101

Fitina za Wahhabi Zafichuliwa

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

FITINA ZA WAHHABI ZAFICHULIWA

Kimeandikwa na:

Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Kimetafsiriwa na:

Dr. Muhammad Kanju

Kimetolewa na Kimechapishwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania

S.L.P. 20033 Dar es Salaam - Tanzania

Haki za kunakili imehifadhiwa na:Bilal Muslim Mission of Tanzania

ISBN 9976 956 89 4

Toleo ya Kwanza: 1994 Nakala: 2000Toleo ya Pili 1996 Nakala: 2000Toleo ya Tatu: 1997 Nakala: 1000Toleo ya Nne 1999 Nakala: 1000Toleo ya Tano: 2001 Nakala: 1000Toleo ya Sita: 2003 Nakala: 1000Toleo ya Saba: 2005 Nakala: 5000

Kimechapwa na::ALLIED PUBLISHERS PRIVATE LTD

NEW DELHI - INDIA

Kimetolewa na Kuchapishwa na::BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

S.L.P 20033DAR ES SALAAM - TANZANIA

YALIYOMO

Dibaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 1Utangulizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 2

HUU NI USHI‘A

Maana na Asili ya Ushi‘a . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 5Hadithi ya Vizto Viwili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .13Msingi wa Imani wa Shi‘a Ithna ‘ashariya . . . . . . . . . . . . . . . . . . 19Daraja ya Muhammad (s.a.w.w.) na Ahli zake (a.s.) . . . . . . . . . 23Al-Hashawiyah Wahhabiya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .25

UCHAMBUZI WA KIJITABU“WHAT IS SHI‘AISM?” (USHI‘A NI NINI?)

Umasuma wa Maimamu: . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 29Imani ya Sunni kuhusu Ismah ya Mitume . . . . . . . . . . . . .29Imani ya Shah Waliullah, Shah ‘Abdu ’l-‘Aziz, Muhyiddin Ibn Al-‘Arabi na wengineyo kuhusu Ismat ya Maimamu 12 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .33Tahreef katika Al-Futuhat . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .36Mwishilizo wa Utume . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .38

Tahreef . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 40Baadhi ya mifumo ya Wahhabi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .40Itikadi ya Shi‘a . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 42Mwelekeo wa Shi’a . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .48Hadith za Sunni . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .50Mwelekeo wa Sunni . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 52

Hadith . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 55Nyororo ya dhahabu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .57

Bada’ . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 63Maana ya Bada’ . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 63 Dhabibu ya Nabii Isma‘il . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 63Alivyopewa Tawrat Nabii Musa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .64Imam Fakhruddin ar-Razi na Bada’ . . . . . . . . . . . . . . . . . . 67Az-Zamakhshari na Bada’ . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 68Al-Baydawi na Bada’ . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .69Mungu wa Wahhabi alia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .69

Sahaba . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 70Maana ya Sahaba . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .70Itikadi ya Sunni kuhusu Sahaba . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 71Shi‘a hufuata mwongozo uliotolewa katika Qur’an na Hadith . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 71Aya ya Qur’an 48:18 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 74Azimio la Mulla ‘Ali al Qari na Tahreef ya Wahhabi . . . . 76

Fatwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 78

Taqiyah . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .80Maana sahihi ya Taqiyah . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 80Taqiyah katika ahadith na Tafsir ya Qur’an . . . . . . . . . . . .80Imam as-Suyuti . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 82Imam Fakhruddin ar-Razi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .83Imam al-Bukhari . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .85Tangazo la Mtume (s.a.w.w.) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 85Taqiyah ni kinyume cha Nifaq . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .86Mwandishi wa Wahhabi afanya Taqiyah bila sababu . . . .87

Hitimisho . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .88

1

DIBAJI

Tunamshukuru Allah (s.w.t.), kwa Baraka za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Watukufu Ahlul-Bait (a.s.) kwa kutujaalia kuweza kufanikisha juhudi zetu hizi katika kuchapisha toleo la saba la kitabu hiki “Fitina Za Wahhabi Zafichuliwa.”

Kitabu kilichopo mikononi mwako ni tafsiri ya moja ya ma’andishi ya Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (r.a.). Kitabu hiki kimekuwa maarufu katika ulimwengu wa Ki-Islamu na kilitafsiriwa na kuchapishwa na Taasisi mbali mbali kwa lugha ya Kiingereza, Kiurdu na Kiarabu.

Sababu iliyoifanya Bilal Muslim Mission isimamie kazi hii ni kama zile za mwanzo, ambayo inatokana na maombi ya watu wengi kutoka Afrika ya Mashriki kututaka tuchapishe Kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili.

Hii ilitufanya tutafsiri na kuchapish kitabu hiki ili watu wazungumzao kiswahili waweze kuelewa na kufahamu zaidi juu ya suala hili na fitina hizi za maadui wa Uislamu.

Bilal Muslim Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa mfasiri wa kitabu hiki Ndugu Dr. Mohammad Kanju na wale wote ambao kwa juhudi zao toleo hili la saba la kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi mwao na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au nyingine katika kazi zetu za Tabligh. Tunamuomba Allah (s.w.t.) awal-ipe malipo mema hapa Duniani na baadaye huko, Akhera.

20 Juni, 2005 Sayyid Murtaza RizviDar es Salaam Bilal Muslim Mission

4

2

UTANGULIZI

Hivi karibuni nimepata habari ya kijitabu cha Kiingereza kiitwacho “What is Shi‘aism?” (Ushi‘a ni Nini?), kilichochapishwa Nairobi na kusambazwa Afrika ya Mashariki kote na Wahhabi. Makusudio makubwa ya maandishi kama haya ni kupanda mbegu za chuki na mtengano baina ya Waislamu katika Afrika ya Mashariki na kwingineko. Jumuiya ya Shi‘a inaelewa wazi juu ya uchochezi huu; na hatukutaka kusisitizia upotofu huu kwa kuandika jibu lao. Wahhabi hupokea amri zao kutoka familia ya Saudi ambao wao wanamilikiwa na White House (Ikulu ya Marekani), huko Washington (Mji mkuu wa Marekani); na kama kila mtu anavyojua, ni sera iliyotangazwa na Washington na vibaraka wake kwamba Uislamu ni adui wao nambari moja. Kwa hiyo, wanataka kuuvunja Uislamu kwa njia zozote zile ziwezekanazo, na kwa bahati mbaya, akina Khalid, akina Fahad akina Mubarak na vikaragosi vyao wanacheza ngoma yao.

Tunahisi kwamba kujibu uchafu huu tutakuwa tunacheza juu ya mikono ya hao maadui wa Uislamu. Ni hisia hizi ndizo ambazo zimetuweka kimya kwa muda mrefu. Lakini sasa tumefikia hatua ambapo ukimya unatafsiriwa kama ni unyonge, kwa hiyo ufafanuzi kidogo juu ya kijitabu hiki haitakuwa vibaya.

Kitu kingine kilichotuzuia kujibu ilikuwa ni upofu wa waandishi hawa. Hawaangalii vitabu vya Shi‘a; wanaendelea tu kuzungumza yaliotapikwa na wazee wao; halafu huyahamishia kwenye makaratasi; (yaani vitabu) wakifikiria kuwa wameushinda Mlima Everest. Mamia, kama sio maelfu ya majibu yametolewa kwa vitabu vyao, lakini waandishi hawa hawajathubutu hata kuyaangalia. Na dhana hii huzidi kuchanganya kama Mwandishi ana ujinga kama Mwandishi wa kijitabu hiki tunachokijadili, Mwandishi asiyejulikana kwa jina wala asili. Hakuna mateso makubwa kwa Mwanafunzi wa dini kama kulazimishwa kuzungumza na mtu ambaye hana ilimu kama huyu. Hata hivyo pamoja na kutopenda kwangu nimeamua kuyaendea mateso haya, na “ni kwa Allah tu ndiko nashitakia huzuni na masikitiko yangu.”1

Kijitabu “Ushi‘a ni nini”, kimeandikwa bila mpangilio, na kufuata 1 Qur’an 12:86.

3

taratibu yake hiyo kungeweza kusababisha marudio yenye kukera.

Katika majibu haya, nimeshughulikia nukta zote za msingi katika hali ambayo si ya jazba kiasi ilivyowezekana, na kupuuza lugha ya matusi ambayo Mwandishi ameitumia kwa Mashi‘a. Ni wale ambao hoja zao ni dhaifu ndio hujaribu kufidia udhaifu huo kwa kuwatusi wapinzani wao.

Mwanzo kabisa nimeweka moja ya makala zangu za zamani, “Meaning and Origin of Shi’aism” (Maana na Asili ya Ushi‘a) na vifungu vichache muhimu vyenye kuelezea kwa ufupi itikadi na imani ya msingi ya Shi‘aIthna ‘Ashari. Hii itamsaidia msomaji kutofautisha baina ya kweli na masingizio yasiyo na msingi ya Mwandishi huyu asiyejulikana wa kitabu hiki cha Wahhabi.

Kabla sijagusa vichwa vya habari vya kijitabu hicho, hapa nataka kuweka wazi kwamba nimeandika (kitabu hiki) kwa wale wanaotafuta ukweli na ambao wako tayari kuupokea (kwa nia njema) bila chuki wala dhana zilizopandikizwa. Siandiki kwa ajili ya wale ambao mantiki zao ni kama hizi zifuatazo:-1. Kulaani masahba ni ukafiri na yeyote anayejitia katika kuwalaani

ni kafiri.2. Amir Mu’awiya alianza kumlaani Amirul Mu’minin Ali (Binamu,

Mkwe na Sahaba wa Mtume (s.a.w.w.) na Khalifa wa nne miongoni mwa Khulafa-e-Rashidin(waongofu) wa Kisunni) katika khutba za Ijumaa na Iddi mbili, na laana hii iliendelea kwa zaidi ya miaka 90 katika dola ya ki-Islam kutoka Sindh mpaka Hispania na kutoka Afrika hadi Uturuki.

3. Kwa hiyo Amir Mu’awiyah alikuwa ni Muumini muaminifu na Sahaba aliyeheshimiwa sana, pia ni Khalifa wa Mtume (s.a.w.w.)

Watu kama hao ni bora wasisome kitabu hiki. Namuomba Allah Subhanahu Wa Ta’ala akifanye kitabu hiki kuwa nuru na mwongozo kwa Ummah wa Kiislam katika siku hizi za giza.

Bihaqqi Muhammadin wa ‘alihi ‘t-tahireen.

Dar es Salaam Sayyid Saeed Akhtar Rizvi24th Septemba, 1993

HUU NI USHI‘A

5

MAANA NA ASILI YA USHI‘A

Mwelekeo wa imani ya Shi‘a umeelezewa na Waandishi wengi wasio wa Ki-Islamu kama dhehebu potovu la Ki-Islamu lililo kinyume na Uislamu wa asili. Hivyo wanadokeza kwamba Ushi‘a ni upotofu wa Ki-Islamu uliokuja baadae. Hivi kwa uhakika hii ni kweli au ni kampeni tu za kuuponda Ushi‘a? Hapa unatolewa ushahidi kutoka vitabu vya Sunni vyenye kuthibitisha kuwa Ushi‘a ni Uislamu asilia.

Maana ya Ushi‘a

Neno Shi‘a )شيعة( limetokana na neno la Kiarabu at-tashayyu )التشيع( lenye maana ya kufuata. Kulingana na al-Qamus na Lisanu ’l-‘Arab, marafiki na wafuasi wa mtu wanaitwa Shi‘a wake. Kulingana na Taju ’l-‘urus, kikundi cha watu wanoafikiana juu ya jambo (lolote) wanaweza kuitwa “Shi‘a.” Neno hili hutumika sawa sawa kwa umoja na wingi, vile vile hutumika sawa sawa kwa wanaume na wanawake.

Katika Qur’ani imetumiwa kwa wafuasi wa Mitume wa Allah (s.w.t.)

(a) Katika kisa cha Musa (a.s.) inasema hivi:-ي من عدوه

ذي من شيعته ع ال

ذذا من عدوه فاستغاثه ال ـ ذا من شيعته وه ـ ه

Huyu ni katika Shi‘a wake na yule ni katika adui zake, yule ambae alikuwa Shi‘a wake alimuomba msaada juu ya yule adui yake.2

(b) Katika kisa cha Nuh (a.s.) inasema hivi:-براهيم

وإنذ من شيعته ل

Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi (Shi‘a) lake.3

Kamusi za Kiarabu baada ya kutoa maana ya kawaida ya neno Shi‘a, kwa kawaida huongeza: “Jina hili kijumla hutumika kwa wale wenye mapenzi na kumfuata Ali (a.s.) na watu wa nyumbani kwake, na imekuwa ndio jina lao makhsusi”.4

2 Qur’ani 28:15.3 Qur’ani 37:83.4 Al-Qamus, Juzuu ya 2; at-Turayhi, Majma‘ul ’l-Bahrayn, Juzuu ya 2 uk. 539; Ibn

al-Athir al-Jazari, an-Nihayah, toleo la Misri, [1383/1963], Juzuu ya 2 uk. 519-520.

6

Shaykh al-Mufid (aliyekufa 413 A.H. / 1022 M.) ameeleza kwamba wakati neno Shi‘a linapotumika na Sarufi yenye kuainisha ‘al’ (al-Shi‘a) basi ina maana ya “kundi pekee lenye kumfuata Imam Ali (a.s.) kwa mapenzi na imani (itikadi) na kwamba alikuwa ni Imamu baada ya Mtume (s.a.w.w.) bila mwonya wowote....”5

Kwa ufupi, Shi‘a wamepata jina hili kwa sababu wanamfuata Imam Ali (a.s.) na kizazi chake Maasumin, na kupuuza madai ya watu wengine ya Uimamu. Kama itakavyoelezwa baadae, ni Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe aliyewapa jina hili wafuasi wa Ali (a.s.).

Chanzo Cha Ushi‘a

Asili ya Ushi‘a ni sawa sawa na ile ya Uislamu. (Kwa maana Ushi‘a ndio Uislamu na Uislamu ndio Ushi‘a). Tofauti kubwa iliyo baina ya Masunni na Mashi‘a ni kuhusu mshika makamu baada ya Mtume wa Uislamu. Masunni huwamini kwamba Abu Bakar ndiye aliyekuwa mshika makamu wa kwanza; Mashi‘a huwamini kwamba Ali ndiye mshika makamu wa haki wa kwanza. Kama msomi asiye na chuki akichunguza matangazo ya Mtume (s.a.w.w.) kama yalivyoandikwa na Wanachuoni wa Kisunni katika tafsir zao za Qur’ani, hadithi za Mtume (s.a.w.w.), wasifu na tarekh (historia), hana budi kukubali kwamba alikuwa ni Mtume mwenyewe ndiye muanzilishi wa Ushi‘a.

Tangazo la kwanza la kubaathiwa (Utume wa Muhammad (s.a.w.w.)) limeandamana wakati mmoja na tangazo la ukhalifa la kwanza kutolewa kwa Ali (a.s.). Tukio hilo linajulikana kama “karamu ya ndugu wa karibu.” Vifungu vinavyohusu habari hii vimenukuliwa hapa kutoka kitabu cha Tarikh cha at-Tabari:Ali (a.s.) alisema “wakati Aya ‘na uwaonye jamaa zako wa karibu’6 iliposhushwa kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) aliniita mimi na akaniamrisha kutayarisha sa‘ moja (kiasi cha kilo 3) cha chakula na niwakaribishe ukoo wa Abdu’l Muttalib ili apate kuzungumza nao. Walikuwa karibu watu arubaini, miongoni mwao walikuwepo ami 5 al-Mufid, Shaykh, Awa’ilu ’l-Maqalat (Qum: Toleo la 2, 1370 A.H.) uk. 2-3.6 Qur’ani 26:214.

7

zake Abu Talib, Hamza, Abbas na Abu Lahab. Kisha Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akatoa khutba isemayo:-‘Enyi watoto wa Abdu’l Muttalib! Simjui mtu yeyote katika bara-Arabu yote ambaye amewaletea watu wake kitu kilicho bora zaidi kuliko kile nilichokuleteeni mimi. Nimekuleteeni mema ya hii Dunia na Akhera. Na Allah (s.w.t.) ameniamrisha nikuiteni ninyi kwayo. Ni nani basi miongoni mwenu atakayenisaidia katika jambo hili, kwa masharti kwamba atakuwa ndugu yangu, wasii wangu na Khalifa wangu miongoni mwenu?’”

Ali aliendelea kusema: “Hakuna hata mmoja aliyejibu; hivyo nilisema (ingawa nilikuwa mdogo kuliko wote katika umri): ‘Mimi, ewe Mtume wa Allah! nitakuwa msaidizi wako katika kazi hii.’ Basi Mtume (s.a.w.w.) akaweka mkono wake kwenye shingo yangu na kusema: ‘Hakika huyu ni ndugu yangu, wasii wangu na Khalifa wangu miongoni mwenu. Msikilizeni na mumtii.’ Waliokuwa kwenye mkutano wote wakaamka, huku wakicheka na kumuambia Abu Talib kwamba Muhammad ameamrisha yeye kumsikiliza mtoto wake na kumtii.”7 7 At-Tabari, Muhammad bin Jarir, Tarikh, Juzuu 3 (Laden: E.J.Brill, 1882-1885)

uk. 1171-1173. Ni kitu cha kushangaza kwamba katika Tarikh ya at-Tabari toleo la Misri (Kairo) 1939 (ambao inadaiwa kuwa imechekiwa na kile cha toleo la Laden) yale maneno muhimu “wasiyyi wa Khalifati” (Wasii na Khalifa wangu) yamebadilishwa kuwa “kadha wa kadha.” Masikitiko yalioje kuona ulimwengu wa usomi kutoa mhanga uaminifu wake kwa ajili ya siasa. Ni lazima itajwe hapa kwamba hadithi hii pamoja na maneno yale imesimuliwa na wanachuoni wa Kisunni thelathini, au zaidi, Wanahistoria, Muhaddithina na Mufassirina wa Qur’ani. Imam Ahmad bin Hanbal ameisimulia hadithi hii katika Musnad yake (Juzuu ya 1. uk.111) pamoja na sanad hii ifuatayo (1) Aswad bin Amir kutoka kwa (2) Sharik, kutoka kwa (3) al-A‘mash kutoka kwa (4) al-Minhal, kutoka kwa (5) Ibad bin Abdullah al-Asadi, kutoka kwa (6) Ali. Sasa (1), (3) na (5) ni miongoni mwa wasimuliaji wa hadithi wa al-Bukhari na Muslim, ambapo (2) ni miongoni mwa wasimuliaji wa hadithi wa Muslim na (4) ni miongoni mwa wale wa al-Bukhari.

Vile vile Ahmad bin Shu’ayb an-Nasa’i ambaye kitabu chake cha Sunan ni kimoja miongoni mwa vitabu sita sahihi vya rejea vya hadithi za Masunni, amesimulia hadithi hii kutoka kwa Ibn Abbas katika kitabu chake al-Khasa’is uk. 6.

Kwa rejea zingine za hadithi hii, tazama al-Muraja’at cha Abdul Husayn Sharafu d-‘Din (Barua ya 20-23). Hii ni kitabu muhimu sana cha Ki-Shi‘a cha wakati huu; kimechapishwa mara nyingi huko Iraq, Iran, Lebanon na Kuwait. Tarjuma yake ⇒

8

Hii ilikuwa ni wakati wa mwanzo kabisa.

Katika siku za mwisho za uhai wake, Mtume (s.a.w.w.) alitangaza katika sehemu inayoitwa Ghadir Khum, kati ya Makka na Madina, kwamba Ali alikuwa ndiye Khalifa wake na Kiongozi wa Waislamu. Tukio hili limeandikwa na wanachuoni wengi wa Kisunni. Imam Ahmad bin Shu‘ayb an-Nasai (amekufa 303 A.H./915-16 M) amesimulia tukio hili kupitia Sanad (nyororo) mbali mbali za wasimuliaji wa hadithi katika kitabu chake al-Khasa’is, moja wapo ikiwa kama ifuatavyo:-

Abu ’t-Tufayl alisema kwamba Zayd bin Arkam alisema, “wakati Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anarudi toka Hijja yake ya mwisho na akapumzika penye bwawa (Ghadir) la Khum akasema: ‘Inaelekea kama vile nimeitwa (kurejea kwa Mola) nami nimekubali wito huo. Na nakuachieni miongoni mwenu vitu vizito viwili vyenye thamani, kimoja ya hivyo ni kikubwa kuliko kingine: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul Bayt wangu (Kizazi changu). Hivyo angalieni jinsi mtakavyojikhusisha navyo baada yangu kwa sababu vitu hivyo havitatengana mpaka vitakapokuja kwangu kwenye chemchem (ya ‘Kauthar’ siku ya hukumu). Mimi ni mwenye kutawalia (walii) mambo ya kila muumini.’ Wakati anasema hivyo aliunyoosha mkono wa Ali (a.s.) na akasema, ‘Yeyote yule ambaye mimi ni mwenye kumtawalia mambo yake, huyu (Ali) ni mwenye kumtawalia mambo yake. Ee! Allah! Mpende mwenye kumpenda Ali, na uwe adui kwa kila mwenye kumfanyia uadui yeye.”

Abu ’t-Tufayl anasema: “Nilimuuliza Zayd, ‘maneno haya uliyasikia kutoka kwa Mtume wa Allah (s.w.t.)?’ akasema: ‘Hakuna mtu aliyekuwa mahala pale ila alimuona kwa macho yake na kumsikia kwa masikio yake.’”8 Hadithi hii inajulikana kama hadithi ya vizito viwili vyenye thamani.

Katika kitabu hicho hicho, Imam an-Nasa’i ananukuu hadithi kutoka ⇐ ya Kiurdu ‘Din-e-Haqq’ ilichapishwa Kujhwa (Saran) India; ambapo baadae ilitafsiriwa kwa Kiingereza kwa jina la ‘The Right Path’ na Mohammad Amir Haider Khan na hivi karibuni kimechapishwa na Peermahomed Ebrahim Trust, Karachi. (Tafsiri ya Kiingereza tangu wakati huo kimechapishwa mara nyingi huko Iran, Uingereza na Marekani).8 An-Nasa’i, al-Khasa’is uk. 15.

9

kwa Zayd bin Arkam ambayo ina maneno haya ya Mtume (s.a.w.w): “Je! Mimi sina mamlaka kwa Muumini kuliko alivyo kwa nafsi yake?” Wote wakajibu: “Kwa hakika! Ewe Mtume wa Allah, Tunashuhudia kwamba wewe unayo mamlaka juu ya kila Muumin kuliko nafsi yake.” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Basi hakika ambaye yeye namtawalia mambo yake (Mawla), huyu vilevile ni mwenye kumtawalia mambo yake.” Wakati anasema hivyo aliunyoosha mkono wa Ali.9 Hadithi hii inajulikana kama, “Hadithi ya Wilayya.”

Hadithi za “Vizito Viwili vyenye thamani” na “Mawla” ziko pamoja na zimesimuliwa mara nyingi sehemu mbali mbali na mamia ya wahadithiaji (muhadithina). Mwanachuoni mashuhuri wa Kiwahhabi, Nawwab Siddik Hassan Khana wa Bhopal (India) anasema: “Hakim Abu Sa‘id anasema kwamba hadithi za ‘Vizito Viwili vyenye thamani’ na ‘Mawla’ ni hadithi mutawatir,10 kwa sababu idadi kubwa ya masahaba wa Mtume wamezisimulia kiasi kwamba Muhammad bin Jarir ameziandika hadithi hizi mbili kwa nyororo (asnad) tofauti sabini na tano za Wasimuliaji.”11

Abdu’l-Husayn Ahmad al-Amini ameainisha wapokezi wa hadithi hii, na akakuta miongoni mwao wako sahaba wa Mtume (s.a.w.w.) mia moja na ishirini, na themanini na nne ni tabi‘in (wafuasi wa masahaba). Idadi ya muhaddithiin wa Kisunni ambao wameisimulia inafikia mia tatu na sitini. Vitabu maalumu mia mbili na sitini (vingi vikiwa katika juzuu nyingi) vimeandikwa na wanazuoni wa Kishi‘a na Kisunni kwa ajili ya hadithi hii tu.12

Asili ya Jina

Tunapoona kwamba baina ya matukio haya mawili, Mtume (s.a.w.w.) 9 An-Nasa’i, al-Khasa’is uk. 16. 10 Mutawatir ni Hadithi iliyosimuliwa na watu wengi katika kila ngazi, kiasi

ambacho mtu hawezi kuitilia shaka kuhusu usahihi wake.11 Siddik Hassan Khan Minhajul-Wusul uk. 13.12 Tazama al-Amin, al-Ghadir J.1, ambacho kimeshughulikia suala hili pekee. Hii

ni ni kitabu kingine muhimu cha Ki-Shi‘a cha wakati huu. Juzuu kumi na moja zilichapishwa kabla ya al-Amini kufariki mwaka 1969. Kimechapishwa mara nyingi huko Iraq, Iran na Lebanon. Nimeona tafsiri yake ya Kiajemi. Marehemu Sheikh Muhammad Mustafa Jawhar, wa Karachi, alitafsiri juzuu ya kwanza katika Kiurdu lakini ikapotea wakati ikwa kwenye mashine ya uchapishaji. Sasa tafsiri nyingine ya Kiurdu ya juzuu ya kwanza imechapishwa huko India.

10

mara kwa mara alikuwa akiwaashiria wafuasi wa Ali kama Mashi‘a, tunalazimika kukubali kwamba sio imani ya Kishi‘a tu, bali hata jina (hilo) limeanzishwa na Mtume mwenyewe. Hadithi zifuatazo zinanukuliwa kutoka rejea za Kisunni:-

Ibn ‘Asakir anasimulia kutoka kwa Jabir bin Abdullah kwamba alisema: “Tulikuwa pamoja na Mtume (s.a.w.w.) wakati Ali alipokuja (hapo tulipokuwa). Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, hakika huyu (Ali) na Shi‘a wake ndio wenye kufuzu siku ya ufufuo.’ Kisha Aya ifuatayo ikashushwa. “Hakika wale walioamini na kutenda mema, basi hao ndio wema wa viumbe. (Qur’ani 98:7)”13

At-Tabarani anasema kwamba, Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali: “Ewe Ali! Hakika utakuja mbele ya Allah, wewe na Shi‘a wako hali ya kuwa mmeridhika (na Allah) na hali ya kuwa mnaridhia kwa Allah.”14

Kuna hadithi nyingi kutoka kwa wasimuliaji wengi ambazo wanachuoni wa Kisunni wasingeweza kuzipuuza. Hivyo walijaribu kuzifanya hadithi hizi zioane na upande wao. Kwa mfano baada ya kunukuu hadithi hizi, Ibn Hajar al-Makki anaandika hivi: “Na Shi‘a wa Ahlul Bayt ni Ahlu’s-Sunnah wa’l-Jamaa (yaani Sunni) kwa sababu ni wao waliowapenda Ahlul Baty kama ilivyoamrishwa na Allah na Mtume wake. Ama wengine, basi wao ni maadui (wa Ahlul bayt).”15

Dai hili lilirudiwa tena na Shah Abdu ’l Aziz Dehlawi ambaye anasema: “Ni lazima ieleweke kwamba Shi‘a wa kwanza (ambao ni

13 As-Suyuti, Jalalu’d-Din (amekufa 910/1504 – 05) katika Tafsiri yake ad-Durrul-Manthur, J. 6 uk. 379. Anasimulia hadithi kama hii kutoka kwa Ibn Abbas na Ali kadhalika katika sehemu hiyo hiyo; Al-Khuwarizmi (amekufa 569/1173-4) katika al-Manaqib.

Hadithi nyingine za Mtume (s.a.w.w.) zitamkazo kwamba Shi‘a wa Ali watafuzu siku ya kiyama zinasimuliwa na Wanachuoni wa Kisunni kutoka kwa Abdullah, Abu Rafi, Jabir bin Abdullah, Ibn Abbas na Ali; Mingoni mwa wanachuoni hawa ni at-Tabarani katika kitabu chake al-Mu‘jam al-Kabir, Ahmad bin Hanbal katika al-Manaqib yake, Ibn Mardawayh al-Kanji ash-Shafi’i katika kitabu chake Kifayatu ’t-Talib na wengine wengi.14 Ibn Athir katika an-Nihayah; Ibn Hajar al-Makki katika as-Sawa‘iqu ’l-Muhriqah

(Misri, Hakuna tarehe) uk. 92. Anasimulia hadithi nyingi kuhusu suala hili.15 as-Sawa‘iqu ’l-Muhriqah.

11

Sunni na Tafadhiliyya) katika siku za zamani walijulikana kama Mashi‘a.Wakati Ghulat na Rawafidh, Zaydiyyah na Ismailiyyah walipochukuwa jina hili kuwa lao...... Sunni na Tafadhiliyyah hawa kulitaka jina hili kwa upande wao, na kwa hivyo wakajichukulia jina la Ahlu ’s-Sunnah wa’l-Jamaa.”16

Madai kama haya hayastahili kujibiwa. Lakini baada ya kuona mukhtasari wa tafsiri ya Kiarabu ya Tuhfah umechapishwa hivi karibuni huko Misri, na nukuu hapa maoni ya mwanachuoni mwingine wa Kisunni, Ubaydullah Amritsari, ambaye baada ya kunukuu madai hayo hapo juu katika kitabu chake Arjahu’l-matalib, Amristsari anasema: “Kusema kwamba hapo mwanzo Sunni walikuwa wakijulikana kama Shi‘a ni madai yaliyotupu, kwa sababu hakuna uthibitisho unaoweza kupatikana. Ingelikuwa masunni walikuwa wakiitwa Shi‘a, basi angalau baadhi ya viongozi wa Kisunni wangelijulikana kwa jina hili kabla ya kuja kwa Zaydiyyah (120 A.H.). Aidha, kama Sunni wangelijulikana kwa jina hili, Zaidiyyah na Ismailiyyah, wasingeweza kulivumilia jina hili kuwa lao (kwa sababu ya uadui uliokuwepo) na wangejichagulia jina lingine.”17

Mashi‘a wa Kwanza

Wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.) neno Shi‘a lilikuwa linatumika kabla ya yote kwa Masahaba wanne wakubwa walioheshimiwa: Salman al-Farsi, Abu Dharr Jundab bin Junadah Al-Ghifari, Miqdad bin Aswad al-Kindi na Ammar bin Yasir.

Kashfu ’z-Zunun (J.3), ananukuu kutoka Kitabu ’z-Zinah cha Abu Hatim Sahal (kadhaa) bin Muhammad Sajastani (alikufa 205 A.H.): “Katika siku za uhai wa Mtume (s.a.w.w.) neno Shi‘a lilikuwa linatajwa kwa kuwaashiria watu wanne: Salman al-Farsi, Abu Dharr Ghaffar (Kadhaa), Miqdad bin Aswad al-Kindi, na Ammar bin Yasir.”18

16 Shah ‘Abdu ’l-Aziz Dehlawi, Tuhfah-e-Ithnâ-‘ashariyyah, Nawalkishor Press, Lucknow, hakuna tarehe; uk. 4, 11, 59.

17 ‘Ubaydullah Amritsari, Arjahu ’l-Matalib, (Lahore: Toleo la 2) uk. 608 (ambayo imechapishwa kimakosa kama 164).

18 Kama ilivyonukuliwa na Hasan al-Amin katika Islamic Shi’ite Encyclopaedia J.1 (Beirut 1968) uk. 12-13.

12

Hawa ndio waliokuwa Shi‘a wa kwanza, na huo ndio uliokuwa mwanzo wa Imani ya Shi‘a chini ya uongozi mpole na usimamizi wa Mtume wa Uislamu mwenyewe.

13

HADITH ATH-THAQALAYN(HADITHI YA VITU VIWILI VYENYE THAMANI)

Katika Sura iliyotangulia imetajwa hadithi muhimu ya “Vitu Viwili vyenye thamani” (ath-thaqalayn) na “ambaye mimi ni mwenye kutawalia mambo yake na Ali ni mwenye kutawalia mambo yake” (al-Wilayah). Kwa hadithi ya pili, maelezo ya kutosha yametolewa kwenye kitabu changu, Imamate (cha Kiingereza uk. 62-81). Na kuhusu hadithi ya kwanza, na nakuu baadhi ya rejea (pamoja na marekebisho) kutoka “The Right Path”, tafsiri ya Kiingereza ya al-Muraja’at.

Mtume mtakatifu (s.a.w.w.) amesema:“Enyi watu, nakuachieni miongoni mwenu vitu viwili ambavyo mkivifuata, hamtapotea kamwe baada yangu, navyo ni kitabu cha Allah na Ahlul-Bayt wangu.”19

Vile vile alisema:“Nimekuachieni miongoni mwenu vitu fulani na kama mtakuwa na mapenzi navyo hamtapotea asilani; Vitu hivi ni Kitabu cha Allah, ambacho ni kama kamba iliyonyooka kutoka mbinguni mpaka ardhini, na watoto wangu, yaani Ahlul-Bayt wangu. Viwili hivi havitatengana mpaka vinifikie mimi katika chemchem ya Kawthar (huko Peponi) Basi, chukueni tahadhari ya jinsi mtakavyojihusisha navyo.”20

Vile vile alisema:“Nakuachieni miongoni mwenu vitu viwili vizito, Kitabu cha Allah na Ahlul-Bayt wangu; na viwili hivi kamwe havitatengana mpaka vinifikie kwenye Hawdhi.”21

19 Imetolewa taarifa na Tirmidhi na Nasa’i kupitia kwa jabir na kunakiliwa kutoka kwao na Al-Muttaki wa India mwanzo wa Sura ya “Kushikamana”, katika kitabu chake, Kanzu ’l-Ummal toleo la 5 chapa ya Beirut, 1405/1985 Juzuu 1 uk.172.

20 Hadithi Na. 874 katika Sahih al-Tirmidhi kama ilivyosimuliwa na Zayd ibn al-Arkam, Kanzu’l Ummal Juzuu 1 uk. 173.

21 Imam Ahmad ibn Hanbal, Musnad, J. 5, uk. 182, na J. 5, uk. 189 mwishoni; At-Tabarani, al-Mu‘jam al-Kabir kutoka kwa Zayd ibn Thabit; Kanzu ’l- ‘Ummal J. 1, uk. 172; Al-Hakim, Mustadrak, J. 3, uk.148, pamoja na maelezo kwamba hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa vipimo vilivyofuatwa na Masheikh wawili (yaani, Muslim na Bukhari) ingawa hawakuijumlisha katika vitabu vyao; Dhahabi, Talkhis al-Mustadrak.

14

Vile vile alisema:“Hivi punde nitaitwa na nitakuacheni, lakini nakuacheni miongoni mweni vitu Viwili Vizito, Kitabu cha Allah Azza wa Jallah na kizazi changu. Kitabu cha Allah ni kama kamba ambayo imening’nia kutoka mbinguni mpaka ardhini, na kizazi changu ambao ni Ahlul-Bayt. Allah Mjuzi wa mambo ananiambia kwamba viwili hivyo kamwe havitaachana mpaka vinifikie kwenye Hawdhu. Hivyo kuwenu waangalifu jinsi mnavyokwenda nao baada yangu.”22

Wakati Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) alipokuwa anarudi (toka Makka kwenda madina) baada ya Hijja yake ya mwisho (hijat’l-wida = hijja ya kuaga) alifika mahala paitwapo Ghadir Khum, alisimama hapo na akasema:“Inaelekea kama nimeitwa na ninakwenda zangu. Hata hivyo nakuachieni miongoni mwenu vizito viwili, kimoja kati ya hivyo ni kikubwa kuliko kingine. Ni Kitabu cha Allah Azza wa Jallah na watoto wangu. Basi kuweni waangalifu na jinsi mtakavyojihusisha navyo baada yangu. Viwili hivyo havitaachana mpaka vinifikie katika chemchem ya Kawthar.”

Aliendelea kusema:“Mola, Azza wa Jallah ni Mwenye kutawalia mambo yangu na mimi ni mwenye kutawalia mambo ya kila Muumin wa kweli.”Kisha akashika mkono wa Ali kwa mkono wake na akasema:“Ni (yaani Ali) mwenye kutawalia mambo ya wale niliokuwa mimi nawatawalia. Ee! Allah wapende wale wenye kumpenda Ali na wachukie wale wenye kumchukia yeye...”23

22 Imam Ahmad ibn Hanbal, kutoka kwenye hadithi iliyo simuliwa na Abu Sa’id al-Khudri katika njia mbili, katika Musnad yake, J. 3, uk. 17 na uk. 26. Pia imeandikwa na Ibn Abi Shaybah, Abu Ya’li na Ibn al-Sa’id kutoka kwa Abu Sa’id; Kanzu ’l-‘Ummal, J. 1, uk. 185 hadithi Na. 944; pia tazama hadithi Na. 945 & 946.

23 Al-Hakim kutoka kwa Zayd ibn al-Arkam, Al-Mustadrak Juzuu 3, uk. 109 pamoja na maoni kwamba hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa vipimo vilivyokubaliwa na Masheikh wawili (yaani Muslim na Bukhari) ingawa hawakuiandika kwa ukamilifu. Vile vile imepokewa kupitia rejea nyingine kutoka kwa Zayd ibn al-Arkam na kuandikwa katika Juzuu 3, uk. 533 ya Mustadrak pamoja na maoni kwamba ni sahihi, ingawa Mashekhe wawili hawakuiandika. Dhahabi vile vile ameiandika katika kitabu chake Talkhis kwamba ni sahihi.

15

Abdullah ibn Hantab alisimulia kwamba Mjumbe wa Allah alituhutubia sisi kule Juhfah akisema: “Je, mimi sina mamalaka zaidi juu yenu ninyi kuliko mliyo nayo wenyewe juu ya nafsi zenu?” Wakasema, “naam, kwa hakika.” Kisha akasema: “Nitawataka ninyi muwajibike kwa ajili ya vitu viwili, yaani, Kitabu cha Allah na kizazi changu.”24

Hadithi zote hizi sahihi zenye nguvu (za kihoja), zinazothibitisha kwamba ni wajibu kufuata Qur’ani na Ahlul-Bayt, sio hadithi za hivi hivi; zimerudiwa mara nyingi na zimesimuliwa na Masahaba ishirini au zaidi wa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kupitia rejea mbali mbali. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amerudia maneno haya tena na tena (na sio sehemu moja na mara moja tu, bali mara nyingi na sehemu mbali mbali) bayana, kuonyesha kwamba ni lazima kuwafuata na kuwatii Ahlul-Bayt (a.s.). Alitoa tangazo hili wakati wa Hijja ya muago, siku ya Arafa, pale Ghadir Khum, wakati wa kurudi kutoka Ta’if na Madina katika Mimbar-Msikitini. Mwisho ni wakati akiwa yu mgonjwa hali ya kukata roho kitandani na chumba kimejaa Masahaba wake, alisema:-“Enyi watu! Hivi karibuni nitaondoka kutoka hapa, na ingawa nimekwisha kuelezeni hivyo, ninarudia mara nyingine tena kwamba, nakuachieni pamoja nanyi vitu viwili, yaani, Kitabu cha Allah na Kizazi changu, ambao ni Ahlul-Bayt wangu.” Kisha alinyanyua mkono wa Ali na kusema:“Tazameni huyu ni Ali, yuko pamoja na Qur’an na Qur’an iko pamoja naye. Hakuna mtengano kamwe baina ya viwili hivyo, mpaka vinijie kwenye chemchem ya Kawthar.”25

Kundi kubwa la watu mashuhuri watokanao na Madhehebu ya Ki-Sunni wameikubali hadithi hii kama usia na hati ya mwisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hata Ibn Hajar, baada ya kuiandika Hadithi al-Thaqalayn (hadithi ya vizito viwili) aliitolea maelezo akasema:-“Hadithi ya kushikamana (yaani na vizito viwili) imepokewa

24 Al-Tabarani ameindika Hadithi hii kama ilivyotajwa na ‘Allamah al-Nabahani katika kitabu chake Arba’in al-Arba’in, na Allamah al-Suyuti katika kitabu chake Ihya’ al-Mayt.

25 Tazama Kitabu cha Ibn Hajar, al-Haythami al-Makki, as-Sawa‘iqu ’l-Muhriqah, Sura ya 9.

16

kupitia rejea nyingi, na zaidi ya Masahaba ishirini wameisimulia.” Kisha kitambo kidogo akasema: “Hapa wasi wasi unakuja, na ni kwamba, wakati hadithi hii imepokewa kupitia rejea mbali mbali; wengine wanasema kwamba maneno haya yalisemwa wakati wa Hija ya mwisho, wengine wanasema yalisemwa Madina wakati Mtume (s.a.w.w.) yu mgonjwa kitandani akikaribia kukata roho na chumba kikiwa kimejaa Masahaba, bado wengine wanasema alizungumza maneno haya Ghadir khum au wakati anarudi kutoka Ta’if. Lakini hakuna ubishani kwa vile inawezekana kwamba, kwa kuchukulia umuhimu na ukubwa wa Qur’ani na Ahlul-Bayt pamoja na msisitizo wa jambo hili mbele ya watu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huenda alirudia maneno haya katika mara zote hizi ili yeyote ambaye hakuyasikia kabla huenda akayasikia sasa.”26

Zaidi ya hayo, kwa vile Ahlul-Bayt ni wenye uzito mbele ya Allah kama ilivyo Qur’an, basi Ahlul-Bayt wana sifa sawa na Qur’an. Kama Qur’an ni kweli kutoka mwanzo mpaka mwisho, na bila utata wowote ndani yake, na kama inavyopasa juu ya kila Mwislamu kutii amri zake, hivyo lazima vile vile Ahlul-Bayt wawe wakweli, wakamilifu na viongozi waadilifu ambao amri zao lazima zifuatwe na wote. Kwa hiyo hakuna kukwepa kukubali uongozi wao na kufuata itikadi na imani yao. Waislamu wanalazimika kwa maneno ya Mtume (s.a.w.w.) kuwafuata wao na sio mtu mwingine yoyote. Kama ambavyo haiwezekani kwa Mwislamu kuipa mgongo Qur’an au kushika njia nyingine ambayo ni tofauti, hivyo wakati Ahlul-Bayt (a.s.) wanaelezewa kwa maneno yasiyoshaka kwamba wao ni sawa kwa uzito na muhimu kama ilivyo Qur’an, basi mwelekeo huo huo lazima ufuatwe kwa heshima ya mwenendo wao, na haiweze kuruhusiwa kuwapa mgongo na kufuata watu wengine.

Katika kusema kwake Mtume:- “Nakuachieni miongoni mwenu vitu viwili, kama mtashikamana navyo (vyote viwili) hamtapotea kamwe; na vitu hivyo ni Kitabu cha Allah na watu wa nyumbani kwangu.” Mambo ya kushikamana navyo (hivyo vitu viwili) lazima yatizamwe kwa kuchunga sana. Inaonyesha wazi kwamba yeyote atakaeshikamana navyo vyote kama viongozi wake, ataokolewa kutokana na kupotea. Hivyo basi, kama mtu atachukuwa kimojawapo tu, bila ya kuchukuwa na kingine kama mwongozo, atapotea. Nukta 26 as-Sawa‘iqu ’l-Muhriqah, Sura 11, kichwa cha habari ndogo 1 uk. 89.

17

hii bado inaonekana wazi kwa kuyatizama mazungumzo ya Tabarani ambayo yana amri ya zaidi:“Chunga! Na usiende mbele yao au nyuma yao, kwa njia yoyote ile utaharibikiwa; na usijaribu kuwafundisha kwani wao wanajua zaidi kuliko wewe”.

Ibn Hajar anachukukuliwa kwamba maneno haya yanaonyesha kwamba Ahlul-Bayt ambao walikuwa wenye sifa hizo wanayo daraja ya juu sana kuliko watu wote.27

Hadithi nyingine ambayo itamlazimu kila Mwislamu kuwafuata Ahlul-Bayt na kutokuwakubali wengine kama viongozi wa mambo ya dini ni ile ambayo Mtume (s.a.w.w.) amesema: (Kama ilivyosimuliwa na Abu Dharr al-Ghifari):“Tazama! Ahlul-Bayt wangu ni sawa sawa na Safina ya Nuhu, mwenye kuipanda ataokolewa, na atakaye ipa mgongo ataangamia.”28

Bado hadithi nyingine inatueleza kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema:- “Ahlul-Bayt wangu ni kama lango la Kutubia la wana wa Israili,29 mwenye kuingia humo atakuwa amesamehewa.”30

Hadithi nyingine ni kama ifuatavyo:-“Nyota huwalinda viumbe waishio Duniani kutokana na kuzama majini (kufa maji) na Ahlul-Bayt wangu ni walinzi wa wafuasi wangu kutokana na fitina (katika mambo ya dini). Hivyo, kundi lolote miongoni mwa wa Arabu lipingalo Ahlul-Bayt wangu (katika masuala ya dini) litatawanyika kwa kutokuelewana na kuwa kundi la shetani.”31

Kwa hiyo hadithi hizi hazina shaka yoyte. Haiwezekani kuwa na njia nyingine isipokuwa kuwafuata Ahlul-Bayt na kuacha upinzani wote juu yao. Uwazi na maneno yasiyo na shaka ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametuelekeza kuhusu mambo haya katika hadithi zilizotajwa 27 as-Sawa‘iqu ’l-Muhriqah, sura ihusuyo wosia wa Mtume uk. 136.28 Imam Hakim, Al-Mustadrak J. 3, uk. 151.29 Qur’an, 2:57-58.30 Al-Tabarani, Al-Mu’jam Al-Aswat (hadithi na 18) kama ilivyosimuliwa na Abu

Sa’id; Al-Nabahani Arba’in uk. 216.31 Imam Hakim, Al-Mustadrak J. 3, uk. 149 kama ilivyopokelewa na Ibn Abbas, na

maelezo kwamba hadithi hii ni sahihi, lakini haikuandikwa na Mashekhe wawili, Muslim na Bukhari.

18

hapo juu, hayawezi kupitwa au kuwa sawa katika lugha nyingine ile.Hapa Ahlul-Bayt wametajwa kwa pamoja. Neno hili linahusika na Ahlul-Bayt wote. Lakini jina lenyewe linatumika kwa wale tu ambao ni hoja za Allah na kushika nafasi ya Uimamu kwa amri Yake (s.w.t.), kama ilivyothibitishwa na dalili za akili na hadithi. Wasomi wanachuoni wa Ki-Sunni hulikubali hili pia. Kwa mfano, Ibn Hajar anaandika katika kitabu yake Sawa‘iqu ’l-Muhriqah: “Baadhi ya watu hufikiria kwamba Ahlul-Bayt ambao Mtume (s.a.w.w.) amewataja kama walinzi ni wale watu wasomi miongoni mwa Ahlul-Bayt, kwa vile uwongofu waweza kupatikana kupitia kwao tu. Wao ni kama nyota kupitia kwao tunaongozwa katika njia iliyo sawa. Na kama nyota zingeondolewa tungejikuta uso kwa uso na Ishara za Allah (s.w.t.) kama alivyoahidi (yaani siku ya kufufuliwa). Hii itatokea wakati Imamu Mahdi atakapo kuja, kama ilivyotajwa katika hadithi, na Nabii Isa (a.s.) atasali nyuma yake, Dajjal atauawa, kisha Ishara za Allah (s.w.t.) zitatokea moja baada ya nyingine.”32

Katika pahala pengine Ibn Hajar anaandika: “Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) aliulizwa itakuwa vipi hali ya watu baada ya Ahlul-Bayt?” akajibu:“Hali yao itakuwa kama ile ya punda ambaye mfupa wake wa mgongo umevunjika.”33

Unajua vizuri sana, kwamba hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) isemayo kwamba Ahlul-Bayt ni sawa na Safina ya Nuhu, hutufikisha kwenye uwamuzi wa kwamba, wale ambao wameichukua imani yao na kuwafuata wataokolewa kutokana na adhabu ya moto, ambapo wale waliowapa mgongo mwisho wao utakuwa kama yule aliyejaribu kuokoa maisha yake kwa kupanda juu ya mlima, pamoja na tofauti moja tu, kwamba yeye (yaani mtoto wa Nuhu) alizama majini (alikufa maji), watu hawa watazamishwa kwenye moto wa jahannam. Na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutumia mfano wa lango la kutubia (yaani la wana wa Israil) huonyesha kwamba kama lilivyo lango hilo, hivyo hivyo Ahlul-Bayt nao ni udhihirisho kwa utukufu na mamlaka ya Allah (s.w.t.) Ambaye Kwake tutajisalimisha na kutoa utiifu wetu kiunyenyekevu.32 as-Sawa‘iqu ’l-Muhriqah, Sura ya 11 uk. 91.33 as-Sawa‘iqu ’l-Muhriqah, uk. 143.

19

MSINGI WA IMANI WA SHI‘A ITHNA-‘ASHARIYA

Katika istilahi za Kishi‘a, misingi ya imani huitwa Usul-e-Deen (yaani mizizi ya Dini). Usul-e-Deen ziko mitano; mitatu inaitwa mizizi ya Dini ya Uslamu. (misingi mikuu ya Uislamu) nayo ni hii:

1. Tawheed - mani ya umoja wa Mwenyezi Mungu.2. Nubuwwat - Imani juu ya Mitume.3. Qiyamat - Kuamini Siku ya Hukumu.

Miwili iliyobakia inaitwa Usul-e-Iman, Misingi ya Imani. Nayo ni:

1. ‘Adl - Uadilifu wa Mwenyezi Mungu.2. Imamat - Mshika Makamu - Mrithi wa Mtume.

Mtu mwenye kuamini mizizi hii mitano anaitwa Shi‘a Ithna ‘Ashari. Shi‘a kama huyo huamini kwamba:

1. Tawheed: Kuna Mungu mmoja tu, wa milele. Hana mwanzo wala mwisho, ni mwenye kujitosheleza. Mwenye Enzi na nguvu na ana uwezo juu ya kila kitu na kila jambo, ni Mwenye kujua yote, hakuna kilicho siri Kwake. Ana hiari juu ya mambo yote, halazimishwi. Ni Mwenye kutambua, na ni Mwenye kuona kila kitu, ni Mwenye kusikia kila sauti, Yuko kila mahali, Yeye anaona na kusikia kila kitu ingawa hana jicho wala sikio. Hana mshirika wala mwenzi, wala hana mtoto yeyote au mke. Hakutengenezwa wala hakubuniwa kwa kitu chochote cha maada. Hana mwili wala sehemu mahala pa kuwepo, hadhuriwi na kitu chochote kinacho husiana na mwili. Haongozwi na wakati, mabadiliko au vitu kama hivyo. Haonekani, Hajaonekana, na wala Hataonekana si hapa Duniani wala Akhera. Sifa zake hazikutengwa na dhati Yake.Husema kweli na ni Mkweli. Haingii kwenye mwili wowote, Hahitaji kitu chochote, na hafanyi ubaya. Ni Yeye aliyeumba Mbingu na Ardhi na ni Yeye Mwenye kuzihifadhi na kuziruzuku.

2. ‘Adl: Allah ni Muadilifu, hafanyi dhulma kwa yeyote yule. Ametuamrisha nasi kuwafanyia uadilifu viumbe wenzetu, lakini

20

Yeye Mwenyewe hatufanyii uadilifu tu, bali hutufanyia hisani pia. Ametuumba kwa ajili ya kumuabudu Yeye tu, ili tupate ukamilifu wa kiroho kupitia kwayo. Ukamilifu huo wa Kiroho unatuwezesha sisi kuwa karibu na Allah.

Kwa lengo hili, Ametupa uhuru na hiari yakutaka na kuchagua. Kama tukichagua kwa hiari yetu (wenyewe) njia iliyonyooka (iliyowekwa na Allah) tunayo yakini ya kupata furaha ya milele katika Akhera na utukufu kwa Rehma za Allah.

3. Nubuwwat: (Utume) kutuonyesha njia iliyonyooka, Allah (s.w.t.) alikuwa anatuma wawakilishi wake kwa wanadamu. Wao wanaitwa Nabii au Rasul. Ni wajibu kuamini utume wa Mitume iliyopita pamoja na Mtukufu Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.).

Wamekuja jumla ya Mitume Ambiyaah na Mitume Mur-salu 124,000 kuanziana Adamu (a.s.) na kuishia na Muhammad (s.a.w.w.). Mitume wote walikuwa Ma’sum (wasiotenda dhambi yeyote). Vile vile walikuwa hawana upungufu wowote katika mwili na tabia ambazo zaweza kuleta karaha kwa watu. Muhammad, Mtukufu Mtume wa Uislamu ndiye wa Mtume wa Mwisho (hakuna tena Mtume baada yake), yeyote anayedai Utume baada yake ni muongo na mlaghai.

Mtume Mtukufu wa Uislamu (s.a.w.w.) alipaa (kwenda) mbinguni katika Miraji. Qur’an ni neno la Allah. Hapajakuwa na mabadiliko, kupungua au kuongezeka katika Qur’ani. Hadithi ni rejea sahihi za Shari’ah (mambo yanayohusu Dini).

Ni wajibu kuamini kuulizwa maswali kaburini kupitia kwa Munkar na Nakir, kwamba ni kweli Kuminywa kwa kaburi, ni kweli Malaika, Shetani na Majini ni kweli.

4. Imamat: Kuwaongoza watu katika njia iliyonyooka (Sirat) na kuhifadhi Dini ya Uislamu, Allah aliwateuwa washika makamu wa Mtume wa Uislamu kumi na wawili, mmoja baada ya mwingine. Wanaitwa Maimamu. Imamu kilugha ni kiongozi. Wa kwanza wao alikuwa ni ‘Ali bin Abu Talib (a.s.), na wa mwisho

21

wao ni al-Mahdi (a.s.). Maimamu wote ni Ma’sum (wasio tenda dhambi wala kukosea).

Majina ya maimamu kumi na wawili ni kama yafuatayo:-

Imam Mahdi, Imam wa kumi na mbili yuko hai, lakini amefichwa (yuko ghaibu) na macho yetu hayamuoni kwa amri ya Allah (s.w.t.). Atajitokeza Allah (s.w.t.) atakapo mruhusu, na kuanzisha ufalme wa Allah (s.w.t.) katika ardhi. Itakuwa karibu na mwisho wa ulimwengu, wakati utakapoeneza haki na usawa katika ulimwengu, wakati utakapo kuwa umejaa dhulma na uonevu.

5. Qiyamat: Baada ya hapo kitakuja Qiyama, Siku ya kufufuliwa, Siku ya Hukumu. Siku moja ulimwengu huu utafikia mwisho. Watu wote watakufa; kisha watu wote watafufuliwa na kuulizwa imani na matendo yao. Watu wenye imani sahihi na kufanya matendo mema watawekwa peponi; ambapo watu wenye imani potofu wa-takwenda Motoni. Siku ya Hukumu ni kweli na haina shaka ipo. kuhama kwa Roho (kuingia kwenye mwili mwingine) ni wazo potofu. Kila mtu atalipwa kutokana na matendo yake, mema au mabaya. Mizan (Mizani), Hisab (hesabu ya amali), na Sirat (Njia, Daraja iliyo juu ya Moto wa Jahannamu) ni ukweli; Watu watapewa hati za amali kwa mikono yao ya kulia au kushoto. Shafa’at (Shufaa au maombezi) ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) ni ukweli. Kutubia ni wajibu. Pepo na Moto vipo hata hivi hapa.

1. ‘Ali bin Abu Talib 2. Hasan bin ‘Ali3. Husain bin ‘Ali4. ‘Ali Zaynul Abideen bin Husain5. Muhammad Baqir bin ‘Ali Zaynul Abideen6. Ja‘far Sadiq bin Muhammad Baqir7. Musa Kazim bin Ja‘far Sadiq8. ‘Ali Riza bin Musa Kazim9. Muhammad Taqi bin ‘Ali Riza10. ‘Ali Naqi bin Muhammad Taqi11. Hasan Askari bin ‘Ali Naqi12. Muhammad Mahdi bin Hasan Askari

22

Kujua na kuamini Usul-e-Deen (Mizizi ya Dini) iliyotajwa hapo juu ni kitu cha kwanza na muhimu sana kwa mtu. Kama ilivyoelezwa hivi punde kuipuuza humtupa mtu kwenye adhabu isiokoma ya moto wa jahannam. Ikiwa mtu haamini Usul-e-Deen (Mizizi ya Dini), basi matendo yake yote ya ibada hayakubaliwi na Allah (s.w.t.).

23

DARAJA YA MUHAMMAD (S.A.W.W.) NA AHLI ZAKE

Kwa mujibu wa Shi’a, Shafi’i na Masunni wengine, wengi wanaamini kwamba wakati Allah (s.w.t.) Alipotaka kuumba viumbe, Aliumba kwanza nuru ya Muhammad (s.a.w.w.). Hadithi ya Shi’a inayozungumzia habari hii inapatikana katika kitabu cha Biharu ’l-anwar, juzuu ya 15. Hapa ninanukuu tu kutoka rejea za Sunni kwa kukamilisha hoja dhidi ya Wahhabi wanaoamini kimakosa kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa sawa na wanadamu wengine.

Al-Qastalani (aliyekufa 923 H.) alisimulia hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana na mada hii kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah al-Ansari na ‘Ali (a.s.).34

Al-Mas’udi (aliyekufa 346 H.) alisimulia hadithi ndefu kutoka kwa ‘Ali (a.s.) inayosema kwamba, Allah aliumba kabla ya yote Nuru ya Muhammad; kisha akaiambia ule Nuru:“Wewe ni mteuliwa na ni Amin (mdhamini) wangu, Nuru na mwongozo wangu. Kwa sababu yako wewe nataka kuumba ardhi na mbingu, nitaweka thawabu na adhabu, na kuumba Pepo na Moto.” Hadithi iliendelea kusimulia kuhusu A’ali zake Muhammad (s.a.w.w.), kuumbwa kwa Malaika, roho na ulimwengu. Kisha inasimuliwa Ahadi iliyochukuliwa kutoka Nafsi (za binadamu) ambayo inakusanya imani ya Mungu mmoja na kukubali utume wa Muhammad (s.a.w.w.).35

Hii ndio sababu Ibn Abbas anasimulia kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mimi nilikuwa Mtume wakati Adam yuko baina ya Roho na Mwili.”36 Yaani Adamu akiwa katika hatua ya mwanzo ya kuumbwakwake.

Nuru ya Muhammad iliipamba Arsh ya Allah (s.w.t.). Baada ya muda mrefu sana kupita Adam alipoumbwa, Nuru hiyo iliwekwa kwenye kipaji chake cha uso wake. Iliendelea na safari yake kizazi baada ya kizazi, kupitia Mitume wengi na Mawasii wao, mpaka ilipofikia kwa Nabii Ibrahim (a.s.). Kutoka kwa Ibrahim ilikwenda kwa mwanawe mkubwa Nabii Ismail (as).34 al-Qastalani, al-Mawahibu ’l-Ladunniyah, J. 1, uk. 5, 9, 10.35 al-Masu’di, Maruju ’dh-dhahab.36 at-Tabarani, al-Mu‘jam al-Kabir; al-Khasa’is al-kubra, J. 1, uk. 4.

24

Wathila ibn al-Asqa alisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Hakika Allah alimchagua Ismail kutoka kizazi cha Ibrahim; na alimchagua Banu Kinanah kutoka kizazi cha Ismail; na alimchagua Quraysh kutoka kwa Banu Kinanah; na alimchagua Banu Hashim kutoka Quraysh; na akanichagua mimi kutoka Banu Hashim.”37

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Jibril aliniambia: ‘Nimeangalia katika Ardhi kutoka mashariki mpaka magharibi, lakini sikuona mtu yoyote aliyemzidi (kwa ubora) Muhammad; na nimeangalia katika Ardhi kutoka mashariki mpaka magharibi lakini sikuona kizazi kilicho bora kama kizazi cha Hashim.”38

Mtume alisema: “Mimi na Ali tulikuwa Nuru moja mbele ya Allah (s.w.t.) miaka kumi na nne elfu kabla ya kuumbwa Adam. Wakati Adam alipoumbwa Nuru ile iliwekwa kwenye kiuno chake. Hivyo Allah (s.w.t.) alikuwa akiihamisha kutoka viuno bora kwenda matumbo tohara ya uzazi (yaani kwenda kwa akina mama watoharifu) mpaka Allah (s.w.t.) akaiweka kwenye kiuno cha Abdu’l-Muttalib. Kisha Allah (s.w.t.) akaigawanya sehemu mbili, sehemu moja ikaenda kwenye kiuno cha Abdullah na sehemu nyingine ikaenda kwenye kiuno cha Abu Talib. Kwa hiyo Ali anatokana na mimi na mimi natokana na yeye, nyama yake ni nyama yangu na damu yake ni damu yangu; mwenye kumpenda yeye anafanya hivyo kwa kunipenda mimi, na mwenye kumchukia yeye anafanya hivyo kwa sababu ananichukia mimi.”39

Shi’a, Shafi’i na hanafi wote kwa pamoja wanaamini kwamba jadi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka Abdullah mpaka Qidar ibn Ismail na kutoka Ismail mpaka Adam (a.s.) walikuwa ni wenye imani ya

37 Sahih at-Tirmidhi; amesema hadithi hii ni sahihi.38 Abu ‘l-Fida’, at-Tarikh.39 ‘Ubaydullah Amritsari, Arjahu ‘l-matalib, (toleo la kwanza 1340 H. uk. 458-463).

Amenukuu hadithi nane, zenye kuhitilafiana kidogo, na maana hii kutoka Muhadithiin mbali mbali wa Kisunni, wakiwemo akina Ibn Marduwayh, Al-Khwarizmi, Ibnu ’l-Maghazili, Al-Khatib Al-Baghdadi, al-Hamwayni, Muhammad ibn Yusuf al-Kanji ash-Shafi‘i, Abu Hatim na Abu Muhammad Ahmad bin ‘Ali Al-‘Asimi n.k. Baadhi ya hadithi hizi zinasema: “hivyo (Allah (s.w.t.)) alinifanya mimi kuwa Mtume na akamfanya Ali Wasii wangu (yaani mrithi wangu).”

25

kweli. Waliamini Mungu Mmoja tu na hawakushirikisha na chochote, na kwa uaminifu mkubwa na imani walifuata dini za haki za wakati wao. Kutoka Qidar mpaka Abdullah wote hawa walifuata Shari’ah ya Nabii Ibrahim (a.s.) ambayo ni Dini aliyowaamrisha Allah kuifuata.

Mwanachuoni mashuhuri wa ki-Shafi’i, Imam Jalalu ’d-deen as-Suyuti (aliyefariki mwaka 911 H) ameandika vitabu tisa juu ya mada hii, na amethibitisha pasi na shaka yoyote kwamba jadi yote ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) walikuwa ni wenye imani ya kweli. Mwanachuoni mashuhuri (Muhaddithiin) wa ki-Hanafi, Sheikh ‘Abdu ’l-Haqq Dehlawi ameandika hivi: “Wazazi wote wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka Adam mpaka Abdullah walikuwa tohara na wasafi kutokana na uchafu wa ukafiri na shirki. Haiwezekani kwa Al-lah (s.w.t.) kuweka Nuru tukufu (ya Mtukufu Mtume) katika giza na sehemu chafu, yaani katika kiuno cha mtu kafiri au kwenye tumbo la mwanamke kafiri. Aidha ingewezekanaje kwa Allah (s.w.t.) kuwaadhibu jadi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika Siku ya Hukumu na hivyo kumdhalilisha mbele ya walimwengu!”40

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe amesema: “Nilikuwa wakati wote nikihamishwa kutoka viuno vya watu wasafi kwenda kwenye matumbo ya wanawake safi.”41

Kwa marejeo za Kishi‘a, angalia Biharul-anwar, J.15.

Al-Hashawiyah Wahhabiya

Imani ya Wahhabi ni kinyume kabisa na imani ya ki-Islam. Wahhabi wanasema kwamba wazazi wa Mtume Mtukufu na babu zake walikuwa wanaabudu masanamu na ni makafiri. (Allah (s.w.t.) atukinge na hilo). Wahhabi wataona matokeo ya unafiki huu Siku ya Hukumu wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) atakaposimama mbele ya Allah (s.w.t.) akilalamika dhidi yao kwa maneno yao ya uchonganishi ya ukafiri dhidi ya wazazi na babu zake. Je, Muhammad ibn ‘Abdu ’l-Wahhab anaweza kuwaokoa Mawahhabi kutokana na ghadhabu ya Muhammad ibn Abdullah (s.a.w.w.) Siku hiyo?40 Madariju ’n-nubuwwah.41 ‘Ubaydullah Amritsari, Arjahu ’l-matalib, uk. 526-528.

26

Sasa kwa vile msomaji ameona kwa mpangilio (mfupi) kuwa Ushi‘a una maana gani na ni kipi Shi‘a wanaamini, wakati sasa umefika kuangalia shutuma zisizo na msingi zilizotolewa dhidi yao (Shi‘a) katika kijitabu kidogo cha Nairobi cha Mwandishi asiyejulikana.

Awali ya yote ni lazima kutaja kuwa Wahhabi ni al-Hashawiyah wa leo, au tuseme kwamba imani zao na maoni yao ni sambamba mia kwa mia na yale ya waliokuwa wakiitwa al-Hashawiyah. Al-Hashawiyah limetokana na neno al-hashw, (yaani mambo yasiyojulikana hakika yake, ni dhaifu na kuingizwa katika Dini). Jina hili linatumika kwa wale ambao wanakubali na kuamini hadithi zote ambazo zimeletwa kwenye Uislamu na watu ambao sio waaminifu. Wanaamini kwa maana ya kilugha tu maneno ya hadithi zote zilizohusishwa na Mtume (s.a.w.w.) na Sahaba zake bila kuzitafsiri kwa maana yake sahihi. Hata kama hadithi ni ya kuzua (kughushiwa) (lakini mzushi wa hadithi hiyo amechukua tahadhari kuiwekea wapokezi wazuri) wanakubali bila kujali kama maneno yake yanaafikiana na Qur’an au hadithi mutawatir au zilizo kubalika, au hapana. Muhaddithiina wengi wa Ki-Sunni walikuwa Hashawiyah.

Ahmad ibn Yahya al-Yamani (amekufa 840 H) anaandika hivi:“al-Hashawiyah: Jina hili linatumika kwa wale ambao “wanasimulia hadithi dhaifu, yaani ambazo zilipenyezwa na Zanadiqah katika semi za Mtukufu Mtume na wanazikubali bila kuzitafsiri tena, na wenyewe wanajiita As-habul-hadith and Ahlus-sunnah wal Jama’ah… Kwa pamoja wanaamini katika Jabr na tashbih, (yaani Allah analazimisha kufanya matendo na anafanana na viumbe). Huamini vile vile kuwa Mungu ana mwili na umbo, na kusema kwamba anavyo viungo mbali mbali kama mikono na miguu……”42

Abul Fath Muhammad ibn ‘Abdul-Karim ash-Shahristani (467-548 H) ameandika hivi katika kitabu chake Al-Milal wan-Nihal:-“Na kundi la As-habul-hadith, al-Hashawiyah wameonyesha wazi imani yao ya Tashbih (Allah kufanana na viumbe wake).... kiasi ambacho walifikia kusema kwamba wakati mmoja Allah macho yake yalimuuma, hivyo Malaika wakaenda kumuangalia; na kwamba 42 Ahmad ibn Yahya al-Yamani, Kitab al-Munyah wal Amal, fi sharh al-Milal wan

Nihal, chapa ya 1988, uk. 114.

27

alilia wakati wa mafuriko ya Nuhu, mpaka macho yakawa mekundu; na kwamba Arshi inatoa mlio wa kuomboleza chini Yake (kwa sababu ya uzito Wake) kama tandiko jipya la ngamia; na kwamba Amezidi Arshi kwa ukubwa mpaka kufikia vidole vinne kwa pande zote.”43

Hakuna haja ya kuonyesha kwamba ufafanuzi na maelezo haya yanawahusu moja kwa moja Wahhabi ambao wanajiita wenyewe Ashabul-Hadith or Ahlul-hadith na mara nyingi hujifanya kama Masunni, na siku hizi wanajiita wenyewe Ansaru ’s-Sunnah.

43 Ash-Shahristani, al-Milal wan Nihal, imepigwa chapa pambizoni mwa Kitabul Fasl cha Ibn Hazam, uk. 141.

UCHAMBUZI WA KIJITABU“WHAT IS SHI‘AISM?”

(USHI‘A NI NINI?)

29

UMA’SUM WA MAIMAMU :

Mwandishi wa kijitabu “What is Shi‘aism?” (Ushi‘a ni nini) ametoa hojanne kuonyesha kuwa mashi‘a ni Makafiri. Hoja ya nne kwa mujibu wake yeye ni kama zifuatavyo:“Shi‘a wanamini kuwa Maimamu wao hawakosei na hawana dhambi. Tabia na sifa hizi ni makhususi kwa ajili ya Mitume na Wajumbe wa Mwenyezi Mungu tu (s.w.t.).”

Maoni: Mwandishi huyu asiyejulikana hana habari kwamba jamaa zake wa ki-dini, yaani Wahhabi, hawaamini hata Ismah (kutokukosea na kutokuwa na dhambi) ya Mitume pia. Sitaki kunukuu hadithi za Sahih al-Bukhari zenye kumuonyesha Mtume Mtukufu wa Uislamu katika mwanga ulio mbaya mno. Ingawa usemai wa Kiajemi unasema kwamba: “Kunukuu neno la kikafiri sio ukafiri,” lakini imani yangu hainiruhusu mimi hata kunukuu hadithi zile potofu ambazo zimewapaWakristo na Myahudi silaha mikononi kuushambulia Uislamu na Mtukufu Mtume wake (s.a.w.w) kwa kutumia kitabu hiki cha Sahih al-Bukhari.

Mbali na hayo, Wahhabi huamini wazi wazi kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) si chochote bali ni kama kinara tu kwa Waislamu; na kwamba alikuwa akitoa amri kwa kutegemea Ijtihad yake. Kwa maneno mengine yeye alikuwa kama Mujtahid tu. Na kila mtu anaelewa kwamba Mujtahid anaweza wakati mwingine kufikia uamuzi ulio sawa ambapo wakati mwingine anaweza akafanya makosa. Kutokana na imani hizo, vipi anadai kuwa Mitume, na hususan Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa Ma’sum? (Asiye na dhambi na asiyekosea?)

Ni wazi mwandishi huyu asiyejulikana, kama si kutokuelewa dini yake vizuri, basi ametenda dhambi ya Taqiyyah kwa kuficha imani yake ya asili.

Imani ya Sunni kuhusu Ismat ya Manabii :

Na kama ilivyo itikadi ya Sunni, (hapa nanukuu kutoka vitabu viwili vyenye kutegemewa) kuhusu suala hili:1. Mwanachuoni mashuhuri ‘Allamah at-Taftazani (Sa‘du ’d-Deen

Ma‘ud ibn ‘Umar al-Ash‘ari ash-Shafi‘i) ameandika katika Sharu ’l

30

Maqasid hivi:“Madhehebu yetu ni kwamba Mitume hawafanyi dhambi kubwa yoyote ile baada ya kuba’athiwa (kupewa Utume) katika hali yoyote ile, (yaani si kwa kukusudia au kwa bahati mbaya) na hawafanyi dhambi ndogo kwa makusudi. Wanaweza kutenda madhambi madogo bila kukusudia, lakini hawadumu wala kuendelea kutenda dhambi hizo, bali hukanywa na hukanyika.”44

Katika maneno mengin (Allamah at-Taftazani anatueleza kwamba) Mitume wanaweza kufanya madhambi makubwa kabla ya kuba’thiwa.

2. Mulla ‘Ali al-Qari-Hanafi anaandika hivi:-“Mitume ni Ma’sum kutokana na uongo, hasa kuhusu mambo ya Shari’ah na kufiksha amri za dini na mwongozo wa Ummah, kwa makusudi (kwa mujibu wa ijma‘) na bila ya kukusudia (kutokana na maoni ya wengi).

Ama kwa madhambi mengine yote kuna maelezo kidogo kama ifuatavyo:-i. Mitume ni Ma’sum kutokana na ukafiri kabla na baada ya

kuba’thiwa, kwa mujibu wa ijma‘.ii. Vivyo hivyo, Mitume ni Ma’sum kutokana na kutenda madhambi

makubwa makusudi, kwa mujibu wa maoni ya Waislamu walio wengi; lakini al-Hashawiyyah wanakataa.

iii. Kama Mitume wanaweza kutenda madhambi makubwa bila kukusudia; walio wengi wanasema; wanaweza.

iv. Ama kwa madhambi madogo, wengi wanasema, Mitume wanaweza kutenda dhambi hizo makusudi, kinyume na ambavyo al-Jubba’i na wafuasi wake wanavyosema.

v. Wanachuoni wote kwa pamoja wanasema kwamba mitume wanaweza kutenda dhambi ndogo bila kukusudia, isipokuwa kwa vitu visivyo na maana kama kuiba kipande cha mkate, au kupuguza kidogo kipimo cha nafaka; lakini wanachuoni watafiti wameongeza sharti moja kwamba wanaonywa na wanakuwa na tahadhari. Hata hivyo, masuala yote hayo hapo juu yanahusu kipindi cha baada ya kupokea Wahyi. Ama kipindi kabla ya hicho, hakuna uthibitisho kuonesha kwamba hawawezi kufanya dhambi ndogo katika kipindi hicho. Lakini Mu’tazili hawakubaliani na hili (yaani, kwa

44 at-Taftazani, Sharu ‘l-Maqasid, chapa ya Beirut (1409 / 1989) J. 5, uk. 51.

31

mujibu wa Mu’tazili, Mitume hawawezi kufanya dhambi ndogo hata kabla ya Wahyi.)

vi. Na Shi‘a wanasema kwamba Mitume hawawezi kufanya dhambi yoyote, kumbwa au ndogo, kabla ya kupokea Wahyi au baada yake.45

Chunguza maelezo yote haya ya imani ya kweli ya Masunni katika suala hili, na angalia maelezo ya wazi ya Hashawiyyah (yaani, Mawahhabi) wanaamini kwamba Mitume wanaweza kufanya dhambi kubwa kwa makusudi. Kisha angalia jinsi alivyo mdanganyifu mwandishi huyu Wahhabi asiyejulikana anavyojifanya kwamba anaamini katika ‘ismah ya Mitume na Wajumbe wa Allah.

Ni ukweli uliothibiti wa historia ya Ki-Islamu kwamba Makhalifa wao wote sio Ma’sum; walikuwa si wenye kuepukana na dhambi au makosa. Ili kuwalinda kutokana na ukosoaji wamemteramsha chini Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) kutoka kwenye nguzo ya ‘ismah, na kama ilivyotajwa hapo juu, Imamu wao al-Bukhari amechangia sana katika kumtweza Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.).

Umeona kwamba wanazuoni wa Ki-Sunni wanafahamu na wanakiri kwamba imani ya Shi‘a kuhusu ‘ismah ya Mitume ni nzito mno na kwamba kwa mujibu wa Shi‘a Mitume walikuwa hawana dhambi na hawafanyi makosa kuanzia mwanzo wa kuzaliwa kwao mpaka mwisho wa maaisha yao, na walikuwa ni Ma’sum kutokana na madhambi makubwa na madogo.

Kwa hali hiyo basi, kwa sababu tunaamini Mitume Ma’sum tunasema (kama Qur’an na hadithi zinavyotuongoza) kwamba, warithi wa Mtume (s.a.w.w.) vile vile lazima wawe Ma’sum. (Kwa hoja zetu na thibitisho za ‘ismah ya Mitume na Maimamu, tazama vitabu vyangu hivi, “Prophethood” na “Imamate” [Tarjuma kwa lugha ya Kiswahili ya vitabu hizo ni “Utume” na “Uimamu”] vinayopatikana kutoka Bilal Muslim Mission of Tanzania).*

Lakini Wahhabi wanaamini Mtume ambaye alistahili kutenda 45 Mulla Ali al-Qari, Sharu ’l-fiqhi ’l-akbar, chapa ya Beirut (1404 / 1984), uk. 93.* Neno la mchapishaji: vile vile tazama The Infallibility of the Prophets in the Qur’an cha Sayyid Muhammad Rizvi [tarjuma kwa lugha ya Kiswahili ya kitabu hiki ni Ismah ya Mitume katika Qur’ani]. Zote zinapatikana kutoka Bilal Muslim Mission.

32

madhambi makubwa na madogo. Kwa hali hiyo, hawana budi kuamini watu wanaokosea na wasio Ma’sum kama warithi wake.

Mwandishi huyu asiyejulikana anaendelea kuandika hivi: “Shah Waliullah Dehlavi katika Kitabu chake “Tafheemat e Ilahiyah” (uk. 2444) ameliondoa pazia kwa kusema. Hakika hawaamini (yaani Shi‘a) Mwisho wa Utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.); ingawa hawaamini ukomo wa Utume wa Muhammad (s.a.w.w.) lakini bado wanaushuhudia kwa nguvu sana.”

Ni kweli kwamba Shah Waliullah Dehlavi anadai kwamba imani ya Shi‘a ni batili kwa sababu wanawaona Maimamu wao kuwa ni Ma’sum ingawa wanaamini kwamba Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa ndiye mwisho wa Mitume.

Mengi yanaweza kusemwa kuhusu kitabu hiki, At-Tafhimatu ’l- Ilahiyah, na madai yake ya kiburi na jeuri ambayo huonyesha tabia ya majivuno ya mwandishi wake, lakini hapa sio pahala pakuzungumzia suala hili. Kama mtu akisoma kitabu hiki ataona kwamba matamshi yake ambayo yanaonyesha majisifu, hayana tofauti na yale ya Mirza Gulam Ahmad Qadiani. Lakini Shah alikuwa hodari zaidi kwa kuficha madai yake chini ya kivuli cha tasawwuf. Hata hivyo hebu turudi kwenye maudhui yetu.

Madai ya Shah Waliullah kwamba Madhehebu ya Shi‘a ni batili yanaeleweka. Kila mtu miongoni mwa Madhehebu 73 za Ki-Islamu anaamini kwamba ni Madhehebu yake tu ndio iliyo ya haki, na nyingine 72 ni batili. Lakini Waislamu hawasemi kwamba Madhehebu nyingine ni Kafir. Hata Shah Waliullah amejizuia kutumia neno hili dhidi ya Shi‘a. Mtoto wake mashuhuri, Shah ‘Abdu ’l-‘Aziz anasema kwamba mtu mmoja alimuuliza baba yake (Shah Waliullah) kama Shi’a walikuwa wazushi. Baba yake (badala ya kujibu moja kwa moja) akaelezea maoni mbali mbali ya wanafikih (Wanasheria wa mambo yaDini) wa ki-Hanafi kuhusiana na suala hilo. Yule mtu hakutosheka, na akamtaka Shah atoe maoni yake mwenyewe. Baada ya kupewa jibu kama lile la kwanza, aliondoka akiwa amejaa hasira, na inasemekana alisema kwamba Shah Waliullah mwenyewe ni Shi‘a.46

46 Manazir Ahsan Gilani, Tadhkirah-e-Hazrat Shah Waliullah, Karachi, 1959, uk. 198-199.

33

Imani ya Shah Waliullah, Shah ‘Abdu ’l-‘Aziz, Muhyiddin Ibn Al-‘Arabi na wengineyo kuhusu ‘Ismat ya Maimamu 12:

Vyovyote vile iwavyo. Sasa hebu tuangalie hoja kuu ya Shah Waliullah kwamba itikadi ya ‘ismah ya Maimamu wetu 12 haiingiliani na itikadi ya kukoma kwa Utume wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hakuna haja ya kutazama mahali popote pale. Ni kitu cha kushangaza sana, Shah Wa-liullah Dehlavi mwenyewe katika kitabu hiki hiki (kilichonukuliwa na huyu mwandishi asiyejulikana) At-Tafhimatu ’l-Ilahiyah ametaja sifa nne za kiroho kwa Maimamu wetu kumi na wawili kama ifuatavyo:-

1. ‘Ismah2. Hikmah3. Wajahah4. Qutbiyat Batiniyah (kuwa chimbuko la kiroho).

Ili kutoa mwanga tu kwa yale anayosema, ninafasiri sehemu ya maandishi yake kuhusu sifa ya Wajahah:-“Ewe ndugu! Nimekueleza moja tu katika elfu kuhusu Wajahah. Kama mja akiwa Wajih (mwema sana, mteule), anakuwa mwenye kupendeza na kamili. Kisha kila hatua anayochukua inakuwa ni tendo zuri; kama akisogea au akila tonge la chakula, ni tendo zuri; akipanda mnyama, kila hatua ya Farasi wake ni tendo zuri; wakati akilala kugeuka kwake upande wa kulia na kushoto, yote hayo yanakuwa ni matendo mazuri, Allah hukubali kutoka kwake matendo hayo machache zaidi, ambayo kutoka kwa wengine haikubaliwi.

“Na anakuwa kipenzi cha Allah, na chochote alichokiumba Allah kakiumba kwa ajili yake. Na ‘ismah inapokamilika, matendo yake yote yanakuwa haqq yenyewe (haki, sawa sawa). Sisemi kwamba matendo yake yanatokea kwa mujibu na haqq; Bali (nasema kwamba) matendo yake yenyewe ni haqq (ni tabia yake); (zaidi) sana haqq ni kitu am-bacho huonekana (kama mwanga) kutoka matendo hayo; kama miali kutoka juani. Na Mtume wa Allah (s.w.t.) ametaja cheo hii wakati yeye aliomba kwa Allah Ta’ala kuhusu ‘Ali, akisema: “Ya! Allah! Igeuze haqq pamoja na yeye kokote atakakogeukia”; na hakusema mgeuze (‘Ali) kokote haqq inakogeukia.” (Juzuu 2, uk. 19).

34

Mtu mmoja Mirza Hasan ‘Ali aliaandika barua ndefu kwa Shah ‘Abdu ’l-‘Aziz Muhaddith Dehlavi, akipinga jinsi baba yake maarufu alivyosadikisha sifa hizi nne zilizotajwa hapo juu kwa “Hazaraat A’immah Ithna ‘ashar ‘Alayhumussalaam” (watukufu Maimamu kumi na mbili, amani iwe juu yao), ambapo ‘ismah, kwa mujibu wa Sunni haikubaliwi kwa wengine ila kwa Mitume, Wajumbe na Malaika; Na jinsi yeye (Shah ‘Abdu ’l-‘Aziz Dehlavi) alivyothibitisha haya katika Risalah yake wakati akielezea imani ya baba yake.

Swali na maelezo ya majibu ya Shah ‘Abdu ’l-‘Aziz yamechapishwa kwenye “Fatwa Shah ‘Abdu ’l-‘Aziz.” Haitawezekana kutafsiri maelezo yote kwenye kijitabu hiki kidogo, lakini baadhi ya maneno yananukuliwa hapa kuonyesha kwa ujumla maana ya majibu yake.Anasema:-“‘Ismah ina maada mbili: Kwanza: Kutokuwezekana kutenda dhambi,ingawa mtu anao uwezo wa kufanya hivyo. Maana hii kwa mujibu wa Ijma‘ ya Ahlus-Sunnah imetengwa kwa ajili ya Mitume na Malaika. Pili: Kutotenda dhambi yoyote, ingawa mtu anaweza akafanya hivyo. Hakuna ugumu katika fikra hii; na maana hii inaitwa “mahfuziyyat” (kuhifadhiwa) katika lugha ya kisufi... maana hii haikutengwa kwa Mitume. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliomba ‘ismah hii wakati alipowaombea Ahlul-Bayt wake, kwa maneno haya: “Ya! Allah! Weka uchafu mbali nao na uwatoharishe kwa utakaso.”

“Hikmah yenye manufaa ni elimu yenye manufaa. Kama ikisomwa (kutoka kwa mtu) haiitwi hikmah... Ikiwa elimu hiyo ni (kiroho) kipaji alichopewa mtu moyoni mwake, inaitwa hikmah, iwe inahusika na imani, matendo au maadili. Hii pia haikutengwa kwa Mitume ... Ndio maana imekuja katika hadithi Tukufu: ‘Mimi ni nyumba ya hikmah na Ali ni mlango wake;’ na imekuja katika hadithi nyingine inayojulikana sana: ‘Mimi ni Jiji la Elimu na Ali ni mlango wake.’ Na elimu katika hadithi hizi ina maana hii hasa (yaani elimu ya Ki-Mungu)”.

“Wajahah ina maana kwamba Allah hushughulika na baadhi ya waja Wake katika hali ambayo hurudisha nyuma uovu wa maadui kutoka kwao, na kuonyesha usafi wao kutokana na masingizio ya kasoro na kushindwa... Imethibitishwa kuhusu ‘Ali Murtaza (Allah awe radhi

35

naye) wakati Mtume (s.a.w.w) alipoomba kwa ajili yake: Ya! Allah! Geuza haqq kokote anakogeukia; na hakusema Mgeuze kokote haqq inakogeukia.”

“Na Qutbiyat Batiniyah ina maana kwamba Allah (s.w.t.) huchagua baadhi ya waja wake, ili kwamba upendeleo wa ki-Mungu unawafikia wao kwanza binafsi na moja kwa moja, na kisha kutoka kwao huenda kwa wengine, hata kama mpokeaji wa baadae hakujifundisha au kupokea chochote moja kwa moja kutoka kwao. Kwa mfano, mionzi ya jua hufika ndani ya nyumba kupitia dirisha; kwanza dirisha linamulikwa, na kisha vitu vingine hung’arishwa kupitia mwanga wa anga.”47

Kwa njia hii, itikadi ya ‘ismah na sifa nyingine za Maimamu wetu kumi na wawili (a.s.) imesadikiwa na Shah Waliullah Dehlavi na kuthibitishwa pamoja na hoja na Shah ‘Abdu ’l-‘Aziz Dehlavi. Tunayo haki ya kuwauliza Wanachuoni hawa wawili mashuhuri, iwapo wao wenyewe waliamini katika ukomo wa Utume wa Muhammad (s.a.w.w) au hapana?

Imani ya ‘ismah kwa Maimamu wetu kumi na wawili haikuishia kwa wanachuoni hawa wawili waliotajwa hapo juu, ambao imetokea kuwa walikuwa miongoni mwa maadui wakali wa Shi‘a. Hata kabla na baada yao, wanachuoni wa Ki-Sunni walikuwa wakitaja na kuonyesha itikadi hii. Kwa mfano, Shaykh Muhyiddin ibn Al-‘Arabi Al-Undulusi (kafa 638 H) ameandika katika kitabu chake maarufu, Al-Futuhat Al-Makkiyah:“Elewa kwamba Mahdi (Allah awe radhi naye) ni lazima atadhihiri. Lakini hatadhihiri mpaka ulimwengu utakapojaa maonevu na dhuluma; kisha ataijaza haki na uadilifu; na kama hakutakuwa na zaidi ya siku moja (ya maisha) ya Dunia, Allah atairefusha siku hiyo vya kutosha ili imtoshe Khalifa huyu kutawala. Na yeye (Imam Mahdi) anatokana na kizazi cha Mtume wa Allah (s.w.t.) kutokana na na watoto wa Fatimah (Allah awe radhi naye); Mhenga wake ni Husain bin Ali bin Abi Talib; baba yake ni Hasan Al-‘Askari (mwana wa Imam Ali Al-Naqi, mwana wa Imam Muhammad Al-Taqi, mwana wa Imam Ali Al-Ridha, mwana wa Imam Musa Al-Kadhim, mwana wa Imam Ja‘far Al-Sadiq, mwana wa Imam Muhammad Al-Baqir, 47 Shah ‘Abdu ’l-‘Aziz Dehlavi, Fatwa ‘Azizi, Dehli (India), haina tarehe uk. 126-128.

36

mwana wa Imam Zainul Abedeen Ali, mwana wa Imam Husain, mwana wa Imam Ali bin Abi Talib); Jina lake ni jina la Mtume wa Allah. Waislamu watafanya Bay’at (Kiapo cha Utii) naye baina ya Rukn na Maqam (yaani Rukn Yamani na Maqam Ibrahim ndani ya Ka’bah); atakuwa kama Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kwa umbile, na chini yake kwa tabia, kwa sababu hakuna anayeweza kuwa (sawa kwa tabia) kama Mtume wa Allah (s.w.t.), kama Allah mwenyewe alivyosema: Hakika wewe (Muhammad) unatabia njema kabisa..... Atagawa mali kwa usawa na atafanya uadilifu kwa Ummah... Msaada (kutoka kwa Allah) utakuwa mbele yake; atafuata nyayo za Mtume wa Allah (s.w.t.), na hatafanya kosa lolote; kutakuwa na Malaika akayemsaidia ingawa yeye mwenyewe hatamuona ...”48

Zingatia maneno haya “na hatafanya kosa lolote; kutakuwa na Malaika akayemsaidia..”

Baadae, Mwanachuoni mwingine mwenye kujulikana sana wa

48 Al-Futuhat al-Makkiyah, Sura ya 366, Maneno haya ya Shaykh Muhyiddin ibn Al-‘Arabi (amekufa in 638 H) imenukuliwa na wanachuoni wengi wanao heshimiwa wa Ki-Sunni na wa Ki-Shi‘a wa Uturuki, Misri na India. Mashuhuri miongoni mwao ni:-a. Shaykh ‘Abdul Wahhab as-Sha‘rani, (898- 973 H.) katika Kitabu chake

Al-Yawaqit wal Jawahir, (alichokimaliza katika Rajab, 955, yaani miaka 18 kabla ya kufa kwake), Misri. 1307 H, J. 2, uk.145, ikachapishwa tena Darul Ma‘rifah, Beirut;

b. Shaykh Muhammad As-Sabban ash-Shafii (amekufa 1206 H.), katika kitabu chake Is‘afu ’r-Raghibeen, Misri, 1312 H, uk. 142; vile vile kimechapishwa pembezoni mwa kitabu Mashariqu ’l-Anwar, (ilichotajwa hapa chini);

c. Shaykh Hasan Al-‘Adawi Al-Hamzawi (amekufa 1303 H.) katika kitabu chake Mashriqu ’l-Anwar, Matba‘at Al-‘Uthmaniyah, Istanbul, 1307 H;

d. Sayyid Hamid Husayn Al-Musawi (amekufa 1306), katika Kitabu chake Istiqsa‘u ’l-Ifham, Lucknow, J.2

Tahreef ndani Al-Futuhat: Weka maanani rejea zote hizi za Ma-Ulama wenye kuheshimiwa kama hawa, na kisha tazama katika Al-Futuhat kilichochapishwa Misri mwaka 1339 katika juzuu nne. Utaona kwamba wachapishaji wamebdilisha (yale) maneno, “Mhenga wake ni Husain” na (kuandika) Mhenga wake ni Al-Hasan; na kisha wakaondoa mlolongo wote wa kizazi kuanzia na maneno, “baba yake ni Hasan Al-‘Askari” na kumalizia mistari minne baadae, kwa (maneno) “mwana wa Imam Ali bin Abi Talib.” Kwa masikitiko tahrif kama hizi zimekuwa mpangilio wa kawaida katika vitabu vyote vya zamani vinavyochapishwa Misri na baadhi ya nchi za Kiislam tangu miaka 100 au zaidi.

37

Ki-Sunni Sufi, Maulana ‘Ali Akbar Maududi, aliandika hashiyah juu ya Nafahat, ambamo ameandika hivi:“Shaykh Abu ’l-Hasan ash-Shadhili (r.a.) amesema kwamba Qutb49 ina alama kumi na tano kwa vile (kwa mfano) anasaidiwa na ‘ismah (kutokuwa na dhambi), rahmah (huruma), khilafah na niyabah (umakamu) na anasaidiwa na wale malaika wanaobeba Arshi, na ukweli wa utu wake (Hakika ya dhati ya Mwenyezi Mungu) inathibitika kwake na anashikilia (anakuwanazo) tabia za ki-Ungu n.k... Kwa hiyo, Madhehebu yao hao wanaoamini kwamba watu wengine wasiokuwa Mitume wanaweza kuwa Ma’sum imethibitishwa... Ukweli kwamba Mahdi (r.a.) aliyeahidiwa yupo (anaishi) na yeye ni Qutb baada ya baba yake Al-Hasan al-‘Askari (Allah awe radhi nao) kama yeye alikuwa Qutb baada ya baba yake, na hivyo mpaka Imam ‘Ali ibn Abi Talib (Allah (s.w.t.) atupe heshima kupitia kwao) inaonyesha kwamba sifa hii (ya Qutbiyat) imetengwa kwao tu (yaani maimamu 12) kwani tangu Qutbiyat imekuja kwa babu yake, ‘Ali ibn Abi Talib mpaka imemalizikia kwake (Mahdi) - sio kabla ya hapo. Sasa Qutb yeyote anayepata daraja hii, anaipata kama naibu wake - kwa sababu yeye (Mahdi) amefichwa kwenye macho ya watu wa kawaida na hata watu maalum (ingawa hakufichwa kutoka kwenye macho ya watu watukufu sana ...). Kwa hiyo ni jambo lisiloepukika kwamba, kila Imam kutoka Maimamu hawa kumi na wawili ni lazima awe Ma’sum.”50

Na karne iliyopita (karne ya 14) Mwanachuoni mashuhuri anayejulikana sana wa Ki-Sunni Maulana Wahidu ’z-Zaman wa Hydrabad Deccan ameandika hivi:“Maoni sahihi ni kwamba Aya hii (ya utakaso) imekusanya watu hawa watano tu, (yaani Mtume, Ali, Fatima, Hasan na Husain) ingawa katika matumizi ya ki-Arabu, neno Ahlul-Bayt linatumika kwa wake vile vile. Watu wengine wanathibitisha kwa Aya hii kwamba watu hawa watano walikuwa ni Ma’sum. Lakini kama sio Ma’sum, basi kwa hakika walikuwa Mahfuz (walio hifadhiwa kutokana na kutenda dhambi au makosa).”51

49 Baadhi ya maelezo ya Qutb yametolewa na Shah Waliullah, kama ilivyonukuliwa hapo awali.

50 Maulana ‘Ali Akber Maududi, al-Mukashafat (Hashiya juu ya Nafahat), chini ya jina ‘Ali ibn Sahl al-Isfihani, kama ilivyonukuliwa katika Istiqsa‘u ’l-Ifham, J. 2.

51 Wahiduzzzaman Khan, Anwaru ‘l-lughah, Banglore, kifungu cha 22 uk. 51.

38

Hivyo, hawa ndio Maimamu wetu kumi na wawili, ambao ‘ismah yao inakubaliwa hata na maadui wetu wakali. Walilazimika kuwa Ma’sum kwa sababu Mtume, ambaye walimrithi, alikuwa Ma’sum.

Wale ambao kwao Mtume hakusalimika na madhambi na makosa, wametosheka na viongozi ambao hawakuwa Ma’sum. Inashangaza kuona watu kama hawa wakitulaumu ati kwa nini tunawaamini Maimamu hawa Ma’sum!! Hatukufunga mlango wa Ushi‘a kwa mtu yoyote kama wanatuonea wivu kwa sababu ya Maimamu wetu Ma’sum, wanakaribishwa kuingia kwenye kundi la Mashi‘a na wao vile vile watapata uongofu kutoka kwa viongozi hawa hawa Ma’sum.

Mwishilizo wa Utume:

Muandishi huyu asiyejulikana anasema: “Itikadi ya Shi‘a ya Uimamu si chochote bali ni kuendelezwa kwa Utume, ambao kwa kweli umepewa jina tofauti tu. Lakini kuna nini katika jina, ikiwa nia na vilivyomo ni ile ile?”

Yeyote anayetaka kujua itikadi yetu kuhusu Khatmun Nabuwwat (ku-koma kwa utume) ni budi asome kitabu changu “Muhammad (s.a.w.w.) ni Nabii wa Mwisho” au cha Kiingereza “Muhammad (s.a.w.w.) is the last Prophet” ambavyo vinapatikana kutoka Bilal Muslim Mission of Tanzania. Maneno machache yananukuliwa kutoka kitabu hicho (cha Kiingereza) kwa rejea rahisi: “Wakati ubinadamu ulipofikia hali hiyo, Mwenyezi Mungu alituma sheria za mwisho ambazo zingetumiwa na watu wote hadi siku ya mwisho wa dunia. Baada ya Muhammad Mustafa (saww) hapakuwa na haja tena ya sheria mpya zozote; wala hapakuwa na haja tena ya nabii au mjumbe yoyote mpya kutoka kwa Mungu. Na ilikuwa kwa sababu hii kwamba yeye (Mtume Muhammad (s.a.w.w.)) alitangazwa na Mwenyezi Mungu kuwa ni Mwisho wa manabii wote.”

“Bila shaka, haja ya mfasiri wa Qur’ani Tukufu na mwenye kulinda sheria za dini itakuwepo daima. Lakini Mwenyezi Mungu alimteua Maimamu kwa lengo hili, baada ya Mtume wa Mwisho. Mfululizo wa Utume ukakomea hapo na ndipo mfumo mpya wa uongozi wa dini, unaojulikana kama ‘Imamat’ kuletwa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:- ‘Wana wa Israeli, mitume walikuwa wakiwaongoza;

39

alipofariki mtume, mwingine alichukua mahali pake. Lakini hakuna mtume baada yangu, na hakika watakuwepo Makhalifa’.”

Sasa huyu Mwandishi asiyejulikana budi amuulize Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Lakini kuna nini kwenye jina wakati nia na vilivyomo ni ile ile?” (Lakini kwa kweli nia na vilivyomo sio ile ile, kama ilivyowazikwenye rejea zilizotolewa hapo juu).

Mwandishi huyu asiyejulikana ametumia uk. 7-13 wa kijitabu chake akinukuu baadhi ya maneno kutoka vitabu mbali mbali vya Kishi‘a kuonyesha kwamba uimamu mbele za Mshi‘a ni kuendelea kwa uongozi wa dini (Kiroho) baada ya Mtume wa mwisho; na Mashi‘a wanaamini kwamba Imam lazima awe Ma’sum (asiyetenda dhambi) na Mansus min Allah (aliyeteuliwa na Allah). Kama mwandishi huyu asiyejulikana asili yake, hapendi itikadi hii, angezikana hoja zilizotolewa na Waandishi hao. Kama hakuona vitabu vilivyochapishwa Iran, Pakistan au India, hakika atakuwa ameona kitabu changu “Imamate” ambapo kutoka humo amenukuu sentensi moja tu katika uk. 10 wa kijitabu chake. Kitabu changu hicho kina kurasa 188; zote zinahusu suala hili (la Uimamu). Na mada ya ‘ismah na kuteuliwa na Allah, huanzia katika ukurasa 39 na kuendelea mpaka ukurasa wa 105. Ningefurahi kama mwandishi huyu angejaribu kukanusha yoyote kati ya hoja zangu. Lakini hakuwa na ushujaa wa kufanya hivyo; bali aliendelea tu kudai kwamba itikadi hii ya Shi‘a ni kinyume na itikadi ya Sunni. Sawa, kila mtu anajua kwamba kuna (ulimwengu wa) tofauti nyingi kati ya itikadi ya Shi‘a na Sunni kuhusu uimamu na ukhalifa. Sasa kwa nini apate tabu kwenye nukta hii. Kama anafikiria kuwa itikadi ya Shi‘a ni potofu, angepaswa kuzikana hoja zetu. Lakini hakuleta hoja yoyote, na hivyo hakuna kitu cha kujibu.

Na zaidi ya hoja zilizoandikwa juu ya ‘ismah katika kitabu changu, nimeandika uthibitisho wa Shaykh Muhyiddin ibn al-‘Arabi, Maulana ‘Ali Akbar Maududi, Shah Waliullah Dehlavi, Shah ‘Abdu ’l-Aziz Dehlavi and Maulana Wahidu ’z-Zaman Hyderabadi kwamba Maimamu wetu kumi na mbili walikuwa Ma’sum. Kama Shi‘a ni Makafiri kwa sababu ya itikadi hii, vipi kuhusu hawa wanachuoni thabiti wa Ki-Sunni? Walikuwa ni Waislamu? Au nao vile vile walikuwa makafiri?

40

TAHREEF

Baadhi ya mifumo ya Wahhabi :

Hoja ya kwanza, kwa maoni yake ni hii:-“Imethibitishwa na ukweli kwamba, wao wanakubaliana na itikadi kwamba kuna Tahreef katika Qur’an. Mashi‘a wote wa zamani au wa sasa, Maimamu wao na madhehebu mbali mbali za Kishi‘a kwa pamoja wanakubaliana juu ya itikadi hii. Kwa ajili hiyo Mashi‘a ni makafiri kwa msingi wa ijma‘.”

Mahali pengine anaandika hivi:-“Waanzilishi wa dini ya Shi‘a tangu zama za kuweka msingi wake wamepita katika awamu tatu za kihistoria. Awamu ya kwanza, hakuna hata mmoja miongoni mwa Mashi‘a aliyeshikilia itikadi ya kwamba Qur’an ni kamili na bila ya mabadiliko. Hata hivyo, katika awamu ya pili, ni wanachuoni wanne tu miongoni mwa Mashi‘a ambao kwa njia ya Taqiyah walitangaza kuwa hakukuwa na Tahrif katika Qur’an.”

“Walikuwa ni (1) Abu Jaffar Sani Muhammad bin Ali bin Hussain bin Mussa bin Bayyabah Allama Sadduqh, aliyefariki mwaka 381 A.H. (2) Sharif Murtaza Abdul Qasim Ali bin Hussain bin Hassanain bin Mussa Baghdadi, mwandishi wa kitabu ‘ilmul Huda, aliyefariki mwaka 436 A.H. (3) Shaikh at-Taifa Abu Jaffar Muhammad bin Hussain bin Ali Toousi Mufasir, aliyefariki mwaka 460 A.H. (4) Abu Ali Tabrisi Aminuddin Fazal bin Hussain bin Tazal Mashudi, mwandishi wa Tafsir Majmah al-Bayan, aliyefariki mwaka 548 A.H

“Hii ni kusema, katika awamu ya pili kuanzia mwaka 261 A.H. hadi 548 A.H. ni wanachuoni wanne tu wa Kishi‘a ambao hawakuamini kuwa kulikuwa na Tahrif katika Qur’an. Hata hivyo, kwa vile usemi wao haukuwa katika misingi ya hoja na ilikuwa kinyume na zile hadithi za Dini ya Kishi‘a zisizokatizwa, Wanachuoni wa Kishi‘a wa awamu ya pili walipuuza usemi na utafiti wao.”

Katika kunukuu kifungu cha kwanza mwandishi huyu ametumia maneno ambayo kwayo amewalaumu maimamu wetu kwa ukafiri. Na’udhu billah. Naamuulize Shah Waliullah na Shah ‘Abdu ’l-‘Aziz

41

kama mtu anyewatukana Maimamu (a.s.) kumi na mbili wa Kishi‘a kwa maneno mabaya kama haya kama ni Muislamu au Kafir. Au na aulize swali hilo hilo kwa Kiongozi wake Manzoor Ahmad Nu‘mani. Jibu lake litakuwa pia ni kipimo kwa Uislamu wake Manzoor Ahmad Nu‘mani.

Mwandishi huyu pia hajui kwamba mwanzishi wa Ushi‘a si mwingine bali ni Mtukufu Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.) kama ambavyo msomaji atakuwa ameona katika makala ya “Maana na Asili ya Ushi‘a” mwanzoni mwa kitabu hiki.

Awamu za Kihistoria anazozitaja ni ubunifu wake mwenyewe au pengine ubunifu wa kikundi chake. Hata hivyo, hajui kwamba Wanachuoni wanne aliowataja walikuwa ni viongozi wa Jumuiya ya Kishi‘a katika nyakati zao, na kwamba maandishi yao yanaheshimiwa katika ulimwengu wa Kishi‘a hadi leo.

Vile vile hawezi hata kuyaandika majina yao sawa sawa, na nina hakika hajaviona vitabu vyao kamwe.

Anaandika hivi:-“(1) Abu Jaffar Sani Muhammad bin Ali bin Hussain bin Mussa bin Bayyabah Allama Sadduqh”

Maelezo: Kuniyah yake ilikuwa Abu Ja‘far: hakuna neno ‘Sani’ ndani yake; Babu mzaa babu yake alikuwa Babuwayh (sio Bayyabah), na anajulikana kama ash-Shaykh as-Saduq (sio Allamah Sadduqh).

“(2) Sharif Murtaza Abdul Qasim Ali bin Hussain bin Hassanain bin Mussa Baghdadi, author of ‘ilmul Huda”.

Maelezo: Maneno “Mwandishi wa ‘ilmul Huda” ni ya ajabu sana. ‘Alamu ’l-huda (Bendera ya uongozi) ilikuwa ni cheo cha Sharif al-Murtaza. Mtu huyu asiye elewa alidhani ni kitabu chake, na hata hivyo hakuweza kulitamka sawa sawa na akaligeuza ‘Alam kaifanya ‘ilm. Kisha kuniyah yake ilikuwa Abul Qasim (sio Abdul Qasim); Baba yake Sharif al-Murtaza alikuwa ni Abu Ahmad al-Husayn ibn Musa; mwandishi huyu asiye na ujuzi ameongeza jina “bin Hassanain” baina yao.

42

“(3) Shaikh at-Taifa Abu Jaffar Muhammad bin Hussain bin Ali Toousi Mufasir”

Maelezo: Shaykhu ’t-Ta’ifah baba yake alikuwa akiitwa al-Hasan (sio Hussain).

“(4) Abu Ali Tabrisi Aminuddin Fazal bin Hussain bin Tazal Mashudi, mwandishi wa Tafsir Majmah al-Bayan”

Maelezo: Jina lake na pia la babu yake lilikuwa “Fazl” (sio Fazal wala Tazal) na baba yake alikuwa al-Hasan (sio Hussain); sikuweza kutam-bua ni neno gani ambalo mwandishi huyu asiye na ujuzi amelibadili-sha kuwa “Mashudi.” Jina la (kitabu hicho cha) Tafsir ni Majma‘u ’l-Bayan, sio Majmah al-Bayan.

Mifano hii inatosheleza kuonyesha kiwango cha elimu cha mtu huyu. Vile vile, nampa changamoto aandike majina ya hao wanachuoni wa Kishi‘a wa hiyo awamu anayoiita ni ya pili ambao walipuuza maneno na utafiti wao.

Hata hivyo, natuliangalie suala lililo mbele yetu. Kwanza nitanukuu baadhi ya vipengele kutoka kwenye vitabu vyetu vyenye kuhusu suala hili la Tahrif, kisha tuone vitabu vya kisunni vinasemaje kuhusu suala hili.

ITIKADI YA SHI‘A:

Kwanza, itikadi yetu kuhusu Qur’an inaweza kuonekana kwenye rejea zifuatazo toka kwenye kitabu chetu kiitwacho Kitabu ’l-I‘tiqadat (kitabu cha itikadi) kilicho andikwa na Shaykh as-Saduq Abu Ja‘far Muhammad ibn ‘Ali ibn Husayn ibn Musa Babuwayh, (“Mwanachuoniwa kwanza” aliyetajwa hapo juu):“Itikadi yetu ni kwamba, Qur’an ambayo Allah ameiteremsha kwa Mtume wake Muhammad (s.a.w.w.), ni ile ile iliyoko kati ya majalada mawili (daffatayn); na ni ile ile iliyomo mikononi mwa watu, wala sio zaidi ya hiyo.”

Kisha anasema:

43

“Na anayethubutu kusema kwamba sisi tunasema ni zaidi ya hiyo ni muongo.”

Kisha anatoa baadhi ya sababu za itikadi yetu ya kwamba Qur’an sio zaidi ya kitabu kilichomo mikononi mwa watu. Sababu hizo ni kama zifuatazo:-a. Hadithi zinazoelezea thawabu za kila sura ya Qur’an.b. Hadithi zenye kueleza thawabu za mwenye kuisoma Qur’an yote.c. Ruksa ya kusoma Sura mbili katika Rakaa moja (kwenye Sala ya

Nafilah)d. Kukatazwa kusoma sura mbili katika Sala za Faradhi.

“Yote haya yanaweka wazi kile tulichokisema kuhusu Qur’an na kwamba idadi ya ujumla yake ni ile ile iliyomo mikononi mwa watu. Kadhalika kilichosimuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kukataza kuisoma Qur’an yote kwa usiku mmoja na kwamba hairuhusiwi kumaliza Qur’an yote chini ya siku tatu. Haya yote pia yanathibitisha tulichosema.”

Kisha akizungumzia Ahadith Qudsiyah, (Ambazo pia zimeteremshwa na Allah lakini sio sehemu ya Qur’an) anasema:-“Tunasema kwamba sehemu kubwa ya ufunuo iliteremshwa, lakini sio kama sehemu ya Qur’an, na kwamba kama ingekusanywa yote, ukubwa wake bila shaka ungekuwa sawa na Aya kumi na saba Elfu. Na hii, kwa mfano, ni kama alivyosema Jibra’il kumuambia Mtume (s.a.w.w.): ‘Hakika Allah anakuambia, Ewe Muhammad: Wafanye wema viumbe wangu kama vile ninavyofanya Mimi’; na ni kama maneno yake, ‘Kuwa muangalifu na watu wenye chuki na uadui wao’; na ni kama maneno yake, ‘Ishi Maisha Marefu kiasi utakavyo, lakini hatimae utakufa; na penda chochote unachotaka, lakini utakujatenganishwa nacho; na fanya utakalo, kwani (mwishoni) utakujalikuta’; na ‘Utukufu wa Muumini ni sala yake ya usiku, na hadhi yake ni katika kujizuia kuwaudhi watu’; na kama usemi wa Mtume (s.a.w.w.): ‘Jibra’il alikuwa akinihimiza kuosha meno yangu mpaka nikadhani meno yangu yataanguka, na alikuwa akinihimiza kuhusu jirani mpaka nikadhani atawafanya miongoni mwa warithi, na alikuwa akinihimiza kuhusu mwanamke mpaka nikadhani hastahili kupewa talaka, na aliendelea kunihimiza kuhusu mtumwa

44

mpaka nikafikiri kwamba ataweka muda wa mwisho ambao ukiisha basi aachiwe huru’; na kama maneno ya Jibra’il wakati Mtume alipokwisha maliza vita vya Khandaq: ‘Ewe Muhammad! Hakika Allah anakuamuru kwamba usisali al-‘Asr ila katikati ya Banu Qurayzah’; na kama usemi wa Mtume (s.a.w.w.): ‘Mola wangu ameniamuru niwatendee watu wema kama alivyo niamuru kuswali Sala za Faradhi’; na kama maneno yake: ‘Sisi Mitume tumeamrishwa kuongea na watu kulingana na kiwango chao cha kuelewa mambo...”

Anaendelea kunukuu Ahadith Qudsiyah za namna hii nyingi na anamalizia akisema:-“Kuna maelezo mengi namna hii, ambayo yote ni ufunuo lakini hay-akuletwa kama sehemu ya Qur’ani; vinginevyo, kwa hakika yangeingi-zwa kwenye Qur’an na sio kuachwa.”52

Hii inatoka kwenye kitabu kimoja tu. Uthibitisho mwingine wenye kueleza kuwa hakukuwa na nyongeza ndani ya Qur’an au upungufu kutoka kwenye Qur’ani unapatikana na kuelezewa wazi wazi kwenye mamia ya vitabu vyetu vya hadithi, tafsir na itikadi.

Sasa tuangalie alichokiandika mfasiri wetu, ash-Shaykh Abu ‘Ali al-Fazl ibn al-Hasan at-Tabrisi (a.r.) kwenye utangulizi wake wa kitabu chake Tafsir Majma’u ’l-bayan:-“Inakubalika bila ya ikhtilafu kwamba hakuna nyongeza kwenye Qur’an. Ama kuhusu upungufu, kikundi kimoja miongoni mwa wenzetu katika dini (yaani Mashi‘a) na vile vile kundi la al-Hashawiyyah53 litokanalo miongoni mwa Sunni wamesimulia hadithi inayosema kwamba kuna mabadiliko na upungufu ndani ya Qur’an. Lakini Madhehebu iliyo sahihi ya wenzetu katika dini inalipinga hilo. Na ndilo lililoungwa mkono na al-Murtaza (Allah aitukuze Roho yake); na ameandika kwa kina juu ya suala hili katika kitabu chake kiitwacho Jawabu ‘l-masa’ili ‘t-Tarabalasiyat.” Kisha anataja baadhi ya nukta zilizotolewa na as-Sayyid Murtaza, kwa kifupi kama ifuatavyo:-

“Kwamba Qur’ani imesimuliwa kisawa sawa (ni ukweli na) inajulikana kama tujuavyo Miji Mikubwa, mambo makubwa, 52 Shaykh as-Saduq, Kitabu ’l-I‘tiqadat, sura ya ‘itikadi juu ya kiasi cha Qur’ani’.53 Imeelezwa kuwa Wahhabi ndio al-Hashawiyyah wa sasa.

45

matukio muhimu, halikadhalika na vitabu mashuhuri na mashairi yaliyosimuliwa ya Waarabu. Ukweli ni kwamba sababu za kuwasilisha na kuihifadhi Qur’ani zilikuwa zenye nguvu sana, na hadhari ikawekwa juu ya Qur’an kwa kina zaidi kuliko ile ilyopewa kwa mambo mengine hapo juu. Tahadhari (iliyochukuliwa) kwa upande wa Qur’ani haiwezi kulinganishwa na vitu vilivyopita, kwa sababu ni muujiza wa utume, chanzo cha elimu ya Shari’ah na kanuni za dini. Wanachuoni wa Ki-Islam wamefanya jitihada zao za juu kuilinda na kuihifadhi mpaka wakashika maana ya kila maelezo yake: irabu zake, kisomo chake, herufi zake na aya zake. Itawezekana vipi kitu chochote kibadilishwe au kiondolewe ndani yake pamoja na unyofu wa uangalifu na tahadhari makini?

“Vile vile yeye (Allah aitakase roho yake) amesema: Elimu ya kutafsiri Qur’ani na sehemu zake ni sawa sawa na ile ya kuisimulia Qur’an nzima katika usahili wake na uwasilishaji wake. Ni sawa na kile kinachojulikana kuhusu vitabu vingine vinavyojulikana vyema, kama kitabu cha Saybwayh na kile cha al-Muzni... Kama mtu ataingiza sura mpya katika vitabu hivi, mara moja itajulikana, itabainika na kugundulika kwamba ni uwongo... Na tunajua kwamba tahadhari na uangalifu katika kuiwasilisha Qur’ani (kwa watu) ulikuwa makini zaidi na kuaminika kuliko ilivyotumika kuwasilisha kitabu cha Saybwayh na ukusanyaji wa mashairi ya washairi.”

“Vile vile yeye (r.a.) anasema: Hakika Qur’ani ilikuwa katika mkusanyo na muundo wa utungo wakati wa kipindi cha Mtume wa Allah (s.a.w.w.), katika hali hii hii inayoonakana leo. Uthibitsho ufuatazo umetolewa kwa ajili hiyo: (1) Qur’ani ilikuwa ikisomwa na kuhifadhiwa yote moyoni katika siku hizo, kiasi kwamba Mtume wa Allah (s.a.w.w) aliteua kikundi cha Masahaba kuihifadhi moyoni. (2) Ilikuwa ikiwasilishwa (mara kwa mara) na kusomwa mbele ya (Mtume (s.a.w.w.) (3)Kikundi cha Masahaba kama ‘Abdullah ibn Mus’ud na Ubayy ibn Ka’b na wengine wameisoma Qur’an kuanzia mwanzo mpaka mwisho mara nyingi mbele ya Mtume (s.a.w.w.). Mambo yote haya yanathibitisha wazi wazi kwamba (Qur’an) ilikuwa imekusanywa na kupangwa, na sio kwamba ilitawanyika na bila mpangilio.

46

“Vile vile amesema kwamba hao Mashi‘a na Hashawiyah ambao wamekwenda kinyume cha itikadi hii, upinzani wao hauna uzito wowote wa kufikiriwa, kwa sababu maoni haya yanatoka kwa baadhi ya wapokezi wa hadithi ambao wamesimulia baadhi ya hadithi dhaifu ambazo walifikiria kuwa ni sahihi, na hadithi hizo hazina nguvu ya kushinda ukweli ulio wazi, (yaani, ukweli kabisa unaojulikana wazi kwamba, Qur’an haikubadilishwa, hauwezi kupuuzwa kwa sababu ya hadithi dhaifu kama hizi).”54

Nimenukuu kwa urefu kidogo kutoka katika vitabu vya as-Saduq (r.a.) na at-Tabrasi (r.a.), yaani cha kwanza na cha mwisho vya wanachuoni wanne waliotajwa na mwandishi (huyu) asiyejulikana. Na nukuu ya mwisho ina baadhi ya hoja zilizotolewa na as-Sayyid Murtaza ‘Alamu’l-huda, Ulamaa wa pili aliyetajwa katika (kijitabu) “Ushi’a ni Nini?”

Sasa soma tena nini mwandishi huyu asyejulikana alichosema:-“Hata hivyo, kwa vile maelezo yao hayakujengeka katika misingi ya hoja, na yalikuwa kinyume na hadithi za dini ya Kishi’a zisizokatizwa,Wanachuoni wa Kishi‘a wa awamu ya pili walipuuza maelezo na utafiti woa.”

Unaweza ukaamua iwapo maandishi yao yalijengeka katika misngi ya hoja au hapana. Na je, anaweza kutueleza ni akina nani hao wanachuoni wa awamu ya pili ambao walipuuza utafiti wao? Mwandishi huyo aasiye na ujuzi hana habari na hajui daraja walizokuwa nazo, na walizonazo wanachuoni hawa katika jumuiya ya Shi‘a.

Umeona vipi hoja zenye nguvu walizozitoa na vipi walivyozitupilia mbali hadithi za Tahrif zilizowasilishwa na baadhi ya (wanachuoni) Mashi‘a na Masunni.

Na katika mwanga huu nawakaribisha wasomaji wajiunge nami ili tuombe laana ya Allah iwashukie waongo.55

Vile vile anadai kwamba:-54 Majma‘u ’l-bayan, chapa ya Beirut, J. 1, uk. 30-31.55 Qur’an, 3:61.

47

“Allama Bahrul Uloom Farangi Mahal (viyo hivyo) mapema alitoa Fatwa inayosema kwamba Shi‘a ni Waislamu, lakini baada ya kuiona Tafsir Majmah-al-Bayan ilikuja mbainikia kwamba Mashi‘a wanakubali maoni ya Tahrif katika Qur’an.

“Matokeo yake alitoa Fatwa kuhusu ukafiri wa Shi‘a na akaandika: Ambaye kwamba anakubali itikadi ya Tahrif katika Qur’an hivyo dhahiri ni kafir.”

Wasomaji wameona jinsi gani Tafsir Majma‘u ’l-bayan inavyokanusha wazo la Tahrif katika Qur’an. Habari zizoandikwa kuhusu Bahrul Uloom ni kitu kilichobuniwa tu na yeye mwenyewe. Hata hivyo tunakubaliana na yule mwanachuoni wa Ki-Sunni kwamba yoyote mwenye kuamini Tahrif ya Qur’an yuko nje ya dini ya Uislamu - yeyote yule awaye.

Vile vile mwandishi huyu asiyejulikana hajui kwamba, Tafsir Majma‘u ’l-bayan ilichaguliwa na wanachuoni wa al-Azhar na kuchapishwa chini ya usimamizi wao huko Kairo.

Kizuizi chake kikubwa ni kule kutokujua kwake - sio tu vyanzo vya Shi‘a bali hata na vitabu vyake mwenyewe vya hadithi na Tafsir. Vinginevyo hakuna Sunni ambaye amesoma vitabu vyake mwenyewe vya hadithi na Tafsir (yaani, vya wanachuoni wa Kisunni) atathubutu kuandika upuuzi kama huu.

Nina uhakika kwamba kamwe hakukiona kitabu cha Bahrul Uloom Farangi Mahal; sio tu amenukuu visivyo Fatwa ya Bahrul Uloom, bali pia hajui jina la kitabu chake hicho sawa sawa ambacho amekirejelea katika ukurasa wa 29. Ningeweza kurekebisha kosa lake (kama nilivyofanya hapo juu kuhusu majina ya waandishi wa Ki-Shi‘a na vitabu vyao). Lakini ninaliacha kama lilivyo na ninamtaka (nampa changamoto) alete kitabu chochote cha Bahrul Uloom kiitwacho Fatawah al-Rahmat, na kunukuu maneno hasa (halisi) ya kitabu hicho.

Naam hakika, ziko hadithi za Tahrif katika baadhi ya vitabu vya Ki-Shi‘a kama ilivyo katika vitabu vya Ki-Sunni. Lakini mwelekeo wa Ki-Shi‘a kwa hadithi kama hizo hutofautiana kabisa na mwelekeo wa Ki-Sunni. Kwanza ngoja niandike kitu kuhusu mwelekeo wetu.

48

MWELEKEO WA SHI‘A:

Kuna utungo wa mwanzo kabisa wa hadithi za Shi‘a ambao kwa pamoja unaitwa “Vitabu vinne vya mwanzo”- al-Kafi, Man la yahdurhu ’l-faqih, Tahdhibu ’l-ahkam na al-Istibsar. Ingawa vitabu hivi vinaheshimiwa sana, Shi‘a kamwe hawaji viita “Sihah” (yaani sahihi). Kwa hiyo, Mash‘a hazijazuiwa au kufungwa na hadithi yoyote iliyoandikwa humo kwa sababu tu imo katika moja ya vitabu hivyo vinne. Bali huzihusisha hadithi zote zizomo katika vitabu hivyo na kipimo (Mitihani) makini kama vile asnad (wapokezi) wake na dirayah, na kupima kama hadithi (hiyo) iliyotolewa inakubaliana na Qur’an (yaani isiyopingana na Aya yoyote ya Qur’an), hadithi zikubaliwazo za Ma’sumin (Mtume, Bibi Fatimah na Maimamu 12) na matukio yajulikanayo. Kama hadithi itapita vipimo hivi vigumu basi inakubaliwa. Kama sivyo inatafsiriwa vingine katika njia inayokubalika, ikishindwa inapuuzwa (na) (kutupwa) moja kwa moja.

Ni lazima itajwa hapa kwamba sehemu kubwa ya hadithi zinazohusu tahrif zina kasoro na ni dhahifu kama ambavyo nyororo (sanad) za wapokezi wake zinavyohusika. Hata hivyo, baadhi ya hadithi hizi zaweza kuchukuliwa kuonesha kwamba kulitokea tafsiri potofu katika baadhi ya aya, na kutoa maana isiyo sahihi. Kundi lingine ka hadithi linaweza kutafsiriwa kwa urahisi kwa kutaja maneno ya maelezo ya Makari (wasomaji wa Qur’an) yaliyoko kwenye pambizo.

Lakini bado kunabakia hadithi nyingi ambazo haziwezi kufafanuliwa katika njia yoyote ya hizi. Na wanachuoni wetu bila kusita wamezipuuza kwa sababu zinakwenda kinyume na Qur’an na Sunna, na ziko kinyume na ijma‘ ya umma, kwamba kamwe hakujakuwa na maongezo au upungufu ndani ya Qur’an.

Marhum as-Sayyid Al-Khoui (r.a.) ameandika juu ya kuhifadhi Qur’an kutokana na Tahrif katika kitabu chake Tafsir al-Bayan kutoka uk. 213-278 ambamo ndani yake amebainisha kila hadithi, za Sunni na Shi‘a kuhusu suala hili. Rejea fupi mbili kutoka kwa wanachuoni wa Shi‘a zizoandikwa humo ni kama hivi ifuatavyo:-

“Muhaqqiq al-Kalbasi alisema: Hadithi zote hizi zinazozungumzia

49

tahrif ziko kinyume na ijma‘ na hivyo si za kutegemewa (ispokuwa kwa idadi ndogo sana ya watu waliozembea).”

“Mufasir wa al-Wafiyah, Muhaqqiq al-Baghdadi, ameeleleza wazi wazi, kwa kunukuu kutoka Muhaqqaq al-Karaki (ambaye ameandika kijitabu kizima kuhusu suala hili) kwamba: ‘Hadithi zinazozungumzia tahrif ama lazima zitafsiriwe vingine au zipuuzwe.’ Hadithi yoyote ambayo inakinzana na Qur’an na hadithi zinazo kubalika na ijma‘, lazima zitupwe kama hazina nafasi ya kutafsiriwa vingine, au maelezo ya kuthibitisha.”56

Hadithi iliyoandikwa katika al-Kafi inanukuliwa hapa kutoa mfano wa vipi tunamaanisha tunapozungumza kutafsir vingine au maelezo ya kuthibitisha:-

“Abu Abdillah (a.s.) alisema:“Qur’an iliyoletwa na Jibril (a.s.) kwa Muhammad (s.a.w.w.) ni Aya Kumi na Saba Elfu.”57

Maelezo ya ash-Shaikh as-Sadiq (r.a.) katika kitabu chake Kitabu’l-I‘tiqadat, kuhusu kiasi cha Wahyi kwamba zilikuwa ni Hadith Qudsi, inaweza kuchukuliwa kama tafsir ya hadith hii.

Kama mtu hayuko tayari kuyakubali maelezo haya kwa sababu hadithi inazungumzia “Qur’an”, basi hana budi, bali kuitupa hadithi hii bila kusita, kwa sababu idadi hii ni kubwa, mara tatu kuliko idadi yenyewe hasa ya aya za Qur’an.

Mwandishi huyu asiyejulikana baada ya kunukuu hadithi hii ya al-Kafi, anaonyesha wasi wasi kwamba:-“Hii ina maana kwamba kwa (msimamo wa) Shi‘a, theluthi mbili za Qur’an hazipo katika mzunguuko (zimepotea).”

Hata kama tukiikubali hadithi hii katika maana yake ya nje, aya zilizopotea zitakuwa kidogo sana kulioko idadi iliyotajwa na Khalifa wa pili Umar ibn al-Khatab. Yeye alisema:-“Qur’an ina herufi milioni moja na ishirini na saba elfu (1,027,000); 56 As-Sayyid Al-Khoui, Tafsir al-Bayan, chapa ya Kuwait, 1399 H/1979 M. uk. 253.57 Al-Kulayni, Al-Kafi, 1388 H. J. 2, uk. 463.

50

mwenye kuzisoma pamoja kwa utulivu na kuzingatia, atapata kwa kila herufi mke mmoja kutoka kwa Mahural-ain” (wanawake wa Peponi).58

Lakini taarifa zilizoko ni kwamba kuna herufi mia mbili na sitini na saba elfu na hamsini na tatu (267,053) ndani ya Qur’an, kama inavyoonekana kwenye matoleo mengi ya Qur’an, ambapo imetolewa maelezo ya idadi ya herufi za alfabeti mwishoni. Hii ina maana kwamba kwa Sunni robo tatu (3/4) ya Qur’an imepotea. Tunamuomba mwandishi huyu asiyejulikana atueleze hizi herufi 759,947 zilizobakia zimekwenda wapi?

Huenda ni kwa sababu hii, mtoto wa khalifa wa pili Abdallah ibn Um-mar alikuwa akisema:- “Mmoja wenu anasema, ‘ninayo Qur’an yote,’ na nini anachojua ni ipi iliyo yote; Hakika sehemu kubwa ya Qur’an imepotea; bali hana budi aseme: ‘Nimepata kilichokuja kutoa mwanga kutokana nayo.”59

HADITHI ZA SUNNI:

Haiwezekani kutoa maelezo ya sura, Aya, Sentensi na semi zote ambazo hadithi za Sunni zinasema zilizopotea wakati Qur’an ilipokuwa inakusanywa. Mifano michache ya dhahiri ni kama hii ifuatayo:-

1. Sura ya 33 (al-Ahzab) inasemekana kuwa na Aya 200 au karibu ya 300 hivi, ambapo zote inasemekana zimepotea ispokuwa 73. Madai haya ya aya 200 anahusishwa nayo Ummul Mu’mineen ‘A’ishah:-“Imesimuliwa na Abu ‘Ubayd katika al-Faza’il na ibn Al-Anbari na ibn Marduwayh kutoka kwa ‘A’isha kwamba amesema: “Sura ya al-Ahzab ilikuwa ikisomwa wakati wa Mtume (s.a.w.w.) aya mia mbili, lakini wakati wa Uthman alipoandika Qur’an hakuweza kupata zaidi ya zilizopo sasa.”60

Lakini kuna Aya 73 katika Sura ya hii.

58 As-Suyuti, Al-Itqan, chapa ya Dehli. J. 1, uk. 93.59 As-Suyuti, Al-Itqan, J. 2, uk. 32.

Tafsir Ad-Durru ’l-manthur, J. 2, uk. 298.60 Al-Itqan, J. 2, uk. 32; Ad-Durru ’l-manthur, J. 5, uk. 170-180.

51

Hudhayfah alisema Aya 70 zimepotea kutoka kwenye Sura hii.61 Lakini Ubayy ibn Ka’b alisema kwamba Sura hii ilikuwa sawa na, au hata zaidi kuliko, Sura ya al-Baqarah.62 Vile vile tabi’i, Ikrimah amenukuliwa akisema hivyo hivyo.63

Sura ya al-Baqarah ina Aya 286. Ina maana kwamba, kwa mujibu wa Masahaba hawa aya 213 au hata zaidi zimepotea, pamoja na aya ya kurujumiwa (Kupigwa mawe).

2. Sura ya tisa at-Tawbah: Inadhaniwa kwamba 2/3 au 3/4 ya Sura hii imepotea. Taarifa hii inatoka kwa Hudhayfah al-Yamani:-“Hudhayfah (r.a.) alisema: “Ile ambayo mnaiita Surat at-Tawbah ni Sura ya adhabu; kwa jina la Allah haikumuacha mtu yoyote ila imemtweza; na nyinyi mnaisoma moja ya nne yake tu.”64

Sahaba huyo huyo anasema katika hadithi nyingine: “Hamuisomi (Surah at-Tawbah) hata thuluthi yake.” Yaani zaidi ya thuluthi mbili zimepotea.65

Imam Malik ibn Anas, Imam wa dhehebu la Sunni-Malik, aliulizwa ni kwa nini hakuna Bismillah..... katika Sura hii. Alisema: “Ilipotea pamoja na sehemu zake za mwanzo, kwa sababu imethibitishwa kwamba ilikuwa sawa na sura al-Baqarah kwa urefu.”66

Lakini kuna aya 127 tu katika Sura hii ndani ya Qur’an, ambapo sura Al- Baqarah ina Aya 286.

Nafikiri hakuna haja ya kutaja Sura za Sunni za al-Khall‘ na al-Hafd, na Sura nyingine iliyokuwa sawa na Sura al-Baqarah, ambapo vitabu vya Sunni vinasema zilipotea kabisa; mbili za mwanzo zimeandikwa na Ubayy ibn Ka’b katika Qur’an yake na Abu Musa al-Ash‘ari67 na ya tatu ilisahauliwa na Abu Musa Al-Ash‘ari.68

61 Ad-Durru ’l-manthur, J. 5, Uk .180, akinukuu kutoka al-Bukhari, At-Tarikh.62 Al-Itqan, J. 2, uk. 32;63 Ad-Durru ’l-manthur, J. 5, uk. 179.64 Ad-Durru ’l-manthur, J. 3, uk. 208; Al-Itqan, J. 2, uk. 34;65 Ad-Durru ’l-manthur, J. 3, uk. 208.66 Al-Itqan, J. 1, uk. 86;67 Al-Itqan, J. 1, uk. 86-87;68 Ibnu ’l-Athir, Jam’u ‘l-usul. Misri, 1370 H., J. 3, uk. 8.

52

Mamia ya hadithi za tahrif kubwa au ndogo zinasimuliwa katika vitabu vya Ki-Sunni na (kutoka kwa) watu wengine wakubwa na mashuhuri, kama Masahaba hawa wafuatao:- ‘Abdullah ibn ‘Abbas, ‘Abdullah ibn ‘Umar, ‘Abdullah ibn Mas’ud, ‘Abdur-Rahman ibn ‘Awf, Zayd ibn Arqam, Jabir ibn ‘Abdullah, Buraydah, Maslamah ibn Makhlad, Abu Waqid al-Laythi, Ummul-Mu’mineen Hafsah, Ummul-Mu’mineen Ummu Salimah, na shangazi wa Abu Amamah ibn Sahl, pamoja na nyongeza ya Tabi’i ‘Ikrimah.

Hadithi hizi zinapatikana katika: Sahih al-Bukhari, Sahih Muslim, Sunan Abi Dawood, Sahih Tirmidhi, Sunan Nasai, Sunan al-Bayhaqi, Musnad cha Imam Ahmad ibn Hanbal, Muwatta’ cha Imam Malik, Tarikh cha Imam al-Bukhari, Fathul Bari (Sharh cha Sahih Bukhari cha Ibn Hajar al-‘Asqalani), Tafsir Ad-Durru ’l-Manthur na Al-Itqan (vyote vya as-Suyuti) and Kanzu ’l-‘Ummal. Yeyote mwenye shauku ya kuziona hadithi hizi na atizame kitabu changu (cha urdu), Itmam-e-Hujjat, Faizabad (India), 1986.

Kwa ufupi vitabu vya hadithi vya Ki-Sunni vina hadithi nyingi za namna hiyo. Lakini kuna tofauti ya msingi baina ya Madhehebu hizi mbili kuhusu mtazamo na fikra juu ya hadithi kama hizi. Nimeandika mwanzo maoni ya Shi‘a kuhusu hadithi hizi. Sasa hebu tuone Sunni wana lipi la kusema:

MWELEKEO WA SUNNI:Mwelekeo wa Sunni kuhusu hadithi hizi umeshawishiwa na imani yao Kwamba hadithi zote zilizoko katika Sihah Sittah (vitabu sita sahihi hadithi), na hususan zile zinazopatikana katika Sahih Al-Bukhari na Sahih Muslim, zote ni sahihi.

Imam Nawawi (631-676 A.H) anaandika katika kitabu chake Sharh cha Sahih Muslim:-“Ukweli ni kwamba ummah kwa ridhaa umekubali (sahih hizi mbili Bukhari na Muslim) imetufanya tujue kwamba ni wajibu kutenda yaliyoandikwa katika vitabu hivi viwili, na kwa ujumla, hii imekubaliwa kwa pamoja. Watu wanahiari kutenda katika Khabar-ul-Wahid zinazopatikana katika vitabu vingine, mbali na hivi viwili kama Sanad za wapokezi ni sahihi, na (hata hivyo) italeta dhana tu

53

yenye nguvu. Na ndio hivyo hivyo kwa (hizo) Sahih mbili; lakini hivi viwili vinatofautiana na vitabu vingine, kwamba yote yaliyomo mwenye vitabu viwili (Bukhari na Muslim) ni sahihi, na hakuna haja ya kuzipima, bali ni wajibu kuzifuata bila masharti; lakini kwa hadithi zilizomo kwenye vitabu vingine hazitafuatwa mpaka uaminifu wao (wapokezi wake) umechunguzwa na kuonekana kuwa unatimiza masharti ya hadithi sahihi.”

Kukubali huku blangeti lisilo na masharti kwa hadithi zinazopatikana katika vitabu hivi kumewalazimisha Sunni kukubali nadharia ya (Naskhut-tilawah) ufutaji wa usomaji; yaani wanaamini kwamba usomaji wa baadhi wa aya ulifutwa (kuondolewa ndani ya Qur’an) ingawa sheria zilizomo katika baadhi ya aya hizo zinaendelea kutumika. Mifano miwili inayojulikana sana na aya zinazodhaniwa hivyo ni Aya ya kupigwa mawe na aya ya kunyonya (maziwa ya mama) mara kumi au mara tano, ambazo zinapatikana katika Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim na vitabu vingine.

Kwa kutaka kujua “aya ya kupiga mawe” tazama vitabu hivi:-Sahih al-Bukhari, J. 4, uk. 179, 265;Sahih Muslim, J. 3, uk. 1317;Musnad Ahmad Ibn Hanbal, Misri, J. 1, uk. 40;Sunan Ibn Majah, Egypt, J. 2, uk. 853;Muwatta’ Imam Malik, J. 2, uk. 623.

Kwa kutaka kujua “aya ya kunyonya” tazama vitabu hivi:-Sahih Muslim, J. 4, uk. 167; ad-Durru ’l-Manthur, J. 2, uk. 135.

Na hadithi ya Sahih Muslim inasema wazi wazi:“Ummul Mu’mineen Aisha anasema: ‘Kulikuwa na Aya miongoni mwa Aya za Qur’ani iliyoteremshwa inasema: ‘kunyonya mara kumi kunakojulikana hufanya mtu kuwa mahrim’ (ndugu wa kunyonya). Kisha ilinasakhiwa (ilifutwa) na kunyonya mara tano, na Mtume wa Allah (s.w.t.) alifariki na zikawa (bado) ni miongoni mwa aya za Qur’ani zinazosomwa.”69

Swali linakuja: Nani aliyekuwa na haki ya kufuta aya ya Qur’an baada 69 Sahih Muslim, J. 4, uk. 167; ad-Durru ’l-Manthur, J. 2, uk. 135.

54

ya Mtume kufariki?

Ndio maana as-Sayyid Abul Qasim Al-Khoui (r.a.) amesema:-“Na ni wazi kwamba nadharia ya “ufutaji wa usomaji” wa aya (Naskhut-tilawah) ni imani haswa ya kubadilishwa na kuondolewa kwa aya kutoka kwenye Qur’an.”70

Maelezo zaidi ya wazi ni hadithi aliyoisimulia na Ummul-Mu’mineen Aisha kwamba, karatasi lililokuwa na aya za kupigwa mawe kwa (mzinifu) na kunyonya kwa mtu mzima lilikuwa chini ya mto wa kitanda cha Mtume. Wakati alipokufa, na watu walikuwa wanashughulikia mazishi, mbuzi aliingia na akala lile karatasi. Na hivyo ikawa imepotea kabisa.71

Sasa huyu mwandishi asiyejulikana asili yake hana budi asome tena majina ya Masahaba hao, Matabi’in na Maimam ambao wamesimulia hadithi hizi; na majina ya hao Muhaddithin na Mufassirin ambao wameandika hadithi hizi kwenye vitabu vyao. Baada ya hapo itamkwe ile Fatwa ya ‘Allama Bahrul Uloom, ambayo ameinukuu katika ukurasa wa 25 wa kijitabu chake: “Yeyote ambaye kwamba anaunga mkono mwelekeo wa Tahrif katika Qur’ani, huyo dhahiri ni kafir.”

Hongera!!

70 As-Sayyid Al-Khoui, Tafsir al-Bayan, uk. 224.71 Imam Ahmad ibn Hanbal, al-Musnad, Misri, 1313 A.H. J. 6, uk. 269; Sunan Ibn

Majah, uk. 626; Ibn Qutaybah; Ta‘wilu Mukhtalafi ‘l-ahadith, Beirut, 1409/1989. uk. 372; ad-Durru ’l-Manthur, J. 2, uk. 135.

55

HADITHI

Mwandishi huyu asiyejulikana, anaandika chini ya kichwa cha habari: “kukataliwa kwa hadithi”:-“Shi‘a wana vitabu vyao vya hadithi; hata hivyo maneno ya Mtume (Sallallahu alayhi Wasallam) katika vitabu hivyo si zaidi ya asilimia tano; asilimia tisini na tano iliyobakia mna maneno na matendo ya Maimamu wao. Katika istilahi za Kishi‘a, “Hadithi” ni mazungumzo, matendo au khutuba ya Imam. Hivyo Mashi‘a wamevunja mawasiliano yote na Uislamu wa Mtume (Sallallahu alayhi Wasallam) ambaye wakati wa Hijja ya muago (Hijjat’l-widaah) alisema:“Ninawaachieni vitu viwili miongoni mwenu; kama mtavishikilia vizuri hamtapotea kamwe. Navyo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah zangu.”

Mna mambo mengi ya kushangaza katika nukuu hii fupi.

Hebu tuanze na ufafanuzi wa hadithi. Hadithi hata katika istilahi za Ki-Sunni haziishii kwenye “mazungumzo ya simulizi, matendo au ‘Taqrir’” ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) bali hujumuisha mazungumzo ya Masahaba wake na Tabi’in vile vile.

Hivyo hivyo katika istilahi za Ki-Shi‘a ina maana ya mazungumzo, matendo au Taqrir ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) binti yake Fatimah na Maimamu kumi na wawili (a.s.) (yaani Ma’sum 14) au simulizi yake.

Sasa ni juu ya msomaji kuamua kama maneno ya Masahaba na wafuasi wao (ambao ilikubaliwa kuwa sio Ma’sum) ni yenye kukubalika zaidi, au yale ya Bibi Fatimah na Maimamu 12 ambao ‘ismah yao inakubaliwa hata na viongozi wakubwa wa Usunni kama SShah Waliullah Dehlavi, Shah ‘Abdu ’l-‘Aziz Dehlavi na wengineo. Hii ni mbali na ukweli kwamba wanne katika kundi hili - Bibi Fatimah, Ali, Hassan na Husein (a.s.) walikuwa nao ni Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Mwandishi huyuyu asiyejulikana, ametoa ufafanuzi wa hadithi kwa maneno haya:“Katika istilahi za Kishi‘a, hadithi ina maana ya mazungumzo, matendo au khutba ya Imam.” Umeona kwamba sio Maimamu

56

tu, bali hata kabla yao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Bibi Fatimah ambao mazungumzo, matendo na Taqrir au simulizi yake ndio ambayo huitwa Hadithi. Chakushangaza sana ni tafsiri yake ya Taqrir kuwa ni khutuba, ambayo inaonyesha kutokujua kwake hata Madhehebu yake mwenyewe na istilahi zake, kwa sababu neno hili Taqrir kwa kawaida hutumiwa na Madhehebu zote, na lina maaha hii:“Kama mfuasi akifanya kitu mbele ya Mtume au Imam, na Mtume au Imam hamkatazi kufanya hivyo (pamoja nakuwa katika hali ya kuweza kumuongoza mfuasi huyo kama angetaka kufanya hivyo), ile idhini yakimya iliyodhihirika bila ya kunena itathibitisha usahihi wa kitendo cha mfuasi huyo.” Hii ‘idhini ya kimya’ huitwa ‘Taqrir’ neno ambalo mwandishi huyu asiye na ujuzi amelitafsiri kuwa ni ‘Khutuba.’

Anadai kwamba 95% ya hadithi za Shi‘a zinatoka kwa Maimamu. Kuna yoyote anayeweza kukubali madai ya mtu ambaye hajapata kuona hata kitabu chochote cha hadithi za Shi‘a? Ni mtu asiyeelewa ukweli kwamba, Maimamu wetu kamwe hawazungumzi kwa matamanio yao. Chochote walichokisema ni simulizi za hadithi zilizopokelewa kutoka kwa baba zao waliowatangulia, wasafi na wasio na dhambi. Kwa vile ukweli huu ulikuwa unajulikana kwa watu wote, kulikuwa hakuna haja kwa wao kurefusha hadithi zao kwa kutaja sanad za wapokezi.

Mtu mmoja ambaye alikuwa hana habari na ukweli huu alimuuliza Imamu Muhammad al-Baqir (a.s.) kuhusu hadithi “anazozitoa bila kutaja nyororo za wapokeaji.” Imamu (a.s.) akasema: “wakati ninaposimulia hadithi bila kutaja nyororo (sanad) za wapokezi, basi sanad yangu (kwa hadithi hiyo) ni baba yangu (Imam Zaynu ’l-‘Abedeen a.s.) kutoka kwa babu yangu (Imam al-Husayn a.s.) kutoka kwa baba yake (Imam ‘Ali a.s) kutoka kwa Mutukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka kwa from Jibra’il kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.).”72

Matamshi kama haya yametolewa na Imam Ja‘far as-Sadiq (a.s.) kuhusu hadithi zake.73

Salim ibn Hafsah anasema: “Wakati Abu Ja‘far Muhammad al-Baqir ibn Ali (Zainul-Abedeen) (a.s.) alipofariki, niliwaambia swahiba zangu: ‘Nisubirini, ili niende kwa Abu Abdillah Ja‘far (as-Sadiq) 72 al-Mufid, Kitabu ’l-Irshad, Tehran, 1377, uk. 250; Al-Majlisi, Biharu ’1-Anwar,

chapa mpya, J. 46, uk. 28873 al-Mufid, Kitabu ’l-Irshad, uk. 257; Al-Kafi, J.1, uk. 42.

57

ibn Muhammad (Al-Baqir) (a.s.) kumhani (kutoa rambi rambi).’ Nilikwenda nyumbani kwake na kutoa rambi rambi. Kisha nikasema: ‘Sisi ni wa Allah na Kwake tutarejea. Naapa kwa Allah, mtu kama huyu amefariki, alikuwa akitoa hadithi zake husema: ‘Mtume wa Allah (s.w.t.) amesema,’ alikuwa haulizwi wapokezi baina yake na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Hapana, naapa kwa Allah! hataonekana mfano wake tena!” (Kusikia hivi) Abu Abdillah (Imam Ja‘far as-Sadiq) (a.s.) alikaa kimya kidogo; kisha akasema: “Allah (s.w.t.) amesema: Hakika yule ambaye atatoa sadaka hata kama ni kipande cha tende, nitaifanya ikue kwa ajili yake kama mmoja wenu anavyomlea ndama wake wa farasi, mpaka ninaifanya kubwa kwa ajili yake kama mlima wa Uhud.” Kisha nikarudi kwa swahiba zangu na nikasema: ‘Kamwe sijaona kitu cha ajabu zaidi kama hiki. Tulikuwa tunafikiria kwamba maneno ya Imam Abu Ja‘far Muhammad al-Baqir (a.s.) kama haya: “Mtume wa Allah (s.w.t.) amesema” bila kutaja wapokezi baina yake kwamba yalikuwa kitu kikubwa sana, na sasa Abu Abdillah (Imam Ja‘far as-Sadiq a.s.) ameniambia mimi, “Allah (s.w.t.) amesema”, bila wapokezi baina yake.”74

Hivyo wakati Maimam wetu wanapo zungumza, sanad zao kuunganika mpaka kwa Allah (s.w.t.) kunajulikana na kueleweka na wasikilizaji wake; na hawakuwa na haja ya kutaja majina yale matakatifu mara kwa mara. Hii ndio maana mshairi mmoja amesema:“Kama unataka kujichagulia madhehebu ambayoitakukinga na moto Siku ya Kufufuliwa. Basi yaweke kando maoni ya fualani na fualani huyu na yule. Na wapende na wafuate watu wale ambao simulizi na hadithi zao (huenda kama hivi):“Ameisimulia Babu yetu kutoka kwa Jibril (a.s.) kutoka kwa Allah (s.w.t.) Muumba.”

Ni kwa kiungo hiki kitukufu kilichobarikiwa kwamba, kama itanenwa kwa sababu fualani na Maimamu wetu, huchukuliwa kama hazina ya thamani yenye manufaa ya kiroho.

Nyororo ya Dhahabu:Muhaddithina wengi wamesimulia kwamba Imamu wetu wa nane 74 al-Mufid, Al-Amali, uk. 90; Al-Majlisi, Biharu ’l-Anwar, chapa mpya, J. 47, uk. 27

na 337.

58

Abu’l-Hasan ‘Ali Riza (a.s.) alikuwa anapita kutoka Nishapur kuelekea Marv, Muhaddithina mashuhuri wawili, Abu Zar‘ah ar-Razi na Muhammad ibn Aslam at-Tusi walimpokea wakiwa pamoja na idadi kubwa ya Wanachuoni na wanafunzi wa fiqh, hadith na dirayah. Muhaddithina hawa wawili wakasema:- “Ewe Sayyid Mtukufu, mtoto wa Masayyid ambao walikuwa Maimamu, tunakuomba kwa haqq ya baba zako watoharifu waliotangulia na babu watukufu, utuonyeshe uso wako uliobarikiwa na utusimulie hadithi kupitia kwa baba zako, kutoka kwa babu yako Muhammad (s.a.w.w.) ambayo tutakukumbuka kwayo.” Imam alisimamisha kipando chake na akaamuru watumishi wake wapandishe pazia juu ya howdah yake; hivyo watu wakafurahi kuona sura yake iliyobarikiwa; alikuwa na kamba ya meno mawili iliyofika mabegani mwake. Watu wote wa daraja mbali mbali walisimama pale na kumuangalia, wengine walikuwa wakilia, wengine machozi yanawatoka, wengine waliweka mashavu yao kwenye ardhi na baadhi wakibusu kwato za nyumbu wake. Kisha wanachuoni na wanasheria waliowaomba watu wanyamaze, wakisema: “Sikia na sikilizeni na tulieni kimya ili mpate kusikia mambo yanayo kunufaisheni, na msitusumbue na kulia kwenu kwingi na kutokwa na machozi.” Baada ya hapo Imam (‘Ali) Ar-Riza alisema:-“Alinisimulia mimi baba yangu Musa al-Kadhim kutoka kwa baba yake Ja‘far as-Sadiq, kutoka kwa baba yake Ali Zainu’l-Abedeen, kutoka kwa baba yake Al-Husain Shahid wa Karbala, kutoka kwa baba yake Ali ibn Talib kwamba amesema: ‘Amenisimulia kipenzi changu na furaha ya macho yangu, Mtukufu Mtume wa Allah (s.w.t.) kutoka kwa Jibril kwamba amesema: ‘Nimesikia Allah (s.w.t.) akisema: Kalimah ya “Lailaha Illallah,” ni ngome yangu na mwenye kuitamka huingia kwenye ngome Yangu, na mwenyekuingia ngome Yangu anakuwa salama kutokana na adhabu Yangu’.” Kisha pazia lilishushwa juu ya howdah na aliendelea kidogo, halafu akasema: “(Inategemea) kwa masharit yake, na mimi ni katika shariti zake.”

Hadithi hii iliandikwa siku hiyo mahala hapo na waandishi zaidi ya ishirirni elfu.75 ni moja ya hadithi zinazokubaliwa kwa pamoja na Masunni na Mashi‘a, na inasimulia na wanachoni wa madhehebu

75 Ash-Shaykh As-Saduq, ‘Uyunu Akhbar ‘r-Rida, Beirut, 1404/1984. J. 2, uk. 143-145. Hashim Ma’ruf al-Hasani, Siratu ’l-Aimmati ’l-ithna ‘ashar, Beirut, 1406/ 1986, J. 2, uk. 386-7.

59

zote. Muhaddith mashuhuri wa Ki-Sunni Abu Nu‘aym al-Isfihani ameisimulia katika Kitabu chake kinachojulikana sana Hilyatu ’l-awliya’; na halafu akaandika: “Hadithi hii imethibitishwa na (ni) mashuhuri, pamoja na sanad hii, kwa riwayah (simulizi) za watu watoharifu kutoka kwa baba zao wasafi.” Kisha akaongeza: “Baadhi ya watangulizi wetu miongoni mwa Muhaddithina walikuwa wakisema baada ya kutaja sanad ya wasimuliaji hawa: ‘Kama asnad (nyororo ya wapokeaji) hii angesomewa mwendawazimu basi atapona’.” Ibn Hajar al-Haythami al-Makki alisema kwamba imani hii imeelezwa na Imam Ahmad ibn Hanbal.76 Kwa kawaida, asnad hii inajulikana kwa Muhaddithina (wataalam wa hadithi) kama, silsilatu ’dh-dhahab (nyororo ya dhahabu).

Bila shaka sasa mwandishi huyu asiyejulikana, huenda akaelewa ni kwa nini haikuwa lazima kwa Maimamu wetu kutaja katika maneno mengi sanad zao mpaka kwa Mtume (s.a.w.w.), kwa vile ilikuwa inaeleweka kwa kila mtu kwamba chochote walichosema kimechukuliwa kutoka kwa Mtukufu babu yao Mtume wa Allah (s.a.w.w).

Nitakuwa sijatoka nje maudhui, nikitaja kwamba hadithi yenye maana kama hii imesimuliwa kwa “Silsilatu ’dh-dhahab” ndefu (Nyororo ndefu ya dhahabu) kunzia na Imamu wetu wa kumi na mbili (a.s.), na si mwingine bali ni Shah Waliullah Muhaddith Dehlavi, ambaye anaandika katika kitabu chake, “Al Fazl al-Mubeen fi al-Musalsalat min hadith al-Nabi al-Amin”:-“Nasema: Ibn Uqlah amenipa ijazah (ruhusa) ya kusimulia yale yote yaliyokuwa na ruhusa ya kusimulia. Na nimeona katika al-Musalsalat yake, Musalsal hadithi, ambamo ndani yake kila wasimuliaji wake wanazo sifa za kuwa na ubora wa kipekee. Yeye (Ibn Uqlah r.a.) amesema: ‘Kanijulisha mimi, mwenye cheo kikuu kisicho kifani wa wakati huu ash-shaykh Hasan ibn ‘Ali al-‘Ujaymi, kutoka kwa Hafidh wa wakati wake Jamaluddin al-Babili, kutoka kwa mtu mwenye kutegemewa wa wakati wake Muhammad al-Hijazi al-Wa‘iz, kutoka kwa Sufi wa wakati wake ash-Shakh ‘Abdul Wahbab ash-Sha’rawi, kutoka kwa Mujtahid wa wakati wake Jalaluddin as-Suyuti, kutoka kwa Hafidh wa wakati wake Abu Nu’aym Rizwan al-‘Uqba, kutoka wa Qari (msomaji) wa wakati wake ash-Shams Muhammad ibn al-Juzwi, kutoka kwa Imam Jalaluddin Muhammad ibn Muhammad al-Jamal 76 as-Sawa‘iqu ’l-Muhriqah.

60

Zahid wa wakati wake, kutoka kwa Imam Muhammad ibn Mas’ud Muhaddith wa Fars katika wakati wake, kutoka kwa Shaykh wetu Isma‘il ibn Muzaffar ash-Shirazi mwanachuoni wa wakati wake, kutoka kwa ‘Abdus Salaam ibn Abi’r-Rabi‘ Hanafi Muhaddith wa wakati wake, kutoka kwa Abu Bakr ‘Abdullah ibn Muhammad ibn Shapur al-Qalanasi Shaykh wa wakati wake, kutoka kwa ‘Abdu ’l-‘Aziz ibn Muhammad al-Adami Imamu wa wakati wake, kutoka kwa Sulayman ibn Ibrahim ibn Muhammad ibn Sulayman mtu aliye na kipawa zaidi kuliko kawaida wa wakati wake, kutoka kwa Ahmed ibn Muhammad ibn Hashim al-Baladhuri Hafidh wa wakati wake, ambaye alisema kwamba: “Ametuhadithia sisi Muhammad (Al-Mahdi) ibn al-Hasan (Al-‘Askari) ibn ‘Ali (al-Hadi), Imamu aliyefichwa wa wakati wake ambaye alisema: (Baba yangu) al-Hasan (Al-‘Askari) ibn ‘Ali (Al-Hadi), kutoka kwa baba yake (Imam ‘Ali Al-Hadi) kutoka kwa babu yake (Imam Muhammad At-Taqi) kutoka kwa babu yake mkubwa ‘Ali ibn Musa ar-Riza, kutoka kwa baba yake Musa Al-Kazim ambaye alisema: ‘Ametusimulia sisi baba yangu (Imam) Ja‘far as-Sadiq, (ambaye amesema) ametusimulia sisi baba yangu (Imam) Muhammad al-Baqir, (ambaye amesema) ametusimulia sisi baba yangu ‘Ali ibn al-Husayn Zaynu ’l-‘Abedeen as-Sajjad, (ambaye amesema) ametusimulia sisi baba yangu al-Husayn Bwana wa Mashahid, (ambaye amesema) ametusimulia sisi baba yangu father ‘Ali ibn Abi Talib Bwana wa Mawalii, ambaye amesema: ‘Ametupa habari sisi Bwana wa Mitume Muhammad ibn Abdullah (s.a.w.w.) ambaye amesema: ‘Amenipa habari mimi Jibril Bwana wa Malaika, ambaye amesema kwamba, Allah (s.w.t.) amesema: “Hakika Mimi ni Allah hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Mimi; yoyote yule anayeikubali Tawheed (Umoja) Yangu ataingia kwenye ngome Yangu atakuwa salama kutokana na adhabu Yangu.”77

Kufikia hapa ni lazima kuelekeza mawazo ya wasomaji kwenye ukweli ufuatao:-Kwanza: Shah Wahyullah Dehlavi anasimulia hadithi kutoka kwa Imam wa 12 wa Shi‘a Ithna-‘ashariya ambaye hadithi iliyosimuliwa inamuelezea kama “Imam aliyefichwa wa wakati wake.” Vipi anasimulia kwa ijazah hadithi hiyo, kama haamini kuwepo kwa Imam huyo, ambaye amamtolea hadithi kupitia kwa babu zake maarufu waliotangulia mpaka kwa Mutukufu Mtume (s.a.w.w)?77 Shah Waliullah, Al Fazl al-Mubeen, kama ilivyonukuliwa katika Istiqsa‘u ’l-ifham.

61

Pili: Kama ilivyonukuliwa mapema, Mirza Hasan Ali katika swali lake na Shah ‘Abdu ’1-‘Aziz Dehlavi katika majibu yake ya kina, wametumia maneno, شر عل�یہم السلام نا ع� ئمہ ا �ش� نرات ا� Watukufu Maimamu Kumi na Mbili) ح�Amani iwe juu yao). Ina maana kwamba wao vile vile wanaamini kuwepo kwa Imamu wetu wa kumi na mbili, na wote wameonyesha unyenyekevu mkubwa na heshima kwa Maimamu hawa; kiasi kwamba wametumia kwa ajili yao neno “Amani iwe juu yao.” (Alayhima Salaam).

Tatu: Maulana Ali Akbar Maududi, kama alivyo Shah Waliullah, Shah ‘Abdu ’1-‘Aziz na Shaykh Muhyiddin ibn Al-‘Arabi, Shaykh ‘Abdul Wahhab Sha’rani na wengine wengi, waliamini kwamba Imamu wetu wa kumi na mbili (ambaye ni mtoto wa Imamu wa kumi na moja (a.s) na aliyezaliwa 255 A.H.) ni Qutb wa wakati wake, na rehema zote za Allah huwafikia viumbe kupitia kwake; na kwamba yeye, kama babu zake waliomtangulia mpaka kwa ‘Ali (a.s) ni Ma’sum, asietenda dhambi na asieokosea; na fadhila hii imetengwa kwa Mtukufu Mtume, Fatimah bint yake na kwa watu hawa kumi na mbili tu wa Umma huu.

Pamoja nakuwa na sifa hizo hapo juu, kamwe hakuna Shi‘a aliyesema, kuandika au hata kufikiria kuwa ‘Ali (a.s.) au watoto wake walikuwa na fadhila kubwa zaidi kuliko Mtume wa Allah (s.w.t.) kama mwandishi asiyejulikana asili yake anavyo washutumu Mashi‘a kuamini (hivyo) (tazama kijitabu chake uk. 22). Mwandishi huyu haelewi kwamba, mbele ya macho ya Mashi‘a, ubora na sifa za Maimamu (a.s.) msingi wake unatokana na ubora na sifa za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Maneno kama haya yasiyo na maana yoyote, hayastahili kujibiwa. Bali budi tuseme “Laana ya Allah iwe juu ya waongo.”

Kabla ya kufunga nukta hii ni lazima tutaje kwamba hata kama Maimamu wetu wasingeweka wazi, kwamba chochote walichosema kilikuwa hasa usemi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) uliokuja kwao kupitia baba zao watukufu waliowatangulia, tulikuwa tunalazimka kuyakubali maneno yao na kufuata uongozi wao. Kwa nini? Kwa sababu ya hadithi mutawatir ya “Vizito Viwili vyenye thamani” ambayo inakubaliwa na wote, Sunni na Shi‘a, kama tulivyotaja mwanzoni kwa ufupi.

62

Si jambo geni kuona maadui zetu wako tayari kukubali na kufuata maneno ya maelfu ya watu wasio Ma’sumin - sio Masahaba tu, bali hata wafuasi wao kama ‘Ikrimah, Mujahid, al-Hasan al-Basri na wengineo;bali hukataa kukubali na kufuata maneno ya Maimamu Ma’sumin wa Ahlul-Bayt ambao kwa uwazi kabisa Mtume (s.a.w.w.) aliwalinganisha kwa cheo kama sawa sawa na Qur’an.

Ni kwa ajili ya watu wa namna hii kiakili, kwamba Imam Ja‘far as-Sadiq (a.s.) alisema mbele ya baadhi ya watu wa kutoka Kufa: “Ajabu iliyoje watu wansema wamepata elimu yote kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) na wanatenda kwa mujibu wake na wameongozwa (nayo), na wakati huo huo wanafikiri sisi, watu wa nyumba yake hatukupata elimu yoyote kutoka kwake, wala kuongozwa sawa sawa katika njia iliyonyooka, ambapo sisi ni watu wake na kizazi chake!! Ilikuwa ni katika nyumba yetu ufunuo (Qur’ana) uliletwa kwake, na kutokana na nafsi zetu elimu iligawanywa kwa watu. Unafikiri kwamba wao walipata elimu na waliongozwa wakati sisi tukabakia wajinga na tukapotea? Hakika hiyo haliwezekani.”78

78 Biharu ’l-Anwar, J. 26, uk. 158.

63

BADA’

Mwandishi huyu asiyejulikana anaandika kama hoja yake ya pili ya ukafiri wa Mashi’a anaandika hivi:-“Kwa mujibu wa itikadi ya Shi’a, Allah anapasika na Bada. Yaani kusema elimu ya Allah hubadilika mara kwa mara kwa sababu Allah hajui kikamilifu chanzo cha mambo na matokeo yake.”

Maoni: (Huu) tena ni udhihirisho wa mwandishi huyu wa kutokujua kwake. Hebu kwanza niweke wazi nini maana ya Bada’:- Mtu yeyote mwenye akili timamu anajua kwamba elimu ya Allah kamwe haiwezi kuwa na makosa. Katika maneno mengine, ni kwamba hakuwezi kuwa na mabadiliko katika elimu ya Allah. Kinyume chake ni elimu waliyopewa Malaika na Mitume kutoka kwa Allah. Elimu yao japo ni kamili zaidi na sahihi kuliko viumbe wote, bado sio kamili ukilinganisha na elimu ya Allah. Kwa rehema za Allah daima huwajaza tena na tena kwa usahihi na ukamilifu wa elimu zao.

Vile vile tunajua kwamba Allah mara kwa mara huwaweka waja wake kwenye mitihani na majaribu. Vipo visa vingi katika Qur’an, ambavyo vinaeleza kwamba wakati mwingine Allah katika rehema na hekima Zake, huonyesha sehemu tu ya mpango wake wa baadae kwa Malaika na Mitume wanaohusika. Wanajulisha juu ya mpango wake mpaka hatua fulani tu, na elimu ya hatua ya baadae haionyeshi kwao kabla.

Kabla ya kuendelea mbele, hebu ngoja nitoe hapa mifano miwili kutoka kwenye Qur’an Tukufu:

Dhabihu ya Nabii Isma‘il:Nabii Ibrahim alionyeshwa kwenye ndoto kuwa alikuwa anamtoa dhabihu mtoto wake wa pekee kwa mapenzi ya Allah. Na ilivyokuwa ni ndoto, lazima alionyeshwa jinsi alivyokuwa anamuuwa Isma‘il. Lazima alijiona yeye mwenyewe akiifunga mikono na miguu ya mtoto wake, kujifunga yeye mwenyewe kitambaa cha macho kisha akaweka kisu juu ya koo la mtoto na kuanza kuchinja. Kwa hali hiyo hakuweza kuona ni nani au nini hasa kilichokuwa kinachinjwa kwa vile macho yake yalikuwa yamefunikwa. Kwa kuona ndoto hiyo aliamini kwamba anatakiwa amchinje mwanae Ismail katika hali hiyo (aliyoiona kwenye

64

ndoto). Hivyo aliufanya mgumu moyo wake ili amtoe dhabihu mtoto wake wa pekee.

Mtoto aliisikia (hii ndoto) na alijitayrisha kutolewa dhabihu kwa unyenyekevu kwa amri ya Allah. Baba na mtoto wote walikuwa tayari kutoa muhanga kila kitu kwa jina la Allah. Nabii Ibrahim alifanya kama alivyoota mwenyewe anafanya: alifunga mikono na miguu ya mtoto na kumlaza katika mwelekeo unaotakiwa, na mwenyewe akajifunga kitambaa cha macho, akaweka kisu na alikata koo. Baada ya kuondoa kitambaa kwenye macho yake, alimuona Isma‘il anatabasamu na pembeni yuko Kondoo amechinjwa badala yake.

Nabii Ibrahim alidhani ameshindwa mtihani aliopewa. Lakini alifanya kwa usahihi kabisa yale aliyoona yeye mwenyewe akifanya kwenye ndoto. Hakika Allah hakumjulisha matokeo ya hatua ya mwisho. Kama Ibrahim angejua kwamba Isma‘il ataokolewa au Isma‘il angejua kwamba ataokolewa, basi kusingekuwa na maana yoyote ya kuonyesha (waliofanyiwa). Kusingekuwa na hali yoyote ya kuonyesha kukubali kwao kutoa dhabihu chochote kwa jina la Allah. Hivyo, Allah alimuonyesha Ibrahim katika ndoto yake matukio kwa hatua fualani tu, lakini alimuacha bila kujua (kitakachotokea katika) hatua ya mwisho. Na kwa vile hawakujua matokeo, Ibrahim na Isma‘il walikuwa tayari kuonyesha kukubali kwao jinsi walivyotii amri ya Allah, hata kama ikiwa ni katika kutoa muhanga maisha yao na maisha ya wapenzi wao kwa jina la Allah.

Kama wangejua matokeo tokea mwanzo, basi mtihani huu usingekuwa na maana.

Alivyopewa Tawrat Nabii Musa:Mfano mwingine unahusu Nabii Musa na ufunuo wa Tawrat. Nabii Musa alipewa amri kwenda Mlima Sinai, afunge kule siku thelathini kwa matayarisho ya kupokea mbao za Tawrat. Siku ya thelathini alipiga mswaki meno yake na akaenda mlima wa Sinai. Kule aliulizwa na Allah ni kwanini alipiga mswaki meno yake. Alieleza kwa vile alikuwa akija sehemu takatifu, aliona ni bora ajitengeneze kuwa nadhifu na msafi. Allah akamuambia kwamba harufu ya mdomo wa mtu aliyefunga ilikuwa ni nzuri mbele ya Allah kama harufu ya misk

65

na ambari. Na kisha aliambiwa kurudi kwenye sehemu yake aliyokuwa anakaa na afunge siku kumi zaidi, kisha aje Mlima wa Sinai bila ya kupiga mswaki meno yake. Hivyo ilikuwa ni siku ya arubaini ndipo alipopewa mbao za Tawrat.

Allah alijua tangu mwanzo kuwa Musa atakuja baada ya kupiga meno yake mswaki, na atatakiwa kufunga siku kumi zaidi. Lakini hakuna aliyeambiwa habari hizi, si Musa wala Waisraili. Wala Musa hakuambiwa kabla kwamba asipige mswaki meno yake katika siku ile ya thelathini.

Wakati Allah anapozungumzia juu ya elimu yake, Anaeleza muda wote wa usiku arubaini kwa pamoja:“Na (kumbukeni) tulifanya ahadi na Musa siku arubaini. Kisha nyinyi (Banii Israel) mkafanya (sanamu ya) ndama (kuwa Mungu wenu) baada ya kuondoka (Musa) na hivyo mkawa madhalimu.”79

Na ambapo anapozungumzia juu ya elimu ya Musa, Anataja siku thelathini na siku kumi kwa mbali mbali.“Na tulifanya ahadi na Musa kwa siku thelathini na tukazikamilisha kwa (siku) kumi (zaidi), hivyo ukakamilika muhula wa Mola wake (wa) siku arubaini.”80

Sababu zilizoacha isitolewe taarifa mapema ziko wazi kutokana na tabia ya Banii Israel ambao kwa sababu ya kuchelewa kwake siku kumi, waliacha kumuabudu mwenyezi Mungu mmoja wa kweli na wakaanza kuabudu sanamu ya ndama. Kisa hiki kinaelezewa kwa uzuri zaidi katika Aya ya Qur’an ifuatayo:-“Allah akasema (kumuambia Musa): ‘Tumewatia mtihani watu wako baada yako; na Samiri amewapoteza’. Hivyo Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu (na) masikitiko. Aksema: ‘Enyi watu wangu! Je, Mola wenu hakukuahidini ahadi nzuri? Je, umekuwa mrefu kwenu (muda wa) ahadi hiyo au mlitaka ikushukieni ghadhabu kutoka kwa Mola wenu, hivyo mkavunja ahadi na mimi?’ Wakasema: ‘Sisi hatukuvunja ahadi yako kwa khiyari yetu...’ Na yeye (Samiri) akawatolea ndama, kiwili wili tu kinachotoa sauti (kinapopigwa na upepo) Na wakasema: ‘Huyu ndiye Mungu wenu na Mungu wa Musa. 79 Qur’an, 2:51.80 Qur’an, 7:142.

66

Lakini (Musa) amesahau.’”81

Hebu fikiria Jumuiya yote ya maelfu ya Masahaba wa Mtume mkubwa (Musa (a.s.)), mbele ya mshika makamu na mrithi wake Harun, kuacha njia ya kweli ya dini na kuanza kuabudu sanamu, kwa sababu tu, Musa alichelewa kwa siku chache, mtihani huu wa imani usingeweza kufanyika kama Allah (s.w.t.) angemueleza Musa kuwa alipaswa kukaa siku arubaini; au kama angeelezwa kabla kuwa asipige mswaki meno yake siku thelathini.

Hii ndio maana ya Bada’. Sasa ni wapi inasemwa kuwa elimu ya Allah (s.w.t.) hubadilika (eti) kwa sababu Allah (s.w.t.) hajui kwa ukamilifu sababu (ya mammbo) na mwisho wa matokeo yake?

Jina la Bada’ na maana yake, vyote vinatokana katika Qur’an. Allah (s.w.t.) anasema: “...Na yaliwadhihirikia kwao kutoka kwa Allah ambayo hawakuwa wakiyafikiria.”82

Hii ndio maana ya Bada’ na neno hili hutumika wakati Allah (s.w.t.) anapofanya kitu kitokee kwa viumbe ambacho hawakukitazamia.

Mabadiliko hutokea katika elimu ya kiumbe, sio kwa ile ya Allah (s.w.t.).

Mwandishi amenukuu hadithi kutoka al-Kafi, kutoka kwa Imamu ‘Ali ar-Ridha (a.s.) kwamba:-“Allah hakumpeleka Mtume yoyote yule, ile kwamba atangaze kuwa pombe ni haramu, na kwamba ni lazima aelewe kwamba Allah anapasika na Bada’ (Makususdio ni kwamba kama hali mpya itatokea itamfanya Allah kubadilisha makusudio yake)”.

Hadithi hii katika al-Kafi inasema hivi tu: “Allah (s.w.t.) kamwe hakumpeleka Mtume yoyote yule, bali na makatazo ya vileo (pombe) na uthibitisho kwa Allah wa Bada’”83

Mwandishi huyu asiyejulikana ametoa maana isiyo kabisa ya bada’ 81 Qur’an, 20:85-88.82 Qur’an, 39:47.83 al-Kulayni, Al-Kafi, Al-Makatabah Al-Islamiyah, Tehran, 1388, J. I, uk. 115.

67

katika mabano na kaiwekea alama nukuu hiyo ili kuwachanganya wasomaji, ambao wanaweza wakafikiria kuwa, maana iliyotajwa ni sehemu ya hadithi yenyewe!

Ni kwa watu kama yeye ambao Allah anasema katika Qur’an: “Hakika miongoni mwao kuna kundi linalopinda kitabu kwa ndimi zao ili mpate kuyaona kuwa ni sehemu ya kitabu, ambapo si sehemu ya kitabu..... na wanasema uongo dhidi ya Allah hali ya kuwa wanajua.”84

Kama huyu mwandishi asiyejulikana kweli ameiona al-Kafi, angelisoma hadithi zifuatazo ambazo zimeandikwa kabla ya hadithi aliyoinukuu: “Abu ‘Abdillah (a.s.) alisema: ‘Hakuna Bada’ inayotokea kwa Allah kwakitu chochote, bali ni kwamba hicho kilikuwa katika elimu yake kabla ya kutokea.”

“Abu ‘Abdillah (a.s.) alisema: “Hakika Bada’ haitokei kwa Allah kwa sabau ya ujinga.”

“Mansur ibn Hazim anasema: “Nilimuuliza Abu ‘Abdillah (a.s.): ‘Inaweza ikatokea kitu leo ambacho Allah (s.w.t.) hakikuwa katika elimu yake jana?’ (yaani yawezekana Awe hajui kuwa kutatokea kitu kama hicho)? Alisema: ‘Hapana. Allah (s.w.t.) Amfedheheshe yeyote mwenye kusema hivyo.’ Nilisema: ‘Hebu niambie, hivi si kwamba vile ambavyo vimekwisha tokea na ambavyo vitatokea mpaka siku ya kufufuliwa viumbe, vyote viko katika elimu ya Allah (s.w.t.)?’ Alisema: ‘Hakika, hata kabla ya kuumbwa kwa viumbe.’”85

Kwa kawaida hii ni imani ya Masunni waliowengi, ingawa hawaiti Bada’. Ina maana kwamba wao pia wanaikubali maana hii, ingawa wanatofautiana nasi katika jina. Kwa mfano tizama kutoka rejea zifuatazo kutoka Mufassirina watatu wa Ki-Sunni.1. Imam Fakhruddin ar-Razi anaandika chini ya Ayah: “Allah hufuta

atakayo na kuthibitisha (ayatakayo). Na asili ya kitabu iko kwake.”86

“Kuna misemo miwili kuhusu aya hii: Kwanza: Ile ambayo ni ya 84 Qur’an, 3:78.85 Al-Kafi, uk. 115.86 Qur’an, 13:39.

68

kijumla (iliyozunguuka) mambo yote, kama uwazi wa maneno unavyohitaji. Wanasema kwamba Allah hufuta riziki na kuiongeza; na hivyo hivyo ni katika suala la kifo na sa’adah (furaha) na shaqawah (misiba) na imani na kufr. Hii pia ni imani ya Sahaba wa Mtume ‘Amr ibn Mas’ud; na (Sahaba) Jabir ameisimulia hadithi hii kutoka kwa Mtukufu (s.a.w.w.).

Pili: Kwamba imewekwa maalumu kwa baadhi ya vitu, na vipo vipengele vingi kwayo: (1) Kufuta na kuandika kunahusu katika uondoaji (kufuta) wa amri iliyotangulia na kuleta amri nyingine mahali pake... (8) Inahusu riziki, na balaa na majanga, kwamba Allah anaandika haya katika kitabu na kisha huyaondoa kwa maombi na sadaqah (sadaka) na jambo hili lina kusihi kwa mtu kujiambatanisha bila hesabu kwa Allah (s.w.t.)... (10) Hufuta Anachokitaka katika amri Zake bila kumjulisha yeyote dhamira hiyo, kwa sababu anayo Mamlaka kamili kutoa amri kama Atakavyo, na anao uwezo kamili wa kuumba na kuumbua. Kumpa uhai na kifo, kufanya utajiri au umasikini, kiasi kwamba hakuna mhata mmoja katika viumbe wake ambaye ansifika na ghayb yake.”87

2. Allama Az-Zamakhshari anaandika chini ya Aya, “Na hakuna ambaye umri wake umerefushwa basi umri wake (huo) wala chochote hakikupunguzwa kwa maisha yake, bali yote yako kwenye kitabu. Hakika haya ni rahisi kwa Allah.”88

“Ina maana hatuongezi au kupunguza maisha ya mtu. Bali imeandikwa katika kitabu. Yaani imeandikwa kwenye (Lawh) kwamba: ‘Kama mtu huyo atafanya hajj (kwenda hija) au kashiriki katika jihad, basi umri wake utakuwa miaka 40; na kama atafanya vyote (Hija na jihadi), basi umri wake utakuwa miaka (60). Hivyo kama atakusanya vyote viwili (Hija na Jihadi) na akafikia umri wa miaka 60, basi umri wake utakuwa umerefushwa, na kama atafanya kimoja (yaani Hija au Jihad) na hakufikisha zaidi ya miaka 40, basi ina maana kwamba umri wake ulifupishwa kutoka kiwango cha mwisho cha miaka 60. Na ni hakika hii ambayo Mtume wa Allah alitamka katika usemi wake: “Hakika Sadaka na tabia njema kwa jamaa wa karibu (ndugu) hufanya nyumba kuwa na watu wengi na kuongezeka 87 Imam Ar-Razi, Tafsir Mafatihu ’l ghayb.88 Qur’an, 35:11.

69

maisha.”89

3. Mufassir al-Kadhi al-Baydawi anaandika hivi chini ya Aya hiyo hiyo:-

“Inasemekana kwamba kuongezeka na kupungua kwa umri wa mtu hutokea kwa sababu mbali mbali ambazo zimeandikwa katika Lawh. Kwa mfano, inaweza kuandikwa ndani yake (katika Lawh) kwamba, kama Amr akifanya hija, basi umri wake utakuwa miaka 60; vinginevyo utaishia katika miaka 40.”90

Mwandishi huyu asiyejulikana (inavyoelekea) hajui dini yake, wala maandishi ya ma-Ulamaa wake. Achilia mbali maandishi, hawezi hata kuyataja vizuri majina ya vitabu vya wanachuoni wa Ki-Sunni, na amejichukulia mwenyewe jukumu la kuandika juu ya Shi‘a!

Kama kweli huyu Mwandishi asiyejulikana anatamani kuona wenzake wa dini (Ahlul hadith al-Hashawiyyah) wanavyoamini kuhusu elimu na maamuzi ya Allah, hana budi kusoma taarifa ya Abul Fath Muhammad ibn ‘Abdul-Karim ash-Shahristani (467-548 A.H.) ilimenukuliwa katika uk. 26-27 wa kitabu hiki:-“Na kundi la As-habul-hadith, al-Hashawiyah wameonyesha wazi imani yao ya Tashbih (Allah kufanana na viumbe wake)..... kiasi ambacho walifikia kusema kwamba wakati mmoja Allah macho yake yalimuuma, hivyo Malaika wakaenda kumuangalia; na kwamba alilia wakati wa mafuriko ya Nuhu, mpaka macho yakawa mekundu;” na kwamba Arshi inatoa mlio wa kuomboleza chini Yake (kwa sababu ya uzito Wake) kama tandiko jipya la ngamia; na kwamba Amezidi Arshi kwa ukubwa mpaka kufikia vidole vinne kwa pande zote.”91

Kwa nini Allah atokwe na machozi wakati wa mafuriko ya Nuh? Ali-kuwa hajui matokeo yake wakati alipopeleka mafuriko? Si budi huyu mwandishi asiyejulikana naye aonyeshe huruma zake kwa mungu wake kama inavyodhaniwa (kwamba) malaika wamefanya?

89 Az-Zamakhshari, Tafsir Al-Kashshaf.90 al-Baydawi, Tafsir.91 Ash-Shahristani, al-Milal wan Nihal, imepigwa chapa pambizoni mwa Kitabul

Fasl cha Ibn Hazam, uk. 141.

70

SAHABA

“Hoja ya tatu ya ukafir wa Shi’a” inatolewa na mwandishi huyu asiyejulikana kwa maneno haya:-“Shi‘a wanaamini katika ufisadi kuwashutumu (kutukana, kuwalaani) Masheikh wawili (yaani Sayyidna Abu Bakr na Sayyidna Umar r.a.) na kuanzisha lawama zisizo na kweli dhidi ya usafi (chastity) wa Sayyidina (vivyo hivyo) Aisha (r.a.).”

Maoni: Kabla ya kuandika chochote juu ya hoja hii, ni lazima kueleza kwamba, kamwe hakuna Shi‘a aliyesema, kuandika au kueleza chochote dhidi ya usafi (chastity) wa Ummu’l-Muuminina ‘A’isha. Mtu huyu bila shaka hajui kwamba neno “chastity” kiujumla linatumika kwa “kujiepusha kukutana kimwili isivyo halali.” Sisi Mashi‘a hatuwezi kufikiria katika maneno kama hayo kuhusu “Mama wa waumini” yeyote, au kwa ajili hiyo kuhusu mke yeyote wa Mtume yeyote awe yeye ni mke wa Nuh au wa Lut (as). Hakika hatuwezi kuwazuia Wahabbi katika kujiingiza katika mazungumzo machafu kama haya. Mashi‘a watakubali kwa moyo wote kwamba, yeyote atakeyezusha lawama dhidi ya usafi (chastity) wa mama wa waumini ‘A’isha ni kafiri. Ni wazi kwamba lawama kama hizo zitakwenda kinyume na hukumu iliyo wazi ya Qur’an, na hivyo itakuwa ni sawa na kutokuamini Kitabu cha Allah (s.w.t.).

Tukija kwenye cheo cha Sahaba wa Mtume (s.a.w.w.) kuna tofauti ya msingi kati ya mtizamo wa Sunni na ule wa Shi‘a.

Kwanza, hebu tuangalie nini maana ya ‘Sahaba.’ Kwa mujibu wa vitabu vya Sunni, Sahaba ni mtu ambaye baada ya kuukubali Uislamu amemuona Mtume angalau mara moja, hata kama hakupata kuzungumza na Mtume, wala kusikia hadithi yoyote kutoka kwake, wala kupigana jihadi yoyote ile chini ya Mtume; ili mradi tu amekufa akiwa kama Mwislamu. Ufafanuzi huu unawachanganya wale ambao hawakuweza kumuona Mtume kwa sababu ya upofu.92

Na jina hili (Sahaba) linawahusu wale wote walioukubali Uislamu hata kama imani bado haijaingia nyoyoni mwao, hata kama walikuwa wanafiki.92 Ibn Hajar Al-‘Asqalani, Al-Isabah, uk. 10.

71

Kwa maneno mengine, Arabia yote ilkuwa imejaa Masahaba.

Hivyo basi, kwa mujibu wa itikadi ya Sunni Sahaba wote walikuwa waadilifu na wacha Mungu. Wamepachika hadithi kwa Mtume (s.a.w.w) ambayo hujenga msingi wa imani yao: “Sahaba wangu ni kama nyota, yeyote yule mtakaemfuata mtaongozwa sawa sawa.” Hivyo wanaamini kwamba Sahaba wote walikuwa waadilifu.

Mtazamo huu kwa pande zote unapingana na Qur’an na hadithi za Mtume (s.a.w.w.), achilia mbali ukweli kwamba matukio ya kihistoria moja kwa moja hayakubaliani na hili.

Ama kuhusu Qur’an, kigezo cha ubora ni imani ya mtu binafsi, matendo mema na uchaji, kama inavyoonekana katika mamia ya aya, si kitu kama mtu huyo alikuwa ni Sahaba au la. Vile vile Qur’an inasema katika sura at-Tawbah (iliyoteremshwa mwaka wa 9 A.H. mwaka mmoja na nusu tu, kabla ya Mtume kufariki): “Na kutoka miongoni mwa wale Waarabu ambao wanakaa pembezoni mwenu mna wanafiki. Kutoka miongoni mwa watu wa madina; wamebobea katika unafiki, wewe Mtume huwajui. Tutawaadhibu mara mbili kisha watarudishwa katika adhabu kubwa.”93

Pengine mtu anaweza akasema aya hii inawahusu wanafiki. Lakini wanafiki walikuwa vile vile wanahisabiwa miongoni mwa Masahaba, hasa ukichukulia kwamba unafiki wa wengi wao ulikuwa haujulikani hata kwa Mtume mwenyewe. Hata hivyo hapa tunanukuu aya chache tu (kati ya nyingi) ambazo zimeelekezwa kwa waumini miongoni mwa Masahaba:“Enyi mlio amini! Mna kitu (udhuru) gani mnapoambiwa: ‘Nendeni (kupigana) katika njia ya Allah mnainamia ardhi kwa uzito kabisa, je, mmekuwa radhi na maisha ya dunia kulinganisha na ya akhera? Lakinistarehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya akhera si (chochote) lakini kidogo tu. Kama hamtakwenda atakuadhibuni kwa adhabu inayoumiza, na ataleta watu wengine badala yenu, wala hamtamdhuru Allah chochote na Allah ni muweza juu ya kila kitu.”94

“Sema: kama baba zenu na wana wenu na ndugu zenu na wake 93 Qur’an, 9:101.94 Qur’an, 9:38-39.

72

zenu na jamaa zenu na mali mlizochuma na biashara mnazoogopa kuharibikiwa, na majumba mnayoyapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allah na Mtume wake na kupigania dini yake, basi ngojeni mpaka Allah alete amri yake; na Allah hawaongozi watu waasi.”95

“Enyi mlioamini! Msimfanyie khiyana Allah na Mtume wake, wala msikhini amana zenu na hali mnajua.”96

“Kama alivyokutoa Mola wako katika nyumba yako kwa haki, na kundi moja la walioamini halipendi. Wakabishana nawe katika haki, baada ya kubainika (na wakaenda huku wanachukiwa) kana kwamba wanasukumwa katika mautu na huku wanaona.”97

“Lo! Nyinyi mnaitwa mtoe (mali) katika njia ya Allah, na kuna wengine katika nyie mnafanya ubakhili! Basi afanyae ubakhili anaufanyia ubakhili huo kwa (kuidhuru) nafsi yake mwenyewe. Na Allah ni mkwasi, na nyinyi ndio mafakiri. Na kama mkirudi nyuma, ataleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.”98

Ama kuhusu hadithi za Mtukufu Mtume, chache zifuatazo zinatolewa hapa kufafanua suala hili:1. Imesimuliwa na Masahaba, Talha ibn ‘Abdullah, Ibn ‘Abbas na

Jabir ibn ‘Abdullah kwamba Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) aliendesha ibada ya mazishi kwa ajili ya mashahidi wa Uhud; na Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) alisema: “Mimi ni shahidi kwa ajili ya hawa” Abu Bakr (r.a.) akasema: “Ewe Mjumbe wa Allah! Je, sio kwamba ndugu zetu hawa wameukubali Uislamu kama sisi, na wamepigana jihadi kama tulivyofanya sisi?” Yeye (yaani, Mtume s.a.w.w.) akasema: “Hakika! Lakini hawakula chochote kutoka kwenye malipo yao, na sijui nyinyi mtakachofanya baada yangu.” Machozi yalimtoka Abu Bakr na akasema: “Je, sisi tutabakia baada yako wewe!”99

Imam Bukhari anasimulia kutoka kwa al-‘Ula’ ibn al-Musayyab kutoka

95 Qur’an, 9:25.96 Qur’an, 8:27.97 Qur’an, 8:5-6.98 Qur’an, 47:38.99 Al-Waqidi, Kitabu ’l-maghazi, J. I, uk. 310.

73

kwa baba yake kwamba alisema: “Nilimkuta (Sahaba) al-Bara’ ibn ‘Azib (r.a.) na nikasema “Baraka kwenu! Nyinyi mlioishi na Mtume (s.a.w.w.) na mkafanya bay’ah yake (kiapo cha utii) chini ya mti.” Akasema: “Ewe mtoto wa ndugu yangu! Hujui tuliyoyafanya baada yake.”100

2. Sahaba, Ibn ‘Abbas alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema (pamoja na mambo mengine), katika hadithi kuhusu Siku ya Hukumu: “Na hakika watu wengine katika Ummah wangu wataletwa na kupelekwa upande wa kushoto (yaani upande wa moto); hivyo nitasema: “Ewe Mola wangu hawa ni Sahaba wangu.” Lakini nitaambiwa: ‘Kwa hakika hujui waliyoyafanya baada yako, waliendelea kuyapa mgongo juu ya visigino vyao kuanzia mwanzo tu ulipowaacha.’ Kisha nitasema kama alivyosema mtumishi mwema (yaani Nabii Isa): ‘Na nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa nao, na uliponichukua, wewe ukawa mchungaji juu yao, na wewe ni shahidi juu ya kila kitu....’”101

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Hakika mtapelekwa upande wa kushoto Siku ya Kiyama, hivyo nitasema: ‘Mpaka wapi?’ Na nitaambiwa: ‘Mpaka Motoni, kwa jina la Allah!’ nitasema: ‘Ewe Mola wangu hao ni Sahaba zangu.’ Lakini nitaambiwa: ‘Hakika hujui walichokifanya baada yako; hakika walitoka nje ya Uislamu tokea wakati ulipoachana nao!’ Kisha nitasema: ‘Motoni hao! Motoni kwa hao waliobadilisha mambo baada yangu!’ Na sidhani kama kuna atakaeokolewa kutokana nao isipokuwa wachache tu kama mifugo isio na mchungaji.”102

Hadithi zenye maana kama hii hii zimesimuliwa na Masahaba Abu Bakrah103 na Abu ‘d-Darda.104

Pamoja na mamia ya Aya na Hadithi zinazowakosoa Masahaba wengi, bado Sunni wanakataa kuangalia kwa makini kila Sahaba ili kujua kama kweli Sahaba huyo anafaa kufuatwa au la. Kwao kila Sahaba anastahiki kufuatwa.100 Sahih al-Bukhari, J. 5, uk. 195; Imam Malik, Al-Muwatta, J. 2, uk. 462.101 Musnad Ahmad ibn Hanbal, chapa ya Misri. J. I, uk. 235.

(Aya iliyonukuliwa ni kutoka katika Sura ya Al-Maidah, aya ya 117).102 Sahih al-Bukhari, J. 7, uk. 209; J. 4, uk.94 na 156; Sahih Malik J. 7, uk. 66.103 Musnad Ahmad ibn Hanbal, J. 5, uk. 50104 Majma’u ‘z-zawaid, J. 9, uk. 367.

74

Namna yao ya kuhoji inafuata njia hii ifuatayo:- wanachukua Aya inayosifu abaadhi ya Sahaba na kuihusisha kwa wote bila kufikiria shuruti zake na mipakayake.

Kwa mfano:“Kwa hakika Allah amewapa radhi Waislamu walipofungamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawapa kushinda kwa zama za karibu.”105

Kama ukitafakari sana juu ya aya hii, utaona kwamba sio tangazo la jumla la furaha kwa wale wote waliofanya bay’ah kwa nyakti zote zijazo. Kwa maneno mengine, haisemi kwamba: Allah alikuwa radhi na wale wote waliokula kiapo cha utii kwako. Imeweka mipaka kwa waumini tu na hata kwao ni kwa muda maalumu tu, “wakati walipokula kiapo...” Ni wazi kwamba, wale ambao hawakufanya bay’ah au wale ambao sio waumini wa kweli wako nje ya mipaka ya aya hii. Na sio hili tu; aya iliyotangulia inaiweka aya hii katika mtazamo ulio wazi:“Bila shaka wale wanaofungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Allah. Mkono wa Allah uko juu ya mikono yao, Basi avunjae ahadi (ya kiapo hiki) anavunja kwa kuidhuru nafsi yake, na atekelezae aliyomuahidi Allah, Atamlipa malipo makubwa.”106

Hivyo kuna shuruti nyingine ya muhimu sana hapa: Wale waliofanya bay’ah hawatakiwi waivunje. Shurti hii ya nini, ikiwa Sahaba wote waliofanya bay’ah chini ya mti, walikuwa na kinga ya kutoivunja?

Kiapo kilichofanywa chini yamti, kilikuwa na sharti maalumu moja; “Kwamba hawatakimbia kutoka uwanja wa vita.”107

Na Qur’an yenyewe ni shahidi kwamba karibu wote walivunja kiapo hiki siku ya vita vya Hunayn miaka miwili baada ya kiapo hiki. Allah (s.w.t.) Amesema:- “Bila shaka Allah amekunusurini katika mapigano mengi, na siku ya Hunayn (pia), ambapo wingi wenu ulikupandisheni kichwa! Lakini haukukufaeni chochote, na ardhi ikawa dhiki juu yenu, ingawa ilikuwa yenye wasaa, kisha mkageuka mkarudi nyuma (mkakimbia).”108

105 Qur’an, 48:18.106 Qur’ani, 48:10.107 Musnad Ahmad ibn Hanbal, J. 3, uk.192; Tarikh Tabari, J.3, uk. 87.108 Qur’an, 9:25.

75

Vitabu vya hadithi na historia vinasema wazi kwamba katika vita vya Hunayn, ambavyo Sahaba kumi elfu (pamoja na wale waliofanya bay’ah chini ya mti) walishiriki, wote walikimbia isipokuwa wanne walibakia imara, watatu kati yao ni kutoka jamaa zake Mtume, Banu Hashim (‘Ali ibn Abi Talib, ‘Abbas ibn ‘Abdul Muttalib na Abu Sufyan ibn al-Harith ibn ‘Abdul Muttalib) na mmoja kutoka ukoo mwingine (‘Abdullah ibn Mas’ud).109

Kwa mujibu wa hadithi nyingine, ‘Aqil ibn Abi Talib, Zubayr ibn al-‘Awwam, ‘Abdullah ibn Zubayr ibn ‘Abdul-Muttalib na Usamah ibn Zayd vile vile walibakia imara.

Mtume (s.a.w.w.) alimuambia ami yake ‘Abbas kuwaita Waislamu warudi. Alishangaa ni vipi sauti yake itafikia kundi la watu wanaokimbia. Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba, Allah (s.w.t.) ataifanya sauti yake kuwafikia, haidhuru ni umbali gani wameshakwenda. Hivyo, ‘Abbas akaita kwamaneno haya aliyofundishwa na Mtume (s.a.w.w): “Enyi kundi la Ansar, Enyi watu wa mti wa Samurah...” (mahali walipokula kiapo miaka miwili iliyopita).110

Kwa kumbia huku kutoka uwanja wa mapambano, wote (isipokuwa wanne au nane waliotaja hapo juu) wamevunja kiapo chao, na hivyo hawezi kuwa pamoja katika habari nzuri ya radhi ya Mwenyezi Mungu. Lakini Masunni wanakataa kuangalia dalili hizi wazi.

Hili ni suala refu (yaani linahitaji maelezo marefu), lakini hapa nimeonyesha tu tofauti ya msingi wa mtazamo kati ya Sunni na Shi‘a.

Hata hivyo, “hatumtukani kwa upotovu” mtu yoyote; tunarudia tu yaliyosemwa ndani ya Qur’ani, hadithi na historia. Na tunatumia maneno yale yale kwa kila kikundi ambayo Qur’ani na hadithi imeyatumia kwao.

Lakini hebu tuchukulie, kwa ajili ya hoja tu kwamba lawama zinazotolewa na mwandishi huyu asiyejulikana dhidi ya Mashi‘a ni za kweli, na kwamba kweli wanawatukana Masheikh hawa wawili 109 Tarikh al-Khamis, J. 2, uk. 113; As-Sirah al-Halabiyah, J. 3, uk. 255.110 Ibn Sa’d, At-Tabaqat Al-Kubra, Beirut, hakuna tarehe, J. 4, uk. 18-19.

76

(Abu Bakr na Umar), na kisha tuangalie kama kweli kufanya hivyo (kuwatukana) ni sababu ya kuwatangaza kuwa (Shi‘a) ni makafiri.

Ibn Taymiyyah, Sheikhul Islam wa Wahhabi, ananukuu kikundi cha wanachuoni wa Kisunni kama ifuatavyo:-“Na kutukana tu mtu yoyote asiyekuwa Mtume si lazima kumfanye mtukanaji huyo kuwa ni kafiri; kwa sababu baadhi ya wale waliokuwepo wakati wa Mtume (yaani Sahaba) walikuwa wanatukanana, lakini hakuna hata mmoja aliambiwa ni kafiri kwa sababu ya kitendo chake hicho hivyo: na (vile vile) kwa sababu sio wajibu kuwa na imani kwa Sahaba maalum; hivyo kumtukana yoyote katika yao hakumuondoi (mtu) kwenye imani ya Allah na kitabu chake na Mtume wake na Siku ya Mwisho.”111

Na wazi zaidi ni maneno ya Mullah ‘Ali al-Qari ambaye anaandika katika Kitabu chake Shrahal-Fiqh-al-akbar:-“Kumtukana Abu Bakr na Umar sio kufr, kama Abush-Shakur as-Salimi kwa usahihi kabisa alivyothibitisha katika Kitabu chake, at-Tamhid, Na ni kwa sababu ya msingi huu hii (wakudai kwamba kuwatukana Shaykhayn ni kufr) haikuthibitishwa, wala maana yake kuthibitishwa.”

“Hii ni kwa sababu kwa hakika kumtukana Mwislamu ni fisk (dhambi, uovu) kama inavyothibitishwa na hadithi iliyo sahihi, na kwa ajili hiyo Masheikh hawa (Abu Bakr na Umar) watakuwa sawa sawa na Waislamu wengine katika kanuni hii; na vile vile kama tukichukulia kwamba mtu fulani amewaua Masheikh hawa wawili au hata wakwe zao wawili (yaani Uthman na ‘Ali), wote hao kwa pamoja, hata hivyo kutokana na (imani ya) Ahlus-Sunnah wal-Jama’ah, atakuwa hakutoka nje ya Uislamu (yaani hatakuwa kafir); na tunajua kwamba kutukana si vibaya sana kama kuua...”112

111 Ibn Taymiyyah, As-Sarimu ’l-maslul, 1402/1982; uk. 579 (iliyochapishwa na ‘Alama ’l-kutub).

112 Mulla ‘Ali Qari, Shrahal-Fiqh-al-akbar, (1) Matba ‘Uthmaniyah, Istanbul, 1303, uk. 130, (2) Matba‘ Mujtaba’i, Dehli, 1348, uk. 86, (3) Malba‘ Aftab-e-Hind, India, hamna tarehe, uk. 86.

Tume nukuu hapa matoleo matatu ya zamani yaliyochapishwa Uturuki na India. Sasa toleo jipya limechapishwa na Darul Kutubil ‘Ilmiyah, Beirut, mwaka 1404 H./ 1984 M. ambalo inadaiwa kuwa ni “toleo la kwanza,” na kutoka humo kurasa ⇒

77

Matamshi haya mawili ya wanachuoni wakubwa wa Ki-Wahhabi na wa Ki-Hanafi, inatosha na zaidi kuonyesha msingi usio wa kweli (kwa mwandishi huyu) kwa kile anachokiita hoja.

⇐ nne (pamoja na maandishi hayo hapo juu) zimeondolewa. Kipande kilichofutwa kina maneno yale na pamoja na haya kwamba: wale wanao amini kuwa Allah ana mwili hao kwa hakika ni makafiri kutokana na Ijma‘ bila tofauti yoyote ya maoni. Ni wazi kauli hii huwatoa Wahhabi nje ya Uislamu, kwa sababu wao wanaamini kuwa Allah ana mwili, kama ilivyoelezwa mapema.

Kisha kurasa 21/2 zenye majadiliano kama inaruhusiwa kumlaani (لعنت) yazid (mtoto wa Muawyyah aliyeshika Ukhalifa baada ya baba yake, na ambaye anahusika na kifo cha Imam Husain (a.s.) mjukuu wa Mtume (s.a.w.w.)). Mullah ‘Ali Qari amenukuu baadhi ya wanachuoni wa Ki-Sunni wakisema kwamba, Yazid amekuwa kafiri kuanzia muda ule ule alipotoa amri ya kuuawa kwa Imam Husein (a.s.); lakini yeye (Mullah ‘Ali Qari) mwenyewe anaruhusu laana kwa maneno haya tu:-“Allah amlaani aliye muua Husain au alikuwa radhi na hilo.” Hata haya yalikuwa maneno machungu yasiyokubalika kwa Wahhabi ambao wanamuita Yazid “‘Amiru ’l-mu’mineen”!!!

Uongo huu mweupe kwamba toleo la Beirut ndio la kwanza na Tahrif hii ya kuondoa (baadhi ya kurasa na maneno) inaonyesha uaminifu na ukweli wa Wahhabi!!!

78

FATWA

Mwandishi huyu asiyejulikana ameandika Fatwa na hadithi chache za kutunga kueleza kwamba “Rafidha” au Shi‘a ni Kafir.

Kuhusu hadithi hizi, wasomaji wataona ni jambo la kushangaza kwamba hakuna mtu mwingine ila Sheikh wa Kiwahabi Shaykhul Islam, Ibn Taymiyyah pekee alieeleza kwamba ahadithi zote ambazo neno “Rafidha” limetumika ni za kubuni. Anaandika hivi:-“Kwa sababu neno Rafidhah limeanza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye mwaka 105 A.H. Kwa hiyo inafahamika wazi (kabisa) kwamba aahadithi zote ambazo ndani yake neno “Radidha” limetumika ni za Uongo (za kubuni).”113

Sasa natuzijie Fatwa za baadhi ya Sunni au waandishi wa ki-Wahhabi au Mufti. Ni nani aliyewaambia watu hawa kwamba tunayajali japo kidogo tu maoni na mawazo yao? Uislamu na Imani yetu sisi imeambatana na Allah Subhanahu wa Ta’ala kupitia kwa Muhammad (s.a.w.w.) na kizazi chake, ambao ndio warithi wake halali. Kwa nini tujali kuhusu watu ambao hawakuunganishwa na hiki “Kiungo cha Dhahabu?” Tunamshukuru Allah kwamba Uislamu wetu ni wa asili, haukuchafuliwa na imani za Kipagani za watu hawa.

Je, Abu Dharr al-Ghifari, Sahaba aliyeheshimika sana, aliomuomba Uthmani Ibn Affan hati ya uthibitisho kwa ajili ya Imani yake?Je, ‘Amr ibn al-Humuq al-Khuza’i and Rushayd al-Hajari walihitaji hati yoyote kutoka kwa Ibn Ziyad?Je, ‘Ammar ibn Yasir alipewa uthibitishoi wowote na Mu’awiyah?Je, Mitham al-Tammar alihitaji kibali chochote kutoka kwa Ibn Ziyad?Je, Imam Husayn alikuwa anahitaji hati yoyote ya uthibitisho toka kwa Yazid?

Hivyo kwa nini sisi Mashi‘a tujali wanachosema hawa wafuasi wa Mu’awiyah, Yazid na Ibn Ziyad kuhusu sisi?

Imamu wetu ‘Ali alikuwa na “Imani kamili” kama Mtume (s.a.w.w.) alivyokwisha tangaza katika vita ya Khandaq.114 Kwa hiyo sisi Mashi‘a 113 Ibn Taymiyyah, Minhaju ’s-sunnah, chapa ya zamani, J. I, uk. 8.114 Arjahu ’l-matalib, uk. 219-220.

79

wa ‘Ali tumejawa na Imani kiasi kwamba, ikiwa neno “kufur” “li-nahusishwa na sisi, “Kufur” inakuwa nzuri sana na yenye kustahiki kupongezwa machoni pa Allah, na Allah anasifia ubora wake. Anase-ma katika Qur’an kuhusu waumini kama sisi hivi:-“...Basi, anayemkataa (yakufur) Shetani na akamuamini Allah, bila shaka yeye ameshika kishiko chenye nguvu kisichovunjika...”115

Sisi Mashi‘a wa ‘Ali tumesikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu wakati aliposema:-“Hakika nyinyi muna mfano mzuri kwa (Nabii) Ibrahimu na wale waliokuwa pamoja nao: walipowaambia jamaa zao: Kwa yakini sisi tu mbali nanyi, na hayo mnayoyaabudu kinyume cha Allah; tunakukataeni (kafarna bikum), na umekwisha dhihiri uadui na bughudha ya daima kati yetu na ninyi mpaka mtakapomwamini Allah peke Yake…”116

Kwa kufuata “Mfano huu mzuri” sisi Mashi‘a wa ‘Ali tunatoa ujumbe huo huo kwa hawa Ma-Mufti wenye kujiwekeza na wafuasi wao. Ikiwa watasema sisi sio waumini, basi dunia naijue kwamba sisi hatuwaamini Ma-Mufti hawa, hatuamini uongo wao, hatuamini unafiki wao, na wala hatuamini Uislamu wao wa Kimarekani.

115 Qur’an, 2:256.116 Qur’an, 60:4.

80

TAQIYAH

Mwandishi wa Kitabu “Ushi‘a ni Nini?” Ameandika katika ukurasa wa 15, chini ya kichwa cha habari “Taqiyah”:-“Nifaaq au unafiki ndio chimbuko la dini ya Shi‘a. Kwa ujanja kabisa, wanauita unafiki huu Taqiyah yenye maana ya ruhusa ya mtu kuficha imani yake ya kweli kwa ajili ya manufaa.”

Maoni: Ni rahisi kutoa maana isiyo sahihi ya neno na kisha ukalirundika matusi mengi juu yake. Taqiyah ni istilahi ya Qur’an: ina maana ya ruhusa ya kuficha imani ya kweli ya mtu, sio kwa ajili ya manufaa, lakini kama kuna hatari kwa maisha ya mtu mwenyewe, mali au heshima yake au ya muumin mwingine. Ruhusa hii imeanzishwa na Qur’an, imefuatwa na Masahaba wakubwa wenye kuheshimiwa na inakubaliwa na Waislamu wote, Mashi‘a na Masunni kwa pamoja.

Lakini mwandishi wa kijitabu kile yuko nje ya duru la Uislamu kwa hiyo hajui mambo haya. Haelewi kwamba sio “dini” ya Shi‘a tu, lakini ni “dini” ya Waislamu wote.

Ningependa kutoa rejea chache tu hapa kutoka kwenye Qur’an, vitendo vya Masahaba, tafsir, hadithi na maandishi ya Wanachuoni wenye kuheshimiwa wa Kisunni.

Kutoka Kwenye Qur’an:

ن يمان ولكن مذ

به مطمئ بالره وقل

ك

من أ

ذمن كفر بالله من بعد إيمانه إل

ن الله ولهم عذاب عظيم ١٠٦ كفر صدرا فعليهم غضب مح بال ش

“Ambaye anamkufuru Allah baada ya imani kwake (ni muongo) isipokuwa yule ambaye amelazimika ambapo moyo wake umetulia juu ya imani (hana cha kuhofu). Lakini yule Allah anayekifungua kifua chake kwa ukafiri, basi juu yao ghadhabu kutoka kwa Allah na wanayo kwao adhabu kubwa.”117

Aya hii ya Qur’an inazungumzia kisa cha ‘Ammar bin Yasir (r.a.), Sahabi aliyeheshimiwa, wakati alipolazimika kusema baadhi ya 117 Qur’an, 16:106.

ۦ

81

maneno dhidi ya Uislamu ili kujiokoa kutoka kwa makafiri wa Kikureishi.

Makuraishi walimuuwa kinyama shahidi Yasir na mkewe Sumaiyyah kwa sababu tu ya Imani yao. Walikuwa mashahidi wa kwanza wa Uslamu. Wakati wazazi wake walipouwawa, akajifanya kuukana Uislamu na hivyo akaokoa maisha yake. Mtu mmoja akaja kumuambia Mtume (s.a.w.w.) kuwa ‘Ammar amekuwa kafir. Mtume (s.a.w.w.) akasema “Kamwe; hakika nyama na damu ya Ammar... vimeathiriwa na imani ya kweli.” Kisha, ‘Ammar akaja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) huku akilia kwa uchungu kwamba ilikuwa atoe maneno maovu dhidi ya Uislamu ili aweze kuponyoka kwenye makucha ya makafiri. Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza: “Uliuhisi vipi moyo wako?” ‘Ammar akasema: “Ulikuwa imara katika Imani.” Mtume akamwambia asiwe na wasi wasi na akamshauri kuyarudia tena maneno hayo ikiwa makafiri hao watamuuliza tena kufanya hivyo.

Na haikuwa Mtukufu Mtume tu aliyependezewa na chaguo hili la ‘Ammar (r.a.), fursa hii aliyoitumia ‘Ammar (r.a.) Hata Mwenyezi Mungu alithibitisha kitendo chake hiki katika aya ya Qur’an iliyonukuliwa hapo juu.

Tukio hili limetajwa takriban kwenye vitabu vyote vya tafsir chini ya aya hii. Kwa mfano:Tafseer Ad-Durru ’l-Manthur cha Imam as-Suyuti. J. 4, uk. 132.Tafseer Al-Kashshaf of az-Zamakhshari, chapa ya Beirut J. 2, uk. 430.Tafseer Kabir cha Imam ar-Razi.

Aya nyingine:-

لك فليس من مؤمنين ومن يفعل ذ

ولاء من دون ال

كفرين أ

مؤمنون ال

يتذخذ ال

ذل

مصير ٢٨ الله ال

ركم الله نفسه وإل ن تتذقوا منهم تقاة ويذ

أ

ذء إل الله ف ش

ماوات وما ف و تبدوه يعلمه الله ويعلم ما ف السذأ فوا ما ف صدوركم ل إن ت

قء قدير ٢٩ ش

ك رض والله ع ال

“Walioamini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao (wa kuwapa

82

siri zao) badala ya (Waislamu wenzao) na atakaefanya hivyo, basi hatakuwa na chochote mbele ya Allah, ila (ikiwa mnafanya urafiki nao au juu juu tu hivi) kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Allah anakutahadharisheni na adhabu yake. Na marejeo ni kwa Allah. Sema: Kama mkificha yaliyomo vifuani mwenu au mkiyadhihirisha, Allah anayajua, na anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo ardhini, na Allah ni mwenye uwezo juu ya kila kitu.”118

Sababu ya ruhusa bii imeelezwa katika aya hii yenyewe. “Sema: Kama mkificha yaliyomo vifuani mwenu au mkiyadhihirisha Allah anayajua”.

Hapa Allah (s.w.t.) anawahakikishia Waislamu kwamba Imani ni kitu cha kiroho kilichounganishwa na moyo; na kama imani ndani ya moyo wako ni imara, basi Allah anakuwa radhi na wewe iwe imani hiyo umeidhihirisha au umeificha. Yote ni sawa kwa Allah, kwa sababu Allah anazijua siri zako zilizofichika, na hata wakati kama ukificha imani yako kwa makafir Allah anaijua na kuitambua.

Vile vile zipo aya nyingine, lakini hatutaki tupoteze muda mwingi katika suala hili.

Sasa (tuchukue) baadhi ya maelezo toka kwenye vitabu vya Tafsiri:-Imam as-Suyuti anaandika, miongni mwa mambo mengine, chini ya aya hii kwamba:-

إل قوله: إبن عباس ف العوفي عن أبي حاتم من طريق وإبن إبن جرير وأخرج أن تتقوا منهم تقاة: فالتقية باللسان - من حل ع أمر بتكلم به وهو معصية لله فيتكلم به مخافة الناس وقلبه مطمئ باليمان فإن ذلك ل يضره إنما التقية باللسان ... وأخرج عبد بن حيد عن الحسن قال: التقية جائزة إل يوم القيامة - وأخرج عبد عن أبي رجاء أنه كان يقرأ: إل أن تتقوا منهم تقية - وأخرج عبد بن حيد عن

قتادة أنه كان يقرؤها: إل أن تتقوا منهم تقية بالاء.“Na Ibn Jarir na Ibn Abi Hatim wamesimulia kupitia kwa al-‘Awfi kutoka kwa Ibn ‘Abbas (kwamba alisema kuhusu aya hii): ‘Hivyo

118 Qur’an, 3:28-29.

83

Taqiyah ni kwa ulimi. Yoyote atakayelazimishwa kusema kitu ambacho ni cha utovu wa utii wa Allah (s.w.t.) na husema hivyo kwa sababu ya hofu ya watu hao ambapo moyo wake umebakia imara katika imani, haitamletea madhara, hakika Taqiyah ni katika ulimi tu.’

“. . .Na ‘Abd Ibn Hamid amesimulia kutoka kwa al-Hasan (al-Basiri) kwamba amesema Taqiyah ni halali mpaka siku ya ufufuo. Na ‘Abd (Ibn Hamid) amesimulia kutoka kwa Abu Raja’ kwamba alikuwa akisoma ‘illa an tattaqu minhum taqiyatan’; na ‘Abd Ibn Hamid amesimulia kutoka kwa Qatadah kwamba alikuwa akisoma hivyo taqiyatan - pamoja na ya.”119

Hivyo unaona hapa neno ‘Taqiyah’ linavyotajwa kwa kupendelewa ndani ya Qur’an. Na mwandishi huyu asiyejulikana anasema taqiyah ni ukafiri!!

Imam Fakhruddin ar-Razi ametaja baadhi ya kanuni zinazohusu Taqiyah chini ya aya hii, ambazo baadhi yake zinatolewa hapa:-

الموالة إنما تجوز فيما يتعلق بإظھار أنھا للتقية﴾ الثالث ﴿الحكم والمعاداة، وقد تجوز أيضا فيما يتعلق بإظھار الدين. فأما ما يرجع إلی الغير کالقتل والزنا وغصب الموال والشھادة بالزور وقذف المحصنات

وإطلاع الکفار علی عورات المسلمين، فذلك غير جائز البتة.

مع تحل إنما التقية أن علی يدل الآية ظاھر ابع﴾ الر ﴿الحكم الکفار الغالبين إل أن مذھب الشافعي رضي الله عنه أن الحالة بين المسلمين إذا شاکلت الحالة بين المسلمين والمشركين حلت التقية

محاماة علی النفس.

جائزة ھي وھل النفس، لصون جائزة التقية الخامس﴾ ﴿الحكم 119 as-Suyuti, ad-Durru ’l-manthur, J. 2, uk. 16 - 17.

84

مال »حرمة لقوله صلى الله عليه وسلم بالجواز، فيھا أن يحكم يحتمل المال لصون المسلم کحرمة دمه« ولقوله صلى الله عليه وسلم »من قتل دون ماله فھو شھيد« ولن الوضوء، فرض بالغبن سقط بيع إذا والماء المال شديدة إلی الحاجة وجاز القتصار علی التيمم دفعا لذلك القدر من انقصان المال، فکيف

ليجوز ھھنا والله أعلم.

أول في ثابتا کان الحكم ھذا مجاھد: قال السادس﴾ ﴿الحكم السلام لجل ضعف المؤمنين فأما بعد قوة دولة السلام فلا، وروی القيامة، يوم إلی للمؤمنين التقية جائزة قال: أنه الحسن: عوف عن

وھذا القول أولی، لن دفع الضرر عن النفس واجب بقدر المکان.

“Kanuni ya Tatu: Taqiyah inaruhusiwa katika mambo yahusianayo na udhihirisho wa urafiki au uadui; na vile vile imeruhusiwa katika mambo yanayohusiana na kutaja dini yao. Lakini ni dhahiri hairuhusiwi katika mambo yanayo athiri watu wengine, kama kuuwa, zinaa, kupora mali, kushuhudia uwongo, kusingizia mwanamke aliyeolewa (kuwa kazini) au kuwapa habari makafiri kuhusu sehemu dhaifu katika ulinzi wa Waislamu.

“Kanuni ya Nne: Aya ya Qur’an inaonyesha wazi kwamba Taqiyah inaruhusiwa (ukiwa) pamoja na makafiri wenye nguvu. Lakini kwa mujibu wa madh-hab ya Imam Shafi‘i (Allah amuwiye radhi) kama hali katika (madhehebu mbalimbali) ya Waislamu inafanana na hali kati ya Waislamu na makafir, basi Taqiyah (kwa Waislamu vile vile) inaruhusiwa kwa kulinda maisha ya mtu.

“Kanuni ya Tano: Taqiyah inaruhusiwa kwa ajili ya ulinzi wa maisha. Swali ni kwamba iwapo inaruhusiwa kwa ajili ya ulinzi wa mali, uwezekano ni kwamba hiyo pia yaweza kuruhusiwa, kwa sababu Mtume (s.a.w.) amesema: ‘Heshima ya mali ya Mwislamu ni sawa sawa na heshima ya damu yake,’ na vile vile Yeye (s.a.w.) amesema: ‘Ambaye

85

atauawa katika kutetea mali yake atakuwa amekufa kifo cha kishahidi’; na vile vile kwa sababu mtu huihitaji sana mali yake; Ikiwa maji yanauzwa kwa bei kubwa wudhu hauwi wajibu na mtu anaweza kusali kwa kutayamam kuepusha hasara ile ndogo ya mali, hivyo kwa nini kanuni hii isitumike hapa? Na Allah anajua vizuri.

“Kanuni ya Sita: Mujahid amesema kwamba hii kanuni (ya Taqiyah) ilikuwa ikitumika katika mwanzo wa Uislamu, kwa sababu waumini walikuwa wanyonge wakati ule. Lakini sasa kwa vile dola la Kiislam limepata nguvu na imara, taqiyah hairuhusiwi tena. Lakini ‘Awfi amesimuulia kutoka kwa al-Hasan (al-Basri) kwamba amesema: Taqiyah inaruhusiwa kwa Waislamu mpaka siku ya ufufuo. Na maoni yanakubalika zaidi kwa sababu ni wajibu kuondoa aina zote za madhara kutoka kwa mtu mwenyewe kadiri iwezekanavyo.”120

Kutoka Kwenye Ahadith: Imam Al-Bukhari ameandika sura nzima, Kitabul Ikrah, juu ya mada hii ya kulazimishwa, ambamo, pamoja na mambo mengine anaandika hivi:-

أن تتقوا منهم تقاة من أكره وقلبه مطمئ باليمان ... وقال: إل

قول الله تعال: إل

وهي تقية ... وقال الحسن: التقية إل يوم القيامة... وقال النبي صلى الله عليه وسلم: العمال بالنية.

“Na Allah amesema: ‘Isipokuwa mnapotaka kujilinda wenyewe dhidi yao kwa kuwahofia’. Na hiyo ni Taqiyah................ Na Hassan (Basir) amesema: ‘Taqiyah ni mpaka siku ya ufufuo’. Na Mtume (s.a.w.) amesema: ‘Matendo yanatokana na nia’.”121

Ndiyo Mtume (s.a.w.) ameainisha wazi wazi kabisa kwa kusema:

ل دين لمن ل تقية له.“Ambaye hana Taqiyah hana Dini.”122

120 Imam ar-Razi, Tafsir Mafatiu ’l-ghayb Beirut, Toleo ya 3, J. 7, u. 13.121 Sahih al-Bukhari, chapa ya Misri, J. 9, uk. 24-25.122 Mulla ‘Ali Muttaqi, Kanzu ’l-‘Ummal, Beirut, Toleo ya 5., 1405/1985, J. 3, uk. 96,

hadith no. 5665.

86

Ni wazi kwamba (chimbuko la) Taqiyah ni sehemu ya Dini ya Ki-Islamu, iliyowekwa na Qur’an na kuthibitishwa na hadithi za Mtume, yenye kukubaliwa kikamilifu na wanachuoni wa Ki-Sunni na Mufassirin (wafasiri), na kufuatwa na Masahaba wenye kuheshimiwa. Na sasa mtazame mwandishi huyu asiyejulikana anayesema Taqiyah ni nifaaq au unafiki! Hakika si kwamba tu yeye mwenyewe ni mnafiki, bali moja kwa moja yeye ni kafiri kwa sababu amemlaumu Mtume (s.a.w.w.) na Masahaba wake wenye kuheshimiwa kuhimiza na kufanya nifaaq!! Astaghfirullah! Kumbuka kwamba kutokana na hadithi ya Mtume adui huyu wa Taqiyah sio Mwislamu kamwe (Hana Dini).

Ukweli ni kwamba Taqiyah ni kinyume cha unafiki. Kumbuka Imani na Kufr wakati vikionekana na ilani yao yaweza kugawanya katika makundi manne tu:-1. Imani sahihi ya Kiislamu kwa moyo na ilani yake katika maneno.

Hii ni Imani ya wazi.

2. Imani dhidi ya Uislamu kwa moyo na ilani ya kinyume cha Imani ya Kiislamu katika maneno. Hii ni Kufur ya wazi.

Makundi haya mawili ni mbalimbali kwa kila lingine, na hayawezi ku-changanywa katika sehemu moja.

3. Imani dhidi ya Uislamu kwa moyo lakini ilani ya Uislamu katika maneno. Hii ni Nifaq (unafiki).

4. Imani sahihi ya Uislamu kwa moyo lakini ilani ya kinyume cha Imani ya Uislamu katika maneno. Hii ni Taqiyah.

Makundi haya mawili (Nifaq na Taqiyah) nayo kadhalika ni mbalimbali kwa kila lingine, na kamwe hayapatikani katika sehemu moja.

Kwa maneno mengine, anayepinga Taqiyah ni mnafiki kama mwandishi huyu asiyejulikana.

87

Imam ar-Razi pia ameeleza wazi hitilafu hii katika Tafsir yake kwa maneno yafuatayo:-

ويضمر اليمان يظهر الي فالمنافق القلب ف بما العتبار أن إلي إشارة هذا الكفر كافر والمؤمن المکره الي يظهر الكفر و يضمر اليمان مؤمن والله أعلم

بما ف صدور العالمين.“Hii inaelekeza kwenye ukweli kwamba (katika mambo haya) umuhimu hutolewa tu kwa kile kilichofichwa ndani ya moyo. Mnafiki anaeonyesha imani na kuficha kutokuamini kwake ni kafir, ambapo Muumin ambaye kwa kulazimika, anaonyesha kutokuamini na akaficha imani ni Muumin, na Allah anayajua vizuri yaliyofichika mioyoni mwa wote.”123

Kama mtu atataka kujua zaidi juu ya somo hili, itambidi asome kijitabu changu, ‘Taqiyah’ [Kwa lugha ya Kiswahili soma ‘Taqiyah ni Nini’] kinachopatikana kutoka Bilal Muslim Mission, S.L.P. 20033, Dar es Salaam au S.L.P. 10396. Nairobi.

Kabla ya kufunga Sura hii ningependa kumuuliza mwandishi huyu asiyejulikana, kwamba ni kwa nini hakutaja jina lake katika kijitabu chake? Je, (hiyo) sio Taqiyah? Na kwamba vile vile (ni Taqiyah) ambayo haina sababu yoyote? Kenya ni nchi huru na hakungekuwa na hatari kwa maisha yake, heshima au mali yake kama angeandika jina lake kama mwandishi. Kwa hiyo Taqiyah ni aibu kama itafanywa na mtu asiye Wahhabi kulinda maisha yake kutokana na ushenzi wa Wahhabi; lakini inapendeza sana kama ikifanywa na Wahhabi bila sababu yoyote!!

123 Tafsir Mafatiu ’l-ghayb, chini ya Aya ya 19:10

88

HITIMISHO

Mwandishi huyu asiyejulikana amechusha kurasa nyingi dhidi ya anachokiita “kaulimbiu za uwongo za Umoja na Undugu.” Anatukana wale Ahlu-Sunna ambao wanaunga mkono Shi‘a kwa maneno haya: “Wjinga ambao wanatazamia Ma-ulamaa kuleta kaulimbiu za undugu na kuzua msingi mmoja na jukwaa lililo sawa la uelewano wa undugu pamoja na Shi‘a.”

Hili ni lengo moja hasa la kijitabu hiki (“Ushi‘a ni Nini?”) na lengo moja la malengo ya mamia na maelfu ya vitabu, vijitabu, makala na fatwa ambazo mashine za uchapishaji za Wahhabi huchochea kila siku katika lugha za Kiarabu, Urdu, Kiingereza, Kituruki na kiasi kidogo kwa lugha nyingine za sehemu mbali mbali za ulimwengu.

Wanadai kuwa wao ni wafuasi wa Qur’an na wanatumia mabilioni ya pesa za mafuta (Petrodollars) kuwazuia Waislamu ulimwenguni kuungana pamoja, ambapo Allah (s.w.t.) anasema:-“Na shikamaneni na kamba ya Allah pamoja wala msifarikiane.”124

“Na mtiini Allah na Mtume wake wala msogombane, msije mkavunjika mioyo na kupoteza nguvu zenu, na vumilieni, bila shaka Allah yuko pamoja na wenye kuvumilia.”125

Ni lengo la kweli kwamba pamoja na msisitizo wote huu wa umoja, Waislamu wamegawanyika katika makundi mengi hivyo. Hata hivyo ni wajibu wetu kuokoa chochote kile tunachoweza, kutokana na mashambulizi haya ya mgawanyiko na ugomvi. Mwito wa kusimama uliotolewa na Iran kwa Waislamu ulimwenguni kuungana umetegemea amri hii ya Allah (s.w.t.). Lakini bahati mbaya, maadui wa Uislam wameponda ile maana yake na kuwatisha Waislamu wasioshuku kwa kusingizia nyendo mbaya kwa watu hawa wakweli wasio na kombo.

Kuna njia tatu za kuwazeka kwa umoja wa Waislamu. Mbili ya hizo ni kama ifuatavyo:-124 Qur’an, 3:103.125 Qur’an, 8:46.

89

1. Umoja katika Itikadi:- Kwamba Waislamu wote budi wakubali itikadi namna moja tu; na

2. Umoja katika Kanuni za Shari’ah:- Kwamba wote wafuate mtindo mmoja wa matendo ya ibada, na hivyo hivyo katika mambo kama yanamhusu mtu binafsi, kijamii, fedha na kanuni za adhabu.

Ni wazi kwamba njia zote hizi ni muhali kufanyika siku hizi. Umoja wa Itikadi na Shari’ah hautapatikana mpaka atakapodhihiri Imam Al-Mahdi (a.s.).

Sasa kunabakia njia ya tatu ya umoja, nayo ni umoja katika kuwakabili maadui wa Uislamu. Ina maana kwamba Waislamu wote wasimame bega kwa bega kulinda maadili ya Uislamu, ardhi za Waislamu, heshima ya Waislamu na maisha ya Waislamu. Hawana budi kusahau mgawanyiko wa tofauti katika kuukabili Uyahudi (Zionists), ukomonisti na Ubepari. Kama hawatasimama pamoja, hakika watanyongwa pamoja. Tazama nini kinatokea huko Kashmir na India, jinsi Bosnia inavyochinjwa kikatili na Wakristo wa Croats na Serbs, maelfu ya wanawake wa Kiislamu wamenajisiwa. Lakini wanyang’anyi wa fedha za mafuta, wanautumia utajiri huu wa Waislamu kuhami mazizi ya wanyama ya London yasifungwe! Wanyama wana thamani sana kuliko Ummah wa Ki-Islamu...wa Bosnia, kashmir, Burma na Azerbaijan.

Kufuja mamilioni ya dola (fedha) za kimarekani kwa usiku mmoja kwenye meza za kamari huko Las vegas (Marekani) ni muhimu zaidi kuliko kupunguza maumivu na tabu za Waislamu wasiojiweza wa Iraq,Bangladesh, Somalia na Albania. Na ukweli kwamba Tajikistan imeangukia tena mikononi mwa Wakomunisti wakorofi haiwafanyi wajisikie vibaya.

Bahati mbaya, Wahhabi... au hasa koo za watawala wa Arabuni (ambayo kwa makosa huitwa Saudi Arabia), Kuwait na Bahrain hawajali Qur’an na hadithi zinavyosema kuhusu haki ya Muislamu juu ya Waislamu wengine. Juhudi zao za mwanzo na mwisho ni kuokoa falme zao na Usheikh wao kutokana na ghadhabu za watu wao. Wanajua kwamba hakuna Muislamu mzuri anayeweza kuunga mkono ufuska wao, unywaji wao pombe wa dhahiri na sherehe zao za kamari.

90

Wanaelewa wazi kwamba hakuna mtu mwenye akili zake anayeweza kuukubali uonevu wao, tawala zao za kidhalimu na mpangilio wao wa kuwasaga Waislamu wasio Wahhabi. Kwa kushinikizwa na ukweli huu,wanatafuta hifadhi kutoka kwa mabwana zao wa magharibi (Ulaya na Marekani). Wanapuuza maonyo yaliyotolewa na Allah (s.w.t.), kwamba wasiwainamie Mayahudi na Wakristo, wasitafute msaada wao, bali wategemee kikamilifu kwa Alah (s.w.t.) tu peke yake, kama Aya zifuatazo zinavyoeleza wazi wazi:-“Na Mayahudi hawatakuwa radhi nawe wala Wakristo mpaka ufuate mila (dini) yao. Sema: “Hakika uwongozi wa Allah ndio uwongozi (wa kweli)”126

“Enyi Mlioamini msiwafanye maadui zangu na adui zenu kuwa marafi-ki; mtawafanyia mapenzi na hali ya kuwa wamekwisha kanusha yaliyo kujieni ninyi kutokana na haki...”127

“Walioamini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya waumini. Na atakayefanya hivyo, basi hatakuwa na chochote (cha kufanya) mbele ya Allah...”128

“Enyi mlioamini! Msiwafanye makafiri kuwa marafiki badala ya Waumini. Mnataka awe nayo Allah hoja dhahiri juu yenu?”129

“Enyi Mlioamini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa marafiki: ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu atakayefanya urafiki huo nao, basi huyo atakuwa pamoja nao. Hakika Allah hawaongozi watu madhalimu.”130

Lakini watawala hawa wa Kiwahhabi wameuza nafsi zao kwa akina Reagan, Bush, na Clinton; na kinachohuzunisha zaidi wametoa Bara Arabu kwa wingi sana kwa wawekezaji vitega uchumi ambao ni maaduiwa wazi wa Uislamu.

126 Qur’an, 2:120.127 Qur’an, 60:1.128 Qur’an, 3:20.129 Qur’an, 4:144.130 Qur’an, 5:51.

91

Tangu karne kumi zilizopita, nguvu za Waulaya na Wamarekani zilikuwa zikitangaza kwamba Uilsamu ulikuwa adui yao nambari moja. Baada ya kuanguka himaya ya Kirusi, gazeti la Sunday Times (London) liliaandika katika mwezi wa mei 1991 katika safu yake ya mhariri kwamba, kwa vile nchi za magharibi zimemaliza jukumu hili, “sasa” lazima budi kukusanya nguvu zake na kuzielekeza “Mashariki ya kati” (Soma: “dhidi ya Uislamu”). Kilichotokea mapema tu baada ya hapo, ilikuwa ni kufungukwa kwa macho kwa wale ambao huenda walikuwa na mawazo, kwamba nchi za magharibi zinasimama juu ya “Demokrasi” na “haki za binadamu” na kulinda maadili haya.

Marekani imeshutumu wazi wazi kuwa Uislamu ni adui yake nambari moja. Askofu mkuu wa Canterbury George Carey, katika ziara yake ya hivi karibuni (1993) nchini Tanzania aliwasema kwa kishindo Waislamu wenye msimamo thabiti (wao wanawaita Waislamu wenye siasa kali, au msimamo mkali, wengine wanawaita wenye imani kali) kuwa tishio kwa amani duniani.

Na Amerika na washirika wenzake wanawapa moyo (nguvu) vibaraka wao walioko mashariki ya kati na majasusi (walioenea) kila mahali kufuta Uislamu katika uso wa dunia. Na kwa hakika, kwa kutaka kuufanya Ummah ulale usingizi wakaongeza neno, “Fundamentalist”. Kabla ya Uslamu (Neno hili ni la Kiingereza, maana yake ni “mtu mwenye kushikamana vizuri na itikadi yake;” lakini ni kwa bahati mbaya sana neno hili hutumiwa kwa maana ya “Waislamu wakorofi”, “Siasa kali,” “Imani kali” au afadhali kidogo wengine huwaita “Wenye Msimamo mkali, hata hivyo maana zote hizi ni za kuwapakaza Waislamu matope waonekane wabaya mbele za watu).

Masheikh (Wafalme / Masultani) hawa wa nchi hizi zenye mafuta, wana kiboko chenye nguvu sana cha kuweza kuzifanya nchi za Ulaya na Marekani kusalimu amri kwa wapendavyo; kama Imam Hafiz Ismet Saphic wa Sarahevo (Bosnia) - ambaye binti zake watatu waliuwawa wakati wakingojea kwenye foleni ya kugawiwa mikate - alisema, “kama nchi za Ki-Islamu zitoazo mafuta zingesimamisha misafara yao kusafirisha mafuta kwa siku moja tu, nchi za Magharibi zitaweza (mara moja) kubadilisha msimamo wao.”131

131 The Muslim News, London, 30/7/1993.

92

Lakini hawana moyo wa kutumia silaha hii waliyopewa zawadi na Allah (s.w.t.) dhidi ya nchi hizi za Magharibi, kwa sababu wanajua wazi kwamba kudumu kwao kunategemea matakwa ya Marekani.

Watawala hawa wa Ki-Wahhabi wanafikiri Mataifa haya ya Magharibi (Ulaya na Marekani) ni marafiki wa Sunni. Hakuna kinachozidi upumbavu huu. Nguvu hizi si za marafiki wa Sunni wala maadui wa Shi‘a. Ni za marafiki tu wa maslahi zao na maadui kwa wale wote wanoonyesha (hata) madhara madogo tu juu ya maslahi yao.

Kama wanaupenda Usunni, basi kwa nini waliamuru jeshi la Uturuki kunyakua madaraka wakati Arbaken (Muislamu wa Kisunni) alishinda uchaguzi? Kwa nini walilishawishi jeshi la Algeria kufuta uchaguzi wakati ushindi wa Waislamu ulikuwa unaonekana wazi. Kwa nini John Major (Waziri Mkuu wa Uingereza) anaambiwa ameandika barua kwamba hataki serikali yoyote ya Ki-Islamu (ya Ki-Sunni Bosnia) katika nchi za Ulaya?

Sitaki kuhangaikia sana upande huu wa siasa za miliki za Masheikh hawa walio kinyume na watu, bali tu, wanachokifanya dhidi ya Uislamu kwa ujumla ni kuumiza moyo zaidi.

Katika bidii ya kuwapendeza mabwana zao walioko White house (Ikulu ya Marekani) na White hall (Ukumbi wa Bunge la Marekani) wanajiingiza katika vitendo ambavyo vinaweza kuiangusha ngome ya Uislamu.

Mfano mmoja ni hii fitina inayoendelea sasa hivi ya kuupiga vita Ushi‘a. Wahhabi wanafikiri kwamba kuwalaumu Shi‘a, tuseme kwa, kuamini Tahrif ya Qur’an tukufu, kutaharibu mtazamo wa imani ya Shi‘a, hawajui kwamba kufanya hivyo nikutikisa msingi mzima wa Uislamu (ambalo kwa kweli hilo ndilo lengo la wafadhili wao wa Ulaya na Marekani). Hebu tuangalie suala hili ili tuelewe mchezo wa nchi za Magharibi katika sura yake ya kweli ya mateso (hasa ya dini).

Maulamaa wa Kiislamu, Shi‘a na Sunni kwa pamoja, hawakuamini kwamba kulikuwa na upungufu, nyongeza au uondoshaji katika Qur’an. Hakuna mwanachuoni mwenye akili zake wa madhehebu

93

yoyote ambaye anailaumu madhehebu nyingine kuwa inaamini tahrif ya Qur’an. Kwa hakika wamekuja mara kwa mara baadhi ya Maulamaa wa pande zote mbili ambao walijiingiza katika kupakaza matope dhidi ya madhehebu nyingine, bila kuelewa kwamba ikiwa hadithi inapatikana katika kitabu sio lazima ikubaliwe na kundi hilo. Hadith kama hizo (yaani za Tahriif) zimebakia zimezikwa katika vitabu hivyo, na zilikuwa hazitangazwi kwa sababu hakuna hata mtu mmoja aliyetegemeza imani yake kwazo.

Mambo yalibadilika ghafla tu mwaka 1979, wakati taifa la Iran chini ya Uongozi wa marehemu Ayatullah al-Khomeini (r.a.) walipofanikiwa kusimamisha serikali ya kweli, ya kwanza, ya Ki-Islamu katika ardhi (Duniani), karne nyingi baada ya nyakati za Maimamu.

Lau ingekuwa Mapinduzi ya Iran yangeleta serikali inayomilikiwa kutoka nje kwa kufuata malengo ya itikadi za magharibi au mashariki, kwa furaha kubwa ingekubaliwa au angalau ingevumiliwa na hao waliojichagua wenyewe na kujiita wadhamini wa demokrasi. Lakini, kinyume kwa mapatano ya hekima, iliamua kufuata mlengo wa Ki-Islamu. Kisha wakaanzisha wito wa umoja wa Ki-Islamu. Kwa kusimama dhidi ya wale wote walio kinyume na Uislamu bila kujisalimisha kwa yoyte isipokuwa kwa Allah (s.w.t.), Ayatullah Khomeini na Uongozi wa Irani walipata upendo mkubwa usioshindika katika Ummah wa Ki-Islamu Ulimwenguni kote, kuanzia Morocco mpaka Phillipines na kutoka Ulaya mpaka Marekani. Watu waliokanyagwa wakaona kwa macho yao kwamba, watu wasio na silaha mikono mitupu wameishinda milki yenye nguvu sana za kivita katika Mashariki ya kati. Iliwapa moyo mpya watu wanao onewa hata katika nchi zisizo za Ki-Islamu, kama Afrika ya kusini. Kwa kuenea upesi kwa mawazo ya Khomeini, kuliishitua Marekani “Bwana mwenye amri kubwa juu ya kabila zote za Magharibi (Ulaya)”. Walianza kupigana vita dhidi ya Irani kwa kupitia mawakala wao, kupitia vyombo vya habari na katika siasa.

Na kwa upande mwingine, wakawafanya wateja wao katika Saudi Arabia na Kuwait waamini kwamba mwito wa umoja wa Ki-Islamu ni hatari ya kifo ya falme zao. Kwa kuamrishwa na mabwana zao, Mawahhabi walianzisha vita kali ya propoganda za chuki dhidi ya

94

mawazo ya Khomeini, Iran na Ushi‘a. Kalamu za vibaraka zikaanza kutoa vitabu (vya kuvuruga), makala na vijitabu (vyenye kuelezea mambo ya Dini) dhidi ya Shi‘a, wakisema kwamba Shi‘a walikuwa mushrik, wanayo Qur’ani yao, na wanaamini kuwa Qur’ani hii waliyonayo Waislamu imebadilishwa na ni pungufu. Baadhi ya waajiriwa wao wakubwa walikuwa Ihsan Ilahi Zaheer nchini Pakistan na Manzoor Ahmad No’mani na Abul Hasan ‘Ali Nadwi nchini India. Wa mwisho kutajwa ni mtu wa ajabu. Kitambo kirefu kabla ya mapinduzi (ya Iran) alikuwa anaonekana kama shujaa wa umoja wa Uislamu. Alikuwa mwenyekiti wa Muslim Personal Law Board (chombo cha kusimamia sheria za Ki-Islamu) nchini India na mwanachuo wa Kishi‘a kama Naibu wake. Lakini na yeye vile vile alikuwa ni mpokeaji wa Zawadi za Faisal wa ukoo wa kifalme wa Saudia. Na haukupita muda likatokea tangazo lisemalo, “La si mashariki wala magharibi, Uislamu mzuri” lililotolewa kutoka Iran, kisha yeye mwenyewe akajiunga na kundi linalopinga umoja.

Inaonekana kwamba sauti zinazotoka kwenye midomo yao ni sauti za mabwana zao, na majambia ya mayahudi yanayochovywa kwanye damu za Waislamu hutumika kwa ajili ya kalamu zao.

Kitabu kilichoandikwa na mawakala hawa, kinaweza kuwa kimeandikwa kwa Urdu, Kiarabu au lugha nyingine yoyote, lakini baada ya miezi michache tu kitakuwa kimesha tafsiriwa katika lugha zote kubwa za ulimwengu wa Ki-Islamu, na kuvifanya vipatikane kila mahali, na vile vile kuvigawanya bure kwa Mahujaji (wanaokwenda kuhiji Makka).

Mawakala hawa wa Uislamu wa Kimarekani walioletwa ili kuficha ukweli, wanafanya hivyo ili kudhoofisha Iran na kuzuia mapinduzi ya Iran yasiweze kuwahamasisha “vijana wa Ki-Islamu”. Kama Abul Hasan ‘Ali Nadwi mwenyewe alivyokubali katika utangulizi wa kitabu kimoja. Lakini haya ndio ukweli makusudio ya mabwana zao Mayahudi-Wakristo maadui wa Uislamu? Hakika, “Siyo”. Wajanja wa Ki-Islamu wa Kimarekani, wamefukua baadhi ya hadithi za tahreef za Kishi‘a zilizozikwa ndani ya vitabu, kwa lengo kwamba Shi‘a watalipiza kwa kutangaza hadithi kama hizo zinazopatikana katika vitabu vya Sunni, na hivyo kuifanya Qur’an kuwa na kasoro, na imani

95

ya Uislamu katika ufunuo huo wa mwisho itakuwa imeharibika, matokeo ni Uislamu kukosa nguvu yake.

Maandishi haya ya kujitweza yatawapatia wahubiri wa Kikristo silaha imara za kutikisa na kutatanisha imani ya Uislamu juu ya Qur’an. Wana matumaini kwamba, kwa njia hii Waislamu wengi watashawishika kuukubali Ukristo na hata wale ambao hawatabakilika (kubatizwa) hawatabakia kuwa Waislamu wa kweli, wala hawatafuata kitabu ambacho usahihi wake unatiliwa mashaka.

Inasemekana kwamba Glandstone wakati mmoja alisimama ndani ya Bunge (la Uingereza) na nakala ya Qur’an mkononi mwake na akatamka kwamba, “Maadamu Waislamu wanafuata kitabu hiki basi Waingereza hawataweza kuwatawala”. Aliwashauri watu wake kutumia kila hila kutikisa imani ya Waislamu ndani ya Qur’ani.

Mwenendo huu wa kikafiri umefanikiwa nchni Uturuki, Misri, Tunisia, Alegeria na nchi nyingi zinazojiita za Kiislamu ambako mbegu maalumu (chotara) ya Waislamu mbali mbali imeanguliwa ambayo inaonekana kuwa mbaya (yenye madhara) kwa Uislamu na Qur’an. Mbegu hii ilikuwa karibu ifanikiwe nchini Iran vile vile kwa hisani ya utawala wa Pahlavi. Lakini mpango huu ulishindwa, kwa sababu ya viongozi wa dini chini ya uongozi wa marehemu Ayatullah al-‘Uzma Khomeini, na kwa sababu ya imani ya dini waliyokuwa nayo Ummah wa Iran. Sasa maadui wa Uislamu wanatumia propaganda hii ya tahrif kufanikisha lengo lao hilo.

Hivi ndivyo walivyopanga. Lakini Allah (s.w.t.) anasema:-“Wanataka kuzima nuru ya Allah kwa vinywa vyao, na Allah atakamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia.”132

Kwa Ujumla, Mawahhabi wanapinga umoja wa Uislamu ambao Al-lah ameusisitiza sana, na wamewafanya Mayahudi na Wakristo kuwa marafiki na wasaidizi wao kitendo ambacho Allah amekikemea sana, na hivyo katika sehemu nyingi, kukikataza.

132 Qur’an, 61:8.