10
KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 1 Kumbuka ! Watalaamu waliyosomea theologia hawawezi kujibu maswali yote, usitegemee kuwanayo wewe ! Nyaraka: Maswali ya Fasili ya Maandiko wakati huu (The Hermenutical Questions) ”Tunapoleta” mafundisho ya wakati ule kuja kueleweka katika mazingira ya sasa tunasema tunafanya ”hermeneutics” maana yake ni kufafanua maandiko katika mda wetu. Kazi hii kidogo inaelekea kuwa kubahatisha kuliko kazi ya ”exegesis” . Exegesis inaweka mipaka yake lakini hermeneutics inawekwa mipaka na yule anayehubiri. Inatokana na ufahamu wake juu ya andiko anayoifafanua. Kunanini ambayo ni mafundisho ya ”kimazingira”? Kunanini ambayo haina mipaka ya mda (hali ile ni sawa na hali ya leo).

KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 1 · moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu”. Yote hayo ni mafundisho kwa kila mkristo katika kila hali. KUFAFANUA MAANDIKO -

  • Upload
    dolien

  • View
    315

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 1 · moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu”. Yote hayo ni mafundisho kwa kila mkristo katika kila hali. KUFAFANUA MAANDIKO -

KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 1

• Kumbuka ! • Watalaamu waliyosomea theologia hawawezi kujibu maswali yote,

usitegemee kuwanayo wewe !

• Nyaraka: Maswali ya Fasili ya Maandiko wakati huu (The Hermenutical Questions) • ”Tunapoleta” mafundisho ya wakati ule kuja kueleweka katika

mazingira ya sasa tunasema tunafanya ”hermeneutics” maana yake ni kufafanua maandiko katika mda wetu.

• Kazi hii kidogo inaelekea kuwa kubahatisha kuliko kazi ya ”exegesis” . Exegesis inaweka mipaka yake lakini hermeneutics inawekwa mipaka na yule anayehubiri. Inatokana na ufahamu wake juu ya andiko anayoifafanua. • Kunanini ambayo ni mafundisho ya ”kimazingira”? • Kunanini ambayo haina mipaka ya mda (hali ile ni sawa na hali

ya leo).

Page 2: KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 1 · moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu”. Yote hayo ni mafundisho kwa kila mkristo katika kila hali. KUFAFANUA MAANDIKO -

KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 2

• Fasiri tunayoifanya sisi sote • Sote tunafasiri, mazoea yetu, mafundisho mbali mbali tuliyoyapata katika maisha yetu.

Mengine tunafanya makusudi mengine bila kujua. Mengine kwa ajili ya kufaidika kidogo. (inawezekana ikafaidi kanisa au mtu binafsi) Sababu mbali mbali inatufanya tuelewe fungu fulani ngumu kwa jinsi fulani.

• Ni muhimu kuelewa kua mafungu yenye matatizo siyo mengi sana, yaliyo mengi ni rahisi kuelewa na haitupi matatizo. Kama mfano tuangalie ”fungu za matatizo” chache:

• 2Tim 2:3 inamuhusu kila mkristo lakini 4:13 hakuna anayeifuata leo kama mfano wa maisha.. Tukienda 1Tim 5:23. ”Tokea sasa usinywe maji tu......” tunashituka katika makanisa fulani hiyo tunasema inamuhusu Timoteo binafsi. Lakini 2Tim 3:14-16 tunasema inatuhusu sote ingawa waraka wote imeandikwa kwa mtu mmoja Timoteo .

• Baadhi wanapata msingi wa kubatiza watoto katika 1Kor 1:16; 7:14 au Kol 2:11-12, wengine wanashindwa kukubaliana na msingi huo, maana wanashindwa kuona nguvu za msingi huo katika fungo hizo.

• Wanao tilia uzito mafundisho ya hiari, wanapata matatizo na mistari ya Rum 8:30; 9:18-24

• Biblia yetu imeja mistari ambayo tunaweza kuelewa kwa jinsi mbali mbali.Wakati tunapotaka kuelewa maana na kwa jinsi gani andiko fulani inatuhusu kuna taratibu za kufuata.

Page 3: KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 1 · moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu”. Yote hayo ni mafundisho kwa kila mkristo katika kila hali. KUFAFANUA MAANDIKO -

KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 3

• KANUNI YA KWANZA • Maandiko hayawezi kubadili maana ! • Mfano:

• 1Kor 13:10; ”Lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabadilika”. Sasa kuna wanaoamini iliyokamili iliingia wakati tulipopewa agano jipya. Kwa hiyo hakuna nafasi ya 1Kor 14 na vipawa vya Roho mana yenyewe yanaweza kutumika katika taratibu sizizo kamili. Kwa hiyo wanasema eti vipawa vya Roho zimepitwa na wakati zilifanya kazi kwa kipindi tu. Lakini Paulo hakuwa na kusudi hilo,

• Kwanza katika makanisa yetu tunaona kwamba vipawa vinafanya kazi.

• katika historia yote ya wakristo, wakristo wametumia vipawa vya Roho, kwa kujengana, kwa kupiga vita yule mwovu, na kwa kupata kufahamu mapenzi ya Mungu.

• Pia waliyopewa barua hii hawakutegemea kwamba Agano Jipya kama kitabu itapatikana. Na barua za namna hii kawaida yake ni kama inashugulikia matatizo ya watu kwa kuwaeleza kwa njia itakayoweza kuwasaidia kufahamu na kurekibiisha maisha yao.

Page 4: KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 1 · moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu”. Yote hayo ni mafundisho kwa kila mkristo katika kila hali. KUFAFANUA MAANDIKO -

KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 4

• KANUNI YA PILI • Tunapoishi katika mazingira sawa sawa na wale waliopata barua

yenyewe, tunaweza ”kutumia” mafundisho yale moja kwa moja.

• Mfano: • ”Wote wametenda dhambi, kwa neema momeokoka, jivikeni

moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu”. Yote hayo ni mafundisho kwa kila mkristo katika kila hali.

Page 5: KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 1 · moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu”. Yote hayo ni mafundisho kwa kila mkristo katika kila hali. KUFAFANUA MAANDIKO -

KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 5

• TATIZO YA ”MAFUNDISHO MAPANA” • Je inawezekana kutoa mafundisho tofauti na mafundisho ya asili. Yaani mafundisho

yaliyokusudiwa na mwandishi?

• Mfano 1Kor 3:16-17

• Fungo hii inahusu kanisa la Korintho, lakini pia inaonyesha kanuni inayosema kwamba kila Mungu alichokitenga kwa ajili yake kwa njia ya Roho wake kuingia pale ni kitakatifu. Anayeharibu hicki kitu au huyu mtu anajiweka chini ya hukumu ya Mungu. (Anaweza akasamehewa, lakini maana yake ni huwezi ukawasumbua watu wake bila kupata hukumu yake). Ni muhimu kuona kwamba fungo hiii haihusu watu fulani fulani inahusu kanisa, kanisa la mahali. Kuna sehemu nyingine inayohusu kumpotosha mtu mmoja, binafsi. (Matt 18:6, Mk 9:42; Luk 17:2) Lakini fungo hii ya 1Kor, haituruhusu kuiweka kama mafundisho ya ubinafsi baali ni ya kanisa.

• mfano 2: 1Kor 3:10-15

•Fungo hii inahusu thamani ya kazi yetu, kwamba tutajenga juu ya msingi uliyowekwa katika Biblia, injili. Imeandikwa kwamba yeye ajengae vibaya ataokolewa ”lakini ni kama kwa moto” ”Ataponea chupu chupu” Maandiko hayo tuyaeleweje? Inamaana kwamba wokovu ni wa milele? Maana yake ni kwamba ukiokolewa huwezi kuanguka tena. Au inasema kwamba wokovu ni wa neema hautegemei matendo? Maana yake ukijenga vizuri au vibaya haitadhuru wokovu wako, uki fanya kazi sana au kidogo hakuna tofauti...

Page 6: KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 1 · moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu”. Yote hayo ni mafundisho kwa kila mkristo katika kila hali. KUFAFANUA MAANDIKO -

KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 6• Tatizo ya maandiko yanayohusu mazingira ya wakati ule tu (Matatizo tunayoshindwa

kuyatambua leo) • Kuna maandiko yanayo husu mazingira karne ya kwanza tu. Zingine yanaweza yakawa

na maana kwetu lakini ni kama mara chache matatizo kama hayo huonekana. Tufanyeje vifungu vya namna hiyo?? Je, vinawezakutupa chochote cha maana?? Au tuziache tu..?

• Mfano:

• 1Kor 11:17-22; Kulewa na vinywaji vya ushirika, au Gal 5:2: Kulazimisha waumini kutahiriwa. Matatizo ya namna hiyo sisi hatuna kabisa

• Tatizo ambayo ingeweza kuwepo lakini siyo kawaida inaweza kuwa kwamba wakristo fulani wakakataa kua Paulo alikuwa mtume 1Kor 9:1-23, au kama tunaweza kula chakula kilichotolewa kama sadaka kwa miungu 10:23-11:1.

• Tutumieje sehemu , maanadiko, kama hayo? Tunapotafuta kujua ujumbe itabidi tuende kwa hatua mbili. • 1.Kwanza lazima tufanye ”*exegeses” nzuri na ya makini tuweze kuelewa maana ya

fungu yenyewe wakati ule. Mara nyingi tunapofanya hivi tunaweza kuelewa kanuni fulani ambayo inaweza kutumika leo.

• 2.Kanuni hiyo tunahitaji kuitumia katika mazingira yake, hatuwezi kuitumia kama tunavyoamua bali lazima iwe katika ”situation” sawa na wakati ule.

Page 7: KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 1 · moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu”. Yote hayo ni mafundisho kwa kila mkristo katika kila hali. KUFAFANUA MAANDIKO -

KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 7• Tuchambueje mistari ya ”kimazingira” ?

• Kwanza lazima tuweze kufahamu kama fungu tunalolisoma ni ”lenye maana” au sivyo. • Mfano: Maandiko yanayo husu, chakula na vinywaji mara nyingi ni vya

kimazingira na si rahisi kuzichukua na kufuata moja kwa moja. • Tukiweza kuangalia na kugawa maandiko katika sehemu inayohusu maadili na

mazingira tutakua tumepiga hatua. Yanayohusu maadili ni muhimu kwetu yanayohusu mazingira hazina uzito sana. Ku tumia au kutokutumia divai kama kinywaji ni swala la kimazingira.

• Kuna sehemu ya ”urodha ya madhambi” mfano Rum 1:29-31; 1Kor 5:11; 6:9-10; 2Tim 3:2-4 hizo sehemu si rahisi kulinganisha na tatizo, au dhambi za siku hizi. Leo tunamatatizo yetu kutokana na mazingira na maisha tuliyonayo. (Urefu ya mavazi ya wasichana, tai, suruale, helene, marashi, kujipaka..... Uhusiano ya wavulana na wasichana, ”beachlife”..) Matatizo haya siyo rahisi kuunda kanuni fulani na kuifuata katika kila hali, na kabila ya watu.

• Ni muhimu tu kukumbuka kwamba yule aliye huru kuliko mwenzake katika swala fulani asimuhukumu mwenzake, na pia asiye huru sana asimhukumu mwenzake. Tuheshimiane tumuachie Mungu hukumu. Si kazi yetu kupima utakatifu wa watu, na kujilinganisha.

Page 8: KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 1 · moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu”. Yote hayo ni mafundisho kwa kila mkristo katika kila hali. KUFAFANUA MAANDIKO -

KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 8

• Matatizo ya tofauti ya mazingira • Hapa nafuata muongozo, au mashauri kidogo yanayoweza kutusaidia katika

kuchambua lililolamuhimu na lisilolamuhimu sana kufuatana na maelezo ya hapo juu.

• 1.Kwanza tuangalie ni nini ambayo ni msingi wa mafundisho ya Bibilia, na ni nini ambayo inakua pembeni kidoga na kina. Tuta ”focas” kwenye Injili na kuiweka wazi kina cha Injili. Pia itabidi tusiruhusu maswala ya kimazingira kutuongoza katika ufahamu wetu wa injili. Mambo ya umuhimu sana ni: Kuanguka kwa binadamu, Jinsi mungu alivyookoa ulimwengu kwa neema yake, Kwamba Yesu atarudi mara ya pili na kadhalika. Lakini Busu takatifu, mavazi ya mwanamke, strukture ya utumishi na kadhalika siyo muhimu sana na inaweza kua tofauti hapa na pale.

• 2.Kuna kanuni za maadili ambayo katika kila mazingira inakubaliwa. Mfano: Kutokuishi katika uwasherati, uasi, ulevi, vitendo vya kibasha, wizi, ubahili na kadhalika (1Kor 6:9-10) Vitu vingine kama kuoshana miguu, busu takatifu, kula iliyotolewa katika madhabahu ya miungu, mavazi ya wanawake / wanaume, kuoa aukajikalia pekee kama Paulo, au kama mwanamke anaweza kufundisha kanisani haimo katika maadili yanayokubaliwa na wote.

Page 9: KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 1 · moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu”. Yote hayo ni mafundisho kwa kila mkristo katika kila hali. KUFAFANUA MAANDIKO -

KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 9• 3.Katika baadhi ya mafundisho Agano Jipya ina zungumza lugha moja. Kwa mfano:

Upendo ni msingi wa kila kitendo ya kikristo, usilipize kisasi. Siyo vizuri kuanzisha ugomvi, kuua, kuiba, uasherati, usenge, kulewa.....

• Lakini saa nyingine tunaona kwamba lugha inabadilika. Kwa mfano: Jinsi wanawake wanaweza kushika uongozi katika kanisa. Rum 16:1-2 Fibi ni mshemasi, Rum 16:7 Yunia (Mwanamke) anatajwa pamoja na mitume Rum 16:3 Priska (mwanamke) ni msaidizi wa Paulo na anatajwa kabla ya Akila (mwanaume) hiyo inaonyesha kwamba alimzidi katika cheo.

• Tusiruhusu fungu moja kutuongoza katika kanuni zetu kama kunasehemu nyingine ambayo inapinga sehemu hii ya kwanza. Wakati mafundisho yanapishana nasi tuelewe kwamba Mungu aliruhusu iwe hivyo na bila shaka sababu yake ni kwamba anapenda tuelewe kwamba pia kanuni zinaweza kupishana, labda sababu ya mazingira... Hapo inabidi tutumuie hekima yetu.

• 4.Sehemu moja ambayo inahusu mazingira ya pale ni 1Kor 11:2-16, Nywele za mwanamke ziwe badala ya mavazi mst15.. Jamani hapa kwetu hiyo haiwezekani. (iwapo wengine wanajitahidi iwe hivyo..) Na kwetu kama mwanamke mswidish akija amejiifunika kichwa ingeleta maswali mengi katika wanaohudhuria ibada hiyo.. Mavazi ya kule yanaweza yasifae hapa na mavazi ya hapa yanakua ya kimaajabu kule. Hakuna kanuni ya mavazi ya kikristo....

Page 10: KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 1 · moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu”. Yote hayo ni mafundisho kwa kila mkristo katika kila hali. KUFAFANUA MAANDIKO -

KUFAFANUA MAANDIKO - HERMENEUTICS 10• 5.Agano jipya haina msimamo juu ya utumwa. Lakini wanawake katika kanisa

waliinuliwa sana kuliko wanawake katika ”dunia” wakati ule. Waandishi wa kimataifa hawakuwa na msimamo juu ya usenge, lakini Agano Jipya inayo, na inapinga kabisa kitendo hiki. Utumwa na haki ya mwanamke watu wa mataifa walikua na misimamo yao, lakini kwa upande wa wanawake watu wa kanisa wakafuata njia tofauti na watu wa mataifa.

• 6.Mwanamke wakati ule na mwanamke wa sasa kuna tofauti sana na siyo ajabu kabisa. Hata tukiangalia katika ulimwengu wetu wa leo mwanamke katika nchi fukani anaweza kujiendeleza bila shida wakati mwanamke mwenzake katika nchi nyingine (au kanisa) anapata shida kweli. (Kuna inchi ambayo wanawake wanatawala katika kila hali) Mazingira ya wakati ule inawezekana inasababisha mistari kama ya 1Tim 2:9-15.

• Uongozi usiyofaa hauwezi ukadumu, wanaachishwa kazi (katika nchi ya kawaida) Rum 13 ni vigumu kulielewa leo. Demokrasia ilikua kitu ambacho hawakuijua wakati ule, lazima kumtii mkuu. (vipi hapa)7

• 7.Halafu tukumbuke kuwa wanyenyekevu, lazima tukubali kwamba kuna visehemu katika Biblia yetu ambayo ni vigumu kuelewa maana yake . Tusikatae hiyo hali. Ni muhimu sanatuwe wazi katika kujadiliana na wakristo wenzetu, na kuheshimiana katika sehemu zile ambayo tumezielewa tofauti na wenzetu.