40
(MITAZAMO YA WASHIRIKI WA WARSHA) Mtazamo Wangu WARSHA YA WAVIU WASHAURI ILIYOFANYIKA MWANZA, MEI 2014 Chapisho hili lilisimamiwa kwa Ruzuku au Mkataba wa Ushirika Namba 542GGH000436-04, unaofadhiliwa na Kituo cha Kudhibi na Kuzuia Magonjwa. Maudhui yaliyomo ni wajibu wa waandishi na hayawakilishi maoni rasmi ya Kituo cha Kudhibi na Kuzuia Magonjwa au Idara ya Afya na Huduma za Binadamu.

Mtazamo Wangu - agpahi.or.tzagpahi.or.tz/phocadownload/Waviu_Washauri_Book.pdf · (MITAZAMO YA WASHIRIKI WA WARSHA) Mtazamo Wangu WARSHA YA WAVIU WASHAURI ILIYOFANYIKA MWANZA, MEI

  • Upload
    others

  • View
    28

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

(MITAZAMO YA WASHIRIKI WA WARSHA)

Mtazamo Wangu

WARSHA YA WAVIU WASHAURI ILIYOFANYIKA MWANZA, MEI 2014Chapisho hili lilisimamiwa kwa Ruzuku au Mkataba wa Ushirika Namba 542GGH000436-04, unaofadhiliwa na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia

Magonjwa. Maudhui yaliyomo ni wajibu wa waandishi na hayawakilishi maoni rasmi ya Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa au Idara ya Afya na Huduma za Binadamu.

MTAZAMO WANGU © Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative

Kitalu Na. 373, Mtaa wa Mtitu, Barabara ya Umoja wa Mataifa, Upanga Mashariki, S.L.P. 38252, Dar es Salaam, Tanzania. Simu: +255 22 150790, Faksi: 25 22 2152748

Na:Kitalu Na. 152 &154, Barabara ya Kenyatta, Majengo, Shinyanga.

S.L.P.: 1368 | Shinyanga. Simu: +255 28 2764005

Haki zote zimehifadhiwa

Toleo la Mei 2014

Maelezo yalitotumika katika kitabu hiki, ni maandiko halisi yaliyoandikwa na WAVIU Washauri. Shirika limeboresha kwa kuyachapa maelezo hayo.

Warsha ya WaVIUWashaUrI

Victoria Palace, Mwanza, 20-22 Mei, 2014

Mtazamo Wangu

i

ii

iii

Yaliyomo

Orodha ya Vifupisho...................................................................................... iv

Dibaji.......................................................................................................... v

Utangulizi.................................................................................................... 1

shukurani.................................................................................................... 3

WaVIU WashaUrI

Maximilian Msengi................................................................................ 4

Daudi abdallah...................................................................................... 5

Mashauri Charles................................................................................... 6

Daniel richard....................................................................................... 6

happiness Malamala................................................................................ 7

hellena Ng’hyama................................................................................... 8

amos Molongwe..................................................................................... 9

Ziara ya kutembelea Bohari ya Dawa, Kanda ya Ziwa, Mwanza............................ 10

Joyce Philimon..................................................................................... 12

sebastian Ngusa.................................................................................... 12

Ziara ya kutembelea Bohari ya Dawa, Kanda ya Ziwa, Mwanza............................ 13

sitta sakasaka...................................................................................... 15

Magreth Masalu..................................................................................... 16

hamis shigella...................................................................................... 17

Kanzaga Fabian..................................................................................... 18

regina anthony................................................................................... 19

Cosmas shimba..................................................................................... 20

Grace andrea....................................................................................... 22

Daudi Marco.......................................................................................... 23

Victoria Joseph.................................................................................... 24

Paul Ngasa........................................................................................... 25

Felista Bilia.......................................................................................... 26

Philip singili......................................................................................... 27

agatha Venance ................................................................................... 28

Modester Magedi................................................................................... 29

Gregory Paulo....................................................................................... 30

hitimisho..................................................................................................... 31

Matukio katika picha.................................................................................... 32

iv

Orodha ya Vifupisho:arV - antiretroviral Drug (Dawa za kufubaza VVU)

CDC - Centres for Disease Control and Prevention

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa

CTC – Care and Treatment Centre (Vituo vya Utoaji huduma ya Tiba na Matibabu)

LTF - Lost to follow (Mteja aliyepotea katika huduma)

MDGs - Millennium Development Goals

(Malengo ya Maendeleo ya Milenia)

MIssaP - Missed appointment (Mteja aliyekosa mahudhurio)

MsD - Medical stores Department (Bohari ya Dawa)

NaCOPha - The National Council for People Living with hIV/aIDs Tanzania

(Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU na UKIMWI)

NMsF III - National Multi-sectoral strategic Framework III

(Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI III)

PMTCT - Prevention of Mother to Child Transimission

(Kuzuia Maambikuzi ya VVU Kutoka kwa Mama Kwenda kwa Mtoto)

rCh - reproductive and Child health (afya ya Uzazi na Mtoto)

UKIMWI – Upungufu wa kinga mwilini

VPP - Voluntary Pulled Procurement (Manunuzi ya pamoja kwa hiari).

VVU – Virusi vya UKIMWI

v

Dibaji:

Miaka ya hivi karibuni, Tanzania imepata mafanikio katika mapambano dhidi ya UKIMWI kupitia utekelezaji wa miradi ambayo inatekelezwa na wadau mbalimbali pamoja na Wizara ya afya.

Kutokana na jitihada hizo, kiwango cha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kimeonekana kupungua kutoka 5.7% mwaka 2008 hadi kiwango kinachokadiriwa kuwa 5.1% mwaka 2012 (Utafiti wa Viashiria vya UKIMWI na Malaria wa mwaka 2011/2012)1.

Licha ya mafanikio yanayoonekana katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, unyanyapaa na ubaguzi umekuwa ukidumaza jitihada za kutokomeza UKIMWI nchini. hii ni dhahiri kuwa unyanyapaa katika huduma za afya na kwingineko vinachangia kukwamisha ufikiwaji na utumiaji wa huduma kinga, tiba na matunzo pamoja na tabia chanya zinazomzuia mtu asijiweke katika hatari ya kutopata huduma za afya.

Kwa kulitambua hilo, aGPahI ikaamua kuanzisha programu ya kuwatumia WaVIU Washauri katika kupiga vita unyanyapaa na ubaguzi ili kufanikisha adhma ya mtu asijiweke katika hatari ya kutopata huduma ya afya.

Ili kuweza kupambana na unyanyapaa na ubaguzi katika huduma ya afya, WaVIU wanatakiwa kujengewa uelewa kamili juu ya kujitambua kuwa wao ni nguzo muhimu katika kupiga vita unyanyapaa.

Ni imani yangu kwamba uanzishwaji wa programu hii ya kuwaelimisha WaVIU italeta ufanisi katika jitihada zilizopo za mapambano ili kutokomeza UKIMWI nchini Tanzania.

Mwisho ningependa kuwakumbusha kuwa, Tanzania bila UKIMWI inawezekana!

………………………………………………..

Laurean Rugambwa BwanakunuMkurugenzi Mtendaji.

1 Kwa kiingereza ‘Tanzania HIV and Malaria Indicator Survey 2011/2012’

MTAZAMO WANGU | 1

Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) yameainisha kuwa moja ya lengo ni kuzuia na kupunguza maambukizo mapya ya virusi vya UKIMWI. aGPahI kama shirika mojawapo linaloshiriki katika jitihada za kuzuia na kupunguza maambukizi mapya ya VVU nchini Tanzania, limeazimia kuhakikisha lengo hili la milenia linatimia.

aGPahI inafanya kazi kwa kushirikiana na halmashauri katika mikoa ya shinyanga, simiyu na Geita katika kutoa huduma ya tiba na matibabu, kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na uzazi wa mpango.

Katika utelekezaji wa kazi zake, aGPahI hushirikiana pamoja na WaVIU washauri waliopo katika vituo mbalimbali vya utoaji huduma ya tiba na matibabu (yaani CTC) vilivyopo katika zahanati na hospitali. WaVIU hao hujitolea katika kufanya kazi mbalimbali kama vile:1. Kusaidia katika shughuli za CTC kama vile kupanga mafaili, kutafuta na kupanga

mafaili ya wateja na kupima uzito siku za huduma2. Kutoa elimu sahihi kuhusu UKIMWI, na inapobidi kuwapeleka watu kwa mshauri

mtaalamu ili kupata elimu zaidi,3. Kutoa ushuhuda wa uzoefu wao kama watu wanaoishi na maambukizi ya VVU na

watumiaji wa dawa kwa ajili ya ufuasi sahihi wa dawa kwa wenzao,4. Kutembelea wagonjwa majumbani,5. Kutafuta wateja waliopotea,6. Kutoa rufaa kwa wagonjwa kutoka katika jamii ili kurudi katika kituo cha afya kupata

huduma.7. Kuanzisha na kusimamia vikundi vya WaVIU na Watoto wanaoishi na maambukizi ya

VVU.

Kwa kuthamini kazi za WaVIU washauri, aGPahI iliandaa warsha ya siku tatu (3) ili kuwaongezea uwezo, elimu, ujuzi na kubadilishana uzoefu wa kazi zao za kujitolea. Warsha hii ilifanyika Mwanza kuanzia tarehe 20-22 mwezi Mei mwaka 2014.

aGPahI kupitia Kitengo cha Mawasiliano na Huduma za Mkoba kwa Jamii kwa kushirikiana na Kitengo cha Huduma Unganishi kwa Jamii ndio walioandaa warsha hii. Katika siku 3 za warsha, WaVIU washauri walipata mada mbalimbali kama vile:1. Umuhimu wa kuwa MVIU wa kujitolea, faida na changamoto zake, 2. Kazi za MVIU anayejitolea,3. Ufuatiliaji wa wateja waliopotea,4. Uzoefu wa MVIU katika ngazi ya taifa, kazi zinazofanywa na changamoto zinazojitokeza,5. Ufahamu juu ya Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NMsF III). Kujua vipaumbele

na maeneo ambayo yana ufadhili wa kusaidia vikundi,6. Kufahamu jinsi ya kuandaa maandiko ya halmashauri - kwa maeneo ambayo

yametengewa fedha,7. Uhamasishaji wa watoto kujiunga kwenye vikundi.

Watoa mada katika warsha hii walikuwa Bwana Vitalis Makayula, Mwenyekiti kutoka Baraza

Utangulizi

2 | MTAZAMO WANGU

CECILIA YONA – KITENGO CHA HUDUMA UNGANISHI ZA JAMII

JANE SHUMA – KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA ZA MIKOBA.

la Taifa la Watu wanaoishi na VVU na UKIMWI (NaCOPha)2, Dkt. Gastor Njau, Meneja wa Miradi kutoka aGPahI, Jane shuma, Mratibu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma za Mkoba kwa Jamii, aGPahI pamoja na Cecilia yona, Ofisa Miradi wa Kitengo cha Huduma Unganishi kwa Jamii, aGPahI.

Mbinu zilizotumika katika uendeshaji wa warsha hii ni utoaji wa mada, maswali na majibu na majadiliano kwa makundi. Pia WaVIU walitembelea Bohari ya Dawa (MsD) ya Kanda ya Ziwa, Mwanza pamoja na hospitali ya rufaa ya Bugando kwa lengo la kujifunza. Kadhalika, WaVIU washauri waliwezeshwa kuandika mpango kazi ambao utawasaidia katika utendaji kazi pindi wanaporudi katika maeneo yao ya kazi. Kabla ya kukamilisha warsha, WaVIU waliombwa waandike mitazamo au maoni yao kuhusu warsha na nini kiboreshwe. hivyo basi, kurasa zinazofuata ni mitazamo na maoni ya WaVIU ikiambatana na picha zao. Mitazamo hiyo imewekwa katika muundo wa kijitabu.

asanteni sana na furahieni kusoma kitabu hiki.

2 The National Council for People Living with HIV/AIDS Tanzania

MTAZAMO WANGU | 3

Shukurani

shukurani ziwaendee wafadhili wetu Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) kwa kuwezesha kuchapisha kitabu hiki.

Pia tunawashukuru watu mbalimbali waliochangia katika uandishi wa kitabu hiki.

Mwisho, tunalishukuru Baraza la Kiswahili la Taifa (BaKITa), kupitia Idara ya Lugha na Fasihi, kwa kukisoma kitabu hiki na kutupa Ithibati.

4 | MTAZAMO WANGU

Maximilian MsengiKijiji: NgalilaCTC anayohudumia: Kituo cha afya Ngulyati Halmashauri ya Mji wa BariadiMkoa wa Simiyu

UtangULizi:Natoa shukurani za dhati kwa Meneja wa aGPahI wa Mkoa wa shinyanga pamoja na wafanyakazi wenzake kwa kunipatia mwaliko wa kuhudhuria warsha ya siku tatu kuanzia tarehe 20 – 22 Mei 2014 mkoani Mwanza. Pia nawashukuru wanawarsha wenzangu kwa kunichagua kuwa Mwenyekiti katika warsha hii. Ninawashukuru sana.

Mimi Maximilian J. Msengi, MVIU mshauri wa kujitolea kutoka CTC ya Kituo cha afya cha Ngulyati. Elimu niliyoipata nimeielewa na nitawajibika na kutekeleza kadiri ya uwezo wangu kwa kufanya mambo yafuatayo:i. Kutoa mwitiko wa warsha kwa watoa huduma wa

afya wa CTC ya Ngulyati.ii. Nitaandaa mpangokazi.iii. Naahidi kutekeleza yote nitakayopanga.

Matarajio yangu:1. Warsha ya WaVIU washauri wa kujitolea iwe

endelevu na ifanyike mara kwa mara.2. Warsha ni nzuri, inatuongezea maarifa

mapya na juhudi za utendaji kazi.3. Tunabadilishana uzoefu wa utendaji

kazi.4. Pia tumefahamiana na kutambuana.

Natanguliza shukurani zangu.Mawasiliano yangu ni: 0682 962010 na 0768 762099

4 | MTAZAMO WANGU

MTAZAMO WANGU | 5

Daudi AbdallahKijiji: MwabuzoCTC anayohudumia: Zahanati ya MwabuzoWilaya ya MeatuMkoa wa Simiyu

Kuhusu warsha ya WaVIU, mtazamo wangu

ni kuwa:1. WaVIU Washauri wameongeza uelewa

juu ya shughuli zao.

2. Klabu za ariel zitaanzishwa kwa wingi

katika vituo vya CTC na vikundi vya

WaVIU.

3. huduma za CTC zinazotolewa zitakuwa

bora zaidi.

Nashukuru kwa shughuli zinazofanywa na

aGPahI kwa kuwezesha warsha hii.

MTAZAMO WANGU |

6 | MTAZAMO WANGU

Kijiji: IgulwaCTC anayohudumia: Hospitali ya wilaya ya Bukombe Wilaya ya Bukombe.Mkoa wa Geita.

Daniel Richard

Mtazamo wangu katika warsha hii ya WaVIU washauri ni jinsi ya kuhudumia wagonjwa kuanzia

uhamasishaji katika jamii kuanzia ngazi ya vitongoji katika vipimo vya awali. Unasihi

ni jambo la msingi ili kupunguza makali ya VVU katika jamii nzima ili kuwarejesha

watu kupima kwa hiari. Nitaendelea kuhamasisha katika CTC niliyopo, nitaendelea kuhamasisha mpaka mwisho

wa maisha yangu.

Ninatoa shukurani kwa wawezeshaji.

Mashauri Charles

Mtazamo wangu kuhusu warsha ya WaVIU washauri:1. WaVIU washauri watakwenda kutekeleza majukumu

yao ipasavyo, ikiwamo:(a) Ufuatiliaji wa watoro wa huduma

za CTC na PMTCT.(b) Kwenda kuanzisha Klabu za ariel

katika CTC za wilaya, vituo vya afya na zahanati.

(c) Kuboresha huduma zinazotolewa katika CTC.

Mwisho:Nashukuru shirika la aGPahI na wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kufanikisha warsha hii.

Happiness Malamala

Kijiji: ChamboCTC anayohudumia: Hospitali ya wilaya ya UshetuHalmashauri ya wilaya ya Ushetu.Mkoa wa Shinyanga.

6 | MTAZAMO WANGU

MTAZAMO WANGU | 7

Happiness MalamalaKijiji: SomandaCTC anayohudumia: Hospitali ya SomandaHalmashauri ya Mji wa Bariadi.Mkoa wa Simiyu

Mtazamo wangu wa warsha ya WaVIU washauri

iliyofanyika katika Mkoa wa Mwanza ni kuwa

nimefufahi na pia nimepanua elimu toka kwa

WaVIU washauri wenzangu.

Natoa shukurani za dhati kwa Meneja wa aGPahI

wa Mkoa wa shinyanga pamoja na wafanyakazi

wenzake kwa kunipatia mwaliko wa kuhudhuria

warsha kama hii katika Mkoa wa Mwanza. Pia

nawashukuru wana warsha wenzangu kwa

kunichagua kuwa mtunza muda katika warsha

hii.

MTAZAMO WANGU | 7

8 | MTAZAMO WANGU

Hellena Ng’hyamaKijiji: KabaleCTC anayohudumia: Kituo cha Afya ZagayuHalmashauri ya wilaya ya Itilima.Mkoa wa Simiyu

Nimefurahi kushiriki katika warsha hii kwani inasaidia kuimarisha vikundi, kuwakumbuka wenzetu walio na maambukizi ya VVU na UKIMWI na kuwahamasisha wajiunge kwenye vikundi. Bila kuwasahau watoto ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ya kujikinga na afya zao, kuwatembelea katika jamii zao na kuwaelewesha kuhusu umuhimu wa kujiweka wazi.

Mimi ninao wajibu wa kuwaelimisha wanakikundi wenzangu juu ya yale niliyojifunza hapa ambayo ni:

1. Kuhudhuria kliniki ya WaVIU pamoja na kuwaleta watoto CTC, kupima pamoja na kuchukua dawa.

2. hivyo mimi nitayafanyia kazi haya niliyojifunza katika warsha hii na nitaendelea kushiriki katika vikundi kama kawaida.

asante sana na Mungu awabariki.

MTAZAMO WANGU | 8

MTAZAMO WANGU | 9

Warsha hii ambayo imeandaliwa na aGPahI hapa Mwanza, ni kwa ajili ya watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ambao pia ni wasidizi wa kujitolea (lay counsellors) katika CTC mbalimbali katika mikoa ambayo aGPahI inafanya kazi.Kwa hiyo, lengo la Warsha hii ni kuwaongezea uwezo WaVIU washauri ili kuboresha huduma ya matunzo na matibabu wa WaVIU.

Katika warsha hii, nimekutana na WaVIU wanaohudumia mikoa mitatu ambayo ni shinyanga, simiyu na Geita. Tuliweza kubadilishana mawazo mbalimbali, tulijifunza kuhusu uhamasishaji wa WaVIU wasikose kwenda kliniki na pia utumiaji mzuri wa dawa. Pia tumejifunza shughuli zetu za kufanya pale CTC, kama vile:1. Kupanga mafaili2. Kufanya usafi3. Kupima uzito

Pia tulijifunza namna ya kumrudisha mgonjwa aliyepotea kuhudhuria kliniki, namna ya kuunda vikundi na namna ya utunzaji mzuri wa dawa tunazotumia sisi WaVIU. asante sana na sisi wana warsha tunashukuru.

Amos MolongweKijiji: ByunaCTC anayohudumia: Kituo cha Afya ByunaHalmashauri ya wilaya ya Bariadi.Mkoa wa Simiyu.

MTAZAMO WANGU | 9

10 | MTAZAMO WANGU

siku ya tarehe 21 Mei 2014, majira ya asubuhi, WaVIU washauri walitembelea ofisi za Bohari ya Dawa (MsD) – Ofisi za Kanda ya Ziwa, Mwanza. WaVIU washauri walipokewa na Meneja wa Kanda, Bwana Byekwaso Tabura ambaye aliwaeleza kuwa Bohari ya Dawa ni taasisi iliyopo chini ya Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la kununua, kutunza na kusambaza dawa kwenda kwenye vituo vyote vya afya na hospitali za dini. (sheria Na. 13 ya mwaka 1993).

aliendelea kusema kuwa, kipindi cha nyuma (2004-2008) Bohari ya Dawa ilikuwa inanunua dawa kutoka kwa wafadhili mbalimbali. Lakini kadiri muda ulivyozidi kupita wafadhili wamekuwa wakinunua dawa wenyewe na kuwapatia Bohari ya Dawa. Njia kuu ambayo wafadhili wanatumia kununulia dawa inaitwa Voluntary Pulled Procurement (VPP).

Kwa hiyo, Bohari ya Dawa huhusika sana na kutoa oda ya dawa na vifaa vya hospitali kwa mashirika makubwa ya maendeleo/wafadhili ambayo hufanya manunuzi. hata hivyo, taasisi hii imekuwa na changamoto za kifedha mara kwa mara na hivyo kusababisha Bohari ya Dawa kupata misaada mingi kupitia wadau na mashirika mbalimbali yenye mapenzi mema. Kwa mfano, taasisi imekuwa ikipata ufadhili wa ununuzi wa dawa za aina mbalimbali kama vile dawa za kufubaza VVU (arV), vitendanishi, ununuzi wa magari ya kusambaza dawa, sehemu ya kuhifadhi dawa n.k.

Bwana Tabura pia alitumia muda mwingi kujibu maswali ya WaVIU washauri ambayo yaligusa nyanja za ubora wa dawa, sababu za kubadilishiwa dawa mara kwa mara na uhifadhi mzuri wa dawa. Pia aligusia mkakati uliopo wa Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii wa kutaka dawa zote zisambazwe hadi ngazi

ya Zahanati na si kupitia kwa hospitali za Wilaya. sambamba na mkakati huo ni kutaka oda za Zahanati ziwe zinaenda moja kwa moja Bohari ya Dawa na si kupitia katika hospitali za Wilaya.

Meneja wa Kanda alimalizia kwa kutaja changamoto chache zinazowapata, ukiacha fedha. Miundombinu ya barabara si mizuri hasa wakati wa kipindi cha mvua hivyo changamoto huwa ni kubwa kwenye usambazaji wa dawa. hii husababisha ucheleweshwaji wa usambazaji wa dawa. Changamoto nyingine ni bei za vitendanishi pamoja na dawa za kufubaza VVU ni ghali sana. Kwa hiyo ni jukumu letu kuhakikisha zinatumika kiusahihi na kwa uangalifu.

Mwisho kabisa, WaVIU washauri walitembezwa ndani ya Bohari ya Dawa na kujionea jinsi ambavyo dawa zinahifadhiwa. Meneja wa Kanda alikuwa pamoja nao kwa ajili ya kutoa maelekezo ya kina.

ziara ya kutembelea Bohari ya Dawa,Kanda ya ziwa, Mwanza

Baadhi ya dawa ambazo zimekwisha fungwa kwa ajili ya kupelekwa katika Hospitali ya Kahama mkoani Shinyanga.

MTAZAMO WANGU | 11

Meneja wa Kanda, Bwana Byekwaso Tabura (mwenye koti la kahawia) akitoa ufafanuzi kwa WAVIU washauri waliotembelea Bohari ya Dawa.

12 | MTAZAMO WANGU

Joyce PhilimonKijiji: LuguluCTC anayohudumia: Hospitali ya SomandaHalmashauri ya Mji wa BariadiMkoa wa Simiyu

Kuhusu warsha hii, ninaishukuru sana aGPahI kwa kunipa elimu hii. Nimejua namna ya kufuatilia wagonjwa waliopotea na jinsi ya kuwasiliana nao.

Mimi ni MVIU Mshauri, ninaushukuru uongozi wa aGPahI kwa kunipeleka kwenye Bohari ya Dawa Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kujifunza. Nimejua namna dawa zinavyotunzwa, kuna nyingine zinahitaji sehemu ya ubaridi na zingine zinatunzwa sehemu yenye joto kiasi.asante.

Sebastian NgusaKijiji: GullaCTC anayohudumia: Kituo cha Afya LalagoWilaya ya Maswa.Mkoa wa Simiyu

12 | MTAZAMO WANGU

Ni furaha yangu mimi sebastian Ngusa kupata fursa ya kushiriki mafunzo ya WaVIU washauri. Nitaelimisha jamii inayonizunguka kwa kujitolea kwa moyo mmoja baada ya viongozi wa warsha hii kunijengea uwezo wa kuwahudumia wenzangu waliopo CTC na pia nimepata bahati ya kuweza kujifunza matumizi sahihi ya dawa kutoka kwa Meneja wa Bohari ya Dawa ya Kanda ya Ziwa (Mwanza).

MTAZAMO WANGU | 13

Sebastian Ngusa

siku ya alhamisi, tarehe 22 Mei 2014, WaVIU washauri walipata fursa ya kutembelea hospitali ya rufaa ya Bugando, Kitengo cha CTC. Kwa WaVIU wengi, hii ilikuwa ni mara yao ya kwanza kufika katika hospitali hii ya rufaa ya Kanda ya Ziwa.

WaVIU Washauri walipofika CTC walipokelewa na Dkt. Irene Massawe ambaye ndiye alikuwa mwenyeji wao. Walipata matembezi yenye maelezo kutoka katika vitengo mbalimbali vya CTC kama vile chumba cha mapokezi, chumba cha daktari, chumba cha unasihi na chumba cha kutolea dawa. Pia waliweza

kukaa pamoja na WaVIU washauri wa CTC ya Bugando, kuzungumza, kupeana uzoefu wa kazi, changamoto na mbinu za kutatua changamoto hizo.

WaVIU Washauri walifurahishwa sana na ziara hii haswa kutambua kuwa changamoto walizonazo katika CTC zao pia zipo katika CTC ya hospitali ya rufaa ya Bugando. hivyo, kitendo cha kukutana na WaVIU Washauri wenzao, kuzungumza na kubadilishana uzoefu, ilikuwa ni faraja sana kwao. Kama inavyoonekana kwenye picha zifuatazo.

Picha ya kushoto: Dkt. Irene Massawe (aliyenyoosha mkono) akitoa maelezo kwa WAVIU washauri.

WAVIU washauri wakisikiliza maelezo kwa makini.

ziara ya kutembelea CtC ya Hospitali ya Rufaa ya Bugando – Mwanza.

14 | MTAZAMO WANGU

WAVIU Washauri wa CTC ya Bugando, Leonard Muhoja na Yasinta Ndibalema (waliosimama)wakieleza uzoefu wao.

MTAZAMO WANGU | 15

Sitta SakasakaKijiji:KisesaCTC anayohudumia: Zahanati ya KisesaWilaya ya MeatuMkoa wa Simiyu

Mtazamo wangu:Kwanza kabisa nimefurahi sana kufika katika warsha hii ili kubadilishana Mawazo na WaVIU wenzangu ambao wanatoka katika vijiji, wilaya pamoja na mikoa mbalimbali. Katika warsha hii:(a) Nimejifunza zaidi kuhusu matumizi ya dawa za arV pamoja na madhara ya

kutokunywa dawa.(b) Nimejifunza jinsi ya ufuatiliaji wa akina Mama na watoto ambao wameacha kutumia

dawa za kupunguza makali ya VVU ili warudi CTC.(c) Pia nimejifunza majukumu ya kazi yangu katika CTC, pamoja na mpangokazi katika

utekelezaji wa shughuli zangu, kuunda vikundi vya watu waishio na maambukizi ya VVU ikiwa ni pamoja na vikundi vya akina mama na klabu za watoto.

Katika matembezi mbalimbali ya kujifinza, sikuwahi kuwa na ndoto ya kutembelea CTC ya Bugando. Nilipofika hapo, niliongezewa elimu juu ya unasihi, ufuatiliaji wa watoro na kuunda vikundi vya watoto na watu wazima.

Kwa kweli niliyofundishwa nitakwenda kuyafanyia kazi katika CTC yangu ninakotoka. Nashukuru kwa wakufunzi wangu kunielimisha.

Majukumu ya WaVIU:(a) Kutembelea wagonjwa majumbani ili kutoa ushauri kwa

mteja MVIU na familia zao. (b) Kuwapeleka wateja kwa Mshauri Mtaalamu.(c) Kutoa elimu sahihi kuhusu virusi vya UKIMWI.(d) Nimejifunza mambo mengi ambayo mimi nilikuwa

bado suyajui kabla ya kuhudhuria warsha. hii ndio mara ya kwanza.

Matarajio yangu, ninaomba kila baada ya mwaka mmoja tuwe tunakumbushana katika utekelezaji wa kazi kwani kuna tofauti kubwa kati ya uelewa wa wagonjwa na elimu ya jinsi ya kuzuia maambukizi ya VVU. Kwa sasa ninayo hamasa ya kutembelea wagonjwa katika CTC na pia rCh.

16 | MTAZAMO WANGU

Magreth MasaluKijiji: Mwamoto - NkololoCTC anayohudumia: Zahanati ya NkololoHalmashauri ya wilaya ya Bariadi.Mkoa wa Simiyu

Mimi binafsi namshukuru Mungu kwa kuweza kunikumbuka katika warsha hii. Nimeweza kukutana na wawezeshaji kutoka ngazi ya Mkoa hadi Taifa na vilevile kukutanishwa na WaVIU wenzangu kutoka simiyu, shinyanga na Geita.

Vilevile nimeweza kujifunza mambo mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali katika mikoa hii. Nimeweza kupelekwa kwenda kujifunza mambo mengi mazuri katika CTC ya Bugando na kuona sehemu ya kuhifadhia dawa zetu za kufubaza VVU kwenye bohari ya dawa.

Namshukuru Mungu na naomba tena aGPahI izidi kunikumbuka katika warsha yoyote na niko tayari kwenda popote pale.

MTAZAMO WANGU | 17

Hamis ShigellaKijiji: BwendamwizoCTC anayohudumia: Kituo cha Afya IboyaWilaya ya Mbogwe.Mkoa wa Geita

Nimefurahia sana kuhudhuria katika warsha hii. Nimejifunza mengi sana. Kwanza nimetembelea Bohari ya Dawa ya Kanda ya Ziwa. hii ni bohari ya kutunzia dawa. Kwa maana hiyo nitafanya kazi kwa moyo mmoja. Nitajituma kwenda kuhamasisha wagonjwa vijijini pamoja na majumbani kwao .Nimefurahi kutembelea CTC ya hospitali ya rufaa ya Bugando. Nimeweza kujifunza juu ya kumshauri mgonjwa anayeishi na maambukizi ya VVU. Nimefika chumba cha kutolea dawa katika CTC ya Bugando na kuona shughuli zao na pia usafi wa mazingira ya CTC.asante.

18 | MTAZAMO WANGU

Kanzaga FabianKijiji: SegeseCTC anayohudumia: Zahanati ya SegeseWilaya ya MsalalaMkoa wa Shinyanga

Mtazamo wangu kuhusu warsha ya WaVIU washauri ni kwamba:

1. Nimepata uelewa namna hospitali ya rufaa – Bugando Medical Centre inavyotoa vizuri huduma endelevu za matibabu na ushauri, pamoja na changamoto zilizopo kwa WaVIU washauri katika kutafuta watu waliopotea kwenye huduma. Lakini bado nimefurahishwa na jitihada zao pamoja na mpangilio mzuri wa ofisi za CTC.

2. Pia, katika eneo lingine la Bohari ya Dawa (MsD), nimefarijika kuona dawa zikiwa katika utunzwaji wa hali ya juu, na umakini wa Bohari ya Dawa katika shughuli mbalimbali za uagizaji na usambazaji wa dawa katika Kanda ya Ziwa, pamoja na utatuzi wa changamoto zinazotokea kama vile vitendanishi vya maabara (HIV testkits, reagents for CD4 machine, TB/LP, OIs, ARVs n.k.). Lakini wamekuwa wakipigana kufa na kupona kutafuta wafadhili ili kupata vifaa tiba, dawa na vitendanishi ambavyo huwezesha kutoa huduma isiyo na upungufu nchini Tanzania hususan katika Wilaya ya Msalala.

3. aGPahI imeniongezea uelewa na uwezo kielimu na kutumia elimu niliyoipata katika kuongeza ubora wa huduma za watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

4. aGPahI imenikutanisha na WaVIU washauri kutoka mkoani shinyanga, simiyu na Geita na nimebadilishana nao uzoefu katika masuala ya ufuatiliaji wa wazazi na watoto ili waendelee kuhudhuria katika

huduma endelevu, ushauri na matibabu.

18 | MTAZAMO WANGU

MTAZAMO WANGU | 19

5. Warsha hii imenifanya kunufaika kwa masuala mengi yanayohusu nchi yangu juu ya mapambano ya dhati na ya makusudi ya kupunguza kama si kuondoa /kumaliza kabisa maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI na vifo visivyo vya lazima kwa watu waishio na maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Nakualika ndugu Mtanzania ambaye wewe kwa sasa vipimo bado vinaonyesha haujaambukizwa jisimamie, jilinde usiambukizwe kabisa.

Na kwa wewe uliyepima ukakutwa unaishi na VVU na UKIMWI, jihadhari na maambukizi mapya. Tanzania bila maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI inawezekana.

Naishukuru aGPahI kwa mafunzo haya na pia namshukuru Mwenyekiti wa NaCOPha ndugu Vitalis Makayula kwa kuwa pamoja nasi.

Mungu awabariki.

Regina AnthonyKijiji: KabaleCTC anayohudumia: Hospitali ya Wilaya Meatu (Mwanhuzi)Wilaya ya MeatuMkoa wa Simiyu

Kwanza nashukuru kwa warsha hii iliyofanyika jijini Mwanza. Imeniwezesha kufahamiana na wenzangu wanaoishi na VVU wanaotoka sehemu mbalimbali za mikoa ya shinyanga, simiyu na Geita. Pia warsha hii imeniwezesha kufika Bohari ya Dawa ya Kanda ya Ziwa na hospitali ya rufaa ya Bugando.Ninaahidi kufanya yafuatayo:1. Kutoa elimu niliyoipata hapa kwa wenzangu

yaani wahudumu wenzangu.2. Nitawaelimisha kuhusu utumiaji wa dawa za

kufubaza VVU kwa usahihi.3. Nitaelimisha vikundi vya watoto wanaoishi na

VVU.4. Kuwatembelea wateja wanaotoroka katika

huduma bila kuchoka. Mwisho naliomba shirika la aGPahI kutupa fursa ya kutupeleka sehemu mbalimbali za kutembelea CTC ili kupata uzoefu zaidi.Nashukuru, asanteni.

MTAZAMO WANGU | 19

20 | MTAZAMO WANGU

Cosmas ShimbaKijiji: Senani CTC anayohudumia: Kituo cha Afya IkindiloHalmashauri ya wilaya ya Itilima.Mkoa wa Simiyu

Mimi ni Cosmas shimba. Kwa mtazamo wangu katika warsha hii niliyoweza kushiriki kwa kweli imenipa changamoto nyingi sana. Kwanza kabisa, ninalishukuru shirika la aGPahI kwa kuweza kuniteua kuja kushiriki warsha hii. Kwangu mimi ndio mara yangu ya kwanza, nasema asante sana. Nimeweza kukutana na watu wanaotoka sehemu mbalimbali ambao nilikuwa sijawahi kukutana nao ingawa wengine nilikuwa nawasikia kwenye vyombo vya habari, yaani redio na Televisheni.

Changamoto1. Nimeweza kukutana na Mwenyekiti wa Baraza la

Taifa la Kudhibiti UKIMWI (NaCOPha) ambaye amenipatia mchango mkubwa sana katika suala zima la mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI. Kwa kweli ni changamoto nyingi nilizojifunza kutoka kwake. Nimepata hamasa na uelewa mkubwa wa kiakili punde nitakaporudi nyumbani nitakuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya VVU/ UKIMWI kwenye CTC yangu na jamii nzima inayonizunguka kupitia mafunzo haya.

2. Ninalishukuru tena shirika la aGPahI kupitia Dkt. Njau kwa kuweza kunikutanisha na watangazaji wa redio mbalimbali hapa nchini ikiwamo redio sibuka, rFa na sahara Communications ambao nilikuwa nawasikia kwenye vipindi vya redio na Televisheni. Lakini kupitia mafunzo haya, nimeweza kuonana nao ana kwa ana, akiwamo Bwana Faraja wa redio sibuka, Bwana William Bundala wa rFa na Deborah Mpagama wa sahara Communications. Kwangu mimi hii imekuwa faraja na bahati ya pekee kabisa.

MTAZAMO WANGU | 21

3. Nimebahatika kutembelea Bohari ya Dawa Kanda ya Ziwa (MsD) ambapo napo nilikuwa sijawahi kufika. Nimejifunza mambo mbalimbali kama vile dawa zinavyoingia, zinavyutunzwa na zinavyosambazwa. Vilevile tukafanya kikao na baadhi ya wafanyakazi wa Bohari ya Dawa akiwamo Meneja wa Kanda na mmoja wa Maofisa waandamizi ambao walitueleza mambo mengi kuhusu namna wanavyopokea, kutunza na kusambaza dawa hizo. Baada ya maelezo, washiriki walipata muda wa kuuliza maswali na tukajibiwa na kuridhishwa na majibu hayo.

4. Nilibahatika tena kutembela hospitali ya rufaa ya Bugando. Napo nimejifunza mambo mengi mazuri kama vile:

Wagonjwa wanavyopokelewa kwenye CTC yao pamoja na kuwaandikisha kwenye Pre ART register3, ART register4. Lakini pamoja na hayo, kuna changamoto nyingi wanazokumbana nazo kwa sababu wateja wao wengi wanakuwa ni watu wa kutoka sehemu mbalimbali za nchi hususani mikoa ya mbali.

hii inawawia ugumu namna ya kuweza kuwafuatilia na kuwarudisha kwenye huduma kwani wengi wao wanatumia anwani zisizo sahihi, kuandikisha jina tofauti na mahali wanapoishi. Lakini pamoja na hayo, nimejifunza mbinu wanazotumia kuwapata MIssaP na LTF.

Vilevile elimu inatolewa ya kutosha kwa wateja wao na kuwapa moyo wa kuweza kuhamasisha kuendelea na dawa. hatimaye, wateja wanajiweka wazi kwa kuongea ule ukweli pamoja na namna wanavyotumia dawa. Pia WaVIU washauri wa Bugando wana mbinu nzuri za ufuatiliaji, hata wakimkosa mteja mara ya kwanza hawakati tamaa.

Matarajio:Mara baada ya warsha hii, ninatarajia kwenda kufanyia kazi mbinu nilizojifunza hususani namna CTC ya Bugando inavyorudisha wateja waliopotea na kuacha dawa. hii ndio itakuwa kazi yangu mojawapo kwenye CTC yangu.Mwisho natoa shukurani zangu za mwisho kwa aGPahI kwa kunikumbuka katika warsha hii ili niweze kujifunza mengi zaidi. asanteni sana.

3 Pre-ART register - Rejesta ya wagonjwa ambao hawajaanza dawa4 ART register - Rejesta ya wagonjwa walio kwenye dawa

22 | MTAZAMO WANGU

Grace Andrea

Mimi ni MVIU mshauri wa CTC ya Chela. Kwanza tunalishukuru sana shirika la aGPahI kwa semina hii.

Katika mada ya ufuatiliaji wa mama na mtoto, mimi kama MVIU nilijisikia vizuri kuwa na sisi tuna haki kama watu wengine.

Wakati wa warsha hii, nimefanikiwa kutembelea Bohari ya Dawa ya Kanda ya Ziwa (MsD) na kujifunza kuhusu utumiaji wa dawa. Pia tulivyofika katika CTC ya hospitali ya rufaa ya Bugando tumejifunza mambo mengi sana kwa mfano:

1. Namna ya utoaji wa dawa, mapokezi mazuri kwa wagonjwa.

2. Watu wenye TB kukaa sehemu yao wenyewe. Mimi niliona ni vizuri sana.

3. CTC ya Bugando wanapanga mafaili vizuri na kwa namba, hii inarahisisha kupata faili kwa urahisi na kuweza kugundua ni watu gani na wangapi hawaji kwenye huduma.

Tunashukuru sana aGPahI kwa moyo wenu.

Kijiji: Ntundu CTC anayohudumia: Kituo cha Afya ChelaHalmashauri ya wilaya ya MsalalaMkoa wa Shinyanga

22 | MTAZAMO WANGU

MTAZAMO WANGU | 23

Kijiji: MwamabuCTC anayohudumia: Zahanati ya DutwaHalmashauri ya wilaya ya Bariadi.Mkoa wa Simiyu

Kwa mtazamo wangu, katika warsha hii niliyopata fursa ya kushiriki, imenipa changamoto nyingi sana. Kwanza kabisa ninalishukuru shirika la aGPahI kwa kuweza kuniteua kuja kushiriki katika mafunzo haya. Kwangu mimi ni mara yangu ya kwanza na ni bahati ya pekee kwa kunitambua na mimi mtu wa Dutwa kuja kwenye warsha kama hii.

Nimebahatika kukutanishwa na watu au wanawarsha wa wilaya mbalimbali ambao sikutarajia kukutana nao. Tumeweza kubadilishana uzoefu. Pia nimekutana na watangazaji wa radio mbalimbali ambao nilikuwa nawasikia tu redioni.

Kuhusu hii warsha, nimebahatika kutembela Bohari ya Dawa (MsD) Kanda ya Ziwa, Mkoa wa Mwanza. Nimejifunza mambo mbalimbali kama vile dawa zinavyotunzwa na zinavyosambazwa. Pia, tukafanya kikao na Meneja Mkuu Kanda ya Ziwa – MsD Mwanza.

Nimetembelea hospitali ya Bugando na tukaona huduma za CTC zinavyotolewa. Kwa kweli nimependa juhudi zao kwani wanajitahidi kuongea na wagonjwa wa CTC na rCh na kushauri wagonjwa walioacha dawa na kuwarudisha waendelee na matibabu. Pia wanatoa elimu kwa mama na watoto na akina baba kupima kwa hiari, kuwapa elimu ya VVU na UKIMWI na jinsi ya kujikinga na maambukizi mapya.

Daudi Marco

24 | MTAZAMO WANGU

Victoria JosephKijiji: UyovuCTC anayohudumia: Kituo cha Afya UyovuWilaya ya Bukombe.Mkoa wa Geita.

Mimi ni mzazi wa familia yenye watoto wanne (4), wa kiume mmoja (1) na wa kike watatu (3). Nimefurahia suala la kujitolea baada ya kuchaguliwa na shirika la aGPahI kushiriki kwenye warsha hii kuanzia tarehe 20 hadi 22 Mei jijini Mwanza ili kujifunza zaidi kuhusu kujitolea katika kituo changu cha CTC ya Uyovu – Bukombe.Mimi ni mwanachama wa kikundi cha akina Mama Tubadilike – Uyovu. Kikundi ambacho hata aGPahI wanakitambua. Kikundi hiki kimenibadilisha kwa kiwango kikubwa , nimesimama kidedea kuwashawishi akina Mama wengi wabadilike na wawe na msimamo imara wa kujitolea hasa kwa wajane waathirika, watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.Kitu kilichonivutia katika warsha hii ni uamuzi wa busara wa kutupeleka Bohari ya Kanda ya Ziwa- Mwanza kujifunza jinsi dawa zinavyoingizwa pamoja na utunzaji wake. Tulikutana na Meneja wa Bohari wa Kanda ya Ziwa na kitu kilichonifurahisha ni pale ambapo Meneja alipotufafanulia kuwa dawa zinatosheleza kwenye CTC zetu isipokuwa tatizo ni ufuatiliaji wa wahusika wenyewe. Inatakiwa kila CTC iweke oda ya mahitaji yake kila baada ya miezi mitatu kabla ya dawa kuisha. Kitu kingine kilichonifanya niwe na moyo wa kujitolea katika CTC yangu ni pale tulipopelekwa ziara hospitali ya rufaa ya Bugando. hapo nilipata kitu cha ziada cha kuweza kufundisha wenzangu wasiwe watoro wa dawa na wasikwepekwepe kutumia dawa za kufubaza VVU kwani watapata shida baadaye.Pia nilifundishwa jinsi ya kutafuta watoro walioacha kutumia dawa. hapo ndipo nilizidi kuwa na moyo wa kujitolea hasa Mtaalamu mmoja anayeitwa Dkt. Irene Massawe wa hospitali ya rufaa ya Bugando kutueleza umuhimu wa kujitolea. hivyo nawaasa akina mama wenzangu kwa kusema kuwa kujitolea kuna manufaa.

MTAZAMO WANGU | 25

Paul NgasaKijiji: MalampakaCTC anayohudumia: Kituo cha Afya MalampakaWilaya ya MaswaMkoa wa Simiyu

Mtazamo wangu katika warsha hii ya WaVIU washauri ni kwamba nimefurahishwa sana na kujengewa uwezo kuhusu elimu hii ya kutokomeza maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Pia nitajitolea kuelimisha jamii inayonizunguka kwa WaVIU wenzangu na watoto walio CTC. Nitatoa ushauri rCh na kufuatilia watoto waliopotea yaani LTF.

Pia nalishukuru shirika la aGPahI kwa ushirikiano wao mzuri na serikali ya Tanzania na wadau mbalimbali wa afya.

Ningependa kuwaasa wote ambao hawajapima, mpime ili msije mkakaa upande huu ambao tupo sisi ambao tunaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Napenda kumshukuru Meneja wa Bohari ya Dawa ya Kanda ya Ziwa kwa kutuelimisha juu ya utunzaji wa dawa. Napenda pia kuishukuru hospitali ya rufaa ya Bugando Kitengo cha CTC kwa elimu yao nzuri ya ushauri – haswa Dkt. Irene Massawe.

Mwisho nawaasa Watanzania wote wajitokeze kupima afya zao.

Mawasiliano yangu ni: 0684 12 57 06

MTAZAMO WANGU | 25

26 | MTAZAMO WANGU

Felista BiliaKijiji: MwamapalalaCTC anayohudumia: Zahanati ya MwamapalalaHalmashauri ya wilaya ya Itilima.Mkoa wa Simiyu

Ninapenda kwanza kutoa shukurani zangu za dhati kwenu wana aGPahI kwa msaada wenu mnaozidi kutusaidia tangu aGPahI ilipoanza hadi leo. Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu awabariki sana na kuwazidishia mara mia. Nimejifunza mengi kutoka kwenu wana aGPahI na asanteni kwa kunialika kwenye warsha kwani sijawahi kuhudhuria warsha kama hii.

Nimejifunza mengi, mmenipeleka Bohari ya Dawa na CTC ya Bugando. Nimejifunza kwa kuona kwa macho yangu, basi na mimi nimekuwa mbegu kwenye kikundi changu cha JIVU. Maana ya JIVU ni: Jamii inayoishi na Virusi vya UKiMWi – Mwamapalala.

Pia nimefurahi kukutana na WaVIU wenzangu wa sehemu mbalimbali. asanteni sana wawezeshaji wote.

MTAZAMO WANGU | 27

Philip SingiliKijiji:KishapuCTC anayohudumia: Kituo cha Afya cha KishapuWilaya ya Kishapu.Mkoa wa Shinyanga

Mtazamo wangu kuhusu warsha kwa washauri WaVIU ni:

shirika la aGPahI limejikita sana kuboresha afya ya watoto pamoja na familia zao. Kwa hiyo, kwa mtazamo wangu, tangu lianze kutoa huduma zake, shirika limeweza kwa kiasi kikubwa kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia huduma za PMTCT. Mafanikio hayo yameonekana kupitia vituo vya rCh.

Vilevile shirika hili limetoa mchango mkubwa sana katika kutoa elimu ama mafunzo kwa watoa huduma ngazi ya jamii na vituo. hiyo ni kuhakikisha tu huduma bora dhidi ya mapambano ya virusi vya UKIMWI inawezekana.

Warsha hii imeweza kunipatia mwanga wa kuelewa uvumi wa dawa feki za kufubaza virusi vya UKIMWI. hii imetokana na kutembelea moja kwa moja MsD (Bohari ya Dawa) Kanda ya Ziwa na kufanya mahojiano kupitia Meneja wa Kanda. Tuliweza kuulizia maswali mbalimbali kuhusiana na Bohari ya Dawa inavyosimamia usalama wa dawa na utunzaji wake na hili nililishuhudia jinsi bohari inavyotunza dawa zake vizuri. Pia nimefahamu kuwa Bohari ya Dawa ni mali ya wananchi.

Kwa ufupi, kupitia warsha hii nimeweza kutembelea hospitali ya rufaa ya Bugando na kuona jinsi wauguzi na wahudumu WaVIU wanavyojitahidi kutoa huduma katika CTC ya Bugando. Nimejifunza mengi kupitia ziara hiyo. Nimepata uzoefu mbadala wa kufuatilia wateja waliopotea CTC kwa kupitia watoa huduma wanaotumia wenzetu wa CTC ya hospitali ya rufaa ya Bugando.

Vilevile kuna umuhimu wa kuwa na Klabu za ariel za watoto katika CTC, kwani kufanya hivyo kunawafanya watoto kuongeza mahudhurio na kuongeza ufuasi wa dawa.

Mwisho nasema, asante kwa waendesha warsha hii.

MTAZAMO WANGU | 27

28 | MTAZAMO WANGU

Agatha Venance

Kwanza ninayo furaha kubwa kwa warsha hii iliyofanyika kuanzia tarehe 20/05/2014 hadi tarehe 22/05/2014 katika Mkoa wa Mwanza.Warsha hii imewalenga watu wanaoishi na VVU na UKIMWI, jinsi ya kuondokana na unyanyapaa na kuwa watu wa kujitolea binafsi katika jamii zetu.

Katika warsha hii nimejifunza kuwa mwelewa katika kuishi na watu walio na maambukizi ya UKIMWI.

Tumepata fursa ya kutembelea Bohari ya Dawa Kanda ya Ziwa (MsD) na tumeona sehemu ya kutunzia dawa. Pia tumepata nafasi ya kutembelea CTC ya hospitali ya rufaa ya Bugando ambako tumeona wenzetu

wanavyofanya kazi ya kufuatilia watu waliopotea na namna ya kuanza mazungumzo na huyo

mtu aliyepotea na kumsogeza kimawazo karibu na mimi.

Kwa hiyo, ninayo furaha kwa shirika la aGPahI kwa mafunzo haya kwani tumeweza kuvuna ambacho wawezeshaji wametupandia. Tunaomba tena aGPahI msikate tamaa, mwendelee kutuletea

semina nyingine ili tuweze kujifunza zaidi au kuwa wataalamu zaidi.

asanteni.

Kijiji: Ikunguigazi CTC anayohudumia: Zahanati ya Ikunguigazi Wilaya ya MbogweMkoa wa Geita

28 | MTAZAMO WANGU

MTAZAMO WANGU | 29

Modester MagediKijiji: UlowaCTC anayohudumia: Kituo cha Afya UshetuHalmashauri ya Wilaya ya UshetuMkoa wa Shinyanga

Mtazamo wangu kuhusu warsha ya WaVIU washauri ni:Mimi ni MVIU na naishi kwa matumaini. Mpaka sasa nimejifunza mengi sana kutoka kwa wawezeshaji wa shirika la aGPahI, mwezeshaji kutoka NaCOPha na pia kubadilishana mawazo juu ya mambo mbalimbali kutoka kwa WaVIU wenzangu.Pia tumetembelea Bohari ya Dawa ya Kanda ya Ziwa (MsD). Tumesikia mengi kutoka kwa Meneja wa Bohari ya Dawa na tumeona jinsi wanavyotujali kuhusu dawa zetu za kufubaza makali ya VVU.Tumepata uelewa ni jinsi gani dawa na vitendanishi vya maabara vinavyopatikana au

vinavyonunuliwa kutoka nchi za nje. Tumeshuhudia uboreshaji wa majengo ya kutunzia dawa. Pia tumejifunza mengi kutoka aGPahI kwa mfano ufuatiliaji wa watoro majumbani, kutafuta akina mama waliopotea na kuwarejesha kwenye kliniki zao na kuwashauri kujiunga na vikundi vya akina mama vilivyopo kwenye CTC zao.Nimeweza kushiriki kwenye mahojiano na waandishi wa habari kutoka radio Free africa (rFa) na radio sibuka. Tumetembelea CTC ya hospitali ya rufaa ya Bugando ambapo tumewakuta WaVIU wenzetu wakiwa kazini pamoja na washauri wao wataalamu. Tulipata fursa ya kutembea vitengo mbalimbali vya CTC ambapo tumeona wahudumu wanavyofanya kazi kwa juhudi. Tumejifunza mengi sana kutoka Bugando na WaVIU washauri wa Bugando CTC wametushirikisha changamoto zao na jinsi wanavyojitahidi kuzitatua. Pia, tumefurahi kuona utoaji mzuri sana wa elimu pale Bugando CTC.Mwisho, nawashukuru sana shirika la aGPahI kwa kutujali na kutukumbuka katika Warsha hii nzuri iliyofanyika Mwanza.Kwa kweli imetutia nguvu na tutaendelea kufanya kazi katika CTC zetu kwa uelewa mzuri tulioupata kutoka kwenye warsha. Ninaamini tutatekeleza haya kwenye vituo vyetu tutakaporudi.Ninawatakia safari njema wawezeshaji wetu na Mungu awabariki nyote.asanteni.

MTAZAMO WANGU | 29

30 | MTAZAMO WANGU

Gregory PauloKijiji: IbojaCTC anayohudumia: Kituo cha Afya cha UkuneHalmashauri ya Wilaya ya UshetuMkoa wa Shinyanga

Mtazamo wangu kuhusu warsha ya WaVIU washauri ni kwamba nimejifunza mambo mengi sana ikiwamo mafanikio ya utekelezaji wa mkakati wa pili, changamoto mbalimbali katika eneo la kinga, eneo la matunzo, matibabu na msaada, mazingira wezeshi, ufuatiliaji wa fedha, kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na pia majukumu yangu kama MVIU mshauri, yakiwamo:(a) Kutoa elimu sahihi ya VVU na UKIMWI katika kliniki na jamii

inayotuzunguka.(b) Kusaidia shughuli za CTC (kufanya usafi, kupanga mafaili ya wateja

na kupima uzito.(c) Kutoa ushauri kwa mteja MVIU pamoja na familia zao na

inapohitajika kuwapeleka kwa mshauri mtaalamu.(d) Kutembelea wagonjwa majumbani ili kutoa ushauri kwa familia

na wagonjwa wa muda mrefu pia kutafuta wateja (watu wazima, akina mama na watoto) waliopotea ikiwamo kutoa rufaa kwa wagonjwa kutoka katika jamii ili wakapate huduma katika kituo cha afya.

Kutoa uzoefu au ushuhuda wangu binafsi kama mtu anayeishi na VVU na kushuhudia matumizi sahihi ya Dawa za kufubaza VVU. Pia nitahamasisha jamii katika masuala yanayohusu afya (kupima afya mapema na kuendelea kuhudhuria kliniki bila kukosa na kuwahamasisha WaVIU kujiunga na vikundi vya WaVIU ili kusaidiana na kuweza kupunguza unyanyapaa na kuwasiliasha taarifa ya kazi katika kituo cha huduma ya afya cha karibu nami). Kutoa elimu ya afya katika klabu ya watoto wanaoishi na virusi vya UKIMWI, kutambua na kutoa taarifa ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu.Mwisho napenda sana kuwashukuru wafanyakazi wa aGPahI kwa kutuwezesha katika warsha hii kwani nimejifunza mambo mengi sana. Nimetembelea Bohari ya Dawa ya Kanda ya Ziwa na kujifunza mambo mengi ambayo nilikuwa siyajui. Pia, nimetembelea hospitali ya rufaa ya Bugando, nako pia nimeweza kubadilishana uzoefu na WaVIU washauri wenzangu.shukurani kwa wawezeshaji wetu. asanteni.

MTAZAMO WANGU | 31

HitiMiSHOWarsha ya siku tatu ilikuwa ndiyo chanzo cha mitazamo iliyoandikwa kwenye kitabu hiki. Washiriki walikuwa wachangamfu na walionekana kupenda kufahamu mambo mbalimbali kutokana na maswali mengi waliyouliza. Pia, wengi wao walikuwa huru kutoa uzoefu wao kwa manufaa ya washiriki wenzao.

aGPahI imeona manufaa ya kuwa na warsha kama hii. hivyo, shirika linatarajia siku zijazo kuwa na warsha nyingine zaidi ili WaVIU wengi zaidi wapate kufaidika. aGPahI imejifunza kuwa kwa kadiri kiwango cha unyanyapaa kinavyoendelea kupungua, ndivyo WaVIU wanavyojiweka wazi kuhusu hali zao za afya na kuwa wafuasi wazuri wa dawa. shirika limejifunza kuwa, utumiaji wa kundi hili katika kufuatilia WaVIU walioacha dawa unaweza kuwa njia bora ya kuwarudisha tena kwenye huduma.

asanteni sana!

32 | MTAZAMO WANGU

Matukio katika picha

Wasiliana nasi:Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative

Kitalu Na. 373, Mtaa wa Mtitu, Barabara ya Umoja wa Mataifa, Upanga Mashariki, S.L.P. 38252, Dar es Salaam, Tanzania | Simu: +255 22 150790 | Faksi: 25 22 2152748

Na:Kitalu Na. 152 &154, Barabara ya Kenyatta, Majengo mkoani Shinyanga.

S.L.P.: 1368 | Shinyanga | Simu: +255 28 2764005