64
UMOJA NA MAPENDO GAZETI LA MAFRATERI WA JIMBO KATOLIKI SINGIDA TOLEO LA KWANZA 2013.

UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

  • Upload
    others

  • View
    5

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

UMOJA NA MAPENDO GAZETI LAMAFRATERI WA JIMBO KATOLIKI SINGIDA

TOLEO LA KWANZA 2013.

Page 2: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

UMOJA NA MAPENDO GAZETI

TOLEO LA KWANZA 2013

UMOJA NA MAPENDO NI GAZETI LA KILA MWAKA LINALOTOLEWA NA MAFRATERI WA JIMBO KATOLIKI

SINGIDA KWA LENGO LA KUJUZA, KUELIMISHA NA KUTAFAKARISHA.

KWA YEYOTE ANAYEHITAJI NAKALA AWASILIANE NA: UMOJA NA MAPENDOMAFRATERI JIMBO KATOLIKI SINGIDA P.O.BOX 487 SINGDA.

Page 3: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 3

YALIYOMO1.Utanguli.......................................................................................... 4

2.Mafrateri hongereni kwa kuanzisha gazeti..................................... 6

3.Mwaka wa Imani: Dalili na athari za kutetereka kwa Imani........... 7

4.Be courageous, open and sincere.................................................. 8

5.Uhai Singida Umoja na Mapendo................................................... 9

6.Utume wa walei katika kanisa........................................................ 13

7.Vijana na maisha ya uchumba........................................................ 19

8.Sala inalipa..................................................................................... 23

9.Jicho langu...................................................................................... 27

10.Haya mateso!............................................................................... 30

11.Utume kwa watoto....................................................................... 33

12.Yesu mfano wa kuigwa katika uinjilishaji...................................... 35

13.Rehema kamili katika mwaka WA imani....................................... 41

14.Fumbo la uhai wa Binadamu....................................................... 42

15.Aliye na masikio na asikie............................................................. 43

14.Why do Catholics use Holy water................................................. 47

15.The word of God and the Eucharist.............................................. 48

16.Chama changu kina nini?............................................................. 49

17.Faida yenye hasara....................................................................... 55

Page 4: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 4

UTANGUZI

Umoja na Mapendo ni kiitikio cha kauli mbiu, salamu na moto

ya Jimbo letu Katoliki Singida am-bacho ni Uhai Singida-Umoja na Mapendo ni msingi, mhimili, asili na chanzo chetu wanafunzi wa upadre-Mafrateri kupata nguvu na mwamko wa kuanzisha gazeti ambalo tumea-mua kulipa jina lake “UMOJA NA MAPENDO GAZETI”. Lengo hasa la kuanzisha gazeti hili ni kujijengea utamaduni wa kusoma, kuandika na kutoa tafakari mbalimbali kwa njia ya kuandika ili tuweza kuwapelekea watu habari njema ya neno la Mungu katika nyanja za kiimani, kimaadili na kijamii. Msingi wake ni kuchua hatua na kutekeleza mapango wa kanisa juu ya uinjilishaji mpya.

Tunaposema Uinjilishaji Mpya hapa haina maana ya kuhubiri Injili mpya kinyume na hii tunayoifahamu bali ni kupeleka Injili kwa watu kwa kutumia mbinu mpya na za kisasa kadiri ya mazingira ili kwamba ujumbe wa neno la Mungu uweze kuwafikia watu walipo katika maz-ingira yao walipo kwa kutumia njia na mbinu ambazo kwao zinakua rahisi kupokea na kuelewa ujumbe

wa neno la Mungu na kumfahamu Yesu Kristo aliye njia, ukweli na uzima wetu. Hapa lazima tuchukue angalisho na tuelewe kuwa kutumia njia na mbinu mpya haina maana ya kuibadili Injili au maandiko ma-takatifu kulingana na mazingira ya watu. Hapa tunamaana ya kutumia njia ambazo zinazotuwezesha ku-wafikia watu wote, vijana, watoto na wazee walio na elimu ya juu ka-bisa, ya wastani na walio na elimu duni. Uandishi ni moja ya njia za kuwafikishia watu ujumbe hususani wasomi na walio na weledi wa kuso-ma na kuandika. Tumeamua kuanza rasmi katika mwaka huu wa imani ili tuweza kuangalia mwenendo wa imani yetu kama wakristo. Wazo hili limechukua muda mrefu tangu tulipolijadili kwa mara ya kwanza mwaka 2007. Lakini kutokana na ukosefu wa vitendea kazi kama vile “computer” na utaalamu ni jinsi gani tungeweza kufanya kazi hii iweze kukubalika na kuwafaa watu hatukuweza kuanza. Kwa mawazo na maelekezo ya watu wengine na kadiri tulivyozidi kuwa weledi tuka-ona kuwa tukijaribu tunaweza ku-fanya kitu kizuri cha kuwafaa watu. Tumethubutu, tumeweza na hivi leo tumeanza rasmi katika mfululizo wa kutoa gazeti kama hili ambalo lita-kua la kila mwaka.

Baada ya utangulizi huu hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mun-gu, kwanza kwa zawadi ya Uhai

Page 5: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 5

aliotujalia ili tumjue, tumpende, tumtumikie na mwisho tuweze kufi-ka kwake Mbinguni. Pili kwa zawadi kubwa ya wito wa kuwa wakristo am-bayo ndiyo njia ya kutufikisha kwake na zaidi sana kutuita kwa namna ya pekee katika wito huu mtakatifu wa kuwa makasisi na watenda kazi ka-tika shamba lake pasipo mastahili yetu. Tunamshukuru pia kwa kutu-linda, kutuongoza, kutupatia neema na Baraka zake na hivyo kuwa hivi tulivyo na kutuwezesha kutoa kwa mara ya kwanza gazeti hili kwani Mungu asipoujenga mji waujengao wanafanya kazi bure.

Tunamshukuru sana aliyekua Asko-fu wa Jimbo letu katoliki Singida na sasa ni msimamizi wa kitume jim-boni mwetu Baba na Mlezi wetu Mhashamu Askofu Desiderius Rwo-ma kwa kukubali wazo letu, kututia moyo kuwa tunaweza na yeye mwe-nyewe kuchangia kwa kiasi kikubwa kwa hali na mali katika kufanikisha kutoa gazeti hili. Tunasema asante sana Baba Mungu akujalie neema na Baraka zake uzidi kudumu katika utume wako.

Tunaushukuru pia uongozi mzima wa jimbo letu katoliki Singida kwa kukubali na kutupa Baraka zote za kutoa gazeti hili. Shukrani hizi ziende hasa kwa aliyekua mkuru-genzi wetu wa miito Pd. Aloisi Moss, Msarifu wetu wa jimbo mheshimi-wa Pd. Edward Mapunda, aliyekua

Makamu wa Askofu na sasa ni msaidizi wa msimamizi wa kitume jimboni mheshimiwa Pd. Francis Lyimu pamoja na Mkurugenzi wetu wa miito kwa sasa Pd. Gabriel Choda wote katika umoja wao pamoja na mapadre wote tunasema asanteni sana kwa moyo wenu wa kibaba kwa kututia moyo kuwa tunaweza.

Hatuna budi kujishukuru wenyewe pia kujipongeza kwa kazi hii am-bayo kwayo tunajiendeleza kiakili na kiroho. Hata hivyo kazi hii ni tun-da la mikono ya wanadmu ambaye si mkamilifu na hivyo inaweza kuwa na mapungufu ndani yake, hivyo ili iweze kuwa kazi bora tunakaribisha maoni, mapendekezo na masahi-hisho ili kazi hii iweze kuwa na man-ufaa kwa kanisa mahalia la Singida na hata kwa watu wengine pia ka-tika kuendeleza kazi ya uinjilishaji kwa sifa na utukufu wa mwenyezi Mungu.

Asanteni sana Mungu awabariki nyote.

Na Frt. Paschal D.J. Ighondo Mwaka nne Teolojia

Page 6: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 6

MAFRATERI HONGERENI KWA KUANZISHA GAZETI

Mafrateri wa Singida, pongezi zangu pateni,Nilijua mnaweza, kuanza lenu gazeti,Hilo sasa limetoka, wote sasa lisomeniKiu ya gazeti zima, soma na lipe habari

Histori mmejenga, ya gazeti lenu hiliTupe yenu ya busara, yahu mwaka wa imaniTujue yote kwa kina, imani tuishi vipiKiu ya gazeti zima, soma na lipe habari

Na miito kuipenda, zenu mbinu tupasheni,Dung’unyi nayo Diagwa, vijana wafurikeniUsista na uburuda, wengi kuupokeeniKiu ya gazeti zima, soma na lipe habari

Gazeti hili kuchapa, vijisenti lahitajiFrateri wako waomba, msaada kuwapeniVipaji waweze kuza, Frateri walo shuleni Kiu ya gazeti zima, lipeni zako habari.

Na: Askofu Desiderius M. RwomaMsimamizi wa Kitume

Jimbo la Singida.

Page 7: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 7

Ushirikina ndiyo dalili kuu ya kutetereka kwa imani.

Ushirikina huu upo katika jamii na hata miongoni mwa wale wanaom-wamini Kristo. Ukatili wa kinyama wa maalbino, biashara ya viungo vya binadamu, mauaji ya vikongwe kwa visingizio mbalimbali, safari za ungo, imani katika tiba za masharti ya kishirikina kama vile kutoa kafara za watu au kufanya tendo la ndoa kinyume na maumbile na kuvunja baadhi ya amri za Mungu kwa imani potofu kuwa kwa njia hiyo atafaniki-wa katika biashara, kupata ajira au uchimbaji wa madini, kufaulu miti-hani au kupata mchumba. Tiba hizi zenye masharti kama hayo ni uvun-jifu wa amri ya kwanza ya Mungu, hazina tija na ufanisi katika maisha ya kikristo zaidi ya kumuathiri mtu mzima kiroho na kimwili. Ufyekaji wa mashamba ya migomba na mi-buni ya wanaodhamiwa kuwa ni wa-chawi na watu wanaojiita “vifaru”, dhana ya uwepo wa wataalamu wa kufanya mvua inyeshe wakati wa ki-angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo wazi za uwe-po wa ushirikina.

Vichochezi vya ushirikina ni umaski-ni unaompelekea binadamu, kukosa elimu, afya na maisha bora Katika hali hii ya umaskini binadamu ana-badilika na kuingia katika utaratibu wa bendera fuata upepo.

Mkristo huanza kubadilika kulinga-na na nguvu za ushawishi wa upepo wa maoni ya watu binafsi au wahu-biri wa dini zinazozaliwa kila kuki-cha wanaodai wana majibu muafaka ya matatizo yake yote.

Matatizo ya kiroho au kimwili ya-napomfika maskini anajikuta hana nguvu za kiuchumi, elimu-dini na elimu-dunia yakutosha kumwezesha kusimama imara na kutolea uamuzi fumbuzi na sahihi kwa changamoto za maisha yake. Matokeo yake mtu wa aina hii hupotoshwa kirahisi. Hu-kimbilia huduma iliyokaribu naye. Hubadili dini kwa kupewa zawadi chambo, ahadi ya kupewa fedha na wengine hukimbilia nguvu za giza na kupiga ramuli wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo watapata jawabu muafaka kwa matatizo yao.

TAMAA YA MALI NA UPAGANI WA KIMAGHARIBI NI KICHO-CHEZI KINGINE CHA USHIRIKINA. Tamaa ya mali wakati wetu huu inapandikizwa nchini kwa njia ya utandawazi na baadhi ya madhehe-bu ya kidini au makundi ya wasomi walioathiriwa na maisha ya tamaa ya mali na upagani wa kimagharibi dhidi ya dini zisizounga mkono uta-jiri unafumbia macho uwepo wa ta-baka za maskini na matajiri. Tamko hili la Kristo kuwa…ni rahisi zaidi

MWAKA WA IMANI: DALILI NA ATHARI ZA KUTETEREKA KWA IMANI

Page 8: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 8

kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufame wa mbinguni…” (Mk.10:25) haliwafurahishi matajiri wa dunia hii, watu binafsi na madhehebu ya dini zisizomwamini Mungu wa kweli aghalabu kwa kusukumwa na tamaa ya mali huwavuta watu kwa ahadi za kutajirika kimiujiza, maombezi ya kufuta nuksi na kumaliza haraka matatizo yao mengine ya kiroho au kimwili. Labda hii ndiyo sababu in-ayopelekea wakristo kutafuta ku-jua na wengine kuhofu malengo ya “freemasoni” na kile kinachodaiwa kuwa ni dini ya waabudu shetani (devil worship).

Ukiangalia kwa makini makundi ya aina hii hudai yanahitaji huduma au wanachama wa dini yao watangulize malipo ya “chochote” au wapeleke “shukrani “ baada ya kupata vingi-nevyo walichopa-mali au tiba wata-vipoteza au matatizo yao yataware-jea na hali yao itakuwa mbaya zaidi na hapatakuwepo tena uwezekano wa kupata tena alichopoteza.

Waamini wapendwa, “SIMAMENI IMARA KATIKA IMANI YA KWELI” ya Kanisa Moja, Takatifu, Katoliki na la Mitume.

Na: Askofu Desiderius M. Rwoma

Msimamizi wa KitumeJimbo la Singida.

BE COURAGEOUS, OPEN AND SINCERE

Fr. Gabriel C. Choda -Vocation Director, Singida Diocese

Reflection on Mt. 4: 1-11This part of the Gospel is full of sym-bolism. Jesus our Saviour is led by the Spirit into the desert after his bap-tism in the Jordan to confront Satan. Jesus must go into the desert before the beginning of his public ministry because the source of the problems of this world is Satan. Satan`s role is to mislead, to dehumanize and to turn us away from God. In the Bible the desert has always been seen as the home of evil. Jesus enters it for forty days and walks out victorious-ly. He conquers evil, he conquers the desert. “HE SHOWS US THE WAY TO THIS STRENGTH.”

The desert is where good and evil battle. The Israelites spent forty years there to be formed and shaped into God’s people. They entered the

Page 9: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 9

desert with a sense of purpose and unity. They were on a mission to find and live in the Promised Land. They should have grown stronger on the journey. Instead, they became divid-ed, tired and confused. They were not the people they imagined they were. The desert is important to a Seminarian, to a Priest, to us all for exactly the same reason. We are not the people we think we are. We have our illusions, our idols and security blankets. Without them we see that we are quite little, very poor and empty. The desert gives us the abil-ity to find out who we are and who God is. We can then come to God with a more realistic picture of our-selves.

Dear Seminarians, dear Priests and dear leaders of this magazine, Vic-tory is possible but the battle will not be easy. My prayer for us all is that: Be courageous, open and sin-cere, Don’t give up. St. Paul tells the Romans that “the love of God has been poured forth in our hearts by the Holy Spirit, who has been given to us” (Rom 5:5). This love embraces all in the Church and beyond it.

Yours Sincerely Fr. Gabriel C. Choda Vocation Director, Singida Diocese

UHAI SINGIDA UMOJA NA MAPENDO

Frt. Anselm Matungwa

Ni fursa nyingine kwetu sisi waamini wa Jimbo Katoliki la

Singida kuweza kutafakari tena juu ya kauli mbiu yetu ya Uhai Singida Umoja na Mpendo. Nilipokuwa natafakari nilijikuta nimetwaliwa juu sana kiroho kwani neno “uhai” kwetu sisi sote ni neno la kina sana. Nilijaliwa kuwa Singida kwa mara ya kwanza nilipohitimu kidato cha sita mnamo 2006, niliona mengi ya kuvutia. Ni mwezi wa tano sasa. Mambo niliyozoea kuyajua kwa na-dharia tu katika vitabu na kufikirika kwangu niliweza kuyaona kwa ma-cho yangu mwenyewe bila kutumia miwani wala darubini.

Mandhari ya asilia, na kilimo cha alizeti nilichokuwa nikisoma ka-tika vitabu, punda wa kufanya kazi, magari ya kukokotwa na wanyama, kama ng’ombe wa kulima na kubeba mizigo, sehemu baadhi tambarare na miti mingi ya asili, kilimo cha jadi cha mahindi, uwele, mtama na ulezi ni baadhi katika kutaja ambavyo ni thamani na mali na aina yakuvutia

Page 10: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 10

nilivyokuwa sijashudia toka awali. Hii ilinivutia sana. Siwezi sahau magari ya kukokotwa na wanyama kama ng’ombe na punda. Kwa mara ya kwanza nilishuhudia, wanyama waliofundishwa na kuongozwa na watu wa rika zote, watoto wa miaka sita na wazee wa miaka sabini. Haya yote yalikuwa mageni kwangu na yalikonga hisia zangu katika hali ya furaha na kunihakikishia kuwa kuna uhai hapa singida.

Uhai huu ni juu ya mandhari ya ardhi, viumbe vyote, hai na visivyo hai vinavyomzunguka binadamu; wanyama, mimea, mawe, udongo mzuri wenye rutuba, hali safi ya hewa na binadamu mwenyewe. Hivi vyote ni vizuri sana na vyote ni mpango wa Mwenyezi Mungu. “…Mungu aliona kila alichokiumba kuwa ni kizuri sana...” (Mwanzo 1.31). Hapa tunafumbuliwa macho kuwa uhai wa kila kiumbe watoka kwa Mungu. Mimea na wanyama tu-naowatumia kwa kufanya kazi zetu, uzuri wa anga na hali ya hewa tu-nayoifurahia, na uhai tunaoufurahia hapa Singida unatiririka kutoka kwa Mungu mwenyewe. Uhai huu una-husu maisha yetu hapahapa duni-ani. Ni uhai wa asili unaoonekana wazi, hauhitaji uthibitisho maana ni ukweli uliowazi na sisi wenyewe ni mashahidi wa mambo haya yote tunayoyaona. Ni kutokana na umoja na ushirikiano wa Utatu Mtakatifu binadamu alipata uhai huu, wadudu

kama mchwa, viroboto na kunguni nao wakapata uhai. Kwa umoja wa Mungu mmoja katika nafsi zake tatu yaani Baba, Mwana na Roho Mtakatifu uhai ukawepo tena ni ma-tokeo ya upendo wa Mungu mwe-nyewe. Mungu akasema; “Natum-fanye mtu kwa sura na mfano wetu wenyewe…” (Mwanzo. 1:26). Hivyo basi binadamu wote; mwanamke na mwanaume, kikongwe na kijana ni wamoja kwani wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu mwenyewe.

Umoja ni ushirikiano, mshika-mano, na makubaliano ya kunia

kitu kimoja kwa uwazi utokao ndani ya kila nafsi ya mtu. Umoja pia ni mfanano, kuwa na mtazamo wa pamoja na kudhamiria kwa pamo-ja. Mfano wetu watoka kwa Mungu mwenyewe, “…natufanye mtu kwa mfano wetu…” (Mwanzo 1:26). Sisi ni matokeo ya umoja wa Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, hatimaye tukapata uhai. Hivyo basi sisi ni wamoja kwani sisi ni matun-da na matokeo ya Umoja wa Nafsi tatu za Mungu Mmoja. Kutokana na mapendo yake Mungu aliye mmoja nafsi tatu, tuko na uhai wa mwili na roho hapahapa duniani. Lakini, bin-adamu alivyo ni kiumbe dhaifu maa-na alipopewa zawadi hii ya uhai ha-kutimiza masharti na wala hakusita kumkaidi Mungu na kupoteza uhai (Mwanzo 2:17). Mungu naye hakus-ita kumuadhibu Adamu na Eva kwa kukosa usikivu (Mwanzo 3:14). Kwa

Page 11: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 11

kuwa Mungu ni uhai, Umoja na ni Upendo halisi, chanzo, chemchemi na mwanzo wa kila uhai, kwa upen-do hakusita kumrudishia uhai bina-damu kwa kuituma nafsi yake ya pili ndiye Yesu Kristu aje kumkomboa binadamu “...Baba alimtuma awe Mkombozi wa ulimwengu…anaishi katika muungano na Mungu…” Wae-brania 4:14-15.

Uhai tuliojaliwa tunaweza kuupote-za kwa ukaidi wetu kwa Mungu, kwa kufanya shughuli zisizo halali, kama vile wizi, unyang`anyi, ushirikina na kwa kutokubali majukumu yetu kama wazazi, watoto, walezi, wal-imu na wafanyakazi katika kazi zetu. Uhai wetu tutausalimisha kwa kuuishi upendo na kuwatumikia wengine kwani tukiupoteza uhai wetu kwa ajili ya wengine, tutau-salimisha na kuulinda. Mfano kwa kujishusha ili wengine watukuzwe, kutii amri, kutumikia wengine ku-liko kutumikiwa, kupenda wengine kuliko kupendwa, kuanza kusalimia wengine kuliko kusalimiwa, kusaid-ia wengine katika shida mbalimbali za hali na mali, kuombea wengine, kushuhudia mazuri kuliko mabaya na kutotakia wenzetu kupatwa na mabaya. Umoja wetu Wanasingida, kijimbo, kiparokia, katika kigango, na kwenye jumuiya zetu na zaidi sana katika familia zetu; ushamiri, ustawi, unawiri, uonekane na watu wasio wa jamii yetu na jumuia zetu, wasio wakatoliki, ili waongoke

waige mazuri kutoka kwetu, wap-ate mfano mwema, na mafunzo ye-nye mwelekeo kutoka kwetu. Umoja na mapendo miongoni mwetu na kati ya wengine basi uonyeshe uhai wetu tulionao kiroho maana ndio kiashirio na kielelezo cha kuishi kwa Mungu ndani mwetu. Umoja wetu uwe chumvi katika dunia na katika jamii tunamoishi. Chunvi huongezea chakula chetu ladha ili tunapokula chakula hicho tuweze kuishi na tuwe na uhai. “…ninyi ni chumvi ya dunia…” Mt. 5:13.

Dunia inapata giza kwa matendo yetu yasiyompendeza Mungu. Ma-janga mengi yanayoikosesha dunia amani, tamaa za mamlaka na mad-araka, mali na pesa haya yote saba-bu ni ukosefu wa umoja na mapendo duniani. Hakuna kutumikiana, ubin-afsi umetawala katika kujinufaisha matokeo yake ni vita vya wenyewe kwa wenyewe, madhara yake watu wasio na hatia kama watoto, vikon-gwe, wazazi na waamini wa Mungu hupoteza uhai.

Dunia inahitaji mwanga wa kufuku-za giza na kuweka mambo waziwazi, kufukuza ubinafsi ili kutetea amani, umoja, utaifa na upendo miongoni mwetu. Wakristu wa Singida tuen-delee kuwa wamoja katika Mungu na kufukuza mgawanyiko wa udini katika taifa letu kwani ni jukumu letu sote kwani tukiwa wamoja Kris-tu yuko ndani mwetu aliyemwanga

Page 12: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 12

na nuru ya ulimwengu. Matendo yetu yawe mazuri yenye umoja, upendo, ukweli, utii, unyenyekevu, ukomavu wa kiimani, uvumilivu na kuchukuliana, ukarimu kwa wasio wa itikadi na imani zetu na ukar-imu kwa wageni, kuomba na kuwa na moyo wa shukrani kwa Mungu, kujali wengine, utu wema na ubi-nadamu. Haya yote yaongozwe na maisha ya kupokea sakramenti na kujenga tabia ya kusoma neno la Mungu na hasa katekisimu yetu ya kanisa katoliki. Hivi ndivyo kuwa mwanga katika ulimwengu ili watu waone matendo yetu mema wamtu-kuze Mungu aliye mbinguni.

Mara nyingi tunashindwa kufanya vizuri kwakukosa umoja na map-endo. Penye nia pana njia, tukip-enda na kunuia pamoja tutashinda wala hatutashindwa. Hakuna aliye nuia na kupenda kwa nia nzuri ku-fanya jambo akashindwa. Mfano, tukiipenda ardhi yetu tutaitunza na kuithamini, tukipenda mazingira mazuri tutayatengeneza na kuyal-inda, tukihitaji hewa safi kwa ajili ya uhai wetu tutailinda na kuitunza pia kuijali na tutaifurahia.

Vivyohivyo tukipendana sisi kwa sisi katika Kristu tutathaminiana tangu aliyemdogo tumboni mwa mama tutamlinda, wazee na wakon-gwe tutawaheshimu na kulinda uhai wao na kuwatumikia kwa pamoja.

Ndugu zangu, basi tupendane na kuulinda uhai wetu kiroho pia kim-wili maana binadamu ni mwili na roho. Tupendane na kutunza tunu zile Mungu alizomjalia binadamu. Ardhi, misitu, wanyama, udongo na zaidi sana uhai wetu. Kuombeana na kutakiana amani, kufarijiana katika shida mbalimbali na mengine ma-zuri kama hayo. “Ikiwa mimi Bwana na mwalimu wenu nimewatawaza miguu, imewapasa nanyi kutawad-hana…” Yon. 13:3 hayo ni maneno ya Bwana wetu Yesu Kristu mwe-nyewe akiwasisitizia mitume wake juu ya upendo wa kutumikiana kwa upendo wa unyenyekevu.

UHAI SINGIDA……..NA Frt. Anselm Matungwa mwaka wa pili teolojia Seminari kuu ya Mtakatifu Agustino Peramiho-

Songea

Page 13: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 13

Frt Pashal Ighondo

Walei ni waamini wote walio-batizwa isipokuwa wale we-

nye Daraja Takatifu na wenye hali ya kitawa iliyokubaliwa na kanisa. Kwa ubatizo waamini wote wanait-wa kuwa watakatifu na wanakua kiungo cha mwili wa kristo yaani kanisa (Rom 12:4-5), mawe hai ya kuujenga mwili wa kristo na hekalu la Roho Mtakatifu anayefanya kazi ndani ya kila mmoja akimjalia vipaji na karama zake kwa ajili ya manufaa ya jumuiya na taifa lake Mungu ili kwayo Mungu atukuzwe na mwana-damu atakatifuze (1kor. 12:11, 2Pet 1:1). Hivyo kila mmoja anatumwa kwenda kutangaza habari njema kwa mataifa yote (Mt 28:18-20).

Hivyo basi sisi sote tuliobatizwa tunaitwa na kutumwa kutangaza neno la Mungu kwa namna na jinsi mbalimbali kadiri Roho Mtakatifu anavyotujalia. Utume wa walei ndio kushiriki utume wa kanisa lenyewe uletao wokovu na kuutimiza huo utume ni agizo ambalo wote wana-

pewa na Mungu mwenyewe kwa njia ya ubatizo na kipaimara. Jukumu hili ni la kikuhani na kiibada, kinabii na ushuhuda (LG 30-36).

Utume huu wa walei unajidhihirisha wazi kuwa unatoka kwa Mungu kwa tendo la uumbaji: “Mungu akasema, na tufanye mtu kwa sura na mfano wetu akatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na wanyama wa nchi kavu…Mungu akawabariki, akawaambia zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha” (Mwz 1:26, 28). Kwa maneno haya ya uumbaji tumepewa jukumu la ku-endeleza kazi ya Mungu hapa dun-iani. Mtume Paulo anatuambia; “Tena mjitahidi kutulia na kutenda shughuli zenu na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, hamtakuwa na lazima ya kuwategemea wengine kwa mahitaji yenu” (1Thes 4:11-12). Huu ni utume wetu tunaoupata kwa ubatizo, kwenda ulimwenguni pote kuwafanya mataifa wafuasi wake Kristo (Mt 28:19-20). Baba Mtakati-fu Yohane Paulo II, analiasa kanisa la Afrika akisema kuwa; Wakristo wa Afrika wanapaswa kuwa na jukumu la kujitegemea na kujiendesha we-nyewe. Hiki ndicho kinachosisitiz-wa na sheria ya Kanisa namba. 222: “Christ’s faithful have the obliga-tion to provide for the needs of the Church, so that the Church has

UTUME WA WALEI KATIKA KANISA

Page 14: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 14

available to it those things which are necessary for divine worship, for works of the apostolate and of charity and for the worthy sup-port of its ministers.”

Hili jukumu linaweza kutimizwa na waamini walei kwa namna na njia tofauti kadiri ya mpango wa Mungu kwa kila mtu. Njia mbalimbali za kulitegemeza Kanisa ni uwajibikaji wa waamini katika kutimiza nyajibu na majukumu yao kama walei ka-tika kuendeleza kazi ya utangazaji wa Injili kwa watu wote ni pamoja na zaka, sadaka, shukrani misa, ma-toleo, shukrani ya mavuno na mi-chango mbalimbali.

Zaka ni moja ya kumi ya mapato yote ya mwaka. Hivyo ni amri ya Mungu kumpa yeye mwenyewe iliyo haki yake (Walawi 27:30-33; Kumb 14:22). Hii inawezakuwa moja ya kumi ya mifugo, mazao au pesa. Zaka inaweza kujumlisha mi-chango yote iliyowekwa na kanisa. Kanisa letu linatulea kwa kuweka viwango vya kuanzia kima cha chini. Wengi wetu tunabaki katika kiwango tulichowekewa. Hii in-akuwa kutimiza wajibu na si kutoa shukrani zako kwa Mungu. Tukiwa watu tuliokomaa katika imani yetu tunapswa kunyayuka katika imani na mapendo kwa Mungu tukim-tolea shukrani zetu bila kufuata vi-

wango tulivyowekewa bali kutoa kwa ukarimu na Baba yetu aonaye sirini atatujaza. Sheria zinatudai kima cha chini kabisa mfano kanisa linaposema pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa pasaka jiulize kama ni kweli wewe wakati wa Pasaka ndio unapokea, basi utakua hujui bado umuhimu wa Ekaristia. Tena kwa kutotoa kwetu moja ya kumi kikamilifu ni wizi na udanganyi-fu. Ndugu zangu je ni kitu kidogo mwanadamu kumwibia Muumba wake? Hatujajifunza kwamba Mun-gu hadanganyi wala hadanganyiki? Mara nyingi tunajichumia laana kwa sababu tunamwibia Mungu. Ukosefu wa mvua, majanga mbal-imbali, wadudu waharibifu, ukosefu wa mzunguko wa pesa katika miji na vijiji vyetu na fanaka mbalim-bali wakati mwingine ni matokeo ya kumwibia Mungu (Malaki 3:6-12). Mwenyezi Mungu hufungua madi-risha ya Baraka kadiri ya ukarimu wetu kwake. Tazameni wazee wetu wa imani walivyobarikiwa (Mwz 14:18-20; 28:20-22).

Nani anapaswa kulipa zaka?Mkristo yeyote aliyefikisha umri wa miaka 18 anawajibika kulipa zaka kwa makuhani wa Bwana. Watoto pia wanaweza kulipiwa na wazazi ikiwa ni moja ya wajibu wa wazazi wakatoliki kuwalea watoto wao ka-tika maisha ya kikristo. Kumbe kwa

Page 15: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 15

namna hii watoto wetu wanajifunza kumtolea Bwana kwa heshima ya jina lake. Ndio maana ni vyema sana kuwepo utaratibu katika parokia zetu kuwa kila jumuiya siku ya ku-wasilisha zaka familia nzima inan-yanyuka na kila mmoja anatamka toka Baba hata mtoto wa mwisho.

Sadaka ni kile kinachotolewa na kuteketezwa kwa heshima ya Mun-gu, ili laana zifungwe na neema na baraka zifunguliwe. Sadaka kubwa na halisi ya sadaka zote ni ya Kristo msalabani (1Kor 5:7). Hii ndio kafara yenye nguvu ajabu. Misa ndio tam-biko kubwa kushinda matambiko yote. Ndiyo maana Padri Kabla ya kuanza mageuzo (kutambika) anat-ualika wote: “salini ndugu ili sadaka yangu na yenu ikubaliwe na Mungu Baba mwenyezi.” Neema na baraka tunazopata katika adhimisho la Misa Takatifu ni lazima kwanza mtu uwe katika moyo wa sala na ibada na ku-nyanyua moyo kwa Mungu, ujitoe kabisa nafsi yako pamoja na Kristo kwa Mungu kama Mzaburi anavyo-tuambia; “sadaka yangu Ee Mugu ni moyo mnyoofu, uliopondeka” (Zab 51:17). Kwa hiyo katika misa tu-napaswa kutoa mioyo yetu pamoja na vyote tulivyonayo yaani sehemu ya mali zetu kama ishara ya nje ya sadaka yetu ya moyoni. Pesa na mali tunazotoa tunaziita sadaka kwa sa-babu ni kile kinachotolewa kuwak-

ilisha sadaka ya ndani. Sadaka hii haipimwi kwa wingi bali kwa moyo si wingi wala ziada. Ni kutoa kilicho cha thamani kwako mbele ya Mungu wako ndiyo maana Yesu anamsifia Mjane kwa sababu ya kutoa vyote alivyokuwa navyo; moyo na nafsi yake vyote anamtolea Mwenyezi na kumtegemea kabisa. Lakini wen-gine walitoa vilivyo vya ziada. Hivyo sadaka ni kumtolea Mungu vilivyo vya thamani kama shukrani kwake kwa mema yote aliyotutendea.

Shukrani misa: Sadaka tunayotoa wakati wa misa ni sehemu ya tendo zima la kutuunganisha sisi na sadaka ya Yesu msalabani anayotolea kwa mikono ya padre nasi tunatolea mi-oyo yetu kwa kutoa mali zetu kama ishara ya sadaka yetu ya moyo. Ka-tika Ibada ya Misa takatifu sisi tu-naungana na Kristo anayejishusha na kuwa nasi katika maumbo ya mkate na divai yaani mwili na damu yake mwenyewe-Ekaristi Takatifu. Hivyo hatuna budi basi kumshukuru Kristo kwa upendo wake mkubwa aliotuonyesha kukubali kujishusha kwetu kukaa nasi ili atuokoe. Kazi yetu ni kutubu na kubadili maisha pia kutoa mali yetu kuonyesha shukrani zetu ndio maana tunatoa sadaka ya pili-shukrani.

Page 16: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 16

Matoleo: Tukisoma Kumbukumbu la torati 12:6 tunaelezwa wazi kuwa waamini wanapaswa kutoa matoleo ya hiari wanavyoona kadiri ya ma-hitaji ya kanisa ya wakati huo, wa-jisikie kwa hiari kumtolea Mungu ili Injili iweze kwenda mbele nahivyo watatimiza wajibu wao wa kuihu-biri injili.

Shukrani ya mavuno: Wakati wa Agano la kale shukrani ya mavuno iliitwa pia mavuno mapya. Zamani wazee wetu baada ya kuvuna wal-ipeleka sehemu ya mazao yaliyo bora kwa mtambikaji na sehemu nyingine kwa mtemi ili kujipatia Ba-raka na neema. Kwetu sisi Wakristo mtemi wetu ni Yesu na mtambikaji wetu ni Yesu kwa mikono ya pa-dre. Tukivuna mavuno mapya kabla hutujayatumia ni vyema kupeleka kwa Bwana anayetuwezesha ku-vuna hayo yote. Hivyo basi mavuno ya mwanzo tulete kwanza Hekaluni makuhani wayabariki tuache seh-emu kwa matumizi ya Kanisa na kingine tupeleke tukatumie kwa shukrani. Kama wewe si mkulima basi sehemu ya faida za biashara au sehemu ya mshahara na posho pamoja na zawadi kwa mwaka pele-ka kwa aliyekuumba na anayeku-wezesha siku zote. Tujiwekee hazi-na mbinguni tusiwe kama tajiri yule mpumbavu (Rej Lk 12:16). Basi leteni malimbuko yenu ya mavuno

kwa makuhani nao watayabariki na sehemu kidogo inakwenda kuchan-ganywa na akiba ya nyumbani.

Changizo: Kwa kuwa gharama za kuendesha shughuli za kanisa ni kubwa sana hivyo kuna aina ya ku-jitoa kwa njia ya changizo-huu ni utoaji kwa njia ya michango mbal-imbali ili kufanikisha shughuli zi-nazojitokeza kwa wakati. Inaweza kuwa ni ujenzi wa Kanisa, upanuzi, ukarabati wa ofisi na mengine kama hayo. Aina hii mara nyingi hubuni-wa na viongozi wa parokia, kigango au jimbo kwa kutegemea hitaji ili kufikia lengo.

MATUMIZI YA MAJITOLEA YA WAAMINI

Majitoleo ya waamini yanatumi-ka katika uendeshaji wa shughuli mbalimabali za kichungaji kama vile: Mahitaji ya Misa na Ibada mbal-imbali kama mishumaa, umeme, maji, hostia na divai. Kwa Chakula na mahitaji ya mapadre (1Kor 9:13; Hes 18:8), mafuta na matengenezo ya vyombo vya usafiri, ukarabati au ujenzi wa nyumba, ofisi au kanisa, asilimia fulani inakwenda jimboni ambayo ni pamoja na masomo ya wanafunzi wa upadre na mapadre kadiri ya mahitaji ya jimbo, chakula cha waseminari wadogo vikao vya kichungaji na matumizi mengineyo. Pia hutumika kwa kutoa huduma

Page 17: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 17

kwa maskini, wafungwa na wahi-taji mbalimbali. Hapa labda tuseme kidogo wapo Wakristo wanaofikiri kuwa wanaweza wao kama wao kwenda na kumsaidia maskini. Licha ya kuwa kusaidia wahitaji ni wajibu wa kila binadamu ni muhimu kutoa ili Kanisa kwa nafasi yake lifanye mambo hayo kama lilivyokabidhiwa na Kristo.

Kwanini Wakatoliki hatujitumi kutoa?:

Kwanza tumedekezwa na wamision-ari nasi tumejidekeza: Wamisionari walipoingia kwa mara ya kwanza petu kutuletea habari njema walitu-letea pia mahitaji ya kimwili kama vile nguo, sabuni, chakula na hudu-ma za afya. Kwa wakati huo ilikuwa sawa kabisa kwani tulikuwa nyuma sana kimaendeleo ya uchumi pia elimu na hivyo tulihitaji kweli msaa-da. Lakini leo hii tukitathimini kwa undani tumekwisha endelea vya ku-tosha. Sasa ni wajibu wetu kulitege-meza kanisa. Sisi ndio Baba na Mama wa Kanisa. Sasa kilema walichotua-chia wamisionari kinatutafuna hata leo katika mambo mbalimbali si ma-jitoleo ya pesa na mali pekee hata katika maisha yetu kijamii. Kutege-meza Kanisa ni tatizo. waamini wamezoea kutoa Tsh.100/= au amejitahidi 200/= ukiwaambia waongeze ifike Tsh.500/= hata 1000/= na kuendelea wanasema

dini imekuwa ghali mno. Wakati wa ulipaji zaka ukifika, waamini waki-himizwa kutoa fungu la kumi la mali zao wanasema wao ni maskini sana hivyo viwango ni vikubwa mno. La-kini si kwamba simu zao zinakosa vocha, moja moto moja baridi hawa-kosi, kuchangia harusi zaidi ya Tsh 25,000/= na sare juu lakini hizo hazikosekani. Wengine wanajiu-liza “kwani zaka hiyo ina kazi gani? Mbona zamani wakati wa maparoko wazungu hakukuwa na usumbufu huu? Ukiwaomba waamini kujitolea kazi fulani za maendeleo ya Kanisa, kwa mfano, kuchimba msingi au ku-kusanya matofali watauliza “kuna posho?” wengi watatoa udhuru ili kukwepa na wengine watathubutu kushawishi wengine kuwa BADO MAPEMA SANA KUFANYA KAZI BILA MALIPO.

Bahati mbaya sana hata baadhi ya viongozi wetu wengine wamekum-bwa na ugonjwa/ulemavu huu. Wanadiriki kuwatetea Wakristo wa parokia zao wasilipe zaka au wasi-toe sadaka kwa viwango vinavyoki-dhi eti Wakristo hawa ni maskini hali zao ni duni hawana kitu. Ndugu zangu hakuna mtu maskini ambaye hana cha kumpa Mungu wake isi-pokua aliyekwisha kufa ambaye anahitaji msaada wa sala zetu.

Page 18: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 18

Sababu ya pili ni kukosa ukereketwa.

Wakristo wakatoliki tumekosa uk-ereketwa wa kweli na Kanisa letu mahalia. Hatuoni uchungu wa kuo-na tunarudi nyuma, tunasali kwe-nye nyumba ya Mungu iliyochoka wakati sisi tunaishi kwenye majum-ba mazuri (Rej. Hag 1:2-11), hatujali kuona Makuhani wake Bwana waki-hangaika na usafiri au chakula. Hebu tuamke!! Inashindikana nini mmoja kusema ataweka kochi katika nyum-ba ya Mapadri, mwingine rangi seh-emu fulani, meza ya chakula, vyom-bo jazeni, vinywaji, chakula, mavazi ya misa, siborio hata kisipungue kitu Injili iende mbele wakati huo tunabadili maisha yetu. Tusitoe ki-dogo bali tutoa kwa ukarimu (2Kor 9:6-9). Sadaka huleta baraka (Mdo 9:36-43), tena ukijitoa wakfu pamo-ja na mali yako utakuwa umejiwekea hazina mbinguni (Mt 6:19-21; Lk12: 33-34) Hivi tunaitii Injili ya Kristo (2Kor 9:13-15), tunajiwekea mifuko isiyochakaa (Lk 12:33-34).

Utajiri wa mali asilia uliopo viji-jini: Wachache wanaweza kuanza kusingizia Ooh! sisi huku kijijini tuko nyuma kwani uwezo wetu ni mdogo ukilinganisha na mjini. Sisi ni maskini sana hatuna pesa ndio maana tuko nyuma ila tangu nikue sijawahi ona mwamini mfugaji aki-toa ng’ombe hata mmoja kama zaka au shukrani. Wakristo tunao utajiri mkubwa sana kama: - Ng’ombe, Mbuzi, Kuku, Bata, mazao kama: mahindi, dengu, mtama, karanga, papai, vitunguu, mawese, mbogam-boga, mayai na mengine mengi ali-yotujalia Mungu. Wote huu ni utajiri mkumbwa ambao Mwenyezi Mungu ameuweka vijijini basi nasi tumrud-ishie kwa furaha. Sasa Kama kuna utajiri mkubwa namna hii sio mjini sio vijijini sasa tatizo ni nini?

TAFAKARI CHUKUA HATUA UJIPATIE NEEMA NA BARAKA KWA KUENDELEZA KAZI YA UENEZAJI WA HABARI NJEMA KWA WATU

WOTE!

Na Frt Paschal Ighondo-Mwaka wa Nne Teolojia Seminari Kuu

Segerea

Page 19: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 19

VIJANA NA MAISHA YA UCHUMBA

Frt. Joseph Lyanga1. MAANA YA UCHUMBA

Kuna maana mbalimbali za neno Uchumba: Uchumba ni makubalia-no ya pande mbili baina ya mwa-namume na mwanamke wanaotaka kuoana. Uchumba ni hali ya watu wawili, mwanaume na mwanamke, wenye umri unaokubalika kijamii na wenye akili timamu kujitayar-isha kwa maisha ya ndoa. Uchumba ni kipindi cha matayarisho ya ndoa kati ya mwanaume na mwanamke ambapo hao wawili wanaamua kwa hiari yao na upendo wao kufanya matayarisho ya fungamano la kui-shi pamoja. Uchumba ni kipindi cha matayarisho ya mwanaume kum-wacha baba yake na mama yake na kuandamana au kuambatana na mwanamke kwa lengo la kuwa mwili mmoja (Mwa 2:23-24). Uchumba unawaunganisha mtu mme na mke wasiokuwa na uhausiano wa kiu-koo na wanaotarajia kukaa pamoja kama mume na mke (Katika baa-dhi ya makabila kuna utaratibu unaokubalika kwa watu wa ukoo mmoja kuoana, kama vile binamu, watoto wa baba mkubwa na mdo-go lakini uchumba wa namna hii

ni nadra sana na hauungwi mkono kutokana na sababu mbalimbali za kibayolojia. Uchumba ni kipindi am-bacho wachumba (mwanamume na mwanamke) wanakitumia kwa ajili ya kupata elimu ambayo inawatam-bulisha jinsi ya kuingia, kuishi na kudumu katika maisha ya ndoa siku zote za maisha yao. Mchumba (wachumba) ni mwanamume ali-yepeleka posa au mwanamke ali-yepelekewa posa na kukubaliwa na wazazi. Kwa kawaida wachumba ni watu waliokubaliana kuoana baada ya taratibu zinazoendana na mila na tamaduni za mahali kukamilika.

2. SIFA ZA UCHUMBAMuda usizidi walau kipindi cha mwaka mmoja au mmoja na nusu lakini kisichukue muda mrefu mno au mfupi mno. Kipindi mwanaume na mwanamke kufahamiana kwa mfano kutambulishana kwa wazazi wao au ndugu wengine. Viashiria vya fungamano huwasilishwa, kwa mfano mahari kadri ya mila na des-turi ya mahali na kabila. Kipindi cha kujenga na kuimarisha upendo na heshima kati ya watarajiwa, wakiin-goja kwa hamu siku yao ya ndoa. Kuchunguza kwa undani hali yako binafsi na kumchunguza mwenzako kwa lengo la kugundua kasoro za kitabia, magonjwa ya kurithi, ulema-vu, umri, elimu zaidi sana kuchun-guza UPENDO wa kweli. Kipindi cha kueleza mambo wanayoyapendelea na wasiyoyapendelea kwa uwazi

Page 20: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 20

bila kificho. Ni kipindi ambacho wachumba huweka mipango yao ya baadaye kwa uwazi; kwa mfano kazi, familia (ni watoto wangapi wazae na wapishane miaka mingapi waki-tumia njia asilia kuweka mpishano wa uzazi). Kipindi cha kuweka baya-na misimamo kuhusu mapato yao na kuelezana kwa uwazi mapato ya kila mmoja. Katika kipindi hiki wa-chumba hujiweka sawa kisaikolojia kwamba huyu ndiye na siyo mwing-ine nitakaye kaa naye maisha yangu yote. Ni kipindi ambacho wachum-ba hupata mafunzo na maelekezo kuhusu maisha ya ndoa kulingana na taratibu za mila na desturi za ma-hali kwa mfano kuhudhuria semina mbambali za uchumba.

3. MWANZO WA UCHUMBATuanze sehemu hii kwa kunukuu maneno kutoka katika kitabu cha Wimbo ulio Bora 3:1-4 ambayo ni; “Usiku nikiwa kitandani mwangu, niliota namtafuta nimpendaye moyoni mwangu; nilimtafuta, lakini sikumpata. Nilienda nikazunguka mjini, barabrani na hata vichochoro-ni, nikimtafuta Yule wangu wa moyo, nilimtafuta lakini sikumpata. Walin-zi wa mji waliniona walipokuwa wa-nazunguka mjini. Basi nikawauliza “Je, mmemwona mpenzi wangu wa moyo?” Mara tu nilipoachana nao, nilimwona mpenzi wangu wa moyo; nikamshika wala sikumwachia aon-doke, hadi nilipompeleka nyumbani kwa mama yangu, hadi chumbani kwake Yule aliyenizaa”.

3.1. NIAUchumba huanza na nia ya mwa-naume na mwanamke kutamani ndoa, yaani kumtafuta mpenzi wa kuoa au kuolewa. Matamanio hayo ni hali aliyoiweka Mungu ambayo yameumbwa kimaumbile au silika ya mvutano wa urafiki wa kudumu na upendo wa kweli kati ya mtu mume na mtu mke. “Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye” (Mwa.2.18). Na hivyo hupelekea mvulana au msi-chana kumtafuta mwenzi kwa lengo hilo. Hatimaye mvulana akimwona msichana kwa macho, akili na moyo hufanya mipango ili wakutane ma-hali fulani kwa maongezi. Katika hali ya aibu mtu huyo anaweza kuandika akiomba nafasi hiyo au akamtumia rafiki yake au wa yule mwenzake ili awasilishe ombi la kukutana. Katika miaka ya hivi karibuni, umezuka mtindo wa baadhi ya wanawake kuwaomba wavulana uchumba. Ka-tika baadhi ya watu hapa duniani ni kawaida kwa wanawake kuomba uchumba kwa wanaume kwa mfano kwa wahindi. Kwa vyovyote vile, ombi hutanguliwa na nia.

3.2. MUNGUKwa vile mtu huyu anamtafuta mwenzi wa maisha, yafaa sana kum-kimbilia Mungu kwa ajili ya kum-womba msaada. Chaguo la mwenzi wa maisha laweza kuwa zuri kama Mungu ameshiriki katika uchaguzi huo. Hivyo mchumba hanabudi kusali, kufunga na kuomba kwa

Page 21: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 21

imani ili Mungu amsaidie katika ua-muzi unaotarajia kuufanya. Mfano wa sala ya kumwomba Mungu ili kumpata mchumba mwema. “Ee Mwumba wetu, umewaunganisha watu katika ndoa takatifu. Nami na-tamani kupokea sakramnenti hiyo na kushirikiana na mwenzangu wa ndoa maisha yangu yote. Kwa hiyo nakuomba Ee Bwana unisaidie kuch-agua kwa hekima, nimpate mchum-ba mwema, safi, mwaminifu; nifuate zaidi uzuri wa roho kuliko wa uso na tabia njema kuliko umaridadi. Mioyo yetu iwe ya kulingana, nia zetu zipatane, tupate kuishi pamoja kwa amani na kulea jamaa kwa ku-kuheshimu wewe na kupata baraka zako Amina”. 3.3. KUKUTANA MARA YA KWANZAJiulize kwanza nikutane naye kwa lengo gani? Awe nani kwangu; Mchumba au rafiki? Matendo ya baa-dae ya watu hawa yanategemea sana maswali haya. Si jambo rahisi kuon-gea na mtu umpendae kwa lengo la kuoa au kuolewa naye. Kama huyo unayetarajia kukutana naye hakuku-weka moyoni au hata akilini mwake; unaweza ukakosa maneno ya kuon-gea naye. Kwa kawaida mwanaume ndiye anayeanza kuongea (au vingi-nevyo kwa kadri ya mila husika). Mwanaume asitarajie kupata jibu la ndiyo au hapana siku hiyo hiyo. Msi-chana ataomba atoe jibu siku ny-ingine. Kwa nini? Msichana anataka kupata ushauri kwanza kutoka kwa

wazazi, ndugu na marafiki, kufanya upelelezi juu yake kwani hana haki-ka kama maneno hayo hajamwam-bia msichana mwingine, kuchungu-za tabia yake na kujenga uhusiano zaidi kwa sababu uamuzi atakaotoa ni wa kudumu, hivyo anaogopa asije akajutia baadae.

3.4. MAHANGAIKO NA WASIWASIBaada ya kukutana mara ya kwanza, kinafuata kipindi cha mahangaiko zaidi: Mvulana anakuwa na maswali lukuki kichwani mwake. Kwa mfano, anaweza kujiuliza: Je, nitakubaliwa ombi langu au litakataliwa au labda ana mchumba mwingine? Msichana naye anajiuliza: huyu mwanaume hana msichana au mwanamke mwingine kweli? Je, ananipenda kweli au ananidanganya? Je, huyu si kama wale wengine walionidan-ganya? Tena anapata wasiwasi zaidi anapoona wavulana au wanaume wengine wanamtafuta; hali kadha-lika kwa msichana au mwanamke. Hivyo kila mmoja anakuwa ana-jiuliza nimfuate yupi, na nimwache yupi? Je, nikimpenda huyu atani-tunza milele? Wasiwasi unazidi zaidi kama kabla ya uchumba huo alikuwa na uhusiano wa “kimap-enzi” na mwanaume (au wanaume) kwa ahadi kuwa angemwoa lakini akajikuta ameachwa peke yake. Kwa wanawake ambao siyo tu walikuwa na “wapenzi” bali pia walizaa, suala la uchumba linaleta wasiwasi na mahangaiko makubwa zaidi. Mwa-

Page 22: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 22

naume aliyewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke (au wanawake) wengine anapata shida ya kuwa na mfungamano wa dhati, au upendo wa dhati. 3.5. KUKUTANA MARA YA PILIMuda tangu kukutana mara ya kwanza hadi mara ya pili unatege-mea matashi ya msichana husika.Yaweza kupita siku moja, mbili, juma moja au majuma mawili au hata mwezi mmoja na zaidi. Hiki ni kipindi muhimu cha kutafuta majibu yatokanayo na wasiwasi na mahan-gaiko. Ni kipindi ambacho msichana na mvulana hutafuta kupata taarifa zaidi kuhusu mwenzake. Hiki ni kama kipindi cha kungoja matokeo baada ya kufanya mtihani. Kipindi hiki ni vizuri kitumike kumwomba Mungu, aongoze njia, alete jawabu la kweli. Ni kipindi kigumu mno kwa wanaohusika, hivyo mkim-bilie Mungu daima katika kipindi hiki chote. Unaweza kusali hivi: Ee Mungu Baba wa mbinguni, wewe ulimchagua Yosefu kuwa Baba mlishi wa Yesu kristu, na kwa njia ya Bikira Maria ukawaletea binadamu mkom-bozi. Basi nami Ee Mungu natarajia kumpata mchumba ambaye atakuwa Mwenzi wangu wa maisha. Maisha yetu ya pamoja yatuletee ukombozi, yatuwezeshe kukufikia wewe Mun-gu. Unijalie Mwanga wa roho wako ili nipate jibu sahihi kwa mtu huyu aliyenijia/aliyeugusa mtima wangu akitaka/nikitaka awe/niwe mchum-

ba wangu/wake. Je, kweli Ee Mungu huyu ndiye upendae awe mume/mke wangu katika maisha yangu? Nakushukuru Ee Mungu kwani ka-tika kipindi hiki kabla sijakutana nae utakuwa umenisadia kupata jibu sahihi. Nakuomba hayo kwa njia ya kristo Bwana wetu. Amina.

Siku ya kukutana mara ya pili msi-chana (Kwa kadiri ya desturi za makabila mengi ya kibantu) anatoa jibu la NDIYO AU HAPANA kwa ombi la mvulana. Ndiyo au hapana ya msi-chana hutolewa baada ya kupata taarifa ya uhakika juu ya mvulana.Taarifa hizo zaweza kuwa juu ya; tabia yake, muungwana, mcheshi, mkimya, mhuni, mchoyo, mkarimu, mpole, mwenye hasira, mwenye chuki, mlevi, mlafi, msengenyaji, mwenye majungu, umri wake je, afya yake, kuna historia ya magonjwa ya kurithi katika ukoo wake, mtu wa kazi au la, kuna tetesi au taarifa za hakika kuhusu masuala ya ushiriki-na? Ndiyo au hapana yake huweka uhusiano mpya katika watu hao wawili. Jibu la hapana huvunja uhu-siano, na jibu la ndiyo hudumisha uhusiano.

Na Frt. Joseph Lyanga- Mwaka wa kwanza Teolojia Seminari kuu ya

Mtakatifu Agustino Peramiho-songea

Page 23: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 23

SALA INALIPA

Frt. Simon Mdanku

Tafakari ya ndani juu ya umuhimu wa sala katika maisha yetu ya

kila siku kama wafuasi wa Kristo ni ya lazima. Tukiulizana swali ya kw-mba: Je wajua jinsi ya kusali? Hakika wengi bila shaka tungeweza kush-angazwa na swali hilo na tungeweza kujibu kwamba nimejifunza kusali siku nyingi zilizopita na sasa nasali kila siku. Najua Sala za asubuhi, sala za jioni, sala ya kanisa (The Liturgy of the Hours) na licha ya hapo nasali rozari na pia nahudhuria maadhi-misho ya Misa Takatifu. Hakika jibu la namna hii laonyesha kabisa nia njema ya mtu ambaye yuko tayari kuishi maisha mema ya kikristo na hasa kusali daima, ni juhudi njema. Lakini hatutegemei tu kusali, bali kusali vyema. Jambo hili yamkini ni tatizo kubwa kwetu sisi wakristo tu-lio wengi. Hivyo pamoja na kuwa na imani ya sala tunapaswa kujihusisha na ubora na umuhimu wa sala. Ndu-gu zangu, mitume wenyewe walisali na kwa kuwa walikuwa ni waebra-nia waaminifu walidhani kuwa wal-isali vyema, walijua zaburi pamoja

na sala nyingine na pia walikwenda hekaluni mara nyingi kadiri ya she-ria, lakini walipomwona Yesu akiwa anasali kwa undani walitambua kwamba walihitaji kitu kingine zai-di katika sala na hivyo wakajisikia kumuomba, “Bwana tufundishe ku-sali” Luka 11:1.

Hivyo ndivyo inavyotupasa kufanya kwa maana hata kama tungejua ku-sali kwa namna gani, bado daima kuna nafasi ya kuimarisha sala yetu. Daima usitosheke na namna unavyojisikia kwamba unafahamu namna ya kusali. Pindi utakapopata nafasi ya kujichunguza kwa makini utagundua kuwa unajua kidogo sana juu ya sala. Kusali vyema daima kunahitaji msaada wa Mungu kwa kuwa sala ni zawadi ya Mungu na pia ni matunda ya juhudi zetu. Yesu ali-tuambia, “…bila mimi hamwezi ku-fanya chochote” (Yohana 15:5). Tu-napaswa kusikiliza na kuhamasika tunachoambiwa na Maandiko Mat-akatifu juu ya sala; “usiwe mlegevu wa kusali” Ybs. 7:10. Pia mafundisho mbalimbali ya kanisa yanaweza ku-tusaidia zaidi katika maisha yetu ya sala hasa tunapofanya tafakari juu ya mwaka wa imani kwamba kris-to ndiye mlango wa kweli ambapo kila mmoja wetu anapaswa kupitia. Tufungue mioyo yetu kwa Mungu kwa sababu anatungoja na kutuita ana hamu ya kukaa nasi lakini mara kadhaa haoni juhudi zetu za kupen-da kumkaribisha.

Page 24: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 24

Tazama jinsi alivyomfanyia Zakayo mambo mema: “Na Yesu alipofika mahali pale, alitazama juu akam-wambia; Zakayo, shuka upesi kwa maana leo imenipasa kushinda nyumbani mwako” (Luka 19:5). Hebu fikiri kama ingekuwa ni wewe unaitwa na Yesu kwa jina lako fu-lani, na pia anakuambia leo hii na-taka kushinda nyumbani mwako, ni furaha gani ambayo ungekuwa nayo. Sisi pia tunapaswa kumwalika mwe-nyezi Mungu kwa furaha. Sala yetu naamini bila shaka itapata msuku-mo mkubwa kama kila tunapotaka kusali tunakumbuka kuwa Mungu anatusubiri tushuke juu ya mti kama Zakayo na kutuita. Kwa kujua kuwa tunatamaniwa na kuitwa na Mungu, bila shaka nasi kwa upande wetu tutapatwa na hamu na kiu ya Mun-gu. Tamaa hii yetu ya Mungu itafan-ya sala yetu iwe ni ya furaha na uwe ni muda wenye matunda. Tutakuwa kweli tayari kujibu kwa ukarimu kwa lolote ambalo Bwana atatuhi-taji kama alivyofanya Zakayo.

KUKAA KIMYA NA KUSIKILIZANakumbuka vyema sana nilipokuwa bado seminari ndogo padre mtoa mafungo katika utaratibu ambao tulikuwa nao seminarini aliwahi kusema na hiyo kwangu ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kusikia maneno hayo, alisema “Silence is the best friend who never be-trays” ambayo kwa tafsiri yangu ya kawaida inasema kuwa “ukimya ni

rafiki yetu mkubwa ambaye kamwe hawezi kutusaliti”. Maneno haya ni yakini na sitaki kuyapinga kwa maa-na nimeonja matunda yake mengi sana mpaka sasa, lakini tunatakiwa kwenda zaidi na kujua pia namna ya kumsikiliza Mungu tunapokuwa ka-tika hali hii ya ukimya.

Kwa kweli wakati tunapoongea na watu, hatuongei wakati wote. Yatu-pasa kuwaachia pia wenzetu nafasi ya kuongea. Hivyo ndivyo inavy-otakiwa katika sala. Tusiongee tu wakati wote tunapokuwa katika sala bila kusimama. Tunatakiwa pia kuwa na muda wa kukaa kimya ili tuweze pia kumsikiliza Mungu ili sala zetu ziwe kweli maongezi na majadiliano kati yetu na Mungu kama tunavyosema, sala ni kuon-gea na Mungu. Mara nyingi inakuwa kinyume chake kwani tunajikuta sisi ndio tunakuwa waongeaji peke yetu bila kumpa Mungu nafasi ya kusema nasi na matokeo yake tunajikuta tu-naishiwa ya kusema na badala yake tunajikuta tayari tumeshatawanya mawazo mbali sana na sala zetu. Hivyo basi muda wa utulivu unahi-tajika kabla na wakati wa sala. Si rahisi vile mtu ambaye ametoka ka-tika mazungumzo au shughuli fulani na papo hapo akaingia moja kwa moja katika sala: mtu huyu kamwe hatakuwa na utulivu au ukimya wa ndani. Hebu tujiulize maswali ya-fuatayo: Je, nimezoea kujiandaa kabla ya sala, ziwe za jumla au bi-

Page 25: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 25

nafsi? Wakati wa sala, nikingundua ya kuwa mawazo yangu yanakwen-da nje ya sala, je ninafanya nini? Je ninakata tamaa ya kuendelea na sala? Au ninakuwa mtulivu na kui-kubali hali na mapungufu yangu na pia namtumainia Mungu kwa msaada anaonipatia wa kufanya sala zangu ziwe bora na za maana zaidi? Wakati moyo wangu ukiwa katika mahangaiko mathalani mara baada ya kutofautiana na wengine au nikijisikia ya kuwa nimekosewa na kwa wakati huo ninaona vigumu kusamehe au wakati nikikabiliwa na uwoga na wasiwasi, ninafanya nini? Je ninajaribu kusahau masumbuko yote hayo? Au ninatoa mambo hayo kwa Mungu, ili aviponye vidonda hivi vilivyo ndani ya moyo wangu na hivyo kuupunguza uvuto uliopo ndani yangu kwa ajili ya mazingira mazuri ya sala? Je ninapokea sakra-menti ya Upatanisho inayotuponya dhambi zetu na majeraha mbalim-bali ambayo kwayo yanaweza kuwa ni kikwazo katika kutaka kuwa na utulivu katika sala? Ninaamini maswali hayo yatakupa tafakari ya kutosha ili kujiweka vyema na ku-tokata tamaa katika sala. Kamwe hatuwezi tukamwamuru mwenyezi Mungu afuate matarajio yetu kwam-ba ni namna gani tungependa Mun-gu atutendee bali tumwache Daktari atende kazi yake bila kumshurut-isha atufundishe kwanza sayansi ya dawa husika kabla hajatutibu.

KUTAFUTA MUDA WA SALAKwa tulio wengi kupata muda wa sala sio kazi rahisi, tunakabiliana mno na shughuli mbalimbali tangu asubuhi na mapema tunapoamka mpaka usiku. Ndugu zangu katika utaratibu huu itakuwa vigumu kwetu sisi kupata wakati wa kusali. Kuna usemi wa kiafrika usemao; “kwenda katika nyumba ya anayependwa, hakuna mlima”. Hivyo shughuli hizo zote zisikupe taabu, we anza ma-zoezi ya kufanya sala kila siku, anza hatua baada ya hatua usifanye pa-para nawe baada ya mazoezi ya siku kadhaa hakika utajikuta umeanza kuiva katika sala kwa maana Mungu anaona nia yako iliyo njema ya kum-tumikia yeye hakika atakupa nguvu, kwani kristo mwenyewe anasema, “Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo, mimi nimeushinda ulimwengu” Yn.16:33. Hivyo ndivyo Kristo anavyotutangazia ushindi wetu juu ya ulimwengu wenye shu-ghuli nyingi ambazo zinatufanya tu-kose muda wa kuongea naye.

Kristo akiwa anaona mateso makali yatakayompata anaamua kujitenga na wanafunzi wake na kwenda ku-sali. Haya yote kristo anayatenda ka-tika hali yake ya kimwili aliyokuwa nayo na ndio maana anawaambia wanafunzi wake, kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi lakini mwili ni dhaifu. Yesu anakuwa katika mahangaiko makali sana lakini kamwe anabaki katika

Page 26: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 26

sala daima. Nasi katika shughuli zetu yatupasa kutosahau nafasi ya sala (Mt.26:36-46). Tunatiwa moyo wa kutafuta muda wa sala tukikum-buka kwamba, muda huu hautanu-faisha tu ukuaji wa kiroho, bali pia utatusaidia katika mafanikio ya shu-ghuli zetu za kila siku. Uzoefu unatu-eleza kwamba, baada ya muda mzuri wa sala, utaonja amani ya moyo na shughuli zingine zote huenda vizuri kinyume chake nafsi itakusuta ya kwamba hujatimiza vyema wajibu wako wa kiroho na badala yake uta-onja ukavu mkubwa rohoni ambayo pengine itakusababisha kukosa amani. Kama unakumbuka vyema jiulize ile siku ambayo ilikupasa uende kusali lakini ukapuuzia kwa sababu ya shughuli za kila siku, hivi ulijisikiaje? Mlio wengi mtaniambia mlikosa amani na baadhi kwa kuto-taka tu kukubaliana nami mtasema hakukuwa na shida yoyote, lakini kwa sababu dhamiri yako husema ukweli mara nyingi, ingenipa jibu la walio wengi hata kama wewe umea-mua tu kukataa ukweli.

Mtakatifu Inyasi wa Loyola anatu-kumbusha kwamba yatupasa kuzin-gatia muda wetu uleule wa sala hata kama pale tunapojisikia tuko katika ukavu wa kiroho, kukosa hamu au mvuto wa kutaka kusali, kujisikia uchovu wa ndani kabisa rohoni mwetu. Hali hii inapotupata mara nyingine yatupasa kuichukulia kati-ka mtazamo chanya kama ni namna

ambayo Mwenyezi Mungu anatu-taka tuoneshe upendo wetu kwake katika hali ya ukomavu maana ni katika hali hii ndipo na juhudi zetu za kutaka kujumuika tena na Mungu zinapoanza kujitokeza tena lakini pia kuna hatari ya kutoweza kutam-bua hili na matokeo yake tukapoteza kabisa uhusiano wetu na Mwenyezi Mungu kwa kukata tamaa. Daima tu-tambue Mungu wetu ni chemchemi iliyojaa upendo na huruma nyingi.

Wapendwa wangu nigependa kuwa-kumbusheni matunda ambayo tut-aweza kuyapata endapo tu tutatam-bua umuhimu wa sala na kuifanya kuwa ni sehemu yetu ya kwanza kabisa katika maisha, sala inatufan-ya kuwa wana wa Mungu, inainua mwenendo wetu mwema wa kuishi, kutambua vile Mungu anavyotu-penda na pia kurudisha upendo wa Mungu kwetu na pia katika sala tu-napata msamaha kwa makosa yetu.

Na Frt. Simon MdankuMwaka wa Tatu Falisafa Seminari

kuu Peramiho-Songea

Page 27: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 27

JICHO LANGU

Frt. Felix M. A Muna

Ni kawaida kwamba mara nyingi binadamu huwa na tabia ya ku-

fanya jambo lolote kutokana na mfa-no fulani ambao alishawahi kuuona, kusikia ama kuwahi kukutana nao binafsi ama kwa kutenda. Mara ny-ingi hali hii humpata kila mtu husu-sani awapo katika umri wa utotoni. Kadiri anavyoendelea katika ukuaji wake, mtu huyu huweza kukutana na changamoto mbalimbali na hivyo huwa katika wakati mzuri zaidi wa kujifunza mambo mengi zaidi. (The more you expose yourself the more you learn). Hii ni sawa na kusema kwamba binadamu hujifunza ku-tokana na mazingira yake, ndio kusema pia, Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Tabia ya mtu ni kitu cha msingi sana katika mahusiano na watu wengine. Nasema hivyo nikiwa na maana kwamba, tabia yake ndiyo itakayo-mfanya huyu mtu aweze kuishi aina fulani ya maisha; na kushirikiana na baadhi ya watu tu huku akibagua wengine. Hii haina maana kwamba

yeye anapenda kuwabagua ila tabia haziendani. Ndege wanaofanana hu-ruka pamoja. Kumbe basi tabia yake ndiyo itakayotupa ruhusa tuseme na tumtangaze kuwa ni: mwema, mwovu, mchawi, mpagani, mchoyo, anadharau, mlevi, fisadi, mcha-Mungu, hana mwelekeo au mvivu. Tungeweza kusema hayo yote kwa kuangalia matendo yake tu. Lakini ukweli ni kwamba matendo yake yanatokana na tabia yake ambayo imo ndani mwake na ndiyo inayoon-goza matendo hayo ya nje. Hivyo basi matendo yake yanabaki kwetu kama kielelezo tu cha ukweli uliomo ndani mwake yaani tabia (internal struggle or conflicts to reveal reality outside).

Je, tumlaumu mtu kwa kuwa na ta-bia fulani ama nzuri ama mbaya? Ni swali gumu lakini kama binadamu ni muhimu sana kujiuliza ili kusudi tuweze kuona nini kimekosekana na nini kifanyike. Pia kukumbusha-na juu ya tabia zetu tukianzia kwa mtu binafsi na katika jamii kwa ujumla. Kwa jicho la haraka haraka, sidhani kama kuna mtu atakayepin-gana nami kwamba, mtu mwenye tabia nzuri anastahili kupongezwa. Tukigeuka nyuma kidogo tunaweza kujiuliza tena Je, ni lazima hiyo ta-bia watu wote wakubaliane kuwa ni nzuri? Hapa huwa ninakumbuka usemi huu, tenda wema uende zako,

Page 28: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 28

na pia, “Hakuna aliye mwema ila Mungu pekee” (Mk10:17-18). Kwa nini pawepo na usemi kama huu? Kwa sababu binadamu daima yupo katika mapambano na kila waka-ti anawaza na kutenda tofauti na wakati uliopita. Pamoja na hayo yote isiwe ni kigezo cha kusema kwamba hatuwezi kutambua tabia njema ya mtu na hivyo tusimpongeze. Lengo la kumpongeza mtu ni kuonesha kwa wengine mfano bora wa kuig-wa na hivyo kuisaidia jamii kutam-bua mwelekeo unaofaa. Mathalani kumpatia zawadi mwanafunzi kwa kufaulu mitihani yake vizuri, huwa-fanya na wengine waweze kujifunza kwa bidii zaidi. Kumbe basi tunaona kwamba ni vizuri na ni jambo jema kujenga utamaduni wa kuponge-zana pindi tunapopata mafanikio katika jambo fulani.

Tukirudi kwa upande wa pili wa swali letu hapo juu (tabia mbaya), na yenyewe inakuwaje? Mtu anapo-zaliwa huwa hana tabia yoyote am-bayo tunaweza kusema kwamba ni nzuri au mbaya. Kumbe basi tabia yake kwa kiasi kikubwa hutokana na mazingira yake ya ukuaji [malezi na vinasaba vyake] pamoja na watu anaoishi nao hususani angali bado mtoto. Mtu huyu, pamoja na yule mwema, wote hatuwezi kuwalaani au kuwapongeza peke yao. Hii ni kwa sababu si wao peke yao waliamua

kuwa hivyo bali pia malezi yao kwa ujumla. Tujiulize je, malezi yao yali-kuwa ya namna gani, tuliwajengea msingi au mtazamo upi wa maisha? Siku hizi kumeibuka tuhuma nyingi sana kutoka kwa wazazi au walezi au jamii kuwa watoto au vijana wa siku hizi wamepotoka. Sipingani sana katika swala hilo ingawa siku-wahi kuwaona enzi zao walipokuwa vijana, lakini bila shaka utakubali-ana na mimi kuwa; mwembe huzaa tunda liitwalo embe, mchungwa hu-zaa chungwa na kila mti kwa kadiri ya asili na taratibu zake. Labda ni-waulize ninyi wazazi na wakulima, wakati hii hali na mwelekeo huu unaanza mlikuwa wapi? Na kwa nini hamkuchukua hatua yoyote mapema! Hata sasa! Cha kujivunia ni kwamba, walau sasa mmesha-gundua kwamba kuna tatizo linalo hitaji utatuzi wa haraka. Pamoja na hayo mimi huwa nabaki kuwashan-gaa kwamba, kila mtu anajitahidi kukwepa jukumu hili akimrushia mwingine mpira huu. Hivi huu mpi-ra utachezwa kwa kurushiana hivyo mpaka lini basi?

Niwakumbushe tu japo kwa kifupi, huu ni wakati wa kufanya jambo chonde chonde, malezi bora ni msingi wa maisha bora na maadili mema katika jamii yetu ya sasa na ile ijayo. Wazazi nawasihi tukum-buke kwamba, kuzaa si kazi, kazi ni

Page 29: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 29

kulea, tena si kulea tu, bali ni aina ipi ya malezi? Wengi wetu tusikiapo malezi, tunaweza kufikiri ni kuwa-patia watoto wetu; chakula, mavazi, na malazi peke yake. Labda niwa-habarishe kuwa malezi hayaishii hapo tu. Tukiishia hapo ni sawa kabisa na mtu aliye jenga nyumba yake bila kuweka madirisha, mil-ango, samani mbalimbali, pengine hata kupaka rangi. Siku hizi vijana wengi hujikuta wakivutika zaidi ku-fuatilia kile wanachokiita “starehe” bila hata kufahamu “background” yake. Vijana hawa huwa katika ha-tari kubwa zaidi kwao binafsi na hata kwa kizazi kitakachotokana na wao. Hii ni kwa sababu hawaku-jiandaa na pia hawakuwa na kiona mbele (hawajui). Lakini yanini ku-hangaika na kitu usichokijua? Eti wewe kijana mwenzangu. Mwisho wa siku unaanza kujuta na kujifariji eti si mimi! ni shetani! Ni wazazi! – Hawakuniambia wakati hukuwahi hata kuwashirikisha.

Kwanini lakini binadamu ana ta-bia ya hivi? Kila upande upo huku ukilaumu na kunyoshea wengine kidole kana kwamba wewe ni “the best of all”.

Siri kubwa zaidi ni kujifahamu kwanza binafsi, pili kufahamu kizuri ni kipi, tatu kufanya kizuri na ku-washirikisha wengine kufahamu na kutenda mazuri kama Bikira Maria-kumtembelea Elizabeth (tendo la pili la Rozari ya Furaha).

Kumbe basi ni jukumu letu sote, watoto, vijana, wazazi au walezi na viongozi wa pande zote mbili (dini na serikali), kuwa pamoja katika malezi na katika kujenga jamii bora, kiroho na kimwili. Tukumbuke pia kuwa hizi ni zama za ukweli na uwazi, kumbe tusikubali kuficha uovu tukijua kuwa utatuumbua siku moja. Mfano mzuri ni EPA na Richmond. Hali kadhalika tutambue kuwa ukweli au uzuri au ubora au wema ni gharama, ila ni gharama yenye faida kubwa zaidi sasa na wakati ujao. Hivyo ni wakati wangu mimi na wewe kuchagua kipi bora; kupata faida ya leo na kesho tu, au kutumia gharama kubwa kwa faida itakayodumu?

Frt. Felix M. A MunaMwaka Tatu Falisafa Seminari

Kuu Ntungamo Bukoba

Page 30: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 30

HAYA MATESO!

Frt. Abel Sifaeli

Mateso ni hali ya maumivu ayapatayo mtu katika mwili.

Maumivu haya yanaweza kuwa ya wastani au makali sana. Mateso huwaza kumfanya mtu aathirike kisaikolojia au hata wakati mwing-ine apoteze uwezo wake sahihi wa kufikiri na kutoa maamuzi ka-tika mambo yahusuyo maisha yake mwenyewe na hata kwenye jamii aishimo. Nimekuwa nikijiuliza mara nyingi hivi ni kwa nini wema na waovu hupata majaribu na mateso yaleyale? Kwetu sisi wakristo waka-toliki tunaamini kwamba “Mungu ni upendo” na pia Mungu anaweza kila kitu (ni mweza yote). Kwa kawaida ukimpenda mtu unatamani apate pia mafanikio ambayo yatamfanya awe mwenye furaha ndivyo Mungu Baba yetu anatupenda upeo kuliko sisi tunavyompenda yeye mwenyewe. Anapenda tupate tunu zilizo njema na zitakazo tufanya wenye furaha. Kinachonishangaza ni kwamba Mungu huyu anayedai kwamba nimweza wa kila kitu na anatupen-da kwanini anaruhusu mateso na majanga mengi hivi kutokea katika

ulimwengu wetu wa sasa? Kama vile njaa, magonjwa, mafuriko, vita na mengine mengi. Je! hii ina maana kuwa Mungu anatudanganyi kwam-ba anatupenda?

Asili ya mateso: Kuhusu hasa chanzo cha mateso kwa binadamu tunapaswa kwenda zaidi kwe-nye mafundisho ya kanisa pamoja na Maandiko matakatifu. Mungu alipoumba ulimwengu na vyote vilivyomo, aliviona kuwa ni vyema na vizuri, (Mwa1:31). Kifo, mateso na mahangaiko ambayo yapo hapa ulimwenguni ni matokeo ya dhambi za mwanadamu za kukosa utii (Rom 5:12). Binadamu wa kwanza alium-bwa katika hatua nne ambazo zi-namfanya awe na amani na utulivu. Kwanza binadamu ameummbwa katika uhusiano mwema na Mungu. Pili, uhusiano kati yake yeye mwe-nyewe ili aweze kutawala hisia zake. Amepewa akili, utashi na uhuru wa kufanya maamuzi yamuhusuyo. Tatu, uhusiano kati ya mwanadamu na mwanadamu mwenzake. Nne, uhusiano kati ya mwanadamu na viumbe vilivyoumbwa na Mwe-nyezi Mungu. Vitu na viumbe vyote vilivyoumbwa isipokuwa malaika viliwekwa chini ya mwanadamu avi-tawale, avitunze na avitumie. Mungu hakumuumba mwanadamu ili afe au ateseke. Mungu alimuumba mwana-damu akampatia zawadi ya neema ya utakaso na akampatia amana uz-ima wa milele. Kutokana na kukosa utii, mwananadamu alitenda dham-

Page 31: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 31

bi na kuvunja agano lilokuwa kati yake na Mungu. Kutokana na ma-tokeo ya dhambi, adhabu ya kifo na mateso ikaingia ulimwenguni. Hapo ndipo binadamu alipopoteza zawa-di ya neema ya utakaso na uhakika wa kumwona Mungu uso kwa uso. Hivyo mateso na mahangaiko ni ma-tokeo ya dhambi za mwanadamu.

Kwanini tunapatwa na mateso: Kuna baadhi ya watu wanaoamini kwamba mateso na mahangaiko yanayowapata watu hapa Duniani hayana maana yoyote. Lakini waka-toliki huamini mateso na mahan-gaiko kwao yana maana. Wakatoliki wanaamini Mungu ndiye mpaji wa yote. Hivyo wakati mwingine Mungu huruhusu mateso na majaribu kwa lengo lakutupatia zawadi ambayo nikubwa zawadi. Wakati mwing-ine huruhusu majaribu na mateso kwa lengo la kutuepusha na maovu. Mungu wakati wote hurusu kiumbe chake kijaribiwe kulingana na uw-ezo kilichonacho, jaribu haliwezi kuzidi uwezo wa kiumbe kustahimi-li. Pia Mungu amempatia mwana-damu utashi na uhuru wa kushinda majaribu.

Kwanini Mungu anarusu mateso na mahangaiko?

Kujibu swali hili kwanza tunapas-wa kuangalia kwanini mwana-damu yuko hapa duniani: Mungu ametuumba ili tushiriki uzima wa milele. Mungu ametuumba ili tuweze

kushiriki furaha ya uzima wa milele.Uzima huu wa milele ndio kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu huko mbiguni. Lengo msingi la maisha yetu hapa duniani ni lile lile kama la wazazi wetu wa kwanza Adamu na Eva waliowekwa katika bustani ya Edeni. Wakati huu wa maisha yetu Mungu hutuacha tujaribiwe ili kupi-ma imani yetu na uaminifu wetu kwake. Mateso yote tunayopata hapa duniani ni dawa ya kutuponya. Ugonjwa hatari kwa roho ya bina-damu ni dhambi. Dhambi hututenga na Mungu na kuharibu uhusiano huu kabisa. Niafadhali kuteseka ka-tika ulimwengu huu kuliko kufurahi sasa na kuikosa furaha ya milele, (Mt 5:29-30). Mungu huruhusu majari-bu na mateso kwasababu zifuatazo: Mungu anataka kutujaribu: Mungu huruhusu majaribu ili kupima imani yetu kwake na upendo tulio nao kwake. Je tunampenda Mwenyezi Mungu kwasababu yeye ni mpaji au kwasababu yeye ni rafiki yetu na Baba yetu. Mungu huruhusu majari-bu ili kutupima tunamtumikia nani, (Ayubu 1:6-12.).

Mungu anatufundisha, anatufanya wanyenyekevu na tuishi pia kwa haki. Kama baba humwonya mwa-naye kwa kumpa adhabu ili awe mwema. Je Mungu hapaswi pia kutufundisha kwa kutupatia adhabu pale tunapokosea ili turudi katika njia iliyo sawa? Mateso na majaribu anayoyaruhusu Mwenyezi Mungu yana lengo zuri. Mateso na majaribu

Page 32: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 32

hayo huzaa matunda yaliyomema kwa wale ambao watakua wamey-apokea kwa nafasi chanya (Ayubu 12:5-11). Mwenyeheri Papa Paulo II anasema, mateso yana lengo la kutuletea ukombozi, yanamrudishia mtu uzuri wa kale yule atakaye tam-bua huruma ya Mungu na kutubu.Watakatifu wengi wamepitia mate-so kwa kuyapokea vyema wame-fanywa wana wa Mungu. Mateso yanatupatia nafasi ya kumpenda Mungu, kumtukuza na kushiriki ka-tika kazi yake ya ukombozi. Nafasi mbalimbalia za majaribio zinazo-tupata tukizipokea kwa mtizamo chanya, zinatuweka karibu zaidi na mwenyezi Mungu. Mtakatifu Paulo anatuambia kwamba “Sasa naya-furahia mateso niliyonayo kwa ajili yenu…” (Kol 1:24). Hivyo basi yatu-pasa pia kuteseka kwa ajili ya wen-zetu ili wawezepia kuupata uzima wa milele.

Tutawezaje kushiriki mateso ya Kristu: Kwakuwa tumeunganish-wa pamoja na Kristu, mateso yetu pia yameunganishwa pamoja naye, na tunashiriki katika kazi yake ya ukombozi. Basi tu mwili mmoja katika Kristu…na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia na-cho, kiungo kimoja kikitukuzwa, vi-ungo vyote hufurahi pamoja nacho” (1Wakorinto 12:12-27). Mateso ya Kristo yanapozidi kwetu ndivyo hivyo faraja yetu inavyozidi kwa njia ya Kristo. Hivyo tunaalikwa kushiri-ki katika kazi ya ukombozi iliyo kazi

kuu kuliko kazi zote. Wale ambao wanashiriki kikamilifu katika kazi ya ukombozi wanajitunzia wenyewe hazina mbinguni isiyoharibika. Ma-jaribu na mateso yanayotukumba kila mara inatubidi kuyapokea kwa imani. Tunapaswa kumwomba Mungu atujalie neema zake ili tu-weze kufahamu katika uhalisia kile anachokihitaji kutoka kwetu. Ujum-be wa Mungu tunaweza kuupata sawasawa kwa kuzingatia haya: Ku-chunguza moyo ilikuona kama upo katika imani. Kutolea mateso na majaribu yote kwa Mungu. Sala ni muhimu. Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Kumshuku-ru na kumsifu Mungu kwa kushiriki (sisi) mateso pamoja na Yesu Kristo. Mateso na mahangaiko tunayoya-pata hapa duniani si kwasababu tu wadhambi bali Mungu huyaruhusu ili tupate tunu iliyo njema zaidi. Mungu alituumba na kutupatia uh-uru na utashi, akatuacha tutumie vipawa hivi katika kumfuata yeye. Wakati mwingine hupima imani yetu kama tuko imara kwa kumua-cha shetani atujaribu (Ayu 1:1-2: I-13). Silaha kubwa kabisa katika kuyashinda majaribu ni kujikabihdi mbele ya Mungu na kusali ilituweze kushinda majaribu hayo. Kwahiyo tunaalikwa kuyashinda majaribu na mateso kwa sala na tafakari.

Na Frt. Abel SifaeliMwaka wa pili Teolojia Seminari

kuu Kipalapala-Tabora

Page 33: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 33

UTUME KWA WATOTO

Frt. Patrick Myuku

“Waacheni watoto wadogo waje kwangu msiwazuie; kwa maana wa-toto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.” (Mk 10:14). Ni maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo akithibit-isha kuwa watoto nao ni wateule wa neno la Mungu katika kusikiliza na kuishi Ukristo. Watoto ni mfano mzuri wa kuigwa hasa maisha ya utoto yaliyojaa upole na unyenyeke-vu. Utume wa watoto ni ushiriki wa watoto katika kueneza ufalme wa Mungu katika maisha ya wanadamu kwa njia ya kuhubiri neno la Mun-gu na kuwa mashuhuda wa ukweli kwa njia ya maneno na matendo yao. Kwa njia ya ubatizo, sisi sote tunapewa wajibu wa kuwa mitume. Kazi ya kuwa mitume ni kutumwa au kupeleka habari njema ya ufalme wa Mungu kwa watu wote. Watoto nao huitwa kuwa mitume wa neno la Mungu kwa mataifa yote.

Katika dhamira hii ya utume kwa watoto, hatuna budi kutambua kuwa utume wa watoto unakabiliwa na changamoto ambazo huwafanya watoto wasitambue kuwa wanayo-

nafasi ya kufanya utume katika umri wao wa utoto. Ni jukumu la familia kuwafundisha watoto wao juu ya imani ya Kikristo na kuwaingiza katika dhana nzima ya moyo wa ki-misionari, moyo ambao utawafanya walitumikie Kanisa kwa nguvu zao zote kwa vipindi vijavyo vya maisha yao, yaani nafasi yao kama vijana na watu wazima

Kama kuna kitu ambacho Mkristo anapaswa kufanya katika kuweke-za elimu au maarifa ni kwa mtoto, hasa anapokuwa katika maisha ya utoto. Hiki ni kipindi ambacho ta-bia ya mwanadamu huundwa kwa kiasi kikubwa. Mafunzo ya kipinidi hiki ni msingi au mhimili wa maisha ya baadaye. Ni wakati ambako akili huweza kujifunza kwa urahisi zaidi na kuelewa zaidi. Wahenga wetu wanatuambia kuwa, ‘Samaki mkun-je angali mbichi’, na Waingereza wanatuambia kuwa; ‘You cannot teach an old dog new tricks’ (hu-wezi kumfunza mbwa mzee mbinu mpya). Misemo hii miwili inatuku-mbusha kwamba uelimishaji wa watoto unapaswa kufanyika mape-ma kwa uzoefu kuwa kuchelewa kufanya hivyo itakuwa vigumu sana au kutowezekana kabisa katika utu uzima. Katekesi kwa watoto yafaa kufanywa kwa makini zaidi kwani ndio msingi wa maisha yajayo.

Hakika watoto ni Kanisa la sasa, kesho na vizazi vijavyo. Wazazi,

Page 34: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 34

walezi na Kanisa, tunapaswa ku-wekeza kwa watoto. Taifa lolote ma-kini duniani hutambua umuhimu wa kurithisha maarifa kwa watoto. Ni wajibu wetu wazazi, kuwarithisha watoto moyo wa utume, moyo wa kulitumikia kanisa katika kuhakiki-sha Kanisa litakuwa na wafuasi wa-liokomaa kiimani, imani ambayo imekuzwa tangu utotoni. Hatuna budi kuungana na maneno ya Mwe-nyeheri Baba Mtakatifu Yohane Paulo II aliyoyatoa katika baraza kuu la Umoja wa Mataifa, October 2, 1979 kwamba; No country on earth, no political system can think of its own future otherwise than through the images of these new generations that will receive from their parents the manifold heritage of values, du-ties, and aspirations of the nation to which they belong and of the whole human family. (Hakuna taifa lolote dunia, hakuna mfumo wowote wa kisiasa ambao unaweza kufikiria juu ya maisha yake yajayo isipokuwa katika sura za watoto ambao wata-pokea na kurithishwa na wazazi wao juu ya thamani, wajibu na matarajio ya nchi zao juu ya yote yahusuyo ja-mii ya wanadamu). Endapo Kanisa na familia hazitatilia mkazo umri huu muhimu, ni dhahiri kuwa taifa letu na kanisa letu halitafanikiwa vizuri katika kujibu changamoto zi-nazokabili imani yetu na jamii zetu kwa sasa na vizazi vijavyo.

Waswahili wanatuasa kuwa; “Ukio-na vyaelea ujue vimeundwa.” Ni

ukweli tunapaswa tuoneshe juhu-di zetu kwa kuwapa watoto wetu katekesi inayowafanya watambue utume wao kama watoto. Maisha mazuri yapatikanayo kwa wafuasi wajao yatatukumbusha kuwa vi-takavyoelea tuliviunda. Katekesi husika kwa watoto, lazima Kanisa na wazazi waungane kikamilifu. Fa-milia ndiyo kanisa la nyumbani na Shule ya katekesi ya kwanza kwa watoto. Uundwaji wa dhamiri zenye mioyo ya ukereketwa wa utume hu-zaliwa katika familia, mafundisho ya Makatekista, vyama vya kitume, Ju-muiya Ndogondogo za Kikristo, ma-fundisho ya upokeaji wa sakramen-ti, katekesi shuleni na ushiriki wa Misa Takatifu kwa watoto jumapili na siku zingine zilizopangwa. Kwa kawaida, mafanikio huwa hayashuki kutoka hewani, bali hupatikana kati-ka juhudi na mipango mizuri. Malezi tajwa juu yatafanya watoto wawe waelewa wa imani yao mapema na kuwa mashuhuda wa injili.

Tunapaswa kuwa na mikakati ya kuhakikisha kuwa, tunawavuta wa-toto ili wapate kufurahia utoto wao na kulipenda kanisa katika kutoa utume wao vizuri katika kipindi cha sasa na hata kwa miaka ijayo. Maz-ingira ya kuwavuta ni kama vile; kuwasomesha (elimu ya kidunia na kidini), kuimarisha zaidi vyama vya kitume (Utoto Mtakatifu, Legio Mariae, Shirika la Mtakatifu Aloisi Gonzaga na mengine) katekesi en-

Page 35: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 35

delevu, semina na warsha mbal-imbali, uanzishwaji wa michezo na mashindano mbalimbali, kuwaha-misisha kuhudhuria matukio mbal-imbali ya kiliturujia na uimarishaji wa huduma mbalimbali kwa wato-to. Mazingira haya yataleta ladha na uhai zaidi kwa watoto ambao nao wanajukumu la kuinjilisha.

Wajibu wa watoto katika utume wao ni utumikiaji katika Misa Takatifu, kusoma neno la Mungu na nyajibu paswa katika Misa Takatifu hasa kwa Misa zinazokuwa za watoto, ku-wasaidia wagonjwa na kuwatembe-lea, kuwa mashuhuda wa matendo mema, kuwaheshimu wazazi wao, na kuwa wajenzi wa Kanisa kwa sasa na kwa vizazi vya baadaye. Endapo hatutawaandaa watoto wetu ka-tika malezi ya Kikristo, hatupaswi kutegemea muujiza wenye neema bali muujiza ambao ni maafa kwa maisha ya Ukristo na jamii zetu. Fa-milia makini, taifa makini, watu ma-kini hawafanyi vitu kwa kubahatisha bali hutumia njia sahihi, mipango sahihi kufikia vitu muhumu vita-kavyokidhi matakwa ya jamii zao. Ni lazima tuwekeze vyakutosha ka-tika watoto wetu kwa kuwafundisha mapema nafasi yao kama Kanisa la leo, kesho na urithishwaji wa vizazi na vizazi.

Frt. Patrick MyukuMwaka wa Nne Teolojia Seminari

Kuu Kipalapala

YESU MFANO WA KUIGWA KATIKA UINJILISHAJI

Frt. Melkior Mtitu

Awali ya yote nipende kurejea mwito wa Maandiko Matakati-

fu, kwani ni kutoka humo tunapata mwongozo wa kuijua na kuiishi Imani yetu kupitia mapokeo na mamlaka ya Kanisa. Kwa kawaida katika uinjilishaji, Kristo ndiye anay-etangazwa na wale walio wake ali-yewachagua (Yohane 15:16) ili wa-pate kuwa viongozi wa kila mmoja, na wala asije tokea mmoja ambaye atawakosesha wale wamwaminio (Mk 9:42). Kumbe kila mwamini ana jukumu la kuwa kama chumvi na taa katika kuhakikisha yale aliyotaka Kristo yanamfikia kila mhitaji. Mhi-taji huyu hujumuisha watu wote, iwe wa umri mdogo ama mkubwa, Mkristo ama si Mkristo na wa taifa lolote bila kujali rangi (Mt 28:19-20).

Pamoja na kwamba kuna viongozi wa kuongoza kondoo wa Kristo, ha-wafanyi hivyo kwa kutegemea nguvu zao wenyewe bali wanamtegemea Kristo aliye mfano wetu kwani Yeye alisema, "Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi yangu. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo atazaa ma-

Page 36: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 36

tunda mengi, maana bila Mimi ha-muwezi kufanya chochote”, (John 15:5). Kumbe katika uinjilishaji wao wanapata mfano kwa Yesu. Sisi waamini wote tunawajibu huohuo wa kutenda kadiri na alivyofundisha Kristo ndio maana anasema “Nime-wapeni mfano, ili nanyi pia mfanye kama nilivyowafanyieni” (John 13:15).

Tukiangalia maisha ya Yesu tunam-wona akiwa katika mazingira tofau-ti tofauti bila kujali urahisi ama ugu-mu wa mahali hapo. Naye pamoja na kufundisha mambo yamhusuyo, alimfanya Mungu Baba apate kujuli-kana kwetu kupitia Yeye aliye ndani yake. Kutokana na umoja huo usi-ogawanyika anawaombea wafuasi wake wawe na umoja katika yale yote aliyowaagiza kutenda na up-endo kati yao ili wapate kutambu-lika kama alivyosema “Mkipendana watu wote watajua kwamba ninyi ni wanafunzi wangu”(John 13:35).

Hivyo basi, pamoja na kwamba tu-naweza tukajifunza namna ya ku-fanya uinjilishaji toka kwa mitume na wafuasi wake (Mdo 15:7), kwa ustadi zaidi tunaweza tukajifunza mengi toka kwake Kristo kwani Yeye alisema tujifunze toka kwake (Mt 11:29), na hapa si tu namna ya kuhubiri bali hata ya kuhudumia ja-mii kwa namna mbalimbali.

KWA NINI BASI TUJIFUNZE TOKA KWA YESU?

Yesu ni Neno wa Mungu na aliku-wapo toka milele. Yeye ni Mungu na Mtu kweli. Aliuvaa ubinadamu pasi-po dhambi wala udhaifu wowote ili tupate kujifunza kuwa wakamilifu toka kwake. Hivyo tuna haja kabisa ya kumfahamu na kumfanya atam-bulike, kwani yeye ni mwanga wa kweli wa kuwaangazia watu. Tuna-ona mitume waliulizwa kama nao walitaka kuondoka wakajibu tuende wapi Bwana wewe unayo maneno ya uzima wa milele (Yn 6:67-69). Si hivyo tu, mitume walienda na kukaa naye na kuona alivyotenda (Yn 1:39).Kumbe tuna kila sababu tosha za kwenda kwa Yesu kila mara kuchota elimu yenye kuigwa. Pia anasisitiza kuwa tunayopaswa kujifunza yote yanayotoka kwa Baba (Yn 8:28).

Tupo katika ulimwengu wenye changamoto nyingi kwa sasa am-bapo Imani yetu inayumba hasa katika mioyo ya waamini. Kuna mawimbi mengi toka ndani kama vile kukata tamaa na kukosa hamu ya kuyaishi mafundisho na ya nje kama vile mfumo hasi wa sasa kupi-tia utandawazi unafisha imani ya watu na kudunisha uinjilishaji.

Kwa ubatizo wetu tumekuwa wa-fuasi wa Kristo na tumepewa maju-kumu ya kutimiza kwani tumeuvaa ukuhani wa jumla hivyo tujifunze yafuatayo toka kwa Yesu aliye Ku-hani na Katekista Mkuu.

Page 37: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 37

Yesu katika familia ya NazaretiTunajifunza mengi kutoka kwa wa-zazi wa Yesu waliomkomaza mtoto wao kimaadili, kielimu na kidini hadi akakua katika kimo na hekima.Walitimiza wajibu wao kama wazazi kuona mtoto wao anashiriki kazi mbalimbali kama vile useremala na matukio muhimu ya kidini mfano kwenda kusali Yerusalemu. Yesu alipobaki huko wazazi walichu-kua hatua ya kumtafuta na walim-kuta hekaluni akiwa na wazee wa kanisa (Lk2:48-52). Ni swali la ku-jiuliza katika zama zetu hizi wazazi tunatimiza wajibu uleule? Ama tu-melegeza kamba katika malezi kwa kiasi fulani kutokana na kazi nyingi tunazokuwa nazo? Hatukanyi wala kuonya inapopasa wakati Maandiko yanatutaka tufanye hivyo? (2 Tim 4:2). Je sisi wazazi tunaiga mfano mwema wa wazazi hawa? Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya wazazi wanaenda kanisani na kuwaacha watoto nyumbani bila sababu ya msingi hata kufuatilia mienendo yao. Watoto hawa tunawakuta kati-ka mazingira hatarishi kwa imani na maadili yao. Hii ni dalili mojawapo inayoonesha jinsi walezi na wazazi walivyokata tamaa katika malezi ya watoto na hivyo kuendekeze wa-toto kukosa heshima, nidhamu na mwelekeo chanya wa maisha. Katika mwaka huu wa Imani tuamuke basi na kuwajibika ipasavyo hasa kwa kuwasaidia watoto wetu waweze kukua katika maadili mema ya dini na kijamii.

Yesu katika malezi ya watotoTunamuona Yesu akiwaalika watoto waende kwake ili wapate kupokea mafundisho na kuwajengea fikra njema toka utotoni ili wakue katika kumwelekea Mungu (Mt 19:14).Kisha anawahoji wazazi ni vitu gani wanavyowapa watoto wao? Je ni vile vinavyowajenga ama vile vina-vyowabomoa? (Mt7:9-11). Tunawe-za kujihoji hapa kama kweli tume-kua mstari wa mbele kuwafundisha watoto Imani ya dini yetu na kuwa-sisitiza kusoma Biblia au tunawaa-chia wengine wafanye kazi hiyo?

Siku hizi wazazi tumetumbukia ka-tika kutoa kipaumbele kwa watoto kupata elimu dunia bora na kusa-hau kuwa kama haijajengwa katika msingi imara wa kimaadili utoka-nao na dhamiri iliyo njema, haita-mfaa kitu. Hii ni kutokana na upepo uliopo sasa wa mawazo mkengeuko ambayo yanawayumbisha vijana na wanashindwa washikilie wapi. Elimu-dunia kwa upande mwing-ine imemfumba macho kijana kush-indwa kutamani elimu-dini (Lk 11:52). Ndio maana tunaona jinsi vijana wanavyokosa pa kujishikiza kwa kuwa hawajapata kufundwa katika elimu iliyo kweli toka uto-toni. Wengine hata wanadiriki ku-tokwenda kanisani kusali wakidai kupoteza muda na kutopata mafaa yoyote, badala yake wanajiingiza zaidi katika maisha ya anasa zai-di. Vijana wamejikita zaidi katika ulimwengu wa kutafuta vituambao

Page 38: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 38

umepoteza wengi, mfano kujiin-giza katika freemasonry ama mi-kataba ya kishirikina kusudi apate pesa ili awe na maisha bora kwa nje.Laiti watoto na vijana wangelimjua Elimu (YbS 16:24) wangelienenda katika uadilifu (1Yn3:17). Hivyo basi tuwalee na tuwajengee watoto wetu tabia ya kumcha Mungu aliye msingi wa elimu yote (Meth 1:7). Tukifanya hivyo katika mwaka huu wa Imani watoto na vijana wataku-wa na tamaa ya kuijua Imani yao na kujikita katika kuiishi na hivyo wat-akuwa na msimamo imara popote pale watakaposimama wenyewe.

Yesu na utume wa woteTunamwona Yesu akiwahudumia watu wa aina mbalimbali; maskini, wadhambi, wakoma, wenye magon-jwa, wajane, wafiwa, wanandoa hata matajiri, wema na wakosefu. Wote aliwahudumia kwa usawa na haki hakujali tofauti zao za kipato wala rangi au utaifa, (Mt 11:5). Kumbe lengo zima la utume wa Yesu lili-kuwa ni kuupa thamani utu wa mtu na kumwokoa kila mwanadamu (Yn 6:39). Hata katika masuala ya uka-rimu Yesu aliwajali sana wasio na kitu, kwani hata wao wanapaswa kualikwa kushiriki matukio mbal-imbali ya kijamii (Lk14:13). Ndio maana Yesu aliambatana nao na ku-waonesha kwamba wana haki sawa na wengine katika jamii. Yatupasa sisi Wakristo katika kipindi hiki cha Mwaka wa Imani tuchote namna ya utume wa Yesu katika kuhudumia

wengine. Tuchunguze ni wapi tume-bagua na ni wapi tumeweka nguvu zaidi na kwa nini? Je tunaaangalia zaidi utu wa mtu au tunalenga kile alichonacho ambacho ndo tunatege-mea kukipata?. Wahenga wanase-ma, “Mkono mtupu haulambwi”, ni usemi amabao umekithiri vich-wani mwa walio wengi hasa zama hizi, hata kuathiri Uinjilishaji wetu. Pamoja na kwamba Yesu aliwaamin-isha mitume kuwa wasiwe na shaka watakula nini au watavaa nini, na kuwapa wajibu wanaohudumiwa, isichukuliwe kama kigezo msingi katika kuangalia maslahi ya mwili, bali roho kwanza mengine baadaye.

Yesu na na Utawala wa sheriaUtume wa Yesu ulijikita katika she-ria mpya ya upendo inayomwongo-za mtu awe na mahusiano mema na Mungu wake na jirani zake, na wala si ile inayowafanya watu kuwa wa-tumwa na aliikosoa ilipohitajika, (Yn 7:23). Yesu alidiriki hata kukemea viongozi waliotenda kinyume na haki za kila mmoja, (Lk 11:42-43). Kumbe hata sasa Kanisa halipaswi kunyamaza wala kukawia kukemea uongozi unaotaka kuweka sheria kandamizi na kusahau kwamba madaraka walio nayo yatoka kwa Mungu. Kanisa linahimiza kwamba “Taasisi za kibinadamu zikinze kwa ujasiri kila mtindo wa utumikishaji wakijamii na wa kisiasa, na pia ziz-itetee haki za msingi za wanadamu walio chini ya dola yoyote” (GS 1412)

Page 39: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 39

Yesu na mitumeYesu aliwafanya wanafunzi wake kuwa marafiki zake, akawashiriki-sha makuu ya Mungu (Mt 11:25) ambayo wenye hekima na akili wali-fichwa. Aliwaasa kwa kila jambo wanalotenda walitende kwa Jina lake (Mt 18:20). Na aliwaahidi kuwa nao hadi ukamilifu wa dahari. Kum-be ni kutokana na ukaribu wa pekee waliokuwa nao mitume waliweza kumtambua Yesu katika mazingira fulani fulani na hasa katika kuu-mega mkate. Hii ni sawa na kushiriki sakramenti na kusali daima.

Siku hizi, wengi wamekata tamaa ya kupokea sakramenti kutokana na sa-babu mbalimbali ama za kutokujali au kutofundishwa umaana wa sakra-meti hizi katika maisha yao. Moyo wa kusoma Maandiko umepungua hata kwa baadhi ya waamini, lakini hili ni jambo linalowezekana kureke-bishwa ili tusije tukawa kama wale wanaopokea Neno la Mungu kwa muda na kisha tunarudi kulekule nyuma. Neno la Mungu lahitaji kuta-fakariwa kila mara ili liweze kue-leweka mioyoni mwa watu. Ndio maana Origeni anakiri kuwa kila aya katika Biblia ina fumbo ndani mwake, hivyo si kazi rahisi kuielewa Biblia hivihivi bila kuchukua wasaa wa kufanya tafakuri. Mitume nao walikiri kutokuelewa kwa nini Yesu alisema kwa mifano. Lakini Yesu aliwahakikishia kuwa wao wame-jaliwa kuzifahamu siri za ufalme wa mbinguni. (Mt 13:10-12). Hii ni

kutokana na ukaribu waliokuwanao mitume na Yesu.

Changamoto kwetu tuliyonayo sasa, ni kuona jinsi wenzetu wa madhe-hebu mengine na Uislamu wana-vyojitahidi kufanya mashindano ya weledi juu ya Maandiko, lakini sisi tumebaki nyuma. Yatupasa sasa nasi kuamka na kuanzisha kitu cha nam-na hiyo kwa watoto wetu kuanzia katika familia na jumuiya zetu, shule za msingi hadi kitaifa ili tujenge ta-bia ya kusoma na kutafakari Biblia vema, nayo hii itatujengea ujasiri wa kujibu swali lolote ambalo tutau-lizwa juu ya imani yetu (1Pt 3:15).

TUFANYE NINI BASI?Kwa namna mbalimbali kanisa lina-jitahidi katika kutoa huduma za ki-jamii kama vile, huduma afya, elimu, malazi na kusaidia wenye shida mbalimbali kama vile walemavu bila ubaguzi sawa na Yesu alivyo-fanya. Pia kupitia mikutano mbalim-bali, kama vile, kongamano la vijana ulimwenguni ambalo mwaka huu limefanyika Brazil, tafakari juu ya mwaka wa Ekaristi, Mtume Paulo, Jumuiya ndogondogo, Upadre na sasa wa Imani. Yafaa kuendeleza ari ya Baba Mtakatifu (Pope Emeritus) Benedikto wa XVI ambaye ametaka kuturudisha katika mzizi wa imani yetu. Amekiri kuona changamoto zinazolikumba Kanisa Katoliki am-bamo ni pamoja na kuanza kulegea kwa imani katika nchi mbalimbali. Lakini anatoa heko kwa Kanisa

Page 40: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 40

la Afrika kuwa “The future of the Church is In Africa”, akimaanisha kuwa Kanisa la baadaye li katika Af-rika. Hii ni kutokana na Uchungaji wa Maaskofu wa Afrika na moyo wa imani wa Waafrika, pamoja na aliyoyaona katika safari yake aliyoi-fanya nchini Angola.

Wahenga wanasema, “Mgema akisi-fiwa tembo hulitia maji”, Wakristo tuangalie usemi huu usije kuwa kweli katika maisha yetu. Pamoja na kwamba tumeona jinsi vijana baadhi na watu wengine walivyo-poteza moyo wa sala. Ni wasaa wetu sasa kuwaendea katika maeneo yao na kuwatia moyo ili wapate kurudi kundini.

DALILI ZA KUZIDI KUIMARIKA KWA IMANI

Kuongezeka kwa vikundi vya kwa-ya hasa vile za Vyuo vikuu na vya ualimu, ambavyo kwa kupitia uim-baji kwa namna moja au nyingine zimeweza kuamusha na kuitangaza Imani yetu kwa watu wa rika zote. Watoto nao hawapo nyuma ambao ndio Kanisa la Kesho, wakiwakil-ishwa na Watoto wa Shirika la Ki-papa la Utoto Mtakatifu. Ongezeko la majarida mbalimbali na vipindi vya redio juu ya imani na maadili ni wazi kuwa imani inazidi kuimarika. Kuongezeka kwa idadi ya vijana wa-naopenda kujiunga na seminari na utawa nayo ni dalili ya kukua kwa imani na hata mabadiliko kijamii

yanajionesha kupitia kazi zao. Ni jukumu la kila mwamini kuwaunga mkono wanapoona wafanyakazi ka-tika shamba la Bwana wakiongeze-ka. Wawata katika Kanisa nao wana mchango mkubwa kweli katika kum-wagilia miito mitakatifu. Majimbo mbalimbali kama vile Singida, Mbu-lu, Bukoba, Tabora na Iringa nayo yana Vyuo vya Katekesi ambayo ni nafasi mojawapo kwa waamini kupata mafundisho mbalimbali ya Kanisa, pamoja na Biblia. Hivyo basi Imani yetu yaweza kujengwa imara mioyoni mwa waamini ili waweze kujua ni nini wanachoamini, wana-chopaswa kuamini na kwa nini wa-naamini hivyo.

Uwepo wa vyama mbalimbali vya kitume kama vile WAWATA, VIWA-WA, TYCS, Moyo Mtakatifu Wa Yesu, Lejio Mariae, Painia, Utoto Mtakati-fu na vikundi vingine kama Pro-Life, Focolare, Scout, Karismatiki Kato-liki navyo vina nafasi kubwa katika uinjilishaji vinaonesha kukua kwa imani. Ni changamoto kwetu katika nyakati za sasa kufahamu na kufuta dhana ya kwamba Lejio Mariae, Moyo Mtakatifu wa Yesu na Painia si vyama vya watu fulani tu bali ni vya wote, hata chama cha Utoto Mtakat-ifu kisionekane kuwa ni chama cha wasichana tu.

Page 41: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 41

HITIMISHOTumeona jinsi Yesu anavyotupa mfano wa namna ya kuenenda kwetu katika Uinjilishaji kwa ku-muiga Yeye. Yatupasa kujiuliza mas-wali mengi na kuyatafutia majibu hasa tunapouenzi mwaka wa Imani, na tuweke mikakati ya namna gani kwa pamoja na kila mmoja kwa na-fasi yake tutaifikishaje Imani yetu sehemu mbalimbali.

Wote kwa ujumla, yatupasa kumu-unga mkono Papa aliyestaafu (Pope Emeritus) Benedikto wa XVI kwa jitihada zake za kuweka mkazo ka-tika kusoma vema Biblia Takatifu, Katekisimu ya Kanisa Katoliki na Mtaguso Mkuu wa Vatikano II. Ni kutoka humo tunapata miongozo mbalimbali ya maisha, kidini, ki-maadili na kijamii. Na ndimo tu-napopata kujua kanisa linasema nini juu ya Imani yetu. Pamoja na mafundisho mbalimbali ya mababa wa Kanisa msingi wake ni Biblia na Katekisimu Katoliki. Hivyo basi ni wajibu wa waamini kuyasoma yale yote ambayo Kanisa linasisitiza na kufundisha.

Frt. Melkior Mtitu-Mwaka wa Pili Teolojia Seminari Kuu

Kipalapala.

REHEMA KAMILI KWA MWAKA WA IMANI 2012/2O13

UTANGULIZI

Askofu Desiderius M. RwomaMsimamizi wa Kitume

Jimbo la Singida.

Baba mtakatifu, Benedict XVI mwaka jana, hakutangaza mwa-

ka WA imani. alifungu pia upatika-naji WA rehema kamili zinazoen-dana na maadhimisho ya mwaka WA imani katika nyakati mbalimbali kwa waamini kama inavyoelezwa hapa chini.

MASHARTI:1. Toba kamili.2. Kuungama.3. Kupokea Ekaristi Takatifu.4. Kusali kwa nia za Baba Mtakatifu: Baba yetu, kanuni ya imani na kusali kwa Bikira Maria na Mitume.

JINSI YA KUADHIMISHA MWAKA WA IMANI

a) KUSOMA NENO LA MUNGU (Biblia Takatifu, Nyaraka za Baba Mtakatifu na Maaskofu) na kurejea mara kwa mara Mtaguso WA II WA Vatikano na Katekisimu ya Kanisa Katoliki.

Page 42: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 42

b) KUSHIRIKI HIJAWASIO WAGONJWA: washiriki ibada kwa kusali katika nafasi mbalimbali takatifu au mahali ulipobatizwa na kurudia ahadi za ubatizo. nafasi hizo ni kama: Kanisa kuu la Roma, Kanisa Kuu na vituo vya hija vya Taifa au Jim-bo, Katakumbu na kadhalika.

WAGONJWA: Washiriki kiroho kwa kuunganisha mawazo yao na waamini hasa wakati ule Baba Mtakatifu au Maaskofu, kwa msaada WA TV au ra-dio, wanaposali Baba yetu, kanuni ya imani na sala nyingine huku wakim-tolea Mungu mateso yao.

FAIDA YA KUSHIRIKIa) Kupata huruma ya Mungu katika ondoleo la dhambi.b) kuondolewa adhabu kwa walio to-harani

KATIKA MWAKA WA IMANI JIEPUSHE NA UJINGA HUU

1. kutokumjua Kristo kama Binada-mu-kwamba alikuwa Mungu-mtu.2. Kukataa kumjua Kristo na ma-fundisho yake.3. Kutokumruhusu Kristo kuunda maisha yako katika utamaduni WA jamii4. Kotojua Katekisimu ya Kanisa Ka-toliki na maandiko Matakatifu.5. Kutomruhusu Kristo kuwa mhunzi WA utamaduni na Sanaa.6. Kutothamini au kubeza yaliyo ya Kimungu.7. Kutangulia sana wakati.

FUMBO LA UHAI WA BINADAMU

uhai wa mwandamu asili yake ni Mungu. Uhai huu kwetu sisi huanzia tumboni

mwa mama na hukaa humo kwa kawaida na kama hakuna hitilafu ya kimaumbile kwa miezi 9. Uhai wa binadamu huanza tangu pale mbegu ya baba, yai la mama na roho ya Mungu vinapoungana. Uhai huu hudumu hadi kifo cha binadamu. Akiwa tumboni hukua, hujimudu, husikia, huonja, hupata huzuni na huonyesha furaha, ndiyo maana “….mara tu Elizabeti aliposikia sauti ya Ma-ria, kitoto kichanga tumboni mwake Elizabeti kikaruka kwa furaha…” Lk 1:41, pia tunaso-ma; “…Watoto hao wakashindana tumboni mwake Rebeka, naye akasema, kama hivi ndivyo mambo yalivyo, ya nini kuishi?” Mwa 25:22. Hivyo tangu kutungwa mimba hadi ku-zaliwa binadamu anakua kimwili, kivionjo na kiakili na ni Mungu peke yake ndiye mwenye kutenda kazi hiyo ambayo hakuna binadamu awezaye. Na huu ndio muujiza mkuu kwani hata wanasayansi waliobobe wameshindwa kabisa kujua na hata kupima jinsi binadamu anavyokua, siyo tu tumboni bali hata baada ya kuzaliwa kama anavyoshuhudia Mzaburi; Maana wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, uliunga tumboni mwa mama yangu. Mifupa yangu haikusitirika kwako, nilipoum-bwa kwa siri, nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi, macho yako yaliniona kabla sijakamilika; chuoni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa-jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, nafsi yangu yajua sana. (Zab.139:13-16). Ni zawadi tuilinde na kuitunza...AMINA

Na Frt Paschal D.J. Ighondo

Page 43: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 43

ALIYE NA MASIKIO NA ASIKIE

Frt. Richard Mateleka

Ndugu zangu katika Kristu, Uhai Singida Umoja na mapendo!

Kwa upendo wa dhati kabisa kwenu wakristu wenzangu wa Jimbo Kato-liki Singida napenda kutumia maka-la hii fulpi kutoa mawazo yangu juu ya ukristu wetu zama hizi za sasa. Ndugu zangu, maneno yaliyotumika kwa Kichwa cha makala hii yali-kuwa yakitumiwa na Bwana wetu Yesu Kristu kila alipotaka kusisitiza jambo fulani kwa wafuasi wake pin-di alipokuwa akiwafundisha, Mfano, ni katika Injili za (Mt. 11:15, 13:9, 13:43 na Mk, 4:9).

Maneno haya aliyoyatumia Yesu Kristu katika mafundisho yake ya-natualika sisi wakristo wa leo kum-sikiliza Yesu Kristu katika neno lake kiimani katika Mungu, kimaadili katika jamii zetu na kisheria ka-tika mamlaka mbalimbali husu-sani serikali zetu. Kwa namna hiyo, mafundisho ya Bwana wetu Yesu Kristu yana nafasi kubwa sana kwa maisha yetu ya kikristu kijimbo na ulimwengu mzima kwa ujumla. Kwa ufupi kabisa nimeamua kugawa mafundisho ya Yesu Kristu katika

makundi matatu nayo ni haya ya-fuatayo:-

Maisha ya Upendo kwetu soteKwa hakika kati ya maneno yanay-otajwa na watu wengi walau kila siku, ni neno UPENDO. Neno UPEN-DO hutamkwa na rika tofauti na ka-tika maana tofauti. Kwa mtazamo wa kikristu neno UPENDO ni kubwa na lenye maana iliyotukuka; maandiko yanatuambia kuwa “Mungu ni Up-endo, na mwenye kuishi katika up-endo, anaishi ndani ya Mungu na Mungu anaishi ndani yake” (1Yoh. 4:16b). Hata hivyo, kusema tu kuwa Mungu ni Upendo haitoshi, maana tunawajibika kuishi kama atakavyo Mungu, yaani kuishi fadhila ya Up-endo kwake Yeye Mungu na jirani zetu. Maana hiyo ndiyo Amri Kuu, “Umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na roho yako yote na kwa akili zako zote. Hiyo ndiyo amri kuu, tena ya kwanza. Na ya pili ni sawa na hiyo; umpende mwenza-ko kama unavyojipenda mwenyewe” (Mt. 22:37-39).

Pamoja na hayo yote, bado Bwana wetu Yesu Kristu anatudai tuwap-ende hata adui zetu, (Mt. 5:44-45). Upendo wetu kwa jirani zetu na maadui wetu ni sawa na sadaka ya Yesu Kristu msalabani, maana alijinyenyekeza mwenyewe akawa mtii mpaka mauti, yaani mauti ya msalabani (Filp. 2:8), ndiyo maana Mtakatifu Ursula anasema “haku-na upendo bila sadaka”. Kwa hiyo,

FUMBO LA UHAI WA BINADAMU

uhai wa mwandamu asili yake ni Mungu. Uhai huu kwetu sisi huanzia tumboni

mwa mama na hukaa humo kwa kawaida na kama hakuna hitilafu ya kimaumbile kwa miezi 9. Uhai wa binadamu huanza tangu pale mbegu ya baba, yai la mama na roho ya Mungu vinapoungana. Uhai huu hudumu hadi kifo cha binadamu. Akiwa tumboni hukua, hujimudu, husikia, huonja, hupata huzuni na huonyesha furaha, ndiyo maana “….mara tu Elizabeti aliposikia sauti ya Ma-ria, kitoto kichanga tumboni mwake Elizabeti kikaruka kwa furaha…” Lk 1:41, pia tunaso-ma; “…Watoto hao wakashindana tumboni mwake Rebeka, naye akasema, kama hivi ndivyo mambo yalivyo, ya nini kuishi?” Mwa 25:22. Hivyo tangu kutungwa mimba hadi ku-zaliwa binadamu anakua kimwili, kivionjo na kiakili na ni Mungu peke yake ndiye mwenye kutenda kazi hiyo ambayo hakuna binadamu awezaye. Na huu ndio muujiza mkuu kwani hata wanasayansi waliobobe wameshindwa kabisa kujua na hata kupima jinsi binadamu anavyokua, siyo tu tumboni bali hata baada ya kuzaliwa kama anavyoshuhudia Mzaburi; Maana wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, uliunga tumboni mwa mama yangu. Mifupa yangu haikusitirika kwako, nilipoum-bwa kwa siri, nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi, macho yako yaliniona kabla sijakamilika; chuoni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa-jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, nafsi yangu yajua sana. (Zab.139:13-16). Ni zawadi tuilinde na kuitunza...AMINA

Na Frt Paschal D.J. Ighondo

Page 44: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 44

ndugu zangu wakristu kwa kuishi upendo kwa Mungu na jirani zetu kwa hakika watu watatutambua sisi kuwa ni wafuasi wa Bwana wetu Yesu Kristu (Yoh. 13:35).

Kuikiri Imani yetu Katoliki kwa uthabiti

Fadhila ya Imani ni moja kati ya fa-dhila tatu za kimungu ambazo ni muhimu katika maisha yetu wakris-tu. Katika maandiko matakatifu tu-nasoma mahali pengi kuwa kabla Yesu Kristu hajawaponya wagonjwa mbalimbali walioletwa kwake aliuli-za juu ya Imani ya mgonjwa au wale waliomsaidia kumleta kwake. “Wat-aka nikutendee nini? Naye akasema, ‘Bwana nipate kuona”, Yesu akam-wambia, “Ona, Imani yako imek-uponya” (Lk. 18:41-42). Maneno ya Yesu “wataka nikutendee nini?”, yanapima Imani ya mwombaji ki-pofu ambaye naye alikiri kuwa Kris-tu anauwezo kweli wa kumponya upofu wake. Hivyo basi, “Imani hii ya kweli, isiyotikisika ni mojawapo ya majaribu makubwa ya upendo ambao tunaweza kutoa kwa Yesu” – Mtakatifu Ursula.

Ndugu katika Kristu, Imani pe-kee haitoshi kutustahilisha kuwa warithi wa uzima wa milele. Imani yetu inapaswa iambatane na ma-tendo mema kwa jirani zetu hasa wale wahitaji kama yatima, wajane, wazee, maskini, wagonjwa, wale-mavu n.k. Mtume Yakobo anasema

“Ndugu zangu, yafaa nini mtu akise-ma ana Imani, lakini hana matendo? Je, Imani hiyo yaweza kumuokoa?” (Yak. 2:14). Maneno haya, Imani na mapendo ni vitu viwili visivyoweza kutenganishwa kama pande mbili za sarafu. “Basi, kama mwili bila roho umekufa, vile vile Imani bila maten-do imekufa” (Yak. 2:2b). Mwaka huu wa Imani uwe chachu katika maisha yetu ya kikristu, kama vile “chachu kidogo ichachuavyo donge lote la unga” (Filp. 5:9). Kumbe tusikubali hata kidogo mwaka huu wa Imani upite bila mabadiliko ya kiimani ndani yetu.

Ni kweli kabisa kwamba nyakati zetu hizi tunakumbwa na changamoto nyingi ambazo zinachangia mno na kwa kiasi kikubwa utepetevu wa Imani yetu katoliki. Tunashuhudia viongozi wa dini wakipoteza maisha kwa kupigwa risasi (Fr. Evarist Mushi –Zanzibar), wakristu kuchomwa moto (Nigeria), mashambulio ya mabomu katika mikusanyiko ya Ibada (Parokia ya Olasiti – Arusha), makanisa au nyumba za Ibada ku-chomwa moto (Dar-es-Salaam, Misri – Makanisa ya Orthodox) na sehemu nyingine. Haya yote yanachangia kwa kiasi kikubwa kufanya wakris-tu wakatoliki kudhoofika kiimani. Matumini ya kudumu katika Imani yetu tunayapata kutoka kwa Yesu Kristu Mwenyewe anaposema kuwa “Nawaambieni ninyi, rafiki zangu, msiwaogope wenye kuua mwili, na

Page 45: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 45

zaidi ya hayo hawana la kufanya” (Lk. 12:4). Wewe na mimi tunapas-wa kumwogopa Mungu awezaye kututupa Jehanamu, awezaye kuua roho na mwili. Mtume Petro naye anaongeza kwa kusema “wapend-wa, msihangaike mkijaribiwa kama kwa mchomo wa moto. Kupatwa na hayo ni jambo la kawaida. Bali fura-hini mnaposhiriki mateso ya Kristo, mpate kufurahi na kushangilia pia wakati utukufu wake utakapofunu-liwa” (1Pet. 4:12-13).

Pamoja na mateso mbalimbali tu-nayoshiriki na Kristu, wito wa ku-tolipa kisasi umekuwa ukitolewa na viongozi wetu wa dini, viongozi wetu wa kiroho ili kutunza heshi-ma ya Kristu na wafuasi wake. Kila tunapotaka kurudisha kisasi kwa mabaya tuliyotendewa, tusikie sauti ya Yesu Kristu katika dhamiri zetu isemayo “Rudisha upanga wako ma-hali pake maana wote wachukuao upanga wataangamia kwa upanga” (Mt. 26:52). Basi tuwewatulivu, wa-vumilivu, imara na thabiti katika Imani yetu, “msilipe mabaya kwa mabaya, wala matusi kwa matusi bali barikini maana Mmeitwa kurithi ba-raka” (1Pet. 3:9) na mtu aliye thabiti mpaka mwisho ndiye atakayesali-mika (Mt. 10:22). Hata hivyo, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa juhudi mbalimbali zinazochu-kuliwa na viongozi wetu wa kanisa kuhakikisha Imani katoliki inapata mizizi thabiti kwa waamini wao.

Mafundisho ya Katekesi ni juhudi za dhati zinazochukuliwa kuimarisha Imani katoliki kwa wakristu wa rika zote. Maana twajua kuwa Katekesi ni kuelimisha katika Imani ya wa-toto, ya vijana, na watu wazima kwa kuwapatia mafundisho ya kikristu, ambayo kwa kawaida hutolewa, kwa mtiririko na mpangilio unaogu-sa maisha kwa lengo la kuwaingiza katika maisha yote ya Kikristo.

Ndugu zangu, madhulumu, mateso na changamoto zote za kiimani ziwe kama ngazi ya kupanda kuelekea mbinguni. Tunapaswa “tupige mbio kwa uthabiti katika mashindano yaliyowekwa mbele yetu” (Ebr. 12:1b). Tusonge mbele bila kurudi nyuma kuikiri imani yetu Katoliki iliyowekwa kwa misingi ya Mitu-me watakatifu. Na kwa kweli lililo jema kwa sasa katika maisha yetu ya kiimani ni kumwomba Mungu atuongezee Imani kama walivyo-fanya mitume wa Bwana wetu Yesu Kristu (Lk. 17:5). Kwa kutimiza yote yatupasayo tutaimba wimbo wa maandamano tukielekea mbin-guni kwa sauti tukisema “Nalifurahi waliponiambia, ‘twende nyumbani kwa Bwana” (Zab. 122:1), kwa ajili ya kupokea tuzo yetu ya kupiga vita vilivyo vizuri na imani kuilinda.

Kuishi Kwa Matumaini Kwa MunguFadhila hii ya matumaini hutubidis-ha kuamini hapa duniani. Mambo tuyatarajiayo hapo baadae ni pamoja

Page 46: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 46

na yale yanayobainishwa katika sala ya Nasadiki – Yesu Kristu, atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu; nao ufalme wake hautakuwa na mwisho, tunatumaini juu ya ufufuko wa wafu na uzima wa milele ijayo. Amina (Rej. Misale ya Waumini, Uk. 378-379). Kumbe, yatupasa kujiandaa kwa ujio wa pili wa Bwana wetu Yesu Kristu; ndiyo siku ya hukumu ya wazima na wafu, “Hapo wafu waliomo katika Kristu watafufuka kwanza. Halafu sisi tu-liochwa wazima tutarushwa pamoja nao mawinguni kumkuta Kristo an-gani” (1Thes. 4:16b-17).

Tukumbuke kuwa matumaini yetu ya kuurithi ufalme wa Mungu na uzima wa milele vinatudai kufanya juhudi ya kuishi fadhila za Imani na mapendo. Bwana wetu Yesu Kristu anatuuliza swali msingi juu ya matu-maini yetu ya ujio wake, akasema “la-kini Mwana wa Mtu atakapokuja, Je, atapata Imani duniani?” (Lk. 18:8). Ni swali ambalo kila mmoja wetu anapaswa kulijibu kwa nafsi yake, ili pindi ajapo Bwana akute imani kwa kila mmoja wetu. Tunapaswa kusali sana bila kuchoka ili Mungu atu-saidie na kutuimarisha katika Imani kwa ajili ya matumaini yajayo, kama yasemavyo maandiko, “Nia yetu ndi-yo kila mmoja wenu afanye bidii hiyo hiyo mpaka mwisho afikie ukamilifu wa matumaini, msije mkachoka, bali mpate kuwa wafuasi wa wale wa-lio warithi wa ahadi kwa sababu ya

Imani yao na uvumilivu wao” (Ebr. 6:11-12). Matumaini yetu yatatimia tukimwelekea Mwenyezi Mungu, Yeye aliye asili ya kila kilicho chema machoni petu kwa vile vinavyoone-kana na hata visivyoonekana. Mt. Ur-sula anasema “tutafute wakati wote umoja wa Mungu……katika kazi tu-elekeze mawazo yetu kwa Mungu, kama maua yanavyoelekea jua.” Hivyo basi, wakati tungali duniani maisha yetu yanatakiwa kuungana na Mungu “tukingojea heri tunay-otazamia na ufunuo wa utukufu wa Mungu mkuu na wa Mwokozi wetu Yesu Kristu (Tit. 2:13).

Basi, ndugu zangu, kwa kuhitimisha hatuna budi kubaki imara katika Imani na mapendo kwa ajili ya uz-ima wetu wa milele hapo baadaye. Magumu tuyapatayo yaimarishe Imani yetu kwa Kristu, kwani ni nani anayeweza kututenga na Upendo wa Kristo? Je, ni matatizo au shida au dhuluma, njaa, kukosa nguo, hatari au upanga? (Rom. 8:35). Kwa hakika majibu ya maswali haya ni kwamba hakuna kitutengacho na Kristu. “Kwa hiyo, ndugu zangu wapendwa, muwe thabiti na imara. Endeleeni kuifanya kazi ya Bwana siku zote mkijua ya kuwa taabu yenu katika Bwana si bure” (1Kor. 15:38).

Na Frt. Richard Mateleka-Mwaka wa Tatu Falisafa Seminari Kuu

Kibosho

Page 47: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 47

In the Catholic the Church we find the Holy water Font at the door

and the faithful when entering in the church dip their fingers into it and sprinkle some drops on the ground and then bless themselves by mak-ing the sign of cross.

Why do we Catholics use Holy wa-ter before entering the church?

It is due to the following reasons; Holy water reminds us of the waters of the red sea which the people of Israel walked before entering in the red sea. Holy water also reminds us of the water of baptism which opened for us the gate to the house of being God’s children. When Cath-olics bless themselves by the Holy water the words of the prophet Eze-kiel becomes true; “The Lord says this…. I will sprinkle clean water upon you to cleanse you….’’ (Ezek 36:25).

Why do we sprinkle Holy water on the ground before blessing ourselves? When we sprinkle Holy water on the ground we remember our dead people and feel that we

are together with them, because we do believe in the communion of saint that means we believe in the communion of the dead and the liv-ing wherever they may be here on earth, in purgatory, or already in the glory of heaven. Also, by doing so the Holy water becomes like a visible bond between them and us. It makes us feel one with them and belong together. As Saint Paul says whether we live or die we belong to the Lord (Rom 14:8). So the Holy water helps to remain us in touch with God and our dead people.

What makes Holy Water holy?Holy Water is the water blessed by the priest. He prays over the wa-ter and asks God to strengthen the faith of all those who are going to use it. Sometimes the Priest adds salt to the water; this reminds faith-ful that they should become tasty to the world and preserve their faith in God.

Oswald HIRMER, Our Joy in Being Catholic, Pauline’s Publications Af-rica, Marian mission Press, Wash-ington D.C 1991.

By Frt. Gallus Mpako-3rd Year Philisophy- Ntungamo

Major Seminary

WHY DO CATHOLICS USE HOLY WATER BEFORE ENTERING THE CHURCH?

Page 48: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 48

The sacrament is an efficacious sign representing an invisible

and an instrument of invisible real-ity. Sacrament cannot be experience by our senses but only faith. The word of God and Eucharist are two things united they cannot be sepa-rated. They are inseparable. The word of God helps us to know Jesus. The relationship between the word and sacraments takes deeper mean-ing when we turn to the celebration of the Eucharist. The unity between the word and Eucharist is grounded in then witness of scripture (Jn6:6), where can we buy some bread for this people to eat…here Jesus want-ed to feed his people with his body and blood (Eucharist).

Here we see that Jesus is the bread of the life which feed us daily. This always happens in the celebration of the Liturgy (Holy mass). First we proclaimed the word and we en-counter Jesus in the breaking of the bread. In underlying comparison be-tween Jesus and Moses who speaks to Yahweh face to face with

God as man talking to his friend (Ex 33: 11), in the discourse of bread, Jesus speaks of the gift of the God which Moses obtained for His peo-ple-manna in the desert also Jesus in the Holy mass we feed on the Liv-ing God, himself that we truly eat the bread from heaven (Eucharist).

St. Luke gives us a clear example to us when the disciples were on the way to Emmaus (Lk 24:13-35) and helps us to reflect further on the link between, the two, that is the word and the holy meal (Eucharist) which were done by Jesus himself. The scriptural readings in the Litur-gy of the word, we hear God-Logos speaking to us and in the Liturgy of Eucharist, and the Logos becomes our sacred meal. The two distinctive but inseparable the listening and understanding the word of the God –Jesus rightly help us to recognize Jesus in the breaking of bread. This opens up our eyes of faith –their eyes were opened and they were influenced to remain with Jesus, but Jesus left them… (Lk24:31).

THE DISCTINCTIVE BUT INSEPARABLETHE WORD OF GOD AND EUCHARIST

Frt. Higinius Julius Daghoo

Page 49: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 49

Therefore we as Christians we must understand both the word and the Eucharist that the two are bound together, and we cannot understand one without the other. However faith is required as st. Anselim says, (“Es-sential/necessary for understand-ing alone nothing without faith) “Fides querens intellectum”. That means, faith seeking understanding or in other words l believe in order to understand. The word opens up our eyes to understand the Eucha-rist because the scripture illumines and explain the mystery of the Eu-charist that is Death and the resur-rections of Jesus. BENEDICT XVI Apostolic Letter Ver-bum Domine 2012

By Frt. Higinius Julius Daghoo 2nd

year of philosophy-Ntungamo Major Seminary

CHAMA CHANGU KINA NINI?

Frt Patrick Sebastian

Chama ni umoja wa watu wenye nia fulani kwa umma. Umoja wowote ambao unaundwa lazima uwe na shabaha na shabaha hiyo isiwe kinyume na sheria za nchi.

Binadamu ana viungo vingi lakini viungo hivyo pia umoja wao huwezi kupingana hata siku moja hivyo kama viungo vilivyo na umoja basi vyama ama wanachama wanapaswa kuwa na umoja ili kutimiza shabaha ya chama. Swali la kujiuliza katika dunia ya tatu vyama vyake ama wa-nachama wana umoja unaotakiwa na kanuni zao. Napenda kusema malengo ya chama, makosa yanay-ojitokeza katika chama na wajibu wa chama.

MALENGO YA CHAMAChama cha siasa kinapoamua kushiriki katika uchaguzi mkuu huwa kina nia ya kuongoza umma kufikia maisha yaliyo bora kwa watu. Mfano chama cha TANU kilipo kuwa kinaundwa kilikuwa na lengo moja tu, ambalo lilikuwa ni kuitoa serikali ya mkoloni wa Kiingereza na mambo yote yaliyokuwa yakien-

Page 50: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 50

dana na tabia ya kikoloni. Swali la kujiuliza, vyama vya siasa vya sasa hapa Tanzania malengo yao nini? TANU ni chama ambacho kweli kweli kilikuwa na nia ya kuwafanya Watanganyika kuwa huru kutoka kwenye mikono ya mkoloni. Ukiso-ma kazi nyingi kama vile vitabu vya chama cha TANU pamoja na maazi-mio yake utaona kweli kulikuwa na watu wenye nia ya kuongoza watu wawe na maisha bora. Mfano Azi-mio la Arusha lilikuwa na matamko rasmi yenye kuonyesha malengo ya TANU.Azimio la Arusha lasema: “Tumeonewa kiasi cha kutosha; Tumenyonywa kiasi cha kutosha.Tumepuuzwa kiasi cha kutosha, unyonge wetu ndio uliotufanya tu-nyonywe, tuonewe na kupuuzwa sasa tunataka mapinduzi, mapin-duzi ya kuondoa unyonge ili tusion-ewe tena tusinyongwe tena na wala tusipuuzwe tena”

Je sauti ya TANU kupitia Azimio la Arusha unaionaje? Je chama gani cha siasa kwa muda huu kina maneno ya kuonesha uchungu dhidi ya shida za raia wake? Chama cha TANU ki-likuwa na na sera ambazo ziligusa maisha ya raia wake pia kilikuwa na sera ambazo zilikuwa zinaandaa watu kufurahia nchi yao. Sera kama vile elimu ya kujitegemea, vijiji vya ujamaa. Moja ya maneno yaliyohi-miza vijiji vya ujamaa ni “Mtu pe-kee hakawii kufikia kikomo cha uw-ezo wake. Ni uwezo wa mtu pamoja na wenzake ambao hauna kikomo. Binadamu wanapotaka maende-leo makubwa huwa hawana budi

waweke juhudi zao pamoja. Na kuna njia mbili tu za kuweka juhu-dii zetu pamoja kwa kufunzwa kazi pamoja au kwa kufanya kazi pamo-ja.Tunaweza kufunzwa kazi pamoja kwa manufaa ya mfuga watumwa au bepari au tunaweza kufanya kazi pamoja kwa manufaa yetu we-nyewe. Ni dhahiri kwamba tutati-miza shabaha zetu hizi ikiwa msingi wa maisha ya Watanzania utakuwa ni vijiji vya ujamaa, ambamo watu wanaishi pamoja na kufanya kazi pamoja kwa faida ya Taifa zima”. Je ni chama gani kwa sasa ambacho kinawahimiza watu wake kuishi kwa pamoja wakiwa nawanafurahia maisha katika nchi yao?

MAKOSA YANAYOJITOKEZA KWENYE VYAMA VYA SIASA

Kuwepo Kwa Makundi Ndani Ya Chama: Kundi lao na kundi letu haya makundi husababisha chama cho-chote kufikia malengo. Tuone mwili wa binadamu unavyofanya kazi. Mwili una viungo vigi lakini viungo hivyo kila kimoja hufanya kaz i yake kadiri ya sheria za mwili. Kiungo kimojawapo pindi kinaposhindwa kufaya kazi inavyopaswa basi mwili wa binadamu huyu utabadilika jina na kuitwa kilema au ugonjwa kama macho hayataona basi binadamu huitwa kipofu. Pia kama binadamu huyo hana pua basi ataitwa toinyo, hivyo endapo chama kitakuwa na makundi basi chama hicho kitaitwa chama cha wendawazimu kwa saba-bu hawawezi kusikilizana pindi wa-napopanga mipango ya maendeleo.

Page 51: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 51

Mara nyingi sababu zinazosaba-bisha makundi ni elimu, uwezo wa kipato na madarka. Kutokuelewana miongoni mwetu ni jambo la kibina-damu hivyo tukieleweshana hatuna budi tuelewane, mfano kama ukim-weleza mtu jambo hakusikilizi kisha na wewe ukaenda kuharibu masikio kwa kuweka pamba masikio ili usisikie yale unayoelezwa na yule uliyemweleza hakukusikia wewe basi huo ni wendawazimu kwa sa-babu hutaki watu waelewane ndani ya chama. Ni vizuri kufuata kanuni za chama na za nchi ili kuweza kuti-miza shabaha ya umoja wetu. Kuo-na kosa la mtu mwingine ni rahisi kuliko kuona makosa ambayo mtu mwenyewe anayatenda. Hivi 2 na 3 ni 5 lakini mimi naweza kusema ni sita 6. Majibu haya yote ni sawa laki-ni kama hukupewa alama sahihi ni kujumlisha ama kuzidisha endapo alama sahihi ni kujumlisha jibu sa-hihi ni Tano 5 na endapo mimi ni-taendelea kulazimisha jibu liwe sita ni kosa kwa sababu sijafuata kanuni inayopaswa kutumika ili kufikia jibu sahihi.

Ni vizuri tukaongozwa na kanuni tulizojiwekea ili kufikia malengo ya vyama vyetu sio kuongozwa na fikra zetu. Mawazo yetu ndiyo yanayosa-babisha kuwepo na makundi ndani ya chama. Mara nyingi fikra zetu daima huwa na maslahi binafsi na sio maslahi ya jumuiya ama chama.Daima tabia ya ukweli huwa ni nzuri sana maana huwa haichagui aliyes-ema ukweli ni mtu wa namna gani mtoto, msomi ama la. Ukweli we-

nyewe huwa unabaki palepale. Mfa-no kama mtoto anakueleza moto unaunguza lakini wewe ukadharau hayo maneno yake ukashika moto huo, Upenda usipende utakuunguza tu. Hapo ndipo utakumbuka ushauri wa mtoto kuwa moto unaunguza.Hivyo viongozi na wataalamu wa vyama wanapswa kupokea mashau-ri yale yenye maslahi kwa umma na sio ya mtu binafsi ama kikundi ki-dogo cha watu wenye choyo.

Kutokupenda Kuelimika: Mara nyingi wanachama wengi hujiona kuwa wanaelewa kila kitu na ha-wataki kuendelea kujielimisha kwa mambo ambayo hawayajui huona kuwa kuelimika ni hadi ukasome hapo ndipo imani yao inasema huyu mtu amesoma, zaidi ya hayo wale waliosoma nao hutumia vibaya elimu yao kwa kuwakandamiza wale wasio soma na hata kudiriki kusaini mikataba kwa maslahi binafsi. Moja ya kanuni ya mwana TANU inasema “Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu wote na kutumia elimu yan-gu kwa faida ya wote”. Hivyo ndugu zangu wananchi ni vizuri kutambua kuwa elimu ni uwezo wa mtu ku-weza kutambua jema na baya katika jamii kudumisha ama kulitokomeza kama lina madhara kwa umma. Mara nyingi ukitaka kupima mtu aliyeelimika na ambaye hajaelimika utaona yule asiyeelimika huwa na majibu mepesi kwa mambo makub-wa. Mfano kwa sisi wa dunia ya tatu tupo maskini, atakueleza wakoloni ni chanzo cha umaskini katika nchi zetu kama hivyo kwa nini sasa kila

Page 52: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 52

mara Marais wa dunia ya tatu hu-enda Ulaya kuwaalika hao waliotut-awala waje kuwekeza pasipo aibu anasema bila uwekezaji hatuwezi kuendelea. Ndugu wananchi hali hii huzuia akili zetu kutafuta su-luhisho la matatizo yetu. Mwana-falsafa mmoja wa Kiyunani aliwael-eza wanafunzi wake kuwa mwanzo wa kujifunza ni pale ambapo hujui, lakini sasa wale wenye madaraka kufahamu chanzo cha umaskini na kupata jibu la haraka kuwa ili tuen-delee lazima tuende Ulaya tukawaite waje kuwakeza katika nchi za dunia ya tatu huu ni uwezo wa viongozi wetu wa kufikiri. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema anashangaa sana maji kutoka nchi kavu kuelekea ba-harini mahali ambapo kuna maji mengi”. Na mimi nashangaa kuona mwekezaji kuchukua kiasi cha shi-lingi 700 kitanzania na nchi inachu-kua shilingi 300 tu, hivi huyu mtu anasema bila uwekezaji hatuwezi kuendelea anamaanisha nini? Je kuna uwezekano wa tajiri wa dunia ya tatu kweda kufungua kiwanda cha kutengeneza magari huko Japan ama China. Tafuta majibu.

Viongozi wa chama kuweni wakweli katika kutatua matatizo ya jamii. “Chama ambacho nia yake ni kuwa daktari wa matatizo ya jumuiya hakina budi kiwe na tabia ya kujua matatizo yenyewe sababu za mata-tizo hayo na dawa yake. Bila kujua matatizo na sababu za matatizo hayo hatuwezi kujua dawa yake”. Kutokuelimika hufanya wanachama kutotumia akili zetu kufikia malen-

go yetu. Hivyo basi ni vizuri kutumia akili zetu vizuri ili kuleta faida kwa umma. Chuki ndani ya chama ama nje ya chama

Chama cha TANU kilikuwa huru ku-wachukia viongozi wa serikali ya kikoloni na tabia zao, kwa sababu wakoloni walikuwa wanawanyan-yasa Waafrika kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Lakini leo hii hatuwezi kusimama na kuhutubia umma kuwa chama fulani sio kizuri kwa sababu chama hicho ni chama ambacho ki-naongozwa na watu ambao ni ndu-gu zetu ama rafiki zetu. Sasa kama tutaanza kusimama majukwaani na kuanza kuwatukana na kuwake-jeli viongozi wake na wanachama wao tutaonekana tumeishiwa sera, wakati lengo la chama ni kuelimisha watu ili wawe na maisha mazuri sio kuanza kusema chama kingine, sisi tuuze sera zetu hapo tutaonekana watu ama chama chenye maana kwa jamii. Hasa kilicho madarakani hata siku moja hakina sababu ya kuzun-gumza chama kingine, kwani wao ndio wamepewa dhamana ya kuon-goza umma. Kama kitaanza kujadili chama pinzani huo ni upuuzi tu.

Mwindaji hurusha mshale porini kwa lengo la kupata shabaha ya ki-toweo ndege ama swala na akimko-sa huufuata huo mshale kwa kuwa haukupotelea mbali. Aliurusha kwa lengo la kupata kitoweo, hivyo wana-chama wao wanapaswa kuhangaika na shida na majibu ya shida za jamii sio shida za chama pinzaniama ku-fuata matakwa ya mtu binafsi. Kama

Page 53: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 53

tutafanya kazi ya kuhangaika na up-inzani huo ni mwanzo wa kuishiwa na nguvu.

Chama pinzani kazi yake ni kuelim-isha umma. Ili uweze kupata maisha mazuri sio kueleza ubaya wa chama ama watu wa chama kile na vion-gozi wake ama kutengeneza chuki dhidi ya chama tawala na umma.Kwa kufanya hivyo utasababisha umma kutoshirikiana na serikali yao katika kuleta maendeleo kwa manufaa yao.

Mara ngapi viongozi wa upinzani hushawishi raia kutoshiriki shu-ghuli za maendeleo na kusema serikali ina fedha huo ni utoto na hauna maana. Tukumbuke maneno ya mwalimu Nyerere “Maendeleo ya nchi huletwa na watu hayaletwi na fedha. Fedha ni matokeo sio msingi wa maendeleo”. Hivyo wanasiasa wanapaswa kuelimisha watu kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo yao sio wasubiri ser-ikali ilete maendeleo katika nchi yao. Hakuna serikali hata moja dun-iani ambayo inaweza kugawa fedha kwa raia wake.

Kukosa udadisi na uzalendo Baadhi ya wanachama hawana uda-disi wala uzalendo kwa kuwajibika ili kuweza kuleta faida kwa umma.Pindi linapotokea janga kwenye nchi hasa nchi za malofa huo ndio wakati wa watu wenye madaraka wanavyoweza kujipatia umaarufu na utajiri usiokuwa wa maana. Hali hii kila kiongozi hutafuta jibu lisilo

la uhakika ili apate chake cha ku-fanya afurahie maisha yake yeye na jamaa zake mfano mwaka 2006 nchi ya Tanzania ilikumbwa na ukame ambao ulikuwa wakati wa wanachama kupata chao, waziri mmoja aliweza kugeuza maamuzi ya baraza zima kuwa mawazo yake. “Serikali ilitaka kukodisha mitambo kwa kampuni ya CDC Globele, ser-ikali ilitaka wapunguze kipindi cha ukodishaji mitambo washushe zaidi bei yao ya umeme na wawe tayari kuzalisha umeme hadi Mei 2006 ilipeleka ujumbe tofauti kabisa kuwa, serikali inafuta mpango wa kukodisha mitambo kutoka kwao Kwa kuwa yule aliyepewa mamla-ka akatumia vibaya mamlaka yake ndivyo alivyosababisha hadi Waziri mkuu kujiuzulu kutokana na tatizo la ukame ulioikumba nchi yetu.Hivyo ukifanya kosa moja jua kosa linalofuata linaweza kuleta madhara kwa umma kama ilivyosababisha kampuni hewa kulipwa fedha bure za umma kiasi cha shilingi milioni 152 kwa siku kwa taarifa zilizotole-wa na kamati teule ya bunge. Hivyo wale wenye madaraka ni vizuri kuheshimu malengo ya wanachama kwa manufaa ya umma.

Urafiki au kutokuwajibikaMambo ya urafiki katika chama hurudisha nyuma maendeleo ama hufanya malengo ya chama yash-indwe kufikiwa. Kwa sasa vyama vimekuwa kama umoja wa majan-gili amabao kazi yao ni kutopenda watu wote wawe na maisha mazuri kwa hata wale wanaojitokeza wazi-

Page 54: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 54

wazi wamehujumu uchumi wa nchi hakuna chochote kinachoweza ku-fanyika. Enzi za chama cha TANU kulikuwa hakuna lele mama kama kweli umebainika umefanya kosa la uhaini ama umehujumu uchumi hakuna cha urafiki wewe ni sheria na kanuni zinafanya kazi sio kuan-galia yale uliyoyafanya mzuri huko nyuma ndiyo uendelee kuumiza raia wetu. Mfano Bibi Titi ni mwanamke aliyepigania uhuru na Mwalimu Ny-erere lakini baada ya uhuru alianza kuwa mpinzani wa chama cha TANU kwani alipinga Azimio la Arusha lil-iloundwa mwaka 1967. Mwalimu hakujali ule uzuri wake wa mwanzo na uafiki wakati wa kudai uhuru alitupwa mahakamani na kubainika kuwa anakosa la uhaini kosa hilo lilimfanya kufungwa kifungo cha maisha jela. Pia Oscar Kambona huyu alikuwa ni rafiki mkubwa wa Mwalimu Nyerere na alikuwa ni waziri wa uchumi na mambo ya nje naye alilazimika kuikimbia nchi kutokana na kupinga Azimio la Ar-usha, hivyo Mwalimu aliweza kuwa makini na kanuni ya chama chake kisiwe chama cha majangili ambao wamemfukuza mkoloni kisha watu wachache waanze kufaidi matunda ya uhuru. Je swali la kujiuliza Chama gani sasa ambacho wanachama wake wakibainika kuwa ni wahuju-mu uchumi ama wahaini kinaweza kufanya yale yaliyofanywa na Mwal-imu? Kila kitu ni chema kutokana na uumbaji wa Mwenyezi Mungu endapo kitatumika kadiri ya asili yake na taratibu zake. Lakini kama hakitatumika kadiri ya taratibu kitu

hicho kitakuwa ni hatari kwa jamii zake. Silaha ni nzuri kama itatumi-wa kwa malengo la kujilinda dhidi ya maadui lakini kama ikitumiwa kuua hata rafiki zako basi silaha hiyo haitakuwa na maana yoyote kwako. Hivyo vyama vyote vya sia-sa ni vizuri kama vitaweza kufanya kazi zake kwa manufaa ya umma lakini kama vitageuka na kuwa-kandamiza wananchi vyama hivyo havitakuwa na maana yoyote. Hivyo chama chochote kinachotaka kushi-ka dola kiwe na wajibu wa kuangalia maslahi ya umma na sio ya chama. Zamani wabunge walikuwa wanach-aguliwa kwa ajili ya kuwakilisha wa-nanchi sasa wamekuwa wanawakil-isha chama na wameacha wananchi.Kibaya zaidi sasa wapo waliojijen-gea kwenye vichwa vyao chama fu-lani ni cha dini fulani haya mawazo yatoke haraka kwenye vichwa vyetu kwasababu ni mawazo yenye chuki na fitina.

Na Frt Patrick SebastianSeminari Kuu ya Kibosho, Mwaka

wa III Falsafa

Page 55: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 55

FAIDA YENYE HASARA

Frt. Gariel Masaka

Maisha ni fursa ambayo Mwe-nyezi Mungu ametupatia

sisi wanadamu. Kila mwanadamu ameumbwa kwa makusudi fulani. Hakuna mwanadamu awaye yote am-baye ameumbwa ili aishi kwa niaba ya mtu mwingine au aishi kama kivuli cha mtu mwingine. Huwezi kusema eti mimi naishi kwa niaba ya fulani. Mun-gu hajapungukiwa kiasi hicho. Ndani ya fursa ya maisha/uhai kuna fursa zingine nyingi ambazo humjia mwan-adamu. Mara nyingi fursa huonekana kuwa ndogo sana wakati inakuja na huonekana kuwa kubwa wakati ina-ondoka. Ndio maana utamsikia mtu akisema, “Ningejua… ningefanya …!” Ukimsikia mtu anasema hivyo ujue tayari fursa imetumika vibaya! Fursa ikitumika vizuri huleta mafanikio ka-tika safari ya maisha ya hapa duniani. Maisha ni safari, safari ni mwendo ambao huleta mabadiliko. Mabadil-iko maishani yaweza kuwa mazuri au mabaya. Mabadiliko mazuri ni “faida” lakini mabadiliko mabaya ni “hasara”. Juhudi na maarifa huleta mafanikio/faida maishani; ndiyo maana siku zote

tunasisitizwa kufanya kazi kwa bidii ndipo tuone/tupate mafanikio. Katika hilo mtume Paulo anatuambia, “Asiye fanya kazi na asile” (2 The 3:10). Pamo-ja na kwamba “faida” ni kitu kizuri, ni manufaa au mafaa ya jambo fulani lakini faida hiyo hiyo yaweza kuwa kitu kibaya iwapo itapelekea mata-tizo maishani yaani hasara maishani. Hiyo ina kuwa ni faida lakini ndani yake ina hasara ndio maana tukaiita faida yenye hasara. Faida inayopa-tikana pasipo kumshirikisha Mungu ni faida yenye hasara. Lakini pia mtu anaweza kumshirikisha Mungu katika kutafuta faida au mafanikio maishani lakini anapofanikiwa anakula bila kumkumbuka tena Mungu ambaye ndiye aliyemwezesha mtu huyo kuwa na mafanikio mathalani mafanikio ka-tika utajiri. Ndio maana utakuta mara nyingi sana mtu anaweza kukumbuka kusali kabla ya kula lakini baada ya kula hakumbuki kusali tena na wakati mwingine hata vyombo alivyovitumia anaweza kuviacha pale pale.

Katika Katekisimu ya Kanisa Kato-liki, kuna swali huuliza hivi; “Mungu ametuweka duniani tufanye nini?” Kwa maneno mengine swali hili linata-futa sababu ya Mungu kutuumba. Jibu la swali hilo katika Katekisimu hiyo hiyo ni hili, “Mungu ametuweka duni-ani ili tumjue, tumpende, tumtumikie na mwisho tupate kufika kwake mbin-guni”. Kumbe hapa tunaweza kutam-

Page 56: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 56

bua moja kwa moja kuwa hapa duni-ani hatukuletwa kwa bahati mbaya, uwepo wetu si wa bahati nasibu. Mara nyingi utamsikia mtu akisema, “Nime-jikuta tu nimefanya hivi, sikutegemea jamani!” Ieleweke kwamba, katika suala la uumbaji, Mungu hakujikuta tu ametuumba, hakutuumba kwa ba-hati mbaya ndiyo maana kuna hizo sababu kuu nne ambazo kwazo tuko duniani. Tumetoka kwake na kwake tutarudi. Ni wazi kwamba sababu ya nne yaani ya kufika kwake mbinguni, inategemea sana hizi sababu tatu za mwanzo ambazo ni kumjua, kumpen-da na kumtumikia. Katika maisha ya mwanadamu kwa hali ya kawaida tu huwezi kumpenda mtu usiyemjua. Kwa vyovyote vile utampenda mtu au utamchukia mtu ama baada ya ku-muona yeye mwenyewe au kumsikia au kuona kazi zake au kwa kusikia tu habari zake, ndipo utaweza kusema nampenda huyu au nampenda yule. Ndiyo maana katika hilo sisi wana-damu huwa tunapenda kitu au tu-nampenda mtu kwa sababu fulani. Kumbe sababu ya kwanza kabisa ya kumjua Mungu ndiyo inayotupelekea tumpende. Tukimjua tutampenda na tukimpenda tutamtumikia na tukim-tumikia vizuri kadiri ya mapenzi yake tutafika kwake mbinguni.

Katika makala yetu ya leo napenda tut-afakari zaidi kuhusu sababu mbili kati ya hizo nne tajwa hapo juu. Tutafakari

juu ya kumtumikia na kufika kwake mbinguni. Nimechagua hizi mbili sio kwamba zile zingine mbili (kumjua na kumpenda) hazihitajiki la hasha! Zina-hitajika sana lakini kwa leo hebu tuzi-chambue hizi mbili za mwisho yaani kumtumikia na kufika kwake mbin-guni. Zaidi sana hii sababu ya tatu ya kumtumikia Mungu ndiyo wazo kuu la leo.

Tunatambua kwamba binadamu ni mwili na roho. Vyote hivyo viwili vi-nahitaji chakula ili viweze kuwa imara. Hata hivyo ikumbukwe kuwa chaku-la cha mwili si chakula cha roho na chakula cha roho si chakula cha mwili. Lakini vyoye viwili vinamtegemea mhusika wa huo mwili yaani binadamu mwenyewe. Pilika pilika za kila siku za mwanadamu zinalenga katika kunu-faisha ama mwili na roho kwa pamoja au wakati mwingine hulenga kushi-bisha kimojawapo. Kwa bahati mbaya sana mara nyingi binadamu amekuwa akiutumikia zaidi mwili wake mwe-nyewe kuliko roho yake mwenyewe. Binadamu wamejiweka katika nyanja mbalimbali sana za kumtumikia Mun-gu. Hii ni pamoja na miito mbalimbali mitakatifu kama vile Upadre, Utawa (wakike na wakiume) pamoja na Ndoa. Pia katika kumtumikia Mungu kuna miito mingine ambayo tunaweza kuiita “Miito-kazi”. Miito-kazi ni kama vile udaktari, ualimu, kazi mbalimbali za ufundi, kilimo na biashara bila ku-

Page 57: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 57

sahau uongozi wa kidini, kisiasa na ki-jamii. Katika yote haya binadamu ana-tumika na kutumikia. Katika kutumikia au kutumika huku, binadamu huweza kupata faida, mafaa au manufaa yato-kanayo na kazi yake. Manufaa haya ni pamoja na mshahara wa kazi, mavuno mazuri shambani au faida kubwa kati-ka biashara. Kwa kifupi manufaa haya au faida hii yaweza kupelekea utajiri mkubwa wa kidunia na kupelekea kuzisahau roho zetu na hatima yake kumsahau Mungu ambaye ndiyo hiyo roho. Kama ambavyo nimeeleza hapo juu kuwa wengi wetu tunashughulikia zaidi mwili kuliko roho.

Hebu muone huyu: Kuna mtu mmoja wa mahali fulani alisikika akisema, “kesho siendi kanisani kwa sababu leo umeme umekatika siku nzima sijaen-da saluni”. Mtu mwingine aliyekuwa karibu naye akamwambia, “Ni heri kuingia mbinguni ukiwa na jicho moja kuliko kuwa na macho mawili halafu ukatupwa jehanamu.” Kimsingi ha-tusemi watu waende kanisani wakiwa wachafu isipokuwa kila jambo fulani lifanywe kwa wakati wake kwa kupima uzito wake kadiri ya mapenzi ya Mun-gu. Kukosa kusali eti kisa hujaenda saluni au hujafua nguo! Huo naweza kusema ni ugonjwa wa akili. Hivi hiyo jumapili kwani imefika ghafla? Au mtu mwingine anasema siendi kanisani kwa sababu sina wa kumwachia duka langu! Eti hela zitanipita jamani siwezi

kufunga duka! Mtu wa namna hii ndi-ye anayemkumbuka Mungu wakati wa shida tu.

Ndugu zangu ni kweli kabisa katika maisha ya kila siku tunatumikia na kutumika lakini tujiulize, Je! Tunam-tumikia nani na kwa namna gani? Tu-natumikaje? Ndugu msomaji ukipata muda jaribu kufanya utafiti mdogo tu, nenda katembelee maeneo ya sokoni au stendi yoyote iliyo karibu nawe halafu angalia watu walivyo bize kiasi cha kutosalimiana wao kwa wao. Waangalie kwa makini halafu jaribu kutathimini hatima ya kila kitendo kin-achofanyika hapo. Je! Ni kweli hatima yake ni kufika mbinguni kama Mungu anavyotudai? Yaani huyu anasema hiki! Yule anaimba! Huyu anacheka! Yaani tu basi walau kila mtu yuko bize katika kutumika au kutumikia jambo fulani!

Mtume Paulo anapotuambia kuwa asi-yefanya kazi na asile. Ni kweli kabisa anahimiza bidii ya kazi, kila mtu ale kwa jasho lake bila uvivu wowote. Ni vema na haki kwamba tunafanya na tu-napata faida au manufaa. Sasa mbona tukisha fanikiwa tunamsahau Mungu? Kutajirika kidunia na halafu kumsahau Mungu ni faida yenye hasara. Faida au mafaa ambayo ni zao la kutumika au kutumikia mara nyingi yametupelekea tuvae miwani ambayo haipitishi mwanga hata kidogo, yaani tunakuwa

Page 58: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 58

gizani katika mwanga. Mwanga upo lakini sisi tupo gizani. Tuna macho la-kini hatuoni! Tuna masikio hatusikii! Tuna pua hatunusi! Kuipata dunia yota na kuikosa mbingu ni faida yenye hasara. Kimsingi faida yenye hasara ni hasara.

Yesu anapotuambia kuwa ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia ufalme wa mbinguni (Mk. 10:24-25) hamaan-ishi kwamba masikini wote wasio na chakula wala mavazi wala sehemu za kulala ndio wataenda mbinguni, hap-ana! Pia hamaanishi kwamba matajiri wote wa kidunia wataenda jehana-mu/motoni, hapana! Jibu liko hapa, “Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni wao” (Mt 5:3). Maskini wa roho maana yake roho safi na nyeupe isiyo na mawaa mbele ya Mwenyezi Mungu. Ndugu yangu, um-asikini wa kimwili sio tiketi ya kwenda mbinguni wala utajiri wa kidunia sio kizuizi cha kwenda mbinguni. Isi-pokuwa jambo la msingi hapa kuan-galia ni kwamba, katika hali yoyote ile ya maisha uliyonayo ambayo yaweza kuwa ni utajiri au umaskini jiulize, Je! Umempa Mungu nafasi kiasi gani ka-tika hiyo hali uliyonayo? Usijeshangaa ukaishi kwa taabu sana hapa duniani na mbingu ukaikosa, yaani unapanda kwa machozi na unavuna kwa ma-chozi.

Waswahili husema “mchumia juani hulia kivulini” lakini mimi nasema hivi, tusipo kuwa makini tutachumia juani na tutalia juani.

Nimesema kuwa si utajiri au umas-kini wa kimwili/kidunia ndio chanzo cha kwenda au kuikosa mbingu. Mtu aweza kuwa tajiri sana akajiona yeye ndiye muweza wa yote na hamhitaji Mungu katika maisha yake. Hali kad-halika, mtu aweza kuwa maskini sana kiasi cha kuona kuwa Mungu hana nguvu tena ya kumsaidia hivyo hamhi-taji tena Mungu maana anaona hana msaada wowote kwake. Watu hawa wote wawili hawawezi kwenda mb-inguni. Ndiyo hawawezi kwenda kwa sababu hawamtambui Mungu na ha-wafanyi juhudi yoyote ya kumtafuta. Hawajampa Mungu nafasi. Huku ni kukata tamaa.

Kwa kweli Mungu mwenyewe ndiye mtoa vyote alivyonavyo binadamu. Yeye ndiye anaruhusu kutajirika kwa mtu. Mtu hawezi kutajirika bila Mun-gu. Lakini sasa tujiulize, kama Mungu ndiye anaruhusu kutajirika kwa mtu, kwa nini tena anasema si rahisi tajiri kwenda mbinguni? Ina maana ametoa utajiri ili wanaoupata wasiende mb-inguni? Mbona anasema ametuumba ili baadae tufike kwake? Jibu la mas-wali haya yote ni hili: Ni kweli kabisa Mungu ndiye mtoa wa vyote, ni kweli kabisa Mungu anaruhusu utajiri, ni

Page 59: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 59

kweli kabisa Mungu anapenda sote baada ya kuishi hapa duniani baadae tukaishi naye mbinguni. Sasa anapo-tuonya juu ya utajiri anatuweka wazi kwamba, utajiri wa kidunia ni moja ya kishawishi kikubwa sana kinachoweza kumfanya mtu asiione njia ya mbingu-ni. Ukisoma kwa makini fundisho hilo, Yesu hasemi kuwa matajiri hawatain-gia ufalme wa Mungu, hasemi kuwa matajiri hawawezi kuingia ufalme wa Mungu; anasema “Ni rahisi kwa nga-mia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia ufalme wa Mun-gui” (Mk 10:25). Hilo neno “rahisi” linamaana kubwa sana, kwa maneno mengine tungeweza kusema si rahisi tajiri kuingia ufalme wa Mungu. Kuse-ma “si rahisi” haimaanishi kuwa “hai-wezekani”. Inawezekana sana tu! Ila inahitajika neema ya Mungu ili kua-chia utajiri wa kidunia kwa ajili ya sifa na utukufu wa Mungu.

Katika maisha ya kawaida mwana-damu anapokuwa ametajirika tayari hupenda aendelee kuwa tajiri zaidi na zaidi, hapendi kufirisika, hapendi kabisa kuona mali zake zikipungua. Ndio maana atajitahidi kwa gharama yoyote kulinda utajiri wake. Wengine wako tayari hata kuua wengine kwa lengo la kulinda utajiri wa kidunia. Imeonekana mara myingi baadhi ya watu wanaulinda utajiri wa kidunia kuliko hata wanavyolinda usafi wa roho zao. Naomba ieleweke kuwa

kulinda uhai wa kimwili haina maana ya kulinda uhai wa kiroho. Katika hilo utakuta mtu yuko tayari kufa akitetea mali yake kuliko kufa akitetea imani yake (kufia dini/ kufa shahidi kiimani). Ugumu wa tajiri kuingia mbinguni unakuja kwamba, tajiri huyu anam-sahau Mungu kabisa kwa sababu ya utajiri wake, anamsahau Mungu kwa sababu ya mafanikio yake. Muone kijana huyu, yuko tayari kuamwacha Mungu kwa sababu ya utajiri. Rejea Mk 10:17-27 hasa aya ya 22, “wala-kini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi”. Mali inamfanya mtu amwache Mungu. Anaifaidi dunia lakini anaikosa mbin-gu. Hiyo ni faida yenye hasara. Hasara nyingine ni kwamba katika mafanikio huwa kuna “ubinafsi”. Angalia mfano huu rahisi; Mwanafunzi anapofaulu mtihani husema ni juhudi zake mwe-nyewe. Utaskia akisema, “nilisoma sana aise usiku na mchana bila kulala ndio maana nimefaulu”. Haya sasa sikia anavyosema anapofeli mtihani; Ah! Hakufundishwa vizuri, oh! Hatuna vitabu! Hatukumaliza mtaala! Hatuna walimu! Yaani visingizio chingu nzima. Hata siku moja hasemi kuwa amefeli kwa sababu ya uzembe wake. Ni kweli kabisa mara nyingi tunapofanikiwa kimaisha hatukumbuki tulikotoka. Tunabaki kufurahia tu mafanikio tuli-yopata mpaka tunamsahau aliyefani-kisha hayo.

Page 60: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 60

Kusahau tulikotoka ni chanzo cha kusahau aliyetutoa huko. Kama uki-kumbuka kuwa wakati wa mateso ulimwomba Mungu akusaidie, kumbe utakapo fanikiwa kama utakumbuka nyuma ni wazi utamkumbuka ali-yekusaidia na hivyo utamshukuru na kuendelea kuangana naye. Wakati wa masika wengi huomba Mungu alete mvua, lakini wanapovuna husa-hau kumrudishia shukrani Mwenyezi Mungu. Walau moja ya kumi ya ma-pato. Yaani linakuwa ni jambo la ajabu sana, unakuta kwa mfano waamini kwa hiari yao wenyewe kabisa bila kulazimishwa wanaamua muomba misa kwa ajli ya kuomba mvua ili wa-pate mazao. Hapo wanamkumbuka Mungu wakati wa shida. Sawa ni kitu kizuri maana yeye mwenyewe alise-ma, “Ombeni mtapewa, tafteni mta-pata, bisheni hodi mtafunguliwa,…” Sasa ndugu yangu Mungu anakupatia mvua unavuna vizuri, kwa nini sasa unasubiri ulazimishwe kumshukuru Mungu? Yaani unakuta mtu anatoa shukrani ya mavuno huku amenuna utafkiri kiasi kwamba ardhi aliyoilima ni yake, mvua ni yake na nafaka ni zake. Tunamkosea sana Mungu. Mtu anapata mazao mazao gunia mia moja halafu cha ajbu kabisa shukrani ya mavuno anatoa debe moja! Ni aja-bu sana! Kwa kweli utajiri ni kitu kizuri sana kama mtu atautumia kwa ajili ya sifa na utukufu.

Ikitokea umetajirika, mshukuru Mun-gu kwamba kakupatia kitu cha kuweza kutoa kwake. Tunashindwa kumfuata Mungu kwa sababu ya mafanikio ya kidunia (Mt 19: 16-30; Mk 10:23; Lk 18:18-30).

Ndugu yangu jaribu kufanya utafiti kadiri uwezavyo halafu utaona ni watu wangapi wamebadilika kitabia baada ya kupata mafanikio fulani maishani. Wengine wakishafanikiwa hata kusalimia wenzao huwa ni shida, wanataka wao ndio wasalimiwe tu! Wanajiona kuwa wao ndio kila kitu. Wanandoa wengi walipokuwa mas-kini wameishi vizuri tu kwa upendo na amani lakini walipotajirika tu! Mambo yakaharibika, ugomvi kila siku hauushi ndani ya nyumba, mganga wa kienyeji amekuwa ndiye muungu wao mlinzi. Yaani kwa kifupi utajiri kwao ime-kuwa ni chanzo cha matatizo. Hiyo ni faida yenye hasara. Yesu ametuonya; “Angalieni, jilindeni na choyo maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyonavyo.” (Lk 12:15). Barua ya Paulo kwa Timotheo inase-ma, “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wame-farakana na imani na kujichoma kwa maumivu mengi.” (1 Tim 6:10). Pia rejea (Ybs 13:1-8) utaona mitego ya tajiri mwenye kiburi.

Page 61: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 61

Hali kadhalika Yoshua bin Sira anatu-patia ujumbe huu: “Mwanangu, mbona unazidi kujishughulisha na kazi nyingi? Afanyaye haraka kuongeza mali hataepuka hatia. Ukijihimiza ku-fuata utajiri hutapata, wala ukiutafuta hutauona. Kuna mtu ajitahidiye na ku-fanya kazi na kujihimiza; walakini kwa kadiri iyo hiyo huenda nyuma. Kuna aendaye polepole na kuhitaji msaa-da, na kukosa nguvu, naye yu mas-kini kabisa; walakini macho ya Bwana yamemtazama kwa hisani, akampand-isha kutoka unyonge wake, akamwi-nua kichwa chake na kumkweza nao wengi wakastaajabu kwa kumwona. Mema na mabaya, uzima na mauti, umaskini na utajiri, hayo yote yatoka Bwana. Ukarimmu wa Bwana hukaa pamoja na mwenye haki, na hisani yake itamfanikisha daima. Kuna aji-tajirishaye kwa werevu na kujinyima, na hii ndiyo thawabu yake; asemapo, “nimeona raha na sasa ntakula ma-pato yangu”, yeye hajui baada ya siku ngapi atawapisha wengine na kufa.” (Ybs 11:10-19). Pia waweza kusoma (Zab 49:17-19, 127:1-2; Mit 11:24; Isa 47:5; Ayu 27:16-23; Mhu 2:21-23; Lk 12:16-21).

Mungu ametuchagulia kazi fulani au hali fulani ya maisha akijua kwamba hali hiyo au kazi hiyo ndiyo inatufaa sisi kutufikisha kwake. Kwa sababu hiyo kila mtu anapaswa kuipokea hali aliyonayo na zaidi sana kuomba

neema zake Mungu ili kati hali yoyote ile ya maisha tutakayo kumbana nayo tuone wema na upendo wa Mungu. Kama Mungu amekupatia talanta moja, usiifukie tafadhali. Mungu ame-kuumba na anakujua vizuri kabisa ku-liko unavyojijua ndio maana akakupa kile ambacho ni saizi yako na amba-cho kwa kweli ukikitumia vizuri kita-kufikisha mbinguni. Tambua kwamba kama Mungu amekupatia mbegu ya mtama, siku ya mavuno hawezi ku-kudai mazao ya mzabibu! Atakudai kile alichokupa uzalishe. Au tuseme kwamba umepewa mzigo wenye kiasi cha uzito wa kilo kumi ukapewa na bajaji ya kubebea huo mzigo. Sasa cha ajabu kwa tama tu ya mali unaenda kuongeza mizigo mingine yenye uzito wa tani 1000, wakati huo huo chombo chako cha usafiri ni bajaji, hivi utabe-baje? Matokeo yake mzigo uliopewa hautaubeba na ile uliyoiongeza nayo haitabebeka. Hasara tupu! Ninacho-taka kusema ni kwamba pale tulipo ndipo tumtumikie Mungu, yaani tum-tumikie Mungu katika hali zozote zile tunazokumbana nazo. Tusisubiri ku-fikia hali Fulani ya maisha ndipo tuan-ze utumishi. Kama Mungu ameamua umtumikie katika hali ya umaskini, basi vumilia tu atakuonesha njia ya kumfikia yeye kupitia huo huo umas-kini ulio nao.

Mafanikio ya maisha wakati mwingine hutuweka mbali na Mungu. Tazama

Page 62: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 62

mfano wa mwana mpotevu (Lk 15:11-32), mwana huyu anapopewa urithi na babaye, anajiona kuwa mkamilifu, hahitaji kukaa karibu na babaye, ana-jiona kuwa anaweza kujitegemea, hamhitaji baba tena ndio maana ana-safiri nchi ya mbali akaishi mwenyewe huko (Lk 15:13). Alipoona amemaliza alivyo kuwa navyo ndipo anakumbuka tena kurudi kwa babaye (Lk 15:18). Sasa ndugu msomaji nadhani uanwe-za kuona jinsi mafanikio yanavyoweza kumpa mtu kiburi cha kujiona anawe-za kufanya chochote bila kumtege-mea mwingine. Ndivyo tunavyokuwa mbele ya Mungu, yeye daima ni mka-rimu, anatoa bila kupungukiwa, tu-napomwomba mafanikio mathalani utajiri, anapotupatia tunasafiri nchi ya mbali, tunamsahau kabisa, hata salamu (yaani sala) hatumtumii. Tu-napoishiwa ndipo tunamkumbuka na tunarudi tena kuomba anatupa-tia. Fundisho jingine hapa ni kwamba tukikaa katika Mungano na Mungu hatutapungukiwa daima.

Mungu anahusika zaidi na sisi, na sio mafanikio tuliyonayo maishani. Ma-fanikio tuliyonayo yanapaswa kutufaa sisi tu kutupatia wokovu. Kama ma-fanikio au utajiri ulionao hakusaidii kumuona Mungu, basi hiyo ni faida yenye hasara. Una faida ndiyo kwa maana ya mafanikio/utajiri wa ki-dunia lakini una hasara kwa sababu mafanikio yako au utajiri haukufikishi

kwa Mungu, utajiri wako unakutenga na Mungu. Ndiyo maana tukasema fai-da ya namna hii ni hasara. Faida yenye hasara kimsingi ni hasara taslimu. Kuna wimbo unaitwa “Bila Mungu ni bure” tutauona mwishoni mwa makala hii. Yesu daima katika neno lake haachi ku-tukumbusha, “Tafuteni kwanza ufalme wa Mungu, mengine yote mtayapata kwa ziada” (Lk 12:31; Mt 6:33). Na mahali pengine anatuambia, “Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia na kuu-rithi uzima wa milele.” (Mt 19:29; Lk 18:29-30; Mk 10:29-30).

Jambo la mwisho la kuzingatia ni kwamba wakati wa kufa kwetu, ma-fanikio ya kidunia au vyeo vya mtu pamoja na elimu yake haitahesabiwa mbele ya Mungu, utaalamu wa kuon-geea lugha mbalimbali za dunia hii au kuwa na vyeti vya elimu ya juu, vyote hivyo na ufahari wowote ule wa ki-dunia hautafaa kitu iwapo vyote hivyo havitatuweka karibu na Mungu (Soma 1 Kor 14:1-40). Jamani utajiri kwa we-nyewe sio mbaya ila itategemea unau-tumiaje. Kama Mungu anakujalia ma-fanikio/utajiri maishani ni jambo zuri, mshukuru sana yeye na kasha tumia utajiri huo kwa sifa na utukufu wake. Saidia wasio jiweza, tumia utajiri huo ukusaidie kufikisha injili kule ambako kutokana na umaskini ilikuwa vigumu

Page 63: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 63

kuifikisha. Huo ndio uinjilishaji mpya. Tukifanya hivyo, utumishi wetu utaku-wa na mafanikio duniani na mbinguni. Tutaweza kumjua Mungu, kumpen-da, kumtumikia na mwisho tutafika kwake Mbinguni. Hilo ndilo kusudio hasa la Mungu kutuumba sisi. Ndiyo maana alimtuma mwanae wa pekee ili kila amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele (Yn 3:16). Uzima wa milele hatuwezi kuupata kama hatufanyi juhudi ya kurudi kwake.

Basi tumalizie tafakari yetu hii kwa kuimba wimbo ufuatao ambao um-etungwa na Mrema S. F. M. Juni 2006. Wimbo unaitwa BILA MUNGU NI BURE.

1.Nilihangaika huku na huku mimi nikatafuta furaha; [nikifikiria kwamba furaha ipo kwenye mali, nikifikiria kwamba furaha ipo kwenye utajiri]2

KIITIKIO:[Lakini nimegundua (tena) nimejua ya kwamba, Mali, utajiri bila Mungu ni bure.]2

2. Nilihangaika huku na huku mimi nikatafuta amani; [nikifikiria kwamba amani ipo kwenye mali, nikifikiria kwamba amani ipo kwenye utajiri]2

3. Nilihangaika huku na huku mimi nikatafuta faraja; [nikifikiria kwam-ba faraja ipo kwenye mali nikifikiria kwamba faraja ipo kwenye utajiri]2

4. Nilihangaika huku na huku mimi nikatafuta upendo; [nikifikiria kwam-ba upendo upo kwenye mali, nikifikiria kwamba upendo upo kwenye utajiri]2

5. Nilihangaika huku na huku mimi nikatafuta fadhili; [nikifikiria kwam-ba fadhili ipo kwenye malinikifikiria kwamba fadhili ipo kwenye utajiri]2

{Nota za wimbo huu, Rejea: Mku-sanyo-Nyimbo Seminari Kipalapala M-NSK Namba 9 Uk. 80}

Na Frt. Gabriel MasakaMwaka wa pili Teolojia

Page 64: UMOJA NA MAPENDO - The Catholic Diocese of Singidasingidacatholicdiocese.co.tz/documents/Umoja na Mapendo Gazeti.pdf · angazi na kunyesha siku anayotaka ni dalili nyingine zilizo

Umoja na Mapendo Gazeti 64