Upload
others
View
12
Download
1
Embed Size (px)
Citation preview
The University of Dodoma
University of Dodoma Institutional Repository http://repository.udom.ac.tz
Humanities Master Dissertations
2014
Usawiri wa mwanamke katika tamthiliya
teule za Penina Muhando
George, Grace
Chuo Kikuu cha Dodoma
George, G. (2014). Usawiri wa mwanamke katika tamthiliya teule za Penina Muhando (Tasnifu).
Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.
http://hdl.handle.net/20.500.12661/1990
Downloaded from UDOM Institutional Repository at The University of Dodoma, an open access institutional repository.
USAWIRI WA MWANAMKE KATIKA TAMTHILIYA TEULE ZA
PENINA MUHANDO
Na
Grace George
Tasnifu Iliyowasilishwa kwa Ajili ya Kukamilisha Masharti ya Shahada ya Uzamili
ya Sayansi ya Jamii katika Fasihi ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dodoma
Chuo Kikuu cha Dodoma
Oktoba, 2014
i
ITHIBATI
Aliyetia sahihi hapa chini anathibitisha kuwa amesoma na hapa anapendekeza kwa Chuo
Kikuu cha Dodoma, kukubali kupokea tasnifu hii: Usawiri wa Mwanamke katika
Tamthiliya Teule za Penina Muhando katika kukamilisha matakwa ya shahada ya uzamili
katika fasihi (MA Kiswahili) ya Chuo Kikuu cha Dodoma.
……………………………………………………..
Prof. Frowin Paul Nyoni
(MSIMAMIZI)
Tarehe……………………………………
ii
IKIRARI NA HAKIMILIKI
Mimi, Grace Martin George, ninathibitisha kwamba tasnifu hii ni kazi yangu mwenyewe
halisi na haijawasilishwa wala haitawasilishwa katika Chuo Kikuu kingine chohote kwa ajili
ya kutunukiwa Shahada nyingine yoyote.
Sahihi………………………………………..
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuzalisha, kunakili, wala kusambaza sehemu
yoyote ya tasnifu hii kwa namna yoyote bila kibali cha maandishi kutoka kwa
Mwandishi au Chuo Kikuu cha Dodoma.
iii
SHUKURANI
Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa uhai, uzima na afya njema
hata nikaweza kufanikisha kazi hii, bila matatizo yoyote yale ya kiafya. Pia aliyenipa
akili na ufahamu wa kufanikisha kazi hii na kufikia hapa nilipofikia.
Pili, namshukuru msimamizi wangu Profesa Frowin Paul Nyoni ambaye ni Mkuu
wa Skuli ya Sanaa na Lugha katika Chuo Kikuu cha Dodoma kwani yeye ndiye
aliyekuwa mhimili mkuu katika kufanikisha kazi hii, amekuwa nami bega kwa bega
ili kuhakikisha kazi hii inafikia kiwango hiki. Licha ya shughuli nyingi lakini
alijitolea muda wake mwingi katika kunisahihisha na kunikosoa pale nilipokwama.
Nauthamini sana mchango wake, Mungu ambariki.
Tatu naishukuru sana familia yangu akiwemo mama yangu mzazi Bi Maria na baba
yangu kwa kukubali kunipeleka shule bila kujali umri na uwezo wako kifedha.
Mungu awaongezee siku za kuishi duniani. Pia nawashukuru kaka zangu na dada
zangu wote ambao hawakusita kunishauri na hasa kunisikiliza na kunitimizia
mahitaji yangu ya shule. Mungu awabariki sana.
Nne nawashukuru sana Profesa Penina Mhando, Profesa Imani Sanga, Daktari
Vicensia Shule, Daktari Mona Mwakalinga na Mwalimu Mtiro wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam kwa kunipa mchango na maarifa pamoja na kunihimiza kukamilisha
tasnifu hii maana haikuwa kazi rahisi. Nauthamini sana mchango wao na
ninawaombea heri na fanaka katika siku za maisha yao yote.
iv
Mtu mwingine muhimu sana ni Daktari Elias Manandi Songoyi. Shukrani zangu za
dhati zimfikie kwani aliweza kunielekeza namna ya kutafuta mada ya kufanyia
utafiti. Akiwa darasani alisisitiza kutofautisha mambo yanayohusu jamii, yaani
sosholojia na yale ya fasihi, akahimiza kuwa tusichanganye vitu hivyo viwili. Hii
ilinisaidia kupata mada ambayo ndiyo iliyofanyiwa utafiti huu.
Zaidi ya hao nitumie nafasi hii kumshukuru Daktari Rafiki Sebonde. Huyu ni
mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Wakati wa mafunzo ya darasani
alinifundisha namna ya kuandika utafiti kwa kunipa mwongozo wa kuchanganua
mambo muhimu yanayotakiwa kuwemo katika utafiti kwa kufuata mpangilio
unaokubalika, pia jinsi mtafiti anavyotakiwa kuwa wakati wa kukusanya data hasa za
uwandani. Daktari alinifanya nijiamini na hii ilinisaidia sana katika kufanikisha
utafiti wangu. Mungu ambariki sana.
Pia, ninamshukuru sana Prof. V. Lakshmanan kwa kunifundisha kuhusu nadharia za
fasihi. Katika utafiti huu sikupata mahangaiko yoyote kwani tayari nilishamakinika
katika uchaguzi na upembuzi wa nadharia ambazo zimeniongoza kufanya utafiti huu.
Siwezi kuwasahau wanafunzi wenzangu wa Shahada ya Uzamili wa mwaka (2014)
kwa ushirikiano wao katika majadiliano mbalimbali ya kitaaluma. Fidelis
Kyarwenda, Steven Jeremia, Ally Azizi kwa kutaja baadhi tu.
Shukrani zangu za pekee ni kwa wahadhiri wote walionifundisha katika Chuo Kikuu
cha Dodoma, Shahada ya uzamili, hata kunifanya kuwa mahiri katika lugha yangu ya
Kiswahili niipendayo sana. Mungu awabariki wote kwa pamoja.
v
Nichukue nafasi hii kumshukuru mume wangu mpenzi kwa dhati kabisa, Bwana
Colman Temba kwa kunitia moyo na kunifadhili kwa hali na mali wakati wote wa
masomo yangu tangu Shahada ya Awali na sasa Shahada ya Uzamili. Na hiki ni
kithibitisho tosha kuwa tasnifu hii si mali yangu binafsi bali ni yetu sote na Mungu
ambariki sana.
Pia, ninawashukuru sana watoto wangu Gift Colman na Ian Colman kwa
kunivumilia wakati wote wa masomo kwani muda mwingi niliutumia katika kazi
zangu na kushindwa kutekeleza kikamilifu jukumu la kuwaangalia wao. Pia watoto
hawa walikuwa msaada mkubwa kwangu hasa katika kuchapa kazi zangu
mbalimbali za kimasomo katika ngamizi.
vi
TABARUKU
Kazi hii ninaitabaruku kwa mama yangu mpenzi na baba yangu Bibi na Bwana
Msacky na ndugu zangu wote, Lucy, Devotha, Agatha, Simon, Veronica, Emanuel,
Flora na Joachim, kwani walijitoa bila kuchoka ili nisome kadri nitakavyo. Pia kwa
kunipa muda mzuri wa kujisomea, kunipa ushauri pale nilipochoka, kuniamini na
kuniombea hata nilipokuwa mbali na nyumbani. Asanteni na Mungu awabariki na
kuwapa afya na maisha marefu.
vii
IKISIRI
Utafiti huu umejadili kuhusu Usawiri wa Mwanamke katika Tamthiliya Teule za
Penina Mhando. Tatizo lililojenga utafiti huu ni kutokana na hali ya kila siku ya
waandishi wa tamthiliya za Kiswahili wakiwemo wanaume, kumkweza mwanaume
kinafasi na kimajukumu na kumshusha mwanamke, hivyo utafiti huu ulijikita
kuchunguza nafasi ya mwanamke katika tamthilia teule za Penina Muhando.
Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani kwa kuchunguza kazi mbalimbali ili kupata
ruwaza ya jumla kuhusu nafasi ya mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijinsia,
pia vitabu teule ambavyo ni Hatia (1972) na Nguzo Mama (1982) vimesomwa na
kuchunguzwa kwa makini na kuona jinsi mwanamke alivyochorwa. Mahojiano
yalifanyika ili kupata mawazo mbalimbali kuhusu mada ya utafiti. Pia umeongozwa
na nadharia ya Ufeministi. Hivyo utafiti huu umebaini kuwa kuna tofauti kubwa za
kimajukumu kati ya mwanaume na mwanamke. Kwa upande mmoja mwanamke
amechorwa kwa mtazamo hasi na chanya yaani ameonekana ni kiumbe duni,
mnyonge, na hivyo kuendelea kumdharau, kumkejeli na kumdhihaki. Kwa upande
mwingine mwanamke amechorwa kama mshauri, mlezi, mbunifu, mvumilivu na mtu
mwenye huruma na ushirikiano katika jamii. Pia utafiti huu umebaini kuwa zipo
athari mbalimbali zinazosababishwa na uchorwaji wa mwanamke katika tamthilia.
Athari mojawapo ni kuigwa kwa matendo machafu ambayo yanasababisha
kudharaulika na kuendelea kukandamizwa kwa wanawake. Hivyo basi kutokana na
matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa katika jamii nafasi ya
mwanamke na mgawawanyo wa majukumu huwa tofauti na mwanaume kwa sababu
ya mila na tamaduni mbovu ambazo humchukulia mwanamke kama kiumbe duni
wakati wote ingawa uhalisia wa sasa hauko hivyo.
viii
YALIYOMO
ITHIBATI ....................................................................................................................................... i
IKIRARI NA HAKIMILIKI ................................................................................................ ii
SHUKURANI ............................................................................................................................... iii
TABARUKU ................................................................................................................................ vi
IKISIRI.. ....................................................................................................................................... vii
YALIYOMO .............................................................................................................................. viii
ISTILAHI ZILIZOTUMIKA KATIKA UTAFITI HUU .......................................... xi
ORODHA YA VIFUPISHO VILIVYOTUMIKA ....................................................... xii
SURA YA KWANZA: UTANGULIZI WA UTAFITI ................................................. 1
1.1 Usuli wa Tatizo la Utafiti ..................................................................................................... 3
1.2 Tamko la Tatizo la Utafiti .................................................................................................... 7
1.3 Malengo ya Utafiti ................................................................................................................. 9
1.3.1 Lengo Kuu ............................................................................................................................ 9
1.3.2 Malengo Mahsusi ................................................................................................................ 9
1.4 Maswali ya Utafiti ............................................................................................................. 10
1.5 Umuhimu wa Utafiti ............................................................................................................ 10
1.6 Nadharia ya Utafiti .............................................................................................................. 11
1.6.1 Nadharia ya Kifeministi .................................................................................................. 11
1.7 Mipaka ya Utafiti .................................................................................................................. 19
1.8 Hitimisho................................................................................................................................. 19
SURA YA PILI: MAPITIO YA MACHAPISHO MBALIMBALI KUHUSU
MWANAMKE ............................................................................................................................ 20
2.0 Utangulizi ............................................................................................................................... 20
2.1 Mwanamke katika Fasihi ya Kiswahili .......................................................................... 20
2.1.1 Mwanamke Wakati wa Umwinyi/ Ukoloni............................................................... 25
2.1.2 Mwanamke Baada ya Uhuru ......................................................................................... 26
2.2 Mapitio ya Machapisho Mbalimbali kuhusu Mwanamke ....................................... 28
2.3 Hitimisho................................................................................................................................. 35
SURA YA TATU : MBINU ZA UTAFITI ...................................................................... 36
3.0 Utangulizi .............................................................................................................................. 36
3.1 Eneo la Utafiti........................................................................................................................ 36
3.2 Mbinu za Ukusanyaji wa Data .......................................................................................... 36
ix
3.2.1 Uchambuzi wa Matini ..................................................................................................... 37
3.2. 2 Mahojiano / Usaili ........................................................................................................... 37
3.3 Usampulishaji na Njia za Usampulishaji ....................................................................... 38
3.4 Vyanzo vya Data................................................................................................................... 39
3.4.1 Vyanzo vya Data za Msingi ........................................................................................... 39
3.4.2 Vyanzo vya Data Fuatizi................................................................................................. 39
3.5 Vifaa katika Ukusanyaji wa Data ................................................................................... 40
3.5.1 Kalamu na Shajara ............................................................................................................ 40
3.5.2 Dodoso ................................................................................................................................. 40
3.5.3 Ngamizi (Kompyuta) ....................................................................................................... 41
3.5.4 Kinyonyi .............................................................................................................................. 41
3.5.5 Tepurikoda .......................................................................................................................... 41
3.5.6 Kamera ................................................................................................................................. 42
3.6 Mbinu ya Uchanganuzi wa Data ..................................................................................... 42
3.7 Hitimisho................................................................................................................................. 42
SURA YA NNE: UWASILISHAJI, UCHAMBUZI NA MJADALA WA
MATOKEO YA UTAFITI .................................................................................................... 43
4.0 Utangulizi .............................................................................................................................. 43
4.1 Historia ya Penina Muhando ............................................................................................. 44
4.2 Hatia (1972) ........................................................................................................................... 46
4.2.1 Utangulizi ............................................................................................................................ 46
4.2.2 Uwasilishaji na Uchambuzi wa Data .......................................................................... 49
4.2.2.1 Mwandishi Alivyomsawiri Mwanamke katika Tamthilia ya Hatia (1972)
kwa upande Chanya katika Nafasi na Kimajukumu .......................................................... 49
4.2.2.2 Mwandishi Alivyomchora Mwanamke katika Tamthilia ya Hatia (1972)
kwa upande Hasi katika Nafasi na Kimajukumu ............................................................... 54
4.2.3 Mjadala na Dhamira Zilizoibuka Kutokana na Uchorwaji wa Mwanamke
katika Tamthiliya ya Hatia (1972) ......................................................................................... 60
4.3 Nguzo Mama (1982) ............................................................................................................ 70
4.3.1Utangulizi ............................................................................................................................. 70
4.3.2Data na uchambuzi wake ................................................................................................. 73
4.3.3Mwanamke Alivyochorwa katika Tamthiliya ya Nguzo Mama (1982) kwa
Upande Chanya ............................................................................................................................ 73
x
4.3.4 Mwanamke Alivyochorwa katika Tamthiliya ya Nguzo Mama (1982) kwa
Upande Hasi ................................................................................................................................ 81
4.3.5 Mjadala wa Dhamira Zilizojitokeza Kutokana na Uchorwaji wa Mwanamke
katika Tamthiliya ya Nguzo Mama (1982) ........................................................................... 87
4.4 Athari za Uchorwaji wa Wahusika Wanawake katika Kazi za Fasihi ................. 92
4.6 Hitimisho................................................................................................................................. 96
SURA YA TANO: MUHTASARI WA MATOKEO YA UTAFITI ,
MAPENDEKEZO, NA HITIMISHO ............................................................................... 98
5 .0 Utangulizi .............................................................................................................................. 98
5.1 Muhtasari wa Mpangilio wa Tasnifu .............................................................................. 98
5.2 Muhtasari wa Matokeo ya Utafiti ...................................................................................... 100
5.4 Mapendekezo ....................................................................................................................... 102
5.4.1Mapendekezo kwa Watafiti........................................................................................... 102
5.4.2Mapendekezo kwa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ................................... 102
5.4.4Mapendekezo kwa Jamii ................................................................................................ 103
5.4.5 Mapendekezo kwa Waaandishi wa Tamthiliya ...................................................... 103
5.5 Hitimisho............................................................................................................................... 104
MAREJELEO ........................................................................................................................... 105
VIAMBATANISHO ............................................................................................................... 109
xi
ISTILAHI ZILIZOTUMIKA KATIKA UTAFITI HUU
Athari: Ni matokeo yanayotarajiwa, mawazo au hisia anazopata mtangazaji
au msikilizaji
Dhamira: Ni kiini cha jambo au habari iliyosimuliwa au kuandikwa, hasa katika
fasihi.
Jinsia: Ni mahusiano ya kijamii kati ya mwanaume na mwanamke. Pia
jinsia ni ile hali ya kuwa na maumbile ya kike au ya kiume. Katuli
(2002) anaelezea kwamba jinsia ni tabia za kijamii, kiutamaduni na
kisaikolojia ambazo zinamtambulisha mtu kama mwanaume au
mwanamke.
Taswira: Picha ya mwanamke inayojitokeza baada ya matumizi mbalimbali ya
semi, ishara, lugha katika kazi za kifasihi.
Tamthiliya: Ni mchezo wa kuigiza au kazi ya kisanaa iliyoandikwa kwa lengo la
kuigizwa jukwaani ili kufikisha ujumbe Fulani kwa hadhira.
Usawiri wa mwanamke: Ni wahusika wanaotumika kueleza jambo katika kazi za
kifasihi, wasifu wao, tabia zao, lugha zao, itikadi zao, vionjo vyao,
na hata mitazamo yao.
Ni hali ya kuonyesha matendo na mienendo ya wahusika katika kazi
ya kifasihi.
xii
ORODHA YA VIFUPISHO VILIVYOTUMIKA
Dkt: Daktari wa Falsafa
EAJA: Equal Access to Justice Act
FPA: Kitengo cha Sanaa za Maonyesho ( Fine Perfoming Art)
M.A: Masters of Arts (Shahada ya Uzamili katika Sanaa)
Prof: Profesa
TATAKI: Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
TGNP: Tanzania Gender Networking Program ( mtandao wa jinsia Tanzania)
TUKI: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
uk: Ukurasa
1
SURA YA KWANZA
UTANGULIZI WA UTAFITI
1.0 Utangulizi
Utafiti huu unahusu Usawiri wa Mwanamke katika Tamthiliya Teule za Penina
Muhando. Utafiti umechunguza kazi mbili za Penina Muhando ambazo ni Hatia
(1972) na Nguzo Mama (1982), na kuona namna zinavyomsawiri mwanamke na
kuweka wazi mgawanyo wa majukumu.
Sura hii imepitia vipengele mbalimbali ambavyo vinatoa maelezo ya utangulizi wa
mwelekeo wa utafiti huu. Vipengele hivyo ni pamoja na usuli wa tatizo, tamko la
tatizo la utafiti, malengo ya utafiti. Vipengele vingine katika sura hii ni maswali na
umuhimu wa utafiti huu, pamoja na nadharia iliyotumika.
Tamthiliya ni moja kati ya tanzu kubwa muhimu za fasihi andishi. Tanzu nyingine za
fasihi andishi ni ushairi na riwaya. Mtunzi wa tamthiliya husawiri mawazo kwa
maongezi ya wahusika na kwa kujenga migongano na mijadala baina ya wahusika
hao. Tamthiliya hutungwa kwa ajili ya kuigizwa, hivyo mawazo huwekwa katika
matendo na mazungumzo.
Tamthiliya ina historia ndefu sana. Ilianza katika mataifa ya nje, hususani huko
Ulaya ambayo ndiyo imeathiri sana tamthiliya ya Kiswahili. Kihistoria ilichipuka
kutokana na mambo matatu ambayo ni miviga na viviga vya kijamii na kidini
pamoja na tendi na misahafu ya kidini, umathilishaji wa maisha ya kawaida kwa ajili
ya burudani, maonyo au michezo na sanaa za maonyesho za kijadi kama vile ngoma
na dansa.
2
Tamthiliya kama utanzu wa fasihi andishi katika lugha ya Kiswahili ililetwa Afrika
Mashariki na wakoloni (Bertoncini, 1989). Mgeni kutoka Uingereza aliyejihusisha
na uigizaji hapo mwanzo mwaka (1957) alikuwa Graham Hyslop aliyetunga michezo
ya kuigiza kama Akilimali (1945), Afadhali Mchawi (1957) na Mgeni Karibu (1957).
Mmojawapo wa wanafunzi wake ni Henry Kuria aliyetunga tamthiliya ya
Nakupenda Lakini (1957). Baadaye waandishi wengine walifuata kama vile
Gerishon Ngugi aliyetunga tamthiliya ya Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi (1961).
Wafula (1999) anasema kuwa baadhi ya tamthiliya zilitungwa moja kwa moja
katika lugha ya Kiswahili ilhali nyingine zilitafsiriwa kutoka lugha ya Kiingereza na
lugha nyingine za kigeni. Kwa mfano, Morrison (1966) alitafsiri mchezo wa kuigiza
ulioitwa “Mchuuzi Muungwana”.
Waandishi wengi wa tamthiliya wamekuwa wakiandika maudhui ya kazi zao
kulingana na matukio yaliyotendeka na yanayotendeka katika jamii. Hivyo hutumia
mbinu mbalimbali za kisanii ili kufikisha ujmbe kwa jamii.
Miongoni mwa waandishi wa tamthiliya za Kiswahili ni Amandina Lihamba,
Ebrahim Hussein, Emanuel Mbogo, Balisidya Ndyianao na Penina Muhando ambao
wametumia mbinu hizo ili kuweka sawa maudhui yao katika jamii na kueleza
matatizo mbalimbali na uozo uliopo katika jamii. Maudhui katika tamthiliya nyingi
yanamsawiri mwanamke kama kiumbe duni hata katika majukumu ilionekana
kwamba kuna kazi ambazo hawezi kuzifanya kwamba ni za mwanaume tu.
Kutokana na kudunishwa huko ilisababisha mwanamke ajisikie vibaya na kujiona
kwamba kuna mambo ambayo hawezi kuyafanya katika jamii. Hii ndiyo sababu
3
mtafiti amekuwa na hamasa za kufanya utafiti kuhusu Usawiri wa mwanamke
katika tamthiliya Teule za Penina Muhando.
1.1 Usuli wa Tatizo la Utafiti
Mwanamke katika kazi mbalimbali za fasihi amechorwa kwa mtazamo tofautitofauti.
Katika riwaya za Kezilahabi Rosamistika (1971) tunaona kuwa mwandishi
anamtumia mhusika Rosa kama mhusika mkuu wa riwaya yake. Mwandishi
amemchora Rosa katika picha ya kusikitisha, kwani amechorwa katika hali ya
kunyanyaswa, kama Malaya, kama chombo cha starehe na biashara. Hivyohivyo
katika riwaya za Mohamed (1976) Nyota ya Rehema mwandishi pia kaonyesha jinsi
mhusika wake huyo ambaye ndiye mhusika mkuu katika riwaya hiyo jinsi
anavyonyanyaswa yeye na mama yake.
Pia uchorwaji wa mwanamke katika magazeti kipengele cha hadithi fupi kimekuwa
mstari wa mbele kumchora mwanamke katika mtazamo hasi. Haya aliyaona Nkya
(2004) alipofanya uchunguzi katika magazeti ya Mzalendo na Sunday News ya
nchini Tanzania. Aliona kuwa magazeti haya yalimchora mwanamke kama malaya,
chombo cha starehe, mdhaifu na chanzo cha dhambi katika jamii. Katika miaka ya
sabini, Besha (1976) alitafiti hadithi hizo zinazoandikwa kwenye magazeti mengine
na kupitia baadhi ya nyimbo zilizoimbwa katika vituo vyetu vya redio. Alihitimisha
kwa kutoa picha kwamba, mwanamke anachorwa kama mwovu, mshawishi,
anayewapotosha wanaume. Katika baadhi ya hadithi alipata dhana nyingine ya kuwa,
mwanaume alionekana kama mtu bora, anayetawala mkewe hasa katika ndoa.
4
Chaligha (2011) amefanya utafiti kuhusu jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika
katuni mnato. Katika utafiti wake naye ameonyesha jinsi mwanamke
anavyodhalilishwa kwa kuchorwa akiwa amevaa nusu uchi, mwanamke kama mtu
asiyekuwa na haki ya kupata elimu, mwanamke kama chombo cha starehe kwa
mwanaume. Hivyo basi yeye amegundua kuwa wasanii wengi wanaojihusisha na
sanaa ya katuni mnato ikiwa kama mojawapo ya kazi za kifasihi wanapochora katuni
mwanamke anachorwa kwa mtazamo hasi tu na mwanaume huchorwa kama mtu
mstaarabu, aliyeelimika na mwenye kuvaa mavazi mazuri ya heshima.
Senkoro (1982:84) anaeleza kuwa, historia ya kunyanyaswa na kugandamizwa kwa
mwanamke katika jamii ni ndefu. Inarudi nyuma hadi wakati jamii ilipogawanyika
katika matabaka mbalimbali. Hata hivyo ufuatiliaji huo wa kihistoria haujaweka
kando ukweli kuwa katika baadhi ya jamii kulikuwepo vipindi vya kihistoria
ambavyo wanawake walitawala kisiasa, kiuchumi na kimadaraka kwa jumla. Mara
nyingi katika jamii, mgawanyiko kati ya jinsia ya kiume uligeuka kuwa mgawanyiko
kati ya matabaka mara jamii ilipogawanyika kati ya wale waliomiliki nyenzo na njia
zote za uchumi, ambao walikuwa wanaume, na wale ambao hawakuwa na chochote
isipokuwa jasho lao na wengi wao wakiwa wanawake. Anaendelea kueleza kuwa
kuanzia wakati huo basi, mwanamke alilazimika kumtegemea mwanaume
aliyezitumia nguvu hizo kufanya lolote juu ya mwanamke.
Pia usawiri wa mwanamke katika kazi za fasihi, sanaa na katika jamii umeelezwa na
wataalamu mbalimbali wa fasihi kwa namna tofauti tofauti. Profesa Penina Muhando
kwa maelezo yake mwenyewe mbele ya mtafiti tarehe 11.11.2013, anaeleza kuwa,
kihistoria mwanamke amenyanyasika sana na alionekana kuwa hana sauti kwa
5
mwanaume, yeye ni wa kusikiliza kila kitu anachosema na anachotaka mwanaume.
Anaendelea kusema kuwa, wakati wao wanashughulikia suala la jinsia (gender)
mwanamke alikuwa hana sauti, hata wakati wa kuajiriwa mwanamke alikuwa
hapewi nyumba lakini mwanaume alipewa nyumba. Nanukuu maelezo yake, “hata
wakati tunaajiriwa sisi mwanamke alikuwa hapewi nyumba lakini kwa kazi hiyohiyo
na elimu hiyohiyo kwa mwanaume alikuwa akipewa nyumba”.
Muhando anaona kuwa, katika taasisi mbalimbali mwanamke hata akiwa ana elimu
kiasi gani au ana kiwango cha elimu sawa na mwanaume bado anadharaulika na
kuonekana kuwa hawezi. Anasema kuwa huo ndio unyanyasaji wenyewe. Muhando
anamalizia kwa kusema kuwa, mwanamke katika jamii athaminiwe na kuonekana
kuwa na yeye ni mtu anayeweza kuleta mabadiliko na sio wanaume tu. Pamoja na
mwanaume kuonekana kuwa yeye ndiye mleta maendeleo lakini bila mwanamke pia
bado hayo maendeleo hayajakamilika.
Fasihi ya Kiswahili tangu zamani imewasawiri wanawake kama watumwa. Katika
tenzi za awali mathalani Utendi wa Mwanakupona na hata Mashairi ya Muyaka, sura
tunayoipata ni ile inayomfanya mwanamke chombo cha kutumiwa na mwanaume ili
kijifurahisha. Taswira hii iliathiriwa kwa kiasi kikubwa na mfumo wa kimwinyi.
Wosia ulio katika Utendi wa Mwanakupona ni wa kuwadunisha na kuwahubiria
wanawake wakubali kuwatumikia na kuwaabudu wanaume. (Ndungo 19850).
Balisidya (1982:8) anaeleza kuwa, Mwanamke katika jamii ya watanzania
anatazamwa kama chombo cha starehe kwa wanaume. Anaendelae kueleza kuwa
6
mtazamo huu haumpi heshima mwanamke kama mzazi bali chombo muhimu kwa
mwanaume cha kujitosheleza haja zake za kimwili.
Baada ya nchi za Afrika Mashariki kujipatia uhuru wake waandishi wa fasihi ya
Kiswahili waliibua, kutumia na kufuata mtindo wao wa uandishi wa kazi zao
uliotofautiana na ule uliozoeleka katika kuwelezea wanawake. Pia chambuzi,
tahakiki na tafiti mbalimbali zilizofanywa na baadhi ya wataalam zimezidi
kumkandamiza mwanamke kwa kumchora kama kiumbe dhaifu. Kwa kupitia
Momanyi (2000) tumeona kuwa uchorwaji wa mwanamke katika kazi za Shaaban
Robert, amegundua kuwa mwanamke amechorwa katika mtazamo hasi yaani kiumbe
tegemezi kwa mwanaume.
Utafiti huu umelenga kuchambua “Usawiri wa Mwanamke katika Tamthiliya Teule
za Penina Muhando”. Mwandishi huyu amechaguliwa kwa kigezo cha umahiri wake
katika kumchora mwanamke kwa namna tofautitofauti kulingana na jinsi au matendo
wanayofanyiwa katika jamii zetu. Pia mwandishi huyu ni mwanafasihi ambaye
anashughulikia maswala ya harakati za ukombozi wa mwanamke ulimwenguni. Pia
tamthilia hizo teule zimechaguliwa kwa sababu ni kati ya kazi zake nyingi ambazo
maudhui yake yanaonyesha mambo maovu na mema anayofanyiwa mwanamke
katika jamii zetu. Pia tamthiliya hizo ni kazi yake ya kwanza yaani Hatia (1972)
ambayo aliandika kabla ya kujiingiza katika maswala ya jinsia na Nguzo Mama
(1982) ni kazi yake ya zama hizi za harakati za ukombozi wa mwanamke duniani.
Tamthiliya zote hizo zimezungumzia maswala ya mwanamke na wahusika wake
wakuu ni wanawake.
7
Katika kipindi cha 1971-1984 jamii ilikuwa katika mhemko wa utekelezaji wa
Azimio la Arusha hivyo basi ni kwa kupitia kipindi hiki waandishi wengi waliweza
kutoa dukuduku zao kuhusu mwanamke. Hivyo, ni muktadha wa kipindi pia ndio
uliotusaidia au uliotusababisha tukachagua tamthilia hizo. Hata hivyo utafiti huu
ulitegemea sana kumwona mwandishi huyu wa kike alivyomchora mwanamke
katika kipindi cha nyuma na alivyomchora mwanamke katika kipindi hiki.
Kwa upande mwingine katika kazi nyingi za fasihi ya Kiswahili mhusika wa kike
anaonekana kuwa kivutio kwa waandishi wengi wa riwaya, tamthilia, mashairi na
hata kwa wasanii wanaojihusisha na uchoraji wa katuni na magazeti kwani
humtumia mwanamke kama chombo cha starehe. Haya yameonekana wazi kwa
kupitia utafiti huu na tafiti mbalimbali kuwa picha ya mwanamke katika fasihi ni
hasi wakati inapolinganishwa na mwanaume. Hii sio sahihi, kwani pamoja na
mwanamke kuwa na wajibu wa kuzaa, kunyonyesha nakadhalika pia anao wajibu wa
kufanya kazi nyingine ambazo zinaingiza kipato katika familia, jamii na taifa kwa
ujumla.
1.2 Tamko la Tatizo la Utafiti
Tamthiliya ni fasihi pana na inayoitazama jamii na kuielezea kwa namna ya utofauti.
Hutumia lugha ya kuigiza ikiambatana na matendo ili kufikisha ujumbe kwa jamii.
Kumekuwa na harakati nyingi zinazoendelea kuhusu kumkomboa mwanamke, siyo
Tanzania pekee bali ulimwenguni kote. Tangu Umoja wa Mataifa utangaze kwamba,
mwaka 1975 ni mwaka wa wanawake duniani, juhudi mbalimbali zimekuwa
zikifanywa kuwakomboa wanawake kutokana na ukandamizwaji na udhalilishwaji.
Harakati zinazofanywa ni pamoja na kuwepo kwa mikutano ya hadhara, mikutano ya
8
kimataifa kama vile Beijing, kampeni za kitaifa, kuwepo kwa siku ya wanawake
duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe nne Machi.
Watafiti pamoja na wahakiki wachache wamezungumzia kidogo suala la usawiri wa
mwanamke katika tamthiliya. Mfano Wegesa (1994) alitafiti kuhusu “mwanamke
katika tamthiliya za Ebrahimu Hussein” ambazo ni Alikiona, Wakati Ukuta,
Kinjekitile, Mashetani, Arusi na Kwenye Ukingo wa Thim. Wegesa aligundua kuwa,
tamthiliya zote kwa pamoja zimemsawiri mwanamke kama mnyonge, muasherati,
chipukizi wa kisiasa, mdhaifu na tegemezi kwa mwanaume.
Mtiro (2005) alitafiti kuhusu “Taswira ya mwanamke katika tamthilyia mbili za
Kitanzania ambazo ni: Alikiona na Machozi ya Mwanamke, katika utafiti wake
akagundua kuwa, katika tamthiliya ya machozi ya mwanamke, mwanamke
amesawiriwa kama mzazi na mlezi katika jamii na familia kwa jumla, asiye na haki
ya kuwatembelea wazazi wake, kiumbe kinachodhulumiwa na kugandamizwa,
mwanamke kama mtu asiyepinga suala la wanawake kutopigania haki zao. Wakati
katika tamthiliya ya Alikiona, mwanamke amesawiriwa kama mzinzi na asiye
mwaminifu katika ndoa yake, mwongo, kiumbe duni na mwenye tamaa.
Mwakalinga (2003) amezungumzia nafasi ya mwanamke katika filamu za
Kitanzania. Yeye anaeleza kuwa, mwanamke lazima ajiamini kwa kile
anachokifanya na kuonyesha juhudi zake katika kazi mbalimbali za kisanaa, kijamii
na kiuchumi ili aweze kupata thamani katika jamii kama ilivyo kwa wanaume.
Shule (2004) amefanya utafiti juu ya mchango wa filamu katika harakati za
kupunguza unyanyasaji wa kijinsia na hatari zinazoweza kusababisha UKIMWI.
9
Katika utafiti wake ameonyesha jinsi filamu zinavyoweza kusaidia kuwaelimisha
vijana wa kiume katika kuzuia unyanyasaji wa kijinsia ambao ni mojawapo ya
mambo yanayoweza kusababisha kuenea kwa maambukizi ya UKIMWI.
Senkoro (2009) ameeleza kwa ufupi jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika
vipengele vichache tu kama vile kejeli na dhamira. Aidha, wataalamu hao
hawajamchambua mwanamke katika tamthiliya teule za Penina Muhando kama
mhusika mkuu katika tamthiliya hizo. Tatizo lililojenga utafiti huu ni kutokana na
hali ya kila siku waandishi wa kiume wa tamthiliya za Kiswahili kumkweza
mwanaume kinafasi na kimajukumu na kumshusha mwanamke. Aidha wataalam hao
hawajamchambua mhusika mwanamke jinsi alivyosawiriwa na mwandishi
mwanamke katika kazi za kifasihi. Hivyo utafiti huu unakusudia kuchunguza usawiri
wa mwanamke katika tamthiliya za Hatia na Nguzo Mama za Penina Muhando.
1.3 Malengo ya Utafiti
Malengo katika utafiti yako ya aina mbili yaani lengo kuu na malengo mahususi.
1.3.1 Lengo Kuu
Kuchunguza usawiri wa mwanamke katika tamthiliya teule za Penina Muhando.
1.3.2 Malengo Mahsusi
Malengo mahsusi katika utafiti ni haya yafuatayo;
i. Kubainisha nafasi ya mwanamke katika tamthiliya za
Hatia na Nguzo Mama kwa jumla.
10
ii. Kuchambua namna wahusika wa kike
walivyochorwa kwa mujibu wa mgawanyo wa
majukumu katika tamthiliya hizo.
iii. Kuchunguza athari zinazotokana na usawiri wa
mwanamke katika tamthiliya za Hatia na Nguzo
Mama.
1.4 Maswali ya Utafiti
i. Nini nafasi ya mwanamke katika tamthiliya za
Hatia na Nguzo Mama.?
ii. Je, wahusika wa kike wamechorwaje kwa mujibu
wa majukumu katika tamthiliya hizo?
iii. Ni athari gani zinazopatikana kutokana na usawiri
wa mwanamke katika tamthiliya za Hatia na Nguzo
Mama?
1.5 Umuhimu wa Utafiti
Kazi yoyote ile ya fasihi hubeba ujumbe ndani yake. Hata kama ujumbe huo
haujaelezwa kinagaubaga lakini bado hubaki kuwa ujumbe. Asiyeelewa akiuliza
haitwi mjinga bali hupatiwa jibu. Tamthiliya kama kazi ya fasihi kwa vyovyote vile
imesheheni ujumbe uliokusudiwa kufikishwa kwa jamii. Inatarajiwa kuwa kazi hii
itawasaidia watafiti wengine kutafiti zaidi juu ya tamthiliya na hasa katika vipengele
ambavyo havijaguswa kwa undani, kama vile migogoro, dhamira, falsafa za
wanatamthiliya, mtindo, muundo, mandhari na matumizi ya lugha. Kwa kufanya
hivyo, uwanja mpana utaachwa kwa watafiti wengine kutafiti suala hili kiundani na
kuandika ikiwezekana hata vitabu. Hili litasaidia kuwa na marejeo mengi. Utafiti
huu unategemewa kuleta matumaini mapya kwa waandishi hasa wanawake katika
11
tamthiliya. Waandishi hao wataandika zaidi na zaidi kwa kuwa watajiona wako sawa
na waandishi wengine wa kazi za kifasihi, na hivyo watafanya vizuri zaidi hasa
baada ya kugundua kwamba kazi zao ni za thamani kwa wanazuoni na watafiti.
Wasomaji nao wanatarajiwa kugeuzwa mtazamo wao wa awali kuhusu uchorwaji
wa mwanamke katika tamthiliya kwa kuwa wengi huzisoma na kuziacha tu bila
kufuatilia ujumbe uliomo ndani yake, bila kuchukua hatua za makusudi za
kubadilisha mwenendo ikiwa ni mbaya.
1.6 Nadharia ya Utafiti
Wamitila (2008) anaeleza kuwa, “nadharia ni maarifa ya kitaaluma ambayo msomaji
au mhakiki anapaswa kuyajua na kuyafahamu kabla ya kuianza kazi yake”. Pamoja
na hivyo nadharia pia ni maarifa ambayo inatupasa kuwa nayo kabla ya kujihusisha
na kazi yoyote ile ya uhakiki. Pia nadharia ni maarifa ambayo yanamwezesha
msomaji kupanua uelewa wake na kwa njia hiyo, kuboresha usomaji wake na
kuifanya kazi ya fasihi.
Sehemu hii inafafanua uteuzi wa nadharia inayoongoza utafiti huu katika ukusanyaji
na uchambuzi wa data. Uchanganuzi wa nadharia unatokana na jinsi nadharia
yenyewe inavyobainisha mahusiano baina ya mwanamke na mwanaume katika
jamii. Utafiti huu unaongozwa na nadharia ya Ufeministi kwa kuona kuwa inaweza
kujibu na kuongezea upungufu uliojitokeza katika tahakiki zilizotangulia.
1.6.1 Nadharia ya Kifeministi
Ufeministi ni nadharia na mtazamo wa dunia. Kama nadharia, Ufeministi ni mfumo
wa mawazo yanayofasili, na yanayoelezea mambo yanayohusiana na uhusiano wa
12
kijinsia na uwepo wa mwanamke. Felluger (1998) anaeleza kwamba nadharia ya
Ufeministi inatafuta kuondoa nadharia za utawala wa mwanaume ili kuweka bayana
dosari za asili, na upofu wa jinsia.
Mafeministi wanaendeleza mikabala mipya, kutoa fasili ya mwanamke na ukweli
kuhusu mwanamke.
Naye Tsikataa (1991) anafafanua zaidi kwamba, Ufeministi ni utambuzi wa ubaguzi
wa kimfumo dhidi ya wanawake katika uwanja wa jinsia na katika kujitoa kufanya
kazi kuyakabili mabadiliko yaliyopo katika jamii. Anazidi kueleza kwamba, baada
ya wanawake kuona kwamba wamewekwa katika daraja la mwisho kwenye ngazi
zote za maaamuzi, kama vile siasa, uchumi na katika ngazi ya jamii, ndipo
walipoamua kupambana ili waweze kujikomboa wenyewe.
Mwanzoni mapambano hayo yalipigwa vita, lakini kuanzia miaka ya 1800 mpaka
1900 madai yao mengi, kama vile haki ya kupiga kura, na kupata nafasi katika ngazi
ya uchumi na jamii yalipitishwa. Walionekana kwamba wana haki kubwa kushiriki
katika kuzalisha maarifa kama walivyo na haki ya kuwa sehemu ya maarifa hayo.
Nadharia ya Kifeministi ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1792 huko Ulaya. Kwa
mujibu wa Ma Humm na Walker (1992), historia ya nadharia ya ufeministi inaweza
kugawanywa katika vipindi vitatu. Kipindi cha kwanza kilikuwa kati ya karne ya 19
na mwanzoni mwa karne ya 20, kipindi cha pili kilitokea katika miaka ya 1960 na
1970. Kipindi cha tatu kilianzia miaka ya 1990 mpaka sasa. Wanazidi kueleza
13
kwamba nadharia ya Ufeministi ilianzia kwenye harakati za mafeministi za
kujikomboa.
Licha ya Humm na Walker kuelezea chimbuko au mwanzo wa kuibuka kwa
nadharia ya ufeministi lakini Mackinnon (1991) anafafanua zaidi na kueleza
kwamba, Ufeministi ni nadharia ya kwanza kuibuika kutokana na watu ambao
walivutiwa nayo. Yaani ni nadharia iliyoibuliwa na kundi la watu waliovutiwa na
mustakabali wake. Anazidi kueleza kwamba zipo sababu nne zilizofanya suala la
ukombozi wa mwanamke liwe la kisiasa. Kwanza kabisa ni wanawake kama kundi,
wanatawaliwa na wanaume kama kundi, na mwanamke mmoja anatawaliwa na
mwamaume mmoja. Pili, wanawake wamefanywa kuwa tegemezi katika jamii na sio
kwa sababu za asili ya mtu au za kibaolojia. Tatu mgawanyo wa majukumu, ambao
unahusisha jinsia unamuweka mwanamke katika kiwango cha juu cha kazi zisizo na
hadhi. Hali ya kutokuthamini kazi azifanyazo mwanamke imetawala katika jamii
nyingi na jamii humwona mwanamke hata hisia zake binafsi ni za kiegemezi. Nne,
tangu matatizo ya mwanamke yalipojulikana kuwa sio ya mtu mmoja bali ya
wanawake wote, na hayawezi kutatuliwa na mtu binafsi, ndipo suala hili likawa la
kisiasa zaidi.
Hata hivyo Cox (1965) anaeleza kwa kuweka wazi jinsi nadhaharia ya Ufeministi
ilivyoibuka kwa kusema kwamba, nadharia ya Kifeministi ilianzishwa kama njia ya
kujadili matatizo ya wanawake ambao hudhaniwa kuwa na hadhi ya chini, katika
jamii nyingi duniani.
14
Katuli (2002) ni mtaalamu mwingine anayeelezea mgawanyiko wa mafeministi, na
kueleza kwamba mafeministi wamegawanyika katika makundi manne ambayo ni
mafeministi wa Kiradikali (wenye siasa kali), Mafeministi wa Kiliberali (wenye
kutaka mabadiliko), mafeministi wa Ki-Marx na mafeministi wa nchi za dunia ya
tatu. Ijapokuwa kila kundi lina msimamo na kanuni zake, lakini lengo la makundi
hayo bado ni moja tu la kumkomboa mwanamke.
Pamoja na maelezo hayo ya wataalamu hao hapo juu hata hivyo katika miaka ya
1900, wanawake wengi walianza kuandika vitabu akiwemo Mary Wollstencecraft,
aliyeandika Vindication of the Right of Women (1792) na A Room of One’s Owns,
kilichoandikwa na Virginia Woolf (1929). Mwingine ni Sarah Gremke aliyeandika
Anti Slavery Leader na makala yake ya “Letters on the Equality of Sexes and the
Condition of Woman” (1938). Gremke aliandika kuhusu asasi za dini zenye sheria
ngumu zinazomnyayasa na kumkandamiza mwanamke.
Naye Simone de Beauvoir katika kitabu chake cha Second Sex (1949) anashambulia
asasi kongwe ambazo zinaonekana kuwa mhimili mkubwa wa udhalilishaji wa
wanawake ambazo ni ndoa, dini, na utamaduni. Anazidi kueleza kuwa asasi ya ndoa
inampa mwanaume nafasi kubwa ya kupanga na kuamua juu ya familia na
kumwacha mwanamke kama chombo tu. Dini nayo anaieleza kuwa ni asasi ambayo
ina maagizo na amri ambazo ni ngumu na zinazomkandamiza mwanamke kwani
zinamtaka kunyenyekea.
Pia Bond (2000) anashadidia asasi ya utamaduni na kusema kwamba kipengele cha
utamaduni ni kipengele pekee kinachotengeneza mazingira ya kumkandamiza
15
mwanamke asifikie ngazi za juu za uongozi. Anazidi kueleza kwamba katika suala la
uongozi wanaume wengi hawaamini kwamba mwanamke ataweza kuongoza vizuri
kabisa na kufanya maamuzi sahihi na yanayostahili.
Sanjari na maelezo ya Bond na de Beauvoir kuhusu asasi zinazomkandamiza
mwanamke, York na wenzake (1991) katika moja ya kanuni zao wanafafanua
kwamba, watu wanaokandamizwa tu ndio wanaoweza kusema juu ya ukandamizwaji
wao, ni wao tu wanaoweza kuelezea tajiriba zao na kutoa mchanganuo ambao
hautapinga jitihada zao, na sio wakandamizaji. Ina maana kwamba mwanaume
hawezi kutetea haki za mwanamke isipokuwa kama na yeye anajua kwamba
mwanamke anaonewa na mifumo iliyopo katika jamii.
Wamitila (2002:157) anasema, utamaduni anaokulia mwanamke unachangia katika
kumdidimiza katika hali ya unyonge. Utamaduni huo unamfanya mwanamke
ajichukulie kuwa ni kiumbe duni. Baada ya kukubali hali hiyo mwanamke anaishia
kuwa chombo cha kutumikishwa na kuendeleza utamaduni huo hasi katika jamii.
Ndoa nia taasisi mojawapo ya kitamaduni inayoendeleza ukandamizaji wa
mwanamke. Asasi hiyo imejengwa kwenye imani kuwa mwanaume ana uwezo
mkubwa katika nyanja mbalimbali na kuishia kumwangalia mwanamke kama
chombo tu.
Katika kufafanua nadharia ya ufeministi Wamitila anasema kuwa tamaduni jamii
yenye mfumo dume huegemea upande wa kiumeni, yaani mwanaume anatukuzwa
huku mwanamke akikandamizwa. Utamaduni huo unawapitishia wanajamii wake
mila ambazo zinajitokeza kwenye sanaa ya lugha yake. Utamaduni umeumbwa kwa
16
namna ya kumkandamiza mwanamke katika nyanja zote za maisha. Wanawake
katika jamii zao hususani za Kiafrika, wanachukua mitazamo inayoendeleza itikadi
hii ambayo ni hasi. Kwa jinsi hii huweza kudharau jinsia zao wenyewe na kukosa
moyo wa kujiamini kwa wandishi wa kike, hii ni mojawapo ya jinsia iliyoathirika na
mfumo dume. Nadharia hii ya Ufeministi wa Kiafrika ni muafaka katika kuchambua
na kubainisha ukweli wa mtazamo ya Kifeministi.
Palmer (1983) anasema kuwa jamii ya kitamaduni inamuumba mwanamke ambaye
anataka kujikomboa na kujijua lakini ambaye bado anaamini misingi ya mila na
desturi kuhusu nguvu aliyonayo mwanamke katika jamiii. Hivyo kutokana na
maelezo haya tumetumia mkabala huu wa Kifeministi kuonyesha namna mwanamke
anavyochorwa katika fasihi ya Kiswahili huku tukiangalia mwandishi mwanamke.
Kama ilivyo mitazamo mingine ya kijamii, Ufeministi una mizizi yake katika siasa
ya ukombozi kwa hivyo nadharia hii iliongoza katika harakati za ukombozi wa
mwanamke zilipopamba moto kunako miaka ya sitini ( hasa Marekani). Baadhi ya
mambo yaliyozingatiwa na muungano huu ni kuunda upya uhalisia wa mwanamke
kwa kupunguza na kudhihirisha miundo ya kijadi ambayo inamtukuza mwanaume
na kumkandamiza mwanamke.
Kwa kuelewa hayo hapo juu, Scott (1986:1053) anasema:
wananadharia wamefanya busara sana kubadilisha msimamo
wao kwa kuanza kutumia jinsia pahala ukike hasa
wanaporejelea mahusiano ya jinsia hizi mbili katika utaratibu
wa jamii. Bila shaka wamegundua kuwa wanawake na
wanaume hufafanuliwa kwa kurejeanana basi hapana ufafanuzi
17
wa upande wowote ule utakaofuzu iwapo watatenganishwa.
(tafsiri yetu)
Mawazo ya Scott yanaelekea kufafanua ukweli uliopo kuwa wanaume na wanawake
ni viumbe walio na uwezo sawa na ambao husaidiana katika majukumu yao ya
kijamii japokuwa kimaumbile ni tofauti.
Donnely (2009), yeye anadai kwamba wanawake wahusika katika katuni inatakiwa
wachorwe kwa kuonesha kuwa wanaweza. Donnely alivutiwa na wanakatuni na
wachoraji wanawake wa zamani ambao walichora katuni zilizopinga mfumo dume.
Ijapokuwa katuni hizo ziko kwa namna ya kuchekesha lakini ndani yake zina ujumbe
mzito uhusuo mgawanyo wa majukumu kati ya wanawake na wanaume, na jinsi
mwanamke anavyochorwa katika jamii. Donnely ameonesha vizazi viwili tofauti
ambapo mwanamke alitazamwa kwa namna tofauti. Mwanzoni kabisa alionekana
kama mtu asiye na vigezo vya kupata kazi ila anafaa kuwa mama wa nyumbani tu na
chombo cha starehe kwa mwanaume. Lakini kilifika kipindi ambacho mwanamke
naye alitoka na kwenda kutafuta kazi huku akijiamini kwamba anaweza. Mwaka
1977 alimuona mwanamke akihesabiwa kama mama wa nyumbani asiyeweza
kufanya kazi ya kuingiza kipato bali alionekana kama mfanyakazi mkuu nyumbani.
Naye Kiango (1992) anasema kwamba mkanganyo kuhusu nafasi ya mwanamke
husababishwa na ukosefu wa itikadi murua za uchambuzi. Anasema:
Kulegalega na kukanganyikiwa kwa waandishi kuhusu
nafasi ya mwanamke kunatokana na kukosekana kwa
itikadi murua ya uchambuzi. Kukosekana kwa itikadi
hiyo ndiko kunakomfanya mwanamke apewe picha
isiyo nzuri na iliyo potofu. (uk 84-89).
18
Kutokana na tamthilia alizozichambua yaani ya Uasi, Mke Mwenza, Nakupenda
Lakini, Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi, na Jirani Kanyolewa, Kiango anaeleza
kwamba maendeleo katika teknolojia yanategemewa vile vile kuathiri nafasi ya
mwanamke katika jamii. Anafafanua zaidi kwamba katika kazi kadha wa kadha za
kifasihi mwanamke anachorwa kama kitega uchumi au chombo cha kuleta faida kwa
mwanaume. Hii inatokana na kukosekana kwa itikadi murua za kichambuzi ambazo
zitamweka mwanamke katika mtazamo chanya. Nadharia ya Ufeministi itatumika na
itamsaidia mtafiti kuchambua na kuelezea nafasi ya mwanamke katika fasihi ya
tamthiliya na mwitikio wa mafeministi juu ya uchorwaji wa wanawake.
Manufaa muhimu ya nadharia ya Ufeministi ni kule kuzungumzia masuala ya
wanawake na kupigania usawa miongoni mwa wanadamu na kuonyesha udhaifu wa
mfumo dume.
Nadharia inayoongoza utafiti huu ni kitengo kimoja cha Ufeministi ambao ni
Ufeministi wa Kiafrika. Hii ni nadharia inayojaribu kuelezea matatizo
yanayowakabili Waafrika, kisababishi cha matatizo yao na jinsi wanavyoweza
kujiepusha nayo. Kwa mfano Chukwuma (1994) anasema kuwa utambuzi wa
mapambano ya mwanamume wa Kiafrika, utambuzi wa kutokuwa na usawa na
matatizo ya mafundisho ya mila za ukoloni, kuwepo kwa Ufeministi kumeangalia
utamaduni wa Mwafrika na uasili wake katika kumchunguza mwanamume na
mwanamke. Davies na Grave (1986) wametoa mchango wao kuwa wameshikilia
utambuzi wowote wa mwanamke wa kiafrika, jamii yake na ukweli wa kihistoria
lazima vizingatiwe.
19
Kwa hivyo azma kuu ya Ufeministi hasa Ufeministi wa Kiafrika ni kusoma upya
kazi za fasihi ili kusisitiza umuhimu wa vipengele vilivyopuuzwa na wahakiki wengi
au ambavyo hawangeviona kwa sababu walikuwa wanafanya kazi katika nadharia za
kijadi zinazomtukuza mwanaume. Hivyo nadharia hii ndiyo iliyoongoza utafiti huu
kwa kuwa inazungumzia masuala yanayohusu wanawake na namna ya kutatua
matatizo yanayowakwamisha. Pia imetupa mbinu mbadala inayotumika katika
kumkuza mhusika wa kike. Hivyo utafiti huu ni njia mojawapo ya kumnusuru
mwanake na kumpa nyenzo na njia ya kupigana nayo katika nyanja mbalimbali iwe
matatizo yake kijijini, mjini, katika ndoa na hata kazini.
1.7 Mipaka ya Utafiti
Utafiti huu umejikita katika kuchunguza usawiri wa mwanamke katika kazi teule za
Penina Muhando. Kazi hizo ni Hatia (1972) na Nguzo Mama (1982). Uteuzi wa
tamthiliya hizi umefanywa kwa sababu ni kazi ambazo wahusika wake wakuu ni
wanawake, pia zimeandikwa na mwandishi wa jinsia ya kike na pia kigezo cha
wakati kimezingatiwa. Hivyo mtafiti ameangalia ni jinsi gani mwandishi mwanamke
alivyomsawiri mhusika mwanamke.
1.8 Hitimisho
Katika sura hii tumeeleza utangulizi kwa jumla kuhusu utafiti, usuli wa tatizo la
utafiti, tamko la tatizo la utafiti. Pia kiunzi cha nadharia kinachoongoza utafiti huu
kimebainishwa katika sura hii. Aidha malengo ya utafiti, maswali ya utafiti na
umuhimu pamoja na mipaka ya utafiti vimejadiliwa. Kwa hiyo sura ya pili inajadili
kwa kina mapitio ya machapisho mbalimbali yanayohusiana na mwanamke.
20
SURA YA PILI
MAPITIO YA MACHAPISHO MBALIMBALI KUHUSU MWANAMKE
2.0 Utangulizi
Katika sura hii mtafiti amefanya mapitio ya machapisho mbalimbali yanayohusiana
na utafiti huu. Mtafiti amegundua kuwa machapisho haya ni muhimu kwani
yamemwongoza kubaini pengo la utafiti ambalo halijafanyiwa kikamilifu na watafiti
wengine. Mwishoni mwa sehemu hii limeoneshwa pengo hilo lililoshughulikiwa na
mtafiti wa utafiti huu.
2.1 Mwanamke katika Fasihi ya Kiswahili
Katika fasihi ya Kiswahili, taswira ya mwanamke imejitokeza katika namna
mbalimbali, katika kufanya hivi tunajaribu kudhihirisha ni kwa kiasi gani nafasi na
wajibu wa mwanamke wanaopewa na waandishi hawa unaambatana na itikadi na
imani kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii za Kiafrika.
Katika Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi (1961) na Nakupenda Lakini (1957),
mwanamke amesawiriwa kama bidhaa ya kuchuma pesa. Wazee wanadai kiasi
kikubwa sana cha mali kama mahari. Kama bidhaa wanawake huuzwa na
kununuliwa. Katika Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi, Muriithu anamweleza Ronaldo:
MURIITHI: nilipokuwa kijana nilimpenda mama yako, alafu
nikamnunua. Sasa mimi ni mzee ndipo sasa naenda
kumuuza Wangare ambaye ni mali yangu. Nawe
utakapokuwa mzee utakuwa ukila nyama kama zile
tunazokwenda kula, heri mungu akujalie upate kununua mke
(uk 80).
21
Maneno hayo yanatudhihirishia kuwa mwanamke hakuwa na heshima yoyote katika
jamii hii. Hivyo mwanaume aliyekuwa na hela aliweza kununua mwanamke yoyote
anayempenda katika utamaduni wa kijadi, msichana hakupewa uhuru wa
kujichagulia mchumba aliyempenda. Mbaabu (1985:28-29) katika Uasi (1989) baba
yake Riziki alitaka kumchagulia binti yake mchumba. Nyamawi wa rika lake
anamuona Riziki kama bidhaa ya kuuzwa kwa wenye pesa wala si kwa John, kijana
maskini asiyeweza kulipa mahari.
Chande anasema
(Kwa John)------ Nisingekukataza kutembea na binti yangu kijana
lakini kama ujuavyo wazee wako maskini hawana cha kunipa ,ikiwa
nia yako ni kumuoa Riziki. Riziki sitaki madeni na wasiokua na
kitu.Watanipa nini? (uk 13).
Vivyo hivyo Sita wa Zabibu Chungu (1985) hakubali kuolewa na Shekh Zabibu,
mzee ambaye walimchagulia, Sita anatoroka siku ya harusi na kuolewa na Makuu,
kijana ambaye walipendana kama Chande wa Uasi, Bi Radhia wa Zabibu Chungu,
hajali hisia za binti yake cha muhimu sana kwake ni ile mali watakayoipata baada
ya mahari kulipwa.
Hapa tunaona jinsi mahari katika jamii za Kiafrika ilivyotumiwa kumkandamiza
mwanamke. Mtoto wa kike hakuwa na hadhi yoyote katika jamii. Hakuthaminiwa
na watu kwa sababu atakapoolewa angebadilishwa na mifugo au pesa. Hali hii
alimdhalilisha sana mtoto wa kike na kumtoa utu. Ilimfanya aonekane kama mali ya
mumewe ambaye alimnunua na anamtunza na anamtumia anavyopenda.
22
Kwa mujibu wa tamaduni za Kiafrika wa kijadi dhima na nafasi ya mwanamke ni
jikoni. Nafasi hii ya mwanamke inajidhihirisha wazi katika tamthiliya, mfano
Mulwa katika Bunami (1984), Rehema na Eda wanapika na kukamua ng‟ombe tu.
Katika Ukame (1983), Mosi na Bintiye Nawo humkamua ng‟ombe na kumpikia
Mzee Heri tu. Utamaduni wa jamii hizi ulimnyima mwanamke nafasi ya kushiriki
katika mambo mengine ya nje ya mazingira ya nyumba.
Maonevu ya kitamaduni yanawafanya wazee wasione faida yoyote katika
kumuelimisha mtoto wa kike. Katika Jirani Kanyolewa (1975) msichana Chadi
licha ya kufaulu mtihani wake vizuri hana matumaini ya kuendelea na masomo
kwani wazazi hawaoni haja ya kumwelimisha. Katika Ukame, Nema alikoseshwa
nafasi ya kusoma ili kaka yake Mambo asome. Kwa maoni ya mzee Heri, Nema
ambaye ni mwanamke hangeisaidia familia yake. Hali hii inamfanya mwanamke
kuoneka kama mtu duni, asiye na usawa na mwanaume. Imani hii imetokana na
hali kwamba mtoto wa kike anapoolewa hufaa jamii ya mumewe kuliko jamii yake
mwenyewe. Katika riwaya za Euphrase Kezilahabi, kama Rosa Mstika (1971),
Kichwa Maji( 1974), Dunia Uwanja wa Fujo (1975) na Gamba la Nyoka (1978)
anaendeleza falsafa ya jamii yake kongwe kuhusu mwanamke. Falsafa hii
inamchukulia mwanamke kuwa kiumbe duni aliye chini ya utawala wa mwanaume.
Katika Rosa Mistika, Regina anapatwa na mateso mengi lakini hawezi kumwacha
mumewe Zakaria kwa sababu ya watoto. Katika utamaduni na mila za Kiafrika
mwanamke akishaolewa anapaswa kuyakabili yote yanayompata kwa unyenyekevu
(Ngocbo 1986:149), katika uhusiano wao Regina hathubutu kumuuliza Zakaria
chochote. Zakaria anapoziiba pesa za karo ya mtoto ya
23
shule alizozipata Regina kwa kumuuza ng‟ombe wake na kuzinywa pombe, Regina
anaogopa kumuuliza, bali anasononeka tu kwa mawazo. Katika maelezo yake
Kezilahabi anasema,:
Katika kijiji cha Namagondo hapakuwa na mwanamke aliyekuwa
akipigwa karibu kila juma kama Regina. Wanawake wengi kijijini
walijiuliza kwanini hakutaka kumwacha bwana wake. Wengi walimwona
mjinga.(uk 7)
Kutokana na hali hii tunamwona Regina kama mfano wa mwanamke aliyekubali hali
yake kama mjaaliwa. Mungere wa Dunia Uwanja wa Fujo, anaonyesha
unyenyekevu kwa mumewe kwa kila hali. Bintiye anapopata mimba na kuadhibiwa
na baba yake, Mungere hamtetei anabaki analia tu pembeni. Wahusika hawa
wanachorwa katika hali ya kuridhika na hali na nafasi zao. Ni taswira za aina hii
huzua maoni kuwa, Kezilahabi ni mwandishi anakatisha tama ukombozi wa
mwanamke.
Hizi ni taswira ambazo hazimsaidii mwanamke aliyedunishwa kujifahamu na
kujitafakari juu ya hali yake. Badala yake zinazomfanya kuamini kuwa nafasi duni
anayoishikilia katika jamii ni majaaliwa.
Taasisi nyingine ya kitamaduni inayomkandamiza mwanamke ni utawala. Baadhi ya
jamii huwatawisha wasichana wao, kwa kuwafungia ndani ya nyumba ili wasitoke
nje na wasionekane na wavulana mpaka siku ya ndoa. Katika Utengano (1980 ) Said
A Mohamed anatuonyesha jinsi hali ya utawa inavyomtesa mwanamke Maimuna
aliyenyimwa uhuru wa kutoka nje na alimtii baba yake bila kupinga. Kwa kuzidiwa
na kero na kushindwa kuvumilia, aliasi utawa huu na kuingilia ukahaba. Katika
24
Buriani, Eda na Rehema wametawishwa nyumbani. Rehema analalamika kuwa baba
yao hawapeleki katika mikutano ya sherehe ili wakapate kubadilisha mazingira. Hali
hii ya utawa ilimnyima mwanamke fursa ya kwenda nje na kukabiliana na hali halisi
ilivyo. Kama ilivyodhihirika katika Utengano, mwanamke anapoasi utawa huu
hujikuta katika maovu yanayomdhalilisha sana.
Katika Machozi ya Mwanamke (1977) Madahiro anamchukulia mwanamke kuwa
chombo cha kuzalisha mali. Hii ndio sababu inayomfanya aamue kuoa wake wengi.
Pesa anazozipata kutokana na mauzo ya tumbaku anazitumia kwa manufaa yake
binafsi. Mwanamke hana haki ya kumiliki mali anayoizalisha. Hapa tunaona jinsi
ndoa inavyotumiwa kuwanyonya na kuwanyanyasa wanawake. Katika muktadha
huu wanawake huonekana kama wanyama wa huduma, kwa jinsi ambavyo
wanatumikishwa na waume zao mashambani.
Mbali na kazi za shamba, mwanamke anafanya kazi zote za nyumbani kama kutafuta
kuni, kufua nguo, kupika, kuteka maji, kumpashia mumewe maji na kumwandalia
chakula. Hapa tunaona kuwa Madahiro hana huruma wala utu, anawafanya wake
zake kama watumwa. Mume akishamnunua mke kwa mahari, anakuwa mali yake na
hivyo anamtumia apendavyo.
Katika Mke Mwenza, Gange ameoa wasichana ambao wakishirikiana na watoto
wanatosha kuhudumia mashamba yake. Badala ya kuajiri wafanyakazi anaoa wake
wengi ili apate watu wa kufanya kazi, faida inayotokana na kazi yao yeye huitia
mfukoni.
25
Hivyo basi tunatarajia kwamba picha ya mwanamke katika kazi za fasihi, kama
inavyojadiliwa hapo juu japokuwa hizo ni baadhi tu ya kazi chache za fasihi
zilizomsawiri mwanamke kwa namna hiyo zinatuangazia kuhusu picha ya
mwanamke. Taswira tulizozipata zinaambatana na nafasi na majukumu waliyopewa
wanawake katika utamaduni wa jadi katika kazi hizo. Baadhi ya picha hizo
zinajitokeza katika kazi nyingine za kifasihi za sasa na katika jamii zetu kwa jumla.
Hapo tumetumia mifano michache tu na hivyo inatupa misingi ya kuangalia Penina
Muhando ambaye naye ni mwandishi wa kike jinsi alivyowachora wahusika wake
wa kike katika tamthiliya za Hatia na Nguzo Mama.
2.1.1 Mwanamke Wakati wa Umwinyi/ Ukoloni
Katika kipindi hiki, tabaka tawala la kimwinyi lilitawala njia zote za kiuchumi na
kitamaduni. Hali ya mwanamke haikubadilika. Wanawake waliokuwa katika tabaka
la watwana walifanyishwa kazi nyingi kwa masaa marefu, bila malipo yoyote mbali
na kutumiwa kama vyombo vya kukidhi haja na uchu wa wanaume. Wanawake
waliokuwa katika tabaka la mamwinyi vilevile, walikandamizwa na waume zao
ambao waliwachukulia tu kama chombo cha kuzaa na kifaa kilichopenda mapambo
ya kuvutia wanaume (Nzomo 1987:114).
Hali hii ilimfanya mwanamke abaki kwenye nafasi duni sana katika jamii, nafasi ya
chini ya kuonekana, kujiona na kujikubali kuwa pambo la kuufurahisha moyo na
jicho la mwanaume (Senkoro 1987:24).
Mfumo wa urithi kwa upande wa baba ambao ulitokana na ugawaji wa kazi kwa
misingi ya ujinsia, uliwafanya wanaume kuwa bora zaidi na waliokua warithi wa
26
mali yote katika jamii, katika hali hii mwanamke alipewa nafasi ya pili, nyuma ya
mwanaume kazi zake za kushona zilidunishwa kwa vile hazikuleta faida kubwa
kama vile kazi za wanaume za kufuga na kuwinda (Reed 1983:70). Mabadiliko haya
ya kijamii, ambayo yaliletwa na mabadiliko katika utaratibu wa mfumo wa
kiuchumi, yalikuwa na athari kubwa kwa upande wa wanawake. Sifa yake katika
jamii kuanza kupungua. Alianza kudunisha na kupuuzwa (Reed 1970:240) na katika
kipindi hiki mifumo mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni
ilimnyima mwanamke haki yake. Mwanaume aliyekuwa na wanawake wengi
alipewa hadhi ya juu, kwani wanawake walichukuliwa kama mali. Mwanamke
alitarajiwa kufanya kazi zote za shambani na nyumbani. Kwa upande mwingine
mwanaume alipewa wajibu wa kulinda usalama, kujenga nyumba, kuchunga mifugo,
kuwinda na kutayarisha konde. Ingawa mwanamke alifanya kazi nzito shambani
mazao yalipopatikana alinyimwa haki ya kuyamiliki na faida iliyopatikana pia
alinyimwa. Mumba (1990:2) anasema kuwa, katika jamii zilizoendelea urithi
ulikuwa kwa upande wa baba, mwanamke alipewa nafasi duni, nafasi ya kurithi
mali yoyote ilikuwa kwa baba. Wakati huo mwanamke hakuruhusiwa kurithi
chochote mumewe alipofariki. Mwanaume aliyekuwa ameoa alipofariki mali yake
iligawiwa watoto wa kiume. Mjane naye na mali yake yote na watoto alirithiwa na
ndugu wa kiume wa mumewe. Ikiwa ndoa ililazimika kuvunjika mwanamke
aliondoka na watoto walibaki kwa baba yao (Reed 1970:24) na (Ngcobo 1986:144).
2.1.2 Mwanamke Baada ya Uhuru
Wanawake kama wanajamii walipigania uhuru wakitarajia kwamba
utakapopatikana hali yao hii ya maisha ingekuwa bora zaidi. Matarajio haya
hayakutimia, kwani baada ya mkoloni kuondoka, ukoloni uliendelea kwa sura
27
nyingine na mwanamke aliendelea kunyanyaswa. Waafrika waliochukua mamlaka
walijinyakulia mashamba yaliyokuwa mikononi mwa wakoloni, viongozi
waliwatumia wanyonge kulima katika mashamba hayo ili na wao waweze
kujitajirisha hivyo wanyonge wakiwemo wanawake waliendelea kunyanyaswa hata
baada ya uhuru. Hatamu za uongozi zilichukuliwa na wanaume, wanawake
walisahauliwa. Wanawake waligundua kuwa kupatikana kwa uhuru hakukuleta
mabadiliko yoyote kwa kundi lao hili. Hawakushirikishwa katika kutoa maamuzi
kwa maswala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi na hata maswala yanayowahusu wao
wenyewe. Madaraka makubwa nyumbani au serikalini yalipewa mwanaume.
Mipango yote ya maendeleo haikumuhusisha mwanamke. Baada ya muda
wanawake waliona haja ya kunyanyuka na kupigania haki zao (Wipper 1970:4-6).
Kufika miaka ya sabini, harakati za kujikomboa mwanamke zilipamba moto.
Umoja wa mataifa ukiongoza shughuli hizi za ukombozi ulitangazwa mwaka 1975
kuwa mwaka wa kina mama ulimwenguni. Kulionekana haja ya kupigania uhuru wa
kiuana, usawa katika malezi ya watoto, uhuru wa kiuchumi na kisiasa pamoja na
kisheria. Hapa usawa utakuwa na maana kuwa mwanamke atakuwa na uhuru wa
kuyaendeleza maisha yake na kujiendeleza bila vikwazo vyovyote (West
1975:9).Vyama na makundi mbalimbali ya kina mama viliundwa ili kupigania usawa
huu. Mengi yamefanywa na makundi haya kuangazia umuhimu wa mwanamke
kama jamii. Mikutano mingi imewahi kufanywa na mapendekezo mengi yakatolewa
kuhusiana na swala la kuyaboresha maisha ya mwanamke. Kufikia sasa baadhi ya
mapendekezo haya yametekelezwa kwa kiasi fulani, kama vile kuwapo wanawake
wa nafasi katika elimu, siasa na hata sheria. Hata hivyo mengi bado yanatarajiwa
kutoka kwa serikali za Kiafrika (Wipper 1970:8).
28
2.2 Mapitio ya Machapisho Mbalimbali kuhusu Mwanamke
Chaligha (2011) alitafiti kuhusu, “Usawiri wa mwanamke na mgawanyo wa
majukumu kujinsia katika fasihi picha ya katuni mnato za Kiswahili”. Alibaini kuwa,
mwanamke katika sanaa ya katuni anakandamizwa kwa kiasi kikubwa. Mwanamke
bado hajapewa muonekano chanya japo zipo katuni chache ambazo zimemuonyesha
kwa mtazamo chanya. Katika asasi nyingi mwanamke hukandamizwa na
kudunishwa na vyombo mbalimbali hususani katika suala la utoaji mahari, elimu
duni, uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa. Chanzo cha hayo ni mfumo dume uliopo
katika jamii. Pia mwanamke ameonekana hana maadili mema ila ni mtu wa
kugeuzwa na tamaduni wa kigeni ulioingia nchini. Yote haya yamesababishwa na
mwanamke kukosa urazini kuhusu haki zake.
Sanga (2011) naye katika tasnifu yake amechunguza usawiri wa mwanamke katika
utanzu wa nyimbo za kizazi kipya Tanzania. Muziki huo hutawala sana matangazo
ya redio na vyombo vingine vya habari ambavyo vina nguvu katika kujenga
mtazamo wa kijamii juu ya mambo mbalimbali. Ameonyesha kuwa taswira ya
mwanamke katika nyimbo za kisasa anachorwa kwa udhalili na zaidi mwanamke
anachorwa kama mwenye kuwa na tamaa ya starehe na mwenye kukosa uaminifu.
Hivyo basi, kazi ya Sanga itatoa mwanga mkubwa katika utafiti huu katika kupata
usawiri wa mwanamke na mgawanyo wa majukumu katika tamthiliya kwa kuangalia
kwa jicho la kipekee na kihistoria katika kazi nyingine.
Naye Rosalind (2010), mwanamama mcheshi katika makala ya “Ack! Cartoonists
and Feminsts Quarrel Over Demise of Cathy” (yaliyochapwa tarehe 20/8/2010)
anafafanua kwamba, katika magazeti ya katuni ya miaka ya 1975, wanaume tu ndio
29
waliochorwa kwa mtazamo chanya lakini wanawake walichorwa kama akina mama
wa nyumbani au wasichana wauza baa au hoteli. Anamsifu Cathy na kusema ni
mwanakatuni mfeministi aliyefungua ukurasa mpya kwa kuanza kumchora
mwanamke kwa mtazamo chanya. Anaeleza kwamba wanawake waandishi
walipewa nafasi ya pili katika kuhariri katuni lakini wanawake hawakujali ndipo
wakaamua kuandika na kuchora kupitia wavuti na tovuti. Kwa hakika Rosalind
hakujadili nafasi ya mwanamke kiundani ila aliandika tu makala kuhusiana na nafasi
ya mwanamke mwanakatuni katika fani ya uandishi na uchoraji. Hakuchambua
nafasi ya mwanamke mhusika kama alivyochorwa katika tamthiliya. Hata hivyo kazi
ya Rosalind ni muhimu katika kupata ufafanuzi wa nafasi ya mwanamke katika
uhariri na pia itatoa mwanga wa kuwaelewa wanawake na jinsi wanavyoielezea
nadharia ya Kifeministi ambayo ndiyo itakayotumika katika kuongoza tasnifu.
Soko na Senkoro (2009) wameeleza kwa kifupi nafasi ya mwanamke katika katuni
za michezo. Wanadhihirisha hilo kwa kueleza kwamba nafasi ya mwanamke katika
fasihi picha ya katuni mnato za michezo ni ndogo sana na hata hivyo wamechorwa
kikejeli na kwa mabezo. Hawa wamemwangalia mwanamke katika kipengele kimoja
tu cha michezo, lakini si katika vipengele vingine vya kijamii. Hata hivyo makala
yao itatoa mchango mkubwa sana katika utafiti huu kwani kejeli, sitiari na dhihaka
ndivyo vipengele vinavyobeba ujumbe ambao unaelezea nafasi ya mwanamke katika
fasihi tamthiliya.
Omari (2008) “Katika Makala ya Fasihi Simulizi na Jinsia” ametafiti nyimbo za
watoto na kuona jinsi mwanamke na mwanaume wanavyosawiriwa. Baadhi ya
30
nyimbo alizofanyia utafiti ni Kula Mbakishie Baba, Nitakusemea kwa Baba, Gari la
Baba, Namsaka Mke Wangu, Tumenye Machungwa na Watoto Wangu eh.
Usawiri wa mwanamke katika nyimbo za watoto ni kwamba baba ni mtu wa
kutoshinda nyumbani na ni mpiganaji. Nyimbo nyingi za watoto zinaonyesha kuwa
baba au mwanaume ni mtu ambaye mara nyingi hakai nyumbani kwani mwanamke
ndiye anayepaswa kukaa nyumbani na kufanya kazi za kifamilia ikiwa ni pamoja na
kumwandalia mwanaume na watoto.
Omari (2008) anaendelea kueleza kuwa, nyimbo nyingi za watoto zinaonyesha kuwa
baba ni mtu wa kuogopwa na ni mkali. Dhana hii inatumika sana katika kuwatisha
watoto pindi wakifanya kosa kwa kuambiwa, “Nitakusemea kwa Baba”. Watoto
wanaposikia hivyo huwa wanaogopa sana. Pia katika utafiti wake anatuonyesha
kuwa, baba ndiye mmiliki wa mali na mwanamke ni mtu ambaye hawezi kujimudu
kimaisha.
Utafiti uliofanywa na Omari kuhusu usawiri wa mwanamke na mwanaume katika
nyimbo za watoto umeonyesha kumdhalilisha mwanamke na kumpa sifa chanya
mwanaume. Hii inatoa taswira kwamba hata watoto wamejengewa imani kwamba
wanawake siku zote ni wanyonge. Utafiti wa Omari umempa mtafiti mchango
mkubwa sana katika utafiti huu.
McCabe (2007), alifanya mahojiano kwa njia ya baruapepe na Jacky Fleming,
mwanakatuni wa Uingereza ambaye alianza kuchora katuni kuhusiana na ufeministi
mwaka 1978. Fleming katika mahojiano hayo, anaeleza kwamba wakati wote
31
wanawake walichorwa vibaya katika vyombo vya habari. Anasema kwamba, kwa
wanawake hazikuwa habari za kuvutia kabisa kama mwanaume anavyoona vibaya
kwa mwanamke kumfanya asiwe na uwezo wa kuzalisha watoto. Hata hivyo
madhumuni ya mahojiano hayakuchambua nafasi ya mwanamke katika jamii kama
mhusika katika kazi ya katuni, bali kutaka kujua nafasi ya mwanamke mwandishi na
mtazamo wa kifeministi. Ijapokuwa mahojiano hayo hayakuchambua nafasi ya
mwanamke katika fasihi ya tamthiliya lakini yamemsaidia mtafiti kuelewa kwa
haraka nafasi ya mwanamke na jinsia katika tamthiliya za Hatia na Nguzo Mama
zilivyochorwa na wasanii wa kike au wa kiume.
Shule (2004) amefanya utafiti juu ya mchango wa filamu katika harakati za
kupunguza unyanyasaji wa kijinsia na hatari zinazoweza kusababisha UKIMWI.
Katika utafiti wake ameonyesha jinsi filamu zinavyoweza kusaidia kuwaelimisha
vijana wa kiume katika kuzuia unyanyasaji wa kijinsia ambao ni mojawapo ya
mambo yanayoweza kusababisha kuenea kwa maambukizi ya UKIMWI. Stadi hii
inatoa mwanga juu ya mambo au majanga ya jamii yanavyoweza kuingizwa kwenye
tamthiliya na kutumika kama njia ya kuifundisha au kuikanya jamii.
Mwakalinga (2003) amezungumzia nafasi ya mwanamke katika filamu za
Kitanzania. Anaeleza kwamba wanawake wanastahili kusawiriwa katika mtazamo
chanya ili kuwasilisha picha sahihi ya wanawake wa Kiafrika. Wanawake pia
wanatakiwa kuandika hadithi zao wenyewe, na kutengeneza na kusimamia filamu
zao wenyewe. Utafiti wa Mwakalinga unasaidia kuonyesha jinsi ambavyo kazi za
kifasihi zimekuwa zikiwasawiri wanawake na mambo yanayotokea kwenye jamii.
32
Unasaidia pia katika kutuongoza kuona nafasi mbalimbali za mwanamke katika
tamthiliya za Hatia na Nguzo mama.
Ndungo (1998) alitafiti suala la kiuana katika methali za Gikuyu na Kiswahili.
Utafiti huo ulitilia mkazo matumizi ya lugha ya kitamathali katika methali na
misemo. Ingawa maoni ya Ndungo kuhusu uchorwaji wa mwanamke katika fasihi
simulizi siyo tofauti na wale waliomtangulia, ameonyesha kuwa utamaduni na
malezi huchukua nafasi muhimu katika kuunda na kuimarisha itikadi na mielekeo ya
jamii kuhusu wanawake. Hivyo hata jamii nayo inahusika katika kumkandamiza
mwanamke katika fasihi, tukiangalia jamii aliyokulia mwandishi kama ilikuwa ya
kumdunisha mwanamke basi hata katika kazi zake aghalabu atamdunisha
mwanamke. Hivyo basi Ndungo ametoa mchango maridhawa kwa watafiti wapya.
Pia utafiti wake umetuwezesha kuziba baadhi ya mapengo yaliyokuwepo hapo
awali, kwa kutuangazia picha ya mwanamke kama ilivyo katika fasihi na matumizi
ya lugha ya Kiswahili kwa jumla. Kufika sasa kulingana na tafiti hizo imebainika
kuwa mwanamke anaonewa na kuchukua nafasi ya pili baada ya mwanaume. Hivyo
mwanamke ni kiumbe duni anapolinganishwa na mwanaume, hata hivyo tafiti hizi
hazikumchambua mwandishi mwanamke jinsi alivyomchora mhusika mwanamke
kitu ambacho kimemsukuma mtafiti kufanya utafiti huu.
Lughano (1989) amehakiki usawiri wa mwanamke katika riwaya nne za Euphraise
Kezilahabi. Kulingana naye ni mwandishi wa kiume ambaye anakatisha tama
ukombozi wa mwanamke. Maoni ya Lughano ni kwamba Kezilahabi anaendeleza
falsafa ya jamii yake kongwe kuhusu mwanamke, falsafa ambayo inamchukulia
mwanamke kuwa kiumbe duni aliye chini ya utawala wa mwanaume. Utafiti huu pia
33
umetusaidia sana katika utafiti wetu kwani maoni yake yameweza kuendeleza
mawazo yetu kuhusa usawiri wa mwanamke katika tamthiliya teule za Penina
Muhando.
Chesaina (1987) amehakiki jukumu na usawiri wa wahusika wa kike katika
tamthiliya zilizoandikwa katika lugha ya kiingereza, Kifaransa na Kiswahili.
Amewachukua waandishi wa kike na wa kiume na kuwalinganisha, huku akitoa hoja
kwamba waandishi wa kike wanatofautiana kwa kiasi kikubwa jinsi
wanavyowasawiri wahusika wa kike. Hoja yake kuu ni kuwa wanaume
wanapoandika juu ya masuala ya kike wanakumbana na vikwazo kutokana na hali
kwamba wao wenyewe hawajakumbana na dhuluma hizi binafsi kwa hivyo
hawawezi kuipenya nafsi ya mwanamke. Hoja zake zimetufaa katika utafiti wetu,
kwani zimetusaidia katika kubainisha jinsi Penina Muhando alivyoweza kumchora
mwanamke.
Senkoro (1982), amehakiki wahusika wa kike katika riwaya ya Kezilahabi, Dunia
Uwanja wa Fujo (1975). Pia Senkoro (1987) anagusia kwa ufupi uchorwaji wa
wahusika wa kike katika fasihi ipatikanayo katika mfumo wa kibepari. Maoni yake
ni kwamba katika fasihi inayopatikana katika mfumo huu, mwanamke huonyeshwa
kama pambo la kutamaniwa na mwanaume au kama kiumbe duni ambaye jukumu
lake kuu liko kitandani. Uhakiki wake unatofautiana na wa kwetu kwani
hakuchambua kazi yoyote maalum ya kifasihi. Hata hivyo baadhi ya maoni
anayotoa yametufaa katika utafiti huu.
34
Mbughuni (1982) ameandika makala kuhusu taswira ya mwanamke katika riwaya za
Tanzania. Anatoa hoja kuwa taswira inayoendeleza kuhusu mwanamke katika
riwaya za Tanzania ni za aina mbili. Ya kwanza ni ile ya Hawa wa biblia ambaye
anawakilisha uovu wote katika jamii, mchoyo, shetani na mlaghai. Taswira ya pili
inamweka mwanamke jikoni, akiwa anatawaliwa na mwanaume. Wakati Mbughuni
amejifunga kwenye riwaya za Kitanzania sisi tumeshughulikia tamthilia za
mwandishi wa Kitanzania vilevile. Hivyo basi kazi yake hiyo imetusaidia sana katika
utafiti wetu.
Siyo hao tu waliomjadili mwanamke bali hata waandishi wengine ambao
wameandika riwaya, tamthilia na ushari. Waandishi hao ni pamoja na Mwanakupona
binti Mshamu aliyeandika Utenzi wa Mwanakupona uliochapwa na kuhaririwa na
Nabahany (1972). Mshamu katika utenzi wake anasisitiza maadili mema na jinsi
mwanamke anavyotakiwa kuishi na mumewe. Anatakiwa awe mnyenyekevu,
mwelekevu na msikivu pale mwanamume anaposema au kutoa amri fulani.
Utendi huu umeleta mwanga katika utafiti huu hasa katika vipengele vya maadili,
utamaduni na dini. Kazi hii kubwa ya Mshamu imeleta mwanga hasa katika
utamaduni na dini, ambazo ni asasi kongwe zilizomuonea, zilizomtweza na
kumnyanyasa mwanamke.
Waandishi wengine ni pamoja na Nawal El Saadawi aliyeandika riwaya ya Woman
at Point Zero (1983), Elieshi Lema aliyeandika riwaya ya Parched Earth (2001), na
Ama Ata Aidoo aliyeandika riwaya ya Changes (1991). Hawa ni waandishi
wanawake waliomchora mwanamke
35
kama jamii ilivyomhesabu. Hata hivyo mwanamke katika riwaya hizo anaonesha
harakati za kujikomboa na kujitoa katika kunyanyaswa, kuonewa na kuwa tegemezi
kwa mwanaume,anaondoka na kujitafutia maisha ya uhuru wake yeye mwenyewe.
Kazi za wanawake wanafasihi hawa, zitajenga utafiti huu katika kushadidia data za
msingi ambazo zitachunguza usawiri wa mwanamke katika fasihi ya tamthiliya za
Hatia na Nguzo Mama.
2.3 Hitimisho
Mapitio haya yametoa mwanga kwa mtafiti kuhusu usawiri wa mwanamke katika
tamthiliya za Hatia, na Nguzo Mama kwani usawiri wake haukuelezewa kiasi cha
kueleweka vizuri katika jamii, na hivyo imempa mtafiti uwanja mpana wa kujadili
usawiri huo katika tamthiliya na kuchambua mgawanyo wa majukumu kijinsia
katika jamii kama tamthiliya hizo zilivyobainisha.
Sura inayofuata inahusu mbinu mbalimbali za utafiti zilizotumika katika utafiti huu
pamoja na mbinu zilizotumika kuchambua na kuwasilisha data za utafiti.
36
SURA YA TATU
MBINU ZA UTAFITI
3.0 Utangulizi
Sehemu hii inahusika na mbinu mbalimbali za utafiti zilizotumiwa na mtafiti ili
kupata data na mbinu ambazo zilitumiwa kuzichambua na kuziwasilisha data hizo
kulingana na mada ya utafiti.
3.1 Eneo la Utafiti
Utafiti huu ulifanyikia uwandani na maktabani. Mtafiti alikwenda Chuo Kikuu cha
Dar es salaam, katika kitengo cha sanaa za maonyesho (FPA) kuwahoji wahadhiri
watano ambao ni Profesa Penina Muhando, Daktari Imani Sanga, Daktari Vicensia
Shule, Daktari Mona Mwakalinga na Bw Mtiro. Maktaba zilizotumika ni Maktaba
Kuu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma, Taasisi ya
Taaluma za Kiswahili (TATAKI), Mtandao wa Jinsia, Taasisi ya Taaluma ya
Maendeleo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mapitio ya vitabu pia yalifanywa katika
Makavazi ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia,
mtafiti alitumia njia za kielektroniki kwa ajili ya kupata makala mbalimbali na
baadhi ya data za upili ambazo zilisaidia kukamilisha utafiti huu.
3.2 Mbinu za Ukusanyaji wa Data
Data za msingi zilipatikana katika tamthiliya teule za Penina Muhando ambazo ni:
Hatia (1972) na Nguzo Mama (1982). Mtafiti kachagua tamthiliya hizo kwa sababu
ni mojawapo ya tamthiliya ambazo hazijafanyiwa tafiti za kina kuhusu taswira
zinazojitokeza kuhusu mwanamke. Pia, tamthiliya hizo wahusika wake wakuu ni
wanawake. Pia, data fuatizi zilipatikana katika majarida, tasnifu, vitabu, makala na
37
machapisho mbalimbali yaliyogusia suala la tamthiliya kwa jumla, ikiwa ni pamoja
na yale yaliyogusia usawiri wa mwanamke katika fasihi na katika kazi ambazo si za
kifasihi pamoja na mahojiano yaliyofanyika kwa mwandishi mwenyewe na
wataalamu wa fasihi.
3.2.1 Uchambuzi wa Matini
Uchambuzi wa matini ni mbinu inayojumuisha uchambuzi wa majarida, magazeti
pamoja na matini za mazungumzo ambazo hazijaandikwa (Kothari 2008). Katika
utafiti huu mbinu hii ilitumika kupata data za msingi pamoja na za upili. Mtafiti
alisoma kazi teule, machapisho na nyaraka mbalimbali ambazo zilimpatia data za
msingi na data za upili zilizomsaidia mtafiti katika utafiti huu.
3.2. 2 Mahojiano / Usaili
Mahojiano ni njia ya kupata data inayohusisha maswali na majibu yanayofanywa
kwa mazungumzo kati ya mtafiti na mtafitiwa (Kothari 2008). Kwa mujibu wa
King‟ei na Kisovu (1987) wanaeleza kuwa, mahojiano ni mbinu inayotumika katika
utafiti wa Fasihi Simulizi ambapo mtafiti huweza kukutana ana kwa ana na
watafitiwa kwa njia zingine na kuuliza maswali kuhusu habari anayoitafiti. Pia
mtafiti anaweza kufafanuliwa jambo fulani lenye utata ili aweze kulifahamu vizuri.
Mbinu hii ilimsaidia mtafiti kupata taarifa za msingi zinazohusiana na mada ya
utafiti. Kwa upande wa uwandani njia ya mahojiano huru ilitumika, na katika
mahojiano hayo nyenzo iliyotumika ni dodoso. Faida ya kutumia mahojiano ni
kupata taarifa za msingi kwa haraka. Pia ilimsaidia mtafiti kupata data nyingi na
thabiti zilizosaidia kufanikisha utafiti huu. Kazi ya mahojiano ilifanywa na mtafiti
38
katika maeneo ya utafiti yaliyopendekezwa.Wahojiwa walitakiwa kujibu maswali
yaliyoandaliwa na mtafiti kwa maelezo au kwa kuandika.
3.3 Usampulishaji na Njia za Usampulishaji
Sampuli ni sehemu ya populesheni ambayo mtafiti alitumia katika ukusanyaji wa
taarifa zilizomsaidia kufikia malengo ya utafiti. Mtafiti alitumia mbinu ya
usampulishaji nasibu, lengwa na holela, ambapo kila mhusika anapewa nafasi sawa
ya kuchaguliwa na kujumuishwa katika sampuli. Katika utafiti huu mtafiti
aliwachagua wawakilishi hao kulingana na jinsi wanavyokidhi haja na malengo ya
utafiti bila kuzingatia jinsi zao. Sampuli hiyo ilichaguliwa kiholela kutoka katika
makundi yote yaundayo jamii tafitiwa ili kutoa fursa kwa kila mlengwa kutafitiwa.
Sampuli hiyo ilihusisha tamthiliya mbili ambazo ni Hatia na Nguzo Mama.
Wahadhiri watano kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliobobea katika
taaluma ya Fasihi ya Kiswahili walihojiwa ili kupata taarifa zaidi zilizomsaidia
kukamilisha utafiti huu. Mtafiti alitumia tamthiliya za Hatia na Nguzo Mama na
sababu hasa ya kuteua tamthiliya hizo imetokana na malengo ya tasnifu yenyewe
ambapo tamthiliya hizo wahusika wake wakuu ni wanawake. Pia mwandishi huyu
amechaguliwa kwa kigezo cha umahiri wake katika kumchora mwanamke kwa
namna tofautitofauti kulingana na jinsi au matendo wanayofanyiwa katika jamii zetu
za kila siku. Pia mwandishi huyu ni mwandishi mwanamke ambaye ni
mwanaharakati katika maswala ya jinsia kuhusu ukombozi wa mwanamke na
amewahi kufanya kazi katika mashirika yanayoshughulikia maswala ya mwanamke.
39
3.4 Vyanzo vya Data
Data zilizochambuliwa zilitoka katika vyanzo mbalimbali, hata hivyo, data za msingi
zilitoka katika tamthiliya za Hatia na Nguzo Mama za Penina Muhando. Data fuatizi
zimetoka katika machapisho mbalimbali yaliyosomwa maktabani na mahojiano
yaliyofanywa na mtafiti kwa wataalamu na waandishi wa tamthilia. Vifuatavyo ni
vyazo vya data za msingi na vyanzo vya data fuatizi.
3.4.1 Vyanzo vya Data za Msingi
Data zilizokusanywa na kutumika katika utafiti huu ni data za msingi na data za
upili. Data za msingi ni data zilizokusanywa na mtafiti kutoka uwandani kwa lengo
la kujibu maswali ya utafiti. Data hizi huwa ni taarifa ambazo ni mpya na za awali
katika tarehe ya kuchapishwa (Kamuzora, 2008). Data za msingi katika tasnifu hii
zilipatikana kwa kusoma tamthiliya ya Hatia na Nguzo mama ili kuchunguza usawiri
wa mwanamke katika tamthilia hizo.
Vitabu vya tamthiliya za Hatia na Nguzo Mama vilinunuliwa ili kupata data za
msingi. Vyanzo hivi vimesaidia katika upatikanaji wa data za msingi ambazo
zimejenga usuli wa tatizo la utafiti.
3.4.2 Vyanzo vya Data Fuatizi
Data za upili zinafafanuliwa na Kamuzora (2008:143) kuwa, ni data zipatikanazo
kutoka katika data zilizokusanywa na watu wengine kwa madhumuni mengine na
katika vyanzo vya kifasihi. Data hizi humilikiwa na mtu mwingine na si mwandishi
wa sasa. Huwa zimekwishatokea katika nyaraka zingine. Maandiko na machapisho
40
mengine kutoka kwa wataalamu na wachambuzi wa kazi za fasihi zihusuzo
tamthiliya lengwa zilisomwa na data za upili kupatikana.
Vyanzo vya data fuatizi ni vile vilivyotokana na makala mbalimbali zilizosomwa,
kama vile tasnifu, vitabu, majarida na katika makala zilizopatikana katika tovuti na
wavuti na maktabani pamoja na mahojiano na mwandishi na wataalamu wa fasihi.
Data hizi zimesaidia kushadidia data za msingi zilizotumika katika tasnifu hii, na
kusaidia kutimiza malengo ya utafiti na kujibu maswali ya utafiti. Uchambuzi wa
matini ni njia iliyotumika katika vyanzo fuatizi.
3.5 Vifaa katika Ukusanyaji wa Data
Ili kukamilisha utafiti huu, vifaa au nyenzo mbalimbali zilitumika kukusanya data
uwandani na maktabani kama vile kalamu za wino, shajara, ngamizi (kompyuta)
kinyonyi, dodoso, hojaji, kamera na kinasa sauti. Nyenzo hizi zilimsaidia mtafiti
kupata data zisizo za kiidadi, yaani data zilizochambuliwa kwa maelezo kuhusu
Penina Muhando. Ufafanuzi wa vifaa hivyo ni:
3.5.1 Kalamu na Shajara
Ni vifaa vilivyotumika maktabani na uwandani, mtafiti alichukua nukuu muhimu
wakati wote alipokusanya data katika maeneo mbalimbali na kuziandika kwenye
shajara kwa kutumia kalamu.
3.5.2 Dodoso
Ni orodha ya maswali yaliyotumika katika kuwasaili watafitiwa. Mtafiti anakuwa na
maswali ambayo yanamwongoza wakati wa kufanya utafiti (Kothari 2008). Katika
utafiti huu, mtafiti alitumia dodoso katika mahojiano aliyoyafanya na watafitiwa
41
waliopo katika maeneo yaliyopendekezwa. Watafitiwa hao walishiriki kwa moyo wa
ukarimu katika kujibu maswali ya dodoso hizo na baadaye alizifanyia uchambuzi ili
kuona kama zimejibu maswali ya utafiti na hatimaye kukidhi malengo ya utafiti huu.
3.5.3 Ngamizi (Kompyuta)
Hiki ni kifaa muhimu katika kufanya utafiti kwani licha ya kuwa data za maktabani
na uwandani zimehifadhiwa humo, pia kilitumika kama sehemu ya maktaba tembezi
au maktaba ya kidijitali ambapo mtafiti aliweza kupata fursa ya kusoma nyaraka
zinazohusiana na utafiti wake pamoja na kupata maelezo kuhusu nadharia
iliyotumika. Hivyo basi, ngamizi imetumika katika kipindi chote cha utafiti yaani
kuanzia wakati wa maandalizi ya utafiti, wakati wa kuchanganua data na wakati wa
kuandaa ripoti ya utafiti huu.
3.5.4 Kinyonyi
Ni kifaa ambacho kilitumika kutunza nakala tepe (soft copy) zilizohusiana na utafiti
huu. Kifaa hiki ni muhimu katika zoezi zima la utafiti kwani kilitumika tangu
mwanzo wa utafiti huu mpaka sasa kazi imekamilika. Hata baada ya kukamilika kwa
utafiti, kinyonyi kimetumika kuhifadhi ripoti nzima ya utafiti huu. Matumizi ya kifaa
hiki huenda sambamba na matumizi ya ngamizi. Hivyo, ngamizi na kinyonyi
hutegemeana.
3.5.5 Tepurikoda
Ni kifaa kinachotumika katika kunasa na kurekodi sauti wakati wowote katika
muktadha wote ule. Katika utafiti huu, tepurikoda ilitumika uwandani ambako
42
mtafiti alirekodi mahojiano baina yake na watafitiwa. Taarifa zilizorekodiwa katika
tepurikoda zilitumika katika uchambuzi wa data katika utafiti huu.
3.5.6 Kamera
Ni kifaa kilichotumika katika kupata taarifa mbalimbali ambazo haziko katika
maandishi kwa mfano picha za wahojiwa na maeneo mbalimbali ambayo
yanahusiana na mada husika.
3.6 Mbinu ya Uchanganuzi wa Data
Data zote zimechanganuliwa kwa mkabala usio wa kiidadi yaani ule wa maelezo. Hii
ni kwa sababu utafiti huu haukuhusisha takwimu. Pia, data zimepangwa kulingana
na malengo na maswali ya utafiti, hii ni kwa sababu mtafiti alitaka uchanganuzi wa
data hizo ulandane na malengo ya utafiti, sambamba na kujibu maswali ya utafiti. Ili
kurahisisha zoezi la upangaji kulingana na malengo na maswali, data zote zimepewa
msimbo ili kuiweka tasnifu katika mtiririko na mpangilio mzuri. Data zote
zilizoambatanishwa kama vielelezo zimechambuliwa kila moja kwa nafasi yake, ili
kurahisisha uchakataji. Pia, data fuatizi zimenukuliwa pale ilipobidi ili kuthibitisha
uchambuzi wa data za msingi.
3.7 Hitimisho
Mbinu hizo ndizo zilizotumika katika kupata data zilizochambuliwa katika utafiti
huu. Data hizo zimejibu maswali ya utafiti na matokeo yake ndiyo yametimiza
malengo ya utafiti na hivyo tatizo la utafiti limetatuliwa na pengo la mapungufu
limezibwa japo kwa sehemu au kutoa mwanga juu ya tafiti zijazo. Sura inayofuata
inahusu uwasilishaji na uchambuzi wa data.
43
SURA YA NNE
UWASILISHAJI, UCHAMBUZI NA MJADALA WA MATOKEO YA
UTAFITI
4.0 Utangulizi
Sura hii inahusu uwasilishaji na uchambuzi wa data. Tromp na Kombo (2006:110)
wanasema, uchambuzi wa data ni kuchunguza kwa undani data na kuzitolea
hitimisho. Uwasilishwaji wa data kwa mujibu wa waandishi hawa ni namna ya
kupangilia data ili ziweze kueleweka vizuri. Uwasilishwaji umefanywa kwa mbinu
ya ufafanuzi kulingana na malengo mahsusi ya utafiti. Sura hii imeshughulikia
mambo matatu yanayoakisi malengo yetu, kila jambo tumejadili kwa kina kuakisi
data zilizokusanywa uwandani kwa kutumia mbinu za mahojiano na mapitio ya
maandiko. Pia nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika imetumika.
Kuna mitazamo miwili katika tasnifu hii, mtazamo hasi na mtazamo chanya, kwa
maana kwamba, Penina Muhando katika tamthiliya zake za Hatia na Nguzo Mama
kamchora mwanamke kama mtu anayeweza yeye mwenyewe hata asipowezeshwa.
Lakini pia kwa upande mwingine ameonyesha jinsi gani wanaume wanavyomtazama
mwanamke kama kiumbe dhaifu kinachomtegemea mwanaume kwa kila kitu hata
kimawazo. Pia ameonyesha jinsi mwanamke alivyobebeshwa mambo yote maovu
katika jamii.
Pia utafiti huu umebainisha majukumu anayopewa mwanamke katika jamii na jambo
la tatu tumejadili athari zinazotokana na usawiri wa mwanamke katika kazi za
kifasihi. Sehemu hii imejadili tamthiliya mbili za Penina Muhando ambazo ni Hatia
44
(1972) na Nguzo Mama (1982). Mwisho ni sura ya tano ambayo ina muhtasari wa
tasnifu nzima, matokeo ya utafiti, mapendekezo na hitimisho.
4.1 Historia ya Penina Muhando
Penina Muhando alizaliwa 03/03/1948 wilayani Kilosa katika mkoa wa Morogoro
nchini Tanzania. Kwa upande wa kabila, anasema kuwa mama yake alikuwa Mnguu
kutoka Tanga na baba yake ni Mkaguru kutoka Morogoro. Penina Muhando,
alisoma katika shule mbalimbali za Tanzania na mwaka 1971 akapata shahada ya
kwanza. Baada ya kumaliza masomo hapo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, aliajiriwa
hapo hapo chuoni kusomesha Sanaa za Maonesho. Mwaka 1973 alitunukiwa
Shahada ya Uzamili ya Sanaa za Maonyesho na mwaka 1983, Muhando alipata
Shahada ya Uzamivu ya Falsafa ya Sanaa za Maonyesho hapo hapo Dar es Salaam
na kupanda madaraja hadi kufikia hadhi ya Profesa. Penina Muhando pia ni
mwanamke wa kwanza Tanzania kushika wadhifa wa Afisa Taaluma katika Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam.
Licha ya kuwa mhadhiri hapo chuoni, Penina alitumia muda wake mwingine
kuandika tamthiliya na kumfanya kuwa mmoja kati ya waandishi waliofanikiwa sana
katika uandishi wa sanaa za maonesho. Aidha, baada ya kuolewa na Bwana Mlama,
Penina alibadili jina la ubini wake na kwenda kwenye jina la mumewe hivyo kuitwa
Penina Mlama. Hata hivyo, kwenye kazi zake mbalimbali bado ameendelea
kulitumia jina lake la Penina Muhando. Katika maisha yake na mumewe Penina
amebahatika kupata watoto wawili. Kwa sasa ni mjane.
45
Mwandishi huyu kwa sasa amerudi tena katika Chuo Kikuu cha Dar es Salam
kusomesha, baada ya kupumzika kwa muda kutokana na kutingwa na majukumu ya
ukurugenzi katika asasi zinazojishughulisha na masuala ya wanawake. Baadhi ya
asasi hizo na mashirika hayo yasiyokuwa ya kiserikali aliyoyafanyia kazi ni
Foundation for African Women Educationalist (FAWE), shirika lenye makao makuu
jijini Nairobi Kenya, na pia asasi isiyo ya kiserikali iitwayo Campaign for Female
Education (CAMFED) Tanzania, yenye makao yake makuu huko Cambridge,
Uingereza.
Penina Muhando ni mojawapo wa wasomi wa kujivunia kutoka katika Chuo Kikuu
cha Dar es salaam na Tanzania kwa jumla, kwa maana ni msomi aliyesomea nchini
Tanzania, kuanzia shule ya msingi, sekondari mpaka Chuo Kikuu aliposomeshwa
Shahada ya Kwanza, ya Pili mpaka Shahada ya Udaktari wa Falsafa katika Sanaa za
Maonesho.
Penina Muhando ameandika kazi mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza
zote zikiwa na mchango mkubwa kwenye Fasihi Andishi hususani kwenye utanzu
wa tamthiliya. Baadhi ya kazi hizo ni: Hatia (1972), Tambuaeni Haki Zetu (1973),
Heshima Yangu (1974), Pambo (1975), Modern African Theatre with Special
Emphasis on East Africa (1975), Nguzo Mama (1982), Lina Ubani (1984), The
Challenge to the African Writers Today (1990), Culture and Development: The
Popular Theatre in Africa (1991), Gender Responsive Pedagogy: a Teacher’s
Handbook (2005). Kati ya kazi zilizotajwa hapo juu za kitamthiliya ni: Hatia
(1972), Tambueni Haki Zetu (1973), Heshima Yangu (1974), Pambo (1975), Talaka
si Mke Wangu (1976), Nguzo Mama (1982) na Lina Ubani (1984).
46
Profesa Penina Muhando mwandishi wa Hatia na Nguzo Mama akiwa katika
mahojiano na mtafiti ofisini kwake Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam tarehe
11/11/2013.
4.2 Hatia (1972)
4.2.1 Utangulizi
Katika utangulizi, tunaona kuwa, Hatia ni mchezo unaotuonyesha matatizo
yanayowakabili wanawake wanapoishi kwenye mazingira yenye msingi tofauti na ile
waliyolelewa nayo. Cheja ni mfano wa wasichana wengi Tanzania ya leo ambao
waendapo kuishi mjini na hali wamelelewa kijijini hutumbukia katika udanganyifu
wa kimjini ambao baadaye huwaletea matatizo wao pamoja na jamii zao.
Tamthiliya hii ya Hatia inaweza kumfaa mtu wa kiwango chochote kwa kuwa
inahusu maisha ya watu wengi katika jamii na hasa vijana. Mwandishi amedhihirisha
umahiri wake kwa kuonyesha jinsi jamii zetu zinavyowakandamiza wanawake na
kuwaweka katika nafasi duni.
47
Ni dhahiri kuwa mambo yanayozungumzwa katika tamthiliya hii, kwa hakika ni
mambo ambayo wanafanyiwa wanawake wengi katika jamii tunazoishi.
Tamthiliya ya Hatia (1972) ina jumla ya maonesho sita yenye kurasa 41. Onesho la
kwanza lina kurasa tisa. Ni onesho lililoonesha jinsi wasichana wanaotoka kijijini
wanavyokubali kudanganywa na wanaume wa mjini. Mwanamke anakubali
kushawishiwa na vijana wa mjini bila kujua kuwa kuna madhara, na bila kufanya
uchunguzi wa kina kwa vijana hao. Mfano mzuri ni mhusika Cheja ambaye
alidanganywa na Juma muuza samaki na kisha kukubali kufanya naye mapenzi.
Onesho la pili lina kurasa chache zaidi ya onesho la kwanza. Lina jumla ya kurasa
sita tu. Linaonesha juhudi za akina mama katika kushirikiana katika kazi mbalimbali
ili waweze kuyamudu maisha. Licha ya hayo, pia linaonesha jinsi mwanamke
anavyoweza kumshauri au kutoa ushauri katika mambo mbalimbali katika jamii. Hii
inaonesha kuwa, ushauri wa mwanamke katika familia au jamii ukifuatwa basi ni
wazi kuwa unaweza kuleta mafanikio. Mfano mzuri ni Mwanamke II
anavyomshauri Bw Chowe kuchukulia mambo taratibu, kutafakari na kufuata
utaratibu wa jamii zao.
Katika onesho hili la pili ndipo tunaonyeshwa jinsi mwanamke alivyo na ushirikiano
katika jamii na mshauri wa mambo mbalimbali katika jamii. Hapa mwanamke
amepewa nafasi ya kumshauri mwanaume, amesawiriwa kama mtu mwenye busara
hata katika kuamua na kufanya maamuzi mbalimbali.
48
Onesho la tatu lina jumla ya kurasa nane. Katika onesho hili ndipo tunaoneshwa
jinsi mila na desturi za jadi zinavyotenga mwanamke katika maamuzi. Mfano mzuri
ni Bi Chowe na mwanae Cheja kutokushirikishwa katika kikao cha wazee ambacho
kililenga kuzungumzia matatizo yaliyotokea katika familia yao. Pia, hapa
mwanamke anaonekana kama kitega uchumi kwa kuwa wazee wamekaa na kupanga
malipo ya Cheja bila kumshirikisha yeye mwenyewe.
Onesho la nne lina jumla ya kurasa sita. Katika onesho hili tunaoneshwa jinsi mila
na desturi za jadi zinavyotumika katika kuamua mambo. Waapishaji wanajiandaa
kwa ajili ya shughuli ya uapishaji. Kutokana na hali ya usasa na kuelimika, Sembuli
anakataa kuapishwa kwa kuwa haamini mambo hayo. Japokuwa alisingiziwa, lakini
haamini kama mila zao zinaweza kuhakikisha hilo. Hapa tunaoneshwa pia shughuli
hii ya uapishaji inafanywa na wanaume tu.
Onesho la tano lina kurasa tatu. Ndilo onesho lenye kurasa chache kuliko yote.
Katika onesho hili, tunaonyeshwa udhaifu wa mwanamke, pia tunaonyeshwa jinsi
mwanamke anavyoweza kukata tama na kufanya maamuzi ya kujiua. Mfano mzuri
ni mhusika cheja baada ya kuona vita imepamba moto kijijini anataka kujinyonga.
Pia katika onesho hili tunooneshwa jinsi mwanamke alivyosawiriwa kama mlezi.
Mfano ni Bi chowe kumtafuta mwanae kwa bidii zote ili aweze kumwokoa na mauti
kwani atamtunza yeye na mtoto wake atakayezaliwa.
Onesho la sita lina kurasa tisa sawa na onesho la kwanza. Onesho linapoanza,
wanaonekana familia zote mbili zilivyoumizwa. Vita hivi vilikuwa vita vikubwa
sana maana watu waliumia sana. Hapa ndipo mwanamke amesawiriwa kama mtu
49
mwongo katika jamii, kwa kuwa kasababisha vita kutokea kwa kusema uongo.
Mfano mzuri ni mhusika Cheja ambaye kutokana na ujinga wake wa kuyavamia
maisha ya mjini kusababisha kupata ujauzito na kisha kumtaja mtu asiyehusika kuwa
ndiye aliyehusika na ujauzito huo.
4.2.2 Uwasilishaji na Uchambuzi wa Data
4.2.2.1 Mwandishi Alivyomsawiri Mwanamke katika Tamthilia ya Hatia (1972)
kwa upande Chanya katika Nafasi na Kimajukumu
Ushirikiano
Mwanamke amechorwa kama mtu mwenye ushirikiano katika jamii. Mwandishi
amedhihirisha hili kwa kumtumia mwanamke wa I, mwanamke wa II na mwanamke
wa III pamoja na Bi. Chowe katika uk. wa 10, wanaposema kuwa:
MSIMULIZI: Kijiji kimoja katika wilaya ya Kilosa. Saa za mchana. Nje ya
nyumba ya Bwana Chowe, wanawake watatu wanatwanga
mahindi huku wakiimba wimbo wa kutwanga. Mmoja wao
Bi Chowe na wengine majirani.
Bi. Chowe: Jamani tayari yameiva. Tupepete sasa. Hivyo basi Muhando
anatuonyesha namna wanawake wanavyoshirikiana katika
jamii. Ili kurahisisha kazi wanakutana kwa pamoja na
kufanya kazi kwa kushirikiana ili waweze kumaliza mapema.
Mtafiti ameona kuwa, wanawake hupenda sana kushirikiana katika kazi mbalimbali
ambazo zinaleta maendeleo yao kiuchumi. Kama alivyoeleza Daktari Vicensia Shule
kuwa, wanawake wengi wa miaka hii ya karibuni wamekuwa na ushirikiano
mkubwa sana kiasi kwamba maisha yao yanabadilika kutoka katika hali ya
unyanyaswaji na waume zao. Anaendelea kusema kuwa, kutokana na ushirikiano
huu wa akina mama wameweza kuanzisha vikundi mbalimbali vya uwekezaji na pia
50
kujiunga na vyama mbalimbali katika ujasiriamali. Anaeleza kuwa kutokana na
ushirikiano wanaoonyesha wanawake, na manufaa ya kushirikiana kwao, wanaume
nao wameshawishika nao kujiunga na vyama mbalimbali kitu ambacho kinafanya
vyama hivyo viwe vya watu wote. Bila kuchagua wanawake na wanaume.
Anamalizia kwa kusema kuwa, ushirikiano katika jamii ni kitu muhimu sana. Umoja
ni nguvu utengano ni dhaifu
Uvumilivu
Mwanamke amechorwa kama kiumbe mvumilivu katika maisha na hata katika ndoa
yake. Hii inajidhihirisha katika uk. wa 13, anaposema kwamba:
Bw. Chowe: Acha kuniletea upuuzi hapa. Alikwambia atakuja? (Bi. Chowe
anatingisha kichwa). (Anafoka.) kwanini hukumuuliza. Vipi
yeye anafanya kutoroka na kuwasumbua akina Sembuli? Jambo
la aibu na wewe unalichekelea kama mpumbavu. Mwite hapa
Cheja sasa hivi aeleze nini kimemtorosha. Wanawake wengine
kumbe wajinga. (Bi Chowe bado amesimama ameshangazwa na
hasira za mume wake). Upesi kamlete mtoto wako kabla
ghadhabu yangu haijavuka kiwango. Shenzi kabisa.
Bw. Chowe: Hivyo wewe unajua maana ya kwenda kuleta kitu. Nimesema
nenda kamlete hapa. Punda wee! Kama kuna mambo
mmeyapanga na mtoto wako leo mtanieleza au mtaniona.
Katika uk. wa 14, mwandishi anaendelea kusema kuwa:
Bw. Chowe: hapana mama yangu. Nilifahamu hili litoto lijinga sana. Lakini
limeharibiwa na limama Lake. Sisi kwenye ukoo wetu
hatuko namna hii. Haya yanataka mpaka yapigwe ndipo
yaseme. Lakini kama ni kupiga tu kwangu si kazi hasa kwa
jambo kama hili. (Anawatishia) leo nyie, nyie! (kwa
mwanamke wa II) mama yangu; mimi na Sembuli
tunaaminiana halafu leo hili litoto linatoroka hata bila
kuaga. Kwani wamekufanyia uovu nao. ( kwa sauti) sema!
Sema! Au nitakukong‟ota sasa hivi (anainua fimbo).
51
Pamoja na kuwa Cheja kweli kafanya makosa, lakini lawama zote pamoja na matusi
anabebeshwa mama yake. Licha ya kutukanwa, Bi Chowe amevumilia na kufuata
kila analoambiwa na mume wake.
Mtafiti amegundua kuwa, wanawake wana asili ya uvumilivu katika mioyo yao.
Kwani pamoja na mateso yote ayapatayo mwanamke katika ndoa, mara nyingi
huyavumilia wala hakimbii mateso hayo. Profesa Imani Sanga na Bw Mtiro kwa
pamoja mawazo yao yanafanana. Wote waliona kuwa mwanamke ni kiumbe
mvumilivu sana katika maisha kuliko mwanaume. Wanasema kuwa, pamoja na
mateso yote ayapatayo mwanamke ikiwa ni pamoja na kupigwa, kutukanwa,
kudhalilishwa pamoja na kusalitiwa hasa katika ndoa wanavumilia. Mtiro alitoa
mfano jinsi mwanamke katika jamii za Kikurya anavyopigwa na mume wake lakini
sio rahisi mwanamke akimbie bali huvumilia ili aweze kuwalea watoto wake.
Mshauri
Pia mwanamke kachorwa kama mshauri mzuri katika jamii. Hili linajidhihirisha
dhahiri katika uk. wa 13-14, mwandishi anaeleza kuwa:
Mwanamke II: Baba mkimchukulia polepole atasema. Mbona
nyumbani ndiko alikokimbilia.
Mwanamke II : Hapana, baba, hapana. Usiyachukulie mambo kwa
ghadhabu. Usijihangaishe kumtafuta unaweza
usimwone. Na nani ajuae, kwenye jiji kubwa kama
Dalisalama lolote linaweza likutokee. Baraza letu la
wazee mbona lipo na wewe ukiwa mmoja wao.
Yafanyeni mashtaka haya kimila tu.
52
Mwanamke II: Isiwe mambo harakaharaka. Hata hao wazee wenyewe
si ajabu wengine wako wako makazini kwao kama
mkutano ni leo hawataweza.
Mwanamke II: Vumilia tu baba. Yote yategemea baraza litakapokutana.
Kutokana na maelezo hayo ni wazi kabisa kuwa mwanamke ni mshauri mzuri sana
katika jamii. Bwana Chowe alitaka kuchukulia mambo kwa pupa lakini kutokana na
ushauri wa mwanamke wa pili alipunguza hasira na kisha kufuata utaratibu
unaotakiwa.
Mlezi
Mwanamke amechorwa kama mlezi na mtu mwenye huruma. Mfano mzuri ni Bi
Chowe alivyokuwa analia kuhusu ujauzito wa mwanae na kuhangaika kumwokoa
alivyotaka kujinyonga. Haya yanajidhihirisha katika uk. wa 31 kuwa:
Bi. Chowe: Uuuuuuuuuuuu! Uuuuuuuuuuuuuuuu! Mie, ooooooooo
maskini mie (mara hiyo mzee wa 1 na 2 wanafika tena
wanakimbia kutoka upande walioelekea mwanzo
wanashtuka kumwana Bi. Chowe.)
Mzee 2: Nini tena jamani?
Mzee 1: Kuna jambo lolote lililotokea?
Bi. Chowe: Eee wazee wangu, mimi leo sijui Mungu kanionaje.
Namtafuta Cheja kapotea.Watoto wamesema wamemwona
ametoka ameshika kamba. Uuuuuu! Labda anataka kwenda
kujinyonga.
Mzee 2 : Jamani huyu mtoto vipi lakini?
Bi. Chowe: Cheja mwanangu angekaa tu hata huyo mototo nitalea
mimi. Niacheni nimtafute upesi kabla hajajiua. (Anatoka
mbio)
53
Licha ya mwanamke kuonekana kama mshauri pia mwanamke amechorwa kama
mtu mwepesi kuomba msamaha. Hii inajidhihirisha katika uk. wa 38, Cheja
anaposema kuwa:
Cheja: Nimesema mwacheni. Iliyobaki naomba mnisamehe.
Mnisamehe wazee wangu, hasa mzee Sembuli, mnisamehe.
Hivyo basi, mwandishi amemwonyesha mhusika Cheja kama mfano mzuri wa
mwanamke baada ya kugundua kuwa amekosa amejirudi na kuomba msamaha.
Mbunifu
Mwanamke kachorwa kama mtu mbunifu na mwenye uwezo wa kujitegemea bila
msaada wa mwanaume. Mwandishi anadhibitisha haya katika uk. wa 39, anaposema
kuwa:
Cheja: Juu ya maisha yangu niachieni mimi mwenyewe. Nitakwenda
Majogo.
Bi. Chowe: Uende wapi tena? Utulie nyumbani sasa. Unaanza kusema nini
tena?
Cheja: Ndio mama. Nitakwenda majogo nijiunge na hao walioanzisha
kijiji kipya.
Nitashirikiana nao katika kazi nijitegemee.
Kutokana na maelezo hayo basi, ni dhahiri kuwa mwanamke anaweza kujitegemea
mwenyewe hata bila kumsubiri mwanaume amletee.
Mtafiti amegundua kuwa, mwanamke pia akidhamiria jambo anaweza. Sio kwamba
mwanamke humtegemea mwanaume kwa kila kitu, bali wanawake nao wana juhudi
mbalimbali ambazo zinachangia au zinatoa mchango mkubwa katika familia.
54
4.2.2.2 Mwandishi Alivyomchora Mwanamke katika Tamthilia ya Hatia (1972)
kwa upande Hasi katika Nafasi na Kimajukumu
Rahisi kushawishika
Mwanamke amechorwa kama mtu ambaye ni rahisi kushawishika. Mfano mzuri ni
Cheja. Hii inaonekana wazi katika uk. wa 8 asema kuwa:
Juma: Lahaula! Unafanya nini mahali kama hapa peke yako?
Unatoka wapi na unakwenda wapi?
Cheja: Popote. Juma nimekuwa nikikutafuta hii wiki ya pili.
Nimefika nyumbani kwako lakini nimeambiwa
ulishahama. Nimejaribu sana kukupata ulipo bila
mafanikio.
Juma: (Anahamaki) Vipi nini? Kitu gani kinakufanya unitafute hivyo?
Cheja: Haa, Juma mpenzi. Ni wewe kweli unauliza kwa nini
ninakutafuta! Hayo yote tuyaachilie mbali. Nina jambo
kubwa la kukuambia, Juma.
Juma: (Akimkodolea macho) jambo gani?
Cheja: (polepole) Juma yale mambo ya siku ile. Nina mimba.
Kutokana na hayo, mwandishi anaonyesha kuwa, Cheja kashawishiwa na Juma na
kisha kufanya naye mapenzi na hatma yake ni ujauzito ambao Juma hataki hata
kusikia. Anamkataa, anasema kuwa yeye hahusiki. Cheja alitoka kijijini na kuvamia
maisha ya mjini. Matokeo yake kashawishiwa na Juma naye akakubali kwa haraka
bila kuwaza kuwa wanaume wengi wa mjini ni matapeli na ni waongo. Yeye alitaka
tu kutimiza haja zake na kisha kumwacha.
Kitega Uchumi
Mwanamke amechorwa kama kitega uchumi katika jamii. Haya yanadhihirika wazi
katika uk. wa 11 pale mwandishi anaposema kuwa:
55
Bi. Chowe: Ndugu yangu wee! huyo mkami kwani ni mtu wa kuoa hivi
karibuni? Anangojea mali ya dada yake ndio aoe nayo.
Hapa mwandishi anatuonyesha kuwa, mtoto wa kike katika jamii ni kama
kitegauchumi kinachotegemewa na familia. Endapo mtoto wa kike akiolewa,
watapata fedha na vitu ambavyo vitawasaidia katika familia. Kama ilivyoonekana
kwa mhusika Cheja ambaye ni binti, na Mkami ni kijana ambaye anategemea kuoa
endapo dada yake ataolewa na kutolewa mahari na ndipo sehemu ya mahari hayo
itolewe kwa ajili ya Mkami.
Daktari Vicensia Shule, Daktari Mona Mwakalinga na Profesa Imani Sanga kwa
pamoja mawazo yao kuhusu mwanamke kama kitega uchumi yanafanana.
Wameeleza kuwa suala la mwanamke kuonekana kama kitega uchumi ni la muda
mrefu hasa katika kipengele cha mahari.
Wazazi wengi wanawaozesha watoto wao wakiwa katika umri mdogo lengo lao ni ili
wapate mali kupitia mtoto huyo. Imeonekana kuwa ni tatizo kubwa kwa jamii
nyingi za Kiafrika kumbadilisha mtoto wa kike na vitu kwa lengo la kujinufaisha
kimaisha. Wao wameona kuwa kutokana na mila na desturi za jamii zetu
zinasababisha mwanamke kuwa kitega uchumi katika familia
Chombo cha Starehe
Mwanamke amechorwa kama chombo cha starehe katika jamii. Katika uk. wa 1-9
mwandishi anaonyesha haya anapoeleza kuwa:
Cheja: Haa, Juma mpenzi. Ni wewe kweli unaniuliza kwa nini
ninakutafuta! Haya yote tuyaachilie mbali, nina jambo
kubwa la kukuambia Juma.
56
Juma: Una mimba? Yangu mimi.
Juma: Unasema upange na nani? Kama una maana upange na mimi,
tafadhali sana dada tusiingiliane. Yanakuhusu wewe
mwenyewe.
Kwa maelezo hayo, mwandishi anaonyesha kuwa, Juma hakuwa anampenda Cheja
bali haja yake ni kupata starehe yake aliyokuwa anaihitaji. Alihitaji kuburudika tu na
kuondoka, lakini ujauzito ulipotokea hakutaka hata kusikia, anadai yeye hahusiki.
Mtafiti amegundua kuwa, mwanamke anakuwa kama chombo cha starehe kwa
mwanaume kwa sababu mwanaume akishafanya anachokitaka mambo
yatakayotokea baadaye kama ujauzito hujidai hahusiki. Lakini wakati anamtaka ili
kukamilisha haja zake hujidai anampenda kumbe lengo lake ni kumchezea tu ili
akamilishe haja na starehe yake. Wanawake wengi wakishaambiwa na mwanaume
kuwa anampenda, basi hujikuta akisahau kila kitu na kumwona huyo mwanaume
kuwa ndiye wa maana kwake. Mara nyingi wanawake husahau yatakayotokea
baadaye. Majuto huja baadaye na kukumbuka mapenzi aliyokuwa akipewa na ndipo
huanza kuiona dunia ni mbaya.
Mwongo
Mwanamke amechorwa kama mtu mwongo, tapeli na asiyekuwa mwaminifu ambaye
anadanganyika. Kwa kudhihrisha hili, katika uk. wa 8 na 14 mwandishi anasema
kuwa:
Cheja: Sasa nyumbani nitasema nini ikiwa wewe hapa unanikana?
Juma: Aaa (kwa uovu) hivyo ndiyo shida yako? Waambie kosa hilo
limetendwa na mwajiri wako.
Juma: Tena basi. Wewe tazama. Yule bwana Sembuli mnatoka naye
kijiji kimoja kwa hiyo wazazi wako wanamfahamu. Licha
ya hayo unaishi nyumbani kwake.
57
Mwandishi anaonyesha jinsi Cheja alivyo mjinga anashawishiwa kwenda kusema
uongo naye anakubali bila kufikiria juu ya kumsemea uongo mtu ambaye hajatenda
kosa hilo. Mwandishi anaendelea kudhihirisha hili kwa kueleza kuwa:
Cheja: (kwa kusita hali akiwa bado katazama chini) Bwana Se….
Bwana Sembuli alinikosea kwa nguvu na sasa mimi ni
mjamzito.
Hivyo basi, mhusika Cheja anakubali kusema uongo ili mtoto atakayemzaa apate
matunzo na yeye mwenyewe kutunzwa, kitu ambacho si haki yake.
Mwanamke kama Chombo cha Biashara
Mwanamke amesawiriwa kama chombo cha biashara katika jamii. Hii
imejidhihirisha pale ambapo wazee wanapanga mali wanazotakiwa kulipwa na
Sembuli, uk. wa 18, anasema kuwa:
Mzee Chimaisi: Haya sasa basi kama alivyokuwa akisema mzee mwenzetu
hapo mwanzo, adhabu ya Sembuli ni malipo. Na kama
ilivyo jadi yetu malipo yenyewe ni sehemu tatu kwa vile
ametumia nguvu. Kwanza malipo ya wazazi, pili, malipo
ya msichana mwenyewe, na tatu malipo ya kumtunza
mtoto atakapozaliwa. Sasa basi tuanze malipo ya wazazi.
Kwa muktadha huu, tunaona kuwa mwanamke anafanywa kama chombo cha
biashara katika jamii, hasa wanafamilia kujipatia kipato kikubwa kwa kupitia ya
mtoto wa kike.
58
Mwanamke hana Maamuzi
Mwanamke amesawiriwa kama mtu ambaye hana maamuzi na asiyeweza
kushirikishwa katika vikao vya kufanya maamuzi. Mwandishi ameonyesha haya
katika uk. wa 21, anasema kuwa:
Mzee 1: Wazee sasa mnataka kujidharau wenyewe pamoja na jadi yetu.
Mna maana kusema kuwa sisi wazee wote hapa na mvi zetu
tumeshindwa na jambo hili hata tumwite mwanamke, tena
msichana mdogo, aje aseme? Mliona wapi mambo kama haya
jamani?
Kwa maana hiyo, tunaona wazi kabisa jinsi tamaduni zinavyozidi kumkandamiza
mwanamke na kumnyima haki ya kutoa mawazo.
Mwanamke Kama Mtu wa Kukata Tamaa
Mwanamke amechorwa kama mtu ambaye hukata tamaa kwa haraka. Hii
imejidhihirisha kaitka uk. wa 30-31, mwandishi anaposema kuwa:
Cheja: (anatoka mafichoni pake na kukimbilia upande wa pili)
lazima nijinyonge wasije wakanikuta wakaniuliza.
Nitasemaje?
Hii inaonyesha kuwa ni rahisi sana mwanamke kukata tamaa anapopatwa na
matatizo makubwa, kama mhusika Cheja anavyotaka kujiua kutokana na matatizo
yaliyompata.
Utafiti huu umeona kuwa, mwanamke ni mtu ambaye hawezi kukabiliana na
vikwazo katika maisha bali ni rahisi sana kukata tamaa kutokana na mambo
anayoyapata katika jamii. Na mara nyingi maamuzi huwa ni kujinyonga au kujiua
kwa njia yoyote ile.
59
Mwanamke kama Mtegemezi
Mwanamke amechorwa kama kiumbe dhaifu, bila mwanaume hawezi. Mwandishi
ameonyesha haya katika uk. wa 36, anaposema kuwa:
Cheja: (kwa uchungu) yaani kweli, Juma. Imekuwa si kitu kwako
litakalonipata baadaye.
Hunifikirii nitamfanyaje mtoto. Uk. wa 9.
Mwandishi anaedelea kusema kuwa:
Cheja: …..lakini nilidhani kwa kufanya vile mtoto wangu atapata
matunzo kama watoto wengine. Mimi mwenyewe ningepata
matunzo kama wengine. Uk. wa 38.
Hii ni wazi kabisa kuwa, mwanamke bila mwanaume hawezi kuyakabili maisha.
Ndio maana mhusika Cheja akaamua kukubali kumsingizia Bwana Sembuli ule
ujauzito ili aweze kupata matunzo.
Mwanamke kama Kiumbe Kinachonyanyasika
Mwanamke amesawiriwa kama kiumbe kinachonyanyasika na kunyanyaswa na
mwanaume. Hii imejidhihirisha katika uk. wa 13, anaposema kuwa:
Bw. Chowe: Hivyo wewe unajua maana ya kwenda kuleta kitu.
Nimesema kamlete hapa. Punda wee! Kama kuna mambo
mmeyapanga na mtoto wako leo mtanieleza au mtaniona.
Hapa mwanamke ananyanyasika kwa kutukanwa matusi na mumewe, jambo ambalo
linasikitisha kwa kuwa anatukanwa wakati kosa katenda mwingine. Mwanamke
ameonekana kama chanzo cha matatizo yaliyotokea katika familia ya bwana Chowe.
60
4.2.3 Mjadala na Dhamira Zilizoibuka Kutokana na Uchorwaji wa Mwanamke
katika Tamthiliya ya Hatia (1972)
Ukombozi wa Mwanamke
Suala la ukombozi wa mwanamke limekuwa likijadiliwa na waandashi wa kazi za
fasihi toka zama za kale, kuwa mwanamke anakabiliwa na matatizo ya
kukandamizwa, kunyanyaswa na kunyimwa haki zake. Muhando katika tamthiliya
ya Hatia amejadili matatizo yanayomkabili mwanamke na mbinu za kukabiliana na
matatizo hayo. Kwa mfano, Cheja anapewa mimba kisha anakanwa na kutelekezwa
na Juma kijana anayeishi mjini. Katika kutatua matatizo kama haya, Muhando
anaamini kuwa jamii iungane kuwaelimisha vijana wanaofanya uhalifu kama huo.
Ijapokuwa zoezi hilo ni endelevu kwani halitafanyika kwa siku moja. Zingatia
maongezi yafuatayo:
Sembuli: Cheja akishanieleza juu ya kijana huyu nitafanya chini juu
impate. Halafu nitajaribu kwa njia zozote kumwelewesha
ubaya wa maisha anayoendesha…
Mzee 3: Lakini kama kijana mwenyewe ni muhuni tu wa mjini
atayasikiliza maneno yako?
Sembuli: Itachukua siku nyingi na njia nyingi pia kubadilisha
mwenendo huu… uk. 40
Utafiti huu umegundua na kuona kuwa, suala la ukombozi wa mwanamke ni suala la
kimchakato. Mwanamke pekee ndiye anayeweza kujikomboa mwenyewe na sio
kusubiri mwanaume kumkomboa. Mtafiti amegundua kuwa, mwanamke anapaswa
kujishughulisha katika kazi mbalimbali na sio kuchagua kazi ndipo aweze
kujikomboa katika nyanja mbalimbali za maisha.
61
Profesa Imani Sanga katika mahojiano na mtafiti yaliyofanyika tarerhe 08/11/2013,
anasema kuwa, mwanamke ili aweze kujikomboa asijione kuwa ana tofauti na
mwanaume kimajukumu katika jamii, anapaswa kufanya shughuli zote zilizopo
katika jamii ili aweze kuchangia katika kuinua uchumi pamoja na shughuli zote za
kimaendeleo. Mwanamke anapaswa apate elimu sawa na wanaume, ajishughulishe
katika kazi mbalimbali. Anaendelea kusema kuwa, hata siku hizi wanawake hupiga
vinanda makanisani au sehemu za ibada, pia ni waweka hazina pamoja na
waongozaji wa kwaya au nyimbo. Kwa upande mwingine anasema kuwa kampeni
hizi za ukombozi wa mwanamke, zimesaidia sana kuwafanya wanawake wajitambue
na kujinasua katika unyanyaswaji. Vilevile anadai kuwa, ni kwa kiasi kidogo sana
kwa sasa zile kazi ngumu na za kutumia nguvu zinaonekana kuwa za wanaume, ila
kwa kiasi kikubwa wanawake wameweza kujikomboa hata kiuchumi.
Hata hivyo mafeministi wa Kimarx wanasema kwamba kinachotakiwa ni kuwaweka
wanaume na wanawake katika daraja au tabaka moja yaani asiwepo aliye mkuu au
bwana kwa mwenzake. Kwa mtazamo wao ni kwamba kazi zinazomhusu
mwanamke zinabaki kuwa zile zile lakini ikitokea anataka nafasi katika ngazi ya
jamii basi kusiwepo na matabaka.
Mwanamke katika Kufanya Maamuzi
Uwakilishi wa Wanamke ni mdogo sana popote pale maamuzi yanapofanyika bila
kujali ngazi au taasisi inayohusika. Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) (2001;44-
45), wanaeleza kwamba, tofauti ni kubwa kati ya wanawake na wanaume katika
masuala ya jamii yanayojitokeza serikalini katika ngazi ya uongozi na ufanyaji wa
maamuzi. Licha ya ukweli kwamba, katiba ya mwaka 1977 pamoja na kufanyiwa
62
marekebisho mwaka 1984 inatoa haki sawa kwa wanawake na wanaume, kupiga
kura na kutumikia umma, bado uwakilishi wa wanawake ni mdogo sana.
Ufanyaji wa maamuzi katika ngazi ya kaya bado sio wa kidemokrasia, kwani
wanawake na watoto hawahusishwi.
Umasikini
Suala la umasikini na hali ngumu ya maisha ni tatizo ambalo huwakumba watu
mijini na vijijini. Katika tamthiliya ya Hatia, Muhando amejadili suala la umaskini
na jinsi linavyowakatisha tamaa watu na kujiona wanyonge siku zote. Kwa upande
mwingine, watu wa vijijini huamua kwenda mijini kutafuta kazi ili kupambana na
umasikini lakini kuna msemo usemao „mjini kisomo‟ kwani watu wengi
wanaokimbilia mijini hukumbana na masaibu na kushindwa kukabiliana nayo. Kwa
mfano Cheja kapewa ujauzito na kutelekezwa hivyo kuongeza umaskini katika
familia. Rejea maongezi ya Bi Chowe; „…Kwanza hii yote shauri ya umaskini tu.
Mwanangu asingekwenda kufanya kazi Dalisalama…‟ Uk 10.
Mwanamke Kama Mlezi
Muhando amemchora mwanamke katika nafasi mbalimbali, katika Hatia amemchora
mwanamke katika nafasi mbalimbali kama mzazi, mlezi wa watoto, msimamizi wa
masuala ya familia ikiwemo kuandaa chakula, kwa mfano Bi. Chowe, Mwanamke I
na II ni wazazi na walezi wa familia.
Mtafiti amegundua kuwa, katika tamthiliya kinamama ni watu wenye bidii katika
kulea watoto na watu wenye huruma. Mfano mzuri ni Bi Chowe alivyokuwa akilia
63
baada ya kuambiwa kuwa Cheja ni mjamzito. Pia alijitoa katika kumlea yeye
mwenyewe pamoja na mtoto atakayezaliwa.
Dkt Vicensia Shule katika mahojiano yaliyofanywa tarehe 08/11/2013 pamoja na
mtafiti anasema kuwa, katika jamii zetu, wanawake ndio wenye jukumu kubwa la
kuwalea watoto iwe wa kike au wa kiume. Anaendelea kusema kuwa, iwapo mtoto
wa kike akiharibikiwa au akipata matatizo kama vile mimba na kuacha shule au
kufeli, basi lawama zote hupewa mama. Baba anaona kuwa mwenye makosa ni
mama na hivyo lawama zote hupewa mama. Licha ya akina mama wengi kuwa pia
na jukumu la kuleta kipato katika jamii au familia, lazima ahakikishe kuwa anawapa
watoto malezi bora.
Hivyo basi utafiti huu umeona kuwa, mwanamke anajukumu kubwa la kulea familia
licha ya kuwa na shughuli nyingine mbalimbali za kuleta kipato katika jamii.
Mwanamke ameonekana kuwa, muda mwingi huwa na watoto tofauti na baba.
Unyanyaswaji
Kwa upande wa pili mwanamke amechorwa kama kiumbe duni asiyejitambua,
anakandamizwa na ananyimwa haki. Hivyo wanaume hutumia mwanya huo
kumchukulia mwanamke kama mtu asiyekuwa na msaada wowote katika familia na
jamii kwa jumla. Kwa mfano, Juma anampa ujauzito Cheja baadaye anamkana na
kumtelekeza. Halikadhalika, Bw. Chowe anamdhalilisha mwanamke kwa maneno
yafuatayo:
Mimi kila siku nawaambia watoto wa kike ovyo sana
mnabisha…Acha kuniletea upuuzi hapa … Jambo la aibu na
64
wewe unalichekea kama mpumbavu…Jamani wanawake
wengine kumbe wajinga…shenzi kabisa…punda wee! uk. 12
na 13
York na wenzake (1991) wanaeleza kwamba, tofauti kubwa kati ya mwanamke na
mwanaume mbali na jinsi, ni ile ya mwanamke kunyanyaswa, na mwanaume ndiye
mnyanyasaji. Wanazidi kueleza kwamba, mwanaume hashiriki kabisa katika
kunyanyaswa ila yeye ndiye anayefaidika. Hiyo ndiyo sababu wanawake walitaka
kujikomboa wenyewe bila kuwashirikisha wanaume, kwani walijiona wao ndio
waathirika wakubwa wa unyanyasaji.
Unyanyasaji na usaliti wa kimahusiano umechorwa kimzaha ili kuishambulia asasi
ya ndoa ambayo imepoteza heshima yake. Kuhusu suala hili, mafeministi Leathwood
Carole na Hay Valeria (2006), wanasema kwamba sababu sio kukandamizwa bali
kuelewa kuwa maisha ya kiukandamizwaji aishiyo mwanamke hayasababishwi na
ujinsia tu bali pia na ubaguzi, umri, na utabaka. Urazini huo ndio uliomuinua Bi
Chowe kuamua kuvumilia matusi aliyokuwa anatukanwa na mume wake mbele ya
wanawake wenzake.
Msanii yeyote yule hufanya sanaa yake kulingana na mazingira yaliyomzunguka
kama asemavyo Kezilahabi (1983:230) katika Makala ya Semina za Kimataifa ya
Waandishi wa Kiswahili III, anasema kwamba:
Waandishi wengi waliofanikiwa ni wale waliowaweka
wahusika wao chini ya misingi ya mazingira
wanayoyaelewa na hasa yale ya kabila lao, ili kuweka
hadharani tatizo la kitaifa.
65
Waandishi wanavyomchora mwanamke katika hali ya kunyanyaswa na kuumizwa
kila mara hutokana na hali halisi waionayo katika mazingira halisi
yanayowazunguka. Na hili linathibitishwa na mafeministi wanaosema kwamba,
wanawake wote wanaishi katika hali ya kunyanyasika lakini ni wajibu wa kila
anayenyanyasika kujikomboa (York na wenzake 1991).
Mwanamke kama Chombo cha Starehe
Pia mwanamke anaonekana kuwa mwili wake ni chombo cha starehe kwa
mwanaume. Free Encyclopedia inaeleza jinsi mwili wa mwanamke unavyohusishwa
na udunishwaji kwamba mwanamke ni kama kitu/kifaa, mali, na hata bidhaa
inayoweza kubadilishwa miongoni mwa wanaume. Tamaa ya mapenzi inamfanya
mwanaume kutokuridhika na mke wake, hivyo miili ya wanawake anaifanya kama
bidhaa ambayo inaweza kubadilishwa tu na kwa wakati wowote.
Katika tamthiliya ya Hatia, mhusika Juma ameonekana kumdanganya Cheja kuwa
anampenda na hatima yake Cheja kukubali kufanya naye mapenzi, kumbe lengo la
Juma ni kujifurahisha na kutimiza haja zake na sio kuwa anampenda Cheja. Mtafiti
amegundua kuwa, wanawake wengi hutumiwa kama chombo cha kumstarehesha
mwanaume na kutimiza haja za wanaume kwa kufanya nao mapenzi wakijua kuwa
wanapendwa kweli. Jambo hili limezungumziwa pia na Dkt Vacensia Shule katika
mahojiana na mtafiti tarehe 08/11/2013. Anaeleza kuwa wanawake wengi
wanadanganyika kuwa wanapendwa bila kufanya utafiti kuwa kama ni upendo wa
ukweli. Hivyo hujikuta tayari wameshamkubalia mwanaume, lakini lengo la
wanaume ni kutaka kutimiza haja zao au hamu yao ya mapenzi na baada ya hapo
hawana tena habari na mwanamke huyo bali huishia kumtafuta tena mwanamke
66
mwingine. Anaendelea kusema kuwa, wanaume huwachezea wanawake kwa kufanya
nao mapenzi ili tu kutimiza haja zao na kutaka kujua mwili wa kila mwanamke
wanayemwona ili kupata tu starehe.
Mwanamke kama Kitega Uchumi
Tamthilia hii pia inatuonyesha kuwa, hadhi ya wasichana katika jamii imejikita
katika uwezekano wa kuwatumia kupata mali. Hivyo mabinti ni vitega uchumi
miongoni mwa jamii nyingi za kiafrika. Binti hathaminiwi kwa kuwa ni binadamu
mwenye uwezo na nguvu. Katika jamii nyingi za Kiafrika, wanawake wanaishi kwa
ajili ya watu wengine hususani mwanaume. Kama si baba basi kaka au ndugu wa
kiume. Mfano mzuri Mkami, ni mwakilishi bora wa imani kuwa mwanamke ni
kitega uchumi kwa manufaa ya mwanaume.
Katika tamthiliya hii Mkami anathibitisha imani inayowafanya wanawake
wadunishwe katika jamii. Maneno yafuatayo yanathibitisha:
Mkami : (kwa haraka) Ng‟ombe saba, mbuzi tisa na kuku watatu.
Mzee Chimaisi: (huku akicheka) Babu vipi? Unataka ujipatie ng‟ombe
wa kuolea hapohapo?
Mkami: Ndio, kwanza huyu dada yangu angeolewa vizuri angepata
zaidi ya hizo. Uk. wa 18
Mtafiti amegundua kuwa, wanawake wamepewa hadhi ya chini kwa kuwa,
wanadhalilishwa mno. Wanadhalilishwa kwa kuwa miili yao na utu wao unatumiwa
katika kuipatia familia kipato. Pia mwanamke anaweza kutumia mwili wake ili
kuweza kupata mahitaji mbalimbali ya kijamii na kujikimu kimaisha. Hii
inasababisha kushusha utu wake na thamani yake katika jamii.
67
Mwanamke katika Utamaduni
Katika utamaduni mwanamke amechorwa pia kwa hali ya kudhalilishwa, kuaibishwa
kuonewa, kunyanyaswa na kukandamizwa. Kwa kuwa mwanamke tangu kale
utamaduni ulimtaka awe mtu mnyenyekevu, mtiifu kwa mumewe, basi ameendelea
kunyanyasika na kudhalilishwa. Simone de Beauvoir (1972) ni miongoni mwa
wanawake wanaoipiga vita mitazamo ya kitamaduni inayomuona mwanamke kama
kiumbe dhaifu.
Utamaduni ndio unaoweka alama zinazoonesha nafasi na majukumu ya mwanamke
na mwanaume. Kipengele cha utamaduni kinatengeneza mazingira ya
kumkandamiza mwanamke asifikie ngazi za juu za uongozi kwani wanaume
hawaamini kama wanawake wanaweza kuwaongoza vizuri kabisa na kuyatimiza
maamuzi ya wanaume na wanawake kwa usawa. Siku zote wanaume wanapata
mashaka juu ya uongozi wa mwanamke katika suala la uongozi (Bond, 2000). Pia
huweka alama ambazo hulingana na uthamani wa kijinsia. Hapa basi, wanaume ni
wanajamii walio katika tabaka la juu na wanawake katika tabaka la chini. Kwa
mfano kazi zinazofanywa na wanawake hazionekani kuwa ni muhimu wala kuwa ni
kazi za kimaendeleo. Hata kama zikionekana kuwa muhimu, muonekano huo
hauelezewi katika ngazi ya jamii isipokuwa katika ngazi ya familia tu. Rosaldo
(1974), anaona kuwa mwanamke wakati wote anachorwa katika mtazamo hasi na
haoni kama kweli kuna ukumbozi wa jinsia ya kike kutokana na mfumo wa utawala
wa kiutamaduni ambao unamilikiwa na wanaume.
Mtafiti amegundua kuwa, kutokana na utamaduni au jadi ya Mwafrika, mwanamke
inambidi avumilie yote yanayotokea akiwa kwa mume wake. Mfano mzuri ni Bi
68
Chowe ambaye anavumilia manyanyaso yote ya mumewe kwa sababu ya matatizo
yaliyompata Cheja. Kutokana na utafiti huu tumeona kuwa, ni vigumu mwanamke
aliyekulia katika utamaduni au jadi ya kiafrika kuyakimbia matatizo yatakayompata
akiwa kwa mumewe. Yampasa ayakabili na kuvumilia kwa kuwa hawezi kuondoka
tena.
Mwanamke kutolewa mahari wakati anaolewa ni jambo la kiutamaduni katika jamii
nyingi za Tanzania na labda Afrika. Mahari inaweza kuonekana kama ishara ya
umoja kati ya familia mbili na wengine wanadai kuwa ni ishara ya kuaminiana na
haina tofauti na mila za Kimagharibi za kuvishana pete (FEMA, 2010). Lakini suala
hili la kiutamaduni linamfanya mwanamke kuwa mfungwa au mtumwa wa
mwanaume hivyo kushusha hadhi ya mwanamke na kumfanya awe mali ya
mwanaume. Kama asemavyo Balisidya (1982), fasihi simulizi inadhihirisha kwamba
mwanamke alifundishwa tangu kale. Tena anajua kwamba akiisha kutolewa mahari
hawezi kumkimbia mume wake wala familia ya mume wake hata kama ataonewa,
atanyanyaswa na kukandamizwa. Lakini hata hivyo inampasa kuvumilia tu pale pale
kwani yuko kwenye kifungo cha mahari ambayo wazazi wake hawawezi kuilipa
tena.
Utafiti uliofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania
(TAMWA), kama walivyonukuliwa na timu ya FEMA (2010), umehusisha ulipaji
mahari na unyanyasaji wa wanawake. Utafiti huo umeonesha kuwa unyanyasaji huo
unaohusishwa na mahari ni kama vile wasichana kukatishwa masomo ili waolewe,
kuvumilia vipigo na kupoteza haki ya kumiliki mali.
69
FEMA (2010) wanasema kuwa, ijapokuwa ni utamaduni wa Watanzania na
Waafrika kwa ujumla kwamba, wanawake baada ya kuolewa wanatarajiwa
kuhudumiwa na kulindwa na waume zao, lakini matokeo yake wanawake sasa
wanakuwa hawana mamlaka katika jamii, wamebakia majumbani, na kuzaa watoto.
Pia utamaduni unamnyanyasa mwanamke kwa sababu mwanaume katika jamii
nyingi habebi wala kufanya kazi yoyote ile ambayo inaonekana kuwa ni ya akina
mama. Wengine wanahofia kuchekwa na wengine ni ujeuri tu na kukosa huruma.
York na wenzake (1991) wanaelezea ukombozi wa mwanamke katika mojawapo za
kanuni za ukombozi wa mwanamke kwamba:
Wanawake wote wanashiriki katika unyanyaswaji
mmoja tofauti kubwa kati ya wanawake na wanaume
(mbali na ujinsia) ni kwamba unyanyasikaji wa
wanawake ni maalumu kwa faida ya wanaume ambapo
wanaume ndio wanyanyasaji. [Tafsiri yangu]
Umoja na Ushirikiano
Katika tamhiliya ya Hatia (1972) mwandishi anaonyesha jinsi wanawake walivyo na
umoja na ushirikiano katika mambo mbalimbali. Mfano ni katika wanawake wa kijiji
cha Bi Chowe wanavoshirikiana katika kutwanga mahindi. Hii imejidhirisha katika
uk. wa 10 anaposema
MSIMULIZI: kijiji kimoja katika wilaya ya Kilosa. Saa za mchana.
Nje ya nyumba ya Bana Chowe. Wanawake watatu
wanatwanga mahindi huku wakiimba wimbo wa
kutwanga. Mmoja wao ni Bi. Chgowe na wengine ni
majirani.
70
Mwandishi huyu amemchora mwanamke kama mtu anayependa ushirikiano katika
jamii. Hii ni wazi kabisa kuwa wanawake hujibidiisha katika kazi mbalimbali ili
kuweza kuondoa umaskini na pia ili waweze kujikomboa wao wenyewe. Mtafiti
amegundua kuwa, akina mama katika tamthilia hii wamechorwa kama watu wenye
umoja katika kufanya mambo mmbalimbali katika jamii.
4.3 Nguzo Mama (1982)
4.3.1 Utangulizi
Katika tamthiliya hii mwandishi anasema kuwa, toka Umoja wa Mataifa kutangaza
kwamba mwaka 1975 ni mwaka wa wanawake duniani, juhudi mbalimbali
zimekuwa zikifanywa kuwakomboa wanawake kutokana na ukandamizwaji na
udhalilishwaji. Je harakati hizi ambazo zimeendelea toka wakati huo mpaka sasa
zimepata mafanikio na matatizo gani? Nguzo Mama ni tamthiliya inayochambua
matatizo yanayowakabili kina mama katika juhudi zao za kuendesha harakati hizi za
kujikomboa. Kwa kupitia tamthiliya hii ndipo tutagundua au tutaona kama harakati
hizi zimeleta manufaa au la.
Tamthiliya ya Nguzo Mama (1982) ina maonesho manne yenye jumla ya kurasa 59.
Tamthiliya hii imeundwa hivi kwamba, onesho linalobeba dhamira kuu limepewe
nafasi zaidi. Katika kuhakikisha hilli, onesho la kwanza lina kurasa kumi tu ndilo
onesho fupi kuliko yote. Ni onesho linaloelezea juhudi mbalimbali zinazofanywa
na akina mama wa Patata katika kujaribu kusimamisha Nguzo Mama. Kila
mwanamke kuwa na wazo tofauti na mwenzake akiamini moja kwa moja kuwa,
ndilo litakalofaa kuinua Nguzo Mama. Mfano, Bi. Moja anapendekeza dhahabu,
fedha, uturi na maua. Bi. Pili kwa upande wake anaonelea jembe lenye mpini mrefu
71
au mfupi, chungu mdomo mdogo au kikapu cha gogo. Bi. Tatu, lake ni mabenzi,
mavolvo, ST au SU yote hayo ni mawazo tu ya akinamama katika kukabiliana na
kuinua Nguzo Mama. Pamoja na kuwepo kwa mawazo mazuri ya akina mama
wanakwamishwa na baadhi yao kama akina Bi. Nane. Pia katika onesho hili wapo
wawakilishi wa wanawake wenye fikra pevu mfano mzuri uk wa 7 pale Bi Nne
anaposema: “Bora tufanye mikutano, badala ya maandamano, maazimio tutoe na
sana tuyatangaze”.
Onesho la pili lina kurasa zaidi ya kwanza lina kurasa 19. Ndilo onesho refu kuliko
mengine. linaonesha visa na vituko zaidi katika kumwandaa msomaji kufahamu
matatizo wanayokutana nayo wanawake, katika juhudi za kusimamisha Nguzo
Mama. Ni onesho linaloelezea juhudi mbalimbali zinazofanywa na wanawake
katika kuinua Nguzo Mama. Mfano, uk. wa 12 Bi. Nane anasema: “Mnajua
NGUZO MAMA haiwezi kusimama mpaka tuivute kwa kamba”. Bi. Nane
anajaribu kutoa maarifa ambayo yatasaidia kuinua Nguzo Mama. Mwandishi
anatuonesha kuwa, wakati akina mama wanajaribu kuinua Nguzo Mama kuna
wengine wanajaribu kukwamisha zoezi hili kutokana na chuki zao. Kwa mfano,
katika uk. wa 13 tunaoneshwa Bi. Nne akisema: “Aaa! Kaanza Bi. Nane mambo
yake. Alikaa wapi? NGUZO MAMA ilipoletwa hatukumwona hapa, wala kwenye
maandamano hakuja. Sasa watu wanapanga mambo vizuri ndio anajidai. Alikuwa
wapi siku zote, acheni! tupeni kwamba hizo”.
Katika onesho hili la pili ndipo tunapooneshwa kuwa, wanawake wamechorwa
kama wajasiriamali wanaojishungulisha na miradi midogomidogo itakayoweza
kuleta maendeleo. Mfano tunaoneshwa Bi. Pili akipika na kuuza pombe katika
72
kilabu. Pamoja na kufanikiwa kwa Bi. Pili kupata pesa kidogo nyumbani
anakumbana na kikwazo cha maendeleo ambaye ni mume wake. Wanawake
wanaonesha hili kwa kusema kuwa, “Si Sudi mume wa Bi. Pili aliyetaka pesa zote
za pombe apewe”. Wanawake wengine katika ujasiriamali ni Bi. Moja na wenzake
wanafuma vitambaa, wengine mikeka na wengine mapambo ya meza. Licha ya
kufuma na kwenda kuviuza sehemu mbalimbali anatokea Bi. Tano ambaye, ni
mvivu wa kuuza vitambaa kwa madai eti hawezi kuwabembeleza wateja. Pia
mwanamke amechorwa kama mtu anayeona umuhimu wa elimu Bi. Nne
anatambua umuhimu wa elimu hasa pale anaposema: “pia somo la ushonaji
litatiliwa mkazo mashuleni.”
Mwanamke amechorwa kama kiongozi mbaya, mfano mzuri tunaupata kutoka
kwa Mwenyekiti ambaye baada ya kuletewa mashtaka na Bi. Nne kuhusu Bi Nane
yeye aliyachukua kama yalivyo, kwa kuamua kesi yeye na Bi. Nne pasipo
kuwashirikisha wajumbe wengine. Vilevile mwanamke amechorwa kama mtu
mwenye chuki kwa mfano, Bi nne ambaye alipeleka mashtaka ya uongo kwa
Mwenyekiti kwa lengo la kutaka kumgandamiza Bi. Nane.
Onesho la tatu lina jumla ya kurasa 16 ni onesho linalofuata kwa urefu baada la
onesho la pili. Limepewa urefu huu ili kujenga na kusisitiza umuhimu wa ukombozi
kwa mwanamke. Tangu mwanzo tunaandaliwa kumuona mwanamke Bi. Msimulizi
akisimulia yale matukio yote yanayotokea katika harakati za ukombozi wa
mwanamke. Bi. Msimulizi anaonekana kukerwa na vikwazo mbalimbali
vinavyokwamisha kusimama kwa Nguzo Mama kama vile tamaa ya Bi. Moja
kutamani kanga na hivyo kuacha kuvuta Nguzo Mama, kukosekana kwa
73
ushirikiano, kutumikishwa kwa wanawake, ukahaba unaofanywa na Bi. Sita,
dhuluma zinazofanywa na Kiando na Makande dhidi ya shemeji yao. Kuwa kuna
kila sababu ya kuteketeza vikwazo hivyo kwani, vinachangia kurudisha nyuma
maendeleo ya wanawake na kamwe hayatawezekana mpaka vigingi hivi vyote
vitokomezwe.
Onesho la nne lina jumla ya kurasa 15 tu. Limepewa urefu huu ili kuendeleza
kusisitiza ukombozi wa wanawake. Onesho linapoanza tunakutana na Bi. Msimulizi
ambaye anasema: “sana walifadhaika hasa yeye Bi Nane wakarudi majumbani
roho zinasononeka. Asubuhi na mapema vitandani bado wamo la mgambo likalia”.
Moja kwa moja tunapatanishwa kuwa, katika onesho lilopita kuwa, Bi. Nane
amewashinda kesi akina Mwenyekiti na Bi. Nne katika onesho hili tunaoneshwa
kuwa, juhudi za kuinua Nguzo Mama bado zinaendelea na zimeshika kasi. Ndipo
wanawake wanapogundua kuwa, juhudi hizi zinahitaji ushirikishwaji wa jamii
nzima wakiwemo wanaume na watoto wote. Kujitenga kwa akinababu, nako
kunakwamisha maendeleo na kuwepo kwa wasaliti katika jamii zetu
kunakwamisha kusimama kwa Nguzo Mama
4.3.2 Data na uchambuzi wake
4.3.3 Mwanamke Alivyochorwa katika Tamthiliya ya Nguzo Mama (1982)
kwa Upande Chanya
Mwanamke kama Mbunifu
Mwanamke amechorwa kama mtu anayetafuta njia na mbinu mbadala zitakazosaidia
katika kufanikisha kupata ukombozi wa mwanamke. Mwandishi amedhihirisha hili
kwa kuwatumia Bi. Moja na Bi.Tatu. Mfano, Bi. Moja anaposema ( uk. wa 1):
74
BI. MOJA : “Tukupambe kwa dhahabu
Au tukupambe kwa fedha
Wanja hina na uturi
Tukupambeje maua”
Naye Bi Pili anasema katika uk. wa 2
BI. PILI: “Jembe gani unataka
Mpini mrefu au mfupi
Chungu mdomo mdogo
Au kikapu cha kigogo
Tukupambeje maua”
Hivyo basi, Muhando anatuonesha namna wanawake wanavyohamasika na
ukombozi wao, kila mmoja akijaribu kutoa wazo lake, akiamini kuwa ndilo
litakalosaidia kusimama kwa Nguzo Mama.
Mwanamke kama Mlezi
Mwanamke amechorwa kama mzazi na mlezi. Mfano dhahiri ni Bi. Saba, alikuwa na
watoto watano, aliowazaa na kuwalea yeye mwenyewe. Baadaye alikuja
kunyang‟anywa watoto hao na ndugu wa marehemu mumewe. Hili linajihidhirisha
pale, Bi. Msimulizi anaposimulia (uk. wa 44):
Bi. MSIMULIZI: “Alipoona wanawe wote watano
Mdogo miaka mitatu
Wanaswagwa kama mbuzi”.
Pia, Bi. Pili naye ni kiwakilishi cha mazazi na mlezi bora. Aliwalea watoto wake
pamoja na mumewe vizuri. Mpaka jamii yote ikawa inampongeza kwa malezi yake.
Mfano ni Chizi, ambaye alitambua juhudi za Bi. Pili katika kuilea familia yake kwa
kuwapikia chakula, kufua nguo na kulima. Pia, alijihusisha na upikaji wa pombe
uliomuwezesha kupata kipato kidogo cha familia. Tazama uk. wa 59 pale Chizi
anaposema:
75
CHIZI: “Mke kujipatia awe kama Bi. Pili
Nguo anifulie na pombe anipatie
Ambaye taabu yote atakubali
Watoto anizalie na pia anilelee
Chakula anilimie na pia anipikie”
Mwanamke katika Kujikomboa
Mwanamke amechorwa kama mtu anayeona na kutambua umuhimu wa ukombozi
wa wanawake.
Hivyo anahimiza jamii nzima kushirikiana kwa pamoja katika kutafuta ukombozi
wa mwanamke. Hili linajihidhirisha uk. wa 59 pale Bi. Nane anaposema:
Bi. NANE: “Tushirikishe wanaume pia
NGUZO MAMA ina faida kwa wote”.
Bi . Nane anawataka wanawake wenzake wawashirikishe wanaume katika harakati
zao. Hii ina maana kwamba, jamii nzima inahitajika kushiriki katika ukombozi wa
wanawake. Pasipo kujali jinsia, umri wala watoto, wote kwa pamoja wanahitajika
ndipo Nguzo Mama itasimama.
Mwanamke pia amechorwa kama mwanaharakati katika kutafuta ukombozi wa
mwanamke. Mfano Bi. Msimulizi anaposema (uk. wa 5)
BI. MSIMULIZI: “Haraka wakaivamia hao wabeba wana
Nguzo kutaka kusimamisha”
Kutokana na maneno hayo tunaonyeshwa kuwa, kila mwanamke anaguswa na
harakati zinazofanywa ili kuweza kuwakomboa wanawake isipokuwa Nguzo
Mama ni nzito inahitaji jamii nzima ishiriki ndipo mafanikio yatakapopatikana.
76
Mwanamke amechorwa kama mtu anayejitegemea na anayeweza kujimudu
kimaisha pasipo kuwa tegemezi kwa mtu mwingine. Hili linajidhihirisha katika uk.
wa 42 pale Bi.Tatu anapomwambia Bi. Nne:
Bi NNE: “Unasemaje hivyo kwa kuwa wewe una kazi ya mshahara
Hata ukiachwa unajitegemea”.
Muhando amemsawiri mhusika Bi. Nane kuwa, ni mwanamke msomi na aliyepata
bahati ya kuajiriwa. Anapokea mshahara unaomuwezesha kujikimu kimaisha na
kuondokana na utegemezi katika jamii.
Mwanamke ni Msomi
Mwanamke amechorwa kama msomi, anayetambua umuhimu wa elimu aliyonayo na
kisha anajaribu kuitumia vizuri, kwa kuwaelimisha wanawake wenzake namna ya
kuweza kuinua Nguzo Mama. Kwa mfano, Muhando amemtumia mhusika Bi. Nane
kwa kumuonesha kuwa, ndiye mwanamke msomi aliyemudu kuitumia elimu yake
ipasavyo. Hili linajihidhihirisha katika uk. wa 10 pale mwandishi anaposema
MWANDISHI: “Anaingia Bi Nane, haimbi. Amevaa nguo za kisasa.
Ameshika vitabu vipatavyo sita hivi. Anakwenda kwa
mwendo wa kikazi. Anafika pale kwenye NGUZO MAMA
anaimba, anafunua vitabu vyake na kusoma hapa na pale
Katika kufunua vitabu vyake Bi. Nane, mwandishi anataka kutupa taswira ya kuwa
Bi. Nane pamoja na kugundua umuhimu wa elimu aliyonayo alipenda kurejelea
vitabuni ili kupata maarifa zaidi yatakayosaidia kusimamisha Nguzo Mama.
77
Vilevile, mhusika msichana naye ni kiwakilishi cha wasomi. Msichana huyo
amevaa sare za shule na anakwenda shule ili kutafuta elimu anayoamini kuwa
itakuwa ni ufunguo wa maisha yake.
Hay (2006) kama alivyonukuliwa na Pullen anaeleza kwamba elimu hasa elimu ya
juu katika hisia au mawazo ya vijana wanawake haipo, kwani hufikiri kwamba
haiwahusu. Anaona ni vema utamaduni huo uvunjwe miongoni mwa mabinti
wadogo kwani wote wanastahili elimu sawa na vijana wa kiume. Hata kama mtoto
huyo wa kike alipenda kusoma sana lakini ataishia kupenda na kutamani tu bila
kutimiza tamaa yake ya kutaka kusoma.
Mwanamke kama Mshauri
Mwanamke amechorwa kama mtu anayetoa ushauri na kuwatia wenzake moyo
kuwa, wasikate tamaa katika kusimamisha Nguzo Mama badala yake watafute
mbinu sahihi itakayo wawezesha kuinua Nguzo Mama. Hili linajidhiirisha uk. wa
11 Bi. Msimulizi anaposema:
BI. MSIMULIZI : “Tamaa tusikate tutafute maarifa”.
Bi. Msimulizi anawataka wanawake wenzake kuwa, wasikate tamaa katika
kusimamisha Nguzo Mama isipokuwa inawabidi wakae chini washauriane nini cha
kufanya.
Bi. Nane naye ni mhusika mwanamke aliyesawiriwa kama mtu anayetoa maarifa
kwa wenzake akiamini kuwa, maarifa hayo huenda yakasaidia kusimamisha Nguzo
Mama. Hili linajidhihirisha uk wa 12 pale Bi Nane anaposema
BI. NANE: “Basi, tusikilizane, mnajua NGUZO MAMA
78
haiwezi kusimama mpaka tuivute kwa kamba.
Hebu njooni mchukue hizi kamba tuzifunge
kwenye NGUZO MAMA halafu kila mmoja avute”.
Bi. Nane anaamini kuwa, kamba ikitumika katika kuvuta Nguzo Mama basi
itasimama. Hayo ni baadhi tu ya maarifa aliyojaribu kuyatoa Bi. Nane kwa
wanawake wenzake.
Mwanamke amesawiriwa kama mtu anayesikitishwa na kusononeshwa kwa
kukosekana kwa ushirikiano miongoni mwa wanawake wenzake. Kwani kuwepo
kwa jambo hili kunachelewesha kusimama kwa Nguzo Mama. Hili
linajidhihirisha uk. wa 13 pale Bi. Nane anaposema
BI. NANE: “Jamani vipi tena mbona mnaondoka?
(Ameshangaa na kamba zake mikononi.)
NGUZO MAMA hii haitasimama”.
Hivyo basi, Bi. Nane anaonesha kuwa, ni dhahiri Nguzo Mama haitaweza
kusimama mpaka vigingi vyote vitokomezwe, ikiwemo kutokuwepo kwa umoja
na ushirikiano miongani mwa wanawake wenzake. Kwani Waswahili wanasema,
kidole kimoja hakivunji chawa. Pia umoja ni nguvu utengano ni dhaifu.
Mwanamke kama Mjasiriamali
Mwanamke amechorwa kama mjasiriamali. Kwa mfano, Bi. Pili ambaye ni
mhusika mwanamke anajishunghulisha na upikaji wa pombe ili kuweza kujipati
maendeleo ya familia yake. Hili linajihidhirisha uk. wa 14 pale Bi. Msimulizi
anaposema:
BI. MSIMULIZI: “kaamua Bi. Pili
Pombe kujipikia na kilabuni kuiuza
79
Pesa akipata, pesa msema kweli
na NGUZO MAMA itasimama”.
Mwandishi anatuonesha kuwa, Bi. Pili anajishughulisha na upikaji wa pombe
unaomwezesha kupata pesa kidogo zinazosaidia kulea familia yake vyema. Licha
ya pesa anazopata mumewe anamlazimisha ampe.
Baadhi ya wanawake wa Patata kama vile Bi. Moja na wanawake wengine nao
walikuwa ni wajasiriamali wanaojishughulisha na miradi midogomidogo kama
vile ufumaji wa vitambaa, mapambo ya nyumba na usukaji mikeka. Baada ya
kufuma na kusuka mikeka walikwenda kuviuza sehemu mbalimbali. Kutokana na
juhudi hizo walijipatia pesa kidogo ambayo waliamini kuwa, ingewasaidia katika
harakati za kuinua NGUZO Mama. Mfano katika uk. wa 17 unatudhihirisha
miradi hiyo ya kina mama, mfano mzuri ni pale Bi Msimulizi anaposema:
BI. MSIMULIZI: “Anaingia Bi. Moja na akina mama wengine
wanatandika mikeka na kukaa. Kila mmoja
anafuma kitu fulani wengine vitamba vya meza,
wengine mapambo ya nyumba wengine wanasuka
mikeka”.
Mwanamke kama Mpiga Vita Suala la Uvivu
Mwanamke amechorwa kama mtu anayepiga vita vikali suala la uvivu, kwani
linarudisha nyumba maendeleo ya wanawake na jamii kwa ujumla. Hili
linajihidhirisha uk. wa 18 pale Bi. Moja anaposema:
BI. MOJA : “Hata haiwezekani! Sema tu hukwenda
Nakwambia uvivu unaturudisha nyuma sisi”.
80
Bi. Moja ni kielelezo cha wanawake wanaopiga vita suala nzima la uvivu,
kwa kumwambia Bi. Tano kuwa, biashara inahitaji kubembeleza. Hivyo basi, ili
ukombozi wa wanawake upatikane hatuna budi kutupilia mbali tabia ya uvivu.
Mwanamke kama Mvumilivu
Mwanamke amechorwa kama mtu anayeweza kukabiliana na vikwazo pamoja
na matatizo mbalimbali yanayoweza kumpata katika jamii. Kwa mfano Bi.
Nane aliweza kuwakabili vyema mwenyekiti pamoja na Bi. Nne, kwa mashtaka
ya uongo ambayo Bi. Nne aliyapeleka kwa mwenyekiti. Mfano katika uk. wa
23 unatudhihirisha Bi. Nane alivyoweza kuyakabili matatizo yaliyompata;
anasema:
BI. MSIMULIZI: “Hasira zikampanda Bi Nane
lakini vyema akizitawala
mdomo akauma neno lisije mtoka”
Hivyo basi, tunaonyeshwa kuwa, Bi. Nane aliwasikiliza mwenyekiti na Bi. Nne
na mwisho akagundua kuwa, wote wawili walikuwa na hila juu yake. Na ndipo
alipowajibu kwa busara namna mambo yanavyopaswa kuendeshwa. Kisha
mwenyekiti na Bi. Nane wakabaki midomo wazi wasijue la kufanya.
Mwanamke kama Mchapakazi
Mwanamke amechorwa kama mchapakazi anayejibidisha katika kufanya kazi ili
kuweza kulea familia yake vyema. Hili linajihidhihirisha katika uk. wa 36, pale
Bi. Pili anaposema:
BI. PILI: “Nimefua mchana huu. Asubuhi si nilidamkia
shambani. Kurudi shambani kwanza nikapikia
81
watoto, maji hakuna, nikaenda kuyachukua”
Muhando anatuonyesha kuwa, aghalabu mwanamke amekuwa akichapa kazi za
nyumbani peke yake tena bila ya kupumzikia. Akitoka shambani anawapikia
watoto wake chakula. Anapaswa pia kwenda kuchota maji. Bila shaka alikuta
nyumba na vyombo ni vichafu ataanza kusafisha nyumba na kuosha vyombo.
4.3.4 Mwanamke Alivyochorwa katika Tamthiliya ya Nguzo Mama (1982) kwa
Upande Hasi
Kiumbe anayenyanyaswa
Mwanamke kama kiumbe kinachonyanyasika katika jamii. Kutokana na kuwepo
kwa mfumo dume unaowagandamiza kwa kuwafanya ni wazazi tu na mambo
muhimu hawawahusishi. Mfano uk wa 4 ni pale Bi Msimulizi anaposimulia:
BI. MSIMULIZI: “Wabeba wana vibaya walinyanyasika
wakaonekana si watu ingawa jamii waliikuza”
Inaonekana katika jamii ya Patata, wanawake walidharauliwa na kunyanyaswa.
Walikuwepo tu kwa sababu ya kuzaa. Hawakutambua umuhumi mwingine wa
kuwepo kwa wanawake katika jamii yao.
Mwanamke amechorwa kama mtu anayefanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo
kunyang‟anywa pesa pamoja na kupigwa na mumewe. Hili linajidhihirisha uk.
wa16 pale Sudi anapomwambia Bi. Pili:
SUDI: “Wee! Hawara zako ndiyo wanakutia jeuri unaninyima
pesa toa pesa sasa hivi (Anampiga Bi. Pili anakimbia
huku analia)”
82
Bi. Pili alipata pesa kidogo kutokana na pombe aliyokuwa anaipika na kuiuza.
Lakini bado dume hilo lilizoea kulelewa na halikuridhika, likataka kuzitawala pia
pesa za Bi Pili. Huu ni uonevu uliokithiri katika jamii nyingi za kiafrika.
Pia, mwanamke amechorwa kama mtu anayefanyiwa dhuluma kwa
kunyang‟anywa vitu vyote alivyoachiwa na marehemu mumewe, wakiwemo na
watoto wake watano. Hili linajidhihirisha uk. wa 43 pale Bi Saba anaposema:
BI. SABA: “Nitawaambia mara ngapi
ndugu yenu amekufa hela zote mmechukua,
watoto wote mmeninyang‟anya, vitu vyote
mmechukua, bado mnaniambia nimechukua hela”.
Bi. Saba mara baada ya kufiwa na mumewe, ndugu wenye uchu na tamaa ya
kumiliki mali walijitokeza na kumnyang‟anya kila kitu. Hii ni dhuluma kubwa
aliyofanyiwa Bi. Saba ambapo haina budi kukomeshwa na kutokomezwa kabisa
katika jamii tuliyo nayo sasa. Ili kwamba wajane wanaoachwa waweze kujua kuwa
wataendelea vipi na maisha na sio kuanza kuwaza watakavyoanza maisha upya.
Tuangalie mfano kutoka katika uk. wa 43 jinsi BI SABA anavyoshangaa baada ya
kuwaona shemeji zake wamerudi tena kuchukua mali:
BI SABA: “Haa! Shemeji mmerudi kuchukua hata kitanda!
Hata sufuria! Nitalala wapi na nitapikia wapi jamani!”.
Mwanamke kama Mtegemezi
Mwanamke amechorwa kama kiumbe duni, kisichoweza kujitegemea chenyewe bila
nguvu ya mwanaume. Na hivyo kuwa tegemezi kwa mume wake kwa kila kitu. Hili
linajidhihirisha katika uk wa 41 pale Bi. Tatu anaposema:
BI TATU: “ Siyo utani ndugu yangu. Tunakwenda kwenye pati na
mume
83
wangu leo saa moja. Lazima nipalilie unga kwa baba
watoto wangu ati. Nitakula nini”.
Hapa tunapata picha kuwa, Bi Tatu siyo kwamba amekwenda kwenye pati na
mumewe kwa kupenda, isipokuwa asingekwenda angenyimwa pesa kwa ajili ya
mahitaji ya watoto pamoja na mahitaji yake binafsi. Kwa maana kwamba mumewe
angekataa kutoa huduma za nyumbani. Hivyo mwanamke anafuata kila kitu
anachotaka mumewe kutokana na kuwa yeye ndiye ameshikilia maisha yake, na
kuwa akikataa kufuata anayoyataka mumewe basi huduma hizo asingezipata. Wakati
umefika kwa wanawake kizinduka kutoka usingizini na kukataa kuwa tegemezi kwa
mume.
Utamaduni unavyomkandamiza Mwanamke
Mwanamke amechorwa kama mtu anayegandamizwa na mila potofu zinazoruhusu
mwanamke kunyang‟anywa mali alizoachiwa na mumewe. Kuwa mwanamke
anapofiwa na mumewe anapaswa kutaja mali zote walizokuwa wamechuma na
marehemu kwa ndugu wa marehemu. Hii sio haki kwa kuwa mali hizo wametafuta
mke na mume, na sio vizuri ndugu wa mwanaume kwenda kuzidai. Hili
linajidhihirisha uk. wa 43, Makange anapomwambia Bi. Saba kuwa:
BI. SABA: “Umeficha mali ya ndugu yetu
mwanamke wewe. Huogopi hata waliokufa!”
Kutokana na tamaa na uchu wa mali waliyonayo ndugu wa mume wa Bi Saba
wanaamini kuwa, kuna mali nyingine zimefichwa. Wanataka mali ambazo
hawajazitolea jasho. Hivyo basi umefika wakati ambapo sheria inafaa ichukue
mkondo wake na sio kuogopa waliokufa. Wanajaribu kumpa Bi Saba imani potofu
ya kuogopa waliokufa. Kama kufa kafa mmoja na mali ilichumwa na wote wawili
84
hivyo inapaswa mali zilizosalia kumilikiwa na kuendelezwa na aliyebaki ambaye
naye ameshiriki kuchuma mali hizo.
Mwanamke kama Msaliti
Mwanamke amechorwa kama msaliti. Pale ambapo, licha ya kutambua kuwa
mhusika Chizi ni mtoto wa kaka yake lakini kwa makusudi anaamua kusema kuwa,
hamfahamu na anamkataza asimuite shangazi. Hili linajidhihirisha uk. wa 50, Bi
Tatu anapomwambia Chizi kuwa:
BI. TATU: “Usiniite shangazi, toa balaa lako hapa
ukirudi nitakuitia mbwa akuume”.
Bi Tatu amemkataza Chizi asimwite shangazi na isitoshe anamtishia kuwa,
atamwitia mbwa, hii ni hali ya kukataa majukumu ya kifamilia ambayo inapaswa
kupigwa vita vikali katika jamii zetu kwani inarudisha nyuma maendeleo katika
jamii.
Mwanamke kama Chombo cha Starehe
Mwanamke amechorwa kama chombo cha starehe. Ambaye anajihusisha na biashara
ya ukahaba, ambapo amegeuza mwili wake kuwa kama bidhaa iuzwayo sokoni
inayosubiri mnunuzi aje ili anunue. Mfano mzuri ni mwanamke kahaba ambaye ni
Bi Sita. Hili linajidhihirisha katika uk wa 8 pale mwandishi anaposema kuwa:
MWANDISHI: “Wakati wimbo unaendelea anaingia Bi. Sita haimbi.
Anaingia kwa miondoko ya kikahaba na amevaa
kikahaba”.
Kuvaa kikahaba kwa Bi Sita kunatudhihirishia kuwa yuko sokoni. Ameamua
kuanika biashara yake ili wanunuzi wafike na kuinunua. Hapa mwandishi
anatuonyesha kuwa wanawake wanategemewa kupata maendeleo kwa kujiuza.
85
Vile vile mwanamke amechorwa kama chombo cha starehe, kilichopo kwa ajili ya
kumstarehesha mwanaume. Mfano mzuri ni pale Bi Sita anapomwambia Bi Tano
katika uk wa 39:
BI. SITA: “ Mwambie mumeo ashike yake kwanza
alinifuta yeye mwenyewe. Wewe ulikuwa wapi?”
Licha ya Bi. Sita kutambua kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mume wa Bi. Tano,
kamwe hakujali. Kwani amekubali kufanywa kama chombo cha starehe kwa
kuchezewa na kisha kuachwa, kwani alijua kabisa kuwa mumewe Bi. Tano ana mke
na sio kwamba anataka kumwooa ila ni tamaa tu za kutimiza haja zake za kimwili.
Mwenye Wivu
Mwanamke pia, amechorwa kama mtu mwenye wivu, fitina na chuki binafsi. Na
hivyo kuchangia kukwamisha juhudi za ukombozi wa mwanamke. Mfano mzuri ni
mwanamke mwenye fitina, wivu na chuki binafsi ambaye ni Bi. Nne, ambaye mara
kwa mara anaonekana kutokukubaliana na mawazo ya Bi. Nane hata kama
anafahamu kuwa yana manufaa huyapinga. Hili linajidhihirisha katika uk. wa 13, Bi.
Nne anaposema kuwa:
BI. NNE: “Ha! Mnafanya nini
nani kawaambia mfanye hivi? Ndio nini hii?”
Kila juhudi inayopigwa na wanawake anatokea Bi. Nne na kuwarudisha nyuma.
Hivyo basi, ili ukombozi wa mwanamke uweze kupatikana kuna kila sababu ya
kupiga vita wivu, fitina na chuki.
86
Mvivu
Mwanamke amechorwa kama mvivu, asiyewajibika ipasavyo katika kufanya kazi
inayoweza kuleta maendeleo ya mwanamke. Hili linajidhihirisha katika uk. wa
19 pale Bi. Tano anaposema:
BI. TANO: “Kila nilipokwenda wananiambia wameshanunua vya
kutosha.sasa mimi ningewalazimisha!”
Bi. Tano ni mwanamke mzembe na mvivu asiyependa kuwajibika katika kufanya
kazi. Haoni tatizo hata kidogo kwa kukosa wateja wa kununua vitambaa vyake.
Wanawake kama Bi. Tano ndiyo wanaokwamisha upatikaji wa maendeleo ya
wanawake kwani hawapendi kujishungulisha.
Mwanamke kama Mtu mwenye Tamaa
Mwanamke amechorwa kama mtu mwenye tamaa ya vitu vidogo vidogo kama
vile kanga. Hili linajihidhirisha uk. wa 35 pale Bi. Moja anapomwambia Shabani:
BI. MOJA: “Kama ulijua kufika sasa hivi nipe hela za kanga bwana.
Meli hii hainikosi leo utanipa hela hizo kanga nikakate.
Mwezi wa tatu huu kanga sizijui”.
Muhando anatuonesha kuwa, Bi. Moja ni kiwakilishi cha wanawake wenye tamaa
ya vitu vidogovidogo kama kanga. Inavyoonekana Shabani hana hela hizo za
kununulia kanga.
Lakini Bi. Moja anamlazimisha mwisho wake ni kutokea kutokuelewana. Hivyo
basi mwandishi anaitaka jamii kuacha kuwa na tamaa ya vitu visivyo vya lazima
kwa sababu ndivyo vyanzo vya kukwamisha maendeleo ya jamii kwa ujumla.
87
Mwanamke Kama Mpinga Maendeleo
Mwanamke amechorwa kama mtu asiye na ushirikiano na wenzake na ndiye
chanzo cha kukwamisha maendeleo. Hili linajidhihirisha katika uk. wa 41 pale Bi.
Tatu anaposema
BI. TATU: “Jamani mie naondoka. Mnaiona volvo hiyo
imenifuata mie”
Bi. Tatu hana ushirikiano na wanawake wenzake wakati wa kuinua Nguzo Mama
yeye Volvo inamfuata na hivyo anaamua kuiacha Nguzo Mama na kwenda
kupata Volvo.
Mfano mwingine wa mwanamke asiye na ushirikiano na wenzake ni Bi Sita
ambaye yeye mikononi yake ati ni laini hivyo hawezi kuinulia Nguzo Mama.
Hili linajidhihirisha uk. wa 41 pale Bi. Msimulizi anaposimulia:
BI. MSIMULIZI : “Naye yule Bi. Sita alienda zake kimoja.
Kamwe hakurudi kuigusa Nguzo Mama sikuzoea
kazi Ngumu Mama mie mikono yangu laini
mwenyewe nategemea. Leo nitashika kamba
mikononi kutwaniza.
Halafu hicho chakula nitategemea nini?”
4.3.5 Mjadala wa Dhamira Zilizojitokeza Kutokana na Uchorwaji wa
Mwanamke katika Tamthiliya ya Nguzo Mama (1982)
Ukombozi wa Mwanamke
Usawiri wa mhusika mwanamke katika tamthiliya ya Nguzo Mama (1982) umeweza
kujenga dhamira ya ukombozi wa mwanamke. Tumeoneshwa kuwa, mwanamke
amekuwa akitafuta ukombozi wake kwa kutafuta maarifa zaidi juu ya kuinua
Nguzo Mama. Vilevile mwanamke kama Bi. Pili amekuwa akijishungulisha na
88
kupika pombe na wanawake wengine wakisuka mikeka, vitambaa vya meza pamoja
na mapambo ya ndani. Juhudi zote hizi zimekuwa zikifanywa ili kuhakikisha kuwa,
Nguzo Mama inasimama.
Umoja na Ushirikiano
Kama Waswahili wasemavyo, umoja ni nguvu, utengano ni dhahifu. Hivyo basi,
usawiri wa muhusika mwanamke umeweza kujenga dhamira ya umoja na
ushirikiano. Mwandishi anatuonesha kuwa, ili Nguzo Mama iweze kusimama
hakuna budi jamii yote kushirikiana katika suala nzima la kuinua Nguzo Mama. Hili
linajihidhirisha wazi pale mwandishi anaposema uk. wa 58. “Bila umoja
hatutafanikiwa kitu”.
Muhando anaitaka jamii kushirikiana kwa pamoja katika suala la kuinua Nguzo
Mama kwani wakiachiwa wanawake wenyewe kamwe hawataweza kuinua Nguzo
Mama bali anachokitaka ni watu wote kuona umuhimu wa kuinua Nguzo Mama.
Udunishwaji, Unyanyaswaji na Ugandamizaji wa Wanawake katika Jamii
Usawiri wa mhusika mwanamke umeweza pia kujenga dhamira hii, kwa maana
kwamba, wanawake wameoneshwa kama wahusika wanaogandamizwa na
kudunishwa katika jamii wanamoishi. Kwa mfano, mwanamke kama Bi. Saba
alinyang‟anywa mali zake zote alizoachiwa na marehemu mumewe ikiwa ni pamoja
na watoto wake wote watano. Tena mwandishi anatueleza kuwa, watoto wake
aliwalea Bi. Saba kwa shida sana huku baba yao akiwa analewa pombe.
Unyanyasaji pia tunauona kwa Bi. Pili ambaye alikuwa anauza pombe lakini pesa
yote aliyoipata kwenye pombe hiyo alinyang‟anywa na mumewe Sudi tena kwa
89
kupigwa kipigo kikali. Udunishwaji wa wanawake, tunauona pia kwa Bi. Pili
ambaye licha ya kujishughulisha na upikaji pombe wanaume kama Totolo
walionekana kumdharau kwa kutoamini kuwa, Bi Pili naye anaweza kupika pombe.
Mfano dhahiri unajihidhirisha katika onesho la pili uk. wa 14 pale Totolo
anapomwambia Bi. Pili:
TOTOLO: “Lo! Hata na wewe Bi. Pili siku hizi unapika pombe
kwa maana hiyo,
Totolo alitegemea kazi hiyo ifanywe na mwanaume na siyo mwanamke. Ndiyo
maana hata kushangaa kwake kunaonesha ni kumdharau Bi. Pili.
Uongozi Mbaya
Udikteta unaoneshwa kuwa ni zao la uongozi mbovu uliopo kwenye jamii ya wana
Patata. Viongozi kama mwenyekiti wa kamati ya mashauri wamesawiriwa kama
madikteta. Wanafanya wajisikiavyo au vile waambiwavyo na watu wao wa karibu,
bila kufuata misingi na miongozo waliyowekewa na katiba za jamii zao.
Mwenyekiti wa kamati ya mashauri anatumia vitisho kumlazimisha Bi. Nane
kusema asichokijua ili mradi tu yeye ni kiongozi. Pia, mwenyekiti anaonesha
udikteta wake pale alipotaka kuamua kesi aliyosikiliza upande mmoja tu wa
mashtaka, tena maelezo hayo kapewa wakati mshtakiwa hayupo.
BI. MSIMULIZI: “……Vipi mtu atakubali kutoa ushauri kutumia vitisho!
kufuata maelezoya mshtaki peke yake tena yaliyoelezwa
wakati mshtakiwa hakuwepo vipi mtu atamshauri
mshtakiwa bila kujua mawazo yake” …uk. wa 24.
Pia Muhando anaonesha jinsi udikteta uliokithiri unavyitawala jamii ya Patata, yaani
mtu mmoja anaweza kuamua maamuzi yanayotakiwa kufanywa na kamati nzima.
Mfano ni pale Mwenyekiti wa kamati ya mashauri alipounda kamati ya watu wawili
90
ili wamshtaki Bi. Nane. Uongozi mmbaya pia umewakilishwa na Bi Saba ambaye
licha ya kuwa kiongozi hajui hata nini maana ya Nguzo Mama, mpaka Chizi
anamshangaa.
Uvivu na Uzembe
Utafiti huu umegundua kuwa mwanamke amesawiriwa kama mvivu na mzembe.
Mfano ni pale wanawake wa Patata waliposhindwa kuinua nguzo mama. Wakati
walipokuwa wanafanya kazi hiyo, wanawake wengine wakawa wanategeana na
kusababisha kushindwa kuinuka kwa Nguzo Mama. Bi. Moja anaacha kuvuta kamba
na kuanza kuongea na Bi Tano kuhusu kanga ambazo kwa muktadha waliokuwepo
wasingepaswa kuzungumzia mambo hayo. Anauliza wapi wamenunua kanga naye
B. Tano anaanza kumweleza kuwa, ni kwa Mwarabu na pia anamtahadharisha
kuwa, anapaswa kuwahi la si hivyo zitakwisha. Mara B.i Moja anaacha kuvuta
kamba na kuondoka ili kuziwahi kanga. Mara Bi Nane anashtuka na kuuliza,
BI. NANE: “sasa jamani Bi. Moja anakwenda wapi tena!! Bi. moja
akiwa mbali anajibu, Aaa !! jamani nitarudi lakini,
kanga hizi sizikosi” uk. wa 34.
Bi. Sita naye amesawiriwa kama mwanamke asiyewajibika na asiyejali umuhimu wa
kazi za maendeleo, kwani naye baadaye anaacha kuvuta kamba na kumfuata
mwanaume eti kwa sababu tu alimkonyeza ili amfuate licha ya umuhimu uliopo
kwenye kuinua Nguzo Mama.
Bi. Tatu naye kwake Nguzo Mama si mali kitu zaidi ya mume na sherehe, hivyo
anawasusia wenzake kamba na kukimbilia kwenye Volvo lililomfuata na kuelekea
kwenye pati ambayo kwake ni muhimu zaidi kuliko Nguzo Mama.
BI. TATU: jamani mie naondoka mnaiona Volvo hiyo imenifuata mie.
91
Sio utani ndugu yangu. Tunakwenda kwenye pati na
mume wangu leo saa moja lazima nipalilie unga kwa
watoto wangu ati. Nitakula nini” uk. wa 14.
Hata viongozi nao wanaonekana wababaishaji na waliojaa maneno matamu
mdomoni pasipo uwajibikaji kwa vitendo. Bi. Nne kama kiongozi naye anaondoka
kwenye kazi muhimu itakayowezesha maendeleo ya wanawake kupatikana na
kwenda kwenye vikao na kupiga soga bila utekelezaji. Mtafiti amegundua kuwa,
wanawake wenyewe ndio wanaokwamisha maendeleo yao wenyewe kutokana na
wivu, uvivu na uzembe kama ilivyobainika katika tamthiliya ya Nguzo Mama.
Utegemezi wa Mwanamke
Utafiti huuu umeliangalia suala la utegemezi wa wahusika wanawake kwa wanaume
kwa mawanda mapana. Mtafiti amegundua kuwa, tamthiliya ya Nguzo Mama
(1982) imemsawiri mwanamke kama kiumbe kisichokamilika katika mazingira ya
kipekee kijinsia. Mwanamke anamtegemea mwanaume katika masuala mbalimbali,
hususani kiuchumi na katika masuala yakifamilia na kijamii kwa jumla. Mfano ni
katika uk. wa 14 pale Bi. Tatu anaposema:
Bi. Tatu: Siyo utani ndugu yangu tunakwenda kwenye pati na
mume wangu leo saa moja.Lazima nipalilie unga kwa
baba watoto wangu.
Mwanamke amedunishwa kwa kuonekana kuwa tegemezi kwa mwanaume kwa
kuwa, mwanaume anamlisha yeye na watoto. Siyo kuwa Bi. Tatu anakwenda
kwenye pati na mume wake kwa kupenda au kwa ridhaa yake mwenyewe bali kwa
kumpendezesha mume wake na kumridhisha ili atoe pesa za matumizi. Hii ni kwa
lengo la kumbembeleza ili apate unga, maana asipokwenda unga atapata wapi!
92
4.4 Athari za Uchorwaji wa Wahusika Wanawake katika Kazi za Fasihi
Utafiti huu umebaini athari mbalimbali zinazopatikana kutokana na usawiri wa
wahusika wanawake katika tamthiliya za Hatia na Nguzo Mama. Athari zenyewe
zaweza kuwa mbaya au nzuri. Usawiri wa wahusika hawa katika kazi za kifasihi
unaweza kuleta athari kubwa kwa kizazi kijacho kwani wanajenga hisia kuwa huo
ndio mtindo bora wa maisha. Kazi hizi zinaposomwa na vijana wa siku hizi
zinaweza kuwavutia kuiga tabia na mwenendo wa wahusika hao.
Dkt Vicensia Shule alisema kuwa, athari mojawapo itokanayo na usawiri chanya wa
wahusika wanawake katika kazi za kifasihi ni kuwa wanapozisoma kazi hizi
wanaona kuwa wanawake nao wanapewa kipaumbele na wanathaminiwa katika
jamii. Hata hivyo ameendelea kusema kuwa, mwanamke anapothaminiwa na
kupewa nafasi katika hizi kazi za kifasihi, msomaji anapoisoma kazi hiyo huwa na
hamasa ya kutaka kuonyesha juhudi zaidi katika jamii ili wapate nafasi ya kuendelea
kuthaminiwa zaidi. Ameendelea kueleza kuwa, mwanamke anaposoma kazi ya
kifasihi iliyoandikwa na mwanamke na kuona nafasi na majukumu waliyopewa
wanawake hususani katika tamthiliya moja kwa moja husababisha wanawake wengi
kuanza kuandika kazi mbalimbali za kifasihi au kujiunga na vyama mbalimbali vya
wanawake ili nao kujiunga katika kupinga hali ya unyanyasaji wa wanaume kwa
wake zao. Pia, anasema kuwa, nafasi na majukumu wanayopewa wakina mama
katika kazi za kifasihi husaidia kutoa hamasa zaidi katika jamii na kwa wanawake
kwa jumla katika kutetea harakati za ukombozi wa mwanamke.
Hivyo basi utafiti huu umegundua kuwa, athari mojawapo ya kutumia taswira
chanya kuhusu mwanamke katika kazi za kifasihi hususani tamthiliya, inasaidia sana
93
katika kuwafanya watazamaji au wasomaji hasa wanawake kujitambua na kuweza
kuongeza juhudi zaidi katika kupigania haki na ukombozi wa mwanamke kifikra na
hata kiuchumi.
Profesa Penina Muhando katika mahojiano na mtafiti yaliyofanyika tarehe
11/11/2013, naye amesema kuwa usawiri chanya wa mhusika mwanamke katika kazi
yoyote ya kifasihi husababisha au huleta matokeo chanya kwa msomaji au kwa
mtazamaji kama ni tamthiliya. Anaendelea kueleza kuwa, wanawake wengi hasa wa
vijijini hawajatambua haki zao kama vile suala la elimu na mambo mengine ya
kijamii na kifamilia kwa jumla. Katika suala la elimu amesema kuwa, asilimia
kubwa ya wanawake wa vijijini hawajui kuwa elimu ni haki yao, ila wanapotazama
tamthiliya au kusoma tamthiliya kwa wale wanaojua kusoma, hasa kipindi hiki cha
utawandazi ulioenea hadi vijijini kwa sasa, wamegundua kuwa wao wana haki ya
kupata elimu kama ilivyokuwa kwa wanaume. Alitoa mfano kuwa, kwa sasa
wasichana wengi wanakataa kuolewa au kuachishwa masomo na pia wengine
hudiriki hata kutoroka kwa kupinga suala zima la unyanyasaji wa wanawake katika
nyanja mbalimbali katika jamii zao. Ameendelea kusema kuwa, wanawake wengi
wamejitambua na kuchukua hatua za kukataa manyanyaso ya wanaume kama vile
kulazimishwa kuolewa wakiwa na umri mdogo, kukeketwa nakadhalika.
Tumeona kuwa kwa kiasi kikubwa kazi hizi za kifasihi zimesaidia sana katika
kuzindua akili za wanawake katika jamii na kujitambua, pia wanawake wengi
wamejikita katika kujishughulisha na kazi mbalimbali katika jamii ilimradi tu na
wao wainue kipato chao pamoja n kuilea familia kwa jumla.
94
Mtafiti amegundua kuwa, mwanamke anaweza kubadilisha mwenendo na
kujithamini pale anaposoma kazi ambazo zina mtazamo chanya juu yake.
Kutokakana na utafiti huu tumeona kuwa kuna funzo kubwa sana kwa wasichana na
akina mama kwa jumla. Suala la elimu ni jambo ambalo limeonekana kuwasisimua
watu wengi kwa kuona kuwa elimu ndicho chombo pekee kinachoweza kuleta
ukombozi wa mwanamke. Katika tamthiliya ya Nguzo Mama mwanafunzi amewatia
hamasa akina mama kwa kumwona amebeba vitabu na amevalia sare za shule. Licha
ya mwanafunzi, pia mwalimu naye amekuwa kishawishi kizuri kwa wakina mama
wa Patata. Msomaji au mtazamaji wa tamthiliya hiii hupata msukumo na hamasa za
kuona umuhimu wa elimu katika jamii.
Pia usawiri au uchorwaji wa mwanamke kwa upande chanya katika kazi za kifasihi
husaidia kuhamasisha wasomi kufanya utafiti. Hivi sasa baada ya utafiti mwingi
kufanyika umeweza kuamsha hamu ya watu kuandika kazi mbalimbali zinazohusu
mwanamke katika kazi za kifasihi.
Kwa kufanya utafiti jamii itafahamu mambo yaliyomo katika tamthiliya hizo na
matatizo yote yaliyomo katika jamii na jinsi ya kutatua.
Pia athari mbaya zinazotokana na usawiri au taswira hasi za wanawake katika kazi
za fasihi zimejitokeza kama ifuatavyo:
Utafiti huu umegundua kuwa, mwanamke anaposawiriwa katika hali ya uhasi,
matokeo yake ni kusababisha matatizo makubwa katika jamii kama vile vita
nakadhalika. Mfano mzuri ni mhusika Cheja katika tamthiliya ya Hatia (1972) jinsi
95
alivyozua vita kwenye kijiji kizima, watu wamepigana, wameumizana na hata
kusababisha hela nyingi kupotea katika matibabu.
Dkt Mona Mwakalinga ameeleza kuwa, athari zinazoweza kujitokeza kutokana na
usawiri hasi katika kazi za kifasihi hususani katika tamthiliya ni wasomaji kuiga
matendo mabaya yanayoigizwa au wanayosoma katika kazi hizo. Aliendelea kueleza
kuwa, mwanamke hupenda kuiga mambo si kawaida yake kufanya kwa wengine.
Alitoa mfano kuwa, hasa kwa kipindi hichi tulichonacho cha utandawazi.
Mwanamke katika kazi ya kifasihi amechorwa kavaa mavazi mafupi au
yanayomwacha wazi sehemu zake za mwili. Msomaji au mtazamaji wa tamthiliya
huweza kuiga matendo machafu ambayo yameonyeshwa kuwa mwanamke ndiye
anayefanya ili kuvutia wanaume.
Bw Mtiro naye ameeleza athari mojawapo ni kuwa msomaji au mtazamaji wa
tamthiliya hujenga dhana potofu kuwa mwanamke ni mtu wa kujiremba tu, ni mtu
wa kumtegemea mwanaume tu, ni mtu wa kumfurahisha mwanaume tu, ni mtu wa
kukandamizwa tu, ni mtu ambaye hawezi kufanya maamuzi katika jamii au katika
familia yake na ni mtu malaya tu. Anaendelea kueleza kuwa, watu wengi hasa
wanaume wanaposoma kazi hizi au kuzitazama hujaribu au kuwapeleka wake zao
kama walivyoona au kama walivyosoma katika kazi hizo. Hata katika majukumu
msomaji au mtazamaji hutoka na dhana potofu kuwa majukumu ya mwanamke ni
kupika, kufua na kulea familia ikiwa ni pamoja na mume.
Utafiti huu umeona kuwa, uchorwaji hasi wa mwanamke katika tamthiliya
husababisha kukata tamaa kwa wanawake na madhara yake anaishia kujinyonga au
96
kujiona kuwa hana thamani katika jamii. Mwanamke mara nyingi ameonekana ni
mtu wa kukata tamaa katika maisha. Uchorwaji huu wa mwanamke kama kiumbe
dhaifu cha kukata tamaa haraka husababisha mtazamo hasi kwa wasomaji na
watazamaji kuona kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu na mara nyingi mwisho wake
wanaonekana sio wa mafanikio tofauti na wanaume.
Hivyo basi, waandishi wengi wa kazi za kifasihi husana kazi zao kulingana na jamii
au matendo yanayofanyika katika jamii zao. Hivyo husababisha watu wa utamaduni
mwingine au wa jamii nyingine wanaposoma kazi hizo kuiga matendo
yanayofanywa na jamii nyingine bila kujua madhara yake.
4.6 Hitimisho
Sura hii ya nne imefanya jitihada ya kuyajibu maswali ya utafiti. Katika sura hii
mtafiti ameelezea jinsi mwandishi anavyoweza kumsawiri mwanamke kutokana na
vitendo mbalimbali wanavyofanyiwa wanawake katika jamii na jitihada
wanazofanya wanawake katika jamii mbalimbali, na kwa kadri atakavyotaka ujumbe
uifikie jamii kuhusu mwanamke. Hii inatokana na kwamba mwanamke kutumiwa
kueleza mambo hasi na wakati mwingine katika upande wa chanya na hivi ndivyo
ilivyojitokeza kati tamthiliya tulizozijadili. Ambapo mwandishi wa tamthiliya ya
Hatia (1972) na Nguzo Mama (1982) ametumia taswira mbalimbali kuelezea maovu
yanayotendwa na wanaume juu ya wanawake pamoja na harakati zinazofanywa na
mwanamke katika kujikomboa. Katika tamthiliya hizi taswira ya mwanamke
imetumika katika pande zote mbili yaani hasi na chanya. Pia katika sura hii mtafiti
amebainisha dhamira mbalimbali zilizojitokeza katika tamthiliya teule zilizojadiliwa
kwa lengo la kuonyesha uhusiano wa moja kwa moja na usawiri wa mwanamke.
97
Katika uchambuzi wa data uhusiano huo umeshadidiwa na nadharia ya Ufeministi
ambayo imekuwa mhimili mkubwa katika kuchakata data zilizopatikana. Sura
ifuatayo itaelezea muhtasari wa kazi zima, ikiwa ni pamoja na maoni na
mapendekezo ya mtafiti kwa mwandishi, jamii na waandishi wachanga wa kazi za
fasihi.
98
SURA YA TANO
MUHTASARI WA MATOKEO YA UTAFITI , MAPENDEKEZO, NA
HITIMISHO
5 .0 Utangulizi
Utafiti huu ulikuwa na lengo la kuchunguza jinsi mwanamke alivyochorwa katika
tamthiliya teule za Penina Muhando. Katika sura hii, muhtasari wa sura
zilizotangulia umetolewa. Kila sura imeelezwa kwa kifupi ili kuweka wazi kile
kilichofanyika katika utafiti. Vilevile, sura hii inatoa maoni na mapendekezo
yanayoweza kufanyiwa utafiti na wanazuoni wengine kwa kina zaidi na kuhusu
tamthiliya. Nadharia iliyotumika ni nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika. Muhtasari
wa matokeo ya Utafiti uliongozwa na maswali matatu ya utafiti ambayo ni:
i. Nafasi ya mwanamke imesawiriwa vipi katika
tamthiliya za Hatia na Nguzo Mama?
ii. Je, wahusika wa kike wamechorwaje kwa mujibu wa
majukumu katika tamthiliya hizo?
iii. Ni athari gani zinazopatikana kutokana na usawiri wa
mwanamke katika kazi za kifasihi?
5.1 Muhtasari wa Mpangilio wa Tasnifu
Tasnifu hii ilihusu jinsi mwanamke alivyochorwa katika tamthiliya teule za Penina
Muhando. Tasnifu hii ina sura tano, ambapo sura ya kwanza inahusu utangulizi wa
jumla wa tasnifu zima, usuli wa tatizo ambao kwa kifupi, historia ya tamthiliya kwa
ujumla katika dunia na Tanzania. Usuli huo unafafanua maendeleo ya tamthiliya na
jinsi wanawake walivyozungumziwa. Tatizo la utafiti limeelezewa sanjari na
malengo ya utafiti ambayo yamegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni
lengo kuu na malengo mahususi ambayo yako matatu. Malengo hayo matatu
99
yamezalisha maswali ya utafiti ambayo nayo yako matatu. Maswali hayo
yamejibiwa katika uchanganuzi wa data na hivyo malengo ya utafiti yakatimizwa.
Katika sura hii pia nadharia iliyotumika imefafanuliwa, ambayo ni nadharia ya
Kifeministi. Katika sura hii pia umuhimu wa utafiti umeoneshwa na kuelezea jinsi
wataalamu mbalimbali, wasomaji na watafiti Watakavyofaidika. Mwishoni mwa
sura hii ya kwanza kuna mpangilio mzima wa utafiti. Katika kurasa za kwanza
istilahi na msamiati mbalimbali umefafanuliwa ili kutoa utata kwa wasomaji na
watafiti wengine. Pia vifupisho vya maneno yaliyotumika vimeandikwa kwa kirefu
katika sura hii.
Sura ya pili inatoa historia za waandishi wa kazi zilizoteuliwa na mtafiti katika
utafiti huu, wanawake katika fasihi na wanawake katika jamii. Pia mtafiti ametalii
maandiko mbalimbali yaliyotumika kujenga hoja madhubuti iliyofanya utafiti uwe
muhimu. Kigezo kilichotumika katika maandiko haya ni cha kutalii tafiti zilizohusu
waandishi na jinsi kazi zao zilivyofanyiwa utafiti na hii imemsaidia mtafiti kubaini
pengo ambalo watafiti wengine hawajalifanyia kwa kina.
Sura ya tatu ya tasnifu hii inaelezea mbinu mbalimbali za utafiti zilizotumika
kukamilisha tasnifu hii. Mbinu hizo ni pamoja na eneo la utafiti, usampulishaji, vifaa
vya utafiti sambamba na vyanzo vya data za msingi na vyanzo vya fuatizi. Utafiti
huu ulifanyikia katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam kuwahoji baadhi ya wataalam wa Fasihi ya Kiswahili, Makavazi ya Taasisi
ya Taaluma ya Kiswahili (TATAKI) na Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Maandiko mbalimbali yalisomwa. Uchambuzi wa data za utafiti huu ulizingatia
nadharia ya Ufeministi.
100
Katika sura ya nne ya tasnifu ndipo data zilipochanganuliwa. Uchanganuzi wa data
hizi ndio uliojibu maswali ya utafiti sambamba na kutimiza malengo ya utafiti
yaliyokusudiwa. Data zote zilizopatikana katika kazi teule za Penina Muhando,
maktabani na kwa wataalam wa fasihi ya Kiswahili zilichambuliwa na kuweka
bayana usawiri wa mwanamke katika tamthiliya teule za Hatia (1972) na Nguzo
Mama (1982). Mgawanyo wa majukumu kijinsia pia umeelezewa kwa uwazi kwa
kushadidiwa na hoja mathubuti na faafu za wataalamu mbalimbali waliofanya
kuhusu mwanamke. Sura hii imeongozwa na nadharia moja yaani ya ufeministi.
Mwisho tasnifu hii imejengwa na sura ya tano ambayo inatoa muhtasari wa tasnifu
nzima, inahitimisha na kutoa mapendekezo kwa watafiti, wataalamu, wasomaji/jamii
na waandishi wa tamthiliya.
5.2 Muhtasari wa Matokeo ya Utafiti
Lengo kuu la kazi hii lilikuwa kuchunguza jinsi mwanamke alivyochorwa katika
tamthiliya teule za Penina Muhando. Kutokana na uchambuzi wa data, matokeo ya
utafiti yanaonyesha kuwa tamthiliya zote mbili, Hatia na Nguzo Mama zimeonyesha
taswira mbalimbali ambazo zinaakisi masuala mbalimbali ya maisha kuhusu
mwanamke katika jamii na jinsi au mtazamo na muonekano wa mwanamke katika
jamii.
Katika utafiti huu, imegundulika kwamba nafasi ya mwanamke katika tamthiliya,
mwanamke anakandamizwa kwa kiasi kikubwa. Mwanamke bado hajapewa
muonekano chanya japo zipo taswira chache ambazo zimemuonesha mwanamke
kwa mtazamo chanya ambapo mwanamke ameonekana kama mtu mwenye
ushirikiano, mlezi na mwenye jitihada za kujikomboa pamoja na mwenye ushauri na
101
busara katika jamii. Katika baadhi ya asasi mbalimbali mwanamke ameonekana
kukandamizwa na kudunishwa na vyombo vya sheria, suala la utoaji mahari, elimu
ndogo kuhusu uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa na mfumo dume uliopo katika
jamii. Pia mwanamke ameonekana hana maadili mema ila ni mtu wa kugeuzwa na
utamaduni wa kigeni uliongia nchini. Yote haya yamesababishwa na mwanamke
kukosa urazini kuhusu haki zake. Hali hiyo ndiyo iliyowaamsha wanawake
mafeministi kuanza harakati za kujikomboa ili waweze kutokana na hali ya
kugandamizwa.
Katika swali la kwanza tumegundua kuwa, mwanamke kapewa nafasi mbalimbali za
uzuri na ubaya katika tamthilia za Hatia (1972) na Nguzo Mama (1982).
Katika upande wa mgawanyo wa majukumu, mwanamke ameonekana kuwa hawezi
kufanya kazi ambayo ni ya mshahara sawa na mwanamume. Pia mwanamke
anaonekana kuachiwa kazi zote za nyumbani ambazo hazina ujira wowote. Kazi hizo
hazithaminiwi kuanzia ngazi ya familia mpaka ngazi ya jamii, kama zilivyo za
wanaume. Hata ikiwa mwanamke amepata kazi lakini mshahara wake hauwezi
kulingana na wa mwanaume, mwanamke analipwa mshahara mdogo zaidi kwa kuwa
anaonekana kuwa hawezi.
Utafiti huu umetoa mchango ambao umeleta changamoto mpya katika fasihi
tamthiliya na katika jamii kwa ujumla. Pia umetoa changamoto katika tafiti nyingine
za kifasihi hasa katika usawiri wa mwanamke katika kazi nyingine za kifasihi.
Kwa upande mwingine, utafiti huu umetoa mwanga kwa wanawake waandishi wa
fasihi na wale wasio wa fasihi ila wanaandika kuhusiana na wanawake, kwani
102
tasnifu imeweza kugusa pande zote za kifasihi. Pia umewasaidia wanawake kujua
uthamani wa kazi zao katika jamii kwani wanafikisha ujumbe waliokusudia katika
jamii kwa njia ya fasihi kwa kuandika na kuigiza majukwaani kama ilivyo kwa
waandishi wengine wanavyofikisha ujumbe kwa njia ya maandishi.
5.4 Mapendekezo
Tasnifu hii ilihusu usawiri wa mwanamke katika tamthiliya teule za Penina
Muhando, ambazo ni Hatia (1972) na Nguzo Mama (1982). Kazi za kifasihi zipo
nyingi na zote zinatumia wahusika katika kufikisha ujumbe wake kwa jamii.
5.4.1 Mapendekezo kwa Watafiti
Kwa kuwa tasnifu ilijikita katika kuangalia wahusika wanawake katika tamthiliya,
itakuwa vema kwa watafiti wengine kuchunguza tamthiliya na kuandika makala,
majarida, na vitabu vingi kabisa ili marejeo yawe mengi. Pia ni muhimu watafiti
wengine wakafanya uchunguzi wa tamthilia kuangalia wahusika wa kiume ili kuona
kama kuna wanaume waliosawiriwa kama wanawake.
Vilevile wahusika wanawake katika tamthiliya wamechorwa kwa namna tofauti na
wasanii tofauti. Ni vema kuwachunguza wanatamthiliya na kuchunguza ujumbe wao
kisha tuweze kupata falsafa, mtazamo na msimamo wao ili kuona mchango wake
katika jamii.
5.4.2 Mapendekezo kwa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)
Wanawake ni watu walio duni mbele ya wanaume kwani jamii ndivyo inavyowaona.
Uduni wao ndio unaowafanya wasipate kazi za kuajiriwa kwa wingi kama walivyo
103
wanaume. Ingawa jamii imeanza kufunguka na kuona umuhimu wa mwanamke
katika ngazi zote lakini hata katika ajira walio wengi hawapati haki, malipo na nafasi
sawa na wanaume. Hii ni kwa sababu wanaume hawaamini kama wanawake
wanaweza kama wanaume wanavyoweza. Kutokana na tatizo hili, Mtandao wa
Jinsia nchini Tanzania unapaswa utambue kwamba hata wanawake wanaweza hata
kama wasipowezeshwa. Mtandao unapewa changamoto ya kuhimiza mabadiliko ili
mwanamke naye apate fursa sawa na mwanaume.
5.4.4 Mapendekezo kwa Jamii
Katika tamthiliya zilizotafitiwa imegundulika kwamba wanawake kwa sehemu
kubwa wamekejeliwa kutokana na jinsi walivyo, na jinsi jamii inavyowatazama na
inavyowachukulia. Pengine kejeli juu ya mwanamke inasababishwa na muonekano
wa matendo yake ndani ya jamii kuwa si mazuri. Hivyo inapaswa waelewe kwamba
fasihi au sanaa nyingine ni kioo cha jamii kinachoonesha mwenendo mzima wa watu
ndani ya jamii. Aidha wanatakiwa kubadilika na kuwa na mwenendo mzuri ili
maadili mema yaweze kuonekana kwao na wawe mfano wa kuigwa. Hata hivyo
jamii inatakiwa ipambane na suala la umalaya kwa kuwapatia wanawake kazi zenye
malipo mazuri kwani inaonekana kuwa machangudoa wengi wanafanya biashara
hiyo kwa sababu hawana kazi zinazoweza kuendesha maisha yao.
5.4.5 Mapendekezo kwa Waaandishi wa Tamthiliya
Tasnia ya uandishi wa tamthiliya imepanuka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na
kipindi cha nyuma mara baada ya Tanganyika kupata uhuru. Waaandishi wengi wa
tamthiliya aghalabu wanamchora mwanamke kama kichekesho, mtu aliyekosa
ustaarabu, kahaba na aliyekosa maadili, duni, mnyonge, tegemezi asiyeweza
104
kujitegemea mwenyewe, mtawaliwa na mjinga asiye na elimu. Aidha waandishi wa
tamthiliya inatakiwa wabadilike kulingana na wakati kwani wanawake walio wengi
wamestaarabika na wamesoma. Idadi ya wanawake waliosoma kwa sasa sio sawa na
ya miaka ya nyuma ambapo ilihitajika wapate elimu ya ngumbaro ndipo waonekane
wamesoma. Waandishi wa tamthiliya wanapaswa kumchora mwanamke katika
taswira ambazo zitamkweza mwanamke hasa tukizingatia wakati na majira
tuliyonayo kuhusu suala la ukombozi wa mwanamke. Hilo litawasaidia wanawake
kujitambua zaidi na kujua wajibu wao katika jamii, tofauti na sasa ambapo kila siku
wanakutana na tamthiliya au kazi zinazoudhalilisha utu wao. Hivyo basi mwanamke
asionekana kwa mabaya zaidi bali kwa mema pia maana yapo mengi yanayofanywa
na wanawake yanaweza hata kuzidi yale ya wanaume.
5.5 Hitimisho
Wanawake wanaweza ikiwa watawezeshwa na hata bila kuwezeshwa ikiwa
watapewa nafasi ya kuweza. Kama jamii itaona umuhimu wa kuwapa madaraka na
mamlaka ya kuongoza na kusimamia kazi katika sehemu nyeti pia. Maendeleo
yanaweza kutokea katika nchi ikiwa wanawake watapewa nafasi sawa na wanaume
katika sekta zote za uongozi yaani kuanzia nafasi ya Urais, Uwaziri, Ubunge, Jeshi,
na Uongozi wa sehemu nyingine mbalimbali, na sio kama sasa wanavyopewa tu
katika baadhi ya sekta.
105
MAREJELEO
Bader Z. (1974), “Social Condition of the Peasant Women in Zanzibar and Pemba.”
Paper No, 18 iliyowasilishwa katika semina ya Wanawake Brulap, Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam.
Balisidya, M.L (1982), “The Image of Woman in Tanzania Oral Literature: A
Survey” Katika. Mulokozi (mh), Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa
Kiswahili, Juzuu 49/2. Uk. 08.
Birkett, J na Elizabeth H. (1991) (wah), Determined Women: Studies in the
Construction of Female subject 1900-90, London, The Macmillan Press
Ltd.
Bond, S (2000), “Culture and Feminine Leadership”, katika Women Power and the
Academic From Rhetoric to Reality. New York, Berghahn Books.
Davenport(1900),www.sanseverrting.wordpress.com/2008/01/30/guy_davenport_the
_writer_as_cartoonist. 12/04/2013, Saa 12:00 Jioni
Eckman, F. na O‟Sullivan (1988)
http://www.ncbi.nlm.nihgox/pmc/articles/PMC.2223159#bhan
05/04/2013 saa 6:35 Mchana
El Saadawi (1983), Woman at Point Zero. Egypt, Zed Books.
Felluger, D.F (1998), “Undegraduate Introduction to Critical Theory” http://
scout.cs.wisc.edu/scout/report/socsci/ 11/05/2013, Saa 8:12 Mchana.
Hughes, D.M (2000), Men Create the Demand; Women Are the Supply. Lecture on
Sexual Exploitation Queen Sofia Center, Valencia, Spain November 2000
Universit of Rhodes Island.
Ilumoka A.O (1994), African Women’s Economic, Social and Cultural Rights.
Philadelphia, University of Pennsylvania Press.
Kayoka, C.M (200), The Woman in Kiswahili Literature: A Feminist Approach. Dar
es Salaam, The Open University of Tanzania.
Kezilahabi, E (2003), “Mandhari na Wahusika”, katika Makala za Semina ya
Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili 111 Fasihi. Dar es Salaam, Taasisi
ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Uk.84-89
Kiango, S.D (1982), “Tamthilia za Kiswahili: Dhamira Chapwa na Usuli katika
Uchapwa” katika Mulokozi (Mh) Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa
Kiswahili Juzuu 49/2.
Kiango S.D (1992), “Taswira ya Mwanamke katika Tamthilia za Kiswahili za
Kenya” katika Ibrahim, S. (Mh) Baragumu, Jarida la Kiswahili Juzuu
Namba 1.
106
King‟ei, K. na C.N.M Kisovi (2005), Msingi wa Fasihi Simulizi. Nairobi, Kenya
Literature Bureau.
Mackinnon, C.A (1991), Toward A Feminist Theory of the State. London, Havard
University Press.
Mbilinyi, M na Ophelia M (1980), Women and Development in Tanzania: An
Annotated Bibliography. Addis Ababa EtiopiaECA/ Ford Foundation.
Morris, P (1993), Literature and Feminism. Oxford Black.
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) (2001), Kuelekea Kwenye Usawa: Taswira ya
Mwanamke Tanzania. Dar es Salaam, SARDC.
Mulokozi, M. M (1996), Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam, Chuo
Kikuu Huria Tanzania.
Mulokozi, M.M. na Kahigi, K.K (1979), Kunga za Ushairi na Diwani Yetu.
Dar es Salaam, Tanzania Publishing House.
Mlama, P .(1976), Hatia, . Dar es Salaam: East African Publishing House.
Mlama, P. (1982), Nguzo Mama. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
Mtiro, C (2005), The Image of Women in two Tanzanian Plays, A case of Alikiona
and Machozi ya Mwanamke, Unpublished M.A Dissertation, Universty
of Dar es Salaaam,
Nabahany, A. (1972), (mh) Utenzi wa Mwanakupona. Nairobi, Heinemann
Ndomba, R.G.S (2001), “A Study on Cartoons Language in Tanzanian Newspapers:
A Sociolinguistic Stylistic Perspective.” B. A Desertation paper LL 300,
University of Dar es Salaam.
Nicholas, J. (2005), A Shelf of Our Own; Creative Writing and Australian Literature.
Australia, Australian Book Review.
Noordin M.M (2008), “Nadharia ya Ufeministi wa Kiislamu katika Fasihi ya
Kiswahili” katika Ogechi N.O, na wenzake Nadharia katika Taaluma ya
Kiswahili na Lugha za Kiafrika. Eldoret Kenya, Moi University Press.
Nyerere, Mwalimu JK (1967),”Socialism and Rural Development” Dar es Salaam.
Ngugi, G. (1961), Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi. Nairobi: East Africa Publishing
House.
Okin, S.M (1995), “Inequality between the Sex in Different Cultural Context” katika
Women Culture and Development: A Study of Human Capabilities.
Nussbaum, M na Jonathan, G. (wah) Clarendon Press Oxford
Pullen, C. (2006), Marxist against Feminists on Education. London
107
Rasaldo, M.Z (1974), “Women Culture and society: A Theoretical Overview in
Michelle Zambalist”. katika Rosaldo and Liuise L. (wah) katika Women
Culture and Society, Stanford University Press.
Sanga, Imani. (2001), Construction of Gender and Gender Roles in Religious Choirs
in Dar es Salaam. Unpublished MA Dissertation. University of Dar es
Salaam.
Sen, A. (1995), “Gender Inequality and Theories of Justice” katika Women Cultural
and Development: A Study of Human Capabilities. Nussbaum, M, C na
Jonathan G (wah). Clarendon Press-Oxford.
Senkoro F.E.M.K (1987), Fasihi. Dar es Salaam, Press and Publicity Centre.
Senkoro, F.E.M.K (2008), “English is not our Mother Land; Anecedotal Discussions
and Views on the Language Question in Tanzania”, katika LOITASA
Reflecting on Phase I and Entering Phase II. E&D Vision Publishing
Limited. Dar es Salaam.
Soko, N na Senkoro, F.E.M.K (2009), “Engendered Sports Coverage in Zambia and
Tanzania”. Paper for Presentation in the Forthcoming CODESRIA
Gender Symposium. Cairo Egypty
Shule,V. (2004), “Effective Video Film Reducing Young Mens Gender Violence
and Other .H.I.V Risk Behaviours”, (Unpublished M.A Theatre Arts
Dissertation) University of DSM.
Taib A.H (2008), “Mkabala wa Kiislamu katika Uchanganuzi na Uhakiki wa Fasihi
ya Kiswahili”, katika Ogechi N.O na wenzake (wah) Nadharia katika
Taaluma ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika. Eldoret Kenya, Moi
University Press.
UNDP (1996), Womeni in Africa Profile of Leadership A Mandate For Change.
UNDP Regional Bureau for Africa UNDP 1 UN Plaza New York.
UNESCO.(1988)http://portal.unesco.org/ci/en/ev,php_URL_ID=14786&URL_DO=
TOPIC&URL_SECON=201.html. 25/04/2013
Wamitila, K.W (2002), Uhakiki wa Fasihi, Misingi na Vipengele vyake, Nairobi,
Phoenix Publishers.
Wegesa B. B. N. (1994). Mwanamke Katika Tamthiliya za Ebrahim Hussein:
Shahada ya Uzamili ya Falsafa katika Idara ya Kiswahili Chuo Kikuu cha
Moi (Haijachapwa).
York, J. na wenzake (1991), “We are the Feminists That Women Have Warned Us
About” katika Gunew, S (mh) A Reade in Feminists Knowledge
Zerbisias A. (2010), “Ack! Cartoonists and Feminists Quarrel Over Demise of
Cathy.”
108
http://www.thester.com/living/columnists/94657_zeerbisias_antonia. Published on
Friday August, 20 ,2010.. 18/04/2013, Saa 1:10 Jioni.
109
VIAMBATANISHO
KIAMBATANISHO (a)
Hojaji kwa mwandishi
1. Je, unaitwa nani? Taja majina yako kamili.
2. Umezaliwa mwaka gani?
3. Umeolewa?
4. Je wewe ni kabila gani?
5. Je, mmebahatika kuwa na watoto wangapi?
6. Je, ni kazi zipi umewahi kufanya za kijamii tofauti na kazi za kifasihi?
7. Kwa sasa unafanya kazi gani?
KIAMBATANISHO (b)
Hojaji kwa wataalamu wa Fasihi ya Kiswahili na Sanaa
1. Mwanamke amezungumziwa vipi katika kazi za kifasihi ulizowakuzisoma?
2. Umewahi kusoma kitabu chochote cha Profesa Penina Muhando?.
3. Wanawake wametumika vipi katika matukio mbalimbali ya kijamii?
4. Ni kwanini waandishi wengi huwatumia wanawake katika matukio mabaya?
5. Mwanamke kasawiriwa vipi katika kazi za Penina Muhando?
6. Unajisikiaje unaposoma kazi ya kifasihi na kuona taswira zinazomdhalilisha
mwanamke?
7. Ni athari gani zinazotokana na usawiri wa mwanamke katika kazi za kifasihi?
8. Kwa sasa mwanamke anaonekana vipi katika kazi za kifasihi na katika jamii
ukilinganisha na kipindi cha nyuma?
110
ORODHA YA PICHA
Picha mbalimbali kuonyesha wataalamu waliohojiwa na mtafiti
Pichani ni Mtafiti pamoja na Profesa Penina Muhando mwandishi wa
tamthilia za Kiswahili wakiwa katika mahojiano katika Chuo Kikuu cha Dar
es salaam tarehe11/11/2013.
Profesa Penina muhando akiwa ofisini kwake wakati wa mahojiano mnamo tarehe
11/11/2013 katika ofisi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
111
Pichani ni Profesa Penina Muhando mwandishi wa tamthiliya ya Hatia na
Nguzo Mama akimkaribisha mtafiti ofisini kwake siku ya mahojiano tarehe
11/11/2013.
Profesa Imani Sanga akiwa ofini kwake na mtafiti siku ya mahojiano tarehe
08/11/2013, akimpatia mtafiti baadhi ya makala zake alizoandika kuhusu
mwanamke.
112
Daktari Mona Mwakalinga akiwa pamoja na mtafiti ofisini kwake baada ya
mahojiano katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 05 /11/2013.
Pichani ni daktari Vicensia Shule akishukuriwa na mtafiti ofisini kwake
tarehe 08/11/2013 baada ya mahojiano.
113
Pichani ni Mwalimu Mtiro akimdadavulia kwa kina mtafiti kuhusu usawiri
wa mwanamke katika kazi za kifasihi tarehe 18/11/2013.
Pichani ni Mwalimu Mtiro akiwa katika mahojiano na mtafiti ofisini kwake
tarehe 18/11/2013.