20
UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe Mussa Shekinyashi [email protected] 0714 80 75 65 0743 98 98 29

UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

  • Upload
    others

  • View
    8

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe

Mussa Shekinyashi

[email protected]

0714 80 75 65

0743 98 98 29

Page 2: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Utangulizi

Ngoswe penzi kitovu cha uzembe ni tamthiliya maarufu sana ambayo imewahi kuigizwa katika redio Tanzania na katika majukwaa mbalimbali hapa nchini. Ni tamthiliya ambayo imeundwa vyema katika vipengele vya fani na maudhui. Ameteua lugha nzuri na yenye mvuto kwa wasomaji yenye mbinu za kifasihi zilizosheheni, muundo wenye mtiririko mzuri, unaoakisi kuanza kuchipuka kwa matukio mpaka kilele cha matukio. Wahusika wamebeba vyema uhusika wao mfano Ngoswe.

Ameibua dhamira kuhusu mambo yanayoigusa jamii ya leo kama vile uzembe, madhara ya ulevi, uzembe kazini, suala la matabaka kati ya mjini na vijijini. Mtazamo, falsafa na msimamo wake ni kulenga kuibadilisha jamii na kuleta maendeleo.

Page 3: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Vipengelevya

Maudhui

Page 4: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Dhamira

Page 5: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Ukosefu wa Elimu

Mwandishi anatumia wahusika wake kuonesha tatizo la kukosekana kwa elimu miongoni mwa wanajamii. Mhusika Mzee mitomingi hajui kusoma. Hii inaonekana pale Ngoswe anapomkabidhi kiitambulisho asome lakini anashindwa.

Pia watoto katika kijiji kile hawaendi shule. Watoto wa Mitomingi na wale wa Mama Mjane hawasomi bali hufanya kazi za nyumbani na shamba tu.

Kwa upande mwingine, mhusika Jimbi kutofahamu tarehe yake ya kuzaliwa ni ishara tosha kwamba katika kijiji hiki watu hawafahamu kusoma na kuandika.

Mwisho wahusika kukataa kuhesabiwa kwa kuwa waliamini kuwa kuhesabiwa ni kurogwa. Hii inadhihirisha kuwa wananchi hawajui maana na umuhimu wa sensa.

Page 6: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Mapenzi ya Ulaghai

Mapenzi ya ulaghai ni yale ambayo mmoja kati ya wapenzi anakuwa hana ukweli katika uhusiano husika.

Mwandishi wa tamthiliya hii anaonesha uwepo wa mapenzi ya ulaghai miongoni mwa vijana.

Anamtumia mhusika Ngoswe anayemlaghai Mazoea ili aweze kutoroka kwa wazazi wake.

Katika jamii yetu kuna vijana walaghai wa mapenzi.

Page 7: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Imani Potofu

Dhamira hii inaibuka kupitia Mama Mjane anayeficha watoto ili wasihesabiwe.

Katika mawazo yake aliamini kuwa wanaohesabu watu ni wachawi. Mbali na hilo mhusika huyu aliamini kuwa mumewe alikufa kwa kurogwa.

Imana hizi zipo miongoni mwa wanajamii. Hapa mwandishi anaiakisi jamii kwa jicho pevu na kuikosoa.

Page 8: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Athari za Ulevi

Wanaume wengi hujihusisha na vitendo vya ulevi wa pombe.

Tabia hii inaathari nyingi kwa familia na jamii kwa ujumla. Mwandishi anamtumia mhusika Ngoswe kuonesha athari ya pombe.

Hii imejitokeza pale Ngoswe anapochoma karatasi za kuhesabia watu.

Pia Ngoswe na Mitomingi kushindwa kufanya kazi siku iliyofuata.

Hii inadhihirisha namna pombe inavyoweza kuwa chachu ya uzembe na kurudisha maendeleo nyuma.

Page 9: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Umasikini

Mfumo mzima wa maisha katika kijiji kile unaonesha kuwa wanachi wa kijiji kile ni masikini.

Kukosekana kwa elimu, kukosekana kwa huduma za afya, shule kuwa mbali na makazi ya watu na imani za kishirikina ni moja ya mambo yanayoashiria umasikini.

Mwandishi anasawili hali halisi ya vijiji vingi nchini Tanzania kupitia hali hizi.

Page 10: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Mapenzi Chanzo cha Uzembe

Dhamira hii inajidhihirisha kupitia mhusika Ngoswe ambaye anapoteza takwimu za serikali kwa sababu za mapenzi.

Vijana wengi kwenye jamii yetu hupoteza muda mwingi kwenye masuala ya mapenzi.

Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii.

Page 11: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Nafasi ya Mwanamke katika Jamii

Mlezi wa familia: mhusika Mama Mazoea na Mama Mainda

Kama kiumbe asiye na maamuzi sahihi: kitendo cha mama Mazoea kushindwa kuwakanya Mazoea na Ngoswe alipowakuta Kisimani.

Kama kiumbe asiye na msimamo: Mazoea

Kama mtu anayedharauliwa: Kitendo cha Mitomingi kumfokea mke wake mbele ya mgeni

Page 12: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Ndoa za Mitala

Utamaduni huu umebainishwa kupitia familia nyingi ndani ya tamthiliya hii.

Mwandishi anaonesha kuwa wanaume wengi katika kijiji kile wameoa mke zaidi ya mmoja.

Hajaonesha wazi kuwa utamaduni huu ni mbaya ingawa haushauriwi sana katika jamii.

Hii ni kwa sababu za kiuchumi na kiafya (kuenea kwa magonjwa ya zinaa)

Page 13: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Kukosekana kwa Huduma za Kijamii

Huduma muhimu za kijamii ni kama shule na hospitali.

Katika mazungumzo ya wahusika inabainishwa kwamba huduma za kijamii kama shule, hospitali na huduma nyingine za kijamii zipo mbali na makazi ya watu.

Hii inadhihirisha ukosefu wa huduma za kijamii jambo linaloashirikia umasikini miongoni mwa wananchi katika kijiji kile.

Page 14: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Vipengele vingine vya

Maudhui

Page 15: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Ujumbe

Mapenzi ni chanzo cha uzembe katika jamii yetu

Kukosekana kwa elimu kunarudisha nyuma maendeleo

Imani za kishirikina ni adui wa maendeleo

Ni vizuri kufikiri kabla ya kutenda

Pombe ni adui mkubwa wa ustawi wa maendeleo ya binadamu

Mshika mawili moja humponyoka

Njia ya muongo ni fupi. Mazoea kumdanganya mama yake.

Kuwa na msimamo husaidia kuepuka vishawishi.

Page 16: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Migogoro

Mgogoro kati ya Jimbi na Mitomingi baada ya jimbi kusahau siku ya kuhesabiwa akatuma watoto shambani.

Mgogoro kati ya Ngoswe na Mzee Jimbi wakigombania idadi ya miaka ya mzee Jimbi

Mgogoro kati ya mazoea na Mama Mazoea baada ya mazoea kuchelewa kurudi mtoni

Mgogoro kati ya Mitomingi na wakinamama wajane baada ya kuficha watoto wasihesabiwe

Mgogoro nafsia aliokuwa nao ngoswe baada ya kumkaribisha mama Mazoea ndani akidhani ni Mazoea.

Mgogoro nafsia aliokuwa nao Ngoswe baada ya kuchoma karatasi kwa ulevi

Page 17: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Muendelezo…

Mgogoro kati ya Mzee Mitomingi na Mama Mazoea baada ya Mazoea kuitwa na baba yake kisha akadanganya kuwa alikuwa anamsuka mama yake.

Mgogoro kati ya Mitomingi na wake zake baada ya Mazoea kutoroshwa.

Mgogoro kati ya Ngoswe na Mitomingi

Mgogoro wa nafsi aliokuwa nao Ngoswe baada ya karatasi zake kuchomwa moto.

Mgogoro kati ya Ngoswe, Mitomingi na Serikali.

Mgogoro wa kitabaka kati ya mijini na vijijini

Page 18: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Falsafa

Mwandishi anaamini kuwa ni vigumu kwa mwandamu kuchanganya mapenzi na kazi.

Anafafanua kwamba katika hali kama hiyo kimoja kitafanywa vizuri zaidi ya kingine.

Anamtumia mhusika Ngoswe aliyepoteza hesabu ya watu kwa sababu za uzembe wa kimapenzi.

Pia anaamini kuwa elimu inanafasi ya kutatua matatizo ya kijamii. Jamii ikielimika basi maendeleo yatatokea kwa urahisi.

Page 19: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Mtazamo na Msimamo

Mwandishi anaiangalia jamii katika mtazamo yakinifu.

Anabainisha masuala yanayoigusa jamii waziwazi.

Mwisho anapendekeza masuluhisho ya masuala hayo.

Huu ni msimamo wa kimapinduzi kwa kuwa unalengo la kujenga jamii mpya.

Page 20: UHAKIKI wa NGOSWE Penzi Kitovu cha Uzembe€¦ · Mwandishi anawakumbusha vijana juu ya hatari ya kuchanganya mambo mawili wakti mmoja kupitia dhamira hii. Nafasi ya Mwanamke katika

Asanteni kwa kunisikiliza