185
i TOLEO MAALUM ZIADA YA GAZETI LA KENYA, NO. 63 JAMHURI YA KENYA ZIADA YA GAZETI LA KENYA, 2005 NAIROBI, AGOSTI 22, 2005 YALIYOMO Ukurasa Katiba mpya ya Kenya iliyopendekezwa…………………………….1 Iliyoandikwa na kuchapishwa na Mwanasheria Mkuu kuingana na Kifungu 27 cha Sheria ya Kurekebisha Katiba ya Kenya (CAP 3A ya Sheria za Kenya) IMECHAPISHWA NA KUTANGAZWA NA MCHAPISHAJI WA SERIKALI, NAIROBI

Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

  • Upload
    others

  • View
    22

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

i

TOLEO MAALUM ZIADA YA GAZETI LA KENYA, NO. 63

JAMHURI YA KENYA ZIADA YA GAZETI LA KENYA, 2005

NAIROBI, AGOSTI 22, 2005

YALIYOMO

Ukurasa Katiba mpya ya Kenya iliyopendekezwa…………………………….1

Iliyoandikwa na kuchapishwa na Mwanasheria Mkuu kuingana na Kifungu 27 cha Sheria ya Kurekebisha Katiba ya Kenya (CAP 3A ya Sheria za Kenya)

IMECHAPISHWA NA KUTANGAZWA NA MCHAPISHAJI WA SERIKALI, NAIROBI

Page 2: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

ii

MPANGILIO WA IBARA

UTANGULIZI

SURA YA KWANZA

MAMLAKA YA WANANCHI NA UKUU WA KATIBA

1. Mamlaka ya wananchi 2. Ukuu wa Katiba

3. Sheria za Kenya

SURA YA PILI

JAMHURI

4. Kutangaza Jamhuri 5. Eneo 6. Usambazaji mamlaka 7. Mji Mkuu 8. Uenezaji vyombo vya Dola

9. Lugha 10. Taifa na Dini 11. Alama za Kitaifa 12. Siku za Kitaifa

SURA YA TATU

MAADILI YA TAIFA, KANUNI NA MALENGO

13. Maadili ya Taifa, kanuni na malengo

SURA YA NNE

URAIA

14. Kanuni za kijumla za uraia 15. Kudumisha uraia uliopo 16. Kupata uraia 17. Uraia wa kuzaliwa 18. Uraia na ndoa 19. Uraia wa kuandikishwa 20. Watoto wa kulelewa na watoto wanaopatikana Kenya 21. Uraia maradufu 22. Kunyang’anywa uraia 23. Makaazi 24. Wajibu wa Raia

Page 3: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

iii

25. Sheria kuhusu uraia

SURA YA TANO

UTAMADUNI

26. Kanuni kuhusu utamaduni 27. Tume ya Taifa ya Utamaduni 28. Siku ya Utamaduni

SURA YA SITA

SHERIA YA HAKI ZA BINADAMU

Sehemu ya Kwanza – Kanuni za Jumla kuhusu Sheria ya Haki za Binadamu

29. Haki za kimsingi na uhuru 30. Matumizi ya Sheria ya Haki za Binadamu 31. Utekelezaji wa haki na uhuru 32. Utekelezaji wa Sheria ya Haki za Binadamu 33. Mamlaka ya mahakama kulinda na kutekeleza Sheria ya Haki za Binadamu 34. Mipaka ya haki

Sehemu ya Pili – Haki za Kimsingi na Uhuru

35. Haki ya kuishi 36. Usawa 37. Uhuru wa kutobaguliwa 38. Jinsia 39. Wazee katika jamii 40. Vijana 41. Watoto 42. Familia 43. Watu wenye ulemavu 44. Heshima za binadamu 45. Uhuru na usalama wa mtu 46. Utumwa, kazi za utumwa na kulazimishwa 47. Faragha 48. Uhuru wa dini, imani na maoni 49. Uhuru wa kutoa maoni 50. Uhuru wa vyombo vya habari 51. Kupata habari 52. Uhuru wa kushirikiana 53. Mikusanyiko, maandamano, kuchochea migomo na malalamiko 54. Haki za kisiasa 55. Uhuru wa kwenda utakako na makaazi 56. Wakimbizi na hifadhi 57. Uhuru wa biashara, kazi na taaluma 58. Hifadhi ya haki ya mali 59. Mahusiano ya kazi 60. Ruzuku ya jamii

Page 4: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

iv

61. Afya 62. Elimu 63. Makaazi 64. Chakula 65. Maji 66. Usafi 67. Mazingira 68. Lugha na utamaduni 69. Haki za wateja 70. Utawala wa haki 71. Kupatikana kwa huduma za mahakama 72. Haki za watu waliotiwa nguvuni 73. Kufanyiwa kesi ya haki 74. Haki ya watu walio kizuizini 75. Hali ya hatari

SURA YA SABA

ARDHI NA MALI

76. Tume ya Jinsia 77. Tume ya Haki za Kibinadamu na Haki za Kiutawala 78. Kanuni za sera ya ardhi 79. Ukabidhi na uainishaji wa ardhi 80. Ardhi ya Umma 81. Wageni kumiliki ardhi 82. Usimamizi wa matumizi ya ardhi 83. Tume ya Taifa ya Ardhi 84. Sheria za ardhi

SURA YA NANE

MAZINGIRA NA MALIASILI

85. Kanuni na majukumu kwa mazingira 86. Kulinda mazingira 87. Kuhifadhi mazingira 88. Utekelezaji wa haki za mazingira 89. Matumizi na uendelezaji wa maliasili 90. Mikataba kuhusu maliasili 91. Tume ya Taifa ya Mazingira 93A. Sheria kuhusu mazingira

SURA YA TISA

UONGOZI NA UAMINIFU

92. Majukumu ya uongozi 93. Kushika wadhifa afisini 94. Nidhamu kwa maafisa wa Serikali 95. Mali za maafisa wa Serikali

Page 5: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

v

96. Vikwazo dhidi ya shughuli 97. Tume ya Maadili na Uaminifu 98. Sheria ya uongozi

SURA YA KUMI

UWAKILISHI WA WATU

Sehemu ya Kwanza – Mfumo na Utaratibu wa Uchaguzi

99. Misingi ya jumla 100. Chaguzi 101. Kusajiliwa kama mpiga kura 103A. Kuondolewa kwenye usajili kama mpiga kura 102. Kupiga kura 103. Wagombea wa kujitegemea 104. Wagombea bila kupingwa 105. Uwakilishi katika mashirika ya kimataifa

Sehemu ya Pili – Tume ya Uchaguzi na Mipaka

106. Kuundwa kwa Tume na kazi zake 107. Mipaka ya maeneo ya uchaguzi 108. Kuweka mipaka ya utawala

Sehemu ya Tatu – Vyama vya Kisiasa

109. Kanuni za kimsingi 111A. Wajibu na kazi za vyama vya kisiasa 110. Udhibiti 111. Mfuko wa vyama vya kisiasa 112. Madhumuni ya Mfuko 113. Vyanzo vingine vya fedha 114. Hesabu na ukaguzi 115. Usimamizi 116. Nidhamu ya chama 117. Vikwazo dhidi ya matumizi ya rasilmali za umma

SURA YA KUMI NA MOJA

BUNGE

Sehemu ya Kwanza – Kuundwa kwa Bunge na Wajibu wake

118. Kuundwa kwa Bunge 119. Utekelezaji wa mamlaka

Sehemu ya Pili – Muundo na Ujumbe katika Bunge

120. Ujumbe wa Seneti 121. Ujumbe wa Baraza la Taifa 122. Sifa na kutokuwa na sifa kwa wajumbe

Page 6: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

vi

124A. Makundi yaliyotengwa 123. Kuchaguliwa kwa Wabunge 124. Kuwa wazi nafasi ya Mbunge 125. Uamuzi wa suala kama mtu ni mjumbe

Sehemu ya Tatu – Maafisa wa Bunge

126. Spika na Naibu wa Spika wa Bunge 127. Usimamizi Bungeni 128. Kiongozi wa Upinzani 129. Makarani na wafanyakazi wa Bunge

Sehemu ya Nne – Utungaji Sheria na Utaratibu Bungeni

130. Utekelezaji wa uwezo wa kutunga sheria 131. Miswada ya Fedha 132. Mjadala katika Ukumbi mwingine 133. Idhini ya Rais na kuwasilishwa 134. Kuanza kutumika kwa sheria 135. Haki ya kulalamikia Bunge 136. Akidi 137. Lugha rasmi Bungeni 138. Kupiga kura Bungeni 139. Maamuzi ya Seneti 140. Kudhibiti utaratibu 141. Uwezo wa kuitisha ushahidi 142. Wananchi kupata nafasi na kushiriki 143. Uwezo, haki na kinga

Sehemu ya Tano – Mengineyo

144. Masjala ya Sheria 145. Makao ya Bunge 146. Muhula na kuahirishwa Bunge 147. Tume ya Huduma ya Bunge

SURA YA KUMI NA MBILI

MAMLAKA YA UTENDAJI

Sehemu ya Kwanza – Kanuni na Mfumo wa Mamlaka Tendaji ya Kitaifa

148. Kanuni za mamlaka ya utendaji 149. Muundo wa Mamlaka Tendaji ya Kitaifa

Sehemu ya Pili – Rais na Naibu Rais

150. Mamlaka ya Rais 151. Majukumu ya Kitaifa ya Rais 152. Majukumu ya kisheria ya Rais 154A. Mipaka ya uwezo wa Rais 153. Maamuzi ya Rais

Page 7: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

vii

154. Haki ya kupiga kura na wakati wa uchaguzi wa urais 155. Sifa za kufaa na kutofaa kuchaguliwa Rais 156. Utaratibu wa uchaguzi wa Rais 157. Masuala kuhusu uhalali wa uchaguzi wa urais 158. Kushika madaraka ya urais 159. Muhula wa Rais madarakani 160. Kinga ya Rais dhidi ya mashtaka 161. Kumwondoa Rais kwa sababu ya kutoweza kazi 162. Kushitakiwa na kuondolewa kwa Rais 163. Afisi ya Rais kuwa wazi 164. Uwezo wa msamaha wa Rais 165. Afisi ya Naibu Rais 166. Afisi ya Naibu Rais kuwa wazi 167. Majukumu ya Naibu Rais 168. Kufariki kabla ya kushika madaraka 169. Malipo na marupurupu ya Rais na Naibu Rais

Sehemu ya Tatu – Waziri Mkuu na Baraza la Mawaziri

170. Waziri Mkuu 171. Uteuzi wa Waziri Mkuu 172. Muhula wa kuwa madarakani 173. Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu 174. Kuondolewa kwa Waziri Mkuu 175. Mawaziri na Naibu Mawaziri 176. Katibu wa Baraza la Mawaziri 177. Maamuzi, majukumu na uwajibikaji wa Baraza la Mawaziri 178. Utoaji wa majukumu 180A. Kutokuwepo kwa Naibu Rais, Waziri Mkuu, Manaibu wa Waziri Mkuu, Mawaziri na

Naibu Mawaziri ndani ya Jamhuri 179. Makatibu Wakuu 180. Kuteuliwa na kufutwa kazi kwa Makatibu Wakuu

SURA YA KUMI NA TATU

MFUMO WA MAHAKAMA NA SHERIA

181. Kanuni na muundo wa uwezo wa mahakama 182. Mfumo wa ngazi za mahakama na usimamizi wake 183. Uhuru wa mahakama 184. Mahakama ya Juu 185. Mamlaka ya kisheria ya Mahakama ya Juu 186. Mahakama ya Rufaa 187. Mamlaka ya Mahakama ya Rufaa 188. Mahakama Kuu 189. Mamlaka ya Mahakama Kuu 190. Mamlaka ya usimamizi ya Mahakama Kuu 191. Uteuzi wa majaji 192. Sifa za kuteuliwa kuwa Jaji 193. Muda wa kazi za majaji 194. Kuondolewa afisini

Page 8: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

viii

195. Mahakama za chini 196. Mahakama za Kadhi 197. Mamlaka ya kisheria ya mahakama za Kadhi 198. Tume ya Huduma ya Mahakama 199. Majukumu ya Tume ya Huduma ya Mahakama 200. Mwanasheria Mkuu 201. Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma 202. Wakili wa Umma 203. Kuondolewa afisini

SURA YA KUMI NA NNE

SERIKALI ZILIZOSAMBAZIWA MAMLAKA

Sehemu ya Kwanza – Mfumo na Kanuni za Serikali Zilizosambaziwa Mamlaka

204. Malengo ya serikali kusambazwa 205. Kanuni ya serikali iliyosambaziwa mamlaka 206. Ushirikiano baina ya Serikali katika ngazi mbalimbali 207. Kugawanya majukumu 208. Mgongano wa sheria 210A. Usimamizi wa wilaya za mijini na maeneo ya miji 210B. Kusimamishwa kwa Serikali ya Eneo au Wilaya 210C. Marufuku kuchaguliwa katika ngazi ya Taifa na ya serikali zilizosambaziwa mamlaka

Sehemu ya Pili – Maeneo

209. Serikali za Maeneo 210. Mabaraza ya kutunga sheria za maeneo 211. Kamati tendaji ya eneo 212. Uchaguzi wa mkuu na naibu mkuu wa eneo 213. Uchaguzi wa meya na naibu meya wa Nairobi 214. Shughuli za kamati za mamlaka tendaji za maeneo

Sehemu ya Tatu – Wilaya

215. Serikali za Wilaya 216. Mamlaka ya kutunga sheria ya baraza la wilaya 217. Uchaguzi wa madiwani wa wilaya 218. Kamati tendaji ya wilaya 219. Uchaguzi wa gavana na naibu wa gavana wa wilaya 220. Shughuli za kamati tendaji ya mamlaka ya wilaya

Sehemu ya Nne – Kata

221. Serikali za Kata 222. Mabaraza ya Kata 223. Msimamizi wa Kata

Sehemu ya Tano – Jumla

224. Muda wa afisi

Page 9: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

ix

225. Uwezo wa kuita mashahidi 226. Haki, kinga na uwezo wa kufikia na kushiriki kwa umma 228A. Usawa wa jinsia na uanuwai 228B. Serikali wakati wa mpito 227. Uongozi na uadilifu 229A. Uchapishaji wa sheria 228. Masharti yatakayowekwa na Sheria za Bunge

Sehemu ya Sita – Masharti ya Muda

229. Kustahiki kuchaguliwa au keteuliwa katika serikali zilisombaziwa mamlaka 230. Taratibu na mipango ya ndani ya serikali zilisombaziwa mamlaka 231. Uchaguzi wa meya na naibu wa meya wa Nairobi 232. Uchaguzi wa madiwani wa wilaya 233. Uchaguzi wa mabaraza na wasimamizi wa kata

SURA YA KUMI NA TANO

FEDHA ZA UMMA

Sehemu ya Kwanza – Fedha za Umma na Usimamizi wa Mapato

234. Kanuni na malengo ya fedha za umma na usimamizi wa mapato

Sehemu ya Pili – Uwezo wa Kutoza Kodi na Kugawa Mapato

235. Kutoza kodi 236. Utozaji wa kodi 237. Fungu la Fedha za Taifa kwa serikali zilizosambaziwa mamlaka 238. Utungaji Sheria

Sehemu ya Tatu – Mifuko ya Fedha za Umma

239. Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali 240. Utoaji wa fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali 241. Mfuko wa Mapato ya Serikali zilizosambaziwa mamlaka 242. Mfuko wa Dharura

Sehemu ya Nne – Kukopa

243. Ukopaji wa Serikali 244. Ukopaji wa serikali zilizosambaziwa mamlaka 245. Deni la Umma 246. Serikali zinapodhamini mikopo

Sehemu ya Tano – Bajeti

247. Kanuni 248. Makadirio ya mwaka ya Taifa 249. Mswada wa mgawanyo na matumizi ya mapato 250. Bajeti ya mwaka ya serikali zilizosambaziwa mamlaka

Page 10: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

x

Sehemu ya Sita – Usimamizi wa Fedha

251. Ununuaji bidhaa na huduma za umma 252. Hesabu na ukaguzi wa taasisi za umma 253. Kudhibiti hazina 254. Msimamizi wa Bajeti 255. Mkaguzi Mkuu

Sehemu ya Saba – Taasisi

256. Mamlaka ya Mapato ya Taifa 257. Tume ya Mgawo wa Mapato 258. Benki Kuu ya Kenya 259. Majukumu ya Benki Kuu 260. Baraza la Uchumi na Jamii

SURA YA KUMI NA SITA

HUDUMA KWA UMMA

Sehemu ya Kwanza – Huduma kwa Umma

261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi wa Umma 263. Uwezo na majukumu 264. Ajira katika serikali zilizosambaziwa mamlaka 265. Himaya kwa maafisa wa umma 266. Tume ya Uajiri wa Waalimu 267. Tume ya Huduma za Afya

Sehemu ya Pili – Huduma ya Kenya ya Kurekebisha Tabia

268. Kuundwa 269. Mkurugenzi Mkuu

SURA YA KUMI NA SABA

USALAMA WA TAIFA

Sehemu ya Kwanza – Vyombo vya Usalama vya Taifa

270. Kanuni na malengo 271. Vyombo vya usalama vya Taifa 272. Kuundwa kwa Baraza la Usalama la Taifa 273. Majukumu ya Baraza la Usalama la Taifa

Sehemu ya Pili – Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi

274. Kuundwa 275. Uamrishaji Jeshini

Page 11: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

xi

Sehemu ya Tatu – Huduma ya Upelelezi ya Taifa

276. Kuundwa 277. Baraza la Upelelezi la Taifa

Sehemu ya Nne – Huduma ya Polisi ya Kenya

278. Kuundwa 279. Malengo na majukumu 280. Inspekta Jenerali 281. Tume ya Huduma ya Polisi

Sehemu ya Tano – Huduma ya Polisi wa Utawala

282. Kuundwa 283. Majukumu 284. Kamanda Jenerali

SURA YA KUMI NA NANE

TUME ZA KIKATIBA

285. Kutumika kwa Sura 286. Malengo na uhuru wa Tume 287. Kushirikishwa 288. Wajumbe wa Tume 289. Wafanyakazi wa Tume 290. Majukumu ya Jumla ya Tume 291. Mikutano ya Tume 292. Kuondolewa afisini 293. Fedha za Tume 294. Taarifa za mwaka na nyinginezo 295. Tume nyingine za kikatiba 296. Tume ya Haki za Kibinadamu na Haki za Kiutawala 297. Tume ya utekelezaji wa Katiba 298. Tume ya Jinsia 299. Tume ya Mishahara na Malipo

SURA YA KUMI NA TISA

MAREKEBISHO YA KATIBA

300. Marekebisho ya Katiba 301. Marekebisho yatakayofanywa na Bunge 302. Marekebisho ya Katiba kupitia Raia

SURA YA ISHIRINI

MASHARTI YA KIJUMLA

303. Utekelezaji wa Katiba 304. Kufasiri Katiba

Page 12: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

xii

305. Fafanuzi

SURA YA ISHIRINI NA MOJA

MASHARTI YA MPITO NA YANAYOTOKANA NA KUIDHINISHWA KATIBA HII

306. Sheria inayotokana na kuidhinishwa Katiba hii 307. Mpito 308. Tarehe ya kutekelezwa 309. Kufuta

JEDWALI

Jedwali ya Kwanza Maeneo, wilaya na sehemu za jiji Jedwali ya Pili Alama za Kitaifa Jedwali ya Tatu Viapo vya Taifa na matamko ya dhati Jedwali ya Nne Mgawanyo wa majukumu baina ya Serikali ya Taifa na

ngazi za Serikali zilizosambaziwa mamlaka Jedwali ya Tano Uwezo wa kutoza kodi Jedwali ya Sita Sheria zitakazotungwa na Bunge Jedwali ya Saba Masharti ya mpito na yanayotokana na kuidhinishwa Katiba hii

Page 13: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

13

UTANGULIZI

Sisi, watu wa Kenya - TUKITAMBUA utukufu wa Mola muumba wa vyote: TUKIWASTAHI wale wote waliopambana kishujaa kuleta uhuru na haki nchini mwetu: TUKIJIVUNIA uanuwai wa kikabila, kitamaduni na kidini, na tukidhamiria kuishi kwa amani na umoja kama taifa moja huru lisilogawanyika: TUKIHESHIMU mazingira asili tuliyorithi na tukikata kauli kuyadumisha kwa manufaa ya vizazi vijavyo: TUKIJITOLEA kulea na kulinda maslahi ya kila mmoja, familia na jamii katika taifa letu: TUKITAMBUA matumaini ya Wakenya wote ya kuwa na Serikali ambayo imejengwa katika misingi muhimu inayothamini uhuru, demokrasia, haki ya kijamii na utawala wa sheria: TUKITEKELEZA haki yetu isiyotengeka ya uhuru ili kuamua aina ya utawala wa nchi yetu na tukiwa tumeshiriki kikamilifu katika utaratibu wa kuandaa Katiba hii: TUNAIKUBALI, tunaiidhinisha na tunajipa Katiba hii wenyewe na kwa vizazi vyetu vijavyo.

MUNGU IBARIKI KENYA

Page 14: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

14

SURA YA KWANZA

MAMLAKA YA WANANCHI NA UKUU WA KATIBA

Mamlaka ya wananchi 1. (1) Mamlaka yote makuu ni ya wananchi wa Kenya na yanaweza kutekelezwa

tu kulingana na Katiba hii.

(2) Wananchi watatekeleza uwezo wa utukufu wao kwa njia ya moja kwa moja au kupitia kwa wawakilishi wao watakao teuliwa kidemokrasia.

(3) Mamlaka ya wananchi yametolewa kwa vyombo vya Serikali vifuatavyo vitakavyotekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba -

(a) Bunge, na mifumo ya kisheria katika serikali za wilaya;

(b) Mamlaka ya nchi, na mifumo ya mamlaka katika serikali za wilaya;

(c) Mahakama na mahakama nyingine huria; na

(d) Tume za kikatiba na afisi za Taifa;

Ukuu wa Katiba 2. (1) Katiba hii ndiyo sheria kuu ya Jamhuri na inalazimu tawala zote za

serikali na watu wote kote katika Jamhuri.

(2) Uhalali na uthabiti wa Katiba hii hauwezi kupingwa na au mbele ya mahakama yoyote au chombo chochote cha Serikali.

(3) Sheria ambayo inapingana na Katiba hii ni batili kwa kiwango cha ukinzani huo na kitendo chochote au utendaji unaopingana na Katiba hii si halali.

(4) Mtu au kikundi cha watu wanaweza kuwasilisha malalamiko katika Mahakama Kuu ili kutangazwe kuwa sheria fulani inapingana na au inakiuka Katiba hii;

(5) Mahakama Kuu ikitoa tamko chini ya Ibara ndogo (3), inaweza pia kutoa amri nyingine inayohitajika ili kutekeleza tamko hilo.

Ulinzi wa Katiba 3. (1) Kila mtu anawajibika kuheshimu na kulinda Katiba hii.

(2) Juhudi yoyote ya kuunda mfumo mwingine wa serikali usiofungamana na Katiba hii si halali.

Sheria za Kenya 3A. (1) Sheria za Kenya zinajumuisha Katiba hii na kila kilichotajwa hapa

ambacho kinakubaliana na Katiba hii -

Page 15: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

15

(a) sheria zilizotungwa chini ya Katiba hii;

(b) sheria zilizotungwa na Bunge zinazotumika mara tu kabla ya tarehe ya kuanza kutekeleza Katiba hii;

(c) sheria nyengine yoyote ambayo ilikuwa inatambuliwa na mahakama kama ni sehemu ya sheria za Kenya, kabla ya tarehe ya kuanza kutekeleza Katiba hii;

(d) sheria za kibinafsi za watu wa Kenya;

(e) kanuni ambazo zinajulikana kama sheria za jumuiya ya madola au nadharia ya uadilifu kama zinavyohusu katika mwenendo na taratibu za mahakama;

(f) sheria za Jumuiya ya Afrika Mashariki; na

(g) sheria za kimataifa, na makubaliano ya kimataifa yanayohusu Kenya.

Page 16: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

16

SURA YA PILI

JAMHURI

Kutangaza Jamhuri 4. (1) Kenya ni Jamhuri iliyo dola huru.

(2) Jamhuri ya Kenya imejengwa katika misingi ya utawala bora chini ya demokrasia ya vyama vingi, utawala shirikishi, uwazi na uwajibikaji, mgawanyo na utenganishaji wa madaraka, kuheshimu kwa haki za binadamu, uhuru wa kimsingi na utawala wa sheria.

Eneo 5. (1) Eneo la Jamhuri ya Kenya ni lile linalotambuliwa na sheria ya kimataifa.

(2) Jamhuri imegawanywa katika wilaya na sehemu nyinginezo kama zitakavyo aagizwa na Sheria ya Bungea;

(3) Kila wilaya itagawanywa katika sehemu nyinginezo kama itakavyoagizwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

Usambazaji Mamlaka 6. (1) Utukufu wa mamlaka ya watu utatekelezwa katika -

(a) Ngazi ya taifa;

(b) Ngazi ya wilaya;

(2) Serikali katika kila ngazi ni tofauti, zinategemeana, kushauriana na kujadiliana.

Mji Mkuu 7. (1) Mji Mkuu wa Kenya ni Nairobi.

(2) Vyombo vyote vya taifa vitasambazwa katika maeneo yote kwa uadilifu.

Uenezaji Vyombo vya Dola 8. Dola itaeneza vyombo vya serikali zote wilayani ili kuhakikisha -

(a) Upatikanaji wa huduma za serikali na uajiri kwa usawa;

(b) Mawasiliano mema baina ya vyombo vya serikali na wananchi.

Lugha 9. (1) Lugha ya Taifa ya Kenya ni Kiswahili.

(2) Lugha rasmi za Kenya ni Kiswahili na Kiingereza na hati zote

rasmi zitaandikwa kwa lugha hizo mbili.

(3) Dola itaheshimu na kulinda lugha tofauti za wananchi wa Kenya.

Page 17: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

17

(4) Dola itahimiza maendeleo na matumizi ya Breli na njia nyingine zozote zinazofaa kwa mawasiliano ya vipofu na watu wenye ulemavu mwingine.

Taifa na Dini 10. (1) Taifa na dini vinatenganishwa.

(2) Hapatakuwa na dini ya Taifa.

(3) Dola itazichukulia dini zote kwa usawa.

Alama za Kitaifa 11. Alama za taifa za Jamhuri ni kama zilivyo katika Jadweli ya Pili; na ni -

(a) bendera ya taifa;

(b) wimbo wa taifa;

(c) nembo; na

(d) muhuri wa taifa.

Kama zilivyoainishwa katika Jedwali ya Kwanza.

Siku za Kitaifa 12. (1) Sikukuu za kitaifa zitakuwa -

(a) Juni 1 - Sikukuu ya Madaraka

(b) Oktoba 20 - Sikukuu ya Mashujaa

(c) Disemba 12 - Sikukuu ya Jamhuri

Page 18: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

18

SURA YA TATU

MAADILI YA TAIFA, KANUNI NA MALENGO

Maadili ya Taifa, kanuni na malengo 13. (1) Maadili ya Taifa, kanuni na malengo yanajumuisha -

(a) ukuzaji wa umoja wa kitaifa na kujitolea kwa raia wake kwa mwito wa utaifa na uzalendo;

(b) utambuaji wa uanuwai wa wananchi wake na ulinzi wa tamaduni za jamii zake;

(c) uendelezaji wa ushiriki wa wananchi katika masuala ya kitaifa na kufanikisha ugawaji, na usambazaji wa mamlaka;

(d) hakikisho la kuwepo kwa utawala ulio wazi na uwajibikaji wa maafisa wa serikali, maafisa wa umma, vyombo vya serikali na vya umma;

(e) kuchukua hatua za thabiti za kuondoa aina zote za rushwa;

(f) hakikisho kuwa wananchi wanapata haki kwa wakati unaofaa kutoka kwa vyombo vya sheria vilivyohuru, visivyopendelea, vyenye ustadi na visivyo ghali mno;

(g) utambuaji wa mchango wa jumuiya za wananchi katika utawala na kusaidia juhudi zao katika kuhakikisha uwajibikaji wa Serikali;

(h) ulinzi na ukuzaji wa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi na kuendeleza utu wa watu binafsi na jamii;

(i) hakikisho la kushiriki kikamilifu kwa wanawake, watu wenye ulemavu, jamii zilizotengwa na raia wengine wote katika maisha ya nchi katika miktadha ya kisiasa, kijamii na kiuchumi;

(j) utekelezaji wa kanuni ya kwamba hakutakuwa na zaidi ya theluthi mbili za watu wa jinsia moja katika mashirika kwa kuteuliwa au kuchaguliwa;

(k) utatekelezaji hatua kwa hatua wa kanuni kwamba angalau asilimia tano ya wajumbe wa mashirika kwa kuchaguliwa au kuteuliwa ni watu wenye ulemavu;

(l) utambuaji wa majukumu maalum ambayo Taifa, jamii na wazazi wanayo kwa watoto na itahakikisha na kudumisha familia na taasisi ya ndoa;

(m) uwajibikaji katika kutimiza haki za kijamii na kuwatimizia Wakenya wote mahitaji ya kimsingi na mazingira salama;

Page 19: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

19

(n) utambuaji, uendelezaji na ukuzaji wa nafasi ya, sayansi na teknolojia;

(o) uondoaji wa tofauti za kimaendeleo baina ya maeneo ya nchi na sekta za jamii;

(p) ufanisi katika usimamizi wa maliasili za taifa kwa manufaa ya wananchi;

(q) utambuaji ya majukumu ya jamhuri kwa vizazi vijavyo vya Wakenya kwa kufuata sera za usimamizi endelevu wa mazingira; na

(r) ukuzaji wa umoja wa Afrika na wa ulimwengu na itajitolea kutumikia amani na mshikamano wa kimataifa.

(s) ushirikiano na ushikamano na jamii ya kimataifa katika kufuatilia kupatikana amani ya kimataifa.

(2) Maadili ya Taifa, kanuni na malengo yaliyomo katika Sura hii yanatumika kwa vyombo vyote vya serikali, maafisa wa serikali, maafisa wa umma, raia na vyombo vya kibinafsi pale ambapo chombo kimojawapo -

(a) kinatumia na kuifafanua Katiba hii au sheria nyingine yeyote; au

(b) kinatumia, kinaunda, au kutekeleza maamuzi ya sera.

Page 20: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

20

SURA YA NNE

URAIA

Kanuni za kijumla za uraia 14. Kila raia -

(a) anastahiki kupata haki, fursa na faida za uraia kwa mujibu wa Katiba hii;

(b) ana haki sawa ya kupata paspoti ya Kenya na kupata hati yoyote ile ya usajiliwa na ya utambulisho inayotolewa na serikali kwa raia; na

(c) ana kiwango sawa cha majukumu ya uraia.

Kudumisha uraia uliopo 15. Kila mtu ambaye alikuwa raia wa Kenya kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba

hii atabaki kuwa raia wa Kenya.

Kupata uraia 16. (1) Uraia unaweza kupatikana kwa njia ya kuzaliwa, kusajilishwa, au

kuandikishwa.

(2) Kila mtu ambaye hakuwa raia wa Kenya kabla ya kuanza kutumika Katiba hii, lakini ambaye angekuwa raia wa Kenya kama Katiba hii anaweza kutuma maombi ya kusajiliwa kama raia wa Kenya kwa kufanya maombi.

Uraia wa kuzaliwa 17. (1) Kila mtu aliyezaliwa Kenya, atakuwa raia wa kuzaliwa ikiwa, mama ama

baba yake –

(a) alikuwa raia wakati wa tarehe ya kuzaliwa mtu huyo; au

(b) alipata uraia tarehe kumi na mbili Decemba mwaka wa

sitini na tatu. (2) Mtu aliyezaliwa nje ya Kenya ni raia ikiwa, wakati wa kuzaliwa kwake,

ima baba au mama wa mtu huyo alikuwa -

(a) raia aliyezaliwa Kenya; au

(b) raia kwa kusajilishwa au kuandikishwa.

(3) Ikiwa mzazi mmojawapo alifariki kabla mtu huyo hajazaliwa, kwa madhumuni yote ya Sura hii, uraia wa mzazi huyo wakati wa kifo unatumika kama kwamba mzazi huyo aliendelea kuishi hadi mtu huyo alipozaliwa.

Page 21: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

21

Uraia na ndoa 18. (1) Mtu aliyefunga ndoa na raia wa Kenya kwa kipindi kisichopungua miaka

saba anaweza kutuma maombi kusajiliwa kama raia wa Kenya.

(2) Uraia haupotei kwa njia ya ndoa au talaka.

Uraia wa kuandikishwa 19. Mtu ambae ni mkaazi halali wa Kenya kwa kipindi kisichopungua miaka saba

mfululizo, na ambaye atatimiza masharti yaliyowekwa na Sheria iliyotungwa, anaweza kuomba kuwa raia wa Kenya kwa kuandikishwa.

Watoto wa kulelewa na watoto wanaopatikana Kenya 20. (1) Mtoto anayepatikana Kenya ambaye anaonekana yuko chini ya umri wa

miaka minane, ambaye utaifa wake na wazazi wake hawajulikani, atachukuliwa kuwa raia wa Kenya wa kuzaliwa.

(2) Mtoto ambaye si raia na ambaye analelewa na raia wa Kenya anaweza kutuma maombi ya kusajiliwa kuwa raia.

Uraia maradufu 21. (1) Mtu ambaye ni raia wa kuzaliwa -

(a) hapotezi uraia wake kwa ajili ya kupata uraia wa nchi nyingine ana haki ya kurejeshewa uraia akiomba.

(b) anaweza kuomba kurejeshwa uraia, ikiwa mtu huyo alipoteza uraia kwa ajili ya kupata uraia wa nchi nyingine.

Kunyang’anywa uraia 22. Mtu ambaye ni raia kwa kusajilishwa au kwa kuandikishwa, au ambaye uraia

wake umepatikana kwa kupitia kusajiliwa au kuandikishwa kwa mtu mwengine, anaweza kunyang,anywa uraia, ikiwa uraia huo ulipatikana kwa njia ya udanganyifu, wasilisho la uongo au kuficha taarifa muhimu.

Makaazi 23. (1) Watu wafuatao wanaweza kuingia na kuishi Kenya mradi tu wametimiza

masharti yaliyowekwa na Sheria ya Bunge yanayohusu kuingia nchini na kuishi -

a. aliyekuwa raia hapo awali;

b. mke ambaye si Mkenya au mjane au mume ambaye si Mkenya ama mjane wa raia wa Kenya; na

c. mtoto wa raia wa Kenya.

(2) Bunge litatunga sheria itakayosimamia uingiaji na ukaazi nchini Kenya kwa makundi mengine ya watu na kueleza haki ya wakaazi wa kudumu.

Page 22: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

22

Wajibu wa raia 24. (1) Raia wote wana wajibu wa -

(a) kupata ufahamu wa masharti ya Katiba hii na kudumisha maadili na malengo yake;

(b) kuheshimu, kutetea na kuilinda Katiba hii na sheria;

(c) kuendeleza demokrasia, utawala bora, na utawala wa kisheria;

(d) kutekeleza haki yao ya kupiga kura na kushiriki katika namna nyingine za shughuli za kisiasa;

(e) kujitahidi kukuza umoja wa kitaifa na kuishi kwa amani na wengine;

(f) kushirikiana na vyombo vya kutekeleza sheria ili kudumisha sheria na utengamano;

(g) kulipa kodi zote kwa mujibu wa sheria;

(h) kujiepusha na vitendo vya rushwa; na

(i) kushiriki katika kazi kwa manufaa ya jumla na kuchangia katika maendeleo ya taifa;

(j) kukuza uwezo wao kadri wanavyoweza kwa kupata maarifa, kuendelea na elimu na ukuzaji wa taaluma;

(k) kuchangia maendeleo ya jamii wanakoishi;

(l) kuendeleza maisha na maslahi ya kifamilia na kuwajibika katika muktadha wa familia;

(m) kulinda na kutunza mali ya umma dhidi ya uharibifu na ubadhirifu;

(n) kulinda mazingira na kuhifadhi maliasili;

(o) kuelewa na kukuza nafasi ya Jamhuri katika jamii ya kimataifa na kujitahidi katika kupatikana Umoja wa Afrika.

(2) Wajibu ulioagizwa na Ibara ndogo (1) utatekelezwa kwa usawa kama inavyofaa kwa watu wasiokuwa raia.

Sheria kuhusu uraia 25. Bunge litatunga sheria -

(a) kuweka taratibu ambazo mtu anaweza kuwa raia;

(b) kuruhusu mtu kukana uraia wake kwa hiyari;

(c) kuweka taratibu za mtu kunyang’anywa uraia wake chini ya Ibara 22; na

(d) kwa jumla kutekeleza masharti ya Sura hii.

Page 23: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

23

Page 24: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

24

SURA YA TANO

UTAMADUNI

Kanuni kuhusu utamaduni 26. (1) Katiba hii inatambua utamaduni kama msingi wa taifa, ustaarabu,wa

pamoja wa watu wa Kenya na jamii zake, pia ni chimbuko ambalo nyanja zote binafsi na maisha ya jumla yanaegemea na hasa -

(a) unathibitisha maadili na misingi ya Katiba isiyoandikwa ya jamii za Wakenya, utamaduni wao wa kale, juhudi zao na matumaini yao ya baadae;

(b) inatambua na kulinda malengo muhimu na maadili ya utamaduni pamoja na kuthamini kwamba utamaduni ndio msingi wa kulea fahari ya taifa na utambulisho;

(c) inaonyesha na kuthibitisha utukufu pekee na ubarizi wa watu wa Kenya na jamii katika kuchangia na kushirikiana katika utamaduni wa dunia.

(2) Serikali -

(a) itakuza kuelewana, kustahimiliana, na kuthamini uanuwai wa kijamii;

(b) itaheshimu, itahifadhi, italinda na itaendeleza turathi za Kenya, na hasa utamaduni wake, maeneo na mambo ya kale, kihistoria, kidini, kitakatifu, kimachimbo na mwahala mwengine mwenye umuhimu.

(c) itakuza:

(i) utafiti na sera ya elimu ambayo inakuza utamaduni na maadili ya kitamaduni, itakayowezesha watu kujenga hulka madhubuti, miiko na misingi ya imani;

(ii) aina zote za tamaduni za taifa kupitia fasihi, sanaa, sherehe za kitamaduni, sayansi, mawasiliano, habari, vyombo vya habari, machapisho na maktaba na turathi nyingine za kitamaduni;

(d) itaunga mkono na kukuza utekelezaji unaofaa wa tiba za kisasa na za jadi;

(e) itatambua nafasi ya sayansi na teknolojia asilia katika maendeleo ya taifa;

(f) itaunga mkono, itakuza na kulinda teknolojia asilia, na haki miliki ya kitaaluma za watu wa Kenya.

Page 25: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

25

(g) Kupitia sheria, itahahakikisha kwamba jamii zinapata fidia au malipo kwa matumizi ya tamaduni zao na turathi za utamaduni;

(h) Itakuza, inapowezekana, matumizi ya mifumo ya kilimo cha kiasili, vyakula na vinywaji vya kiasili.

(i) Kupitia sheria itatambua na kulinda umilikaji wa mbengu za kiasili na mimea tofauti, sifa zake za kigenetiki au nyinginezo tofauti na matumizi yao katika jamii za Kenya.

Tume ya Taifa ya Utamaduni 27. (1) Inaundwa Tume ya Taifa ya Utamaduni.

(2) Tume hiyo itakuwa chombo kikuu cha Serikali katika kutimiza kanuni na malengo ya Sura hii, na hasa -

(a) itashauri kuhusu masuala ya sera na utekelezaji wake kuhusiana na utamaduni;

(b) kufanya, kuendeleza utafiti na kuandika kuhusu tamaduni za Kenya, pamoja na historia ya taifa na sheria za mila;

(c) itakuza na kulinda utamaduni na makumbusho ya kihistoria, maliasili zinazohusu utamaduni kwa manufaa ya jamii ambazo ni muhimu kwao turathi hizo, na kwa ajili ya taifa;

(d) kufanya kazi nyengine kama zinavyoweza kuelezwa na sheria na kwa ujumla kutekeleza malengo ya Sura hii.

(3) Bunge litatunga sheria kutekeleza masharti ya Ibara hii.

Siku ya Utamaduni 28. Tarehe 26 Desemba itakuwa ni sikukuu ya Utamaduni.

Page 26: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

26

SURA YA SITA

SHERIA YA HAKI ZA BINADAMU

Sehemu ya Kwanza - Kanuni za Jumla Kuhusu Sheria ya Haki za Binadamu

Haki za kimsingi na uhuru 29. (1) Sheria ya Haki za Binadamu ni nguzo muhimu ya serikali ya kidemokrasia

ya Kenya na ni msingi wa sera za kijamii, kiuchumi na kitamaduni;

(2) Madhumuni ya kutambua na kulinda haki za binadamu ni kuhifadhi utu wa watu binafsi na jamii na kuendeleza haki za kijamii pamoja na kutambua vipawa vya binadamu wote;

(3) Haki na huru zilizotolewa katika sura hii –

(a) ni asili kwa kila mtu na hazitolewi na serikali;

(b) haziondoi haki nyinginezo ambazo hazikutajwa moja kwa moja katika Sura hii; na

(c) zinategemea tu upeo uliotolewa katika Sura hii.

Matumizi ya Sheria ya Haki za Binadamu 30. (1) Sheria ya Haki za Binadamu inahusika katika ufafanuzi wa sheria zote na

inahusisha vyombo vyote vya serikali na watu wote;

(2) Kila mtu atanufaika na haki na uhuru kwenye Sheria ya Haki za Binadamu, kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo, kutegemea hali ya haki yenyewe.

(3) Wakati wa kutekeleza kanuni ya Sheria ya Haki za Binadamu, mahakama -

(a) itaendeleza sheria kwa namna ambavyo sheria hiyo haitaathiri haki au uhuru huo;

(b) itafuata ufafanuzi ambao unapendelea zaidi utekelezaji wa haki au uhuru; na

(c) inaweza kuweka masharti ya kisheria ili kuweka mipaka ya uhuru kwa namna ambayo haitoathiri Ibara ya 34.

(4) Katika kufafanua Sheria ya Haki za Binadamu, mahakama au mahakama maalum, au Tume au mamlaka yeyote -

(a) itaendeleza maadili yanayodhihirisha jamii iliyowazi na yenye demokrasia kwa misingi ya hadhi ya utu, usawa, haki na uhuru;

Page 27: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

27

(b) itaendeleza makusudio, lengo na madhumuni ya Sheria ya Haki.

(5) Katika kufafanua au kutumia haki maalum ama uhuru, iwapo serikali itadai kwamba haina rasilmali kutekeleza haki ama uhuru, chombo chochote cha serikali, mahakama yoyote, mahakama maalum au kikao itaongozwa na kanuni kwamba -

(a) ni wajibu wa Serikali kuonyesha kwamba hakuna rasilmali;

(b) katika kugawa rasilmali, serikali ina wajibu wa kutoa kipaumbele katika kuhakikisha kuwa haki kwa kiwango inafikiwa kwa mujibu wa hali iliyopo, ikiwa ni pamoja na udhaifu wa vikundi au watu wanaodai kuvunjiwa haki zao; na

(c) mahakama, mahakama maalum, tume au mamlaka nyingine haitoweza kutoingilia uamuzi wa vyombo vya serikali kuhusu mgao wa rasilmali zilizopo, kwa kisingizio tu kuwa mahakama, mahakama maalum, tume au mamlaka nyingine ingeweza kufikia maoni tofauti.

Utekelezaji wa haki na uhuru 31. (1) Ni wajibu wa msingi kwa kila chombo cha serikali kuzingatia, kuheshimu,

kulinda, kukuza na kutekeleza haki na uhuru uliomo katika Sura hii, ifaavyo, katika utekelezaji wa uwezo na majukumu yao.

(2) Dola itachukua hatua za kisheria, sera na hatua nyinginezo kutimiza ufanikishaji wa haki zilizohakikishiwa katika Ibara ya 60, 61, 62, 63, 64, 65 na 66.

(3) Ibara zilizotajwa katika ibara ndogo (2), hazitamaanisha kuilazimisha Serikali kutekeleza majukumu kupita kiasi cha uwezo wa Serikali.

(4) Dola itatambua nafasi ya jumuiya za wananchi raia katika kuendeleza na kulinda haki na uhuru katika Sheria ya Haki za Binadamu.

(5) Dola itatimiza majukumu yake yote ya kimataifa kuhusu haki za binadamu, na kwa ajili hiyo Serikali -

(a) itatoa taarifa kwa wakati kwa vyombo vya kimataifa vya haki za binadamu juu ya utekelezaji wa mikataba ya haki za binadamu na mikataba mengine;

(b) itachapisha taarifa za serikali zinazokusudiwa kuwasilishwa na serikali kwa taasisi za kimataifa na za kanda zinazohusika na utekelezaji wa mikataba ya haki za kibinadamu; na

(c) itasaidia mijadala ya umma na kushiriki kwa jumuiya za wananchi katika taarifa hiyo kabla ya kuimaliza na

Page 28: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

28

kuiwasilisha kwa mamlaka za kimataifa zinazosimamia utekelezaji wa mikataba ya haki za binadamu, kimataifa na ya kanda;

(6) Maoni na mapendekezo ya vyombo vya kimataifa yanayohusu majukumu ya kimataifa yatawasilishwa kwa wananchi, na serikali itatoa taarifa Bungeni kuhusu, kama na jinsi inavyodhamiria kutekeleza mapendekezo hayo.

Utekelezaji wa Sheria ya Haki za Binadamu 32. (1) Mtu aliyeorodheshwa katika Ibara ndogo (2) ana haki ya kuilalamikia

Tume ya Haki za Binadamu na Haki za Kiutawala na kufungua mashtaka katika mahakama akidai kwamba haki kwenye Sheria ya Haki za Binadamu imekataliwa, imevunjwa, imekiukwa au kutishiwa kuvunjwa.

(2) Kwa ajili ya Ibara ndogo (1), watu watakaolalamika mbele ya Tume au kwenda mahakamani ni -

(a) mtu anayejiwakilisha kwa maslahi yake mwenyewe;

(b) mtu anayewakilisha mwingine asiyeweza kujiwakilisha kwa jina lake;

(c) mtu anayewakilisha wanachama wa, au kwa maslahi ya, kikundi au tabaka au watu;

(d) mtu anayewakilisha kwa ajili ya maslahi ya umma; na

(e) jumuiya inayowakilisha maslahi ya wanachama wake.

(3) Kwa ajili ya Ibara ndogo (1), Jaji Mkuu ataweka kanuni za ya utaratibu zitakazo tosheleza vigezo vifuatavyo -

(a) kwamba haki za kufungua mashtaka zilizotolewa kwenye Ibara hii zimetimizwa;

(b) kwamba taratibu za kuwezesha kusikiliza kesi zimepunguzwa;

(c) kwamba mahakama, huku ikizingatia masharti ya haki ya adala asilia, haitazuilika bila ya sababu za msingi kwa kisingizio cha mahitaji ya kitaaluma;

(d) kwamba hakuna ada itakayotozwa ya kuanzisha mashtaka chini ya Ibara hii; na

(e) kwamba mashirika ama watu wenye taaluma maalum wanaweza, kwa idhini ya mahakama kusimama mbele ya mahakama kama rafiki wa mahakama.

Mamlaka ya mahakama kulinda na kutekeleza Sheria ya Haki za Binadamu 33. (1) Mahakama Kuu ina mamlaka ya kusikiliza maombi ya (fidia) kitulizo

kutokana na ukiukaji wa Sheria ya Haki za Binadamu.

Page 29: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

29

(2) Bunge litatunga Sheria ili kutoa mamlaka ya kusikiliza kesi zinazostahiki kwa mara ya kwanza ili kusikiliza maombi juu ya vitulizo kwa sababu ya ukiukaji wa Sheria ya Haki za Binadamu.

(3) Katika suala lolote linalowasilishwa mahakamani kulingana na Ibara ya 32, mahakama inaweza kuidhinisha faraja inayofaa, ikiwa ni pamoja na -

(a) amri ya kukataza;

(b) tamko la kuthibitisha haki;

(c) tamko la ubatili wa Sheria yoyote inayokiuka Sheria ya Haki za Binadamu na haina uhalali kwa mujibu wa Ibara ya 34;

(d) amri ya fidia dhidi ya serikali au mtu yeyote anaehusika na ukiukaji haki; na

(e) amri kuhusiana na mapitio ya mahakama.

(4) Katika kesi dhidi ya mamlaka ya umma kwa kukiuka haki za binadamu, mahakama inaweza isitoze gharama dhidi ya mdai au mlalamikaji ila tu mahakama itakapoamua kwamba kesi hiyo ilikuwa haina uzito, inayoudhi au isiyo na msingi wowote.

Mipaka ya haki 34. (1) Haki au uhuru uliofafanuliwa katika Sheria ya Haki za Binadamu unaweza

tu kuwekewa mipaka -

(a) kutokana na mpaka au ufafanuzi uliowekwa moja kwa moja kwenye sharti lenye haki au uhuru huo, na kutokana na mpaka wa sheria inayotumika kwa jumla; na

(b) kwa kiwango ambacho mipaka hii ni ya kadiri na ya haki katika jamii yenye uwazi na ya kidemokrasia yenye kuheshimu utu wa binadamu, usawa na uhuru, yanapozingatiwa mambo yote yakiwemo pamoja na -

(i) aina ya haki;

(ii) umuhimu wa madhumuni ya mipaka;

(iii) hali na upeo wa mipaka;

(vi) umuhimu wa kuhakikisha kuwa kunufaika na haki na uhuru wa mtu binafsi hakuhatarishi haki na uhuru wa wengine.

(v) uhusiano baina ya mipaka na madhumuni yake; na ikiwa kuna njia nafuu zisizokuwa za kutimizia madhumuni hayo.

(vi) Ulinzi wa usalama wa kitaifa, usalama wa umma, nidhamu ya umma, uadilifu wa umma au afya ya umma.

Page 30: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

30

(2) Licha ya masharti ya Ibara ndogo (1), sharti katika sheria -

(a) ni batili inapohusu sheria iliyopitishwa au kurekebishwa

baada ya tarehe ya kuanza kutumika, isipokuwa kama sheria hiyo imeeleza kwamba, sheria hiyo imeeleza hasa madhumuni na nia ya kuwekea mipaka haki au uhuru huo pamoja na aina na upeo wa mipaka hiyo.

(b) haitafasiriwa kuiwekea mipaka haki au uhuru ulioelezwa katika sheria ya haki za binadamu isipokuwa maelezo hayo yawe wazi na hasa kuhusu haki au uhuru ambao utawekewa mipaka na aina na upeo wa mipaka hiyo.

(3) Licha ya masharti ya Ibara ndogo (1) katika sheria -

(a) haitotafsiri kuiwekea mipaka haki au uhuru ulioelezwa katika Sheria ya Haki za Binadamu isipokuwa maelezo ya wazi na maalum kuhusu mipaka ya haki au uhuru huo na namna na aina ya upeo wa mipaka ya sheria;

(c) haitoiwekea mipaka haki au uhuru ulioelezwa katika sheria ya Haki za Binadamu kwa ajili ya kuziondosha kutoka kiini cha haki za msingi au za lazima.

(3) Serikali ama mtu yeyote anaetaka kuthibitisha kwamba mpaka fulani unaruhusiwa, ana wajibu wa kuthibitisha mahakamani, katika mahakama maalumu ama kikao kingine kwamba matakwa ya Ibara hii yametimizwa kikamilifu.

(4) Masharti ya Sura hii kuhusu usawa yataelezwa kwa upeo mahsusi unaodhamiriwa tu kwa ajili ya utekelezaji wa Sheria ya Kiislamu kwa waumini wa dini ya Kiislamu kuhusiana na mambo ya binafsi, ndoa, talaka na urithi.

Sehemu ya Pili – Haki za Kimsingi na Uhuru

Haki ya kuishi 35. (1) Kila mtu ana haki ya kuishi isipokuwa kama itakavyoagizwa na Sheria ya

Bunge.

(2) Maisha ya mtu yanaanza wakati wa utungaji mimba.

(3) Utoaji mimba hautaruhusiwa ila tu kama utakavyoagizwa na Sheria ya Bunge.

Usawa 36. (1) Kila mtu yuko sawa mbele ya sheria na ana haki sawa ya kulindwa na

usawa wa kunufaika na sheria.

Page 31: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

31

(2) Usawa unajumlisha kunufaishwa kikamilifu na kwa usawa wa haki zote na uhuru wote.

Uhuru wa kutobaguliwa 37. (1) Serikali haitabagua moja kwa moja ama kwa njia isiyokuwa ya moja kwa

moja dhidi ya mtu ye yote kwa sababu yoyote, iwe ni jamii, jinsia, ujauzito, ndoa, kabila au hali ya kijamii, rangi, umri, ulemavu, dini, dhamira, imani, utamaduni, mavazi, lugha ama kuzaliwa.

(2) Mtu hatabagua moja kwa moja au kwa hali isiyo ya moja kwa moja dhidi ya mtu mwingine kwa sababu yoyote kufuatana na Ibara ndogo (1).

(3) Mtu hatalazimishwa kuonyesha au kueleza kabila au jamii yake.

(4) Licha ya Ibara ndogo (1), Serikali itachukua hatua za kisheria na nyinginezo zitakazojumuisha, ingawa hazitoishia tu kwenye mipango na sera za upendeleo maalum za kuwanufaisha watu binafsi ama makundi yaliyokosa fursa, iwe ni kwa matokeo ya ubaguzi katika siku zilizopita, lakini hatua zo zote zitazochukuliwa -

(a) zitatoa manufaa ya kutosha kulingana na mahitaji halisi ya kimsingi; na

(b) zitaruhusiwa kufuatana na Ibara ya 34.

(5) Bunge litapitia upya mipango na sera za vitendo vya upendeleo vilivyoelezwa katika Ibara Ndogo (4) baada ya kila miaka kumi.

Jinsia 38. (1) Wanawake na wanaume wana haki ya kutendewa sawa, pamoja na haki ya

kupata fursa sawa katika siasa, uchumi na shughuli za kijamii.

(2) Wanawake na wanaume wana haki ya kurithi, kufikia kuweza kupata na kusimamia rasilmali.

(3) Sheria, tamaduni, desturi ama mila zo zote zinazodhalilisha hadhi ya utu, ustawi na maslahi ama hali ya wanawake na wanaume zimepigwa marafuku.

(4) Licha ya Ibara ndogo (1) Serikali -

(a) italinda wanawake na haki zao, kwa kuzingatia hali zao maalum na jukumu lao la kuwa mama katika jamii; na

(b) itatoa nafasi zinazotosheleza na fursa ya kuendeleza maslahi ya wanawake ili kuwawezesha kufikia upeo wa vipawa vyao na maendeleo.

Wazee katika jamii 39. (1) Wazee katika jamii wana haki ya kuendelea kufaidi haki zote na uhuru

kama ilivyofafanuliwa katika Sheria ya Haki za Binadamu.

Page 32: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

32

(2) Serikali itachukua hatua za kisheria na kisera ili kuhakikisha

haki za wazee za - (a) kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii;

(b) kufuatilia maendeleo yao binafsi;

(c) kuwa huru kutokana na aina zote za ubaguzi na unyanyasaji;

(d) kuendelea kumiliki maisha yao, ikiwa ni pamoja na haki ya kujiamulia wenyewe kuhusiana na maswala yao ya kijamii, kiuchumi na kisiasa; na

(e) kupata huduma mwafaka na msaada wa familia na Serikali.

(3) Bunge litatunga sheria ya kuunda baraza kufafanua na kushauri kuhusu sera na mipango ya wazee katika jamii wanaohitaji malezi na ulinzi. jamii.

Vijana 40. (1) Vijana ni sehemu muhimu ya jamii na wana stahiki kufaidi haki na uhuru

kama zilivyoelezwa katika Sheria ya Haki za Binadamu, kwa kuzingatia mahitaji yao maalum.

(2) Serikali itachukua hatua za kisheria na nyingine, ikiwa ni pamoja na, lakini hazitoishia tu na, sera na mpango wa upendeleo maalum ili kuendeleza maslahi ya vijana.

(3) Hatua zinazorejewa katika Ibara ndogo (2) ni pamoja na zile zitakazohakikisha kuwa vijana -

(a) wanafikia elimu na mafunzo bora na yenye manufaa;

(b) wanashiriki katika utawala;

(c) wanafikia ajira zitakazowanufaisha;

(d) wanapata fursa za kutosha katika maisha ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kwingineko;

(e) wana uhuru wa kushirikiana na wengine ili kuendeleza maslahi yao halali;

(f) wanalindwa kutokana na utamaduni, mila, jadi, au mazoea yanayodhalilisha heshima au ubora wa maisha; na

(g) wanaishi maisha yasiyokuwa na ubaguzi, unyonyaji au unyanyasaji.

Watoto 41. (1) Watoto wana hadhi maalum katika jamii.

(2) Ni jukumu la wazazi wao, ukoo, jamii na serikali kuwalea, kuwalinda na kuwaelimisha watoto.

Page 33: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

33

(3) Watoto wote, iwe wamezaliwa ndani au nje ya ndoa, wako sawa mbele ya sheria na wana haki sawa chini ya Katiba hii.

(4) Maslahi ya mtoto ni muhimu zaidi katika kila jambo linalohusu mtoto.

(5) Mama na baba yake mtoto, wawe wamefunga ndoa au la, wana jukumu sawa la kulinda na kuyakidhi mahitaji ya mtoto.

(6) Kila mtoto ana haki -

(a) ya kupewa jina na uraia tangu kuzaliwa na kusajilishwa anapozaliwa;

(b) ya kupata malezi ya wazazi au malezi mbadala yanayofaa ikiwa mtoto ametenganishwa na wazazi wake;

(c) ya kupata elimu ya msingi, bila malipo na ya lazima;

(d) ya kulindwa kutokana na ubaguzi, desturi na mila za kitamaduni zenye kumdhuru, kumnyonya, kumpuuza au kunyanyasa;

(e) ya kulindwa kutokana na aina zote za dhuluma na kazi yo yote inayohatarisha maisha ama kuharibu maslahi ya mtoto;

(f) ya kupata lishe bora ya kutosha, makaazi, huduma za afya za kimsingi na huduma za kijamii;

(g) ya kuwa huru kutokana na adhabu ya viboko au aina nyingine za ukatili, nguvu na kutendewa matendo yasiyo ya kibinadamu shuleni na katika taasisi nyinginezo zinazoshughulikia huduma kwa watoto;

(h) kutoshiriki katika uhasama au kuajiriwa katika vita vya silaha na walindwe kutokana na migogoro ya vita vya silaha;

(i) kutokamatwa au kutiwa kizuizini isipokuwa kama kufanya hivyo ni hatua ya mwisho, na pale ambapo mtoto ametiwa nguvuni au kizuizini ashughulikiwe kwa namna ambayo haitodhalilisha heshima na utu wa mtoto na inayozingatia haki za mtoto, pamoja na, lakini haitoishia katika haki ya -

(i) kuwekwa kizuizini humo kwa muda mchache iwezekanavyo;

(ii) kutenganishwa na watu wazima waliopo kizuizini;

(iii) kupewa huduma za kisheria na Serikali; na

(iv) kushughulikiwa na kutunzwa katika hali inayojali ulemavu kama upo, jinsia na umri;

(j) kuwa na wakili aliyewekwa na Serikali kwa gharama ya Serikali katika mashtaka yanayomhusu mtoto, endapo dhuluma itaweza kutokea; na

Page 34: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

34

(k) kujua uamuzi unaomwathiri mtoto, kutoa maoni na maoni haya yazingatiwe, kwa kutilia maanani umri na kukomaa kwa mtoto pamoja na hali ya maamuzi.

(7) Watoto wenye mahitaji maalum, wanastahiki uangalizi maalum wa serikali na jamii.

(8) Serikali ina wajibu wa kuchukua hatua za kutekeleza kisheria na kiutawala masharti ya Katiba hii na ya mikataba ya kimataifa na viwango kuhusiana na haki za mtoto.

Familia 42. (1) Familia ni msingi wa kimaumbile na ni kitengo muhimu katika jamii na

uti wa mgongo wa taratibu za kijamii.

(2) Kila mtu mzima ana haki-

(a) ya kuoa au kuolewa na mtu wa jinsia tofauti kulingana na maridhiano ya wanaohusika; na

(b) ya kuanzisha familia.

(3) Mtu hataoa au kuolewa na mtu wa jinsia yake.

(4) Wale wanaooana wanastahiki haki sawa katika ndoa, wakati wa kuoana, na katika kuvunja ndoa yao.

(5) Bunge litatunga sheria inayotambua -

(a) ndoa zilizotimizwa chini ya mila yoyote au taratibu za kidini, sheria za familia au binafsi;

(b) Sheria ya binafsi pamoja na za familia zinazofungamana na watu wenye kufuata dini fulani,

kwa kiwango ambacho ndoa hizo au utaratibu unaolingana na Katiba hii.

Watu wenye ulemavu 43. (1) Watu wenye ulemavu wana haki ya kufurahia haki zote na uhuru wote

uliotajwa katika Sheria ya Haki za Binadamu na kushiriki kikamilifu katika jamii kama wengine.

(2) Watu wenye ulemavu wana haki ya -

(a) kupewa heshima na kuheshimiwa utu wao pamoja na kutendewa, kuitwa na kutajwa, kirasmi au katika muktadha wa binafsi, kwa njia au maneno yasiyokuwa ya dharau au kudhalilisha;

(b) kupata elimu na kuifikia katika taasisi za elimu na nyenzo za kuwasaidia watu wenye ulemavu ambazo vimechanganywa

Page 35: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

35

pamoja katika jamii kwa jumla kulingana na mahitaji ya watu wenye ulemavu;

(c) kufikia sehemu zote, kwenye usafiri wa umma, kwenye vyombo vya habari na mawasiliano;

(d) matumizi ya lugha ishara, Breli pamoja na njia nyingine zifaazo za mawasiliano;

(e) kushiriki katika kutoa maamuzi katika ngazi zote;

(f) kurithi, kupata haki na kumiliki mali;

(g) kufikia vifaa na nyenzo za kuwawezesha watu wenye ulemavu kuondokana na vipingamizi vinavyotokana na ulemavu wao;

(h) kutendewa na kupata nafasi katika shughuli zote za maisha ambazo ni adilifu na sawa na zinazolingana na watu wengine katika jamii.

(3) Dola itachukua hatua za kisheria na nyinginezo kuhakikisha watu wenye ulemavu wananufaika kutokana na haki zilizoko katika Ibara ndogo (2).

(4) Sheria na hatua za kisera zilizohakikishwa katika Ibara ndogo (3) zitaweka masharti maalum kwa wanawake wenye ulemavu.

Heshima za binadamu 44. (1) Kila mtu ana heshima na haki ya maumbile ya kuthaminiwa na

kuheshimiwa na kulindwa utu wake.

(2) Haki ya maumbile ya kuthaminiwa utu wa kila mtu -

(a) ni pamoja na haki ya mazishi ya maiti ya marehemu kwa heshima; na

(b) inaendelea kwa mabaki ya marehemu baada ya mazishi.

Uhuru na usalama wa mtu 45. Kila mtu ana haki ya uhuru na usalama wake ambao ni pamoja na haki ya -

(a) kutonyimwa uhuru bila ya sababu za msingi au za kisheria;

(b) kutowekwa kizuizini bila kushtakiwa, isipokuwa wakati wa hali ya hatari ambapo kuwekwa kizuizini huidhinishwa kwa masharti ya Ibara ya 74;

(c) kutohusishwa na aina zote za fujo za umma au za watu binafsi;

(d) kutoteswa kwa njia yoyote, iwe kimwili au akili; na

(e) kutopewa adhabu ya kupigwa viboko au kutendewa au kuadhibiwa kikatili, kinyume na kibinadamu au kwa kudhalilishwa.

Page 36: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

36

Utumwa, kazi za utumwa na kulazimishwa 46. (1) Hakuna mtu atakayewekwa utumwani au kufanyishwa kazi ya utumwa.

(2) Hakuna mtu atakaefanyishwa kazi ya kulazimishwa.

Faragha 47. Kila mtu ana haki ya faragha ambayo inajumuisha haki ya -

(a) kutopekuliwa mwili au makazi;

(b) kutochunguzwa mali;

(c) kutokamatwa milki;

(d) kutotoa habari zinazohusu familia yake au mambo yake ya faragha kuulizwa au kutangazwa bila sababu au ulazima au; na

(e) kutoingiliwa mawasiliano yake ya faragha.

Uhuru wa dini, imani na maoni 48. (1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kuamini, dini, mawazo, itikadi, imani na

maoni.

(2) Kila mtu ana haki, ima kibinafsi au pamoja na wengine katika jamii, katika hadhara au faragha kudhihirisha dini, imani kwa kuabudu, kutii, pamoja na kutekeleza ibada kwa siku ya sala.

(3) Kila jumuia ya kidini ina haki ya kutumia gharama zao kuanzisha na kuendesha mahali pa elimu na kutoa mafunzo ya kidini kwa waumini wake katika kutoa elimu hiyo.

(4) Ufuasi wa kidini na mafunzo ya kidini yanaweza kutolewa na taasisi za serikali au taasisi zinazosaidiwa na serikali ikiwa –

(a) zitaendeshwa kwa msingi wa usawa; na

(b) mahudhurio ya ufuazi au mafunzo ya dini ni kwa hiari.

(5) Mtu asikatazwe kujiunga na taasisi yoyote au ajira au huduma yozote au kufaidika na haki yoyote kwa sababu ya imani ya dini yake.

(6) Mtu asilazimishwe –

(a) kula kiapo kinachopingana na dini ya mtu huyo au imani yake au kinachoeleza imani ambayo mtu huyo haifuati;

(b) kula kiapo kwa namna ambayo ni kinyume cha dini au imani ya mtu huyo au kinachoeleza imani ambayo mtu huyo haifuati;

(c) kupokea mafunzo ya kidini au kushiriki au kuhudhuria sherehe ya kidini au kufuata siku ya mapumziko au ufuasi unaohusiana na dini ambayo si ya mtu huyo;

(d) kufanya, kufuata au kufanyishwa kitendo cha kidini au ada;

Page 37: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

37

(e) kutaja itikadi ya kidini ya mtu huyo; au

(f) kufanya kitendo kingine chochote ambacho ni kinyume na dini au itikadi ya mtu huyo.

Uhuru wa kutoa maoni 49. (1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kutoa maoni, ambao ni pamoja na -

(a) uhuru wa kupokea na kutoa habari au maoni;

(b) uhuru wa ubunifu wa kisanaa, pamoja na mavazi; na

(c) uhuru wa kielimu na uhuru wa utafiti wa kisayansi.

(2) Haki inayotajwa katika Ibara ndogo (1) haihusishi -

(a) propaganda ya kivita;

(b) uchochezi wa ghasia; au

(c) kuchochea chuki ambayo -

(i) inahusu kusingizia wengine ili kusababisha madhara; au

(ii) yenye kuhusiana na ubaguzi unaokatazwa chini ya Ibara ya 37.

Uhuru wa vyombo vya habari 50. (1) Uhuru na uwezo wa kutoingiliwa kwa vyombo vya utangazaji vya

elektroniki, maandishi na vyombo vya habari vya uchapishaji vya aina zote unahakikishwa.

(2) Serikali haiwezi -

(a) kuzuia na kudhibiti, au kuingilia, mtangazaji, mtayarishaji, mtoaji au msambazaji wa gazeti lolote au katika uenezaji wa habari kupitia chombo chochote; au

(b) kumnyanyasa au kumwadhibu mtu yeyote kama huyo kwa, fikra au maoni yoyote au yaliyomo katika matangazo au uenezaji kama huo.

(3) Vyombo vya utangazaji vya elektroniki na vingine vya habari vina uhuru wa kuanzishwa kufuatana na utaratibu wa kupewa leseni ambao -

(a) upo ili kuhakikisha kuzingatia kanuni muhimu za masafa ya angani na ishara nyingine za mawasiliano; na

(b) ni huru na haudhibitiwi na serikali, maslahi ya kisiasa au kibiashara.

(4) Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali vitakuwa huru na bila upendeleo na vitatoa nafasi na uwezo kwa ajili ya kuwakilisha maoni na mawazo yanayotofautiana.

Page 38: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

38

(5) Bunge litatunga sheria ambayo -

(a) inatoa masharti yanayofaa ya kugawa muda wa kuwa hewani katika vyombo vya utangazaji vya serikali au vingine vilivyoteuliwa kwa ajili ya vyama vya kisiasa kwa jumla au wakati wa kampeni za uchaguzi;

(b) inasimamia uhuru wa kutangaza kuhakikisha kampeni ya huru za uchaguzi;

(c) inaruhusu uundaji wa chombo huru kisichothibitiwa kiserikali wala kisiasa, na kinachowakilisha maslahi ya sehemu zote za jamii na kitakachoweka viwango vya vyombo vya habari na kunadhimu na kufuatilia utekelezaji wa viwango hivyo.

(6) Utekelezaji wa haki zilizoainishwa katika Ibara hii unaambatana na wajibu na majukumu maalum, na utakuwa chini ya -

(a) mipaka au vizuizi vilivyoainishwa na katiba hii;

(b) heshima ya haki na hadhi ya wengine, na

(c) udumishaji wa uadilifu, mamlaka na uhuru wa mahakama, taratibu za kisheria na usimamizi wa haki.

Kupata habari 51. (1) Kila raia ana haki ya kupata -

(a) habari zilizoko mikononi mwa Serikali; na

(b) habari zozote alizo nazo mtu mwingine ambazo zinahijitaka katika kutekeleza au kulinda haki au uhuru wowote.

(2) Kila mtu ana uhuru wa kudai masahihisho au kuondolewa mbali taarifa za uongo au za kupotosha zinazomwathiri mtu.

(3) Dola itachapisha na kusambaza habari zozote muhimu zinazohusu taifa.

(4) Bunge litatunga sheria kuhakikisha kuwa watu wanaweza kupata habari.

Uhuru wa kushirikiana 52. (1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kushirikiana na wengine.

(2) Haki hizo zinajumuisha uundaji, uendeshaji na kuendelea kuwapo kwa mashirika.

(3) Mtu hatalazimishwa kujiunga na jumuiya ya aina yoyote.

(4) Serikali itachukua hatua za kisheria na kisera kuendeleza na kuhimiza jumuiya zishiriki katika kutoa maamuzi na usimamizi wa masuala ya umma katika ngazi mbili za serikali.

(5) Sheria yoyote inayohitaji jumuiya za wananchi kujisajili, au kudhibitiwa, itaeleza kwamba -

Page 39: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

39

(a) usajili utahitajika tu ikiwa pana sababu nzuri za kufanya hivyo;

(b) usajili utakuwa mikononi mwa vyombo huru visivyodhibitiwa na Serikali au uongozi wa kisiasa;

(c) ada yoyote inayotozwa haitakuwa zaidi ya inayohitajika kulipia gharama za lazima za utataribu wa usajili;

(d) endapo kusajiliwa unahitajika chini ya aya kutakuwa na haki ya usajili, ila tu kama pana sababu muhimu ya kuzuia;

(e) viwango vyovyote vya maadili vinavyolenga jumuiya vitawekwa kwa kuzishirikisha jumuiya hizo;

(f) taratibu za kufuta usajili zihakikishe kuwepo kwa fursa ya kujitetea na kukata rufani katika mahakama maalum iliyo huru.

Mikusanyiko, maandamano, kuchochea migomo na malalamiko 53. Kila mtu ana haki ya kukutana, kuandamana, kuchochea mgomo kwa amani bila

silaha na kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka ya umma bila ya kuomba ruhusa.

Haki za kisiasa 54. (1) Kila raia yuko huru kufanya maamuzi ya kisiasa, ambayo ni pamoja na

haki ya –

(a) kuunda, au kushiriki katika kuunda chama cha kisiasa;

(b) kushiriki katika harakati za, au kusajili wanachama wa chama cha kisiasa; na

(c) kufanya kampeni ya chama cha kisiasa au kwa ajili ya kisiasa.

(2) Kila raia ana haki ya uchaguzi huru, wa haki na wa mara kwa mara kwa-

(a) uchaguzi wowote kwa chombo cha umma nafasi zake zinazochaguliwa au afisi yoyote iliyoundwa chini ya Katiba hii; na

(b) wadhifa wa chama chochote ambamo raia huyo ni mwanachama.

(3) Kila raia ambaye ni mtu mzima ana haki kulingana na sheria inayohusika –

(a) kusajiliwa kama mpiga kura na kupiga kura kwa siri katika uchaguzi unaotajwa kwenye Ibara ndogo (2); na

(b) kugombea nafasi katika afisi ya umma, au afisi katika chama cha kisiasa ambacho yeye ni mwanachama, na akichaguliwa, atashika nafasi.

Uhuru wa kwenda utakako na makaazi 55. (1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kwenda atakako.

(2) Kila mtu ana haki ya kuondoka Kenya.

Page 40: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

40

(3) Kila raia ana haki kuingia, kubaki na kuishi kokote katika Kenya.

Wakimbizi na hifadhi 56. (1) Mtu aliyekimbilia nchini Kenya hawezi kurudishwa au kupelekwa katika

nchi nyingine endapo mtu huyo ana sababu za kweli za kuogopa kuteswa katika nchi hiyo au kutendewa vyenginevyo hata kumfanya astahiki kuchukuliwa kama mkimbizi.

(2) Bunge litatunga sheria ya kulingana na sheria za kimataifa na kawaida zinazohusiana na watu wanaotafuta ukimbizi au hifadhi nchini Kenya.

Uhuru wa biashara, kazi na taaluma 57. (1) Kila raia ana haki ya kuchagua biashara yake, kazi au taaluma.

(2) Taratibu za biashara, kazi au taaluma zinaweza zikasimamiwa na

sheria.

Hifadhi ya haki ya mali 58. (1) Kwa mujibu wa Ibara ya 83 na 84, kila mtu ana haki ya kupata mali na

kuimiliki ama kibinafsi au kwa ushirika na wengine mahali popote nchini Kenya.

(2) Bunge halitatunga sheria inayoiruhusu serikali au mtu binafsi -

(a) kumnyang’anya mtu

(i) mali yoyote kiholela;

(ii) kiholela kumnyang’anya mtu haki kwenye mali hiyo au maslahi yake; au

(b) kuweka mpaka au kwa njia yoyote kuzuia mtu kunufaika na haki yoyote chini ya Ibara hii kwa msingi wowote uliowekwa na Ibara ya 36(1).

(3) Serikali haitamnyang’anya mtu mali ya aina yoyote, maslahi ama haki, katika mali isipokuwa uchukuwaji ya aina hiyo -

(a) uwe inatokana na kupata ardhi au kuwa na maslahi katika ardhi ama kubadilishana maslahi katika ardhi au hati ya umiliki ardhi kuambatana na Sura ya Saba; au

(b) iwe inachukuliwa kwa madhumuni ya umma au maslahi ya umma na inatekelezwa kwa mujibu wa Katiba hii au Sheria iliyotungwa na Bunge ambayo -

(i) inahitaji kutolewa kwa malipo ya mara moja na kamilifu ya fidia ya haki kwa mtu huyo, kabla ya mali hiyo kuchukuliwa; na

(ii) inaruhusu mtu yeyote aliye na maslahi au haki ya kumiliki mali hiyo, haki ya kwenda mahakamani.

Page 41: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

41

(4) Maagizo yanaweza kuwekwa kuwalipia fidia watakaotwaliwa ardhi walioikalia kwa nia njema hata kama hawana hati miliki ya ardhi hiyo.

(5) Haki inayotambuliwa na kulindwa na Ibara hii haihusishi mali yoyote ambayo imepatikana kupitia njia isiyo ya halali.

Mahusiano ya kazi 59. (1) Kila mtu ana haki ya mahusiano mazuri ya kazi.

(2) Kila mfanyakazi ana haki ya -

(a) malipo ya haki;

(b) masharti yenye kukubalika ya kufanya kazi;

(c) kuunda, kujiunga na, au kushiriki katika shughuli na mipango ya chama cha wafanyikazi; na

(d) kugoma.

(3) Kila mwajiri ana haki ya -

(a) kuunda na kujiunga na chama cha waajiri; na

(b) kushiriki katika shughuli na mipango ya chama cha waajiri.

(4) Kila chama cha wafanyakazi na chama cha waajiri kina haki ya -

(a) kuamua usimamiaji wake, mipango na shughuli zake;

(b) kupanga, kuunda na kujiunga na shirikisho.

(5) Kila chama cha wafanyakazi, chama cha waajiri na mwajiri ana haki ya kufanya mapatano ya jumla.

Ruzuku ya jamii 60. (1) Kila mtu ana haki ya ruzuku ya jamii.

(2) Serikali itatoa malipo ya hifadhi ya jamii kwa watu ambao hawawezi kujikimu pamoja na wale wanaowategemea.

Afya 61. (1) Kila mtu ana haki ya afya njema, inayojumuisha haki ya huduma

za afya, na pia kupata huduma ya afya ya uzazi.

(2) Hakuna mtu atakayenyimwa matibabu ya dharura.

Elimu

62. (1) Kila mtu ana haki ya kupata elimu.

(2) Dola itaandaa mpango wa kutekeleza haki ya kila mtoto kupata elimu ya lazima ya malezi na ya msingi, bila malipo na katika kufanya hivyo itazingatia mahitaji ya watoto wenye mahitaji maalum.

Page 42: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

42

(3) Dola, itachukua hatua zitakazofanya elimu ya sekondari na ya baada ya sekondari, hatua kwa hatua, kupatikana na kufikiwa.

(4) Kila mtu ana haki ya kuanzisha na kuendeleza, kwa gharama yake mwenyewe, taasisi za elimu zenye kujitegemea kufuatana na matakwa yaliyowekwa na Katiba hii na kwa kufikia viwango vilivyowekwa na sheria.

Makaazi 63. Kila mtu ana haki ya kumwezesha kupata kuwa na makaazi ya kufaa na

anayomudu kuyalipia .

Chakula 64. Kila mtu ana haki ya kutokumbwa na njaa na kuweza kupata chakula cha kutosha

chenye ubora unaokubalika.

Maji 65. Kila mtu ana haki ya kupata maji ya kutosha yenye ubora unaofaa.

Usafi 66. Kila mtu ana haki ya usafi wa kiwango kinachokubalika.

Mazingira 67. Kila mtu ana haki ya -

(a) mazingira yaliyo salama kwa maisha na afya;

(b) kuwa na mazingira yaliyo hifadhiwa, kwa manufaa ya vizazi vilivyopo na vijavyo, kupitia hatua za sheria na hatua nyingine ambazo –

(i) zinazozuia uchafuzi na uharibifu wa ikolojia;

(ii) zinazoimarisha uhifadhi; na zinazohakikisha maendeleo endelevu ya kiikolojia na matumizi ya maliasili huku maendeleo ya kiuchumi na kijamii yakiimarishwa; na

(a) ya kupata habari bila malipo kuhusu hali ya mazingira.

(b) kufidia hasara inayotokana na kukiukwa haki zinazo tambuliwa na Ibara hii.

Lugha na utamaduni 68. (1) Kila mtu ana haki ya kutumia lugha na kushiriki katika utamaduni

anaoupenda.

(2) Mtu anayetokana na jamii yenye utamaduni au lugha fulani, hawezi kunyimwa haki, pamoja na watu wengine wa jamii hiyo -

(a) kufurahia utamaduni wake na kutumia lugha yake; au

Page 43: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

43

(b) kuunda, kujiunga au kuendeleza vyama vya kitamaduni na lugha pamoja na vyombo vya jumuiya nyengine za wananchi.

(3) Hakuna mtu atakayemlazimisha mwingine kufanya au kutekeleza desturi au tambiko zozote za kitamaduni.

Haki za wateja 69. (1) Wateja wana haki ya -

(a) kupata bidhaa na huduma zinazofaa;

(b) kupata taarifa muhimu ili waweze kunufaika kikamilifu kutokana na bidhaa na huduma;

(c) kulindwa afya zao, usalama na maslahi yao ya kiuchumi; na

(d) kulipwa fidia kwa madhara yanayotokana na kasoro zinazotokana na bidhaa au huduma.

(2) Ibara hii itatumika kwa bidhaa na huduma zinazotolewa na vyombo vya umma au watu binafsi na makundi.

(3) Bunge litatunga sheria ya kuwalinda wateja na kusimamia matangazo ya biashara yaliyokweli, ya haki na wa heshima.

Utawala wa haki 70. (1) Kila mtu ana haki ya kitendo cha utawala kinachofanywa kisheria bila ya

kuchelewa, kwa ufanisi, uadilifu, kilicho halali na chenye utaratibu wa haki.

(2) Kila mtu ambaye haki zake zimeathiriwa na kitendo cha kiutawala ana haki ya kupewa sababu za kitendo hicho kimaandishi.

(3) Bunge litatunga sheria kutekeleza haki katika Ibara ndogo (1) na sheria hiyo itatoa uwezo wa marejeo ya matendo ya utawala kwa mahakama, au pale inapofaa, kwa tume huru na isiyopendelea.

Kupatikana kwa huduma za mahakama 71. (1) Kila mtu ana haki ya kutaka mzozo wowote unaoweza kuamuliwa kwa

kutumia sheria kuamuliwa kupitia kusikizwa katika mahakama iliyowazi au, inapofaa, mahakama maalum huru, tume au mamlaka nyingine.

(2) Ada yoyote yanayotakikana kulipwa na mtu chini ya Ibara ndogo (1) itakuwa ya nafuu na haitatumika kama pingamizi ya kupata haki.

Haki za watu waliotiwa nguvuni 72. (1) Kila mtu anayetiwa nguvuni ana haki ya -

(a) kufahamishwa mara moja kwa lugha na kwa namna anayoifahamu –

(i) sababu ya kutiwa nguvuni

Page 44: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

44

(ii) haki ya kubakia kimya; na

(iii) athari za kutobakia kimya;

(b) kubakia kimya

(c) kuwasiliana na wakili wake na watu wengine ambao msaada wao unahitajika;

(d) kutolazimishwa kukiri, au kukubali lolote linaloweza kutumiwa kama ushahidi dhidi yake na ikiwa mtu huyo kwa hiyari yake anachagua mwenyewe kukiri, afanye hivyo mahakamani au mbele ya hakimu;

(e) kuwekwa mahala tofauti na wafungwa wanaotumikia kifungo;

(f) kufikishwa mbele ya mahakama haraka iwezekanavyo, lakini isiwe baada ya saa arobaini na nane tangu alipokamatwa; au si baada ya siku ya kwanza ya mahakama baada ya saa arobaini na nane kama saa arobaini na nane yatatimia baada ya saa ya mahakama au siku ambayo ni ya mahakama kwa kawaida.

(g) baada ya kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza baada ya kukamatwa, kufanyiwa mashtaka au kufahamishwa, sababu ya kuendelea kuwekwa kizuizini, au kuachiliwa; na

(h) kuachwa huru kwa kuweka rehani au dhamana kabla ya kufanyiwa mashtaka, isipokuwa kuwe na sababu inayolazimisha iwe vinginevyo.

(2) Hakuna mtu yeyote atakayekuwa rumande kwa kosa ikiwa adhabu ya kosa hilo ni faini pekee au kifungo kisichozidi miezi sita.

Kufanyiwa kesi ya haki 73. (1) Kila mtuhumiwa ana haki ya kufanyiwa mashtaka ya haki

yanayojumuisha -

(a) kuchukuliwa kutokuwa na hatia hadi ithibitishwe kinyume chake;

(b) kufahamishwa shtaka na maelezo kamili ili kujibu;

(c) kuwa na muda na nyenzo ya kutosha kujitayarisha utetezi;

(d) kufanyiwa mashtaka ya hadhara mbele ya mahakama iliyoundwa na Katiba hii;

(e) mashtaka kuanzishwa na kukamilishwa bila ya kucheleweshwa kusiko sababu ya maana;

(f) kuweko wakati anaposhtakiwa;

(g) kuchagua, na kuwakilishwa na wakili, na kufahamishwa, ipasavyo kuhusu haki hii;

Page 45: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

45

(h) kuwa na wakili aliyetolewa kwa mshtakiwa na serikali na kwa gharama ya serikali, ikiwa yaonekana hatotendewa haki asipopewa wakili huyo, na kufahamishwa kikamilifu kuhusu haki hii;

(i) kubaki kimya na kutotoa ushahidi wakati mashtaka yanapoendeshwa;

(j) kutoa na kupinga ushahidi;

(k) kutolazimishwa kutoa ushahidi unaoweza kumtia hatiani;

(l) kupata usaidizi wa mkalimani bila kuhitajika kulipia ikiwa mshtakiwa haelewi lugha inayotumiwa kuendesha mashtaka;

(m) kutohukumiwa kwa kutenda au kutotenda kitendo ambacho wakati huo hakikuwa -

(i) kosa nchini Kenya; au

(ii) tendo la jinai chini ya kanuni za jumla za sheria zinazotambuliwa na mifumo maarufu ya sheria au sheria ya kimataifa.

(n) kutoshtakiwa kwa kosa la kutenda au kutotenda ambalo mtu huyo alikuwa amekwisha kuachiwa huru au kuhukumiwa;

(o) kupata adhabu ndogo zaidi kati ya adhabu zinazoweza kutolewa ikiwa adhabu iliyotolewa imebadilishwa kati ya kipindi ambacho kosa hilo, limefanywa na wakati wa kuhukumu; na

(p) kukata rufaa, au kufanyiwa mapitio na mahakama ya juu.

(2) Licha ya Ibara (1)(m)(i), mahakama inaweza kumuadhibu mtu kwa sababu ya kutotii mahakama hata kama kitendo au kutotenda kulikosababisha utovu huo, na adhabu iliyopendekezwa havijaelezwa katika sheria iliyoandikwa.

(3) Kwa minajili ya Ibara ndogo (1), taarifa hiyo kwa mtu itatolewa kwa lugha ambayo mtu huyo anaielewa.

(4) Ushahidi uliopatikana kwa njia inayokiuka Sheria ya Haki za Kibinadamu ikiwa kuchukuliwa kwake kutafanya mashtaka kutokuwa ya haki au utaathiri utawala wa haki.

(5) Mtu anayeshtakiwa kwa kosa ambalo si katika makosa ambayo mahakama inaweza kuendesha kesi kwa utaratibu wa muhtasari, atakuwa na haki, akiomba, ya kupata nakala ya mwenendo wa kesi.

(6) Mshtakiwa ana haki ya kupata nakala ya kumbukumbu ya mwendo wa kesi ndani ya kipindi cha siku kumi na nne baada ya kuhitimisha kesi kwa malipo ya ada inayokubalika kwa mujibu wa sheria.

Page 46: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

46

(7) Mtu aliyehukumiwa kwa kosa la jinai na ambaye rufaa yake imetupiliwa mbali na mahakama ya juu anayoruhusiwa kukata rufaa, au na kukata rufaa, katika muda unaoruhusiwa wa rufaa, anaweza kuiomba mahakama ya juu kufungua mashtaka mapya ikiwa ushahidi mwingine mpya na muhimu umepatikana.

(8) Bunge, kutumia sheria litatoa masharti kuongoza mahakama katika wadhifa wake kuhusiana na watu kupuuza maagizo ya mahakama.

Haki za watu walio kizuizini 74. (1) Mtu aliyewekwa kizuizini chini ya sheria, awe amehukumiwa au la,

ataendelea kuwa na haki zake za kimsingi chini ya Katiba, isipokuwa haki hiyo iwe haiambatani na madhumuni ya kuwa kizuizini.

(2) Bunge, kutumia sheria, litaagiza watu waliokizuizuini wahudumiwe kibinadamu, kwa kutilia maanani mikataba ya kimataifa kuhusu haki za binadamu.

Hali ya hatari 75. (1) Hali ya Hatari inaweza tu kutangazwa kulingana na Ibara ya 144(3) na

ikiwa tu -

(a) Jamhuri inatishiwa kivita, kuvamiwa, uasi wa jumla, vurugu, maafa ya kimaumbile au hali nyingine za dharura; na

(b) kutangaza huko ni muhimu katika kukabiliana na hali ya hatari iliyotangazwa.

(2) Tangazo la hali ya hatari, na sheria zozote zilizotungwa au hatua nyingine zilizochukuliwa ambazo ni matokeo ya tangazo hilo, litakuwa na nguvu iwapo -

(a) kwa matazamio; na

(b) isizidi siku kumi na nne kutoka siku ya tangazo hilo, isipokuwa kama Bunge litaamua kuongeza muda wa tangazo.

(3) Bunge linaweza kuongeza muda wa tangazo hilo la hali ya hatari-

(a) kwa azimio lililopitishwa -

(i) kufuatia mjadala Bungeni; na

(ii) kwa walio wengi kama ilivyoelezewa kwenye Ibara ndogo (4); na

(b) kwa muda usiozidi miezi miwili baada ya kila tangazo.

(4) Kuongezewa muda huko kwa hali ya hatari kwa mara ya kwanza kutapitishwa kwa kura za kuunga mkono za asilimia sitini na tano ya

Page 47: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

47

wabunge, na ongezeko la muda mwengine utakaofuata litapitishwa kwa kura za kuunga mkono zisizopungua asilimia sabini na tano ya wabunge.

(5) Mahakama Kuu inaweza kuamua uhalali wa -

(a) kutangazwa kwa hali ya hatari;

(b) kuongezwa muda kwa tangazo la hali ya hatari; au

(c) sheria yoyote ambayo imetungwa au hatua nyingine ilizochukuliwa, kufuatia tangazo la hali ya hatari.

(6) Sheria yoyote iliyotungwa kufuatia tangazo la hali ya hatari inaweza kukiuka Sheria ya Haki za Kibinadamu endapo tu -

(a) kukiuka huko kunahitajika na hali hiyo ya hatari; na

(b) sheria -

(i) inaambatana na majukumu ya Jamhuri chini ya sheria ya kimataifa inayohusiana na hali ya hatari;

(ii) ilingane na Ibara ndogo (7); na

(iii) ichapishwe katika Gazeti la Serikali haraka iwezekanavyo baada ya kutungwa

(7) Sheria iliyotungwa na Bunge inayoruhusu mamlaka ya tangazo la hali ya hatari, au sheria iliyotungwa au hatua zinazochukuliwa kufuatia tangazo lolote lile, haitaruhusu au haitoidhinisha ulipaji fidia kwa serikali, au mtu yeyote, dhidi ya kitendo chochote kinachokiuka sheria.

Sehemu ya Tatu – Tume za Haki za Binadamu

Tume ya Jinsia 76. (1) Kwa ajili ya Ibara 38, inaundwa Tume ya Jinsia.

(2) Majukumu ya Tume hiyo ni -

(a) kuendeleza usawa wa jinsia na haki kwa ujumla, na kuratibu na kufanikisha mielekeo ya jinsia katika maendeleo ya taifa;

(b) kutekeleza wajibu wowote kama utakavyoagizwa na Sheria, na kwa ujumla, kutekeleza malengo ya Ibara hii.

(3) Bunge, kutumia sheria, litaweka masharti mahususi ya kuwezesha utekelezaji wa mambo yanayohusiana na Ibara hii.

Tume ya Haki za Kibinadamu na Haki za Kiutawala 77. (1) Inaundwa Tume ya Haki za Kibinadamu na Haki za Kiutawala.

Page 48: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

48

(2) Kwa mujibu wa maagizo ya Katiba hii, majukumu ya Tume hii ni -

(c) kuendeleza ulindaji wa, na heshima kwa ajili ya haki za binadamu na kuimarisha utamaduni wa haki za binadamu;

(d) kufuatilia, kuchunguza na kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa haki za binadamu katika nyanja zote za maisha katika Jamhuri;

(e) kuchukua hatua kuhakikisha kuwa fidia inayotosha imetolewa ikiwa haki za binadamu zimekiukwa;

(f) kupokea malalamiko kuhusu matumizi mabaya ya cheo, kutendewa visivyofaa, kunyimwa haki, au mwenendo wa ufisadi, usiohalali, wenye kudhulumu au usio wa haki;

(g) kuhusu haki za binadamu, kuanzisha uchunguzi wake yenyewe au kutokana na malalamiko, uchunguzi na utafiti na kutoa mapendekezo ya kuimarisha utendaji kazi wa vyombo vya Serikali; na

(h) kutekeleza wajibu wowote kama utakavyoagizwa na sheria, na kwa ujumla, kutekeleza malengo ya Ibara hii.

3) Bunge, kutumia sheria, litaweka masharti mahususi ya kuwezesha utekelezaji wa mambo yanayohusiana na Ibara hii.

Page 49: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

49

SURA YA SABA

ARDHI NA MALI

Kanuni za sera ya ardhi 78. (1) Ardhi ni rasilmali kuu ya Kenya na pia msingi wa maisha ya wananchi na

itahifadhiwa, kutumiwa na kusimamiwa kwa njia ambayo ni adilifu, ya kufaa, ya kiuzalishaji na endelevu.

(2) Serikali itafafanua na kuifanyia marekebisho mara kwa mara sera ya kitaifa kuhusu ardhi ikihakikisha kanuni zifuatazo –

(a) usawa wa kupata ardhi na rasilmali nyingine zinazohusu ardhi;

(b) ulinzi wa haki za ardhi kwa wote wanaomiliki ardhi; wanaoitumikia na wanaoishi mahali hapo kwa nia njema;

(c) usimamizi wa rasilmali za ardhi kwa njia endelevu na ya uzalishaji;

(d) usimamizi wa ardhi ambao ni wazi na wa kufaa katika matumizi ya fedha;

(e) kuhifadhi kwa njia ya kufaa na kulinda mazingira ya maeneo ya kiikolojia ambayo ni nyeti; na

(f) kuondoa katika sheria, taratibu, mila na desturi zinazowabagua wanawake kuhusiana na ardhi na milki katika ardhi; na

(g) kuhimiza jamii kusuluhisha mizozo ya ardhi kwa njia inayokubalika kijamii, kwa mujibu wa Katiba hii.

Ukabidhi na uainishaji wa ardhi 79. (1) Ardhi yote nchini Kenya ni ya wananchi wa Kenya kwa pamoja, wakiwa

kama taifa, jamii au watu binafsi.

(2) Ardhi yote nchini Kenya imeanishwa kama ya umma, ya jamii au ya binafsi.

Ardhi ya umma 80. (1) Ardhi ya umma ni -

(a) ardhi ambayo wakati wa kuanza utekelezaji wa Katiba hii ni ardhi iliyo mikononi mwa serikali kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge;

(b) ardhi ambayo kwa uhalali imo katika mikono ya serikali, inayotumiwa, au inayokaliwa na wizara, idara au mamlaka ya wilayani isipokuwa ardhi ambayo inakaliwa kwa kukodishwa;

(c) madini yote kama ilivyofafanuliwa na sheria;

Page 50: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

50

(d) ardhi iliyoingia mikononi mwa Jamhuri kwa njia ya kuirudisha au kuisalimisha;

(e) ardhi ambayo umiliki wake wa kibinafsi au kijamii hauwezi kuthibitishwa kisheria;

(f) ardhi ambayo mrithi wake hawezi katika njia za kisheria kutambuliwa;

(g) misitu ya serikali isipokuwa iliyotajwa katika Ibara ya 81(2) (e), na maeneo ya asili ya maji, mbuga za wanyama, hifadhi ya wanyama na hasa maeneo yanayohifadhiwa;

(h) barabara zote na njia zilizo wazi na ambazo zilizoainishwa na Sheria iliyotungwa na Bunge;

(i) mito yote, maziwa na maeneo mengine ya maji kama ilivyoelezwa na Sheria iliyotungwa na Bunge;

(j) eneo la mipaka ya bahari ya eneo la nchi na pia eneo la ardhi iliyochini ya bahari;

(k) ardhi yote baina ya alama ya maji yaliyojaa na yaliyotoka;

(l) ardhi yote isiyoainishwa kama ya binafsi au ya jamii kwa mujibu wa Katibu hii; na

(m) ardhi yoyote iliyotangazwa kuwa ya umma na Sheria iliyotungwa na Bunge.

(2) Ardhi ya umma, iliyoainishwa chini ya Ibara ndogo ya (1)(a), (b), (d), (e) na (f) itakabidhiwa serikali ya wilaya kama amana kwa watu wa wilaya hiyo na itasimamiwa kwa niaba yao na Tume ya Taifa ya Ardhi.

(3) Ardhi ya umma iliyoainishwa chini ya Ibara ndogo ya (1)(c) na (g) hadi (m) itakabidhiwa na kuwa mikononi mwa serikali kama amana kwa watu wa Kenya na itasimamiwa kwa niaba yao na Tume ya Taifa ya Ardhi.

(4) Ardhi ya umma haitotolewa au kutumiwa isipokuwa kwa mujibu wa sheria itakayofafanua aina na masharti ya kutolewa au kutumiwa.

Ardhi ya jamii 81. (1) Ardhi ya jamii itakabidhiwa na itakuwa mikononi mwa jamii

zinazotambuliwa kwa mujibu wa ukabila, utamaduni na maslahi ya jamii.

(2) Kwa mujibu wa Ibara ndogo (1) “ardhi ya jamii” ni pamoja na -

(a) ardhi yote ambayo imeshikiwa amana na serikali zilizosambaziwa mamlaka;

(b) ardhi yote ambayo imeandikishwa kisheria kwa jina la wawakilishi wa kikundi kwa mujibu wa masharti ya sheria yoyote iliyotumika;

Page 51: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

51

(c) ardhi yote inayoshikwa, inayosimamiwa na kutumiwa na jamii maalum kama misitu ya kijamii, maeneo ya kulisha mifugo au mahali pa ibada (hekalu);

(d) ardhi yoyote iliyopewa jamii maalum kwa utaratibu wowote wa kisheria;

(e) ardhi ya jadi ambayo kidesturi inamilikiwa na jamii za wawindaji-wakusanyaji; na

(f) ardhi yoyote nyingine iliyotangazwa kama ya jamii na Sheria iliyotungwa na Bunge,

lakini haitajumuisha ardhi ya umma kama ilivyoelezwa katika Ibara ya 79.

(3) ardhi yoyote ya jamii ambayo haijasajiliwa itakuwa chini ya serikali za wilaya kwa niaba ya jamii.

(4) ardhi ya jamii haitatolewa au kutumiwa isipokuwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge ambayo itaeleza aina na mipaka ya haki ya watu wa kila jamii mmoja moja na kwa ujumla..

(5) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya utekelezaji wa Ibara hii.

Ardhi ya binafsi 82. Ardhi ya binafsi inajumuisha -

(a) ardhi ambayo imesajiliwa na kumilikiwa na mtu bila masharti au ardhi inayomilikiwa na mtu kwa kukodisha; na

(b) ardhi yoyote ambayo imetangazwa kuwa ni ardhi binafsi na Sheria iliyotungwa na Bunge.

Wageni kumiliki ardhi 83. (1) Mtu ambaye si raia anaweza kumiliki au kutumia ardhi kwa msingi wa

kukodishwa tu, na ukodishaji huo kwa vyovyote, hautazidi miaka tisini na tisa.

(2) Mkataba, hati ya kumiliki au uhawilishaji au utaratibu wowote unaompa mtu asiyekuwa raia umilikaji wa ardhi kwa zaidi ya miaka tisini na tisa, ni batili.

(3) Ifikapo tarehe ya kuanza kutumika Katiba hii, umilikaji wowote wa ardhi kwa kipindi cha zaidi ya miaka tisini na tisa, wa mtu asiyekuwa raia utakoma, na umilkaji wa ardhi hiyo utaregeshwa kwa serikali, na serikali itamkodishia ardhi hiyo mtu huyo kwa muda mwengine wa miaka tisini na tisa.

(4) Bunge litatunga sheria kuwezesha utekelezaji wa Ibara ndogo (3).

Page 52: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

52

Usimamizi wa matumizi ya ardhi 84. (1) Serikali ina uwezo wa kusimamia matumizi ya ardhi yoyote, maslahi, au

haki ya ardhi kwa madhumuni ya ulinzi, usalama wa umma, mwongozo, afya ya umma, upangaji wa matumizi ya ardhi, au maendeleo au matumizi ya mali.

(2) Serikali itahimiza na kuwezesha kuwepo kwa hali inayofaa ya

kijamii, kiuchumi, kisiasa na kisheria kwa ajili ya uendelezaji na usimamizi wa mali.

(3) Serikali itahakikisha -

(a) kuanzishwa kwa mfuko wa maendeleo ya nyumba ili kuwezesha watu wa Kenya kupata kuwa na nyumba zaidi na zilizo bora; na

(b) utungaji wa, na urekebishaji kila mara wa sera ya taifa ya nyumba kwa madhumuni ya kuongeza, kudhibiti, na kusimamia nyumba za taifa zilizoko.

(4) Bunge litatunga sheria -

(a) kuitaka serikali na mashirika yanayohusika pamoja na serikali zilizosambaziwa mamlaka kuhimiza matumizi yanayokubalika, yasiyoghali na teknolojia ya kati inayofaa, vifaa vya ujenzi, ubunifu, na mbinu katika sekta ya mali, mradi tu matumizi yake hayaathiri vibaya au kudhuru watu na mazingira; na

(b) inayohakikisha kuwa uwekezaji mkubwa wa mali unanufaisha jamii na uchumi wake.

Tume ya Taifa ya Ardhi 85. (1) Inaundwa Tume ya Taifa ya Ardhi.

(2) Majukumu ya Tume ya Taifa ya Ardhi ni -

(a) kusimamia ardhi ya umma kwa niaba ya serikali zilizosambaziwa mamlaka;

(b) kutengeneza na kupendekeza kwa serikali sera ya kitaifa ya ardhi;

(c) kushauri serikali na serikali zilizosambaziwa mamlaka kuhusu mipango ya sera kwa ajili ya maeneo maalum ya Kenya, kuhakikisha kwamba maendeleo katika ardhi ya jamii na ya binafsi yanaambatana na mpango wa maendeleo wa eneo hilo.

(d) kuchunguza mizozo ya umilikaji wa ardhi, makaazi na upatikanaji wa ardhi ya umma katika eneo kama ilivyoainishwa kisheria;

(e) kushauri serikali kuhusu na kusaidia katika utekelezaji wa mpango kamili kwa ajili ya usajili wa hati ya umiliki wa ardhi kote nchini Kenya;

Page 53: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

53

(f) kufanya utafiti unaohusiana na ardhi na matumizi ya maliasili, na kutoa mapendekezo kwa mamlaka inayohusika;

(g) kuanzisha uchunguzi wake yenyewe au kutokana na malalamiko ya mtu, au watu, au taasisi nyingine kuhusu dhuluma katika ardhi hivi sasa na pia wakati uliopita na kuhakikisha kupatikana suluhisho linalofaa;

(h) kuwezesha kushiriki kwa jamii katika kutunga sera ya ardhi;

(i) kuhimiza utekelezaji wa mifumo ya jadi iliyokubalika ya kusuluhisha mizozo ya ardhi;

(j) kutathmini kodi ya ardhi na ada za mali katika eneo lolote lililoelekezwa na sheria;

(k) kufuatilia na kuchunguza majukumu kuhusu upangaji wa matumizi ya ardhi kote nchini;

(l) kukusanya, na mara kwa mara kuzipitia upya sheria zote zinazohusu ardhi; na

(m) kuanzisha mapitio ya sheria zote za sekta ya matumizi ya ardhi kulingana na sera ya taifa ya ardhi.

(3) Tume ya Taifa ya Ardhi itaanzisha afisi kote nchini Kenya.

Sheria za ardhi 86. (1) Bunge litatunga sheria -

(a) kurekebisha, kuziweka pamoja na kuzitathmini sheria za ardhi zilizoko;

(b) kurekebisha sheria ya matumizi ya ardhi katika maeneo kwa mujibu wa sera ya ardhi ya taifa;

(c) kusimamia njia za kubadilisha matumizi ya ardhi kutoka aina moja hadi nyingine;

(d) kusimamia utambuaji na uhifadhi wa mali za waliooana na hasa nyumba wanayoimiliki waliooana ima wakati wa ndoa yao au baada ya kutalikiana;

(e) kuwezesha uthibitishaji wa ardhi inayomilikiwa kwa manufaa ya jamii yoyote na mtu yeyote au shirika, na kupewa ardhi hiyo kwa jamiii zinazoistahiki;

(f) kulinda, kuhifadhi, na kuruhusu ufikiaji usio mipaka wa ardhi ya umma;

(g) kuwezesha mapitio ya utoaji wa ardhi ya umma ili kuthibitisha au kufafanua uhalali wake;

Page 54: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

54

(h) kuwezesha kupewa makaazi watu wasiokuwa na ardhi na makaazi pamoja na kujenga upya makaazi yasiyo rasmi mashambani na mijini;

(i) kuanzisha mfuko wa ardhi ili kuwezesha raia kupata ardhi kwa njia ya uadilifu;

(j) kuwalinda wanaomtegemea marehemu kupata maslahi katika ardhi pamoja na kulinda maslahi ya mke au mume katika kuikalia ardhi;

(k) kuanzisha akiba ya ardhi ili kuwezesha kupatikana kwa ardhi kwa matumizi ya umma; na

(l) kuamua kiwango cha juu na chini cha ardhi yenye rutuba inayoweza kumilikiwa na mtu.

(2) Bunge litaamua kauli kuhusu tarehe ya mwisho ya ukaguzi unaoamriwa chini ya Ibara ndogo (g).

Page 55: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

55

SURA YA NANE

MAZINGIRA NA MALIASILI

Kanuni na majukumu kuhusu mazingira 87. Serikali -

(a) itaheshimu utaratibu wa kiasili na jamii za kiikolojia, pamoja na kuhifadhi makaazi, mimea na wanyama;

(b) itahakikisha matumizi endelevu, utumiaji, usimamizi na uhifadhi wa mazingira na maliasili na ugawaji sawa wa manufaa yatokanayo;

(c) itahakikisha kwamba maadili ya kitamaduni na kijamii yanayofuatwa kidesturi na jamii za Wakenya kwa ajili ya maendeleo endelevu ya mazingira na maliasili yanazingatiwa;

(d) itaidhinisha nchini maafikiano na mikataba ya kimataifa na baina ya nchi kuhusu uhifadhi wa mazingira;

(e) itahakikisha kwamba mipango na matumizi ya mazingira yanazingatia maeneo yaliyonyuma kimaendeleo na wenyeji wake;

(f) itaendeleza uhifadhi wa nishati na matumizi ya kudumisha vyanzo vya nishati;

(g) itazuia kuchafuliwa kwa mazingira na uharibifu wa ikolojia;

(h) itatenga rasilmali ya kutosha ili kurudishwa katika hali yake na kukarabati maeneo yaliyoharibika na yale yanayokumbwa na maafa ya mara kwa mara ili yaweze kukalika na kuzalisha; na

(i) itahakikisha kufikia na kudumisha idadi ya miti itakayochukua angalau asilimia kumi ya eneo la ardhi ya Kenya.

Kulinda mazingira 88. Kila mtu ana wajibu wa kushirikiana na vyombo vya serikali na watu wengine -

(a) kuhakikisha maendeleo endelevu ya kiikolojia na matumizi ya maliasili;

(b) kuheshimu, kuhifadhi na kulinda mazingira;

(c) kuzuia au kuacha kitendo kinachodhuru mazingira;

(d) kuamrisha mamlaka inayohusika kuchukua hatua kuzuia au kuacha kitendo au kutotenda kitendo ambacho kinaharibu mazingira; na

(e) kudumisha mazingira safi, salama na yenye kudumisha afya njema.

Page 56: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

56

Kuhifadhi mazingira 89. Katika matumizi na usimamizi wa mazingira, Serikali -

(a) italinda maliasili ya kinasaba na anuwa ya kibayolojia;

(b) itazuia uharibifu na kuhimiza kutumia upya;

(c) itaanzisha mifumo ya kutathmini athari za mazingira, ukaguzi wa mazingira, na ufuatiliaji mazingira;

(d) itahimiza kushiriki kwa umma;

(e) italinda na kukuza hakimiliki na vipaji vya wazalendo kuhusiana na wa anuwai ya bayolojia na maliasili ya kinasaba katika jamii; na

(f) itahakikisha kuwa viwango vya mazingira vinavyotekelezwa katika Jamhuri ni viwango vinavyokubalika kimataifa.

Matumizi na uendelezaji wa maliasili 90. (1) Serikali itahakikisha ulinzi, usimamizi, uimarishaji na maendeleo

endelevu ya maliasili na-

(a) itaazimia kuongeza uzalishaji na mapato;

(b) itafanya utafiti mwafaka kuhakikisha kuongezeka kwake;

(c) itafutilia mbali desturi za biashara zisizo za haki katika uzalishaji, utengenezaji, ugawaji na uuzaji;

(d) itanadhimu usafirishaji wa nje na uagizaji wa maliasili nyingine;

(e) itanadhimu uasili wake, ubora, njia za uzalishaji, uvunaji, na utengenezaji;

(f) itafutilia mbali taratibu na shughuli zinazoweza kuhatarisha au kuzuia kuwepo maliasili; na

(g) itazitumia kwa manufaa ya watu wa Kenya.

Mikataba kuhusu maliasili 91. (1) Mapatano ya kibiashara yanayohusu utoaji wa haki au kibali cha, au kwa

niaba ya, mtu yeyote, pamoja na serikali kwa mtu mwengine kuvuna maliasili ya Kenya, yaliyofikiwa baada ya Katiba hii kuanza kufanya kazi, sharti yaidhinishwe na Bunge.

(2) Bunge linaweza, kupitia sheria iliyoungwa mkono na thuluthi mbili za wabunge wote, kusamehe aina yoyote ya mapatano kutokana na masharti ya Ibara ndogo (1).

Tume ya taifa ya mazingira 92. (1) Inaundwa Tume ya Taifa ya Mazingira.

Page 57: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

57

(2) Tume ya Taifa ya Mazingira ndiyo itakuwa chombo kikuu cha Serikali katika kutekeleza kanuni na malengo ya sura hii, na hasa -

(a) itahakikisha ulinzi, uhifadhi, na usimamizi wa mazingira;

(b) itaendeleza haki, usawa na ugawaji wenye kukubalika, na utumiaji wa mazingira na maliasili;

(c) itafanya utafiti kuhusu mazingira na maliasili;

(d) kushauri Serikali na serikali zilizosambaziwa mamlaka kuhusu taratibu za sera kwa ajili ya usimamizi wa mazingira na maliasili na udhibiti wa makaazi ya binadamu;

(e) kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa sera ya taifa ya mazingira;

(f) itashajiisha ushiriki wa wananchi, mjadala na maoni kabla ya mapatano ya kimataifa, mikataba na makubaliano ambayo yana athari kwa mazingira haijaidhinishwa.

(g) itatekeleza wajibu wowote kama utakavyoagizwa na sheria, na kwa ujumla, kutekeleza malengo ya Ibara hii.

Sheria kuhusu mazingira 93. Bunge litatunga sheria -

(a) kuhakikisha kwamba mali asili zinakuzwa kiendelevu kwa maslahi ya Kenya kwa jumla na kwa maslahi ya wakaazi wa eneo maliasili hiyo ipo;

(b) kuweka matumizi na usimamizi wa mali asili kwa serikali zilizosambaziwa mamlaka ambapo mali asili hio ipo;

(c) kunadhimu, uvunaji endelevu, utumizi, usimamizi na ugawaji wa haki wa manufaa yanayotokana na maliasili;

(d) kulinda haki miliki na taaluma na vipaji asili vya wenyeji katika uanuwai wa kibiolojia na kupata maliasili kinasaba;

(e) za uhifadhi wa misitu, mbuga za wanyama, hifadhi na maficho, fukwe na maeneo ya chem chem za maji na kukuuza utalii wenye kuhifadhi ekolojia;

(f) kuzuia kutoa zaidi maeneo ya hifadhi kwa watu isipokuwa tu ikiwa utowaji huo unaambatana na misingi ya kuimarisha usimamizi endelevu na unaleta faida kwa jamii;

(g) kuhakikisha kwamba matumizi ya ardhi na sera za mazingira zinawekwa kwa kuhami kilimo na ardhi ya mbugani dhidi ya uharibifu wa mazingira;

(h) kutekeleza kanuni ya “mchafuzi alipe” na kuhakikisha kwamba utupwaji na uhifadhi wa vitu visivyotakiwa kimazingira

Page 58: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

58

pamoja na mabaki ya hatari na vifaa vya kivita ikitiliwa maanani haja ya mazingira safi, salama na yenye afya.

(i) kuhakikisha kwamba utoaji wa mionzi yenye kudhuru na ghasia katika mazingira zinadhibitiwa ili kutimiza masharti ya mazingira safi, yenye afya na salama;

(j) kupunguza mgongano baina ya binadamu na wanyama pori; na

(k) kutoa fidia kwa hasara ya kupoteza maisha ya mwanadamu, majeruhi, hasara na uharibifu wa mali binafsi.

Page 59: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

59

SURA YA TISA

UONGOZI NA UAMINIFU

Majukumu ya uongozi 94. (1) Ukuu wowote wa mamlaka ya watu uliyopewa afisi ya Serikali -

(a) ni amana ya umma itakayotekelezwa kwa njia ambayo -

(i) inafungamana na madhumuni na malengo ya Katiba hii;

(ii) inadhihirisha heshima kwa watu;

(iii) inaleta heshima kwa taifa na staha kwa afisi; na

(iv) inaendeleza imani ya umma katika uadilifu wa afisi; na

(b) inakabidhi afisa huyo wa serikali jukumu la kuhudumia watu kwa unyenyekevu.

(2) Kanuni elekezi za uongozi na uadilifu ni pamoja na -

(a) uteuzi kwa misingi ya uaminifu, uwezo wa ustahiki, au kuchagua katika chaguzi huru na za haki;

(b) kutoa maamuzi yasiyo na upendeleo, ambayo hayaathiriwi na unasaba, upendeleo, au sababu nyingine zisizofaa;

(c) kuhudumia kwa kujitolea kwa maslahi ya umma;

(d) kutangaza maslahi ya kibinafsi yanayoweza kupingana na wajibu wa umma;

(e) uaminifu na uadilifu katika kutekeleza wajibu wa umma; na

(f) uwazi na uwajibikaji kwa umma katika maamuzi na vitendo; na

(g) nidhamu na kujitolea katika kuhudumia watu.

Kiapo ama tamko la dhati la afisi 95. Kabla ya kushika wadhifa afisini au kutekeleza majukumu yoyote ya afisi, kila

mtu aliyechaguliwa au kuteuliwa kushika afisi ya Serikali ataapa na afuate kiapo au tamko la dhati la afisi kwa njia na namna ilivyoelezwa na Jedwali ya Pili au Sheria iliyotungwa na Bunge.

Nidhamu kwa maafisa wa Serikali 96. (1) Afisa wa serikali, wakati wowote, atakuwa na mwenendo wa namna

ambayo atajiepusha na -

(a) mgongano wowote baina ya maslahi ya kibinafsi na majukumu ya umma au rasmi;

(b) kuhatarisha maslahi ya umma au rasmi kwa sababu ya maslahi ya kibinafsi; au

Page 60: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

60

(c) kudhalilisha afisi au cheo chake.

(2) Afisa wa serikali -

(a) hatatumia afisi ya Serikali moja kwa moja au vinginevyo au uwezo wa afisi hiyo kwa maslahi ya kibinafsi, au kupata maslahi mengine yasiyo stahiki kutoka kwa mtu yeyote;

(b) hatatafuta au kupokea mali, zawadi au manufaa ya aina yoyote kama kishawishi au rushwa kwa ajili ya upendeleo au utekelezaji au kutotekeleza wajibu rasmi;

(c) hatatafuta au kupokea mkopo wa kibinafsi au kunufaika katika hali ambazo zinaweza kuonekana kuathiri uadilifu wa afisa huyo wa Serikali;

(d) hatatumia vibaya fedha za umma au kwa ubadhirifu au kuharibu, kinyume na sheria, mali ya umma;

(e) hatatumia rasilmali, mali au vifaa vya umma ili kuomba michango kutoka kwa umma kwa madhumuni yoyote yasiyokuwa rasmi;

(f) hatatumia uwezo wa afisi yake kunyanyasa kijinsia au kimwili mtu yeyote, au kujaribu kupata fadhila za mapenzi au kupata maslahi mengine yasiyostahiki kutoka kwa mtu yeyote; au

(g) hataamuru mtu mwingine -

(i) kufanya jambo lililokatazwa na Ibara hii kwa maslahi ya afisa huyo wa serikali; au

(ii) kufanya kitendo kisicho halali.

(3) Ikiwa afisa wa Serikali amehukumiwa kwa hatia inayohusiana na masuala yaliyorejewa na Ibara hii afisa huyo ataachishwa kazi.

(4) Mtu aliyefutwa kazi au kuondolewa kutoka afisi ya Serikali kuambatana na Katiba hii au kwa sheria ya kukiuka Sura hii atazuiwa kupewa kazi nyingine katika afisi yeyote ya umma.

Mali za maafisa wa Serikali 97. (1) Afisa wa Serikali atawasilisha taarifa ya maandishi kwa Tume ya Maadili

na Uaminifu kwa utaratibu na namna itakavyoamuliwa na Tume, au ilivyoagizwa na sheria, akitaja mali, rasilmali, na madeni yake, ya mkewe au mumewe, na ya watoto wake ambao hawajaoa au kuolewa ambao hawajafikisha umri wa miaka kumi na minane -

(a) mara tu akiwa afisa wa Serikali;

(b) kila mwaka wakati akiwa afisa wa Serikali;

(c) akiacha kuwa afisa wa Serikali.

Page 61: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

61

(2) Zawadi au msaada kwa afisa wa Serikali katika shughuli ya umma au rasmi ni zawadi kwa Jamhuri, na itawasilishwa Serikalini kama inavyohitajika, na kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Vikwazo dhidi ya shughuli 98. (1) Afisa aliyeajiriwa kwa kazi ya kudumu katika Serikali hatashika wadhifa

mwengine wenye faida au mshahara.

(2) Rais, Naibu Rais na afisa yeyote wa serikali aliyeteuliwa hatakuwa na wadhifa katika chama cha kisiasa.

(3) Afisa wa serikali aliyestaafu na anayepokea malipo ya uzeeni kutoka kwa mfuko wa umma hatakuwa na zaidi ya vyeo viwili kama mwenyekiti, mkurugenzi au mwajiriwa wa -

(a) kampuni inayomilikiwa, au inayodhibitiwa na serikali; au

(b) chombo cha serikali.

(4) Afisa mstaafu wa Serikali hatapokea malipo mengine yoyote kutoka kwa mfuko wa umma isipokuwa vile ilivyoagizwa na Ibara ndogo (3).

Tume ya Maadili na Uaminifu 99. (1) Inaundwa Tume ya Maadili na Uaminifu.

(2) Tume ya Maadili na Uaminifu ndio itakuwa chombo kikuu cha Serikali katika kutekeleza kanuni na malengo ya Sura hii, na hasa -

(a) kupokea na kuhifadhi taarifa zilizoagizwa katika Sura hii;

(b) kuhakikisha utiifu wa, na utekelezaji wa, masharti ya Sura hii;

(c) kupokea na kuchunguza malalamiko kuhusu kutotii Sura hii na, ikifaa, kupeleka malalamiko kwa mamlaka yanayohusika kwa kuchukuliwa hatua;

(d) kuweka mikakati ya kuzuia ufisadi, pamoja na kutoa miongozo kwa vyombo vya Serikali; na

(e) kutekeleza majukumu mengine yatakayoagizwa na sheria, na kwa ujumla, kutekeleza malengo ya Sura hii.

(3) Tume haitachunguza jambo lolote lililoko mahamakani au katika mahakama maalumu.

(4) Tume itaanzisha na kudumisha daftari ambamo rasilmali na madeni ya maafisa wa Serikali yatasajiliwa.

(5) Tume itaweka daftari ya rasilmali na madeni ya maafisa wa Serikali wazi kwa kukaguliwa na umma.

Sheria kuhusu uongozi 100. Bunge litatunga sheria kwa ajili ya -

Page 62: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

62

(a) kuanzisha taratibu za utekelezaji thabiti wa Sura hii;

(b) kuweka viwango vya adhabu ambavyo vitaweza kutolewa kwa kukiuka masharti ya Sura hii; na

(c) kuweka masharti mengine yoyote yatakayohitajika ili kuhakikisha uendelezaji wa kanuni za maadili ya uongozi na uadilifu yaliyowekwa katika Sura hii.

Page 63: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

63

SURA YA KUMI

UWAKILISHI WA WATU

Sehemu ya Kwanza – Mfumo na Utaratibu wa Uchaguzi

Kanuni za jumla 101. Mfumo wa uchaguzi utatosheleza kanuni zifuatazo –

(a) uhuru wa raia kutekeleza haki zao za kisiasa chini ya Ibara 54;

(b) usawa wa jinsia katika vyombo vilivyochaguliwa kama ilivyoagizwa na Ibara 13(1)(j);

(c) uwakilishi wa watu walemavu kama ulivyoagizwa na Ibara 13(1)(k);

(d) uwakilishi sawa wa watu kwa ujumla pamoja na wafanya kazi na vijana;

(e) uchaguzi wa haki ambao –

(i) hauna fujo, vitisho, ushwawishi usiofaa na rushwa;

(ii) utaendeshwa na chombo huru; na

(iii) utasimamiwa katika njia iliyoadilifu, isiopendelea

upande wowote, angavu, iliyosahihi na yenye kuajibika.

Chaguzi 102. Bunge litatunga sheria kutoa masharti ya -

(a) idadi ya majimbo ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa Bunge kwa Tume ya Uchaguzi na Mipaka.

(b) utaratibu wa uteuzi wa wagombea uchaguzi;

(c) usajili wa kuendelea wa raia kama wapigaji kura;

(d) namna ya kuendesha na kusimamia uchaguzi na kura za maoni;

(e) usajili wa, na kupiga kura kwa, raia waishio nje ya Kenya; na

(f) mambo mengine yanayohusu uchaguzi na kura za maoni, kama bunge litakavyoamua.

Kusajiliwa kama mpiga kura 103. (1) Raia anastahili kusajiliwa kama mpiga kura katika chaguzi au kura za

maoni iwapo wakati wa tarehe ya maombi ya usajili, raia huyo ametimiza umri wa miaka kumi na minane na ana sifa nyingine kama zitakavyoelezwa na sheria.

Page 64: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

64

(2) Raia mwenye sifa za kusajiliwa kama mpiga kura, atasajiliwa katika kituo kimoja pekee.

(3) Mipango ya usimamizi wa usajili wa wapiga kura na utaratibu wa kuendesha uchaguzi hautomnyima haki raia anaestahiki kupiga kura na kugombea uchaguzi.

Kuondolewa kwenye usajili kama mpiga kura 104. (1) Raia ataondolewa kutoka kwenye usajili kama mpiga kura katika uchaguzi

au kura za maoni kwa sababu zozote zitakazoelezwa na sheria.

(2) Suala kama raia hastahiki kusajiliwa kama mpiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni litaamuliwa na Mahakama Kuu.

Kupiga kura 105. Katika kila uchaguzi Tume ya Uchaguzi na Mipaka itahakikisha kwamba -

(a) utaratibu wa upigaji kura ni mwepesi;

(b) sanduku la kura litakapotumiwa, litakuwa lenye kuonyesha;

(c) kura zilizopigwa zitahesabiwa, zitaorodheshwa na kutangazwa na afisa msimamizi wa kituo mara moja kwenye kituo cha kupigia kura.

(d) matokeo ya vituo vya kupigia kura yanajumlishwa waziwazi na kutangazwa mara moja na afisa msimamizi wa kura;

(e) mipango maalum imefanywa ili Vikosi vya Ulinzi wa Kenya, Polisi ya Kenya, Polisi Tawala, wafanyakazi wa Balozi za Kenya, raia walio nje ya Kenya, wafungwa, maafisa wa uchaguzi, na wagonjwa mahospitalini wapate nafasi ya kupiga kura; na

(f) miundo na taratibu zinazofaa kuondoa mienendo yote mibaya ya uchaguzi, pamoja na uhifadhi wa usalama wa vifaa vyote vya uchaguzi imewekwa.

Wagombea wa kujitegemea 106. Kwa mujibu wa Ibara ya 117 na masharti yaliyowekwa kwa ngazi mbalimbali za

serikali iliyosambaziwa mamlaka, mtu ana haki ya kusimama kama mgombea wa kujitegemea katika uchaguzi wa bunge au katika serikali za wilaya, ikiwa mtu huyo -

(a) ni raia wa Kenya;

(b) hajakuwa mwanachama wa chama cha kisiasa kilichosajiliwa kwa muda wa miezi sita kabla ya tarehe ya uchaguzi anaougombea;

(c) amesajiliwa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka kama mgombea wa kujitegemea na ametimiza masharti ya sheria ya maadili yaliyotayarishwa na Tume kwa wagombea kama hao; na

Page 65: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

65

(d) ameteuliwa na idadi ifuatayo ya wapiga kura waliosajiliwa katika jimbo la uchaguzi ambalo mtu huyo anataka kugombea -

(i) ikiwa ni kiti cha Bunge, wapiga kura elfu moja waliosajiliwa;

(ii) ikiwa ni kiti cha baraza la wilaya, wapiga kura mia tano waliosajiliwa; na

Wagombea bila kupingwa 107. Iwapo mgombea mmoja tu wa ubunge au wa baraza la wilaya ndiye

aliyependekezwa, mgombeaji huyo atatangazwa kuwa amechaguliwa.

Uwakilishi katika mashirika ya kimataifa 108. Kwa kufuatana na mikataba inayohusika na maafikiano ya kimataifa, Bunge

litatunga sheria itakayoongoza uchaguzi na uteuzi wa wawakilishi wa Jamhuri katika vyombo vya kisheria vya Kimataifa.

Sehemu ya Pili – Tume ya Uchaguzi na Mipaka

Kuundwa kwa Tume na kazi zake 109. (1) Inaundwa Tume ya Uchaguzi na Mipaka.

(2) Tume ya Uchaguzi na Mipaka ina wajibu wa -

(a) usajili wa kuendelea wa wapiga kura;

(b) uwekaji mipaka ya maeneo ya uchaguzi;

(c) uendeshaji na usimamizi madhubuti wa uchaguzi na kura za maoni;

(d) uendelezaji wa chaguzi na kura za maoni, ambazo ni huru na zenye usawa;

(e) usajili na usimamizi wa vyama vya kisiasa;

(f) usimamizi wa Mfuko wa Fedha wa Vyama vya Kisiasa;

(g) usuluhishaji wa utatanishi mdogo wa uchaguzi;

(h) uendelezaji wa elimu ya wapiga kura na utamaduni wa demokrasia; na

(i) kuwezesha uchunguzaji, ufuatiliaji, na utathmini wa uchaguzi;

(j) kupendekeza mipaka ya utawala, pamoja na uwekaji, upitiaji na ubadilishaji wa mipaka ya wilaya na vitengo vyengine kata; na

(k) kuhakikisha kwamba wagombea wote wa urais, ubunge, na baraza la wilaya wanatimiza mahitaji na sifa zote za kugombea uchaguzi; na

Page 66: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

66

(l) wadhifa mwengine wowote kama itakavyoagizwa na sheria ya bunge.

Mipaka ya maeneo ya uchaguzi 110. (1) Tume ya uchaguzi na Mipaka itatangaza majina na mipaka ya maeneo

kwa ajili ya uchaguzi wa Bunge.

(2) Katika kuweka mipaka ya maeneo na kuyapa majina, Tume ya Uchaguzi na Mipaka -

(a) itazingatia uwiano na usawa wa wanaoishi katika eneo na kuhakikisha uwakilishaji unaotosha katika sehemu ya mijini na mashambani kusikokuwa na watu wengi;

(b) itashauriana na washikadau wote, na

(c) itazingatia historia, uanuai na ushikamano wa eneo kwa kutilia maanani -

(i) idadi ya watu na mikondo ya ongezeko;

(ii) sifa za kijiografia na vituo vya mijini;

(iii) maslahi yanayojumuisha jamii na uhusiano wa kihistoria, kiuchumi na kitamaduni;

(iv) njia za mawasiliano; na

(v) haja ya kuhakikisha kila eneo la uchaguzi wa Bunge lote limo katika wilaya moja.

(3) Tume kila baada ya kipindi kisichozidi miaka kumi inaweza kurekebisha na kubadilisha majina na mipaka ya maeneo ya uchaguzi.

(4) Majina na maelezo ya mipaka ya maeneo chini ya Ibara ya ndogo (1) yatachapishwa katika Gazeti, na yataanza kutekelezwa Bunge likivunjwa baada ya uchapishaji huo.

(5) Mtu anaweza kuomba Mahakama Kuu kupitia upya uamuzi wa Tume uliofanywa chini ya Ibara hii.

Kuweka mipaka ya utawala 111. (1) Tume ya Uchaguzi na Mipaka katika kutekeleza kazi zake chini ya Ibara

ya 108(2)(j) itazingatia uwezekano, uendelevu, na uthabiti wa eneo, wilaya au kata, kwa kutia maanani -

(a) idadi ya watu na eneo;

(b) uhusiano wa kihistoria na kitamaduni;

(c) uchumi wake na maliasili; na

(d) malengo na kanuni za serikali za wilaya.

(2) Tume inaweza kupendekeza kwa Bunge -

Page 67: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

67

(a) ili kubadili mipaka ya mikoa, wilaya au kata; au

(b) ili kufutilia mbali na kuunda maeneo mapya, wilaya au kata.

(3) Kabla ya kutoa pendekezo lolote chini ya Ibara hii, Tume

itashauriana na mamlaka ya wilaya inayohusika pamoja na washiriki wote wanaohusika.

Sehemu ya Tatu – Vyama Vya Kisiasa

Kanuni za kimsingi 112. (1) Chama cha kisiasa kitakuwa na -

(a) sura ya kitaifa;

(b) uongozi uliochaguliwa kidemokrasia;

(c) lengo la kuendeleza na kudumisha umoja wa kitaifa;

(d) utii wa kanuni za kidemokrasia za utawala bora na kuendeleza na kudumisha utaratibu wa demokrasia katika chama kupitia uchaguzi wa mara kwa mara, ulio huru, na wenye usawa;

(e) heshima kwa haki za wengine kushiriki katika shughuli za kisiasa, pamoja na watu wenye ulemavu, wafanyakazi, na jamii ndogo nyinginezo;

(f) uendelezi na heshima za haki za kibinadamu, usawa wa jinsia na uadilifu;

(g) uendelezi wa malengo na kanuni za Katiba hii na utawala wa sheria;

(h) heshima na kukiri maadili ya vyama vya kisiasa.

(2) Chama cha kisiasa hakiwezi -

(a) kuanzishwa kwa msingi wa dini, lugha, rangi, kabila, jinsia, au ueneo ama kijihusisha kutumia propaganda yenye msingi wa mambo yoyote kati ya hayo;

(b) kushiriki, au kuhimiza matumizi ya nguvu au kutisha wanachama wake, waungaji mkono au wapinzani wake au watu wengine;

(c) kuanzisha au kudumisha wanamgambo wenye sifa za kijeshi au jeshi la mgambo au vikundi kama hiyo; au

(d) kushiriki katika rushwa au aina nyingine ya ufisadi.

Page 68: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

68

Sheria kuhusu vyama vya kisiasa 113. Bunge litatunga sheria za usimamizi wa vyama vya kisiasa ambazo zitaeleza

kuhusu –

(a) udhibiti wa vyama vya kisiasa;

(b) majukumu na wadhifa wa vyama vya kisiasa;

(c) usajili na usimamizi wa vyama vya kisiasa kwa mujibu wa Ibara 109(2)(e);

(d) kuanzisha na kusimamia mfuko wa vyama vya kisiasa kwa mujibu wa Ibara 109(2)(f);

(e) hesabu na ukaguzi wa vyama vya kisiasa;

(f) nidhamu ya vyama vya kisiasa;

(g) vizuizi dhidi ya matumizi ya mali ya umma kuendeleza maslahi ya vyama vya kisiasa; na

(h) mambo mengine yoyote yatakayoonekana muhimu kwa usimamizi wa vyama vya kisiasa.

Page 69: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

69

SURA YA KUMI NA MOJA

BUNGE

Sehemu ya Kwanza – Kuundwa kwa Bunge na Wajibu wake

Kuundwa kwa Bunge 114. Linaundwa Bunge la Kenya.

Utekelezaji wa mamlaka 115. (1) Mamlaka ya utungaji sheria katika Jamhuri yamekabidhiwa Bunge.

(2) Bunge linadhihirisha uanuwai wa tamaduni na kuwakilisha matakwa ya wananchi, kwa kutekeleza mamlaka yao kupitia -

(a) kutunga sheria;

(b) kujadiliana na kuamua masuala yanayowahusu wananchi;

(c) kutafakari na kupitisha mabadiliko katika Katiba hii;

(d) kuidhinisha na kugawa mapato miongoni mwa viwango vinne vya Serikali na kuidhinisha matumizi ya fedha za Serikali na za idara za Serikali;

(e) kuhakikisha uadilifu katika kugawa maliasili ya taifa na fursa miongoni mwa sehemu na jamii za Kenya;

(f) kuchunguza na kusimamia vitendo vya vyombo vya serikali;

(g) kutafakari na kuidhinisha mikataba ya kimataifa;

(h) kuidhinisha uteuzi, inapohitajika kufanya hivyo kwa mujibu wa Katiba hii au sheria;

(i) kuangalia upya tabia ya Rais madarakani, Naibu Rais na maafisa wengine wa Serikali wakiwa madarakani na inapohitajika, kuanzisha hatua za kuwaondoa mamlakani; na

(j) kuidhinisha matamko ya hali ya hatari na vita.

(3) Mtu au chombo kengine isipokuwa Bunge, hakitakuwa na uwezo wa kutunga masharti yenye nguvu za kisheria nchini Kenya, isipokuwa kwa mujibu wa mamlaka yaliyotolewa na Katiba hii au sheria.

Sehemu ya Pili – Muundo na ujumbe katika Bunge

Ujumbe wa Bunge 116. (1) Bunge litakuwa na -

(a) mjumbe mmoja aliyechaguliwa kutoka kila eneo la uchaguzi kwa mujibu wa sheria;

Page 70: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

70

(b) mwanamke mmoja aliyechaguliwa kutoka maeneo maalum ya uwakilishi wa wanake yatakayotengwa kulingana na sheria;

(c) idadi ya wajumbe watakaoteuliwa na vyama vya kisiasa kulingana na idadi ya kura zilizopigiwa kila chama katika uchaguzi, kufuatilia orodha zilizowasilishwa na vyama vya kisiasa vilivyopigania uchaguzi;

(d) Mwanasheria Mkuu, ambaye atakuwa mbunge kwa sababu ya afisi yake;

(e) Spika, ambaye atakuwa mbunge kwa sababu ya afisi yake; na

(f) Mawaziri watakaoteuliwa chini ya Ibara 168(5), ambao watakuwa wabunge kwa sababu ya afisi zao.

(2) Wajumbe waliotajwa katika Ibara ndogo (1)(c) watajumuisha -

(a) wajumbe wenye ulemavu, ambao idadi yao itakuwa sawa na asilimia tano ya jumla ya ujumbe wa bunge, ambapo thuluthi moja ya hao walemavu watakuwa wanawake;

(b) idadi ya wajumbe sawa na asilimia tano ya ujumbe wa bunge ambao watateuliwa na vyama vya kisiasa kuwakilisha maslahi maalum, pamoja na vijana na wafanyi kazi; na

(c) idadi ya wajumbe kama itakavyohitajika kuhakikisha kwamba si zaidi ya thuluthi mbili za wabunge ni wa jinsia moja.

(3) Mjumbe aliyetajwa katika Ibara ndogo (1)(c) na (2) atahudumu kama mjumbe kwa muhula mmoja tu.

(4) Bunge litatunga sheria kuwezesha utekelezaji wa Ibara hii.

Sifa na kutokuwa na sifa kwa wajumbe 117. (1) Isipokuwa mtu ambaye hana sifa za kuchaguliwa kwa mujibu wa Ibara

ndogo (2), mtu anaweza kuwa mbunge ikiwa mtu huyo -

(a) ni raia;

(b) amesajiliwa kama mpiga kura;

(c) ametimiza mahitaji ya sifa za kielimu na kimaadili kama yalivyoagizwa na Katiba au sheria; na

(d) kama ni mgombea uchaguzi wa kiti cha Bunge -

(i) ameteuliwa na chama cha kisiasa; au

(ii) ikiwa ni mgombea anayejitegemea, anaungwa mkono na angalau wapiga kura elfu moja katika eneo la uchaguzi linalohusika kama ilivyoagizwa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka.

(2) Mtu atakosa sifa za kuwa Mbunge, ikiwa mtu huyo -

Page 71: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

71

(a) anashikilia wadhifa wa afisi ya serikali au ya umma, usiokuwa ubunge;

(b) hana akili timamu;

(c) ni muflisi ambaye hajasamehewa;

(d) anatumikia hukumu ya kifungo kisichopungua miezi sita;

(e) alikuwa, kwa muda wowote katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, alitumikia hukumu ya kifungo cha muda usiopungua miaka mitatu kwa uhalifu alioufanya kwa kosa linalotambuliwa chini ya sheria ya Kenya;

(f) ameondolewa katika afisi ya Serikali au ya umma kwa sababu ya utovu mkubwa wa nidhamu; au

(g) amepatikana kwa mujibu wa sheria kuwa alitumia vibaya afisi ya Serikali au umma au kwa namna yeyote kukiuka kanuni za Sura ya 9.

(3) Mtu hapotezi sifa ya kuwa mbunge chini ya Ibara ndogo (2) isipokuwa iwe uwezekano wote wa rufaa, au kupitia upya hukumu ya kifungo au uamuzi umekamilika.

Kuchaguliwa kwa Wabunge 118. (1) Uchaguzi wa wabunge utafanywa siku ya Jumanne inayotangulia siku

ishirini na nane kabla ya muhula wa Bunge.

(2) Wakati wowote itakapotokea nafasi ya mjumbe wa Bunge kuwa wazi -

(a) Spika ataiarifu Tume ya Uchaguzi na Mipaka kwa maandishi ndani muda wa siku ishirini na moja baada ya nafasi hiyo kuwa wazi; na

(b) kwa mujibu wa Ibara ndogo (3), uchaguzi mdogo utafanywa ndani muda wa siku tisini baada ya nafasi hiyo kuwa wazi.

(3) Uchaguzi mdogo hautafanywa ndani ya muda wa miezi mitatu kabla ya uchaguzi mkuu.

Kuwa wazi nafasi ya Mbunge 119. (1) Nafasi ya mbunge itakuwa wazi -

(a) ikiwa mbunge amejiuzulu nafasi yake kwa kumwandikia taarifa Spika;

(b) ikiwa mtu huyo hatastahiki kuchaguliwa kwa mujibu wa Ibara ya 117(2);

(c) ikiwa Bunge limemaliza muda wake;

(d) ikiwa mbunge hakuhudhuria vikao vinane vya Bunge bila ruhusa ya maandishi, kutoka kwa Spika, wakati wowote Bunge

Page 72: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

72

linapokaa, na ameshindwa kutoa maelezo yanayotosheleza kwa kamati inayohusika;

(e) ikiwa mbunge ameondolewa kisheria kwa mujibu wa Ibara ya 96;

(f) ikiwa mbunge amekihama chama chake cha kisiasa alichosimamia alipokuwa mgombea uchaguzi wa ubunge; au

(g) ikiwa, baada ya kuchaguliwa na kuingia Bungeni kama mbunge wa kujitegemea, mbunge huyo anajiunga na chama cha kisiasa.

(2) Uundaji au ufutaji wa muungano ambao chama cha mwanachama kimejiunga, ama ufutaji wa chama cha kisiasa au muungano wa zaidi ya vyama viwili, hakutachukuliwa kama kukihama chama madhumuni ya Ibara ndogo (1)(f).

Uamuzi wa suala kama mtu ni mjumbe 120. (1) Mahakama Kuu itasikiliza na kuamua swali kama -

(a) mtu yeyote amechaguliwa au kuteuliwa kihalali kama mbunge; au

(b) kiti cha mjumbe yeyote kimekuwa wazi.

(2) Swali lililotajwa katika Ibara ndogo (1) litasikilizwa na kuamuliwa ndani ya muda wa miezi sita baada ya tarehe ya kuwasilisha malalamiko.

Sehemu ya Tatu - Maafisa wa Bunge

Spika na Naibu Spika wa Bunge 121. (1) Kutakuwa na -

(a) Spika wa Bunge, atakayechaguliwa kuambatana na Kanuni za Bunge, miongoni mwa watu wenye sifa za kuchaguliwa wabunge lakini si miongoni mwa wabunge; na

(b) Naibu Spika wa Bunge atakayechaguliwa kuambatana na Kanuni za Bunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni wajumbe wa Bunge.

(2) Afisi ya Spika au Naibu Spika itakuwa wazi -

(a) wakati Ukumbi wa Bunge unapokutana mara ya kwanza baada ya uchaguzi;

(b) ikiwa afisa anayehusika amekosa sifa kwa mujibu wa Ibara ya 117(2);

(c) ikiwa Bunge litaamua kwa azimio linaloungwa mkono na kura za wajumbe wasiopungua asilimia sabini na tano;

(d) ikiwa anayeshikilia nafasi hiyo atakufa;

Page 73: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

73

(e) ikiwa mtu huyo amejiuzulu kutoka nafasi yake kwa kuandikia Bunge.

Usimamizi Bungeni 122. (1) Katika kila kikao cha Bunge -

(a) Spika anaongoza; au

(b) ikiwa Spika hayupo, Naibu Spika ataongoza; au

(c) ikiwa Spika na Naibu Spika hawapo, mjumbe mwingine anaweza kuchaguliwa ili aongoze.

Kiongozi wa Upinzani 123. (1) Kutakuwa na kiongozi wa Upinzani atakayechaguliwa na chama kikubwa

zaidi au muungano wa vyama vya Bunge ambavyo havikuunda Serikali.

(2) Kuhusu uendeshaji wa shughuli katika Bunge, Kiongozi wa Upinzani -

(a) atakuwa na cheo baada ya Rais, Naibu Rais, Waziri Mkuu na Spika; na

(b) ana haki ya kushiriki katika hafla zote za kiserikali; na

(c) ana haki ya kuwa wa pili kujibu, baada ya Waziri Mkuu kuhusu hotuba ya Rais kwa Bunge.

(3) Kanuni za Bunge zitahakikisha kuwa kiongozi wa upinzani anashiriki ipasavyo katika Bunge.

Makarani na wafanyakazi wa Bunge 124. (1) Kutakuwa na Karani wa Bunge atakayeteuliwa na Tume ya Huduma za

Bunge, kwa idhini ya Bunge.

(2) Afisi ya Karani na afisi za wafanyakazi wake zitakuwa afisi katika huduma ya Bunge.

(3) Kulingana na Ibara ndogo (4), Karani atastaafu anapofikia umri wa miaka sitini na tano.

(4) Bunge linaweza kumtoa Karani kwa azimio linaloungwa mkono na kura za asilimia isiyopungua sitini na tano ya wajumbe wote wa Bunge.

Sehemu ya Nne – Utungaji Sheria na Utaratibu Bungeni

Utekelezaji wa uwezo wa kutunga sheria 125. (1) Bunge litatumia uwezo wake wa kutunga sheria kupitia Miswada

iliyopitishwa na Bunge na kuidhinishwa na Rais.

(2) Mswada unaweza kuwasilishwa Bungeni na mjumbe yeyote, au kamati ya Bunge.

Page 74: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

74

(3) Kila Mswada wa sheria unaowasilishwa Bungeni utakuwa na maelezo, yatakayoelezea -

(a) mipaka au upunguzaji wa haki katika sheria ya haki za binadamu au taathira nyinginezo za kikatiba;

(b) taathira za kifedha; na

(c) ushirikishaji wowote wa umma katika kuandaa Mswada huo.

(4) Kamati inayohusika -

(a) itaamua kuhusu namna na kiwango cha kushiriki kwa umma kwa kila Mswada unaowasilishwa Bungeni; na

(b) itawezesha ushirikishaji huo na kuhakikisha utekelezaji wake kikamilifu.

(5) Bunge litatoa wakati wa kutosha wa kujadili Miswada.

Miswada ya Fedha 126. (1) Mswada wa fedha unaweza kuwasilishwa na Waziri pekee.

(2) Katika Sura hii, “Mswada wa fedha” unamaanisha Mswada ulio na masharti yanayoshughulikia -

(a) kuweka, kufuta, kusamehe, kurekebisha au kudhibiti kodi;

(b) kutoza malipo kutoka Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali ama mfuko mwingine wowote wa Serikali au kubadilisha au kufuta sheria za utozaji wowote wa malipo hayo;

(c) maidhinisho, upokeaji, uhifadhi, uwekezaji, kutoa ama kuchunguza fedha za umma;

(d) msaada wa pesa kwa mtu yeyote au mamlaka ama ubadilishaji au ufutiliaji mbali msaada huo;

(e) kukusanya ama kudhamini mkopo wowote au kurudisha malipo kama hayo; au

(f) jambo lolote linalotokana na yoyote kati ya mambo hayo.

(3) Katika Ibara ndogo (2) maelezo “kodi”, “pesa za umma”, na “mkopo” hazijumlishi kodi yoyote, pesa za umma au mikopo inayochangishwa na serikali zilizosambaziwa mamlaka.

Idhini ya Rais na kuwasilishwa 127. (1) Bunge likipitisha Mswada, Spika atauwasilisha Mswada huo ili

uidhinishwe na Rais ndani ya siku kumi na nne.

(2) Ndani ya siku kumi na nne baada ya kupokea Mswada huo, Rais -

(a) ataidhinisha Mswada;

Page 75: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

75

(b) atakataa kuidhinisha Mswada huo;

(3) Rais anapokataa kuidhinisha Mswada, Rais, ndani ya siku kumi na nne ya kukataa huko, atawasilisha taarifa kwa Spika kurudisha Mswada huo uzingatiwe tena na Bunge huku akioonyesha vipengele maalum ya Mswada huo au sababu ambazo, kwa maoni ya Rais, zinahitajia Mswada kuzingatiwa tena na Bunge, pamoja na mapendekezo yake Rais ya marekebisho.

(4) Iwapo Rais amerudisha tena Mswada Bungeni kwa mazingatio zaidi, Bunge -

(c) litaweza kubadilisha Mswada wa sheria kwa kuzingatia pingamizi zilizoelezwa na Rais; ama

(d) litaweza kupitisha Mswada wa Kisheria kwa mara ya pili bila marekebisho.

(5) Bunge likibadilisha Mswada, Spika atauwasilisha upya kwa Rais ili kuidhinishwa.

(6) Ikiwa Bunge, baada ya kutilia maanani maoni ya Rais, litapitisha Mswada kwa mara ya pili kwa kura zilizoungwa mkono na thuluthi mbili ya wajumbe wote, bila ya marekebisho -

(a) Spika atauwasilisha upya kwa Rais ndani ya siku saba; na

(b) Rais atauidhinisha Mswada huo ndani ya siku saba.

(7) Ikiwa Rais atakataa kuuidhinisha Mswada ndani ya mda ulioelezwa na Ibara ndogo (1), itachukuliwa kwamba Mswada huo umeidhinishwa baada ya kumalizika mda huo.

Kuanza kutumika kwa sheria 128. (1) Mswada ukishapitishwa na kuidhinishwa na Rais -

(a) utachapishwa katika Gazeti ndani ya siku saba tangu uidhinishwe;

(b) utaanza kutumika kuanzia siku ya kumi na nne tangu uchapishwe kwenye Gazeti isipokuwa kama sheria imeeleza vinginevyo.

(2) Sheria inayotoa moja kwa moja maslahi ya kifedha kwa wabunge haitaanza kutekelezwa mpaka Bunge lililopitisha sheria hiyo livunjwe.

(3) Ibara ndogo (2) haihusishi maslahi waliyonayo Wabunge kama wananchi.

Haki ya kulalamikia Bunge 129. Kila mtu ana haki ya kulalamikia Bunge, kutunga, kubadilisha au kufuta sheria

yoyote.

Akidi 130. Akidi ya Bunge ni asilimia thelathini ya wajumbe wote wa Bunge huo.

Page 76: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

76

Lugha rasmi Bungeni 131. Lugha rasmi za Bunge zitakuwa ni Kiswahili, Kiingereza na lughaishara.

Kupiga kura Bungeni 132. (1) Ila iwe imeelezwa vinginevyo katika Katiba hii, suali lolote

lililowasilishwa ili kuamuliwa Bungeni litatolewa uamuzi kwa wingi wa wajumbe waliohudhuria na kupiga kura katika Bunge.

(2) Kuhusu suali litakalopendekezwa kwa uamuzi katika Ukumbi wowote -

(a) Spika hatokuwa na kura;

(b) wajumbe walio wabunge kwa ajili ya afisi zao hawatakuwa na kura; na

(c) iwapo kura zitakuwa sawa basi suali hilo litashindwa.

(3) Kura ya mjumbe anayepiga kura juu ya suali ambapo mjumbe huyo ana maslahi moja kwa moja ya kifedha, haitahesabiwa.

Kudhibiti utaratibu 133. (1) Kwa mujibu wa Katiba hii, Bunge -

(a) litadhibiti utaratibu wake na litaweka kanuni zake kwa ajili ya uendeshaji bora wa vikao vyake;

(b) litaunda kamati kwa namna na kwa madhumuni ya jumla au malengo maalum kadiri itakavyoona na litadhibiti taratibu za kamati yoyote ya aina hiyo.

(2) Vikao katika Bunge havitokuwa batili kwa sababu tu –

(a) kuna nafasi wazi ya ujumbe wake; au

(b) kuwapo au kushiriki kwa mtu yeyote asiyestahiki kuhudhuria au kushiriki kwenye vikao vya Bunge.

Uwezo wa kuitisha ushahidi 134. Katika kutekeleza majukumu yake -

(a) Bunge au kamati yake yoyote, linaweza kumwita Waziri au mtu yeyote mwenye mamlaka katika afisi ya umma ama watu binafsi ili kuwasilisha maelezo au kuja mbele yake kutoa ushahidi;

(b) Kamati ya ukumbi wowote inaweza kumshirikisha mjumbe yeyote wa Bunge au kuajiri watu wenye sifa ili kusaidia katika utekelezaji wa majukumu yake; na

(c) Bunge au kamati yake yoyote, litakuwa na uwezo wa Mahakama Kuu -

Page 77: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

77

(i) kuhakikisha mahudhurio ya mashahidi na kuwahoji baada ya kula kiapo, kukiri au vinginevyo;

(ii) kulazimisha utoaji nyaraka; na

(iii) kutoa agizo au ombi kuwahoji mashahidi ng’ambo.

Wananchi kupata nafasi na kushiriki 135. (1) Bunge -

(a) litaendesha shughuli zake kwa uwazi, na kufanya vikao vyake na vya kamati zake, hadharani; na

(b) litafanikisha kushiriki kwa wananchi katika masuala ya kutunga sheria na shughuli nyingine za Bunge na kamati zake.

(2) Licha ya Ibara ndogo (1), hatua muafaka zinaweza kuchukuliwa -

(a) kudhibiti wananchi kupata nafasi, pamoja na vyombo vya habari kufikia Bunge na kamati zake; na

(b) kuwezesha mtu yeyote kupekuliwa, na inapowezekana, kukatazwa kuingia au kutolewa Bungeni.

(3) Bunge halitawazuia wananchi, au vyombo vya habari vyovyote kuhudhuria kwenye vikao au kamati zake chini ya ibara hii isipokuwa iwe ni haki na kuna sababu za kutosha kufanya hivyo katika jamii yenye uwazi na demokrasia.

Uwezo, haki na kinga 136. (1) Kutakuwa na uhuru wa kuzungumza na mjadala Bungeni na uhuru huo

hautoingiliwa au kuhojiwa katika mahakama yoyote.

(2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Bunge, Bunge linaweza kutoa uwezo, haki na kinga kwa Bunge, kamati zake pamoja na wajumbe wake.

Sehemu ya Tano – Mengineyo

Masjala ya Sheria 137. (1) Bunge litaunda -

(a) Masjala ya Sheria ya umma, ambayo itawekwa kwa lugha zote rasmi, katika maandishi ya kuonekana na ya Breli, chini ya ulinzi wa Spika wa Bunge; na

(b) utaratibu wa ziada kuhusu kuanza kutumika, uchapishaji na usambazaji wa sheria.

(2) Nakala ya kila sheria itahifadhiwa kwa usalama kwenye Masjala ya Sheria.

Page 78: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

78

(3) Nakala ya sheria iliyowekwa kwenye Masjala, na iliyoidhinishwa na karani kuwa ni sahihi, ni ushahidi wa kutosha wa masharti ya sheria hiyo.

(4) Pakitokea mgongano baina ya nakala za sheria za lugha tofauti, nakala iliyotiwa sahihi na Rais au kwa niaba ya Bunge au baraza la serikali iliyosambaziwa mamlaka ndio itakayokuwa na nguvu.

(5) Serikali itahakikisha kuwa sheria zinapatikana na kufikiwa -

(a) kwenye maktaba zote za umma; na

(b) katika Breli na njia nyingine za mawasiliano kwa ajili ya watu

wenye ulemavu wa kuona au mwingine.

Makao ya Bunge 138. (1) Kwa mujibu wa Ibara ndogo (2), makao ya Bunge yatakuwa Nairobi.

(2) Kikao cha Bunge kitafanyika sehemu yoyote ndani ya Kenya na kitaanza wakati ambao utaagizwa na Bunge.

(3) Kila bunge jipya linapochaguliwa, Rais, kupitia tangazo kwenye Gazeti, atateua mahali na tarehe, si zaidi ya siku saba baada ya kumalizika muda au muhula wa Bunge lililopita kwa kikao cha kwanza cha Bunge jipya.

Muhula na kuahirishwa Bunge 139. (1) Muhula wa Bunge ni miaka mitano kuanzia tarehe ya kikao cha kwanza

baada ya uchaguzi.

(2) Wakati wowote Jamhuri ikiwa katika vita, Bunge linaweza kuamua mara kwa mara, kwa azimio lililoungwa mkono kwa kura zisizopungua asilimia sitini na tano za wabunge wa kila Ukumbi, kuongeza muda wa Bunge kwa miezi isiyozidi sita kwa wakati mmoja.

(3) Muhula wa Bunge hautaongezwa chini ya Ibara ndogo (2) -

(a) kwa zaidi ya miezi kumi na miwili; au

(b) kabla ya muhula wake kumalizika baada ya uchaguzi kufanywa kwa mujibu wa Ibara ya 118(1).

(4) Kwa mujibu wa Ibara hii, Bunge litaahirishwa mnamo siku ya thelathini Novemba, kila mwaka, na kikao kinachofuata kitaanza mnamo Jumanne ya kwanza ya Februari mwaka unaofuata.

Tume ya Huduma ya Bunge 140. (1) Inaundwa Tume ya Huduma ya Bunge ambayo itakuwa na -

(a) mwenyekiti na naibu mwenyekiti waliyechaguliwa na Tume hiyo kutoka miongoni mwa wajumbe walioteuliwa kwa mujibu wa aya (b);

Page 79: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

79

(b) wajumbe saba walioteuliwa na Bunge kutoka miongoni mwa wajumbe wake ambao-

(i) wanne watateuliwa kutoka chama au muungano wa vyama vinavyounda Serikali, ambapo angalau wawili kati yao watakuwa wanawake; na

(ii) watatu watateuliwa na chama au muungano wa vyama visivyounda Serikali, ambapo angalau mmoja kati yao atakuwa mwanamke; na

(c) wajumbe wawili wa jinsia tofauti walioteuliwa na Bunge miongoni mwa watu ambao si wabunge na wana uzoefu wa masuala ya umma.

(2) Mjumbe wa Tume hii ataacha afisi -

(a) ikiwa mtu huyo ni mbunge-

(i) kutokana na muda wa Bunge kumalizika;

(ii) ikiwa ataacha kuwa mbunge; au

(iii) ikiwa hali itatokea kwamba, endapo hangekuwa mbunge hangestahiki kuchaguliwa hivyo;

(b) Ikiwa mtu huyo ni mjumbe wa kuteuliwa, baada ya kubatilishwa uteuzi wake na Bunge.

(3) Tume hii itakuwa na majukumu yafuatayo -

(a) kutoa huduma na vifaa ili kuhakikisha utendakazi bora na thabiti wa shughuli za Bunge;

(b) kubuni nyadhifa katika huduma za bunge na kuteua na kusimamia maafisa katika nyadhifa hizo;

(c) kutayarisha makadirio ya kila mwaka na matumizi ya fedha (yatakayogharamiwa na Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali) ya huduma ya Bunge na kudhibiti wa kibajeti wa huduma hiyo;

(d) kutekeleza pekee au kwa ushirikiano na mamlaka nyinginezo zinazohusika, kuendeleza fikra kamili ya demokrasia ya bunge; na

(e) kufanya mambo mengine -

(i) muhimu kwa maendeleo ya wabunge na watumishi wa Bunge; au

(ii) yaliyoagizwa na au chini ya Sheria.

(4) Katika kutekeleza uwezo wake au kutenda kazi zake chini ya Katiba hii, Tume haitakuwa chini ya muongozo au amri ya mtu au mamlaka yeyote.

Page 80: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

80

Page 81: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

81

SURA YA KUMI NA MBILI

MAMLAKA YA UTENDAJI

Sehemu ya kwanza – Kanuni za Mamlaka ya Tendaji

Kanuni za mamlaka ya utendaji 141. Uwezo wa Mamlaka ya utendaji utatekelezwa -

(a) kwa faida na manufaa ya watu na jamii za Kenya kwa njia

ambayo inaambatana na kanuni za kuwahudumia watu; na

(b) kwa njia ambayo inaambatana na madhumuni na malengo ya

Katiba hii na sheria.

Mamlaka Tendaji ya Rais

142. Mamlaka tendaji ya Jamhuri yamekabidhiwa Rais.

Sehemu ya Pili – Rais na Naibu Rais

Mamlaka ya Rais 143. (1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri.

(2) Rais atakuwa -

(a) ndiye Mkuu wa Taifa, Kiongozi wa Serikali, Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama wa Taifa;

(b) ni kielelezo cha umoja wa kitaifa, na ana wajibu wa –

(i) kuendeleza na kuimarisha umoja wa taifa;

(ii) kulinda ukuu wa Jamhuri;

(iii) kuendeleza na kuheshimu anuwai ya watu na jamii za Kenya; na

(c) ataitii, atailinda, na ataiheshimu Katiba hii na atahakikisha ulinzi wa haki za kibinadamu na haki za kimsingi na utawala wa sheria.

(3) Uwezo wa Rais utatekelezwa kwa mujibu wa Katiba hii na sheria.

Majukumu ya Kitaifa ya Rais 144. (1) Rais -

(a) atahutubia ufunguzi wa kila Bunge jipya lililochaguliwa;

(b) atahutubia kikao maalum cha Bunge mara moja kwa kila mwaka;

Page 82: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

82

(c) anaweza kuhutubia Bunge wakati mwingine wowote;

(d) mara moja kwa kila mwaka, -

(i) atatoa taarifa, katika hotuba yake kwa taifa juu ya hatua zote zilizochukuliwa na maendeleo yaliyopatikana katika kufanikisha malengo ya taifa, maadili na kanuni zilizowekwa katika Sura ya Tatu; na

(ii) atawezesha kuchapishwa katika Gazeti kwa undani hatua na maendeleo yaliyotajwa katika Ibara ndogo (1).

(2) Rais kwa mujibu wa Katiba hii atateua na anaweza kufuta uteuzi wa -

(a) Waziri Mkuu;

(b) Manaibu wawili wa Waziri Mkuu;

(c) Mawaziri;

(d) Manaibu waziri;

(e) Mtumishi mwingine yeyote wa Serikali au wa Umma ambaye Katiba au Sheria inamlazimu Rais kuteuwa, kufuta kazi au kumtoa afisini.

(f) Watumishi wengine wa umma ambao watateuliwa na Rais kwa mujibu wa Katiba au sheria.

(3) Baada ya idhini ya Baraza la Mawaziri, Rais anaweza -

(a) kutangaza hali ya hatari, kwa masharti ya Ibara ya 76; au

(b) kutangaza vita.

(4) Rais anaweza kuteua Tume za Uchunguzi.

(5) Licha ya Ibara ndogo (4), Tume ya Uchunguzi itakaoteuliwa kwa mujibu wa Ibara 204 (2), itateuliwa tu baada ya kuidhinishwa na Bunge.

(6) Rais atawasilisha ripoti ya tume ya uchunguzi iliyoteuliwa chini ya Ibara ndogo (4) mbele ya Bunge ndani ya siku ishirini na moja ya ya Rais kuipokea ripoti hiyo.

(7) Rais anaweza, baada ya kuidhinishwa na Bunge, kutia sahihi mikataba ya kuruhusu Jamhuri kufungamana na mikataba kulingana na Ibara 115 au makubaliano ya kimataifa.

(8) Rais -

(a) baada ya kuidhinishwa na Bunge, atateua makamishna wakuu, mabalozi, wawakilishi wa kidiplomasia na ukonseli;

(b) atapokea wawakilishi wa ukonseli na wakidiplomasia wa kigeni;

(c) atatoa msamaha chini ya Ibara ya 166; na

Page 83: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

83

(d) kufuatana na Sheria ya Bunge, atatunuku heshima kwa niaba ya wananchi na Jamhuri.

(9) Rais -

(a) atahakikisha kwamba wajibu wa kimataifa wa Jamhuri unatekelezwa kupitia utekelezaji wa mawaziri wanaohusika na kuwasilisha ripoti ya utekelezaji kwa Bunge kila mwaka;

(b) ataheshimu uhuru, kutopendelea kwa, na hadhi za maafisa wa serikali, mahakama, Tume za Kikatiba na vyombo vyengine vilivyoundwa na sheria na kuhakikisha kupatikana kwa na utekelezaji wao kama ilivyodhamiriwa na Katiba hii.

(10) Kwa mujibu wa Katiba hii na sheria nyengine yeyote, uwezo wa kubuni au kuanzisha na kufuta afisi za Jamhuri ya Kenya, wa kuteua na kufuta nyadhifa hizo, zimekabidhiwa Rais.

(11) Teuzi chini ya Ibara ndogo (10), zitaidhinishwa na Bunge.

Mipaka ya uwezo wa Rais 145. (1) Ibara ya hii itatumika kwa mtu anaeshikilia afisi ya Rais au aliyeruhusiwa

kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, kutekeleza uwezo wa Rais -

(a) katika kipindi kuanzia tarehe ya kura ya mwanzo katika uchaguzi wa Rais, na kumalizia pale Rais mteule atakaposhika madaraka.

(b) iwapo Rais hayupo kwa muda mfupi au anashindwa kutekeleza kazi zake, kama ilivyoelezwa na Ibara ya 160.

(2) Katika kipindi kilichotajwa na Ibara ya ndogo (1), mtu ambaye Ibara ya hii inamhusu hatotekeleza uwezo wa Rais kuhusiana na -

(a) upendekezaji au uteuzi wa majaji wa mahakama za juu za kumbukumbu;

(b) pendekezo, uteuzi au kufuta kazi afisa yeyote ambae anahitajika na Katiba hii au sheria kuteuliwa na Rais;

(c) uwezo wa kutoa msamaha; na

(d) uwezo wa kutoa tunzo za heshima kwa niaba ya wananchi wa Jamhuri ya Kenya.

Maamuzi ya Rais 146. Uamuzi wa Rais chini ya mamlaka ya Katiba hii au sheria nyingine yoyote

utakuwa kwa maandishi na utakuwa na muhuri na sahihi ya Rais.

Uchaguzi wa urais 147. (1) Uchaguzi wa Rais utakuwa kwa kupiga kura, na ni haki ya mtu mzima

mwenye umri wa kupiga kura kushiriki, kwa njia ya kura ya siri, na

Page 84: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

84

utafanywa kulingana na Sehemu hii na kwa Sheria yoyote ya Bunge inayodhibiti uchaguzi wa urais.

(2) Uchaguzi wa urais utafanywa -

(a) wakati mmoja na ule wa bunge chini ya Ibara 118 (1); au

(b) katika mazingira yaliyokusudiwa na Ibara ya 161.

Sifa za kufaa na kutofaa kuchaguliwa Rais 148. (1) Mtu anastahiki kupendekezwa kama mgombea wa urais ikiwa mtu huyo -

(a) ni raia wa Kenya kwa kuzaliwa;

(b) ana sifa za kuwa mgombea uchaguzi wa Bunge; na

(c) ameteuliwa -

(i) na chama cha kisiasa kilichosajiliwa; au

(ii) kama mgombea wa kujitegemea na wapiga kura wasiopungua elfu kumi wanaojumuisha angalau wapiga kura mia moja waliosajiliwa, kutoka kila wilaya.

(2) Mtu hatofaa kuteuliwa kuwa mgombea wa urais akiwa mtu huyo-

(a) anatii taifa la kigeni;

(b) anafanya kazi au anashikilia wadhifa wowote katika afisi ya huduma za umma, ikiwemo afisi ya jaji, hakimu au afisi nyingine ya mahakama, au afisi katika Jeshi la ulinzi la Jamhuri au katika mamlaka ya serikali ya wilaya;

(c) ni mjumbe wa Tume ya kikatiba;

(d) ni mgombea wa uchaguzi kama mbunge;

(e) amefukuzwa au kuondolewa katika afisi au amesita kuwa na afisi chini ya Ibara 96; au

(f) hastahiki kusimama kama mgombea wa ubunge.

Utaratibu wa uchaguzi wa Rais 149. (1) Ikiwa mgombea mmoja tu ndiye aliyeteuliwa kuwa Rais, basi mgombea

huyo atatangazwa kuwa Rais.

(2) Ikiwa watu wawili au zaidi wameteuliwa, basi uchaguzi utafanywa katika kila jimbo la uchaguzi kumchagua Rais.

(3) Katika uchaguzi wa urais -

(a) watu wote waliosajiliwa kama wapigakura katika uchaguzi wa ubunge wana haki ya kupiga kura;

Page 85: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

85

(b) uchaguzi utafanywa kwa kura ya siri mnamo siku iliyotajwa katika Ibara ya 156, kwa wakati, pahala na kwa namna ambayo itaelekezwa na au chini ya Sheria iliyotungwa na Bunge; na

(c) baada ya kuhesabu kura kwenye vituo vya kupigia kura, Tume ya Uchaguzi na Mipaka itatangaza matokeo.

(4) Mgombea wa Urais atakayepata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote zilizopigwa kwenye uchaguzi huo, na pia amepata, si chini ya asilimia ishirini na tano ya kura zilizopigwa katika zaidi ya nusu ya wilaya, atatangazwa kuwa Rais.

(5) Endapo hakuna mgombea aliyechaguliwa, uchaguzi mpya utafanywa ndani ya majuma matatu baada ya uchaguzi uliopita, na katika uchaguzi huo, wagombea watakuwa tu –

(a) mgombea aliyepata kura nyingi zaidi; na

(b) mgombea wa pili kupata kura nyingi zaidi,

na mgombea atakayepata kura za juu ndiye atakayetangazwa kuwa Rais.

(6) Uchaguzi wa urais utafutiliwa mbali na uchaguzi mpya kufanywa ikiwa mgombea -

(a) hajateuliwa kabla ya kumalizika muda uliopangwa kwa ajili ya kuwasilisha uteuzi;

(b) amekufa mnamo siku ya, au kabla ya, siku ya uchaguzi yenyewe kufanyika au kupangwa kufanyika; au

(c) ambaye angeweza, ila tu sababu amekufa, kutangazwa kwamba amechaguliwa kama Rais, kufa baada ya uchaguzi kuanza lakini kabla hajatangazwa kuwa amechaguliwa Rais.

(7) Uchaguzi mpya utafanywa kwa mujibu wa Ibara ndogo (6) ndani ya siku sitini za muda wa uchaguzi uliopita wa urais, kumalizika.

(8) Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka atawasilisha taarifa ya maandishi ya matokeo ya uchaguzi wa urais kwa Rais aliyopo madarakani na kwa Jaji Mkuu ndani ya siku saba baada ya uchaguzi kumalizika.

(9) Endapo mtu aliyechaguliwa Rais ni mbunge, Tume ya Uchaguzi na Mipaka itatangaza kiti cha mtu huyo cha ubunge kuwa wazi na kunako siku thelathini, itaanda uchaguzi katika eneo hilo la ubunge kujaza nafasi hiyo.

Masuala kuhusu uhalali wa uchaguzi wa urais 150. (1) Mtu anaweza kuwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Juu kupinga

kuchaguliwa kwa Rais mteule.

Page 86: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

86

(2) Malalamiko yatawasilishwa ndani ya siku saba baada ya tarehe ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa urais, na Tume ya Uchaguzi na Mipaka.

(3) Mahakama ya Juu ndani ya siku saba baada ya malalamiko kuwasilishwa itatoa uamuzi wake.

Kushika madaraka ya urais 151. Rais mteule -

(a) atashika madaraka ya urais -

(i) Jumanne ya kwanza baada ya siku ishirini na moja kumalizika tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais na Tume ya Uchaguzi na Mipaka; au

(ii) ndani ya siku saba baada ya uamuzi wa Mahakama ya Juu kuhusu malalamiko kuhusiana na uchaguzi huo yaliyowasilishwa chini ya Ibara ya 150; na

(b) atashika wadhifa wake kwa kula na kutii –

(i) kiapo au tamko la dhati la utiifu; na

(ii) kiapo cha utiifu au tamko la dhati la utekelezaji wa majukumu ya afisi,

kama ilivyoagizwa katika Jedwali ya Pili, mbele ya Jaji Mkuu au Jaji ya Mahkama ya Juu mnamo tarehe ambapo kipindi cha ya Rais aliyepo kinamalizika.

Muhula wa Rais madarakani 152. (1) Rais atakuwa madarakani kwa muhula usiozidi miaka mitano, kuanzia

tarehe ya kushika madaraka ya uongozi.

(2) Mtu hatoshika madaraka ya urais kwa zaidi ya mihula miwiili.

(3) Mtu atakayeshikilia madaraka ya urais kwa kutumikia mfululizo kwa angalau miaka miwili unusu atachukuliwa kuwa ametumikia muhula kamili.

Kinga ya Rais dhidi ya mashtaka 153. (1) Hakuna mashtaka yoyote ya jinai yatakayoanzishwa au kuendelezwa

katika mahakama yoyote dhidi ya Rais akiwa kazini au mtu anayetekeleza wadhifa wa afisi hiyo.

(2) Hakuna mashtaka yoyote ya madai yatakayoanzishwa katika mahakama yoyote dhidi ya Rais au mtu anayetekeleza wadhifa wa afisi hiyo wakati akiwa kazini kuhusiana na kitu chochote kilichotendwa au kutotendwa katika kutekeleza uwezo wao chini ya Katiba hii.

Page 87: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

87

(3) Iwapo sheria imewekwa ambayo inaweka muda maalum ambao mashtaka yanaweza kufunguliwa dhidi ya mtu, muda wote ambapo mtu alikuwa ni Rais au kufanya kazi za Rais hautazingatiwa katika kuhesabu muda uliowekwa na sheria hiyo.

(4) Kwa mujibu wa Ibara hii, Rais yuko chini ya Katiba na Sheria.

Kumwondoa Rais kwa sababu ya kutoweza kazi 154. (1) Mbunge anaweza, katika kikao chochote cha Bunge, kupendekeza hoja ya

kumwondoa Rais madarakani kwa kushindwa kufanya kazi kutokana na sababu ya ugonjwa wa kimwili au kiakili.

(2) Ikiamuliwa na zaidi ya nusu wajumbe wote wa Bunge kwamba suala la afya ya kimwili au kiakili ya Rais kutekeleza majukumu ya afisi yake linapaswa lichunguzwe, Spika, atamwarifu Jaji Mkuu ambae ndani ya siku saba za uamuzi huo, atateua tume maalum ya madaktari watano kwa mujibu wa sheria za Jamhuri –

(a) wanne kati yao watateuliwa na Bodi ya Matabibu na Madaktari wa Meno; na

(b) mmoja atateuliwa na Rais au jamaa yake wa karibu au mtu wa familia ya Rais,

Ili wachunguze jambo hilo.

(3) Bunge likiamua kuwa suala la uwezo wa Rais kiakili au kimwili kutekeleza majukumu yake lichunguzwe, Rais ataendelea kutekeleza wajibu wake hadi mtu mwingine ashike wadhifa wa Rais, au tume maalum iliyoteuliwa chini ya Ibara ya ndogo (2) itoe taarifa kwamba Rais hawezi kutekeleza wadhifa wake, chochote kitakachotokea kwanza.

(4) Iwapo Jaji Mkuu hatoteua tume hiyo maalum ndani ya muda uliowekwa chini ya Ibara ya ndogo (2), Spika atateua tume hiyo maalum ndani ya siku saba.

(5) Tume hiyo maalum litachunguza na kutoa taarifa -

(a) kwa Jaji Mkuu ndani ya siku kumi na nne ya uteuzi na kupeleka nakala moja kwa moja kwa Spika; au

(b) kwa Spika ndani ya siku kumi na nne ya uteuzi wa tume hiyo maalum iliyoteuliwa na Spika.

(6) Jaji Mkuu au Spika, kulingana na hali itakavyokuwa, atathibitisha kwa maandishi na ataiwasilisha shahada pamoja na taarifa ya tume hiyo maalum mbele ya Bunge.

(7) Pale ambapo taarifa ya tume hiyo maalum inaeleza kwamba Rais anaweza kumudu kufanya kazi zake, Spika ataliarifu Bunge.

Page 88: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

88

(8) Ikiwa tume hiyo maalum imetoa taarifa kuwa Rais hawezi kutekeleza majukumu, Bunge likiungwa mkono na kura za zaidi ya nusu ya wajumbe wote, litaidhinisha uamuzi wa Tume hiyo na baada ya kuidhinisha huko Rais atatoka afisini.

Kushitakiwa na kuondolewa kwa Rais 155. (1) Mbunge anaweza, wakati wowote, kuwasilisha kwa maandishi, kwa

Spika, ilani aliyoitia saini Mbunge huyo, akieleza kwamba ana nia ya kupendekeza kushtakiwa Rais kwa sababu ya -

(a) kukiuka vibaya masharti ya Katiba hii; au

(b) mwenendo mbaya unaoathiri maslahi ya Jamhuri au mwenendo ambao umeipatia sifa mbaya afisi ya Rais,

na kueleza kwa ukamilifu sababu hizo.

(2) Spika, ikiwa Bunge, -

(a) linakutana wakati huo au limeitwa kukutana, anaweza kuwasilisha hoja kwa Bunge ili ishughulikiwe ndani ya siku saba; au

(b) halikutani, atalitaka kukutana ndani ya kipindi cha muda wa siku ishirini na moja baada ya kufahamishwa kuhusu hoja hiyo ili liishughulikie.

(3) Ikiwa hoja chini ya Ibara ya ndogo (2), itapitishwa na zaidi ya asilimia

hamsini ya wabunge wote, Bunge, kulingana na kanuni za Bunge, litachagua kamati maalum yenye wabunge kumi na tatu kuchunguza jambo hilo.

(4) Kamati hiyo maalum itachunguza suala hilo na itatoa taarifa ndani ya siku kumi kwa Bunge kama kuna ithibati kuhusu madai hayo dhidi ya Rais.

(5) Rais atakuwa na haki kuhudhuria na kuwakilishwa mbele ya kamati hiyo maalum wakati wa uchunguzi.

(6) Ikiwa kamati hiyo maalum itaarifu kuwa madai yoyote dhidi ya Rais hayana ithibati, hakuna hatua zaidi itakayochukuliwa chini ya Ibara ya hii kuhusu madai hayo.

(7) Ikiwa kamati hiyo maalum itaarifu kuwa madai yoyote dhidi ya Rais yametolewa ithibati, Bunge itapiga kura ya kumuondoa Rais, na Rais atatenguliwa madarakani ikiwa asilimia sabini na tano ya wajumbe watapiga kura kuunga mkono madai ya kumuondoa Rais.

Afisi ya Rais kuwa wazi 156. (1) Afisi ya Rais itakuwa wazi endapo mhudumu wa afisi hiyo –

(a) amefariki;

(b) amejiuzulu kwa kumuandikia Spika; au

Page 89: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

89

(c) ametolewa madarakani chini ya Katiba hii.

(2) Afisi ya Rais itakapokuwa wazi, Naibu Rais atachukua majukumu ya Urais.

(3) Ikiwa afisi za Rais na Naibu Rais zitakuwa wazi, Spika atachukua majukumu ya afisi ya Rais.

(4) Ikiwa pana nafasi kwa mujibu wa Ibara ya ndogo (3), Tume ya Uchaguzi na Mipaka itaitisha uchaguzi wa urais ndani ya siku sitini tokea nafasi hiyo kuwa wazi kwa uchaguzi wa Naibu Rais.

Uwezo wa msamaha wa Rais 157. (1) Kutakuwa na uwezo wa msamaha wa Rais utakaotolewa baada ya

kufanywa maombi na mtu yeyote kwa Rais kufuatana na ushauri wa kamati iliyotajwa katika Ibara ya ndogo (3), na uwezo huo wa msamaha hautokasimiwa kwa mtu yeyote.

(2) Bunge litatunga Sheria za kuunda vigezo vitakavyotumiwa na Kamati ya Ushauri iliyotajwa katika Ibara ya ndogo (3) katika kuandaa ushauri wake kwa mujibu wa Ibara ya ndogo (1).

(3) Ili kutekeleza uwezo wa msamaha chini ya Ibara ndogo (1), kutakuwa na Kamati ya Ushauri ya Uwezo wa Rais wa Msamaha, ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao -

(a) Mwanasheria Mkuu;

(b) Waziri anayehusika na Huduma ya Kenya ya Kurekebisha

(c) Tabia;

(d) daktari wa utabibu aliyeteuliwa na Halmashauri ya Madaktari wa Matibabu na Madaktari wa Meno;

(e) kiongozi wa huduma ya majaribio;

(f) mtu aliyeteuliwa na Tume ya Haki za Kibinadamu na Haki za Kiutawala;

(g) watu watatu, kila mmoja wao awe ameteuliwa na mashirika yanayowakilisha dini za Kikristo, Kiislamu na Kihindu; na

(h) Wakili mmoja aliyefanya kazi kwa angalau miaka kumi na mitano, aliyeteuliwa na Chama cha Wanasheria wa Kenya.

(4) Wajumbe wa Kamati ya Ushauri walioteuliwa kwa mujibu wa Ibara ndogo (3), (c), (e), (f) na (g) wataendelea kuwa wajumbe wa Kamati ya Ushauri, mradi waendelee kuwa na sifa, kwa mda wa mwaka mmoja na wanaweza kuendelea tena na ujumbe wao kwa awamu mbili zaidi za mwaka mmoja.

(5) Kamati ya Ushauri inaweza kufanya kazi licha ya kuwa na nafasi tupu katika ujumbe wake.

Page 90: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

90

(6) Kamati ya Ushauri inaweza kudhibiti utaratibu wake wa kufanya kazi.

(7) Katika kutekeleza uwezo uliotolewa na Ibara ndogo (1), Rais anaweza -

(a) kutoa msamaha kwa mtu aliyehukumiwa kwa hatia, bila masharti au kwa masharti halali;

(b) kuahirisha kwa kipindi maalum ama kisicho maalum, utekelezaji wa adhabu iliyotolewa kwa mtu;

(c) kubadilisha adhabu kwa kutoa adhabu isiyokali kwa kosa alilofanya mtu; au

(d) kupunguza adhabu yote au sehemu ya adhabu aliyopewa mtu kwa kosa alilofanya.

(8) Kamati ya Ushauri inaweza kuzingatia maoni ya waathirika wa kosa wanapofikiria kupendekeza kwamba Rais atumie uwezo wake wa msamaha.

Afisi ya Naibu Rais 158. (1) Kutakuwa na Naibu Rais wa Jamhuri.

(2) Kila mgombea katika uchaguzi wa urais atamteua mtu, aliye na sifa zote za kustahiki kuchaguliwa kuwa Rais, kama mgombea wa Naibu Rais.

(3) Tume ya Uchaguzi na Mipaka haitaandaa uchaguzi tofauti wa Naibu Rais lakini itamtangaza mgombea aliyeteuliwa na mtu atakayechaguliwa kuwa Rais, kuwa amechaguliwa Naibu Rais.

(4) Endapo mtu aliyechaguliwa Naibu Rais ni mbunge, Tume ya Uchaguzi na Mipaka itatangaza kiti cha mtu huyo cha ubunge kuwa wazi na kunako siku thelathini, itaanda uchaguzi katika eneo hilo la ubunge kujaza nafasi hiyo.

(5) Mtu atakayetangazwa kuchaguliwa kuwa Naibu Rais atakula kiapo au kutoa tamko la dhati na kiapo au tamko la dhati kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya afisi yake, kama ilivyoagizwa kwenye Jedwali ya Pili, mbele ya Jaji Mkuu au Jaji wa Mahakama ya Juu.

(6) Muhula wa Naibu Rais utaanza wakati Rais anapochukua madaraka na utamalizika -

(a) wakati Rais afuataye anapochukua madaraka; au

(b) Naibu Rais anapokuwa Rais; au

(c) kwa kujiuzulu, kufariki ama kuondolewa madarakani.

Page 91: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

91

(7) Naibu Rais anaweza kujiuzulu wakati wowote kupitia kwa taarifa ya maandishi kwa Rais na kujiuzulu huko kutaanza tarehe na wakati uliowekwa kwenye taarifa yake, au ikiwa hakuna tarehe na wakati kwenye maandishi, kuanzia saa sita mchana mnamo siku ifuatayo.

(8) Masharti ya Ibara ya 154 na 155 kuhusu kuondolewa kwa Rais madarakani na kushtakiwa kwa Rais, pamoja na mabadiliko yanayostahiki, yatatumika kwa afisi ya Naibu Rais.

(9) Naibu Rais hatashika madaraka kwa zaidi ya mihula miwili.

(10) Mtu atakayekuwa Naibu Rais kupitia Ibara 159 na ambaye kwa mfululizo ameendelea kushika madaraka ya Naibu Rais kwa angalau miaka miwili unusu katika kipindi cha urais atachukuliwa kuwa amehudumu muhula kamili.

Afisi ya Naibu Rais kuwa wazi 159. (1) Afisi ya Naibu Rais itakuwa wazi –

(a) ikiwa mhudumu wa afisi hiyo amefariki au kujiuzulu;

(b) ikiwa mhudumu wa afisi hiyo ametolewa madarakani chini ya

Katiba hii;

(c) endapo mhudumiwa wa afisi hiyo amechukua madaraka ya

Rais chini ya Ibara ya 156; au

(d) wakati ambapo mtu anaefuatia kuchaguliwa kama Naibu Rais anachukua mamlaka yake.

(2) Ikiwa afisi ya Naibu Rais ni wazi, Rais atamteua mgombea aliye na sifa zinazohitajika kuambatana na Ibara ya 158 ashike wadhifa wa Naibu Rais.

(3) Uteuzi chini ya Ibara ndogo (2) utakuwa wa maandishi na utakabidhiwa Spika wa Bunge ndani ya kipindi cha siku kumi na nne za afisi kuwa wazi.

(4) Bunge linaweza, kwa kupitisha azimio lililoungwa mkono na thuluthi mbili ya wajumbe wa Bunge, kuidhinisha mtu aliyeteuliwa chini ya Ibara hii kuwa Naibu Rais.

(5) Ikiwa Bunge halitaidhinisha uteuzi huo chini ya Ibara ndogo (4), Rais atateua tena chini ya Ibara ndogo (2).

(6) Ikiwa Bunge halitaidhinisha uteuzi chini ya Ibara ndogo (5), Rais atateua mtu kuwa Naibu Rais.

(7) Mtu ambaye uteuzi wake umeidhinishwa chini ya Ibara ndogo (4) au ameteuliwa kama Naibu Rais chini ya Ibara ndogo (6), atashika wadhifa kwa utaratibu uliofafanuliwa katika Ibara ya 158(5).

Page 92: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

92

(8) Muhula wa Naibu Rais anayeidhinishwa chini ya Ibara hii utaanzia siku Naibu Rais anaposhika madaraka na utakamilika kwa njia iliyofafanuliwa katika Ibara ya 158(6).

Majukumu ya Naibu Rais 160. (1) Naibu Rais atakuwa msaidizi mkuu wa Rais katika kutekeleza majukumu

ya Rais.

(2) Naibu Rais atatekeleza majukumu aliyopewa na Katiba hii, na majukumu mengine yoyote anayoweza kupewa na Rais.

(3) Naibu Rais atatekeleza wajibu kwa niaba ya Rais ikiwa Rais ni mgonjwa au endapo hayupo nchini kwa muda.

Kufariki kabla ya kushika madaraka 161. (1) Ikiwa mtu aliyechaguliwa kuwa Rais atafariki kabla ya kuchukua

madaraka, mtu aliyetangazwa kuwa Naibu Rais atakuwa Rais na afisi ya Naibu Rais itakuwa wazi.

(2) Ikiwa mtu aliyetangazwa kuchaguliwa kuwa Naibu Rais atafariki kabla ya kushika madaraka, afisi ya Naibu Rais itatangazwa kuwa wazi baada ya mtu aliyetangazwa kuchaguliwa kuwa Rais kuchukua madaraka.

(3) Ikiwa watu wote wawili waliotangazwa kuchaguliwa kuwa Rais na Naibu Rais watafariki kabla ya kushika madaraka, Spika atashikilia madaraka ya Rais na Tume ya Uchaguzi na Mipaka itaandaa uchaguzi mpya ndani ya kipindi cha siku sitini tangu kifo cha pili.

Malipo na marupurupu ya Rais na Naibu Rais 162. (1) Rais na Naibu Rais watalipwa malipo na marupurupu yao kutoka Mfuko

Mkuu wa Fedha za Serikali.

(2) Malipo, marupurupu na stahiki za Rais au Naibu Rais hazitabadilishwa kwa namna ambayo itawaathiri vibaya wakati wakiwa wanashikilia nafasi zao au wakistaafu.

(3) Marupurupu ya kustaafu yanayostohili kulipwa Rais na Naibu Rais wastaafu, pamoja na nyenzo nyingine wanazopata hazitabadilishwa kwa namna ambayo itawaathiri vibaya katika uhai wao.

Sehemu ya Tatu – Baraza la Mawaziri

Uteuzi na Majukumu ya Waziri Mkuu 163. (1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri, ambaye atateuliwa na Rais

kulingana na masharti ya Sehemu hii.

(2) Waziri Mkuu atawajibika kwa Rais na, chini ya muongozo au amri ya Rais kwa ujumla -

(a) atakuwa kiongozi wa shughuli za serikali bungeni;

Page 93: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

93

(b) atatekeleza au kusababisha kutekelezwa kazi nyingine kama atakavyoamrishwa na Rais;

(c) itatekeleza majukumu mengine kama yanavyoagizwa na Katiba

hii na majukumu mengine kama Rais atakavyompatia.

(3) Ikiwa Waziri Mkuu hayupo, Naibu mmoja wapo wa Waziri Mkuu, aliyeteuliwa na Waziri Mkuu atatekeleza majukumu ya Waziri Mkuu.

Uteuzi wa Waziri Mkuu 164. (1) Ndani ya siku saba tangu kuitisha vikao vya Bunge, baada ya uchaguzi, au

ikihitajika kujaza nafasi ya Waziri Mkuu, isipokuwa wakati wa kura ya kutokuwa na imani, Rais atampendekeza mbunge mmoja kuteuliwa kama Waziri Mkuu.

(2) Baada ya kupokea pendekezo kutoka kwa Rais kuambatana na masharti ya Ibara ndogo (2), Spika ataitisha kikao cha Bunge na kulijulisha kuhusu uteuzi uliopendekezwa na Rais.

(3) Ndani ya siku saba baada ya Spika kupokea pendekezo kutoka kwa Rais, Spika ataitisha upigaji kura katika Bunge kuidhinisha kuteuliwa kwa mtu aliyependekezwa na Rais.

(4) Kura inayotazamiwa katika Ibara ndogo (3) itapita iwapo itaungwa mkono na kura za zaidi ya asilimia hamsini ya wajumbe wa Bunge.

(5) Iwapo Bunge halitaidhinisha uteuzi wa mtu aliyependekezwa na Rais, Rais atampendekeza Mbunge mwengine kuteuliwa kama Waziri Mkuu.

(6) Ikiwa hakuna yeyote kati ya watu walioelezwa katika Ibara ndogo (1) na (5), ambaye ameidhinishwa na Bunge kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, Rais atamteua Mbunge mwengine awe Waziri Mkuu.

Muhula wa kuwa madarakani 165. Muhula wa Waziri Mkuu utaendelea hadi -

(a) Waziri Mkuu anapofariki, anapojiuzulu, au anapoondolewa madarakani; au

(b) mtu mwingine anayeteuliwa Waziri Mkuu baada ya uchaguzi anapochukua madaraka.

Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu 166. (1) Waziri Mkuu anaweza kujiuzulu kutoka madarakani kwa kuwasilisha

taarifa ya maandishi kwa Rais.

(2) Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu kunaanza -

(a) tarehe na wakati uliowekwa kwenye taarifa hiyo, ikiwa paliwekwa tarehe na wakati; au

Page 94: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

94

(b) saa sita mchana siku ifuatayo siku ilipowasilishwa, ikiwa vinginevyo.

Afisi ya Waziri Mkuu na Mawaziri kuwa wazi 167.Afisi ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu, Waziri au Naibu Waziri itakuwa wazi -

(a) Rais anapoamuru hivyo;

(b) ikiwa mhudumu wa afisi amefariki au kujiuzulu; au

(c) wakati mtu mwengine aliyeteuliwa kuchukua afisi hiyo

anapochukua madaraka.

Baraza la Mawaziri 168. (1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri litakalojumuisha -

(a) Rais;

(b) Naibu Rais;

(c) Waziri Mkuu;

(d) Manaibu wawili wa Waziri Mkuu;

(e) Mawaziri;

(f) Mwanasheria Mkuu; na

(g) Kiranja Mkuu wa Serikali Mbungeni.

(2) Mwanasheria Mkuu na Kiranja Mkuu wa Serikali Bungeni, watakuwa mawaziri kutokana na afisi zao.

(3) Kutakuwa na idadi ya mawaziri kama itakavyoamuliwa na Bunge au ikiwa hakuna masharti yoyote ya Bunge, idadi itakayoamuliwa na Rais.

(4) Rais atateua manaibu wawili wa Waziri Mkuu, Mawaziri na Naibu Mawaziri.

(5) Rais anaweza kuteua idadi isiyozidi asilimia ishirini ya mawaziri kutoka watu ambao si wabunge lakini ambao wanastahiki kuwa wabunge.

(6) Mtu atakayeteuliwa Naibu Waziri Mkuu, Waziri au Naibu Waziri -

(a) anaweza kujiuzulu kwa kuwasilisha taarifa kwa maandishi kwa Rais; na

(b) ataendelea kuwa afisini hadi -

(i) anapofariki, anapojiuzulu, au anapoondolewa kwenye madaraka; au

(ii) mtu mwingine anapoteuliwa kuchukua wadhifa huo baada ya uchaguzi wa Bunge.

(7) Kujiuzulu kunakoelezwa katika Ibara ndogo (3) kunaanzia -

Page 95: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

95

(a) tarehe na wakati uliotajwa kwenye taarifa kama ipo; au

(b) saa sita mchana siku ifuatayo siku ilipowasilishwa, ikiwa vinginevyo.

Katibu wa Baraza la Mawaziri 169. (1) Kutakuwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri.

(2) Katibu wa Baraza la Mawaziri atateuliwa na Rais kwa idhini ya Bunge.

(3) Afisi ya Katibu wa Baraza la Mawaziri itakuwa afisi ya umma.

(4) Katibu wa Baraza la Mawaziri -

(a) atakuwa na dhamana ya afisi ya Baraza la Mawaziri;

(b) atakuwa na jukumu, kwa mujibu wa maelekezo ya Baraza la Mawaziri, la kupanga shughuli na kuweka kumbukumbu za Baraza la Mawaziri.

(c) atawasilisha maamuzi ya Baraza la Mawaziri kwa watu wanaohusika au mamlaka; na

(d) kutekeleza wajibu wowote mwingine kama atakavyoelekezwa na Baraza la Mawaziri.

(5) Katibu wa Baraza la Mawaziri -

(a) anaweza kuondolewa madarakani na Rais; au

(b) anaweza kujiuzulu kutoka afisini kwa kutoa taarifa ya maandishi kwa Rais, na taarifa ya kujiuzulu inaanza kufanya kazi mara tu Rais akiipokea.

(6) Mara tu Serikali mpya ikikabidhiwa madaraka, mtu anayefanya kazi ya Katibu wa Baraza la Mawaziri ataacha kushika wadhifa huo.

Maamuzi, majukumu na uwajibikaji wa Baraza la Mawaziri 170. (1) Baraza la Mawaziri litakutana angalau mara moja kwa mwezi.

(2) Akidi ya mkutano wa Baraza la Mawaziri itakuwa nusu ya wajumbe wa Baraza la Mawaziri.

(3) Uamuzi wa Baraza la Mawaziri utakuwa kwa maandishi.

(4) Uamuzi wa Baraza la Mawaziri hautokuwa halali na hautotekelezwa ila ukiwa na sahihi na Rais.

(5) Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wanawajibika kwa ujumla na pia

kibinafsi, kwa Bunge kwa ajili ya–

(a) utekelezaji wa uwezo wao na utekelezaji wa majukumu yao;

(b) usimamizi na utekelezaji wa sheria walizopewa.

Page 96: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

96

(6) Waziri atahudhuria vikao vya Bunge, au Kamati ya Bunge atakapotakiwa kufanya hivyo, na kujibu maswali yoyote kuhusu suala lolote alilokabidhiwa kushughulikia.

(7) Wajumbe wa Baraza la Mawaziri watatoa taarifa kamilifu na ya kawaida kwa Bunge kuhusiana na mambo yaliyopo katika mamlaka yao.

Ugawaji wa majukumu 171. Rais -

(a) atatoa na kuhamisha majukumu kwa ajili ya utekelezaji na usimamizi

wa sheria yoyote ya Bunge kwa -

(i) Naibu Rais;

(ii) Waziri Mkuu;

(iii) Naibu Waziri Mkuu;

(iv) Waziri;

(v) Naibu Waziri; na

(b) anaweza kumpa Naibu Rais, Waziri Mkuu, Naibu Waziri, Naibu

Waziri Mkuu, Waziri au Naibu Waziri uwezo au kazi pale ambapo muhudumu ya afisi hiyo hayupo kazini au kwa muda hawezi kufanya kazi zake au kutekeleza uwezo wake.

Sehemu ya Nne – Maafisa Wengine wa Serikali

Makatibu Wakuu 172. (1) Inaundwa afisi ya Katibu Mkuu, ambayo ni afisi ya umma.

(2) Kila Wizara ya Serikali itakuwa chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu.

Kuteuliwa na kufutwa kazi kwa Makatibu Wakuu

173. (1) Katibu Mkuu atateuliwa na Rais na kuidhinishwa na Bunge.

(2) Katibu Mkuu -

(a) anaweza kuondolewa madarakani na Rais; au

(b) anaweza kujiuzulu kutoka wadhifa wake kwa kutoa taarifa ya maandishi kwa Rais, na kujiuzulu huko kutaanza taarifa hiyo itakapopekelewa Rais.

Mwanasheria Mkuu 174. (1) Inaundwa Afisi ya Mwanasheria Mkuu, itakayokuwa afisi ya huduma ya

umma.

(2) Mwanasheria Mkuu atateuliwa na Rais na kuidhinishwa na Bunge.

Page 97: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

97

(3) Sifa za mtu anayestahili kuteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu, ni kama zile za anayestahiki kuteuliwa katika afisi ya Jaji Mkuu.

(4) Mwanasheria Mkuu ndiye mshauri mkuu wa kisheria wa Serikali.

(5) Mwanasheria Mkuu atakuwa na wajibu wa -

(a) kuandika, kupitia, na kupendekeza kuidhinishwa (au vinginevyo), maafikiano, mapatano, mikataba na nyaraka kwa jina lolote zitakavyoitwa ambazo Serikali ni mshiriki au Serikali ina maslahi, kama ilivyofafanuliwa na Sheria.

(b) kuwakilisha Serikali mahakamani au kwenye kesi nyingine za kisheria ambapo Serikali ni mshiriki, isipokuwa kesi za jinai; na

(c) kutunga sheria, pamoja na sheria ndogo, kwa niaba ya Serikali.

(6) Mwanasheria Mkuu atakuwa na mamlaka, kwa idhini ya mahakama, kuhudhuria mashtaka ya madai ambapo Serikali si mshiriki, kama rafiki wa mahakama;

(7) Mwanasheria Mkuu ataendeleza, atalinda na utadumisha utawala wa sheria na kulinda maslahi ya umma.

(8) Uwezo wa Mwanasheria Mkuu unaweza kutekelezwa na yeye mwenyewe au kupitia maafisa wa chini yake watakaotekeleza kama walivyoagizwa kijumla au kimahsusi na Mwanasheria Mkuu.

(9) Katika kutekeleza wajibu wake, Mwanasheria Mkuu hataelekezwa au kudhibitiwa na mtu au mamlaka yoyote.

(10) Mwanasheria Mkuu atakuwa madarakani kwa muhula wa miaka mitano na atastahiki kuteuliwa tena kwa muhula mmoja mwengine wa miaka mitano.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma 175. (1) Inaundwa Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma itakayokuwa afisi

katika huduma ya umma.

(2) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma atateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya Huduma za Umma na kwa kuidhinishwa na Bunge.

(3) Sifa ya mtu anayestahiki kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ni sawa na sifa za mtu anayestahiki kuteuliwa kama jaji wa Mahakama Kuu.

(4) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma atakuwa na uwezo wa kumwelekeza Inspekta Generali wa Huduma ya Polisi ya Kenya kuchunguza taarifa au madai ya makosa ya jinai.

Page 98: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

98

(5) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma atatekeleza uwezo wa Serikali wa kushtaki na anaweza -

(a) kuanzisha na kuendesha mashtaka ya jinai dhidi ya mtu yeyote mahakamani (isipokuwa mahakama ya kijeshi) kwa ajili ya hatia inayodaiwa kufanywa;

(b) kuchukua na kuendesha mashtaka yoyote ya jinai yaliyoanzishwa katika mahakama yoyote (isipokuwa mahakama ya kijeshi) yaliyotokana au kuendeshwa na mtu mwingine au mamlaka, kwa kibali cha mtu huyo, au mamlaka; na

(c) kuambatana na Ibara ndogo (6), kusimamisha wakati wowote kabla hukumu haijatolewa mashtaka yoyote ya jinai yaliyoanzishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma au kuchukuliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma chini ya aya (b).

(6) Iwapo usimamishaji ulioelezwa katika Ibara ndogo (5)(c) unatokea baada ya mshtakiwa kukamilisha utetezi wake, mshatakiwa ataachiliwa huru.

(7) Bunge linaweza kupitia Sheria, kutoa uwezo wa kushitaki kwa mamlaka nyingine mbali na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.

(8) Uwezo wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma unaweza kutekelezwa na yeye mwenyewe au kupitia maafisa wa chini yake watakaotekeleza kama walivyoagizwa kijumla au kimahsusi.

(9) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma hatahitaji -

(a) idhini ya mtu yeyote wala mamlaka ili kuanzisha taratibu za mashtaka ya jinai; na

(b) katika utekelezaji wa uwezo wake au wajibu wake, na hataelekezwa au kudhibitiwa na mtu yeyote au mamlaka.

(10) Katika kutekeleza uwezo wake chini ya Ibara hii, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ataongozwa na maslahi ya umma, nia ya utekelezaji wa haki na haja ya kuzuia matumizi mabaya ya taratibu za kisheria.

(11) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma atakuwa madarakani kwa muhula wa miaka kumi na hatastahiki kuteuliwa tena.

Wakili wa Umma 176. (1) Inaundwa afisi ya Wakili wa Umma itakayokuwa afisi kwa huduma ya

umma.

(2) Wakili wa Umma atateuliwa na Rais kufuatia mapendekezo ya Tume ya Huduma ya Umma pamoja na idhini ya Bunge.

(3) Sifa za kuteuliwa kama Wakili wa Umma ni kama zile zinazohitajika kwa uteuzi wa Jaji wa Mahakama Kuu.

Page 99: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

99

(4) Kuambatana na Ibara ndogo (5), Wakili wa Umma atatoa ushauri wa kisheria na uwakilishi kwa watu wasioweza kumudu kugharamia huduma za kisheria.

(5) Bunge litatunga Sheria ambayo itaweka masharti kuhusu -

(a) usimamizi wenye kufaa, wenye matokeo na usimamizi na uendeshaji wenye uwazi wa afisi ya Wakili wa Umma;

(b) vigezo vitakavyotumika vya watu wanaostahiki kupewa msaada wa kisheria; na

(c) kuchapisha habari za kuwepo kwa msaada wa kisheria.

(6) Uwezo wa Wakili wa Umma unaweza kutekelezwa na yeye mwenyewe au kupitia maafisa wa chini yake watakaotekeleza kama watakavyoagizwa kijumla au kimahsusi na Wakili wa Umma.

(7) Katika kutekeleza wajibu wake, Wakili wa Umma hataelekezwa au kudhibitiwa na mtu au mamlaka yoyote.

(8) Wakili wa Umma atakuwa madarakani kwa muhula wa miaka kumi na hatastahiki kuteuliwa tena.

Kuondolewa afisini 177. (1) Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma au Wakili wa

Umma wanaweza kuondolewa afisini kwa sababu tu -

(a) kushindwa kutekeleza kazi zake za afisi kutokana na udhaifu au kimwili au kiakili;

(b) kukiuka masharti yaliyowekwa katika Sura ya Tisa;

(c) kufilisika;

(d) kutokumudu kazi; au

(e) mwenendo mbaya katika utendakazi au vinginevyo.

(2) Mtu anayetaka Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma au Wakili wa Umma kuondolewa madarakani anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa Tume ya Huduma ya Umma ambayo, licha ya Ibara ya 275(2)(b), atawasilisha kwa maandishi akieleza msingi wa kutaka afisa anayehusika kuondolewa madarakani.

(3) Tume ya Huduma ya Umma itachunguza malalamiko na ikitosheka kuwa yanadhihirisha msingi chini ya Ibara ndogo (1), atampelekea Rais malalamiko hayo.

(4) Ndani ya siku kumi na nne baada ya kupokea malalamiko, Rais atamsimamisha kazi afisa anayehusika, na -

(a) Ikiwa ni Mwanasheria Mkuu, atateua mahakama

maalum yenye -

Page 100: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

100

(i) Spika kama mwenyekiti;

(ii) majaji watatu wanaohudumu au waliohudumu kama Jaji Wakuu au Jaji kwenye Mahakama ya Juu kabisa katika mfumo wa kisheria wa Jumuiya ya Madola; na

(iii) watu wengine watatu wenye uzoefu wa masuala ya umma; na

(b) ikiwa ni Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma au Wakili wa Umma atateua mahakama maalum yenye -

(i) wajumbe wanne kutoka miongoni mwa watu ambao ni au wamewahi kuwa majaji wa Mahakama za Juu za kumbukumbu au wanastahiki kuteuliwa kama majaji wa Mahakama za Juu za kumbukumbu;

(ii) wakili mmoja mwenye uzoefu wa angalau miaka kumi na mitano aliyeteuliwa na Chama cha Wanasheria cha Kenya; na

(iii) watu wengine wawili wenye uzoefu wa masuala ya umma.

(5) Mahakama maalum itachunguza suala hilo na kutoa taarifa kuhusu ukweli na kutoa mapendekezo kwa Rais, atakayechukua hatua kuambatana na mapendekezo ya mahakama maalum.

(6) Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma au Wakili wa Umma aliyesimamishwa kazi chini ya Ibara ndogo (4) atastahili kupewa malipo na marupurupu yake hadi atakapoondolewa afisini.

(7) Mahakama maalum iliyoundwa chini ya Ibara ndogo 4(b) itachagua mwenyekiti kutoka miongoni mwa wajumbe wake na mahakama maalum zilizoteuliwa chini ya Ibara ndogo (4)(a) na (b) katika shughuli nyingine zote zitakuwa na jukumu la kujiwekea taratibu zao.

Page 101: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

101

SURA YA KUMI NA TATU

MFUMO WA MAHAKAMA NA SHERIA

Kanuni na muundo wa uwezo wa mahakama 178. (1) Uwezo wa mahakama unatokana na watu na utatumiwa na mahakama

pamoja na mahakama maalum kwa jina lao na kuambatana na mila, desturi na malengo yao, na kwa mujibu wa Katiba hii na sheria, kwa manufaa ya umma.

(2) Uwezo wa mahakama umekabidhiwa mahakama tu na mahakama maalum zilizoundwa chini ya Katiba hii.

(3) Katika kutekeleza sheria, mahakama zitaongozwa na kanuni kwamba -

(a) haki itafanywa kwa wote bila kuzingatia hadhi yao;

(b) haki haitacheleweshwa;

(c) fidia ya kutosha itatolewa kwa walioathirika na makosa;

(d) kupatanisha, kusuluhisha na kuamua makundi yanayozozana na kutumia mahakama za jadi, inapofaa, kutaendelezwa;

(e) haki itatolewa bila kuzingatia masuala ya kiutaratibu ya kitaaluma; na

(f) madhumuni na kanuni za Katiba hii zitalindwa na kuendelezwa.

(4) Katika utekelezaji wa majukumu, mahakama na maafisa wake na watu wanaohusika katika utekelezaji wa haki –

(a) watajitahidi kutoa huduma ya hali ya juu kwa umma;

(b) watazingatia kanuni zilizofafanuliwa katika Sura ya Tisa; na

(c) wataendelea kujielimisha kuhusiana na maendeleo ya kisasa katika sheria.

(5) Serikali itatoa raslimali zinazohitajika pamoja na fursa kuwawezesha watumishi wa Mahakama kutoa huduma ya kiwango cha juu.

Mfumo wa ngazi za mahakama na usimamizi wake 179. (1) Mahakama inajumuisha majaji wa mahakama za juu za kumbukumbu, na

maafisa wengine wa mahakama.

(2) Mahakama za kiwango cha juu za kumbukumbu ni Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufaa, na Mahakama Kuu.

(3) Mahakama za chini ni -

Page 102: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

102

(a) Mahakama za Mahakimu, Mahakama za Kikristo, Mahakama za Kadhi, Mahakama za Kihindu na mahakama nyingine za kidini;

(b) Mahakama za kijeshi;

(c) mahakama za kimila;

(d) mahakama nyengine za mashinani zitakazoundwa na sheria iliyotungwa na Bunge; na

(e) mahakama nyingine zozote zilizoundwa na zilizo chini ya Mahakama Kuu;

(4) Bunge, kwa kutunga sheria, litaunda mahakama yenye uwezo wa kusikiliza na kuamua kesi zinazotokana na waajiri na waajiriwa.

(5) Inaundwa Afisi ya Msajili Mkuu wa Mahakama na afisi nyingine za wasajili kama zitakavyoanzishwa na Tume ya Huduma ya Mahakama;

(6) Msajili Mkuu wa Mahakama atakuwa ndiye msimamizi mkuu na afisa mdhamini wa mahakama.

Uhuru wa mahakama 180. (1) Katika kutekeleza mamlaka ya mahakama, Idara ya mahakama itatekeleza

kazi zake kufuatana na Katiba na sheria pekee, wala haitadhibitiwa au kuongozwa na mtu mwingine au mamlaka yoyote.

(2) Afisi ya jaji wa mahakama ya juu ya kumbukumbu haitafutwa wakati yupo mtu alieshika madaraka ya kiti hicho cha jaji.

(3) Matumizi ya uendeshaji wa shughuli za Idara ya mahakama, ikiwa ni pamoja na malipo na marupurupu, yanayolipwa au kuhusiana na watumishi wa Idara ya mahakama, yatatoka kwenye Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali.

(4) Malipo na marupurupu, yanayolipwa, au kuhusiana na wafanyikazi wa Idara ya mahakama, hayatabadilishwa kwa namna ambayo itawaathiri vibaya.

(5) Afisa wa Idara ya mahakama hatashtakiwa kwa kitendo au kesi kuhusiana na kitu alichokifanya kwa nia njema katika kutekeleza majukumu yake.

Jaji Mkuu 181. (1) Inaundwa afisi ya Jaji Mkuu ambaye atakuwa kiongozi wa Idara ya

mahakama.

(2) Kwa mujibu wa Ibara ya 192 (1), Jaji Mkuu atatumika kwa kipindi cha miaka kumi au hadi afikishe umri wa miaka sabini, chochote kitakachotokea kwanza.

Page 103: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

103

(3) Kama Jaji Mkuu hajafikisha umri wa miaka sabini wakati wa kumalizika kipindi cha miaka kumi kilichotajwa katika Ibara ndogo (5), anaweza -

(a) kustaafu, endapo amefikisha umri wa miaka sitini;

(b) kuendelea kufanya kazi kama jaji wa Mahakama ya Juu, hata kama kuna idadi ya majaji inayohitajika katika Mahakama ya Juu; au

(c) kujiuzulu kazi yake.

Naibu Jaji Mkuu 182 Inaundwa afisi ya Naibu wa Jaji Mkuu ambaye atakuwa msaidizi mkuu wa

Jaji Mkuu.

Mahakama ya Juu 183. (1) Inaundwa Mahakama ya Juu, itakayokuwa na -

(a) Jaji Mkuu, ambaye ndiye rais wa Mahakama;

(b) Naibu Jaji Mkuu, atakayekuwa makamu wa rais wa mahakama;

(c) majaji wengine wasiopungua watano na wasiozidi saba.

(2) Mahakama ya Juu itakuwa imekamilika kwa ajili ya shughuli zake ikiwa na majaji watano.

(3) Mahakama ya Juu itakuwa Nairobi.

Mamlaka ya kisheria ya Mahakama ya Juu 184. (1) Mahakama ya Juu -

(a) ina uwezo wa kipekee wa kushughulikia kesi za asili -

(i) kuhusu kesi za uchaguzi wa urais; na

(ii) kuhusu masuala ya utaratibu wa kumshtaki Rais;

(b) itakuwa na uwezo wa kusikiliza rufaa kutoka Mahakama ya Rufani au kutoka mahakama nyingine au mahakama maalum kama ilivyoagizwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

(2) Rufaa za Mahakama ya Rufani zitakwenda Mahakama ya Juu -

(a) ambayo itakuwa na haki kuhusu kesi inayohusu tafsiri au matumizi ya Katiba hii; na

(b) kesi yoyote nyingine ambayo Mahakama ya Rufaa au Mahakama ya Juu imethibithisha kwamba inahusu jambo lenye umuhimu wa jamii.

(3) Mahakama ya Juu haitafungika na maamuzi yake wa awali kama ni katika maslahi ya haki na maendeleo ya sheria na sayansi na falsafa ya sheria isifungike na maamuzi hayo.

Page 104: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

104

(4) Licha ya masharti ya Ibara ya 183(2) uamuzi uliofanywa kwa mujibu wa Ibara ndogo (3) unaweza kufanywa tu na kikao cha mahakama ambamo majaji wote wa Mahakama ya Juu watashiriki.

(5) Mahakama nyingine zote zitalazimika kufuata maamuzi ya Mahakama ya Juu.

Mahakama ya Rufaa 185. Mahakama ya Rufaa inajumuisha rais wa Mahakama ya Rufaa na idadi ya majaji

wengine na itaongozwa na kusimamiwa kama itakavyoagizwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

Mamlaka ya Mahakama ya Rufaa 186. Mahakama ya Rufaa ina mamlaka kisheria kusikiliza rufaa kutoka kwa

Mahakama Kuu na mahakama nyingine zozote au mahakama maalum zilizoanzishwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

Mahakama Kuu 187. Mahakama Kuu inajumuisha na Jaji Kiongozi wa Mahakama na idadi ya majaji

wengine na itaongozwa na kusimamiwa, kama itakavyoagizwa na Sheria itakayotungwa na Bunge.

Mamlaka ya Mahakama Kuu 188. (1) Kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 184(1)(a) Mahakama Kuu ina

mamlaka asilia yasio mpaka, kuhusu -

(a) kesi za jinai na za madai, na

(b) masuala yote kuhusu ufafanuzi na utekelezaji wa masharti ya Katiba hii; na

(c) Mamlaka mengine ya rufaa au asilia, kama itakavyopewa na au Sheria iliyotungwa na Bunge.

(2) Kwa minajili ya kutekeleza mamlaka ya Mahakama Kuu chini ya Ibara ndogo (1), Jaji Mkuu anaweza kuunda vitengo vya Mahakama Kuu vyenye mamlaka ya kusikiliza na kuamua mambo maalum, ikiwa ni pamoja na mizozo inayohusu mazingira na makaazi katika matumizi ya, na hati ya kumiliki ardhi.

Mamlaka ya usimamizi ya Mahakama Kuu 189. (1) Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya usimamizi wa mahakama za chini

na juu ya mtu yeyote, chombo au mamlaka inayotekeleza wajibu wa kisheria, au kama wa kisheria, lakini si juu ya Mahakama ya Juu ya kumbukumbu.

Page 105: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

105

(2) Kwa minajili ya Ibara ndogo (1), Mahakama ya Juu inaweza kuitisha kumbukumbu za mahakama za chini au mtu, chombo au mamlaka kama ilivyotajwa katika Ibara ndogo (1) na inaweza kutoa amri yoyote na maelekezo inayohisi yanafaa kuhakikisha usimamizi wa haki unafanyika bila upendeleo.

Uteuzi wa majaji 190. Nafasi yoyote katika afisi ya Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu, au Jaji mwingine wa

Mahakama ya Juu ya kumbukumbu itajazwa na mtu aliyeteuliwa na Rais kwa mapendekezo ya Tume ya Huduma za Mahakama, na utaidhishwa na Bunge.

Sifa za kuteuliwa kuwa jaji 191. (1) Jaji Mkuu na majaji wa Mahakama ya Juu watateuliwa kutoka miongoni

mwa watu -

(a) ambao wamehitimu kama mawakili nchini Kenya au katika nchi nyingine yenye mfumo wa sheria ya Jumuiya ya Madola kwa angalau miaka kumi na tano, na ambao –

(i) wanatumikia au wamehudumu kama Majaji wa Mahakama ya Rufaa au Mahakama Kuu; au

(ii) ni mawakili wa kibinafsi au walioandikwa na Huduma ya Umma; na

(b) wana uwezo wa kitaaluma ulivyodhihirishwa na sifa za kielimu na umahiri katika fani ya sheria au utumishi ya umma; na

(c) wana mwenendo wenye uadilifu na uaminifu wa kiwango cha juu.

(2) Majaji wa Mahakama ya Rufaa watateuliwa kutoka kwa watu walio na -

(a) uzoefu wa angalau miaka kumi na miwili nchini Kenya au katika nchi nyingine yenye mfumo wa sheria ya Jumuiya ya Madola –

(i) kama Jaji wa Mahakama ya Rufaa au Mahakama Kuu; au

(ii) kama mawakili wa kibinafsi au walioandikiwa na Huduma ya Umma;

(b) uwezo wa kitaalamu kama ilivyodhihirishwa na sifa za kielimu na umahiri wake katika fani ya sheria au utumishi wa umma; na

(c) mwenendo wenye uadilifu na uaminifu wa hali ya juu.

(3) Majaji wa Mahakama Kuu watateuliwa kutoka kwa watu walio na -

(a) uzoefu angalau wa miaka kumi nchini Kenya au katika nchi nyingine yenye mfumo wa sheria ya Jumuiya ya Madola –

(i) kama mahakimu waliohitimu kitaaluma; au

Page 106: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

106

(ii) kama mawakili wa kibinafsi au walioandikiwa na Huduma ya Umma;

(b) uwezo wa kitaaluma unaodhihirishwa na sifa za elimu na umahiri katika fani ya sheria au utumishi wa umma; na

(c) uaminifu na uadilifu wa kiwango cha juu.

Muda wa kazi za majaji 192. (1) Jaji ataastafu anapotimiza umri wa miaka sabini.

(2) Baada ya kufikia umri wa kustaafu, ikiwa kuna kesi ambazo ziliwasilishwa mbele ya jaji wa mahakama za juu za kumbukumbu, kabla kufikisha umri wa kustaafu, anaweza kuendelea kufanya kazi kwa muda wa miezi sita ili kumwezesha jaji kutoa uamuzi, au kutekeleza jukumu lingine kuhusiana na kesi hizo.

Kuondolewa afisini 193. (1) Jaji katika mahakama ya juu ya kumbukumbu anaweza kuondolewa afisini

kutokana na -

(a) kushindwa kutekeleza majukumu ya afisi yake kutokana na udhaifu wa mwili au akili;

(b) kukiuka maadili ya kazi za ujaji kama zilivyowekwa kwa ajili ya Mahakama za Juu za kumbukumbu na Sheria iliyotungwa na Bunge;

(c) kufilisika;

(d) kutomudu kazi za ujaji;

(e) kuwa na mwenendo katika utekelezaji wa kazi za ujaji au vinginevyo; au

(f) kutofuata kanuni za Sura ya Tisa.

(2) Mtu anayetaka jaji wa mahakama ya juu ya kumbukumbu aondolewe madarakani anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa Tume ya Huduma za Mahakama, ambayo, licha ya Ibara ya 275(2)(b), atawasilisha kwa maandishi, akieleza madai ambayo yanaeleza sababu za kutaka jaji huyo aondolewe madarakani.

(3) Tume ya Huduma za Mahakama itazingatia malalamiko na ikitosheka kuwa yana msingi chini ya Ibara ndogo (1), itampelekea Rais malalamiko hayo.

(4) Ndani ya siku kumi na nne baada ya kupokea malalamiko hayo, Rais atamsimamisha Jaji kazi, ikisubiriwa hatua ya Rais kwa mujibu wa Ibara ndogo (5), na huku akitenda kwa kufuata ushauri wa Tume ya Huduma za Mahakama -

(a) ikiwa ni Jaji Mkuu, atateua mahakama maalum yenye -

Page 107: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

107

(i) Spika kama Mwenyekiti;

(ii) majaji watatu wanaohudumu au waliowahi kuhudumu kama Majaji Wakuu au Majaji ya Mahakama ya Juu kabisa katika nchi inayofuata mfumo wa sheria ya Jumuiya ya Madola; na

(iii) watu wengine watatu wenye uzoefu wa masuala ya umma; na

(b) Ikiwa ni jaji mwingine asiyekuwa Jaji Mkuu, atateua mahakama maalum yenye -

(i) wajumbe wanne kutoka miongoni mwa watu ambao ni au wamewahi kuwa majaji wa mahakama za juu za kumbukumbu au wanastahiki kuteuliwa kama majaji wa mahakama za juu za kumbukumbu, lakini vyovyote hawajawahi kuwa wajumbe wa Tume ya Huduma za Mahakama katika miaka mitatu iliyopita; na

(ii) watu wengine watatu wenye uzoefu katika masuala ya umma.

(5) Mahakama hiyo maalum itachunguza suala hilo na kutoa taarifa kuhusu ukweli pamoja na kutoa mapendekezo kwa Rais, atakayechukua hatua kufuatana na mapendekezo ya mahakama hiyo maalum.

(6) Jaji aliyesimamishwa kazi chini ya Ibara ndogo (4) ataendelea kulipwa nusu ya malipo na marupurupu yake hadi atakapoondolewa afisini.

(7) Mahakama maalum iliyoundwa chini ya Ibara ndogo 4(b) itachagua mwenyekiti kutoka miongoni mwa wa wajumbe wake, na mahakama maalum zilizoteuliwa chini ya Ibara ndogo (4)(a) na (b) zinaweza, kwa mujibu wa Katiba hii, kujiwekea taratibu zao.

Mahakama za chini 194. (1) Bunge, kupitia Sheria ya Bunge -

(a) litaanzisha mahakama za kijeshi na mahakama nyingine zilizo chini ya Mahakama Kuu; na

(b) litazipa mamlaka ya kisheria na majukumu.

(2) Hakimu au Kadhi hataondolewa afisini, isipokuwa baada ya uamuzi wa Tume ya Huduma za Mahakama kwa misingi iliyowekwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

Mahakama za Kidini 195. (1) Zinaundwa Mahakama za Kikristo, za Kadhi na za Kihindu.

(2) Bunge linaweza, kupitia Sheria, kuanzisha mahakama zingine za kidini.

Page 108: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

108

(3) Mahakama za Kikristo, za Kadhi na za Kihindu na mahakama nyingine mtawalia -

(a) zitakuwa na wasimamizi wakuu, Kadhi Mkuu na idadi ya wasimamizi wengine au makadhi, wote wakifuata imani ya dini inayohusika mtawalia; na

(b) zitapangwa na kusimamiwa kama itakavyoamriwa na sheria ya Bunge inayozihusu.

(4) Mahakama za Kikristo, za Kadhi, za Kihindu na nyingine za dini zitakuwa na mamlaka ya kuamua masuala ya dini zao kuhusu hali ya kibinafsi, ndoa, talaka, pamoja na masuala yanayotokea baada ya talaka, na mirathi katika kesi ambazo pande zote mbili zinazohusika zinafuata imani ya dini inayohusika kama itakavyoagizwa na sheria ya Bunge.

Tume ya Huduma ya Mahakama 196. (1) Inaundwa Tume ya Huduma ya Mahakama ambayo itakuwa na -

(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa mwenyekiti;

(b) Jaji mmoja wa Mahakama ya Juu atakaechaguliwa na majaji wa Mahakama ya Juu;

(c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufaa atakayechaguliwa na majaji wa Mahakama Rufaa;

(d) Jaji mmoja wa Mahakama Kuu atakayechaguliwa na Majaji ya Mahakama Kuu;

(e) Mwanasheria Mkuu;

(f) mawakili wawili wenye uzoefu wa angalau miaka kumi na mitano mfululizo watakaoteuliwa na Chama cha Wanasheria wa Kenya; na

(g) mtu mmoja aliyeteuliwa na Tume ya Huduma ya Umma.

(2) Msajili Mkuu wa Mahakama atakuwa Katibu wa Tume hiyo.

(3) Mjumbe wa Tume hiyo, isipokuwa aliyeteuliwa chini ya Ibara 1(a) na (e), atashika wadhifa kwa kipindi cha miaka mitano na wanaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Majukumu ya Tume ya Huduma ya Mahakama 197. (1) Majukumu ya Tume ya Huduma ya Mahakama ni -

(a) kuhakikisha na kuendeleza uhuru na uwajibikaji wa Idara ya mahakama na usimamizi wa haki wenye ufanisi, matokeo na uwazi;

(b) kupendekeza kwa Rais watu wa kuteuliwa kuwa majaji;

Page 109: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

109

(c) kupitia upya na kutoa mapendekezo kuhusu masharti ya kazi ya majaji, mahakimu na maafisa wengine wa Idara ya mahakama, isipokuwa mishahara na malipo;

(d) kumshauri Rais kuhusu wajumbe wa mahakama maalum waliotajwa katika Ibara ya 193(4);

(e) kuteua, kuchukua hatua za kinidhamu na kuwaondoa wasajili, mahakimu na maafisa wengine wa Idara ya mahakama ikiwa ni pamoja na wahudumu wasio wanasheria kama itakavyoelezwa na Sheria iliyotungwa na Bunge;

(f) kutayarisha na kutekeleza mipango ya elimu na mafunzo kwa majaji, mahakimu na maafisa wa Idara ya mahakama na wahudumu wasio wanasheria; na

(g) kuishauri serikali kuhusu kuongeza ufanisi katika usimamizi wa haki.

(2) Katika kuteua au kufuta wasimamizi wa mahakama za kidini, Tume itamshauri kiongozi wa mahakama ya dini inayohusika.

Page 110: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

110

SURA YA KUMI NA NNE

SERIKALI ZILIZOSAMBAZIWA MAMLAKA

Sehemu ya Kwanza –Mfumo, Malengo na Kanuni za KusambazaMamlaka

Malengo na kanuni za kusambaza mamlaka 198. (1) Malengo na kanuni za usambazaji mamlaka ni -

(a) kuhakikisha utekelezaji wa kidemokrasia na uwajibikaji katika kutekeleza ukuu wa mamlaka;

(b) kuimarisha umoja wa kitaifa kwa kutambua uanuwai;

(c) kutoa uwezo wa kujiongoza kwa wananchi katika ngazi zote na kuimarisha kushiriki kwa wananchi katika utekelezaji wa mamlaka ya dola;

(d) kutambua haki ya jamii za wenyeji kusimamia mambo yao na kuunda mitandao na jumuiya za kusaidia katika usimamizi huo na kudumisha uendelezaji wake;

(e) kuendeleza maendeleo ya kijamii na kiuchumi na utoaji wa huduma zilizo karibu na zinazoweza kufikiwa kote nchini Kenya;

(f) kuhakikisha ugawaji ulio sawa wa rasilmali za kitaifa na za kienyeji kote nchini Kenya, na kuweka masharti maalum yanayolenga maeneo yaliyoachwa nyuma kimaendeleo; na

(g) kufanikisha usambazaji wa vyombo vya dola na majukumu.

(2) Watu na vyombo vyote vinavyotekeleza uwezo na majukumu kwa mujibu wa Sura hii sharti vizingatie malengo yaliyofafanuliwa na Ibara hii.

Kitengo/sehemu/eneo la usambazaji mamlaka 199. Wilaya ndio kitengo/sehemu/eneo muhimu ya usambazaji mamlaka.

Ushirikiano baina ya Serikali na serikali za wilaya 200. (1) Serikali na seriikali za wilaya -

(a) zitatekeleza uwezo na majukumu yao kwa namna ambayo itaheshimu hadhi ya taasisi na haki na majukumu ya ngazi mbili hizo za serikali;

(b) ziitasaidia, zitaunga mkono na kushauriana na ngazi nyingine na, inapofaa, kutekeleza sheria zilizotungwa katika kila ngazi; na

(c) zitawasiliana kwa ajili ya kubadilishana taarifa, kuratibu sera, usimamizi na uimarishaji wa uwezo.

Page 111: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

111

(2) Serikali na serikali za wilaya zitashirikiana katika kutekeleza majukumu na, kwa lengo hilo, zinaweza kuunda kamati za pamoja na mamlaka za pamoja.

(3) Mzozo baina ya Serikali na serikali ya wilaya au baina ya serikali za wilaya, utasuluhishwa kwa taratibu zitakazotolewa na sheria ya Bunge

(4) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo (3), sheria itakayotungwa na Bunge itaweka utaratibu wa kutatua migogoro baina ya serikali na serikali kwa njia ya upatanishi, usuluhishi au kukubaliana.

Kugawanya majukumu 201. (1) Isipokuwa ambapo imefafanuliwa vinginevyo na Katiba hii au kupitia

sheria, uwezo na majukumu ya ngazi mbalimbali za serikali yanapatikana katika Jedwali ya Tatu.

(2) Kila serikali ya wilaya itagawa utoaji wa huduma zake na majukumu mengine ya serikali kwa kuyasambaza, kama iwezekanavyo na inavyofanikisha.

(3) Ikiwa uwezo na majukumu yametolewa na Serikali kwa serikali ya wilaya, mipango itawekwa kuhakikisha kuwa fedha zinazohitajika kwa utekelezaji wa shughuli hiyo zinahamishwa ipasavyo, ili kufanikisha uwezo na majukumu.

(4) Jukumu lililotolewa kwa Serikali na serikali ya wilaya litakuwa ni jukumu miongoni mwa majukumu yanayoingiliana katika kila moja ya serikali hizo, na endapo kunamgongano, jukumu la Serikali la kitaifa litakuwa na nguvu.

(5) Jumuiya, muungano na mitandao wa jumuiya au vijiji katika mfumo wa kazi na uwezo wao kisheria, na pia vitakuwa na haki ya kujiendesha kama ilivyoelezwa na sheria ya kitaifa.

Mgongano wa Sheria 202. Panapokuwa na mgongano kati ya sheria kuhusu masuala yaliyo chini ya

mamlaka yanayolingania ngazi mbili za Serikali, sheria ya kitaifa itakuwa na nguvu kuliko ya wilaya.

Usimamizi wa maeneo ya mijini ndani ya wilaya 203. (1) Bunge, kupitia sheria, litatoa masharti kwa ajili ya uongozi na usimamizi

wa maeneo ya mijini yaliyoko wilayani.

(2) Sheria chini ya Ibara ndogo (1) -

(a) itaweka vigezo vya kufafanua baina ya –

(i) maeneo ya mijini yaliyomo wilayani; na

(ii) sehemu za vijijini zilizoko wilayani;

Page 112: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

112

(b) itaweka vigezo na taratibu za kubadilisha hali kutoka sehemu ya vijijini katika wilaya hadi kuwa eneo la mjini ndani ya wilaya;

(c) itaweka vigezo vya kugawanya eneo ndani ya wilaya kuwa ni eneo la mjini;

(d) itabuni misingi ya utawala na usimamizi wa maeneo ya mijini yaliyoko wilayani, ambayo itazingatia matakwa maalum ya Mji Mkuu wa Taifa na miji mingine mikubwa;

(e) itawezesha wananchi katika maeneo ya miji kushiriki katika kazi za utawala wa wilaya ambamo yamo.

(3) Sheria hiyo inaweza -

(a) kuagiza namna za utambuzi wa aina mbali mbali za maeneo ya miji katika wilaya na;

(b) kutunga masharti zaidi kwa ajili ya utawala bora zaidi wa maeneo ya miji ndani ya wilaya.

Kusimamishwa kwa Serikali ya Wilaya 204. (1) Serikali ya Wilaya inaweza kusimamishwa -

(a) kwa hali ya dharura inayotokana na ugomvi wa ndani au vita; au

(b) kwa kutomudu kazi kulikokithiri au matendo ya rushwa au kushindwa kufuata maadili yaliyowekwa na Sheria ya Bunge kuhusiana na serikali ya Wilaya.

(2) Serikali ya Wilaya haitosimamishwa chini ya Ibara ndogo (1)(b) isipokuwa Tume ya uchunguzi iliyoteuliwa kulingana na Ibara 144(5) imechunguza shutuma dhidi yake, na imetoa shauri yake kwa Rais kwamba serikali hiyo ya wilaya isimamishwe.

(3) Ikiwa Tume ya uchunguzi chini ya Ibara ndogo (2) itapendekeza kwamba serikali hiyo ya wilaya isimamishwe, Rais ataisimamisha serikali hiyo ya wilaya.

(4) Wakati wa kusimamisha chini ya Ibara hii matayarisho yatafanywa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za serikali hiyo ya wilaya kwa mujibu wa sheria itakayotungwa na Bunge.

(5) Kusimamishwa chini ya Ibara hii hakutoendelea zaidi ya siku tisini ambapo katika muda huo uchaguzi mpya wa baraza la wilaya linalohusika utafanywa.

Marufuku kuchaguliwa katika Serikali na katika serikali ya wilaya 205. Isipokuwa iwe imeagizwa vinginevyo katika Katiba hii, mtu hatoshika afisi ya

umma au ya kuchaguliwa kwa wakati mmoja katika Serikali na serikali ya wilaya.

Page 113: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

113

Sehemu ya Pili – Baraza la Kitaifa la Serikali za Wilaya na Mabaraza Mengine

Kuundwa na majukumu ya Baraza la Kitaifa la Serikali za Wilaya na Babaraza Mengine 206. (1) Linaundwa Baraza la Kitaifa litakalojulikana

Serikali za Maeneo 211. (1) Inaundwa katika kila eneo, serikali yenye Baraza la eneo mamlaka ya

utendaji ya eneo.

(2) Eneo la Nairobi litasimamiwa kama Jiji Kuu la Taifa, kwa mujibu wa Sheria itakayotungwa na Bunge.

Mabaraza ya kutunga Sheria za Maeneo 212. (1) Baraza la kutunga sheria la eneo -

(c) lina wajumbe wanne (wasiokuwa wajumbe wa baraza la wilaya) waliochaguliwa kutoka kila wilaya ya eneo na baraza la wilaya hiyo;

(d) liko madarakani kwa miaka mitano; na

(e) lina uwezo wa kupitisha sheria yoyote inayofaa, au inayohusika na, utekelezaji wa uwezo na ufanikishaji wa majukumu yaliyopewa eneo;

(2) Katika kuchagua wajumbe wa baraza la eneo, baraza la wilaya litazingatia uanuwai unaopatikana wilayani.

(3) Mjumbe katika baraza la eneo atakuwa na uwezo wa kuhudhuria mikutano ya baraza la wilaya lililomchagua na kushiriki katika majadiliano yake lakini hana haki ya kupiga kura kuhusu jambo lolote.

Kamati tendaji ya eneo 213. (1) Mamlaka ya serikali ya eneo yanatekelezwa na kamati tendaji ya eneo,

yenye -

(a) mtendaji mkuu wa eneo na naibu mtendaji mkuu watakaojulikana kama -

(i) isipokuwa eneo la Nairobi, mkuu wa eneo na naibu mkuu wa eneo; na

(ii) katika eneo la Nairobi, meya na naibu wa meya, na watachaguliwa kwa mujibu wa Ibara ya 214 au 215, kama itakavyohitajika; na

(b) wajumbe wengine walioteuliwa na mtendaji mkuu wa eneo kwa idhini ya baraza la eneo.

Page 114: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

114

(2) Idadi ya wajumbe watakaoteuliwa chini ya Ibara ndogo 1(b) haitazidi thuluthi moja ya wajumbe wa baraza la eneo.

(3) Iwapo mtendaji mkuu ni mgonjwa au hayupo, naibu mtendaji mkuu atatekeleza kazi, uwezo na shughuli za mtendaji mkuu wa eneo.

Uchaguzi wa Mkuu na Naibu Mkuu wa Eneo 214. (1) Mkuu na naibu mkuu wa eneo watachaguliwa na jimbo la uchaguzi lenye

wajumbe wote wa baraza la wilaya waliochaguliwa katika eneo.

(2) Mjumbe wa Baraza la Uchaguzi lililoundwa chini ya Ibara ndogo (1) hawezi kuchaguliwa awe mkuu au naibu mkuu wa eneo.

(3) Katika uchaguzi chini ya Ibara ndogo (1) -

(a) mgombea atakayepata thuluthi mbili za kura zote atatangazwa kuchaguliwa;

(b) ikiwa hakuna mgombea aliyepata idadi hiyo ya kura -

(i) upigaji kura kwa mara ya pili utaendeshwa, ambapo wagombea ni yule aliyepata idadi kubwa zaidi na wa pili kupata idadi kubwa katika upigaji kura wa kwanza; na

(ii) mgombea atakayepata kura nyingi zaidi katika upigaji kura wa pili atatangazwa kuchaguliwa.

Uchaguzi wa meya na naibu meya wa Nairobi 215. Meya na naibu wa meya watachaguliwa kwa mujibu wa Sheria itakayotungwa na

Bunge, kwa wingi wa kura za wapiga kura waliosajiliwa na wanaotimiza mahitaji kuhusu makaazi katika eneo kama ilivyoagizwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

Shughuli za kamati za mamlaka tendaji za maeneo 216. (1) Wajumbe wa kamati ya mamlaka tendaji ya maeneo, mwenyekiti wao

akiwa mtendaji mkuu, wana wajibu wa kutekeleza mamlaka kuhusu shughuli na uwezo katika eneo.

(2) Wajumbe wa kamati ya mamlaka tendaji ya eneo wanawajibika kwa pamoja, na kila mmoja wao, kwa baraza la kutunga sheria la eneo katika utekelezaji wa uwezo na wajibu wao.

Sehemu ya Tatu - Wilaya

Serikali za wilaya 217. Inaundwa serikali katika kila wilaya, yenye baraza na mamlaka tendaji za wilaya.

Mamlaka ya kutunga sheria ya baraza la wilaya 218. (1) Mamlaka ya kutunga sheria za wilaya yamekabidhiwa baraza la wilaya.

Page 115: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

115

(2) Baraza la wilaya linaweza kupitisha sheria zozote zinzoafaa, au zinazohusika katika ufanisi wa utekelezaji wa uwezo na shughuli zilizopewa Baraza la Wilaya.

(3) Baraza la wilaya lina uwezo wa kudumisha uangalizi juu ya kamati tendaji ya mamlaka ya wilaya na vyombo vingine vyovyote vyenye mamlaka ya utekelezaji vilivyoundwa na sheria za baraza la wilaya.

(4) Baraza la wilaya linaweza kupendekeza kwa baraza la kutunga sheria la eneo kuhusu jambo lolote ambalo lipo nje ya uwezo wa baraza la wilaya lakini ambalo limo ndani ya uwezo wa kutungiwa sheria na baraza la kutunga sheria la eneo.

(5) Baraza la wilaya linaweza kutayarisha mipango na sera kwa ajili ya usimamizi wa utumiaji wa rasilmali za wilaya na kwa maendeleo na usimamizi wa miundo mbinu na taasisi za wilaya.

Uchaguzi wa madiwani wa wilaya 219. (1) Baraza la wilaya lina -

(a) mjumbe mmoja aliyechaguliwa katika kila wodi yenye mipaka, kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge baada ya kuzingatia mapendekezo ya Tume ya Uchaguzi na Mipaka;

(b) idadi ya wajumbe wa viti maalum, wote wakiwa wanawake, kama inavyohitajika ili kuhakikisha kuwa angalau thuluthi moja ya wajumbe wa baraza ni wanawake, waliochaguliwa baada ya wajumbe kutangazwa wamechaguliwa chini ya aya (a); na

(c) idadi ya wajumbe wa makundi na jamii zilizotengwa, pamoja na watu wenye ulemavu, wazee na vijana, mradi tu angalau wawili ni watu wenye ulemavu, kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

(2) Hakuna lolote katika Ibara hii linalomzuia mwanamke aliyegombea uchaguzi bila kufanikiwa chini ya Ibara ndogo (1)(a) kugombea kiti maalum chini ya Ibara ndogo (1)(b).

(3) Baraza la wilaya linachaguliwa kwa muhula wa miaka mitano.

Kamati tendaji ya wilaya 220. (1) Mamlaka tendaji ya wilaya yanatekelezwa na kamati tendaji ya mamlaka

ya wilaya yenye -

(a) gavana na naibu gavana wa wilaya; na

(b) kuambatana na Ibara ndogo (2), wajumbe wengine

walioteuliwa na gavana kwa idhini ya baraza la wilaya.

(2) Idadi ya wajumbe walioteuliwa chini ya Ibara ndogo (1)(b) haitazidi -

Page 116: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

116

(a) thuluthi moja ya idadi ya wajumbe wa baraza la wilaya; au

(b) watu kumi.

(3) Iwapo gavana wa wilaya ni mgonjwa au hayupo, naibu wa gavana atatekeleza kazi, uwezo na dhamana za gavana wa wilaya

Uchaguzi wa gavana na naibu gavana wa wilaya 221. (1) Gavana na naibu wa gavana wa wilaya watachaguliwa katika uchaguzi na

watashiriki kama wagombea wenza, na wapiga kura waliosajiliwa na waliotimiza mahitaji yanayohusu makaazi katika eneo kama ilivyoagizwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

(2) Gavana na naibu gavana wa wilaya watakuwa madarakani kwa muhula wa miaka mitano na kila mmoja wao anaweza, kama anastahiki, kuchaguliwa tena kwa muhula mwingine.

(3) Mjumbe wa kamati tendaji ya wilaya asiye gavana au naibu wa gavana wa wilaya anaweza kuondolewa madarakani kwa azimio lililopitishwa na baraza la wilaya.

Shughuli za kamati tendaji ya mamlaka ya wilaya 222. (1) Kamati tendaji ya mamlaka ya wilaya -

(a) itatekeleza sheria zilizotungwa na baraza la wilaya;

(b) itatekeleza wilayani sheria za kitaifa na za maeneo kwa mujibu wa sheria;

(c) itaratibu shughuli za usimamizi wa wilaya na idara zake; na

(d) itaratibu shughuli za kata na za jamii wilayani.

(2) Bila kuwekea mpaka uwezo wa baraza la wilaya, kamati tendaji ya mamlaka ya wilaya inaweza kutayarisha na kuanzisha mapendekezo ya sheria ili kuidhinishwa na baraza.

(3) Kamati tendaji ya mamlaka ya wilaya ina uwezo na shughuli nyengine kwa mujibu wa Katiba hii au sheria ya taifa au ya eneo.

(4) Wajumbe wa kamati tendaji mamlaka ya wilaya wanawajibika kwa pamoja na kila mmoja wao kwa baraza la wilaya katika utekelezji wa uwezo na shughuli zao.

(5) Kamati tendaji ya mamlaka ya wilaya -

(a) itafanya kazi kwa mujibu wa Katiba hii;

(b) itatoa kwa baraza la taifa taarifa kamili na za mara kwa mara kuhusu masuala yanayodhibitiwa na kamati ya mamlaka ya wilaya.

Page 117: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

117

Sehemu ya Nne – Kata

Serikali za Kata 223. (1) Inaundwa serikali katika kila kata, itakayokuwa na baraza na kamati

tendaji za kata.

(2) Msimamizi wa kata anawajibika kwa baraza la kata katika utekelezaji wa uwezo na shughuli za afisi yake.

Mabaraza ya Kata 224. (1) Baraza la kata lina wawakilishi waliochaguliwa na wapiga kura

waliotimiza mahitaji yote ya makazi kwenye kata kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

(2) Uchaguzi kwa ajili ya Ibara ndogo (1) utaendeshwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge, na inayohakikisha kwamba idadi sawa ya wanaume na wanawake wamechaguliwa.

Msimamizi wa Kata 225. (1) Msimamizi wa kata ndiye mwenye mamlaka ya utekelezaji katika kata, na

anachaguliwa na wapiga kura wa kata, kwa mujibu wa Sheria ya wilaya.

(2) Msimamizi wa kata atakuwa madarakani kwa muhula wa miaka mitano na anaweza, akistahiki, kuchaguliwa kwa muhula mmoja mwingine.

Sehemu ya Tano – Jumla

Muda wa afisi 226. Kuambatana na masharti maalum ya Sura hii, mtu atashika -

(a) afisi ya kuchaguliwa kwa muhula wa miaka mitano na anaweza, akistahiki, kuchaguliwa kwa muhula mwingine; na

(b) afisi ya kuteuliwa kwa muhula wa miaka mitano na anaweza, akistahiki, kuteuliwa tena kwa muhula mwingine.

Uwezo wa kuita mashahidi 227. Baraza la kutunga sheria la eneo au la wilaya -

(a) lina uwezo wa kumuita mtu yeyote kufika mbele yake au kamati yake ili kutoa ushahidi au maelezo; na

(b) kwa minajili ya aya (a), lina uwezo wa Mahakama Kuu katika -

(i) kushurutisha mahudhurio ya mashahidi na kuwahoji kwa kiapo, kwa tamko la dhati au vinginevyo;

(ii) kulazimisha uwasilishaji wa nyaraka; na

(iii) kutoa ombi ili kuwahoji mashahidi nchi za ng’ambo.

Page 118: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

118

Haki, kinga na uwezo wa kufikia na kushiriki kwa umma 228. Ibara ya 144 na 145 zitatumika kwa mabaraza ya maeneo, ya wilaya na ya kata

kama zitakavyotumika katika bunge la taifa.

Usawa wa jinsia na uanuwai 228A. (1) Wajumbe wa bunge, baraza au kamati tendaji iliyoundwa chini ya Sura

hii, wakati wowote, haitakuwa na zaidi ya thuluthi mbili ya jinsia moja.

(2) Sheria itatungwa na Bunge kuhakikisha kwamba jamii na uanuwai wa utamaduni katika eneo, wilaya au mahali unadhihirika katika vyombo vya kutunga sheria na vya utendaji wa majukumu katika eneo, wilaya au mahali.

(3) Bila ya kupunguza uwezo wa Ibara ndogo (2), sheria lazima iainishe njia za kuwalinda jamii ndogo katika wilaya.

Serikali wakati wa mpito 228B Iwapo uchaguzi wowote unaelekea kufanywa kuunda Bunge au baraza katika

Sura hii, Bunge au baraza lilioko litaendelea kuwa na uwezo wa kuendelea na shughuli hadi hapo litakapoundwa upya baada ya uchaguzi.

Uongozi na uadilifu 229. Wajumbe wa bunge, baraza au kamati zilizoundwa katika Sura hii watatenda kwa

mujibu wa kanuni zilizoagizwa katika Sura ya Tisa.

Uchapishaji wa sheria 229A. (1) Sheria au sheria ndogo ambayo imetungwa na baraza la kutunga sheria la

eneo au wilaya au kata, na kamati tendaji haitokuwa na nguvu za kisheria mpaka ichapishwe katika Gazeti.

(2) Sheria za ngazi ya taifa, eneo na wilaya zinaweza kuweka masharti mengine kuhusiana na uchapishaji wa sheria za serikali zilizosambaziwa mamlaka.

Masharti yaliyoagizwa na Sheria ya Bunge 230. (1) Bunge litatunga sheria yenye sharti kuhusu masuala yote muhimu au

yanayofaa ili kuwezesha utekelezaji wa Sura hii, pamoja, na hasa, sharti la -

(a) uhamishaji kiawamu, kwa kipindi kisichozidi miaka mitano tangu tarehe ya kuidhinishwa, uwezo na majukumu yaliyotolewa na Ibara ya 209, kutoka kwa Serikali Kuu hadi kwa serikali zilizosambaziwa mamlaka;

(b) utawala wa Nairobi, kama makao makuu ya taifa, na wa miji mingine;

Page 119: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

119

(c) ukasimu wa madaraka kutoka ngazi moja ya serikali hadi nyingine, pamoja na ukasimu wa uwezo wa kisheria kutoka Serikali Kuu hadi serikali za maeneo na za wilaya kuhusiana na masuala yanayofafanuliwa katika aya zifuatazo za Ibara hii kupitia Sheria iliyotungwa na Bunge, masharti ya kanuni ya ukasimu na urudishaji wa madaraka hayo uliokasimiwa;

(d) namna ya uchaguzi na uteuzi wa watu, na kuondolewa kwao katika serikali zilizosambaziwa mamlaka, pamoja na sifa za wapiga kura na wagombea;

(e) utaratibu wa bunge, mabaraza na kamati tendaji za mamlaka, pamoja na uenyekiti, idadi ya vikao, akidi na upigaji kura; na

(f) kusimamisha bunge, mabaraza na kamati tendaji za mamlaka.

(2) Sheria iliyopitishwa kwa ajili ya Ibara ndogo (1), itaweka masharti kwa madhumuni ya masuala yaliyowekwa katika sehemu ya Sita ambayo -

(a) yanaunga mkono kanuni za usambazaji mamlaka; na

(b) yana maelezo kamili,

kama masharti ya Sehemu hiyo.

Sehemu ya Sita – Masharti ya muda

Kustahiki kuchaguliwa au kuteuliwa katika serikali zilizosambaziwa mamlaka 231. Hadi sharti linalohusika lipitishwe kupitia Sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili

ya Ibara ya 230, mtu atastahiki kuwa mjumbe wa bunge, baraza au kamati tendaji katika Sura hii ikiwa mtu huyo -

(a) anastahiki kuwa mjumbe wa Baraza la Taifa; au

(b) amekuwa mkaazi katika eneo, wilaya au kata mfululizo kwa kipindi cha miezi kumi na miwili mara tu kabla ya tarehe ya uchaguzi au uteuzi.

Taratibu na mipango ya ndani ya serikali zilizosambaziwa mamlaka 232. (1) Hadi sharti linalohusika lipitishwe kupitia Sheria iliyotungwa na Bunge

kwa ajili ya Ibara ya 230, kila bunge, baraza au kamati tendaji iliyoundwa katika Sura hii inaweza, kupitia azimio, kusimamia utaratibu wake na mipango ya ndani.

(2) Uwezo uliotolewa na Ibara ndogo (1) ni pamoja na uwezo wa kuweka sharti linalohusu -

(a) uteuzi na uchaguzi, na uondoaji wa watu kama maspika na manaibu spika;

(b) kuitisha vikao, idadi na uenyekiti wa mikutano; na

Page 120: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

120

(c) akidi na upigaji kura mikutanoni.

Uchaguzi wa meya na naibu wa meya wa Nairobi 233. Hadi sheria inayohusika kutungwa na Bunge kwa ajili ya Ibara ya 215 -

(a) utaratibu wa kupiga kura chini ya Ibara hiyo utakuwa sawa na uchaguzi mdogo wa Baraza la Taifa; na

(b) masharti ya makaazi kwa ajili ya Ibara hiyo ni kwamba mtu awe mkaazi wa eneo kwa kipindi cha miezi kumi na miwili mfululizo mara tu kabla ya tarehe ya uchaguzi.

Uchaguzi wa madiwani wa wilaya 234. Hadi sheria inayohusika itungwe na Bunge kwa ajili ya Ibara ya 219(1) -

(a) wodi za kila wilaya ni wodi zilizoko kabla tu ya tarehe ya kuanza kutumika;

(b) idadi ya wajumbe wanaowakilisha makundi na jamii zilizotengwa ni idadi iliyo karibu sana na asilimia ishirini ya idadi ya wajumbe waliotajwa katika Ibara ya 219(1)(a); na

(c) Utaratibu wa kuendesha uchaguzi wa wajumbe wa baraza la wilaya utakuwa kama ilivyoamuliwa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka.

Uchaguzi wa mabaraza na wasimamizi wa kata 235. (1) Hadi sheria inayohusika itungwe na Bunge kwa ajili ya Ibara ya 224(2),

utaratibu wa kuendesha uchaguzi wa wajumbe wa baraza la kata ili kuhakikisha kwamba idadi sawa ya wanawake na wanaume wamechaguliwa utakuwa kama ulivyoamuliwa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka.

(2) Hadi sharti linalohusika litungwe kupitia sheria ya wilaya kwa ajili ya Ibara ya 225 (1), utaratibu wa kuendesha uchaguzi wa wanachama wa baraza la kata utafanywa kama ilivyoamuliwa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka.

Page 121: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

121

SURA YA KUMI NA TANO

FEDHA ZA UMMA

Sehemu ya Kwanza – Fedha za Umma na Usimamizi wa Mapato

Kanuni na malengo ya fedha za umma na usimamizi wa mapato 218. Lengo la msingi la mfumo wa fedha za umma na usimamizi wa mapato katika

Jamhuri ni kuhakikisha -

(a) uzalishaji wa mapato unaofaa na ulio madhubuti;

(b) ufuataji wa kanuni za uwazi na uwajibikaji na kutii sheria pamoja na udhibiti unaofaa na uangalizi juu ya mikopo na matumizi;

(c) ukusanyaji wa mapato kwa usawa, na ugawaji wa rasilmali na mapato ya taifa na ya mashinani kote katika Jamhuri kwa kuzingatia mahitaji maalum ya makundi na jamii zilizotengwa;

(d) utekelezaji wa kanuni za ujumla, uadilifu katika mambo ya kodi na kukusanya kodi kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi.

(e) kwamba utozaji wa kodi utazingatia mzigo wa kodi ya moja kwa moja kwa watu;

(f) kwamba manufaa na mizigo ya mikopo na matumizi ya fedha za umma imegawanywa kwa usawa baina ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;

(g) kuhakikisha kuwa bajeti na taratibu za bajeti zinakuza uwazi, uwajibikaji na usimamizi wa kifedha unaofaa, wa uchumi, madeni na sekta ya umma; na

(h) kwamba hesabu za fedha za umma zinakaguliwa na kutolewa taarifa mara kwa mara.

Sehemu ya Pili – Uwezo wa kutoza kodi na kugawa mapato

Kutoza kodi 219. (1) Hakuna mtu au mamlaka inayoweza -

(a) kutoza kodi, ada au malipo kwa niaba ya Serikali au serikali ya wilaya isipokuwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa; na

(b) kuondoa au kubadilisha kodi, ada au malipo yoyote yaliyowekwa na sheria isipokuwa pale ambapo sheria imeruhusu kufanya hivyo.

Page 122: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

122

(2) Sheria inayoruhusu kutoa msamaha wa kodi yoyote, ada au malipo itahitaji kwamba taarifa ya msamaha huo na sababu yake ihifadhiwe, iwasilishwe na kuarifiwa Mkaguzi Mkuu.

Uwezo wa kutoza kodi 220. (1) Uwezo wa Serikali na serikali za wilaya, wa kutoza kodi na kukusanya

mapato umefafanuliwa katika Jedwali ya Nne.

(2) Uwezo wa serikali za wilaya wa kutoza kodi na kukusanya mapato hautatekelezwa kwa namna ambayo itahatarisha sera ya taifa ya kiuchumi, shughuli za kiuchumi nje ya mipaka ya wilaya au usafiri wa bidhaa, huduma, fedha au kazi nchini.

(3) Wakati Serikali na serikali ya wilaya au kati ya serikali mbili au zaidi za wilaya zina uwezo wa kutoza au wa kukusanya mapato kuhusu chanzo kimoja, ugawaji unaofaa wa uwezo huo na majukumu utafanywa na Sheria itakayotungwa na Bunge.

(4) Hakuna lolote katika Ibara hii linalozuia ugawaji wa mapato yaliyokusanywa chini ya Ibara hii kati ya Serika na serikali ya wilaya au kati ya serikali mbili au zaidi za wilaya zenye uwezo wa kutoza kodi au uwezo na majukumu wa kukusanya mapato kuhusu chanzo kimoja.

Ugawanyaji wa fedha za Taifa 221. Kwa mujibu wa nyenzo katika Ibara ya 240 -

(a) Serikali itazingatia sawa katika kugawanya mapato ya fedha kati ya Serikali na serikali za wilaya; na

(b) kila serikali ya wilaya –

(i) ina haki ya kupata fungu kwa uwadilifu la mapato ya kitaifa; na

(ii) inaweza kupata ruzuku ya kusawazisha au mgawo mwingine kutoka mapato ya Serikali ima kwa masharti au bila masharti;

(c) mapato ya ziada yaliyokusanywa na serikali ya wilaya hayatopunguzwa kutokana na sehemu yake ya mapato yaliyokusanywa kitaifa, au kupunguzwa kutoka kwenye mgawo iliyopewa kutoka kwenye mapato ya Serikali;

(d) Serikali haina wajibu kufidia serikali ya wilaya ambayo haikusanyi mapato sawa na uwezo wake wa hazina na misingi na vyanzo vya kodi; na

(e) fungu la mapato yaliyokusanywa kitaifa litahamishiwa serikali ya wilaya bila kuchelewa na bila kupunguzwa, isipokuwa kama uhamishaji umezuiwa chini ya Ibara ya 236(2) au upunguzaji

Page 123: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

123

unaofanywa kuondowa majukumu ya serikali ya wilaya kwa Serikali.

Sehemu ya Tatu – Mifuko ya Kuwekea Fedha za Umma

Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali 222. (1) Unaundwa mfuko utakaojulikana kama Mfuko Mkuu wa fedha za Serikali.

(2) Kuambatana na Ibara ndogo (3), fedha zote zinazokusanywa au zinazopokewa kwa madhumuni ya, au kwa niaba ya, au kwa amana ya Serikali zitalipwa katika Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali.

(3) Fedha zilizotajwa katika Ibara ndogo (2) hazihusishi fedha zozote -

(a) ambazo zitalipwa katika hazina ya umma iliyowekwa kwa madhumuni maalum chini ya Sheria iliyotungwa na Bunge; au

(b) ambazo zinaweza kuhifadhiwa na chombo cha serikali katika ngazi ya Taifa au wilaya, kilichozipata kwa madhumuni ya kulipia matumizi ya chombo hicho, chini ya Sheria iliyotungwa na Bunge.

Utoaji wa fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali 223. (1) Fedha hazitatolewa kwenye Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali

isipokuwa -

(a) kulipia matumizi yatakayolipwa kutoka kwenye mfuko kwa mujibu wa Katiba hii au Sheria iliyotungwa na Bunge; au

(b) wakati ambapo suala la fedha hizo linapoidhinishwa na Sheria ya Matumizi ya Fedha au Sheria ya Matumizi ya Ziada.

(2) Fedha hazitatolewa kutoka kwenye hazina yoyote ya umma ya Serikali ila zile za Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali, isipokuwa suala hilo la fedha liwe limepitishwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

(3) Fedha hazitatolewa kutoka kwenye Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali au hazina yoyote ya umma ya Serikali isipokuwa utoaji huo uwe umeidhinishwa na Msimamizi wa Bajeti.

Mfuko wa Mapato ya serikali za wilaya 224. (1) Unaundwa Mfuko wa Mapato kwa kila serikali ya wilaya, ambamo fedha

zote zitakazopatikana au kupokewa, kwa madhumuni au kwa niaba ya, au kwa amana ya serikali ya wilaya, isipokuwa fedha zilizoagizwa kutowekwa humo na Sheria iliyotungwa na Bunge, zitalipwa.

(2) Fedha zinaweza kutolewa tu kwenye Mfuko wa Mapato ya serikali ya wilaya -

(a) ambapo imeidhinishwa kwa mujibu wa sheria ya matumizi ya serikali ya wilaya; au

Page 124: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

124

(b) kama matozo ya moja kwa moja kutoka kwenye Mfuko wa Mapato yaliyoidhinishwa na Sheria iliyotungwa na Bunge au sheria ya serikali ya wilaya.

Mfuko Wa Dharura 225. Kutakuwa na mfuko utakaoitwa Mfuko wa Fedha za Dharura na utendakazi wake

utakuwa kwa mujibu wa sheria itayotungwa na Bunge.

Sehemu ya Nne – Kukopa

Ukopaji wa Serikali 226. (1) Serikali inaweza kukopa kutoka chanzo chochote.

(2) Serikali haitoweza, kwa niaba yake au kwa niaba ya taasisi nyingine ya umma, mamlaka au mtu, kukopa fedha, kudhamini mkopo au kupokea msaada, isipokuwa kama masharti ya mapatano hayo yamewasilishwa na kuidhinishwa kwa uamuzi wa Bunge.

(3) Fedha zote zilizopokewa kutokana na mapatano yaliyotajwa katika Ibara ndogo (2) zitawekwa kuwa, ni sehemu ya, Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali au mfuko mwingine wa fedha za umma ulioanzishwa kwa ajili ya mapatano hayo.

(4) Ndani ya muda wa siku saba baada ya Bunge, kwa azimio, likiomba, Waziri anayehusika na fedha atawasilisha Bungeni habari zinazohusu mkopo ambao in dharura kuonyesh -

(a) kiwango chote cha madeni kwa kuonyesha kiwango kilichokopwa na riba iliyolimbikizwa;

(b) mpango uliowekwa kwa ajili ya kulipa mkopo;

(c) matumizi ya mkopo; na

(d) hatua zilizochukuliwa kulipa mkopo huo.

(5) Kwa minajili ya Ibara hii, neno “mkopo” linajumuisha fedha zozote zilizokopwa ama kutolewa kwa Serikali kwa masharti ya kurejeshwa au kulipwa na aina yoyote ya kukopa au kukopesha ambapo fedha kutoka kwa Mfuko Mkuu ama hazina yoyote ya umma zinaweza kutumiwa au zinatakiwa kutumia kwa malipo ama kulipia.

Ukopaji wa serikali za wilaya 227. (1) Serikali ya wilaya inaweza kutafuta mikopo kwa ajili ya maendeleo au

matumizi ya kawaida kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

(2) Sheria iliyotungwa na Bunge iliyotajwa katika Ibara ndogo (1) inaweza kuidhinishwa tu baada ya mapendekezo yote ya Tume ya Mgawo wa Mapato kuzingatiwa.

Page 125: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

125

(3) Serikali ya wilaya haiwezi kukopa bila kwanza kupata idhini ya bunge lake.

Deni la Umma 228. (1) Kwa kufuata Ibara ndogo (2), deni la umma la Jamhuri litalipwa kutokana

na Mfuko Mkuu.

(2) Sheria itawekwa na Bunge kwa ajili ya kulipia deni lote au sehemu ya deni la Jamhuri kutoka Mifuko mingine ya umma.

(3) Kwa minajili ya Ibara hii, deni la umma ni pamoja na riba ya deni hilo, mfuko wa kulipia madeni kwa ajili ya deni hilo, gharama zake, matozo na gharama ambayo zinazotokana na usimamizi wa deni hilo na dhamana ambazo bado hazijalipwa na Serikali.

(4) Jumla ya viwango vilivyokopwa katika mwaka wa fedha na Serikali na serikali zote za wilaya hazipaswi kuzidi asilimia fulani ya jumla ya pato la Taifa kama itakavyoagizwa katika Sheria ya Bunge.

Serikali zinapodhamini mikopo 229. (1) Sheria itakayotungwa na Bunge itaweka masharti ambayo yatalizimu

Serikali na serikali za wilaya inapoweza kudhamini mkopo.

(2) Sheria itakayotungwa na Bunge iliyotajwa katika Ibara ndogo (1), inaweza kuidhinishwa tu baada ya mapendekezo ya Tume ya Mgawo wa Mapato kuzingatiwa.

(3) Ndani ya miezi miwili baada ya kila mwaka wa fedha, Serikali na serikali ya wilaya itachapisha taarifa ya dhamana ilizotoa kwa mwaka huo.

Sehemu ya Tano – Bajeti

Kanuni 230. Bajeti za Serikali na serikali za wilaya zitakuwa na -

(a) makadirio ya mapato na matumizi yanayotofautisha baina ya matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo;

(b) mapendekezo ya kugharimia upungufu unaotarajiwa kwa kipindi kinachohusika; na

(c) mapendekezo yote kuhusu kukopa na aina nyingine za dhima ya umma itakayoongeza deni la umma mwaka unaofuata.

Makadirio ya mwaka ya Kitaifa 231. (1) Waziri anayehusika na fedha atawasilisha Bungeni katika tarehe isiyozidi

miezi miwili kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha -

(a) makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha unaofuata; na

Page 126: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

126

(b) mpango wa mikakati ya maendeleo wa kipindi kisichopungua miaka mitatu (au kwa kipindi kirefu zaidi kwa mujibu ya Sheria ya Bunge) pamoja na maelezo kamili ya sera za hazina za fedha zilizotayarishwa na Waziri anayehusika na fedha akishirikiana na Waziri anayehusika na mipango na maendeleo ya Taifa.

(2) Waziri anayehusika na fedha ataweka katika makadirio ya mwaka, kifungu maalum cha bajeti kwa ajili ya maendeleo ya sehemu na jamii zilizotengwa.

(3) Mkuu wa idara yoyote inayosimamia hesabu zake, chombo cha Serikali, au Tume ama Shirika ambalo limeundwa chini ya Katiba, atawasilisha angalau miezi mitatu kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha, makadirio ya usimamizi na maendeleo ya matumizi na makadirio ya mapato ya mwaka unaofuata kwa Waziri anayehusika na fedha.

(4) Makadirio yaliyotayarishwa chini ya Ibara ndogo (3) yatawasilishwa mbele ya Bunge na Waziri anayehusika na mambo ya fedha bila ya kubadilishwa, lakini pamoja na mapendekezo yoyote yatakayotolewa na Tume ya Mgawo wa Mapato.

(5) Wakati wowote kabla Baraza la Taifa kutafakari makadirio ya mapato na matumizi yaliyowasilishwa kwake au kwa mamlaka ya Waziri anayehusika na mambo ya fedha, kamati inayohusika ya Bunge itajadili na kuyarekebisha makadirio hayo na kutoa mapendekezo yanayofaa Bungeni.

(6) Kamati hiyo iliyotajwa katika Ibara ndogo (5), italazimika, katika kujadili na kurekebisha makadirio, kutafuta mapendekezo ya umma na ya Baraza la Uchumi na Jamii, na mapendekezo hayo yatazingatiwa wakati kamati hiyo itakapotoa mapendekezo yake Bungeni.

Mswada wa mgawanyo na matumizi ya mapato 232. (1) Katika kila mwaka wa fedha, Waziri anayehusika na mambo ya fedha,

atawasilisha Bungeni Mswada wa kugawa mapato uliotokana na mapendekezo ya Tume ya Mgawo wa Mapato na Mswada huo utagawa mapato yaliyokusanywa na Serikali kwa ngazi mbili za serikali.

(2) Kwa msingi wa Mswada wa kugawa mapato uliopitishwa na Bunge chini ya Ibara ndogo (1), kila ngazi ya serikali itatayarisha na kupitisha Miswada yake ya bajeti na matumizi.

(3) Wakati makadirio ya matumizi ya Serikali, isipokuwa matumizi yanayotozwa katika Mfuko wa Fedha za Serikali kwa mujibu wa Katiba au Sheria iliyotungwa na Bunge, yameidhinishwa na Bunge, yatajumuishwa kwenye Mswada, utakaojulikana kama Mswada wa Matumizi ya Fedha, ambao utawasilishwa Bungeni ili kuwezesha utozaji kutoka kwa Mfuko Mkuu wa viwango vinavyohitajika kuyakimu

Page 127: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

127

matumizi ya viwango hivyo kwa madhumuni yaliyobainishwa kwenye Mswada huo.

(4) Ikiwa, katika mwaka wowote wa fedha -

(a) fedha zilizoidhinishwa kwa shughuli yoyote ile chini ya Sheria ya Matumizi ya Fedha hazitoshi ama mahitaji ya matumizi yametokea ambayo hayakuwa yamepangiwa kiwango katika Sheria hiyo; au

(b) kwamba fedha zote zimetumiwa kutoka kwenye Mfuko wa Dharura kwa sababu hakuna fedha zilizoidhinishwa kwa ajili hiyo,

makadirio ya ziada yanayoonyesha jumla ya fedha zinazohitajika ama zilizotumiwa yatawasilishwa Bunge, na ikiwa ni kuhusu matumizi ya ziada, ndani ya kipindi cha muda wa miezi minne baada ya kutoa kwa mara ya kwanza fedha hizo.

(5) Jumla ya fedha zinazohitajika au kutumiwa kwa makadirio ya ziada, ambapo fedha zilizotengwa hazikutosha, hazitazidi asilimia kumi ya fedha zilizoidhinishwa hapo awali na Bunge kwa madhumuni hayo katika kipindi hicho cha mwaka huo wa fedha, lakini Bunge linaweza katika hali maalumm, kuidhinisha asilimia kubwa zaidi.

(6) Ikitokea kwamba, katika mwaka wowote wa kifedha, kadirio la ziada ama makadirio ya ziada yameidhinishwa na Bunge kwa mujiby wa Ibara ndogo (2), Sheria ya Matumizi ya Fedha za Ziada itawasilishwa Bungeni katika mwaka wa fedha unaofuatia mwaka huo wa fedha ambao unahusiana na makadirio hayo, ili kutoa idhini ya fedha hizo zilizoidhinishwa kwa madhumuni yaliyobainishwa katika makadirio hayo.

(7) Masharti ya Ibara 231(5) yatatumika katika makadirio yaliyotayarishwa chini ya Ibara ndogo (4).

(8) Pale ambapo sheria ya kuidhinisha matumizi kwa ajili ya mwaka wa fedha haijaidhinishwa, au kuna uwezekano wa kutoidhinishwa wakati wa kuanza mwaka huo wa fedha, Bunge linaweza, kuidhinisha kifungu cha matumizi kutoka Mfuko Mkuu (ambacho hakitazidi kwa jumla nusu ya makisio ya matumizi kwa mwaka huo wa fedha ambayo yamewasilishwa Bungeni), kwa ajili ya kukidhi matumizi ya lazima ili kutekeleza huduma za Serikali katika mwaka huo mpaka Mswada sheria ya Matumizi itakapoidhinishwa, lakini fedha zozote zilizotoka kwa njia hiyo zitajumuishwa katika vifungu tofauti kwa huduma mbali mbali ambazo fedha hizo zilitolewa kwa mujibu wa sheria ya matumizi.

Bajeti ya mwaka ya serikali za wilaya 233. Bunge litaagiza kupitia sheria -

Page 128: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

128

(a) muundo wa mipango pamoja na bajeti za serikali zote za wilaya;

(b) yaliyomo ndani ya mipango na bajeti za serikali zote za wilaya, vikiwemo vyanzo vya mapato na namna matumizi yanayopendekezwa yatakavyofuata mpango wa Taifa na makadirio ya kifedha;

(c) wakati ambao mipango na bajeti za serikali za wilaya zitakapowasilishwa; na

(d) hali na namna ya ushauriano baina ya Serikali na serikali serikali za wilaya wakati wa kuandaa mipango na bajeti.

Sehemu ya Sita – Usimamizi wa Fedha

Ununuaji bidhaa na huduma za umma 234. (1) Wakati chombo cha Serikali au taasisi nyingine ya umma katika ngazi

yoyote ya serikali inapofanya mkataba kwa ajili ya ununuzi bidhaa au huduma, itafanya hivyo kuambatana na mfumo ambao ni wa haki, wenye usawa, na uwazi na wenye ushindani, na usio na gharama kubwa.

(2) Sheria iliyotungwa na Bunge itaweka mfumo ambamo sera zinazohusiana na ununuzi na utoaji zitaweza kutekelezwa na zitazingatia yote au baadhi ya yafuatayo, kuhusu -

(a) aina ya kupendekezwa katika kugawanya mikataba;

(b) himaya na uendelezaji wa watu, aina ya watu, au makundi ya watu ambao hapo awali walikuwa wamenyimwa fursa kwa mashindano yasiyo ya haki au ubaguzi;

(c) vikwazo dhidi ya makandarasi wasiofanya kazi zao kwa utaratibu uliodhibitiwa kitaaluma, mapatano ya kandarasi au sheria; na

(d) vikwazo dhidi ya watu ambao wamekwepa wajibu wao wa kulipa kodi, au wana hatia ya vitendo vya ufisadi au ukiukaji mkubwa wa sheria na mienendo ya haki ya kuajiri.

Hesabu na ukaguzi wa taasisi za umma 235. (1) Katibu Mkuu anayesimamia wizara na msimamizi mkuu wa idara au

shirika la umma kila mmoja anawajibika kwa Bunge kuhusu fedha za wizara hiyo, idara au shirika la umma.

(2) Hesabu za serikali zote na vyombo vya serikali zitakaguliwa na Mkaguzi Mkuu.

(3) Hesabu za afisi ya Msimamizi wa Bajeti na Mkaguzi Mkuu zitakaguliwa na kutolewa taarifa na mhasibu mwenye sifa za kitaaluma na ambae atateuliwa na Bunge.

Page 129: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

129

(4) Ikiwa mtu yeyote katika huduma ya umma, ikiwemo afisi ya kisiasa, ataamuru au ataidhinisha matumizi ya fedha za umma kinyume na sheria, masharti au maagizo, mtu huyo atawajibika kwa hasara yoyote itakayotokana na matumizi hayo na atalazimika kulipa hasara hiyo, iwe mtu huyo bado yuko afisini au hayuko.

(5) Sheria iliyotungwa na Bunge itaeleza jinsi ya kuweka kumbukumbu na ukaguzi wa hesabu za serikali za wilaya, na kuelezea hatua nyengine kwa ajili ya kuhakikisha utendaji bora na uwazi katika usimamizi wa fedha.

Kudhibiti hazina 236. (1) Sheria itakayotungwa na Bunge itaunda chombo cha Serikali ya Taifa

kitakachoitwa Hazina Kuu na itaagiza hatua zitakazohakikisha uwazi na udhibiti na matumizi katika kila ngazi ya serikali.

(2) Hazina Kuu, kwa maafikiano na Waziri anayehusika na fedha, inaweza kusimamisha uhamishaji wa fedha kwa chombo cha Serikali au taasisi ya umma kwa sababu tu ya ukiukaji mkubwa wa taratibu za kifedha, au ukiukaji wa kifedha wa mara kwa mara, wa taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Ibara ndogo (1).

(3) Uamuzi wa kutohamisha fedha uliofikiwa kwa mujibu wa Ibara ndogo (2), hautazuia uhamishaji wa zaidi ya asilimia hamsini ya fedha za kitengo chochote cha serikali ya wilaya.

(4) Uamuzi wa kutohamisha fedha uliofikiwa kwa mujibu wa Ibara

ndogo (2) - (a) hautazuia uhamishaji wa fedha kwa muda unaozidi siku sitini;

na

(b) unaweza kutekelezwa mara moja, lakini utakoma kuanzia nyuma, ila ikiwa ndani ya siku thelathini baada ya tarehe ya uamuzi huo, Bunge litaidhinishe kwa azimio.

(5) Bunge linaweza kutoa upya uamuzi wa kukomesha kuhamisha fedha chini ya Ibara ndogo (2), kwa siku zisizozidi sitini kwa wakati mmoja.

(6) Kabla Bunge halijaidhinisha au kutoa upya uamuzi wa kukomesha uhamishaji wa fedha -

(a) Msimamizi wa Bajeti atatoa taarifa Bungeni; na

(b) serikali ya wilaya inayohusika, chombo cha Serikali, au taasisi ya umma itafahamishwa ukiukaji huu na itapewa fursa ya kujibu madai dhidi yake mbele ya kamati ya Bunge.

Msimamizi wa Bajeti 237. (1) Kutakuwa na Msimamizi wa Bajeti atakayeteuliwa na Rais na

kuidhinishwa na Bunge.

Page 130: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

130

(2) Ili mtu kuteuliwa kuwa Msimamizi wa Bajeti, mtu huyo atakuwa -

(a) ni mhasibu aliyehitimu kitaaluma na awe mwenye uzoefu usiopungua miaka kumi na ujuzi katika uchumi na usimamizi wa fedha; na

(b) mtu mwenye hulka ya uaminifu na uadilifu.

(3) Msimamizi wa Bajeti atakuwa madarakani kwa muhula cha miaka mitano na anaweza, akiwa na sifa, kuteuliwa kwa muhula mwingine mmoja.

(4) Msimamizi wa Bajeti atasimamia utekelezaji wa bajeti kama ilivyoidhinishwa na Serikali na serikali za wilaya kwa -

(a) kuhakikisha kwamba fedha zinatumiwa kwa matumizi yaliyoagizwa au kama ni fedha zilizotoka Mfuko wa Dharura, kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge iliyotajwa katika Ibara ya 225;

(b) kutoa hesabu kamili ya matumizi halisi na sio makadirio ya matumizi;

(c) kutoa ushauri wa kitaaluma kwa kamati za fedha za Bunge; na

(d) kufanya kazi kwa karibu na Hazina Kuu, idara na Wizara.

(5) Ndani ya kipindi cha miezi miwili baada ya kila mwaka wa fedha kumalizika, Msimamizi wa Bajeti atawasilisha Bungeni taarifa ya shughuli za afisi ya Msimamizi wa Bajeti mnamo mwaka huo wa fedha.

(6) Ndani ya kipindi cha miezi mitatu baada ya kuwasilisha taarifa hiyo iliyo katika Ibara ndogo (5), Bunge litajadili na kutafakari taarifa hiyo na kuchukua hatua zinazofaa.

(7) Katika kutekeleza majukumu yake, Msimamizi wa Bajeti hataelekezwa wala kudhibitiwa na mtu ama mamlaka yoyote.

(8) Sababu na utaratibu wa kumwondoa mwanatume wa Tume ya kikatiba kama ilivyoagizwa katikba Ibara ya 277, yatatumika pamoja na marekebisho yanayofaa, kwa Msimamizi wa Bajeti.

(9) Malipo na marupurupu ya Msimamizi wa Bajeti yatatolewa kwenye Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali.

Mkaguzi Mkuu wa Fedha 238. (1) Kutakuwa na Mkaguzi Mkuu atakayeteuliwa na Rais na kuidhinishwa na

Bunge.

(2) Ili mtu kuteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu, mtu huyo awe -

(a) ni mhasibu aliyehitimu kitaaluma na awe mwenye uzoefu usiopungua miaka kumi na ujuzi mkubwa wa ukaguzi wa fedha za umma;

Page 131: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

131

(b) mtu mwenye hulka ya uaminifu na uadilifu.

(3) Mkaguzi Mkuu atakuwa madarakani kwa muhula wa miaka mitano na anaweza, akiwa na sifa, kuteuliwa kwa muhula mwingine mmoja.

(4) Mkaguzi Mkuu atafanya kazi ya -

(a) kukagua hesabu za Serikali na za serikali za wilaya na mashirika ya Serikali; na

(b) kuthibitisha kwamba fedha zote zilizoidhinishwa na Bunge au kukusanywa na ngazi yoyote ya serikali na kugawanywa, zimetumiwa ipasavyo, na matumizi hayo yanawiana na mamlaka ya uwezo wake na kwamba matumizi ya pesa yalidhibitiwa, kutumika inavyofaa na kwa ufanisi; na

(c) ndani ya miezi sita baada ya mwisho wa kila mwaka wa fedha, kukagua na kutoa taarifa ya mwaka huo wa fedha, kuhusu -

(i) hesabu za umma za kitaifa na za serikali za wilaya;

(ii) hesabu za mifuko yote na mamlaka za Serikali na za serikali za wilaya;

(iii) hesabu za mahakama zote;

(iv) hesabu za Tume zote zilizoundwa na Katiba hii;

(v) hesabu za Bunge;

(vi) hesabu za vyama vya kisiasa zinazogharimiwa na fedha za umma;

(vii) hesabu za taasisi zozote zinazogharimiwa kutoka fedha za umma; na

(viii) deni la umma.

(5) Ndani ya kipindi cha miezi mitatu baada ya kuwasilisha taarifa iliyoelezwa kwenye Ibara ndogo (4)(c), Bunge litajadili na kutafakari taarifa hiyo na kuchukua hatua zinazofaa.

(6) Sheria iliyotungwa na Bunge itaagiza uwekaji wa kumbukumbu na ukaguzi wa hesabu wa serikali za wilaya, na kuagiza hatua nyingine za kupata usimamizi wa fedha uliobora na wazi.

(7) Katika kutekeleza majukumu yake, Mkaguzi Mkuu hatowajibika au kudhibitiwa na mtu yeyote au mamlaka yoyote.

(8) Sababu na utaratibu wa kumwondoa mwanatume wa Tume ya kikatiba kama ilivyoagizwa katikba Ibara ya 277, yatatumika pamoja na marekebisho yanayofaa, kwa Mkaguzi Mkuu.

(9) Malipo na marupurupu ya Mkaguzi Mkuu yatatolewa kwenye Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali.

Page 132: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

132

Sehemu ya Saba - Taasisi

Mamlaka ya Mapato ya Taifa 239. (1) Inaundwa Mamlaka ya Mapato ya Taifa.

(2) Mamlaka hii ina wajibu wa kukusanya mapato ya Serikali, isipokuwa kama ilivyoagizwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

(3) Muundo, majukumu, na shughuli za mamlaka ni kama ilivyoagizwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

Tume ya Mgawo wa Mapato 240. (1) Inaundwa Tume ya Mgawo wa Mapato.

(2) Tume hii itakuwa na watu wafuatao watakaoteuliwa na Rais -

(a) mwenyekiti;

(b) wawakilishi kumi na sita wa serikali za wilaya, walioteuliwa na Kikao cha Kitaifa cha Serikali za Wilaya;

(c) watu wawili walioteuliwa na Bunge;

(d) Katibu Mkuu katika wizara inayohusika na fedha; na

(e) Msimamizi wa Bajeti.

(3) Jukumu muhimu zaidi la Tume hii ni kuchunguza msingi wa mgawo wa mapato ya rasilmali ya Taifa na kuhakikisha kuwa mgawo huo ni wa uadilifu baina ya -

(a) Serikali na serikali za wilaya ;

(b) serikali za wilaya ; na

(c) ikihitajika, misaada inayotolewa kwa masharti au bila masharti.

(4) Tume -

(a) itatoa taarifa kwa Serikali na serikali za wilaya kuhusu mgawo wa mapato ya Taifa kwa ngazi mbili za serikali;

(b) itapitia mara kwa mara mapendekezo hayo ili kuhakikisha kuwa yanabadilika na hali; na

(c) itasuluhisha na kuamua mizozo inayohusu mipango ya fedha baina ya Serikali na serikali za wilaya.

(5) Katika mapendekezo yake, Tume -

(a) italenga kufafanua na kuendeleza vyanzo vya mapato katika ngazi mbili za serikali kwa madhumuni ya kuhimiza uwajibikaji wa kifedha na kuzisaidia serikali za wilaya hadi zifikie uwezo wa kujitegemea kifedha; na

Page 133: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

133

(b) kutoa mapendekezo ya kitendo cha upendeleo.

(6) Katika mapendekezo yake kuhusu ugawaji wa mapato ya kitaifa, Tume itazingatia -

(a) maslahi ya kitaifa;

(b) kiasi chochote kinachofaa kutengwa kuhusia na deni la kitaifa na majukumu mengine ya kitaifa;

(c) mahitaji na maslahi ya Serikali, yanayotegemea vigezo halisi;

(d) umuhimu wa kuhakikisha kuwa wilaya zinaweza kutoa huduma za msingi na kutekeleza wajibu wake;

(e) uwezo wa kifedha na ufanisi katika wilaya;

(f) mahitaji ya kimaendeleo na mengineyo katika wilaya;

(g) tofauti za kiuchumi ndani ya, na miongoni mwa wilaya kwa ajili ya masawazisho ya kifedha na haja ya kuwa na usawazishaji wa kifedha;

(h) umuhimu wa kitendo cha upendeleo;

(i) umuhimu wa uchumi bora zaidi katika kila wilaya;

(j) majukumu ya wilaya kwa mujibu wa Sheria za kitaifa;

(k) matarajio ya kuwapo migawo ya mapato thabiti na ya kubashirika; na

(l) umuhimu wa kuchukua hatua za wepesi katika kukabiliana na mambo ya dharura na mambo mengine ya muda, na hali nyingine zinazotokana na vigezo sawa na madhubuti.

(7) Mapendekezo ya Tume yanaweza kubadilishwa na Serikali kwa idhini ya Bunge.

(8) Sheria iliyotungwa na Bunge itahakikisha kuweko kwa taratibu na shughuli za Tume na kuagiza mfumo wa kutekeleza sera iliyotajwa katika Ibara ndogo (3).

(9) Tume itakuwa na majukumu mengine kama ilivyoagizwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

(10) Katika kutekeleza wajibu wake, Tume itazingatia kanuni, vigezo, utaratibu, masharti na mifumo ya kuhakikisha kuwa kuna ugawaji sawa wa mapato ya taifa na maliasili kama ilivyoagizwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

(11) Kila mwaka, kabla ya kupita Januari 31, Tume itaandaa taarifa, kwa mujibu wa masharti yaliyotungwa na Sheria ya Bunge, ikidhihirisha mapendekezo yake kuhusu mgawo wa mapato ya taifa kwenye ngazi zote mbili za serikali na kuwasilisha taarifa hiyo Bungeni ili iidhinishwe.

Page 134: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

134

(12) Mapendekezo ya Tume kama yalivyobadilishwa chini ya Ibara ndogo (7), yanazishurutisha serikali zote na yatabainishwa katika bajeti zote na utozaji kodi na sera nyingine za sheria.

Benki Kuu ya Kenya 241. (1) Inaundwa Benki Kuu ya Kenya.

(2) Benki Kuu ya Kenya ndiyo mamlaka pekee ya kutoa sarafu za Kenya.

(3) Mamlaka ya Benki Kuu ya Kenya yapo katika Halmashauri itakayokuwa na Gavana, Naibu Gavana na wajumbe wengine wasiozidi watano.

(4) Wajumbe wa Halmashauri -

(a) watateuliwa na Rais na kuidhinishwa na Bunge; na

(b) watakuwa madarakani kwa mujibu wa Ibara ya 273(5) na kwa muhula wa miaka mitano na wanaweza, wakiwa wanasifa, kuchaguliwa tena kwa muhula mmoja zaidi.

(5) Ili kuteuliwa kama Gavana mtu sharti awe na utaalamu, uzoefu na ujuzi katika mambo ya kiuchumi, usimamizi wa fedha au uhasibu na awe mtu mwenye hulka ya uaminifu na uadilifu.

(6) Gavana wa Benki Kuu atakuwa ndiye mwenyekiti wa Halmashauri.

(7) Katibu Mkuu wa Hazina Kuu atakuwa katika Halmashauri hiyo kwa sifa ya afisi yake.

(8) Sababu na utaratibu wa kumwondoa mwanatume wa Tume ya kikatiba kama ilivyoagizwa katikba Ibara ya 277, yatatumika pamoja na marekebisho yanayofaa, kwa Halmashauri hiyo.

Majukumu ya Benki Kuu 242. (1) Benki Kuu ya Kenya -

(a) itaendeleza na kudumisha thamani ya sarafu ya Jamhuri;

(b) itatoa noti na sarafu;

(c) itakuwa kama benki na mshauri wa fedha wa Serikali;

(d) itaendesha sera za fedha za Serikali kwa taratibu zinazoambatana na masharti ya kisheria yanayohusika kwa maslahi ya maendeleo ya kiuchumi yenye usawa na uendelevu katika Jamhuri;

(e) itahimiza na kuendeleza maendeleo ya kiuchumi, na matumizi bora ya rasilmali za Jamhuri, kupitia utendakazi mwema wa shughuli za benki na mfumo wa madeni; na

(f) itafanya shughuli nyingine kwa mujibu wa Sheria zisizopingana na Ibara hii.

Page 135: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

135

(2) Katika kutekeleza majukumu yake, Benki Kuu ya Kenya itatii Katiba hii na haitaelekezwa au kudhibitiwa na mtu au mamlaka yoyote.

(3) Noti na sarafu zitakazotolewa na Benki Kuu ya Kenya zinaweza kuwa tu na picha ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kenya au taswira nyigine zinazoonyesha au kuashiria Kenya au sura yoyote ya Kenya.

Baraza la Uchumi na Jamii 243. (1) Linaundwa Baraza la Uchumi na Jamii litakalokuwa na watu tisa

walioteuliwa na Rais, kwa msingi wa sifa, lakini kwa kuzingatia uanuwai wa watu wa Kenya, na idhini Bunge.

(2) Watu watakaochaguliwa kwenye Baraza hilo -

(a) watakuwa wamehitimu na wenye uzoefu katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii; na

(b) hawatalemea upande wowote watakapochagulia katika Baraza hilo.

(3) Majukumu ya Baraza hilo yatakuwa -

(a) kuishauri Serikali na Bunge katika mambo ya uchumi na jamii yanayowahusu wananchi wa Kenya;

(b) kuishauri serikali kuhusu uundaji, utekelezaji, ufuatiliaji na utathmini wa sera za mikakati ya uchumi na jamii;

(c) kutafakari na kutoa taarifa kwenye Bunge kuhusu athari za kiuchumi, kijamii, za sheria na mapendekezo ya bajeti yanayowasilishwa Bungeni;

(d) kufuatilia hatua za maendeleo ya hali za Wakenya na jinsi yanavyoathiri hali yao ya kimaisha, hasa, hali ya maisha ya walio maskini na wale walio katika hali ngumu; na

(e) majukumu mengine kama yatakavyoagizwa na Sheria ya Bunge.

(4) Kwa mujibu wa Ibara hii, Bunge litatunga sheria -

(a) kunadhimu namna Baraza litakavyotekeleza majukumu yake; na

(b) kueleza aina ya taarifa, yaliyomo, pamoja na namna ya kuiwasilisha kwenye Baraza.

Sheria kuhusu utozaji wa kodi 244. (1) Kuambatana na Ibara ya 220, Bunge litatunga sheria kunadhimu utozaji

wa kodi na uwezo mwingine wa ukusanyaji wa mapato wa serikali za wilaya, na ugawaji wa mapato na utoaji wa misaada kwa serikali za wilaya.

Page 136: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

136

(2) Sheria ya Bunge iliyotajwa katika Ibara ndogo (1) inaweza kuidhinishwa tu baada ya Tume ya Ugawaji wa Mapato na Waziri anayehusika na serikali za wilaya kushauriwa na mapendekezo yao kuwasilishwa Bungeni.

(3) Sheria ya Bunge iliyotajwa katika Ibara ndogo (1), itazingatia -

(a) maslahi ya taifa;

(b) masharti yoyote ambayo yamewekwa kwa minajili ya deni la taifa na majukumu mengine ya kitaifa;

(c) mahitaji na maslahi ya serikali;

(d) haja ya kuhakikisha kuwa serikali za wilaya zinaweza kutekeleza shughuli zilizokabidhiwa;

(e) uwezo wa hazina na ufanisi wa serikali za wilaya;

(f) mahitaji ya kimaendeleo na mahitaji mengine ya serikali za wilaya;

(g) tofauti za kiuchumi miongoni mwa serikali za wilaya, yakiwemo mahitaji ya sehemu zilizotengwa;

(h) majukumu ya serikali za wilaya kuambatana na sheria za kitaifa;

(i) matarajio ya kuwapo migawo ya mapato thabiti na ya kubashirika; na

(j) mahitaji ya dharura au ya muda.

Page 137: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

137

SURA YA KUMI NA SITA

UTUMISHI WA UMMA

Sehemu ya Kwanza - Utumishi wa Umma

Maadili na kanuni za utumishi wa umma 245. (1) Maadili na kanuni zinazoongoza utumishi wa umma ni pamoja

na - (a) kudumisha na kuendeleza viwango vya juu vya maadili ya

kitaaluma;

(b) kuendeleza matumizi ya rasilmali katika njia iliyo thabiti, inayofaa na ya kiuchumi;

(c) utoaji huduma bora usiopendelea, ya haki na yenye usawa;

(d) kuhimiza watu washiriki katika utaratibu wa kutayarisha sera;

(e) kushughulikia mahitaji ya watu wakati yanapotakikana kwa wepesi na katika muda unaofaa;

(f) kujitolea katika utekelezaji wa sera na miradi ya umma.

(g) uwajibikaji katika vitendo vya usimamizi vilivyotekelezwa na vilivyoachwa;

(h) uwazi unaostawishwa kutokana na umma kupata maelezo sahihi na kwa muda unaofaa;

(i) kwa mujibu wa aya (k), sifa ndio msingi katika uteuzi na upandishaji vyeo;

(j) nafasi za kutosha na fursa sawa katika uteuzi, mafunzo na maendeleo kwa waume na wake kwa usawa, na watu wa makabila yote; na

(k) uwakilishaji wa uanuwai wa jamii za Kenya, watu wenye ulemavu na jamii ndogo na zilizotengwa katika muundo wa huduma kwa umma katika ngazi zote.

(2) Kanuni za utumishi wa umma zilizotajwa hapo juu zinatumika katika -

(a) huduma za umma katika ngazi mbili za Serikali;

(b) huduma za umma katika vyombo vyote vya Serikali; na

(c) huduma za umma katika mashirika yote ya umma.

Tume ya Utumishi wa Umma 246. (1) Inaundwa Tume ya Utumishi wa Umma.

Page 138: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

138

(2) Kutakuwa na katibu wa Tume ambaye atakuwa mtendaji mkuu na atateuliwa na Rais kwa mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma na kwa idhini ya Bunge.

(3) Katibu wa Tume atashika madaraka kwa muhula wa miaka mitano na anaweza kuchaguliwa tena kwa muhula mmoja zaidi wa miaka mitano.

Uwezo na majukumu 247. (1) Uwezo na majukumu ya Tume ni -

(a) kuunda na kufuta afisi, isipokuwa kama kuna masharti tofauti katika Katiba hii;

(b) isipokuwa kama kuna masharti tofauti katika Katiba hii, kuteua watu watakaochukua madaraka chini ya Katiba hii, au sheria nyingine yoyote, kuteua au kuteua kwa muda watu kufanya kazi katika huduma za umma, kuthibitisha uteuzi na kuchukua hatua za nidhamu na kuondoa watu wanaofanya kazi katika afisi hizo;

(c) kuchunguza, kufuatilia na kutathmini mpangilio, usimamizi na mienendo ya wafanyi kazi wa huduma za umma;

(d) kuhakikisha utendaji thabiti na wenye matokeo bora katika utendaji wa huduma kwa umma;

(e) kuhakikisha kwamba taratibu zinazohusu uajiri, uhamishaji, upandishaji vyeo, na hatua za kinidhamu za wafanyikazi zinaambatana na maadili na kanuni kama zilizowekwa katika Ibara ya 13 na 245;

(f) kuyapitia upya makubaliano na masharti, ya kazi, na kanuni kuhusiana na sifa za maafisa wa umma, na kuendeleza nguvukazi katika huduma ya umma na kutoa mapendekezo kwa serikali kuhusiana na hayo;

(g) kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Ibara ya 279 na kutathmini kiwango cha utekelezaji wa maadili na kanuni kama zilivyowekwa katika Ibara ya 13 na 245;

(h) kusikiliza na kuamua rufani kuhusu masuala ya utumishi wa umma kutoka kwa serikali za wilaya; na

(i) kutekeleza majukumu mengine kwa mujibu wa Katiba hii au Sheria iliyotungwa na Bunge.

(2) Tume inaweza, kwa masharti ambayo itayaweka kwa maandishi, kukabidhi mamlaka yake yoyote na majukumu yake chini ya Ibara hii kwa mjumbe au wajumbe wa Tume, au kwa afisa, shirika au mamlaka inayohudumia umma.

(3) Ibara ndogo (1) haitatumika kwa afisi zifuatazo za utumishi wa umma -

Page 139: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

139

(a) afisi za dola;

(b) afisi ya Balozi, au mwakilishi yeyote mkuu wa Jamhuri katika taifa lingine;

(c) afisi ambazo ya mwanatume wa Tume ya kikatiba;

(d) afisi katika serikali ya wilaya; na

(e) afisi yoyote ya huduma kwa serikali ya wilaya, ila ikiwa inahusu rufaa katika Ibara ndogo (1)(h).

(4) Mtu hatateuliwa chini ya Ibara ndogo (1) kufanya kazi kama mhudumu wa binafsi wa Rais au Rais mstaafu, bila idhini ya Rais au Rais mstaafu.

(5) Bunge litatunga sheria ili kuboresha utendakazi wa Tume hii.

Ajira katika serikali za wilaya 248. Serikali ya wilaya ina wajibu wa kuajiri, kuteua, kupandisha cheo, kuhamisha na

kufuta kazi watu katika utumishi wake wa umma kwa kuzingatia mfumo wa taratibu zilizosawa na viwango kwa mujibu ya Sheria iliyotungwa na Bunge.

Himaya kwa maafisa wa umma 249. Afisa wa Umma -

(a) hatoonewa ama kubaguliwa kutokana na utekelezaji wa wajibu wake kwa mujibu wa Katiba au sheria nyingine yoyote; au

(b) hatofutwa kazi ama kuondolewa katika madaraka au kuteremshwa madaraka ama kuadhibiwa kwa vyovyote vile bila ya kufuata utaratibu wa sheria.

Tume ya Huduma ya Walimu 250. (1) Inaundwa Tume ya Huduma ya Walimu.

(2) Majukumu ya Tume ya Huduma ya Walimu yatakuwa ni -

(a) kusajili walimu waliohitimu mafunzo; na

(b) kwa mujibu wa Ibara ya 248 -

(i) kuandikisha na kuajiri walimu waliosajiliwa;

(ii) kuwapangia sehemu za kazi walimu walioajiriwa na Tume ili watoe huduma katika shule yoyote ya umma na taasisi nyingine;

(iii) kuwapandisha vyeo na kuwahamisha walimu;

(iv) kuwachukuliwa walimu hatua za kinidhamu;

(v) kuwafuta ajira walimu huyo; na

(vi) kutekeleza majukumu mingine yoyota ya Tume hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Bunge.

Page 140: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

140

(3) Tume itapitia upya viwango vya elimu, ufundishaji na uwezo wa kufundisha unaofaa kwa watu wanaoingia katika huduma ya ufundishaji na upatikanaji wa walimu pamoja na kuishauri Serikali kuhusu masuala ya taaluma ya ualimu.

Tume ya Huduma za Afya 251. (1) Inaundwa Tume ya Huduma za Afya.

(2) Majukumu ya Tume ya Huduma za Afya ni -

(a) kusajili wahudumu wa afya waliohitimu;

(b) kwa mujibu wa Ibara ya 248 -

(i) kuandikisha na kuajiri wahudumu wa afya;

(ii) kuwapangia sehemu za kazi wahudumu wa afya walioajiriwa na Tume ili watoe huduma katika hospitali yoyote ya umma au taasisi nyingine; na

(iii) kuwapandisha vyeo na kuwahamisha maafisa hao;

(c) kuhakikisha ukuzaji wa nguvukazi na viwango na maadili ya kitaaluma katika huduma ya afya;

(d) kuhakikisha usajili wa wataalamu wote kwenye sekta ya afya;

(e) kufanya ukaguzi wa afya na utafiti;

(f) kuhakikisha usimamizi unaofaa wa kiufundi, pamoja na kupata huduma na vifaa;

(g) kusimamia fedha za huduma ya afya; na

(h) kutekeleza majukumu mengine yoyote yaliyoagizwa na Tume kwa mujibu ya Sheria iliyotungwa na Bunge.

Tume ya Mishahara na Malipo 252. (1) Inaundwa Tume ya Mishahara na Malipo.

(2) Majukumu ya Tume ya Mishahara na Malipo ni -

(i) kuweka na kurekebisha mishahara na marupurupu ya maafisa wote wa serikali, maafisa wa umma, na wajumbe wa Tume zote za kikatiba;

(j) kusawazisha mishahara na marupurupu ya maafisa wote wa Serikali, maafisa wa umma wakiwemo maafisa wa Serikali za wilaya, na waajiriwa wa mashirika ya Serikali; na

(k) kutekeleza majukumu menginine chini ya Katiba hii au kwa mujibu wa Sheria ya Bunge.

Page 141: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

141

Sehemu ya Pili - Huduma ya Kenya ya Kurekebisha Tabia

Kuundwa kwa Huduma ya Kenya ya Kurekebisha Tabia 253. (1) Inaundwa Huduma ya Kenya ya Kurekebisha Tabia.

(2) Malengo ya Huduma ya Kenya ya Kurekebisha Tabia ni kuhakikisha -

(a) kuwekwa salama kwa watu walioko magerezani na katika hali ya kibinadamu;

(b) kusimamia wahalifu katika jamii wanaotumikia kifungo cha nje ya magereza na walio chini ya uangalizi; na

(c) kuwarekebisha wahalifu ili kuwawezesha kurudia maisha yenye manufaa katika jamii.

(3) Bunge litatunga Sheria -

(a) kuanzisha utaratibu unaotosha kwa uwajibikaji na utawala wa Huduma ya Kenya ya Kurekebisha Tabia;

(b) kuunda mpangilio wa uongozi, usimamizi na utendakazi wa Huduma ya Kenya ya Kurekebisha Tabia; na

(c) kwa jumla kudhibiti Huduma ya Kenya ya Kurekebisha Tabia.

Mkurugenzi Mkuu 254. (1) Inaundwa afisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Kenya ya

Kurekebisha Tabia.

(2) Mkurugenzi Mkuu atateuliwa na Rais kwa ushauri wa Tume ya Utumishi wa Umma na kwa idhini ya Bunge.

(3) Mkurugenzi Mkuu atashika madaraka kwa muhula wa miaka mitano na anaweza kuteuliwa tena kwa muhula mmoja zaidi wa miaka mitano.

(4) Mkurugenzi Mkuu –

(a) naweza kuondolewa madarakani na Rais; au

(b) anaweza kujiuzulu kutoka madarakani kwa kumuandikia Rais, na kujiuzulu huko kutatekelezwa mara tu Rais akipokea barua hiyo.

Page 142: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

142

SURA YA KUMI NA SABA

USALAMA WA TAIFA

Sehemu ya Kwanza – Vyombo vya Usalama vya Taifa

Kanuni na malengo 255. (1) Usalama wa Taifa ni kulinda mipaka ya Kenya, watu wake, mali zao,

uhuru, na maslahi mengine ya kitaifa dhidi ya vitisho vya ndani na nje.

(2) Usalama wa taifa la Kenya utakuzwa na kuhakikishwa kwa mujibu wa kanuni zifuatazo -

usalama wa taifa utategemea mamlaka ya Katiba hii na Bunge;

usalama wa taifa utatekelezwa kuambatana na sheria, ikiwemo na sheria ya kimataifa, na kwa kuheshimu sana utawala wa sheria, demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa kimsingi;

vyombo vya usalama vitaheshimu uanuwai wa tamaduni katika jamii mbali mbali za Kenya katika kutekeleza kazi zake; na

uajiri katika vyombo vya usalama vya taifa utadhihirisha uanuwai wa watu wa Kenya kwa idadi iliyo sawa.

Vyombo vya usalama vya Taifa 256. (1) Vyombo vya usalama vya Taifa ni -

Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi wa Kenya;

Huduma ya Upelelezi ya Taifa;

Huduma ya Polisi wa Kenya; na

Huduma ya Polisi wa Utawala.

(2) Lengo kuu la vyombo vya usalama vya taifa na mfumo wake ni kulinda usalama wa watu wa Kenya na mali yao, na mamlaka ya nchi, amani, umoja wa taifa na kudumisha heshima ya mipaka ya Jamhuri.

(3) Katika utendaji wa kazi zao, vyombo vya usalama vya taifa na kila mtumishi wa vyombo hivyo -

hatalemea upande wowote;

hataendeleza maslahi yoyote ya chama cha kisiasa au lengo lolote; ama

hataathiri maslahi ya kisiasa au lengo la kisiasa ambalo ni halali chini ya Katiba hii.

Page 143: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

143

(4) Hakuna mtu atakayeunda chombo kinachohusiana na usalama wa taifa isipokuwa kama ilivyoidhinishwa na Katiba hii au kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

(5) Vyombo vya usalama vya taifa vitakuwa chini ya mamlaka ya raia.

(6) Bunge litatunga sheria kuweka majukumu, mpangilio na usimamizi wa vyombo vya usalama vya taifa.

Kuundwa kwa Baraza la Usalama la Taifa 257. (1) Linaundwa Baraza la Usalama la Taifa litakalokuwa na -

Rais;

Naibu Rais;

Waziri Mkuu;

Waziri anayehusika na ulinzi;

Waziri anayehusika na mambo ya nje;

Waziri anayehusika na usalama wa ndani; na

Mwanasheria Mkuu.

(2) Rais ataongoza mikutano ya Baraza na iwapo Rais hayupo, Naibu Rais ataongoza, na iwapo Naibu Rais hayupo, Waziri Mkuu ataongoza.

(3) Rais anaweza kumualika mtu yeyote kuhudhuria mkutano wa Baraza hilo.

(4) Kutakuwa na katibu wa Barala la Taifa la Usalama ambaye atateuliwa na Rais.

Majukumu ya Baraza la Usalama la Taifa 258. (1) Baraza la Usalama wa Taifa -

(a) litahakikisha kuwa sera za ndani ya nchi, za kigeni na za kijeshi zinazohusu usalama wa taifa zinafungamana ili kuwezesha vyombo vya usalama kushirikiana kikamilifu;

(b) litatathmini na kupima malengo ya uwajibikaji wa utendaji na hatari kwa Jamhuri kuhusiana na uwezo wa kijeshi uliopo au unaowezekana; na

(c) litaanzisha na kuzingatia sera zinazohusu maslahi ya pamoja kwa vyombo vya usalama vya taifa, na kuimarisha usimamizi kwenye vyombo hivyo;

(2) Baraza la Usalama wa Taifa linaweza, Bunge likiidhinisha -

(a) kupeleka majeshi nje ya Kenya kwa -

(i) kusaidia shughuli za amani za kimataifa na za kanda;

(ii) Baraza la Usalama wa Taifa linaweza, Bunge likiidhinisha

Page 144: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

144

(b) kuidhinisah kuletwa majeshi ya kigeni nchini Kenya.

(3) Baraza la Usalama wa Taifa litatoa taarifa Bungeni kila mwaka kuhusu hali ya usalama ya Jamhuri.

Sehemu ya Pili – Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi

Kuundwa kwa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya 259. (1) Vinaundwa Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi vitakavyokuwa na -

Jeshi la Kenya la Nchi Kavu;

Jeshi la Kenya la Anga; na

Jeshi la Kenya la Wanamaji.

(2) Hakuna mtu atakayeruhusiwa kuanzisha kikosi cha kijeshi ama chenye hadhi ya kijeshi isipokuwa kama ilivyoagizwa na Katiba hii.

(3) Linanundwa Baraza la Ulinzi litakalokuwa na -

Waziri anayehusika na ulinzi, atakayekuwa mwenyekiti;

Naibu Waziri anayehusika na ulinzi, atakayekuwa Makamu Mwenyekiti;

Mkuu wa Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi wa Kenya;

Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu;

Kamanda wa Jeshi la Anga; na

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji; na

Katibu Mkuu katika Wizara inayohusika na ulinzi.

(4) Baraza la Ulinzi litateua katibu wake.

(5) Baraza la Ulinzi litakuwa na wajibu wa jumla wa sera, kudhibiti na usimamizi wa Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi vya Kenya pamoja na majukumu mengine yanayoweza kuagizwa na Bunge kwa mujibu wa Sheria.

Uamrishaji jeshini 260. (1) Rais, kwa ushauriano na Baraza la Ulinzi, atateua Mkuu wa Vikosi vya

Ulinzi wa Kenya, Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu, Kamanda wa Jeshi la Anga na Kamanda wa Jeshi la Wanamaji.

(2) Bila kuathiri uwezo wa Rais kama Amri Jeshi Mkuu, Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Kenya na Makamanda wa Majeshi watatekeleza amri zao kwa Vikosi vya Ulinzi wa Kenya na kutekeleza majukumu mengine yatakayoidhinishwa na Bunge kwa mujibu Sheria.

Page 145: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

145

Sehemu ya Tatu – Huduma ya Upelelezi ya Taifa

Kuundwa 261. (1) Kunaundwa Huduma ya Upelelezi ya Taifa.

(2) Rais, kwa idhini ya Baraza la Taifa, atateua Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Upelelezi ya Taifa.

(3) Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Upelelezi ya Taifa atakuwa madarakani kwa muhula wa miaka mitano na atastahiki kuteuliwa tena kwa muhula mwingine wa mwisho wa miaka mitano.

(4) Mkurugenzi Mkuu –

(a) anaweza kuondolewa madarakani na Rais;

(b) anaweza kujiuzulu kutoka madarakani kwa kumuandikia Rais, na kujiuzulu huku kutatekelezwa mara tu Rais atakapoipokea barua hiyo.

(5) Mkurugenzi Mkuu atakuwa na amri juu ya Huduma ya Upelelezi wa Taifa na atatekeleza majukumu mengine kama Bunge litakavyoagiza kisheria.

(6) Huduma ya Upelelezi ya Taifa itakuwa na wajibu juu ya upelelezi na ujasusi ili kuendeleza usalama wa taifa, kulinda Katiba, maslahi ya dola na ustawi wa watu wa Kenya, na itatekeleza majukumu mengine kama Bunge litakavyoagiza kisheria.

(7) Katika kutekeleza majukumu yake, Huduma ya Upelelezi ya Taifa itaheshimu haki za binadamu, haki za msingi na utawala wa sheria.

(8) Hakuna huduma ya upelelezi, isipokuwa Huduma ya Upelelezi ya Taifa, ya Polisi wa Kenya au kitengo cha Upelelezi cha Vikosi vya Ulinzi wa Kenya, itaundwa ila kwa sheria.

Baraza la Upelelezi la Taifa 262. (1) Linaundwa Baraza la Upelelezi la Taifa lenye -

(a) Waziri anayehusika na usalama na upelelezi nchini, atakayekuwa mwenyekiti;

(b) Waziri anayehusika na mambo ya nje;

(c) Waziri anayehusika na fedha;

(d) Mwanasheria Mkuu; na

(e) Mtu anayeongoza Utumishi wa Umma.

(2) Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Upelelezi ya Taifa atakuwa Katibu wa Baraza la Upelelezi la Taifa.

(3) Majukumu ya Baraza la Upelelezi ni -

Page 146: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

146

(a) kushauri Huduma ya Upelelezi ya Taifa kuhusu masuala yote yanayohusu -

(i) sera ya usalama wa taifa na upelelezi;

(ii) usimamizi wa huduma;

(iii) matumizi ya kifedha ya huduma hiyo; na

(b) majukumu mengine kama itakavyoagizwa na Bunge kwa mujibu wa sheria.

Sehemu ya Nne - Huduma ya Polisi ya Kenya

Kuundwa 263. (1) Kunaundwa Huduma ya Polisi ya Kenya.

(2) Huduma ya Polisi ya Kenya ni huduma ya polisi ya taifa, na mgawo wa majukumu yake utaratibiwa ili kuzingatia muundo wa usambazaji wa mamlaka.

(3) Bunge litatunga sheria ili kutekeleza ibara hii.

Malengo na majukumu 264. (1) Huduma ya Polisi ya Kenya -

(a) itajitahidi kufikia viwango vya juu vya kitaaluma na nidhamu;

(b) itaondoa ufisadi;

(c) itazingatia kanuni zilizofafanuliwa katika Ibara ya 256(3);

(d) itaheshimu na kuzingatia viwango vya haki za kibinadamu, uhuru wa kimsingi na utawala wa sheria;

(e) itafuata kanuni za uwazi na uwajibikaji;

(f) itajenga na kukuza uhusiano mwema baina yake na jamii; na

(g) itaratibu, itasimamia, na itadhibiti mashirika yote ya usalama ya kibinafsi na yanayohusiana na serikali ili kuhakikisha usalama na amani nchini Kenya.

(2) Huduma ya Polisi ya Kenya itafanya Kazi na jamii ili kuhakikisha -

(a) kudumisha sheria na nidhamu;

(b) kuzuia na kupeleleza uhalifu;

(c) usalama wa watu;

(d) kulinda maisha na mali;

(e) kulinda haki na uhuru;

(f) mazingira salama na yenye amani; na

Page 147: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

147

(e) kusaidia waathirika wa uhalifu na ghasia.

Inspekta Jenerali wa Huduma ya Polisi ya Kenya 265. (1) Rais atateua Inspekta Jenerali wa Huduma ya Polisi ya Kenya.

(2) Inspekta Jenerali atakuwa madarakani kwa muhula mmoja wa miaka mitano.

(3) Inspekta Jenerali atakuwa na amri juu ya Huduma ya Polisi ya Kenya na atatekeleza majukumu mengine kama atakavyoagizwa na Bunge kwa mujibu wa sheria.

(4) Inspekta Jenerali -

(a) naweza kuondolewa madarakani na Rais; au

(b) anaweza kujiuzulu kutoka madarakani kwa kumuandikia Rais, na kujiuzulu huko kutatekelezwa mara tu Rais akipokea barua hiyo.

(5) Inspekta Jenerali hataondolewa madarakani isipokuwa kwa mapendekezo ya mahakama maalum iliyoteuliwa na Rais yenye -

(a) Jaji wa Mahakama Kuu, atakayekuwa mwenyekiti;

(b) mwenyekiti wa Tume ya Huduma ya Polisi; na

(c) mtu mwingine mwadilifu aliyehudumia umma kwa utumishi bora.

Tume ya Huduma ya Polisi 266. (1) Inaundwa Tume ya Huduma ya Polisi.

(2) Tume ya Huduma ya Polisi itakuwa na -

(a) mtu anayestahiki kuteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu;

(b) maafisa wa polisi wawili waliostaafu, mmoja kutoka kila Huduma;

(c) watu watatu waadilifu waliohudumia umma kwa utumishi bora;

(d) Inspekta Jenerali wa Huduma ya Polisi ya Kenya; na

(e) Kamanda Jenerali wa Huduma ya Polisi wa Utawala.

(3) Rais atateua Mwenyekiti miongoni mwa wajumbe walioteuliwa chini ya Ibara ndogo (2).

(4) Tume ya Huduma ya Polisi itateua katibu wake.

(5) Majukumu ya Tume ya Huduma ya Polisi ni - (a) kuajiri na kuteua watu watakaofanya kazi, kushika nafasi kwa

muda na kuamua kuhusu kupandisha vyeo katika Huduma;

Page 148: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

148

(b) kuendelea kupitia upya maswala yote yanayohusu viwango au sifa zinazohitajika kwa watumishi wa Huduma;

(c) kuendelea kupitia upya maswala yote yanayohusu mishahara, marupurupu na hali na masharti mengine katika Huduma;

(d) kudhibiti nidhamu, pamoja na kusikiliza na kuamua rufani za watu wa Huduma; na

(e) kutekeleza majukumu mengine yaliyoagizwa na Katiba hii au kwa mujibu wa Sheria ya Bunge.

(6) Katika Ibara hii “Huduma” ina maana ya Huduma ya Polisi ya Kenya na Huduma ya Polisi wa Utawala.

Sehemu ya Tano – Huduma ya Polisi wa Utawala

Kuundwa kwa Huduma ya Polisi wa Utawala 267. (1) Inaundwa huduma itakayoitwa Huduma ya Polisi wa Utawala.

(2) Huduma ya Polisi wa Utawala ni huduma tofauti na Huduma ya Polisi ya Kenya.

(3) Huduma ya Polisi wa Utawala itapangwa kwa namna itakayozingatia usambazaji wa mamlaka.

(4) Huduma ya Polisi wa Utawala itakuwa huduma chini ya Tume ya Huduma ya Polisi.

Majukumu ya Huduma ya Polisi wa Utawala 268. (1) Huduma ya Polisi wa Utawala itafanya kazi na watu ili -

(a) kuhifadhi na kudumisha amani ya umma; na

(b) kuzuia uhalifu.

(2) Polisi wa utawala -

(a) wanaweza kuwakamata wahalifu na kufanya mambo yote yanayohitajika ili kudumisha amani ya umma na kulinda haki za binadamu na uhuru; na

(b) watazingatia kanuni zilizofafanuliwa katika Ibara ya 256(3) na 264(1).

Kamanda Jenerali wa Huduma ya Polisi wa Utawala 269. (1) Rais, kwa idhini ya Bunge, atateua Kamanda Jenerali wa Huduma ya

Polisi wa Utawala.

(2) Kamanda Jenerali wa Huduma ya Polisi wa Utawala atakuwa madarakani kwa muhula mmoja wa miaka mitano.

Page 149: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

149

(3) Kamanda Jenerali wa Polisi wa Utawala atakuwa na amri juu ya Huduma ya Polisi wa Utawala na atatekeleza wajibu mwingine kama ilivyoagizwa na Bunge kwa mujibu wa sheria.

(4) Kamanda Jenerali

(a) naweza kuondolewa madarakani na Rais; au

(b) anaweza kujiuzulu kutoka madarakani kwa kumuandikia Rais, na kujiuzulu huko kutatekelezwa mara tu Rais akipokea barua hiyo.

Page 150: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

150

SURA YA KUMI NA NANE

TUME ZA KIKATIBA

Kutumika kwa Sura 270. Sura hii inatumika kwa Tume zote za Kikatiba, isipokuwa ambapo sharti maalum

limewekwa vinginevyo katika Katiba hii.

Malengo na uhuru wa Tume 271. (1) Malengo ya Tume za Kikatiba ni -

(a) kulinda ukuu wa wananchi;

(b) kudumisha utiifu miongoni mwa vyombo vyote vya serikali kwa kanuni za demokrasia na maadili; na

(c) kuhakikisha uimarishaji wa kikatiba, kwa kuhami majukumu muhimu ya demokrasia ili yasiathiriwe visivyofaa, yasichezewe, na yasiingiliwe kati.

(2) Tume za Kikatiba -

(a) zinawajibika kwa Katiba pekee na sheria;

(b) ni huru na hazielekezwi au kudhibitiwa na mtu yeyote au mamlaka; na

(c) hazitapendelea upande wowote na zitatekeleza majukumu yake bila hofu au upendeleo ama ubaguzi.

(3) Kwa kadri inayofaa, Tume ya Kikatiba -

(a) itaanzisha matawi katika ngazi zote za serikali zilizosambaziwa mamlaka; na

(b) itatoa huduma zake kwa wananchi bila malipo.

Kushirikishwa kwa Tume 272. Tume ya Kikatiba ni chombo chenye hadhi ya kisheria.

Wajumbe wa Tume 273. (1) Tume ya Kikatiba itakuwa na wajumbe wasiopungua watatu na wasiozidi

tisa.

(2) Isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo na Katiba hii, wajumbe wa Tume ya Kikatiba -

(a) watainishwa na kupendekezwa kama itakavyoelezwa na sheria iliyotungwa na Bunge, kwa kuzingatia kanuni za upendeleo maalum;

(b) watateuliwa na Rais; na

Page 151: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

151

(c) wataidhinishwa na Bunge.

(3) Ili kuteuliwa mjumbe wa Tume ya kikatiba mtu sharti -

(a) awe na sifa mahsusi zinazohitajika kwa Tume hiyo na zilizofafanuliwa katika Katiba hii; na

(b) awe na sifa na uzoefu unaofaa.

(4) Mjumbe wa Tume ya Kikatiba anaweza kuajiriwa kwa ajira ya kudumu au kwa muda.

(5) Mjumbe wa Tume ya Kikatiba -

(a) isipokuwa awe ni mjumbe kwa wadhifa wake -

(i) atakuwa madarakani kwa muhula wa miaka mitano na anaweza kuteuliwa kwa muhula mmoja zaidi wa miaka mitano; na

(ii) atastaafu akitimiza miaka sitini na mitano;

(b) isipokuwa awe amekuwa mjumbe kwa wadhifa wake au wa muda, hatakuwa na cheo kingine chenye maslahi au malipo moja kwa moja au vinginevyo, ama ajira nyingine ya umma au ya kibinafsi,; na

(c) atafuata kanuni zilizofafanuliwa katika Sura ya Tisa.

(6) Mjumbe wa Tume ya kikatiba hatachukuliwa hatua au kushitakiwa kwa jambo au kitu alichokifanya kwa nia njema katika utekelezaji wa jukumu lake kama mjumbe.

(7) Wajumbe wa Tume ya Kikatiba watachagua mwenyekiti miongoni mwao -

(a) katika kikao cha kwanza cha Tume; na

(b) itakapolazimu kujaza nafasi katika afisi hiyo.

Wafanyakazi wa Tume 274. Tume ya kikatiba itaajiri wafanyakazi itakaohitaji ili kutekeleza majukumu yake.

Majukumu ya jumla ya Tume 275. (1) Tume ya Kikatiba itaelimisha umma kuhusu wajibu, madhumuni na

majukumu yake na -

(a) inaweza yenyewe kufanya uchunguzi, au kutokana na malalamiko yaliyotolewa na mwananchi;

(b) ina uwezo wa Mahakama Kuu -

(i) kutoa hati za wito; na

Page 152: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

152

(ii) kulazimisha mahudhurio ya shahidi ili kutoa hati kwa minajili ya uchunguzi wake;

(c) kuwasilisha kesi katika Mahakama Kuu kuwa mtu anadharau Tume;

(d) ina uwezo wa kupatanisha, kusuluhisha na kushauriana; na

(e) kwa kadri inavyoruhusiwa na sheria, inaweza kutoa fidia au kutoza faini.

(2) Malalamiko kwa Tume ya Kikatiba yanaweza kuwasilishwa na mtu yeyote anaestahiki kulalamika chini ya Ibara ya 32(1) na (2) -

(a) kwa maandishi akionyesha sababu za malalamiko yake na ithibati zake; au

(b) malalamiko yakiwasilishwa kwa mdomo, ambapo tume itayaandika na kutiwa sahihi na afisa wa Tume.

(3) Tume ya Kikatiba inaweza, pamoja na majukumu yaliyoidhinishwa na Katiba hii, kutekeleza majukumu mengine kama itavyoagizwa na Bunge kwa mujibu wa sheria.

Mikutano ya Tume 276. (1) Mikutano ya Tume ya Kikatiba ni halali hata kama pana nafasi tupu kati

ya wajumbe wake.

(2) Tume ya Kikatiba inaweza, ikizingatia Katiba hii na sheria ya Bunge, kuweka utaratibu wake.

Kuondolewa afisini 277. (1) Mjumbe wa Tume ya Kikatiba anaweza kuondolewa afisini kwa sababu tu

ya -

(a) kutoweza kutekeleza wajibu wa kazi yake kutokana na ugonjwa wa kimwili au kiakili;

(b) utovu wa nidhamu katika kutekeleza majukumu ya afisi hiyo au vinginevyo;

(c) utumiaji mbaya wa afisi au ukiukaji wa kanuni za Sura ya Tisa;

(d) kufilisika; au

(e) kutomudu kazi.

(2) Mtu anayetaka mjumbe wa Tume ya Kikatiba kuondolewa kwa sababu yoyote iliyoko kwenye Ibara ndogo (1), anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa Bunge na aonyeshe sababu za malalamiko yake.

(3) Bunge litachunguza malalamiko na likitosheka kwamba yana sababu chini ya Ibara ndogo (1), litampelekea Rais malalamiko hayo.

Page 153: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

153

(4) Baada ya kupokea malalamiko hayo chini ya Ibara ndogo (3), Rais -

(a) atamsimamisha kazi mjumbe huyo akisubiri matokeo ya malalamiko hayo; na

(b) atateua tume maalum kwa mujibu wa Ibara ndogo (5).

(5) Tume maalum itateuliwa na Rais na itakuwa na -

(a) mwenyekiti, ambaye ana cheo au alikuwa na cheo cha jaji wa Mahakama ya Juu ya kumbukumbu, katika Jamhuri;

(b) angalau watu wawili wanaostahiki kuteuliwa kama Majaji wa Mahakama Kuu; na

(c) mjumbe mwengine mmoja anayeweza kuchunguza mambo yanayohusu sababu hasa za kuondolewa madarakani.

(6) Tume hiyo maalum itachunguza jambo hilo, na itatoa taarifa kuhusu mambo hayo na itoe pendekezo kwa Rais, ambaye atachukua hatua kulingana na pendekezo hilo ndani ya siku thelathini.

(7) Wakati mjumbe amesimamishwa kazi chini ya Ibara hii, mjumbe huyo anastahiki kuendelea kupokea mshahara na marupurupu yake.

Fedha za Tume 278. (1) Fedha za Tume ya Kikatiba ni pamoja na -

(a) pesa zilizotengwa na Bunge kwa ajili ya Tume; na

(b) pesa nyingine zozote zilizopokelewa na Tume katika utekelezaji wa majukumu yake.

(2) Matumizi ya usimamizi wa tume ya Kikatiba pamoja na malipo na marupurupu yanayolipwa, au yanayohusu, watu wanaohudumia Tume yatatoka Mfuko wa Fedha za Serikali.

(3) Tume ya Kikatiba itawasilisha vitabu na hesabu za fedha kwa Mkaguzi Mkuu ili kukaguliwa, ndani ya miezi mitatu baada ya mwaka wa fedha.

(4) Mkaguzi Mkuu atawasilisha, ndani ya miezi mitatu baada ya kuwasilishiwa vitabu na hesabu za fedha, taarifa ya hesabu kwa Rais na Bunge.

Taarifa za mwaka na nyinginezo 279. (1) Tume ya Kikatiba itawasilisha taarifa kwa Rais na Bunge, ndani ya miezi

saba baada ya mwaka wa fedha

(2) Taarifa hiyo itakuwa na -

(a) maelezo kuhusu utekelezaji wake katika kufikia malengo yake;

(b) maelezo kuhusu shughuli zake za mwaka na matarajio ya shughuli za baadaye; na

Page 154: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

154

(c) taarifa ya Mkaguzi Mkuu.

(3) Bunge linaweza, wakati wowote, kuiomba Tume ya Kikatiba kuipelekea taarifa kuhusu jambo lolote.

(4) Rais ataijibu taarifa ya Tume hiyo kwa kuandikia Bunge ambalo litajadili taarifa hiyo pamoja na maelezo ya Rais.

(5) Taarifa ya Tume ya Kikatiba chini ya Ibara hii inaweza kukubalika mahakamani kama ushahidi.

Tume nyinginezo 280. Bunge linawza kwa kupitia sheria kuunda Tume nyingine yoyote ikihitajika

SURA YA KUMI NA TISA

MAREKEBISHO YA KATIBA

Marekebisho ya Katiba 281. (1) Pendekezo la kurekebisho Katiba hii linalohusu -

(a) ukuu wa Katiba;

(b) mipaka ya Kenya;

(c) mamlaka ya wananchi;

(d) kanuni na maadili ya Jamhuri;

(e) Sheria ya Haki za Binadamu;

(f) muda wa kushika Urais;

(g) uhuru wa Idara ya mahakama na Tume za Kikatiba;

(h) majukumu ya Bunge;

(i) maadili na kanuni za kusambaza mamlaka; au

(j) masharti ya Sura hii,

litapitishwa kwa mujibu wa Ibara ya 282 au 283, na kuidhinishwa na wananchi katika wingi wa kura ya maoni iliyopigwa kwa ajili hiyo.

(2) Rekebisho la Katiba hii ambalo halikutarajiwa katika Ibara ndogo (1), litapitishwa ima na -

(a) Bunge, kwa mujibu wa Ibara ya 282; au

(b) watu na Bunge, kwa mujibu wa Ibara ya 283.

Marekebisho yatakayofanywa na Bunge 282. (1) Mswada wa kurekebisha Katiba hii -

Page 155: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

155

(a) hauwezi kushughulikia jambo lingine lolote isipokuwa marekebisho yatokanayo na sheria itokanayo na mswada huo;

(b) hautasomwa kwa mara ya pili katika Bunge, mpaka angalau siku tisini baada ya tarehe ya kusomwa mara ya kwanza kwa mswada katika Bunge; na

(c) utakuwa umepitishwa na Bunge pale ambapo Bunge limepitisha mswada huo, utakaposomwa mara ya pili na ya tatu, kwa wingi wa zaidi ya thuluthi mbili ya kura za wajumbe wote wa Bunge.

(2) Bunge litatangaza mswada wa kurekebisha Katiba hii, na kufanikisha majadiliano ya umma kuhusu mswada huo.

(3) Bunge likipitisha mswada wa kurekebisha Katiba hii, Spika atawasilisha kwa Rais -

(a) hati ya kuthibitisha kwamba mswada umepitishwa na Bunge kwa mujibu wa Ibara hii; na

(b) mswada huo uidhinishwe na uchapishwe.

(4) Ndani ya siku thelathini baada ya mswada huo kuidhinishwa na Bunge, Rais ataiidhinisha na atasababisha uchapishwe, kwa mujibu wa Ibara ndogo (5).

(5) Ikiwa mswada wa kurekebisha Katiba hii unapendekeza rekebisho lililotarajiwa katika Ibara ya 281(1), Rais -

(a) kabla ya kuidhinisha mswada huo, ataiomba Tume ya Uchaguzi na Mipaka kupigisha kura ya maoni ya Kitaifa ili kuidhinisha mswada huo; na

(b) ndani ya siku thelathini baada ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka kuthibitisha kwa Rais kuwa mswada umekubaliwa kwa wingi wa kura za raia waliopiga kura ya maoni, ataidhinisha mswada huo na kusababisha uchapishwe.

Marekebisho kupitia kura ya maoni 283. (1) Rekebisho la Katiba hii linaweza kupendekezwa kwa pendekezo la raia

walio wengi kwa kuwekwa saini na angalau wapiga kura milioni moja waliosajiliwa.

(2) Pendekezo la raia la rekebisho la Katiba hii linaweza kuwa katika umbo la pendekezo la jumla au katika rasimu ya Mswada wa sheria ulioandaliwa.

(3) Ikiwa pendekezo liko katika umbo la pendekezo la jumla, wapendekezaji wa hoja hiyo iliyoungwa mkono wataiandaa kama Mswada wa sheria.

(4) Wapendekezaji wa hoja ya marekebisho iliyoungwa mkono watawasilisha rasimu ya Mswada wa Sheria na saini za kuunga mkono kwa Tume ya

Page 156: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

156

Uchaguzi na Mipaka, ambayo itathibitisha kwamba pendekezo hilo linaungwa mkono na wapiga kura milioni moja waliosajiliwa.

(5) Ikiwa Tume ya Uchaguzi na Mipaka imetosheka kuwa pendekezo hilo linatosheleza mahitaji ya Ibara hii, Tume itawasilisha rasimu ya Mswada huo katika kila Baraza la Wilaya ili kutafakari ndani ya kipindi kisichozidi miezi mitatu baada ya tarehe ya kuwasilishwa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka.

(6) Baraza la Wilaya likiidhinisha rasimu ya Mswada huo, mwenyekiti wa wilaya atawasilisha nakala ya Mswada huo kwa Spika, na hati ya kuthibitisha kwamba baraza hilo la wilaya limeidhinisha.

(7) Rasimu ya Mswada wa Sheria ikiidhinishwa na wingi wa mabaraza ya wilaya, itawasilishwa Bungeni mara moja, ambapo Bunge litaushughulikia mswada kwa mujibu wa Ibara ya 282.

(8) Bunge likipitisha Mswada huo, utawasilishwa kwa Rais ili aidhinishe kwa mujibu wa Ibara ya 282(4) na (5).

(9) Ikiwa Bunge halikupitisha mswada huo, mswada utawasilishiwa raia katika kura ya maoni.

(10) Ikiwa wingi wa raia waliopiga kura kwenye kura ya maoni chini ya Ibara ndogo (9) wameunga mkono mswada huo, itachukuliwa kwamba umepitishwa na Bunge na itawasilishwa kwa Rais ili auidhinishe.

Page 157: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

157

SURA YA ISHIRINI

MASHARTI YA JUMLA

Utekelezaji wa Katiba 284. Masharti ya Ibara ya 31 na 32 yatatumika, na mabadiliko yakilazimu, kwa ajili ya

utekelezaji wa masharti mengine ya Katiba hii.

Kufasiri Katiba 285. (1) Katiba hii itafasiriwa kwa njia ambayo -

(a) inaendeleza malengo, maadili na kanuni zake;

(b) inakuza haki za kibinadamu na uhuru wa kimsingi na utawala wa sheria;

(c) inaruhusu ustawishaji wa sheria; na

(d) inachangia utawala bora.

(2) Ikiwa pana mgongano baina ya matoleo ya lugha mbalimbali ya Katiba hii, toleo la Kiingereza litatumika.

(3) Isipokuwa maelezo yakihitaji vinginevyo, wajibu au madaraka yaliyopewa Bunge na Katiba hii ili kuunda, kuwezesha au kuagiza jambo lolote au kitu yatatekelezwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

(4) Kila sharti katika Katiba hii litafasiriwa kwa msingi wa ufafanuzi kwamba sheria daima inajieleza, na kwa hivyo, pamoja na mambo mengine -

(a) uwezo uliotolewa au wajibu ulioagizwa na Katiba hii unaweza kutekelezwa au kufanywa, kadri hali inavyohitaji, na mtu aliyekalia kiti chenye madaraka yanayohusika au kilichopewa wajibu;

(b) marejeo yoyote katika Katiba hii au sheria yoyote nyengine kwa mtu aliyekalia kiti chini ya Katiba hii ni pamoja na marejeo kwa mtu anayetekeleza kihalali majukumu ya afisi hiyo kwa wakati wowote;

(c) marejeo katika Katiba hii au sheria yoyote nyengine kuhusu afisi, chombo cha Serikali, au mahali palipotajwa katika Katiba hii, itasomeka kwa mujibu wa mabadiliko rasmi yanayohitajika ili yatumike katika hali hiyo; na

(d) marejeo katika Katiba hii kuhusu afisi, shirika au chama ni marejeo kuhusu afisi hiyo, shirika au chama, au endapo afisi hiyo, shirika au chama haipo tena, basi itahusu chombo kilichorithi mahali hapo au kilichosawa na chombo hicho.

(5) Katika Katiba hii, isipokuwa maelezo yaeleze vinginevyo -

Page 158: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

158

(a) kama neno au usemi umefafanuliwa katika Katiba hii, tofauti yoyote ya sarufi au usemi unaofanana na neno hilo au usemi una maana inayokubaliana, utasomeka kwa fasiri na mabadiliko yanayohitajika na muktadha huo; na

(b) neno “pamoja na” lina maana “pamoja na, lakini si maana hiyo pekee” na neno “inajumuisha” ina maana “inajumuisha lakini si maana hiyo pekee”.

(6) Wakati wa kuhesabu muda baina ya matukio mawili kwa sababu yoyote chini ya Katiba hii, ikiwa muda huo unafafanuliwa -

(a) kwa siku, siku ambapo tukio la kwanza limetokea haitahesabiwa na siku ambapo tukio la mwisho limetokea itahesabiwa;

(b) kama miezi, mwisho wa kipindi ni mwanzo wa siku ya mwezi unaohusika -

(i) wenye idadi sawa na siku kama tarehe ambapo kipindi kilianza, kama mwezi huo una tarehe inayofanana; au

(ii) ambayo ni siku ya mwisho ya mwezi huo, vinginevyo; au

(c) kama miaka, kipindi kinamalizika mwanzoni mwa tarehe ya mwaka unaohusika inayofanana na tarehe ya kipindi kuanza.

(7) Kama kipindi kilichotengwa na Katiba hii kwa sababu yoyote ni siku zisizozidi sita, Jumapili na siku za mapumziko hazitahesabiwa wakati wa kuhesabu muda.

(8) Ikiwa, katika hali mahsusi, kipindi kilichotengwa na Katiba hii kwa sababu yoyote kinamalizika siku ya Jumapili au siku ya mapumziko, kipindi kitajumuisha siku inayofuata ambayo si Jumapili au siku ya mapumziko.

(9) Kama hakuna wakati mahsusi uliowekwa wa kutekeleza wajibu, wajibu huo utatekelezwa bila kucheleweshwa kusikofaa, na kila fursa inapojitokeza.

(10) Ikiwa mtu yeyote au chombo cha Serikali kina mamlaka chini ya Katiba hii kuongeza muda uliotengwa na Katiba hii, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo katika sharti linalotoa mamlaka hayo, yanaweza kutekelezwa kabla au baada ya kumalizika kipindi hicho.

(11) Agizo katika hii kuwa mtu yeyote au mamlaka hatokuwa chini ya amri au mwelekezo wa mtu mwengine yeyote au mamlaka katika kutekeleza majukumu yeyote chini ya Katiba hii haitafahamika kuwa inazuia mahkama kutekeleza mamlaka yake kuhusu swali lolote, ikiwa mtu huyo au mamlaka ametekeleza majukumu hayo kwa mujibu wa Katiba hii au sheria nyengine yoyote.

Page 159: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

159

Fafanuzi 286. Katika Katiba hii, isipokuwa maelezo yakihitaji vinginevyo -

“mtu mzima” ni mtu aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane;

“kitendo cha upendeleo” ni pamoja na hatua yoyote iliyokusudiwa kuondoa au kupunguza ukosefu wa usawa au kunyimwa kwa maksudi au kukiukwa kwa haki au uhuru;

“rekebisha” ni pamoja na geuza, ondoa, batilisha, tengua, futa, badilisha, ongeza au tofautisha, yote kabisa au sehemu yake;

“mtoto” ni mtu ambaye hajatimiza umri wa miaka kumi na minane;

“jumuia ya wananchi” ni ujumla wa makundi yaliyojipanga, na kila kundi linashirikishwa na masharti ya hiari na halifungamani na serikali;

“Mfuko Mkuu wa Fedha za Serikali” ni mfuko ulioundwa na Ibara ya 222;

“Tume ya Kikatiba” ni tume iliyoundwa kwa ajili hiyo na Katiba hii;

“ulemavu” ni pamoja na hali ya mwili, hisia, akili, saikolojia, au kulemaa kwingine, hali au ugonjwa ambao unaonekana na watu wengi katika jamii kuwa una athari kubwa au ya muda mrefu katika uwezo wa mtu kufanya kazi yake ya kila siku;

“Wilaya” inamaanisha mujawapo ya wilaya zilizogawanywa katika Kenya kwa mujibu wa sheria ya Bunge;

“hati” ni pamoja na chapisho, au kitu kilichoandikwa, kilichosemwa au kilichochorwa juu ya kitu chochote kwa njia ya herufi, michoro au alama au kwa njia zaidi ya moja ya hizo, inayokusudiwa kutumiwa kwa lengo la kuhifadhi kitu hicho;

“tarehe ya kutekeleza” ni tarehe ya Katiba hii kuanza kutumika;

“utungaji sheria” ni kutunga Sheria au sheria ndogo;

“ruzuku ya kusawazisha” inamaanisha ruzuku inayotolewa na Serikali Kuu kwa serikali ya wilaya kwa kutoa kiwango maalum kwa wilaya ambazo zilizowachwa nyuma kimaendeleo na itagemea namna serikali ya wilaya au kitengo kingine chochote kimebaki nyuma ya kiwango cha kitaifa cha wastani kwa huduma fulani;

“mwaka wa fedha” inapotumiwa kwenye muktadha wa -

(a) serikali, ni kipindi cha miezi kumi na miwili inayomalizika Juni thelathini au siku nyingine yoyote iliyoagizwa na Bunge; au

(b) mtu yeyote, ni kipindi cha miezi kumi na miwili inayomalizika mnamo tarehe itakayoamuliwa na mtu huyo;

Page 160: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

160

“Gazeti” ni Gazeti la Kenya linalochapishwa kwa idhini ya Serikali, au ziada ya Gazeti la Kenya;

“Serikali” ni Serikali ya Taifa;

“afisa wa mahakama” ni mtu mwenye madaraka kamili au ya muda katika afisi ya msajili, naibu msajili, hakimu, afisi msimamizi wa mahkama ya kidini au Kadhi.

“Kenya” ni eneo la mipaka ya Jamhuri;

“sheria” ni sheria iliyotungwa na Bunge au sheria iliyotungwa na baraza la wilaya na inajumuisha amri, sharti, sheria ndogo za mji, mtaa, au chama, tangazo, au sheria nyingine kama hiyo iliyotungwa kwa mamlaka ya utungaji sheria;

“mzee katika jamii” ni mtu mwenye umri wa miaka sitini au zaidi;

“mtu” ni pamoja na kampuni, shirika, au chama kilichoshirikishwa chenye hadhi ya kisheria au kisicho na hadhi ya kisheria;

“chama cha kisiasa” ni mjumuiko wa watu waliojiunga kwa ajili ya madhumuni yaliyokusudiwa katika Ibara ya 112;

“uwezo” ni pamoja na fursa, mamlaka au hiari;

“afisa wa umma” ina maana ya mtu anaeshika au anaeshikilia kwa muda afisi katika huduma ya Serikali au huduma ya umma, ambapo malipo yake yanalipwa moja kwa moja kutoka Mfuko Mkuu au moja kwa moja kutokana na fedha zilizotengwa na Bunge;

“huduma ya umma” ni mkusanyiko wa watu wote, isipokuwa maafisa wa Serikali, wanaotekeleza jukumu katika chombo cha Serikali;

“malipo na marupurupu” inajumuisha mishahara, posho na haki zinazotokana na malipo ya binafsi kwa ajili ya afisi, ikijumuisha pensheni, kiinua mgongo au malipo mengine yanayolipwa wakati wa kustaafu.

“Jamhuri” ina maana ya Jamhuri ya Kenya.

“Dola” inapotumika kama nomino, ina maana ya ujumla wa afisi, vyombo na vitu vinavyohusisha Serikali ya Jamhuri chini ya Katiba hii.

“afisi ya Serikali” ni afisi iliyobuniwa chini ya Katiba hii;

“afisa wa Serikali” ni mtu anayekalia kiti cha afisi ya serikali iliyoaanzishwa chini ya Katiba hii, au iliyoanzishwa na kupewa madaraka hayo na sheria, na kwa ajili ya Sura ya Tisa inajumuisha afisa wa umma;

“chombo cha serikali” ni Tume, afisi, wakala au chombo kingine kilichoundwa kwa mujibu wa Katiba hii na chenye jukumu katika Jamhuri;

“kuandika” ni pamoja na kuchapisha, kupiga picha, lithografia, kupiga chapa, njia nyingine yoyote ya kuwakilisha au kunukuu maneno kwa namna inayoonekana, na Breli; na

“vijana” ni jamii ya watu katika Jamhuri, na kila mmoja wao -

Page 161: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

161

(a) ametimiza umri wa miaka kumi na minane; na

(b) hajatimiza umri wa miaka thelathini na mitano.

Page 162: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

162

SURA YA ISHIRINI NA MOJA

???, MASHARTI YA MPITO NA YANAYOTOKANA NA KUIDHINISWHA KATIBA HII

Sheria inayotokana na kuidhinishwa Katiba hii 287. (1) Pale ambapo Bunge linahitajika kutunga sheria kusimamia jambo fulani,

Bunge litapitisha sheria hiyo kwa muda uliowekwa katika Jedwali ya Tano, kuanzia tarehe ya utekelezaji.

(2) Licha ya Ibara ndogo (1), Bunge linaweza, kwa azimio linaloungwa mkono na kura ya angalau thuluthi mbili ya wajumbe wote, kuongeza mda uliowekwa kuhusiana na jambo lolote chini ya Ibara ndogo (1), kwa mda usiozidi mwaka mmoja, katika itakavyoamuliwa na Bunge.

(3) Uwezo wa Bunge uliokusudiwa chini ya Ibara ndogo (2), unaweza kutekelezwa –

(a) mara moja tu; na

(b) katika hali za kipekee kama itakavyothibitishwa na Spika.

(4) Kwa ajili ya Ibara ndogo (1) na (2), Mwanasheria Mkuu akishauriana na Tume ya Utekelezaji wa Katiba, atatayarisha na kuwasilisha Bungeni miswada itakikanayo, haraka iwezekanavyo, ili kuwezesha Bunge kupitisha sherio hiyo ndani ya muda uliowekwa.

(5) Iwapo Bunge haijapitisha sheria ndani ya muda uliowekwa chini ya Ibara ndogo (1) au (2), mswada kama ulivyowasilishwa chini ya Ibara ndogo (4), utachukuliwa kuwa umepitishwa siku inayofuata siku ya mwisho ya muda uliowekwa katika Jedwali ya Tano au mda uliozidishwa chini ya Ibara ndogo (2).

(6) Ibara ndogo (4) haiathiri utekelezaji wa haki yeyote chini ya Ibara ndogo (1), au chini ya Ibara 125 au 129.

Mpito 288. ??? , Masharti ya Sheria ya mpito na yanayotokana yaliyowekwa katika Jedwali

ya Sita yataanza kutekelezwa siku ambayo Katiba hii itaanza kutumika.

Tarehe ya Kutekelezwa 289. Katiba hii itaanza kutekelezwa tarehe itakapoidhinishwa na Rais.

Kufuta 290. Katiba iliyopo kabla ya utekelezaji wa Katiba hii itafutwa kuanzia tarehe ya

utekelezaji huo.

Page 163: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

163

JEDWALI YA KWANZA

(Ibara ya 11)

ALAMA ZA KITAIFA

(a) Bendera ya Taifa

Zingatia: Vipimo vyote viliyotolewa si sharti viwakilishe vipimo maalum na ni ya uwiano

tu. Maelezo: Chane tatu kubwa za upana sawa zenye rangi, kuanzia juu hadi chini, nyeusi, nyekundu, na kijani na kutenganishwa na chane nyembamba nyeupe, na ngao yenye ulinganifu na mikuki mieupe juu yake katikati.

Page 164: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

164

(b) Wimbo wa Taifa 1 1 Ee Mungu nguvu yetu O God of all creation Ilete baraka kwetu Bless this our land and nation Haki iwe ngao na mlinzi Justice be our shield and defender Natukae na udugu May we dwell in unity Amani na uhuru Peace and liberty Raha tupate na ustawi Plenty be found within our borders 2 2 Amkeni ndugu zetu Let one and all arise Tufanye sote bidii With hearts both strong and true Nasi tujitoe kwa nguvu Service be our earnest endeavour Nchi yetu ya Kenya And our Homeland of Kenya Tunayoipenda Heritage of splendour, Tuwe tayari kuilinda Firm may we stand to defend 3 3 Natujenge taifa letu Let all with one accord Ee, ndio wajibu wetu In common bond united Kenya istahili heshima Build this our nation together Tuungane mikono And the glory of Kenya Pamoja kazini The fruit of our labour Kila siku tuwe na shukrani. Fill every heart with thanksgiving

Page 165: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

165

(a) Nembo (b) Muhuri wa Kenya

Page 166: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

166

JEDWALI YA PILI

(Ibara ya 95)

VIAPO VYA TAIFA NA MATAMKO YA DHATI

KIAPO AMA TAMKO LA DHATI LA UTIIFU WA RAIS/ KAIMU RAIS NA NAIBU RAIS Mimi,……..………., nikitambua kikamilifu wajibu huu mkuu wa wadhifa wa Rais/Kaimu Rais/Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya, ninaapa/natamka kwa dhati ya kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya Kenya; kwamba nitatii, nitahifadhi, nitalinda na kutetea Katiba ya Kenya, kwa mujibu wa Sheria, na sheria nyingine zote za Jamhuri; na kwamba nitalinda utukufu na heshima, uadilifu na hadhi ya watu wa Kenya. (Ikiwa ni kiapo: Ee Mungu nisaidie). KIAPO AMA TAMKO LA DHATI LA UTEKELEZAJI KAZI YA AFISI YA RAIS/ KAIMU RAIS Mimi,……………naapa/natamka kwa dhati kwamba kwa ukweli na kwa kujitolea nitawatumikia wananchi na Jamhuri ya Kenya katika afisi ya Rais/Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kenya na kwa kujitolea, nitatekeleza wajibu na majukumu ya afisi ya Rais/Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kenya na kuwafanyia haki watu wote kwa mujibu wa Katiba kama ilivyowekwa, na sheria za Kenya, bila uoga, upendeleo, upendo au nia mbaya. (Ikiwa ni kiapo: Ee Mungu nisaidie). KIAPO AMA TAMKO LA DHATI LA UTEKELEZAJI KAZI YA AFISI YA NAIBU RAIS Mimi,…………..naapa/natamka kwa dhati kwamba kwa ukweli na kujitolea nitawatumikia wananchi na Jamhuri ya Kenya katika afisi ya Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya; na kwa kujitolea nitatekeleza wajibu na majukumu ya afisi ya Naibu Rais, kwa uwezo wangu wote; kwamba daima nitakapohitajika nitatoa, kwa uaminifu na ukweli, ushauri na maoni kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya; kwamba nitatenda haki kwa wote bila uoga, upendeleo, upendo au nia mbaya, na kwamba kwa vyovyote sitatoa siri, kwa masuala ninayoyafahamu kutokana na majukumu na wajibu kuwa siri yangu, isipokuwa ikiwa ni lazima katika utendakazi wangu kama Naibu Rais na kwamba nitatekeleza wajibu wangu wa afisi kwa makini na uangalifu na kwa uwezo wangu wote. (Ikiwa ni kiapo: Ee Mungu nisaidie).

Page 167: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

167

KIAPO AMA TAMKO LA DHATI LA UTEKELEZAJI KAZI YA AFISI YA WAZIRI MKUU/KAIMU WAZIRI MKUU

Mimi,……………naapa/natamka kwa dhati kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Kenya; kwamba nitatii na kutetea Katiba ya Kenya na sheria nyingine zote za Jamhuri ya Kenya; kwamba daima nitawatumikia wakati wote kwa ukweli na vizuri wananchi wa Jamhuri ya Kenya; kwamba ninaahidi kulinda afisi ya Waziri Mkuu/Kaimu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kenya kwa heshima na hadhi kuu; kwamba nitakuwa mshauri mkweli na mwaminifu kwa Rais; kwamba sitatoa siri kwa namna yoyote ile, kwa yale ninayoyafahamu katika utekelezaji wa majukumu yangu na nitahifadhi siri, isipokuwa ikiwa ni lazima katika utendakazi wangu kama Waziri Mkuu/Kaimu Waziri Mkuu; na kwamba nitatekeleza wajibu wangu wa afisi kwa makini na uangalifu na kwa uwezo wangu wote. (Ikiwa ni kiapo: Ee Mungu nisaidie). KIAPO AMA TAMKO LA DHATI LA UTEKELEZAJI KAZI YA AFISI YA NAIBU WAZIRI MKUU/WAZIRI/NAIBU WAZIRI Mimi,………………nikiwa nimechaguliwa Naibu Waziri Mkuu/Waziri wa Kenya/Naibu Waziri, naapa/natamka kwa dhati kwamba daima nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Kenya, na kwamba nitatii, nitaheshimu, nitalinda na kutetea Katiba ya Kenya na Sheria nyingine zote za Jamhuri; na nitawatumikia kwa dhati na ukweli watu na Jamhuri ya Kenya katika afisi ya Naibu Waziri Mkuu/Waziri/Naibu Waziri; na kwamba ninajitolea kuilinda afisi yangu kama Waziri Mkuu/Waziri/Naibu Waziri kwa heshima na hadhi kuu; kwamba nitakuwa mshauri mkweli na mwaminifu kwa Rais katika usimamizi mwema wa masuala ya umma ya Jamhuri ya Kenya; kwamba sitatoa siri kwa namna yoyote ile kwa yale ninayoyafahamu katika utekelezaji wa majukumu yangu na nitahifadhi siri, isipokuwa ikiwa ni lazima kwenye utendakazi wangu kama Waziri Mkuu/Waziri/Naibu Waziri na kwamba nitatekeleza wajibu wangu wa afisi kwa makini na uangalifu na kwa uwezo wangu wote. (Ikiwa ni kiapo: Ee Mungu nisaidie). KIAPO AMA TAMKO LA DHATI LA UTEKELEZAJI KAZI YA AFISI YA KATIBU MKUU Mimi,………………..., nikiitika mwito wa kutekeleza majukumu ya Katibu Mkuu, naapa/natamka kwa dhati, kwamba isipokuwa kwa idhini ya Rais, sitaelezea kwa namna yoyote ile hali au yaliyomo katika shughuli, utaratibu au nyaraka za Baraza la Mawaziri nilizokabidhiwa kuzihifadhi, isipokuwa ikiwa ni lazima katika utendakazi wangu kama Katibu Mkuu. (Ikiwa ni kiapo: Ee Mungu nisaidie).

Page 168: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

168

KIAPO KWA JAJI MKUU/NAIBU JAJI MKUU, MAJAJI WA MAHAKAMA YA JUU, MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA NA MAJAJI WA MAHAKAMA KUU Mimi,…………………, (Jaji Mkuu/ Naibu Jaji Mkuu, Jaji wa Mahakama ya Juu, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jaji wa Mahakama Kuu, naapa/natamka kwa dhati kwamba kwa uaminifu nitatumikia watu na Jamhuri ya Kenya na nitafanya haki bila ya kupendelea upande wowote kwa mujibu wa Katiba ilivyowekwa na Sheria na desturi za Jamhuri bila uoga, upendeleo, upendo, nia mbaya yenye madhara, ubaguzi au ushawishi wa kisiasa, kidini au athari nyingine. Katika utekelezaji wa majukumu ya Mahakama niliyopewa kila wakati, na kadri ya ujuzi na uwezo wangu, daima nitahifadhi, nitalinda, nitasimamia, nitatekeleza na kutetea Katiba ili kulinda hadhi na heshima ya idara mahakama na mfumo wa haki nchini Kenya na kuendeleza haki, uhuru, umahiri na uadilifu wake. (Ikiwa ni kiapo: Ee Mungu nisaidie). KIAPO/TAMKO LA DHATI LA MBUNGE Mimi, …………………………, nikiwa nimechaguliwa mjumbe wa Bunge naapa/natamka kwa dhati kwamba nitakuwa mwaminifu na mkweli kwa watu na Jamhuri ya Kenya; kwamba nitatii, nitaheshimu, nitatetea, nitadumisha na nitalinda Katiba ya Jamhuri ya Kenya; na kwamba nitatekeleza wajibu wangu kama Mbunge kwa uaminifu na uangalifu. (Ikiwa ni kiapo: Ee Mungu nisaidie) KIAPO CHA SPIKA/ NAIBU SPIKA Mimi,………..……….., nikiwa nimechaguliwa kuwa Spika/Naibu Spika, naapa/ natamka kwa dhati kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu wa kweli kwa watu na Jamhuri ya Kenya; kwamba kwa uaminifu na uangalifu nitatumika kama Spika/Naibu Spika; kwamba nitatii, nitaheshimu, nitatetea, nitadumisha na nitalinda Katiba ya Jamhuri ya Kenya, na kwamba nitatenda haki kwa kila mtu kwa mujibu wa Katiba ya Kenya na sheria na desturi za Bunge bila woga au upendeleo, upendo au nia mbaya. (Ikiwa ni kiapo: Ee Mungu nisaidie).

Page 169: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

169

JEDWALI YA TATU

(Ibara 209(1))

MGAWANYO WA MAJUKUMU BAINA YA SERIKALI YA TAIFA NA ZA WILAYA

Sehemu ya 1 – Serikali ya Taifa

1. Mambo ya kigeni, sera ya kigeni, na biashara ya kimataifa.

2. Kwa ushauriano na wilaya, matumizi ya maji ya kimataifa na rasilimali za maji.

3. Uhamiaji na uraia.

4. Uhusiano baina ya dini na Dola.

5. Sera ya lugha na kuendeleza lugha rasmi na za kiasili.

6. Ulinzi wa taifa na matumizi ya huduma za taifa za ulinzi.

7. Usalama wa taifa, pamoja na -

(a) kuweka viwango vya uajiri, mafunzo ya polisi, na matumizi ya huduma ya polisi;

(b) sheria ya jinai; na

(c) huduma za kurekebisha tabia.

8. Mahakama.

9. Sera ya taifa ya uchumi na mipango.

10. Sera ya fedha, sarafu, benki (pamoja na uwekaji mkuu wa sarafu), ushirikishaji na udhibiti wa benki, bima, na huduma za fedha.

11. Takwimu za taifa, na tarkimu za sensa za idadi ya watu, uchumi na jamii kwa jumla.

12. Haki za mali ya kitaaluma.

13. Viwango vya uajiri.

14. Kulinda wateja, pamoja na viwango vya ruzuku ya serikali na mipango ya malipo ya uzeeni kwa wataalamu.

15. Ruzuku ya jamii na sera ya malipo ya uzeeni.

16. Sera ya elimu, viwango, mitalaa, mitihani na kutoa hati za kuanzisha vyuo vikuu.

17. Vyuo vikuu vya, taasisi za elimu na taasisi nyingine za utafiti na masomo ya juu, na shule za kitaifa za upili na taasisi za elimu maalum.

18. Kuendeleza michezo na elimu ya michezo.

Page 170: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

170

19. Uchukuzi na mawasiliano, inayojumuisha -

(a) wa barabarani;

(b) ujenzi na udhibiti wa barabara kuu za taifa;

(c) viwango vya ujenzi na udumishaji wa barabara nyingine vinvyowekwa na wilaya;

(d) reli;

(e) njia za bomba;

(f) usafiri baharini;

(g) bandari na vivuko;

(h) mambo yanahusu usafiri wa vyombo vya angani;

(i) usafiri wa anga za mbali;

(j) huduma ya posta;

(k) mawasiliano ya simu; na

(l) matangazo ya redio na televisheni.

20. Ujenzi wa kitaifa.

21. Sera ya nyumba.

22. Kanuni za jumla za mpango wa ardhi na uratibu wa mpango wa wilaya.

23. Kulinda mazingira na maliasili kwa lengo la kuunda mfumo wa kudumu na maendeleo endelevu, inayojumisha -

(a) uvuvi, uwindaji na ukusanyaji;

(b) kulinda wanyama na maishapori;

(c) kulinda maji, kupata maji tosha ya masazo, uhandisi wa maji, na usalama wa mabwawa; na

(d) kudhibiti uchafuzi wa hewa, makelele, na usumbufu mwingine wa kijamii na matangazo ya biashara ya nje.

24. Vituo vya afya vya Taifa vya rufaa.

25. Kukabili maafa.

26. Kumbukumbu za kitaifa na mambo ya kale yenye umuhimu wa kitaifa.

27. Chaguzi za kitaifa.

28. Sera ya afya.

29. Sera ya ukulima.

30. Sera ya matibabu ya wanyama.

Page 171: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

171

31. Sera ya nishati inayojumuisha umeme na usambazaji wa gesi na usimamizi wa nishati.

32. kukuza uwezo wa utenda kazi na kutoa msaada wa kiufundi katika wilaya.

33. Uwekezaji wa umma.

34. Kasino, kamari na michezo mingine ya Taifa.

35. Sera ya utalii na maendeleo.

36. Jukumu lingine lolote ambalo halikutajwa na Katiba hii au sheria ya Bunge.

Sehemu ya Pili: Serikali za Wilaya

1. Isipokuwa ambapo Katiba au sheria zimeagiza vinginevyo, uwezo na majukumu ya serikali ya wilaya katika sehemu yake yote ya utekelezaji, itakuwa -

(a) kubuni sera za wilaya;

(b) kuweka viwango vya wilaya;

(c) kuweka mipango ya wilaya;

(d) kusimamia na kutathmini utekelezaji;

(e) uzalishaji, usimamizi na utoaji huduma za wilaya;

(f) ukuzaji, utendakazi na ukarabati wa miondo msingi na huduma za wilaya;

(g) kufanikisha na kusawazisha udhibiti wa shughuli katika wilaya; na

(h) kukuza uwezo wa utendakazi.

2. Kilimo, kinachojumisha -

(a) mimea na ufugaji;

(b) viwanja vya kuuzia wanyama;

(c) vichinjio vya wilaya;

(d) udhibiti wa magonjwa ya mimea na wanyama; na

(e) uvuvi.

3. Huduma za matibabu wilayani, zinazojumisha -

(a) vituo vya afya na maduka ya madawa wilayani;

(b) huduma za gari za kubebea wagonjwa;

(c) kuendeleza huduma ya afya ya msingi;

(d) kutoa leseni na kudhibiti vituo vya kuuza chakula kwa umma;

(e) huduma za madawa ya wanyama (lakini si kudhibiti taaluma);

Page 172: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

172

(f) makaburi, afisi za mazishi, na tanuu za kuchomea maiti;

(g) kuondoa takataka, jaa za taka, na kutupa takataka ngumu.

4. Kudhibiti uchafuzi wa hewa, makelele, na usumbufu mwingine wa kijamii na matangazo ya biashara ya nje;

5. Shughuli za kitamaduni, burudani za umma na vifaa vya umma, zinazojumuisha -

(a) kasino na michezo mingine ya kamari;

(b) mbio;

(c) leseni za pombe;

(d) sinema;

(e) sinema za video na kukodisha;

(f) maktaba;

(g) makumbusho;

(h) michezo na shughuli na vifaa vya kitamaduni; na

(i) viwanja vya mapumziko, ufukweni na vifaa vya starehe.

6. Usafiri wilayani unajumuisha -

(a) barabara za wilaya;

(b) taa za barabarani;

(c) magari na kuegesha;

(d) uchukuzi wa umma barabarani;

(e) vivuko na bandari, lakini si udhibiti wa kimataifa na meli za taifa, na mambo yanayohusiana na hayo.

7. Udhibiti na ustawi wa wanyama, ikijumuisha -

(a) leseni za mbwa; na

(b) huduma za mahali pa wanyama kuishi, kutunzwa na kuzikwa.

8. Maendeleo ya biashara na udhibiti, ikujumuisha -

(a) masoko;

(b) leseni za biashara (lakini si kudhibiti taaluma);

(c) upimaji ardhi na uchoraji ramani;

(d) mipaka na kuweka;

(e) taratibu za biashara za makaazi;

Page 173: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

173

(f) utalii wa ndani; na

(g) vyama vya ushirika.

9. Mipango na maendeleo wilayani, inajumuisha -

(a) Takwimu; na

(b) ardhi.

10. Elimu ya shule za malezi, msingi na sekondari, elimu maalum, vyuo vya ufundi vijijini, vituo vya sanaa ya nyumbani na huduma za malezi ya watoto.

11. Utekelezaji wa sera ya serikali ya kitaifa kuhusu maliasili na uhifadhi wa mazingira, inayojumuisha -

(a) uhifadhi wa udongo na maji; na

(b) misitu.

12. Ujenzi wilayani na huduma, inaojumuisha -

(a) usimamizi wa maji ya dhoruba katika sehemu zilizojengwa; na

(b) huduma za maji na usafi.

13. Polisi na huduma za kuzima moto na kukabili maafa.

14. Kudhibiti madawa ya kulevya na sinema chafu.

15. Kuhakikisha na kusimamia jamii na kata kushiriki katika utawala wa kiwango cha mashinani na kusaidia jamii na kata kuendeleza uwezo wa kiutawala kwa ajili ya matumizi thabiti ya madaraka na majukumu na kushiriki katika utawala mashinani.

Page 174: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

174

JEDWALI YA NNE

(Ibara ya 220)

UWEZO WA KUTOZA KODI

Sehemu ya Kwanza: Uwezo wa kutoza kodi wa Serikali ya Taifa

Serikali ya Taifa inaweza kukusanya, kwa njia ya kodi, ushuru, ada na malipo -

(a) kodi ya mapato;

(b) kodi ya nyongeza;

(c) kodi ya shirika;

(d) kodi ya forodha;

(e) ushuru wa bidhaa za ndani;

(f) kodi ya mauzo ya jumla;

(g) ushuru wa stampu wa kitaifa;

(h) kodi ya bahati nasibu za kitaifa na mipango kama hiyo;

(i) kodi ya uchukuzi wa barabara, anga, reli na maji;

(j) kodi ya nyumba na mali nyingine zinazomilikiwa na Serikali ya Taifa;

(k) ada za leseni zinazotolewa na Serikali ya Taifa;

(l) ada za mahakama, faini na utwaliwaji wa mali;

(m) stakabadhi za kubadilishana;

(n) ada za kusajili magari na ada za leseni ya kuendesha gari;

(o) ada za mali asili;

(p) ada za bidhaa za serikali na huduma; na

(q) kodi nyingine zilizoidhinishwa na sheria ya Kitaifa.

Sehemu ya Pili: Uwezo wa serikali za wilaya kutoza kodi

Serikali wilaya inaweza kukusanya, kwa njia ya kodi, ushuru, malipo ya ziada, ada, na malipo

mengine yanayojumuisha -

(a) malipo ya ziada ya jumla kwa msingi wa kodi yoyote, ada au ushuru

uliotozwa na sheria ya kitaifa lakini si msingi wa kodi ya mapato ya

Page 175: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

175

mashirika, malipo ya nyongeza (VAT) na ushuru wa forodha na

ushuru wa bidhaa za ndani;

(b) ada ya matumizi ya ardhi;

(c) ada ya kilimo;

(d) ada za matumizi ya mali ya serikali ya wilaya;

(e) kodi ya mali na malipo ya ziada ya huduma zinazotolewa na au kwa

niaba ya wilaya;

(f) ada za leseni, zikiwemo ada za leseni za pombe, ada za soko na ada za

uchuuzi;

(g) ada ya kibali cha biashara;

(h) kodi ya burudani;

(i) malipo ya udumishaji wa barabara wilayani;

(j) kodi ya hoteli na mikahawa katika wilaya;

(k) ada ya kuingilia mbuga za hifadhi za wanyama;

(l) kodi ya uchukuzi;

(m) kodi ya kuegesha;

(n) kodi nyingine, ushuru, malipo ya ziada, ada na malipo kama wilaya

inavyoagizwa kutoza mara kwa mara na Sheria ya Kitaifa; na

(o) kodi nyingine, ushuru, malipo ya ziada, ada na malipo ambayo

hayakutengewa kiwango cha Serikali ya Taifa pekee.

Page 176: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

176

JEDWALI YA TANO

(Ibara ya 287(1))

SHERIA ZITAKAZOTUNGWA NA BUNGE

SURA NA KICHWA CHA IBARA IBARA MUDA

ULIOWEKWA SURA YA NNE URAIA Uraia kwa kuandikishwa 19 Miaka miwili Uraia maradufu 21(3) Miaka miwili Makao 23(2) Miaka miwili Sheria kuhusu uraia 25 Miaka miwili SURA YA SITA SHERIA YA HAKI ZA BINADAMU Kutekeleza haki na uhuru 31(3) Miaka mitatu Mamlaka ya mahakama kutetea na kutekeleza Sheria ya Haki

33(2) Miaka mitatu

Wazee katika jamii 39(3) Miaka miwili Watoto 41(8) Mwaka mmoja Familia 42(5) Miaka mitatu Watu wenye ulemavu 43(3) Miaka mitatu Uhuru wa vyombo vya habari 50(5) Mwaka mmoja Kufikia habari 51(4) Miezi sita Uhuru wa kushirikiana 52(4) Mwaka mmoja Wakimbizi na hifadhi 56(2) Mwaka mmoja Haki ya wateja 69(3) Miaka mitatu Utawala wa haki 70(3) Miaka mitatu Kufanyiwa kesi kwa haki 73(8) Miaka mitatu Haki za watu walio kizuizini 74(2) Miaka mitatu Tume ya Jinsia 76(3) Miaka mitatu Tume ya Haki za Kibinadamu na Haki za Kiutawala

77(3) Miaka mitatu

SURA YA SABA ARDHI NA MALI Ardhi ya jamii 81(5) Miaka miwili Usimamizi wa matumizi ya ardhi 84(4) Miezi sita Sheria kuhusu ardhi 86 Miaka miwili SURA YA NANE MAZINGIRA NA MALIASILI Sheria kuhusu mazingira 93 Miaka miwili

Page 177: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

177

SURA NA KICHWA CHA IBARA IBARA MUDA ULIOWEKWA

SURA YA TISA UONGOZI NA UADILIFU Sheria ya uongozi 100 Mwaka mmoja SURA YA KUMI UWAKILISHI WA WATU Uchaguzi 102(1) Mwaka mmoja Uwakilishi katika mashirika ya kimataifa

108 Mwaka mmoja

Udhibiti wa Vyama vya Kisiasa 113 Mwaka mmoja SURA YA KUMI NA MOJA BUNGE

Uanachama wa Bunge 116(3) Mwaka mmoja Masjala ya sheria 137 Mwaka mmoja SURA YA KUMI NA MBILI MAMLAKA YA NCHI Uwezo wa Rais kuhurumia 157(2) Mwaka mmoja Wakili wa Umma 176(5) Miaka miwili SURA YA KUMI NA TATU MFUMO WA MAHAKAMA NA SHERIA Mfumo wa ngazi za mahakama na usimamizi wake

179 Mwaka mmoja

SURA YA KUMI NA NNE SERIKALI ZILIZOSAMBAZIWA MAMLAKA Ushirikiano na uhusiano kati ya Serikali ya Taifa na serikali za wilaya

200(3) Mwaka mmoja

Usimamizi wa maeneo ya miji katika wilaya

203(1) Mwaka mmoja

Kusimamishwa kwa muda kwa serikali ya wilaya

204(3) Mwaka mmoja

Kubuniwa na majukumu ya Kikao cha Taifa cha serikali za wilaya na vikao vingine

206(4) Mwaka mmoja

Uchaguzi wa wajumbe wa baraza la wilaya

209(1) Mwaka mmoja

Sharti litakaloidhinishwa na Bunge 217 Mwaka mmoja SURA YA KUMI NA TANO FEDHA ZA UMMA Utozaji ushuru 220 Mwaka mmoja Mfuko wa Dharura 225 Mwaka mmoja Kukopa kwa serikali za wilaya 227 Mwaka mmoja Serikali zinapodhamini mikopo 229 Mwaka mmoja Bajeti ya mwaka ya serikali 233 Mwaka mmoja

Page 178: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

178

SURA NA KICHWA CHA IBARA IBARA MUDA ULIOWEKWA

zilizosambaziwa mamlaka Kununua bidhaa na huduma za umma 234(2) Mwaka mmoja Hesabu na ukaguzi wa taasisi za umma 235(5) Mwaka mmoja Kudhibiti Hazina 236(1) Mwaka mmoja Mhasibu Mkuu 238(6) Mwaka mmoja Mamlaka ya Mapato ya Taifa 239(3) Mwaka mmoja Tume ya Mgawo wa Mapato 240(8) Mwaka mmoja Baraza la Uchumi na Jamii 243(4) Mwaka mmoja Sheria kuhusu utozaji ushuru 244(1) Mwaka mmoja SURA YA KUMI NA SITA HUDUMA KWA UMMA Mamlaka na wajibu 247(5) Miaka miwili Ajira katika serikali za wilaya 248 Miaka miwili Kuundwa kwa Huduma ya Kenya ya Kurekebisha Tabia

253(3) Miaka miwili

SURA YA KUMI NA SABA VYOMBO VYA USALAMA WA TAIFA Vyombo vya Usalama wa Taifa 256(6) Mwaka mmoja Kuundwa kwa Huduma ya Polisi ys Kenya

263(3) Mwaka mmoja

Page 179: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

179

JEDWALI YA SITA

(Ibara 288)

MASHARTI YA MPITO NA YANAYOTOKANA NA KUIDHINISHWA KATIBA HII

Sehemu I - Jumla

Haki, majukumu na wajibu wa serikali 1. Haki zote na wajibu, bila kuzingatia chanzo chake, wa serikali au Jamhuri, uliopo

mara tu kabla ya tarehe ya kutekelezwa Katiba hii, utaendelea kuwepo kama haki na wajibu wa Serikali ya Jamhuri chini ya Katiba hii.

Sheria zilizoko 2. Sheria zote zilizoko mara tu kabla ya tarehe ya kutekelezwa katiba hii zitaendelea

kuwepo na zitafasiriwa pamoja na mabadiliko, marekebisho, ufafanuzi, matumizi kwa kadri ihitajikavyo kwa ajili ya kuafikiana na Katiba hii.

Baraza la Taifa 3. Baraza la Taifa lililoko mara tu kabla ya kuanza kutumika Katiba hii litaendelea

kuwepo kama Bunge kwa madhumuni ya Katiba hii kwa kipindi chake ambacho hakijamalizika na ndani ya miezi sita baada ya kuanza kutumika Katiba hii, itasahihisha Nidhamu za Bunge kwa mujibu wa Katiba hii.

Uchaguzi mdogo 4. Uchaguzi mdogo utakaofanywa baada ya kuanza kutekelezwa Katiba hii

utafanywa kwa mujibu wa Katiba hii.

Vyama vya kisiasa 5. (1) Chama cha kisiasa kilichoko mara tu kabla ya kuanza kutumika Katiba hii,

kitatimiza mahitaji ya usajili wa chama cha kisiasa ndani ya miezi kumi na miwili ya kuidhinishwa kwa sheria inayowezesha usajili wa vyama vya kisiasa.

(2) Ikiwa baada ya kukamilika kwa kipindi cha miezi kumi na miwili, chama cha kisiasa hakitakuwa kimetimiza mahitaji ya sehemu ndogo (1), chama hicho cha kisiasa kitafutwa mara moja kama chama cha kisiasa, na mtu yeyote mwenye cheo cha kuchaguliwa kwa msingi wa kudhaminiwa na chama hicho, ataendelea na cheo hicho lakini atakuwa mwanachama wa kujitegemea.

Mamlaka ya Utendaji 6. (1) Watu wanaoshikilia afisi ya Rais na Makamu wa Rais mara tu kabla ya

kuanza kutumika Katiba hii wataendelea kuhudumu kama Rais na Naibu Rais, mtawalia, kwa mujibu wa Katiba hii hadi kufanyika uchaguzi wa kwanza chini ya Katiba hii.

Page 180: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

180

(2) Masharti ya Ibara 163, 164, 168(1)(c), (d) and (g), 168(2), (3), (4) and (5) yatatekelezwa baada ya uchaguzi wa kwanza chini ya Katiba hii.

(3) Mtu anayeshikilia wadhifa katika Baraza la Mawaziri, mara tu kabla ya tarehe ya kuanza kutumiwa Katiba hii, ataendelea kushika wadhifa huo chini ya Katiba hii.

Afisi zilizopo 7. (1) Mtu ambaye mara tu kabla ya kutekelezwa Katiba hii anafanya kazi au

kukaimu afisi iliyoundwa na Katiba iliyoko kabla ya tarehe ya kutekelezwa Katiba hii, ataendelea kufanya kazi au kukaimu afisi hio kama kwamba ameteuliwa na Katiba hii.

(2) Mtu yoyote ambaye mara tu kabla ya tarehe ya kutekelezwa Katiba hii alikuwa na cheo au amekaimu cheo katika afisi ya umma iliyoundwa chini ya sheria yoyote iliyoandikwa, mradi tu inaafikiana na Katiba hii, ataendelea kuwa na cheo au kukaimu cheo katika afisi hiyo kama kwamba ameteuliwa katika cheo hicho chini ya Katiba hii.

(3) Masharti ya Ibara hii hayataathiri uwezo aliopewa mtu au mamlaka yoyote chini ya Katiba hii ili kufuta afisi au kuwaondoa watu kutoka afisi hiyo.

(4) Utaratibu wa kuteua watu ili kujaza nafasi zinazotokana na matokeo ya utekelezaji wa Katiba hii utaanza mnamo tarehe ya kutekelezwa Katiba hii na kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

(5) Ikiwa mtu ameondoka afisi aliyokuwemo kabla ya tarehe ya kuanza kutekelezwa Katiba hii, na afisi hiyo imehifadhiwa au kuundwa kwa mujibu wa Katiba hii, mtu huyo anaweza, akistahiki, kuteuliwa tena, kuchaguliwa au vinginevyo ili achukue madaraka ya afisi hiyo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

(6) Mtu aliyetajwa katika sehemu ndogo (1), (2) na (5), atawasilisha kwa Tume ya Maadili na Uaminifu, hati na ushahidi unaohitajiwa na Sura ya Tisa ndani ya siku thelathini tangu kuteuliwa kwa Tume hiyo.

Kiapo cha uaminifu kwa Katiba hii 8. Siku ya kutekelezwa Katiba hii, Rais na afisa yeyote wa Serikali au mtu

mwengine ambaye, kabla ya tarehe ya utekelezaji, alikuwa ameapa au ametamka tamko la dhati la afisi kwa mujibu ya Katiba iliyokuwako kabla ya tarehe ya utekelezaji, au ambaye anatakiwa aape au atamke kwa dhati kwa mujibu wa Katiba hii, ataapa au kutamka kwa dhati inavyohitajika kwa mujibu wa Katiba hii.

Urithi wa taasisi, afisi, mali na madeni 9. (1) Kama sharti la Katiba hii limebadilisha jina la afisi au taasisi iliyopo mara

tu kabla ya kuanza kutekeleza Katiba hii, afisi au taasisi hiyo kama ijulikanavyo kwa jina jipya itakuwa mrithi wa kisheria wa afisi au taasisi iliyotajwa kwanza.

Page 181: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

181

(2) Madeni yote, mali na rasilmali nyinginezo, zilizokuwepo au kukabidhiwa Serikali au Jamhuri au vinginevyo mara tu kabla ya kuanza kutekeleza Katiba hii, zitaendelea kuwepo au kukabidhiwa baada ya tarehe ya kuanza kutekeleza Katiba hii.

(3) Kwa madhumuni ya sehemu hii, Mamlaka ya Mapato ya Kenya iliyokuweko mara tu kabla ya tarehe ya kutekeleza Katiba hii itaendelea kuweko kama Mamlaka ya Mapato ya Taifa inayorejewa katika Ibara ya 239.

Malipo ya uzeeni, kiinua mgongo na marupurupu mengine 10. Sheria inayohusu malipo ya uzeeni, kiinua mgongo au malipo mengine ya binafsi

kwa wale wanaoshikilia afisi za kikatiba itakuwa ndiyo sheria iliyokuwa ikitumika wakati ambapo marupurupu hayo yalipotolewa, au sheria nyingine iliyoko katika tarehe ya baadaye ambayo haimuumizi mtu huyo.

Hatua za mahakama na masuala yanayosubiri uamuzi 11. (1) Isipokuwa iagizwe vinginevyo chini ya Katiba hii, shughuli zote za

kimahakama zinazosubiri mahakamani au katika mahakama maalum, zitaendelea kusikilizwa na zitaamuliwa na mahakama hiyo au mahakama kama hiyo au mahakama maalum yaliyoanzishwa na Katiba hii;

(2) Isipokuwa iagizwe vinginevyo chini ya Katiba hii, suala au utaratibu wowote ambao, mara tu kabla ya mwanzo wa utekelezaji wa Katiba hii unasubiri uamuzi wa Tume iliyoko ya kikatiba, afisi au mamlaka utaendelea mbele ya Tume hiyo au nyingine kama hiyo, afisi au mamlaka iliyoundwa na Katiba hii.

Adhabu ya kutandikwa viboko 12. Kila hukumu ya kutandikwa viboko iliyotolewa na mahakama yoyote mara tu

kabla ya utekelezaji wa Katiba hii, itaondolewa na haitatekelezwa.

Tume ya Utekelezaji wa Katiba 13. (1) Inaundwa Tume ya utekelezaji wa Katiba itakayokuwa na -

(l) mwenyekiti; na

(m) wajumbe wengine wanane.

(2) Jukumu la Tume ni -

(a) kufuatilia, kufanikisha, na kusimamia maendeleo ya utaratibu wa sheria za utawala kama inavyohitajika ili kutekeleza Katiba hii;

(b) kuwasilisha taarifa mara mbili kwa mwaka kwa Rais na Bunge kuhusu -

(i) maendeleo ya utekelezaji wa Katiba hii kwa wakati unaofaa; na

Page 182: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

182

(ii) vikwazo vyovyote dhidi ya utekelezaji wa Katiba hii kwa wakati unaofaa;

(c) kufanya kazi na mwenyekiti wa kila Tume ya Kikatiba hii ili kuhakikisha kwamba maagizo na malengo ya Katiba yanaheshimiwa.

(3) Tume hii itavunjwa tarehe itakayoamuliwa na Bunge, ambayo sio chini ya miaka mitano tangu tarehe ya kutekelewa.

Kuteuliwa kwa Tume 14. (1) Tume ya Maadili na Uaminifu na Tume ya Utekelezaji wa Katiba

zitaundwa ndani ya kipindi cha siku tisini baada ya tarehe ya utekelezaji wa Katiba hii.

(2) Ndani ya kipindi cha miezi tisa ya kuundwa kwa Tume ya Maadili na Uaminifu na Tume ya Utekelezaji wa Katiba, Tume zifuatazo zitaundwa kulingana na utaratibu huu -

(a) Tume ya Kugawa Mapato;

(b) Tume ya Huduma ya Bunge;

(c) Tume ya Huduma ya Mahakama;

(d) Tume ya Huduma ya Polisi;

(e) Tume ya Huduma kwa Umma;

(f) Tume ya Haki za Kibinadamu na Haki za Kiutawala;

(g) Tume ya Jinsia;

(h) Tume ya Uchaguzi na Mipaka;

(i) Tume ya Mishahara na Malipo;

(j) Tume ya Taifa ya Ardhi;

(k) Tume ya Huduma ya Walimu;

(l) Tume ya Taifa ya Mazingira;

(m) Tume ya Huduma ya Afya; na

(n) Tume ya Taifa ya Utamaduni.

Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Juu 15. Utaratibu wa kuteua Majaji wa Mahakama ya Juu utaanza na kukamilishwa ndani

ya kipindi cha siku tisini, baada ya kuteuliwa kwa Tume ya Huduma za Mahakama.

Page 183: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

183

Ukiukaji wa haki za binadamu za wakati uliopita 16. Bunge litaidhinisha sheria kuipa Tume ya Haki za Kibinadamu na Haki za

Kiutawala, ndani ya kipindi cha miezi sita ya utekelezaji wa Katiba hii uwezo wa -

(a) kuchunguza hali zote za ukiukaji wa haki za binadamu na mtu yeyote au kundi la watu kabla ya kuanza kutekelezwa kwa Katiba hii;

(b) kuchunguza sababu za migogoro ya kijamii, pamoja na vifo vya halaiki, mauaji ya kisiasa, vita vya kikabila na kubainisha wale waliohusika;

(c) uwezo wa kufanya mapendekezo yanayofaa kuhusu -

(i) kuwashtaki wale waliohusika;

(ii) malipo ya fidia kwa waliodhulumiwa;

(iii) upatanisho; na

(iv) kufidia.

Ardhi ya jamii 17. Hadi jamii zitakapoainishwa na hatimiliki zao zitakaposajiliwa, ardhi ya jamii

itakuwa ndani ya kabidhi ya Tume ya Taifa ya Ardhi kwa niaba ya jamii.

Elimu ya raia 18. Kuanzia tarehe ya kutekeleza Katiba, Serikali kupitia vyombo vyake

vinavyohusika, itaanza utaratibu wa kuendesha na kufanikisha elimu ya raia kuhusu Katiba hii kwa watu wa Kenya katika lugha rasmi na lugha zao za asili.

Rekebisho la Sura ya Kumi na Tano 19. Utaratibu wa kubadilisha Katiba hii ulioagizwa katika Ibara ya 281(1), utatumika

kwa Sura ya Kumi na Tano kwa miaka mitano kuanzia tarehe ya kutekeleza.

Sarafu 20. Hakuna kitu katika Ibara ya 242(3) litakaloathiri uhalali wa sarafu na noti

zilizotolewa kabla ya tarehe ya utekelezaji.

Sehemu II – Usambazaji wa Mamlaka

Wilaya 21. Hadi sheria itakapopitishwa kwa mujibu wa Ibara 5, wilaya kwa madhumuni ya

Katiba hii zitakuwa ni zile wilaya zilizoko mara tu kabla ya tarehe ya kutekeleza Katiba hii.

Mamlaka ya mitaa 22. (1) Mamlaka yote ya mitaa iliyoundwa chini ya sheria ya serikali ya mitaa

(Sura 265) iliyokuwepo mara tu kabla ya kuanza kutumika Katiba hii

Page 184: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

184

itaendelea kuwepo hadi utekelezaji wa muundo mpya chini ya Sura ya Kumi na Nne kama ilivyoagizwa na Sheria itakayotungwa na Bunge.

(2) Bunge litatunga sheria inayorejewa katika sehemu ndogo (1) ndani ya mwaka mmoja tangu tarehe ya Katiba hii kuanza kutumika.

(3) Madiwani wote wa mamlaka za mitaa iliyofafanuliwa katika sehemu ndogo (1) wataendelea kuwa madiwani baada ya Katiba mpya kuanza kufanya kazi hadi uchaguzi uitishwe kwa mujibu wa sheria inayorejewa katika sehemu ndogo (1).

(4) Kabla ya kutungwa kwa sheria chini ya Ibara 5, kata zilizoko mara tu kabla ya kuanza kutumika Katiba hii ni kata zilizotajwa katika Ibara hiyo, na mipaka kama ilivyokuwa.

Utawala wa Mikoa 23. (1) Baada ya kuanza kutekelezwa sheria iliyotajwa katika Ibara ya 217 na

ndani ya miezi sita baada ya uchaguzi uliotajwa katika sehemu ya 22, mfumo wa utawala wenye Machifu Wasaidizi, Machifu, Wakuu wa Tarafa, Wakuu wa Wilaya, na Wakuu wa Mikoa, unaojulikana kama Utawala wa Mikoa, utavunjwa na Serikali itatoa maelekezo mapya kwa maafisa wote wa umma wanaohudumu chini ya mfumo huo.

(2) Mnamo tarehe ya kuanza kutumika Katiba hii, mali zote zilizoko chini ya Serikali ya Taifa na zilizoko katika mikoa, wilaya, tarafa na kata zitakuwa mali ya umma.

(3) Hadi wakati ambapo serikali za wilaya zitakapoundwa, rasilmali zote zilizoko chini ya mamlaka ya mitaa mara tu kabla ya tarehe ya kuanza kutumika Katiba hii, hazitahamishwa au kuondolewa kwa njia nyingine yoyote bila idhini ya maandishi kutoka kwa Serikali ya Taifa, na uhamisho wowote usiokuwa na idhini hiyo si halali.

Sharti kuwekwa na sheria ya Bunge 24. Bunge, kupitia kwa sheria, litaweka masharti ya -

(a) uhamisho wa taratibu wa uwezo na majukumu ulizopewa serikali za wilaya kwa mujibu wa Ibara ya 201, kwa muda usiozidi miaka mitano tangu tarehe ya kutekelezwa Katiba hii kutoka Serikali ya Taifa hadi serikali za wilaya; na

(b) ukabidhi wa uwezo kutoka kiwango kimoja cha Serikali hadi kingine, ukiwemo ukabidhi kutoka Serikali ya Taifa hadi serikali za wilaya, uwezo wa kutunga sheria na masharti ya uhamishaji na urejeshaji wa uwezo uliowakilishwa.

Page 185: Rasimu ya Katiba ya Kenya,2004 Edited after publishing, 1 ...constitutionnet.org/sites/default/files/KEL-003.pdf · 261. Maadili na kanuni za utumishi wa umma 262. Tume ya Utumishi

185

Kustahiki kuchaguliwa au kuteuliwa katika serikali za wilaya 25. Hadi sharti linalohusika lipitishwe kupitia Sheria iliyotungwa na Bunge, mtu

atastahiki kuwa mjumbe wa bunge la wilaya baraza la wilaya lililobuniwa katika Sura ya Kumi na Nne, ikiwa mtu huyo -

(a) anastahiki kuchaguliwa kuwa mbunge;

(b) amekuwa mkaazi katika wilaya hiyo kwa mda wa kipindi cha miezi kumi na miwili mara tu kabla ya tarehe ya uchaguzi au uteuzi huo.

Taratibu na mipango ya ndani ya serikali za wilaya 26. (1) Hadi sharti linalohusika lipitishwe kupitia Sheria iliyotungwa na Bunge

kwa ajili ya Ibara ya 218, kila bunge la wilaya, au baraza la wilaya lilioundwa katika Sura ya Kumi na Nne, inaweza, kupitia azimio, kusimamia utaratibu wake na mipango ya ndani.

(2) Uwezo uliotolewa na sehemu ndogo (1) unajumuisha uwezo wa kuweka sharti linalohusu -

(a) uteuzi na uchaguzi, na uondoaji wa watu kama maspika na manaibu spika;

(b) kuitisha vikao, idadi na uenyekiti wa mikutano; na

(c) akidi na upigaji kura mikutanoni.

Uchaguzi wa meya na naibu wa meya wa Nairobi na miji mingine 27. Hadi sheria inayohusika kutungwa na Bunge, kuhusu uchaguzi wa meya au naibu

wa meya wa Nairobi na jiji lingine lolote -

(a) utaratibu wa kupiga kura utakuwa sawa na uchaguzi wa Bunge; na

(b) masharti ya makaazi kwa ajili ya uchaguzi kama huo ni kwamba mtu awe mkaazi wa eneo kwa kipindi cha miezi kumi na miwili mara tu kabla ya tarehe ya uchaguzi.

Uchaguzi wa wajumbe wa bunge la wilaya 28. Hadi sheria inayohusika itungwe na Bunge kwa ajili ya Ibara ya 209(1) -

(a) wodi za kila wilaya ni wodi zilizoko kabla tu ya tarehe ya kuanza kutumika; na

(b) utaratibu wa kuendesha uchaguzi wa wajumbe wa bunge la wilaya utakuwa kama ilivyoamuliwa, katika hali hiyo, na Tume ya Uchaguzi na Mipaka.