53
#IlalaTupoVizuri MIAKA MITANO YA MAFANIKIO YA AWAMU YA TANO. HOSPITALI YA WILAYA KIVULE AUTI YA ILALA ISSN 0856-9711 TOLEO NA.12 JULAI 2020 S JARIDA LA AFYA: SHUGHULI ZA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA ELIMU SEKONDARI UFAULU UMEONGEZEKA KWA KASI KUBWA LENGO LA KUTOKOMEZA UMASKINI IFIKAPO 2030 ELIMU YA MSINGI: ONGEZEKO LA UFAULU KWA DARASA LA SABA

S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

  • Upload
    others

  • View
    6

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

1# I l a l a Tu p o V i z u r i

MIAKA MITANO YA MAFANIKIO YA AWAMU YA TANO.

H O S P I TA L I YA W I L AYA K I V U L E

AUTI YA ILALAISSN 0856-9711 TOLEO NA.12 JULAI 2020

SJARIDA LA

AFYA:SHUGHULI ZA UTOAJIWA HUDUMA ZA AFYA

ELIMU SEKONDARIUFAULU UMEONGEZEKAKWA KASI KUBWA

LENGO LA KUTOKOMEZAUMASKINI IFIKAPO 2030

ELIMU YA MSINGI:ONGEZEKO LA UFAULUKWA DARASA LA SABA

Page 2: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

2

HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA

KITENGO CHA HABARI, UHUSIANONA MAWASILIANO

Sauti ya Ilala

Kwa Mawasiliano;

Tangaza nasi kupitia;

Wote Mnakaribishwa+255 713 493 797 / +255 715 428 855

Ilala_Manispaa

Sau t i y a I l a l a

1# I l a l a Tu p o V i z u r i

MIAKA MITANO YA MAFANIKIO YA AWAMU YA TANO.

H O S P I TA L I YA W I L AYA K I V U L E

AUTI YA ILALAISSN 0856-9711 TOLEO NA.12 JULAI 2020

SJARIDA LA

AFYA:SHUGHULI ZA UTOAJIWA HUDUMA ZA AFYA

ELIMU SEKONDARIUFAULU UMEONGEZEKAKWA KASI KUBWA

LENGO LA KUTOKOMEZAUMASKINI IFIKAPO 2030

ELIMU YA MSINGI:ONGEZEKO LA UFAULUKWA DARASA LA SABA

Page 3: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

3

Sau t i y a I l a l a

1# I l a l a Tu p o V i z u r i

MIAKA MITANO YA MAFANIKIO YA AWAMU YA TANO.

H O S P I TA L I YA W I L AYA K I V U L E

AUTI YA ILALAISSN 0856-9711 TOLEO NA.12 JULAI 2020

SJARIDA LA

AFYA:SHUGHULI ZA UTOAJIWA HUDUMA ZA AFYA

ELIMU SEKONDARIUFAULU UMEONGEZEKAKWA KASI KUBWA

LENGO LA KUTOKOMEZAUMASKINI IFIKAPO 2030

ELIMU YA MSINGI:ONGEZEKO LA UFAULUKWA DARASA LA SABA

SAUTI YA ILALABODI YA WAHARIRI

MWENYEKITI

MSANIFU WA JARIDAFEROOZ KILLAH

MCHAPISHAJI

BI. TABU SHAIBU

JARIDA LA

Mhariri

Jarida hili hutolewa na:Kitengo cha Habari, Uhusiano

na MawasilianoS.L.P 20950, DAR ES SALAAM, TANZANIA

OFISI YA MKURUGENZI1 MTAA WA MISSION

SIMU: 2128800 2128805

WEBSITE: www.ilalamc.go.tzEMAIL: [email protected]

WAJUMBENEEMA NJAU - Mhariri MsaidiziHASHIM JUMBE - Mwandishi

RODNEY MALONGO - Mwandishi

Uongozi na Diraya Maendeleo

UK - 07

Ilala kinara wa ukusanyaji wa Mapato Tanzania

UK - 12

Manispaa ya Ilala na Sera ya Hapa Kazi Tu.

UK - 13

Zifahamu Kata 36 zaManispaa ya Ilala

UK - 16

Uboreshwaji wa Huduma za AfyaUK - 31

Ongezeko la Samani na Miundombinu

UK - 40

Kwa kipindi cha Miaka Mitano 2015 - 2020

UK - 45

UK - 51 UK - 52

Hongera Mkurugenzi na Wako wasaidizi

UK - 43

Lengo la kutokomeza umaskini 2030

UK - 47

Ongezeko la Ufaulu ndani ya Manispaa

UK - 44

Shukrani kwa Mkurugenzi kutupeleka Mafunzoni

UK - 50

UK - 35

01.UTAWALA 02.MAPATO 03.SERA

04.KATA 05.AFYA

07.ELIMU MSINGI

10.MAFANIKIO

13.BARAZA LA MADIWANI 14.DMDP

08.SHAIRI

11.MALENGO

09.ELIMU SEKONDARI

12.ULINZI NA USALAMA

06.HABARI PICHA

Yaliyomo:

KIUTA

Page 4: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

4

Katika hatua za ukuaji wa viumbe hai kunahusisha mabadiliko ndani yake ambayo huwa na mahitaji zaidi na ya kimsingi ili kuweza kukabiliana na mabadiliko hayo. Mageuzi, mabadiliko ya kiuchumi pamoja na maboresho mbalimbali katika utoaji wa huduma za kijamii ndani ya Taifa la Tanzania katika kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia 2015 hadi 2020 chini ya uongozi wa Rais John Pombe Maghufuli yanatokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa kwa kila ngazi ya kiutawala.

Katika ngazi ya serikali za Mitaa utekelezaji wa moja kwa moja umefanyika kwakuwa zimesimamia na kutekeleza maagizo mbalimbali ya Serikali. Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imetekeleza maelekezo na maagizo ya Serikali ya awamu ya tano (5) kwa kuandaa mipango na bajeti.

Utoaji wa huduma bora za kijami umechangia ongezeko la idadi ya watoto wanaopata elimu ya awali, msingi na sekondari kupitia sera ya elimu bila malipo iliyoenda sambasamba na ongezeko la miundombinu ya elimu. Tutakubaliana sote kuwa ile hoja ya kupata wataalam wa ndani elimu bure ndilo jibu lake. Ongezeko la vituo vya kutolea huduma za Afya kumepunguza idadi ya vifo vya mama wajawazito na watoto kutoka 93 mwaka 2015 na kufikia kina mama 21 mwaka 2020 sawa na asilimia 44.

Eneo lingine muhimu lililochangia mafanikio ni mabadiliko katika eneo la usimamamizi wa Rasilimali watu. Watumishi wameweza kupata haki na stahiki zao ikiwemo kupandishwa vyeo/madaraja ambapo jumla ya watumishi 6722, wamepandishwa vyeo sambamba na marekebisho wa mishahara yao.

Ujenzi wa ofisi za Kata za Buyuni, Liwiti na Bonyokwa, pamoja na ofisi za Mitaa za Nyebulu na Mzinga umelenga kusogeza huduma karibu na wananchi.Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa imetoa elimu na kuwajengea uwezo watumishi kuzingatia maadili ya kiutumishi na kupunguza malalamiko yaliyokuwa yamekithiri katika utoaji wa huduma.

Miundombinu ya barabara, madaraja, vivuko, utunzaji wa mazingira, mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, rushwa, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi pamoja na uwajibikaji wa viongozi kumerudisha imani ya wananchi kwa Serikali yao. Katika Manispaa ya Ilala kupitia mradi wa DMDP maisha ya watu yamebadilika ujenzi wa barabara za lami, uwekaji wa taa za barabarani, ujenzi wa masoko na mifereji wa mvua kumeongeza thamani ya maeneo hayo. Maeneo hayo ni pamoja na Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, na Gongo la Mboto. Mifumo ya kielektroniki katika kutekeleza majukumu ya utoaji wa huduma mbalimbali ikiwemo malipo ya kodi kumechangia katika udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato kwenye zahananti zote 27, Vituo vya afya vya. Mara baada ya kuanza kutumika Kwa mfumo wa GoTHOMIS kiasi kilichokusanywa katika maeneo ya kutolea huduma za afya kimeongezeka.

TAHARIRI

Page 5: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

5

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa wilaya ya Ilala Mheshimiwa Ng’wilabuzu Ndwata Ludigija amefanya ziara ya kikazi jimbo la Ukonga na kufanikiwa kutatua kero ya mgogoro wa shule iliyokuwa ikiwasumbua wananchi wa mtaa wa Gulukakwalala Gongalamboto jimbo la ukonga, kufuatia ujenzi wa mradi wa reli ya mwendo kasi yaani standard gauge iliyo katiza katika eneo la shule ya msingi Gulukakwalala na kupelekea kuvunjwa kwa shule hiyo.

Akiilezea kero hiyo mmoja wa wananchi wa mtaa wa bwana Jofrey Joseph amesema, “uongozi wa serikali ya mtaa Gulukakwalala uliwaambia kuwa shule yao itavunjwa ili kupisha ujenzi wa mrdi wa reli ya standard gauge na watoto waliokuwa wakisoma shule hii wataamishiwa kwenye shule ya jirani ili kupisha ujenzi wa shule mpya ya Gulukakwalala na kisha kurushwa kwenye shule yao punde tu ujenzi ukikamilika, lakini hali imekuwa tofauti baada ya kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo mpya ambapo uongozi wa serikali ya mtaa umebadilisha matumizi ya shule hiyo na kuifanya kuwa ENGLISH MEDIUM SHOOL bila ya kuwashiriksha wananchi na bado watoto wao wamekuwa wakisoma kwenye shule ya uhamishoni ambayo ipo mbali na makazi yao”

Akijibu kero hiyo Mkuu wa Wilaya ya llala Mh. Ludigija amesema, “Baraza la Madiwani lilikaa na kukubaliana hivyo kwa sababu asilimia kubwa ya Wananchi waliohamishwa kupisha ujenzi wa shule wameyahama maeneo hayo na kuhamia mbali hivyo baraza likakubaliana kuweka english medium school, lakini kwakuwa bado kuna wanafunzi ambao wanasoma uhamishoni au maeneo ya jirani na kwa kuwa wananchi wa mtaa huo bado wanahitaji kuandikisha watoto zao darasa la kwanza hivyo serikali imeamua kuigawanya shule hiyo mpya ya english medium ili kuwawezesha kuanzishwa upya kwa shule ya msingi Gulukakwalala na watoto wanaosoma uhamishoni kurudi

UFUATILIAJI NA UTATUZI WA KERO ZA WANANCHI

Page 6: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

6

kwenye shule yao ya nyumbani na pia kuwezesha kusajiliwa kwa watoto wa darasa la kwanza katika eneo hilo”

Aidha kero nyingine zilizozungumziwa na wananchi wa mtaa wa Gulukakwalala ni pamoja na mazingira hatarishi kuishi yanayotokana na mto msimbazi, pamoja na kukosekana kwa kampuni ya urasimishaji ardhi katika maeno hayo ya Gulukakwalala mbapo mkuu wa wilaya kupitia mtaalam wa ardhi aliyeambatana naye kwenye ziara hiyo waliwahakikishia wananchi hao kuwa kero hiyo tayari imefika kwenye idara yao na mchakato wa kupatia ufumbuzi umekwisha anza.

Akihitimisha kikao hiko na wananchi mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Ludigija amewasihi wananchi wa eneo hilo kutokubali kutumika vibaya na watu wenye nia ovu dhidi ya maendeleo ya jamii na uchumi wa taifa hili hususani katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu, kwani kufanya hivyo kunaweza hatarisha maendelo ya nchi na kurudisha nyuma juhudi za kimaendeleo zinazo fanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Mh. Raisi Dkt. John Magufuli.

Page 7: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

7

Na Mwandishi wetu

Uongozi ni mamlaka au karama anayopewa mtu kuwaonyesha watu njia kwa vitendo. Kipimo cha uongozi ni namna ambavyo kiongozi anaweza kuleta ushawishi kwa watu na kufikia maendeleo yaliyotarajiwa.

Katika matoleo ya jarida hili tutakuwa na mfululizo wa makala kuhusu uongozi kama itakavyokuwa ikizungumziwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Jumanne Shauri. Hii ni sehemu ya kwanza ya makala hiyo;

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bwana Jumanne Shauri anaanza kwa kuongelea namna ambavyo kiongozi bora anatakiwa kuwa ili kufanikisha malengo yake anayoyapanga katika kuhudumia watu anaowaongoza.

Akihojiwa na mwandishi wa jarida hili Mkurugenzi amesema kiongozi lazima awe na dira itakayo muwezesha kupanga mpango mkakati ili kukamilisha dira hizo kwani viongozi waliofanikiwa hutengeneza dira na kufanikiwa katika uongozi wao kupitia dira walizoziweka.

Dira ni nini?

Dira ni kifaa cha kutambua mwelekeo hivyo dira inapaswa kuonesha muelekeo wa kiongozi wapi alipotoka na ndoto anazotaka kuzifikia. Dira ndio nguzo kuu ya kiongozi itakayo mwezesha kufanikisha malengo yake kupitia mipango ya kimkakati atakayo iweka kwa kulinganisha dira yake na ndoto zake.

UONGOZI NA DIRA YA MAENDELEO

Page 8: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

8

Na sio tu kwa kiongozi bali mtu yoyote ili afanikiwe malengo yake lazima awe na dira na ndoto ili apate muelekeo wa nini anakitaka kukifikia na pia kutengeneza mikakati ya kufikia jambo lake. Katika kuliongelea hilo Bwana Shauri alisema “hata wanafunzi wakitaka kufaulu masomo yake lazima aweke dira kwamba anataka kufikia ufaulu gani mathalani ufaulu wa daraja la kwanza kisha aweke mikakati ni namna gani anaweza kufikia mafanikio hayo”.

Pia Mkurugenzi anasema ” mtu huwezi kukurupuka tu na kusema leo unataka kukimbia mbio za riadha kama hauna maandalizi hivyo ni lazima ujiandae kwa muda hata miezi sita au ndani ya mwaka mmoja ndipo uweze kushiriki riadha na kufanikiwa kushinda”

DIRA ZA VIONGOZI TANZANIATangu awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi Tanzania, viongozi wake wote walikua na dira waliozitumia katika kuhudumu muda wote wa uongozi wao na kufanikisha mengi kwa kufuata dira hizo.

Tangu nchi ipate uhuru mpaka sasa Tanzania ina awamu tano za uongozi na awamu zote viongozi wake walihudumu kwa mafanikio makubwa kwa kutumia dira za maendeleo na walitengeneza mipango ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ya kimkakati ya kufikia dira hizo

Awamu ya kwanza ya uongozi Tanzania chini ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ulikua na dira ya kupiga vita umasikini, maradhi na ujinga ili kuhakikisha kila mtanzania anakua na maisha bora.

Hayati Mwl. Julius Kambarage NyerereAwamu ya Kwanza

Mhe. Ally Hassan MwinyiAwamu ya Pili

Dkt. Jakaya Mrisho KikweteAwamu ya Nne

Dkt. John Pombe MagufuliAwamu ya Tano

Hayati Benjamin William MkapaAwamu ya Tatu

Page 9: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

9

Dira hiyo ilifanikiwa na kuwafanya wananchi kuondokana na ujinga kwa kufanya elimu kuwa bure ili watanzania wote waweze kusoma hata kama wana hali ya umasikini. Watoto pia walipata nafasi ya kufundishwa na walimu wa UPE na kupata elimu ya msingi iliyowasaidia kujua kusoma na kuandika.mwalimu Julius Nyerere aliamzisha elimu ya kujitegemea kuanzia shule za msingi mpaka sekondari na vyuoni huku lengo la elimu hiyo likiwa ni kuondoa ujinga pamoja na kuwafanya watanzania wasiwe wageni wa mazingira yao na kuyatumia vyema ili kuweza kujiingizia kipato kwa shughuri mbalimbali za kiuchumi kama kilimo, uvuvi pamoja na useremala.

Katika suala la kuondoa umasikini Mwalimu Nyerere alianzisha taasisi ya chakula na lishe. Mapema kabisa wakati Dunia ikiwa bado haijui mchango wa lishe bora kwa watoto na hapa Afrika Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza kabisa kuanzisha kituo maalumu cha kutafiti na kuishauri serikali juu ya lishe ya watoto na watu wake kwa ujumla (Tanzania Food and Nutrition Centre). Mpaka leo Tanzania inaheshimika duniani kote kwa kuwa na wataalamu wabobezi katika lishe. Mataifa mengi duniani kote huja hapa nyumbani kujifunza namna kituo chetu cha chakula na lishe kinavyochagiza mipango makini ya afya ya ulaji serikalini na kwa wananchi

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru amewahi kusema kuwa mwalimu Julius Nyerere ndio muasisi wa bima ya afya ya jamii mwaka 1962.Profesa Mseru ameeleza hayo Oktoba 11, 2019 wakati akizungumza katika kongamano la siku mbili la kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililoandaliwa na taasisi ya uongozi kwa ushirikiano na UDSM. Amesema japo Serikali wakati huo hakikuwa kubwa kama sasa, lakini Nyerere alijua mahitaji ya wananchi na changamoto wanazozipata katika matibabu yao kwa kutokuwa na utaratibu huo. .

Lakini pia katika kupigana vita na adui umasikini mwalimu Julius Kambarage Nyerere alianzisha falsafa ya ujamaa na kujitegemea lengo kuu la falsafa hii lilikuwa ni kulifanya taifa la Tanzania kuwa na uchumi wa kujitegemea na kutokuwa ombaomba kwa mabeberu. Kufuatia dhima hiyo mwalimu nyerere alikuja na mipango mkakati mbalimbali ya kuhakikisha sera ya ujamaa na kujitegemea inafikia malengo kwa kumfaidisha kila mtanzania ambapo alianzisha mipango mbalimbali ikiwemo mashamba ya vijiji, pamoja na kuanziaha viwanda ili kuwezesha upatikanaji wa ajira miongoni mwa watanzania ili kuweza kupata kipato cha kujikimu kimaisha.

kwa upande wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi alikuja na Dira ya kuikomboa nchi katika hali mbaya ya kiuchumi ya nchi yetu kutokana na athari ya vita ya Kagera wakati huo hiyo kuja na kauli mbiu ya RUKSA. Dira hiyo iliangazia kupigania wanyonge na watu wa hali ya chini kwani alitoa ruksa kwa shughuli zote halali zilizokatazwa kufanywa kufanyika bila kuvunja sheria za nchi. Dira hiyo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Rais wa awamu ya tatu Hayati Benjamin Mkapa yeye aliongoza Tanzania chini ya Sera ya ubinafisishaji akilenga Taifa la Tanzania liweze kuingia katika uchumi wa kati katika maendeleo yake. Akiwa madarakani Rais Mkapa alibinafsisha baadhi ya mashirika yanayomilikiwa na Serikali na akatumia sera ya soko huru. Dira yake ilipata msaada wa Benki ya Dunia na shirika la fedha duniani IMF na kuwezesha baadhi ya madeni ya nje ya Tanzania kufutwa. Aidha Mhe. Mkapa alifanya juhudi za kupambana na ufisadi zilizopelekea kuundwa kwa jukwaa la wazi lililoitwa Tume ya Rais juu ya ufisadi iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba na kuongeza msaada katika mapambano hayo.

Page 10: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

10

Awamu ya nne ya Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ilikuja na dira ya maisha bora kwa kila mtanzania kwa kuzingatia anapitia na kuboresha kila sekta ili watanzania wote wanufaike na nchi yao kwa kuwa na maisha bora kuanzia daraja la juu mpaka wananchi wa daraja la chini. Mipango hiyo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani watanzania wengi maisha yao yalibadilika na kuwa bora. Maboresho yalifanyika kwenye sekta ya ulinzi na usalama, huduma za kijamii na sekta ya utalii pamoja na uwekezaji sekta nyengine muhumu zenye kuleta maendeleo chachu kwa maisha bora ya watanzania.

Rais wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kupitia sera ya HAPA KAZI TU ametekeleza dira alizoziweka tangu aanze kuhudumu katika kipindi chake na kuhakikisha dira zilizowekwa na Maraisi wa awamu zilizopita zinafikiwa kikamilifu.

Katika kukamilisha sera na dira yake Rais Magufuli anaamini kwamba viwanda vitakua nguzo katika taifa ili kuleta uchumi ulio bora huku ukitengeneza ajira kwa Watanzania wengi. Rais Magufuli amezidi kujikita katika misingi ya baba wa Taifa katika kujenga vituo vingi vya afya ili kutokomeza adui ambae ni maradhi, kaboresha shule nyingi na kujenga na ameweza kutekeleza sera ya Elimu Bure ili kila mtoto wa kitanzania aweze kusoma.

Sambamba na hayo Shauri aliongelea Viongozi wakubwa Duniani ambao walikua na dira katika uongozi wao zilizosababisha kufikia mafanikio viongozi hao ni pamoja na Mao Zedong wa China, Mahatma Gandhi wa India na Martin Luther King wa Marekani.

Mahatma Gandhi alikuwa mwanasheria, mwanafalsafa na mtetezi wa haki za binadamu na kiongozi wa juu wa siasa nchini India.Ghandi alifanya kazi kwenye shamba la miwa nchini Afrika Kusini lakini aliweka dira kwamba akirudi nchini kwake atahakikisha India inapata uhuru. Aidha aliporejea India aliweka mipango ya kimkakati kwa kutumia mbinu ya uasi wa kiraia usio wa vurugu ulioisaidia india kupata uhuru na kuhamasisha mavuguvugu kadhaa ya haki za kiraia na uhuru Duniani.

Naye Mao Zedong alikua ni kiongozi wa Jamhuri ya watu wa China kuanzia mwaka 1949 na kiongozi wa chama cha kikomunisti cha China tangu 1935 hadi kifo chake 1976. Katika hatua za mwanzo siasa yake ya kiuchumi ilisababisha njaa na vifo vingi wakati wa utekelezaji lakini maono na ndoto za Mao zilikua ni kuipeleka China katika uchumi ambao sasa tunauona. China imekua nchi ambayo ina uchumi wa juu kutokana na sera iliyowekwa na Mao.

Martin Luther King alikua na dira na ndoto kuwa ipo siku moja Marekani itaongozwa na mtu mweusi na ndoto hiyo ilitimia kwani mnamo mwaka 2009 hadi mwaka 2017 Nchi ya marekeni iliongozwa na mmarekani mweusi Barack Hussein Obama akiwa kama raisi wa awamu ya 44 kupitia chama cha Democratic.

Page 11: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

11

HITIMISHO

Katika kuhitimisha sehemu hii ya kwanza ya makala Mkurugenzi Jumanne Shauri ametolea mfano jinsi kiongozi wa Taifa letu Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza Dira kwa vitendo baada ya kuahidi kufika kwenye uchumi wa kati kabla ya mwaka 2025 na hatimaye kufikia malengo hayo ndani ya mwaka 2020, na kusema kuwa hayo yote yamewezakana ndani ya muda mfupi kutokana na ukweli kuwa kiongozi wetu wa Nchi alipoingia tu madarkani aliingia na sera yake ya HAPA KAZI tu na kuja na mipango ya kimkakati ya kutimiza sera hiyo kwa kuanzisha na kufufua viwanda ili kutoa fursa ya ajira kwa kila mtanzania.

Aidha Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala alieleza kwa upande wa Halmashauri ataendelea kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato na kubuni vyanzo vipya ili kufikia asilimia mia moja ya makadirio yaliyowekwa ambapo fedha hizo zitakuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika sekta ya Afya Bwana Shauri amelenga kuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha kunakuwepo na miundombinu rafiki kwa wanannchi kuanzia Zahanati, Kituo cha Afya na hospitali.

Hali kadhalika katika Sekta ya Elimu chini ya uongozi wake atahakikisha Halmashauri inakuwa na vyumba vya kutosha vya madarasa, samani, nakuongeza idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kuanzi darasa la awali, msingi na sekondari.

Vile vile Halmashauri imelenga kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa 10% ya mapato ya ndani mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Katika kuwezesha wananchi wa Manispaa ya Ilala Kupitia mikopo itokanayo na asilimia kumi ya mapato ya ndani Bwana Shauri analenga katika uanzishaji wa Viwanda vidogo vidogo pamoja na uzalishaji wa bidhaa italenga kuwezesha upatikanajio wa ajira kwa wananchi.

Page 12: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

12

ILALA KINARA CHA UKUSANYAJI MAPATO KATIKA HALMASHAURI ZA TANZANIA.

Na Mwandishi Wetu

Katika Serikali ya awamu ya tano chini ya Jemedari Dkt . John Joseph Pombe Magufuli na adhima yake kubwa ya kutoa huduma bora kwa wananchi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imejikita na kutekeleza kwa ufanisi mkubwa ukusanyaji wa mapato ambayo ndiyo chagizo kubwa linalofanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Halmashauri imeweka mikakati thabiti ya kuhakikisha Ukusanyaji mapato unatekelezeka kwa asilimia 100% kwa Kuimarisha ukusanyi wa mapato kwa kuongeza vyanzo vipya vya mapato na kupanua wigo wa walipa kodi ili kuongeza uwezo wa serikali wa kugharamia huduma za Kijamii na Kiuchumi.

Kwa kipindi cha Januari 2016 hadi Juni 2020 Halmashauri imelenga kuboresha takwimu za walipakodi, Kununua vitendea kazi hususani magari ya kufuatilia mapato na vifaa vya ki-elekitroniki (point of sale-POS) vya kupokelea mapato.

Katika kipindi kinacholengwa, magari 10 madogo ya ufuatiliaji mapato yamenunuliwa. Aidha mfumo wa malipo kwa kutumia mitandao ya benki za CRDB, NMB, zinatumika na mashine za ki-electroniki (Point of Sales-POS) 680 za kukusanyia mapato zimenunuliwa na zitumika maeneo mbalimbali ya utoaji wa huduma kama vile Vituo vya afya, masokoni, makampuni ya kukusanya taka na ofisi za Kata. Uboreshaji watakwimu za walipakodi unaendelea. Ulipaji wa kodi kwa huduma mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri zinasogezwa karibu zaidi na wananchi kwa kuanzia na Kata ya Buguruni. Miradi ya kimkakati ya ujenzi wasoko la Kisutu na machinjio ya Vingunguti inatarajia kuongeza mapato mara itakapokamilika.

Jedwali la ukusanyaji wa Mapato.

Aidha pamoja na ukusanyaji mkubwa wa mapato kwa miaka mitano, Halmashauri imeweza kuthibiti matumizi ya mapato hayo kwa kuwa na matumizi bora na kupata hati safi kwa miaka minne mfululizo ambayo ni katika mwaka wa fedha 2015/2016 hadi 2018/2019.

Jedwali hili linaonyesha jinsi ufanisi wa ukusanyaji wa mapato unavyoongezeka kwa miaka mitano (5)

Page 13: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

13

Na Rosetha GangeHapa kazi tu,ni falsafa ,msemo au kauli mbiu iliyoanzishwa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr.John Joseph Pombe Magufuli mwaka 2015 wakati wakampeni zake za kuwania kiti cha urais.Hata hivyo baada ya kufanikiwa kuingia madarakani amekuwa akiitumia kauli mbiu hii kwa kutekeleza kwa vitendo kwa kuwataka wananchi kufanya kazi wakati kwa manufaa yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kupitia Idara ya maendeleo ya jamii na vijana imekuwa mstari wa mbele katika kuitekeleza kauli mbiu hii kwa kuwawezesha vijana kwa njia mbalimbali ii kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo katika nchi.

Katika Manispaa ya Ilala, Idara ya Maendeleo ya Jamii imepewa jukumu la kuifikia jamii hususani kuiwezesha kiuchumi kwa kuzingatia umri,rika, jinsia na bila kujali ubaguzi wa rangi, utaifa,kabila, mila na desturi. Pia idara ya Maendeleo ya Jamii ina jukumu la kuleta ustawi na maendeleo ya jamii kuanzia mtu mmoja mmoja,vikundi na jamii kwa ujumla.Hii yote ni katika kuendana na kauli mbiu ya hapa kazi tu.

Uwezeshaji wa wananchi katika kukabiliana na changamoto ya kiuchumi.

Ili kuendana na sera ya hapa kazi tu ya Mhe.Rais, Manispaa ya Ilala katika kipindi cha 2015-2020 imefanikiwa kusimamia zoezi la utoaji mikopo kwa viundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ikiwa ni pamoja na kusajili vikundi mbalimbali vya kiuchumi na kijamii.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imekuwa ikitekeleza agizo la serikali linalotokana na azimio la bunge lililotolewa mwezi Agosti 1993 kifungu cha 17 kidogo cha kwanza cha sheria ya “exchequer na Audit ordinance cap” 439 ya mwaka 1961.Agizo hili lilizitaka Halmashauri zote nchini kutenga na kupeleka asilimia kumi (10%) ya mapato yanayotokana na vyanzo vya ndani kwenye mfuko wa kuendeleza wanawake na vijana kwa mgawanyo wa asilimia 5% wanawake na asilimia 5% vijana.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilipoanzishwa mwaka 2000 ilikuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa agizo hilo kwa kuanzisha mfuko huo .Mwaka 2014, Halmashauri iliingia makubaliano na Benki ya wananchi wa Dar es salaam (DCB) yaliyolenga kuitumia benki hiyo kukopesha fedha.Lengo kuu ikiwa ni kuimarisha urejeshaji wa mikopo na utoa mbinu za biashara kwa wanufaika wa mfuko huo kwa kipindi hicho ambapo ilikuwa ni wanawake na vijana.

Katika kuwawezesha wananchi wafanye kazi na katika kuendana na falsafa ya hapa kazi tu,katika mwaka wa fedha 2015/2016,Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilichangia kiasi cha shilingi bilioni moja,milioni mia mbili kumi na mbili na mia tisa elfu tu.(1,212,900,000) katika kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi.Mwaka 2016/2017 ilichangia kiasi cha shilingi bilioni moja,milioni mia sita na nne laki moja themanini na tatu elfu mia nane arobaini na tano (1,604,183,845) na mwaka 2017/2018, Halmashauri ilichangia kiasi cha shilingi bilioni nne milioni mia mbili sabini na nane laki sita themanini na tatu elfu mia nane arobaini na tano(4,278,683,845).

MANISPAA YA ILALA NA SERA YA HAPA KAZI TUU.

Page 14: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

14

Mwitikio wa wanawake na vijana ulikuwa mkubwa katika kuchangamkia fursa hizo na hivyo kuendana na falsafa ya hapa kazi tu ili kuweza kujikwamua kiuchumi.Miradi na vikundi mbalimbali vilipewa mikopo ambavyo ni pamoja na ushonaji, ufumaji, mama na baba lishe, utengenezaji wa batiki na sabuni za maji na miche, ukulima wa mboga mboga, kuuza nafaka, genge, ufugaji na bodaboda. Jumla ya vikundi vilivyokopeshwa mpaka kufikia 2018 ni vikundi 289 na wanufaika ni 12,564.

Katika bajeti ya 2019/2020,Halmashauri ilipanga kutoa mikopo kwa vikundi 150 vya wanawake na 150 vya vijana katika Manispaa ya Ilala ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi na kusimamia usajili wa Asasi na vikundi 100 kiuchumi na kijamii.

Vile vile Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeendelea kuungana na serikali ya awamu ya tano kuelekea uchumi wa viwanda kwa vitendo na kufanya kazi kwa bidii, pamoja na kutoa mikopo bila riba kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kwa mgawanyo wa asilimia 4%.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,chini ya kitengo cha uratibu na usajili wa vikundi imefanikiwa kusajili vikundi mbalimbali na kuwakopesha jumla ya shilingi bilioni moja na milioni mia nane sitini na tano na laki moja (1,865,100,000).Fedha hizi zilitolewa kwa mgawanyo wa shilingi bilioni moja milioni mia moja hamsini na mbili laki nne na hamsini(1,152,450,000) zilizokwenda kwa wanawake,shilingi milioni mia nne themanini na sita na laki nne(486,400,000) zilitolewa kwa vijana na shilingi milioni mia mbili ishirini na sita laki mbili na hamsini elfu(226,250,000) zilitolewa kwa watu wenye ulemavu.

Hii yote ni katika kuunga mkono falsafa ya Mheshimiwa Rais iliyowataka wananchi wafanye kazi kwa bidii katika kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na pia kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Ili kuhakikisha mchango wa sekta ya viwanda katika pato la taifa unaongezeka na kufikia malengo ya dira ya taifa ya maendeleo 2025, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilianzisha na kusimamia viwanda vidogo vodogo na vya kati na kuanzisha shughuli mbalimbali ili kuwa kwamua wananchi kiuchumi kama ifuatavyo;

Imeanzisha viwanda vidogo vidogo,vya kati na vikubwa kwa njia ya vyombo ya habari, semina ,mikutano,mafunzo na makongamano kwa wananchi na wadau pamoja na kujenga mahusiano na miji rafiki nje ya Tanzania.

Imefanikiwa kuboresha mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji kwa kuimarisha miundo mbinu ya usafiri na usafirishaji kama barabara za juu za makutano ya Tazara.

Ugawaji wa vitambulisho vya wajasiliamali kwa wafanyabiashara wadogo vinavyopatikana kwa gharama ya shilingi 20,000 umesaidia kwa kiwango kikubwa kuinua uchumi na kipato cha wafanyabiashara wadogo pamoja na familia zao.

Page 15: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

15

Vilevile upatikanaji wa vitambulisho hivi umesaidia kuamsha ari kubwa kwa wafanyabiashara kuchapa kazi kwani ule usumbufu uliokuwepo mwanzo wa kutozwa kodi haupo kama zamani.

Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020, ibara ya (132) imehakikisha watoto wanalindwa dhidi ya uonevu, ukatili, udhalilishaji, utumikishwaji na mila potofu.

Watoto 428 wamepatiwa elimu juu ya kujilinda kupitia kamati ya ulinzi na utokomezaji wa ukatili kwa watoto na wanawake.Aidha kamati mbalimbali zimeundwa kwa mujibu wa mwongozo mpya wa kitaifa kwa kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya watoto na wanawake.

Aidha kupitia Ibara ya (137) Manispaa ya Ilala imeanzisha uraghibishi wa vijana waweze kujiajiri kwa kuthamini kazi nyingine za mikono,kilimo,ufundi,michezo,sanaa na kazi nyingine za kitaaluma .Vijana wamewezeshwa kwa kupewa mafunzo ya ujasiliamali na kuweza kujiajiri. Aidha katika mwaka 2019/2020 ilijitahidi kutenga bajeti ili kuweza kuimarisha, kudhibiti na kuratibu matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Vile vile kupitia dawati la jinsia na watoto,Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi juu ya madhara yatokanayo na kutenda vitendo vya ukatili kwa watoto na wanawake ikiwa ni pamoja kusambaratika familia na kuongezeka kwa watoto wa mitaani,jambo linalohatarisha maisha yao na kuyumba kwa uchumi wa nchi kwani badala ya hao waliofanyiwa ukatili na kuamua kuondoka katika kaya zao kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya nchi watabaki kuwa wazurulaji mitaani hivyo maendeleo ya nchi yatadolora.

Hali kadhalika wananchi wamekuwa wakipewa elimu kuripoti matukio yote ya ukatili wa kijinsia yanayojitokeza katika jamii ili kuweza kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Kwa ujumla Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kiwango kikubwa imejitahidi kutekeleza kwa vitendo sera ya Mheshimiwa Rais ya hapa kazi tu kwa kuwawezeha wananchi wake katika nyanja tofauti tofauti hasa ya kiuchumi ili kuweza kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na cha Taifa zima kwa ujumla hali iliyopelekea hivi karibuni nchi yetu kuwa miongoni mwa mataifa matano duniani kutangazwa na benki ya dunia kuwa nchi yenye uchumi wa kati.Hii yote inatokana na wananchi kuwa na mwitikio mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii.

Page 16: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

16

• HUDUMA ZA KIJAMII ZAZIDI KUBORESHWA • UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI WASHIKA KASI AWAMU YA TANO

Na mwandishi wetuHalmashauri ya Manispaa ya Ilala inundwa Na Kata 36 na mitaa 159. Katika kipindi cha miaka mitano (5) ya uongozi wa serikali ya awamu ya Tano mafanikio mengi ya huduma yamepatikana na kuboresha maisha ya wakazi wa Manispaa ya Ilala. Katika makala hii ndugu msomaji utraweza kuzifahamu Kata zinazounda Manispaa ya Ilala na miradi iliyotekelezwa.

1. KATA YA MCHAFUKOGEKata ya Mchafukoge iko katika tarafa ya Kariakoo, Kata hii inapakana na Kata ya Kisutu, Kivukoni, Gerezani, Kariakoo na Jangwani. Ina mitaa miwili Mtaa wa Kitumbini na Mchafukoge. Kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012 Kata hii inakadiriwa kuwa na wakazi 10688 shughuli kuu ya wakazi wa Kata hii ni biashara na ajira binafsi huku wakazi wake wengi kwa zaidi ya asilimia 90 wakiwa watanzania wenye asili ya bara la Asia.

Katika Kata hii ndipo ambapo ujenzi wa soko la Kisasa la Kisutu unafanyika ambalo baada ya kukamilikwa kujengwa litakuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 1500 Ikilinganishwa na soko la awali lilikuwa na wafanyabishara 337 wana mradi wa Ujenzi Ofisi mpya ya Kata unaotekelezwa na Mkandarasi ELIMACO TANZANIA LIMITED kwa kiasi cha Tshs.38,368,709.84/=, wana Mradi wa uboreshaji kisima cha maji kinachotumiwa na Ofisi ya Kata. Huduma za kijamii zinazopatikana katika Kata hii kwa upande wa afya Hospitali ya Mnazimmoja, na ina shule moja ya Sekondari Jamhuri Sekondari .

36ZA MANISPAA YA ILALA;

KUTOKA KATA

Kivutio cha magorofa marefu ndani ya Kata ya Mchafukoge

Page 17: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

17

2. KATA YA MSONGOLAKata ya Msongola ipo upande wa kusini wa Manispaa ya Ilala imepakana na Wilaya ya Mkuranga na Manispaa ya Temeke. Ina jumla ya wakazi 46,989 wanaume wakiwa 22,401 na wanawake 24,584. Kaya zaidi ya 10,418. Kaya ya Msongola ina jumla mitaa tisa (9) ambayo ni Yangeyange, Mbondole, Kitonga, Mkera, Sangara, Kiboga, Mvuleni, Kidole na Uwanja wa Nyani. Wananchi wa Kata hii wanajishughulisha na shughuli za kilimo na ufugaji na biashara ndogondogo.

Miradi mbalimbli ya kimaendeleo imetekelezwa katika kata hii ambayo ni Ujenzi wa Zahanati ya Luhanga uliogharimu Tshs. 69,900,000/=, Ujenzi wa Ofisi ya Walimu Yange Yange umegharimu Tshs. 20,000,000/= jumla ya gharama za miradi yote ni Tshs.89,000,000/=.

3. KATA YA BONYOKWAKata ya Bonyokwa inaundwa na mitaa mitatu (3) ambayo ni Mtaa wa Bonyokwa, Mtaa wa Kisiwani na Mtaa wa Msigwa. Kata hii ilipatikana kutokana na kugawanywa kwa kata ya ambapo imepakana na Kata ya Segerea, kwa upande wa magharibi na Kata ya Kimara iliyopo Manispaa ya Ubungo, kwa upande wa kusini inapakana na Kata ya Kinyerezi na kwa upande wa Kaskazini inapakana na Kata ya Kisukuru.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Kata ya Bonyokwa inakadiriwa kuwa na jumla ya watu 19,089 wakiwemo wanaume 8,579 na wanawake 10,513.

Miradi ya maendeleo iliyotekelezwa; katika Kata hii ni Ujenzi wa Ofisi ya Kata uliogharimu shilingi Tshs.114,131,075/=, Ujenzi wa matundu ya vyoo katika Shule ya msingi Bonyokwa umegharimu shilingi Tshs.14,000,000/=, Umaliziaji wa Ofisi ya Serikali ya mtaa wa Msingwa umegharimu shilingi Tshs.18,000,000/=, Ukarabati wa Ofisi ya walimu katika shule ya msingi Bonyokwa umegharimu shilingi Tshs.12,500,000/=, na Ujenzi wa kuchoma taka na kizimba katika Zahanati ya Bonyokwa umegharimu shilingi Tshs.4,500,000/=.

4. KATA YA KINYEREZIKata ya Kinyerezi imepakana na Kata ya Pugu Manispaa ya Ilala, Kata ya Kwembe Manispaa ya Ubungo, Mashariki imepakana na Kata ya Ukonga, Gongolamboto kwa upande wa kaskazini, imepakana na Kata ya Bonyokwa, Kata hii ni miongoni mwa Kata 36 zinazounda Manispaa ya Ilala ina jumla ya mitaa sita ambayo ni Kinyerezi, Kibaga, Kanga, Kifuru, Kwalimbanga na Kichangani.

Miradi ifuatayo imetekelezwa katika Kata hii kama ifuatacyo; ujenzi wa vyumba vitatu(3) vya madarasa Shule ya Msingi Kinyerezi umegharimu shilingi Tshs.62,000,000/=. ujenzi wa matundu sita ya vyoo umegharimu shilingi Tshs.6,6000,000/=, Ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa Shule ya Msingi JICA umegharimu shilingi 37,500,000/=, Ujenzi wa chumba kimoja cha darasa Shule ya Msingi Zimbili umegharimu shilingi Tshs.12,500,000/=, Ujenzi wa darasa moja Kinyerezi Sekondari umegharimu shilingi Tshs.17,884,000/=, Ujenzi wa madarasa sita Kinyerezi Annex Sekondari umegharimu shilingi Tshs.200,000,000/= na Ujenzi wa matundu 22 ya vyoo Kisungu Sekondari ambao umegharimu shilingi Tshs.60,000,000/=.

Page 18: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

18

5. KATA YA CHANIKA

Kata ya Chanika ina wakazi wapatao 43,912 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi 2012 na Kaya 11,123 imepakana na Kata ya Buyuni, kusini imepaka na Zingiziwa , magharibi imepakana na Msitu wa Kazimzumbwi na Mashariki imepaka na Msongola. Ina mitaa nane (8) ambayo ni Mtaa wa Vikongoro, Nguvu Mpya, Ngwale, Tungini, Lukooni, Kidugalo, Yongwe na Virobo.

Huduma za Kijamii

Kata ya Chanika ina Shule moja ya Sekondari iitwayo Nguvu Mpya na Shule tano za msingi ambazo ni Chanika, Tungini, Lukooni, Kidugalo, Yongwe, Vikongoro na Kidugalo. Jumla ya vikundi 24 Wanawake, Vijana na Wenyeulemavu wamepatiwa mikopo.

6. KATA YA KISUKURU

Kata ya Kisukuru ni miongoni mwa Kata 36 zinazounda Manispaa ya Ilala, Kata hii upande wa Kaskazini inapakana na Kata za Makuburi na Kimara zilizopo Manispaa ya Ubungo, Upande wa Kusini inapakana na Kata ya Segerea iliyopo Manispaa ya Ilala, Upande wa Mashariki inapakana na Kata ya Kimanga na Magharibi inapakana na Kata ya Bonyokwa zote zipo Manispaa ya Ilala ina Mitaa mitano ya Serikali.

Huduma za kijamii;

Kata ya Kisukuru ina Shule za Msingi nane(8) ambapo saba ni za watu binafsi na moja ni ya Serikali ambazo ni Magoza, Agness Michael, Mount Zion, Sabisa, Amani ACCT, Lusasaro, Tigo Hane na Mwenyeheri Anuarite. Pia ina Shule za Sekondari nne ambapo tatu ni za binafsi na moja ya Serikali ambazo ni Magoza, Kisukuru Regent, Segerea Hill na Mwenyeheri Anuarite.

Uwepo wa Hospitali ya Mama na Mtoto - KOICA

Page 19: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

19

7. KATA YA KITUNDA

Kata ya Kitunda ni miongoni mwa Kata 36 katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Mkoa wa Dar es salaam ina jumla ya mitaa minne ambayo ni Mtaa wa Relini, Kitunda Kati, Kiyombo na Kipera kwa upande wa Mashariki inapakana na Buza iliyopo Manispaa ya Temeke, Magharibi inapakana na Kata ya Mzinga, kaskazini inapakana na Kata ya Kipawa, na Kusini inapakana na Kata ya Kivule ina jumla ya watu wapatao 32,188 kati ya hao wanaume ni 15,451 na wanawake ni 16,731 na kaya 7442.

Katika Kata hii wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwa ni Kilimo cha mbogamboga na matunda , Waajiriwa na Serikali na Taasisi Binafsi, Ufugaji na Biashara wana miradi wanayoitekeleza ambayo ni Choo cha wanafunzi Shule ya Msingi Kiyombo umegharimu shilingi Tshs.20,000,000/=, Ujenzi wa choo matundu kumi (10) Shule ya Msingi Kitunda umegharimu shilingi Tshs.20,000,000/= na Ujenzi wa vyumba vinne (4) vya madarasa Shule ya Sekondari Kitunda umegharimu shilingi Tshs.50,000,000/=.

Mwamko wa wananchi kuchangia maendeleo;

Katika kuleta chachu ya maendeleo wananchi katika Kata hii walitoa mchango wao kwa kuchangia wa kiasi cha shilingi 1625,000/= kwa ajili ya ujenzi wa mtaro uliopo Kiyombo Mennonite. Aidha wamechangia shilingi 3,446,000/= kwa ajili ya Ujenzi wa Sekondari ya Kitunda.

8. KATA YA KIVULE

Kata ya Kivule ina wakazi 36,031 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 na kuna kaya 8149, kaskazini imepakana na Kata ya Kipunguni, kusini imepaka na Kata ya Msongola, Magharibi imepakana na Kata ya Majohe na Mashariki imepakana na Kata ya Mzinga. Ina mitaa minne ambayo ni Kerezange, Bombambili, na Kivule.

Huduma za kijamii

Kata hii ina Shule nne(4) za Msingi ambazo ni Kivule, Serengeti, Misitu na Bombambili shule za msingi za binafsi ni Zawadi, Daddy, Click na Kananura pia zipo shule nne(4) za sekondari za serikali za Misitu, Kerezange, Kivule na Abbuy Jumaa shule mbili(2) za binafsi za sekondari ni Messac na Mbonea Kuna Zahanati moja visima viwili vya maji na vingine vya Dawasco.

9. KATA YA LIWITI

Kata ya Liwiti kwa upande wa Mashariki imepakana na Kata ya Tabata , upande wa Magharibi imepakana na Kata ya Segerea, upande wa Kaskazini imepaka na Kata ya Kimanga na upande wa kusini imepakana na Kata ya Vingunguti na Kipawa. Ina jumla ya wakazi 51,300 ambapo wanaume ni 23,278 na wanawake ni 28,022. Kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ina mitaa minne (4) na mitaa yote ina watendaji.

Page 20: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

20

10. KATA YA MNYAMANI

Kata ya Mnyamani Ina jumla ya watu 58,360. Kata hii ilitokana na kugawanywa kwa Kata ya Buguruni.

11. KATA YA PUGU

Kata ya Pugu iko umbali wa kilomita ishirini na moja (21) kutoka mjini na ipo kusini Magharibi mwa Jiji la Dar es Salaam na umbali wa kilomita tano (5) kutoka Kisarawe Mjini, Mkoa wa Pwani. Kata ya Pugu imepakana na Kata ya Gongolamboto, Kata ya Buyuni na Kata ya Majohe. Ina jumla ya wakazi 59,029 Na mitaa mitano (5) ambayo ni Kinyamwezi, Mustafa, Kigogo A, Kigogo B, na Bombani.

Huduma za kijamii;

Kata ya Kipunguni ina jumla ya Shule za msingi sita (6) kati ya hizo shule nne(4) ni za serikali shule hizo ni Pugu Kajiungeni, Kigogo Fresh, Kinyamwezi na Bombani za Binafsi ni Kabby academy na Majority. Shule za Sekondari ni tatu (3) shule mbili zikiwa ni za Serikali ambazo ni Pugu na Kinyamwezi Sekondari na binafsi ni Magnus Sekondari, imetekeleza mradi wa Ujenzi wa vyumba sita vya madarasa Kinyamwezi Sekondari uliogharimu Tshs milioni 90.

12. KATA YA SEGEREA

Kata ya Segerea ina mitaa minne (4) ambayo ni Segerea, Migombani, Ugombolwa na Machimbo imepakana upande wa mashariki na Kata ya Liwiti, Magharibi Kinyerezi na Kisukuru, Kaskazini Kimanga na Kusini Kipawa. Ina jumla ya wakazi 43,878 wakiwemo wanawake 25,242 na wanaume 18,636 jumla ya kaya ni 9574 kwa mujibu ya sensa ya watu na makazi mwaka 2012.

Katika Kata hii wananchi wanajishughulisha na ujasiriamali mdogo mdogo ambao wanafanya biashara za bidhaa mbalimbali na wachache wameajiriwa Serikali na Mashirika Binafsi.

Huduma za kijamii

Kata ya Segerea ina jumla ya Shule nne (4) za Serikali ambazo mbili (2) ni Sekondari ina zahabati moja(1)

13. KATA YA UPANGA MASHARIKI

Kata ya Upanga Mashariki ni mojawapo kati ya Kata 36 za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Ipo mashariki mwa Wilaya yetu ikipakana na Kata za Upanga Magharibi, Jangwani, Kisutu na Kivukoni. Kata hiyo ina jumla ya wakazi 13,059 ambapo wanaume wakiwa 6,233 na wanawake 6,826. Kata ya Upanga Mashariki ina mitaa miwili ambayo ni Mtaa wa Kibasila na Mtaa wa Kitonga.

Wadau wachangia Shughuli za kimaendeleo;

Shughuli mbalimbali za kimaendeleo zimetekelezwa katika kata hii kupitiaambazo ni ujenzi wa barabara ya Longido kwa kiwango cha lami kwa kilomita 0.56 ambayo imegharimu million

Page 21: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

21

400 kutoka kwa wananchi na Upakaji wa Rangi na Ujenzi wa Kizimba cha Taka katika Shule ya Msingi Upanga kwa uhisani wa Samakiba Foundation ambao ni muunganiko wa Ali Kiba na Samatta.

Unic Finance wamekarabati Chumba cha zana kinachowekewa vifaa na walimu na vilevile wamejenga sehemu ya kunywea maji wameweka mabomba, Mabohora nao wamejenga sehemu za kupaki magari katika mitaa ya Magore, Mvumi, Alykhani na Kibasila. Lotary Charity ambayo ni Organization ya Hindu (BASIC CHARITY HINDU) wamekarabati Shule ya Maktaba yote.

14. KATA YA KIVUKONI

Kata ya Kivukoni ina jumla ya wakazi 6742 ambapo Wanaume ni 5331 wanawake ni 3211.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka2012. Kata hii kwa upande wa Mashariki inapakana na bahari ya Hindi na upande wa Magharibi kata ya Kisutu, Kaskazini ina pakana na Kata ya Upanga Mashariki, Kusini bahari ya Dar es Salaam. Kata hii ina Mitaa 2 ambayo ni Mtaa wa Kivukoni na Mtaa wa Seaview. Sehemu kubwa ya wakazi wanaoishi katika kata hii ni watumishi katika Sekta ya Umma na mashirika mbalimbali. Baadhi ya wakazi wajiajiri wenyewe kwenye biashara.

15. KATA YA BUGURUNI

Buguruni ni kata inayoundwa na Mitaa minne (4) ambayo ni Malapa, Madenge, Mivinjeni na Mtaa wa kisiwani. Kwa upande wa Magharibi imepakana na kata ya Mnyamani, Mashariki imepakana na kata ya Ilala, Kaskazini Magharibi imepakana na kata ya Tabata, upande wa kaskazini Imepakana na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na upande wa kusini imepakana na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.

Kata ya Buguruni ina mitaa minne ina jumla ya wakazi 67,253 ikiwa wanaume ni 31,338 na wanawake 35,915 kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

Usafiri wa Kivuko kwa wananchi

Page 22: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

22

Huduma za kijamii

Kata ya Buguruni ina shule tano (5) za msingi

Miradi ya maendeleo

Miradi ya maendeleo iliyotekelezwa inajumuisha ujenzi wa madarasa Shule ya Sekondari Buguruni moto uliogharimu Tshs.200,000,000.00 umaliziaji wa jengo la wazazi na ununuzi wa vifaa tiba kituo cha Afya Buguruni umegharimu Tshs.300,000,000.00 Ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi kisiwani na ujenzi wa matundu 10 ya vyoo katika shule ya Msingi Hekima umegharimu Tshs. 46,600,000.00 .

16. KATA YA BUYUNI

Kata ya Buyuni ina mitaa nane (8) ambayo ni Buyuni, Zavara, Mgeule, Mgeule juu, Kigezi, Kigezi chini, Taliani na Nyeburu na ina idadi ya wakazi 35,341 wanawake 18,645 na wanaume 16,696. Kata hii imetokana na kugawanywa kwa Kata ya Chanika mwaka 2015

Shughuli kuu za kiuchumi za wakazi wa kata ya Buyuni ni Biashara ndogondogo, Ujasiriamali, Kilimo cha Biashara pamoja na ufugaji kuku.

Miradi ya maendeleo;

Miradi iliyotekelezwa katika Kata hii ni pamoja na ujenzi wa madarasa 2 shule ya msingi nyeburu ambao umegharimu Tshs 34,000,000. Ujenzi wa ofisi ya Kata umegharimu Tshs 118,640,000, Ujenzi wa matundu 12 ya vyoo shule ya msingi Zavara umegharimu Tsh 24,000,000, Ujenzi wa madarasa 2 shule ya msingi Buyuni II umegharimu Tshs 20,000,000, Ujenzi wa matundu 10 ya vyoo shule ya msingi Nyeburu umegharimu Tshs 20,000,000. Kata ya Buyuni ina shule za msingi 5 ambazo ni shule ya Msingi Buyunu II, shule ya Msingi Nyeburu, Shule ya Msingi Kigezi, Shule ya Msingi Mgeule na shule ya Msingi Zavara shule za sekondari zilizopo ni Nyeburu na Buyuni na zote ni za Kata.

17. KATA YA GEREZANI

Kata ya Gerezani ni kata ya mjini iliyopo tarafa ya Kariakoo Kata ya Gerenzani ina mitaa miwili ya kiserikali. Gerezani Mashariki na Gerezani Magharibi. Kata ya Gerezani imepakana na Kata ya Mchafukoge upande wa Mashariki, upande wa Magharibi imepakana na Kata ya Ilala, upande wa Kaskazini imepakana na Kata ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. Kata ya Gerezani ina jumla ya kaya 1816 kwa mujibu wa sensa ya 2012 wanaume ni 3767 na wanawake ni 3509.

Shughuli kubwa za kiuchumi Kwa wakazi wa kata hii ni biashara kubwa na ndogondogo. Pia kuna vikundi vya uzalishaji Mali vya wanaume na vijana zaidi ya 20, Vya ushirika kama DASICO na vya binafsi.

Page 23: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

23

Huduma za kijamii

Kata ina Zahanati moja, Shule mbili(2) za awali Gerezani na Uhuru Wasichana, ina shule za msingi tatu(3) ambazo ni shule ya msingi Gerezani, Uhuru Wasichana na Mchanganyiko. Shule za Sekondari ni nne (4) Benjamini Mkapa, Gerezani, Uhuru Mchanganyiko na Dar es Salaam.

18. KATA YA KARIAKOO

Kata ya Kariakoo ni miongoni mwa Kata kumi zinazofanya kitovu cha Jiji yaani CDB Kata hii ina mitaa mitatu(3) ambayo ni Kariakoo Kaskazini, Kariakoo Magharibi, na Kariakoo Mashariki. Shughuli kubwa za kiuchumi zinazofanyika katika Kata ya Kariakoo ni Biashara (kuuza na kununua madukani), Upangishaji na Upangaji wa nyumba, Ubadilishanaji wa fedha, huduma za Hoteli, Migahawa, Baa na Soko. Kwa mujibu wa sense ya Taifa ya watu na takwimu ya mwaka 2012 ina wakazi wapatao 13,780.

Huduma za kijamii

Kata ina Shule mbili za msingi shule ya Msingi Lumumba inayomilikiwa na serikali na shule ya binafsi moja ambayo ni Qiblatain.

19. KATA YA KIPUNGUNI

Kata ya Kipunguni ni mpya yenye mitaa minne (4) Mtaa wa Kipunguni B, Machimbo, Amani na Kitinye. Jumla ya wakazi katika Kata hii ni 72191 ambapo wanawake ni 29325 na wanaume 42866.

Kata ya Kipunguni ina jumla ya shule sita (6) za msingi shule mbili (2) ni serikali ambazo ni Kipunguni na Kilimani.

Soko kubwa la wafanyabiashara katikati ya Jiji

Page 24: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

24

20. KATA YA KIWALANI

Kata ya Kiwalani ni moja ya Kata 36 zinazounda Halmashauri ya Manipsaa ya Ilala. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Kiwalani ina wakazi wapatao 49422 ikiwa na wanaume 23722 na wanawake 25700 katika kaya 13053. Kata ya Kiwalani imepakana na Kata nne ambazo tatu zipo wilaya ya Ilala na moja ni wilaya ya Temeke. Mnazi mirefu upande wa Mashariki, Vingunguti upande wa Kaskazini, Kipawa upande wa Magharibi, Yombo Vituka imepakana na Temeke upande wa Kusini. Kata ya Kiwalani ina mitaa mitatu ya Utawala ambayo ni mtaa wa Yombo, Mtaa wa Kigilagila, Mtaa wa Kiwalani.

Huduma za kijamii

Kata hii inazo shule Saba (7) za msingi na zahanati nane (8) zahanati mbili (2) ni za serikali na zahanati sita (6) ni za binafsi. Shughuli za kiuchumi katika kata hii ni biashara ndogondogo, ufugaji na kilimo cha bustani.

21. KATA YA MAJOHE

Kata ya Majohe ipo tarafa ya Ukonga Jimbo la Ukonga. Kata ya Majohe ina Mitaa mitano ambayo ni Viwenge, Kivule, Kichangani, Rada na Mjimpya. Kata ya Majohe imepakana na kata ya Gongolamboto, Kivule, Kipunguni, Pugu, Msongola na Buyuni. Kata ya Majohe ina jumla ya watu wapatao 103,397 ambapo wanaume ni 48,520 na wanawake ni 54,872 na jumla ya kaya 24,520.

Shughuli za kiuchumi zinazofanyika katika Kata ya Majohe ni ujasiriamali wa biashara ndogondogo, ufugaji na kilimo cha mbogamboga.

Miradi mikubwa ya kimaendeleo iliyotekelezwa katika Kata hii ni pamoja na Ujenzi wa mradi mkubwa wa maji katika Mtaa wa Kichangani uliogharimu Sh 229,667,087.50. Mradi wa ujenzi wa soko Mtaa wa Rada uko katika hatua za awali.

22. KATA YA MCHIKICHINI

Kata ya Mchikichini inaundwa na mitaa mitatu(3) Mtaa wa Msimbazi Bondeni, Mtaa wa Ilala Kota na Mtaa wa Misheni ina jumla ya wakazi 33,311 kwa mujibu wa sense ya mwaka 2012.

Huduma za kijamii

Kata hii Ina shule moja (1) ya msingi na shule moja (1) ya Sekondari

Miradi ya maendeleo iliyotekelezwa

Miradi mbalimbali ya kuboresha utoaji wa huduma imetekelezwa ikiwemo nukarabati wa jingo la Ofisi ya Kata na ujenzi wa ofisi ya Diwani, ujenzi wa jengo la utawala la shule ya msingi Mchikichini pamoja na ukarabati wa soko la Kigogo Sambusa

Page 25: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

25

23. KATA YA UKONGA

Kata ya Ukonga ni moja kati ya Kata 36 za Manispaa ya Ilala. Kata ya Ukonga ina mitaa mitano ambayo ni Mtaa wa Mwembe Mdafu, Mtaa wa Mazizini, Mtaa wa Markazni, Mtaa wa Mongo la Ndege na Mtaa wa Sabasaba jumla ya wakazi katika Kata hii ni 129,774.

Huduma za Kijamii

Kata ya Ukonga ina jumla ya shule za msingi za Serikali nane (8) ambazo ni Ukonga Jika, Mzambarauni, Gongolamboto, Jeshini na Mongolandege. Vilevile kuna shule za msingi sizizo za Serikali nne (4), shule hizo ni Markaz, Islamic na St Ferese.

24. KATA YA MZINGA

Kata ya imetokana na kugawanywa kwa Kata ya Kitunda mwaka 2015 na ina jumla ya mitatu ambayo ni Mzinga, Mwanagati na Magole upande wa Magharibi inapakana na Kata ya Kivule na kusini inapakana na Kata ya kitunda.Kata ya Mzinga ina jumla ya watu wapatao 38,654 kati yao wanaume ni 18,764 na wanawake ni 19,800 na kaya ni 12,853. Shughuli za kiuchumi

Wakazi wa kata hii wanajishughulisha na kilimo cha mbogamboga na matunda, waajiriwa na Serikali na Taasisi binafsi, ufugaji na biashara. Miradi mbali mbali ya kimaendeleo iliyotekelezwa ni ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Mwanagati, na viwili vya sekondari, Mradi wa maji, Ujenzi wa msingi kituo cha Afya, Ujenzi wa Ofisi ya Kata, Kuweka umeme kisima cha maji magole, na Umailiziaji wa Ofisi ya Mtaa wa Mzinga.

Mchango wa wananchi katika shughuli za maendeleo

Katika kuongeza chachu ya maendeleo katika Kata ya Mzinga, wananchi wamechangia Tshs 4,800,00/= kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Mwanagati kutoka Buza mpaka mpakani mwa kata ya Mzinga na Kitunda, wamechangia kiasi cha Tshs 13,475,650/= kwa ajili ya Ujezni wa Kituo cha Polisi kilichopo Mwanagati, wamechangia Tshs 2,560,000/= kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya mtaa wa Magole na pia wamechangia Tshs 9,000,000/= kwa ajili ya kivuko cha Mtaa wa Magole.

25. KATA YA TABATA

Kata ya Tabata inaundwa na Mitaa nane (8) ambayo ni Tabata, Mandela, Msimbazi, Kisiwani, Tenge, Msimbazi Magharibi, Matumbi na Mtambani. Kijiografia kwa upande wa mashariki inapakana na Kata ya Buguruni, magharibi inapakana na Kata ya Kimanga, kaskazini ni Wilaya ya Ubungo na kusini ni Liwiti na Vingunguti. Kwa mujibu wa sense ya Taifa ya mwaka 2012 kata hii ina jumla ya wakazi 74,742 kati yao wanawake ni 38,833 na wanaume ni 35,909 jumla ya Kaya ni 19,527 kwa makadirio inakadiriwa kuwa na watu 84,000 na Kaya karibia 22,000.

Miradi iliyotekelezwa ni upanuzi wa chumba cha maabara ya zahanati ya Tabata A kwa gharama ya sh. 22,000,000/=.

Page 26: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

26

26. KATA YA VINGUNGUTI

Kata ya Vingunguti imepaka na Kata ya Kipawa, Kata ya Liwiti, Kata ya Mnyamani na Kata ya Minazi Mirefu imeundwa na mitaa sita ambayo ni Mtaa wa Mtambani, Mtaa wa Kombo, Mtaa Kata ya Vingunguti ni miongoni mwa Kata 36 zinazounda Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. wa Majengo, Mtaa wa Mtakuwa, Mtaa wa Miembeni, Mtaa wa Butiama ina jumla ya wakazi wasiopungua 82,169 wanaume 40,542 wanawake 41,627 na idadi ya Kaya 21,868.

Shughuli za Kata hii ni Biashara ndogondogo, Mama Lishe, Baba Lishe, Ushonaji nguo na masofa ya kienyeji, Maduka makubwa na madogo, Shughuli za machinjio, Bodaboda (Usafirishaji). Kata hii ina vikundi mia moja kumi na saba (117), Wanawake vikundi sabini na tisa (79), vijana vikundi thelathini na sita (36), walemavu vikundi viwili (2). Shule ya Sekondari ni moja, Shule za msingi tano kati ya hizo nne ni za Serikali na moja ni binafsi pia Shule za awali zipo tano kati ya hizo nne ni za Serikali na moja ni binafsi.

Pia Kata hii imejenga Ujenzi wa Madarasa, Ukarabati wa Soko la kwa Simba na Ujenzi wa Barabara ya Buguruni kwa Mnyamani, ina Zahanati moja ya Serikali ambayo ni Zahati ya Vingunguti na Zahanati za Binafsi zipo tatu ambazo ni Emara Dispensari, Afya Bora, Mtambani Dispensari.

27. KATA YA ZINGIZIWA

Kata ya Zingiziwa imetokana na kugawanywa kwa kata ya Chanika, upande wa kusini imepakana na Wilaya ya Kisarawe,upande wa kaskazini imepakana na kata ya Chanika,upande wa mashariki inapakana na Kata ya Msongola,upande wa magharibi inapakana na Msitu wa Kazimzumbwi.

Kata hii ina mitaa minne [4] ambayo ni Lubakaya, Zogoalia, kimwani, Gogo, Nzasa, Somela, Zingiziwa, Ngobedi. Ina jumla ya wakazi 75,946 wanaume ni 34,251 wanawake ni 41,695 jumla ya kaya ni 9278. Wakazi wa kata ya Zingiziwa hujishughulisha na kilimo na ufugaji ambapo tayari kuna vikundi vinne(4) vya uzalishaji mazao na vikundi vitatu(3) vya wafugaji.

Huduma za kijamii

Kata ya Zingiziwa ina jumla ya shule tatu [3] za sekondari na shule tano [5] za msingi za serikali.

28. KATA YA JANGWANI

Kata ya Jangwani ina jumla ya Mitaa minne (4) ambayo ni Mtaa wa Ukombozi, Mtaa wa Mnazi Mmoja, Mtaa wa Mtambani A, na Mtaa wa Mtambani B.

Kata ya Jangwani imepakana na Kata ya Kariakoo na Kata ya Mchafukoge upande wa mashariki, Upande wa Magharibi inapakana na Manispaa ya Kinondoni, Upande wa kaskazini inapakana na Kata ya Upanga Magharibi na Upanga Mashariki na Upande wa Kusini inapakana na Kata ya Mchikichini.

Page 27: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

27

Kata ya Jangwani ina jumla ya Shule mbili (2) ambazo ni Shule ya Msingi Mnazi Mmoja na Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja.

29. KATA YA KIMANGA

Kata ya Kimanga Ina mitaa mitano (5) ambayo ni Kimanga, Tembomgwaza, Sokoine, Darajani na Twiga. Ina jumla ya wakazi 56,182 wanaume 26,487 na wanawake 26,695 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.

Huduma za kijamii;

Kata ya Kimanga ina shule za msingi nne (4) za serikali ambazo ni Kimanga A, Tumaini, Kisukuru, na Darajani na shule mbili (2) za binafsi ambazo ni Kamene na Andrews.Pia ina shule mbili(2) za sekondari za binafsi na shule moja(1) ya sekondari ya Serikali.

Miradi ya maendeleo

Kata imewreza kutekeleza miradi ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa matundu (10) ya vyoo katika shule ya msingi Kimanga. Kata imepanga kujenga ofisi ya Kata na stendi ya mabasi Kimanga

30. KATA YA KISUTU

Kata ya Kisutu ina jumla ya wakazi 8308. Kiutawala inaundwa na mitaa miwili (2) Mtendeni na Kisutu.

Shughuli za kiuchumi;

Wakazi wa Kisutu wanajishughulisha na shughuli za Biashara, Ujasiriamali na watumishi wa serikali.

Ofisi ya Klabu ya Yanga

Page 28: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

28

31. KATA YA PUGU STESHENIKata ya Pugu Station ina mitaa mitatu ambayo ni Kichangani, Pugu Station na Mtaa wa Bangulo. Kata hii ina jumla ya wakazi 28,368 ambapo Kichangani wanaume ni 2,700 na wanawake ni 2765 Pugu Station wanaume ni 3,793 na wanawake ni 3,843 Bangulo wanaume ni 7,120 na wanawake 8,147.

Huduma za kijamiiKata ya Pugu imetekeleza miradi ya maendeleo. Jumla ya sh. 307, 254,042/= zimetumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ambayo ni ujenzi wa Ofisi ya Kata Mtaa wa kichangani 121,254,042, Ukarabati wa Ofisi ya Mtaa na ujenzi wa choo Mtaa wa Bangulo umegharimu TShs 10,000,000, Ujenzi wa Zahanati Mtaa wa Bangulo Umegharimu TShs 100,000,000, Ujenzi wa madarasa manne Shule ya Msingi Pugu Station Mtaa wa Pugu Station umegharimu TShs 68,000,000, kuezeka madarasa mawili Shule ya Msingi Bangulo Mtaa wa Bangulo umegharimu TShs 8,000,000.

32. KATA YA ILALA

Kata ya Ilala ina jumla ya wakazi 31,083 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 . Kati ya hao wanaume ni 15,242 na wanawake 15 ,841 jumla ya kaya zilizopo kata hii ni 7771, na jumla ya nyumba ni 2600. Kwa upande wa kaskazini inapakana na Kata ya Kigogo Manispaa ya kinondoni. Ina jumla ya Mitaa.

Huduma za kijamii

Kata ya Ilala ina shule tisa(9) za msingi kati ya hizo shule sita (6) ni za serikali na shule tatu(3) ni za binafsi. Pia katika kata hii zipo shule tano (5) za sekondari ambazo mbili (2) ni za watu binafsi na sekondari tatu (3) ni za serikali;. Juhudi zinaendelea Ili kuwa na Zahanati tayari eneo limekwishapatikana.

Usafiri wa treni kati ya eneo la mjini kati hadi Pugu

Page 29: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

29

33. KATA YA UPANGA MAGHARIBI

Kata ya Upanga Magharibi ni miongoni mwa kata 36 katika Manispaa ya Ilala. Kata ya Upanga Magharibi ina mitaa mitatu (3) Charambe,Fire na Mtaa wa Mfaume. Kata hii imepakana na Bahari ya Hindi kwa upande wa Magharibi. Upande wa Mashariki imepakana na Kata ya Jangwani, Upande wa Kaskazini imepakana na Kata ya Upanga Mashariki, na upande wa Kusini imepakana na Kata ya Hananasifu pamoja na Kata ya Magomeni zote za Manispaa ya Ubungo. Katika Ujenzi huo wa Madarasa mawili ya awali, Shule ya IST imetoa shilingi milioni mbili, laki sita, elfu kumi na tano na mia tisa (Tsh:2,615,000,900) na Tilima alitoa mifuko hamsini (50) ya cement wananchi nao walijitolea nguvu kazi kwenda kuchimba misingi, Mpaka sasa Ujenzi huo wa madarasa ya awali uko katika hatua ya msingi.

34. KATA YA KIPAWA

Kata ya kipawa Ina jumla ya mitaa 6 ambayo ni Mji mpya, Karakata, Uwanja wa Ndege, Mogo, Stakishari, na Kipunguni. Kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012, kata ya kipawa inajumla ya wakazi 74,180 wakiwemo wanaume 35,866 na wanawake 38,314.

Huduma za kijamii

Kata ya kipawa kuna shule za msingi tano na sekondari mbili. Aidha Ina zahanati 12.

Ujenzi wa Kituo cha magonjwa ya milipuko

Miongoni mwa mambo ambayo yametekelezwa ni ukarabati wa kituo cha afya upande wa umeme na maji huku akiendelea na ujenzi wa eneo kwa ajili ya kutumika endapo patatokea magonjwa ya mlipuko na ujenzi huo ukigharimu jumla ya shilingi milioni 300. Ushiriki wa wananchi katika shughuli za kimaendeleo; wananchi wake kwa kujitolea na kushirikiana kujenga barabara za zege ambazo ziligharimu milioni 800. Kadhalika wamefanikiwa kujenga barabara ya Mombe huku huduma ya maji ya Dawasco ikiwa imefika katika mitaa ya kata ya Kipawa na wananchi wamekuwa wakifurahia huduma hiyo.

Kiwanja kipya cha ndege - TERMINAL 3 eneo la Kipawa

Page 30: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

30

35. KATA YA GONGOLAMBOTO

Kata ya Gongolamboto, Ina jumla ya mitaa 4 ambayo ni; mtaa wa Gongolamboto, mtaa Ulongoni A, Ulongoni B, na mtaa wa Gulukakwalala.

Huduma za kijamii;

Kata hii Ina shule za msingi za serikali 6 ambazo ni Ulongoni, mwangaza, maarifa, gulukakwalala, ushindi, na Gongolamboto JICA. Shule za binafsi ni; Highmount, Rugwa, Highlight, na Gofu, comrade Shule za sekondari za serikali ni tatu(3) ambazo ni; Ulongoni, Juhudi A, Juhudi jeshini, shule za binafsi za sekondari ni 2 ambazo ni highview na St. Thomas zahanati za serikali ni mbili (2) . Pia kata ya Gongo la mboto ilifanikiwa kujenga shule ya secondary Juhudi Kwa wanafunzi wa kidato cha tano (5) na sita (6) jambo ambalo limesababisha wanafunzi wa kidato cha nne (4) wanaofanya vizuri kujiunga na shule hiyo. Shughuli za kiuchumi zinazofanyika katika Kata hii ni biashara kubwa na ndogo.

Miradi ya maendeleoKata ya Gongolamboto Kwa kiasi kikubwa imenufaika na barabara za lami zilizojengwa kupitia mradi wa DMDP kwenye mitaa ya kata hiyo jambo ambalo litasababisha maeneo mengi kupitika kwa urahisi hata katika kipindi cha mvua na kupunguza foleni baadhi ya maeneo ya Gongo la mboto pamoja na kuunganisha barabara ya kwenda kinyerezi. Aidha kiasi cha shilingi milion152 kimeelekewa katika ujenzi wa ofisi ya kata hiyo.

Kutokana na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa SGR Shule ya Msingi Mikongeni na zahanati viliathirika hivyo serikali ililipa fidia ya shilingi milioni 800 ambazo zimetumika kujenga madarasa 23 ya kisasa ya shule ya msingi Pugukakwalala. Aidha shilingi milioni 500 zimetolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Gulukakwalala.

36. KATA YA MINAZI MIREFU

Kata ya Minazi Mirefu ni kata mpya iliyotokana na kugawanywa kwa Kata ya Kiwalani ina jumla ya wakazi 39,850 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

Shughuli za kiuchumi katika kata hii ni kilimo cha mbogamboga na vibarua walioajiriwa kwenye viwanda vilivyopo kata kata hii. Kata hii Ina shule moja (1) ya sekondari

Uwezeshaji wa wananchi kiuchumi

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeendelea kuwawezesha wananchi wake kiuchumi kupitia asilimi kumi (10) ya mapato yake ya ndani Kwa kila mwaka. Mgawanyo wa asilimia ni asilimia (10) ni kama ifuatavyo; 4% wanawake, 4% Vijana na 2% Watu Wenye Ulemavu.

Katika kipindi cha miaka mitano (5) 2015 hadi 2020 jumla ya Tshs. 10,709.364,166 zimetolewa Kwa ajili ya kuwezesha wananchi kiuchumi ambapo jumla ya vikundi vilivyopata mkopo ni 2,742 kati yao vikundi 1,699 ni wanawake, vikundi vya vijana ni9 973 na wenye ulemavu vikundi 99. Vikundi mbalimbali kutoka katika kata 36 zimeweza kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo hiyo ambapo wameweza kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya usindikaji wa vyakula, viwanda vidogovidogo (uzalishaji wa bidhaa mbalimbali), Kilimo cha teknolojia Kisasa cha bila udongo (hydroponic farm) usafirishaji na uchukuzi (coster, uba, bajaji na bodaboda). Jumla ya bajaji 247, bodaboda 117, Uba 2, Coster 2 na Canter 1 vimetolewa.

Page 31: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

31

Halmashauri ya manispaa ya Ilala kupitia idara ya afya inafanya usimamizi wa shughuli mbalimbali kwa kushirikiana na timu ya uendeshaji wa huduma za afya ikiongozwa na Mganga Mkuu. Katika kipindi cha miaka mitano ya Serikali (2015-2020), manispaa ya Ilala imejenga vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya vinavyomilikiwa na serikali.

Shughuli za utoaji wa huduma za afya.

Katika kipindi cha mwaka 2015-2020, Hospitali mpya za wilaya 67 zimejengwa zenye thamani ya Shilingi Bilioni 100.5.Ongezeko hili la hospitali 67 zinafanya kuwa na jumla ya hospitali za wilaya 144.

Kati ya hospitali hizo 67 za wilaya zilizojengwa ,mojawapo ni hospitali ya wilaya ya Ilala iliyopo Kivule,ujenzi wa Hospitali hii ni mkakati wa serikal na jitihada zake katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake na kupunguza adha katika kupata huduma za afya.

Ujenzi wa hospitali ya Kivule umekuja kufuatia iliyokuwa Hospitali ya Wilaya ya Amana kupandishwa hadhi na kuwa Hospitali ya mkoa, hivyo Wilaya ya Ilala kukosa Hospitali ya Wilaya jambo lililowalazimu wananchi wa Wilaya hii hususani wanaoishi maeneo ya pembezoni mwa mji kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya katika hospitali ya Mnazi Mmoja.

Kutokana na adha ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya hususani akina mama wajawazito ambao wengi wao wanakuwa kwenye hatari ya kupoteza maisha kutokana na kuchelewa kupata huduma zinazostahili, serikali ya awamu ya tano kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ikaamua kujenga hospitali ya Wilaya iliyopo Kivule.

Ujenzi wa hospitali ya Kivule umelenga kuongeza nafasi kwa ajili ya wagonjwa kupata huduma za afya kwa urahisi, lakini pia ni utekelezaji wa sera ya taifa inayosisitiza kila wilaya kuwa na hospitali yenye hadhi ya wilaya.

Sambamba na hilo,hospitali hii ina madaktari bingwa na wataalamu wenye weledi wa kutosha ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Amana hivyo kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.

Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kivule umesaidia wananchi wa kata mbalimbali zinazoizungua Kata hiyo kunufaika pia huduma za Afya na huduma za kibingwa na rufaa,kama kata ya Msongola,Kitunda,Kipunguni,Majohe na kata ya Mzinga.

Hospitali hii ilianza rasmi kutoa huduma za afya mnamo mwezi June 2020 ,na gharama za ujenzi wa Hospitali hii umegharimu jumla ya Shilingi Bilioni 1.5,fedha kutoka Serikali kuu na unajumuisha majengo saba (7) ambayo ni jingo la utawala,jingo la wazazi,jengo la mionzi,jingo la ufuaji,jingo la stoo ya dawa na jingo la maabara.

HUDUMA ZA AFYA ZABORESHWA.

Page 32: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

32

Sambamba na ujenzi wa vituo vya afya, vituo vya kutolea huduma za afya vinapata mgao wa dawa kutoka bohari kuu ya dawa (MSD) .Vilevile kupitia makusanyo ya fedha yanayopatikana kupitia uchangiaji wa huduma zinazotolea vituo vya afya vimeweza kuendelea kujinunulia dawa muhimu.

Huduma ya Afya ya uzazi na mtoto.

Manispaa ya Ilala kupitia mpango wa Taifa wa kupunguza vifo vya kina mama na watoto iliendelea kutoa huduma bora ya afya ya uzazi na mtoto katika kipindi cha 2015-2020.Katika kuhakikisha mama na mtoto wanapata huduma bora wakati wote, mpango huu ulifanikiwa ulifanikiwa kuvifikia vituo vya kutolea huduma vipatavyo 92 ambavyo vinamilikiwa na serikali na watu binafsi.

Huduma zinazotolewa nampango huu ni pamoja na upimaji wa ukuaji na maendeleo ya mtoto,upimaji wa mam wajawazito sambamba na huduma za uzuiaji wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Vilevile Manispaa ya Ilala katika kipindi cha miaka mitano imerahisisha suala la upimaji na tiba ya magojwa yanayotokana na kujamiiana kama vile kaswende na magonjwa ya malaria kwa mama na wajawazito.

Katika miaka ya nyuma kulikuwa na ongezeko kubwa la magonjwa ya kujamiiana katika jamii.Na kulikuwa na muamko mdogo katika suala la kupima ili kuweza kupata matibabu,kwani kutokana na kasumba iliyopo miangoni mwa wanajamii wengi inaonekana mtu akigundulika na ugonjwa kama kaswende ni aibu kwake .Hivyo endapo atajigundua na ugonjwa huo,hawezi kwenda kituo cha afya kupata matibabu yaliyo sahihi.

Tofauti na sasa ambapo Manispaa ya Ilala kupitia wadau mbalimbali,asasi za kiraia na sekta binafsi zinazojishughulisha na masuala ya afya imekuwa ikitolewa elimu katika jamii kwa njia tofauti tofauti kama majarida mbalimbali,vipeperushi,makongamano na semina mbalimbali juu ya magonjwa mbalimbali ya kujamiiana kama kaswende na kisonono,kuwa ni magonjwa ya kawaida kama magonjwa mengine na endapo mtu atajihisi au kuona ana dalili za magonjwa hayo asijisikie aibu na kujifungia ndani bali afike katika kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu mara moja ili kuweza kupata ushauri wa kitaalam,kupima na hatimaye kupatiwa matibabu yaliyo sahihi endapo atathibitika kuwa na maambukizi ya magonjwa hayo.

Aidha Manispaa ya Ilala imefanikiwa kutoa chanjo Kwa watoto na mama wajawazito kwa kipindi chote cha miaka mitano na pia uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi umekuwa ukifanywa mara kwa mara ili kuweza kubaini dalili ya saratani.

Kutokana na utafiti uliofanywa na shirika la afya duniani (WHO) 2010, inaonesha kuwa Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake wengi duniani.Takwimu zinaonesha kuna wanawake 260,000 duniani kote wanafariki kutokana na saratani hii. Nchini Tanzania, wastani wa wanawake 6241 huugua saratani ya mlango wa kizazi ambapo 4355 kati yao hufa.

Page 33: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

33

Wizara ya Afya, jinsia, wazee na watoto mwaka 2018 ilizindua chanjo ya shingo ya kizazi ambayo hupewa mabinti wa miaka 9-14 ili kuweza kuzuia uwezekano wa kupata maambukizi ya saratani hii.Na toka imeanzishwa imeonesha matokeo chanya kwani kumekuwa na muitikio mkubwa katika jamii kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hii.

Katika kuhakikisha vifo vya akina mama vitokanavyo na saratani vinapungua, Manispaa ya Ilala kupitia Idara ya Afya imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha walengwa wote wa chanjo hizi wanafikiwa kupitia vituo vyote vya kutolea huduma za Afya na kwa muda sahihi.Hii yote inaonesha jinsi gani huduma ya afya ya uzazi ilivyoimarika katika Manispaa ya Ilala.

Kupungua Kwa Vifo vya kina mama na watoto.

Manispaa ya Ilala katika kipindi cha miaka mitano(2015-2010) imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kupunguza vifo vya kina mama na watoto kwani imekuwa ikitoa mafunzo ya mara kwa mara kwa watoa huduma za afya yanayohusiana na utoaji huduma bora na huduma za dharura kwa kina mama wajawazito na watoto.

Kutokana na ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya mwaka 2015/2016 inaonesha kuwa, nchini Tanzania kuna vifo vya uzazi 556 katika kila vizazi hai 100,000.Ili kuweza kufikia malengonya maendeleo endelevu ya millennia kuhusu afya ifikapo mwaka 2030 ya kuwa na raia wenye afya bora,ni jukumu la kila mmoja kuhamasisha akina mama wajawazito kuhudhuria kliniki katika kipindi chote cha ujauzito na kujifungua.

Katika kupunguza vifo vya kina mama na watoto Manispaa ya Ilala kupitia Idara ya Afya, ilitoa vitendea kazi kwa watoa huduma pamoja na kuhakikisha huduma za magari ya kubebea wagonjwa (Amulance) zinatolewa muda wote.Vilevile iliwapatia mafunzo kwa vitendo watoa huduma za afya ya uzazi na mtoto.

Sambamba na hayo ilifanikiwa kuhamasisha akina mama na jamii kwa ujumla umuhimu wa kuanza kliniki mapema na umuhimu wa wajawazito kuwahi hospitali mara wapatapo tatizo na kujifungulia katika vituo vya afya.

Udhibiti wa ugonjwa wa Ukimwi.

Katika kuhakikisha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi yanapungua nchini, serikali imejitahidi kutunga sera na kubuni mikakati mbalimbali. Mwaka 2018 Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alizindua mkakati maalum wan ne wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI 2018/19-2022/23 ukiwa na lengo la kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75% ifikapo 2020 na asilimia 85% ifikapo mwaka 2023.Vilevile mkakati huo ulizinduliwa kwa lengo la kupunguza vifo vinavyohusiana na Ukimwi kwa asilimia 50% ifikapo mwaka 2020 na asilimia 70% ifikapo mwaka 2023 na kupunguza unyanyapaa na ubaguzi ifikapo 2023 na kuelekea utokomeza kabisa ifikapo 2030.

Page 34: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

34

Mwaka 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kupitia kamati ya Ukimwi ilifanikiwa kutoa elimu Kwa wanajamii hususani vijana juu ya ugonjwa wa Ukimwi, kuhamasisha matumizi ya kinga (condom) katika nyumba za wageni n.k.

Vilevile Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, mashirika na sekta tofauti tofauti kwa kiwango kikubwa imefanikiwa katika utoaji na ufuatiliaji wa dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARV’S) na kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.Huduma hizi hutolewa chini ya usimamizi na uratibu wa Wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa kushirikiana na tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania.

Magonjwa ya Mlipuko.

Manispaa ya Ilala imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na homa ya dengue.Upuliziaji wa dawa wa mara kwa mara katika vyoo na sehemu zote zinazoweza kuzalisha wadudu,ulikuwa ukifanyika ili kuweza kuua vimelea vya wadudu wanaoweza kuambukiza magonjwa ya mlipuko.

Vilevile Manispaa ilifanikiwa kufanya ukaguzi wa majengo ya vyakula ili kuhakikisha hali ya usafi katika majengo inakuwepo muda wote.Aidha elimu ya afya juu ya udhibiti wa ugonjwa wa kipindupindu ilikuwa ikitolewa mara kwa mara hivyo kuifanya jamii kuepukana na shughuli zote zinazoweza kupelekea mlipuko wa magonjwa hayo.

Kwa ujumla Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kipindi cha miaka mitano yaani 2015-2020 imefanikiwa sana kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake lengo kuu ikiwa ni kuwa na jamii yenye ustawi na afya bora kwani wananchi hawawezi kuwa na afya duni wakawa na uwezo wa kufanya kazi.Ili kuendana na falsafa ya “Hapa kazi tu”, inatakiwa wananchi wawe na afya njema.Ndio maana serikali inajitahidi kutoa huduma bora za afya ili wananchi waweze kufanya kazi kwa bidii bila kikwazo chochote.

Page 35: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

35

Ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya kimkakati

Ukarabati wa madarasa - S/Msingi G/Mboto Jica

HABARI PICHA

Shule mpya - S/Msingi Kibadeni

Bweni la wasichana - Jangwani

Page 36: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

36

Utoaji wa Elimu kwa wakulima na wafugaji - NANENANE 2020

Utoaji wa elimu kwa wanafunzi wa shule ya awali

Maumbo ya Kilimo cha mjini

Page 37: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

37

Madarasa - S/Msingi Kibadeni

Madarasa - S/Sekondari Bonyokwa

S/Sekondari Minazi Mirefu

S/Msingi Kimwani

Vyoo - S/Msingi Vikongoro

Page 38: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

38

Kituo cha mafunzo ya wakulima na wafugaji - Kinyamwezi

Ofisi ya walimu - S/Msingi Kinyamwezi Annex

Ofisi ya walimu - S/Msingi Kimwani Ofisi ya walimu - S/Msingi Buyuni

Page 39: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

39

Wa kwanza Kulia Mkurugenzi akimkabidhi Mwekahazina (katikakati) funguo na kadi za magari ya kukusanyia mapato, wa kwanza kushoto ni Afisa Usafirishaji wa

Manispaa

“Ambulance” - Hospitali ya Mnazi Mmoja Magari ya kukusanyia mapato

Ujenzi wa soko jipya la Kisutu

Page 40: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

40

Na Mariam HassanNi wazi kuwa tokea Mh. Dkt. John Pombe Magufuli kuingia madarakani, Serikali ya awano ya tano ilianza utekelezaji wa ahadi ya Rais ya kuhusu elimu bure waTanzania wengi wamekua na muamko wa kuwaandikisha watoto wao katika shule za Msingi..

Kupitia sera hiyo ya Elimu bure, Serikali imehakikisha wananchi wake wamefuta ujinga kwa kwenda kuwaandikisha watoto wa kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba. Kutokana na hiyo sera Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeshirikiana na Serikali ya awamu ya tano ili kufikia uchumi wa kati wa nchi kwa kuhakikisha wanafunzi wengi wanajiunga darasa la kwanza mpaka la saba.

Sera ya elimu bure imefanya wanafunzi wengi wa elimu ya msingi kufaulu vizuri kwenda kidato cha kwanza mpaka cha nne kutokana na uboreshaji wa miundombinu kama madarasa, madawati, vyoo, majengo ya utawala na kufanya elimu msingi kupata mafanikio mengi kwa kipindi cha miaka mitano kama anavyoeleza Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala Bi. Elizabeth Thomas.

Uandikishaji wa wanafunzi waongezeka

“Uandikishaji wa wanafunzi katika kipindi cha miaka mitano (2015-2020) umeongezeka kwa asilimia kubwa. Uandikishaji kwa wanafunzi darasa la kwanza mwaka 2015 tuliandikisha wanafunzi elfu ishirini na moja mia saba sabini na nane (21778) kulinganisha na sasa mwaka 2020 ambapo tuliandikisha wanafunzi elfu thelathini mia nane na sitini na saba (38067)”

Ongezeko la Shule

Bi. Elizabeth Thomas anaendelea kusema kuwa kumekua na ongezeko la shule katika kipindi hiki cha miaka mitano (2015-2020).

“Shule za awali zimeongekeza kwani mwaka 2015 kulikua na shule 83 lakini sasa 2020 kuna shule za awali mia moja na ishirini (120). Shule za msingi nazo zimeongezeka kutoka mia moja kumi na moja (111) mwaka 2015 mpaka shule mia mia moja na ishirini na moja (121) vilevile kulikua na vitengo vitano vinavyotoa elimu maalum lakini sasa kuna vitengo kumi na mbili vinavyotoa elimu kwa walemavu.

MAKALA YA ELIMU MSINGI

Page 41: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

41

Ongezeko la ufaulu kwa darasa la saba

“Mwaka 2015 ufaulu ulikua asilimia 82 lakini mpaka mwaka 2019 ufaulu umeongezeka mpaka asilimia 93. Pia kwa upande wa darasa la nne ufaulu unaendelea kuongezeka kila mwaka. Kutokana na ufaulu huu Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inaonekana kufanya vizuri katika mitihani hiyo ya kumaliza Elimu Msingi.

Kutokana na hayo mafanikio katika Idara ya Elimu Msingi imefanya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa kioo cha maendeleo katika Halmashauri nyingine za ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa na kuifanya Manispaa kujizolea tuzo nyingi za ufaulishaji wanafunzi pamoja na michezo kimkoa, kiwilaya, na kitaifa pia kuwa mfano bora wa kuigwa na Manispaa nyingine.

Ongezeko la samani na miundominu

Bi. Elizabeth Thomas anasema kumekua na ongezeko la samani katika kipindi hiki cha miaka mitamo (2015).

“Idadi ya madarasa imeongezeka kwani mwaka 2015 kulikua na madarasa 1465 lakini mpaka kufikia 2019 kulikua na madarasa 1822.

Page 42: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

42

Vyoo vya wanafunzi mwaka 2015 vilikua 2034 ila mpaka kufikia 2019 vilikua 3524. Vyoo vya walimu mwaka 2015 vilikua 30 mpaka kufikia 2019 vilikua 79. Kwa upande wa ofisi za walimu mwaka 2015 zilikua 56 ila mpaka mwaka 2019 ofisi zilikua 82 na nyumba za walimu mwaka 2015 zilikua nyumba 150 lakini mpaka sasa 2019 nyumba ziko 158”

Upande wa michezo

Katika miaka mitano 2015-2020 imeshinda michezo ya Umitashumta mkoa mara nne pia imeshinda usafi wa mazingira mara nne kimkoa.

Page 43: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

43

Asubuhi kumekucha, na jua linachomoza,

Kila kilichojificha, nuru inakiangaza

Macho nikiyapekecha, siwezi kuona giza

Hongera Mkurugenzi, na wako wasaidizi

Sitaki kusema sana, nisije nikajikweza

Nimeyaona bayana, mengi mkitekeleza

Mmefanya kwa mapana, ilani kutekeleza

Hongera Mkurugenzi, na wako wasaidizi

Hii awamu ya Tano, kweli mmefanya kazi

Kuongeza makusanyo, mnahitaji pongezi

Ilala ni ya mfano, Manispaa ya kazi

Hongera Mkurugenzi, na wako wasaidizi

Nimetembea Kivule, Chanika hadi Kigezi

Niliyoyaona kule, mwasitahiki pongezi

Tena nawapa kongole, ubora wa yenu kazi

Hongera Mkurugenzi, na wako wasaidizi

Bilioni Miambili, ambazo mmekusanya

Mjionee fahari, kwa kazi mliyofanya

Hii ni njema shughuli, moyoni inapopenya

Hongera Mkurugenzi, na wako wasaidizi

Ujenzi wa madarasa, barabara Zahanati

Mkautengea pesa, mradi wa Vingunguti

Vibovu vyenye makosa, vyote mmekarabati

Hongera Mkurugenzi, na wako wasaidizi

Miradi ya madaraja, maji na makaravati

Kinyerezi kwa Muhoja, Majohe na Mwanagati

Ulongoni jino moja, sasa wamepanda chati

Hongera Mkurugenzi, na wako wasaidizi

Shule mmeshazijenga, msingi na sekondari

Mipango mliipanga, kutekeleza kwa hari

Kariakoo Upanga, Ukonga-Sitakishari

Hongera Mkurugenzi, na wako wasaidizi

Kusini Kaskazini, pande zote Tanzania

Utendaji wa makini, wote wameuelewa

Kwa kweli jipongezeni, Ilala Manispaa

Hongera Mkurugenzi, na wako wasaidizi

Nina ya kusema mengi, wino umeniishia

Mliyoyafanya mengi, mfano mnatiliwa

Bidii, kazi sipingi, heri ninawaombea

Hongera Mkurugenzi, na wako wasaidizi

Mtunzi: Shabani M. Yusuph

Afisa Mazingira

Manispaa ya Ilala

SHAIRI: HONGERA MKURUGENZI NA WAKO WASAIDIZI

Page 44: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

44

UTOAJI WA ELIMU YA SEKONDARI Na Mariam Hassani,

Mafanikio ni neno lenye maana pana na maana sawa na neno Maendeleo , kwa tafsiri tunaeza sema ni kupiga hatua moja kwenda nyingine . Maana halisi ya mafanikio inategemea unazungumzia mafanikio ya kitu gani inaweza kuwa ya binafsi, kiuchumi, kiteknolojia, kijamii kwa tafsiri hiyo ni kwamba kila aina ya mafanikio itakua na maana yake ambayo ni mahususi kwa maana hiyo tu .

Lakini unawezaje kuzungumzia au kuyapata mafanikio ya kitu bila kuyahusisha na Elimu, ili mtu aweze kuboresha maisha yake au kupata mafanikio lazima awe na elimu ya kitu hivyo Elimu ndio kitu cha msingi ambacho kinamuwezesha mtu kujitambua na kufikia malengo au mafanikio ya kitu Fulani.

Aidha , Ili elimu iweze kuleta mabadiliko ya kweli ya kimaendeleo ni lazima iwe bora hivyo Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kupitia Idara yake ya Elimu Sekondari imekuwa ikibuni mikakati mbalimbali ili kufanikisha malengo iliyojiwekea katika utoaji wa elimu kulingana na Sheria, Kanuni, Taratibu, na Miongozo mbalimbali iliyopo. Hadi sasa Idara hii imepata mafanikio mengi kwa kipindi cha miaka mitano (5) 2015-2020 kama anavyoelezea Kaimu Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilala, Bw. Stephen Petro

‘Uboreshaji wa Miundombinu na Samani’

Kwa miaka mitano (2015-2020) tulikuwa na shule 49 ila kwa sasa tuna shule 54, vyumba vya madarasa vimeongezeka kwa asilimia 50%, vyoo navyo vimeongezeka kwa asilimia 30% pia shule zilizojengwa zimekidhi kiwango cha elimu bure kwa wananchi pia ongezeko la madawati limeongezeka kwa asilimia 60%.

‘Ongezeko la wanafunzi mashuleni’

Tangu kuanza kwa elimu bure bila malipo tumefanikiwa kuwa na ongezeko la wanafunzi mwaka 2015 tulikuwa na wanafunzi elfu arobaini na tatu mia nane ishirini na tisa (43829) lakini mpaka kufikia sasa 2020 tuna wanafunzi sabini na moja elfu na saba (7107).

‘Ufaulu umeongezeka kwa kiasi kikubwa’

Kwa ujumla matokeo ya Mtihani wa kumaliza Elimu Sekondari na vyuo umeongezeka kwa kipindi cha miaka mitano (2015-2020) ufaulu kwa kidato cha pili (2015) ulikuwa ni asilimia 87.5% lakini mpaka (2019) ulifikia asilimia 91.81%, upande wa kidato cha sita (2015) ulikuwa asilimia 66.46% lakini mpaka (2019) ufaulu ulifikia asilimia 75.2%, upande wa kidato cha sita (2015) ulikuwa asilimia 96% lakini mpaka (2019) ufaulu ulikuwa 98%.

Kwa upande wa michezo UMISETA tumefanikiwa kufanya vizuri katika ngazi mbalimbali Kimkoa, Kiwilaya na Kitaifa

Mafanikio hayo katika Idara ya Elimu Sekondari imefanya Idara za Manispaa nyingine kuiga mfano kutoka kwa Manispaa ya Ilala kwa kuwa kufanya vizuri sana na kuwa mfano bora wa kuigwa kwa kutekeleza vizuri ilani ya Serikali kwa kufuata maagizo yote ya Mheshimiwa Rais.

Page 45: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

45

Na Mwandishi Wetu

Nchini Tanzania, Sekta ya Kilimo ni muhimili wa maendeleo ya uchumi. Sekta hii inachangia kiasi cha nusu ya pato la Taifa na hivo kuifanya sekta ya muhimu nchini na kwa kulitambua hilo, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kupitia idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika imehakikisha inatoa mafunzo, fursa na uboreshaji wa miundominu kwa wakulima.

Katika kipindi cha miaka mitano (2015-2020), Manispaa ya Ilala kupitia Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza majukumu yake katika upande wa kilimo ambayo ni kuhamasisha, kutoa ushauri na mafunzo kwa wakulima kuhusu kilimo cha mjini, teknolojia za kisasa zinazotumika katika kilimo na pia kuboresha miundombinu kwaajili ya wakulima na kuhakikisha wanafanya kilimo chenye tija ili kujiinua kimaisha.

MAFANIKIO YA SEKTA ZA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA

Jengo la Kituo cha Kata cha Rasilimali Kilimo Kinyamwezi ambalo limejengwa kwa makadirio ya gharama ya shilingi 109,337,161 Fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri

Page 46: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

46

Upande wa Ushirika: Ushirika umesaidia kukuza na kupatikana mitaji ya wajasiriamali walio sekta rasmi na isiyo rasmi, kuanzishwa kwa biashara ndogo na kubwa, kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo, kustawisha sekta ya uchukuzi na usafirishaji, kuimarisha masoko ya mazao ya mifugo na kilimo cha mjini pamoja na kuongeza ajira rasmi na zisizo rasmi.

Katika kipindi cha miaka mitano (2015-2020) kumekua na ongezeko la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) kutoka Vyama 201 mwaka 2015/2016 mpaka Vyama 277 mwaka 2019/2020 ambalo ni ongezeko la 27.4%. Pamoja na hayo, Idadi ya wanachama waliojiunga na kunufaika na huduma za SACCOS imeongezeka kutoka idadi ya wanachama 82676 Mwaka 2015/2016 hadi kufikia idadi ya wanachama 114919 mwaka 2019/2020 ambapo ni ongezeko la 39%. Pia Hisa/mtaji wa wanachama uliowekezwa umeongezeka kutoka Tshs.4,548,192,424/= Mwaka 2015/2016 hadi kufikia Tshs 4,925,736,552 mwaka 2019/2020 ambalo ni ongezeko la 8.3%.

Aidha, akiba/uwekezaji wa wanachama umeongezeka kutoka Tshs.83, 730,280,132/= Mwaka 2015/2016 hadi kufikia Tshs 92,705,833,735/= mwaka 2019/2020 ambalo ni ongezeko la 10.7%. Mikopo iliyotolewa kwa wanachama wa vyama vya Akiba na Mikopo imeongezeka kutoka Tshs. 117,531,423,706 Mwaka 2015/2016 hadi kufikia Tshs. 132,227,855,247 Mwaka 2019/2020 ambapo ni ongezeko la asilimia 4.8%

Vilevile Idara iliandaa mafunzo Kwa wanachama 90850 ambapo walipata elimu ya ushirika kulinganisha na mwaka 2015/2016 ambapo wanachama waliopata mafunzo walikua 62007 tu.

Ofisi ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika imepanga kuendeleza mafanikio yaliyopatikana kwa muda wa miaka 5 iliyopita ili kuyaendeleza na kuyaboresha kwa kiwango cha 50% kwa miaka 5 ijayo.

Washiriki kutoka vyama ya Ushirika Manispaa ya Ilala katika mafunzo ya kujijengea uwezo

Page 47: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

47

Na Hashim Jumbe

Kupitia lengo namba moja la kutokomeza umasikini lililomo kwenye ajenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, Serikali zinahimizwa kutafuta mbinu mbadala kuwawezesha wananchi kupitia miradi mbalimbali kujikwamua na umasikini ifikikapo mwaka 2030.

Tanzania ni nchi mojawapo ambapo Serikali imechukua jukumu la kutoa elimu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na kutoa muongozo kwa wananchi na kuwapatia fursa za ujasiriamali kupitia miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji wa nyuki.

Katika kipindi cha miaka mitano (2015-2020) Manispaa ya Ilala kupitia kitengo cha nyuki kimefanikiwa Kwa kiasi kikubwa kutimiza malengo iliyojiwekea pamoja na kusimamia utekelezaji wa sera ya nyuki katika Halmashauri na kutoa mafunzo kwa wafugaji juu ya mbinu za kisasa

Kaimu Mkuu wa kitengo Bi. Nitikey Mwakabende anasema kuwa katika miaka mitano hii waliweza kutoa elimu kwa wafugaji wa nyuki wengi kulinganisha na miaka ya nyuma.

“Manispaa ya Ilala ina maeneo machache ya ufugaji wa nyuki kutokana na ukuaji wa haraka wa mji hivyo tuliweza kutoa elimu kwa wafugaji ikiwemo kutoa huduma za ugani kwa Jamii katika Manispaa ya Ilala ambapo jumla ya watu 306 walipata mafunzo ya ufugaji nyuki kwa njia za kisasa.

Vilevile tuliweza kuwapa elimu ya njia mbalimbali za ufugaji wa nyuki. Ufugaji sio lazima uwe kwenye mizinga unaweza kufuga kwenye magudulia, kwenye mbao, magogo nk. Kwahiyo huwa tunawasihi kuwa wasiogope kuingia kwenye ufugaji wa nyuki kwani ni ufugaji usio na gharama kabisa” alisema bi. Mwakabende.

Shughuli za ufugaji nyuki zilizotekelezwa

Moja ya mashamba yanayofuga nyuki katika Manispaa ya Ilala ni Shamba la mfano lililo chini ya Manispaa lililopo Zingiziwa ambapo ndani ya shamba hilo kulitekelezwa miradi ifuatayo

Ujenzi wa banda moja la nyuki

Ununuzi wa mizinga ya nyuki 25

Ujenzi wa choo kimoja kwaajili ya wafanyakazi na wageni

Kutengeneza barabara kwenye mipaka ya shamba kwaajili ya tahadhari ya moto.

LENGO NAMBA MOJA LA KUTOKOMEZA UMASIKINI 2030

Page 48: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

48

Mashamba mengine ya ufugaji wa nyuki yaliyopo katika Manispaa ya Ilala ambayo ni ya watu binafsi ni Pugu Stesheni ambapo kuna mashamba 2, yaliyokuwa chini ya vikundi vya Vikoba na Mazingira lenye mizinga 6 na lingine likiwa chini ya Mazingira na Ufugaji nyuki lenye mizinga 10. Pia kikundi Women Life Foundation kilichopo Tabata kina mizinga 2, Mama Gogomoka wa Msongola mwenye mizinga 10, Joseph Manzi wa Chanika mwenye mizinga 30 pamoja na Obadia Kweba Chanika Nzasa mwenye mizinga 5 na kufanya jumla ya mizinga ya nyuki kuwa 88.

Mavuno ya asali na nta:

Asali na Nta ni mazao yatokanayo nyuki. Je wajua kuwa Nta ni zao la nyuki litokalo katika mwili wa nyuki kwenye matezi yaliyopo katika sehemu ya chini ya tumbo la nyuki kibarua. Na haitokani na mimea? Pia nta hutumika Kama malighafi katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kama vile mishumaa, polishi ya samani, viatu, vipodozi na kadhalika hivyo kuifanya iwe bidhaa adhimu.

Mwaka 2016 jumla ya lita 880 za asali zilivunwa zenye thamani ya sh.6, 880,000/= na nta lita 344 yenye thamani ya sh.4, 472,000/=. Mwaka 2017 jumla ya lita 860 zilivunwa zenye thamani ya sh.8, 600,000/= na nta lita 344 yenye thamani ya sh. 4,472,000/=. Mwaka 2018 lita zilizovunwa ni 860 zenye thamani ya sh.10,320,000/= na nta lita 430 zenye jumla ya sh. 6,450,00/= na mwaka 2019 zilipatikana lita 880 za asali zenye thamani ya sh.10,560,000/= pamoja na nta lita 440 zenye thamani ya sh.6,600,000/=

Ndugu Paul Nyangwa ambaye ni mfugaji lakini pia ni mjasiriamali wa mazao ya nyuki kutoka Pugu Stesheni anasema kuwa ufugaji wa nyuki hasa uuzaji ya asali na nta umemsaidia kwa kiasi kikubwa kujikwamua kimaisha.

Banda ya nyuki lililo chini ya Manispaa lililopo Msongola

Page 49: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

49

“Ufugaji wa nyuki na uuzaji wa asali umenisaidia kwa kiasi kikubwa kujikwamua. Nimeweza kujenga nyumba na pia nawasomesha wanangu kwa biashara hii hii. Lakini ukiacha uuzaji wa asali pia ninatengeneza mizinga na kuwauzia watu. Kwahiyo natoa ushauri kuwa watu wasiogope kuwekeza kwenye biashara hii kwani ukiwa mvumilivu mafanikio yapo”

Kwa mafanikio haya ni wazi kuwa kitengo cha nyuki cha Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kimefanikiwa kwa asilimia kubwa katika kipindi hiki cha miaka 5 (2015-2020) katika kutoa mafunzo na kuboresha miundombinu na kuhakikisha wafugaji wanatekeleza shughuli zao.

Page 50: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

50

Na Rodney Malongo

Askari Polisi waliomaliza kozi ya mafunzo ya uongozi wa Polisi Wasaidizi wamemshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ndg. Jumanne Shauri kwa kuwapeleka kwenye mafunzo na kumuahidi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa.

Akitoa shukrani hizo kwenye ofisi ya Mkurugenzi kwa niaba ya polisi hao, Staff Sergeant Christian Mwanjonde alisema kuwa wanashukuru kwa kupata mafunzo hayo kwani yatawasaidia kuwajengea uwezo na ufanisi kazini.

“Mafunzo yalienda vizuri na wote tumemaliza na tumerudi salama. Idadi ya Wahitimu Polisi Wasaidizi waliopandishwa vyeo kutoka Sergeant kwenda Staff Sergeant ni wawili na waliopandishwa kutoka Koplo kwenda Sergeant ni wanne.” alisema Staff Sergeant Christian Mwanjonde

Waliopandishwa kutoka Sergeant kwenda Staff Sergeant ni AP 1104 S/Sgt Christian Mwanjonde na AP 870 S/Sgt Adamu F. Tesha. Waliopandishwa kutoka Koplo kwenda Sergeant ni AP 849 Sgt Ayoub L. Chale, AP 852 Sgt Osward M. Musasa, WAP 1108 Sgt Neofila J. Kali na WAP 1105 Sgt Jane J. Lyimo.

Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ndg. Jumanne Shauri aliwapongeza polisi hao kwa kumaliza mafunzo na kuahidi kuzidi kuwapeleka wengine nao wakapate mafunzo.

Mafunzo hayo yalianza rasmi tarehe 31/08/2020 na kumalizika tarehe 02/10/2020 huko Kidatu mkoani Morogoro yakiwa na lengo la kuwajengea askari uwezo ili kuongeza ufanisi kazini sambamba na kuwapandisha vyeo.

ASKARI POLISI WAMSHUKURU MKURUGENZI KWA KUWAPELEKA KWENYE MAFUNZO

ULINZI NA USALAMA

Page 51: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

51

BARAZA LA MADIWANI 2015-2020

Page 52: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

52

DMDPDar es Salaam Metropolitan Development Project

Barabara ya Chacha

Soko la Bombom

Kisima cha maji - Mongolandege

Page 53: S Sa laJARIDA LA AUTI YA ILALA · 2021. 1. 18. · ilala_manispaa sau ti ya ila la 1 #ilala t upov izur i miaka mitano ya mafanikio ya awamu ya tano . hos pit ali ya wil aya kivul

Sau t i y a I l a l a

54

SIMU NA: 21288002128805

FAX NA: 2121486

OFISI YA MKURUGENZI1 MTAA WA MISSIONS.L.P 20950DAR ES SALAAM

M U O N E KA N O WA M AC H I N J I O YA K I S A S A - V I N G U N G U T I

I l a l aTup oVizu r i

Ilala MunicipalIlala Municipal#[email protected] f