16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1153 SAFAR 1436, IJUMAA , NOV. 28-DES. 4, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Wanasiasa, magazeti wanapandikiza ugaidi Wabaya kuliko watuhumiwa ugaidi Tujifunze kutoka Kenya na ATPU yao Kama tukifuata nyayo, tumeangamia Vigogo wa Mamlaka kamili waunguruma 'Ndio’ itaangamiza lengo la Mapinduzi Wahoji ile sababu ya kumtoa mkoloni Hakuna maendeleo kwa mfumo uliopo SHEIKH Ponda Issa Ponda. MZEE Salum Rashid, Katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi. Uk. 3 Dhulma ilishashtadi… Ya Escrow ni tabia Uk. 2 BAADHI ya Waislamu wakiwa nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam wakiendelea na dua wakati kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda ikiendelea kuunguruma ndani ya Mahakama hiyo Novemba 26, 2014. Sheikh Ponda ashinda kesi Mahakama Kuu Uk. 8

ANNUUR 1153.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

ISSN 0856 - 3861 Na. 1153 SAFAR 1436, IJUMAA , NOV. 28-DES. 4, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

Wanasiasa, magazeti wanapandikiza ugaidi

Wabaya kuliko watuhumiwa ugaidiTujifunze kutoka Kenya na ATPU yaoKama tukifuata nyayo, tumeangamia

Vigogo wa Mamlaka kamili waunguruma

'Ndio’ itaangamiza lengo la MapinduziWahoji ile sababu ya kumtoa mkoloniHakuna maendeleo kwa mfumo uliopo

SHEIKH Ponda Issa Ponda.

MZEE Salum Rashid, Katibu wa kwanza wa Baraza la

Mapinduzi. Uk. 3

Dhulma ilishashtadi… Ya Escrow ni tabia

Uk. 2

BAADHI ya Waislamu wakiwa nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam wakiendelea na dua wakati kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda ikiendelea kuunguruma ndani ya Mahakama hiyo Novemba 26, 2014.

Sheikh Ponda ashindakesi Mahakama Kuu

Uk. 8

2 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Habari

W A I S L A M U n c h i n i wameaswa kuwa makini na propaganda ya dhana ya Jihadi kwani ni mipango maalum ya Mataifa ya Ulaya inayowalenga Waislamu katika kutekeleza vita dhidi ya Uislamu.

Tahadhari hiyo imetolewa na Muhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro, Mwalimu Suleiman Filambi, akizungumza katika kipindi cha Mwangaza wa Jamii kinachorushwa na Radio Imaan, ya Mjini Morogoro.

Filambi amesema, jamii ya Wais lamu hiv i sasa inapaswa kuiangalia dhana ya Jihadi kwa umakini zaidi kuliko kukurupuka jambo ambalo linaweza kuwaingiza Waislamu katika mtego uliokusudiwa na watunga sera dhidi ya Uislamu na Waislamu.

“Tatizo lililopo hivi sasa ni kwamba, jamii inayolengwa ambayo ni ya Waislamu, wengi wao hawafahamu kuwa wanalengwa na hizi propaganda zinazoendelea za uwepo wa Jihadi katika Mataifa ya Afrika”. Alisema Mwl. Filambi.

Alisema, kuibuka kwa mitandao ya kijamii hivi sasa, imekuwa ni tatizo kwa Waislamu wengi hususani kwa vijana kwani wamekuwa w a k i i p a k i p a u m b e l e wanadhani kuwa kwa kusoma madai fulani kupitia mitandao hiyo ndio inatosheleza kupata ufumbuzi wa masuala na matatizo ya Waislamu.

“Matokeo yake Waislamu wenyewe kwa wenyewe wameingia katika mgongano w a k i m t a z a m o , w a p o ambao wanatafsiriwa kuwa hawataki Jihadi na wengine wanaonekana wanataka Jihadi, sasa wananyoosheana v ido le” . Al i sema Mwl . Filambi.

Alisema, hivi sasa Waislamu w a m e w a w e k a k a n d o

Njama za makafiri kuangamizaWaislamu kupitia jihad bandiaNa Bakari Mwakangwale wanazuoni wanaoelewa

masuala ya Uislamu, bali wanaamini za id i mada zitolewazo katika mitandao, na fat’wa anayoikuta huko ndio unakuwa msimamo wake.

Akasema Mwalimu Filambi kuwa hilo ni tatizo kubwa linaloweza kuwaangamiza Waislamu.

Filambi alisema, Waislamu wanapaswa kuzama zaidi katika mafunzo ya Uislamu kutoka kwa wanazuoni wenye taaluma ya masuala ya dini na si kwa tafsiri ya juu juu tu kisha wakachukua maamuzi na kuanza kuyafanyia kazi.

Fi lambi, a l isema kwa kawaida watengeneza agenda au mada za kuwagonganisha Waislamu, huwa wanaangalia p a l i p o n a m wa n ya wa kuwagonganisha Waislamu na hutumia njia hiyo kwa kujinasibisha na Uislamu kwa lengo la kuwavuruga.

Akinukuu maelezo ya Profesa Hamza Njozi, katika Bunge la Katiba, alisema kwa haya yanayoendelea nchini huivi sasa hadhani kama Tanzania inaweza kuwa salama, kwa sababu agenda zinawekwa na mabwana wakubwa hivyo Uislamu unakuwa ni njia tu kama daraja la kuwafikisha katika ajenda zao.

Kwa sababu, alisema baada ya vita na Warusi, mabwana wakubwa hao walitangaza wazi kuwa, vita iliyobaki ni dhidi ya Uislamu kwa sababu ndio dini pekee inayoweza kuwa kikwazo katika malengo yao.

A k i t o a m a o n i y a k e kutokana na hali ilivyo sasa hususani kwa Waislamu Abdallah Waziri, alisema Uislamu ni dini ya kiutu zaidi kwani umefundisha kuishi na mtu hata asiyekuwa Muislamu.

A l i s e m a , Wa i s l a m u wanapaswa kufahamu na kujifunza kutoka kwa Mtume Muhammad (s a w), kwani

aliweza kuishi na Mayahudi, Washirikina pamoja na hila zao za ukandamizaji dhidi ya Waislamu na Uislamu.

“Mfumo wa Kiislamu sio fikra za mtu binafsi bali kuna mfumo rasmi ambao Mwenyezi Mungu a m e u s h u s h a a m b a o unapatikana katika Qur an, na si vinginevyo. Hivyo linapokuja suala kuhusu Uislamu ni lazima litolewe fat ’wa na wanazuoni si kila mmoja anaweza kutoa msimamo, jambo ambalo l i n a w e z a k u w a i n g i z a Waislamu katika matatizo makubwa.” Alisema Ust. Waziri.

Akasema, uk ianga l ia suala zima la Jihadi, kuwa linatafsirika zaidi katika Sira, kwamba katika matukio yaliyogusa Waislamu na Uislamu Mtume (s a w) alifanya nini, na inapolazimu kwenda kupigana Mtumie, alitumia vigezo, adabu na Sharia zipi.

Alitolea mfano sakata la kundi la Boko Haram la nchini Nigeria, linalosadikiwa kuwa lipo katika Jihadi, akasema katika Uislamu hakuna Jihadi ya kuwateka wanawake (mabinti) na kuuwa watu hovyo kama magaidi na maharamia.

Katika uhai wake, Al-Maruhum, Mwalimu Jafari Siraji, aliwahi kuwataka Waislamu kuwa makini sambamba na kuchukunguza mwenendo wa matukio ya n a y o s h a j i h i s h wa n a Waislamu au Uislamu, kisha kurejea katika sira na Fiqh, kwamba Mtume (s a w) aliyaendea vipi masuala ya Jihadi.

Katika makongamano yake mbalimbali Mwalimu Siraji, alikuwa akieleza kuwa kilichopo hivi sasa ni mitego iliyotengenezwa na makafiri kisha kuiingiza kwa Waislamu wakilenga kuwashawishi na kuwaingiza katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

KATIKA maadili ya Kiislamu, ni mwiko mtu kudhulumu au hadhulumiwa.

Ni marufuku kumdhulumu mtu kwa kigezo chochote kile, hata kama unatofautiana naye katika imani. Wala mtu asikubali kudhulumiwa na yeyote awaye.

H i i n i k w a s a b a b u dhulma kwa a ina zake zote imeharamishwa na kukaripiwa vikali kabisa ndani ya Qur’ani tukufu na suna ya Mtume (Hadithi)

“ M s i d h u l u m u w a l a msidhulumiwe.” [2:279].

“ N a a t a k a y e d h u l u m u miongoni mwenu, tutamuonjesha adhabu kubwa.” [25:19].

“ N a A l l a h h a wa p e n d i madhalimu.” [3:57]

Na Allah amesema tena katika hadithi Quds,

“Enyi waja wangu, hakika Mimi nimej iharamishia dhulma na n imei fanya (dhulma) kuwa ni yenye kuharamishwa baina yenu, b a s i m s i d h u l u m i a n e . ” (Muslim).

Hiyo ni baadhi ya mifano tu katika Qur’an Tukufu na Hadith za Mtume Muhammad (s.a.w), ambayo kwa pamoja ndio muongozo sahihi katika maisha ya Muislamu na binadamu wote kwa ujumla.

Hapa unaonekana utukufu wa hali ya juu wa Uislamu, dini ya haki, uadilifu na usawa. Hakika hii ni dini ambayo inayochukia dhulma na madhalimu na inaamrisha uadilifu, kufanya hisani na inakataza uchafu na uovu na dhulma.

K a m a m w a n a d a m u angekubali kutii na kukua katika maadili ya dini, maadili kama haya yanayokataza kikamilifu dhulma miongoni mwa wanadamu kat ika maisha yake yote duniani, basi ni wazi haki ingeshtadi kat ika jami i na yeyote anayedhulumu angetahayari.

Tunaweza tukaielezea na kuianisha dhuluma kuwa ni kile kitendo cha mtu au kikundi cha watu kuchupa mipaka ya Allah (sw) na kuitumia au kuikalia haki ya mtu au watu wengine bila uhalali.

Na mara nyingi dhulma hufanyiwa mnyonge au dhaifu asiyeweza kujinusuru nayo. Dhulma hutokana na kiza kilichoko moyoni mwa mtu, na kiza hiki ndicho kinachomzuia kuiona haki na kuhesh imu haki ya mwenziwe. Akachukua kitu kisichokuwa chake, iwe cha mtu binafsi, cha serikali (jamii), bila ya kuona vibaya.

Ukosefu wa mwongozo na imani ya dini ni jambo jingine linalofanya dhulma iongezeke. Wanaodhulumu hufanya hivyo kwa kibri na jeuri yao ya kimamlaka waliyo

Dhulma ilishashtadi… Ya Escrow ni tabia

nayo juu ya watu wengine.Katika hali kama hii ,

l a u m o y o wa d h a l i m u ungelikuwa na nuru, basi angeweza kuzingatia haki ya wengine na kuziheshimu na asingelikuwa na ujasiri wa kumdhulumu yeyote.

Zipo dhulma za aina tatu. Kuna dhulma hupatikana k w a m j a k u m k u f u r u Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumshirikisha. Dhuluma ya mja kwa nafsi yake na kuna dhuluma ya mtu kwa wenziwe au kwa viumbe v ing ine vya Mwenyez i Mungu.

Aina hii ya tatu ya dhuluma hasa ndio tunayokusudia kuielezea hapa, ambayo h u p a t i k a n a p a l e m t u atakapowafanyia maudhi wenziwe kwa kuwavunjia heshima au kuchukua mali zao. Iwe ni kwa nguvu alizo nazo, kwa ukwasi alio nao, kwa cheo alicho nacho, kwa elimu aliyo nayo au kwa roho yake mbaya tu ya kibinafsi na choyo.

Dhulmati huyu anaweza kufanya dhulma hata kwa kuwadhuru watu katika miili au hisia zao, kwa kutwaa mali zao pasi na uhalali au haki.

H a ya n d i o m a t a t i z o ya l iyotus ibu hiv i sasa , ambapo watu waliopewa dhamana na Watanzania, watachukua mabilioni ya fedha isipo haki ambapo pesa hizo zingetumika kwa kununulia madawa na kutoa huduma nyingine za kijamii. Kwenye huduma kama ya umeme, wananchi wanajikuta wakilipa gharama kubwa, kumbe katika gharama hizo, wamejumlishiwa pia na zile fedha za wizi na zinazotumika kifisadi badala ya kuboresha huduma na kupunguza gharama za uendeshaji. Ndio haya tunayosikia ya akaunti ya Tegeta Escrow.

T u k u m b u s h e k u w a dhuluma hizi hazikuanza leo. Ni tabia ya muda mrefu kwa watendaji wa serikali na wenye mamlaka, ambao nafs i zao z inaongozwa na tamaa, choyo, ubinafsi uliopindukia kiasi kwamba sasa kudhulumu imekuwa jambo la mazoea na tabia.

Watanzania wanakumbuka vyema sakata la ununuzi wa ndege ya Rais katika awamu ya Rais Benjamin Mkapa na lile la rada na vijisenti vya ‘chenji’ yake.

Katika Awamu hii ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete muendelezo wa dhulma kubwa uliendela ambapo masalia ya walafi walikuja na mpango mwingine wa kudhulumu kupitia akauti ya madeni ya Nje (EPA). Katika kashfa hii, dhulma k u b w a i l i f a n y w a n a wateule wachache dhidi ya

Watanzania, kufuatia wateule hao kutumia mamlaka yao kuiba fedha nyingi, zaidi ya bilioni mia moja katika akauti hiyo.

Haukupita muda, dhulmati w e n g i n e w a k a k w a p u a mabilioni ya fedha kupitia mikataba mibovu na ya wizi katika kashfa ya Richmond.

Hatujakaa sawa, hivi karibuni tu, watu wakatumia mwanya wa operesheni ya Taifa ya kupambana na ujangili , kudhulumu kwa kukwapua mifugo ya wafugaji, kukwapua fedha zao kupi t ia rushwa za kulazimisha nk. Wengine waliokaidi kudhulumiwa wakaishia kupoteza mifugo yao na baadhi yao kuteswa barabara.

Tuseme tu kwamba, haya yamekuwa mazoeya, kwamba sasa dhulma ni jambo la kawaida kwa baadhi ya wanasiasa na viongozi wetu.

We n g i h a w a a m i n i k i na wamejaa tamaa za fisi. Wanapata madaraka kupitia migongo ya Watanzania, halafu wanatumia nafasi tulizowapa kudhulumu ili kukidhi tamaa zao huku wakiwaumiza Watanzania zaidi ya milioni 46.

Pamoja na jitihada za Bunge kujaribu kuwabana, badi tatizo halionekani kwisha kwa kuwa wanaodhulumu wa l i s h a k o s a m i o y o ya imani katika dini, (hawana mwongozo wa k id in i ) , wameonja tamu ya dhulma na wameshazoea.

Katika mioyo yao, hakuna h u r u m a wa l a m a a d i l i . Zaidi wanaonyesha wapo kinadharia zaidi kuliko vitendo.

Hata hivyo awali tuliona dawa sahihi iliyoonekana kuwa mwarobaini wa dhulma inayofanywa na viongozi

na wenye mamlaka dhidi ya wananchi, ilikuwa ni rasimu ya katiba iliyokuwa imependekezwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba.

Kwa sababu Rasimu ya Warioba ilikuwa ni rasimu iliyowapa wananchi mamlaka zaidi ya kuwasimamia na kuwawajibisha viongozi wao.

Hata hivyo walengwa w a l i t a m b u a h i l o n a kuivunjavunja na kuondoa kabisa ile azma ya rasimu ya kuwawajibisha dhulmati.

Bila ya kuwa na katiba inayowawajibisha wenye mamlaka na viongozi, hatudhani kama Bunge letu la sasa pamoja na kuonyesha jitihada zake za kudhibiti walafi hawa, wa t a f a n i k i wa k u o n d o a mazoea yaliyokwishajengeka kwa watendaji wakubwa serikalini kuwadhulumu wananchi.

3 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014Habari

Vigogo wa Mamlaka kamili waungurumaIMEELEZWA kuwa kura ya ‘Ndio’ kwa katiba inayopendekezwa itaviza malengo yote ya mapinduzi na kuleta maangamizi Zanzibar kama nchi.

Aidha, Zanzibar isitarajiwe kuwa na maendeleo ya kiuchumi, kama hali itabaki kama ilivyo Wazanzibari wakiwa wametiwa kwapani na serikali ya muungano, ambayo inatajwa kuwa ndiyo ya Tanganyika iliyojivika koti la Tanzania katika muungano wa serikali mbili.

Hayo ni katika hoja zilizotolewa katika kongamano lililofanyika mapema wiki hii katika Hoteli ya Bwawani ambapo ilielezwa kuwa imekuwa bahati mbaya kwamba Zanzibar imekosa mtetezi hivi sasa kwa vile Rais amekuwa akisimamia zaidi masilahi ya CCM.

“Ikiwa Rais atalichukulia hili kichama na sio ki-nchi na ikafika kupigwa kura ya maoni, wafahamu kwamba sote tupo katika jahazi moja pengine viongozi wao kwa maslahi yao binafsi, wanahisi wawe hewallah bwana kwa lolote wanaloambiwa Dodoma. Ndugu zangu wanachama wa CCM, nawaheshimu sana na naheshimu msimamo wao na kuchagua chama wanachotaka, lakini nawasihi katika hili watafanya makosa makubwa kama watasema Ndio.”

Mzee Rashid anasema akishangaa kuwa watu walokwenda mbio kutaka Muingereza awaachie nchi yao hadi wakaachiwa kukafanyika Mapinduzi, lakini hali hiyo imebadilika kwa kuwa Zanzibar hivi sasa haina mamlaka yoyote kinyume na dhamira yake ya Mapinduzi na watu hawalioni hilo.

Mzee Salum Rashid ambaye alikuwa Katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi, alisema Wazanzibari wengi hawaridhishwi na mambo yanavyokwenda na kutaka kurejeshwa mamlaka ya Zanzibar na sio wananchi tu bali hata viongozi wakiwemo Baraza la Mapinduzi na kuna nyaraka mbali mbali ambazo zinaitaka Tanganyika kurejesha mambo mbali mbali Zanzibar.

“ Z a n z i b a r i we n c h i h u r u , tuligombania uhuru na tunagombania mamlaka hivi sasa, sio kwa sababu ya ukorofi, lakini tunafanya hivyo kwa sababu ya kurejesha hali ya uchumi wa Zanzibar, tunataka kurejesha hali ya vijana wetu kuwainua katika ajira na kuifanya nchi vizuri, kurejesha mfumo wa elimu, kurejesha afya bora na mambo mengine ambayo sasa hayapo kutokana na hali ya uchumi,” alisema.

“Zanzibar bila ya mamlaka kamili na bila ya sera mbadala haiwezi kusonga mbele na kama Zanzibar inataka kuendelea, basi ifuate mfano wa Mauritius na isifate mfano wa Tanganyika,” alisema huku akishangiriwa kwa makofi.

Katibu huyo wa zamani wa Baraza la Mapinduzi, amesema, mchakato wa katiba umeifanya Zanzibar isiwe na msemaji wake katika kipindi hiki muhimu cha historia ya visiwa hivi.

Akizungumza katika kongamano hilo la kitaifa lililoandaliwa na Kamati ya watu sita ya kusimamia Maridhiano ya kisiasa lililofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani,

Na Salma Alghaithiyyah. aliwanasihi Wazanzibari kuinusuru nchi yao katika kipindi hiki cha kutafuta katiba.

“Mimi nilifikiria wakati huu wa mchakato, Rais wa muungano ambaye anawakilisha Tanganyika na Rais wa Zanzibar watafanya mazungumzo kwa kila khatua ambayo wote ni viongozi wakubwa wa chama cha CCM, watafanya mazungumzo ili kutupatia katiba na mamlaka kamili kama tulivyokusudia, lakini wamefanya mazungumzo kama viongozi wa CCM, sasa jee huu utaratibu ni mwafaka? Jee, hii katiba ya nchi au ni katiba ya chama?” Alihoji.

Alisema ukitizama zile tunu za taifa ni sera za Chama Cha Mapinduzi, na sio za taifa ambapo, Rashid aliwaonya Wazanzibari kabla ya kufanya maamuzi ya kupiga kura ya ‘Ndio’ itakayoitosa nchi yao, wanapaswa kufahamu kwamba hizi ni nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar zilizoungana miaka 50 iliyopita.

“Zanzibar mwaka 1963 Muingereza alipokata shauri ya kutupa uhuru wetu, vyama vyote viwili tulitakiwa watu saba tukaandika katiba ya uhuru wa 1963, lakini Zanzibar hawaitaki, eti ilikuwa imetaja Sultan kwa nini haibadilishwi badala ya Sultani tukaweka Rais katiba hiyo iliandikwa na Afro Shirazi na Hizbu, ilitoa haki za binaadamu kwa kila raia, uteuzi kila miaka mitatu baada ya mapinduzi ikatubidi sisi tusimamishe katiba kwa kuwa hatukuweza kuitekeleza maana serikali ya kimapinduzi haiwezi kutekeleza katiba.”

Alisema kwa wakati ule khatima ya Zanzibar haikuweza kuamuliwa na chama kimoja, lakini khatima ya Zanzibar ilikuwa iamuliwe na vyama vyote na Wazanzibari wote na ndio maana Wazanzibari wote

waliheshimika na kuamua jambo la nchi yao.

Alisema, Zanzibar inapaswa kutetea mamlaka yake na kukataa kuamuliwa na Dodoma kwa kuwa Zanzibar ina mamlaka yake na haihitajiki kuamuliwa jambo lake Uingereza wala Dodoma.

“Mamlaka ya Zanzibar ni muhimu na wala sio u-CUF Mzanzibari kuitetea nchi yake”, alisisitiza Katibu huyo wa zamani wa Baraza la Mapinduzi.

Alisema katiba ni jambo muhimu sana na sio jambo la kuchezea, sio la maskhara au la mzaha.

Rashid anasema anashangaa kuwa watu walokwenda mbio kutaka Muingereza awaachie nchi yao hadi wakaachiwa kukafanyika Mapinduzi, lakini hali hiyo imebadilika kwa kuwa Zanzibar hivi sasa haina mamlaka yoyote kinyume na dhamira yake ya Mapinduzi.

Katibu huyo wa zamani alisema Wazanzibari wengi hawaridhishwi na mambo yanavyokwenda na kutaka kurejeshwa mamlaka ya Zanzibar na sio wananchi tu bali hata viongozi wakiwemo Baraza la Mapinduzi na kuna nyaraka mbali mbali ambazo zinaitaka Tanganyika kurejesha mambo mbali mbali Zanzibar.

K wa u p a n d e wa k e B wa n a Mohammed Mugheiry (Eddy Riamy) ametuma salamu zake kwa Rais wa Zanzibar ambapo alisema Dk. Shein anavurugiwa nafasi yake na hao wapambe wake ambao wanafanya kampeni chini kwa chini kumuangusha ambapo huenda Mkoa wa Kaskazini na kupachua bendera za Uamsho lengo ni kumchafulia Rais Dk. Shein ili aonekane uongozi wake una matatizo.

“Wanaokwenda kushusha bendera ili watu waichukie serikali yako ndio wabaya, lakini wewe umeshika

kuitukana Kamati ya Maridhiano kila ukipanda jukwaani na wale wanaokwenda kuandika Maskani Kisonge kuwa Wapemba wahame na waondoke, ndio hao hao watu wako ambao wanakwambia wewe mwenyewe uhame”, alisema Eddy Riamy.

“Mimi nikitiwa ndani, mwengine anyanyuke aseme hatufai tusikubali, lakini hatukubali katiba yetu ya Zanzibar iharibiwe na tutakwambia hatufai kwa sababu gani wamekwenda Dodoma kutaka katiba yetu ya Zanzibar ifutwe?” Alisema na kuhoji.

Aidha Eddy al isema “CCM Z a n z i b a r wa n a p a n d a k a t i k a majukwaa na kuwatukana Waarabu tu, lakini wanasahau kwamba akina (Mheshimiwa Wziri Mkuu) Pinda, (Waziri Wiliam (Lukuvi) na (Mheshimiwa Spika wa Bunge) Anna Makinda, wanakwenda Oman huko huko kwa Waarabu huku akina Shamhuna wakibaki kazi yao kubeba mikoba”.

Akizungumza katika Kongamano hilo, Masoor Yussuf Himid, alisema lazima Wazanzibari waache woga na kukataa kuwachonganisha Wazanzibari kwani Maridhiano ni kheri na Mwenyeenzi Mungu amehimiza umoja na mshikamano.

“ K u n a wa t u wa z i t o l a k i n i wanaogopa kuzungumza kwa kuwa wapo katika nyadhifa za serikali, ukiwaambia wanasema wakati haujafika, lakini tunawaambia wakati ni huu wa kusema na tusisubiri kufa”, alisisitiza Mansoor.

Mansoor amesema wanaoimba Mapinduzi Daima, bila ya kuyafanyia kazi kwa kuleta uhuru na maendeleo, hao ni wanafiki kwa sababu lengo la mapinduzi ni uhuru na kuleta mamlaka ya Zanzibar.

Inaendelea Uk. 4

Sheikh Ponda ashinda kesi Mahakama KuuMAHAKAMA KUU ya Tanzania imefuta hukumu iliyokuwa imetolewa awali na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Mei mwaka jana dhidi ya Sheikh Ponda Issa Ponda, ambayo ilimtia hatiani na kumhukumu kifungo cha nje na watuhumiwa wenzake wengine 49 wakiachwa huru.

U c h a m b u z i w a h o j a zilizowasilishwa, umeifanya Mahakama Kuu kufuta hukumu i l i y o k u w a i m e t o l e w a n a Mahakama ya Kisutu na kwa sasa Sheikh Ponda yuko huru, hana hatia yeyote kwa mashtaka ambayo ameshtakiwa.

Hukumu hiyo iliyotolewa kufuatia rufaa iliyowasilishwa mahakamani hapo na wakili wa upande wa utetezi Juma Nassor.

Mahakama i l i toa sababu takriban sita za kupinga hukumu iliyomtia hatiani Sheikh Ponda katika Mahakama ya Kisutu.

“Kwa bahat i nzuri rufaa hiyo imekubalika, hoja zetu zimeonekana ni za msingi, Jaji

Na Seif Msengakamba amekubaliana nasi kwamba ushahidi ambao ulitolewa katika mahakama ya Kisutu, umebainika kwamba hapakuwa na ushahidi wowote unaoweza kuthibitisha shitaka ambalo ametiwa hatiani, la kuingia katika eneo lililokuwa na migogoro kule Markaz Chang’ombe kwa kutumia nguvu”. Alisema Wakili Nassor jana mahakamani hapo.

Kwa msingi huo, Mahakama Kuu iliridhika kwamba kwa ushahidi uliokuwa umetolewa, haukuonyesha kuwa kulikuwa matumizi ya nguvu.

Hukumu ya Jaj i Shangwa ilikwenda mbele zaidi na kuona kwamba Sheikh Ponda, pamoja na Waislamu ambao walikuwa wamefika Markazi Chang’ombe, walitumia njia mbalimbali za kidiplomasia kwa maana ya kuongea na huyo ambaye ndiye aliyenunua eneo hilo, pamoja na kuchukua namba ya simu ya shahidi namba tano Bw. Othmani kwa ajili ya kufanya mazungumzo.

A l i s e m a , m a z u n g u m z o yalifanyika katika Msikiti wa Mtambani kwa hali ya utulivu mpaka pale polisi walipokuja

kuwakamata wale Waislamu kule Chang’ombe.

Sababu nyingine iliyokuwa hoja ya msingi ya kufuta hukumu ya Sheikh Ponda iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu, ni kwamba kesi ile ilikuwa inahusu mgogoro wa ardhi na haikustahili kuwa kesi ya kijinai.

Wakili wa utetezi Juma Nassoro, alisema kimsingi jeshi la Polisi lilipaswa kumshauri mlalamikaji aende katika mahakama ya ardhi ili akathibitishe uhalali wa eneo lake, na kama kuna mtu alikuwa anapaswa kushtakiwa, basi alipaswa kushitakiwa katika mahakama ya ardhi kwa maana ya kesi ya madai.

A i d h a , i l i o n e k a n a k u wa M a h a k a m a y a K i s u t u haikujielekeza katika kuweka mizani sawa kwa washtakiwa wote, yaani fare trial.

Ilionekana kuwa kutokana na ushahidi uliokuwepo, hapakuwa na sababu yeyote ya kuwaachia washitakiwa arobaini na tisa kwa ushahidi ule ule uliotumika kuwaachia washitakiwa wengine,

4 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014Makala

Kufungwa Misikiti KenyaMlolongo wa njama dhidi ya WaislamuSawa Wazayuni kule Baytul Muqaddas

KATIKA nchi kama Jamhuri ya Kenya uhuru wa kuabudu ni jambo ambalo limekuwa likiheshimiwa na ndio maana ukienda katika nchi hiyo utakuta kuna dini mbalimbali. Wananchi wa dini mbalimbali wamekuwa wakiishi kwa amani kwa miaka nenda rudi na hatujasikia vita vya kidini katika nchi hiyo. Mfano wa wazi ni kupata makanisa hata katika miji ambayo kimsingi ni ya Waislamu kama Mombasa. Uhuru wa kuabudu umepelekea kuweko utitiri wa makanisa na hata makanisa sasa yameondoka katika mkondo wa nyumba za ibada na kuwa miliki za watu. Kwa maana kwamba, makanisa sasa nchini Kenya ni sehemu ya vitega uchumi vya wahubiri. Nyote bila shaka mmesikia mkasa wa hivi karibuni wa utapeli katika kanisa moja huko Kenya. Kali zaidi ni ule mkasa wa Embakasi, Nairobi ambapo mhubiri alimnunua dada mmoja na kumuahidi kumlipa kitita kizuri cha pesa. Alichotakiwa kufanya dada huyo ni kuja akiwa amepindisha mdomo ambapo mhubiri baada ya kufanya maombi na mikogo ya hapa na pale, dada hunyoosha mdomo wake na mhubiri hupayuka kwa nguvu HALELUYA, KWA JINA LA YESU, AMEPONA.

Tab’ani kesi kama hizo ziko pia nchini Tanzania, Uganda na kwingineko Afrika Mashariki, ingawa kwa Kenya masuala ya kutapeliwa waumini makanisani yamekithiri. Nimedokeza hayo ili kutoa taashira ya jinsi Wakristo walivyokuwa na uhuru wa kufanya mambo yao pasi na kubughudhiwa kinyume kabisa na Waislamu.

Tukio la kufungwa misikiti minne ya Mussa, Sakina, Swafaa na Minaa huko Mombasa Kenya hivi karibuni na polisi ya nchi hiyo kutoruhusu waumini kutekeleza ibada zao za kila siku katika misikiti hiyo, ni habari ambayo ilimgusa kila Mwislamu mwenye dhamira safi. Sababu inayotolewa na vyombo vya usalama vya Kenya ya kuhalalisha hatua hiyo ya kufunga misikiti katika Kaunti ya Mombasa ni kwamba, hatua hiyo imechukuliwa katika mlolongo wa vita dhidi ya ugaidi na sababu za Kiuslama. Kwa mujibu wa polisi, misikiti hiyo imekuwa ikitumiwa kueneza misimamo mikali ya kidini na vitendo vya ugaidi. Taarifa ya polisi imedai kwamba, imepata silaha pia katika misikiti hiyo. Waislamu wa Kenya na hata wa nchi nyingine ambao wanapinga kufungwa misikiti hiyo wanasema kuwa, kufungwa kwa misikiti hiyo kunaweza kuchochea hisia za chuki na kuwafanya vijana kuwa na siasa kali. Aidha wanasema hizo ni harakati zisizokubalika na zinaweza kuongeza hali hiyo kwa kuwaudhi vijana zaidi na kushadidisha hisia miongoni mwao kwamba, serikali iko dhidi yao, hivyo kuwafanya kuwa na siasa kali zaidi. Wenye mtazamo huo wanahoji kwamba, kama misikiti hiyo ina kamati zake zinazoongozwa na viongozi ambao mipango yao ni kuingiza ajenda za siasa kali na kuwaandikisha vijana kwa ajili ya kuwapeleka Somalia kujiunga na kundi la al-Shabab, kwa nini serikali isingeingilia kati kuhakikisha kamati hizo zinabadilishwa badala ya kufunga misikiti hiyo? Je hatua hiyo sio kinyume kabisa na uhuru? Kwa nini waumini wengine wa Kiislamu

Na Salum Bendera

wanyimwe haki ya kwenda kufanya ibada katika misikiti hiyo kwa sababu ya makosa ya watu wachache?

Bila shaka uamuzi wa busara ungeweza kutumika nao ni serikali kusaidia kamati hizi kutwaa tena udhibiti wa misikiti hii kuliko kuifunga.

Swali ambalo limekuwa likiulizwa na wengi ni kwamba, kufunga misikiti hiyo kunamaliza ugaidi au kutashadidisha? Je walioshambulia bari la abiria Mandera na kuua watu 28 wasio na hatia walikuwa waumini wa misikiti ya Mussa, Sakina, Swafaa au Minaa?

Jambo jingine linalolalamikiwa na Waislamu wa Mombasa na wa Kenya kwa ujumla katika kadhia nzima ya kufungwa misikiti minne ya Mussa, Sakina, Minaa na Swafaa ni jinsi polisi wanavyovamia misikiti hiyo na kuingia na viatu katika nyumba hizo za ibada. Kitendo cha polisi hao kuingia na mabuti yao na kuivunjia heshima misikiti hiyo hata kama ni kwenda kukamata magaidi, hakikubaliki hata kidogo. Msikiti ni nyumba tukufu ya ibada na polisi wanapoingia katika maeneo hayo hata kama wanakwenda kumkamata gaidi aliyejificha humo wanapaswa kuheshimu nyumba hizo za ibada na kuacha kujeruhi hisia za Waislamu. Hatua hiyo ya polisi ya Kenya haina tofauti na hujuma na vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu zinazofanywa na askari wa utawala wa Kizayuni kila siku huko Baytul Muqaddas. Jeshi la Israel huvamia msikiti mataktifu wa al-Aqswa kibla cha kwanza cha Waislamu huko Palestina na kuingia na viatu, jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa kila kona ulimwenguni.

Ni kutokana na ukweli huo ndio maana Waislamu kote Afrika Mashariki wanalitathmini suala la kufungwa misikiti minne ya Mombasa kwamba, ni katika mlolongo ule ule wa kuwaandama Waislamu lakini katika kivuli cha kisingio cha kupambana na ugaidi. Vita ambavyo jiwe lake la msingi liliwekwa na Marekani baada ya mashambulio ya

Septemba 11.Mwenyekiti wa Baraza Kuu

la Waislamu nchini SUPKEM, Profesa Abdul-Ghafur Al-Busaidy akizungumzia sakata la kufungwa misikiti hiyo alisema, ingekuwa jambo la busara kama serikali ingeketi kwenye meza ya mazungumzo na viongozi wa kaunti na wa kidini nchini Kenya ili kulitafutia ufumbuzi jinamizi la ugaidi na vijana kushawishiwa kujiunga na makundi yenye misimamo mikali,

badala ya kuvamia maeneo ya ibada na kuwakamata waumini kiholela. Matamshi hayo yaliungwa mkono na Khelef Khalifa Mwenyekiti wa Shirika la Kiislamu la Kutetea Haki za Binadamu nchini Kenya (MUHURI), ambaye alisisitiza kuwa, ugaidi ni suala la idiolojia ambalo linafaa kutafutiwa ufumbuzi kwa kutumia sera za kiaidiolojia.

Hakuna Mwislamu wa kweli anayeunga mkono kutumiwa maeneo ya ibada kuendeshea harakati za kufurutu ada; kwani Uislamu unapinga suala zima la misimamo ya kupindukia ambayo imekuwa ikitumiwa vibaya na watu wenye fikra finyu na uelewa mbaya kuhusiana na Uislamu na kadhia nzima ya jihadi katika Uislamu. Fikra za kuua watu bila sababu au kwa kuwa sio Waislamu au kwa sababu hawajui kutamka shahada mbili na mikasa mingine kama hiyo inayonukuliwa kufanywa na baadhi ya makundi ya kigaidi kama ya al-Shabab Somalia, Daesh Iraq, Jabhat al-Nusra Syria na kwingine, ni fikra na mitazamo finyu na potofu na ambayo haikubaliwi na mafundisho sahihi ya Uislamu. Hata hivyo haya yote bado hayalalalishi vitendo vinavyofanywa na polisi ya Kenya vya kuvamia misikiti kiholela, kuivunjia heshima kwa kuingia na viatu na kuwakamata waumini kiholela pasi na ya sababu kwa tuhuma za ugaidi na mengineyo.

Mbona makanisa yanayotapeli waumini kila leo nchini Kenya hayafungwi? Kwani sheria sio msumeno? Au ndio chambilecho Waswahili, mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu?

MOJA ya Misikiti iliyofungwa nchini Kenya hivi karibuni.

Sheikh Ponda ashinda kesi Mahakama KuuInatoka Uk. 3ukamtia hatiani mshitakiwa Sheikh Ponda.

Pia kulikuwa na hoja kwamba ushahidi wa kielelezo ambacho kilidaiwa kuwa Sheikh Ponda alikiri makosa, ulikuwa sio ushahidi wa kweli na hakuna kielelezo ambacho Sheikh Ponda alipokiri makosa kwa mashitaka ambayo al ishitakiwa kuwa aliingia kwa nguvu huko Markaz Chang’ombe.

Hivyo , i l ionekana kuwa Mahakama ya Kisutu ilikosea kusema kwamba Sheikh Ponda alikiri makosa.

Kwa ujumla Jaji alizichukua sababu zote hizo na nyingine na kuziweka katika hoja moja kwamba je, kulikuwa na ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Sheikh Ponda kwa mashitaka ambayo a l iyoshi takiwa na kuhumiwa?

Mwisho ndipo Jaji alichambua ushahidi na ikathibitika kwamba ushahidi ule haukutosha na haikupaswa kumtia hatiani na hatia ile imefutwa na rasmi.Katika kushrehesha hukumu hiyo, Jaji Shangwa alimwelezea Sheikh Ponda kuwa yeye ni zaidi ya Sheikh, kwani ni yake ya kutetea haki za Waislamu ni sahihi.

J a j i S h a n g w a a l i s e m a anavyofahamu, ni kweli katika Uislamu mali ya Wakfu haiuzwi. Alifafanua kuwa anavyofahamu Mujahidina katika Uislamu, ni

mtu ambaye yuko radhi kuitetea dini yake, jambo ambalo alisema kuwa ni sahihi kabisa.

Hivyo alimshauri baada ya kumaliza suala lake, akafungue kesi ya madai katika mahakama ya ardhi kudai haki ya Waislamu ambayo ni wakfu.

Hata hivyo, bado Sheikh Ponda ataendelea kukabiliwa na kesi nyingine dhidi yake iliyofunguliwa katika mahakama ya Morogoro.

Imeelezwa kuwa Sheikh Ponda hawezi kuwa huru kwa sasa maana ya kutoka mahabusu baada ya kushinda rufaa yake, kwasababu kule Morogoro jeshi la Polisi limemshitaki tena kwa kosa jingine wakidai kwamba alifanya uchochezi mjini Morogoro na vile vile amekiuka mashariti ya hukumu ya mahakama ya Kisutu.

Wa k i l i wa J u m a N a s s o r alisema hizo zilikuwa kesi mbili tofauti, lakini kushinda rufaa ya Mahakama Kuu ni jambo ambalo linaathiri kesi ya Morogoro, kwa kuwa kimsingi tayari inaonekana shitaka la kukiuka hukumu ya Mahakama ya Kisutu halitakuwepo tena.

Wakili huyo alisema kuwa wataichukua hukumu ya rufaa yao kutoka Mahakama Kuu na kuipeleka Morogoro ili kunaiomba mahakama hiyo, nayo vile vile kwa mujibu na kadiri sheria itakavyoruhusu kumwachia huru mteja wao.

5 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014Habari za Kimataifa

JOPO lililoteuliwa na mahakama kutoa maamuzi katika jimbo la Missouri nchini Marekani juu ya polisi aliyemuua kijana wa miaka 17 huko Marekani, limeamua kutomfungulia mashitaka ofisa huyo wa polisi, ambaye alimpiga risasi na kumuuwa kijana mweusi asiyekuwa na silaha Michael Brown, yapata miezi minne iliyopita.

Baada ya maamuzi hayo kutangazwa, hali katika mji wa Ferguson imekuwa tete huku waandamanaji wakitupia mawe na chupa magari ya polisi na mengine kuchomwa moto, huku Polisi nao wakijibu kwa kutumia gesi ya kutoa machozi.

Ghasia hizo zilifuatia tangazo la mwendesha mashitaka wa kitongoji cha Missouri, Robert McCulloch, Jumatatu usiku wiki hii kutangaza kwamba jopo hilo halikuona sababu yoyote ya kumfungulia mashitaka polisi Darren Wilson.

Wilson alikuwa ofisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuuwa kijana Michael Brown Agosti 9, 2014.

Mauaji hayo yalisababisha mvutano mkali kati ya wakazi ambao wengi wao ni jamii ya watu weusi wa eneo la St. Louis, ambalo hufanyiwa doria na polisi ambao wengi wao ni Wazungu.

Baada ya maamuzi kutangazwa Jumatatu usiku, familia ya Michael Brown ilisema kwamba wamesikitika sana.

Mawakili wa Darren Wilson w a l i s e m a j o p o l a m a j a j i walioteuliwa limekubaliana kwamba hatua za polisi huyo zilifuata sheria na taratibu za polisi.

Wakati machafuko katika eneo la Ferguson huko Marekani yakiwa bado hayajapoa kutokana na afisa huyo wa polisi kumpiga risasi na kumuua kijana asiye na silaha, habari nyingine zinasema Polisi katika jimbo la Cleveland wamemuua kwa kumpiga risasi mtoto wa kiume mwenye mri wa miaka 12 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Tamir Rice, alipigwa risasi katika viwanja vya michezo vya Cudell Commons Park Jumamosi, baada ya kumtaka asalimishe silaha aliyokuwa akiichezea kwa kuwatishia watu, Cleveland.com imeripoti.

Polisi walisema Rice alishika bunduki yake kiunoni alipotakiwa ajisalimishe na walidhani alikuwa akichomoa silaha ya kweli.

Hata hivyo mnyetishaji wa taarifa za Rice kuwa na silaha na kutishia watu, alisema silaha hiyo ilionekana kama si halisi.

Huu ni mzuka wa polisi kuua watoto MarekaniMuuaji hana kesi, vurumai zatawalaWamuua mwingine wa miaka 12

Polisi kumwona kijana huyo akipeleka mkono kiunoni kutoa ‘silaha’ yake walimpiga risasi mbili tumboni.

“Kwanini wasingemtishia,” Gregory Henderson alihoji katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia mauaji ya mwanaye.

“Alipigwa risasi mara mbili, sio mara moja na mwishowe hakuna aliyepiga risasi miguuni, walimpiga sehemu za juu za mwili.”

Ofisa huyo wa polisi alidai kuwa, alimpiga risasi kijana huyo baada ya kuchomoa silaha

yake na kudai kuwa alitishia kumshambulia, hivyo alifyatua risasi ili kujilinda.

Hata hivyo watu waliokuwepo karibu na tukio hilo walisema kuwa mtoto huyo mdogo, hakuwa amemtishia kwa njia yoyote ofisa huyo wa polisi, si kwa maneno na wala si kwa vitendo.

Kuanzia Agosti 9 mwaka huu, mji wa Ferguson na miji mingine ya Marekani imegeuka uwanja wa maandamano makubwa na ghasia, raia wakilalamikia ukatili wa polisi wa nchi hiyo dhidi ya raia.

JAMHURI ya Kiislamu ya Iran imezindua ndege nyingine isiyo na rubani (drone) ya kisasa kabisa iliyotengenezwa nchini humo, ambayo inaweza kutumika katika operesheni za upelelezi.

Drone hiyo iliyopewa jina la Ababil-3 imezinduliwa katika siku ya nne katika Maonyesho ya saba ya Kimataifa ya Sekta ya Vyombo vya Anga nchini humo, katika kisiwa cha Kish katika ghuba ya Uajemi Kusini mwa Iran.

Taarifa zinaeleza kuwa Drone hiyo inaweza kuruka kwa saa nane mfululizo katika eneo lenye ukubwa wa kilomita 250 na kupaa kwa umbali wa futi 15,000 juu angani, huku ikituma picha katika kituo cha mbali.

Wiki iliyopita, Iran pia ilizindua drone nyingine inayoshabihiana

na ile ya Marekani iliyolazimishwa kutua Iran miaka mitatu iliyopita.

Drone hiyo ya Iran inashabihiana na ile ya Marekani ya RQ-170 isiyoonekana kwenye rada.

Mwezi Septemba, Iran ilionyesha drone yake nyingine iliyotengenezwa na wataalam wa ndani wa nchi hiyo iliyoitwa 'Sadeq 1', katika maonyesho ya kijeshi katika hifadhi ya mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, marehemu Imam Khomeini, huko kusini mwa Tehran.

Sadeq 1 ina uwezo wa kuruka umbali wa kwenda juu angani wa futi 25,000 kwa mwendo kasi sana (supersonic speeds).

D r o n e z a I r a n z i m e k u wa zikitengenezwa kwa ajili ya majaribio ya rada na mifumo ya ki-electronic na kwa ajili ya kutathmini mafunzo.

Katika siku za hivi karibuni, taifa

hilo limeelezwa kuwa limepiga hatua kubwa katika maendeleo ya viwanda vya usafiri wa anga, hasa katika kubuni na kuunda ndege zisizokuwa na rubani.

Wakati huo huo Iran leo imezindua chanjo iliyotengenezwa hapa nchini katika sherehe iliyohudhuriwa na Rais Hassan Rouhani.

Chanjo hiyo ya watoto ina uwezo wa kukinga magonjwa matano hatari ambayo ni pamoja na Homa ya Haemophilus-B, Kifaduro, Pepopunda, Hepatitis B na Dondakoo.

Maafisa wa Iran wamesema wana uwezo wa kuzalisha asilimia 60 ya chanjo zinazohitajika nchini humo.

Shirika la Afya Duniani WHO, limeitaja Iran kuwa nchi iliyofanikiwa zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati katika kuwapa watoto chanjo ya ugonjwa wa kupooza, Polio. (www.almanar.com)

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameunga mkono juhudi za kuundwa nchi huru ya Palestina.

Akihutubia vyombo vya habari, Ban Ki-moon, amelaani j inai zilizofanywa na majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vya siku 50 katika eneo la Ukanda wa Gaza na kusisitiza juu ya umuhimu wa kuungwa mkono kimataifa kukarabatiwa eneo hilo.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali mapigano yanayoendelea huko Baitul Muqaddas hasa suala la kuvunjiwa heshima matukufu ya Waislamu katika eneo hilo takatifu.

Ameongeza kuwa, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zilizoghusubiwa licha ya kuwa si wa kisheria, bali unazuia pia kupatikana amani na utulivu katika eneo hilo.

Wakati Katibu Mkuu UN akitaka kuundwa Taifa huru la Wapalestina, Misri kwa upande wao wanakoleza kitanzi cha mzingiro kwa Wapalestina hao.

Hii ni kutokana na kitendo cha Jeshi la Misri kutangaza kuwa limeharibu njia za chini kwa chini zaidi ya elfu moja na mia nane zinazounganisha eneo la mpaka wa nchi hiyo na Ukanda wa Ghaza.

Taarifa ya jeshi la Misri imedai kuwa, hatua hiyo imechukuliwa ili kuzuia kile kinachodaiwa kuwa ni kuingia makundi ya wanamgambo wa kigaidi nchini humo.

Jeshi la Misri l inadai kuwa makundi 13 ya kigaidi yakiwemo ya Answar Baitul Muqaddas, al Qaeda na mengineyo yamekuwa na harakati za kuingiza silaha nchini humo, kwa lengo la kutoa mafunzo kwa wanamgambo wa makundi hayo waliomo ndani ya ardhi ya Misri.

Naye Majidi al Basyuni, Naibu Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani wa Misri ameeleza kuwa, maeneo ya Sinai yamekuwa yakitumiwa na makundi ya kigaidi yanayofanya njama za kutaka kujitenga na ardhi ya Misri.

Moon aunga mkono kuundwa taifa huru la Palestina

Michael Brown (picha ndogo) aliyeuawa na askari wa Marekani (mwenye picha kubwa).

Iran yazindua drone nyingine

6 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014Makala

KATIKA ngazi za kitaaluma, mwanataaluma wa Chuo Kikuu anayefanya kazi yake ipasavyo na kwa weledi, anaweza kupanda kufikia ngazi ya Profesa Mshiriki (Associate Professor ) katika kipindi cha miaka 9 tangu aajiriwe Chuo Kikuu. Aidha, inamchukua miaka 3 zaidi kufikia ngazi ya Profesa Kamili (Full Professor ). Inapotokea mwanataaluma akajinadi kuwa kafundisha Chuo Kikuu zaidi ya miaka 38 na wakati huo huo akabakia kama Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecturer), basi hii ina tafsiri mbili tu, kwamba mhusika ni dhaifu sana au mvivu mno.

Ni kweli kwamba kuna fani ambazo ni vigumu kufanya utafiti na kuandika machapisho yanayoweza kumpandisha mtu kufikia ngazi za uprofesa katika kipindi kifupi. Tafiti nyingine huchukua muda mrefu na ni za gharama mno. Hata hivyo, tafiti hizi si zile za sayansi ya siasa (Political Science). Huhitaji fedha nyingi wala muda mrefu kufanya utafiti na kuandika machapisho yanayohusu hali ya siasa nchini. Inatosha kusikiliza redio na kuandika paper. Huo ndio ukweli!

Nimelazimika kuanza na utangulizi huu ili kuweka bayana upotoshaji unaofanywa na baadhi ya wanataaluma ambao hujiita wataalam na wachambuzi wa siasa, kupitia vyombo mbalimbali vya habari huku wakijua wazi kuwa uwezo wao kitaaluma ni mdogo. Vyuo Vikuu vyote duniani vinaongozwa na kauli mbiu ya “You either publish or you perish” yaani andika/chapisha au ufe kitaaluma. Kimsingi, mwanataaluma ambaye haandiki au kuchapisha ni mfu kitaaluma.

Kwa bahati mbaya sana, baadhi ya watu waliokufa kitaaluma kutokana na kutokuandika machapisho kwenye majarida ya kimataifa wameona njia bora ya kuwalaghai Watanzania kuwa ni wakali kitaaluma, ni kukimbilia kwenye vyombo vya habari na kujifanya wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii. Jiulize, huo uchambuzi kwa nini wasiupeleke kwenye majarida ya kimataifa? Ni wazi kuwa hawawezi kuthubutu kwa kuwa wanajua kuwa uchambuzi huo ni dhaifu, hauna viwango na hauwezi kukubalika.

Dr Benson Bana ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwanataaluma h u y u m z e e n i m i o n g o n i mwa watu wanaopenda sana kuonekana kwenye vyombo vya habari wakifanya kile wanachodai wenyewe kuwa ni uchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii. Hata

Dk. Bana, ni udini tu au udhaifu wako kitaaluma?Na Majidi Mussa Kimaro, Arusha hivyo, mara nyingi uchambuzi wa

mwanataaluma huyu umekuwa ukikosolewa na watu wengi katika jamii kutokana na kulalia upande mmoja au kukosa hoja zenye mashiko.

Katika mtandao mmoja wa kijamii, mmoja wa wachangiaji aliwahi kuandika hivi kumhusu Dr Bana:

“Mtu kama huyu Benson katika nchi ni hatari sana kuliko watu wanavyotambua. Huyu ni mropokaji anayefundishwa au kujipendekeza ili aendelee k u t i m i z a m a l e n g o y a k e y a k i p r o p a g a n d a k a m a anavyotumwa na '---'. Report zake ni za kuegemea mlengo wa chama kilicho madarakani na siku zote ametoa report sizizoungwa mkono na sehemu kubwa ya jamii yetu, labda wasomi anao wadanganya kwa ufundishaji wake. Si mchambuzi mkweli. kwa umri wake ni janga kwa wasomi wadogo wanaomtizama. Simply said benson is a ccm puppet.”

M c h a n g i a j i m w i n g i n e akaandika: “Jamaa nilimsikiliza na nikamshangaa mpaka mwanangu akaniuliza....Baba unafikiri nini? Ama kweli jamaa ni janga kwa wanafunzi wake na Taifa letu.”

Mwingine naye akaandika hivi: “Kimsingi nimekuwa nikitilia shaka wakati wote uchambuzi wa huyu dk. Kumbuka tafiti zenye kuhusu mvuto wa viongozi, hata maoni yake juu ya kujivua gamba kwa RA ni utata mtupu. Nashukuru kwa taarifa kwamba m d a u n i m we n ye m l e n g o wa CCM, hivyo nimetambua ni kwanini uchambuzi wake unaonekana kubeba upande mmoja na kuponda mwingine kiaina. Hatari sana kwa wasomi kama hawa kutosimamia kweli. Wakati utawaumbua.”

Mwingine akamkejeli Dr Bana: “Uchambuzi wa BANA utadhania ni uchambuzi uliofanywa na bibi (nyanya) yangu kule kijijini ITIMBI.”

Dr. Bana ni mwalimu wangu. Hata hivyo, naomba nikiri kuwa sikuwahi kumwelewa hata siku moja katika ufundishaji wake! Ufundishaji wake zaidi ulikuwa wa ubabaishaji. Huwezi kumweka Dr. Bana katika kundi la magwiji kama kina Profesa Issa Shivji, Haroub Othman, Mwesiga Baregu na hata wanafunzi wake kama kina Dr. Bashiru Ali. Na hii ndio sababu sishangai kuwa kwa nini katika kipindi cha miaka 38 anayodai kufundisha Chuo Kikuu ameshindwa kusogea kutoka ngazi moja hadi nyingine.

Maoni ya Dr. Bana kufuatia waraka wa Wizara ya Elimu wa tarehe 11 Novemba 2014 uliotaka wanafunzi katika vyuo vikuu kupewa haki yao ya kikatiba ya kufanya ibada kwa siku za Ijumaa

na Jumamosi kama ilivyo kwa siku za Jumapili, ni ushahidi mwingine juu ya uwezo mdogo wa Mhadhiri huyu katika kupambanua mambo. Inaonesha dhahiri kuwa Daktari huyu ni mvivu wa kujenga hoja na anasukumwa zaidi na chuki, choyo na hisia badala ya kuzingatia ukweli na uhalisia wa mambo.

Katika kupinga waraka wa serikal i Bana anadai kuwa wanafunzi wake siku za Ijumaa na Jumamosi hawezi kuwakatalia kwenda kuabudu. anaongeza “Hili si suala la Serikali kutoa waraka – ni la mwafaka kati ya mwalimu na mwanafunzi.”

Inawezekana kwamba Mwalimu wangu Bana amebadilika siku hizi (tofauti na ninavyomfahamu mimi) - kwamba siku hizi anajali haki ya wengine kuabudu kama yeye.

Hata hivyo, kama si kwa makusudi, basi mwalimu wangu amekurupuka. Hakusoma waraka husika na kujua chimbuko lake. Kwamba kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanafunzi na viongozi wa dini kwamba wananyimwa haki ya kuabudu. Shughuli za masomo ikiwemo mitihani inapangwa kwa makusudi nyakati za Ibada. Mahafali katika vyuo vingi yanaanza saa sita siku za Ijumaa na maombi ya kubadili hali hii yamekuwa yakigonga mwamba! Hoja kwamba yeye anawaruhusu wanafunzi wake kuabudu haiwezi kumaliza tatizo. Je; ruhusa ya Bana pekee ndio suluhu ya ubaguzi

wa kidini unaofanywa dhidi ya baadhi ya wanafunzi Tanzania?

Ningemuelewa vizuri sana Dr. Bana kama angechukulia changamoto hii kama eneo la utafiti ili kupata ukweli juu ya utekelezaji wa haki ya kuabudu vyuoni badala ya kukurupuka na hoja zilizochoka.

Bana anadai kuwa eti “Serikali inachokoza jambo ambalo tayari lina utamaduni wake. Kwamba inapotoa mwongozo maana yake inafanya wengine nao wadai.” Anaongeza kuwa eti “kinachofanywa sasa ni kutoa jini kwenye chupa.” Sielewi kwamba Bana anakusudia nini anaposema utamaduni wake. Utamaduni upi? Wa kuwanyima uhuru wa kuabudu baadhi ya watu? Hivi kuna tatizo gani serikali kukumbusha taasisi zake kufuata sheria na taratibu kwa kuwapa wananchi haki zao za msingi? Leo Serikali ikitoa waraka kukemea rushwa na uzembe kazini, Bana atadai kuwa jini anatolewa kwenye chupa kwa kuwa tayari kuna utamaduni wa rushwa?

Bana anaonyesha chuki za wazi dhidi ya waislamu anapodai kuwa “Haya mambo yanaweza kuibua hisia za makundi kama ya Waislamu wenye msimamo mkali kuibuka na kudai Ijumaa isiwe siku ya kazi. Watataka wapumzike kama wenzao wanaopumzika Jumapili, ndio maana nasema hili jambo halipaswi kuingiliwa na serikali, liachwe walimu na wanafunzi wenyewe waone

PROFESA Issa Shivji.

Inaendelea Uk. 7

7 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014Makala

Dk. Bana, ni udini tu au udhaifu wako kitaaluma?Inatoka Uk. 6namna ya kulitekeleza.”

Huo ni uchambuzi wa mtu mwenye PhD! aliyefundisha Chuo Kikuu kwa miaka 38! Hawezi kuona kwamba hapa hana hoja zaidi ya ubaguzi wa wazi na chuki iliyotamalaki! Kwani hamna Wakristo wenye siasa kali? Kama si unafiki, mtu mwenye chuki kama huyu kweli atamruhusu Muislamu akafanye ibada? Hivi dawa ya kuzuia mtu asidai kitu ni kuhakikisha kuwa unamkandamiza na kuhakikisha kuwa hapati haki yake ya msingi? Kwa hoja kiwete kama hizi, hivi ni jarida (Journal) lipi litakubali paper (maandiko) ya Dr Bana?

Dr Bana anauliza “mbona miaka kumi iliyopita haya mambo hayakuwepo?” Eti hakumbuki Waislamu kudai jambo hili! Kama ni kweli kwamba Bana hakumbuki, basi ni dhahiri kwamba akili yake imechoka kiasi kwamba kuendelea kwake kubaki Mlimani huku akilipwa mshahara ni kitendo cha kuliibia taifa. Madai ya wanafunzi Waislamu kuruhusiwa kufanya ibada ni ya kihistoria, lakini yamekuwa yakipuuzwa bila sababu za msingi.

Hata hivyo, ni kujidhalilisha pale msomi wa PhD anayejifanya mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii anapotaka kutuaminisha kuwa hatutakiwi kushughulishwa na mambo ambayo hayakuwepo siku za nyuma. Kwa hoja yake anataka tuamini kwamba hata yeye anajishangaa kuvaa viatu kwa kuwa miaka 50 iliyopita

mguu wake ulikuwa haujui kiatu! Kwamba anashangazwa na mchakato unaoendelea wa katiba kwa kuwa haukuwepo miaka kumi iliyopita! Hii ndiyo hoja ya msomi kweli? Kwa hoja mfu kama hizi, kwa nini asibaki kwenye ngazi moja ya kitaaluma kwa zaidi ya miaka 20?

Namheshimu sana Mwalimu wangu Dr Bana. Hata hivyo, s i t a m t e n d e a h a k i e n d a p o sitamkumbusha kuwa anapwaya mno kitaaluma, na kwamba pengine alipotea njia na kujikuta katika fani ya uwanataaluma. Ndio maana hata wanafunzi wake wengi aliowafundisha wako mbali katika ngazi za taaluma kulinganisha naye. Pengine anaamini kuwa maoni yake kupitia vyombo vya habari yanamjengea umaarufu. Ukweli ni kwamba maoni haya yanammaliza na kuanika udhaifu wake mbele ya jamii. Kwa hali hiyo itabidi mwalimu wangu aendelee kusherehekea miaka 30 ya kuwa mhadhiri mwandamizi mkongwe zaidi hapa Tanzania.

Mwisho, kama mdau naunga mkono hatua ya wizara kutoa waraka unaoelekeza vyuo vikuu kuzingatia haki na uhuru wa watu kuabudu. Haiwezekani wakati Taifa linalia na mmomonyoko wa maadil i , wawepo watu wanaowanyima raia wengine uhuru wa kuabudu. Hamna dini inayoruhusu ufisadi, rushwa, wizi, ulevi, umalaya, uuaji nk. Na haya ndiyo maradhi makubwa yanayolisumbua Taifa letu.

H I S T O R I A z a d i n i , zinatufahamisha kuwa, kila Mwenyezi Mungu alipoleta Mtume au Mitume, (Manabii), waharibifu chini ya ibilisi wali ingil ia kat i kuharibu miongozo ya Mwenyezi Mungu aliyopitishia kwa Mitume hao. Baada ya uharibifu huo, Mwenyezi Mungu alituma mjumbe mwingine. Na kama vile mlezi wa mototo, humwanzisha mtoto shule kwa darasa la kwanza nakuendelea, ndivyo Mwenyezi Mungu alivyowaletea wanadamu ujumbe kulingana na nyakati zao.

Ujumbe wa Nabii Musa a.s ulivurugwa mara nyigi, na wavurugaji waliamini kuwa wataufuta kabisa, ili sheria zao ziwe ndizo zinazo tawala. Mfano mdogo ni wa mfalme wa Ugiriki na wa Rumi waliotaka imani zao ndio zitawale. Ni pamoja na wana wa Israeli kuibadilisha Torati na kutengeneza kitabu chao cha Talmudi. Hiyo ndiyo maana Nabii Isa (Yesu) A.S. akawa hakusomeshwa katika chuo chochote, bali Mwenyezi Mungu alimjuvya el imu i l iyokuwa katika Torati na ndiyo maana hakupewa kitabu, bali alipewa Injili (Mahubiri) yaliyotoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia kichwani kwake:

“Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyafuati mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.” (Yohana 5:30.)

Waandishi, Mafarisayo na Masadukayo, walishtuka na kukasirika baada ya kuona kuwa anawahubiri sheria zile zile za Torati ambazo waliamini wamezivuruga sana, kwa kuwa alikuwa akiwaambia kuwa:

“Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au Manabii la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amini, nawaambia, m p a k a m b i n g u n a n c h i zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya Torati haitaondoka, hata yote yatimie.” (Mathayo 5:20.)

Ndiyo maana wakapanga mbinu za kumwuuwa mapema tu baada ya kukabidhiwa Utume akiwa na miaka 30 kwa kuwa walihofia kua akiendelea kuishi wataumbuka. Na kwa kuwa Yesu hakuwa na kitabu, mahubiri yake ya miaka mitatu hayakuandikwa akiwepo, wakiamini kuwa wakimuuwa mafundisho yake yatakuwa ndio mwisho:

“Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi. Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini ; na Warumi wa t a k u j a , wa t a t u o n d o l e a

Huyu mnyama kutoka ardhini mnyama gani?Na Khaitib Juma Mziray mahali petu na taifa letu. Mtu

mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani mkuu mwaka ule, akawaambia, ninyi hamjui neno lolote wala hamfikiri yakwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa nzima.” (Mathayo 11:40-50)

“ H a p o B w a n a Y e s u a l i p o s u l i b i wa , i l i d h a n i wa kwamba dini ya Kikristo hapana budi itakoma mara moja. Yeye Kristo alikuwa hakuwaachia wanafunzi wake chuo chochote alichokiandika, wala Imani (Creed) yoyote aliyoitengeneza.” (Historia ya Kanisa, cha Canon H.J.E. Butcher, uk. 1.)

Ndiyo maana, ile dhana hiyo ya kufutika mafundisho ya dini itokayo kwa Mwenyezi Mungu ikamilike, Paulo alipewa kazi ya kuwasaka wale wanafunzi wa Yesu ili wauawe wasije wakaendeleza yale mafundisho yake. Wa kwanza kuuawa, ni Stefano; wanafunzi wakatawanyika na kukimbilia nchi za jirani, Paulo akaomba kibali cha kwenda kuwasaka:

“ L a k i n i S a u l i ( Pa u l i o ) , akazidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana (Yesu), akamwendea Kuhani Mkuu, akataka apewe barua za kwenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, i l i akiona watu wa njia hii (wanaofuata mafundisho ya Yesu), waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.” (Matendo. 9:1-2.)

Biblia na historia ya Kanisa, vinatuonesha kuwa, mwanafunzi wa Yesu a l iyei twa Yohana M t a k a t i f u , wa l i s h i n d wa kumwuwa; au ni kwa mipango ya Wa r u m i , Wa ya h u d i n a Wagiriki hicho ni kizungumkuti, maana kazi kubwa ya mambo yanayoihangaisha dunia hii, yal ipangiwa huko, na dini iliyokusudiwa, ikaanzishiwa huko, kama nilivyo nukuu hapo juu. Na yule mwuwaji mkuu wa wanafunzi wa Yesu, akawa ndiye mkufunzi mkuu. Na injili zake zikawa ndizo za kwanza kutolewa na kufundishia dini:

“Bali, kinyume cha hayo, walipoona yakuwa nimekabidhiwa Injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa;…” (Galatia 2:6-10.)

“Ndugu zangu, nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwanadamu, hata hivyo l ik i isha kuthibi t ika , hakuna mtu alibatilishaye, wala kuliongeza neno.” (Gal 3:15)

Paulo amewaandikia wafuasi wake huko Glatia mnamo mwaka wa 57, A.D. yeye akiwa Efeso au Makedonia. Utangulizi wa barua kwa Wagalatia; Biblia ya Imprimatur.

“Mkumbuke Yesu Kris to aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo Injili yangu.” (1.Timotheo 2:8.)

Paulo amemwandikia Timotheo mwaka wa 65, A.D. akiwa Rumi, na ndizo zilizo fundishia Ukristo kabla ya hizi Injili nne tunazoziona katika Biblia hivi leo.

Injili na Ufunuo wa Yohana viliandikiwa gerezani, katika visiwa vya Patimo Yohana akiwa gerezani. Sina hakika kuwa, mfungwa huyu aliyeshindikana kuuawa kwa lengo la kufuta mafundisho ya Yesu; ilitokea nini askari wamruhusu kuandika yale yaliyokuwa yamekataliwa, na waandishi , Mafarisayo, Masadukayo na Makaisari wa Ugiriki na Rumi. Lakini ngoja waandishi watusaidie:

“Wanafunzi wengi hudhani ya kwamba kitabu hiki kiliandikwa kwenye mwaka wa 95 (A.D.) na Yohane Mtume, alipohamishwa na wakubwa wa Dola katika k i s i wa k i i t wa c h o Pa t m o . Wengine husema yakwamba hakikuandikwa na Yohane mwenyewe, ila mfuasi wake fulani. Sababu ni kwamba lugha

ni tofauti na lugha ya Injili, ijapo mawazo ni ya Yohane. Wengine husema ya kwamba kitabu kiliandikwa na Yohane akisaidiwa na karani ambaye hakutawala sana lugha ya Kigiriki.”

Utangulizi wa Ufunuo wa Yohane; Bibli ya Imprimatur.

Ufunuo huu umebeba madhila mengi , yal iyo, yanayo na yatakayoikumba dunia hii, iwe ni kwa maana halisi ya Ufunuo, au kwa ufunuo wa kupangwa kwa ajili ya kuwadhulumu wanadamu na kuwaangamiza viumbe kwa jumla, chini ya kivuli cha dini:

“Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, lilikuwa na vichwa saba na pembe kumi,…nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi na Shetani.” (Ufunuo 12:1-17)

“Kisha nikaona mnyama alitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.” (Ufunuo 13:1-4)

Itaendelea toleo lijalo

8 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014Makala

NINGEPENDA kuanza kwa kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu wale waliodhulumiwa uhai wao kwa kupigwa risasi katika tukio la mwishoni mwa wiki kule Kenya. Katika tukio hilo tunaambiwa kuwa watu wanaodhaniwa kuwa ni magaidi waliteka basi na kuuwa watu 28.

Aidha, nawapa pole wale ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu ambao wamekatizwa uhai wakiwa safarini kuelekea Nairobi. Taarifa za vyombo vya habar i z ina fahamisha kuwa basi lililokuwa likielekea Nairobi, lilipofika katika mji wa Mandera, ulio mpakani na Somalia, lilivamiwa na kutekwa na watu wenye silaha. Taarifa zaidi zinadai kuwa watekaji hao waliwatenganisha Waislamu na Wakristo kisha wakawauwa Wakristo 28, waliokuwa kati ya abiria 60 wa basi hilo.

Waliwajua vipi Wakristo? Baadhi ya vyombo vya habari vikasema kuwa waliwataka watu wote watamke Shahada mmoja mmoja, walioshindwa wakatambulika kuwa ni Wakristo. Magazeti mengine yakasema kuwa abiria waliambiwa kusoma Qur’an, walioshindwa kusoma japo sura au aya yoyote, wakatambulika kuwa sio Waislamu.

“The hijackers demanded the 60 passengers aboard recite the Shahada, a tenet of Islam. The 28 -- 19 men and nine women -- who were unable to recite the passage where shot to death.” (Agence France-Presse reported)

Wakati AFP wakisema kuwa abir ia wali takiwa kutamka Shahada, BBC wao walikuwa na haya ya kusema:

“Gunmen separated out non-Muslims by asking passengers to read from the Koran, officials and witnesses said. Those who failed were then shot in the head.”

Ripoti ya polisi Kenya ni sawa na ile ya AFP ambapo Mkuu wa Pol is i , David Kimaiyo, alisema kuwa waliouliwa ni wale walioshindwa kutamka Shahada.

Taarifa ya haraka haraka ya polisi, wanasiasa na vyombo vya habari, zilidai kuwa wahusika wa shambulio hilo ni ‘Mujahidina’ wa al-Shabab, wengine wakisema ni ‘magaidi’ wa al-Shabab.

Sababu zilizotolewa ni mbili, moja ni kwamba pamoja na ile sababu ya siku zote kwamba wanafanya mashambulizi hayo kulipiza kisasi kutokana na hatua ya serikali ya Kenya kupeleka jeshi Somalia, lakini sababu nyingine imeta jwa kuwa wanal ipiza kisasi kwa tukio la wiki iliyopita ambapo polisi walivamia Msikiti Mombasa, wakauwa kijana mmoja na kuwakamata wengi kwa mamia. Katika operesheni hiyo, iliyomalizika kwa kupigwa kufuli misikiti minne na kuwa marufuku kupiga Adhana na kuswali au kufanya Ibada yoyote katika Misikiti hiyo, polisi walidai kuwa

Wanasiasa, magazeti wanapandikiza ugaidi

Wabaya kuliko watuhumiwa ugaidiTujifunze kutoka Kenya na ATPU yaoKama tukifuata nyayo zao, tumeangamia

Na Omar Msangi

wamekamata shehena kubwa ya silaha msikitini.

K wa u p a n d e wa k e R a i s

Uhuru Kenyatta amesema kuwa wanachotaka magaidi hao wa al-Shabab ni kupandikiza vita

ya kidini baina ya Waislamu na Wakristo. Na hiyo ni kutokana na jinsi walivyoendesha shambulio hilo kwamba waliwalenga abiria Wakristo tu.

Kwa upande mwingine baadhi ya vyombo vya habari vikadai kuwa al-Shabab wamedai katika mtandao wao kwamba wanauwa Wakristo kwa sababu walifurahia kitendo cha polisi kuvamia Misikiti na kuifunga.

Taarifa ya serikali ya Kenya imesema kuwa harakati za kuwasaka na kuwaangamiza washambuliaji hao zinaendelea na kwamba jeshi la Kenya limefanikiwa kushambulia na kuangamiza baadhi ya kambi za magaidi ambapo al Shababu 100 wameuwawa. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa ya Makamo wa Rais wa Kenya William Ruto.

Hata hivyo inadaiwa kuwa msemaji mmoja wa al-Shabab aliyetajwa kwa jina la Abdi Aziz Abu Mus'ab, amekanusha madai hayo ya Ruto na kusema kuwa ni uwongo mtupu.

"Our mujahedeen are safe and didn't face any attack whatsoever after the successful operation they carried out by the grace of Allah," amenukuliwa Mus'ab akidaiwa kuongea na Al Jazeera.

Kwa upande wake serikali ya Marekani haraka haraka ililani shambulio hilo na kusema kwamba ipo pamoja na Kenya katika kupambana na magaidi wa al-Shabab.

"The United States condemns in the strongest terms today's horrific attack in Kenya by the terrorist group al-Shabab against innocent civilians."

Alisema Bernadette Meehan ambaye ni msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa (National Security Council) la Marekani.

"The United States stands with our Kenyan partners in the effort to counter the threat of terrorism and affirms our ongoing commitment to working with all Kenyans to combat these atrocities."

Bibie Bernadette Meehan, aliongeza katika taarifa aliyoitoa huko Washington.

Kinachoelezwa katika habari hii kwanza ni kufahamishwa juu ya kuwepo magaidi wa al-Shabab na pili juu ya ubaya wao na ukatili wao. Na hilo huelezwa kupitia tukio lao la kuuwa abiria 28. Lakini katika hilo kuna kitu kinapandikizwa, sio tu kwamba magaidi hao ni Waislamu, lakini magaidi wanaolenga kuwaangaza Wakristo na hivyo kuchochea vita ya kidini, baina ya Waislamu na Wakristo.

Taarifa hizi zinatufahamisha pia jinsi serikali ya Kenya ilivyojizatiti kupambana na magaidi wa al-Shabab, lakini pia jinsi Sekali ya Marekani inavyoguswa na jambo hili na azma yake ya kushirikiana na Wakenya katika kupambana na magaidi.

Yapo mambo kadhaa hapa ya kutizama. Kwanza ni kuwa yapo makosa makubwa yamefanywa

Inaendelea Uk. 9

TAARIFA za wiki hii kutoka Nigeria zinafahamisha kuwa washambuliaji wawili wa kike wa kujitoa muhanga (suicide bombers), walilipua bomu katika soko lililojaa watu katika mji wa Maiduguri, na kuuwa kwa uchache watu 45.

Taarifa ya Shirika la Habari la AFP ikidai kunukuu mashuhuda waliokuwa eneo la tukio ilidai kuwa wasichana wadogo chini ya miaka 20 waliokuwa wamevalia hijabu walijilipua katikati ya watu sokoni hapo.

Japo hakuna kikundi hadi sasa kilichodai kuhusika na shambulio hilo, vyombo vya usalama vya Nigeria vinadai kuwa watuhumiwa watakuwa ni Boko Haram.

Tukio hilo linakuja baada ya miaka mingi kwa serikali ya Nigeria na vyombo vyake vya dola kutangaza hatua kali za kupambana na Boko Haram, lakini pia na kuwekewa bajeti kubwa ya

Wataalamu wa kupambana na magaidi watatuangamiza

Na Omar Msangi msaada kutoka Marekani kwa ajili hiyo.

Shambulio hilo linakuja pia wakati mji huo na Jimbo zima la Borno lipo chini ya hali ya hatari (state of emergency) kutoka Mei mwaka jana.

“US Government Sent Nigeria $20 Million To Fight Boko Haram Since 2012”, hiyo ni taarifa ya mwandishi Clement Ejiofor, ambaye anaeleza kuwa mwaka 2012 serikali ya Marekani ilitoa Dola milioni 20 sawa na Naira (pesa ya Nigeria) bilioni 176 (N3.176 billion) kwa ajili ya kusaidia polisi, idara za usalama na jeshi kupambana na Boko Haram.

Bajeti hiyo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, lakini zaidi ikiandamana na mafunzo ya kijeshi na kikachero, yakiwemo mazoezi ya pamoja na uundaji wa vikosi maalum. Hata hivyo, sote hali tunaiona. Kama ilivyo kwa Yemen, Pakistan na Afghanistan, msaada huo haujaweza kuondoa

Inaendelea Uk. 9

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta. MAKAMU wa Rais William Ruto

9 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014Makala

Wanasiasa, magazeti wanapandikiza ugaidi

Inatoka Uk. 8huko nyuma na wanasiasa wetu, ambayo ndiyo yanayopelekea kupandikiza kitisho katika nchi zetu. Na kikishapandikizwa, kikakubalika kwamba kipo, hizi kauli za polisi, jeshi, Rais wa nchi kwamba ‘tutapambana vikali na magaidi’, ni kauli za bure tu. Hazina maana yoyote. Kadiri watakavyojidai kupambana, ndivyo na ugaidi wenyewe utakavyoongezeka. Mfano wala haupo mbali, upo kwa Goodluck Jonathan na Boko Haram yake.

Aliwahi kusema aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Robert Finlayson "Robin" Cook , kwamba, al-Qaida ni magaidi wa kubuni na wa kutumiwa na mabeberu kwa malengo yao. Mabeberu wakiacha mkakati huo wa kutumia magaidi katika mipango yao, na ugaidi unaporomoka siku hiyo hiyo. Huo ndio ukweli. Sio kwa ATPU au jeshi la Kenya kukaza buti kupambana na magaidi.

Nigeria walikaza sana buti toka Boko Haram walipokuwa wakidaiwa kuwa wanarusha mabomu ya mafuta ya taa na baruti za kutengeneza kienyeji, sasa wana magari ya kivita na mizinga ya kutungulia ndege! Swali ni je, wamezipata wapi silaha hizi? Zimetoka wapi na zimeingia vipi Nigeria hadi kuwafikia?

Al-Shabab halikuwa tatizo la Kenya, Uganda, TanzaniaInafahamika wazi kuwa pamoja

na matatzo waliyokuwa nayo Somalia, vita vyao havikuwa tatizo la Kenya, Uganda, Zanzibar wala Dar es Salaam, ukiacha tatizo la wakimbizi kama walivyo wale kutoka Rwanda, Burundi na Congo DRC. Inafahamika pia kuwa juhudi zote za inayoitwa Jumuiya ya Kimataifa kuleta amani Somalia, zilikwama. Na inafahamika kuwa ni Wasomali weyewe hatimaye waliofanikiwa kurejesha amani kama CCM na CUF walivyofanikiwa kuleta muafaka Zanzibar ikatulia, wakati huko nyuma miafaka yote iliyopata baraka na iliyosimamiwa na serikali ya muungano na ile Jumuiya ya Kimataifa, ikasainiwa kwa mbwembwe ilikwama.

Ni jambo linalofahamika wazi pia kwamba hawa ‘wanaotoa machozi kuwalilia Wakenya waliouliwa’ na wanaosema kuwa watakuwa bega kwa bega na Kenya kupambana na magaidi, ndio waliovuruga amani iliyochipua Somalia na ikawa ndio sababu ya kuibuka al-Shabab. Lakini inafahamika wazi pia kuwa ilikoanzia al-Shabab, ni wananchi wa Somalia waliokuwa wakipinga serikali waliyoita kibaraka iliyoweka na wale walioondoa serikali yao ya umoja iliyoweza kurejesha amani na usalama Somalia.

Lakini kilichotokea ni kuwa wakati al-Shabab na serikali ya mpito (Transitional Federal Government-TFG), ilikuwa ni

tatizo la Somalia, tukasomeshwa na mabeberu kuimba kuwa al-Shabab ni magaidi wanaohusiana na a l -Qaidah. Tukaupokea

wimbo tukaimba kwa juhudi na mbwembwe nyingi bila maarifa wala kutumia akili japo kidogo. Matukio yakapatikana ya kudaiwa

kuthibitisha hilo.

Shambulio la WestgateShopping Mall Nairobi

Yapo matukio mengi ambayo ilidaiwa kufanywa na magaidi wa al-Shabab likiwemo lile shambulio la Kampala tarehe 11 Julai, 2010 ambapo watu 74 walikufa na wengine 70 kujeruhiwa wakati wapenzi wa mpira wakitizama mechi za kombe la dunia. Lakini hayo tuyaache kwanza tutizame la Westgate Shopping Mall, Nairobi. Tuliambiwa magaidi kati ya 10 na 15 kutoka Somalia waliigia Kenya wakiwa na gari lililosheheni silaha wakaingia katika kituo hicho maarufu cha kibiashara na kuanza kuuwa watu. Walivamia tarehe 21 Septemba 2013, na kudumu katika jengo hilo hadi 24 Septemba ambapo ilidaiwa kuwa watu 67 waliuliwa na wengine zaidi ya 175 kujeruhiwa.

Polisi, vikosi maalum vya polisi, Idara za Usalama za Ndani na Nje ya Kenya na jeshi la Kenya, wote hao walikuwa katika operesheni ya kukabiliana na ‘magaidi’ hao 15 kutoka Somalia! Vifaru na silaha nyingine nzito za kijeshi, vikaonekana vikiranda na kuzingira Nakumati. Na tunaambiwa kuwa kituo hicho cha kibiashara kinamilikiwa na raia wa Israel. Lakini pia wapo Wayahudi kwa uchache wanne ambao wamekodi katika jengo hilo wakiendesha migahawa. Zaidi ni kwamba, Kenya ina makubaliano na Israel ya kiulinzi na hivyo makachero wa mwanzo kuingia katika operesheni hiyo ya kukabiliana na ‘magaidi’ 15 kutoka Somalia, walikuwa makachero wa MOSSAD. (Tazama: International Business Times)

Hata hivyo, vikosi vyote hivyo havikufanikiwa japo kukamata au kuuwa hata gaidi mmoja na kuonyesha mai t i yake ! Magaidi wakafanya waliyofanya, wakajiondokea zao wakaacha h u k u n y u m a w a n a j e s h i , serikali na wananchi wa Kenya, wakiparurana kuwa badala ya kupambana na magaidi, wanajeshi walikuwa wakipora mali na kulewa. Picha zikasambazwa k u o n y e s h a w a l i c h o k u w a wakifanya wanajeshi hao wakiwa ndani ya Nakumati. (Pflanz, Mike. "Kenyan army admits that soldiers looted Westgate during siege". London. Retrieved 29 October 2013.)

Taarifa za kuingia magaidi Nakumati, Westgate, Nairobi, zilipambwa na kusindikizwa na visa vyingi vilivyonogeshwa zaidi na vyombo vya habari vikiwa vile vilivyopigiwa zumari kuonyesha jinsi ‘magaidi’ hao al-Shabab walivyokuwa katili kwa Wakrsito. TV na magazeti yakaandika na kupamba kwamba magaidi hao walikuwa wakiwapa mateka wao mtihani, anayefaulu kuthibitisha kuwa ni Muislamu anaachwa, a n a ye f e l i a n a p i g wa r i s a s i

Wataalamu wa kupambana na magaidi watatuangamizaInatoka Uk. 8tatizo la ugaidi wa Boko Haram. Inakuwa kana kwamba kila unapopewa msaada zaidi, ndio ugaidi unavyoongezeka na magaidi kuwa na uwezo mkubwa zaidi.

Tuliambiwa kuwa kule Iraq walitumia “Salvador Option” na tunafahamu kilichotokea pale walipokamatwa makachero wawili wa Uingereza wakijifanya ni magaidi wa Mehdi Army wa kujitoa muhanga. Hakuna namna nyingine unaweza kuelewa kitendawili hiki cha Boko Haram, zaidi ya kutizama uhusiano wa ugaidi wa Iraq na matukio hayo ya “Salvador Option”.

Kule Mombasa tumeambiwa kuwa polisi walivamia msikiti kwa sababu kulikuwa na taarifa za ki-intelijensia kuwa kuna silaha na watu wanaojifunza ugaidi. Ukifanya harakati kama zile, kwa maana ya kuvamia msikiti na kisha kuufunga na kupiga marufuku watu kuswali, jambo ulilo na uhakika nalo ni kuwa litazuka zogo na vijana (Waislamu) wanaweza kuja juu kutaka kulipiza kisasi.

Swali ni kuwa kwa nini polisi walifanya harakati ile wakijua matokeo yake?

Lakini mara baada ya tukio hilo, tunaambiwa kuwa magaidi

wa al-Shabab wameuwa abiria 28 Wakristo baada ya kufanya zoezi la kuwatambua wakisafiri katika basi. Na tunaambiwa kuwa al-Shababu hao ambao wamejitaja kama Mujahidina, wanafanya hivyo kulipiza kisasi uvamizi wa misikiti kwa madai kuwa Wakristo walifurahia Waislamu walipovamiwa na polisi. Hapa kuna mambo mawili. Ukisema kuwa waliofanya ni Mujahidina, watu hao hawawezi kuwa Waislamu kwa sababu hakuna mahali popote katika mafundisho ya Uislamu panapo ruhusu jambo hilo kufanyika. Hata kwa kutumia lile tukio la Mombasa kuwa ni hasira, wanalipiza kisasi, bado haipo katika hukumu za Kiislamu.

Lakini ukirudi katika tukio la Mombasa na jinsi lilivyofuatana na hili la kuuliwa abiria na hoja zinazotolewa, na ukizingatia madai ya watu wa Mombasa kuwa polisi wanapandikiza silaha Msikitini, na ukizingatia pia kuwa hakuna Muislamu anayeweza kufanya unyama huo kwa jina la Uislamu, wa kushusha abiria wasio na hatia na kuwapigha risasi za kichwa, tukio hili linakuwa tata kama lile la Westgate. Bali itabidi uchunguzi ufanyike kujua, nani kauwa abiria hawa 28 Wakristo?

Human Rights Watch na Inaendelea Uk. 10 Inaendelea Uk. 10

WATU 28 wanaodaiwa kuuliwa na magaidi nchini Kenya.

10 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014Makala

Wanasiasa, magazeti wanapandikiza ugaidi

Inatoka Uk. 9kichwani. Lakini tukaambiwa pia kuwa hata watoto wadogo wakithibitika kuwa ni Wakristo, walikuwa wakibamizwa vichwa vyao katika ukuta au mikono yao kukatwa ikachongwa na kufanywa kalamu za kuandikia huku damu ikifanywa wino. Vyombo vya habari vikasherehesha sana habari hizi.

K wa h i y o , m p a k a t u k i o l i n a m a l i z i k a , i s h a w e k w a ‘ushahidi’ kuwa wapo magaidi wanaoitwa al-Shabab weye uwezo wa kushinda polisi, Idara ya Usalama ya Kwenya na Jeshi lote la Kenya likipewa msaada kutoka Israel na Uingereza! Lakini maadhali tuliambiwa kuwa walikuwepo makachero wenye silaha nzito wa MOSSAD na wale wa Uingereza (na Marekani?), ni kwamba tukio liliweka muhuri pia kuwa magaidi hao ni hatari mno kiasi kwamba hata wazito hao wa kidunia katika vita na ukachero, hawana ubavu wa kukabiliana nao!

Maadhali ushaweka msingi huo, na maadhali ushakubali kuwa una kitisho hicho cha ugaidi wa kiwango hicho, katika ulimwengu huu wa Vita dhidi ya Ugaidi, yaliyosalia au tuseme yatakayokuja kufanyika baadae ili kuendeleza ‘vita ya wenyewe mabeberu’ dhidi ya ugaidi, wala hutakuwa na udhibiti nayo. Huo ndio ukweli. Ndio pale nikasema kuwa kauli ya Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake William Ruto, wala hazina maana yoyote. Silaha zitaendelea kupatikana Misikitini, iwe ni kwa njia ya kupandikizwa (dubious terrorism sting tactics-Dubious Entrapment ), kwa maana ya kughilibu baadhi ya watu au kuwanunua na kuwafanyisha vitendo vitakavyothibitisha kuwa kuna ugaidi. Na kwa sababu hiyo, matukio yanayodaiwa ya Wakristo kutenganishwa na Waislamu, kisha Wakristo kuuliwa, yataendelea kuwepo.

I le kukubali propaganda kuwa al-Shabab wanaopambana na majeshi ya uvamizi ya Ethiopia yaliyovamia nchi yao na kuweka serikali kibaraka, ni magaidi hatari kwetu; kosa namba moja. Vile tulivyopokea shambulio la Westgate, pamoja na utata wote ulioligubika kama inavyoelezwa katika ile makala ya Jicho Pevu (KTN), kosa la pili la msingi. Mtu anadaiwa kupigwa risasi ya mgongoni, lakini picha inamwonyesha hana damu inayotiririka, bali doa tu jekundu inakodaiwa kupita risasi. Lakini zaidi anatembea. Ajabu ya mambo. Kwa ujasiri mkubwa tv zinaonyesha na magazeti yaliandika na kusherehesha, ikiwa ni pamoja na yule aliyedaiwa kupigwa risasi ya kisigino, lakini soksi haina damu na anatembea mwenyewe!

Kuuliwa Masheikh

Kenya yamefanyika mauwaji

mengi ya viongozi wa kidini. Taarifa za uhakika zinaonyesha kuwa viongozi hao waliuliwa na kikosi maalum cha kupambana na magaidi (Anti Terror Police Unit-ATPU), lakini serikali inasema haijui nani kafanya mauwaji hayo. Au pale wanapokiri kuwa Sheikh kauliwa na ATPU, basi wanadai kuwa ‘Sheikh’ huyo alikuwa gaidi aliyeuwawa wakati akirushiana risasi na polisi, wakati ukweli wa mambo Sheikh huyo alivamiwa nyumbani kwake akapigwa risasi za karibu kichwani. Hata wanawake waliovaa hi jabu wamedaiwa kuwa na silaha na kupambana na polisi!

Kuna na haya ya juzi ambapo baadhi ya watu wanadai kuwa polisi walifanya kupandikiza silaha walizodai kuzikamata msikitini na kisha kuvamia. Na wanaodai haya sio watu wa mitaani tu. Hata ile Tume ya Haki za Binadamu Kenya, imekuja na madai hayo pia na kuonya kuwa matumizi ya njia hizo chafu, zitaiangamiza Kenya.

Hapa kwetu kumekuwa na mtindo, chambilecho, nyimbo m b a ya h a i m b i w i m wa n a . Atasimama mwanasiasa katika jukwaa, iwe la kisiasa au la kidini na kuwafananisha, kwa mfano Masheikh wa UAMSHO na Boko Haram. Au atazungumza katika namna ambayo, anakazia uwepo wa kitisho cha magaidi, iwe al-Qaida au al-Shabab. Katika masiku ya hivi karibuni, ukaja na mtindo mwingine wa kuchochea chuki na uhasama baina ya Waislamu na Wakristo. Tuliwahi kutangaziwa hapa kwamba ulinzi wa polisi utaimarishwa makanisani ili kuwalinda Wakristo wakati wa ibada. Ilimuradi linapandikizwa jambo ambalo katika hali halisi ya maisha mitaani halipo kabisa.

Sasa tuna hiyari, kujifunza k u t o k a K e n ya n a N i g e r i a tusalimike au tukimbilie jahazi linalozama ambalo nadhani wenzetu watakuwa wanataka kutafuta namna ya kutoka kujinusuru, lakini hawaioni.

Walisema wasomi na maprofesa kutoka Nigeria waliokuwa katika ile semina ya Muslim University of Morogoro (MUM), kuwa mkisharuhusu hali kama hii kujengeka, basi mmekwisha kwa sababu yaliyobaki mtakuwa hamna udhibit i nayo. Kila siku watapatikana watu wa kushambulia, kulipua na kuuwa watu, wala hamtajua nani kafanya, ila mtatangaziwa kuwa ni al-Shabab (Boko Haram).

Ser ikal i na vikosi vyake i k i s h a r u h u s u y o t e h a y a yakafanyika, inakuwa kama mnyama aliyekiwisha zingwa na chatu, hana pa kutokea tena.

Hiyo ndiyo ha l i . Kenya imezama wala haitoki. Labda wanasiasa watanabahi na wakae kitako na kuja na mkakati mpya, lakini sio huu wa Ruto na afande David Kimaiyo.

Wataalamu wa kupambana na magaidi watatuangamizaInatoka Uk. 9Columbia Law School, wamefanya utafiti na kutoa ripoti ya kurasa 214 waliyoipa jina "Illusion of Justice: Human Rights Abuses in US Terrorism Prosecutions”.

N d a n i y a r i p o t i h i y o w a n a o n y e s h a j i n s i F B I wanavyotumia njia mbovu na zisofaa (Dubious Entrapment Arrests/terrorism sting tactics.) kuwatia katika jinai ya ugaidi watu ambao wala hawakuwa na mawazo ya kufanya uhalifu huo.

Ripoti hiyo inaeleza kwa undani jinsi serikali ya Marekani inavyowahujumu Waislamu na kuwachonganisha na jamii ya Wakristo. Na hiyo ni kwa sababu ya kuwafanyia vitendo vingi vya ‘entrapment’ na kuwatangaza kuwa ni magaidi.

“The report also shows how government tactics are antagonizing American Muslims. "The U.S. government has on the one hand claimed that American Muslim communities are essential partners, while at the same time placing them under surveillance and treating them as suspects. The impact of those practices has been quite serious, alienating some communities and leading to fear and suspicion in places like mosques and community centers that should be places of refuge." (Andrea Prasow, deputy Washington director for HRW)

Kama tutakumbuka vizuri katika matukio yote yaliyowahi

kutokea hapa nchini yenye harufu ya ugaidi likiwemo lile la kuuliwa Padiri Zanzibar na lile la kulipuliwa bomu kanisani Arusha, tuliambiwa kuwa wazoefu FBI wanakuja kutusaidia. Lakini ripoti ya Human Rights Watch inatuambiwa kuwa:

“The FBI will identify someone who fits a possible terrorist profile; urge that person to participate in an attack; provide the necessary materials; then, finally, make an arrest. In many of the sting operations we examined, informants and undercover agents carefully laid out an ideological basis for a proposed terrorist attack, and then provided investigative targets with a range of options and the weapons necessary to carry out the attack. Instead of beginning a sting at the point where the target had expressed an interest in engaging in illegal conduct, many terrorism sting operations that we investigated facilitated or invented the target's willingness to act before presenting the tangible opportunity to do so."

Ufupi wa maneno ripoti hiyo inasema kuwa ni makachero wa FBI wanaowatia watuhumiwa wazimu wa kufanya ugaidi na pia kuwasaidia kwa vifaa watu hao na kisha baadae baada ya kuweka ushahidi, ndio huwakamatisha. Na kwamba wala hawasubiri kumpata mtu ambaye anaonekana kuwa na mawazo ya kigaidi, bali wao ndio hupandikiza mawazo

Inaendelea Uk. 12

BASI linalodaiwa kutekwa na magaidi na kuua abiria 28 Wakristo.

11 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014Makala

NIKIWA kama mgeni mwalikwa katika Haqika ya kijana wetu mmoja (Allah sw amuhifadhi ) maeneo ya Nsumba jijini Mwanza, ulizuka mjadala juu ya umuhimu wa Jihadi. Mmoja kati wageni waalikwa alizusha mjadala mkubwa wa kuwalaumu wasomi wanaobeza j ihadi akisema hapa namnukuu:

“ K u p i n g a , k u b e z a , a u kudhihaki jihadi ni ukafiri na anayefanya hivyo anaingia kwenye ukafiri. Wamezuka watu na magazeti yao waliyoyapa majina ya Allah, eti kazi yao ni kuwabeza vijana wanaofanya hijra sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya jihadi hawajui Uislamu utasimama kwa mambo matatu (i) imani (ii) hijra (iii) jihadi? Someni vizuri dini.” Mwisho wa kumnukuu.

Hoja katika mjadala haijawahi kuwa Jihad na nafasi yake katika Uislamu. Hakuna Muislamu aliyetamka Shahada ambaye atapinga Jihad. Kusema kuwa kuna watu wanapinga Jihad ni upotoshaji. Kinachohojiwa ni je, wanayofanya Boko Haram, ni Jihad?

Wiki iliyopita tuliambiwa kuwa IS wamechinja watu 18, lakini wameweka pia katika mtandao wao cl ip ya video ambapo wapiganaji wa IS wanaburura maiti za watu waliowaua mitaani. Wamefunga maiti katika pikipiki kwa kamba ndefu , ha la fu wanapita kwa kasi mitaani, maiti zikibururwa nyuma ya pikipiki huku watu wakisimama na kushangaa. Swali ni je, haya ya IS ni Jihad?

Kwa anayetaka kujua ukweli, ushahidi upo wa kutosha kuwa IS wanapewa mafunzo, pesa na silaha kutoka Marekani na NATO, na hata majeruhi wao wanatibiwa katika hospitali za Israel. Na moja ya picha katika mitandao na magazeti ya Israel anaonekana Waziri Mkuu wa Israel, Binyamin Netanyahu akiwatembelea baadhi ya majeruhi hao katika hospitali za Israel.

Je, USA, NATO, Israel, inaweza kusimama bega kwa bega na Mujahidina kusimamisha Dola ya Kiislamu?

Kama hilo linawezekana, basi tungeona hilo likitokea Libya na Afghanistan. Lakini walioitwa wa p i g a n a j i wa K i i s l a m u , walitumika kufanikisha malengo ya mabeberu, sasa Libya ni vurugu tupu. Mabeberu wanavuna mafuta bila ya kuwa na serikali madhubuti ya kuwadhibiti japo walipe kodi.

Hivi kuwahamasisha watu kuuwa na kupora mali za kafiri, ndio Jihad? Wapi yanapatikana mafundisho hayo katika Uislamu.

Abu Baghdadi anayedaiwa kuwa Amir wa IS aliibukia katika gereza la Bucca (biggest U.S. detention camp in Iraq) mwaka 2009 alikokuwa akishikiliwa na askari wa Marekani waliokuwa Iraq. Siku alipoachiwa alimuaga mkuu wa kambi ile, Col. Kenneth King akimwambia, “tutaonana

Hoja sio Jihad, tusipotosheNa Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.New York” (‘I’ll see you guys in New York).

K a m a n d a K e n n e t h K i n g anasema hakuwa ameelewa alichomaanisha Abu Baghdadi kwa wakati ule. Alikuja kuelewa alipokuja kuona kuwa kapewa tenda ya kuongoza ISIS walio “foot soldiers” na “intelligence assets” wa ubeberu wa Marekani na Israel.

Pengine na sisi turudi nyuma tutizame, hawa ‘Akhiy’ wetu, walio makamanda wetu na wanaotuhimiza kuwa na AK-47 nyumbani, kama hatuna tuuze TV tununue, wameibuka kutoka wapi? Miaka mitatu, minne hadi mitano nyuma, walikuwa wapi? Tuvinjari mpaka kule Mabatini, tuulize, ipi rekodi ya maisha yao? Na pengine kama tutaweza kufuatilia tutafute tujue, walipopotea kwa muda, walikuwa wapi kabla ya kuibuka wakiwa ‘wamezaliwa upya’? Wamesoma na kupata mafunzo haya ya Jihad wanayotuhimiza kutoka wapi?

Mwenendo wa maisha ya Mtume (s.a.w) ulijijenga katika kile wataalamu wamekiita (six C ) mambo sita yanayofasiri m w e n e n d o w a m a i s h a ambayo ni, kwanza, Concience ( d h a m i r a ) . D h a m i r y a o iliwapelekea wakatulea katika kile wanachokiamini. Dhamira iliwaambia iko siku Uislamu utasimama hivyo hawakukubali kuvuka hatua moja kwenda nyingine.

M t u m e ( s . a . w ) a l i p o k e a maagizo kutoka kwa Allah s.w akayafundisha vilivyo ndani ya miaka mitatu tena kwa siri katika Darul- Arkamu ( nyumba ya Arkamu ). Malengo na matarajio

ya Mtume (s.a.w) ilikuwa ni kuiona jamii siku moja ikitoka kwenye giza totoro, na yeye Mtume ( s.a.w) kapewa jukumu la kuwawashia taa.

Hivyo ndivyo Mtume (s.a.w) na maswahaba zake na dhamira zao ziliwapelekaea kuwatoa watu katika madhila makubwa. Kabla hatujaingia kipengele cha pili, tujitazame dhamira zetu sisi vijana tunaohemkwa kupigana jihadi. Hivi ni kweli kijana dhamira yako imetulia kabisa kwamba familia yako umeifundisha Uislamu na wanaujua na kuufuata Uislamu vizuri, sasa wanakiendea kila kipengele cha maisha yao kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume (s.a.w)? Wanachuma na kutumia mali zao kama alivyofundisha Mtume? Wanalala na kuamka kama alivyofundisha Mtume? Wanakula na kutembea kama Mtume? Hawadhulumu katika biashara na mengine kama hayo?

Ni muhimu sana kijana wa Kiislamu kujiuliza maswali haya kwani ndivyo s i l s i la iliyowavukisha Mtume (s.a.w) na maswahaba zake (r.a), vinginevyo ni kuvuka hatua na kuvuka hatua hasara zake ni kubwa katika jamii.

Ni hatua hii pekee iliyompelekea Mtume (s.a.w) akamwandaa mtu wa kuingia naye hatua ya pili. Kijana wa Kiislamu, hebu vuta hisia Mtume (s.a.w) kamfikisha pahala Abubakari (r.a) yuko tayari kutoa mali yake yote kwa ajili ya Allah (s.w) hata alipoambiwa na Mtume (s.a.w) anatakiwa kuhama pamoja naye alionyesha utayari wa hali ya juu. Kijana wa Kiislamu, unanye Abubakari wako wa kuhama naye? Angalia Abubakari alivyoiandaa familia yake Asmaa binti Abubakar (r.a) anapeleka chakula pangoni usiku anakutana na maadui wanamtafuta Mtume (s.a.w) na

baba yake, wanamuuliza rejea majibu aliyowajibu binti yule alivyoandaliwa kwa silabasi ya Mtume (s.a.w). Wewe unae Asmaa wako ?

La p i l i nn i Compass ion –(Huruma) maandalizi hayo yaliwapelekea wakaharumiana kwa kiwango cha juu sana. Hawakukubali kufanya jambo lolote lenye kuleta maangamizi katika jamii hata walipoingia katika mapambano. Huruma i l i wa p e l e k e a wa k a c h u n g a mipaka katika mapambano. H a w a k u w a d h u r u w a l e wasiohusika. Hayakuwagusa wazee, watoto, wanawake na nk Hawakuharibu miundo mbinu yoyote. Sote ni mashahidi katika hizi zinazodaiwa kuwa jihadi za IS, Jabhat Islamia, Boko Haram na watu kama hao, zinazoendelea. Kwa watu kukosa huruma tunashuhudia maangamizi makubwa kwa watu wasiohusika. Tunashuhudia uharibifu mkubwa wa miundo mbinu. Hii ndiyo tofauti kubwa kati ya jihadi ya kweli na ile bandia, isiyokuwa na dhamira nzuri wala malengo ya Kiislamu.

Kuna kitu kinaitwa Courage-kwa maana ya ushujaa au uthubutu. Kwa vile walijiandaa vyema na walihakikisha wanayepambana naye ndio adui halisi wa Dini yao, walionyesha ushujaa wa hali ya juu lakini pia walifikia uwiano wa wingi uliotajwa katika Kurani wa mmoja kumi.

J i n g i n e l a m u h i m u n i Consideration, yaani kufikiri kabla ya kutenda. Mtume (s.a.w) akiwa kwenye maandalizi , kila akipima nguvu za waumini a n a g u n d u a b a d o s i y o z a kupambana, aliwasubirisha. Hata pale walipotokea baadhi ya Waislamu wanataka mapambano, bado aliwasubirisha kwani akiona viwango bado kwa kulinganisha na nguvu ya makafiri. Leo sisi vijana tukiambiwa tufikiri vizuri hii jihadi ya kurushiwa silaha na Amerika akidai amekosea, tunaambiwa ina lengo la kutufanya tujiangamize wenyewe, tunaporomosha matusi, kutukanana Waislamu kwa hoja kuwa baadhi yetu wanapinga jihad!

C nyingine inasimama kwa neno Control, ikimaanisha kujidhibiti. Pamoja na hali iliyowakabili Waislamu wakati wa Mtume ya kuteswa sana na makafiri, walijidhibiti na kujizuiya hadi walipoona kuwa sasa wanaweza kuwakabili. Walizuiya mikono yao wakabaki kuzidisha ibada na Da’wa kupata waumini wengi zaidi.

Confidence, inamaana ya kujiamini. Mtume (s.a.w) na swahaba zake waliamini kwa kufuata utaratibu wa mafundisho ya Allah, iko siku kafiri atakuwa chini na Uislamu utakuwa juu. Na ndicho kilichotokea ndani ya miaka 23. Sisi kwa kutokujiamini, kijana una miaka arobaini, hata siku moja hujawahi kuwaita majirani zako ukawaambia kuhusu uzuri wa Uislamu, wala maisha yako hayajawa kigezo chema kwa majirani wasio Waislamu waupende Uislamu kwa tabia zako njema, utu na uadilifu wako.

12 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 201412 Barua/Mashair

Kalamu nimeishika, gaidi kumbaini, Batini alofichika, mumtambue bayani, Si mwingine Amerika, ukipenda marekani, Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA. Kwa jahara huoneka,yuna kiu ya amani, Kumbe yu gaidi fika, ukijasusi kwa ndani, Kwa ngozi alojivika, muhali kumbaini, Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA. Mipaka yuaivuka, hata ya ughaibuni, Kwa majeshi kupeleka, ya vita ulimwenguni, Katu damu kumwagika, hajutii ya insani, Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA. Kwa 'ishuze' za kupika, dunia ameiwini, Sasa yuaaminika, kwa kila anolibuni, Dunia yaghururika, kwa puyaze kuamini, Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA. Aula ikakumbuka, IRAQ alokibuni, Katu hazikuoneka, silaha alozibuni, Kwalo ikighafilika, atazidi kuiwini, Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA. Kwa sasa yuaibuka, na la tenge tahanani, Yu tena akurupuka, kwa kunadi hadharani, Si jingine kwa hakika, la Syria tambueni, Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA. Eti yuna uhakika, na ushahidi mezani, Bilhaki kwa hakika, kwayo mimi siamini, Kwa la IRAQ kupika, yu bado mwamuamini? Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA. IRAQ alitamka, tena kwa kujiamini, "Ndanimwe zimefichika, silaha ziso kifani", Na nembo kuzipachika, "za hilaki kwa insani", Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA. Ikaja kubainika, kwa ukaguzi makini,Kwa wakaguzi kuweka, mambo yote hadharani, "Adaicho Amerika,sicho tulokibaini", Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA. Mara akawakiuka, kwa wake ufirauni, Kwa majeshi kupeleka , angani na ardhini, Umma ukahujumika, kwawo wake 'uhaini', Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA. Wanawake kwa hakika, wakahiliki vitani, Na watoto kadhalika, pasi na kosa jamani, Namba 'wani' nikimweka, yu gaidi ni kosani?, Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA.

Naanza kumhimidi, Mola wangu SUBHANA,Yu pweke tena wahidi, aso mke wala mwana,Mwenye aali weledi, kwa ghaibu na bayana,UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI.

Insani hatuna budi, kutafakari kwa kina,Kwa kila letu kusudi, la siri na la bayana,La kinywa na la fuadi, si kunga kwa SUBHANA,UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI. Uongozi njema sudi, kwa anolenga 'ubwana'Hukazana kwa juhudi, kukwepa nongo utwana,Lengole ni kufaidi, si dhima kwa SUBHANA,UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI.

Jambole kulisanidi, vyovyote atang'ang'ana,Kwa uvumba au udi, ili liweze kufana,Hata kama kwa kutadi, mipaka ya SUBHANA,UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI.

Ahadi ataahidi, lukuki tena mwanana, Keshoye huzikaidi, na nyingine huzikana,Kuulizwa hana budi, na Allahu SUBHANA,UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI.

Kitini hanayo budi, hugeuka kuwa 'bwana',Husimika yake jadi, ya asili huikana,Kwa kujitenga baidi, na mila ya SUBHANA,UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI.

Hujali wake mradi, wa juzi, leo na jana, Japo ni wa kifisadi, huhisi wa kiungwana,Kwa ya kwake itikadi, u mwema kwa SUBHANA, UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI.

'ESCROW' walofaidi, wang'oke kwenye dhamana, Wafilisiwe nukudi, na mali walozivuna, Na mwisho hapana budi, na kortini kuwabana,SI TUNU YA UFISADI, UONGOZI NI AMANA.

ABUU NYAMKMOGI- MWANZA.

UFISADI WA VIONGOZI AKAUNTI YA 'ESCROW'

GAIDI NAMBARI 'WANI'!

Wataalamu wa kupambana na magaidi watatuangamizaInatoka Uk 10hayo. Na zaidi ripoti inasema:

“Some of the people targeted suffer from mental illness or financial problems. It said they were given the motive and the means to commit crimes they might never have ever considered.”

Na ripoti ya HRW inanukuu kesi mbi l i ambapo baada ya Majaji kusikiliza kesi na ushahidi uliowasilishwa na FBI, walikuwa na haya ya kusema:

“…of one suspect, that only the government could have succeeded in making a terrorist out of him -- because his "buffoonery is positively Shakespearean in scope…."The government came up with the crime, provided the means, and removed all relevant obstacles."

Hawa ni Majaji wa New York kat ika i le kesi mashuhuri ambapo vijana wanne Waislamu walituhumiwa kutaka kudungua ndege ya kijeshi na kulipua synagogue la Wayahudi.

K a m a h a w a n d i o wataalamu wanaowapa mafunzo ATPU wetu, tutawaamini vipi polisi wa Kenya katika zile habari zao kuwa wamekamata s i l a h a m s i k i t i n i . Tutawaamini vipi ATPU w a k i t u a m b i a k u w a magaidi wameuwa abiria Wakristo 28. Kwanini tusiwe na wasiwasi kuwa yaweza kuwa ni moja ya zile “Sting Operations”.

T u f a h a m u k u w a k w a m t i n d o h u u unaozungumzwa katika ripoti ya Human Rights Watch, kwamba:“The government came up with the crime, provided the means, and removed all relevant obstacles", huenda ndio unaosababisha leo Nigeria kuzama katika tope la Boko Haram, lakini ndio pia utakaoitosa Kenya, na sisi huku iwapo tutafuata nyayo.

Yapo maneno hapa yanataka kuta fakar i kwa kina kidogo. Hebu yasome. Human Rights Watch wanasema:

“Some of the people targeted suffer from mental illness or financial problems. It said they were given the motive and the means to commit crimes they might never have ever considered.”

Ambapo maana yake ni kuwa hawa ‘marafiki z e t u n a wa t a a l a m u wetu wa kutegemewa’ k a t i k a k u p a m b a n a n a u g a i d i , m o j a ya mbinu wanazotumia

ni kuwatafuta vi jana m a a d h u r a w a l i o punguwani kidogo, kama wavuta bangi vile na wenye matatizo ya kipesa. Hawa hujazwa fikra za ugaidi, kulipua mabomu na ‘Jihad feki’ halafu ndio baadae hukamatwa ikadaiwa kuwa ni magaidi Waislamu.

Sasa kwa mtindo huu, kama tutakwenda na mtizamo kuwa hawa vijana ndio maadui hatari wa amani ya nchi yetu, kadiri tutakavyofanya o p e r e s h e n i z a kuwakamata na kuwatesa, h a i t a t u s a i d i a s a n a . Haitatusaidia kwa sababu tutakuwa tunahangaika na majani, wala si matawi tukiacha shina na mizizi yake ikiendelea kunawiri na kuzalisha matawi zaidi na zaidi. Vijana maadhura na wenye shida ya pesa wa t a e n d e l e a k u we p o . Tusipohangaika na huyu a n a y e wa t u m i a k a t i k a “Sting Operations” zake, kinyume chake tukamfanya ndio wa kutusaidia katika kupambana na magaidi, itakuwa sisi, kwa maana ya serikali na vyombo vyake vya dola pamoja na wale watuhumiwa wa ugaidi, wote tutakuwa sawa tu mbele ya mabeberu hawa. Tutakuwa tunatumiwa na kufadhiliwa kila mmoja kwa namna yake, lakini kwa kutimiza lengo lile lile. Kupandikiza ugaidi na kuleta machafuko katika nchi zetu kwa manufaa ya mabeberu.

Yapo maneno mengine ya kuzingatia sana katika ile ripoti ya HRW. Sikiliza i n a v y o s e m a k a t i k a kipande hiki cha ripoti:

“In many of the sting operations we examined, informants and undercover agents carefully laid out an ideological basis for a proposed terrorist attack, and then provided investigative targets with a range of options and the weapons necessary to carry out the attack. Instead of beginning a sting at the point where the target had expressed an interest in engaging in illegal conduct, many t e r ror i sm s t ing operations that we investigated facilitated or invented the target's willingness to act before presenting the tangible opportunity to do so."

Leo ukisikia kwa mfano anasimama mtu, Ustadh/Sheikh msikitini anahimiza watu kuwa na silaha kwa

aj i l i ya kupambana na makafiri au Wakristo au hata kwenda Somalia, mtu huyu anasimama katika misikiti miwili, mitatu na anadumu kwa mas iku kadhaa, bila ya vyombo husika kuchukua hatua, kwa nini Waislamu wasiwe na wasiwasi kuwa ni katika zile zile mbinu za ‘marafiki zetu FBI ’ za “dubious entrapment?” Rejea ile ripoti ya HRW iliposema: “The government came up with the crime, provided the means, and removed all relevant obstacles."

Kama walivyosema HRW, “Sting Operations” hizi ndio zinapandikiza ugaidi. Pili, zinawatia uhalifu Waislamu il i serikali ipate kuwahujumu. Na tatu, inawachonganisha na wananchi wenzao wa dini nyingine na hatimaye kuleta machafuko katika nchi.

K u f u a t i a t u k i o l a k u u l i w a a b i r i a 2 8 Wakristo, Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa waliofanya mauwaji hayo wanalenga kuleta vita ya kidini baina ya Waislamu na Wakristo. Kwa muda mrefu, Kenya imekuwa mshirika wa karibu wa vyombo ya usalama vya Marekani katika kupambana na ugaidi kuliko ilivyo Tanzania. Washirika hao ndio wanaowapa mafunzo na kuwafadhili ATPU. HRW nao wanatuambia kuwa ‘washirika na marafiki hao wa Kenya’ kat ika kupambana na ugaidi , kawaida yao ni kupandikiza ugaidi ili kuwanasa magaidi na hufanya mambo ambayo yanaleta uhasama baina ya Waislamu na Wakristo.

Kauli ya Rais Kenyatta na ile ya Makamu wake William Ruto, haitawasaidia Wakeya kubaki salama kama ambavyo ile ya Goodluck Jonathan na mabilioni ya Dola anayopewa kutoka Washington, haijasaidia N i g e r i a h a d i s a s a kuondokana na kitisho cha Boko Haram.

K e n ya k u l i k u wa n a migogoro sugu ya kikabila kutokana na suala nyeti la ardhi, lakini sio hii ya kidini na ugaidi. Wajitizame u p ya k wa m a k i n i . L a kama wamekubali kuwa s e h e m u ya “ D u b i o u s Entrapment Arrests na Sting Operations” za ki-FBI, hakuna wa kuwasaidia wala wasitafute mchawi.

13 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014TANGAZO

Bismillahir Rahmanir Rahiim

ISLAMIC PROPAGATION CENTRENAFASI ZA KIDATO CHA KWANZA – 2015

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Kwanza kwa shule zifuatazo:• Mkuzo Islamic High School - Bweni tu - SONGEA• Kirinjiko Islamic Sec. School - Bweni tu – SAME - KILIMANJARO• Nyasaka Islamic Sec.School - Bweni tu - MWANZA• Ubungo Islamic High School - Kutwa tu – DAR ES SALAAM

1. Shule hizi ni za Kiislamu, zenye lengo la kuwapa watoto elimu bora na kuwalea kwa malezi mazuri ya Kiislamu.

2. Masomo yanayofundishwa ni haya yafuatayo:Elimu ya Dini ya Kiislamu, Usomaji Qur’an na mafunzo yake, Hadithi za Mtume(s.a.w), Lugha ya Kiarabu, Kiswahili, English, Basic Mathematics, Physics, Chemistry, Biology, Geography,

History, Civics, Book – keeping na Commerce.

3. Patakuwa na mtihani tarehe 29/11/2014 saa 2:00 asubuhi katika vituo mbali mbali kote nchini. Muombaji anaweza kufanyia mtihani katika kituo chochote.

4. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 28/11/2014.

5. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.

6. Pia, fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa atakayepata fomu kupitia tovuti (download) atatakiwa kulipia wakati wa kurejesha siku ya mtihani.

• Arusha -OfisiyaIslamicEducationPanel,JamboPlastic,Ghorofaya2mkabalana msikiti Mkuu Bondeni : 0763 282 371/ 0783552414.

• Kilimanjaro - Moshi: Msikiti wa Riadha : 0654 723 418. - Same Juhudi Studio mkabala na Bank ya NMB Same: 0757 013344.

- Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 - Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054. - Ugweno – Kifula Shopping Centre- Yusuph Shanga : 078458776.

• Tanga - Twalut Islamc Centre – Mabovu Darajani : 0715 894111/0789 410914.- Uongofu Bookshop: 0784 982525

- Korogwe: SHEMEA SHOP : 0754 690007. - Mandia Shop - Lushoto: 0782257533.

• Mwanza - Nyasaka Islamic Secondary School : 0717 417685/0786 417685.-OfisiyaIslamicEducationPanel–MtaawaRufijimkabalanaMsikitiAl-Amin0785086770.

• Musoma-OfisiyaIslamicEdPanel-MtaawaKarume,NyumbaNa.05:0784721015/0765024623• Kagera -Bukoba:AlhudaCaféKwamzeeKinobekaribunaofisizaTRA.:0684701175.• Shinyanga - Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa ya Shinyanga Mjini :0752180426

-KahamaofisiyaAN–NUURKaribunamsikitiwaIbadhi:0753993930.

• Dar es Salaam - Ubungo Islamic High School : 0712974428/0712033556.-OfisiyaIslamicEd.Panel–Temeke-MsikitiwaNurulYakin:0655144474.

• Morogoro - Wasiliana na Ramadhani Chale : 0715704380.• Dodoma - Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0718 661992.• Singida -OfisiyaIslamicEducation.Panel–karibunaNurusnackHotel:0786425838/0784928039.• Manyara -OfisiyaIslamicEd.Panel–MasjidRahma:0784491196

• Kigoma - Msikiti wa Mugera – Mwandiga: 0714 717727. - Kibondo – Islamic Nursery School: 0784 442860. - Kasulu: Murubona Isl.SS: 0714710802.

• Lindi - Wapemba Store: 0784 974041/0783 488444/0653 705627.

• Mtwara - Amana Islamic S.S: 0715 465158/0787 231007.

• Songea - Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU : 0713249264/0683670772. - Mkuzo Islamic High School : 0717348375.

• Mbeya -OfisizaIslamicEducationPanelUhindini–0785425319.

• - Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209/0785425319. .

• Rukwa - Sumbawanga: Masjid TAQWA: 0717082 073.

• Tabora - Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566.

• Iringa - Madrastun – Najah: 0714 522 122.

• Pemba -Wete: Wete Islamic School : 0777 432331/0712772326.

• Unguja - Madrasatul – Fallah: 0777125074. • Mafia -OfisiyaUst.YusufuAllyjiraninamsikitimkuu:0773580703.• Handeni-NassoroMafiga:0782105735/0657093983

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU – WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

MKURUGENZI

WABILLAH TAWFIIQ

1

14 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014Makala

CHAKULA ambacho ni bora k a b i s a k wa m t u m m o j a , kinaweza kuwa sumu baridi kwa mtu mwingine, na kumletea madhara endelevu katika maisha yake. Kwa muktadha huu basi, hakuna chakula bora kwa kila mtu! Chakula ni bora kwa mtu kama baada ya kukitumia mwili utakipokea vizuri, ukafyonza virutubisho, na kikasaidia kuimarisha afya ya mlaji.

Ni vigumu kujua aina ya chakula inayokufaa, bila kujua jinsi mwili wako unavyochakatua chakula. Kimsingi wataf i t i wamebaini makundi makuu matatu ya watu kuhusiana na jinsi miili inavyochakatua chakula. Kundi la kwanza ni la wachakatuaji wa protini. Hawa miili yao inakubaliana zaidi na vyakula vya protini. Kwa watu wa kundi hili vyakula vya wanga, na hususan vile vilivyochakatuliwa na kuchujwa kwa kiwango kikubwa (highly processed and refined), ni sumu baridi ambayo itawapelekea kuugua maradhi mengi ya kimfumo.

Kundi la pili ni la wachakatuaji wa wanga. Hawa miili yao inakubaliana zaidi na vyakula vya wanga. Kwa watu wa kundi hili vyakula vya protini, na hususan vile vilivyochakatuliwa n a k u h i f a d h i wa k wa a j i l i ya kuwa na muda mrefu wa matumizi, ni sumu baridi ambayo itawapelekea kuugua maradhi mengi ya kimfumo. Kundi la tatu ni la wachakatuaji wa vyakula vya protini na wanga kwa viwango sawa. Kundi hili kidogo lina bahati kwa maana halidhuriwi kwa wepesi na vyakula vilivyoko katika yale makundi mawili ya mwanzo.

M o j a y a m a g o n j w a y a n a y o s a b a b i s h w a n a mkanganyiko huu katika kula ni ugonjwa wa kisukari. Mchakatuaji wa protini anapokula chakula cha wanga, kasi ya kuchakatua wanga huo ni kubwa mno ikilinganishwa na mlaji mwenzake ambaye ni mchakatuaji wa wanga. Kasi hiyo hupelekea kiwango cha sukari kinachoingia katika mzunguko wa damu ndani ya muda mfupi kuwa kikubwa sana. Kutokana na hali hii kongosho hulazimika kufanya kazi ya ziada kuzalisha kiwango kikubwa cha insulin (homoni ya kuondoa sukari kwenye damu na kuipeleka kwenye seli ili itumike kutengenezea nishati), ili kukabiliana na ongezeko hilo.

Hali hii ikijirudia rudia mara kwa mara kongosho huchoka na kuanza kufanya kazi chini ya kiwango; au wakati mwingine vipokezi vya sukari katika seli (receptors) hushindwa kuendana na kasi ya kuletewa sukari kwa ajili ya matumizi ya seli, na

Chimbuko la maradhi ya kisukari ni chakula kisichofaaNa Juma Kilaghai huishia kuikataa sukari hiyo.

Hali hii kitaalamu hujulikana kama insulin resistance, au pingamizi dhidi ya insulin kwa tafsri isiyo rasmi. Kuna baadhi ya nyakati yote mawili hutokea kwa wakati mmoja, yaani kongosho linafanya kazi chini ya kiwango, na pia mgonjwa anakabiliwa na pingamizi dhidi ya insulin.

Hivi karibuni imebainika kuwa moja ya sababu kubwa sana zinazopelekea vipokezi vya seli vikashindwa kupokea sukari inayoletwa ni uvimbe mwako (inflammation). Vichocheo vya kusababisha uvimbe mwako kwenye seli viko vingi lakini baadhi ya hivi ni vyakula tunavyokula kila siku. Vyakula hivi ni pamoja na sukari, wanga uiliochakatuliwa kwa kiwango kikubwa, na mafuta ya mbegu (alizeti, ufuta, karanga, pamba, mawese, nakadhalika) yanapotumiwa kwa aji l i ya kupikia. Sababu nyingine ni maambukizi ya vimelea vya maradhi mbalimbali.

Wataalamu wameyagawanya magonjwa ya kisukari katika makundi makuu matatu. Makundi haya ni:

1. Kisukari cha aina ya kwanza (type 1 diabetes). Hiki ni kisukari kinachojitokeza mapema (kwa kawaida kabla ya mtu kufika miaka 40), mara nyingi ikiwa ni katika kipindi cha utoto na ujana wa chini ya miaka 20. Katika aina hii ya kisukari mwili wa mhusika unaacha kuzalisha kabisa homoni ya insulin na hivyo kumlazimu mgonjwa kuishi kwa kudunga sindano za insulin kila siku.

2. Kisukari cha aina ya pili (type 2 diabetes). Kiashiria kikubwa katika aina hii ya kisukari ni kwamba mwili hauzalishi insulin ya kutosheleza mahitaji, au vipokezi (receptors) vya sukari katika seli havifanyi kazi kwa kiwango kinachotakiwa. Zaidi ya asilimia 90 ya wagonjwa wote wa kisukari duniani wanaugua aina hii ya kisukari.

3 . Kisukar i cha u jauzi to (gestational diabetes). Hiki ni kisukari kinachowakumba baadhi wanawake pale wanapokuwa wajawazito. Wakati wa ujazito baadhi ya wanawake huwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye mzunguko wa damu kuliko inavyotakiwa na wanaweza wakalazimika kutumia matibabu ili wasidhurike. Kutotambua kuweko kwa kisukari hiki na kukitibu kunaweza kusababisha matatizo wakati wa kujifungua. Moja ya madhara ya aina hii ya kisukari ni kuzaliwa watoto wenye miili mikubwa kuliko kawaida.

Kisukari ni ‘ugonjwa’ unaotisha. Ni ‘ugonjwa’ unaotisha kutokana na sifa zake. Sifa hizi ni pamoja na kutokuwa na dawa ya uhakika, kumlazimisha mgonjwa abadilishe

mwenendo wake wa maisha kwa kiasi kikubwa, kusababisha mlolongo wa madhara mengine kibao ya kiafya ndani ya mwli, kuongeza gharama za maisha kwa mgonjwa, na ile hali ya kugeuka kuwa janga la kijamii.

Tunasema kisukari hakina dawa ya uhakika kwa kuwa ulimwengu wa tiba za kisasa umeshindwa kuja na dawa za aina hiyo hadi sasa. Dawa zilizoko ni zile za kumsaidia mgonjwa kushusha sukari iliyolundikana kwenye damu yake, ili iende katika viwango vinavyokubalika. Hata hivyo historia inaonyesha kuwa baadhi ya dawa hizi siyo salama, na hatima yake zinamsababishia mtumiaji madhara mengine ya kiafya ikiwa ni pamoja na kumwongezea uwezekano wa kupoteza maisha.

Avandia (rosiglitazone) ni moja ya dawa hizo. Mauzo ya dawa hii ambayo enzi zake ilikuwa ni moja ya dawa maarufu sana za kifamasia kwa ajili ya ugonjwa wa kisukari, yalifikia kiasi cha dola za Kimarekani bilioni 3.2 mnamo mwaka 2006. Baada ya hapo ziliibuka taarifa za kitafiti kwamba dawa hi i i l ikuwa inasababisha madhara makubwa ya kiafya kwa mtumiaji kama vile ongezeko la hatari ya shambulizi la moyo (heart attack), wepesi wa kuvunjika mifupa na hususan ile ya mikononi juu ya kiwiko, uharibifu wa macho, kiharusi na uharibifu wa ini kutokana na ongezeko la sumu. Inakadiriwa kuwa ndani ya Marekani peke yake kati ya mwaka 1999 na mwaka 2006 dawa hii ilisababisha mashambulizi ya moyo (heart attacks) na vifo kati ya 60,000 na 200,000.

Japokuwa baadhi ya matatibu wa dawa za asili na zile za tiba mbadala wanadai kuwa wanatibu ugonjwa huu, madai haya yanapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari. Ni kweli kuwa mtu anaweza kuwa na dawa ya kuondoa sababu moja au zaidi

ya kisukari na hivyo kumsaidia mtumiaji kuondokana na dalili zote za ugonjwa huo. Hata hivyo hii haina maana kwamba dawa hiyo itamtibu kila mgonjwa wa kisukari. Kwa kifupi ni kwamba kundi la wenye kisukari kilichosababishwa na sababu zinazoguswa na dawa husika watapona, na wengine wenye kisukari kilichosababishwa na sababu zisizoguswa na dawa hiyo hawatapona.

Mazoea yana tabu sana . Tulio wengi hatuli chakula kwa kuzingatia kanuni za afya bali tunakula kwa ajili ya mazoea na kulenga ladha. Mgonjwa wa kisukari mwenye nia ya kuidhibiti hali hiyo analazimika kuachana kabisa na kula kwa mazoea na kulenga ladha. Anatakiwa ajue kuwa vyakula vyote vya wanga, na hususan vile vilivyochakatuliwa kwa kiwango kikubwa, vina madhara makubwa kwake na anatakiwa kuviendea kwa tahadhari kubwa. Hali hii huwa ni chanzo kikubwa cha kufadhaika kwa baadhi ya watu ambao wamepata ugonjwa wa kisukari. Baadhi yao huuliza kwa ghadhabu : ‘sasa utakula nini???!’ na kuendelea kula vyakula vyao walivyozoea huku wakisaidiwa kisaikolojia na kimwili na vidonge wanavyopewa hospitalini na madaktari wao. Waathirika wengi wa madawa kama avandia ni wale wanaoangukia katika kundi hili.

Kisukari pia kinatisha kwa kuwa kinasababisha mololongo wa matatizo mengine kibao ya kiafya. Matatizo haya ni pamoja na uharibifu wa macho unaotambulishwa na magonjwa kama glaucoma (uharibifu wa neva za jicho), cataracts (ukungu kwenye lenzi ya jicho), retinopathy (uharibifu mkubwa katika retina ya jicho), nakadhalika. Matatizo ya miguu yanayotambulishwa na magonjwa kama neurapathy ( m a u m i v u ya t o k a n a y o n a u h a r i b i f u wa m i s h i p a ya

Inaendelea Uk. 15

15 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014 MAKALA/TANGAZO

Chimbuko la maradhi ya kisukari ni chakula kisichofaaInatoka Uk. 14

fahamu), ulcers (vidonda sugu), gangrene (mkusanyiko wa tishu zilizokufa kutokana na kutofikiwa na mzunguko wa damu), nakadhalika. Matatizo mengine ni yale ya magonjwa ya ngozi na magonjwa ya moyo.

Faraja ya ugonjwa wa sukari ni kuufatilia kwa makini. Hii ina maana kuwa ni muhimu kufanya kipimo kila siku, ikiwezekana hata mara mbili au tatu kwa siku. Kutokana na hali hii gharama za kuufuatilia ugonjwa huu ni kubwa na huathiri kwa kiasi kikubwa hali ya kiuchumi ya mgonjwa. Kwa mfano tu, hivi sasa katika zahanati na vituo vingi vya afya, gharama za kupima kisukari kwa mara moja ni kati ya shilingi 2,000.00 na shilingi 2,500.00. Unapomwambia mtu apime mara tatu kwa siku maana yake atumie kati ya shilingi 6,000 na shilingi 7,500.00 kila siku!

Mwisho kisukari kinatisha kwa sababu taratibu kinaonekana kunyemelea hadhi ya kuwa ni janga kubwa sana la kijamii. Katika pande zote za dunia kisukari kinaongezeka badala ya kupungua. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, dunia inatarajiwa kuwa na wagonjwa wa kisukari 366,000,000 mwaka 2030 kutoka wagonjwa 171,000,000 waliokuwepo mwaka 2,000. Hili ni ongezeko la aslimia 53! Tanzania, ambayo mwaka 2,000 ilikuwa na wagonjwa 201,600 inatarajiwa kuwa na wagonjwa 605,000 mwaka 2030, ikiwa ni ongezeko la 66.7%

Hata hivyo janga la kisukari linaoonekana kuzikumba zaidi zi le nchi ambazo raia wao wanapendelea mno vyakula vya wanga katika mitindo tofauti- soda, pasta, doughnut, keki, mikate, lambalamba, nakadhalika. Nchi kama Italy uwiano kati ya Wataliano wanaoumwa kisukari na wale ambao hawaumwi ni 1:14!. Inawezekana sababu kubwa ikawa ni piza, pasta na spaghetti. Hivi ni vyakula vinavyotengenezwa kwa ngano na Wataliano wanavifakamia kwa wingi.

Marekani uwiano wao ni 1:17. Hii nayo ni jamii ambayo imelogewa soda, doughnut, chips, pizza, na vyakula vingine vya wanga vilivyochakatuliwa kwa kiwango cha juu. India uwiano wao ni 1:39. Hawa nao ni mabingwa wa vitu vitamu. Wahindi ni wafakamiaji wa tamutamu za kila aina na sifa kuu ya tamutamu hizi ni wingi wa sukari, ngano, mafuta na rangi.

Tanzania ina uwiano wa 1:238. Huu ni uwiano mzuri sana ukilinganisha na nchi tulizotangulia kuzitaja. Sababu ya uwiano huu mzuri ni nini wakati kimsingi sehemu kubwa ya Watanzania ni wala wanga zaidi kutokana na hali zao za kiuchumi?

Nadhani sababu kubwa ni ukweli kwamba Watanzania wengi ni wakaazi wa vijijini na kimsingi pamoja na kwamba sehemu kubwa ya chakula chao ni wanga, lakini kutokana na sababu za kiuchumi, wanalazimika kuula wanga huo katika mfumo ambao haujachakatuliwa.

Kuepukana na ugonjwa wa kisukari ni muhimu kufanya kipimo cha kutambua aina ya mwili wako katika kuchakatua vyakula (metabol ic typing test) na iwapo utagundulika kuwa wewe ni mchakatuaji wa protini, haraka uchukue hatua za kupunguza kwa kiwango

kikubwa ulaji wa wanga, na hasa ule ambao umechakatuliwa kwa kiwango kikubwa. Nafasi ya wanga (kwa ajili ya kuzalisha nishati ya matumizi ya mwili) ichukuliwe na mafuta bora ya kula – nazi, siagi, samli, zaituni. Nafasi ya wanga kwa ajili ya kujaza tumbo ichukuliwe na mboga mchanganyiko za majani, na pale ambapo uwezekano upo, sehemu kubwa ya mboga hizo iwe mbichi (salad). Mafuta ya kawaida (yale tuliyoyazoea) tunaweza kuendelea kuyatumia (siyo kwa kupikia) bali kwa kupambia saladi (salad dressing).

Aidha kama wewe tayari ni

mgonjwa wa kisukari, utanufaika sana kwa kuondoa wanga uliochakatuliwa katika orodha ya vyakula vyako na ukaingiza wanga ambao haujachakatuliwa, tena kwa kiwango kidogo sana kama mbadala wake. Kwa ajili ya kuupatia mwili nishati punguzo hilo la wanga lichukuliwe na ongezeko la mafuta bora ya kula – nazi, siagi, samli, na zaituni. Aidha nafasi ya kushiba ichukuliwe na wingi wa mchanganyiko wa mboga za majani, ikiwezekana sehemu kubwa ya mboga hizi iwe mbichi (salad).

K a m a i l i v y o k w a y u l e anayelenga kukwepa kuugua kisukari, mafuta ya kawaida (yale tuliyoyazoea) tunaweza kuendelea kuyatumia (siyo kwa kupikia) bali kwa kupambia saladi. Ushauri huu kuhusu mafuta ni kinyume kabisa na ushauri mnaopatiwa na madaktari wenu kuhusu mafuta ya kula. Hata hivyo kisayansi ndio ushauri sahihi. Mungu akipenda post yetu ijayo itazungumzia jambo hili kwa kina ili kuliweka katika mazingira ya kueleweka zaidi.

Herbal Impact1574/144 Mosque Street ,

Kitumbini, Dar es Salaam. P.O. Box 70949, Dar es Salaam, Tanzania.

Tel: +255 (22) 2134757Mobile: 0754281131/065528113

1/0779281131/0686281131E-mail: enterprisesnovel@

yahoo.com.

Sifa na masharti ya kujiunga Muombaji atimize sifa na masharti yafuatayo:(i) Awe Muislamu aliye tayari kuishi Kiislamu(ii) Awe anajua kusoma Qur’an kwa ufasaha.(iii) Awe amemaliza juzuu ya 1 na 2 ya Maarifa ya Uislamu, Darasa la Watu

Wazima kabla ya kujiunga.(iv) Awe na uwezo wa kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili kwa ufasaha.(v) Awe amehitimu darasa la saba au kidato cha nne na awe anafundisha

madrasa au kipindi cha dini katika shule za Msingi au Sekondari.• Patakuwanausailinamtihanisikuyatarehe29/11/2014saa2:00asubuhi

katika chuo cha Ubungo na Kirinjiko na katika vituo mbalimbali vya mitihani kote nchini.• Mwishowakuchukuafomunitarehe28/11/2014.• Fomuinalipiwashilingi5,000/-tu.

Fomuzinapatikanakatikavituovilivyoorodheshwaukurasawa13wagazetihili.MKURUGENZI

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

NAFASI ZA KUJIUNGA NA KOZI FUPI YA UALIMU KATIKA VYUO VYA UBUNGO NA KIRINJIKO-2015

16 AN-NUURSAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 201416 MAKALA

AN-NUUR16 SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Soma gazeti la

AN-NUUR kila Ijumaa

KESI dhidi ya watuhumiwa wa ugaidi ambayo awali i l i w a s i l i s h w a k a t i k a Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita, imefikishwa Mahakama Kuu ya Tanzania Jumatatu wiki hii Novemba 24 ikiwa chini ya Jaji Twaibu Faudhi.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 4 mwaka huu, baada ya mawakiliwa wa upande wa Jamhuri kuiomba mahakama hiyo kuwapa muda wa kuleta majibu ya maombi yaliyoletwa na upande wa utetezi katika mahakama hiyo.

Jaji Faudhi alikubaliana na hoja ya upande wa Jamhuri na kuwaamuru kuleta majibu yao Novemba 28.

Wakili wa upande wa utetezi, Abubakari Salim, alimwelezea mwandishi wa gazeti hili baada ya kuahilishwa kwa kesi hiyo kuwa, upande wa Jamhuri ulioongozwa na wakil i Peter Njike, awali waliomba kupewa muda zaidi wa kuleta majibu ya maombi ya upande wa ute tez i yaliyowasilishwa mahakami hapo.

“Wamepewa tarehe 28 Novemba walete majibu yao na sisi kama tuna hoja za nyongeza, tumetakiwa kuleta Desemba 1 na shauri litasikilizwa Desemba 4 mwaka huu”. Alisema Wakili

Watuhumiwa ugaidi, kesi yaanza Mahakama Kuu DarSheikh Mselemu azushiwa kifo!

Na Seif Msengakamba

huyo.W a k a t i k e s i y a

wa t u h u m i wa h a o wa ugaidi ikianza kusikilizwa, k u l i k u w a n a t a a r i f a z i l izokuwa z imezagaa katika mitandao ya simu kuwa Sheikh Mselem Ali Mselem amefariki.

Uzushi huo uliibuka siku ya Jumanne, ikiwa ni siku moja baada ya watuhumiwa hao, akiwemo Sheikh Mselem kurejeshwa rumande kutoka Mahakama Kuu ambapo kesi yao ilikuwa ikisikilizwa.

Taarifa hizo zilikuwa zikisambazwa kwa njia ujumbe mfupi wa simu na katika mitandao ya kijamii.

Gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao, Abdalah Juma, ambaye naye alisema yeye yupo Zanzibar.

Hata hivyo aliwasiliana

n a m a wa k i l i we n z a k e waliokuwa Dar es Salaam ambao walimhakikishia kwamba Sheikh Msellem alikuwa salama.

“Taarifa hizo za mitandao ya simu na kijamii ni za uzushi na uvumi unaoenezwa bila kuchunguzwa. Niwatoe hofu Waislamu juu ya afya ya Sheikh Mselemu, afya yake ni safi na imeimarika na inaendelea vizuri.”

W a k i l i h u y o aliwahakikishia Waislamu akiwaomba watul ie na kuwataka kutosikiliza taarifa zisizokuwa rasmi na ambazo hazijachunguzwa.

“Kila mmoja atakufa, ya nini umzushie mwenzako hali ya kuwa yu hai”, alihoji Wakili Juma.

Alisema watuhumiwa wote walifika mahakamani na afya zao zinaendelea vizuri hivyo kuwataka Waislamu kuendelea kuwa na subra.

Hujuma kwa Waislamu zazidi kupamba motoMaduga aachiwa kwa mashartiAlidaiwa kufadhili magaidi MoroAtakiwa kuripoti polisi miaka 2

b a l i n i w a t u h u m i w a kwamba Serikali ilikuwa inawatuhumu tu na wao ni wajibu hoja kujitetea”. Alisema Sheikh. Mwinge.

K i o n g o z i h u y o w a Waislamu Mkoani humo, alisema ilibainika Mahakana hapo kuwa Waislamu hao walikamatwa na watu wa uchunguzi wa mabomu wa Kimataifa, ambao ndio wanaendelea na zoezi hilo kwa sasa hata hivyo hakuna ushahidi wowote uliotolewa kwa tuhuma hizo.

A l i p o u l i z w a k a m a Waislamu hao walipata nafasi ya kujitetea juu ya tuhuma hizo, Sheikh Mwinge, alisema, kutokana na upande wa mashitaka kuweka wazi kuwa haikuwa kesi hawakuwa na papara ya kutafuta Wakili kwa ajili ya utetezi au wao wenyewe kujitetea.

W a i s l a m u h a o wameachiliwa kwa mashariti kadhaa kufuatia upande wa mashitaka kuiomba Mahakama, miongoni mwa mashariti hayo kuwataka w a s i f a d h i l i M a g a i d i , wasiwasaidie na wasitoe msaada wa kifedha kuwapa magaidi.

Aidha, Mahakama hiyo iliombwa iwatake Waislamu hao kuwa walinzi wa amani kwa muda wa miaka mitatu, sambamba na mashariti magumu ambayo yatatolewa na Mahakama.

M a s h a r i t i m e n g i n e yametajwa kuwa, kila mjibu maombi (mtuhumiwa) alitakiwa kusaini mkataba wa udhamini wenye thamani ya Shilingi Milioni tatu, sambamba na wadhamini watatu huku wakitakiwa kuripoti kituo cha Polisi kwa RCO, kila baada ya miezi mitatu.

Sheikh Mwinge, alisema mashariti yote yalitimizwa kwa watuhumiwa hao kwa kusaini mkataba wa kulinda amani na dhamana ya shilingi milioni tatu kwa maandishi pia walipatikana wadhamini watu kwa kila mmoja s iku hiyo hiyo Mahakamani hapo, baada ya Mahakama kukubaliana na upande wa mashitaka.

“ L a k i n i M a h a k a m a ilipinga muda wa miaka mitatu na badala yake ikawapa miaka miwili . Kwa hiyo kwa mujibu wa makubaliano hayo ya

Na Bakari Mwakangwale

kimahakama, wataanza kuripoti kwa RCO, kuanzia Februari 25, 2015, kwa hiyo tokea jana (Jumatatu wiki hii) wakawa huru.” Alisema Shkh. Mwinge.

A k i z u n g u m z i a kamatakamata hiyo ya Serikali na kuwahusisha na Ugaidi, Sheikh Muwinge, alisema hayo ni matunda y a Ta n z a n i a k u u n g a mkono sheria ya Ugaidi, kwa madai ya kupiga vita Ugaidi bila kujua gaidi wanayemkusudia ni nani.

“Mchakato ule wa sheria ya Ugaidi matokeo yake ndio haya na kwa kutokana na hali ya Waislamu tuliyonayo sasa na kanuni za sheria hiyo, ni wazi kwamba Waislamu tupo katika kuti kavu ndani ya nchi yetu”. Alisema Muwinge.

“Kubwa niseme kwamba utulivu unahitajika, subra inahitajika hekma inahitajika katika suala zima la kufikisha ujumbe wa Mwenyez i M u n g u , v i n g i n e v y o tunaweza kujikuta tunaingia katika mitego iliyokusudiwa k w e t u . ” A l i s e m a n a kutahadharisha.

Sheikh Waziri Maduga, na Wais lamu wengine wanne walikamatwa usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne ya wiki iliyopita, k i s h a w a l i s a f i r i s h w a hadi Jijini Dar es Salaam, ambapo Novemba 23, 2014 ( Jumapili) walirudishwa Mjini Morogoro na hatimaye Novemba 24 (Jumatatu wiki hii) walifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Morogoro.

W a i s l a m u h a o walikumbwa na kadhia hiyo ni Sheikh Waziri Amani Maduga (Kiongozi wa Kiislamu), Othman Saidi Masanga (Dereva SUA), Shabani Ramadhani Mussa, A l l y A h m a d a K a h e n a (wafanyabiashara Sokoni Morogoro) , Msagomora Faraji Msagomora, wote wakiwa n i wakazi wa Morogoro.

Sheikh Waziri Maduga, ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Daarul Hijra iliyopo Mafisa Mjini Morogoro, ambayo inaendesha na kusimamia Shule za Awali na Msingi za Taasisi hiyo, pia Shekh Maduga, ni muhadhiri wa Dini ya Kiislamu.

MWENYEKITI wa Taasisi ya Kiislamu ya Daarul-Hijra ya Mjini Morogoro, Sheikh Wazir i Amani Maduga, ameachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Morogoro baada ya kukamatwa kwa tuhuma za Ugaidi.

M b a l i y a S h e i k h Maduga, pia Mahakama hiyo imewaachia Waislamu

wengine wanne, Jumatatu ya wiki hii ambao walikamatwa pamoja naye mapema wiki iliyopita wakiwa katika shughuli zao mjini huo.

Hatua hiyo imefikiwa na Mahakama hiyo, baada ya upande wa mashitaka ( S e r i k a l i ) k u i e l e z a Mahakama kuwa Waislamu hao sio washitakiwa bali ni wajibu maombi.

Akiongea na An nuur, A m i r wa B a r a z a K u u la Jumuiya na Taasisi za

Kiislamu, Mkoani humo, S h e i k h A y o u b S a l i m Muwinge, alisema taarifa kutoka Mahakani hapo zilieleza kuwa, upande wa mashitaka unawatuhumu W a i s l a m u h a o k w a kujihususha na Magaidi, kwa kuwahifadhi na kuwapa msaada wa kifedha.

“Tuhuma zao zinahusishwa na masuala ya Ugaidi, lakini katika maelezo yao upande wa mashitaka wamesema kwamba si washitakiwa

SHEIKH Mselem (katikati).