Upload
others
View
7
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
1
RIPOTI YA KAMATI YA FEDHA, BIASHARA NA KILIMO YA
BARAZA LA WAWAKILISHI - ZANZIBAR
2011/2012
SEHEMU YA KWANZA
1.0. UTANGULIZI
Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo imeundwa kwa mujibu wa Kanuni ya 108 ya Baraza la
Wawakilishi la Zanzibar toleo la mwaka 2011, ikiwa na majukumu yafuatayo:-
a) Kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Kamati yaliyotolewa kwenye ripoti ya Kamati ya
mwaka uliotangulia.
b) Kufuatilia utekelezaji wa Sera na Mipango ya Wizara husika kadri Spika atakavyoelekeza kwa
mujibu wa malengo yaliyowasilishwa Barazani wakati wa usomaji wa Bajeti na hotuba
nyengine za Waziri alizotoa Barazani.
c) Kuchambua mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Wizara husika ya mapato na
matumizi ya kila mwaka.
d) Kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Kitaifa na Miradi ya Wananchi ya Wizara
husika.
e) Kuchunguza na kufuatilia mapato ya Serikali ya Wizara husika
f) Kufikiria jambo lolote litakalopelekwa kwake na Spika.
g) Kuchambua ahadi zote za Wizara zilizo chini ya Kamati kama zitavyokuwa zikitolewa katika
Baraza na kufuatilia utekelezaji wa ahadi hizo.
h) Kufikiria Miswada ya Sheria itakayopelekwa kwake na Spika
Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo imepangiwa kufuatilia utekelezaji wa malengo hayo katika
Wizara zifuatazo:-
a) Wizara ya Nchi (OR) Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo.
b) Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko
c) Wizara ya Kilimo na Maliasili.
Kamati ilifanya kazi zake za kawaida ikiwa na Wajumbe wafuatao:-
1. Mhe. Salmini Awadh Salmini - Mwenyekiti
2. .Mhe. Abdalla Mohamed Abadalla - Makamo Mwenyekiti
3. Mhe Mahamoud Mohamed Mussa - Mjumbe
4. Mhe. Bikame Yussuf Hamad - Mjumbe
5. Mhe Rufai Said Rufai - Mjumbe
6. .Mhe. Raya Suleiman Hamad - Mjumbe
7. Mhe. Mlinde Mabrouk Juma Mjumbe
8. Ndg. Amour Mohamed Amour - Kati bu
9. Ndg. Shemsa Maabad Mohamed - Katibu
Kamati imefanya kazi zake kwa muda wa Wiki nane (8) kama ilivyo utaratibu wake katika kufuatilia
utekelezaji wa kazi zake katika Wizara, Idara na Mashirika mbali mbali ya Serikali.
Kamati imefanya kazi hizo za kufuatilia utekelezaji wa malengo ya bajeti kama ilivyoainishwa
katika vitabu vya bajeti za Wizara husika, kazi ya ufuatiliaji ilifanyika Unguja, Pemba na Tanzania
Bara kwa Taasisi ambazo ni za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au hata zile za Serikali ya
Jamhuri ya Muungano kwa lengo la kupata kujifunza na kupata uzoefu.
2
SEHEMU YA PILI
2. 0. UTEKELEZAJI WA MALENGO YA WIZARA
2.1. WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI
2.1.1. IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI
MIRADI
Katika mwaka wa Fedha wa 2010/2011 Idara inasimamia na kuratibu utekelezaji wa programu na miradi
ya maendeleo ifuatayo:
i) Mradi wa Kuimarisha Huduma za Kilimo – ASSP
ii) Mradi wa Kuimarisha Huduma za Mifugo – ASDP-L
iii) Mradi wa Usarifu Mazao ya Kilimo.
iv) Mradi wa Miundombinu ya Masoko, Uongezaji thamani na huduma za Fedha vijijni (MIVARF)
MALENGO YA IDARA
a) Kufanya mapitio ya Sera ya Kilimo, Misitu, Mbegu na Hakimiliki za wavumbuzi.
b) Kusimamia na kuimarisha ukusanyaji wa Takwimu za uzalishaji wa mazao ya chakula, biashara
na maliasili.
c) Kusimamia utekelezaji wa mpango Mkuu wa Utafiti na Dira ya Elimu kwa wakulima.
d) Kukusanya mapato ya Tsh. 1,293,774,000/-
e) Kutayarisha na kutoa nakala 2,000 za Jarida la Mkulima.
f) Kuchapisha matokeo ya Tafiti mbalimbali za kilimo.
UTEKELEZAJI WA MALENGO
Hadi mwezi Disemba 2011 kazi ya mapitio ya awali ya Sera ya Kilimo hayajaanza.
Rasimu ya mwanzo ya Sera ya Misitu imewasilishwa kwa wadau.
Rasimu ya mwanzo ya Sheria ya Hakimiliki ya uvumbuzi wa mbegu mpya imekamilika na iko
kwenye ngazi ya Wizara.
Wizara imekusanya jumla ya Tsh. 234,849,615 hadi Novemba, 2011.
Nakala 1000 za Jarida la Mkulima zimechapishwa.
MRADI WA UIMARISHAJI MIUNDOMBINU YA MASOKO, UONGEZAJI THAMANI YA
MAZAO NA HUDUMA YA FEDHA VIJIJINI (MIVARF)
Mradi huu unatekelezwa katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar na umetengewa jumla ya
fedha USD 162 milioni sawa na Tanzania Shilingi 247.1 bilioni ikiwa ni fedha za mkopo kutoka Mfuko
wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo IFAD, AFDB na AGRA. Utekelezaji unafanyika kitaifa na
umeanza Julai 2011 na utadumu kwa miaka saba (2011/12 – 2017/18).
MALENGO YA MRADI
a) Ujenzi wa mfumo na miundombinu ya masoko mradi utasaidia katika maeneo yafuatayo:
(i) Ujenzi wa masoko Wilayani yatakayokuwa na huduma za uhifadhi wa bidhaa
zinazoharibika.
(ii) Ujenzi wa Viwanda viwili vya kuzalisha barafu kimoja Unguja na kimoja Pemba.
(iii) Ujenzi wa barabara za mashambani kuunganisha maeneo yote ya uzalishaji na barabara
kuu kwa lengo la kurahisisha kuyafikia masoko na utoaji wa huduma za kilimo.
b) Utoaji mafunzo na uwezeshaji katika usarifu wa bidhaa za kilimo. Mradi utasaidia.
(i) Kuimarisha vikundi vya wajasiriamali katika usindikaji na usarifu wa bidhaa za kilimo.
(ii) Kutoa mafunzo ya usarifu na usindikaji bidhaa za kilimo kwa wakulima, wajasiriamali
na watoaji huduma za usarifu na usindikaji bidhaa za kilimo.
c) Kuanzisha mfumo wa utoaji wa huduma za kifedha vijijini na Mradi utasaidia
(i) Kutayarisha sera ya upatikanaji wa huduma za fedha kwa wakulima na wajasiriamali
wadogo wadogo.
(ii) Kuanzisha na kuwezesha taasisi za kijamii za utoaji huduma za fedha vijijini.
3
UTEKELEZAJI WA MALENGO
Kwa kupitia fedha za wahisani ambazo ni TShs. 168, 209,860.00 kazi zifuatazo zimefanyika:
Uzinduzi na utambulisho wa Mradi.
Kuunda Timu ya Uratibu wa Mradi – Zanzibar
Kutambulisha Mradi kwa Kamati ya Kisekta ya Usimamizi.
Kutambulisha Mradi kwa Viongozi wa Wizara, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara.
Kutambulisha Mradi kwa Kamati ya Ushauri na Utekelezaji wa Mradi za Mikoa na Wilaya.
Kununua samani na vitendea kazi.
Matumizi ya uendeshaji wa ofisi.
Kwa kupitia fedha za wahisani ambazo ni TShs. 48, 389,400.00 kazi zifuatazo zimefanyika
Kufanya matengenezo ya Ofisi za Mradi.
Utafiti wa mfumo wa masoko ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.
Ununuzi wa vipuri vya gari.
Ununuzi wa vitendea kazi
Matumizi ya Uendeshaji wa Ofisi.
2.1.2. IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI
MALENGO YA IDARA
a) Kutayarisha mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi (Training Master Plan) utakaoonesha
maeneo ya vipaumbele katika fani za Wizara.
b) Kuimarisha utendaji katika uhifadhi wa kumbukumbu zikiwemo taarifa za wafanyakazi na
rasilimali za Wizara (data base).
c) Kutayarisha mpango mkakati (strategic plan) wa miaka mitatu wa Idara kwa lengo la
kuimarisha ufanisi wa kazi.
d) Kuhakikisha mali za Serikali zilizomo ndani ya Wizara zinatunzwa na kupatiwa hati miliki.
UTEKELEZAJI WA MALENGO
i) Utayarishaji wa mpango mkakati (strategic plan) wa miaka mitatu umekamilika, kwa
upande wa mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi bado unaendelea. Hata hivyo baadhi ya
vipengele vya mpango mkuu wa mafunzo vimeanza kukamilika (Training Master Plan)
kama:
Kuunda Kamati ya mafunzo ya Wizara.
Kukusanya taarifa za elimu na fani walizonazo.
Kufanya uchambuzi wa taarifa zilizokusanywa, mpango huu unatarajiwa kukamilika
ifikapo Machi, 2012.
ii) Ukamilishaji hati miliki wa Rasilimali za Wizara umeanza kwa kukamilisha mambo
yafuatayo:-
Upimaji wa mashamba na vituo vya utafiti kama Kijichi, Kizimbani, Selem, Bambi na
maeneo ya chuo cha kilimo kizimbani umekamilika pamoja na kupatiwa michoro yake.
Aidha umefanyika upimaji wa maeneo yaliyozunguka nyumba zilizo chini ya Wizara
kama Mbweni, Mazizini, Saateni pamoja na Ofisi za ASSP/ASDPL Maruhubi.
Kwa upande wa vipando (vya usafiri) tayari vimekwisha orodheshwa na hivi sasa hatua
za kufanya usajili kwa ajili ya kupata nambari mpya unafanyika ili hatimae litayarishwe
daftari la kumbukumbu (Registration Book), mfano wa vyombo hivyo ni gari, pikipiki,
trekta, vespa
n.k.
4
CHUO CHA KILIMO KIZIMBANI
MALENGO
i. Kutoa mafunzo ya cheti kwa wanafunzi 140 mwaka wa kwanza na wa pili
ii. Kujenga bweni la wanafunzi kupitia Miradi ya ASSP/ASDP-L.
iii. Kutoa mafunzo kwa wakulima 500 kwa mabonde matatu ya mpunga.
iv. Kukamilisha usajili wa Chuo kwa Baraza la Vyuo vya Ufundi Tanzania.
UTEKELEZAJI WA MALENGO
Lengo limevukwa ambapo kwa sasa wanafunzi 156 wanaendele na masomo.
Ujenzi wa Bweni unaofadhiliwa na ASSP/ASD-L upo katika hatua za kupata mkandarasi
baada ya kufunguliwa zabuni
Mafunzo yametolewa kwa wakulima 337 wa mabonde ya Mtwango, Weni na Mangwena.
Chuo tayari kimeshasajiliwa na kupatiwa Hati Na. REG/ANE/027.
2.1.3. IDARA YA KILIMO
Idara hii ina jukumu kubwa la kusimamia maendeleo ya wakulima, kutoa pembejeo za kilimo na
upatikanaji wa mbegu na dawa.
MALENGO YA IDARA
i) Uongezaji tija wa kilimo cha mpunga wa juu.
ii. Kuimarisha soko la ndani la mchele.
UTEKELEZAJI WA MALENGO
Wizara tayari imeshanunua tani 141 za mbegu kwa wakulima wa ndani na ziada ya tani 160
zitanunuliwa Tanzania Bara ili kufikia mahitaji ya wakulima kwa msimu huu ambayo ni Tani
355. Hatimae mbegu zitauzwa kwa wakulima kwa bei ya Sh. 200/- tu kwa kilo ikiwa ni bei ya
ruzuku kwa wakulima.
Jumla ya tani 490 za mbolea pamoja na lita 20000 za dawa zimeagizwa ili kuwahi msimu
lakini hadi mwezi Disemba, 2011 bidhaa hizo zilikuwa bado hazijawasili.
Jumla ya tani 3.4 za mbegu aina ya NERICA imezalishwa katika kituo cha kilimo Bambi na
zimesambazwa kwa wakulima
UDHIBITI WA INZI WA MATUNDA
MALENGO YA IDARA:
i) Kuwaelimisha wakulima 1,500 juu ya mbinu za kilimo bora.
ii) Kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa Mabibishamba/Mabwanashamba ili kuweza
kubadilishana utaalamu ikiwemo kuwapeleka katika maonesho ya nane nane Tanzania Bara.
iii) Kutayarisha makala 15 na vipeperushi 600 na kupatiwa wakulima.
vi) Kutayarisha vipindi 60 vya redio na 37 vya TV na kuvirusha hewani.
iv) Kununua gari tano kwa lengo la kufanikisha utoaji wa huduma za elimu kwa wakulima.
5
v) Kuendeleza kazi za karantini na ukaguzi wa mazao.
vi) Kuzalisha na kusambaza tani 12 za mbegu za mahindi na mtama tani 5 na jamii ya kunde
tani 8.
vii) Kununua na kusambaza mbolea tani 1,090 (545 TSP na 545 Urea).
xi) Kutoa huduma za kilimo cha matrekta kwa kushirikiana na wenye matrekta binafsi pamoja
na kutengeneza matrekta mabovu 29 na zana zake.
UTEKELEZAJI WA MALENGO
Hatua mbali mbali za udhibiti wa inzi wa matunda ikiwemo kusambaza mitego ya inzi. Tokeo kuanza
kazi ya udhibiti wa inzi wa matunda jumla ya mitego 65,000 imenunuliwa na kusambazwa katika sehemu
mbali mbali za mashamba na Mijini Unguja na Pemba.
Kazi ya kusambaza mitego ya inzi ilikuwa ikidhaminiwa na mradi wa MACEMP lakini kuanzia mwaka
2010/2011, Idara imeanza tena kutegemea Bajeti ya Serikali ambapo kwa mwaka wa fedha 2011/2012,
hadi Januari 2012, Idara imeshatumia jumla ya TShs. 75, 793,495/= kwa kazi za utekelezaji kama
ifuatavyo:-
1. Ununuzi wa dawa.
2. Usambazaji wa mitego 20,000 Wilaya Kaskazini “A” na “B” na Wilaya ya Micheweni
Pemba.
3. Ufuatiliaji na ubadilishaji wa dawa.
4. Maslahi ya wafanyakazi.
5. Gharama za Usafiri.
6. Kufanya tathmini juu ya kiwango cha uharibifu toka kuanza kuweka mitego. Tathmini
ya mwisho inaonesha kuwa kiwango cha uharibifu kimepungua kutoka asilimia 70
mwaka 2008, asilimia 43 mwaka 2010 hadi kufikia asilimia 30 mwaka 2012.
2.1.4. IDARA YA MISITU NA MALI ZISIZOREJESHEKA
Idara hii ina jukumu la kulinda na kuhifadhi misituya asili, kuratibu upatikanaji wa maliasili
zisizorejesheka na upatikanaji wa mbegu na miche bora ya miti ya mazao ya biashara, matunda, misitu na
mapambo.
MALENGO YA IDARA i. Kuzalisha miche 500,000 na ujenzi wa mabanda ya kuzalisha miche.
ii. Kutoa elimu ya upandaji na uendelezaji mikarafuu na kufanya sensa ya mikarafuu kwa Wilaya saba
(3 kwa Unguja na 4 kwa Pemba)
UTEKELEZAJI WA MALENGO
i. Idadi ya miche 240,000 imeoteshwa kwa Unguja na Pemba. Ujenzi wa mabanda mapya haukuanza.
Wakati elimu ya kuendeleza zao la karafuu imetolewa.
ii.Kuhusu sensa ya mikarafuu; kilichofanyika ni makisio tu ya kazi yenyewe ambayo ni Sh.303, 131,352
2.1.5. IDARA YA UMWAGILIAJI MAJI
Idara hii imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuyaendeleza mabonde ya mpunga kwa kuimarisha
miundombinu yake kama vile uchimbaji wa visima, matengenezo ya njia na ujenzi wa misingi ya maji.
MALENGO YA IDARA
Kusimamia ujenzi wa miundombinu mipya ya umwagiliaji maji kwa ekari 237. Kazi hii
itafanyika kupitia Mradi wa TASAF na JICA.
Kujenga mtaro mkuu wa mita 500 na kujenga matuta katika ekari 25 bonde la Koani.
6
Kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa mabwana/mabibishamba 40 Unguja na Pemba.
Kusomesha wafanyakazi wawili Msc na wanane kiwango cha Diploma.
Kutoa mafunzo kwa wakulima 120 wa bonde la Kibokwa.
Kutayarisha vishamba 10 vya maonesho, kuongeza u taalamu kwa wakulima wa mpunga na
mboga mboga katika mabonde ya umwangiliaji maji.
Ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji maji katika maeneo mawili ya vituo vya uzalishaji
mbegu ekari 65 ambapo Kibonde Mzungu ekari 40 na Ole ekari 25.
UTEKELEZAJI WA MALENGO
Serikali imetoa jumla ya Tsh.4, 165,000/- kwa ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa msingi wenye
urefu wa mita 100 kwenye bonde la Kinyakuzi. Kwa upande wa bonde la Weni lenye ukubwa
wa hekta 16, jumla ya Shilingi 2, 100,000/- zilitolewa na zilitumika kwa ununuzi wa mawe kwa
ajili ya kukarabati banio (Spillways) kazi hiyo imekamilika kwa asilimia 90.
Kwa upande wa bonde la Makombeni ambalo kwa sasa kuna mradi unaofadhiliwa na Serikali ya
Japan wa JP 5 Bonde hilo linahitaji jumla ya Tsh. 238,280,000/- na Wafadhili wametoa jumla
ya Tsh.113,725,000/-, SMZ mchango wake ni Tsh. 12,500,000/- na sehemu iliyobaki ni nguvu
za wakulima ambayo ni karibu Tsh. 112,000,000/- ambazo zinaweza kuongezeka zaidi ya
hapo.Kazi ya uchimbaji wa kisima imekamilika lakini hata hivyo transforma na umeme bado
haujafika na pia matengenezo ya barabara ya kuingilia bondeni ambayo kwa wakati wa mvua
inakuwa ni vigumu kupitika hasa kwenye kilima bado haujafanyika. Mradi huo ambao ulikuwa
umalizike Januari, 2010.
Kisima cha Bumbwisudi kimechimbwa na majaribio ya wingi wa maji yamaefanyika. Jumla ya
Tshs 26, 000,000/- kutoka TASAF zimetumika.
Mitaro ya saruji mita 500 Bumbwisudi na mita 500 Uzini imejengwa na jumla ya Tsh
30,000,000/- kutoka TASAF zimetumika kwa kazi hiyo.
Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha kifusi mita 100 umefanyika Bumbwisudi jumla ya Tshs
3,000,000/-kutoka TASAF zimetumika.
Vyanzo vya maji vya mto mawe Kikobweni na Kianga vimepandwa miti na kupigwa matuta ya
kuzuia mmong‟onyoko wa ardhi. Jumla ya Tsha 5, 000,000/-zimetumika kutoka TASAF.
.
Majaribio ya kumwaga na kupima wingi wa maji kisima cha Makombeni yamefanyika jumla ya
Tshs 700,000/- zimetumika kwa kazi hiyo.
Usafishaji wa kisima Tibirinzi umefanyika na jumla ya Tshs 700,000/- zimetumika.Kisima
kimepunguza kuzalisha maji na mpango wa Badea wa idara ni kuchimba kisima chengine.
Pampu mpya na transfoma zimewekwa katika bonde la Saninga Jumla ya Tshs 30,
000,000/zimetumika kwa kazi hiyo.
Banda la kupumzikia wakulima wa bonde la Saninga tayari limefikia kwenye linta ambapo
Serikali imetoa Tsh.4, 795,000/- kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi na kazi nyengine ni
nguvu za wakulima wenyewe.
Ukarabati wa mtaro mita 60 Mtwango umefanyika jumla ya Tshs 1, 000,000/- za SMZ na jamii
zimetumika.
Pampu ya kisima cha umwagiliaji maji cha Uzini imetengenezwa na inafanya kazi , jumla ya
Tsh 6,000,000/- zimetumika kwa kazi hiyo.
7
Ujenzi wa tuta unaendelea kwa ajili ya kuzuia uingiaji wa maji ya bahari katika bonde la
mpunga Mziwanda unaendelea na jumla ya Tshs 50, 000,000/- za SMZ zimetumika.
.
Vijishamba darasa 10 (kumi) vimetayarishwa vya maonesho Unguja na Pemba jumla ya
Tshs.,000,000/-zimetumika.
2.2. 0WIZARA YA BIASHARA VIWANDA NA MASOKO
2.2.1. IDARA YA BIASHARA NA UKUZAJI MASOKO
Idara ya Biashara, Viwanda na Masoko kwa mwaka wa fedha 2011/2012 imepangiwa kutekeleza
malengo yafuatayo:-
i) Kuendeleza, kuimarisha mazingira bora ya ukuzaji Biashara, kwa kuufanyia mapitio makubwa mfumo
wa utoaji leseni za biashara nchini.
ii) Kuwasilisha Serikalini kwa mazingatio rasimu za sheria mpya za ushindani, mizani na vipimo na
sheria ya biashara.
iii) Kuanza utekelezaji wa sheria ya viwango ya Zanzibar.
iv) Kuendelea kutafuta masoko ya ndani na nje ya bidhaa zinazozalishwa hapa Zanzibar.
v) Kukusanya mapato ya Tsh.30, 000,000.00, kutokana na kazi za ukaguzi wa vipimo.
UTEKELEZAJI WA MALENGO
Kazi ya utekelezaji wa Sheria ya Viwango bado haijaanza .Hata hivyo Wizara imeshapatiwa
majengo mawili kwa ajili ya maabara na Ofisi.Serikali inaendelea na hatua za uteuzi wa
mtendaji mkuu.Aidha ununuzi wa vifaa, samani za ofisi na uajiri wa wataalamu wengine
utafanyika baada ya kuajiriwa mtendaji mkuu.
Mapitio ya mfumo wa leseni yamekamilika na utungaji wa rasimu ya sheria kwa ajili hiyo
unaendelea. Rasimu hiyo inakusudia kuifuta sheria ya leseni Nam.3 ya 1983 inayotumika hivi
sasa.
Mapitio ya Sheria zinazohusiana na ushindani na kumlinda mtumiaji, mizani na vipimo na sheria
ya biashara.
Wizara imesitisha kuendelea na taratibu hizi mpaka pale sheria mpya ya leseni itakapokuwa
tayari. Kwani sheria hiyo pamoja na mambo mengine itaelekeza mfumo wa utoaji vibali, usajili
na mambo mengine yanayohusiana na biashara.
Kusimamia uendeshwaji wa biashara halali kwa kuimarisha ufuatiliaji wa ubora wa vipimo na
mizani na kumlinda mtumiaji.
i) Kazi za Ukaguzi
Idara kwa kipindi cha Julai hadi Desemba, 2011 jumla ya mizani 919, Pampu za mafuta 15,
gari za kubebea mafuta 6, Underground tank na flow meter moja vilikaguliwa kwa Unguja na
Pemba. Kiasi cha Tsh. 10,920,500/- ambazo ni asilimia 33.64 ya lengo.
Maduka 1151, maghala 38 na viwanda 6 vimekaguliwa na bidhaa zenye thamani ya Tsh. 6, 677,
6000/- zimeharibiwa ambazo zilikutwa zikiwa tayari zimepitwa na wakati au kuharibika.
ii) Usimamizi wa bei za bidhaa muhimu za chakula.
Wizara imeanza utekelezaji wa kanuni za kusimamia bidhaa na huduma za biashara za mwaka
2011. Kanuni hizo pamoja na mambo mengine zimeweka utaratibu maalum wa uwekwaji wa
bei za bidhaa hizo muhimu.
Katika ufuatiliaji wa masoko ya ndani,Wizara imeratibu ushiriki wa wajasiriamali katika
maonesho ya kimataifa ya saba saba ambapo wajasiriamali 50 walishiriki,Maonesho ya nane
nane wajasiriamali 8, maonesho ya ujio wa Prince Charles wajasiriamali 8, maonesho katika
Mkutano wa Sita wa Baraza la Biashara (ZBC) Wajasiriamali 20 na maonesho ya Wasiria
ambapo wajasiriamali 10 walishiriki.
8
Kwa upande wa masoko ya Nje Wizara imeratibu ushiriki wa maonesho ya Jua kati
yaliyofanyika Rwanda ambapo wajasiriamali sita walishirik.Aidha Wizara imewapatia mafunzo
juu ya mbinu za kisasa za utafutaji wa masoko ambapo Mjasiriamali mmoja alipelekwa nchini
Afirika ya Kusini chini ya udhamini wa Shirika la Biashara la Dunia (WTO) na Wajasiriamali
wawili nchini China kwa udhamini wa Serikali ya China.Aidha Wizara imetoa mafunzo ya
usarifu wa ngozi na utafutaji wa masoko kwa bidhaa zinazotokana na ngozi ambapo
wajasiriamiali 23 wanashiriki mafunzo hapa Zanzibar.
Uwanja wa Kimataifa wa Maonesho ya Biashara
Katika kuhakikisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendeleza ukuwaji wake wa
Uchumi kupitia Biashara; imeliandaa eneo la uwanja wa Maoneshao ya Kimataifa liliopo
Nyamanzi, Wilaya ya Magharibi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Eneo hilo limewekwa alama yaani (becon) na kinachosubiriwa ni kutolewa Zabuni kwa ajili ya
kuliendeleza katika:-
i) Kutayarisha michoro ya matumizi ya ardhi (land use plan)
ii) Kutayarisha michoro ya kihandisi
iii) Kutayarisha gharama za mradi
Hata hivyo hadi mwishoni mwa mwezi wa Disemba zabuni hiyo haijatangazwa.
ZIARA YA KAMATI KATIKA SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS)
Katika kuhakikisha kuwa Serikali ya Mapinduzi inaweka taasisi ya kudhibiti ubora wa bidhaa
zinazotumiwa na Wananchi (ZBS). Kamati ilipata fursa ya kutembelea Shirika la Viwango Tanzania
(TBS) kwa lengo la kupata uzoefu ili kuweza kushauri Serikali juu ya suala hilo.
Shirika la Viwango Tanzania awali ililianzishwa kupitia Sheria ya Viwango Nam 3 ya mwaka 1975 na
kuanzishwa tena upya kwa sheria Nam 2 ya 2009, ambayo imeongeza nguvu na uwezo wa Shirika katika
kuchukua hatua mbalimbali kama vile kuondoa bidhaa hafifu zilizoko sokoni ,kufuta leseni,kuwepo kwa
utaratibu wa marejesho na/au faida,kuweka taratibu za kuharibu bidhaa duni au kuzirudisha zilikoagizwa
na kutozwa faini.
Miundombinu
Shririka la TBS limekuwa na majengo ya kisasa yenye kukidhi haja iliyopo yakiwemo majengo yenye
Maabara za upimaji bidhaa na yenye vifaa vya kisasa,majengo ya Afisi na wataalamu wenye sifa mbali
mbali katika taaluma ya sanyansi na kwa sasa lina jumla ya Wafanyakazi 195.
ZIARA YA KAMATI KATIKA DEPORT YA MTONI
Kamati imefanya ziara katika Deport za Mtoni kutokana na kuwepo ukosefu wa mafuta unaojitokeza
mara kwa mara.Katika ziara hiyo ambapo Kamati ilipata nafasi ya kuzungumza na uongozi wa Kampuni
zote tatu zinazojishughulisha na uagizaji wa mafuta Kampuni hizo ni GAPCO, United Petroleum (UP)
na Zanzibar Petroleum(ZP) na kupata changamoto zifuatazo ambazo ndizo zinazopelekea ukosefu huo
wa mafuta.:-
Urasimu mkubwa katika bandari ya Dar-es –Salam .Kutokana na kubadilika kwa sheria ya
EURA ambayo inaruhusu muagizaji mmoja tu wa mafuta kutoka nje ya Nchi na kuziuzia
Kampuni mbalimbali za mafuta kumesababisha kuwepo na foleni kubwa jambo ambalo
linapelekea meli ndogo hasa zinazotoka Zanzibar kuchelewa kuyapata mafuta hayo kwa wakati
,ambapo Kampuni ya GAPCO ndio wanaochukua Dar-es-Salaam.
.
Kupigwa marufuku uingizwaji wa mafuta kwa kutumia njia ya meli kwa meli ambapo njia hii
inapelekea kufanyika kwa magendo ya mafuta kwa wingi sana na kuikosesha Serikali mapato
yake.Utaratibu huo unafanywa na Kampuni ya United Petrolium na Zanzibar Petrolium (ZP)
9
TARATIBU ZA KULIFUNGA SHIRIKA LA MAGARI
Hatua za kulifunga shirika zinaendelea kwa kutayarisha mafao ya wafanyakazi kwa kuzingatia
mabadiliko ya mishahara.,na kwa maana hiyo hati inatayarishwa ya kuzingatia deni na maslahi ya
Wafanyakazi .Hati hiyo inatarajiwa kuwasilishwa kwa Mheshimiwa Rais baada ya kukamilishwa kwa
kazi hizo.
SHIRIKA LA TAIFA LA BIASHARA (ZSTC)
Shirika la Taifa la Biashara limefanyiwa marekebisho katika muundo na uendeshaji wake.Katika kukidhi
haja hiyo sheria Nam 11 ya mwaka 2011 ilitungwa ikiainisha majukumu ya msingi ya
Shirika.Halikadhalika mpango kazi wa shirika umeandaliwa na ulitarajiwa kuwasilishwa Serikalini
mwezi Feburuari 2012.
Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar ndilo lenye jukumu kubwa la ununuzi wa zao la karafuu kutoka
kwa wakulima wa Zanzibar. Zao ambalo ndio tegemeo kuu la kiuchumi kwa Taifa. Itakumbukwa
kwamba katika misimu ya mavuno ya karafuu iliyopita ununuzi wa karafuu ulikuwa ni mdogo sana kwa
Shirika pamoja na kuwa kulikuwa na mavuno ya kuridhisha lakini inaonekana wakulima wengi walikuwa
hawapeleki karafuu zao ZSTC kwa madai ya kwamba bei inayotolewa ni ndogo na hivyo wakulima
waliziuza kwa wafanyabiashara wa magendo.
Hali Halisi ya Ununuzi
Katika msimu ulioanzia mwezi Julai, 2011 Serikali kupitia ZSTC ilipandisha bei mara tatu kwa kipindi
cha kisichozidi miezi mitatu, ambapo bei iliyokuwapo ya Sh. 5,000/- kwa kilo ya karafuu ya daraja la
kwanza ilipanda hadi Sh.10, 000/- na baadae kuwa Sh. 12,000/- na kwa sasa [Septemba 2011] imefikia
Sh. 15,000/-.
Kwa kipindi cha miezi mitano Julai hadi Novemba, 2011 Shirika lilikadiria kununua tani za karafuu
2,165 kwa thamani ya Tshs 32.475bilioni kwa Unguja na Pemba,ambapo kwa kipindi hicho manunuzi
halisi yalikuwa ni jumla ya tani 2695.3335 zenye thamani ya Tshs 40,204,6,39500 ikiwa ni ziada ya
kuvukwa kwa lengo hilo kwa asilimia 24%. Kwa upande wa mauzo hadi kufikia tahere 30 Novemba
2011 Shirika limeweza kuuza jumla ya tani 2018.76 za karafuu zenye thamani ya USD 27.500,160
ambapo wastani wa bei ni kati USD 13.647.
Hali ya Magendo
Kwa ujumla suala la usafirishaji wa magendo ya karafuu Kisiwani Pemba limepungua kwa kiasi kikubwa
kwani idadi ya karafuu zinazopelekwa ZSTC inadhihirisha ukweli huo. Kipindi cha kuanzia mwezi Julai
hadi Septemba, 2011 jumla ya karafuu zenye uzito wa kilo 878 zilikamatwa.
Malalamiko Pamoja na kazi nzuri inayofanywa na wafanyakazi wa Shirika katika kutoa huduma kwenye vituo hivyo
Kamati ilipokea malalamiko yafuatayo:
Wakulima/wauza karafuu wanawalalamikia wachukuzi juu ya kuwatoza fedha nyingi kwa ama
kuwabebea mazao yao au kuwasafishia na kuwasindikia karafuu zao. Bei ya cheti cha kuchukulia
mazao inatofautiana kati ya Mkoa wa Kusini na Kaskazini (Mkoa wa Kusini ni Sh. 500/- wakati
Kaskazini ni Sh. 1,000/- kwa cheti kimoja)
Bado wakulima wana wasiwasi juu ya ubora wa mizani zinazotumiwa na Shirika kuwa ni za
kizamani lakini vile vile wakulima wenyewe baadhi yao wanashindwa kuzisoma wakati wa
kupimiwa karafuu zao.
Vipimo vya uzito wa gunia vilikuwa vinababaisha kati ya gunia lenye uzito wa kilo moja na lile
lenye uzito kilo moja na nusu. Halkadhalika uzito wa kipimo cha robo kilo ya karafuu nacho
kifanyiwe malipo. Utoaji wa vibali vya kusafirishia karafuu kutoka Wilaya moja kwenda nyengine
umekuwa na tatizo.
Majengo ya baadhi ya vituo vya kuuzia karafuu yako katika hali mbaya na hayana hata vyoo.
10
2.3.0. WIZARA YA NCHI (OR) FEDHA NA MIPANGO YA MAENDELEO
2.3.1. IDARA YA MHASIBU MKUU WA SERIKALI
MAJUKUMU
Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali ina majukumu makubwa ya kuitunza Hazina ya Serikali, kusimamia
mwenendo wa Deni la Taifa, kudhibiti mapato na vilevile kusimamia shughuli za kihasibu na Ukaguzi wa
Ndani kwa kuhakikisha kwamba taratibu na sheria zote zinazohusika zinafuatwa katika suala zima la
kudhibiti mapato na matumizi ya Serikali.
MALENGO YA IDARA
Katika kipindi cha mwaka 2011/2012 Idara ilipanga kutekeleza mambo yafuatayo:
(i) Kufanya jumuisho la Hesabu na kuliwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali.
(ii) Kuendelea kutoa kipaumbele kwa malipo ya mishahara, malipo ya Wastaafu na malipo mengineyo.
(iii) Kuendelea kutoa mafunzo (Muda mfupi na Muda mrefu)
(iv) Kusimamia Deni la Taifa.
UTEKELEZAJI WA MALENGO YA IDARA
Katika suala zima la jumuisho la Hesabu za Serikali ni kwamba Idara imekwisha kamilisha hesabu
kutoka kwenye Wizara zote na ipo katika hatua za mwisho na ilitarajiwa kuliwasilisha jumuisho hilo
kabla ya mwezi wa Disemba, 2011.
Kwa upande wa malipo ya mishahara, zoezi limeendelea kama kawaida na kwa wakati ikiwa ni pamoja
na mabadiliko ambayo yalianzia mwezi wa Oktoba, 2011. Mabadiliko hayo ambayo ni makubwa kiasi
yameleta changamoto kiasi lakini hata hivyo Serikali imeweza kukabiliana nazo. Aidha Serikali
inaendelea kuwalipa mafao Wastaafu ikiwa ni pamoja na viinua mgongo na pencheni zao kwa wakati
muwafaka, ambapo hadi kufikia mwezi wa Novemba, 2011 imeweza kuwalipa wastaafu wote waliostaafu
hadi mwezi wa Agosti, 2011. Na hivyo jumla ya Tsh.2.186 Billioni zimetumika kulipa viinua mgongo
vya wastaafu 351. Madai ya Wastaafu wa miezi ya Septemba, Oktoba na Novemba, 2011 yalikuwa ni
Tsh. 896 Milioni na yalitarajiwa kulipwa mwezi wa Disemba, 2011 na Januari, 2012.
Wakati huohuo suala la matumizi mengineyo (Other Charges) kwa kipindi cha miezi mitano (Julai –
Novemba) jumla ya Tsh. 2, 237, 597,000/- sawa na asilimia 41 zilitolewa kupitia Wizara na Taasisi
mbalimbali za Serikali. Deni la Taifa nalo limefikia Tsh. 186.25 Billioni hadi mwezi Novemba, 2011
hiyo ilikuwa ni sawa na asilimia 19.63 ya pato la Taifa. Kiwango hicho kwa Nchi zinazoendelea kama
yetu huwa hakitishi sana.
Wakati Deni la Ndani kwa mwezi huo wa Novemba lilikuwa limefikia Tsh.43.46 Billioni sawa na
asilimia 23 ya Deni lote, ikiwa ni ziada ya Tsh.7.12bil. Ikilinganishwa kama ilivyokuwa kwa mwezi wa
Juni,2011 ambapo kiwango kilikuwa ni Tsh.36.34 billioni. Deni la Nje nalo limeongezeka kwani hadi
kufikia mwezi wa Novemba, 2011 lilifikia Tsh. 142.79 bilioni sawa na asilimia 76.66 (USD 86.23mil)
ikiwa ni ziada ya Tsh.17.37 bilioni kwani mwezi wa Juni, 2011 Deni lilikuwa Tsh.125.42 bilioni (USD
79.39Mil).
Deni hili la Nje limeongezeka kutokana na sababu mbili kuu za msingi ambazo ni:-
a.) Kuingizwa kwa fedha katika Miradi
b.) Mabadiliko ya thamani ya Shilingi ya T anzania ikilinganishwa na zile za kigeni.
2.3.2. IDARA YA BAJETI
MALENGO YA IDARA
i) Kukamilisha maandalizi ya mfumo wa Program Based Budgeting na kuanza kutumia rasmi
mfumo huo wa bajeti katika mwaka wa fedha wa 2012/2013.
ii) Kusimamia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2011/2012.
iii) Kutoa muongozo wa mafunzo maalum kwa Wizara na Taasisi mbali mbali za Serikali.
11
UTEKELEZAJI WA MALENGO
Katika kutekeleza suala la utayarishaji, utekelezaji na ufuatiliaji wa bajeti ya Serikali. Taasisi
zimepatiwa ruzuku kwa asilimia 100. Jumla ya fedha kwa ruzuku hizo ni Tshs 3,170,576,666/-
ambazo zilipewa Taasisi zifuatazo :-
i) Bodi ya Mapato Zanzibar
ii) Mfuko wa Barabara
iii) Chuo cha Utawala wa Fedha Chwaka
iv) Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali
v) Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar
Muongozo wa kwanza umetayarishwa na umeshatolewa kwa Wizara sita pamoja na Mafunzo
kwa Wizara hizo, ambapo walengwa katika mafunzo hayo ni Makatibu
Wakuu,Wakurugenzi,Viongozi wa ndani wa Wizara ya Nchi (OR)Fedha ,Uchumi na Mipango
ya Maendeleo na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Fedha zilizotumika katika kufanikisha
kazi hiyo ni jumla ya Tshs 25,281,900/-.
2.3.3. IDARA YA UTUMISHI NA UENDESHAJI
MALENGO YA IDARA
i) Kuanza maandalizi ya Ofisi Pemba
ii) Kuendelea na utekelezaji wa mapendekezo ya Mshauri Mwelekezi ya kuwajengea uwezo
wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo.
iii) Kuwapatia wafanyakazi 83 wa Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo mafunzo
ya muda mrefu na mfupi ndani na nje ya nchi;
iv) Kuandaa mafunzo ya ndani (In house training) kwa wafanyakazi 60 kwa lengo la kuwaongezea
uwezo, ujuzi na uzoefu katika utendaji wa kazi zao.
UTEKELEZAJI WA MALENGO
Maandalizi ya Ujenzi wa Ofisi ya Wizara Pemba yalianza lakini kwa bahati mbaya ujenzi huo
haukufikia hatua ya kukabidhiwa kutokana na makosa ya kiufundi yaliyotokea na kuathiri
kiwango kikubwa jengo hilo na kupelekea kusitishwa kwa kazi ya ujenzi.
Mpaka ujenzi unasitishwa gharama zilizotumika ni jumla ya Tshs 736,826,936/-.Wizara tayari
wameshapatiwa kiwanja chengine katika eneo la Gombani na iko katika hatua ya kuingia
mikataba na Idara ya Ujenzi Michenzani.
Wafanyakazi wamepatiwa mafunzo ya muda mrefu ni 13 na muda mfupi 34 fedha zilizotumika
katika kazi hiyo ni jumla ya Tshs 404,206,007/-.
2.3.4. IDARA YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ-DSM
MALENGO YA IDARA
Idara ina majukumu ya kuratibu shughuli mbalimbali za kiuchumi na maendeleo baina ya SMZ na
Wizara za SMT ikiwa ni pamoja na kuratibu ushirikiano wa kiuchumi baina ya SMZ na Ofisi za Kibalozi
pamoja na taasisi za Umoja wa Mataifa zenye Ofisi zake Dar es Salaam.
UTEKELEZAJI WA MALENGO
Suala la kuratibu na kukuza ushirikiano.
Katika kipindi cha mwezi wa Novemba hadi Disemba 2011, Idara iliomba jumla ya Tsh. 14,589,000/-
kwa kazi ya kuratibu na kukuza ushirikiano na kuingiziwa TSH. 1,000,000/-.Kazi iliyofanyika ni
kushiriki kwenye vikao vya uteuzi wa waombaji wa masomo ya juu katika fani mbali mbali chini ya
ufadhili wa Nchi ya Serbia na kazi nyengine iliyofanyika ni kuhudhuria mkutano wa maandalizi ya
Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika.
12
Suala la kuendeleza na kuimarisha uwezo wa Utawala wa rasilimali watu.
Hadi kufikia mwezi wa Disemba, 2011 Idara haikuweza kuingiziwa fedha ilizoomba (Tsh. 8,000,000/-)
na hivyo lengo hilo halikuweza kutekelezwa.
Suala la kuweka mazingira bora ya utendaji kazi ili kuleta ufanisi wa kazi.
Fedha zilizoingizwa kwa kazi hii ni jumla ya Tsh.21, 000,000/- kati ya 37,000,000/- zilizoombwa. Fedha
hizo zimewezesha kumpatia mafunzo mfanyakazi mmoja, kufanya matengenezo kwa gari moja na baadhi
ya huduma nyengine ndogondogo.
2.3.5. IDARA YA UHAKIKIMALI NA MITAJI YA UMMA
MALENGO YA IDARA
Idara imepanga kutekeleza majukumu yafuatayo:
i) Kukamilisha tathmini ya mali za kudumu na kukamilisha uandaaji wa Daftari la mali za
kudumu za Serikali.
ii) Kuendeleza uhakiki wa mali za Serikali katika Wizara na Taasisi za Serikali.
iii) Kusimamia na kuratibu ufunguji wa hesabu za mwaka katika mashirika ya Serikali
iv) Kusimamia ununuzi na uondoaji wa mali za Serikali kwa mujibu wa sheria.
v) Kuendelea kusimamia sheria ya manunuzi No 9 ya mwaka 2005 na sheria ya Mitaji ya
Umma No 4 ya mwaka 2002.
vi) Kuendelea kuwajengea uwezo watendaji katika masuala ya ununuzi Serikalini.
vii) Kufanya ukaguzi katika manunuzi yanayofanywa na taasisi za Serikali.
viii) Kuanzisha Daftari maalum la wakandarasi na watoa huduma nyengine wenye sifa za
kupewa kazi hizo Serikalini.
ix) Kufanyia tathmini mashirika ya umma na kuishauri Serikali juu ya marekebisho yake.
UTEKELEZAJI WA MALENGO
Kuhusu lengo la kuendeleza uhakiki wa mali za Serikali na uanzishwaji wa Daftari la mali hizo
katika Wizara na Taasisi za Serikali.
Taratibu za kupata kampuni ya kufanyaka kazi ya kutathimini na uanzishwaji wa Daftari la
mali za Serikali zimekamilika na kazi hiyo imefanyika kwa asilimia 40.
Kazi ya kutengeneza nyaraka za manunuzi na miongozo yake inaendelea na imefanyika
kwa asilimia 50, fedha zilizotumika ni jumla ya Tshs 550,000/-
Idara imefanya semina nne Unguja na Pemba kwa wadau wote wa sheria ya manunuzi na
uondoshaji wa mali za Serikali,fedha zilizotumika ni Tshs 2,200,000/-
Kazi za ukusanyaji taarifa za manunuzi zinaendelea na zimeshafanyika kwa asilimia
75,fedha zilizotumika ni Tshs 750,000-/
Ripoti ya mwaka ya ukaguzi wa mali kazi na huduma za Serikali katika Wizara na Taasisi
za Serikali imetayarishwa kwa asilimi 60.
Idara imeweza kufanya uchanganuzi wa mahesabu kwa mashirika ya Bandari, Utalii na
Benki ya Watu wa Zanzibar, fedha zilizotumika ni Tshs 550,000/-na kazi hiyo imefanyika
kwa asilimia 75.
Kazi ya kuweka kumbukumbu za udhibiti wa mitaji na hisa za uwekezaji wa Serikali
inaendelea, jumla ya fedha zilizotumika Tshs 250,000 na kazi imefanyika kwa asilimia 50.
Miradi ya ujenzi wa Ofisi za Serikali inaendelea kwa kuanza matayarisho ya ujenzi kwa
Ofisi zifuatazo; Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu , Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu, Jengo la E-Government, Katiba na Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
fedha zilizotumika Tshs 716,968,282/-.
Tathmini ya mali za Serikali.Kazi hiyo mshauri mwelekezi ameshapatikana na kazi
itaanza katika kipindi cha robo ya tatu.
MFUKO WA HIFADHI YA JAMII
MALENGO YA MFUKO
Mfuko umekusudia kufanyia mageuzi makubwa mfumo wa hifadhi ya jamii.Chini ya Mfuko huu
sheria ya ZSSF itafanyiwa marekebisho ili iweze kwenda sambamba na mageuzi hayo.
13
UTEKELEZAJI WA MALENGO
Uwekezaji wa muda mfupi
Dhamana za hazina kupitia BoT zenye thamani ya Tshs 1,141,905,000/- zimenunuliwa na faida
iliyopatikana ni Tshs 43,628,179/-
Jumla ya Tshs 17,450,000,000/- zimewekezwa katika akiba za benki za muda maalum na faida
iliyopatikana ni Tshs 1,509,279,339/-
Fedha zilizowekezwa katika majengo na kodi iliyopatikana ni Tshs 1,552,907,518/-.
Uwekezaji wa muda mrefu:
Fedha zilizowekezwa kupitia TANRE zilikuwa 1,413,226,000/- hakuna gawio lililofanyika
hadi kufikia Disemba 2011.
Fedha nyengine zimewekezwa katika majengo na kodi ambazo ni Tshs 5,423,197,461/-. Na
faida iliyopatikana ni Tshs 112,706,000/-
Fedha zilizowekezwa katika dhamana za Serikali kupitia BoT ni Tshs 27,459,753,880/-
faida iliyopatikana ni Tshs 1,851,275,635/-
Thamani ya Vipande vya UTT ni Tshs 1,027,024,184/- na thamani ya vipande hivyo
iliongezeka kwa Tshs 25,620,315/- kwa kipindi cha miezi mitatu (Oktoba hadi Disemba,
2011).
Thamani ya hisa za TPCC ni Tshs 677,697,280/- thamani ya hisa hizo imeongezeka kwa
Tshs 6,516,320/- kwa kipindi cha (Oktoba hadi Desemba 2011).
Hisa za NMB ni Tsh 1,384,294,700/- hadi Disemba 2011 hakujakuwa na ongezeko la
thamani ya hisa hizo.
Hisa za CRDB ni 1,299,037,680/- hadi Disemba 2011 hakujakuwa na ongezekao la thamani
ya hisa hizo.
Jumla la Tshs 16,585,394,737/- zimekopeshwa kwa taasisi tofauti za Serikali na faida
iliyopatikana ni Tshs 198,795,223.33/- hadi kufikia Disemba 2011 .Fedha hizo
zimekopeshwa kwa Taasisi zifuatazo:-
ZRB, Tshs 3, 785, 394,737/-na faida iliyopatikana ni Tshs 136, 459,892/-
ZSTC, Tshs 12, 000, 000,000/- na faida iliyopatikana ni Tshs 62, 335,331/-
ZIPA, Tshs 800, 000,000/- hakuna faida iliyopatikana hadi Kamati inapatiwa maelezo
haya.
Jumla Tshs 7, 500, 000,000/- zimewekezwa kwenye dhamana za SMZ.
Thamani ya Vipande vya Jikimu Fund ni Tshs 1, 983, 524,181 hadi kufikia Disemba 2011
thamani ya vipande hivyo imepungua kwa Tshs 12, 434,542.02/- Gawio la Tshs 71,
725,894.80 limepatikana. Mfuko unatarajia faida ya Tshs 2, 221, 247,620/- katika uwekezaji
wake wa muda mrefu hadi Disemba 2011.
Ulipaji wa mafao.
Mfuko umekuwa ukiendelea kulipa mafao ya uzee, mafao ya urithi pamoja na mafao ya ulemavu. Jumla
ya Wanachama 114 wamelipwa mafao yao katika kipindi cha Oktoba 2011 hadi Disemba 2011 dhidi ya
lengo lililowekwa la Wanachama 201.Hii ni sawa na asilimia 54 ya lengo na Jumla ya fedha zilizotumika
ni Tshs 532, 951,022/-
Uwekaji wa Kumbukumbu
Mfuko unaendelea kutekeleza miradi ya kuboresha uwekaji wa kumbukumbu za Mfuko kwa kutumia
mifumo ya TEHAMA) ICT). Katika utekelezaji wa miradi hiyo mpango mkakati mkuu wa TEHAMA wa
miaka mitano uliandaliwa na kuanza utekelezaji wake mwaka 2009.Kati ya miradi saba ya ICT
iliyotarajiwa kutekelezwa mitano imeshaanza na imo katika hatua mbali mbali za utekelezaji.
14
MAMLAKA YA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA BIMA (TIRA)
Jukumu kubwa ni kusimamia shughuli za Bima ambazo zinatolewa na Kampuni mbalimbali za Bima
hapa nchini.
Kazi zake
Miongoni mwa kazi zake ni pamoja na Usajili wa Kampuni za Bima na Madalali, Usajili wa Mawakala
na Wakadiriaji Hasara, Ukaguzi wa Kampuni za Bima na Ushughulikiaji wa Malalamiko ya Wateja na
Wadau wengine wa Bima.
Utekelezaji.
Usajili wa Kampuni za Bima na Madalali kwa Upande wa Zanzibar.
Jumla ya kampuni nne za Bima zilizosajiliwa chini ya Sheria ya Bima hadi kufikia tarehe 31 Disemba,
2010 , ambazo ni Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC), Jubilee Insurance Company (T) Ltd, National
Isurance Corporation (T) Ltd na African Life Assurance Company.
Jumla ya Madalali wa Bima waliosajiliwa hadi kufikia tarehe 31 Disemba, 2010 na wanafanya shughuli
zao Zanzibar ni kumi na nne (14).
TUME YA PAMOJA YA FEDHA.
Tume ya Pamoja ya Fedha ilianzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka wa 1977, Ibara ya 134 na kuanzishwa kwa Sheria ya Tume hii ya mwaka 1996 (Sura ya 140).
MAJUKUMU YA TUME.
Miongoni mwa majukumu ya Tume ni :-
a) Kuchambua mapato na matumizi yanayotokana na, au yanayohusu utekelezaji wa Mambo ya
Muungano, na kutoa mapendekezo kwa Serikali zote mbili kuhusu mchango na mgao wa kila mojawapo
wa Serikali hizo;
b) Kuchunguza kwa wakati wote mfumo wa shughuli za fedha za Jamhuri ya Muungano na pia uhusiano
wa mambo ya kifedha kati ya Serikali mbili;
c) Kutekeleza majukumu mengine ambayo Rais ataipatia Tume au kama Rais atakavyoagiza, na kwa
mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.
UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU
Katika kutekeleza majukumu yake Tume imefanya stadi mbalimbali zikiwa kama ni ushauri wa
kitaalamu kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania (SMT) Miongoni mwa stadi hizo ni kuhusu:-
UHUSIANO WA KIFEDHA BAINA YA SMT NA SMZ.
Uchambuzi wa masuala ya fedha yanayohusu mambo ya Muungano.
Vyanzo vya Mapato ya Muungano.
Uimarishaji wa Sera za Bajeti na fedha baina ya SMZ na SMT.
Usimamizi wa Deni la Taifa baina ya SMT na SMZ.
MAPENDEKEZO. i) Vigezo vya kugawana Mapato na Kuchangia Gharama za Muungano.
ii) Marekebisho ya Sheria ya Tume ya Pamoja ya Fedha.
iii) Muongozo wa Uendeshaji wa Akaunti ya Fedha ya Pamoja.
iv) Kuimarisha mfumo wa Bajeti na Fedha baina ya SMT na SMZ.
v) Utaratibu wa kushughulikia ushauri unaotolewa na Tume kwa Serikali mbili.
vi) Marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa Bidhaa.
15
BENKI YA POSTA TANZANIA. Benki ya Posta Tanzania (TPB) imeanzishwa kisheria mwaka 1992 ikiwa ni Taasisi iliyopewa leseni na
Benki Kuu ya Tanzania ambayo inajiendesha kama taasisi ya Fedha (Non-bank Financial Insititution),
madhumuni makubwa yakiwa ni:-
Kukusanya amana za wateja.
Kuendesha shughuli zote zinazoendeshwa na mabenki ya biashara.
Kutoa huduma bora za kibenki kwa mujibu wa Sheria za Mabenki na Taasisi za Fedha nchini.
UTEKELEZAJI WA MALENGO.
Benki imepanga kutekeleza mambo yafuatayo:-
i) Kuongeza mtaji wa benki kutoka Tsh.6.7 Bilioni mwaka 2010 na kufikia Tsh. 11.6 mwaka 2011.
ii) Kuongeza amana za Wateja kutoka asilimia 20 hadi asilima 30 kwa kila mwaka, ambapo kw a
mwaka 2011 ilifikiwa.
iii) Kupunguza hasara zinazotokana na shughuli za kibenki ikilinganishwa na mapato, uwiano huo
usizidi asilimia 2 kwa mwezi.
iv) Kuongeza tija na ufanisi na uzalishaji wa faida kutoka Tsh. 3.5 milioni mwaka 2010 na kufikia
Tsh. 5.47 milioni kwa mwaka 2011.
Mgawanyo wa Hisa.
Mgawanyo wa hisa na umiliki wa benki hadi Novemba, 2011 ni kama ifuatavyo:-
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni asilimia 75.2
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni asilimia 7.5
Shirika la Posta Tanzania lina asilimia 22.0 na
TP&TC SACCOs ni asilimia 6.5
Mikopo.
Benki ilianza kutoa mikopo mwaka 1998, Mikopo inayotolewa ni ya; Biashara, Watumishi wa Umma,
Mikopo midogo midogo na Mikopo ya Uwezeshaji.
Hadi kufikia mwezi wa Novemba, 2011 jumla ya Tsh .62, 972.7 milioni zimetolewa, kati ya hizo Tsh.
1,2037 milioni zimetolewa kwa Tawi la Zanzibar.
BENKI YA WATU WA ZANZIBAR LTD.
Tawi la Kariakoo – Dar es Salaam
Katika kuimarisha shughuli zake PBZ imeanza kutoa huduma Tanzania Bara kuanzia tarehe 29/4/2011
kwa ufunguzi wa Tawi lake liliopo Mtaa wa Kariakoo DSM , Tawi ambalo linatoa huduma zote za
kibenki zinazopatikana hata kwenye matawi mengine yote.
Maendeleo yake.
Tangu kuanzishwa kwake (Tarehe 29/4/2011) hadi Novemba, 2011 limeweza kuweka amana za Wateja
Tsh. 6,084,465,849/- na kutoa mikopo ya Tsh. 11,055,245,000/- kati ya hizo 1,700,000,000/- ni kwa ajili
ya mkopo wa Biashara.
Tawi la Huduma za Benki ya Kiislamu (Islamic Division).
Katika kutanua wigo wa Biashara, Benki pia imefungua tawi la huduma za Kiislamu ambalo
lilifunguliwa rasmi na kuanza huduma hizo Tarehe 10/12/2011.
Maendeleo yake.
Katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja tangu kufunguliwa benki imeweza kuwa na wateja 190 na
kuweka amana za Tsh. 306 milioni.
16
BENKI YA WATU WA ZANZIBAR TAWI LA CHAKE CHAKE-PEMBA.
Amana za Wateja.
Jumla ya Tsh 7,951.62 milioni zimewekwa kama amana za wateja hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2011
katika Tawi la Benki la Chakechake zikiwemo Tsh.4,540 milioni kama akiba (Saving), Tsh.3,137.56
milioni kama biashara (Current), Tsh. 274.06 milioni ni ya Muda maalum (Fixed). Wakati amana
nyenginezo zilikuwa na thamani ya Tsh.0.88 milioni.
Utoaji wa Mikopo.
Kwa upande wa Mikopo kwa wafanyakazi Tawi la Benki la Chakechake kwa kipindi cha kuanzia Julai,
2010 hadi Juni, 2011 limetoa mikopo kwa wafanyakazi 3,171 yenye thamani ya Tsh. 7,425 milioni.
Wakati kwa upande wa mikopo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi (AK na JK) hadi kufikia Juni, 2011
wananchi waliofaidika na mikopo hiyo ni 201 kwa thamani ya Tsh.329.211 milioni. Ukilinganisha na
waliopata fursa hii katika kipindi kilichoishia Juni, 2010 idadi ya wananchi waliopata ni 188 kwa mkopo
wenye thamani ya Tsh.407.396 milioni.
Utoaji wa mikopo ya JK na AK imesitishwa kwa muda kutokana na kujitokeza kasoro ambazo
zimelifanya zoezi hili kuwa gumu hasa wakati wa marejesho ya mikopo hiyo. Hivyo Benki inasubiri
maelekezo kutoka kwa W izara ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa maelekezo na utaratibu mzuri
utakaowezesha mikopo hiyo kutolewa na kurejeshwa bila ya matatizo.
Faida ya Tawi.
Tawi la Benki la Chakechake linajiendesha wenyewe kwenye mapato na matumizi na kwa kipindi hadi
kufikia Tarehe 30 Juni, 2011 limeweza kupata faida ya Tsh. 125.63 milioni.
Aidha linaimarisha huduma zake kwa kutumia mtandao wa Benki (Banking Computer Software) ambao
unamruhusu mteja kuweza kupata huduma ya kutoa na kuweka fedha zake tawi lolote la Benki ya Watu
wa Zanzibar.
Katika kuendeleza huduma hizo na kupunguza msongamano kwa wateja Benki imeanzisha huduma
kwenye vituo vya Wete na Mkoani halikadhalika kumeanzishwa huduma za ATM kwa miji ya
Chakechake ATM tatu, Wete ATM moja, Mkoani ATM moja na Konde ATM moja.
Ujenzi wa Jengo Jipya.
Katika kufanikisha lengo la kutoa huduma bora kwa wateja Benki imejenga jengo jipya lenye uwezo
mkubwa wa kutoa huduma hizo kwa ufanisi. Jengo ambalo limekabidhiwa rasmi Tarehe 29 Septemba,
2011. Jengo lina sehemu mbili, moja inatoa hudumma za Benki za kawaida (Conventional) sehemu
nyengine ni kwa ajili ya huduma za kibenki za Kiislam.
Taratibu za benki hizi za Kiislamu na mawazo ya wengi ni kuwa labda benki ile ni ya watu maalum.
Utaratibu wa utoaji wa mikopo nao unahitaji mafunzo maalum ambayo pia yanaihusisha Benki Kuu ya
Tanzania ikiwa kama dhamana wa kusimamia benki kwa mujibu wa Sheria.
.
Benki Kuu ya Tanzania (BOT)
Benki Kuu ndio yenye jukumu la kusimamia benki zote zilizopo Tanzania, katika kufanya hivyo na
pamoja na mambo mengine inayozingatia ni suala zima la utoaji wa leseni ya biashara hiyo.
Benki kuu kupitia Tawi lake la Zanzibar imekuwa mshauri mzuri katika mambo yanayohusiana na
uchumi. Ushauri huo hutolewa kupitia tafiti mbalimbali zinazofanywa pamoja na kushiriki katika vikao
mbalimbali vya Kamati za kitaalamu kama vile Kamati ya kuweka Ukomo wa matumizi ya fedha (
ceiling committee) na Vikao vya matayarisho na maendeleo ya MKUZA.
Tafiti ambazo zinafanyika ni zile zinazohusiana na:
Sekta ya Viwanda.
Mfumko wa bei na Chakula.
Utafiti wa zao la Mpira.
17
SHIRIKA LA BIMA LA ZANZIBAR.
Shirika la Bima la Zanzibar ni moja kati ya kampuni 29 zilizosajiliwa na Kamishna wa Tanzania kwa
lengo la kutoa huduma za Bima katika mfu mo wa biashara huria ulianzia mwaka 1998.
UTELEZAJI WA MALENGO.
Katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2011 liliweka lengo la kukusanya jumla ya
Tshs..10,500,000,000/- fedha zilizokusanywa ni jumla ya Tshs 9,006,790,797/-sawa na asilimia 86 ya
lengo, mapato hayo yalitokana na aina za bima zifuatazo:-
i) Bima ya gari Tshs 8,106,111,717/-
ii) Bima ya moto Tshs 324,470,000/-
iii) Bima ya Meli Tshs 231,149,080/-
iv) Bima mchanganyiko Tshs 345,060,000/-
Uwekezaji wa fedha za Shirika.
Hadi kufikia Disemba 2011 Shirika limewekeza jumla ya Tshs 5,084,102,000 /- kama ifuatavyo:-
1) Makao makuu – uwekaji wa fixed deposit ni Tshs 1,619,102,000/- (FBME na
EXIM Bank)
2) Uwekaji wa dhamana za Serikali –Tshs 2,665,000,000/-.(BoT)
3) Kanda ya Pwani Tshs 800,000,000/-(BoA, Commerce, Africa Bank na DTB)
Katika mradi wa ujenzi, Shirika linatarajia kukamilisha mradi wake wa ujenzi wa ghorafa tano ujenzi huo
ulitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi March 2012, ambapo uligharimu jumla ya Tshs 2.9
bilioni.Hatahivyo Shirika halijaweza kukamilisha azma yake ya kuanzisha huduma za bima zinazoendana
na maadili ya kiislamu (TAKAFUL).
(KANDA YA PWANI). Ofisi ya Shirika la Bima Zanzibar – Kanda ya Pwani inasimamia matawi yote yaliyoko Tanzania Bara,
ambayo ni Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma.
UTEKELEZAJI WA MALENGO.
Katika kipindi cha Januari hadi Disemba, 2011 Ofisi ya Kanda ya Pwani ilipangiwa kukusanya jumla ya
Tsh.5, 684,950,000 na kutumia jumla ya Tsh.814, 157,597/- kwa uendeshaji wa Ofisi.
Hadi kufika mwezi Novemba, 2011 jumla ya Tsh.3, 988,551,556/- zilikusanywa. Mapato hayo ni sawa na
asilimia 70 ya lengo. Wakati matumizi yalikuwa Tsh.692, 033,957.79 sawa na asilimia 85 ya bajeti
iliyowekwa.
Katika suala la ulipaji wa madai ya wateja; jumla ya Tsh. I, 940,286,500/- zilitumika.
Mengineyo (Uwekezaji wa Fedha Taslim)
Hadi kufikia Novemba, 2011 Ofisi ya Kanda ya Pwani iliweza kuwekeza jumla ya Tsh.800, 000,000/-
ambapo kwenye Bank of Africa na Africa Bank Corporation kila moja wamewekeza Tsh.30, 000,000/-.
BODI YA MAPATO ZANZIBAR.
Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) ilianzishwa chini ya sheria Namba 7 ya mwaka 1996 kama taasisi ya
ukusanyaji mapato ya Serikali yatokanayo na vyanzo vya ndani. Bodi ya Mapato ilianza kazi rasmi
mnamo mwezi Septemba, 1998.
UTEKELEZAJI WA MALENGO.
Katika kuyafikia malengo iliyowekewa; Bodi ya Mapato Zanzibar inasimamia Sheria zifuatazo:-
a) Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) nambari 4 ya mwaka 1998.
b) Sheria ya Kodi ya Mahoteli (Hotel Levy) nam. 1 ya mwaka 1995.
c) Sheria ya Kodi ya bidhaa za Mafuta ya Petroli nam. 7 ya mwaka 2001.
18
d) Sheria ya Kodi ya Ushuru wa Stempu nam. 6 ya mwaka 1996.
e) Sheria ya Ada ya huduma ya Bandari na Viwanja vya Ndege nam. 2 ya mwaka 1999.
f) Sheria ya leseni za biashara ya mwaka 1983.
g) Sheria ya Kodi ya Majengo.
h) Sheria ya Usimamizi wa Kodi nam 7 ya mwaka 2009.
Mbali ya kusimamia sheria hizo, Bodi ya Mapato Zanzibar imepewa uwakala wa kusimamia ada na kodi
zilizokuwa zinasimamiwa na Taasisi nyengine hapa Zanzibar ambazo ni:-
• Leseni za Udereva
• Leseni za njia,
• Usajili wa vyombo vya moto na
• Kodi ya Ardhi
UTEKELEZAJI WA MALENGO YA UKUSANYAJI WA MAPATO.
Bodi ya Mapato Zanzibar ilikadiriwa kukusanya mapato yenye jumla ya Tshs. 71.2 bilioni kwa kipindi
cha Julai – Januari, 2011/2012 kutokana na vyanzo mbalimbali inavyovisimamia.
Makusanyo halisi kwa kipindi hiki cha miezi saba ni Tshs.71.3 bilioni, ambazo ni sawa na asilimia
100.08 ya makadirio kwa kipindi husika
MUHTASARI WA MAKADIRIO NA MAKUSANYO HALISI KWA MUJIBU WA VYANZO
KWA KIPINDI CHA MIEZI SABA JULAI - JANUARI, 2011/2012
KIANZIO
JULAI - JAN
2010/2011
JULAI - JAN
2011/2012
JULAI - JAN
2010/2011
JULAI - JAN
2011/2012
JULAI -
JAN
2010/20
11
JULAI - JAN
2011/2012
VAT&EXCISE DUTY 31.40 34.90 27.70 33.90 88.20 97.13
K/MAFUTA 13.70 16.00 13.50 14.80 98.50 92.50
K/NYENGINEZO 16.60 20.30 16.30 22.60 98.20 111.33
JUMLA 61.70 71.20 57.50 71.30 93.13 100.08
MAKUSANYO HALISI (BIL.
TZS) ASILIMIA YA
UTEKELEZAJI
MAKADIRIO YA
MAKUSANYO (BIL. TZS)
Kiutekelezaji kianzio cha VAT na Exercise Duty kwa pamoja vimeweza kukusanya jumla ya Tshs.33.9
bilioni ikilinganishwa na makisio ya Tshs.34.9 bilioni sawa na asilimia 97.13 na kianzio cha kodi za
mafuta kilichokadiriwa kukusanya jumla ya Tshs.16.0 bilioni na makusanyo halisi ni Tshs.14.8 bilioni
sawa na asilimia 92.50 na kianzio cha kodi nyenginezo kimekusanya Tshs.22.6 bilioni ukilinganisha na
makisio ya Tshs.20.3 bilioni sawa na asilimia 111.33.
Ikilinganishwa makadirio ya kipindi cha miezi Saba (Julai – Januari), katika mwaka 2011/12 ya Tshs.
71.2 bilioni na makusanyo halisi yaliyofikiwa ya Tshs. 71.3 bilioni kunajitokeza ongezeko la makusanyo
kwa kiasi cha Tshs. 0.1 bilioni sawa na asilimia 0.08 ya makadirio.
19
Ikilinganishwa kiwango cha makusanyo ya Tshs. 57.5 bilioni kilichofikiwa katika kipindi cha Julai -
Januari, 2010/11 na kiwango cha Tshs. 71.3 bilioni kilichofikiwa katika kipindi cha Julai - Januari,
2011/12 kunajitokeza ongezeko la makusanyo ya Tshs. 13.8 bilioni.
MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA.
Kodi zinazosimamiwa na TRA Zanzibar:
Idara ya Kodi za Ndani ya TRA Zanzibar inasimamia ukusanyaji wa mapato chini ya sheria namba 11 ya
mwaka 2004 ya kodi ya mapato ambayo inahusisha kodi ya makampuni (Corporate tax) kodi za zuio
(Withholding Taxes), faida halisi kwa kuuza rasilimali (Capital gain), Kodi ya Mapato ya mtu binafsi na
kodi kwenye marupurupu ya ajira.
Aidha Idara hiyo inasimamia kodi ya kuendeleza ufundi stadi (Skill development levy) chini ya sheria
namba 8 ya mwaka 2006.
Idara ya Forodha inasimamia ukusanyaji wa mapato chini ya sheria ya Forodha ya Afrika Mashariki ya
mwaka 2004, ambayo inatoza kodi ya Forodha kwa Bidhaa zinazotumika moja kwa moja na mlaji. Pia
Idara inakusanya kodi ya ushuru wa bidhaa chini ya sheria ya kodi ya bidhaa.
Aidha, Idara inakusanya ushuru wa Bidhaa kwa mafuta ya kuendeshea vyombo vya moto na mitambo,
kwa sheria ya mafuta. Pia Idara ya Forodha inasimamia ukusanyaji wa kodi ya VAT kwa bidhaa
zinazoingia nchini kwa mujibu wa sheria namba 4 ya mwaka 1998.
MAKISIO YA MAPATO KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012.
Kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 Mamlaka ya Mapato Tanzania ofisi ya Zanzibar ilipangiwa
kukusanya Shilingi 100,581 milioni ambazo ziliongezeka kwa asilimia 32 kuliko mapato halisi ya
Shilingi 76,335 milioni yaliyokusanywa katika mwaka wa fedha 2010/2011. Kati ya makisio hayo ya
shiling 100.581 milioni, Idara ya Forodha na Ushuru ilipangiwa kukusanya Shilingi 49,442.3milioni na
idara ya Kodi za Ndani ilipangiwa kukusanya shilingi 51,138.8 milioni.
Kwa kipindi cha miezi 7 cha kuanzia Julai – Januari Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Zanzibar ilipangiwa
kukusanya shilingi 57,805.1 milioni ambapo Idara ya Kodi za Ndani ilikisiwa kukusanya Shilingi
28,879.6 milioni na Idara ya Forodha ilikisiwa kukusanya Shilingi 28,925.5 milioni.
MAPATO HALISI KATIKA KIPINDI CHA JULAI – JANUARI
Mapato halisi yaliyokusanywa na Mamlaka ya Mapato kwa kipindi cha Julai – Januari katika mwaka huu
wa fedha wa 2011/2012 ni Shilingi 49,780.5 milioni sawa na utekelezaji wa asilimia 86 ukilinganisha na
makisio ya kipindi hicho.
Mapato yaliyokusanywa kwa kipindi hichi cha mwaka huu wa fedha wa 2011/2012 yameongezeka kwa
asilimia 20 ukilinganisha na kipindi kama hicho cha mwaka wa fedha uliopita wa 2010/2011. Mwaka
uliopita kipindi kama hicho Mamlaka ya Mapato ilikusanya shilingi 41,355.1milioni.
Idara ya Forodha imevuka lengo la kipindi hicho cha miezi Saba kwa takriban asilimia 109 baada ya
kukusanya shilingi 31,485.9 milioni. Aidha, Idara ya Kodi za Ndani haikufikia lengo la kipindi hicho
baada ya kukusanya Shilingi 18,294.6 milioni dhidi ya lengo la Shilingi 28,879.6 milioni. Utendaji huu
ni wa asilimia 63.
Sababu kubwa ya kutofikia lengo kwa Idara ya Kodi za Ndani – Zanzibar kumechangiwa na
kutohaulishwa kwa Shilingi 10,500 milioni za PAYE kwa kipindi cha Julai – Januari 2012 zinazotokana
na watumishi wa Taasisi za Muungano zilizopo Zanzibar. Ilitegemewa kuwa PAYE ya Watumishi wa
Taasisi za Muungano waliopo Zanzibar ingelipwa kwa TRA Zanzibar kutoka Hazina Tanzania Bara
katika mwaka wa Fedha wa 2011/2012. Hata hivyo, matatizo ya kisheria yamekwamisha utekelezaji wa
azimio hilo.
20
Jadueli namba 1: Ulinganisho wa utekelezaji kiidara katika mwaka wa fedha wa 2011/2012 na
2010/2011.
Idara
2010/2011
2011/2012
Makisio Hali Halisi Asilimia Makisio Hali Halisi Asilimia
Forodha 23,214.0 26,082.8 112 28,925.5 31,485.9 109
Kodi za
Ndani
15,638.0 15,272.5 98 28,879.6 18,294.6 63
Jumla Kwa
TRA
Zanzibar
38,852.0 41,355.3 106 57,805.1 49,780.5 86
MFUKO WA BARABARA.
MFUKO WA BARABARA – ZANZIBAR.
Makusanyo.
Kwa mwaka wa fedha 2011/2012 Mfuko ulikadiria kukusanya jumla ya Tsh. 6.432 bilioni na ambapo
kwa kipindi cha miezi minne (Julai hadi Oktoba, 2011) jumla ya Tsh. 1,797 bilioni ambazo ni sawa na
asilimia 28 ya makadirio. Mfuko umepokea Tsh. 1,424 bilioni.
UTEKELEZAJI WA MALENGO.
Jumla Tsh.1, 322 bilioni zililipwa kwa kazi za barabara pamoja na malipo ya ununuzi wa lami na Grader
Kalavati za Kiongele, pamoja na usafi wa Barabara.zikiwa ni asilimia 24 ya makadirio ya mwaka.
Barabara zilizotengenezwa kwa fedha hizo; kwa upande wa Unguja ni:-
Mwanakwerekwe – Nyumba Mbili, Soko la Mchina – Mbuyu Mnene, Kiboje -- Mabonde ya Mpunga,
Kiyashange – Kijijini.
Kwa upande wa Pemba ni uwekaji wa tabaka la lami barabara ya Weni – Wete, mambo mengine ni
uzibaji wa viraka na usafi wa barabara.
MRADI WA UJENZI WA AFISI.
Ujenzi wa Afisi ya Mfuko wa Barabara „White Villa‟ iliyopo Kikwajuni upo katika hatua za mwisho
kukamilika na ilitarajiwa kufunguliwa kwenye sherehe za Mapinduzi ya Januari, 2012.
Jengo hilo ambalo linajengwa na Mkandarasi „Rans Company Ltd‟ na kusimamiwa na Mshauri M/S
Yasser Consultant, na linajengwa kwa gharama ya Tsh. 696,575,000/- na Mjenzi huyo hadi mwezi
Disemba, 2011 ameshalipwa jumla ya Tsh.390,819,000/- kukiwa na bakaa ya Tsh.305,756,000/-.
Lengo la baadae la Mfuko ni kuweka mitambo ya kisasa ya ulinzi (CCTV Camera), ununuzi wa
Genereta la dharura na kwa kushirikiana na Baraza la Manispaa itajenga maegesho ya magari na bustani.
MAMLAKA YA UKUZAJI VITEGA UCHUMI.
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA KAZI ZA AFISI YA ZIPA.
MAJUKUMU YA JUMLA.
Kwa ujumla kazi zinazotekelezwa zianatajwa katika Sheria ya uwekezaji No.11 ya Mwaka 2004, lakini
kazi hizo kwa ufupi ni kama ifuatavyo:-
Mamlaka ndicho chombo pekee cha Zanzibar cha kushughulikia ukuzaji vitega uchumi pamoja
na kazi zote zitazopelekea kufanikisha uwekezaji wa aina zote za vitega uchumi.
21
Mamlaka ina wajibu wa kudumisha uhusiano wa Wawekezaji, Serikali na Mamlaka nyengine
zinazohusika na uwekezaji.
Mamlaka ni dhamana wa utawala, udhibiti na uendeshaji wa Bandari huru na Maeneo huru ya
Uchumi.
Mamlaka ina wajibu wa kutekeleza kazi nyengine zenye kufanikisha kufikia malengo ya
uwekezaji.
MALENGO YA MAMLAKA.
a. Kujenga maghala matatu katika eneo huru la Amani na matatu katika eno la Bandari
huru ya Maruhubi
b. Kufanya” Master plan “kwa eneo la Fumba.
c. Kukamilisha taratibu za mradi wa jengo la kitega uchumi la Mamlaka Pemba.
d. Kufanya ukarabati wa mfumo w a maji taka katika eneo la Amani.
e. Ujenzi wa uzio wa ukuta katika eneo la Bandari Huru Uwanja wa Ndege.
UTEKELEZAJI WA MALENGO.
Mamlaka inatekeleza kazi ya ujenzi wa Maghala kwa kushirikiana,ambapo Wawekezaji
wanajenga wenyewe maghala na kukatwa gharama hizo kwa mujibu wa makubaliano.
Mamlaka inafanya mawasilianao na mshauri elekezi kutoka kampuni ya Phills Internationa
kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Mkuu (Master plan) wa uendelezaji wa maeneno ya
Fumba, Chaleni na Myamanzi.
Mamlaka imetafuta mshauri wa ujenzi na kazi ya tathmini inaendelea .Aidha kazi za
kujenga ofisi za muda za mamlaka zimeanza katika sehemu ya kiwanja cha Tibirinzi.
Ukarabati wa mfumo wa maji taka Amani hatua za awali za kufanyia marekebisho ya
michirizi imefanyika.
Taarifa ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2011/2012.
Katika kipindi cha miezi sita (Julai-Disemba) jumla ya Tshs 809,287,454.77 zilikusanywa kutoka vyanzo
tofauti vya mapto na Tshs 150,000,000.00/- ni ruzuku kutoka Serikalini, hivyo jumla ya makusanyo ni
Tshs 959,287,454.77/- ambazo ni sawa na asilimia 49.76 ya makadirio ya mwaka mzima.
Tathmini ya maombi ya miradi.
Jumla ya miradi kumi na sita(16) yenye thamani ya mtaji wa makisio ya USD 71, 421,300 iliidhinishwa
katika kipindi cha Julai –Disemba 2011. Kati ya miradi hiyo mitano ni ya hoteli, minne ni ya viwanda,
minne ya kilimo, miwili ya huduma na mmoja ni wa mawasilianao .Jumla ya Tshs 24, 718,000.00/-
zimetumika katika kazi hiyo.
Kuwajengea uwezo wa Wafanyakazi.
Jumla ya Wafanyakazi 9 wamepatiwa fursa ya kushiriki katika mafunzo ndani na nje ya nchi juu ya
mambo mbali mbali yanayohusu kazi zao kwa lengo la kuwaongezea taaluma na uwezo wao wa
kutekeleza majukumu yao ya kazi. Jumla ya Tshs 62, 977,070.00/- zimetumika.
Kutangaza fursa za uwekezaji.
Mamlaka ilitangaza fursa mbali mbali za uwekezaji kwa kufanya ziara za uenezi ,kushiriki katika
mikutano ya kikanda naya kimataifa ya uhamasishaji.Aidha makala mbali mbali katika magazeti kama
vile kwenye SACD directory,Tanzania Review,pamoja na uchapaji wa diary na kalenda ,ziara zimefaywa
katika Nchi zenye viwanda vya usindikaji samaki (Syscheles na Maldives) ili kujifunza na kushajihisha
wenye viwanda kuja Zanzibar,jumla ya Tshs 25,951,154.40 zimetumika kwa kazi hiyo.
22
Kukuza teknolojia ya habari.
Tovuti ya www.zanzibarinvest.org imetafsiriwa kwa lugha ya kichina mwelekeo sasa ni kuwa na lugha
ya kirusi na kituruki, jumla ya Tshs 5, 700,000/- zimetumika.
Uimarishaji miundo mbinu (maji).
Mamlaka imesafisha kisima cha maji safi na kuweka pampu mpya ya kusukuma na kuvuta maji,
Tshs.7,000,000/- zimetumika.
Uimarishaji miundo mbinu (barabara).
Idara ya Ujenzi na Matengenezo ya Barabara imeshalipwa jumla ya Tshs 84,670,000/- kwa ajili ya ujenzi
wa barabara ya maeneo huru ya Amani na Maruhubi.
Ukarabati wa Maghala.
Mamlaka imefanya matengenezo ya maghala mawili hapo Amani Industrial Park (call center,) na
Maruhubi ghala linalotumiwa na kampuni ya Sham limited fedha zilizotumika ni jumla ya Tshs
115,566,910/-.
Kwa upande wa Pemba katika kipindi cha April-Juni, 2011 Afisi ilitumia Jumla ya Tshs 11,361,900 kwa
kazi za kawaida, taarifa imeelezwa kuwa hakuna mapato yoyote yaliyokusanywa katika kipindi hiki.
HALI YA UWEKEZAJI KWA KIPINDI CHA APRIL-JUNI (PEMBA).
Kwa kipindi cha April hadi Juni mradi mmoja ulisajiliwa.Wamiliki wa mradi huo ni Bwana Isaias Jose
Pena na Bwana Morin raia wa Uhispania na Bwana Rune.
Katika maeneo ya Micheweni hadi kamati ilipofika katika ofisi za ZIPA Pemba bado hakujawa na
mwekezaji yeyote aliyejitokeza.
Shughuli kuu iliyofanyika ni ukaguzi wa mara kwa mara kwa ajili ya kuangalia usalama wa maeneo.
Hata hivyo baada ya kuzungumza na wawekezaji ambao wamejenga maghala ya kuhifadhi mwani
kwenye maeneo hayo kukamilika, Afisi ya ZIPA Pemba imefanya utaratibu wa kuyapima na kuyawe
kea “Bicons”.
OFISI YA MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI.
MALENGO YA IDARA
Miongoni mwa malengo yaliyopangwa na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu kwa kipindi cha mwaka wa fedha
wa 2011/2012 ni kama yafuatayo:-
(a) Kufanya tathmini juu ya hali ya ukuaji wa ukadiriaji wa Pato la Taifa kwa mwaka 2011
(b) Ukamilishaji wa matayarisho ya Sensa ya Watu na makaazi.
(c) Utekelezaji wa mpango mkuu wa Takwimu Tanzania.
(d) Kuendeleza kazi za mradi wa ZANSTAT na mchakato wake kwa awamu ya Pili.
UTEKELEZAJI WA MALENGO.
Takwim za Quarterly – GDP.
Idara imekamilisha ukadiriaji kwa mwaka wa kwanza na robo ya pili (April – Juni, 2011), robo ya tatu
inaendelea sambamba na kazi za ukusanyaji wa takwimu za Economic Survey.
Sensa ya Watu na Makaazi ya Mwaka 2012. Moja ya matayarisho ya Sensa hii ni utayarishaji wa ramani za Maeneo ya Kuhesabia Watu katika Mikoa
yote ya Tanzania na kutayarisha ramani hizo katika mfumo wa Geographical Information System kwa
kutumia Digitalization System. Kwa upande wa Zanzibar kazi ya kutenga maeneo kwa Mikoa yote
mitano imemalizika. Jumla ya maeneo 5,397 ya kuhesabia Watu yametengwa kwa ajili ya Sensa hiyo
ikilinganishwa na maeneo 2,062 ya mwaka 2002.
Matayarisho mengine yaliyofanyika ni kuandaa miongozo mbalimbali ikiwemo Muongozo wa Sensa
pamoja na kuunda kamati mbali mbali za kusimamia kazi za Sensa.
23
Aidha kumefanyika Sensa ya majaribio ambapo maeneo 44 yalitengwa kwa madhumuni hayo, nayo ni
katika Mikoa ya Arusha, Kigoma, Dar es Salaam, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Mtwara, Njombe na
Pwani kwa upande wa Tanzania Bara, na kwa upande wa Zanzibar jumla ya maeneo SITA yalihusishwa,
maeneo MANNE yalikuwa katika Shehia ya Chukwani, Unguja na maeneo MAWILI yalikuwa kwa
Shehia za Sizini na Maziwa Ng‟ombe , Pemba.
Aidha mradi wa Zanzibar Statiscal System Project umeanza kutekelezwa kwa lengo la kubadilisha
mfumo wa Takwimu Zanzibar na kuwezesha kutoa Tawimu zilizo bora na zinazokwenda na wakati.
SEHEMU YA TATU
3.0. HITIMISHO.
Baada ya Kamati kukamilisha kazi yake ya ufuatiliaji katika Wizara husika, ilitoa ushauri, maoni na
kuziagiza Idara na Taasisi zinazohusika kama ifuatavyo:-
3.0.1. WIZARA YA NCHI (OR) FEDHA, UCHUMI NA MIPANGO YA MAENDELEO.
MAONI/MAAGIZO YA KAMATI.
1. .Serikali zote mbili zisimamie utekelezaji wa utaratibu wa kuhakikisha kuwa kodi ya mapato
(income tax) kwa Wafanyakazi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaoishi
Zanzibar kodi yao ya Mapato (PAYE) iwe inakusanywa Zanzibar kupitia Bodi ya Mapato
Zanzibar kama wakala .
2. Utaratibu wa ukusanyaji kodi ya visa ubadilishwe kwani utaratibu unaotumika hivi sasa
hauoneshi uhalisia wa mapato halisi sambamba na idadi ya wageni wanaoingia Nchini.
3. .Suala la magendo ya mafuta linahitaji msukumo wa pamoja kati ya vyombo vyote vya ulinzi,
bandari na Wananchi kwa ujumla, wavuvi na wale wanaotumia bandari zisizo rasmi.
4. Elimu itolewe kwa Wafanyabiashara ikiwa na msisitizo wa kuhakikisha kuwa kila mfanya
biashara anatoa risiti bila ya hata kuombwa na mteja au kuweka masharti ya kupunguza bei
iwapo mteja hatapatiwa risiti.
5. Utaratibu uandaliwe wa kuanzisha mfumo wa utoaji risiti uliounganishwa na mtandao
(electronic receipt) ambao utamuwezesha kila mfanyabiashara kuwa na risiti.
6. Kuwe na udhibiti mzuri wa ukusanyaji wa kodi za mahotelini ili kuwe na uwiano ulio na idadi
sawa ya Wageni wanaoingia Zanzibar na kulala mahotelini na mapato halisi
yanayokusanywa.Aidha mapato yanayokusanywa yaendane na viwango vya mahoteli yenyewe.
7. TRA Zanzibar iangalie sana malipo ya ushuru unaotolewa ili kusiwe na malipo ya tofauti ya
ushuru huo iwapo bidhaa itasafirishwa kupelekwa Tanzania Bara.
8. Sheria Nam 6 ya mwaka 1996 ya “stamp duty” ifanyiwe marekebisho ili kuwe na uwezekano wa
kuweka kiwango maalum cha kodi ya mapato badala ya makisio.
9. Serikali iweke kipaumbele wa ujenzi kwenye miundo mbinu katika maeneno huru ya uchumi
ili iwe ni kivutio kwa Wawekezaji.
10. Mamlaka inayosimamia utoaji wa huduma za Bima (TIRA) iangalie vyema kanuni zake hasa ile
inayohusiana na umiliki wa mali zisizohamishika (Fixed Assets) ili kampuni zinazotoa huduma
za Bima ziweze kumiliki wenyewe majengo ya Afisi badala ya kukodi.
24
11. Shirika la Bima la Zanzibar likamilishe taratibu zake za kuanzisha Bima inayoendana na maadili
ya Kiislam (TAKAFUL).
12. Serikali izitumie kikamilifu takwimu zinazotolewa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali kwa ajili ya
kuweka vipaumbele, Miradi na Mipango mingine ya Maendeleo.
13. Bado wananchi wanashindwa kufahamu kwa undani madhumuni ya Takwimu na suala zima la
kuhesabiwa (Sensa) hivyo elimu zaidi inahitajika kutolewa kwa Wananchi ili waweze kutoa
taarifa kwa usahihi .
14. Kamati inaagiza kuwa Bodi ya Mapato Zanzibar ihakikishe kuwa inawatambua na kuwasajili
Wafanyabiashara wote wakubwa na wadogo.
15. Kamati inaagiza kuwa Wafanyabiashara wote kuwa wanafanya mauzo katika maeneo ya
biashara na wanatoa Ankara za kodi kwani hivi sasa walipa kodi wengi hawatoi risiti
wanapofanya mauzo.
3.0.2. WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI.
MAONI / USHAURI /MAAGIZO YA KAMATI
1. Sheria na kanuni zinazohusiana na makosa ya uharibifu wa misitu na maliasili nyengine zipitiwe
upya kwani inaonekana adhabu zilizowekwa ni ndogo kiasi cha kutomtia khofu anayetenda
makosa..
2. Elimu zaidi iongezwe juu ya matumizi bora ya gesi na majiko mengine ambayo yanapunguza
matumizi ya kuni.
3. Upandaji wa mikarafuu mipya uwe ni mkakati wa makusudi kwa Wizara na isimamie kwa
karibu zoezi hili, hasa katika makuzi ya mikarafuu hiyo. Kila mwaka kuwe na takwimu halisi
inayoonesha idadi ya iliyopandwa, iliyokuwa vizuri, maeneo yaliyoonesha kiwango kizuri cha
ukuaji na yale ambayo hayakufanikiwa pamoja na sababu za kitaalamu zenye matokeo hayo.
4. Chuo cha Kilimo Kizimbani kizidi kuendelezwa ili kiwe miongoni mwa vyuo vya kilimo
vinavyotoa elimu hiyo kwa kiwango cha shahada (Degrees).
5. Wakulima wapatiwe mbegu bora za mpunga zinazozalishwa kwa wakati ili wawahi msimu wa
kilimo.
6. Wizara itayarishe maombi ya fedha Serikalini mapema ili fedha hizo zipatikane kwa wakati wa
msimu unaoendana wa kilimo.
7. Wakulima wapelekewe matrekta mapema kwa ajili ya kulima na kuburuga.
3.0.3. WIZARA YA BIASHARA VIWANDA NA MASOKO.
MAONI/USHAURI/MAAGIZO YA KAMATI.
1. Kuna haja ya kuwaelimisha wakulima umuhimu wa kuwepo kwa wachukuzi na
majukumu yao ili ipatikane njia muafaka itakayoondosha mgongano kati yao.
2. Kamati inazishauri Serikali za Wilaya kuwa na uwiano wa bei za vyeti vya mazao kati
ya Halmashauri moja na nyengine.
3. Kamati inalishauri Shirika kuangalia uwezekano wa kununua aina nyengine ya mizani
ya kisasa zaidi (Digital) ili kuondosha wasiwasi wa baadhi ya wakulima wanaouza
karafuu juu ya uwezo wa mizani zilizopo sasa.
25
4. Suala la kusafirisha karafuu kutoka Wilaya moja kwenda nyengine zikiwa mbichi au
kavu, Kamati inashauri bado Serikali iliangalie kwa makini na iandae utaratibu mzuri
wa kutoa vibali ili vibali hivyo visitoe fursa ya upelekwaji wa karafuu mahala pengine
pasipostahiki.
5. Kamati inashauri kufanyiwa matengenezo majengo ya vituo vya ununuzi wa karafuu
pamoja na ujengwaji wa vyoo.
6. Bado hakuna uwiano wa bei za bidhaa hasa za vyakula zinazouzwa katika sehemu
moja , hivyo Wizara haina budi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha
kwamba yale makubaliano ya bei kati yao na Wafanyabiashara yanatekelezwa kama
walivyokubaliana.
7. Juhudi za makusudi zifanyike ili kujua idadi sahihi ya maghala na maduka
yanayouzwa bidhaa kwa jumla na reja reja.
8. Zabuni kwa ajili ya matayarisho ya uwanja wa Kimataifa wa Maonesho ya Biashara
itangazwe mapema ili matumizi na gharama za eneo hilo zifahamike na walengwa.
9. Ukarabati wa Maghala ya kuhifadhia chakula cha akiba ya Nchi pamoja na
matayarisho mengine yanayohusiana na uhifadhi huo kwa mujibu wa sheria ufanyike
haraka ili angalau mwakani maghala hayo yaweze kutumika kwa kuhifadhia chakula
cha akiba.
10. Wizara isimamie suala la uhifadhi wa mafuta ya Nchi kwa ajili ya mafuta ya dharura.
11. Wizara iharakishe kufanya marekebisho ya sera ya viwanda ili iendane na wakati na
iwe na vivutio kwa wawekezaji katika Sekta ya Viwanda.
12. Kamati inaagiza Wizara kuwaajiri Wafanyakazi wa ukaguzi wa bidhaa wenye ujuzi wa
kutosha na kuwapatia vitendea kazi.
13. Elimu zaidi inahitajika kwa Wajasiriamali ili waweze kutengeneza bidhaa zitakazoweza
kukabiliana na ushindani katika masoko.