Upload
ilala
View
337
Download
6
Embed Size (px)
DESCRIPTION
Manispaa ya Ilala yazindua kampeni ya usafi
Citation preview
1
HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu wananchi
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala katika kutekeleza jukumu la
kuweka mazingira safi ya eneo lake imekuwa ikikabiliana na
changamoto mbalimbali za uchafuzi wa Mazingira. Changamoto
hizo zimesababisha kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko kama
kipindupindu na kuharisha. Pamoja na changamoto hizo shughuli
za usafi wa Mazingira katika Manispaa ya Ilala zinaendelea
kutekelezwa kulingana na sheria na taratibu. Hivyo kila
mwananchi anapaswa kuzingatia sheria na taratibu hizo za
kutunza Mazingira.
Kama nilivyoeleza kuwa zipo changamoto zinazozuia jitihada za
kuiweka Manispaa katika hali ya usafi miongoni mwa hizo ni hizi
zifuatazo; uchafuzi wa Mazingira unaotokana na vyombo vya
usafiri, uoshaji holela wa magari, utupaji ovyo wa taka,
2
uunganishaji wa maji taka katika mifereji ya wazi, magari mabovu
yaliyoegeshwa kwa muda mrefu, ujenzi usiofuata taratibu ambao
husababisha miundombinu ya maji ya maji ya mvua kushindwa
kufanya kazi. Maelekezo yanatolewa kuwa kila chombo cha
Usafiri wa Umma na watu binafsi kinatakiwa kuwa chombo cha
kutupia taka na abiria yeyote katika chombo cha usafiri haruhusiwi
kutupa taka nje. Atakayebainika kutupa taka nje atachukuliwa
hatua yeye binafsi na chombo chake cha usafiri.
Kwa wamiliki wa magari wote wanashauriwa kupeleka magari
yao katika maeneo yaliyoruhusiwa (Washing bay). Adhabu
itatolewa kwa yeyote atakayebainika kuosha gari katika
sehemu isiyoruhusiwa. Muda wa siku saba (7) unatolewa
kuanzia tarehe 1/12/2015 kwamba wenye wagari mabovu
wawe wameondosha magari hayo.
Nachukua fursa hii kuwafahamisha kuwa, atayekiuka taratibu za
usafi na kusababisha uchafuzi wa Mazingira atachukuliwa hatua za
kisheria ikiwemo kulipa faini ya papo kwa papo. Kwa mara
nyingine Manispaa inasisitiza kuwa, mwananchi yeyote
atakayesadia kumkamata mchafuzi wa Mazingira atalipwa asilimia
hamsini ya faini iliyotozwa kutoka kwa mchafuzi huyo.
3
Jitihada za kujenga uelewa wa masuala ya usafi wa mazingira kwa
wananchi zinaendelea ambapo Manispaa imeanzisha utaratibu wa
matangazo ya mtaani kwa kutumia gari maalum la matangazo.
Vilevile kwa kutumia vipindi vya television na redio ambapo
makosa ambayo yanayosababisha mtu kupewa adhabu ya uchafuzi
yamekuwa yakibainishwa na inaaminika kuwa elimu inayotolewa
inajenga uelewa kwa kila mwananchi kulinda na kutunza
mazingira yanayomzunguka.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inao mkakati endelevu wa usafi
na Mazingira. Mkakati huu unalenga kubadili sura ya Jiji la Dar es
Salaama ili liwe lenye mazingira safi na salama, pia unalenga kwa
kila mwananchi kujiona kuwa anawajibika moja kwa moja katika
Mkakati huu. Aidha mkakati unahimiza kuwa na wakandarasi
walio na uwezo wa kutoa huduma iliyo bora ya kusafisha na
kuzoa taka inayozingatia viwango.
Kutokana na siku ya maadhimisho ya siku ya uhuru tarehe 9
Disemba, kuelekezwa itumike kwa shughuli za usafi na utunzaji
wa Mazingira maandalizi yamefanyika na shughuli za kusafisha
mazingira zimeanza katika kata zote za Manispaa ya Ilala. Kila
mtendaji wa mtaa, na kata kwa kushirikiana na kamati zao za usafi
na Mazingira, wametakiwa kuandaa utaratibu wa kusafisha
4
maeneo yao. Kila mkazi wa Manispaa hii anaelekezwa
kushirikiana na wananchi wenzake kuhakikisha anasafisha
mazingira yanayo mzunguka na kwamba zoezi hili ni endelevu.
Manispaa ya Ilala inaendelea kuwakumbusha wananchi wake
kuwa, kwakuwa tayari tumetangaziwa kuwepo mvua za El nino na
Wataalamu wa hali ya Hewa, ambazo zitanyesha maeneo
mbalimbali ya nchi hii ikiwemo na maeneo ya Jiji la Dar es
salaam Tunawahimiza wananchi wote wa Manispaa hii kusafisha
mifereji na mitaro ya maji ya mvua inayowazunguka. Halmashauri
kwa kushirikiana na taasisi mbali mbali imeanza kusafisha
mifereji na mitaro yote ya maji ili kuepuka mafuriko yasiyokuwa
ya lazima. Shime Wanachi mnasisitizwa kutotupa taka ovyo katika
mifereji ya wazi ili kuepusha kuziba kwa mifereji hiyo.
Asanteni kunisikiliza
Isaya M. Mngurumi
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala