Upload
others
View
59
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
1
ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI
ZANZIBAR
MHE. PANDU AMEIR KIFICHO - SPIKA
1.Mhe. Balozi Seif Ali Iddi MBM/Makamo wa Pili wa
Rais/Kuteuliwa na Rais
2.Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini MBM/Waziri wa Nchi, Afisi
ya Rais na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi/Jimbo la
Dimani.
3.Mhe. Omar Yussuf Mzee MBM/Waziri wa Nchi, Afisi
ya Rais, Fedha, Uchumi na
Mipango ya Maendeleo/
Kuteuliwa na Rais
4.Mhe. Haji Omar Kheri MBM/Waziri wa Nchi, Afisi
ya Rais, Utumishi wa Umma
na Utawala Bora/Jimbo la
Tumbatu
5.Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji MBM/Waziri wa Nchi, Afisi
ya Makamo wa Kwanza wa
Rais/Kuteuliwa
6.Mhe. Mohammed Aboud Mohammed MBM/Waziri wa Nchi, Afisi
ya Makamo wa Pili wa
Rais/Kuteuliwa
7.Mhe. Abubakar Khamis Bakary MBM/Waziri wa Katiba na
Sheria/Jimbo la Mgogoni.
8.Mhe. Rashid Seif Suleiman MBM/Waziri wa
Miundombinu na
Mawasiliano/Jimbo la Ziwani.
9.Mhe. Ali Juma Shamuhuna MBM/Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali/Jimbo la
Donge
10.Mhe. Juma Duni Haji MBM/Waziri wa
Afya/Kuteuliwa
2
11.Mhe. Zainab Omar Mohammed MBM/Waziri wa Ustawi wa
Jamii na Maendeleo ya Vijana,
Wanawake na
Watoto/Kuteuliwa
12.Mhe. Said Ali Mbarouk MBM/Waziri wa Habari,
Utamaduni, Utalii na
Michezo/Jimbo la Gando
13.Mhe. Ramadhan Abdalla Shaaban MBM/Waziri wa Ardhi,
Makaazi, Maji na
Nishati/Kuteuliwa.
14.Mhe. Suleiman Othman Nyanga MBM/Waziri wa Kilimo na
Maliasili/Jimbo la Jang‟ombe
15.Mhe. Nassor Ahmed Mazrui MBM/Waziri wa Biashara,
Viwanda na Masoko/Jimbo la
Mtoni
16.Mhe. Abdillah Jihad Hassan MBM/Waziri wa Mifugo na
Uvuvi/Jimbo la Magogoni
17.Mhe. Haroun Ali Suleiman MBM/Waziri wa Kazi,
Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi na Ushirika/Jimbo la
Makunduchi
18. Mhe. Shawana Bukheti Hassan MBM/Waziri Asiyekuwa na
Wizara Maalum/ Jimbo la Dole
19. Mhe. Haji Faki Shaali MBM/ Waziri Asiyekuwa na
Wizara Maalum/Jimbo la
Mkanyageni
20.Mhe. Machano Othman Said MBM/Waziri Asiyekuwa na
Wizara Maalum/Jimbo la
Chumbuni.
21.Mhe. Othman Masoud Othman Mwanasheria Mkuu
3
22.Mhe. Issa Haji Ussi Naibu Waziri wa
Miundombinu na
Mawasiliano/Jimbo la Chwaka
23.Mhe. Zahra Ali Hamad Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali/Nafasi za
Wanawake
24.Mhe. Dr. Sira Ubwa Mamboya Naibu Waziri wa
Afya/Kuteuliwa na Rais
25.Mhe. Bihindi Hamad Khamis Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Utalii na
Michezo/ Nafasi za Wanawake
26.Mhe. Haji Mwadini Makame Naibu Waziri wa Ardhi,
Makaazi, Maji na
Nishati/Jimbo la Nungwi
27.Mhe. Thuwaybah Edington Kissasi Naibu Waziri wa Biashara,
Viwanda na Masoko/Jimbo la
Fuoni
28.Mhe. Mtumwa Kheir Mbarak Naibu Waziri wa Kilimo na
Maliasili/Nafasi za Wanawake
29. Mhe. Mohammed Said Mohammed Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi/ Jimbo la Mpendae
30.Mhe. Abdalla Juma Abdalla Jimbo la Chonga
31.Mhe. Abdalla Moh‟d Ali Jimbo la Mkoani
32. Mhe. Ali Mzee Ali Kuteuliwa
33.Mhe. Abdi Mosi Kombo Jimbo la Matemwe
34.Mhe. Ali Abdalla Ali Jimbo la Mfenesini
35. Mhe. Ali Salum Haji Jimbo la Kwahani
36.Mhe. Amina Iddi Mabrouk Nafasi za Wanawake
4
37. Mhe. Asaa Othman Hamad Jimbo la Wete
38.Mhe. Asha Abdu Haji Nafasi za Wanawake
39.Mhe. Asha Bakari Makame Nafasi za Wanawake
40.Mhe. Ashura Sharif Ali Nafasi za Wanawake
41.Mhe. Bikame Yussuf Hamad Nafasi za Wanawake
42.Mhe. Farida Amour Mohammed Nafasi za Wanawake
43.Mhe. Fatma Mbarouk Said Jimbo la Amani
44.Mhe. Hamad Masoud Hamad Jimbo la Ole
45.Mhe. Hamza Hassan Juma Jimbo la Kwamtipura
46.Mhe. Hassan Hamad Omar Jimbo la Kojani
47.Mhe. Hija Hassan Hija Jimbo la Kiwani
48.Mhe. Hussein Ibrahim Makungu Jimbo la Bububu
49.Mhe. Ismail Jussa Ladhu Jimbo la Mji Mkongwe
50.Mhe. Jaku Hashim Ayoub Jimbo la Muyuni
51.Mhe. Kazija Khamis Kona Nafasi za Wanawake
52.Mhe. Mahmoud Muhammed Mussa Jimbo la Kikwajuni
53.Mhe. Makame Mshimba Mbarouk Jimbo la Kitope
54.Mhe. Mansoor Yussuf Himid Jimbo la Kiembesamaki
55.Mhe. Marina Joel Thomas Kateuliwa na Rais
56.Mhe. Mbarouk Wadi Mussa Jimbo la Mkwajuni
57.Mhe. Mgeni Hassan Juma Nafasi za Wanawake
58.Mhe. Mlinde Mbarouk Juma Jimbo la Bumbwini
5
59.Mhe. Mohammed Haji Khalid Jimbo la Mtambile
60.Mhe. Mohammed Mbwana Hamad Jimbo la Chambani
61.Mhe. Mussa Ali Hassan Jimbo la Koani
62.Mhe. Mohamedraza Hassanali Mohamedali Jimbo la Uzini
63.Mhe. Mwanaidi Kassim Mussa Nafasi za Wanawake
64.Mhe. Mwanajuma Faki Mdachi Nafasi za Wanawake
65.Mhe. Nassor Salim Ali Jimbo la Rahaleo
66.Mhe. Omar Ali Shehe Jimbo la Chake-Chake
67.Mhe. Panya Ali Abdalla Nafasi za Wanawake
68.Mhe. Raya Suleiman Hamad Nafasi za Wanawake
69.Mhe. Rufai Said Rufai Jimbo la Tumbe
70.Mhe. Saleh Nassor Juma Jimbo la Wawi
71.Mhe. Salim Abdalla Hamad Jimbo la Mtambwe
72.Mhe. Salma Mohammed Ali Nafasi za Wanawake
73.Mhe. Salma Mussa Bilali Nafasi za Wanawake
74.Mhe. Salmin Awadh Salmin Jimbo la Magomeni
75.Mhe. Shadya Mohamed Suleiman Nafasi za Wanawake
76.Mhe. Shamsi Vuai Nahodha Jimbo la Mwanakwerekwe
77.Mhe. Subeit Khamis Faki Jimbo la Micheweni
78.Mhe. Suleiman Hemed Khamis Jimbo la Konde
79.Mhe. Ussi Jecha Simai Jimbo la Chaani
80.Mhe. Viwe Khamis Abdalla Nafasi za Wanawake
81.Mhe. Wanu Hafidh Ameir Nafasi za Wanawake
Ndugu Yahya Khamis Hamad Katibu wa Baraza la Wawakilishi
6
Kikao cha Kumi na Saba – Tarehe 8 Julai, 2013
(Kikao kilianza saa 3:00 asubuhi)
DUA
Mhe. Naibu Spika, (Ali Abdalla Ali) alisoma Dua
TAARIFA
Mhe. Naibu Spika: Waheshimiwa Wajumbe, kabla ya kuanza shughuli zetu
asubuhi kuna taarifa ya mechi iliyochezwa jana baina ya Timu ya Baraza la
Wawakilishi Sport Club na wenzetu wa Uhamiaji. Matokeo ni kwamba Timu
ya Baraza Sport Club imeshinda mabao mawili na Uhamiaji hawakupata kitu.
Wafungaji wetu wa mabao hayo ni moja amefunga Mhe. Ussi Jecha Simai na
goli la pili amefunga mtendaji wetu Fuad Rashid Omar. (Makofi)
Kwa matokeo hayo, sasa tumeingia nusu final na tunampongeza kocha wetu
Sumbu na anasema yako matumaini ya kuchukua kombe timu yetu. (Makofi)
MASWALI NA MAJIBU
Nam. 131
Wafungwa na Mahabusu Kunyimwa Haki ya Kutoa Maoni na Habari
Mhe. Jaku Hashim Ayoub – Aliuliza:-
Mhe. Naibu Spika, kabla kujibiwa swali langu Nam. 131 naomba kwa
heshima na taadhima nitoe utangulizi kwa ruhusu yako Mhe. Naibu Spika.
Kesho au kesho kutwa tunategemea kuwa na mwezi mtukufu wa Ramadhani
na serikali kwa kuwathamini wananchi wake katika mwezi huo Mtukufu wa
Ramadhani imeondoa msamaha wa kodi zote ikiwemo mchele, sukari na unga
wa ngano. Kwa hivyo, ombi langu kwa serikali kwamba isimamie vizuri zoezi
hili ili wananchi waweze kufaidika.
Vile vile katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani tumeshuhudia mavazi ya
rusha roho katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani. Kutokana na hali hiyo,
naiomba serikali kupitia kwako Mhe. Naibu Spika, kwamba itoe tamko rasmi
kabisa kwa mavazi hayo kwa muda huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani
yawe basi.
7
Kifungu cha 18(1) cha Katiba za Zanzibar ya mwaka 1984 kinatoa haki kwa
kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na
kutafuta kupokea na kutoa habari kupitia chombo chochote, bila ya kujali
mipaka ya nchi na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(a) Je, kwa nini wafungwa na mahabusu wananyimwa haki ya
kuzungumza na vyombo vya habari visiwani Zanzibar.
(b) Wizara ina mpango gani wa kuhakikisha haki za wafungwa na
mahabusu za kutoa maoni inazingatiwa kwa mujibu wa Katiba ya
nchi.
(c) Wafungwa wangapi na mahabusu Zanzibar ambao walipata haki ya
kutoa maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba mpya ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Mhe. Waziri wa Nchi, (OR) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi –
Alijibu:-
Mhe. Naibu Spika, kabla sijajibu swali la Mhe. Mwakilishi naomba ku-
respond au kuzungumza kidogo kuhusu mambo aliyoyazungumza. Mhe.
Naibu Spika, ni kawaida kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inapokaribia
mwezi Mtukufu wa Ramadhani huwa inatoa msamaha wa vyakula muhimu
kama vile unga wa ngano, mchele na sukari kila mwaka tunasamehe kodi.
(Makofi)
Sasa namuomba sana Mhe. Mjumbe kupitia kwako Mhe. Naibu Spika, akiwa
mfanyabiashara, basi tuitumie vizuri fursa hiyo ili wananchi wetu waweze
kuona unafuu wa punguzo hilo linalotolewa na serikali kwa makusudi.
Kuhusu ombi lake la pili sote tunafahamu kwamba nchi yetu ni ya Kiislamu
kwa taratibu zetu pamoja na mila zetu. Vile vile huwa tunakumbushana tu kila
mwaka inapokaribia mwezi Mtukufu wa Ramadhani huwa tunarekebisha
mpaka wakati ule wa kuondoka kazini.
Pia nyumba zote za starehe, mikahawa pamoja na restaurants zinafungwa na
hali hiyo ni kawaida, isipokuwa nazidi kuwakumbusha tu wananchi wenzangu
na hayo ni ya kawaida na tunazidi kukumbusha na sote tutekeleze wajibu
wetu kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mhe. Naibu Spika, baada ya utangulizi huo kwa niaba ya serikali. Sasa
naomba kumjibu swali lake Nam. 131 lenye vifungu (a), (b) na (c) kama
ifuatavyo:-
8
(a) Mhe. Naibu Spika, fursa ya kuwasiliana baina ya wanafunzi ama
mahabusu na jamaa zao na watu wengine wowote ikiwamo hawa
aliowataja waandishi wa habari, zilizokuwepo kwa mujibu wa sheria
Chuo cha Mafunzo ni ya kuandika barua, ambazo hutuma kwa ndugu
na jamaa na ile ya kuonana uso kwa uso na watu ambao yeye
mwenyewe ameomba kuwaona au jamaa na ndugu watakaofika
kumuona.
(b) Serikali huwa inatoa ruhusa maalum pale inapotokea haja ya
wanafunzi wa mahasubu kutoa maoni kwa mujibu wa Katiba. Kwa
mfano, serikali ilipokea maombi kutoka Tume ya Mabadiliko ya
Katiba ya kutaka kupokea maoni kutoka kwa wanafunzi na
mahabusu ambao wamo katika Vyuo vya Mafunzo vilioko Kisiwani
Pemba. Kwa hivyo, maombi hayo yalikubaliwa na wanafunzi na
mahabusu walipata fursa ya kutoa maoni yao.
(c) Jumla ya wanafunzi watano na mahabusu saba wa Chuo cha
Mafunzo Zanzibar walipata haki ya kutoa maoni yao katika
mchakato wa kuandaa Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba mpya ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Jaku Hashim Ayoub:Mhe. Naibu Spika, ahsante pamoja na majibu
ambayo ametoa Mhe. Waziri kutokidhi swali la msingi.
(a) Je, gereza la Kiinua Miguu lina wanafunzi ama mahabusu wangapi,
mpaka wakapewa nafasi watu wawili kutoa maoni.
(b) Katika swali langu la msingi nimeuliza kwa nini wafungwa na
mahabusu wananyimwa haki ya kuzungumza na vyombo vya habari
wakati haki yao kwa mujibu wa kifungu cha 18(1) cha Katiba ya
Zanzibar.
Mhe. Waziri wa Nchi, (OR) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi:
Mhe. Naibu Spika, nafikiri nilisema kwenye majibu ya swali mama (a),
kwamba fursa ya kuwasiliana baina ya wanafunzi ama mahabusu na jamaa
zao na watu wengine pamoja na waandishi wa habari ni kwamba wao
wenyewe kwa mujibu wa Sheria ya Chuo cha Mafunzo wao waandike barua
ambazo huduma kwa ndugu na jamaa zao kuonana uso kwa uso na watu
ambao yeye mwenyewe ameomba.
Sasa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo (Kiinua Miguu) hawakuitumia fursa
hiyo, yaani hawajawahi kwa taarifa nilizonazo, isipokuwa walioomba ni
wanafunzi watano na mahabusu saba wa Chuo cha Mafunzo cha Wete Pemba,
9
ambao hao ndio waliomba na fursa hiyo wakapatiwa. Kwa hiyo, hakuna tatizo
isipokuwa wafuate zile taratibu za kuomba tu.
Mhe. Makame Mshimba Mbarouk: Mhe. Naibu Spika, ahsante kwa kunipa
fursa hii ya kuuliza swali la nyongeza pamoja na majibu mazuri ya Mhe.
Waziri. Kwa hivyo, nadhani huko nyuma kulikuwa na serikali inawapelekea
mahabusu magazeti pamoja na redio kwa ajili ya kusikiliza mambo ya
ulimwengu yanavyokwenda.
Je, utaratibu huu upo unaendelea na kama hauendelei, basi kwa nini
tusiendeleze kuwapatia vitu kama hivyo ili kuweza kujua ulimwenguni kuna
nini.
Mhe. Waziri wa Nchi, (OR) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi:
Mhe. Naibu Spika, ni kweli na hasa kutokana na haki za binadamu
zilivyoashiria siku hizi ulimwenguni watu kama hawa mahabusu
aliozungumza wanapaswa wapewe fursa za magazeti. Kwa kweli nina hakika
fursa ya redio na televisheni wanayo na sina hakina na magazeti, basi
nitafuatilia na nione kama hawapewi basi na hiyo tunaiingiza.
Mhe. Shadya Mohammed Suleiman:Mhe. Naibu Spika, ahsante sana kwa
kunipatia nafasi ya kuweza kumuuliza Mhe. Waziri swali moja la nyongeza.
Mhe. Waziri nataka kufahamu wastani wa wanafunzi na mahabusu.
Mhe. Waziri wa Nchi, (OR) na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi:Mhe. Naibu Spika, ni kawaida kwenye Vyuo vyetu vyote vya
Mafunzo huwa tunao mahabusu wengi zaidi ya wanafunzi na hiyo ndio trend
ya wastani kwa jumla tuliyonayo siku zote. Kwa kweli haijawahi kutokea
tukawa na wanafunzi na mahabusu idadi sawa.
Hali hii zaidi inatokana na kwamba kesi zile huwa zinachelewa kukamilika,
kwa hiyo mahabusu wale wanakwenda na kurudi na uchungu bado
haujakamilika. Sasa mpaka tarehe ya leo 08 Julai, 2013 kuna mahabusu
wapatao 223 na wanafunzi 98 na utaona uwiano na mara nyingi trend
inakwenda hivyo.
10
Nam. 36
Upatikanaji wa Ving’amuzi
Mhe. Hassan Hamad Omar – Aliuliza:-
Tulipata kusikia ndani ya vyombo vya habari kwamba Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar itapata msaada wa ving‟amuzi laki mbili na kuvigawa kwa
wananchi kwa thamani ndogo sana, kisha tukasikia vitauzwa kwa thamani ya
shilingi 50,000/= sasa shilingi 75,000/= na malipo yaende katika taasisi za
AGAPE badala ya wizarani.
(a) Je, hali hii ya kutatanisha imesababishwa na nini na ukweli ni upi.
(b) Je, huoni kuweka thamani kubwa ya bei ya king‟amuzi kutapelekea
wananchi wengi ambao idadi kubwa ni wanyonge washindwe
kufaidi haki ya kupata habari kupitia televisheni.
(c) Je, kuna ubaya gani kuendelea kubakia na analogue na king‟amuzi
ikabaki kuwa ni hiari.
Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo – Alijibu:-
Mhe. Naibu Spika, nakushukuru na naomba nimjibu Mhe. Mwakilishi swali
lake Nam. 36 kama ifuatavyo:-
(a) Mhe. Naibu Spika, serikali kupitia Wizara ya habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo haijawahi kutangaza kwamba itapata msaada wa
wa ving‟amuzi laki mbili na kuvigawa kwa wananchi kwa thamani
ndogo sana au bure.
Kwa kweli tulichokitangaza ni kwamba ving‟amuzi vitakavyoletwa
vitaanza kuuzwa kwa bei ya shilingi 50,000/= kwa king‟amuzi
kimoja, na kwamba hadi leo king‟amuzi kinachorushwa matangazo
ya digital Zanzibar kinauzwa kwa shilingi 50,000/= kila kimoja,
labda hapo baadaye kitakapopanda kwenye kiwanda basi na sisi
tutalazimika kupandisha na kuwaarifu wananchi.
Mhe. Naibu Spika, isipokuwa gharama za ziada za matumizi ya
king‟amuzi chenyewe baada ya kukinunua ndio kimefanya jumla
yake gharama hizo zifikie shingi 73,000/= kama ifuatavyo:-
(i) Bei ya ununuzi wa king‟amuzi ni shilingi 50,000/=
11
(ii) Gharama ya kutanguliza malipo ya muda wa
mwezi mmoja ni shilingi 8,000/=
(iii) Gharama ya usajili na uunganishaji kwenye
mtambo mkuu head hand ni shilingi 15,000/=.
Kwa hivyo, hiyo ndio inayofanya jumla iwe
shilingi 73,000/=
Mhe. Naibu Spika, baada ya ujenzi wa miundombinu ya digital ya
Serikali kukamilika pamoja na kupata maarifa ya uendeshaji wa
miundombinu hiyo. Kwa kweli wizara yangu imetiliana mkataba wa
uendeshaji wa miundombinu hiyo ya digital ya Serikali na mjenzi wa
miundombinu hiyo Kampuni ya AGAPE kwa muda wa miaka
miwili.
Moja ya masharti ya mkataba huo ni kuwa Kampuni ya AGAPE
itafute yenyewe mkopo wa ununuzi na uuzaji wa ving‟amuzi hivyo
na ndio maana malipo ya ununuzi wa king‟amuzi yanakwenda kwa
taasisi ya AGAPE badala ya wizara.
(b) Mhe. Naibu Spika, si kweli kwamba bei ya king‟amuzi hicho ni
kubwa kuliko ving‟amuzi nyengine na zaidi ukitilia maanani
kwamba kiwango cha king‟amuzi chetu kina fursa za matumizi ya
internet kuweza kurikodi vipindi na kutumika katika matangazo ya
High Definition Digital hapo baadae kutoka Standard Digital kwa
hivi sasa.
Mhe. Naibu Spika, naomba niwaambie Waheshimiwa Wajumbe wa
Baraza lako hili tukufu, kwamba king‟amuzi hichi kwa hapa nchini
hivi sasa basi ndio pekee chenye hadhi ya kurusha matandao wa
Standard Digital na pia High Definition Digital. Vile vile kwa hali
ya king‟amuzi hicho popote Tanzania king‟amuzi hicho basi
hakiuzwi chini ya shilingi 110.
(c) Ubaya wa kubakia katika mfumo wa matangazo ya Analogue ni
kwamba,
(i) Moja tutakuwa tunavunja makubaliano ya nchi hizi
za Afrika ya Mashariki kwamba ikifika mwezi wa
Januari 2013 zianze kurusha matangazo ya digital
katika nchi zetu.
(ii) Ikiwa sisi Zanzibar tutabakia katika mfumo wa
matangazo ya Analoue na nchi za jirani ziingie
12
katika mfumo wa matangazo ya digital, kuna
uwezekano wa mawingi yetu ya matangazo ya
analogue yakaingiliwa na kuchafuliwa na
matangazo ya digital ya nchi jirani na hivyo
kukosa kabisa matangazo ya televisheni katika
nchi yetu.
Mhe. Hassan Hamad Omar: Ahsante sana Mhe. Naibu Spika, kwa kunipa
fursa ya kumuuliza waziri swali la nyongeza. Mhe. Naibu Spika, pamoja na
majibu mazuri ya Mhe. Waziri naomba nimuulize swali lenye (a) na (b).
Mhe. Naibu Spika, ni kweli kwamba siku hizi hali ya upatikanaji wa
matangazo katika king‟amuzi cha ZBC umeimarika.
(a) Mhe. Waziri alisema kutakuwa na channel 36, mbona kuna channel
20 tu.
(b) Nasikia kuna utaratibu wa kutumia satellite, kwani kuna njia ngapi
za digital na kwa nini sisi tukatumia hii ya ving‟amuzi.
Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo: Mhe. Naibu
Spika, swali lake la (b) ni la kiufundi sana, lakini nitajaribu kulifafanua.
Kwanza ni kweli kwamba tulitangaza tutatoa channel 36 na hivi sasa tunatoa
channel 20.
Sababu yake ni kwamba tumeweka transmitter mbili kwa kila kituo katika
vituo vyetu sita, lakini kwa sababu ya uzoefu wa nchi jirani, Kenya na
Tanzania walipoingia digital moja kwa moja mwezi wa Januari mwaka huu
wananchi wa nchi hizo walizua vurugu kubwa Kenya walienda Mahkamani
wakazuwia utaratibu huo, kwa sababu nchi ya Kenya ilifunga matangazo ya
analogue moja kwa moja wakarusha matangazo ya digital. Kwa hivyo,
wananchi kwa kweli walipata usumbufu mkubwa na Mahkama ikaingilia kati.
Kwa upande wa Bara mpaka leo kuna tatizo kubwa. Sasa sisi kuzuia hilo
tukaamua twende kwa pamoja digital na analogue kwa mpigo. Katika hili
channel moja ya digital inaweza kurusha matangazo mpaka channel 20,
frequency moja mpaka 20, transmitter moja ya digital inarusha mpaka
channel 20. Kwa hivyo, transmitter moja tumeiweka kwa ajili ya digital na
moja tumeiweka kwa ajili ya analogue. Sasa tunatumia transmitter moja
tunarusha channel 20.
Hii transmitter nyengine tumeiacha kwa ajili ya wananchi ambao hawajapata
ving‟amuzi ili waweze kufaidi Mhe. Naibu Spika, fursa za matangazo, ndio
maana yake hatujazima ile ya analogue tukizima tutafika channel zile zile 36-
13
40. Kwa hivyo, tumefanya hivyo makusudi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba
wananchi wetu ambao hawajapata ving‟amuzi bado wanaendelea kufaidi
matunda ya kupata matangazo kwa sababu ni haki ya Kikatiba.
Suala la pili Mhe. Naibu Spika, kama nilivyosema ni suala la kiufundi kidogo
lakini ni kwamba kuna njia tatu za kurusha matangazo ya digital. Njia ya
kwanza ni ya kutumia satellite, tatizo lake hii capital cost yake ni kubwa sana,
kwa hiyo kwa hali yetu tukaona tusianze huko. Gharama yake ni kubwa lakini
pia matangazo yake yana tendency ya kuingiliwa na hali ya hewa, wale watu
wenye madishi kama Arabic Set na watu wengine wanaona wakati mwengine
hali ya hewa. Kwa hivyo, gharama yake ni kubwa kidogo hii ya pili.
Aina ya pili ni ya kutumia cable kama Zanzibar Cable lakini tatizo lake ni
kwamba itumike kwa eneo dogo. Sasa tabu sana kwa Zanzibar Cable kutoa
cable hapa mpaka Makunduchi, kwa hivyo inatumika kwa njia ndogo. Mhe.
Naibu Spika, sisi tumekusudia kwamba digital yetu itumike nchi nzima
ikiwemo Micheweni na Makunduchi. Kwa hivyo, hii isingetufaa.
Aina ya tatu ni hii terrestrial ambayo inatumia kwa minara tofauti, ndiyo
ambayo sisi tumeamua kutumia hiyo lakini zote zinatumia ving‟amuzi Mhe.
Naibu Spika.
Mhe. Mbarouk Wadi Mussa: Mhe. Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa
nafasi na mimi nimuulize Mhe. Waziri swali la nyongeza. Mhe. Waziri, azma
ya mapinduzi ya Zanzibar ilikuwa ni moja kuwaletea wananchi wake
maendeleo na moja kati ya maendeleo ni kuanzisha ile television ya rangi
kuweza kupata habari nchi mbali mbali na kuona badala ya ile redio kwa
kusikia. (Makofi)
Sasa wananchi wetu wa Zanzibar wengi wao ni maskini na hili linajulikana
kabisa. Mhe. Naibu Spika, unapoanzisha kitu kama hichi inabidi wanunue,
haoni kwamba atakuwa anakwenda kinyume na ile azma ya mapinduzi ya
kuwapatia habari wale wananchi ya television kwa sababu watakuwa hawana
uwezo kwa kununua kile king‟amuzi.
Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo: Mhe. Naibu
Spika, kwamba ni kweli azma ya serikali ni kuwapatia wananchi matunda ya
mapinduzi na shughuli ya television, yaani mtandao ni moja katika shahaba
hiyo.
Lakini sio kweli kwamba wananchi wa Zanzibar hawawezi kumiliki
king‟amuzi. Mhe. Naibu Spika, wananchi wa Zanzibar wanaweza kumiliki
14
television shilingi 200,000/= sasa king‟amuzi cha shilingi 50,000/= kwa nini
wasiweze, kwa kweli itakuwa haiwezekani.
Vile vile ni mfumo kwamba haiwezekani tuendelee kubakia analogue ni
lazima twende katika digital, kwa sababu dunia nzima inaelekea huko, kwa
hivyo hatuwezi kuwaambia Wazanzibari bakieni analogue, tutapitwa na
itakuwa hata hayo matangazo hatuyaoni, yaani technology imetulazimisha
kwenda huko Mhe. Naibu Spika, na wala hakuna njia nyengine.
Kwa hivyo, hatuwezi vyenginevyo na sisi hizo serikali kwa uwezo wake wa
kibajeti hatuwezi kugawa ving‟amuzi kila nyumba bure na hiyo
haitawezekana. Lakini ninachosema kwamba tunajitahidi kuona kwamba
wananchi wetu tunajaribu kufidia kama nilivyosema king‟amuzi hichi katika
soko la kawaida ni shilingi 120,000/= na zaidi. Mhe. Naibu Spika, sisi
tumejaribu kuhakikisha kwamba wananchi wetu wanapata ving‟amuzi katika
bei hiyo.
Mhe. Salma Moh’d Ali:Mhe. Naibu Spika, nakushukuru pamoja na majibu
mazuri ya Mhe. Waziri naomba nimuulize swali la nyongeza. Mhe. Naibu
Spika, ni kweli kuna taarifa ya uhakika kwamba digital hapa Unguja imeanza
vizuri, lakini kwa upande wa Pemba hata pale Chake Chake kwenye mnara
wa television basi matangazo yake huwa ni ya kukatakata na baadhi ya siku
hayapatikani kabisa.
(a) Kutokana na hali hiyo, namuomba Mhe. Waziri anifahamishe je nini
sababu ya tatizo hili.
(b) Wananchi wa Pemba wategemee tatizo hili litatatuka lini.
Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo: Mhe. Naibu
Spika, ni kweli kwamba digital Pemba haijatulia nakiri hilo na niombe radhi
kwa wananchi wa Pemba kwamba tunaendelea na jitihada zetu na zitafika
pahala.
Kwa kweli sababu kubwa ni kwamba tulipo-design huu mtandao tuli-design
mawimbi yapeperushwe kwa kutumia mkonga na kwamba microwave link
zibakie kama akiba endapo mkonga utaharibika. Mhe. Naibu Spika, kwa
bahati mbaya mkonga haujawa tayari na kwa hivyo tunatumia ule utaratibu
wa akiba wa microwave link.
Kwa hivyo, Pemba inapata signal kutoka mnara wa Nungwi kwenda mnara
uliopo Kichunjuu, ili signal ionekane vizuri lazima makawa yaliyo juu ya
minara yaonane line of site yaonane, na kukiwa na upepo kidogo ikinyumba
15
basi digital nayo inayumba na hiyo ndio tendency iliopo Nungwi kwamba
kuna upepo mkubwa na kwa hiyo digital ikiyumba kidogo basi na hali ya
matangazo inayumba Pemba.
Mhe. Naibu Spika, hiyo ndio hali halisi na tunajitahidi mpaka juzi Jumapili
mimi mwenyewe nilikwenda Nungwi kwenye mnara kuona namna gani
wahandisi wanajaribu kuweka hali sawa, lakini wamejaribu kidogo na
nimeambiwa kwamba hali kidogo imetengemaa na hiyo ndio hali halisi.
Vile vile mategemeo yetu ni kwamba itakapofanyakazi mkonga wa taifa basi
hali hii itatengemaa vizuri na kwa mujibu wa Mhe. Waziri wa Nchi, (OR),
Utumishi wa Umma na Utawala Bora juzi katika bajeti yake alitwambia
kwamba baada ya muda mfupi wametia mkataba na Kampuni ya ZANTEL, ili
mkonga wa taifa ufanye kazi na hali hiyo ikiwa tayari basi na wananchi
Pemba watapata matangazo bila ya kukatika hata kidogo.
Nam. 123
Ujenzi wa Nyumba ya Daktari katika Hospitali ya Chake Chake – Pemba
Mhe. Rufai Said Rufai – Aliuliza:-
Kwa kuwa kuna taarifa kwamba Hospitali ya Chake Chake ina tatizo la
daktari wa tiba (Doctor of Medicine MD) na kwa kuwa kuna taarifa kuwa
wizara iko tayari kupeleka daktari wa fani hiyo, lakini kikwazo kikubwa
kilichopo ni nyumba ya kuishi daktari.
Je, ni lini serikali italipatia ufumbuzi tatizo hilo.
Mhe. Naibu Waziri wa Afya – Alijibu:-
Mhe. Naibu Spika, kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mhe. Mwakilishi swali
Nam. 23 kama ifuatavyo:-
Ni kweli kwamba Hospitali ya Chake Chake kuna madaktari bingwa wa
maradhi ya kawaida (physician), daktari wa magonjwa ya wanawake
(Obstretics and Gynecologist), daktari wa watoto (Pediatrition) na daktari
bingwa wa upasuaji (Surgeon). Lakini hao ni wageni na mzalendo ni wa
mkataba. Kwa taratibu za ugawaji wa wafanya kazi kwa mahitaji (minimum
requirement) katika mahospitali yetu, kila hospitali inatakiwa iwe na daktari
mzalendo ili kuwa dhamana wa hospitali husika.
16
Daktari aliyekubalika ni daktari wa kawaida MD (General Doctor of
Medicine). Mhe. Naibu Spika, sio kweli kwamba kukosekana kwa nyumba
kumekwamisha kupatikana kwa MD ila hawapo kwa sasa wa kupangiwa
huko, pindipo wakipatikana watapangiwa na pa kukaa patapatikana.
Mhe. Rufai Said Rufai: Mhe. Naibu Spika, nashukuru na naomba nimuulize
swali moja la nyongeza Mhe. Naibu Waziri. Mhe. Naibu Spika, kuna taarifa
kwamba nyumba ya kukaa daktari ipo ambayo aliyokuwa akikaa daktari
dhamana wa Hospitali ya Chake Chake. Lakini sasa imewekwa mtumishi wa
serikali wa kawaida. Je, kwa kufanya hivyo ni kuboresha huduma ya afya au
ni kurudisha nyuma huduma hiyo.
Mhe. Naibu Waziri wa Afya: Mhe. Naibu Spika, kwa uwelewa wangu mimi
kuhusu nyumba iliyopo Chake-Chake anayekaa ni clinical officer kwa level
yake lakini kwa vile ndio daktari aliyopo, kwa hivyo tumempa hiyo nyumba
pindi akitokea daktari akipatikana tutamuondosha yule tutampa yule
anayestahiki.
Mhe. Saleh Nassor Juma: Ahsante Mhe. Naibu Spika, pamoja na majibu
mazuri ya Mhe. Naibu Waziri wa Afya naomba niulize swali moja dogo sana
la nyongeza. Kwa kuwa malengo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
kiasi kikubwa ni kupunguza vifo vya mama na mtoto. Na kwa kuwa umekiri
hapa kwamba daktari bingwa pale Chake-Chake hayupo, hospitali ambayo
inahudumia asilimia kubwa ya wakaazi wa kisiwa cha Pemba.
a) Je. Mhe. Naibu Spika, kuendelea kuiacha hospitali ile kukosa daktari
bingwa ni pia lengo la Melennium goals kufikia kupunguza vifo vya
mama na watoto katika Zanzibar.
b) Kwa kuwa kila siku wanafunzi wa Zanzibar wana graduate katika
vyuo Vikuu vya Mambo ya Afya na Wazanzibari katika graduation
hizo wamo. Je ni lini kwa sababu ulisema akipatikana daktari
utapelekwa kule, sasa ni lini utampeleka daktari katika hospitali ya
Chake-Chake kwa vile wana graduate siku hadi siku katika vyuo
vikuu vya nchi hii.
Mhe. Naibu Waziri Afya: Mhe. Naibu Spika, naomba kujibu swali la
a) Ni kweli vifo vya mama na watoto vinatakiwa vikingwe na hilo ndio
lengo la serikali.
Chake Chake nimesema pana madaktari wengi akiwemo daktari wa
wanawake akiwemo na daktrari wa watoto. Kwa hiyo suala hilo hata
17
wananchi wengi wameshakwenda madaktari hao wapo, isipokuwa ni
hao wa kigeni, lakini wote ni mabingwa.
b) Mhe. Naibu Spika, tunasomesha madaktari wengi, nje na ndani ya
nchi, wanakuja na kuondoka wengine wanakaa. Kuna utaratibu
tumeupanga kwamba kila hospitali pawe na daktari wa aina fulani.
Tunayemtaka na tunayemzungumza hapa ni daktari atakayekuwa
dhamana kwenye hospitali husika. Hospitali za Wilaya zote
zinatakiwa ziwe na daktari dhamana mzalendo. Sasa
watakapokuwepo tutapanga, Hospitali ya Micheweni, Chake-Chake,
Vitongoji, Mkoani na Hospitali ya Wete, wakija tutapanga lakini
tunategemea labda mwaka huu watakuja madaktari wengi, kwa
sababu wapo wanaomaliza Muhimbili, tutahakikisha tunafanya hivyo
na kwa Unguja tutapeleka Kivunge na Makunduchi.
Nam. 23
Upatikanaji wa Maji Safi na Salama Kijiji cha Jitenge, Kojani
Mhe. Hassan Hamad Omar - Aliuliza:-
Kwa kuwa kumekuwa na kero na usumbufu mkubwa sana kwa wananchi wa
Kijiji cha Jitenge Maziwani Jimbo la Kojani kwa kukosa maji safi na salama
kwa muda mrefu. Pamoja na juhudi zinazochukuliwa na Mwakilishi na
Mbunge wa jimbo hilo na Halmashauri ya Wilaya ya Wete bado huduma hiyo
ni kikwazo kupatikana.
a) Je, Mhe. Waziri nini kinachokwamisha juhudi hizi.
b) Je, ni lini wananchi wa kijiji cha Jitenge Maziwani watarajie
kupata huduma hii muhimu ya maji safi na salama.
Mhe. Naibu Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati - Alijibu:-
Mhe. Naibu Spika, naomba kumjibu Mhe. Waziri swali lake Nam. 23 kama
hivi ifuatavyo:-
(a) Mhe. Naibu Spika, kijiji cha Jitenge awali kiasi kama miaka
sita iliyopita kilikuwa kinatumia huduma ya maji kwa kutumia hand
pump kwa msaada wa UNICEF. Huduma hii ilikuwa inapatikana bila
ya usumbufu wowote. Halmashauri ya Wilaya ya Wete, Mbunge na
Mwakilishi walichangia mipira nchi tatu kasorobo kupitia maziwani
ambapo pia kulikuwa na matatizo ya maji. Kwa bahati mbaya mipira
18
hiyo ilikuwa ni midogo kwa Kijiji cha Jitenge, namuomba Mhe.
Mwakilishi na Halmashauri wawe na moyo wa kuchangia huduma
hiyo ya maji ili kupatikana mipira yenye kiwango kama ushauri wa
Mamlaka utakavyotolewa.
(b) Mhe. Naibu Spika, kwa kijiji cha Ziwani najua mipira
iliyotolewa na Mhe. Mwakilishi iko chini ya kiwango Class C
ambapo husababisha kupasuka mara kwa mara. Ningemuomba Mhe.
Mwakilishi ashirikiane na Mamlaka yetu ya maji tawi la Pemba ili
kuhakikisha kwamba mipira inayotafutwa ni mipira yenye kiwango
na kuzuia uvujaji huo wa mara kwa mara.
Mhe. Hassan Hamad Omar: Ahsante sana Mhe. Naibu Spika, pamoja na
majibu mazuri ya Mhe. Naibu Waziri wa Ardhi, Makaazi na Nishati, naomba
nimuulize swali la nyongeza kama hivi ifuatavyo.
Mhe. Naibu Waziri utakubaliana na mimi kama juhudi ya Mbunge wangu wa
Jimbo la Kojani pamoja na Halmashauri ya Wilaya tumefanya juhudi kubwa
sana. Lakini mpaka hivi ninavyozungumza maji Jitenge hayapatikani.
Wananchi hawa wa kijiji cha Jitenge walishakusudia kwamba wamekwenda
sambamba na jina lao kwamba jitenge kweli wametengwa. Ndio maana
tukapeleka nguvu kubwa wakataka kujitoa katika jimbo hili na kuomba
sehemu nyengine wakajiunge. Tukawashajihisha wabaki katika jimbo na
Inshallah kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na jitihadi ya serikali watapata
huduma.
Nataka uniahidi ni lini kero lile litamalizika na wananchi wa jitenge watapata
maji.
Mhe. Naibu Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati: Mhe. Naibu
Spika, nimshukuru tena kwa mara nyengine kwa msaada wao yeye pamoja na
Mhe. Mbunge kwa kushirikiana nasi katika kuchangia huduma hii. Kwa hivyo
wananchi hawa wa Jitenge sitaki niseme lini, lakini namuomba tushirikiane
tena mimi na yeye pamoja na Mamlaka yangu ili kwenda kushughulikia hili
tatizo. Namuhakikishia kwamba tutakaposhirikiana basi wananchi hao
wataipata huduma hii na tatizo hilo litawaondokea.
Mhe. Subeit Khamis Faki:Nakushukuru sana Mhe. Naibu Spika, kwa kunipa
fursa nimuulize Mhe. Naibu Waziri swali la nyongeza.
Mhe. Naibu Spika, katika kuwatatulia wananchi kero ya maji serikali
imefanya jitihada ya kila aina ili kupunguza kero la maji katika nchi yetu ya
Zanzibar. Kwa kuwa mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani tunaoingia kesho
19
kutwa, ni vyena wananchi kuwapunguzia kero zaidi hasa katika huduma hii
ya maji, kwa sababu watu wanakuwa wana thaumu na kwenda mabondeni
kujitwika ndoo kwenye mabonde na kupandisha kwenye milima inakuwa ni
tatizo zaidi. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanzisha huduma ya kusaidia
wananchi pale ambapo wananchi hawapati maji kwa upande wa Unguja kuna
magari maalum ya maji yanawapelekea wananchi kuwasaidia ili
kuwapunguzia usumbufu.
(a) Je, namuuliza Mhe. Waziri katika kipindi hichi cha Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani wamejipanga vipi na kule kuona katika
sehemu za vijiji ambavyo hawapati maji kuna magari maalum
yanawapelekea wananchi ili kuwapunguzia usumbufu katika mwezi
huu mtukufu wa Ramadhani.
(b) Je, na kama hivyo sivyo ni lini watajipanga zaidi ili
wananchi waepukane na matatizo hayo.
Mhe. Naibu Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati: Ahsante Mhe.
Spika, kama alivyozungumza Mhe. Mwakilishi kwamba tunao utaratibu wa
kuwasaidia wananchi wale ambao huduma ya maji safi na salama
haijawafikia katika vijiji vyao, hususan katika kipindi hichi cha mwezi wa
Ramadhani. Namuomba Mhe. Mwakilishi aelewe kwamba huduma hii sio
kwa Unguja tu nilisema Zanzibar. Kwa hiyo tunafanya Unguja na Pemba.
Bado Wizara yangu kupitia Mamlaka ya Maji itaangalia vile vijiji ambavyo
huduma hiyo haipo hasa kwa mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani basi
itaendelea kuwasaidia kama ilivyowasaidia katika miaka mengine.
Mhe. Saleh Nassor Juma: Ahsante sana Mhe. Naibu Spika, kunipatia fursa
ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mhe. Naibu
Waziri naomba niulize swali hilo kama ifuatavyo.
Kwa kuwa wananchi wa Jitenge katika jimbo la Kojani wameendelea na
wataendelea kukosa maji pale. Kwa sababu juzi tu Mhe. Waziri wakati
anajibu swali pale alisema tunategemea maji ya visima virefu ambavyo sasa
hivi maji yanakosekana kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na yataendelea
kukosekana. Kwa hivyo hili tatizo linaonekana litaendelea.
Kwa kuwa tatizo hili litaendelea kuwepo sio Jitenge tu lakini Vitongoji, Wawi
na hata hapa maskini hapa Mji Mkongwe nao maji ni tatizo. Sasa vipi pale
Jitenge Mhe. Waziri kwa sababu serikali inaonekana haina uwezo wa
kupeleka maji.
20
(a) Je, ni lini mtakwenda kuwafundisha kupeleka elimu ya
kuvuna maji ya mvua ili kama wenzao Bara wanavyovuna
maji ya mvua. Hii elimu ya kuvuna maji ya mvua ni lini
mtaipeleka Jitenge ili watu waweze kufaidika na hii taaluma
ya kupata maji ya kuvuna ya mvua.
(b) Kwa kuwa kila kukicha serikali yetu inashindwa kufanya
ubunifu wa kupata maji. Maana juzi tuliambiwa vile vile hamuwezi
kuyageuza maji ya bahari na kuwa maji safi ya kutumia. Je, ni lini
Mhe. Naibu Waziri mtajenga mitambo hii kutibu maji (Water
treatment plans) ambazo zitatusaidia haya maji taka kuyageuza
kuwa maji mazuri ya kutumia kama wanavyofanya wenzetu katika
nchi za Ghuba na hata hizi nchi nyengine katika Jangwa la Sahara.
Ni lini mtajenga mitambo ya kutibu maji ili na sisi tuondokana na
hili tatizo.
Mhe. Naibu Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati: Mhe. Naibu
Spika, kuhusu kujenga mitambo hiyo aliyoizungumza basi inategemea hali ya
fedha ambayo itaingia katika mamlaka yangu. Ni suala ambalo linahitaji
gharama, kwa hivyo serikali iko tayari kulishughulikia hili lakini vile vile
inaangalia hali ya fedha itakavyowezesha kufanya mitambo hiyo.
Vile vile suala la Jitenge, bado narejesha kauli kwamba Wizara yangu
itaangalia zaidi jinsi gani ya kuwasaidia wananchi wa Jitenge. Lakini bado
nimesema naomba sana mashirikiano mimi pamoja na Mhe. Mwakilishi
tushirikiane kisha tuangalie njia gani ya kuliondosha tatizo la wananchi wa
Jitenge kuhusiana na suala la maji.
Mhe. Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati: Mhe. Naibu Spika,
pamoja na majibu mazuri ya Mhe. Naibu Waziri naomba kuongezea majibu
ya ziada kutokana swali la Mhe. Saleh Nassor Juma kama hivi ifuatavyo.
Mhe. Naibu Spika, katika suala la maji Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imefanya jitihada kubwa kabisa na ndio maana imebuni miradi mingi mipya
hivi sasa ambayo tayari ili katika kiwango cha kutekelezwa ambacho
tunategemea tukifika mwakani kwenye mwezi wa Septemba na Oktoba hali
ya maji katika Zanzibar itakuwa ni nzuri, tuna matumaini makubwa sana.
Kwa hivyo, hasa haya maeneo ambayo kweli yana matatizo maji tunategemea
kwamba tukifika mwakani hali ya maji katika maeneo hayo pia itakuwa
imeshakuwa nzuri kabisa kuliko ilivyo hivi sasa.
Anapozungumzia suala la water treatment plans nadhani kwa Zanzibar
hatujafika kiwango hicho kwa sababu tatizo letu kubwa ni kuwa na pampu au
21
vyanzo vya maji vya kutosheleza. Hivi sasa hivi kuna miradi ya kuongeza
vyanzo vya maji vingi sana, kwa sababu bado ardhini inaonesha dalili
kwamba kuna maji mengi, maji yaliopo hapa juu ndiyo yameathirika sana na
tabia ya nchi, lakini ardhini inaonesha kuna maji mengi. Kwa sababu kila
kisima kinachochimbwa kinatoa maji ya kutosha kabisa.
Kwa hivyo napenda kumwambia kwamba haijafikia kiwango hicho cha
kufanya water treatment plans hapa Zanzibar, lakini tutegemee miradi yetu
hii inayoendelea sasa hivi italeta mafanikio. Kuna mradi mkubwa sasa hivi wa
Ras al Khaimah ambapo wanachimba visima katika maeneo mbali mbali na
wanapata mafanikio makubwa sana kwamba maji wanayakuta mengi sana.
Tukitoka hapo labda angetwambia Mhe. Mwakilishi kwamba bado tuna
reserve ya maji kubwa katika upande wa Magharibi wa Kisiwa cha Unguja
kuelekea Mainland, huko kuna reserve kubwa sana ya maji ambayo nayo
tukifanya maarifa na tukipata wahisani pamoja na sisi wenyewe tunaweza
tukayapata maji hayo tukayatumia kwa matumizi. Zanzibar ina bahati ya
kuwa ni kisiwa chenye maji matamu sana na tunaweza tukayaendeleza ikiwa
uwezo utakuwepo. Ahsante sana.
HOJA ZA SERIKALI
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya kwa
Mwaka wa Fedha 2013/2014
Mhe. Waziri wa Afya: Kabla sijaanza naomba nieleze kwamba kutokana na
ukubwa wa hotuba yangu nimeruhusika kwa mujibu wa Kanuni kifungu cha
96 (2) kuweza kusoma muhtasari angalau nisizidi masaa mawili. Kwa hivyo
nitakaposoma nitakuwa kila mara nawaejesha Wajumbe kwenye hichi kitabu
chengine, kwa hivyo naomba nisome muhtasari tu ili ninusuru wakati.
Bismillahi Rahmani Rahim.
Utangulizi
Mhe. Naibu Spika, naomba kutoa hoja kwamba sasa Baraza lako tukufu likae
kama Kamati ya Matumizi ili liweze kupokea, kujadili, kuchangia na
mwishoe liidhinishe makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya
kwa kazi za kawaida na kazi za maendeleo, kwa mwaka wa fedha 2013/2014.
Mhe. Naibu Spika, kwanza sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba
wa vyote viliomo nchi kavu, baharini na angani kwa kutupa afya njema
ambayo imetuwezesha kukutana mara nyengine tena katika kikao hiki
muhimu cha bajeti.
22
Mhe. Naibu Spika, sasa naomba kumpongeza Mhe. Dr. Ali Mohamedd Shein,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pamoja na
Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Rais kwa uongozi wao wa
busara na wenye kutumia hekma nyingi kuiongoza nchi hii, hivyo kuendelea
kuwa ya amani na utulivu. Aidha, nawashukuru kwa mara nyengine tena
kutokana na maelekezo yao wanayoyatoa kupitia vikao vya kila robo mwaka,
mikutano ya kawaida au ziara za kikazi ambayo huwa na lengo la kuimarisha
utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa nchi hii.
Mhe. Naibu Spika, wewe mwenyewe pamoja na wajumbe wako wa Baraza
hili, mmekuwa na mchango mkubwa kwenye vita vya kupambana na maradhi
visiwani mwetu. Fikra na mawazo yenu na hata nguvu mnazozitoa majimboni
mwenu kiujumla au kwa mtu mmoja mmoja zimechangia kwa kiasi kikubwa
kwenye mapambano dhidi ya maradhi mbali mbali yanayowaathiri wananchi.
Kwa niaba ya uongozi na watendaji wote wa Wizara ya Afya tunawashukuru
kwa kujumuika nasi kwenye shughuli hii pevu na muhimu. Haya yote
mnayoyafanya yanatuongezea ujasiri wa kutekeleza majukumu yetu kwa
ufanisi bila ya kuchoka. Tunakuombeni muendelee kuwa nasi bila ya kurudi
nyuma au kukata tamaa, kwani mpiganaji mzuri ni yule asiyevunjika moyo au
kukata tamaa.
Mhe. Naibu Spika, kazi zinazofanywa na Kamati za Baraza la Wawakilishi
zinazisaidia sana sekta katika kutekeleza majukumu yake. Hivyo napenda
kuishukuru Kamati ya Maendeleo na Ustawi wa Jamii ya Baraza la
Wawakilishi iliyomaliza muda wake chini ya Mwenyekiti Mhe. Amina Iddi
Mabrouk, kwa kipindi chote cha kazi zake Kamati ilikuwa ikitoa maelekezo
na ushauri kwa Wizara ambao ulisaidia kwa kiasi kikubwa kutekeleza
majukumu yake ya utoaji wa huduma za afya ikiwemo kinga na tiba kwa
wananchi wa Zanzibar. Vile vile napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza
Mwenyekiti mpya wa Kamati Mhe. Mgeni Hassan Juma kwa kuteuliwa
kuiongoza kamati hii muhimu, ni matumaini yangu tutashirikiana kwa pamoja
katika kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha wanapata huduma stahiki za
afya kwa shughuli zake za kila siku pamoja na zile iliyojipangia kutekelezwa.
Majukumu ya Wizara
Mhe. Naibu Spika, majukumu makuu ya Wizara ya Afya ni haya yafutayo:
a) Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sera, sheria, mikakati,
mipango na miongozo ya utoaji wa huduma za afya,
23
b) Kutoa huduma za kinga, tiba na marekebisho ya tabia kwa
jamii,
c) Kusimamia maendeleo ya taaluma kwa wafanyakazi wa ngazi
mbali mbali wa sekta ya afya,
d) Kusimamia upatikanaji wa raslimali (fedha, nguvu kazi, vifaa
na madawa) katika kufanikisha utoaji wa huduma,
e) Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa taasisi na wizara juu ya
umuhimu wa afya ya jamii,
f) Kusimamia na kudhibiti ubora na usalama wa chakula, dawa
na vipodozi,
g) Kufanya uchambuzi na kutoa ushauri kwa jamii juu ya
matumizi bora ya kemikali,
h) Kusajili wataalam wa kada mbali mbali za afya,
i) Kusimamia uendeshaji wa hospitali za binafsi, maduka ya
madawa pamoja na kuratibu shughuli za matibabu ya asili,
j) Kuchukua tahadhari za haraka kukabiliana na maradhi ya
miripuko.
Muhtasari wa Mafanikio ya Wizara
Mhe. Naibu Spika, katika kipindi cha mwaka 2012/2013 wizara imepata
mafanikio mazuri katika utendaji kutokana na kazi zake za maendeleo, baadhi
ya mafanikio hayo ni pamoja na:
a) Kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka 285 kwa kila
vizazi hai 100,000 mwaka 2011 kufikia 221 kwa kila vizazi
hai 100,000 mwaka 2012,
b) Kuanzisha chanjo mpya dhidi ya maradhi ya kuharisha
(Rotavirus) na chanjo dhidi ya homa ya uti wa mgongo
(Pneumococcal),
c) Kupungua kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa
makundi maalumu.
24
i. Wanaume wanaojamiiana kutoka 12.3% mwaka 2008 na
kufikia 2.6% mwaka 2012,
ii. Watumiaji wa madawa ya kulevya kwa njia ya kujidunga
sindano kutoka 16% mwaka 2008 hadi 11.3% mwaka
2012.
d) Kuendelea kwa kasi kubwa ya ujenzi wa jengo la Mradi
Shirikishi wa Mama na Mtoto liliopo Kidongo Chekundu.
e) Kupitishwa sheria za afya ya jamii na wataalamu wa afya ya
mazingira katika Baraza la Wawakilishi. Sheria hii itakuwa
kichocheo katika kuimarisha afya ya jamii na kuepusha
maradhi yanayosababishwa na mazingira yasio salama.
f) Kuanzisha mfuko maalumu wa fedha kwa ajili ya huduma za
afya wilayani (District Health Services Basket Fund), ili
kuimarisha utoaji wa huduma katika vituo vya afya.
g) Kumalizika ujenzi wa jengo la Bohari Kuu ya Dawa
Maruhubi,
h) Kuanzisha utaratibu wa kufuatilia majumbani wagonjwa
wanaogundulika na malaria ndani ya siku tatu,
i) Kukamilika ujenzi wa majengo mapya ya maabara katika
hospitali za Wete, Chake-Chake na Micheweni,
j) Kupunguza msongamano wa jamaa wa wagonjwa
wanaolazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja,
k) Kuongezeka kwa asilimia ya mama wajawazito
wanaojifungua chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya
kutoka asilimia 47.1 mwaka 2011 kufikia 51.3 mwaka 2012,
l) Kukamilika kwa matengenezo makubwa ya nyumba tisa za
wafanyakazi zilizoko Kivunge.
Utekelezaji Kifedha
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Wizara ilipangiwa
kuchangia jumla ya Tsh. 805,500,000 kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.
Kufikia mwezi wa Machi 2013, kiasi cha Tsh. 366,020,263 (45.4%)
25
zilikusanywa. Aidha wizara iliidhinishiwa jumla ya Tsh. 18,234,000,000 kwa
ajili ya kazi za kawaida, mishahara, maposho na ruzuku. Kati ya hizo Tsh.
3,946,000,000 kwa Kazi za Kawaida. Hadi kufikia Machi 2013, jumla ya Tsh.
2,385,944,437 (60.46) zilikwishatolewa, kwa upande wa mishahara na posho
Tsh. 13,731,080,000 ziliidhinishwa na hadi kufikia Machi, 2013 jumla ya
Tsh. 10,475, 486,742 (76.29) zilitolewa na Tsh. 556,920,000 ziliidhinishwa
kama Ruzuku kwa Chuo cha Taaluma za Afya – Mbweni ambapo kufikia
Machi Tsh. 172,956,000 (31.06) tayari zilikwishatolewa. Miradi ya
Maendeleo ilitengewa jumla ya Tsh. 2,731,600,000, kufikia Machi 2013
jumla ya Tsh. 724,251,400 (26.5%) zilitolewa.
Mhe. Naibu Spika, naomba uniruhusu nieleze utekelezaji kwa mchanganuo
wa kila Idara, fedha zilizotengwa na kuingizwa hadi kufikia Machi kwa
mwaka 2012/2013 na zilizotengwa kwa mwaka 2013/2014. Ufafanuzi wake
unaonekana kiambatisho namba 17.
Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2012/2013
Mhe. Naibu Spika, katika mwaka 2012/13, Wizara ilitekeleza majukumu yake
kwa kuzingatia Malengo ya Milenia, Dira ya Maendeleo (2020), Mkakati wa
Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini II (2010), Sera ya Afya (2011)
pamoja na maazimio mengine ya kitaifa na kimataifa. Maeneo
yaliyotekelezwa ni haya yafuatayo kwa ufupi:
Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (NCD)
Mhe. Naibu Spika, magonjwa yasio ya kuambukiza yanaonekana kuongezeka
kwa kasi katika visiwa vya Zanzibar kwa miaka ya karibuni. Magonjwa hayo
ni pamoja na shindikizo la damu, kisukari, saratani na magonjwa mengine
sugu ya mapafu ikiwemo pumu n.k. Kwa kuona umuhimu wa kukabiliana na
hali hiyo, Wizara imeanzisha Kitengo cha kupambana na magonjwa hayo
ikiwa na lengo la kupunguza kasi ya ongezeko la magonjwa yasiyo ya
kuambukiza na kusimamia utekelezaji wa mikakati yenye lengo la
kukabiliana na magonjwa hayo.
Mhe. Naibu Spika, utafiti wa kuweza kubaini hali halisi ya kutambua
mahitaji ya taaluma, vitendea kazi pamoja na raslimali umefanyika kwa vituo
vya afya 34 vya daraja la pili vinavyotarajiwa kuanzisha huduma za maradhi
yasioambukiza, hospitali 4 za vijiji na hospitali 3 za wilaya. Pia matayarisho
ya mpango mkakati wa kupunguza kasi ya maradhi hayo yameanza
sambamba na urushaji wa vipindi mbali mbali vya televisheni na redio na
kuandikwa makala ya magazeti kuhusiana na maradhi hayo.
26
Mhe. Naibu Spika, kwa ufafanuzi na kwa urefu na wa-refer wajumbe kuanzia
kifungu namba 2.1.0 hadi 2.1.3 ya hotuba yangu iliyomo ndani ya kitabu.
KITENGO CHA KUFUATILIA MWENENDO WA MARADHI
Mhe. Naibu Spika, wizara kwa mwaka wa fedha 2012/2013 imeweza
kufuatilia mienendo ya maradhi mbali mbali ikiwemo magonjwa ya miripuko
kama vile kuharisha damu, ugonjwa wa kutafunwa na mbwa, ugonjwa wa
surua, ugonjwa wa tetekuanga, ugonjwa wa kuharisha kwa kawaida na
ugonjwa wa neoanatal tetanus. Kazi hii imefanywa baada ya kupokea taarifa
za kila wiki juu ya hali ya maradhi maalum kutoka vituo vyote vya Serikali.
Aidha katika kuimarisha mfumo huo wakuu wa vituo hivyo na wataalamu
wanaoshughulika na ukusanyaji wa taarifa „Infectious Diseases Weekly
Ending‟ (IDWE) katika ngazi ya wilaya walipatiwa mafunzo juu ya ufuatiliaji
wa maradhi kwa kila wiki.
Mhe. Naibu Spika, katika mwaka 2012/2013 kulitokea mripuko wa maradhi
ya kuharisha huko Bumbwini, ufuatiliaji ulifanywa ili kujua ukubwa wa tatizo
kwa kufanya utafiti wa kina (Operational Research). Matokeo ya utafiti
yalibainisha kwamba asilimia 33.3 ya waliougua walitumia maji yasiyokuwa
safi na salama na asilimia 66.7 walikula dagaa lisilokuwa salama. Mbali na
hayo kwa kushirikiana na Timu ya Afya ya Wilaya sampuli ya choo (Stool
Sample) ilichukuliwa kwa wagonjwa watatu na matokeo yake yalionesha
kuwa kuna vijidudu vijulikanavyo „Vibrio Parahaemolytica‟, ambavyo
vinapatikana kwa njia ya kula vyakula vya pwani (Sea food). Sambamba na
hilo ufuatiliaji pia ulifanyika katika sehemu mbali mbali, matokeo ya maradhi
yaliyogundulika kwa mgawanyo wa umri na kwa Wilaya yanaonekana katika
kiambatisho namba 1 na 2 ya hotuba yangu na maelezo zaidi kuhusu
ufuatiliaji wa maradhi yanapatikana kifungu namba 2.2.0 hadi namba 2.2.6.
MARADHI YASIYOPEWA KIPAUMBELE
Mhe. Naibu Spika, uchunguzi juu ya maradhi yasiyopewa kipaumbele
yakiwemo kichocho, minyoo matende na mabusha ulifanyika. Kwa upande
wa kichocho jumla ya watu 1,299 kutoka sehemu mbali mbali
walichunguzwa. Kati yao watu 928 waligunduliwa kuwa na ugonjwa sawa na
asilimia 71 na kwa wale waliogunduliwa na maradhi walipatiwa tiba. Aidha
tafiti kwa ajili ya kuimarisha njia za mapambano dhidi ya kichocho, minyoo
na matende zilifanyika ikiwa pamoja na kufanya tathmini za mwenendo wa
maradhi ya kichocho katika skuli 48. Aidha katika mzunguko wa pili wa
ulishaji dawa za kichocho na minyoo, jumla ya wananchi 1,183,154
waliorodheshwa kula dawa hizo, kati ya hao wananchi 976,122 walikula dawa
sawa na asilimia 83.
27
Mhe. Naibu Spika, ugonjwa wa matende ni moja ya ugonjwa unaowasumbua
wananchi hasa wa Wilaya ya Kusini. Kwa mantiki hii uchunguzi mdogo kwa
watu 32 ulifanyika ambapo ni mtu mmoja tu ndiye alionekana kuwa na
vimelea. Vile vile huduma za maradhi haya zinaendelea kwa kupokea
wagonjwa walioathirika zamani na kupatiwa mbinu za kuweka uvimbe katika
hali ya usafi (home based care).
Mhe. Naibu Spika, ufafanuzi kamili wa kitengo hiki unapatikana katika
kifungu 2.3.0 hadi 2.3.6 cha hotuba yangu.
KITENGO CHA AFYA BANDARINI
Mhe. Naibu Spika, katika kuzuia kusambaa kwa maradhi kutoka nchi hadi
nchi, ukaguzi kwa vyombo vya usafiri na abiria (uwanja wa ndege na
bandarini) ulifanyika. Jumla ya vyombo vya usafiri (meli kubwa, boti na
majahazi) 2,063 vilipangwa kukaguliwa, kati ya hivyo, vyombo 2,066 (102%)
vilikaguliwa Unguja na kwa Pemba ni 29. Ukaguzi ulibainisha kuwa vyombo
31 havikuwa katika hali ya usafi hivyo vilifanyiwa ufukizwaji (fumigation) na
vyombo 30 vimefanyiwa hatua za usafi (upuliziaji/mitego). Aidha abiria
450,704 wa kawaida na 188,622 wa kigeni walikaguliwa. Maelezo zaidi
kuhusu kazi zilizofanywa na Kitengo cha Afya bandarini yanapatikana katika
kifungu 2.4.0 hadi 2.4.7 ya hotuba yangu.
KITENGO CHA HUDUMA ZA MATIBABU YA MACHO
Mhe. Naibu Spika, uchunguzi na utibabu wa macho ulifanyika kwa wanafunzi
2,665 wa Skuli za Jambiani, Kizimkazi Mkunguni, Matemwe, Kidutani
Maandalizi, Kisiwandui na Skuli ya Kidongo Chekundu. Kati yao wanafunzi
587 walipatiwa matibabu na kupewa miwani. Pia askari polisi 69 wa
Hanyegwa Mchana walichunguzwa, kati yao askari 51 walipatiwa miwani na
18 walitibiwa macho. Jumla ya miwani 445 za kusomea ilitolewa kupitia
huduma za masafa katika sehemu mbali mbali. Kiambatisho namba 3 cha
hotuba kinajieleza zaidi.
Mhe. Naibu Spika, kutokana na ukosefu wa daktari bingwa wa macho kwa
watoto hapa nchini, kwa mashirikiano makubwa na Kitengo cha Matibabu ya
Macho kwa watoto cha Muhimbili (MCBI). Kitengo kimeweka utaratibu wa
kuwapeleka watoto wenye matatizo makubwa ya macho huko Muhimbili au
madaktari hao bingwa wa Muhimbili kuja hapa nchini na kutoa huduma
zinazostahili. Kupitia mpango huu kwa kipindi cha Julai hadi Machi, 2013
jumla ya watoto 131 walipatiwa matibabu na madaktari hawa kati ya hao 32
walifanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho na presha ya macho.
28
Mhe. Naibu Spika, ufafanuzi kamili wa kitengo hiki unapatikana katika
kifungu 2.6.0 hadi 2.6.6 cha hotuba yangu.
KITENGO CHA AFYA YA WAFANYAKAZI
Mhe. Naibu Spika, katika kuhakikisha afya ya wafanyakazi, jumla ya
wafanyakazi 2,364 (Unguja 2,030 na Pemba 334) kutoka taasisi mbali mbali
zinazohusisha chakula walichunguzwa afya zao na kubainika maradhi mbali
mbali ikiwemo pumu, UKIMWI, homa ya tumbo (typhoid), homa ya ini kwa
wafanyakazi 108. Wafanyakazi hawa walifanyiwa utaratibu wa kupatiwa
matibabu. Kiambatisho namba 4 kinatoa ufafanuzi na maelezo zaidi
yanapatikana kifungu namba 2.7.0 hadi namba 2.7.3.
Mhe. Naibu Spika, maelezo zaidi ya utekelezajii wa kitengo hiki yanapatikana
katika kifungu 2.7.0 hadi 2.7.3 cha hotuba yangu.
KITENGO CHA LISHE
Mhe. Naibu Spika, katika kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa tezi shingo
(Goitre) yanayosababishwa na ukosefu wa madini joto ambayo hupatikana
kwenye chumvi maalumu, wizara imechapisha na kusambaza vitabu 1,000
vya kanuni ya chumvi kwa maafisa wa ngazi mbali mbali. Halikadhalika
ulishaji wa matone ya vitamin A na dawa za minyoo kwa watoto walio na
umri wa miaka mitano ulifanyika na kubainika kushuka kwa ulaji wa matone
hayo kutoka asilimia 95% hadi 61.5% kitaifa. Sababu kubwa iliyopelekea
kushuka kwa kiwango hiki ni pamoja na kubadilisha mikakati ya utekelezaji
wa kazi hii ambapo kwa sasa kazi inafanywa kwa kupitia huduma za kawaida
(routine services) badala ya kutolewa kwa mfumo wa kampeni kama
ilivyokuwa hapo zamani.
Mhe. Naibu Spika, ufafanuzi kamili wa kitengo hiki unapatikana katika
kifungu 2.8.0 hadi 2.8.4 cha hotuba yangu.
Mhe. Naibu Spika, kwa ujumla Idara ya Kinga na Elimu ya Afya imeelezwa
kwa urefu kuanzia ukurasa wa 5 mpaka ukurasa wa 18 wa hotuba yangu.
HUDUMA ZA TIBA
HOSPITALI ZA WILAYA
Mhe. Naibu Spika, huduma za tiba kwa hospitali tatu za Wilaya na nne za
Vijiji, ziliendelea kutolewa kama kawaida. Hospitali hizi zimefanyiwa
matengenezo na kupatiwa vifaa mbali mbali. Kwa upande wa matengenezo;
29
Hospitali ya Abdalla Mzee ilitengenezewa mfumo wa maji safi, Hospitali ya
Chake-Chake imefanyiwa matengenezo makubwa katika sehemu inayotoa
huduma za viungo; Hospitali ya Wete wodi ya wanaume na kliniki ya watoto;
ukarabati mkubwa wa nyumba tisa za daktari na ujenzi wa ukuta umefanyika
katika hospital ya Kivunge. Katika Hospitali ya Micheweni kumetengenezwa
chumba cha kuhifadhia dawa na mfumo wa maji safi umetengenezwa katika
Hospitali ya Vitongoji. Aidha kwa upande wa vifaa kama X-ray, mashine ya
Ultra Sound na ECG pamoja na vitanda na magodoro vilinunuliwa kwa
baadhi ya hospitali.
Mhe. Naibu Spika, napenda kuliarifu Baraza lako tukufu kwamba maabara ya
hospitali ya Chake-Chake imechaguliwa kuwemo kwenye maabara 18
zilizomo nchini Tanzania ambazo ziko kwenye ubora (quality), jambo hili
linatia matumaini makubwa katika utoaji wa huduma za maabara katika
hospitali hii. Sambamba na hili wafanyakazi wa maabara hiyo wamepatiwa
mafunzo ili waweze kutoa huduma kwa kiwango kinachostahili.
Mhe. Naibu Spika, ufafanuzi kamili wa Hospitali za Wilaya unapatikana
katika kifungu 3.1.0 hadi 3.9.1 cha hotuba yangu.
HUDUMA ZA UZAZI KATIKA HOSPITALI ZA IDARA YA TIBA
Mhe. Naibu Spika, akinamama kujifungulia katika hospitali ni moja kati ya
mikakati inayochangia kupunguza vifo vya akinamama vitokanavyo na uzazi.
Kwa kipindi cha Julai 2012 hadi Machi 2013, jumla ya wajawazito 9,176
walilazwa katika hospitali hizo. Kati ya hao wajawazito 7,782 walijifungua
kwa njia ya kawaida na akinamama 522 walijifungua kwa njia ya upasuaji.
Akinamama 20 walifariki dunia kutokana na sababu mbali mbali kama kifafa
cha mimba, kutokwa na damu kwa wingi na mengineyo. Ufafanuzi wa hali ya
uzazi unaonekana katika kiambatisho namba 6.
MPANGO WA DAMU SALAMA
Mhe. Naibu Spika, kwa kipindi cha mwaka 2012/2013, jumla ya unit za damu
6,127 (77%) zilikusanywa ambapo lengo lilikuwa kukusanya unit 8,000.
Aidha, wizara kwa kushirikiana na wadau mbali mbali itaendelea na jitihada
za kuwahamasiha wananchi juu ya umuhimu wa kuchangia damu. Kwa
maelezo zaidi naomba watu wasome ukurasa namba 24 hadi 25.
MATIBABU NJE YA NCHI
Mhe. Naibu Spika, shughuli ya kusimamia matayarisho ya usafirishaji
wagonjwa nje ya nchi baada ya kushindikana kimatibabu ndani ya nchi nalo
30
ni jukumu la Idara ya Tiba. Kwa mwaka wa fedha 2012/2013 jumla ya
wagonjwa 223 walitathminiwa na Bodi (Medical Board), Hadi kufikia Machi
2013 jumla ya wagonjwa 144 ndio waliosafirishwa nje ya nchi. Vile vile
wagonjwa 45 walipelekwa Tanzania Bara. Jumla ya Tsh. 990,248,168
zilitumika kwa huduma hiyo ambazo zimepita kiwango cha fedha
zilizotengwa kwa mwaka 2012/2013 ambazo jumla zilikuwa ni Tshs.
335,000,000. Hali hii inaathiri kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa kazi
nyengine za wizara.
Mhe. Naibu Spika, maelezo zaidi ya utekelezaji wa Idara yaTiba yameelezwa
kuanzia kifungu 3.0 mpaka 3.13.3 ambavyo vinavyopatikana ukurasa wa 19
mpaka ukurasa wa 25 wa hotuba yangu.
IDARA YA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA
Mhe. Naibu Spika, jukumu muhimu la idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja ni
kutoa huduma za uchunguzi na matibabu kwa wagonjwa ikiwemo huduma za
rufaa, pamoja na mambo mengine, Idara hii kupitia hospitali zake za Mnazi
Mmoja, Mwembeladu na Hospitali ya Wagonjwa wa Akili K/Chekundu hutoa
mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa kada mbali mbali za afya wanaotoka
katika Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya na vyuo vya afya vya binafsi na
skuli ya madaktari ya Zanzibar inayoendeshwa kwa msaada wa Cuba.
Mhe. Naibu Spika, nia ya Serikali ni kuifanya Idara hii kuwa taasisi yenye
kujitegemea (Semi Autonomous) ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa
huduma. Katika kufanikisha hilo rasimu ya sheria ya kuanzisha taasisi hiyo
imeshaandaliwa na imo katika mchakato wa kujadiliwa katika vikao husika.
HOSPITALI YA MNAZI MMOJA
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013 hospitali imeweza
kuendesha huduma za afya kupitia kambi maalum kwa kushirikiana na
madaktari bingwa kutoka nchi ya Spain na Ujerumani. Hadi kufikia Machi
2013 jumla ya wagonjwa 296 waliohndumiwa na madaktari bingwa kutoka
Spain na Ujerumani, kati yao 60 walifanyiwa upasuaji. Wagonjwa 47
walionwa na madaktari kutoka Ujerumani na wagonjwa 19 walifanyiwa
upasuaji ukiwemo wa hyrocephulus, spinal bifida repair yaani uti wa
mgongo, lamine ctomy pamoja na maradhi mengine. Aidha huduma za
wagonjwa wa nje na wa kulazwa zinapatikana katika kiambatisho namba 8 za
kliniki maalum ikiwemo macho, masikio, koo namba 9 na uzazi namba 10.
Mhe. Naibu Spika, mbali na utoaji wa huduma hospitali pia imefanikiwa
kutekeleza mambo yafuatayo:
31
a) Kuweka mtambo wa oxygen kwenye chumba cha upasuaji
(theatre), wodi ya wagonjwa mahututi (ICU), wodi ya wazazi (maternity)
na chumba cha dharura;
b) Mashine ya kisasa ya kufanyia operesheni (minimal access
surgery) imewekwa kwenye chumba cha upasuaji;
c) Kufungua kituo cha meno cha tabasamu (smiling center) kwa
mashirikiano na wataalamu kutoka China na madaktari wazalendo
wa Zanzibar kwa kufanya marekebisho kwa midomo yenye kasoro;
d) Mfumo wa kuweka kumbukumbu za wagonjwa kwa kutumia
kompyuta (Electronic medical Record System) umeanzishwa
hospitalini hapo;
e) Kuifanyia ukarabati mdogo wodi ya wazazi na chumba cha
wagonjwa wa dharura.
Mhe. Naibu Spika, huduma za kujifungua ni moja ya huduma inayopewa
kipaumbele katika hospitali hii, kwa mwaka 2012/13 Wizara imekuwa
ikitekeleza agizo la Mhe Rais la kutoa huduma hizo bila ya malipo wakati
wote vifaa vya kutolea huduma hiyo vilipopatikana. Katika kipindi cha Julai
2012 – Machi 2013, jumla ya wajawazito 5,503 walijifungua kwa njia ya
kawaida (normal delivery), wajawazito 1,042 walijifungua kwa njia ya
upasuaji na wajawazito 24 walifariki dunia kutokana na sababu mbali mbali,
takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wajawazito waliofariki imepanda kutoka
20 kwa mwaka 2011/2012. Kwa ufafanuzi zaidi angalia kiambatisho namba
10. Maelezo ya kina kwa hospitali hii yanapatikana ukurasa 26 hadi 30 katika
hotuba.
HOSPITALI YA WAGONJWA WA AKILI (Kidongo Chekundu)
Mhe. Naibu Spika, kuanzia Julai 2012 hadi Machi 2013, jumla ya wagonjwa
wa nje 4,522 walipatiwa matibabu (2,314 ni wanaume na 2208 ni wanawake).
Aidha, wagonjwa waliolazwa ni 230 (152 ni wanaume na 78 ni wanawake),
mgonjwa mmoja alifariki dunia. Idadi ya wagonjwa waliolazwa imeongezeka
kwa wagonjwa 54
.
Mhe. Naibu Spika, moja kati ya changamoto niliyoieleza katika Baraza hili
katika hotuba ya Wizara ya mwaka 2012/13 ni msongomano wa ndugu na
jamaa wa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hii. Tatizo hili limekuwa ni
la muda mrefu na hatua kadhaa zimekuwa zikichukuliwa ili kutoa fursa kwa
madaktari kupata muda na wasaa mzuri wa kuwahudumia wagonjwa. Kwa
32
sasa wizara imeajiri kampuni ya ulinzi ili kudhibiti uingiaji ovyo wa watu
hospitalini. Napenda kutumia fursa hii kuwaomba wananchi kushirikiana na
uongozi wa hospitali ili utaratibu huu mpya uliowekwa kwa manufaa yetu
pamoja na wagonjwa waliolazwa ufanikiwe.
Mhe. Naibu Spika, Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja imeelezwa kwa urefu
kuanzia vifungu 4.0 mpaka 4.3.3 kwenye ukurasa wa 25 mpaka 32 wa hotuba
yangu.
OFISI YA MFAMASIA MKUU
Mhe. Naibu Spika, upatikanaji wa dawa muhimu na vifaa tiba ni moja ya eneo
muhimu kwa sekta ya afya ingawa bado upatikanaji wake haukidhi mahitaji
halisi, kwa mwaka wa fedha 2012/2013,wizara imepokea jumla ya Tsh.
271,441,649 kwa ununuzi wa dawa na zana za tiba kutoka mfuko mkuu wa
serikali kati ya Tsh. 1,500,000,000 zilizotengwa. Kwa upande wa washirika
wa maendeleo jumla ya dawa zenye thamani ya Tsh. 3,550,857,320
zilipatikana. Kiambatisho Namba 12 kinatoa ufafanuzi.
Mhe. Naibu Spika, ili kuondokana na kutokuwa na uhakika wa upatikanaji wa
dawa, Wizara imekubaliana na Shirika la Maendeleo la Denmark
(DANIDA), kuanzisha Mfuko maalum wa dawa muhimu (Essential Medicine
Fund) ambao utaruhusu washirika wengine wa maendeleo kuweza kujiunga
na mfuko huo na kuwa na „Account‟ maalum ambayo itafunguliwa. Katika
mchakato huo Shirika la DANIDA limekubali kuchangia Shilingi za
Kitanzania bilioni mbili (bilioni 2) Katika kufanikisha azma hii Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inatakiwa kuchangia Shilingi milioni mia tano (500,
000,000). Fedha hizo ni kwa ajili ya dawa muhimu (100 items) ambazo
zinatumika kuanzia ngazi ya vituo vya afya hadi katika Hospitali za Wilaya,
vijiji na hospitali ya Mnazi Mmoja.
Mhe. Naibu Spika, utaratibu maalum wa kuzinunua dawa muhimu
„Framework contract‟ utatumika kutoka mfuko wa dawa. Tayari mtaalam
elekezi yupo nchini katika kusaidiana na wataalamu wetu ili kufanikisha azma
hii. Kwa upande wa dawa za ziada ambazo zinatumika zaidi Hospitali kubwa
za wilaya na Mnazi Mmoja hizi zitanunuliwa kwa kutumia bajeti ya Serikali
ya bilioni 1.5 ambazo ni kati ya bilioni 2.1 zilizotengwa kwa ajili ya ununuzi
wa dawa kwa bajeti ya mwaka 2013/14, pia utaratibu wa Framework
Contract utatumika.
Mhe. Naibu Spika, mbali na mafanikio niliyoyaeleza, Ofisi ya Mfamasia
Mkuu wa Serikali ilikabiliwa na changamoto zifuatazo katika utekelezaji wa
kazi zake zikiwemo:
33
a) Fedha za ununuzi wa dawa zinazotolewa na Serikali huwa hazitoshi na
upatikanaji wake huwa chini ya kiwango kilichopangwa kwenye bajeti
kwa wakati zinapotakiwa.
b) Kuwepo kwa ucheleweshaji wa dawa kutoka Bohari ya Dawa ya Dar es
Salaam (Medical Store Department). Kwa kipindi cha mwaka uliopita
2012/2013, dawa za miezi mitatu ambazo zilitakiwa zifike Januari 2013,
dawa hizo zilifika mwezi wa Mei 2013, na dawa zilizopatikana zilikuwa
ni asilimia 40 tu ya dawa zote zilizoagizwa, hivyo kufanya dawa nyingi
kukosekana katika vituo vya afya. Hili ni moja kati ya tatizo sugu kwa
uagizaji wa dawa za wizara yetu. Mfumo huu ndio uliotulazimisha
kutafuta mfumo mbadala niliouelekeza katika maelezo yaliyotangulia
hapo juu.
Mhe. Naibu Spika, Idara ya Mfamasia imeelezwa kwa ukamilifu kuanzia
kifungu 5.0 mpaka 5.0.8 vilivyo kwenye ukurasa wa 32 mpaka 35 wa hotuba.
BOHARI KUU YA DAWA
Mhe. Naibu Spika, katika kuhakikisha ubora na uimara wa huduma za
usambazaji dawa na vifaa tiba, Idara inaendelea kuimarisha mfumo wa
usambazaji kulingana na mahitaji (Pull System) kutoka vituo vya afya 19 hadi
kufikia 98 (Unguja 56 na Pemba 42) ambayo sawa na asilimia 71 ya vituo
vyote vya afya. Kupitia mfumo huu mahitaji halisi ya dawa na vifaa tiba
hubainishwa na kituo cha afya husika kwa mashirikiano na Timu ya Afya ya
Wilaya.
Mhe. Naibu Spika, mafunzo yanayolenga usimamizi mzuri wa dawa
yalitolewa kwa wasimamizi wa dawa kutoka Timu za Afya za Wilaya. Katika
mwaka wa fedha 2013/2014, Bohari Kuu ya Dawa inatarajia kuongeza idadi
ya vituo vya afya vinavyoagiza dawa kulingana na mahitaji (Pull System)
kutoka 98 hadi kufikia vituo vyote (144).
Mhe. Naibu Spika, Idara ya Bohari Kuu ya Dawa imeelezwa kwa ukamilifu
kuanzia kifungu 6.0 mpaka 6.0.4 vinavyopatikana kwenye ukurasa wa 35
mpaka 37 wa hotuba.
MKEMIA MKUU WA SERIKALI
Mhe. Naibu Spika, Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanya
uchunguzi wa vielelezo 405 vinavyotoka katika taasisi mbali mbali zikiwemo
Jeshi la Polisi, Vikosi vya SMZ na watu binafsi. Mbali ya uchunguzi wa
vielelezo, Ofisi ya Mkemia Mkuu imefanikiwa kufanya ununuzi wa kemikali
na vifaa vya maabara kwa ajili ya kazi za uchunguzi. Kiambatisho namba 13
34
kinatoa ufafanuzi wa idadi ya sampuli zilizochunguzwa na Idara ya Mkemia
Mkuu wa Serikali.
Mhe. Naibu Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013/2014 ili kufikia
kuwa na maabara ya kisasa na yenye vifaa vya uhakika na kupata ufanisi
mkubwa wa kufanikisha kazi zake ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali
imejipangia kuongeza ujuzi wa wafanyakazi wa maabara kwa kuwapatia
mafunzo ya ziada ya nadharia na vitendo, vile vile ofisi inategemea kuandaa
rasimu ya sheria ya kemikali pamoja na kuanzisha utafiti wa kisayansi ili
kudhibiti uharibifu wa mazingira unaohusiana na matumizi ya kemikali.
Mhe. Naibu Spika, Idara ya Mkemia Mkuu imeelezwa kwa ukamilifu kuanzia
kifungu 7.0 mpaka 7.0.3 ndani ukurasa wa 37 mpaka 38 wa hotuba yangu.
IDARA YA SERA, MIPANGO NA UTAFITI
Mhe. Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2012/2013, wizara imekuwa
ikiendelea na mchakato wa kuangalia njia mbadala za kugharamia huduma za
afya. Timu ya wataalamu kutoka taasisi za SMZ zimekuwa zikishirikiana kwa
pamoja katika mchakato huu, moja kati ya mapendekezo yaliyoridhiwa ni
kuendelea na taratibu za kuanzisha bima ya afya. Hatua zilizofikwa hadi sasa
tayari uchambuzi yakinifu umeshafanyika juu ya utayari wa wananchi
kuhusiana na bima ya afya na mafunzo kwa timu ya wataalamu yamefanyika
kwa msaada wa mtaalamu kutoka Shirika la Afya Duniani.
Mhe. Naibu Spika, mapitio ya Mpango Mkakati wa tatu wa Wizara
yamefanyika, mapitio haya yameenda sambamba na kufanya tathmini ya kina
(Situation Analysis and Response) ya utekelezaji wa mpango mkakati wa II
wa miaka mitano iliyopita (2006/07-2010/11). Katika kuimarisha utayarishaji
mipango kazi na upatikanaji wa ripoti kwa wakati na kwa urahisi, wizara
imeanzisha programu maalumu ya mtandao (Web Based Planning and
Reporting Tool).
Mhe. Naibu Spika, Idara ya Sera, Mipango na Utafiti imeelezwa kwa
ukamilifu kuanzia kifungu 8.0 mpaka 8.0.6 kwenye ukurasa wa 38 mpaka 41
wa hotuba.
IDARA YA UTUMISHI NA UENDESHAJI
Mhe. Naibu Spika, uhaba wa wafanyakazi hasa wenye fani za kitaalamu
umekuwa ni tatizo la muda mrefu kwa wizara. Napenda kueleza kwamba kwa
mwaka 2012/13, wizara iliidhinishiwa nafasi mpya za ajira 816 hadi sasa ni
nafasi 366 tu ndizo zilizokwisha jazwa (asilimia 45). Hali hii pia
35
imechangiwa na kutokuwepo kwa wataalam wa afya wenye kiwango
kinachotakiwa waliomaliza na kuomba ajira.
Mhe. Naibu Spika, jumla ya wafanyakazi 101 wameweza kustaafishwa
kutokana na kufikia umri wa kustaafu (Unguja 62 na Pemba 39), na
wafanyakazi 28 walifariki dunia. Aidha wizara imefanikiwa kuziomba na
kupewa kibali cha kuzijaza nafasi hizo, na hatua za kuajiri wafanyakazi
wengine zinaendelea. Sambamba na hilo wizara imeimarisha mfumo wa
takwimu za rasilimali watu (HRIS), mfumo ambao umeiwezesha wizara
kupitia kamati ya mgawanyo wa wafanyakazi kuweza kuweka uwiano wa
wafanyakazi katika ngazi zote za huduma.
Mhe. Naibu Spika, wizara imeandaa mapendekezo ya rasimu ya maposho ya
kufanya kazi katika mazingira hatarishi na maposho ya dhamana kwa
wafanyakazi wanaostahiki kupatiwa maposho hayo na rasimu hizo
zimeshawasilishwa Wizara ya Utumishi na Utawala Bora kwa hatua za
utekelezaji.
Mhe. Naibu Spika, kupitia Idara hii mpango mkuu wa mafunzo kwa
wafanyakazi utakaokuwa ni kiongozi katika kupeleka wafanyakazi
masomoni umekamilika. Pia Idara imefanikiwa kupeleka masomoni
wafanyakazi na wanafunzi katika vyuo mbali mbali kwa mafunzo ya muda
mrefu na muda mfupi, ndani na nje ya nchi ambapo jumla ya wafanyakazi
226 kati yao 115 wanawake na 111 wanaume wamepatiwa mafunzo ya
muda mrefu. Wafanyakazi 14 walipatiwa mafunzo ya muda mfupi. Aidha
Jumla ya Wafanyakazi 82 wamerudi masomoni wakiwemo madaktari
bingwa wa fani ya moyo, upasuaji na usingizi.
Mhe. Naibu Spika, utekelezaji wa Idara ya Utumishi na Uendeshaji
umeelezwa kwa ukamilifu kuanzia kifungu 9.0 mpaka 9.2.5 kwenye ukurasa
wa 41 mpaka 44 wa hotuba yangu.
TAASISI MAALUM ZA WIZARA YA AFYA
CHUO CHA TAALUMA ZA SAYANSI ZA AFYA
Mhe. Naibu Spika, Chuo hiki kina jumla ya wanafunzi 588 wa kada mbali
mbali ambao wanaendelea na masomo, kati ya hao wanaume ni 315 na
wanawake ni 273. Aidha wanafunzi 408 (wanawake 242 na wanaume 166)
wanatarajiwa kumaliza masomo yao ifikapo Juni 2013. Katika juhudi za
kukuza viwango vya elimu inayotolewa, chuo kimeweza kupitia mitaala
miwili ya fani za Afisa Tabibu na Afisa Afya ya Jamii na Mazingira. Sanjari
36
na hilo walimu 11 wamepelekwa masomoni ili kukidhi mahitaji ya elimu
inayotolewa.
Mhe. Naibu Spika, maelezo zaidi juu ya taaluma ya sayansi ya
afya yanapatikana kifungu kumi moja mpaka kumi
moja tano.
Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi
Mhe. Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2012/2013 bodi ilifanya ukaguzi
katika hospitali na vituo vya afya 68, kati ya hivyo, vituo vya afya 10
vilisimamishwa kutoa huduma kutokana na uchakavu wa majengo, madaktari
dhamana kutokwenda kikawaida vituoni huko na uhaba wa wafanyakazi
wenye sifa, vituo hivyo vilivyozuiliwa ni Hundi Clinic, Almanac Dispensary,
Mahonda Medical Centre, Mwembemakumbi Dispensary, Huduma
Dispensary, Salama M. Centre,Maryam Clinic, Bububu Dispensary, Kiponda
Medical Clinic na Magogoni Dispensary yaani Huruma, kati ya hizo hospitali
tisa ziliruhusiwa kuendelea kutoa huduma baada ya kurekebisha mapungufu
yaliobainika na kuridhiwa na Bodi.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha uliopita Bodi iliweza kutekeleza
majukumu yake ya kusimamia ubora na usalama wa chakula
a) Kuendelea kufanya mikutano ya pamoja na wamiliki wa
hospitali binafsi ili kuimarisha huduma zinazotolewa na
hospital hizo;
b) Kufanya marekebisho ya sheria na miongozo ya kuendesha
hospitali binafsi;
c) Kuendelea kufanya ukaguzi katika Hospitali na vituo vya afya
binafsi.
Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi
Mhe.Naibu Spika, Bodi imefanya ukaguzi wa maduka 637 ya chakula ya
jumla na rejareja, kati ya 600 yaliyopangwa, maghala saba ya kuhifadhia
chakula, hoteli 129, mikahawa 67, viwanda sita vya chakula, supermarket 6
maduka ya kuuzia nyama 146, maduka 84 ya dawa na 21 ya vipodozi, ghala
moja la kuhifadhia dawa, machinjio tisa, mazao ya baharini kilogram 15.5 na
jumla ya lita 136,243 za maziwa ya ng‟ombe, katika ukaguzi huo, hatua
zilichukuliwa katika kuondoa matatizo yaliyogundulika
37
Mhe. Naibu Spika, Maabara ya Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi
ilichunguza jumla ya sampuli 1,045 za Chakula, kati ya sampuli hizo, 1,035
zilikua salama na Sampuli 10 hazikufaa kwa matumizi ya binadamu. Aidha,
Sampuli 25 za dawa zilichunguzwa, Sampuli 16 zilipasi na sampuli tisa
zilifeli. Sampuli 31 za dawa za mitishamba ambazo zote zilionekana zinafaa
kwa matumizi ya binaadamu pia zilichunguzwa.
Mhe. Naibu Spika, hatua mbali mbali zilichukuliwa kwa waliobainika na
kasoro baada ya ukaguzi huo uliofanyika ikiwemo kupewa maelekezo ya kuja
kusajili biashara zao, kupewa muda wa kuweka bidhaa katika mpangilio
mzuri ndani ya maduka, kuhamasisha wafanyakazi kuchunguza afya zao
kutenganisha bidhaa za chakula na vipodozi.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2013/2014 Bodi imeanzisha rasmi
ofisi inayoshughulikia Mfumo wa Utoaji wa Huduma Bora (Quality
Management System). Aidha, Bodi imedhamiria kufuata na kutekeleza
miongozo ya kimataifa ya utoaji wa huduma bora kama ilivyoainishwa
kwenye “IS0 900I:2008 na Muongozo wa Huduma kwa wateja (ZFDB
Service Client Charter).
Mhe. Naibu Spika, pamoja na mafanikio hayo lakini Bodi bado inakabiliwa
na changamoto ya kuwepo kwa bandari na njia zisizo rasmi, jambo ambalo
linapelekea kuingizwa kwa bidhaa nchini zilizo chini ya kiwango. Naomba
mamlaka husika na serikali kwa ujumla kulitatua suala hili kwa manufaa ya
wananchi. Kutokana na tabia ya baadhi ya wafanya biashara kuleta bidhaa
zenye kiwango pungufu, bodi imeagizwa kupitia upya sheria ya bodi na
kuleta marekebisho ya mabadiliko yake katika Baraza lako kabla ya
kumalizika kikao hiki cha bajeti.
Mhe. Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2013/2014, Bodi imejipangia
kutekeleza kazi kuu zifuatazo:-
a) Kuendelea kushiriki kikamilifu katika Mpango wa Uwiano wa
Usajili wa Dawa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki;
b) Kujenga Ofisi mpya za Bodi katika eneo la Mombasa Zanzibar;
c) Kusimamia marekebisho ya Sheria ili kuifanya Bodi kuwa
Mamlaka kamili.
Baraza la Wauguzi
Mhe. Naibu Spika, jumla ya wauguzi na wauguzi wasaidizi 71 walisajiliwa
hadi kufikia mwezi Machi 2013 na kupewa leseni za utendaji kazi. Wauguzi
watano waliokwenda kinyume na maadili ya kiuguzi walichukuliwa hatua za
38
kinidhamu kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kutohudhuria kazini bila
ya kuwa na sababu maalum.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka 2012/13, Baraza limeifanyia marekebisho
sheria ya Baraza la Wauguzi na Wakunga ya mwaka 1986 baada ya kubainika
mapungufu katika sheria hiyo. Kwa sasa sheria imo katika mchakato wa
kujadiliwa katika vikao mbalimbali.
Mhe. Naibu Spika, katika kipindi cha mwaka 2013/2014 Baraza limejipangia
kutekeleza yafuatayo:-
a) Kutayarisha miongozo mbali mbali ya utoaji wa huduma za
uuguzi na ukunga;
b) Kukamilisha marekebisho ya sheria ya Baraza la Wauguzi na
Wakunga;
c) Kusaidia katika mchakato wa kuanzisha Jumuiya ya Wakunga
Zanzibar.
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala
Mhe. Naibu Spika, kazi zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 ni
usajili na ukaguzi wa maduka 30 ya dawa za tiba asili na mbadala Pia
waganga 153, kliniki 10, (nane kwa Unguja na mbili Pemba), wasaidizi
waganga 38 na vilinge 92 vilifanyiwa usajili.
Mhe. Naibu Spika, wizara imekuwa ikifanya ufuatiliaji wa karibu katika
kuona sekta hii haiendi kinyume na matakwa ya sheria. Hivyo waganga wa
jadi na ambao sio waganga na wale ambao hawakufuata sheria za uuzaji wa
dawa za asili walidhibitiwa kwa kushirikiana na askari polisi pamoja na
vyombo vya habari ili kubainisha taarifa zao. Hatua nyengine zilizochukuliwa
ni kuziteketeza dawa hizo na kudhibiti matangazo ambayo yapo kinyume na
taratibu za Baraza. Aidha, hatua pia zilichukuliwa kwa wale walioonekana
kuuza dawa katika sehemu za miskiti, barabarani na sehemu ambazo
hazikubaliki na baraza hivyo ukaguzi wa mara kwa mara ulifanyika.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2013/2014 kazi kuu zifuatazo
zitatekelezwa na Baraza.
a) Kuendelea kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa tiba asili na
utumiaji mbaya wa dawa za tiba asili na tiba mbadala kwa baadhi ya
waganga kupitia vyombo vya habari na vipeperushi;
b) Kujenga uhusiano mzuri kati ya madaktari wakisasa
(Biomedical Practitioners) na waganga wa asili (Traditional healers);
c) Kuendelea kusajili waganga wa tiba asili pamoja, maduka na
vituo vya afya vya tiba asili na mbadala;
39
d) kuendelea kufanya ukaguzi wa waganga wa tiba asili na
wauzaji wa dawa misikitini.
Maabara ya Afya ya Jamii – Pemba
Mhe. Naibu Spika, maabara ya Afya ya Jamii (P H L – I d C) ni Taasisi
inayohusika na kufanya tafiti pamoja na kufanya uchunguzi yakinifu wa
sampuli kutoka maabara mbali mbali za hapa nchini. Pia, maabara hii
huangalia nyendo za maradhi mbali mbali yanayoathiri afya ya jamii na
kubuni mbinu za kuyadhibiti. Katika mwaka 2012-13 maabara ilipokea
sampuli 156 (101 Unguja na 55 Pemba) za makohozi na kuzifanyia uhakiki.
Kati ya hizo sampuli 30 (23 kutoka Unguja na 7 Pemba) zilionekana
kuambukizwa na kifua kikuu.
Mhe. Naibu Spika, mafanikio mengine yaliyopatikana ni kuanza kufanya
kipimo cha kuotesha vidudu na kuangalia dawa mjarabu kwa vidudu (Culture
and Sensitivity) kwa sampuli za hospitali kama vile choo kikubwa, mkojo,
damu, CSF, HVS na nyenginezo.
Mhe. Naibu Spika, kwa upande wa hudumia za akinamama wajawazito na
watoto wachanga (Cord care and Pregnant Study), jumla ya watoto wachanga
23,202 wamepatiwa huduma stahiki. Vile vile jumla ya akina mama
wajawazito 2,064 walitambuliwa. Kati ya hao 1,767 wameshaorodheshwa
tayari kwa kupatiwa huduma zikiwemo kupima mapigo ya moyo (BP) na
mkojo mara tatu kabla ya kujifungua na mara mbili baada ya kujifungua.
Mhe. Naibu Spika, napenda kuliarifu baraza lako tukufu kuwa maabara hii pia
inasaidia kutoa mchango mkubwa katika kuwapatia ajira vijana wetu kwani
mbali ya kada muhimu zilizomo ndani ya maabara hii ambao ni wafanyakazi
waliomo ndani ya wizara ya afya maabara pia hutoa ajira za muda mfupi na
muda mrefu. hadi sasa jumla ya wafanyakazi tisini 90 wanafanya kazi katika
mabara hii. Halikadhalika zaidi ya wanawake 80 kutoka shehia zote za Pemba
wameshafanyiwa usaili.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka ujao wa fedha maabara itaendelea kufanya
utafiti kuhusiana na kichocho utakaohusiana na DNA, kuenedelea na utafiti
wa minyoo ikiwemo kupima ubora wa dawa mbali mbali zitakazoweza kuwa
bora zaidi kwa kutibu maradhi hayo.
MIRADI YA MAENDELEO
Mradi wa Kusaidia Kupunguza Vifo Vitokanavyo na Uzazi
40
Mhe. Naibu Spika, mafanikio yaliyopatikana kwa mradi huu kwa mwaka
2012/2013 ni pamoja na kukamilika kwa matengenezo ya Kituo cha Afya cha
Bogoa na kuanza matengenezo ya Kituo cha Afya Wesha.
Mheshimiwa Spika, mradi umewapatia mafunzo ya muda mfupi hapa nchini
wafanyakazi 95 juu ya “Community Participation in Health” na wafanyakazi
50 kwa mafunzo ya “Emerging Health Problems and Medical Procedures”.
Mafunzo haya yaliwashirikisha wafanyakazi kutoka vituo vya afya na
hospitali za vijiji.
Mhe. Naibu Spika, katika baraza lako la mwaka 2012/2013 wizara yangu
ilitoa taarifa ya maendeleo mazuri yanayoendelea kwenye ujenzi wa jengo la
wagonjwa wa Akili liliopo Hospitali ya Wete Pemba na kujenga matumaini
ya kukabidhiwa jengo baada ya miezi mitatu. Bahati nzuri wakati ujenzi
ukiendelea ilionekana kasoro ya kutokuwepo eneo la kutolea huduma za kazi
za “Occupational Therapy”, hali hii ilisababisha hatua za haraka kuchukuliwa
kwa kufanya marekebisho yanayostahiki. Kwa hivi sasa ujenzi unaendelea
na unatarajiwa kumalizika wakati wowote kuanzia hivi sasa.
Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 mradi utakamilisha
majukumu yafuatayo:-
a) Kufanya matengenezo makubwa ya jengo la huduma za uzazi
na watoto katika hospitali ya Wete pamoja na kulipatia vifaa na
samani;
b) Kulipatia vifaa na samani jengo la huduma za magonjwa ya
Akili Pemba baada ya ujenzi kukamilika;
c) Kujenga vituo vya afya na nyumba za wafanyakazi
Mzambarauni Pemba na Mwera Unguja pamoja na kuvipatia
vifaa;
d) Kufanya matengenezo ya vituo vya afya Wingwi na Tundaua;
e) Kugharamia mafunzo ya muda mfupi kwa wafanyakazi sita wa
mradi;
f) Kufanya tathmini ya mwisho na kufunga mradi.
Mradi Shirikishi wa Afya ya Uzazi na Mtoto
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/ 2013, mradi uliweza kufanya
utafiti mdogo juu ya upatikanaji wa huduma za dharura za uzazi (EmONC
assessment) katika vituo 79 Unguja na Pemba. Lengo ni kuziimarisha huduma
katika vituo vyote vya afya ili mama wajawazito waweze kuzifikia huduma
hizo kiurahisi. Utafiti huo utasaidia katika kuwa na mipango madhubuti yenye
muelekeo katika kuimarisha huduma za uzazi.
41
Mhe. Naibu Spika, jumla ya watoa huduma 80 Unguja na Pemba wamepatiwa
mafunzo ya utoaji wa huduma za uzazi wa mpangilio ya nadharia na vitendo,
jumla ya vipandikizi 2,752 vimenunuliwa na kusambazwa kwenye vituo na
hospitali kwa lengo la kurahisisha watendaji kuyatumia mafunzo hayo
kivitendo. Mafunzo mengine yaliyotolewa yalihusu namna ya kutoa huduma
za haraka kwa mtoto mchanga (Neonatal Resuscitation), kwa wafanyakazi 25
kwa kila wilaya. Mafunzo haya yalikwenda sambamba na ununuaji wa vifaa
(newborn resuscitation kits & suction machines) kwa ajili ya huduma hizo.
Mhe. Naibu Spika, mapitio ya mpango wa kuharakisha kupunguza vifo
vitokanavyo na uzazi na watoto (Road Map Review) ulifanyika. Ripoti ya
mapitio inaonesha kwamba kuna mafanikio na changamoto. Miongoni mwa
mafaniko yaliopatikana ni kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi kutoka
vifo 285 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2011 hadi kufikia vifo 221 kwa
kila vizazi hai 100,000 mwaka 2012.
Mhe. Naibu Spika, kwa upande wa changamoto zilizojitokeza katika mapitio
hayo imegundulika kwamba mkakati huu haukusambazwa ipasavyo hasa
katika ngazi za chini; ikiwemo ngazi ya wilaya, vituo vya afya na ngazi ya
jamii, na hata usimamizi wake haukufikia kiwango kilichokusudiwa ingawa
jitihada zilitumika kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa mzuri.
Mhe. Naibu Spika, Ujenzi wa Jengo la ofisi ya kitengo shirikishi unaendelea
kwa kasi, na linatarajiwa kumalizika mwanzoni mwa mwaka wa fedha
2013/2014. Jengo hili linategemewa kufunguliwa Rasmi wakati wa
maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Aidha, gari mbili za
kubebea wagonjwa (Ambulances) zilinunuliwa kwa ajili ya hospitali ya Wete
na Makunduchi.
Mhe. Naibu Spika, mafunzo ya matibabu ya magonjwa ya watoto kwa njia ya
uwiano “Integrated Management of Childhood Ilnesses (IMCI)” kwa njia ya
elimu masafa kwa wahudumu kumi na tisa kutoka vituo mbali mbali vya
Unguja na Pemba yametolewa. Ufuatiliaji baada ya mafunzo hayo ulifanyika
katika vituo 17 kwa Unguja na 11 kwa Pemba. Vile vile mafunzo ya IMCI
kwa njia ya elimu masafa (e- Learning) yalitolewa kwa walimu (Training Of
Trainers) 15 wa Chuo cha Sayansi za Afya pia mafunzo msasa ya IMCI
yalitolewa kwa watendaji 33 kutoka wilaya ya kati.
Mhe. Naibu Spika, hadi kufikia sasa jumla ya vituo 137 vinatoa huduma za
kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kati ya
hivyo, vituo 64 vipo Pemba na 73 Unguja. Katika mwaka 2012, akina mama
wajawazito 46,221 walipatiwa ushauri nasaha na kupimwa afya zao. Kati ya
hao kina mama 281 sawa na asilimia 0.6 waligunduliwa kuwa na
42
maambukizo ya VVU. Halikadhalika kati ya watoto 148 waliochunguzwa
watoto saba waligunduliwa na maambukizo ya VVU sawa na asilimia 4.7%.
Huduma za Chanjo
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka 2012/2013 kiwango cha chanjo kitaifa
kimeshuka kutoka asilimia 96 ya mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 90 ya
mwaka 2012. Kupungua kwa kiwango hiki kitaifa kumechangiwa sana na
kushuka kwa kiwango cha chanjo katika Wilaya za Mkoani, Chake Chake,
Micheweni, Kaskazini “A‟ na Kaskazini “B”, wilaya ambazo zilichanja chini
ya asilimia 80. Pia ufinyu wa fedha za kuendeshea kazi za chanjo, ufuatiliaji
mdogo wa kazi za chanjo na matatizo ya upatikanaji wa umeme (TUKUZA)
kwa vituo vya Afya vya Pemba ni sehemu ya changamoto iliyoshusha chanjo.
Ufafanuzi unaonekana katika kiambatanisho namba 15.
Mhe. Naibu Spika, napenda kuliarifu Baraza lako tukufu kwamba, katika
kukabiliana na maradhi yanayozuilika kwa chanjo, wizara imefanikiwa
kuanzisha chanjo mbili mpya za “Rotavirus” ambayo inakinga maradhi ya
kuharisha na „Pneumococcal‟ yenye kukinga maradhi ya homa ya kichomi na
ya uti wa mgongo. Hivyo katika kufanikisha utowaji wa chanjo hizo, jamii
pamoja na watoa huduma wa afya walihamasishwa ili kuzielewa na hatimae
kuzikubali chanjo hizo.
Mhe. Naibu Spika, katika kuhakikisha kuwepo kwa uhifadhi mzuri wa chanjo
unaokubalika, wizara imeanza kufanya matayarisho ya ujenzi wa chumba cha
mtambo wa baridi huko Pemba. Mchoro na ramani ya ujenzi huo tayari
imeshaandaliwa, zabuni imeshatangazwa, kutathiminiwa na mkandarasi
ameshachaguliwa. Ujenzi huu utagharamiwa kwa mashirikiano baina ya
Serikali na Shirika la kimataifa la kuhudumia watoto (UNICEF).
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2013/2014 mradi huu unalenga
kutekeleza kazi kuu zifuatazo:
a) Kufanya uhamasishaji na kujenga uwezo juu ya huduma za uzazi,
maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa mama wajawazito, uzazi wa
mpangilio na huduma rafiki kwa vijana Unguja na Pemba;
b) Kuimarisha mfumo wa mawasiliano wa huduma za afya ya uzazi kwa
kina mama wajawazito na watendaji wa afya kwavituo vyote vya afya;
c) Kufanya mafunzo kwa wahudumu wa afya juu ya huduma za afya ya
uzazi na mtoto ikiwa ni pamoja na huduma za uzazi za dharura (EmOC)
na huduma za chanjo;
43
d) Kununua dawa za uzazi wa mpangilio pamoja na ununuzi wa chanjo na
vifaa vyake. Kutoa chanjo ya pepopunda katika skuli za Sekondari
Unguja na Pemba;
e) Kufanya tafiti zinazohusiana na masuala ya chanjo (Operational
research);
f) Kufanya Uhakiki wa takwimu za chanjo (DQS);
g) Kukamilisha kuchapisha na kusambaza muongozo wa utoaji huduma za
chajo kwa wachanjaji;
h) Kuanzisha dozi ya pili ya chanjo ya surua (measles second dose) na
kutoa chanjo nyengine za kawaida.
i) Kutoa mafunzo juu ya Matibabu ya Watoto wachanga na maradhi ya
kuharisha kwa watoa huduma za watoto kwa Pemba.
j) Kuanzisha mikakati ya kuondoa kabisa maambukizi ya VVU kwenda
kwa mtoto.
Mradi Shirikishi wa Ukimwi, Kifua Kikuu na Ukoma
Mhe. Naibu Spika, Mradi Shirikishi wa UKIMWI, Kifua Kikuu na Ukoma ni
muunganisho wa miradi miwili yote yenye lengo la kusimamia, kuratibu na
kutoa huduma za tiba na kinga dhidi ya maambukizo ya UKIMWI, kifua
kikuu na Ukoma.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, wizara ilifanya utafiti
wa kutathmini mwenendo wa maambukizo ya VVU kwa makundi matatu
hatarishi; wanaume wanaojamiiana (MSM), wanawake wanaofanya biashara
ya ngono (FSW) na watumiaji wa dawa za kulevya kwa kujidunga sindano
(IDUs) pamoja na kujua idadi yao kwa kila kundi (size estimation). Matokeo
ya awali ukilinganisha na mwaka 2007 yanaonyesha kwamba hali ya
maambukizo ya VVU kwa wanaume wanaojamiiana yamepungua kutoka
asilimia 12.3 (2007) hadi asilimia 2.6 (2012), wanaojidunga sindano za
madawa ya kulevya yamepungua kutoka asilimia16 (2007) hadi asilimia 11.3
(2012). Aidha, wanawake wanaofanya biashara ya ngono maambukizi
yameonekana kupanda kutoka 10.8 (2007) hadi asilimia 19.3 (2012).
Mhe. Naibu Spika, katika kufikia lengo la kuwapatia dawa za kupunguza
makali ya VVU (ARV) bila malipo kwa watu wanaoishi na VVU, hadi kufikia
Machi 2013 jumla ya watu 6,906 wanaoishi na VVU walikuwa tayari
wameshasajiliwa kwenye kliniki 10 (6 Unguja na 4 Pemba), miongoni mwao,
watu 4,090 (59.2%) wanatumia dawa za ARVs, kati yao watoto ni
392(9.6%).
Mhe. Naibu Spika, ili kuimarisha huduma za tiba katika maabara zinazotoa
huduma za uchunguzi wa UKIMWI, mradi ulipokea mashine tatu mpya za
44
CD4 ambazo zimepelekwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Mwembeladu
na Kivunge. Aidha mashine aina mbili za “Haematology na Chemistry”
zilipokelewa na kupelekwa katika hospitali za Micheweni, Makunduchi na
Mwembeladu.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/13, mradi huu ulifanya
ufuatiliaji na kubaini kasoro mbali mbali za kiutendaji katika baadhi ya
hospitali zinazotoa huduma ya tiba ya UKIMWI. Hali hiyo ilipelekea mradi
kufanya mafunzo maalum ya vitendo ya siku mbili yaliyohusu Ushauri juu ya
ufuasi wa dawa na Ujazwaji wa Madaftari na ripoti za robo mwaka. Kliniki
ambazo watendaji wake walipata mafunzo haya ni Al – Rahma, Kivunge,
Makunduchi kwa Unguja, na Micheweni na Mkoani kwa Pemba.
Mhe. Naibu Spika, moja ya lengo la mradi huu kwa mwaka wa fedha
2012/2013 ilikuwa ni kuanzisha huduma ya chanjo ya kujikinga na
maambukizi ya homa ya ini aina ya “B” (Hepatitis B Vaccine) kwa watu
wanaoishi na VVU. Azma hii imeanza kutekelezwa kwa kutoa chanjo hiyo
kwa kundi la wanaotumia madawa ya kulevya kwa njia ya kujidunga sindano
na wale walioko katika utafiti wa maradhi hayo katika kliniki ya Mnazi
Mmoja.
Mhe. Naibu Spika, chanjo hizo zimetolewa katika nyumba sita (6) kati ya
saba (7) maalum za kurekebisha tabia (sober houses) zilizopo Unguja.
Takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya watu 233 waliopimwa katika nyumba
hizo 221 (95%) hawakugundulika na virusi vya homa ya ini “B”na hivyo
wanastahiki kupatiwa chanjo ya homa hiyo, miongoni mwao watu 59 (27%)
walipata angalau dozi moja, 40 (18%) walikamilisha dozi mbili na watu 30
(14%) tu ndio walioweza kukamilisha dozi tatu za chanjo hiyo. Hii ni
kutokana na ugumu uliojitokeza wa kuwafikia watu hao.
Mhe. Naibu Spika, kwa wale wanaofanyiwa utafiti katika kliniki ya huduma
na Tiba ya UKIMWI katika hospitali ya Mnazi Mmoja, jumla ya wagonjwa
1,571 wameshaorodheshwa katika utafiti huo. Kati yao watu 558
wameshapata chanjo ya kujikinga na ugonjwa huo na 56 ambao
wamegunduliwa na ugonjwa wa homa ya Ini B walianzishiwa dawa.
Mhe. Naibu Spika, moja ya mkakati wa kupambana na maradhi haya thakili
ni kuhimiza utumiaji wa mipira ya baba wakati wa kujamiiana. Katika
kuhakikisha kuwa wahitaji wanapata mipira hiyo bila malipo, mradi
umesambaza jumla ya mipira ya baba 34,700 katika vituo vya Afya,
waelimishaji rika, hotelini, majumba ya starehe pamoja na jumuiya zisizo za
Serikali (NGOs).
45
Mhe. Naibu Spika, kwa upande wa huduma za Kifua Kikuu, jumla ya watu
280 waligunduliwa kuwa na maradhi hayo, kati yao 243 (86.8%) walitibiwa
na kupona. Wanaume 172 (61.43%) na Wanawake 108 (38.57%). Vile vile
huduma za ufuatiliaji majumbani zilifanyika kwa wagonjwa 18. Aidha watu
169 ambao ni jamaa wa wagonjwa hao pia walipatiwa elimu juu ya namna ya
kujikinga. Katika nyumba hizo 18 kumepatikana watoto 21 ambao
wameanzishwa dawa za kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa
kipindi cha miezi sita. Pia wakati wa zoezi hili vipeperushi 367 vimegawiwa
kwa watu waliopatiwa elimu.
Mhe. Naibu Spika, kwa upande wa huduma za maradhi ya ukoma jumla ya
watu 97 waligundulika na maradhi haya (wanawake 32 na wanaume 65), kati
yao wagonjwa sita walikuwa na ulemavu grade 2. Aidha, ununuzi wa vifaa
vya kutengenezea miguu bandia na kiatu chake ulifanyika kwa walioathirika
na Ukoma. Aidha jumla ya watu 169 ambao ni jamaa wa wagonjwa
walipatiwa elimu ya afya juu ya maradhi hayo.
Mhe. Naibu Spika, mkakati mwengine unaotumika katika kupambana dhidi
ya maradhi haya ni kuelimisha jamii namna ya magonjwa haya
yanavyoambukizika na njia za kujikinga. Kwa mwaka 2012/13, jumla ya
vipeperushi 32,531 vimechapishwa kwa ajili ya kuelimisha jamii, kati ya
hivyo, 10,000 – vinalenga katika kushajiisha jamii juu ya umuhimu wa
kupima kabla ya ndoa na vipeperushi 20,000 vinahusu Huduma ya ushauri
nasaha na upimaji kwa wagonjwa wanaofika vituo vya afya na hospitali na
vipeperushi 2,531 vilihusu kujinga na maradhi ya kifua kikuu na ukoma. Pia
vipindi saba vya Televisheni na redio vilirushwa heweani.
Mhe. Naibu Spika, licha ya juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Wizara ya
Afya, bado suala la UKIMWI ni tatizo, hivyo juhudi makhsusi za pamoja
zinahitajika katika kupambana na maradhi haya thakili. Mkazo zaidi
unatakiwa katika kuondosha unyanyapaa kwa wanaoishi na VVU/UKIMWI,
kupiga vita imani potofu juu ya mipira ya baba au mama (kondomu),
kuongezeka kwa waganga wanaowashawishi wagonjwa kutumia dawa za
kienyeji badala ya ARVs na changamoto za kutoa huduma za tiba kwa
makundi maalum.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2013/14 mradi huu umeazimia
kutekeleza kazi kuu zifuatazo:
a) Kuendelea kuimarisha tiba na ushauri kwa kuwapatia dawa za kupunguza
makali ya VVU (ARV) kwa watu wanaoishi na VVU bila malipo kwa
wananchi wote wanaostahiki kutoka asilimia 60% mwaka 2013 kufikia
asilimia 65 mwaka 2014;
46
b) Kuimarisha na kuongeza huduma za ushauri nasaha na upimaji kutoka
vituo 87 mwaka 2013 kufikia 100 mwaka 2014 na kuhakikisha nyenzo
na vifaa vinapatikana kwa wakati;
c) Kuendelea kuimarisha tiba na ushauri kwa kuwapatia dawa za
kupunguza makali ya VVU (ARV) kwa watu wanaoishi na VVU bila
malipo kwa wananchi wote wanaostahiki kutoka asilimia asilimia 60%
2013 kufikia asilimia 65% mwaka 2014;
d) Kuendelea kutoa taaluma zaidi ya maradhi ya UKIMWI kwa watendaji
wa afya wa Unguja na Pemba katika sehemu zao za kazi (mentor
couching) kuhusiana na tiba kwa kutumia dawa za ARV, uzuiaji wa
maambukizo ya mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) na ushauri nasaha wa
kujikubalisha matumizi ya dawa (adherence counseling) na kuwahudumia
makundi maalum;
e) Kupanua huduma na tiba kwa makundi maalum ili kuwapatia huduma za
karibu na bora makundi hatarishi ya kuambukizwa na VVU;
f) Kuendelea kushirikiana na Idara ya madawa ya Kulevya na kurekebisha
tabia kuanzisha utoaji wa huduma na tiba na kuwapatia dawa kwa
watumiaji 200 wa madawa ya kulevya;
g) Kutekeleza mpango wa tiba kama kinga kwa baadhi ya makundi ya watu
watakaogundulika na VVU (watu wa makundi maalum, mama wajawazito,
watakaogundulika ya kuwa na VVU na homa ya ini pamoja na wenza);
h) Kufanya ukaguzi wa huduma za ushauri na upimaji wa VVU na kwa kwa
huduma za wagonjwa wanaolazwa na wanaotibiwa katika hospitali ( PITC na
VCT).
Mradi wa Kuipandisha Hadhi Hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa ya Rufaa
Mhe. Naibu Spika, mradi huu unalenga katika kuipandisha hadhi hospitali hii
kuwa ya Rufaa kwa Zanzibar, ambapo itatoa huduma za rufaa zitakazo
kwenda sambamba na mpango mkakati wa hospitali hii. Huduma hizo ni
pamoja na kuongeza miundo mbinu, wataalamu (specialist) na huduma za
kitalaamu kama vile upasuaji wa moyo (cardioverscular surgery), upasuaji
wa maradhi ya mgongo na ubongo (neurosurgical services), na huduma za
maradhi ya figo (Dialysis).
Mhe. Naibu Spika, katika mwaka wa bajeti 2012/13, wizara iliazimia kuanza
matayarisho ya zabuni kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi wa kuipanua
hospitali hii kwa mashirikiano na Uholanzi. Napenda kuliarifu Baraza lako
tukufu kuwa siku ya tarehe 18/2/2013 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na
Serikali ya Uholanzi ziliwekeana saini mkataba wa makubaliano wa kuanza
kuutekeleza mpango kazi wa mradi huo. Aidha hatua za awali za matayarisho
ya utekelezaji wa mpango mkakati huo umeshaanza.
47
Mhe. Naibu Spika, miongoni mwa mambo muhimu yaliomo katika mradi huu
ni ujenzi wa kliniki za maradhi maalumu zitakazo endeshwa na madaktari
bingwa, wodi ya kina mama ya kujifungulia na baada ya kujifungua na
chumba cha huduma za dharura (Emergency Units/casuality). Eneo
lilotengwa kwa ajili ya ujenzi huu ni katika majengo ya zamani ya kiwanda
cha dawa. Sambamba na hilo ukarabati wa jengo la Mapinduzi mpya
unaendelea na uko katika hatua za mwisho.
Mhe. Naibu Spika, uchache wa upatikanaji wa fedha za maendeleo umeathiri
zaidi utekelezaji wa shughuli za mradi huo, ambapo hadi sasa idara
imeshindwa kununua tanuri la kuchomea takataka kifaa ambacho ni muhimu
sana katika kufanikisha usafi na ubora wa huduma. Hata hivyo, wizara
imepata fedha kutoka mfuko wa msamaha wa madeni wa Kimataifa (MDRI)
fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya ununuzi wa tanuri la kuchomea taka
(incinarator), mobile X-ray,na vifaa vya uchunguzi wa saratani. Zabuni kwa
ajili ya ununuzi huo imeshatangazwa.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2013/2014, mradi huu umejipangia
kutekeleza kazi kuu zifuatazo:-
a) Kutekeleza mradi wa ORIO;
b) Kujenga jengo litakalotoa huduma za maradhi ya figo (Dialysis);
c) Kujenga jengo la wodi ya watoto;
d) Kujenga jengo litakalotoa huduma za upasuaji wa maradhi ya mgongo na
ubongo (neurosurgical services) ambalo litajumuisha chumba cha upasuaji
(theatre), chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), klinik pamoja na wodi;
e) Kuendelea kuwapatia wafanyakazi mafunzo ya matibabu kwa huduma
mpya zinazotaka kuanzishwa kama vile kansa na mafigo (Dialysis);
f) Kufanya matengenezo ya miundo mbinu na ununuzi wa vifaa tiba.
Mradi wa Kudhibiti Malaria Zanzibar
Mhe. Naibu Spika, mradi huu unalenga katika kutoa huduma za kinga na tiba
dhidi ya ugonjwa wa malaria. Juhudi mbali mbali zinazotumika katika
kutokomeza ugonjwa huu ni pamoja na kuanzisha kampeni ya Maliza Malaria
Zanzibar ambayo imepelekea mafanikio makubwa katika nchi yetu.
Mhe. Naibu Spika, kazi za ufuatiliaji na ukaguzi zilifanyika katika vituo vya
afya 142 Unguja na Pemba kati ya 202 vilivyopangwa kukaguliwa,
(vikiwemo vya serikali na binafsi) kwa lengo la ukaguzi huu ni kuangalia
zaidi namna ya uchunguzi na matibabu ya malaria yanavyotolewa kwa
kuzingatia miongozo iliyokubalika.
48
Mhe. Naibu Spika, napenda kuliarifu baraza lako tukufu kuwa katika kipindi
cha Julai 2012 hadi Machi 2013, hali ya upatikanaji wa dawa za malaria kwa
wagonjwa waliogundulika kuwa na malaria ulikuwa ni mzuri na hakukuwa na
upungufu wa dawa hizo. Wagonjwa wengi waliopatiwa huduma hiyo
waliweza kutumia dawa hizo bila ya kuwaletea madhara ya aina yoyote
isipokuwa wagonjwa 17 tu waliripotiwa kupata matatizo madogo madogo
kama vile matatizo ya ngozi, kuhara na kutapika, matatizo ambayo hayakuwa
na uhusiano na dawa za malaria.
Mhe. Naibu Spika, upigaji wa dawa ya majumbani kwa maeneo maalum ya
wilaya za Magharibi, Kati, Kusini, Chake Chake, Wete, Mkoani na
Micheweni, ambayo yalibainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa
malaria. Katika zoezi hili jumla ya nyumba 28,463 zilipangiwa kupigwa
dawa, kati ya hizo nyumba 26,900 sawa na asilimia 94.5 zilifanikiwa kupigwa
dawa. Haya ni mafanikio makubwa ya zoezi hili, ambapo Shirika la Afya
duniani linasisisitiza angalau asilimia 80 ya nyumba zote ziwe zimepigwa
dawa.
Mhe.Naibu Spika, katika kuangalia uimara wa dawa za majumbani dhidi ya
mbu wanaoambukiza malaria, aina tano za dawa za majumbani zilifanyiwa
uchunguzi, ili kubaini uwezo wake wa kuuwa mbu wa malaria. Dawa
zenyewe ni Bendiocarb, permethrine, deltamethrine, DDT, na labda
cyhalothrine. Aidha dawa aina ya Bendiocarb, pyrethroids na DDT
zimeonesha kuwa na nguvu kubwa kabisa ya kuangamiza mbu wa malaria,
hata hivyo tahadhari zinahitajika ili kuweza kulinda nguvu ya dawa hizo.
Dawa za permethrine na deltamethrine zilionesha kuwa na nguvu ndogo ya
kuuwa mbu wa malaria. Kwa sasa dawa inayoendelea kutumiwa ni aina ya
Bendiocarb.
Mhe. Naibu Spika, shughuli za uchunguzi wa malaria ziliendelea kama
kawaida ambapo jumla ya watu 71,584 walichunguzwa damu kwa njia ya
darubini miongoni mwao, 213 sawa na asilimia 0.31 waligunduliwa kuwa na
vimelea vya malaria. Kwa upande wa uchunguzi kwa njia ya haraka (mRDT),
jumla ya wagonjwa 72,591 walichunguzwa malaria kwenye vituo tofauti
Unguja na Pemba, kati ya hao wagonjwa 321 (0.44%) waligundulika kuwa na
vimelea vya maradhi hayo.
Mhe. Naibu Spika, mfumo wa ukusanyaji wa taarifa za malaria, kupitia simu
za mkononi umesaidia kuweza kuwafuata wagonjwa wa malaria katika
sehemu wanazoishi mara tu taarifa hizo zinapofika sehemu husika. Kwa
kipindi cha bajeti hii jumla ya wagonjwa 370 waliripotiwa. Ufuatiliaji
ulibainisha kuwa asilimia 38 walikuwa na kumbukumbu za kusafiri nje ya
Zanzibar katika kipindi cha mwezi uliopita. Hali hii inaonesha kuwepo
49
umuhimu wa kuwachunguza wageni wanaoingia Zanzibar kupitia baharini na
angani. Ufuatiliaji pia ulifanyika kwa familia zilizoripotiwa kuwa na
wagonjwa, hivyo watu 1,385 walichunguzwa, kati yao 69 walionekana kuwa
na vimelea sawa na asilimia tano na kupatiwa tiba sahihi kwa wakati.
Mhe. Naibu Spika, kazi za kufuatilia mwenendo wa mbu waenezao ugonjwa
wa malaria katika maeneo teule (sentinel sites) Unguja na Pemba ilifanyika.
Kwa upande wa Unguja maeneo yaliyo husika ni Mwera Chaani Bumbwini
na Malindi. Kwa Pemba ni Bopwe, Vitongoji Uwandani na Tumbe.
Mhe. Naibu Spika, matokeo kwa ujumla yanaonesha kuwa idadi ya mbu wa
malaria wamepungua ukilinganisha na miaka ya nyuma kabla ya upigaji dawa
wa majumbani na ugawaji vyandarua. Hata hivyo tabia ya mbu inaonekana
kubadilika ambapo inakisiwa asilimia 70 ya mbu hao wanauma nje usiku wa
mapema kuanzia saa moja mpaka saa tano, kipindi ambacho wananchi wengi
wanakuwa nje wakiongea au kujipumzisha, Kutokana na changamoto hii njia
za ziada za kumaliza malaria zinahitajika zikiwemo za kuangamiza viluilui
katika maeneo yenye madimbwi na mabonde ya maji.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka 2013/2014, mradi umejipangia kutekeleza
kazi kuu zituatazo:-
a) Kuchunguza uimara wa dawa za safu ya kwanza ya kutibu
malaria (dawa za mchanganyiko);
b) Kuendelea kufuatilia mwenendo wa maradhi ya malaria kwa
kufanya tafiti zitakazojitokeza ambazo zitakazopelekea kuleta maamuzi
yatakayosaidia kuendeleza mbele kampeni ya maliza malaria Zanzibar;
c) Ugawaji wa vyandarua katika mpango endelevu;
d) Kuangalia uimara wa viuwatilifu (Chemicals) dhidi ya mbu
wanaoneza malaria.
Mradi wa Ujenzi wa Bohari Kuu ya Dawa
Mhe. Naibu Spika, mradi wa Ujenzi wa Bohari Kuu ya Dawa una lengo la
kuwa na ghala kubwa na la kisasa ambalo litakuwa na uwezo mkubwa wa
kuhifadhi dawa kwa ajili ya hospitali na vituo vya afya Unguja na Pemba.
Mhe. Naibu Spika, kama nilivyoeleza katika hotuba ya mwaka wa fedha
2012/2013 kuwa wizara ilikuwa inajenga jengo kwa ajili ya Bohari kuu ya
Dawa. Napenda kuliarifu Baraza lako tukufu kwamba jengo hilo limemalizika
na kufunguliwa rasmi na Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein siku ya tarehe 6/01/2013. Kupatikana kwa
ghala hii kumewezesha uhifadhi wa dawa na vifaa tiba kuwa ni wa uhakika na
50
salama, kwani ghala hili limewekewa mitambo maalum wa kutambua
ubadhirifu wowote ambao unaweza kutokea.
Mhe. Naibu Spika, mambo mengine yaliyofanywa katika kuimarisha ghala hii
ni pamoja na ununuzi wa samani za ofisi, kompyuta, folk-lift pamoja na
jenereta kubwa na jipya la kusambazia umeme wakati wa dharura. Sambamba
na hilo, ujenzi wa kantini kwa huduma za vyakula utakamilika wakati wowote
kuanzia hivi sasa.
Mhe. Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2013/2014 mradi umejipangia
kutekeleza kazi kuu zifuatazo:-
a) Kujenga Bohari Kuu ya Dawa Pemba;
b) Kununua gari kwa ajili ya usambazaji wa dawa na ukaguzi;
c) Kuongezwa kwa folk-lift, kwani mpaka sasa ipo moja tu.
Mradi wa Kustawisha Siha za Wazanzibari
Mhe. Naibu Spika, mradi huu unalenga kuhamasisha jamii juu ya masuala
yanayohusu afya ili waweze kujikinga na maradhi yakiwemo ya kuambukiza
na yasiyo ya kuambukiza pamoja na mambo hatarishi.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, jumla ya vipindi 81
vimetangazwa kupitia redio na televisheni vyenye nia ya kuhamasisha jamii
katika masuala mbali ya afya ikiwemo uchangiaji wa damu kwa hiari,
umuhimu wa matone ya Vitamin A kwa watoto chini ya umri wa miaka
mitano, matumizi ya chumvi yenye madini joto, uanzishwaji wa chanjo mpya
ya kuzuia maradhi ya kuharisha na chanjo ya kukinga maradhi ya uti wa
mgongo na namna ya kujikinga na maradhi yasiyo ya kuambukiza.elimu ya
afya kuhusiana na usafi wa mazingira ilitolewa katika skuli 120 Unguja na
Pemba.
Mhe. Naibu Spika, vikundi 10 vya mazoezi vilipatiwa elimu juu ya umuhimu
wa kufanya mazoezi na wanavikundi walipata fursa ya kupimwa afya zao na
kufahamishwa uwiano wa urefu na uzito ili waweze kujua maendeleo ya afya
zao. Kwa mantiki hiyo hiyo ya kujikinga na maradhi yasiyo ya kuambukiza,
wananchi walihamasishwa kuepukana na matumizi ya pombe na tumbaku
pamoja na kuzingatia ulaji bora ambao una lishe kamili. Zoezi hili lilifanyika
kwa kubandika matangazo na mabango 3,000 kwenye mitaa, maskuli na
masokoni. Pia gari za abiria 40 zilibandikwa stika kwa kuhamasisha juu ya
athari zitokanazo na matumizi ya sigara na tumbaku.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2013/2014 mradi huu umejipangia
kutekeleza kazi zifuatazo:
51
a) Kufundisha waganga 30 wa kienyeji waliosajiliwa kwa siku
mbili juu ya sababu hatarishi na ugunduzi wa mapema wa maradhi
yasioambukiza;
b) Kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa kwa shule za msingi za
Unguja na Pemba;
c) Kuendelea kutoa elimu ya afya juu ya maradhi ya kuambukiza
na yasiyo ya kuambukiza kwa kutumia vyombo vya habari;
d) Kubuni na kusambaza vipeperushi mbali mbali vinavytoa elimu
ya afya juu ya kujua dalili na kujiepusha na maradhi ya kuambukiza na
yasiyoambukiza;
e) Kuhamasisha jamii juu ya uchangiaji wa damu salama ili iweze
kusaidia kwa haraka kwa wagonjwa watakaohitaji kusaidiwa damu;
f) Kundelea kufuatilia mienendo ya taarifa mbalimbali ya
magonjwa katika jamii;
g) Kununua mitambo ya uchapishaji wa vielimishaji jamii.
Mradi wa Kupandisha Hadhi Hospitali za Vijiji na Wilaya
Mhe.Naibu Spika, mradi huu una jukumu kubwa la kuongeza majengo,
kuongeza vifaa na kukarabati majengo yaliyopo pamoja na vitendea kazi ili
kuzipandisha hadhi hospitali za vijiji kuwa za Wilaya na Wilaya kuwa za
Mikoa.
Mhe. Naibu Spika, hospitali ya Abdalla Mzee imo katika mpango wa
kujengwa upya na kuwa na hadhi ya hospitali ya Mkoa wa Kusini Pemba na
kuwa na hadhi ya rufaa kwa Pemba na yenye uwezo wa kulaza wagonjwa
160. Hospitali hii itajengwa kwa msaada mkubwa kutoka Jamhuri ya Watu
wa China na itakuwa ni ya kisasa yenye uwezo wa kutoa huduma za
wagonjwa mahututi (ICU), huduma za dharura (accident and emergency) na
huduma za uchunguzi wa CT Scan.
Mhe. Naibu Spika, hadi hivi sasa wizara imeshafanya makisio ya gharama za
nyumba zitakazovunjwa ili kutoa nafasi kwa ujenzi huo kuendelea. Jumla ya
Tsh. 1.2 bn zitatumika kwa ajili ya kazi ya kuwalipa fidia watu
watakaobomolewa nyumba zao. Hadi kumalizika kwake ujenzi huo
utagharimu jumla ya RMB 70, 000,000 ya Jamhuri ya Watu wa China sawa
na Tsh. 18.6 bn. Kazi inayoendelea hivi sasa ni kukamilisha ramani pamoja
kufanya gharama ya vifaa vya hospitali na mradi huu unatarajiwa kuanza
rasmi mwaka ujao wa fedha unaoanza July 2013.
Mhe. Naibu Spika, katika kufanikisha malengo yake kwa mwaka 2013/2014
mradi umejipangia kutekeleza kazi kuu zifuatazo:-
a) Kuanza ujenzi wa hospitali ya Abdalla Mzee;
52
b) Kutengeneza chumba cha upasuaji katika hospitali ya Kivunge;
c) Kufanya matengenezo ya wodi ya wanawake na wanaume
katika hospitali ya Micheweni.
Mradi wa Mabadiliko ya Sekta ya Afya
Mhe. Naibu Spika, mkutano wa Saba wa mwaka wa Mapitio ya Sekta ya Afya
(7th AJHSRM) ambao uliwashirikisha wadau mbali mbali wakiwemo
washiriki wa maendeleo umefanyika. Mkutano huu uliibua mafanikio
yaliyopatikana pamoja na changamoto kwa mwaka uliopita. Mambo
yaliyoibuliwa yanajumuisha kubadilisha muelekeo wa sera kwa kuyapa
kipaumbele maeneo ambayo yamekuwa ni changamoto kwa jamii mfano
maradhi yasio ya kuambukiza na kuweka nguvu zaidi katika huduma za
watoto wachanga (neonatal care).
Mhe. Naibu Spika, ziara ya Kimasomo kwa viongozi wa Wizara ya Afya
pamoja na wataalamu mbali mbali nchini Rwanda yenye lengo la kujifunza
namna ya utekelezaji wa mfumo wa kutathmini ufanisi wa utendaji wa kazi
katika vituo vya afya na Hospitali (Performance Based Finance) imefanyika.
Ziara hii itasaidia sana katika kuanzisha mfumo huu hapa kwetu kwa kutumia
uzoefu uliopatikana.
Mhe. Naibu Spika, kujitathmini katika kazi yeyote ni jambo la msingi ili
kuona huduma zinazotolewa zinakidhi kiwango. Kufanikisha azma hii
muongozo wa kufanya tathmini ya utekelezaji wa kazi (Performance
Assessment Tool) katika Wilaya na Vituo vya Afya ulitayarishwa, sambamba
na kupatiwa mafunzo kwa madaktari dhamana wa Wilaya na wakuu wa vituo
vya afya. Baada ya mafunzo hayo zoezi la ufuatiliaji linaendelea kufanyika ili
kubaini kama, muongozo huo unafuatwa na huduma zinazotolewa zimefikia
viwango.
Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya Mkemia Mkuu
Mhe. Naibu Spika, lengo kuu la mradi huu ni kujenga maabara kubwa na ya
kisasa pamoja na kuipatia vifaa ambavyo vitaipelekea maabara hii kuweza
kutoa huduma za uchunguzi wa kitaalamu kwa sampuli mbali mbali
zinazowasilishwa.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, wizara imekamilisha
ukarabati mkubwa wa jengo la Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali liliopo
Maruhubi, kuipatia samani pamoja na vifaa vya kisasa vya kufanyia
uchunguzi ili kuongeza ufanisi wa kazi zake.
53
Mhe. Naibu Spika, katika kuongeza ufanisi wa watendaji wafanyakazi
wawili wa maabara hii wamekwenda nchini Uturuki kwa kubadilishana
uzoefu wa kitaalamu wa uendeshaji wa maabara.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2013/2014 mradi umejipangia
kujenga majengo mapya ya Maabara za kisasa Unguja na Pemba.
Mradi wa Chuo cha Madaktari Zanzibar (Zanzibar Medical School)
Mhe. Naibu Spika, chuo cha Madaktari kinatoa mafunzo ya udaktari kwa
mashirikiano makubwa na Chuo Kikuu cha Matansas, Cuba. Kwa sasa chuo
kana jumla ya wanafunzi 50 (38 kwa Unguja na 12 Pemba).
Mhe. Naibu Spika, katika mwaka 2012/2013, niliahidi kushirikisha madaktari
wazalendo katika kutoa taaluma ya afya katika chuo hiki. Napenda kuliarifu
Baraza hili tayari madaktari wawili wazalendo wanasaidiana na madaktari wa
Cuba katika kutoa taaluma chuoni hapo.
Mhe. Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014 chuo kitaendelea kutoa taaluma
ya udaktari kwa wanafunzi wote wanaosoma katika chuo hiki.
Mradi wa Kuimarisha Huduma za Afya Wilayani
Mhe. Naibu Spika, Timu za afya za wilaya ni kiungo kikuu cha utekelezaji wa
shughuli za utoaji wa huduma za afya kati ya wizara ya afya, program na
vitengo vya wizara, vituo vya afya, wadau wengine na jamii kwa ujumla.
Timu hizi zina jukumu la kusimamia utekelezaji wa huduma mbali mbali za
afya zinazotolewa katika vituo vya afya ikiwemo wafanyakazi, majengo na
vifaa. Kwa mwaka wa fedha 2012/2013 wizara iliamua kuanzisha mfumo
maalum wa kuendesha kazi za timu hizi ambapo mfuko maalum wa pamoja
wa fedha (District Health Servises Basket Fund) uliazishwa.
Mhe. Naibu Spika, utumiaji wa huduma za afya wilayani ni kiashiria muhimu
katika kupima utumiaji wa huduma hizo. Katika mwaka 2012 kwa wastani
Wilaya sita (Chake-Chake na Wete kwa Pemba: Kati, Kaskazini A, Kusini na
Mjini kwa Unguja) zilionekana kuwa na utumiaji mzuri wa huduma za afya
ambapo kila mtu mmoja alitembelea mara moja au zaidi. Kiwango hiki ni
zaidi ya kiwango kinachopendekezwa na Shirika la Afya Ulimwenguni
ambapo inakadiriwa kwamba mwanadamu yeyote anatakiwa kwenda kituo
cha afya kwa ajili ya kupata huudma angalau mara moja kwa mwaka. Hali hii
inaamaanisha kwamba wananchi wengi wanapatiwa huduma za afya katika
vituo vya afya vilivyopo.
54
Mhe. Naibu Spika, utekelezaji wa shughuli katika wilaya hizi unatofautiana
kutegemeana na mazingira na mahitaji halisi ya wilaya husika. Kwa mwaka
wa fedha 2012/2013, Siku za Afya za Vijiji zilifanyika katika Shehia 50 za
Unguja na Pemba. Katika Siku hizo huduma mchanganyiko za afya zilitolewa
kwa wanavijiji, wananchi waliweza kuchunguzwa afya zao kwa kupimwa
maradhi ya Shinikizo la damu, Kisukari, Saratani ya Shingo ya kizazi na
matiti, VVU, Kifua Kikuu, Macho na meno. Tiba ilitolewa kwa wale
waliostahiki na kwa wale waliokuwa na hali mbaya walipatiwa rufaa.
Mhe. Naibu Spika, katika kuimarisha elimu ya afya mashuleni, mafunzo ya
ukufunzi (TOT) juu ya uhusiano wa ugonjwa wa kifua kikuu na VVU kwa
walimu kupitia vituo vya walimu (Teacher‟s Centre) yalitolewa. Walimu
hawa walitakiwa kutoa taaluma kwa klabu za wanafunzi (School Clubs)
pamoja na wanafunzi wa madarasa) na hatimae klabu hizo hutakiwa
kuwaelemisha wenzao (elimu rika). Vile vile, elimu kuhusu umuhimu wa
chanjo ya Pepo Punda imetolewa kwa wanafunzi wa sekondari shamba na
mijini wengi wao waliitikia wito na kupatiwa chanjo hiyo mara tu baada ya
mafunzo hayo kutolewa.
Mhe. Naibu Spika, ukaguzi wa majengo kama vile mikahawa na skuli
umefanyika na imeonekana kuwa hali ya mazingira ni mbaya hususan maeneo
ya vyoo. Pia, wahudumu walikaguliwa afya zao na kupewa ushauri wa kiafya.
Aidha, akina mama lishe na wauza mikahawa wamepewa elimu ya usafi
binafsi (personal hygiene) na utaratibu wa kutayarisha chakula pamoja na
usafi wa mazingira. Hali ambayo itasaidia katika kupunguza kasi ya maradhi
mbali mbali.
Mhe. Naibu Spika, uhamasishaji kwa wakunga wa Jadi, wahudumu wa uzazi
wa mpango na watu maarufu umefanyika kwa kupewa elimu juu ya umuhimu
wa kuhudhuria kliniki za mama waja wazito ndani ya wiki 16. Wadau hao
walielezwa huduma mbali mbali zinazotolewa katika hudhurio la mwanzo na
za marudio pia walitakiwa kuwashajihisha kina mama kujifungua katika
Vituo vya Afya na kufata utaratibu uliowekwa wa kuhudhuria kliniki mara tu
baada ya kujifungua kwa kuchunguza afya zao na kupewa matone ya Vit-A
pamoja na watoto kuanza chanjo.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka 2013/14 kazi zifuatazo zitatekelezwa:-
a) Kuendelea kufanya ufuatiliaji katika vituo vya afya;
b) Kuendelea na kusimamia matengenezo madogo madogo ya
vituo vya afya na hospitali za vijiji;
c) Kuendela kutoa mafunzo ya afya kwa wafanyakazi wa vituo na
hospitali za vijijii (mafunzo juu ya kumhudumia mtoto
55
kulingana na muongozo wa IMCI, Afya ya mama na mtoto) ili
waweze kutoa huduma zinazoendana na miongozo ya utoaji
wahuduma za afya ya kitaifa na kimataifa;
d) Kuendelea kutoa huduma ya afya ya jamii kupitia njia mbali
mbali ikiwemo huduma za mkoba katika maeneo ya Tumbatu,
Kijini, Kinuni, Kisiwa Panza, Fundo).
CHANGAMOTO
Mhe. Naibu Spika, kama nilivyoeleza kuwa, mafanikio makubwa
yamepatikana katika utekelezaji wa majukumu ya wizara kwa kipindi cha
mwaka 2012/2013. Hata hivyo, Wizara ya Afya bado inakabiliwa na
changamoto nyingi ambazo zinahitaji mashirikiano yetu sote kuweza
kuzitatua.
Mhe. Naibu Spika, miongoni mwa changamoto hizi ni bajeti iliyopangwa na
kuidhinishwa huwa haiendani na utoaji wa fedha kutoka Serikali Kuu, hivyo
huathiri utekelezaji wa kazi za kawaida na za maendeleo. Matumizi baada ya
kumalizika kikao cha bajeti kama hiki huombwa Ofisi ya Rais Fedha na
Mipango ya Maendeleo kwa mfumo wa kila robo mwaka na wizara hujiwekea
vipaumbele kwa mujibu wa mahitaji tuliyonayo, lakini bado maombi hayo
hayapatikani kwa wakati na huwa hayalingani na kile kilichoombwa kwa kazi
za kawaida na maendeleo. Hiyo changamoto moja Mhe. Naibu Spika,
inayotusumbua.
Mhe. Naibu Spika, moja katika mkakati wa Wizara ya Afya ni kuimarisha
huduma za afya wilayani na vijijini. Hata hivyo, utekelezaji wa mkakati huu
hauendani na kasi ndogo ya serikali ya kuimarisha madaraka wilayani ya
Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, tunaiomba serikali
kukamilisha taratibu zilizobakia ili tuende sambamba na utoaji bora wa
huduma za afya wilayani na vijijini.
Mhe. Naibu Spika, ujenzi wa vituo vya afya vinavyoanzishwa na wananchi
bila ya kufuata utaratibu bado ni tatizo kutokana na ufinyu wa bajeti ya afya
na ukosefu mkubwa wa wafanyakazi wanohitajika kuvihudumia vituo hivyo
wakati vinapomalizika. Taarifa tuliyonayo hivi sasa kuna vituo 28
vilivyoanzishwa ambavyo vinahitaji wataalamu, dawa na vifaa mambo
ambayo ni changamoto kubwa kwa wizara yetu. Kama nilivyosisitiza katika
hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya ya mwaka 2012/2013, kwa mara nyengine
tena, naomba kutoa wito kwa viongozi na wananchi kujihusisha zaidi katika
kujenga nyumba za wafanyakazi na kununua dawa, vifaa na tiba mbadala ya
kufikiria kujenga vituo vipya vya afya ambapo tulivyonavyo vinatosha.
56
Mhe. Naibu Spika, kutokamilika kwa mfumo madhubuti unaowalazimisha
wafanyakazi kubakia makazini hasa wale ambao wanaopelekwa masomoni
wa kada za kitaalamu, kunapelekea wafanyakazi kutorudi au hata wale
waliokuwepo kukimbia. Kwa mfano, katika kipindi hiki jumla ya
wafanyakazi 32 wa kada tofauti hawajarejea katika sehemu zao za kazi wakati
serikali imelipia gharama kubwa za kuwasomesha.
Mhe. Naibu Spika, gharama kubwa za huduma za maji na umeme imekuwa ni
tatizo kwa uendeshaji wa vituo vya afya vijijini na hata kwa hospiatali zetu za
wilaya na rufaa. Ukubwa wa tatizo hili unatokana na Shirika la Umeme na
Mamlaka ya Maji kulipisha vituo vya afya na hospitali kama ni kampuni za
kibiashara, jambo ambalo linapelekea kutumia fedha chache tulizonazo kwa
kazi za kawaida na maendeleo kulipia umeme, ambazo zingetumika kwa
shughuli nyengine. Nachukua fursa hii kuzitaka taasisi husika kulizingatia
suala hili na kulipatia ufumbuzi.
Mhe. Naibu Spika, kushuka kwa kiwango cha chanjo kitaifa ni moja katika
tatizo sugu linalotusumbuaWizaraya Afya. Kushuka kwa kiwango cha chanjo
kitaifa ni tatizo lililojitokeza hasa katika wilaya ambazo zilichanja chini ya
kiwango cha asilimia 80. Hali hii imepelekea kuibuka kwa maradhi ya surua
ambayo yalikuwa hayapo kwa watoto, maradhi ambayo ni tishio kwa taifa.
Hivyo nawaomba wananchi wenzangu kupitia hotuba hii kwa pamoja
tushirikiane kuwashajihisha akinamama na baba kuwapeleka watoto wao
kuchanjwa kwani janga la maradhi yakitokea huwa hayachagui sura wala
kabila wala kijiji.
MALENGO YA WIZARA YA AFYA KWA MWAKA 2013/2014
Mhe. Naibu Spika, Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2013/2014
imejipangia kutekeleza mambo makuu yafuatayo:-
a) Kuhakikisha upatikanaji wa dawa, vifaa, tiba na vitenganishi
vyenye ubora na usalama katika ngazi zote;
b) Kuimarisha utoaji wa elimu ya afya kwa jamii ili kupunguza
kiwango cha maradhi ya kuambukiza na yasiyokuwa ya
kuambukiza;
c) Kuendeleza mashirikiano na Wizara ya Utumishi wa Umma ili
kupata ufumbuzi wa motisha za wafanyakazi wa afya na
wafanyakazi wanaofanya kazi katika mazingira magumu;
d) Kuendelea kutoa mafunzo ya kada mbali mbali za afya kwa
wafanyakazi;
e) Kuanzisha mkakati wa muda mrefu wa vyanzo mbadala vya
rasilimali fedha kwa ajili ya kutolea huduma za afya;
57
f) Kuimarisha na kusimamia shughuli za utafiti, tathmini na
ufuatiliaji wa taarifa za afya katika ngazi zote;
g) Kuimarisha miundombinu ya afya ikiwemo ujenzi wa Hospitali
ya Abdalla Mzee na upanuzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja;
h) Kukamilisha mpango mkakati wa afya wa III na kuufanyia
mahitaji yake kifedha;
i) Kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika ngazi za wilaya
kupitia mfuko wa fedha wa pamoja wa wilaya (District Health
Services Basket Fund) ikijumuisha Hospitali za Wilaya,
Hospitali za Vijiji na Vituo vya Afya.
HITIMISHO
Mhe. Naibu Spika, mafanikio yaliyopatikana ya kutoa huduma bora za afya
kwa wananchi kulitegemea mashirikiano makubwa yaliyokuwepo ndani ya
wizara hii. Hili halikuwa jukumu la mtu mmoja, kwa mustakbala huo, sina
budi kuwapongeza viongozi wote ndani ya wizara ikiwa ni pamoja na Naibu
Waziri wangu Dr. Sira Ubwa Mamboya, Katibu Mkuu, Wakurugenzi na
Wakuu wote wa vitengo/sehemu zilizomo ndani ya wizara, kwa mashirikiano
makubwa waliyonipa na tuliyofanya pamoja.
Mhe. Naibu Spika, nathamini mchango mkubwa wa wafanyakazi wa ngazi
zote za ndani ya wizara kwa kufanya kazi bila ya kuchoka kwani
wanakabiliwa na changamoto nyingi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Hali hii imeniwezesha kufanikisha utekelezaji wa majukumu yangu kwa kiasi
fulani kwa urahisi sana. Aidha, nathamini mchango na mashirikiano kutoka
kwa taasisi nyengine za serikali katika kusaidia upatikanaji wa huduma za
afya visiwani mwetu.
Mhe. Naibu Spika, huduma za afya zimekuwa zikitolewa kwa mashirikiano
na sekta binafsi (Private Sector), pamoja na jamii ya Wazanzibari na
wananchi wote. Wizara yangu itakuwa mchoyo wa fadhila pindipo
haitaipongeza sekta hii kwa mchango wao katika kutoa huduma. Hali hii
imesaidia wizara yangu katika kufanikisha utekelezaji wa jukumu lake la
kuipatia jamii huduma inayostahiki. Aidha, wizara inaishukuru jamii ya
Wazanzibari na wananchi wote kwa ujumla kwa mashirikiano na michango
yao katika utoaji na upokeaji wa huduma za afya.
Katika kipindi chote cha utoaji wa huduma za afya, serikali za nchi marafiki,
mashirika ya kitaifa na kimataifa pamoja na watu binafsi yalikuwa sambamba
na wizara yangu, hivyo kutoa mashirikiano makubwa pamoja na misaada ya
hali na mali ili kuhakikisha afya za jamii za watu wetu zinaimarika.
58
Mhe. Naibu Spika, nitakuwa sikuzitendea haki taasisi zote hizo pindipo
sikutoa shukurani zangu za dhati kwao, nawaomba wasichoke kwa vile safari
ya kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wetu ingali ndefu na inahitaji
mashirikiano yetu sote. Nachukua fursa hii adhimu kuwashukuru wote hasa
WHO, UNICEF, UNFPA, UNDP, WORLD BANK, ADB, JHIEPIGO,
GLOBAL FUND, USAID, DANIDA, ICAP, HIPZ, CLINTON FOUNDATION,
SAVE THE CHILDREN, IVODE CANERI na ITALIAN FOUNDATION. Pia
shukurani ziende kwa nchi marafiki za Cuba, Italy, Marekani, Oman, China,
Israel, Turky, Misri, France, India, Netherland, Uingereza na wote ambao
sikuwataja katika orodha huu.
Mhe. Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2013/2014 Wizara ya Afya
imepangiwa kuchangia jumla ya Shilingi 924,000,000 kwenye Mfuko Mkuu
wa Serikalii kiambatisho namba 16 kinaonesha ufafanuzi. Pia wizara
imepangiwa kutumia Shilingi 5,764,000,000 kwa kazi za kawaida, Shilingi
1,368,000,000 ikiwa ni ruzuku na Shilingi 14,186,000,000 kwa mishahara na
maposho. Kiambatisho namba 17 kinaonesha ufafanuzi. Kwa kazi za
Maendeleo wizara imepangiwa kutumia jumla ya Shilingi 6,333,000,000
kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali, Shilingi 37,257,128,000 misaada na Shilingi
5,078,489,000 ikiwa ni Mikopo kutoka nje. Kiambatisho namba 18
kinaonesha ufafanuzi.
Mhe. Naibu Spika, utekelezaji wa majukumu ya wizara yangu yanategemea
kwa kiasi kikubwa kupitishwa kwa hotuba yangu hii ya bajeti. Kwa mintarafu
hiyo nategemea Baraza lako tukufu limeipokea, litaijadili, kuichangia na
mwishoe litapitisha bila ya mashaka ili wizara yangu iweze kuwapatia
wananchi huduma bora za afya na hatimae kuimarisha afya zao. Naomba
Mhe. Naibu Spika, Baraza hili liidhinishe jumla ya Shilingi 21,318,000,000
kwa Kazi za Kawaida, Ruzuku, Mishahara na Maposho. Pia naomba Baraza
liidhinishe jumla ya Shilingi 6,333,000,000 kwa Kazi za Maendeleo kutoka
serikalini na Shilingi 37,257,128,000 ikiwa ni ruzuku kwa washirika wa
maendeleo, Shilingi 5,078,489,000 mkopo kutoka kwa washirika wa
maendeleo.
Mhe. Naibu Spika, kwa heshima kubwa na taadhima na kwa idhini yako
naomba kutoa hoja.
(Hoja ilitolewa iamuliwe)
59
Kiambatisho Nam 1: Mwenendo wa Maradhi kwa Mgawanyo wa
Umri 2012/13
Kiambatisho Nam 2: Mwenendo wa Maradhi kwa Mgawanyo wa
Wilaya
60
Kiambatisho Nam 3: Takwimu za Wagonjwa Walioonekana kupitia
Uchunguzi wa Vijijini kwa mwaka 2012/13
61
Kiambatisho Nam 4: Matatizo yaliyogunduliwa Wakati wa Uchuguzi wa
Afya za Wafanyakazi
62
Kiambatisho Nam 5: Wagonjwa wa Nje na Ndani Katika Hospitali za
Idara ya Tiba Julai, 2012 - Machi, 2013
63
Kiambatisho Nam 6: Taarifa ya Hali ya Uzazi Katika Hospitali za
Idara ya Tiba, Julai, 2012 – Machi, 2013
Kiambatisho Nam 7: MAHUDHURIO YA WAGONJWA KATIKA
KLINIKI ZA MARADHI MAALUM KWA HOSPITALI ZA IDARA YA
TIBA, July 2012 - March 2013
64
Kiambatisho Nam 8: Mahudhurio ya Wagonjwa wa Nje, Waliolazwa
na Waliofariki Katika Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja, Julai 2012 -
Machi 2013
65
Kiambatisho Nam 9: Mahudhurio ya Wagonjwa Katika Kliniki za
Maradhi Maalum Katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Julai 2012, - Machi,
2013
Kiambatisho Nam 10: Taarifa ya Hali ya Uzazi Katika Wodi ya
Wazazi kwa Hospitali za Mnazi Mmoja na Mwembeladu Julai, 2012 –
Machi, 2013
66
Kiambatisho Nam 11: Kambi zilizofanywa na ZOP kuanzia Julai
2012- Machi 2013
Kiambatisho Nam 12: Thamani ya Dawa na Zana za Tiba
Zilizopatikana (Julai, 2012 – Machi, 2013)
67
Kiambatisho Nam 13: Idadi ya Sampuli Zilizochunguzwa Julai 2012 -
Machi 2013
68
69
Kiambatisho Nam 14: Wanafunzi waliorudi Masomoni,
Julai 2012 – Machi 2023
Cadre
Level
Grand
Total
Certificate
Diploma
Advanced
Diploma
Degree
Post
Grade
Diploma
Masters
pHd
Accounting 1 1
AMO 2 2
Anaethetic
Nurse
6 6
Biomedical
Technician
8 8
Chemist 1 1
DDS 2 2
Dental
Surgery
1 1
Economic &
Nutrition
1 1
ENT 2 2
Entomology
& Vector
Control
1 1
Guidence &
Councelling
1 2 3
Internal
Medicine
1 1
M.B.B.S 4 4
Medical
Imaging
4 4
Medical
Laboratory
2 2
Nursing 16 1 17
Oncology 1 1
Paediatrics 1 1
Procurement 1 1
Psychology
&
Counseling
2 2
Public
Health
4 4
70
Reproductive
Health
1 1
Social Work 1 1
Vector
Control
1 1
Grand Total 14 4 6 38 1 4 1 68
Kiambatisho Nam 15: Taarifa ya Huduma ya Chanjo kwa Watoto
chini ya Mwaka mmoja Julai 2012 - Mach 2013
71
Kiambatisho Nam 16: Fedha Zilizotengwa na Kukusanywa kwa
Kipindi cha Julai 2012- Machi 2013 na Mapendekezo ya Makusanyo
2013-2014
Kasma Maelezo ya
Mapato
Makadirio
2012/2013
Makusanyo
Julai-Machi
2012/2013
Asilimia
Mapendekezo
ya Makadirio
ya Mapato
2013/2014
4 IDARA YA MIPANGO NA UENDESHAJI
142126
Huduma za
Maabara ya
Mkemia
Mkuu
1,000,000.00 - -
-
JUMLA
NDOGO
1,000,000.00 - -
-
6 IDARA YA KINGA
142238
Shahada ya
maradhi ya
kuambukiza
15,000,000.00
7,249,000.00 48.33
16,000,000.00
142260
Huduma za
daktari na
orodha wa
wafanyakazi
na abiria
14,000,000.00
8,416,000.00 60.11
15,000,000.00
JUMLA
NDOGO
29,000,000.00
15,665,000.00 54.02
31,000,000.00
7 IDARA YA TIBA UNGUJA
142261
Malipo ya
X-Ray na
uchunguzi
wa damu
20,000,000.00
11,597,000.00 57.99
20,000,000.00
JUMLA
NDOGO
20,000,000.00
11,597,000.00 57.99
20,000,000.00
0801- IDARA YA TIBA PEMBA
72
142261
Malipo ya
X-Ray na
uchunguzi
wa damu
10,000,000.00
1,511,000.00 15.11
3,000,000.00
JUMLA
NDOGO
10,000,000.00
1,511,000.00 15.11
3,000,000.00
145000 MICELLANIOUS REVENUES
145002 Mapato
mengineyo
35,000,000.00
45,072,800.00 128.78
70,000,000.00
JUMLA
NDOGO
35,000,000.00
45,072,800.00 128.78
70,000,000.00
145000 1501 M/MMOJA HOSPITAL
145001 Mapato
mengineyo
710,500,000.00
292,174,463.00 41.12
384,000,000.00
Huduma za
haraka -
-
-
416,000,000.00
JUMLA
NDOGO
710,500,000.00
292,174,463.00 41.12
800,000,000.00
JUMLA
KUU
805,500,000.00
366,020,263.00 45.44
924,000,000.00
Kiambatisho Nam 17: Fedha Zilizotengwa na Kuingizwa kwa Kazi za
Kawaida kwa kipindi cha julai 2012- machi 2013 na makadirio 2013-2014
73
74
Kiambatisho Nam 18: Fedha Zilizotengwa na Kuingizwa kwa Kazi za
Maendeleo kwa Kipindi cha Julai 2012-Machi 2013 na Makadirio 2013-
2014
Mhe. Hassan Hamad Omar (Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya
Maendeleo ya Wanawake na Ustawi wa Jamii): Mhe. Naibu Spika, kwa
ruhusa yako naomba kusoma hotuba ya maoni ya Kamati ya Maendeleo ya
Wanawake na Ustawi wa Jamii kuhusiana na bajeti ya Wizara ya Afya kwa
mwaka wa fedha 2013/2014.
Mhe. Naibu Spika, awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu
kwa kuturuzuku uhai na afya njema na kutuwezesha kukutana tena leo hii
kwa madhumuni ya kuwatumikia wananchi wetu na manufaa ya taifa letu kwa
ujumla.
75
Pili napenda nikushukuru wewe binafsi kwa kuniruhusu kusimama mbele ya
Baraza lako tukufu kwa niaba ya Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na
Ustawi wa Jamii, kuwasilisha maoni ya Kamati kuhusiana na makadirio ya
mapato na matumizi ya kazi za kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha
2013/2014.
Mhe. Naibu Spika, napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Waziri wa Afya,
Naibu Waziri, pamoja na watendaji wote wa wizara kwa mashirikiano yao
waliyotupa wakati wa kupitia na kuichambua bajeti ya wizara, kwa kweli
mashirikiano yao yamefanikisha kumaliza kazi hii kwa wakati na kwa ufanisi
mkubwa.
Sitokuwa nimetenda haki hata kidogo iwapo nitakosa kuwashukuru na
kuwapongeza Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawi
wa Jamii kwa kazi nzuri waliyoifanya hadi kuniwezesha leo hii kusimama
mbele ya Baraza lako tukufu kuwasilisha maoni ya Kamati juu ya Makadirio
ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2013/2014. Naomba
niwatambue kwa kuwataja majina wajumbe wa Kamati kama hivi ifuatavyo:-
1. Mhe. Mgeni Hassan Juma Mwenyekiti
2. Mhe. Hassan Hamad Omar M/Menyekiti
3. Mhe. Abdi Mosi Kombo Mjumbe
4. Mhe. Ali Salum Haji Mjumbe
5. Mhe. Farida Amour Moh'd Mjumbe
6. Mhe. Mwanaid Kassim Mussa Mjumbe
7. Mhe. Mohamed Mbwana Hamad Mjumbe
8. Ndg. Maryam Rashid Ali Katibu
9. Ndg. Asha Said Mohamed Katibu
Mhe. Naibu Spika, baada ya utangulizi huo, naomba kutoa maoni ya Kamati
kuhusiana na Bajeti ya Wizara ya Afya.
Jengo la Ofisi Kuu – Pemba
Mhe. Naibu Spika, Kamati yetu imesikitishwa na hali ya Wizara ya Afya
Pemba kukosa ofisi yake. Ofisi Kuu Pemba imekuwa haina jengo kwa muda
mrefu na inatumia chumba kimoja kidogo kilichopo katika hospitali ya Wete;
hali ambayo hairidhishi kwani chumba hicho kinakuwa hakikidhi haja kwa
matumizi ya wizara nzima. Afisa Mdhamini anashindwa kuwa karibu na
wasaidizi wake mbali mbali kutokana na ufinyu wa ofisi.
76
Mhe. Naibu Spika, Kamati inaiomba serikali kutatua tatizo la ofisi ya wizara
Pemba. Kiukweli Kamati haikuridhika na hali ya ufinyu wa ofisi kwa sababu
utekelezaji wa majukumu ya wizara unakuwa ni mgumu.
Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba katika Hospitali na Vituo vya Afya
Pemba
Mhe. Naibu Spika, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ni muhimu katika
hospitali na vituo vya afya, lakini Kamati ilipotembelea vituo vya afya na
hospitali mbali mbali ilibaini upungufu mkubwa wa dawa na vifaa tiba.
Sambamba na hilo, Kamati ilifanya mahojiano na timu nne za afya Pemba
zilizopo katika Wilaya ya Micheweni, Wilaya ya Wete, Wilaya ya Chake
Chake na Wilaya ya Mkoani; nazo zilikiri kuwa upatikanaji wa dawa na vifaa
tiba ni tatizo katika wilaya zao.
Mhe. Naibu Spika, kutokana na umuhimu wa huduma za afya na dawa,
Kamati inaishauri Wizara kutafuta kampuni nyingine ya kuagiza na kuingiza
dawa nchini badala ya kutegemea ghala kuu ya dawa ya Dar es Salaam pekee
MSD (Medical Store of Dar es Saalam) ambao nao huchangia uhaba wa
upatikanaji wa dawa katika hospitali na vituo vyetu vya afya katika muda
unaotakiwa.
Kuhusu Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
Kamati haikuridhishwa na utekelezaji wa miradi unaondeshwa na wizara.
Katika bajeti ya wizara ya mwaka wa fedha 2012/2013, wizara ilijipangia
kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo. Kamati imebaini utekelezaji
usio wa ufanisi katika programu shirikishi ya afya ya mama na mtoto, mradi
wa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na mradi wa kuvipandisha hadhi
vituo vya huduma za afya. Malengo ya miradi hiyo hayakuweza kufikiwa
kikamilifu.
Mhe. Naibu Spika, katika utekelezaji wa programu shirikishi ya afya ya mama
na mtoto ambayo ilikusudia kujenga vyumba vya baridi na kufanya ukarabati
wa ofisi ya chanjo Pemba. Kamati ilisikitishwa sana kuwa utekelezaji wake
haukuweza kufanyika na hakukuwa na sababu za msingi kwani fedha za
wahisani ziliingizwa na kushindwa kufanyiwa kazi katika muda
uliokusudiwa. Kitendo hichi ni kuwavunja moyo wahisani wetu na Kamati
inamtaka waziri atoe maelezo juu ya jambo hili.
Pia Kamati inaiagiza wizara katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2013/2014
kuhakikisha kuwa wanafanya ujenzi wa haraka wa vyumba vya baridi pamoja
na ukarabati wa Ofisi ya Chanjo, kwani chanjo zote kwa upande wa Pemba
77
zinahifadhiwa katika ofisi hiyo, kuendelea kuchelewa kufanya ujenzi
kutapelekea kutokuwa na uhakika wa usalama wa chanjo zetu pamoja na
wafanyakazi wanaohudumia ofisi hiyo.
Mhe. Naibu Spika, katika mradi wa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi,
Wizara ilikusudia kufanya matengenezo katika vituo vya afya vya
Mzambarauni na Wesha kwa upande wa Pemba na kwa Unguja Kituo cha
Afya Mwera. Vituo vyote hivyo vilikosa kukarabatiwa katika kipindi husika,
ukarabati uliofanyika ni wa Kituo cha Afya cha Bogoa pekee ambacho
utekelezaji wake ulikuwa wa tangu bajeti ya mwaka wa fedha 2011/2012.
Aidha, katika mradi wa kuvipandisha hadhi vituo vya huduma za afya, lengo
lake lilikuwa ni kufanya utanuzi wa majengo ya Hospitali ya Kivunge na
Micheweni pamoja na ununuzi wa vifaa mbali mbali kwa ajili ya utoaji mzuri
wa huduma za afya katika hospitali hizo. Utekelezaji wake haukuwa wa
kuridhisha.
Mhe. Naibu Spika, Kamati inaitaka serikali kuingizia fedha wizara kwa
wakati ili iweze kutekeleza mipango yake iliyojipangia ikiwemo utekelezaji
wa miradi kwa lengo la kuimarisha huduma za afya nchini na kuinua sekta hii
muhimu.
Idara ya Utumishi na uendeshaji
Mhe. Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2012/2013, idara ilikamilisha
mpango mkuu wa mafunzo kwa wafanyakazi ambao utekelezaji wake utaanza
kutumika rasmi katika mwaka huu wa fedha. Kamati inaipongeza wizara kwa
kuweza kukamilisha mpango huo muhimu ambao utasaidia katika kupunguza
upungufu mkubwa wa wafanyakazi wa afya katika kada mbali mbali kwa
hospitali na vituo vya afya.
Katika nchi yetu tumekuwa na upungufu mkubwa wa madaktari wa
magonjwa ya akili, madaktari wa X-ray, madaktari wa magojwa ya damu na
madaktari wa kensa. Kamati inaishauri wizara katika mpango mkuu wa
mafunzo kwa mwaka wa fedha 2013/2014 kuwahimiza wafanyakazi
watakaoenda masomoni kuchukua fani zilizokuwa pungufu katika nchi yetu
na pia kuwepo na motisha maalumu kwa watakaokubali kuchukua fani hizo.
Mhe. Naibu Spika, pia Kamati inaisisitiza wizara kusimamia vyema mfumo
wa takwimu za rasilimali watu, mfumo ambao husaidia katika kupangia
wafanyakazi sehemu za kazi kwa mujibu wa mahitaji. Wizara imekuwa
inakabiliana na changamoto ya wafanyakazi wengi wa afya kutopendelea
kufanya kazi vijijini na badala yake kupendelea zaidi kubakia mijini pekee.
78
Mhe. Naibu Spika, Kamati inaiomba wizara ijitahidi kusimamia maslahi ya
wafanyakazi na ihakikishe inasimamia ipasavyo mapendekezo ya rasimu ya
maposho kwa wafanyakazi wanaofanya kazi katika mazingira ya hatarishi na
pia kuwazingatia wale wanaofanya kazi katika mazingira ya vijijini
yaliyokosa huduma muhimu. Kufanya hivyo, kunaweza kuwavutia
wafanyakazi wetu kubakia katika ajira na kupunguza idadi kubwa ya
wafanyakazi wanaokimbia kufanya kazi vijijini na katika nchi yetu kwa
ujumla.
Idara ya Sera, Mipango na Utafiti
Mhe. Naibu Spika, Kamati inapongeza jitihada zinazoendelea kufanywa na
idara katika mchakato mzima wa kuanzisha bima ya afya kwa wananchi.
Kiukweli bima hiyo ni muhimu na itawasaidia wananchi kuwa na uhakika wa
kupata huduma za afya kila watakapokuwa wanasumbuliwa na maradhi mbali
mbali.
Mhe. Naibu Spika, kumekuwa na wananchi ambao hushindwa kuhudhuria
katika hospitali na vituo vya afya kutokana na kushindwa kumudu gharama za
afya. Kamati ina matumaini makubwa kwamba kuanzishwa kwa bima ya afya
kutawawezesha wananchi walio wanyonge kufaidika na huduma za afya kwa
kadri watakavyokuwa wanazihitajia.
Kamati inaisisitiza wizara kuendelea na hatua mbali mbali zinazohusiana na
kukamilika kwa bima hiyo na pia kuandaa utaratibu mzuri ambao utapelekea
kupatikana kwa huduma kwa wepesi na kunufaisha wananchi wote.
Idara ya Kinga na Elimu ya Afya
Mhe. Naibu Spika, miongoni mwa majukumu ya idara ni kukinga na
kukabiliana na maradhi ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza. Katika
miaka ya hivi karibuni, katika visiwa vya Zanzibar kumekuwa na ongezeko
kubwa la magonjwa yasio ya kuambukiza ikiwemo shindikizo la damu,
kisukari, saratani na magojwa mengine sugu ya mapafu kama vile pumu.
Kamati inaipongeza wizara kwa kuweza kufanya utafiti katika hospitali nne
za vijiji na hospitali tatu za wilaya na kuweza kubaini hali halisi ya magonjwa
na kutambua mahitaji ya taaluma, vitendea kazi na rasilimali watu.
Mhe. Naibu Spika, kitengo cha kupambana na magonjwa yasio ya
kuambukiza kinaendelea kusimamia utekelezaji wa mikakati ya kukabiliana
na magonjwa hayo na Kamati inasisitiza wizara, pamoja na kuwepo kwa
79
kitengo, kuendelea kuusimamia muongozo wa matibabu ya magonjwa
yasioambukiza ili uweze kukamilika na kuanza kutumika.
Aidha, kwa upande wa maradhi ya malaria, Kamati inapenda kuipongeza
wizara kwa jitihada wanayoendelea kuchukua ya kudhibiti maradhi hayo.
Kamati iliweza kujionea wenyewe kisiwani Pemba, Shehia ya Tumbe kuwa
ugonjwa wa malaria katika kijiji hicho umeweza kutokomezwa. Kamati
inaiomba wizara kuendelea na juhudi ya kudhibiti maradhi ya malaria ili
yasije yakaibuka tena kwa kuendela kutoa elimu ya kinga ya maradhi hayo.
Kamati ina matumaini makubwa kuwa idara itaendelea kufanya vizuri katika
majukumu yake mbali mbali kutokana na ongezeko la bajeti kutoka shilingi
milioni mia mbili thalathini na moja (231,000,000) katika mwaka wa fedha
2012/2013 mpaka kufikia milioni mia tatu hamsini (350,000,000) katika
mwaka huu wa fedha.
Idara ya Tiba
Mhe. Naibu Spika, idara hii inajumuisha Hospitali za Wilaya na Vijiji na pia
inasimamia mradi wa kupandisha Hospitali za Vijiji na Wilaya. Kiujumla
hospitali zetu zinakabiliana na changamoto za msingi ikiwemo hali mbaya ya
upatikanaji wa dawa na vifaa, uchakavu wa majengo, uchache wa
wafanyakazi, kuwepo kwa madeni makubwa ya maji na umeme, kukosekana
kwa uzio katika vituo vya afya, walinzi na kadhalika.
Mhe. Naibu Spika, Kamati inaitaka serikali kuisadia wizara katika
kukabiliana na changamoto hizi. Kamati imeweza kushuhudia uchakavu na
ufinyu wa majengo katika hospitali zetu za vijiji na wilaya. Kwa upande wa
Hospitali ya Vitongoji Pemba, maabara, wodi na nyumba za madaktari
zimekuwa ni chakavu na hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa sio mzuri.
Mhe. Naibu Spika, Kamati inaona kama kweli ile azma ya serikali ya
kuzipandisha hospitali za vijiji kuwa za wilaya na zile za wilaya kuwa za
mkoa inafikiwa, lazima serikali ihakikishe inaongeza fedha, majengo, vifaa na
vitendea kazi katika hospitali hizo.
Mradi wa Kuimarisha Huduma za Afya Wilayani.
Mhe. Naibu Spika, utekelezaji wa mradi huu unategemea ufanisi mkubwa wa
Timu za Afya za Wilaya pamoja na mfumo ulioanzishwa na wizara wa
kuendesha kazi za timu za wilaya ambapo Mfuko maalum wa pamoja wa
fedha (District Health Services Basket Fund) hutumika katika kuwapatia
fedha timu hizo.
80
Kamati imegundua kuwa utaratibu unaotumika wa kuwapatia fedha Timu za
Afya za Wilaya bado haujafahamika kwa timu zewenyewe na hivyo
kupelekea timu hizo kukosa fedha kwa wakati. Kamati inaiomba wizara
kuendelea kutoa elimu juu ya mfumo uliyoanzishwa ili maafisa wa timu za
afya za wilaya wapate fedha kwa wakati na pia wapewe madaraka ya
kuzitumia fedha kwa kufanikisha kazi zao.
Mhe. Naibu Spika, timu za afya za wilaya zimeweza kufikia vituo mbali
mbali vya afya na kuona utekelezaji wa huduma zinazotolewa katika vituo.
Mbali na jitihada za kufikia vituo hivyo, timu hizo ziliweza kugundua
changamoto zilizopo kama ufinyu wa vituo, upungufu wa wafanyakazi,
kukosekana kwa uzio katika vituo, madeni makubwa ya umeme na maji,
matokeo ya uvamizi na wizi na ukosefu wa vifaa tiba.
Mhe. Naibu Spika, Kamati inaiomba Serikali kuisaidia wizara katika
kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo ili hatimae huduma za afya za wilayani
ziweze kuimarika.
Hitimisho
Mhe. Naibu Spika, Wizara ya Afya kwa bajeti ya mwaka 2012/2013 imepata
mafanikio katika baadhi ya maeneo huku ikiwa bado baadhi ya maeneo
yanahitaji kufanyiwa kazi. Kamati yetu kiujumla haijaridhika kabisa na
uingizwaji wa fedha katika Wizara ya Afya kwa matumizi ya kazi za kawaida
na kazi za maendeleo. Uingizwaji wa fedha usioridhisha unaendelea
kuikwamisha wizara katika kutekeleza majukumu yake. Hivyo Kamati
inaiomba Serikali kuipa kipaumbele wizara kwa kuingizia fedha ipasavyo ili
iweze kutekeleza majukumu yake.
Mhe. Naibu Spika, baada ya maelezo hayo, nawaomba Wajumbe wenzangu
wa Baraza lako Tukufu, kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi ya
mwaka wa fedha 2013/2014 jumla ya Tshs 21,318,000,000 kwa kazi za
kawaida, ruzuku, mishahara na maposho na Tshs 6,333,000,000 kwa kazi za
maendeleo.
Mhe. Naibu Spika, nawashukuru sana kwa kunisikiliza na kwa niaba ya
Kamati naunga mkono hoja na naomba kuwasilisha. Ahsante sana. (Makofi).
Mhe. Jaku Hashim Ayoub: Mhe. Naibu Spika, kabla ya yote sina budi
kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyeniwezesha kusimama hapa na kuweza
kutumia pumzi zake alizoweza kuniazima.
81
Baada ya hapo Mhe. Naibu Spika, nataka nimshukuru Mhe. Rais wa Zanzibar
Dr Ali Moh'd Shein kwa kuwajalia wananchi wake wa visiwa vyake Unguja
na Pemba kwa kuthibitisha hilo Mhe. Naibu Spika, hata katika uteuzi wake
wa Mawizira sijui karibu nane au kumi Wizara ya mwanzo alianzia ni Wizara
ya Afya si kama herufi imeanzia (A), hii ni muhimu kwa wananchi wake wa
Zanzibar.
Ushahidi wa hilo Wajumbe wako humu katika Baraza hasa mimi mmoja
ambaye nilikuwa sipati jibu kwa muda mrefu suala la ada ya uzazi. Nilikuwa
nikizungumza kwa muda mrefu na nikathubutu kusema ndani ya Baraza hili
kuna watu wanaweka vitu vyao rehani ikiwemo bangili, simu zao za mkononi,
vyombo vya dhahabu hospitali chini pale ili kupata vitu vya kwenda
kujifungua. Lakini majibu nikayapata hapa mbele kwa Naibu Waziri
hayaridhishi lakini namshukuru Mhe. Dr Ali Moh'd Shein kulipitai hilo na
akaliona suala la ukweli kwa kujali wanancchi wake na kuweza kuliondoa.
Namshukuru sana.
Mhe. Naibu Spika, itakuwa si mwingi wa fadhila kama sijakushukuru wewe
kwa kunipa nafasi hii kuwa wa mwanzo kuchangia kwa siku ya leo.
Mhe. Naibu Spika, kabla ya kuanza mchango wangu kwanza nitataka maelezo
katika sehemu karibu 15.
(1) Ni lini kitengo cha X-ray kitakuwepo huduma muda wa massa 24, ni
kitengo muhimu. Mimi binafsi nimeshakupigiwa simu karibu mara tatu
mpaka nne karibu saa nne usiku mpaka tano nakwenda pale hapana mtu na
kitengo hichi kinalipiwa hivyo mwanzo nitahitaji maelezo.
(2) Sehemu ya Theater ni sehemu muhimu sana, sehemu ya operesheni
nitahitaji maelezo vile vile ni lini mtaweka madaktari masaa 24
kuhudumia kitengo kile. Kunatokea ajali mara nyingi usiku na watu
wanapoteza maisha yao Mhe. Naibu Spika.
(3) Sehemu ya Uzazi bado ni kitendawili mpaka juzi mimi naondoka
pale Mhe. Naibu Spika, pana matatizo, baadhi ya vifaa kuna upungufu. Kuna
nyuzi hizi hata juzi nilizungumza aina ya viclen, mimi ningeomba
zingetengwa pesa kama milioni moja zikanunuliwa, wizara kama haina pesa
akija kujifungua yule mtu atalipia zile ada ndogo ndogo. Lakini inakuwa
usumbufu mgonjwa kenda pale kaingia saa tisa za usiku mtu kishabeba
mimba miezi tisa kufika pale kitu kile hakipo, ni hatari kubwa hii.
(4) Hii inanisikitisha mpaka hivi sasa asubuhi natoka huku Hospitali ya
Mental. Mimi nataka nielewe ile Hospital au ward, milioni mbili
kwa mwezi wanazopewa Mhe. Naibu Spika, ni ndogo sana. Hizi
milioni mbili zigawe kwa mia si zitakuwa sh. 700/= tu kwa siku
atakula kweli mgonjwa yule, si tunawaumiza sisi wenyewe hizo
82
shilingi milioni mbili Mhe. Naibu Spika, hazifiki kwa wakati.
Nitahitaji maelezo hapo Mhe. Waziri.
(5) Kuna upungufu wa walinzi na hicho kimekuwa kilio cha muda mrefu
hata kwenye kamati iliyoongozwa na Mhe. Mwenyekiti mtetezi wa
wanyonge Mhe. Hija Hassan Hija tulitembelea na suala hilo
tukalikuta na tukatoa maagizo.
(6) Risk Allowance za madaktri Hospitali ya Mnazi Mmoja tumepiga
kelele muda mrefu nazo hatujapata taarifa hadi muda huu. Wale watu
wanafanyakazi katika hali hatarishi.
(7) Kuna course za madaktari leo mwezi wa nne mpaka sasa hivi Mhe.
Naibu pika, bado hawajatiliwa kweli ndio wataweza kufanyakazi wale kwa
moyo mkunjufu wala sibahatishi atakapokuja hapa atanieleza Mhe. Waziri.
(8) Jengo la Kitengo cha Macho ni bovu Mhe. Hija Hassan Hija alipiga
kelele sana hapa na hivi sasa kunahatarisha usalama wa lile jengo lenyewe
lilivyo, na hili nitahitaji maelezo.
(9) Mhe. Naibu Spika, mgonjwa anapofika pale kunako sehemu ya
kupokea mgonjwa panakuwa na vigari vya kupakiwa mgonjwa na kupelekwa
juu, leo kuna kigari kimoja tu na hakiendi. Mhe. Naibu Spika, shilingi ngapi
kigari kile kinahitaji au tuwaajiri watu wenye nguvu wachukue wagonjwa
kwa mikono yao wawapeleke juu kule. Nitahitaji maelezo hapo.
(10) Hospitali ya Mnazi Mmoja tangu ilipojengwa mwanzo wake mpaka
leo yale madirisha yanatia huruma yanahitaji bajeti ya shilingi ngapi
ukapita pale chini unamuona mgonjwa anachungulia.
(11) Lini Hospitali ile ya Mnazi Mmoja itakuwa inategemewa kuitwa
hospitali ya Rufaa lakini mimi naona kama ni ndoto.
(12) Ningeomba watendaji wakuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja
wakiongozana na Waziri mwenyewe na Mhe. Naibu Waziri, Katibu
hebu wafanye siku wawapitie wale wagonjwa wakawakague mle
wakaona tatizo ni nini. Aibu Mhe. Naibu Spika, utakaa tu na ma-files
yako juu ya meza yako huwezi kufanya kazi namna hiyo ulifuate file
machozi. Pahali panatia huruma Mhe. Waziri, Naibu Waziri, Katibu
Mkuu na majuzi magharibi saa moja au hivi mbili taa moja
wanatumia madaktari wawili, daktari anatoka pake anakwenda kwa
mweziwe kukaa kufuata taa, bulb imeungua kiza, utendaji kwa kweli
mbovu wa Wizara ya Afya haya mengine hayahitaji bajeti ni
kujituma tu na kujitolea.
(13) Kamati imepita Mhe. Naibu Spika, niliagiza watafutiwe usafiri wa
basi wale mpaka leo hakuna.
Sasa sehemu yangu itahitaji maelezo Mhe. Waziri sasa nitakwenda kwenye
mchango wangu.
Mhe. Naibu Spika, utaratibu unaofanywa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja,
utaratibu huu ni mzuri unasaidia kupunguza msongamano katika hospitali.
Tatizo linakuja katika Vituo vya Afya, hivi zitatoa huduma vipi wakati
83
vitendea kazi havina. Vituo havina mahitaji ya huduma za saa 24 si kutiana
changa la macho Mhe. Naibu Spika, huku. Tufanye jambo tuambizane
wananchi wanatusikia huku usije kufika hapaliwi tukadanganyana. Mtu
anatoka kwenda Mnazi Mmoja anafuata daktari na akifika hayupo kenda kula
mbatata za urojo nje.
Jambo jengine hawa wanafunzi wa Chuo cha Afya kufanya majaribio kwenye
miili ya wagonjwa kama ni majaribio hichi kitu ni hatari, kufanya mazoezi ya
vitendo kwa wagonjwa hii hatari Mhe. Naibu Spika.
Mhe. Naibu Spika, nije kwenye Kitengo cha Dharura. Mpaka sasa Hospitali
ya Mnazi Mmoja haina kitengo cha haraka na dharura. Hili ni tatizo Mhe.
Naibu Spika, wagonjwa wanapopata ajali mshituko wa moyo wakiletwa hapo
wanasubiri masaa kadhaa bila ya kutokea daktari, hayo hayataki hata tochi
Mhe. Naibu Spika, hii inatokana na kutokuwepo kitengo maalumu cha
kushughulikia wagonjwa wa dhahura. Mhe. Waziri atueleze ni lini hospitali
itakuwa na kitengo cha huduma ya dharura.
Nije katika utaratibu wa ulinzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja huu ni wa
kupongezwa na wa kupigiwa mfano. Lakini kampuni gani iliyopewa jukumu
lile na utaratibu wa kupewa kazi ya ulinzi inakuwaje pale. Leo tuna vikosi
vyetu vingeweza kulinda ili kupunguza gharama. Bajeti yenyewe iliyoko
Wizara ya Afya ni ya kusikitisha na kutia huruma na ningeomba sana
Wajumbe wenzangu mimi nimechangia mwazo nina sababu zangu.
Lakini kwa kweli haikidhi tusiwalaumu tu watendaji hawa ndio ukweli
usiofichika, tutamsukumia makombora Mhe. Waziri, Naibu Waziri, Katibu
Mkuu lakini Serikali haiko makini kwa suala hili. Tutapiga makelele mpaka
tutachoka. Hawawezi kulaumika Wizara ya Afya tunawabebesha mzigo
ulikokuwa si wao lakini wapewe nyenzo. Leo kweli zimekatwa pesa za meli
haielekei hasa. Nilipiga kelele sana hapa lakini na Mwanyezi Mungu
alipitisha rehema zake yakajakuonekana ukweli wake, Mwenyezi Mungu
amrehemu Mhe. Hassan Mtondoo amlaze mahali pema peponi naye alipiga
kelele sana hapa.
Mhe. Naibu Spika, ukurasa wa 87 Kazi za kawaida Ruzuku bilioni 6.3 ni kazi
za maendeleo. Hii kweli Wizara ya Afya ni Wizara nyeti kwa nchi hii.
Waheshimiwa Wajumbe tusiwalaumu sana wafanyakazi wa wizara hii, hoja
mimi naomba tuirudishe Wizara ya Afya wakajipange tena.
Mimi si mgeni wa suala hilo nimeshapata majukumu na nishatukanywa kwa
wizara hii. Mwaka juzi kuingia tu mwanzo Wizara ya Afya ilirejeshwa
akataka kushitakiwa muandishi wa habari nikawaambia msimshitaki yeye,
nishitakini mimi ndio niliyezungumza shilingi milioni mia tatu wameshindwa
kutenga miaka miwili mitatu, ulitokea mtihani mzito. Kilitokea ugonjwa wa
kipindupindu tumefadhiliwa na watu wawili tu na mmoja ameshatangulia
mbele ya haki na mmoja yupo, hatuwezi kuchukua rehani maisha ya watu na
kuna magonjwa mengine Mhe. Naibu Spika, huwezi kujua wakati gani
yatakuja kuonekana.
84
Mfano huu Mhe. Naibu Spika, Wizara ilipanga kutumia shilingi bilioni 5.7
kwa kazi za kawaida na bilioni 14.1 kwa mishahara na posho ni bilioni 6.3
kwa kazi za maendeleo, katika Mfuko Mkuu wa Serikali. Wakati ruzuku za
wahisani ni bilioni 1.3 Mhe. Naibu Spika, ukiangalia fedha zilizotengwa za
bajeti kwa mwaka 2012/2013 kiwango cha fedha kilichoingizwa utaona
Wizara ya Afya ina tatizo kubwa la Fedha wanazoomba katika makisio ni
ndogo.
Mfano kiambatanisho namba 17 Idara ya Mfamasia Mkuu wa Serikali,
makadirio ni bilioni 1.5 hadi Machi imeingiziwa milioni 271.4 sawa na
asilimia 17.55. Idara ya Utumishi na Uendeshaji Pemba makadirio shilingi
mia moja sitini na tano milioni, hadi Machi wameingiziwa shilingi milioni 64,
hebu nambie Mhe. Naibu Spika. Mkemia Mkuu Pemba milioni 20 makadirio
hadi Machi kaingiziwa shilingi nne laki tisa. Tutakwenda kweli, sawa na
asilimia 24.6.
Idara ya Mipango Unguja makadirio ni milioni mmoja thalathini na mbili hadi
Machi wamepewa shilingi milioni 41.3. Bajeti hii tunapitisha na posho na
vikao lakini matumizi ya kuwezesha kuondoa kero katika huduma ya afya
bado ufumbuzi haujapatikana.
Mhe. Naibu Spika, ripoti ya Utelezaji wa Malengo ya Wizara katika kipindi
cha Oktoba mwaka jana inaonesha wahisani wameanza kuondoka na hili ni
tatizo kubwa, litaloweza kutu-cost sisi. Sasa hivi wahisani wameshaza
kufunga virago ambao walikuwa wachangiaji wakubwa wa madawa.
Mhe. Naibu Spika kuna ripoti hii ambayo ni ya kusikitisha Ripoti ya
Utekelezaji wa Malengo Wizara ya Afya katika kipindi cha Oktoba mpaka
Disemba katika mwaka uliopita jumla bilioni 1.2 zilihitajiwa hazikupatikana
katika mfuko, badala yake zilipatikana shilingi mia 530 milioni sawa na
asilimia 25, kiwango ambacho Mhe. Naibu Spika, ni kidogo sana. UNICEF
walikuwa wachangie shilingi milioni mia moja na sitini milioni hawakutoa
kitu, Global Fund hawakutoa kitu, DANIDA walikuwa watoe shilingi bilioni
1.1 wametoa shilingi milioni mia 500 na DANIDA nasikia wako njiani mwaka
2014 wanaondoka.
Wizara hapa lazima iongeze pesa katika kitengo cha madawa. Kama
hatukuwa makini tutapiga makofi tu hapa tutakuwa tunabeba jukumu.
Kitengo hichi kiongezwe mara mbili kutokana na bajeti iliokuwepo hivi sasa
lazima iongezwe mara mbili. Vyenginevyo narudia tena yale yale
tutawalaumu watendaji wa Wizara ya Afya, Waziri, Naibu Waziri, Katibu
Kuu na Wakurugenzi bila ya kuwa na nyenzo za kazi hawawezi kufanyakazi
hawa.
Lakini jambo la kusikitisha Mhe. Naibu Spika, kama wanavyosema
Waswahili kuwa anayebebwa na yeye mwenyewe hujikaza. Serikali nao hapa
ilitakiwa ichangie hadi Disemba shilingi milioni 150 lakini kwa mshangao
imetoa milioni 30 tu. Ndipo niliposema kwamba anayebebwa naye hujikaza.
Serikali ilikuwa inatakiwa itoe mfano na anayekuja naye aone haya.
85
Mhe. Naibu Spika, mfuko huu ndio unaotoa huduma muhimu za tiba hasa za
Chanjo za Mama Wajawazito na Watoto. Kama fedha hazipatikani kutoka wa
wahisani mfumko wa dawa safari hii ukutakuwa mkubwa, upangiwe dawa za
kutosha iwekwe mara mbili bajeti yake.
Mhe. Naibu Spika, ukurasa wa 49 chombo hiki kina umuhimu sana kwa
sababu bila ya wauguzi hospitali inakuwa haijakamilika. Lakini jambo la
kusikitisha wauguzi wetu wamekuwa wakivunjwa moyo na viongozi wetu.
Hivi majuzi tu wauguzi hawa walifanya sherehe lakini cha kusikitisha na cha
kutia aibu hakuna kiongozi hata mmoja wa Wizara ya Afya aliyekwenda
kujumuika nao, si Waziri, si Naibu Waziri wala si Katibu Mkuu si
Wakurugenzi ilikuwa ni siku wa wauguzi duninai. Kwa unyonge mkubwa
sana kwa sababu Mhe. Waziri na Naibu Waziri hawakushirikishwa
hawakupewa taarifa katika maazimisho hayo na kusababisha mgeni rasmi
kugoma kusoma hotuba yake, ilikuwa Maisara juzi hapa Mhe. Naibu Spika.
Nije katika Bodi ya Chakula na Vipodozi ukurasa wa 47. Mhe. Naibu Spika,
nazungumza ukaguzi wa maduka, maghala na chakula, hoteli na mikahawa.
Lakini cha kusikitisha Zanzibar hivi sasa kuna tatizo kubwa la kuanza kuuza
vyakula vilivyokwisha muda wake hasa vya makopo, utakuta pale Darajani
soda tatu za kibati zinauzwa elfu moja badala ya soda ile moja shilingi elfu
moja.
Mhe. Naibu Spika, nije katika hii hospitali yetu inayotaka kuitwa ya Rufaa.
Narudia tena itakuwa ni ndoto. Nije katika sehemu ya watoto. Mhe. Naibu
Spika, hivi sasa kitanda kimoja wanalala watoto watatu, mabomba ya vyoo
hayafanyi kazi sehemu ya watoto hiyo viti vya madaktari hazisemeki. Mhe.
Naibu Spika, kuna dawa hii ya vidonda inaitwa Povidon haipo, kuna dawa ya
mtoto inaitwa Ventolin haipo na muhimu sana mtoto anapopata ajali au
kaletwa mtu pale inaitwa manitol drop haipo katika ward ya watoto. Nirudi
katika sehemu ya ICU pale kuna vein machine ni mbili tu katika sehemu hiyo
ambapo vitanda sita vilivyokuwepo. Ndio nikasema bado ICU haijakamilika
na hiki kitengo ni muhimu mashine hizi za mapigo ya moyo mbili tu ndio
zinazofanyakazi na vitanda ni sita.
Mhe. Naibu Spika: Zimebaki dakika tano.
Mhe. Jaku Hashim Ayoub:Mhe. Naibu Spika, kuna kitengo hiki cha EEG,
hichi kinatoa huduma kwa masaa matatu tu na siku zenyewe ni Jumatatu,
Jumanne na Jumatano, saa 2 mpaka saa 5 hichi kitengo ni muhimu na kazi
zake ni kubwa.
La mwisho Mhe. Naibu Spika, wagonjwa wetu wanapokwenda pale wanapata
tabu kuingia hospitali ya Mnazi Mmoja. Wale wana haki yao hospitali au
wizara iandae utaratibu maalum wa kuwatafutia pahali wakajifiche wale watu
wanapata mvua, jua. Kwa hivyo na hapa nitahitaji maelezo. Mhe. Waziri pale
wasifukuzwe tu wale watu wana wagonjwa wao hawakutaka kuja kutembea
pale shida ndio iliyowaleta pale na matatizo.
86
Kuna kitengo cha Chanjo, hivi majuzi kimefanya kazi mwaka jana
wafanyakazi hawa walilipwa mshahara huko mashamba walinipa salamu
niwaulizie watapata chochote au hawapati au wamejitolea fisabilillahi. Kwa
hayo, Mhe. Naibu Spika, sitounga mkono hoja hii na Wajumbe wenzangu
nakunasihini sana kila anayeinuka hapa aitizame bajeti hii ni ndogo sana.
Narudia tena tusiwategemee wahisani, wahisani wameshaanza kukunja virago
bajeti hii naomba kila anayekuja hapa tuirudishe mpaka ijipange tena Serikali.
Vyenginevyo tutakuwa tunawatesa wananchi tu tunawalaumu tena watendaji
hawa bila ya kupewa nyenzo hawawezi kufanya kitu. Kila anayeinuka hapa
nasaha zangu asiunge mkono bajeti hii mpaka ikajipange tena Serikali, fedha
ni ndogo walizopewa hizi hazifanyi kitu, tutawalaumu bure na tutaendelea
kulaumu. Ahsante sana Mhe. Naibu Spika. (Makofi).
Mhe. Makame Mshimba Mbarouk: Mhe. Naibu Spika, ahsante sana na
mimi kuweza kunipa nafasi hii niwe mtu wa pili kwa kuweza kuichangia
bajeti hii ya Wizara ya Afya.
Mhe. Naibu Spika, mimi siku zote napenda panapo zuri niseme zuri na
panapo baya niseme ubaya.
Lakini nimshukuru sana Mhe. Waziri wangu leo kwa mara ya kwanza na
kukiri kusema kwamba bado hatujawa na Hospitali ya Rufaa tutapokamilika
ndipo tutakuwa na Hospitali ya Rufaa. Hapo Mhe. Waziri nakushukuru sana
kuwa zile kauli zetu tunazosema kumbe mnakuwa mnaziona lakini
mnatupinga kwa kuwa mawaziri tu ndio wenye uwezo wa kusema.
Mhe. Naibu Spika, mara nyingi sana husema kuna wizara haiko makini katika
utendaji wake kuwatekelezea kwenye bajeti. Hilo ni kweli sio siri wizara hizi
ambazo ni muhimu sana na tuwaongozee sana wizara zile zinazoshughulika
na jamii, kutowaingizia bajeti kamili bila ya kuwapunguzia Mhe. Naibu
Spika, ni kweli inakuwa hitilafu kubwa na kasoro zinajitokeza katika utendaji.
Mhe. Naibu Spika, hilo mimi nakiri na naiomba sana na mtu ambaye
aliyechukua nafasi ya Waziri wa Fedha alione hilo suala, ili waweze
kuwakamilishia hawa watu. Kwa kusema tu Mhe. Naibu Spika, ukweli ulivyo
nimesikitika sana na fungu hili la kasma hii ya likizo. Kifungu 21104 kama
kweli macho yangu naona kama kuna milioni moja ya likizo. Sasa sijui vipi
hiyo Mhe. Naibu Spika, hapa ni kuwachezea na kuwafanyia utani
wafanyakazi wa Wizara hii ya Afya.
Lakini la kusikitisha zaidi labda inawezekana hii ni mia moja lakini kwa
niliovyoona hii ni milioni moja ya likizo amepewa Mhe. Waziri kwa wizara
yake. Sasa hili mimi naomba sana liangaliwe ndio maana nikasema kuwa
tunawatania au tunawachezea hawa wenzetu katika wizara hii. Sasa Mhe.
Waziri utakuja kunisahihisha kama ni milioni mia moja au milioni moja,
mimi binadamu leo sikuvaa miwani, kwa hiyo baadae kifungu hicho cha
kasma cha likizo.
Mhe. Naibu Spika, niende ukurasa wa 11 Kitengo cha Afya Bandarini. Mimi
naomba sana Mhe. Waziri tuwe serious na kitengo hichi kwa kukisaidia vifaa
87
vyote vinavyohusika vinavyokwenda na wakati vya uchunguzi na upembuzi.
Tunaomba sana hichi tukipe kipaumbele nacho kwa kuwa walinzi wa
kuangalia matatizo ya mwanzo yanayoingia nchini. Sasa kama leo
hatutokuwa na vifaa vya kisasa itakuwa kazi yetu bure na tutasema kuwa
haina maana kitengo hicho kuwepo hapo.
Lakini Mhe. Naibu Spika, ukurasa wa 14 sehemu ya huduma Kitengo cha
Macho. Mhe. Naibu Spika, hawa
Nam.607
IMESAHIHISHWA
Mhe. Makame Mshimba Mbarouk: (Anaendelea) ukurasa wa 14 sehemu ya
huduma ya kitengo cha macho. Mhe. Naibu Spika, niwashukuru sana hawa
kuanzia ma-experts wetu wa hapa Zanzibar pamoja na wataalamu wa Kichina.
Mhe. Naibu Spika, ni mahodari sana na wanajitahidi sana kuwaokoa wenye
matatizo ya macho ambayo yanatuingia mara kwa mara kutokana na vyakula
tunavyokula ni vibovu.
Mhe. Naibu Spika, kwa kweli wanajitahidi sana na wanajaribu kuokoa macho
yetu ili kuweza kuona, lakini ukiiangalia ile sehemu yao ni ya hatari zaidi na
niliisemea sana mwaka jana katika bajeti yao. Hivi sasa nimeambiwa
wameshahamishwa wanapelekwa sijui Kibweni kule. Mhe. Naibu Spika, lile
jengo linakwenda na maji. Pamoja na hayo naomba sana Mhe. Waziri
tuwaangalie kwa ufanisi zaidi na kuweza kuwatekelezea mahitaji yao.
Mhe. Naibu Spika, hiki kitengo ni muhimu na kina zana za kisasa na
hazitakiwi kutembezwa huku na huku, ukizipeleka huku na huku mwisho
zitakuwa na matatizo katika ufanyajikazi wake, hazitakiwi ziondolewe mara
kwa mara, zinatakiwa zikikaa pahali iwe zimekaa pale pale. Hili ni moja
ambalo tuliangalie kwa uangalifu na kwa umakini kabisa jengo hili tufanye
kila hila na ikiwezekana, kuna mafungu mengine makubwa humu
tuyapunguze ili tuwarudishie watu wa Hazina watusaidie kutuwekea fungu
jengine kwa kufuata pale marekebisho ya haraka sana katika kitengo hiki.
Mhe. Naibu Spika, nikiendelea na huduma ambazo zina umuhimu sana hasa
katika hospitali yetu hii, niingie katika ukurasa wa 25 kuhusu Idara ya
Hospitali ya Mnazi Mmoja. Mhe. Naibu Spika, kuna mambo mengi sana
yametajwa humu kwenye kifungu hiki, hospitali ya Mnazi Mmoja yenyewe,
huku kuna Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja yenyewe.
88
Nakwenda huku na huku Mhe. Naibu Spika, kote nitachangia, litakalokuwa la
huku wataligawa wenyewe na litakalokuwa la huku wataligawa wao. Mhe.
Naibu Spika, hapa ndipo nilipokuwa nataka kusema, naomba sana niseme
kwa unyonge sana na kutokana na hali yetu. Mimi siendi kule Hospitali ya
Mnazi Mmoja kwa umbea, wala si sehemu ya kusema kuna disko, wala sio
sehemu ya kusema kuna swimming pool, niende nikakoge na wala sisemi kule
niende nikaangalie rusha roho. Mhe. Naibu Spika, nakwenda kule kwa
matatizo ya wananchi wetu, naomba sana nieleweke. Kuna mambo nayaona
mimi mwenyewe kabisa.
Mhe. Naibu Spika, mimi nina uzoefu mmoja, hili nasema Mwenyezi Mungu
kanijaalia. Sikusoma kama walivyosoma watu lakini mtu niletewe wa PhD na
mimi elimu yangu niliyoipata kwenye vibanda vya Baja, basi nitamshinda wa
PhD. Kwa sababu kitu chochote Mhe. Naibu Spika, ukikikubali ndani ya nafsi
yako tayari wewe unapata kujua. Kitu chochote tu Mhe. Naibu Spika,
ukishakikubali basi na kile kitu kinakukubali ndani ya nafsi yako kwa nini
usijue, neno dogo utaweza kulijua kubwa.
Mhe. Naibu Spika, mimi siku moja nilisema hivi, naomba sana nimnukuu
babu yangu Mhe. Juma Duni, alikasirika tu lakini hakutaka kupata ukweli,
pamoja na mimi aliniambia sikutaka ukweli, lakini nakubaliana nayo hiyo ni
sawa. Mimi ni kama wakili namchokoza mtu wangu ili nione points zake
atakuja kunijibu vipi.
Katika Hansard hii nimshukuru sana babu Juma Duni, nilifikiria atanitia
makosani. Amejibu vizuri sana na kwa uangalifu, kumbe yale yote
niliyoyasema yako juu ya alama na yako sahihi. Kwa nini nikasema hivyo.
Mhe. Naibu Spika, Mhe. Waziri alisema humu kuhusu shuka la kuwawekea
wagonjwa kwenye theatre, aliniambia kuwa hivyo vitu vipo na Babu Juma
usidanganywe, nina ushahidi tosha. Nilikuwa na mgonjwa wangu alikuwa na
matatizo ya mkojo, nilikwenda kusikiliza kwa nini leo huyu hakufanyiwa
upasuaji. Jibu likatoka unamuona huyu tunamtoa, imekosekana nguo ya
kufunikiwa. Sasa niseme uongo kwa kutaka nini Babu Juma, wananiambia
hivi na nimeona. Mimi nilifikiria kwa sababu kuna mambo mawili katika
upasuaji, inawezekana presha imepanda labda kwa kitu hicho mgonjwa
anaweza akarejeshwa. Lakini jambo la pili nguo zikikosekana sio kanzu ya
kuchukua nyumbani ukaipeleka pale ukamfunika. Kuna taratibu zake, haiwi
viatu tu katika eneo lile unaambiwa uvuwe, je nguo uichukuwe nyumbani
ulete pale, utaongeza virus.
Kwa hivyo, Mhe. Naibu Spika, naomba sana tunapowaambia hawa mawaziri,
hebu wakae wafikiri huyu mtu kaniambia ni kweli hili jambo au basi tu. Mhe.
89
Waziri mimi sitaki nafasi yako ya Uwaziri wa Afya, siutaki hata siku moja
nikuambie, wala sitaki nafasi ya Naibu Waziri wa Afya siitaki. Leo babu
Juma ukisema unajiuzulu na naibu wako jiuzuluni, lakini mimi siitaki nafasi
hiyo, si mchezo. Mhe. Naibu Spika, nakuomba sana kwamba watufahamu.
Mhe. Naibu Spika, Hospitali yetu ya Mnazi Mmoja ina mapungufu sana tena
makubwa sana. Mwenzangu alipitia, sasa na mimi naingia ndani. Mhe. Naibu
Spika, kulikuwa na kitanda cha upasuaji kimoja kilikuwa kibovu na
waniambie, nimekiona kitanda kinakokotwa kinaletwa juu. Haya niambieni,
sisi leo tunakusaidieni. Sio vibaya ukiniambia kweli mheshimiwa kitanda
kibovu lakini Wizara ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo
haikunitilia pesa nikakamilisha, nitakuwa mimi nampigia debe nani?
nakupigia debe wewe kuikamata serikali, kwa nini isikutilie fedha kwenye
jambo hilo. Hamtaki kukubali hivyo.
Mhe. Naibu Spika, leo humu kuna ukurasa ambao Mhe. Waziri anasema
kuwa bado anatafuta fedha za kutaka kununua vifaa vya uchunguzi wa
cancer, hapa ndipo ninapokuja, hili suala linanisikitisha sana. Babu Juma
ukubali na picha ninazo mpaka leo zile mashine naomba bora mkazipeleke
kwenye ma-scrape kule mkauze, nakubaliana hilo kuwa mpaka leo mashine
zile hazina catalogue, catalogue iliyoletwa hailingani na mashine. Babu Juma
unaogopa nini?
Juzi mama Waziri pale Bi. Fatma Mjasiri alikubali nilipomchokoza suala
kama hili kwa walemavu dawa zao zimechakachuliwa. Akakubali, akawa
wazi pale. Kwa hivyo, leo nataka uwe wazi na wewe. Amekwenda Makamu
wa Kwanza wamempiga changa la macho, amekwenda Makamu wa Pili
mmemdanganya, bado mpaka leo mashine zile Mhe. Waziri kubali kosa
liseme na likubali kuwa kweli alipewa mtu tender siye ambaye ni maalum
kwa masuala kama yale, haya ndio yanayotuuma sisi. Unaambiwa mashine
zimechunika, mashine zikachunike mpaka leo zisifanye kazi, tia rangi kama
zimechunika ili zifanyekazi.
Mhe. Naibu Spika, nataka nikuambia sasa hivi sijui ni mara ya ngapi mimi
nalipa fedha ya kwenda kuchunguzwa wananchi wangu wa Jimbo la Kitope.
Mimi naomba sana Mhe. Waziri kama hamtaki mimi nije kule hospitali basi
nendeni Jimbo la Kitope, kawaambieni huyu mtu hatumtaki asije hospitali
kuwauguzeni, tutakutibuni sisi, basi mimi sitofika hospitali. Lakini
haiwezekani nione fedha za wafadhili zinaletwa kwa makusudio ya
kuwasaidia wananchi wetu waliokuwa katika hali ngumu, halafu baadae watu
tu wakajichumie matumboni wakila, mimi sikubaliani na Babu Juma.
90
Babu Juma mimi hili silikubali kabisa tena munipe sababu maalum kubwa
sana, pamoja na kuwa wewe umeniambia kuwa nithibitishe rushwa. Hapa
automatically sio lazima rushwa useme fulani, mpaka leo hii mwaka jana
naisema hadithi hiyo hiyo na wewe unaniahidi kuwa utachukua tume kutoka
Dar es Salaam na mimi utaniita pale niangalie. Je, umeniita, hujaniita. Sasa
mimi nitasema nini, nitasema rushwa ipo, kwa nadharia hiyo nitasema rushwa
ipo. Lakini kwa nini Mhe. Waziri asiitwe yule mtu aliyeleta vile vifaa
tukamwambia hivi, bwana wee! vifaa havijakamilika, kuna visu hamna na
kuna kitu fulani hamna katukamilishie, kwani mnaona tabu gani kama sio
nadharia ya rushwa, kwa sababu atawaambia wale nipeni na mimi
nilichokupeni asilimia 10, ndio ugumu na mvutano wenyewe uko hapa. Babu
Juma usione tabu njoo niambie Mwenyezi Mungu atakupa fungu lako, usione
tabu usiwaweke hawa watu wabaya.
Sasa hayo ndio tunayolalamika sisi wananchi tumeshika msahafu pale na
tukasema kuwa tutawatendea wananchi kwa kila haki yote, Ewe Mwenyezi
Mungu nisaidie, ogopa hiyo na leo ulianza kwa Bismillah. Sasa nitaomba
ulianza kwa kutaja jina la Mwenyezi Mungu kuwa ulisema ripoti yako ni ya
uhakika na utajibu maneno ambayo ni ya uhakika moja hilo. Naomba sana
Mhe. Naibu Spika, tuweke kanuni kando kama itawezekana zile mashine
ziletwe na zikiletwa hapa kama zikiwa complete mimi naomba Mhe.Naibu
Spika, nitajiuzulu niko tayari kuliachia jimbo, ziletwe hapa mashine,
wanasheria kama wapo, hiyo sheria kanuni kuweka kando mashine ziletwe,
sasa naomba Baraza lako tukufu Mhe. Naibu Spika, mashine ziletwe ndani ya
ukumbi huu ili tuone nasema kweli au fitna tu, utaniangalia Mhe.Naibu Spika,
angalia hilo suala.
Mhe. Naibu Spika, sasa niende katika insulin. Leo nimekuja na quality za
insulin ninazitoa kwa heshima yako. Hii insulin ambayo waliyoizoea
wagonjwa na hii insulin ambayo tumeipigia kelele, hebu iangalieni sample
nyie wenyewe mtaona ipi big quality, materials na vitu viliomo humu
automatical utaona, leo nasema hii hapa. Mimi nauliza kitu kimoja
Mheshimiwa wangu hapa nakwenda kidogo kidogo sasa hivi. Mhe. Naibu
Spika, kule kuna kitengo maalumu, mimi juzi nilivyosema sikimtaja daktari
gani anayehusika sikusema katika Hansard yangu tafuteni lakini nilisema kwa
uchungu tu. Mimi naamini sababu zipi Mhe. Waziri, ukaitisha tenda bila ya
kumuona daktari muhusika na wagonjwa wako ukawaambia jamani eeeh!
tunatoa tenda ya insulin ambayo sasa hivi na ile ya zamani hatuitaki tena, ni
sababu zipi uje unipe sababu.
Mhe. Naibu Spika, mimi nashangaa sana, utakuta mtu engineer wa nyumba,
engineer wa kutengeneza barabara za reli, wewe unataka kutengeneza
barabara, unafikiria unakwenda kuwauliza wale engineers wa nyumba na
91
engineer wa reli utapata jibu, hupati jibu hata siku moja, kwa sababu kuwa
wale sio specialist wa mambo kama yale. Naomba sana Babu Juma
wasikuchanganye nisikilize mimi. Unajua sasa hivi hii dawa imeshaathiri
watu na tena nakwambia sikwambii kwa uficho na watafute hawa wazee
wako tayari hata ukiwapigia simu, hii dawa imeshawaathiri watu na pale kwa
nini nyinyi mnataka mtu akenda kuchukua dawa aandike namba ya simu kwa
sababu gani, haidhuru ndio utaratibu wa kuchukua dawa, lakini kwa nini?
Mhe. Naibu Spika, naomba sana Mhe. Waziri Babu Juma sikupingi sana
lakini naomba sasa nisome Hansard yako kama hivi;
"Mhe. Spika, naomba niwaeleze na nimueleze Mhe. Mshimba
kwamba hao aliowaeleza hawa kwamba ni mabingwa wa tiba hii ya Dr.
Kaushid na Professor Sawi niliwaita mimi"
Mhe. Naibu Spika, naomba unisikilize kwa makini hapo. Narudia tena hii ni
Hansard ya Mhe. Waziri wa Afya alipokuja kunijibu. Mhe. Waziri alikubali
kwa maana hiyo kuwa kweli kikao cha tarehe 12 kilikuwepo, nimshukuru
kwa hilo. Anasema aliwaita yeye mwenyewe kutafuta ushauri wa kitabibu,
hawakuitwa na daktari wa kisukari kama ilivyoelezwa. Mimi sikusema hivyo.
Lakini sawa na iwe hivyo hivyo, nilipofanya kikao hicho na wataalamu wa
wizara ambao nao ni madaktari kama huyo wa kisukari akiwemo Katibu
Mkuu mwenyewe na Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja na daktari
wetu huyo wa kisukari wote walikuwepo wakati wa mjadala wa Dk. Kaushid,
aliulizwa swali la moja kwa moja. Je, wewe mtaalamu wa tiba dawa hii inafaa
au haifai. Dk. Kaushid alishindwa kutupa jibu la moja kwa moja kwamba
haifai. Hakutoa jibu la moja kwa moja kuwa haifai au inafaa. Lakini sasa
sikiliza kitu chengine kinakuja.
Isipokuwa alisema kwa baadhi ya nchi kama USA, Uingereza na WHO
hawajathibitisha. Sasa si ndio walimwengu hao, si ndio wenye nchi hao WHO
nani asiyewajua, USA nani asiyeijua, Uingereza nani asiyeijua. Amekiri yeye
mwenyewe babu yangu namshukuru sana kwa maelezo yake ya Hasarnd hii
humu. Lakini naendelea na kikao baada ya kikao tulimuomba atuletee ushauri
wake kwa maandishi. Alikaa kimya hata baadae kumuhimiza mara mbili.
Namshukuru sana Babu Juma Duni, alimuhimiza huyo Professor anasema
kuwa baada ya mkutano wake na mimi nilimuomba aniletee ripoti yake,
mwishowe aliniletea ripoti hiyo kwa mtandao na wala hakuitia saini na ndio
maana Mhe. Mshimba aliyopewa na anaitumia kwamba ndicho kielelezo cha
udhaifu wetu wa kukataa ushauri wa bingwa.
Babu Juma umefanya haraka Mhe. Waziri, ungesubiri ile barua ya mtaalamu
alete
92
Mhe. Naibu Spika: Umwite Mhe. Waziri.
Mhe. Makame Mshimba Mbarouk: Aaah! Babu Juma, samahani.
Mhe. Naibu Spika: Babu Juma mwite mitaani huko.
Mhe. Makame Mshimba Mbarouk: Ahsante. Mhe. Waziri nakushukuru
sana kumbe hujahamaki, naendelea na maelezo yangu.
Mhe. Naibu Spika, mimi namuambia Mhe. Waziri ilikuwa yeye asubiri
kwanza.
Kifungu chengine,
"Mhe. Spika, baada ya kupata maelezo ya kitabibu ya wizara iliomba
tena ushauri kwa wasimamizi wa kujadili dawa ya Serikali ya Muungano
hapa kwetu Zanzibar, wao kwa pamoja walijibu kwamba dawa hii
imesajiliwa".
Hee! huyu msimamizi ndio professor. Kumbe kapata ushauri kwa
wasimamizi sio kwa wale wataalamu aliowaita yeye mwenyewe kwa mujibu
wa kupata jibu. Hapa namuomba sana Mhe. Waziri sina nia mbaya na yeye,
sitaki nikuzuilie fungu lakini hapa nakuzuilia fungu na mshahara wako
nauzuia kutokana na maelezo haya yameniudhi sana Mhe. Waziri Babu Juma.
Samahani nimekuzoea babu yangu.
Mhe. Naibu Spika, hapa ndipo nitakapoweza kuzuia fungu ili kuweza kupata
ufafanuzi wa kutosha. Mhe. Naibu Spika, nina wagonjwa ambao tayari dawa
hiyo imewadhuru, nikisema Bwana Juma Ame Juma wa Chukwani na yeye
dawa hii imemdhuru, Bibi Safia Mohamed miaka 40 wa Kikwajuni na yeye
dawa hii imemdhuru na amesema kuwa dawa hii hatoweza kuitumia kuntum.
Naomba sana Mhe. Waziri usiambiwe jambo ukalikubali moja kwa moja bila
ya kupata ushauri, nakuomba sana ukae na washauri wako husika wataalamu
wetu kabla hawajatukimbia ili ukae nao kuliko watu wengine.
Kwa sababu Mhe. Waziri tulichokifanya kimoja serikali ambacho ni kibaya
sana Mhe. Naibu Spika, Mkurugenzi wa Mnazi Mmoja ni specialist wa
mambo ya usingizi, tuna Surgery ambapo yeye ni Mkurugenzi, tuna Katibu
Mkuu ni professor, ni daktari anajulikana wapi na wapi. Leo tunakwenda
kumpa Ukatibu Mkuu, hapa tumefanya kosa moja kubwa sana serikali, lakini
ndio mambo tumefanya tu na ukiangalia hospitalini hatuna tena wengine
baada ya hao, sio kama hatuna hatuna. Unafikiria watakalia wapi, watakalia
juu kwenda kwa serikali wale wenzao watawakandamiza.
93
Mhe. Naibu Spika, kuhusu mafao ya madaktari wetu. Wenzetu Bara sasa hivi
wanapata mishahara mizuri, naomba sana Mhe. Waziri aangalie mafao yao.
Mhe. Naibu Spika, kuna matatizo ya orderlies na nurses. Hawa huduma ya
kwanza wanaanza wao, halafu baadae ndio anaitwa daktari muhusika.
Mhe. Naibu Spika, kuhusu risk allowance yao hawa, mwenzangu kishaisema
sitaki niirejee. Kuna watu wanapata matatizo na wengine wanapata TB katika
utibabu mpaka leo haki zao wanashindwa kupewa. Mhe. Waziri tunaomba
sana hilo suala lazima Mhe. Naibu Spika
Mhe. Naibu Spika: Bado dakika tano.
Mhe. Makame Mshimba Mbarouk:Namalizia. Mhe. Naibu Spika, nilisema
kuwa ma-nurses, ma-ordelies bado na madaktari wenyewe tugeuke, hizi
scheme of services bado hazijakidhi haja kwa wao wana kazi kubwa,
wanafanyakazi masaa 24 na wanajitahidi kadri ya umaskini wao pamoja na
kuwa hawana vitendea kazi. Naomba sana Mhe. Naibu Spika, kwamba hili
suala liongezwe fungu ili Mhe. Waziri aweze kuwasaidia hawa watu ili
wapate kufanyakazi kwa uangalifu sana.
Mhe. Naibu Spika, inasikitisha sana kama hamtowaangalia hawa watu wetu.
Sasa hivi niwashukuru sana kuwa kuna baadhi ya nguo zimeoneshwa kuwa
zimerudishwa kwenye makontena. Lakini Mhe. Waziri vyakula bado, sijui
kama ule unga mpaka leo kama umesharejeshwa? Mimi siogopi kusema
bwana, kama ule unga haujaondoshwa bandarini kauondoweni bwana, mimi
siogopi kusema kwa sababu nawatetea wananchi, wananchi ndio wamenileta
hapa ili niwatetee wao, tena mwenye kununa, asiyenuna shauri yake. Lakini
nitasema jambo la ukweli, kama ule unga haujaondoshwa basi uondoweni,
kwa nini mmeweza kurudisha mitumba ya nguo na mitumba ya friji kwa
sababu haiko katika quality, mshindwe kuuondoa unga, uondoweni bwana,
mimi siogopi kabisa, nasema uondoweni mara moja tusije tukafa
Wazanzibari. Wazanzibari tunapata maradhi kutokana na vitu sio standard,
ndio maana cancer zinakuwa nyingi, mnatafuta nini, msitafute kitu hamna
utafiti wa kutafuta. Vyakula vibovu vimekwisha muda wake, mnatuleta tule
hapa Wazanzibari tufe. Sasa unafikiria vipi, ni lazima hiyo tunasema kwamba
ishirikishwe.
Mhe. Naibu Spika, kwa kukidhi muda wako, mimi naomba sana kuwa
wananchi wangu waangalie wale member wa sukari, hii ndio tunaitaka, hii
chukuweni wenyewe, tunaitaka hii dawa, hii dawa ndio quality, dawa
iliyomzowea mwenyewe mgonjwa anaitaka hii, msimlazimishe mwachieni
94
huru, waachieni wenyewe watumie, Usiitishe tender bila ya kuwaita wenyewe
wanaohusika, hilo ndio kosa lenyewe Mhe. Waziri.
Mhe. Naibu Spika, kwa hayo machache naizuia bajeti hii, sitomruhusu Mhe.
Waziri atumie. Mhe. Waziri sitomruhusu atumie mpaka anipe maneno
mazuri, asikubali kufuata maneno ya wataalamu ajiangalie mwenyewe katika
qualification zake. Maana yake wakati mmoja Mhe. Naibu Spika, ngoja
kidogo alikuwa akipenda kusema zamani madudu, kumbe madudu yamo
kwenye wizara yake. Lugha hii akipenda sana kuitumia Mhe. Waziri na mimi
nilikuwa nikiwapenda zamani watu wangu hawa watatu. Mhe. Haji Faki
Shaali wakati ule tukishirikiana naye katika kujibu maneno yake, Mhe.
Abubakar Khamis walikuwa wakijibu vizuri wakati ule.
Sasa na sisi Mhe. Waziri zamu yako kuwa madudu yamo ndani ya wizara
yako. Mhe. Naibu Spika, naondoa shilingi yangu, ahsante.
Mhe. Suleiman Hemed Khamis: Mhe. Naibu Spika, nakushukuru kwa
kunipatia nafasi na mimi kuweza kutoa mchango wangu katika wizara hii
kubwa sana ambayo imepewa majukumu makubwa sana ya utekelezaji.
Mhe. Naibu Spika, niseme kwa ufupi kwamba Wizara hii ya Afya ina
majukumu ya kusimamia utoaji wa huduma za afya, ikiwemo kutoa ushauri
wa wagonjwa, kutoa elimu ya afya na kutoa matibabu. Haya ni moja katika
majukumu ya Wizara hii ya Afya na ni majukumu makubwa.
Mhe. Naibu Spika, mimi nilitegemea kwamba wizara hii kubwa iliyo na
majukumu mazito, nilitegemea kwamba Mhe. Waziri wa Fedha, Uchumi na
Mipango ya Maendeleo tutakuwa naye hapa, kwa sababu kuizungumza
wizara hii, bila ya kuwepo Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango ya
Maendeleo sio jambo zuri, kwa hapa pana matatizo makubwa katika
kuyatekeleza majukumu haya. Kwa hivyo, nasikitika kwamba Waziri wa
Fedha hayupo ili asikie kilio cha watu waliokuwemo humu ndani. Kwa hivyo,
pamoja na kutoa ushauri, pamoja na elimu na utibabu. Pia utakuta kwamba
utibabu huu umo ndani ya nchi lakini pia wizara inahusika na utoaji wa
utibabu wa nje na inaonesha kwamba wizara hii haina ubaguzi, inafanyakazi
zake vizuri bila ya kuwa wanaotaka kuhudumiwa wana ubaguzi wa aina
yoyote, watu wanatolewa huduma sawa kwa sawa, haki sawa kwa
wote.(Makofi)
Mhe. Naibu Spika, inatoa huduma za kinga vile vile na maradhi ya
kuambukiza ambayo ni majukumu makubwa sana, inaangalia pia vifo vya
watoto wachanga ambao haya yanatokana na mama zao wakati wa
kujifungua, wanakabiliwa na matatizo makubwa sana hasa watoto wachanga.
95
Vile vile wanahitaji katika fedha hii kuwa iwe nyingi lazima kuwe na vifaa
vya kutosha na inavyoonesha baada ya kuisoma hii kwamba katika kupewa
kiwango cha fedha ni kidogo sana hakitoshi kabisa. Hii ni wizara kubwa na
inahitaji fedha nyingi ili kuweza kufanikisha malengo ya wizara hii.
Mhe. Naibu Spika, katika mambo mengine ambayo nahisi yana jukumu
kutokana na maradhi mbali mbali ya homa kali sana, pamoja na hayo mengine
ambayo tumepata taarifa hapa kwamba kesi za Ukimwi katika nchi hii
zimekuwa ni nyingi bado zinaendelea, pamoja na wao kusema kwamba
zinapungua, lakini wakati huo huo bado kesi zinaendelea kwa wingi, pamoja
na kusema kwamba kesi za wagonjwa 6,906 wamesajiliwa kwenye clinic 10,
ambazo sita zikiwa hapa Unguja na nne zikiwa Pemba. Wagonjwa 4,000
wanatumia dawa za ARV na watoto ambao ni wengi sio chini ya watoto 392,
bado wanaendelea kupata matibabu kutokana na mama zao.
Mhe. Waziri hili suala ni zito na ni gumu kabisa. Je, hawa watoto ambao
tayari wamekwishaonekana wanahifadhiwa vipi watoto hawa katika suala hili
zima, maana watoto sio kidogo ambao tayari wamezaliwa 392 ni watoto
wengi sana, ni juhudi gani ambazo zinachukuliwa kuwasaidia watoto hawa
katika maisha yao ya baadae.
Mhe. Naibu Spika, kwa sababu inaonekana kutokana na suala hili ni lazima
wizara isaidie kwa vyovyote vile kutokana na hali hii watoto ambao tayari
wamezaliwa na maradhi haya ya Ukimwi.
Jambo jengine Mhe. Naibu Spika, ambalo nataka nilizungumzie na Mhe.
Waziri kalisema kwenye ripoti yake kuhusu masuala haya ya madawa ya
kulevya, ambayo bado vijana wetu wengi sana wanajiingiza katika mambo
haya na bado inaonesha kwamba vijana hawajaamua kuwacha suala hili.
Suala la madawa ya kulevya linaendelea kwa wingi sana na maambukizo
yanakuwa ni mengi sana. Hapa inaonesha kwa upande wa wanaume ni
asilimia 2.6 wanaendelea na mambo haya na kwa upande wa wanawake
ambao ndio wengi zaidi sio chini ya asilimia 19.3. Hii inaonesha kuwa suala
hili bado siku baada ya siku maradhi haya yanaendelea, au wale vijana
ambao ni injection drug user na hawa pia wako wengi sio chini ya asilimia
11.3.
Mhe. Waziri katika masuala haya kuna mpango gani wa kuweza kuwasaidia
hawa vijana au hamasa gani mnachukua katika kuwasaidia vijana wazidi
kuacha tabia hii ya madawa ya kulevya na kujidunga sindano ambapo
maambukizo yanakuwa kwa wingi.
96
Mhe. Naibu Spika, tumeambiwa katika ripoti yako kwamba maradhi haya ya
madawa ya kulevya ambapo vijana wanaojidunga sindano wanapata homa
kali sana ya ini. Je, Mhe. Waziri katika masuala haya ni vijana wangapi
ambao wamejitokeza wenye masuala haya ya homa hizi kali za ini.
Mhe. Naibu Spika, suala jengine ambalo nataka kulizungumzia ni maradhi
haya ya ukoma ambayo mara nyingi tunaambiwa bado yako na yanaendelea.
Lakini siku za nyuma katika uchunguzi imeonekana kwamba watu hawa
hawana mambo ya kuambukiza na wameachiwa huru kutembea wanakotaka
na
Nam.908
IMESAHIHISHWA
Mhe. Suleiman Hemed Khamis: (anaendelea) hawana mambo ya
kuambukiza na wameachiwa huru kutembea wanakotaka.
Lakini hapa kwa taarifa zake Mhe. Waziri maradhi ya ukoma inaonekana
bado wapo wamechunguzwa si chini ya watu 97, ambao wamechunguzwa na
kuonekana na maradhi hayo, watu hao kiasi 65 ni wanaume na 32 ni
wanawake. Kwa kweli zamani tuliambiwa maradhi haya hayapo na wala
hayaambukizi.
Mhe. Naibu Spika, namuomba Mhe. Waziri wakati atakapokuja hapa atupe
maelezo kwamba ni kweli kuwa haya maradhi kwa sababu watu hawa
wameachiwa huru kama kule Pemba sehemu za Kinyasini, hawa watu
wanatembea wanachanganyika na wananchi, wanakula vyakula pamoja na
zamani tuliambiwa hawana maambukizo na ndio maana katika haki za
binadamu wameachiliwa wawe huru. Lakini je, hii hali inayojitokeza baada
ya uchunguzi na utafiti inaonekana kwamba watu hawa ni wengi sana.
Kwa hivyo, ni hatua gani ambazo atazichukua Mhe. Waziri juu ya watu kama
hawa ili kupunguza matatizo ya ugonjwa kama huu wa kuambukiza ambao
tuko nao bega kwa bega.
97
Vile vile ninataka kujua kutoka kwa Mhe. Waziri kupitia kwako Mhe. Naibu
Spika, kwa hapa Unguja tunao pharmacist wengi sana na pharmacies ziko
nyingi sana hapa Unguja na kule Pemba ziko pharmacies pia. Lakini jambo la
kustaajabisha ni kwamba hatuna pharmacist, ambapo sisi watu wa Pemba
hatuhitaji kuwa na pharmacist kule, kwa sababu pharmacies ziko nyingi
lakini wao hawako. Kwa hivyo, hilo Mhe. Naibu Spika, naomba kuelewa na
kupata maelezo japo kidogo.
Mhe. Naibu Spika, kuna maradhi ambayo Mhe. Waziri aliyazungumza hapa.
Kwa mfano, maradhi ya kichocho, minyoo na matende. Sasa hapa katika
ripoti yake Mhe. Waziri alizungumzia kwamba maradhi hayapewi
kipaumbele, yaani hayamo kwenye priority amekusudia nini kusema kwamba
maradhi haya hayamo kwenye priority. Kwa kweli maradhi haya tunayo sisi
binadamu, kama vile maradhi ya matende, minyoo kwa watoto wetu pamoja
na kichocho kwa wale wanaokoga kwenye mito. Mhe. Naibu Spika, kila moja
katika hili ukiliangalia ni zito ambalo linatuhusu sisi na wala sijui taaluma
gani ambayo inayotoka.
Mhe. Naibu Spika, mimi nilitaka kwenye mambo mengi haya ya maradhi
nisingependelea kama pale anapotoa taarifa si vibaya kusema kwamba
television na redio zipo zinatoa maelezo. Lakini mimi naona kuna kitu
ambacho ni cha msingi zaidi ambapo itaweza kutoa elimu ya kutosha kwa
wananchi ili ambayo tuliyokuwa tukitumia zamani kwa njia ya mobile. Njia
hii ndio ya pekee kijiji hadi kijiji kuweza kuwaelezea wananchi kujua nini
tatizo liliopo kwa maradhi ambayo husika. Kwa hivyo, nadhani kuondoka
kwa Mobile Cinema na hili ni suala ni zito na hivi sasa ndio maradhi yanazidi.
Kwa mfano, tunajua hii kichocho ni life cycle and where to break it na
kukatika kwake ni kuondosha makonokono.
Lakini kwenye taarifa zake hakutuambia Shehia ngapi ambazo
zimetembelewa, yaani katika kila jimbo imeelekeza watu wangapi, kwa
sababu kila mahala kuna mito ya kutosha na kuzaliwa kwa makonokono kwa
sababu makonokono wapo wengi na hawa ndio wanaosababisha maradhi ya
kichocho. Kwa maana hiyo, hatujui ni maeneo gani ambayo tayari
yameshatembelewa na watu wamepewa elimu ya kutosha.
Mhe. Naibu Spika, suala la minyoo ni jambo muhimu sana kwa wananchi na
bado taarifa zake kwa wazazi bado halijapewa kipaumbele, namna ya kuwa
na usafi wa vyakula, mazingira na watoto kuweza kuhifadhiwa vizuri.
Mhe. Naibu Spika, nataka kumwambia Mhe. Waziri kwamba suala la
matende kwa kule Pemba halikuonekana upande wa Kaskazini na zamani
tuliambiwa matende yako sana upande wa Kusini Pemba. Je, kwa nchi nzima
98
hasa imeonekana maeneo gani maradhi haya kwa sababu zamani maradhi
haya yalikuwa yakijulikana kwa maeneo maalum. Kwa hivyo, inawezekana
kutokana labda infection ya mazingira ndio iliyochangia kwamba watu sasa
wanaendelea kupata maradhi haya.
Mhe. Naibu Spika, prevention is better than cure, kuhifadhi ni bora kuliko
kutibu, kwani kutibu ni gharama kubwa sana. Sasa kama tutakuwa na njia ya
kuhifadhi maambukizo ya matende basi itakuwa ni bora zaidi kwa sababu
binadamu yeyote anapopata matende inakuwa hata mwendo unabadilika,
maisha yanabadilika, uwezo wa kufanyakazi hana.
Kwa hivyo, hili ni suala muhimu na Mhe. Waziri ameeleza hapa kwamba
hayakupewa kipaumbele. Mhe. Naibu Spika, namuomba Mhe. Waziri wakati
atakapokuja hapa basi alizungumzie suala hili kwa nini akazungumzia
maradhi haya hayakupewa kipaumbele.
Nikiendelea na mchango wangu sasa naomba nizungumzie kuhusu suala zima
la Kitengo cha Bandarini. Mhe. Naibu Spika, ameelezea Mhe. Waziri
kwamba amefanya ukaguzi wa baadhi ya meli kuhakikisha kwamba mnafika
kwa ajili ya kutoa huduma kwa meli tofauti hapa Unguja. Lakini suala
amelizungumza vizuri sana na wala hakuficha ule ukweli katika kuangalia
suala hili, pia bado linaonekana kwamba kuna baadhi ya vyombo vyengine
hawafuati utaratibu wa kuweka usafi wa meli zao, ambapo inabidi nyinyi
mukafanye fumigations kwenye meli hizi.
Mhe. Naibu Spika, nataka kumuuliza Mhe. Waziri kwamba kwa nini hawa
watu hawataki kufanya usafi wa meli zao na kwa nini watu hawa iwe kuna
ulazima wa kuangaliwa usafi wao, kwani usafi ni wao na wao ndio
wanaolazimika kufanya hivyo. Sasa kama watu hawataki je, upande wake ni
hatua gani ambazo wanachukua kuhakikisha kwamba usafi wa meli zao upo.
Vile vile naomba kushauri kitu kimoja kama inawezekana, kwa sababu wizara
yako ina kazi nyingi za kufanya na hana muda wa kutosha, kwa nini hatoi
mafunzo kwa wale na wao wakapewa namna ya kufanya fumigations katika
meli zao, badala ya watu wake kuondoka na kwenda kuifanyakazi ile,
napenda kutoa ushauri huo kama unafaa.
Katika mambo yaliyozungumzwa hapa kwa Zanzibar matatizo bado
yanaendelea kuibuka kwa wingi, yaani matatizo ya maradhi ya macho. Mhe.
Naibu Spika, suala la ugonjwa wa macho linakuwa ni tatizo kubwa sana na
zamani tulikuwa tunategemea matatizo ya macho ni kwa watu wazima. Lakini
hivi sasa inaonekana kwamba maradhi ya macho kwa watoto yamekuwa ni
99
mengi sana na suala hili limekuwa ni gumu katika utekelezaji wake, kwa
sababu lina gharama.
Mhe. Naibu Spika, hivi sasa naomba anieleze Mhe. Waziri kwamba hana
daktari bingwa wa macho, je hii ni kweli. Kwa hivyo, namuomba Mhe.
Waziri wakati atakapokuja hapa kufanya majumuisho, basi anieleze hivi ni
kweli hana daktari bingwa wa macho. Hali hii ina maana kusema kwamba
madaktari wa macho mpaka tukapate kutoka Muhimbili, sasa kama hatuna
basi wizara ijitayarishe kwa kuweka madaktari bingwa wa masuala ya macho.
Kwa kweli mara nyingi inaonesha tunasafiria madaktari kutoka Muhimbili au
nchi za nje. Sasa nataka kujua kutoka katika wizara yake ni lini hasa
atajipanga kuona na yeye badala ya kupata watu kutoka nje katika utibabu wa
macho, basi Serikali ya Zanzibar au Wizara ya Afya inahudumia suala hili
kwa watoto na watu wazima.
Jambo la mwisho pia nataka kujua angalau ile kupanda kwa ugonjwa huu wa
macho. Je, unapungua huu ugonjwa wa macho au unazidi kuendelea. Sasa
kama ugonjwa wa macho unazidi kuendelea ni hatua gani ambayo atachukua
zaidi ya kutoa mafunzo kwa watu ambao wanaoathirika na ugonjwa wa
macho, kwa sababu hivi sasa operations za macho wenye watoto wa macho
zimekuwa nyingi sana kuanzia watu wa zima mpaka watoto wadogo.
Mhe. Naibu Spika, pia ninalo suala jengine ambalo nataka kumueleza Mhe.
Waziri kwamba suala la lishe, ambalo hili ni suala la utapiamlo, hali hii
inatokana kwetu sisi ngazi ya jamii. Kwa hivyo, tunataka kujua suala hili la
utapiamlo ambapo lishe haipatikani ya kutosha amechunguza nini katika suala
hili na utafiti gani mkubwa ambao ameufanya na nini anaweza kuwasaidia
wananchi katika suala lenyewe, yaani atawaambia nini wananchi na
amegundua kitu gani, kwa sababu ni lazima katika suala hili la utapiamlo kwa
watoto wetu ni jambo muhimu, kwa sababu hawa ndio nguvu kazi wa kesho.
Sasa ikiwa jamii yetu kubwa ina suala zima la utapiamlo, basi nafikiri suala
hili ni vyema likachukuliwa hatua. (Makofi)
Katika suala la huduma za uzazi na kupunguza vifo kwa akinamama
linaendelea. Lakini inaonesha kwamba huduma hizi kwa kweli ni nyingi sana,
yaani kutokana na idadi ya hospitali zetu tulizonazo nchi nzima, basi hospitali
ni nyingi na kila hospitali hata ndogo unayoifikia wewe tuache hii ambayo
hivi sasa ni kubwa sana, lakini hata hospitali ndogo basi huduma hii
inahitajika. Kwa mfano, katika vijiji vyetu kutokana na kila masafa ya meli
tano hivi sasa kuna hospitali na tunatarajia wazazi watakuwa wanakwenda
katika hospitali hizi.
100
Je, Mhe. Waziri kupitia kwako Mhe. Naibu Spika, kiasi gani atatusaidia
kuweza kupunguza vifo hivi vya wazazi ambao wanatoka katika maeneo ya
mbali na kuweza kufika katika hospitali ambapo mara nyingi kesi kama hizi
na wala sina haja ya kumficha kwamba zinafanyiwa refer kutoka hospitali
ndogo kwenye hospitali kubwa. Kwa mfano, wazazi waliopo Konde
wanategemea labda Hospitali ya Micheweni lakini mara nyingi wanafanyiwa
refer Mkoani.
Kwa hivyo, ninachotaka kuzungumzia Mhe. Waziri kwa Hospitali ya
Micheweni ni kubwa na mara nyingi sisi tunapata kesi pale Konde ambapo
wazazi wanataka kupelekwa Hospitali ya Chake-Chake. Sasa nadhani ni
vyema na ile Hospitali ya Konde nayo ifikiriwe, kwa sababu akichunguza
yeye mwenyewe basi anajua kwa idadi ya watu tulionao pale Konde, basi
wanahitaji kuwa na gari yao ya kuwasaidia kuwapeleka Chake-Chake. Je, ni
lini Mhe. Waziri atafikiria na Hospitali ya Konde kuwawekea gari ya kuweza
kuwafanyia kesi za rufaa badala ya kupeleka mbali.
Mhe. Naibu Spika, katika suala hili linakuja swali kwa wazazi kuhusu
upasuajia. Kwa kweli mimi nataka kujua tu Mhe. Naibu Spika, kwamba nini
na sababu au chanzo cha kufanyika operation namna hizi kwa wazazi, tuulize
labda ni ukosefu wa damu. Vile vile kama suala hili linajulikana hawa
wanawake mara nyingi wanafika katika Clinic, yaani kila baada ya kipindi
fulani wanaambiwa waje.
Sasa kama kulikuwa na matatizo ya wanawake kwa nini ifikie hadi kufanyiwa
operation sababu hasa huwa nini. Mhe. Naibu Spika, ikiwa kama kulikuwa na
sababu kabla kwa nini mzazi au watu wake waliokuja na mzazi hawaambiwi
wajitayarishe kwa namna kadha mpaka inafika hadi wanawake kufanyiwa
operation. Mhe. Naibu Spika, namuomba Mhe. Waziri wakati atakapokuja
kufanya majumuisho basi anisaidie kunielezea kama ni suala la damu au
linatokana na matatizo mengine.
Vile vile tunataka kujua kuhusu suala zima la maradhi ya kifafa cha mimba
kwa wazazi. Kwa kweli maradhi haya yanakuwa vipi na hayana matibabu na
kwa nini yanatokezea wakati mwanamke anapotaka kujifungua na precaution
gani ambazo mwanamke anatakiwa azichukue kabla hajajifungua na hilo pia
tunataka kulijua.
Mhe. Naibu Spika, katika mambo mengine ambayo nataka nitoe mchango
wangu ambapo linatukumba Zanzibar na nikisema Zanzibar ninamaanisha ni
Unguja na Pemba maradhi ya kisukari. Maradhi haya yamechukua namba
kwa Zanzibar, hivi sasa hata watoto wadogo wanaozaliwa wengi wanakuwa
101
labda kwa sababu ya urithi kutokana na wazazi wao wenye ugonjwa wa
kisukari, lakini maradhi ya kisukari ni mengi sana hapa Zanzibar.
Je, Mhe. Waziri kupitia kwako Mhe. Naibu Spika, katika utafiti wa wizara
yake ni kitu gani ambacho amegundua hasa na tatizo liko na ikiwa lipo tatizo
tufanye nini. Sasa hii advise kama hii najua labda pengine mara nyengine
unaipeleka kwenye kutoa huduma katika redio au television. Kwa hivyo,
tuelewe kisiwa cha pili kilichopo kule suala la redio na television usilipe uzito
mkubwa sana, kwa sababu hakuna kinachoonekana wala hakuna taarifa na
hiyo television yenyewe haifanyikazi sawa sawa, yaani mara inaonekana na
wakati mwengine haionekani. (Makofi)
Mhe. Naibu Spika, pamoja na kujinasua kwamba huduma nyingi anazipeleka
kwenye redio na television na hizo hazitufiki. Kwa hivyo, je kwa upande
wake kwenye suala hili la kisukari ambalo ni common disease kwa Zanzibar,
je tunafanya nini au tunakwenda wapi Wazanzibari. Kwa kweli hivi sasa ni
wagonjwa wa kisukari pamoja na ugonjwa wa macho yote haya ni matatizo
makubwa sana.
Hata hivyo, sasa naomba nizungumzie kuhusu vyakula ambavyo tunategemea
hawa wagonjwa hasa hasa kwa wagonjwa kuweza kupatiwa hizi dawa
ambazo ni dawa zao wa ugonjwa wa kisukari zinapatikana hapa, lakini wakati
mwengine hazipatikani, maana tunasikia hapa kuna watu wanayo Society au
Chama cha Wagonjwa wa Kisukari, je, suala hili liko vipi.
Maradhi mengine ni kuhusu pressure ambalo pia linahangaisha watu.
Matatizo ya Wazanzibari hivi sasa kila unayemsikia anasema ana ugonjwa wa
miguu, yaani kila wakati watu wanazungumza habari ya ugonjwa wa miguu
inauma na haitembei sawa sawa na hapa tatizo nini.
Mhe. Naibu Spika, tumuombe Mhe. Waziri aina ya nyakula tunavyotumia
pengine inawezekana tayari contaminated au vimeshapitiwa na wakati ama
kuna matatizo ambapo vyakula hivi si vizuri kwetu sisi, basi aweze kutushauri
kwamba vyakula fulani si vizuri na tuweze kutumia zaidi natural foods, yaani
vyakula ambavyo vinatoka katika mashamba.
Suala jengine ambalo nataka kulizungumzia ni mental case, yaani wagonjwa
wa akili. Mhe. Naibu Spika, katika nchi yetu hivi sasa ya Zanzibar, ukitembea
katika miji utawaona vijana wengi sana wamepungua akili, yaani akili
imeharibika na idadi ya vijana hivi sasa inaongezeka barabarani na ni wengi
sana. Kutokana na hali hiyo, tunategemea labda serikali itakuwa na mpango
maalum wa kuwadhibiti hawa vijana ambao wanazurura barabarani ambao
akili zao kidogo si barabara.
102
Hata hivyo, kwa hapa Unguja namuomba Mhe. Waziri kupitia kwako Mhe.
Naibu Spika, aweze kuitembelea Hospitali yake ya Wagonjwa wa Akili
upande wa wanaume na ule wa wanawake. Kwa kweli hali si ya kuridhisha
hata katika chakula hali sio nzuri. Vile vile vijana wanakuwa ni wengi zaidi
kuliko watu wengine. Kwa hivyo, namuomba Mhe. Waziri suala hili alifanyie
utafiti wa kutosha, kwa sababu naona kama hii Hospitali ya Wagonjwa wa
Akili ni wengi sana kwa pande zote mbili, yaani wanawake na wanaume. Sasa
Mhe. Waziri tupe hasa nini matatizo ya hospitali hii ambapo huduma kidogo
haziridhishi.
Mhe. Spika, tunataka kujua kwa nini Pemba mpaka leo hospitali hii
haijamalizika ni miaka mingi imeombwa hospitali hii na bado hospitali hii
haijapatikana. Kwa kweli suala hili linanishangaza hii huduma kutoka Pemba
kuja hapa Unguja ni nzito sana, huduma kama hii ya mgonjwa wa akili
kumchukua mtu binafsi na kuja naye hapa kwa gharama zake yeye
mwenyewe ni nzito sana.
Lakini zamani ninavyojua mimi Mhe. Naibu Spika, huduma hii ilikuwa kuna
mashirikiano baina ya mzazi mwenye mtoto mgonjwa pamoja na wizara yake
hushirikiana bega kwa bega kumsafirisha kutoka Pemba na kumleta Unguja,
na hivi sasa anaachiwa mzee peke yake.
Suala hili ni zito tena ni gumu sana na linahitaji gharama kubwa sana
kuwasafirisha, kwa sababu huwezi kumsafirisha mgonjwa wa akili mtu
mwenyewe peke yake lazima awepo mtu kama askari wa kuweza kumu-ascot
mpaka hapa. Kwa kweli jambo hili wizara hii kwa upande wa Pemba
haifanyiki kazi hiyo, unapokwenda kudai masuala haya wanakwambia
jitegemee wewe mwenyewe. Hii Mhe. Waziri ndio hali halisi ilivyo.
Mhe. Naibu Spika: Mhe. Mjumbe malizia dakika 20 zimekwisha.
Mhe. Suleiman Hemed Khamis: Mhe. Naibu Spika, ahsante. Masuala
mengine ni kuhusu maslahi ya wafanyakazi.
Mhe. Naibu Spika, kuhusu maslahi ya wafanyakazi bado mpaka hivi sasa
mishahara midogo na ndio maana katika wizara yake wafanyakazi aliowataja
kiasi 32 wameondoka katika wizara yake. Kwa kweli suala hili ni gumu tena
ni zito sana. Kwa hivyo, ni vyema alichunguze suala hili kwa nini watu
wanaacha kazi wanaondoka vijana baada ya kuingia kazini, nadhani
inaonekana kwamba ni maslahi ni madogo. (Makofi).
103
Mwisho Mhe. Naibu Spika, naomba hili linimalizie kwenye jimbo langu
kwamba nataka nimwambie Mhe. Waziri kupitia kwako kwamba mimi ninao
upungufu wa wazalishaji, kwa sababu wazalishaji waliopo ni kidogo
hawatoshi na huduma zinakuwa ni nzito.
Pili Mhe. Naibu Spika, kuhusu call allowance. Kwa hiyo, hapa zaidi ya miezi
mitatu au minne hawa wakunga au wazalishaji hawapati haki zao. Kwa hivyo,
ninamuomba Mhe. Waziri kupitia kwako Mhe. Naibu Spika, kwamba suala
hili la call allowance waweze kulipwa kwa wakati. (Makofi)
Jambo jengine laboratory hatuna mtu ambaye anashughulikia mambo ya
ndani, pia hatuna mlinzi wa kuweza kulinda Hospitali yetu ya Konde ambayo
inahitaji mlinzi tuwe naye.
Mhe. Naibu Spika, nakushukuru na mimi kwa kunipa nafasi ya kuweza kutoa
mchango wangu katika suala hili.
Mhe. Naibu Spika: Waheshimiwa Wajumbe, sasa tunamalizia dakika kumi
na nyengine kumi kipindi cha jioni. Mhe. Asaa Othman Hamad.
Mhe. Asaa Othman Hamad: Mhe. Naibu Spika, nikushukuru na mimi
kunipa muda huu uliobaki na kukubali kwamba itakuwa nakudai.
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kuniwezesha mimi na wenzangu
siku hii kufika kwenye jengo lako hili tukufu tukiwa wazima wa afya.
Mhe. Naibu Spika, bajeti ya mwaka huu tulisema ni ya huduma ya wananchi
wa Zanzibar. Sasa kama hivyo ndivyo basi tulitarajia bajeti zinazofuata
zinakwenda kwenye mtiririko wa kauli hiyo iliyotangulia mwanzo.
Mhe. Naibu Spika, leo tunajadili Wizara ya Afya ambayo ina umuhimu kwa
maisha ya watu wetu, pia kwa taifa hili kuwa na watu wenye afya bora. Mhe.
Naibu Spika, fedha zilizotengwa kwa wizara hii hazikidhi mahitaji ya
kuendesha wizara lakini pia kuyafikia malengo waliyojiwekea. Kwa hivyo,
nianze kwa kumshukuru Mhe. Waziri pamoja na watendaji wake, pia
niishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa dawa za watoto, chanjo na
kuharisha na huko tumeona mambo yamekwenda vizuri. Hata hivyo, kuna
mapungufu Mhe. Naibu Spika yanayokatisha tamaa.
Vile vile na mimi niungane na waliotangulia kwanza Mhe. Naibu Spika,
serikali haitutendei haki Baraza lako, kwamba leo tunajadili wizara kama hii
na hata nyengine isiyokuwa hii Mtendaji Mkuu wa Shughuli za Serikali ndani
ya Baraza hili halipo, Waziri wake Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais hayupo
104
na Waziri wa Nchi, (OR), Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo naye
hayupo. (Makofi)
Mhe. Naibu Spika, angalau basi kwa taratibu za Mabunge haya ya
Commonwealth mtu kama huyo anapokuwa hayupo basi Wabunge
wanaarifiwa nani anachukua nafasi ile, lakini tunasimama ni sisi na waziri na
naibu wake. Kwa hivyo, Mhe. Naibu Spika, katika hili tunaomba sana serikali
ione umuhimu wa watu hawa kuwemo kwenye chombo hichi.
Mhe. Naibu Spika, nitakuwa na maswali kwa Mhe. Waziri na nitamuomba
anisikilize kwa makini kwa sababu ninataka majibu sahihi. Kwanza nimuulize
Mhe. Waziri katika wizara yake hii kuna mpaka wa utendaji kwa watendaji
wenyewe pia kwa maslahi ya watendaji baina ya Unguja na Pemba.
Kwa kweli tunalalamika na kupiga kelele madaktari wetu wazalendo
wanaondoka na mwenzake waziri aliyeondoka wa wizara hii alikuwa
anatuambia wala serikali ihatomzuia mtu anayetaka kuondoka. Lakini
chochote kinachotendeka kina sababu. Mhe. Naibu Spika, Hospitali ya Jimbo
langu ya Wete tunao upungufu mkubwa wa wafanyakazi.
Katika hili Mhe. Waziri asijekuja na jibu la nyumba, hospitali inazo nyumba
zake, isipokuwa wamewagaiya watu ambao si wa hospitali waliokuja pale
kusaidia wakakosa makaazi na badala yake tukaambiwa sisi tuwape nyumba
kwa ajili ya kukaa madaktari waliokuja mwaka jana. Kwa maana hiyo,
nyumba ya Hospitali ya Wete ipo wamewapa wasiokuwa wafanyakazi wa
hospitali na matokeo yake wanaokuja kusaidia watu pale wanakosa makaazi.
Kwa hivyo suala la nyumba lisijekuwa ni jibu. (Makofi)
Mhe. Naibu Spika, tunao upungufu mkubwa wa wafanyakazi wetu na hata
yale maeneo nyeti kama vile theater. Kwa hivyo, kunahitajika kikosi
kikamilike kwa wakati unaohitajiwa na hapa kuna tatizo.
Mhe. Naibu Spika, kama muda umefika basi naomba nisite na Inshaallah nije
nianze Hospitali ya Wete kwa wakati muafaka.
Mhe. Naibu Spika: Waheshimiwa Wajumbe, ninawashukuru na sasa
tunaakhirisha kikao chetu hadi saa 11:00 za jioni.
(Saa 7:00 mchana Baraza liliakhirishwa mpaka saa 11:00 jioni)
105
(Saa 11:00 jioni Baraza lilirudia)
(Majadiliano Yanaendelea)
Mhe. Asaa Othman Said: Nakushukuru kwa mara nyengine Mhe. Naibu
Spika, baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha jioni hii
tukiwa wazima wa afya. Mhe. Naibu Spika, tulifikia Wete Hospitali. Hospitali
hii ina wafanyakazi kidogo sana. Ni kidogo sana kwa idadi yao na ni kidogo
hasa kwa yale maeneo ambayo yana umuhimu mkubwa siku hadi siku. Mfano
wa hilo ni ile theatre, ina nurses watatu na daktari wao mmoja wa akina
mama kwa magonjwa haya ya akina mama. Hawa anayekwenda likizo ni
mtihani, lakini hawa wao wasihudhurie misiba wala furaha. Hawa wanaingia
saa 1:30 asubuhi lakini ni masaa 24.
Kazi za theatre, zinaeleweka. Mhe. Naibu Spika, kilio cha wafanyakazi wa
sekta hii Pemba ni wao kutengwa kutopewa hizi allowances na hizi wanazoita
call. Lakini kilichofanyika hapa hapa kuzingatiwa mazingira ya kule Pemba.
Pemba wao ni kidogo kwa idadi yao na ndio hao hao wanaoingia call, hawana
shift, hawana chochote. Sasa palipotajwa malipo ya call wakatajwa madaktari
na specially kule hakuna na huyo aliyekuwepo hapewi kitu.
Nilianza mchango wangu kwa kuuliza Mhe. Waziri, watendaji wako ndani ya
Wizara yako Unguja na Pemba umeweka mpaka wa stahili. Mhe. Naibu
Spika, huyu gyner ambaye ni mzalendo, muungwana huyu, huyu ni mchaji wa
Mungu, hapewi zaidi ya mshahara wake lakini ni usiku na mchana anatumika.
Mhe. Naibu Spika, nilisema na naendelea kusema kwamba wafanyakazi ni
kidogo. Mhe. Waziri kilio hichi alikisikia akawaleta wengi, tatizo aliloliona
yeye akataja nyumba. Nasema nyumba ni tatizo nalikubali, lakini sikubaliani
naye kwa nini zile ziliopo zao wao wenyewe Wizara ya Afya mbona
wamezigawa kwa watu waliokuwa sio wa sekta ya Afya. Mhe. Waziri
angeleta kilio hichi baada ya kuishiwa na kile alichonacho. Lakini tumekuja
kuliona kumbe kuna tatizo kubwa zaidi kuliko nyumba na ndio maana
wafanyakazi Pemba hawakai. Mfanyakazi aliyehitimu siku moja, kada moja,
chuo kimoja na mwenzake aliyekuwepo Unguja lakini hawalingani mishahara
yao. Kuna upendeleo, kuna ubaguzi katika hili na hili ndilo linalowahamisha
wafanyakazi.
Mhe. Naibu Spika, tulikuwa na daktari wa watoto alikuwa anasoma na
mwenzake nchi moja Afrika Mashariki, akaja Pemba, alipokuwa anasafiri
kuja Unguja kutizama mazingira ya kazi na wenzake na malipo, akaligundua
hili. Alipolalamika akaambiwa Nabii Muhammad alizaliwa Makka na alihajj
106
na weye kama unayataka haya hapa na wewe hajj na kweli aliondoka Pemba
hayupo, yuko wapi? Mhe. Waziri akitaka nitamwambia yuko wapi.
Sasa mimi nauliza hivi kumbe ni kwa makusudi yanafanywa haya ili kusudi
kule wahame? Wakikuwepo kule hawalipi kodi ya Serikali? Wananchi wa
kule Pemba hawalipi kodi ya serikali hii? Kwa nini wafanyiwe hivi?
Kuwasumbua watendaji hawa si wao tu lakini pia wanawasumbua na
wananchi wa Kisiwa kile cha Pemba.
Mhe. Naibu Spika, madaktari wa magonjwa mbali mbali ukiacha huyu wa
magojwa ya akina mama, hatuna Wete, kuna hawa ma - VSO wanatajwa
wapo, wanatusaidia, lakini bado tatizo ni kubwa, hakuna daktari wa mifupa
hapa, kwa watoto ndio huyu Mcuba yupo anasaidia, na wengine wengi
hawapo, kumbe kuna tatizo. Mhe. Waziri nitakuomba miye uje utufafanulie
tatizo ni nini hasa linalokwamisha kwa nini kule Pemba wasipelekwe
madaktari wa fani tofauti kuwasaidia wananchi wa kisiwa kile.
Mhe. Naibu Spika, Mhe. Waziri alikuwa na kikao na Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar. Wafanyakazi wakapeleka kilio chao hichi, Mhe. Waziri na
watendaji wake alibeba ahadi, akazitaja wiki mbili kulishughulikia.
Namuomba leo kutoka siku hiyo hadi leo ni wiki ngapi sasa? Waliotajwa na
Wizara kwamba hao ndio wanaostahiki kulipwa hizi call ni madaktari na hao
mabingwa, lakini narudia kusema kuna haja ya kuyatizama mazingira halisi
ya kule Pemba. Hawa watu hawana shift, hawana likizo, kwa sababu ni lazima
aende akaokoe maisha ya mtu.
Mhe. Spika, kuna mwenzetu sijui kama nikimtaja na yeye hatohamishwa
huko aliko, ndiye anayetusaidia kwa nguvu zake zote Kamanda wa Chuo cha
Mafunzo. Karibuni hii gyner huyu mzalendo alikuwa likizo, kazi yote ya pale
ilikuwa inamuangukia bwana huyu, Mwenyezi Mungu atamlipa malipo
anayoyajua yeye mwenyewe. Huyu hana mapumziko, wakati wake wa
mapumziko tunauchukua sisi, hajui matembezi anakuja kutoa msaada pale,
mbali ya wale anaowaokoa jamaa zangu wanapoletwa na vitanda kutoka
kwao wanapovuka pale jirani.
Mhe. Naibu Spika, hali halisi na hivyo vitendea kazi vya dharura navyo
hapana. Kuna tatizo pia la uingizwaji na ucheleweshwaji wa pesa. Magonjwa
ya sukari sasa hivi ni tatizo kubwa, hawa wanatakiwa wachangiwe lakini
wanatofautiana uzito wa ugonjwa wenyewe. Anaambiwa na daktari wake kwa
wiki aripoti mara tatu ama zaidi ya hapo. Hali ya maisha kiuchumi ya kwetu
ni mbaya sana. Hili ndio pale niliposema kutowepo mtendaji Mkuu wa
shughuli za serikali humu ndani hatutendewi haki na serikali. Kwa sababu
hapa nilikuwa na lugha zaidi ya kuizungumza, serikali itoe jibu.
107
Suala la mama waja wazito. Mhe. Naibu Spika, pamoja na kauli ya Mhe. Rais
bado tatizo lipo. Kinachopelekwa hakikidhi haja na bado tunaendelea kuzaa.
Anapofika mama kutaka kujifungua saa ile wanamdai vifaa vya kujifungulia
hili ni tatizo. Mhe. Naibu Spika, labda utayabeba wewe mwenyewe leo.
Nadhani niwaombe Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza lako Tukufu kwanza
tuzuie bajeti hii kutoipitisha, tena tuizuie kwa nia njema kabisa, hadi pale
serikali itakapotoa jibu juu ya masuala tunayoyauliza. Hatuna nia ya
kuikomoa wizara wala mtu mwengine yoyote. Nia yetu ni kuwatendea haki na
mema Wazanzibari wote.
Mhe. Naibu Spika, mpaka kitabu hiki cha bajeti jaduweli la 17 limenipa picha
ya haya ninayoyasema kuna mpaka mkubwa utolewaji wa fedha baina ya
Unguja na Pemba. Hii siyo haki, sijui wanakomolewa Wapemba wenyewe
ama anakomolewa Waziri wa Wizara hii, nashindwa kupata jibu sahihi. Ndio
maana nikasema ningefurahi zaidi kama angekuwepo Mtendaji mkuu wa
shughuli za serikali akatusaidia katika haya.
Mhe. Naibu Spika, scheme za wafanyakazi za wenzao Pemba zimekama,
wanaambiwa wao ni wengi sana. Za wenzao Unguja zimetekelezwa,
kitendawili hichi Mhe. Waziri hebu njoo utusaidie utakaposimama, kwa nini
iwe hivi? Wale mabingwa na madaktari hawapo, lakini hata simu nayo
haithaminiwi. Wote hawa ni wafanyakazi wa wizara hii hii.
Mhe. Spika, kuna jengo Wete pale la magonjwa ya akili limetelekezwa, Mhe.
Waziri tunaomba utupe ufafanuzi kulikoni. Wanaokuja kutizama ndugu zao
waliolazwa hospitali hawana sehemu ya kukaa. Hospitali yenyewe haina uzio,
tatizo linalowapata watendaji sasa ni kutoa huduma huku watu waliokuja
kutizama wagonjwa wakishuhudia kinachoendelea, matokeo yake
wanabebeshwa lawama wafanyakazi wa hospitali kumbe lawama sio yao
wao. Hili nalo ni tatizo lipo, tunakuomba utupe muhtasari wa majibu, naomba
sana. La kwanza ni lile la mpaka nililouliza, upo haupo? Na kama upo kwa
nini? Ushahidi kwamba kuna mpaka vielelezo vya bajeti ya kitabu chako,
lakini na maelezo niliyonayo.
Mhe. Naibu Spika, la mwisho orodha aliyoiomba Mhe. Rais, baada ya
kulalamika wenzetu hawa hawana pesa za kulipa call nina majina 86, majina
haya hayana hata jina moja kutoka Pemba, kwa sababu nilizozitaja. Lakini
namuomba sana Mhe. Waziri wale kule wanafanya kazi zaidi ya hawa hapa.
Hawa waliyokuwemo kwenye orodha hii kwa maana hawana muda wa
mapumziko wao. Theatre ina watu watatu, daktari ni mmoja, akitoka saa 9:30
anarudi tena saa 12, saa 12 anatoka tena baada ya sala ya Alfajiri. Huyu mtu
unasema humlipi call kwa sababu yeye sio specialist, hivi tukueleweje,
108
haiwezekani! Hapa ni lazima serikali huko mlikopeleka orodha hii mpeleke
nyengine kwa maelezo stahiki kusudi na wao waweze kupata taasisi zao kama
wenziwao wanavyopata.
Mhe. Naibu Spika, nakushukuru kwa muda wangu uliopungua lakini angalau
umeu - consider baada ya hayo nasema siipitishi miye bajeti hii na nawaomba
Waheshimiwa Wawakilishi bajeti hii isipite kwanza hadi pale serikali
itakapotoa kauli thabiti kuhusu kauli ya mwanzo bajeti hii ni kwa ajli ya
huduma kwa wananchi wa Zanzibar. Nakushukuru.
Mhe. Abdalla Juma Abdalla: Nakushukuru Mhe. Naibu Spika, kwa kupata
nafasi hii niweze kueleza machache katika makadirio na mapato katika sekta
hii muhimu sana katika jamii yetu. Nitajitahidi kadiri inavyowezekana
kufuata maelekezo yako Mhe. Naibu Spika, nisitumie muda mwingi. Kwa
sababu hiyo basi sitaki nipongeze ila nataka niende kwenye mada moja kwa
moja.
Nitakachokianzia Mhe. Naibu Spika masikitiko, nasikitika kidogo na sisikitiki
na Wizara hii, lakini nasikitika na mwenendo wa Wizara ya Fedha katika
kuingiza fedha hizi ambazo fedha chache tulizozikadiria kutoziruhusu
zipelekwe katika sekta ya afya. Lakini mwenendo wa kuzipeleka unakuwa ni
wa kusuasua sana. Ukifunua ukurasa wa 32 kuna Ofisi ya Mfamasia Mkuu,
imeelezwa hapa katika nukta, paragrafu 502 kwamba fedha iliyoidhinishwa
katika bajeti ya mwaka huu tunayomaliza ilikuwa ni bilioni moja mia tano na
arubaini na saba milioni kwa ajili ya dawa, hiyo ni portion ya serikali, maana
na wafadhili na wao wanachangia.
Mhe. Naibu Spika, kilichotiwa hadi kufikia mwezi wa Machi ni shilingi mia
mbili na sabini na moja milioni, hiyo ni asilimia ndogo sana ni kama asilimia
nafikiri 18. Lakini kwa kifupi Mwanasheria Mkuu huwa anasema tukamcheka
hapa kwamba hatuko serious. Lakini hii inaonesha kweli hatupo serious,
maana hakuna sekta muhimu, hata ukisoma MKUZA moja katika malengo ni
kuimarisha afya na siha za watu, lakini kwenye MKUZA tunaandika vile
wakati wa ku - practise sasa unafanya kitu kama hichi.
Mhe. Naibu Spika, na mimi nataka niungane na Mhe. Asaa kwamba kwa
kweli kuna haja ya bajeti hii kwanza kuirudisha ili tuone wenzetu Wizara ya
Fedha wanatoa umuhimu wa kutosha kwa sekta muhimu kama hii. Hatuwezi
kujenga nchi tukiwa na watu wagonjwa. Watu wanaumwa, Wazanzibari
tunaumwa kwa asilimia kubwa, leo serikali yenyewe haipeleki pesa kwa ajili
ya tiba. Mimi nadhani si jambo zuri hata kidogo. Kuna haja ya kuwa wakali
kidogo Waheshimiwa katika hili. Kwa sababu jamii yetu ina watu wanyonge
hakuna mmoja anayeweza kujihudumia mwenyewa kwa afya. Lazima huu
109
msaada wa serikali upatikane 100%. Kwa hivyo mimi kwanza nataka nitoe
lawama zangu hizo kali sana.
Pili nijaribu kuangalia hichi kitabu cha bajeti ya programu, nikaenda kwenye
programu Nam. 3 ambayo inahusu Sera ya Afya, Utawala na Uendeshaji.
Lakini hiyo ina programu mbili ndogo ndogo. Ile programu ya 3(b) inasema
ni Sera, Mipango na Utafiti, sasa haja yangu hapa ni huu utafiti.
Mhe. Naibu Spika, jamii yetu imeelemewa sana na maradhi ambayo
yanaongezeka kila siku, yamekuwa maradhi maarufu sana tena maradhi sugu
sana. Kwa mfano maradhi ya Kisukari, ni tatizo kubwa sana sasa hivi,
utafikiri ni vile maleria zamani. Ukienda kwenye clinic ya wagonjwa wa
kisukari ni kubwa sasa kuliko maradhi mengine, kuna maradhi ya moyo, kuna
maradhi ya Kiharusi. Imekuwa ni jambo la kawaida sasa hivi, maradhi ya
figo, saratani na maradhi ya miguu. Ni maradhi ambayo yanatusumbua sana
Wazanzibari.
Mhe. Naibu Spika, nadhani kitengo cha utafiti sasa watwambie Wazanzibari
tuna tatizo gani? Maana kama tunakula vyakula visivyofaa watwambie
kwamba ukila chakula hiki ndio maana ya tatizo hili, lakini tukiendelea
kunyamazia hili basi siku moja tutakuja kujikuta hapa sote ni walemavu.
Maana yake sasa hivi nusu ya watu ni karibu walemavu, kila mtu anakwenda
tata kama anajifundisha kutembea sasa hivi kwa matatizo ya miguu na
wengine wamekondeana kwa sukari. Sasa nadhani ni vyema kitengo hiki
kifanye kazi kwa bidii sana, haya matatizo tujue sababu ni kitu gani,
yanatuvamia sana maradhi haya.
Nikiacha hilo Mhe. Naibu Spika, sasa niende kwenye tatizo jengine kubwa na
sugu sana, kama tunavyojua jamii yetu ina watu wanyonge sana, haya
matatizo niliyoyataja mengi yao kwa mfano kama maradhi ya moyo, saratani,
kiharusi ni maradhi ambayo hayatibiki ndani ya nchi, hata maradhi ya miguu
waliyo na mbawa zao huruka kidogo kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutibu
miguu. Tatizo tulilonalo jamii yetu ni wanyonge sana.
Mhe. Naibu Spika, katwambia Mhe. Waziri kwa mwaka uliopita katumia
karibu milioni 900 kwa ajili ya kusafirisha watu kupeleka nje kwa matibabu.
Hiyo ukiangalia wale wagonjwa wanaohitaji kwenda nje haifiki hata asilimia
3% wanaopelekwa. Watu ni wengi, uwezo wa serikali wa kusafirisha watu
kupeleka nje ni mdogo sana, kwa hivyo wanabakia masikini za Mungu kufa
hivi hivi wakijiona. Masikini ya Mungu huwezi kumwambia aende kwa fedha
zake akatibiwe India hata siku moja, kama hajapata msaada wa serikali
hawezi kwenda. Tunawaona humu wanapita miskitini wakiombaomba pesa,
wana matatizo na unamuhisi kwamba huyu sasa anaelekea kwenye kaburi
110
hana vya kufanya. Pengine maisha yake yangeokolewa kama angekuwa na
pesa za kupelekwa nje.
Tatizo ni kubwa na nilikuwa naiomba serikali ikae iumize vichwa sana, tena
tuwe na nia ya makusudi kabisa, kwamba zile huduma zinazofuatwa kule nje
kwa nini hatufanyi utaratibu tukazipata hapa ndani ya nchi. Kwa mfano
tunaweza kusomesha kama wale mabingwa wanaotibu kule India tukawa na
mabingwa wenye taaluma zile wakatusaidia hapa. Kama kuna vifaa
wanavyovitumia kule India vikanunuliwa vikawepo hapa, japo ni ghali lakini
tukiwa na nia na tukaweza kutoa taaluma kwa wananchi wakatufahamu wao
wenyewe watachangia. Lakini kwa hivi tunavyokwenda tutapoteza watu kila
siku.
Nikiacha hilo Mhe. Naibu Spika, sasa niendelee na lawama zangu. Lawama
nyengine ni tatizo la wataalamu wetu kuondoka katika nchi. Nakumbuka
ukisoma kitabu cha Mhe. Waziri kaiweka hii kama changamoto. Kweli
tunawasomesha watu kwa pesa za wanyonge, masikini za Mungu wagonjwa
hohe hahe, lakini mtu akishapata taaluma unamkuta yuko karibu basi yupo
Dar-es-Salaam, lakini mara nyingi utawakuta wapo nje kabisa. Kwa upande
mmoja mimi nawalaumu sana kwa sababu waliowafikisha pale au
zilizowafikisha pale ni pesa za wanyonge za masikini. Walipaswa kwa
vyovyote vile kuwa wazalendo kusaidia jamaa zao. Lakini maslahi ya
kibinafsi yanawachukua wanaisaliti jamii yao. Mimi nawanasihi sana, tamaa
za kibinafsi hazitotufikisha mbali katika kujenga jamii yetu, kwa hivyo
wabakie kwanza watusaidie katika nchi.
Kwa upande wa pili lawama zangu nazilenga serikalini. Serikali kuna haja ya
kuangalia kwa makusudi hawa wataalamu ni mali sana. Ukitaka kujua kama
ni mali wao aondoke leo tu hapa kesho utamtafuta Dar-es-Salaam
keshaajiriwa zamani, watu wanatafuta. Sasa kile kinachotafutwa na wenzetu
na sisi tukitunze. Kwa hivyo nadhani wataalamu si watu wengi sana katika
jamii, hebu serikali ijipange kuhakikisha kwamba wataalamu hawa
hawaondoki wanabakia. Wanaweza wakalinganisha hivi kwani Dar-es-
Salaam wanawalipa shilingi ngapi, basi kile anacholipwa Dar-es-Salaam hebu
na sisi tumlipe hapa asiondoke. Mimi nadhani hilo tukilifanya tunaweza
kubakisha wataalamu wengi sana hapa.
Mhe. Naibu Spika, mimi mara nyingi huwa napenda kutoa mfano mmoja.
Mimi nilikuwa na mgonjwa wangu binafsi akawa na tatizo la moyo.
Nikampeleka Abdalla Mzee, wakanambia huyu mpeleke Unguja tatizo lake ni
kubwa. Nikaja naye Mnazi Mmoja wakanambia huenda ukawa na safari ya
India kwa tatizo lake. Nikaanza kushtuka kweli kweli maana pesa za
kumpeleka India mgonjwa wangu sina. Lakini wakanambia kwa kuanzia hebu
111
nenda kwa dokta mmoja pale Dar-es-Salaam anaitwa Lowakatare. Mimi
nikamfuata Lowakatare, kabla ya kufika kwa yule dokta Lowakatare yule
karani wake tu, alimpima yule mgonjwa kwanza akanambia huyu mtoto tatizo
analo kweli, lakini kwa ninavyoliona ni dogo na halihitaji kwenda nje ya nchi,
lakini nenda kwa daktari.
Basi nikampeleka kwa daktari akamfanyia vipimo akanambia sikupi hata
panadoli, tatizo hili ni dogo sana kaa nae baada ya mwaka mmoja niletee tena
nimpime. Moja kwa moja lile tatizo likaondoka. Sasa nikasema basi Zanzibar
nzima wameshindwa kugundua hili tatizo kuwa si kubwa wananipeleka India,
kama sikupita huku ningesema nakwenda India moja kwa moja ingekuwaje.
Yule karani aliyenambia hivyo ni mtoto wa Kizanzibari alivyonisikia nasema
tu akaniuliza wewe ni Mpemba wa wapi. Nikamwambia Chake-chake, na
yeye akaniambia anatoka huko huko Chake Chake. Huyu tungekuwa naye
hapa angetusaidia mangapi, hatukuwatunza wanatukimbia Mhe. Naibu Spika.
Sasa mimi naihusia sana Serikali tusione gharama ya kuwatunza hawa
wataalamu, hebu tuwapeni pesa wakae hapa watusaidie.
Jambo jengine Mhe. Naibu Spika, ni tatizo hili ambalo Mhe. Naibu Waziri,
amelieleza kwa sababu sekta ya afya ni sekta ya huduma haizalishi, hii sekta
inatoa tu huduma, sasa kuna haja ya kusaidiwa na sekta nyengine.
Amelalamika sana Mhe. Waziri kwamba analipishwa umeme katika kiwango
kile ambacho wanalipishwa wafanyabiashara na yeye hafanyi biashara, yeye
anatoa huduma. Shirika la Umeme ni Shirika la Serikali, hata Mamlaka ya
Maji ni Mamlaka ya Serikali, walipaswa kufanya huruma fulani kutoa offer
kwa hospitali, wasilete bili kama wanam-charge mtu mwengine anayefanya
biashara. Hii nadhani kuna haja kwa Serikali kulifanyia kazi vile vile tukaona
kama Shirika la Umeme basi angalau ile bili inakwenda nusu nusu kule sio
kamili, na hata Mamlaka ya Maji vile vile iwasaidie hawa wenzetu waweze
ku-save pesa kidogo za kusaidia hizi huduma za wananchi wetu.
Jambo jengine ambalo nilisema niliseme kidogo Mhe. Naibu Spika, ni kuhusu
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala. Hii sekta inakuwa sasa katika nchi
yetu na nadhani kuna mambo mawili muhimu ya kufanya, na nakumbuka
niliwahi kusema mwaka hivi kwamba kuna haja sasa Wizara ya Afya ikaweka
kitengo maalumu na ikiwezekana kukawa na mtaala maalumu wa kusomesha
madaktari wetu mambo haya ya tiba asilia au tiba mbadala, kwa sababu
visiwa vyetu vimezungukwa na miti, na wataalamu walionusanusa kidogo
wanasema miti yote iliyotuzunguka hapa ni dawa ya maradhi mamoja au
mengine, tatizo letu hatuwezi kugundua mjiti ni dawa ya kitu gani na uzuri wa
dawa hizi sio chemical, ni miti shamba haileti athari kubwa ndani ya miili
yetu, lakini bahati mbaya wengi wetu hatujui.
112
Mhe. Naibu Spika, nilikuwa nadhani kuna haja ya hili kulipa umuhimu, lakini
kwa upande wa pili hizi tiba asilia zinaanza kutumika hapa katika nchi na ni
sekta inayokuwa, maduka ya madawa ya asili yako mengi sasa, sasa khofu
yangu inakuja kuna miti mengine kwa mfano kama muarubaini; muarubaini
wanasema asili ya kuitwa hivyo ni kwa sababu unatibu maradhi arubaini,
lakini ule mjiti wenyewe una sumu na ukiikosea kipimo sumu yake badala ya
kutibu inaweza kukuletea madhara.
Sasa ndio inakuja ule umuhimu wa kupata wataalamu wanaoweza kuchuja ile
dozi hasa iwe kiasi gani ili akiweza kutumia ule mjiti basi uweze kumtibu
badala ya kumdhuru. Nafikiri tungefanya hivyo tukaweza kuitumia miti yetu
iliyotuzunguka hapa pengine hata hili tatizo la kuhangaika madawa ya
hospitali lingepungua kwa kiwango kikubwa, kuna haja ya kuelimisha
madaktari wetu na wao watoe taaluma kwa wananchi, maana yake sifa ya
mjini huu kama umeshaujua wewe ah! Si lazima uende kwa daktari,
ukishikwa na tumbo unazunguka nyuma kachimbe mti fulani unakunywa
mambo yamekwisha, umeshapunguza gharama za kwenda hospitali,
ushampunguzia daktari adha ya kwenda kutatua maradhi yako. Sasa na hili
nafikiri ni jambo muhimu sana kwa sababu mazingira yetu yanaruhusu hii
miti tunayo mengi sana.
Mhe.Naibu Spika, kama nilivyokwambia kwamba nitajitahidi kuutumia muda
wako vizuri sitatumia muda mwingi sana naomba niseme jambo la mwisho.
Hili nataka ni-quote kiambatanisho nambari kumi na saba, sikufurahi sana na
mgao wa fedha unavyokwenda kati ya Unguja na Pemba. Nilikuwa nasoma
hapa kwa mfano kitengo cha tiba Unguja ukiangalia kiambatanisho nambari
kumi na saba kiko ukurasa wa 104, kitengo cha tiba kiko Unguja na Pemba,
sasa Unguja makadirio ya fedha ilikuwa ni 435,000,000/= hapa ziliingizwa
zaidi ya hizo, paliingizwa 1,093,699,000/= ni sawa sawa na asilimia 250,
lakini kitengo hicho hicho Pemba kilikadiriwa 213,000,000/= lakini
zilizoingizwa 96,000,000/= sawa sawa na asilimia 45 hayalingani, kule kuna
asilimia 250 pengine kulikuwa na sababu ya msingi naomba ufafanuzi, lakini
hapa ukitizama utaona kama kule Pemba kumeachwa nyuma kidogo.
Mhe. Naibu spika, ukiangalia Mkemia Mkuu Unguja, makadirio yalikuwa ni
99,000,000/= zikapatikana 38,848,000/= ni sawa na asilimia 39, lakini
Mkemia Mkuu Pemba ilikadiriwa 20,000,000/= zikapatikana 4,000,000/=
sawa sawa na asilimia 24, sijui kuna tatizo gani mpaka mtiririko unakuwa
hivi? Na ukiangalia Idara ya Utumishi na Uendeshaji kwa hapa Unguja ni
347 zikapatikana 223 sawa na asilimia 64, lakini Idara hiyo hiyo Pemba
ilikadiriwa 165 zikapatikana 64 sawa na asilimia 39 yaani iko nyuma, na
ukiangalia hizi ni huduma ambazo bila ya shaka ziwe sawa, sasa kwa graph
113
hii inaonekana kama kule Pemba inawezekana kama Waziri ana sababu za
msingi labda.
Baada ya kusema haya nMhe. Naibu Spika, nataka nisisitize kwamba kwa
kweli sisi Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi tukijipanga vizuri tunaweza
kuilazimisha Serikali ikaweza kutia fedha za kutosha katika Wizara hii
muhimu. Sasa mimi nawaomba wenzangu kwa hili tuwe serious kwa
kumtegemea babu Juma tu na Dkt. Sira wanaweza wakashindwa kuishawishi
Wizara ya Fedha ikatia fedha za kutosha. Kwa hiyo kazi kwetu. Ahsante
Mhe. Naibu Spika.
TAARIFA
Mhe. Naibu Spika: Kabla sijaendelea na wachangiaji niliowataja, naomba
nitoe taarifa kwamba kuna ndugu yetu anaitwa Keith R. Weghorst ambae ni
raia wa Marekani amepata kibali cha serikali kufanya utafiti hapa Zanzibar,
na kwa sababu utafiti wanaoufanya unahusu mambo ya Bunge, Ndugu Keith
ameruhusiwa na uongozi wa Baraza kukusanya taarifa anazozihitaji kutoka
kwa Waheshimiwa Wajumbe. Kwa maana hiyo Waheshimiwa Wajumbe
tunapewa taarifa kwamba ndugu huyu atakuwepo hapa kwa ajili ya kufanya
mahojiano na baadhi yetu, mahojiano hayo yanaweza kufanywa ama na yeye
mwenyewe au anatumia watafiti wasaidizi ambao mmoja ni Ndugu Abdalla
Ali Abeid na wa pili ni Ndugu Riziki Pembe Juma, ambao wapo hapa katika
ukumbi huu leo hapa juu.
Kwa hivyo Waheshimiwa tunaomba tutoe ushirikiano kipindi tutakapohitajika
kufanya mahojiano hayo. Halkadhalika naomba muwatambue watafiti
wasaidizi hao ambao ni Ndugu Abdalla Ali na Ndugu Riziki naomba
wasimame, hao ndio wanaomsaidia utafiti kwa hivyo tuwape mashirikiano.
Waheshimiwa Wajumbe niendelee na uchangiaji ninamshukuru Mhe. Abdalla
katumia muda mzuri, Waheshimiwa Wajumbe tuko nyuma siku 4 katika
bajeti yetu hii, kwa hivyo naomba leo twendeni vizuri ili kesho asubuhi
tuimalize hii tuingie bajeti nyengine.
Mhe. Ismail Jussa Ladhu: Mhe. Naibu Spika, awali ya yote naomba nianze
kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu subhanahu wataala kwa kunijaalia mimi
na sisi sote uhai na uzima tukaweza kuendelea na shughuli zetu hapa, Mhe.
Naibu Spika, ninakushukuru na wewe kwa kunipa nafasi hii na mimi
kuichangia bajeti hii ya Wizara ya Afya. Tatu naomba nimpongeze Mhe.
Waziri wa Afya Mhe. Juma Duni Haji kwa uwasilishaji mzuri wa hotuba yake
asubuhi hii ya leo.
114
Mhe. Naibu Spika, mimi naomba nianze kuwa kusema kwamba mimi binafsi
na kwa niaba ya wananchi ninaowawakilishi hapa wa Jimbo la Mji Mkongwe
ninaikataa na siiungi mkono bajeti hii ya Wizara ya Afya. Mhe. Naibu Spika,
tofauti na zile Wizara nyengine ambazo nilizikataa kwa sababu ya matatizo
mbali mbali. Hii naikataa ili kupeleka ujumbe kwa serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwamba haturidhiki na jinsi wanavyocheza na afya za wananchi
wetu.
Mhe. Naibu Spika, tunajadili bajeti muhimu sana hapa na yule ambaye
tungepaswa kumpa ujumbe wetu hasa Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo hayupo lakini hata Kiongozi wa
Shughuli za Serikali katika Baraza hatunaye hapa na sisi hatuna taarifa ni nani
Kaimu Kiongozi wa Shughuli za Serikali katika Baraza hili. Kwa sababu ni
kawaida katika mabunge ya Jumuiya ya Madola anapoondoka kiongozi wa
serikali anakuwepo kaimu wake. Sasa Mheshimiwa nasikitika sijui kama
tutakayoyasema yatakuwa yanafika ndiko na yatapata ufumbuzi au itakuwa
ndio kama kawaida yetu, business as usual; tunafanya kazi kama tulivyozoea.
Mhe. Naibu Spika, tuliposomewa bajeti kuu ya serikali katika ukurasa wa 31
wa kitabu cha hotuba ya bajeti ya serikali tuliambiwa kwamba bajeti ya
mwaka ujao wa fedha ni bajeti ya huduma za jamii kwa wananchi wa
Zanzibar. Mimi Mheshimiwa mimi naona haya ni maneno ya kisiasa tu,
maneno ya kisiasa kutaka kuwafurahisha wananchi na kutucheza shere sisi
Wawakilishi wao katika Baraza hili. Kwa sababu hali halisi Mhe. Naibu
Spika, haioneshi hivyo na si tu haioneshi hivyo kwa makisio au makadirio ya
bajeti hii, maana makadirio yanaweza kuwa ni mazuri sana na nakumbuka
alipokuwa akiichangia bajeti kuu Mhe. Naibu Waziri wa Afya aliipongeza
kwamba Wizara ya Afya mara hii imetengewa zuri. Lakini fungu hili
lilikuwemo katika nambari likiwa halitokezi katika uhalisia lina faida gani
kwa wananchi wa Zanzibar na afya zao.
Mhe. Naibu Spika, katika mtiririko wa uingizwaji fedha katika kitabu hiki cha
bajeti ya Waziri wa Afya. Wizara ya Afya ni katika Wizara iliyopewa
vipaumbele vya chini kabisa na serikali hii. Kwenye afya za wananchi wetu
kwenye maisha yao halafu tunakuja hapa tunawadanganya kwamba ni
huduma za jamii. Na hili Mheshimiwa si kwa mwaka huu tu mwaka huu
limetafutiwa lugha ya kisiasa kwamba ni bajeti ya huduma za jamii. Lakini
mwaka jana, mwaka juzi, tunaendelea kuambiwa hivyo hivyo kwamba
kipaumbele cha bajeti zetu moja ni afya, na kama utakumbuka Mhe. Naibu
Spika, tulipokuwa katika semina kule tuliambiwa kwamba uwekezaji katika
sekta moja inabidi ufanyike kwa muda mrefu ili tija ionekane. Sasa tija katika
Wizara ya Afya na sekta ya Afya hatuioni.
115
Mhe. Naibu Spika, wenzangu wamesoma hapa kiambatanisho namba 17
kilichoko ukurasa wa 104 wa hotuba ya Waziri, ukitizama Ofisi Kuu Pemba
bajeti imeingizwa asilimia 35.52, mipango Unguja asilimia 31.29, Kinga
Unguja asilimia 37.37, Tiba Unguja asilimia 251.43 ndio pahala pekee
palipovunja rekodi hapo. Tiba Pemba hiyo hiyo tiba tizama huyu ndumila
kuwili. Pemba asilimia 45.19 Unguja ni 251.43 Pemba asilimia 45.19.
Mkemia Mkuu Pemba asilimia 39.24, hospitali ya Mnazi Mmoja asilimia
63.89, Mkemia Mkuu Pemba asilimia 24.90, Utumishi na Uendeshaji Unguja
asilimia 64.04, Utumishi na Uendeshaji Pemba asilimia 39.90, Mfamasia
Mkuu wa serikali asilimia 17.55.
Mhe. Naibu Spika, tunacheza shere na maisha ya watu ukitizama kama
ingelikuwa Wizara ya Afya yenyewe inatoa msukumo chini ya mwenye bajeti
hii ambaye ni Katibu Mkuu wizara kwamba kipaumbele chake ni Utumishi na
Uendeshaji sio afya za wananchi, na ndio maana bajeti imejitokeza vizuri
sana katika Utumishi na Uendeshaji tena Unguja sio Utumishi na Uendeshaji
Unguja na Pemba, Unguja. Mhe. Naibu Spika, hali hii inasikitisha sana. Sasa
ninajiuliza mimi kwamba katika uhalisia huu bajeti hii tunampitishia Waziri
wa Afya tunampitishia nambari, zikamsaidie nini nambari hizi?
Mhe. Naibu Spika, bajeti hii ina matatizo mengi sana kwa upande wa fedha za
kawaida ni hivyo. Ukija katika fungu la maendeleo ukurasa 105 wameandika
hapa vichekecho vikubwa Mhe. Naibu Spika, kwenye jumla huku chini
asilimia fedha walizopata ni 332, hii inakuonesha jinsi gani katika Wizara ya
Afya kwenye utawala kumefeli, Katibu na timu yake wamefeli kazi. Yaani
jumla ya bajeti yake asilimia kajumlisha zile asilimia 13, 54, halafu jumla
kapata asilimia 332 tungekuwa tunaogelea kwa maisha mazuri ya afya katika
Zanzibar tungekuwa tunapata bajeti ya maendeleo asilimia 332. Yaani
utawala wa Wizara ya Afya umeshindwa hata kufanya hesabu ukatupa
asilimia halisi.
Mhe. Naibu Spika, mimi nimefanya hesabu, bajeti halisi ambayo pesa
iliyopatikana ni 724,251,400 kati zilizokadiriwa bilioni 2,731,600,000 ni sawa
na asilimia 26.5 basi. Hapa wanatuandikia ati asilimia 332, mtawala huyu ana
timu yake ya wataalamu, wameandaa kitabu sijui kwa miezi mingapi pale
katika Baraza la Wawakilishi tena kilikosewa ukabandikwa ukurasa juu yake
kwamba hii ndio sahihi isharekebishwa marekebisho yale ndio haya Mhe.
Naibu Spika, tuliyoletewa hapa, are we serious? Yuko wapi Mhe. Rashid Seif
ilikuwa nimuulize leo.
Mhe. Naibu Spika, nasema tena hatuko tayari kuhudumia afya za wananchi
wetu. Mhe. Naibu Spika, inanisikitisha sana huu muda ulionipa leo ni mdogo
sana kwa madudu yaliyokuwemo katika Wizara hii. Mhe. Naibu Spika, ili
116
kuonesha hali halisi ya uingizaji wa fedha nimeazima hapa kutoka katika
kamati iliyopita ya Ustawi wa Jamii makadirio ya matumizi ya fedha na
uingizwaji wake kwa mwezi wa Oktoba/Disemba kwa kazi za kawaida, kwa
kazi za kawaida iko hapa Mhe. Naibu Spika, na kwa kazi za maendeleo iko
hapa ukitizama ni aibu Mheshimiwa sina haja ya kusoma kifungu kimoja
kimoja, kwa sababu nitakuwa ninawapotezea watu muda na mimi nitapoteza
muda wangu. Lakini suala la jumla tu Mheshimiwa kwa Oktoba mpaka
Disemba kuonesha kwamba serikali hii haijali afya za wananchi wake katika
uingizwaji wa fedha.
Makadirio ya kazi za kawaida ilikuwa ni 18,234,000,000, lakini matumizi
halisi 2012, 2013 Oktoba mpaka Disemba ni 3,918,867651, wapi bilioni 18,
wapi bilioni 3 walizoingiziwa.
Mhe. Naibu Spika, katika fedha za maendeleo zilikuwa jumla yake kwa
miradi tofauti kwa kipindi hiki cha Oktoba/Disemba mwaka 2012 zilikuwa
ziwe 2,731,600000, lakini kilichoingizwa ni 192,251400. Kweli tunawajali
wananchi wetu Mheshimiwa, hiyo ndio uchambuzi wa bajeti. Tunaambiwa ati
bajeti ya huduma za jamii kwa wananchi wa Zanzibar tunachezwa shere na
wanachezwa shere wananchi wa Zanzibar Mhe. Naibu Spika.
Mhe. Naibu Spika, nikitoka hapo hilo nimetoa picha halisi tuone kwamba
tunadanganyana humu ndani ya Baraza. Niseme jengine Mheshimiwa kabisa
nimwambie Mhe. Waziri wa Afya kabla sijaingia katika nukta zangu hasa
akakae na watendaji wake wa Wizara ya Afya waliotoka Pemba waliokuja
katika hiki kikao cha bajeti, kuonesha hii aliyoizungumza Mhe. Asaa na
akaigusia Mhe. Abdalla Juma kwamba kuna double standard katika utendaji
wa Wizara hii, watendaji wamekuja hata posho katika kikao hiki cha Baraza
la Wawakilishi kinachoendelea wapo juu hapo Mhe. Naibu Spika, wao
hawakufikiriwa. Halafu tunasema kwamba tunajali usawa wa wananchi,
tunajali huduma zao.
Mhe. Naibu Spika, nikitoka hapo katika kitabu chake cha hotuba Mhe. Waziri
kataja changamoto, na mimi ninampongeza katika hili Mhe. Waziri wa Afya
ndio Waziri pekee ambaye tangu nimeingia Baraza hili katika hotuba yake
siku zote kunakuwa na sehemu ya changamoto, yeye mwenyewe anatwambia
changamoto ambazo anazikabili. Mhe. Naibu Spika, katika changamoto hizi
kazungumzia suala la madaktari na wafanyakazi au watumishi wa sekta ya
afya kuondoka nchini, liko katika ukurasa wa 81.
Mhe. Naibu Spika, madaktari wataendelea kutukimbia na watumishi wengine
wa serikali kwa sababu hatujali maslahi yao. Mimi najiuliza kila siku Mhe.
Spika, na juzi nilipochangia hapa nilisema katika Wizara ya Utumishi wa
117
Umma, hivi Zanzibar kuna madaktari wangapi hao waliokuwa wana sifa
zilizotimia za udaktari tukawa tunashindwa kuyafanya maslahi yao yakawa
bora wakabakia wakatumika kilillahi katika nchi hii? Tuna Wakurugenzi
mamia tunajua kulinda maslahi yao, tuna mameneja chungu nzima tunalinda
maslahi yao, tuna Makatibu Wakuu sijui kumi na ngapi sasa tunalinda
maslahi yao, tuko Wawakilishi, tuko Mawaziri tunalindana maslahi yetu,
lakini huyu ambaye tunampa dhamana ya kutetea afya zetu, wangapi
Mheshimiwa hivyo serikali ingeweza kufanya maamuzi leo ikasema daktari
inamlipa mshahara na stahiki kama anazolipwa Mkurugenzi wa Idara
tungepoteza nini sisi? Leo katika bajeti hii kumetengwa bilioni 17.5 ili
kwenda kurekebisha mishahara, niliuliza hapa tunashindwa kuchangia Mhe.
Naibu Spika, tunapouliza tupeni basi mchanganuo wa marekebisho yenu ya
mishahara tuchangie vizuri tunaambiwa aa tunajiandaa, tunapanga
tutakwambieni, hakuna maelezo kwa Wawakilishi wa wananchi.
Mhe. Naibu Spika, leo tunamlipa daktari wetu sisi hapa MD unamlipa shilingi
laki sita kwa mwezi anapoanza huyu baada ya makato ya kodi anabakia laki
nne tisiini elfu. Assistance Medical Officer analipwa kama laki tano
akishakatwa kodi anabakia kama na laki nne. Lakini hata specialist wenye
ma-PHD hao tunamlipa laki nane Mhe. Naibu Spika, hivyo tunategemea
kweli hawa watakuwa na moyo kujituma wakati wanaona huku kuna
watendaji wengine tunakumba tu? Tunajenga matabaka katika nchi hii. Kuna
tabaka la wala nchi ambao wananchi wanatuona ni sisi wanasiasa na kuna
tabala la wavuja jasho wananchi huko wanaoteseka wakiwemo madaktari
wetu kama hawa Mhe. Naibu Spika.
Mhe. Naibu Spika, leo tunapenda kulinganisha mambo na Tanganyika mbona
katika hili hatulinganishi. Mhe. Naibu Spika, wenzetu katika bajeti hii kuanzia
tarehe 1 Julai, daktari anayeanza kazi na nnayo pay slip hii hapa atakuwa
analipwa milioni moja laki moja na elfu mbili, baada ya kukatwa PSPF, Kodi
ya Mapato, na makato mengine anabakia na laki nane elfu moja mia tano na
hamsini na nane hii hapa Mhe. Naibu Spika. Wameongezewa ndani ya bajeti
hii kwa asilimia 65 ili kukimbia watu wasiondoke ndani ya nchi. Sisi
tunaimba tu siasa kila siku wanaondoka, wanaondoka, sasa tunachukua hatua
gani kuwalinda wako wangapi nilisahau kusema Mheshimiwa. Mhe. Waziri
wa Afya anakuwa muungwana sana atwambie ukweli humu ndani, kwamba
yeye kafika pahala kagonga mwamba katika Wizara ya Fedha na Wizara ya
Utumishi wa Umma, kwamba alifika kusema kwamba nitagoma nao
madaktari wakifika kugoma kwa sababu hamuwalindii maslahi yao.
La kusikitisha Mhe. Naibu Spika, kwamba ilifika pahala katika kikao cha
Makatibu Wakuu kulijadili hili, Katibu Mkuu wao wa Wizara ya Afya badala
ya kuwatetea madaktari wake anakasirika kwamba kwa nini kunafikiriwa
118
maslahi ya madaktari wake. Mimi naona jambo la ajabu Mhe. Naibu Spika,
nilitegemea yeye awe mstari wa mbele maana wengine wanakuja kwetu
wakitu-lobby wakitushawishi tuwajengee hoja hapa mambo yao yawe mazuri.
Huyu naambiwa katika Kikao cha Makatibu Wakuu kakasirika. Mheshimiwa
tunawapenda na yeye anatoka katika fani hii hii anayajua mambo yalivyo
halisi.
Mhe. Naibu Spika, nimetaja hapa kwamba specialist tunamlipa laki nane,
hapo Tanganyika tu specialist analipwa zaidi ya milioni mbili halafu atabakia
hapa afanye kazi gani. Lakini kuna mambo yao ya posho zao Mhe. Naibu
Spika. Kuna call allowance posho ya wito mfanyakazi yoyote wa serikali
taratibu tulizoziweka mwisho kazini saa tisa na nusu akifanya kazi zaidi ya
hapo akiitwa maana yake alipwe posho. Leo mna maposho maalum chungu
nzima katika mabuku haya, lakini madaktari yao hatuyatambui, wanafanya
kazi katika mazingira ya hatari, kuna risk allowance haipo wanafanya kazi
hawana usafiri wanataka wapewe posho la usafiri transport allowance haipo.
Nyumba za madaktari mfano tunagawana sisi kwa sisi wao sasa inabidi
wapewe posho ya nyumba, posho ya nyumba hawapewi, zimetoka baada ya
kelele zetu fedha mwaka jana zimetoka toka kufika mwaka huu zimekwama.
Imekuwa kila kitu cha kusukuma tu mpaka watishwe, mbona yetu sisi
hatungoji tukatisha tukapewa maslahi yetu?
Mhe. Naibu Spika, naambiwa katika bajeti hii hakuna kifungu cha kuwalipia
ndio maana inabidi wanakamatia kamatia ndani ya bajeti kwa nini? Uongozi
wa Wizara ya Afya katika ngazi watendaji Katibu Mkuu na wenzake kwa nini
hawalifikirii hili, tumeona bajeti ya Utumishi na Uendeshaji imenona, kwa
Unguja asilimia 65 wamefika wao lakini nyengine asilimia 17. Ndio maana
ukakuta kipaumbele chao siku zote kwenye kutaka kusafiri kwenda katika
mikutano ya kimataifa, hakuna kukosekana bajeti siku zote bajeti ipo
wanakwenda tu safari, lakini pesa kulipwa daktari hakuna Mhe. Naibu Spika.
Mhe. Naibu Spika, wako ma-orderly, wako wauguzi leo mshahara huu mkia
wa mbuzi tunaomlipa halafu hata kumuwekea chakula wengine wanaweza
kufanya kazi masaa 24 pale anaingia mtu leo anatoka kesho hata chakula
haikewi posho, hata kuwekea chakula haekewi. Huo mshahara mkia mbuzi
tunaomlipa huo atoe akatafute chakula ajilishe mwenyewe anaihudumia nchi,
anaihudumia serikali pale. Mbona sisi katika masemina yetu tunaweka
maposho na viburudishaji kwa nini tunajenga matabaka katika nchi hii,
kwamba ukiwa mwanasiasa tu wewe au mtendaji mkubwa katika serikali
wewe maslahi yako mazuri lakini hawa wanaotumika kuijenga hiyo nchi
tunawasahau maslahi yao? Watwambie watendaji.
119
Mhe. Naibu Spika, zilipendekezwa hizo allowance au posho na marekebisho
ya mishahara namalizia ninayo mengi lakini nitajitahidi kufupisha.
Wamepeleka mapendekezo yao ninazo nyaraka zao hapa zote zimekaa juu ya
meza ya Katibu Mkuu hazisongi mbele, kuna Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tukiwauliza hapa hakuna majibu,
halafu tunalalamika wanakimbia, watakimbia wote Mhe. Naibu Spika, hao.
Mhe. Naibu Spika, jengine ninasikitika sana na muda leo ni mazingira yao ya
kufanyia kazi; leo Rais Mhe. Naibu Spika, katangaza kama huduma za
kujifungua ni bila ya malipo, lakini hali halisi haiko hivyo kwa sababu bajeti
yenyewe haipo. Leo hawa wamesema wanahatarisha maisha yao
unawafungua watu wanatwambia leo wanafunguliwa wengi wengine unakuta
kwa mfano wanaathirika na ukimwi, anakwenda pale anacheza na mgonjwa
kama yule yeye hana kinga ya aina yoyote hata ile posho ya kumkinga
hawana. Lakini tunawalaumu wao na huko nje mtu hajui anatukana daktari tu,
anatukana wauguzi kumbe hatujawapelekea huduma. Wanakuja watu wa
shamba pale hawana pa kupata vitu, anakwenda kufanya nini? Ndio hayo
aliyosema Mhe. Jaku wanaishia kuweka rehani vitu vyao, kwa sababu
unamwambia kwamba huduma bure na ameshasikia katika tangazo la redio na
televisheni, lakini hali halisi akienda pale unaambiwa kuna post operation
dawa hakuna, hakuna sindano hakuna chochote zote anaambiwa kanunue hizi,
kama suala la Ambulance hakuna mafuta mradi hakuna chochote Mhe. Naibu
Spika, leo unaambiwa ukifika pale kuna machupa ya JIK kama unataka
kufanya biashara ya machupa ya JIK ukayachukue hospitali yalivyojaa, kwa
sababu wanaambiwa wakayatafute wao, hakuna chochote kilichokuwa pale,
nini kipaumbele chetu?
Mhe. Naibu Spika, hivi ninavyozungumza oxygen hakuna hospitali, kuna
mgonjwa naambiwa tangu Jumamosi anataka kufanyiwa upasuaji mpaka
dakika hii tunazungumza hajafanyiwa kwa sababu hakuna oxygen theatre
chumba cha upasuaji. Mhe. Naibu Spika, kisa nini bajeti imekwisha
wanaambiwa wasubiri mpaka bajeti mpya, maisha ya watu, hivyo Serikali
imeshindwa na mpango wa vipi kuhudumia hichi kipindi cha mpito baina ya
bajeti iliyopita na bajeti mpya.
Mhe. Naibu Spika, matatizo yako mengi muda huu hata ungenipa saa nzima
mimi siyamalizi yaliyokuwepo katika Wizara ya Afya.
Niseme haraka haraka Mhe. Naibu Spika, nizungumzie suala la matibabu ya
nje ya Zanzibar, tunaambiwa bajeti yake imezidi mno iliyokisiwa, iko katika
ukurasa wa 24 wa kitabu cha Mhe. Waziri. Mhe. Naibu Spika, wanatuambia
bajeti hiyo awali ilipangwa kutumia 335,000,000/= lakini imetumia
990,244,168/=. Mhe.Naibu Spika, ilipokuja Serikali hii tuliambiwa maneno
120
mengi katika kuongeza vitengo pale katika hospitali ya Mnazi Mmoja
kuifanya hospitali ya rufaa, yangelikuwa haya yanashughulikiwa, haya
mabilioni yanayokwenda kila siku kusafirisha wagonjwa nje yangelikuwa
yanatumika kuimarisha huduma tukanunua vifaa, tukawalipa madaktari,
ingelikuwa hizi shughuli zinafanyika hapa hapa Zanzibar, lakini tutaendelea
kila siku kutumia mabilioni kupeleka watu nje, na huko mpaka pengine
ujuane na mtu upate kupenya kwenda huko mbele lakini ndani ya nchi
yenyewe huduma mbovu kabisa.
Mhe. Naibu Spika, nimalizie kwa sababu ya muda ni suala la miradi hii.
Mimi nataka kutoa pendekezo kwamba ukitizama orodha ya miradi ya
maendeleo ni mingi sana, sasa mimi najiuliza mwisho wa mwaka huu fedha
zinazoingizwa ndio kama nilivyoeleza hapa tunategemea wahisani ambao
wenyewe wanaondoshwa, kwa hiyo matokeo yake yote imepata hichi asilimia
10 asilimia 15 hakuna moja linalofika popote, kwa nini Wizara ya Afya
isichague miradi kwa mfano michache ikaingiziwa fedha kikamilifu
ikaonekana tofauti yake, ikakamilishwa ikaonekana tofauti yake, lakini kuna
orodha tele, si kuonesha uhodari Mhe. Naibu Spika, kuja hapa kuonesha
miradi ya maendeleo 10 sijui nini, lakini mwisho wa mwaka hakuna hata
moja iliyofika hata asilimia 10 ya hatua yake, huo si utaratibu.
Kwa hivyo Mhe. Naibu Spika, niseme nimesikitika sana na hali hii, nasikitika
sana hatuwajali madaktari wetu wauguzi wetu, leo mmeacha kuzungumzia
hali ya wananchi wetu kwa sababu kama haya hatuyahudumii, hao wananchi
wetu wataendelea kuimba kila siku na sisi tutapiga kelele kila siku hapa lakini
mwisho itakuwa hakuna kinachopatikana kwa sababu hatuwatunzi
tunawadhalilisha, tunadharau maslahi yapo kwetu sisi tu watendaji na
wakubwa wa Wizara ya Afya. Mhe. Naibu Spika, naomba sana hilo moja la
pili la Serikali ije kujibu kuhusu uingizaji wa fedha kama hatukulipatia
jawabu hili Mhe. Naibu Spika, mimi bajeti hii siipitishi na naomba wenzangu
hii tusiipitishe tupeleke ujumbe Serikalini kwamba sisi tunajali afya za
wananchi kuliko wanavyojijali wao ambao zaidi wanajali safari zao za
kwenda nje kila siku, kazi yao wakubwa kusafiri, haijawahi kukosekana bajeti
ya kusafiri Mhe. Naibu Spika, hata siku moja kwa hiyo bajeti hii hatuipitishi
mpaka tupate jibu la Serikali, si Waziri wa Afya, maana yeye ndiye aliyekuwa
haingiziwi fedha, ila Serikali Kuu ije itujibu hapa.
Mhe. Naibu Spika, narejea kusema siipitishi bajeti hii, siiungi mkono hata
siku moja itarudi kwao. Ahsante.
Mhe. Kazija Khamis Kona: Ahsante Mhe. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi
na mimi ya kusimama hapa kuchangia machache. Kwanza kabisa
nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia afya njema tukakutana hapa
121
tena leo jioni hii kuendelea na ujenzi wa taifa letu. Vile vile nimpongeze
Mhe. Waziri, kwa juhudi anazozichukua katika Wizara yake. Mhe. Naibu
Spika, kwa kuanzia mimi nitaanzia ukurasa wa 5 Kitengo cha Kupambana na
Magonjwa yasiyoambukiza.
Mhe. Naibu Spika, kitabu chake kilieleza magonjwa ambayo yasiyoambukiza
ni sukari, saratani na shinikizo la damu na pumu. Sasa nimuombe Mhe.
Waziri, maradhi haya sijui Wizara yake imefanya utafiti wa kugundua chanzo
kinachosababisha maradhi haya na nimuombe vile vile kama utafiti
haujafanyika basi Wizara yake ichukue jitihada ya kufanya utafiti ili
wananchi wetu wapewe kuwa maradhi haya yanasababishwa na nini?
Mhe. Naibu Spika, kwa kuendelea naenda na hospitali ya Kivunge. Mhe.
Naibu Spika, kabla ya hapo kwanza ninataka ninukuu ukurasa wa kumi na tisa
kifungu cha tatu zero moja kinasema:
"Idara hii inajumuisha hospitali tatu za Wilaya, hospitali ya Chake
Chake, Hospitali ya Abdalla Mzee, Hospitali ya Wete na hospitali nne
za vijiji ambazo ni hospitali ya Makunduchi na Kivunge".
Hapa nadhani Mhe. Waziri, naomba anifafanulie, kwa sababu hospitali ya
Kivunge mara tunaambiwa ya Wilaya na leo hapa naona tunaambiwa wa
vijiji. Kwa hiyo Mhe. Waziri, hapa mimi nataka aje anifafanulie aniwekee
wazi kuwa hospitali ya Kivunge na ya Makunduchi hospitali ya vijijini au za
Wilaya. Halafu Mhe. Naibu Spika, niende hospitali ya Kivunge kwanza
nimshukuru Waziri hospitali ile kwa kutujengea ukuta mzuri uliozuia
kuingiza wanyama, lakini Mhe. Waziri, jengo lile ukuta ule umeujenga mpaka
leo hii bado halijawekwa lango la geti pale, jambo ambalo ni sawa sawa na
kuwa hujafanya kitu kwa sababu pale pako wazi kama wadudu wanaingia,
wanyama wanaingia, hivyo nimuombe Mhe. Waziri, alikamilishe hili ili
tuondokane na usumbufu wa wanyama.
Mhe. Naibu Spika, hapo hapo hospitali ya Kivunge Mhe. Waziri, naomba aje
anihakikishie kwa sababu tumesikia fununu ya kwamba hospitali ya Kivunge
baadhi ya huduma zinafanywa na walinzi, sasa Mhe. Waziri, naomba uje
unihakikishie suala hili ni kweli au laa? Halafu Mhe.Naibu Spika, suala hili
kama lipo basi nimuombe Mhe. Waziri, ya kwamba siku yoyote suala la
kupewa watu ambao taaluma hawana, kwa hiyo suala hili ni tatizo, itakuja
kutokea athari kwa wananchi wetu pamoja na Serikali yetu. Naomba Mhe.
Waziri, suala hili alifanyie kazi kwa kina kama alijue namna gani ya kutatua
na kama hawa walinzi wanafanya hivyo basi awaambie waache mara moja na
kama hospitali ina upungufu wa wataalamu hao basi Mhe. Waziri, awapeleke
wataalamu hao katika hospitali hiyo.
122
Mhe. Naibu Spika, niendelee na hospitali ya Mnazi Mmoja, kwanza leo hapa
nimelisikia tamko ya kwamba Hospitali ya Mnazi Mmoja haijawa kuwa
hospitali ya rufaa, lakini huko nyuma Mhe. Naibu Spika, tuliambiwa hospitali
ya Mnazi Mmoja ni hospitali ya rufaa, sasa jee tulikubali sisi lipi? Hospitali
bado haijawa ya rufaa au vipi?
Mhe. Naibu Spika, hospitali hii tunayosema ambayo Mhe. Waziri, leo
maelezo yake alisema haijakamilika ya kuwa ni hospitali ya Rufaa ina
mashaka mengi au matatizo mengi na ndio maana nadhani akaogopa kutoa
uthibitisho kamili kama hospitali ya rufaa kwa sababu haijakamilika kiurufaa
ndio akachelea kulisema hilo.
Sasa Mhe, Naibu Spika, hospitali hii ya Mnazi Mmoja ina matatizo kiasi
fulani au tuseme madaktari wetu wana matatizo kiasi fulani, sio wote baadhi
ya madaktari. Kwa sababu nikasema hilo Mhe. Naibu Spika, mgonjwa
anatolewa hospitali ya Wilaya au ya Vijiji ntakuja kufafanuliwa, analetwa
hospitali ya Mnazi Mmoja ya Rufaa. Lakini mgonjwa yule Mhe. Naibu
Spika, akishafika hospitali ya Mnazi Mmoja anapewa transfer ya hospitali
binafsi, suala hili lipo si kwa mgonjwa mmoja wala wawili. Kwa hiyo Mhe.
Naibu Spika, aje atuambia Mhe. Waziri, hivi kweli ni haki mgonjwa
kuondolewa hospitali ile hospitali yao ambayo wanachangia kadi na
imewekwa kuwahudumia wao wananchi leo atolewe hospitali ile apelekwe
hospitali ya binafsi, hii kweli ni haki?
Mhe. Naibu Spika, Mhe. Waziri hapa aje anifafanulie na anieleze vizuri ili
nifahamu na kama kweli suala hili lipo na mimi naona lipo haswa kwa sababu
mimi mwenyewe nimelishuhudia achukue hatua zinazostahiki ili madaktari
hawa maana sawa sawa na kusema wanawaiba wagonjwa kwa kwenda
kuwatibu hospitali zao, sasa huu wizi wanaoufanya madaktari wetu Mhe.
Waziri, aufanyie utafiti, upo mimi nishaufanya utafiti upo, sasa na yeye
afanye utafiti ili athibitishe ikisha na hatua achukue.
Halafu Mhe. Naibu Spika, Mhe. Waziri, kitabu chake hapa alieleza namba 5
ya kwamba wana tatizo na daktari bingwa wa macho, kwa sasa hivi daktari
bingwa anatoka Bara hospitali ya Muhimbili. Sasa hapa nimuombe Mhe.
Waziri, afanye jitihada zake na sisi tuwe hawa madaktari bingwa wa matatizo
haya ya macho ili tuondokane na usumbufu wa kuwapeleka wagonjwa wetu
Bara au kumtoa daktari kumtoa Bara.
Mhe. Naibu Spika, Mhe. Waziri alisema ya kwamba hospitali ya Mnazi
Mmoja bado msongomano upo kutokana na watu wanakaa kuwasikiliza
wagonjwa wao au kuwasubiri. Suala hili Mhe. Naibu Spika, halitaondoka
123
hasa kwa wale wenye waja wazito, kwa sababu mtu akiwa na mja mzito huwa
roho yake inampaparika anataka awe karibu nae, sasa nimuombe tu Mhe.
Waziri, hawa wenye kukaa kuwasubiria wagonjwa wao awatafutie sehemu
maalumu ili wakae kwa kusubiri wagonjwa wao au kusikiliza taarifa za
wagonjwa, maana saa nyengine utaambiwa mgonjwa wako fulani jamaa yake
yuko wapi, sasa akiwa hayupo pale itakuwa tatizo.
Sasa nije Wodi ya Wazazi Mhe. Naibu Spika. Wodi ya Wazazi nayo ina
matatizo yake, ina matatizo tena makubwa, halafu katika Wodi hii ya Wazazi
nimuombe au niiombe Serikali au Wizara, Wodi hii kusiwe na Wakunga wa
kiume, kwa sababu nimewashuhudia mimi mwenyewe mle muna Wakunga
wanaume, wasafishaji wanaume na wanawake walivyo jamani wakaumwa
tunajijua wenyewe, kila mtu anakaa anavyojaaliwa na Mungu, sasa kwa kweli
tunakashifika na hayafai kuyasema niliyoyaona hospitali, lakini ninamuomba
Mhe. Waziri, hili alifanyie kazi, hivi jamani ndio tuseme kweli hawapo
Wakunga wanawake ambao waliosomea fani hii. Mhe. Waziri, hili kwa
wanawake wanatukashifu wanaume, kwa hiyo tuiombe Serikali au Wizara
suala hili lishughulikiwe tuwe na Wakunga wanawake, wasafishaji mle ndani
wanawake, halafu pia niwaombe madaktari wetu watumie lugha iliyokuwa
laini wakati wanapowashughulikia wagonjwa hasa waja wazito
wanapokwenda kujifungua, waondokane na lugha za kuwakemea na lugha
zilizokuwa chafu.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja.
Mhe. Abdalla Mohamed Ali: Ahsante Mhe. Naibu Spika, na mimi kunipa
fursa alasiri hii kuzungumza machache kuhusiana na mpango huu wa
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya.
Mhe. Naibu Spika, kidogo baada ya kupitiapitia mpango huu ningependa
nipate maelezo kidogo kwa sababu kuna vifungu hasa katika Idara ya Kinga,
vote 220101 ya gharama za simu. Mwaka jana kitengo hichi kilikuwa na
kama 1,000,000/=, lakini mwaka huu nikiangalia gharama zake zimefikia
karibu 14,000,000/=, sasa najiuliza kulikoni katika Idara hii ya Kinga kiasi
kwamba kwa mwezi wastani wa 1, 000, 00/= na kitu. Lakini pia kuna vote
220202 ununuzi wa zawadi, pia naona kifungu hichi nacho kimenona sana,
kwa sababu mwaka uliopita kilikuwa kina 500,000/= lakini mwaka huu kuna
11,000,000/= sasa sijui zawadi hizi wanapewa wageni wanapoondoka wale
wenzetu kutoka Cuba au vipi nataka nipate maelezo zaidi.
Jengine Mhe. Naibu Spika, katika hilo ni kwamba Idara ya Tiba Unguja. Idara
hii katika Vote 211120 kuna medical allowance, sasa kwa hapa Unguja
medical allowance, destination yake ni 21,000,000/=, lakini Idara hii ya Tiba
124
Pemba, destination yake ni 96,000,000/= sasa mawazo yangu mimi ni
kwamba kama ni wafanyakazi imani yangu Unguja wapo wengi zaidi kuliko
Pemba, je ni vipi huku Pemba iwe hii vote inachukua fedha nyingi zaidi
kuliko hapa Unguja.
Mhe. Naibu Spika, niendelee kidogo kutoa mchango wangu katika Wizara hii.
Ukiangalia kitabu hiki Mhe. Naibu Spika, utaona kuna jengo zuri sana ambalo
tunalitarajia kuwa ni Hospitali ya Rufaa ya Abdalla Mzee, Mkoani Kisiwani
Pemba. Hili ni jambo zuri sana na labda tungeipongeza Serikali kuona sasa
upo umuhimu wa kuwa na Hospitali kama hizi. Isipokuwa Mhe. Naibu Spika,
ni kwamba hivi sasa huwa mara nyingi bajeti zetu zinakwenda kwa programu
na matatizo yetu makubwa ni madaktari, na tunapokuwa na maendeleo kama
haya bila ya shaka huwa tunayakamilisha kwa kupata zana zote na moja kati
ya zana hizo ni madaktari. Sasa labda niulize katika programu zetu
tunazozifanya je tumeandaa utaratibu wa kupata madaktari ambao labda
baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali hii wataweza kuhudumia
hospitali ile.
Mhe. Naibu Spika, kwa nini ninasema hivyo, ni vizuri kwamba Makomredi
wenzetu toka mwaka 1969 wanatusaidia katika kuiendesha hospitali hii ya
Abdalla Mzee Mkoani, lakini hivi sasa Mhe. Naibu Spika, ni kuwa hospitali
hii haina daktari mzalendo, kwa maana hiyo wenzetu wamebadilika kiuchumi,
sasa inapofika wakati wa likizo huwa kipindi kirefu madaktari hawa hawapo
inawezekana siku nyengine mwezi mmoja na ziada. Ikifikia kipindi hicho
Mhe. Naibu Spika, huwa tunapata tabu sana, sasa sijui Mhe. Waziri, hilo
tunalijua kwamba hawa wenzetu wanaotusaidia kwa hali na mali, kuna wakati
huwa wanaondoka na kuiacha hospitali bila ya madaktari, ingawaje siku
nyengine huwa tunaelezwa huwa tunapata madaktari kutoka sehemu
nyengine, lakini hii mimi kwa mawazo yangu haitoshelezi.
Hivyo ningeomba katika utaratibu utakaokuja hivi sasa basi tuhakikishe
kwamba daktari mzalendo anakuwepo akasaidiana na wale wenzetu au
watakapokuwa hawapo basi yeye atafanya kazi yake kama kawaida.
Lakini Mhe. Naibu Spika, pia niseme kwamba tunapokuwa na miradi ya
maendeleo kama hii bila ya shaka kutakuwa na negative au positive aspect na
negative zake. Mhe. Naibu Spika, katika utanuzi wa hospitali hii bila ya
shaka kutatokea watu ambao wataathirika, na kwa ujumla ni wale watu ambao
wanakuwa wapo karibu na eneo la hospitali hii. Mara nyingi watu kama
hawa huwa wanafanyiwa malipo compensation ya vijumba vyao, lakini la
kushangaza kwamba tunapofanya tathmini ya majumba haya huwa Mhe.
Naibu Spika, tunaangalia ile bati aidha na yale matofali tu hatuangalii
mengine.
125
Hivi sasa hata kama mtu utamlipa pengine thamani ya nyumba yake
10,000,000/= itakuwa ni thamani ya kile kijumba, bado hatujazingatia
kwamba mtu yule anahitaji kiwanja akiondoka pale ili apata kujijengea hiyo
nyumba nyengine. Sasa kinachotokea ni kwamba malipo tunayowapa
wananchi wetu yanakuwa ni kidogo hayawasaidii kuweza kupata kujenga, ku-
replace zile nyumba zao ambazo zimevunjwa.
Kwa hiyo ningeomba wakati wa kufanya tathmini kama hii na wao wenyewe
tukawashirikisha, tusiwaache wakawa wapo pale tukawapalekea tu wewe
tathmini ya nyumba yako ni kiasi fulani, lazima tukae pamoja tufanye
tathmini na tukubaliane tuone kwamba na hawa wameridhika na sio tu
kwamba Serikali inataka kufanya jambo fulani kwa hiyo unawajibika
uondoke japo kwa shingo upande. Nafikiri wote ni raia wa nchi hii na
wanahitaji na wao kupewa haki zao ili wajione wanatunzwa na kuthaminiwa
katika nchi yao.
Mhe. Naibu Spika, labda niende kidogo katika kitengo cha huduma za damu
salama. Ninachokijua ni kwamba hichi ni kitengo kimoja muhimu sana kwa
hivi sasa, kwa sababu hakuna mtu yeyote ambaye anakwenda hospitali
akaambiwa wewe unatakiwa utoe damu au unatakiwa usaidie damu kwa njia
moja au nyengine, isipokuwa kitengo hiki ndicho kinachosimamia kusambaza
damu kwa hospitali zote zilizopo. Lakini kila nikiangalia nahisi kwamba
labda kitengo hichi sisi kama ni Serikali hatujakipa umuhimu wa kipekee,
kwa sababu sioni fungu ambalo limeingizwa au ruzuku yoyote na
tumewaachia wahisani tu watu ambao tunajua fika kwamba mchango wao
umeanza kupungua. Sasa nafikiri kulikuwa na haja kubwa sana hivi sasa
kuona kwamba kitengo hichi kina umuhimu wa pekee, na hivyo kupatiwa
fedha ili kuweza kujiendesha, tusiwaachie peke yao hawa Wahisani, siku
ambayo watasimama basi na sisi angalau tuwe tushaanza kutembea japo
kupiga mbio hatujaweza lakini kutembea tumeshaanza.
Mhe. Naibu Spika, sasa niendelee kidogo katika kitengo cha Mkemia Mkuu
wa Serikali. Mimi nafikiri kama Wizara ingelikuwa ina umakini basi hapa
ndio ingelianzia ile prevention kwa sababu utumiaji wa vyakula na vipodozi
na mambo mengine ndio unasababisha mengi katika matatizo tuliyonayo.
Lakini kitengo hichi bado hatujakipa umuhimu wake, nafikiri tungeangalia
kwa kina sasa tukajua kwamba tukikiendeleza kitengo hichi basi ni moja kati
ya kinga, tutakuwa tumeanza njia moja ya kuwakinga wananchi wetu na
maradhi, kwa hiyo zile fedha ambazo labda tunazitenga katika kununulia
madawa zingelipungua.
126
Kama sijakosea Mhe. Naibu Spika, jana nilipitia gazeti moja linalotoka
Tanzania Bara na nikaona kwamba kuna kitengo kinachoshughulika na
mambo kama haya, wao wamepiga marukufu au wameona kwamba kuna
matatizo katika utumiaji wa mafuta ya OKI, nikawa najiuliza kwa nini watoe
ripoti kama ile, wakati kwetu sisi hapa hakuna ripoti yoyote inayoeleza.
Imani yangu ni kwamba tajiri aliyekwenda kununua mafuta yale basi na tajiri
mwengine alitokea katika kisiwa cha Zanzibar na yeye akaleta mafuta kama
yale. Lakikni matokeo hapa sisi tunaendelea na hakuna taarifa yoyote lakini
kule kwa wenzetu taarifa imeshatoka kwamba mafuta haya hayana ubora wa
kutumia mwanaadamu. Sasa labda kuna ushirikiano wowote kati ya vitengo
vyetu hivi viwili vinavyoshughulika na mambo haya ya vyakula na vipodozi
na mengineyo ili linapotokea suala kama hili upande mmoja ikawa taarifa, na
sehemu nyengine imefika na labda taarifa sio kufika tu lakini ikawa
imekubalika itumike ipasavyo.
Mhe. Naibu Spika, labda niende tena kidogo katika Vituo vya Afya. Mimi
nafikiri hapa tumesahau kwamba mpango wa Serikali ni kueneza vituo vya
afya vijijini. Tunashukuru kwamba kila kona unayopita unavikutia vituo hivi,
lakini la kushangaza baada ya kukutia kile kikapu wanachopimiwa watoto
basi hukutii chengine, dawa hakuna, vifaa vyengine hamna, na sehemu
nyengine hata huyo daktari pengine anakaa meli sita ndio anafika au hayupo
kabisa.
Kwa hiyo hapa nahisi Wizara ingeangalia kwa kina kwamba hivi sasa kuna
umuhimu wa vituo hivi kwa vile tuna Bohari Kuu ya Madawa basi navyo
vikapata mgao wa kutosha, ili tukajua kweli ile thamani ya kuvijenga vituo
hivi ipo.
Mhe. Naibu Spika, vituo vyengine tulivyonavyo vinafikia hata milioni mia
mbili, mia tatu thamani yake lakini ni jambo la aibu kuona unakwenda katika
kituo kile huduma unazozipata ni chache mno, sasa Wizara hilo ilione na
tukijaaliwa mwaka unaofuata basi tuone sehemu hizi nazo zinapatiwa huduma
zinazostahili. Lakini baada ya kusoma ripoti hii nimegundua kwamba kuna
ongezeko kubwa la kutoona yaani wananchi wanapungua nuru ya macho hasa
nilipoisoma ile ripoti ya Hanyengwa Mchana, katika askari 59 waliofanyiwa
kuna waliopewa miwani na kuna waliopewa dawa, hii inamaanisha kwamba
hivi sasa hili ni moja katika matatizo makubwa yanayowasumbua wananchi
wetu, sasa labda Wizara imeshaandaa utafiti wowote ikaweza kutusaidia
wananchi tuepukane na mambo haya angalau ukatwambia ongezeko hili
limesababishwa na tatizo moja, mbili, tatu, pengine nina imani kwamba labda
vyakula tunavyokula inawezekana ikawa ndio sababau, kama bado basi
ningeishauri Wizara kama ilivyofanya tafiti katika kitengo katika mradi wa
malaria, basi na hapa ukaanza utafiti mapema, kwa sababu moja katika
127
matatizo sugu yanayokuwa kwa wingi hivi sasa ni wananchi kutoona, hasa hii
iliyotueleza kwamba kuna watoto maskulini, sasa sijui watakuwa wanasoma
vipi. Ingawaje njia za kisasa zipo lakini kinga ni bora kuliko tiba. Mhe. Naibu
Spika, nakushukuru.
Mhe. Salma Mohammed Ali: Mhe. Naibu Spika, nakushukuru sana kwa
kunipa nafasi, lakini kwanza nataka nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa
kuniwezesha kusimama hapa na kuchangia hotuba hii. Mhe. Naibu Spika,
sasa nitarudia kukushukuru wewe sana kwa kunipa nafasi, tena nasema ni
nafasi ya upendeleo. Kwa sababu Mhe. Naibu Spika, kisa cha kusema hivyo
leo mimi sijaleta karatasi ya kutaka kuchangia, kwa hivyo naamini huo ni
upendeleo au kuna mmoja humu aliyenipendelea nichangie basi akaniandikia
kikaratasi. Nakushukuru sana Mhe. Naibu Spika. (Kicheko)
Mhe. Naibu Spika, sasa naomba nitumie nafasi hii kumpongeza sana Mhe.
Waziri kwa jinsi alivyoisoma hotuba yake, na vile vile nampongeza zaidi kwa
pale alipotueleza kuwa kaweza kupunguza msongamano wa jamaa wa
wagonjwa wanaolazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Mhe. Naibu Spika, hili ni jambo zuri kwa sababu haipendezi kwenda wodini
muda wote ikawa mmejaa watu, hata daktari anashindwa kufanya kazi ya
kuhudumia wale wagonjwa. Lakini Mhe. Naibu Spika, hapa naomba
nimuulize Mhe. Waziri tayari keshajitayarisha? Kwa sababu naamini watu
wengine wanaokaa mle huwa wanaingia kwa kuwahudumia wale wagonjwa
wao, hakuna hata mmoja anayependa mgonjwa wake aidha akae na kinyesi
kwa muda mkubwa au adhalilike. Sasa ikiwa Mhe. Waziri keshajipanga basi
mimi nitamshukuru sana kwa sababu tunaona hospitali za wenzetu tukienda,
mgonjwa unaingia kwa masaa kumtizama lakini unamkuta hali yake
inaridhisha. Kwa sababu zile huduma za usafi na kila kitu anafanyiwa.
Kwa hivyo, namuomba Mhe. Waziri aliangalie hili kwanza, tayari anao
wafanyakazi wa kutosha wa kufanya hizo kazi? Asije akawazuia watu kuingia
kuwasaidia wagonjwa wao wakati yeye hana uwezo wa kuwahudumia.
Mhe. Naibu Spika, sasa nataka niende ukurasa wa 32, hapa pana Ofisi ya
Mfamasia Mkuu naomba ninukuu Mhe. Naibu Spika. “Ofisi ya Mfamasia
Mkuu wa Serikali ina jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu,
vifaa, tiba pamoja na kusimamia matumizi sahihi ya dawa. Katika kulifikia
lengo hili, Ofisi ya Mfamasia Mkuu imepewa dhamana ya kufanya makisio na
kuratibu ununuzi wa dawa na vifaa, kufanya ukaguzi kwenye Hospitali na
Vituo vya Afya ili kuhakikisha utumiaji sahihi wa dawa”.
128
Sasa Mhe. Naibu Spika, katika kiambatanisho nambari 17 ukurasa wa 104,
Makadirio yaliyopangwa ni shilingi 1,547,000,000/-, zilizopatikana ni shilingi
271,000,000 tu sawa na asilimia 17. Sasa namuomba Mhe. Waziri
atakapokuja atwambie hizi asilimia 17 kweli zinaweza kutekeleza haya
majukumu yaliyopangwa ya Mfamasia Mkuu.
Mhe. Naibu Spika, nataka niende kwenye kiambatanisho hicho hicho, fungu
0701 Tiba Unguja, fedha zilizopatikana ni asilimia 251.43. Lakini
kiambatanisho hicho hicho fungu 0801 Tiba Pemba fedha zilizopatikana ni
asilimia 45. Sasa namuomba Mhe. Waziri hapa akijasimama anambie ni
sababu zipi na kwa nini Idara ni moja ya Tiba Unguja ipate asilimia 251 na ya
Tiba Pemba ipate asilimia 45? Namuomba akija anipe sababu, kwa sababu
ingelikuwa angalau ni idara mbali mbali tungelisema vyengine, lakini idara
moja Tiba Unguja na Tiba Pemba, hapa asilimia 251 kule asilimia 45.
Namuomba Mhe. Waziri atwambie hili. Kwa sababu hapa ni kuwavunja
moyo wananchi wataona upande mmoja wanabaguliwa.
Sasa Mhe. Naibu Spika, nataka niende kwenye kiambatanisho Nam. 18
kifungu 60008. Mhe. Naibu Spika, hapa pana programu ya kudhibiti malaria.
Mhe. Naibu Spika, hapa tumeelezwa kwamba imepata asilimia 19 tu hiyo
programu ya kudhibiti malaria.
Mhe. Naibu Spika, hili ni tatizo kwa sababu malaria yalikuwa yamepungua
kwa asilimia kubwa, lakini hivi sasa Mhe. Naibu Spika, malaria yashaanza
kurudi, ingawa ukienda hospitali ukiangaliwa damu unaambiwa huna malaria,
lakini ukiondoka tayari dose ya malaria unapewa. Kwa nini upewe dose ya
malaria kama huna malaria, ni kwa kuwa tayari yameshaanza kurudi. Sasa
namuomba Mhe. Waziri anambie hapa hivi kweli wakiondoka tu hawa
wafadhili haya malaria ndio yanarudi, inaonesha serikali haiko tayari kwa
sababu ukisaidiwa lazima kile ulichosaidiwa ukithamini. Leo wanaondoka
wafadhili hawajafika kwao wanasikia Zanzibar malaria tayari.
Mhe. Naibu Spika, hili linasikitisha tena naiomba serikali ijizoweshe hasa
ikifadhiliwa ikubali ule ufadhili. Serikali yetu haijajiweza, sasa
ikishafadhiliwa ule ufadhili waupokee si kwa kuwa akishaondoka mtu tena
basi. Hivyo kweli wewe umejengewa nyumba yule aliyekujengea mpaka
kufagia aje akufagilie? Mhe. Naibu Spika, serikali ijizoweshe hasa, ifanye
makusudi kujizowesha kuthamini nguvu za wenzetu, si kwa kuwa
wameshatusaidia tuache zipotee, hivyo kweli sisi kila siku tutasaidiwa jambo
lile lile tu, keshokutwa wanakuja wafadhili wengine ati wanakuja kupambana
na malaria, haipendezi, waje watusaidie kwa mengine.
129
Mhe. Naibu Spika, sasa nataka niende kwenye Maabara ya Jamii Pemba. Kwa
kweli mimi hapa nasikitika sana, hii ni bajeti ya tatu nimo katika Baraza hili,
katika hotuba hatujaona hata pesa ndogo inayotengwa kwa maabara hii. Mhe.
Naibu Spika, hilo ni tatizo, ndio hapo hapo tulipozowea kufadhiliwa
tukajiachaacha na wakishaondoka waliotufadhili hatujui kuendeleza.
Mhe. Naibu Spika, mimi Wafanyakazi wa Wizara ya Afya huwasikia sana
kuwa maabara hii haitengewi fedha na kazi zake Mhe. Waziri katueleza, wana
kazi kubwa wanazofanya tena nzuri, lakini leo serikali haiwafikirii hata
kidogo ikiwa hawajajizowesha leo hao wafadhili wakiondoka hawa wataweza
kweli. Mhe. Naibu Spika, yote hayo niliyosema namuomba Mhe. Waziri
akinyanyuka anijibu.
Sasa nataka niende kwenye ukaguzi wa abiria Bandarini na Airport. Mhe.
Naibu Spika, mimi hapa nina masikitiko makubwa, kwa sababu katika airport
ya Pemba katika ziara ya Kamati tulikwenda hicho kijumba kilichoandikwa
pale mlangoni „Afya‟; Mhe. Naibu Spika, mimi mwenyewe kama ni choo basi
ningelitafuta vya kukaa, nikae vipi niweze kujisaidia hicho chumba kilivyo,
maana ile kujisaidia ningeliona wasi wasi nikatafuta vya kukaa. Chumba
kibovu, madirisha hakina, hapana madaktari na hata ile panadol haipo. Sasa
namuomba Mhe. Waziri akija na hili anambie pale kweli ni Kituo cha Afya au
pana maandishi tu ya afya.
Vile vile nataka nije katika tatizo kubwa linalotukabili wanawake na
wanaume, lakini wanawake tumezidi ugonjwa wa kensa. Mhe. Naibu Spika,
hili ni tatizo ni ugonjwa mgumu, ugonjwa uliokuwa matibabu yake ni ghali na
wananchi wetu tunawajua hali zao. Matibabu yake hayapatikani hapa petu
mpaka uende kwa wenzetu. Sasa namuomba Mhe. Waziri anambie ana
mpango gani wa kutusaidia? Tunateketea! Kwa sababu uwe unaumwa malaria
tu peke yake basi utakuwa wewe tayari unaangamia huna kitu je, leo ugonjwa
kama ule unaoambiwa mpaka upate mamilioni ya kutibiwa, shilingi elfu mbili
mtu hanayo, lazima Wizara ya Afya hili walitizame tunateketea!
Sasa hivi wanawake wengi kila mmoja utamsikia nina kensa ya kizazi. Kwa
hivyo, namuomba Mhe. Waziri walitizame hili kila mmoja na uwezo wake au
aliyekuwa hana uwezo akishaumwa ndio basi.
Halafu katika ukurasa wa 69. Mhe. Naibu Spika, hapa nimekuta mfumo wa
ukusanyaji wa taarifa za malaria kupitia simu za mkononi. Namuomba Mhe.
Waziri anifahamishe vizuri kwa sababu mimi sijaisikia hii, sijui humu vijijini
wana watu wao mtu akishaumwa anatoa zile taarifa au ni mgonjwa
mwenyewe. Namuomba hapa akija anifahamishe ili tujue huu utaratibu na sisi
130
tuweze kuutumia. Kwa sababu pengine kuna watu walio na malaria wengi
lakini hawajajua huu utaratibu.
Suala jengine ambalo nataka nilizungumzie Mhe. Spika, ni kwamba pale
Wawi pana Hospitali hii ama nawapongeza sana Mhe. Waziri kwa huduma
wanazozitoa hasa za mama na watoto. Lakini Mhe. Naibu Spika, aliyepo pale
sijui ni daktari au ni nesi lakini ni mmoja, akiumwa yule basi ile kazi
haifanyiki pale. Hii miezi ya nyuma Mhe. Naibu Spika, alikuwa yuko likizo
kama miezi mitatu alikuwa anatoka daktari aidha kutoka Gombani au Jeshini
na akija pale kwa siku moja kwa wiki, ukienda wanawake na watoto pale
wanasokoteana. Hebu Mhe. Waziri pale atuongezee mtu, mtu mmoja huyu
atakayefanya kazi kuanzia asubuhi mpaka saa tisa hapumziki na maslahi ndio
kama hayo yanayosemwa kila siku hayapo; hivyo Mhe. Naibu Spika, si
kuwarejesha nyuma wafanyakazi?
Namuomba Mhe. Waziri apatizame pale kile kituo ni cha jeshi na huyo
aliyepo wamempeleka wao kutoka Wizara ya Afya, lakini watuongezee mtu,
wanawake na watoto wanahangaika sana kufika toka alfajiri. Mtu akishasali
tu anatoka kwake kukimbilia kuweka foleni na atarudi saa saba au nane. Kwa
hiyo Mhe. Waziri, nakuomba na hapo utusaidie.
Mhe. Naibu Spika, jengine ambalo nataka niliseme kidogo ni kuhusu
madaktari. Naomba Mhe. Naibu Spika, madaktari wajijue kama ni madaktari
na kazi zao ni tofauti na wafanyakazi wengine. Kwa sababu wao wanafanya
kazi na wagonjwa, na mgonjwa vile ukimpokea vizuri au ukizungumza nae
vizuri basi peke yake ile huwa keshapata faraja, yale maradhi yanaanza
kupungua. Lakini ikiwa mgonjwa utampokea vibaya na kumpa maneno
mabaya basi hata kama utampa ile dawa yeye atajisikia ni mnyonge tu. Kwa
hivyo, namuomba Mhe. Waziri awape semina madaktari, wajue kama kazi
wanazofanya wao ni tofauti na wafanyakazi wengine, wao wana kazi nzito
kukaa na wagonjwa, na si semina tu hata maslahi yao yaboreshwe kwa sababu
ndio wameshatajwa wana kazi nzito.
Lakini pia Mhe. Naibu Spika, katika hizo kazi tunawaomba wale waliokuwa
wanatusaidia kule katika kujifungua wasitumie maneno yaliyokuwa sio. Mhe.
Naibu Spika, hata kutoka roho kila mmoja na vile anavyotoka, na kujifungua
kila mmoja na anavyojifungua, ikiwa mtu atapiga makelele sema naye
umwambie huo si utaratibu mzuri ni aibu hiyo, lakini kumkaripia
ukamwambia hizo starehe zako uliniita haipendezi, hakuna asiyejua kama
jambo lile ni la starehe, lakini kwa nini umwambie mtu pale maneno ya
kashfa.
131
Mhe. Naibu Spika, namuomba Mhe. Waziri atoe semina sana kwa
wafanyakazi wake kwa kweli wana kazi ngumu na wanahitaji wafikiriwe hata
kwa maposho, lakini pia na kauli zao ziwe nzuri kwa wagonjwa.
Mhe. Naibu Spika, jambo moja linalowavunja moyo wanawake na
wakajifungulia nyumbani na wakahatarisha maisha yao ni hili. Wakati
mwengine Mhe. Naibu Spika, unakuta watoto waliokuwa hata hawajaolewa
wanakujibu maneno hayo, wewe mwenyewe unaona aibu kuwatizama
anakwambia haya ilikuwaje uliniita hiyo siku hiyo, haya kwani lazima
nikuite.
Mhe. Naibu Spika, nakushukuru sana, namuomba Mhe. Waziri anijibu hoja
zangu.
Mhe. Nassor Salim Ali: Ahsante Mhe. Naibu Spika, na mimi kunipa nafasi
hii ya kuchangia kidogo Hotuba ya Bajeti ya Wizara hii ya Afya. Mhe. Naibu
Spika, kwanza nichukue fursa hii kukupongeza wewe kwa kunipa nafasi hii.
Aidha, pia nimpongeze Mhe. Waziri pamoja na Katibu Mkuu na watendaji
wote wa Wizara ya Afya kwa kuweza kufanya kazi ngumu na ndefu na nzito
ya afya ambayo inagusa jamii yote ya Wazanzibari.
Aidha, pia nimpongeze sana kwa dhati kabisa Rais Dr. Ali Mohamed Shein
kwa kuweza kusimamia vyema serikali yetu au serikali yake inayoongoza
kwa kuwapa miongozo mawaziri wake na watendaji katika kuleta huduma
zilizo bora. Vile vile nimpongeze kwa jana kutangaza kwamba ataleta
mishahara mipya kwa wafanyakazi wa serikali na nina imani kwamba
wafanyakazi wa Wizara hii ya Afya basi na wao watakuwa wamefurahia suala
hili. Nampongeza sana Mhe. Rais.
Mhe. Naibu Spika, nije katika ukurasa wa 31 wa kitabu cha Mhe. Waziri
Hospitali ya Wagonjwa wa Akili, Kidongochekundu. Mhe. Naibu Spika,
mbali na uboreshaji wa majengo mbali mbali katika hospitali ile bado kuna
matatizo makubwa ambayo yapo katika hospitali ile. Mhe. Naibu Spika, kwa
kweli kuna jambo la kusikitisha sana kuona kwamba hospitali ile ambayo
inawagusa jamii yetu, ndugu zetu kuona kwamba bado ina matatizo ya
masuala ya usafi na kuna matatizo ya wadudu ambao wakiwemo kunguni na
wadudu wengine ambao wanaleta matatizo katika hospitali ile. Hili lalamiko
limetujia sisi na vile vile kuthibitisha kuwa kuna tatizo hili.
Lakini cha kusikitisha sana Mhe. Naibu Spika, kuona kwamba kuondoa
matatizo ya kunguni ambapo karatasi ninayo ya bajeti ya kuweza kuja
kufanya utibabu wa kuondoa kunguni katika hospitali ile ni takriban kama
shilingi laki tatu na nusu. Hii ni aibu na ni jambo la kusikitisha sana,
132
ningemuomba sana Mhe. Waziri kufuatilia suala hili kuhakikisha kwamba
ndugu zetu, jamaa zetu, wanaondokana na matatizo ya wadudu kama vile
kunguni katika Hospitali ile ya Wagonjwa wa Akili pale Kidongochekundu.
Mhe. Naibu Spika, nije katika ukurasa wa 30 Hospitali ya Wazazi
Mwembeladu. Nitoe pongezi kubwa sana kwa Waziri pamoja na watendaji
wake katika kusimamia vyema na kufuata miongozo na ushauri tuliokuwa
tukiutoa hapa katika Baraza lako tukufu. Mhe. Naibu Spika, katika vikao
mbali mbali vilivyopita tulizungumzia suala la matatizo ya madaktari, lakini
tunashukuru kwamba kumepelekwa madaktari wawili na Waziri ametueleza
hapa ambao wamepelekwa pale na ambao wamesaidia kuondoa matatizo
makubwa yaliyokuwa yanaikabili hospitali ile.
Mhe. Naibu Spika, katika kitabu hiki naomba uniruhusu kusoma, “Kufikia
Machi 2013, jumla ya kinamama 4,067 walilazwa na akinamama 3,498
walijifungua kwa njia ya kawaida na hakuna mzazi aliyefariki dunia. Aidha,
hospitali hii hushughulikia huduma ya mama na mtoto pamoja na kutoa
huduma za VVU na UKIMWI.
Mhe. Naibu Spika, kuweza kuwazalisha akinamama takriban elfu nne na
kuweza kutotokea kifo hata cha mtu mmoja hii ni hatua kubwa na ni hatua ya
kupongezwa. Kwa kweli mimi kwa dhati kabisa nampongeza Mhe. Waziri
pamoja na watendaji wake na madaktari wetu kwa kusimamia vyema na
kuweza kutoa huduma zilizo bora katika hospitali ile. Lakini bado pia ipo haja
ya kuweza kuongeza bidii na kuongeza huduma zilizo bora zaidi katika
hospitali ile.
Mhe. Naibu Spika, nije Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ukurasa wa 246
katika kitabu kikuu. Ukifungua katika kifungu cha 2000201 Chakula na
Vinywaji. Mhe. Naibu Spika, nataka maelezo wakati Waziri atakapokuja,
atupe maelezo sahihi kuona kwamba katika fungu hili kwa mwaka 2012/2013
kulikuwa na jumla ya shilingi 3,475,000/-, lakini katika bajeti ya mwaka huu
2013/2014 kuna jumla ya shilingi 15,266,000/-. Sasa ukitoka katika mwaka
jana shilingi 3.4 milioni na hivi sasa ni 15.2 milioni kweli ni kiongezeko
kikubwa. Kwa hivyo, akija atupe maelezo sahihi Mhe. Waziri.
Vile vile ukija katika kitabu kikubwa kile cha kurasa 247 kifungu 220517
Utayarishaji wa Mpango wa mwaka wa Bajeti. Mhe. Naibu Spika, katika
bajeti ya 2012/2013 kulikuwa na shilingi 6,900,000; lakini ukija katika bajeti
ya mwaka huu 2013/2014 kuna shilingi 20,000,000/-. Ni vyema Mhe. Waziri
akija atufafanulie atupe maelezo kutoka shilingi 6,900,000 mpaka shilingi
20,000,000.
133
Mhe. Naibu Spika, baada ya kusema hayo nije katika Kituo cha Afya cha
Rahaleo. Kituo cha Afya cha Rahaleo ni kituo ambacho kimekuwa kikitoa
huduma na kuweza kusaidia jamii katika masuala mbali mbali yakiwemo pia
ya UKIMWI. Na kituo kile hapo zamani kilikuwa kikisaidiwa sana na
Agakhan Foundation. Lakini taarifa tulizonazo kwamba tayari Agakhan
Foundation wanataka kuondoa mkono wao katika kusaidia kituo kile. Sasa
nilikuwa nataka maelezo kwamba hili ni kweli? Na kama ni kweli basi
wamejipanga vipi ili kuweza kukiendeleza kituo kile ambacho kinasaidia sana
jamii ambayo imo katika Wilaya hii ya Mjini.
Lakini vile vile kituo kile kinahitajika kufanyiwa ukarabati na kuweza
kukiendeleza na kukiweka katika hali nzuri na kuweza kusaidia jamii.
Lakini Mhe. Naibu Spika, nije katika kitabu cha Mhe. Waziri ukurasa wa 50,
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala.
Mheshimiwa katika Baraza lako hili tukufu kupitia Kamati ya Maendeleo ya
Wanawake na Ustawi wa Jamii katika kipindi kilichopita kilitoa maelekezo
haya ili kuweza kupata taarifa ya waganga asilia au waganga wa tiba wa
Kichina. Kama Mhe. Waziri unakumbuka Makamo Mwenyekiti Mhe. Hija
Hassan alitamka hapa Barazani na kusema tupate taarifa sahihi za tukio
ambalo lilitokea pale kwa waganga wa jadi hawa wa Kichina kwamba kuna
mama mmoja au mzalendo Mzanzibari alipoteza maisha yake katika kipindi
kile ambacho tulizungumza kwenye Baraza lililopita. Lakini mpaka leo
hatujapata taarifa au maelezo yoyote kuhusiana na uchunguzi au taarifa za
wenzetu hawa ambao wanashughulika na tiba asilia za Kichina. Kwa hivyo, ni
vyema atakapokuja atupe taarifa ya uchunguzi umefikia wapi kuhusiana na
suala lile.
Mhe. Naibu Spika, baada ya kusema hayo naunga mkono kwa asilimia mia
moja, lakini vile vile namuomba Mhe. Waziri atupe yale ambayo nimetaka
kuyajua. Baada ya kusema hayo Mheshimiwa nakushukuru sana.
Mhe. Subeit Khamis Faki: Nakushukuru sana Mhe. Naibu Spika, usiku huu
kunipa na mimi fursa nichangie hotuba hii ya bajeti ya Wizara ya Afya
ambayo ni wizara muhimu sana.
Mhe. Naibu Spika, kwanza napenda nishukuru na kumpongeza Mhe. Makamu
wa Pili wa Rais kwa kuweza kusaidia Hospitali ya Micheweni vitanda pamoja
na magodoro 40. Nampongeza sana kwa uzalendo wake na kuona kwamba
kuna haja ya kuisaidia Hospitali hiyo na akafanya hivyo, namuomba
Mwenyezi Mungu amjaalie awe na moyo pale anapoona kunastahiki kusaidia
atusaidie tena.
134
Jambo la pili, pia napenda niipongeze Wizara ya Afya kwa kushirikiana na
wafadhili kwa kujenga maabara nzuri ya Micheweni kwa ajili ya kusaidia
Hospitali ya Micheweni pamoja na wananchi wa Wilaya ya Micheweni kwa
ujumla. Lakini pamoja na pongezi hizo muhimu, sasa napenda niwaambie
Wizara ya Afya kama pamoja na kutujengea maabara nzuri sana lakini
maabara ile inahitaji kupata madaktari wazuri ili iweze kufanya kazi vizuri.
Kwa sababu kujenga maabara ni kitu kimoja kimekamilika lakini kuweka
madaktari wakaweza kufanya kazi vizuri ni kitu chengine. Kwa hivyo,
namuomba Mhe. Waziri aone kwamba kuna haja ya kuweka madaktari wazuri
ili ile maabara iliyopo pale iweze kufanya kazi vizuri.
Pia niwaombe watendaji wa hii Hospitali ya Micheweni kuitunza sana ile
maabara, kufanya kazi kwa kuitunza na kuishughulikia vizuri ili iweze
kudumu na kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi.
Mhe. Naibu Spika, suala jengine ninalotaka kuzungumza nafikiri kipindi
kilichopita nilizungumza sana katika bajeti mbili zilizopita; na bajeti hii
nitazungumza tena. Mhe. Naibu Spika, Hospitali ya Micheweni kabla ya
kuazimia kuwa ifanywe kama Hospitali ya Wilaya, basi ilikuwa inafanya kazi
kama Hospitali ya Wilaya. Kwa hivyo, kipindi kilichopita nilisema kwamba
hospitali yetu ni ndogo haitoshi na leo napenda nikumbushe tena.
Namuomba Mhe. Waziri afanye kila jitihada anazozijua lakini hospitali yetu
ya Micheweni haitoshi ni ndogo mno. Kwa sababu ni dhahiri anaona kwamba
kuna kipindi inakuwa mpaka vile vyumba vya madaktari vinakuwa ni
hospitali.
Sasa namuomba Mheshimiwa kuwa kuna kila haja ya kuboreshwa zaidi
kuongezwa wodi za kulazwa wagonjwa hasa ukizingatia kwamba wodi za
kulazwa watoto pamoja na watu wazima ziko pamoja. Kwa hivyo, kuna haja
ya kutenganisha wodi za watoto zikawa ziko mbali na zile za wazee ziwe
mbali. Sasa namuomba Mhe. Waziri aone kwamba hospitali yetu ni ndogo na
ni ndogo sana na haitoshi. Namuomba Mhe. Waziri hili alione na alifanyie
kazi.
Mhe. Naibu Spika, suala jengine ni kwamba kule Micheweni kulitayarishwa
chumba cha upasuaji kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Micheweni, kwa
sababu hospitali zilizopo za upasuaji kwa Pemba ziko mbali mno na
Micheweni. Kwa hivyo, kwa makusudi kukatengenezwa chumba kizuri kwa
ajili ya upasuaji. Sasa chumba kile kipo lakini sasa matatizo tuliyonayo ni
kwamba chumba kile kifanye kazi basi, ile sehemu ya upasuaji ifanye kazi
hasa ukizingatia kwamba kumtoa mzazi Micheweni mpaka ukimfikisha
Mkoani au Chake Chake basi kwa kweli hali inakuwa ni taabani sana au
135
pengine anaweza akakata roho njiani kwa sababu ya umbali zaidi wa
kumsafirisha kumpeleka kule.
Sasa azma ile ya kuona kama kuna haja ya kufanyiwa upasuaji kule
Micheweni basi ikamilike madaktari tayari wapo wanasoma. Lakini sasa zile
zana za kupasulia hakuna kwa mfano hakuna mashine ya ganzi na vifaa
vyengine vya upasuaji havipo. Kwa hiyo, namuomba Mhe. Waziri kupitia
wizara yake waone kwamba sasa kuna haja ya ile azma ikamilike.
Mhe. Naibu Spika, suala jengine nitakalolizungumza ni suala la madereva wa
hospitali. Mhe. Naibu Spika, madereva wetu nao wana kazi ngumu sana. Kwa
hiyo, naomba na wao wafikiriwe. Aidha watengewe hata maposho ya ziada
kwa sababu wanafanya kazi mpaka usiku, mtu anakuwa saa nyengine
keshakuwa nyumbani kwake anapigiwa simu kuna mgonjwa anataka
kupelekwa hospitali, kama kwetu sie anataka kupelekwa Chake Chake au
Mkoani inabidi atoke usiku kwa ajili ya kumuwahisha ngonjwa hospitali.
Kwa hiyo, Mhe. Naibu Spika, naomba na hawa madereva waangalie kwa
jicho la huruma kabisa, kwa sababu na wao wana kazi ngumu sana. Aidha
watengewe maposho ya ziada ya kupewa na wao ili waweze kufanya kazi
zetu vizuri zaidi.
Mhe. Naibu Spika, suala jengine nitakalolizungumza ni suala la aidha
wanapotokea wagonjwa wa dharura wa ghafla yaani kwa mfano kama wale
waliopata ajali. Mhe . Naibu Spika, hawa wagonjwa wakipata ajali
wanachukua muda mkubwa kupata matibabu. Sasa mgonjwa keshapata ajali
na akawa bado anakaa muda hajapata matibabu inakuwa wale wenye
wagonjwa hawaridhiki na wanapiga kelele sana na wanailaumu Serikali.
Kwa hiyo, naomba Mhe. Waziri aone kama kuna haja ya kuweka kitengo
maalum inapotokea dharura ili waweze kutibu watu kwa haraka haraka sana,
ikiwa kipo basi kitayarishwe zaidi kiimarishwe zaidi, kama hakipo basi aone
kama kuna haja ya kukiweka ili wagonjwa wetu wakipata matatizo ya ghafla
waweze kutibiwa mara moja ili waweze kuwahiwa na kupata nafuu. Maana
mgonjwa siku nyengine damu zinatoka nyingi lakini anakaa muda mkubwa
hajapa matibabu, kwa hiyo yule mgonjwa anaona kama ni dharau. Kwa hiyo
naomba Mhe. Waziri kama hakipo kitengo hichi basi kiwekwe na kama kipo
basi kiimarishwe ziadi ili kiweze kufanya kazi zaidi.
Mhe. Naibu Spika, suala hili ni suala jengine nimeona humu la Mkemia Mkuu
kwa upande wa Pemba. Basi sijui kama Pemba kuna Mkemia Mkuu, lakini
nimeangalia nimeona kama yuko Mkemia Mkuu Pemba. Lakini nilipoangalia
kwenye Mkemia Mkuu Pemba nimeona vifungu vyote vya fedha
136
ninavyoviangalia ni ziro mpaka mwisho kabisa nimeona kuna total ya milioni
20. Sasa sijui yeye huku Pemba hana kazi za kufanya mpaka ikawa mote ni
ziro tu au kwa nini iwe hivi. Kwa hiyo, naomba hili labda atakapokuja Mhe.
Waziri anitolee ufafanuzi ili nifahamu zaidi.
Suala jengine nimeona huku kwenye kifungu 1501 Hospitali ya Mnazi
Mmoja. Nimeangalia sasa kwenye kifungu hichi 263185 kuna mfumo wa
pamoja wa usimamizi wa Kitaifa, kuna milioni hamsini laki tisa na thalathini
na mbili. Sasa mimi huu mfumo wa pamoja wa kitaifa mimi sijaujua ni
mfumo gani na fedha ni nyingi sana na bahati nzuri au bahati mbaya
2011/2012 hamna 2012/2013 hamna. Lakini 2013/2014 ndio ipo hiyo milioni
hamsini kwenye huo mfumo wa pamoja wa usimamizi wa kitaifa. Kwa hiyo,
naomba Waziri labda atakapokuja kufanya majuisho anifahamishe ili na mimi
niujue huu usimamizi wa kitaifa ni upi.
Mhe. Naibu Spika, kwa hayo machache nakushukuru sana. (Makofi).
Mhe. Naibu Spika: Ahsante nakushukuru na wewe Mheshimiwa kwa kujali
muda.
Mhe. Mussa Ali Hassan: Ahsante Mhe. Naibu Spika, kwa kuweza kunipa
nafasi ya kuweza kuchangia Bajeti hii ya Wizara ya Afya.
Vile vile namshukuru Mhe. Waziri pamoja na watendaji wake kuhusu
shughuli nzuri za wizara hii.
Mhe. Naibu Spika, nataka nimuhakikishie kwamba kazi zake ni nzuri tena ni
nzuri sana. Isipokuwa kwa leo nachangia katika kifungu namba 3 ukurasa wa
21 kuhusu Hospitali ya Mkoa wa Kusini Unguja.
Mhe. Naibu Spika, kwa kweli Mkoa wa Kusini hivi sasa una matatizo
makubwa sana kuhusu upatikanaji wa madawa kwa wagonjwa wetu wa Mkoa
mzima kwa hivi sasa. Hospitali nyingi za Mkoa wetu zina matatizo ya
madawa. Kwa hivyo, namshauri Mhe. Waziri ajitahidi sana kuipa kipaumbele
Mkoa wa Kusini kuweza kupata madawa hasa yale muhimu ambayo yana
ugumu kupatikana katika Mkoa wetu ni madawa ya Ukimwi pamoja na
Sukari.
Kwa hivi sasa akiweko mgonjwa wa Ukimwi inabidi afuatilie masafa ya
mbali sana ili kuweza kupata dawa, au mgonjwa wa sukari inabidi afuate
mafasa makubwa sana ili apate madawa kwa ajili ya maradhi ya sukari, na
ukitizama magonjwa haya ni magonjwa sugu ambayo kutibika kwake ni
kugumu. Kwa hivyo, namshauri Mhe. Waziri aipe kipaumbele Mkoa wa
Kusini Unguja ili iwe na madawa hasa zile hospitali zake ziko mbali sana.
137
Vile vile namshauri Mhe. Waziri Mkoa wa Kusini ina Wilaya zake kubwa
sana kwa hivyo, atusaidie tuweze kuwa na hospitali ya Wilaya ili rufaa
zipatikane katika Wilaya hasa katika maeneo nyeti kuweza kujengwa
Hospitali ya kisasa tukavijivunia katika Mkoa wa Kusini hasa Wilaya ya Kati
na sehemu nzuri tunazo kwa kumsaidia angelifanikisha katika maeneo mapya
ya mji mpya Tunguu na akaweza kuweka Hospitali ya Wilaya ya Mkoa wa
Kusini Unguja.
Vile vile namshauri Mhe. Waziri kwa kweli katika Mkoa wa Kusini kuna
hospitali ziko mbali mbali sana hasa ukitizama ukivuka kabisa ambayo iko
katika kijiji cha Uzi Ng‟ambwa. Kwa kweli Uzi Ng‟ambwa kuna matatizo
hasa kwa vile ni kisiwa kuvuka kwake ni shida wananchi wanapata tabu sana
kuweza kufuatia hospitali masafa makubwa ili kuhami afya zao.
Kwa kweli Uzi Ngambwa hivi sasa kuna aibu sana kwa Wizara ya Afya. Hivi
sasa hospitali ipo lakini kwa kweli haina daktari hata mmoja, sielewi hii
inakuja kwa nini au Mhe. Waziri amesahau kupeleka madaktari kule na kama
amesahau kwa kweli namkumbusha, na kama amepeleka aelewe kwamba
madaktari Uzi Ng‟ambwa hawaendi kufanya kazi kwa sababu ni kisiwa na
kiko mbali.
Kwa kweli inasikitisha sana kwa sababu tunayo nyumba nzuri ya madaktari
lakini ukienda kwa hivi sasa wanalala mbuzi na kondoo hamna daktari sielewi
hili suala lina faida gani kupoteza pesa za Serikali kuweza kujenga nyumba
kama ile ni nzuri hata mimi sina, na yeye Waziri na hakika hana kama ile ya
Uzi lakini utakuta hivi sasa inalala wanyama kama hao sijui kuna faida gani?
Na kama amepeleka daktari na kama haendi namuomba Mhe. Waziri achukue
hatua ya kumfungulia mashtaka daktari huyo kwa sababu amepoteza pesa za
Serikali kuweza kujengwa nyumba ile kwa ajili ya madaktari, lakini hivi sasa
hakuna daktari hata mmoja.
Kwa kweli ukienda kunasikitisha sana madaktari wake ni wale wa huduma ya
mwanzo peke yake utakuta watu wa Uzi Ng‟ambwa hivi sasa wana kilio
kikubwa sana hata kama daktari anataka kwenda gari ile inayogeuza tu Uzi
Ng‟ambwa ndio ile ile ndio anakwenda na ile ile anarudia ile ile, sielewi kama
yupo kwa kweli kama ndivyo alivyoweka mkataba. Kwa kweli Mhe. Waziri
akija anieleze sababu gani zilizosababisha kwamba Uzi Ng‟ambwa hakuna
daktari hadi hivi leo.
Mhe Naibu Spika, kwa kweli hivi sasa sina zaidi ya kuchangia isipokuwa
nachangia kifungu 4.3 ukurasa wa 31 kuhusu Hospitali ya wagonjwa wa akili.
Kwa kweli namshukuru sana Mhe. Waziri kwa hesabu yake na kitabu chake
kuanza kukisoma nimeona kwamba ametibu wagonjwa wa akili katika
138
Hospitali ya Mental ya Kidongochekundu wagonjwa 4522. Kwa kweli nampa
hongera sana. Kwa kweli watu wa Unguja sasa hivi kama walivyokuwa
wagonjwa wa Malaria karibu kutakuwa hakuna wagonjwa wa akili.
Lakini nasikitika sana Mhe. Waziri katika kitabu chake sikuona kwamba
ametibu mgonjwa hata mmoja katika Hospitali ya Pemba. Sasa nataka
nimuulize Pemba hakuna wagojwa wa akili? Na kwa nini Pemba sikuona
kwamba iko Hospitali ya wagonjwa wa akili nimekwenda sana Pemba lakini
sijaiona hospitali ambayo imewekwa kwamba hii ina jina la wagonjwa wa
akili.
Mhe. Waziri naomba akija anisaidie kunijuilisha kwamba wagonjwa wa akili
wa Pemba wanatibiwa wapi ama kule Pemba hakuna mgonjwa wa akili hata
mmoja? Lakini nikitembea njiani nawakuta tuseme wale wote ni wala unga tu
wale. Kwa hivyo, Mhe. Waziri akija nataka anieleze kwamba wagonjwa wa
akili Pemba wanatiwa wapi na katika kitabu chake naona amesahau hakutia
hata mgonjwa mmoja ambaye ametoka Pemba ametibiwa wapi au wote
wanakwenda nchi za nje. Mhe. Waziri ukija naomba unisadie suala hili kama
si hivyo mimi nitaondoa shilingi yangu katika bajeti yako.
Mhe. Naibu Spika, kwa kweli mchango mkubwa kwa hivi sasa unakwenda
katika Hospitali zetu za Rufaa za hapa Mjini Zanzibar. Namshukuru Mhe.
Rais wa Zanzibar kuweza kutoa wagonjwa wote wanaozaa pale kwamba
wasitoe chochote. Hili nalipongeza sana lakini tu tuhuma zinazokwenda hivi
sasa kama ni za kweli Mhe. Waziri katika hospitali yako, kwa kweli hivi sasa
inavyosemekana kwamba wazazi wetu wanapokwenda kujifungua
wakimaliza kujifungua wanaambiwa wachangie chupa ya Jik sijui Mhe.
Waziri kama hili suala unalifahamu na kama hulifahamu basi ujue wazazi
wetu wanatoa chupa ya Jik sijui hii Jik inafuliwa mashuka au Jik hii
inakwenda wapi.
Kwa kweli, Mhe. Waziri nisikupe muda mgumu sana isipokuwa tu
nakupongeza sana katika shughuli zao lakini naomba utakapofika hapa yote
niliyoyasema nataka uhakikishe kwamba unayajibu si hivyo naondoa shilingi
katika bajeti yako.
Kwa kweli mimi na wananchi wangu wa Jimbo la Koani naunga mkono hoja
hii mia kwa mia ahsante sana.
Mhe. Viwe Khamis Abdalla: Ahsante sana Mhe. Naibu Spika, kwa kunipa
fursa hii usiku huu nikaweza kuchangia Hotuba ya Mhe. Waziri wa Afya.
139
Mhe. Naibu Spika, nichukue nafasi hii nimpongeze Mhe. Waziri kwa
uwasilishaji wake mzuri wa hotuba yake. Mhe. Naibu Spika, pia nataka
nimpongeze Mhe. Afisa Mdhamini kwa kutekeleza vizuri majukumu yake.
Mhe Naibu Spika, naomba nichangie katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Hospitali ya Mnazi Mmoja ni Hospitali ya Rufaa. Lakini hospitali ile haina
usafi. Kwa hivyo, naomba nimwambie Mhe. Waziri alisimamie vizuri suala
hili la usafi. Kwa sababu usafi ni muhimu katika mazingira yote anayoishi
binaadamu.
Mhe. Naibu Spika, nikitoka hapo niende kwenye hospitali ya Vitongoji. Mhe.
Naibu Spika, Hospitali ya Vitongoji ni hospitali inayotumiwa na wananchi
ambao wako kwenye vijiji; tukiangalia kijiji cha Ole, Kiuyu Minungwini,
Vitongoji yenyewe. Lakini Mhe. Naibu Spika, hospitali hii ina uchunguzi wa
damu ya Malaria tu haina vifaa vyovyote vile mgonjwa akiwa anapokuwa
anashindikana na tatizo lolote lazima apelekwe Chake Chake, na huko Chake
Chake unaweza ukaenda pale ushapelekwa kama umepelekwa usiku
unawekwa mpaka asubuhi ili kwa kuweza kupatiwa vipimo. Mhe. Naibu
Spika, nimuombe Mhe. Waziri suala hili alishughulikie ili hospitali ya
Vitongoji iweze kupatiwa vifaa.
Mhe. Naibu Spika, nikitoka hapo niende katika Hospitali ya kijiji cha Kiuyu
Minungwini kituo cha Afya. Mhe. Naibu Spika, kituo hichi cha Afya kwa
kweli ni kituo cha miaka mingi sana tayari kimeshaanza kufanya ufa hakiwezi
kutekeleza huduma yake, namuomba Mhe. Waziri aje anieleze ni lini kituo
kile kitajengwa kipya au kitafanyiwa ukarabati.
Mhe. Naibu Spika, nikitoka hapo niende kwenye ukurasa wa 57 Huduma za
Chanjo. Mhe. Naibu Spika, katika kitabu hichi kimeeleza kama katika
huduma za chanjo za kupunguza maradhi Pemba haikufanikisha kutokana na
umeme wa Tukuza. Sasa namuomba Mhe. Waziri aje anieleze hivi kweli
Wizara nzima ya Afya inashindwa na pesa ya kununua umeme wa Tukuza.
Mhe. Naibu Spika, nikitoka hapo niende kwenye Ajira za Madaktari ambao
wana utaalamu wa kusafisha matatizo ya kibofu cha Mkojo. Kutokana na
tatizo linalowasumbua wananchi kisiwani Pemba tatizo hili limeenea sana
katika Wilaya ya Chake Chake. Unapokwenda pale hospitali ya Chake Chake
ukifika tu ukiwa na matatizo haya ya kibofu cha mkojo wanakuingiza mpira
na baadae kukusababishia matatizo makubwa sana, namuomba Mhe. Waziri
katika ajira atakazoajiri mwaka huu watafute daktari ambaye atakuwa na
utaalamu wa kuweza kuliondoa tatizo hili na linawasumbua zaidi kina baba.
140
Mhe. Naibu Spika, kwa kuwa muda wako nauthamini sana naomba niunge
mkono hotuba ya Mhe. Waziri, lakini nikimuachia suala langu la Kituo cha
Afya cha Kiuyu Minungwini.
Mhe. Salmin Awadh Salmin: Ahsante sana Mhe. Naibu Spika, kunipa nafasi
hii na mimi nikaweza kuchangia mawili matatu katika Hotuba hii ya Mhe.
Waziri wa Afya Mhe. Juma Duni Haji kuhusu Makadirio ya Mapato na
Matumizi kwa mwaka 2013/2014.
Mhe. Naibu Spika, Wizara hii ya Afya ni Wizara muhimu sana kwa ajili ya
maendeleo ya Afya ya wananchi wa Zanzibar. Kama tunavyofahamu Mhe.
Naibu Spika, kipindi hiki au katika zama hizi kumekuwa na maradhi mengi
yanayowakabili wananchi, na hii inatokana na mambo mbali mbali ambayo
wataalamu wetu wamekuwa wakitueleza ikiwemo masuala mazima ya
vyakula vyetu hivi tunavyovila. Kwa hivyo, wizara hii ni muhimu na kwa
sababu inabeba uhai wa wananchi wa Zanzibar.
Mhe. Naibu Spika, wenzetu hawa wamekuwa wakijitahidi kuhudumia
wananchi wa Zanzibar na kuhakikisha kwamba Afya zao zinaimarika kila
siku. Lakini tatizo tuliloliona ambalo tatizo hili mimi nashindwa kuelewa sijui
nimlaumu nani na kwa sababu mambo haya yanategemeana na hali halisi ya
uchumi wetu. Sote tunafahamu Wajumbe wa Baraza hili kwamba hali ya
Uchumi wa nchi yetu kwa kweli si nzuri na hii mimi nadhani inapelekea
kutupa tabu namna ya kugawana hii rasilimali fedha tuliyo nayo. Kwa sababu
mapato yetu ni madogo lakini mahitaji yetu ni makubwa. Lakini hata hichi
kidogo ambacho tunakipata nacho kinaonekana hatukitumii uzuri.
Kwa hivyo, Mhe. Naibu Spika, mimi nathubutu kusema kwamba sijui
nimlaumu nani, na kwa sababu ukiangalia migawanyo tunayogawana katika
wizara mbali mbali basi utakuta fedha zinazotolewa au mgao unaotolewa basi
haufikii yale malengo ambayo tumelenga. Sasa nasema Mhe. Naibu Spika,
kwamba sijui nimlaumu nani sijui niilaumu Wizara ya Fedha? sijui nimlaumu
Waziri wa Afya au Mawaziri wengine, sijui nimlaumu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, kwa sababu huwezi kutekeleza malengo kama rasilimali
fedha ulizopewa ni chache. Tunabakia hapa kulaumiana.
Lakini Mhe. Naibu Spika, mimi ninaloliona kwetu sisi wana siasa na wenzetu
watendaji tuisimamie Serikali tuhakikishe kwamba uchumi wetu unakua,
mapato yetu yanakuwa vianzio vyetu vya mapato vinaongezeka ili tuweze
kupata fedha za kuweza kutekeleza mahitaji yetu, vyenginevyo kila siku
tutakuwa tunalaumiana bure hapa.
141
Mhe. Naibu Spika, katika Bajeti ya mwaka uliopita na katika bajeti hii ya
mwaka huu Mhe. Waziri wa Fedha pia alituambia katika mambo yaliyoekewa
kipaumbele ni masuala ya Afya. Lakini ukiangalia mimi nimeangalia fedha za
maendeleo zilizotengwa na zilizopatikana. Lakini nimeangalia fedha za
matumizi ya usoni zilizotengwa hadi kupatikana hadi kufikia mwezi wa
Machi nafikia pahala sijui nimlaumu nani.
Kwa hivyo, Mhe. Naibu Spika, mambo haya yanahitaji kuangaliwa kwa
umakini sana, tutakuja kufika pahala tutalaumiana wengine wanataonekana
wabaya, lakini kumbe tatizo upatikanaji wa fedha, waswahili wamesema
"Maskini hapendi mwana". Msemo huu una umuhimu mkubwa sana, kwa
sababu wewe unapokuwa masikini huna huwezi kufanya mambo mengine
yoyote yale hata nyumbani kwako Mhe. Naibu Spika, ukiwa huna fedha basi
matumizi yako yataoana na kipato chako. Pengine ungependa kila siku ule
biriani nyumbani kwako, lakini fedha huna utafanyaje. Kwa hivyo, masikini
hapendi mwana pengine ungependa mtoto wako kila anapokwenda skuli
aondoke na shilingi elfu kumi. Lakini unampa shilingi mia tano si kwa sababu
humpendi lakini fedha ulizokuwa nazo ndio kwa kiasi kile ulichokuwa nacho.
Kwa hivyo, Waheshimiwa Wajumbe wenzangu wa Baraza hili lazima tufike
pahala hili tulizingatie kwa umakini, vyenginevyo tutakuwa tunanyosheana
vidole, Waziri mbaya, Katibu Mkuu mbaya, kumbe rasilimali fedha tuliokuwa
nayo ni chache.
Mjumbe mwenzangu hapa Mhe. Ismail Jussa Ladhu alisema kwamba katika
kikao cha Makatibu wakuu anapinga kuwaongeza madakatari mimi sifikirii
kama jambo hili linaweza likawa sifikirii, kwamba Katibu Mkuu asifanye
mbinu zozote za kuona madaktari wake wanapata maslahi makubwa, mimi
sidhani kama kuna Katibu Mkuu wa aina hiyo pengine ni dhana tu. Kwa
sababu maslahi yote ya wafanyakazi wa Serikali yapo katika Idara ya
Utumishi, na juzi tulikuwa tunasema hapa tunaitaka Serikali kupitia Wizara
ya Utumishi ijaribu kuangalia na kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa
Serikali wakiwemo madaktari.
Sasa tunapofika pahala tukalaumiana mimi naogopa sana tusije kufika pahala
tukamgombanisha Katibu Mkuu na madaktari wake. Mimi leo ukinambia
kuwa Spika, anazuia maslahi yangu sina urafiki na Mhe. Spika, halkadhalika
binaadamu yoyote atakaposikia fulani anazuia maslahi ya mtu mwengine
urafiki huo utakuwa haupo.
Kwa hivyo, tusije kujenga dhana kwa madaktari wetu kwamba Katibu Mkuu
anazuia maslahi ya madaktari, kwa kweli tutakujamfikisha pahala pabaya na
si jambo zuri. Suala la maslahi ya wafanyakazi yako chini ya Wizara ya
142
Utumishi, na mara zote wenzetu watumishi wanatwambia hata Mhe. Rais
anasema mara zote kwamba ataongeza maslahi ya wafanyakazi pale hali
itakaporuhusu. Safari hii ametenga fedha bilioni 17 kwa ajili ya maslahi ya
wafanyakazi.
Hata jana Mhe. Rais kwenye mkutano uliofanyika Kibanda Maiti alisema na
alirudia kwamba atajitahidi kadiri ya uwezo wake kuhakisha maslahi ya
wafanyakazi yanaboreshwa kila hali itakaporuhusu. Sasa nadhani tuzingatie
haya maelezo yanayotolewa na Viongozi wetu tusije kufika pahala tukaona
kuna mtu anajaribu kumzuia mwengine.
Mimi nakubaliana sana na Wahehimiwa Wajumbe wenzangu kwamba bado
maslahi ya madaktari yanahitaji kuboreshwa, na hapa walipo Mhe. Naibu
Spika siko wanakotoka, sote mashahidi, madaktari wanatoka hali mbaya ziadi
huko nyuma kabla wakati wa Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein na wameweza
kurekebishiwa maslahi yao katika hatua hii waliopo, haidhuru hawawafikii
wenzao wa Tanzania Bara, lakini maslahi ya madaktari yameboreshwa.
Siwezi kutaja takwimu hapa, lakini sote tunafahamu kwamba maslahi ya
madaktari yameboreshwa na serikali itakapopata uwezo itaboresha zaidi ili
yawe bora zaidi, na mimi nakubaliana sana na Waheshimiwa Wajumbe
wanaosema madaktari ni muhimu, pamoja na umuhimu wa wafanyakazi
wengine lakini madaktari ni muhimili muhimu sana.
Mhe. Naibu Spika, nakubaliana na wazo la Mhe. Ismail Jussa Ladhu kwamba
madaktari wanastahiki kulipwa mishahara yao, ili angalau ioane na
Wakurugenzi na huu ni juu ya umuhimu wa kada hii waliyonayo. Kwa hivyo,
Mhe. Naibu Spika, hali yetu kwa kweli ya kifedha isije ikafika pahala
tukaanza kuzozona wenyewe kwa wenyewe, sote keki ya taifa tunaijua, keki
yetu tunayoipata hapa tunaijua, namna tunavyogawana tunajua.
Takwimu hizi ambazo wenzetu wa Wizara ya Afya wametuletea asilimia 30,
35, 17 sijui asilimia ngapi, hakuna hata eneo moja lililokiuka zaidi ya asilimia
hizi za namna ya utekelezaji. Kwa hivyo, tusije tukafika pahala tukalaumiana
katika hili, lakini pia tusije tukawalaumu zaidi wenzetu wa Wizara ya Fedha,
Uchumi na Mipango ya Maendeleo kwa sababu ndio keki tuliyokuwa nayo,
fedha tulizokuwanazo hatuwezi zote tukaielekeza eneo moja, lazima
tugawane kidogo kidogo. Hata mzee wetu muasisi Marehemu Mzee Abeid
Aman Karume alisema kwamba bora tugawane kidogo kidogo kuliko kuja
kugombania kilichopo. Kwa hivyo, hiyo ni misemo ambayo ni sahihi waasisi
wetu wametueleza kwamba kidogo tulichokuwanacho basi tugawane kidogo
kidogo, kuliko kuja kuwa na kingi tukaanza kugombania.
143
Mhe. Naibu Spika, kuhusu utaratibu unaofanywa wa kuwapeleka wagonjwa
katika maeneo katika hospitali ya Mnazi Mmoja. Kwa kweli Mhe. Naibu
Spika, wenzetu wamekuwa na utaratibu kwa upande mmoja naweza kusema
ni mzuri, lakini kinachoonekana bado Hospitali ya Mnazi Mmoja
hawajajipanga katika hili. Kumekuwa na utaratibu ambao sasa hivi
unalalamikiwa na wananchi walio wengi. Wagonjwa wanapofika katika
Hospitali ya Mnazi Mmoja wanaulizwa, wewe umetokea wapi. Anajibu mimi
natokea Magomeni, anaambiwa nenda Kidongo Chekundu au nenda Nyumba
za Wazee. Ni sawa, lakini je Wizara ya Afya wamekiandaa vipi kitu kile
kidogo kilichopo. Unapomwambia mgonjwa aende kituo cha Mental pale au
mgonjwa wa Magomeni aende kituo cha Fuoni, au unapomwambia nenda
katika kituo cha Sebleni, hicho kituo umekiandaaje, au yule mgonjwa
unayempeleka kule kile kituo umekiandaaje? Kwa sababu sio suala la kwenda
tu ni suala la huduma ambayo ataipata kule. Kwa hivyo, wananchi wetu
wamekuwa wakitulalamikia sana juu ya utaratibu huu, wamesema utaratibu
huu hauwapi faraja.
Mimi nadhani Hospitali ya Mnazi Mmoja isipunguze msongomano wa eneo
lile kwa utaratibu huu, maana yake wananchi wetu watakuja kuonekana
kwamba tunawatelekeza na ni jambo ambalo sio zuri. Unamtoa katika
hospitali ya Mnazi Mmoja ambapo mwenyewe alitegemea kwamba atapata
matibabu, halafu unamwambia nenda katika kituo cha Sebleni, Sebleni
hakuna daktari, hakuna huduma nyengine yoyote. Kwa kweli utaratibu huu
nadhani ni mapema mno. Ni vyema Wizara ya Afya ikaviandaa hivi vituo
kwa ajili ya kupokea wagonjwa, ikiwemo kuwa na madaktari na vifaa vya
kutosha.
Mhe. Naibu Spika, sidhani kama vituo hivi vya karibu vingekuwa na huduma
ya kutosha, kama mwananchi angetoka Magomeni akaenda zake Mnazi
Mmoja, sidhani. Lakini wananchi wanatoka katika maeneo haya wakitegemea
kwamba Mnazi Mmoja ndiko kwenye huduma ambayo wanaweza kuipata.
Kwa hivyo, suala hili Mhe. Waziri nasema kwamba bado linahitaji uliangalie
kwa makini zoezi hili, ni zuri linaweza likapunguza msongomano katika
Hospitali yetu ya Mnazi Mmoja, hospitali ya rufaa. Lakini hivi vituo ambavyo
tunawapeleka wagonjwa wetu vimeandaliwa.
Leo Mhe. Naibu Spika, ukienda katika kituo cha Fuoni ambacho kinahudumia
maeneo yote yale, sijui utafikiria pana kitu gani. Ni kituo kinachobeba
wagonjwa wengi, kituo ambacho kimechukua eneo kubwa. Kwa hivyo, Mhe.
Waziri jambo hili linalalamikiwa sana na ninaamini utaliona na utachukua
hatua zinazostahiki juu ya jambo hili.
144
Jengine Mhe. Naibu Spika, ni suala hili ambalo wenzangu pia wamelisema ni
juu ya utaratibu huu wa kwenda kuwaangalia wagonjwa. Mimi ninaongeza
nyama katika hili, maana kichwani mwangu lilikuwepo, japokuwa hupendi
Mhe. Naibu Spika, lakini najaribu kuongeza nyama.
Mhe. Naibu Spika, kwa kweli katika Hospitali ya Mnazi Mmoja hakuhitaji
vurugu ambazo zinasababisha mambo mengi. Lakini sasa vurugu zile badala
ya kuwemo mule ndani, sasa vurugu zinakuja barabarani, kwa sababu wale
wanaokwenda kuwaangalia wagonjwa wao hawapati nafasi ya kuingia ndani,
matokeo yake wanazagaa huko barabarani. Hii inatokana na nini Mhe. Naibu
Spika, kwa sababu bado hawajaamini kuwa wagonjwa wao wanaweza
kuhudumiwa ipasavyo. Sote tunajua kwamba tuna upungufu wa dawa, wakati
mwengine mgonjwa anaandikiwa dawa yuko kitandani, lakini wale wa
kwenda kununua ile dawa wako nje, matokeo yake mgonjwa yule anakua
hapati huduma ya kutosha, hiyo ndio hofu yao. Laiti wagonjwa wale
wangekuwa wanapata huduma ya kutosha mule ndani ya ward, mna
wahudumu wa kutosha, mgonjwa anapotaka kwenda chooni anasaidiwa, basi
sidhani kama watu wangekuwa wanakwenda kurundikana, kwa sababu
wangekuwa na matumaini makubwa juu ya huduma inayotolewa mule katika
Hospitali yetu ya Mnazi Mmoja.
Kwa hivyo, ni suala zuri, lakini kama nilivyotangulia kusema lile la mwanzo,
tunatakiwa kwanza tujipanga vizuri sana ili tuone kwamba mambo haya
yanayotuletea matatizo katika jamii yetu yanaondoka.
Mhe. Naibu Spika, Mhe. Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango ya
Maendeleo hayupo, na Mkuu wa Shughuli za Serikali pia hayupo, kama
alivyosema Mhe. Ismail Jussa. Lakini ombi langu Mhe. Naibu Spika, katika
bajeti hii ya mwaka 2013/2014 waiangalie sana Wizara ya Afya, pamoja na
ufinyu wa bajeti au pamoja na keki ndogo tuliyonayo, lakini waiangalie sana
Wizara ya Afya na kwa sababu Wizara ya Afya ndio kwenye uhai. Ukiwa na
nguvu kazi ambayo haiwezi kufanya kazi kutokana na maradhi basi huwezi
kupata maendeleo na sote Wazanzibari ni wagonjwa, asiyeugua hiki ana hiki,
hakuna hata mmoja ambaye yuko mzima kwa asilimia 100 sote tuna maradhi
na sote tunahitaji kukimbilia hospitalini.
Kwa hivyo, Mhe. Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kama
Kaimu yupo, namuona Kaimu yupo wa Wizara ya Fedha, Uchumi na
Mipango ya Maendeleo Dk. Mwinyihaji tunakuomba sana takwimu hizi
zilizojitokeza katika bajeti hii, basi mwakani kuonekana mabadiliko.
Tusizungumzie suala la asilimia 17 au asilimia 20. Kama tunakusudia
kwamba Wizara ya Afya ni kipaumbele, basi kwa kadiri tunavyoweza ile sura
ya kipaumbele iweze kuonekana. Sio lazima kwamba kwa asilimia 100, lakini
145
angalau Wajumbe wako wa Baraza la Wawakilishi waone kwamba kweli
hapa kipaumbele kimewekwa, lakini kilishindikana kutekelezwa kwa asilimia
100 kwa sababu ya ufinyu wa bajeti, lakini kwa hivi takwimu zilivyo
inaonesha dhahiri kwamba hakuna kipaumbele ni haya mambo ya
kubabaishana babaishana tu, lakini hakuna kipaumbele katika bajeti hii.
Kwa hivyo, kipaumbele lazima kionekane Mhe. Naibu Spika, Wizara ya
Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo ni lazima iweke fedha za kutosha
kwa ajili ya huduma za wananchi. Tunasubiri bajeti ya mwakani, mimi
niwaombe Waheshimiwa Wajumbe wenzangu, pamoja na kwamba Mhe.
Ismail Jussa rafiki yangu anasema haiungi mkono kwa asilimia 100. Lakini
mimi nadhani tuiunge mkono hii bajeti ya Mhe. Juma Duni, kwa sababu
tutakuja kumalizika, kama hatutoipitisha bajeti hii, maana yake tutawamaliza
wananchi wetu.
Tuiunge mkono bajeti hii ili angalau japo hizo panadol waweze kuzipata.
Sasa kama hatutoipitisha bajeti hii ya Wizara ya Afya, maana yake hakuna
huduma yoyote itakayotolewa. Kwa hivyo, tuiunge mkono bajeti hii ipite,
lakini lazima serikali iangalie sana eneo hili ni muhimu, eneo la madaktari,
maslahi ya madaktari ni muhimu, eneo la madawa ni muhimu, eneo la
huduma za afya ni muhimu.
Kwa hivyo, Mhe. Naibu Spika, kwa kuwa muda wako unamalizika na mimi
maelezo yangu yanamalizika kwamba naunga mkono bajeti hii ya Wizara ya
Afya kwa masharti kwamba mambo haya ambayo yanaonekana ni kasoro,
basi serikali iyaangalie na sisi Inshaallah Mwenyezi Mungu akitujaalia bajeti
mwakani tupo, tutaiangalia.
Lakini kubwa zaidi Mhe. Juma Duni uelewe kwamba wewe ndio dhamana wa
wizara hii, wewe ndiye mas-ul na hili huwezi ukalikwepa, kwa sababu
matatizo yaliopo hapa hawezi kuteremka kule Katibu Mkuu na Mkurugenzi
kuja kujibu, utakayejibu ni wewe. Kwa hivyo, wewe ndiye mas-ul wa Wizara
ya Afya, wewe ndiye dhamana wa Wizara ya Afya. Matatizo yote
yanayojitokeza wewe ndiye utakayejibu kwa niaba ya serikali. Kwa hivyo,
hili nalo Mhe. Waziri ulijue. Sisi hatumkamati mtu mwengine hapa,
tutakukamata wewe, tukitaka kuwawajibisha basi tutakuwajibisha kwanza
wewe katika hili. Kwa hivyo, huwezi ukakwepa lawama yoyote itakayotokea
katika wizara hii, wewe ndiye mas-ul.
Baada ya maelezo haya Mhe. Naibu Spika, naunga mkono hoja na niwaombe
Waheshimiwa Wajumbe wenzangu waunge mkono, ili tuendeleze mbele
mambo yetu, ahsante sana Mhe. Naibu Spika.
146
Mhe. Naibu Spika: Mhe. Salmin Awadh Salmin tunakushukuru.
Waheshimiwa Wajumbe, nilizungumza katika kipindi cha jioni kwamba hivi
sasa tuko nyuma kwa siku nne ya bajeti yetu, na nikazungumza wanaotaka
kuchangia walete mapema ili tujipange. Kwa bahati mbaya sasa hivi
nimepokea majina sita kwa mfululizo na tumeshasema kwamba kesho
asubuhi Mhe. Waziri anajumuisha.
Kwa hivyo, niwaombe Waheshimiwa Wajumbe wafuatao walete michango
yao asubuhi kwa maandishi ili Waziri wakati wa maswali aweze kutafuta
majawabu, hivyo tunawataka radhi sana, nao ni;
1. Mhe. Mohamed Mbwana Hamad
2. Mhe. Salma Mussa Bilali
3. Mhe. Mohamed Haji Khalid
4. Mhe. Farida Amour Mohamed
5. Mhe. Mahmoud Muhammed Mussa
Waheshimiwa Wajumbe, kesho asubuhi tukijaaliwa tukimaliza maswali,
wamebakia wachangiaji wawili. Mhe. Bi Panya Ali Abdalla na Mhe.
Mwanajuma Faki Mdachi. Wao walileta majina tangu asubuhi.
Baada ya hapo tutamwita Mhe. Naibu Waziri na baadae tuwaite mawaziri
wanaotaka kumsaidia. Baada ya maelezo hayo nawashukuru kwa
mashirikiano yenu. Naakhirisha kikao chetu mpaka kesho siku ya Jumanne
tarehe 09/07/2013 saa 3:00 barabara za asubuhi.
(Saa 1: 45 usiku Baraza liliakhirishwa hadi tarehe 09/07/2013 saa 3:00
asubuhi)