16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1055 RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Moyo, Rashid wapasua jipu la muungano Wahoji uhalali wake. Hati ya awali yatakiwa Karume, Komandoo nao wapigilia msumari Hawajaona ‘faida kiuchumi’ ila kudharauliwa Tanganyika na Zanzibar wakutane katika AU HIVI majuzi Waislamu walilalamika wakidai kuwa Baraza la Mitihani limechakachua matokeo yao ya mtihani. Hizi ni shutuma nzito kwa nchi yoyote inayojali raia wake na inayopenda kudumisha amani ya kweli. Shutuma kama hizi si CCM wana sera za udini Wamerithi toka kwa Mwalimu Nyerere Rais Kikwete, Shukuru wanauendeleza vizuri kutumia ujanja ujanja wa kuzizima chini kwa chini, bali ni suala ambalo serikali inatakiwa ijisafishe wazi wazi ili kuondoa chuki ambazo zinaendelea kujilimbikiza. Na wale wote waliohusika, ni lazima wawajibishwe kwa mujibu wa sheria. (Soma makala uk. 8, 9) MUHIMU hapa ni kuona kwamba ‘tumekuwa’ kuwa na Dini ya Kiislamu kwa karne nyingi sana na sasa kila mtu anajua kwamba Uislamu si dini tu peke yake, lakini imechimba zaidi hata katika tabia, silka na hulka zetu. Sisi ni Waislamu kwanza - Waziri Waislamu tumeungana zaidi kwa lugha yetu moja na kuwa sote ni wamoja. Wajibu wetu wa kwanza ni kuunganisha umoja wetu huu (wa Kiislamu) kwa misingi nilioieleza. (Mh. Abubakar Khamis Bakary- Soma Uk. 13) WANANCHI wa kijiji cha Chwaka, Kusini Unguja wamewaomba Rais Jakaya Kikwete na Dk Ali Mohamed Chwaka wataka Rais Kikwete kuirejeshea Zanzibar mamlaka Wampa changamoto nzito Dr. Shein Na Mwandishi Wetu Shein, kushughulikia suala la Zanzibar kurejeshewa mamlaka yake kamili kama ilivyokuwa kabla ya kuungana na Tanganyika. Ombi hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano wa wazi wa Baraza la Katiba Zanzibar (BAKAZA) wakati likitoa elimu ya Katiba kwa wananchi wa kijiji hicho. Huo ni mfululizo wa Baraza Inaendelea Uk. 4 Barabara ya Yasser Arafat yazinduliwa Dar es Salaam Uk. 2 DKT. Salmin Amour DKT. Amani Karume WANASIASA wakongwe waliyokuwa katika Serikali ya Mapinduzi, wakati wa kuundwa kwa Muungano huo, Bw Salum Rashid (kushoto) na Bw Hassan Nassor Moyo, Habari Uk. 4.

ANNUUR 1055.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: ANNUUR 1055.pdf

ISSN 0856 - 3861 Na. 1055 RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

Moyo, Rashid wapasua jipu la muunganoWahoji uhalali wake. Hati ya awali yatakiwaKarume, Komandoo nao wapigilia msumariHawajaona ‘faida kiuchumi’ ila kudharauliwaTanganyika na Zanzibar wakutane katika AU

HIVI majuzi Waislamu wal i la lamika wakida i kuwa Baraza la Mitihani limechakachua matokeo yao ya mtihani.

Hizi ni shutuma nzito kwa nchi yoyote inayojali raia wake na inayopenda kudumisha amani ya kweli.

Shutuma kama hizi si

CCM wana sera za udiniWamerithi toka kwa Mwalimu NyerereRais Kikwete, Shukuru wanauendeleza

vizuri kutumia ujanja ujanja wa kuzizima chini kwa chini, bali ni suala ambalo serikali inatakiwa ijisafishe wazi wazi ili kuondoa chuki ambazo zinaendelea kujilimbikiza.

Na wale wote waliohusika, ni lazima wawajibishwe kwa mujibu wa sheria. (Soma makala uk. 8, 9)

MUHIMU hapa ni kuona kwamba ‘tumekuwa’ kuwa na Dini ya Kiislamu kwa karne nyingi sana na sasa kila mtu anajua kwamba Uislamu si dini tu peke yake, lakini imechimba zaidi hata katika tabia, silka na hulka zetu.

Sisi ni Waislamu kwanza - Waziri

Waislamu tumeungana zaidi kwa lugha yetu moja na kuwa sote ni wamoja.

Wajibu wetu wa kwanza ni kuunganisha umoja wetu huu (wa Kiislamu) kwa misingi nilioieleza. (Mh. Abubakar Khamis Bakary-Soma Uk. 13)

WANANCHI wa kijiji cha Chwaka, Kusini Unguja wamewaomba Rais Jakaya Kikwete na Dk Ali Mohamed

Chwaka wataka Rais Kikwetekuirejeshea Zanzibar mamlaka

Wampa changamoto nzito Dr. SheinNa Mwandishi Wetu Shein, kushughulikia suala

la Zanzibar kurejeshewa mamlaka yake kami l i kama ilivyokuwa kabla ya kuungana na Tanganyika.

Ombi hilo l i l i tolewa mwishoni mwa wiki iliyopita

kwenye mkutano wa wazi wa Baraza la Katiba Zanzibar (BAKAZA) wakati likitoa elimu ya Katiba kwa wananchi wa kijiji hicho.

Huo ni mfululizo wa Baraza Inaendelea Uk. 4

Barabara ya Yasser Arafat yazinduliwa Dar es Salaam

Uk. 2

DKT. Salmin Amour DKT. Amani Karume

WANASIASA wakongwe waliyokuwa katika Serikali ya Mapinduzi, wakati wa kuundwa kwa Muungano huo, Bw Salum Rashid (kushoto) na Bw Hassan Nassor Moyo, Habari Uk. 4.

Page 2: ANNUUR 1055.pdf

2 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Habari

BARABARA iliyo karibu na makazi ya Balozi wa Dola ya Palestina, jijini Dar es Salaam imepewa j ina la Yasser Arafat . Hafla ya uzinduzi wa barabara hiyo iliongozwa na Bw Richard Chengula aliyemuwakilisha Meya wa Kinondoni Mheshimiwa Yusuf Mwenda.

Baada ya kufunua bango la barabara hiyo, Bw Chengula alisema wananchi waliamua kuipa barabara hiyo jina la Yasser Arafat kwa kuzingatia kuwa kiongozi huyo wa Pa les t ina a l ikuwa mtu mashuhuri duniani, pamoja na jitihada zake za kuimarisha

Barabara ya Yasser Arafat yazinduliwa Dar es Salaam

uhusiano wa kirafiki baina ya Tanzania na Palestina.

Alisema barabara hiyo itawakumbusha wananchi kuwa Tanzania i l ikuwa miongoni mwa nchi ya kwanza kuitambua Dola ya Palestina.

Naye Balozi wa Dola ya Palestina, Dr Nasri Abujaish alisema alifurahi sana na kuwashukuru wananchi wa Tanzania kwa uamuzi wao wa kuipa barabara hiyo jina la Bw Yasser Arafat ambaye alikuwa mwanzilishi wa Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Rais wa kwanza wa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina na Rais wa kwanza wa Dola ya Palestina.

Akasema, sababu muhimu zaidi ya uamuzi huu ni

kuwa Rais Arafat alikuwa rafiki mkubwa wa Tanzania, akitembelea nchi hii mara kadha kwa mwaliko wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Baadae mshikamano huu uliendelezwa kwa mialiko ya Rais Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

Balozi Abujaish akaongeza kwa kusema: “Katika jiji la Ramallah ambao ni makao makuu ya Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina, tumeanzisha mchakato wa kuzindua Mtaa wa Mwalimu Nyerere. Kwa kufanya hivyo tutakuwa na Mtaa wa Mwalimu Nyerere nchini Palestina na Mtaa wa

Yasser Arafat hapa nchini Tanzania.”

“Ni matumaini yetu kuwa hatua hizi tulizochukua zitaendeleza na kuimarisha kumbukumbu za viongozi w e t u w a k u u h a w a i l i waendelee kukumbukwa na vizazi vijavyo”.

Balozi alisema Wapalestina w a t a m k u m b u k a A r a f a t kwa vile ndie aliyeanzisha vuguvugu la ukombozi wa Palestina kutokana na uvamizi wa Israel.

Arafat atakumbukwa pia kwa sababu anawakilisha dira yetu ya kitaifa na ukombozi wa taifa letu la Palestina

“ H i v i l e o m o t o aliouwashaYassir Arafat umezaa matunda kutokana na kukubalika kwa Dola ya

Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN). Tunasikitika kuwa yeye hayupo nasi kushuhudia mafanikio hayo. Hata hivyo kumbukumbu zake zitaendelea kubaki mioyoni mwetu, na harakati za ukombozi zitaendelea hadi kufikia uhuru kamili wa nchi yetu na hatimae kukubalika kwa Palestina kama mwanachama kamili wa UN”

Balozi Abujaish alisema President Arafat na chama cha PLO walikuwa karibu sana na taifa la Tanzania na chama cha CCM. “Wapalestina leo wana faghari kwa uhusiano huu wa kihistoria baina ya mataifa yetu na wananchi

wetu. Ni matumaini yetu kuwa uhusiano huu utaendelezwa na kuimarishwa,” aliongeza

“Ni kwa sababu uhusiano huu umetokana na mshikamano wenu wa dhati na Wapalestina ambao wanapambana na uvamizi na ukandamizaji wa Israel nchini mwao. Kwa kweli nyinyi Watanzania mmechukua msimamo huu dhidi ya ukoloni wa Israel sawa na mlivyofanya wakati ule wa utawala wa makaburu kule Afrika Kusini. Kwa hili tunawashukuru sana kwa moyo wetu wote,” alimalizia Balozi Abujaish.

(Habari hizi ni kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha Palestina Tanzania 24 January 2013.)

Balozi wa Dola ya Palestina, Dr Nasri Abujaish (kushoto) na Bw Richard Chengula aliyemuwakilisha Meya wa Kinondoni Mheshimiwa Yusuf Mwenda.

KUANZIA jana usiku, Waislamu sehemu mbalimbali nchini na maeneo mengine duniani, wamekuwa katika sherehe za Maulidi ya Mazazi ya Mtume (saw).

Wa k a t i S h e r e h e h i z i zikiadhimishwa, yapo mambo inabidi Waislamu kujiuliza na kuona ni vipi wananufaika na ujio wa Mtume Muhammad (s.a.w). Kwanza ni kuwa, kwa muda mrefu sasa Waislamu wa nchi hii wamekuwa na madai na hata kulalamika k w a m b a w a n a b a g u l i w a na kudhulumiwa haki zao. Wanadai kuwa kumekuwa na mfumokristo ambao uliasisiwa toka wakati wa ukoloni ambao ndio umekuwa sababu ya wao kudhulumiwa haki zao kama wananchi.

Kwa upande mwingine wanada i kuwa Wakr i s to wamehodhi fursa za elimu, ajira na madaraka serikalini na katika taasisi za umma kutokana na upendeleo wanaopewa chini ya mfumokristo. Kwa maelezo yao wenyewe, Waislamu wa nchi hii wanajiona kama raia daraja la pili.

Swali ni je, mafundisho ya Uislamu, mafundisho ya Mtume wanayesherehekea uzao wake, yanawasaidia vipi Waislamu kujinasua na hali hii? Kama kuja kwa Mtume Muhammad (s.a.w) kumetajwa kuwa ni Rehma kwa walimwengu, je, Rehma hii, inawasaidiaje Waislamu wanaodai kubaguliwa na kuonewa? Katika jumla ya mafundisho aliyokuja nayo Mtume (s.a.w) ni kuwa Waislamu wasidhulumu na wala wasikubali kudhulumiwa. Je, hii hali ya kulalamika miaka yote hii kwamba wnaabaguliwa na kudhulumiwa, ni katika Uislamu? Mbona inakuwa kinyume na mafundisho ya Mtume? Kwa nini Waislamu waendelee kulalamika wakati dini yao inawakataza wssikubali kudhulumiwa? Je, dhulma itaondoka kwa kulalamika?

Tuseme kuwa yapo masuala ya kisera ambayo yamekuwa yakiwaletea Waislamu nchini athari kubwa na mbaya kiasi cha kuuingiza umma katika mateso makubwa. Kwa hakika Waislamu kwa sasa wana kila sababu ya kujikita zaidi katika masuala hayo ya kisera ili kuhakikisha wanakuwa huru katika Uislamu wao dhidi ya sera zinazotawala nchini.

Waislamu wanakabiliwa na tatizo la kukosa uhuru wa kuabudu. Uhuru wa kuwa na Jumuyia rafiki za kimaendeleo, uhuru wa kuitumikia dola i n a y o k u w a m a d a r a k a n i kutokana na kufunikwa na

Maulid itukomboemfumokristo nk.

K i p i n d i h i k i c h a kusherehekea uzao wa Mtume (s.a.w) ndio wakati hasa wa kutafakari, ni hatua zipi za kuchukua kuhakikisha kuwa katika yale wanayopalalamikia angalau ikija maulidi nyingine mwakani, basi waweze kusema kuwa hili na lile limeondoka

Hivi sasa kuna hizi harakati zinaendelea za Katina mpya, ni kipindi ambacho tunaona kila Muislamu anatakiwa kufuatilia kwa karibu mchakato huu wa katiba kuhakikisha kwamba Waislamu wanakomboka katika kitanzi cha kukosa uhuru wa kuabudu kulingana na imani yao kwa kigezo cha katiba.

Kama ni mahakama ya kadhi, kujiunga na taasisi za kijamii na kiuchumi kama OIC, kuwa huru siku za ibada ya Ijumaa, kuwa huru kuvaa kwa heshima hata katika maeneo ya kiserikali, (Hijab, kofia n.k., kuwepo mfumo huru halali wa kiutendaji serikalini, kupewa ruzuku kama watu wa inami nyingine nk.

Haya ni masuala ya msingi ya kufanyiwa kazi kipindi hiki cha mchakato wa mabadiliko ya katiba.

Hata hivyo, jambo muhimu sio kuwekwa katiba au sharia kwani hata katiba ya sasa inapinga ubaguzi. Muhimu kwa Waislamu ni kujenga ile dhamira ya kukataa kuonewa na wakawa tayari kulisimamia hilo na kwa gharama yoyote.

Hata kama i takuwepo katiba nzuri, lakini Waislamu wenyewe wakawa hawa hawa ambao wanaona dhulma ya wazi katika taasisi kama ya Baraza la Mitihani, lakini hawaonekani kuchukua hatua madhubuti na makini kuondoa dhulma hiyo, huna vya kuwasaidia. Hao wataendelea kudhulumiwa na kuonewa hata kukiwa na katiba nzuri kiasi gani.

Ha ta kama ku takuwa na katiba nzuri kiasi gani, lakini Waislamu wenyewe wakawa hawa hawa ambao mtu akiwa mwanasiasa, msomi, mfanyabiashara aliyefanikiwa na afisa wa serikali, anajiona hana la kupigania Uislamu na Waislamu ila huona kuwa hilo ni jukumu la ‘wanaharakati’, bado itakuwa kazi ngumu kwa Waislamu wa nchi hii kuepukana na dhulma.

Ni matarajio yetu kuwa tutasherehekea Maulid huku tukitafakari jinsi Mtume (s.a.w) alivyowakomboa Waislamu kutoka makucha ya madhalimu wa Makkah ili nasi tupate kujikomboa.

Page 3: ANNUUR 1055.pdf

3 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013Habari

RAIS Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, a m e o m b a k u p a t i w a hati halisi (Original) ya Muungano wa Tanganyika n a Z a n z i b a r a m b a y o imetiwa saini na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume.

Ombi hilo la Karume limekuja kufuatia utoaji wake wa maoni mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, makamo Mwenyekiti Assa Rashid na wajumbe wengine aliyokutana nayo juzi nyumbani kwake Mjini Unguja.

Karume alisema yeye hana hati ya Muungano na hajawahi kuiona na iwapo Tume hiyo inayo hati hiyo, basi angeomba kupatiwa kwani ni Wazanzibari wengi wanahitaji kuiona hati hiyo ambayo ni mkataba kati ya nchi mbili zenye mamlaka kamili kila moja na zilizoungana mnamo mwaka 1964 kila nchi ikiwa huru.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya tume hiyo, kimesema Karume mbali ya kutaka kupatiwa hati ya Muungano lakini pia alisema anaunga mkono kuwepo kwa Muungano wa Mkataba ambao kila nchi itakuwa na mamlaka yake kamili na kisha

Karume ataka Hati halisi ya Muungano

Na Alghaithiyyah Zanzibar,

RAIS Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume.

MAKAMU wa kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharif Hamad.

kufuatia huo na mfungamano wa mkataba ambapo alisema Zanzibar kwa takriban miaka 50 sasa imekuwemo katika Muungano lakini imekuwa hainufaiki kiuchumi ndani ya Muungano huo.

Aidha Karume alisema yeye yupo tayari kuongoza kipindi cha mpito iwapo kutakuwepo na kipindi hicho kutoka Muungano huu uliopo

na kuingia wa Maktaba pale alipoulizwa na Mjumbe wa Tume hiyo, Salim Ahmed Salim ambaye alionesha khofu yake na uzoefu wa chaguzi zinazofanyika nchini kwamba zinakuwa na machafuko.

K a r u m e a l i s e m a hakuna machafuko yoyote yatakayoweza kutokezea katika kipindi hicho cha mpito na iwapo Rais aliyekuwepo m a d a r a k a n i h a t a w e z a

kusimamia na hatajiamini kwa hilo, basi yeye anaweza kuchukua nafasi hiyo ili aweze kusimamia hilo na akaahidi kwamba hali itakuwa shuwari na kuivusha Zanzibar katika machafuko kama alivyoweza kusimamia Maridhiano kati ya vyama vikuu vya CCM na CUF mwanzo hadi mwisho wake.

Karume ambaye amekuwa rais kwa miaka 10 Zanzibar, amesema amepata uzoefu m k u b w a s a n a k a t i k a kipindi cha uongozi wake akiwa madarakani ambapo ameshuhud ia Zanz iba r ikidhoofika kiuchumi wakati upande wa pili wa Muungano ukinufaika zaidi.

Amesema , n i waka t i mwafaka kupitia katiba mpya watu kuwa wazi na kusema ukwel i kwa kubainisha kero na matatizo yote ya Muungano ili hatua za lazima zichukuliwe katika kuwaletea wananchi katiba iliyo nzuri na yenye usawa wa nchi mbili zilizoungana na zenye hadhi sawa.

“Karume alisema wazi wazi kwamba kwa kipindi

cha miaka 10 ameshuhudia mengi sana katika suala zima la maslahi ya Zanzibar, lakini pia alisema sasa ni zama mpya za ukweli na uwazi na kwa hali iliyofikia sasa hakuna njia nyengine zaidi ya kila nchi - Zanzibar na Tanganyika - kurejesha mamlaka yake kitaifa na kimataifa na kisha nchi hizo mbili kushirikiana kupitia Muungano wa Mkataba kati yao, hivyo ndivyo alivyosema M h e s h i m i w a K a r u m e ” kilisema chanzo chetu cha habari.

H a t a h i v y o K a r u m e aliwaambia wajumbe wa tume hiyo kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliotiwa saini na Mwalimu Nyerere na Mzee Karume ulikuwa na heshima hapo zamani na ukiheshimiwa sana lakini kumekuwepo na dharau fulani ambazo z i m e k u w a z i k i f a n y w a na viongozi na baadhi ya watendaji jambo ambalo linadhoofisha Muungano huo na kusababisha malalamiko makubwa miongoni mwa pande mbili hizo.

C h a n z o c h e t u c h a habari kimesema kwamba Makamishna wa Tume ya Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Joseph Warioba, wamemwambia k w a m b a k a t i y a w o t e waliotoa maoni hadi sasa waliouchambua Muungano kinaga ubaga ni yeye Dk. Amani Karume na Maalim Seif.

Chwaka wataka Rais Kikwete kuirejeshea Zanzibar mamlakahilo katika kutoa elimu ya Katiba kwa wananchi wa Zanzibar.

Akizungumza kat ika mkutano huo, mmoja wa Wazee wa Chwaka, Fadhil Mussa Haji alisema suala la kuunganisha nchi lilifanywa na watu wawili, Mwalimu Nyerere na Mzee Karume na wote hawapo tena.

Akasema, ni jukumu la viongozi waliopo madarakani kulishughulikia suala hilo.

“Mwalimu Nyerere na Mzee Karume waliunganisha nch i kwa kuamua wao wenyewe na kisha Mzee Karume akaja uwanjani kutuuliza mnakubali union watu wakaitikia…kwa kuwa alijua hakuna atakayeweza kupinga kwa wakati ule,” alisema na kuongeza:

”Lakini sisi hatujakubaliana na hayo tokea wakati huo…sasa kilichobaki tunamuomba Rais Kikwete na Rais Shein wao ndio wapo madakarakani wa tu re j e shee mamlaka na hadhi ya Zanzibar,”

Inatoka Uk. 1 alisema Mzee Fadhil, huku akishangiliwa na vijana waliohudhuria mkutano huo.

Mzee Fadhil alisema yapo baadhi ya mambo ambayo yameingizwa katika orodha ya mambo muungano bila ya ridhaa ya Wazanzibari.

Ha ta h ivyo akasema kuwa baadhi ya Wazanzibari wenyewe ndio walishiriki kuizamisha nchi yao kutokana n a t a m a a n a k u p e n d a madaraka, jambo ambalo alisema hivi sasa linawafanya wajute:

“ N i s i s i w e n y e w e tumefanya na tumetaka tutendewe hivi kwa sababu sisi tulikuwa tumeshapata uhuru wetu hapa mwaka 1963, lakini ni Wazanzibari wenyewe wakaleta mapinduzi na kuukataa ule uhuru halali,” alisema na kufafanua:

”Sasa tunasema hizi tamaa na kupenda madaraka sasa hivi ndivyo vitu vinavyotuadhibu sote katika nchi yetu kwa tamaa za hao wachache waliyokuwa wakituamulia,” alisema Mzee Fadhil.

A l i t o a m f a n o k w a viongozi wa Wazanzibari walivyojikaanga kwa mafuta yao wenyewe: “Ni tamaa ndizo zilizosababisha nchi kutokuwa na hadhi na mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake,” alisema Mzee Fadhil.

Alisema ni tamaa ndiyo zilizofanya kuporwa mamlaka kamili ya Zanzibar na hivyo kubakisha nchi kukosa uwakilishi hata kwa yale mambo ya Zanzibar, ambayo sio ya muungano yanavyokosa uwakilishi wa Wazanzibari katika nchi za nje:

”Wakati umefika sasa kwa kila mmoja kufahamu kwamba mamlaka ya Zanzibar yanahitaji kuheshimiwa na kupiganiwa na kila raia ili hadhi ya Zanzibar irudi,” alisema Mzee Fadhil.

Ak i toa maon i yake alipendekeza Katiba mpya iweke bayana mamlaka ya Zanzibar na rais wake, kwani alisema hivi sasa rais wa Zanzibar, hana hadhi ya kweli kama itakiwavyo kwa rais wa nchi.. RAIS Jakaya Mrisho Kikwete.

Page 4: ANNUUR 1055.pdf

4 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013Habari

Moyo, Rashid wapasua jipu la muunganoTUME ya mabadil iko Katiba mpya, imeelezwa kuwa Baraza la Mapinduzi h a l i k u s h a u r i w a w a l a kush ir ik i shwa kat ika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ulioundwa Aprili 26, 1964.

Wanasiasa wakongwe waliyokuwa katika Serikali ya Mapinduzi, wakati wa kuundwa kwa Muungano huo, Bw Salum Rashid na Bw Hassan Nassor Moyo waliiyambia Tume hiyo, walipokuwa wakitoa maoni yao Maisara, mjini Zanzibar.

K a t i k a m a o n i y a o walisema: Tangu awali katika kuundwa Muungano, kulikosekana uhalali, licha ya kuwa umedumu kwa miaka hamsini huku kukiwa na malalamiko kadhaa ya wananchi.

Wa k i z u n g u m z a k w a pamoja, Wanasiasa hao waliunga mkono kuwepo kwa Muungano, lakini walishauri mfumo mpya wa Muungano wa Mkataba, ili kila nchi kuwa na mamlaka yake kamili:

“Kwa hali ilivyo miaka 50 ya Muungano kushindwa kutatua mambo mbali mbali, mfumo pekee unaofaa kwa sasa na kwa kizazi hiki ni Muungano wa Mkataba. Utaratibu wake utajulikana baadae,” walisema Wanasiasa hao.

Bwana Nassoro Moyo alisema Serikali ya Muungano, isiogope maoni ya wananchi kwani kwa takriban miaka 50 matatizo ya Muungano yameshindwa kutatuliwa na njia pekee kwa sasa ni kukubali kubadilisha mfumo wa Muungano huo.

“Tukiwa na mfumo mpya wa Muungano, utakwenda sambamba na wakati huu ambao idadi kubwa ya wananchi wameamka na kuona kuna matatizo katika Muungano wetu,” alisema Mzee Moyo.

Mzee Moyo a l ikuwa Waziri wa kwanza wa Sheria wa Serikali ya Muungano, na Bwana Salum Rashid alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.

Kwa pamoja , wazee hao wakongwe wa siasa za Zanzibar, walishauri kuwepo kwa Muungano l ak in i walisisitiza, ili kuimarisha Muungano kwa nchi zote mbili, ni kusikilizwa kwa maoni ya wananchi ambao wanataka aina mpya ya Muungano wa Mkataba.

“Sisi ndiyo tul ikuwa

Na Alghaythiyah, Zanzibar

na dhamana wakati ule na tulitakiwa tuunganishe Serikali kwa kuimarisha udugu na kuimarisha uchumi wetu, bahati mbaya sasa kuna kero, mimi siziiti kero naita ni matatizo, ni wakati wake kuondoshwa”, alisema na kubainisha:

“Msimamo wangu ni Serikali ya Mkataba na ndiyo ninavyoamini na naamini kwamba huu muungano tulionao ni Muungano wa Mkataba, hili siyo jambo jipya, Mwalimu Nyerere na Mzee Karume walitia saini ya Mkataba, hili sio jambo jipya,” alisisitiza Mzee Moyo.

Moyo alitaka kurudishwa kwa utaratibu wa zamani, ili Rais wa Zanzibar aendelee kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Tanzania , akimaanisha Muungano huo ni wa Tanganyika na Zanzibar.

Naye , Ka t ibu Mkuu wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi, Mzee Salum Rashid ambaye alikuwa Dar es Saalm na Mzee Karume siku ya kusainiwa Mkataba wa Muungano, alisisitiza kuwepo kwa Muungano wenye maslahi kwa wananchi wa nchi zote mbili.

“Serikali ya Muungano isiwe na woga wa kuvunjika kwa Muungano. Hilo sio jambo kubwa na wala siyo jambo geni, baadhi ya nchi za Afrika ziliwahi kuungana, na Muungano ukavunjika,” alisema na kufafanua zaidi akisema:

“Sioni jambo zito kuvunjika kwa Muungano, mbona Muungano wa Senegal na Gambia ulivunjika na wote walikuwa ni wanachama wa Umoja wa Afrika na hakuna jambo lolote lililotokea,” alisema Bw Salum Rashid.

A l i s e m a w a n a n c h i wanaotaka Muungano wa Mkataba, hawamaanishi kuvunja Muungano, bali

wanataka mfumo mpya wa Muungano ili kuirudishia Zanz ibar, mamlaka na madaraka yake kamili.

A l i s e m a i f a h a m i k e kwamba, kuwa nje ya Serikali siyo sababu ya kuwa ni fursa ya kuzungumza hayo, lakini wakati ule likizungumzwa suala la Muungano, ilikuwa inaonekana ni uhaini.

A l i s e m a k w a s a s a haiwezekani tena kuburuzwa na hasa v i jana . Hivyo matumaini yake kwa tume hiyo ni makubwa.

“Naamini watafanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa na maoni ya wananchi ambayo wameyatoa kwa Tume, yatatekelezwa,” alisema Bw Salum Rashid.

Alisisitiza kuwa Muungano wa Mkataba ndiyo sahihi kwa sasa na hakuna sababu ya viongozi kuogopa hilo, Wazanzibari na hasa vijana wanataka nchi yao kuwa na mamlaka kamili.

M z e e M o y o n a Rashid, wote wawili kwa pamoja wamewatoa hofu Wazanzibari kuhusu utendaji wa Tume hiyo, na walisema wanaiamini kwamba itafanya kazi yake kwa uadilifu, bila upotoshaji.

Tume hiyo inayongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba na Katibu wa Tume, Assa Rashid tayari imeshachukuwa maoni ya baadhi ya viongozi wakuu, pamoja na Marais wastaafu wa Serikali ya Zanzibar.

Viongozi waliyokwisha toa maoni yao ni pamoja na Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Rais Mstaafu Dk Salmin Amour, Dk Amani Abeid Karume na baadhi viongozi wengine wa Serikali ya Zanzibar..

Wakati huo huo Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe Amani Abeid Amani Karume amesema kwamba wakati wa siku za mwanzoni, Muungano

ulikuwa wa heshima na usawa kati ya Zanzibar na Tanganyika lakini kadiri siku zinavyokwenda unachukua sura ya nchi moja -Tanganyika – kuuhodhi Muungano huo dhidi ya Zanzibar.

Akasema akiwa Rais kwa kipindi cha miaka 10 ameshuhudia mengi dhidi ya maslahi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Dr. Karume amesema hayo waka t i alipokutana na Tume ya Jaji Warioba na kutoa maoni yake juu ya Katiba Mpya.

Katika maoni yake Dr. Karume amesema kuwa hizi ni zama mpya za uwazi na ukweli na kwa hali iliyofikia sasa, hakuna njia nyengine zaidi ya kila nchi – Zanzibar na Tanganyika – kurejesha mamlaka yake (sovereignty) kitaifa na kimataifa na kisha nchi hizo mbili kushirikiana kup i t i a Muungano wa Mkataba kati yao.

N a y e R a i s M s t a a f u aliyemtangulia Dr. Amani, Mheshimiwa Dr. Salmin Amour, maarufu ‘Komandoo’, katika maoni yake ameieleza Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwamba anataka kuona Zanzibar na Tanganyika kila moja ikiwa ni nchi yenye mamlaka kamili ndani na nje na kisha zishirikiane kwa mfumo wa ushirikiano kama ule uliopo baina ya nchi za Afrika kupitia Umoja wa Afrika (AU).

D k . S a l m i n A m o u r amesema msingi wa umoja wa nchi za Afrika umetokana na mashirikiano kati ya vyama vya ukombozi chini ya PAFMECA.

Akasema Umoja wa Vyama vya Ukombozi vya Afrika Mashariki na Kati (PAFMECA) ulitambua haja ya nchi za Afrika kuungana baada ya uhuru, lakini kwa msingi wa kuheshimu mamlaka ya k i l a nch i (sovereignty) na mipaka yake.

Hivyo, akataka mahusiano mapya kati ya Zanzibar na Tanganyika yazingatie msingi huo ambao ndiyo pia uliojenga misingi ya Umoja wa Afrika (African Union).

K w a m b a k a m a n i muungano, basi Tanganyika na Zanzibar wakutane katika Umoja wa Afrika.

Kwa upande mwingine b a a d h i y a w a n a n c h i w a m e p o n d a h o j a z a wanaozungumzia udogo wa Zanzibar kwamba ni kikwazo cha kusimama kama nchi wakisema kuwa wachukue mfano wa Cape Verde ambayo hivi karibuni katika mchezo wa mpira imecheza na kutoka sare na nchi kubwa ya Afrika ya Kusini.

“Cape Verde ni nchi ndogo yenye watu wasiofika laki sita, lakini juzi hapa katika michezo ya Afrika imecheza ikiwa na bendera yake na kutoka sare na Afrika ya Kusini nchi kubwa yenye watu zaidi ya milioni 52.” Amesema mtoa maon i mmoja.

“Watizame Singapore, nchi ndogo kuliko Zanzibar na ilikuwa imeungana na Malaysia, lakini ilijitenga na sasa ipo mbali kimaendeleo, h u w e z i k u i l i n g a n i s h a na Unguja i l iyo katika muungano, kwa hiyo hoja sio udogo wa nchi wala muungano, ni dhamira na mipango ya nchi katika kujiendeleza, sisi Zanzibar dhamira tunaweza kuwa nayo, lakini hiyo mipango tunaiweka na kuitekeleza vipi chini ya makucha ya muungano wakati hata OIC tulikatazwa kujiunga ili tusinufaike na misaada ya Benki ya Kiislamu isiyo na riba.” Amesema mwananchi huyo ambaye hata hivyo hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

Bw Hassan Nassor MoyoBw Salum RashidDKT. Salmin Amour DKT. Amani Karume

Page 5: ANNUUR 1055.pdf

5 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013Habari za Kimataifa

KIONGOZI wa chama cha ‘Harakati ya Israel’ Bi. Tzipi Livni, amesema kuwa serikali ya Qatar imetoa kiasi cha dola milioni tatu kumsaidia Waziri Mkuu wa utawala wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwenye kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo Jumanne Januari 22.

Livni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Israel ameongeza kuwa, chama cha Yisrael Beytenu, kinachoongozwa na Avigdor Lieberman, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nchi za Nje wa Israel, nacho pia kimepokea dola milioni mbili na nusu kutoka serikali ya Qatar, ikiwa ni msaada wa kampeni ya uchaguzi mkuu huo.

Kwa upande mwengine, Chanel ONE ya Televisheni ya Israel imetangaza juu ya kuwepo mahusiano ya karibu kati ya Livni na mke wa Emir wa Qatar.

Kwa miaka kadhaa sasa Qatar, imekuwa na mahusiano ya kibiashara na mashirika ya Kizayuni na mashirika hayo yamekuwa na ofisi zake nchini humo.

Mashirika hayo yamekuwa yakitumiwa kama mwanzo wa kuwepo mahusiano ya kisiasa kati ya pande mbili na kuandaa safari za pande mbili za viongozi wa Qatar na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wakati baadhi ya nchi za Kiarabu zikijizatiti kusaidia utawala huo wa kizayuni, vitisho vya Israel dhidi ya msikiti wa al Aqsa bado vinaendelea, na mara hii mjumbe wa chama kinachoitwa “Yisrael Beiteinu” ameutaka utawala wa Israel kuulipua msikiti huo.

Matamshi hayo yanaonyesha ukubwa wa hatari zinazoukabili msikiti huo, ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.

P a i r L e p i d , m k u u w a chama kingine cha Kizayuni ambacho kinaunga mkono siasa za kupenda kupora ardhi na kijipanua za utawala wa Israel, amekosa haya na soni usoni kiasi cha kuthubutu kutangaza kuwa, Quds utakuwa mji mkuu wa utawala huo haramu.

Matamshi hayo yanatolewa katika hali ambayo, Avigdor Lieberman, waziri wa zamani wa mashauri ya kigeni wa Israel pia amesisitiza juu ya kupanuliwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina, hasa kwenye mji wa Baitul Muqaddas.

Kwa ujumla matamshi hayo ya viongozi wa utawala wa Kizayuni yanabainisha kuendelea malengo yao ya uharibifu dhidi ya msikiti wa al Aqsa na pia harakati za kutaka kuudhibiti mji wa Baitul Muqaddas.

Njama za Israel dhidi ya msikiti huo zimeingia katika kipindi cha hatari zaidi na kuna uwezekano

HAO NDIO WAARABU!

Qatar yatoa mamilioni ya dola kuisaidia IsraelWenye mpango wa kuipoteza Al Aqsa nao wamo

wa kutekelezwa mipango miovu ya kutaka kukiharibu kikamilifu kibla hicho cha kwanza cha Waislamu.

Wazayuni wanatumia njia tofauti za kuuharibu msikiti wa al Aqsa ikiwa ni pamoja na kuchimba mashimo mengi na njia za chini ya msikiti huo mtukufu na kando kando yake.

Vitendo hivyo kwa kweli vina lengo la kuzidhoofisha kuta za msikiti wa al Aqsa ili eneo hilo takatifu liweze kuharibika kwa mtikisiko mdogo tu wa ardhi au mripuko.

Hivi karibuni ilifichuliwa kuwa, moja ya mashirika ya kijasusi ya utawala wa Kizayuni linalojulikana kwa jina la ‘Kaj” lilifanya kikao na marubani wa Kizayuni kuwashawishi wadodoshe bomu kwenye msikiti huo.

Tangu kuundwa utawala huo pandikizi katika ardhi za Palestina hadi hivi sasa, msikiti mtukufu wa al Aqsa umeshashambuliwa mara kadhaa na Wazayuni.

Mwaka 1969 Wazayuni wenye misimamo mikali wakiongozwa na Dennis Michael Rohan, waliuchoma moto msikiti huo wa kihistoria, hatua ambayo iliratibiwa na makundi ya watalii kwa ushirikiano na viongozi wa Tel Aviv.

Katika tukio hilo, mita mraba zisizopungua 200 za dari ya msikiti huo ziliharibiwa na kuanguka kabisa, pande tano za kuba la msikiti huo ziliungua na mimbari yenye thamani kubwa iliyojengwa miaka 800 iliyopita, iliteketea kabisa kwa moto.

Huku mji wa Baitul Muqaddas na msikiti wa al Aqsa ukikabiliwa na duru mpya ya vitisho na

njama za utawala wa Kizayuni, fikra za walio wengi duniani wanaitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti na za haraka za kupambana

MSIKITI wa al Aqsa

Mahakama ya Gambia imemuhukumu kifungo cha miaka 10 gerezani Ensa Badjie, Mkuu wa zamani wa Jeshi la Polisi la Gambia (IGP) baada ya kumku ta na hatia ya kushiriki kwenye magendo ya dawa za kulevya, wizi na ufisadi.

H a l i k a d h a l i k a m a h a k a m a h i y o imemkuta Ensa Badjie na hatia ya kutumia vibaya madaraka yake. Mkuu huyo wa zamani wa jeshi la polisi la Gambia alitiwa mbaroni wiki iliyopita na makachero wa polisi wa nchi hiyo.

Taar i fa z inasema kuwa, Ensa Badjie tayari ameshaanza kutumikia adhabu ya k i fungo hicho pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu wa jeshi la polisi waliohukumiwa adhabu mbalimbali za vifungo.

IGP Gambia jela miaka kumi

na utawala huo, wakiamini kwamba, kucheleweshwa suala hilo kutaifanya Israel kuendelea na hatua zake hizo za uharibifu bila ya woga.

URUSI imeanza kufanya mazoezi makubwa ya jeshi lake la majini katika bahari za Mediterranean na Bahari Nyeusi, karibu na Syria ambayo inakabiliwa na mashambulizi ya magenge ya waasi.

Mazoezi hayo yameelezwa kuwa ni makubwa zaidi kufanywa na Jeshi la Majini la Urusi kwa miongo kadhaa.

Taarifa rasmi ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kuwa, mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika katika utaratibu wa vikosi vya ulinzi vya Urusi wa mwaka 2013, wa kujiimarisha kiulinzi na kuzingatia zaidi suala la kufanya kazi kwa pamoja vikosi vya nchi hiyo, kutoka manowari zake mbalimbali zinapokuwa katika eneo la maji la mbali.

Mazoezi hayo ya Jeshi la Majini yataendelea hadi Januari 29 na kufanya majaribio ya silaha na mbinu tofauti za kivita.

Urusi imekuwa ikizilaumu nchi za Magharibi kwa kuchochea mauaji na uasi nchini Syria, na kusababisha kushuhudiwa machafuko tangu katikati ya Machi 2011.

Raia wengi na maafisa usalama wa serikali ya Syria wameuawa katika machafuko hayo.

Urusi yafanya mazoezi makubwa ya kijeshi Syria

Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi Bw. Sergei Lavrov, ametupilia mbali ombi la nchi za Qatar na Uturuki za kui taka Moscow imshawishi Rais Bashar Assad wa Syria aondoke madarakani na kusisitiza kwamba, kiongozi huyo hatang’atuka madarakani.

Ameongeza kuwa, suala la kuondoka madarakani Rais Assad haliko mikononi mwa serikali ya

Moscow. Bw. Lavrov amesema, hakuna

sababu zozote za kuwepo uadui wa serikali za Uturuki na Qatar dhidi ya serikali ya Damascus, kwani nchi hizo zilikuwa na mahusiano mazuri na serikali ya Syria.

Lavrov amesisi t iza kuwa, mgogoro wa Syria kamwe hauwezi kumalizwa kwa njia za kijeshi na kwamba, njia pekee ya kutatua mzozo huo ni kuketi kwenye meza ya mazungumzo.

URUSI imeanza kufanya mazoezi makubwa ya jeshi

Page 6: ANNUUR 1055.pdf

6 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013Makala/Tangazo

S H U K R A N I z o t e anastahiki mwenyezi Mungu Rehema na Amani zimfikie Mtume wetu Muhamad na masahaba zake na wanaomfuata ama baada ya utangulizi huu.

Hakika Uislam ni dini inayohimiza msamaha na uwepesi na inatosha kwa jina la dini ya uwepese na msamaha. Na maana ya hanafia ni msimamo na msamaha yaani ni dini nyepesi inayotekelezeka amri zake, hivyo basi Uislamu umekuja ili kutia nguvu vyanzo vya msamaha wa kuacha ubabe kuvuka mipaka na siasa kali na kuhimiza kuishi na watu wote kwa wema na yanayotilia nguvu zaidi ni maneno ya mtume (S.A.W) kwa hakika nimetumilizwa ili nitimize tabia njema na msamaha ni miongoni mwa vyanzo vya tabia nzuri na ndio tabia ya juu zaidi ilio nzuri.

Msamaha ni shina na chanzo cha tabia nzuri Qur-ani imezungumzia hilo pale mwenyezi Mungu alipowaamrisha waja wake kusamehe na kuwa wapole akasema “hataki mwenyezi m u n g u k u k u w e k e e n i ugumu” pia akasema tena “Anataka mwenyezi Mungu kwenu wepesi na wala hataki kwenu ugumu”

Amesema tena “anataka m w e n y e z i m u n g u awapunguzieni kwenu mambo magumu na aya za msamaha ni nyingi hazidhibiiki.

Na vilevile qur-ani imemihimiza mtume (S .A .W) aishi na waislamu kwa tabia ya msamaha na maana yake ni kukubali uwepesi wa tabia zao na kuyabea makosa yao na kuwasamehe wanapoteleza.

Amesema Mwenyezi M u n g u w a s a m e h e n a waamrishe mema na wapuuze wa j inga” na akasema kumwambia mtume (SAW) na kwa Rehema toka kwa mwenyezi Mungu umekuwa laini kwao na lau ungekuwa mwenye moyo mbaya na chuki wangekukimbia wote uliokaribu nao wasamehe

DR. EMAD RABIE

Uislam unahimiza kusamehena waombee msamaha na washauri katika mambo” na msahama kwa maana yake pana zaidi ina maana ya uwepesi kwa watu hadi wapinzani na kuwasamehe na kuishi nao kwa ulaini na upole na uwepesi na kukubali nyuzuru zao na kupokea yale wanayokosea. Hivyo basi ni lazima kwa kila muislamu kuishi kwa tabia ya musamehe kwa watu wote bila ya kubagua kati ya Muislamu na asiye Muislamu katika mambo yote ya maisha ya kila s iku amesema mtume ( S . A . W ) “ A m r e h e m u mwenyezi Mungu mtu a m b a y e h u s a m e h e anapouza na anaponunua na anapokopesha” na uzuri ulioje juu ya maneno ya mshair i huyu mwenye hekima nitailazimisha nafsi yangu kusamehe kila kosa.

Hata kama nitafanyiwa makosa mengi zaidi akasama mwengine:-

Ananisamehe mimi mtu mjinga kwa maneno mabaya ninachukia kumjibu yeye anataka ujinga mimi nataka upole ni sawa na kijiti cha kibiriti zawadi yake ni kuunguzwa na kuishi na watu kwa msamaha na viumbe vyote kwa kuna faida kubwa nazo ni:-

Ta b i a y a k u s a m e h e inakuwani mwenendo wa kueneza mapenzi kati ya watu.

Huondoa chuki na choyo moyoni mwa muislamu.

Msamaha ni wito wa kikazi na ni mfano mzuri wa kuigwa kwa kueneza Uislam kati ya wasio waislam na dalili kubwa juu ya hilo ni kuenea Uislam katika nchi nyingi za Afrika na Ulaya bila ya vita au kuuana. Kwa hak ika umeenea Uislam katika nchi hizi ni kwa matokeo ya tabia ya kusamehe waliokuwa nao Waislam wafanya biashara na watalii katika nchi hizi pale walipoona watu uzuri wa tabia zao na ukubwa wa msamaha wao waliingia k a t i k a U i s a l a m k w a kuupenda na kuridhia na kutii bila ya kulazimishwa au kuteswa nguvu na mifano ya Kiislam katika jambo hili la kusamehe limejaa katika vitabu vya historia na sira (Mwenendo) wa mtume (S.A.W) haitutoshi kuyataja katika makala hii ambayo ni ndogo.

Kwani kuyataja kwake inahitaji vitabu vingi na wakati mrefu yatosha tutaje

mifano michache iliyoenea na ni mashuhuri masikioni mwa wasikilizaji pale alipoingia mtume kuikomboa maka na kuwasamehe watu wa makka ambao walimuadhibu

yeye na masahaba zake. Hakuongeza la kusema

isipokuwa aliwambia “Enyi watu wa makka hivi mnadhani mimi nitakufanyeni nini nyinyi?” wakasema kheri

ndugu mwema na mtoto wa ndugu mwema”

Akasema “Nendeni na nyinyi mupo huru” (S.A.W)

Baadhi ya Viongozi waliotoa mada mbali mbali meza kuu wakiwa katika Kongamano la kidini lililoandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Kimisr Markaz cha jijini Dar es salaam kongamano hilo lilifanyika Jijini Arusha na kuhudhuriwa na washiriki 180 hivi karibuni.

Jumuiya ya wataalamu wa kiislamu Tanzania ( TAMPRO) kwa kushirikiana na Jumuiya ya wanazuoni Tanzania (Hai-atul – Ulamaa) wana watangazia waislamu wote kuhudhuria katika Hafla ya ugawaji Zakka.

Siku: JumapiliTarehe: 27/01/2013Mahali: Lamada hotelMuda: saa 2:30 ( Asubuhi) – Saa 6:30 mchana

Zakka ya mwaka huu imelenga kuwasaidia kina mama Wajane Masikini/ Mafukara 15 na Wanafunzi 15 wasio na uwezo.

Kwa mawasiliano zaidi piga simu: 0716 776226, 0713 208585, 0754 434968.

Wote mnakaribishwa.

TAMPRO BAITUL- MAAL

Page 7: ANNUUR 1055.pdf

7 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013Makala

INGAWA bado kuna ubishi kwa serikali yetu, kuendelea kuisujudia Dar es Salaam na kupuuzia ulazima wa kukuza na kuendeleza mikoa mingine kiuchumi, lakini ukweli unaendelea kubaki kuwa, watu wataendelea kumiminika kutoka mikoa mingine na kujazana Dar es Salaam.

W a t u w a m e k u w a wakitiririka Dar wakiamini kuwa hapo ndipo l i l ipo jicho la serikali kihuduma na kimaendeleo. Wanaamini kwamba Dar ndiko mahali ambako kuna fursa zaidi za kimaisha na mahali ambako mtu anaweza akajishughulisha na chochote na ukaambulia chochote.

Hali hii ni matokeo ya serikali kuweka mazingira ya huduma za jamii, kimaendeleo na kiuchumi katika eneo moja na kuyaacha maeneo mengine yakisuasua.

Kwa mfano , Dodoma ndiko yalipo Makao Makuu ya Chama Tawala na Serikali, lakini katika uhalisia wake, Dodoma ni Makao Makuu

Kupeleka gesi Dar ni kuhujumu malengo ya Mtwara Corridor

Na Shaaban Rajab

RAIS Mstaafu, Benjamin William Mkapa

jina, vigoda bado vipo Dar es Salaam. Wenye vigoda wanaona kuhamia Dodoma ni sawa na kuchukua ‘uamuzi mgumu’.

Yote hayo ni kwa sababu Dodoma pamoja na cheo kizuri cha Makao Makuu, lakini kama ilivyo mikoa mingine, inaonekana haina mazingira yanayowashawishi serikali kuhamia huko.

Pamoja na kwamba kasumba hii ya serikali imeifanya Dar kuwa na mrundikano mkubwa wa watu kiasi cha kuelemea miundo mbinu ya jiji hili, bado inaonekana kukosekana m i k a k a t i k a b a m b e y a kuwafanya Watanzania kuona fahari kubaki katika mikoa yao na kuendelea na shughuli zao za uchumi na kimaendeleo.

Hivi sasa kuna sakata la wananchi wa mkoa wa Mtwara uliopo Kusini mwa Tanzania, ambao wanashinikiza serikali kutumia gesi inayozalishwa mkoani humo, kuwa chachu ya kuwanyanyua kiuchumi na kimaendeleo badala ya kuivuna na kuielekeza Dar es Salaam.

Wana Mtwara wanaamini kuwa gesi iliyopo itakuwa chachu ya maendeleo mkoani

humo kiasi cha kuwafanya Watanzania kutoka mikoa mingine, kuwa na hamu ya kwenda kuishi na kufanya kaz i zao Mtwara kama wanavyokimbilia jijini Dar es Salaam hivi sasa.

Sote tunakumbuka ule mpango wa kufungua malango ya kiuchumi unaoitwa Mtwara Corridor. Mpango huu ulikuwa na maana ya ku fungua kiuchumi maeneo kwa ajili ya uwekezaji na miundombinu ili kuhudumia maeneo ya ndani Kusini (Land Locked Area) yaani Mtwara, Lindi, Ruvuma hadi nchi jirani za Malawi na Zambia.

Mkakati huu ulichagizwa zaidi na Rais wa awamu ya tatu Mzee Benjamin William Mkapa, kiasi cha kuanza kuleta sura ya matumaini hususan kwa watu wa mikoa ya Kusini.

Kugunduliwa kwa gesi huko Songosongo na Mnazi Bay, kuwepo kwa bandari yenye kina kirefu cha asili ya Mtwara, kilimo cha zao la korosho, matunda, utengenezaji wa chumvi, madini ya nishati kama makaa ya mawe huko Kiwira, madini vito huko Lindi, Tunduru, Jasi, Gypsum n.k, maliasili zote hizi ni kichocheo muhimu cha maendeleo ya kiuchumi kwa ukanda huu na kwa taifa kwa ujumla.

M t w a r a u k i w a m k o a unaoongoza kwa zao la korosho, unahitaji viwanda vya kubangulia zao hilo (processing factories) ili kuliongezea thamani na wakati huo huo kuongeza pato kwa mkulima. Baadhi ya viwanda vinafanya kazi lakini vingi vimesimamisha uzalishaji na kugeuzwa maghala.

Ta y a r i M t w a r a k u n a wawekezaji wa viwanda ambao wameshaanza uwekezaji wao. Kwa mfano hivi sasa kuna ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Dangote, kuna mpango wa kujengwa kiwanda kikubwa cha mbolea, ambacho kitatumia umeme mwingi.

Kunahitaji viwanda vya chumvi, migodi ya madini kama kule Tunduru itahitaji umeme, migodi ya makaa ya mawe Kiwira kadhalika. Ruvuma na L ind i ko t e kunahitaji umeme wa uhakika kwa ajili ya uwekezaji ambao umeshaanza kuonekana.

Gesi ya Msambiati imeleta matumaini ya kuwepo nishati ya kutosha kwa ajili ya kuendesha shughuli zote hizi za kiuchumi katika eneo hilo. Uwekezaji wote huu utahitaji umeme wa kutosha na wa uhakika katika eneo lote la Mtwara Corridor hapo baadae, ili kukidhi haja ya uwekezaji katika eneo hilo.

Kuitoa gesi Mtwara na kuisafirisha hadi Dar es Salaam ili eti iweze kuzalisha umeme wa uhakika katika gridi ya

Taifa na kuleta nishati ya kudumu katika viwanda vya Dar es Salaam, ni sawa na kusaliti matarajio ya uwekezaji mkubwa ka t ika Mtwara Corridor.

Ni vyema serikali ikaona haja ya kufua umeme na kuuingiza gridi ya Taifa kutokea huko huko Mtwara, na ukasambaa mikoa mingine ikiwemo Dar. Hatua hii pia ni bora zaidi kiusalama kwani hata Ubungo Electric Plant ikikwama iwe ni kwa tufani au maafa, basi kunakuwepo na chaguo la chanzo kingine cha umeme, nao ni kutoka Mtwara Electric Plant.

Kwa kufanya maamuzi ya busara katika kuvuna na kutumia rasilmali zilizopo mikoani, na kwa kuweka mikakati ya kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kiuchumi mikoani, ni wazi kwamba utafika wakati watu badala ya kurundikana Dar, wakatamani kwenda Mtwara , L indi , Kigoma, Kagera na mikoa mingineyo, kwa kuwa zile fursa zilizokuwa zikionekana Dar pekee huko nako zitakuwepo.

Kwa kifupi , hatua hi i inaiwezesha mikoa nayo kuwa ‘Economic Hub’ kama Dar japo inaweza isiwe sawa kwa kipindi kifupi.

Hivi sasa serikali imeamua kujenga bandari mpya huko Mwambani katika jiji la Tanga, ni hatua ya kimaslahi kiuchumi kwa taifa na ya kimaendeleo kwa Watanzania. Hatua hii bila shaka ni nzuri na hata kistrategia inakubalika.

Kwa kujengwa bandari ya kisasa Tanga, ni wazi kwamba kutarahisisha kupokea na kusafirisha bidhaa nyingi katika maeneo ya Kaskazini mwa nchi na katika nchi jirani za Uganda, Rwanda na Burundi, na DRC.

Hata hivyo wakati wa ujenzi wa bandari ya Tanga ukiwekwa bayana, serikali pia imeeleza kuwa imeingia makubaliano na Kampuni ya Ujenzi (Merchants Holding Company), kutoka China kwa ajili ya ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu, alishasema kuwa makubaliano ya awali yalifanyika Septemba 5 mwaka jana na kwamba, u jenzi wa bandar i h iyo utakwenda sambamba na uendelezaji wa miradi mingine inayoambatana na ujenzi wa bandari hiyo kwenye Eneo Maalumu la kiuchumi la Bagamoyo (SEZ).

Dkt. Nagu alisema kikosi kazi cha kampuni ya Merchants Holding Company, kitasimamia miradi itakayojumuisha ujenzi wa barabara itakayounganisha bandari hiyo, pamoja na ujenzi wa reli itakayounganisha bandari hiyo na reli ya kati na

TAZARA.Waziri alichagiza zaidi

kuwa miradi hiyo itatekelezwa kwenye maeneo hayo maalum ya kiuchumi, hivyo ni mradi wenye umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya Taifa ikizingatiwa kwamba bandari hiyo mpya itasaidia kupunguza msongamano wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, ambayo alidai tayari imekaribia ukomo wake wa kupanuliwa.

Dkt. Nagu alibainisha kwamba bandari mpya ya Bagamoyo i t akuza kwa kiasi kikubwa ushindani wa Tanzania kikanda na Kimataifa kwa kuwa itaongeza uwezo wa kuhudumia shehena za mizigo kutoka na kwenda nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Congo (DRC), na Malawi.

Alisema kadhalika mapato yatokanayo na biashara ya kimataifa yataongezeka na kuongeza fursa za ajira hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi wa nchi.

Binafs i s idhani kama kulikuwa na ulazima sana kiuchumi kujenga Bandari ya mpya Bagamoro kwa sasa kuliko ile ya Mtwara. Kujengwa kwa Bandari Bagamoyo, ni kama tawi tu (subsidiary) kwa bandari ya Dar es Salaam. Zaidi ni kwamba zitakuwa eneo moja, kwa maana hakuna nafuu yoyote kiusafirshaji inayoweza kupatikana kiuchumi zaidi ya ile inayotajwa ya kuondoa msongamano bandari ya Dar es Salaam.

Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zingetosha kujenga uchumi kwa njia ya bandari. Si Bagamoyo. Kwa kutengemaa bandari za Tanga na Mtwara, ingetosha kupunguza msongamano uliopo katika Bandari ya Dar. Shehena za DRC, Rwanda, Burundi, Uganda ni rahisi na nafuu iwapo zitapita katika bandari ya Tanga kuliko Dar au hiyo ya Bagamoyo.

S h e h e n a z a M a l a w i , Zambia na maeneo maalum ya uwekezaji ya Kusini mwa nchi zingesafirishwa kwa urahisi na kwa unafuu zaidi kwa kupitia Bandari ya Mtwara, ambayo tunaona kimaslahi ya kiuchumi ndiyo ingestahili kupewa kipaumbele ikilinganishwa na hiyo inayojengwa Bagamoyo!

Kiuchumi tunaona maamuzi yaliyofanywa na serikali hayakuwa na tofauti na ya wale walioamua kuing’oa reli ya Nachingwea –Mtwara, i l iyojengwa mahsusi na wakoloni wa Kiingereza kwa ajili ya kusafirisha mazao ya karanga na korosho.

Ni vyema serikali ikajali zaidi mipango ya kiuchumi i n a y o k i d h i v i g e z o v y a kiuchumi na kimaendeleo kuliko mipango inayokidhi sababu na haja za kisiasa.

Page 8: ANNUUR 1055.pdf

8 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013

Makala

S I A S A n i m c h e z o mchafu, na ukitafakari zaidi kuhusu msemo huu, utagundua kwamba w a n a s i a s a n i w a t u wachafu na hutakiwi kuwaamini hata siku m o j a . M w a n a s i a s a yeyote haijalishi anaapa kwa kutumia Qur’an au Bibilia, madhali ni mwanasiasa hata kiapo chake haki f ik i kwa mungu. Wengi wapo kama popo, akifika msikitini ameshika tasbihi, na akiingia kanisani amevaa msalaba!

Binadamu ameumbwa na ubinafsi wa kujipendelea, wakati wowote na popote pale alipo hata akipata fursa ya kuamua, basi hatasita kujipendelea. A t a j i p e n d e l e a k w a kuonyesha kwamba yeye ni bora zaidi kuliko wale waliomzunguka. Wakati m w i n g i n e a n a w e z a k u j i p e n d e l e a k w a kudhihirisha kwamba imani yake ni bora kuliko imani ya wengine, au mila za kabila lake ni bora kuliko zingine nakadhalika. Imani za udini katika nchi yetu zina historia ndefu mno licha ya kwamba wanasiasa na serikali zao zimekuwa zikikataa kwamba hakuna ubaguzi wa udini katika nchi hii. Kulingana na utafiti wangu hulka za udini pia zimechangia k u l i n d a n a k u j e n g a desturi za kulindana: mtu anakosa ambalo kwa mujibu wa sheria anastahili kuwajibishwa kwa kufikishwa mbele ya haki, lakini kwa vile ni muumini mwenzio, basi unamlinda, na huku ukizingatia kigezo kwamba ukimfukuza utapunguza idadi ya waumini katika safu ya uongozi wako. Imeshawahi kutokea mtu amekosa lakini kigezo cha iman i za k id in i kikamlinda asifukuzwe kazi bali akahamishiwa i d a r a n y i n g i n e i l i akajirekebishe!

Wa k a t i m w i n g i n e udini unatumika kama njia mbadala ya kuugawa umma ushindwe kusimama kwa pamoja kama taifa kutetea mahitaji muhimu na maslahi kwa taifa (Divide and Rule).

Taifa hili ni la Waislamu na Wakristo ukiwagawa wakawa hawapendani,

Je, wana Sera za Udini?

Na Dr. Noordin Jella

w a n a g o m b a n a n a kuchukiana, basi wanakuwa hawana uwezo wowote wa kuukemea utawala wala kuuwajibisha pale wanapoenda kinyume na taratibu zilizowekwa; n a k w a m a a n a h i i w a t a w a l a w a n a w e z a k u f a n y a w a t a k a v y o wanajua hakuna nguvu ya umma ya pamoja ya kuwawajibisha. Hii katiba tunayoitafuta hivi sasa tungekuwa tumeshaipata miaka mingi iliyopita tangu enzi za Nyerere, lakini tumegawanywa na tumegawanyika.

M w a k a 1 9 9 2 tulipoanzisha mfumo wa vyama vingi vya kinafiki, ni wanasiasa hao hao

wal iokuwa ser ikal in i waliokuwa mustari wa mbele katika zoezi hilo la kuviunda vyama vya upinzani, na walipomaliza kuviunda wao hao hao ndiyo walianza kutuambia kwamba hiki ni chama Wais lamu na k i le n i chama cha Wakristo au chama fulani ni chama cha kikabila nakadhalika! Ilimradi tu wametugawa na kweli tumegawanyika.

Tatizo la Udini ni tatizo sugu na lina historia ndefu katika nchi hii, na tatizo hili hakulianzisha Dr. Kikwete licha ya kwamba watu wengi wanalalamika kwamba Kikwete ana Udini. Udini aliuanzisha Mwalimu Nyerere mwenyewe hata

kabla nchi haijapata uhuru toka kwa Waingereza, na kauli ya kwanza ya Udini aliitoa Nyerere akiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja mjini Dar es Salaam aliposema “Hapa nipo Mkristo peke yangu” wakati akitoa kauli hiyo alikuwa amezungukwa na baadhi ya wanaharakati wa chama cha TAA waliokuwa wanapigania uhuru wa nchi hii ambao wote walikuwa ni Waislamu.

Wakati watu wanashauku ni namna gani wanaweza k u p a t a u h u r u y e y e hakuf iki r ia umuhimu wa uhuru kwanza, bali alifikiria Udini! Pamoja na kwamba hakuna anayejua dini nzuri ni ipi? Au

pamoja na kwamba hakuna aliyechagua azaliwe na dini gani, nikiwa na maana kwamba wote tumefuata dini walizokuwa nazo wazazi wetu, ingawa kuna wachache ambao wamevuka barabara na kujiunga na dini nyingine kwa sababu za ndoa, uchumi, ushawishi fulani au maamuzi tu ya mtu mwenyewe. Kulingana na uelewa wa viongozi wetu tangu nchi hii ipate uhuru, ni kwamba kila mtawala alijitahidi kuwasogeza maumini wenzie karibu na yeye kadri ilivyowezekana, kwa mfano: Nyerere alipoingia Ikulu kwanza inasemekana aliandika Waraka wa kuwaagiza viongozi wa wizara ya elimu kutoa kipaumbele kwa wanafunzi wa Kikristo, na baada ya kufanya hivyo akahakikisha kwa vitendo kwamba anawapendelea Wakristo kwa kila hali.

Hii ni vita kubwa sana, pamoja na kwamba siyo vita ya kutumia bunduki au mapanga lakini ni vita ambayo imeweza kudumu kwa zaidi ya miaka 50 sasa; pamoja na kuwepo kwa vita hii, lakini hakuna kiongozi hata mmoja utakayemuuliza kuhusu vita hii akubali kwamba kuna vita! Kuna msomi mmoja wa Uingereza al ikuwa anaitwa Isac Newton ambaye aligundua t a r a t i b u z a m w e n d o (principles of motion): moja ya taratibu hizo inasema “Kila kitendo kina jibu lake” (Every Action has Reaction). Nimetumia taratibu za Newton ili nielezee kwamba Mkiristo akimtoa Muislamu kwa maana ya kwamba ni Muislamu, basi Waislamu wengine walioko ndani ya System hiyo hiyo wanajibu mapigo chini kwa chini; Muislamu akimtoa Mkiristo na kumuweka Muislamu kwa maana za kidini, basi Wakristo waliopo ndani ya System hiyo hiyo wanajibu mapigo ya chini kwa chini. Wewe kama ni Mkiristo, u k a m c h a g u a Wa z i r i Mkristo au wewe kama ni Muislamu ukamchagua Waziri Muislamu bado hujafanya kitu kwa vile waziri si mtendaji bali waziri ni mzungumzaji, lakini wanaopika mambo huko jikoni huwajui kama

RAIS Jakaya Kikwete. Dkt. Shukuru Kawambwa (Waziri)

Inaendelea Uk. 9

Page 9: ANNUUR 1055.pdf

9 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013Makala

Je, wana Sera za Udini?Inatoka Uk. 8

ni Waislamu au Wakristo! Hii ni vita ya kipuuzi na

inabidi vita hii ikomeshwe m a r a m o j a , k w a v i l e tukiendelea na ustaarabu huu tutajikuta siku moja tunatoana ngeu. Tusihusishe mahitaji muhimu ya binadamu na imani za kiroho. Kila binadamu bila ya kujali imani yake ya kidini anahitaji kula, kunywa, kuvaa, elimu bora na mengineyo. Hivyo kuhusisha imani za kiroho na mahitaji muhimu ya binadamu, ni kumkufuru mungu.

Watu wengi wanamlaumu sana Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwamba ni mtu anayeendekeza udini, lakini kwa nini tumlaumu Kikwete tusiilamu CCM na system yake! Si tunasema kwamba Rais ni taasisi, kama hivyo ndivyo sioni kama tutakuwa sahihi kumlaumu Kikwete, mimi nawaombeni hebu mvute kumbukumbu zenu mkumbuke kukua na kuenea kwa Udini tangu nchi hii imepata uhuru mwaka 1961 hadi leo, ingawa nafahamu kwamba Watanzania tuna k u m b u k u m b u d h a i f u ; hatukumbuki jana wala hatuna habari na kesho, isipokuwa tunaiona leo tu kwa vile ipo mbele ya macho yetu, lakini pamoja na lawama hizo, Kikwete huyo huyo anaonekana vita ya udini imemshinda kwa vile Wakristo wana vyuo vikuu zaidi ya 15 hapa nchini, wakati Waislamu wana Chuo Kikuu kimoja.

Waislamu wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kuhusu ahadi ya Mwalimu Nyerere ya kuwapa Wakristo upendeleo, lakini wamekuwa wakipuuzwa kama wanachosema siyo kitu muhimu! System ya Nyerere (serikali ya CCM) imekuwa na tabia ya kupuza sana wananchi wake. Unaweza ukatoa hoja nyeti sana kwa manufaa ya jamii, lakini wakajikausha kwa kukaa kimya kama vile unachokidai hakina maana!

Mtu wa kwanza katika s e r i k a l i k u z u n g u m z i a kubaguliwa Waislamu katika elimu alikuwa Professor Kighoma Malima, lakini Mzee Mwinyi hakuchukua hatua zozote wala kukemea ‘kwa vile ubaguzi huo umewekwa na mwenye nchi. Sasa hivi yupo Rais Kikwete na Maalimu Shukuru Kawambwa hawataki kuuweka hadharani

ubaguzi huo wala kuukemea. Wanaogopa wakiukemea wanaweza kuwa kat ika matatizo makubwa, kwa vile mwenye nchi aliacha wosia kwamba anataka kulipa Kanisa “A better chance.”

Mimi naona kwa mwenendo huu tunazidi kuongeza baruti kwenye mbegu ya chuki iliyopandwa na Mwasisi wa Taifa hili Mwalimu Nyerere. Nyerere amepanda mbegu ya chuki ya udini kati ya Waislamu na Wakristo na kama tusipotumia busara kuing’oa mbegu hii kuichoma moto na kuifukia baharini, basi nchi hii siku za usoni itawaka moto!

Hivi majuzi Waislamu walilalamika wakidai serikali wamechakachua matokeo yao ya mtihani ya kidato cha Nne/Sita! Hizi ni shutuma nzito sana kwa nchi yoyote inayojal i ra ia wake na inayopenda kudumisha amani ya kweli, na shutuma kama hizi si vizuri kutumia ujanja ujanja wa kuzizima chini kwa chini, bali ni suala ambalo serikali inatakiwa ijisafishe wazi wazi ili kuondoa chuki ambazo zinaendelea kujilimbikiza; na wale wote waliohusika ni lazima wawajibishwe kulingana na mujibu wa sheria.

Mwaka 2007 nilipokuwa nafundisha kule Chuo Kikuu Mzumbe siku moja

ni l ikuwa nasahihisha mtihani wa wanafunzi wangu wa mwaka wa ta tu ambao n i l ikuwa nawafundisha somo la Quantitative Economics (Mahesabu ya Uchumi); w a k a t i n a s a h i h i s h a mtihani huo akauona mwalimu mwenzangu

ambaye alikuwa Mhadhiri M w a n d a m i z i . M a r a akaanza kushangaa eti kumbe ninajua hesabu! A k a a n z a k u s t a a j a b u inakuwaje mimi Muislamu ninajua hesabu?

Mara akawaita walimu wengine nao wakaanza kushangaa kama yeye

alivyokuwa anashangaa! Mimi nikaona labda kwa vile ni walimu wenzangu, labda walikuwa wanafanya utani, lakini cha kushangaza nikaona gumzo hilo likawa refu na baada ya hapo ikawa inaendelea minong’ono ya chini kwa chini! Na wengine wakaanza kuniita Abdala, wakati hilo siyo jina langu!

Je, kama ningekuwa ni Bhudist au sina dini yoyote ningewekwa kwenye kundi gani!? Ningekuwa juu ya Ukristo au ningekuwa chini ya Uislamu!? Je, Watanzania bado hamjakubali kwamba Nyerere ka tupumbaza? S a s a k a m a M h a d h i r i Mwandamiz i wa Chuo Kikuu anaweza kustaajabu kwamba kumbe Muislamu anaweza kujua hesabu!? Hivi imani ya kiroho na uelewa au ufahamu wa mtu vinahusiana nini!? Ina maana Professor wa hesabu Mkiristo akibadili dini na kuwa Muislamu hesabu zote kichwani zinayeyuka na kuwa muuza machungwa?

Ndugu zangu Watanzania, Nyerere ametufanya kitu k ibaya sana , na kama tusipotumia busara tutakuja kuchinjana kama kuku kwa imani za kijinga ambazo hazitofautiani na imani za kishirikina.

Mimi binafsi ni muhanga wa sera za Udini, naamini kwamba sera na vigezo hivi hivi vya udini ndivyo vimetumika kuvipiga vita na kuviagandamiza vitabu vyangu ndani na nje ya nchi. Wanakitengo wakitumia desturi na mila zao zile zile za Udini za kwamba kwa nini Muislamu aandike vitabu vingi kiasi hiki (Vitabu 33)? Vitabu hivi vinaweza k u o n e k a n a k w e n y e mitandao kama vile www.amazon.com, www.google.com, na mingineyo (tafuta Noordin Jella).

Udini umeleta chuki za kijinga ambazo zimepuuza kabisa kitu kinachoitwa uzalendo. Leo Muislamu amefanya kitu kizuri, Wakristo wanakipinga; kesho Mkiristo naye atafanya kitu kizuri kwa taifa hili lakini Waislamu watakipinga..

(Dr. Noordin Jella (Ph.D. in Economics)

Former Lecturer of Mzumbe, Open & KIU – Dar, Un ivers i t i e s . Currently: Freelance Journalist & Seasonal Political Analyst

Email: [email protected] Mobile: +255 782 000 131)

NAPE Nnauye, Katibu Mwenezi CCM

RAIS Jakaya Kikwete (katikati), Rais mstaafu Zanzibar, Dkt. Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu mstaafu Yusuph Makamba.

Page 10: ANNUUR 1055.pdf

10 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013Makala

(Januari 2013 - Mtandao wa kupashana habari)

MTU mwingine wa hatari ambaye alikuwa na nafasi katika kuundwa kwa mpango wa kupambana na uasi nchini Irak alikuwa Kamishna wa zamani wa polisi jijini New York Bernie Kerik (aliyepigwa picha akiwa Chuo cha Polisi cha Baghdad amezungukwa na walinzi) ambaye mwaka 2007 alifunguliwa mashitaka katika mahakama ya shirikisho (serikali kuu) kwa makosa 16 ya jinai.

Kerik alikuwa ameteuliwa na utawala wa Bush wakati uvamizi wa Irak ulipoanza mwaka 2003 kusaidia katika kuunda upya na kutoa mafunzo kwa jeshi la polisi Irak. Wakati akiwa hapo kwa muda mfupi mwaka 2003, Bernie Kerik - ambaye alishika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Ndani kwa muda - alifanya kazi ya kuunda makundi ya kigaidi ndani ya jeshi la polisi la Irak. “Akiwa amepelekwa kuinua majeshi ya usalama Irak kufikia hali inayostahili, Kerik alijifanya ‘waziri wa muda wa mambo ya ndano wa Irak.” Washauri wa Uingereza walimwita ‘terminator ’ wa Baghdad, kwa mujibu wa jarida la Salon, Desemba 9, 2004.

C h i n i y a u o n g o z i w a Negroponte kwenye Ubalozi wa Marekani mjini Baghdad, wimbi la mauaji yaliyojificha ya raia na kuuawa kwa kulengwa yalikuwa yameanza. Wahandisi, madaktari, wanasayansi na wasomi pia walilengwa.

M w a n d i s h i w a v i t a b u na mchambuzi wa masuala ya kimataifa , Max Fuller ameonyesha kwa undani vitendo vya kinyama vilivyofanywa chini ya mpango wa kupambana na ugaidi ulioendeshwa na Marekani.

Kuzuka kwa makundi ya mauaji kuliarifiwa mara ya kwanza mwezi Mei (mwaka 2005) ....makumi ya miili ilionekana imetupwa ovyo bila kificho ... katika maeneo yasiyokaliwa na watu mjini Baghdad. Waliouawa walikuwa wamefungwa pingu, wakafungwa kitambaa usoni na kupigwa risasi kichwani, na wengi walionyesha dalili za kuwa waliteswa vibaya.

Ushah id i huo u l ikuwa unatosha kwa Chama cha Wanazuoni wa Kiislamu (AMS), ambacho hasa kinaunganisha wanazuoni wa ki-Sunni, kutoa taarifa ambako walitoa tuhuma kuwa majeshi ya usalama chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na Brigedi ya Badr, ambayo mwanzoni ilikuwa tawi la kijeshi la Baraza Kuu la

Ugaidi wenye ‘sura ya kiutu’: Historia ya vikundi vya mauaji Marekani -2

Na Profesa Michel Chossudovsky

Mapinduzi ya Kiislamu nchini Irak (SCIRI), kuwa wanahusika na mauaji hayo. Pia waliituhumu Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kuendesha ugaidi wa dola (kwa mujibu wa Financial Times, gazeti mashuhuri la Uingereza).

M a k o m a n d o o w a polisi pamoja na Brigedi ya Mbwamwitu walikuwa wanasimamiwa na mpango wa kupambana na ugaidi wa Marekani, katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Irak.

Makomandoo wa polisi waliundwa chini ya uangalizi wenye uzoefu na wapiganaji dhidi ya ugaidi wa Marekani, na kuanzia mwanzo walifanya operesheni za pamoja na vikosi maalum na vya siri vya jeshi la Marekani, kwa mujibu wa taarifa za usalama wa taifa la shirika la habari la Reuters.

Mshirika muhimu katika kukua kwa Makomandoo Maalum wa Polisi alikuwa James Steele, mshirika wa zamani wa vikosi maalum vya Jeshi la Marekani ambaye alionja vita huko Vietnam kabla ya kuendelea mbele, kusimamia ujumbe wa kijeshi wa Marekani nchini El Salvador wakati wa kilele cha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.....

Mchangiaji mwingine wa Marekani alikuwa yule yule Steven Casteel ambaye, alikuwa ofisa mwandamizi zaidi mshauri katika Wizara ya Mambo ya Ndani alipuuzia taarifa zenye ushahidi kamili wa uvunjwaji usio na mipaka wa haki za binadamu kama ‘uvumi na vijembe.’ Kama Steele, Casteel alipata uzoefu katika Amerika ya Kusini, kwa upande wake akishiriki katika kumtafuta

maporini mbabe wa madawa ya kulevya Pablo Escobar katika vita dhidi ya madawa nchini Colombia miaka ya 1990......

Alichofanya Casteel huko nyuma ni muhimu kwa sababu aina hii ya kukusanya taarifa za kijasusi na kutayarisha orodha za watu wa kuuawa ni sehemu mahsusi ya kile Marekani inachofanya inaposhi r ik i katika programu za kupambana na ugaidi na kunadhihirisha uwiano wa kile kilichotokea na kuonekana kana kwamba ni mauaji ya mtawanyiko, yanayotokea ghafla tu.

Mauaji haya ya halaiki y a n a y o r a t i b i w a r a s m i yanaendana na kile kinachotokea Irak, Pia yanaendana na kile k inachofahamika kuhusu Makomandoo wa Polisi Maalum, ambayo ilifukwa kuipa Wizara ya Mambo ya Ndani uwezo wa kutumia vikodi maalum vya wapiganaji (kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani). Ili kuendana na nafasi hiyo, makao makuu ya Makomandoo wa Polisi yamekuwa ndiyo kitu cha kamandi maalum ya kitaifa, udhibiti, mawasiliano, kituo cha uendeshaji kumpyuta na ujasusi, kwa usimamizi wa Marekani (kwa mujibu wa Max Fuller, aliyetajwa juu).

Maandalizi ya mwanzo y a l i y o f a n y w a c h i n i y a Negroponte mwaka 2005 yalitekelezwa chini ya mrithi wake, Balozi Zalmay Khalilzad. Robert Stephen Ford alihakikisha uendelezaji wa mradi huo kabla ya kuhamishwa kuwa Balozi wa Marekani nchini Algeria mwaka 2006, na pia aliporudi Baghdad kama naibu balozi, mwaka 2008.

Operesheni ‘Contra wa

Syria’: Kujifunza kutoka uzoefu wa Irak

Uigaji wa kutisha nchini Irak wa ‘mpango wa Salvador’ chini ya Balozi John Negroponte umekuwa ‘mfano wa kuigwa’ wa kuunda Contras wa ‘Jeshi Huru la Syria.’ Robert Stephen Ford bila shaka alihusika na utekelezaji wa mradi wa Contra wa Syria, baada ya kurudishwa Baghdad kama naibu mkuu wa kituo (ubalizi) mwaka 2008.

Nia nchini Syria ilikuwa ni kuunda migawanyiko kati ya makabila-dini ya Walawi, Wasuni, Washia, Wakurdi, Wadruze ba Wakristo. Wakati hali ya Syria ni tofauti kabisa na ile ya Irak, kuna maeneo yanayofanana kabisa kuhusu njia za kufuata ambako mauaji na utisho mwingine vinafanyika.

Taarifa iliyochapishwa na jarida la Ujerumani, Der Spiegel, kuhusu vitendo vya kikatili vilivyofanywa katika mji wa Homs nchini Syria zilithibitisha mpangilio wa kufanya mauaji ya watu wengi kikabila, n a mauaji nje ya mkondo wa sheria yanayofanana na yale yaliyofanywa na makundi ya mauaji yaliyoundwa na Marekani nchini Irak.

Watu wa Homs walikuwa muda wote wana i twa n i ‘wafungwa’ (Washia, Walawi) na ‘wahaini.’ Wanaoitwa ‘wahaini’ ni raia wa Kisuni katika maeneo yanayoshikwa na waasi mijini, ambao wanaonyesha kutokukubaliana au upinzani kwa utawala wa vitisho wa Jeshi Huru la Syria (FSA).

‘Tangu kiangazi kilichopita (2011), tumewakatilia mbali watu karibu 150, ambao ni karibu asilimia 20 ya wafungwa wetu,” anasema Abu Rami (wa FSA)..... Lakini wauaji wa Homs wamekuwa wakihangaikia zadi wahaini katika makundi yao wenyewe na siyo wafungwa wa kivita. “Kama tunamkamata Msuni akifanya ujasusi, au kama raia anayahaini mapinduzi, tunafanya chap chap,” anasema mpiganaji huyo. Kwa mujibu wa Abu Rami, brigedi ya kuzika ya Hussein imewaua wahaini kati ya 200 na 250 tangu kuanza kwa uasi, kwa mujibu wa Der Spiegel, Machi 30, 2012.

Mradi huo ulihitaji mkakati m a a l u m w a k u s a j i l i n a kuwafunza askari wa kukodiwa. Vikundi vya mauaji ikiwa ni pamoja na wafuasi wa Salafi wa Lebanon na Jordan viliingia Syria kwa mpaka wake wa kusini, na Jordan katikati ya mwezi Machi 211. Sehemu ya kazi ya msingi (kufikia hapo) ilikuwa imeshafanyika kabla ya Robert Stephen Ford kuwasili Damascus mwezi Januari 2011.

Balozi Ford akiwa Homs mwanzo wa Julai 2011

Kuteuliwa kwa Ford kama

Balozi wa Marekani nchini Syria kulitangazwa mapema 2010. Mahusiano ya kibalozi yalikuwa yamevunjwa mwaka 2005 baada ya kuuawa kwa (aliyekuwa Waziri Mkuu wa Lebanon) Rafik Hariri, ambako Washington iliilaumu Syria kwa mauaji hayo/ Ford aliwasili nchini Syria takriban miezi miwili kabla ya kuanza kwa uasi.

Jeshi Huru la Syria (FSA)Washington na washirika

wake walirudia nchini Syria vielelezo vikuu vya ‘Mkakati wa Salvador nchini Irak,’ na kufikia kuundwa kwa Jeshi Huru la Syria (FSA) na vikundi vyake tofauti vya uasi ikiwa ni pamoja na kikundi mwanachama wa Al Qaeda cha brigedi za Al Nusra.

Wa k a t i k u u n d w a k w a Jeshi Huru la Syria (FSA) kuliotangazwa Juni 2011, kusajili na kutoa mafunzo kwa askari wa kukodiwa kutoka nje kulianzishwa kitambo kabla. Katika maeneo mengi, Jeshi Huru la Syria ni vungavunga tu. Linainuliwa na vyombo vya habari vya Magharibi kama chombo ha l i s i cha kijeshi kilichoundwa kutokana na askari wengi kuyakimbia majeshi ya serikali. Idadi halisi ya waliokimbia jeshi la serikali haikuwa muhimu au ya kutosha kuunda mfumo halisi wa jeshi, wenye mamlaka za utawala na udhibiti.

FSA siyo jeshi halisi la watu wa fani hiyo, ila ni mkusanyiko au mtandao wa brigedi tofauti za ugaidi, ambao wanaunganisha pamoja vikundi vya kijeshi vinavyojitegemea, vikifanya opereseni sehemu tofauti za nchi.

Kila moja kati ya vikundi hivi vya kigaidi inafanya kazi kivyake. FSA haina mfumo mmoja wa kutoa amri na kudhibiti kinachotokea, na kuwasiliana na vikundi tofauti vya kijeshi. Vikundi hivi vinaelekezwa na vikosi maalum na mawakala wa usalama wa Marekani na NATO ambao wamepachikwa katika mifumo ya vikundi kadhaa husika.

Vikosi hivi maalum (vyenye mafunzo ya hali ya juu) katika mapigano (wengi wao ni waajiriwa wamakampuni binafsi ya ulinzi) wanawasiliana kila mara na vituo vya upelelezi wa kijeshi vya Marekani na washirika wake wa NATO, pamoja na Uturuki. Vinaelekezwa na vikosi maalum (vikiwemo SAS ya Uingereza na askari wa miavuli wa Ufaransa) na makampuni binafsi ya ulinzi na usalama yenye mikataba na NATO na makao makuu ya Jeshi la Marekani (Pentagon). Kwa hili, taarifa zinathibitisha kukamatwa na serikali ya Syria kwa waajiriwa 200 hadi 300 wa makampuni binafsi ya ulinzi ambao walikuwa katika vikundi vya uasi.

(itaendelea)

Page 11: ANNUUR 1055.pdf

11 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013Makala/Tangazo

Kuna ki jana mmoja aliwahi kuishi katika nchi hii, na huyu kijana alikuwa anaitwa Edward Moringe Sokoine. Kijana huyu alikuwa anatoka kabila la Wamasai. Sokoine aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hii na alipokuwa Waziri Mkuu alikuwa mtu wa kwanza kumrekebisha Nyerere hadharani kwa kusema “Tusiseme Zidumu Fikira za Mwenyekinti wa CCM, Bali Tuseme Zidumu Fikira Njema za Mwenyekiti wa CCM”; Ujasiri huu ulikuwa siyo wa kawaida, ilikuwa si rahisi kwa mtu yeyote kumkosoa Nyerere, Nyerere alikuwa hakosolewi, harekebishwi na wala hashauriki, alikuwa Mungu Mtu! Sokoine alipokuwa Waziri Mkuu alianzisha kampeni ya kupambana na “Wahujumu Uchumi” kwa wakati huo au kwa sasa tunawaita “ M a f i s a d i ” , S o k o i n e aliwahi kuwapa baadhi ya vigogo wa serikali siku saba warudishe pesa za wananchi shilling million sitini (Tsh. 60,000,000) za wakati huo ambapo dollar moja ya Kimarekani ilikuwa Shillingi 20. Vigogo hao walidaiwa kumuuzia Lord Rajipar Meli ya serikali na pesa hazikuonekana. Basi Sokoine katika kampeni zake za kupambana na Ufisadi akawapa siku saba kwa kuwaambia k u w a a n a w a p a S i k u Saba warudishe Pesa za Wananchi, la wakishindwa atawapeleka Radio Tanzania wakawaambie Watanzania kwa Njia ya Radio Pesa Zao wamezipeleka Wapi?; Mimi Naenda Dodoma Kuhutubia Bunge, Nikirudi Nipate Majibu”.

Kwa baha t i mbaya kabla ya siku saba kutimia Sokoine alifariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea huko Dakawa – Morogoro a k i t o k e a B u n g e n i Dodoma.

Watanzania wenzangu k a m a m m e y a s a h a u haya naomba mtafute kumbukumbu kwenye maktaba za Radio Tanzania na Magazeti ya Tanzania w a k a t i h u o ( U h u r u ,

Je, Nyerere ni kikwazo cha katiba ya umma?-3Na Dr. Noordin Jella

MWALIMU Julius Kambarage Nyerere

Mzalendo, Daily News & Sunday News); nakumbuka yali tangazwa kwenye taarifa ya habari wakati huo na kwenye magazeti yote yaliandika.

Sokoine alipofariki ndipo harakati za kupambana na Ufisadi za kweli zilipoishia hapo na kuzikwa rasmi nje kidogo ya mji wa Morogoro kando ya njia ya kwenda Dodoma, na baada ya hapo yakaendelea maneno yale yale ya majukwaani tu ya kulaani na kukemea rushwa na ufisadi bila ya vitendo!

Je , wa le wakubwa wenzangu wa l ioku la chumvi nyingi kama mimi, haya wanayakumbuka, au yakitokea haya walikuwepo Ughaibuni!? Ina maana Nyerere alikuwa hajui kwamba Kawawa ameuza meli ya Wananchi kwa Shillingi million sitini? Wakati nchi ilikuwa na meli moja tu! Sasa wale wanaosema angekuwepo Nyerere haya yanayotokea yasingetokea, naomba waseme au wajibu hoja hii.

Leo hii tunashangaa u f i s a d i w a k a w a i d a unaofanywa na baadhi ya mawaziri na viongozi wa umma. Sokoine alipofariki ufisadi huo wa kutisha

ukaisha kimya kimya hakuna aliyejitokeza kuhoji swala hilo tena!

Ndugu zangu Watanzania kabla hatujafikiri kesho k u t a k u w a j e , l a z i m a tukumbuke jana kulikuwa vipi. Huwezi kufanya utabiri wa hali ya uchumi (economical prognosis) wa mwaka kesho kama huna takwimu za mwaka jana. Ukitaka kufanya utafiti wa jambo lolote lile, ni lazima kwanza uelewe kitu kinachoitwa “Chanzo cha Tatizo” au kwa jina la Kiingereza “Background of Problem”. Bila kujua chanzo cha tatizo la Ufisadi la nchi hii, hata tufanye nini au hata tumpate nani, au kitawale chama gani, ha tu taweza kumal iza ufisadi.

Rais Mwinyi aliukuta ufisadi, akauacha na Rais Mkapa naye akaukuta na kuendeleza yale waliofanya watangulizi wake kwa vile Katiba ni ile ile na watu ni wale wale. Rais Kikwete naye hawezi kumaliza Ufisadi hata tungelala barabarani mwaka mzima, h a w e z i k u b a d i l i s h a chochote kwa vile yeye ni mzungumzaji tu lakini System anayoisimamia ni System ile ile ya Nyerere na chama chake kile kile

cha CCM. Enzi za Nyerere pamoja na Tanzania kuwa na wasomi wengi waliokuwa wamefika vyuo vikuu, lakini katika uchaguzi mkuu wa Urais, Nyerere alikuwa anagombea na “Kivuli” yaani kwamba hakuna mtu mwingine mwenye sifa za kugombea nafasi ya Urais na yeye, na chini ya picha yake kulikuwa na neno “Ndiyo” na chini ya kivuli kulikuwa na neno “Hapana”. Hivyo ukichagua neno ndiyo Umemchagua Nyerere, na ukichagua neno hapana pia Umemchagua Nyerere! Huyo nd iye Nyerere n i l iyekuwa ninamjua mimi.

Jambo la kushangaza ni kwamba katika nafasi za Ubunge walikuwepo w a g o m b e a w a w i l i wawili wakiwakilishwa na alama ya “Jembe na Nyumba”. Nakumbuka Nyerere watu walikuwa wanamtania wanamwita “ H a a m b i l i k i ” y a a n i Nyerere ni mtu aliyekuwa hapendi ushauri wa mtu yeyote yule. Wanaomjua Nyerere vizuri wanasema huwezi kumkalisha chini umshauri, hatakusikiliza, ukitaka atumie ushauri

wako unatakiwa aidha uandike uache wazi aje asome bila wewe kuwepo, au uwepo chumba cha pili uongee kwa nguvu asikie lakini usijue kama anakusikiliza.

Nyerere aliwahi kwenda Marekani kuomba msaada wa chakula wakati wa Rais Ronald Reagan, Rais huyo wa Marekani alimshangaa kwa nini apate shida ya kuomba chakula wakati Tanzania ni nchi yenye rutuba na mito mingi. Nyerere alidai hana wataalam wazuri wa Uchumi. Reagan alimshauri kwamba ampe wakulima watano (5) wa Kimarekani waje walime chakula cha kuwatosha Watanzania wote na kingine wauze nchi za nje. Nyerere alikataa akasema yeye ni Mjamaa hataki Mabepari.

( M a k a l a h i i imeandikwa na Dr. Noordin Jella (Ph.D. in Economics)

Former Lecturer of Mzumbe, Open & KIU – Dar, Univers i t ies . Currently: Freelance Journalist & Seasonal Political AnalystEmail: norjel [email protected] Mobile:

+255 782 000 131)

Inapenda kutoa shukran zake za Dhati kwa mahujaji wote waliosafiri na Ahlul-daawa.

Pia inatangaza kua imeandaa safari ya Umra Mfungo wa Saba ni sawa na machi 11 2013 kwa Gharama ya Dola 1450 tu.

Inaendelea kuandikisha mahujaji kwa Mwaka 2013. Wale watakao jiandikisha na kufanya malipo mapema watapata punguzo maalumu la bei.

Usisahau Ahlu Daawa Hajj kwa Bei nafuu na huduma bora.

Kwa mawsiliano piga simu zifuatazo.

Dar es salaam: 0773 724444, 0715 786101 na kwa Zanzibar 0777 417736, 0777484982.

AHLU-DAAWA HAJJ

Page 12: ANNUUR 1055.pdf

12 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013Barua/Shairi

R I WAYA y a S h a m b a la wanyama (1945), ni moja kati ya kazi nzuri kabisa za kibunifu katika Tasnia ya fasihi andishi hapa duniani. Riwaya hii ambayo iliandikwa na Muingereza ambaye ni maarufu kwa jina la George Orwell, ni mtiririko wa sitiari (allegory) unaoakisi dhana nzima ya ujamaa wa kidemoskrasia katika tawala mbali mbali za kidunia.

Kazi hii yenye ubora, ladha na mvuto usiochosha, inahusu kisa cha dola la wanyama. Wanyama ambao kwa pamoja walikubaliana kuungana na kuishi kwa misingi ya usawa na haki. Moja kati ya kanuni hizo za usawa, ilikubaliwa kwamba hakuna mnyama mmoja a t a k e m d h u r u m n y a m a mwengine ama kwa kumla, kumpiga, kumdhulumu na hata kumuuwa. Kanuni hii ilipita na ikaandikiwa kauli mbiu (slogan) isemayo ‘Wanyama wote ni sawa’!

Kwa muda baada ya kanuni hii kupitishwa na kukubaliwa na wanyama wote, wanyama wadogo wadogo na wale waliokuwa waathirika wa vitimbi, viteweji na mateso ya wanyama wakubwa, walihisi kupata faraja kubwa kwa kuhakikishiwa usalama wao. Imani yao hii ilichangiwa na kuona kauli ile mbiu ikiimbwa na kuandikwa kila kona ya dola lao lile kiasi ya kumfanya kila mnyama

NANUSA HARUFU YA ‘GEORGE ORWELL’ MCHAKATO WA KATIBA

Written by Stonetown (Kiongozi) // 19/01/2013 // Makala/Tahariri // 5

Comments

aamini kile anachokiona katika kauli mbiu ile.

Wa s w a h i l i h u s e m a ‘Taa haachi mwiba wake’. Haikutimia wiki, kuna baadhi ya wanyama hasa ndege, walianza kuona dalili mbaya katika jamii yao. Moja ya dalili hio ni kupotea kwa baadhi ya wanyama katika mazingira ya kutatanisha. Kwa lugha nyepesi, kuna baadhi ya wanyama walianza kuwala wengine kimya kimya kila siku.

Wa n y a m a w a d o g o walipogundua usaliti huu walirudi kwa mkubwa wao kushitaki na kusimulia masikitiko yao juu ya kitendo hiki cha uvunjifu wa amani, na usalama wa wanyama katika dola yao. Kwa bahati mbaya walipofika mahala pa mashtaka na kueleza makosa yao, waliona ile kauli mbiu imebadilishwa kidogo kutoka ilivyokuwa mwanzo.

Awali kauli ilisomeka ‘Wanyama wote ni sawa’, lak in i sasa inasomeka ‘Wanyama wote ni sawa, lakini baaadhi ya wanyama, ni sawa zaidi kuliko wengine’! Kisa hichi kikaishia hapo. Kumalizika kwa kisa hiki ndipo tunapopata nadharia hiyo niliyoitumia katika kichwa cha makala hii hapo juu, ambayo ni moja ya nadharia maarufu duniani kwa sasa. Yaani nadharia ya ‘Ki-Orwelli’.

N i m e w a j i b i k i w a n a kuandika kwa kusema kuwa kwa namna mchakato mzima wa maoni ya katiba unavyokwenda, nanusa harufu ile ile waliyoinusa wanyama wadogo kama mimi katika ‘Shamba la

wanyama’ . Haru fu ya kwamba kuna baadhi ya wanyama ni sawa kuliko wengine. Na hii si tuhuma kutoka katika ombwe la uwazi, bali ina kila aina ya ithibati na visherehesho vya kuutilia shaka mapema mchakato huu wa katiba nchini.

Nilitegemea iwapo maoni ya katiba yalilenga kukusanya maoni ya wananchi, kwa haki na usawa, na ili yanipe imani kuwa haki itatendeka, basi yalikuwa yafanywe kwa wanachi wote bila kuweka tabaka (strata/ social classes). Hii ni kutokana na ukweli kwamba katika mchakato wa katiba, wananchi wote, wake kwa waume, wakubwa kwa wadogo, viongozi na waongozwa, mashehe na mapadiri, wanasiasa na majeshi, wote kwa pamoja ni wananchi walio sawa. Na mchakato wa katiba ulikuwa uanze na kauli mbiu hiyo ya ‘ Wananchi wote ni sawa mbele ya haki na sheria’!

Kuwe na usawa kwamba, maoni ya katiba yafanyike kama vile tunavyofanya uchaguzi. Yapitie kimajimbo au maeneo ya ukazi wa wananchi . Sasa maoni yakifika j imbo ambalo kiongozi mkuu wa nchi au mstaafu anapoishi, basi hio ndio iwe zamu yake ya kwenda kutoa maoni hapo kwao. Kwa mfano, ikiwa Rais wa Zanzibar anaishi Mbweni, basi maoni yakifika jimbo la eneo hilo, iwe ndio zamu yake ya kutoa maoni na wananchi sawia, ijapokuwa atapewa nafasi ya kwanza kufanya hivyo,

Moyoni ‘na dukuduku, na wa ‘dili’ si wa dini,Wendao huko na huku, na vilembavyo vichwani,‘Kipyora kizumbukuku, dhidi ya WANAZUONI,Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ? Nahitaji mbayana, anieleze kiini,Cha wao kuwatukana, MAULAMAA wa DINI,Walounena BAYANA, UKWELI wa QUR-ANI,Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ? Wakajitoa MUHANGA, na kutupwa GEREZANI,Si kwa kusaka ‘FARANGA, bali RADHI za MANANI,MASHEIKH wa kubananga, LENGOLO hasa ni nini,Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ? Wamponda ALBANNA, MWANAZUONI makini,Harakatize mwanana, asozifahamu nani,Watueleze bayana, walofanya wao nini,Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ? Kadhalika MAUDUDI, ‘WAMRADDI’ hadharani,Mithili ya ‘MURTADI, hali ni MWENZA safuni,Kubwa kwao ni ‘KURADDI’, WENZA wao WAUMINI,Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ? Waaidha na QUTUBI, MUHANGA wa GEREZANI,Kwa ya DINI yake HUBBI, akanyongwa KITANZINI, Kwazo zao TAASUBI, WAMKUFURISHA DINI’Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ?

Wawaita MAJAHILI, eti WASOJUA DINI,Si NAHARIi si LAILI, tena KADAMNASINI,Kama hawa MAJAHILI, WAO tuwaite NANI,Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ? ‘TAF-HIMU QUR-ANI’, ni TAFSIRI ya NANI,‘FI-DHWILALI QUR-ANI, MFASIRI wake NANI,Kama si WAO ni NANI,’ WAPONDAJI’ NIJUZENI,Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAKENGEUSHI ?

ABUU NYAMKOMOGIMWANZA.

MASHEIKH AU WAPOTOSHAJI ?

Inaendelea Uk. 14

1118 sqm - 4 Milion, 1261 sqm 5 milion, 1348 sqm 5.5 milion, 674 sqm 3 milion, 848 sqm - 3.4 milion, 510sqm - 1.5 milion, 516sqm - 2 milion, 522sqm - 2 milion, 523sqm - 2 milion, 646sqm - 2.6 milion, 656sqm - 2.6 milion, 474sqm 1.8 milion, 456 sqm 1.8 milion, 538 sqm 1.8 milion, 469sqm 1.9 milion, 406 sqm 1.6 milion, 356sqm 1.5 milion, 399sqm 1.6 milion, 359sqm 1.5 milion, 612sqm 3 milion.

Vipo Barabara ya Kongowe-SogaKilomita moja toka barabara ya

Morogoro.

Simu No.0755 090 754/0715 090 754.

Viwanja vilivyopimwa vinauzwaKongowe Kibaha

Page 13: ANNUUR 1055.pdf

13 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013Makala

Alhamdulillahi Wahdahu Lasharikalahu, waswalatu wasalamu ala Nabiyina Muhamad (S.A.W), amma baadau

M h e s h i m i w a M u f t i , mtoto wa jongoo alipotaka kutembea alimuuliza mama yake aende vipi? Atangulize mguu upi mwanzo, lakini jibu alilolipata kwa mama yake ni kumwambia “nenda mwanangu nenda”.

Mheshimiwa Mufti na Waheshimiwa wazee wetu na masheikh wetu, na mimi nimewekwa katika mtihani huo huo. Sioni haja ya kutoa hotuba ya uzinduzi wa Baraza la Ulamaa mbele ya visima vya elimu ya dini yetu. Chochote nitachokisema basi si zaidi ya tone moja la chumvi ndani ya bahari ya elimu yetu ya dini. Naomba kwa Uradhi wenu mniruhusu niseme machache ambayo yatakuwa na kasoro nyingi mbele ya wazee mliobobea katika misingi ya dini. Nawaombeni radhi sana kwa hayo.

HISTORIA YA ZANZIBAR NA UISLAM

Mapema tu , mnamo karne za nyuma watu wa kale kama vile Sumerians, Assyrians, Hindus, Egyptians na Waarabu wa Kusini walitembelea mwambao wa Afrika ya Mashariki ambapo wal ikutana na makabila ya kienyeji kama vile Wahadimu, Wapemba na Watumbatu. Waarabu hawa, hasa kutoka Ghuba ya Uajemi (Persion Gulf) ndio walioanza kuuleta Uislamu na Wazanzibari wakaikubali kwa dhati dini hii.

Wanah i s to r i a weng i wanaamini kuwa Uislamu umeingia mapema kabisa katika mwambao wa Afrika ya Masha r ik i . Waka t i mwanahistoria maarufu wa Moroko Ibun Battuta alipotembelea eneo hili alikuta wakazi wake ni Waislamu na Kiarabu ndio lugha ya fasihi kwa biashara.

Mnamo mwaka 1503 Zanz iba r i l i ka l iwa na Wareno lakini katika karne ya 17 kulikuwa na ghasia k a t i k a m w a m b a o h u u ikiwemo Pemba. Mwaka 1652 Waarabu waliivamia Zanzibar na wal i i t eka Mombasa, Pemba na Kilwa mnamo mwaka 1698 na

Aliyosema Waziri wa Katiba na SheriaMheshimiwa Abubakar Khamis Bakary

1699. Visiwa vyote vikawa chini ya Imam wa Muscat Seyyid Said bin Sultan, Mwanzilishi wa Zanzibar na zao la karafuu. Yeye ndie aliyekuwa kiongozi. Mnamo mwaka 1804 akauhamisha mji mkuu wa Oman kutoka Muscat kuja Zanzibar na katika mwaka 1832, Zanzibar sasa ilijulikana kisiasa, kibiashara na kidini. Mbali na mabadiliko ya kiutawala kuanzia mwaka 1861, 1869 na 1872 lakini ilipofika mwaka 1891 Zanzibar ilikuwa na utaratibu wake kamili wa Serikali na Sir Lioyd Mathews ndiye aliyekuwa Waziri wa Kwanza (First Minister) na mweka hazina (Treasurer).

Muhimu hapa ni kuona kwamba Zanzibar imekuwa na Dini ya Kiislamu kwa karne nyingi sana na sasa kila mtu anajua kwamba Uislamu Zanzibar si dini tu peke yake, lakini imechimba zaidi hata katika “culture”, tabia, silka na hulka zetu. Waislamu hapa Zanzibar ni zaidi ya asilimia 98% na tumeungana zaidi kwa lugha yetu moja na kuwa sote ni wamoja. Wajibu wetu wa kwanza wa Baraza hili ni kuunganisha umoja wetu huu kwa misingi nilioielezea hapo juu.

SHERIA YA MUFTISheria ya Mufti , Na.

9/2001 inaanzisha Afisi ya Mufti pamoja na maafisa wengine wa Afisi hiyo. Kazi za Mufti zimeelezwa vyema katika kifungu cha 9(1) ikiwa ni pamoja na kutoa “fat-wa” ambapo katika kutekeleza kazi hii anaweza akashauriana na Ulamaa wa Zanzibar. Kifungu cha 15(1) cha sheria hiyo kimempa uwezo Waziri muhusika kufanya kanuni. Chini ya uwezo huo kwa tangazo maalum la Serikali Na. 52/2011 kumeanzishwa Kanuni za Baraza la Ulamaa ambapo chini ya kanuni ya 3 itakuwa ni chombo cha ushauri na kitajulikana kama ni Baraza la Ulamaa. Baraza hilo litaongozwa na Mufti atayekuwa Mwenyekiti na Wajumbe wafuatao:-

i. Sheikh mmoja kwa kila Wilaya atayeteuliwa na Waziri kwa kushauriana na Mufti.

ii. Masheikh wanne (4) kutokana na ujuzi wao pia watateuliwa na Waziri baada ya kupata mapendekezo ya

majina yasiyopungua sita (6) kutoka kwa Mufti.

iii. Naibu Mufti, Kadhi Mkuu, Naibu Kadhi Mkuu, Katibu Mtendaji Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana na Mwalim Mkuu Chuo cha Kiislam ambao wao wanaingia kutokana na wadhifa wao.

Makatibu wa vikao hivi watakuwa Katibu wa Mufti na Msaidizi wa Katibu wa Mufti. Baraza hili kwa mujibu wa kanuni ya 5 linatakiwa likutane angalau mara mbili kwa mwaka na wanaweza kufanya kikao cha dharura pale inapohitajika. Mufti chini ya kanuni ya 5(2) anaweza kuunda kamati maalum itayoshughulikia tatizo lililojitokeza ila ni lazima atilie maanani suala zima la uwakilishi katika kamati hiyo, na kwamba maamuzi ya kamati hiyo yanaweza kukuba l iwa , kutenguliwa au kufanyiwa marekebisho fulani katika kikao cha Baraza zima la Maulamaa.

KAZI ZENUWazee wetu, Masheikh

na Maulamaa wetu, wajibu wenu na kazi zenu zipo chini ya kanuni ya 7 ya Kanuni za Baraza la Ulamaa ambayo inasema:

“Kaz i ya Ba raza n i kumshauri Mufti juu ya masuala ya

Kiislam yaliyowasilishwa

kwake kwa kutolewa fat-wa na kufanya kazi nyengine litakazopewa na Mufti”.

Kazi zenu ni ngumu na zinahitaji uadilifu mkubwa, kujitolea, haki na ukweli. Ndio maana Imamu Ibnu Qaym amewaita wanachuoni kuwa ni watia saini (signatory) kwa niaba ya Mwenyezi Mungu. Sina wasi wasi hata chembe wa mambo haya juu yetu. Naamini na sote tunakubali kuwa Baraza limepata wajumbe wenye elimu, busara na hekma, waadilifu na wakweli; na hivyo basi msingi mkubwa wa mafanikio wa kazi zenu na wajibu wenu tunao. Haya sote tunayaelewa pale Mwenyezi Mungu alipotutanabahisha katika Suratul Al-Ahzab kwa kutukumbusha kuwa tutawakal kwa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa mlinzi na kuwa sote tulioamini tumuogopeni Mwenyezi Mungu na tuseme maneno ya kweli.

Tunapoyafanya hayo kwa uadilifu, ukweli na haki kama ilivyo kawaida yenu, na tukavuta subra katika mitihani ambayo tutaipata wakati wa kutekeleza majukumu haya; basi Mwenyezi Mungu atazidi kuwa nasi. Mwenyezi Mungu mwenyewe anatukumbusha katika Qur-ani yake, katika Suratul Asr kuwa Binaadamu yuko katika hasara isipokuwa

wale walioamini na wakafanya vitendo vizuri na wakausiana kufuata haki na wakausiana kushikamana na subira (yaani) kustahamiliana. Jukumu hili nalo ni kubwa na ni zito lakini ndio wajibu wetu, na ni lazima kulifanya. Tukilifanya kwa misingi tuliyoielezea hapo juu basi nasi tutakuwa katika kundi la wataokuwa na kheri, Inshaalla Mwenyezi Mungu atujaalie kila la kheri, na kulitekeleza jukumu hilo zito kwa njia ile anayoipenda Mwenyezi Mungu. Ammin.

MABADILIKO YA TABIA YA BAADHI YA WAUMINI

M h e s h i m i w a M u f t i , Waheshimiwa Maulamaa v i s i w a v y e t u h i v i vimekumbwa na wimbi kubwa la mabadiliko ya baadhi ya waumin. Ni ukweli usiopingika kuwa wakati wetu umekuwa na wasemaji wengi sana wanaozungumzia mambo ya kiislamu tokea mambo ya USULI hadi ya FURUU mambo haya yote yanahitaji elimu ya kina na hekimu kubwa hali ya kuwa wao sio Ahli wa ilmu. Bahati mbaya kila msemaji hupata wasikilizaji, mashabiki na hata waenezaji na wenye kuyanusuru maneno hayo. Hali hii imeleta mtafaruki mkubwa baina yetu, ikazaa migongano na hat imae makundi yenye kupingana ambayo yameidhoofisha dini na jamii yetu. Ni kweli Uislamu haukuweka tabaka la watu wadini na wasio wa dini, lakini pia haukuwacha mambo shaghala baghala. Mtume Muhammad (S.A.W) amesema “wanachuoni ndio warithi wa Mitume”. Tunajua kuwa umoja wetu wa Kiislam na mshikamano wetu wa sasa unaaza kumong’onyoka.

Kwa maana hiyo tujitahidini kufuata na kuhimizana maagizo ya Qur-ani:-

“Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi

Mungu nyote kwa pamoja na wala musifarikiane”

H a t a k a t i k a h a d i t h i tunatanabahishwa kwamba

“ H a k i k a m f a n o w a Waislamu katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kurehemeana kwao ni sawa sawa na kiwiliwili kimoja’’

Ni wajibu wenu mlio hapa, kuyajadili mambo kama haya

Inaendelea Uk. 14

MUFT wa Zanzibar

Page 14: ANNUUR 1055.pdf

14 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013Makala

Aliyosema Waziri wa Katiba na SheriaInatoka Uk. 13na mengine zaidi ya haya ili mumshauri Mufti ipasavyo. Kamba hii ya Mwenyezi Mungu ambayo sasa waislam wanaanza kuihujumu inahitaji kulindwa isikatwe katwe. Nyinyi Baraza la Ulamaa ndio walinzi wetu. Roho zetu, macho, nafsi tamaa na kiu ya waislam wema zinawatazama nyinyi. Naamini kwa uwezo w a M w e n y e z i M u n g u mtafanikiwa kuielezea dini yetu kwa njia ya fat-wa na njia nyingi nyenginezo kwa kuielemisha jamii, kwa maslahi yetu na kizazi chetu na dini yetu.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kuwa kuna vyuo (maahad) vingi vinavyotoa elimu bora na vyuo hivyo vina walimu wazuri Unguja na Pemba. Hata hivyo kwa kukosekana umoja wa vyuo hivyo imekuwa tabu kwa mwanafunzi anaemaliza thanawi kujiunga na vyuo vikuu vyetu pamoja na kuwa vyuo vya nje wanakubaliwa. N a t u m a i m t a m s h a u r i Mufti ili tuone namna gani tutaunganisha maahad zetu na kuwawezesha wanafunzi wake kunufaika na vyuo vikuu vyetu katika fani zao. Sadaka hazianzi nje bali kuanzia nyumbani.

UHURU WA DINI /KUABUDU NA HAKI ZA MTU

Bila shaka Uislamu ni dini iliyotoa uhuru mkubwa kwa mwanaadamu kiasi cha Allah kukataza watu kulazimishwa kufuata dini. Uhuru ndio unaomtofautisha mwanadamu na malaika. Hata h ivyo uhuru huo umeambatana na majukumu kwani hakuna uhuru usio na mipaka . Kikawaida Uislamu unaangalia zaidi dhima (majukumu kuliko uhuru). Amesema Mtukufu, Subhanahu Wataala kuwa (na naapa) kwa nafsi na kwa aliyeitengeneza. Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake. Bila shaka a m e f a u l u a l i y e i t a k a s a (nafsi yake) na bila shaka amehas i r ika a l iye iv iza (Suratu Ash-Shams aya 7-10). Ili kujenga utawala wa sheria, haki na kulinda amani na utulivu nchi yetu inaamini dhana ya uhuru na haki za binadaamu. Kwa tafsiri iliyo rahisi ni kweli kifungu cha 18(1) na (2) cha Katiba kinachotowa uhuru wa maoni, kifungu cha 19(1), (2) na (3) kuhusu uhuru wa mtu kuamini dini atakayo na kifungu cha 20(1) kuhusu

uhuru wa kuj ikusanya, vinaruhusu watu au waumini kufanya wanayotaka kwa kisingizio cha Katiba yetu ya Zanzibar.

Ni kweli vifungu vyote hivyo vinatoa uhuru wa muumini yeyote kufanya kile anachohisi ndani ya maoni yake. Lakini muumin huyo huyo anatakiwa asisome baadhi ya vifungu tu kwa maslahi yake, lakini avisome vifungu vyote vinavyohusiana na maudhui inayohusika. Sasa, kwa maana hiyo ukisoma vifungu vya Katiba vya 18, 19 na 20 ni lazima usome kwa pamoja na kifungu cha 23(1), (2), (3) na (4) pamoja na kifungu cha 24(1) kama vinavyojielezea hapo chini:

“23(1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na Sheria za Zanzibar, kuchukua hatua za kisheria k a m a z i l i v y o w e k w a , kuhakikisha hifadhi ya Katiba na Sheria za nchi.

(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Zanzibar, mali ya nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuheshimu mali ya mtu mwengine.

(3) Watu wote watatakiwa na sheria kulinda vizuri mali ya Zanzibar na kwa pamoja kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu na kuendesha uchumi wa Zanzibar kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadae ya Taifa lao.

(4 ) Ki la Mzanz ibar i ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi, kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa Zanzibar……….”

“24(1) Haki na Uhuru wa binadamu ambayo misingi yake imeorodheshwa na Katiba hii haitatumiwa na mtu mmoja kwa namna ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma na inaweza kubanwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi iwapo tu kibano hicho ni lazima na kinakubalika katika mfumo wa kidemokrasia……..”

Masheikh wetu, misingi hii ya Katiba naamini itawasaidia sana katika kazi zenu ambapo baadhi ya waumini hutumia v i b a y a u h u r u w a o n a kusababisha fujo, kuingilia mali ya umma na kadhalika. Hivi sivyo na ni wajibu wetu sote na zaidi Baraza lenu tukufu kuwaelimisha sana waumini wa aina hii misingi mizuri ya dini, silka, tabia na khulka zetu za kiislam ambazo siku zote zinataka

na zinasisitiza umoja, udugu na amani. Na sisi tunatakiwa kwanza tuitakie amani nchi yetu ya Zanzibar kama fundisho tulilopewa na baba yetu Ibrahim (AS) kwanza alipoiombea nchi yake amani na baadae akaiombea iwe na riziki na baraka. Kazi kubwa tunayo na hiyo ni changamoto kwenu, na ndilo jukumu lenu na wajibu wenu mwengine. Inshaalla Mwenyezi Mungu atawasaidia. Ammin.

MWISHONinafahamu kuwa Baraza

hili la Ulamaa lililopo mbele yangu ni la pili. Baraza lililopita ambalo lilikuwa chini ya Mufti aliyepita Almarhum Sheikh Harith Bin Khelef bin Khamis, Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi amin – limemaliza muda wake. Napenda kuchukuwa fursa hii kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kwa niaba yangu binafsi kuwashukuru sana sana wajumbe wa Baraza hilo na kuwatakia kila la kheri

katika maisha yao. Napenda pia niwaombee malazi mema peponi wale wajumbe wetu wengine waliotangulia mbele ya haki wakiwemo Sheikh Mussa Makungu, Sheikh Ali Khatib Mranzi, Sheikh Abdulrazak Othman Juma, Sheikh Ali Mwinyi Kombo (Wilaya ya Kati) na Sheikh Suleiman Haji (Wilaya ya Mjini) na Sheikh Simai Daima ambao juhudi zao wakati wa uhai wao na hususan walipokuwa wakilitumikia Baraza lililopita zilionekana vizuri sana.

Pia nawashukruru sana Mwanasheria Mkuu wa Ser ikal i , Kamishna wa Polisi na Mkuu wa Usalama ambao na wao kwa nafasi zao walikuwa ni wajumbe wa kualikwa kutokana na hali ya mivutano mingi ya kidini iliyokuwepo wakati huo. Wazee wetu kwa uelewa wao wanatuambia:

“Paukwa Pakawa’yaani penye kuondokwa

hukaliwa. Ninafuraha kusema Baraza la Ulamaa la kwanza limemaliza muda wake na

limeshaondoka ingawa bado wamo wajumbe amabo wanaendelea baadhi yao wakiwa wameingia njiani na wengine wameingia mwanzo. N a t u m a i u z o e f u w a o utawasaidia sana wajumbe wapya . Nyinyi ml iopo hapa sasa mnajaza pengo lililowachwa wazi na wao. Sina wasi wasi hata chembe kwamba pengo hilo limejazwa vizuri na halina mwanya, ninawaombeni muendeleze zaidi kazi hizi za Baraza ili Zanzibar irejee kama enzi za zamani kwa kutambulika kuwa ndio chimbuko la dini yetu kwa Afrika ya Mashariki, Kati na Kusini. Nawakumbusha hadithi isemayo “Nyote ni wachunga na nyote mtaulizwa kuhusu ki le mnachokichunga”. Inshaalla, Mwenyezi Mungu a tuwaf ik i sh i e , na tuwe wachunga wema. Ammin.

(Hii ni hotuba ya Waziri wa Katiba na Sheria wakati wa uzindizi wa Baraza la Pili la Maulamaa tarehe 19. 01. 2013 katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi.)

Nanusa harufu ya ‘George Orwell’ mchakato wa katiba

Inatoka Uk. 12lakini utaratibu uwe hivyo.

Na nilitegemea iwe hivi kwa watu wote nchi nzima. Wa Bagamoyo akatowe maoni kwao, alie Dar es Salaam atatoa maoni hapo jimboni kwake, alie kambini kwa jeshi bila shaka kambi hio haiko angani, aende jimbo ilipo kambi hio akatoe maoni. Na kwa mpangilio kama huu angalau tungeweza kuamini kwamba mchakato wa katiba una sura ya usawa na hivyo haki haichezi mbali.

L a k i n i n i j a m b o l a kushangaza sana kuona tume ya Katiba inapitia majumbani mwa viongozi na wastaafu, wizara, idara, na mashirika ya Serikali, na halafu pengine hata taasisi za kidini, ili kukusanya maoni. Utaratibu huu unaleta matabaka kwa wananchi. Na asili na maumbile ya mfumo wa kitabaka duniani dumu daima hautendi haki. Huu ndio uhalisia wa nadharia na mifumo yote ya kitabaka duniani.

Kwa mujibu wa mwenendo

wa mchakato huu wa katiba unavyoendeshwa, wa kuanza kijumba hodi, unaonesha wazi kuwagawa wananchi na kuwafanya wasiwe sawa mbele ya haki. Binadamu ni mtu aliemumbwa na fikra, akili, na maarifa. Unapomleta mtu kama Mkapa jimboni kutoa maoni na wanachi wengine, hata akizomewa, watu watahisi kuwepo kwa usawa. Na unapompa siku yake pekee tena nyumbani kwake, unaanza kuuumba dudu moja baya mno la ubaguzi na ngazi refu ya utabaka baina ya wananchi na wakubwa wao.

Taswira inayojengeka machoni mwa wananchi hivi sasa, kwa tume kuanza kupitia watu binafsi majumbani kukusanya maoni yao, eti tu kwa sababu ni wakubwa, haina mustakabali mzuri. Haina kwa sababu tafsiri iko wazi ya utaratibu kama huu. Iko wazi hata kwa kujiuliza swali dogo tu. Hivi kweli maoni waliyotoa

wananchi wote wa Zanzibar, yanawezajae kuyapindua maoni aliyoyatoa Mkapa na Mwinyi? Sipati picha!

Yaani, hivi kweli maoni ya wananchi wa kawaida yatasikil izwa bora kwa kulinganisha wingi wao kuliko ukubwa na maoni ya wenye cheo, kauli, na nguvu katika nchi hii? Hili si kweli, maana tumeona katika chaguzi nyingi hapa nchini, ambapo sauti ya wananchi walio wengi ikipinduliwa na kauli ya mtu mmoja. Hili liko wazi kama sabuni ya mche!

Na ndio hapa ninapoona kuwa ile kauli mbiu isemayo ‘Watu wote ni sawa mbele ya haki na Sheria’ ikibadilika na kusomeka ‘Watu wote ni sawa mbele ya haki na sheria, lakini baadhi ya watu, ni sawa zaidi kuliko wengine’. Kwa hali hii naanza kukosa imani na kutawaliwa na ruwaza za nadharia ya ‘Ki-Orwell’ ninapautazama mchakato mzima wa katiba hapa nchini unavyokwenda.

Natoa hoja.

Page 15: ANNUUR 1055.pdf

15 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013Makala

KAMA Waislamu, tunapaswa kuendelea kufanya harakati z e t u z a k u s i m a m i s h a dini na kupigania haki katika jamii hata kama w a t a w a l a w a n a j a r i b u kutusambaratisha. Jinsi gani tutajilinda dhidi ya mashinikizo tunayopata kutoka kwa maadui wa Uis lamu; ni Sunna na sehemu ya Sira. Hili ni eneo muhimu ambalo Waislamu hatukuliendeleza vya kutosha.

Hekima ya Kuhama Makka vs. Kanuni ya Kuikomboa: Si vigumu kufikiria sababu hasa zilizomfanya Mtume Muhammad (saw) ahame kutoka Makka kuelekea Madina katika nyakati zile ngumu. Ni jambo la kawaida na linaloeleweka vyema kwamba mtu anaweza kutafuta maisha bora zaidi. Lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu hakufanya hivyo. Badala yake alisisitiza kuendeleza harakati zake mjini Makka.

Washir ikina wal imtaka afanye miujiza, wakisema kama kweli wewe ni Mtume, kwa nini huwezi kubadilisha vilima vya Safa na Marwa kuwa dhahabu? Walimtaka pia awaonyeshe k i t a b u k i l i c h o a n d i k w a kikiteremka kutoka mbinguni! Lakini kadri walivyomdhihaki, ndivyo alivyozidi kupigania ukweli na haki na kufichua uovu wao.

Kisha kukawa na uvumi na propaganda chafu dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Makka nzima ikajaa propaganda chafu za Maqurayshi dhidi ya Muhammad (saw) na wafuasi wake. Eneo lote la Rasi ya Arabuni likavuma kwa taarifa potofu kuhusu Muhammad na Waislamu, na zikaenda mbali zaidi mpaka Afrika na maeneo mengine. Taarifa potofu za kumpinga Muhammad (saw) zilifikia kilele chake wakati wa Ibada ya mwaka ya Hijja, wakati watu walipokuja Makka kutoka eneo lote la Arabuni. Watu wa Makka walikutana na Walid bin Mughira, mkuu wa ukoo fulani, ili kujadiliana jinsi ya kumdhalilisha Muhammad (saw) katika kipindi hiki cha Hijja. Baadhi yao walishauri kwamba Muhammad awas i l i shwe kama mhubiri, lakini Walid aliwajibu kwamba Muhammad hazungumzi lugha ya wahubiri. Baadhi yao walishauri kwamba Muhammad atangazwe kuwa ni mwendawazimu, lakini Walid alikataa hili kwa sababu Muhammad hakufanana kabisa na mwendawazimu au mtu aliyechanganyikiwa. Wengine wakafikiria kumshutumu kwa uchawi, lakini Walid alikataa kwa sababu hakukuwa na ushahidi wa hilo. Hatimaye walikubaliana kusema kwamba Muhammad anazungumza maneno ya ajabu ambayo yanaweza kutenganisha ndugu,

Mtume amenyooka, harakati zetu zimepinda-2Na Said Rajab

kuvunja ndoa na kuharibu familia.

Makka ilikuwa imepakana na h imaya mbi l i kubwa, Wafursi na Warumi, kwa hiyo Maqurayshi walijaribu kusisitiza kwamba Muhammad alikuwa akifundishwa Qur’an na kijana mmoja wa Kikristo aliyeitwa Jabr. Habari hizi zilisambaa sana na hatimaye zikajibiwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe:

“Na bila shaka tunajua kwamba wanasema: “Yuko mtu anayemfundisha” (Lakini lugha ya yule wanayemuelekezea (kuwa anamfundisha Mtume) ni ya kigeni na, hii lugha inayotumika katika Qur’an) ni lugha ya Kiarabu bulbul” Qur(15:103).

Kufuat ia hoja h iyo ya Mwenyezi Mungu, wakuu wa Makka wakatangaza kwamba Muhammad si mtu wa Makka - maneno anayosema yanatoka vyanzo v ing ine na yeye ameshikamana zaidi na vyanzo hivyo kuliko alivyoshikamana na utamaduni wake, lugha yake ya asili na dini ya mababu zake. Lakini pamoja na yote hayo, Mtume wa Mwenyezi Mungu hakufikiria hata mara moja kubadili kitovu cha Uislamu kutoka Makka kuelekea sehemu nyingine.

Maqurayshi, ambao ndiyo waliodhibiti madaraka mjini Makka, hawakukata tamaa kumfukuza Muhammad (saw) kutoka Makka, ikiwa ni pamoja na kupambana naye kwa njia zote. Hatimaye wakaamua kumuwekea vikwazo yeye na ukoo wake. Wakuu wa Makka wa l ikuba l i ana kumtenga Muhammad (saw) na ukoo wa Bani Hashim na Bani Abdul Mutallib. Hii maana yake hakuna aliyeruhusiwa kufanya nao biashara wala kuoleana nao. Na hati maalumu ya kuwatenga ikabandikwa kwenye Ka’abah.

Maqurayshi na washirika wao walidhani kwamba hatua hii ya kumtenga Muhammad na jamaa zake kutoka katika

maisha ya Makka kungeleta tija zaidi kuliko mikakati yao ya awali. Hali hii iliendelea kwa takriban miaka miwili au mitatu hivi. Maqurayshi walitarajia kwamba watu wa ukoo wa Mtume wangeanza kumkacha Muhammad (saw), na hata baadhi ya Waislamu wangeachana na Uislamu. Mwisho wake, Muhammad angebaki mpweke, aliyetengwa na jamii na asiyepata msaada wowote.

Licha ya yote hayo, Mtume wa Mwenyezi Mungu hakusalimu amri. Bado hakufikiria kukimbia na kuhamisha kiti cha Uislamu kutoka Makka kwenda kwenye ngome ny ing ine . Bada la yake, aliibuka kutoka kwenye changamoto hizo na dhamira kubwa zaidi ya kuikomboa Makka.

Habari hizi za Mtume wa Mwenyezi Mungu na watu wake kutengwa kiuchumi na kijamii zikaenea eneo zima la Arabuni. Na watu wenye akili timamu wakaanza kutambua kwamba kuna jambo si la kawaida kuhusu huyu mtu Muhammad.

Vipi Mtume wa Mwenyezi Mungu na wafuasi wake na watu wa ukoo wake waliweza kuhimili kutengwa kule? Walikimbilia eneo moja pembezoni mwa Makka, ambapo waliteseka sana na maumivu ya kukosa chakula na mahitaji mengine muhimu. Kuna wakati walikosa kabisa chakula.

W a i s l a m u h a w a h a w a k u r u h i s i w a h a t a kuzungumza na watu wengine. Ruhusa pekee waliokuwa nayo ni miezi mitukufu ya (al -Ash-hur al-Hurum), ambapo Mtume wa Mwenyezi Mungu angeenda Ka’aba na kuwaeleza Waarabu wanaotoka nje ya Makka maana ya Uislamu.

Vikwazo hivi dhidi ya Mtume na watu wake vikaleta huruma kutoka kwa watu wengine wa Arabia. Wengine walimsikiliza

na wakaitikia vizuri wito wake. Wengine walimpelekea chakula na maji kwa siri. Hali hii iliendelea kwa takriban miaka mitatu, ndipo vijana watano wa Makka walipoibuka na kutamka hadharani kwamba vikwazo hivi ni upotofu mkubwa. Vijana hawa walitafuta namna ya kuondoa lile tangazo lililowekwa kwenye Ka’aba.

Siku hiyo, mmoja wao akaenda kwenye Ka’aba na kuwahutubia watu akisema: “Oh Watu wa Makka! Tunakula na kusaza na tunavaa, wakati Bani Hashim wanaangamia bondeni pembezoni mwa Makka, hawawezi kununua wala kuuza! Sitatulia mpaka tangazo lile la kuwatenga kwenye Ka’aba lichanwe”. Aliposikia hivi, Abu Jahl akajibu kwa sauti: “Wewe ni muongo! Na kwa hakika tangazo lille halitachanwa!”

Kisha kijana wengine wanne wakasogea mbele kuunga mkono kile kilichosemwa na mwenzao. Abu Jahl akatambua kwamba vijana hawa watano walikuwa wakiwakilisha kundi kubwa la watu pale Makka. Kupambana nao kungeleta matatizo makubwa Makka. Kwa hiyo, tangazo lile likashushwa na kuchaniliwa mbali, na Mtume wa Mwenyezi Mungu na watu wake wakaruhusiwa kurejea Makka.

Tangu pale, Maqurayshi wakatambua kwamba hakuna kitu kitakachoweza kumzuia Muhammad (saw) kueneza ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kufanya kile ambacho Allah (sw) anataka kwenye ardhi. Kipengele cha ushujaa katika Sira ya Mtume wa Mwenyezi Mungu , kup i t i a ma tuk io kama haya katika maisha yake, hakizingatiwi kabisa na wale wanaopanga harakati za Kiislamu leo. Wanadhani akili

na uoni wao pekee vinatosha!Inawezekana vipi watu

hawaoni jinsi maamuzi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu yalivyokuwa imara na yenye kufuata kanuni kule Makka? Ni kweli, kulikuwa na majaribio mawili ya kutafuta msaada au ukimbizi nje ya Makka, Habashah na Ta’ if. Lakini majaribio haya ya kupunguza madhila ya Waislamu wa awali Makka, hayakuwa mbadala wa kuikomboa Makka.

U s h a h i d i w a h i l o n i kwamba, wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu alipoasisi dola ya Kiislamu Madina, bado alielekeza nguvu zake katika kuikomboa Makka. Katika miaka yake kumi Madina, Mtume aliandaa jeshi kubwa, yeye mwenyewe akishiriki mapigano, akapambana vita ya kuikamata Makka na Ka’aba, ili ziwe ngome ya Mamlaka ya Kiislamu. Wapi pengine, wakati Mwenyezi Mungu mwenyewe ameshasema:

“Kwa yakini nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ibada) ni ile iliyoko Bakkah (Makka), yenye baraka na uongozi kwa ajili ya walimwengu wote” Qur(3:96).

Tatizo la Waislamu sisi wa leo, hatutaki kubanwa na ‘Model’ hii ya harakati za Mtume wa Mwenyezi Mungu katika kusimamisha dini ya Allah hapa duniani. Sisi tunataka kubuni dira zetu za harakati, ambazo ni nadharia zaidi kuliko uhalisia. Kama kuna kipengele cha kisiasa na kijamii katika Sunnah, ambacho Mtume wa Mwenyezi Mungu ametuachia kama urithi, basi ni ukombozi wa Makkah. Sijui vipi tunasahau Sunnah hii kubwa kabisa ya Mtume!

Ni ukwel i u s io f i ch ika kwamba mji wa Makkah ndiyo kitovu cha Waislamu duniani. Makkah, ndiko alikozaliwa Mtume, ndiko alikoanza harakati zake, ndiko inakofanyika Ibada ya Hijja, ambayo ni nguzo ya Uislamu, Makkah ni Qiblah cha Waislamu. Ndiyo maana Mtume wa Mwenyezi hakuwa tayari kuiona Makkah ikiwa mikononi mwa Washirikina.

Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa na chaguo la kuikwepa Makkah, na kukamata ardhi nyingine kubwa tu, katika eneo la Arabuni au nje ya hapo, lakini hakuzingatia chaguo hilo. Badala yake, aliamua kupambana, kuteseka na kuipigania Makkah kwa hali zote. Hapa kuna funzo kubwa jinsi Mtume alivyodumu katika ajenda muhimu, hata mazingira yakiwa magumu kiasi gani. Hakuhama kwenye ajenda! Alibadili mbinu tu ya kufikia lengo, lakini ajenda ni ile ile.

Page 16: ANNUUR 1055.pdf

16 AN-NUURRABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR16 RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013

MAULID MUBARAK!

SHURA ya Maimamu Mtwara imetoa kauli ikiorodhesha madhila waliyofanyiwa watu wa Mikoa ya Kusini na kusema dhulma sasa basi.

Kat ika kau l i h iyo wamesema kuwa katika kipindi cha ukoloni wa Wajerumani (1885-1917), “wananchi wa mikoa ya Kusini walitumika kama nguvu kazi ya kuendeleza maeneo mengine yenye migodi na mashamba.”

Wa k a s e m a , w a t u walinyang’anywa ardhi zao na kulazimishwa

Masheikh Mtwara sasa wasema ubaguzi basi

Hizi sio zama za kufanywa manambaWaeleza walivyoporwa mashine ya maji

Na Mwandishi Wetu kuacha familia zao na kwenda Kufanya kazi kwa nguvu katika mashamba ya mikonge mikoa ya Tanga na Kilimanjaro ambapo walikuwa wakijulikana kwa j ina maarufu la manamba.

“Katika sura hii, Mikoa ya Kusini iliachwa bila kuendelezwa ili iwe kitovu cha kutoa wafanyakazi (manamba) wa kutumika kat ika mashamba ya wakoloni katika maeneo mengine ya nchi. Ushiriki wa watu wa Mtwara katika Vita ya Majimaji ilikuwa ni kielelezo cha kupinga d h u l m a d h i d i y a o . ” Wamesema Masheikh.

Waki fa fanua za id i

wamesema kuwa ukoloni wa Mwinge reza nao uliendeleza dhulma hiyo ambapo Mtwara ilitengwa kama eneo linalostahili kubaguliwa na kuhujumiwa kimaendeleo.

“Katika utawala wa Waingereza, mwendo ulikuwa ni uleule. Mikoa ya Kusini ilitengwa na kubaguliwa kiuchumi. Mwandishi wa Kifaranza Libenow (1971) katika kitabu chake Colonial Rule and Political Development in Tanzania: The Case of Makonde ukurasa wa 11 anaandika kwamba waingereza waliita Mtwara kuwa ni “Cinderella Region of a Cenderalla Territory”

yaani eneo lililotengwa/kubaguliwa la ukanda uliotengwa/kubaguliwa.”

Wa k a s e m a k u w a ilikuwa matarajio kwamba baada ya uhuru ubaguzi huo ungekoma lakini haikuwa hivyo.

W a k i t o a m f a n o wakasema kuwa pamoja na kuwa “Mtwara ina Bandari yenye kina kirefu katika Afrika ya Mashariki yote, lakini mpaka sasa mipango ya kuiendeleza imekuwa ni kizungurumkuti.”

Kwa upande mwingine w a k a s e m a k u w a “ Wananchi wa Mtwara na Kusini kwa ujumla wanazidi kulia tu na kusuasua kwa ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Lindi-Dar es Salaam. Wanazidi kuumia wanapoona ile mikoa inoyoheshimiwa na serikali ikiwa na Barabara nzuri zinazopitika tena ujenzi wake umekamilika kwa muda mfupi sana. Miaka minane ya Mh. Rais Kikwete zile kilomita 60 za barabara kutoka Ndundu mpaka Somanga hazijaisha lakini gesi anataka kuiwekea bomba na mradi ukamilike kwa miezi 18.”

Aidha , “Wananch i wameshuhudia reli ya kusini iking’olewa bila sababu za msingi na huku ikijulikana kuwa reli ni moja ya miundombinu muhimu katika kuchochea uchumi na maendeleo ya jamii kwa ujumla. Wananchi wa Mtwara wameshuhudi mashine ya maji Kitangali Newala ikiondolewa na kupelekwa Dodoma ambayo ilikuwa msaada kutoka Finland.”

Wakizidi kuorodhesha dhulma Masheikh hao wakasema kuwa “wananchi

wa Mtwara wameshuhudia k iwanda cha samaki Mtwara kikiondolewa na kupelekwa Dar es Salaam (na) wameshuhudia taa za mwanga mkali za uwanja wa ndege Mtwara ziking’olewa na kupelekwa Arusha.”

Ni katika hali hiyo Masheikh hao wanasema kuwa wanaungana na wananchi wa Mtwara k u p i n g a g e s i a s i l i a k u p e l e k w a D a r e s Salaam.

Katika kutilia mkazo madai yao wakanukuu maandiko matakatifu wakisema kuwa “Kwa hakika MwenyeziMungu anaamrisha uadilifu, na kufanya ihsani, na kuwapa jamaa (na wengineo), na anakataza uchafu na uovu, na dhuluma. Anakunasihini i l i mpa te ku fahamu (mfuate)” (Qur’an 16:90)

Na kwamba amesema Mtume (s .a .w) kuwa “mwenye kuuona uovu, basi na auondoshe kwa m k o n o w a k e , k a m a akishindwa basi atumie ulimi wake kushajiisha u o v u u o n d o k e n a akishindwa, basi achukie moyoni mwake na huko kuchukia n i udhai fu wa imani”. (Bukhari na Muslim)

W a k a h i t i m i s h a w a k i s e m a k u w a “wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa muda mrefu wamekuwa wakichukia t u m i o y o n i m w a o maovu na madhila yote waliyokuwa wakifanyiwa na serikali, lakini sasa imefika wakati tuseme na tudhihirishe maovu hayo waziwazi ili asaa viongozi wajirekebishe na wawafanye uadilifu.”

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akisalimiana na Muft Sheikh Issa Shaaban Simba. (Picha kutoka Maktaba yetu)

Mhariri na watendaji wa gazeti la AN-NUUR wanawatakia

Waislamu Sherehe njema za Mazazi ya Mtume (S.A.W.)