MUHTASARI KUHUSU SHERIA YA PSSSF
CARE INTERNATIONAL
DAR ES SALAAM
09/11/2018
UAMUZI WA SERIKALI KUHUSU KUUNGANISHA MIFUKO YA PENSHENI
❑Tarehe 20 Oktoba, 2017 Serikali ilipitisha uamuzi kwa ajili ya:
➢kuunganisha Mifuko ya Pensheni ya PSPF, LAPF, GEPF na PPF na
kuunda mfuko mmoja PSSSF ajili ya Watumishi wa Umma.
➢Kuufanyia marekebisho Mfuko wa NSSF ili uwe Mfuko
mahsusi kwa ajili ya wafanyakazi wa Sekta binafsi na sekta
isiyo rasmi.
MALENGO YA KUUNGANISHA MIFUKO YAPENSHENI
❑Hatua ya kuunganisha Mifuko ya Pensheni ililenga:
➢Kupunguza gharama za uendeshaji;
➢Kuwa na mfumo wa mifuko ya pensheni inayozingatia masharti ya ajira;
➢Kuimarisha Mifuko ya Pensheni ili kuiwezesha kutoa mafao zaidi kwa
wanachama kama ilivyoanishwa kwenye Mkataba wa ILO
➢Kuweka utaratibu wa kukabiliana na tatizo la upotevu wa ajira kwa
wanachama kwa kuanzisha Fao la Upotevu wa Ajira; na
➢Kuboresha huduma kwa wanachama wa Mifuko ya Pensheni.
▪ Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma Na.2 ya Mwaka 2018 ilipitishwa na
Bunge la Jamhuri ya Muungano tarehe 31 Januari, 2018
▪ Sheria inauunganisha Mifuko minne ya pensheni ambayo ni PSPF, PPF, GEPF NA LAPF na kuunda
Mfuko mmoja wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
▪ Sheria ya PSSF imesainiwa tarehe 8 Februari, 2018 na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali la
Tarehe 9 Februari, 2018.
▪ Sheria iliaanza kutumika tarehe 1 Agosti, 2018 na hiyo ndiyo tarehe rasmi ya kuanza kwa Mfuko wa
PSSSF
▪ Kanuni za utekelezaji wa Sheria ya PSSSF zimekamilika na zimekwishatangazwa katika Gazeti la
Serikali kwa sasa taratibu za uchapaji zinaendelea katika Ofisi ya Mpiga Chapa wa Serikali
▪ Sheria hiyo imegawanyika katika sehemu kuu Kumi na Moja.
KUTUNGWA KWA SHERIA YA PSSSF
MAMBO MUHIMU YALIYOZINGATIWA KWENYE SHERIA
❑Kuanzisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Vif. 49
& 6 PSSSF Act
❑Kubainisha kwa uwazi jumla ya mafao 7 yatakayolipwa na PSSSF Kifungu cha
29 PSSSF &21 NSSF
❑Kuweka utaratibu bora na ulio rahisi wa wanachama wa mifuko inayounganishwa
kuhamia kwenye mfuko mpya pasipo kuathiri mafao yao na uendelevu wa mfuko
mpya…”cut off date”. Vif. 5 PSSSF & 95 NSSF
❑Kuainisha viwango vya uchangiaji na namna ya uchangiaji katika mfuko mpya
(15% kwa 5%).
❑Kuweka bayana kuwa mafao na michango ya wanachama haitatozwa kodi
kama ilivyokwisha bainishwa katika sheria za kodi. Vif. 47 &56;
MAMBO MUHIMU YALIYOZINGATIWA…contd
❑Kuweka mfumo madhubuti utakaohakikisha mwanachama anapata mafao kwa wakati
kama ifuatavyo:
➢kuweka mfumo rahisi na mfupi wa mashauri ya madai ya michango mahakamani
(summary proceedings).
➢Kuweka mfumo wa makosa ya jinai na kuwezesha wanasheria wa Mfuko
kuendesha mashauri hayo pale watakapoidhinishwa na DPP
➢Kuimarisha mfumo wa ukaguzi maeneo ya Kazi
➢Kuzuia mali za mfuko kukamatwa kwa amri ya mahakama
➢Kuweka masharti yatakayomwezesha mwanachama kutumia mafao yake
kujipatia mikopo ya nyumba (home mortgage);
MAMBO MUHIMU YALIYOZINGATIWA…contd
❑Kuanzisha fao la upotevu wa ajira (unemployment benefit)
❑Kuongeza wigo wa wanachama wa mfuko mpya kwa kuwatambua wafanyakazi
wote waliopo kwenye mashirika ambayo serikali ina hisa kuwa wanachama wa
mfuko huo.
❑Kuainisha muundo wa bodi ya wadhamini ili kuzingatia uwakilishi wa waajiri na
wafanyakazi.
❑Kuboresha masharti kuhusu mafao ya majaji na viongozi wengine waandamizi wa
serikali ambao wanashika nafasi za kikatiba kwa kutenganisha mafao yao ya
pensheni na stahili nyingine wanazopata wakati wa kustaafu.
MAMBO MUHIMU YALIYOZINGATIWA…contd
❑inatoa fursa kwa mwanachama anayetumikia kifungo jela
kushirikishwa juu ya namna bora ya mafao yake yatakavyotumika
ikiwa ni pamoja na kutunza familia yake akiwa anaendelea kutumikia
kifungo kwa kuiandikia bodi ya mfuko na bodi itafanyia maamuzi
kwa kuzingatia taarifa ya mfungwa husika;
❑Imeainisha kipindi cha mpito na mambo yanayopaswa kusimamiwa
na kutekelezwa katika kipindi hicho;
❑Kumpa mamlaka Waziri mwenye Dhamana ya Hifadhi ya Jamii
kutunga kanuni za utekelezaji wa sheria hiyo
USALAMA WA MICHANGO, MAFAO NA RASILIMALI ZA MIFUKO
❑Masharti ya Sehemu ya Kumi Sheria ya PSSSF yanatambua, yanalinda na kuhamishia katika
Mfuko wa PSSSF yafuatayo:
➢ Mikataba iliyoingiwa na Mifuko iliyounganishwa
➢Mashauri ya nidhamu yaliyofunguliwa na mifuko iliyounganishwa
➢Wanachama, wastaafu na wanufaika
➢Mifuko ya Hiari iliyokuwa chini ya Mifuko iliyounganishwa
➢ Rasilimali na Madeni ya mifuko iliyounganishwa
➢ Haki na wajibu wa Mifuko iliyounganishwa
➢ Vitega uchumi na Miradi
➢Madai ya Mafao;
➢Mashauri yaliyopo mahakamani
MAMBO MUHIMU…UANACHAMA
• Mfuko wa PSSSF unaundwa na wanachama
wafuatao:
• wafanyakazi wote watakaoajiriwa
kwenye Utumishi wa Umma baada ya
tarehe 1 Agosti, 2018;
• waliokuwa wanachama wa mifuko
iliyounganishwa (PSPF, LAPF, PPF na
GEPF) mpaka tarehe 31 Julai, 2018 bila
kujali sekta walizopo.
• wafanyakazi wote watakaoajiriwa
kuanzia tarehe 1 Agosti, 2018 kwenye
makampuni au mashirika ambako Serikali
inamiliki zaidi ya asilimia 30 ya hisa za
kampuni.
• Mfuko wa NSSF utahudumia wanachama
wafuatao:
• Wafanyakazi walioajiriwa katika sekta
binafsi;
• Wafanyakazi wa kigeni walioajiriwa
Tanzania Bara;
• Wafanyakazi walioajiriwa katika Taasisi za
kimataifa zinazofanya kazi Tanzania Bara;
• Wafanyakazi waliojiajiri katika Sekta isiyo
rasmi;
• Kundi lingine lolote kama ambavyo
Mheshimiwa Waziri atakavyoona inafaa
baada ya kushauriwa na Mamlaka.
MAMBO MUHIMU…UKUSANYAJI MICHANGO
• Viwango vya Uchangiaji (Kif. 18)
• PSSSF: Mwajiri – 15%, Mfanyakazi 5%
• NSSF: Mwajiri – 10%, Mfanyakazi 10%
• Mwajiri anaweza kuchangia kiwango kikubwa
Zaidi
• Mshahara utakaozingatiwa kufanya makato
ya michango katika Mfuko.
• PSSSF: -Posho
• NSSF: +Posho na marupurupu mengine anayopata
mfanyakazi
• Wafanyakazi ambao walikuwa wanachama
wa Mifuko iliyounganishwa (GEPF, LAPF, PPF
na PSPF), ambao mshahara uliokuwa
unatumika pamoja na viwango vya uchangiaji,
endapo vinatofautiana na masharti ya Sheria
ya Mfuko wa PSSSF, kwa Kipindi chote cha
Mpito, wataendelea kutumia mshahara na
viwango vya uchangiaji vilivyokuwa
vinatumiwa na Mifuko yao ya zamani, mpaka
watakapojulishwa vinginevyo na Mfuko.
MAMBO MUHIMU…UKUSANYAJI MICHANGO
• Michango yote iliyowasilishwa katika Mifuko iliyounganishwa kabla ya
Tarehe 01 Agosti, 2018 itazingatiwa kana kwamba imewasilishwa katika
Mfuko wa PSSSF.
• Ili kulinda na kutetea maslahi ya mwanachama, sheria mpya ya PSSSF
imeweka faini ya kiwango cha Asilimia 1.5 ya michango iliyocheleweshwa
na endapo mwajiri ataendelea kuchelewesha michango, tozo itaendelea
kutozwa kwa utaratibu wa riba dundulizi (compound interest).
MAMBO MUHIMU…ULIPAJI MAFAO
• Umri wa kustaafu: Kuanzia miaka 55 (hiari)
hadi miaka 60 (lazima)
• 60 – 65 kwa kada maalumu za kitaaluma
• Sheria PSSSF imeongeza mafao mapya
• Fao la Upotevu wa ajira; na
• Fao la Ugonjwa.
• Mafao kuto tozwa kodi
• Malipo ya mafao hata kama mwajiri atakuwa
hajawasilisha michango
• Kuboresha mafao ya warithi mara baada ya
mwanachama/mstaafu kufariki
• Kuboresha masharti ya Fao la Uzazi
• Sheria ya PSSSF (Kif. 43) kinaweka mtiririko wa
hatua za Mwajiri, Mfuko na Mwanachama
katika kulipa mafao ya pensheni.
• Mwajiri kutoa notisi ya kustaafu miezi 6 kabla
ya Tarehe ya kustaafu
• Mwanachama kufungua madai ya mafao
• Tozo ya 5% dhidi ya Mfuko kwa kuchelewesha
kulipa mafao
UKOKOTOAJI WA MAFAO
CARE INTERNATIONAL
DAR ES SALAAM
09/11/2018
MAFAO YA HIFADHI YA JAMII
MAFAO YA MUDA MREFU
• Pensheni ya Uzeeni
• Fao la Ulemavu
• Fao la Warithi
MAFAO YA MUDA MFUPI
• Fao la Upotevu wa Ajira
• Fao la Ugonjwa
• Fao la Uzazi
• Mkopo wa Nyumba
MAMBO YALIYOZINGATIWA KATIKA KANUNI
• Vigezo na ukokotoaji wa Malipo ya Mafao ya Pensheni;
• Ukokotoaji wa Mafao Maalum ya Mkupuo (Special Lumpsum);
• Ukokotoaji na Utoaji wa Mafao ya Kupoteza uwezo wa kufanya kazi
kutokana na ulemavu au Ugonjwa (Invalidity Benefit);
• Utoaji wa Mafao ya Kifo (Death Gratuity)
• Ukokotoaji na Utoaji wa Mafao kwa Warithi; (Survivors Benefits)
• Utoaji wa Mafao ya Upotevu wa Ajira (Unemployment Benefit);
• Ukokotoaji wa Mafao ya Malipo ya Ugonjwa (Sickness benefit);
• Utoaji Mikopo ya nyumba kwa wanachama (Home Mortgage).
A) VIGEZO NA UKOKOTOAJI NA MALIPO YAMAFAO YA PENSHENI
• Kanuni ya 4 na 5 zimeweka vigezo anavyostahili mwanachama ili alipwe mafao ya pensheni kama
ifuatavyo:-
• mwanachama awe amechangia kwa kipindi kisichopungua miezi 180 (miaka 15)
• ametimiza umri wa kustaafu wa lazima (60) au hiari (55)
• Kanuni ya 8 (1) imeonesha namna ya ukukotoaji wa mafao ya pensheni kama ifuatavyo:-
• Pensheni nzima (Full pension)
• 1/580 x jumla ya miezi ya uchangiaji x mishahara (APE);
• Mkupuo (Commuted pension)
• 1/580 x jumla ya miezi ya uchangiaji x mishahara (APE) x 12.5 x 25%
• Pensheni ya mwezi
• 1/580 x jumla ya miezi ya uchangiaji x mishahara x 75% x 1/12
JEDWALI 1: MALIPO YA PENSHENI KWAMWANACHAMA
Mshahara wa mwezi (TZS) 1,000,000
Kiwango cha uchangiaji 20%
Muda wa Uchangiaji (miezi) 420 Miaka 35
Jumla ya Michango (TZS) 84,000,000
Kikotoo cha zamani Kikokotoo kipya
Mkupuo (TZS) 71,612,411 35,806,205
Pensheni ya mwezi (TZS) 371,847 557,771
Kiwango kilicho ongezeka (TZS) 185,924
Muda wa kuishi (miaka) 15.5 15.5
Jumla ya pensheni ya mwezi 69,163,542 103,745,406
Jumla ya mafao yote 140,775,953 139,551,611
B) UTHAMINISHAJI WA MAFAO YA PENSHENI(INDEXATION);
• Kanuni ya 11 imeeleza namna ambavyo mafao ya pensheni yatakavyo thaminishwa ambapo mambo
yafuatayo yatazingatiwa:-
• mafao yaongezwa kwa asilimia 50 ya mfumuko wa bei,
• mfumuko wa bei uwe kati ya asilimia 1 mpaka 10.
• mfumuko wa bei ukiwa zaidi ya asilimia 10 uthaminishaji wa mafao utakua asilimia 5
• mfumuko wa bei ukiwa chini ya asilimia 1 kutakua hakuna uthaminishaji.
• Uthaminishwaji utafanywa kila baada ya miaka 3
PENSHENI ILIYOAHIRISHWA(DEFERRED PENSION)
• Kanuni ya 12 inaweka utaratibu wa mwanachama aliyechangia zaidi ya miezi 180 na
yupo chini ya umri wa kustaafu kuhairisha pensheni yake kutokana na sababu zifuatazo;
• Atachaguliwa kwenye nafasi ya kisiasa;
• Kupunguzwa kazi;
• Mabadiliko ya muundo wa taasisi;
• Kufutwa kwa ofisi.
• Mwanachama atalipwa kwa mujibu wa kanuni ya 8 malipo ya mkupuo na kisha kulipwa
pensheni ya mwezi pindi atakapo fikisha umri wa kustaafu
C) UKOKOTOAJI WA MAFAO MAALUM YAMKUPUO (SPECIAL LUMPSUM);
• Kanuni ya 13 imebainisha kuwa wanachamba ambao hawatakuwa na sifa za kulipwa pesheni
watalipwa Mafao Maalum ya Mkupuo
• Mafao Maalum ya Mkupuo yatakua ni jumla ya michango ya mwanachama iliyolipwa kwenye
Mfuko pamoja na riba iliyofafanuliwa kwenye kanuni hizi za mafao.
D) KIMA CHA CHINI CHA PENSHENI
• Kanuni ya 14 imefafanua kuwa kima cha chini cha pensheni kuwa kisiwe chini ya asilimia 40 ya
mshahara wa sekta ya ajira ya mwanachama anayestaafu.
E) UKOKOTOAJI NA UTOAJI WA MAFAO YA KUPOTEZAUWEZO WA KUFANYA KAZI KUTOKANA NA ULEMAVU AU
UGONJWA (INVALIDITY BENEFIT);
• Kanuni YA 16 imebainisha kuwa malipo ya kupoteza uwezo wa kufanya kazi kutokana na
ulemavu au Ugonjwa (Invalidity Benefit) yatalipwa kwa kuzingatia kanuni ya 8 ya malipo ya
pensheni.
• Malipo haya hayatakiwi kuwa chini ya asilimia 30 ya wastani wa mshahara wa mwaka
ukigawanya kwa 12.
• VIGEZO
• Awe amefukuzwa kazi kutokana na ugonjwa usiotokana na kuumia kazini
• Awe amepoteza uwezo wa kufanya kazi usiotokana na kuumia kazini
• Awe chini ya umri wa kustaafu kwa hiari;
• Awe amechangia kwenye mfuko si chini ya miezi 36, ambapo miezi 12 iwe kabla ya kupata majanga haya.
F) MAFAO YA KIFO (DEATH GRATUITY)
• Kanuni YA 17 inabainisha kuwa endapo mwanachama atafariki akiwepo kazini na
amechangia chini ya miezi 180 (miaka 15) wategemezi wake watalipwa mafao ya Kifo.
• Wategemezi hao watalipwa mkupuo maalum au mshahara bora, yoyote itakayokua
kubwa
• UTARATIBU
• Mjane/mgane atalipwa asilimia 40 ya mafao haya na kama wapo zaidi ya mmoja mafao haya
yatagawanywa sawa;
• Watoto watalipwa asilimia 60 iliyobaki na yatagawanywa sawa kwa watoto wote;
• Kama hakuna watoto mjane/magane atalipwa asilimia 100 ;
• Kama hakuna mjane/mgane watoto watalipwa asilimia 100;
• Kama kuna watoto wapo shuleni mgawanyo kwa watoto utagawanya nusu ambapo nusu moja itatumika
kulipia ada na itasimamiwa na mfuko, na nusu nyingine itagawanywa sawa kwa watoto;
• Mahakama inaweza kubadilisha mgawanyiko huu kwa sababu
G) UKOKOTOAJI NA ULIPAJI MAFAO KWA WARITHI
• Kanuni ya 18, Mafao ya warithi (Survivor benefits) yatalipwa kwa mwanachama
aliyechangia kwa kipindi kisichopungua miezi 180 na yatalipwa kama ilivyo
ainishwa kwenye kanuni ya 8 ya ulipaji wa mafao ya pensheni.
• Kanuni ya 19: Vigezo vya malipo ya mafao ya warithi
• Mjane/mgane mwenye umri zaidi ya miaka 45 au chini na ana watoto chini ya miaka 15;
• Mtoto mwenye umri wa miaka 21 aliyepo masomoni au chini ya miaka 18;
• Watoto wa mwanachana asiyekua na mjane/mgane; au
• Kwa wazazi wa mwanachama aliyefariki bila watoto au mjane/mgane.
H) UTOAJI WA MAFAO YA UPOTEVU WA AJIRA
• Kanuni ya 20 imebainisha kuwa mafao ya upotevu wa ajira yatakuwa sawa na
asilimia 33.3 ya mshahara wa mwezi wa mwanachama aliyepoteza ajira.
• Kanuni 21; Muda wa ulipaji wa mafao ya upotevu wa ajira;
• Mafao haya yatalipwa kwa kipindi kisichozidi miezi 6 kwa mwaka na mwanachama
atalipwa kwa kipindi kisichozidi miezi 18 katika kipindi chote cha ajirA;
• Kama mwanachama atakua hajapata ajira baada ya miezi 18 anaweza kumuandikia
Mkurungenzi Mkuu kuomba kuhamisha michango yake kwenda kwenye Mfuko wa
hiara wa chaguo lake na anaweza kuendelea kuchangia katika mfuko huo
• Michango hiyo ya mwanachama itakua ni sawa na malipo ya mkupuo maalum ukitoa
mafao ya upotevu wa ajira aliyokwisha kulipwa
• Kwa mwanachama aliyechangia chini ya miezi 18 atalipwa asilimia 50 ya
michango yake
• Kama mwanachama atakosa ajira baada ya miezi 18 baada ya malipo haya
kukoma, ataweza kubadilisha michango yake kwenda kwenye Mfuko wa hiari wa
chaguo lake kwa kumuandikia Mkurungenzi Mkuu kuomba kuhamisha michango
hiyo na anaweza kuendelea kuchangia katika mfuko huo
• Michango hiyo ya mwanachama itakua ni sawa na malipo ya mkupuo maalum
ukitoa mafao ya upotevu wa ajira aliyokwisha kulipwa
..... Muda wa ulipaji wa mafao ya upotevu wa
ajira;
I) UKOKOTOAJI WA MAFAO YA MALIPO YAUGONJWA
• Vigezo vya kulipwa mafao ya malipo ya ugonjwa; kanuni ya 22 imeainisha
vigezo vya kulipwa fao hili kama ifuatavyo:-
• Mwanachama awe mgonjwa au amepata ajali isiyotokana na kuumia kazini;
• Awe chini ya umri wa kustaafu kwa hiari;
• Awe amechangia kwenye mfuko angalau kwa miezi 36 ambapo miezi 12 iwe
imechangiwa kabla ya kuugua.
• Kiwango cha Mafao ya Malipo ya Ugonjwa
• Kanuni ya 24 imebainisha kuwa kiwango cha Mafao ya Malipo ya Ugonjwa kuwa ni
sawa na asilimia 40 ya mshahara wa mwezi kabla ya kuugua na atalipwa kwa muda
wa miezi mitatu
J) UTOAJI WA MIKOPO YA NYUMBA (HOME MORTGAGE)
• Kanuni ya 24 imebainisha kwamba kila mwanachama wa mfuko ana haki ya
kutumia mafao yake kama dhamana ya kupata mkopo wa nyumba.
• Kanuni 25; Vigezo vya kupata mkopo wa nyumba
• Awe ni mwanachama wa mfuko husika;
• Awe amechangia kwenye mfuko si chini ya miaka 10;
• Muda wa malipo usizidi kipindi cha uchangiaji wa lazima; na
• Awe mtanzania.
• Mfuko utaingia makubaliano na benki ili mwanachama aweze pata mkopo huu
na usizidi asilimia 50 ya mafao ya mda mrefu ifuatavyo:-
• Mkupuo maalum kwa mwanachama aliyechangia pungufu ya miezi 180
• Pension nzima kwa mwanachama aliyechangia zaidi ya miezi 180
SHUKRAN