24
INTER-AFRICAN COMMITTEE Kvinnefronten / Wanawake mbele Norway + + + + + + + + + + + + + + + + + + +++ + + +++ + + +++ + + +++ + + +++ + + +++ + + +++ + + MUHTASARI WA WATATHMINI NA MAPENDEKEZO TANZANIA Gro Therese Lie, Ellen Alexandra Lothe na Chiku Ali Chama hamasisha dhidi ya ukeketaji wa wanawake

iac swahili.indd

  • Upload
    vanque

  • View
    262

  • Download
    4

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: iac swahili.indd

I N T E R - A F R I C A N C O M M I T T E E

Kv i n n e f r o n t e n / Wa n a w a k e m b e l e N o r w a y

++++

+

++

+

+ ++++

+

++

+

+

+ + + + ++ + + + +

+ + + + ++ + + + +

+ + + + +

+ + + + ++ + + + +

M U H T A S A R I W A W A T A T H M I N I N A M A P E N D E K E Z O

T A N Z A N I A

Gro Therese Lie, Ellen Alexandra Lothe na Chiku Ali

C h a m a h a m a s i s h a d h i d i y a u k e k e t a j i w a w a n a w a k e

Page 2: iac swahili.indd
Page 3: iac swahili.indd

INTER-AFRICAN COMMITTEE

Page 4: iac swahili.indd

IAC National Committee: Kilimajaro Inter-African Committee

P.O. Box 6539, Moshi, Tanzania

Simu: +(255) 27- 52 038/- 51 121

IAC Chapter: Dodoma Inter-Africa Committee

P.O Box 759, Dodoma, Tanzania

IAC Headquaters: c/o ECA, P.O.Box 3001, Addis Ababa, Ethiopia

Simu: + (251) 1-44 32 73. Simu/fax: -51 57 93

e-mail: [email protected]

IAC Liaison Off ice, Geneva: [email protected]

www: iac-ciaf.ch

INTER-AFRICAN COMMITTEEChama hamasisha dhidi ya ukeketaji wa wanawake, Tanzania

Muhtasari wa Utendaji na Mapendekezo

By Gro Therese Lie, Ellen Alexandra Lothe na Chiku Ali

Bergen/Oslo/Singida, Desemba 2004

© Kvinnefronten/Wanawake mbele Norway

Mada imepata msaada kutoka kwa OD/FOKUS/Norad

Mtoaji: Kvinnefronten/Wanawake mbele Norway

Osterhaugsgata 27

0183 Oslo, Norway

Simu/fax: + (47) 22 20 64 00

e-mail: [email protected]

www.kvinnefronten.no

www.fokuskvinner.no

Matayamisho: Camilla Løland na Thera Mjaaland

Picha: Gro Th. Lie, Anne Røthing, Agnete Strøm na Målfrid Utne

Mada hii imetafsiriwa Kiswahili kutoka katika Kiingereza na: Hadija Samma

Kime tolewa na Allkopi

Page 5: iac swahili.indd

INTER-AFRICAN COMMITTEE

CHAMA HAMASISHA DHIDI YA UKEKETAJI WA WANAWAKETANZANIA

Page 6: iac swahili.indd

6

Page 7: iac swahili.indd

”Hii ni mila na desturi – sio rahisi kubadilisha mawazo ya watu.”

Page 8: iac swahili.indd

8

Page 9: iac swahili.indd

Fahirisi

1 MUHTASARI WA WATATHMINI 11

2 HITIMISHO NA MAPENDEKEZO 17Hitimisho 17Mapendekezo 19

Picha katika ukurasa wa mbele,kushoto zinaonyesha maigizo ya vijana wa Samumba, huko wilaya ya Singida, wakiigiza kuhusu ukeketaji wakati wa mkutano uliyofanywa na IAC wa kuhamasisha hapo kijijini kama inavyoonyeshwa katika picha zifuatazo.

Page 10: iac swahili.indd

10

Page 11: iac swahili.indd

11

1Muhtasari wa watathmini

Tathmini hii imefanyika kwa maagizo kutoka Norad kupitia FOKUS kwa ajili na faida ya chama cha wanawake mbele wa Norway. Lengo letu limekuwa ni kutathmini kazi za chama mwanvuli wa muungano wa kamati za Waafrika, chama kisicho cha kiserikali, juu ya nchi 28 katika bara la Afrika. Chama mwanvuli hiki kinajulikana kama; IAC.

IAC imekuwa ikipokea misaada ya kifedha kutoka katika chama cha wanawake cha Norway kupitia FOKUS tangu mwaka wa 1998. Tanzania ilicha-guliwa kuwa nchi mojawapo katika kutathimini ubora wa shughuli za IAC kwa njia shirikishi ya kimaelezo. Ilisadikiwa kuwa Tanzania ni nchi ambayo inaweza kuonyesha na kutoa mfano bora wa kiuhalisi katika mafunzo yatolewayo na IAC kiundani zaidi. Hii ni kwa sababu Tanzania ina mifano tofauti katika vitendo vya ukeketaji wa wanawake. Tanzania inaonekana kuwa na uzoefu wa kutumia njia mbalimbali katika kukabiliana na changamoto tofauti dhidi ya vitendo vya ukeketaji wa wanawake. Zaidi, shughuli za IAC nchini Tanzania ziko katika awamu tofauti na huendeshwa kwa utaratibu na mbinu tofaouti kufuatana na sehemu na watu wake.

Dhumuni kubwa la tathmini hii ni kutoa habari muhimu kuhusu ujuzi halisi, fikira na maoni kuhusu pambano la ukeketaji na kutumia mada hii kama mfano kwa kazi hii siku za baadaye utakaotumiwa na wahamasishaji washughulikao kwenye ngazi tofauti katika shughuli za IAC mikoani na kitaifa, na kimataifa.

Tathmini hii ilifanywa, nchini Tanzania kuanzia tarehe 25 Juni hadi Julai 6 mwaka 2004, na kikosi cha watu watatu wakiongozwa na Gro Th. Lie, profesa katika kituo cha utafiti na uhamasishaji wa afya (HEMIL) na idara ya saiko-lojia katika chuo kikuu cha mji wa Bergen. Mwengine ni Ellen Alexandra Lothe, mhadhiri na profesa mshirika katika chuo cha wauguzi cha Lovisenberg Deaconal Oslo, pamoja nao ni Mtanzania aliyeishi miaka mingi nchini Norway, Chiku Ali, msanii, mwanasiasa na mkereketwa mwenye ujuzi wa muda mrefu, katika haki za wanawake hususani na masuala ya ukeketaji wa wanawake Singida, Tanzania na Bergen, Norway. Watathmini hawa walifanikiwa kukusanya habari kama ilivyo-

Page 12: iac swahili.indd

12

kusudiwa, kwa kuwahoji wahusika walengwa, katika vikundi tofauti tofauti na pia kwa kushiriki katika mijadala. Walitembelea matawi tofauti na kuwahoji viongozi wa vikundi hivi katika ngazi tofauti kuanzia kitaifa mpaka vijijini. Walipokea mtazamo mpana uliyoambatanisha maoni ya IAC Tanzania na jinsi chama kinavyofanya kazi zake. Viongozi wahusika hufuata kwa namna ya changamoto katika ngazi zote na katika vitongozi mbalimbali kwa lengo la kuwania kupata ujuzi wa mila bora za uhamasishaji, na afya bora.

Hivyo basi, utendaji wa shughuli za IAC unaafiki na kuhusisha utaratibu wa viwango tofauti na ushirikisho wa sekta tofauti katika kurejesha mila bora za mbinu za uendelezaji wa afya.

Lengo la IAC ni kuwa na ushiriakano mzuri baina ya wananchi, na haswa miongoni mwa vijana. Mathalani, viongozi wa IAC Tanzania wanafuatilia utaratibu wa kuunganisha vyama kwa kusudi la kuwahusisha viongozi wote wa vijijini katika kazi yao ya kupambana na ukeketaji.

Timu ya tathmini ilipokea habari kuhusu mabadiliko yanasababisha faida na ugumu kwa lengo la kuboresha shughuli zihusianazo na suala la ukeketaji wa wanawake. Habari nyingi za muhimu zilijitokeza. Wananchi wamepata mwamko mkubwa na kuonyesha kuelewa undani wa vita dhidi ya ukeketaji mpaka hii leo. Wananchi wengi wanaelewa kuwa ukeketaji wa wanawake unasababisha hatari katika afya za wanawake, na ni upingaji wa sheria katika harakati za ya kutetea haki za binaadam. Jamii husika nyingi zimewacha tabia ya ukeketaji. Lakini kikosi cha tathmini kimegundua kwamba tabia hii bado inaendelea kisirisiri. Na ni tatizo kubwa sana. Hii inaonyesha kwamba jamii nyingi, dhidi ya juhudi kubwa za kuhamasisha, bado hazijaelewa umuhimu wa kuacha tabia hii ya ukeketaji.

Hata hivyo, kwa upande mwingine inaonyesha kwamba, wanafunzi wanaji-funza kuhusu madhara ya tabia hii shuleni. Kitu ambacho kinaleta matumaina na pole pole vijana sasa wanaweza kuzungumza na jamii zao kuhusu madhara ya tabia hii pamoja ili kushawishi kuweza kuepuka ukeketaji. Miiko yote kuhusu jambo hili la ukeketaji imevunjwa katika familia kadhaa. Vijana wametunga nyimbo na michezo kwa marika yote kuhusu jambo hili. Haya ni maendeleo muhimu ambayo yametokana na kazi muhimu na ya ufafanuzi ifanywayo na IAC.

IAC imeweza pia kuhamasisha wananchi vijijini kusudi waweza kutoa habari kuhusu madhara haya ya ukeketaji kwa wale walio karibu yao na kwa umma kwa ujumla. Chama hiki pia kinaushirikiano mkubwa na wahudumu katika vituo vya afya kwa ajili ya kusambaza madhara ya ukeketaji kwa jamii, ushirikiano na askari na vyombo vya kisiasa kwa njia ya kuwatumia wabunge wawakilishi.

Vile vile kuna ushirikiano mkubwa na vyombo vya habari kwa malengo ya kutumia vyombo hivyo kama njia ya kuwashawishi wanasiasa na viongozi wa kitaifa. Hii ni muhimu kwa sababu wanasiasa na viongozi wengine wa kitaifa wanaelewa mambo yanayoendelea miongoni mwa wananchi na wanauwezo wa kuweka kipengele cha ukeketaji katika risala zao za kitaifa.

Page 13: iac swahili.indd

13

Hata hivyo, kampeni za uhamasishaji pia hubeba madhara ambayo hayaku-tabiriwa. Watu wanajua kuwa ukeketaji ni mila ambayo imekatazwa. Hivyo basi wanaifanya kisirisiri huko vijijini na mara nyingi huwafanyia wasichana wadogo na hata wakati mwingine, mpaka watoto wachanga wa kike. Hili ni jambo la kusikitisha kwa sababu linaongeza madhara kiafya katika maisha yote ya hawa watoto na kwa upande mmoja hili zoezi la siri ni sababisho la kwamba kazi ya kutokomeza ukeketaji inakuwa ngumu sana. Hii ina maana kwamba, kwa upande mwingine kazi hii ya kupigania dhidi ya ukeketaji inakuwa muhimu zaidi sasa kuliko hapo awali. Imekuwa dhahiri kuwa mabadiliko ya msimamo mara nyingi huwa hayaendani na mabadiliko ya tabia ( maneno mengi utekelezaji kidogo). Watu lazima waelewe kuwa mabidiliko ya tabia kwa kuonyesha kwa vitendo, ni muhimu katika maisha yao. Hata hivyo, ni lazima ieleweke kwamba swala la ukeketaji ni swala pingamizi na ni tatizo zito katika jamii huko vijijini.

Dhara lingine ambalo linajitokeza kuletwa na kampeni hii ni kuwa wasichana na wanawake waliokeketwa hupakwa alama ya aibu na wenzao katika vijiji vyao. Mbeleni, wasichana ambao walikuwa hawakukeketwa walikuwa wakipata aibu kwa sababu walikuwa hawaonekani kama ‘wazima’ na hivyo basi ilikuwa ngumu kwao kuolewa, au pia kukubaliwa na jamii. Ajabu sasa ni kwamba aibu imepin-duliwa na kubandikwa kikundi kile ambacho zamani ndicho kilichokuwa ‘sawa’. Na hivyo basi leo hii makapera wengi wanadai hawataki kuoa wanawake walio keketwa. IAC inakumbana na pambano la aina mpya na imeonelea kuwa mbinu ya awali ya uhamasishaji iliyokuwa inatumika haiwezi kutumika milele.

Hii ni hisia kwamba IAC inalazimika kutafuta na kubadilisha mbinu mpya kulingana na mienendo inayokwenda na wakati, ili kukabili hili tatizo jipya lililojitokeza. Pambano moja kuu ni kuhakisha kwamba jamii inahamasishwa ili kuwaona wasichana na wanawake waliokeketwa wanachukuliwa kama binadamu wanaotumikia jamii vyema na wala sio watu tofauti wenye kasoro.

Mada hii inaeleza na kupendekeza vipengele bora katika shughuli za IAC, changamoto na mapambano dhidi ya ukeketaji na jinsi ya kukabiliana na zoezi katika changamoto hizi kufuatana na vigezo muhimu vya tathimini hii. Mwelekezo umewekwa zaidi katika mambo yenye kukubalika na kutekelezwa kulingana na mtazamo wa uhamasishaji wa afya ya jamii . Madhumuni hasa ni kuweka wazi mapambano yanayoikumba IAC. Uwazi katika kazi hii ya mapambano dhidi ya ukeketaji umeonekana kwa kiasi kutokana na mahojiano na watoa habari maalum, kwa kiasi kutokana na mazungumzo yaliyoshirikisha pande tofauti tofauti. Bila kusahau majadiliano baada ya michezo ya kuigiza na nyimbo zilizochezwa wakati wa mikutano iliyohusu ukeketaji.

Page 14: iac swahili.indd

14

Watathmini wangependa kuhitimisha kwa kueleza kuwa IAC Tanzania ni chama shupavu na imara chenye malengo, muamko na maoni muhimu bila kusahau wanachama wake wachachamavu wanaojitolea kwa dhati katika ngazi zote. Hata hivyo, watathimini wangependa kuhitimisha kwa kutoa mapendekezo yafuatayo:

• Endelezeni mbinu tofauti katika utendaji kazi kufuatana na hali halisi ya makundi tofauti ya watu. Hii mnaweza kufanya kupitia changamoto, warsha na majadiliano kwa kushirikisha matawi tofauti, na hivyo basi kuimarisha na kubo-resha ujuzi wa wahamasishaji.

• Tieni nguvu kazi ya kuwapa vijana uwezo wa kujitegemea ulio mkubwa zaidi katika kampeni zenu. Wapeni vijana uwezo! Wanahitaji ustadi, ujuzi katika mbi-nu hususani katika kufanya kazi na wazee, viongozi wa dini na wanasiasa katika jamii zao.

• Endeleeni na uendelezaji wa taratibu mpya katika maadili ya ukeketaji amabazo zitatimiza matakwa ya ukeketaji dhidi ya ukeketaji. Endeleeni kuendeleza kanu-ni mbalimbali za kimila bila kuhusisha ukeketaji. Wajumulisheni wazazi katika upangaji wa mikakati, mintarafu, hususani katika zile mila muhimu zinazoeli-misha jamii.

• Andaeni mikutano ya hadhara. Wapeni matumaini watu ili waeleze historia zao katika mihadhara, wabadilishane mawazo na uzoefu kwa kushirikiana na wale waliokuwa na matatizo kama wao.

• Imarisheni mbinu zenu za ukusayaji na uendelezaji wa habari zinazoeleweka. Ushahidi mwingi kuhusu madhara ya ukeketaji yanahitajika. Andikeni chini changamoto dhidi ya mapambano haya!

• Toeni kipaumbele katika elimu na mashuleni. Elimu na maarifa ndio vizingiti muhimu katika mapambano ya kukabiliana na ukeketaji.

• Kabilianeni na uwongo na mila potofuzinazoambatana na gonjwa la ‘lawalawa’! Endelezeni zaidi na ushirikiano wa wauguzi, manesi na vituo vya afya katika jambo hili!

• Pigeni vita doa la kutenga ambalo wanapatiwa watoto na wanawake ambao tayari wamekwisha keketwa. Ndio, ni muhimu kwamba ukeketaji lazima uma-lizike katika mila zetu, lakini hii isiwe kienzo cha kusababisha wale ambao wa-likwisha keketwa watengwe na kutiwa doa na jamii. Kumbukeni kwamba jamii hujengwa na wanajamii wote kwa kujumuika.

Page 15: iac swahili.indd

15

• Imarishani nguvu zenu kwa ushirikiano. Tembeleaneni vijijini, jipeni moyo kwa pamoja!

• Jengeni ushirika vijijini ili kukinga na kusuluhisha kutoelewana na matatizo ya (au matatizo yanayoweza kutokea) ndani ya ushirika.

• Endelezeni uhusiano pamoja na viongozi wa vijijini ambao huonekana ni

usaidizi bora kwa wakeketaji wa zamani.

• Endelezeni zaidi ushiriakiano baina ya IAC na vitongoji vyote za jamii.

• Imarisheni matumizi ya vyombo vya habari vinvyoweza kuonyesha ujumbe mathalani kwa kutumia runinga na filamu.

• Wahamasisheni wanasiasa na wabunge wenu.

• Ongezeni changamoto za uhamasishaji kwa wanaohusika na ukeketaji. Makabiliano tofauti yanahitaji mbinu tofauti za ufatiliaji.

• Tumieni watu wa vijijini!

• Hamasisheni watu wafanyiwe uchunguzi wa mara kwa mara.

Tunatumaini kwamba mapendekezo yetu yataeleweka kufuatana na ugunduzi tulioupata: ya kwamba IAC Tanzania ni chama muhimu chenye mambo mengi ya kujivunia na kupendeza katika muungano chama mwanvuli juu ya kamati za Waafrika. Pia chama hiki kina wanachama (waume kwa wake) waliojitolea, shupavu na mashujaa waliodhamiria kupambana na jambo ambalo linachukua muda mrefu kubadilishwa na linalohutaji utulivu na kujitolea. Kupambana na ukeketaji ni kazi ngumu. Tunaisifu Tanzania kwa kujitolea kuhakikisha jamii ya ijayo itakuwa haina shida hii ya ukeketaji wa wasichana na wanawake wa Tanzania.

Page 16: iac swahili.indd

16

Page 17: iac swahili.indd

17

2Hitimisho na mapendekezo

Hitimisho Lengo kubwa la tathimini hii lilikuwa ni kusambaza na kutoa maelezo kwa kiundani kuhusiana na kazi za IAC katika kuhamasisha haki za msingi za wanawake na kuleta mabadiliko katika jamii kwa njia ya uelimishaji na ufahamishaji, au kuleta mwamko kutoka kwa wahamasishaji wa IAC kupitia ngazi na maeneo mbalimbali. Kwa ujumla dhumuni kubwa katika tathimini hii ni kutafuta njia ya kupambana na changomoto kuhusu jinsi gani shughuli za chama zitaendelezwa, kwa kushirikiana pamoja katika vita dhidi ya vitendo vya ukeketaji, kwa kutumia njia ya tathimini shirikishi. Watathimini walifanikiwa kupata tathimini zilizohitajika. Kwa kutumia mbinu ya kuteua washiriki waliokuwa na habari zilizohusiana na madhumuni ya tathimini. Mijadala na mahojiano yalifanyika kwa wanawake wahusika ambao pia wako katika mstari wa mbele katika shughuli za IAC, kuanzia ngazi za vijiji na za kitaifa nchini Tanzania, vijana wa jinsia zote, watu waliokuwa wakifanya vitendo vya ukeketaji, watu wa marika yote ambao wameshahamasika katika kuleta mabadiliko na wanachama wa IAC, watu mashuhuri na muhimu vijijini na mikoani, viongozi wa dini na wazee, pamoja na mkurugenzi mtendaji wa chama cha waandishi wahabari cha wanawake nchini Tanzania, TAMWA. Baada ya mahojiano na mijadala, wanatathimini walihitimisha kuwa IAC ni chama imara kilicho na malengo na mtazamo imara wa utendaji na chenye wanachama wenye ari ya kujitolea na walio wachachamavu katika pembe na ngazi zote nchini.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1984 mpaka hivi sasa chama cha IAC kina kamati za kimataifa katika nchi 28 barani Afrika. Kamati hizi za kimataifa zimegawanywa katika makundi kufuatana na viwango vya utendaji na changamoto zinazokabiliana nazo. Hivi karibuni kamati ya IAC ya Tanzania limechaguliwa kuwa ni kundi katika kifungu cha kwanza kwa jinsi lilivjoonyesha utendaji bora katika kuratibu na kuandaa mapambano dhidi ya ukeketaji. Wahamasishaji wake wanafahamu umuhimu katika kuhamasisha makabila husika nchini Tanzania kuhusiana na madhara yatokanayo na vitendo vya ukeketaji, na pia jinsi ya kuwawezesha vijana ili kushiriki katika kupinga vitendo hivi. Kamati ya IAC nchini Tanzania inaongozwa na wanawake wanajitolea kwa hali na mali (na baadhi

Page 18: iac swahili.indd

18

ya wanaume pia) ambao wameweza kuleta mafanikio katika kazi zao. Sambamba na kuwa kazini wamekuwa pia wakifanya tathimini ya shughuli zao na kufanyia kazi matokeo ya tathimini zao na marekebisho katika kazi zao. Viongozi hawa wanatambua changamoto zilizopo katika kukabiliana na makabila tofauti nchini. Matatizo haya ni pamoja na kuwepo kwa tofauti kubwa za mtazamo kuhusiana na suala la ukeketaji miongoni mwa vizazi tofauti. Pia kuna muelekeo wa tatizo kuhusiana na changamoto inayoonyesha umuhimu wa kushirikiana kwa pamoja katika mapambano haya kwa watu wa aina zote nchini Tanzania. Hii ina maana kwamba jinsi ya kuhusisha watu wa marika yote, jinsia zote, na viongozi wa kidini na kisiasa katika ngazi ya chini,mkoa na taifa. Hivyo basi IAC imeweza kujumuisha watu wa pande tofauti tofauti katika kazi zake, kuanzia wanawake waliokeketwa na wale ambao bado hawajakeketwa. Wanaume pia wamejumuishwa. Kwa kifupi hili ni jambo linalostahili sifa kubwa.

Japo IAC imepata mafanikio makubwa, chama hiki kinatambua kwamba kuna mapambano makubwa siku za usoni. Hii ni kwa sababu ya hali ya mada hizi ambazo kwa desturi huwa ni nyeti ambazo zimekuwako kwa muda mrefu na hivyo basi jamii huwa na ugumu wa kukubali mabadiliko. Chama hiki kinatambua vile vile ugumu wa kujua uzito wa tatizo la ukeketaji (hasa kwa sababu zoezi hili linafa-nyika kwa siri na wahusika hutoa taarifa isiyo halali). Hivyo basi ni vigumu sana kuweza kukagua matokeo ya kazi ya utendaji dhidi ya kujitolea vilivyo. Ilihali, IAC inatambua ugumu wa kazi inayofanya na pengine huwenda ikachukua kizazi kizima mpaka kufikia jamii isiyo na ukeketaji Tanzania nzima. Kwa vile wametabiri hali hii, wanaendelea kuongeza ujuzi wa kulikabili tatizo la ukeketaji na kuhakikisha kufanikiwa katika utendaji wa kazi zao huku wakijaribu kufuata njia ambazo zinaambatana na kueleweka kulinganisha na hali ya vijiji wanavyo-fanya navyo kazi kusudi waweze kuboresha pambano la ukeketaji. Hii ni pamoja na juhudi za kuweza kuhamasisha watu wa sehemu husika katika kuelimisha nama ya kupambana dhidi ya ukeketaji.

Licha ya kufanya kazi zinazoleta matokeo mazuri na pia kuwa na wanachama wahamasishaji wanaojitolea kwa hali na mali, kamati ya IAC, Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto na matatizo mbalimbali. Chama hichi kinaathiriwa na uchumi duni kama vilivyo vyama vyengine visivyo vya kiserikali (NGO) vinavyokabiliwa na uduni huu wa kiuchumi. Uchumi duni unachangia pingamizi dhidi ya utendaji na wahamasishaji wake. Katika muktadha huu Chama hiki kinastahili sifa na ni jambo la kutia moyo kuona jinsi wanachama wameweza kuungana na kuendelea kufanya kazi yao kwa kujitolea kwa hali na mali dhidi ya vipingamizi vikubwa. Vile vile ni sifa kubwa kuona jinsi wasivyokata tamaa za utendaji wa kazi zao licha ya kupata upinzani mkubwa, kubughuziwa na kukanwa na hata kutishiwa maisha yao wanapokwenda vijijini kuwahamasisha kuhusu suala hili nyeti la ukeketaji. Kwa kifupi basi wahamasishaji na wakereketwa

Page 19: iac swahili.indd

19

hawa wanastahili sifa ya ujasiri kwa kuwa ni mashujaa katika mapambano haya dhidhi ya ukeketaji.

Mapendekezo

Sisi watathmini tumefurahishwa na kuridhishwa sana na kazi inayofanywa na kamati ya IAC, Tanzania. Kwa jinsi hii tungependa kuwapatia maneno ya kutia moyo: Endeleeni na mienendo yenu ya kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa, viongozi wa dini, wazee, vijana na jamii! Endeleeni kuwaelimisha wasichana kuhusu sheria zilizopo na ambazo zitawalinda dhidhi ya ukeketaji! Tayarisheni vijana kusudi waweze kujitetea wenyewe! Endeleeni na kazi ya kuwaangalia na kuwalea ”wasichana-watorokao-ukeketaji”! Endeleeni kutumia elimu mashuleni kama sehemu za kubadilisha jamii!

Hata hivyo ni muhimu kusisitiza kwamba Kamati ya IAC, Tanzania, inakumbana na vikwazo muhimu tofauti tofauti ambavyo vinahitaji kuelezwa na kufafanua katika jitihada ya kutafutia uvumbuzi na masuluhisho kupatikana. Hivyo basi, watathmini wangependa kutoa mapendekezo yafuatayo:

• Endelezeni mbinu tofauti katika utendaji kazi zinazoweza kutumika kwa makundi tofauti ya watu.

Hii mnaweza kufanya wakati wa changamoto, warsha na majadiliano kwa kushi-rikisha matawi mbalimbali na hivyo basi kuimarisha na kuboresha ujuzi wa wahamasishaji. Endeleeni kuongeza mbinu za uhamisashaji wakati mkiangalia jinsi gani vikundi vya makabila tofauti vinaweza kusaidiana katika mapambano haya kusudi juhudi hii iimarike na iweze kudumu. Ni vyema pia kujaribu kutafuta mbinu amabazo vijana wataweza kuwakabili wazee wa makabila yao bila kusaba-bisha mgogoro. Jifunzeni na mgundue mbinu mpya. Sambazeni vyombo vya uelimishaji katika wilaya zenu.Wekeni mwamko na nia mpya za kufanya kazi na kuwaelimisha watu. Vijana wangependa wapate njia mpya na mbinu mpya za makabiliano, elimu na ukufunzi kupitia changamoto na warsha.

• Wapeni vijana uwezo mkubwa zaidi katika kampeni zenu.

Wapeni vijana nyenzo! Kwani wanajamii huko vijijini wanashuhudia jinsi gani kumekuwa na tofauti kubwa baina ya wazee wenye kufuata mila na desturi za jadi, na maadili na mafunzo wafuatayo vijana wa sasa. Hivyo basi, kuna haja ya kuimarisha na kutilia mkazo kazi kwa vijana. Suala la vijana linatakiwa kuchu-kuliwa maanani na kuangaliwa kupitia mtazamo wa pande zote za jamii. Vijana

Page 20: iac swahili.indd

20

wanahitaji ujuzi katika mbinu za kukabiliana, hasa, na viongozi wa dini, wazee na wanasiasa. Makabiliano yao lazima yawe kwenye kiwango cha kujumuisha. Tumieni usambazaji wa habari kupitia runinga na video katika kuelimisha vijana. Usambazaji wa aina hii umeonyesha mafinikio makubwa miongoni mwa vijana katika mapambano dhidi ya ukeketaji katika sehemu mbalimbali. Endelezeni wingi wa sekta ya vikundi vinavyohusisha vijana (yaani wanaume kwa wanawake), pia endelezeni kazi inayohusisha vijana kwa wazee. Endelezeni elimu iliyotayarishwa kwa madhumuni ya kuelimisha watu mapambano yenu. Shirikisheni kwa mialiko maafisa wa maendeleo kwenye jamii na pia viongozi wa kanisa.

• Endeleeni na upanuaji wa taratibu mpya dhidi ya ukeketaji.

Tengezeni vipindi vya uhamisishaji wa jamii kwa kutumia sinema\video kwa nia ya kubadili vitendo vya ukeketaji. Video hizi zikionyeshwa kwa wananchi zinaweza kuwa ni changamoto na kichocheo katika kuleta mabadiliko katika jamii! Kwa vile ukeketaji wa wasichana ni njia mojawapo pekee ya usambazaji wa mila na elimu asili kwa jamii tumieni wazee kutafuta njia zingine za kutoa elimu hiyo kwa wasichana.Hii ni muhimu kwa sababu wazee wangependa wasichana wawe na tabia nzuri na wajue mila pia. Vile vile usambazaji wa elimu asili ya mila kutoka kwa wazee hadi kwa vijana itaimarisha hali ya maisha ya pamoja katika jamii na pia itaimarisha uhusiano miongoni mwa vizazi tofauti. Sherehe (kama unyago) inayotoa ujuzi wa mila na tabia njema za jamii wakati huo huo ikiwa inakemea ukeketaji, inaonekana ina mafanikio makubwa miongoni mwa jamii. Waelezeni wazazi watafute taratibu zengine za kushangilia mila zenu. Waalikeni na wahusisheni katika upangaji na mipango ya elimu dhidhi ya taratibu isiyohusisha ukeketaji.

• Andaeni mikutano ya hadhara.

Wapeni moyo matumaini watu ili wapate mwamko wa kueleza historia zao katika mihadhara. Wapeni nafasi ya kubadilishana mawazo na wazoefu waliokuwa na matatizo kama wao (wakereketwa). Wananchi wa vijijini hupenda kusikia hadithi za mafanikio hivyo basi zienezeni miongoni mwa wanavijiji. Kwa makusudi ya kuwabadilisha watu mawazo ni muhimu muweze kuwahusisha wabunge, viongozi wa kisiasa na watendaji. Wanawake wanaojitokeza hadharani na kusema “mimi nimekeketwa na nimepata madhara makubwa kwa sababu hii!” wanachangia kuelezea tajriba yao ya maisha wanaweza kuwafanya watu waseme “tumesema wazi wazi ya kuwa tungependa kusimamisha jambo hili na hivyo basi wanawake wa vijiji vyote ni muhimu kujitokeza hadharani!”

Page 21: iac swahili.indd

21

• Imarisheni mbinu zenu za ukusanyaji na uendelezaji wa habari zenye ukweli.

Ushahidi mwingi kuhusu madhara ya ukeketaji unahitajika. Imarisheni kwa kuweka kumbukumbu changamoto nyeti dhidi ya mapambano haya! Utafiti wa ukeketaji unaonyesha kuwa kuna udhaifu katika utafiti mzuri kuhusu mila hii. Wanachama wa IAC wana mada na vielelezo vingi kuhusu tatizo hili. Husisheni wodi za wazazi na wakunga wa jadi, kwa sababu wasichana wengi watawasiliana nao wakati wa mimba na kujigungua.

• Toeni kipaumbele kwa elimu na shule.

Kutokupata elimu na maarifa ndio vizingiti vikubwa katika mapambano ya kukabi-liana na ukeketaji. Umma lazima uelewe kwa nini ukeketaji lazima utokomezwe. Sheria inayokataza ukeketaji wa watoto wa kike haiwezi kufanya kazi yake iwapo watu hawajui kwa nini jambo hili limekatazwa. Elimisheni vijana kwani msipo-waelimisha hawatakuwa na akili ya kuweza kugundua baya na kulitenganisha na zuri katika kuendesha maisha yao. IAC lazima ishirikiane na mashule. Angalieni sababu zinazo fanya vijana kuacha shule na mziunganishe na matatizo ya jamii. Pamoja na yote, mtaona ya kuwa watoto wengi wana maisha magumu, licha ya haki zinazowatetea; kwa mfano, ukiangalia watoto yatima na jinsi wanavyotumika kinyume cha haki zao kwa kufanyishwa kazi nyingi nyumbani.

• Kabilianeni na uwongo na imani za kale kuhusu ugonjwa wa ‘lawalawa’!

Endelezeni zaidi ushirikiano wa wauguzi na vituo vya afya katika jambo hili! Madaktari na wafanyi kazi wa hosiptali wanahakikisha kuwa ’lawalawa’ ni ugonjwa unaosababishwa na uchafu na unaweza kutibiwa. Kufuatana na imani potofu, ’lawalawa’ inatumika mara nyingi kuhalalisha ukeketaji na kwa hivyo inataikiwa ipatiwe nafasi kubwa katika mapambano dhidi ya ukeketaji. Wauguzi wanatakiwa wawe mstari wa mbele na wachukue pambano la kuelimisha jamii kwa kujitolea.

• Imarishaneni nguvu zenu.

Tembeleaneni vijijini mpeane moyo! Hii itasaidia kutia moyo watendaji wa sehemu tofauti tofauti. Ni muhimu mjulishe umma kwamba kuna makabila mengi ambayo yanafanya tohara kwa watoto wa kike na hivyo basi ni lazima kabila husika zishiri-kiane. Pangeni mabaraza, changamoto na warsha tofauti tofauti. Oneni umuhimu wa kutolewa kwa mgawo wa msaada wa usafiri, baiskeli, vyombo vya ofisini na posho za kila siku kwa watendaji. Watendaji hutembea kwa muda mrefu kwa

Page 22: iac swahili.indd

22

makusudi ya kugawanya elimu unyeti kuhusu mada hii. Hivyo basi wao huenda njaa na kuchoka kwa sababu ya ukosefu wa uchumi bora. Ni lazima kusaka suluhisho kwa tatizo hili ama sivyo chama hiki kitakimbiwa na hawa watendaji waliojitolea kwa sababu ya uchovu na ukosefu wa kutiwa moyo.

• Kijengeni chama vijijini ili kukinga na kusuluhisha kutoelewana na matatizo ya (au matatizo yanayoweza kutokea) ndani ya chama.

Uhusiano mzuri unaweza kupatikana kupitia mikutano ya kitaifa inayoweza kukusanya matawi yote ya chama. Pia kuna haja ya kufunua idara ndani ya chama hiki itakayojihusisha tu na usuluhishaji wa mizozo katika kutoa mawaidha yanayofaa kwa wasichana na jamii wanapokuwa wanaotafuta msaada na mawaidha.

• Endelezeni njia bora katika kuwasaidia na kuwatia moyo wakeketaji walioacha kufanya kazi ya ukeketaji wa wanawake.

Iambieni jamii iwakubali na iwasaidie katika kutafuta njia zengine lisha kwa jamii zao kusudi wasipate matatizo ya kifedha kwa kutoifanya kazi yao, la sivyo wataen-delea na kazi yao kisiri siri. Toeni shahada za vyeti vinavyoonyesha ya kuwa wahusika wameacha kazi ya ukeketaji, hasa vyeti vilivyo na picha kisha mwafanyie karamu ya kuwatunukia.

• Endelezeni zaidi ushiriakiano baina ya IAC na vitongoji vyote vya jamii.

Ushirikiano bora na utendaji unahitajika katika sekta vitongoji vyote vya jamii, bila kusahau zahanati, na wauguzi, viongozi wa kisiasa, viongozi wa dini na vyama vinavyofanya kazi zinazohusiana na haki za binadamu, haki za wanawake na haki za watoto.

• Imarisheni matumizi ya vyombo vya habari vinavyoweza kuonyesha ujumbe kupitia runinga na filamu.

Tengezeni video zinazoonyesha taratibu zengine za mila! Jambo hili litawatia moyo walengwa ili waweze kubadilisha njia zao. Elimisheni umma kupitia video. Tumieni redio na runinga kusudi muwafikie watu wengi katika sehemu tofauti. Shirikianeni na wasanii na waandishi ambao wanaweza kutafsiri ujumbe wa IAC kupitia nyimbo, mashairi na tamthilia kwa ajili ya kusambazisha ujumbe huo kwenye vyombo vya habari.

Page 23: iac swahili.indd

23

• Wahamasisheni wabunge wenu.

Elimisheni wanawake kwa wanaume katika mambo ya sheria ili waweze kuwasaidia wale ambao wameathiriwa na ukeketaji. Kuna haja ya kuanzisha idara itakayohusika na maswala ya kisheria hasa ya mambo ya wanawake! Kuna haja ya mawakili wa kuwatetea wale wanaokataa kukeketwa. Pia watu wanofanya kazi na polisi na mahakama wanahitaji mafunzo.

• Ongezeni changamoto za uhamasishaji kwa walengwa.

Makabiliano tofauti yanahitaji mbinu tofauti za ufatilizi. Ni ngumu kusikilizwa kama unafanya kazi ya kusimamisha ukeketaji, na ni ngumu zaidi kuweza kufanya watu wabadilishe mienendo yao. Matakwa ya wamaasai ni tofauti kulinganisha na makabila mengine na hivyo wamasaai wanaweza kuhitaji kuhamasishwa zaidi kushinda makabila mengine.Ukeketaji umechimba mizizi katika mila za kimaasai na hivyo basi ni ngumu sana kubadilisha imani zao japokuwa vifo miongoni mwa wasichana ni vingi sana. Olaiboni (watemi) wa wamasaai ndio wanaofanya uamuzi na ni lazima wafahamishwe madhara ya ukeketaji. Mkihamasisha vijana bila ya kuwahusisha Olaiboni itakuwa hamna faida itakoyopatikana. Kwa kifupi viongozi wote lazima wafahamishwe madhara ya ukeketaji. Wanawake kwa kawaida huwa hawajui sheria zinazowahusu, hivyo ni inapaswa mtengeneze mafunzo na kuwae-lekeza kuhusu husika kufuatana na uwezo wao wa kuelewa.

• Tumieni watu wa vijijini!

Tumieni watu wa vijijini wanojua lugha na mila za makabila yao na wenye kufahamu watu wa jamii zingine zilizolengwa kwa undani zaidi. Hii ni muhimu katika kujenga uaminifu na kuleta maelewano. Hamasisheni na wafundsheni madhara ya ukeketaji watu wale ambao mara nyingi ndio wanaoheshimika na kusikilizwa katika jamii. Jaribuni mpange elimu yenu kwa marika kwa sababu kimila ni vigumu kwa wazee kuwasikiza vijana na kwa vijana pia ni vigumu kuzungumza na wazee kuhusu mada nyeti zinazohusiana na mila na desturi zetu. Kabilianeni na wanasiasa wa vijijini, viongozi wa dini na watu wanaoheshimika vijijini. Sikilizeni kila mawaidha ya watu wa vijijini yanayohusiana na mbinu zenu. Hamasisheni kila kitongoji! Watendaji wa IAC ni watumwa wa mabadiliko na hivyo basi lazima mfanye kazi pamoja nao na pia pamoja na vikao vya wilaya. Wapeni nguvu na uwezo watu wenyewe ambao ni walengwa waje na masuluhisho ya matatizo yao.

Page 24: iac swahili.indd

24

• Hamasisheni watu wafanyiwe uchunguzi wa mara kwa mara.

Hamasisheni katika kiwango cha kitaifa na cha vijijini kusudi kuweko na sheria inayowalazimisha watu kupeleka watoto wao hospitali kwa uchunguzu wa mara kwa mara. Hamasisheni kutokea ngazi za chini mpaka ngazi za juu, ili wote wanao-husika waweza kufanya zoezi la kusisitiza sheria itakayowaruhusu wauguzi kwenye vituo vya afya kuwaangalia na kuwachunguza watoto wanaoletwa kupimwa afya vituoni.