62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ______________________________________________________ _______ Kongamano la Jubilei ya Miaka 75 ya TUKI Tarehe 4 – 7 Julai, 2005 METHALI ZA KIUTANDAWAZI 1 / 62

METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili

­­­_____________________________________________________________

Kongamano la Jubilei ya Miaka 75 ya TUKI

Tarehe 4 – 7 Julai, 2005

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1 / 62

Page 2: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

John P. MbondeUtangulizi

Katika kuziainisha methali, watu hupenda kuziita kuwa hizi ni zaasili ya jamii fulani kama vile ya Kihispania na zile ni za Kiafrikaau hizi ni za Kimaasai na hizo ni za Kingoni n.k. Aina hii yamethali, jamii huzidai kuwa ni za asili ya jamii yake (kabilafulani), na hivyo, huzifanya kuwa ni mali yake kiutamadunikama zilivyo mila na desturi tofauti mbalimbali katika jamii hiyohusika. Kumbe kati ya methali hizo zote, baadhi yake hutumikamahali pote duniani. Aina hii ya methali zitumikazo mahali pengiduniani, ingawa huundwa katika lugha tofauti mbalimbali nawakati mwingine kwa mipangilio yake ya maneno hutofautiana,lakini maana yake huwa ni ileile.

Ni kwa mantiki hiyo, nimeamua kuziita Methali za Kiutandawazi.Nafahamu pia kwamba baadhi ya wanataaluma wangependakuziita ni Methali za Kimataifa. Jina lolote linaloweza kutumika kuainisha methali hizo, halinautata wala mjadala kwa kuwa zinatumika miongoni mwamataifa mengi duniani kote. Kamwe methali hizo siyo mpyawala za ajabu wala hazina hadhi ya milenia ya tatu kwamaumbile, bali ni zilezile ambazo zimezoeleka katika matumiziya kila siku. Ila inawezekana kwamba zinaweza kuwa za asiliya jamii fulani zilizoanza kuzitumia, au hupendelea kuzitumiamara nyingi zaidi kuliko jamii nyingine kwa msukumo wa

2 / 62

Page 3: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

mazingira. Kwa mfano, lugha ya Kispanishi ina utajiri mkubwasana wa methali kuliko lugha nyingi duniani. Hali kadhalika,Kichina kimefaulu kuhifadhi methali zake kwa wingi tangu karnena karne.

Madhumuni ya kuzikusanya na kuzihifadhi pamoja nikurahisisha upatikanaji wake. Fauko ya hayo, huu ni wakatimuafaka wa kuzijengea uhalali na hadhi yakinifu methali zakiutandawazi ili kwenda sambamba na maendeleo endelevu yakisayansi na kiteknolojia. Ifahamike wazi kuwa bado suala hilolinahitaji kufanyiwa tafiti za kina kirefu ili kuboresha dhana hiyo.

Mwenendo wa methali za kiutandawazi hautofautiani na ule wamethali za kawaida. Ni dhahiri kuwa baadhi ya vigezo vyakubainisha methali za kiutandawazi ni ile tabia ya taswira zakimataifa zilizobebwa nazo. Baadhi ya methali huhusishwa navitu vya eneo dogo la nchi, lakini zile za kiutandawazi hazinamipaka. Kwa mfano, Waarabu wa Pemba hujuana kwavilemba. Pemba ni kisiwa katika bahari yaHindi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilemba nivitambaa wafungazo vichwani. Tabia ya kufunga vilemba vyaaina hiyo, hujitokeza huko Pemba miongoni mwa Waarabukatika mashamba ya karafuu. Ingawa maana ya ndani yamethali hii yaweza kabisa kuwa ya kimataifa, yaani yakiutandawazi. Mathalani, wazungu watawapendelea wazunguwenzao. Ufinyu wa methali za mahali ni sawa na jinsi aina

3 / 62

Page 4: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

fulani za mila hutawala jamii ndogo ya mahali hapo tu. Kumbemethali Wapiganapo tembo, nyasihuumia (When elephants fight, the reeds get hurt), hii ni methali ya kiutandawazi.

Kwa upande mwingine, baadhi ya methali huwa hazitumiki kilasiku, katika ufinyu au utandawazi wake, badala yake huwazimebaki katika vitabu tu. Ukweli ni kwamba hata baadhi yamisamiati katika kamusi za aina zote za lugha, hubaki katikavitabu kwani matumizi yake ni ya nadra mno kwa sababu aubila sababu za kimsingi. Na kila zinapotumika husikika kuwa ningeni katika masikio ya wasikilizaji wake. Hata nchini Tanzaniaambako ni chimbuko la historia ya Kiswahili, hususan Zanzibar,kwa namna moja au nyingine, Waswahili hao, si hoja kama niwasomi au watu wa kawaida, wanaposikia mtu akitumiamsamiati au istilahi iwayo utawasikia wakishutumu, “Kiswahilicha siku hizi ni kigumu, jamani! Afadhali ya Kiingereza.” Vivyohivyo, iwapo Mwiingereza msomi akitumia misamiatiisiyotumika katika maisha ya kila siku ya jamii ya Waingereza,wanaposikia hayo hulaani na kusema, “Kiingereza cha wasomiwa siku hizi ni kigumu (bombastic).

4 / 62

Page 5: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Nini maana ya methali?

Methali ni lugha nyepesi ipenyayo moja kwa moja katika mioyoya wasikilizaji. Aidha, methali au misemo huondoa wingu auukungu katika mawasiliano ya kisayansi na ya teknolojia nzitoza kitaaluma. Pia, methali ni kielelezo cha utashi wa uhai wajamii husika, historia na falsafa ya utu wa binadamu, hekima nabusara. Mwanafasihi mashuhuri katika Afrika, Chinua Achebe,katika kitabu chake Things Fall Apart (1959: 7) anaandika, “Methali ni mafuta ya mawese ambayo kwayo maneno huliwa.”Kauli hii ikizingatiwa barabara huyafanya maandishi kukubalikakuwa ni fasihi, maana matumizi ya methali na fani nyinginehukoleza simulizi kama tui la nazi na viungo mbalimbali kamavile vitunguu, nyanya, zinavyoifanya mboga iwe na riha naladha tamu zaidi. Methali ni njia ya mkato ya kuelimisha,kuadilisha, kukosoa na kuelekeza jamii, husuan vijana katikakuzingatia tunu za jadi kwa kina ndani ya mazingira ya asili yajamii.

5 / 62

Page 6: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

“Methali ni aina ya usemi nzito na ambao unakusudiwakusema jambo maalumu lakini ya fumbo. Usemi huumzito mara nyingi hukusudiwa kumuonya, kumuongoza,na kumuadilisha mwanadamu. Kwa umbile la nje methalihuwa na muundo maalumu, muundo wenye baadhi(pande) mbili. Upande mmoja wa methali huwa unaelezamazoea au tabia ya mtu au kitu juu ya utendaji wa jambo;na upande wa pili unaeleza matokeo yatokanayo namazoea hayo au tabia hiyo ambayo imeelezwa katikaupande wa kwanza.” (S. Y. A. Ngole na Lucas N.Honero, Fasihi- Simulizi Methali: Kitabu cha pili, (uk viii)TUKI, DUP 1981.

Lugha ya Kiswahili ni tajiri sana kwa semi zake. Licha yamethali, kuna misemo, misimu, nahau. Tofauti na methalimisemo ni tungo zitumiazo picha, ishara na tamathali kuelezakitu au wazo kwa kifupi, ili litolewe maadili au maonyo au sifafulani. Kumbe vitendawili ni semi fupifupi za fumbo zenyekutumia picha, tamathali na ishara kueleza wazo lililofichikaambalo ndilo jawabu la fumbo. Kwa mfano, Koti la mzeehalikosi chawa.

6 / 62

Page 7: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Na kwa upande wa misimu ni semi ndogondogo za kuibuka nakufifia au kufa kabisa ambazo huzushwa katika mazingirafulani, hufa baada ya mazingira yale kutoweka. Kwa mfano, Klabu ya Simba ilishinda kwa kishindo cha tsunami.(This coinagewas heard by the author while travelling in Dar es Salaamcomuters known as “Daladala” hence I personally call suchsayings as “Daladala Philosophy” which associate withcontemporary events such as ‘tsunami’ impact in which Simbasoccer club beat their long time rival, the Younger soccer clubwith such impact as that of tsunami). Pia, matumizi yamsimu, k.m. Mambo! Poa!Huu ni msimu uliochipua na kuchanua miaka hii ya karibuni,ambao nao siku itafika utanyauka na kufa. Hata Rais waawamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Benjamin William Mkapa ameondokea kuupendana kuutumia mara nyingi sana anaposalimiana na wananchikabla ya kuzungumza au kuwahutubia. Akisha sema, “Mambo!”Hadhira humkubalia kwa mkupuo mmoja, “Poa!”

“Methali hutupa maarifa;

hutupa ukweli kwa kifupi;

7 / 62

Page 8: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

hufanana katika lugha mbalimbali za nchi kadha zaulimwenguni;

hutumika hasa na wazee kufundisha vijana na watoto,hali ya maisha duniani.” Kutoka katika Utangulizi wakitabu 500 Haya Proverbs kilichotungwa na Nestor, H.Byera, EALB (1978).

Aidha, kuna ufafanuzi wa aina mbalimbali kutoka kwawanataaluma wa nyakati mbalimbali kuhusu dhana “methali”.Katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu 1981: 165 “Methali ni kifungucha maneno yanayotumiwa pamoja kisanii kwa njia ya kufumbaau kupigia mfano na ambacho kinachukua maana ndefu napana kuliko maneno yenyewe yanayotumiwa; muhtasari wamaneno ya kisanii wenye maana pana k.v. Mcheza kwao hutunzwa.”Kuna baadhi ya hadithi nyingi huanza na methali na kumaliziakwa methali. Kwa mfano, katika kitabu kilichotungwa naKayombo, Innocent Kapilima, Hadithi za Babu Zetu wa Tanganyika,TMP (1959), ametumia mtindo huo wa kuanza na ‘methali’ nakumalizia na methali katika kusimulia hadithi zake.

Zipo methali nyingi ni za Kiafrika pale zinapohusisha na ishara

8 / 62

Page 9: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

au vitu vipatikanazo katika mazingira yao. K.m. “Jifya mojahaliinjiki chungu.”

1.

Nini Maana ya Utandawazi?

Dhana ya utandawazi ilizuka mwishoni mwa miaka ya 1980 nakushamiri miaka ya 1990 na kuwa changamoto katika nyanjambalimbali. Utandawazi ni upanukaji kwa kina kirefu zaidi nakusambaa kwa masafa marefu mahusiano miongoni mwa jamiimbalimbali mintarafu uhalisia wa maisha, kuanzia yale yaustawi wa jamii hadi yale ya harakati za kujikimu, kiuchumi,kiutamaduni, kiulinzi, kibiashara, kiuwekezaji, kimawasiliano,kiteknolojia na kuufanya mchakato mzima kuipelekea dunia iwemithili ya kijiji kimoja kidogo. Mvuvumko huo wa kiutandawazikiuchumi na kiutamaduni umeipa Marerkani nafasi ya kasikubwa ya katika kuhodhi na kudhibiti mageuzi hayo.

9 / 62

Page 10: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

“Kwa ufafanuzi wa jumla, dhana utandawazi inamaanishakuifanya dunia nzima ionekane

kama kijiji kimoja kwa kupanuka kwake kimawasiliano,kijamii na kiuchumi katika uhalisia

wa mambo ulivyo katika nyanja mbalimbali kama vileuchumi, utamaduni, biashara,

uwekezaji, kiteknolojia hata kiroho. Kutokana na welewahuu inadaiwa kwamba uchumi wa

dunia umo katika mchakato wa kuoanishwa kwa kuvunjamipaka na nguvu za kiuendeshaji

kuwa kitu kimoja.” S.M.Rugumamu, GlobalizationDemystified, DUP(2005).

10 / 62

Page 11: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Waandishi wengine, kama vile C.K. Omari, Prof. E. Kezilahabina W.D. Kamera wanasisitiza katika vitabu vyao Misemo naMethaliToka Tanzania (Kitabu cha I&II):

“Misemo na Methali zimejaa wingi wa hekima namafundisho yanayoweza kutumika katika

kufafanua utamaduni wa jamii, muundo na mfumo wake,siasa yake, uchumi na mazingira

yake.”

1.

Mantiki ya Methali za Kiutandawazi

11 / 62

Page 12: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Nimeorodhesha baadhi tu ya methali zenye hadhi yautandawazi na kuelezea kwa kifupi kwa lugha ya Kiswahili naKiingereza, ingawa ingependeza sana kama tafsiri yakeingeweza kuwa katika lugha ya Kifaransa, Kijerumani, Kichinana katika lugha zingine za kimataifa. Ukweli huu wa methali zakiutandawazi unaenda sambamba kama alivyoandika HellenByera Nestor katika utangulizi: “…methali hufanana katikalugha mbalimbali za nchi kadha za ulimwenguni.”Hapa mwandishi huyo kwa kutumia dhana ‘hufanana’ kimsingialimaanishwa kuwa baadhi ya methali hutumika mahali pengiduniani ingawa ni kwa lugha tofauti lakini maana iliyobebwakatika maudhui yake ni ileile.

Zimepangwa kwa kuzingatia alfabeti ya Kiswahili. Methali zakiutandawazi ni changamoto kwa upande wa maendeleo yamawasiliano ya kiuhusiano miongoni mwa mataifa. Ikumbukwekwamba madai kwamba methali za kiutandawazi asili yake niUlaya au Marekani kama inavyodaiwa katika masuala menginemengi ya kiutamaduni na kihistoria. Utajiri uliomo katika methaliza kiutandawazi kamwe usimithilishwe na utajiri au maendeleomengine ya kisayansi na kiteknolojia kutoka katika nchi tajiriduniani na kwenda nchi maskini duniani!

Ni matumaini yangu kwamba mkusanyiko huu wa methali zakiutandawazi utatoa changamoto kwa wanataaluma kujengawigo mpana na kukita katika kina kirefu cha uchambuzi na

12 / 62

Page 13: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

upembuzi yakinifu.

4.0 Changamoto

Watu binafsi, serikali na taasisi mbalimbali zinaendelea kupaniakatika kukikuza Kiswahili. Kutokana na hali halisi ya baadhi yamethali kuweza kupotea miongoni mwa jamii mbalimbali zaKiafrika, mpango maalumu umeanzishwa ili kuweza kuziandikana kuzitolea maelezo methali za makabila mbalimbali ya Afrikakwa kuandika vitabu kadha wa kadha. Mradi huo ambao kilamwezi hutoa methali moja kutoka nchi moja ya Kiafrika,unaweza kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kamaulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings andStories Website : www.afriprov.org .

Hali kadhalika, kuna vitabu vingi vya methali vilivyoandikwa nawatunzi mbalimbali duniani. Katika mradi nilioutaja hapo juu,jitihada zimefanywa na kila mwandishi katika kukumekusanya

13 / 62

Page 14: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

methali zisizopungua mia moja za jamii yake kwa shabaha yakuzihifadhi ili zisije zikapotea. Mradi wa methali adimu zaKiafrika ulioanza mwaka 1999 ilimradi kusalimisha methali namisemo ambayo iko hatarini kupotea, hadi 2004 ulikuwaumefaulu kuzikusanya na kurudufu vijitabu kumi na tatu. Kunategemeo kubwa kupata ongezeko kubwa kabla ya mwisho wamwaka huu 2005.

5.0 Hitimisho

Tunaposherehekea Jubilei ya Miaka Sabini na Tano (75) yamchakato wa kukistawisha Kiswahili (The Inter-TerritorialLanguage [Swahili] Committee iliyoundwa 1930hadi Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI), iliyopandishwahadhi mwaka 1964), bado safari ni ndefu. Juhudi mbalimbalizilifanywa na serikali hata ikaunda Baraza la Kiswahili la Taifa(BAKITA) 1967; Idara ya Kiswahili-Chuo Kikuu cha Dar esSalaam 1970; Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni,Zanzibar 1979. Na wakereketwa waasisi walianzisha Chamacha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA) tangu

14 / 62

Page 15: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

miaka mingi kabla ya kupata Uhuru mwaka wa Tanganyika.Kiswahili hutumika katika nchi nyingi duniani; hufundishwakatika taasisi na vyuo vikuu kadha wa kadha duniani; hutumikakatika vituo vya redio na televisheni nyingi duniani; aidha, nimoja ya lugha rasmi za Umoja wa Afrika (AU).

Zifuatazo ni baadhi tu ya methali za kiutandawazi:

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Ada ya mja hunena muungwana ni kitendo

15 / 62

Page 16: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Kutokana na tabia ya kibinadamu, mtu hutambulika kwauungwana wake kwa vitendo vyake wala siyo kwa mavazi,maumbile au maneno ayasemayo.

Public opinion maintains, a gentleman is judged by his actions.(Manners make man; or Handsome is as handsome does).

1.

Akili ni nywele kila mtu ana zake

Akili za watu ni za aina nyingi na ni tofauti kama vile nywele zakila binadamu ni tofauti. Brains are like hair, every humankindhas her/his own kind.

16 / 62

Page 17: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Baada ya dhiki faraja

Baada ya shida huja raha.

After hardship comes relief. (Every cloud has a silver lining;After storm comes a calm).

1.

Bandubandu huisha (humaliza) gogo

Hata gogo liwe kubwa namna gain, unapolichanachana mwisho

17 / 62

Page 18: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

gogo hilo humalizika.

Chip! Chip! Finishes the log. (Little strikes fell great oak.Constant dripping wears away a stone).

1.

Chanda chema hufikwa (huvishwa) pete

Jambo jema husifiwa na hushangiliwa ili liweze kufana zaidi. Niwana kama kidole kizuri kinapovalishwa pete ili kizidikupendeza.

A handsome finger gets a ring put round it.

18 / 62

Page 19: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Chema chajiuza kibaya chajitembeza

Kitu kizuri huonekana bila ya kunadiwa, lakini kibaya hupigiwadebe ili kukitangaza.

A good thing sells itself, a bad thing advertises itself for sale.(Good wine needs no bush).

1.

Dalili ya mvua ni mawingu

19 / 62

Page 20: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Ishara ya kuwa mvua itanyesha hivi punde ni mawingu meusimakubwa. Na yasipokuwepo mawingu haiwezi kunyesha. Halikadhalika, katika juhudi zako waweza kujua mapema kamautafanikiwa.

Clouds are the sign of rain. (Morning shows the day as thechildhood shows the man. Cunning events cast their shadowsbefore. No smoke without fire).

1.

Damu ni nzito kuliko maji

Watu wa ukoo mmoja husaidiana sana katika matatizo yaokuliko marafiki au jamaa wa mbali.

Blood is thicker than water.

20 / 62

Page 21: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Elimu haina mwisho

Elimu ni za aina nyingi. Kila siku maarifa ya aina mpyayanagunduliwa na kuzuka, hivyo haiwezekani kuielewa elimuyote duniani.

Education has no limits. (One has to continue to learn all his/herlife time).

1.

Elimu ni bahari

Elimu ni pana hivi sawa na upeo wa bahari ambayo huelezwana kusambazwa miongoni mwa binadamu.

21 / 62

Page 22: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Education is like an ocean which spread all over the horizons ofpeople’s life.

1.

Fadhili za punda ni mashuzi

Shukrani za mtu mjinga ni kumtukana yule aliyemtendeamema.

The gratitude of a donkey is a breaking of wind.

22 / 62

Page 23: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Fimbo ya mbali haiuwi nyoka

Fimbo iliyo karibu nawe ndiyo ikufaayo wakati inapotokeashida. Methali hii inalenga kuwatanabaisha watu kuwabinadamu anapopata shida ni watu walio karibu naye ndiowatakaomsaidia.

A stick in the hand is the one that kills a snake.

1.

Ganda la muwa la jana, chungu kaona kivuno

23 / 62

Page 24: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Ganda la jana la muwa huwa limekauka, lakini chunguanapolipata huona ni mavuno maridhawa. Maana asiyezoeakuwa nacho, akipatapo hata kama ni kitu duni au hafifu namnagani na kidogo, hushangilia. Mathalani, kukengeuka kwamaadili kwa vijana barani Afrika na kuzamia tamaduni za kigeni.

The skin of yesterday’s sugar-cane is a whole harvest of an ant.

1.

Gonga gogo usikie mlio wake

Ukitaka kujua mlio wa gogo, lipige na usikilize. Hili lina maanakuwa yakupasa kulichunguza jambo kwanza kabla yakulihukumu (kulikabili).

24 / 62

Page 25: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Knock a log in order to hear the sound it makes.

1.

Haba na haba hujaza kibaba

Ukiweka akiba kidogo ya kitu kila mara, mwishoni utakuwa naakiba kubwa. Mwanzo wa makubwa ni madogo.

Little by little fills up the measure. (Little drops of water, littlegrains of sand, make a mighty ocean and a pleasant land).

25 / 62

Page 26: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Harakaharaka haina baraka

Jambo lifanywalo harakaharaka, haliwezi kufana. Mambolazima yaende kwa kuzingatia mchakato wenye mpango nataratibu madhubuti.

Hurry, hurry, has no blessing. (More haste, less speed).

1.

Iliyopita si ndwele, ganga ijayo

26 / 62

Page 27: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Mambo yaliyopita, yasishughulikiwe sana, bali tujizatitikuyakabili na kuyadhibiti yale yajayo.

That which has passed is not a diease, cure what is coming.

1.

Iwapo nia, njia hupatikana

Mtu anapofanya dhamira ya dhati ya kutaka kulitekeleza jambo,hawezi kukosa njia ya utekelezaji.

Where there’s a will, there’s a way.

27 / 62

Page 28: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza

Chochote usichokifahamu vizuri huwezi kukieleza kwa ufasaha.

A matter of which you are ignorant is like a dark night.

1.

Jogoo la shamba haliwiki mjini

Jogoo lililozoea kuishi shamba, likihamishiwa mjini hushindwakuwika kwa sababu ya mabadiliko ya mazingira yake. Maana,

28 / 62

Page 29: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

ye yote aliye ugenini yampasa kufanya mambo kwa tahadhari ilikulingana na mazingira ya hapo.

The country cock does not crow in the town.

1.

Kata pua uunge wajihi

Mtu akikata pua yake kwa ajili ya kujirembesha anakuwaanaiharibu sura yake zaidi.

Cut off your nose to mend your face. (Keep up appearanceseven at the price of losing your property. Cut off your nose tospite your face).

29 / 62

Page 30: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Kidole kimoja hakivunji chawa

Mtu mmoja peke yake hawezi kutenda mengi. Umoja ni nguvuna utengano ni udhaifu.

One finger cannot kill a louse.

1.

Kuishi kwingi kuona mengi

Kuishi katika dunia kwa muda mrefu humpa mtu nafasi ya

30 / 62

Page 31: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

kujifunza mengi. Tuwaheshimu wazee kwa vile wanawezakutushirikisha katika mang’amuzi mengi yenye hekima nabusara.

To live long is to see much.

1.

La kuvunda halina ubani

Harufu mbaya ya kitu kilichooza haiwezi kufichika au kuzuiwakwa kufukizia ubani. Hali kadhalika, jambo lililoharibikahalifichiki.

There is no incense for something rotting (it is impossible toconceal its evil odour).

31 / 62

Page 32: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Lililoandikwa ndilo liwalo

Lile aliloliweka Mungu litendeke, halishindwi kutendeka kamaalivyolipanga. Hii ina maana kuwa Mwenyezi Mungu ni muwezawa yote, hivyo alipendalo hutokea vivyo hivyo. Hakunaawezaye kushindana na matakwa (mapenzi) ya Muumba.

That which is written (by God) is what is (i.e. must surely cometo pass).

1.

Maji yaliyomwagika hayazoleki

32 / 62

Page 33: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Maji yakisha mwagika haiwezekani kuyazoa au kuyakusanyatena. Yaani, jambo likiharibika huwa limeharibika, hata kamalikitengenezwa kamwe halitaweza kuwa kama lilivyokuwa hapoawali.

If water is spilt, it cannot be gathered up.

1.

Milima haikutani, lakini binadamu hukutana

Milima haina uwezo wa kukutana, lakini binadamu wakiwa haihuweza kukutana hata baada ya kuwa mbalimbali kwa mudamrefu. Hii ni methali inayotumika katika kutiana moyo wakatiwanapoagana kwamba wakijaliwa watakutana. Pia hutumikakatika kuwaonya watu kuacha tabia ya kuwatendea vibayawengine kwani huenda wao pia wakatendewa hivyo siku zausoni.

33 / 62

Page 34: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Mountains do not meet, but people meet each other.

1.

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo

Malezi umpatiayo mtoto huwa ni msingi wa mustakabali wake.Maisha ya mtu yanategemea sana msingi wa malezialiyoyapata tangu angali mchanga. Ni vigumu kwa mtu kuachatabia aliyoizoea katika makuzi yake.

As you bring up the child, so he/she will be.

34 / 62

Page 35: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Njia mbili zilimshinda fisi

Kutokana na tamaa yake kubwa, fisi alijaribu njia mbili yakushoto na kulia, lakini alishindwa. Mwangata mbili, mojahumpokonya.

Two ways failed the hyena.

1.

Nyumba usiyolala ndani yake hujui ila zake

35 / 62

Page 36: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Mtu hufahamu tu mambo ya nyumba ambamo amelala. Nijambo la kijinga kwa mtu kujifanya kuwa anaelewa mamboambayo kwa yamkini hayaelewi.

You cannot know the defects of a house you have not slept in.It is the wearer who knows where the shoe pinches.

1.

Ombaomba huleta unyonge

Tabia ya kuombaomba vitu humfanya mwombaji kuwamnyonge au duni. Mlegevu, mzembe, goigoi na mvivukuwategemea watu wengine, maana hana bidii ya kujitafutiariziki yake kwa kufanya kazi mwenyewe. Mtegemea cha ndugu,hufa maskini.

36 / 62

Page 37: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Begging makes somebody become inferior.

1.

Ondoa dari uezeke paa

Acha kujenga dari mpaka umalize kuezeka. Mtu anatakiwakwanza kufanya jambo lililo muhimu kwanza kabla ya mengineyasiyo muhimu.

Remove the ceiling in order to thatch the roof.

37 / 62

Page 38: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Panapofuka moshi pana moto

Moshi ni ishara ionyeshayo uwepo wa moto. Watuwanaogombana mara kwa mara si ajabu kuwa siku mojawataingia vitani na kusababisha maafa.

Where there is smoke there is fire.

1.

Paka akiondoka, panya hutawala

38 / 62

Page 39: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Paka na panya ni maadui wakubwa. Paka hutishia sana uhaiwa panya kwa kuwakamata na kuwala nyama. Kwa jinsi hiyo,paka anapoondoka, panya hupata nafasi ya kufanya vitu vyaobila ya kuwa na hofu yoyote. Ndivyo ilivyo kwa wafanyakazi,endapo mkubwa wao akiondoka, walio chini hujiona kuwa huruna hufanya mambo wapendavyo.

When the cat goes away, mice do reign. When the cat’s away,the mice do play.

1.

Penye watu wengi hapaharibiki neno

Mahali ambapo kuna watu wengi hapaharibiki neno. Walipowatu wengi hubadilishana mang’amuzi na hivyo fikira na nguvuzao hukusanywa pamoja ili kulitengeneza jambo. Penye wengipana Mungu ambaye ni muweza wa yote.

39 / 62

Page 40: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Where there is a gathering of people nothing goes bad. Wherethere are many people, there God is (Vox populi vox Dei).

1.

Radhi ni bora kuliko mali

Kupata radhi ya wazazi ni bora kuliko kupata mali. Baraka yawazazi haiwezi kupatikana hivihivi tu, lakini mtu anawezakutafuta mali wakati na mahali popote. Kwa hiyo, yatupasakuwatii wazazi (wakubwa) wetu ili watubariki ndipo hatatutafutapo mali au riziki huwa tumekwisha pata baraka yamafanikio maishani kutoka kwa wazazi.

Blessings are better than wealth.

40 / 62

Page 41: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Rahisi haihalisi

Kitu au bidhaa ipatikanayo kwa bei poa ni kitu hafifu hivyo huwasi kizuri na hakifai. Cheap things are not worthy spendingmoney on them.

1.

Sikio halilali njaa

Hapana siku ipitayo bila ya sikio kusikia maneno fulanifulaniyawe mabaya au mazuri. Hivyo sikio halilali bila ya kusikianeno.

41 / 62

Page 42: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

An ear does not go to sleep hungry (there’s always plenty ofgossip).

1.

Sumu ya neno ni neno

Moto huzimwa kwa maji na pia neno humalizwa na neno.Likizuka neno au jambo linalowafanya watu kulisema sana auuvumi fulani, ule uvumi huendelea hadi pale uvumi mwinginetofauti utakapotokea. Basi, hapo watu husahau ule uvumi wakwanza wakaushika ule uvumi mpya.

The poison for a word is a word. Tit for tat.

42 / 62

Page 43: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Tamaa mbele, mauti nyuma

Mtu mwenye tamaa nyingi mwishowe hupatwa na misibamibaya. Anayetanguliza tamaa na ubinafsi mbele ajue hanamwisho mzuri.

Desire first, death afterwards (i.e. No one ever thinks of thepossibility of death when concentrating on achieving a particularend). Man proposes, God disposes.

1.

Taratibu ndio mwendo

43 / 62

Page 44: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Mwendo wa polepole ndio ufaao. Yaani, jambo lolote lile halinabudi kufanywa kwa kuzingatia kanuni.

Slowly is indeed the way to walk. He that goes slowly goessurely. Hasten slowly. Slow but sure.

1.

Uchungu wa mwana, aujua mzazi

Mzazi ndiye anayepata uchungu mwingi zaidi ya watu woteanapomzaa mtoto wake. Yaani mwenye kuthamini kituchochote kile ni yule mwenye kitu hicho. Kwani ni yeye ndiyealiyetaabika katika kukitafuta na kukipata.

The labour of childbirth is known to the mother.

44 / 62

Page 45: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Ukiona vinaelea, vimeundwa

Ukiviona vyombo vya kusafiria vinaelea juu ya maji, ujuekwamba ni matokeo ya juhudi na maarifa ya watuwaliovitengeneza. Kizuri chochote ukionacho, ufahamukimepatikana kwa bidii na jasho na siyo kwa miujiza.

If you see vessels afloat, remember that they have had to bebuilt.

1.

Usipoziba ufa, utajenga ukuta

45 / 62

Page 46: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Usipoukarabati ufa kwenye ukuta mapema, ukuta utabomokana hivyo utalazimika kuujenga ukuta tena. Usipolirekebishakosa dogo tangu mwanzo, utapata hasara kubwa hatimaye.

If you do not fill up a crack, you will have to build a wall. A stitchin time saves nine.

1.

Vita havina macho

Wakati wa vita mtu ye yote yule anaweza kuumizwa, kuuawaau kupata madhara ya aina yoyote ile. Ni vema kujiepusha navita.

War has no eyes (i.e. it kills indiscriminately).

46 / 62

Page 47: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Vita vya panzi furaha ya kunguru

Panzi wanapopigana na kuuana kwa wingi ni furaha ya kungurukwani hupata chakula chao kwa urahisi. Hali kadhalika, maafaya wanyonge huweza kuwa furaha ya wakubwa.

A fight between grasshoppers is a joy to crows.

1.

Wapiganapo tembo, nyasi huumia

47 / 62

Page 48: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Ndovu wawili wakipigana, husababisha nyasikukanyagwakanyagwa na kuharibika. Yaani viongozi wawiliwanapopigana wanaoumia ni wafuasi au watu walio chini yahimaya zao. Wakati mataifa makuu mawili (k.m.Warusi naMarekani wakati wa vita baridi) yanapopigana, mataifa madogondiyo yanayoumia.

Where elephants fight, the reeds get hurt.

1.

Ya kale hayapo

Yale yaliyotokea zamani yamekwisha na yanapaswakusahauliwa. Hapana haja ya mtu kuwa na kifundo cha moyokwa ubaya aliofanyiwa hapo zamani.

48 / 62

Page 49: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

The ancient (things) are no longer with us. Let bygones bebygones.

1.

Yote yang’aayo si dhahabu

Si kila kionekanavyo kinameremeta ni dhahabu. Kwani vikovingi ving’aavyo, lakini ambavyo si dhahabu na ni vya thamanindogo mno kuliko dhahabu. Usikipende kitu kwa uzuri wake wanje, bali ukichunguze sana ili ujue ubora wake. Uzuri wamkakasi ndani kipande cha mti.

All that glitters, do not think it is gold.

1.

Ziba mwanya, asipite panya

49 / 62

Page 50: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Ukisha kugundua mwanya wa panya, fanya hima ili uuzibe ilipanya wasifanye mazoea ya kuutumia mwanya huo. Mathalani,serikali ikisha gundua mwanya wa bidhaa za magendo hainabudi kuharakisha kuuziba mwanya ili kuondokana na ugumu wakulikabili tatizo hilo baada ya kuzoeleka na walanguzi seuze nawafanyabiashara ya magendo.

Seal the small path so that the rats should not create the habitof using it.

1.

Zimwi likujualo halikuli likakwisha

Shetani akujuaye hakuli akakumaliza. Watu wa jamii au ukoomoja hawadhuriani kabisa. Endapo wakifanya hivyo, basihuhesabika kuwa ni wachawi.

50 / 62

Page 51: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

A devil that knows you will not devour you completely.

Vitabu vya Rejea

1.

Ahmed Ndalu & Kitula G. King’ei, Kamusi yaMethali za Kiswahili, EAEP (1989).

51 / 62

Page 52: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

2.

Charlotte and Wolf Leslau, African Proverbs,The Peter Pauper Press, NY (1962).

3.

Farsi, S.S., Swahili Sayings, EALB

4.

Healey, Joseph G., Towards an AfricanNarrative Theology, Paulines Publications Africa (1996); Once Upon a Time in Africa: Stories of Wisdomand Joy,Orbis Books (2004); African Stories for Preachers and Teachers, Paulines Publications Africa(2005); Kueneza Injili kwa Methali, Benedictine Pulications Peramiho (1984).

52 / 62

Page 53: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

5.

Johnson, Frederick, Swahili-English Dictionary& English-Swahili Dictionary, OUP(1939).

6.

Kalugila, Omushumba Leonidas, Emigani naEbikoikyo,North Western Publishers, Bukoba (1992).

7.

Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora,Kugundua Mbegu za Injili,Benedictine Peramiho Publications (1993).

8.

53 / 62

Page 54: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Madam, Swahili-English Dictionary, (1894).

9.

Mayoka, J.M., Nahau za Kiswahili, MathewsBookstore & Stationers, Dar es Salaam,Tanzania.

10.

Mbonde, J. P., Wisdom from Ngoni Proverbs,privately duplicated (2004).

11.

Muwanga, Aminieli Stephano, Methali kwaPicha,Utamaduni Publishers (1984).

54 / 62

Page 55: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

12.

Ngole S.Y.A. & Honero Lucas N. (Wahariri),Fasihi Simulizi Methali (kitabu cha Pili(TUKI) DUP (1981).

13.

Nestor, Hellen Byera, 500 Haya Proverbs,East Africa Literature Bureau (1978).

14.

Omari,C.K., Kezilahabi, E., and Kamera,W.D., Misemo na Methali Toka TanzaniaKitabu cha 1 (Toleo Jipya 2000) & Kitabucha 2(Toleo Jipya 2004) Mathews Bookstore &Stationers, Dar es Salaam, Tanzania.

55 / 62

Page 56: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

15.

Rugumamu, Severine M., GlobalizationDemystified: Africa’s Possible DevelopmentFutures, DUP(2005).

16.

Scandinavian Institute of African Studies: Swahili Proverbs from East Africa,Uppsala (1977).

17.

TUKI: Kamusi ya Kiswahili Sanifu, OUP(1981).

18.

56 / 62

Page 57: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

TUKI: Kiswahili cha Utandawazi, DUP

19.

TUKI: Kamusi ya Kiswahili Sanifu (toleo lapili), OUP (2004).

20.

Wamitila, K.W., Kamusi ya Methali,Longhorn Publishers, (2001).

21.

Wanjohi, Gerald Joseph, Under One Roof-The Gikuyu Proverbs; & The Wisdom andPhilosophy of African Proverbs: The GikuyuWorld-View,Paulines Publications Africa (1997)

57 / 62

Page 58: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Note: This paper was originally delivered duringthe 75th anniversary of TUKI or the Institute ofKiswahili Research (1930-2005) at theUniversity of Dar as Salaam, Tanzania (4 th

-7th

July, 2005). The author decided to select only51 proverbs that are commonly used aroundthe globe. Hence, he calls them "globalproverbs." Actually, globalisation as a processcommenced many centuries ago. Think of theearly travellers such as Christopher Columbus,Vasco da Gamma, missionaries, slavery andslave trade, the First and Second World Warsand other periods and other events. Oneevidence is Negro-Americanism with itscomplexity of cultures. But globalisation takes anew face in the development of economy andculture particularly science and technology incommunication. The third millennium appearsto have overshadowed the entire meaning ofglobalisation. The

58 / 62

Page 59: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

contextulisationof each global proverb varies according to itsenvironment and culture. But those of Africanorigin have their flavor or touch notched in eachone of them:

e.g. Proverbs are the daughters ofexperience (Sierra Leone); A proverb is thehorse of

conversation: when the conversation lags, aproverb will revive it (Yoruba); A wise man

59 / 62

Page 60: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

who knows proverbs reconciles difficulties(Yoruba).

Indeed, these few selected global proverbs inthis paper are intended to represent all thosethat which are universally or popularly usedand/or recognised. Most of these globalproverbs have diversified origins: some of themoriginated from Africa, and some from Europeand many others from Asia.

60 / 62

Page 61: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

J. P. Mbonde

Retired civil servant (teacher/headmaster);a graduate from Sydney University,Australia and the De Montfort University,UK; Freelance journalist; author of severalbooks; Analyst of both oral and writtenAfrican Literature; EducationalConsultant; a regular book reviewer; hastraveled all over the globe on academicsand study tours.

P.O. Box 3479, Dar es Salaam, Tanzania,East Africa.

Email: [email protected]

61 / 62

Page 62: METHALI ZA KIUTANDAWAZI - African Proverbs, … kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website : . Hali kadhalika,

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Revised 23 August, 2005

62 / 62