27
Manusura Nakala Maalum SWAHILI: SURVIVORS-SE

Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

  • Upload
    others

  • View
    9

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

ManusuraNakala MaalumSWAHILI: SURVIVORS-SE

Page 2: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

1

Haujambo, Nusura!

Kitabu hiki ni chako pekee. Kimejaa mawazo ya kuwaza

na mambo ya kufanya. Kitakusaidia kupona na kukua.

Janga hili la ugonjwa wa Covid-19 limeathiri watu wote kwa njia tofauti.Hivyo kitabu chako kitakuwa tofauti

na vitabu vya watu wengine wote. Ni kitabu chako binafsi!

Jina langu ni

Mimi ni Nusura

Page 3: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

2 3

Kuishi kwa Usalama

Unaweza kujihisi una wasiwasi au unaogopa. Hivyo ni sawa.

Manusura wakati mwingine huogopa.Kuna mambo mengi ya ajabu

katika dunia hii kubwa na pana. Lakini pia kuna mambo ya kuogofya.

Mafuriko ya maji, vita, ajali za gari na sasa kuna janga hili la ugonjwa

unaoenea kwa kasi ulimwenguni kote.

Andika mambo machache yanayokupa wasiwasi kuhusu janga hili la ugonjwa

wa Covid-19 hapa chini.

Page 4: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

4 5

“Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa! Ningeruka niende mbali kupumzika.

Ningalitorokea mbali sana na kukaa jangwani;

ningaliharakisha kwenda mahali pa salama, mbali na tufani kali na dhoruba.”

Mwandishi mmoja alikuwa na uoga sana alipoelezea matamanio haya:

– Zaburi 55:6-8

Page 5: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

6 7

Je, ushawahi kuwa na matamanio kama hayo?Je, unatamani nini unapoogopa?

Ninapoogopa, ninatamani ...

Andika au uchore matamanio yako

hapa chini.

Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote.

Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi

wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu. Kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi ndani

ya maisha yetu, hivyo ndivyo faraja yetu inavyofurika kwa njia ya Kristo.

2 Wakorintho 1:3-5

Page 6: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

8 9

Mawaidha kwa Manusura

Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako pa salama.

Chukua Hatua!

Tunga wimbo. Nyimbo ni bora sana za

kusaidia watu kuacha kuhisi uoga.

Hapa kuna wimbo kutoka kwa Biblia:

Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani?

Bwana ni ngome ya uzima wangu, nimhofu nani?

Zaburi 27:1

Nawa mikono yako mara kwa mara kwa maji na sabuni;

Usisimame karibu sana na watu wengine;

Jaribu sana usijiguse macho, mapua na mdomo;

Ukihisi kuwa na homa, kukohoakohoa, au una shida kupumua, waulize wazazi au walinzi wako kuongea na daktari.

Cheza michezo kwenu nyumbani badala ya kwenda kucheza na marafiki.

Jikinge kutokana na virusi vya Covid-19 kwa njia hizi:

Page 7: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

10 11

Kuomba Msaada

Unaweza kuhisi kuzidiwa na mambo.Hivyo ni sawa.

Manusura wanahitaji msaada wakati mwingine.

Inaweza kukatisha tamaa wakati hauwezi kwenda nje au hauna yeyote wa kucheza naye.

Unaweza kuhisi kuchoka au kuhuzunika. Inaweza kuwa vigumu kuelezea unavyohisi.

Inaweza kuwa vigumu kupokea msaada kutoka kwa watu.

Watu walio maishani mwako wanataka kukusaidia. Lakini hawatajua jinsi ya kukusadia usipowaambia unachohitaji,

hivyo ... WAAMBIE!

Page 8: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

12 13

“Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba:“ ‘Baba yetu uliye mbinguni,

Jina lako litukuzwe. Ufalme wako uje.

Mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.

Utupatie riziki yetu ya kila siku. Utusamehe deni zetu,

kama sisi nasi tulivyokwisha kuwasamehe wadeni wetu.

Usitutie majaribuni, bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu.’ ”

Mathayo 6:9-13

Alisema hivi:

Mwombe Mungu kile unachohitaji!

Yesu alitufundisha jinsi ya kuomba msaada kwa Mungu.

Page 9: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

14 15

Tunaweza kumwomba Mungu msaada wakati wote.

Lifanye ombi lililo ukurasa ufuatao kuwa lako kwa kujaza maneno yako.

Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu, moyo wangu umemtumaini yeye,

nami nimesaidiwa. Moyo wangu unarukaruka kwa furaha

nami nitamshukuru kwa wimbo.

Zaburi 28:7

Mungu, ahsante kwa kunipenda sana.

Leo najihisi hivi:

kwa sababu ya:

Nahitaji msaada wako. Tafadhali:

Asante kwa yafuatayo:

Page 10: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

16 17

Mawaidha kwa Manusura

Wafahamishe watu mambo unayohitaji. Wafahamishe jinsi wanavyoweza kukusaidia.

Fanya ombi lako binafsi. Muulize Mungu kukulinda wewe na jamaa wako. Mshukuru kwa kukulinda.

Kuwa msaidizi.Angalia kama kuna mtu anayehitaji msaada.Unaweza kusaidia katika kazi za nyumbani

kama kusafisha nyumba au kuosha vyombo. Mtu huhisi vizuri anaposaidia!

Kumbuka unaweza kuomba msaada unapohitaji.

Chukua Hatua!

Page 11: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

18 19

Zaburi 10:14

Kuhisi Faraja Unaweza kuhisi huzuni. Hivyo ni sawa.Manusura wakati mwingine wanahuzunika.

Unaweza kuhisi kumkosa mtu aliyefariki.Unaweza kufikiria sana kuhusu mambo yalivyokuwa mbeleni.

Unaweza kuwa hautambui unahisi aje hasa.

... wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni,

umekubali kuyapokea mkononi mwako.

Page 12: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

20 21

Heri wale wanaohuzunika, maana hao watafarijiwa.

Heri walio wapole, maana hao watairithi nchi.

Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watatoshelezwa.

Heri wenye huruma, maana hao watapata rehema.

Heri walio na moyo safi, maana hao watamwona Mungu.

Heri walio wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu. Heri wanaoteswa kwa sababu ya haki, maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.

Mathayo 5:4-10

Yesu alisema,

Page 13: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

22 23

Je, ni mambo gani unapenda kuyafanya?

Je, unapenda kukimbia kasi sana?Je, unapenda kutafuta wadudu wa aina mbalimbali?

Je, unapenda kuchora picha?

Tengeneza orodha ya Mambo Muhimu ya KufanyaAndika mambo unayopenda kuyafanya hapa.

Mambo Muhimu ya Kufanya

Page 14: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

24 25

Mawaidha kwa Manusura

Mwambie mtu anayekupenda jinsi unavyohisi. Ni msaada kwako kuelezea mawazo yako na hisia zako.

Mwambie Mungu kuhusu huzuni yako.Mwombe akufariji moyoni. Tazamia baraka.

Fanya jambo moja katika orodha yako ya Mambo Muhimu ya Kufanya.

Chukua Hatua!

Tengeneza Kijisanduku cha Hisia

Tafuta kijisanduku kama katoni.

Rembesha kijisanduku kwa rangi au kalamu au chochote kitakachokifanya kionekane spesheli.

Jaza kijisanduku na vitu vinavyokufurahisha. Vinaweza kuwa vijibarua au vitu vinavyokukumbusha kuhusu mambo mazuri yanayotendeka kila siku.

Unapohuzunika, toa kijisanduku chako cha hisia na ujifurahishe kwa vitu vilivyomo.

Page 15: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

26 27

Kuachilia

Waweza kuhisi hasira.Hivyo ni sawa.Manusura huhisi hasira wakati mwingine.

Waweza kuona kama maisha hayana haki.Unaweza kukasirika kwa kutoweza kwenda nje.

Unaweza kutamani mambo yawe tofauti.

Unaweza kuchora picha ya uso ulio na hasira kama unahisi hasira.

HRRR!

Page 16: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

28 29

Ni sawa kukasirika, lakini ni bora zaidi kuachilia hasira.

Mara nyingi tunahitaji kumsamehe mwenzetu kwa

jambo alilotenda likatuumiza.

Kwa hiyo, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao sana, jivikeni moyo wa huruma,

utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. Vumilianeni na kusameheana mtu akiwa

na lalamiko lolote dhidi ya mwenzake. Sameheaneni kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi.

Wakolosai 3:12-13

Basi ndipo tutaweza kuachilia hasira zetu.

Kuishi vile Mungu anapenda ni kuwa na uwezo wa kuwasamehe watu na kuachilia hasira yako.

Page 17: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

30 31

Wakati mwingine, unataka kupiga mayowe kwa sauti

kubwa ili umalize hasira yako.

Tengeneza mrija wa kupigia mayowe.

2. Weka mdomo wako kwa mwisho mmoja wa mrija.3. Weka mkono wako juu ya mwisho mwingine wa mrija.4. Vuta pumzi ndani kabisa.5. Piga mayowe kwa muda na kwa sauti kubwa uwezavyo.

1. Kunja kitabu hiki au kingine kwa namna hii:

Page 18: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

32 33

Mawaidha kwa ManusuraWasamehe watu. Mwombe Mungu akupeuwezo wa kuwasamehe watu waliokukosea.

Zungumza na mtu mzima unayeweza kumwamini jinsi unavyoweza kuthibiti hasira yako.

Achana na hasira. Tumia mrija wako wa kupigia mayowe.

Chukua Hatua!Namna rahisi za kuepuka hasira isiyofaa.Jifanye kuwa mtu huyo mwingine. Nini kinabadilika unapotazama mambo kwa mtazamo wa mtu mwingine?

Unapokasirika, vuta pumzi tatu kwa nguvu kabla ya kufanya lolote.

Lala usingizi wa kutosha.

Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua lisichwe mkiwa

bado mmekasirika.

Waefeso 4:26

Nenda Usameheane!

Page 19: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

34 35

Kupata Njia ya Mawasiliano

Unaweza kuhisi upweke.Hivyo ni sawa.Manusura wakati mwingine huhisi upweke.

Unaweza kuhisi kama dunia ni kubwa nawe u mdogo sana sana.

Unaweza kuwa unamkosa mtu unayempenda. Unaweza kuwa mbali na rafiki zako au jamaa wako.

Ikiwa kuna mtu unamkosa, andika jina lake hapa.

Andika jina lake kwa mfano ambao unakukumbusha mtu huyo.

Unaweza kuliandikwa lirembeke, au liwe la kipekeeau liwe KUBWA KABISA au dogo sana.

Page 20: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

36 37

Baba wa yatima, mtetezi wa wajane,ni Mungu katika

makao yake matakatifu.Mungu huwaweka

wapweke katika jamaa,huwaongoza wafungwa wakiimba,bali waasi huishi katika nchi kame.

Tangu pale mwanzo kabisa wa ulimwengu, Mungu alisema kwamba si vyema

kwetu kuwa pekee.

Kuwa rafiki!

Zaburi 68:5-6

Ili kuishi maisha mema, kunahitajika jamii nzima.

Page 21: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

38 39

Ikiwa unahisi upweke, wasiliana na watu walio karibu nawe.

Kuwa mbunifu sana!

Njia nzuri sana ya kuwasiliana na watu ni kuwaandikia barua.

Barua utakayoandika itakuwa njia ya kuwasiliana na mtu fulani.

Unaweza kuandika barua ya shukrani, barua ya kutia mtu moyo,

barua ya kumweleza umemkosa,

au barua ya jambo lingine lolote upendalo.

Page 22: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

40 41

Mawaidha kwa ManusuraTazama walio karibu nawe, na umshukuru Mungu kwa ajili ya watu wa ajabu unaoishi nao.

Jaribu kuwasiliana na mtu fulani kwa kuandika kijibarua.

Chukua Hatua!

Jifundishe kuwapenda wale walio karibu nawe kwa upendo ulio kama hivi:

Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni wivu, hauna majivuno, hauna kiburi. Haukosi kuwa na adabu,

hautafuti mambo yake, haukasiriki upesi, hauweki kumbukumbu ya mabaya.

Upendo haufurahii mabaya bali hufurahi pamoja na kweli.

Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.

Upendo haushindwi kamwe.1 Wakorintho 13:4-8

Page 23: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

42 43

Wakati Janga Hili Litaisha Mungu kwetu sisi ni kimbilio

na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.Kwa hiyo hatutaogopa,

hata kama dunia ikiondolewanayo milima ikiangukia

moyoni mwa bahari.Hata kama maji yake

yatanguruma na kuumuka,milima nayo ikitetemeka

kwa mawimbi yake.Zaburi 46:1-3

Haujui janga hili litaendelea kwa muda gani.Lakini unaweza kumtegemea

Mungu atakupitisha. Kwa wakati huu, unaweza kuanza kupanga unachotaka

kufanya litakapopita! Andika orodha ya mambo unayotaka kufanya hapa:

Page 24: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

44 45

Biblia inatuambia:

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee,

ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Yohana 3:16

Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu baada

ya siku tatu, na Yesu bado yuko hai leo!

Isaya 53:4

Yesu anataka umwamini na umpe maisha yako ili uweze kuwa naye milele. Ikiwa uko tayari

kumpa Yesu moyo wako, omba ombi hili:

Bwana Yesu,

nafahamu kwamba unanipenda, na ulikufa msalabani kwa ajili yangu.

Naomba msamaha kwa mambo yale mabaya niliyoyatenda.

Kutoka leo nataka kuishi kwa ajili yako.

Tawala maisha yangu ninapojifunza kukutumaini na kukufuata.

Ahsante kwa kuwa Mwokozi wangu!

Amen.

Hakika alichukua udhaifu wetuna akajitwika huzuni zetu...

Page 25: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

46 47

Page 26: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

48

Page 27: Manusura - Biblicadownloads.biblica.com/free-resources/Swahili/Swahili... · 2020. 7. 7. · Omba. Unaweza kuzungumza na Mungu wakati wowote unapoogopa. Yeye anaweza kuwa mahali pako

ManusuraTM Nakala Maalum Hakimiliki © 2020 na Biblica, Inc.

Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.

The SurvivorsTM Special Edition (Swahili)Copyright © 2020 by Biblica, Inc. All rights reserved worldwide.

Maandiko ya Biblia yamenakiliwa kutoka kwaNeno: Biblia TakatifuTM

Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 na Biblica, Inc.Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.

ISBN: 978-1-62337-391-7