View
241
Download
0
Category
Preview:
Citation preview
8/19/2019 Rais Magufuli Ahudhuria Ibada Ya Pasaka Azania Front
1/2
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
T RIF KW VYOMBO VY H B RI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi
watanzania kuendelea kuwa wamoja na kushirikiana kuijenga nchi yao, badala ya
kubaguana.
Rais Magufuli ametoa wito huo leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Usharika wa Azania Front Jijini Dar es salaam, ambako amesali ibada ya
Pasaka pamoja na waumini wa kanisa hilo.
Amesema Mwenyezi Mungu alimtoa mwanae wa pekee Yesu Kristo kuja
kuikomboa dunia bila kuwabagua wanadamu, vivyo hivyo nasi binadamu tunapaswa
kutobaguana, iwe kwa dini zetu, makabila yetu, mitazamo ya kisiasa na hata rangi
zetu.
Aidha, Rais Magufuli amewakumbusha watanzania kufanya kazi kama ambavyo
vitabu vitakatifu vinasisitiza umuhimu wa kufanya kazi, na amebainisha kuwa
Tanzania yenye neema inawezekana endapo kila mtu atazingatia kufanya kazi.
“Tukifanya kazi hatuhitaji hata misaada kutoka nje nchi hii ina neema nyingi. Kwa
kweli tukifanya kazi kwa bidi nchi yetu inapaswa kuwa inatoa misaada kwa nchi
nyingine n sio kuomb mis d kutok nchi nyingine” Amesisitiza Dkt. Magufuli.
Rais Magufuli ambaye amesali kwenye kanisa hilo kwa mara ya kwanza tangu
achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini ikiwa ni mara
yake ya nne kusali katika kanisa hilo hata kabla ya kuwa Rais, amewaomba
watanzania kuendelea kuliombea Taifa lao na pia kumuombea yeye ili afanikiwe
kutekeleza jukumu kubwa na zito la kuiongoza nchi.
http://www.ikulu.go.tz/http://www.ikulu.go.tz/http://www.ikulu.go.tz/http://www.ikulu.go.tz/
8/19/2019 Rais Magufuli Ahudhuria Ibada Ya Pasaka Azania Front
2/2
Pamoja na kuongoza maombi ya kumuombea Rais Magufuli na Mkewe Mama
Janeth Magufuli waliohudhuria ibada hiyo, Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya
Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Malasusa amempongeza Rais Magufuli kwa tabia
yake ya kupenda kuhudhuria ibada na kuwasihi viongozi wengine kupenda ibada.
Askofu Malasusa ameuelezea ufufuo wa Yesu Kristo kuwa jambo la kuleta
matumaini, na hivyo amepongeza mwelekeo wa nchi kwa sasa, huku akisema Kanisa
linaona matumaini kwa Taifa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
27 Machi, 2016
Recommended