gani utatumika kufiki-sha madai hayo haijawekwa wazi na hai-jaeleweka au kuelezwa kama huu ni uamuzi ambao una baraka za Barala la Mawaziri. Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uje-rumani Deutsche Welle Dkt. Mwinyi amesema kuwa ataiandikia Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ili kuona ni namna gani jambo hili litafiki-shwa kwa serikali ya Ujerumani.

Vita vya MajiMaji vilipokwisha kwa nguvu za kijeshi na matumizi ya njaa kama silaha ya vita wapiganaji 75,000 wa Kiafrika waliuawa na wananchi wengine kati ya 200,000-300,000 walikufa sababu ya njaa iliyotokana na vita. Gharama ya vita ilikuwa kubwa siyo kwa uhai tu lakini jamii kubwa iliondokewa na nguvu kazi kubwa kwa muda mfupi na kusababisha kuvunjika kujiamini miongoni mwa wananchi kilicho kilichosababisha kwa kiasi kikubwa kutafuta uhuru kwa njia ya amani wakati wa Mwalimu Nyerere nusu karne baadaye.

Pichani juu sehemu ya mashujaa wa vita vya Maji Maji baada ya vita wakinyongwa kwa amri ya Serikali ya Mjerumani ikiwa ni fundisho dhidi uasi.

Chini sehemu hiyo hiyo walionyongewa mashujaa wa Maji Maji inavyoonekana leo. Sehemu ya mti wa ku nyongewa bado upo umesimama pamoja na kamba zake.

Page 9: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

Machi 13, 2017 ZAMAMPYA 9

Somo la Utawala

Je, mtumishi au kiongozi anaweza kupingana na uongozi wa juu yake hadharani kwa jambo kubwa na akabakia kuwa kiongozi?

KBaada ya Donald Trump kuchaguliwa kama Rais wa 45 wa Marekani siyo watu wote ndani ya serikali yake na kwenye chama chake walikubaliana naye. Kuna ambao walimpinga kuanzia alipotaka kugombea na wengine walimpinga baada ya kuchaguliwa. Ndani ya serikali yake kuna watu ambao waliikataa misimamo mbalim-bali ya kiutendaji na kisera ya Trump kiasi kwamba hawakuwa tayari kufanya naye kazi.

Misimamo ya Trump ambayo imewak-waza wengi ni pamoja na ile inayohusiana na sera zake za uhamiaji, mazingira, ulinzi na usalama na hata mambo yanayohusi-ana na tabia yake ambayo baadhi ya watu wanaiona ni ya kibabe na yenye kutukuza mfumo dume. Tangu aingie madarakani wapo wafanyakazi na watendaji mbalim-bali ambao waliamua kuachia kazi zao – wengine wakiwa wametumikia muda mrefu tu – ili kupinga kufanya kazi chini ya mtu ambaye hawamkubali kisera na kita-bia. Nitatoa mifano michache tu.

Edward Price – Msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa na Afisa wa CIA. Yeye ali-jiuzulu kupinga jinsi Trump alivyotoa nafasi kwa mshauri wake wa mikakati kuingia katika Baraza la Usalama na kuwaondoa baadhi ya majenerali. Akiandika kwenye gazeti la Washington Post, Price anasema hakudhania kuwa angefikia uamuzi wa kutoka CIA lakini sababu ya Trump aliamua kuachia ngazi. Hakuwa tayari kufanya kazi chini ya Rais ambaye anapuuzia taarifa za kiinteligensia.

Mustafa Ali – Afisa katika Idara ya Mazin-gira ya Marekani (EPA) ambaye alitumikia idara hiyo kwa miaka ishirini aliamua kuji-uzulu wiki iliyopita kupinga mpango wa Trump kukata bajeti ya idara hiyo. Chini ya Trump bajeti yake ya mwaka huu kwa idara hiyo itakatwa kwa karibu asilimia 25

jambo ambali Ali hakuwa tayari nalo na aliona amepingana mno kimtazamo na Rais wake na hivyo aliamua kujiuzulu.

Mifano hiyo miwili ni ya watu wa seri-kalini; wapo wengine wengi pia. Ndani ya chama chake vile vile wapo watu ambao walimkosoa Trump na hawakuwa tayari kuendelea naye ndani ya chama. Mifano miwili hapa inatosha kuitoa.

Beth Fukumoto – Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani kwenye jimbo la Hawaii aliamua kujiondoa ndani ya chama cha Republican kufuatia shinikizo la viongozi wa chama chake baada ya yeye mara kadhaa kumkosoa Rais Donald Trump. Kwenye maandamano ya wanawake yali-yofanyika Januari 21 (siku moja tu tangu Trump aapishwe) Fukumoto alizungumza kwenye maandamano hayo na kumuita Trump mbabe. Chama chake kilijaribu kumuasa lakini hakuwa tayari kunyamaza na hivyo kuamua kuhama meli.

George Willis – Mmoja wa sauti za wahafidhina wa Marekani ambaye alikuwa maarufu sana na kwa muda mrefu akian-dika makala mbalimbali za kisiasa. Mshindi wa tuzo ya Pulitzer na mwandishi wa muda mrefu aliamua kuachana na Republican. Trump mwenyewe aliandika kwenye mtan-

Wasiokubaliana na Magufuli CCM Wajiondoe Wenyewe?

“Ili waheshimiwa ni lazima wao wenyewe wajiheshimu; lakini

pia wao wenyewe wawe wa kwanza

kuonesha kuwa wane-heshimu wengine”

SWALI LA NYONGEZA NA M.M MWANAKIJIJI

dao wa Twitter kupuuzia kujiondoa kwa George Willis.

Mifano hii ya aina mbili inanirudisha kwenye kichwa cha habari. Kuna watu-mishi na watendaji ndani ya Serikali ya Rais Magufuli ambao hawakubaliani naye – ama kifalsafa au kiutendaji au hata kiitikadi lakini bado wanataka kuendelea kuwa watumishi. Vile vile ndani ya Chama cha Mapinduzi.

Wengi tunakum-buka jinsi gani katika Mkutano Mkuu wa CCM uliompitisha mgombea wake wa Urais mwaka 2015 jinsi mbele ya Mwenyekiti Kikwete na uongozi wa juu wa chama hicho kundi la wajumbe liliposimama kuimba ‘Tuna imani na Lowassa’ wakionesha kukasirishwa na kitendo cha Kamati Kuu kuengua jina la Lowassa na hivyo kutengeneza njia nyeupe kwa John Magufuli. Ni wazi kuwa wajumbe wale hawakuwa na imani na Magufuli na walijionesha hivyo wazi. Siyo Magufuli tu kwa kuimba kwao walikuwa hawana imani na Kamati Kuu.

Tunakumbuka jinsi baada ya taarifa ya aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Nape Nnauye kutangaza majina yali-yopitishwa kwenda kwa Mkutano Mkuu jinsi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Sofia Simba na Adam Kimbisa walivyosimama kupinga jinsi ukataji wa jina ulivyofanyika. Wote walikuwa wanajulikana ni mashabiki wa Lowassa. Wengi tunakumbuka jinsi Sofia Simba katika kumpamba Lowassa alisema mwaka 2009 wakati akimtetea Lowassa bungeni; maneno ambayo ali-yekuwa mjumbe wa Kamati ya Richmond Lucas Selelii aliyaita yanafaa kwenye “kitch-en party”.

Lakini pia tukumbuke kuna wengi walio-jitokeza kwa maelfu kumuunga mkono Lowassa katika safari yake ya “matumaini” kuelekea Ikulu. Wengi walijiunga naye na wakaja hata na msemo wa “ulipo tupo” na Lowassa alipokatwa jina lake wengi wali-tarajia maelfu waliofuatana naye kwenye safari ya kutafuta wadhamini wange-amua kuungana naye huko kwa jirani. Na inawezekana hili lilitokea kwenye sanduku la kura kwani kupata kura milioni 6 si jambo dogo na halijawahi kufikiwa na mgombea yeyote wa upinzani. Hata hivyo, hawa-

kumfuata kwa kuamua kuachana na CCM na kwenda CHADEMA kama yeye.

Hapa ndipo hoja yangu inapokuja. Wengi waliomuunga mkono Lowassa na ambao hawajawa mashabiki wa Magufuli walipas-wa kuonesha kwa vitendo imani yao kwa Lowassa. Hili ni kweli kwa wabunge ambao wanaonekana wazi kumpinga Magufuli na sera yake; mfano mzuri ni watu kama Hus-sein Bashe. Bashe ni mwanasiasa kijana na machachari na labda ni miongoni mwa wachache ambao wameweza kuikosoa seri-kali ya Magufuli Bungeni. Ni wazi baada ya kashkash aliyopewa juzi kuelekea Mkutano Mkuu wa CCM umempa somo muhimu. Siyo yeye tu hata mpambe wa kampeni ya Magu-fuli na Mbunge wa Geita Mjini Bw. Msukuma naye amepata somo.

Kama hawa wote na wengine – wabunge na wajumbe wa ngazi mbalimbali za CCM – wanaamini kabisa kuwa nchi inaelekea kubaya chini ya Magufuli, kama kweli

wanaamini Magufuli anaongoza vibaya nchi kwa kusigina Katiba au kuwa na ubabe fulani, hawapaswi kusema na kubakia; wanapaswa

kusema na kujiuzulu. Kujiuzulu huko

siyo woga wala hofu; kujiuzulu huku ni misi-mamo kutofautiana. Nimewahi kuandika mara nyingi sana huko nyuma hasa kwenye masuala ya CHADEMA kuwa endapo viongozi wajuu wanatofautiana ama na chama chao au na uongozi wa juu wa chama chao hawawezi kusema “wanapinga” halafu wakataka kuba-kia kwenye vyeo vyao. Ni kanuni ya kawaida tu kuwa unapopinga-

na na bosi wako kwenye jambo la msingi tena hadharani ni muhimu wakati huo huo ukajitan-gaza kujiuzulu nafasi yako.

Ni matumaini yangu kuwa viongozi wote wa CCM wa ngazi zote na hata walioko Bungeni au serikalini ambao hawakubaliani na Magu-fuli kama Rais au na uongozi na sera zake kama kiongozi mkuu wa chama wanapaswa kujiuzulu nafasi hizo mara moja. Hawawezi kuendelea kukalia nafasi wakati hawaamini katika ajenda, sera au mwelekeo unaotolewa na kiongozi wao.

Kutokujiuzulu ni kuwa kinyonga wa kisiasa. Viongozi hawa hawawezi kutaka kubadilika badilika rangi kila kiongozi mwingine anapoin-gia ndani ya chama. Walitaka kuwa hivi wakati wa Mkapa, wakawa vile wakati wa Kikwete na sasa wanataka kuwa na rangi nyingine wakati wa Magufuli. Kama wanaamini katika misimamo yao na katika tofauti ya msingi baina yao na Rais/mwenyekiti wao. Ni jukumu lao kujiuzulu nafasi zao.

Nje ya hapo, ni jukumu la Rais na Mwenyekiti wa chama chao kuhakikisha kuwa wanaondole-wa ndani ya chama na serikali. Hii ni matunda ya demokrasia, ni zao la utawala wa pamoja na wa msimamo mmoja. Kama huamini ambayo chama kinaamini na kinataka kutekeleza ni jukumu lako kujiondoa. Ukweli huu siyo kwa CCM tu bali hata kwa vyama vingine vya kisiasa au vya kijamii. Kama hukubaliani na viongozi wako wakuu au kiongozi wako mkuu, ni jukumu lako kusema kuwa hukubaliani naye, na uki-shasema hadharani hukubaliani naye basi jambo moja tu limebakia kufanya.

Kujiuzulu. (Pichani juu Rais Magufuli akihutubia Mku-

tano Maalum wa CCM, Jumapili mjini Dodoma. Picha na Issa Michuzi)

Niandikie: [email protected]

Page 10: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

10 ZAMAMPYA Machi 13, 2017

Dkt. Joseph Ng’weshemi MDUtanguliziWanawake na watoto wamekuwa

ni waathirika wakubwa wa ukatili wa kingono katika jamii nyingi ikiwemo Tan-zania. Matokeo ya utafiti wa mwaka 2009 uliofanywa na UNICEF ikishirikiana na CDC pamoja na MUHAS nchini Tanzania na kuchapishwa mwaka 2011 ujulikanao kama “Tanzania Violence Against Children Survey, 2009” ulibainisha kuwa kila wan-awake watatu kati ya kumi (27.9%) wenye umri kati ya miaka 13 mpaka 24 nchini Tanzania waliripotiwa kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikia umri wa miaka 18. Ambapo pia asilimia 13.4% ya vijana wa kiume wa umri huo nao walitoa taarifa za kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikia umri wa miaka 18.

Ukatili wa kingono ni mojawapo ya aina za ukatili wa kijinsia ambapo isipo dhibitiwa hupelekea athari kubwa kwa muathirika na hata kwa taifa zima kwa ujumla. Ukatili wa kingono una athari nyingi sana ikiwamo Kuambukizwa maradhi kama ukimwi, mimba zisizotarajiwa, maumivu ya kimwili na kisaikologia pamoja na unyanyapaa.

Makala hii inalenga kuongeza ufahamu juu ya uwezekano mkubwa uliopo wa kuzuia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi “VVU” kwa waathirika wa ukatili wa kingo-no na uwepo wa huduma hii katika vituo mbalimbali vya Afya nchini Tanzania, na pia kuongeza hulka ya kutafuta huduma hii miongoni mwa waathirika wa ukatili wa kingono.

Kinga ya Maambukizi ya VVU ni nini?Kinga ya Maambukizi ya VVU ijulikanayo

kitaalamu kama “HIV Post Exposure Pro-phylaxis” (PEP), ni kinga ambayo hutolewa mapema kwa kusudio la kuzuia hatari ya Maambukizi ya VVU. Kinga hii inahusisha kuanza umezaji wa dawa za kinga mapema iwezekanavyo (ndani ya masaa 72 “Siku tatu”) baada ya tendo moja la ukatili wa kingono ili kuzuia uwezekano wa kusam-baa kwa VVU mwilini na hatimaye kuzuia

maambukizi. Ukweli huu kuhusu Kinga ya VVU:-• Nihudumayadharuraambayo

hutolewa ndani ya masaa 72 na sio zaidi baada ya tendo moja la ukatili wa kingono. Kinga inapotolewa mapema kabisa ni bora zaidi kwa ufanisi wa kinga.• Hutolewa kwa watu ambao

hawana Maambukizi ya VVU kabla ya uka-tili wa kingono, hivyo ni lazima kupima na kubaini hali ya Maambukizi ya awali kabla ya kuanzisha kinga. Endapo mwathirika wa ukatili wa kingono atakutwa na Maam-

MAKALA: MASAA 72 YA KUPATA KINGA YA HIV KWA WAATHIRIKA WA UKATILI WA NGONO

“Ukatili wa kingono ni mojawapo ya aina za ukatili wa kijinsia

ambapo usipod-hibitiwa hupeleka athari kubwa kwa

muathirika”

AFYA NA TIBA

bukizi ya awali ya VVU hataweza kupatiwa kinga ya VVU.• Itatolewamfululizokwasiku28,na

inaweza kusitishwa kabla ya siku 28 endapo mtuhumiwa wa ukatili wa kingono atat-hibitaka bila ya shaka kutokuwa na Maam-bukizi ya VVU.• Hutolewakwamuathirikawaukatili

wa kingono endapo hali ya Maambukizi ya mtuhumiwa wa ukatili wa kingo hajulikani.• HudumahiiyakingayaVVUhutole-

wa katika vituo vyote vya Afya vyenye kliniki za kutolea tiba kwa waathirika wa VVU na Ukimwi “CTC” na pia baadhi ya kliniki za afya ya kinga ya mama na mtoto (PMTCT) nchini Tanzania.

Je ninaweza kutumia kinga ya VVU baada ya ngono isiyo salama? • Kingahiihutumikanyakatizadharu-

ra tu, kwamfano ndani ya masaa 72 baada ya ukatili wa kingono.• KingayaVVUsichaguosahihikwa

watu wenye mahusiano mengi ya kingono yasiyo salama na huweza kupelekea usugu wa matibabu ya VVU pindi tiba ya VVU inapo-hitajika.• NjiaborazakujiepushanaMaam-

bukizi ya VVU ni zile ambazo zina tukinga kwanza na Maambukizi (protect against exposure). Kama vile kushiriki ngono na

mpenzi mmoja aliye salama, matumizi sahihi ya kondom, n.k.

Je nani wengine wanao stakili kupewa kinga dhidi Maambukizi ya VVU?• WatumishiwaAfyaambaobahati

mbaya wamepata ajali ya vifaa vyenye ncha kali ambavyo vina damu/vimiminika kutoka kwa wagonjwa.• Watumiajiwamadawayakulevywa

mara baada ya kuchangia sindano au uchan-giaji wowote wa sindano usiokuwa wa hiari.

Kwakuwa ukatili wa kingono umekuwa uki-ripotiwa kwa kiwango cha chini sana, hali hii imepelekea takwimu za kitafiti juu ya ukubwa wa tatizo hili kutofautiana kwa kiwango kikub-wa. Idadi ndogo sana ya waathirika wa uka-tili wa kingono inayofanikiwa kupata Kinga dhidi ya Maambukizi ya VVU inatokana na usiri mkubwa unaosababishwa na unyanyapaa kwa waathirika ambao wangeweza kuzuia kupata Maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Tusaidie wahanga wa ukatili wa kingono kupata kinga dhidi ya VVU kwa wakati.

Page 11: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

Machi 13, 2017 ZAMAMPYA 11

“Waziri Mkuu Asante”

Inawezekana kabisa vurugu nyingi za kisiasa zilikuwa zinatokana na watu kupata viroba kirahisi rahisi?

Sasa ukiingia uwanja wa Taifa amani ni kubwa sana tofauti na zamani, ushahidi mkubwa ni mechi ya watanii wa jadi Yanga na Simba hilikwisha salama bila uvunjifu wa miundombino au amani, ukiwa kwenye vyombo vya usafiri mbalimbali sasa amani ni kubwa sana, maofisini amani ni kubwa na tele kwa kila mtu, lakini ata ajali nchini kwa mujibu wa Jeshi la Usalama Baraba-rani linasema hakuna kabisa ajali kipindi hiki kwa siku kama zamani, yote haya ni matokeo ya kupiga marufuku pombe aina ya viroba na serikali ya awamu hii.

Jana siku ya Ijumaa kwenye mkoa wa Arusha, kulikuwa na mkutano mkubwa sana wa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema (pichani) na wananchi wake tangu atoke jela ya Gereza la Kisonga, Jijini Arusha.

Alikuwa huko mahabusu kwa kesi ili-yokuwa ikimkabili siku nyingi kiasi, iliyom-pelekea kukosa dhamana kwa takribani miezi minne, kwasababu mbalimbali za

uendeshaji kesi kwenye Mahakama ya

Arusha, kisha alifanikiwa kutoka kwa dha-mani hapo majuzi.

Alihitisha mkutano wa mbunge na wananchi wake kwa muktadha mbalim-bali kupitia PA, mabango na mitandao ya kijamii, kwa malengo mbalimbali ali-yoyakusudia na wananchi walijitokeza kwa wingi kiasi tofauti na zamani kwa kumsikili-za hiyo jana.

Agenda kuu ya mkutano mpaka mku-tano unamalizika ilikuwa ni kuisema serikali hii ya Dkt John Magufuli tu, kuwa inaon-goza nchi hii kidikteta, kutofata katiba, kuingilia kesi zake na mambo mengi mabaya kwa maono ya waliopewa nafasi

ASANTE SERIKALI KWA KUZUIA VIROBA, SASA AMANI KILA KONAFIKRA HURU: FREDY MASOLWA

ya kusema neno kwenye mkutano huo na yeye mbunge.

Agenda ya taarifa za kimaendeleo ya Arusha kwa wananchi toka yupo Jela mpaka sasa hakuongelea kabisa, hakuu-liza wala kushauri njia za kusonga mbele kimaendeleo na Arusha yao, lakini Mkuu wa Mkoa wa Arusha alipata kidogo miwashow-asho toka kwa mbunge huyu.

Mkutano ulianza kwa amani kubwa na kumalizika kwa amani kubwa sana.

Jana nimeona wananchi mkutanoni hasa vijana wakiwa watulivu sana, wakishan-gilia kwa tahadhari kubwa sana na mau-mivi makuwa mwili mwao ya upendo kwa mbunge wao.

Jana nimesikiliza hoja mbatata kiasi toka kwa waongehaji wote, lakini sijaona hoja kinzani na mvurugano za huko nyuma toka kwa mbunge wa Arusha, ingawa hoja mbatata hazikuwa na maono ya kimaende-leo lakini zilitengeneza staha kwake, vion-gozi na wananchi mbalimbali kwenye mku-tano huo waliongea kwa mpurulano na sio “Vuta Nkuvute”

Jana nimemuona wanachama wenye nguvu kubwa kuliko Mh. Lowasa, kwenye chama cha Chadema, Mwema Sepetu “Sepenga”, akitema cheche kwa sauti ya Peoplessssssssss na hoja za kibashite.

Jana nimeona amani iliyoja nuru na heri kubwa sana maeneo ya mkutano muda wote, huku askari wakiwa hawana kazi ya kutuliza ghasia mbalimbali. Jana nimeona watu wakielekea kwenye mkutano kwa utaratibu na kutoka kwa utulivu uliojuu ya mstari wa sita kwenye goli la adui.

Jana sijaona agenda ya maendeleo kwa jimbo la Arusha kama maji, elimu, miun-dombinu, afya, mazingira na kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo hasa jimbo lake, kama nilivyoona kwa jimbo la Mh. Zito Kabwe kwa wananchi wake akiwaomba wapande kwa wingi miti ya Mawese ili-wapate mapato kwa kukuza uchumi wa jimbo lake kwenye mkutano wake hapo jana huko Kigoma Mjini.

Jana sijaona mashuti ya ndani ya kumi na nane, kwasababu Mh. Lema alikuwa ni mtu aliyetulia sana kimawazo, kiakili na ata kimatamshi yake kila wakati. Asante sana Waziri Mkuu kwa kuzui Viroba nchi nzima.

Kilio changu kikubwa hapo jana sijaona vyombo vywa habari wakirusha tukio hili aise, kama TV kubwa nchi ya IVT hawakuru-sha kabisa habari ya mbunge huyu, kwenye kipindi chochote huku imani yangu niki-amini mkoani Arusha wana ofisi yao na waandishi wengi tu, mpaka habari kuu ya

saa mbili sikuona, kwani Mh. Godbless Lema ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani Nchin nje na Ubunge wake. Asante Waziri Mkuu

Kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii sijaona habari ikichukua nafasi yake kwa kasi ya kibashite au mambo kadha wa kadha. Asante Waziri Mkuu

Television mbalimbali nyingine sijaona habari hii ikipewa nguvu ya juu, kwani sio tukio dogo hili la Mandela wa Arusha kuachiwa kwa takribani miezi minne akiwa kwenye nondo za mahabusu ya Gereza Korofi la Kisonga hapo Arusha, na sijajua kwanini hawajarusha. Asante Waziri Mkuu

Kwenye Radio mbalimbali sijaona kabisa habari hii ikiwa kubwa kwenye vipindi vywao, kwani kulikuwa na wana-chama nguli wa CDM, Wema Sepetu kwenye mkutano huo, kwahiyo matarajio yangu ingekuwa habari kubwa sana huko. Asante Waziri Mkuu.

Asante sana akaunti za mitandao ya kijamii za Bavicha na Chadema Kanda ya Kaskazin, kwa kurusha mubashara tukio hili lakini picha hazikuwa safi ingawa sauti ilikuwa safi sana. Asante Waziri Mkuu.

TANZANIA YA SASA

Tuendele na kasi ya kuchakata Viwanda kila sehemu vidogo mpaka vikubwa, kwa kasi ya urasmishaji malighafi kuwa bidhaa ghafi au kamili. Twendeni mashambani au maporini tukalime mvua inanyea vizuri tu, tupate mazao tuchakate kwenye viwanda kama malighafi kisha bidhaa na vitu sahihi kwa fedha sahihi

Majimboni kwetu tuanzishe mashamba darasa kwa watu waliofanikiwa kibiasha-ra, kiujasiriamali, kikazi au kimaendeleo, tuweke VICOBA sahihi sio vya watu 30 tu, kisha tuviweke wasimamizi wazuri kupitia SACCOS za kila kata, mpaka SACCOS ya jimbo kupitia mfuko wa maendeleo wa Jimbo.

Utaona wananchi wakitengeneza dha-mani ya mazao yao au biashara zao kuwa kubwa, na wewe kama mbunge au jimbo kukusanya ushuru wa malighafi, bidhaa na vitu, kisha kuwarudishia wananchi kwa njia ya madawa kwenye zahanati zao, elimu na miundombinu.

Tuanzishe kamati za watalamu washauri kila jimbo kwa uongozi huu ni rahisi kuwapita China kwa miaka ya 2025. Siasa ni maisha ya kila siku ya wanadamu, tuipe mipaka kwa kufanyakazi kwa nguvu na hali zaidi.

Pole sana Lema kwa masahibu mbalim-bali, karibu uraiani na jimbo kwako.

Leo nipo macho kabisa wala sio ndoto hii. Asante Waziri Mkuu. Mwisho!

0715 011 406!

Page 12: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

12 ZAMAMPYA Machi 13, 2017

PAUL MPAZI: Mteja anapokuwa si mfalme tena!Huduma kwa mteja inapokuwa in huruma kwa mteja!

Na. Paul Mpazi

HUDUMA KWA wateja ni mfululizo wa shu-ghuli iliyoundwa ili kuongeza kiwango cha mteja kuridhika - yaani, hisia kuwa bidhaa au huduma imekutana na matarajio ya mteja. Msisitizo hapa ni “mteja kuridhika” Katika ofisi mbalimbali hasa zenye mlengo wa kibiashara mara nyingi kuna

kitengo hiki kinachotakiwa kuhakikisha wateja wanapa-ta msaada wa maelekezo au ushauri. Maelekezo haya yamekuwa yakitole-wa katika namna ambayo mhudumu na mhudu-miwa wanazungumza kwa

lugha ya “kirafiki” zaidi ili kuweza kuleta ufanisi wa kile anachokitarajia mteja. Katika utafiti wa muda mfupi niliou-fanya nimegundua kuwa kumeanza kuwa na tofauti kubwa kati ya huduma kwa wateja katika maeneo mbambali. Huduma inayotolewa kwa mteja ambaye shughuli iliyompeleka pale ni kuweka fedha au kuli-pia huduma fulani imekuwa ni nzuri naya ukarimu wa hali ya juu sana kuliko yule anayefika ofisni hapo kufuatilia malipo yake. Kwa mfano, mteja anayeingia katika ofisi ya bima kulipia bima mali yake anapokele-wa vizuri sana na kwa ukarimu wa hali

ya juu kuliko mteja anayeingia katika ofisi hiyo hiyo kuomba kulipwa baada ya mali yake kuharibika katika mazingira yasiyozuilika (Mfano gari linapopata ajali). Hali hii, kama nilivyotoa mfano wa shirika la bima hapo juu; ipo kwa kiasi kikubwa sana katika mashirika ya mifuko ya kijamii kama NSSF, PSPF, LAPF n.k. Je, wateja kwao ni wale wanaokuja kuweka tu na sio wanaokuja kuchukua?. Kwa nini wanasahau kuwa alichokiweka huyo mteja ndicho kinachowafanya wao wawe hapo?. Kwa nini wanasahau kuwa alichokiweka mteja huyo ndicho anachokuja kuchukua? Kwa nini wanasahau kuwa alichokiweka huyo mteja ndicho kinachowafanya wao wawe hapo?. Kwa nini wanasahau kuwa alichokiweka mteja huyo ndicho ana-chokuja kuchukua? Kwanini wasimpe heshima na staha mteja ambaye anakuja kuchukua fedha ZAKE kama vile wanavyo-mchangamkia na kumfanya ajisikie kweli ni ‘mfalme’ wakati anapokuja na kuwekeza?

Kwanini wasiseme basi mteja ni “mfalme wakati wa kuweka fedha ili wakati wa kuchukua yeye ni kabwela?”

Najiuliza tu.

FAO Signs a17.5m Pact With Tanzania to Improve Food SecurityTanzania has continually suffered food insecurity almost every year()The Food and Agriculture Organisation (FAO) on Monday signed a minimum of 17.6 million U.S. dollars Country Programming Framework (CPF) with Tanzania. The signing event was held here between the FAO Country Representative, Fred Kafeero, and Tanzania’s Permanent

Secretary in the Ministry of Agriculture, Livestock and Fisheries, Eng. Mathew Mtigumwe.

According to Kafeero, the implementa-tion of the CPF is to be financed through partnerships with development partners, the government of Tanzania, South-South cooperation programmes and joint One UN programmes.

The programmes would help in improv-ing agriculture, food security, nutrition and natural resources management in the coun-try over the next four years.

  Kafeero said that the framework guides FAO support and partnership with the gov-ernment of Tanzania from 2017 to 2020 in the context of UN Development Assistance Plan (UNDAP II) 2016-2021.

“It draws lessons from the previous CPF and it takes into account the findings and recommendations of the evaluation of FAO’s

contribution to the United Republic of Tan-zania 2014-2016.

“It also seeks to strengthen collaboration with key stakeholders and development partners supporting the government of Tanzania,’’ he said.

Explaining the UN body’s contribution and expected results under the framework, the FAO Representative highlighted the four mutually reinforcing priorities of the CPF.

 This which include evidence-based agri-culture policy, planning, investment and sector coordination; increasing agricultural production, productivity for food and nutri-tion security.

Others are improving market access for increased incomes; and strengthening resilience to natural and man-made threats and crises.

“Implementation of the priorities will be through working in partnership with central and local governments by specific linkages and coordination with agriculture line ministries; collaboration with non-state

NEWS HEADLINESTanzania Urged to Reconsider Its Refugee Response

ProcessMSF

Pressure is mounting in Tanzanian refu-gee camps as the flow of refugees from Burundi continues on a large scale. January saw the largest rate of new arrivals in a single month since May 2015, with nearly 19,000 people crossing the border into Tanzania, according to the UNHCR.

Some 290,000 refugees, over three-quar-ters of whom are Burundian, are crammed

into three overstretched camps: Nyarugusu, Mtendeli and Nduta.

Nduta camp – already full in November last year – is now overflowing and is cur-rently home to 117,000 people, more than double its intended capacity. With between 600 and 1,000 people arriving per day, it is expected the camp will reach 150,000 by mid-April.

David Nash, head of mission for MSF, emphasises the urgent need to identify a site for a fourth camp and establish it imme-diately.

“MSF has repeatedly called for this, but we are still not seeing concrete action being taken,” he says. “Although agencies have begun to scale up assistance, the humanitar-ian response still does not match the rate of new arrivals. With insufficient shelter avail-able, people are forced to spend more time in overcrowded communal shelters, where the risk of disease is much higher.”

As refugees arrive, medical pressures grow

In Nduta camp, where MSF is the main health provider, medical teams have seen a fourfold increase in the number of out-patient consultations. Malaria is the major concern and with the rainy season putting additional pressure on already overcrowded and unsanitary living conditions, there has been an explosion in cases. In January alone, MSF treated nearly 17,000 people for the dis-ease in Nduta and Nyarugusu camps. Diar-rhoea, respiratory tract infections, and skin

conditions are also very common among refugees.

Sexual and reproductive health services are in high demand in Nduta. Deliveries more than doubled during the last four months of 2016, and over 400 babies were born in January. Young children, pregnant women and new mothers are particularly vulnerable to illness.

“There is a real fear that we may witness a health crisis if crowding gets worse and facilities are unable to meet the needs of people arriving,” says Nash.

Refugee status under threatEfforts to meet the shelter, medical and

hygiene needs of refugees will also need to take into consideration the recent decision by the Tanzanian government to revoke the prima facie status of Burundian refugees arriving into the country.

Since the emergency began in April 2015, all Burundians arriving into Tanzania have been automatically granted refugee status. The decision to change this approach means new arrivals will now have their refugee status determined individually, a process that may affect the humanitarian assistance that can be made available to them.

“Tanzania in recent years has generously hosted hundreds of thousands of refugees fleeing acute crisis,” Nash says. “International donors need to drastically increase their sup-port to this crisis. At the same time, the Tan-zanian Government must ensure it continues to respect refugee conventions and provide safe refuge for as long as people continue to flee. We again call for a rapid scale-up of aid to support the ever-increasing number of refugees entering Tanzania.”

Iraq Forces Dis-lodge ISIS From Mosul Main Gvt Building

(REUTERS) Elite Iraqi security forces dis-lodged Islamic State militants from the main government building in Mosul on Tuesday,

their last major city stronghold in Iraq, an Iraqi spokesman said.

A special Rapid Response team stormed the Nineveh governorate building and the surrounding government complex in an overnight operation, Lieutenant Colonel Abdel Amir al-Mohammadawi, a spokes-man for the elite interior ministry unit, told Reuters.

“They killed tens from Daesh,” he said, referring to the Islamic State group by one of its Arabic acronyms.

Recapturing the site would help Iraqi forces attack the militants in the nearby old city center and mark a symbolic step toward restoring state authority over Mosul, even though the buildings are destroyed and not being used by Islamic State.

The battle for Mosul, which started in mid-October, will enter a more complicated phase in the densely populated old city, where, the Iraqi military believes, several thousand militants are among the remain-ing civilian population. Aid agencies esti-mated that 750,000 civilians remained at the start of the latest offensive.

Page 13: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

Machi 13, 2017 ZAMAMPYA 13

Na. M. M. MwanakijijiSURA YA 2

SSURA YA PILINilikuwa nimelowa jasho; mwili bado uli-

kuwa unatetemeka. Kila nilivyofikiria moyo ulinilipuka. Koo lilikuwa limekauka nikiwa na kiu ya pipa la maji. Nilikuwa nimetem-bea kwa mwendo wa haraka sana toka pale ofisini hadi makutano ya Barabara ya Maktaba na Bibi Titi Mohammed. Sikuwahi kutembea kwa haraka namna hiyo kama nilivyotembea hivyo tangu nilipokuwa shule ya Msingi Nyanguge miaka ile. Nili-tamani kukaa chini kupumzika lakini sikua-mini kama nilikuwa na muda wa kufanya hivyo. Toka ofisini barabara ya Madaraka hadi nilipokuwepo nilikuwa nimetembea kwa muda mfupi sana. Sikutaka kusimama pale; mfukoni nilikuwa na shilingi elfu ishirini tu. Nilikuwa na mamilioni benki na nikapata wazo la kwenda ATM yoyote ili-yokuwa karibu nichukue hela kidogo kabla mambo hayajawa mabaya zaidi. Nilikata kushoto kuelekea barabara ya Morogoro. Nilikuwa na akaunti yangu mojawapo kwenye benki ya Barclays na lilikuwa ni kusudio langu kufika pale mara moja. Kelele za magari yaliyokuwa yanaenda huku na kule sikuzijali; mara mbili hivi nili-jikuta narushiwa matusi na makonda wa daladala kwa sababu walinikosakosa.

Akili yangu ilikuwa inazunguka kuliko pia; bado nilikuwa katika hali ya kutoamini kwani yaliyotokea kama saa moja kabla niliona kama ni ndoto fulani ambayo ningeweza kuzinduka. Kwa kadiri nili-vyokuwa natembea ndivyo nilivyojua kuwa sikuwa ndotoni; nilikuwa kwenye tukio lililokuwa linaendelea kutokea wakati ule.

Nilipoingia pale benki kitu cha kwanza niliomba chupa ya maji. Kabla sijaenda kwenye kaunta kujaribu kutoa hela kidogo. Nilitumia tai yangu iliyokuwa mfukoni kuji-pangusa uso wakati nakunywa maji. Niliso-gea mbele ya kaunta ya dada wa benki na kumkabidhi kitambulisho changu pamoja na fomu ya rangi ya njano ya kuchukulia fedha. Alichukua vyote hivyo na kuanza kuingia kwenye mtandao wao kuangalia akaunti yangu na kunipatia fedha zangu.

Nilikuwa nimezama kwenye mawazo hata sikumuuona dada yule alipoondoka pale dirishani. Niligundua kuwa hakuwe-po wakati namuona akija pale dirisha la kuchukulia fedha na mtu ambaye nilimtam-bua kuwa ni menewa wa tawi lile la benki.

“Vipi kuna tatizo” niliwawahi kabla hawa-jasema kitu

“Samahani Vicent, kuna tatizo kidogo katika kuifungua akaunti yako” alisema Meneja ambaye nilikuwa nafahamiana naye kwa muda mrefu tangu nifungue akaunti yangu pale.

“Iddi, kuna shida gani ni kwa akaunti zote au yangu tu?” niliuliza kwa udadisi.

“Sasa hivi ni akaunti yako tu” alisema Iddi Mchonde. Mchonde alikuwa ni mtu wa makamu ambaye alikuwa amenyoa nywele zake zote kipara. Alikuwa mfupi na mwenye kitambi kidogo ambacho kama kitaachwa kinaweza kuwa ni shida mbele ya safari. Alivyonipa jibu hilo niliuma midomo yangu kutafakari kwa sekunde chache. Kabla sijasema lolote aliniwahi.

“Naomba uje ofisini ili tuweze kufuatilia makao makuu kugundua kuna tatizo gani” alisema.

Nilipiga hesabu za haraka haraka nikaona kuna mtego hapo. Nilishaona filamu nyingi ambazo zinatoa mafunzo ya vitu kama hivi; mara nyingi hakuna jema hapo. Mawazo yangu yalikatishwa ghafla baada ya kuona gari la polisi likiingia katika eneo la benki

ile; meneja hakuweza kuona kwani ilikuwa upande ambao alikuwa ameupa mgongo.

Niliamua kumshukuru na kumwambia kuna mahali ninaenda nitarudi tena baadaye labda tatizo litakuwa limetatuliwa. Sikutaka kupoteza muda nilibeba chupa yangu ya maji macho yangu yakiwa yanaelekea upande wa lile gari la polisi. Sikujua lilikuwa linafuata nini pale na sikutaka kujua lakini akili yangu yote ilikuwa inapiga ving’ora vya tahadhari. Nilitoka kwenye eneo la benki na mara moja kuchepukia upande mwingine wa jengo lile kuelekea barabarani ambako nilikuwa nimetokea. Nikashika tena baraba-ra ya Bi Titi Mohammed kuelekea makutano yake na mtaa wa Uhuru.

Nilipofika kituo cha basi cha Baridi pale nikadandia kibajaji kuelekea mtaa wa Uhuru. Nilimuambia yule kijana anipeleke hadi tawi la NBC mtaa wa Samora. Akili yangu ilikuwa inaenda kasi sana; sikuwa nafikiria kitu kingine chochote isipokuwa uwezekano kuwa akaunti zako zote zinawe-za kuwa zimepigwa stop na kama ni hivyo wapi nitaweza kupata fedha. Nilikuwa na kiasi kikubwa cha fedha taslimu nyumbani. Akaunti yangu nyingine iliyokuwa na fedha za Kitanzania ilikuwa pale; niliombea tu kuwa kilichonikuta kule Barclays kisirudie na kuwa ilikuwa ni bahati mbaya tu ya mifumo yao na siyo kitu kingine chochote.

Dakika chache za kupishana na mabasi na magari ya kila namna nilifika pale NBC. Jambo la kwanza lililonishtua ni uwepo wa magari mawili ya polisi. Nilitembea mbali na pale benki nikiwa ninaangalia kwa mach-ale. Kengele zangu za tahadhari ziliendelea kupiga kelele. Inawezekana hakikuwa kitu chochote lakini sikutaka kujaribisha kuona; nilijua natafutwa na wanaonitafuta wame-amua kubana kila kinachoweza kubanwa kikabana.

Nilimwomba dereva wa bodaboda kuniteremsha makutano ya Azikiwe na Samora. Nilikuwa najisikia njaa maana tangu ile asubuhi nilipopata kifungua kinywa sikuwa nimekula chakula chochote na nilihitaji muda wa kufikiria vizuri nini cha kufanya. Hela kidogo niliyokuwa nayo mfukoni ingenitosha kwa chakula na labda ikibidi hata kujilaza kwenye hoteli mahali fulani. Lakini nilihitaji hela na mahali pekee nilipojua kwa uhakika palikuwa na hela tas-limu ni nyumbani kwangu. Nilifikiria kuwa kama polisi walikuwa wananitafuta kwa hakika watakuwa wameshafika nyumbani kwangu au wananitegea nifike.

Katika kutafakari nini cha kufanya kati ya kumpigia simu Rita au mwenyewe kwenda pale nyumbani niliona lililokuwa salama zaidi ni kupiga simu nijue hali ilivyo pale nyumbani kuliko kwenda na kujikuta nime-jiingiza mwenyewe mtegoni hasa baada ya yale matukio ya mapema mchana kwenye benki. Nilikuwa nafahamku kuwa polisi na vyombo vya usalama wanaweza kumfuatilia mtu kwa kutumia simu yake ya mkononi kwani teknolojia ya GPS ambayo simu zina-tumia kuelekeza mahali inaweza pia kutu-miwa kujua simu ya mtu iko wapi.

Nilitembea baada ya kushuka kutoka kwenye mtaa wa Samora hadi nilipofika Dia-mond Plaza; kulikuwa na mgahawa mmoja pale ambao nilikuwa napenda kwenda wakati wa mchana nikaingia kimya kimya kuagiza chakula wakati napanga mkakato wa nini la kufanya. Wakati nasubiria chakula nilichomoa simu yangu na kutoa sim card yangu pamoja na memory card nyingine ambayo ilikuwa na picha na video mbalim-bali. Nilitoa betri kutoka kwenye simu kuhakikisha kuwa imezimika kweli. Nili-fanya hivyo bila kuonekana na mtu yeyote na nilipomaliza kula tu nikaenda kutupa simu yenyewe kwenye pipa la takataka lili-lokuwa pale nje ya mgahawa; nilitupa betri baada ya kuvuka upande wa pili mtaa wa Mirambo kuelekea Barabara ya Sokoine.

Nilitembea kwa muda kuelekea barabara ya Sokoine lakini muda wote ule akili yangu ilikuwa inazunguka kama pia kichwani mwangu, nilikuwa nahema, nimechoka lakini pia nikiwa nashuku kila gari lililopita karibu karibu yangu. Sikutaka kusimama hadi nifike kwenye kituo cha mabasi Mwendokasi pale Mirambo inapokutana na ile ya Kivukoni. Sikuwahi kutembea maisha yangu yote kama nilivyotembea siku hiyo.

Sijui ni kitu gani kilininong’oneza kuan-galia upande wa pili wa barabara. Inaweze-kana ni mizimu, hisia ya machale au ni bahati tu; macho yangu yalimuona mtu ambaye ni kama nilikuwa nimemuona mara nyingi siku ile na sikumtilia maanani. Hata hivyo, kumuona tena pale kulinifanya moyo ush-tuke kidogo. Alikuwa ni kijana hivi labda kama miaka ishirini na tano lakini siyo wa kuzidi miaka thelathini. Alikuwa amevaa suruali ya jeans na viatu vya raba za Nike. Alikuwa amevaa tsheti nyeusi na miwani ya jua. Kilichonifanya nimuangalie ni kuwa mtu huyo huyo nilimuona mara ya kwanza wakati nakimbia kutoka ofisini baada ya kufukuzwa kazi. Nilimuona tena wakati natoka benki ya ya Barclays na baadaye nina uhakika wa asil-imia mia moja alikuwa mbele yangu wakati bajaji inanishusha pale Azikiwe na Samora. Lakini kumuona kwangu tena umbali wa kama mita hamsini tu kulitokea si kwa bahati mbaya; macho yetu yaligongana kwa sekunde kadhaa na mara moja niligundua kuwa alikuwa ananitazama mimi.

Nilipoepusha macho yangu kujaribu kufikiria nifanye nini nilishtushwa na mlio wa gari lililofunga breki mbele yangu kabisa. Nilirudka pembeni kujaribu kujiepusha nalo nikidhani limekosea njia. Kilichofuatia kilitokea kwa haraka, sikupata hata muda wa kuufanya ubongo wangu ufuatilie kwa makini kwani pamoja na kukutwa na hofu ya ghafla, wazo la kuwa naelekea kufa lilinijia kwa ghafla vile vile. Sikujua ni nini kilitokea. Ninachokumbuka ni kuwa baada ya lile gari kufunga breki kitu pekee nilichoweza kuki-ona ni kuwa lilikuwa ni gari aina ya Toyota Landcruiser mpya kabisa ikiwa na vioo vili-vyotiwa giza.

Mlango wa mbele wa abiria na ule wa nyuma wa upande wa kushoto ilifunga kwa wakati mmoja; watu wawili ambao walikuwa ni mapandakizi ya watu walitokea kwenye kila mlango na kabla sijajua nini kinafuatia mmoja alikuja nyuma yangu na mara moja nikahisi mdomo wa bastola.

“Ingia kwenye gari!” aliniamuru. Nilianga-lia kama kuna mtu yeyote ameona. Sidhani kama watu waliokuwepo pale walielewa nini kinatokea.

“Nimefanya nini kwani” nilijaribu kuu-liza huku nikijizuia kuingia kwenye lile gari. Ndipo yule mtu mwingine alipokuja mbele yangu na kunipiga ngumi tumboni iliyoni-fanya niiname kwa maumivu makali. Nilijihisi kutapika kwa ghafla. Kabla sijainuka wote wawili walinusukuma mzoba mzoba kuin-gia kwenye mlango wa nyuma wa abiria na mmoja akaingia upande wa kushoto kwangu. Wakati huo huo mlango ule wa abiria upande wa kulia nyuma ya dereva ulifungulia na yule jamaa niliyekuwa nimemuona mwanzoni; aliyekuwa amevaa suruali ya jeans na tsheti nyeusi aliingia na kufunga mlango. Jamaa mwingine aliyetoka upande wa mbele wa abiria naye aliingia kwenye kiti chake na mtu mwingine aliyekuwa dereva nilimuona aki-ondoa mguu wake kwenye breki.

Kabla sijafungua mdomo wangu; jamaa mwenye tsheti nyeusi alinichomeka sindano shingoni na mara moja nilihisi usingizi mzito ukinijia. Nilijaribu kufungua mdomo kupiga kelele sikuweza. Nilijaribu kujifurugusa siku-

weza. Niiliishiwa nguvu. Nilijikuta napiga kelele moyoni tu.

“Mungu nisaidie”

SURA YA 3

Kama ukungu ukifunguka mbele yangu ndivyo nilivyojikuta nafumbua macho yangu taratibu. Nilijihisi nimechoka kama mtu aliyetoka kulala usingizi wa muda mrefu. Koo langu lilikuwa limekauka kiasi kwamba nilivyojaribu kumeza mate nili-hisi maumivu. Niligundua mara moja kuwa sikuweza kunyanyua mikono yangu kwenye kiti nilichokaa na nilipojaribu kunyanyuka sikuweza vile vile. Niliguna kidogo kwa maumivu kwenye mikono yangu nilipo-jaribu kuilazimisha kunyanyuka. Nilikuwa nimefungwa kwa kamba kwenye kiti hicho. Miguu yangu pia ilikuwa imefungwa kamba. Niliweza kuhisi mpwitopwito wa damu ikip-ita katika mishipa yangu ikifuata mdundo wa moyo wangu.

“Bosi! Anaamka jamaa” nilisikia sauti nisi-yoifahamu ikizungumza kwa sauti ya juu. Nilijitahidi zaidi kufungua macho yangu kuangalia mahali nilipo na niko na kina nani. Hata hivyo ukungu ule uliniishia na nikaweza kuona vizuri; niliinua kichwa changu kuangalia niko mahali gani.

“Aha nakuja mara moja” sauti nyingine ilimuitikia yule wa kwanza na kukapita ukimya kidogo wakati tunamsubiria huyo bwana. Macho yangu yalinipa taarifa mbalimbali japo nilijaribu kuzipa kila aina ya tafsiri ili kupata maana. Sakafuni kulikuwa na makaratasi yaliyochafuka na kuzagaa kila mahali; hakukuwa na sehemu ambayo hai-kuwa na makaratasi hayo. Niliweza kuona makabati yaliyovunjika yakiwa na makarata-si na mafaili yaliyochakaa. Kutoka nilipoku-wa nimekaa niliweza kuona viti nane vya plastiki vya rangi ya njano. Mwanga pekee uliyokuwa ukiingia ndani ya jengo hilo uli-tokea kwenye madirisha makubwa manne yaliyokuwa yamefunikwa na mapazia manne yakitenganishwa na mlango mmoja. Jengo lilikuwa limechaa na sikuweza kusikia kitu chochote. Nilipojaribu kuangalia juu niliona dari lililokuwa na alama za kuvuja huku sehemu ya dari hiyo ikiwa imebomoka na kuning’ingia. Niliweza kugundua harufu kali kama ya uchafu uliokaa pale muda mrefu nilipoangalia mbele zaidi kwenye hilo jengo kubwa niliweza kuona milango miwili midogo iliyokuwa na maandishi ya maneno ya matusi matusi; niliamini kuwa inaweze-kana kule kulikuwa chooni au sehemu fulani ambapo uchafu ulikuwa ni maskani yake. Nilijitahidi kujiinua kidogo nikae sawa lakini yale maumivu mikononi yalirudi tena. Aliyekuwa amenifunga alikuwa amepania kweli kunifunga nisitikisike.

“Vicent, Vicent, Vicent” sauti nzito ilisikika nyuma yangu na hyo aliyesema alinipiga piga taratibu mgongoni kama rafiki yangu fulani hivi. Sikuweza kusema kitu. Alikuja mbele yangu. Sikutambua wala sikujua yeye ni nani; nilihisi kulikuwa na watu wen-gine aliokuwa nao japo idadi yao sikuweza kuibaini mara moja ila nilikuwa na uhakika ukiongoza yule aliyemuita na wale tulio-kuwa ndani ya gari basi hakukuwa na watu chini ya watano pale.

“Kwanini ulikimbia kazini asubuhi?” alin-iangalia na kunikazia macho akiniacha nim-patie jibu.

“Aah aah” nilijaribu kutafuta maneno lakini sikuweza mara moja maana sikujua ni jibu gani lingeweza kutoshelesha swali nililoulizwa. Lakini zaidi mimi mwenyewe sikuwa nimefikiria swali hilo zaidi.

ITAENDELEA TOLEO LIJALO

RIWAYA: SIKU YA MKOSI - 2

Page 14: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

Ciliquamet velent lore vel ing exero cor iustionse eu

14 ZAMAMPYA Machi 13, 2017

KICHUYA UMETOA FUNZO SIKU YA YANGA NA SIMBAKuna mambo mengi ya kujifunza lakini haya makubwa zaidi

Na. Joseph MandalaKabla sijaendelea na makala hii naomba

kukiri na kusema kuwa Yanga kwangu mimi walikurupuka kumpisha Hans Van Pluijm sio kwakuwa wamefungwa na Simba hapana ila sababu ilionifanya nikiri na kukubali kuwa Yanga walikuwa sahihi kwa kumpa nafasi George Lwandamina. Sababu zangu kwa Hans Van Pluijm kumpi-sha George Lwandamina zilikuwa tatu, Namba sita (Kiungo mkabaji), Maamuzi ya kimfumo na kuwa na viungo wachache. Kwangu mimi kadi ya Jonas Mkude ilikuwa ni chanzo cha kutokujua maamuzi ya kim-fumo ya Hans Van Pluijm maana baada ya kutoka kwake hakuna badiliko la kimfumo lililofanyika na kuruhusu Simba au Joseph Omog kuendelea na mipango yake ya kimfumo kuikabili Yanga na mwisho wa siku Simba wanapata sare, suala la Joseph Omog ni hadithi ilioanzia pale Azam Sports Club lakini Joseph Omog amebakia mshin-di wakati wote dhidi ya Yanga kimfumo. Kadi ya Besele Bukungu imeendelea kuwa sindano ndani ya kidonda katika fikira zangu juu ya uamuzi wa kimfumo dhidi ya George Lwandamina maana baada ya kutolewa kwa beki huyu Yanga au kocha George Lwandamina alien-delea kubaki na mfumo uleule kwa maana ya mfumo wa mwanzo wa 4:4:2. Pamoja na Simba kuwa pungufu wakati huo tukumbuke Thabani Kamusoko akiwa yupo nje na ndani alikuwepo Jus-tine Zulu huku alipoingia Juma Said Makapu wachezaji ambao ni viungo wakabaji, mpaka alipoingia Juma Maha-dhi bado Yanga kimfumo walibakia kuwa vilevile kosa ambalo alikuwa amelifanya Hans Van Pluijm siku ya 01.10.2015. Tutakubaliana na mimi kuwa kucheza mfumo wa 4:4:2 wachezaji kwa kila idara wanapaswa kuwa timamu kim-chezo na mfumo huu uondoa ush-irikiano wa kiuchezaji na kubakia na ushirikiano wa kimfumo kiuchezaji. Ukiangalia Yanga beki zao zilikuwa sawa yaani Haji Mwinyi, Abdul, Kelvin Yondani na Andrew Vicent na kikubwa hali ya mchezo ilikuwa kubwa sana kwa Andrew Vicent na hapa kiufundi mimi nilianza kuliona kosa la kimsingi juu ya ucha-guzi kati ya Canavarro na Andrew Vicent kucheza mbele ya viungo hatari walio na washambuliaji aina ya Ajib na Mavugo na uchaguzi sahihi ulikuwepo kama mfumo wa 4:4:2 ungeendelea kufanya kazi lakini baada ya Thaban Scara Kamusoko kutoka na mfumo wa 4:4:2 ulipaswa kubadilika. Yanga walifungwa na Simba kwa matumizi sahihi na maamuzi ya viungo wa Simba maana ndio waliokuwa na uwezo wa kuamua mfumo na aina ya mpira baada ya kuingia kwa Ndemla na Kichuya wali-wafuata Yanga waliokuwa wamekaa golini

UTAMADUNI SANAA BURUDANI

kwao kimfumo maana bado walikuwa katika mfumo mama wa 4:4:2 na katika ya uwanja walikosa mtu wa kusambaza mpira maana nilishindwa kuelewa baada ya Tha-bani Kamusoko kutoka nje ya uwanja pia Haruna Nyonzima alienda likizo ya wapi? Kitu ambacho nashindwa kuelewa George Lwandamina alikuwa wapi kukiona na kufanya maamuzi ya kimfumo maana Juma Said Makapu si mwepesi wa kupokea na kugawa mpira kama Thabani Kamusoko. Nilipoona Thabani Kamusoko kushindwa kuendelea na mchezo nilikuwa Dodoma Carnival nilimgeukia swahiba yangu na kumwambia tuondoke mpira umeisha na Simba wameshinda maana nilijua kuwa hakuna mchezaji aliekuwa na uwezo wa kutoa huduma kama yake na Yanga waliku-wa wazuri kupitia kwa Thabani Kamusoko kitu ambacho hata George Lwandamina alishindwa kutoa suluhisho la mgongo wa timu ya Yanga dhidi ya viungo wa Simba. Swali hili hakuna asiejua kuwa Joseph Omog ni muumini wa matumizi ya viungo katika mchezo wowote na hiki alishawahi kuku-tana nacho Hans Van Pluijm wakati Joseph Omog akiwa Azam Sports Club na Simba pia. Kichuya ameendelea kutoa funzo la kuwa Yanga wanahitaji kuwa na viungo wengi na wa aina mbili yaani viungo wa kushambulia

wa aina mbili wakusaidia kufunga, wakufun-ga na aina nyingine ni wakulinda wanaofa-nana kiuwezo na tatizo la viungo ndio tatizo lililosababisha Yanga kukosa mafanikio katika kombe la shirikisho hatua ya makundi. Katika makala zangu zilizopita niliwahi kusema kuwa sina muda wa kumpa Obrey Chirwa kama mfungaji mzuri jambo hili nimeendelea kukubaliana nalo maana kufun-ga ni sanaa ya maamuzi ya utumiaji wa sanaa ya kufunga pamoja na kazi nzuri ya kusababi-sha penati na kadi nyekundu bado aliendelea kutoa ushirikiano mdogo kwa Amis Joselyn Tambwe kitu ambacho kiliigharimu timu sana pamoja na kuwa sifa kubwa ya mshambuliaji ya mwanzo ni uchoyo ila sio katika mchezo mkubwa unaohitaji nafasi za kufunga ambazo utokea mara chache sana au kufanya makosa ya kukaba ya Vicent Dante, Bukun-gu na Lufunga lazima utapata adhabu tu. Tutaendelea kuikumbusha Yanga na hasa kocha kuhusu matumizi ya wachezaji dhidi ya timu pinzani au aina ya wachezaji Fulani matu-mizi ya Said Makapu na Vicent Dante yalikuwa na changamoto kubwa katika mchezo wa uli-opita hasa kwa aina ya wachezaji wa Simba. Laudit Mavugo anapata nafasi ya kupiga kichwa ,ingekuwa dhidi ya Canavarro au Bossou lile lisingetokea maana ndani ya kisanduku cha goli huwa hatukabi kwa nafasi ila mtu kwa mtu na ndio tabia ya

Vincent Bossou na Canavarro au ilikuwaje Obrey Chirwa ageuke mbele ya Bukungu au mbele ya Lufunga na kusababisha matatizo yale ya penati na kadi nyekundu. Hapa kuna kitu cha kujifunza kikub-wa kuwa kuna wachezaji kiuwezo hawastahili kuchezea vilabu hivi. Oni na taa nyekundu imewaka jang-wani ni nani anaizima au ataizima? Kuwa mwisho wa kutamba kwa Yanga kumefika na kweli wahenga walisema “Ngoma iki-vuma sana upasuka” na Hakuna Marefu yasio na mwisho kiufupi hali si shwari pale jangwani ndani na nje ya uwanja pole sana ndugu yangu George Lwan-damina maana hali ya utulivu kuipata kwa sasa pale jangwani ni shida sana. Lakini hili ndio kilio cha kila siku kuwa pamoja na kuwa na wafadhili Simba na Yanga zinapaswa kuendeshwa kitaalamu na sio kwa mtindo huu, sababu kubwa ya Yanga kufungwa ni kukubali kumtegemea Yusuph Manji kama mfadhili kwa kila kitu kifedha, baada ya mfadhili huyu kupata matatizo ilikuwa sio rahisi kiungwana kuon-gelea mada ya fedha na mchezo badala ya tatizo lililopo na Yanga kukosa fedha kwa ajili ya kambi na maandalizi kwa ujumla. Ukiangalia kwa utafiti mzuri utagundua kuwa chanzo kimeanzia mbali sana na ni pale Yanga Yetu ilipokataliwa kukodishwa timu na tangia pale mambo mengi ndani ya Yanga kifedha kimtazamo hayaendi sawa japo wahusika wanakanusha hili. Swali dogo tu kama Yanga Yetu inge-pewa timu au mchakato ungekuwa unaenda vizuri tatizo la Donald Ngoma na Vicent Bossou lingekuwepo? TFF wanapaswa kuendesha vilabu hivi kisasa na sio kijima au kiubepari maana fursa zipo za timu hizi kutengeneza pesa ila inabakia kuwa kitendawili pamoja na kuwepo kwa matumizi makubwa ya SMARTPHONES nchini. Naomba kuwapa mwanga kuwa Yanga wasipokuwa makini safari yao kima-taifa itaishia kwa Zanaco , kwa wale tulioangalia uwezo wa Zanaco tuta-hitaji kuweka pembeni siasa zetu hizi. Pia kuna kitu cha kujadili kimapana sana hivi Haruna Nyonzima kila mchezo dhidi ya Simba huwa wapi? Japo wakati Thabani Kamusoko akiwa ndani alionesha uhai japo kwangu anabakia kuwa mchezaji wa mechi ndogo au Simba ndio timu inayojua sana kumficha Haruna japo siwezi kumlaumu. Dida kwa goli la mwisho ila pongezi ziende kwa Shiza Kichuya. YANGA MALIZENI MATATIZO YA WACHEZAJI WENU LIGI BADO.

Page 15: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

Machi 13, 2017 ZAMAMPYA 15

Page 16: Wengine wafukuzwa, wavuliwa uongozi, wakaripiwa · Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia), Sofia Simba (katikati) na Adam Kimbisa (Kushoto) walipojitokeza kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya

16 ZAMAMPYA Machi 13, 2017

AIFUNGIA KRC MAGOLI KAMA SHEREHENahodha wa timu ya taifa Mbwana Samatta azidi kung’ara kimataifa.

Na. Tizzo ChumaNAHODHA WA timu ya Taifa ya soka ya Tan-zania - Taifa Stars Mbwana Samatta amezidi kung’ara katika soka la mataifa baada ya kuendelea kuifungia timu ya KRC ya Ubel-giji magoli kama vile anafanya sherehe.

Mchezaji huyo mshambuliaji wiki iliyopita Alhamisi aliipachikia timu yake mabao mawili maridadi katika mashindano ya UEFA raundi mtoano dhidi ya timu ya Gent ya Ubelgiji vile vile. Timu hizo mbili ambazo zinafukuzana katika ligi ya daraja la kwanza ya Ubelgiji zilijikuta zikicheza mchezo wa mashambu-lizi ya nguvu lakini ni Genk ya kina Samatta ambayo hadi timu zinakwenda mapumziko ilikuwa inaongozwa kwa mabado 4-1.

Mabado hayo yalifungwa na Omar Colley, Mbwana Samatta na Jere Uronen.

Baada ya mapumziko timu hizo ziliendelea kushambuliana lakini ilikuwa ni KRC Genk ya kina Samatta iliyoendelea kufanya ukweli na ukweli ulifanywa na mchezaji huyo wa Kitanzania pale alipoipatia timu yake bao la

DAR-ES-SALAAM, MKUU wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Bw. Paul Makonda ameanzisha zogo jingine ambalo limezua mjadala mkubwa kitaifa pale alipoendelea kuwataja watu mbalimbali ambao amedai kuwa kwa namna moja au nyingine wanahusika au kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.

Kutajwa kwa Manji na Makonda kume-lirudisha tena jina la mmoja wa wafanya-biashara wakubwa nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga mbele ya wananchi. Hii si mara ya kwanza kwa Manji kutajwa na baadhi ya watu mashuhuri na mara zote amekuwa akijitetea vikali.

Safari hii vile vile Manji aliitisha kikao na waandishi wa habari akilaani vikali kutajwa na Makonda na kuwa yeye mwenyewe ata-jipeleka mwenyewe polisi bila kusubiri siku ambayo aliambiwa aende yaani Ijumaa. Manji alienda jana Alhamisi ambapo alitu-

mia muda wa karibu masaa sita akizung-umza au kuhojiwa na polisi.

Manji alilaani vikali kitendo cha Makonda kumuita aende polisi kwani amemvunjia heshima yake na jina lake. Akizungumza kwa hasira Manji alidai kuwa kuhusishwa kwake na masuala ya madawa ya kulevya kunaweza kumletea matatizo hasa ana-posafiri na timu yake ya Yanga.

“Huwezi kuniita mimi kama mbwa” alisema Manji.

Pamoja na Manji watu wengine mashuhuria mbao walitajwa katika awamu ya pili ya orodha ya Makonda ni pamoja na mhubiri na mchungaji maarufu nchini Askofu Joseph Gwajima ambaye naye ali-takiwa kujipeleka polisi.

Hadi hivi sasa ni wasanii kadhaa ambao Makonda aliwataja wiki iliyopita ambao tayari walienda kukutana naye polisi na baadhi yao kufikishwa mahakamani ambapo nane kati yao wamewekwa chini ya uangalizi maalum.

Haijulikani hata hivyo ni lini Manji atafun-gua kesi dhidi ya Makonda kwa kumchafua jina lake.

Makonda tayari ameshajiingiza kwenye kile kinachoonekana ni matatizo baada ya kuitwa na Bunge la Jamhuri ya Muun-gano kutokana na madai ya kulidhalilisha na hivyo Bunge kwa kauli moja bila kujali vyama likaamua kutoa wito wa kibunge (summons) ili Makonda aende kujieleza mbele ya Kamati ya Uongozi wa Bunge.

MANJI ATAJWA NA MAKONDA SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA

Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amtaja Yusuf Manji katika harakati zake za kupambana na madawa ya kulevya Mkoani Dar-es-Salaam

Na. Mwandishi Wetu

ZAMAMPYA michezoSAMATTA ANG’ARA

tano la sherehe. Hadi mechi inaisha KRC Genk ilikuwa na mabao 5-2.

Kama hiyo haitoshi katika ligi ya Ubel-giji siku ya Jumapili, Mbwana Samatta tena aliongoza kufungua kapu la magoli pale alipopachika bao la kwanza dhidi ya Westerlo. Genk ilishinda mchezo huo kwa mabao 4-0. Mechi ya marudioano ya mashindano ya UEFA itafanyika Ijumaa ijayo na kama Genk itashinda itakuwa ni mara ya kwanza

kuingia robo fainali za mashindano hayo yanayoangaliwa na mamilioni ya watu pote duniani na ambayo huwa na wachezaji karibu wote maarufu wa Ulaya na wale wa nchi za kigeni wanaocheza soka Ulaya. Hii ni mara ya kwanza kwa mchezaji wa Kitanzania kushiriki mashindano hayo makubwa duniani.

Mbwana Samatta akishangilia bao la timu yake siku ya Alhamisi