9
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA TAARIFA YA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI NDG: PAUL C. MAKONDA KWA WAANDISHI WA HABARI 28 th -February-2015 Ndugu waandishi wa habari kwanza ninashukuru sana kwa kuitikiwa wito wangu wa kuzungumza nanyi leo.Kama mnavyojua,ni siku chanhe tu tangu nilipoteuliwa na nimeona vyema nipate muda wa kuwaeleza mambo kadhaa kwa undani ili kuleta uelewa mpana kwa wanakinondoni ili tuweze kufanikisha dhamira yetu ya kujiletea maendeleo. Kusudi langu kubwa katika muda wote nitakaokuwa hapa kama mkuu wa wilaya ni kuona kuwa wananchi wa Kinondoni wanapiga hatua katika nyanja mbalimbali za maendeleo na haki inatendeka katika uendeshaji wa shughuli zetu za kila siku. Katika kufanikisha azma yangu pamoja na watendaji wengine wa wilaya ya Kinondoni;mipango nitakayoitekeleza itagawanywa katika ile ya muda mfupi, mipango ya kati na mipango ya muda mrefu.Ningependa 1 OFISI YA MKUU WA WILAYA KINONDONI 1 MTAA WA MINAKI, S. L. P. 9583, 14881 DAR ES SALAAM. WILAYA YA KINONDONI Anwani ya Simu: 2170169/2170183 Unapojibu tafadhali Taja:

Taarifa Ya Mkuu Wa Wilaya Ya Kinondoni Kwa Waandishi Wa Habari

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Taarifa Ya Mkuu Wa Wilaya Ya Kinondoni Kwa Waandishi Wa Habari

Citation preview

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAOFISI YA WAZIRI MKUUTAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

WILAYA YA KINONDONIAnwani ya Simu: 2170169/2170183Unapojibu tafadhali Taja:Kumb. Na. AB.22/236/01/40OFISI YA MKUU WA WILAYA KINONDONI1 MTAA WA MINAKI,S. L. P. 9583,14881 DAR ES SALAAM.27 Februari, 2015

TAARIFA YA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI NDG: PAUL C. MAKONDA KWA WAANDISHI WA HABARI 28th-February-2015Ndugu waandishi wa habari kwanza ninashukuru sana kwa kuitikiwa wito wangu wa kuzungumza nanyi leo.Kama mnavyojua,ni siku chanhe tu tangu nilipoteuliwa na nimeona vyema nipate muda wa kuwaeleza mambo kadhaa kwa undani ili kuleta uelewa mpana kwa wanakinondoni ili tuweze kufanikisha dhamira yetu ya kujiletea maendeleo.Kusudi langu kubwa katika muda wote nitakaokuwa hapa kama mkuu wa wilaya ni kuona kuwa wananchi wa Kinondoni wanapiga hatua katika nyanja mbalimbali za maendeleo na haki inatendeka katika uendeshaji wa shughuli zetu za kila siku.Katika kufanikisha azma yangu pamoja na watendaji wengine wa wilaya ya Kinondoni;mipango nitakayoitekeleza itagawanywa katika ile ya muda mfupi, mipango ya kati na mipango ya muda mrefu.Ningependa kuyazungumzia maeneo sita yafuatayo kama ndio dira ya utendaji kazi kwa wakati huu.1.ARDHIKinondoni ni moja ya wilaya ambayo inakabiliwa na changamoto kubwa sana ya migogoro ya ardhi.Asili ya migogoro hii inatokana hasa na mgongano wa uhalali wa umiliki pamoja na uvamizi wa maeneo ya wazi yaliyotengwa maalumu kwa shughuli za jamii. Changamoto hii ni ya muda mrefu na natambua juhudi nyingi zilizofanyika katika kutatua hili.Moja ya mkakati wangu ni kufanya utatuzi unaohusisha taasisi zote muhimu ili kufupisha mlolongo unaowapotezea muda walioko kwenye migogoro na kuhakikisha mwenye haki anapewa haki yake bila kuyumbishwa.Ili kufanikisha hilo ninatangaza rasmi kuitenga siku ya kila iumaa kuwa siku maalumu ya kukutana na wananchi na kusikiliza matatizo yanayohusiana na Ardhi.Utaratibu huu utaanza tarehe 6 mwezi wa 3,na zoezi la uandikishaji wa wale wanaohitaji kusikilizwa matatizo yao utaanza saa 3 kamili asubuhi.Ili kupata ufumbuzi usio na shaka kamati ndogo itakayohusika katika kushughulikia matatizo haya itaundwa na -Mimi Mwenyewe nkiwa kama mwenyekiti-Katibu tawala wilaya(DAS) akiwa ni katibu-Mwanasheria wa Manispaa-Afisa Mipango miji-Afisa ArdhiIli kufanya zoezi hili liwe na ufanisi na mafanikio ningeomba wananchi wafuate utaratibu kuanzia ngazi za watendaji wa chini kabla ya kufikisha katika ofisi yangu na pia kila muhusika ahakikishe amekuja na vielelezo vyote halali vinavyoweza kutumika katika kufikia uamuzi.

2.MAJIChangamoto ya upatikanaji wa maji katika wilaya ya kinondoni inazidi kukua kutokana na ukuaji wa kasi wa idadi ya watu na ubadhirifu unaofanywa na baadhi ya watu kwa kujiunganishia maji isivyo halali na pia kuharibu miundo mbinu ya maji.Mara tu nilipoingia ofisini nimeviagiza vyombo husika kutathmini changamoto zilizo katika miundo mbinu yetu kunakosababisha upotevu wwa asilimia 54 ya maji yote yanayosambazwa katika wilaya ya Kinondoni.Pia mkakati maalumu umeshandaliwa wa kuwatambua,kuwaumbua na kuwachukuliwa hatua za kisheria wale wote waliojiunganishia maji kinyume cha taratibu na sheria. Nimewaagiza DAWASCO kwa kushirikiana na viongozi wa mtaa kuanza zoezi la kutambua wahujumu wa miundo mbinu ya maji mara moja.Ili kuendelea kubaini changamoto zinazotukabili na kutafuta njia mbadala za kutatua,tarehe 10 Marhi tutakuwa na ziara maalumu kutembelea maeneo yanayozalisha maji ya mitambo ya Ruvu na Mlandizi. Hii itatusaidi kupata ufumbuzi wa kudumu wa changamoto zinazotukabili. 3.ELIMUKati ya maeneo ambayo Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekuwa akiyapa msisitizo sana ni eneo la Elimu.Na ni vyema tukatambua kuwa elimu ni muunganiko wa Walimu,Maabara,WanafunzI,Majengo na Vitabu.Kama wilaya tumepiga hatua sana kwani mwaka 2005 tulikuwa na shule za sekondari 5 na kwa sasa tuna sekondari 49,hii ni hatua kubwa sana.Kila siku zinavyokwenda,wastani wa mwalimu kwa wanafunzi unazidi kupungua.Ingawa kwa sasa wastani wetu wa 1:65 uko juu kuliko maeneo mengi. Hii ni kutokana na ukweli kuwa Wilayah ii ni kivutio kwa wananchi wenngi kutoka maeneo mbalimbali ambao wanahamia Wilayani hapa kwa sababu za kiuchumi na kufuata huduma nzuri za kijamii. Bado tunafanya juhudi ya kufikia wastani unaokubalika wa mwalimu 1 kwa wanafunzi 45(1:45).Kwenye eneo la vitabu tumeendelea kujiimarisha na hivi karibuni tumepokea vitabu 77,280 ambavyo vimepelekea uwiano wa vitabu vya hesabu na mwanafunzi uwa 1:1 na ule wa vitabu vya hesabu na baiolojia kuwa 1:2.Kama tunavyotambua kuwa Mh.Rais amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha ujenzi wa maabara kwa ajilil ya mafunzo ya vitendo kwa masomo ya sayansi. Hii ni muhimu kwa kuwa katika kuelekea uchumi wa kati kama dira ya maendeleo ya Taifa 2025 inavyosema,ni muhimu kujenga wigo mpana wa wataalamu wa mambo ya sayansi. Idadi kubwa ya wanafunzi wapatao 402500 katika wilaya ya kinondoni inaashiria umuhimu wa kipekee wa kuongeza kasi ya ujenzi wa maabara pia. Ili kufanikisha azma hii nitaendelea kuweka msukumo wa ujenzi wa maabara zaidi kwa kuzingatia kuwa tangu kuanza kwa kampeni hii ya ujenzi wa maabara halmashauri imetumia takribani bilioni 4.7 katika ujenzi wa maabara 126. Katika miezi mitatu ijayo tunakusudia kukamilisha ujenzi wa maabara katika shule zote za kinondoni.Katika kufanikisha azma ya kuwa na walimu wenye motisha katika wilaya yetu,nitaendelea kuwa mstari wa mbele na kusukuma hoja za walimu katika kuwapatia mambo yao muhimu.

4.AFYA NA USAFIKama wilaya tunakabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye sekta ya afya zinazohitaji kufanyiwa kazi kwa haraka. Kwa kushirikiana na wataalamu wa halmashauri tutaanda mpango wa pamoja(comprehensive plan) ili kutambua na kuyatafutia ufumbuzi matatizo yaliyokubuhu katika eneo hili.Wilaya ya Kinondoni inakabiliwa na changamoto kubwa ya uchafu.Ningependa kupongeza kampeni na mikakati iliyofanywa huko nyuma katika kuhakikisha kuwa tatio la uchafu linatatuliwa. Tatizo kubwa linalotukabili kwa sasa ni umbali kati ya dampo la Jiji lililopo Pugu Kinyamwezi na mahali takataka zinapotoka. Ukizingatia jiografia ya wilaya yetu baadhi ya maeneo ni umbali wa kilometa 60 au zaidi hadi dampo. Hiki ni kikwazo kikubwa katika juhudi zetu za kusafisha Manispaa yetu. Katika kukabiliana na hilo tumeanza kutafakari pamoja na mamlaka nyingine za wilaya namna tunavyoweza kubadilisha taka kuwa bidhaa zenye thamani kama vile mbolea ama karatasi.Teknolojia ya namna hii inapatikana na itaifanya taka kuwa kitu cha thamanai kama ambavyo chupa za plastiki zimekuwa za thamani.Mara baada ya kujadiliana kwa kirefu na wataalamu husika taarifa rasmi itatolewa namna ya ufanikishaji wake. 5.BARABARABado kumekuwa na changamoto kubwa ya barabara katika wilaya ya kinondoni inayosababisha misongamano na wakati mwingine baadhi ya barabara kushindwa kupitika kabisa.Katika kukabiliana na tatizo hili nimekusudia kufanya mambo mawili ya msingi:Moja ni kushughulikia kwa kikamilifu miundombinu inayoambatana na barabara(mitaro);kuanza kuikarabati kabla ya kipindi cha mvua hakijaanza.Pili ni kufanya matengenezo na kuendeleza ujenzi wa barabara za mchepuko(feeder roads) ili kupunguza msongamano katika barabara kuu.Ningependa kutumia fursa hii kutoa wito kwa wananchi wanaoishi mabondeni kuhama mara moja ili kuepusha maafa yanayoweza kuwakabili katka majira ya mvua.6.AJIRA NA MICHEZO.AjiraKatika ajira kusudi langu kubwa ani kubadilisha mtazamo wa wafanyabiashara wadogowadogo watambue kuwa chochote wanachokifanya leo ni njia yao ya kuelekea katika ndoto zao kubwa. Hii itamaanisha kuchukulia biashara zao kwa umakini na kuheshimu kazi hiyo.Mtazamo huu utakapofanikiwa juhudi zangu kubwa zitakuwa katika kuwaandalia program mbalimbali katika makundi yao husika(Vijana,Wazee,Wanawake n.k) ili kuwapatia mafunzo mahsusi kulingana na taaluma zao.Kundi la wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kwa jina la wamachinga,kwa kushirikiana na watendaji wakuu wa halmashauri(Mstahiki Meya na Mkurugenzi) tunawaandalia mkakati wa maalumu wa kuboresha biashara zao utakaowafanya kuwa marafiki na sio maadui wa serikali yao. Hii ni pamoja na kuendelea kuboreshwa kwa masoko yaliyopo sasa kwa kufanywa ya kisasa zaidi, kujengwa masoko mengine mapya na upanuzi wa soko la kisasa la sim2000. Hatua hizi zitaongeza uwezo wa Manispaa wa kuwa na nafasi nyingi zaisi kwa wajasiriamali kwa wilaya yetu.MichezoKatika juhudi za kuendeleza michezo katika wilaya ya Kinondoni kutakuwa na mashindano maalumu ya Kinondoni Cup yatakayohusisha kuanzia ngazi ya chini.Kwa ushirikiano maalumu wa vyama vya michezo ya wanaume na ile ya wanawake hivi karibu wapenzi wa michezo watatangaziwa rasmi ufunguzi wa mashindano mbalimbali.Katika vipaji vya Muziki mkakati maalumu wa kuwasaidia vijana ambao tayari wana nyimbo zao ila wamekosa uwezo wa kurekodi ,watashindanishwa na 20 watakaokuwa bora watapata nafasi ya kufadhiliwa kupelekea kufanya rekodi na pia kuwatangaza katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni.Mchakato huu mzima utahusisha watendaji wa wlaya ya kinondoni,mashirika mbalimbali na watu binafsi.

Ningependa kumalizia kwa kusema kuwa;mafanikio ya shughuli za kila siku za kinondoni zinategemea sana na uhodari wa watumishi wa umma katika nyanja za walimu,askari,makarani n.k.Nikiwa kama kiongozi wa wilaya ningependa sana kuwa na muda maalumu pamoja na watumishi wa umma ili kujadili mambo yanayowahusu wao kwa umaalumu wao.Mara baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya mkakati huu,awamu itakayofuata itakuwa na lego kubwa la kuwafikia kundi hili.Mwisho kabisa napenda kuwashukuru waandishi wote wa habari,na napenda kuchukua nafasi hii kuomba ushirikiano wenu katika kuwaletea wananchi wa Kinondoni maendeleo.Mungu Ibariki Africa,Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Kinondoni,Ahsanteni kwa kunisikliiza.

1