16
1 W aziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe ameitambulisha Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Mamlaka kwa wafanyakazi na kuitaka Mamlaka kutoa ushirikiano ili kuboresha utendaji kazi. Dk. Mwakyembe alitoa rai hiyo katika mkutano wake na wafanyakazi uliofanyika Bandari ya Dar es salaam katika Ghala la Nafaka hivi karibuni. Bodi hiyo mpya yenye wajumbe nane itafanya kazi chini ya Mwenyekiti wake Bw. Raphael Mollel. Wakurugenzi wengine wa Bodi ni Bw. Said Salum Sanko, Bw. John Ulanga, Bw. Jaffer Machano, Eng. Julius Mamiro, Dk. Hilderbrand Shayo, Dk. Jabir Kuwe Bakari, Bi Caroline Temu Kavishe na Bi Asha Nassoro. Akinukuu Waziri Mwakyembe alisema Ripoti ya Benki ya Dunia (WB) Bandari ya Dar es salaam ndiyo inayofanya vibaya zaidi katika Bandari zote TANZANIA PORTS AUTHORITY www.tanzaniaports.com | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email: [email protected] Toleo Namba 16 21 - 27 Januari, 2013 Na Mwandishi Wetu Inaendelea Uk. 2 Ukaguzi wa abiria kwenda ZNZ lazima Uk. 7 Dar Port yaendeleza mvua ya vikombe mara tatu mfululizo Uk.11 EU yaridhishwa na utendaji Bandari ya Dar es Salaam Uk.5 Ili kutatua kero hizi na kuifanya Bandari ifanye kazi kwa ufanisi Dk. Mwakyembe aliwataka wafanyakazi kushirikiana na Bodi mpya, huku akiahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili. za ukanda wa Afrika Mashariki huku ikigubikwa na tuhuma za urasimu, wizi na vitendo vya rushwa. ENEO LA MAPOKEZI NI KWA AJILI YA WAGENI Wafanyakazi wanakumbushwa kwamba eneo la Mapokezi ni kwa ajili ya Pia ikumbukwe ni wajibu wa kila mfanyakazi kujali wageni wetu kwa kutoa kauli nzuri na Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na wafanyakazi wa TPA. Picha Uk. 3

TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

1

����������������� ���������������

Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe ameitambulisha Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Mamlaka kwa wafanyakazi na kuitaka Mamlaka kutoa ushirikiano ili kuboresha utendaji kazi.

Dk. Mwakyembe alitoa rai hiyo katika mkutano wake na wafanyakazi uliofanyika Bandari ya Dar es salaam katika Ghala la Nafaka hivi karibuni.

Bodi hiyo mpya yenye wajumbe nane itafanya kazi chini ya Mwenyekiti wake Bw. Raphael Mollel. Wakurugenzi wengine wa Bodi ni Bw. Said Salum Sanko, Bw. John Ulanga, Bw. Jaffer Machano, Eng. Julius Mamiro, Dk. Hilderbrand Shayo, Dk. Jabir Kuwe Bakari, Bi Caroline Temu Kavishe na Bi Asha Nassoro.

Akinukuu Waziri Mwakyembe alisema Ripoti ya Benki ya Dunia (WB) Bandari ya Dar es salaam ndiyo inayofanya vibaya zaidi katika Bandari zote

TANZANIA PORTS AUTHORITY

www.tanzaniaports.com | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email: [email protected] Toleo Namba 16 21 - 27 Januari, 2013

Na Mwandishi Wetu

Inaendelea Uk. 2

Ukaguzi wa abiria kwenda ZNZ lazima

Uk. 7 Dar Port yaendeleza mvua ya vikombe mara tatu mfululizo

Uk.11EU yaridhishwa na utendaji Bandari ya Dar es Salaam

Uk.5

Ili kutatua kero hizi na kuifanya Bandari ifanye kazi kwa ufanisi Dk. Mwakyembe aliwataka wafanyakazi kushirikiana na Bodi mpya, huku akiahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

za ukanda wa Afrika Mashariki huku ikigubikwa na tuhuma za urasimu, wizi na vitendo vya rushwa.

ENEO LA MAPOKEZI NI KWA AJILI YA WAGENIWafanyakazi wanakumbushwa kwamba eneo la Mapokezi ni kwa ajili ya

Pia ikumbukwe ni wajibu wa kila mfanyakazi kujali wageni wetu kwa kutoa kauli nzuri na

Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na wafanyakazi wa TPA. Picha Uk. 3

Page 2: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

2

Uteuzi

Inatoka Uk. 1

“Nina imani na Bodi hii mpya, nawasihi mshirikiane nayo, na mfanye kazi kwa bidii ili kurudisha heshima ya Bandari,” alisema Waziri huku akishangiliwa na wafanyakazi.

Kuhusu tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa Bandari ya Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe aliahidi kuzishughulikia ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wafanyakazi wote wanaohusika na vitendo viovu iwapo itathibitishwa hivyo.

“Hakuna atakayeonewa, tutachunguza na ikithibitika

kuna tatizo, wahusika watashughulikiwa.

Dk. Hilderbrand ShayoBi. Caroline Temu Kavishe

Bw. John Ulanga

Bw. Jaffer MachanoEng. Julius MamiloMakamu Mwenyekiti wa Bodi

Dk. Jabir Kuwe Bakari Bi. Asha Nassoro

Bw. Raphael MollelAliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi

Page 3: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

3

Elimu

Bw. Said Salum Sauko

kiwango kimeongezeka kutoka bilioni 28 kwa mwezi hadi bilioni 42 kwa mwezi huku ikitarajiwa kuwa mapato hayo yataongezeka.

Katika mkutano huo Wafanyakazi walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali na kupatiwa majibu ya ufafanuzi kutoka kwa Mhe. Waziri, Menejimenti pamoja na viongozi wa DOWUTA waliohudhuria mkutano huo.

Baadhi ya tuhuma zinazowakabili wafanyakazi waliosimamishwa kupisha uchunguzi ni pamoja na kufungua kampuni zao binafsi, kuzipatia zabuni za kuhudumia bandari na kuingia mikataba upya bila kufuata sheria.

Waziri Mwakyembe alipongeza hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Menejimenti kuongeza ufanisi na ukusanyaji wa mapato ambapo hivi sasa

Sehemu ya wafanyakazi wakimsikiliza Mhe. Waziri wa Uchukuzi.

Page 4: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

4

Elimu

Wahitimu ambao ni wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari katika Idara ya Uhandisi na Utekelezaji wakiwa katika picha ya pamoja katika mahafali ya 13 ya

Chuo cha Bandari wa kwanza kushoto ni Esau Challe, Ahmed Kipande, Hassan Ahmed, Edius Kinunda, Kennedy Mweisabula, Stella Mutayabalwa, na Nuhu Urio.

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari waliohitimu kozi ya Stashahada ya Shipping and Port Management katika chuo cha bandari wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutunikiwa vyeti vyao. Wakwanza kushoto ni Esau Challe, Asha Jabir, Hidaya Ramadhani, Esther Mushi, Celina Saimon, Edesius Elias Kinunda,, Fatuma Kajugus na Zuhura Nyarubindo wote kutoka idara ya Utelekezaji bandari ya Dar es Salaam.

�������

Na Mwandishi wetu

Chuo cha Bandari k i n a t e g e m e a kuanza kutoa

mafunzo katika ngazi ya Shahada ya Kwanza (Bachelor’s degree) katika fani za “Shipping and Port Management” na “Maintenance Management”.

Mpango huu unategemewa kuanza rasmi kipindi cha mwaka wa masomo cha 2013/2014 - 2014/2015.

Wakati huohuo chuo hicho kinategemea kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka

wanafunzi 1,300 hadi 1,800 mara baada ya kudahili wanafunzi wa kozi mbalimbali katika ngazi ya cheti mwezi Machi, 2013.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Bandari, Bw. Kassim Chamshama wakati wa Mahafali ya 13 ya Chuo yaliyofanyika katika viwanja vya chuo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

“Chuo cha Bandari hivi sasa kina idadi ya wanafunzi 1,300 na tunategemea idadi hii

Inaendelea Uk. 8

Page 5: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

5

Pongezi

Umoja wa Ulaya (EU) umepongeza jitihada zilizofanywa na Mamlaka kufanyia kazi mapendekezo mbalimbali ambayo waliyoyatoa Oktoba mwaka 2011 kuboresha ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.

Pongezi hizo zimetolewa na Balozi wa EU, Filiberto Sebregondi kwa niaba ya ujumbe wa mabalozi na kundi la wafanyabiashara 23 wakati walipotembelea Bandari hiyo.

Mbali na kusifu hatua zilizochukuliwa, Balozi Filberto Sebregondi pia alisifu taarifa ya TPA kwa kuielezea kuwa imejitosheleza na imebainisha vizuri hatua zilizochukuliwa

kutekeleza mapendekezo ya umoja huo wakati wa ziara yao ya awali.

“Tumefurahi kuona mambo mengi ambayo tulishauri yafanyiwe kazi mwaka jana yamepatiwa ufumbuzi na sisi tunaridhika na hali ilivyo sasa tungependa wafanyabiashara, wanaotumia Bandari hii nao wapate fursa ya kutoa maoni yao kuhusu uboreshaji zaidi

ili kuifanya Bandari hii kuwa ni kituo chenye ushindani na ufanisi zaidi,” amesema Sebregondi.

Ziara hiyo iliyojumuisha mabalozi wa EU na wafanyabiashara pia ililenga kuangalia utoaji wa huduma na usalama wa abiria wanaosafi ri kati ya Dar es Salaam na Zanzibar ambapo ujumbe huo ulitembelea eneo la abiria wanaokwenda Zanzibar na kujionea utaratibu mzuri uliopo wa abiria wa kwenda Zanzibar.

Ujumbe wa EU ulibaini changamoto mbalimbali zilizokuwa zinaikabili Bandari ya Dar es Salaam mwaka jana ikiwa ni pamoja na muda mrefu wa kutoa mzigo, matumizi ya kalamu na karatasi badala ya Tehama mambo ambayo yamefanyiwa kazi na kupelekea kuongezeka kwa ufanisi.

Naye Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe aliwahakikishia mabalozi hao kwamba Wizara na Mamlaka tayari zimekwishachukua hatua madhubuti kuboresha Bandari kama vile kuhakikisha usalama wa abiria na mizigo na upimaji wa mizigo na usimamizi

Na: Focus Mauki

Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akiwaongoza Mabalozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya hapa nchini (EU) walipotembelea Bandari ya Dar es Salaam.

Inaendelea Uk. 6

Page 6: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

6

Pongezi

wake, kudhibiti uwezo wa boti kusafi risha abiria, ulinzi na ukaguzi unaofanywa kwa mashine za kisasa pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara wa boti za kusafi risha mizigo.

“Tumefanya maboresho makubwa sana katika Bandari hii kama vile kupunguza muda wa kuhudimia meli, matumizi ya vifaa vya kisasa, kufunga mashine ya ukaguzi wa abiria, kuweka maboya ya kutosha ya uokozi na kubwa zaidi ni kuboresha sheria zetu ili kila jambo linalofanyika lifuate sheria,” alifafanua Waziri.

Sheria yetu hairuhusu kusajili meli yenye umri wa zaidi ya miaka 15 na sasa kule Zanzibar sheria kama hii itaanza kutumika rasmi ili tuwe na uwiano.

“Kule Zanzibar hakuna sheria ya kutosajili meli yenye umri wa zaidi ya miaka

15, muswada upo katika Baraza la Wawakilishi na tunategemea mwakani

Januari au Februari utajadiliwa ili tuwe na uwiano sawa wa sheria hii kwa bara na visiwani,” aliongeza Dk. Mwakyembe.

Katika kipindi cha mwaka mmoja Mamlaka imefanikiwa kuboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kupakia na kupakua mizigo.

Ili kuongeza kasi ya kuhudumia mizigo Mamlaka inatumia mifumo mbalimbali ya mtandao wa kompyuta (ICT) kama vile ‘Harbour view system’ ambao umeanza kufanya kazi tangu Juni 2010, mfumo wa ‘Cargo sytem’ ulioanza kufanya Aprili 2011 na ‘Billing sytem’ ambao unaotumika tangu Januari 2011.

Mbali na haya kumekuwepo na hatua za kuelimisha umma na hasa wateja kuwasilisha nyaraka sahihi za mzigo mapema zifanyiwe kazi kabla ya mzigo husika haujafi ka bandarini kampeni inayofahamika kama ‘dokumenti kwanza mzigo baadae’.

Mamlaka pia imechukua hatua za kufanya kazi kwa muda wa saa 24 ili kuendana na kasi ya ongezeko la mzigo kuongeza ufanisi.

Kwa upande wa vifaa vya utendaji kazi TPA mpaka sasa imenunua kreni 3, Reach stackers 3, Empty handlers 4, trekta kubwa 6, terminal trekta 4, matrela ya kubeba kontena 12 pamoja na mashine moja ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7 hadi kufi kia ICD 9 zote zikiwa na uwezo wa kuhudumia kontena 11,730.

Bandari kavu (CFS) kwa ajili ya kuhudumia magari nazo zimeongezeka kutoka 3 zikiwa na uwezo wa kuhudumia magari 4,950 hadi kufi kia 4 zenye uwezo wa kuhudumia magari 5,250.

Mamlaka pia imeongeza eneo la NASACO linalofahamika kama

Meneja Utekelezaji wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Patrick Namahuta (mwenye njano) akifafanua jambo kwa Mabalozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya walipotembelea Bandari ya Dar es Salaam kujionea utekelezaji unavyofanyika. (wa pili kulia) ni Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe na kushoto ni aliyekuwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Joseph Msaky.

Inatoka Uk. 5

Inaendelea Uk. 16

Page 7: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

7

Usalama

Abiria wote watakaosafi ri kwenda Zanzibar pamoja na mizigo yao watalazimika kukaguliwa kwa kutumia mashine ya kisasa ili kudhibiti usalama wao pamoja na wa mizigo.

Mashine hiyo ambayo imeanza kutumika kwa muda mrefu sasa inasimamiwa na Kitengo cha Ulinzi cha Mamlaka ambapo ukaguzi utafanyika kwa abiria pamoja na mizigo yote kabla ya kuruhusiwa kuendelea na safari.

Matunda ya mashine hii ni jitihada za Mamlaka kuboresha huduma zake pamoja na usalama wa abiria wote wanaotumia meli kwenda Zanzibar.

Na: Mwandishi wetu

Mashine hiyo aina ya Smiths Heimann X-ray imefungwa katika eneo la kuingilia abiria bandarini.

Abiria ataingilia geti kubwa ambapo atafanyiwa ukaguzi wa kawaida wa tiketi, kitambulisho chake na baadae atalekea katika mlango wa kuingilia chumba kilichofungwa mashine hiyo.

Lengo la kufungwa kwa mashine hii ni kuboresha huduma ya usafi ri wa majini kwa kuimarisha

ulinzi na usalama wa abiria pamoja na mizigo yao.

Kutokana na matumizi ya mashine hii wasafi ri wote watapaswa kukata tiketi zao mapema angalau saa moja kabla ya safari na mara baada ya kukata tiketi waelekee moja kwa moja katika milango ya ukaguzi.

Mashine hii inatumika kwa utaratibu kama ule uliopo katika viwanja vyetu vya ndege ambapo pia huu ni utaratibu wa kawaida katika maeneo mengine mbalimbali ulimwenguni wenye lengo la kuimairsha ulinzi na usalama wa abiria pamoja na mizigo yao.

Mashine hii inatarajiwa kuboresha huduma kwa kupunguza muda wa ukaguzi wa abiria na mizigo yao, lakini kubwa zaidi kuhakikisha Bandari yetu inapitisha mizigo salama kwa abiria na mali zao.

Vifaa vyote vya hatari kama vile silaha za moto, visu pamoja na aina zote za bidhaa za milipuko havitaruhusiwa isipokuwa kwa vibali maalumu.

Page 8: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

8

Pongezi

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dk. Harrison Mwakyembe ameipongeza Kamati ya kuboresha Bandari ya Tanga kwa jitihada zake za kuboresha Miundombinu ya reli na barabara ili mizigo iweze kupitishwa kwa wingi kupitia bandari

ya Tanga.

Dk. Mwakyembe aliyasema hayo alipokutana na wadau mbalimbali wa Kamati ya uboreshaji wa bandari ya Tanga katika hoteli ya Mkonge mjini Tanga.

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya uboreshaji wa bandari ya Tanga Bwana Isdory Temba alimuomba Waziri awafahamishe sababu

zinazopelekea ucheleweshwaji wa uendelezaji wa Bandari mpya ya Mwambani, kwani wamekaa muda mrefu bila kujua nini kinachoendelea katika utekelezaji wake.

Bwana Temba na Kamati yake iliomba uboreshwaji wa miundombinu ya reli ili irahisishe kusafi risha mizigo kupitia bandari ya Tanga.

itaongezeka kufi kia wanafunzi 1,800 wakati tutakapoanza kudahili wanafunzi wa kozi mbalimbali katika ngazi ya cheti mwezi Machi mwaka 2013,” alisema Bw. Chamshama.

Chamshama ameongeza kwamba pamoja na mafanikio ya ukuaji wa idadi ya wanafunzi na mitaala husika chuo kinakumbana na changamoto mbalimbali kama vile upungufu wa vyumba vya madarasa, bwalo la kulia chakula, ukumbi wa mikutano na viwanja vya mafunzo na michezo.

Idadi ya wahitimu na kozi katika mabano ni wahitimu

131 (Stashahada ya “Shipping and Port Management”),

Akijibu hoja hiyo Waziri alisema “mikakati ya kuijenga bandari mpya ya Mwambani inafanyika na pia Serikali ina mikakati ya kuboresha miundo mbinu hiyo ya reli na inafanyiwa kazi hivyo naomba muwe na subira”. Alimalizia Dkt. Mwakyembe na kuiomba Kamati hiyo kuendelea na kutafuta mbinu zaidi za kuboresha bandari ya Tanga.

Na Cecilia Korassa

Inaendelea Uk. 16

Inatoka Uk. 4

wahitimu 23 (Stashahada ya “Engineering Maintenance”), na wahitimu 29 (Stashahada ya “Clearing Forwarding and Port Management”).

Katika ngazi ya Cheti, yaani Basic Technician Certifi cate kulikuwa na kozi nne ambapo idadi ya wahitimu ilikuwa 215 (“Basic Technician in Shipping and Port Operations”), wahitimu 56 wa (“Basic Technician Certifi cate in Clearing Forwarding and Port Operations”, wahitimu 60 (“Basic Technician Certifi cate in Public Relations and Marketing”) na wahitimu wa 3 wa (“Basic Technician Certifi cate in Engineering Maintenance”).

Chuo cha Bandari kimesajiliwa na Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA) na vilevile Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi yaani National Council for Technical Education (NACTE). Kutokana na kusajiliwa huko Chuo kimeweza kutoa mafunzo kuanzia ngazi ya kwanza hadi ya tatu chini ya VETA na ngazi ya nne yaani “NTA level 4, 5, na 6” chini ya NACTE.

Naye mgeni rasmi katika mahafali hayo Mkurugenzi wa Ofi si ya Rais (Utumishi), Bw. William Ngunda amekipongeza chuo kwa jitihada zake za kuhakikisha kinaendesha kozi nyingi za uhakika pamoja na kuvutia walengwa wengi zaidi.

Page 9: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

9

Wastaafu

EX-NASACO maalumu kwa ajili ya kuhudumia kontena.

Mbali na matumizi ya Kurasini Oil Jet (KOJ), Mamlaka imeanza kutumia boya jipya la Single Point Mooring (SPM) ambalo lina uwezo wa kuhudumia mafuta kwa kiwango cha tani 150,000, boya hili limeanza kufanya kazi rasmi Novemba 15.

Katika kujali muda wa wateja wake Mamlaka pia imeanzisha kituo kimoja cha kuhudumia wateja ambacho kinafahamika kama ‘One Stop Centre’.

Kuendeleza Michezo

Mkuu wa Bandari ya Tanga Bwana Awadhi Masawe amewashukuru wafanyakazi wastaafu katika bandari hiyo kwa mchango walioutoa bandarini hapo wakati wa utumishi wao huku akiwasihi kutumia vema

mafunzo waliyopata ili kujinufaisha kimaisha.

Washiriki wa semina walifundishwa jinsi ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu, elimu kuhusiana na mikopo, ujasiriamali,uwekezaji,matumizi ya fedha za pensheni na elimu juu ya mifuko ya hifadhi za jamii.

Akisoma risala kwa niaba ya wastaafu Bi Rita Mzee aliushukuru uongozi nzima wa Bandari kwa kuwapatia mafunzo waliyoyaelezea kuwa ni mchango mkubwa baada ya kustaafu, huku wakiomba mafunzo kama hayo yawe endelevu kwa wastaafu wajao.

Mkuu wa Bandari ya Tanga Bwana Awadhi Masawe alifunga mafunzo hayo kwa kuwatunukia vyeti wastaafu hao na kuwasifu kwa mahudhurio mazuri.

Na Jackson Kaheza – Mwanafunzi mafunzo kwa SAUT

Inatoka Uk. 6

Mkuu wa Bandari ya Tanga Bwana Awadhi Massawe akimkabidhi cheti cha kuhitimu Semina ya Wastaafu Bibi Joyce Mtaua wa Idara ya Rasilimali Watu Bandari ya Tanga.

Maboresho haya yote pamoja na mengine yameongeza tija katika Bandari ya Dar es Salaam kama vile kupunguza muda wa Meli kupakia au kupakua mzigo, kontena, magari na bidhaa nyingine. Ili kuhakikisha mizigo ya wateja inakuwa salama Mamlaka inatekeleza mkataba wa ‘ISPS code’ na kuhakikisha yale yote yanayopendekezwa yanatekelezwa ili kufi kia vigezo na masharti ya mkataba huo na kuifanya Bandari kuwa salama.

Page 10: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

10

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wamebainisha kuwa Bandari ya Dar es Salaam ni kiungo muhimu cha soko la Afrika Mashariki.

Hayo yalisemwa na Mh. Abubakar Zam Abubakar ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya mahusiano na nchi jirani na utatuzi wa migogoro iliyoteuliwa na Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wakati wa ziara fupi katika Bandari ya Dar es Salaam.

Ziara ya wabunge hao katika Bandari ya Dar es Salaam ilikuwa na dhumuni la kukagua utekelezaji wa itifaki ya soko la pamoja ikiwa ni pamoja na kujua changamoto mbalimbali zinazoikumba Bandari ya Dar es Salaam katika shughuli zake za utekelezaji.

“Tumeamua kuja kujionea wenyewe ili kujifunza na kufahamu changamoto katika utekelezaji wa itifaki ya soko la pamoja ili bunge kupitia kamati iliyounda iweze kujua na kujadili changamato hizo na kuzitafutia ufumbuzi” alisema Mh. Makongoro Nyerere.

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Meneja wa Bandari Bi. Apolonia Mosha Meneja wa Bandari Msaidizi (Utekelezaji) Bibi Winnie Mulindwa, alishukuru

Na: Innocent Mhando

Masoko

Kaimu Meneja wa Kitengo cha Mafuta cha Kurasini Oil Jetty (KOJ) Capt. Andrew Matillya akifafanua jambo kwa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki walipofanya ziara fupi Bandari ya Dar es Salaam.

Page 11: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

11

Masoko

Kamati hiyo kwa kutembelea Bandari na kueleza kwamba Mamlaka iko katika mpango wa kuboresha huduma zake kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ubadilishaji wa mfumo wa Boya la kupakua mafuta (SPM) Mjimwema, ujenzi wa Bandari ya Mbegani, kuboresha gati na 1 -7 kwa kuchimba na kupanua kina kufi kia mita 12.

Mpango mwingine ni pamoja na matumizi ya TEHAMA zaidi katika kazi za utekelezaji ili kupunguza muda wa meli kusubiri kuhudumiwa kuongeza maeneo ya kuhifadhi mizigo (yards), kuboresha utaratibu wa kuhudumia makasha, ukaguzi wa mizigo na uboreshaji wa usalama wa mizigo bandarini.

Akijibu baadhi ya maswali ya wajumbe wa kamati hiyo waliotaka kufahamu hatua zinazochukuliwa kukabiliana na upotevu wa vifaa vya

magari yaingiayo bandarini Bibi Mulindwa alisema wateja wanashauriwa kukagua fomu inayoitwa “Vehicle Discharging Inspection Transfer Tally (VDITT) ili kujihakikishia kama magari yao yana vitu vilivyoorodheshwa kabla ya kuleta malalamiko.

Ujumbe huo ulitembelea maeneo mbalimbali ya Bandari ikiwa ni pamoja na TICTS na kuhitimisha kwa kutembela Kurasini Oil Jetty (KOJ) na Kitengo cha mizigo mchanganyiko.

Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Bi Apolonia Mosha akizungumza na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakati walipotembelea Bandari hiyo.

Page 12: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

12

Mafunzo

Afi sa Mwandamizi Rasilimali watu ambaye pia ni mratibu wa Mafunzo wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Bw. Ernest Mwesiga amesema kwamba zoezi

la uendeshwaji wa semina ya jinsi ya kumjali mteja `Customer Care` linamhusu kila mfanyakazi wa Mamlaka.

Hayo aliyasema hivi karibuni wakati wa mafunzo kwa wafanyakazi wa Bandari zote ya siku tatu yaliyofanyika katika Hoteli ya Livingstone mjini Bagamoyo, Pwani.

Akifafanua jinsi zoezi hilo litakavyokuwa, Mwesiga alisema: “…zoezi hili litakuwa endelevu na litafanyika kila mwaka. Aidha litajumuisha wafanyakazi wa Bandari zote na litakuwa linafanyika bila kuzingatia mhusika anatoka kitengo gani na anafanya kazi gani.”

Lengo la mafunzo hayo kwa mujibu wa Bw. Mwesiga ni

kuwawezesha wafanyakazi kutoa huduma bora kwa wateja na kuongeza ufanisi zaidi.

“Mteja akipata huduma bora akaondoka ameridhika itamfanya siku nyingine aweze kurudi tena,” alisema.

Afi sa huyo aliwataka wanasemina hao kuyafanyia kazi yale yote waliyofundishwa pindi warudipo katika sehemu zao za kazi.

Nao wafanyakazi waliopata fursa ya kuhudhuria semina hiyo walisema kwamba wanaomba muda uongezwe kwani siku tatu ni muda mfupi

na mambo ya kujifunza ni mengi.

Pia waliushukuru uongozi wa Mamlaka kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani wameweza kujifunza mambo mengi na kupata uelewa zaidi jinsi ya kutoa huduma bora kwa wateja, pia kuweza kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo pindi wawapo kazini.

Semina hiyo iliendeshwa na Mkufunzi George Mungai kutoka Goal getters Consultants ambapo mada kuu ilikuwa ni jinsi ya kumhudumia na kumjali mteja.

Na: Cartace Ngajiro na Evetha Claudio

Pichani ni Wanasemina baada ya kumalizika kwa semina katika Hoteli ya Livingstone (Malaika) Bagamoyo.

Page 13: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

13

Bandari ya Dar es Salaam imenyakua vikombe 8 vikitokana na ushindi katika michezo ya mpira wa miguu, pete, kamba, bao, na riadha katika mashindano

yanayokutanisha Bandari zote nchini “Interport Games” Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni katika tafrija fupi iliyofanyika ukumbi wa Harbors Club Kurasini.

kufanya kazi kwa bidii.

Bandari ya Dar es salaam ni kinara wa michezo hiyo katika vipindi vitatu mfululizo huku ikiibuka ushindi wa jumla na vikombe lukuki.

Tafrija hiyo iliyokuwa ya aina yake ilihudhuriwa na wakuu wa idara mbalimbali ambapo mgeni rasmi alikuwa Meneja Utekelezaji Bw. Patrick Na-mahuta, kwa niaba ya Kaimu Meneja wa Bandari.

“Nawapongeza wanamichezo kwa kujituma na kucheza kwa nidhamu kubwa. Ila muendele na mazoezi ili muwe wakakamavu na mwepukane na magonjwa madogo madogo,” alisema Bw. Namahuta.

Namahuta aliwaasa wanami-chezo hao kuchapa kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi na kuboresha huduma katika Ban-dari ya Dar es Salaam ambayo ni lango kuu la biashara.

Pamoja na mambo mengine wanamichezo kupitia risala yao kwa mgeni rasmi

walipendekeza mpira wa miguu uchezwe dakika 90 kwa mujibu wa Shirika la Kabumbu Duniani (FIFA).

Walipendekeza pia vifaa vya michezo vitolewe mapema ili kuboresha michezo hiyo na kuwepo kwa zawadi

ya mfungaji bora kwani ndio chachu ya kuwafanya wachezaji kujituma wawapo kiwanjani.

Hafl a hiyo ilipambwa na maigizo ya wafanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam pamoja na muziki.

Na: Innocent Mhando

Michezo

Vikombe 8 vilivyokabidhiwa kwa Meneja Bandari kutoka katika michezo ya mpira wa miguu, kamba, bao, riadha, mpira wa pete.

Page 14: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

14

Elimu

Bandari ya Dar es Salaam imejiongezea wataalam zaidi waliohitimu katika

fani za Mawasiliano na Sheria ambao kwa upande mwingine wanatazamiwa kutumia ujuzi wao ili kuleta ufanisi wa kazi katika shughuli za kila siku katika Bandari na Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa Ujumla.

Peter Millanzi ambaye ni Afi sa Mawasiliano Mwandamizi katika Bandari ya Dar es Salaam ametunikiwa Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma (Masters Degree in Mass Communication) katika chuo cha Mtakatifu Augustino Tanzania Tawi la Dar es Salaam na Athuman Mkangara Shahada ya Kwanza ya Sheria (BA in Laws) katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania).

Katika mahojiano na mwandishi wa gazeti hili Millanzi aliishukuru Mamlaka kwa kutoa fursa kwa wafanyakazi wake kujiendeleza kielimu na kuiomba Mamlaka kuwapatia ruhusa maalumu wanaojisomea ifi kapo kipindi cha mitihani ili kupata muda mwingi wa maandalizi pasipo kupunguzwa siku za likizo. Kwani kwa sasa wafanyakazi wengi wanaosoma hutumia siku zao za likizo kwa ajili ya kipindi cha mitihani hivyo kukosa kabisa muda wa kwenda likizo kwani siku zao huwa zinaishia kipindi cha mitihani.

Millanzi pamoja na mambo mengine alitaja changamoto mbalimbali alizokumbana nazo wakati akiwa mwanafunzi ni pamoja na

kipindi cha mitihani inalazimu kuchukua likizo kwani inakuwa vigumu kufanya kazi na wakati huohuo kujisomea pamoja na kutokupata muda wa kujisomea kwa ajili ya mtihani. “Muda mwingine inalazimu kujisomea mpaka usiku

�������������������������

Na: Innocent Mhando

Peter Milanzi, Afi sa mawasiliano Mwandamizi

katika Bandari ya Dar.

Athuman Mkangara.Afi sa Biashara Mwandamizi.

Mwenyekiti DOWUTA.

Edesius Kinunda akiwa na Essau Chale kutoka kitengo cha Utekelezaji wakiwa katika mahafali ya 13 Chuo cha Bandari.

Inaendelea Uk. 15

Page 15: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

15

Malenga

Ema nipe karatasi, Na kalamu niazime,Niandike kwa nafasi, Nilo nayo niyaseme,Shairi chapa upesi, Gilawa mi nimtume,Leonard wa Mpemba, Uwakili kahitimu.

Asojua namjuza, Ndani ya zetu Bandari,Askari kaanza, Bandari alipojiri,Taaluma kaongeza, Hakika yeye ni jasiri,Leonard wa Mpemba, uwakili kahitimu.

Sifa kajiongezea, Kakataa kubabaishwa,Kitabu amebukua, Daraja kapandishwa,Sheria amesomea, Hadi joho amevishwa,Leonard wa Mpemba, uwakili kahitimu.

Tangazo amelitoa, Kwa wote wafanyakazi,OFA amejitolea, Mwenye shida ya kikazi,Mhuri awagongea, Bure bila ya ajizi,Leonard wa Mpemba, uwakili kahitimu.

Ujuziwe ni adhimu, Ndani ya yetu Bandari,Hongera kwa ukarimu, Kwa Bandari ni fahari,Wewe kwetu ni muhimu, Sifazo sawa johari,Leonard wa Mpemba, uwakili kahitimu.

Shime kwa wafanyakazi, Tumtumie Mpemba,Kwa yale tusomaizi, Tupeleke kwa Mpemba,Naye bila pingamizi, Kortini atatamba,Leonard wa Mpemba, uwakili kahitimu.

Mdikang’andu ARS (GHOSHI-JA-MBAZI)Tanga Port Control TowerMob: 0715 390684

sana na asubuhi uamke mapema kuwahi ofi sini na kusababisha ugumu katika utendaji kazi”. alisisitiza Millanzi.

Pamoja na changamoto hizo Millanzi amewashauri wafanyakazi wenzake wanapokuwa na muda kujiendeleza kielimu wafanye hima kwani hatua hiyo itaongeza ufanisi kiwandani pamoja na kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kutoka kwa nchi zilizoendelea.

“Elimu haina mwisho, na elimu ni kama mtu anayepanda mlima kwani kadri anavyozidi kupanda juu ndipo anavyozidi kuongeza wigo wa kuona eneo kubwa zaidi kwa hiyo mtu unavyozidi kujiendeleza ndio unavyozidi kuongeza upeo mkubwa katika kujua mambo mengi zaidi na kupata upeo mkubwa wa utendaji kazi”, alisema Millanzi.

Kwa upande wake Mkangara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi DOWUTA Tawi la Dar es Salaam ametoa wito kwa wafanayakazi wenzake wa Mamlaka kujiendeleza kielimu pasipo kujali umri wao ili kuweza kupanua uwezo wao wa kuelewa na kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi kwani dunia ya sasa inahitaji watu wasomi. “Wafanyakazi lazima wajiendeleze kielimu na wenye umri mkubwa pia wasiogope wengine wanajiona wana umri mkubwa wanaingia na hofu ya kuingia darasani na kujiendeleza kielimu”. Alisema Mkangara

Mkangara akaongeza kwa kusema kuwa kusoma wakati anafanyakazi ni changamoto kubwa aliyokumbana nayo wakati wote, “kuweza kufanya yote inawezekana kinachotakiwa ni kugawa na kubana muda wa kusoma na kufanya kazi na wakati mwingine kuingia gharama wewe mwenyewe ili kuweza kuhakikisha mambo yote yanakwenda kwa wakati”.

Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni lango kuu la biashara inawalazimu wafanyakazi wake kujiendeleza kielimu ili kutoa huduma bora ili kuendana na hali halisi ya soko linavyoenda pamoja na kukabiliana na upinzani uliopo kutoka bandari za nchi jirani.

Inatoka Uk. 14

Page 16: TPA Gazeti Issue 16 January 2013 - Tanzania€¦ · ya X-ray ya kufanyia ukaguzi wa mizigo. Pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya ICD kwa ajili ya kuhudumia kontena kutoka ICD 7

16

Michezo

Uongozi wa Chama cha Kuweka na

Kukopa Bandarini Saccos umewataka wafanyakazi wa Bandari kujiunga na Chama hiki.

Akiongea na mwandishi wa gazeti hili, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho ndugu Mataro Kikoba alisema, Saccos Bandarini ni Chama ambacho kina faida kubwa kwa wafanyakazi kwa kuwapa maendeleo makubwa.

Alisema, Bandari Saccos inatoa mikopo mbalimbali ambayo imekuwa mkombozi mkubwa kwa wafanyakazi ambao tayari ni wanachama wa Saccos hii.

Mikopo ambayo hutolewa na Chama hiki ni pamoja na mikopo ya maendeleo, mikopo hii huanzia milioni moja na laki tano na kuendelea, na

mwanachama hukatwa kuanzia mwaka mmoja na kuendelea.

Makamu Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa mkopo mwingine utolewao ni mkopo wa shule, ambapo Mwanachama hupata mkopo huu kila mwaka na mkopo huu ni wa shilingi milioni moja tu, na mwanachama hukatwa kwa mwaka mmoja tu.

Vile vile alisema kuna mkopo wa dharula, mkopo huu ni shilingi laki tano tu, na mwanachama

huweza kukatwa kwa miezi sita.

Chama cha Saccos bandarini kinayo mikakati mbali mbali ambayo imelenga kuwakwamua wanachama toka katika lindi la umasikini. Chama kimeamua kuanzisha mradi wa kuwapatia wanachama wake viwanja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba bora. Mpango huu ni endelevu kwa kadri mapato ya Chama yatakavyokuwa yanaongezeka.

Mkakati mwingine ni ule wa kuanzisha benki ya Saccos ili Chama kiwe na uwezo mkubwa wa kukopesha wanachama wake.

“Chama cha Ushirika huu kilisajiliwa rasmi tarehe 23 Agosti, 1968 na Msajili wa vyama vya Ushirika Tanzania kwa kupata hati ya usajili inayotambulika.

Hivyo basi, wafanyakazi msiwe na wasiwasi wowote kwani chama hiki kipo kishe ria kabisa”. Alisema ndugu Kikoba.

Na: Bernard James

Ndg. Mataro Kikoba

“Napenda kuwapongeza kwa kupanua wigo wa kozi na kupokea wanachuo wengi kutoka nje ya Mamlaka kuliko ndani ya Mamlaka,” aalisema Ngunda.

Ngunda ameongeza kwamba sasa Chuo kimepanuka kitaifa na kinaweza kuhudumia Sekta mbalimbali za Uchukuzi, Uendeshaji wa Vyombo na Uhandisi jambo linalokipa hadhi ya kuwa ni chuo cha Taifa na Kimataifa cha Wananchi wote wa Afrika Mashariki.

“Nimeambiwa kuwa mmeweza kubuni kozi ya Zimamoto na Usalama na mnakamilisha mchakato wa kuanzisha kozi ya Usalama na Ulinzi sasa nawaasa muendelee kuwa wabunifu ili muweze kukidhi mahitaji ya soko hususani katika sekta ya Uchukuzi na sekta nyinginezo,” alisema Ngunda.

Chuo cha Bandari ni mojawapo ya vyuo vikongwe hapa nchini ambavyo vinasifi ka kwa kuzalisha rasilimali watu ya kutosha kwa ajili ya Bandari nchini na Sekta nyingine za Uchukuzi.

Inatokea Uk. 8