4
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA Simu: 255-22-2114615, 211906-12 Barua pepe: [email protected] Barua pepe: [email protected] Tovuti : www.foreign.go.tz Nukushi: 255-22-2116600 20 KIVUKONI FRONT, P.O. BOX 9000, 11466 DAR ES SALAAM, Tanzania. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Safari za Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete Nje ya Nchi Wizara imesikitishwa na taarifa za uongo zilitolewa katika vyombo vya habari kuwa Mhe. Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uongozi wake wa miaka 10 ametumia Shilingi trilioni 4 kwa ajili ya safari za kikazi nje ya nchi, ambazo ni wastani wa bajeti nzima ya wizara kwa miaka mitano (5). Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kutoa ufafanuzi kuwa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, kiasi kikubwa kabisa cha bajeti kuwahi kutengwa kwa ajili ya safari za Viongozi Wakuu yaani Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ni shilingi

Ziara Za Rais JK

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Ziara Za Rais JK

Citation preview

Page 1: Ziara Za Rais JK

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Simu: 255-22-2114615, 211906-12

Barua pepe: [email protected] pepe: [email protected] : www.foreign.go.tzNukushi: 255-22-2116600

20 KIVUKONI FRONT, P.O. BOX 9000,

11466 DAR ES SALAAM, Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Safari za Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete Nje ya Nchi

Wizara imesikitishwa na taarifa za uongo zilitolewa katika vyombo

vya habari kuwa Mhe. Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania katika uongozi wake wa miaka 10

ametumia Shilingi trilioni 4 kwa ajili ya safari za kikazi nje ya nchi,

ambazo ni wastani wa bajeti nzima ya wizara kwa miaka mitano

(5).

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda

kutoa ufafanuzi kuwa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani mwaka

2005, kiasi kikubwa kabisa cha bajeti kuwahi kutengwa kwa ajili

ya safari za Viongozi Wakuu yaani Rais, Makamu wa Rais na

Waziri Mkuu ni shilingi bilioni 50 ambazo zilitengwa kwa Mwaka

wa Fedha 2014/2015 kwa ajili ya Idara ya Itifaki. Kwa miaka

mingine yote wastani umekuwa ni kati ya shilingi bilioni tano hadi

25 kulingana na mahitaji ya idara hiyo.

Page 2: Ziara Za Rais JK

Ifahamike kuwa kiasi hicho cha shilingi bilioni 50 ni bajeti nzima

ya Idara ya Itifaki, ambapo kuna fungu maalum kwa ajili ya ziara

za viongozi. Fungu hilo linagharamia makundi makuu matano

kama ifuatavyo:

1. Kundi la Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa

Taasisi na Walinzi;

2. Kundi la Makamu wa Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au

Wakuu wa Taasisi na Walinzi;

3. Kundi la Waziri Mkuu wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au

Wakuu wa Taasisi na Walinzi;

4. Kundi la Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nje ya nchi

wanapotembelea Tanzania; na

5. Kundi la Wajumbe Maalum wanaokuja nchini kuleta taarifa

muhimu kwa Rais.

Makundi yote haya hugaramiwa na Serikali kupitia Wizara ya

Mambo ya Nje ndani ya bajeti ya Idara ya Itifaki kifungu cha Ziara

za Viongozi.

Aidha uandaaji wa bajeti ya Wizara chini ya Idara ya Sera na

Mipango unahusisha wadau wengine nje ya Wizara kama vile

Kamati ya Bunge ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na

hupitishwa kila mwaka na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania.

Page 3: Ziara Za Rais JK

Tunapenda kuwaatahadharisha wananchi juu ya watu wanaotoa

taarifa za uongo kwa madhumuni ya kujenga chuki dhidi ya

Serikali. Ikumbukwe kuwa ziara za viongozi zinazoratibiwa na

Wizara ya Mambo ya Nje zina mafanikio makubwa kwa nchi na

Watanzania kwa ujumla.

Wizara inaandaa taarifa ya ndefu ya utekelezaji wa majukumu ya

Wizara, changamoto na mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi

cha miaka kumi ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete

ambayo itatolewa kwa umma kwa lengo la kutoa elimu zaidi.

MWISHO.

Imetolewa na:Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,17 Septemba 2015