Upload
others
View
3
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
iUwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
Je, Watoto Wetu Wanajifunza?Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki
Agosti 2012
ii Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
Hakimiliki: Uwezo & Hivos/Twaweza, 2012.
Sehemu yoyote ya chapisho hili inaweza
kunakiliwa kwa namna nyingine yoyote
kwa madhumuni yasiyo ya kibiashara kwa
kuzingatia kuwa chanzo kitatajwa na nakala
mbili zitumwe kwenda kwenye anwani iliyopo
hapa chini.
Uwezo Afrika Mashariki ilipo Twaweza
Barabara ya Lenana, ACS Plaza ghorofa ya 3,
S.L.P 19875 00200 Nairobi, Kenya
Simu: +254 203861372/3/4
Barua pepe: [email protected]
1Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
Shukrani 2
Muhtasari 3
Utangulizi 4
Tafiti za Uwezo 6
Matokeo Muhimu 10
Hitimisho 21
VIAMBATISHO
KIAMBATISHO A 24
KIAMBATISHO B 25
KIAMBATISHO C 26
KIAMBATISHO D 27
KIAMBATISHO E 28
KIAMBATISHO F 29
YALIYOMO
2 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
Uwezo ni sehemu ya Twaweza, ambayo ni asasi huru ya Afrika Mashariki inayokuza upatikanaji wa taarifa kwa watu, kuwawezesha wananchi kuchukua hatua pale walipo na kuboresha matokeo ya utoaji huduma katika eneo lote la Afrika Mashariki. Data kwa ajili ya ripoti hii zilikusanywa kwa ushirikiano na Asasi ya wanawake Watafiti
wa Elimu ijulikanayo kama “Women’s Education Reseachers of Kenya (WERK)” wakiongozwa na John Mugo, Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) ukiongozwa na Suleman Sumra na Jukwaa la Taifa la Asasi zisizo za kiserikali la Uganda-the Uganda National NGO Forum (UNNGOF) likiongozwa na Richard Ssewakiryanga.
Ripoti hii imeandaliwa na kuwekwa pamoja na Sam Jones, ambaye pia ametumia umakini mkubwa katika kuhakiki usahihi wa data zilizotolewa humu. Youdi Schipper wa Uwazi-Twaweza alitoa msaada wa kiufundi na kiuchambuzi. John Mugo, Benjamin Piper and Njora Hungi walitoa ushauri wa kina ambao umezingatiwa sana kuboresha ripoti hii. Msaada wa uhariri ulitolewa na Hannah-May Wilson na Mtemi Gervas Zombwe. Kazi ya kutafsiri ripoti hii imefanywa Robert Sizya. Mwongozo wa jumla na kuhakiki ubora ulitolewa na Sara Ruto na Rakesh Rajani.
Kazi za Uwezo na Twaweza zinachangiwa na wafadhili makini na wapenda maendeleo, wakiwemo Mfuko wa Hewlett, DFID, Sida, SNV, Hivos na Banki ya Dunia. Matokeo na mapendekezo yaliyomo humu kimsingi hayawakilishi maoni ya yeyote kati ya washirika hawa.
Data zote zilizotumika katika ripoti hii zimechukuliwa kutoka kwenye ripoti ya Uwezo 2011 na tafiti za kitaifa zilizofanyika hapo awali na zinaweza kupatikana kwenye tovuti yetu ya www.uwezo.net.
Shukrani
3Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
Muhtasari
Ripoti hii inajumuisha, inalinganisha na inawasilisha muhtasari wa taarifa za matokeo ya utafiti wa kitaifa wa Uwezo 2011 wa nchi za Kenya, Uganda na
Tanzania bara. Tafiti hizi ni tafiti kubwa zaidi za aina yake kuwahi kufanyika Afrika. Yapata watoto 350,000 katika kaya zaidi ya 150,000 katika maeneo ya nchi hizi tatu walipimwa uwezo wao katika stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu kwa ngazi ya darasa la pili. Darasa la 2 linawakilisha ngazi ya chini ya umahiri unaotarajiwa baada ya mtoto kumaliza miaka miwili ya elimu ya msingi.
Jambo kubwa lililogundulika ni kwamba licha ya mafanikio makubwa katika kupanua wigo wa upatikanaji wa elimu ya msingi, ujuzi halisi katika kusoma na kuhesabu umebaki kuwa duni nchi zote za katika ukanda huu. Japokuwa watoto kwa sasa wameandikishwa shuleni kwa idadi kubwa mno kuliko awali, lakini hawajifunzi stadi za msingi zinazotarajiwa wajifunze katika ngazi za madarasa yao na katika umri wao. Kwa kubainisha, tathmini za Uwezo zimegundua kwamba:
(a) Zaidi ya watoto wawili kati ya kila watoto watatu walioandikishwa katika ngazi ya Darasa la 3 Afrika Mashariki walishindwa kufaulu majaribio ya kawaida ya Kiingereza, Kiswahili na Hesabu yaliyotungwa kwa kiwango cha ngazi ya Darasa la 2;
(b) Kuongezeka kwa ubora katika stadi za msingi za kusoma na kuhesabu kunaongezeka polepole sana wakati watoto wanapopanda madarasa katika mfumo wa elimu, ikimaanisha kwamba ubora wa kujifunza umebaki kuwa duni kwa ngazi zote za shule ya msingi;
(c) Ziko tofauti kubwa za wastani wa ufaulu wa majaribio miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki. Ingawa matokeo ya jumla kwa ngazi zote ni duni, wanafunzi wa Kenya wanafanya vizuri zaidi katika kusoma na kuhesabu. Watoto wa Uganda wanafanya vibaya zaidi katika ngazi za chini lakini polepole wanashika kasi na kuwapita watoto Wakitanzania wanapofikia ngazi ya darasa la 6 na kuendelea;
(d) Kuna tofauti za msingi kwenye ufaulu wa majaribio miongoni mwa wilaya na wilaya katika nchi zote za Afrika Mashariki, huku kukiwa na tofauti kubwa katika nchi na nchi kwa nchi zote tatu;
(e) Kuna tofauti ndogo za ufaulu wa majaribio kati ya wavulana na wasichana: tofauti za kijinsi hazionekani kuwa kubwa katika miaka ya mwanzoni ya elimu;
(f) Maskini wanafanya vibaya kila mahali; watoto wanaotoka katika kaya zenye hali duni kiuchumi na kijamii hufanya vibaya katika majaribio yote na katika umri wa rika lolote; na
(g) Wanafunzi wanaosoma katika shule binafsi (zisizo za serikali) wanafanya vizuri zaidi kuliko wanafunzi wanaosoma shule za umma (za serikali) katika nchi zote tatu, tofauti hii imeonekana zaidi Tanzania.
Matokeo haya yanaonyesha picha ya kutisha ya hali ya elimu katika Afrika Mashariki, na yamekuwa yakikosolewa na baadhi ya watu eti yanaleta jina baya katika maendeleo ya elimu. Methodolojia ya Uwezo, muundo wa sampuli, zana zetu na mchakato mzima vimekuwa vikifanywa kwa mashauriano na wataalam wa kitaifa na kimataifa, na kuhakikiwa kwa umakini. Maelezo ya kina kuhusu methodolojia na mkusanyo kamili wa data pia vinapatikana kwa wote. Ukweli wa kwamba matokeo ya utafiti ya mwaka 2011 kwa sehemu kubwa yanaendana na yale ya utafiti wa mwaka 2009/10 unazidi kuonyesha kwamba methodolojia na menejimenti ya Uwezo ni thabiti, imara na inaaminika. Uwezo inakaribisha uchunguzi zaidi na changamoto zenye ushahidi wa msingi, kwa kuwa zitazidi kuimarisha utafiti.
Mwisho, japo matokeo ya utafiti yanatia wasiwasi, bado zipo sababu za kuwa na matumaini. Kwanza, sehemu zote Afrika Mashariki, Ziko baadhi ya shule na wilaya zinafanya vizuri licha ya kukabiliwa na vikwazo vya aina ileile sawa na sehemu zingine. Shule na jamii hizi zinajenga vyanzo muhimu vya ufumbuzi na majawabu ya jinsi ya kuboresha kujifunza kwa watoto. Pili, kuna dalili zinazoonesha wazi kuhama kwa mjadala wa umma na kuelekea kujikita kwenye ubora na matokeo ya kujifunza, na kuuliza maswali makini ambayo yanaweza kusaidia maamuzi ya kisera na kupata thamani kubwa kutoka katika uwekezaji uliopo sasa. Tatu, kidunia kunaongezeko la kufanyia majaribio uvumbuzi na ubunifu ili kuchochea kujifunza ambako kunaweza kuinufaisha Afrika Mashariki, tukichagua na kuamua kwa makini.
Fursa ya kumsaidia kila mtoto ili ajifunze ipo. Na ripoti hii ina lengo la kuwataarifu fursa hiyo.
4 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
Utangulizi
5Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
Mwanzoni mwa karne, mawaziri wa elimu kutoka katika nchi 100 duniani walionyesha dhamira ya dhati ya kutoa elimu bora ya msingi kwa watoto
wote, tena bure pasipo malipo kwenye Kongamano la Elimu la Dunia (World Education Forum) lililofanyika huko Dakar, Senegal.1
Hususan, wajumbe walikubaliana:“Kuhakikisha kwamba kufikia mwaka 2015 watoto wote, hasa wasichana, watoto walio mazingira magumu, na wale walioko katika makundi madogomadogo, wanaandikishwa bila malipo na kuhitimu elimu ya msingi yenye ubora.” (Lengo la 2)
Pia walidhamiria:“Kuboresha nyanja zote za ubora wa elimu na kuhakikisha masuala yote yahusuyo elimu yanaboreshwa ili matokeo ya kujifunza yanayotambulika na kupimika yafikiwe kwa wote, hasa katika kusoma na kuhesabu na stadi za msingi za maisha.” (Lengo la 6)
Maazimio haya yalipata mwitikio kote Afrika Mashariki, na kuleta ari mpya ya msisitizo kwenye elimu ya msingi. Kutokana na hayo, maendeleo makubwa yamefikiwa kwa kuongezeka uandikishwaji wa watoto katika shule za msingi katika ukanda mzima. Ushahidi kutoka katika tafiti mbalimbali za kaya, ikiwa ni pamoja na zilizoelezwa hapa, unaonesha kwamba hadi sasa hivi ongezeko la karibu 90% ya watoto wenye umri wa kwenda shule wameandikishwa katika shule za msingi nchini Kenya, Tanzania na Uganda (tazama kiambatisho A). Hata hivyo, licha ya mafanikio haya makubwa, kuna tatizo ambalo limeendelea kuongezeka, nalo ni kwamba watoto wako shuleni lakini hawajifunzi. Wakati upatikanaji wa elimu umeongezeka, ubora wa elimu inayotolewa umebaki kuwa palepale na kwa kweli unaweza ukawa umeshuka zaidi.
Tofauti na takwimu za uandikishwaji wa watoto shuleni, data zilizo wazi kwa wananchi kuhusu matokeo ya kujifunza kama vile stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu zinapatikana kwa nadra sana. Kiini cha hamasa inayochochea jitihada za Uwezo ni kuziba pengo hili, na kusaidia kuhamisha mlengo wa umma na sera kutoka kwenye vitendeakazi/nyenzo za kielimu kwenda kwenye matokeo ya kujifunza.
1 Mawaziri husika wa Elimu kutoka Uganda na Tanzania walishiriki mkutano huu. Kujua orodha nzima ya uwakilishi kwenye mkutano huu huko Dakar angalia: www.unesco.org/education/efa/wef_2000/listpartwef.pdf
1. Utangulizi
Tangu mwaka 2009, Uwezo imefanya utafiti mpana wa kitaifa katika kaya kupima na kutathmini hali halisi ya ujuzi katika stadi za msingi za kusoma na kuhesabu kwa watoto wenye umri wa kwenda shule sehemu zote nchini Kenya, Tanzania na Uganda. Kwa kigezo cha kuyafikia maeneo kijiografia, tafiti hizi zinawakilisha tafiti huru kubwa zaidi zilizopo leo zinazopima matokeo ya elimu katika nchi zote tatu.2
Lengo la ripoti hii ni kulinganisha na kuwasilisha muhtasari wa matokeo ya utafiti wa Uwezo wa awamu ya pili wa kutathmini hali ya ujifunzaji ambao ulifanyika mwaka 2011 nchini Kenya, Tanzania (bara), na Uganda. Ripoti hii imepangiliwa kama ifuatavyo: Sehemu ya 2 inawasilisha tafiti za Uwezo kwa kifupi; Sehemu ya 3 inawasilisha matokeo muhimu ya utafiti; Sehemu ya 4 ni hitimisho kwa ufupi. Habari zaidi pia zinapatikana kwenye viambatisho kadhaa (tazama kisanduku hapa chini).
Kiambatisho A kinatoa data mahususi zaidi za Afrika Mashariki
Viambatisho B, C na D vinatoa matokeo maalum ya nchi kwa wastani wa alama zilizofikiwa katika majaribio, zikiwa zimetofautishwa kimadarasa (ngazi) wanayosoma, ki-makundi madogo madogo ya watu na ki-wilaya.
Kiambatisho E kinatoa mifano ya majaribio ya kusoma na hesabu yaliyotumika katika utafiti.
Kiambatisho F kinatoa matokeo kamili ya nafasi za ufaulu kwa wilaya za Afrika Mashariki.
Mwisho, matokeo yaliyowasilishwa katika ripoti hii yanatofautiana kidogo ukilinganisha na ripoti maalum za kila nchi kwa awamu zote mbili za tafiti wa Uwezo. Hii ni kwa sababu data zimechujwa kikamilifu, uzani mpya wa sampuli umekokotolewa ili kuakisi kwa ukaribu sifa za kiwango cha idadi ya watu, na masahihisho yamefanyika kwa uchunguzi uliokosekana ili kuimarisha ulinganifu kwa kipindi fulani. Wakati makadirio yako tofauti kidogo, bado hakuna tofauti kubwa kiasi cha kutufanya tubadilishe ripoti zetu za awali.
2 “Huru” ina maana kwamba utafiti haukufanywa au kuchambuliwa na taasisi/wakala wa serikali(umma)
6 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
Taf iti za Uwezo
7Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
Tafiti za Uwezo za kupima matokeo ya kujifunza zilianza kufanyika Kenya mwaka 2009, ikafuatiwa na Tanzania na Uganda mwaka 2010. Tafiti hizi ziliunda duru ya
kwanza ya tafiti za Uwezo (na hapa, inatajwa kama “Uwezo 1”). Tafiti zilifanyika tena katika nchi zote tatu mwaka 2011 na kuwakilisha duru ya pili ya zoezi hili (na hapa, inatajwa kama “Uwezo 2”).
2.1 Maeneo yaliyofikiwa na tafitiDuru zote mbili, Uwezo 1 na Uwezo 2 zilitumia mbinu ambazo zilitoa uwakilishi wa kitaifa wa sampuli za kinasibu kwa idadi ya watu waliokusudiwa (watoto wenye umri wa kusoma shule ya msingi na kuendelea, ikiwemo watoto wenye umri wa miaka 16.) Hii inamaanisha kwamba takwimu zilizohesabika kutoka kwenye tafiti hizi zinaweza kutumika katika kufuatilia kiwango cha ufaulu na matokeo ya kujifunza katika ngazi ya kitaifa, na pia zinaweza kutumika katika kulinganisha wakati mwingine tena inapohitajika. Sampuli pia zinauwakilishi wa ngazi ya wilaya, ambayo ina maana kwamba ulinganishi unaweza kufanywa kati ya wilaya na wilaya ndani ya nchi na kati ya nchi na nchi.
Tofauti kuu kati ya Uwezo 2 na Uwezo 1 ni kwamba awamu ya pili ilifikia idadi kubwa ya wilaya katika kila nchi, na kaya na watoto wengi zaidi kwa ujumla. Faida kuu ya kufikia eneo kubwa zaidi maana yake ni kuongeza usahihi kwenye matokeo, inatuwezesha sisi kuchunguza tofauti ya matokeo kati ya wilaya moja moja nyingi zaidi. Jedwali la 1 linatoa maelezo ya jumla ya maeneo yaliyofikiwa katika duru zote mbili katika kila nchi. Kuongezeka kwa maeneo yaliyofikiwa kati ya Uwezo 1 na Uwezo 2 ni kubwa; idadi ya wilaya zilizochaguliwa imepanda kutoka kwenye 38% hadi 90% ya wilaya zote katika ukanda (sasa inajumuisha wilaya zote za Tanzania bara na Uganda) na idadi ya watoto waliofikiwa imeongezeka maradufu (kwa kuchukua nchi zote tatu pamoja). Katika nchi zote mbili Tanzania na Uganda ambazo zilikuwa na idadi ndogo ya maeneo yaliyochaguliwa katika awamu ya kwanza ukilinganisha na maeneo yaliyochaguliwa Kenya, idadi ya watoto waliopimwa imekuwa karibu mara tatu zaidi. Hii inafanya tafiti za Uwezo kuwa moja ya tafiti zenye sampuli kubwa zaidi kuwahi kufanyika katika ukanda huu.
2. Taf iti za Uwezo
Nchi Duru Wilaya % Shule Vijiji Kaya Watoto
Kenya1 (Sept/Okt 2009) 70 44 2,029 2,029 33,760 79,693
2 (Feb/Mach 2010) 122 77 3,474 3,628 55,843 131,971
Tanzania1 (Mei 2010) 38 32 1,010 1,077 18,952 37,683
2 (Mach/Apr 2011) 119 100 3,709 3,825 59,992 114,761
Uganda1 (Aprili 2011) 27 34 748 792 12,412 32,882
2 (Apr/Mei 2011) 79 99 2,115 2,360 35,481 101,652
JumlaUwezo 1 135 38 3,787 3,898 65,124 150,258
Uwezo 2 320 90 9,298 9,813 151,316 348,384
Vidokezo: safu zote (ukiacha safu ya Nchi, Duru, ‘%’) zinataja idadi ya vitu vilivyofanyiwa sampuli na kubakia katika kundidata baada ya kuchujwa; safu ya ’%’ inahusu idadi ya wilaya katika sampuli kati ya wilaya zote katika nchi; idadi ya shule zilizofanyiwa sampuli mara nyingi ni pungufu kidogo kuliko idadi ya maeneo ya kuhesabia (vijiji) kwa kuwa si maeneo yote ya kuhesabia yanakuwa na shule ndani yake.
Chanzo: data zimekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 1 na Uwezo 2.
Jedwali la 1: Maeneo yaliyofikiwa wakati tafiti za Uwezo 1 na Uwezo 2
8 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
Mbinu ya utafiti wa Uwezo imechukuliwa kutoka katika shirika lijulikanalo kwa lugha ya kiingereza kama “the Annual Status of Education Report (ASER – tazama www.asercentre.org) ikimaanisha Ripoti ya Mwaka ya Hali ya Elimu. Kama ilivyo Uwezo, ASER ni tathmini ya mwaka ya kitaifa ya kupima uwezo wa watoto wenye umri kati ya miaka 6-16 katika kusoma na kuhesabu. Katika matokeo yaliyotolewa mwezi Januari 2012, ASER waliandika kuwa wamefanya tathmini katika wilaya 558 na kuzifikia shule 14,283, kaya 327,372 na kuwapima watoto 633,465 nchini India.
2.2 Muundo wa Utafiti wa UwezoManeno machache ya kitaalam yamewekwa katika mpangilio kuhusu muundo wa tafiti za Uwezo, pia jinsi gani matokeo yanapaswa kutafsiriwa (ufafanuzi wa kina zaidi wa masuala haya unaweza kupatikana katika ripoti yetu ya kitaalam). Kwanza, tafiti zote zimefuata ngazi tatu za hatua za uchaguzi sampuli kinasibu, kwa kufanya: (1) uchaguzi wa wilaya (sehemu) kwa uchaguzi sampuli rahisi wa kinasibu, huku kila wilaya imepewa welekeo sawa wa kuchaguliwa; (2) uchaguzi wa maeneo ya kuhesabia (vijiji) kuendana na uwiano wa ukubwa wa idadi ya watu; na (3) uchaguzi wa kaya katika kila eneo la kuhesabia kwa uchaguzi sampuli uliopangiliwa. Muundo huu unahakikisha kuwa utafiti ni kiwakilishi cha kitaifa na wilaya kwa watoto wote wenye umri kati ya miaka 6 na 16 (au miaka 7 na 16 kwa Tanzania) na watu gani ni wakazi katika kaya wakati wa utafiti (ukiacha wanaoishi katika taasisi). Uzani wa sampuli umekokotolewa kuendana na muundo wa sampuli na kujumuisha marekebisho yaliyokwishafanyika hapo mwanzo ili kuhakikisha uzani sahihi wa tofauti za umri uliofikiwa katika utafiti.
Pili, kwa kuzingatia mahesabu ya takwimu zilizowasilishwa hapa, uzani wa sampuli umetumika kote. Pale ambapo data zimekusanywa kutoka katika nchi zote tatu matokeo yanapimwa kwa ukubwa wa idadi kamili ya watu wa nchi hizi. Ukiweka kiutofauti, matokeo yaliyokusanywa yanaweza kusomwa kama wastani makadirio ya mtoto wa Afrika Mashariki (yaani, ambayo yamechaguliwa kinasibu kutoka Kenya, Tanzania au Uganda). Kutokana na ukubwa wa sampuli uliotumika katika duru zote za utafiti, hakika, tofauti zote katika makadirio kwa kila takwimu zilizotolewa katika makundi madogo madogo zina umuhimu kitakwimu katika ngazi za kawaida.
Mwisho, kumbuka kitu cha kuzingatia kuhusu jinsi ya kusoma matokeo kutoka kwenye majaribio ya kusoma na hesabu yaliyotumika katika tafiti za Uwezo. Kusema kwa dhati, alama za majaribio zilizofikiwa zinatoa makisio lakini haikosi kuwa huu ndiyo uthibitisho kamili wa ‘uwezo halisi’ wa watoto
au kiwango cha maendeleo yao katika kujifunza. Kama ilivyosemwa katika Uwezo mwaka 2010:33 “ili kutathmini kujifunza, kiwango cha mabadiliko, mtu atahitaji kudhibiti maarifa ya watoto tangu wanapoanza maisha ya kujifunza shuleni kwa Kenya, Uganda na Tanzania”. Katika uwasilishaji wa matokeo yetu kipekee tunajikita kwenye viwango vya ufaulu katika majaribio ya kusoma na kuhesabu.
Tunafanya hivyo kwa sababu kupima viwango hivi vya ufaulu kuna uhusiano wa moja kwa moja kuhusu matakwa ya mtaala na sera – watoto walioandikishwa katika ngazi ya darasa la tatu au zaidi wanapaswa kufaulu majaribio yaliyoandaliwa kwa ngazi ya darasa la 2. Sehemu ya watoto wanaoshindwa kufikia kiwango hiki wanaonesha pengo lililopo katika kujifunza. Kuongezeka kwa ukubwa wa pengo hili ndiyo msingi wa motisha wa tafiti za Uwezo, na tunaendeleza shabaha yetu dhahiri kwenye Nyanja hii katika ripoti yetu ya sasa.
2.3 Majaribio ya Kusoma na KuhesabuMaudhui ya tafiti za Uwezo yameelezwa katika ripoti maalumu ya kila nchi na kwenye tovuti ya Uwezo. 4Kwa kila kaya iliyotembelewa, vifungu vya maswali kadhaa viliulizwa kwa mkuu wa kaya ili kukusanya taarifa za msingi kuhusu kaya hiyo (kwa mfano, idadi ya wakazi na umiliki wa rasilimali kwa kila kaya). Pamoja na hayo, jaribio fupi la kusoma na kuhesabu lilitolewa kwa kila mtoto katika kaya hiyo mwenye umri wa kati ya miaka 6 na 16.
Wakusanya taarifa pia walijaza taarifa za kina zaidi kumhusu kila mtoto ikiwemo zinazoeleza kama anakwenda shule na anasoma darasa la ngapi. Jaribio la kusoma linalopima ujuzi wa kusoma na ufahamu katika lugha ya Kiingereza lilifanyika. Katika nchi zote tatu, lugha ya Kiingereza inafundishwa kama somo kuanzia darasa la 1 na hakika ni lugha inayotumika katika mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi kwa Kenya na Uganda. Pamoja na hayo, kwa Tanzania na Kenya (lakini si kwa Uganda) jaribio jingine la kusoma lilifanyika katika Kiswahili. Katika majaribio haya ya stadi za kusoma, watoto waliulizwa kutambua herufi kutoka katika alfabeti, kusoma neno, kusoma aya, na kusoma na kuelewa hadithi fupi.
Katika majaribio ya hisabati, watoto waliulizwa kutambua namba na kuhesabu, na pia kufanya hesabu za msingi. Hapa chini ni mfano wa majaribio wakati Kiambatisho E kinaonyesha seti kamili ya majaribio kwa kila nchi ya kusoma (Kiingereza na Kiswahili) na majaribio ya hisabati yaliyotumika katika duru ya utafiti wa Uwezo 2011.
3 Uwezo 2011. Je, Watoto Wetu Wanajifunza? Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki. www.uwezo.net
9Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
Majaribio yote yaliandaliwa kwa kufuata mtaala wa ngazi ya Darasa la 2 kwa kila nchi, ambao ni kiwango kinachotarajiwa kufikiwa baada ya mtoto kutimiza miaka miwili ya elimu ya msingi. Hivyo basi, ili kuthibitisha kwamba viwango bora vya elimu vinazingatiwa, mtu angetarijia kwamba wanafunzi wote wanaosoma Darasa la 3 au zaidi waweze kujibu maswali yote kwa usahihi kabisa. Hii inatajwa kama ‘kufaulu’ katika uwasilishaji wa matokeo hapa chini. Majaribio yanaakisi mtaala wa taifa wa kila nchi. Kutokana na tofauti za msisitizo katika mitaala ya kitaifa, majaribio yaliyotumika katika tafiti siyo kwamba yanalingana kabisa.
Kwa hiyo, hayawezi kulinganishwa kwa usawa kabisa – kwa maana ya ngazi ya “kufaulu” kwa Kenya sio lazima iwe sawa na ngazi ya “kufaulu” kwa Tanzania. Hivyo ripoti hii inapaswa kutazamwa kama kipimo cha uwezo wa watoto wa ngazi ya Darasa la 2 kwa mujibu wa mtaala wa nchi yao. Hii haijalishi uchambuzi wa majaribio unaonesha kwamba yanafanana zaidi kuliko kutofautiana kwake. Ngazi katika jaribio la kusoma hazibadiliki, wakati tofauti chache tu zipo kwenye jaribio la hisabati katika nchi zote tatu. Ili kusaidia kuonesha ulinganifu katika nchi zote tatu, ni maswali yanayofanana tu katika tafiti zote ndiyo yamejumuishwa katika matokeo ya pamoja ya ujuzi wa kusoma na kuhesabu. Kwa mfano, kwa kuwa madaraja ya kufaulu hayatolewi kwa ngazi ya Darasa la 2 nchini Tanzania, data hizi hazijawasilishwa katika uchambuzi huu.
Jedwali la 2: Sampuli ya Majaribio ya Uwezo Afrika Mashariki mwaka 2011
10 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
Matokeo Muhimu
11Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
Kulingana na matokeo ya Uwezo 1 (angalia Ukweli namba 8), Uwezo 2 inathibitisha kwamba ujuzi wa stadi za kusoma na kuhesabu kwa watoto wa shule za msingi ni duni katika eneo lote la ukanda wa Afrika Mashariki. Kielelezo cha 1, ambacho kinabeba nchi zote tatu kwa pamoja, kinaonesha asilimia ya watoto wa shule ya msingi walioandikishwa katika ngazi ya Darasa la tatu ambao wanaweza kufaulu kila jaribio kati ya majaribio matatu yaliyoandaliwa kwa kiwango cha ngazi ya darasa la 2 yaliyojumuishwa katika dodoso la utafiti4. Pamoja na hayo, kielelezo pia kinaonyesha asilimia ya wanafunzi wa Darasa la 3 katika ukanda ambao walifaulu majaribio yote mawili, la maswali ya kusoma katika lugha yao ya taifa ya kufundishia (Kiingereza kwa Kenya na Uganda; Kiswahili kwa Tanzania) na maswali ya (kawaida) ya hisabati – maana yake, hii inapima uwiano wa walioweza kufaulu majaribio yote mawili kwa pamoja.5
4 Data maalum za kila nchi za viwango vya kufaulu majaribio zimetolewa kwenye Viambatisho B, C na D..
5 Maswali ya kawaida ya ujuzi wa kuhesabu ni yale yaliyojumuishwa kwenye majaribio katika kila nchi na kila duru ya utafiti. Yako (kwenye mpangilio wa kuongezeka kwa ugumu): Kutambua namba; Kujumlisha; Kutoa; na kuzidisha.
Kielelezo hiki kinaonyesha kwamba wanafunzi wachache sana walioandikishwa katika Darasa la 3 wanaweza kufaulu kila moja ya majaribio. Kiuhalisia, ni pungufu kidogo ya mmoja kati ya watoto watatu waliweza kufaulu jaribio la Kiswahili (31%) na majaribio ya hisabati (29%), lakini ni mmoja tu kati ya sita alifaulu jaribio la Kiingereza (16%). Vivyo hivyo, ni pungufu ya mmoja kati ya watoto sita aliweza kufaulu majaribio yote mawili ya kusoma na kuhesabu kwa pamoja (15%). Matokeo haya yanaonyesha kwamba kundi kubwa zaidi la wanafunzi hawapati ujuzi mahiri wakati wa kipindi cha miaka ya mwanzoni katika shule za msingi kama inavyotarajiwa katika mitaala ya kitaifa.
3. Matokeo Muhimu
Matokeo haya yanaonyesha kwamba kundi kubwa zaidi la wanafunzi hawapati ujuzi mahiri wakati wa kipindi cha miaka ya mwanzoni katika shule za msingi kama inavyotarajiwa katika mitaala ya kitaifa.
Kiswahili
Ukweli wa 1: Ni chini ya theluthi moja ya watoto Afrika Mashariki wana ujuzi wa kusoma na kuhesabu.
Kielelezo cha 1: Viwango vya kufaulu majaribio kwa watoto walioandikishwa katika Darasa la 3, Afrika Mashariki yote
Vidokezo: “Kwa pamoja” inamaanisha kufaulu maswali ya majaribio yote mawili, (ya kawaida) jaribio la hisabati na maswali ya jaribio la kusoma.
Chanzo: data zimekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 2.
% y
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi
Kiingereza Kwa pamojaHisabati
12 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
Je, matokeo haya duni yanaendelea kuwepo katika ngazi zote za shule ya msingi? Kielelezo cha 2 kinaonyesha viwango vya kufaulu kwa kila jaribio kwa watoto walioandikishwa madarasa ya ngazi za juu zaidi ya Darasa la 3. Kielelezo kinaonyesha kwamba kadri watoto wanavyoendelea mbele katika mfumo wa shule kwenda madarasa ya juu zaidi, viwango vya kufaulu pia vinaendelea kuongezeka kwenye majaribio yote ya ngazi ya Darasa la 2. Hili linatuonyesha kwamba watoto wanajifunza na kupata baadhi ya stadi za msingi, japokuwa si katika wakati uliotarajiwa kama ulivyopangwa na mtaala. Kiwango kikubwa zaidi cha kujifunza kinatokea katika ngazi za juu za shule ya msingi kati ya Darasa la 4 hadi la 5, na Darasa la 5 hadi 6 ikionyesha kwamba watoto wengi wanapata ujuzi wa ngazi ya Darasa la 2 katika miaka ya mwishoni mwa elimu ya msingi.
Kutokana na ngazi ya chini ambayo majaribio yanaandaliwa, inaonyesha kwamba viwango vya kufaulu vinaongezeka polepole sana. Kwa mfano, katika Darasa la 4, yapata nusu tu ya wanafunzi wanaweza kufaulu jaribio la Kiswahili huku viwango vya kufaulu viko chini zaidi katika hisabati na Kiingereza. Ni katika Darasa la 7 tu ndiyo kuna zaidi ya theluthi mbili ya watoto waliofaulu kila jaribio. Hii inaonyesha kwamba ujuzi madhubuti wa watoto wengi katika kusoma na kuhesabu umebaki kuwa chini katika ngazi zote za shule ya msingi. Hofu nyingine ni kwamba idadi kubwa ya watoto wanaojiandaa kufanya mitihani yao ya mwisho ya kitaifa hawajawa na ujuzi katika stadi za msingi za kusoma na kuhesabu.
Kiwango kikubwa zaidi cha kujifunza kinatokea katika ngazi za juu za shule ya msingi kati ya Darasa la 4 hadi la 5, na Darasa la 5 hadi 6 ikionyesha kwamba watoto wengi wanapata ujuzi wa ngazi ya Darasa la 2 katika miaka ya mwishoni mwa elimu ya msingi.
Matokeo ya utafiti duru mbili za zilizopita yamerejewa kwenye matokeo ya ukanda mzima wa Afrika Mashariki. Hata hivyo, ziko tofauti ndogondogo kwa Kenya, Tanzania na Uganda kwa kuzingatia ujuzi katika stadi za kusoma na kuhesabu (matokeo ya majaribio) ya watoto wenye umri wa kwenda shule. Hii imeoneshwa katika kielelezo cha 3, kinachoonesha asilimia ya watoto wenye umri wa miaka kati ya 10 na 16 ambao wanaweza kufaulu kila jaribio (Kiingereza, Kiswahili
na Hisabati), pia majaribio yote ya kusoma na kuhesabu yakijumuishwa pamoja.
Kielelezo kinaonesha kwamba watoto wa Kenya wamefaulu zaidi kuliko watoto wengine wa nchi za Afrika Mashariki katika majaribio yote. Hii inaonekana wazi zaidi katika majaribio ya kusoma. Kiwango cha kufaulu cha watoto wa Kenya katika somo la Kiingereza ni zaidi ya mara mbili ya
Ukweli wa 2: Watoto wawili katika kila watoto 10 wa Darasa la 7 katika Afrika Mashariki hawana ujuzi wa ngazi ya Darasa la 2 katika kusoma na kuhesabu.
Ukweli wa 3: Kuna tofauti kubwa miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki
Kielelezo cha 2: Viwango vya kufaulu majaribio kwa Madarasa kwa watoto walioandikishwa shule, Afrika Mashariki yote kwa pamoja
Vidokezo: namba zilizoko kwenye mhimili mlalo zinataja darasa la 4 na la 7 shule ya msingi. Pia kumbuka kwamba matokeo ya Kiswahili yamejumuisha Kenya na Tanzania tu.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 2.
% z
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi
HisabatiKiingereza Kiswahili
13Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
watoto wa Tanzania (ni asilimia 39 zaidi), na asilimia 29 zaidi ya watoto wa Uganda. Matokeo haya yanaweza kuonesha madhara ya lugha zinazotumika kufundishia kama Kiingereza kinatumika kwa mapana zaidi katika ngazi zote za shule ya msingi. Hata hivyo, hata katika jaribio la Kiswahili, ambacho kinazungumzwa sana Tanzania kuliko Kenya, Wakenya wamefanya vizuri -20% zaidi ya watoto wa Kenya wenye umri wa miaka 10-16 wanafaulu vizuri jaribio la Kiswahili kuliko watoto wa Tanzania. Tofauti iliyopo miongoni mwa nchi hizi tatu ni ndogo sana katika jaribio la hesabu ingawa hata huko nako wanafunzi wa Kenya wanafanya vizuri (kwa wastani) kuliko watoto wa nchi nyingine.
Pointi mbili za ziada zinaweza kusemwa. Kwanza, ikumbukwe kwamba kufaulu vizuri zaidi kwa wanafunzi wa Kenya kunaendana tu na wanafunzi wa nchi nyingine. Kwa ujumla, suala linabaki palepale kwamba katika ngazi ya Darasa la 3 karibu theluthi moja ya wanafunzi wa Kenya (na wanafunzi wachache zaidi wa Tanzania na Uganda) wanaweza kufaulu jaribio la ngazi ya Darasa la 2.
Pili, wakati Kielelezo cha 3 kinaonesha kwamba watoto wa Uganda wanafanya vibaya zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki (isipokuwa katika jaribio la Kiingereza), ziko tofauti ndogo sana kati ya Tanzania na Uganda kama mtu ataangalia ufaulu wa majaribio kwa kila Darasa (angalia Kiambatisho
B hadi D)6 Wanafunzi wa Uganda wanafanya vibaya kwa kulinganisha ngazi za madarasa ya chini, lakini wanaonesha kasi ya kuongeza ufaulu katika ngazi za juu. Kwa mfano, idadi ya watoto wa Uganda ambao wanafaulu katika kusoma na kuhesabu (kwa pamoja) iko chini kuliko Kenya na Tanzania kwa Darasa la 1 hadi la 5. Hata hivyo, kuanzia Darasa la 6 na kuendelea, wanafunzi wa Uganda wanawazidi kidogo katika kufaulu wanafunzi wa Tanzania.
Hivyo, katika Darasa la 7, karibu 90% ya wanafunzi wa Kenya wanafaulu katika kusoma na kuhesabu, majaribio yote mawili (kwa pamoja), ambayo inalinganishwa na 80% ya wanafunzi wa Uganda lakini ni theluthi mbili tu (66%) ya wanafunzi wa Tanzania.
Maelezo yanayoweza kutolewa kuhusu kasi ya kupanda kwa wanafunzi wa Uganda ni matumizi makubwa ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia katika madarasa ya juu ya shule ya msingi (ambako kunaongeza kiwango cha kufaulu katika jaribio la kusoma Kiingereza Tanzania).7
6 Masuala haya pia yamejadiliwa kwa kina katika ripoti kubwa ya kiufundi (tazama www.uwezo.net)
7 High repetition rates in Uganda are indicated in external data sources, such as UNESCO (2011),Global Education Digest 2011: Comparing Educa-tion Statistics Across the World, Montreal: UNESCO Institute for Statistics
...kufaulu vizuri zaidi kwa wanafunzi wa Kenya kunaendana tu na wanafunzi wa nchi nyingine. Kwa ujumla, suala linabaki palepale kwamba katika ngazi ya Darasa la 3 karibu theluthi moja ya wanafunzi wa Kenya (na wanafunzi wachache zaidi wa Tanzania na Uganda) wanaweza kufaulu jaribio la ngazi ya Darasa la 2.
Kielelezo cha 3: Viwango vya kufaulu majaribio kwa watoto wenye umri wa miaka 10-16, kwa kila nchi
Vidokezo: mahesabu yanawahusu watoto wote (wawe wameandikishwa au hawajaandikishwa); “Kwa pamoja” inaonyesha ufaulu kwenye maswali ya aina zote mbili ya hesabu (za kawaida) na maswali ya kusoma katika lugha ya taifa ya kufundishia; jaribio la Kiswahili halikutumika kwa nchi ya Uganda.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 2.
% z
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi
Kiswahili Kwa pamojaKiingereza Hisabati
14 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
Ukweli wa 4: Ziko tofauti kubwa sana katika matokeo ya majaribio kati ya wilaya na wilaya ndani ya kila nchi
Tafiti za Uwezo zina uwakilishi katika ngazi ya wilaya katika kila nchi. Kwa hiyo, inafaa kujali kiwango ambacho ujuzi wa kusoma na kuhesabu unafautiana katika ngazi za wilaya. Hii inaweza kusaidia kubaini maeneo maalum (ya kijiografia) yanayofanya vizuri sana na yanayoshindwa kufanya vizuri ndani ya mfumo wa elimu, ambayo yana umuhimu mkubwa sana wa kuzingatiwa kisera kwa kuwa hali za ndani ya nchi zinatofautiana kati ya mikoa, kama inavyokuwa katika mgawo wa bajeti.
Ili kuchunguza kwa kina swali hili tulitafuta wastani wa kufaulu katika majaribio ya kusoma na kuhesabu kwa pamoja kwa watoto wenye umri wa miaka 10-16 katika kila wilaya. Baada ya hapo, katika kila nchi wastani huu wa viwango vya kufaulu ukapangwa kuanzia wa chini mpaka wa juu kabisa.
Jedwali la 3 limeorodhesha wilaya 10 bora zaidi na wilaya 10 dhaifu zaidi katika ukanda ambazo zinathibitisha kuwepo kwa tofauti kubwa sana kati ya wilaya na wilaya, na kati ya nchi na nchi. –wilaya kumi bora zote ziko Kenya (hasa ukanda wa Kati), wakati kumi dhaifu zaidi zote zinatoka Uganda (hasa ukanda wa Kaskazini).
Matokeo ya ngazi za wilaya pia yanafanya matokeo ya utafiti yawe na tofauti kubwa za ulinganifu katika kufaulu kati ya nchi hizi tatu. Kwa mfano, wilaya inayofanya vizuri zaidi nchini Uganda ilipata 72%, kiasi ambacho ni kikubwa kidogo tu ya kile cha kiwango cha kati cha kufaulu cha wilaya za Kenya.
15Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
Jedwali la 3: Muhtasari wa Wilaya zinazofanya vizuri zaidi na Wilaya zinazofanya vibaya zaidi katika Afrika Mashariki
Nafasi Nchi Mkoa Wilaya% ya ufaulu kwa pamoja
% za Uandikishaji
1 Kenya Central Thika West 92.1 90.7
2 Kenya Central Kikuyu 89.9 97.2
3 Kenya Nairobi Nairobi East 89.4 91.5
4 Kenya Central Nyeri South 88.2 95.7
5 Kenya Central Gatanga 86.9 96.7
6 Kenya Central Kirinyaga 86.7 96.7
7 Kenya Rift Valley Kajiado North 86.4 85.4
8 Kenya Eastern Imenti South 85.6 92.9
9 Kenya Central Ruiru 85.2 86.0
10 Kenya Central Gatundu 85.1 92.6
311 Uganda Northern Amuru 25.3 95.0
312 Uganda Northern Dokolo 23.3 95.7
313 Uganda Western Bundibugyo 22.7 95.3
314 Uganda Eastern Bugiri 22.1 96.9
315 Uganda Eastern Kaliro 20.6 88.0
316 Uganda Northern Amolatar 20.3 94.5
317 Uganda Northern Nakapiripirit 19.4 60.7
318 Uganda Northern Moroto 19.1 61.0
319 Uganda Northern Kaabong 16.9 60.3
320 Uganda Northern Kotido 9.7 40.8Vidokezo: mpangilio wa ngazi umetafutwa kwa kukusanya alama kutoka kwenye alama za majaribio walizopata katika kila wilaya kwa kila nchi; uandikishwaji shule unahusu shule za msingi na sekondari; sampuli zinawahusu watoto wa umri wa miaka 10-16 tu; “Kwa pamoja” inahusu kufaulu katika maswali ya kawaida ya jaribio la hisabati na maswali ya jaribio la kusoma katika lugha ya taifa ya kufundishia shule ya msingi.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 2.
Jedwali la 3a: Muhtasari wa Wilaya zinazofanya vizuri zaidi na Wilaya zinazofanya vibaya zaidi nchini Kenya
Nafasi Mkoa Wilaya% ya ufaulu kwa pamoja
% za Uandikishaji
1 Central Thika West 92.1 90.7
2 Central Kikuyu 89.9 97.2
3 Nairobi Nairobi East 89.4 91.5
4 Central Nyeri South 88.2 95.7
5 Central Gatanga 86.9 96.7
6 Central Kirinyaga 86.7 96.7
7 Rift Valley Kajiado North 86.4 85.4
8 Eastern Imenti South 85.6 92.9
9 Central Ruiru 85.2 86.0
10 Central Gatundu 85.1 92.6
113 Rift Valley Samburu North 41.3 62.9
114 Coast Tana Delta 40.7 84.0
115 Rift Valley Turkana South 40.5 69.2
116 North Eastern Lagdera 40.5 63.4
117 North Eastern Wajir East 37.1 78.8
118 North Eastern Wajir West 36.0 71.6
119 North Eastern Wajir North 35.2 66.2
120 North Eastern Ijara 33.9 58.0
121 Rift Valley Turkana Central 30.8 61.4
122 Rift Valley Samburu East 26.5 47.9“Kwa pamoja” inaonesha wastani wa kiwango cha kufaulu (kwa wilaya) kwenye maswali ya majaribio yote mawili la hesabu (za kawaida) na maswali ya jaribio la ujuzi wa kusoma Kiingereza; mpangilio wa nafasi kwenye ufaulu “wa pamoja”unatokana na kiwango cha kufaulu; uandikishwaji unahusu shule za msingi na sekondari; sampuli zinawahusu watoto wa umri wa miaka 10-16 tu.
Chanzo: imekokotolewa kwa kutumia data za Uwezo 2.
Jedwali la 3b: Muhtasari wa Wilaya zinazofanya vizuri zaidi na Wilaya zinazofanya vibaya zaidi nchini Tanzania
Nafasi Mkoa Wilaya% ya ufaulu kwa pamoja
% za Uandikishaji
1 Arusha Arusha 80.2 96.7
2 Iringa IringaMjini 78.5 89.1
3 Kilimanjaro Moshi Mjini 72.5 86.0
4 Kagera Bukoba Mjini 71.1 90.9
5 Kilimanjaro Rombo 70.2 93.9
6 Morogoro Morogoro Mjini 69.7 86.9
7 Dar es Salaam Temeke 68.8 78.6
8 Mbeya Mbeya Mjini 68.4 95.9
9 Tanga Tanga 66.4 95.7
10 Dar es Salaam Ilala 66.3 90.1
110 Shinyanga Kishapu 31.8 84.3
111 Shinyanga Kahama 31.7 80.3
112 Mtwara Mtwara Vijijini 30.6 82.3
113 Mara Serengeti 29.8 63.9
114 Kigoma Kibondo 28.6 73.1
115 Tanga Kilindi 28.2 83.1
116 Shinyanga Meatu 28.0 87.0
117 Mwanza Ukerewe 27.7 87.9
118 Dodoma Mpwapwa 27.7 81.7
119 Shinyanga Bariadi 25.4 73.8“Pamoja” inaonesha wastani wa kiwango cha kufaulu (kwa wilaya) kwenye maswali ya majaribio yote mawili la hesabu (za kawaida) na maswali ya jaribio la ujuzi wa kusoma Kiswahili; mpangilio wa nafasi umezingatia kiwango cha “pamoja” cha ufaulu; uandikishwaji shule unahusu shule za msingi na sekondari; sampuli zinawahusu watoto wa umri wa miaka 10-16 tu.
Chanzo: imekokotolewa kwa kutumia data za Uwezo 2.
Jedwali la 3c: Muhtasari wa Wilaya zinazofanya vizuri zaidi na Wilaya zinazofanya vibaya zaidi nchini Uganda
Nafasi Mkoa Wilaya% ya ufaulu kwa pamoja
% za Uandikishaji
1 Central Kampala 69.3 94.3
2 Central Wakiso 64.5 92.6
3 Western Mbarara 54.9 93.1
4 Western Bushenyi 52.3 95.6
5 Central Mityana 50.4 96.1
6 Western Kiruhuura 50.0 95.3
7 Central Nakaseke 49.6 95.8
8 Central Luwero 47.7 94.7
9 Western Ibanda 47.4 92.9
10 Central Nakasongola 46.7 97.4
70 Northern Amuru 25.3 95.0
71 Northern Dokolo 23.3 95.7
72 Western Bundibugyo 22.7 95.3
73 Eastern Bugiri 22.1 96.9
74 Eastern Kaliro 20.6 88.0
75 Northern Amolatar 20.3 94.5
76 Northern Nakapiripirit 19.4 60.7
77 Northern Moroto 19.1 61.0
78 Northern Kaabong 16.9 60.3
79 Northern Kotido 9.7 40.8“Pamoja” inaonesha wastani wa kiwango cha kufaulu (kwa wilaya) kwenye maswali ya majaribio yote mawili la hesabu (za kawaida) na maswali ya jaribio la ujuzi wa kusoma Kiswahili; mpangilio wa nafasi unatoakana na kiwango cha ufaulu cha pamoja”; uandikishwaji unahusu shule za msingi na sekondari; sampuli zinawahusu watoto wa umri wa miaka 10-16 tu.
Chanzo: imekokotolewa kwa kutumia data za Uwezo 2.
16 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
Katika baadhi ya wilaya zinazofanya vibaya, watoto wanahudhuria shuleni vizuri kwa uaminifu, hata ambapo hawana kitu kikubwa wanachoweza kuonesha kuwa wamejifunza shuleni.
Data zilizowasilishwa hapo juu zinaonesha mambo mawili zaidi. Katika baadhi ya wilaya, asilimia ya watoto waliofaulu jaribio la Uwezo iko juu kuliko idadi ya watoto walioandikishwa shule. Hii inaweza kumaanisha kwamba kuna idadi ya watoto ambao hawajaandikishwa shule, au wale ambao wanaweza kuwa wamemaliza elimu ya msingi lakini
hawakuendelea zaidi baada ya masomo shule ya msingi, wana ujuzi wa kusoma na kuhesabu katika wilaya zinazoonekana kufanya vizuri. Katika baadhi ya wilaya zinazofanya vibaya, watoto wanahudhuria shuleni vizuri kwa uaminifu, hata ambapo hawana kitu kikubwa wanachoweza kuonesha kuwa wamejifunza shuleni.
Jedwali la 4 linaonesha viwango vya kufaulu, asilimia kumi ya wilaya za mwisho kabisa (yaani ni viwango vya chini kabisa na vya juu kabisa vya asilimia kumi ya wilaya za mwisho), kiwango cha kati cha kufaulu, na kiwango kilichofikiwa cha viwango vya ufaulu cha asilimia kumi ya wilaya bora zaidi (maelezo ya kina zaidi yapo katika Kiambatisho cha 1). Data zinaonesha kwamba wilaya zenye ufaulu wa juu kabisa kwa Kenya zilipata kiwango cha ufaulu kati ya 84% na 92%; Tanzania wilaya za juu kabisa zilikuwa na wastani wa ufaulu cha kati ya 63% na 80%; ambapo Uganda, wilaya za juu kabisa zilipata wastani wa ufaulu kati ya 48% na 70%. Viwango vya kati vya ufaulu vinaonesha kwamba 50% ya wilaya zote za Kenya zilipata wastani wa ufaulu kuanzia 68%; hata hivyo, kwa Uganda, 50% ya wilaya (za kiwango cha kati) zilipata kiwango cha ufaulu cha 34% au pungufu yake.
Matokeo haya yana maanisha nini? Tofauti kubwa ya viwango vilivyofikiwa kwa wastani wa ngazi ya wilaya vinamaanisha kuwepo kwa utofauti wa kijiografia uliodhahiri katika kusoma na kuhesabu ndani ya kila nchi (ki-wilaya). Kwa maneno mengine, ujuzi tarajiwa wa kusoma na kuhesabu wa ‘wastani’ kwa wanafunzi katika kila wilaya unatofautiana kwa kutegemeana na maeneo wanakoishi. Kwa mfano, wilaya bora kabisa kwa ufaulu Tanzania, inapata wastani wa ufaulu waa 80% ukilinganisha na 25% katika wilaya inayofanya vibaya
zaidi, tofauti ya asilimia 55.8
Kwa nyongeza, matokeo haya yanaonesha maeneo kadhaa ya ubora na/au kushindwa katika kila nchi. Kwa Kenya, kiwango kilichofikiwa cha 10% ya wilaya za mwisho kinaonekana kiko juu, hii inaonesha kuwepo kwa idadi ndogo ya wilaya zinazofanya vibaya zaidi (nyingi ni wilaya za ukanda kame katika Bonde la Ufa na ukanda wa Kaskazini Mashariki, (tazama Jedwali 3a). Kiutofauti, japokuwa Tanzania na Uganda zote zina wilaya zenye alama za wastani wa chini sana, mtu atagundua kwamba kiwango kilichofikiwa cha 10% ya wilaya bora zaidi kinaonekana kikubwa.
Hii inaonesha kuwepo kwa idadi ndogo ya wilaya hasa zinazofanya vizuri katika nchi hizi, ambazo zinapatikana katika maeneo ya mijini yenye utajiri au wilaya zenye utajiri wa kilimo. Matokeo ya ngazi ya wilaya pia yanaonesha kuwepo kwa tofauti kubwa za kufaulu kati ya nchi na nchi. Kwa mfano, wilaya bora zaidi kwa kufanya vizuri Uganda ilipata wastani wa ufaulu wa 72%, ambayo ni mkubwa kidogo tu zcha wilaya zenye wastani wa kati nchini Kenya. Hii inamaanisha kwamba karibu nusu ya wilaya za Kenya zinazidi wastani wa ufaulu wa wilaya bora zaidi za Uganda.
8 Kama ilivyoelezwa kwa kina katika ripoti ya kiufundi kiwango cha ku-tokuwa sawa kijiografia kwenye matokeo ya kujifunza kiko juu Tanzania na chini zaidi Uganda, kikipimwa kwa kuangalia tofauti ya ufaulu kiwilaya
Jedwali la 4: Muhtasari wa wastani wa viwango vya kufaulu vya ngazi ya wilaya kwenye majaribio ya kusoma na kuhesabu kwa pamoja, kwa kila nchi
% y
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi
17Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
Sababu mbalimbali zinaweza kuhusishwa na uwepo wa tofauti hizi za ujuzi wa kusoma na kuhesabu miongoni mwa watoto wa Afrika Mashariki. Baadhi yake, ni hali ya maisha kijamii na kiuchumi inamchango mkubwa kuamua ujuzi wa mtoto. Mathalan, kaya zenye kipato cha juu zinaweza kumudu vizuri gharama za mahitaji ya vifaa vya ziada vya kujifunzia (kama vile vitabu na penseli) na pia haziwashirikishi sana watoto katika shughuli za kuzalisha kipato.
Katika kutafiti suala hili, kaya katika sampuli ziligawanywa katika makundi matatu ya hali za kiuchumi na kijamii kulingana na idadi ya maswali rahisi yaliyoulizwa – kama vile rasilimali za kudumu wanazomiliki, kama wana umeme na/au maji safi na salama, na kama mama katika kaya hiyo amepata elimu yoyote rasmi.9 Kwa hakika, huu pekee ndiyo uainishaji ghafi; hata hivyo, mtu ataona kuna tofauti kubwa kati ya makundi ya kiuchumi na kijamii katika matokeo ya kusoma na
9 Ili kuhakikisha kuna ulinganifu, aina tatu za makundi ya kiuchumi zimeta-jwa kwa namna ileile kwa kila nchi katika Ukanda wa Afrika Mashariki. Yaani, siyo makundi maalum ya ki-nchi.
kuhesabu. Hii imeonyeshwa katika kielelezo cha 5, ambacho kinaonesha asilimia ya watoto wenye umri wa miaka 10-16 katika kila kundi la kiuchumi na kijamii (kwa ukanda mzima), ambao wanaweza kufaulu majaribio yote mawili ya kusoma na kuhesabu (kwa pamoja). Kielelezo kinaonesha tofauti kati ya maskini na wasio maskini. Pengo kati ya maskini na wasio maskini ni pointi asilimia 18, wakati pengo kati ya fukara kabisa na wasio maskini ni alama asilimia 27. Hii ina maana kwamba watoto wengi kama mara mbili (karibu watoto 6 kati ya 10 wenye umri wa miaka 10-16) wanaotoka katika kaya zisizo maskini wanaweza kufaulu majaribio yote mawili ukilinganisha na watoto wanaotoka katika kaya fukara kabisa (karibu watoto 3 tu kati ya 10). Data hizi zinadhihirisha kwamba jitihada zinahitajika kwenye elimu ya umma kwa pande zote, ukweli ni kwamba fursa za kuendeleza ujuzi zinatofautiana sana katika Afrika Mashariki.
...jitihada zinahitajika kwenye elimu ya umma kwa pande zote, ukweli ni kwamba fursa za kuendeleza ujuzi zinatofautiana sana katika Afrika Mashariki.
Kielelezo cha 4 kinaonesha asilimia ya wavulana na wasichana wenye umri wa miaka 10-16 katika kila nchi ambao wanaweza kufaulu majaribio yote mawili kusoma na kuhesabu. Kwa nchi zote tatu, kielelezo kinathibitisha kuwepo kwa baadhi ya tofauti za kijinsia.
Kiuhalisi, kwa wastani, wasichana wanawazidi kidogo wavulana katika nchi zote tatu. Tofauti za viwango hivi ziko sawa katika alama za majaribio yote mawili ya kusoma na kuhesabu.
Ukweli wa 5: Kuna tofauti ndogo kati ya wavulana na wasichana katika ujuzi wao wa kusoma na kuhesabu
Ukweli wa 6: Watoto wanaotoka katika kaya maskini zaidi wanafanya vibaya kwenye majaribo katika umri wa rika zote.
Kielelezo cha 4: Viwango vya kufaulu katika majaribio ya kusoma na kuhesabu (kwa pamoja) kwa watoto wenye umri wa miaka 10-16, kwa vigezo vya kijinsia na ki-nchi
% z
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi
Wavulana Wavulana WavulanaWasichana Wasichana Wasichana
18 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
Pengo hili la kujifunza kati ya maskini na wasio maskini linaendelea pia kuonekana katika umri wa kila rika; yaani linaongezeka kwa kiwango cha juu sana. Hii inaonekana katika Kielelezo cha 6, ambacho kinaonyesha viwango vya kufaulu katika majiribio yote mawili pamoja kwa watoto wenye umri wa maalum (kuanzia umri wa miaka 7-16).
Mambo makubwa mawili yanajitokeza hapa. Kwanza, kiwango cha kufaulu cha wasio maskini kimeoneshwa na mstari wa juu (uliounganishwa na pembe tatu) mara zote huwa juu ya mistari mingine miwili, maana yake viwango vya ufaulu mara zote huwa viko juu kwa kundi hili. Katika umri wa miaka 10, kwa mfano, kiwango cha ufaulu miongoni mwa wasio maskini (33%) ni mara mbili ya kile cha maskini ambacho ni (16%) na ni mara tatu zaidi ya kile cha wale masikini zaidi kabisa ambacho ni (10%). Kwa wastani, uduni katika kujifunza utokanao na watoto kutoka katika kaya maskini, ukilinganisha
na watoto kutoka katika kaya zisizo maskini, ni unafanana kwa karibu miaka miwili (na hasa kwa kaya maskini zaidi). Hii ni kwa sababu katika umri wa miaka 12, karibu 34% ya watoto kutoka katika kaya zenye kipato kizuri wanafaulu majaribio yote mawili, ambayo ni sawa na kiwango cha ufaulu cha watoto wenye umri wa miaka 10 wanaotoka katika kaya zisizo maskini.
Pili, mtu atagundua kupanuka kwa pengo kati ya kundi maskini zaidi na makundi mengine kunaongezeka polepole kwa kuzingatia viwango vya kufaulu majaribio (kama ilivyooneshwa katika kielelezo), hasa baada ya umri wa miaka 14. Pamoja na sababu nyingine, hii kutokana na idadi kubwa ya watoto wanaokatisha masomo na idadi ndogo ya watoto wanaoendelea na masomo kwenda shule za sekondari kutoka familia maskini zaidi.10
10 Ni chini ya 4% ya watoto wote kutoka katika kaya maskini zaidi wenye umri wa miaka 10-16 ndio wameandikishwa katika shule za sekondari, ikilinganishwa na 15% ya watoto wanaotoka katika kaya zisizo maskini.
Katika umri wa miaka 10, kwa mfano, kiwango cha ufaulu miongoni mwa wasio maskini (33%) ni mara mbili ya kile cha maskini ambacho ni (16%) na ni mara tatu zaidi ya kile cha wale masikini zaidi kabisa ambacho ni (10%).
Kwa wastani, uduni katika kujifunza utokanao na watoto kutoka katika kaya maskini, ukilinganisha na watoto kutoka katika kaya zisizo maskini, ni unafanana kwa karibu miaka miwili (na hasa kwa kaya maskini zaidi).
Kielelezo cha 5: Kiwango cha ufaulu kwenye majaribio ya kusoma na kuhesabu (kwa pamoja) kwa watoto wenye umri wa miaka 10-16, kwa vigezo vya matabaka ya kiuchumi na kijamii, kote Afrika Mashariki
Kielelezo cha 6: Viwango vya ufaulu katika majaribio ya kusoma na kuhesabu (kwa pamoja), kwa vigezo vya kiuchumi na kijamii na umri, katika Afrika Mashariki yote
% y
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi%
ya
ufau
lu w
a w
anaf
unzi
Wenye kipato kizuri
Wenye kipato kizuri
Umri wa mtoto
Maskini
Maskini
Masikini zaidi
Masikini zaidi
19Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
Kwa kuongezea kwenye tofauti zilizopo katika matokeo ya majaribio ya kusoma na kuhesabu kutokana na maeneo na hali za kiuchumi na kijamii, pia ziko tofauti kubwa zinahusiana na aina ya shule wanazosoma. Hii imeoneshwa na Kielelezo cha 7, ambacho kinaonesha asilimia ya watoto wenye umri wa miaka 10-16 ambao wanaweza kufaulu majaribio yote mawili ya kusoma na kuhesabu (kwa pamoja) kwa kuzingatia iwapo wanasoma shule za serikali (umma) au shule binafsi. Grafu inaonesha kwamba shule binafsi zinatoa viwango vya juu vya ufaulu katika nchi zote. Kwa mfano, kiwango cha kufaulu katika shule za serikali za Tanzania ni ni 47% wakati katika shule binafsi ni 75%. Kwa sehemu, utofauti kati ya Tanzania na nchi nyingine ni kwamba kuna uwezekano unaletwa na idadi ndogo sana ya wanafunzi wanaosoma shule binafsi, hata miongoni mwa wanafunzi wenye kipato kizuri, ikiashiria kwamba huenda wanachagua kimaalum.
Mambo mawili zaidi yanajitokeza katika data hizi. Kwanza, pengo katika matokeo kati ya shule za umma na shule binafsi ni kubwa sana Tanzania kuliko Kenya au Uganda. Hili linaonekana kwenye umbali uliopo kwenye mihimili-grafu kati ya shule za umma na shule binafsi kwenye kielelezo. Kwa Tanzania, wanafunzi wa shule binafsi wanafanya vizuri kwa zaidi ya mara moja na nusu ya wale walioko shule za serikali. Kwa Kenya na Uganda umbali huu ni mdogo zaidi. Pili, bila kujali aina ya shule wanazosoma, tofauti kubwa miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki zinabaki kuwa wazi. Kwa kila aina ya shule (ziwe za umma au binafsi), wanafunzi wa Kenya wanafanya vizuri zaidi kuliko wanafunzi wa Uganda na Tanzania. Zaidi ya yote, kwenye wastani, wanafunzi walioko kwenye shule zinazofanya vibaya za serikali za Kenya bado zinawazidi kwa kufanya vizuri wanafunzi wanaotoka katika shule zinazofanya vizuri zaidi kwa Uganda.
pengo katika matokeo kati ya shule za umma na shule binafsi ni kubwa sana Tanzania kuliko Kenya au Uganda.
Ukweli wa 7: Wanafunzi wanaosoma katika shule binafsi wanafanya vizuri zaidi kuliko wanafunzi wanaosoma katika shule za serikali (za umma)
Mwisho, ni muhimu kuangalia kama duru ya kwanza na ya pili ya tafiti za Uwezo zinatufikisha kwenye hitimisho lilelile, iwapo kumeendelea kuwepo ulinganifu na iwapo umakini wa kutosha umetumika ili kuruhusu ulinganishaji wakati mwingine. Kwa upande wa kwanza, mtu angetarajia matokeo yawe sawa kwa kuwa tafiti zote zilifanyika kwa uwakilishi wa kitaifa na kwa muda wa miaka miwili, (kwa upande wa Kenya) inatenga zile duru mbili, ambazo muundo ni wa muda mfupi kuweza kufikia mabadiliko ya kiwango kikubwa katika
matokeo ya elimu. Kwa upande mwingine, baadhi ya tofauti zinapaswa kutarajiwa, hasa kutokana na idadi kubwa ya wilaya zilizofikiwa katika duru ya pili. Hakika, ripoti ya Afrika Mashariki kwa duru ya kwanza ya tafiti za Uwezo (angalia www.uwezo.net) ilibainisha kwamba kunaweza kukawa na mkingamo kidogo katika matokeo kutokana na ukweli kwamba chini ya nusu ya wilaya zote zilijumuishwa katika sampuli. Kama ilivyobainishwa katika Sehemu ya 2, wasiwasi huu uliangaliwa katika Uwezo duru ya 2 ambayo ilifikia zaidi
Ukweli wa 8: Matokeo ya utafiti wa Uwezo mwaka 2011 kwa kiwango kikubwa yanaendana na yale ya awamu ya kwanza.
Kielelezo cha 7: Viwango vya ufaulu kwenye majaribio ya kusoma na kuhesabu (kwa pamoja) kwa watoto wenye umri wa miaka 10-16, kwa vigezo vya aina ya shule na nchi
% y
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi
Binafsi Binafsi BinafsiUmma Umma Umma
20 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
ya robo tatu ya wilaya zote katika kila nchi, ikimaanisha matokeo ya awamu ya pili ni ya uhakika zaidi.
Kwa kuangalia ukanda mzima (yaani, tukichukua Kenya, Uganda na Tanzania), kielelezo cha 8 kinalinganisha matokeo kati ya duru mbili za tafiti za Uwezo kwenye majaribio ya kusoma (Kiingereza na Kiswahili) na kuhesabu. Kielelezo kinaonesha asilimia ya watoto wenye umri wa miaka 10-16
katika ukanda ambao wanaweza kufaulu kila jaribio. Ni watoto wenye umri wa zaidi ya miaka 10 tu ndiyo wamejumuishwa, kwa kuwa katika umri huu, wanatarajiwa kuwa wametimiza angalau miaka 2 katika elimu ya msingi. Na hivyo, wanapaswa kuwa na uwezo wa kufaulu majaribio. Kielelezo kinaonesha bayana tofauti hizo katika viwango vya ufaulu kati ya duru hizi mbili kuwa ni ndogo.
Ni watoto wenye umri wa zaidi ya miaka 10 tu ndiyo wamejumuishwa, kwa kuwa katika umri huu, wanatarajiwa kuwa wametimiza angalau miaka 2 katika elimu ya msingi. Na hivyo, wanapaswa kuwa na uwezo wa kufaulu majaribio.
Matokeo kutoka katika duru mbili za utafiti kwa kila nchi yanalingana yakichukuliwa tofauti tofauti (Jedwali la 4). Data zinaonesha asilimia ya watoto wenye umri wa miaka 10-16 katika kila nchi ambao walijibu kwa usahihi majaribio ya kusoma na hisabati kwa pamoja. Tofauti ni ndogo, ikiashiria kiwango kikubwa cha ulinganifu kati ya awamu hizi mbili. Hii inaashiria kwamba methodolojia ya utafiti na uongozi inaonekana kuwa imara na ya kuaminika.
Jedwali la 4: Asilimia za wanafunzi waliofaulu majaribio yote mawili la kusoma na hisabati, kwa kila nchi
Duru ya 1 Duru ya 2
Kenya 65.6 69.7
Tanzania 44.3 45.4
Uganda 30.6 37.9
Afrika Mashariki 45.9 49.8
Vidokezo: Duru ya 1 ya tafiti ilifanyika mwaka 2009 (Kenya) na mwaka 2010 (Uganda na Tanzania); Duru ya 2 ya tafiti zote ilifanyika mwaka 2011.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 1 na Uwezo 2.
Matokeo ya majaribio ya kusoma na kuhesabu kwa watoto wenye umri wa miaka 10-16 kwa duru mbili za utafiti wa Uwezo
% y
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi
Kiingereza Hisabati
21Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
Hitimisho
22 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
4. Hitimisho
Ripoti hii ni muhtasari wa matokeo muhimu ya utafiti Uwezo awamu ya pili (Uwezo 2) uliofanyika Kenya, Tanzania bara na Uganda mwaka 2011. Tafitihizi,
ambazo ni kati ya tafiti za kaya zenye sampuli kubwa zaidi kuwahi kufanyika Bara la Afrika, hutoa ushahidi makini kuhusu hali halisi ya ujuzi wa kusoma na kuhesabu wa watoto zaidi ya 100,000 (wenye umri miaka 6-16) katika kila nchi ndani ya nchi tatu, na kwenye wilaya zote katika nchi hizo. Tafiti hizi ni kiwakilishi cha kitaifa, kwa hiyo hutoa msingi mzuri wa kuchunguza viwango/ngazi ya ujuzi na mwenendo wa matokeo ya kujifunza.
Matokeo muhimu ya utafiti wa Uwezo awamu ya 2 yana akisi yale ya Uwezo awamu ya 1. Licha ya mafanikio muhimu katika upatikanaji wa elimu ya msingi eneo lote la Ukanda huu,kunakothibitishwa na kuongezeka kwa uwiano wa uandikishaji, idadi kubwa ya watoto bado hawajifunzi kikamilifu.Katika nchi zote tatu, zaidi ya theluthi mbili ya watoto wa darasa la 3 hawana ujuzi wa msingi wa kusoma na kuhesabu majaribio ya ngazi ya darasa la 2. Aidha, watoto wanapata stadi hizi polepole kadri wanavyopanga madarasa, na watoto wengi hupata ujuzi huo baada ya kukamilisha miaka mitano ya kujifunza au zaidi (badala ya miwili tu).
Tafiti hizi pia zimebainisha matokeo mengine kadha muhimu. Kuna tofauti kubwa kwenye wastani wa alama za ufaulu kati ya nchi na nchi Afrika ya Mashariki. Wanafunzi wa Kenya kufanya vibaya zaidi wakati wa miaka ya mwanzo ya elimu ya msingi, lakini wanaonesha maendeleo ya haraka na kuwazidi kidogo wanafunzi wa Tanzania wanapofikia mwisho wa elimu ya msingi. Pia kuna tofauti kubwa katika wastani wa ufaulu wa majaribio kati ya wilaya na wilaya ndani ya kila nchi. Nchini Kenya kuna idadi ndogo ya sana ya wilaya zinazofanya vibaya zaidi. Nchini Tanzania na Uganda kuna idadi kubwa ya wilaya zinazofanya vibaya sana na idadi ndogo ya wilaya zinazofanya vizuri zaidi.
Tofauti kwenye ufaulu wa majaribio (kati ya mwanafunzi mmoja mmoja na wilaya) ni kutokana na sababu kadhaa. Hata hivyo, jambo muhimu ni kwamba kuna tofauti chache katika alama za ufaulu wa majaribio kati ya wavulana na wasichana, na wasichana wanawazidi kidogo wavulana katika nchi zote tatu. Hata hivyo, watoto kutoka kaya duni kiuchumi na kijamii hufanya vibaya zaidi kwenye majaribio kwa umri wote, jambo linaloashiria kwamba kukosekana kwa usawa kwenye fursa
za elimu ni jambo linaloendelea kuwepo.Pia wanafunzi katika shule binafsi hufanya vizuri zaidi ya wanafunzi katika shule za serikali (umma) katika nchi zote tatu, tofauti ambayo ilionekana zaidi kwa watoto wa Tanzania.
Ripoti ya kiufundi yenye maelezo mengi inatoa uchambuzi wa kina zaidi ya utafiti wa Uwezo (inapatikana kutoka www.uwezo.net ). Pamoja na mambo mengine, utafiti wa siku zijazo utajaribu zaidi kuweka bayana vigezo vya matokeo ya kujifunza na tofauti zake katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Pindi matokeo kama haya yanapotolewa, ni kawaida watu kuuliza ufumbuzi ni nini. Hakika, Uwezo yenyewe imeanzishwa si tukufanya utafiti lakini kuchochea maboresho katika stadi za kusoma na kuhesabu.Hata hivyo, bado tunasita kutoa orodha ya majibu yaliyo tayarishwa; kwa maana, uzoefu unatufundisha ufumbuzi unaonekana dhahiri unaweza usiwe na tija/ au manufaa. Katika mtazamo wetu swali la nini kifanyike linahitaji kuangaliwa kwa umakini mkubwa na uatayari wa kufikiri kitofauti. Katika mtazamo huo, tunapendekeza mambo matano ya kutilia maanani.
• Kutofanya zaidi kilekile tulichozoea kufanya. Katika uso wa matokeo duni, wanasiasa, mameneja elimu na Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) mara nyingi hutoa wito wa kufanya zaidi, au rasilimali zaidi ziwekezwe kwenye shughuli au hatua zile zile za ufumbuzi, wakati tatizo la msingi kiuhalisia inaweza kuwa ni uchaguzi wa shughuli au hatua za ufumbuzi na wala siyo ukosefu wa rasilimali.
• Kusisitiza juu ya ushahidi huru na makini. Sera nyingi na bajeti huamriwa kwa kuzingatia matendo yaliyopita, upendeleo wa kiitikadi au matakwa ya kisiasa. Watunga sera na watawala wa shule wanaweza kufanya vyema kwa kuchunguza ushahidi ufanisi/tija inayoletwa na shughuli/hatua mbalimbali ili kuweka ufahamu mzuri zaidi wa nini kinafanyika na kuleta manufaa.
• Kuzingatia matokeo ya kujifunza badala ya vitendea kazi/vifaa vya elimu. Miongoni mwa wananchi watunga sera vilevile, elimu mara nyingi hutazamwa katika nyanja ya nyenzo/vifaa kama vile madarasa, madawati, vitabu, vilevile kama nyenzo za kibinadamu kama vile idadi ya walimu wenye sifa na wanafunzi waliojiunga. Wakati mambo haya pasipo shaka yanaweza kuchangia kipimo
23Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
cha mwisho cha mafanikio , mawazo na akili zetu zote tunapaswa kuvielekeza kwenye uwezo wa anayejifunza/mwanafunzi, yaani; siyo kuangalia kuna madawati mangapi bali Juma anaweza kusoma.
• Kujifunza kutoka kile kinachoweza kufanyika na kuleta manufaa. Wakati matokeo kiujumla ni mabaya, baadhi ya shule na wilaya hufanya vizuri zaidi kuliko wengine licha ya kukabiliwa na vikwazo vinavyofanana na vya wengine. Mafanikio yao kwa sehemu yanaweza kutokana na fursa za kihistoria na kipato, lakini kunaweza kuwa na sababu nyingine za mafanikio kwa kuangalia menejimenti ya taasisi, jitihada za pamoja na ubunifu ambao wengine wanaweza kuiga.
• Kuchunguza na kufanyia majaribio mawazo mapya. Muundo wa msingi wa ualimu na ufundishaji katika shule nyingi leo haujabadilika sana kwa miongo kadhaa. Inaweza kuwa na maana kujenga utamaduni na nafasi kwa ajili ya mawazo “sumbufu” na teknolojia na kupima kama
uvumbuzi na mbinu tofauti, kama vile malipo unapofanya vizuri, vinaleta manufaa zaidi. Mambo haya matano ya kutilia maanani yako zaidi kwenye namna ya kufikiri na kulikabili tatizo kuliko kuendelea kutoa ufumbuzi kwenye masuala maalum. Na pengine hiyo inaweza kuwa hatua muhimu.
Hakika, wakati miundombinu ya shule imepanuliwa zaidi
na kuendelea kutumia moja ya tano ya bajeti ya taifa bado vinaendelea kutoa matokeo mabaya, changamoto yetu kuu inaweza kuwa iko kidogo kwenye kubainisha sera au kurekebisha utaalamu, kuanzisha mradi mpya au kupata fedha, lakini zaidi inatokana na kushindwa kwa ubunifu na mawazo yetu kuhusu kuboresha elimu. Kama matokeo ya utafiti wa Uwezo yanaweza kuchochea viongozi wa elimu na wananchi pia, wakiwemo walimu na wazazi, kutulia, na kujiuliza kwa kushangaa kama tunafanya kitu sahihi, na badala yake ni kufikiri juu kile kinachoweza kufanyika na kuleta manufaa na namna gani kukifanya, uwezo itakuwa imefanya sehemu kubwa ya kazi yake.
24 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
KIAMBATISHO A: UWIANO WA UANDIKISHAJI SHULE YA MSINGI
Jedwali A1: Muhtasari wa wastani wa viwango vya kufaulu katika majaribio ya kuhesabu na kusoma kwa pamoja kwa ngazi ya wilaya, kinchi
10% Chini Kati 10% Juu
Kenya 26.5 - 50.0 67.6 84.3 - 92.1
Tanzania 25.4 - 33.3 42.8 63.1 - 80.2
Uganda 9.7 - 22.7 34.1 47.7 - 69.3
Vidokezo: 10% za Chini na za Juu zinaonesha wastani wa viwango vya kufaulu kwa wilaya za juu kabisa na za chini kabisa katika kufaulu kwa makundi ya 10% ya wilaya za juu na 10% ya wilaya za chini katika kila nchi.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 2.
Jedwali A2: Asilimia ya watoto wenye umri wa miaka 10-16 waliofaulu majaribio ya Uwezo, kijinsia na ki-nchi
Nchi Jaribio Wavulana Wasichana Tofauti
Kenya Kusoma 72.4 76.6 -4.2
Kuhesabu 70.0 72.9 -2.9
Kwa pamoja 67.7 71.8 -4.0
Tanzania Kusoma 55.2 59.0 -3.7
Kuhesabu 59.9 61.3 -1.4
Kwa pamoja 44.3 46.5 -2.2
Uganda Kusoma 42.9 46.2 -3.3
Kuhesabu 56.6 57.2 -0.5
Kwa pamoja 36.6 39.2 -2.6
Vidokezo: Majaribio ya ‘Kusoma’ yanahusu Kiingereza kwa Uganda na Kenya, na Kiswahili kwa Tanzania; majaribio “kwa pamoja’ ina maanisha wanafunzi ambao wanafaulu majaribio yote mawili ya kusoma na kuhesabu.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 2.
Kielelezo A.1: Uwiano wa watoto walioandikishwa shule za msingi, kwa umri
Vidokezo: kielelezo hiki kinaonesha uwiano wa watoto katika umri uliotajwa ambao wameandikishwa shule za msingi; kumbuka kwamba shule ya msingi kwa Tanzania wanaanza wakiwa na umri wa miaka 7, ambao ni mwaka mmoja baadaye kuliko Uganda na Kenya.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 2.
25Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
KIAMBATISHO B: VIELELEZO NA MAJEDWALI YA NYONGEZA KWA KENYA
Kielelezo B.1: Viwango vya ufaulu majaribio Kimadarasa kwa watoto walioandikishwa shule, nchini Kenya
Kilelezo B.2: Viwango vya ufaulu majaribio ya kusoma na hisabati (kwa pamoja) kwa watoto wenye umri wa miaka 10-16, kwa vigezo vya hali ya kiuchumi na kijamii, nchini Kenya
Kielelezo B.3: Matokeo ya majaribio kwa watoto wenye miaka 10-16, kwa kila duru ya utafiti wa Uwezo, nchini Kenya
Vidokezo: duru za tafiti zimeoneshwa katika namba kwenye mihimili ulalo.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 1 na Uwezo 2.
Vidokezo: matabaka ya hali za kiuchumi na kijamii yamefafanuliwa kwenye maelezo.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 2.
Vidokezo: Namba zilizopo kwenye mihimili ya ulalo zinawakilisha Darasa la 3 hadi la 7 shule za Msingi; ‘Kwa pamoja’ inawakilisha ufaulu wa majaribio yote mawili kusoma kiingereza na kiswahili na hesabu.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 2.
Kiingereza Kiswahili
Hisabati Kwa pamoja
% y
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi
% y
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi
Wenye kipato kizuri Maskini Masikini zaidiKiingereza Kiswahili Hisabati
26 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
KIAMBATISHO C: VIELELEZO NA MAJEDWALI YA NYONGEZA KWA TANZANIA (BARA)
Kiingereza Kiswahili
Hisabati Kwa pamoja
Kielelezo C.1: Viwango vya ufaulu majaribio Kimadarasa kwa watoto walioandikishwa shule, nchini Tanzania
Vidokezo: Namba zilizopo kwenye mihimili ya ulalo zinawakilisha Darasa la 3 hadi la 7 shule za Msingi; ‘Kwa pamoja’ inawakilisha ufaulu wa majaribio yote mawili, kusoma kiingereza na kiswahili na hesabu.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 2.
Kilelezo C.2: Viwango vya ufaulu majaribio ya kusoma na hisabati (kwa pamoja) kwa watoto wenye umri wa miaka 10-16, kwa vigezo vya hali ya kiuchumi na kijamii, nchini Tanzania
Vidokezo: matabaka ya hali za kiuchumi na kijamii yamefafanuliwa kwenye maelezo.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 2.
Vidokezo: duru za tafiti zimeoneshwa katika namba kwenye mihimili ulalo.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 1 na Uwezo 2
Kielelezo C.3: Matokeo ya majaribio kwa watoto wenye miaka 10-16, kwa kila duru ya tafiti wa Uwezo, nchini Tanzania
% y
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi
% y
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi
Wenye kipato kizuri Maskini Masikini zaidi
Kiingereza Kiswahili Hisabati
27Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
KIAMBATISHO D: VIELELEZO NA MAJEDWALI YA NYONGEZA KWA UGANDA
Kielelezo D.1: Viwango vya kufaulu majaribio Kimadarasa kwa watoto walioandikishwa shule, nchini Uganda
Vidokezo: Namba zilizopo kwenye mihimili ya ulalo zinawakilisha Darasa la 3 hadi la 7 shule za Msingi; ‘Kwa pamoja’ inawakilisha ufaulu wa majaribio yote mawili Kusoma Kiswahili na Kiingereza na jaribio la hesabu.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 2.
Kilelezo D.2: Viwango vya kufaulu majaribio ya kusoma na hisabati (kwa pamoja) kwa watoto wenye umri wa miaka 10-16, kwa vigezo vya hali ya kiuchumi na kijamii, nchini Uganda
Kielelezo D.3: Matokeo ya majaribio kwa watoto wenye miaka 10-16, kwa kila duru ya tafiti wa Uwezo, nchini Uganda
Vidokezo: matabaka ya hali za kiuchumi na kijamii yamefafanuliwa kwenye maelezo.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 2.
Vidokezo: duru za tafiti zimeonyeshwa katika namba kwenye mihimili ulalo.
Chanzo: imekokotolewa kutoka kwenye data za Uwezo 1 na Uwezo 2.
% y
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi
% y
a uf
aulu
wa
wan
afun
zi
Wenye kipato kizuri Maskini Masikini zaidi
Kiingereza
Hisabati Kwa pamoja
Kiingereza Hisabati
28 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
KIAMBATISHO E: MIFANO YA MAJARIBIO YA UWEZO YA KUSOMA NA HESABU
Jaribio la Hisabati
Jaribio la Kiingereza
Jaribio la Kiswahili
29Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
Kenya Thika West Central 1
Kenya Kikuyu Central 2
Kenya Nairobi East Nairobi 3
Kenya Nyeri South Central 4
Kenya Gatanga Central 5
Kenya Kirinyaga Central 6
Kenya Kajiado North Rift Valley 7
Kenya Imenti South Eastern 8
Kenya Ruiru Central 9
Kenya Gatundu Central 10
Kenya Githunguri Central 11
Kenya Kiambu Central 12
Kenya Muranga North Central 13
Kenya Nyandarua South Central 14
Kenya Lari Central 15
Kenya Masaba Nyanza 16
Kenya Mbooni Eastern 17
Kenya Nyandarua North Central 18
Kenya Manga Nyanza 19
Kenya Taita Coast 20
Kenya Laikipia East Rift Valley 21
Tanzania Arusha Arusha 22
Kenya Gucha Nyanza 23
Kenya Keiyo Rift Valley 24
Kenya Marakwet Rift Valley 25
Kenya Naivasha Rift Valley 26
Tanzania Iringa Mjini Iringa 27
Kenya Mombasa Coast 28
Kenya Nakuru Rift Valley 29
Kenya Baringo Central Rift Valley 30
Kenya Makueni Eastern 31
Kenya Nakuru North Rift Valley 32
Kenya Baringo North Rift Valley 33
Kenya Mwala Eastern 34
Kenya Buret Rift Valley 35
Kenya Eldoret East Rift Valley 36
Kenya Meru South Eastern 37
Kenya Wareng Rift Valley 38
Kenya Kisii Central Nyanza 39
Kenya Mandera West North Eastern 40
Kenya Sotik Rift Valley 41
Kenya Nandi North Rift Valley 42
Kenya Kangundo Eastern 43
Kenya Nandi Central Rift Valley 44
Kenya Emuhaya Western 45
Kenya Imenti North Eastern 46
Tanzania Moshi Mjini Kilimanjaro 47
Kenya Tharaka Eastern 48
Kenya Mbeere Eastern 49
Kenya Koibatek Rift Valley 50
Kenya Suba Nyanza 51
Kenya Kitui Eastern 52
Tanzania Bukoba Mjini Kagera 53
Kenya Kajiado Central Rift Valley 54
Kenya Nandi South Rift Valley 55
Tanzania Rombo Kilimanjaro 56
Kenya Hamisi Western 57
Kenya Trans Nzoia West Rift Valley 58
Tanzania Morogoro Mjini Morogoro 59
Kenya Yatta Eastern 60
Kenya Embu Eastern 61
Uganda Kampala Central 62
Kenya Kibwezi Eastern 63
Tanzania Temeke Dar Es Salaam 64
Kenya Mwingi Eastern 65
Kenya Butere Western 66
Kenya Rongo Nyanza 67
Tanzania Mbeya Mjini Mbeya 68
Kenya Bungoma North Western 69
Kenya Kisumu West Nyanza 70
Kenya Laikipia West Rift Valley 71
Kenya Marsabit Eastern 72
Kenya Molo Rift Valley 73
Kenya Nandi East Rift Valley 74
Kenya Mandera Central North Eastern 75
Kenya Tigania Eastern 76
Tanzania Tanga Tanga 77
Kenya Nyando Nyanza 78
KIAMBATISHO F: NAFASI ZA UFAULU WILAYA ZA AFRIKA MASHARIKII
Nchi Wilaya Mkoa Nafasi Nchi Wilaya Mkoa Nafasi
30 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
Tanzania Ilala Dar Es Salaam 79
Kenya Rachuonyo Nyanza 80
Kenya Bomet Rift Valley 81
Kenya Kakamega Central Western 82
Kenya Lamu Coast 83
Kenya Teso North Western 84
Kenya Kericho Rift Valley 85
Tanzania Songea Mjini Ruvuma 86
Kenya Bondo Nyanza 87
Kenya Samia Western 88
Kenya Busia Western 89
Kenya Kakamega North Western 90
Uganda Wakiso Central 91
Kenya Trans Nzoia East Rift Valley 92
Kenya Rarieda Nyanza 93
Tanzania Mwanga Kilimanjaro 94
Kenya Taveta Coast 95
Kenya Malindi Coast 96
Tanzania Hai Kilimanjaro 97
Kenya Kyuso Eastern 98
Tanzania Kilolo Iringa 99
Kenya Mt Elgon Western 100
Tanzania Mufindi Iringa 101
Kenya Kakamega South Western 102
Kenya Bungoma East Western 103
Kenya Kuria East Nyanza 104
Tanzania Same Kilimanjaro 105
Kenya Migori Nyanza 106
Kenya Mutomo Eastern 107
Kenya Kilifi Coast 108
Kenya Kisii South Nyanza 109
Kenya Kwanza Rift Valley 110
Tanzania Shinyanga Mjini Shinyanga 111
Kenya Narok North Rift Valley 112
Kenya Igembe Eastern 113
Tanzania Njombe Iringa 114
Kenya Trans Mara Rift Valley 115
Kenya Bunyala Western 116
Tanzania Moshi Vijijini Kilimanjaro 117
Tanzania Ulanga Morogoro 118
Kenya Mandera East North Eastern 119
Kenya Gucha South Nyanza 120
Tanzania Ileje Mbeya 121
Tanzania Makete Iringa 122
Tanzania Pangani Tanga 123
Kenya Kaloleni Coast 124
Kenya Loitoktok Rift Valley 125
Tanzania Kinondoni Dar Es Salaam 126
Tanzania Iringa Vijijini Iringa 127
Kenya Moyale Eastern 128
Kenya West Pokot Rift Valley 129
Kenya Pokot Central Rift Valley 130
Tanzania Kibaha Coast 131
Tanzania Kyela Mbeya 132
Uganda Mbarara Western 133
Kenya Laikipia North Rift Valley 134
Tanzania Kigoma Mjini Kigoma 135
Kenya Teso South Western 136
Tanzania Newala Mtwara 137
Tanzania Dodoma Mjini Dodoma 138
Tanzania Ilemela Mwanza 139
Tanzania Mtwara Mjini Mtwara 140
Kenya Pokot North Rift Valley 141
Tanzania Simanjiro Manyara 142
Tanzania Songea Vijijini Ruvuma 143
Tanzania Lushoto Tanga 144
Tanzania Kisarawe Coast 145
Tanzania Manyoni Singida 146
Uganda Bushenyi Western 147
Kenya Samburu Central Rift Valley 148
Tanzania Tabora Mjini Tabora 149
Tanzania Chunya Mbeya 150
Tanzania Korogwe Tanga 151
Tanzania Musoma Mjini Mara 152
Uganda Mityana Central 153
Kenya Tana River Coast 154
Kenya Isiolo Eastern 155
Tanzania Singida Mjini Singida 156
Tanzania Babati Manyara 157
Kenya Msambweni Coast 158
Nchi Wilaya Mkoa Nafasi Nchi Wilaya Mkoa Nafasi
31Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
Uganda Kiruhuura Western 159
Kenya Narok South Rift Valley 160
Uganda Nakaseke Central 161
Tanzania Nyamagana Mwanza 162
Tanzania Mbeya Vijijini Mbeya 163
Kenya Bungoma South Western 164
Tanzania Hanang Manyara 165
Tanzania Rungwe Mbeya 166
Tanzania Maswa Shinyanga 167
Uganda Luwero Central 168
Tanzania Mbinga Ruvuma 169
Uganda Ibanda Western 170
Uganda Nakasongola Central 171
Tanzania Mafia Coast 172
Tanzania Karatu Arusha 173
Tanzania Mvomero Morogoro 174
Uganda Hoima Western 175
Uganda Kabarole Western 176
Tanzania Mbarali Mbeya 177
Tanzania Kilombero Morogoro 178
Tanzania Arumeru Arusha 179
Uganda Rukungiri Western 180
Tanzania Kiteto Manyara 181
Tanzania Nachingwea Lindi 182
Tanzania Mbulu Manyara 183
Tanzania Kondoa Dodoma 184
Tanzania Ludewa Iringa 185
Uganda Masaka Central 186
Tanzania Kasulu Kigoma 187
Tanzania Mkuranga Coast 188
Uganda Mbale Eastern 189
Tanzania Mpanda Rukwa 190
Tanzania Singida Vijijini Singida 191
Tanzania Bukoba Vijijini Kagera 192
Tanzania Bukombe Shinyanga 193
Tanzania Bagamoyo Coast 194
Tanzania Bunda Mara 195
Uganda Ntungamo Western 196
Tanzania Liwale Lindi 197
Tanzania Namtumbo Ruvuma 198
Uganda Lyantonde Central 199
Kenya Samburu North Rift Valley 200
Uganda Kabale Western 201
Tanzania Lindi Mjini Lindi 202
Tanzania Masasi Mtwara 203
Kenya Tana Delta Coast 204
Kenya Turkana South Rift Valley 205
Kenya Lagdera North Eastern 206
Tanzania Kilwa Lindi 207
Uganda Mpigi Central 208
Tanzania Kwimba Mwanza 209
Tanzania Muheza Tanga 210
Tanzania Kigoma Vijijini Kigoma 211
Uganda Kalangala Central 212
Uganda Kanungu Western 213
Tanzania Misungwi Mwanza 214
Tanzania Urambo Tabora 215
Uganda Jinja Eastern 216
Tanzania Magu Mwanza 217
Uganda Gulu Northern 218
Uganda Mukono Central 219
Tanzania Igunga Tabora 220
Uganda Kasese Western 221
Tanzania Rufiji Coast 222
Tanzania Karagwe Kagera 223
Tanzania Biharamulo Kagera 224
Tanzania Morogoro Vijijini Morogoro 225
Uganda Rakai Central 226
Uganda Isingiro Western 227
Tanzania Kilosa Morogoro 228
Tanzania Uyui Tabora 229
Uganda Kitgum Northern 230
Uganda Busia Eastern 231
Tanzania Geita Mwanza 232
Tanzania Sikonge Tabora 233
Tanzania Lindi Vijijini Lindi 234
Tanzania Iramba Singida 235
Tanzania Handeni Tanga 236
Kenya Wajir East North Eastern 237
Tanzania Ngorongoro Arusha 238
Nchi Wilaya Mkoa Nafasi Nchi Wilaya Mkoa Nafasi
32 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
Tanzania Ngara Kagera 239
Tanzania Ruangwa Lindi 240
Uganda Manafwa Eastern 241
Kenya Wajir West North Eastern 242
Tanzania Mbozi Mbeya 243
Tanzania Tandahimba Mtwara 244
Uganda Kisoro Western 245
Tanzania Dodoma Vijijini Dodoma 246
Uganda Moyo Northern 247
Uganda Kapchorwa Eastern 248
Tanzania Sumbawanga Mjini Rukwa 249
Tanzania Nzega Tabora 250
Uganda Kiboga Central 251
Tanzania Sengerema Mwanza 252
Tanzania Monduli Arusha 253
Kenya Wajir North North Eastern 254
Uganda Sironko Eastern 255
Uganda Bukwo Eastern 256
Tanzania Kongwa Dodoma 257
Tanzania Shinyanga Vijijini Shinyanga 258
Tanzania Muleba Kagera 259
Uganda Arua Northern 260
Uganda Kamwenge Western 261
Tanzania Sumbawanga Vijijini Rukwa 262
Uganda Kyenjojo Western 263
Uganda Pader Northern 264
Uganda Kumi Eastern 265
Kenya Ijara North Eastern 266
Tanzania Nkasi Rukwa 267
Uganda Masindi Western 268
Uganda Soroti Eastern 269
Tanzania Tunduru Ruvuma 270
Tanzania Musoma Vijijini Mara 271
Tanzania Tarime Mara 272
Uganda Lira Northern 273
Uganda Amuria Eastern 274
Uganda Kayunga Central 275
Tanzania Kishapu Shinyanga 276
Uganda Kibaale Western 277
Tanzania Kahama Shinyanga 278
Uganda Buliisa Western 279
Uganda Oyam Northern 280
Kenya Turkana Central Rift Valley 281
Tanzania Mtwara Vijijini Mtwara 282
Uganda Kaberamaido Eastern 283
Uganda Adjumani Northern 284
Tanzania Serengeti Mara 285
Uganda Abim Northern 286
Uganda Bukedea Eastern 287
Uganda Sembabule Central 288
Uganda Mubende Central 289
Uganda Nebbi Northern 290
Uganda Katakwi Eastern 291
Tanzania Kibondo Kigoma 292
Uganda Pallisa Eastern 293
Uganda Butaleja Eastern 294
Uganda Iganga Eastern 295
Uganda Bududa Central 296
Tanzania Kilindi Tanga 297
Uganda Mayuge Eastern 298
Tanzania Meatu Shinyanga 299
Tanzania Ukerewe Mwanza 300
Tanzania Mpwapwa Dodoma 301
Uganda Nyadri Northern 302
Uganda Apac Northern 303
Uganda Yumbe Northern 304
Uganda Koboko Northern 305
Uganda Tororo Eastern 306
Uganda Budaka Eastern 307
Kenya Samburu East Rift Valley 308
Uganda Kamuli Eastern 309
Tanzania Bariadi Shinyanga 310
Uganda Amuru Northern 311
Uganda Dokolo Northern 312
Uganda Bundibugyo Western 313
Uganda Bugiri Eastern 314
Uganda Kaliro Eastern 315
Uganda Amolatar Northern 316
Uganda Nakapiripirit Northern 317
Uganda Moroto Northern 318
Uganda Kaabong Northern 319
Uganda Kotido Northern 320
Nchi Wilaya Mkoa Nafasi Nchi Wilaya Mkoa Nafasi
33Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!
34 Je, Watoto Wetu Wanajifunza? | Ujuzi wa Kusoma na Kuhesabu katika Afrika Mashariki | Agosti 2012
Uwezo Afrika Mashariki ilipo Twaweza
Barabara ya Lenana, ACS Plaza ghorofa ya 3,S.L.P 19875 00200 Nairobi, Kenya
Simu: +254 203861372/3/4Barua pepe: [email protected]
www.uwezo.net
Ripoti hii inajumuisha, inalinganisha na inawasilisha muhtasari wa taarifa za matokeo ya utafiti wa kitaifa wa Uwezo 2011 wa nchi za Kenya, Uganda na Tanzania bara. Takriban watoto 350,000 katika maeneo ya nchi hizi tatu walipimwa uwezo wao katika stadi za msingi za kusoma, kuandika na
kuhesabu kwa ngazi ya Darasa la 2.
Methodolojia ya Uwezo, muundo wa sampuli, zana zetu na mchakato mzima vimekuwa vikifanywa kwa mashauriano na wataalam wa kitaifa na kimataifa, na kuhakikiwa kwa umakini. Maelezo ya kina kuhusu methodolojia na mkusanyo kamili wa data pia vinapatikana kwa wote.
Jambo kubwa lililogundulika ni kwamba licha ya mafanikio makubwa katika kupanua wigo wa upatikanaji wa elimu ya msingi, ujuzi halisi katika kusoma na kuhesabu umebaki kuwa duni katika nchi zote za ukanda huu. Japokuwa watoto kwa sasa wameandikishwa shuleni kwa idadi kubwa mno kuliko awali, lakini hawajifunzi stadi za msingi zinazotarajiwa wajifunze katika ngazi za madarasa waliyofikia na katika umri walionao.
Japokuwa matokeo haya yanaonesha picha ya kutisha ya hali ya elimu katika Afrika Mashariki, bado zipo sababu za kuwa na matumaini. Kwanza, sehemu zote Afrika Mashariki, Ziko baadhi ya shule na wilaya zinafanya vizuri licha ya kukabiliwa na vikwazo vya aina ileile sawa na sehemu zingine. Shule na jamii hizi zinajenga vyanzo muhimu vya ufumbuzi na majawabu ya jinsi ya kuboresha kujifunza kwa watoto. Pili, kuna dalili zinazoonesha wazi kuhama kwa mjadala wa umma na kuelekea kujikita kwenye ubora na matokeo ya kujifunza, na kuuliza maswali makini ambayo yanaweza kusaidia maamuzi ya kisera na kupata thamani kubwa kutoka katika uwekezaji uliopo sasa. Tatu, kidunia kunaongezeko la kufanyia majaribio uvumbuzi na ubunifu ili kuchochea kujifunza ambako kunaweza kuinufaisha Afrika Mashariki, tukichagua na kuamua kwa makini.
Fursa ya kumsaidia kila mtoto ili ajifunze ipo. Na ripoti hii inalengo la kuwataarifu fursa hiyo.