19
OFISI YA RAIS, IKULU MPANGO WA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN GOVERMENT PARTNERSHIP – OGP) Imewasilishwa kwenye Mkutano wa Mashauriano na Wadau 15 Novemba 2011 1

OFISI YA RAIS, IKULU · OFISI YA RAIS, IKULU MPANGO WA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN GOVERMENT PARTNERSHIP – OGP) Imewasilishwa kwenye Mkutano wa

  • Upload
    others

  • View
    26

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

OFISI YA RAIS, IKULU

MPANGO WA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN

GOVERMENT PARTNERSHIP – OGP)

Imewasilishwa kwenye Mkutano waMashauriano na Wadau

15 Novemba 2011

1

Yaliyomo

• Utangulizi

• Chimbuko la Mpango

• Maeneo yanayozingatiwa kwenye Mpango

• Maandalizi ya Mpango wa Tanzania

• Ni maeneo yapi yaingizwe kwenye Mpango waKitaifa?

• Manufaa yaliyopatika kwa Nchi zilizoanza kutekelezaOGP

• Hitimisho

2

Utangulizi

• Tangu tupate Uhuru mwaka 1961 juhudi zimekuwazikifanywa na Serikali katika Awamu zote za kuhakikishawananchi wanahusishwa na kupewa habari kuhusumustakabali wa maisha yao.

• Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara za18(d), 20(1), na 21(2) zinazungumzia ushiriki waWananchi katika kupata habari na kushiriki katikashughuli zinazohusu maendeleo yao.

• Ili kutimiza matakwa haya ya Kikatiba Serikali ilibuniMwongozo wa Utawala Bora unaozingatia misingi yademokrasia, uwazi, uwajibikaji, ushirikishwaji, usawa,utawala wa sheria, na uadilifu.

3

Utangulizi (unaendelea)

• Serikali imeandaa Sera mbalimbali ili kuhakikishamisingi ya Utawala Bora inazingatiwa. Baadhi ya Serahizo ni kama vile Sera ya Afya ya mwaka 2007, Seraya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, Sera ya Maji yamwaka 2002 zinatamka wazi kwamba ushirikishwajiwa wananchi katika upangaji na utekelezaji wa miradiya maendeleo ni muhimu.

• Utekelezaji wa Mpango huu siyo jambo geni machonimwa Watanzania. Lengo la mpango huu nikuimarisha uwazi na uwajibikaji katika utendaji washughuli za Serikali.

4

Chimbuko la Mpango

• Mpango huu wa uendeshaji Serikali kwa uwazi (OGP)ulibuniwa na wadau mbalimbali wakiwemo Serikali,Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kuzinduliwa MjiniNew York Marekani tarehe 20 Septemba 2010.

• Serikali ya Tanzania imeridhia kujiunga katikaMpango huu unaojumuisha Nchi nyingine 45 dunianiambapo Nchi kutoka Afrika ni Kenya, Ghana, Liberiana Afrika ya Kusini.

5

Chimbuko la Mpango - unaendelea

Chimbuko la mpango huu linatokana na changamoto

nyingi kuendelea kujitokeza katika uendeshaji washughuli za Serikali zetu kama vile

• Kuimarisha uadilifu miongoni mwa Watumishi waUmma,

• Matumizi mazuri ya rasilimali za Nchi,

• Kuimarisha usalama wa wananchi

• Uwajibikaji wa kitaasisi

6

Chimbuko (linaendelea)

Mpango unajikita katika maeneo makuumanne:-

– Uwazi

– Ushirikishwaji wa wananchi

– Uwajibikaji

– Teknolojia na Uvumbuzi

Equity Monitoring Report, 2011 7

Chimbuko la Mpango - inaendelea

• Matokeo yanayotarajiwa yako katika maeneomakuu matano:– Kuboreka kwa utoaji wa huduma

– Kuongezeka kwa uadilifu

– Kusimamia ipasavyo matumizi ya mali za umma

– Kuongeza usalama wa wananchi

– Kuongezeka kwa uwajibikaji wa Kitaasisi.

8

Taratibu za Nchi Kujiunga na OGP

• Nchi zilizojiunga zinasaini makubaliano ya kujiunga

• Baada ya kusaini zinaainisha maeneo kwa kushirikianana wadau ambayo zinadhani yataimarisha uwajibikaji nakutayarisha mpango Kazi

• Mpango utakaotayarishwa unawasilishwa kwenyeSekretarieti ya Kimataifa kwa ajili ya kupata uzoefu waNchi zingine shiriki kwenye Mpango

• Utekelezaji pamoja na tathmini unafanyika

9

Hatua zilizofikiwa kwa Tanzania• Kikundi Kazi kimeundwa na Serikali kusimamia

uandaaji wa Mpango wa Kitaifa wa OGP

• Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora,tayariametoa taarifa kwenye Vyombo vya Habari kuhusumkakati wa kutayarisha Mpango huu

• Maelekezo yametolewa kwa kila Wizara kuhakikishainashiriki kikamilifu katika Mpango huu wa ‘OGP’

• TWAWEZA ni mdau muhimu katika maandalizi yaMpango huu.

10

Hatua zilizofikiwa kwa Tanzania• Ili kuweza kujipima kikamilifu, Tanzania imeamua

kuanza kutekeleza mpango huu katika Sekta tatu zahuduma za jamii ambazo ni Afya, Elimu, na Maji

• Ili kushirikisha wananchi wengi zaidi katika kutoamaoni namba ya Wazi na bure ya simu imetolewakwa wananchi kupiga simu au kutuma ujumbe (sms) bila malipo. Namba hiyo ni 0658 - 999222

• Kutoa anwani kwa wananchi wanaotaka kutumia njiaya barua: IKULU, SL.P. 9120 DAR ES SALAAM.

• Kutoa anwani za tovuti: www.mwananchi.go.tz

11

Ni maeneo yapi yaingizwe kwenye Mpangowa Kitaifa?

• Uwazi:– Kuweka utaratibu wa kuyafanya madawati ya

malalamiko yaliyoanzishwa katika Wizara naMamlaka za Serikali za Mitaa yafanye kazi. Hiiitaongeza uwazi katika utendaji wa shughuli zaSerikali

– Kubaini na kuimarisha matumizi ya masanduku yamaoni yaliyopo katika vituo vya kutolea hudumana kuweka utaratibu madhubuti wa kutambuayanavyofanya kazi

12

• Uwazi (inaendelea):– Kupitia upya majukumu ya Bodi na Kamati za

Vituo vya utoaji wa huduma katika Sekta za Afya, Elimu na Maji ili kuzifanya zitekeleze majukumuyake ipasavyo

– Kuweka utaratibu ili kuhakikisha kuwa taarifa zamapato na matumizi zinabandikwa katika Mbao zaMatangazo kwenye ngazi za Halmashauri, Kata, Vijiji, Mitaa na Vituo vya kutolea huduma katikaSekta za Afya, Elimu na Maji

13

• Ushirikishwaji:– Kuweka taratibu madhubuti na rahisi za kufanya

tovuti ya Wananchi iweze kutumika kikamilifu.

– Kupitia upya mfumo wa Upangaji wa Mipangongazi za Msingi kwa kutumia utaratibu wa fursa navikwazo (O&OD) ili uwe rahisi kutumika nawananchi na kuleta matokeo tarajiwa.

– Kupitia upya miongozo na taratibu za uendeshajimikutano ya Mashauriano na Wadau juu yaUpangaji Mipango na Bajeti katika Sekta za Afya, Elimu na Maji kwa lengo la kupata ushiriki mpanazaidi na hivyo kuongeza ushirikishwaji.

14

• Uwajibikaji na Uadilifu:– Kuhuisha Mikataba ya huduma kwa Mteja katika Wizara na

Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuhakikisha yaliyomoyanatekelezwa

– Kuimarisha taratibu zilizopo za ufuatiliaji wa Mapato naMatumizi ya fedha za Umma (Public Exependiture Tracking Survey – PETS) kwa lengo la kubaini thamani ya fedha.

– Kuhuisha vigezo vya utoaji wa ruzuku ya matumizi yaKawaida na Maendeleo katika Halmashauri.

– Kuweka taratibu madhubuti za kusimamia mapato namatumizi ya fedha kwa kutumia ‘Integrated FinancialManagement System’ (IFMS), ambayo imewekwa katikaMikoa, Wizara na Halmashauri zote

15

• Teknolojia na Uvumbuzi:• Kuandaa ramani zinazoainisha vituo/maeneo ya utoaji

wa huduma za maji Nchini ili taarifa hizo zitumikekupanga mipango endelevu ya maji. Utaratibu huuutasaidia wananchi kutoa taarifa kwa viongozi waokuhusu ufanyaji kazi wa vituo vya maji vilivyopo.

• Kuongeza kasi ya matumizi ya TEHAMA katika kuongezaufanisi wa kufundishia na kujifunzia.

• Kuhakikisha teknolojia ya matibabu kwa njia ya masafa(telemedicine) inatekelezwa kama ilivyotarajiwa. Mpangohuu ambao umeanzia ‘Ocean Road Hospital’ utaenezwakatika Hospitali nyingine nchini.

• Kutoa taarifa mbalimbali za utoaji wa huduma (Elimu,Afya, Maji) kwa wananchi kwa kutumia njia ya teknolojiaya habari na mawasiliano kama vile tovuti, simu zamkononi, televisheni, kompyuta, radio na sms.

16OGP Taskforce, Tanzania

Manufaa yaliyopatika kwa Nchi zilizoanza kutekelezaOGP

Uzoefu unaonyesha kwamba Nchi ambazo zimeanza

kutekeleza Mpango wa OGP zimepata mafanikio

makubwa katika kuboresha utoaji huduma na kupiga

hatua kubwa za kimaendeleo. Baadhi ya Nchi zilizopiga

hatua kubwa kimaendeleo kupitia Mpango huu ni:• Mexico – Kupitia CSO ijulikanayo kama FUNDAR ilionyesha

upungufu wa utoaji huduma kwa akina mama ambapoZahanaji zilikuwa hazifunguliwi na haduma za dawahazipatikani. Kwa kutumia matangazo ya CSO hii Wizara yaAfya ilishughulikia tatizo hili na kuokoa maisha ya watu.

Equity Monitoring Report, 2011 17

Manufaa yaliyopatika kwa Nchi zilizoanza kutekelezaOGP (Yanaendelea)

• India – MKSS walihamasisha ubandikaji wataarifa mbalimbali zipatazo laki moja kwenyembao za matangazo zilizosaidia wananchikufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbalikatika Jimbo la Rajasthan

Equity Monitoring Report, 2011 18

HITIMISHO• Mpango huu wa uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa uwazi

utasaidia Taifa letu kuongeza ushirikishwaji wa wananchikatika kuchangia mawazo, maoni, na mapendekezo juu yauendeshaji wa shughuli za kila siku za Serikali. Hatua hiiitasaidia kuongeza uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali zaumma kulingana na vipaumbele vilivyowekwa na hivyokuharakisha maendeleo. Ni vema nafasi hii ikachukuliwa kwauzito wake na wadau wote.

• Asasi za Kiraia (CSOs) zina jukumu la msingi na la kipekeekatika kufanikisha hili. Tushirikiane wote kuendeleza kasi yamaendeleo ya Taifa letu.

• Kwa taarifa zaidi kuhusiana na OGP tafadhali tembelea:www.opengovpartnership.org

OGP Tanzania 19