44
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Aprili 2014 Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

  • Upload
    others

  • View
    16

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-1-

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

Aprili 2014

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)

Page 2: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri
Page 3: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Halmashauri ya Wilaya ya Ilala – Dar es Salaam

Imeandaliwa na Timu ya Sam

Aprili, 2014

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)

Page 4: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri
Page 5: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-5-

SHUKRANI

Kukamilika kwa ripoti hii ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ) katika Wilaya ya Ilala kumetokana na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali katika sekta ya afya. Timu ya UUJ Ilala inatambua na kuthamini kwa kiasi kikubwa juhudi zilizotolewa na wadau hao.

Shukrani za dhati ziende kwa wawezeshaji wa mafunzo haya ambao ni Simon Moshy, Aisha Hamis and Josephine Nyonyi kwa kuratibu mchakato mzima wa mafunzo, uchambuzi, ufuatiliaji pamoja na kutoa mrejesho. Pia shukrani kwa Sikika kwa kufadhili ziara ya uhakiki wa shughuli mbalimbali zilizohitaji uhalalisho, uthibitisho na ufafanuzi kama zilivyoainishwa katika ripoti hii.

Timu inatoa shukrani za kipekee kwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa kutambua umuhimu wa zoezi hili na kulisimamia tangu mwanzo hadi mwisho na hatimaye kukamilika kwa ripoti hii. Pia timu ya UUJ inatoa shukrani kwa ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala hususani Idara ya Afya kwa ushirikiano mkubwa walioutoa na kuwezesha timu kupata nyaraka mbalimbali muhimu kwa ajili ya uchambuzi.

Timu ya UUJ inapenda kuwashukuru watendaji wote wa vituo vya huduma za afya vya manispaa ya Ilala kwa kutoa ushirikiano wakati timu ilipotembelea kujionea huduma na miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo yao.

Shukrani za pekee ziwaendee wajumbe wa Timu ya UUJ wa Wilaya ya Ilala;

Mwenyekiti – Timu ya UUJ/SAM Ilala

Page 6: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-6-

YALIYOMO

Shukrani 2

Yaliyomo 3

Orodha ya Vifupisho 5

Sehemu ya kwanza 6

1.1 Utangulizi 6

1.2 Lengo la zoezi la uuj 6

1.3 Muundo wa timu ya uuj 7

1.4 Wajumbe wa timu ya uuj, 2013 7

Sehemu ya pili 8

2.1 Mafunzo kwa timu ya uuj 8

Sehemu ya tatu 10

3.1 Uchambuzi wa nyaraka 10

3.1.1 Uchambuzi wa mpango mkakati wa afya

(Health strategic plan) 11

3.1.2 Uchambuzi wa mpango kabambe wa

Afya wa halmashauri 2011/12 12

3.1.3 Uchambuzi wa ripoti za utekelezaji wa

mpango kambambe wa afya wa

halmashauri 2011/12 12

3.1 Hoja zilizoibuliwa na ufafanuzi ya menejimenti 13

3.2 Hoja maalum kwa hospitali ya wilaya amana 24

3.3 Hoja maalum kwa ngazi ya vituo vya afya 26

3.4 Hoja maalum kwa ngazi ya zahanati 27

3.5 Hoja maalum kwa ngazi ya jamii 28

3.6 Uchambuzi wa mpango wa ukimwi Wa halmashauri 2011/12 29

Page 7: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-7-

Utangulizi 293.6.1 Hoja zilizotoka katika mpango wa ukimwi wa mwaka 2011/12 29

3.6.2 Shughuli ambazo hazikufanyika na hazikuripotiwa katika

taarifa za utekelezaji 31

3.6.3 Shughuli zilizotekelezwa lakini hazipo katika mpango kazi 31

3.6.4 Mambo makuu yaliyobainika na timu ya uuj 31

Sehemu ya nne 33

4.0 Kutembelea vituo vya huduma 33

4.1 Mafanikio ya halmashauri: 33

4.2 Changamoto katika utoaji wa huduma manispaa ya ilala 37

Sehemu ya tano 43

5.1 Majibu ya halmashauri juu ya hoja za timu ya

UUJ zilizofanyiwa desemba 2013 44

Sehemu ya sita 45

6.1 Hitimisho 45

6.2 Mapendekezo 46

Page 8: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-8-

ORODHA YA VIFUPISHO

SAM/UUJ Social accountability Monitoring/ Ufuatiliaji wa Uwajibikaji wa Jamii

ICESCR International Covenant for Eco – Social and Cultural Rights/Mkataba wa Kimataifa kuhusu Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni

WAVIU Waishio naVirusi vya UKIMWI

VVU Virusi Vya Ukimwi

FGM Female Genital Mutilation (Tohara kwa wanawake-Ukeketaji)

CMAC Kamati ya kudhibiti UKIMWI ya halmashauri

STD Sexually Transmited Diseases (Magonjwa ya zinaa)

CHBG Council Health Block Grant

OC Other Charges

CHMT Council Health Management Team

MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi

MoFEA Ministry of Finance and External Affairs (Wizara ya Fedha na Uhusiano wa nje)

TAMISEMI Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Page 9: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-9-

SEHEMU YA KWANZA

1.1 UTANGULIZIMchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji wa Jamii (UUJ) ujulikanao kama “Social Accountability Monitoring - SAM” ulikusudia kuiwezesha Halmashauri ya Wilaya ya Ilala kuboresha utoaji wa huduma za kijamii hususan sekta afya, ili wananchi wanufaike na huduma hizo kama haki zao za msingi. Kimsingi, Sikika iliiwezesha Timu ya SAM iliyochaguliwa kufanya shughuli ya ufuatiliaji chini ya miongozo sahihi na kufuata sheria. Utekelezaji wake umezingatia sheria; Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia. Sheria ambazo timu imezitumia ni pamoja na Ibara za (11), (12), (14) – (28) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mikataba ya Kimataifa ya Banjul (Africa) na International Covenant for Eco – Social and Cultural Rights (ICESCR – 1976) ambayo yote imejikita katika kuhakikisha kuna uwajibikaji katika kufikia upatikanaji na utoaji wa haki za binadamu na mahitaji ya msingi ya jamii.

1.2 LENGO LA ZOEZI LA UUJLengo kuu la zoezi hili la Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ) ni kuijengea uwezo jamii katika kufanya chambuzi za taarifa mbalimbali pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali inayotekelezwa na sekta ya afya ya serikali. Zoezi hili pia linalenga kuwezesha jamii kuhoji uwajibikaji wa wasimamizi na watoa huduma za umma ili waweze kutoa huduma zinazokidhi mahitaji muhimu na ya msingi kwa jamii kama vile afya, elimu, maji, chakula na makazi.

1.3 MUUNDO WA TIMU YA UUJZoezi la kuunda timu ya UUJ lilifuata hatua mbalimbali ili kuweza kupata uwakilishi kutoka katika makundi mbalimbali ya wananchi. Mikutano ya wananchi katika ngazi ya kata ndiyo iliyotangulia ambapo walipatikana wawakilishi wa wananchi sita (6), wawili wakiwa ni WAVIU. Hii ilifuatiwa na Mkutano wa Baraza la Madiwani ambalo lilichagua wajumbe wawili waliowawakilisha katika Timu ya UUJ. Na kisha mkutano wa wadau uliowashirikisha; Mkuu wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala, Watendaji wakuu wa Halmashauri, Kamati ya Uongozi ya Afya, Watendaji wa Kata, wawakilishi wa kamati za uongozi za vituo vya afya, wawakilishi wa makundi ya kidini, makundi maalum ya watu wenye ulemavu na watu wanaoishi na maambukizi ya VVU. Katika mkutano huo, wawakilishi wa kikundi cha SAM/UUJ walichaguliwa miongoni mwa makundi yaliyokuwepo, kila kundi lilichagua mwakilishi wake na kuunda timu ya watu 15.

Page 10: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-10-

1.4 WAJUMBE WA TIMU YA UUJ, 2013Na. JINA KUNDI WAKILISHA

Richard Zaidi MwananchiDominica Daniel MwananchiRashidi Said MwananchiAngel Alfred MwananchiShomvi Kumburu MwananchiMariam Myugo MwananchiRenatus Luhungu Afisa Mtendaji Kata ya KivukoniAlly S. Itongora AZAKIJohnson Vigero kamati ya kudhibiti UKIMWI ya halmashauriSemeni Segellah Ofisi ya Mganga Mkuu wa WilayaAngelina Malembeka DiwaniRiyami Gharib Diwani-MchikichiniMch. Gilbert Lwoga DiniPeter C. Mwasingi Kamati za usimamizi wa vituo vya hudumaAboubakar Nyundo Bodi ya Huduma za afya ya Wilaya

Page 11: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-11-

SEHEMU YA PILI

2.1 MAFUNZO KWA TIMU YA UUJTimu ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ) ilipata mafunzo ya siku 15. Katika mafunzo hayo, wajumbe wa timu walipata fursa ya kuelimishwa juu ya mfumo mzima wa uwajibikaji wa jamii na kujadili kwa kina hatua tano muhimu za UUJ.

Hatua hizo ni:

Dhana ya utoaji huduma kwa mtazamo wa HAKI za misingi za Binadamu na kuangalia Mahitaji ya Dola/serikali ili kuhakikisha upatikanaji wa haki za msingi za kijamii na kiuchumi zikiwemo huduma za afya.

Mgawanyo wa Rasilimali Na Mpango Mkakati na kuangalia nini maana ya mgawanyo wa rasilimali na Kwanini wananchi wafuatilie mchakato wa mgawanyo wa rasilimali. Timu ya UUJ pia iliangalia mchakato wa Mgawanyo wa rasilimali nchini Tanzania; na kujadili kwa kina mchakato wa maandalizi ya mipango ya muda mrefu, muda wa kati na mipango ya muda mfupi ikiwemo mipango ya mwaka ya afya katika ngazi ya vituo na halmashauri kwa ujumla. Katika mjadala huu, timu ilipata fursa ya kusikia uzoefu wa wajumbe wawakilishi wa kamati za usimamizi wa vituo juu ya namna wanavyoandaa mipango na njia za kuainisha mahitaji ya jamii, muda wa maandalizi na wadau wanaoshiriki katika mchakato wa maandalizi ya mipango ya mwaka ya vituo vya huduma zikiwemo kata. Timu pia ilijifunza hatua zote muhimu kabla kupitishwa mipango ikiwemo mipango kuwasilishwa kwa timu ya Mipango ya halmashauri na hatimaye baraza la madiwani la halmashauri. Pamoja na hayo, timu ilifahamishwa Zana za usimamizi katika kusimamia mgawanyo wa rasilimali.

Usimamizi wa matumizi ni hatua inayohusisha ufuatiliaji wa karibu wa jinsi halmashauri/taasisi inatumia fedha zilizoidhinishwa na kutolewa katika mipango ya wakati husika. Katika hatua hii, wajumbe wa timu ya UUJ walijadili ni umuhimu kusimamia Matumizi na uwajibikaji kwa jamii pamoja na kuangalia Miongozo inayosimamia/kuelekeza matumizi ya fedha za umma na Taarifa za Mifumo ya Usimamizi wa Fedha na wajibu wa kitengo cha Ukaguzi wa Ndani katika kusimamia matumizi sahihi ya rasilimali katika kuzuia/kuepusha matumizi mabaya ya rasilimali ili kufikia upatikanaji wa haki za msingi za binadamu ikiwemo haki ya huduma bira za afya.

Usimamizi wa Ufanisi/Utendaji ambapo timu ilifafanuliwa dhana nzima ya usimamizi wa ufanisi na kujadili maswali muhimu timu ya UUJ wanayopaswa

Page 12: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-12-

kujiuliza: Je, Halmashauri na watoa huduma wanatekeleza shughuli na malengo ya mpango kwa ufanisi na ufasaha? Je, wanawajibika kwa makosa au udhaifu wa mfumo wa Usimamizi wa Utendaji au katika utoaji huduma? Je, Halmashauri zinahakikisha ufikiwaji wa haki za kijamii na kiuchumi kwa kutoa huduma kulingana na rasilimali zilizopo?

Usimamizi wa Uadilifu ni kitendo cha kuwawajibisha watendaji wakuu wa serikali kwa kusimamia maamuzi/shughuli zake ili iweze kuwajibika dhidi ya kanuni za ufanisi, uaminifu na unyoofu katika utendaji kazi wake. timu pia ilijadili Vyombo mbalimbali vya maamuzi na wajibu/mamlaka ya kikatiba ya kidemokrasia katika kusimamia utendaji, hivi ni pamoja na; Bunge/Baraza la madiwani, Taasisi za Ukaguzi ( mf.Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu), Kamati za huduma ya afya na Kamati za UKIMWI

Page 13: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-13-

SEHEMU YA TATU

3.1 UCHAMBUZI WA NYARAKA Mfumo wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii unalenga katika kuhakikisha haki za binaadamu na mahitaji ya jamii yanafikiwa kikamilifu. Mchakato wa uchambuzi wa mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii (UUJ) katika halmashauri ya Manispaa ya Ilala ulifuata hatua zote tano muhimu za mchakato huu. Hatua hizi ni mipango na mgawanyo wa rasilimali, usimamizi wa matumizi, usimamizi wa utendaji, usimamizi wa uadilifu na usimamizi wa uwajibikaji.

Kwa kila hatua ya mfumo, Timu ya UUJ ilifafanuliwa dhima na umuhimu wa kupitia hatua husika katika kuleta uwajibikaji kwa watendaji. Baada ya kufafanuliwa hatua hizo muhimu katika kutekeleza zoezi la UUJ, timu iliwezeshwa kupitia nyaraka/zana zote muhimu katika kila hatua. Nyaraka hizi ni pamoja na mipango ya muda mrefu na muda mfupi mfano mipango mikakati ya halmashauri na ile ya idara ya afya, mipango ya afya na UKIMWI ya halmashauri, ripoti za utekelezaji pamoja na taarifa za vyombo vya usimamizi zikiwemo mihutasari ya kamati ya kudhibiti UKIMWI ya halmashauri (CMAC) na mihutasari ya baraza la madiwani la halmashauri kwa mwaka 2011/12.

Lengo la uchambuzi huu ni kuangalia kama utendaji wa halmashauri kwa kila hatua ya mfumo unahakikisha upatikanaji wa haki za kijamii katika sekta ya afya kwa kutumia rasilimali zilizopo.

Wakati wa uchambuzi wa nyaraka, timu ya UUJ iliainisha maeneo yaliyohitaji Ufafanuzi, uthibitisho na Uhalalisho katika kila hatua na kuyajengea hoja na kuziwasilishwa kwa menejimenti ya afya ya halmashauri (CHMT). Timu ya

Timu ya UUJ iliandaa mkutano wa ndani uliojumuisha wajumbe wa timu ya uendeshaji wa huduma za afya ya halmashauri uliofanyika katika ofiisi ya Mganga mkuu wa Manispaa. Katika mkutano huo timu iliwasilisha hoja zote zilizoibuliwa, hali halisi ya utoaji wa huduma kama ilivyobainika katika ziara ya kutembelea vituo. Timu pia iliwasilisha changamoto na mafanikio ya zoezi kwa hatua zilizokamilika.

Kupitia mkutano huo, Wajumbe wa CHMT waliomba timu ya UUJ iwape muda ili waandae majibu ya hoja nyingine zilizohitaji uchambuzi wa kina.

3.1.1 UCHAMBUZI WA MPANGO MKAKATI WA AFYA (Health Strategic Plan)Manispaa ya Ilala ni moja ya manispaa tatu za jiji la Dar es Salaam, yenye idadi ya watu 637,573. Mpango mkakati wa afya wa Manispaa ya Ilala ni wa miaka mitano

Page 14: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-14-

kuanzia 2011-2016. Mpango huu una Uchambuzi wa kina na umeonesha mazingira ya nje na ndani, Mikataba ya kimataifa na kitaifa, Dira ya Taifa, Umeangalia sera ya taifa. Mpango huu unaonesha uchambuzi wa mahitaji muhimu ya kiuchumi na ya kijamii ingawa mahitaji ya makundi maalum kama wazee, watoto wanaoishi katika mazingira magumu, wanaoishi na VVU n.k hayakuanishwa. Mahitaji ya makundi yaliotambuliwa ni watoto chini ya miaka 5, wajawazito. Mpango umeonesha uhusiano baina yake na mpango mkakati wa halmashauri.

Vilevile Mpango mkakati umeweza kuelezea uwezo wake wa rasilimali watu na changamoto zilizopo kuwa idadi ya watumishi waliopo ni 721 na wale wanaohitajika ni 3721. Umeweza kuonesha uwezo na vipingamizi katika idara ya afya, ikiwa ni pamoja na mapungufu ya utoaji huduma yanayosababishwa na mazingira ya nje (uk 16). Vyanzo vya mapato vimeoneshwa ikiwa ni pamoja na makadirio ya mapato na matumizi. Gharama iliyotengwa kwa kila shughuli pia zimeonekana ukurasa wa 37-41.

Mpango huu wenye Uchambuzi wa kina umeelezea Historia fupi, uwezo wa rasilimali watu, uchumi wa eneo, shughuli za biashara na mgawanyo wa kata, Dira na Dhamira.

Mpango pia umeelezea shughuli zinazotegemewa kufanyika ndani ya kipindi cha miaka mitano na rasilimali zote zinazohitajika. Malengo yalioanishwa yanapimika, (uk 18-23 ).

Hata hivyo, timu imebaini kuwa Mpango Mkakati wa Afya haukuainisha Matatizo ya kiafya yaliyopo halmashauri ikiwemo kipindupindu. Ushiriki wa wadau katika uandaaji wa mpango haukuwekwa bayana isipokuwa wametaja kamati, na bodi kuwa walishirikishwa bila kufafanua ni kwa jinsi gani. Pia fedha kwa ajili ya shughuli za UKIMWI hazikuonyeshwa ndani ya mpango mkakati huo.

3.1.2 UCHAMBUZI WA MPANGO KABAMBE WA AFYA WA HALMASHAURI 2011/12Mpango kabambe wa afya wa manispaa ya Ilala una taarifa muhimu za awali zikiwemo uchambuzi yakinifu wa mahitaji; uwezo wa rasilimali, matatizo ya kiafya, shughuli zinazotakiwa kufanyika na vipaumbele vya halmashauri na zimeonyesha wahusika wanaotakiwa kuzitekeleza. mpango wa afya wa Ilala una taarifa za bajeti/fedha kulingana na shughuli zilizopewa kipaumbele. Malengo yanapimika pia umeweka wazi uwezo/vipingamizi vya utendaji na jinsi ya kutatua vipingamizi (uk 64-69)

Mpango huu pia umehusisha na kufanyia kazi taarifa zilizotokana na mipango iliyopita (imeelezwa katika muhtasari wa taarifa) ingawa baadhi ya taarifa hazijaelezea

Page 15: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-15-

malengo. Mpango wa afya wa wilaya umeelezea uwezo wake wa rasilimali watu na changamoto katika kutekeleza mpango. (uk 64).

Pendekezo: Halmashauri imekuwa na utaratibu wa kuajiri wafanyakazi wa muda (part time basis). Halmashauri ioneshe bajeti ya kuajiri wafanyakazi hao katika mpango wao wa mwaka ili kuonesha juhudi za halmashauri katika kuongeza rasilimali watu ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

3.1.3 UCHAMBUZI WA RIPOTI ZA UTEKELEZAJI WA MPANGO KAMBAMBE WA AFYA WA HALMASHAURI 2011/12Timu ilifanikiwa kupata ripoti za utekelezaji za awamu tatu kwa mihula; Oktoba-Desemba na Januari-Machi na Aprili-Juni 2012.

3.2 HOJA ZILIZOIBULIWA NA UFAFANUZI YA MENEJIMENTI

1. Katika mwaka 2011/12-halmashauri ilianisha Maeneo makuu 11 kwa kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa na serikali. Hata hivyo kuna maeneo mengine ambayo yaliyotengewa fedha huku mengine hayakutengewa, mfano Uzazi na afya ya Mama na mtoto pamoja na magonjwa ya ngono na UKIMWI.

HOJA: Timu inataka kufahamu kwanini maeneo haya hayakutengewa fungu?

Ufafanuzi wa Menejimenti: Hii inatokana na matatizo ya mfumo wa mipango (PLANREP), Baadhi ya vipengele vinakuwepo katika bajeti, ila mfumo wenyewe wa PLANREP hauoneshi fedha hizo katika “summary” ya Bajeti kuu. Mfumo unashindwa kujumlisha kasma zote katika jumla kuu ya bajeti. Kuna tatizo la kuunganisha shughuli mbalimbali kwa kuchukua kazi zisizo sahihi.

(Hata hivyo ilielezwa kuwa mfumo huo umefanyiwa marekebisho kwa sasa)

2. Utofauti wa taarifa za bajeti Katika viambatanisho vya bajeti mahususi ‘Specific budget’ na bajeti kuu ‘Main budget’ ; Fedha za (mfuko wa pamoja) zinatofautiana.

i. Usafi na afya ya mazingira (Environmental Health and Sanitation); kiasi cha shilingi 53,520,000 na 4,039,907 (57,559,907) zilizotengwa kwa ajili ya Usafi wa Maji (water hygiene and sanitation) zimeonekana katika specific lakini katika jedwali la bajeti kuu hazijaoneshwa.

ii. Fedha za UKIMWI katika jedwali la bajeti kuu ni 6,417,500 (CHBG) ila katika bajeti mahususi (specific budget) ni 8,107,500 huku malaria ikiwa ni shilingi 33,986,090/- kutoka 9,986,090/-.

Page 16: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-16-

Health Block Grants

iii. Ustawi wa Jamii: fedha kwa ajili ya rehabilitative support/huduma za utengamao kiasi cha 920,000/- hazikuwepo kwenye main bajeti lakini zimeoneshwa katika specific bajeti.

iv. Majanga na dharura: kiasi cha shilingi 5,275,000/- kwa ajili ya kuwatambua jamii zilizo katka mazingira hatarishi lakini katika bajeti ya jumla kiasi hicho hakikuainishwa (walianisha 10M za uchangiaji).

Hoja: timu inaomba ufafanuzi kuhusu utofauti wa bajeti hizi

Ufafanuzi wa menejimenti: Fedha hizi ni za wadau wa maendeleo ambazo zinaweza kuwa fedha taslim ama huduma. Hivyo, katika jedwali la bajeti kuu vyanzo vyote vya fedha huainishwa ila katika jedwali la bajeti mahususi (specific budget summary) bajeti ya shughuli hizi haiingizwi, ila huingiza fedha kutoka vyanzo vya kapu la pamoja na serikali kuu (mfuko wa pamoja na serikali kuu) tu.

Maoni ya timu: Timu haikuridhishwa na majibu ya menejimenti, hivyo inaomba kupatiwa maelezo ya ziada.

3. Fedha za uchangiaji hazikuainisha kama chanzo kikuu cha fedha.

Ufafanuzi wa menejimenti Halmashauri huandaa vitabu tofauti. Kitabu kinachopelekwa TAMISEMI, na MoFEA haviingizwi fedha za uchangiaji kwa kuwa fedha hizo zikishaingia kwenye akaunti ya wizara itachukua muda mrefu/mchakato mrefu kuomba, hivyo vituo havitaweza kutumia fedha zake kwa wakati. Kitabu cha mkurugenzi ndio huingizwa fedha za uchangiaji. Hivyo, inawezekana timu ya UUJ ilipata kitabu ambacho si cha mwisho na kinachofanyiwa kazi.

4. Kiasi cha 60,000,000/- kilitengwa kwa ajili ya msamaha kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu (exemption and waivers of the vulnerable children). Timu haikuweza kuona kiasi hiki kimepangwa kutumikaje kwani hakikujumlishwa katika jumla ya eneo la kuboresha ustawi wa jamii.

Ufafanuzi wa menejimenti: Hakuna shughuli maalum. Fedha hizi hutengwa ili kutolea huduma za misamaha kwa makundi maalum. MMOH hukadiria fedha kwa ajili ya misamaha kwa mwaka. Kila kituo huweka kumbukumbu za wanaotibiwa kwa misamaha na kuiwasilisha kwa mhasibu wa Halmashauri.

Maoni ya timu: Ni vema mchanganuo huu ukaelezwa ndani ya taarifa kuondoa maswali mengi na kufanya taarifa kuwa wazi.

Page 17: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-17-

5. Utofauti wa jumla ya bajeti za mwaka (planned activities for priority area)

Shughuli 2.3 (jamii): ukarabati wa Buguruni camp, katika muhula wa pili ilioneshwa zimetengwa shilingi 40,920,315/- wakati shughuli hiyohiyo imeonekana kutengewa 30,549,745/- katika muhula wa tatu. Timu inataka ufafanuzi juu ya tofauti hii ya bajeti iliyopangwa kwa mwaka mzima.

Ufafanuzi wa menejimenti: Mara nyingine MMOH huhamisha fedha kutoka katika shughuli moja na kupeleka katika shughuli nyingine, na uhamishaji huu hufanyika katikati ya mwaka wa kiserikali (Desemba). Hivyo fedha hizi kupungua ni kufuatia kuhamishwa fedha kwenda kwenye kasma za shughuli nyingine.

Maoni ya timu: Jibu lililotolewa ni la ujumla sana na halijaainisha bayana kuhusu fedha hizi. Timu ya UUJ inashauri uhamishaji wa fedha unapofanyika uwe na maelezo ya kujitosheleza kuwa zimeelekezwa wapi.

6. Utofauti wa makadirio ya bajeti katika mipango na ripoti za utekelezaji

Shughuli ya kuboresha huduma za mkoba katika maeneo yasiyopewa kipaumbele (underserved area) zilitengewa kiasi cha shilingi 8,500,000/- (MMOH- uk 10) huku ripoti ya utekelezaji imeonesha kuwa fedha zilizotengwa kwa huduma hizo 12,640,000/- (uk 36)

Ufafanuzi wa menejimenti: Kulingana na hali ya wakati, baadhi ya kazi huongezewa fedha au kupunguziwa.

Maoni ya timu: Taarifa za kuhamisha fedha kati ya kasma na vifungu tofauti iwe na maelezo ya kujitosheleza na ya wazi.

7. Matumizi hayalingani na vipaumbele katika CCHP uk 33 wa ripoti ya utekelezaji, jedwali namba 4

Ufafanuzi wa menejimenti: Hoja haijajibiwa.

8. Katika jedwali la bajeti ya muhula wa pili, halmashauri ilionesha kuwa kuna deni la jumla ya shilingi 62,000,000/- kutoka Fedha za serikali kuu Matumizi mengineyo kama salio anzia. Katika muhula huohuo, kiasi cha 39,000,000/- zilitumika kupunguza deni na kubakia kiasi cha 23,000,000/-. Hata hivyo, katika kufunga muhula, ripoti ilionesha kuwa deni lililopo kwa fedha za Block Grant ni kiasi kilekile cha 62,000,000/- kama salio ishia). Kiasi hiki kikalipwa tena katika muhula wa tatu (62,000,000/-), hivyo deni hili lililipwa kwa jumla ya 101,000,000/-.

Page 18: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-18-

Hoja: Timu inaomba ufafanuzi kwanini deni hili lililipwa mara mbili; muhula wa pili (39,000,000/-) na muhula wa tatu (62,000,000/-). Je, halmashauri haikuona tofauti ya matumizi katika fedha za Matumizi mengineyo kutoka chanzo cha fedha cha serikali kuu.

Ufafanuzi wa menejimenti: Kiasi cha shilingi milioni 39,000,000 zilitumika kwa kazi nyingine.

Maoni ya timu: Maelezo hayajajitosheleza kuonyesha shughuli zilizofanyika. Timu inashauri kuwa na maelezo ya kujitosheleza kuelezea matumizi ya fedha.

9. Timu imebaini kuna shughuli zimewekwa bila ufafanuzi wa kilichofanyika na bajeti iliyotumika.

Mfano katika ngazi ya zahanati: shughuli namba 3.1.5; halmashauri imepanga kufanya ukarabati wa majengo na mabango katika zahanati tano bila kufafanua ni kiasi gani cha bajeti kilitumika katika kukarabati majengo na kiasi gani kilitumika kwa kutengeneza mabango. Vilevile ripoti ya utekelezaji haijaonesha ni zahanati zipi zilizokarabatiwa na mabango mangapi yametengenezwa.

Hoja: Timu inaomba mchanganuo wa bajeti pia ifahamishwe ni zahanati zipi zilizokarabatiwa na kupatiwa mabango.

Ufafanuzi wa menejimenti: Mabango yaliyokarabatiwa ni Kivule, Kitunda, Mongo la Ndege, Gulika kwalala na Zingiziwa. Ukarabati wa majengo ulitumia fedha za MMAM. Vituo vya Msongola, chanika, Tabata A, NBC, Kivule na Kitunda vilifanyiwa ukarabati.

Maoni ya Timu ya UUJ: Timu inashauri kuwepo kwa maelezo, na mchanganuo wa kujitosheleza katika kutoa taarifa

10. Shughuli namba 3.1.3: kufanya matengenezo ya magari 2.

Hoja: Timu inataka ufafanuzi juu ya;

- Je, ni magari yapi yalifanyiwa matengenezo? Je, ni magari ya vituo vipi?

- Kiasi gani kilitumika kwa matengenezo ya kila gari?

Ufafanuzi wa menejimenti: Magari hayo ni magari mawili ya chanjo yaliyopo kata ya Chanika na ofisi yam ganga mkuu wa manispaa.

Page 19: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-19-

11. Katika ripoti za utekelezaji, timu imebaini kuwa hakuna uhalisia wa ukamilifu wa miradi kama inavyoonesha katika kipengele cha “hali ya utekelezaji wa shughuli kwa asilimia” (cumulative implementation by percentage). Shughuli moja inaonekana imekamilika kwa asilimia mia moja kwa mihula miwili tofauti. Mfano shughuli namba 9.1.13 (MMOH), kupitia mpango mkakati wa mwaka 2007-2012kwa bajeti ya 4,000,000/-. Muhula wa pili (Oct-Dec 2011), fedha zilizopatikana ni 4,000,000/- na zilizotumika ni 4,000,000/- zote (100%). Muhula wa tatu (Jan-March), shughuli hii ilitekelezwa tena na kiasi cha kilitengwa kwa muhula huu ni shilingi 2,400,000/- . Kiasi kilichotumika ni 360,000/- (15%) na utekelezaji wa jumla ni 100%. Muhula wa nne (April-June) kiasi cha 2,600,000/- kiliripotiwa kupatikana na kutumiwa chote (100%) kwa shughuli hii. Mfano wa shughuli nyingine ni 1.1.2 (Amana Hospitali) na 3.2.3

Hoja: Timu inaomba ufafanuzi juu ya;

i. Utofauti wa hali ya utekelezaji wa shughuli kwa asilimia

ii. Kwanini shughuli hii imetekelezwa kwa fedha zaidi ya bajeti iliyopangwa kwa mwaka? (4,000,000/-).

Ufafanuzi wa menejimenti: Matatizo katika kuingiza taarifa katika mifumo ya kuandaa mipango na ripoti za utekelezaj - Planreps.

Maoni ya timu: Ni vema ofisi ya Mganga Mkuu wa Manispaa ikawa na mfumo madhubuti wa kuhakiki taarifa zake ili kuhakikisha kuwa matatizo hayo hayajirudii hapo baadaye.

12. Shughuli namba 4.1.3 na 4.1.8 (ripoti ya muhula wa pili) imeonesha malipo ya masaa ya ziada na posho ya kazi za ziada yaliyofanyika kwa watumishi wa zahanati 10 zilizopo pembezoni (peripheral dispensaries).

Hoja: Timu inaomba ufafanuzi juu ya utofauti wa malipo haya.

i. Je, ni wafanyakazi wangapi walilipwa posho ya masaa ya ziada? Je, ni vituo gani?

ii. Je, wafanyakazi wangapi walilipwa posho ya kazi za ziada (extra-duty allowances?) Je ni vituo gani?

Ufafanuzi wa menejimenti: Ni vigumu kutenganisha malipo ya saa za ziada na malipo ya kazi za ziada kwa wafanyakazi kwa chanzo tofauti. Hivyo inawalazimu kutenganisha/kubadilidha maneno ili kuweza kupata bajeti itakayotosha kufanya malipo hayo. Jumla ya wafanyakazi 102 wa vituo vilivyopo pembezoni walilipwa.

Page 20: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-20-

13. Katika shughuli namba 4.1.11 (Jamii), halmashauri ilipanga kuwezesha kamati 21 za afya za jamii kuibua vipaumbele jamii na kuandaa mipango kazi yao ifikapo June 2012 kwa gharama ya 3,880,000 ambayo ilitumika yote na utekelezaji ni 100% .

Hoja: Timu ya UUJ inaomba ufafanuzi juu ya;

i. Namna gani vipaumbele vya jamii vinaibuliwa?

ii. Nani anahusika katika mchakato mzima?

iii. Je, ni maeneo gani yalifikiwa? Vipaumbele vipi viliibuliwa na kufanyiwa kazi?

Ufafanuzi wa menejimenti: Hizi ni kazi za kamati za usimamizi za vituo kama ifuatavyo;

i. Vipaumbele vya HFGCs vinaibuliwa na kamati husika kwa kuhusisha mahitaji kutoka kwa jamii kupitia wawakilishi wao. Vipaumbele vya kila kituo huwasilishwa MMOH na wenyevti wa kamati.

ii. Mratibu wa mipango na timu ya CHMT hupokea vipaumbele

iii. Vipaumbele vilivyoibuliwa kutoka kamati za vituo ni :

Ujenzi wa vichomeo taka, ujenzi wa makazi/wodi za TB, ununuzi wa mabenchi Kitunda, ukarabati wa vituo, umeme, uzio (recurrent)

iv. Vipaumbele vya kawadia/dawa huchukuliwa vyote 100% ila na ukarabati, ununuzi wa vifaa (2%) vya miradi ya maendeleo hutegemea bajeti.

14. Katika ngazi ya jamii, halmashauri ilipanga kufanya mikutano mbalimbali kupunguza magonjwa ya kuambukiza katika kata 26 kwa gharama ya 6,400,000/-. Katika ripoti za utekelezaji shughuli hii ilitekelezwa katika muhula wa tatu na kiasi kilichopatikana ni 1,600,000/- na zilizotumika ni 2,600,000/- (25%) huku utekelezaji wa jumla ikiwa ni 4,800,000 (75%). Katika muhula wa nne, ripoti ilionesha kuwa bajeti iliyopangwa kwa ajili ya shughuli hii ni 12,400,000/- na zilizopatikana ni 4,325,000/- ambazo zilipatikana na kutumika zote (100%) huku utekelezaji wa jumla ni 100%.

Hoja: Timu ingependa kufahamu;

i. Kwanini kuna tofauti ya bajeti iliyopangwa kwa shughuli hii.

ii. Ni mikutano ya aina gani ilifanyika na mingapi?

iii. Ilihusisha kina nani? Ni lini mikutano hiyo ilifanyika?

Page 21: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-21-

Ufafanuzi wa menejimenti: Halmashauri hufanya ubadilishaji wa matumizi ya fedha inapofika nusu mwaka (mwezi desemba), kwa kuzingatia masuala mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa fedha. Shughuli iliyopangwa na kutekelezwa kwa fedha hizo ni huduma mbalimbali sio mikutano kama ilivyoandikwa na huduma hizi huhusisha halmashauri na wadau mbalimbali wa maendeleo.

15. Katika mpango wa 2011/12, (shughuli 2.1) halmashauri ilipanga kutoa Elimu ya usafi wa mazingira katika ngazi ya jamii ndani ya kata 26 kwa gharama ya shilingi 5,534,420/-. Katika ripoti za utekelezaji, bajeti ya iliyooneshwa kupangwa ni 12,705,420/-. Ripoti ya muhula wa tatu kiasi cha 3,176,355/- kilipatikana na kilichotumika ni 4,176,355/- (25%). Katika muhula wa nne, bajeti iliyopatikana na kutumika ni 12,705,420/- hicho (100%).

Hoja: Timu inapenda kupata ufafanuzi juu ya :

i. Je, elimu hii ilitolewaje? Nani alihusika? Kwa gharama gani kwa kila kata?

ii. Jumla ya bajeti yote iliyotumika ni tofauti na kilichopangwa.

1. Ufafanuzi wa menejimenti: Elimu hii hutolewa na Maofisa afya kwenye kila kata.

2. Kwenye mfumo wa EPICOR wa zamani hakukuwepo na usimamizi wa maazimio (commitment control), mara nyingine shughuli zinatekelezwa kwa zaidi ya bajeti iliyopangwa.

Maoni ya timu: Jibu halijajitosheleza. Timu inasisitiza umakini katika kutoa taarifa za utekelezaji.

16. Halmashauri pia ilionesha kuwa imetekeleza shughuli ya kuandaa mipango kazi ya jamii kwa shilingi 1,200,000/- (shughuli 6.1).

HOJA: Timu inataka kujua ni mipango gani inaandaliwa? Je, nani anahusika kuandaa mipango hiyo? Timu inaomba uthibitisho

Ufafanuzi wa menejimenti: Ni mipango ya maafisa afya, ila kwa sasa kipengele hicho hakipo sababu jamii hawakuwa wakishirikishwa.

Maoni ya timu: Timu inashauri MMOH ione umuhimu wa kutenga na kutumia fedha katika shughuli ya ngazi ya jamii kama inavyoelekezwa katika miongozo ya uandaaji wa bajeti ya afya.

17. Kuna utofauti wa lugha na namba za shughuli zilizopo katika mpango wa afya (CCHP) na ripoti za utekelezaji, pia ripoti za utekelezaji kwa mihula tofauti. Mfano shughuli namba 4.2 katika mpango ni “ni kuwezesha wafanyakazi 60 katika kozi za muda mrefu za ndani ya nchi ifikapo June 2012” huku shughuli hiyo katika ripoti ya utekelezaji muhula wa 2 (oct-Dec) “ kuimarisha ubakizaji

Page 22: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-22-

kwa wafanyakazi wa afya (HCPs) 20 ifikapo June 2012”.

Ufafanuzi wa menejimenti: shughuli hii imekosewa kuandikwa hata hivyo shughuli zote zinatekeleza azimio/lengo moja.

Maoni ya timu: Timu ya UUJ, inahoji umakini wa uandishi wa taarifa. Ni vema ofisi ya MMOH kuwa na mfumo bora wa kukagua taarifa kabla ya kutolewa kwa matumizi ya umma.

18. Hakuna uhalisia wa shughuli zinazopangwa; mfano shughuli 4.2 kiasi kilichopangwa kwa ajili ya mafunzo ya muda mrefu kwa wafanyakazi 60 na bajeti iliyopangwa ni 7,434,003/-.

Ufafanuzi wa menejimenti: Halmashauri haitoi uwezeshaji mkubwa kwa wafanyakazi mara nyingi hupewa shajala tu (kuanzia 50,000-200,000). Pia sio wafanyakazi wote wanaowezeshwa kwani hilo ni lengo lililowekwa na halmashauri.

19. Baadhi ya malengo hayaendani na shughuli zinazotekelezwa katika malengo hayo. Mfano lengo namba 4 kuwajengea uwezo maofisa afya; huku shughuli 4.2 kuimarisha ubakizaji wa watoa huduma wa afya 20 kwa gharama ya shilingi 3,858,501/-.

Ufafanuzi wa menejimenti: Wamekiri kuwa makosa yamefanyika.

20. Viashiria haviendani na shughuli. Hivyo ni vigumu kupima mafanikio ya shughuli husika. Mfano shughuliNa. 6.1.6 (AMANA) kuwezesha huduma za usafiri ifikiapo June 2012, wa gharama ya shulingi 9,800,000/-. Kiashiria kinachotumika kupima utekelezwaji wa shughuli hii ni “idadi ya wafanyakazi waliohudhuria”

Ufafanuzi wa menejimenti: Makosa ya uchapaji… ilikosewa ilitakiwa kuwa idadi ya wagonjwa waliosafirishwa.

Maoni ya timu: Umakini uongezwe katika kuandaa ripoti.

21. Mchanganuo uliowekwa katika shughuli hauendani na shughuli husika. Mfano shughuli Na. 6.1.6 (AMANA) kuwezesha huduma za usafiri ifikiapo June 2012; inputs ni chakula na vinywaji; gharama 10,000/- idadi 230 hivyo jumla ya bajeti ni 2,3000,000/-.

Ufafanuzi wa menejimenti: Makosa yamefanyika

Maoni ya timu: Timu ya uaandaaji wa mipango ya afya iongeze umakini

Page 23: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-23-

22. Halmashauri imetoa vipaumbele tofauti (priority area) katika mpango kazi na ripoti ya utekelezaji ya Q2. Mfano ustawi wa Jamii katika mpango ilipewa namba 6 katika utekelezaji ni namba 7, Uimarishaji muundo/mfumo wa utendaji ni namba 6 badala ya 8 kama ilivyokuwa katika mpango kabambe. (Uk 33 ripoti ya utekelezaji na Uk 10-14, CCHP)

Maoni ya timu: Maeneo ya vipaumbele yanaweza yakawa tofauti kulingana na mahitaji halisi ya muda husika/kipindi cha utekelezaji

23. Halmashauri haikutumia kabisa fedha katika baadhi ya vipaumbele vikiwemo tiba asilia, ustawi wa jamii na mipango ya kuboresha afya (health promotions).

Ufafanuzi wa menejimenti: Si rahisi shughuli hizo zisifanyike, zilifanyika inawezekana zimeripotiwa katika ripoti za utekelezaji ya mwaka.

Maoni ya timu: Timu haikupatiwa taarifa ya mwaka, na haijaridhishwa na jibu lililotolewa.

24. Kipaumbele cha uimarishaji ustawi wa jamii hakijaoneshwa katika ripoti ya utekelezaji.

Hoja: Je, shughuli za ustawi wa jamii zinatekelezwaje?

Ufafanuzi wa menejimenti: Shughuli zilitekelezwa.

Maoni ya timu: Timu haijaridhishwa na jibu kwani halmashauri hawakuonesha ni jinsi gani shughuli hizo zilitekelezwa.

25. Fedha za MMAM zimeonekana kutolewa lakini hazijatumika katika mihula yote (2-4).

Ufafanuzi wa menejimenti: Hakuna maelezo.

26. Shughuli imeonekana kutekelezwa na fedha yote imetumika, lakini mafanikio ni 0% na maelezo yaliyotolewa ni kuwa shughuli itatekelezwa muhula wa tatu (Uk 37- kufanya mkutano na viongozi wa jamii kuhusu chanjo mpya).

Ufafanuzi wa menejimenti: Makosa katika uandishi.

27. Shughuli zimeelezwa kwa vifupisho ambavyo havipo kwenye orodha ya vifupisho. Shughuli 3.3.4 (mikutano ya uhamasishaji kwa THS kuhusu uboreshaji wa huduma) shughuli imetekelezwa kwa 100% (1,800,000/-) Je mkutano huu ulihusisha kina nani?

Ufafanuzi wa menejimenti: THS-traditional healers. Ni makosa yamefanyika

Page 24: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-24-

28. Timu inaomba Ufafanuzi juu ya shughuli 3.3.2) Mikutano ya kila mwezi na CBHC kwa kiasi cha 3,600,000/-. Je, mikutano hiyo inashirikisha CBHC wa kata zipi?

Ufafanuzi wa menejimenti: CBHC wa halmashauri, na wanatoka katika kata zote za manispaa ya Ilala.

29. Kutokuwepo kwa umakini katika kuandaa ripoti

Ripoti zina makosa mengi, timu inashauri timu ya mipango kuongeza umakini wakati wa kuandaa na kupitia ripoti hizo kabla ya kuidhinishwa na kuanza utekelezaji. Mfano; uk 40, shughuli namba 4.1.1 kufanyia matengenezo na huduma mashine na magari 7 ya halmashauri kwa fedha za kapu la pamoja (4,749,995), fedha zilizorekodiwa kutumika ni 474,995 na mafanikio ya utendaji ni 100%. Timu inaamini tofauti ya fedha zilizorekodiwa ni makosa ya uandishi si vinginevyo.

Ufafanuzi wa menejimenti: Umakini umeongezeka. Timu ya Mipango hupitia kwa pamoja kabla ya kuikamilisha na kuiwasilisha katika baraza na mkoa.

30. Ripoti za utekelezaji hazina taarifa za kina juu ya nini kimefanyika. Mfano kuweka mazingira mazuri ya ofisi kwa wafanyakazi 20 wa idara ya afya (4.1.4). shughuli imefanyika lakini hawakusema ni mazingira gani yaliyoboreshwa.

Ufafanuzi wa menejimenti: Taarifa zinazotolewa katika ripoti ni za jumla, hii inasababishwa na miongozo inayotumika kuandaa taarifa hizi kwani taarifa za kina zinaingizwa katika ripoti za Kamati ya bunge ya usimamizi wa fedha za serikali za Mitaa- LAAC, hatahivyo timu itatoa ufafanuzi katika taarifa zinazokuja.

3.3 HOJA MAALUM KWA HOSPITALI YA WILAYA AMANA

1. Shughuli namba 3.2.4: Fedha za usafirishaji wa vifaa, vifaa tiba kwa gharama ya Tshs.6, 467,850/- (54%) ya fedha za uchangiaji. Fedha zilizotengwa ni 65,000,000/- kutoka mkurugenzi wa halmashauri, 12,000,000/- uchangiaji na 85,000,000/- kutoka vyanzo vingine. Je, dawa zinasafirishwa kwenda wapi?

Ufafanuzi wa menejimenti: Fedha hizo zilitengwa na kutumika kunua dawa, vifaa tiba na vitendanishi na kukodi magari ya kusafirishia kutoka bohari Kuu ya dawa ya Taifa -MSD hadi hospitali ya Amana na kituo cha Damu Salama kwa mwaka mzima.

2. Taarifa za fedha zilizobebwa kutoka muhula uliopita haziainishwa katika ripoti ya utekelezaji. Mfano shughuli 3.3.1 kufanya malipo kwa huduma za ufuaji; bajeti ya mwaka 99,200,000/-, zilizopatikana kwa muhula wa 2 ni 7,316,767/- na zilizotumika ni 42,533,100/-. Timu inataka ufafanuzi kuhusu matumizi ya fedha za ziada 42,533,100/- zimetoka wapi? - Hoja haikujibiwa

Page 25: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-25-

3. Shughuli namba 4.2.1: halmashauri ilipanga kutoa huduma za kiutawala kwa wafanyakazi 260.

Hoja: Je ni huduma gani zinafanyika? (Extra duty na house allowance) - Hoja haikujibiwa

FEDHA ZILIZOVUKA MWAKA (2010/2011)

4. Halmashauri ilipanga kufanya Ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwa jumla ya shilingi 32,039,559 za kapu la pamoja (basket fund). Shughuli hii ilionekana kutekelezwa muhula wa pili tu huku fedha zilizopangwa zikiwa ni 20,000,000/- na zilizotumika ni 12,039,559; wakati matumizi ya jumla yaliyorekodiwa katika ripoti ni 32,039,559/- bila kutoa maelezo juu ya jumla hiyo.

Hoja: Timu inaomba ufafanuzi juu ya matumizi hayo.

Ufafanuzi wa menejimenti: Kwenye mfumo wa zamani, bajeti za shughuli zinaingizwa tofauti na taarifa ya hali halisi ya utekelezaji na matumizi (actual/physical implementation na expenditure), hivyo ni rahisi makosa kutokea.

3.4 HOJA MAALUM KWA NGAZI YA VITUO VYA AFYA

5. Timu ya UUJ imebaini kuwa Shughuli zote za UKIMWI zilizopangwa katika ngazi hii ya huduma hazijatekelezwa.

Ufafanuzi wa menejimenti: Shughuli zote zinazotekelezwa na wadau haziingizwi katika ripoti za halmashauri hivyo hazionekani katika ripoti ya halmashauri.

6. Timu pia ilibaini kuwa malengo yaliyowekwa yanajirudia. Mfano shughuli 4.1.3 kutoa huduma za kiutawala na kiutumishi kwa wafanyakazi 260. Lengo hili linafanana na la Amana hospitali. Timu inataka ufafanuzi wa shughuli zinazofanyika, na je, vituo viwili vya afya vina watumishi 260?

Ufafanuzi wa menejimenti: Jumla ya Wafanyakazi wa vituo vya afya ni 150, idadi iliyotajwa ya wafanyakazi 260 ni kutoka ngazi ya hospital na zahanati hivyo kuna makosa ya kiuandishi yamefanyika.

7. Malipo ya posho kwa vibarua yalitolewa kwa muhula wa 2 kwa fedha za uchangiaji. Hakuna fedha za mkurugenzi na fedha za serikali kuu (Block grant. Je, kuna utaratibu gani wa fedha kutoka kwa mkurugenzi na fedha za serikali kuu? Timu inataka kufahamu juhudi zinazochukuliwa na halmashauri katika kuhakikisha fedha hizo zinatolewa kwa wakati.

Page 26: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-26-

Ufafanuzi wa menejimenti: Fedha za uchangiaji tu ndio zinatumika kulipia. Fedha za mkurugenzi naserikali kuu hawalipi tena vibarua

8. Katika bajeti zilizotolewa kwa Vituo vya afya, timu haikuweza kuona fedha zilizotolewa kwa ajili ya kamati za vituo, kuanda mipango kazi kwa mwaka unaofuata. Timu inataka kufahamu, je maandalizi ya mipango kazi ya vituo yanaanza lini (ratiba). Na je, shughuli hii inatekelezeka vipi bila kuwepo kwa pesa?

Ufafanuzi wa menejimenti: Bajeti ya kamati za vituo zilipangwa katika ngazi ya wilaya (ofisi ya mganga mkuu). Ila kwa sasa shughuli zote za jamii zinapangwa katika ngazi husika.

Maoni ya timu: Umakini katika kufuata miongozo na kanuni uongezwe.

3.5 HOJA MAALUM KWA NGAZI YA ZAHANATIKatika uchambuzi wa mipango na ripoti za utekelezaji ngazi ya zahanati, Timu ya UUJ imebaini kuwa:

9. Shughuli nyingi za uboreshaji wa huduma hazijafanyika; Shughuli zilizofanyika ni za utawala na ubimarishaji wa rasilimali watu.

10. Moja ya shughuli iliyotekelezwa ni kutoa samani na vifaa tiba katika zahanati 3 kwa gharama ya 1,980,000/-.

Hoja ya Timu: Je, samani hizo zilitolewa katika zahanati zipi?

Ufafanuzi wa menejimenti: Wodi ya Pugu, Guluka Kwalala na Kivule kwa gharama ya milioni 19. Miongoni mwa vifaa hivyo ni viti vya wagonjwa.

11. Utengenezaji wa kadi: Ripoti imeonesha kuwa halmashauri ilipanga kutengeneza kadi na kuonesha idadi kwa ngazi ya MMOH tu, hatahivyo ripoti hazikuonesha idadi ya kadi kwa ngazi ya zahanati. Ripoti zimeonesha kiasi cha shilingi 45,000,000/ kilitumika bila kuonesha kadi ngapi zimetengenezwa.

Hoja: timu inataka kujua kadi ngapi zimetengenezwa na zikagaiwa ngapi kwa kila zahanati.

Ufafanuzi wa menejimenti: Kadi zilizotengenezwa kwa milioni 4.5 na sio 45,000,000/- kama ilivyorekodiwa, pia kadi hizo zilisambazwa katika vituo vyote vya halmashauri.

Maoni: Umakini katika utayarishaji wa taarifa na umakini katika kutoa ufafanuzi bila viambatanisho vya kuhakiki.

Page 27: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-27-

3.6 HOJA MAALUM KWA NGAZI YA JAMII12. 7.1.1 Matengenezo na huduma za gari la maofisa afya kwa gharama ya

2,000,000/-

Ufafanuzi wa menejimenti: matengenezo hayo yalifanywa kwa gari la Maofisa afya wa Halmashauri ambalo hutumika kufanyia usimamizi katika kata na mitaa.

13. Mkutano wa mwaka na CHFM na CHMT 20, kwa gharama ya 6,800,000/-. Je, mkutano wa kina nani? Ulihusu nini?

Ufafanuzi wa menejimenti: Ni mkutano wa CHSB (bodi ya halmashauri na kamati za vituo vya huduma za afya) na CHMTs na sio CHFM.

3.7 UCHAMBUZI WA MPANGO WA UKIMWI WA HALMASHAURI 2011/12

UTANGULIZI

Timu ya UUJ ilifanikiwa kuchambua mpango na bajeti ya UKIMWI ya halmashauri kwa mwaka 2011/12 pamoja na ripoti zake za utekelezaji. Katika Uchambuzi huo timu hiyo ilibaini mambo mbalimbali yakiwemo Utofauti wa jumla ya fedha zilizorekodiwa katika mpango wa UKIMWI wa mwaka 2011/12. Katika mwaka huo wa fedha, halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilitegemea kupokea jumla ya shilingi 211,992,000 za kutekelezea shughuli za UKIMWI. Kiasi kilichopokelewa ni 137,760,847 (64.98%) na kilichotumika ni 130,299,875 (94.58%) ya kilichopatikana. Hata hivyo, baada ya kujumlisha fedha zote zilizopokelewa na kuainishwa katika maeneo makuu ya shughuli (Mazingira wezeshi Tshs 65,281,875/- Kinga Tshs 27,698,000/- na huduma, tiba na Misaada Tshs 19,040,972/-) timu imebaini kuwa kuna upungufu wa wa fedha zilizorekodiwa kupokelewa na kiasi halisi kilichopatikana (Tshs 112,020,847/- tofauti ya shilingi 25,740,000 kati ya 137,760,847/-).

Katika uchambuzi huo, Timu ya UUJ ilibainisha hoja zifuatazo ambazo kwa bahati mbaya haikufanikiwa kupata ufafanuzi wa menejimenti kwa wakati.

3.7.1 HOJA ZILIZOTOKA KATIKA MPANGO WA UKIMWI WA MWAKA 2011/121. Shughuli namba A01C01: Halmashauri ilipanga kutoa mafunzo kwa kamati 10

za UKIMWI za mitaa 10 ziweze kutambua wajibu wao na kutumia kiasi shilingi 18,250,000/- kwa siku 60. Hata hivyo mafunzo yalitolewa kwa kamati 10 kwa muda wa siku 10.

Hoja: Timu inataka ufafanuzi juu ya Kamati za Mitaa ipi zilipatiwa mafunzo? Na washiriki wangapi walipata mafunzo hayo?

2. Shughuli namba A01C03: Kutoa mafunzo elekezi kwa siku 3 kwa asasi 40 juu ya ukusanyaji wa takwimu kwa kutumia TOMSHA na kutumia 4,620,000/-.

Page 28: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-28-

Hoja: timu inataka kufahamu ni Asasi gani zilishiriki?

3. Shughuli namba A01C05: Kuwezesha kata 26 kutekeleza shughuli za UKIMWI kwa gharama ya 21,000,000/. Halmashauri ilipokea 26,000,000/- na kutumia fedha zote.

Hoja: Je, kila kata ilipata kiasi gani? Na shughuli gani zilitekelezwa?

4. Shughuli namba A04C01: kuwatambua na kutoa mafunzo ya siku 5 kwa waelimishaji rika 40 kutoka makundi mashoga, madada poa na wanaotumia dawa ili kutoa elimu juu ya ngono salama kwa gharama za 5,550,000/- na kutekelezwa.

Hoja: Waelimishaji rika walipatikanaje? Maeneo gani yalishiriki? Changamoto gani zilizopo katika utekelezaji wa shughuli hii?

5. Shughuli namba A03C01: kutoa huduma tembezi ya kupima, ushauri nasaha katika masoko 10 na maeneo hatarishi kwa gharama ya 11,860,000/-.

Hoja: Je, masoko gani yalifikiwa?

6. Shughuli namba A03C02: Kuwezesha jamii kushiriki katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI dunia kwa gharama 8,685,000/- hata hivyo Shughuli hii haiukuoneshwa katika ripoti ya utekelezaji,

Hoja ya Timu: timu inataka kufahamu kama shughuli hii haikufanyika?

7. Shughuli namba A04C01: Halmashauri ilipanga kutoa mafunzo ya siku 3 kwa watoa huduma ngazi ya jamii (CBHC) 40 juu ya ushiriki wa jamii na ukusanyaji wa takwimu 12,840,000/.

Hoja: Timu inataka kujua watoa huduma wa jamii walioshiriki ni wa kata gani?

8. Shughuli namba A07C01: halmashauri ilipanga kutoa vyakula lishe kwa WAVIU 200 kwa gharama 11,580,000/-.

Hoja: Je, vyakula vilitolewa katika kata gani?

9. Shughuli namba A05C01: kuhamasisha jamii kuhusu ukatili wa jinsia, elimu ya UKIMWI na unyanyapaa kwa kutumia gari ya sinema katika kata 26, kwa gharama ya 10,288,000/- na kutumika zote.

Hoja: Je, kata zipi zilifikiwa? Je, ni maeneo/kata zipi zimeathirika zaidi na tatizo hili? Aidha, ni kipaumbele katika kata zote?

Page 29: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-29-

3.7.2 SHUGHULI AMBAZO HAZIKUFANYIKA NA HAZIKURIPOTIWA KATIKA TAARIFA ZA UTEKELEZAJI

Katika uchambuzi wa mpango na ripoti za utekelezaji wa shughuli za kudhibiti UKIMWI, timu imebaini kuwa kuna shughuli zimeoneshwa katika mpango lakini hazikuripotiwa katika ripoti za utekelezaji bila ufafanuzi wowote. Shughuli hizo ni pamoja na:

10. Shughuli namba A06C01: kutambua vikundi vya WAVIU 100 na watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi 100 ili wasaidiwe, kwa gharama ya 1,360,000/- ila shughuli hii haikuoneshwa katika ripoti za utekelezaji.

11. Shughuli namba A06C01: kutoa vifaa vya shule kwa wanafunzi 100 wenye mahitaji katika kata 26 kwa gharama za 15,600,000/-.

12. Shughuli namba A06C01: Kuwezesha vikundi 5 vya wajane, watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na WAVIU katika kata 26 kwa gharama ya 22,500,000/-. Shughuli hii haikuoneshwa katika ripoti ya utekelezaji.

Hoja ya Timu: timu ilitaka kujua, Je shughuli hizi hazikutekelezwa, aidha kwanini halmashauri haikutoa maelezo yoyote?

3.7.3 SHUGHULI ZILIZOTEKELEZWA LAKINI HAZIPO KATIKA MPANGO KAZI

Timu ya UUJ pia imebaini kuwa kuna baadhi ya shughuli hazikuwepo katika Mpangokazi wa mwaka 2011/12 lakini zilitekelezwa na halmashauri. Shughuli hizo ni pamoja na

13. Shughuli namba A07C05: ununuzi wa seti ya kompyuta (laptop) na vifaa vyake kwa gharama ya 5,245,380/- ambayo iliagizwa katika mwaka wa fedha 2009

3.7.4. MAMBO MAKUU YALIYOBAINIKA NA TIMU YA UUJ

14. Timu imebaini kuwa shughuli zilizowekwa katika mipango ya UKIMWI kwa mwaka 2011/12 sio matatizo halisi yalipo ndani ya jamii.

15. Pia Taarifa za utekelezaji hazina mchanganuo wa kina; mfano hazioneshi shughuli imefanyika lini, wapi na muhusika katika kutekeleza shughuli hiyo.

16. Muuondo wa uaandaaji wa shughuli haueleweki. Hakuna uhalisia wa muda wa kumalizika utekelezaji wa shughuli. Mfano shughuli namba A01C01; muda wa utekelezaji wa shughuli hii ni siku 60. Lakini katika ripoti ya utekelezaji, shughuli hiyo imeripotiwa kutekelezwa kwa siku 3 tu? Kutokuwepo kwa uhalisia wa muda wa utekelezaji wa shughuli kunasababisha maswali mengi kwa anayesoma

ripoti (Timu ya UUJ)

Page 30: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-30-

SEHEMU YA NNE

4. KUTEMBELEA VITUO VYA HUDUMAKutembelea vituo vya huduma, ni hatua mojawapo katika utekelezaji wa zoezi la UUJ. Dhumuni la zoei hili ni kuhakiki hoja zilizotokana na Uchambuzi wa taarifa/nyaraka za halmashauri, vilevile kutoa nafasi kwa timu kutathmini hali halisi ya utoaji wa huduma katia vituo vya umma.

Timu ya UUJ ilifanikiwa kutembelea jumla ya vituo vya huduma za afya 22 ambavyo ni Vituo Hospitali ya Amana, Vituo vya afya (3) ambavyo ni Mnazi Mmoja, Pugu na Buguruni; Zahanati (18) zikiwemo Tabata A, Tabata NBC, Segerea, Kinyerezi, Bonyokwa, Mongolandege, Gongo la Mboto, Guluka kwalala, Vingunguti, Gerezani, Zingiziwa, Msongola, Kivule, Kiwalani, Mvuti, Chanika, Buyuni na Majohe. Timu vilevile ilitembelea Ofisi za kata za Tabata A, Segerea, Ukonga, Buguruni na Kivule.

Katika ziara hiyo, timu ilijifunza mambo mbalimbali yakiwemo mafanikio na changamoto zilizopo katika utoaji huduma ndani ya halmashauri.

4.1 MAFANIKIO YA HALMASHAURI:i. Uwepo wa hali nzuri ya mazingira vituoniTimu inaipongeza halmashauri kwa kuboresha mazingira ya vituuo vya kutolea huduma za afya kwani hali hii huongeza ari na bidii ya kazi kwa wafanyakazi hivyo kuwavutia kubakia vituoni. Miongoni mwa mazingira hayo ni majengo ya kutosha na imara, vifaa kama vile mabenchi/viti vya wagonjwa, baiskeli za wagonjwa. na uwepo wa miundombinu ya kutupia taka yakiwemo mapipa ya taka. Mfano wa vituo hivyo ni zahanati za Mongolandege, Mvuti na Tabata Segerea.

Pichani ni eneo la mapokezi katika zahanati ya Mongolandege

Page 31: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-31-

ii. Uwepo wa chumba maalum kwa ajili ya matibabu ya wazee

Serikali kupitia sera ya afya (2007) imejidhatiti kuboresha huduma za afya kwa makundi maalum yakiwemo wazee, wajawazito na watoto chini ya miaka mitano. Hatahivyo, kumekuwa na malalamiko mengi juu upatikanaji wa huduma hususan kwa wazee yakiwemo kutokuwepo kwa taratibu rasmi za matibabu na gharama kubwa wanazoshindwa kumudu. Hali hii ni tofauti katika zahanati ya Gulukakwalala kwani wazee wote wanaokidhi vigezo vilivyoainishwa katika sera ya afya wanapata matibabu katika chumba maalum kwa utaratibu maalum.

iii. Uwepo wa vichomeo taka

Ingawa baadhi ya vituo havina taka, timu imekuta vichomeo taka vya kutosha katika zahanati ya Vingunguti.

iv. Uhusiano mzuri baina ya kituo, kamati ya usimamizi na ofisi ya kata na Mitaa

Timu inapongeza baadhi ya vituo vyenye uhusiano mzuri kati ya kamati ya usimamizi wa kituo (HFGC) na timu ya uendeshaji ya kituo (wataalam) mfano zahanati ya Kitunda, vilevile ushirikiano mzuri na serikali za mtaa katika shughuli za maendeleo ya zahanati mfano Zingiziwa. Tunaamini kuwa ushrikiano baina ya taasisi hizi ni muhimu katika kuboresha huduma kwa wananchi kwani kimsingi, jukumu kubwa la wote ni kuhakikisha ustawi wa jamii.

v. Utunzaji mzuri wa kumbukumbu za kituo

Timu pia imeridhishwa na uhifadhi mzuri wa kumbukumbu za vituo katika baadhi ya vituo hali inayorahisisha wananchi ama vyombo vya wasimamizi kupata taarifa zote muhimu za kituo zikiwemo mafunzo, taarifa za fedha, dawa na vifaa tiba viliivyopokelewa na kutumika, wagonjwa wanaotibiwa kituoni. Utunzaji mzuri wa kumbukumbu pia unakuza uwazi , uwajibikaji na utawala bora. Vituo hivyo ni pamoja na zahanati ya Zingiziwa, hospitali ya Amana na kituo cha afya cha Mnazi mmoja na Buguruni.

Aidha, timu inaupongeza uongozi wa hospitali ya Amana na vituo vya afya vya Mnazi mmoja na Buguruni kwa kuwa na utaratibu mzuri wa kurekodi maoni na malalamiko ya wateja juu ya huduma zinazotolewa kvituoni hapo. Miongoni mwa masuala yaliyokuwa yakitathminiwa na timu ni uwepo na ufanyaji kazi wa njia za kutolea malalamiko kwa watumia huduma hususan sanduku na/ama chumba maalum cha maoni. Timu pia iliulizia matumizi ya njia hizo na utaratibu unaofuatwa katika kuyakusanya maoni hayo kama vile nani anahusika kufungua masanduku ya maoni, kwa kipindi gani yanafunguliwa, yanarekodiwa wapi pamoja na chombo kinachohusika kutoa maamuzi juu ya hatua za kuchukuliwa kulingana na maoni/malalamiko ya wananchi yaliyokusanywa. Hivyo, katika vituo hivyo, masanduku ya

Page 32: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-32-

maoni hufunguliwa na mkuu wa kituo/katibu pamoja na wajumbe wawili wa kamati akiwemo mwenyekiti. Maoni yote hurekodiwa katika vitabu maalum na kujadiliwa katika vikao vya kamati zikiwemo kutoa mapenndekezo juu ya hatua za kinidhamu dhidi ya mlalamikiwa. Kuwepo vitabu maalum vya kurekodia maoni na hatua za kinidhamu zinazochukuliwa ni njia mojawapo ya kukuza uwajibikaji kwa watoa huduma na uboreshaji wa huduma kwa wananchi.

vi. Uwepo wa ubao wa matangazo

Upashanaji wa taarifa ni changamoto kubwa katika vituo vingi. Lakini, baadhi ya vituo vimekutwa na mbao za matangazo zilizo na taarifa za mapato na matumizi zinazoeleweka , mfano zahanati ya Zingiziwa, Mvuti. Katika zahanati ya Buyuni, timu ilikuta taairifa muhtasari wa kikako cha kamati ya usimamizi wa kituo cha robo mwaka. Timu inapongeza uongozi wa vituo hivyo kwa kuimarisha uwazi na kutoa taarifa hizo muhimu kwa wananchi. Pichani chini ni taarifa za fedha zilizobandikwa katika mbao za matangazo katika zahanati za Mvuti (kushoto) na Kulia ni muhutasari wa kikao cha kamati katika zahanati ya Buyuni.

Page 33: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-33-

4.2 CHANGAMOTO KATIKA UTOAJI WA HUDUMA MANISPAA YA ILALAMbali na Mafanikio tuliyoyaona katika vituo, timu imebaini changamoto nyingi zinazoikabili utoaji wa huduma za afya katika vituo viilivyotembelewa zikiwemo:

i. Kutokuwepo na mafunzo ya utunzaji bora wa kumbukumbu

Hakuna mfumo bora wa utunzaji wa taarifa za kituo hususan rasilimali watu hivyo taarifa nyingine zilikuwa ni za kubuni tu, hii ilioenakana katika vituo 19 isipokuwa vitatu vilivyotajwa kwenye mafanikio.

ii. Kutokuwepo ama ucheleweshwaji wa stahiki za wafanyakazi

Watoa huduma wamelalamikia ucheleweshwaji mkubwa wa stahiki zao zikiwemo posho za masaa ya ziada, likizo na mazingira magumu. Hii ni Changamoto kubwa inayochochea baadhi ya watumishi kutokuzingatia maadili yao ya kazi na wengine kuondoka. Tatizo hili limetajwa kama tatizo sugu katika zahanati zote zilizotembelewa.

iii. Rasilimali watu

Upungufu wa rasilimali watu ni moja ya changamoto kubwa inayoikabili sekta ya afya ikiwemo Manispaa ya Ilala.

iv. Uchakavu wa Miundombinu na majengo

Timu imeshuhudia uchakavu mkubwa wa majengo katika baadhi ya zahanati ikiwemo Bonyokwa na baadhi ya majengo Gulukakwalala. Cha kushangaza zaidi ni kuwa zahanati hizo bado mpya yaani zimejengwa kipindi kifupi kwani uchakavu huo hauendani na muda wa kituo. Kwa timu, hii inamaanisha kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa vituo hivyo kujengwa chini ya viwango vinavyotakiwa.

Page 34: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-34-

Pichani ni sehemu ya paa la jengo la zahanati ya Bonyokwa. Zahanati hii ilifunguliwa mwaka 2009 lakini haikujengwa kwa ubora unaokidhi mazingira kwani dari limeliwa na mchwa, kuna nyufa kwenye kuta na vitasa vya milango vimeharibika.

v. Ukosefu wa uzio katika vituo

Ukosefu wa uzio katika vituo ni suala lilionekana kutopewa kipaumbele na halmashauri. Timu ilishuhudia vituo vingi vikiwa vimejengwa katikati ya makazi ya watu huku vikiwa havina uzio hali inayosababisha muingiliano mkubwa wa shughuli za kijamii na utoaji wa huduma. Vituo hivyo ni pamoja na zahanati za Mojohe, Msongola, Zingiziwa, Bonyokwa, Mongolandege na Gulukakwalala,

Athari zilizotajwa kusababishwa na vituo kukosa uzio ni pamoja na wananchi kuvamia eneo la kituo na kuzuka kwa migogoro ya ardhi baina ya kituo na wananchi hali inayohatarisha usalama wa watumishi na mara nyingine kuwalazimu watumishi kuacha kuishi kwenye nyumba za kituo kwa kuhofia usalama wao mfano zahanati ya Msongola

vi. Ufinyu wa nafasi ya kutolea huduma katika vituo

Kituo cha afya Buguruni ni moja kati ya vituo vinavyohudumia wakazi wengi wa ndani na nje ya manispaa ya Ilala. Hata hivyo, kituo hiki kinakabiliwa na changamoto kubwa ya ufinyu wa nafasi kwani kipo katikati ya makazi ya watu.

Kutokuwepo kwa vyumba vya matibabu vya kutosha huathiri ubora wa huduma ikiwemo misongamano ya wagonjwa na mara nyingine baadhi ya huduma kutolewa sehemu zizizo rasmi. Mfano, katika zahanati ya Kitunda, wataalam hutumia jengo la Kifua kikuu ambalo halijakamilika kama chumba cha mapumziko kwa wagonjwa. Vituo vingine vyenye ufinyu wa nafasi ni pamoja na zahanati ya Gerezani.

Timu ya UUJ pia ilibaini kuwa na changamoto ya viwango vya ramani na ujenzi wavituo vya kutolea huduma, kwani wakati majengo mengine yalikuwa yamejengwa vizuri na nafasi ya kutosha katika vyumba vya kutolea huduma, kuna baadhi ya majengo yalikuwa na ufinyu mkubwa wa nafasi kiasi kwamba msongamano wa wagonjwa na usiri katika kutoa huduma unakuwa mdogo. Ufinyu huu ulionekana katika zahanati ya Chanika ambako wodi ya mapumziko imekuwa ni sehemu ya kujifungulia (labor ward) kutokana na uwingi wa wajawazito (wajawazito 150 kwa mwezi wakati vitanda vilivyopo ni 8 tu ; vya kupumzika 6 na 2 vya kuzalia).

Ufinyu wa vyumba vya kutolea tiba hususan TB hali inayowalazimu huduma hiyo kutolewa nje kwa kuhofia usalama wa afya za watoa huduma, mfano zahanati ya Kiwalani.

Page 35: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-35-

vii. Uchakavu wa Mabango ya Vituo

Miundombinu mingine ni kama uwepo wa mabango yanayoelekeza uwepo wa kituo. Timu ya UUJ ilikuta mabango mawili katika kituo cha Pugu; moja linasema zahanati linguine kitua cha afya, Bango limechakaa sana huko zingiziwa kama inavyoonekana pichani, bango halikuwekwa sehemu ya wazi katika Zahanati ya Vingunguti na kutokuwepo kabisa kwa mabango katika Zahanati ya Bonyokwa.

Pichani: Bango la zahanati ya Zingiziwa

viii. Maji na Umeme

Maji na Umeme ni nishati muhimu katika suala zima la utoaji huduma “bora za afya na inayokidhi mahitaji ya watumiaji”. Kutokupatikana kwa huduma za uhakika za maji na umeme ni kikwazo kikubwa kinachokabili baadhi ya vituo vya huduma wilayani Ilala vikiwemo Zahanati za Kinyerezi na Bonyokwa. Ili kuwezesha utoaji wa huduma, vituo hulazimika kununua maboza, ya maji hali ambayo inayoongeza gharama kubwa za matumizi ya fedha ukiachilia mbali usalama wa maji hayo. Zahanati ya kiwalani inatumia maji ya kisima na hayana mfumo mzuri wa kuyatumia, yanachotwa na ndoo. Kisima cha zahanati ya Mvuti hakijawahi kuwekewa pump hata hivyo zhahanati hiyo huvuna maji ya mvua ambayo hayatoshelezi.

Page 36: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-36-

Kwa upande wa umeme, Zahanati ya Bonyokwa haikukutwa na nishati yoyote ya umeme kama ilivyoonekana kwenye hoja hapo nyuma. Umeme unakatika mara kwa mara katika zahananti ya Kiwalani hivyo wameomba kubadilishiwa line.

ix. Uhaba wa vichomeo taka

Ili kutunza mazingira ya vituo na kuepusha ueneaji wa magonjwa, ni budi kwa kila kituo kuwa na kichomeo taka imara. Hata hivyo, timu imebaini tatizo la Uhaba wa cvichomeo taka katika vituo ilivyotembelewa vikiwemo zahanati za Bonyokwa, Gongo la Mboto, Kiwalani na Gulukakwalala. Pia katika zahanati ya kinyerezi, kichomeo taka kimejengwa karibu mno na majengo ya kutolea huduma hali ambayo inaweza kuleta madhara kwa binadamu kwani moshi wa taka unarudi ndani ya vyumba vya kutolea huduma wakati wa kuzichoma kama inavyoonekana pichani.

i. Ucheleweshwaji wa Dawa na vifaa tiba.

Ucheleweshwaji wa madawa kutoka MSD ilionekana kuwa changamoto kubwa kwa vituo vyote, iliripotiwa katika kituo cha afya cha Pugu kuwa dawa kutoka MSD zinaweza kuchukua hadi miezi sita tangu zinapoagizwa. Pia upatikanaji wa dawa kwa kundi la msamaha uliripotiwa kuwa ni changamoto hasa katika zahanati ya Tabata A, Msongola na kituo cha afya cha mnazi mmoja kwani kundi hilo ni kubwa kuliko uwezo wa kituo kukidhi mahitaji yao.

Pamoja na ucheleweshwaji wa madawa, kulikuwa na changamoto ya uhifadhi mzuri wa dawa kama vile Bonyokwa ambapo timu ilikuta stoo ya madawa haina mashelfu hivyo dawa zinahifadhiwa katika mazingira magumu (ndani ya maboksi) na hivyo

Page 37: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-37-

kupunguza ufanisi wa utunzaji bora wa dawa. Kituo pia hakina maabara ila kimetenga meza kwa ajili ya kufanya vipimo vya malaria kama inavyoonekana kwenye picha.

Chumba cha kuhifadhia madawa (kushoto) na maabara (kulia) katika zahanati ya Bonyokwa.

Ngazi ya kata

• Hakuna ushirikiano wa dhahiri kati ya kata na vituo, hii ilionekana katika

• Kamati za ukimwi haziwezi kutekeleza majukumu yake kutokana na upungufu wa rasilimali fedha.

• Hakuna kumbukumbu ya taarifa

• Kamati za UKIMWI za kata hazina uhuru wa kufanya kazi kufuatana na vipaumbele vyao.

• Mipango ya UKIMWI huwa haiandaliwi katika ngazi ya kata kutokana na kutopatikana kwa pesa.

Page 38: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-38-

SEHEMU YA TANO

5.1 MKUTANO MKUU WA MREJESHO KWA WADAUBaada ya kukamilisha hatua ya mafunzo, Uchambuzi wa nyaraka na hatimaye kutembelea vituo kwa ajili ya kuhakiki wa taarifa, timu iliandaa rasimu ya ripoti ya zoezi zima la UUJ iliyowasilishwa kwa wadau wa afya na UKIMWI wa wilaya ya Ilala katika Mkutano uliofanyika tarehe 12/02/2014.

Mkutano huo ulifunguliwa na Mwenyekiti wa Kamati za Huduma za jamii Mh. Angelina Malembeka ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Kaimu Mkurugenzi Bi Nuru W. Kindamba, Kaimu Mganga mkuu wa Manispaa Dr Willy Sangu. Wadau wengine waliohudhuria ni wenyeviti wa kamati za vituo vya huduma, watendaji wa kata zote za manispaa ya Ilala, waheshimiwa madiwani, wawakilishi wa ofisi ya mkurugenzi na wawakilishi wa ofisi ya Mganga Mkuu wa halmashauri.

Lengo la mkutano huu ni kutoa mrejesho juu ya zoezi zima la UUJ lilivyofanyika zikiwemo mafunzo, Uchambuzi wa nyaraka na hali halisi ya vituo vilivyotembelewa. Kupitia mkutano huu timu pia iliwasilisha changamoto walizokabiliana nazo wakati wa utekelezaji wa zoezi na walichojifunza, na mapendekezo ya timu.

Baada ya ufunguzi, wawakilishi wa timu ya UUJ waliwasilisha hoja zote zilizoibuliwa na timu pamoja na ufafanuzi uliotolewa na menejimenti ya afya na kasha kutoa nafasi ya majadiliano kwa wadau wote waliohudhuria mkutano huo.

5.2 MAJIBU YA HALMASHAURI JUU YA HOJA ZA TIMU YA UUJ ZILIZOFANYIWA DESEMBA 2013Kama sehemu ya majadiliano, mwakilishi wa ofisi yam ganga mkuu alieleza jitihada zilizochukuliwa na Halmashauri kufanyia kazi baadhi ya hoja zilizoibuliwa na timu ya UUJ ambazo zimeshafanyiwa kazi na idara ya afya. Miongoni mwa masuala hayo ni:

A. Ushirikiano wa uongozi wa kituo na Kamati kwenda kwenye Baraza la maendeleo ya kata ni mdogo.

Mapendekezo ya timu: DMO awashirikishe wasimamizi wa kituo na kuwaelekeza kupeleka vipaumbele vyake na kuboresha ushirikiano na Ofisi ya Kata.

Page 39: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-39-

Hatua zizochukuliwa na MMOH:

1. Baada ya mkutano wa mrejesho na CHMTs, ofisi ya mganga mkuu waliandaa mkutano wa muhula na wakuu wa vituo na kujadiliana juu ya changamoto zilizoainishwa na timu ya UUJ. Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni:

• Wakuu wa vituo vya huduma wawe wanahudhuria mikutano ya baraza la maendeleo ya kata na kuwasilisha masuala yote ya vituo hususan changamoto ili zijadiliwe na kuwekewa mikakati ya pamoja, wakati wa supervision, CHMT walikuta wakuu wa vituo vya mfano Msongola, mvuti na mivuleni wamehudhuria mikutano ya baraza la maendeleo ya kata.

• Utunzaji wa taarifa vituoni

• Pia wamewapa rai wakuu kuandaa taarifa za kila robo mwaka kwa usahihi na zipitiwe na kusainiwa kabla ya kuwasilisha MMOH. (kuhuisha leja ya dawa, kuandika na kuyadili malalamiko ya wateja katika kamati. Masanduku ya maoni ni lazima yatengenezwe na kutumika.

2. Kutokuwepo kwa huduma za kuzalisha akina mama wajawazito katika zahanati ya Gerezani

Hatua zizochukuliwa na MMOH:

Halmashauri ilifuatilia na kuona umuhimu wa kutolewa huduma hizo, ila kwa sasa ofisi ya Mganga Mkuu imeshapeleka kitanda cha kujifungulia akina mama wajawazito na huduma zimeanza kutolewa

Mapendekezo ya Wadau

1. Timu/sikika ishiriki katika kipindi cha maandalizi ya mipango ili kuweza kufahamu halmashauri imepanga nini na baadaye waweze kusimamia.

2. Timu ijifunze namna halmashauri inavyofanya kazi ili kuimarisha kazi zake

Page 40: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-40-

SEHEMU YA SITA

6.1 HITIMISHOKazi ya ufuatiliaji wa uwajibikaji Jamii iliyotekelezwa na Timu ya UUJ imeibua hoja mbalimbali ambazo tunaamini ni chachu ya mabadiliko kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala hususan idara ya afya. Timu inaamini kuwa, mchakato huu wa ufuatiliaji uwajibikaji wa jamii una manufaa makubwa kwa jamii na halmashauri kwa ujumla, kwani pamoja na kutoa mafunzo maalumu na kuwajengea uwezo wananchi wa kudai ufafanuzi, uthibitisho na uhalalisho juu ya maamuzi ya watoa huduma, bado mchakato huu umeweza kubainisha changamoto zinazoikabili halmashauri, kitu ambacho ni msaada mkubwa katika kuleta mabadiliko hususan kwenye idara ya afya na utoaji wa huduma za afya kwa ujumla.

Ni imani kubwa ya timu kuwa, ili halmashauri iweze kuwajibika ipasavyo kwa jamii, ni muhimu kwa zoezi hili kufanyika kwa idara zote mara kwa mara. Hivyo basi, kwa imani hiyo, timu inashauri halmashauri kushirikiana na Sikika na wadau wengine kuiwezesha timu iwe endelevu na iweze kufuatilia uwijibikaji kwa jamii katika idara nyingine zote za halmashari lengo likiwa moja tu, kufikia haki za binadamu na kukidhi mahitaji ya jamii.

Katika utekelezaji wa kazi hii, timu ilikutana na changamoto mbalimbali. Changamoto kuu ni upatikanaji wa baadhi ya nyaraka kwa ajili ya zoezi la UUJ, Kushindwa kuhudhuria mafunzo na uchambuzi wa nyaraka kwa baadhi ya wawakilishi.

6.2 MAPENDEKEZOKwa kutambua umuhimu wa zoezi la UUj katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya ndani ya halmashauri ya Manisaa ya Ilala, Timu ya UUJ inashauri yafuatayo:

1. Kuwepo na ushirikiano katika upatikanaji wa nyaraka mapema ili kufanikisha zoezi.

2. Timu inashauri halmashauri izingatie uhalisia wa upatikanaji wa bajeti katika vyanzo vyake ili kupunguza utofauti mkubwa wa bajeti inayopangwa na fedha zinazopatikana hivyo kuathiri utekelezaji wa shughuli zinazopangwa. Hii itasaidia kuwa na uhalisia wa bajeti na kuongeza uwezekano wa kutekeleza shughuli zitakazopangwa kwa asilimia kubwa.

3. Mbali na masanduku ya maoni, kuwe na mfumo wa kutoa maoni kuendana na mazingira halisi tuliyonayo,

Page 41: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-41-

4. Watu wa kata/mtendaji na wengine ambao sio watendaji wa kwenye kituo wahusishwe wakati wa kufungua masanduku ya maoni kwani malalamiko mengine hayatapewa uzito.

5. Kuwe na madodoso kwenye vyumba vya malalamiko.

6. Kamati za afya za vituo zinahitaji kuwezeshwa kuhusu wajibu wao maana kumeonekana na utofauti kati ya kamati moja na nyingine. Mfano, suala la kumchagua mwenyekiti wa kamati ni jukumu la wanakamati lakini kuna maeneo mengine (Kivule) imeonekana kuwa jukumu hilo ni la watu wachache.

7. Motisha kwa watumishi hasa kwa upande wa kupatiwa nyumba, serikali/manispaa itengeneze mfumo wa kuwawezesha kada zote kuweza kuwapa motisha.(eligible &entitled)kwani kuna kada nyingine hazitakaa zifikie kwenye ngazi ya TGSG.

8. Kitengo cha mipango miji na ardhi wahakikishe kuwa mipaka ya vituo vya kutolea huduma inalindwa, na kwa vile ambavyo havijapimwa wahakikishe kuwezeshwa kwa zoezi hilo. i.e haivamiwi.

9. Wafadhili wanaojitolea kuongeza majengo katika vituo vya kutolea huduma wapewe masharti, (Kwa mfano, kujenga foundation itakayoruhusu jengo kwenda juu /kuwa ghorofa. Hii itasaidia kuepusha ufinyu wa nafasi ulioonekana katika baadhi ya vituo vilivyotembelewa).

10. Bodi ya afya ya wilaya iwe inatembelea vituo sio tu kwa kuvitambua ila kwa kuangalia hali ya utekelezaji wa huduma kwa ujumla.

11. Kuhusishwa kwa bodi ya afya ya halmashauri katika kamati ya huduma za jamii za madiwani kutiliwe mkazo.

12. Kamati za UKIMWI za kata ziwashirikishe waganga wafawidhi ili kuboresha utoaji huduma kwa jamii., kwa mfano Mvuti kuna unyanyapaa mkubwa hvyo elimu inahitajika.

Page 42: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri
Page 43: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri
Page 44: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Ilala SAM Report.pdf · MMAM Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ... – (28) za Katiba ya Jamhuri

Ripoti ya SAM Ilala

-44-

Sikika inafanya kazi kuhakikisha usawa katika

upatikanaji wa huduma bora za afya, kwa kutathimini

mifumo ya uwajibikaji katika ngazi zote za serikali.

Nyumba Na.69Ada Estate, KinondoniBarabara ya TunisiaMtaa wa WaverleyS.L.P 12183Dar es Salaam, Tanzania.

Nyumba Na. 340Mtaa wa KilimaniS.L.P 1970Dodoma, Tanzania.Simu: 0262321307Faksi: 0262321316

Simu: +255 22 26 663 55/57 Ujumbe mfupi: 0688 493 882Faksi: +255 22 26 680 15Barua pepe: [email protected]: www.sikika.or.tzBlog: www.sikika-tz.blogspot.comTwitter: @sikika1Facebook: Sikika Tanzania