2
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI HALMSHAURI YA MANISPAA YA ILALA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWA BVR KITS OPERATORS NA WAANDISHI WASAIDIZI KWENYE ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA Afisa Mwandikishaji Manispaa ya Ilala anawatangazia wenye sifa kujitokeza kuomba nafasi ya kazi ya kuwa BVR OPERATORS AU MWANDISHI

Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi Waandishi

  • Upload
    ilala

  • View
    346

  • Download
    6

Embed Size (px)

DESCRIPTION

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Citation preview

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI HALMSHAURI YA MANISPAA YA ILALATANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWA BVR KITS OPERATORS NA WAANDISHI WASAIDIZI KWENYE ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURAAfisa Mwandikishaji Manispaa ya Ilala anawatangazia wenye sifa kujitokeza kuomba nafasi ya kazi ya kuwa BVR OPERATORS AU MWANDISHI MSAIDIZI kwenye zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura.Sifa za Mwombajii. Awe ni Raia wa Tanzaniaii. Awe ni Mkazi wa Manispaa ya Ilalaiii. Awe anajua kusoma na kuandikaiv. Awe na Elimu ya Sekondari na kuendeleav. Awe na Elimu ya kiwango cha cheti na kuendelea ya matumizi ya Kompyuta vi. Awe ni Mkazi wa Kata anayoombea kufanya kaziJinsi ya kutuma maombii. Barua ya maombi iandikwe kwa mkono ikiwa na anuani kamili ya mwombaji na kuambatanishwa na vivuli ya vyeti.ii. Mwombaji ataje Kata anayoishi ambayo anaombea kufanya kazi hiyoiii. Barua za maombi ziwasilishwe Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala (Afisa Mwandikishaji) iliyopo katika makutano ya Barabara ya Mission na Sokoine kwa kutumia anuani ifuatayo;Afisa Mwandikishaji,Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,1 Mtaa wa Mission,S.L.P 20950,11883-Dar es Salaam.N.B Siku ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 19/06/2015 saa 9:30 alasiri. Limetolewa na,Isaya M.MngurumiAfisa Mwandikishaji Manispaa ya Ilala