56
M M K K U U Z Z A A M Mw w o o n n g g o o z z o o k k w w a a L L u u g g h h a a N N y y e e p p e e s s i i Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar Julai 2007

Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

����

MMMKKKUUUZZZAAA

MMMwwwooonnngggooozzzooo kkkwwwaaa LLLuuuggghhhaaa NNNyyyeeepppeeesssiii

Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar

Julai 2007

Page 2: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

ii

Page 3: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

iii ����

Mkakati wa

Kukuza Uchumi na Kupunguza

Umaskini Zanzibar

Julai 2007

Mwongozo kwa

Lugha Nyepesi

MMM KKK UUU ZZZ AAA Umetayarishwa na

Mwamvuli wa Jumuiya Zisizokuwa za Serikali Zanzibar (ANGOZA)

Kwa kushirikiana na

Hakikazi Catalyst

Julai 2007

Page 4: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

iv

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano mkubwa wa wadau mbali

mbali imeandaa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini

Zanzibar unaojulikana kama MKUZA. Mkakati huu wa miaka minne

umepitishwa katika ngazi mbali mbali za serikali na kuzinduliwa Mwezi wa

Machi 2007

Ili waraka huu wa kitaalam uweze kusomwa kirahisi na idadi kubwa ya watu

waliomo ndani na nje ya serikali, hususan wananchi wa kawaida, ilionekana ni

lazima kuandaliwa kwa mwongozo huu wa lugha nyepesi katika lugha ya

Kiingereza na Kiswahili. Chapisho hili, ambalo ni sehemu ya Mkakati wa

Mawasiliano wa MKUZA, litaweza kuwafikia watu wengi zaidi na hivyo

kuwahimiza kushiriki kikamilifu katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na

kutathmini MKUZA. Kwa upande mwingine, chapisho hili litaimarisha umiliki

wa umma wa Mkakati huu.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejidhatiti kushirikiana kikamilifu na wadau

wote ili kuhakikisha kwamba MKUZA unatekelezwa kikamilifu. Kwa

kuzingatia msimamo huu thabiti wa Serikali, ninatoa wito kwa watu wote

kuhakikisha wanasoma chapisho hili kwa makini ili waweze kujenga ufahamu

na hivyo kuweza kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa MKUZA.

Nachukua fursa hii kuwapongeza wote walioshiriki kwa namna moja au

nyingine katika kuandaa chapisho hili la Mwongozo wa Lugha Nyepesi wa

MKUZA. Shukrani za pekee ziende kwa Mwamvuli wa Jumuiya Zisizokuwa

za Serikali (ANGOZA) pamoja na washirika wao shirika la Hakikazi Catalyst

kwa jitihada zao na kujituma katika kuratibu kazi ya kuandaa kijitabu hiki hadi

kukamilika kwake.

Khamis Mussa Omar

Katibu Mkuu

Wizara ya Fedha na Uchumi, Zanzibar

MMM

KKK

UUU

ZZZ

AAA

UJUMBE WA KATIBU MKUU, WIZARA YA FEDHA NA

UCHUMI, ZANZIBAR

Page 5: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

v

Dibaji 1

MKUZA kwa muhtasari

Utangulizi 2

1. Sura ya kwanza: Mpango wa Kupunguza Umaskini Zanzibar (ZPRP) ulipata

mafanikio gani na changamoto zipi zimebakia?

4

Taarifa za awali

Ukuaji wa uchumi

Huduma za jamii

2. Sura ya Pili: Mchakato wa mapitio ya ZPRP ulifanyikaje? 11

Hatua tatu za Mashauriano

Changamoto zilizoibuliwa wakati wa mchakato wa mashauriano

Mambo muhimu yaliyojitokeza wakati wa warsha ya kitaifa

3. Sura ya Tatu: Hali ya ukuaji wa uchumi na ya umaskini hivi sasa ikoje? 12

Hali ya sasa ya ukuaji wa uchumi

Umaskini wa kipato na tofauti ya kimaisha

Ustawi wa jamii

Masuala mtambuka

4. Sura ya Nne: Muundo wa MKUZA 20

Misingi muhimu

Marekebisho ya msingi

Klasta kuu tatu

Klasta 1: ukuaji wa uchumi na upungukaji wa umaskini wa kipato

Klasta 2: Huduma na ustawi wa jamii

Klasta 3: Utawala bora na umoja wa kitaifa

5. Sura ya Tano: Nani atatekeleza MKUZA na vipi? 25

Muundo wa utekelezaji

Majukumu na wajibu wa watekelezaji wakuu

6. Sura ya Sita: Ni jinsi gani ufuatiliaji na tathmini ya MKUZA itafanyika? 27

Sekretarieti ya MKUZA

Ngazi za usimamizi wa MKUZA

Vyanzo vya taarifa

Matokeo ya Msingi ya Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUZA

Changamoto

7. Sura ya Saba: Ugharamiaji wa MKUZA utakuwaje? 30

Raslimali kwa ajili ya MKUZA

Mibadala ya bajeti

Hatari zinazoweza kujitokeza katika Mfumo wa Ugharamiaji MKUZA

• Viambatisho 32

Makundi yaliyo katika hatari na sababu za hali hiyo 33

Shabaha za Utekelezaji, Changamoto Kuu, na Hatua za Utekelezaji 34

MMM

KKK

UUU

ZZZ

AAA

YYYAAALLLIIIYYYOOOMMMOOO

Page 6: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

vi

Maneno muhimu Mifano

Matokeo ya jumla Ni matarajio ya muda mrefu ya kitaifa na kisekta kama yalivyobainishwa katika sera za kitaifa kama vile dira ya 2020. Kwa mfano: Jamii iongozwe kwa utawala wa sheria na serikali yenye kuaminika, uwazi na kuwajibika.

Malengo Tarajio lililokusudiwa katika kufanikisha moja ya matarajio ya jumla. Lengo halihitaji sana kuwepo kwa shabaha na kipindi maalum cha ufanikishaji. Kwa mfano: Hakikisha ujumuisho wa watu katika mchakato wa utawala na wa maendeleo

Shabaha za utekelezaji Haya ni matarajio ambayo yanadhibitiwa kwa muda maalumu uliopangwa wa utekelezaji wa lengo. Kwa mfano: Imarisha kazi za madaraka mikoani katika ngazi ya wilaya.

Changamoto muhimu ziliyoibuliwa

Haya ni matatizo yaliyotajwa katika kupindi cha mashauriano ambayo yanahitaji kushughulikiwa Kama vile: Ugawaji mdogo wa madaraka kwa ngazi za chini

Hatua za utekelezaji Shughuli ambazo wahusika tafauti watazitekeleza ili kuweza kushughulikia changamoto zilizotajwa katika kipindi cha mashauriano. Shughuli hizi pia zimeelekezwa kufanikisha matokeo ya jumla ya utelekezaji. Kwa mfano: Endeleza na tekeleza mkakati wa ugawaji wa madaraka kwa Wizara teule za serikali.

Wadau Hizi ni Wizara, Idara na Mashirika ya serikali. Pia hujumuisha wahusika wasiokuwa wa kiserikali kama vile Jumuiya za kiraia, sekta binafsi na vyama vya wafanyakazi Kwa mfano: Wizara ya kilimo.

VVU Virusi vya UKIMWi

UKIMWI Upungufu wa Kinga Mwilini

MKUKUTA Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania

MKUZA Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar

MMM

KKK

UUU

ZZZ

AAA

MMMAAANNNEEENNNOOO MMMUUUHHHIIIMMMUUU YYYAAALLLIIIYYYOOOTTTUUUMMMIIIKKKAAA KKKWWWEEENNNYYYEEE MMMKKKUUUZZZAAA

Page 7: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

1

Utayarishaji wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA) ulifanyika kwa mashauriano ya nchi nzima yaliyohusisha wadau mbalimbali ikiwemo serikali, sekta binafsi, jumuiya za kiraia, wananchi na washirika wa maendeleo. Hivyo mambo muhimu yanayojitokeza katika mkakati huu ni ushirikishwaji, uoanishaji na ubia wa wadau wote.

MKUZA umetokana na Mpango wa Kupunguza Umaskini Zanzibar (ZPRP) ambao ulilenga sekta maalum zilizopewa kipaumbele. MKUZA kwa upande mwengine umejengwa juu ya klasta (maeneo) tatu ambazo zinazingatia changamoto zilizotolewa wakati wa mapitio ya ZPRP. Mambo yaliyomo katika klasta hizi tatu ndiyo yanayofanya kupatikana kwa marekebisho ya msingi yanayoongoza MKUZA kwa ujumla kama yalivyowekwa katika jedwali la hapa chini.

Klasta 1 Klasta 2 Klasta 3

Ukuaji wa uchumi na upunguzaji umaskini wa

kipato

Huduma na ustawi wa jamii

Utawala bora na umoja wa kitaifa

Matokeo Makuu = ukuaji mkubwa wa uchumi endelevu unaolenga

maskini.

Matokeo Makuu = kuboresha ustawi wa jamii

na upatikanaji endelevu wa huduma bora hususani

kwa maskini na watu walioko hatarini.

Matokeo makuu = jamii inayotawaliwa kwa misingi

ya sheria na serikali inayotabirika, iliyowazi na

inayowajibika.

Kila klasta ina matokeo makuu ambayo yana malengo yake (angalia juu). Klasta hizi kwa jumla zina Malengo 22 ambayo kwa upande wake yamehusiana na shabaha za utekelezaji 93, mambo muhimu (Changamoto) 325 na hatua za utekelezaji 520.

Itakuwepo sekretarieti ambayo itaratibu mchakato wa marekebisho yanayotokea ili kuhakikisha panakuwepo ufuatiliaji na utaratibu wa kutathmini madhubuti.

Mpango wa kina wa mahitaji ya fedha kwa ajili ya MKUZA bado haujaandikwa. Hata hivyo ni muhimu kuzingatia kwamba shabaha na mikakati mingi ya utekelezaji imetokana na mipango ya kisekta iliyopo na ambayo hutengewa fedha katika bajeti

MMMKKKUUUZZZAAA KKKWWWAAA MMMUUUHHHTTTAAASSSAAARRRIII MMM

KKK

UUU

ZZZ

AAA

Page 8: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

2

Huu ni Mwongozo wa lugha nyepesi wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar ambao kwa jina maarufu unaitwa MKUZA. MKUZA ulichapishwa mnamo mwezi Novemba 2006 na umepangwa kuendelea kutoka mwaka 2005 /2006 hadi mwaka 2008/2010. MKUZA unafuatia Mpango wa Kupunguza Umaskini Zanzibar (ZPRP) wa Januari 2002 ambao uliendeshwa kutoka mwaka 2002 hadi mwaka 2005.

Mwongozo huu umeandaliwa ili kufanya fikra za MKUZA ziwafikie watu mbalimbali ili waweze kushiriki vyema katika kupanga, kutekeleza, kusimamia na kutathmini MKUZA kama utakavyojionesha tangu Serikali Kuu hadi ngazi ya Shehia.

Sehemu kuu ya Mwongozo huu imo katika sura saba. Sura ya kwanza inaelezea mafanikio ya ZPRP na changamoto zilizopo.

Sura ya pili inazungumzia mchakato wa mashauriano mbalimbali ambao ulitumiwa kutathmini ZPRP.

Sura ya tatu inaonesha takwimu zilizopo zinazoonesha ukuaji wa uchumi na kiwango cha umaskini wa kipato na usiokuwa wa kipato Visiwani. Uchambuzi huu utatumika kupima mafanikio ya MKUZA.

Sura ya nne inazungumzia muundo wa MKUZA na inaorodhesha sehemu muhimu katika muundo wake yaani klasta zake tatu, matokeo makuu, na malengo yake 22 (angalia kiambatisho kwa taarifa ya kina)

Masuala ya muundo wa MKUZA, usimamiaji wake na tathmini ya utekelezaji yanaoneshwa kuanzia sura ya tano hadi sura ya saba.

Kila mmoja anakaribishwa na kushajiishwa kushiriki katika hatua zinaoendelea katika kubuni, kutekeleza, kusimamia na kutathmini MKUZA. Taarifa za mawasiliano juu ya wapi unaweza kupeleka mawazo yako zimetolewa kwenye gamba la nyuma la mwongozo huu.

Mafanikio ya Mkakati huu

yatategemea zaidi ushiriki wa wadau

wote katika ngazi zote

Hivyo tunapaswa kuungana pamoja

kwa dhati katika mchakato wa

utekelezaji kwa kutumia vizuri na kwa

uadilifu raslimali.

Tufanye kazi pamoja, tutekeleze

Mkakati huu ili kuimarisha maisha ya

Wazanzibar.

Rais Amani A. Karume

Kwenye Mkuza (2007)

.

UUUTTTAAANNNGGGUUULLLIIIZZZIII MMM

KKK

UUU

ZZZ

AAA

Page 9: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

3

Kisanduku 1: Tafiti zilizofanywa

� Mapitio ya Matumizi ya Serikali (PER)

� Tathmini ya nchi juu ya Uwajibikaji wa Kifedha (CFAA)

� Uchambuzi juu ya Hali ya Uchumi Zanzibar

� Utafiti juu ya zao la karafuu � Utafiti juu ya Marekebisho ya Serikali

za Mitaa � Mpango wa Utekelezaji wa Utawala

bora

Mpango wa Kupunguza Umaskini Zanzibar (ZPRP) ulizinduliwa mwezi Mei, 2002. Mpango

huo ulikuwa wa mwanzo wa muda wa kati kwa ajili ya kutekeleza Dira ya Maendeleo 2020

ambao ulilenga katika:

Mpango huu ulilenga katika kukuza uchumi na kuimarisha utoaji wa huduma za jamii. Uchumi ulitarajiwa kukua kwa asilimia 5.0 katika mwaka wa mwanzo, asilimia 5.5 katika mwaka wa pili, na asilimia 6.0 katika mwaka wa tatu.

Ili kutekeleza ZPRP, tafiti mbali mbali zilifanywa kama zinavyoonekana katika kisanduku namba 1. Tafiti hizo zilianisha uimara na mapungufu katika uwajibikaji wa masuala ya fedha, usimamizi wa matumizi ya fedha za umma, na mipangilio ya manunuzi katika sekta ya umma.

Katika kipindi cha utekelezaji wa ZPRP :

Uchumi ulikua kwa kasi ya asilimia 8.6 katika mwaka 2002, asilimia 5.9 katika mwaka 2003 na asilimia 6.4 katika mwaka 2004.

Wastani wa pato la mtu binafsi uliongezeka kutoka shilingi za Tanzania 261,000/= (sawa na dola za kimarekani 276) katika mwaka 2002, na kufikia shilingi za Tanzania 331,000/= (sawa na dola za kimarekani 303) mwaka 2004.

1. Mpango wa Kupunguza Umaskini Zanzibar (ZPRP)

ulipata mafakinio gani na changamoto zipi zimebakia?

Taarifa za awali

Pato la taifa limekuwa

likiongezeka katika kiwango

kinachotia matumaini katika

kipindi cha Mpango wa Kupunguza

Umaskini, lakini ukuaji huo

haujabadilisha hali ya maisha ya

mwananchi wa kawaida kwa

kiwango cha kuridhisha. Nini

kifanyike ili kuimarisha hali za

watu maskini?

ANGOZA (2006)

Ukuaji wa Uchumi

Page 10: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

4

Mfumko wa bei ulifikia asilimia 5.2 katika mwaka 2002, asilimia 9.0 katika mwaka 2003 na asilimia 8.1 katika mwaka 2004. Mfumko huo ulichangiwa zaidi na uzalishaji mdogo wa chakula nchini na ongezeko la bei za chakula kinachoagizwa kutoka nje.

Page 11: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

5

Hata hivyo, bado Zanzibar inakabiliana na changamoto zifuatazo.

� Sekta ya Kilimo

� � (a) ukosefu wa

muundo thabiti wa kuimarisha uhakika wa upatikanaji wa chakula

� (b) kuvamiwa kwa maeneo ya kilimo (c) huduma duni za kilimo kama vile mikopo na elimu kwa wakulima

� (d) miripuko ya mara kwa mara ya maradhi ya mimea na mazao

� (e) bajeti ndogo kwa ajili ya kilimo

� (f) soko duni kwa ajili ya bidhaa za kilimo.

Ongezeko la Idadi ya Watu

Ongezeko la idadi ya watu sio tu kwamba

linaathiri Pato la Taifa katika kuimarisha

pato la mtu binafsi bali pia linachangia

kuendelea kukua kwa ukosefu wa ajira

kwa vijana.

� Sekta ya Viwanda � inakabiliwa na (a) ukosefu wa

miundo mbinu bora ya viwanda kwa kuvutia wawekezaji wa kigeni pamoja na wazalendo (b) ujuzi mdogo wa masuala ya viwanda (c) ucheleweshaji katika kutoa leseni na taratibu za kupata ithibati ya kuweka vitega uchumi (d) bidhaa duni (e) maarifa duni miongoni mwa jumuiya ya wafanyabiashara juu ya namna ya kupata soko.

� Sekta ya Fedha � imekabiliwa na changamoto mbali

mbali zikiwemo viwango vya juu vya riba vinavyofikia kati ya asilimia 13 na 17. Kwa upande mwengine, kiwango cha akiba katika benki kimeshuka mno na kufikia wastani wa asilimia 2.4 tokea mwaka 2002.

� Sekta ya Utalii � (a)

miundombinu duni na isiyofaa kama vile mtandao wa barabara, viwanja vya ndege, nishati ya umeme

� (b) uwezo mdogo wa ukusanyaji mapato

� (c) ujuzi mdogo wa usimamizi wa utalii, mna urithi wa vitu vya kihistoria na vivutio vya utalii.

Sekta ya viwanda ndiyo kichocheo cha ukuaji wa uchumi, lakini tunapaswa kuwa na mazingira mazuri ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi katika sekta hiyo

MKUZA PTF

Page 12: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

6

Skuli bora ni ile ambayo

wanafunzi na wazazi

wana maamuzi katika

uendeshaji wa skuli, pia

nyenzo zinatumika

vizuri na kuna uwazi na

uwajibikaji

Haki Elimu

Eneo hili linazungumzia elimu, afya, maji na usafi wa mazingira, jinsia, hifadhi ya jamii na Utawala Bora.

Elimu Majedwali yafuatayo yanaonesha ongezeko la idadi ya wanafunzi na asilimia ya uandikishaji katika ngazi ya maandalizi, msingi na elimu ya lazima.

Jedwali 1 : Idadi ya wanafunzi na Asilimia ya wanafunzi walioandikishwa

Idadi ya wanafunzi Asilimia ya wanafunzi walioandikishwa

Kiwango

2002 2005 2002 2005

Maandalizi

15,004 18,538 14% 15.9%

Msingi

184,382 208,283 98.1% 101.3%

Elimu ya lazima 225,921 260,615 87.7% 92.6%

Usawa wa kijinsia katika uandikishaji watoto umefanikiwa katika ngazi za elimu ya msingi na ya lazima. Utoaji wa elimu bora pia umepiga hatua kama inavyojionesha kwa kuongezeka kwa viwango vya kupasi kwa kila ngazi kutoka darasa la kumi kwenda darasa la kumi na moja, kutoka darasa la kumi na mbili kwenda la kumi na tatu, na kutoka darasa la kumi na nne kwa wahitimu wenye sifa za kujiunga.

Licha ya mafanikio hayo, bado sekta hii inakabiliwa na changamoto zifuatazo:

Kwa ujumla, ufanisi wa mfumo wa elimu bado haujaridhisha kutokana na sababu kadhaa zikiwemo

� Idadi ndogo ya skuli � Upungufu wa walimu wa sayansi na hisabati � Huduma chache za maabara na vifaa � Upungufu wa zana na vifaa vya kusomea na

kufundishia � Upungufu wa vyoo � idadi ndogo ya walimu wenye sifa � Upungufu wa nyumba za walimu na ukosefu wa

huduma ya usafiri � Mchango duni wa wazazi � Utoaji mdogo wa huduma za kusomeshea pamoja na

kutowajumuisha ipasavyo watu wenye ulemavu.

Huduma za Kijamii

� Bado si watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanaoandikishwa � Kuna tofauti kubwa ya uandikishaji watoto shule kati ya wilaya na wilaya.

Page 13: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

7

Afya

Kwa ujumla ufanisi katika miundo mbinu na utoaji wa huduma katika Sekta ya Afya umeimarika ikiwemo:

Mpango Mkuu wa Kupambana na Malaria pamoja na Mkakati wa Sekta ya Afya kwa ajili ya Kupambana na VVU na UKIMWI umeanzishwa.

Idadi ya vituo vya kuchunguza ugonjwa wa kifua kikuu na ukoma vimeongezeka kutoka 11 mpaka 40 wakati vituo vya huduma za tiba vimeongezeka kutoka 46 hadi 134.

Sera ya Watumishi wa Sekta ya Afya na Mpango wa Miaka Mitano wa Sekta hiyo umekamilika. Vile vile zimeanzishwa huduma za tiba na kinga ya maradhi kwa wafanyakazi wa afya walio katika mazingira hatari kiafya au hali ya kuweza kuathirika na kwa wanaonajisiwa.

Katika miaka ya karibuni, Zanzibar imeshuhudia ongezeko la idadi ya maradhi yasiyoambukiza yakiwemo kisukari, shindikizo la juu la damu, saratani ya shingo ya uzazi, saratani ya ziwa, pumu na kadhalika. Mojawapo ya mambo yanayochangia kwa kiasi kikubwa utoaji duni wa huduma za afya ni upungufu wa wataalamu.

Maji na Usafi wa Mazingira

Huduma za maji salama na usafi wa mazingira zimeimarika kufuatia mafanikio makubwa ya utekelezaji wa miradi 75, ikiwemo (a) uchimbaji wa visima vipya na ujenzi wa matangi ya kuhifadhia maji (b) kuimarisha usimamizi wa taka(c) ujenzi wa vyoo na (d) ukarabati wa mifumo ya michirizi katika Mji Mkongwe.

Huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira imekabiliwa na changamoto zifuatazo:

Changamoto zinazohusiana na mazingira kwa upande wa maji ni (a) uchumvi chumvi wa maji na hatari yauvamizi wa watu katika maeneo ya mwambao (b) uchafuzi wa vyanzo vya maji(c) upungufu wa hifadhi ya maji ya ardhini(d) usimamizi mbaya wa masuala ya ukame na mafuriko (e) ufuatiliaji mdogo wa maji ya ardhini.

� Ujenzi wa vituo sita vipya vya afya na ukarabati wa vituo vyengine hamsini na mbili. � Ukarabati wa vituo kumi vya huduma ya afya na ujenzi wa nyumba kumi za

wafanyakazi � Matanuri ya kuchomea taka za hospitali yamejengwa � Vituo vinne vya afya vimewekewa huduma ya X ray � Upatikanaji wa dawa muhimu kwa afya ya jamii umeimarishwa. � Mkakati wa huduma ya afya ya uzazi kwa mama wajawazito, watoto, vijana,

wanaume na wazee umeandaliwa.

� Usambazaji na ubora duni wa maji mijini na vijijini. � Miundombinu chakavu ya maji. � Upungufu wa wafanyakazi na fedha katika kuendesha shughuli za usambazaji maji

na utunzaji wake. � Ushiriki mdogo wa wadau na ukosefu wa zana za kukusanyia taka pamoja na

ukusanyaji wa taka na kuzisarifu upya. � Ukosefu wa uratibu baina ya shughuli za maji na shughuli za usafi. � Upungufu na ushuhulikiaji mdogo wa michirizi ya maji machafu.

Zanzibar ina vyanzo

vingi vya maji,

inakuaje ikabiliwe na

tatitizo la upatikanaji

wa maji? MKUZA PTF

Page 14: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

8

Suala la upunguzaji wa umaskini

linahitaji muundo mzuri wa utawala

bora ili kuinua hali ya maisha ya

walio maskini katika jamii zetu.

Taasisi zisizo za serikali lazima

zipiganie kuwepo kwa utawala bora

NGORC (2006)

Jinsia na Hifadhi ya Jamii

Licha ya juhudi na hatua maalum za upendeleo za kujumuisha jinsia katika mchakato wa maendeleo bado kumekuwa na changamoto nyingi katika eneo hili ambazo ni pamoja na:

Katika eneo la hifadhi ya jamii suala la kiinua mgongo si tu kwamba halitoshelezi lakini pia haliwafikii wanachama.

Utawala Bora

Mafanikio mengi yamepatikana katika eneo la Utawala Bora Zanzibar. Baadhi ya mafanikio hayo ni vyema kuyataja:

Pamoja na mafanikio hayo, bado sekta ya utawala bora inakabiliwa na changamoto zifuatazo:

Wanawake ni watu

muhimu katika

maendeleo hivyo

wasibaguliwe.

Wawezeshwe.

MKUZA PTF

� � Uwezo wa wafanyakazi wa

mahakama umeimarishwa. � Muafaka baina ya vyama vya

CCM na CUF umekubaliwa kutiwa sahihi na kutekelezwa.

� Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka imeanzishwa. � Uwezo wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali umeimarishwa. � Sheria nyingi ambazo zinakwenda kinyume na misingi ya Utawala Bora

zimefanyiwa mapitio na kurekebishwa. �

� Uendelezaji wa mila zinazokwamisha maendeleo � Suala la jinsia kutojumuishwa kikamilifu katika sera na

mipango ya kitaifa. � Unyanyasaji wa kijinsia bado unaendelea � Ukosefu wa misaada kwa makundi yaliyo katika hatari

kama vile wanawake, vijana, watoto na watu wenye ulemavu.

� Uelewa mdogo juu ya umuhimu wa utawala bora miongoni mwa wananchi. � Uwezo mdogo wa taasisi za serikali katika kutoa huduma, kupanga na kutekeleza

maboresho.

Page 15: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

9

Page 16: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

10

Sura hii inaelezea kwa muhtasari mchakato wa mapitio ya Mpango wa Kupunguza Umaskini Zanzibar. Masuala muhimu yaliyojitokeza katika mchakato huo yalizingatiwa katika kuandaa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA) Madhumuni makuu ya kufanya mapitio ya ZPRP ni: (a) Kupima mafanikio yaliyopatikana na kuainisha mapungufu ya ZPRP na (b) Kutumia mafunzo na maarifa tuliyojifunza ili kusaidia kuandaa Mkakati wa Kukuza

Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA) Mawazo ya kuandaa mpango huu yalibuniwa kwa ubora zaidi kwa kuangaliwa utaratibu wa ukuaji wa uchumi unaowajali maskini sana. Mkakati huu ulitakiwa kuoanisha mabadilikio ya hivi karibuni na mchakato wa kisera kati ya Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na kuzingatia mabadiliko mengine yanayotokea ulimwenguni.

Mbinu zilizotumika katika kufanya mapitio ya ZPRP zilihusisha wadau mbali mbali katika awamu tatu za mashauriano na zilifanyika kati ya mwezi wa Oktoba 2005 na Machi 2006. � Awamu ya kwanza ya Mashauriano: Awamu hii ilihusisha wizara, idara na mashirika mbalimbali, jumuiya za kiraia, watoto, vijana, wanawake, jumuiya za kidini na sekta binafsi. Mikutano ya mashauriano ilifanyika Unguja na Pemba ambapo washiriki waliainisha mafanikio na matatizo ya ZPRP. Awamu ya pili ya Mashauriano Awamu hii ya Mashauriano iliendeshwa na Mwamvuli wa Jumuiya Zisizo za Kiserikali (ANGOZA). Washiriki walikuwa ni vijana, wanawake, wakulima viongozi wa kijamii, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wawakilishi wa vyama vya siasa, watu wenye ulemavu, wajane na wastaafu. Msisitizo katika awamu hii ulikuwa ni kuainisha changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa mpango huo na hatua za kuchukuliwa. Awamu ya tatu ya mashauriano ilijumuisha pamoja wadau kutoka mkutano wa kwanza na wa pili na washirika wa maendeleo ambapo washiriki waliweza kuainisha matokeo, malengo, mikakati ya utekelezaji pamoja na taasisi zitakazotekeleza mikakati hiyo kama ilivyoainishwa katika MKUZA. Vile Vile washiriki walizingatia masuala mtambuka pamoja na Malengo ya Millenia na malengo mengine ya kiulimwengu.

2. Mchakato wa mapitio ya ZPRP ulifanyikaje?

Page 17: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

11

Serikali na Washirika wa Maendeleo

watafanyaje ili kuendeleza utalii na

kuufanya uwalenge maskini na usaidie

mikakati ya kukuza uchumi kwa jamii

za vijijini?

NGORC (2006)

Hali ya sasa ya ukuaji wa uchumi imeongezeka kutokana hasa na mchango wa sekta za huduma ambazo kwa mwaka 2005 zilichangia asilimia 51 ya Pato la Jumla la Taifa. Hii inatokana, zaidi na shughuli zinazohusiana na utalii.

Sekta ya Kilimo bado inaendelea kuwa sekta muhimu ya uchumi, kutokana na ukweli kwamba asilimia 40 ya watu wa Zanzibar wanategemea kilimo kwa maisha yao. Katika mwaka 2002, kasi ya ukuaji wa kilimo ilipungua kwa asilimia -1.5 mwaka 2002, asilimia 4.2 mwaka 2003 na mwaka 2004 ilikuwa asilimia 2.7. Uzalishaji wa karafuu na mazao mengine yanayouzwa nje ya nchi umekuwa ukiongezeka kwa kasi ya wastani wa asilimia 1.2 kwa mwaka. Kupanda na kushuka kwa uzalishaji wa kilimo kunatokana na kilimo cha kutegemea mvua. Thamani ya bidhaa zinazouzwa nje, iliongezeka kutoka shilingi bilioni 7.4 mwaka 2002 hadi kufikia shilingi bilioni 14.2 mwaka 2004. Mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na kukamilishwa kwa sera ya biashara ambayo ina mtazamo wa kuishirikisha sekta binafsi na kuweka mazingira bora ya sheria na kanuni kwa wawekezaji.

3. Hali ya ukuaji wa uchumi na ya umaskini hivi sasa

ikoje?

Hali ya Sasa ya Ukuaji wa Uchumi

Page 18: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

12

Sekta ya fedha nayo ilionesha mafanikio makubwa katika kipindi hicho. Kwa mfano, kulikuwepo na ongezeko la mikopo kwa shughuli za kilimo, biashara na taasisi za mikopo midogo midogo zinaongezeka. Ili kuongeza nafasi za ajira miradi midogo midogo na ya kati (SMEs) iliimarishwa. Hivyo, sekta hii ilitoa nafasi za ajira zipatazo 2,567 kwa kipindi cha mwaka 2002- 2005.

Utafiti wa Kipato na Matumizi ya Kaya uliofanywa mwaka 1991/92, ulionesha kwamba asilimia 61 ya Wazanzibari walikuwa wakiishi chini ya kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi, wakati asilimia 22 waliishi chini ya kiwango cha umaskini wa chakula. Kwa mujibu wa Utafiti wa Kipato na Matumizi ya Kaya uliofanywa mwaka 2004/2005, ilikadiriwa kwamba asilimia 49 ya Wazanzibari wanaishi chini ya kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi, na asilimia 13 wanaishi chini ya kiwango cha umaskini wa chakula.

Umaskini ni mkubwa zaidi katika familia zinazoongozwa na wanawake (51%) kuliko zile zinazoongozwa na wanaume (49%). Umaskini pia unategemea ukubwa wa kaya na kiwango cha elimu ya kiongozi wa kaya. Kuna umaskini mkubwa zaidi maeneo ya vijijini kuliko mijini.

Ajira

Kwa mujibu wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya wa mwaka 2004/05 kiasi cha asilimia 7 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi hawana ajira.

Upatikanaji wa chakula Zanzibar

unategemea sana uzalishaji wa wakulima wadogo wadogo na kwa kiasi kikubwa unategemea chakula kinachoagizwa kutoka nje ya nchi.

Kwa ujumla hali ya upatikanaji wa chakula Zanzibar ni nzuri kiasi isipokuwa wakati wa hali mbaya ya hewa.

Uwezo wa upatikanaji wa chakula ni msingi mkuu wa uhakika wa chakula Zanzibar. Hali hii inategemea sana vipato vya watu. Kikawaida familia nyingi zinashindwa kumudu kupata chakula wanachokihitaji.

Ipo haja ya kuanzisha na kuimarisha mtandao wa huduma ya chakula cha dharura ili kusaidia watu wenye matatizo ya kupata chakula. Vile vile ipo haja ya kuweka mikakati ya muda mrefu ya kuongeza pato la watu wa vijijini.

Lishe duni

Watoto wenye lishe duni, kwa kipimo cha ukuaji usioridhisha (kudumaa), ni tatizo kubwa Zanzibar likiwahusisha asilimia 23 ya watoto wote. Tatizo la lishe duni katika maeneo ya vijijini linaonekana kuwa kubwa zaidi.

Asilimia 7 ya watu wenye uwezo wa

kufanya kazi hawana ajira. Kukosa

ajira kunapelekea ugumu wa kupata

fedha na kuchanganyikiwa kiakili,

hivyo, inahitajika kushajiisha watu

wajiajiri wenyewe, kwani yule

anayepanda mti ndiye anayevuna

matunda yake na asiejituma

hudharaulika.

MKUZA PTF

Umaskini wa chakula ni kipimo cha kutopata mahitaji ya lishe bora.

Umaskini wa mahitaji ya msingi

ni kipimo cha kutomudu kupata mahitaji ya ziada

yasiyokuwa chakula.

Umaskini wa Kipato na Tafauti ya Kimaisha

Page 19: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

13

Elimu

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kwamba asilimia 77 ya wanawake na asilimia 86 ya wanaume wa Zanzibar wanajuwa kusoma na kuandika ukilinganisha na asilimia 67 ya wanawake na asilimia 79 ya wanaume wa Tanzania Bara.

Uandikishaji halisi wa elimu ya msingi uliongezeka kwa kiwango cha asilimia 51 mwaka 1990 hadi kufikia asilimia 79 mwaka 2002 kabla ya kiwango hiki kushuka hadi kufikia asilimia 77 mwaka 2005. Asilimia 23 iliyobakia ni ya watoto wenye umri wa kwenda skuli (miaka 7 - 13) ambao hawakuaandikishwa. Kiwango cha mpito cha elimu ya msingi (darasa la saba kwenda sekondari) kimeongezeka kwa hali ya juu na kufikia asilimia 80 tokea mwaka 1990. Aidha, idadi ya wanafunzi wa kike wanaoendelea na masomo ya sekondari imeongezeka zaidi tokea mwaka 2000 ikilinganishwa na wanafunzi wa kiume.

Katika mwaka 2004, asilimia 80 ya wanafunzi wa kike wa Skuli za Msingi waliendelea na masomo ya Sekondari ikilinganishwa na wanafunzi wa kiume.

Kiwango cha mpito cha sekondari bado kiko chini ingawa kumekuwa na ongezeko kutoka asilimia 10 mwaka 1990 hadi kufikia asilimia 40 mwaka 2004. Mambo yanayochangia tafauti ya uandikishaji wa wanafunzi na kiwango cha mpito ni:

Afya

Kiwango cha umri wa kuishi kilikuwa miaka 47 katika mwaka 1978 hadi mwaka 1988. Takwimu za hivi karibuni zimebainisha kwamba, kiwango hicho kimeongezeka hadi kufikia miaka 57 (wanaume miaka 57 na wanawake miaka 58).

Vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka watoto 99 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai (kwa mujibu wa Sensa ya Watu ya mwaka 1988) hadi kufikia watoto 75 kwa kila watoto 1,000 katika mwaka 1996, watoto 83 mwaka 1999 na kufikia watoto 61 mwaka 2004/2005.

� Uelewa mdogo kwa baadhi ya familia na hata jamii juu ya umuhimu wa elimu � Madarasa yasiyotosheleza yanayopelekea msongamano wa wanafunzi. � Ukosefu wa vifaa muhimu katika maskuli kama vile vitabu,vifaa vya maabara n.k � Upungufu wa walimu wenye ujuzi wa kufundisha watoto wenye ulemavu � Mtizamo duni kwa baadhi ya wazee juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto wenye

ulemavu. � Umbali wa skuli.

Wale waliobahatika

kupata elimu miongoni

mwetu wanajukumu la

kuisaidia jamii kwenye

maeneo wanayoishi

J K Nyerere

Ustawi wa jamii

Page 20: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

14

Msingi mkuu wa maisha ya

furaha ni Afya Bora

MKUZA PTF

Kiwango cha umri wa kuishi kilikuwa miaka 47 katika mwaka 1978 hadi mwaka 1988. Takwimu za hivi karibuni (2002) zimebainisha kwamba, kiwango hicho kimeongezeka hadi kufikia miaka 57 (wanaume miaka 57 na wanawake miaka 58).

Vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka watoto 99 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai (kwa mujibu wa Sensa ya Watu ya mwaka 1988) hadi kufikia watoto 75 kwa kila watoto 1,000 katika mwaka 1996, watoto 83 katika kila watoto 1,000 kwa mwaka 1999 na kufikia watoto 61 kwa kila watoto 1,000 katika mwaka 2004/2005. Vifo vya watoto wachanga chini ya umri wa miaka mitano vimepungua kidogo kutoka 107 katika mwaka 1996 hadi kufikia 101 kwa kila watoto 1000 wanaozaliwa hai katika mwaka 2004/2005. Hali hii kwa kiasi fulani, inatokana na kuongezeka kwa huduma za chanjo katika maeneo mengi. Kwa wastani, katika ngazi ya wilaya, huduma za chanjo kwa watoto imefikia asilimia 88.8. Hata hivyo, vifo vya watoto vimeongezeka kutoka asilimia 34.8 hadi kufikia asilimia 42 katika kipindi hicho. Vifo vinavyohusiana na uzazi bado viko juu Zanzibar. Uwiano wa vizazi vinavyohudumiwa na wakunga wenye ujuzi imeongezeka kutoka asilimia 37 katika mwaka 1996 mpaka asilimia 51 katika mwaka 2004/2005.

Kiwango cha uzazi bado ni cha juu na dawa za uzazi wa mpango hazitoshelezi ingawa matumizi ya dawa hizo yameongezeka kutoka asilimia 16 katika mwaka 2002 hadi kufikia asilimia 18 katika mwaka 2005.

Malaria imeendelea kuwa maradhi yanayoongoza Zanzibar. Asilimia 45 ya wagonjwa 812,520 waliofika hospitali mwaka 2004 waligunduliwa kuwa na maradhi ya malaria. Kiwango cha huduma kwa watoto wa kiume chini ya umri wa miaka 5 wanaotumia vyandarua vilivyotiwa dawa kimeongezeka kutoka asilimia 23.8 mpaka kufikia asilimia 36.8 na kutoka asilimia 18.3 mpaka kufikia asilimia 36.8 kwa watoto wa kike.

Kumekuwa na ongezeko la ugonjwa wa kifua (kikohozi) na homa ya mapafu (nimonia) pamoja na maradhi mengine yanayohusu mfumo wa upumuaji. Maradhi ya kifua yameongezeka kwa asilimia 7 na homa ya mapafu yameongezeka kwa asilimia 6 ya wagonjwa wanaotibiwa hospitalini. Masafa ya kufikia huduma za afya:

Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya kwa mwaka 2004/05 ulionesha kwamba asilimia 96.9 ya wakaazi wanaishi ndani ya kilomita 5 kutoka kituo cha huduma za afya za msingi, wakati asilimia ya watu waliofika na kupata huduma ni asilimia 83.7.

Page 21: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

15

Kuwa na ulemavu haimaanishi

kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi

au kujitegemea. Jamii iwape nafasi

watu wenye ulemavu kutumia uwezo

na vipaji vyao.

MKUZA PTF

Maji na usafi wa mazingira

Wingi na ubora wa utoaji wa huduma ya maji ni suala linalopewa kipaumbele Zanzibar. Hii inatokana na mahitaji ya maji kuongezeka na vyanzo vya maji kuchafuliwa. Ingawa upatikanaji wa huduma ya maji umeongezeka kwa watu wa Zanzibar bado huduma hii ni ya kiwango cha chini katika baadhi ya Wilaya. Asilimia 75 tu ya wakaazi wa mijini na asilimia 51 ya wakaazi wa vijijini ndio wanaopata maji safi na salama ndani ya masafa ya mita 400. Katika sehemu nyingi maji sio salama kwa afya za binadamu.

Usafi wa mazingira: Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya wa mwaka 2004/2005, unaonesha kuwa asilimia 67 ya idadi ya watu wanatumia vyoo bora na vya kisasa. Hali hii inaonesha maendeleo ukilinganisha na ilivyokuwa mwaka 1991 ambapo asilimia 48.3 walikuwa hawana vyoo na asilimia 43 tu walikuwa na vyoo vya mashimo.

Makundi yaliyohatarini (Angalia

kiambatisho 1) ni walengwa muhimu wa MKUZA. Sababu zinazopelekea kuathirika kwa makundi haya ni kutokuwa na uhakika wa chakula na lishe, ufinyu wa kupata raslimali za uzalishaji, ukosefu wa afya bora, ukosefu wa ajira, ukosefu wa huduma za misaada, ukosefu wa huduma bora za elimu, ubaguzi na kutengwa na jamii.

Kwa bahati mbaya, taarifa kuhusu makundi haya mara nyingi zinakosekana na hazijakusanywa kwa utaratibu mzuri. Makisio ya hivi karibuni kuhusu idadi ya watoto yatima yanaonesha kuwa asilimia 0.4 ya watoto wanaishi bila wazazi wao (baba na mama

Masuala Mtambuka (masuala yanayohusu sekta zote)

Masuala mtambuka yanayoelezwa hapa ni haya yafuatayo: Utawala Bora, mazingira, VVU na UKIMWI, na jinsia

Utawala Bora

Serikali ya Mapinduzi na watu wa Zanzibar wanatambua na kuthamini umuhimu wa kukukuza Utawala Bora na umoja wa kitaifa. Utawala Bora na Umoja wa Kitaifa utasaidia kuleta mazingira bora kwa maendeleo endelevu. Katika kuendeleza azma hii, hatua zifuatazo zinahitaji kutiliwa mkazo:

� Kuondoa aina zote za ubaguzi

� Kuandaa mikakati itakayopunguza joto la kisiasa

� Kutoa nafasi zaidi kwa wadau wasio wa serikali

Page 22: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

16

Kisanduku 3: Wadau wasio wa kiserikali � � Jumuiya za Kiraia (CSOs) � Jumuiya za Maendeleo ngazi ya jamii (

CBOs) � Jumuiya za Kidini ( FBOS) � Jumuiya zisizo za kiserikali ( NGOs) � Sekta Binafsi

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2000 – 2005), serikali imeweza kufanya marekebisho mbali mbali ya kiutawala. Mabadiliko haya yamesaidia kuweka mazingira bora ya kukuza uwezo wa kiuchumi kwa watu maskini na pia kuandaa sera za kupunguza umaskini. Marekebisho hayo ni pamoja na mfumo wa sekta ya Umma, serikali za mitaa, mazingira ya kibiashara na usimamiaji wa fedha za serikali.

Serikali pia imechukua hatua mbali mbali za kuendeleza ushirikishwaji wa wadau wengine wasiokuwa wa kiserikali katika majadiliano ya kitaifa na uandaaji wa sera. Hali kadhalika

ushirikiano wa sekta binafsi na serikali umeimarishwa kupitia uanzishwaji wa Baraza la Biashara la Zanzibar.

Kesi zote kuanzia Mahakama za Mikoa hadi kufikia Mahakama Kuu sasa zinaendeshwa na Mkurugenzi wa Mashtaka wa serikali badala ya polisi. Uanzishaji wa Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka wa serikali pia ni hatua iliyokusudiwa ya kuondosha utashi wa kisiasa katika masuala ya mashitaka ambapo hapo awali mashitaka yalikuwa chini ya usimamizi wa Mwanasheria Mkuu. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

imeifanyia mabadiliko Tume ya Uchanguzi ya Zanzibar (ZEC) ili kuruhusu vyama vya kisiasa kupata uwakilishi ndani ya Tume hiyo.

Katika kuendeleza na kulinda haki za binadamu Visiwani Unguja na Pemba sheria mbali mbali zimerekebishwa, kwa mfano Sheria ya Adhabu na Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2004.

Mazingira

Upatikanaji wa vyanzo bora vya maji na usafi wa mazingira umeimarika Zanzibar tangu miaka ya 90. Hata hivyo, baadhi ya vyanzo vya maji vimechafuliwa hususan kutokana na takataka za binadamu.

Katika sekta ya kilimo, mbinu duni za kilimo na usimamiaji wa matumizi ya ardhi umesababisha kupotea kwa tabaka la juu la udongo na kwa hivyo kusababisha mmomonyoko na uchakavu wa ardhi. Vile vile njia za uvuvi zisizo halali (mshale, nyavu za kukokota/juya na matumizi ya baruti) zinasababisha uharibifu wa miamba ya matumbawe na mikoko

VVU na UKIMWI

Takwimu za karibuni juu ya VVU na UKIMWI zinaonesha kwamba asilimia 0.6 ya Wazanzibari wanaishi na VVU. Idadi ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI imeongezeka kutoka watu watatu (3) mwaka 1983 hadi watu 4,652 mwaka 2005. Rika la watu liliopo kwenye hatari ya kuambukizwa ni lenye umri kati ya miaka 20 hadi 49 na hili ndio kundi linalotegemewa sana katika uzalishaji.

Changamoto zinazotukabili ni: (a) kutoa huduma bora za matibabu, kuwasaidia walioathirika na walioathiriwa na VVU na UKIMWI, (b) Kusisitiza mabadiliko ya tabia kwa watu na mkazo zaidi umewekwa kwa yale makundi yaliyo katika hatari ya kuambukizwa.

Mali asili yetu ni urithi tulioachiwa

na mababu zetu, hivyo, tuitunze

kwa maendeleo endelevu kwa ajili

yetu na vizazi vijavyo. MKUZA PTF

Page 23: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

17

Jinsia

Usawa wa kijinsia na kuwaendeleza wanawake ni moja ya mambo muhimu ya kimaendeleo hapa Zanzibar. Wanawake bado wanapewa nafasi duni za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Kadhalika, wanawake hawafaidiki sana kupata: � Huduma bora za elimu na afya � Ardhi na mitaji � Ajira na fursa za masoko

Page 24: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

18

MKUZA ndio mkakati wa kufikia malengo na makusudio ya Dira ya Maendeleo ya 2020. Lengo la dira hiyo ni kufanikisha kuleta maendeleo endelevu ya binadamu na kuondoa umaskini. Katika dira hii umaskini unaelezwa kwamba sio tu ukosefu wa kipato lakini pia unajumuisha ukosefu wa mahitaji ya msingi ya jamii. Muundo huu pia unazingatia kuoanisha mipango na sera nyingine zilizopo Zanzíbar, Tanzania bara na kimataifa.

Katika sura hii tutaangalia misingi halisi inayoongoza MKUZA na marekebisho makuu yanayounganisha MKUZA na shughuli nyengine za maendeleo.

Misingi inayoongoza MKUZA ni kama ifuatavyo:

Umilikishaji wa MKUZA kwa Umma utashirikisha sehemu kubwa ya jamii katika ngazi zote pamoja na kujenga uwezo unaohitajika. Uwajibikaji wa Kisiasa. Dhamira endelevu na msimamo wa kisiasa unahitajika ili kuhakikisha maendeleo ya demokrasia na kuheshimu haki za kibinadamu. Utulivu wa kisiasa, kuvumiliana na sera madhubuti ni mambo muhimu yanayojenga msingi wa uwajibikaji wa serikali kwa wananchi wake.

Uwajibikaji juu ya Marekebisho ya Kijamii, Kiuchumi na ya Kimuundo unafanyiwa kazi katika maeneo haya matatu, ambayo ni (a) Usimamizi wa Fedha na Uchumi (b) Utawala Bora (c) marekebisho ya Kimuundo na kiutendaji.

Mikakati ya Kisekta, Fungamano na Mashirikiano. Mafanikio ya utekelezaji wa mkakati yanalazimisha kuwepo kwa mashirikiano baina ya sekta mbali mbali ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Ubia na Wadau wa Ndani. MKUZA unatoa fursa kwa wadau wa nchini wakiwemo raia, jumuiya za kiraia na sekta binafsi kushiriki katika mjadala wa sera. Usawa. MKUZA umepanga hatua za kufuata katika kupunguza tafauti ya hali ya kimaisha na kuendeleza ustawi wa jamii hasa miongoni mwa watu maskini. Hatua zitachukuliwa kuongeza upatikanaji wa nyenzo za uzalishaji kwa maskini. Vile vile mkazo utatolewa katika kuondosha tafauti za kijinsia zilizopo katika upatikanaji wa huduma jamii katika ngazi za Wilaya na Mkoa. Katika kustawisha maendeleo endelevu ya binadamu mkazo utawekwa katika matumizi bora ya raslimali katika kipindi cha utekelezaji wa MKUZA. Matumizi ya raslimali yatazingatiwa kwa namna ambayo hayataathiri mahitaji ya vizazi vijavyo.

4. Muundo wa MKUZA

Misingi ya MKUZA

Page 25: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

19

Kisanduku 4: Marekebisho yanayoendelea

� Marekebisho ya Matumizi ya Serikali. � Usimamizi wa fedha. na mapato ya

serikalili � Marekebisho ya sekta ya umma � Marekebisho ya sekta ya sheria. Serikali pia imedhamiria kutekeleza mkakati wa msaada wa pamoja kwa Tanzania (JAST)

Uhusiano wa shughuli za uchumi mkuu na uchumi wa kisekta ni muhimu sana katika kufanikisha matarajio na malengo ya MKUZA. sera zinahitajika ili kuhakikisha faida inayotokana na ukuwaji wa uchumi kwa sekta zenye kukuza uchumi kama vile uvuvi, biashara na utalii zinaelekezwa kwa maskini ili kukuza ustawi wao.

Kujumuisha masuala mtambuka. Masuala yanayohusu sekta zote yamejumuishwa katika klasta tatu za MKUZA.

Utekelezaji wa MKUZA unasaidiwa na marekebisho ya msingi katika maeneo ya fedha na usimamizi wa uchumi, utawala bora na muundo wa kiutendaji. Marekebisho haya yataoanishwa na marekebisho ya aina hiyo yaliyokwishaanzishwa Tanzania Bara kama yalivyoainishwa katika kisanduku 4

Utekelezaji madhubiti wa marekebisho haya utasaidia kufanikisha malengo kama yalivyofafanuliwa katika klasta tatu za MKUZA.

Marekebisho ya usimamizi wa kifedha ni muhimu. Marekebisho hayo ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato na uwekaji wa hesabu na ripoti za kifedha za serikali ambayo yote mawili yatasaidia kuwepo kwa utamaduni wa uwazi ambao ni sifa kuu ya utawala Bora.

Marekebisho katika eneo la usimamizi wa uchumi yanakusudia kutekeleza malengo mawili yanayohusiana ambayo ni kuendeleza ukuwaji wa uchumi na kujenga msingi wa kuendeleza Utawala Bora. Marekebisho katika eneo la Utawala Bora yamezingatia (a) kustawisha na kuimarisha demokrasia shirikishi (b) kuimarisha utulivu wa kisiasa na utamaduni wa kuvumiliana. Marekebisho haya yatachochea ukuwaji wa uchumi na ustawi wa jamii.

Marekebisho ya muundo wa taasisi yanakusudia kustawisha na kuongeza mchango wa wadau wasio wa kiserikali katika mchakato wa maendeleo. Marekebisho ya wafanyakazi yanalenga katika kujenga ujuzi muhimu na utaalamu unaohitajika katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kufanya tathmini ya malengo ya MKUZA.

Klasta kuu tatu za MKUZA

MKUZA umegawika katika klasta (Maeneo) tatu kuu ambazo ni utawala bora na umoja wa Kitaifa, huduma za kijamii na ustawi, ukuwaji wa uchumi na kupunguza umaskini wa kipato. Mchoro wa hapa chini unaonesha uhusiano wa karibu baina ya klasta tatu za MKUZA

Marekebisho ya Msingi

Page 26: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

20

Klasta kuu ya MKUZA

Utawala Bora na Umoja wa Kitaifa ndio chimbuko la ukuaji wa uchumi na huduma bora za jamii

Klasta ya kwanza: Ukuaji wa Uchumi na Kupunguza Umaskini wa Kipato

Vyanzo vikuu vya ukuaji wa uchumi ambavyo Zanzibar inakusudia kuvipa msukumo katika kipindi cha utekelezaji wa mpango huu ni kama ifuatavyo: uendelezaji wa wafanyakazi na upatikanaji wa vitendea kazi, kuongeza tija, Kuendeleza Sekta Binafsi, Uwekezaji Katika Soko la Ndani na Uwekezaji Kutoka Nje.

Klasta ya pili: Huduma Na Ustawi Wa Jamii

Kuimarisha huduma na ustawi wa jamii ni mambo muhimu katika kupunguza umaskini. Jamii iliyoelimika na kuwa na afya bora inapelekea kuongezeka kwa uzalishaji, mgawanyo mzuri wa mapato na kuimarika kwa hali ya maisha.

Utawala Bora na Umoja wa Kitaifa

Ukuaji wa

Uchumi na

Kupunguza

Umaskini wa

Kipato

Huduma za

Ustawi wa

Jamii

Marekebisho ya

Msingi

Matarajio ya jumla

� Uchumi endelevu unaowalenga maskini

Malengo

� Kuandaa mazingira mazuri yatakayosaidia ukuwaji wa uchumi endelevu

� Kuendeleza uchumi mkuu endelevu wenye kuzingatia maskini

� Kupunguza umaskini wa kipato na kufanikisha upatikanaji wa uhakika wa chakula.

Ukuaji wa Uchumi na Kupunguza Umaskini

Page 27: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

21

Matarajio ya Jumla

� Kukuza ustawi wa jamii na upatikanaji wa huduma

� endelevu zilizo bora kwa jamii kwa kutilia mkazo

� maskini wanawake na wanaume na watu walio

� katika mazingira � magumu katika jamii.

Malengo

� Kuhakikisha upatikanaji fursa sawa za elimu bora inayooana na mahitaji na inayozingatia jinsia na mazingira.

� Kukuza hali ya afya ikiwemo afya ya uzazi, ustawi wa watoto, wanawake, wanaume na makundi yaliyo katika hatari.

� Kuongeza fursa za upatikanaji wa maji safi na salama ambayo pia watu wataweza kuyamudu hasa watu maskini wanawake na wanaume na makundi yaliyo katika hatari.

� Kuimarisha usafi wa mazingira na mazingira endelevu. � Kutoa fursa ya makaazi ya kutosha na endelevu ya

binadamu. � Kuongeza upatikanaji wa chakula na lishe miongoni mwa

watu maskini zaidi, watoto na makundi yaliyo katika hatari. � Kuimarisha na kueneza huduma za usalama na hifadhi ya

jamii kwa watu wasiopata huduma pamoja na makundi yaliyo hatarini

� Kuendeleza na kuhifadhi urithi wa kihistoria, kiutamaduni na wa asili pamoja na michezo kwaajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamiii.

Page 28: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

22

Klasta ya tatu: Utawala Bora na Umoja wa Kitaifa

Utawala Bora na Umoja wa Kitaifa unajumuisha (a) utawala wa sheria (b) kuwepo kwa demokrasia na mchakato shirikishi (c) kuimarisha haki za binadamu. Misingi mikuu ya utawala bora ni pamoja na kuwa na serikali yenye kuleta mabadiliko, usawa na uwajibikaji katika utekelezaji na utoaji wa maamuzi. Pia unazingatia michakato inayopelekea makundi ya watu na wananchi kueleza mahitaji yao, kuondoa tafauti zao na kudai haki zao za msingi. Haya yanapelekea kuwepo kwa umoja wa Kitaifa.

Matarajio ya jumla

� Kuwa na jamii inayoongozwa kwa utawala wa Sheria na Serikali yenye kutabirika, yenye uwazi na uwajibikaji.

Malengo

� Kuhakikisha ushirikishaji wa watu katika utawala na mchakato wa maendeleo.

� Kuweka ugawaji sawa wa rasilimali za umma, kuimarisha utoaji huduma bora na kurekebisha utumishi wa umma.

� Kuheshimu Utawala wa Sheria na kuweka fursa za kupata haki mahakamani

� Kuimarisha usalama wa raia � Kuongeza uwezo wa taasisi za serikali na watendaji wake. � Kupiga vita rushwa na vishawishi vyake na kuimarisha maadili

ya uongozi. � Kuimarisha Mfumo wa Sheria ili kusaidia ukuaji wa uchumi. � Kuimarisha taasisi za usimamizi na uwajibikaji ikiwemo fursa

za upatikanaji wa habari. � Kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa ajili ya kufuatilia na

kutathmini shughuli na mipango ya Serikali. � Kueneza utamaduni wa Utawala Bora katika ngazi zote. � Kukuza na kuheshimu haki za kibinadamu

Page 29: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

23

Sura hii inaeleza utekelezaji wa MKUZA na kuainisha wajibu wa watendaji wakuu. Utekelezaji wa MKUZA utaongozwa na mfumo wa klasta na Mfumo unaozingatia klasta na matokeo ambao unahitaji uratibu na ushirikiano wa karibu miongoni mwa sekta, Wizara, Idara na Mashirika na watekelezaji wengine wasiokuwa wa kiserikali wanaofanyakazi katika kila kikundi. Utaratibu wa kuratibu na kushirikiana utatoa fursa ya kuimarisha ushirikiano na kuunganisha nguvu wakati wa mchakato wa utekelezaji.

MKUZA utaoanisha na kujifungamanisha na michakato muhimu ya kitaifa

Utekelezaji imara wa MKUZA utategemea zaidi upatikanaji wa raslimali katika kufanikisha vipaumbele vya MKUZA. Mifumo mipya ya ugawaji wa raslimali itaanzishwa na kuwekwa ili kusaidia upatikanaji wa bajeti imara, ufuatiliaji wa matumizi, usimamizi na utoaji taarifa. MKUZA na MKUKUTA tayari umeshafungamanishwa katika mfumo wa mkakati wa aina moja na kuwa na kipindi kimoja cha utelekelezaji (2006 mpaka 2010). Mkakati wa Pamoja wa Misaada Tanzania (JAST)

ni mpango mpya unaotumiwa na Serikali na washirika wa Maendeleo katika kusimamia na kuongeza ubora wa Misaada kwa maendeleo. Utekelezaji wa Mkakati huo unaelekeza kuwepo kwa uoanisho na mafungamano ya michakato ya maendeleo baina ya Zanzibar na Tanzania Bara. Vile vile utahakikisha raslimali za kigeni zinakusanywa na kugawiwa ipasavyo katika sehemu zote mbili za Muungano katika kutekeleza mkakati huo. Washirika wa maendeleo watafanya kazi kwa karibu ili kuoanisha misaada kwa vipaumbele vya Taifa. Kujenga uwezo wa watendaji ni muhimu katika utekelezaji wa MKUZA. Watekelezaji wakuu

katika kila klasta wataainishwa kwa ajili ya mafunzo kupitia mchakato wa Mapitio ya Matumizi ya Serikali (MTEF). Mchakato huu utafungamanisha bajeti za Sekta, matarajio na shabaha za Utekelezaji za MTEFs na MKUZA

5. Nani atatekeleza MKUZA na vipi?

Uhusiano wa serikali na taasisi za kiraia utaongozwa na kujengwa

vizuri zaidi kupitia kukuza uwezo wa kiutendaji na majadiliano ya utetezi wa masuala mbalimbali.

Uwezo wa kiutendaji wa taasisi za kiraia utaimarishwa

kuwawezesha kikamilifu katika michakato ya maendeleo

Muundo wa utekelezaji

Page 30: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

24

Watekelezaji wakuu Majukumu

Baraza la Wawakilishi Kusimamia shughuli za Serikali zinazohusiana na MKUZA

Wizara ya Fedha na Uchumi Mratibu Mkuu wa shughuli zote za MKUZA

Wizara, Idara na Mashirika Kuandaa sera, kusimamia raslimali za umma, utekelezaji na usimamiaji.

Kuongeza ushiriki wa Wizara, Idara na Mashirika

Kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa sekta binafsi

Sekta binafsi Kusimamia shughuli za ukuaji wa uchumi na kuongeza kipato

Kushiriki katika kuboresha utoaji wa huduma za jamii

Jumuiya za Kiraia na Taasisi za Kidini Kushiriki katika kutengeneza Sera na Mipango na kusimamia utekelezaji wa mipango hiyo katika kufikia malengo ya MKUZA

Washirika wa Maendeleo Kutoa misaada ya kifedha na kiufundi

Kushiriki katika michakato ya mashauriano ya Kitaifa.

Wajibu na majukumu ya watekelezaji wakuu wa MKUZA

Page 31: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

25

Muundo, watekelezaji pamoja na hadidu rejea za Mpango Mkuu wa Ufuatiliaji wa MKUZA umefafanuliwa kwenye waraka mwengine. Kwenye sura hii tunazungumzia kwa ufupi kuhusu sekretarieti ya MKUZA, ngazi tatu za usimamizi wa MKUZA, vyanzo vya habari na kisha matokeo tunayotarajia kutokana na mfumo wa ufuatiliaji. Mwisho tunaorodhesha changamoto kadhaa zinazotukabili.

Kamati ya ufundi ya MKUZA ambayo ndiyo inayowajibika na uratibu wa jumla, iko chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi (MoFEA) akisaidiwa na Mratibu wa MKUZA. Mratibu huyo atafanya kazi kwa karibu na makundi manne ya Kitaalamu ya utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Ufuatiliaji wa MKUZA (Tazama Sanduku 5). Makundi hayo ya kitaalamu ni yale yanayohusika na (i) sensa, utafiti na taarifa za kila siku, (ii) Mapitio ya Matumizi ya Serikali (iii) Utafiti, uchambuzi na ushauri, (iv) Mawasiliano

Viashirio vya ufuatiliaji wa maendeleo ya MKUZA vimeandaliwa na vitafanyiwa marekebisho mara kwa mara. Viashirio hivyo vitajumuisha viashirio vikuu vya kila klasta pamoja na viashirio maalumu vya ziada vya kisekta vitakavyotolewa na wadau husika

Baraza la Mawaziri

Baraza litapokea taarifa juu ya shughuli za MKUZA kutoka Kamati ya Kiufundi ya Pamoja ya Wizara kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi ili kuifanyia maamuzi sahihi ya kisera.

Ngazi ya Taifa

IMTC inajumuisha Makatibu Wakuu wa Wizara zote za Serikali na Mwenyekiti wake ni Katibu Mkuu Kiongozi. Makatibu Wakuu ambao Makundi ya Kitaalamu ya Utekelezaji wa MKUZA yapo chini ya Wizara zao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi ambaye Sekretarieti ya MKUZA ipo chini yake watakuwa ni viungo baina ya Ufuatiliaji wa MKUZA na Kamati ya Kiufundi ya pamoja ya Wizara. Hadidu Rejea kwa ajili ya IMTC ni kutayarisha sera na mikakati kwa kutumia ugunduzi wa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya MKUZA na kutoa taarifa kwa Baraza la Mawaziri juu ya maendeleo ya MKUZA.

Ngazi ya Wilaya

Katika ngazi ya Wilaya, Afisa Tawala wa Wilaya ndiye atakuwa Katibu wa timu ya MKUZA Wilayani, ambayo inajumuisha Kamati ya Mipango ya Wilaya. Wajumbe wengine ni Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Wabunge na Madiwani walioko Wilayani. Katika ngazi hii, Mfumo

6. Ni jinsi gani ufuatiliaji na tathmini ya MKUZA

itafanyika?

Kamati ya Ufundi ya MKUZA

Ngazi za usimamizi wa MKUZA

Kisanduku 5: Uanachama wa makundi ya kitaalamu

Wataalamu husika watatoka katika wizara, idara na

mashirika, taasisi za elimu ya juu, Jumuiya za Kiraia,

Washirika wa Maendeleo na Sekta binafsi

Page 32: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

26

wa ufuatiliaji na tathmini utaratibiwa na kusimamiwa na Afisi ya Afisa Tawala wa Wilaya ambayo itawajibika kutoa taarifa kwa Wizara ya Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ.

Kamati ya Mipango ya Wilaya itapanga na kutekeleza shughuli zake kwa mujibu wa MKUZA na Mfumo wake wa ufuatiliaji na Tathmini. Shughuli hizi zitahitaji kuainisha michango na matokeo ambayo yatafuatiliwa na kutathminiwa. Wilaya itaweka viashirio maalum kwa ajili ya shabaha zake za maendeleo na shughuli zake pamoja na zile zilizotayarishwa kwa ajili ya klasta tatu katika ngazi ya Taifa

Kuna ngazi nne za mipango na utoaji maamuzi ndani ya SMZ, kwa hivyo upatikanaji wa habari huanzia katika ngazi hizo kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali ifuatalo

Ngazi Vyanzo

Kitaifa Tafiti na sensa

Wizara, Idara na Mashirika

Tafiti, sensa, takwimu rasmi, na mipango na taarifa za mwaka

Wilaya Tafiti, sensa, Mpango wa Kijamii wa Usimamizi wa Habari na Mfumo wa

Taarifa za Kawaida za wilaya

Shehia Vyanzo vyote hapo juu na buku la Shehia

Vyanzo vya Habari

Page 33: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

27

Sanduku 6: Tathmini Shirikishi ya Utoaji Huduma

Tathmini Shirikishi ya utoaji huduma inatumika katika MKUZA kama njia ya mrejesho kutoka kwa watumiaji

wa huduma. Itapaswa kufanyika kila mwaka ili kufanya tathmini na

matokeo yake yatazisaidia wizara husika kuboresha huduma. Utaratibu

huu utakuwa njia maalum ya kufikisha Sauti za wanyonge kwenye

MKUZA.

Matokeo makuu ya Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa MKUZA

Matokeo yanayotarajiwa kutokana na Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa MKUZA ni pamoja na: (i) Mapitio ya Matumizi Kisekta katika klasta zote tatu, (ii) Taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa MKUZA, na (iii) Taarifa ya Tathmini Shirikishi ya Utoaji Huduma (Tazama sanduku 6)

Changamoto

Changomoto zilizopo zinajumuisha:

� Hifadhi ya Taarifa za Kijamii na Kiuchumi ya Tanzania (TSED) inapaswa kutumiwa na wadau mbali mbali katika kuandaa mipango na sera. Hifadhi hii ya taarifa inahitaji marekebisho ya mara kwa mara pale taarifa mpya zinapopatikana.

� Kujenga uwezo wa Wizara, Idara, Mashirika, vyuo vikuu na taasisi za utafiti. � Kuimarisha Mfumo wa Usimamizi wa Habari katika kila Wizara, Idara, Shirika na

Wilaya ili ziweze kuandaa taarifa za mwaka juu ya upunguzaji wa umaskini kwa kutumia viashirio vilivyokubalika.

� Kufufua mfumo wa kiutendaji na ule wa taarifa za kila siku

� Kuimarisha Mfumo wa Kijamii wa Usimamizi wa Habari na daftari la kijiji katika ngazi ya Shehia.

� Kuwepo kwa ripoti ya Sensa ya Watu ya mwaka 2002 na taarifa juu ya Tathmini ya Matumizi ya Kaya ya mwaka 2004/2005 iliyokusanywa mpaka katika ngazi ya wilaya ni muhimu na zinatakiwa matumizi yake kutoa ramani ya Umaskini Zanzibar na Sura halisi ya Umaskini katika ngazi ya Wilaya

Page 34: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

28

Mambo matatu yanayopaswa kuzingatiwa katika mfumo wa ugharamiaji wa MKUZA ni raslimali kwa ajili ya MKUZA, mibadala ya bajeti, na hatari zinazoweza kutokea.

Ili kufikia matarajio yake, MKUZA unategemea michango kutoka sekta zote pamoja na wadau wote kwa mashirikiano na mafungamano. Hata hivyo, kuanzisha mfumo wa kusaidia muundo huo kunatoa changamoto kubwa.

Muundo wa kugharimia MKUZA unasimamiwa na mambo yafuatayo:

Kutokana na maelezo ya hapo juu ni wazi kuwa ukusanyaji wa raslimali kwa ajili ya kugharimia MKUZA utahusisha wigo mpana zaidi. Hata hivyo izingatiwe kuwa hii si kazi rahisi. Raslimali zaidi zinaweza kutoka katika vyanzo vifuatavyo:

7. Ugharamiaji wa MKUZA utakuwaje?

Raslimali kwa ajili ya MKUZA

� Ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) kwa kiwango cha asilimia 8-10 katika kipindi cha utekelezaji wa Mkakati kinaonesha ufanisi wa ukuaji uchumi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, ukisaidiwa na sekta kuu za uchumi.

� Kiwango cha mfumko wa bei kati ya asilimia 5-6 katika kipindi cha kati kinaonesha kiwango hicho hicho kwa Tanzania Bara na nchi jirani.

� Uwiano wa Kodi katika Pato la Taifa (juhudi za ukusanyaji mapato) kwa kiwango cha asilimia 18.5 kwa mwaka.

Mibadala ya bajeti

� Mapato yatakayotokana na kuoanisha MKUZA na MKUKUTA wa Tanzania Bara sambamba na Mkakati wa Pamoja wa Misaada (JAST)

� Uimarishaji zaidi wa vyombo vya ndani vya ukusanyaji mapato, hususan Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB). Vyombo hivi vitasaidia kutunisha mfuko wa raslimali kwa ajili ya kugharamia MKUZA.

� Kuwasaidia zaidi wadau wa ndani wasiokuwa wa kiserikali ili wasaidie kukuza mfuko wa raslimali.

� Raslimali kutoka nje ya nchi. Juhudi kubwa zinatakiwa kufanyika ili kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje ya nchi. Jambo hili kwa sasa linawezekana kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya uwekezaji.

� Kuzitangaza programu mbali mbali za MKUZA kwa wawekezaji bainifu.

Page 35: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

29

Makadirio ya raslimali yanatarajiwa kuongezeka kutoka shilingi milioni 161,014 kwa mwaka 2005/2006 hadi kufikia shilingi milioni 238,647 mwaka wa fedha 2008/2009. Takriban nusu ya raslimali inatokana na mapato ya ndani ikifuatiwa na mikopo ya miradi na misaada. Gharama za matumizi ya maendeleo zitategemea zaidi raslimali kutoka nje ya nchi.

Hatari zinazoweza kutokea katika Mfumo wa Ugharamiaji wa MKUZA

Hatari zinazoweza kuukabili Mfumo wa Ugharamiaji wa MKUZA ni pamoja na kuyumba kwa Uchumi Mkuu, majanga ya kimaumbile kama vile ukame na mafuriko, maendeleo makubwa katika uchumi wa dunia na kutotabirika kwa mtiririko wa raslimali kutoka nje. Mambo haya yanaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa mpango wa ugharamiaji. Zanzibar haina budi kujikinga na kujiandaa kukabiliana na misukosuko hiyo.

NATUAMINI MCHAKATO WA

MKUZA UTAIJENGEA

UWEZO SERIKALI KUFANYA MAMBO YAKE PASIPO

KUTEGEMEA SANA BAHASHA KUBWA YA HUYU

JAMAA

Page 36: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

30

Kundi lililo katika Hatari Sababu Kuu

Wanawake Ukosefu wa haki ya kudhibiti raslimali kuu za uzalishaji Majukumu ya kimila na kijamii Lishe duni na afya mbaya kwa mama wazazi

Vizuka Mzigo wa kushughulikia mayatima Kuwepo kwa watoto wengi wanaomiliki na kutumia ardhi isiyotosha.

Vijana Ukosefu wa kupata nyenzo za kuzalisha mali Ukosefu wa elimu ya kutosha au elimu ya amali Ukosefu mkubwa wa ajira Ndoa za mapema Majukumu ya kimila na kijamii (kwa wanawake na vijana)

Wazee

Ukosefu wa nyenzo za kuzalisha mali Kukosa uwezo wa kutumia raslimali zilizopo. Kukosekana kwa utaratibu wa misaada ya kijamii Mzigo wa kuwatunza mayatima Afya mbaya

Watoto waliotelekezwa Kuwa miongoni mwa familia kubwa Ukosefu wa misaada ya kijamii na utaratibu wa hifadhi ya jamii. Ukosefu wa chakula na lishe ya uhakika

Mayatima Ukosefu wa mahitaji ya msingi – chakula, makaazi na mavazi. Kuishi na familia kubwa zenye kukosa matunzo ya wazazi. Kuishi na VVU na UKIMWI Ukosefu wa misaada ya kiafya na kielimu Ukosefu wa raslimali zenye kuzalisha Ukosefu wa chakula na lishe ya uhakika

Watu wenye ulemavu Ubaguzi katika familia na jamii kwa jumla Kukosa umiliki wa raslimali kuu kama ardhi Upatikanaji mdogo wa nyumba na usafiri wa umma Kukosekana kwa uwezo wa kujishughulisha katika shughuli za kujipatia mapato.

Watu wanaoishi na VVU na UKIMWI

Ubaguzi na kutengwa kijamii (unyanyapaa) Uwezo mdogo wa kushiriki katika shughuli za kiuchumi Kutopatikana kwa mahitaji ya msingi ya huduma muhimu za afya na matunzo Lishe duni

Maskini wa vijijini na wenye kukosa chakula cha uhakika

Upatikanaji mdogo wa ardhi na nyenzo za kuzalisha mali Vyanzo vidogo vya kujipatia mapato Kuathirika kwa haraka kutokana na majanga ya kimaumbile na yale ya kiuchumi.

Maskini wa mijini na wenye kukosa chakula cha uhakika

Ukosefu mkubwa wa ajira mijini Mazingira machafu na makaazi duni

Chanzo: Taarifa ya Uchambuzi wa Uhakika wa Chakula na Hali halisi ya Lishe (SMZ, 2006)

MMMAAAKKKUUUNNNDDDIII YYYAAALLLIIIYYYOOO KKKAAATTTIIIKKKAAA HHHAAATTTAAARRRIII NNNAAA SSSAAABBBAAABBBUUU

ZZZAAA HHHAAALLLIII HHHIIIYYYOOO

MMM

KKK

UUU

ZZZ

AAA

Page 37: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

31

Katika sehemu hii tunaorodhesha baadhi ya shabaha za utekelezaji, changamoto na hatua za utekelezaji muhimu zilizomo kwenye klasta tatu za MKUZA.

KLASTA 1: UKUAJI WA UCHUMI NA UPUNGUZAJI WA UMASKINI WA KIPATO

LENGO LA 1 - KUANDAA MAZINGIRA MAZURI YA UKUAJI WA UCHUMI

SHABAHA ZA UTEKELEZAJI

CHANGAMOTO HATUA ZA UTEKELEZAJI

1.1.1 Mazingira bora ya uchumi mkuu yawe yamekuzwa

���� Mfumko mkubwa wa bei ���� Mifumo duni ya usimamizi wa fedha

na madeni ���� Uwezo mdogo wa sekta binafsi ���� Uwezo mdogo wa utafutaji raslimali

kutoka nje ya nchi

���� Dhibiti kasi ya mfumko wa bei

���� Tekeleza awamu ya pili ya marekebisho ya huduma za fedha

���� Chukua hatua za kupunguza riba kwenye taasisi zinazokopesha

���� Tafuta raslimali kutoka nje ya nchi ili kuimarisha mazingira ya uchumi na maendeleo

1.1.2 Ukusanyaji wa mapato uwe umeongezeka kutoka 13.8 % ya pato la taifa 2005 hadi 18.5 % ifikapo mwaka 2010

���� Mazingira ya fedha yasiyoridhisha ���� Ukosefu wa sera ya kodi na

uendeshaji mbaya wa masuala ya utozaji kodi

���� Wigo mdogo wa ukusanyaji mapato (kwa mfano mchango mdogo wa mapato kutoka sekta ya utalii)

���� Tekeleza mapendekezo ya utafiti wa vyanzo vya mapato

���� Tayarisha sera ya mapato na kuendeleza programu ya usimamizi wa kodi (TAP)

���� Imarisha muundo na utendaji wa sekta ya utalii

���� Fanya utafiti wa mapato yanayotokana na sekta ya utalii

VVVIIIAAAMMMBBBAAATTTIIISSSHHHOOO MMM

KKK

UUU

ZZZ AAA

Page 38: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

32

SHABAHA ZA

UTEKELEZAJI

CHANGAMOTO HATUA ZA UTEKELEZAJI

1.1.3 Mazingira mwafaka kwa maendeleo ya sekta binafsi kwa kuzingatia miradi midogo na ya kati (SMEs) yawe yameendelezwa.

���� Masharti magumu kwa waombaji wanaotaka kuwekeza

���� Upatikanaji mgumu wa huduma za fedha

���� Matatizo ya upatikanaji wa miundo mbinu, mtaji na wafanyakazi wenye ujuzi

���� Sheria duni za umilikaji wa ardhi ���� Matatizo ya upatikanaji wa

masoko ���� Uratibu duni wa miradi midogo na

ya kati (SMEs)

���� Wezesha Baraza la Biashara kufanya kazi na Mpango wa Kuimairisha Mazingira ya Biashara (BEST) unaotumika Tanzania Bara utumike Zanzibar pia

���� Imarisha mazingira ya biashara na kuwapa motisha wawekezaji

���� Tekeleza sera ya miradi midogo na ya kati

���� Andaa mazingira bora ya sera na sheria kuendeleza sekta binafsi

���� Kukuza uwezo wa ujasiriamali kwa wanawake na wanaume

1.1.4 Ubora wa nguvu kazi uwe umeimarishwa na kasi ya ongezeko la idadi ya watu iwe imepunguzwa

���� Masuala yanayohusu watu hayazingatiwi vya kutosha wakati wa matayarisho ya mipango ya maendeleo

���� Mfumo usioridhisha wa uratibu wa tafiti na takwimu za idadi ya watu na maendeleo

���� Kiwango kikubwa cha ongezeko la watu na uzazi

���� Tekeleza sera ya idadi ya watu na mipango yake

���� Ongeza na imarisha taaluma za wafanyakazi

���� Anzisha programu za kuendeleza taaluma za wafanyakazi wanawake

1.1.5 Upatikanaji wa haki za ardhi uwe umeongezeka

���� Mfumo mgumu wa umilikaji ardhi ���� Utekelezaji hafifu wa mpango wa

matumizi ya ardhi ���� Ongezeko la makaazi yasiyokuwa

na mpango

���� Pitia na kutekeleza sheria zinazohusiana na masuala ya ardhi

���� Imarisha mchakato wa mgawanyo na usimamizi wa ardhi

���� Jamii ijulishwe sera na sheria zinazohusu matumizi ya ardhi

1.1.6 Ongezeko la upatikanaji wa nishati rahisi na endelevu uwe umefikiwa ifikapo mwaka 2010

���� Kukosekana kwa sera na mikakati kuhusu nishati

���� Umeme unaopatikana Unguja hautoshi kutokana na uchakavu wa waya unaoleta umeme kutoka Tanzania Bara ambao tayari umezidiwa nguvu

���� Umeme Pemba ni ghali na upatikanaji wake si wa uhakika

���� Matumizi madogo ya vyanzo mbadala vya nishati

���� Tayarisha na tekeleza sera na mkakati wa nishati

���� Tayarisha makadirio ya mahitaji ya nishati ya muda wa kati na mrefu.

���� Badilisha waya chakavu wa umeme ulioko baharini kutoka Tanzania Bara

���� Unganisha umeme Pemba kutoka Tanga kupitia baharini

Page 39: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

33

Shabaha za utekelezaji Changamoto Hatua za utekelezaji

1.1.7 Mazingira mazuri ya uwekezaji yawe yametayarishwa

���� Mashirikiano hafifu baina ya serikali na sekta binafsi

���� Mazingira ya uwekezaji yasiyoridhisha

���� Urasimu mkubwa katika uwekezaji

���� Kuwepo kwa kodi nyingi na mamlaka nyingi za kodi

���� Anzisha na kutumia kanda maalum za uchumi

���� Anzisha na tekeleza Mpango wa kuimarisha Mazingira ya Biashara (BEST) Zanzibar

���� Andaa taarifa ya uwekezaji kisekta itakayotumika kukuza uwekezaji

���� Tekeleza sera na sheria za uwekezaji

1.1.8 Mfumo endelevu wa usimamizi wa mazingira unaolenga jinsia uwe umetayarishwa

���� Uharibifu wa ardhi na kukithiri kwa uchimbaji wa mchanga na mawe

���� Uchafuzi uliokithiri wa bahari ���� Ukataji wa miti uliopindukia

mpaka na vyanzo vya maji visivyohifadhiwa

���� Endeleza utafiti kuhusu tishio la uharibifu wa mazingira (lililopo na litakalotokea)

���� Hifadhi na karabati vyanzo vya maji na misitu asili

���� Imarisha programu za elimu ya mazingira kwa wanaume na wanawake

���� Endeleza uhifadhi wa mazingira na mahusiano ya viumbe vya baharini

1.1.9 Barabara kuu na ndogo zilizobaki ziwe zimekarabatiwa

���� Mtandao duni wa barabara ndogo za vijijini

���� Tekeleza Mpango Mkuu wa Usafirishaji

���� Jenga na karabati barabara ndogo za vijijini

1. 1.10 Mpango Mkuu wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar uwe umeanzishwa na kutekelezwa na huduma kwenye uwanja wa ndege wa Pemba ziwe zimeimarishwa

���� Kukosekana kwa huduma muhimu za viwanja vya ndege na bandari Zanzibar

���� Andaa na tekeleza Mpango Mkuu wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar

���� Weka huduma bora na endelevu katika uwanja wa ndege wa Pemba

���� Weka huduma bora na endelevu katika bandari za Zanzibar

���� Ongeza ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kuendeleza miundombinu

1. 1.11. Upatikanaji na utumiaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano uwe umekuzwa

���� Upatikanaji duni wa huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

���� Andaa na tekeleza sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

���� Anzisha huduma na mtandao wa kijamii wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Page 40: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

34

Lengo la 2 - ENDELEZA UCHUMI ENDELEVU WENYE WIGO MPANA NA UNAOLENGA MASKINI

SHABAHA ZA UTEKELEZAJI

CHANGAMOTO MIKAKATI YA UTEKELEZAJI

� Kiwango cha ukuaji wa uchumi kiwe kimeongezeka kutoka asilimia 5.6 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 10 mwaka 2010

� Vitega uchumi vichache katika sekta za uzalishaji

� Uhusiano mdogo baina ya sekta na sekta.

� Andaa na kutekeleza mkakati wa ukuaji wa uchumi utakaozingatia jinsia.

� Imarisha na endeleza vitega uchumi katika sekta za huduma na za uzalishaji kama zilivyobainishwa katika mkakati wa ukuaji wa uchumi kama vile uvuvi wa bahari kuu.

� Endeleza uhusiano wa kisekta.

� Maeneo ya urithi wa kihistoria yawe yamehifadhiwa na kutunzwa na wakati huo huo utalii wa kimaumbile na wa kiutamaduni uwe umeendelezwa.

� Utunzaji duni wa maeneo ya urithi wa Kihistoria na ya kiutamaduni.

� Endeleza na hifadhi eneo la Urithi wa Kihistoria na kiutamaduni la Mji Mkongwe.

� Endeleza na hifadhi maeneo ya vivutio vya Utalii.

� Ukuaji wa Sekta ya Kilimo uwe umeongezeka kutoka asilimia 2.4 mwaka 2005 hadi asilimia 6 mwaka 2010.

� Bajeti ndogo inayopewa sekta ya kilimo.

� Upatikanaji mdogo wa huduma za fedha kwa ajili ya sekta ya kilimo mfano mikopo midogo midogo

� Kutegemea kilimo cha mvua. � Uzalishaji mdogo na mfumo

duni wa masoko kwa bidhaa asilia na zisizo asilia zinazosafirishwa nje ya nchi.

� Ongezeko kubwa la wadudu waharibifu wa mazao.

� Ongeza bajeti ya sekta ya kilimo. � Andaa huduma za fedha vijijini na

Imarisha michango ya kilimo. � Hamasisha ushiriki wa sekta

binafsi katika sekta ya kilimo. � Endeleza miradi ya viwanda vya

mazao ya kilimo. � Tekeleza mkakati wa kuendeleza

zao la karafuu � Tekeleza mpango mkuu wa kilimo

cha umwagiliaji. � Toa motisha kwa wakulima wawe

na uzalishaji wa mazao mengi. � Tetea programu za kuendeleza

matumizi ya njia mchanganyiko za uzalishaji na udhibiti wa viumbe waharibifu wa mimea.

SHABAHA ZA UTEKELEZAJI

CHANGAMOTO MIKAKATI YA UTEKELEZAJI

� Upatikanaji wa huduma na fursa za mikopo midogo midogo ya fedha kwa kuzingatia jinsia uwe umeimarika

� Upatikanaji hafifu wa huduma za mikopo midogo midogo

� Imarisha huduma za fedha vijijini zenye kuzingatia jinsia.

� Mazingira bora ya biashara ya nje yawe yameimarika.

� Juhudi ndogo ya kukuza biashara ya nje.

� Uzalishaji mdogo wa bidhaa za kilimo na za viwanda zinazosafirishwa nje.

� Tekeleza mkakati wa kusafirisha bidhaa nje ya nchi.

� Kuza kazi za kituo cha habari za biashara.

� Rahisisha upatikanaji wa soko la nje kwa wanawake na walemavu.

Page 41: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

35

1.2.6 Hoteli za daraja la juu na huduma ziwe zimeongezeka.

� Miundo mbinu duni na ukosefu wa huduma nyengine zinazohusiana na Utalii.

� Uwezo mdogo wa kiutendaji katika huduma za sekta ya utalii.

� Kuza uwezo wa kiujuzi na usiokuwa wa kiujuzi katika nyanja ya ukarimu na ukaribishaji wageni

� Imarisha miundo mbinu na huduma zinazohusiana na utalii.

1.2.7 Ukosefu wa ajira uwe umepunguzwa kutoka kiwango cha asilimia 7 kwa mwaka 2005 hadi asilimia 4 ifikapo mwaka 2010

� Ongezeko la ukosefu wa ajira. �

� Buni na tekeleza mfumo wa habari wa soko la ajira.

� Anzisha, imarisha na saidia biashara ndogo na kati.

LENGO LA 3: PUNGUZA UMASKINI WA KIPATO NA KUWA NA UHAKIKA WA UPATIKANAJI WA

CHAKULA

SHABAHA ZA UTEKELEZAJI

CHANGAMOTO

MIKAKATI YA UTEKELEZAJI

� � �

� Idadi ya watu wanaoishi chini ya kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi kiwe kimepungua kutoka asilimia 49 mwaka 2005 hadi asilimia 25 ifikapo 2010.

� Tija ndogo na fursa chache za kuongeza kipato katika maeneo ya vijijini.

� Imarisha uhusiano baina ya sekta ya kilimo na zisizokuwa za kilimo katika kuongeza kipato na hali ya maisha.

� Imarisha ushiriki wa jamii za vijijini katika shughuli zinazohusiana na utalii.

� Tayarisha mazingira bora kwa ajili ya kuendeleza vitega uchumi vijijini.

� Idadi ya watu wanaoishi chini ya kiwango cha umaskini wa chakula iwe imepungua kutoka asilimia 13 mwaka 2005 hadi asilimia 10 ifikapo mwaka 2010.

� Idadi kubwa ya watu wanaokabiliwa na tatizo la kutokuwa na uhakika wa kupata chakula na lishe.

� Fursa chache za raslimali za uzalishaji kwa wanawake.

� Imarisha hatua zinazolenga kupunguza madhara kwa wanawake na makundi mengine yaliyo katika hatari.

� Anzisha na tekeleza miradi midogo ya kilimo cha umwagiliaji maji.

� Imarisha maisha ya watu kwa kusaidia uendelezaji wa kilimo cha mwani, ufugaji na uvuvi.

� Anzisha programu za viwanda vidogo vidogo vya kusindika na vya kutengeneza vyakula.

KLASTA 2: HUDUMA NA USTAWI WA JAMII

Page 42: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

36

LENGO LA 1 - HAKIKISHA USAWA KATIKA KUTOA ELIMU BORA INAYOZINGATIA JINSIA

Shabaha za utekelezaji

Changamoto Mikakati ya utekelezaji

A. Elimu ya maandalizi na maendeleo 2.1.1 Kiwango cha

uandikishaji kwa skuli za maandalizi kiwe kimeongezeka kutoka asilimia 15.9 katika mwaka 2005 na kufikia asilimia 50 ifikapo 2010

���� Uandikishaji mdogo wa watoto katika skuli za maandalizi.

���� Huduma duni za utunzaji wa mtoto.

���� Hamasisha wawekezaji binafsi na jamii kuanzisha skuli za maandalizi hasa katika maeneo ya vijijini pamoja na maeneo ambayo ni vigumu kufikika.

���� Anzisha madarasa ya skuli za maandalizi katika skuli za msingi.

���� Toa huduma na mafunzo kwa walimu ili waweze kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalum.

B. Elimu ya msingi 2.1.2 Kiwango cha

uandikishaji wanafunzi kiwe kimeongezeka kutoka asilimia 77 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2010.

���� Upungufu mkubwa wa madarasa

���� Uwezo mdogo wa kuchangia fedha kwa maskini na familia zilizo katika hatari

���� Idadi kubwa ya wanafunzi wa kike na wa kiume wanaokatisha masomo.

���� Imarisha mazingira ya skuli na mahusiano mazuri ya kijinsia

���� Kuhamasisha jamii kuwandikisha watoto wenye umri wa kwenda skuli.

���� Hakikisha kwamba wanafunzi wote wakiwemo wenye ulemavu, mayatima na watoto walio katika hatari wanapata elimu bora ya msingi na kumaliza masomo

���� Anzisha njia mbadala ya michango ya skuli kwa maskini na familia zilizo katika hatari

C. Elimu ya sekondari 2.1.3 Kiwango cha

mpito katika mitihani ya kidato cha pili kutoka asilimia 47.6 katika mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 70 mwaka 2010 kiwe kimeongezeka.

���� Mrundikano mkubwa wa wanafunzi katika skuli za sekondari

���� Ukosefu wa vifaa vya maabara, madawa na vitabu vya kiada

���� Ongeza fursa ya upatikanaji wa elimu ya sekondari katika maeneo yaliyokosa huduma za msingi (katika Wilaya zote).

���� Toa motisha kwa sekta binafsi ili waweze kuanzisha skuli nyingi zaidi

���� Hakikisha upatikanaji wa vifaa vya maabara, madawa na vitabu vya kiada

Page 43: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

37

2.1.4 Uwiano wa watoto wa kike wanaoendelea na masomo ya sekondari ya awali na ya juu uwe imeongezeka

� Ufanisi mdogo unaosababishwa na uwezo mdogo wa kuingiza jinsia katika mitaala, njia za usomeshaji na vifaa vya usomeshaji

���� Anzisha elimu ya maandalizi ya ufundi inayozingatia jinsia katika elimu ya sekondari.

D. Sayansi na Teknolojia 2.1.5 Usomeshaji wa

sayansi, hisabati na teknolojia katika skuli uwe umeimarishwa.

���� Matokeo mabaya ya mitihani katika masomo ya sayansi na hisabati hasa wanafunzi wa kike.

���� Upungufu wa wataalamu wa sayansi, hisabati na teknolojia.

� Imarisha msingi wa masomo ya sayansi na hisabati katika skuli na vyuo vya elimu ya juu.

� Weka mipango itakayowavutia na itakayowahamasisha walimu kusomesha sayansi, hisabati na elimu ya ufundi.

Shabaha za utekelezaji

Changamoto Mikakati ya utekelezaji

E. Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika elimu 2.1.6 Fursa za

upatikanaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa ajili ya maendeleo ya elimu ziwe zimeongezeka.

���� Ukosefu wa sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika elimu.

���� Maendeleo duni ya programu za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hasa za serikali na vijijini.

� Anzisha na tekeleza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika sera ya elimu.

� Panua eneo la miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika skuli na katika jamii.

� Tilia mkazo ubia baina ya sekta binafsi na ya umma juu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa ajili ya elimu

F. Elimu isiyo rasmi 2.1.7 Kiwango cha

kujua kusoma na kuandika kiwe kimeongezeka kutoka asilimia 75.8 mwaka (2005) mpaka kufikia asilimia 100 ifikapo mwaka 2010.

���� Idadi ya watu wenye kujua kusoma na kuandika kwa kudodosa miongoni mwa vijana walio nje ya skuli inaongezeka.

���� Asilimia kubwa ya wanawake wasiojua kusoma na kuandika.

� Panua elimu isiyo rasmi kwa njia ya mashirikiano na makundi ya kijamii, jumuiya za kiraia na watu binafsi.

� Toa elimu ya kutosha ya kinga dhidi ya VVU/UKIMWI yenye kulenga jinsia na ya mjumuisho kwa wawezeshaji wa vituo vya elimu visivyo rasmi.

� Anzisha programu mbadala za mafunzo zinazozingatia jinsia kwa ajili ya vijana wasiokuwa skuli.

Shabaha za utekelezaji

Changamoto Mikakati ya utekelezaji

Page 44: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

38

G. Elimu ya Ufundi na Mafunzo 2.1.8 Ujuzi wa

ujasiriamali miongoni mwa vijana uwe umeimarishwa.

���� Ujuzi duni wa elimu ya amali na ujasiriamali miongoni mwa wahitimu.

� Ongeza miundombinu ya mafunzo kwa ajili ya kuendeleza ujuzi na elimu.

H. Elimu ya juu

2.1.9 Uwiano wa idadi ya wahitimu wa Taasisi za Elimu ya Juu uwe umeongezeka

���� Uwezo mdogo wa Taasisi za elimu ya juu

���� Masomo yanayosomeshwa hayaoani na mahitaji ya soko la ajira.

���� Ushiriki mdogo wa wanawake na watu wenye ulemavu katika taasisi za elimu ya juu.

� Ongeza uwezo katika taasisi za elimu ya juu.

� Rekebisha mitaala ya taasisi za elimu ya juu ili iende sambamba na vipaumbele vya Taifa.

� Ongeza nafasi kwa wanawake na watu wenye ulemavu katika taasisi za elimu ya juu.

I. Ubora wa elimu

2.1.10 Ubora wa elimu katika ngazi zote uwe umeimarishwa.

���� Upungufu wa walimu wenye sifa.

���� Uwezo mdogo na ujuzi katika masuala ya jinsia na mbinu shirikishi.

� Ongeza bajeti ya elimu kwa ajili ya maendeleo ya elimu mpaka kufikia asilimia 20 ya matumizi ya Serikali.

� Toa elimu bora, na zana za kujifunzia zenye kuzingatia mahitaji ya kijinsia.

LENGO LA 2 - IMARISHA HALI YA AFYA IKIWEMO AFYA YA UZAZI, USTAWI WA

JAMII KWA WATOTO, WANAWAKE NA MAKUNDI YALIYO KATIKA HATARI

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji

A. Afya ya watoto chini ya miaka mitano 2.2.1 Vifo vya watoto viwe

vimepungua kutoka watoto 61kwa kila watoto 1000 mwaka 2005 hadi watoto 55 ifikapo mwaka 2010.

2.2.2 Vifo vya watoto chini ya

miaka 5 viwe vimepungua kutoka watoto 101 kwa kila watoto 1000 katika mwaka 2005 hadi kufikia watoto71 ifikapo mwaka 2010.

���� Vifo vya watoto chini ya miaka 5 bado ni vya juu.

���� Ugonjwa wa malaria umeenea sana ingawa imeonekana kupungua katika miaka ya karibuni.

���� Ongeza huduma za kinga kwa antijeni.

���� Ongeza matumizi ya vyandarua vilivyotiwa dawa ya muda mrefu,na dumisha utiaji wa dawa kwa vyandarua vilivyokwisha dawa.

���� Imarisha usimamizi wa malaria pamoja na maradhi mengine ya watoto.

���� Imarisha na eneza utoaji wa huduma za kinga kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, Ushauri nasaha na kupima kwa hiari, huduma rafiki kwa vijana na huduma za matibabu ya magonjwa ya zinaa.

���� Shirikisha jamii katika suala kinga pamoja na kampeni.

B. Afya ya Mama na Afya ya Uzazi

Page 45: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

39

2.2.3 Vifo vya mama wajawazito viwe vimepungua kutoka uwiano wa mama wajazito 377 kwa kila 100,000 katika mwaka 1999 mpaka uwiano wa mama wajazito 251 kwa kila 100,000 ifikapo mwaka 2010.

2.2.4 Wazazi wanaopata

huduma ya afya wawe wameongezeka kutoka asilimia 49 katika mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 60 mwaka 2010.

���� Vifo vya mama wajawazito bado vingi

���� Imarisha uwezo wa ujuzi wa wale wanaotoa huduma za ukunga

���� Imarisha fursa ya jamii kupata taarifa na huduma sahihi.

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji

C. Maradhi ya kuambukiza – (I) VVU/UKIMWI 2.2.5 VVU miongoni mwa

wajawazito wenye umri baina ya miaka 15 na 24 viwe vimepungua kutoka asilimia 1 mwaka 2005 hadi asilimia 0.5 mwaka 2010.

2.2.6 Idadi ya watu wenye

uelewa sahihi wa VVU/UKIMWI iwe imeongezeka kutoka asilimia 44 kwa wanawake na asilimia 20 kwa wanaume hadi kufikia asilimia 80 kwa watu wote.

2.2.7 Unyanyapaa katika

masuala ya VVU/UKIMWI uwe umepungua kutoka asilimia 76 mwaka 2005 hadi asilimia 60 mwaka 2010.

���� Muamko mdogo wa jamii juu ya haki ya kufanya mapenzi na afya ya uzazi.

���� Huduma chache za ukunga wa dharura

���� VVU/UKIMWI bado ni

changamoto kubwa kwa Zanzibar.

���� Ongezeko la watu wenye VVU/UKIMWI na magonjwa ya zinaa hasa miongoni mwa wanawake.

���� Matumizi madogo ya huduma zilizopo za kinga na matibabu ya VVU/UKIMWI

���� Panua huduma za dharura za ukunga zikizingatia mahitaji ya makundi ya watu walio katika hatari.

���� Ongeza uwezo wa kitaifa ili kuhakikisha usalama wa afya ya uzazi.

���� Imarisha elimu ya kinga dhidi ya VVU/UKIMWI yenye kuwalenga vijana, wanawake na makundi ya watu walio katika hatari ya kuambukizwa, kama vile watu wenye ulemavu, mayatima na watoto.

���� Imarisha fursa ya jamii kupata taarifa na huduma sahihi kutoka kwa wafanyakazi wa afya.

���� Anzisha na tekeleza mkakati wakutangaza na mawasiliano juu ya VVU/UKIMWI.

���� Jenga uwezo wa jumuiya za kiraia kupambana kikamilifu na VVU na UKIMWI

Page 46: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

40

Shabaha za utekelezaji

Changamoto Mikakati ya utekelezaji

(II) Malaria 2.2.8 Idadi ya

wagonjwa wa malaria iwe imepungua kutoka asilimia 45 mwaka 2004 hadi asilimia 35 mwaka 2010.

���� Kuenea kwa malaria ���� Kuenea ugonjwa na vifo vingi

hasa kwa watoto na wajawazito.

���� Kuchelewa kuchunguzwa hasa katika ngazi ya jamii.

���� Imarisha usimamizi wa kesi maalumu za wagonjwa hasa watoto, mayatima, watoto walio katika hatari na mama wajawazito.

���� Panua huduma za uchunguzi kwa kutumia RDT katika ngazi ya msingi.

���� Imarisha huduma zinazosimamiwa na jamii

(III) Kifua kikuu 2.2.9 Idadi ya vifo

vinavyosababishwa na kifua kikuu iwe imepungua kutoka asilimia 8 hadi 5 ifikapo mwaka 2010.

���� Ongezeko kubwa la ugonjwa wa kifua kikuu.

���� Ongeza udhibiti na usimamizi wa kifua kikuu.

���� Imarisha huduma za uchunguzi kwa ngazi zote.

���� Shirikisha jamii kutumia huduma zilizopo.

D. Maradhi yasiyoambukiza - (NCDs) 2.2.10 Utafiti wa

maradhi makuu yasiyoambukiza uwe umefanywa ifikapo 2010

���� Kuogezeka kwa maradhi na vifo vinavyosababishwa na Maradhi yasiyoambukizwa.

���� Jamii kukosa mwamko juu ya mwenendo wa maisha ya kiafya.

���� Toa zana muhimu na Imarisha usambazaji wa madawa na vifaa vyengine.

���� Imarisha uwezo wa kiutendaji (usimamizi, majengo na watendakazi) kwa ajili ya kushughulikia magonjwa ya akili.

���� Imarisha elimu ya afya na lishe kwa jamii.

LENGO LA 3 - ONGEZEKO LA FURSA YA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI, SALAMA

NA RAHISI

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji 2.3.1 Upatikanaji wa

huduma endelevu za maji kwa maeneo ya mijini uwe umeongezeka kutoka asilimia 75 mwaka 2005 hadi asilimia 90 mwaka 2010

���� Upungufu wa maji safi na salama kwa maeneo ya mijini na vijijini

���� Miundombinu chakavu ya usambazaji maji.

���� Fanya matengenezo ya kawaida ya miundombinu ya usambazaji maji. ���� Imarisha ubia baina ya sekta ya

umma, binafsi na jumuiya zisizo za kiserikali katika utoaji wa huduma ya maji.

���� Imarisha mifumo ya usambazaji maji inayosimamiwa na jamii.

Page 47: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

41

LENGO LA 4 - UIMARISHAJI WA MAJI SAFI NA MAZINGIRA ENDELEVU

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji A. Michirizi na Usafi 2.4.1 Kiwango cha

upatikanaji wa huduma bora za usafi majumbani kiwe kimongezeka kutoka asilimia 67 mwaka 2005 hadi asilimia 83 mwaka 2010.

���� Huduma chache za usafi wa mazingira

���� Huduma chache za michirizi

���� Imarisha usarifu na utupaji wa taka ngumu na taka za hospitali.

���� Anzisha Mamlaka ya kusimamia usafi na hakikisha yanafanya kazi ipasavyo.

���� Kuza ushirikiano wa sekta binafsi na ya umma katika usimamizi wa taka.

B. Mazingira 2.4.2 Uharibifu wa

mazingira uwe umepungua.

���� Uharibifu wa mazingira ���� Ufahamu mdogo wa

masuala ya mazingira

���� Shajiisha upandaji miti ���� Kuza uendelezaji na matumizi ya

nishati mbadala ���� Endeleza matumizi ya mbinu bora

na sahihi za kilimo ���� Hifadhi mfumo wa kimaumbile asilia

wa bahari kwa kuendeleza uvuvi endelevu

LENGO LA 5 - UPATIKANAJI WA MAKAAZI BORA NA ENDELEVU

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji

2.5.1 Mpango sahihi wa matumizi ya ardhi katika ngazi ya jamii na kitaifa uwe umefanyiwa mapitio na kuendelezwa.

���� Mipango duni ya makaazi ya watu katika maeneo ya mijini na vijijini.

���� Ukosefu wa huduma za mikopo kwa ajili ya makaazi

���� Ongeza na imarisha upatikanaji wa makaazi rahisi hasa kwa maeneo ya vijijini na ng’ambo.

���� Anzisha huduma za mikopo kwa makaazi. ���� Shirikiana na sekta binafsi na sekta

zinazotoa huduma, jumuiya za kiraia na washirika wengine katika kuwapatia makaazi bora watu kutoka makundi yaliyokosa huduma za msingi.

Page 48: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

42

LENGO LA 6 - ONGEZA UPATIKANAJI WA CHAKULA NA VIRUTUBISHO

MIONGONI MWA MASKINI, WAJAWAZITO, WATOTO NA MAKUNDI YA WATU WALIO KATIKA HATARI

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji 2.6.1 Utapiamlo kwa

watoto chini ya umri wa miaka mitano uwe umepungua.

� 2.6.2 Kiwango cha

utapiamlo kwa wanawake na wajawazito kiwe kimepungua

���� Kiwango cha utapiamlo miongoni mwa watoto walio chini ya miaka 5 bado ni kikubwa

���� Lishe duni. ���� Mwamko mdogo juu

masuala ya lishe na chakula bora

���� Kiwango kikubwa cha vifo

vya watoto ���� Ukosefu wa virutubisho kwa

watoto walio na chini ya umri wa miaka mitano na waja wazito

���� Endeleza taratibu bora za ulishaji na uwachishaji kunyonya kwa watoto waliochini ya miaka 5

���� Endeleza mikakati ya lishe inayosimamiwa na jamii.

���� Imarisha elimu ya afya inayozingatia lishe

���� Imarisha na panua programu za kuwezesha upatikanaji wa chakula kwa makundi yaliyohatarini wakiwamo wajawazito na watu maskini wanaoishi na VVU na UKIMWI.

LENGO LA 7 - IMARISHA NA PANUA WIGO WA HIFADHI YA JAMII NA MTAJI WA

KIJAMII KWA MAKUNDI YA WATU WALIO KATIKA HATARI

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji 2.7.1 Imarisha mtaji wa

kijamii. � Misaada ya ustawi wa

jamii kwa makundi ya watu walio katika hatari iwe imeimarishwa na kusogezwa

� 2.7.2 Panua wigo wa

hifadhi ya Jamii. � Punguza malimbikizo na

harakisha kulipa mafao ya wastaafu.

� Panua wigo wa miradi ya Ustawi wa Jamii

���� Hatua chache za kusaidia watu waliokosa huduma za msingi na walio katika hatari.

���� Limbikizo kubwa la malipo ya mafao ya wastaafu.

���� Miradi michache ya Ustawi wa Jamii

���� Anzisha na tekeleza programu za kuwawezesha kiuchumi watu waliokosa huduma za msingi na walio katika hatari

���� Imarisha mtandao wa jumuiya za kiraia zenye kutetea na kushughulikia masuala ya watu waliokosa huduma za msingi na makundi ya watu walio katika hatari.

���� Anzisha programu za kulipa malimbikizo ya mafao ya wastaafu.

���� Hamasisha kuanzishwa kwa programu za Hifadhi ya Jamii zinazosimamiwa na Jamii.

���� Rekebisha na Imarisha programu za makazi na huduma nyengine kwa wazee na mayatima.

Page 49: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

43

LENGO LA 8 - KUZA NA HIFADHI URITHI WA KIHISTORIA, KIUTAMADUNI NA

KITAIFA PAMOJA NA MICHEZO KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KIJAMII

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji 2.8.1 Maeneo ya kihistoria

na utamaduni yawe yameendelezwa na kuhifadhiwa ifikapo mwaka 2010.

2.8.2 Vipaji na vifaa vya michezo vilivyo bora viwe vimeimarishwa ifikapo mwaka 2010

���� Kuvurugika kwa mila na utamaduni wa asili

���� Utunzaji duni wa maeneo ya kihistoria na kiutamaduni.

���� Ukosefu wa mikakati ya kuendeleza utamaduni na michezo.

���� Kuza utamaduni wa asili. ���� Kuza utalii endelevu wa kimaumbile,

utamaduni na maeneo ya kihistoria. ���� Endeleza mfumo wa mafunzo kwa

wafanyakazi wa vyombo vya habari, utamaduni na michezo.

���� Kuza na linda Haki Miliki za Wasomi.

2.8.3 Lugha ya Kiswahili katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa iwe imekuzwa ifikapo mwaka 2010

���� Kasi ndogo ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya kitaifa na kimataifa.

���� Imarisha ukuzaji wa Kiswahili kama lugha ya Taifa na Kimataifa

Page 50: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

44

KLASTA 3: UTAWALA BORA NA UMOJA WA KITAIFA

LENGO LA 1 - HAKIKISHA USHIRIKISHWAJI WA UMMA KATIKA UTAWALA NA

MICHAKATO YA MAENDELEO

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji 3.1.1 Upelekaji wa

madaraka Wilayani uwe umeimarishwa.

���� Kasi ndogo ya upelekaji madaraka wilayani

���� Mgawanyo wa madaraka baina ya mamlaka mbali mbali za Serikali hauko wazi

���� Anzisha na endeleza mkakati wa kupeleka madaraka katika ngazi za Wilaya kwa Wizara zilizochaguliwa na Serikali.

���� Fanya mapitio ya mipaka ya mamlaka ya Serikali Kuu na za Mitaa kwa kutumia sheria zilizopo.

3.1.2 Mashirikiano baina ya Sekta ya Umma na Binafsi yawe yameimarishwa.

���� Ushiriki mdogo wa jamii katika masuala ya Serikali.

���� Ushirikishwaji mdogo wa makundi yaliyo katika hatari katika maamuzi.

���� Huduma duni zinazotolewa na sekta ya umma na y a binafsi.

���� Andaa sera ya maendeleo ya jamii.

���� Kamilisha na tekeleza sera ya Jumuiya zisizokuwa za Serikali.

���� Ongeza idadi ya watu kutoka makundi ya watu walio katika hatari katika vyombo vya kutoa maamuzi.

3.1.3 Sera ya hifadhi na urithi wa Taifa iwe imeanzishwa na kutekelezwa

���� Kuwepo kwa sheria na kanuni zisizokidhi mahitaji ya hifadhi na urithi wa taifa.

���� Fanya mapitio na imarisha sheria na kanuni zinazohusiana na hifadhi ya urithi wa Taifa.

���� Andaa na tekeleza sera ya hifadhi ya urithi wa taifa.

LENGO LA 2 - UTOAJI WA HUDUMA ZA JAMII UIMARISHWE NA MAREKEBISHO

YA UTUMISHI WA UMMA YAANZISHWE

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji 3.2.1 Utoaji wa huduma

katika ngazi zote uwe umeimarishwa

���� Raslimali chache zinazowekwa katika sekta ya umma kwa ajili ya utoaji wa huduma.

���� Utekelezaji usiotosheleza wa michakato ya marekebisho ya bajeti.

���� Ongeza bajeti kwa serikali kuu kwa ajili ya utoaji wa huduma. Imarisha uratibu katika uandaaji na utekelezaji wa sera

���� Anzisha na tekeleza Programu ya Maboresho ya utumishi wa Umma

Page 51: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

45

LENGO LA 3 - KUHESHIMU UTAWALA WA SHERIA NA UPATIKANAJI WA HAKI

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji 3.3.1 Mazingira ya kazi

na uwezo wa Mahakama Zanzibar uwe umeimarishwa.

���� Tume ya kurekebisha sheria haifanyi kazi kwa ufanisi.

���� Upungufu wa nakala za sheria na kumbukumbu za kesi.

���� Fursa duni za huduma ya sheria kwa makundi ya watu walio katika hatari.

���� Uendeshaji wa mahakama na huduma ni duni.

���� Imarisha utungaji na urekebishaji wa sheria.

���� Imarisha uchapishaji na ugawaji wa nakala za sheria na kanuni.

���� Endeleza mwamko wa jamii juu ya utawala wa sheria.

���� Endeleza ufanisi na huduma za mahakama

���� Imarisha Tume ya Utumishi wa Mahakama.

���� Imarisha uwezo wa maabara wa huduma za Taifa za uchunguzi

���� Rekebisha mfumo wa sheria za watoto na tenga jela za vijana.

3.3.2 Mazingira ya kazi na uwezo wa Taasisi za Utekelezaji wa sheria Zanzibar yawe yameimarika.

���� Uadilifu mdogo juu ya maadili ya kazi ya uanasheria.

���� Taasisi duni za sheria. ���� Uwezo mdogo wa

kutekeleza sheria.

���� Uwezo wa utendaji na wa upelelezi wa polisi uendeshwe kitaalamu.

���� Imarisha Afisi ya Mwanasheria Mkuu, Afisi ya Mufti na Kamisheni ya Waqf na Mali ya Amana.

���� Imarisha afisi huru ya Mkurugenzi wa Mashtaka.

LENGO LA 4 - USALAMA WA RAIA UIMARISHWE

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji 3.4.1 Amani na utulivu

Zanzibar uwe umeimarika

���� Kuongezeka magendo, madawa ya kulevya na silaha.

���� Uhamiaji haramu. ���� Ukosefu wa boti ya uokozi na

usalama bandarini. ���� Ongezeko la kiwango cha wizi

wa kutumia silaha, wizi na unyanyasaji wa kijinsia.

���� Andaa na tekeleza kampeni dhidi ya kuzuia magendo ya bidhaa.

���� Shirikiana na Tanzania bara kuimarisha utekelezaji wa taratibu za uhamiaji.

���� Ongeza doria za kawaida katika maeneo ya pwani zikiwemo doria za usiku.

���� Andaa programu ya kuzuia makosa ya jinai Zanzibar.

3.4.2 Mfumo wa Usimamizi wa maafa na tahadhari uwe umeimarishwa

���� Usimamizi duni wa majanga ���� Ujuzi mdogo na vifaa duni kwa

ajili ya kukabili na kukinga matokeo ya dharura.

���� Saidia na imarisha kitengo cha usimamizi wa Maafa na anzisha mfumo wa tahadhari.

���� Imarisha idara ya zimamoto na uokozi kwa kuipatia wataalamu na vifaa.

3.4.3 Hatua za kumlinda mlaji ziwe zimeimarishwa

���� Usimamizi duni wa kumlinda mlaji.

���� Mamlaka duni za kusimamia (utoaji leseni n.k.).

���� Imarisha uwezo wa kanuni, uchunguzi na usimamizi wa Bodi ya Kumlinda Mlaji.

Page 52: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

46

LENGO LA 5 - KUONGEZA UWEZO WA TAASISI ZA SERIKALI NA WATENDAJI

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji 3.5.1 Uwezo wa taasisi za

Serikali na watendaji uwe umeimarika.

���� Mazingira duni ya kazi. ���� Ukosefu wa programu za

maendeleo ya mafunzo kwa wafanyakazi wa maeneo muhimu.

���� Udhibiti mkubwa wa maamuzi.

���� Imarisha miundombinu na majengo yaliopo na jenga mapya pale inapohitajika.

���� Imarisha taratibu na uwekaji kumbukumbu katika taasisi za Serikali.

���� Fuata Programu ya Marekebisho ya Utumishi wa Umma.

3.5.2 Masuala ya VVU na UKIMWI katika programu na sera yawe yamejumuishwa

���� Masuala ya VVU na UKIMWI bado hayajajumuishwa kikamilifu katika sera na programu.

���� Ongeza mwamko wa Baraza la Wawakilishi juu ya hali ya VVU/UKIMWI, ikiwa pamoja na wajibu wao katika kushughulikia tatizo hili.

���� Anzisha kanuni za kusimamia shughuli za VVU/UKIMWI, unyanyapaa na ubaguzi wa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI na mayatima katika jamii na sehemu za kazi.

LENGO LA 6 - KUPAMBANA NA RUSHWA NA KUIMARISHA MAADILI YA

UONGOZI

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji 3.6.1 Usawa na haki

katika jamii uwe umeimarika.

���� Ongezeko la rushwa katika sekta ya umma na ya binafsi.

���� Usimamizi mbaya wa fedha za serikali.

���� Uchunguzi dhaifu na uwezo mdogo katika uendeshaji wa kesi za rushwa.

���� Anzisha Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Maadili ya Viongozi.

���� Harakisha upitishwaji wa muswada wa sheria ya kuzuia rushwa na maadili ya viongozi.

���� Tekeleza uingizaji wa kifungu katika sheria ya mwenendo wa jinai kinachohusika na unyanyasaji wa kijinsia.

LENGO LA 7 - KUKUZA MUUNDO WA KISHERIA ILI KUSAIDIA UKUAJI WA

UCHUMI

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji 3.7.1 Sheria za

biashara, taratibu, sera za mazingira na utungaji wa sheria ziwe zimerekebishwa.

���� Kuwepo kwa taasisi tofauti zenye dhamana ya kutoa leseni kwa wafanyabiashara wadogo wadogo.

���� Kesi za kibiashara zinachukua muda mrefu mahakamani kabla ya kukatiwa shauri.

���� Rekebisha na imarisha muundo wa udhibiti wa biashara.

���� Tekeleza na simamia sera ya mazingira na sheria.

���� Imarisha ushiriki wa sekta binafsi katika kuleta maendeleo.

Page 53: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

47

LENGO LA 8 - IMARISHA UANGALIZI NA USIMAMIZI WA TAASISI NA

UWAJIBIKAJI IKIWEMO UPATIKANAJI WA HABARI

Shabaha za utekelezaji Changamoto Mikakati ya utekelezaji 3.8.1 Uwazi na

uwajibikaji uwe umeimarishwa

���� Ukosefu wa uwazi na uwajibikaji wa kutosha kwa viongozi waliochaguliwa.

���� Kutofahamika vyema mfumo wa vyama vingi kumeleta athari mbaya kwa maendeleo.

���� Imarisha elimu ya uraia katika michakato ya kidemokrasia na taasisi; pamoja na michakato ya vyama vingi.

���� Imarisha uwezo wa asasi za kiraia na jamii ili kushiriki katika michakato ya kidemokrasia

���� Wawezeshe wajumbe wa upinzani ili waweze kufuatilia shughuli na sera za Serikali.

3.8.2 Uelewa wa umma na upashanaji habari uwe umeimarishwa.

���� Ukosefu wa vifaa na uwezo unaohitajika katika taasisi za utangazaji.

���� Fursa chache za upatikanaji wa habari juu ya shughuli za Serikali.

���� Njia duni za upashanaji habari katika jamii.

���� Saidia uanzishwaji wa taasisi imara za utangazaji zinazojitegemea na za kitaalamu.

���� Tayarisha na tekeleza sera ya taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

���� Rekebisha Sheria ya Utangazaji ya Zanzibar na mambo mengine muhimu ya kisheria

���� Tayarisha na tekeleza sheria ya uhuru wa habari.

LENGO LA 9 - KUTOA HABARI SAHIHI KWA WAKATI JUU YA UFUATILIAJI NA

TATHMINI YA SHUGHULI ZA SERIKALI NA UTAWALA

Shabaha za utekelezaji

Changamoto Mikakati ya utekelezaji

3.9.1 Ufuatiliaji na tathmini ya shughuli za Serikali uwe umeimarishwa.

���� Hakuna mfumo wa ufuatiliaji na tathmini juu ya shughuli zilizopo za utawala.

���� Taratibu mbaya za uwekaji kumbukumbu na hifadhi ya nyaraka.

���� Kukosekana kufanywa tafiti kwa kipindi maalum na zenye kutoa taarifa za kutosha na kuaminika.

���� Uwezo mdogo wa kufanikisha ukusanyaji wa taarifa na uchambuzi wake.

� Anzisha mfumo wa Ufuatilaji na Tathmini wa Utawala

� Imarisha uwezo wa kutekeleza Ufuatilaji na Tathmini ndani ya Serikali.

� Imarisha uwekaji kumbukumbu na taratibu za usimamizi wa taarifa.

� Imarisha uwezo wa uwekaji nyaraka katika Afisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali.

� Saidia na Imarisha Afisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali.

� Fanya utafiti na anzisha utaratibu unaoongoza matumizi ya matokeo ya utafiti.

Page 54: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

48

LENGO LA 10 - KUENDELEZA TARATIBU ZA UTAWALA KATIKA NGAZI ZOTE

Shabaha za utekelezaji

Changamoto Mikakati ya utekelezaji

3.10.1 Uongozi na uwajibikaji juu ya Utawala Bora kwa ngazi zote uwe umeimarishwa.

���� Kutokuwepo mjumuisho wa taratibu za Utawala Bora katika sera za maendeleo ya taifa.

���� Uratibu duni wa uwajibikaji katika Utawala Bora.

���� Fuatilia utendaji wa Serikali kwa kulinganisha na viashirio vya utawala.

���� Imarisha uwezo wa kuratibu marekebisho ya Utawala Bora na ushiriki wa Jumuiya za kiraia na sekta binafsi katika kuendeleza na kutekeleza mageuzi hayo.

���� Imarisha uwezo wa Idara ya Uratibu wa Utawala Bora.

LENGO LA 11 - KUKUZA NA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA HAKI ZA

BINADAMU

Shabaha za utekelezaji

Changamoto Mikakati ya utekelezaji

3.11.1 Mwamko wa haki za binaadamu na utekelezaji wake uwe umeimarika

���� Uvunjaji wa haki za binaadamu.

���� Uelewa mdogo wa haki za binaadamu na jinsi ya kuzilinda.

���� Hakuna utekelezaji kwa majukumu ya kimataifa yanayohusiana na uhifadhi na uendelezaji wa haki za binaadamu.

���� Kutoshirikishwa ipasavyo, wanawake na watu wenye ulemavu katika shughuli za maendeleo na vyombo vya kutoa maamuzi.

���� Hakikisha Tume ya Haki za Binaadamu inatekeleza majukumu yake Zanzibar.

���� Endesha kampeni za uwelewa wa haki za binaadamu katika sehemu zote za kijamii.

���� Tekeleza Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu.

���� Toa programu za elimu ya umma juu ya haki za binaadamu.

���� Imarisha ushiriki wa wanawake katika vyombo vya kutoa maamuzi katika ngazi na nyadhifa zote na Imarisha shughuli zao za kiuchumi.

3.11.2 Ajira zenye tija na hadhi kwa wote ziwe zimeimarishwa

���� Ubaguzi katika sehemu za kazi.

���� Udhaifu wa usimamizi wa utekelezaji sheria na taratibu zinazoongoza sera za ajira.

���� Kuwepo Unyanyapaa na ubaguzi katika jamii na sehemu za kazi kwa mayatima na watu wanaoishi na VVU/UKIMWI.

���� Tekeleza Mwongozo wa Taifa juu ya Ajira za Watoto.

���� Weka taratibu juu ya utekelezaji wa sheria za kazi.

���� Anzisha mfumo wa kisheria unaoendeleza na kulinda haki za watu wanaoishi na VVU/UKIMWI katika sehemu za kazi na jamii.

Shabaha za utekelezaji

Changamoto Mikakati ya utekelezaji

3.11.3 Utoaji haki kwa wote uwe umeimarika

���� Kuwepo kwa unyanyasaji wa kijinsia/kimapenzi kunarudisha nyuma shughuli za wanawake za kujipatia kipato.

���� Utekelezaji dhaifu wa sheria zilizopo zinazohusu udhalilishaji wa kijinsia.

���� Imarisha uwezo wa mfumo wa Sheria ili kushughulikia kesi nyeti zinazohusu unyanyasaji wa wanawake, watoto na makundi ya watu walio katika hatari.

���� Endeleza na hifadhi haki za watoto. ���� Endesha mafunzo ya uelewa na toa

maelezo ya msingi kuhusiana na kesi

Page 55: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

49

���� Kuwepo kwa ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI.

nyeti zinazohusu wanawake, watoto na makundi ya watu walio katika hatari.

Page 56: Mwongozo kwa Lugha Nyepesi Mkakati wa Kukuza Uchumi na

����

Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na:

Mratibu wa MKUZA Wizara ya Fedha na Uchumi,

S. L. P 1154/874 ZANZIBAR

Simu: (024) 223 1171 Faksi: (024) 223 0546