View
10
Download
0
Category
Preview:
Citation preview
1
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
TAARIFA YA UTENDAJI YA SHIRIKA LA UTAFITI NA
MAENDELEO YA VIWANDA TANZANIA (TIRDO) KWA KAMATI YA
KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA
8 MACHI 2017
2
TAARIFA KUHUSU UTENDAJI WA SHIRIKA LA UTAFITI NA
MAENDELEO YA VIWANDA TANZANIA (TIRDO) KWA KAMATI YA
KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA
1.0 UTANGULIZI
Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) lilianzishwa kwa Sheria
ya Bunge namba 5 ya mwaka 1979 na kuanza kazi zake rasmi tarehe 1 Aprili, 1979.
Sheria hii ilipitiwa na kutangazwa tena na gazeti la Serikali mwaka 2002 (CAP 159 of
2002). Shirika liliundwa ili kufanya utafiti na kutoa huduma za kitaalam ili
kuendeleza viwanda nchini.
2.0 DIRA, DHAMIRA NA MADHUMUNI
2.1 DIRA (VISION)
Shirika la utafiti unaohitajika na wadau, lenye matokeo bora yasiyoharibu mazingira yatakayowezesha ushindani wa viwanda
2.2 DHAMIRA (MISSION)
Kuendeleza utafiti, huduma za kitaalamu na uzalishaji wa bidhaa viwandani kwa kutumia malighafi za hapa nchini na kwa kushirikisha viwanda
2.3 DHUMUNI KUU:
Ni kufanya utafiti (Applied Research), kutoa huduma za kitaalamu viwandani, kukusanya na kusambaza taarifa zinazohusu utaalamu wa viwanda kwa ajili ya kuimarisha na kuongeza uzalishaji bora viwandani.
Aidha, Shirika pia lina dhumuni la kufanya utafiti unaolenga kuongeza thamani ya malighafi inayopatikana nchini na kuzalishwa na viwanda vya ndani kwa malengo ya kuuza nje ya nchi.
3.0 MAJUKUMU YA SHIRIKA
Majukumu ya Shirika ni kama ifuatavyo:-
3.1 Kufanya utafiti wa teknolojia zinazotoka nje ya nchi na za hapa
nchini kwa ajili ya matumizi ya viwanda.
3.2 Kuendeleza na kutoa mafunzo yenye kuwezesha kufanya utafiti wa
kisayansi na kiteknolojia unaoendeleza viwanda.
3
3.3 Kusimamia na kusambaza matokeo ya utafiti unaofanywa hapa
nchini au mahali pengine popote kwa manufaa ya Serikali ya
Tanzania na kutoa tathmini ya utafiti huo katika viwanda.
3.4 Kuanzisha mfumo wa kusajili matokeo ya utafiti unaofanywa nchini
na kuendeleza matokeo ya utafiti huo katika viwanda vyetu.
3.5 Kuanzisha na kuendesha mfumo wa kutunza taarifa za kitaalamu na
kusambaza matokeo ya utafiti wa aina yoyote unaofanywa hapa
nchini kwa niaba ya Serikali.
3.6 Kutoa huduma na ushauri wa kitaalamu Serikalini na katika
mashirika yanayohusika na uzalishaji viwandani, ili kuendeleza
shughuli za viwanda na matumizi ya teknolojia mpya.
3.7 Kushauri na kusaidia Serikali na viwanda kuanzisha mfumo wa
kudhibiti na kuwianisha shughuli za viwandani na kuepusha ama
kupunguza vyanzo vya uchafu wa mazingira wakati wa uzalishaji
viwandani kwa kutumia teknolojia zinazofaa na zinazoongeza
uzalishaji.
4.0 UONGOZI WA SHIRIKA
4.1 Baraza la Shirika:-
Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania linasimamiwa na Baraza la Shirika ambalo limeundwa kwa mujibu wa Sheria. Baraza lina majukumu ya kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Shirika, na kusimamia shughuli zinazofanywa na Menejimenti ya Shirika. Baraza linaongozwa na Mwenyekiti anayeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wajumbe wa Baraza wanateuliwa na Waziri mwenye dhamana ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Mkurugenzi Mkuu ndiye Mtendaji Mkuu wa Shirika na Katibu wa Baraza. Baraza lina wajumbe kumi kutoka Serikalini Taasisi za Umma, na sekta binafsi. Wajumbe wa Baraza waliopo sasa waliteuliwa 1 Novemba 2015 kwa kipindi cha miaka mitatu.
4
JEDWALI 1: WAJUMBE WA BARAZA LA TIRDO
Na. Jina Wadhifa Mahali alipotoka
1. Prof. Idrissa Bilali Mshoro Mwenyekiti Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi
2. Prof. Evelyne Mbede Mjumbe Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
3. Dkt. Hassan Mshinda Mjumbe Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
4. Bi. E.N. Pallangyo Mjumbe Mkurugenzi Msaidizi wa Viwanda Wizara ya Viwanda na Biashara
5. Bw. Bernard Mchomvu Mjumbe FAC Chairperson, P.O. Box 22703, Dar es Salaam
6. Bw. Salehe Selemani Hamadi Mjumbe Mkurugenzi wa Masoko na Biashara za Viwanda, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, P.O. Box 601, Zanzibar
7. Bi. Christina Kilindu Mjumbe Private Sector
8. Ms. Kulthum Mansoor Mjumbe Mchumi, Idara ya Sera na Mipango, TAKUKURU Makao Makuu, P.O. Box 486, Dar es Salaam
9. Bw. Fadhili J. Manongi Mjumbe Mkurugenzi Mkuu, CDE Consulting Ltd. P.O. Box 33025 Dar es Salaam
10 Bi. Fatuma Oloo Mjumbe Mhasibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
11 Prof. Mkumbukwa M. Mtambo Katibu Mkurugenzi Mkuu, TIRDO
4.2 Mfumo wa Menejimenti ya Shirika
4.2.1 Muundo uliopo hapa shirikani ulianza kutumika katika kipindi cha 2007/2008.
(Ona Kiambatanisho A).
4.2.2 Mkurugenzi Mkuu anaongoza kurugenzi ambazo ni:-
a) Utafiti Viwandani
b) Maendeleo ya Uhandisi
c) Elektroniki na tekinolojia ya habari
d) Rasilimali watu na miliki
e) Fedha
4.2.3 Chini ya kurugenzi hizi kuna vitengo vifuatavyo:-
5
(a) Teknolojia ya Kilimo na Kemia ya Viwandani (Agrotechnology and industrial
Chemistry)
(b) Chakula na Teknolojia ya Baiolojia (Food and Biotechnology)
(c) Mazingira na usalama mahali pa kazi (Environmental Technology and
occupational safety)
(d) Teknolojia ya Vifaa vya Kihandisi (Materials Science and Technology)
(e) Teknolojia ya Nishati (Energy Technologies)
(f) Teknolojia ya Nyuzi na Ngozi (Fibre and Leather technologies)
(g) Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Information and Communication
Technologies)
(h) Ufundi wa Vifaa vya Elektroniki (Electronics and Instrumentation
Technologies)
(i) Maendeleo ya Teknolojia na Viwanda vya Mfano (Technology Development
and Pilot plant))
(j) Ushirikishwaji Wadau kutoa huduma (Corporate Services)
(k) Utumishi na Rasilimali Watu (Human Resources)
(l) Miliki na Ukarabati (Estate and Maintenance)
(m) Utawala
5.0 UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA SHIRIKA LA TIRDO
5.1 UTANGULIZI:-
Kwa muda mrefu tangu kuanzishwa kwake shirika la TIRDO kama mashirika
mengine yanayotegemea ruzuku kutoka Serikalini ili kuendesha shughuli zake
Shirika limepambana na changamoto nyingi hasa kutokana na ukosefu wa
fedha. Aidha ukosefu wa fedha pia umesababisha kutokamilika kwa baadhi ya
majengo ambayo yangetumika kama maabara za kufanya utafiti na upimaji
ubora na usalama wa malighafi na bidhaa zinazozalishwa viwandani ili kutoa
ushauri wa kitaalamu kwa wazalishaji.
Pamoja na matatizo hayo, kwa mwaka 2016/17 Shirika limeweza kufanya tafiti
mbalimbali na kutoa huduma za kitaalamu viwandani kwa kutumia fedha za
6
wahisani na fedha za ndani. Baadhi ya Tafiti zinazoendelea ni kama ifuatavyo;
1. Mfumo wa kijani wa usindikaji zao la muhogo usiozalisha taka kwa ajili ya
kuimarisha masoko kwa ajili ya wazalishaji wadogo na wakati, (Greener
cassava processing system leading to zero waste for enhanced
market access by small and medium entrepreneurs). Mradi
unafadhiliwa na USAID ambapo unahusisha kukausha muhogo kwa kutumia
kaushio la jua na kutumia mabaki ya maganda ya muhogo kuzalisha gesi
ambayo inatumika pia katika kaushio nyakati za usiku ama wakati wa mvua.
Mradi wa ukaushaji muhogo na uzalishaji gesi kwa kutumia maganda ya mihogo
2. Mradi wa kuongeza thamani katika taka ngumu za ngozi na kuzalisha bidhaa
mbalimbali za ngozi (Value addition on solid leather waste to produce
leather boards). Mradi ulianzishwa kwa Fedha za Utafiti chini ya COSTECH
na sasa umeingizwa katika bajeti ya Maendeleo ya Serikali.
3. Kujenga uwezo wa kuzalisha kwa biashara uyoga wa kawaida na ule
unaotumika kama dawa (Capacity building for commercial production
of Edible and Medicinal Mushrooms in Tanzania) Mradi unatekelezwa
kwa kushirikiana na chuo cha Hubert Kairuki chini kwa kupitia Fedha za utafiti
chini ya COSTECH.
4. Kutathmini hali halisi ya sekta ya ngozi na nguo nchini (Status of leather
and textile sector in Tanzania). Utafiti huu ulifanyika katika kitengo cha
7
Nguo na Ngozi hapa Shirikani na kuweza kutoa andiko katika majarida ya
kimataifa (Pulication) na pia kuwasilishwa katika mikutano na wadau wa ngozi
nchini.
5. Kutumia mabaki ya mbegu za mafuta katika kutengeneza chakula chenye
protein nyingi (Utilization of Tanzanian oilseed meals to develop high
protein foods and wellness ingrediantes). Utafiti huu unafanyika kwa
kushirikiana na kituo cha Utafiti nchini India – CSIR
6. Kutathmini taka ngumu zitokanazo na usindikaji wa mafuta ya kula kwa ajili
ya kuboresha uzalishaji biogesi itokanayo na kinyesi cha ng’ombe
(Characterization of spent bleaching earth and improvement of
biogas through supplementation of manure). Utafiti huu unafanyika kwa
kushirikiana na CSIR India na umetokana na mahitaji ya viwanda katika
kuongeza thamani katika mabaki yatokanayo na usindikaji mafuta na
kutumika katika kuzalisha bidhaa nyingine na vilevile kutunza mazingira.
7. Uzalishaji wa Citric Acid kutokana na aina mbili za viazi visivyoliwa
(Production of Citric Acid from two Non-Edible yam species) Utafiti
unatekelezwa chini ya makubaliano na Taasisi ya Utafiti nchini India -CSIR
8. Utengenezaji wa mbinu za gharama nafuu za kibiolojia za kutathimini uchafuzi
wa maji katika mito ya nchi za joto za kiafrika (Development of cost
effective biomonitoring methods for assessing water pollution in
tropical Africa rivers, (Julius, Doctoral study)
9. Tathimini ya uchafuzi wa hewa unaosababishwa na ndege katika uwanja wa
kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyeyere (Assessment of
Aviation Emisions at Julius Nyerere International Airport JNIA in
Tanzania and their effects on Air Quality of neighboring community
(Jacqueline Mwenda, Doctoral study).
10. Uchunguzi wa madhara ya mabaki ya viuatilifu katika mazao ya mbogamboga
kwa walaji wa mkoa wa Arusha (Investigating Human Exposure of
8
Pesticides residue through vegetable consumption in Arusha region
(Purificator Andrew, Doctoral study).
Mtambo wa kuchakata taka ngumu za ngozi
Aidha Shirika limetoa na linaendelea kutoa huduma za kitaalamu za Upimaji
ubora wa majaa ya mawe (Coal Quality Testing), Matumizi bora ya Nishati
(Energy Auditing), Mazingira (Environmental Auditing), Upimaji wa
Kihandisi bila kuharibu vifaa (Non Destructive Testing) kwenye mabomba
ya gesi, maji, mabwela (Boilers) na upimaji wa ubora wa vyakula.
Vilevile katika kipindi cha 2016/17 Shirika kwa kutumia wataalamu wake wa
ndani limeweza kutengeneza na kufufua vifaa vya maabara (scientific
equipment) na hivyo kuweza kuokoa Fedha nyingi ambazo zingetuka aidha
kununua vifaa vingine ama kuleta wataalamu kutoka nje ya nchi kufanya
matengenezo. Utaalamu huu ukiendelezwa utaweza kusaidia taasisi nyingine
nyingi za Serikali na hata viwanda kuweza kufufua vifaa na mitambo iliyokufa
na hivyo kuokoa gharama kubwa na muda. Vifaa hivyo ni kama
inavyoonekana katika jedwali;
Na: Kifaa Kitengo
1 Water Bath Chakula na bioteknolojia
2 Distiller Chakula na bioteknolojia
3 Nuve Incubator Chakula na bioteknolojia
4 Stomacher Chakula na
9
bioteknolojia
5 GerhardtKjedahl Kemia ya Viwanda
6 Oxford XRF Mazingira
7. Eltra CHS Analyser Nishati
5.2 MAANDIKO YA MIRADI
Katika kipindi 2016/17 Shirika limefanya juhudi kubwa ya kuandika miradi mbalimbali
ya utafiti, na miradi ya kujenga uwezo (capacity building projects) kwa ajili ya
kutafuta fedha za utafiti na kujenga uwezo wa taasisi. Miradi hiyo iliwasilishwa
Wizara ya Fedha, UNIDO, DANIDA, JICA, WB, USAID, HDIF n.k. Miradi hii imelenga
sekta za Mafuta na Gesi, Makaa ya Mawe, Chuma, Usindikaji vyakula
(agroprocessing), ngozi na TEHAMA. Katika miradi hiyo, DANIDA iliweza
kufadhili mradi wa kutathmini tekinolojia na ubunifu mbalimbali ambao unastahili
kuibuliwa na kuendelezwa kutokana na miradi ya kitafiti iliyofadhiliwa na Danida
Tanzania. Vilevile, miradi mbalimbali ya kutoa huduma za kitaalamu pamoja na
ukaguzi wa viwanda iliandikwa kwa viwanda mbalimbali .
6.0 HUDUMA KWA VIWANDA NA WADAU WENGINE
6.1 UKAGUZI WA VIWANDA VILIVYOKUFA KWA LENGO LA KUSHAURI
SERIKALI
TIRDO kupitia Msajili wa Hazina ilifanya ukaguzi wa viwanda viwili
vilivyofungwa ikiwa ni pamoja na kiwanda cha chai Mponde (Mponde Tea
Factory) na kiwanda cha ngozi Mwanza (Mwanza Tanneries ltd). Ukaguzi huo
ulihusisha pia tathmini ya mitambo na teknolojia zilizopo ili kuweza kushauri
serikali juu ya ufufuaji wa viwanda husika.
Pia, TIRDO kwa kushirikiana na NDC, ilifanya ukaguzi katika kiwanda cha
matairi (General tyre) cha Arusha na TIRDO ina uwakilishi katika kamati ya
Kitaifa ya kushauri kuhusu ufufuaji wa kiwanda hicho.
6.2 UPEMBUZI YAKINIFU KWA UANZISHWAJI WA VIWANDA
(FEASIBILITY STUDIES FOR START UP INDUSTRIES)
TIRDO imefanya upembuzi yakinifu (feasibility study) wa uanzishwaji wa
kiwanda cha kuzalisha viuatilifu (pesticides) Bajuta Arusha, kiwanda cha
10
nyama Sumbawanga na uanzishwaji wa viwanda vya madawa Simiyu. Vilevile
Shirika linategemea kushiriki katika kufanya upembuzi yakinifu katika
uanzishwaji wa kiwanda kikubwa cha chaki Maswa Mkoani Simiyu, kiwanda
cha kusindika nyanya (Tomato paste) mkoani Morogoro na viwanda vingine
vinavyoanzishwa na mifuko ya hifadhi za jamii pamoja na majeshi ya ulinzi na
usalama.
6.3 KUANZISHWA KWA VIWANDA VIWILI VYA MADAWA MKOANI
SIMIYU
TIRDO kwa kushirikiana na Taasisi nyingine nane zimeandaa andiko la
kitaalamu kuhusu uanzishwaji wa viwanda viwili kimoja cha bidhaa za pamba
za mahospitalini na kingine cha kuzalisha dripu mkoani Simiyu. Tayari andiko
limekwisha wasilishwa kwa Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu na kupatiwa
Baraka zote. Inategemewa kuanza kwa upembuzi yakinifu baada ya
kukamilisha taratibu za kifedha na kisheria kati ya NHIF na TIB. Taasisi
nyingine ni pamoja na NDC, TFDA, TBS, TEMDO, NEMC na MSD.
6.4 UPIMWAJI WA UBORA WA MAKAA YA MAWE YANAYOPATIKANA
TANZANIA
Shirika kupitia maabara yake ya makaa ya mawe limeweza kutoa taarifa sahihi
kuhusu ubora wa makaa ya mawe ya Tanzania na hivyo kuweza kutatua
mgogoro uliookuwepo kati ya kiwanda cha simenti cha Dangote na Serikali.
Maabara hii imeweza kusaidia kuepuka hasara kwa Serikali kwa viwanda
kuacha kuagiza makaa ya mawe nje ya nchi na badala yake kutumia makaa
ya mawe ya Tanzania. Maabara inakwenda sambamba na kufanya utafiti wa
nishati mbadala na kubuni tekinolojia za matumizi bora ya makaa ya mawe
viwandani na majumbani. Tayari Wizara ya nishati na madini imekwisha kutoa
agizo la kutaka TIRDO kwa Kushiriana na GST kupima ubora wa makaa ya
mawe nchini, vilevile katika bajeti ya maendeleo ya mwaka 2016/17 lipo
fungu kwa ajili ya kufanya utafiti na kuboresha ‘coal briquettes’ zinazozalishwa
na wajasiriamali wa Tanzania.
11
Maabara ya kupima ubora wa makaa ya mawe TIRDO
6.5 UKAGUZI WA MATUMIZI YA NISHATI VIWANDANI NA MAJENGO YA
SERIKALI (ENERGY AUDITING)
TIRDO inatoa huduma za kitaalamu viwandani amabazo zinalenga kupunguza
gharama za nishati kati ya Asilimia 10 hadi 20. TIRDO imetoa huduma hizo
kwenye viwanda takribani vitano katika mwaka 2016/17.
Ukaguzi wa matumizi ya nishati katika moja ya kiwanda
6.6 UKAGUZI NA USHAURI WA KUZUIA UCHAFUZI WA MAZINGIRA
VIWANDANI (ENVIRONMENTAL AUDITING)
Shirika katika mkakati wa kupunguza uharibifu wa mazingira katika viwanda
vinavyozalisha bidhaa mbalimbali limetoa huduma za upimaji wa viwango vya
hewa zinazochafua mazingira, viwango vya kelele vinavyozidi katika sehemu
mbalimbali ndani ya viwanda na viwango vya vumbi litolewalo wakati wa
12
uzalishaji ndani ya viwanda. Lengo ni kuhamasisha uzalishaji wa bidhaa bora
bila kuchafua mazingira katika viwanda. Huduma zilitolewa katika viwanda vya
sigara, vinywaji baridi, bia, simenti, makaratasi, mbao na mtambo wa kuzalisha
umeme wa Ubungo (Gas Power Plant).
6.7 UPIMAJI UBORA WA VIFAA NA MAJENGO BILA KUHARIBU VIFAA
(NON-DESTRUCTIVE TESTING)
Shirika kwa kushirikiana na kampuni binafsi liliandaa andiko la kufanya kazi ya
uhakiki wa maungio katika bomba la gesi la kutoka Tanga hadi Uganda lakini
halikufanikiwa kukidhi ushindani. Vilevile Shirika kwa kushirikiana na kampuni
ya TASA linaendesha mafunzo ya kitaalamu ya NDT yatakayowezesha wazawa
kushiriki katika sekta ya mafuta na gesi. Kwasasa wafanyakazi watano wa
TIRDO wanaendelea na mafunzo hayo ambapo watakapo hitimu watapatiwa
vyeti vya umahiri hivyo kuweza kutambulika kimataifa.
Kwa mwaka 2016/17 Shirika limehakiki maungio ya kivuko cha MV Njombe
Pamoja na kufanya ukaguzi katika mtambo wa kuzalisha mafuta wilayani Chato.
Uhakiki wa maungio katika kivuko cha MV Njombe kwa kutumia XRay
13
6.8 USALAMA WA VYAKULA MAHOTELINI
Katika kuhakikisha ubora na usalama wa bidhaa za chakula ili kumlinda mteja
shirika limepima sampuli mbalimbali za vyakula na maji ili kuangalia ubora
wake na kuona kama vinakidhi matakwa ya viwango vya kimataifa
vinavyokubalika katika vyakula. Pia wataalamu wametoa huduma za ushauri
kuhusu ubora na usalama wa chakula kwa wasindikaji, na watoa huduma za
hoteli.
6.9 UHAKIKI WA MAABARA (LABORATORY ACCREDITATION)
Ili kuweza kutoa huduma zinazokubalika kimataifa kwa wazalishaji viwandani
Shirika liko katika mkakati wa kupanua wigo wa uhakiki wa maabara yake ya
chakula ili iweze kutoa huduma katika maeneo ya upimaji maji, samaki, asali
na nyama katika viwango vya kimataifa. Maabara hii ya chakula ndiyo pekee
iliyohakikiwa kimataifa kwa TIRDO. Aidha Maabara ya mazingira imekwisha
omba usajili (SADCAS) na kuanza hatua za mwanzo za kufanya ushindani wa
kimaabara (profiency testing) ambao unahitajika katika hatua za kuhakiki.
Inategemewa kwamba maabara hii iweze kuhakikiwa katika upimaji wa maji
safi na maji taka kwa kuanzia na kisha baadae kupanua wigo wa uhakiki.
Maabara iliyohakikiwa ya Chakula
6.10 KUTANGAZA SHUGHULI ZA SHIRIKA (MARKETING)
Katika hatua za kutafuta masoko, Shirika limeshiriki katika maonyesho
mbalimbali ili kujulisha umma juu ya shughuli za Shirika. Maonesho hayo ni
pamoja na maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam, maonesho ya
wakulima “Nanenane” na maonesho ya kwanza ya Viwanda Dar es Salaam.
14
Shirika pia limetoa makala zaidi ya saba katika magazeti mbalimbali nchini
ikiwa ni hatua za kueleza umma wa Watanzania juu ya Shughuli mbalimbali za
Shirika. Aidha Shirika linatafuta fedha ili kuweza kujitangaza zaidi ili Wadau
wote wafahamu shughuli zinazofanywa na shirika.
7.0 UTAWALA
Katika kuboresha huduma za Shirika, Shirika liko katika hatua mbalimbali za
kukamilisha yafuatayo:-
i) Kanuni za Utumishi na Motisha (Staff Regulations and Incentive
Scheme)
ii) Muundo wa Utumishi (Scheme of Service).
iii) Kupitia upya sheria ya Shirika (Review of TIRDO Act)
vi) Kanuni za Fedha (Financial Regulation)
vii) “Land use, feasibility and Business plan”
viii) Muundo wa urishwaji madaraka (Staff succession plan)
Katika kuendeleza watafiti, Shirika liliwapeleka kusoma kozi fupi na za muda
mrefu ndani na nje ya nchi wafanyakazi wake. Wafanyakazi wanne wa Shirika
wanafanya masomo ya Shahada ya uzamivu (PhD) na mfanyakazi mmoja
anafanya mafunzo ya muda mfupi nchini India.
8.0 CHANGAMOTO
Katika kutekeleza majukumu yake Shirika linakabiliana na changamoto
mbalimbali kama vile:-
8.1 Kupata ruzuku ndogo toka Serikalini ambayo:-
i. kuathiri shughuli za utafiti hivyo kutegemea wafadhili tu.
ii. Kushindwa kuboresha na kuhakiki Maabara kuwa na viwango vya
kimataifa
iii. Kushindwa kujenga uwezo wa kutosha kwa wataalamu katika kozi za
utaalamu za muda mfupi (professional training) na mafunzo ya elimu
ya juu (M.Sc. na PhD).
iv. Kushindwa kumalizia majengo yaliyokusudiwa kutumika kwa kazi za
utafiti yakiwemo jengo la teknolojia ya habari na karakana za uhandisi.
15
8.2 Viwango vidogo vya mishahara kwa watumishi ukilinganisha na sekta
nyingine.
8.3 Viwanda vinavyomilikiwa na makampuni ya Kimataifa hutaka kufanyiwa kazi
na mashirika/asasi ambazo huduma zake hutambulika Kimataifa na ziko nje
ya nchi.
9.0 MIKAKATI YA UFUMBUZI WA CHANGAMOTO
9.1 JUHUDI ZA UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA TIRDO
Juhudi za utatuzi wa changamoto zilizopo ni kama ifuatavyo:-
9.1.1 Shirika limendaa maandiko ya Miradi mbalimbali kwa Serikali ili kujenga
uwezo kwenye maabara za metallurgy, kwa ajili ya chuma, energy kwa ajili
ya makaa ya mawe na gesi, na agro-processing kwa ajili ya vyakula (value
addition) kwas asa huduma hizi wadau wanazipata toka nje ya nchi na
kuigharimu nchi kiasi kikubwa cha fedha za kigeni. Kwa kufanya hivyo
mapato yataifanya TIRDO kupunguza kuitegemea Serikali.
9.1.2 Sehemu ya mapato ya Shirika kutokana na huduma kwa wateja hutumika
kuwaendeleza wataalam. Pia shirika kwa kushirikiana na taasisi zingine za
utafiti zinaendelea na juhudi za kuishawishi Serikali iweze kutoa pesa za
kufanyia utafiti ambazo sasa zinatolewa kupitia COSTECH.
9.1.3 Shirika linatekeleza mkakati wa mipango ya maendeleo ‘Corporate
Strategic Plan’. eneo moja ambalo limelenga kulikwamua shirika kifedha ni
mpango wa muda mfupi wa kati na muda mrefu wa matumizi bora ya
ardhi yote ya TIRDO (land use plan, feasibility study and Business plan).
Mpango huo tayari umeanza kutekelezwa kwa kutafuta wadau mbali mbali
kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya uwekezaji.
9.1.4 Kuimarisha uwezo wa kutoa huduma zake kufikia kiwango
kinachotambulika kimataifa kwa kuhakiki maabara.
9.1.5 Juhudi za upatikanaji wa Hati Miliki kwa viwanja viwili ambavyo vina kesi
Mahakamani zinaendelea.
9.1.6 Shirika kuimarisha mashirikiano na taasisi zingine za ndani na nje ya nchi.
16
9.1.7 Kuwaongezea watafiti uwezo (Skills) katika kuandika maandiko ya miradi
(competitive proposal writing).
9.1.8 Shirika kujitangaza kwa wadau wake.
10.0 TIRDO NA MIKAKATI YA AWAMU YA UCHUMI WA VIWANDA
10.1 UTANGULIZI:
Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) limejipanga ili
kuweza kutoa mchango wake katika mikakati ya kukuza uchumi wa viwanda
Tanzania kama inavyoelekezwa na Serikali ya Awamu ya tano. Katika
kutekeleza maelekezo mbalimbali ya serilkali ya Awamu ya Tano yanayolenga
kuwa na uchumi wa Viwanda kwa kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020,
Viwanda vimechangia kwa zaidi ya Asilimia 40% ya ajira Tanzania na pia
Mchango wa Viwanda kwenye Pato la Taifa kuongezeka toka Asilimia 9.9 hadi
Asilimia 15, Shirika limebuni mikakati kadhaa ambayo ikitekelezwa itatoa
matokea chanya na kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya viwanda
Tanzania.
TIRDO imejipanga na imebuni Miradi inayolenga Sekta ya Gesi na Mafuta,
Makaa ya Mawe, Chuma, Usindikaji wa Vyakula, Ngozi na TEHAMA. Miradi
iliyobuniwa ni ile inayolenga kuongeza Pato la taifa, kuongeza ajira na
kuendeleza teknolojia.
Ili kutekeleza hayo, Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania
(TIRDO) limepanga kufanya yafuatayo kwa kipindi cha 2016 – 2020/21 kama
litawezeshwa.
10.1.1 Mchango wa Pato la Taifa kutokana na viwanda kupanda
toka 9.9% hadi 15% ifikapo mwaka 2020.
Katika hili TIRDO imeandaa miradi 21 ambayo katika utekelezaji wake utaleta
tija kwa viwanda na hivyo kuchangia katika ongezeko la pato la Taifa hadi
kufikia 15% mwaka 2020. Miradi hiyo inalenga sekta ya kilimo
(Agroprocessing), sekta ya Ngozi (leather goods), sekta ya mafuta na gesi (oil
17
and gas) na Makaa ya Mawe na Chuma. Miradi hiyo iliwakilishwa Wizarani ili
kuingizwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano.
10.1.2 Sekta ya Viwanda kuongeza ajira kufikia asilimia 40 ya ajira
zote ifikapo 2020
TIRDO kwa kushirikiana na Serikali itaweka kipaumbele kwenye tafiti na
huduma za kitaalamu kwenye viwanda vinavyotumia malighafi zinazozalishwa
hapa nchini kama vile kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili; Viwanda hivyo ni
pamoja na viwanda vya nguo, sabuni korosho, matunda n.k
10.1.3 Mikakati ya kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha viwanda
vikubwa na vya kati na kuweka utaratibu wa kuvilinda dhidi
ya viwanda vya nje
Kwa kutumia wataalam wake, TIRDO itatoa huduma za kitaalam za ushauri
(Feasibility studies) kwa wawekezaji wa viwanda. TIRDO inao uzoefu wa
kutosha na imekuwa ikitumika na Benki ya Rasilimali (TIB) kutoa ushauri kwa
wateja wanaokopa kwa ajili ya kuanzisha viwanda. Hivyo TIRDO itatoa
mchango mkubwa wa kuishauri Serikali na wawekezaji juu ya uanzishwaji wa
viwanda na kuvilinda dhidi ya viwanda vya nje kwa kuhakikisha ubora wa
bidhaa zake ambazo zinazalishwa kwa gharama nafuu.
10.1.4 Kujenga mazingira rafiki yatakayowezesha kupunguza
gharama za uwekezaji na uendeshaji wa viwanda
TIRDO inatoa huduma za kitaalam za matumizi ya nishati na kuweza kusaidia
kupungua gharama za matumizi ya nishati viwandani kati ya asilimia 10 hadi
30. TIRDO imetoa ushauri huo wa kitaalam kwa viwanda na majengo ya
Serikali. Hivyo TIRDO itajitangaza ili kufikia wadau wengi zaidi ili kuhakikisha
viwanda vinazalisha bidhaa kwa gharama nafuu ya Nishati.
TIRDO pia hutoa huduma za kitaalam juu ya kupunguza athari za uchafuzi wa
mazingira ili kupunguza athari ya mazingira zinazotokana na viwanda lakini pia
18
kusaidia viwanda visisimamishe shughuli zake kwa sababu ya uchafu wa
mazingira wanapokaguliwa na wadhibiti wa mazingira kama (NEMC). TIRDO
itajitahidi pia kwenye eneo hili ili wadau wengi waendeshe viwanda bila
kuathiri mazingira na shughuli za uzalishaji.
10.1.5 Kuanzisha viwanda vya msingi vinavyotumia malighafi ya
chuma katika maeneo ya Liganga na Mchuchuma
Katika miradi iliyobuniwa na TIRDO ni ule wa Metallajia (Metallurgy) ambao
unalenga kupima ubora wa malighafi na bidhaa za chuma. Mradi huu
utasaidia wenye viwanda vinavyotumia malighafi ya chuma kuweza kupata
aina ya chuma bora ambazo zinaweza kukidhi ubora wa kimataifa hivyo
kuweza kuongeza soko na kipato. Hii itasaidia kuongeza pato la taifa pia ajira.
Pamoja na hayo, maabara hiyo pia itasaidia sana kuhakikisha kuwa chuma
kinachotumia kwenye nondo za ujenzi wa majumba ya ghorofa zinakuwa bora
na kupunguza athari ya majengo kubomoka hovyo.
10.1.6 Sekta ya viwanda kuongeza fursa za masoko hususan yenye
upendeleo wa ushuru wa forodha
TIRDO ina maabara ya chakula iliyohakikiwa kimataifa ambayo husaidia
kupima ubora wa bidhaa za chakula. Kwa hivyo TIRDO itasaidia sana kuweza
kusaidia katika kuongeza thamani kwa bidhaa na kuweza kupata masoko
mazuri kimataifa. Iwapo itaongezewa uwezo maabara hiyo itapima ubora wa
Bidhaa kama Asali, Maziwa, Nyama, Samaki, Maji n.k. Vipimo ambavyo
vinatambuliwa kimataifa.
10.1.7 Kuendeleza kazi ya ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati hasa vinavyosindika mazao
Maabara ya chakula itasaidia pia kuongeza thamani za bidhaa kwenye
viwanda vodogo na vya kati. Pamoja na hilo, TIRDO itaendelea kubuni
mitambo mbalimbali nafuu kwa wawekezaji wadogo na wa kati
wanaojishughulisha na usindikaji wa mazao (Agroprocessing).
19
10.1.8 Benki ya Rasilimali (TIB) kupanua wigo wa Dirisha Maalumu ili liweze kutoa huduma zake kwenye maeneo yote nchini ikiwemo Tanzania Zanzibar
TIRDO ina mahusiano ya karibu na Benki ya Rasilmali (TIB) na ina
makubaliano (MOU) ya kushirikiana katika kufanya tathmini za viwanda kwa
wale wanaochukua mikopo kwa ajili ya uanzishaji wa viwanda. Kwa hiyo,
TIRDO itakuwa na nafasi nzuri pia kuweza kuishauri Benki na wawekezaji wa
Zanzibar juu ya uanzishwaji wa viwanda. Pamoja na hayo, TIRDO pia ina
mahusiano mazuri ya kikazi na Wizara ya Viwanda na Biashara ya Zanzibar na
Zanzibar State Trading Corporation.
10.1.9 Kuhakikisha kuwa viwanda vilivyopo vinafanya kazi
Ili kuhakikisha kuwa viwanda vilivyopo vinafanya kazi kwa kiwango
kinachokubalika, tathmini ya uwezo wa uzalishaji na teknolojia haina budi
kufanyika. TIRDO kwa kushirikia na taasisi nyingine imejipanga kufanya
tathmini hizo pindi itakapowezeshwa.
10.1.10 Msajili wa Hazina kushughulikia viwanda ambavyo vimeshindwa kufanya kazi.
Ili kuhakikisha kuwa viwanda vilivyokufa wanapewa wawekezaji wenye uwezo,
tathmini ya uwezo wa uzalishaji na teknolojia haina budi kufanyika. TIRDO
ilishawasiliana na Wizara na Msajili wa Hazina kuwa iko tayari kufanya hizo
tathmini kwa kusaidiana na taasisi nyingine za serikali kwani ina utaalam wa
kutosha na imeshawahi kufanya shughuli kama hizo.
11.0 HITIMISHO
Shirika likiwezeshwa kwenye utafiti na kupewa msukumo unaostahili, Shirika
litapiga hatua katika kutatua matatizo yanayovikabili viwanda vyetu kuongeza
uzalishaji na ubora wa bidhaa hivyo kukuza uchumi wa nchi kwani nchi
zilizoendelea pato lake kubwa hutokana na viwanda.
20
MUUNDO WA SHIRIKA
Kiamb. ‘A’
21
KIAMBATISHO B TAFITI ZILIZO FANYIKA TIRDO
1. Kuzalisha “Sodium Alginate” kutokana na kaoli
2. Kuzalisha “Caustic Soda” na kutokana na Magadi
3. Uzalishwaji wa furfural na furane resins kutoka katika mabaki ya pentosan
4. Utengenezaji wa “essential oil” kutokana na majani kama michungwa, michachai
5. Utunzaji wa bidhaa za mbao kwa kutumia gundi iliyozalishwa kutokana na mafuta ya
maganda ya korosho, gundi hiyo pia ilitumika katika utengenezaji wa ‘plywood’ na
‘chipboard’
6. Kuondoa sumu ya Ocharatoxin A katika kahawa. Mradi huu ulifadhiliwa na Jumuiya ya
ulaya, na kutekelezwa katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha
7. Kuboresha uyoga kwa kuzalisha uyoga wenye madini joto na uyoga wa dawa (medicinal
mushroom)
8. Kuboresha unga wa muhogo uliochachushwa (fermented cassava flour) unaozalishwa
kwa njia za asili lengo likiwa ni kuongeza ubora wa bidhaa hiyo, kuongeza udumu (shelf
life) na usafi wa bidhaa, kwa kuondoa sumu aina ya cyanide – uliopelekea
kutengenezwa kwa mashine ya kuchakata muhogo (cassava grating machine). Mashine
hizi zilibuniwa na kutengeneaw kwa ushirikiano kati ya TIRDO na Intermech Engineering
Ltd, na kusambazwa na TIRDO katika mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma na
baada sehemu mbambali ndani na nje ya nchi (e.g. Malawi)
9. TIRDO kwa kushirikiana na “Tropical Pesticide Research Institute” ilifanya utafiti wa jinsi
ya kutunza bidhaa ya mbao kwa kutumia mimea “plant preservative” ambayo
inapatikana hapa hapa nchini ili kulinda bidhaa za mbao kutokana na wadudu na ukungu
(fungus) ambao wanaharibu na kusababisha mbao kulika .
10. Mfumo wa ufuatiliaji wa bidhaa za chakula ambapo ulipelekea kuanzishwa kwa GSI
Tanzania ambayo ni kampuni inayota namba za mstari ‘Bar code’ nchini Tanzania.
11. Kuongeza thamani kwenye taka ngumu zitokanazo na uzalishwaji katika viwanda vya
ngozi (Value addition in leather solid wastes to produce leather boards).
12. Kutumia mazao ya kilimo na mabaki ili kupata nishati mbadala (Industrial Bioconversion
of selected Tanzania crops and residues into value added products using Biotechnology)
13. Makaushio yanayotumia nishati ya Jua Tunnel solar dryer)
22
14. Uboreshaji wa machine za kusaga nafaka kwa kuondoa chembechembe za chuma
zinazochanganyika na unga.
15. Usalama wa mtandao (Cyber Security) kwa mazingira ya Tanzania iliyopelea kuanzishwa
kwa maabara ya ‘Cyber security’ TIRDO.
16. Uzalishaji wa bioethanol kutoka katika mimea ya Dioscorea sansibarensis na Pyrecantha
kaurabasana.
17. Uzalishaji wa biogesi kutokana na taka zitokanazo na usindikaji wa mafuta ya kula
(spent bleaching earth) na kinyesi cha ng’ombe (cow dung manure)
18. Utengenezaji wa mashine ya kukamulia juice ya machungwa iliyofungwa Wilaya ya
Muheza, Tanga.
19. Kutathimini viwanda vinavyoanzishwa na wateja wanaokopa pesa (mtaji) kutoka katika
Benki ya TIB Thathimin imeshafanyika Rombo, Kilimanjaro, Bukoba, Kagera, Pwani,
Arusha, Sumbawanga, Mahonda, Zanzibar, Bunju, Kigamboni, DSM, Kibaha Pwani.
20. Mradi wa kuwasaidia wajasiriamali wa mashamba ya chumvi kuongeza thamani ya zao
la chumvi huko Wawi Pemba, Zanzibar.
21. Mradi wa kutengeneza na kufundisha ukaushaji wa mazao ya kilimo, Mikoa ya Lindi na
Mtwara kwa ushirikiano na FAO.
22. Ufundishaji, utengenezaji na usambazaji wa makaushio ya jua katika mkoa wa Pwani na
shirika la Kibelijiji linalo hudumia wakulima wadogowadogo vijini (VECO).
23. Mradi wa kutengeneza, makaushio ya wajasiriamali wa zao la pilipili, Mikumi, Morogoro
kwa ajili ya kuzuia Tembo waharibifu na kuongeza thamani ya zao hili kwa kushirikana
na ‘World Animal Protection’ ya Nairobi, Kenya.
KIAMBATISHO D
HUDUMA VIWANDANI
1. Upembuzi yakinifu na kutayarisha mpango wa ufufuaji wa kiwanda cha ngozi Mwanza na chai
Mponde Tanga (Mwanza Tanneries na Mponde tea factory)
2. Kupunguza uharibifu wa mazingira katika viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali kwa kutoa
huduma za upimaji wa viwango vya hewa zinazochafua mazingira, viwango vya kelele katika
sehemu mbalimbali viwandani na viwango vya vumbi litolewalo wakati wa uzalishaji viwandani
3. Kupima sampuli mbalimbali za vyakula na maji ili kuangalia ubora wake na kuona kama vinakidhi
matakwa ya viwango vya kimataifa vinavyokubalika katika vyakula
23
4. TIRDO imeshiriki katika mradi wa gesi huko MnaziBay Mtwara mpaka Msimbati kwa kuhakiki
ubora wa bomba linalosafirisha gesi hiyo kwa kupima pasipo kuharibu maungio yote ya bomba
hilo ili kuepusha madhara kwa mazingira na kwa wakazi wa maeneo mbalimbali ambapo bomba
hilo limepita. Bomba hilo lilikuwa lenye urefu wa kilometa 26.
5. Shirika limetoa mafunzo kwa wajasiriamali katika maeneo ya uchomeleaji na pia teknolojia za
uboreshaji chuma viwandani
6. Shirika lilitoa huduma ya ukaguzi wa vifaa vya kihandisi ikiwa ni pamoja na matanki ya mafuta,
vivuko (pantoon), mitambo ya kuzalisha umeme
7. Upimaji wa ufanisi wa majiko ya mkaa na yale yanayotumia mafuta ya mbegu kutoka vikundi
mbalimbali ili kupata matumizi bora ya nishati
8. Matumizi bora ya nishati katika viwanda, majengo ya ofisi na makazi (energy auditing)
9. Mafunzo ya ‘Good manufacturing practices (GMP)’, ‘Good hygine practices (GHP) na ‘Hazard
analysis critical control point’ (HACCP) kwa viwanda vya chakula na wajasiriamali
10. Kufanya upembuzi yakinifu (feasibility study and evaluation) katika viwanda vipya na viwanda
vinavyoongeza uzalishaji chini ya Benki ya Uwekezaji (Tanzania investment Bank)
24
KIAMBATISHO E
TIRDO PROJECTS TO SUPPORT INDUSTRIALIZATION DRIVE
1. TIRDO Industrial Park
Establishment of industrial park at TIRDO facility for incubation and transfer of industrial and agro
technologies
Incubation of entrepreneurs for various agro processing and industrial technologies is necessary to effective
technology transfer. Facility for technology incubation is currently lacking at TIRDO
OBJECTIVE
Industrial park established at TIRDO by 2018
Reverse engineered products for industries and agro-processing
Industrial incubates graduate by 2020 Increased Investment in agro-processing
Increased job creation
Increased government revenue through new investment in agro-processing
2. Petro-Chemical Industries
Petrochemical laboratory at TIRDO
There is no specialized laboratory for the petrochemical industry in Tanzania. Most of the petrochemical
products e.g. fertilizers need tailored quality assurance services to ensure quality products to meet both
national and internal standard requirements
OBJECTIVE
Establish an accredited petrochemical laboratory at TIRDO
Establish database for nutrient requirement in each agricultural zones
Establish quality assurance systems in petrochemical factories
3. Agro-industries
Reducing Chromium in tanneries effluent waste through unit process recycling in Leather Industries
(TIRDO)
A lot of Chromium is disposed in tanneries waste water Leather Industries and is difficult to recover from
tanneries effluent.
This is environmental hazard and adds more expenses in waste water treatment
OBJECTIVE
Determination of residue Chromium in tanneries effluent
Training on Chromium recycling process to tanneries SMMES
Recycling within the tanning processing area
4 Market access of Tanzania Agro- products through accredited testing services (TIRDO)
In adequate accredited laboratory services to support the agro-industry in Tanzania
Most testing services such as residue analysis in honey, meat and milk are sourced outside the country.
These services are expensive and make the Agro-industry in Tanzania less competitive
No single laboratory catering for seafood in all the coastal zone in Tanzania
The Tanzania coast is more endowed with fish than other countries sharing the Indian ocean coast because
of adverse weather (warm and cold current from Mombasa and Mozambique respectively, however this vast
resource is under exploited because of lack of support services
OBJECTIVE
Extend accredited capacity of TIRDO (equipment and human capacity) to include residue analysis,
pesticides residues and mycotoxins analysis
25
Accreditation of food analysis, agro-chemistry environment and health safety laboratories through SADCAS
Establish and accredited a seafood laboratory using the space and expertise available at TIRDO
5 Innovative technologies for reduction of post harvest losses and efficient utilization of resources in the
agro-industry sector (TIRDO)
Post-harvest losses in cereals e.g. rice is about 40% attributed to brokenness, storage pests and
inappropriate technology.
Valuable resources such as rice brand oil and nutraceutical molecules in brand and husk are not tapped due
to lack of appropriate technology.
Increasing rise of people living in cities more rice is being consumed than ever before. Because rice starch is
generally of high glycemic index (GI) , the city dwellers are at risk of health problems associated with high
GI foods including diabetes and cardiovascular diseases
Lack of appropriate processing technologies for small grains such as millet, sorghum and finger millet is
disincentive to cultivate and processing of these draught resistant and highly nutritious cereals
OBJECTIVE
Pilot appropriate handling, drying and di-husking rice to reduce brokenness
Employ molecular techniques to classify Tanzania rice varieties into high and low GI and develop tailored
products for infants and elderly
Develop process for extraction of rice bran oil and blending with conventions oils to produce functional
cooking oils
Extraction and characterization of nutraceutical compounds for rice husk and bran and develop various
nutraceutical products
Develop appropriate technology for processing small grains and develop various products form them
Establish process for biofuel and biofertiliser production from cereal processing waste to result to zero
waste
6 Value Addition on Tanzania vegetable tanned leather using Kaolin from Tanzania (TIRDO)
There is Low quality of hides and skins and poor value addition locally. Vegetable tanned leather
exhibits lower shrinkage temperature. Chrome tanning is associated with environmental degradation
OBJECTIVE
Replacement of traditional tanning by introducing mimosa and aluminium sulphate from kaolin (semi-
metal tanning)
Skills development to SMMEs
Utilization of locally available raw materials to tanning in replacement of imported ones
7 Establishment of accredited leather testing laboratory (TIRDO)
Absence of accredited leather testing laboratory leads to use of health hazardous chemicals in leather
processing. There is also lack of quality assurance practices for exported leather and leather goods.
Rejection or down grading of leather and leather goods in external market is common coupled with lack of
enforcement to tanners to improve quality of their products. Utilization of leather goods with harmful
chemicals to human health is also common in Tanzania
OBJECTIVE
Building and accrediting special leather testing laboratory
Testing and certifying leather and leather goods for internal and external market
Advising tanners about the quality of their leather and ways to improve based on found results after
testing of leather properties
8 Value addition on leather solid wastes to produce leather boards at TIRDO
High production of leather solid wastes in tanneries. It is also Difficult disposing of leather solid wastes as
they contain chromium (hazardous chemical)
OBJECTIVE
Recycling of leather solid wastes to produce leather goods
26
9 Production of fine chemicals and allied products from Cashewnut Shells
Huge amount of cashewnut shells are produced and they are environmental concern. Cashewnut shells are
important resource for industrial chemicals but little is utilized in Tanzania. Fluctuating price of cashew
does not take on board the value of the shells and hence loss to the farmers
OBJECTIVE
Production of cashewnut shell liquid for fibreboard industries
Production of Arcadic acids for chemical industries
Compaction of cashewnut shell for solid waste for bio-energy
10 Coal for Industries and Households
Rural Electrification through Decentralized Small to Medium Scale Electricity Generation Facilities
Using Locally Available Coal and Biomass (TIRDO)
Rural electrification is less than 5%. There is also Poor (electrified) services for health, schools and
water supply leading to Poor economic activities, Rampant diseases from use of fuel wood and
Environmental degradation from intensive use of fuel wood
OBJECTIVE
Provision of clean energy technologies for electricity generation
Utilization of locally available coal and biomass materials
Development and dissemination of local technologies for electricity generation
11 Use of carbonized coal briquettes to substitute charcoal and firewood as cooking fuel in Tanzania
(TIRDO)
Rampant diseases from use of fuel wood. Environmental degradation from intensive use of fuel wood.
Also, there drudgery of women in search of fuel wood
OBJECTIVE
Development of carbonized coal briquettes in substitution of fuel wood and charcoal for household
cooking
Utilization of locally available coal and biomass materials
Development and dissemination of local technologies for household cooking
12 Comprehensive assessment of Tanzania coal quality using accredited laboratory (TIRDO)
Despite the abundant coal deposits, less is on their quality. There is a Danger of utilizing quality
(coking) coal for thermal applications. Technology development is impaired in absence of coal quality
information
OBJECTIVE
Establishment of coal quality databank for Tanzania
Undertaking a detailed sampling and analysis of Tanzania coal
13 Iron and Steel
Development of iron and steel technologies from locally available ore deposits (TIRDO)
Existing ore deposit under-utilized and there is Overdependence on scrap metal for iron and steel
industry. There are also low technological capacity in iron and steel industry, Low quality of iron and
steel products, Low iron and steel per capital consumption and hence low GDP
OBJECTIVE
Capacity development to the TIRDO accredited metallurgical laboratory
Carrying out evaluation of raw materials for iron & steel and other related industries.
Characterization and optimization of raw materials and direct reduction (DR) process parameters for
production of high-grade sponge iron from e.g. Liganga and Maganga Matitu iron ores
Develop appropriate iron and steel technologies for SMEs
Transfer the technology of sponge iron as metallic feedstock in rolling mills and foundries to replace
27
conventional scrap metal
Assist local industries to produce high quality iron & steel products e.g. high strength steel
reinforcement bars
14 Oil and Gas
Enhancing Local Content through skills Development in Welding, Inspection, Fabrication for SMEs
to participate in the emerging oil and gas industry (TIRDO)
Welding and inspection skills are low. Participation of local technicians and entrepreneurs in the oil and
gas industry is low. Almost all services in oil and gas are done by foreign companies. There are no
certification services to local practitioners
OBJECTIVE
Welding and inspection skills development to local technicians and entrepreneurs through accredited
welding services
Establishment of certification programs
15 Industrial services
Provision of Professional Coal Analytical Services for Supporting Industrial Coal Users (Cement,
Paper Mills and Others) and the Proposed Thermal Power Plants (Kiwira, Mchuchuma, and Ngaka)
(TIRDO)
Tanzania coal is analyzed abroad. Results of coal analysis from foreign laboratories is skeptical and is
associated with delays. Also, Tanzania coal quality is less known which poses for cheating in coal export
deals. There is also rampant revenue loss due to adulterated coal quality
OBJECTIVE
Strengthening the technical capacity to the coal accredited laboratory at TIRDO
Dedicating the TIRDO coal laboratory into a reference coal laboratory
16 Improving competitiveness to industries through energy management (TIRDO)
Energy cost to industries consumes up to 40% of total revenue. The high energy cost makes industries not
attractive . The high energy cost makes products not competitive regionally and internationally
OBJECTIVE
Introduce energy management practices to industries
Train the industries to adopt the practices and energy efficient technologies
Energy management skills development to industrialists
17 Revival of privatized industries (TIRDO)
Majority of the privatized industries are said to be marginally contributing to the development agenda. Less
is known on their status and some are said to have shifted their basic role
OBJECTIVE
Undertake an industrial audit to establish the status of the privatized industries
Undertake the needs assessment
Establish a prioritized strategy by taking into consideration of employment, GDP contribution and
contribution to socio-economic development
18 Automatic water Quality Monitoring and Reporting in Aquaculture (TIRDO)
There is inadequate supply of fish to the existing fish processing industries. This is due to the lack of
modern technology in aquaculture. There is a need of establishing automatic monitoring and reporting
systems of aquaculture industry in Tanzania and identification of baseline conditions suitable for
aquatic life.
OBJECTIVE
Establishment of automatic monitoring and reporting system in Tanzania
identification of baseline conditions suitable for aquatic life Environmental impact assessment
28
19 Deployment of Wireless Sensor Networks for Industrial Environmental Monitoring
There is great emission of pollutant gases in manufacturing industries. Currently rudimentary technologies
are employed to monitor industrial pollutants. These technologies are inaccurate and unsafe to users
OBJECTIVE
Establish innovate industrial environmental pollutant gases (CO, O2, CO2, CO, SO2, H2S, NO, NO2, HC
and PM10(Lead)) monitoring base on sensor technology
Awareness creation in the use sensor technology to monitor industrial processors
Transfer of sensor industrial process monitoring technology to SMMES
20 Advanced Cyber Security Training Services (TIRDO)
Critical infrastructure security in Tanzania is insufficient. Media used in banking transaction for industrial
business is not safe. There is lack of awareness of cyber security threats
OBJECTIVE
Training on cyber security issues to raise awareness
To establish security measures in Tanzania industrial firms (major automated industrial)
Development of Industrial application software.
21 Environment
Auditing and valorization of Municipal waste for generation of electricity (TIRDO)
Disposal of municipal waste in most of the big cities in Tanzania is a challenge due to lack of appropriate
systems yet the municipal waste is great bioresource which can be converted to biofuels and biofertiliser
OBJECTIVE
To introduce an innovative system for collection, sorting and classifying municipal waste in organic and
non-organic waste
Building an innovative biogas plant for each municipal Dar-es salaam, Arusha, Mwanza, Tanga, Iringa,
Mbeya, Morogoro
Characterize, pre-treat and produce biogas from the organic fraction of municipal waste
The biogas to used to generate electricity to be fed into the national grid
The biogas slurry to be evaluated for biofertiliser to boot peri-urban vegetable production
Recommended