Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 1 of 25
This booklet on HIV/AIDS was developed by the Tanzania Home Economics Association with support from Our Bodies Ourselves. Other booklets and more information on the project are available at http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania. VIRUSI VYA UKIMWI NA UKIMWI Wakati naongea na mpenzi wangu wa kiume kwenye simu baada ya kuwa
amechukua majibu yake ya vipimo vya ukimwi alikiwa kama mtu anayefanya
mzaha. Halafu aliniambia kuwa majibu yalionyesha kuwa ameathirika. Nilipatwa
na mshangao mkubwa na kufadhaika sana…ila nilishukuru tu kwa kuwa nilitumia
kondomu…Mpaka kufikia wakati huu nimeishapima mara nyingi tu, na
sijaathirika. Na jambo hili limetuzindua mimi pamoja na marafiki zangu wa kike.
Wengi wao nao pia wamepima na wameanza kuwa waangalifu zaidi.
Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza
bila kukoma.
Ni lazima tujipigie kampeni. Hauko peke yako…Hatuna haja ya kuwa na aibu. Ni
muda muafaka sasa tuishi maisha yetu wenyewe.
Ukimwi ni janga la dunia nzima. Kwa wale miongoni mwetu ambao
hatujaambukizwa VVU tunapaswa kujilinda dhidi ya maambukizi haya. Kwa wale
kati yetu ambao tunaishi na VVU/Ukimwi tunahitaji huduma za muhimu na
mitandao ya misaada, tiba bora zaidi, na msaada wa serikali ili tuweze kuishi, na
kadiri tutakavyoweza kuishi na kuzuia maambukizo zaidi kwa wenzi na watoto
wetu. Sote tunahitajika kupigia kampeni uanzishwaji wa huduma za umma za
afya, upatikanaji wa fedha zaidi kwa ajili ya utafiti, na huduma bora zaidi ya afya.
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 2 of 25
Taarifa kuhusu VVU/Ukimwi hubadilika kwa haraka sana. Tafadhali tumia Sura
hii kama msingi wa kukuwezesha kutambua wapi unaweza kupata tiba na taarifa
za ushauri nasaha zinazoenda na wakati.
GONJWA LA UKIMWI UKIMWI ( Upungufu wa Kinga Mwilini) ni ugonjwa uliogunduliwa na wataalam wa
afya nchini Marekani mnamo miaka ya 1980. Hapa Tanzania ugonjwa huu
ulifahamika rasmi mnamo mwaka 1983, na ulianzia mkoa Kagera. Kwa sasa
ugonjwa huu umesambaa mahali pote duniani. VVU (Virusi Vya Ukimwi)
husababisha Upungufu wa Kinga Mwililini (UKIMWI) kwa kushambulia seli za
aina ya T (chembechembe nyeupe za damu za CD4), ambazo ni muhimu kwa
mfumo wa kujikinga wa mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Kwa sababu
kitendo hiki cha kuharibu kinga ya mwili hutokea polepole sana, watu wengi
wanaweza kuishi na virusi hivi kwa muda wa miaka nane mpaka kumi kabla
hawajaugua Ukimwi. Dalili kuwa mtu ameshaanza kuugua Ukimwi ni pamoja na
kupata magonjwa nyemelezi na kiwango cha idadi ya seli aina ya T kushuka
chini ya 200.
Katika miaka ya hivi karibuni, ugunduzi wa dawa za kupunguza makali ya virusi
(ARV) umesaidia watu kuishi miaka mingi wakiwa na virusi vya ukimwi. Viwango
vya vifo vimepungua kwa wale wenye kuweza kuzipata dawa hizi, na
maambukizi ya VVU yamekuwa ugonjwa sugu unaoweza kudhibitiwa. Lakini
licha ya juhudi kubwa za utafiti zinazofanywa, bado hakuna ugunduzi wa kinga
wala dawa ya Ukimwi.
Takwimu zimeonyesha kwamba watu wengi wamepata elimu juu ya Ukimwi na
hivyo kupunguza maambukizo mapya, lakini maambukizi mapya kama elfu
arobaini bado hutokea kila mwaka nchini Marekani, na gonjwa hili linaendelea
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 3 of 25
kuangamiza wengi kwenye maeneo ya nchi masikini duniani, hasa nchi za kusini
mwa jangwa la Sahara, za kusini mashariki mwa bara la Asia, Ulaya mashariki
na kwenye visiwa vya Karibiani. Takwimu pia zimeonyesha kuwa tangu kitabu
hiki kipigwe chapa mwaka 1998, idadi ya watu wazima wanaoishi na virusi vya
ukimwi duniani imeongezeka kutoka watu milioni kumi mpaka milioni 37.8 na
kutoka watoto milioni moja mpaka takriban watoto milioni mbili. Inakadiriwa
kuwa zaidi ya watu milioni 20 tayari wamepoteza maisha kutokana na gonjwa
hili la Ukimwi kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita, na mpaka kufikia mwishoni mwa
mwaka 2003, inakadiriwa kuwa idadi ya watoto wapatao milioni 15 walikuwa
wamepoteza mzazi mmoja au wote wawili kutokana na Ukimwi. Gonjwa hili
limeathiri nguvu kazi ya nchi zinazoendelea kwenye nyanja mbalimbali kama vile
huduma za afya, uchumi na hata tabaka za kijamii kwa ujumla, na bado hakuna
dalili zozote za ufumbuzi wa tatizo hili.
WANAWAKE NA VVU / UKIMWI Mpaka kufikia disemba mwaka 2003, karibia asilimia 50 ya watu waliokuwa
wakiishi na VVU/Ukimwi duniani kote walikuwa ni wanawake. Nchini Marekani,
takriban asilimia 25 ya watu wanaoishi na VVU/Ukimwi ni wanawake. Kati ya
mwaka 1998 na 2002, vipimo vilionyesha kuongezeka kwa maambukizi mapya
kwa asilimia 7 zaidi miongoni mwa wanawake, ikilinganishwa na kupungua kwa
maambukizi kwa asilimia 5 miongoni mwa wanaume nchini humo. Nchini
Marekani na duniani kwa ujumla, wanawake wengi huambukizwa ukimwi kupitia
mahusiano ya kingono na wanaume, na wanawake wa mbari nyingine (wasio
weupe) bado wanaendelea kuongoza katika kupata maambukizi haya. Huku
wakiwa wanawakilisha asilimia 12 tu ya idadi ya watu wote nchini Marekani,
wanawake wa Kimarekani wenye asili ya Afrika wanawakilisha nusu ya
maambukizi mapya yanayotokea nchini humo, na kiwango hiki bado
kinaongezeka kila kukicha. Kwa ujumla viwango vya wanawake vinavyotokana
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 4 of 25
na VVU/Ukimwi vimepungua tangu miaka ya katikati ya 1990, lakini viwango vya
vifi miongoni mwa wanawake wa Kimarekani wenye asili ya Afrika na wa Kilatino
vimebakia juu sana kuliko ilivyo kwa wnawake weupe. (Kwa tarifa zaidi, tazama
“VVU/Ukimwi miongoni mwa Walatino na Watu wa Visiwa vya Pasifiki/Asia”
[W35] kwenye tovuti, www.ourbodiesourselves.org.)
UKWELI AU UONGO
• Wanawake wengi hupata VVu kupitia matumizi ya dawa aina ya IV.
Uongo. Zaidi ya asilimia 70 ya maambukizi ya VVU miongoni mwa wanawake
hutokana na kuambukizwa katika mahusiano yao na wanaume.
Jambo la kushukuru ni kwamba wataalamu wa afya, wanasayansi na
wanaharakati wanatilia mkazo zaidi uhitaji wa kipekee wa wanawake kuhisiana
na VVU/Ukimwi. Wanawake wamekuwa wakijumuishwa zaidi kwenye majaribio
ya kitabibu, ikiwa ni pamoja na kundi kubwa la kitaifa lijulikanalo kama Women’s Interagency HIV Study, ambalo linachunguza kwa namna gani kuongezeka kwa
VVU na matibabu yanawaathiri wanawake. Watoaji wa huduma za afya kwa
sasa wana vifaa bora zaidi vya kuweza kupima dalili za VVU/Ukimwi
zinazohusiana na uzazi, na wanatumia dawa ya kupaka na kifaa maalumu cha
kwenye uke na mlango wa kizazi katika kukinga maambukizi ya kansa ya mlango
wa kizazi yanayoweza kutokana na kuingiliwa na kitu chochote ukeni, kiashiria
cha kipekee kwa wanawake cha Ukimwi. Matibabu mapya yamepunguza idadi
ya watoto wanaozaliwa na maambukizi ya VVU (tazama “VVU na Ujauzito,”
ukurasa wa 304). Na kwenye jumuiya nyingi, wanawake wenye maambukizi ya
VVU na Ukimwi wanasaidiana wenyewe kwa wenyewe, wakifanya kampeni
kuwaelimisha wengine, kufundisha namna ya kujikinga, wakijaribu kurudia hali
yao ya kawaida baada ya kuacha kutumia vilevi, na kupeana matumaini.
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 5 of 25
Kibaiolojia, wanawake wanaweza kuwa katika hatari zaidi ya kuambukizwa
VVU kuliko wanaume kupitia kuingiliwa na mtu wa jinsia nyingine kwa sababu
manii zenye virusi vya ukimwi hubakia kwa muda mrefu zikiwa zimegusana na
ukuta laini wa uke kuliko majimaji yaliyo na virusi yanayotolewa na uke
yanavyobakia kwenye uume. Kuna sababu nyingine pia zinazotuongezea
uwezekano wa kuambukizwa kwa urahisi. Hata kama tuko kwenye mahusiano
na mwanamume mmoja, bado pia tunaweza kuwa kwenye hatari ya
kuambukizwa Ukimwi. Kuna vipindi wanaume wanawashinikiza au
kuwalazimisha wanawake kufanya mapenzi bila kutumia kinga, na wakati
mwingine wanawake husita kuongelea juu ya ngono salama kwa hofu ya
kuumizwa au kuachwa. Hofu ya kupigwa na/au utegemezi kwa mwenzi wa kiume
kiuchumi kunaweza kutuondolea kabisa uwezo wa kujikinga wakati wa kufanya
mapenzi. Utafiti uliofanywa miongoni mwa wanawake wa Kimarekani wenye asili
ya Afrika wa Los Angeles ulionyesha kuwa uwezekano wa wapenzi kutumia
kondomu ulikuwa mdogo kama mwanamke alikuwa anamtegemea mwenzi wake
wa kiume kumlipia pango la nyumba.
Matumizi ya dawa kwa kujidunga kwenye mishipa ya damu – moja kwa
moja, kwa kupitia kushikrikiana sindani, na isivyo moja kwa moja kupitia kufanya
ngono bila kinga na mtumiaji wa kiume – kunachangia kwa kiasi kikubwa
usambazaji wa maambukizi ya VVU kwa wanawake nchini Marekani. Mpaka
kufikia mwishoni mwa mwaka 2002, asilimia 26 ya Wanawake wa nchini
Marekani wanaliokuwa wakiishi na VVU/Ukimwi walikuwa wamepata maambukizi
haya kupitia matumizi ya moja kwa moja ya dawa aina ya IV. Kati ya asilimia 72
ya wanawake wa Kimarekani wanaopata maambukizi kupitia kujamiiana, asilimia
kubwa wamepata VVU kutoka kwa mwenzi wao wa kiume aliyetumia dawa za IV.
Inaweza kuwa vigumu kidogo kwa wanawake wasio weupe, wanawake waishio
kwenye mazingira ya umasikini, na wale kati yetu ambao ni wajawazito au tuna
watoto wanaotutegemea kufaidika na programu bora za tiba. Hata pale
tunapoweza kupata mchanganyiko wa tiba wenye nguvu (tazama “Machaguo ya
Matibabu,” ukurasa wa 302), mahitaji yake ya ratiba za ulaji pamoja na athari
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 6 of 25
zake vinaweza kuleta mazingira magumu kuweza kuzitumia tiba hizi hasa pale
tunapokuwa tumetawaliwa na matumizi ya dawa hizi. Hata hivyo, ugunduzi wa
tiba mpya, ikiwa ni pamoja na kanuni za mlo, mazoezi, michezo n.k. kwa siku
moja, kumerahisisha utoaji wa tiba.
Suala lingine ni kwamba mara nyingi hatufahamu ikiwa wenzi wetu wa kiume
wanafanya mapenzi na wanaume. Uchunguzi iliofanywa hivi karibuni na Kituo
cha Kudhibiti Magonjwa (CDC) umeonesha kuwa zaidi ya moja ya tatu ya
wanaume wa kimarekani wenye asili ya Afrika ambao wameathirika na Ukimwi
walisema waliwahi kufanya mapenzi na wanaume, lakini ni idadi ndogo sana ya
wanawake wenye asili ya Afrika walionekana kufahamu kuwa wenzi wao
walishawahi kufanya mapenzi na wanaume wenzao.
KUJITUNZA
Kwa sababu mbalimbali, huwa hatulipi kipaumbele suala la kujali afya zetu
wenyewe. Umakini mdogo unaoonyeshwa na baadhi ya taasisi za tiba kwa
wanawake – hasa wale wasio wazungu, masikini, wasiokuwa na bima ya afya,
na wale wasioongea kiingereza – bado unatusukuma wengi wetu kuchelewa
kutafuta huduma ya afya na kupima. Tunaweza kutopata matibabu dhidi ya
magonjwa ya zinaa au muwasho wa sehemu za ukeni, kitu ambacho kinaweza
kutuweka katika uwezekano mkubwa zaidi wa kupata VVU pale tunapokutana na
mtu aliyeathirika. Kwa wastani, wanawake wana rasilimali za kiuchumi kidogo
zaidi kuliko wanaume; pia tuko katika uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa wazazi
pekee na waangalizi wa wale wanaoumwa. Baadhi yetu hupata tiba pale tu
watoto wetu wanapoonekana kuwa wameathirika.
Lakini bado tunapaswa kuzijali afya zetu na kufanya juhudi kubadilisha
mfumo mzima unaotukwamisha kufanya hivi. Kuboresha hali ya wanawake juu
ya VVU/Ukimwi nchini Marekani kutatokana na mabadiliko makubwa ya kimsingi
yatakayojikita katika kuondoa umasikini, ubanguzi wa kimbari, na unyanyasaji wa
kijinsia. Mara nyingi sana kunakosekana uungwaji mkono na jamii kwenye vifaa
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 7 of 25
ambavyo tunavihitaji: programu za matibabu za dawa, makazi, lishe ya kutosha,
huduma ya afya, na uangalizi wa watoto. Sote tuna haki ya kuwa na afya bora,
kufurahia kufanya mapenzi bila kuhatarisha maisha yetu, kujijali wenyewe na
kuwajali wengine, na kupata huduma ya afya tunayoihitaji. Wanaharakati wa
VVU/Ukimwi wanaweza kutusaidia kuhakikisha haki hii inapatikana kwa kila
mwanamke. (Kwa maelezo zaidi, tazama “Kujitunza” [W36] kwenye tovuti yetu,
www.ourbodiesourselves.org.)
MAAMBUKIZI YA VVU Maambukizi ya VVU yatafanyika kutoka mtu mmoja hadi mwingine iwapo;
1. Kutakuwapo na ‘idadi’ ya kutosha ya virusi. Giligili za mwili – damu, kilainishi
kitolewacho kabla ya manii, manii, majimaji ya ukeni, na maziwa ya mama –
zinaweza kubeba virusi vya kutosha kuweza kusababisha maambukizi. Mate,
machozi, jasho, mkojo, haja kubwa, na matapishi (isipokuwa vikiwa
vimechanganyikana na damu) havina virusi vya kutosha kuweza kukuathiri.
2. Lazima virusi vipate njia ya kupenya kuingia kwenye mfumo wako wa katika
damu. Virusi vya Ukimwi vinaweza kuingia kwenye mwili wako kupitia utando
telezi ambao unatenganisha uke na njia ya haja kubwa. Vinaweza kuingia moja
kwa moja kwenye damu kwa kupitia kuchangia ya dawa ya IV au ya kujichora
mwili; kwa kupitia kwenye ngozi kwenye sehemu uliyojikata, kidonda, au
mkwaruzo; au kwa kupitia utando telezi ilioko machoni, puani, na kwenye govi na
uwazi wa uume ulioko kwa mbele. Kufanya mapenzi kwa kutumia kinywa,
kulamba na/au kunyonya njia ya haja kubwa, kuingiza kiwiko, kuingiziana vidole,
na kubusiana kwa ndani ya kinywa na ulimi ni vitendo vinavyochukuliwa kuwa na
uwezekano mdogo wa kuambukiza VVU isipokuwa pale tu damu kugusana kwa
damu kutahusishwa.
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 8 of 25
Virusi hivi vinaweza kupenya kiurahisi zaidi katika undando telezi ikiwa kuna
michubuko midogo midogo, uvimbe, au kidonda kilicho wazi vinavyotokana na
maambukizi ya magonjwa. Hivyo basi, uwezekano wako wa kupata Ukimwi, au
wa kumwambukiza mwenzi wako, unongezeka sana Ple unapokuwa na ugonjwa
wa zinaa.
Kwa maelezo zaidi, tazama “Masharti Yanayohusiana na VVU/Ukimwi”
[W37] kwenye tovuti, www.ourbodiesourselves.org.)
KUJIKINGA DHIDI YA VIRUSI VYA UKIMWI
Inawezekana kuishi na VVU kwa miaka mingi bila kuonyesha dalili yoyote kwa
nje, na ndio maana ni muhimu sana kutumia kondomu kila mara unapojamiiana.
NJIA KUU ZA MAAMBUKIZI YA VVU
• Kushirikiana sindano au vitu vyenye ncha kali vilivyo na damu, ikiwa ni
pamoja na kujidunga dawa kama za aina ya IV (heroin, cocaine, speed)
au sindano zinazochangiwa kuchora, kutia chale au kutoga mwili
• Wakati wa ujauzito, kujifungua, na kunyonyesha, kutoka kwa mama hadi
kwa mtoto (tazama “VVU na Ujauzito,” ukurasa wa 304)
• Kuongezewa damu yenye maambukizi ya VVU na bidhaa za damu
(bidhaa hizi kwas asa zinafanyiwa vipimo kikamilifu nchini Marekani hivyo
hatari ni ndogo sana)
KUPATA TIBA HARAKA KUZUIA KUPATA MAAMBUKIZI
Kama unadhani utakuwa umejiweka katika mazingira yanayoweza kupelekea
ukapata VVU, unaweza kupata matibabu kwa haraka, bila ya kusubiri vipimo
kuonyesha uwepo wa VVU mwilini mwako. Watu ambao huchomwa na sindano
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 9 of 25
kwa bahati mbaya kwenye maeneo ya kutolea huduma za afya hutumia aina hii
ya matibabu, yanayoitwa kinga baada ya kuambukizwa. Hii inajumuisha kutumia
dawa ambazo zinatumiwa kwa ajili ya watu wanaoishi na VVU lakini zinazoweza
kuzuia athari za VVU katika hatua za awali. Unaweza kwenda kwenye chumba
za dharura ndani ya saa sabini na mbili (mapema zaidi ni vizuri) baada ya
kuambukizwa VVU na kupata matibabu upesi.Dawa hizo zinazotumiwa katika
dozi ya siku ishirini na nane zinaweza kukugharimu kama dola 1000 hivi, lakini
zina uwezo wa kukukinga usipate maambukizi ya VVU. Bima inaweza
kujumuisha baadhi ya gharama za tiba ya namna hii.
MATUMIZI SALAMA YA SINDANO ZA KUJIDUNGA
Kuchangia sindano, kama ilivyo kufanya ngono isiyo salama, hakusababishi
maambukizi ya VVU moja kwa moja. Hatari ya kuambukizwa itategemeana na
tabia yako mwenyewe. Kwa mfano, ikiwa unachangia sindano na mwenzi wako
mmoja na wote tayari mmepima na kuonekana hamna VVU na ugonjwa wa ini,
basi hamtokuwa kwenye hatari ya kumbukizana. Hatari ya kuambukizwa VVU,
na hepatitis B na C na hutokea pale unapochangia sindano na watu
usiowafahamu au wale ambao hawajapima VVU kuona kama wameambukizwa
au la!
Endapo unajidunga madawa, jaribu kufikiria kupata tiba au kutumia dawa
ambazo sio za aina ya IV (za kunusa au kuvuta). Kama utaendelea kutumia
dawa za aina hii, jaribu kuepuka kuchangia sindano au vitu vingine vyenye ncha
kali na mtu mwingine yeyote. Epuka kurudia kitumia sindano au bomba lake, na
ikiwa utafanya hivi, vioshe vizuri kwa kutumia dawa ya nyumbani ya kusafishia
(kuosha mara tatu kwa kutumia dawa ni vizuri, na halafu suuza tena mara tatu na
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 10 of 25
maji safi). Itakapojitokeza dharura, tumia pombe yoyote kali au mvinyo
kusafishia, lakini sio bora sana kama dawa ya kusafishia. (Tambua kuwa dawa
ya kusafishia haitoua hepatitis C.) Tumia pamba safi isiyotumiwa bado na maji
kila mara unaposafisha. Jaribu kuzitumia programu za kubadilishana sindano
zilizopo kwenye baadhi ya maeneo, na jaribu kuzipigia kampeni ikiwa hazipo
eneo unalioshi. Programu za aina hii zimekuwa na manufaa sana katika
kupunguza maambukizi ya VVU miongoni mwa watumiaji wa dawa kwa
kujidunga.
Kukubali lilikuwa jambo muhimu sana kwangu. Ilinibidi kukubali kuwa nina virusi
hivi na hakukuwa na njia yoyote tena ya kufanya kuviondoa….Siku yangu mbaya
zaidi nikiwa na VVU ni siku yangu nzuri zaidi kwa mara kumi kuliko siku yangu
nzuri zaidi nikiwa mtumiaji mzoefu wa dawa za kulevya.
WASAGAJI: WAKO KATIKA HATARI? Kwa wale miongoni mwetu ambao ni wasagaji tumekuwa tukiambiwa kuwa tuko
katika kundi lenye uwezekano mdogo wa kuweza kuathirika, lakini bado baadhi
yetu hufanya ngono na wanaume, wengine hutumia madawa, wengine tunafanya
biashara ya kuuza miili yetu, wengine wanabakwa, na wengine wanafanya
vitendo hatarishi kama vile kuchangia vifaa vya kufanyia mapenzi na wenzi
ambao bado hawajapima Ukimwi. Uwezekano wa kuweza kupata VVU
unategemeana na mambo tunayofanya, na sio hali ya ujinsia wetu. Kunaweza
kuwa na madhara makubwa kufasili hatari kwa misingi ya kimakundi ya kijamii.
Kwa wale miongoni mwetu ambao wanaishi na VVU au Ukimwi, ni suala la
muhimu kuhakikisha kwamba programu na huduma mbalimbali zinatoa
mazingira ambayo ni salama na yenye kutoa msaada, taarifa na huduma
nyinginezo maalumu kwa wasagaji.
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 11 of 25
DALILI ZA UKIMWI NA UPIMAJI Kulingana na takwimu kutoka Kituo cha Kudhibiti Magonjwa, watu kati ya
180,000 mpaka 280,000 nchini Marekani – takriban robo ya wale walioathirika na
VVU – hawafahamu kama wameathirika. Na ni kwa sababu hii kupima ni suala la
muhimu sana. Ingaw linaweza kuwa jambo la kuogopesha kupima, kadiri
tutakavyopima mapema ndivyo itakuwa rahisi kwetu kuanza matibabu
yanayoweza kuulinda mfumo wetu wa kinga mwili usidurike sana, na kurefusha
maisha yetu kwa miaka kadhaa.
Watu wengi ambao wameambikizwa VVU hupata seti ya dalili za ugonjwa
wa homa ya mafua – kama vile homa kali, kukereketa koo, kuvimba mtoki,
uchovu kupita kiasi na harara – katika mwezi wa kwanza wa maambukizi. Kama
una dalili kama hizi na unadhani labda utakuwa umeambukizwa VVU, ni muhimu
ukapima. Baadhi ya vituo vya afya vinaweza kukupatia matibabu yatakayoweza
kukupunguzia kiwango cha ugonjwa.
Baada ya hiki kipindi cha mwanzo cha mwanzo cha virusi vya ukimwi
mwilini, watu wengi hujisikia wazima kabisa kwa miaka mingine mingi. Lakini
kadiri kinga inavyo pungua mwilini, dalili za ugonjwa na ukimwi hutokea. Hizi ni
pamoja na, kupungua uzito, uchovu, kuvimba mitoki (kwenye shingo, makwapa
na nyonga) na harara. Kutoka jasho usiku, kutokwa vidonda mdomoni, kuumwa
kichwa, kuharisha, na kupoteza hamu ya kula pia kunaweza kutokea. Uwepo wa
maambukizi ya fangasi wa ukeni yanayojirudiarudia, chronic pelvic inflammatory disease, frequently recurring severe genital herpes, au
human papillomavirus (HPV) – virusi ambavyo husababisha veneral warts (condyloma) – unaweza pia kuashiria kuwa maambukizi ya VVU
yameshashamiri na kuwa Ukimwi. Magonjwa nyemelezi, kama vile
Pneumocystis carinii pneumonia (PCP), severe thruss, au lymphoma mara
nyingi hutokea pale mfumo wa kinga ya mwili unapokuwa tayari umeathiriwa
sana na VVU
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 12 of 25
Kufahamu kuwa umembukizwa virusi vya ukimwi ni jambo linaloweza
kubadili maisha yako. Hivyo basi unaweza kutafuta vikundi vya msaada au
washauri nasaa walioko katika eneo lako ambao wanaweza kukushauri juu ya
uamuzi wa kupima, na kutafuta kituo cha kupima ambacho kinatoa ushauri
mzuri.
NI NANI WALIO KATIKA HATARI YA MAAMBUKIZO VIJANA (TENEJA)
Katika dunia watu /vyama walioko chini ya miaka 25 wako katika hatari kubwa ya
kuambukizwa gonjwa hili, inakadiriwa kuwa nusu ya maambukizi yote mapya
duniani ni kwa vijana chini ya miaka 25.
Mwaka 2003, inakadiriwa kuwa watoto 2000 chini ya miaka 15, na watu 6000
kati ya miaka 15 -24 huambukizwa virusi vya ukimwi kila siku.
Duniani kote maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa watoto chini ya miaka 13
hutokana na mama kumuambukiza mtoto wake, hata hivyo uambukizaji toka kwa
mama kwenda kwa mtoto unaendelea kupungua sababu ya usboreshaji wa
madawa wanayopewa akina mama wajawazito.
Wengi wa wasichana huambukizwa virusi vya ukimwi kwa sababu ya ngono, kwa
bahati mbaya hii inatokana na makundi mengi yakiwemo mashirika ya dini
kusisitiza juu ya kuacha ngono na siyo jinsi ya kufanya ngono salama. Jambo
ambalo huwafanya wengi kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo au sehemu ya
haja kubwa ili kukwepa mimba na kutunza ubikra wao, lakini si salama kwa
maambukizi ya virusi vya ukimwi.
WANAOJIDUNGA SINDANO
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 13 of 25
Kuchangia sindano ambazo zimekwisha kutumiwa na waathirika au kufanya
ngono na waathirika ndizo njia kuu ambazo kwako wanawake huambukizwa
virusi vya ukimwi kutokana na utumiaji wa madawa ya mishipa.
Hii ni kwa sababu iwapo sisi wenyewe hatutumii madawa ya kujidunga mishipani,
wapenzi wetu wa kiume wanaweza kuwa wakitumia hivyo kutuambukiza ikiwa
tutafanya ngono isiyo salama.
BIASHARA YA NGONO: Jamhuri ya U.A. Wanahabari, Asikari , mahakama wamekuwa wakiwafungulia
mashitaka wanawake wanao fanya biashara ya ngono na sio wanaume ambao ni
wateja na wanaochangia maambikizi ya Ukimwi, Wanawake ambao
hawajaathirika ni rahisi kuathirika, kwani wanaume wengi wataliapa zaidi fedha
iwapo itakuwa ngono nzembe, na baadhi ya wanawake wanaamini wasichana
wadogo hawajaathirika, kwani wanaume wengi watalipa zaidi fedha iwapo
itakuwa ngono nzembe na baadhi ya Wanawake wanaamini wasichana wadogo
hawajaathirika. Serikali nyingi zinahitaji mamlaka ya kuwapima wanawake
wanaofanya biashara ya ngono walioshikwa wapimwe, bila mamlaka ya
kuwapima wateja wao.Wafanya biashara ya ngono wanatakiwa kutetewa
kisheria na kulindwa, kwani huu ni udhalilishwaji wa haki za Binadamu na
vilevile wawe wamepewa usili wa matibabu.
WANAWAKE WALIO MAGEREZANI Wanawake walioko gerezani, wako katika hatari ya kuambukizwa virusi vya
ukimwi mara tatu zaidi kuliko wanaume walioko gerezani. Na asilimia kubwa ya
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 14 of 25
wanawake walioambukizwa katika nchi ya marekani ni wale walioko gerezani. Na
hapa nchini baadhi ya takwimu zinaonyesha kwamba baadhi ya wanawake
walioko gerezani wameathirika japo idadi yao si kubwa ukilinganisha na wale
ambao hawako gerezani.
Na hii inatokana na hali ngumu ya maisha ya gerezani ya kutopatiwa huduma
bora za matibabu na mazingiria yasiyo ridhisha kiafya. Hata hivyo katika
magereza yale yanayotoa elimu ya kutosha kuhusu virusi vya ukimwi, na elimu
ya kujitambua na kujithamini, wanawake hupokea huduma nzuri na matunzo na
kufuata ushauri wapewao kuliko vile angekuwa nje ya ulimwengu wa gereza.
NINI MAANA YA KIPIMO CHA VVU?
Kuna aina mbalimbali za VVU,vya muda mrefu na mfupi katika kutoa majibu.
Vipimo hivi vyaweza kuwa ni vile vya damu,au utelezi wa mdomono au utandu
ulioki kaitka fizi na mashavu, pia mkojo.
Vipimo vyote hivi vikitumika kwa usahihi hutoa majibu sawa iwapo kuna
maambukizi au la.
NI LINI NAWEZA KUPIMA VIRUSI VYA UKIMWI? Ni vizuri kuchuchukua vipimo vya ukimwi baada yamiezi mitatu tangu siku zile
ulipokuwa mazingira hatarishi.(ulipofanya virusi vya ukimwi kupenya mwilini
mwako. Na kipindi hiki huitwa wondow period(Yaani ni kipindi ambacho mtu
akiambukizwa virusi vya ukimwi mpaka pale virusi vinapoweza kuonekana katika
vipimo). Hata hivyo kama unajihisi umepata maambukizo kwa kuona dalili za
mwanzo mwanzo,na unahitaji kupata dawa mapema ili virusi visiwe visizaliane
kwa wingi mwilini, unaweza kupima muda wowote kabla ya hiyo miezi mitatu.
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 15 of 25
KISA SITARUDI NYUMA TENA.
Kisa hiki kinasimuliwa kwetu na dada Marlene Diaz, anaanza kwa kusema:
“Katiaka siku moja maisha yangu yalibadilika kabisa, sikuwa tu MarleneDiaz, bali
Marlene Diaz mwathirika wa VVU.
Ni katika mwaka 1992,nilipokuwa kwa jumla ya masaa matano (5) mfululizo na
wakati huo nilikuwa na mimba miezi 2 (miwili) Baada ya miezi 6 tangu kubakwa
ndipo nilipima. Nilijawa hisia za uoga siku ya kuchukua majibu ndipo nilipomtuma
shangazi anichukulie majibu yangu. Nilikuwa niko sahihi, majibu yalipotoka
yalionesha kuwa nilikuwa nimeathirika, kwa watati huo nilikuwa na umri wa
miaka 29.
Baada ya hapo ndipo nilianza kupambana na uonevu na unyanyasaji, kwa
bahati wanaharakati dhidi ya ukimwi walinitia moyo sana.
Kwa sasa nimefurahi kwasababu ya madawa ya kurefusha maisha, lakini pia
nina huzuni kwa sababu ya mwanangu Magarita nahii ni kwasababu makampuni
mengi ya kutengeneza madawa haya siyo mengi kwa ajili ya watoto
walioathirika,hivyo watoto hawa hawana matibabu yao sahihi isipokuwa kutumia
dawa za watu wazima walioathirika,na hii ni hatari kubwa.
Mwaka uliopita ulikuwa mbaya sana kwa mwanangu Magarita, alikuwa na miaka
10, akiwa mwenye urefu wa futi tano,alikuwa na uzito wa paundi 59 tu (sawa na
kilogram ) Bahati njema ametumia dawa na sasa idadi ya virusi mwilini mwake
imepungua sana na anaweza kufanya kazi zake vizuri.
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 16 of 25
Katika mtaa ninaoishi vijana wadogo humfanyia dhihaka kwa kumuita majina (
kuashiria kuwa nina ukimwi). Hii huniumiza sana hasa ninapo mfikiria mwanangu
Magarita.
Magarita pia naye ameanza mapambano dhidi ya VVU, katika kuandika mtihani
wake, ameandika juu ya “ Nini maana ya kuishi na virusi vya ukimwi” nahii kwake
umaanisha kujieleza kuwa ndivyo ilivyo wakubali ,wasikubali. Nimefurahi sana
kwa ushujaa wake huo.
Mpaka sas tunajihesabu kuwa miongoni mwa watu wenye bahati; maana shirika
nifanyiapo kazi wamenipa msaada na kunifanya nistahimili hali hii. Nami nasema
tena sitarudi nyuma tena,na siwezi kunyamaza kwa hili, nawe pia usinyamaze
kuhusiana na VVU.
NAWEZA KUFANYA VIPIMO VIPI?
1) DAMU: Hiki ndicho kipimo kilichozoeleka, waweza kupima damu toka kwenye mshipa wa
mkon au kutoka katika kidole na majibu yake waweza kupewa baada ya muda
mfupi tu au mpaka wiki moja baadaye.
Ugonjwa wa Ini pia waweza kupima kea kutumia damu hiyohiyo.
ii) NJIA YA KINYWA NA MKOJO: Kama ilivyo upimaji wa damu, upimaji kwa njia ya kunywa au ugonjwa niwa
hakika,haraka na usioumiza.
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 17 of 25
Kwa kutumia kifaa maalumu,kiasi kidogo cha utando na utelezi ulioko katika
mashavu na fizi hukusanywa na kupimwa na majibu yake hupatikana kuanzia
wiki moja.
Upimaji kwa njia ya mkojo hautumiki sana kwa vile utahitaji pia upimaji wa damu
ya mhusika.
iii) KIPIMO CHA HARAKA
Kipimo hiki hutoa majibu ndani ya masaa 24, kwa njia hii ya kipimo cha haraka,
tone la damu au mate huchukuliwa na kufanyiwa uchungu zaidi.
Njia hii sio nzuri katika kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto
iwapo itafanyika Mama awapo katika uchungu au kujifungua.
NI WAPI NAWEZA KUPIMA
Jambo la kwanza nikuamua je unahitaji usiri yaani kutumia namba Fulani na
wala siyo jina lako ni vizuri kupima katika kliniki za serikali la umma ambazo
zinaweza kukupa ushauri na saha hata baada ya kupokea majibu kitu
ambacho vituo vya kulipia hawatoi ufanyapo vipimo hivo vya usiri ni lazima
ukumbuke kwamba taarifa zako zitaingizwa kwenye jalada lako la afyaaweza
kusaidia kwa baadaye.
pengine utahitaji kuelimishwa zaidi ni kwa jinsi gani uendelee kuishi maisha
yasiyo hatarishi. wahamasishaji, daktari wako, au rafiki wanaweza kukusaidia ili
uishi maisha ambayo hayatakuweka katika hatari ya maambukizi.
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 18 of 25
Na iwapo utakuta umeathirika, kumbuka kwamba watu wanaishi muda mrefu tu
na virusi vya Ukimwi tena maisha bora. Unaweza kuishi na virusi vya ukimwi kwa
muda wa miaka 10 (kumi) bila kuonyesha dalili zozote za maambukizi au bila
kuathirika kikote katika shughuli za maisha.
KUISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI/UGONJWA WA UKIMWI Jambo muhimu kwangu ni kujifunza jinsi ya kuishi na virusi vya ukimwi / ugonjwa
wa ukimwi na jinsi ya kujiamini kwanza. Kumbuka, watu wote watakufa kutokana
na maradhi au sababu mbalimbali, kwanini ufe kabla hujafa? Maisha ni fursa
utakavyoyafanya,kwangu bunafsi sichukulii kuwa na virusi kama hukumu ya kifo.
Ninafahamu ya kwamba jinsi ninavyo jithamini na kujijali kwa kula chakula bora
chenye virutubisho, usingizi wa kutosha,kuhudhuria kliniki,na kumuona daktari
wangu na kuepukana na utumizi wa madawa ya kulevya,nitakuwa salama.
Mwanzo nilifikiri nitakufa lakini sasa naendelea na maisha yangu kama
kawaida.
• Iwapo vipimo vyako vinaonyesha kuwa umeathirika, hii haimaanishi kuwa
unaugua Ukimwi tayari. Ni wakati wa kujifunza na kujijali kiafya zaidi kwa
kula vizuri,kupumzika, na kujilinda dhidi ya magonjwa ya zinaa.
• Jambo jingine litakalo kusaidia ni kutembelea vituo vya afya vinavyotoa
mafunzo juu ya kuishi na ugonjwa huu na pia kutafuta watu wengine
wenye hali kama yako( walioathirika na virusi ili kupeana mawazo.
• Katika kutembelea vituo vya afya tunamaanisha kukagua afya yako kwa
jinsi unavyoonekana kwa nje ( ukaguzi kwa kutoa macho tu) na ukaguzi
kwa kutumia vifaa vya maabara ili kujua yafuatayo:-
1.KUFANYA TATHMIN:
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 19 of 25
Uanapo tembelea kliniki inakufanya kuelewa nia kiasi gani cha CD4 ziko mwilini
mwako na nikiasi gani cha virusi vya ukimwi kiko ndani ya damu yako nah ii
husaidia kupewa dawa zinazoendana na hali yako.
2. CHANJO Chanjo hii hutolewa kwa wale wanaoumwa nimonia( baridi ya bisi-kifua) Donda
ndugu (Tetenus) Mafua, na ugonjwa wa Ini ( Hepatits B)
3. MATIBABU:
• Matibabu ya virusi vya ukimwi yapo ya njia mbalimbali,hivyo mgonjwa
anaweza kupatiwa dawa ARV kwa ajili ya kupambana na virusi
vyenyewe, pia kutibu au kuzuia uambukizo, jinsi ya kujali na kutunza afya
kwa ujumla na jinsi ya kuimarisha kinga ya mwili.
4. MISAADA
• Hapa twaweza kupata msaaada wakutuasa na pia ushauri wa utumiaji wa
vyakula vyenye lishe, na hata msaada wa waaalam.
5. UANGALIZI MAHUSUSI KWA WANAWAKE
• Wanawake walioathirika na virusi vya ukimwi wana matatizo yao
tofauti na makundi mengine hivyo wahitaji uangalizi maalum.
Matatizo hayo ni kama vile uambukizo katika nyonga sehemu za
ukeni, na pia uambukizo katika sehemu za mapafu. Pia wanawake
hao husumbuliwa na saratani nyuma ya ulimi (human papiloma
virusi (HPV) ambayo huweza kuleta saratani.
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 20 of 25
• Kusababisha hivyo basi kipimo huchukuliwa kila baada ya miezi
sita.
UCHAGUZI WA MATIBABU
• Matibabu dhidi ya virusi vya ukimwi na ukimwi hubadilika mara kwa mara
kwa kadri ugunduzi wa kisayansi unavyoendelea juu ya taarifa, na madwa
ya kupambana na virusi vya ukimwi.
MATIBABU YA KITABIBU Hapo mwanzoni matibabu dhidi ya virusi vya ukimwi yalitolewa mapema sana na
kwa wingi ila kupambana na virusi, lakini sasa, vidonge vya ARV hutolewa iwapo
kinga imepungua sana na kiasi cha virusi kimekuwa kikubwa sana.
Dawa hizi za ARV zimegawanyika katika makundi mbalimbali na dawa nyingine
bado zinazidi kuendelea mpaka mwaka 2004 makundi yaliyopo ni kama
ifuatavyo;-
1. Dawa zilizo na mchanganyiko wa sukari/Fosforas/naitrogen
2. Dawa zisizo na mchanganyiko wa sukari au fosiforasi au nitrogen
3. Dawa zilizo na protein
4. Dawa zenye mchanganyiko mbalimbali.
Mpaka sasa kuna aina kumi na tisa na pia kuna mchanganyiko wenye aina mia
moja uitwao cocktails) ili kupunguza idadi ya virusi mwilini na kuongeza kinga ya
mwili.
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 21 of 25
Dawa hizo zimesaidi kupunguza vifo vitokanavyo na ukimwi na kuboresha,
vimesaidia kuboresha hali ya maisha.
MADHARA YA MADAWA HAYA.
• Madawa haya ARV yanaongeza kinga na kupambana na ngezeko la virusi
mwilini, huweza kusababisha madhara yafuatayo;-
• Kichefuchefu, kuhara, uchovu, mifupa kutokuwa imara, na utumikaji
mkubwa wa mafuta mwilini.
• Mtumiaji wa madawa haya ya ARV hueneza kuzidishiwa makali/nguvu na
madawa mengine unayoweza kuwa ukitumia kama vile ya kubanwa kifua,
kuzimia, mafuta kuwa mengi, na vidonge vya kupanga uzazi.
• Pia mtumiaji wa ARV anapaswa kula chakula bora chenye lishe ya
kutosha japo kuwa kwa wasio na kipato kikubwa inaweza kuwa ni shida.
ZINGATIA Usipotumia dawa za ARV kama kuna ulivyo elekezwa mfululizo, unaweza kuwa
na virusi sugu ambavyo vimezoea dawa, hivyo dawa hizo hazitakuwa na msaada
iwapo utaanza kuugua ukimwi halisi.
UANGALIZI WA JUMLA
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 22 of 25
• Mbali na dawa za kitabibu, njia zingine pia zinaweza kutumika katika
kupambana na ongezeko la virusi vya ukimwi, mfano mzuri ni dawa
(mitishamba za kichina, ambazo zinaongeza kinga ya mwili na CD4. Pia
kupunguza kutoka jasho usiku, kichefuchefu kuharisha na kupunguza
maumivu ya mwili kwa ujumla
• Hata hivyo mtumiaji anapaswa kuwa makini anapotumia madawa haya ili
kutoongeza sumu mwilini hasa pale anapotumia madawa ya aina
mbalimbali.
MATIBABU MENGINE
• Nikama vile :
Mazoezi
Yoga
Kukandakanda mwili
Tafakari haya nayo yanaweza kuongeza kinga ya mwili na kuboresha maisha.
VIRUSI VYA UKIMWI NA UJAUZITO: Virusi vya ukimwi vinaweza kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto aidha wakati
wa mimba au kujifungua. Uwapo unahitaji kupata mtoto na unahisi unaweza
kuwa umeambukizwa virusi vya ukimwi ni vizuri kupima kwanza kabla ya kuwa
mjamzito. Kwa wale tayari walio na maambukizo ya virusi vya ukimwi na
wanahitaji kupata watoto dawa za ARV zinatoa matumaini.
• Utafiti mwingine unaonyesha kuwa iwapo mama mjazito atameza dawa za
ARV kabla ya kujifungua, au wakti wa kujifungua atafanyiwa upasuaji
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 23 of 25
tatizo la maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto hupungua kwa
asilimia 2(mbili)
• Pia upimaji wa haraka wa VVU wakati mama anaumwa uchungu/au
anajifungua umesaidia wanawake sana, wanawake ambao hapo mwanzo
hawakujulikana kuwa wana maambukizi ya virusi vya ukimwi, kupunguza
uwezekano wa kuambukiza watoto wao.
Kwa vile mama anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa kunyonyesha ni
vizuri wanawake walio athirika wasinyonyeshe maziwa yao kwa njia ya matiti.
Akina mama hawa pia wanaweza kupata watoto kwa njia ya kufuata au kutumia
desturi au itikadi nyingine au akina mama ambao hawajaathirika lakini wana
wapenzi walioathirika, wanaweza kupata mbegu za kiume kwa njia ya maabara
toka kwa wanaume ambao hawajaathirika.
Watunga sera kuhusu maswala ya ukimwi wanasisitiza kuwa mwanamke
ambaye ana virusi vya ukimwi asiwe mjamzito, na iwapo tayari alikwishakuwa
mjamzito ni vizuri kutoa mimba japokuwa hili ni kinyume cha haki za binadamu
ambaye hudai haki ya kuishi kwa kila mtu na haki ya kufanya maamuzi.
MASUALA/MAAMUZI BINAFSI: Maswali mengi na utata, vimekuwepo kuhusu wanawake walio na virusi vya
ukimwi na kuhusu mambo yao kifamilia. Yafuatayo;-
• Ni vipi kuhusu maisha yangu ki ngono(ngono)?
• Ni nani atawaangalia au kuwatunza watoto wangu nitakapokuwa mgonjwa
sana?
• Je naweza kuimbia familia yangu na marafiki kuwa nina virusi vya ukimwi?
• Vipi kuhusu wafanyakazi wenzangu? Niwambie? Watoto wangu?
• Je watu wakifahamu itakuwaje?
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 24 of 25
• Je nawezaje kukabiliana na hao watoa huduma wasio niheshimu?
• Naweza vipi kupata huduma toka kwa jamii?
• Nawezaje kupata msaada wa kisheria iwapo nitaonewa kwa vile tu nina
VVU.
• Ninakabilije uwezekano wa kufariki?
KUANDAA MALEZI YA WATOTO WETU Japokuwa kumekuwa na madawa yanayosababisha kuishi muda mrefu ni vizuri
kuandaa walezi au watu watakaotunza famila yako kabla ya kuugua sana au
kufariki ili wasisumbuke kwa wakati huo.
JIHUSISHE
Iwapo wanawake walioathirika wataendelea na shughuli zao za kijamii kama
kawaida zitawapunguzia sana kuwa na mawazo na watafarijika katika hisia zao
na upande wa kiroho pia (Mambo ya dini)
Ni katika kipindi ambacho mtu hajaugua sana ndipo aweze kujiunga na vyama
vya watetea haki za waathirika wa ukimwi, na vyama vya kusisitiza upatikanaji
wa huduma bora mahospitalini kwa waathirika na pia kulishilikisha bunge
kutunga sheria za kutetea waathirika, na pia kuwashawishi viongozi wa dini
kuongelea na kuw wazi kuhusu VVU na ukimwi, tena waweze kuwashauri watu
wa rika zote kuhusu janga la ukimwi.
Kwa ufupi kuna mambo mengi sana ambayo wanawake walioathirika na VVU
wanaweza kuyafanya, ikiwa ni pamoja kuwa wafadhili na kuwasaidia wanawake
wengine wasitumie dawazya kulevya au vileo. Kama alivyosema mwanamke
mmoja katika kamati ya kupambana na ukimwi nchini Massachusetts” Iwapo
naweza kuokoa hata mtu mmoja dhidi ya janga hili ni faida kubwa sana”
Virusi Vya Ukimwi Na Ukimwi (“HIV/AIDS”). For more information, see: http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.
Page 25 of 25