4
HISTORIA YANGU Jina langu ni Paulina Shirima.Nimezaliwa katika kijiji cha Ushiri wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro na nina umri wa miaka 40.Baba yangu anaitwa Michael na mama yangu anaitwa Selestina.Katika uzao wetu tumezaliwa watoto saba,watatu wa kiume na wanne wa kike.Mimi nikiwa mtoto wa mwisho kuzaliwa. Wazazi wangu ni wakulima na hupenda kujishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali pamoja na bustani za mboga ambazo hutumika kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani. Kielelezo no 1 P Shirima

Web viewHISTORIA YANGU. Jina langu ni Paulina Shirima.Nimezaliwa katika kijiji cha Ushiri wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro na nina umri wa miaka 40.Baba yangu anaitwa

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Web viewHISTORIA YANGU. Jina langu ni Paulina Shirima.Nimezaliwa katika kijiji cha Ushiri wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro na nina umri wa miaka 40.Baba yangu anaitwa

HISTORIA YANGU

Jina langu ni Paulina Shirima.Nimezaliwa katika kijiji cha Ushiri wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro na nina

umri wa miaka 40.Baba yangu anaitwa Michael na mama yangu anaitwa Selestina.Katika uzao wetu tumezaliwa

watoto saba,watatu wa kiume na wanne wa kike.Mimi nikiwa mtoto wa mwisho kuzaliwa.

Wazazi wangu ni wakulima na hupenda kujishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali pamoja na bustani za mboga ambazo hutumika kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani.

Kielelezo no 1 P Shirima

Mimi nilianza elimu ya msingi mwaka 1983 katika shule ya msingi Ushiri,chini ya uongozi wa mwalimu mkuu

ambaye jina lake ni Mrs Mtenga.Hatimaye nilimaliza elimu yangu ya msingi mwaka 1989,ila kwa bahati mbaya

sikuweza kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari.Hivyo ilinibidi nikae nyumbani na wazazi wangu na

kuwasaidia kazi mbalimbali zikiwemo za ufugaji na kilimo.

Page 2: Web viewHISTORIA YANGU. Jina langu ni Paulina Shirima.Nimezaliwa katika kijiji cha Ushiri wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro na nina umri wa miaka 40.Baba yangu anaitwa

Kutokana na nia yangu ya kutaka kuendelea na masomo,nilikuwa nikimsumbua mama mara kwa mara kuhusu

suala la shule.Baada ya mwaka mmoja kuisha mwaka uliofuata mzazi wangu alinichukulia fomu ya kujiunga na elimu

ya sekondari.Jambo ambalo lilinifanya nijisikie furaha moyoni mwangu. Baada ya siku si nyingi tarehe ya kufanya

mtihani wa usaili iliwadia na siku hiyo niliwahi mapema sana kwenye kituo cha mtihani.Baada ya siku kama kumi

kupita matokeo yalitoka na nikajikuta nimechaguliwa na kuanza kidato cha kwanza.

Maandalizi ya kuandaa mahitaji ya shule yalianza rasmi huku nikiwa na furaha sana na kuahidi kuwa

nitajitahidi sana katika masomo yangu yote.Mwaka 1991 nilijiunga na elimu ya sekondari ya katika shule ya Ugwasi

sekondari iliyoko wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.Shule hiyo ilikuwa ni ya kutwa,pia ilikuwa ya mchanganyiko wa

wasichana na wavulana. Ilikuwa chini ya uongozi wa mwalimu mkuu Mr Leina. Vilevile ilikuwa na mchepuo wa

masomo ya sayansi na art.

Nilipofika kidato cha pili wazazi wangu walishindwa kuendelea kunilipia ada jambo ambalo lilinisononesha

sana nafsini mwangu. Nikawa naenda shule na kufukuzwa kutokana na kushindwa kulipa ada. Hali hiyo ilinifanya

nikae nyumbani na kulima vibarua ili niweze kulipa ada ya shule. Mungu si athumani kwani ni mkubwa na hamtupi

mja wake,nilibahatika kupata mfadhili ambaye alinilipia ada na nikaendelea na masomo. Nilipofika kidato cha pili

nilifanya mtihani na nikafaulu nikaendelea na kidato cha tatu.Mwaka 1994 nilifanikiwa kumaliza elimu ya sekondari

na kubahatika kuchaguliwa kujiunga na chuo cha ualimu Korogwe,mwaka 1995 hadi 1997 nilihitimu mafunzo yangu

ya ualimu.Kwa bahati mbaya wakati huo ajira zilisitishwa.Hivyo sikuajiriwa kwa miaka minne ila nikaamua kujitolea

ili nipate mahitaji yangu.

Mwaka 2002 nafasi za kazi zilitangazwa katika mkoa wa Tanga.Hivyo ilinilazimu kwenda kwenye

usaili.Nikafanikiwa kuingia kwenye ajira mpya na kuajiriwa kama mwalimu wa daraja la III A kwa masharti ya

kudumu.Nilifanya kazi Tanga kwa muda wa miaka mitatu.Hatimaye nilihamia mkoani Kilimanjaro katika wilaya ya

Moshi mwaka 2005 na kuendelea na kazi yangu ya ualimu.

Page 3: Web viewHISTORIA YANGU. Jina langu ni Paulina Shirima.Nimezaliwa katika kijiji cha Ushiri wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro na nina umri wa miaka 40.Baba yangu anaitwa

Kwa sasa nina mume na watoto watatu.Mwaka 2014 niliamua kujiendeleza na masomo ya diploma ya shule

ya msingi katika chuo cha ualimu Marangu,ambapo hadi sasa bado nipo masomoni kwa muda wa miaka miwili.

Mwisho napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wazazi wangu,mfadhili wangu ambaye ameniwezesha

kuwa kama nilivyo sasa na bila kumsahau mume wangu mpendwa kwa kuniruhusu kuja chuoni.