25
34 MAFUNDISHO YA UMISHENI I KUHUBIRI NA KUFUNDISHA Muhtasari: Elekeza kwa mada ilioko hapa chini nayo itakuelekeza kwa mada hiyo. I. Lengo la Kiuzi Hiki II. Ufafanuzi wa Biblia A. Ufasili B. Tafsiri ya Maandiko C. Maana ya Maandiko D. Kutumia Maandiko III. Vifaa IV. Kuhubiri A. Utangulizi B. Kuchagua Mahubiri C. Mahubiri ya Ufasiri 1. Kuchagua Maandiko 2. Kukuza Muhtasari na Maandiko 3. Mazoezi ya Kuwasilisha 4. Kuwasilisha na Maoni D. Mahubiri ya Mada E. Uchunguzi wa Mhusika V. Kufundisha A. Utangulizi B. Somo 1. Ufasiri

MAFUNDISHO YA UMISHENI Imissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KUHUBIRI_NA...34 MAFUNDISHO YA UMISHENI I KUHUBIRI NA KUFUNDISHA Muhtasari: Elekeza kwa mada ilioko hapa chini nayo itakuelekeza

  • Upload
    others

  • View
    43

  • Download
    3

Embed Size (px)

Citation preview

34 MAFUNDISHO YA UMISHENI

I

KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

Muhtasari: Elekeza kwa mada ilioko hapa chini nayo itakuelekeza kwa mada hiyo.

I. Lengo la Kiuzi Hiki II. Ufafanuzi wa Biblia

A. Ufasili B. Tafsiri ya Maandiko C. Maana ya Maandiko D. Kutumia Maandiko

III. Vifaa IV. Kuhubiri

A. Utangulizi B. Kuchagua Mahubiri C. Mahubiri ya Ufasiri

1. Kuchagua Maandiko 2. Kukuza Muhtasari na Maandiko 3. Mazoezi ya Kuwasilisha 4. Kuwasilisha na Maoni

D. Mahubiri ya Mada E. Uchunguzi wa Mhusika

V. Kufundisha A. Utangulizi B. Somo

1. Ufasiri

a. Kiini b. Kifungu kwa kifungu

2. Mada 3. Kuchunguza Mhusika

VI. Habari Zaidi VII. Kazi ya Ziada

A. Hubiri Mahubiri Mawili B. Ongoza Madarasa Mawili

Haki za Kunakili © 2009 Shirika la Mafunzo ya Umisheni. Haki Zimehifadhiwa.

KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

I. Lengo la Kiuzi Hiki

Baada ya kusoma kiunzi hiki cha mafundisho, unafaa:

• Uwe na uwezo wa kufafanua istilahi za kimsingi zinazohusiana na kiuzi hiki.

• Uwe na uwezo wa kuchagua tafsiri ya Biblia isiyo na hitilafu

• Kujua kanuni za kufafanua Biblia

• Kujua vifaa vya kujifunza Biblia

• Kuelewa kanuni za kutoa mahubiri

• Uweze kuchagua mada ya mahubiri

• Uweze kuchagua aina ya mahubiri

• Uweze kupata Maandiko yanayoambatana na mahubiri

• Kujua kukuza muhtasari wa mahubiri

• Kukariri chemshabongo zinazotumiwa katika matumizi ya mahubiri

• Kuweza kutenda kulingana na mahubiri

• Kuelewa baadhi ya njia za kukuwezesha kutoa mahubiri kwa njia inayofaa.

• Kujua hatua zinazohusika katika kutayarisha aina tofauti za mahubiri

• Uweze kuelewa kanuni za kufunza Biblia

• Kuwa umechunguza baadhi ya wavuti zilizo na manufaa katika kuhubiri na kufunza.

RUDI KWA MUHTASARI

KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

II. Ufafanuzi wa Biblia

Lengo la kiuzi hiki ni kutoa muhtasari wa jinsi ya kujifunza Biblia, kuhubiri Biblia, na kufunza Biblia. Mafunzo zaidi yaweza kupatikana katika wavuti na umeorodheshwa hapo chini kwa mada ya “kwa habari zaidi.”

Kabla ya kuhubiri na kufundisha, tunahitaji kuamua yale Maandiko yanamaanisha na jinsi tunavyoweza kutumia Maandiko katika maisha yetu. Na tuchunguze jinsi ya kutafsiri Maandiko.

A. Ufasili

Kamusi ya Merriam-Webster inatupa mwongozo wa matamshi yaliyoandikwa na yakusikiza ili kutusaidia kutamka maneno kwa lugha ya Kiingereza.

http://www.m-w.com/

Katika theolojia, hermeneutics ni sayansi ya kufafanua Maandiko. Fasili ya Maandiko (Exegesis) ni utumizi wa kanuni za kufafanua Maandiko. Ufasiri (Exposition) ni jinsi ya kueleza watu Maandiko. Kwa hivyo mhubiri hutumia kanuni za hermeneutics kufafanua Maandiko ili kueneza mahubiri yanayoeleweka. Tunataka kuepuka isogesis—kujaribu kuweka mawazo yetu kwa Maandiko, au kujaribu kubadilisha Maana iliyo katika Maandiko. Fasili ya maandiko (Exegesis) ni “kusoma kutoka “ kwa Maandiko, na isogesis ni “kusoma ndani ya” Maandiko. Pericope ni kifungu cha Maandiko kilicho na wazo kamili. Wakati mwingine ukurasa katika Biblia waweza kuwa pericope. Wakati mwingine sehemu ya ukurasa au zaidi ya ukurasa mmoja waweza kuunda pericope. Ili tuweze kueleza Maandiko kinaganaga, tunahitaji kutambua mahali pericope inaanzia na mahali inaishia.

B. Tafsiri ya Maandiko

Maandiko ya Biblia ya asili yalikuwa yameandika kwa Kiebrania, Kigriki na Aramaic. Maandiko yametafsiriwa katika lugha nyingi na kutengenezwa upya jinsi lugha zinavyoendelea kugeuka. Ni vyema uweze kuchagua tafsiri isiyo na hitilafu ambayo yaweza kueleweka na watu unaofundisha. Ni lazima tafsiri hiyo iwe imekubalika na makanisa yaliyo na mwelekeo tawala, ikilinganishwa na tafsiri iliyoandikwa na madhehebu ya uasi. Huwa natumia tafsiri ya Union. Habari Njema pia ni tafsiri njema. Kwa Kiingereza huwa natumia New International Version (NIV). Tafsiri nyingine nzuri ni New American Standard, ambayo hutafsiri neno kwa neno. Tafsiri ya King James ni nzuri, ila hutumia lugha ambayo imepitwa na wakati, na kuifanya kuwa gumu

kueleweka. Ni vyema kuchagua kifungu kimoja kama chanzo cha msingi badala ya kubadilisha kutoka kifungu kimoja hadi kingine. Kuwa na chanzo kimoja cha msingi hutuwezesha kukariri Maandiko kwa urahisi. Ungependa kutumia vifaa vya ziada katika masomo yako kwa kutumia tafsiri iliyofafanuliwa- ambayo haifuati utaratibu katika kutafsiri Maandiko ili kuyafanya kuwa rahisi kuelewa. Tafsiri iliyofafanuliwa hutaka kuwa “sawa kabisa” na maandiko ya asili. Kwa sababu Biblia zilizofafanuliwa hazijatafsiriwa neno kwa neno kutoka kwa Maandiko ya asili, sitayatumia kama Maandiko ya msingi. Biblia ya Habari Njema ni tafsiri iliyofafanuliwa. Kama Kiswahili chako siyo sanifu, waweza kutumia Biblia iliyoandikwa kwa lugha ya kimsingi. Biblia inajumuisha Agano la Kale na Agano Jipya, na imeandikwa kwa kutumia misamiati ya kimsingi ya maneno 1,000 pekee.1 Hapo chini kuna mtandao unaoeleza Biblia zilizoandikwa kwa lugha ya Kiingereza, na zimepangwa kulingana na uhalisi wake. Baadhi ya Biblia ni tafsiri ya neno kwa neno na zingine zimefafanuliwa. Tazama chati ya “Tafsiri za Biblia” iliyoko mwisho wa ukurasa wa wavuti huu.

http://preceptaustin.org/inductive_bible_study.htm

C. Maana ya Maandiko

Tafsiri njema ya Biblia hutueleza yale Maandiko yanayosema. Lakini Maandiko yalimaanisha nini nyakati za Biblia? Tumetenganishwa na waandishi wa Biblia na nyakati, Jiografia, na tamaduni. Kifungu nyakati za Biblia chaweza kuwa kilikuwa na maana tofauti na kifungu hicho hicho wakati huu. Kwa hivyo ni lazima tutumie kanuni za kufafanua Maandiko (hermeneutical principles) ili kuamua yale mwandishi wa Biblia alitaka tujue. Zifuatazo ni baadhi ya kanuni zinazotumika kufafanua Maandiko.

1. Biblia ina Mamlaka. Tunaamini kuwa vitabu 66 vya Agano la Kale na

Agano Jipya ni Neno la Mungu lililo na Mamlaka. Mungu alitia msukumo ndani ya waandishi wa Biblia ili kupasha ukweli. 16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. (2 Timotheo 3:16,17)

2. Ni lazima Maandiko yaangaliwe katika muktadha. Tunapojifunza kifungu au pericope, chunguza pia fungu la maneno na kitabu ambacho kifungu hicho kilitolewa. Kiini cha kitabu ni gani? Kwa nini mwandishi aliandika kitabu hicho? Ni nani aliandika Kitabu na alikuwa anaandikia

nani? Kitabu hicho kiliandikwa lini na wapi? Chunguza historia , tamaduni, jiografia na hali ya muktadha.

3. Amua namna (aina ya fasihi). Kitabu au vifungu vya Maandiko ni cha nyimbo, mashairi, unabii, historia, nyaraka, Injili au Sheria? Lugha huwa na maana tofauti kwa aina tofauti.

4. Chukulia maana hasa ya maneno isipokuwa kama kuna sababu ya kuchukulia vingine. Kwa jumla Biblia humaanisha yale inayosema- hasa. Aina na muktadha yaweza kuonyesha kuwa maneno mengine ni ya kitamathali. Biblia inajumuisha sitiari, tashbihi, mithali, istiari na mbalagha. Kwa mfano lugha ya kitamathali imetumika kwa wingi kwenye fasihi ya kutabili mambo ya maafa makubwa yaliyoko katika kitabu cha Ufunuo.

5. Amua maana ya maneno. Mara nyingi ufafanuzi wa Maandiko unahusu kujifunza neno ili kuamua neno hilo lilikuwa na maana gani wakati lilipoandikwa.

6. Fuata kanuni za sarufi. Wanafunzi wa Biblia wanahitaji kuelewa utumizi wa kitenzi, nomino, kivumishi, kielezi, shamilisho halisi na sehemu zinginezo za usemi.

7. Ruhusu Maandiko yafafanue Maandiko. Vifungu vya Biblia vinavyoeleweka hueleza vifungu vya Maandiko visivyo eleweka vizuri. Fikiria maelezo sambamba, kama yale yalioko katika vidokezo vya Injili (Mathayo, Marko na Luka). Tumia marejeo, kama yale yalioko katika Biblia za Marejeo, ili uweze kupata vifungu vilivyo na mada zinazoambatana. Pia Biblia ya upatano na Biblia za Mada husaidia kupata vifungu vinavyoambatana.

8. Kitu kinapotajwa kwa mara ya kwanza chaweza kueleza maana yake mahali pengine popote kitakapotajwa. Jambo likitokea au neno linapotumika kwa mara ya kwanza maana yake huwa inaelezwa. Kwa hivyo angalia kwenye Biblia ya mapatano ili uweze kupata mara ya kwanza ya jambo hili kutokea au kwa neno kutumika.

9. Biblia ni ufunuo unaoendelea. Waandishi wa kwanza wa Biblia hawakuwa na habari nyingi kama vile waandishi wa Biblia waliofuata. Kwa mfano, mafumbo tofauti yalifunuliwa wakati Kristo alikuja kwa mara ya kwanza. Manabii wa Agano la Kale hawakupewa habari kuhusu kanisa. Manabii wa Agano la Kale hawakuelewa kwamba Masiha angekuja duniani mara mbili. Hata kama ufunuo unaendelea, habari zilizotolewa katika Agano la Kale ni muhimu.

10. Tumia vifaa kando na Biblia. Biblia ni maandishi ya msingi ya kujua mapenzi ya Mungu. Lakini vifaa vingine ni muhimu ili uweze kuelewa Biblia na tamaduni za Biblia. Baadhi ya vifaa hivyo vimeorodheshwa katika sehemu ilioko hapo chini.

D. Kutumia Maandiko

Ili uweze kujifunza Maandiko vyema, ni lazima tutumia mafunzo yake. Ni lazima tuongozwe na Maandiko. Kenson Kuba anatoa chemshabongo inayotumika kwa wingi kusaidia kutumia Maandiko. DAMAMK Dhambi – Kunazo dhambi ninazohitaji kukiri? Ahadi – Kuna ahadi ninazohitaji kudai? Matendo/Mtazamo - Kuna mtazamo au matendo nahitaji kutwaa au kuepuka Amri – Kuna amri ninazohitaji kutii? Mifano – Kuna mifano ninayoweza kufuata? Kweli – Kunazo kweli za kuamini? 2

1. 1Kwa habari zaidi kuhusu Biblia katika lugha ya kimsingi, andika kwa Cambridge University Press, New York, New York, USA. 2Kenson Kuba, "Vitabu vya Bure vya masomo ya Uanafunzi ", Masomo ya Uanafunzi kitabu cha 3, ukurasa 21 katika mtandao.

http://biblestudycd.com/books/book3.pdf

RUDI KWA MUHTASARI

KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

III. Vifaa

Vifaa vya mtandao vya kutafsiri Biblia vya bure vyaweza kupatikana katika wavuti ufuatao.

http://www.preceptaustin.org/

Vifaa hivyo vya mtandao katika wavuti ulioko hapo juu vinajumuisha vifaa vifuatavyo:

1. Elekeza kwa mada “Kamusi ya Biblia” Ili uweze kutafuta misamiati ya Biblia, ensaiklopidia na kamusi ya maneno ya Kiebrania na Kigriki.

2. Elekeza kwa mada “Ramani za Biblia” ili ufikie ramani za mahali panapotajwa katika Biblia.

3. Elekeza kwa mada “Ni Giriki Kwangu ” kwa vifaa vitakavyokusaidia kujifunza maneno.

4. Elekeza kwa mada “Tangazo Mfululizo wa Biblia (Bible Commentary)” ili ufikie tangazo zingine nyingi.

Wavuti uliko hapa chini unakuruhusu kupata mada ya Biblia, neno au kifungu cha kumbukumbu katika tafsiri tofauti na katika lugha tofauti. Kwa hivyo inatumika kama Biblia ya mada, Upatano, na hutafuta vifungu vya Biblia kulingana na ukurasa na nambari ya kifungu.

http://www.biblegateway.com/

Nyingi ya vifaa vilivyoko katika mtandao vinapatikana kwa mfumo wa kitabu. Kwa orodha ya vitabu vilivyopendekezwa, tazama “Vitabu vya Bure vya Mafunzo ya Uanafunzi,” Mafunzo ya Uanafunzi kitabu cha 3 katika wavuti ufuatao.

http://biblestudycd.com/

Wavuti ulioko hapa chini ni Kamusi ya Theolojia. Inakuwezesha kuelewa istilahi za kitheolojia, na kueleza imani ya kimsingi ya kanisa.

http://www.carm.org/dictionary.htm

Vifaa vya kujifunza Biblia (baadhi yake zinapatikana bila malipo) vyaweza kupatikana katika:

http://bible.crosswalk.com

Mojawapo ya vifaa vya kujifunza Biblia vinavyopatikana katika wavuti uliko hapo juu ni Biblia ya msambamba (katika lugha saba, ambayo inasaidia sana wakati unatumia Biblia ya kujifunza lugha nyingine). Wavuti ufuatao unatoa habari kuhusu alfabeti za Kiebrania, lugha na tamaduni.

http://www.hebrew4christians.com/

RUDI KWA MUHTASARI

KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

IV. Kuhubiri

A. Utangulizi

Homiletics ni ustadi wa kuhubiri. Homily ni mahubiri. Kazi ya wahubiri ni kueneza Injili – Habari Njema ya Yesu Kristo. Wale ambao hueneza habari isiyo katika Biblia, huwa hawahubiri Injili. Wale ambao hutoa mahubiri ambayo hugeuza Biblia huwa hawahubiri Injili. Wahubiri waaminifu hufuata Roho Mtakatifu wanapoeneza ukweli wa Maandiko. Mara nyingi wachungaji ndio hutoa mahubiri. Kama wewe ni mchungaji, wewe ni mchungaji wa kondoo – washiriki wa kanisa la mtaa. Huwa unawasilisha sio tu maneno ya mahubiri; huwa unawasilisha wewe ni mtu wa aina gani. Una uhusiano wa kipekee na washiriki walioko katika kanisa la mtaa. Wewe pamoja na washiriki ni mwili wa Kristo. Lakini washiriki hukutazamia kwa uongozi na faraja – maneno yaliyo na ufunuo wa Mungu. Hukutazama kama mfano wa kufuata. Mwishowe Kristo ndiye mfano wa kufuata. Lakini kondoo hufuata mchungaji, nao washiriki hufuata mchungaji. Washiriki wanataka kujua ni mambo gani unayoyajua, lakini zaidi ya yote wanataka kujua kama unawajali. Wanataka kujua kwamba unawajali. Baada ya yote, amri zile kuu mbili zinahusu upendo – upendo kwa Mungu na kwa wengine. Mahubiri mengi hufanyika katika mazingira ya upendo unaoendelea kati ya mhubiri na wasikilizaji.

Wahubiri hunena nyakati fulani katika histora, kwa watu fulani, katika mahali fulani. Ukweli wa Maandiko haubadiliki, lakini lugha ambayo inatumiwa kuwasilisha ukweli hubadilika na wakati, na kutoka kwa tamaduni moja hadi nyingine. Kwa hivyo ni lazima muhubiri anene kwa lugha ya moyo wa wasikilizaji. Lugha ya moyo kwa mtu mmoja ni lugha ya kujichagulia kwa mwingine – lugha ambayo hutumika nyumbani. Unapohubiri, ni lazima uhubiri kutoka kwa roho kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Wasikilizaji wanataka kujua kwamba unaamini yale unayohubiri. Unapohubiri, inasaidia ukielekeza maneno yako kwa mtu binafsi, si kwa washiriki wote. Hiyo ni kusema, hubiri kama unazungumza na mtu binafsi. Tazama watu, si kwa ukuta au sakafu. Mahubiri yasichague mtu binafsi, lakini mhubiri awasiliane na mtu binafsi. Maneno ya mahubiri hayaelekezwi kwa mtu mmoja tu. Badala yake maneno ya mahubiri huelekezwa kwa washiriki. Mhubiri hunena kama ananena na mtu mmoja, nao washiriki wengine wanasikiza. Kwa kweli mhubiri atanena kwa sauti kuliko vile anavyoongea na mtu mmoja. Mhubiri aweza kubadili sauti kuliko jinsi anavyobadili akiongea na mtu mmoja. Lakini, bado huhubiri akitazama mtu mmoja, baadaye mwingine, baadaye mtu wa tatu n.k.

Unapotayarisha mahubiri, ni vyema uweze kujadili mahubiri yanayopendekezwa na watu wengine ambao wana ufahamu wa Maandiko kabla ya kuhubiria washiriki. Wakristo wengine huwa na utambuzi na wanaweza kukuonyesha makosa kabla ya kuhubiria washiriki. Wachungaji waweza kukutanika kwa ushirika na kutayarisha mahubiri. Mhubiri aweza kujifunza kutoka kwa wachungaji wengine, lakini mhubiri asinakili mahubiri ya wengine.

30 "Basi kwa sababu hiyo, Mimi ni juu ya manabii hao, asema BWANA, wanaompokonya kila mtu jirani yake maneno yangu. 31 Tazama," mimi ni juu ya manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema,' 32 Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidi watu hawa hata kidogo, asema BWANA. (Yeremia 23:30-32) Kama Mungu amekuita kuhubiri, atakupa maneno ya kunena. Vile unavyozungumza itakuwa tofauti kutoka kwa wengine kwa sababu wewe ni wa kipekee. Mungu alinena kupitia kwa manabii wa Biblia na kila mmoja wao alikuwa na mtindo wake wa kunena na kuandika. Siku hizi, Mungu hunena kupitia kwa wahubiri, na kila mhubiri ana mtindo wa kipekee. Katika kuhubiri, na katika maisha ya Kikristo kwa jumla, ni lazima tuwe wanyenyekevu. Tunapoulizwa maswali ya kitheolojia ambayo hatuna majibu yake, hatuogopi kusema “Mimi sijui.” Tunapokosea katika mahubiri, tuseme tumekosea. Njia bora ya kuongea kuhusiana na maswali magumu ya kitheolojia ni, “Mimi naelewa hivi . . .” Na ni jambo la busara kutohubiri juu ya mambo ambayo hatuna ufahamu wa kutosha juu yake.

B. Kuchagua Mahubiri

Ni lazima wahubiri waelekezwe na Roho Mtakatifu wanapochagua mahubiri. Mungu anaweza kuweka dhana kwenye akili ya mhubiri ambayo inaongoza mhubiri kuhubiri juu ya mada fulani. Unapofuata Roho Mtakatifu kuamua mahubiri, weka maanani mahitaji ya washiriki. Washiriki wanahitaji faraja, onyo, au uongozi katika jambo la kitheolojia? Fikiria juu ya mambo yanayokuhusu, furaha, au utambuzi wa kipekee. Mungu ameweka nini ndani ya roho yako? Omba ili Mungu akupe maneno ya kunena. Unapochagua mahubiri au mfululizo wa mahubiri, chagua aina ya mahubiri: ya ufasiri, mahubiri ya mada, uchunguzi wa mhusika. Katika mahubiri ya ufasiri, mhubiri hueleza ukweli uliko katika vifungu vya Biblia. Katika mahubiri ya mada, mhubiri huchagua mada baadaye hueleza ukweli ulioko katika Biblia

nzima unaohusiana na mada hiyo. Katika mahubiri ya uchunguzi wa mhusika, mhubiri huchagua mhusika mmoja kutoka kwa Biblia baadaye anaeleza kuhusu mhusika huyo.

C. Mahubiri ya Ufafanuzi

Mahubiri ya Ufafanuzi yana manufaa unapowasilisha ukweli wa maandiko kwa kina kuliko mahubiri ya mada au mafunzo kuhusu mhusika. Mnenaji anapoendelea kuhubiri kutoka kwa Biblia nzima, kweli nyingi huelezwa, sio tu kweli zilizoko kwenye mada zilizoteuliwa.

1. Kuchagua Maandiko

Unapoendelea kusoma Maandiko wakati wa masomo yako ya Biblia, kuna vifungu fulani ambazo zinaathiri fikra zako. Waweza kujisikia kuwa kuna hitaji la kueleza wengine vifungu hivyo. Hii ni njia moja ya kuchagua Maandiko. Njia nyingine ya kuchagua Maandiko ni kukariri vifungu vya Biblia, na kusoma Maandiko kila siku; kisha ruhusu Mungu alete Maandiko katika akili yako. Kisha kama vile Roho Mtakatifu anavyokuongoza unene juu ya mada fulani, atakukumbusha Maandiko yanayoambatana na suala hilo. Ikiwa hautakumbuka kumbukumbu ya Maandiko, lakini unaweza kukumbuka maneno machache ya kifungu, waweza kutafuta kifungu hicho kutoka kwa mtandao. Au waweza kutazama kwa kitabu chenye maneno muhimu ya Biblia au Biblia ya mada. Njia ya tatu ya kuchagua vifungu vya Biblia ni kwa kutumia Biblia ya mada au kitabu cha maneno muhimu ya Biblia (concordance) kuangalia fungu la maneno yanayolingana na wazo fulani. Kitabu kubwa chenye maneno muhimu ya Biblia kilichofupishwa na fahirisi za mada zaweza kupatikana nyuma ya Biblia ya mafundisho. Au waweza kutembelea mtandao kutafuta Kitabu pana chenye maneno muhimu ya Biblia na fahirisi za mada.

http://www.biblegateway.com/

Kitabu chenye maneno muhimu ya Biblia na fahirisi za mada yaweza kukuongoza kwa vifungu vya Biblia. Kisha chagua vifungu jitwalia ambazo utatumia kutoa mahubiri. Mara tu unapochagua maandiko, unatakiwa kuamua mwanzo na mwisho wa kifungu au pericope. Kama neno la mwanzo wa kifungu ni neno kama vile “kwa hivyo”, kifungu hicho ni hitimisho la andiko lililotangulia. Kwa hivyo utahitaji kutambulisha kifungu kwa washiriki kwa kutoa muhtasari mfupi wa andiko lililotangulia.

Hata kama unahubiri kuhusu kifungu fulani, wakati mwingine utahitaji kuleta Maandiko ya ziada kwenye mahubiri. Wakati mwingine utahubiri kwa zaidi ya kifungu kimoja. Lakini utataka kulenga mada moja – wazo moja – kwenye mahubiri.

2. Kukuza Muhtasari na Maandiko

Wakati mwingine waweza kupata kuwa una muda mfupi kuliko unaohitaji wa kutayarisha mahubiri. Ni vyema kuweka kando muda wa kutosha wa kujifunza na kutafakari Maandiko. Watu hutoa wakati wao kuja kusikiza mahubiri. Wakati wa mahubiri ni wakati ambao unao usikivu wa kundi la watu au umati wa watu. Maneno yako wakati huo ni ya muhimu sana. Hata kama unataka kufanya utafiti wa mahubiri yako, wakati mwingine, hauna muda. Pengine ulitakiwa kufanya ibada ya wafu au uwe pamoja na mshiriki mahututi. Ni vyema ukiweza kutayarisha mahubiri kadhaa kabla, na kuyaweka kwa ajili ya wakati maalum ambao hautakuwa na nafasi ya kutayarisha mahubiri. Kuna wakati ambao ni lazima utoe mahubiri bila kupata nafasi ya kujiandaa. Njia moja ya haraka ya kukuza mahubiri ya ufasiri ni kama ifuatayo:

a. Omba uongozi wa Roho Mtakatifu.

b. Fikiria washiriki na fursa. Uliza, “Ni nini kitahubiriwa wakati kama huu?”

c. Kama hauna nafasi ya kutosha ya kujitayarisha, chagua kifungu kinachofaa ambacho unaelewa vyema.

d. Tambua muktadha. Kifungu hiki kinatoka katika kitabu gani? Nani aliyeandika Kitabu hicho? Kiini na kusudi la Kitabu ni nini? Kitabu hicho kiliandikwa lini? Kitabu hicho kiliandikiwa nani? Kitabu hicho kiliandikiwa wapi? Paulo, kwa mfano aliandika Nyaraka za Wafilipi akiwa gerezani. Kujua hayo kunatia nguvu maneno yake. “Furahini katika Bwana sikuzote. . .” (Wafilipi 4:4). Kama vile mwandishi wa habari, jiulize maswahili kuhusu kifungu” Nani? Nini? Lini? Wapi? Kwa nini? Jinsi gani?

e. Kama una muda na vifaa, somo kifungu katika zaidi ya tafsiri moja ya Biblia. Weka maanani tofauti zilizoko kwenye tafsiri tofauti.

f. Kuza muhtasari wa mahubiri. Muhtasari utafanana na fahirisi ilioko mwanzo wa kiuzi hiki. Tambua wazo muhimu la kifungu. Kwa jumla, mahubiri katika tamaduni za magharibi huwa na wazo tatu, lakini mahubiri yaweza kuwa na chini au zaidi ya hizo, kulingana na dhana zinazopatikana kwenye kifungu. Mahubiri kwenye tamaduni za

magharibi kwa kawaidia huchukua muda wa dakika 15 hadi 30. Tambua vifungu ambavyo vinahusiana na kila wazo kuu. Unapotoa mahubiri, waweza taka kusoma sehemu ya vifungu au vifungu vyote. Kama kifungu ni kifupi, waweza kusoma kabla ya mahubiri. Au unaweza kusoma vifungu vifaavyo kila unapotaja wazo kuu ya mahubiri.

g. Amua kiini cha kifungu. Kiandike chini. Utataka kuweka mkazo kwa kiini hiki. Unapotoa mahubiri, utataka kurudia kiini, labda ukitumia maneno sawa kwa ajili ya kusisitiza, au labda kwa kutaja kiini tena kwa maneno tofuati.

h. Tambua wazo la kushawishi chini ya kila wazo kuu.

i. Ikiwa una swali kuhusu maana ya Maandiko, tazama vifaa tofauti (kama vile kitabu cha maoni) kilichoorodheshwa hapo juu.

j. Fikiria juu ya kielezo kwa kila wazo. Kwa kawaida kielezo kimoja kwa kila wazo kinatosha. Vielezo hufanya msikilizaji afurahie mahubiri. Vielezo viwe vitu ambavyo washiriki wanaelewa. Vielezo ni daraja kutoka kwa Maandiko ya Biblia hadi kwa maisha ya wasikilizaji. Kwa hivyo jiweke katika nafasi ya wasikilizaji, na uchague vielezo ambavyo wataelewa. Kama itawezekana, lugha inayotumika katika mahubiri iwe mifano thabiti, sio lugha ya dhahania. Watu huelewa na hukumbuka mifano thabiti. Neno “upendo” ni dhahania. Kueleza mama akimpa busu mwanawe ni picha thabiti ya upendo. Kwa hivyo vutia hisia za asili za watu. Unapowasilisha wazo, jiulize, “Hii inakaa aje?” “Inaoja kama nini?” “Inasikikaje ikiguswa?” “Sauti yake iko aje?” “Inanusia aje?”

k. Kuza utangulizi wa mahubiri. Kwa kawaida huwana wakati wa kufikiria kuhusu kiegemeo namuktadha wa kifungu. Kumbuka kwamba washiriki hawajakuwa na wakati kama huo. Kwa hivyo unahitaji kutoa utambulisho ili kuwatayarisha kusikiza ujumbe.

l. Mwanzo kabisa wa mahubiri, ni lazima ueleze unahubiri kuhusu nini.

Ni lazima washiriki wajue kiini. Ni jambo la kuvunja moyo kusikiza kwa zaidi ya dakika chache bila kuelewa jambo ambalo mhubiri anazungumzia. Kwa hivyo mwanzo wa mahubiri, tambulisha kiini chako.

m. Haya ni mahubiri ya ufasiri, kwa hivyo mahubiri yako yaweza kupangwa katika mojawapo ya njia hizi mbili.

• Utangulizi • Ufasiri • Kutumia • Hitimisho • Utangulizi • Ufasiri: Wazo la 1 • Kutumia: Wazo la 1 • Ufasiri: Wazo 2 • Kutumia: Wazo 2 • Ufasiri: Wazo 3 • Kutumia: Wazo 3 • Hitimisho

n. Unapopanga mahubiri, uliza maswali wakati wote, “Kwa hivyo nini?” “Kutakuwa na mabadiliko gani nikitoa mahubiri haya?” Andika jibu lako. Kama hakutakuwa na mabadiliko yo yote ukihubiri mahubiri yako, basi unapoteza wakati wako. Utahitaji kurekebisha mahubiri yako au uchague kifungu kingine.

o. Buni mahubiri ambayo yataelekeza msikilizaji kufanya uamuzi. Unataka wasikilizaji wafanye nini au wafikirie nini kutokana na ujumbe,? Ikiwa kusudi la mahubiri ni kufanya uinjilisti, basi wasikilisaji wanatakiwa kuombwa wampokee Kristo kama Bwana na Mwokozi. Kama mahubiri yamekusudiwa kuwatia moyo kutoa kwa ajili ya maskini, basi msikilizaji aulizwe atoe.

p. Kuwa na ushawishi. Sihi nia ya wasikilizaji. Kiwango cha mahitaji huwapa motisha watu: wanataka chakula, mavazi na makao, na mahitaji haya ya kimsingi yakitimizwa, basi watataka mali au umaizi au mamlaka, au heshima ya kibinafsi2. Elewa ni kitu gani huwapa motisha washiriki fulani. Motisha zingine ni nzuri na zingine ni baya. Biblia hufundisha kuwa tusikimbilie mali na mamlaka , lakini tutafute ufalme wa Mungu, na mahitaji yetu yatatimizwa. Kwa hivyo twaweza kusihi motisha za watu, au kuwashawishi wabadili nia zao.

q. Kuza jinsi ya kutumia mahubiri yako kwa ukamilifu. Tazama chemsabongo DAMAMK hapo juu katika Kutumia Maandiko. Kwanza kabisa mhubiri hufunza watu Maandiko wakati wa ufasiri, na mhubiri huhubiri wakati wa kutumia Maandiko. Ikiwa wewe ni mhubiri, usisahau kuwa mkamilifu kwa kutumia Maandiko.

r. Hifadhi vidokezo vya mahubiri. Labda utahitaji kuvitumia tena wakati na mahali pengine. Labda utahitaji kuhubiri juu ya kiini kama hiki kwa washiriki hawa. Kuna mtu alisema kuwa mhubiri ni lazima ahubiri wazo mara saba ili washiriki waweza kuikubali na kuitumia. Bila shaka, ni kweli kuwa sio kila mmoja kwenye ushirika atakumbuka na kutumia kila kitu mhubiri atakachosema kwa mara ya kwanza.

s. Hubiri kwa njia mabayo ni rahisi kukumbuka. Panga fikira zako, ili uweze kuzikumbuka kwa kutumia maneno machache ya ukumbusho au bila kutumia hata kidogo. Kama hutakumbuka mahubiri, yaweza kuwa vigumu kwa msikilizaji kukumbuka yale utakayohubiri. Ni rahisi kwako na kwa msikilizaji kukumbuka kukumbuka hadithi. Yesu alitumia mithali. Tamaduni nyingi kwanza kabisa hutegemea hadithi kuwafundisha watoto wao. Hadithi huwa zimepangwa kulingana na nyakati - kitendo hufuata wakati hufaao. Waweza kuchagua maneno au fungu rahisi la maneno ili kukukumbusha mambo muhimu ya mahubiri. Kwa mfano, mambo muhimu ya mahubiri yaweza kuwa “tambaa, tembea, kimbia” au “maombi, nguvu, hubiri.” Tumia fungu la maneno ambayo watu wa tamaduni fulani watakumbuka kwa urahisi. Huko Amerika, kuna kipindi cha upelelezi kinachojulikana sana kwenye televisheni nao hutumia fungu la maneno , “Ukweli pekee, mam.”

t. Sehemu ya mwisho ya mahubiri ndiyo sehemu muhimu zaidi. Katika sehemu hii, waweza kufanya muhtasari wa yale uliyoyazungumzia, ukitilia mkazo wazo kuu au kiini cha mahubiri. Baadaye sihi washiriki waweze kufanya uamuzi.

u. Kama hauna ujuzi wa kuhubiri, inasaidia ukiandika mahubiri yako yote kabla. Hii itakusaidia usiwe na makosa mengi ya sarufi, na uweze kuchagua maneno vyema. Waweza kukagua mahubiri na kufanya marekebisho. Inakusaidia kupanga fikira zako vyema. Hata kama kumekuwa na wahubiri wanaofaa katika tamaduni zingine ambao hutoa mahubiri yao kwa kuwasomea washiriki, ni vyema zaidi usiposoma mahubiri yako. Wahubiri wengine waweza kusisitiza mambo fulani kwenye maandiko, na kutumia sehemu za maandiko zilizosisitizwa kama mwongozo wakati wa mahubiri. Kwa kawaida ni vyema zaidi kuhubiri kutoka kwa muhtasari au kuhubiri bila muhtasari. Kuhubiri bila muhtasari kunamruhusu mhubiri kutembea anapotoa mahubiri yake. Inaruhusu mhubiri kutazama

washiriki wake macho kwa macho. Kama utatumia muhtasari, waweza kuuweka ndani ya Biblia, ili uweze kufuata muhtasari huo na pia uweze kusoma Maandiko kutoka kwa Biblia.

v. Urefu wa mahubiri ni tofauti kutoka kwa tamaduni moja hadi nyingine. Usipitishe wakati ambao washiriki wako watasikiza. Washiriki wanapoacha kusikiza, unapoteza wakati wako na wao.

w. Aina nyingine ya mahubiri ya ufasiri ni kueleza kifungu baada ya kifungu. Katika aina hii ya mahubiri hautahitaji kujitayarisha saba kama vile kwa mahubiri mengine yote. Utaratibu huu unasaidia wakati unatoa mahubiri mafupi. (sermonette), au wakati una muda mfupi sana au hauna muda kabisa wa kujitayarisha. Mhubiri husoma kifungu, anaeleza kifungu na kukitumia katika maisha ya kila siku. Baadaye mhubiri anasoma kifungu kingine, anaweza kukieleza/ na kukitumia, kama vile Roho Mtakatifu anavyomwongoza. Mnenaji huongozwa na Maandiko pamoja na Roho Mtakatifu. Vifungu fulani vinafaa kwa aina hii ya ufafanuzi. Vifungu ambavyo vina wazo ambalo linajisimamia katika kifungu kimoja au viwili yafaa zaidi. Mifano ni pamoja na 1 Wakorintho 13 au Mathayo 5:1-16.

3. Mazoezi ya Kuwasilisha

Baada ya kutayarisha muhtasari wa mahubiri pamoja na Maandiko, ni vyema uweze kufanya mazoezi ya kuwasilisha mahubiri. Waweza kupitia mahubiri pamoja na rafiki. Uliza rafiki yako kama ameelewa kila wazo. Uliza rafiki akupe marekebisho anayopendekeza kwa Maandiko na katika kuwasilisha. Waweza kutoa mahubiri mbele ya kioo. Mwanzo wa kazi yake, mhubiri mmoja alikuwa akihubiria miti msituni. Kama una kamera ya kuchukua video au kinasa sauti, inasaidia kurekodi ujumbe wako, baadaye uikague. Fanya mazoezi mpaka uweze kuiwasilisha bila kutumia kumbukumbu. Lakini usijaribu kukariri mahubiri yote. Hii itakunyima uhuru wa kutoa ujumbe. Itafanya mahubiri yasikike kuwa rasmi mno badala ya kuwa inatoka kwa roho. Kariri mambo muhimu peke yake. Afadhali uwachane na mambo yasiyo ya muhimu sana unapowasilisha mahubiri badala ya kuwasilisha kila kitu kwa njia isiyosawishika, na njia rasmi mno. Wachia nafasi Roho Mtakatifu aweze kulete habari mpya kwa hotuba inapowasilishwa. Ni vyema kuweza kujianzia. Watu wengi wana hofu ya kunena mbele za watu. Vitu ambavyo husaidia kushinda uoga wa aina hii ni kama zifuatazo:

• Kuwa tayari. Fahamu yaliyo katika mahubiri. Fanya mazoezi jinsi ya kuwasilisha mahubiri.

• Kuwa mnyenyekevu lakini mkakamavu. Elewa kuwa Mungu amekuita uhubiri, na atakupa kila kitu unachohitaji ili utii mwito.

• Usiige mtu mwingine. Nena kutoka kwa roho yako. Waweza kutumia mbinu kutoka kwa wanenaji wengine maarufu, lakini wewe si nakili wa mnenaji mwingine.

• Tumia vielezo vinavyopendeza na lugha thabiti katika mahubiri yako yote. Wasikilizaji wakiwa wasikivu wakati wa mahubiri, utakuwa na uhakika katika kuwasilisha mahubiri.

4. Kuwasilisha na Maoni

Unapowasilisha ujumbe wako kwa washiriki, ongea kwa sauti ili walio katika viti vya nyuma waweze kusikia. Njia moja ya kuwa na uhakika ni kutazama mtu mmoja aliye nyuma kabisa , na kuongea kama vile unazungumza naye. Badili sauti na mwendo wa hotuba yako, unaposisitiza mambo muhimu. Tua kwa muda kwa wakati ufaao, ili uwape watu nafasi ya kufikiria kuhusu wazo muhimu. Unapotua kwa muda , endelea kutazama wasikilizaji, ukitarajia wafikirie kuhusu yale ambayo umesema. Kuwa na msisimko kuhusu yale unayosema! Kama utaonyesha shauku, wasikilizaji wako watakuwa na shauku. Tumia uhai. Tumia mikono jitwalia. Onyesha washiriki heshima na upendo. Tarajia mema kutoka kwao. Onyesha upendo huu katika hotuba yako na uonyeshe kwa uso wako. Kwa kawaida anza mahubiri kwa tabasamu.

Kuna nyakati ni lazima uonye washiriki kutoka kwa dhambi au kosa. Kuna wakati pia utahitaji kuwatia moyo wale wanaoumia. Kuna msemo unaosema kuwa mhubiri “huumiza walio starehe, na kufariji walioumia.”

Tumia vielelezo jitwalia. Wakati mwingine manabii katika Biblia walieleza jambo kwa kuigiza kisa au kwa kutumia chombo kueleza ujumbe wao. Mbinu hii inafaa hasa wakati unaponena na watoto.

Pata maoni. Waweza kuchagua watu wachache unaoamini na walio na maarifa mkutane nao baada ya kutoa mahubiri ili wakueleze sehemu walizohisi kuwa na nguvu na sehemu dhaifu za mahubiri yako. Kama umeoa, mwenzako anaweza kukupa maoni.

D. Mahubiri ya Mada

Mahubiri ya ufasiri yanajishughulisha na kweli tofauti zinazopatikana katika Maandiko ya Biblia, bali mahubiri ya mada hujishughulisha na mada fulani. Hatua zinazohusika katika kutayarisha mahubiri ya mada ni kama zifuatazo:

1. Kwa maombi chagua mada.

2. Tumia Biblia ya Mada au muhtasari wa mada na kitabu cha maneno

muhimu ya Biblia ili uweze kupata Maandiko yanayoambatana na mada.

3. Kama kuna marejeo mengi juu ya mada hiyo, utahitaji kupunguza mada yako. Kwa mfano, badala ya kuhubiri kuhusu dhambi kwa jumla, unaweza kupunguza mada yako ili iseme, “dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu.” Marejeo ya Biblia yaliyo katika wavuti ilioko hapo juu yaweza kukusaidia kupunguza uchunguzi wako.

4. Somo marejeo yote yanayohusu mada yako, ukiyaangalia kulingana na muktadha.

5. Weka marejeo chini ya mambo machache muhimu ambayo unataka kusisitiza kwenye mahubiri yako.

6. Kutoka kwa kweli utakazowasilisha, amua kiini cha mahubiri yako.

7. Kuza mahubiri mengineyo kama vile ungekuza mahubiri ya ufasiri. Tayarisha utangulizi, wazo la kushawishi, vielezo, hitimisho n.k.

8. Ili kupunguza makosa, pata maoni kutoka kwa Wakristo wenye maarifa kabla ya kuwasilisha mahubiri.

E. Kuchunguza Mhusika

Kuchunguza mhusika au mahubiri yanayoeleza maisha ya mtu ni ufasiri wa maisha ya baadhi ya wahusika katika Biblia. Hatua zinazohusika katika kutayarisha mahubiri haya ni kama zifuatazo:

1. Chagua mhusika wa Kibiblia kwa maombi.

2. Kwa kutumia Biblia ya mada na upatanifu, tafuta marejeo yote ya mhusika huyo. Panga haya kulingana na mfululizo wa nyakati.

3. Soma marejeo ya Maandiko katika muktadha wake.

4. Tafuta maoni kutoka kwa ensaiklopidia ya Biblia, Kamusi ya Biblia, au maelezo ya Biblia kwa habari zaidi kuhusu mhusika katika Biblia. Vifaa katika wavuti vinapatikana hapo juu.

5. Orodhesha matukio makuu katika maisha ya mhusika.

6. Orodhesha mafunzo yaliyofunzwa kupitia kwa maisha ya mhusika.

7. Unaweza kutaka kumwonyesha mhusika kama mtu wa kwanza. Hiyo ni,

unaweza taka kuongea ni kama wewe ndiye Abrahamu au Mariamu (Mama ya Yesu) au mhusika mwingine.

8. Unaweza taka kuonyesha mhusika kama mtu wa tatu.

9. Unapofuatilia maisha ya mhusika, kulingana na mfululizo wa nyakati, inakuwa rahisi kukumbuka mawazo makuu ya mahubiri.

10. Kumbuka kumwonyesha mhusika kwa njia ambayo wasikilizaji watajifunza na kutumia kweli za Kiroho. Kwa mfano, mhusika wa Kibiblia anaweza onyeshwa kuwa mwenye furaha kwa kumtii Mungu au mwenye huzuni kwa kutomtii Mungu.

2Tazama Abraham Maslow’s vyeo vya mahitaji: http://en.wikipedia.org/wiki/Maslow's_hierarchy_of_needs

3Kenson Kuba, “Vitabu vya bure vya Mafunzo ya Uanafunzi,” Kitabu cha mafunzo ya Uanafunzi cha 3, Ukurasa 21 katika mtandao. http://biblestudycd.com/books/book3.pdf

RUDI KWA MUHTASARI

KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

V. Kufundisha

A. Utangulizi

Kanuni nyingi zinazotumika katika hermeneutics pia hutumika katika mafundisho. Kama kuhubiri kunaweza tofautishwa na kufundisha, kwa kawaida kuhubiri kunahimiza kumsihi msikilizaji kufanya uamuzi wakati huo, lakini kufundisha kunahimiza kumjulisha mshiriki ili afanye uamuzi mwafaka baadaye. Msingi wa kufundisha ni uhusiano kati ya mwalimu na wanafunzi. Tunawafunza watu, sio masomo. Wanafunzi wanaompenda mwalimu, wana uwezekano mkubwa wa kujifunza kutoka kwa mwalimu kuliko wanafunzi ambao hawampendi mwalimu. Mbinu za kufundisha hutofautiana kulingana na umri ya wahusika, ukubwa wa kundi, na maarifa ya washiriki. Watu wazima hujifunza vyema wanapohusika katika majadiliano. Kwa hivyo kama kuna walimu wa kutosha, ni vyema kuwafunza watu wazima katika makundi ya watu sio zaidi ya kumi na mbili. Majadiliano kwa kawaida hufanyika katika makundi madogo, lakini mhadhara hutumika vyema kwa makundi makubwa. Kama hakuna walimu wa kutosha wa kufunza makundi madogo, mwalimu anaweza kuwagawanya watu wazima katika makundi madogo ili wajadiliane yale yaliyowasilishwa kwa kundi nzima. Watu wazima wanapokomaa katika imani na maarifa ya Kibiblia, majadiliano zaidi hufanyika na mhadhara hufanyika kwa uchache. Mhadhara unawafaa watoto. Ni wazi kuwa watoto wana usikivu mfupi kuliko watu wazima. Kwa hivyo vitendo vinahitajika kwa watoto. Walimu wanaweza kuwasimulia hadithi. Masomo ya vielezo yanafana kwa watoto wadogo. Mwalimu anaweza kuwaonyesha watoto baadhi ya vifaa kama kijiti, na awaelezee ya kwamba wachungaji hutumia vijiti kuwaongoza kondoo. Mwalimu anaweza kuwaeleza ya kwamba Mungu anatuongoza. Anaweza kutuongoza katika njia ifaayo. Watu wanapokutana kujifunza Biblia, kunafaa kuwa na ushirika na maombi. Kwa hivyo mikutano inaweza anza kwa watu kushiriki shangwe na mahitaji yao. Kama watu katika makundi hawajuani, mwalimu anaweza kuhimiza majadiliano. Mwalimu anaweza kuufungua mkutano kwa kuuliza jambo lisilohusika na funzo la Kibiblia. Mifano ya kuanzisha mazungumzo ni kama ifuatavyo: “Kila mmoja wenu anaweza kutwambia jina lake na jambo linalo kuhusu ambalo hatufahamu?” “Kama ungependa doto yako itimike, doto yako yaweza kuwa gani?”

Washiriki wakiendelea kujuana, hautahitaji kuuliza maswali ya kuanzisha mazungumzo. Badala yake, mwalimu atawauliza kwa kawaida washiriki waweze kushiriki mambo yale yametendeka katika maisha yao katika wiki moja iliyopita. Na watu wanaweza kuuliza maombi. Watu katika kanisa wanatakiwa kuwa kama familia. Mtu akiwa mgonjwa, watu walio katika kundi la kujifunza Biblia wanatakiwa kumtembelea. Ikiwa washiriki wana mahitaji, washiriki wa kundi dogo mara nyingi watajua mahitaji hayo. Ili kudumisha uhai wa washiriki kanisani, na kusaidia kuanzisha ushirika na kukua kiroho, washiriki ni lazima wawe sehemu ya kundi dogo katika mwili wa kanisa.

B. Somo

Kama vile mahubiri, somo la Biblia laweza kuwa la ufasiri, la mada au kuchunguza mhusika.

1. Ufasiri

Somo la ufasiri laweza kuwa la kiini au kifungu kwa kifungu.

a. Kiini

Kanuni nyingi za mahubiri hutumika kwa kutayarisha somo la ufasiri wa kiini. Lakini katika mazingira ya kufunza, washiriki wanaweza kuzungumza na mnenaji na mmoja kwa mwingine. Somo laweza kuwa ndefu kuliko mahubiri.

b. Kifungu kwa Kifungu

Somo la ufasiri wa kifungu kwa kifungu lafaa katika mafundisho kuliko kuhubiri. Kila mmoja wa kundi la mafundisho aweza kuuliza maswali na kuchangia kuhusu vifungu hivyo. Hii huwafanya washiriki kuwa wasikivu na kuhusika katika somo.

2. Mada

Somo la mada huruhusu wanafunzi kujifunza yale ambayo yanahusu kundi hilo. Kwa mfano, kanisa laweza kuamua kufunza washiriki wote wapya theolojia ya msingi. Kwa hivyo somo la mada laweza kutolewa kwa suala kama Utatu Mtakatifu, Kuanguka kwa Mwanadamu, Mafundisho ya Wokovu. Kanuni nyingi sawa na zile zinazotumika katika kutayarisha mahubiri ya mada hutumika kwa kutayarisha masomo ya mada.

3. Kuchunguza Mhusika

Kuchunguza mhusika humruhusu mwalimu kuzoeza washiriki somo. Kwa mfano, mwalimu anaweza kuchunguza wahusika wa kike katika Biblia kwa ajili ya darasa la wanawake.

RUDI KWA MUHTASARI

KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

VI. Habari za Zaidi

Kwa habari za zaidi kuhusu Kujifunza Biblia, Kuhubiri na Kufunza, tazama wavuti ufuatao. Elekeza kwa “Vitabu vya Kujifunza Uanafunzi vya Bure” na uchague Kitabu cha Mafunzo ya Uanafunzi cha 3.

http://biblestudycd.com/

Shule ya Biblia ya Ames inatoa kitabu cha kurasa 259- cha bure kwenye mtandao ambacho kinapeana kanuni za kujifunza Biblia. Tazama “Mitindo bunifu za Kujifunza Biblia” katika wavuti ufuatao.

http://www.amesbible.org/download.html

Elekeza kwa “Wavuti wenye majina ya Masomo ya Biblia” kwa habari muhimu kuhusu hermeneutics na mada nyinginezo katika wavuti ufuatao.

http://www.bible-researcher.com/ Huduma za RBC hutoa mafunzo ya Biblia na Kuishi kwa Mkristo. Ili kujiandikisha lazima mwanafunzi awe na anwani ya imeli na awe na namba ya siri. Enda kwa kiunganishi kifuatacho.

http://cc.christiancourses.com/ Wavuti ufuatao unatoa habari kuhusu kujifunza Biblia. Elekeza kwa “Wavuti wenye majina ya Masomo ya Biblia” arafu uelekeze kwa “hermeneutics.”

http://www.bible-researcher.com/

Ifuatayo ni injini ya kutafuta kwenye mtandao wavuti za Kikristo. Ungependa kuchunguza kutoka kwa wavuti huu kuhusu wavuti zinginezo ambazo zaweza kukusaidia katika huduma yako.

http://www.crosssearch.com/

Kwa mfano, wavuti ulioko hapo juu unatupa kiunganishi kifuatacho, ambao unatoa Mafunzo ya Bure ya Biblia kwa Mtandao kwa watoto.

http://www.ebibleteacher.com/index.html

RUDI KWA MUHTASARI

KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

VII. Kazi ya Ziada

A. Hubiri Mahubiri mawili

Kama unaweza kuipanga, ni lazima uhubiri mahubiri mawili ili kumaliza darasa hili.

B. Ongoza Madara Mawili

Kama unaweza kuipanga, ni lazima ufunze vipindi viwili katika kundi dogo ili kumaliza darasa hili.

RUDI KWA MUHTASARI