52
©  Gulda El Magambo Mkutano kuhusu uwezekano wa kukadiria habari muhimu na majadiliano mengine yenye kuelekea usawa kati ya mume na mke katika miungano ya vijijini na kwenye vyombo vya matangazo visivyo vya ki-serikali katika jimbo la katanga, nchini jamhuri ya kidemocrasia ya congo lubumbashi, tarehe nne hadi nane mwezi wa sita mwaka wa 2007

Mkutano - Food and Agriculture Organization · Ushirika wa vikundi vya maendeleo katika vita dhidi ya kutawanyika kwa ugonjwa wa ukimwi vijijini Mada ya nne [ 33 ] Jinsia na mawasiliano

  • Upload
    others

  • View
    22

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

© G

ulda

ElM

agam

bo

Mkutanokuhusu uwezekano wa kukadiria habari muhimu na majadiliano mengine yenye kuelekea usawa kati ya mume na mke katika miungano ya vijijini

na kwenye vyombo vya matangazo visivyo vya ki-serikali katika jimbo la katanga, nchini jamhuri ya kidemocrasia ya congo

lubumbashi, tarehe nne hadi nane mwezi wa sita mwaka wa 2007

Tarehe nne hadi tarehe nane mwezi wa sita mwaka wa 2007, une fanyika

mjini Lubumbashi, mji nkuu wa jimbo la Katanga, mkutano kuhusu

uwezekano wa kukadiria habari muhimu na majadiliano mengine

yenye kuelekea usawa kati ya mume na mke katika miungano ya vijijini

na kwenye vyombo vya matangazo visivyo kuwa vya kiserikali.

Mkutano huo ulioendeshwa chini ya wongozi wa shirika lenye kutetea

maendeleo ya wa mama wa Katanga (refed-Katanga), ulisaidiwa na

mpango wa dimitra/fao, msinji wa mfalme wa ubelgiji (Fondation

Roi Baudouin), uhusiano na Canada (Coopération canadienne),

uhusiano na Ugerumani ki-afia (gtz-Santé), uhusiano ki-ufundi na

ubelgiji (ctb), unfpa, pnud na pia conafed.

Chaïda hii imetayarishwa kwa msaada wa fedha kutoka uhusia na

Canada (Coopération canadienne) na Fondation Roi Baudouin.

Le Projet Dimitra bénéficie du soutien financier du Service Public Fédéral des Affaires Etrangères, Commerce Extérieur et Coopération au Développement (DGCD) Belgique et de la

Fondation Roi Baudouin.

swahili

© G

ulda

ElM

agam

bo

© D

imit

ra

© G

ulda

ElM

agam

bo

© D

imit

ra

��

fYaliyomo

Utangulizi  [ 2 ]

Machache kuhusu jimbo la Katanga  [ 3 ]

Kwa nini kikao hiki?  [ 4 ]

Washiriki  [ 5 ]

Kufungiliwa rasmi kwa kikao  [ 6 ]

Mada ya kwanza  [ 11 ]

Kumiliki udongo: Matokeo ya uchimbaji madini na mashirika za maendeleo vijijni dhidi ya hali ya kijamii ya wakaaji

Mada ya pili  [ 23 ]

Kutawanywa kwa sheria kuhusu ubakaji na kupiganisha kuto azibiwa kwa wabakaji

Mada ya tatu  [ 27 ]

Ushirika wa vikundi vya maendeleo katika vita dhidi ya kutawanyika kwa ugonjwa wa ukimwi vijijini

Mada ya nne  [ 33 ]

Jinsia na mawasiliano kwa ajili ya maendeleo na njia bora ya kufililia habari muhimu na mawasiliano

Hitimisho kubwa zu kikao  [ 47 ] 

Anuani zetu  [ 48 ]

s

� ��

Utangulizi

Mnamo tarehe 4 hadi 8 za mwezi wa yuni mwaka wa 2007, kumeendeshwa mjini Lubumbashi, mji nkuu wa jimbo la Katanga, kikao kimoja cha kuongeza ujuzi wa kukadiria habari, mawasiliano na jinsia ya mashirika za vijiji na redio za kijamiii za jimbo la Katanga.

Kikao hicho kiliandaliwa na shirika lenye kutetea maendeleo ya wa mama wa Katanga (REFED-Katanga), chini ya hoduma ya kifeza ya projet Dimitra/FAO akisaidiwa na Fondation Roi Baudouin, Coopération canadienne, GTZ-Santé, Coopération technique belge (CTB), UNFPA, PNUD na pia CONAFED.

s

© G

ulda

 El M

agam

bo

� ��

Machache kuhusu jimbo la Katanga

Maelezo machache kuhusu jimbo la Katanga ni kwamba ni eneo kubwa, udongo na ndani ya udongo muna utajiri mingi sana, wakaaji wake ni wakosefu mno na hawana uwezo wa kuhojiana kati yao, njia za mawasiliano na nyumba za uma katika hali mbovu, makabila 50 huishimo.

Jimboni Katanga, hali ya makaaji wanaoishi vijijini ni mbovu sana, hasa zaidi hali ya wanawake. Jimbo hilo lina stahili wangalifu maalum kusudi lipate maendeleo sawa sawa na ya kudumu. Wana wake wapo chini ya uongozi na mamlaka ya wanaume; wanapimiwa vyote na hawakubaliwe kuchunguza faida ya kazi zao. Vivyo hivyo wanakuwa wazaifu kulingana na uhaba wa habari, ubovu wa hali ya matunzo ya afya na malisho mabaya.

Uwingi wa viwanda vya kuchimba madini umepunguza sehemu za udongo wa kuendesha kazi za mlimo. Vinyume vya hali hiyo ni kama vile upungufu na ubovu wa mazao ya mlimo. Kwa ajili ya uchimbaji wa madini vijijini, wanawake wametwikwa mizigo yote ya kazi kwa kuwa walimaji wanaume wameambatana na utafiti wa madini. Inatambuliwa kuzoofika kwa afia ya wamama na ya watoto, na pia kutawanyika kwa ugonjwa wa ukimwi VIH/SIDA.

© O

CH

A D

RC

� ��

Kwa nini kikao hiki?

Ukomo wa mkutano ulikuwa ni kuongeza nguvu za kukadiria habari na mawasilano na pia kuhusu jinsia katika miungano ya vijiji na vyombo vya habari vya kijamii. Viini vya habari mafunzo iliyoyendeshwa kikaoni humo vilichaguliwa na wanamemba wa REFED-Katanga, kwa ajili ya kujibu maswali yafwatayo:

Namna gani kusaidia miungano ya vijiji kusimama imara?Namna gani kutawanya sheria yenye kupinga ubakaji dhidi ya wanawake na kupinga kutoazibiwa kwa mabaya hayo?Namna gani kuhusisha miungano ya vijiji katika miradi za kupiganisha ugonjwa wa ukimwi VIH/Sida?Namna ya kuzidisha miungano ndani ya mifumo na kutumia sana redio za kijamii ambazo ni njia muhimu za kuwasiliana katika jimbo sawa la Katanga?

Mada hayo yote yaligusiwa na wataalam na pia watu wanaendesha wanaoendesha kazi uanjani. Baadaye kukaendeshawa mahojiano katika vikundi vya kazi. Na kiisha kila kikundi kikaandika mapendekezo zake ambazo ziliwekwa pamoja mwishoni mwa kikao.

Kitabu hiki kinarudilia mawazo muhimu yaliyotolewa, mabishano pamoja na mapendekezo ya mkutano ajili ya kuyarudisha mafunzo waliotolewa kwa mafaa ya wote.

••

© D

imit

ra

� ��

Washiriki

Yapata wanakawe na wanaume mia moja toka sehemu mbali mbali za Katanga: Kolwezi, Kalemie, Pweto, Malembankulu, Kasenga, Divuma, Tshamba, Manono, Kamina, Bukavu, Dilolo, Mutshatsha, Kapanga, Kapulula, Kipushi, Kabondo Dianda, Kabongo na Sandoa. 

Wengi wa washirika walikuwa wapasha habari wa redio za kijamii na pia ma-wakili wa miungano ya mashirika za maendeleo vijijini. 

Wamoja wamesafiri mwendo wa siku kumi kabla ya kufikia mahali pa mkutano kwenye jengo la Emmaüs mjini Lubumbashi. Wamama walio kuja na watoto, wamefaidika kupewa mahali pa kuwalinda watoto wao makusudi ya kuwaruhusu kuhuzuria vizuri kikao hicho.

© D

imit

ra

f

Kufunguliwa rasmi kwa kikao Neno la makaribisho na utangulizi wa kikao

Katibu mtendaji wa CONAFED, Kamati kuu ihusikayo na maendeleo ya wanawake ao Comité Femme et Développement

« Kwa nini kuwasiliana? Makusudi ya kuruhusu akina – mama waishio vijijini kufahamisha magumu yanayo wakabili, kugawanya shida na furaha zao. Na ni pia shuruli ya kufikia kukutana na walio mamlaka ao uwezo wa kukomesha magumu hayo. Ni vile vile nafasi inayotolewa kwa wengine ajili ya kubadilishana maoni 

kwa faida ya taifa nzima na ulimwengu kwa jumla. »

© D

imit

raElise Muhimuzi

f

Umuhimu wa ubadilishaji fikra na miungano katika njia za mfumo

Mkurugenzi wa mradi DIMITRA (FAO)

« DIMITRA ni mradi wa habari na mahusiano ambao unatumika pamoja na vikundi vingine vya nyumbani kwa ajili ya kuongeza uwezo wa wakaaji vijijini, hasa zaidi ya wanawake, ikionyesha wazi wazi mchango wao na kutengeza maisha yao na hali yao ya kijamii. »

« Kuungana katika mifumo kunavunja vikwazo vinavyo songa wakaaji vijijini, kuna ruhusu pia kubadilisha maoni kuhusu matatizo na suluhisho kwa kila mojawapo wake, kubadilisha habari, ujuzi na ufahamu hasa zaidi katika jimbo ambamo ukosefu wa kurekebisha mabarabara, umerudisha nyuma uhusiano kati ya wakaaji. » 

© D

imit

ra

© D

imit

ra

Eliane Najros

� ��

f

Kufunguliwa rasmi kwa kikao

Mjumbe wa muungano wa umoja wa mataifa unao husika na mlimo na chakula (FAO) nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

« Muungano wa umoja wa mataifa unao husika na mlimo na chakula, unatia juhudi kwa wekevu juu ya maswala yenye kuelekea wa mama na hasa zaidi kazi wanazozifanya juu ya kustawisha usalama wa chakula na kazi za mlimo. »

« Kikao hiki ni chenyi kuwa na maana sana kwa sababu kinakuja kutia mkazo juu ya kuongeza nguvu za wakaaji na redio za vijiji ajili ya mawasiliano kwa faida ya maendeleo ya vijiji na usalama wa chakula; vyote hivi vikifanywa katika kuheshimu usawa kati ya wanaume na wanawake. »

« Kiongozi mkuu wa FAO alinena ya kwamba majadiliano mema ni mlolongo yenyi kumaanisha vitu viwili: Ni majadiliano, wala sio mtu mmoja

kujitetea binapsi. Bali, watu wote kwa jumba wapewe nafasi ya kusema. »

© D

imit

ra Gana Diagne

� ��

f

Hotuba ya kiserikali

Mheshimiwa Bwana

Waziri mwenye kuhusika na maendeleo ya vijiji wa serikali kuu ya Kinshasa

« Nina matumaini ya kuwa mkutano huu utafungua njia ya kukuza nguvu na ushirika kati ya wakaaji na wajumbe wa kiserkali kupitia vyombo vya habari, zaidi redio za kijamii na za vijiji jimboni Katanga. Nakumbusha mara tena, umuhimu wa kazi za wanawake ambao wanashikilia mazao ya mlimo. Ni wazi kama wanawake ni washirika wa lazima sana katika mwenendo wa kiuchumi, wa kisiasa na wa kijamii, hata kama wengi hawaelewi umuhimu wa ushirika huo. »

Waziri amerudi mara tena kiisha mchana – kati kuhojiana mda mrefu na wanawake saba na pia wanaume watano walio wakilisha wakaaji kutoka vijijini.

s

© D

imit

ra

© D

imit

ra

Charles Mwando Nsimba

���0

Michezo ya kuigiza

Kufunguliwa rasmi kwa kikao kimekamilshwa na mchezo wa kuigiza ulioandaliwa na vijana toka Collège Nzembela ambao walitumia njama zote za kuiga vinyume vya mila fulani fulani.

s

© D

imit

ra

��

f

��

Mada ya kwanza – Kumiliki udongo: Matokeo ya uchimbaji madini na mashirika za maendeleo vijijni dhidi ya hali ya kijamii ya wakaaji

Imeonekana kuwa, mazao ya mlimo yamepunguka kiyasi katika jimbo la 

Katanga kufwatana uregevu wa sheria uchimbaji madini na matokekeo

yake dhidi ya hali ya maisha ya wakaaji: mwenda ruwawa katika uchimbaji

wa madini, kutokeshimu kaki za wakaaji, uhaba wa udongo wa mlimo,

kuharibishwa kwa mazingira, na kadahalika. 

Sheria kuhusu ulinzi wa madini, udongo na miti haikutangazwa kwa 

kirefu kwa faida ya wakaaji. Upotevu umekuwa mwingi hasa zaidi kuhusu 

kuondoshwa vijiji sehemu fulani, matumizi ya watumishi watokao mahali 

pengine, uharibifu wa mazingira, sehemu nyingi za udongo zina chunguzwa 

na mashirika za madini, na kazalika. Uvamiziwa mashirika za kuchimba 

madini ulisababisha uhaba wa udongo wa milimo na pia upungufu wa mazoa 

ya kilimo.

Kuna ngambo moja utawanyaji kwa kiasi kidogo wa sheria fulani (sheria 

kuhusu udongo, madini, pori,…) na ngambo ingine kutohusishwa kwa raia

wakati wa kutayarisha sheria hizo: sheria hizo zinatupilia mbali maslahi za 

wakaaji na pia wanagandamizwa sana katika haki zao. Matokeo mabaya mengi 

yaliweza kuripotiwa, kukiwemo: Baadhi ya vijiji vilivyohamishwa, watumishi 

wengi hutoka mahali pengine. Yafahamishwa vile vile kuwa mwanamke

hashurulishwe katika kazi za kulinda mazao ya mlimo.

�� ��

f

f

Magumu ya pekee ya wamama vijijini. Ukosefu wa kumiliki udongo na kinyume juu ya usalama wa chakula katika eneo la madini sawa vile Katanga

Mtaalam ahusikaye na maswali ya jinsia kwenye chumba cha uhusiano cha Canada (Coopération canadienne)

Kwa kuwa wanawake wapo chini ya mamlaka ya wanaume, hali hiyo inatia mipaka juu ya uwezekano wao kwa kuchunguza rasilimali na faida ya vyote. Wanawake wanaendesha kazi za mlimo juu ya udongo usio wao: vyombo vya kilimo, vifaa na mazao-vyote vinakusudiwa na mabwana zao ao ukoo wao. Hawawezi kuamuru lolote. Pia, wanawake wanatezamiwa sawa vile watumishi wa bure. Kwa ajili ya kutofikilia habari kamilifu pamoja na kuendelea kutumia vifaa vya kilimo vya zamani, wanawake wanwshindwa na kuongeza mazao ya mlimo.

Kufwtana na hali ya wanawake ginsi ilivyo jimboni Katanga, ni sherti kuwepo siasa nyipya kuhusu mlimo na madini, siasa ya ulinzi wa jamii na ya kutetea haki za binadamu. Ni neno la maana pia kuhudumia redio za kijamii ili wanawake wapewe uwezo wa kufikilia habari mhimu na kuongezeana maarifa, hasa kuhusu hatari zinazotokana na uchimbaji madini na pia kuhusu haki zao.

© D

imit

ra

Gul

da E

l Mag

ambo

Marie-Antoinette Saya

�� ��

f

Mada ya kwanza

Matokeo ya uchimbaji madini wa kiviwanda na wa kiasili

Kikundi cha utafuti na matendo juu ya maendeleo ya kudumu na maendeleo ya uchumi mikowani (Groupe ONE)

Makusudi ya kufikiria maendeleo ya kudumu, inatupaswa kupatanisha nguvu za uchumi na siasa nzuri ya kijamii pamoja na uongozi bora.

Uchimbaji wa madini katika viwanda:

Wakati wa Gecamines, wafanyakazi walikuwa wanapewa matibabu ya bure kwenye hospitali. Watoto wao walielimishwa bila tatizo lolote. Watumishi walipewa maji safi, umeme na chakula kingi. Umbalimbali na hayo, maisha ya watumishi wa viwanda vya madini siku za leo, imekuwa mbovu sana. Mifano ni kama hii: 

Mipango ya ki-jamii inayo tetewa haiambatane na matakwa ya wakaaji;Uhusiano baina ya mashirika na mi-ungano ihusikayo na kutimiza kiwango fulani cha kusaidia wakaaji, uhusiano huo hautowe matunda bora;Mipangilio ya ki-serikali kuhusu kazi za viwanda vikuu vya madini, kama inavyo tayarishwa ki-sheria, haiheshimike kamwe;Miungano midogo ya maendeleo vijijini haitambuliwe.

Uchimbaji wa madini kwa kiasili:

Ikiwa kama ni kweli uchimbaji wa madini kwa kiasili inayoendeshwa na watu ki-pekee, umesaidia kupunguza umaskini kwa kuunda kazi, ni vema kutambua kama, shurti za kazi zinaendelea kuwa za hatari sana kwa afia ya wafanya kazi wote kwa jumla, na kwa wanawake na watoto kwa upekee. Ijapo kuwa matunda yanaweza kuwa mazuri, afia ya wanaohusika siyo nzuri hata kidogo.

••

© D

imit

ra

Dolet Nyembo

�� ��

Kukubaliwa kupata habari ni msingi wa siasa nzuri ya ki-jamii. Kupata kufwata habari, ni kadirisho ya kuruhusu watu watetee na kuheshimisha haki zao. Bila habari, hakuna uwezekano wa kujadiliana. Habari ikiwepo, watu wote kwa jumla wanaweza kushiriki katika mazungumzo kwa usawa. Vyombo vya habari ni moja wapo ya kadirisho za kutawanya habari ambayo wakaaji wanayo lazima.

© G

ulda

 El M

agam

bo

�� ��

f

Mada ya kwanza

Kiwanda Anvil Mining kimefanya nini kwa faida ya watumishi wake?

Kiongozi ahusikae na maendeleo ya kijamii na mahusiano kwenye shirika Anvil Mining

Katika shirika Anvil Mining, usawa kati ya mume na nke, unatiwa mkazo ajili ya maendeleo ya wote. Japo hivyo, ginsi vyeo vina pangwa, mwanamke hainuliwe kwenye cheo ao fasi anayostahili. Ndiyo maana, ingefaa shirika Anvil Mining lipange siasa nzuri makusudi ya kuinua wanawake katika kiwanda hicho. Mwanamke ana ujuzi wa kuishi vizuri na watu wote, 

analinganisha vema kiwango cha pesa cha kulisha jamaa lake, analinda uzazi. Mwanamke analipa deni haraka kuliko mwanaume.

Anvil Mining amefanya nini ki-jamii leo?

Shirika hilo limesimika kamati, 45 za maendeleo;Shirika hilo lime jenga shule sita;Soko mbili zilizo jengwa zinatumika;Vyumba kumi vya mikopo vimefunguliwa;Wakaaji elfu mbili wamepewa msaada wa vifaa vya mlimo, wakiwemo 30 asilimia ya wanawake;Mradi wa kisima cha maji safi mkoani Pweto.

Kulingana na kanuni mpya kuhusu uchimbaji wa madini, viwanda vihusikavyo vinapashwa kuweka kumi juu ya mia (10%) ya faida zao katika miradi ya maendeleo vijijini. Ila hakuna mafasirio yoyote iliyotolewa kuhusu”maendeleo vijijini”, kwa ajijli ya kuingiza giza fulani katika mpango huo wa kisheria. 

Kumbuka kuwa migodi ya kuchimbulia madini yanaishi mda wa miaka sita peke yake. Ndiyo maana ni vema kukadiria mawazo juu ya kazi inayopashwa 

•••••

© D

imit

ra

David Kayombo

�6 ��

kuendeshwa kïisha madini kuisha. Kwa hivyo, mi-ungano ya maendeleo, inapashwa kujadiliana ajili ya kupanga miradi yao ya 

maendeleo. Vivyo hivyo mashirika makuu ya madini yanapashwa kupatanisha kazi zao na pia ulinzi wa mazingira makusudi ya kuepuka kuharibu maisha ya watu. 

Kuna uhusiano kati ya Anvil na PACT-Congo (shirika kutoka marekani ambalo linapokea msaada wa USAID kwa ajili ya kusaidia 

maendeleo ya vijiji).

© T

etsh

im

�6 ��

f

Mada ya kwanza

Muundo wa mashirika za maendeleo vijijini

Kiongozi mtendaji wa Prefed (Programme Régional d’Echange et de Formation pour le Développement)

Hakuna mfano pekee kwa kusimika muundo wa shirika la maendeleo vijijini. Mwenyekiti hapashwe kulazimisha sura ya uongozi wake binafsi, bali kusaidia msimamo wa kazi kufwatana na mahitaji za matumikio pamoja na lengo la shirika. Kuhusu mambo ya pesa, ni muhimu kuzamini matumizi angavu ya pesa hizo. Na pia, mashirika za ya maendeleo vijijini 

yapashwa kuwakilishwa katika ngazi za uongozi. Ni vema wanamemba wote wawekeane matumaini. Wakati wa kutoa mchango wao, ni lazima wote watowe kwa kiasi sawa sawa ili wote wajisikie kuwa sawa sawa.

Kamati inapaswa kuacha wazi njia kwa wanamemba ili nao pia waone ginsi shirika lao laongozwa. Katika mikutano, wazaifu wapewe mda wa kusema. Kïisha hapo, wanawake wajitetee na vijana, na mwishowe wanao tabia ya kusikilizwa zaidi, watu wa zamani na wengineo. Hao wote kwa jumla wanapashwa kuwa waangalifu juu ya maoni ya washirika wazaifu waliosema wa kwanza katika mkutano.

Mashirika za maendeleo ya vijiji za kandokando zaweza kujitahidi kukutana mara kwa mara kwa ajili ya kusaidiana na pia kuzungumzia kuhusu matatizo zenyi kuwakumba katika kazi zao. Uwezekano wa kuyaongezea maarifa mashirika za maendeleo vjijijini ni majawapo wa njia zinazo saidia mashirika hizo zidumu milele.

s

© D

imit

ra

Sylvestre Kambaza

�� ��

f

Msaada wa zarura na marekibisho ya mlimo nchini RDC

Mkurugenzi ki-ufundi kwenye Chumba cha kazi za haraka na marekibisho kwenye FAO-RDC

Ukomo ni kustawisha maarifa wa wakaaji vijijini makusudi wawe taratibu na tayari kupiganisha misiba za ulimwengu zinazo sababishwa na watu. Mbinu zitakazotumiwa ni kuokoa, kujenga upya na kustawisha maisha ya watu kupitia mlimo 

na kupunguza hivi unyonge, kuongeza kujitoshelea na kutotegemea misaada ya chakula toka inje.

Wanao husika zaidi ni wanawake na wanaume wanaoishi kwa kazi za mlimo, wavuvi, wakimbizi, watu waishio uhamishoni, watoto wenyi kutatizwa na malisho mabaya, wapiganaji wa zamani, jamaa zinazosimaiwa na wanawaka ao na watoto, jamaa zinazo kabiliwa na ugonjwa wa ukimwi, na kazalika.

Nguzo za mipangilio ya usalama wa malisho ni:

1. Kuokoa maisha:Kustawisha mipango ya uchunguzi na ya kukadirisha hali ya malisho kwa faida ya watu wote na katika vituo vya matunzo kwa upekee;Kuchukuwa mzigo wa watu wasiojiweza, wazaifu.

kazi za kutimiza: Kusimikwa vituo vidogo vya ulinzi wa usalama, kugawa chakula na vyombo mbali-mbali vya mlimo, uchunguzi wa malisho kamilifu.

2. Upunguvu wa mazaifu:Kuongeza njia za kuokoa watu wasiojiweza kwa kuongeza uwezo wa usalama katika malisho;Kuzamini pato ya vifaa vya mlimo ambavyo vya ruhusu wakaaji kutoa mazao;Kuzidisha na kutengeneza ufundi wa mlimo na ule wa ufugo;Kurahisia watu kuwasili katika vituo mnamoendeshwa miradi za mlimo;

•••

s

© F

AO

-RD

C

Michel Ngongo

�� ��

Mada ya kwanza

Kupiganisha magonjwa yenye kushambulia mimea;Kuendesha utetezi wa kupewa udongo kwa vikundi vya watu wasiojiweza.

kazi za kutimiza: kugawa vyombo vya mlimo na chakula, kuendesha majifunzo, kutengeneza njia za vijijini na kutolea chakula kwa wakaaji wanao lazima.

3. Kutia mkazo juu ya kipindi cha mpito:Kufikiria uwezekano wa kuingiza wahusika katika siasa inchini ya kuwahudumia wakaaji wa vijiji;Kuendesha miradi za kuzidisha mbegu na vijiti vyenye kuwa safi;Kuanzisha kazi za kutegeneza upya na kuweka vizuri vyakula;Kuongeazea vyumba vya kazi jimboni za mlimo maarifa;Kutengeneza ma-bonde;Kutetea ufugo na visima vya samaki;Kukarabati barabara na njia za vijijini;Kuzidisha ao kustawisha ufundi wa mlimo na ule wa uvuvi.

kazi za kutimiza: misaada ipewe kwa mashirika za vijini, kutambuwa na kukarabati barabara vijijini, mashirika za maendeleo vivjijini zizzidishiwe nguvu za uongozi, kurekibisha shamba za kutayarishia mimea, kurudishwa katika jamii kwa wapiganaji wa zamani na wasindikizi wao.

••

••••

© F

AO

-RD

 FA

O-R

DC

© F

AO

-RD

C

�0 ��

f

Mada ya kwanza – Kumiliki udongo: Matokeo ya uchimbaji madini na mashirika za maendeleo vijijni dhidi ya hali ya kijamii ya wakaaji

Mapendekezo

Kwa washirika na kwa vikundi vyao:

Waendeshe kampeni za kutolea habari muhimu na mafunzo: kuhusu haki na mapashwa za binadamu, sheria za madini, udongo na mwitu;Kutimiliza jambo la kusawazisha mume na mke: jinsia, kupiganisha mila yenye kurudisha watu nyuma, hasa zaidi kushusha wanawake;Kuziongezea nguvu mi-ungano ya vijijini na vikundi vya nyumbani: kuhusu mafaa ya kujenga vikundi vya maendeleo; kutawanya vyombo vya uongozi wa mashirika, kurudisha matokeyo ya mikutano katika lugha za nyumbani vijijini.

Kwa shirika la raia:

Kufanya vizuri kazi yake ya kuwafuatilia viongozi wa kiserkali: kutetea maslahi ya raiaKuwaongezea wapasha habari maarifa: mafunzo ya kiufundi, kustawisha kazi zao na eneo yenye kupokea matangazo ya vipindi vya redio za kijamii, kuchapwa kwa gaeti ndogo za habari;Matokeo ya mkutano yapashwa kutangazwa kwa faida ya watu wote, kupanga kazi za utetezi: kutia mkazo juu ya mpango wa kutetea madaï ya watu wanao ishi vijijini.

Kwa mashiirika yenye kuchimba madini:

Kuheshimu sheria ya nchi: kuchanga, kufunza na kutumia wafanyakazi kutoka vijijini, kukinga mazingira, kukinga wafanyakazi na jamaa zao ili wasipatwe na magonjwa mbalimbali;Kustawisha mahusiano na wakaaji: kutia mkazo juu ya mahusiliano, kutolea habari muhimu kwa vyombo vya habari vihusikavyo, kutengeneza upya shamba zilizo haribika;

••

�0 ��

Mada ya kwanza

Kufanya mkataba wa kusaidia mashirika za maendeleo, viwanda vya nyumbani na vikundi vya wanawake kuendesha miradi ya maendeleo.

Kwa viongozi wa kiserikali:

Kutezamia upya na kulinganisha sheria: kuhusu udongo, mwitu na madini, kuchunguwa namna ya kulipa hasara ikiwa watu fulani wameguswa na uharibifu wa mazingira;Kuheshimisha mipango yote ya kanuni na sheria za nchi kwa wote;Kuimarisha kazi za kupasha habari vijijini: radio za kijamii za vijiji visilipishwe kodi ama malipo mengine kwa serkali, kukamilisha siasa ya upashaji habari nchini na miradi ya mawasiliano iendeshwe katika vijiji.

Kwa mashirika za kutoa pesa:

Kuimarisha sekta ya mawasiliano: kufundisha wapasha habari, uongozi bora wa redio za kijamii, kushirikisha muongozo mzuri wa vikundi vya wana wake;Kutia mkazo juu ya nguvu na uwezo wa mi-ungano ya maendeleo ya vijiji kupitia vikundi imara;Kutoa mchango kwa uendeshaji wa utetezi kwa ajili ya kuyaweka mbele maslahi ya raia vinapoadaliwa vyombo vya sheria.

••

�� ��

© T

etsh

im

�� ��

fMada ya pili - Kutawanywa kwa sheria kuhusu ubakaji na kupiganisha kuto azibiwa kwa wabakaji

Matatizo yanyi kujitokeza:

Wengi hawa juwe ya kama kuna sheria yenye kuazibu vitendo vya ubakaji zidi ya wanawake na wabinti hasa zaidi katika vijiji na uzaifu katika utumiaji wa sheria hiyo: uhaba wa uhimizaji, kutojulikana kwa sheria, kuto azibiwa, hali mbaya ya majela, uhaba wa vikundi vya kuwasaidia wahanga wa ubakaji, matumikio mabaya ya kazi za sheria;

Mzigo wa mila na asili, ku-oweshwa wa-binti kabla kueneza miaka ya ndoa, ukurungu, imani isiyo kuwa halali, kunyamaa kwa waliobakwa na kubagumliwa kwao, jamii yajihusisha kwa sehemu ndogo sana katika mbinu za kupiganisha ubakaji;

Vikundi mbalimbali vya maendeleo havi shirikiane pamoja;

Ubovu wa hali ya kijamii na ya kiuchumi.

��

f

��

Ujuzi wa UNFPA katika kupiganisha ubakaji na kuto azibiwa nchini RDCongo

UNFPA-Katanga (Fonds des Nations Unies pour la Population)

Ubakaji ki-nguvu ni moja kati ya magumu yenye kukabili afia na ujamii na pia ukiukaji wa haki za binadamu, kama vile haki ya kumiliki afya njema, kimwili na kiakili, haki ya kumiliki maisha. Mnamo mwezi wa julai 2006, kulitangazwa sheria yenyi kutambulisha upya vitendo vya ubakaji kama ukaidi. Ila, inaonekana kuwa sheria hiyo haijulikane ao kutumiwa na vyombo vya sheria kwa ajili ya sababu zisizojulikana. 

Mbele ya mwaka wa 2004, nguvu za kupinga ubakaji zilikuwa zimetawanyika ovyo ovyo kulingana na ukosefu wa uongozi na pia misaada. Ndio sababu, kumeanziliwa mpango wa pamoja kati ya serikali, umoja wa mataifa na mashirika za maendeleo makusudi ya kuleta jibu kwa swali hili la ubakaji na ukosefu wa azabu kwa wabakaji nchini Congo. 

Mitindo mbalimbali ya msaada imetolewa kuhusu afia, sheria, uchumi, usalama na ujamii.

Tufanye nini?

vikundi vitajihusisha na kuwa na zamiri kuhusu hatari za ubakaji na kutoazi-biwa kwa watu wenti kuzaniwa kama ni wabakaji;viongozi wa serikali wanapashwa kuwa taratibu, tayari kujibu na kuleta sulu-hisho kwa matatizo yanayo kabili raia popote;sheria nyipya za kukomesha ubakaji zapashwa kutangazwa;vituo vyenyi kuhusika na ugawaji wa sheria vinapashwa kugaramiwa kwa vyombo vya kazi, vitabu na kwa mafunzo kwa watumishi;inapashwa kuunda vyumba vya kusambishia mahali pote vijijini kwa ajili ya kuruhusu wahanga wa ubakaji kufikilia sheria.

••

© D

imit

ra

Abety Bilanda

��

f

Mada ya pili

Mada ya pili - Kutawanywa kwa sheria kuhusu ubakaji na kupiganisha kuto azibiwa kwa wabakaji

Mapendekezo

Kwa washiriki:

Kurudishia wahusika mambo muhimu yaliyo semwa mda wa mkutano.

Kwa vikundi vya vijijini:

Kusimikwa kwa makundi ya kupiganisha ubakaji pamoja: Kuweka msimamo wa pamoja makusudi ya kuchongea watu walio baka ki-nguvu, kuvunja moyo mipango ya kumaliza mashtaka ya mtindo huo ki-binafsi kuliko kutolea azabu;Kuwasindikiza ki-mashauri walio guswa na ubakaji ki-nguvu: kukataza wasishotwe kidole, watoto wao walio zaliwa kutokana na ubakaji wakubaliwe na walimwengu;Kuendesha utetezi kwenye viongozi wa serikali makusudi ya kusimika vyumba vya kusambisha katika mitaa, kushurulisha vyombo vya habari ajili ya kutangaza makosa za waliotenda maovu ya ubakaji.

Kwa vyumba vya kiserikali, vile vya kipekee na kwa wasaidizi wenyi kutoa pesa:

Kujihusisha kwa vyumba vya kiserikali katika vita dhidi ya ubakaji: kushimikwa kwa vyumba vya masambo katika mitaa mbalimbali;Kujihusisha kwa vyombo vya habari: kuhimiza na kutangaza sheria mpya, kutangaza masambo yote kwenye vyombo vya habari;Kuboresha hali ya kiuchumi na kijamii ya maisha ya wakaaji;Kuimarisha misaada: Kuwaongezea nguvu mashirika zenyi kuendesha kazi katika majimbo zote, kufanya kazi ya pamoja vijijini na kusimika vyumba vya kusambishia katika mitaa mbalimbali.

••

�6 ���6

© D

imit

ra

�6 ��

fMada ya tatu – Ushirika wa vikundi vya maendeleo katika vita dhidi ya kutawanyika kwa ugonjwa wa ukimwi vijijini

Magumu yaliyo tambuliwa:

Kutawanywa kwa habari muhimu na uhimizaji kuhusu ukimwi

visivyotoshelea: uhaba wa zamiri, imani kwa mambo isiyo ya ukweli, 

mila na asili, ubaguzi na kushotewa kidole kwa watu wenye kuwa na 

virusi vya ukimwi wanashotwa kidole, watu wengi hawajuwe hali yao 

ya mwili, woga kujipimisha ili mtu atambua kama hana virusi vya 

ukimwi.

Siasa nchini ya mawasiliano haiambatane kamwe na swala kuhusu

ugonjwa wa ukimwi.

Uzaifu wa kazi za pamoja kati ya vikundi vyenyi kuhusika: serikali, 

vikundi mbalimbali, mashirika zisizo za kiserikali na wasaidizi kifeza.

��

�� ��

f

��

Ujuzi wa GTZ-Santé ya RDC kwa kushurulisha vikundi vya maendeleo vijijini katika kupiganisha ugonjwa wa ukimwi

GTZ-Santé Bukavu

Imetambuliwa ya kama:

ukimwi unagusa zaidi wanawake, na ugonjwa huo unatawanyika zaidi vijijini;unyonge wa watu na vikundi hauwaruhusu kujikinga dhidi ya ukimwi;unyonge wa wanawake na mabinti pamoja na vitendo vya ubakaji waliotendewa vyauongezea ukimwi nguvu za kujitanya upesi.

Kwa ajili ya kukabiliana na ukimwi, GTZ-Santé hutumia mbinu zifuatazo:

kukusanya wahusika (wanawake, vijana) mikutanoni, na vile vile wanamemba wa mashirika za vya maendeleo ya vijiji na pia vikundi vya wasikilizaji;kuongeza maarifa ya washiriki kuhusu ugonjwa wa ukimwi, na njia zake za kujiambukiza kupitia habari muhimu kutoka intaneti, utangazaji wa habari kupitia uchapaji wa gazeti ndogo, mabadilishiano fikra pamoja na ujuzi, kujiunga katika mifumo, na kazalika;kuhimiza watu ili wajipimishe kwa hiari yao kwa ajili ya kutambua vizuri namna ilivyo hali ya afya yao.

Matokeo: Kuundwa kwa vikundi vya wasikilizaji vyenyi lengo la kupiganisha ukimwi, kutangaza habari kupitia gazeti, kuandaa mikutano za kazi pamoja na za mahojiano, kuongoza vikao vya kugawanya fikra kuhusu ukimwi, kuhimize wakaaji kuhusu ubakaji na vinyume vyake, kushawishi watu wajipimishe kwa hiari yao, kuhimiza wanawake wajawazito ili watumie kaze za kuzuia kuambukizwa kwa mtoto na ukimwi wakati wa kuzaliwa na baadaye, kutoa misaada kwa senta za kupana damu kwa bure, na kazalika.

•©

 Dim

itra

Aster Bashige

�� ��

f

Mada ya tatu

Kufungua ulimi kwa kuzungumza kuhusu ukimwi nchini Congo: RDCcompétence

CTB, Coopération technique belge

RDCcompétence anatumia njama za kupekua na kutafakari kuhusu kazi zilizotimizwa na vikundi vya maendeleo vijijini kwa ajili ya kugundua nguvu na uzaifu wanao katika uendeshaji wa kazi hizo. Ni sherti kuwapa watu fursa ya kuzungumzia ugonjwa wa ukimwi ili wapate kuugundua wao kikamilifu wao wenyewe na kujitafutia suluhisho kwa swala lile la ukimwi. 

Mahojiiano yataendeshwa wakati watu wanapopatikana mahali moja, kwa mfano baada ya misa ao kiiisha mkutano fulani. Ulizo litakalogusiwa mara na mara, ni kwamaba watu wanapashwa kujiuliza kama kwa kweli ukimwi ni shida. Baada ya hapo, wajiulize kama mpaka wapi wataonyesha matakwa yao na juhudi ya kupinga ugonjwa huo. Kupi-mwa mwili? Kujuwa hali ya damu?

Ulimwangu wa ujuzi kuhusu kupigana na ugonjwa wa ukimwi unatuomba:

Tuwe na zamiri ya kwamba ugonjwa huo unatuelekea sisi sote maishani mwetu, katika jamaa letu na pia katika kazi zetu;Kuongeza juhudi ajili ya kupunguza unyonge na hatari zenye kuwa mbele yetu siku kwa siku;Kufanya iwezekanavyo ili kila moja wetu atimilize mapashwa yake ya ukingo;Kuelimishwa kutokana na jambo tuliloliona ao kulisikai ao kulitenda binafi na pia kuhojiana na wengine.

••

© T

etsh

im

Sandrine Ruppol

�0 ��

Ushahidi: Jacqueline Naweji Kangaji, REFED Kolwezi

Jacqueline ambaye ni mwuuguzi, alionyesha sanamu zilizo chukuliwa mjini Kolwezi na shirika lake ambalo lajihusisha na kuwahudumia watoto wanaoishi barabarani. 

Washiriki wote walifurahishwa kuona Bi-Jacqueline amekuwepo. Vivyo hivyo alitolea ushahadi wenye maana makubwa. Furaha pia kwa wahuzuriaji mkutano ambao walikuwa wagonjwa pamoja na watoto wao. Mtulivu na mchangamshi, bibi huyu alionyesha kwa wote kama ni mwenye mafaa.

© D

imit

ra

© D

imit

ra

�0 ��

Mada ya tatu

Mafunzo ya kazi za mlimo na mazoezi ya maisha kwa faida ya vijana

Kwa ajili ya kupunguza vinyume vya ugonjwa wa ukimwi unao kabili maeneo za vijiji katika nchi nyingi za Afrika, kiungo cha umoja wa ma-taifa kihusikacho na mlimo na chakula (FAO), kime simika shule za kutolea elimu za mlimo na mambo mengine yenyi kuelekea maisha kwa faida ya vijana. Shule hizo zinalenga kuwaruhusu mayatima, watoto pamoja na vijana wanaokabiliana na unyonge wa namna mbali mbali kujigaramia na kujitoshelea wao wenyewe. Wanaongezewa kupitia shule hizi maaarifa ya kupiganisha maisha ya kila siku pamoja na ujuzi wao katika mlimo.

© F

AO

 / G. B

izza

rri

�� ��

f

Mada ya tatu - Ushirika wa vikundi vya maendeleo katika vita dhidi ya kutawanyika kwa ugonjwa wa ukimwi vijijini

Mapendekezo 

Kwa washiriki na vikundi vyao:

Kuzidisha uhimizaji wa makundi ya watu waishio vijijini: mikutano ya mahojiano na mabadilishiano ujuzi kuhusu kupiganisha ugonjwa wa ukimwi. Kuendesha uvumbuzi mpya na kujumlisha mbinu za vita hiyo dhidi ya ukimwi.

Kwa serikali:

Kuingiza vita dhidi ya ukimwi katika mipango yake na kuipatanisha na mipango mingine anayoiendesha inchini;Kuzidisha maarifa pamoja na vyombo vya utangazaji, hasa redio za kijamii: kuzidisha na kujumlisha vipindi vya redio, kuhudumia kiufundi vikundi vya wasikilizaji, kutumia lugha ya nyumbani katika mahojiano.

Kwa mashirika yenyi kutoa misaada: 

Kushikilia kazi za pamoja: kuheshimia mahitaji kamilifu ya wakaaji wa vijiji kuhusu kupiganisha ukimwi, kushirikisha wasaidizi wengine sawa vile redio na vikundi vya wasikilizaji.

© D

imit

ra

�� ��

fMada ya nne - Jinsia na mawasiliano kwa ajili ya maendeleo na njia bora ya kufililia habari muhimu na mawasiliano

Magumu iliyo tambuliwa:

Uhaba wa njia za kuingia ao za kutoka katika vijiji;

Redio za kijamii zina nguvu ndogo sana kwa kukujitokeza. Redio 

hizo hazitoshelee na vile vile vinakumbwa na uhaba wa vyombo 

vya kazi, mipangilio na vipindi visivyoambatana na mahitaji ya 

wasikilizaji, ukosefu wa fedha na pia wa mafunzo kwa wahimizaji na 

wafundi wa redio hizo;

Wanawake hawa shurutishwe kwa ginsi inavyostahili katika 

uhimizaji na uongozi wa vyombo hivyo vya habari;

Wanawake wanashotwa vidole na kubaguliwa vikali sana kulingana 

na mila na asili za nyumbani;Redio za kijamii hazihusiane.

Mahojiano yameelekea uwezekano wa majadiliano kati ya redio zinazo tangaza habari za maendeleo vijijini, mahusiano kati ya vyombo hivyo vya habari na mi-ungano ya wakaaji na pia, kusimika vikundi vya kukusanyisha wasikilizaji.

••

��

f

��

Kutoelewana kati ya wanawake na wanaume kuhusu ugawaji wa shuguli nchini RDCongo

Mtaalam ahusikaye na maswali ya jinsia kwenye chumba cha uhusiano cha Canada (Coopération canadienne)

Kuna shuguli zinazoambatana na baiolojia ambozo zinajulikana kama ni shuguli za baiolojia zikitegemea kiungo cha mwili (uke ao uume).

Kuna pia kazi za wanaume na wanawake kupitia utalii, dini mbalimbali, majifunzo na kijamii huitwa shuguli za kijinsia, ambazo zinategemea hali katika jamii. 

Uhusiano mdogo kati ya wanawake na wanaume ina matokeo mabaya dhidi ya maendeleo ya wakaaji. Kwa ajili ya kurekibisha hali hiyo, ni vema kuwepo uhusiano 

unaosawanyishwa kulingana na jinsia, na kuboresha hali ya uhusiano wa kipekee kati ya wanawake na wanaume. Mabadiliko hayo yataendeshwa na mwanamke na mwanaume, wote wakaiwa pamoja.

Uelewano mdogo huo kati ya mwanaume na mwanamke na ambao unaotegemea jinsia waweza komeshwa kama kunakusudiwa:

usawa haki: haki zigabuliwe sawa sawa kati ya mme na mke;usawa katika kupewa mshahara: mke na mme waishi katika hali moja ya kijamii;usawa katika bahati za kila mmoja kati yao;usawa wa uwezo na uongozi wa maisha ya kila mmmoja binafsi;kuwa na zamiri, kujiaminia binafsi, na pia wanawake wafikilie rasilimali na uongozi wake.

•••••

© T

etsh

im

Marie-Antoinette Saya

��

f

��

Mada ya nne

Umuhimu wa jinsia katika mawasiliano kwa ajili ya maendeleo

IFASIC, Institut Facultaire des Sciences de l’Information et de la Communication

Kwa kuwa maendeleo inahusu wote, wanawake na wanaume wanastahili kuchanga fikra zao sawa sawa makusudi ya kukamilisha maendeleo na ili ilete faida kwa wote. 

Kwa ajili ya kuingiza jinsia katika mawasiliano kwa ajili ya maendeleo, ni sherti wanawake wapewe nafasi ya kusikilisha sauti yao. Wataweza hivi kuzungumza na kupana maoni yao kuhusu mawsala zenyi kuangalia jamii yao kwa jumla. 

Wanawake, kama vile wanaume, wanapashwa kuwa watumishi wenyi bidii kwa manufaa ya maendeleo, na pia ni wao ndiyo wanafaidishwa na ujio wa maendeleo. 

Ni pia jambo la muhimu kuingiza matatizo ambayo wanayo wanawake kwa kipekee katika mawasiliano: kukomesha umaskini, kutojua kusoma na kuandika, kutomiliki udongo, kutoshiriki kwenyi siasa, ujeuri dhidi ya wanawake, unyonge wa zaidi wa mwanamke kukabiliwa na ugonjwa wa ukimwi, ukosefu wa matunzo na pato kwa kununua dawa, vifo vya wanawake wakati ya kuzaa kwa sababu ya ukosefu wa matibabu ya kawaida wakati wa kujifungua, kutoshiriki kwenyi 

vyombo vya habari kutofikilia mkopo, shida katika impango ya usalama wa chakula, na kadhalika.

Yajulishwa kuwa redio ya kijamii ni njia halali ya kuruhusu watu wote kwa jumla wajitetee. Redio ya kijamii ni chombo cha maelezo YA jamii wala sio chombo cha maelezo KWA watu wote.

© T

etsh

im

© D

imit

ra

Espérance Bayedila

�6 ��

f

Mawasiliano kuhusu jinsia na maendeleo

Mkurugenzi wa mradi Dimitra (FAO)

Mwelekeo wa jinsia huchunguza kazi muhimu zenye kuendeshwa baina ya wanawake na wanaume na pia kulinganisha uwezo wanao binafsi na ndani ya kikundi. Neno jinsia la onyesha kwa uwazi ya kwamba shuguli ziendeshwazo na wanawake na pia wanaume zimetajwa na kupewa na watu wala sizo za kizalikio. Kwa hiyo, hayo yote yaweza kubadilishwa kwa ajili ya kuruhusu ushirika wa wote kwa maendeleo kupitia ngazi mbalimbali; bila kutupilia mbali kama kuna tofauti fulani zilizopo baina ya mwanamke na mwanaume. 

Jinsia iuna msinji wake katika haki za binadamu ambamo kila mtu anastahili achaguwe kinachopendeza maisha yake, bila kutia mkazo juu ya aina ya ki-utu yake. Ndio maana habari kamilifu na mahusiano ni ya muhimu sana.

Kwa ajili ya kuendesha mawasiliano yenyi kulenga maendeleo, mwendeshaji wa mawasiliano anapashwa:

kugusia mambo yenye kuelekea wanawake na wanaume, mambo hayo yanapaswa kuchaguliwa na wanawake na wanaume wenyi kushiriki pamoja;kukusudia sura za wanawake na wanaume zilizo za kweli, za jumla na wala sizo za ufananisho usio na ukweli wowote;kuchungua matatizo ya jinsia kupitia maulizo yafuatayo: nani, nini, wakati gani, wapi na namna gani;kutumia neno jinsia na kukusudia kuliingiza katika maisha yao ya kila siku kwa ajili ya kupasha habari kwa namna inavyofaa na kujizuiza kutangaza habari za kufananisha (jinsia huanza nyumabani mwa kila mtu);kuraisisha ufikiliaji kwa ufahamu na kusaidia mabadiliko ya tabia itimizwe;kutafuta na kutangaza habari mukiwapa kauli wote kwa jumla: wanawake na wanaume.

© D

imit

ra

Eliane Najros

�6 ��

f

Mada ya nne

Kuingizwa kwa mwelekeo wa jinsia katika nyarakati za urekebishaji na ujenzi upya

Mshauri kwenye PNUD (Programme des Nations Unies pour le Développement)

 Kïisha vurugeni, kipindi cha mpito ni wakati wa muhimu na wenyi maffa sana kwa kuimarisha mabadiliko ya uongozi wa kiserkali kwa ajili ya kutimiza usawa kati ya wanawake na wanaume. 

Nchini RDCongo, ni vema kanuni kuhusu uhusiano kati ya mwanamke na mwanaume igeuzwe kuwa sheria. Kanuni hiyo inayokubaliwa na katiba ya inchi inapashwa kujitokeza pia ndani ya mageuzi kuhusu sheria, sekta ya usalama na katika vipindi vyote vya mbinu za uongozi bora humu inchini. Kuhusu uchaguzi, inafaa kuwe kanuni ambayo inasisitiza uwakilishi wa wanawake kwa idadi sawa sawa na wanaume, inafaa sheria ya uchaguzi yenyi mageuzi ya sheria ili mke na mume wawe sawa ndani ya vyama vya kisiasa, mipango ya kisiasa yenyi kuheshimu kanuni ya usawa na katika kushiriki kwa wanawake katika uchaguzi.

Kwa ajili ya kupiganisha umaskini, mwelekeo wa jinsia wapashwa kuingizwa katika miradi yote yenye kuhusu maendeleo ya kijamii na katika miradi ya kutoa mazao ukiwemo mkopo mdogo wa kipesa. Yafaa kujumlisha ushirika wa wanawake katika utekelezaji wa hatua na kuruhusu ushirika wao kama vile washiriki pahali pa kuendelea kuwalinganisha na vikundi vya wanyonge siku zote.

© D

imit

ra

Augusta Angelucci

�� ��

f

Matokeo ya uhaba wa habari na mawasiliano dhidi ya wakaaji vijijini

Ahusikaye na mawasiliano kwenyi shirika FAO-RDC

Mawasiliano humaanisha mololngo wa mazungumzo ya ana kwa ana ao kupitia vyombo vya habari. Inaruhusu washiriki kugawanya habari. Mawasiliano ya muhimu katika kazi za maendeleo.

Ukosefu wa habari unasababisha vinyume vifuatavyo: 

kutofikilia mambo mapya kwa ufahamu;uhaba wa mkutano na majadiliano kati ya watu;uhaba wa habari kuhusu uvumbuzi mpya.

•••

Tizama mifano ya vinyume vya ukosefu wa habari: ginsi matokeo ya uchaguzi imekubaliwa ao hapana, magumu ya kupinga magonjwa yenye kushambulia watu wengi kwa rafla, kuto elewa vema beyi za bizaa kwenye soko, uhaba wa malipizi kwa wenye kutenda maovu, kunyanganya na kusumbuwa watu vijijini.

Namna ya kukomesha hali hii ni kutumia vyombo vya habari vya kijamii vinavyofaa, kama vile redio, taarifa ya habari, gazeti, televisheni, uhimizaji vijijini,… Kupendelea kimoja ao kingine kati ya vyombo hivyo vya habari hulingan na idadi ya wakaaji wenyi kuhusika, ngazi ya pato lao, uwezo 

© D

imit

ra

Phuna Mabika Dakeini

�� ��

Mada ya nne

wanao wa kupokea vyombo vya habari, hali ya elimu ya mlimo, maadibisho ya afia na kazalika.

Vijiji mwa bara la Afrika, redio ndio njia kamilifu ya kutangaza habari na kurahisisha majadiliano. Redio ni chombo 

ambacho kina uwezo wa kukomaza mahusiano kati ya watu wanaoishi pamoja. Redio inasaidia kutosha watu 

katika ujinga. Vivi hivyo, chombo hicho kina ruhusu watu wawe karibu ya viongozi wa serikali.

© T

etsh

im

�0 ��

f

Faida ya kusimika redio katika vijiji

Chumba cha utafuti na utawanyo kwenye FAO

Kufwatana na uhaba wa vyombo vya habari na ugumu wa kuvifikilia (televisheni na gazeti), redio yaaminika leo kuwa ndicho chombo habari cha walio wengi na yenyi kuwa na uwezo wa kusisimua zamiri, kutangaza habari na pia kuhimiza wakaaji vijijini. 

Matumikio yake ya pekee: utumiaji wa lugha za nyumbani, utumiaji wa habari kuhusu mahitaji na pi zenti kutazamia mila za vikundi, mada moja ambamo munaweza kuigizwa habari kuhusu sekta za kiuchumi, za kijamii, za kitamaduni, … 

Ila haziweze pekee yake kufanya lolote kufwatana na magumu mengi ya kisiasa, ya kiuchumi, uhaba wa mafunzo ya wahimizaji na wapasha habari. Ndio maana yafaa kuunda mifumo za redio za kijamii ambamo redio zinapata mahali pa kukutana, kuhojiana, kutenda pamoja na pia kubadilishiana maoni na ujuzi. ©

 Dim

itra

Jaime Almenara Merel

�0 ��

f

Mada ya nne

Redio za kijamii na vikundi vya wasikilizaji katika jimbo la Kivu ya Kusini

SAMWAKI, Sauti ya Mwanamke Kijijini

Ukosefu wa vyombo vya kutawanya habari na mawasiliano unazuia kuinuka kwa mwanamke wa vijiji na inageuka kuwa kinyume kwa maendeleo ya jamii kwa jumla. Redio ya kijamii yaweza kutimiza vizuri kazi hiyo ya kuatawanya habari na kusisimua maedeleo vijijini. Uwepo wa redio ya kijamii vijijini itasukuma mwanamke ashirike katika mipangilio na katika vipindi vyake. Na hiyo itasisismua maendeleo. 

Kikundi cha wasikilizaji ni kukundi cha watu ao shirika ya watu wenyi kujitolea kwa ajili ya kusoma, kusikiliza vipindi vya redio na nia ya kuhojiana na kutenda kwa ajili ya maendeleo. Kikundi hicho kinashurulika zaidi na kazi ya kupekua siku kwa siku habari na vipindi mbalimbali kutoka redio. Vikundi hivyo vinasaidia watu kuelewa taarifa ya habari na kutenda ipasavyo kwa kulet maendeleo ya wanameba wake binafsi na ya mahali waishimo kwa jumla.

Ni kupitia vikundi hivyo ndipo mwanamke wa Kivu ya Kusini anajitetea na kusikilizwa. Magumu yenye kumukabili yanajulikana waziwazi. Ni hapo wanaume na wanawake wanaoishi vijijini wanaitwa wajiunge pamoja makusudi ya kupiganisha kutawanywa kwa ugonjwa wa ukimwi. Kikundi cha wasikilizaji ni cha muhimu sababu kinaruhusu watu waelewe vizuri na kuelewesha wengine.

Jimboni mwa Kivu ya Kusini, vikundi vya wanawake wa vijiji na wapasha habari wa redio za kijamii za hukutana mara kwa mara na kuhojiana kuhusu maedeleo. Mikutano yao hufuatana na ushirika wanaoutarajia na ambao unalenga kutangaza habari kuhusu maendeleo. Kazi zao zaendeshwa katika kukitizamiwa usawa kati ya mwanamke na mwanaume, na ushirika kati ya vikundi hivyo viwili, bila ubaguzi. Kwa jumla, vikundi tisa vya wasikilizaji vimesimikwa mwishoni mwa mwezi wa pili mwaka wa 2007 kwa msaada wa projet Dimitra na Fondation Roi Baudouin.

© D

imit

ra

Adeline Nsimire

�� ��

f

Mitindo mbalimbali ya vipindi vya redio

Chumba cha utafiti na utawanyo kwenye FAO

Kuna mitindo nyingi ya vipindi vya redio: vipindi vya kushirikisha watu wengi, michezo ya kuigiza, mazungumzo, upelelezi, mahojiano, taarifa za habari,  maadibisho, na kazalika. 

Utafiti, uchambuzi na utangazaji mwema unamaanisha kuwa mpasha habari anazingatia mitindo hiyo mbali mbali na pia visima vya kuchtea habari (watu, mashirika,…). Ufundi wa kutafuta habari ni: kuhojiana na mtu, matokeo na pia uchunguzi. Kila kipindi kina vipengele vyake vya pekee. Mahojiano ndiyo ufundi wa utafiti wa habari yenyi kutumikishwa zaidi katika mipango za redio.

© T

etsh

im

Jaime Almenara Merel

�� ��

f

Mada ya nne

Kupata habari kuhusu kazi za mlimo katika miji mikubwa na kandokando zake

Mshauri ahusikaye na kulinda bustani kwenye mradi wa HUP akiwa pia kiongozi k wenye chumba cha SENAHUP mjini Lubumbashi

Mradi HUP unaoendeshwa na FAO makusudi ya kujumlisha mazao ya mlimo na kuyauzisha kwa uwingi sokoni. Shabaha ingine ya HUP ni kutolea wahusika ambao ni watu wasiojiweza waishio mjini na kandokando yake, hasa vikundi vya wanawake na vijana. Ukomo ni kuimarisha usalama katika malisho. 

Mradi wa HUP unaendesha kazi za kuonekana kwa faida ya wanawake ambao wanatimiza kazi mhimu katika mlimo. Mradi huo unaendesha mikutano ya mafunzo na kutolea habari kuhusu maji safi, utumiaji wa dawa za mimea, uongozi wa mazao ya mlimo, kuuzisha, mkopo wa feza na pia maadibisho ya malisho bora,... Inaendesha pia shule shambani. Ukomo ni kuongeza samani ya kazi zinazo fanywa na wanawake ili hali yao irekebishwe ki-jamii na ki-uchumi. 

© B

MH

-L’s

hi/H

UP 

FAO

/RD

C

Grégoire Mutshail

�� ��

Kuhusu metodolojia ya mawasiliano, redio inabaki kuwa chombo chenyi nguvu na chenyi kuomba malipo madogo kwa ajili ya kuwasukumia wakulima wenyi kupatikana mahali pasipo wepesi wa mawasiliano habari muhimu. Pia habari zitaolewa kwenye simu ya mukononi kwa ajili ya kujulishana mabadiliko ya sasa hivi ya bey ya vizaa sokoni.

© D

imit

ra

�� ��

f

Mada ya nne

Mada ya nne - Jinsia na mawasiliano kwa ajili ya maendeleo na njia bora ya kufililia habari muhimu na mawasiliano

Mapendekezo

Kwa washiriki:

Kuunda mahali pa kuendesha mahojiano kati ya redio za kijamii na mashirika za wanawake wa vijiji kwa ajili ya kurusu makundi yaisiyo vijijini kushiriki kwenyi mahojiano na mabadilishaiano fikra na ujuz.Kushawishi na kuimarisha ushirika wa wanawake wa vijiji katika njia za mawasiliano ya kusisimua maendeleo. Mwanamke apewe chombo cha kupokea habari sawa vile redio, ashirikishwe katika vikundi vya wasikilizaji, na pia ahusishwe na mpango wa matayarisho ya vipindi mbalimbali na utangazaji wa vipindi kwenye redio ya kijamiii. Kwa hiyo, kutatengenezwa upya mipangilio ya vipindi ambavyo vitatiliya mkazo shuguli za vikundi.Kutangaza vipindi katika lugha za nyumbani.Kufanya iwezekanavyo kusudi mwelekeo wa jinsia iingizwe katika mipango yote ya redio za kijamii na kuruhusu uwezekano wa wake kupitia kazi zenyi kuendeshwa na vikundi vya wasikilizaji ambavyo vinaongozwa na wanawake.

Kwa kazi za serikali na zile za kipekee:

Kuheshimu na kutumia sheria: uhuru wa upashaji habari, habari kuhusu haki za binadamu, haki za wanawake, wapasha habari wasifungiwe njia ya kupata habari.Kurahisisha kushimikwa kwa redio za maendeleo vijijini na vikundi vya wasikilizaji.Kuzitolea redio za kijamii msaada wa kifedha.

Kwa mashirika yenyi kutoa misaada ya kipesa:

Kusaidia wahusika wenye kuendesha kazi ili wapate ujuzi: Kuunda mahali pa mazungumzo kati ya redio za kijamii na mashirika za wanawake wa vijiji, kusimika vikundi vya wsaikilizaji wakiwemo wanawake wa vijiji kwa idadi sawa sawa na wanaume.Kuhudumia kiufundi na kwa kipesa redio za kijamii na vikundi vya wasiklizaji vya maeneo za vijiji.

••

••

�6 ����

© D

imit

ra

�6 ����

Hitimisho kubwa za kikao

Wahuzuriaji kwenyi mkutano walikubaliana kutowa hitimisho zifuatazo:

Kufikiria kupata habari muhimu na mafunzo: kutawanywa kwa sheria mbalimbali, habari kuhusu haki za binadamu, kupiganisha ugonjwa wa ukimwi, kustawisha siasa ya kuruhusu watu wapewe habari muhimu na kuwasiliana katika maeneo za vijiji nchini kote.

Kuzidisha ujuzi: wa miungano ya maendeleo vijijini na vyumba vya sheria, kuwasiliana katika lugha za nyumbani, kuelimisha wanawake wanaoishi vijijini kujua kusoma na kuandika.

Utetezi na muuungano katika mfumo kupoitia ngazi mbalimbali, ni kama vile viongozi wa asili, viongozi wa makanisa, miungano ya maendeleo, vyumba vya kazi za serikali na wanaotolea pesa.

Ushirika wa vikundi vya nyumbani; kuimarisha ushirika wa wote, kuzidisha mazungumzo kati yao, kuunda miungano, kuendesha matembezi ya kubadilishana maoni na kazalika.

Kutawanya ufahamu: kutangaza habari mpya bila kukawiya na kuwajulisha wanamemba wa ngazi zote matokeo ya kikao hiki.

Kuwa mwangalifu wa jinsia katika njia zote za kazi za maendeleo.

��

Anuani zetu

REFED, Réseau Femme et Développement

Bernadette Kapend

491 Av. Likasi, bâtiment Labo Médical

Lubumbashi, RDC

tél : +243 81 8152771 

e-mail : [email protected] et [email protected]

CONAFED, Comité National Femme et Développement

Elise Muhimuzi

Avenue Mutombo Katshi 7

Commune de la Gombe

B.P. 5.744

Kinshasa, RDC

tél : +243 99 9918406

e-mail : [email protected]

Kuhusu mawasiliano na habari ingine muhimu,

inabidi kujiunga na kikundi cha DIMITRA mjini Bruxelles:

Dimitra

Eliane Najros, Coordinatrice

21, Rue Bréderode

B-1000 Bruxelles

Belgique

tél : + 3225490310

fax : + 3225490314

e-mail :[email protected]

© G

ulda

ElM

agam

bo

© D

imit

ra

© G

ulda

ElM

agam

bo

Mkutanokuhusu uwezekano wa kukadiria habari muhimu na majadiliano mengine yenye kuelekea usawa kati ya mume na mke katika miungano ya vijijini

na kwenye vyombo vya matangazo visivyo vya ki-serikali katika jimbo la katanga, nchini jamhuri ya kidemocrasia ya congo

lubumbashi, tarehe nne hadi nane mwezi wa sita mwaka wa 2007

Tarehe nne hadi tarehe nane mwezi wa sita mwaka wa 2007, une fanyika

mjini Lubumbashi, mji nkuu wa jimbo la Katanga, mkutano kuhusu

uwezekano wa kukadiria habari muhimu na majadiliano mengine

yenye kuelekea usawa kati ya mume na mke katika miungano ya vijijini

na kwenye vyombo vya matangazo visivyo kuwa vya kiserikali.

Mkutano huo ulioendeshwa chini ya wongozi wa shirika lenye kutetea

maendeleo ya wa mama wa Katanga (refed-Katanga), ulisaidiwa na

mpango wa dimitra/fao, msinji wa mfalme wa ubelgiji (Fondation

Roi Baudouin), uhusiano na Canada (Coopération canadienne),

uhusiano na Ugerumani ki-afia (gtz-Santé), uhusiano ki-ufundi na

ubelgiji (ctb), unfpa, pnud na pia conafed.

Chaïda hii imetayarishwa kwa msaada wa fedha kutoka uhusia na

Canada (Coopération canadienne) na Fondation Roi Baudouin.

Le Projet Dimitra bénéficie du soutien financier du Service Public Fédéral des Affaires Etrangères, Commerce Extérieur et Coopération au Développement (DGCD) Belgique et de la

Fondation Roi Baudouin.

swahili