21
Yampasa Muislam ajiandae kufikiwa na mauti kwa kukithirisha (kufanya sana) matendo mema na kujiepusha na makatazo (vilivyoharamishwa). Vilevile mauti yawe akilini mwake, kwa maneno ya Mtume : “Zidisheni kukumbuka kiondoshacho ladha (yaani mauti)”. Hadiyth hii imepokewa na Imaam at-Tirmidhiy na akaithibitisha usahihi wake Imaam al-Albaaniy katika kitabu chake Irwaaul-Ghaliyl uk. 682. Anapofariki Muislam yampasa yule au wale waliopo pale karibu na maiti kumfanyia mambo yafuatayo: 1. Kuyafumba macho ya maiti huyo kwani Mtume aliyafumba macho ya Abu Salamah alipofariki kisha akasema: “Hakika macho yanafuata roho inapotolewa”. Imesimuliwa na Imaam Muslim. 2. Avilainishe viungo vya maiti ili visikakamae. 3. Aifunike maiti hiyo kwa nguo ambayo itasitiri mwili mzima kwa kauli ya mama wa waumini ‘Aaishah:“Hakika alipofariki Mtume alifunikwa kwa nguo iliyomsitiri kote.” Imesimuliwa na Imaam al-Bukhaariy na Imaam Muslim. 4. Waharakishe kuiandaa maiti, kuiosha, kuikafini, kuiswalia na kuizika. Kwani Mtume amesema: “Liharakisheni jeneza…” Imesimuliwa na Imaam al-Bukhaariy na Imaam Muslim. 5. Waizike katika mji au eneo alilofia kwa vile katika vita vya Uhud “Mtume aliamrisha mashahidi wa vita wazikwe pahala pale walipofia wala wasihamishwe”. Imepokewa na Ahlus Sunan (Ma-Imaam Abu Daawuud, an- Nasaaiy, at-Tirmidhiy, Ibnu Maajah) na ameithibitisha usahihi wa Hadiyth hiyo Imaam al-Albaaniy katika kitabu chake cha Ahkaamul Janaaiz uk. 14.

Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

  • Upload
    1300132

  • View
    392

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

Yampasa Muislam ajiandae kufikiwa na mauti kwa kukithirisha (kufanya sana) matendo mema na kujiepusha na makatazo (vilivyoharamishwa). Vilevile mauti yawe akilini mwake, kwa maneno ya Mtume :

“Zidisheni kukumbuka kiondoshacho ladha (yaani mauti)”. Hadiyth hii imepokewa na Imaam at-Tirmidhiy na akaithibitisha usahihi wake Imaam al-Albaaniy katika kitabu chake Irwaaul-Ghaliyl uk. 682.

Anapofariki Muislam yampasa yule au wale waliopo pale karibu na maiti kumfanyia mambo yafuatayo:

1. Kuyafumba macho ya maiti huyo kwani Mtume aliyafumba macho ya Abu Salamah alipofariki kisha akasema: “Hakika macho yanafuata roho inapotolewa”. Imesimuliwa na Imaam Muslim.

2. Avilainishe viungo vya maiti ili visikakamae.

3. Aifunike maiti hiyo kwa nguo ambayo itasitiri mwili mzima kwa kauli ya mama wa waumini ‘Aaishah:“Hakika alipofariki Mtume alifunikwa kwa nguo iliyomsitiri kote.” Imesimuliwa na Imaam al-Bukhaariy na Imaam Muslim.

4. Waharakishe kuiandaa maiti, kuiosha, kuikafini, kuiswalia na kuizika. Kwani Mtume amesema: “Liharakisheni jeneza…” Imesimuliwa na Imaam al-Bukhaariy na Imaam Muslim.

5. Waizike katika mji au eneo alilofia kwa vile katika vita vya Uhud “Mtume aliamrisha mashahidi wa vita wazikwe pahala pale walipofia wala

wasihamishwe”. Imepokewa na Ahlus Sunan (Ma-Imaam Abu Daawuud, an-Nasaaiy, at-Tirmidhiy, Ibnu Maajah) na ameithibitisha usahihi wa Hadiyth hiyo Imaam al-Albaaniy katika kitabu chake cha Ahkaamul Janaaiz uk. 14.

Page 2: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

• Kumuosha, kumkafini, kumswalia na kumzika maiti ni FARDHU KIFAAYAH, yaani ni jambo ambalo baadhi ya waislam wakifanya basi hukumu hiyo hutenguka kwa waliobaki (silazima walifanye). • Ni bora zaidi wamuoshe maiti wale mawasii wake, yaani wale watu waliousiwa na maiti kumuosha. • Kisha baba yake kwa sababu ndie mwenye mapenzi na uchungu kwa mwanae, kisha hufuatia jamaa zake wa karibu. • Mwanamke ataoshwa na wasii wake wa kike, kisha mama yake na halafu binti yake kisha waliokaribu zaidi nae katika jamaa zake. • Mume atamuosha mkewe, kwani Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص alimuambia mama ‘Aishah Haikudhuru ikiwa utakufa kabla yangu basi)) ,ااهنع هللا يضرnitakuosha))…Imesimuliwa na Imam Ahmad. Mke vile vile atamuosha mumewe, kwani Abu Bakr هنع هللا يضر aliusia akifa aoshwe na mkewe. Imetolewa na AbdurRazzaaq. • Mwanamume na mwanamke wanaweza kumuosha mtoto wa chini ya umri wa miaka saba awe wa kike au wa kiume kwasababu utupu wa mtoto huyo hauna hukmu yeyote. • Akifa mwanaume katika kundi la wanawake watupu au akifa mwanamke katika kundi la wanaume, basi haoshwi bali hufanyiwa TAYAMMUM (yaani hutwaharishwa kwa mchanga), ataipiga mikono yake kwenye ardhi ambapo kuna mchanga au udongo kisha ataupangusa uso na viganja vya maiti. • Ni haramu kwa muislamu kumuosha au kumzika kafiri kwa mujibu wa maneno ya Mwenyezi Mungu S.W.T., {{wala usimswalie abadan yeyote katika wao aliekufa...}} {Sura at-Taubah aya na. 84}. Ikiwa imekatazwa kuwaswalia hao makafiri ambalo ndio jambo kubwa zaidi, basi kuwaosha na kuwazika nayo pia yamekatazwa. • Inasuniwa wakati wa kumuosha maiti, kumsitiri utupu wake kwa kumfunika kwa nguo itakayomsitiri na macho ya watu, huenda pia hiyo maiti ikawa katika hali isiyopendeza kuonekana (tazama picha namba 1).

[Maiti ikiwa imelazwa juu ya meza ya kumuoshea na huku imesitiriwa sehemu zake za siri]

PICHA NAMBA 1

• Muoshaji anatakiwa avae gloves kabla ya kuanza kumuosha maiti kisha muoshaji anatakiwa akinyanyue kichwa cha maiti hadi kikaribie usawa wa kukaa kwake na kisha aliminye kwa upole tumbo lake ili litoe uchafu ulioko tumboni na wakati huo huo azidishe kumwagia maji sehemu ya uchafu ili uondoke (tazama picha namba 2).

Page 3: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

[Muoshaji akimnyanyua kidogo maiti na kuliminya tumbo lake kwa utaratibu ili utoke uchafu]

PICHA NAMBA 2

• Kisha avae gloves (vifuniko vya mikono) na ausafishe utupu wa maiti bila ya kuugusa au kuutazama ikiwa maiti hiyo ni ya umri wa zaidi ya miaka saba(tazama picha namba 3).

[Muoshaji akisafisha sehemu za siri za maiti kwa kutumia mpira wa maji akiwa amevaa gloves]

PICHA NAMBA 3

• Kisha apige au aseme Bismillah na kumtawadhisha udhu kama wa swala kama alivyoelekeza Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص kwa wanawake waliokuwa wakimuosha binti yake aitwaye Zaynab, ((Anzeni kuliani mwake wakati mnamuosha na pia sehemu za udhu mwilini mwake)). Ila asiyaingize maji puani, kinywani, masikioni au ndani ya macho yake, bali atumie kitambaa kilichokuwa kidogo na kusafisha meno, ndani ya pua na masikioni mwake.

Page 4: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

• Kisha pia aingize pamba au kitambaa chenye unyevunyevu kwenye masikio yake nakuyasafisha. Inapendeza vilevile asafishe nywele na ndevu za maiti kwa kutumia sabuni,na kisha mwili mzima(tazama picha namba 4 na 5).

[Kichwa cha maiti kikiwa tayari kwa kuoshwa]

PICHA NAMBA 4

PICHA NAMBA 5

• Kisha amsafishe (amuoshe) upande wa kuliani kwake, sehemu za mbele na za nyuma,(tazama picha namba 6 na 7) tena hivyo hivyo upande wa kushotoni kwake kwa hadithi ya Mtume isemayo, ((anzeni kuliani mwake…..)), kisha aendelee kumsafisha hivyo hivyo mara ya pili na ya tatu kwa maneno yake Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص, ((muosheni mara tatu)) na wakati akimuosha aupitishe mkono wake katika mwili wake (maiti) kuusugua ili kutoa uchafu kama upo.

Page 5: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

[Muoshaji akimuosha maiti upande wa mbele wa kulia]

PICHA NAMBA 6

[Muoshaji akimuosha maiti upande wa nyuma wa kulia]

PICHA NAMBA 7

• Muoshaji anaweza kuzidisha zaidi ya mara tatu ikibidi na hata ikizidi mara saba haidhuru.

• Imesuniwa atie KAFUUR (karafuu maiti) katika muosho wa mwisho nayo harufu yake hufukuza vijidudu, Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص amesema ((Tumieni KAFUUR katika muosho wa mwisho)). • Imesuniwa kumuosha maiti kwa maji ya baridi, yatatumika ya moto pale itakapo bidi, kwa

Page 6: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

mfano ikiwa mwili wa maiti una uchafu ambao inabidi yatumike maji ya vuguvugu ndio yatoe uchafu huo. Pia atumie sabuni kuondosha uchafu lakini asitumie nguvu kumsugua asije akamchubua, vilevile atumie kijiti cha meno kusafisha meno ya maiti. • Ni sunna vilevile kupunguza masharubu ya maiti na kukata kucha zake kama ni ndefu, ama nywele za kwapa na sehemu nyingine hizo haziguswi. • Haitakiwi kuchana nywele zake kwani zinaweza kukatika, ama za mwanamke nywele zake hugawanywa au husukwa minyoosho mitatu na kuunganishwa nyuma. • Inapendeza kumpangusa maji na kumkausha baada ya kumuosha. • Ikiwa maiti atatokwa na uchafu wowote (mkojo, kinyesi au damu) baada ya kuoshwa mara saba, basi atawekewa pamba kwenye utupu wake na kisha kuoshwa pale pahala palipoingia najisi na kisha kutawadhishwa. • Endapo kitatoka kitu kichafu baada ya kwisha kukafiniwa basi haipasi tena kumuosha kwa kuepusha usumbufu. • Atakapofariki MUHRIM (mwenye kufanya hajj au umra) basi ataoshwa kwa maji na SIDR kama ilivyotangulia lakini tofauti ni kwamba yeye hatotiwa manukato wala kufunikwa kichwa chake ikiwa ni mwanaume kama alivyosema Mtume S.A.W kuhusu mtu aliyefariki akifanya Hajj, ((msimpake manukato au msimuoshe kwa manukato)) na akasema pia, ((wala msimfunike kichwa chake kwani yeye anafufuliwa siku ya kiama akilabii (yaani akipiga talbiya kwa kusema Labbayka Allahumma Labbayka…))). Hadithi hii imethibitishwa usahihi wake na maimam wote. • Shahidi aliyefariki vitani haoshwi, kwani Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص ((aliamrisha mashahid wa UHUD wazikwe na nguo zao bila kuoshwa)). Hadithi hii imethibitishwa usahihi wake na ma Imam Bukhari na Muslim. Huzikwa shahidi afae vitani na nguo zake baada ya kuondolewa silaha alizokuwa nazo mwilini mwake. Wala haswaliwi kwani Mtume هللا يلص hakuwaswalia mashahidi wa vita vya UHUD ملسو هلآو هيلع• Kiumbe kilichofika miezi minne tumboni mwa mama yake kikitoka kinaoshwa na kinaswaliwa na kinapewa jina kwa kauli ya Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص, ((hakika mmoja wenu anakuwa katika tumbo la mama yake siku arobaini ni tone la manii, kisha anakuwa kipande cha damu mfano wa hivyo (yaani siku arobaini nyingine), kisha kinakuwa kipande cha nyama mfano wa hivyo (yaani siku arobaini nyingine), kisha anatumwa malaika kukipulizia roho)). Imesimuliwa na Imam Muslim. Ama kikiwa kabla ya miezi minne kinakuwa kipande cha nyama kinazikwa pahala popote bila kuoshwa wala kuswaliwa. • Kutopatikana udhuru wa maiti wa kutoweza kuoshwa ima kwa kukosekana maji au mwili wake unakatikakatika hauwezi kuosheka au umeungua kwa moto basi kwa hali hiyo anatakiwa atayamishwe (yaani mtu atapiga matumbo ya viganja vyake katika udongo au mchanga kisha ataupangusa uso na viganja vya maiti). • Inampasa muoshaji amsitiri maiti ikiwa ataona kuna kitu hakipendezi kwa maiti huyo, kama vile uso wake umeharibika au kuna jeraha katika kiwiliwili chake au kovu la kutisha n.k kwani Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص amesema, ((mwenye kumuosha maiti akaficha siri zake, basi Mwenyezi Mungu atamsamehe yeye mara arobaini)). Imesimuliwa na Imam Al Hakim na ikathibitishwa usahihi wake na Imam Albani. • Ni haramu vile vile kuchana nguo wakati wa msiba na kujipiga mashavu au sehemu zozote mwilini kama wafanyavyo mashia wakati wa Muharram kuomboleza kifo cha Imam Al Husayn هنع هللا يضر au kung’ofoa nywele n.k. kwani Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص alikataza kufanya hivyo kwa kusema, ((hawawi miongoni mwetu wale ambao (wanapofiwa) hujipiga vibao mashavuni na kuchanachana nguo zao na kupiga mayowe (na makelele na kulalamika kama walivyofanya watu) wakati wa jaahiliya [kabla ya Uislam])). Muttafaqun ’alayhi (Imepokewa na Imam Al Bukhari na Muslim.

Page 7: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

Yampasa kumkafini maiti na vile vile yapasa gharama za sanda zitokane na mali ya maiti mwenyewe kama alivyosema Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص wakati alipofariki mtu akiwa katika hali ya kuhirimia, ((mkafinini kwa nguo yake)) yaani vazi lake la ihram na huko mkafini (kumpamba) maiti kunatangulizwa kabla ya deni lake kulipwa kama analo na hata kabla ya kuutekeleza wasia wake wa mirathi. • Endapo maiti huyo hakuwa na uwezo wa kuwa na sanda basi jamaa zake wenye kuhusiana naye watakuwa na wajibu wa kuandaa sanda kwa ajili yake. Nao ni watu wake kama baba yake, babu, mwanae wa kiume au mtoto wa mwanae (mjukuu). Na endapo wote hao watashindwa au atakuwa hana jamaa,basi litakuwa jukumu la BAYTUL MAAL, yaani litatolewa fungu kutoka katika hazina ya waislam kama ipo, na kama haipo basi litakuwa jukumu la muislam yeyote aifahamuye hali ya huyo maiti. • Kinachopasa kumkafini maiti ni nguo itakayomsitiri mwili mzima. • Ni sunna kumkafini maiti mwanaume kwa vipande vitatu vya sanda nyeupe kwani Mtume . Hadithi hii ni Muttafaqun ‘Alayhi .(alikafiniwa kwa sanda nyeupe) ملسو هلآو هيلع هللا يلصVipande hivyo vya sanda hutiwa harufu nzuri ya aina ya ubani uliosagwa, kisha hukunjwa moja juu ya nyingine na pia hutiwa kwenye sanda hiyo HANUUT, aina ya unga wenye harufu nzuri ambayo ni maalum kwa maiti na pia husuniwa kufungwa kitambaa chenye pambo ndani yake katika tupu mbili za maiti ili kusitiri na kuzuia eneo lote la utupu wa maiti (tazama picha namba 8), kisha baada ya hapo maiti hulazwa juu ya hiyo sanda iliyotiwa vitu hivyo, hulazwa chale(tazama picha namba 9) kisha huwekwa pamba yenye manukato kwenye matundu ya masikio yake kuzuia kama kutatoka harufu mbaya.

[Vipande vya sanda vikiwa vimetandikwa juu ya meza na kutiwa manukato ya unga tayari kwa maiti kulazwa juu yake]

PICHA NAMBA 8

[Maiti ikiwa imesitiriwa sehemu zake za siri na huku imelazwa chale juu ya meza]

PICHA NAMBA 9

Page 8: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

• Ni sunna kuiweka HANUUT (manukato ya unga) katika maeneo ya matundu yaliyomo usoni mwa maiti kama vile machoni, puani, mdomoni na masikioni na pia juu ya maeneo yote ya sehemu za kusujudia. Pia si vibaya ikiwa kutatiwa HANUUT sehemu za mwili zilizobaki kwa kuwa baadhi ya Maswahaba مهنع هللا يضر walivyofanya hivyo.

• Kisha hufunikwa sehemu ya kulia ya mwili wake kwa kipande cha kwanza cha sanda (kama inavyoonyesha picha na.10),

[Maiti anaanza kufunikwa upande wa kulia kwa kipande cha kwanza cha sanda na kisha utafuatiwa upande wa kushoto vile vile]

PICHA NAMBA 10

kisha hufuatia upande wa kushoto uliobaki wa mwili wake kwa kipande kile kilichobaki cha sanda. Kisha hufunikwa tena hivyo hivyo kwa kipande cha pili na cha tatu cha sanda.Kisha ataondosha ile taulo au kitambaa alichoweka kuusitiri utupu wa maiti mwanzo wakati akimuosha (kama inavyoonyesha picha na.11).

Page 9: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

[Maiti akitolewa taulo au nguo iliyokuwa inamsitiri katika utupu wake kisha akimaliza kufunikwa na vipande vilivyobaki vya sanda]

PICHA NAMBA 11

Kisha sanda hiyo husokotwa mwisho wake na kuanza kufungwa ili isije ikaachia sehemu yeyote na kulegea(kama picha na.12 inavyoonyesha).

[Sanda ya maiti ikisokotwa tayari kwa kufungwa]

PICHA NAMBA 12

Kisha hizo sehemu zilizofungwa zikawa zaning’inia hurejeshwa upande wa kichwani na miguuni na kufungwa kwa pamoja (tazama picha na.13).

Page 10: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

[Mafundo yakiwa yameshafungwa tayari na kurudishwa upande wa mwili wa maiti]

PICHA NAMBA 13

na hufunguliwa mafundo hayo yote kaburini. Na hakuna madhara yoyote endapo mafundo yafungwayo yatakuwa chini ya mafundo saba. Makusudio ya mafundo hayo ni kufanya kule kumkafini maiti kuwe imara.

Baada ya hapo husokota ncha ya hivyo vipande vya sanda na kuvifunga. Nayo hufungwa mafundo saba imara (tazama picha namba 14).

[Maiti ikiwa imeshafungwa madhubuti tayari kwa kuenda kutiwa katika jeneza]

PICHA NAMBA 14

• Vile vile huruhusiwa kumkafini maiti kwa vazi la kawaida kama shuka ya chini (kikoi) na nguo ya juu kama kanzu au shati ila ni bora zaidi kutumia mfumo uliotajwa mbeleni.

• Mwanamke anakafiniwa kwa nguo au vitambaa vitano,kwa shuka IZAAR ambayo huvalishwa chini ya kiwiliwili chake, KHIMAAR au kifuniko cha juu ya kichwa ambayo hushuka hadi kifuani na QAMIYS nayo ni kama kanzu ambayo huwa wazi pembezoni mwake (ubavuni) na vipande viwili vikubwa ambavyo hufunika mwili wake wote kwa ujumla. Swala ya jeneza (maiti) ni FARDHU KIFAAYAH (wanapofanya baadhi ya waislam basi inatosha na si lazima waislam wengine waliobaki kuifanya). • Inasuniwa kwa Imam wakati wa kumswalia maiti asimame kuelekea kichwani mwake akiwa maiti ni mwanaume (tazama picha na.15).

Page 11: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

[Imamu akiwa anaswali huku amesimama akielekea upande wa kichwa cha maiti wa kiume]

PICHA NAMBA 15

na kama maiti ni mwanamke basi asimame kuelekea katikati yake (tazama picha na.16).

Page 12: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

[Imamu akiwa anaswali huku amesimama akielekea katikati ya maiti wa kike]

PICHA NAMBA 16

Hivyo ndivyo alivyofanya Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص, amesimulia hadithi hii Imam Abu Dawud na ameithibitisha usahihi wake Imam Albani katika kitabu chake cha AHKAMUL JANAIZ.

• Ni sunna Imam kuwa mbele ya maamuma, lakini endapo itakosekana nafasi basi maamuma wasimame kuliani na kushotoni kwake naye awe katikati yao. • Atakapoanza kuswalisha imam atasema Audhubillah Mina Shaytwaan Rajiim. Kisha atapiga Takbira nne atanyanyua mikono katika takbir ya kwanza. Kisha si lazima kunyanyua mikono katika takbir tatu zilizobaki kwani maswahaba walifanya hivyo. Na si vibaya kwa mtu kunyanyua vile vile. • Baada ya takbira ya kwanza atasoma Suratul Faatiha na baada ya takbira ya pili atamswalia Mtume kama anavyofanya katika TASHAHUD yaani atasema ((Allahumma swali ‘alaa Muhammad wa’ala aali Muhammad kamaa swalayta ‘alaa Ibraahiym wa’alaa aali Ibrahiyma, Innaka hamiydunmajiyd. Wabaariki a’laa Muhammad….)) Na endapo atafupisha na kusema ((Allahumma swali a’laa Muhammad)) basi pia inafaa Wallahu A’alam. • Kisha baada ya takbira ya tatu anatakiwa amuombee maiti kwa dua zilizothibiti kutoka kwa Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص Miongoni mwa dua hizo ni hii ((Allahummaghfir lahu warhamhu, wa'afihi wa’afanhu, wanaqihi minal khatwaayaa kamaa yunaqa athawbul abyadh minnad danas, waabdilhu daaran khayran min daarihi, wa ahlan khayran min ahlihi, wazawjan khayran min zawjihi, waadkhilhul jannah, waa’idh-hu min ‘adhaabil qabri, wamin ‘adhabi nnaar)). Imesimuliwa na Imam Muslim. • Ama kuhusiana na ASSIQT nacho ni kile kiumbe kilichozidi miezi minne,katika swala kinaombewa msamaha na rehema kwa baba yake kwa kauli ya Mtume هلآو هيلع هللا يلص .((ASSIQT kinaswaliwa na kuombewa msamaha na rehema mzazi wake)) ,ملسوImesimuliwa na Imamu Abuu Dauud na imethibitishwa usahihi wake na Imamu Albani. • Na kisha baada ya takbira ya nne atanyamaza kidogo na kisha atatoa salamu mara moja tu upande wa kulia kama alivyofanya Mtume S.AW. Imesimuliwa na Imam Al Haakim na kuthibitishwa usahihi wake na imam Albani na pia mtu anaweza kutoa salam upande wa kushoto. Tazama kitabu cha AHKAAMUL JANAIZ cha Imam Albani. • Atakayepitwa na baadhi ya takbira basi anatakiwa amfuate imam, mathalan amemkuta imam yuko katika takbira ya tatu basi afanye kila kinachofanywa katika takbira hiyo, nayo ni kusoma dua ya kumuombea maiti kisha baada ya takbira ya nne yeye hatatoa salam bali atapiga takbira na kusoma surat fatiha, na halafu atapiga takbira nyingine na kumswalia Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص na baada ya hapo ndipo atatoa salaam. Hayo yote atayafanya endapo kutakuwa na nafasi, ila akiona jeneza linanyanyuliwa basi ataacha na haidhuru. • Atakayepitwa au kuchelewa kumswalia maiti, basi atamswalia kaburini, wakati anaiswalia maiti kaburini anatakiwa aelekee kibla na kaburi liwe katikati yake na kibla, ataiswalia kama inavyosikiliwa maiti (tazama picha na.17) kama alivyofanya Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص Muttafaqun ‘Alayh

Page 13: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

[Mtu anaonekana akimswalia maiti kaburini kaburi likiwa mbele yake na huku ameelekea kibla]

PICHA NAMBA 17

• Inapendeza vile viele swala ya ghaib, yaani kwa mtu aliyefariki mji au nchi nyingine ikiwa huko aliko hakuswaliwa.

• Waislamu wanaweza kumswalia mtu aliyejiua , jambazi lakini ni bora kiongozi wa waislam wa eneo hilo pamoja na mwanachuoni mkuu wasimswalie kwa kutoa funzo kwa wengine kama hao. • Swala ya maiti inaruhusiwa kuswaliwa msikitini, kama alivyofanya Mtume هلآو هيلع هللا يلص imesimuliwa na Imam Muslim, lakini ilivyo sunna ni kuiswalia pembeni ya msikiti na ni ملسوvizuri kutenga eneo rasmi karibu na msikiti au karibu na makaburi kwa ajili tu ya kuswaliwa maiti ili msikiti usipate madhara ya kuchafuka n.k. Na ubora wa kupatikana eneo karibu na makaburi ni kwa ajili ya kuwarahisishia na kuwafanyia wepesi wazikaji Wallahu A’alam. Ni vizuri kulibeba jeneza kwa pande zake zote nne mabegani (tazama picha na.18).

Page 14: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

[Wazikaji wakiwa wamebeba jeneza ambalo halijazibwa pande zote kama ambavyo inavyopaswa kisunnah]

PICHA NAMBA 18

• Imesuniwa kulipeleka jeneza kwa mwendo wa kasi kiasi, kwani Mtume هلآو هيلع هللا يلص .amesema, ((Lipelekeni jeneza haraka)) ملسو

• Inasuniwa watu wasindikizao jeneza kutembea nyuma , mbele, kuliani na kushotoni mwa jeneza, vyote hivyo vimepokewa kwa matendo ya Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص(SOMA KITABU CHA AHKAAMUL JANAIZ cha Imam Albani) • Ni tendo la kuchukiza mno kwa mtu kukaa chini kabla ya jeneza halijashushwa kwani Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص alikataza kufanya hivyo. • Ni vibaya kuzika maiti katika nyakati tatu ambazo Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص alizikataza, nazo zimesimuliwa katika hadithi aliyoipokea ‘Uqbah bin A’amir هنع هللا يضر aliposema, (Nyakati tatu Mtume alitukataza tusiziswali swala zetu au tusizizike maiti zetu: wakati jua linapotoka (machweo) hadi lichomoze lote yaani lipande. Na jua linapokuwa utosini wakati wa adhuhuri hadi litakapopinda kidogo. Na jua linapozama, hadi lizame lote). Imesimuliwa na Imam Muslim. • Inafaa kumzika maiti usiku au mchana kulingana na wepesi ila tu isiwe katika hizo nyakati tatu zilizotajwa. • Imesuniwa kulifunika kaburi la mwanamke wakati atakapoingizwa ndani yake ili kumsitiri. • Imesuniwa kuanza kumuingiza maiti kaburini kwa upande wa ncha ya kaburi(tazama picha namba 19)

Page 15: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

[Maiti ikiingizwa kaburini na huku kikitangulizwa kichwa chake kuingizwa]

PICHA NAMBA 19

na ikishindikana basi aingizwe kwa upande wa qiblah (tazama picha na. 21).

[Maiti ikiingizwa kaburini kutokea upande wa kibla]

PICHA NAMBA 20

Page 16: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

• Huchimbwa kaburi kwa aina ya AL LAHD (shimo lililomo ubavuni mwa kaburi) nayo ni kuchimba shimo ndani ya kaburi ambalo ni kipimo cha huyo maiti na linakuwa upande wa qiblah na humo ndimo awekwapo maiti. (kama picha na. 22 inavyoonyesha).

[Aina ya kaburi ambalo shimo lake liko ubavuni mwa kaburi upande wa kibla]

PICHA NAMBA 21

• Na hiyo LAHAD ni bora kuliko SHAQ, amesema Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص, ((LAHD ni yetu na SHAQ ni ya wengineo)). Amesimulia Imam Abu Dauud na akaithibitisha usahihi wake Imam Albani katika kitabu chake cha AHKAMUL JANAAIZ uk 145. Na SHAQ ni aina ya shimo kuchimbwa ndani katika kaburi (kama ionyeshavyo picha na.22)

Page 17: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

[Aina ya kaburi ambalo shimo lake limo katikati]

PICHA NAMBA 22

• Ni sunnah kuchimba shimo ndefu ili maiti asalimike na wanyama kama vile kenge na pia kusaidia harufu ya maiti kutokutoka nje kirahisi.

• Mwenye kumuingiza maiti kaburini anatakiwa aseme : (Bismillahi wa 'alaa sunnati au wa 'alaa millati rasulillahi). Imesimuliwa na Imam Abu Dawud na ikathibitishwa usahihi wake na Imam Albani katika kitabu chake Ahkamul Janaaiz uk. 152.

• Watakaoingia kaburini ni mawasii wake (waliousiwa na maiti kumzika) kisha jamaa zake na endapo watakosekana basi muislamu yoyote.

• Ni bora kumweka maiti ndani ya kaburi katika shimo lililomo ubavuni mwa kaburi upande wa kibla kwa kumlaza kwa ubavu wake wa kulia akielekea kibla (tazama picha namba 24) kama alivyosema Mtume (ملسو هلآو هيلع هللا يلص), ((Ka'abah ni kibla chenu mkiwa hai au wafu)). Imesimuliwa na Imam Bayhaqi na imethibitishwa ubora wake na Imam Albani katika kitabu cha Al - Irwaa uk. 690.

Page 18: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

[Maiti akiwa amelazwa kwa ubavu wake wa kulia na kichwa chake kimeelekea kibla]

PICHA NAMBA 23

• Wala kisiwekwe chini ya kichwa chake aina yeyote ya kiegemezo kama vile tofali au jiwe, kwa sababu kitendo kama hicho hakikufanyika wakati wa Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص na pia hakikuachwa kichwa cha maiti wazi ila tu kama amekufa akiwa ni mwenye kuhirimia, yaani yuko katika Hajj kama ilivyotanguliwa kusemwa. Na baada ya kuwekwa kwenye

LAHAD linatakiwa ni hilo LAHAD lizibwe kwa matofali na matundu yatakayobaki yazibwe kwa udongo.

• Imesuniwa baada ya kumaliza kumweka ndani ya shimo la kaburi waislam waliohudhuria wamwage vitanga vitatu vya udongo ndani ya kaburi kwa matendo yake Mtume هللا يلص Imesimuliwa na Imam Ibnu Maajah na ameithibitisha usahihi wake Imam ملسو هلآو هيلعAlbani katika kitabu chake AHKAAMUL JANAAIZ uk 153 (tazama picha na.24).

Page 19: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

[Mzikaji akimwaga ndani ya kaburi vitanga vitatu vya udongo]

PICHA NAMBA 24

• Ni sunna kulinyanyua kaburi, yaani baada ya kufukiwa maiti kaburini lizidi usawa wa ardhi kwa urefu wa kiganja kimoja cha mkono ili lijulikane kuwa ni kaburi na pia watu wasije kupita na kulikanyaga au kukaa juu yake n.k. Na mnyanyuko huo uwe kama nundu ya ngamia (tazama picha namba 25).

Page 20: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

[Kaburi likiwa limenyanyuliwa kiasi ili lijulikane watu wasije kupita juu yake na kulikanyaga]

PICHA NAMBA 25

kisha huwekwa HUSWBAA (changarawe) kama kulivyofanywa katika kaburi la Mtume يلص Imesimuliwa na Imam Abuu Daud ili lijulikane kama kaburi lisije ملسو هلآو هيلع هللاlikakanyagwa au kupitwa juu yake, kisha yamwagiwe hizo changarawe maji, kwa kuwa imepokewa hivyo na katika sunnah imepokewa kwa mapokezi ya kuthibitika ,(Tazama kitabu cha AL-IRWAA Vol 3/206). Pia juu ya kaburi upande wa kichwa cha maiti huweza likawekwa jiwe, kama alivyofanya Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص katika kaburi la Uthmaan bin Madh’uun هنع هللا يضر. Imesimuliwa na Imam Abu Daood na akaithibitisha usahihi wake Imam Albani katika kitabu chake cha AHKAAMUL JANAAIZ uk 155.

• Ni haramu kulijengea kaburi na kuliandika kitu juu yake, au kulikalia juu yake au kuliegemea kwani Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص alikataza kufanya hivyo vyote kwa hadithi iliyosimuliwa na Imam Muslim. • Inachukiza kuzika maiti wawili katika kaburi moja ila iwe ni kwa dharura, mathalan itaruhusiwa endapo maiti watakuwa wamezidi na wazikaji ni wachache au maiti ni wengi na makaburi ni machache, kama ilivyofanywa kwa mashahidi wa vita vya UHUD. Na endapo watazikwa maiti wawili katika kaburi moja basi iwekwe kizuizi cha udongo baina yao. • Ni sunna kuwapelekea jamaa wa maiti chakula kwa kuwa watakuwa na jambo la kuwashughulisha (msiba) na pia watakuwa wameshughulishwa na maiti n.k. Kama alivyowaambia Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص maswahaba zake wakati Jaafar bin Abi Twaalib alipofariki, ((watengenezeeni watu wa Ja’afar chakula kwa kuwa kuna linalowashughulisha)). Amesimulia hadithi hii Imam Abu Dawud na ameithibitisha usahihi wake Imam Albani katka kitabu chake cha AHKAAMUL JAANAIZ uk 167. • Ni jambo la kuchukiza (makrooh) kwa waliofiwa kuwapikia watu chakula kwa kauli ya maswahaba watukufu wa Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص, ((tulikuwa tukichukulia kutengeneza

Page 21: Yampasa Muislam Ajiandae Kufikiwa Na Mauti Kwa Kukithirisha

vyakula na kukusanyika kwa jamaa wa maiti ni katika NIYAAHAH (kuomboleza kwa mayowe na kuongea kuhusu maiti mambo mbalimbali na kutoa sauti za ajabu) )) Imesimuliwa na Imam Ahmad (R.A) na ameithibitisha usahihi wake Imam Albaani (R.A) katika kitabu cha Ahkaamul Janaaiz. • Husuniwa kwa wanaume kuzuru makaburi kwa ajili ya kuwaombea maiti na kupata mazingatio ya mauti (tazama picha namba 26) kwa kauli ya Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص, ((Nilikuwa nimewakataza kuzuru makaburi, ila sasa mnaweza kuyazuru, kwani kuyazuru makaburi kunawakumbusha akhera )). Imesimuliwa na Imam Muslim. Kuna hadithi yenye kuharamisha wanawake kuyazuru makaburi aliposema Mtume هيلع هللا يلص Ni hadithi hasan .((wamelaaniwa wanawake wenye kuyazuru makaburi )),ملسو هلآو(yenye kukubalika), lakini maulamaa wakubwa wa hadithi akiwemo Imam Albani ameeleza kuwa hadithi hii ilifutwa na hadithi iliyopita ya Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص aliposema, ((Niliwakataza kuzuru makaburi ila sasa mnaweza kuyazuru…….)) Hivyo basi baadhi ya maulamaa mashuhuri wa hadithi kwa mujibu wa hadithi ya pili ambayo Mtume ameruhusu kuyazuru, wanaona hakuna kizuizi kwa wanawake ملسو هلآو هيلع هللا يلصkuyazuru makaburi kwani hadithi hiyo haijatofautisha baina ya wanaume na wanawake bali imekuja kwa maneno ya ‘UJUMLA’ yaani ‘NILIWAKATAZA’ na ‘NIKAWARUHUSU’. na pia kuna ushahidi mwingine wa tukio lililosimuliwa na 'Abdullah bin Abi Mulaykah: ((Siku moja 'Aisha رر alikuwa akitokea makaburini, nikamuuliza, 'Ewe mama wa waumini je رررر رررر رunatokea wapi?' Akasema: 'Natokea makaburini kuzuru kaburi la ndugu yangu 'Abdurrahmaan bin Abi Bakr.' Nikasema, 'Je, Mtume ر رر رررر رررر رررر رر ررhakukataza (wanawake) kuzuru makaburi?' Akasema, 'Ndio, kisha aliamrisha (au kuruhusu) kuyazuru.')) Imetolewa na Imam Al Haakim, Al Bayhaqi na Ibn 'Abdil Barri. Amehakikisha usahihi wake Imam Dhahabi na Al Buswayri. Wallahu A’alam! • Anachotakiwa kusema kwa mwenye kuzuru makaburi ni hivi: ((ASSALAAM ‘ALAYKUM DAARA QAUMU MUUMINIYN,WAINNA INSHAALLAH BIKUM LAAHIQUUN)), ((AMANI IWE JUU YENU ENYI WAKAZI WAUMINI, NASI KWA MATASHI YA ALLAH NI WENYE KUWAFUATA)) kutokana na mafunzo yake ملسو هلآو هيلع هللا يلص Imesimuliwa na Imam Muslim. Waislamu wanatakiwa wajichunge na kujihadhari sana kuyatukuza makaburi au kutafuta baraka kutoka hayo makaburi na pia kujipangusa kwayo. Kwani yote hayo yanapelekea katika Shirki!!! • Ni sunna kuomboleza watu waliofiwa kwa kusema, ((Inna lilaahi maa akhadha walahu ma A’atwa, wakulu shay-in ‘indahu bi ajali musammaa, faswbir wahtasib)). Hii dua imethibiti kutoka kwa Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص Muttafaqun ’alayhi. Maana ya dua hii ni (hapana shaka ni chake Mwenyezi Mungu alichokitwaa na ni chake alichokitoa, na kila jambo kwake ni kwa wakati na muda maalum (uliopangwa), basi fanya subira na utaraji malipo) na vile vile Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص akisema, ((Mwenyezi Mungu azidishe ujira wako)) au ((Mwenyezi mungu aufanye bora msiba wako)). • Inaruhusiwa kulia katika msiba bila kuvuka mipaka, kwani Mtume ملسو هلآو هيلع هللا يلص alilia alipofiwa na mwanawe Ibrahim. Mutafaqun ’alayh. Na kulia kwenyewe kusiwe kwa mayowe na NADAB (kulia na huku unataja sifa na mazuri ya marehemu). • Inafaa kwa mfiwa kuomboleza maiti yake, yaani aache biashara yake au safari zisizokuwa na lazima n.k. Na kuomboleza kwenyewe kuwa kwa siku tatu tu isizidi, ila kwa mke aliyefiwa na mumewe, yeye ataomboleza kwa muda wa EDA yake yaaani miezi minne na siku kumi, na akiwa ni mwenye mimba basi hadi atakapojifungua. • Ni haramu kabisa NADAB na NIYAAHA juu ya maiti, NADAB ni kutaja mazuri ya maiti na kuyahesabu, na NIYAAHA ni kulia kwa kupiga mayowe na huku akiongea vitu tofauti kuhusu maiti na kutoa sauti ya ajabu. Hakika kufanya hivyo ni kupingana na QADAR (Mipango ya Mwenyezi Mungu).