33
1 UINJILISTI UFANYAO KAZI Mwongozo wa uinjilisti wa mtu kwa mtu na nyumba kwa nyumba Kimeandikwa na Ken B. Kemper 1011 Aldon Street, Grand Rapids, MI 49509, USA www.vitabuvyakikristo.com

Kimeandikwa na - vitabuvyakikristo.com · Itakusaidia sana ukisoma kila somo na kusoma mistari yote ya Biblia inayotajwa. Pia, ni muhi- mu kutumia maswali yote yaliyopo mwishoni mwa

  • Upload
    others

  • View
    30

  • Download
    5

Embed Size (px)

Citation preview

1

UINJILISTI

UFANYAO KAZI

Mwongozo wa uinjilisti wa mtu kwa mtu na nyumba kwa nyumba

Kimeandikwa na

Ken B. Kemper

1011 Aldon Street, Grand Rapids, MI 49509, USA www.vitabuvyakikristo.com

2

UINJILISTI UFANYAO KAZI

Copyright © 1994 GMI Publications

GMI Publications ina haki zote za ya kitabu hiki. Hairuhusiwi kuchapa na kuuza sehemu yo yote ya kitabu hiki bila ruhusa ya GMI Publications. Vilevile hairuhusiwi kuuza nakala za kikompyuta (digi-tal copies) bila ruhusa ya GMI Publications.

Wahariri – Mch. Albert Juliano Simwanza na Steven Sherman Kama Biblia nyingine hazijatajwa, dondoo zote za kunukuu Biblia zinatumia Swahili Union Version (SUV): Haki miliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa. GMI Publications ni idara ya Grace Ministries International; misheni ifanyayo kazi na dhehebu la Kanisa la Neema (Grace Church) duniani, pamoja na Wakristo wote wanaomwa-mini Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao.

YALIYOMO Utangulizi.................................................................................................................................................................................. 3

1. Uinjilisti wa Mtu kwa Mtu ............................................................................................................................................ 3

2. Maandalizi ya Mwinjilisti ............................................................................................................................................. 8

3. Ujumbe Tunaoshuhudia ............................................................................................................................................ 10

4. Kazi ya Ushuhuda Wako ............................................................................................................................................ 14

5. Vifaa vya Uinjilisti ......................................................................................................................................................... 15

6. Njia ya Kushuhudia ...................................................................................................................................................... 17

7. Kazi za Maombi na Roho Mtakatifu...................................................................................................................... 20

8. Vizuizi vya Kuamini ..................................................................................................................................................... 22

9. Namna ya Kuwaendea Watu ................................................................................................................................... 23

10. Jinsi ya Kutumia Vipeperushi na Maandiko .................................................................................................. 25

11. Kumsaidia Mwongofu Mara Anapokata Shauri ........................................................................................... 27

12. Kumfuata na Kumjenga Aliyeamini ................................................................................................................... 28

13. Kuanza Kufanya Huduma ya Uinjilisti ............................................................................................................. 30

14. Mpango Unaohusisha Kanisa Zima .................................................................................................................... 32

Vitabu Vilivyonisaidia Kuandika Kitabu Hiki ....................................................................................................... 33

3

Utangulizi Kitabu hiki unachoshika mkononi mwako kimetayarishwa ili kikusaidie kufanya kazi ya uin-

jilisti wa siku kwa siku pia utumiwe na Bwana kwa njia ya ajabu. Hakuna kitu kilicho kizuri duniani kuliko kumsaidia mtu aliyepotea ili aipokee njia ya wokovu. Ili uweze kuifanya kazi hii lazima mwinjilisti mwenyewe uwe na uhakika kuhusu imani yako na wokovu wako ndani ya Kristo Yesu. Kitabu hiki kimetolewa kuwasaidia watu wote, wakiwa wazee, vijana, viongozi wa makanisa, akina mama au wasichana, kushuhudia jinsi Kristo alivyowaokoa.

Kitabu hiki kinaweza kutumiwa na mtu akiwa peke yake ili ajifunze namna ya kuwashuhudia wapotevu wanaomzunguka pale alipo au kinaweza kutumiwa na kundi la watu wanaotaka kujua zaidi jinsi ya kuwashuhudia marafiki zao wasio Wakristo wa kweli. Vilevile kitabu hiki kinaweza kutumiwa katika semina ya viongozi, kundi la waaminifu, au katika makanisa kuanzisha kazi ya uin-jilisti au kuimarisha mpango wa uinjilisti wao. Kama masomo haya yatatumiwa katika semina, kuna mwongozo unaohusu jinsi ya kufuata ratiba ya siku sita mwishoni mwa kitabu hiki.

Itakusaidia sana ukisoma kila somo na kusoma mistari yote ya Biblia inayotajwa. Pia, ni muhi-mu kutumia maswali yote yaliyopo mwishoni mwa kila somo na kurudia mambo muhimu kupima kama unajifunza na kukumbuka vizuri. Zaidi ya hayo, ingefaa baada ya masomo machache, ujaribu kuutumia ujuzi unaojifunza kwa kuwashuhudia watu ukiendelea kusoma na kutendea kazi yale unayoyasoma. Maana, kitabu hiki kinalenga matendo ya uinjilisti siyo ujuzi tu. Kama utayaelewa mambo yote bila kutenda ina maana hujaelewa lengo la masomo haya.

Vitu unavyohitaji katika kuanza masomo haya ni Biblia na moyo ulioandaliwa kwa njia ya maombi ili upokee msaada wa Mungu na kuifanya huduma yenye matokeo ya milele! Hakika mam-bo mengi utakayosoma na kujifunza siyo mapya kabisa na ya kushangaza, bali yanaelezwa kwa njia ambayo Mungu hutumia kuleta mafanikio mengi na kulijenga Kanisa Lake.

Yesu Kristo mwenyewe alipokuwa hapa duniani “Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu” (Mt 4:19). Aliwaomba kumfuata na kujifunza tu. Kisha wakatumwa kuifanya kazi ya kuwaongoza wengine. Kwa masomo haya, tufanywe kuwa wavuvi wa watu!

Shukrani kubwa kwa wanafunzi wangu wote wa Tanzania Grace Bible Institute walionitia moyo nikiwafundisha na kufanya uinjilisti huo pamoja nao mwaka 1991-1994. Mungu apokee utu-kufu wote! Matendo 20:24 – Ken B. Kemper

1. Uinjilisti wa Mtu kwa Mtu Kwanza kabisa lazima tuelewe kwamba uinjilisti unaofundishwa katika kitabu hiki ni uinjilisti

wa mtu kwa mtu na nyumba kwa nyumba [personal evangelism]. Usitegemee kujifunza jinsi ya kufanya mikutano mikubwa ya Injili [Crusade] kutokana na masomo haya.

Ingawa mikutano mikubwa huonekana kuwa na faida kubwa, wataalum wamegundua kwamba uinjilisti wa mtu kwa mtu una manufaa na matokeo ya kudumu kuliko mikutano mikubwa. Sababu chache ni hizo:

• Mtu kwa mtu humlenga kila mtu mmoja na mahitaji yake; • Ufuatiliaji wa mtu kwa mtu ni rahisi zaidi; • Maswali na vizuizi vya msikilizaji wa Injili hujibiwa katika uinjilisti wa mtu kwa mtu; • Mtu hujisikia huru nyumbani mwake na kupokea Neno; • Mtu hushindwa kukubali kwa sababu ya kushawishiwa na marafiki au kwa kufuata tu

mkumbo kama kwenye mikutano; • Waliomshuhudia wanaweza kumfundisha na kumshirikisha vizuri zaidi; • Uinjilisti huo unaweza kufanyika na kila mtu (wanaume, vijana, wanawake, n.k.) na siyo

wainjilisti maalum tu wenye uwezo wa kuwahubiria watu wengi hadharani.

4

Uinjilisti mwingi unafanyika siku hizi bila kuleta mabadiliko wala maendeleo yo yote. Uinjilisti wa mtu kwa mtu unaofuata mwongozo wa kitabu hiki kweli utakuwa “uinjilisti ufanyao kazi”.

Kwa sababu hiyo inatupasa kuwa na miongozo mbalimbali katika kueleza huduma hiyo. Afadhali tuanze kwa kueleza uinjilisti wa mtu kwa mtu ni nini na siyo nini. Mwisho tutaweza kufafanua kwa nini tushuhudie.

UINJILISTI WA MTU KWA MTU NI NINI?

Tunaweza kueleza jibu la swali hilo kwa maneno mengi ila kwa urahisi wa kukumbuka, tuya-kariri mambo makubwa mawili.

1. Kumwelezea mtu mmoja mmoja asiye Mkristo Habari Njema za wokovu.

Uinjilisti huo unafanyika kwa mtu mmoja au hata wawili lakini siyo kuwakusanya watu na kuanza kuwahubiria. Uinjilisti huo unahusu mambo yanayomfaa asiye Mkristo. Yaani, anayestahili kuelezwa ni yule ambaye bado hajapata kumkubali Yesu Kristo kama Mwokozi wake na kuokolewa. Aliyeamini na kuokolewa, hata kama siyo mshirika wa dhehebu lako au kanisa lako, hastahili kushuhudiwa wokovu. Aliyetajirika hahitaji kuoneshwa njia ya kutajarika! Wengi siku hizi hufanya hivyo. Huu siyo uinjilisti, bali ni wivi wa samaki waliokwisha kuvuliwa. Nami nina wasiwasi kubwa kama kufanya hivyo kunampendeza Mungu. Makanisa na viongozi wangezitumia nguvu wanazo-tumia kunyang’anyana watu katika kuwashuhudia wale ambao hawajaamini na kuokoka, Mungu angeweza kuleta baraka kuu mno kwa wote!

2. Ni kumwonesha mtu anayesikia Injili jinsi wokovu unavyotimiza mahitaji yake binafsi.

Katika kuieleza Injili kwa mtu mmoja ndipo mwinjilisti anaweza kumlenga hasa msikilizaji na mahitaji yake. Kama katika mazungumzo ya kushuhudia unashindwa kuyagundua mahitaji ya msikilizaji na kumwonesha kwamba kazi aliyoifanya Yesu Kristo msalabani ni kwa ajili ya kuyati-miza mahitaji hayo, basi huduma yako itakuwa kama kusimulia hadithi za kufurahisha tu!

Watu wengi wameshapata kusikia kuhusu Yesu Kristo nao wana msamiati wa mambo ya kikristo, lakini hawajawahi kukutana na Kristo binafsi na madai yake kwao. Hawaoni udhaifu wao na kwamba huo unawazuia kumfikia Mungu Mtakatifu mbinguni. Hiyo ndiyo kazi ya mwinjilisti kuwaelezea jinsi hali yao ilivyo na jinsi mahitaji yao yanapata kutimizwa ndani ya Kristo Yesu na sadaka yake ya uzima.

Ndani ya Injili kuna sehemu nyingi sana. Fikiri kidogo kuhusu mambo yote yaliyotendeka kwako ulipomkiri Kristo kama Mwokozi wako:

• Msamaha wa dhambi zako zote (1Yoh 1:9; Efe 1:7); • Urithi wa ajabu mbinguni pamoja na Bwana (Efe 1:11; 1 Pet 1:4); • Moyo wako ulisafishwa (Zab 51:10); • Nguvu za Mungu mwenyewe ziliingia ndani yako katika utu wa Roho Mtakatifu (Rum 8:9,

10); • Ulipewa mwanzo mpya (2 Kor 5:17); • Ulizaliwa katika familia ya Mungu (Tit 3:5, Yn 1:12); • Ulipata tumaini jipya (Efe 1:12; Tit 3:13); • Ulitiwa muhuri (kuhifadhiwa) na Roho Mtakatifu mpaka siku ya ukombozi (Efe 1:13, 14); • Kazi njema ilianza ndani yako ambayo itamalizika siku ya ukombozi (Flp 1:6); • Ulipata njia ya kuongea na Mungu moja kwa moja (Efe 2:18; Ebr 4:16); • Uliunganishwa na wote walio ndani ya Kanisa lililo Mwili wa Kristo (1 Kor 12:13; Efe 2:14,

15); • Ulipewa uzima tele (Yn 10:10); • Ulipewa uzima wa milele (Yn 3:16; 6:47); • Ulikwepa ghadhabu ya Mungu (Rum 8:1; Yn 3:36); • Ulipata amani na Mungu (Rum 5:1; Efe 1:14); • Ulipata sababu mpya ya kuishi (Flp 1:21; Mdo 20:24); n.k.

5

Kwa kweli wokovu ni utajiri wa ajabu! Utulie, umshukuru na kumsifu Bwana kwa kazi ya ajabu

aliyokufanyia! Sasa unaweza kugundua kwa nini nimeeleza hapo juu kwamba kuna sehemu nyingi za wokovu.

Naamini sana kwamba sehemu moja ya wokovu inakufurahisha zaidi kuliko itakavyofurahisha mtu mwingine, na mtu mwingine ataifurahia sehemu nyingine tofauti. Kazi ya mwinjilisti ni kutafuta hali ya mtu na kumshuhudia kulingana na sehemu zile zinazomhusu ili apate kujua faida ya kuokoka. Naamini kwamba watu wengi hawajaitikia wito wa wokovu kwa sababu wainjilisti hawajafanya ka-zi hii ya kumlenga vizuri msikilizaji na ujumbe wao. Badala yake wahubiri hupenda kuongea wali-yozoea au waliyojifunza shuleni bila kumjali wanayemshuhudia na kujifunza hali zake mbalimbali. Hii imesababisha wafanye uinjilisti usiofanya kazi (usiofanikiwa). Lakini katika kitabu hiki naomba uwe radhi kuchunguza sana hilo suala la uinjilisti linaloyalenga mahitaji na hali ya kila mtu. Hapo ndipo utaufurahia uinjilisti ufanyao kazi.

UINJILISTI WA MTU KWA MTU SIYO NINI?

Njia nzuri ya kukidhihirisha zaidi kitu ni kuonesha kinyume chake. Kwa hiyo itatusaidia kufafanua kidogo mambo ambayo si uinjilisti wa mtu kwa mtu.

1. Si kuhubiri hadharani kwa watu wengi.

Siku hizi wahubiri wamekuwa wengi sana wanaozunguka na vyombo na bendi ili waweze ku-wahubiria watu wengi na kuleta uamsho. Lakini nikiangalia kwa makini nakuta badala ya kuleta uamsho, wanaleta ukinaifu! Kila mtu anasimama na kuyaongea mambo yale yale na kuruka-ruka kuonesha kwamba hapo ndipo kuna Roho wa Mungu. Kwa kweli wengine wanamtumikia Mungu kwa moyo mweupe, lakini ukiwachunguza wengine wanayo makusudi mengine.

Mahubiri ya hadharani yana faida yake. Yanaweza kuwapa watu fikira kuhusu Mungu na Neno lake. Pia, yanasaidia kuuthibitisha uinjilisti wa mtu kwa mtu na kuwapa wainjilisti mlango wa kuanzishia mazungumzo yao katika siku zitakazofuata. Pia, yatambulisha kundi la kanisa ni kundi la namna gani.

Lakini mahubiri haya hayawezi kamwe kuitwa uinjilisti wa mtu kwa mtu, nayo hayalengi na hayafanyi kazi kama uinjilisti wa mtu kwa mtu! Mahubiri haya yanamwaga mbegu kwa watu wote na kutafuta kuwapa watu moyo wa kulisikia zaidi Neno na kuielewa Injili.

Jambo la kushangaza sana siku hizi ni jinsi hata makanisa ambayo hayaukiri wokovu wanaiendesha mikutano ya namna hiyo pia wakieneza ujumbe wao.

2. Si vitendo vinavyofanyika ndani ya kanisa wala kwa Wakristo wengine.

Uinjilisti katika shina lake ni kuwapelekea wapotevu Habari Njema. Huwezi kufanya uinjilisti kwa mtu ambaye alishaokoka. Huku kunaitwa kumwimarisha au kumthibitisha, lakini si kufanya uinjilisti. Kwa sababu kuna watu wengi mno waliopotea, haifai kupoteza muda wa mwinjilisti kwa watu ambao walishaamini. Ni sawa na mkulima ambaye badala ya kwenda kwenye shamba lililoiva na linasubiri kuvunwa anaenda kwenye shamba la mkulima mwenzake ambalo limeshavunwa. Hu-ko ataweza kuokota mabaki tu wakati shamba lake lililoiva linaanza kushambuliwa na ndege na wadudu!

Vilevile kanisani sipo mahali pa kwenda kuvua wapotevu. Kanisani ni mahali pa kuwajenga waongofu na kuwashirikisha wale ambao wameshaokoka ili waimarike; nao waanze kuifanya huduma. Hakuna mvuvi wa samaki anayepanda mtumbwi na kutafuta samaki waliovuliwa na kuwekwa ndani ya mtumbwi mwingine. La, anachukua mtumbwi na anaupeleka baharini ili atupie

6

nyavu zake majini palipo na samaki ambao hawajavuliwa bado. Hali kadhalika na uinjilisti una-osubiri wapotevu wafike kanisani ili washuhudiwe, siyo uinjilisti ufanyao kazi! Lazima mwinjilisti awaendee watu mitaani na nyumbani mwao ili awafikishie Habari hii iliyo Njema kuhusu wokovu.

KWA NINI TUFANYE UINJILISTI?

Lazima tufahamu sababu zetu za kwenda kufanya uinjilisti. Hapo chini nimejaribu kuorodhesha sababu sita zilizo kubwa na za maana ingawa najua kuna sababu zingine nyingi zaidi katika Maandiko Matakatifu.

1. Kumpendeza Mungu na kuonesha upendo wetu kwake.

Tunaposoma Maandiko tunagundua kwamba kushuhudia Habari Njema kunampendeza Mun-gu. Yohana 15:8 inaeleza kwamba Mungu hutukuzwa wakati tunapozaa matunda. Vilevile, 2 Wako-rintho 5:9 inaeleza kwamba popote tulipo shabaha yetu ni kujitahidi katika kumpendeza Mungu. Zaidi ya hayo Mungu alimwuliza nabii Isaya, “Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu?” Ndipo Isaya akajibu, “Mimi hapa, nitume mimi” (Isa 6:8). Naamini kwamba Mungu hupen-dezwa sana tunapojitoa ili tutumwe kushuhudia kwa niaba yake Mungu. Hii inamaanisha tu-meungana naye katika kuokoa ulimwengu. Kwa hiyo, sababu yetu ya kwanza kufanya uinjilisti ni kwamba kushuhudia humpendeza Mungu na kumwonesha upendo wetu kwake.

2. Tuliagizwa kueneza Injili.

Paulo aliyeupokea ufunuo maalum kutoka kwa Kristo Yesu aliweza kutuagiza tuieneze huduma au neno la upatanisho katika 2 Wakorintho 5:18-20. Naamini kwamba hilo ndilo agizo la mwisho kwa wafuasi wake Kristo (na kwa wakati huu) watangaze kuhusu Kristo na kazi yake ya kupatan-isha wanadamu na Mungu kwa njia ya mauti yake msalabani. Vilevile hata Yesu Kristo aliagiza wanafunzi wake waende wakayafanye mataifa yote kuwa wanafunzi katika Mathayo 28:18-20 (Mk 16:15-18). Kwa hiyo sisi kwa agizo lo lote tutakalolishika tunakuta kwamba tunapaswa kuieneza Injili!

3. Upendo wa Kristo unatubidisha.

Katika 2 Wakorintho 5:14 twasoma kwamba “upendo wa Kristo watubidisha”. Halafu vifungu vinavyofuata vinaeleza kuhusu huduma hiyo ya upatanisho; jinsi Kristo alivyotupenda na kujitoa kwetu. Tunapaswa nasi tuwapende wengine na kujitoa kwa ajili yao (1 Yoh 3:16). Vilevile, Paulo alitamka katika 1 Wakorintho 9:16 kwamba, “Ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili!” Paulo aligundua jinsi alivyokuwa kabla hajakutana na Kristo naye alisukumwa na upendo wa Kristo kuwahubiria wengine.

4. Mungu hutumia wanadamu.

Ni ajabu kwamba katika nguvu nyingi za Mungu na uwezo wake wa kuokoa alichagua kuvitu-mia vyombo vilivyo dhaifu kama wanadamu. Mungu angeweza kuwaendea wapotevu kwa njia mba-limbali nyingine. Kwa mfano angeweza kuwatumia malaika, ishara, maono, maandishi ukutani (kumbuka Danieli), sauti ya wanyama (kumbuka Balaamu), au sauti kutoka mbinguni (kumbuka Ubatizo wa Yesu). Lakini mpango wa Mungu kwa leo ni kuitangaza Injili yake akitumia mwanadamu mmoja kumshuhudia mwingine. Chunguza Warumi 10:13-15. Watu hawawezi kuliita jina la Bwana bila kumwamini. Hawawezi kumwamini bila kumsikia. Hawawezi kumsikia bila mhubiri (MWA-NADAMU). Hawawezi kuhubiri bila kupelekwa (WANADAMU TENA). Ibarikiwe miguu ya wana-damu! Mungu amejitengenezea mpango wa ajabu wa kutuhusisha sisi tusiostahili katika kazi yake ya kueneza Injili.

7

5. Uzuri wa ajabu mno wa mbinguni.

Kitu kizuri kinastahili kutangazwa. Kama Wakristo wengi zaidi wangetafakari uzuri wa mbinguni kulingana na hali yetu ya hapa duniani, wangejibidisha katika kuitangaza njia ya kufika huko. Maandiko mengi huonesha baraka zote za mbinguni (Yn 10:10; Efe 1:3; Zab 16:11; Ufu 21:4-11, 18). Watu siku hizi wanatumia muda mwingi kutafakari na kubuni mbinu za kujisafirisha ili wafike Ulaya na Merikani wakati asilimia 99 hawataenda. Ingekuwa bora kutafuta kwa bidii usaf-iri kwa safari yao ya mwisho ambayo itawafikisha katika milele ijayo! Mwanadamu huhangaikia dunia kwa ajlili ya ugonjwa, umaskini, na huzuni nyingi. Tuwatangazie watu kuhusu mahali ambapo mambo hayo hayawezi kuwagusa tena. Tuwaelezee kuhusu mbinguni ili watake kuokoka na kwen-da huko.

6. Mateso na ubaya wa Jehanamu.

Kinyume kabisa cha sababu ya tano ni kwamba wasipochagua kuufuata uzuri wa mbinguni watakuwa wamechagua ubaya na mateso ya Jehanamu. Watu wangefahamu kikamilifu maelezo ya Maandiko Matakatifu kuhusu Jehanamu wangejishughulisha zaidi ili wajiepushe na hali hiyo. Kwanza Jehanamu ni:

a. Hukumu na adhabu - Waebrania 9:27 inaeleza kwamba kila mtu atakufa na baada ya hapo ni HUKUMU. Mathayo 25:46 ineleza kwamba wasioamini “Watakwenda zao kuingia katika ADHABU YA MILELE.” Watu siku hizi hawayaamini Maandiko kwamba Mungu atawahukumu kwa adhabu ya milele. Wanafikiri Mungu atawasamehe tu na hawezi kuwahukumu. Mimi naamini Neno lake Mungu siyo fikira za wanadamu.

b. Mateso - Mathayo 22:13 inaeleza, “Mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” Hakuna anayeweza kutamani mahali hapo! Pia katika Luka 16:23-24 tajiri aliyekufa aliomba sana kwa vile aliteswa sana na moto. Hii ni mifano ya kutuonesha hali ya Jehanamu.

c. Ni ya milele - Soma Mathayo 9:43 na Ufunuo 14:11; 20:10. Mistari yote yaeleza kwamba hali hii ya adhabu na mateso ni ya milele. Wengi wanaamini watateswa kwa muda kidogo halafu watu wakiwaombea au kumhonga padre kiasi cha kutosha, basi wataruka kutoka kwenye mateso kuingia paradiso. Lakini, Neno la Mungu halina hata tone moja la mafundisho haya. Biblia inaeleza dhahiri kwamba kupotea ni kwa milele katika mateso ya ajabu. Kazi ya Shetani ni kudanganya na kuugeuza ukweli wa Neno la Mungu ili watu wasiamini.

Naamini sisi Wakristo tungesaidiwa sana katika uinjilisti wetu tungeweza kwenda kukaa mbinguni kwa dakika moja halafu kwenda Jehanamu kwa dakika moja ili tuweze kupata picha ka-mili ya hali mbili za milele zinazowasubiri wanadamu wote. Tungefanya hivyo tungehubiri kweli Injili! Lakini, Biblia imeshatuelezea wazi; kwa hiyo tushuhudie tunavyofahamu kuwa hiyo hali ni kweli kutoka katika Neno la Mungu. Tukifanya hivyo tutakuwa tunafanya kama Yuda alivyosema, “Waokoeni kwa kuwanyakua katika moto” (Yud 23). MASWALI NA MAJADILIANO

1. Kwa nini ni muhimu tujifunze uinjilisti wa mtu kwa mtu? 2. Uinjilisti wa mtu kwa mtu ni nini? (Taja mambo makuu mawili) 3. Uinjilisti wa mtu kwa mtu siyo nini? (Taja mawili tena) 4. Kwa nini tuufanye uinjilisti huo? 5. Ubaya wa Jehanamu ni nini? (Taja sifa zake tatu)

8

2. Maandalizi ya Mwinjilisti Katika kazi yo yote ambayo mwanadamu huifanya kuna maandalizi. Wengine huamini kwamba

mtu akishajua Yohana 3:16 basi aondoke akaihubiri hiyo hiyo. Je, kama ingekuwa ni kuendesha gari tungemwambia mtu, “Hiki ni moto, kanyaga utaenda”. Halafu tumpe funguo za gari na tumwache aondoke na gari letu la thamani? Hapana, maana atakanyaga na kwenda bila kujua kazi ya usukani wala ya breki. Mwisho wake atagonga kila kiumbe kilicho njiani na atashindwa kusimama hadi ma-futa yatakapoisha! Basi, hali kadhalika tusiharakishe kazi ya uinjilisti hivyo. Maana, ajali nyingi zi-natokea katika mambo ya kiroho kwa sababu hiyo na pia tufahamu kuwa ujumbe tuliokabidhiwa ni wa thamani kuliko ile ya gari.

Kosa moja kubwa linalofanyika kwa wale walio na haraka kuieneza Injili bila kujiandaa, ni kwamba wainjilisti hawa wenyewe hawajapata kubadilika kuwa kielelezo cha ujumbe wao. Kristo aliwaita wanafunzi wamfuate ili wajifunze kwake kisha aliwatuma kuwahubiria wengine. Sisi hatuwezi kuwasaidia wengine kuhusu uzima wa milele mpaka uzima huo umekaa ndani yetu kabisa. Naamini kuna kazi mbili za mwinjilisti, yaani, (1) Kutangaza na (2) Kuthibitisha habari nje-ma ya wokovu. Kutangaza ni rahisi na inawezekana mara moja. Lakini kuthibitisha ni kuonesha mfano wa siku hadi siku jinsi wokovu unavyombadilisha na kumboresha mwanadamu. Kuthibitisha hufanya ujumbe unaotangazwa kuwa hai.

Mapendekezo yafuatayo yaweza kukuongoza unapojiandaa kufanya uinjilisti wa mtu kwa mtu:

1. Uwe mtu wa maombi.

Ukisoma Warumi 10:1 utaona Paulo alisema, “Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe.” Paulo aligundua nguvu za maombi. Mungu hufurahi tunapompelekea hitaji la wokovu wa marafiki zetu. Pia maombi ya kumsihi atu-letee mtu tunayetakiwa kumshuhudia ni maandalizi mazuri kuyafanya. Maombi ndiyo nguvu ya uin-jilisti kwa vile uinjilisti ni kazi ya kiroho siyo ya kimwili.

2. Uwe mnyenyekevu.

Mtu anayefanya huduma ya uinjilisti ili aonekane au atambulike atashindwa kufanya kazi yenye matunda. Wengi katika uinjilisti wa mikutano hufurahishwa na hali ya kuwa mbele ya watu. Lakini uinjilisti wa mtu kwa mtu ni wa siri ukilinganisha na ule wa hadharani. Maana hakuna wanaokufuata ili wakusifu na kuchukua picha jinsi ulivyoingia nyumbani mwa mtu na kumwelezea Habari Njema. Yohana Mbatizaji yu mfano mzuri sana kwetu. Alijiita, “Sauti ya mtu aliaye nyikani” (Yn 1:23). Baadaye, wakati wanafunzi wake walipokuta wengi wanazidi kumwacha na kumfuata Yesu waliona wivu na kumwuliza Yohana kuhusu hali hiyo. Jibu lake limeonesha unyenyekevu unaotakiwa, “Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye (Kristo) hana budi kuzidi, bali mimi kupungua” (Yn 3:30).

Sisi lazima tugundue tu watumishi wa watu tunapowashuhudia (1 Kor 4:5). Watu wenye kiburi hawawezi kuthibitisha Injili kwa wale wanaowahubiria kwa kuwa wanawadharau wale wanaowa-hubiria. Sijui kwa nini siku hizi wahubiri wengi wanaongea kwa ukali wanapoeleza ujumbe wa up-endo na wa ajabu.

3. Uwe mtu mwenye fadhili.

Mtu mwenye fadhili hutafuta nafasi ya kuonesha upendo na fadhili kwa watu wanaomzunguka. Kwa njia hii anathibitisha ujumbe wake. Vilevile watu watakaposikia maneno yake watayathamini na kuyatilia maana kwa vile ameshawashuhudia kwa matendo mema (Mt 5:16).

Ushuhuda hauwezi kuwa kamili tukiwahubiria watu tu bila kuwasaidia pia. Kila wakati, kulin-gana na jinsi Mungu ametujalia, tunpaswa kuyasaidia mahitaji na matatizo yao mengine tukiwafariji na kuonesha uradhi wetu wa kuwasaidia kimwili. Tukiishi hivyo tutajulikana hivyo na mwisho tutakapopata nafasi kumshuhudia Kristo ujumbe wetu utasikilizwa.

4. Uwe mtu wa kujikana na kutanguliza Injili mbele kuliko manufaa ya kimwili.

Mtu hawezi kufanya kazi ya kueneza Injili kikamilifu kama ana mawazo kuhusu faida yake bin-afsi. Maana huduma hiyo haina faida ya kimwili kwa ajili ya mwinjilisti mwenyewe. Bali, huduma inawalenga hasa wapotevu na Mungu. Mwinjilisti hawezi kusaidia mahitaji ya wengine ikiwa macho

9

yake yanajiangalia tu. Atakosa kugundua mahitaji ya wapotevu, nao hawataweza kuitikia ujumbe wake wa wokovu.

Paulo alisema katika 2 Wakorintho 12:15 kwamba alikuwa radhi kutapanya na kutapanywa kwa ajili ya roho za watu. Maana yake ni kwamba alijinyima kwa hiari yake ili watu wapate kusikia Injili na kuokoka. Tunapotanguliza furaha ya dunia hii hatuwezi kutazamia kufanya uinjilisti wenye matokeo yo yote. Yesu mwenyewe aliwaelezea wanafunzi wake kwamba mtu hawezi kushika plau kisha akaangalia nyuma. Mkulima wa namna hii atalima mistari ya ajabu na ya kuleta uharibifu shambani kuliko faida (Lk 9:23).

5. Uwe na imani kubwa katika uwezo wa Bwana kuwaokoa na kuwabadilisha wenye dhambi.

Kutangaza habari hii ya nguvu, lazima sisi wenyewe tuwe tumeshakuwa na uhakika kuhusu uwezo wa Bwana kuokoa ili tuwe kama mtume Paulo aliyesema, “Siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye” (Rum 1:16). Paulo aliamini kwamba Mungu hawezi kushindwa kumwokoa mtu ye yote anayeamini. Je, nasi tunaamini hivyo? Au mara nyingi tunawaza, “Huyu ni mbaya, hawezi kubadilika na kuokoka.” Kumbuka kwamba, “Mungu hapendi mtu ye yote apotee” (2 Pet 3:9).

Paulo mwenyewe alifahamu haya kwa vile yeye alikuwa mwuaji aliyelitesa kanisa kabla hajaokoka. Lakini Mungu aliweza kumwokoa pamoja na ubaya wake wote. Kumbuka hata Musa na Daudi walikuwa wauaji, nao wakapata neema kutoka kwa Mungu wakisamehewa! Je, kuna dhambi kubwa kiasi Mungu hawezi kuisamehe? La! Hasha!

6. Uwe tayari kupiga vita kuwaonesha watu mfano wa faida ya wokovu maishani mwako.

Kwanza lazima wewe mwenyewe uwe umeokoka kweli kweli na uwe na uhakika kuhusu wokovu wako. Pili, wokovu wako unapaswa kuwa umekubadilisha zaidi na zaidi ili uishi namna tofauti na jinsi ulivyoishi kabla hujaokoka. Watu wengi siku hizi hawahitaji maelezo zaidi kuhusu wokovu bali wanahitaji kuona kielelezo chenye kuonesha matokeo mazuri ya wokovu. Kama hatuwezi kuonesha maishani mwetu manufaa ya kuwa Mkristo wa kweli, basi maneno yetu hayatakuwa na maana kwa wengine. Yatupasa kumsogelea Bwana na kuongozwa naye ili wengine waone jinsi ushirikiano wetu na Bwana ni mzuri.

Pamoja na hiyo, tujue hatuwezi kwenda mbele ya watu kama watu tuliokamilika kabisa. Bali, kazi yetu ni kuwaonesha kwamba tunayo nia ya kukua na kujifunza kwa Bwana. Maisha ya kikristo ni vita vya kiroho. Paulo alimwambia Timotheo, “Piga vita vile vizuri vya imani” (1 Tim 6:12). Lazima tuwe tayari kuvaa silaha zote za kiroho ili tuweze kushinda katika vita hivyo (Efe 6:11-18). Tusiwe kama askari aliyeingia vitani bila kuvifahamu vita vyenyewe namna vilivyo wala hakuiandaa hata silaha moja; ukweli huyu hataweza kushinda!

Nafikiri neno kubwa katika somo hili kuhusu maandalizi ya uinjilisti ni kujitoa kabisa kwa Bwana na kujitahidi kuimarika ndani yake ili Yeye aweze kufanya kazi yake ndani yetu na kupitia kwetu. Yote haya ni kusema tuyaangalie maisha yetu na mioyo yetu apendavyo Yeye. Katika hudu-ma hii tukijiendea haiwezi kuleta mafanikio yo yote, bali tukiomba na kuutafuta hasa uongozi wake Mungu, Yeye hatakosa kuyatimiza mapenzi yake.

MASWALI NA MAJADILIANO

1. Kwa nini ni muhimu kuwa na maandalizi katika kazi ya uinjilisti? 2. Kwa nini maombi ni muhimu katika maandilizi hayo? 3. Je, unaweza kujifunza unyenyekevu kwa njia gani? 4. Tunapaswa kuwa na imani kubwa katika nini? Kwa nini? 5. Unaweza kuchukua hatua gani katika kupiga vita ili kuwaonesha watu mfano wa wokovu

maishani mwako? 6. Neno kubwa katika somo hili ni nini?

10

3. Ujumbe Tunaoshuhudia Unaweza kushangaa kwamba somo hili limeingizwa kwenye kitabu hicho. Pengine ungewaza

ujumbe tunaohubiri ni wazi. Sawa, labda kwako wewe ni wazi, na kama ni hivyo ubarikiwe! Lakini nashangaa sana nikizichunguza jumbe mbalimbali ninazosikia siku hizi zinazoenezwa kwa jina la “Habari Njema”. Kwa sababu hiyo inatupasa kulichunguza suala hilo kwa uangalifu na inawezekana utakuta hata wewe umeingia kwenye mtego huo wa kubadilisha ujumbe unaotakiwa kushuhudiwa.

Tuanze kwa kusema kwa kifupi Injili tunayoshuhudia ni nini, halafu tutaziangalia jumbe mba-limbali zinazohuburiwa siku hizi ambazo si Injili za kweli. Mwishoni, tutafafanua ujumbe wa kweli ili wote waweze kuueleza na kuukumbuka bila kuubadilisha.

INJILI TUNAYOPASWA KUIENEZA

Paulo aliieleza Injili kwa kifupi katika 1 Wakorintho 15:1-4 akisema: “Nawaarifu ile injili nili-yowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyohubiri; isipokuwa mliamini bure. Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko.”

Vilevile katika 1 Wakorintho 2:2 alijumlisha ujumbe huo kwa kusema, “Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa.”

Petro aliweza kutoa muhtasari mzuri sana wa Injili katika waraka wake wa kwanza sura ya tatu mstari wa 18 tunaposoma: “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuish-wa.”

Nafikiri tungeweza kuchunguza maandiko mengi zaida lakini jibu letu limeshaonekana kwam-ba ujumbe wetu hasa ni juu ya KRISTO YESU NA KUFA KWAKE KWA AJILI YA DHAMBI ZETU ILI TUPATE KUSHIRIKIANA NA MUNGU. Mambo mengine yanayochanganywa na habari hii siyo Injili ya kweli. Kwa hiyo baada ya kusema hayo tungependa kuzichunguza jumbe mbalimbali zinazo-hubiriwa siku hizi ambazo zinaongeza au kupunguza ujumbe huo tunaopaswa kuutangaza.

INJILI NYINGINE ZINAZOHUBIRIWA SIKU HIZI

mtume Paulo aliowaonya sana watu wa mji wa Galatia alipokuta wameanza kuifuata injili nyingine. Hebu tujifunze umuhimu wa suala hilo kwa kusoma onyo lake:

“Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini ijapokuwa sisi au malaika atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.” (Gal 1:6-9)

Baada ya kusoma onyo hilo tunapata sababu ya kujichunguza ili kuhakikisha injili tunayo-ihubiri ni ya kweli. Maana hatutaki kuingia katika kosa la kuubadilisha ujumbe wa kweli. Katika kuyasikiliza mahubiri ya siku hizi Afrika Mashariki, tumeamua kuorodhesha aina tano za injili zisizo za kweli. Narudia kusema zote hizi zinahubiriwa sasa hivi na wainjilisti mbalimbali ingawa si injili za kweli!

1. Injili ya matendo (sheria).

Hiyo injili inatangaza kwamba kazi ya Kristo Yesu msalabani haikutosha kulipia wokovu wa wako. Inadai ni lazima uongeze masharti fulani ya kanisa lao ili uokoke. Kawaida masharti haya ni kama vile kutoa sadaka, kuhudhuria kanisani, kuungama dhambi, kubatizwa kwa maji, au kufanya matendo mengine ya haki. Lakini Biblia inaeleza wazi katika Waefeso 2:8-9 na Tito 3:5 kwamba hakuna matendo yo yote yanayoweza kukuokoa wala kuchangia wokovu wako. Baadhi ya viongozi wa makanisa hawapendi kumpa Kristo utukufu wake kamili katika uwezo wake wa kuokoa. Ha-wapendi kufanya hivyo kwa sababu wanaogopa waumini wapya wakifahamu Yesu peke yake ame-

11

fanikisha wokovu wao, waumini hawa wapya hawatashiriki shughuli za kanisa kikamilifu wala kuchangia kanisa kama shukrani yao kwa ajili ya mchango wa kanisa katika wokovu wao. Yaani, wanataka waumini wapya kufikiri kanisa limechangia wokovu wao ili wajitoe kanisani kama shukrani. Lakini, kumbe, kanisa halichangii cho chote kwenye wokovu wa mtu.

Wengine wanaweka sheria nyingi zinazohusu vyakula, siku, vinywaji, na hata nguo na nywele wakikosa kuzingatia kwamba, “Hakuna mwenye mwili atakayehesibiwa haki mbele zake kwa maten-do ya sheria” (Rum 3:20; Gal 2:16). Hiyo ndiyo injili mbaya ambayo iliwapata watu wa Galatia na mtume Paulo aliwaonya sana kuhusu hatari ya injili hii.

2. Injili ya kuachana na dhambi na kuwa mtakatifu.

Naamini kwa moyo wangu wote kwamba wanaoihubiri injili hii hawana makusudi mabaya. Lakini wameshindwa kuelewa maana ya kuokoka. Ukiwauliza hawa jinsi ya kuokoka, bila shaka watajibu unahitaji kumwamini Yesu lakini pia wataongeza hitaji la kuachana kabisa na dhambi kwanza. Hapo juu tulieleza Injili ya kweli inasema Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. Katika kuzifia dhambi zetu, aliweza kuondoa adhabu ya dhambi zetu (mauti ya milele) na pia aliweza kutupatia sisi tuliookoka nguvu ya kushinda dhambi tukimruhusu Roho Mtakatifu kututawala kati-ka maisha yetu ya kikristo baada ya kuokoka (Efe 5:18). Wanapokosea katika injili hii ya uongo ni pale wanaposema waliookoka ni wale walioachana na dhambi kabisa. Hakuna mwanadamu anayeweza, katika nguvu zake mwenyewe, kabla hajaokoka, kuachana na dhambi kwanza ili am-wamini Yesu na kuokoka. Ni lazima aokoke akiwa mwenye kutenda dhambi na baada ya kuhuishwa na Kristo katika wokovu wake, ndipo ataweza kutotawaliwa na dhambi.

Wengine wanaohubiri injili hii ya kuachana na dhambi, hudai vilevile, baada ya kuokoka Mkristo hatatenda dhambi tena. Huu, nao, ni uongo mkubwa. Ni kweli mtu aliyeokoka siyo mtumwa tena wa dhambi na kwa kumtegemea Roho Mtakatifu katika maisha yake ataweza kupunguza kiasi cha dhambi katika maisha yake. Lakini mpaka Wakristo watakapopewa miili ya utukufu wa-taendelea kutenda dhambi mara kwa mara kutokana na asili yao ya dhambi.

Uongo huo, wa kusema Wakristo hawatendi dhambi, husababisha wengine kukataa kuokoka kwa sababu ni wazi hata anayewahubiria bado anatenda dhambi. Sababu hata Wakristo wanaen-delea kutenda dhambi ni kwa sababu dhambi inafanyika katika mawazo, moyo, matendo, maneno, makusudi, na hata katika kutofanya kitu fulani kinachopaswa kufanywa (Yak 4:17). Dhambi ni ku-kosa kutimiza mapenzi na makusudi yote ya Mungu. Wakristo wanajitahidi kutimiza mapenzi ya Mungu lakini kutokana na udhaifu wao wanashindwa katika sehemu nyingine mara kwa mara. Dhambi zinatendeka kila siku na watu wote duniani, hata Wakristo. Tazama 1 Yohana 1:8-10,

“Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.”

Kuhubiri injili hiyo inawakatisha tamaa wenye dhambi. Maana mlevi na mwasherati wanakosa kuamini kwa vile wamekuwa watumwa wa tabia zao na hawawezi kuachana na dhambi zao ili waje kwa Yesu. Lakini tukiwaalika kwa Kristo kama walivyo na kuwaonesha kwamba Kristo anaweza kuwapa nguvu ya kushinda dhambi, Injili ya namna hii wataipokea. Tuangalie tusije tukabadilisha maana ya kuokoka na kumfanya aliyetufia awe mwongo!

3. Injili ya raha (starehe).

Injili hii inatangazwa sana kati ya watu walio maskini na wenye kuhangaika wakiwa na mata-tizo mengi. Injili hii huahidi kwamba shida zako zote zitaisha mara utakapomkubali Kristo kuwa Mwokozi wako. Injili hii mara nyingine inaahidi msaada wa kimwili na hata kutarijika na kuachana kabisa na umaskini. Lakini Yesu mwenyewe aliita watu kuachana na mambo ya kidunia akitaka wa-fuate mambo ya kiroho. Kwa mfano alimwambia tajiri kuuza yote na kuwagawia maskini, kisha amfuate.

Ni udanganyifu mkubwa kumwaahidi mtu kwamba mume wake hatampiga tena kama at-ampokea Kristo. Ni kosa kubwa kumwambia mtu kwamba ataanza kula wali kwa nyama akimpokea Yesu Kristo badala ya ugali kwa maharage. Biblia haina injili kuhusu utajiri wala raha za kidunia. Tunachohubiri kutoka Biblia ni kwamba Kristo ataingia ndani yako na kukusaidia kupita katika shida nyingi ulizo nazo. Kristo, ukimruhusu, anaweza kukupa amani katika mateso na ugonjwa ulio

12

nao. Lakini Kristo hajaahidi Wakristo hawatakuwa na matatizo katika dunia hii. Mara nyingine mtu anapookoka ndipo shida zinaanza kuwa kali zaidi kwa vile Shetani ame-

chukia wokovu wake na hutaka kumwangusha. Tusiwadanganye watu ili waumini kwa kuwa wasipotimiziwa ahadi hizo za kimwili watamwacha Kristo mara watakapokutana na ugumu maishani mwao.

4. Injili ya ishara za kimwili.

Injili hii inahubiriwa sana na wahubiri wale wakubwa-kubwa wanaofanya mikutano mikubwa. Mara nyingi wanahubiri vizuri sana, tena kwa usahihi, kuhusu wokovu ulio ndani ya Kristo Yesu bila matendo. Lakini baada ya kualika watu kumpokea Kristo kuwa Mwokozi wao, kwa njia ya imani, nyongeza zingine hutokea.

Kwa mfano, mara nyingine wanasema kwamba watu wataponywa kimwili badala ya kutosheka na jinsi Mungu alivyowaponya kiroho ili wasihukumiwe Jehanamu. Au, wanaanza kuwaombea watu wakitafuta ishara kama kunena kwa lugha ili ioneshe mtu amejazwa na Roho Mtakatifu. Lakini Bib-lia inafundisha karama hii ilitolewa kwa wachache wakati wa mitume, siyo kwa wote (1 Kor 12:30).

Wanadamu wanao ugonjwa mkubwa sana wa kutaka kuona mambo ya kiroho kwa macho yao wenyewe. Kawaida wanataka kuamua wenyewe kuhusu ishara za Mungu. Naamini kabisa Mungu huponya watu siku hizi pale anapotaka yeye. Lakini pia, nimeyaelewa Maandiko Matakatifu kwam-ba ishara hizo zimeisha kutokana na kukamilika kwa Biblia (1 Kor 13:8-12). Hata wanaoamini isha-ra hizo bado zipo leo, wanakubali kwamba haieleweki kwa nini wengi hawawezi kupona na kupata ishara hizo.

Ubaya wa injili hii ni kwamba inapotosha wasikilizaji wengi. Wanapokosa kupata ishara hizo wanaona hawajaokoka kweli kweli. Lakini wokovu hauwezi kuhakikishwa kwa mambo ya kimwili bali unahakikishwa na Roho Mtakatifu ndani yetu akitumia Neno la Mungu (1 Yoh 5:13; Rum 8:16). La kusikitisha zaidi ni kwamba injili hii inasisitiza sana mambo haya ya ishara na mara inaacha Ne-no la Uzima linalookoa.

5. Injili ya kidhehebu.

Injili hii inatangazwa sana. Makusudi makuu ya injili hii ni kuongeza wanachama (washirika) wa kanisa au dhehebu lao. Siku hizi badala ya kuzitanguliza habari za Kristo Yesu na kutaka kuona watu wakiingia katika Kanisa lililo Mwili wa Kristo, wainjilisti wanatangaza uzuri wa dhehebu lao jinsi lilivyo bora.

Wahubiri wa injili hii wanasema mtu amekata shauri hata kama mtu huyu ni mshirika wa ka-nisa jingine aliyeokoka tayari. Wanawabatiza kana kwamba wanapokea wokovu, wakati wanachokifanya ni kubadilisha kadi ya chama chao tu. Wengine wanadai kwamba hakuna waliookoka nje ya dhehebu lao. Nina hakika kwamba wazo hilo linamsikitisha Mungu. Mungu hu-taka waliookoka kuwa ndugu katika Bwana bila kuangalia jina la kanisa lao wala taratibu za ibada zao au hata ubatizo wao.

Waliookoka wanapaswa kuungana na kuzitumia nguvu zao kuwafuata na kuwaokoa wali-opotea kwa kuhubiri Injili ya kweli kuhusu Yesu Kristo. Mungu hajawahi kubuni dhehebu lo lote, wanadamu hupenda kutengana na kuvutana lakini Mungu hutaka umoja. Sisemi tungeweza kuun-gana kuwa kanisa moja, bali tusaidiane katika kazi hii ya kuitangaza Injili ya kweli bila kujali mwongofu atajiunga na dhehebu gani, maadamu ajiunge na Kristo mwenyewe!

Shetani hutumia aina zote hizi tano za injili za uongo kupunguza na kuondoa watu kutoka kati-ka Injili ya kweli kwa kuwa amegundua uwezo wa Injili ya kweli (Rum 1:16). Tujichunguze kuhakikisha tunamhubiri Kristo na kazi yake ya kuokoa na siyo moja wa mitego hiyo iliyotajwa hapo juu. UJUMBE WA KWELI ULIVYO

Kwa matumizi yetu ningependa kueleza kuhusu ujumbe tunaoshuhudia katika sehemu tatu rahisi.

1. Wote ni wenye dhambi na wanastahili kuhukumiwa adhabu.

Mtu asipoweza kugundua upungufu wake na kukubali hali yake ya dhambi inayomfanya kupotea na kutengana na Mungu milele, basi, hataweza kuona hitaji lake la ukombozi. Vifungu vinavyoweza kumsaidia na kumwonesha haya ni: Rum 3:10, 11, 23; Isa 53:6; 1 Yoh 1:8, 10; Efe

13

2:1-3, 5; Rum 6:23; Ebr 9:27; Isa 59:2. Katika kushuhudia ni muhimu kujiunga na msikilizaji na kukubali kwamba wewe mwenyewe ni

mwenye dhambi. Kuonekana huna dhambi itamfanya msikilizaji kujiweka hivyo pia. Mara nyingi itabidi umfafanue maana ya dhambi kwa kuwa wengi wanawaza dhambi ni makosa makubwa tu.

2. Yesu Kristo alikufa ili aziondoe dhambi zetu na atuokoe.

Mtu akishaitambua hali yake ya kupotea na hali yake ya kuwa chini ya adhabu; ndipo utapaswa kumwonesha ukombozi wa Kristo. Mungu alifanya mpango wa ajabu kwa kumtuma Yesu Kristo kuwaokoa wanadamu waliopotea (Rum 5:8; 8:1; 1 Pet 3:18; Yn 3:16; 2 Kor 5:17, 21; Efe 2:4-6; Yn 14:6; Mdo 4:12). Alifanya hivi kwa sababu mtu asingeweza kujiokoa mwenyewe kwa njia yo yote ile (Meth 14:12; Efe. 2:8, 9; Tit 3:5; Isa 64:6; Rum 3:20, 28).

3. Mtu huokoka kwa kuungama na kumwamini (kumpokea) Kristo kama mwokozi wake binafsi.

Hatua hiyo ni ya muhimu kabisa kuonesha kwamba mtu hupata kufaidika na kazi ya Kristo akiungama na kumwamini Kristo kama Mwokozi wake mwenyewe. Kufanya hivyo kunafanya Injili iwe hai kwake. Mistari ya kusaidia ni: Rum 10:9, 10, 13; Yn 1:12; 1 Yoh 5:11, 12; Mt 11:28; 1 Yoh 1:9; Mdo 16:31.

Kwa kuzifuata na kuzijua sehemu hizi tatu za Injili, mwinjilisti huweza kutumia Neno la Mungu kumsaidia mtu ili aweze kuokoka. Vilevile anaweza kumlenga msikilizaji pale ambapo ana mahitaji. Katika maandalizi, ni vizuri kwa mwinjilisti kukariri vifungu vingine au kuweka alama kwenye Bib-lia yake na kuandika maelezo pembeni ya mistari.

Mfano mmoja unaotumiwa sana katika kazi ya uinjilisti ukiwa na mafanikio mengi ni mfano wa daraja. Faida ya mfano huo ni jinsi unavyoweza kuutumia kwa njia mbalimbali kulingana na msikilizaji wako. Chunguza mchoro huu kabla hujaendelea mbele.

MFANO WA DARAJA LA UZIMA

MASWALI NA MAJADILIANO

14

1. Kwa nini ni muhimu kuwa na uhakika wa ujumbe tunaoshuhudia? 2. Injili ya kweli ni nini kwa kifupi? 3. Injili nyingine zinazohubiriwa siku hizi ni zipi? 4. Injili ya raha ni nini? Umewahi kuisikia kwa wainjilisti? 5. Hatari ya injili ya ishara ya kimwili ni nini? 6. Je, Injili ya kweli inafundisha kuacha dhambi? 7. Sehemu kubwa tatu za ujumbe wa kweli ni nini?

4. Kazi ya Ushuhuda Wako Katika ujumbe tunaoshuhudia kifaa kimoja kilicho muhimu ambacho hatujakiongelea ni

ushuhuda wako binafsi. Huo ushuhuda unahusu jinsi Kristo alivyokuokoa wewe. Kwa kueleza ushuhuda wako, unaweza kumsaidia mtu kuona faida ya kuwa Mkristo na jinsi Mungu anavyofanya kazi kuwabadilisha watu wanapookoka.

Soma mwongozo unaofuata ambao unaeleza jinsi ya kuuandika ushuhuda wako. Halafu fuata muundo huo kuuandika ushuhuda wako ukitafuta uwiano katika sehemu zote tatu: (1) Kabla si-jampokea Kristo; (2) Jinsi nilivyompokea Kristo; (3) Tangu nilipompokea Kristo.

1. Simulia ilivyokuwa kwako binafsi, usihubiri. Tumia maneno “mimi” na “yangu” na siyo “wewe”. 2. Tengeneza ushuhuda mfupi. Dakika 3 hadi 5 zinatosha kusimulia ushuhuda wako. 3. Umweke Kristo kuwa kiini au kitovu cha ushuhuda wako. Eleza jinsi Yeye alivyokufanyia. 4. Tumia Neno la Mungu. Kifungu kimoja au viwili tu vya Maandiko hutia nguvu katika ushuhuda

wako. Kumbuka Neno la Mungu lina ukali (Ebr 4:12)! 5. Jaribu kueleza jinsi ulivyofanana na msikilizaji wako kabla hujampokea Kristo na kwa nini uli-

hitaji Mwokozi ili aitambue haja yake ya kuwa na Mwokozi pia. 6. Tumia muundo ufuatao:

USHUHUDA WANGU

(1) Kabla sijamwamini Kristo: ________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

(2) Jinsi nilivyomwamini Kristo: ________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

(3) Tangu nilipomwamini Kristo: ________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

Sasa, fanya mazoezi ya kueleza ushuhuda wako ili uweze kuutumia kuwashuhudia wengine. Omba mtu mwingine akusikilize akijifanya kama yeye ni mpotevu. Hakikisha maneno unayotumia yanaeleweka kwa mtu wa kawaida ambaye haendi kanisani.

Ushuhuda wako unaweza kutumiwa kama utangulizi katika kuanzisha Injili au kutia mkazo katika ujumbe wako unapomwelezea mtu mwingine.

MASWALI NA MAJADILIANO

1. Sehemu tatu kuu za ushuhuda wako ni nini? 2. Kuandaa ushuhuda wako husaidia nini? 3. Unaweza kutumiaje ushuhuda wako kuwashuhudia wengine? 4. Kwa nini siyo vizuri kutumia maneno magumu ya kikristo? 5. Je, umefanya mazoezi ya kuusema ushuhuda wako?

15

5. Vifaa vya Uinjilisti Kila kazi ina vifaa vyake. Fundi seremala siyo fundi bila randa, msumeno, na nyundo. Hali

kadhalika, mwinjilisti asiye na vifaa vya kazi yake anaweza kushindwa kutimiza kazi yake. Lakini kuwa na vifaa havimfanyi mtu afaulu kazi. Maana ukimpatia mtu ye yote mwiko haina

maana ataweza kuijenga nyumba na kunyosha ukuta. Vilevile mtu mwenye vifaa vya uinjilisti asipojifunza na kujizoeza namna ya kuvitumia, haviwezi kumsaidia.

SILAHA YA MWINJILISTI

Hakuna silaha kuu kwa mwinjilisti kuliko Neno La Mungu. Mtu anayetaka kushuhudia lazima alifahamu Neno la Mungu. Yaani aweze kuonesha anayemshuhudia njia ya wokovu kwa kutumia Neno La Mungu. Uwezo wa Maandiko Matakatifu ni mkubwa mno! Waebrania 4:12 inasema kwam-ba, “Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu!” Waefeso 6:17 inaeleza Neno ni “upanga”. Katika vita vya roho za watu lazima tutumie upanga. Ni lazima silaha ya Biblia itumiwe hata kama msikilizaji ha-ziamini nguvu zake! Kwani jeshini, adui akisema haiamini bunduki yangu inaweza kumpiga risasi, ina maana nisiitumie? La, nitamwua na hiyo hiyo asiyoiamini!

Biblia ndiyo mamlaka ya ujumbe wetu. Hata wasipotamka, wanadamu wanaheshimu Neno La Mungu. Ninapotumia silaha ya Biblia inaonesha kwamba ninachoeleza siyo hadithi tu niliyoitunga mimi wala ujanja wangu, bali ni ujumbe kutoka kwa Mungu mwenyewe. Mungu aliahidi katika Isaya 55:11 kuwa, “Ndiyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.”

VIFAA VINGINE VYA UINJILISTI

Kuna vitu vingine vinavyosaidia sana huduma hii ya unijilisti wa mtu kwa mtu. Tuviangalie vi-chache hapo chini:

1. Vipeperushi au sehemu za Maandiko.

Kuwa na maandiko ambayo unayagawa au kuyauza kunasaidia sana jinsi ya kuongea na mtu unapomshuhudia. Mtu hufurahi akipokea kitu, au akiweza kununua kwa bei ndogo, kwa kuwa ata-jisikia umemsaidia kitu. Vilevile anapoachana nawe ataweza kuendelea kujifunza zaidi. Pia, uki-andika jina lako, au la kanisa lako, pamoja na anwani na simu, mtu huweza kukufuata baadaye aki-wa na maswali zaidi au akitaka kukata shauri baada ya kusoma maandiko yale.

Katika historia mafanikio makubwa ya huduma za viongozi wa kikristo yamesaidiwa sana na maandiko. Wengi wamegundua umuhimu wa kuchapisha maandiko ili waelimishe watu jinsi ya kumwamini Kristo na jinsi ya kutembea naye. Kuna watu wengi wanaoshuhudia jinsi maisha yao yalivyobadilika baada ya kusoma maandiko fulani yaliyochoma mioyo yao.

Mwishowe ni vizuri kuwa na maandiko ya kumsaidia yule ambaye atakata shauri na kumpokea Kristo. Yaani masomo ya muumini mpya. Pia ujiandae kuwapa waumini wapya Agano Jipya au Injili ya Yohana kuwasaidia kuanza kukua kiroho mara watakapozaliwa mara ya pili.

Lakini nikuonye, usitumie kama zawadi kuwashawishi watu kukata shauri ili wapokee kitu.

2. Kalamu na daftari au karatasi chache.

Kuwa na vitu hivyo vitakusaidia kuandika jina la mtu uliyemshuhudia pamoja na anwani na simu yake ili uweze kumfuata baadaye na kuona maendeleo yake. Pia, itakusaidia kumwachia jina lako na anwani na simu yako ili akufuate baadaye. Mara nyingine ni vizuri kuandika barua ndogo na kuiacha mlangoni kwa mtu uliyemtembelea ambaye hakuwepo. Pia, unaweza kutunza taarifa ya ka-zi yako, kama vile vizuizi mbalimbali vya walioshuhudiwa, ili uvikumbuke mara utakapowarudia.

3. Mfuko wa plastiki au mkoba.

Mfuko huo unaweza kukusaidia kubeba vipeperushi au vitabu vichache na hata Biblia yako. Kuwa na mfuko huo kutakusaidia kuzuia vumbi na mvua isiyadhuru maandiko yako pia. Mara nyingine watu wana hamu kufahamu uliwaletea nini ndani ya mfuko wako, ndipo utawaonesha maandiko na kuingia katika Injili kirahisi.

16

4. Fedha kidogo.

Kuwa na akiba kidogo kunaweza kusaidia sana, maana mara nyingine utaweza kuanza kazi hiyo na kusahau muda. Ndipo utajikuta uko mbali na nyumbani na njaa imeuma. Ukiwa na fedha kidogo unaweza kujinunulia chai au matunda kuongeza nguvu ya kuendelea na kazi bila kuzuiliwa. Vilevile, mara nyingine utakutana na mahitaji ya unayemshuhudia kama ugonjwa au kilio na uta-weza kuonesha upendo na fadhili kwake kwa vile umejiandaa.

5. Viatu vyepesi.

Kazi ya uinjilisti ni kazi ya askari anayejidharau. Mtu ambaye anataka aonekane vizuri akivaa viatu visivyofaa atashindwa kutembea mbali na mwishoni atashindwa kumshuhudia Kristo kwa wengi. Nafuu kuifahamu kazi hiyo ni ya kutembea na awe askari aliyejitayarisha na viatu vinavyofaa ili afikishe Injili kwa watu wengi zaidi.

Hivi ni vifaa vya uinjilisti vinavyoweza kusaidia ili kazi zifanyike vizuri. Lakini, siyo lazima mtu awe na vifaa hivi vyote kabla hajafanya uinjilisti. Vilevile kuna vifaa vingine ambavyo vinaweza ku-tumiwa ambavyo havijatajwa hapo.

MASWALI NA MAJADILIANO

1. Silaha ya Mwinjilisti ni nini? 2. Kuitumia Biblia unaposhuhudia kunasaidia nini? 3. Vipeperushi vinaweza kusaidia nini? 4. Vifaa vingine ni vipi na kwa nini vinasaidia? 5. Kuna vifaa vingine ambavyo havikutajwa?

MAZOEZI

Fikiri kuhusu mahitaji ya kila mmoja wa watu wafuatao. Kwanza andika mahitaji yake makuu. Halafu fikiri ni kwa njia gani ungeweza kumshuhudia mtu huyu kwa kumlenga jinsi alivyo; yaani, ni sehemu gani ya Wokovu ungeikazia?

Adamu: Mkristo wa Jina tu, anafikiri ameshaokoka lakini anaamini kubaki kwake katika dhehebu lake na kufuata masharti ya kanisa kutamwokoa.

Henry: Alikuwa mshirika wa dhehebu kubwa zamani lakini alikata tamaa na kuacha kusali ali-pokuta hakuna faida sana kwenda kanisani.

Lenodi: Mpagani ambaye hajawahi kuhudhuria kanisani. Hajui kabisa Biblia na anashiriki dini ya asili.

Mariamu: Mshiriki mzuri wa kanisa lakini hajui Biblia ingawa humwamini sana mchungaji wake na dhehebu lake tangu vizazi vitatu. Hapendi kuacha kanisa lake.

Omari: Mwislamu anayelikataa Agano Jipya na uungu wa Kristo. Hashiriki sana dini yake lakini hafurahii ujumbe wa kikristo. Huamini njia nyingine ya kumfikia Mungu.

Amani: Mke wa pili kwa mumewe Ali. Alimchukua baada ya kumpa mimba na anavumilia vurugu za nyumbani mradi anapata chakula na mahali pa kulala. Ni mlevi na anasaidia mradi wa kukoroga pombe. Huogopa kushindwa kuishi maisha matakatifu ya muumini.

17

6. Njia ya Kushuhudia

Mpaka sasa tumejifunza kuhusu maandalizi ya mwinjilisti na ujumbe tunaoshuhudia. Vilevile tumejifunza jinsi ya kutumia ushuhuda wetu kuongeza nguvu katika uinjilisti wetu na mwishoni tumeangalia vifaa vya uinjilisti wa mtu kwa mtu. Kwa hiyo sasa tunastahili kuchunguza utendaji wa uinjilisti wenyewe. Yaani jinsi ya kushuhudia mtu mmoja mmoja au nyumba kwa nyumba. Tutaan-galia somo hili kwa sehemu tatu: (1) Unapoenda kushuhudia na njiani; (2) Unapomfikia mtu mwenyewe na kumshuhudia; na (3) Unapotaka kumaliza na kuachana na mtu uliyemshuhudia. KWENDA KUSHUHUDIA

Katika siku ambayo unataka kuondoka kwenda kuwashuhudia watu fulani kuna mambo mba-limbali ya kukumbuka.

1. Panga timu yako na eneo utakaloendea.

Mkutane kanisani au nyumbani mwa mtu mmoja kati ya timu yako ya uinjilisti. Mwe watu wawili au watatu, mkiwa zaidi mtamwogofya msikilizaji. Pia, mkiwa zaidi ya jinsia moja, lazima wanaume wawe wawili au wanawake wawe wawili kuondoa mawazo mabaya ya watu (yaani msiende mwanaume mmoja na mwanamke mmoja kama siyo mume na mke wake). Timu ya namna hiyo inaweza kukutana na wanawake au wanaume. Ikiwa timu yako ni watu wa jinsia moja basi mlenge hasa watu wa jinsia yenu (yaani kiume kwa kiume na kike kwa kike).

Timu yenu inapaswa kupanga maeneo mnayolenga kushuhudia ili juma linalofuata mweze kuanza huko na kuendelea hadi mmalize sehemu yote mliyoipanga. Ni vizuri kupanga maeneo mta-kayofululiza mpaka umemaliza kijiji au hata mji. Vilevile, mkiwa na mpango itasaidia timu nyingine kulenga maeneo bila kuingiliana au kushindana nanyi.

2. Lazima timu iombe pamoja kabla ya kuwaendea watu.

Kwanza timu yenu inapaswa kujiombea, mkimwomba Mungu kuwatumia kama vyombo safi kueneza Injili. Pili, timu yenu inapaswa kuwaombea wale watakaosikiliza Injili. Kazi ya uinjilisti ni ya kiroho na kuianzisha kwa maombi ni muhimu. Kufanya hivyo kunamkabidhi Mungu kazi yake ya kuokoa roho za watu kama apendavyo Yeye. Pia, kunatukumbusha nguvu zetu zatoka wapi ili tumtegemee Mungu kwa mafanikio.

3. Njiani timu iamue nani atakuwa msemaji na nani atakuwa mshiriki mkimya.

Msiingie nyumba ya mtu bila kufanya maelewano hayo, ingawa mnaweza kuwa na ishara kama kutikisa kichwa au macho kumaanisha mwenzako aanze pale ulipofikia. Bila kufanya hivyo mnaweza kuwa na mvutano katika kueleza Injili mpaka ujumbe hauendi sawa na msikilizaji anatoka bila kuelewa kitu cho chote.

4. Mnapokaribia nyumba ya mtu, au mtu mwenyewe, chunguza kwa siri mazingira ili mpate kugundua ni mtu wa aina gani.

Kufanya hivyo itawasaidia kuanzisha mazunguzo ya kirafiki naye. Vilevile itawasaidia kupata “mwingilio” wa kueleza Injili. Kwa kadiri mnavyomfahamu mtu ndivyo mnavyoweza kumlenga katika mahitaji yake hasa. Kwa mfano akiwa na sanamu ya bikira Mariamu mtagundua dhehebu na imani yake ilivyo, kwa kuona picha za nyumba yake mtafahamu kilicho muhimu kwake, na kwa kunusa harufu ya pombe mtajua ni mtu anayeshiriki au kukoroga pombe, n.k. Hayo yote yatawasaidia kuanzisha mazungumzo yenu. UNAPOKUTANA NA MTU MWENYEWE

Jinsi tunavyokutana na watu na kuongea nao kunaweza kufanya watu wawe na hamu ya kus-ikia ujumbe wetu hadi kuamini au kunaweza kufunga masikio yao na kuwafanya kukataa ujumbe wetu. Kwa hiyo ni muhimu sana tuangalie tunavyoongea nao. Hapo chini ni mapendekezo machache.

18

1. Onesha furaha na tabasamu.

Ni wazi kwamba mtu aliyechangamka anapendwa na watu kuliko anayeonesha kwamba huduma hiyo ni huzuni na mzigo kwake. Basi, onesha kwa sura yako kwamba ujumbe wako ni Ha-bari Njema.

2. Ujitambulishe na upate kumfahamu msikilizaji kwa jina pia.

Hiyo itakusaidia kuongea naye kwa kutumia jina lake. Pia, utakapojitambulisha utaanza kuondoa wasiwasi wo wote alio nao kuhusu wewe. Maana kuanzisha uinjilisti bila kujitambulisha kunamfanya aendelee kujiuliza, “Huyu ni nani anayeongea?” badala ya kumfikiria Kristo Yesu na ujumbe wako.

3. Fanya urafiki naye kwa kuongea kuhusu mambo anayopenda yeye kwanza.

Usiingie nyumba na kuanza kumtwanga na Injili mara moja. Chukua muda kupata kumfahamu yule unayeongea naye. Tafuta kujua kwa urafiki jinsi alivyo. Lakini jiangalie usije ukaonekana kama mpelelezi au polisi! Umfurahishe kwa kusifu mambo yake mazuri. Kwa mfano unaweza kusifu wa-toto, nyumba, mifugo, shamba, picha zilizobandikwa ukutani, n.k. Ukifanya hivyo atapenda kusikili-za ujumbe wako zaidi.

4. Tafuta mwingilio wa kuanzisha Injili kwa njia iliyo na maana kwake.

Katika mambo uliyojifunza juu yake ujitahidi kupata neno la kugeuza mazungumzo yawe juu ya Yesu Kristo na kazi yake. Usitangaze mabadiliko haya, bali uyafanye taratibu ili ionekane kuwa maendeleo ya mazungumzo yako ya kiurafiki. Mwingilio huo utafungua mlango wa kueleza Injili.

5. Ujumbe wako ulenge moyo wake na jinsi alivyo.

Katika mazungumzo yote jaribu kugusa pale anapoumwa kiroho ili aweze kufaidika sana na maana ya wokovu kwake. Usiongee tu mambo ya nje na ya kimwili. Bali weka kiini cha mazungum-zo yenu kuwa mambo ya kiroho.

6. Aliye mshiriki mkimya afanye kazi zake.

Kama uliamua kuwa mshiriki mkimya usifikiri huna kazi wakati mwenzako anaeleza Injli. Kazi zako ni za muhimu sana. Lazima ufuate mazungumzo na uwe macho.

a. Mshiriki mkimya ahakikishe kwamba anayeshuhudia anakaa karibu na msikilizaji ili waweze kusikilizana vizuri na kusoma Biblia pamoja bila shida.

b. Mshiriki mkimya aangalie vurugu zo zote ambazo zinaweza kumvuta akili msikilizaji na kumfanya asisikilize ujumbe. Anaweza kujibu maswali ya wengine yasiyohusika, kucheza na watoto, au kuendeleza kazi ambayo msikilizaji alikuwa akifanya kabla hamjaanzisha mazungumzo naye.

c. Yampasa mshiriki mkimya kusikiliza kwa umakini wakati mazungumzo yanaendelea. Maana anaweza kuombwa kusaidia na kuchangia wakati wo wote. Kama hajasikiliza njiani ata-changanya mambo tu atakapoombwa kuongea.

d. Vilevile, mshiriki mkimya anapaswa kuomba kimoyo moyo wakati Neno la Mungu lin-aelezwa.

Kuwa mshiriki mkimya ni njia nzuri kujifunza jinsi ya kushuhudia. Anayejifunza kushuhudia anapaswa kuchukua nafasi kushuhudia kidogo kidogo hadi anaweza kufanya mwenyewe.

7. Mshuhudiaji aulize maswali kuhakikisha kwamba msikilizaji anafuata.

Si vizuri kuongea kama redio bila kukatika. Unapaswa kuongea kwa upole ukisimama mara kwa mara kumwuliza msikilizaji maswali ili uhakikishe unamlenga vizuri na kwamba anafuata na kuelewa yale unayosema.

8. Kamwe usibishane.

Mazungumzo yote yawe ya kiurafiki. Msipoelewana usiongeze sauti. Nafuu kuacha ujumbe wa upendo ili mtu akukaribishe siku nyingine kuongea tena kwa kuwa Mungu huweza kuutumia ujumbe wako anapobaki kutafakari. Sijawahi kuona mtu akikata shauri baada ya kubishana. Una-weza kushinda mabishano na kupoteza roho wa mtu.

19

UNAPOMALIZA NA KUACHANA

Jinsi unavyomaliza mazungumzo yenu ni muhimu pia. Kuna mapendekezo machache hapa chi-ni:

1. Ujumlishe mambo makubwa.

Kwa kufanya hivyo unamsaidia kuelewa na kukumbuka yote uliyoyazungumza kwa pamoja. Hii ni muhimu kabla hujaendelea na hatua nyingine.

2. Uhakikishe kwamba ameelewa yote.

Umwulize kama kuna sehemu ya mazungumzo ambayo bado hajaelewa au kama anayo maswali juu ya yale mliyoongea. Angalia usikubali maswali yalio mbali na ujumbe wako. Kama kuna sehemu, urudie polepole ukiongeza maelezo au maandiko zaidi ili upate kumsaidia.

3. Umfanye akate shauri juu ya ujumbe wako.

Ni muhimu sana kumfikisha msikilizaji katika mahali pa kuona ni lazima aamue uamuzi fulani. Injli inahitaji kufanyiwa kazi kwa kuwa siyo hadithi ya kufurahisha tu. Umwoneshe faida ya kumpokea Kristo na jinsi ya kumpokea Kristo. Umwulize kama anataka kuamini au kukataa ujumbe huo.

4. Achana kwa maombi na urafiki.

Atake, asitake kukata shauri, ni nzuri kuomba ruhusa kuongoza kwa maombi ukimshukuru Mungu kwa mazungumzo na kumwombea msikilizaji kulingana na jibu lake. Pia, uachane katika hali ya urafiki. Usimfanye kuwa adui ikiwa hataki kuamini, kwani Roho Mtakatifu anaweza kutumia uli-chosema leo kumwongza mbeleni ukiachana kiurafiki.

5. Acha maandiko au kipeperushi na jinsi ya kuwasiliana.

Kwa njia hiyo msikilizaji ataweza kubaki kusoma neno zaidi na kufurahi kwamba ulimpenda hata kumpa zawadi hiyo. Vilevile akiwa na maandiko haya, atajua namna ya kukufuata au kukuita kumsaidia zaidi mbeleni. Isitoshe, maandiko haya yaweza kusomwa na wengine nyumbani mwake pia.

6. Kwa mtu aliyekata shauri ufanye mipango ya kumfuatilia na kumjenga.

Neno hili tutajifunza zaidi katika masomo ya 11 na 12. Kwa sasa, yatosha kusema ni lazima mpango maalum ufanywe na yule aliyeamua kumpokea Kristo kama Mwokozi wake.

Hizi ni sehemu tatu zinazohusu njia au jinsi ya kushuhudia watu mtu kwa mtu na nyumba kwa nyumba. Jitahidi kufuata mapendekezo haya unapoenda kufanya uinjilisti wa mtu kwa mtu na uone kama Mungu atabariki sana kazi yako na kuifanya iwe “uinjilisti ufanyao kazi”. MASWALI NA MAJADILIANO

1. Kwa nini ni muhimu kuangalia jinsi tunavyoongea na watu tunapowashuhudia? 2. Kabla hujafika kwa mtu unayemshuhudia ni muhimu uamue jambo gani? 3. Kazi ya mshiriki mkimya ni nini? 4. Kamwe usifanye nini? Kwa nini? 5. Unapoachana na mtu uhakikishe nini? 6. Kuacha maandiko, jina, na simu namba yako kunasaidia nini? 7. Kwa nini watu waende na timu ndogo badala ya timu kubwa?

20

7. Kazi za Maombi na Roho Mtakatifu Huduma ya Uinjilisti inafanyika kwa njia za kimungu. Matokeo yo yote mazuri ni kwa sababu

Mungu alisaidia yawepo. Hakuna mwanadamu anayeweza kumshurutisha mtu aokoke. Kwa sababu hiyo ni huduma ambayo lazima ifanywe katika mazingira ya kumwomba Mungu sana. Maombi hu-onesha kwamba sisi tunajinyenyekeza chini ya uongozi wa Mungu na kumtegemea aifanye kazi yake tukimtumikia.

Tumeshataja katika sura zilizotangulia kwamba mwinjilisti mwenyewe anapaswa kuwa mtu wa maombi. Vilevile tulieleza kwamba timu ya wainjilisti wanapopanga kwenda kushuhudia ni lazima wafanye maombi kwa ajili yao wenyewe pamoja na wale watakaoshuhudiwa.

Zaidi ya hapo kuna njia nyingine ya kutumia maombi inayoleta mafanikio makubwa sana. Njia hiyo ni kutengeneza Orodha ya Maombi ya Uinjilisti.

ORODHA YA MAOMBI YA UINJILISTI NI NINI?

Orodha ya maombi ni orodha maalum ya majina ya watu unaowafahamu na unataka wapate kumpokea Kristo kama Mwokozi wao. Ni orodha ambayo utaitumia kila siku ikukumbushe ku-waombea ukimwomba Mungu kuwaleta kwa Kristo.

KWA NINI NIWE NA ORODHA YA MAOMBI YA UINJILISTI?

Tukio lenye furaha mno linaloweza kutokea kwako kama Mkristo ni kuona mtu unayemfahamu ameupokea wokovu wa Bwana Yesu Kristo. Jambo la kufurahisha zaidi ni kama ulikuwa unam-wombea mtu huyu kabla hajampokea Kristo. Katika kitabu kimoja mwandishi Leroy Eims alisema, “Ukitaka kuona watu fulani kuja kwa Kristo, nashauri uyaweke majina yao kwenye orodha ya maombi. Halafu uombe Mungu akupe nafasi za kuwashuhudia ukimwomba vilevile kutayarisha mi-oyo yao. Uendelee kuomba hadi Mungu atakapotoa jibu lililoahidiwa.” Mtume Paulo alionesha moyo wake kwa Waisraeli wenzake katika barua ya Warumi aliposema, “Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe” (Rum. 10:1). Siri ya kupata kuona watu wanakuja kwa Kristo ni kuwaombea na kutaka moyoni mwako waokolewe. Kuwa na “Orodha ya Maombi ya Uinjilisti” kutakusaidia kufanya hivyo.

KUTENGENEZA ORODHA YA MAOMBI YA UINJILISTI

1. Mwombe Mungu akupe hekima unapotengeneza orodha yako. 2. Jaribu kuorodhesha majina 5 hadi 10 ya watu wasiomwamini Kristo ambao unakutana nao ma-

ra kwa mara. Hawa wanaweza kuwa majirani, familia, watu kazini, marafiki shuleni, au wengine. Unaweza kuongeza watu kwenye orodha yako wakati Mungu atakapokukumbushia mtu.

3. Tumia karatasi au kadi ndogo kuandika majina haya na uiweke ndani ya Biblia yako ili uione kila mara. Labda utumie kadi hii kama kumbukumbu ya kujisomea Biblia. Anza kuitumia kadi au orodha hii na uwe macho katika kuujenga urafiki na uhusiano na hawa unaowaombea.

Biblia inasema wazi kwamba, “Bwana...hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba” (2 Pet 3:9). Pia tunayo ahadi kwamba tukiuliza kitu cho chote kulingana na mapenzi ya Mungu, Mungu hutusikia, na hutupa (1 Yoh 5:14-15).

Uinjilisti usiofanyika kwa njia ya maombi huonesha kwamba kazi hii ni ya maarifa na siyo ya kiroho. Lakini tunafahamu kwamba uinjilisti ni huduma ya kiroho siyo ya kimwili. Basi, tufahamu kuwa kazi ya kuokoa watu ni kazi ya Roho Mtakatifu.

KAZI YA ROHO MTAKATIFU KATIKA UINJILISTI

Hakuna anayeweza kuokolewa bila Roho Mtakatifu kumwangaza na kumwonesha hitaji lake la wokovu.

Katika Yohana 16:8-11 Yesu Kristo alieleza kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu kumpatia mpotevu ujumbe wa Neno La Mungu. Roho Mtakatifu hutumia ujumbe wa Neno kuhakikisha juu ya dhambi, haki, na hukumu.

Basi, wajibu wa mwinjilisti ni kupanda mbegu ya Neno la Mungu na kuhakikisha ameipanda

21

vizuri akimwagilia kwa maombi. Kuchipuka na kuota kwa mbegu ni kazi ya Roho Mtakatifu. Wen-gine wanajivuna kwa kazi zao za uinjilisti wakijaribu kumnyang’anya Roho Mtakatifu kazi na sifa zake. Haiwezikani. Kufanya hivyo ni hatari sana! Kuna hatari aina mbili zinazotokea unapochukua nafasi ya Roho Mtakatifu katika uinjilisti.

Hatari ya kwanza ni kumlazimisha mtu aamini kabla hajafahamu vizuri wala kuwa na moyo uliofunguliwa na Roho Mtakatifu. Yaani, ni kumshawishi msikilizaji kwa maneno mengi au kum-gandamiza ili atamke “Sawa nimekubali”, wakati moyo wake ungali haujaamini.

Hatari ya pili ni kujivunia matokeo ya kazi ya uinjilisti. Kufanya hivyo haimpendezi Mungu. Kumbuka Paulo alivyowaelezea Wakorintho, “Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kuku-za ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye” (1 Kor 3:6-7). Kumbuka watu wachache wanaokolewa kwa sababu ya kazi ya mwinjilisti mmoja tu.

Kama ndiye Mungu afanyaye kazi hii ya kuokoa, basi tumwachie kazi yake na kuamini Yeye atawaokoa aliowakusudia. Sisi tuendelee kuwa tayari kutumwa naye kama nabii Isaya, “Mimi hapa, nitume mimi!” Tumshukuru na kumsifu Mungu kwa matokeo yo yote katika huduma ya uinjilisti.

MASWALI NA MAJADILIANO

1. Kwa nini maombi ni lazima katika huduma ya uinjilisti? 2. Orodha ya Maombi ya Uinjilisti ni nini? Inasaidia nini? 3. Roho Mtakatifu hufanya kazi gani katika uinjilisti? 4. Wajibu wetu ni nini katika Uinjilisti?

MAZOEZI

Fikiri kuhusu mahitaji ya kila mmoja wa watu wafuatao. Andika mahitaji yao makuu. Halafu fikiri ni kwa njia gani ambayo ungeweza kumshuhudia kwa kumlenga jinsi alivyo; ni sehemu gani ya Wokovu ungekazia?

Yohana - Hana muda wa kwenda kanisani. Anazo shughuli nyingi na kuziacha shughuli zake kutamgharimia kifedha.

Happy - Msichana anayekuwa tayari kusikiliza na kukubali mambo yote bila kutafakari. Anasali na marafiki zake popote wanapopenda.

Albert - Mkristo wa siku nyingi katika kanisa lisilothibitisha wokovu, naye huamini anapoteza wokovu wake anapofanya dhambi. Yaani, hana hakika na wokovu wake.

Neema - Mkristo wa jina tu anayetafuta msaada wa kimwili ndani ya kanisa akitaka faida.

Iddigraf - Msomi mwenye kazi ya kiofisi. Huamini Biblia ni historia tu yenye tafsiri mbalimbali. Huona kwenda kanisani ni kwa maskini na wasio na elimu.

Edigar - Hupenda kuongea Neno la Mungu. Anauliza maswali mengi yasiyohusu Injili na ana-penda kujadili na kubishana bila kuamini.

22

8. Vizuizi vya Kuamini Katika kufanya uinjilisti wa mtu kwa mtu ni lazima utakutana na vizuizi mbalimbali. Maana,

tulijifunza kazi hiyo ni ya kiroho na mpinzani wa mambo ya kiroho yupo. 2 Korintho 10:3-5 inasema, “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.” Shetani hawezi kutulia na kuona wafuasi wake wanavuliwa bila kuinuka na kufanya bidii kuzuia mafanikio katika uinjilisti wako. Ndiyo maana ni lazima kazi ya uinjilisti ifanyike kwa kumtegemea Roho Mtakatifu, nguvu zake za kuokoa, na uwezo wake wa kumshinda adui yule. Kati-ka somo hili tunataka kujifunza jinsi gani Shetani anavyoleta vizuizi ili watu wasiamini. Kazi yetu ni kutumia silaha za roho ili tushinde vizuizi vya Shetani na watu wapate kumtii na kumkiri Kristo kama Bwana na Mwokozi wao.

Sasa tuangalie vizuizi vikubwa vitano halafu tutaweza kuorodhesha vingine tunavyokutana navyo tukiwa kwenye uinjilisti.

1. “Ningependa kuokolewa, lakini nafahamu kwa hakika kwamba nitashindwa kuishi maisha mazuri ya Mkristo wa kweli.”

Mara nyingi mtu unayemshuhudia hawezi kukitamka kizuizi hicho wazi. Anakataa kuamini lakini hasemi kwa nini. Ukigundua hicho ndicho kizuizi kwake ufanye nini? Kwanza ni vizuri kwa kuwa mtu huyu ameshafahamu Mungu hutaka watu kubadilika na kuwa wazuri. Ingawa Mungu huwapokea kama walivyo, anataka kuwafanya wawe wazuri ili wafanane na Yesu Kristo! Tatizo la mtu huyu ni jinsi ambavyo anaona atashindwa kubadilika akijua uwezo wake ni mdogo. Anacho-kosea ni kwamba hajagundua hakuna anayeweza kuishi maisha ya kumpendeza Mungu kwa uwezo wake mwenyewe. Kushinda na kubadilika kunategemea uwezo wa Mungu na kuingiliwa na Roho Mtakatifu. Mtu huyu astahili kufundishwa juu ya kazi ya Roho Mtakatifu na jinsi Mungu anavyowezesha Mkristo kubadilika baada ya kuokolewa akianza maisha ya kumfuata Kristo.

2. “Marafiki na jamaa zangu watanicheka na kunidharau nikiwaambia nimeamini na kuo-kolewa.”

Yesu Kristo aliyajua mawazo haya alipowaambia wanafunzi wake katika Luka 9:26, “Kila ata-kayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu.”

Kizuizi hiki kinaweza kupinduliwa kwa kumweleza msikilizaji mambo yafuatayo:

a. Kukubaliwa na Mungu ni jambo la muhimu kuliko kukubaliwa na wanadamu. Baada ya mi-aka 50 au 100 kibali cha nani kitakuwa muhimu zaidi?

b. Watu wasiomfahamu Kristo kama Mwokozi wao daima watamdharau, maana hata Kristo alidharauliwa. Vilevile Biblia inasema kwamba ujumbe wa Injili ni upuuzi kwa watu wa dunia (1 Kor 2:14) kwa sababu hawauelewi.

c. Nafuu yeye aokolewe kwa sababu atakufa peke yake na atasimama mbele za Mungu peke yake. Atakapobadilishwa, kama Mkristo, ndipo atapata nguvu za kuwashuhudia wale wanaomcheka ili nao pia wapate kuamini badala ya kupotea. Bora asiongozwe na mtu ali-yepotea kuhusu mambo ya kiroho.

3. “Mimi siyo mtu mbaya na siamini kwamba Mungu atanihukumu kama unavyoeleza.”

Mtu huyu ameziamini akili zake na mawazo yake kuliko Neno la Mungu. Kumpokea Kristo hakuji kwa kujiamini bali ni kwa kumwamini Yesu Kristo na Neno Lake. Mara nyingi kizuizi hicho utakisikia kwa wasomi na wenye elimu. Kristo mwenyewe alisema, “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani” (Yn 5:24). Lazima mtu huyu akubali Neno la Mungu zima ni la kweli na kwamba hawezi kuchagua anachotaka kuamini na kuacha asichotaka.

4. “Mimi nimefanya dhambi nyingi na hata ile ‘dhambi isiyoweza kusamehewa’.”

Mtu huyu huhitaji kufafanuliwa kwamba “dhambi isiyoweza kusamehewa” ilikuwa dhambi ya kusema uwezo na ishara za Kristo ziliwezeshwa na Shetani badala ya kuwezeshwa na Roho Mta-

23

katifu. Yaani, ni kumwasi Kristo. Leo anayekataa kumwamini Kristo anamwasi Kristo na akifanya hivyo hadi kufa atapotea milele. Lakini ye yote anayemwamini na kumpokea Kristo anasamehewa dhambi zake zote na anapata kuwa kiumbe kipya (2 Kor 5:17). Hakuna dhambi isiyosamehewa isipokuwa kutoamini.

Soma Zaburi 103:3, 10, 12: “Akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote. Hakututenda sawasawa na hatia zetu, wala kutulipia kwa kadiri ya maovu yetu. Kama mashariki il-ivyo mbali na magharibi, ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.”

VIZUIZI VINGINE VINAVYOSUMBUA

Vizuizi vingine vipo vingi. Angalia vilivyotajwa hapo chini na jaribu kuandika jinsi ya kuvishughulikia na kuvijibu:

1. Unaposhuhudia, mtu mmoja hadi mwingine anaongezeka mpaka umati umepatikana. Hivyo, msikilizaji wako anakosa kusikiliza vizuri na kuamini kwa kuogopa wenzake waliokusanyika.

2. Mtu unayemshuhudia ana shughuli nyingi. Unapoendelea kueleza Injili anachunguza saa yake na kufikiri kuhusu mambo mengine hata kuinuka na kufanya mengine badala ya kufikiria maana ya ujumbe wako.

3. Mtu ameisikia Injili lakini ni jambo geni kwake. Hajaifikiria vya kutosha na hajakomaa katika mawazo yake ili aamini.

4. Mtu anayaogopa mabadiliko magumu ya kuachana na maisha yake ya zamani na pengine hata marafiki zake na familia yake.

5. Mtu amezaliwa katika dini ya wazazi wake na hataki kuiacha dini yake wala kuamini ujumbe wako ingawa dini yake inakataa wokovu duniani.

6. Jaribu kutaja na vizuizi vingine unavyovijua wewe.

MASWALI NA MAJADILIANO

1. Kwa nini tunaweza kuvikuta vizuizi tunapofanya kazi ya uinjilisti? 2. Mtu anayeogopa kuchekwa anaweza kusaidiwaje na hofu yake? 3. Je, mtu anayekataa kuamini ujumbe wa Neno la Mungu anawezaje kushuhudiwa?

9. Namna ya Kuwaendea Watu Mara nyingi sana utasikia makanisa yakihimiza watu kueneza Injili lakini hawawafundishi jinsi

ya kufanya. Kukosa elimu na ujuzi hufanya watu kushindwa katika kazi ya uinjilisti na mara nyingine huleta matokeo ya kugombana badala ya kushuhudia. Naamini kwamba kuna njia chache, ambazo tukizijua, zinaweza kutusaidia jinsi ya kuwaendea watu ili wapate kutusikiliza vizuri.

Kwanza kabisa, ni kurudia yale tuliyojifunza huko nyuma kwamba mwinjilisti ni mwenezaji wa upendo wa Mungu. Kutokana na hali hii, ni lazima mwinjilisti aongee kwa upendo na upole an-apoongea na wote anaowaendea. Nimekuta mara nyingine watu wakishafahamu kuwa unataka ku-washuhudia wanachemka kusudi wajikinge na maneno yako wakitetea hali yao au kanisa lao. Njia ya kufaulu katika kushuhudia watu hawa ni kutochemka wewe mwenyewe na kuwasikiliza kwa upendo na upole. Wasikilizaji watatulia kulingana na jinsi uanvyowaonesha upendo. Hata wasikilizaji wengine watakuheshimu kutokana na hali yako ya upendo wakati mtu unayemshuhudia anakataa ujumbe wako kwa hasira. Lakini kumbuka tulijifunza kutobishana kamwe.

Ninapenda sana kutumia neno “mwingilio” katika kueleza namna ya kufanya uinjilisti. Mwingilio unatumika pale unapozungumza na mtu katika hali ya kujenga urafiki na nafasi ina-patikana kubadili mazungumzo ili uanze kumshuhudia Kristo (mara nyingine bila hata msikilizaji kufahamu). Hii ni njia bora niliyoigundua ya kumfanya mtu awe na hamu kuisikia Injili. Kufanya hivyo humfanya msikilizaji asijisikie kwamba “anahubiriwa”. Miingilio ni mingi sana na hubadilika kulingana na hali ya msikilizaji na mazingira yake. Faida ya kuitumia miingilio ni jinsi ina-vyokuwezesha kuyalenga hasa mahitaji na moyo wa msikilizaji kutoka mwanzo wa mazungumzo yako hadi mwisho wakati unapomshudhudia Injili ya Yesu.

Nimeona mafanikio makubwa kwa wachungaji na wanafunzi wa chuo cha uchungaji (Tanzania

24

Grace Bible Institute) wakitumia njia hii nilipowafundisha mwaka 1991-1994. Wanafunzi, na mimi mwenyewe, tulishangaa kuona katika uinjilisti wa wanafunzi, wastani wa mafanikio yao ulikuwa yapata 20-25%. Yaani, kati ya watu wanne au watano walioshuhudiwa na wanafunzi kwa taratibu hii mmoja alikata shauri! Ni matokeo ya ajabu! Tukumbuke kwamba mbinu na ujuzi hauwezi kuo-koa bali Roho Mtakatifu huokoa. Lakini ni wajibu wetu kujifunza kutumia njia zilizo bora ili Neno La Mungu lipate kusikika vizuri, maana, “Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Rum 10:17).

Watu Watapataje kuamini tukikosea namna ya kuwaendea na kuwahamasisha wausikilize ujumbe wetu wenye maana? Basi tujifunze njia mbalimbali za miingilio zinazoweza kutumiwa na watu wote.

MIINGILIO YA INJILI

1. Njia ya kundi fulani.

Ni vizuri kuwaambia watu kwamba wewe ni mmojawapo wa kundi fulani kama umoja wa vi-jana wa kanisa, au mwanafunzi wa shule fulani, n.k. Kuwaelezea watu hivyo itawasaidia kufahamu kwamba huna makusudi mabaya. Vilevile hawatafikiri wewe ni kichaa anayebisha hodi milangoni mwa watu bila sababu. Watakaposikia wewe ni wa kundi fulani ndipo watafikiri bila shaka ujumbe wako ni wa muhimu kwa kuwa wengi wanashughulika nao. Halafu wenyewe wanaweza kuwa na hamu kujua ni nini chenye umuhimu wa kiasi cha kukufikisha kwao. Hapo ndipo utakapopata nafasi yako ya kuelezea ujumbe wako ulio muhimu sana.

2. Njia ya maandiko.

Unaweza kutembea na vipeperushi au vitabu vya kuuza. Uvioneshe wazi na kuwaelezea watu kwamba umewaletea maandiko mazuri ya kuwasaidia katika maisha yao. Maandiko haya yanaweza kufundisha kusudi la Mungu kwa ajili wanadamu na njia ya kwenda mbinguni.

3. Njia ya ushuhuda wako.

Baada ya kuandaa ushuhuda wako kwa makini, unaweza kuutumia kuingiza Injili. Kwa mfano unaweza kusalimiana na watu na baada ya kufahamiana nao ukasema, “Je, naweza kupata muda mfupi nikuelezee juu ya kitu fulani kilichonitokea ambacho kitakupendeza?” Au, “Ningependa ku-kuambia kuhusu kitu kilichonitokea ambacho ni muhimu kuliko vyote maishani mwangu.”

4. Njia ya watoto.

Mara nyingi watoto wanakuwepo pamoja na wazazi wakati unapowatembelea nyumbani mwao. Utawapendeza wazazi unapoonesha furaha kwa watoto na kuwajali. Kumjali mtoto ni sawa na kuwathamini wazazi wake. Unaweza kuwasifu watoto na kuwapongeza wazazi kwa kazi ngumu ya kulea watoto. Halafu utumie tamko hilo kama mwingilio ukieleza jinsi tunavyozaa watoto na kuwafundisha ili wafanane na wazazi, na ndivyo ilivyo kwa Mungu.

5. Njia ya habari.

Kwa kuzifahamu habari za dunia au za eneo lile unalolitembelea, unaweza kuzitumia habari hizo kama mwingilio wa Injili katika kushuhudia kwako. Kwa mfano unaweza kuzitumia habari za hali ya hewa, vita, mateso, njaa, ajali za magari na ndege, au uvumbuzi mpya. Yote haya yanaweza kutumiwa kuingiza Injili na kuonesha jinsi Injili ni ya muhimu na ya kisasa kulingana na hali ya dunia ilivyo. Hata habari za kanisa, siasa, na wevi zinaweza kutumiwa kama mwingilio.

6. Njia ya dhehebu.

Unaweza kuongea kuhusu madhehebu, jinsi yalivyo mengi siku hizi, na jinsi wote wanavyota-futa ukweli wa Mungu na njia ya kufikia kwake. Au, unaweza kueleza kwamba msingi wa imani ni Neno la Mungu, na kwa sababu hiyo ni bora kuchunguza ujumbe wa Mungu katika Neno lake kuliko kuongea mambo ya kidhehebu. Au, unaweza kueleza kwamba wewe ni wa dhehebu fulani nawe umegundua Injili ya Mungu ambayo siyo ya dhehebu lo lote bali ni ya watu wote.

7. Njia ya kanisa.

Kwa kutumia jina la kanisa lako la mahali unaweza kuvuta watu kutaka kujua zaidi juu ya imani yake. Hasa kama kanisa ni jipya au mnafanya ujenzi katika eneo fulani, hali hii itawaongeza hamu

25

kusikia juu ya imani ya kanisa hilo. Waelewe kuwa katika kanisa lako mmeona umuhimu wa ku-watembelea watu na kuzungumza nao kuhusu imani yenu katika Kristo Yesu.

8. Njia ya uchunguzi kuhusu jinsi watu wanavyosoma Biblia.

Unaweza kuzunguka ukikusanya takwimu kama anayefanya sensa. Unaweza kuuliza: (1) Kama mtu anayo Biblia au sehemu ya Biblia? (2) Kama anaisoma? (3) Kwa taratibu gani anaisoma? (4) Kama anayaelewa anayoyasoma? (5) Kama katika kusoma Biblia ameona na kuyaelewa makusudi ya Mungu kwa wanadamu? Maswali kama haya yaweza kuwaingiza katika Injili kwa urahisi.

9. Njia ya kutumia siku ya sikukuu.

Sikukuu ni siku ya kusherekea kitu fulani. Kwa hiyo kuna maana muhimu kwa siku yenyewe ambayo maana hiyo inaweza kutumiwa kuingizia Injili. Krismasi na Pasaka ni rahisi kutumia upande wa uinjilisti lakini hata nyingine zinaweza kutumiwa kwa mfano: siku ya uhuru, mashujaa, wafanyakazi, muungano, mwaka mpya, wakulima, na hata sikukuu za dini nyingine.

Kwa kuyaangalia mapendekezo yaliyotajwa hapo juu unaweza kuona kwamba njia za kuingizia Injili ni nyingi sana na unapaswa kujizoeza kuzitumia wewe mwenyewe.

Wakati huu nakushauri ujibu maswali yanayofuata halafu ujitahidi kuzunguka na ku-washuhudia watu ukitumia maarifa uliyojifunza hadi hapa katika kitabu hicho. Umtegemee Mungu kwa nguvu na ujasiri na kwa mafanikio yo yote anayokusudia Yeye.

MASWALI NA MAJADILIANO

1. Neno “Mwingilio” lina maana gani katika uinjilisti? 2. Kwa nini ni muhimu kujifunza namna ya kuwaendea watu? 3. Mtu akichemka unapomwendea ni bora kufanya nini? 4. Kama utatumia mwingilio wa ushuhuda wako, unaweza kutumia maneno gani? Toa mfano. 5. Toa mfano wa mwingilio kwa habari za: (1) Ajali ya magari; (2) Hali ya hewa; na (3) Uvumbuzi

mpya.

10. Jinsi ya Kutumia Vipeperushi na Maandiko Kuwa na kifaa hakumaanishi unajua jinsi ya kukitumia. Unaweza kupewa kompyuta nzuri sana

leo lakini ukashindwa hata jinsi ya kuiwasha. Au, unaweza kuitumia vibaya kwa kukosa maarifa na ukaiharibu. Nimeona mara nyingi vipeperushi vikipatikana vinatumiwa vibaya. Maana vipeperushi na maandiko ndiyo kifaa kikuu katika kazi ya uinjilisti wa mtu kwa mtu. Mtu anapotumia vizuri kifaa hiki kinasaidia sana uinjilisti wake kuwa na mafanikio.

Nimeona ni muhimu kuchunguza na kutoa mapendekezo juu ya suala hilo. Kwa maarifa mengi zaidi kuna kitabu kimoja kilichoandikwa na Mchungaji George Verwer kiitwacho Uinjilisti wa Maandiko. (Kituo cha Maandiko Habari Maalum: Tabora, TZ). Kitabu hiki kimezaa mawazo mengi nitakayoeleza hapo chini.

1. Hakikisha una vitabu au vipeperushi.

Unapotumia vipeperushi ni muhimu kufahamu ujumbe wa vipeperushi vyako. Yaani uvisome wewe mwenyewe kwanza kabla hujawapa watu wengine. Siku moja nilipokea vipeperushi kutoka idara fulani na katika haraka yangu nikampa mtu ili vimsaidie kwa kazi yake ya uinjilisti. Kesho yake niliposoma vipeperushi hivyo nilisikitika sana. Maana nilikuja kuona maana ya hivyo vi-peperushi ni kupinga mambo yale yale ninayofundisha kila siku kuhusu wokovu. Kwa hiyo ni mu-himu kuhakikisha maelezo ya vipeperushi vyako kabla hujaanza kuvigawa. La sivyo, unaweza ku-jikuta unagawa traksi yenye injili nyingine isiyo ya kweli. Maana siku hizi kuna mambo ya kila aina yanayochapishwa.

2. Ujue udhaifu na mipaka ya vipeperushi vyako.

Pia ni vizuri kuufahamu udhaifu wa vipeperushi vyako, kama hazimalizi Injili, au hazioneshi jinsi ya kukata shauri. Uwe tayari kueleza ujumbe wake na kuongeza maarifa panapohitajika. Siku hizi vipeperushi vingi vina hadithi nzuri tu. Lazima ujue yale ambayo mtu anayesoma atayafahamu

26

na yale ambayo bado atahitaji kuelewa.

3. Jitambulishe katika maandiko yako.

Andika jina, anwani, na simu yako kwenye vipeperushi unavyogawa, au gonga muhuri wa ka-nisa wenye habari hizo katika vipeperushi vyako. Kwa njia hii mtu huona kwenda wapi kupata msaada zaidi, kuuliza maswali, au kupata nakala zaidi kwa marafiki zake. Usiwe Mwijilisti wa kujificha.

4. Lenga kila mtu unayemgawia.

Unapogawa vipeperushi jitahidi kuvitumia kuongea na kila mtu anayepokea. Usigawe vi-peperushi kama tajiri anayefurahi ugawaji tu. Uvithamini sana vipeperushi vyako na kufanya juu chini kuhakikisha vitasomwa na wanaovipokea. Kitu kinachogawanywa kama takataka kitahesebi-wa kuwa takataka. Uvigawe kwa makini na kuonesha mshangao mkubwa pale mtu anapokataa kupokea. Gawa kwa njia ambayo inaonesha kwamba unapendezwa na wanaovipokea ili wavutwe kuvisoma.

5. Tumia popote uendapo.

Ni vizuri ueleweke kama mgawaji wa maandiko. Ukieleweka hivyo, watu wataanza kukufuata wenyewe ili wapate maandiko na kuusikia ujumbe wako. Unapotembelea benki, posta, ofisi, na kadhalika, uwe na maandiko ili uweze kuongea na ye yote atakayepatikana ukiwa unatumia maandiko kama mwingilio kumwelezea Habari Njema. Kwa sababu nimefanya sana kazi ya kuuza maandiko na kugawa vipeperushi, kuna sehemu nyingine nchini nikipita watu hawakosi kunifuata na kuomba maandiko au kuagizia maandiko fulani.

6. Fuatilia waliogawanywa maandiko.

Kama utapitia sehemu ya mji leo na kuwagawia watu maandiko, basi uwaelezee wasome kwa makini kwa sababu kesho au baada ya siku mbili utapita kuwafuatilia ili ujue walifikirije kuhusu ujumbe wake. Hapo ndipo utaweza kujibu maswali juu maandiko hayo. Pia utaweza kueleza pale ambapo maandiko hayajaeleza. Utakuta wengine wameguswa na ujumbe wa maandiko na Roho Mtakatifu amewaandaa ili wakate shauri lakini hawakujua jinsi ya kufanya.

Hakuna kifaa kinachotumiwa chenye uwezo kama maandiko kwa kazi ya uinjilisti wa mtu kwa mtu. Watu wengi hawapendi kutembea na maandiko, hasa maandiko ya kuuza. Lakini mwuzaji wa vitabu vya kikristo hatambuliki kama mfanyabiashara. Maana ujumbe wa vitabu vyake vinahusu uzima wa milele. Lengo lake katika kuuza vitabu ni kufidia gharama za vitabu na uenezaji wake ili watu wengi wapate kuishiriki huduma hii. Mara nyingine kitu kilichotolewa bure kinahesabiwa kuwa “bure”. Watu siku hizi wanaelewa thamani ya vitu na kwa ujumla wako tayari kuchangia kitu kitakachowasaidia. Kutembea na maandiko kutakufanya upate kuonana na watu wengi na kuweza kushuhudia sana juu ya Kristo Yesu.

MASWALI NA MAJADILIANO

1. Kwa nini maandiko yanakusaidia kufanya uinjilisti? 2. Ukitaka kutumia vipeperushi ufanye nini kwanza? Kwa nini? 3. Je, ni mbaya kuandika jina lako kwenye vipeperushi? Kwa nini? 4. Baada ya kuwapa watu maandiko ni vizuri kufanya nini? Kwa nini? 5. Je, umewahi kuona njia zingine za kuyatumia maandiko? 6. Wewe mwenyewe unapenda kuyatumia maandiko ya namna gani kwa uinjilisti wa mtu kwa

mtu?

27

11. Kumsaidia Mwongofu Mara Anapokata Shauri Tunapofanya kazi hatuwezi kufanya bila kutegemea mafanikio. Ni wakulima wangapi

wanaoenda shambani na kufanya kazi ya kupanda na kutunza mimea bila kutegemea mavuno? Katika kitabu hiki tunajifunza kuhusu “uinjilisti ufanyao kazi”. Kusudi letu katika kazi ya uinjilisti ni kuona mafanikio au mavuno. Lengo la kuieneza Injili ni kuvuta na kupokea walioandaliwa na Bwana kuingia katika familia yake Mungu.

Kama ndivyo, basi, mwinjilisti anapaswa kufanya nini na yule aliyemshuhudia ambaye yu tayari kukata shauri na kumpokea Kristo kama Bwana na Mwokozi wake. Hapo chini kuna mapendekezo ya mambo muhimu ya kufanya.

1. Omba pamoja naye.

Umsaidie msikilizaji kwa kumwombea ili awe na imani ya kumpokea Kristo na kubadilika. Pia, uwe tayari kumwongoza na maombi ya sala ya toba. Sala ya toba ni nafasi yake kumwambia Mungu hitaji lake la wokovu. Yaani, yeye ni mwenye dhambi, anaungama dhambi zake, na anataka kum-wamini Kristo na kazi yake ya ukombozi ili aingie katika familia ya Mungu. Labda utamwongoza ki-fungu kwa kifungu akikuiga, au akiweza amwelezee Mungu mwenyewe. Mara nyingine unaweza kuonesha sala kama imeandikwa mahali fulani kwenye karatasi.

2. Umpongeze sana kwa uamuzi wa busara na muhimu.

Mtu yule sasa hivi amefaulu mtihani wa maisha yake yote. Amezaliwa upya. Ametoka kifungoni mwa Shetani na kuingia katika uhuru wa Mungu! Huyu anastahili pongezi na anastahili kujua ma-laika wanasherehekea mbinguni! Uijenge imani yake kwa kuonesha uamuzi wake ni wa maana sana.

3. Umsaidie kifungu angalau kimoja kuhusu “Uhakika wa Wokovu”.

Vifungu ni vingi lakini napendekeza vinne: Yohana 3:16; 5:24; 6:47; au 1 Yohana 5:11-13. Hivi vyote nimevitumia kumhakikishia mwongofu kwamba kitendo chake cha kuamini ndicho kinachookoa na kumpa uzima wa milele.

Kawaida ufungue Biblia na kuisoma pamoja naye. Ni vizuri akisoma mwenyewe. Halafu um-wulize maswali kama yafuatayo: (1) Kulingana na Neno La Mungu, Je, ukiamini unapata nini? (2) Kupata uzima wa milele unapaswa kufanya nini? (3) Je, sasa hivi umefanya nini? Umeamini kweli? (4) Basi, kuanzia sasa umepata nini? (5) Unajuaje? (6) Neno la Mungu linakuhakikishaje?

Mwisho, ni vizuri umweleze kwamba Shetani hafurahishwi na uamuzi wake na atajitahidi kutia mashaka juu ya wokovu wake ili asiliamini Neno La Mungu. Lakini umwambie asiyategemee mawazo yake (Mith 3:5, 6) bali ategemee Neno la Mungu.

4. Uhakikishe kwamba anayo Biblia au Agano Jipya.

Unapaswa kumwelezea kuhusu umuhimu wa kulisoma Neno La Mungu ambalo ni chakula chake cha kiroho. Umwambie asome sura moja kila siku akianza na kitabu rahisi kama Injili ya Yo-hana.

5. Mfundishe kuhusu umuhimu wa kushirikiana kanisani.

Kuni moja au kaa moja haliwezi kuwaka na kuwa moto. Vilevile ni lazima wakristo washirikiane na kujengana kama familia ya Mungu. Umwambie mahali kanisa lako lilipo na ratiba za ibada zake. Pia ufanye mpango wa kuja kumchukua kwenda kanisani Jumapili. Utakapofika kanisani umfahamishe kwa mchungaji, lakini uwe mwangilifu usije ukamwaibisha.

6. Mpatie masomo ya muumini mpya.

Masomo yanayolenga muumini mpya yatamfaa ili aanze kujifunza mara moja. Kama kanisa lako lina vipindi au darasa kwa ajili ya waumini wapya umtaarifu na umsindikize kwenye vipindi hivyo. Masomo yanayofaa ni kama “Hatua za Kukua Kikristo” yanayotolewa na Uinjilisti wa Maandiko (Box 77 Sumbawanga na Box 1745 Mbeya) au “Haya Yote ni Nini” yanatolewa na World Home Bible League (Nairobi) au mengine kwa Life Ministry (Nairobi).

28

7. Andika jina, anwani, na simu yako na upate jina, anwani, na simu yake.

Hakuna kitu kibaya kama kumwongoza mtu kukata shauri halafu kukosa kumfuatilia. Taarifa kamili ya jina, anwani, na simu itakusaidia kumfuatilia. Pia utaweza kumpa mchungaji au washirika wengine habari hizo ili wamfahamu na kujua anakaa wapi kusudi nao wasaidie katika kumjenga. Usimtambulishe kuwa mwembamba yule mwenye shati nyekundu kidogo.

Mambo yote haya yalioyotajwa hapo juu ni mapendekezo yanayofaa kwa mwongofu mara an-apokata shauri. Yaani, siku hiyo hiyo. Katika sura inayofuata tutaangalia jinsi ya kumfuatilia na kumjenga muumini mpya zaidi baada ya siku hiyo kupita.

MASWALI NA MAJADILIANO

1. Mtu anaweza kuionesha imani yake na kukata shauri kwa njia gani? 2. Vifaa gani vinahitajika kumsaidia mwongofu mara anapokata shauri? 3. Unawezaje kumhakikishia mwongofu juu ya wokovu wake? 4. Kwa nini kufanya hivyo ni muhimu? 5. Ni mambo gani mengine unayopaswa kumfanyia yule anayekata shauri siku hiyo hiyo. 6. Andika mfano wa sala ya toba inayoweza kutumiwa na mtu anayetaka kuamini na kuomba.

12. Kumfuata na Kumjenga Aliyeamini Mtoto anapozaliwa duniani tunafurahi sana na kusherehekea. Wakati mwingine tunacheza na

kula. Huwa tunawataarifu marafiki na familia nzima. Ingekuwaje ikiwa baada ya kusherehekea, wazazi wangemwacha mtoto peke yake kujitegemea wakiendelea na shughuli za maisha bila kumjali. Tungesema wazazi hawa wamepungukiwa akili! Lakini ajabu ni kwamba katika mambo ya kiroho jambo hilo linatendeka sana! Watu wanakata shauri na kuzaliwa kiroho halafu mwinjilisti anaondoka na kuwaacha bila utunzaji wo wote.

Kwa nini kazi hii ya kuwafuatilia na kuwajenga walioamini inaachwa sana bila kufanyika? Mimi napenda kutoa sababu tano nilizogundua mimi.

SABABU ZA KUTOMFUATILIA ALIYEAMINI

1. Hakuna mpango.

Mwinjilisti hakutegemea kwamba mtu angekata shauri na kwa sababu hiyo hakupanga jinsi ya kumfuatilia. Maana amezoea kutupa mbegu tu bila kutazamia mavuno.

2. Kukosa elimu.

Mara nyingine mtu anayeshuhudia hafuatilii waliookoka kwa sababu hajui jinsi ya kuwafuatilia. Hafahamu namna ya kuutunza Mkristo mpya ili asimame imara ndani ya Kristo.

3. Kutojua umuhimu wake.

Wainjilisti wengi wanatambua umuhimu wa kueneza Injili lakini hawajawahi kufikiria kwamba kumwaga mbegu ni mwanzo wa taratibu (process) ndefu. Hawafikiri kuwa wanapaswa kuangalia jinsi ya kumkuza mwongofu. Zaidi hawajaelewa jinsi ilivyo rahisi kwa muumini mpya kuanguka katika imani yake asiposaidiwa.

4. Kukosa uwezo.

Wengine hupenda kushuhudia mbali na nyumbani. Kwa sababu hiyo wakisharudi nyumbani wanakosa uwezo wa kuwafikia wale walioamini tena ili wawasaidie kukua kiroho. Pengine hawana pesa, muda, au hata chombo cha kusafiria ili wawafuatilie tena.

5. Kazi ya ufuatiliaji haina sifa

Unapofanya uinjilisti na watu watatu wanakata shauri, hii ni taarifa nzuri kuwatangazia watu. Kuna hatari kwa wainjilisti kuzoea kushuhudia na kutangaza kanisani idadi ya waliookoka bila kujali malezi yao. Mtu anaweza kusaidia watu 100 kwa mwaka kukata shauri akisifiwa sana kani-sani kwa kazi zake wakati asilimia 90 wamemwacha Bwana kwa vile walikosa ufuatiliaji.

29

Anayefanya kazi ya kuwafuatilia waumini wapya siku hadi siku haonekani na hasifiwi kama mwin-jilisti huyu. Basi, kwa sababu hiyo, watu huacha kazi ya ufuatiliaji na kukimbilia ile ambayo italeta sifa zaidi. Maana, sisi sote tunapenda kupongezwa kwa kazi zetu.

6. Ni kazi ngumu.

Kazi ya kuwafuata na kuwajenga waumini wapya ni kazi ngumu. Kazi hii inatumia muda mwingi. Matokeo ya kazi hii hayaonekani haraka kama kazi zingine. Isitoshe muumini mpya ana-weza kufuatiliwa sana na mwisho aamue kutoendelea katika imani yake. Hapo ndipo kazi ya mlezi inakuwa ngumu zaidi.

UMUHIMU WA KUFUATILIA ALIYEAMINI

Tunaweza kuangalia Maandiko Matakatifu kugundua umuhimu wa kazi hii machoni pa Mungu.

3 Yohana 4 - “Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.”

1 Yohana 2:28; 2 Yohana 8 - “Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunu-liwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibike mbele zake katika kuja kwake. Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu.”

1 Petro 5:2 - “Lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.”

Yohana 21:16 B “Akamwambia tena mara ya pili, ‘Simoni wa Yohana, wanipenda?’ Akamwambia, ‘Ndiyo Bwana wewe wajua kuwa nakupenda.’ Akamwambia, ‘Chunga kondoo zangu.’”

USHAURI KATIKA KUMFUATILIA ALIYEAMINI

Ufuatiliaji unalenga kumfanya muumini mpya akue kiroho na asimame imara katika uhusiano wake na Mungu. Zaidi ufuatiliaji unamsaidia huyu aliyeamini kushirikishwa kikamilifu kanisani na kuanza kufanya huduma za Mungu, hata kuleta wengine kwa Kristo. Kazi ya uinjilisti isiyo na sha-baha hizo inastahili kupangwa upya. Hapo chini ni mambo machache yaliyo muhimu zaidi kwa muumini mpya. Kuna mambo mengine mengi kuliko hayo tu ambayo muumini mpya anapaswa kuyapata ili akomae kiroho. Lakini mambo haya ni yale ya kuanza nayo.

1. Umfundishe kuhusu kuzaliwa mara ya pili na jinsi gani mtu hupata kuzaliwa na Mungu na kuwa Mkristo.

2. Umfundishe jinsi ya kusali (kuomba) kila siku ili awe na mawasiliano na Baba yake wa mbinguni.

3. Umfundishe jinsi na umuhimu wa kusoma Biblia kila siku ili apate chakula cha kiroho. 4. Umfundishe umuhimu wa kuabudu na kushirikiana katika jamii mpya, yaani, kanisa. 5. Umfundishe na kumsaidia kufahamu jinsi ya kushinda dhambi na tabia mbaya siku hadi

siku. 6. Umfundishe jinsi ya kuwashuhudia wengine imani yake kwa uhakika. 7. Umfundishe zaidi kuhusu uhakika wa wokovu wake na usalama wa milele wa wokovu wake.

MASWALI NA MAJADILIANO

1. Kwa nini watu wengi hawafanyi kazi ya kuwafuatilia na kuwajenga waumini wapya? 2. Kati ya sababu zilizotolewa, ni ipi ambayo unafikiri ni sababu kuu? 3. Kuna sababu nyingine zinazozuia ufuatiliaji? Zitaje. 4. Kwa nini ni muhimu kuwafuatilia na kuwajenga waumini wapya? 5. Shabaha kuu za uinjilisti ni nini? 6. Unapaswa kumfundisha muumini mpya mambo gani?

30

13. Kuanza Kufanya Huduma ya Uinjilisti Sasa tumepata mafunzo mengi sana mazuri kuhusu uinjilisti. Mafunzo haya yametolewa kui-

wezesha huduma ya uinjilisti itendeke kwa matendo. Maana, tumeshagundua hitaji kubwa la kum-shuhudia Kristo. Tumejifunza kuhusu maandalizi yake. Tumejifunza kuhusu ujumbe wenyewe tunaoshuhudia. Tumejifunza jinsi ya kuandika na kuutumia ushuhuda wetu. Tumejifunza kuhusu vifaa vya kufanyia uinjilisti. Tumejifunza njia za kushuhudia pamoja na kazi ya maombi na Roho Mtakatifu. Tumejifunza kuhusu vizuizi vya kuamini na jinsi ya kuvitatua. Tumejifunza namna ya kuwaendea watu ili wausikilize zaidi ujumbe wetu. Tumejifunza jinsi ya kutumia maandiko na vi-peperushi. Na mwishoni, tumejifunza jinsi ya kumsaidia mwongofu mara anapokata shauri na namna kumfuatilia na kumjenga baadaye.

Kwa kweli Mungu asifiwe kwa maarifa hayo yote! Lakini kufahamu maarifa ya uinjilisti hakutoshi. Kuyafahamu mambo haya hakuwezi kumsaidia hata mtu mmoja kuokolewa bila wewe KUYATENDEA KAZI. Ukweli ndio huo, mafundisho haya hayatakuwa na uhai mpaka uanze kuya-tumia! Biblia inaeleza, “Aliyepewa mengi atatakiwa mengi.” Kwa kweli umepokea mengi, basi Mun-gu hutaka uyatumie kwa faida ya Kanisa Lake. Unaweza kuanzishaje kufanya huduma ya uinjilisti?

Kwa kuwa wewe mwenyewe uko tayari sasa, unapaswa kuufuata ushauri ufuatao.

1. Fanya uamuzi! Hata kama hakuna mwingine wa kumshuhudia Kristo, wewe ufanye!

Kwa kweli mtu anapoamua hivyo ndipo atafanya kazi kwa nguvu bila kupungukiwa. Mungu atamtumia huyo pia. Maana, unapochunguza Maandiko unakuta Mungu anawaita watu wake na kuwatumia kazini bila kujali utendaji wa wengine. Kila mtu atapewa thawabu kwa jinsi alivyofanya yeye mwenyewe. Thawabu zake hazitegemei matendo ya washirika wengine wa kanisa lake wala matendo ya watu ndani ya familia yake.

Mtu akiwa na hali ya kufanya kazi bila kuwalaumu wengine wasiomsaidia, ataweza kuona wengine wataanza kujitoa kushirikiana naye. Maana, watu wanajifunza sana kwa mifano ya wen-gine na hawakosi kupenda kushiriki kitu kizuri chenye baraka ya Mungu.

Panga ratiba ya kushuhudia. Umwambie Bwana kwamba u tayari kutumiwa kwa kazi ya kui-eneza Injili. Omba akuongoze.

2. Kama watu wachache watapenda kushirikiana katika kushuhudia, tengeneza kikundi cha kudumu katika kushuhudia.

Mapendekezo yafuatayo yatakusaidia kufanya mpango wa kushirikisha wengine katika kushuhudia. Usibane nafasi kwa watu wa aina moja (k. m. vijana, au wanaume tu). Kazi hii inapaswa kufanywa na washirika wote!

a. Weka siku moja maalum au jioni maalum ya kushuhudia kama kikundi au timu. Ni muhimu vilevile kukutana siku nyingine kila juma kwa ajili ya maombi na mafundisho juu ya kushuhudia (k.m. unaweza kupitia kitabu hiki kuwafundisha). Hapo utapata nafasi kukusanya taarifa na kupima maendeleo yenu pia.

b. Panga muda mwingi uwezekanao kushuhudia. Ukitenga saa moja tu kuongea na watu utashindwa kufanya cho chote cha maana. Hata kama una shughuli nyingi, panga jioni moja kwa ajili ya kazi ya uinjilisti na usiruhusu mpango huu kuvurugika.

c. Tembelea watu na mwende nyumba kwa nyumba kwa kufuata mpango. Chora ramani ya kiji-ji, mtaa, au sehemu ya mji na mwanze kupitia mahali mlipochagua kwa taratibu ili mweze kutembelea kila sehemu na kujua mlipopitia na wapi ambapo hamjapitia bado.

d. Fanya yote yawezekanavyo kuwasaidia wanaokata shauri. Hakikisha mpango upo wa ku-wajenga. Msiwaalike tu, bali mwapitie na kuwasindikiza kanisani. Zaidi, mshirikishe muumini mpya katika kundi la marafiki zako.

e. Kumbuka kusudi la huduma ya uinjilisti. Kusudi lenu siyo kuinua jina la kanisa lenu. Mnaen-da kumwinua Yesu Kristo na kumfahamisha kwa dunia ili watu wapate wokovu ndani yake. Kata shauri kwamba hata kama hakuna mafanikio hamwezi kuacha kwenda kushuhudia.

31

KUTUNZA TAARIFA ZA HUDUMA

Hapa Afrika Mashariki nimegundua kwamba watu hawapendi kutoa ripoti kwa huduma zao za kiroho. Wengine wanasema ripoti ni ya kimwili na ya kiroho haipimiki kwa karatasi na wino. Jibu langu ni kuuliza watu, “Huogopa nini?” Pengine wanaogopa kwa kuwa hawafanyi huduma kwa mpango. Ninapotoa taarifa ndipo ninapoweza kuyaangalia maendeleo. Vilevile inaniwezesha kulin-ganisha maendeleo ya mwaka huu na yale ya mwaka jana. Ninaweza kujifunza mengi kutokana na ripoti za huduma. Kupitia hizo taarifa nitajifunza mbinu zinazoleta mafanikio na mbinu zisizofaa. Vilevile kuweka malengo ya mbele hutegemea taarifa ya nyuma. Tunajifunza kwa historia.

Kanisa linapaswa kujua ukuaji wake, jinsi wanavyoshirikisha washirika wake, na pia maende-leo yao katika kushuhudia walio nje ya kanisa. Ni vizuri sana kwa kikundi au kwa mtu anaye-shuhudia kuwa na fomu iliyo rahisi kujaza na kujumlisha matokeo ya huduma yake. Fomu ingetaja tarehe na mwezi na mahali waliposhuhudia. Fomu ingetaja wanaoshuhudia, na walioshuhudiwa pamoja na jinsia yao na kisio la umri wao. Pia ingetaja kama walioshuhudiwa walikata shauri au la. Mwishowe, kama hawakukata shauri, fomu ingeonesha kizuizi chao cha kutoamini, na kama wali-kata shauri, mpango wa kuwafuatilia na kuwajenga (nani na maendeleo yao). Fomu ya namna hiyo ingekuwa rahisi kujaza kila wiki na kisha kujumlisha taarifa kila mwezi au kila baada ya miezi mi-tatu.

Mfano wa ripoti ya taarifa ya uinjilisti ni huo hapo chini. Kwa kujaza fomu hii, kanisa na timu ya wanaoshuhudia wataweza kuhakikisha wanazunguka kwa utaratibu mzuri na kufuatilia wanaosta-hili kufuatiliwa. Itawakumbusha mpango wa kufuatilia wale waliokata shauri na pia itawasaidia katika mpango wa kutembelea tena wengine ambao hawakukata shauri lakini walionesha dalili ya kutaka kujifunza zaidi. Pia, itawasaidia wakati wa kufundishana kutafuta namna ya kushinda vizuizi mbalimbali wanavyokutana navyo. Takwimu nyingine zitaonesha ni watu wa namna gani wanaokuwa tayari kumpokea Yesu, kwa mfano, ni watu wa jinsia gani au wa umri gani.

Fomu hiyo hiyo au nyingine ingeweza kutengenezwa kwa ajili ya kujumlisha mwezi, robo na nusu mwaka, na hata mwaka mzima.

Tarehe__________________ Mahali__________________

Mtu wa 1 Mtu wa 2 Mtu wa 3 Jina Lake? Me, ke? Umri kisio? Aliamini? Kizuizi au Ufuatiliaji?

Mshuhudiaji:________________________________

MASWALI NA MAJADILIANO

1. Ukitaka kuanza huduma ya uinjilisti katika kanisa lako, utafanya nini kwanza? 2. Ukipata kikundi kidogo cha kusaidiana kushuhudia, ungefanya mpango gani pamoja nao? 3. Kwa nini ni muhimu kutunza taarifa? 4. Je, unaweza kuahidi sasa hivi kufuata mapendekezo ya kitabu hiki kuanzisha huduma hii katika

kanisa lako? Kama ndiyo, umwombe Mungu akupe nguvu kuitimiza ahadi yako. 5. Unaweza kuona vizuizi gani katika kufanya mpango wa uinjilisti wa mtu kwa mtu katika kanisa

lako?

32

14. Mpango Unaohusisha Kanisa Zima Kwa vile huduma hiyo ya uinjilisti ni muhimu na ni msingi wa kanisa la Mungu lenye uhai,

mpango huo ungehusu kanisa zima. Maana, tawi moja la kanisa haliwezi kufaulu kuwatangazia watu wote wa wilaya au mkoa mzima. Basi ni kwa njia gani makanisa yangeweza kushirikiana katika kazi hiyo? Tutumie sura hii ya mwisho kuchunguza vizuri swali hilo na kutoa mapendekezo.

Kwanza kabisa, napenda kukupongeza kwa vile umekisoma kitabu hiki hadi hapa. Maana wewe mwenyewe umejifunza na kujiongezea ujuzi. Zaidi, umeshakuwa mwanga wa kuwafundisha wen-gine na kuanzisha mpango wa uinjilisti katika tawi lako na katika makanisa mengine yaliyo jirani, Mungu akikujalia. Kitabu hiki kimeandaliwa ili kitumiwe kwa mafundisho na unaweza kukitumia kufundishia semina kwa ajili ya wainjilisti katika mkusanyiko wa matawi mengi au kwa washirika wachache wa tawi lako la mahali.

Paulo alipomfundisha Timotheo alimweleza hivi, “Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (2 Tim 2:2). Kwa kweli ni wajibu wako kuyatumia yale uliyojifunza na zaidi kuwakabidhi (kuwafundisha) watu waaminifu wafaao (watakaofanya) ambao watawafundisha na wengine pia. Kwa njia hiyo mambo hayo ya Mungu yataenea kwa nguvu!

Kanisa lenye mpango wa kufundisha uinjilisti kwa washirika wake wote, liteue kundi la wain-jilisti wakufunzi. Kanisa, pamoja na wakufunzi hawa, wapange mpango na taratibu za uinjilisti kwa ajili ya makanisa yake. Ndipo wakufunzi hawa watumwe kufundisha wengine katika ngazi mbalim-bali kama vile ngazi ya mkoa au senta (yaani uongozi wa huduma za uinjilisti unaohusu mikusanyi-ko ya matawi zaidi ya moja). Katika kufundisha ngazi hizo, mpango uwekwe kupeleka mafundisho na huduma yenyewe katika kila tawi wakifundisha njia za uinjilisti na wakisimamisha namna huduma itakavyofanyika na jinsi taarifa zitakavyotolewa.

Itasaidia kama makundi ya uinjilisti yataanzishwa katika tawi, senta, na mkoa. Ndani ya ma-kundi haya kamati za unijilisti zingekuwepo za kudumu ili waweze kukutana kila miezi mitatu au nusu mwaka kujengana na kushauriana kuhusu maendeleo na mahitaji ya huduma hiyo. Ingefaa kamati hizo pia zifanye mpango wa kupata mfuko wa fedha kuendeshea shughuli zote za tawi, sen-ta, na mkoa wakitafuta kununua vifaa kama maandiko na vingine. Kamati hizo zikikutana zinaweza kuweka malengo ya uinjilisti katika maeneo yao na pia wanaweza kupanga namna ya kushirikiana katika kulenga vijiji vipya huku wakikumbuka umuhimu wa ufuatiliaji. Hawa vilevile wangeweza kutoa taarifa ya kila mara na kuipeleka kwa mkurugenzi au kamati ya uinjilisti wa kanisa zima.

Kamati hiyo ya uinjilisti wa kanisa zima inahitaji kuwa na wafuatiliaji wa vifaa kama traksi, masomo ya waumini wapya, Biblia na Agano Jipya, na maandiko na masomo mengine.

Muundo mwenyewe wa kushirikiana ungekuwa kama mchoro huu:

Kwa kufuata muundo kama huo, au mwingine unaofanana, kanisa zima linaweza kufaulu zaidi

katika kueneza Injili kupitia watu wao. Mpango wao wa kushirikiana utaongeza nguvu na mafanikio yao wakitegemea uongozi na nguvu za Roho Mtakatifu. Vilevile wataweza kupima maendeleo yao na

33

kuboresha taratibu zao kulingana na habari wanazozikusanya. Makanisa mengi hayana maendeleo kwa vile wameamua uinjilisti ni kazi ya mtu maalum au

kundi maalum ndani ya kanisa na siyo huduma ya watu wote kama tulivyojifunza katika kitabu hiki. Mungu hutaka kila Mkristo kulima na kuvuna katika shamba lake. Ndiyo mpango wake wa kuipele-ka Injili hadi mwisho wa dunia.

Tuachane na mawazo yanayosema uinjilisti lazima uwe na vyombo na mitambo ya kisasa ya bei ghali. Vyombo vyenyewe sivyo vibaya, tena vinaweza kusaidia uinjilisti. Lakini mawazo yanayosema vyombo ni vya lazima ni kinyume na mpango wa Mungu. Maana, mawazo hayo huathiri watu na kuwafikisha katika wazo la kusema, “Bila vyombo basi hatuwezi kushuhudia.” Yesu Kristo na mi-tume wake walikuwa vyombo tosha vya uinjilisti. Nasi tuwe vyombo vya Mungu (2 Tim 2:21) tukipeleka Injili duniani pote! Mungu akubariki!

RATIBA YA SEMINA YA SIKU SITA KWA KUTUMIA KITABU HIKI

Jumatatu Jumanne Jumatano SAA SOMO SOMO SOMO 3:00 - 4:15 Somo #1 Somo #4 Somo #6 4:15 - 4:30 Maswali #1 Maswali #4 Maswali #6 4:30 - 5:00 Pumziko Pumziko Pumziko 5:00 - 6:15 Somo #2 Somo #5 Somo #7 6:15 - 6:30 Maswali #2 Maswali #5 Maswali #7 6:30 - 8:00 Chakula Chakula Chakula 8:00 - 9:15 Somo #3 Mazoezi #1 Mazoezi #2 9:15 - 9:30 Maswali #1 Mazoezi #1 Mazoezi #2 9:30 - 11:00 Kuandaa Injili

na Ushuhuda Mazoezi #1 Huduma #1

Alhamisi Ijumaa Jumamosi

SAA SOMO SOMO SOMO 3:00 - 4:00 Taarifa #1 Taarifa #2 Marudio

4:00 - 4:30 Somo #8 Somo #11 4:30 - 5:00 Pumziko Pumziko Pumziko 5:00 - 6:15 Somo #9 Somo #12 Mipango ya

Kutekeleza 6:15 - 6:30 Maswali #9 Maswali #12 6:30 - 8:00 Chakula Chakula Chakula 8:00 - 9:15 Somo #10 Somo #13 Kufuata Wale

Walioamini

9:15 - 9:30 Maswali #10 Maswali #13 9:30 - 11:00 Huduma #2 Somo #14

JUMAPILI - Kuwapitia waumini wapya na kuwapeleka kanisani na kukaa nao. Kushuhudia

kanisani ulivyojifunza kwenye semina na kumshukuru Mungu kwa yote.

Vitabu Vilivyonisaidia Kuandika Kitabu Hiki

1. Ushuhuda Ufaao na (Evangel Publishing House: Kisumu, Kenya) 1977. 2. Uinjilisti wa Maandiko na George Verwer; Operation Mobilization na (nakala ya Kiswahili - Kit-

uo cha Maandiko Habari Maalum: Tabora, TZ) 1985. 3. Uvuvi wa Watu na William Macdonald; (Emmaus Bible School: Dar es Salaam, TZ). 4. Uinjilisti na D.A. Brown; (Central Tanganyika Press: Dodoma, TZ ) 1967 5. Kukua kwa Kanisa na Dr. Vergil Gerber; (Inland Publishers: Mwanza, TZ) 1978.