9

Tunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili ya kusaidia ...face.dpsk12.org/wp-content/uploads/2014/07/Summer-Learning-Guide_Swahili-FINAL.pdfTunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili

  • Upload
    others

  • View
    34

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Tunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili ya kusaidia ...face.dpsk12.org/wp-content/uploads/2014/07/Summer-Learning-Guide_Swahili-FINAL.pdfTunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili
Page 2: Tunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili ya kusaidia ...face.dpsk12.org/wp-content/uploads/2014/07/Summer-Learning-Guide_Swahili-FINAL.pdfTunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili

asa ni wakati wa kuanza kufikiria juu ya shughuli za msimu wa kiangazi kufanya watoto wako

wajishughulishe, watendaji wakati wa msimu wa kiangazi

Unajua kwamba kama mwanafunzi akiacha kujifunza wakati wa likizo, anaweza kusahau kile

walichojifunza kwa zaidi ya miezi miwili katika kusoma na hisabati? Hii inaitwa hasara ya

kujufunza wakati wa msimu wa kiangazi na inatokea wakati wanafunzi wanasahau kile

walichojifunza zaidi ya mwaka wa masomo. Wanafunzi wanaorudishwa nyuma kwa sababu ya

hasara ya kujifunza wakati wa msimu wa kiangazi kwa mwaka mzima wa masomo yao ya awali

wanaweza kurudi nyuma kwa zaidi ya mika 2.5 nyuma ya wenzao kufikia mwisho wa gredi ya

tano.

Ingawa kuna programu nyingi za msimu wa kiangazi, nyingi zao zina usajili wa mapema, makataa

na nafasi chache. Anza kuuliza kuhusu shughuli za msimu wa kiangazi na programu zipatikanazo

shuleni kwako na katika jumuia yako na wasajili watoto wako kabla ya mwisho wa mwezi Machi.

Kujidunza ni jambo la asili linaloweza kutokea wakati wowote. Kwa mfano mazungumzo ya kila

siku na watoto wako yataongeza kujiamini kwao, kukuza maarifa yao na msamiati, kukuza satadi

zao za mawasiliano, na kukuza uhusiano wako pamoja nao.

Ofisi ya Shughuli za Kifamilia na Kijamii ilishirikiana na walimu kutoka madaraja ya gredi

mbalimbali kutengeneza Shughuli hizi za Kufurahisha kwa Ajili ya Muongo wa Kujifunza wa

Wazazi. Mwongozo huu umejaa shughuli zitakazokusaidia kuwafanya watoto wako

kujishughulisha, mtendaji na kujifunza wakati wa msimu wa kiangazi.

Tunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili ya kusaidia elimu ya watoto wako.

Kwa pamoja tunaweza kuhakikisha kuwa kila mtoto anafanikiwa katika Denver Public Schools.

Shukrazi za pekee kwa walimu wafuatao waliosaidia katika kutengeneza Mwongozo wa Kujifunza:

Park Hill Elementary School: Mary Beth Carlson, Kathleen Isberg, Cheryl Kling, Chris Ando West Leadership Academy: Diego

Romero, Kristin Repaci, Bronwen Forrestal, Margarita Colindres Summer Academy: Lorenza Lara & Alejandra Estrada

S

Page 3: Tunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili ya kusaidia ...face.dpsk12.org/wp-content/uploads/2014/07/Summer-Learning-Guide_Swahili-FINAL.pdfTunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili

GREDI ZA ECE - Chekechea

Shughuli zifuatazo za kuburudisha za Kusoma, Kuandika, Hisabati na Sayansi zitampatia mtoto wako fursa ya fursa ya kufanyia mazoezi

stadi yake ya kufikiri na kukuza uelewa wao wa maneno, ruwaza na ujuzi unaotakiwa ili kufanikiwa shuleni. Shughuli hizi za kujifuna

zinaweza kufanyika nyumbani au sehemu yoyote ile. Jaribu baadhi ya hizi shughuli za kufurahisha kila siku au tengeneza ya kwako!

KUSOMA

Maelezo ya Bidhaa: Kwenye nguo - zimetengenezwa wapi? Kwenye vyakula - vimejumuisha vitu gani?

Kadi za msamiati unazotengeneza za maneno unayoyapenda kutoka kwenye hadithi unayosoma AU unayoizungumzia.

Soma kwa sauti pamoja. Kusoma kwa MWANGWI humaanisha mtu mmoja anasoma kwanza na mtu wa pili anarudia maneno hayo. Kusoma kwa KUIMBA humaanisha mnasoma pamoja kwa wakati mmoja. Zungumza juu ya matini. Umejifunza nini? Ni kitu gani kingine unachotaka kujua?

Angalia picha au vielelezo vingine na kisha soma malelezo ya bidhaa. Je maneno yalifafanua picha au picha ilifafanua maelezo?

Nenda maktaba na tafuta kitabu unachokipenda na kisha kisome. Waambie familia yako kile unachokipenda kuhusiana na kitabu. Bainisha maneno mapya na muulize mtu maana ya hilo neno. Msaidie mwanao ili atengeneze kamusi yake kwenye daftari.

KUANDIKA

Cheza mchezo wa duka la matunda: weka maelezo ya bidhaa,

weka orodha ya matunda.

Mchezo wa mkahawa: andaa menyu, chkua oda & andika tiketi.

Andika mipango yako kila wiki.

Andika kuhusu kipindi cha Televisheni unachokipenda.

Kwa nini unakipenda?

Saidia kupanga mlo wa usiku kwa kuweka orodha ya viambato.

Nenda kwenye hazina ya kuwinda maneno: orodhesha maneno ya

kutafuta.

Waambie familia yako kutaja vitu wanavyovipenda na andika

majibu yao.

Andika hadithi ikijumuisha wanafamilia wote kama wahusika.

HISABATI

Zungumza juu ya hisabati. Kwa mfano: Tuna watoto wawili na watu wazima wawili wanakuja kwenye chakula cha jioni, tutaweka nafasi ngapinkwenye meza?

Kucheza mchezo: kuna vipande 12 katika kila upande wa ubao. Kama utanirusha mara tatu, nitakuwa nimebakiwa na vipande vingapi vya mchezo? Mchezo mwingine unaweza kuwa "Ninafikiria namba." Namba yangu inapoongezwa na 6 inakuwa 10. Namba yangu ni nini?

Pima kisu, uma ana kijiko kwa inchi au sentimita. Onesha kipi ni kirefu/kifupi na kwa kiasi gani?

Wasaidie wanafunzi waelewe nafasi ya namba kwa kujumlisha na kutoa namba ya tarakimu 2.

SAYANSI

Panda na hudumia mbegu mbalimbali ikiwa ni pamoja na maua na mbogamboga. Rekodi taarifa kadri inavyokuwa.

Chunguza jinsi kivuli chako kinavyibadilika wakati wa mchana. Bainisha wadudu na ndege unaowaona kwenye eneo lako. Tafuta

"makazi" yao uwanjani au mtaa wa jirani. Jaribu kutengeneza upya makazi yao "asilia" kwenye boksi la viatu. Jadili vitu vinavyohitajika kwa kiumbe hai kuishi.

Kusanya, linganisha na jadili kuhusu miamba.

Tazama nyota wakati wa usiku. Zingatia mabadiliko katika mwezi na nyota.

Jifunze mchoro wa mwili wa binadamu kisha chora na onesha mifumo yake: (mfumo wa mifupa; upumuaji; mmeng'enyo).

Page 4: Tunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili ya kusaidia ...face.dpsk12.org/wp-content/uploads/2014/07/Summer-Learning-Guide_Swahili-FINAL.pdfTunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili

Shughuli zifuatazo za kuburudisha za Kusoma, Kuandika, Hisabati na Sayansi zitampatia mtoto wako fursa ya fursa ya

kufanyia mazoezi stadi yake ya kufikiri na kukuza uelewa wao wa maneno, ruwaza na ujuzi unaotakiwa ili kufanikiwa

shuleni. Shughuli hizi za kujifuna zinaweza kufanyika nyumbani au sehemu yoyote ile. Jaribu baadhi ya hizi shughuli za

kufurahisha kila siku au tengeneza ya kwako!

Tafsiri za kwenye filamu: Fungua kitufe cha kuonesha tafsiri unapoangalia TV. Wataje wahusika muhimu na elezea tabia zao. Simulia tena hadithi.

Vitabu vya katuni na Riwaya za Michoro: Walinganishe mashujaa tofautitofauti. Nini kinawafanya wawe mashujaa? Wanamtumikia nani? Je kuna mhusika zaidi ya mmoja?

Maelekezo ya chakula: Fuata maelekezo na tengeneza kitu kipya!

Andika msamiati mpya. Majarida na Mtandao: Soma khusu dunia, wanyama, mimea,

na watu maarufu. Watu wanafananaje na wanyama? Kama mimea itatoweka, nini kitatokea?

Barua kutoka nyumbani: andika barua kwa wanafamilia wanaishi nje ya Denver. Wambie wakujibu barua yako.

Andika orodha ya chakula kila wiki. Andika episodi ya kipindi cha Televisheni na wewe ukiwemo. Fanyia utafiti somo lako unalopenda na wasilisha mbele ya

familia yako. Andika orodha ya kazi za numbani kwa wiki nzima. Andika kuhusu kipindi chako kizuri cha Televisheni

unachokipenda. Sema kwa nini unapenda kipindi hicho? Andika ripoti ya hali ya hewa kila siku na uwe mtao taarifa ya

hali ya hewa wa familia yako. Andaa maswali kwa ajili ya usaili. Msaili mtu na andika majibu

kwenye daftari. Linganisha na linganua vipindi viwili vya Televisheni, kipi ni

kizuri zaidi na kwa nini?

Hesabu vitu na vilinganishe Kuna matufaa 15 kwenye mfuko wa lb. 5 kwa $10.99 na machungwa 25 kwenye mfuko wa lb. 10 kwa $10.79. Dili zuri zaidi ni lipi?

Sema muda pamoja. Linganisha saa ya kidijiti na ya kianalogia. Unapokuwa unapika, tumia maelezo ya kupika kutafuta

sehemu (1/4 sukari kwenye kijiko cha chai), au mshirikiane kuongeza marambili mahitaji ya mapishi.

Msaidie mtoto wako kujifunza kugawanya kwa usawa kwa kugawana midoli, chakula na pesa.

Pima pembe na tafuta na tambua pembe mraba nyumbani kwenu.

Tafuta mzingo wa chumba. Ongeza mara mbili urefu, upana kisha zijumlishe.

Pima eneo la chumba: urefu mara upana. Wafundishe watoto wako kuhesabu sarafu na kuweka chenchi.

Angalia nyota wakati wa usiku. Zingatia mabadiliko katika mwezi na nyota.

Tengeneza au chora mfano wa mfumo wa jua. Jifunze jinsi ya kutumia vitu upya na kushiriki katika jumuia

yako. Fanya majaribio na maji: rekodi mvuke wa maji katika dumu la

wazi. Pima msongamano wa vitu kwa kuangalia iwapo vinazama au

kuelea. Tunza daftari la hali ya hewa. Jifunze na andika juu ya ruwaza

ya hali ya hewa. Jifunze mchoro wa mwili wa binadamu kisha chora na onesha

mifumo yake (mfumo wa mifupa; upumuaji; mmeng'enyo).

KUSOMA KUANDIKA

SAYANSI HISABATI

Page 5: Tunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili ya kusaidia ...face.dpsk12.org/wp-content/uploads/2014/07/Summer-Learning-Guide_Swahili-FINAL.pdfTunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili

GREDI ZA ECE - Chekechea

Shule unaweza kuwa imefungwa kwa ajili ya msimu wa kiangazi lakini kujifunza hakukomi. Wakati kuna makambi mengi ya

msimu wa kiangazi, madarasa na programu katika jamii yetu ili kuwaweka watoto wako kujishughulisha na kujifunza kwa

kipindi chote cha msimu wa kiangazi, kuna mambo mengi sana unayowezakufanya kama familia ili kumwezesha mtoto wako

kujifunza na kufanyia mazoezi stadi zao za kufikiri. Jihusishe na shughuli za mwanao katka msimu wa kiangazi ili

kuhskikisha kujifunza kunaendelea. Shughuli zifuatazo za kuburudisha za Kusoma, Kuandika, Hisabati na Sayansi zinaweza

kukusaidi kuanza.

kwa ajili ya msimu wa

Kiangazi

KUSOMA

Panga uzoefu wa familia baada ya kusoma kitabu

kia=nachohusiana na familia.

Shirikisha wengine vitabu vya kusoma kutoka katika nchi

yako ya asili au katika lugha yako ya asili. Unaweza kukusanya

haya matirio na kutengeneza kijitabu.

Andika hadithi yako nzuri kuhusu familia. Ielezee, na isome

kwa kubadilishana Tafakari juu ya simulizi mbalimbali na jadili

mitindo mbalimbali ya kutoa simulizi.

Badilishana kwa kusoma kwa sauti unapokuwa unasoma

matirio kama vile orodha ya chakula au maelezo ya namna ya

kuandaa chakula, ratiba za kazi na matangazo.

Baada ya kusoma kitabu, toa fursa kwa familia kucheza nafasi

za wahusika wa kwenye kitabu.

Tumia teknolojia nyumbani kwako au maktaba ili kupata

vitabu vya kielektroniki (iPod, iPad, iPhone, Smart Phone,

Kindle n.k.)

KUANDIKA

Jichukulie kijitabu kijarida kizuri au kijitabu cha kuandikia.

Andika mawazo yako na kile unachofanya msimu huu wa

kiangazi ili usiweze kusahu! Nunua jarida lisilokuwa na

mistari kwenye kurasa zake ili uweze kuchora na kuandika.

Mara baada ya shule kufungwa, weka orodha ya sehemu

unazotaka kwenda katika musimu huu wa kiangazi.

Endelea kuweka orodha, na weka mkasi kwenye sehemu

ulizokwisha wahi kutembelea.

Anzisha blogu yako kuhusu msimu wako wa kiangazi!

Jaribu kuandika ujumbe mrefu kwa rafiki zako na familia

kupitia Fecebook. Jipime mwenyewe kutumia alama sahihi

za uandishi, matamshi na herufi kubwa ili uweze kujimudu

vizuri.

Fanya utafiti juu ya sehemu unayokwenda kwa ajili ya likizo

na waandikie bodi ya utalii kwa ajili ya kupata taarifa.

HISABATI

Cheza hisabati ya akili kwenye gari Angalia unaweza kupata mangapi kwa usahihi kabla hujafika sehemu unakokwenda.

Tumia adomita ya kwenye gari ili kuajua familia yako inaendesha umbali gani kila siku. Chora jedwali!

Unapokwenda kununua kitu dukani, kokotoa kodi ya mauzo na jaribu kupata chenchi kamili. Angalia kama upo sahihi!

Kadiria upande wa kichwa wa sarafu utaonekana mara ngapi ikiwa utarusha sarafu mara 100. Jaribu hii pia! Nakili majibu yako mezani. Fanya hili jaribio kwa muda na kisha linganisha matokeo yako.

Fungua kibanda cha juisi ya limao! Angalia unaweza kutoza shilingi ngapi kwa kila kikombe ili uweze kupata faida.

Jiwekee muda unapokimbia maili moja. Fuatilia muda wako kila wiki. Chora jedwali la maendeleo yako na angalia jinsi ulivyopiga hatua.

SAYANSI

Fanya majaribia ya kisayansi na mtoto wako:

a. Fanya yai lielee kwenye maji ya chumvi b. Tengeneza kinywaji cha maji ya limao c. Kuchanganya mafuta na maji

Tafuta makala ya kisanyansi na mpatie mwanao aseme kwa ufupi.

Unapokuwa ukiendesha, mwambie mtoto wako atafute maneno ya kisayansi barabarani.

Tembelea Makumbusho ya Denver ya Maliasili na Sayansi.

Weka kambi na mwanao na ongea kuhusu maliasili, na mwambie kwa nini huwezi kuona nyota wakati wa mchana au ukiwa mjini.

Page 6: Tunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili ya kusaidia ...face.dpsk12.org/wp-content/uploads/2014/07/Summer-Learning-Guide_Swahili-FINAL.pdfTunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili

GREDI ZA ECE - Chekechea

Shule unaweza kuwa imefungwa kwa ajili ya msimu wa kiangazi lakini kujifunza hakukomi. Wakati kuna makambi mengi ya msimu wa

kiangazi, madarasa na programu katika jamii yetu ili kuwaweka watoto wako kujishughulisha na kujifunza kwa kipindi chote cha msimu

wa kiangazi, kuna mambo mengi sana unayowezakufanya kama familia ili kumwezesha mtoto wako kujifunza na kufanyia mazoezi stadi

zao za kufikiri. Jihusishe na shughuli za mwanao katka msimu wa kiangazi ili kuhskikisha kujifunza kunaendelea. Shughuli zifuatazo za

kuburudisha za Kusoma, Kuandika, Hisabati na Sayansi zinaweza kukusaidi kuanza.

KUSOMA

Jikite kwenye mazungumzo juu ya matukio ya sasa yanayohusiana na

familia yako, na tafuta taarifa zaidi kwenye magazeti, majarida na

mitandao mingine ya kijamii.

Kabla hujaanza kusoma, elewa kusudi la kusoma matini hiyo ni nini

na zungumza juu ya matarajio uliyonayo juu ya matini hiyo. Baada ya

kusoma, angalia tena kwa ajili ya kuelewa matini.

Tumia teknolojia kukuza programu za kujifunza mtandaoni ukiwa

nyumbani au maabara. Tumia mtandao kupata vitabu vya

kilelektroniki, vyama vya vitabu mtandaoni, majarida na magazeti.

Chagua simulizi ya familia, na jishughulishe katika mazungumzo ya

kujifunza na familia yako ili kujua lengo la simulizi. Badilishana

kusimulia tena simulizi.

Shiriki matirio ya kusoma kutoka nchini kwako au katika lugha yako

ya asili.

KUANDIKA

Ulishawahi kupata barua halisi kwenye sanduku la posta?

Jaribu kumwandikia ndugu yako anayeishi mbali na wewe. Hata

kama tuna Facebook na barua pepe, hakuna kitu kama kupata

barua mikononi mwako!

Insha za kufanya maombi ya chuo mara nyingi huuliza juu ya

mada zifuatazo: tukio muhimu lililobadilisha maisha yako,

kikwazo ulichopaswa kukishinda, au kitu ulichofanya kazi kwa

bidii ili kukipata. Shughulisha ubongo wako msimu huu kwa

kuandika kidogokidogo juu ya mada hizi kwenye daftari. Muda

utakapofika wa kuandika insha hizi, utafurahi sana kwamba

una hizo notisi tayari!

HISABATI

Tunza rekodi ya halijoto kila siku. Kokotoa wastani wa halijoto kila

wiki. Wiki gani iliyokuwa na joto la juu zaidi? Ni mwezi gani ulikuwa

na joto la juu zaidi?

Chunguza matangazo ya maduka kwenye mtandao/dukani/magazeti.

Ni duka gani lenye dili zuri zaidi?

Isaidie familia yako katika kufanya manunuzi ya matunada na mboga.

Kata kuponi na kokotoa kiasi cha pesa utakachobakiwa nacho.

Panga kuwa na chakula cha pamoja na familia yako - kwa bajeti ya

$15.

Tengeneza bajeti ya kila mwezi kwa ajili yako. Tunza angalau 25% ya

kipato chako cha kila mwezi.

Kuwa na rafiki zako kwa ajili ya sherehe za msimu wa kiangazi. Nunua

vitafunwa na panga shughuli. Weka gharama chini ya $2 kwa kila

mtu.

SAYANSI

Fanya majaribio ya kisayansi:

a. Jenga volcano

b. Tengeneza ubao wa karatasi.

c. Safisha sarafu kwa siki

Pika chakula na mzazi wako au mlezi na waulize kuhusu mchakato,

joto, maelekezo, na ufanyaji kazi wake kwa ujumla.

Fanyia kazi matamko ya kama basi (utabiri)...Kama nitapika chakula,

basi sitakuwa na njaa.

Panda bustani ya mbogamboga au maua na andika mambo

uliyogundua. Hakikisha unayamwagilia!

Tazama kipimajoto chako kila siku, na tengeneza jedwali ili

kumwonesha mwalimu wako wa sayansi katika siku ya kwanza

shuleni.

Page 7: Tunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili ya kusaidia ...face.dpsk12.org/wp-content/uploads/2014/07/Summer-Learning-Guide_Swahili-FINAL.pdfTunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili

Jumapili Salama 1. Mfundishe mwanao kusema jina lake kamili. 2. Mfundishe mwanao kusema jina lako kamili 3. Mfundishe mwanao kukariri anwani yako ya makazi - mwoneshe namba ya nyumba ilipo nje ya nyumba na mwoneshe jina la mtaa. 4. Mfundishe mwanao kukariri namba yako ya simu. Kufanyia mazoezi kukariri taarifa muhimu. 5. Jifunze jinsi ya kuvuka barabara salama. 6. Jifunze namna ya kuijokoa pale moto unapotokea. 7. Jifunze kusema "hapana." fanya mchezo ambao mnaulizana kwa kubadilishana ili kufanya mambo yanayochekesha . 8. Cheza mchezo wa kujificha kuwafundisha watoto wako kwa watulivu wakati wanapokutafuta. 9. Mfundishe mwanao mfumo wa ndugu. 10. Mfundishe mtoto wako aina ya dharura na jinsi ya kupiga 911. 11. Jifunze kuomba msaada kwa vitu ambavyo ni vya moto, vikali, vya hatari au vipo juu sana kuvifikia. . 12. Anza masomo ya kuogelea.

Fanya Kitu Jumatatu 13. Panga picha 5 au 6 ili kutengeneza bango au ukurasa wa kitabu. 14. Maziwa yaliyowekewa sukari hutangeneza alama za vidole nzuri. 15. Panda miche ya nje ya nyumba. 16. Kuchimba chambo - ni zoezi zuri kwa stadi nzuri za kuendesha pikipiki na mbinu za kujihami. Wapatie makazi mapya chambo hao karibu na mche uliopanda. 17. Nyoka wa mapovu. 18. Tengeneza jani kuwa kitabu. 19. Paka njia ya bembeni kwa chaki. Isafishe yote kwa maji. 20. Paka rangi kwa kutumia aina tofautitofauti za brashi za kupakia rangi: sweta, ua, pamba, spongi, jani, n.k. 21. Tengeneza kikwazo kwa kutumia pete ya hula, samani zilizoharibika, na maboksi yaliyowazi. 22. Chapisha fulana kadhaa. 23. Tengeneza fimbo ya mazingaombwe kwa kutumia vifaa vyote vinavyopatikana. 24. Jenga nyumba kwa vijiti, kokoto, vifuu, magome ya miti, majani na matirio mengine yanayopatikana nje.

GREDI ZA ECE - Chekechea

Muda wa Kusoma Jumanne 25. Jisajili kwa ajili ya programu ya msimu wa kiangazi ya kusoma kwenye maktaba mahalia. 26. Soma kitabu chini ya mti 27. Soma kitabu chote isipokuwa ukurasa wa mwisho na waulize watoto wako kupendekeza mwisho wa hadithi. 28. Mwambie mtoto wako achague hadithi, na msome pamoja. Ni sawa tu kama sentensi ina urefu wa sentensi moja au mbili. 29. Tengeneza video ya nyumbani ya mtoto wako akisoma hadithi kwa sauti, au ya kwako ukimsomea mtoto wako kwa sauti. 30. Baada ya kusoma kitabu kama vile The Lorax, nenda kaangalie filamu. 31. Soma vitabu kwa kuzingatia mada maalumu, kama bile wadudu, kisha fanya shguli inayohusiana kama vile kuwinda mdudu au kukamata nzi. 32. Mwambie mtoto wako atengeneza ratiba ya msimu wa kiangazi kwa ajili ya familia na soma ratiba kila asubuhi. 33. Tafuta kitabu cha majaribia rahisi ya kisayansi na jaribu baadhi yake nyumbani. 34. Tafuta kitabu kinachumhusu mtu wa kihistoria, na cheza mchezo wa kuvaa nyumbani. Mwambie mtoto wako aandike orodha ya mambo ya kuzingatia katika kuwinda ndege mla mizoga, na hakikisha kuna kila kitu kwenye orodha. 36. Badilishana vitabu unavyovipenda na rafiki zako.

Kupika ni nini? Jumatano 37. Kusaga matunda kwenye blenda. 38. hakuna kuoka vyakula vya shayiri kwenye stovu. 39. Pizza. 40. Kuzamisha ua la rubaruti kwenye blenda 41. Mafini za ndizi 42. Sandiwichi za kuzungusha. 43. Mshikaki wa matunda 44. Supu ya kuku kwenye chungu (chomeka kwenye pochi ili kisiweze kuweka joto ndani) 45. Mashimalo zilizookwa. 46. Mayai na chapati kwa ajili ya chakula cha usiku. 47. Maji ya limao 48. Guacamole.

Kati ya Juni na Septemba watoto wangu wana siku 82 za likizo ya msimu wa kiangazi, na nimewaahidi kuwapa kitu cha kufurahisha kila siku. Hii ina maana kwamba nitahitaji shughuli 82 za msimu wa kiangazi kwa mtoto mmoja mwenye

ulemavu na mtoto mmoja anayekataa kushiriki katika shughuli nyingi. Kitakuwa ni kipande cha keki, sio? Kuazima siku za wiki "Ratiba ya Msimu wa Kiangazi kwa Katoto" kupitia somewhatsimple.com, kuperuzi mtanadoni ili kupata mawazo zaidi

na kuongeza baadhi ya shughuli zangu, hizi ni siku 82 za msimu wa kiangazi za kufurahi na kujifunza.

Page 8: Tunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili ya kusaidia ...face.dpsk12.org/wp-content/uploads/2014/07/Summer-Learning-Guide_Swahili-FINAL.pdfTunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili

Alhamisi ya kutafakari 49. Osha gari pamoja. Hakuna njia ya kupita na hakuna gari? Basi osha mdoli wa gari. 50. Mpigie mtu simu na kumjulia hali. 51. Chukua maua (dandelioni na klova ni sawa) na mpatia mtu ambaye hakuyatarajia. 52. Andika tabia njema kumi za mtu na kisha mpatie kama zawadi. 53. Mwandikie mtu barua ya kushukuru na kisha itume. 54. Toa msaada wa nguo, vitabu na midoli kwa ajili ya matendo ya huruma. 55. Mfundishe mtoto wako kufanya kazi moja ya nyumbani. 56. Mpatie mtu kitu cha kisanaa kilichotengenezwa nyumbani. 57. Kajitolee damu. 58. Kusanya makopo na vyuma na toa msaada pesa uliyopata. 59. Tulia kwa muda na uwakumbuke unaowapenda 60. Mkumbatie mtu anayehitaji kumbatio.

Sehemu fulani Ijumaa ya Kufurahi 61. Kusafisha shamba au bustani ya wanyama. 62. Kucheza uwanjani katika mtaa wa jirani. 63. Makumbusho ya sanaa - angalia kwanza siku ya kuingia bure! 64. Ufukweni. 65. Chukua matunda safi shambani au tembelea soko la mkulima. 66. Endesha treni. 67. Tafuta sikukuu au maonesho ya mtaani. 68. Duka la aisikrimu. 69. Uwanja wa maji ya kububujika.

Jumamosi ya Ujuzi wa Kijamii 73. Simulia hadithi ya utotoni mwako. Mwambie mtoto wake asimulie hadithi kutokana na uzoefu wako wa maisha, ndio, hata kama mwanao hazungumzi. 74. Lala kwenye majani na badilishana kwa kuangalia maoumbo au picha kwenye mawingu. 75. Zunguka na muulize kila mwanafamilia nyumbani swali hilo hilo, kisha shiriki majibu. 76. Angalia picha za zamani za wanafamilia na wataje majina watu wote. 77. Jifunze kufanya hisia mbalimbali na mtoto wako kwa mwonekano wa uso: kawaida, furaha, huzuni, woga, hasira, karaha, mshangao. Badilishaneni na fanya mchezo. 78. Fanyia mazoezi ya kusikiliza kwa kuonesha mwitikio kwa mawasiliano ya bila maneno pekee kwa dakika 1 hadi 5 - kisha badilishana majukumu. 79. Kuwa kioo cha mwingine: iga matendo ya mtu kana kwamba wewe ni taswira ya huyo mtu kwanye kioo kwa dakika moja. Kisha badilishana majukumu. 80. Mchezo Humfuata Kiongozi Chukua nafasi ya kiongozi kwa muda mrefu iwezekanavyo, kisha acha kiongozi mwingine achukue nafasi. 81. Cheza mchezo wa sanamu: mtu mmoja anaganda kama sanamu na mtu mwingine afanye sanamu icheke. Badilishaneni. 82. Endeleza utamaduni wa familia: imba wimbo pamoja, kariri shairi, au fanya mambo fulani ya ufundi.

Kuhusu Karen Wang

Karen Wang ni mzazi wa Urafiki wa Mzunguko. Utakuwa umeshawahi kumwona akijipenyeza kwenye ukumbi wa

kujitolea wa aisikrimu au akisukumwa kwenye siagi na watoto wanaocheka. Ni mtunzi mchangiaje kwenye kitabu

cha

"My Baby Rides the Short Bus: The Unabashedly Human Experience of Raising Kids With Disabilities"

kiungo kwenye makala:

http://www.friendshipcircle.org/blog/2012/06/20/82-summer-activities-for-families-with-special-needs/

GREDI ZA ECE - Chekechea

Page 9: Tunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili ya kusaidia ...face.dpsk12.org/wp-content/uploads/2014/07/Summer-Learning-Guide_Swahili-FINAL.pdfTunathamini kila kitu unachofanya kwa ajili

SSiikkuu HHuurruu 22001155 nnaa SSCCFFDD

Mashirika haya hutoa udahili wa bila malipo kwa wakazi wa Colorado katika siku zilizochaguliwa za mwaka.

Siku Huru 2015 imafadiliwa, kwa kiasi fulani, na raia wa kaunti za Adams, Arapahoe, Boulder,

Broomfield, Denver, Douglas na Jefferson kupitia 0.1% ya mauzo na kodi ya matumizi ya SCFD

Makumbusho ya Sanaa ya Denver Museo de Arte de Denver

Januaryi3 Februari 7 Machi 7 Aprili 4 Aprili 26 (Día de los Niños) Mei 2 Juni 6 Julai 11 Agosti1 Septemba 5 Septemba 12 Oktoba 3 Novemba 7 Disemba 5

Busatani za Kibotania za Denver Jardines Botanicos de Denver

Januari 19 Februari 16 Machi 22 Aprili 22 Julai 21 Agosti 31 Septemba 9 Novemba 13 Novemba 14

Busatani za Kibotania za Denver huko Chatfield Jardines Botanicos de Denver en Chatfield

Januari 6 Februari 3 Machi 3 Aprili 7 Juni 2 Julai 7 Agosti 4 Novemba 3

Kituo cha Denver cha Sanaa za Maonesho Centro de Denver para las Artes Interpretativas

SCFD 10 kwa $10 Kila Jumanne saa 10am, Kituo cha Denver cha Sanaa za Maonesho kitatoa tiketi chache za $10. Viti kumi kwa kila Kampuni yenye Ukumbi wa Sanaa za Maonyesho Katika kituo cha Denver kwa wiki inayokuja itafuzu (hadi maonyesho 25 kwa wiki.) Tiketi zinapatikana kupitia simu (303-893-4100) au kwa kufuata mwenyewe katika jengo la Helen Bonfils Theatre Complex katika ukumbi wa Speer & Arapahoe.

Makumbusho ya Maliasili na Sayansi ya Denver Museo de Naturaleza y Ciencia de Denver Januari 5 Januari 25 Machi 2 Aprili 12 (Earth Day) Aprili 25 (Dia del Niño) Mei 31 Juni 29 Julai 26 Agosti 17 Septemba 27 Oktoba 19 Novemba 9

Bustani ya wanyama ya Denver Zoologico de Denver

Januari 11 Januari 12 Januari 22 Februari 6 Februari 7 Februari 19 Novemba 2 Novemba 13 Novemba 19