67
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mkakati wa Kitaifa wa Kisomo na Elimu kwa Umma (MTaKEU) 2020/2021 - 2024/2025 Januari, 2020

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

  • Upload
    others

  • View
    38

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Mkakati wa Kitaifa wa Kisomo na Elimu kwa Umma (MTaKEU) 2020/2021 - 2024/2025

Januari, 2020

Page 2: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

ii

Yaliyomo

DIBAJI ���������������������������������������������������������������������������������������������������������������������� iv

SHUKURANI ������������������������������������������������������������������������������������������������������������ vi

ORODHA YA VIFUPISHO ���������������������������������������������������������������������������������������� vii

MUHTASARI ����������������������������������������������������������������������������������������������������������� viii

SURA YA KWANZA �������������������������������������������������������������������������������������������������� 1

UTANGULIZI ������������������������������������������������������������������������������������������������������������� 1

1.1 Usuli ........................................................................................................................ 1

1.2 Madhumuni ya MTaKEU ...................................................................................... 4

1.3 Hatua za Uandaaji wa MTaKEU ....................................................................... 4

SURA YA PILI ������������������������������������������������������������������������������������������������������������ 5

UPEMBUZI YAKINIFU WA MAZINGIRA �������������������������������������������������������������������� 5

2.1 Maendeleo ya Kisomo na Elimu kwa Umma Tanzania ................................. 5

2.2 Mifumo ya Kisera Inayozingatiwa katika MTaKEU ...................................... 7

SURA YA TATU ������������������������������������������������������������������������������������������������������� 10

UCHANGANUZI WA UWEZO, UDHAIFU, FURSA NA CHANGAMOTO ������������������ 10

3.1 Muhtasari wa Uchanganuzi ............................................................................10

3.2 Tathmini ya Mazingira ya Ndani ....................................................................10

SURA YA NNE ��������������������������������������������������������������������������������������������������������� 14

DIRA, DHIMA NA MALENGO YA KIMKAKATI ������������������������������������������������������� 14

4.1 Dira .......................................................................................................................14

4.2 Dhima ...................................................................................................................14

4.3 Malengo ya Kimkakati ....................................................................................14

4.4 Malengo ya Kimkakati, Mikakati, Shabaha na Viashiria vya Utendaji.15

Page 3: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

iii

SURA YA TANO ����������������������������������������������������������������������������������������������������� 30

MFUMO WA USHIRIKIANO KITAASISI KATIKA KUTEKELEZA MTaKEU ���������������� 30

5.1 Wahusika wa MTaKEU ......................................................................................30

5.2 Mfumo wa Kitaasisi katika Kutekeleza MTaKEU .........................................31

SURA YA SITA ��������������������������������������������������������������������������������������������������������� 42

UFUATILIAJI, TATHMINI NA MFUMO WA UTOAJI TAARIFA ��������������������������������� 42

6.1 Maelezo ya Jumla ............................................................................................42

6.2 Ufuatiliaji na Tathmini ya utekelezaji wa MTaKEU .....................................42

SURA YA SABA ������������������������������������������������������������������������������������������������������� 44

UWEZESHWAJI WA KIFEDHA NA UENDELEVU WA MKAKATI ������������������������������� 44

7.1 Uwezeshwaji wa Kifedha wa MTaKEU ..........................................................44

7.2 Mikakati ya Kupata Fedha ..............................................................................41

7.3 Makadirio ya Gharama za MTaKEU kwa kipindi cha 2020/2021- 2024/2025 .......................................................................................................45

7.4 Uendelevu katika Utekelezaji wa MTaKEU .................................................49

KIAMBATISHO �������������������������������������������������������������������������������������������������������� 50

Page 4: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

iv

DIBAJI

Upatikanaji wa stadi za kisomo na elimu kwa umma ni jambo la

muhimu katika kuwasaidia wanaume na wanawake wa Tanzania

kuyatawala mazingira yao. Kutokana na umuhimu wa stadi za kisomo

katika kumwezesha mtu kuwa raia mwema, kisomo kimekuwa ni sehemu

ya programu za elimu ya watu wazima nchini. Kwa hiyo, mkakati huu

unalenga kuleta mabadiliko kwa vijana na watu wazima nchini Tanzania,

ambao wanakabiliwa na changamoto zinazotokana na kutokuwa na stadi

za kisomo katika maisha yao ya kila siku. Madhumuni ya mkakati huu

ni kubuni, kuendeleza na kuandaa programu bora za kisomo na elimu

kwa umma zinazowafikia watanzania wengi. Vilevile, umejikita katika

kuhakikisha umahiri unaopatikana unaendelezwa kwa kuimarisha huduma

saidizi za kisomo. Mkakati umebuniwa baada ya kufanya upembuzi

yakinifu wa hali ya kisomo na elimu kwa umma na kwa kuhusisha

watekelezaji mbalimbali wa programu za kisomo na elimu kwa umma

nchini. Mkakati huu unatanabahisha masuala muhimu yaliyobainishwa

na wadau wakuu wa kisomo na elimu kwa umma kama njia ya kusaidia

kushughulikia changamoto za kisomo na elimu kwa umma nchini Tanzania.

Watekelezaji mbalimbali wa shughuli za kisomo na elimu kwa umma kama

vile Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST), Tawala za Mikoa na

Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Wizara,

Idara na Wakala za Umma, mamlaka za serikali za mitaa, asasi za kiraia,

wadau wa maendeleo, vyuo vikuu, Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania,

na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ni washirika wakubwa katika

kubuni na kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kisomo na Elimu kwa Umma

(MTaKEU). Hivyo, unahitajika ushirikiano madhubuti kati na baina ya

wizara na taasisi mbalimbali za serikali katika kuhakikisha utekelezaji

sawia na wenye kuleta tija. Kwa mantiki hiyo, serikali itaendeleza juhudi

Page 5: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

v

zake ili kuhakikisha kwamba kunakuwepo na jamii ya watu walioelimika

na wenye uwezo wa kupata taarifa sahihi ili kuwa na maisha bora na

maendeleo endelevu. Serikali inatambua pia ukweli kwamba ukosefu wa

stadi za kisomo kwa vijana na watu wazima ni kikwazo katika jitihada

za kutimiza agenda za maendeleo ya taifa na malengo ya maendeleo

endelevu kufikia mwaka 2030, ambayo Tanzania imeridhia kuyatimiza

kikamilifu. Kwa hali yoyote ile, Serikali kupitia WyEST itaendelea kuweka

mazingira mazuri yatakayoruhusu wadau mbalimbali kushiriki kikamilifu

katika kutekeleza mkakati huu.

……………………………

Dkt� Lyabwene M� Mtahabwa

Kamishna wa Elimu

Page 6: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

vi

SHUKURANI

Mkakati wa Kitaifa wa Kisomo na Elimu kwa Umma (MTaKEU) ni matokeo

ya juhudi na michango mbalimbali kutoka kwa watu binafsi, mashirika na

wizara za serikali. Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima (TEWW) inatoa

shukurani za dhati kwa wadau wote ambao wamefanikisha maandalizi ya

mkakati huu. Kwa nafasi ya pekee, TEWW inaishukuru Wizara ya Elimu,

Sayansi na Teknolojia (WyEST) kwa kuongoza maandalizi ya mkakati

huu. Maelekezo na msaada ambao umeendelea kutolewa na WyEST

umefanikisha kuandikwa kwa mkakati huu. TEWW inatoa shukurani pia

kwa wataalamu wa ndani ya TEWW, WyEST, na Ofisi ya Raisi - Tawala

za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa mchango na ushauri

wao wa dhahiri ambao umefanikisha andiko hili.

Vivyo hivyo, TEWW inatoa shukurani kwa mashirika mengine na wadau

mbalimbali walioshiriki kwa mchango wao mkubwa mpaka kukamilika kwa

mkakati huu. Pia, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima inatambua mchango

kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,

Taasisi ya Elimu Tanzania, Baraza la Mitihani la Tanzania na Mamlaka ya

Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Mashirika mengine ni pamoja na Bodi ya

Huduma za Maktaba Tanzania, Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, asasi za

kiraia na wadau wa maendeleo.

……………………………

Dkt� Naomi Katunzi

Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi TEWW

Page 7: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

vii

ORODHA YA VIFUPISHO

CCM Chama cha Mapinduzi

MEMKWA Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa

MMEM Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi

MTaKEU Mkakati wa Kitaifa wa Kisomo na Elimu kwa Umma

MTEF Medium Term Expenditure Framework

MUKEJA Mpango wa Uwiano kati ya Elimu ya Watu Wazima na

Jamii

OR-TAMISEMI Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

TEWW Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima

URT United Republic of Tanzania

WyEST Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Page 8: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

viii

MUHTASARI

Serikali ya Tanzania imefanya juhudi kubwa kupambana na tatizo la

kutokujua kusoma, kuandika na kuhesabu nchini. Ipo mikakati rasmi na

isiyo rasmi inayotumika katika kupambana na kutokujua kusoma, kuandika

na kuhesabu nchini Tanzania. Jitihada na mikakati hiyo inayofanywa na

serikali ya Tanzania inaendana na lengo namba 4.6 la Malengo ya

Maendeleo Endelevu ya dunia ambalo linajikita katika “kuhakikisha

kwamba vijana na watu wazima wote, wanaume na wanawake, wanafikia

kiwango cha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu ifikapo mwaka 2030.

Lengo hili linaakisi jitihada za kiulimwengu zinazoendelea za kuzitaka

serikali zote ulimwenguni kuondoa tatizo la kutokujua kusoma, kuandika

na kuhesabu.

Licha ya jitihada zinazofanywa na nchi ya Tanzania kuendeleza fursa

za elimu na kisomo tangu uhuru, matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi

nchini Tanzania (URT, 2012) yanaonesha kwamba, vijana na watu wazima

wenye umri wa miaka 15 na zaidi wapatao milioni 5.5 (22.4% ya idadi

ya watu wote) hawajui kusoma na kuandika. Takwimu hii inatoa picha

kwamba vijana na watu wazima milioni 5.5 bado hawana haki ya msingi

ya kupata fursa za elimu na stadi za kisomo. Kutokujua kusoma na

kuandika ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya mtu binafsi na jamii

kwa ujumla. Hivyo, Mkakati wa Kitaifa wa Kisomo na Elimu kwa Umma

(MTaKEU) ni programu ya miaka mitano kwa kipindi cha 2020/2021-

2024/2025 ambayo imeandaliwa kama mwitikio wa kushughulikia tatizo

hilo. Mpango huu unatambua kisomo kama haki ya msingi kwa maendeleo

ya mtu binafsi, kijamii, kiuchumi na kisiasa.

MTaKEU ni mwongozo ulioandaliwa kwa makusudi kama nyenzo ya

kuongoza wadau mbalimbali ambao wanatekeleza programu za kisomo

Page 9: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

ix

na elimu kwa umma katika ngazi tofauti nchini. Mkakati unatambua

kwamba masuala ya kisomo na elimu kwa umma ni mtambuka na yanahitaji

kufanyiwa kazi na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu ya watu wazima

na elimu nje ya mfumo rasmi. MTaKEU umeandaliwa kutokana na tathmini

ya mahitaji ambayo ilihusisha watu binafsi, serikali, mashiriki ya kiserikali

na yasiyokuwa ya kiserikali, taasisi za elimu na washirika wa maedeleo.

Mkakati unabainisha jitihada za taifa katika kukuza na kuendeleza

kisomo na unahusianishwa na sera, matamko na mikataba ya kitaifa na

kimataifa, kwa kuzingatia uzoefu tulioupitia katika sekta ya elimu tangu

nchi ilipopata uhuru.

Dira ya muda mrefu ya MTaKEU ni kuwa na jamii iliyoelimika na yenye

uwezo wa kupata taarifa sahihi kwa ajili ya kuwa na maisha bora na

maendeleo endelevu. Kuifanya dira hii iwe halisi, mkakati huu umeweka

malengo kadhaa ambayo ni: Kuanzisha programu za kisomo na elimu

kwa umma zilizo bora na zenye manufaa kwa jamii; Kuimarisha mifumo na

programu wezeshi za kuendeleza kisomo na elimu kwa umma; Kuboresha

mifumo ya usimamizi wa takwimu za kisomo na elimu kwa umma; Kuweka

viwango vya sifa za kitaaluma kwa ajili ya programu za kisomo na elimu

kwa umma; Kuandaa zana na vifaa bora vya kufundishia na kujifunzia

katika programu za kisomo na elimu kwa umma; Kujenga uwezo wa

wawezeshaji na waratibu wa programu za kisomo na elimu kwa umma;

Kukuza kazi za utafiti, uvumbuzi na ubunifu katika masuala ya kisomo na

elimu kwa umma. Mkakati huu umeweka pia mikakati mahsusi, shabaha

na viashiria vya utendaji kwa kila lengo.

Mkakati huu unafafanua kwa uwazi mfumo wa utekelezaji; unaonesha

jinsi ufuatiliaji na tathmini vitakavyofanyika; na unafafanua utaratibu wa

kifedha utakavyokuwa katika kufikia malengo. Wakati ambapo WyEST

inakuwa na jukumu kuu la kiuongozi katika utekelezaji wa mkakati huu

Page 10: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

x

kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, wadau wengine wote wanahitaji

kuhakikisha kwamba majukumu yao yaliyobainishwa yanaingizwa

katika mipango na bajeti zao. Hivyo basi, inatarajiwa kwamba MTaKEU

utaongoza juhudi za kukuza na kuendeleza kiwango cha stadi za kisomo

miongoni mwa vijana na watu wazima nchini na kusababisha kuwa na

maisha bora na maendeleo endelevu.

Page 11: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

1

SURA YA KWANZA

UTANGULIZI

1�1 Usuli

Kisomo ni moja kati ya nyenzo kuu za maendeleo na sehemu muhimu ya

stadi za msingi na umahiri unaohitajika kumwezesha mtu kuwa raia mwema.

Huimarisha uwezo wa watu kujishughulisha kwa uhuru na kuongeza uwezo

wao wa kutawala na kubadili maisha yao. Ukosefu wa stadi za kusoma,

kuandika na kuhesabu huwafanya watu kuwa wahanga wa umasikini,

kutengwa kijamii, na kushindwa kupata mahitaji ya msingi na kukabiliwa

na hatari ya kunyimwa haki za kibinadamu. Kwa kutambua umuhimu

mkubwa wa kisomo, tangu mwaka 1948, UNESCO imekuwa ikitazama

kisomo kama haki ya binadamu. Kwa tafsiri rahisi, kisomo humaanisha

uwezo wa kusoma, kuandika na kufanya hesabu za kawaida katika

lugha yoyote kwa kiwango kinachoridhisha. Hata hivyo, katika mkakati

huu, dhana ya kisomo haiishii tu katika uwezo wa kusoma, kuandika na

kufanya hesabu rahisi, bali pia katika kutambua matumizi yake kwenye

maingiliano ya maisha ya siku kwa siku na katika kutatua matatizo ya

maisha ya kila siku.

Tangu mwaka 1961, Tanzania ilipopata uhuru, kutokujua kusoma na

kuandika kumetambuliwa kuwa ni mojawapo ya vyanzo vikubwa vya

umasikini, maradhi, ukandamizaji na unyonyaji katika jamii. Kwa sababu

hiyo, jitihada za kuondoa tatizo la kutokujua kusoma na kuandika kwa watu

wazima zilianzishwa na serikali ya Tanzania miaka ya 1970. Ili kufikia

lengo hilo, serikali ilifanya jitihada mbalimbali zikiwemo za kukusanya

rasilimali zinazohitajika katika utekelezaji wa programu za kisomo kutoka

kwa wafadhili na wadau wengine ndani na nje ya nchi, kuweka muundo

wa usimamizi katika ngazi za chini za jamii pamoja na kutoa mafunzo kwa

Page 12: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

2

waratibu wa elimu ya watu wazima. Walau kila halmashauri au wilaya

ilihamasisha watu wazima kujiunga katika madarasa ya kisomo kwa

ajili ya kujifunza kusoma, kuandika na kufanya hesabu rahisi. Kampeni

za kuelimisha umma ziliandaliwa, kama vile Kazi ni Uhai, Kupanga ni

Kuchagua, Uhuru na Kazi, Wakati wa Furaha, Uchaguzi ni Wako, Chakula

ni Uhai, Mtu ni Afya na Siasa ni Kilimo.

Wizara ya Elimu ya Taifa ilianzisha programu mbalimbali za kuweza

kuwasaidia wanakisomo. Kwa mfano, mtaala wa kisomo cha kujiendeleza

ulianzishwa ukiwa na hatua tatu ambazo ni hatua ya V, VI na ya VII

(baadaye majina yalibadilishwa na kuwa ngazi ya chini, ya kati na ya

juu) ili kuepusha kuzilinganisha na ngazi za shule ya msingi. Mtaala huo

ulibuniwa kwa namna ambayo inajumuisha vipengele vya nadharia na

vitendo. Kipengele cha nadharia, kwa mfano, kilihusisha masomo kama

vile Kiingereza, Kiswahili, Uchumi, Hisabati na Elimu ya Siasa, ambayo

yalifundishwa katika madarasa ya kisomo cha kujiendeleza. Kipengele

cha mafunzo kwa vitendo kilijikita sana katika programu za kazi kama

vile kilimo, maarifa ya nyumbani na ufundi stadi, ambazo zilitolewa katika

vituo maalumu vya elimu ya watu wazima na vyuo vya maendeleo ya

jamii. Kule kujumuishwa kwa kipengele cha mafunzo kwa vitendo katika

mtaala wa kisomo cha kujiendeleza kulichukuliwa kama hatua muhimu ya

kufungamanisha kisomo na uzalishaji.

Masomo ya nadharia na yale ya vitendo yaliambatanishwa katika

programu saidizi ambazo zilijumuisha matumizi ya magazeti ya vijijini,

maktaba za vijijini, programu za kielimu kwa redio na elimu kwa filamu.

Programu hizo zilizinduliwa kwa njia za hadhara ili kuwapatia wanakisomo

taarifa kuhusu elimu kwa vitendo katika kilimo, afya na kazi za ufundi wa

mikono. Lengo kubwa lilikuwa ni kujenga mazingira endelevu ya kisomo

vijijini. Ili kufanikisha hili, magazeti manane ya vijijini yalianzishwa nchini.

Page 13: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

3

Vilevile, maktaba za vijijini zipatazo 3,170 zilianzishwa katika ngazi ya

kata, kila moja ikiwa na wastani wa vitabu 400.

Mikakati hiyo iliyotajwa ilileta mafanikio bayana mnamo miaka ya 1980.

Kwa mfano, Tanzania ilifikia rekodi ya kushuka kwa kiwango cha kutokujua

kusoma na kuandika kutoka 80% mwaka 1961 hadi kufikia 9.6% mwaka

1986. Hata hivyo, tangu kipindi hicho, nchi imeshuhudia kushuka kwa kasi

kwa kiwango cha kisomo. Sensa ya kitaifa ya mwaka 2012 ilionesha kuwa

kiwango cha kutokujua kusoma na kuandika kilifikia 28.4%, maeneo ya

vijijini yakiwa na kiwango kikubwa zaidi ambacho ni 37.7%. Katika kipindi

hicho, kulikuwa na idadi ipatayo milioni 3.5 ya watoto wenye umri wa

kwenda shule na vijana wa kati ya umri wa miaka 7 mpaka 19 waliokuwa

nje ya shule. Pia ilikadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2015, kungekuwa na

watoto na vijana milioni 5 wenye umri wa kuwa shuleni ambao wangekuwa

nje ya shule. Tena, takwimu kutoka Basic Education Statistics of Tanzania

(BEST) ya mwaka 2017 zinaonesha kwamba wanafunzi walioacha

masomo ya elimu ya msingi kwa miaka mitano mfululizo ya 2012, 2013,

2014, 2015 na 2016 walikuwa ni 104,295; 67,037; 84,481; 85,985;

na 117,927 mtawalia. Hali hii inaweza kuchangia katika ongezeko la

kiwango cha idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika nchini.

Kwa kuwa kutokujua kusoma na kuandika ni moja ya vikwazo katika kuifikia

Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025, ambayo inalenga kuugeuza

uchumi wa Tanzania na kuufanya kuwa wa kipato cha kati na maendeleo

ya viwanda ya kiwango cha kati, programu za kisomo na elimu kwa umma

ni muhimu sana. Ni katika muktadha huu kwamba serikali, kupitia Wizara

ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imeandaa huu Mkakati wa Kitaifa wa

Kisomo na Elimu kwa Umma (MTaKEU).

Page 14: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

4

1�2 Madhumuni ya MTaKEU

Mkakati huu unalenga kuimarisha uendeshaji wa programu za kisomo na

elimu kwa umma nchini Tanzania. Utekelezaji wake ni wa miaka mitano

(2020/2021-2024/2025) ukiwa na lengo la muda mrefu la kufuta ujinga

ili kuinua hali ya maisha ya watu. MTaKEU umeandaliwa mahususi kama

mwongozo wa utekelezaji wa mipango na programu za kisomo na elimu

kwa umma nchini.

1�3 Hatua za Uandaaji wa MTaKEU

Mchakato wa uandaaji wa MTaKEU umehusisha watekelezaji mbalimbali

katika ngazi mbalimbali. Kwanza kabisa, Wizara ya Elimu, Sayansi na

Teknolojia iliipatia TEWW jukumu la kufanya upembuzi yakinifu ili kuandaa

rasimu ya mkakati. Upembuzi yakinifu ulifanyika, ukihusisha mikutano

ya mashauriano na wadau wakuu na kwa kuipitia mikakati ya kitaifa

na kimataifa na mipango iliyopo inayohusu kisomo na elimu kwa umma.

Mashauriano yaliyohusisha watu wenye taarifa muhimu wanaosimamia

kisomo na elimu kwa umma nchini pia yalifanyika. Rasimu iliyoandaliwa

ilipokelewa katika ngazi ya wizara kwa ajili ya kupitiwa na kushirikishana

baina ya WyEST na OR-TAMISEMI kabla ya kukamilika kwake kwa ajili

ya utekelezaji.

Page 15: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

5

SURA YA PILI

UPEMBUZI YAKINIFU WA MAZINGIRA

2�1 Maendeleo ya Kisomo na Elimu kwa Umma Tanzania

Tangu mwaka 1961 Tanzania ilipopata uhuru, imekuwa ikifanya juhudi

mahsusi katika kukabiliana na tatizo la kutokujua kusoma na kuandika.

Katika miaka ya 1970, serikali ilizindua kampeni kubwa ya kisomo. Ili

kufanikisha hili, kisomo chenye manufaa, kisomo cha kujiendeleza pamoja

na programu saidizi za kisomo kama vile elimu kwa wafanyakazi,

elimu kwa njia ya filamu, elimu kwa njia ya redio, magazeti ya vijijini

yaliyoendana na mazingira halisi na vyuo vya maendeleo ya wananchi

vilianzishwa. Matokeo yake yalikuwa ni kupungua kwa idadi ya watu

wazima wasiojua kusoma na kuandika kutoka zaidi ya 80% mwaka 1961

hadi kufikia 9.6% mwaka 1986. Hata hivyo, tangu kipindi hicho, mafanikio

haya makubwa hayakudumu kwa muda mrefu kutokana na ugumu wa

hali ya kiuchumi nchini na matokeo ya mabadiliko kisera. Matokeo yake

sekta ndogo ya elimu ya watu wazima iliathirika kwa kiasi kikubwa, na

kusababisha kushuka kwa kasi ya kisomo kama inavyooneshwa kwenye

Mchoro 1.

Mchoro 1: Mwenendo wa Kiwango cha Kisomo 1961-2015

Page 16: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

6

Ili kushughulika na changamoto ya kushuka kwa kasi ya kisomo, Tanzania

imefanya jitihada mbalimbali, mojawapo ikiwa ni kushiriki katika

maadhimisho ya Muongo wa Kisomo wa Umoja wa Mataifa yaliyofanywa

mwezi Desemba 2001 katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa chini

ya kauli-mbiu isemayo “Kisomo ni Uhuru”. Umuhimu wa Muongo wa Kisomo

wa Umoja wa Mataifa ulijikita katika dhana pana ya kisomo kama msingi

wa ujifunzaji endelevu katika maisha yote. Mkazo wake ulikuwa katika

kuonesha uhitaji wa kuimarisha uhusiano kati ya ujifunzaji na elimu ya

mfumo rasmi, nje ya mfumo rasmi na mfumo usio rasmi na uwekaji wa

mazingira ya kisomo kama sehemu ya mikakati ya kukuza na kuinua elimu

ya watu wazima. Tanzania ilijielekeza pia kwa dhati katika kutekeleza

makubaliano na mapendekezo ya Muongo wa Maendeleo Endelevu wa

Umoja wa Mataifa, ambayo yalilenga katika kuhuisha kasi ya kimataifa

ya ujifunzaji na elimu ya watu wazima na kuziba pengo baina ya fikira

na uhalisia wa mawazo kwa upande mmoja na ukosefu wa sera na

mazingira thabiti na ya kimfumo ya kisomo na ujifunzaji wa watu wazima

kwa upande mwingine. Tanzania pia ilikubali kutekeleza makubaliano na

mapendekezo ya CONFINTEA ambayo yalitokana na mkutano uliofanyika

Tokyo (Japani) mnamo mwaka 1972, Paris (Ufaransa) mwaka 1985 na

Humburg (Ujerumani) mwaka 1997.

Mwaka 2001 serikali ilizindua Mpango wa Maendeleo ya Elimu

ya Msingi (MMEM), kwa lengo la kuongeza, miongoni mwa mambo

mengine, utoaji wa elimu bora ulio wa haki na usawa. Utekelezaji wake

ulionesha jitihada za serikali katika kufikia malengo ya Elimu kwa Wote

na Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa. Mwaka

2002, serikali iliona umuhimu wa kuandaa Mpango wa Elimu ya Watu

Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi ndani ya mfumo wa MMEM ili

kutoa fursa kwa kundi kubwa la watoto na vijana walio nje ya mfumo

Page 17: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

7

rasmi wa shule kuweza kupata elimu, na kutatua tatizo la ongezeko la

wasiojua kusoma na kuandika miongoni mwa watu wazima. Mpango huo

ulizingatia changamoto kadhaa katika maeneo ya upatikanaji wa elimu,

ubora, usimamizi, uwezo, ufanisi na rasilimali. Programu muhimu kama vile

Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA) na Mpango wa

Uwiano Kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii (MUKEJA) zilianzishwa

ili kuchangia katika kutatua tatizo hilo. Mnamo mwaka 2010, Tanzania

ilianzisha mpango wa miaka mitano wa Sekta Ndogo ya Elimu ya Watu

Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi 2010/11-2014-2015 kama

jitihada za serikali katika kufanikisha sera ya Elimu kwa Wote, Malengo

ya Maendeleo ya Milenia, Mpango Mkakati wa Kupunguza Umasikini

na Dira ya Maendeleo Tanzania 2025. Mpango huo uliweka msisitizo

katika ufikikaji na uendelezaji, kisomo cha kujiendeleza na elimu endelezi,

utolewaji wa fedha na uendelevu wa programu za elimu ya watu wazima

na elimu nje ya mfumo rasmi. Licha ya kuwepo kwa mafanikio makubwa

katika mikakati na mipango iliyotajwa, kiwango cha idadi ya wasiojua

kusoma na kuandika nchini bado kiko juu.

2�2 Mifumo ya Kisera Inayozingatiwa katika MTaKEU

Uandaaji wa mkakati huu umejengwa juu ya sera na mipango ifuatayo:

2�2�1 Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030

Malengo ya Maendeleo Endelevu ni shabaha zilizokubaliwa miongoni

mwa serikali za dunia kuhusu maendeleo. Yanafuata baada ya Malengo

ya Mendeleo ya Milenia na yanajikita katika agenda za mwaka 2030

za Maendeleo Endelevu. Agenda hii ni mpango wa utekelezaji kwa

ajili ya watu, dunia na hatima ya mafanikio. Mpango huu unalenga

kuimarisha amani ya ulimwengu wote kwa mawanda mapana ya uhuru na

unatambua kwamba kuondoa umasikini wa aina zote ukiwemo umasikini

Page 18: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

8

uliokithiri ni changamoto kubwa sana inayoukumba ulimwengu na ni jambo

muhimu sana linalohitajika kwa ajili ya maendeleo endelevu. Tanzania

imedhamiria kuutekeleza mpango huu kwa kushirikiana na nchi nyinginezo

na wadau mbalimbali.

Lengo la 4 ni mahsusi hasa kwa maendeleo jumuishi ya kisomo na elimu

kwa umma. Lengo la 4.6 linataka “kuhakikisha kwamba vijana na watu

wazima wote, wanaume na wanawake, wanafikia kiwango cha kujua

kusoma, kuandika na kuhesabu ifikapo mwaka 2030.”

2�2�2 Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025

Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 inaelezea mipango ya kitaifa

ya muda mrefu ambayo Tanzania inatamani kuifikia. Pamoja na mambo

mengine, dira hii inalenga kuugeuza uchumi wa Tanzania na kuufanya kuwa

wa kipato cha kati na wa maendeleo ya viwanda ya kiwango cha kati

ifikapo mwaka 2025. Inalenga kuwafikisha watanzania wote katika hali

ya ubora wa juu wa maisha ambao unaweza kufikiwa kwa kutengeneza

jamii ya watu walioelimika vizuri na wanaojifunza, hali ambayo inaweza

kufikiwa kwa njia ya, pamoja na mambo mengine, kukomesha tatizo la

kutojua kusoma na kuandika. Programu za kisomo na elimu kwa umma

zinatoa maarifa na stadi zinazohitajika katika kutatua changamoto za

kimaendeleo kwa umahiri na kiushindani.

2�2�3 Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2015-2020)

Ilani ya uchaguzi ya CCM imejikita katika Dira ya Maendeleo Tanzania

2025. Kwa ujumla, ilani hii (kifungu cha 51 - 52) inaelezea jitihada za

serikali katika kuimarisha uhusiano baina ya elimu rasmi, elimu nje ya

mfumo rasmi na elimu isiyo rasmi katika juhudi za kukuza na kuinua elimu

ya watu wazima kwa lengo la kuunda jamii ya watu walioelimika.

Page 19: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

9

2�2�4 Sera ya Elimu na Mafunzo (2014)

Sera ya Elimu na Mafunzo inasisitiza kujenga jamii ya watu walioelimika

kwa kuongeza fursa za elimu na mafunzo kwa makundi mbalimbali ya

watu, na kuwasaidia walengwa kuhitimu elimu yao katika ngazi husika.

Kupitia sera hii, serikali inaonesha dhamira ya kuandaa miongozo na

mazingira yanayofaa kuhakikisha kwamba elimu na mafunzo, ikiwemo

elimu ya watu wazima, vinatolewa katika ngazi mbalimbali kwa ubora

stahiki na kwa kupitia njia mbalimbali zikiwemo ujifunzaji huria na masafa.

2�2�5 Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu

Takwimu za hivi karibuni kutoka katika ripoti ya Mpango wa Maendeleo

ya Sekta ya Elimu wa 2016/17-2020/21 zinaonesha kwamba Tanzania

ina idadi kubwa ya watoto na vijana walio nje ya shule, na takribani robo

ya watu wazima hawajui kusoma na kuandika. Hivyo basi, kuna haja ya

kuwa na mkakati ulioandaliwa vizuri wa kukabiliana na hali hii.

2�2�6 Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa

Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa ni sehemu moja

katika mabadiliko makubwa ya sekta za umma ambayo yanasisitiza

ugatuaji wa madaraka wenye lengo la kuimarisha ushirikishwaji wa

watu walio katika ngazi za chini. Programu za elimu ya watu wazima

zinatakiwa ziendeshwe katika mifumo hii ya ugatuaji kwa kutoa elimu ya

msingi kwa watoto, vijana na watu wazima walio nje ya shule.

Page 20: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

10

SURA YA TATU

UCHANGANUZI WA UWEZO, UDHAIFU, FURSA NA CHANGAMOTO

3�1 Muhtasari wa Uchanganuzi

Uchanganuzi wa uwezo, udhaifu, fursa na changamoto kwa mkakati huu

umejikita kwenye tathmini ya mazingira ya ndani na ya nje.

3�2 Tathmini ya Mazingira ya Ndani

Tathmini ya mazingira ya ndani imejikita katika uwezo na udhaifu kama

ifuatavyo:

(a) Uwezo

Mafanikio ambayo yanaimarisha utekelezaji wa Mpango wa

Kitaifa wa Kisomo na Elimu kwa Umma yanajumuisha:

i. Kuwepo kwa mfumo wa taasisi za serikali zenye jukumu la

kutelekeza MTaKEU;

ii. Uzoefu wa muda mrefu wa WyEST na mashirika mengine na wabia

kama vile TEWW, Bodi ya Huduma za Maktaba ya Tanzania, OR-

TAMISEMI, vyombo vya habari, vyuo vya mandeleo ya jamii na

taasisi zisizo za kiserikali katika kusimamia programu za elimu ya

watu wazima, zikiwemo programu za kisomo na elimu kwa umma;

iii. Uwepo wa taasisi za kitaaluma zinazoweza kutoa mafunzo

endelevu na kuwajengea uwezo wawezeshaji na viongozi wa

kisomo na elimu kwa umma;

iv. Utayari wa serikali na wanajamii katika kuunga mkono na

kuchangia shughuli za kisomo na elimu kwa umma nchini; na

v. Uwepo wa miongozo ya kisera inayozitaka taasisi zote za umma

kuwa vituo vya programu za kisomo.

Page 21: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

11

b) Udhaifu

i. Uhaba wa programu zinazofaa kwa ajili ya kisomo na elimu kwa

umma;

ii. Uhaba wa mifumo saidizi na programu za kisomo katika ngazi

mbalimbali;

iii. Mfumo usio na ufanisi wa data za kisomo na elimu kwa umma;

iv. Kukosekana kwa zana na mifumo thabiti inayoratibiwa vizuri ya

namna ya kufanya upimaji wa ufundishaji na ujifunzaji wa kisomo

na elimu kwa umma;

v. Mfumo usioratibiwa vizuri wa kuandaa zana na vifaa vya

kufundishia na kujifunzia katika programu za kisomo na elimu kwa

umma;

vi. Kukosekana kwa viwango vya kitaifa vya kutambua weledi wa

wawezeshaji na waratibu wa programu za kisomo na elimu kwa

umma;

vii. Msisitizo hafifu katika kuhimiza kazi za ubunifu na uvumbuzi katika

masuala yanayohusu kisomo na elimu kwa umma;

viii. Uhaba wa tafiti za kina na zinazoratibiwa kwa ufasaha kuhusu

kisomo na elimu kwa umma nchini; na

ix. Utendaji hafifu wa kamati za elimu ya watu wazima na nje ya

mfumo rasmi katika ngazi zote.

3�3 Tathmini ya Mazingira ya Nje

Uchunguzi wa mazingira ya nje umejikita katika masuala ambayo

yanaweza kuathiri MTaKEU katika hali chanya na hasi kutokea nje. Mambo

ambayo yalitiliwa maanani katika tathmini yamejikita katika muktadha

wa kisiasa, mfumo wa sheria na kanuni, mahusiano na ushirikiano na

wadau wengine, kijamii, kiuchumi na kimazingira, ambayo yanaangukia

chini ya fursa na changamoto kama ifuatavyo:

Page 22: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

12

a) Fursa

Utekelezaji wa MTaKEU utawezekana kwa kuzingatia fursa

zifuatazo:

i. Mifumo ya sheria na kanuni: Zipo sera, sheria na programu ambazo zinaongoza na kusaidia utekelezaji wa MTaKEU. Hizo hujumuisha Sera ya Elimu na Mafunzo (1995; 2014); Tamko la Serikali Namba 494 la 17 Disemba, 2010 lililoanzisha OR-TAMISEMI na sheria ya bunge Namba. 12 ya mwaka 1975 inayoipa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) jukumu la kuendesha programu za elimu endelezi, Elimu ya Watu Wazima na elimu nje ya mfumo rasmi;

ii. Uwepo wa jitihada za kimataifa na sera zinazohimiza programu za kisomo katika nchi mojamoja;

iii. Mazingira mazuri ya kisiasa yanayotamani kuwa na jamii ya wasomi kama yanavyodhihirishwa katika maamuzi ya kisiasa, hotuba na katika ilani za vyama vya siasa kama vile Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020;

iv. Utayari wa wadau wengine wa ndani na wa nje ambao wanaweza kushirikishwa katika utekelezaji wa MTaKEU;

v. Uwepo wa taasisi zisizo za kiserikali, taasisi za kijamii, taasisi za kidini, vyama vya siasa na makundi mengine ya kijamii na kiuchumi ambayo yanaweza kuendeleza au kutoa majukwaa kwa ajili ya programu za kisomo;

vi. Uwepo na ongezeko la matumizi ya mitandao ya kijamii, simu za mkononi, vifaa vya huduma za maktaba zinazohamishika na kompyuta;

vii. Uwepo wa walengwa wa programu za kisomo na elimu kwa umma; na

viii. Uwepo wa wadau wenye ari ambao ni muhimu katika kutekeleza,

kuendeleza, kusaidia au kushirikiana katika kutekeleza MTaKEU.

Page 23: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

13

b) Changamoto

Changamoto zinaweza kujumuisha yafuatayo:

i. Mazoea potofu kuhusu tafsiri ya programu za kisomo miongoni

mwa wadau mbalimbali yanaweza kurudisha nyuma utekelezaji

wa MTaKEU; na

ii. Uhaba wa fedha zinazoelekezwa katika kugharamia programu

na mipango ya elimu ya watu wazima.

Page 24: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

14

SURA YA NNE

DIRA, DHIMA NA MALENGO YA KIMKAKATI

4�1 Dira

Dira ya huu Mkakati wa Kitaifa wa Kisomo na Elimu kwa Umma ni “kuwa

na jamii iliyoelimika na yenye uwezo wa kupata taarifa sahihi kwa ajili

ya kuwa na maisha bora na maendeleo endelevu kufikia mwaka 2025.

4�2 Dhima

Dhima ya mkakati huu ni “kubuni, kuendeleza na kuratibu programu za

kisomo na elimu kwa umma zilizo bora na zinazopatikana, na kuhakikisha

kuwa umahiri uliopatikana unakuwa endelevu kwa kuimarisha huduma

saidizi za kisomo”.

4�3 Malengo ya Kimkakati

Mkakati huu una malengo ya kimkakati saba yafuatayo:

i. Kuanzisha programu za kisomo na elimu kwa umma zilizo bora na

zenye manufaa kwa jamii;

ii. Kuimarisha mifumo na programu wezeshi za kuendeleza kisomo

na elimu kwa umma;

iii. Kuboresha mifumo ya usimamizi wa takwimu za kisomo na elimu

kwa umma;

iv. Kuweka viwango vya sifa za kitaaluma kwa ajili ya programu za

kisomo na elimu kwa umma;

v. Kuandaa zana na vifaa bora vya kufundishia na kujifunzia katika

programu za kisomo na elimu kwa umma;

vi. Kujenga uwezo wa wawezeshaji na waratibu wa programu za

kisomo na elimu kwa umma; na

vii. Kukuza kazi za tafiti, uvumbuzi na ubunifu katika masuala ya

kisomo na elimu kwa umma.

Page 25: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

15

4�4 Malengo ya Kimkakati, Mikakati, Shabaha na Viashiria vya

Utendaji

LK 1� Kuanzisha programu za kisomo na elimu kwa umma zilizo bora

na zenye manufaa kwa jamii

Sababu

Uhaba wa programu za kisomo na elimu kwa umma unaashiria uhitaji wa hatua za muda mfupi na muda mrefu kwa kuzingatia masuala makuu mawili: ubora wa programu na jinsi zinavyokidhi mahitaji ya jamii ya kielimu. Ubora wa programu unahusu jumla ya matokeo ya uboreshaji wa uanzishwaji wa vituo vya mafunzo, mgawanyo wa rasilimali, mafunzo yatolewayo kwa wawezeshaji na wasimamizi wa programu lengwa pamoja na kuwajengea morali ya kazi. Programu zinazokidhi mahitaji ya kielimu ya jamii inahusu ubunifu unaozingatia tofauti za muktadha katika kuandaliwa kwake. Vilevile, programu zinazokidhi mahitaji ya kielimu ya jamii zinahitaji ushirikishwaji wa walengwa na wadau katika hatua mbalimbali kuanzia kipindi cha maandalizi hadi wakati wa utekelezaji na pia kuzingatia unyumbufu wa mbinu na njia za utoaji wa mafunzo. Hili linahusisha pia uwepo wa haja ya kupanua mawanda ya utoaji wa programu za kisomo ili zipatikane kwa urahisi kwa vijana na watu wazima

wanaozihitaji, hususani maskini na waliotengwa.

Mikakati

a) Kufanya upembuzi wa mahitaji kwa ajili ya kuandaa programu

bora na zinazokidhi mahitaji ya jamii;

b) Kujenga uelewa kuhusu umuhimu wa programu za kisomo na elimu

kwa umma;

c) Kuandaa miongozo ya utekelezaji wa programu za kisomo na

elimu kwa umma; na

d) Kuhamasisha wadau mbalimbali kuanzisha programu za kisomo

na elimu kwa umma.

Page 26: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

16

Shabaha

i. Kubainishwa kwa mahitaji ya ujifunzaji kwa ajili ya kusaidia

maandalizi ya programu za kisomo na elimu kwa umma zenye

ubora na zinazokidhi mahitaji ya jamii katika wilaya zote kufikia

mwaka 2022;

ii. Kuanzishwa kwa hifadhi ya mahitaji ya kielimu kwa ajili ya

makundi mbalimbali katika kila wilaya kufikia mwaka 2022;

iii. Kuandaliwa kwa kampeni kuhusu masuala mawili ya kitaifa kufikia

mwaka 2025;

iv. Kufanyika kwa kampeni kupitia vyombo vya habari juu ya umuhimu

wa kisomo na elimu kwa umma kufikia mwaka 2025;

v. Kufanyika kwa mikutano, semina au warsha za uhamasishaji

angalau 6 katika kila kata kufikia mwaka 2022;

vi. Kuanzishwa kwa programu moja ya kisomo katika kila wilaya

kufikia mwaka 2022;

vii. Kuanzishwa kwa programu moja ya elimu kwa umma katika kila

wilaya kufikia mwaka 2022;

viii. Kuwepo na kutumika kwa miongozo ya mtaala wa kisomo na elimu

kwa umma kufikia mwaka 2025;

ix. Kuanzishwa kwa programu moja ya elimu kwa jamii kwenye kila

kata ifikapo mwaka 2023;

x. Kuhusishwa kwa wadau watatu katika kuanzisha programu za

kisomo na elimu kwa umma kwenye kila wilaya ifikapo mwaka

2025;

xi. Kuanzishwa kwa kituo kimoja cha kisomo katika kila kata ifikapo

mwaka 2025; na

xii. Kuwepo kwa walengwa milioni mbili walionufaika na programu

za kisomo ifikapo mwaka 2025.

Page 27: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

17

Viashiria vya Mafanikio vya Msingi

i. Uwepo wa ripoti ya tathmini ya mahitaji ya kielimu;

ii. Idadi ya programu za kisomo na elimu kwa umma zilizoandaliwa

katika kila wilaya;

iii. Idadi ya programu za elimu kwa jamii zilizoanzishwa katika kila

kata;

iv. Ongezeko la asilimia ya vijana na watu wazima wanaoshiriki

katika programu za kisomo na elimu kwa umma kila mwaka;

v. Idadi ya vituo vya kisomo vilivyoanzishwa katika kila wilaya;

vi. Idadi ya walengwa walionufaika katika programu za kisomo na

elimu kwa umma;

vii. Kuwepo kwa miongozo ya kisomo na elimu kwa umma inayotumika;

na

viii. Vithibitisho vya kuboreka kwa maisha ya wanajamii.

LK 2� Kuimarisha mifumo na programu wezeshi za kuendeleza

kisomo na elimu kwa umma

Sababu

Ufanisi wa programu za kisomo na elimu kwa umma hutegemea kwa

kiasi kikubwa uwepo wa mifumo na mfululizo wa programu wezeshi zilizo

madhubuti na zenye ufanisi. Tanzania ina historia ya muda mrefu katika

kutumia mifumo wezeshi ya kisomo kama vile maktaba za vijijini, magazeti

ya vijijini na redio. Hata hivyo, mifumo wezeshi hiyo haijatumika kiasi cha

kutosha kuimarisha programu wezeshi za kisomo. Ipo haja ya kutumia

teknolojia mpya na kuendeleza mifumo iliyopo ambayo bado inakidhi

mahitaji kuhakikisha kwamba mifumo wezeshi madhubuti na yenye ufanisi

inakuwepo nchini Tanzania.

Page 28: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

18

Mikakati

a) Kufanya upembuzi yakinifu wa mifumo na programu wezeshi za

kisomo zilizopo;

b) Kuanzisha programu na mifumo wezeshi ya kisomo katika maeneo

ya mijini na vijijini,

c) Kuanzisha maktaba zinazohama katika jamii za wafugaji ambazo

zina kiwango kikubwa cha kutojua kusoma na kuandika;

d) Kushawishi na kujenga uelewa wa jamii juu ya programu na mifumo

wezeshi ya kisomo; na

e) Kuanzisha na kuimarisha uhusiano kati ya programu za kisomo na

elimu kwa umma na vyombo vya habari.

Shabaha

i. Kufanyika kwa upembuzi yakinifu katika wilaya zote kufikia

mwaka 2022;

ii. Kufanyika kwa programu nne za kushawishi na kueneza habari

kuhusu programu na mifumo wezeshi kila mwaka;

iii. Kuwepo kwa maktaba moja ya kijiji iliyosheheni vifaa

vinavyotakiwa katika kila mkoa kufikia mwaka 2025;

iv. Kuanzishwa kwa programu moja ya kisomo kwa njia ya redio

katika kila mkoa ifikapo mwaka 2025;

v. Kuanzishwa kwa programu moja ya kitaifa ya kisomo kwa njia ya

televisheni ifikapo mwaka 2025;

vi. Kuunganishwa kwa vikundi vitatu vya kijamii na kiuchumi katika

programu za kisomo katika kila kata ifikapo mwaka 2025;

vii. Kuanzishwa kwa kituo kimoja cha kisomo cha kujiendeleza katika

kila kata ifikapo mwaka 2025;

Page 29: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

19

viii. Kuimarishwa kwa kiwanda cha uchapaji cha Taasisi ya Elimu ya

Watu Wazima ifikapo mwaka 2025;

ix. Kutumika kwa vyuo vya maendeleo ya wananchi katika kuendeleza

kisomo na elimu kwa umma ifikapo mwaka 2025;

x. Kuanzishwa kwa maktaba moja inayohama katika kila jamii ya

wafugaji ifikapo mwaka 2025; na

xi. Kubuniwa na kutumika kwa programu ya simu za mkononi katika

mipango ya kisomo na elimu kwa umma.

Viashiria vya Mafanikio vya Msingi

i. Vithibitisho vya uwepo wa mifumo na programu wezeshi katika

kila wilaya;

ii. Idadi ya wadau wanaotambua na kudhamiria kusaidia uanzishwaji

wa huduma wezeshi za kisomo;

iii. Idadi ya miundombinu wezeshi iliyojengwa, kukarabatiwa na

kuwekewa samani kwa kuzingatia mahitaji;

iv. Idadi ya programu wezeshi za kisomo zinazofanya kazi katika

jamii;

v. Idadi na asilimia ya walengwa walionufaika na huduma wezeshi

za kisomo;

vi. Kupungua kwa idadi ya watu wanaorejea katika hali ya kutokujua

kusoma na kuandika;

vii. Idadi ya vituo na vikundi vya wanakisomo vilivyoanzishwa na

kuendelezwa kwenye makundi ambayo huwa pembezoni na

yasiyofikika kwa urahisi;

viii. Idadi ya jamii za wafugaji zilizohamasika kujiunga na programu

za kisomo na elimu kwa umma; na

ix. Ongezeko la asilimia ya jamii zinazofikiwa na programu bora za

kisomo na elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari.

Page 30: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

20

LK 3� Kuboresha mifumo ya usimamizi wa takwimu za kisomo na

elimu kwa umma

Sababu

Uendeshaji wa programu za kisomo na elimu kwa umma una sifa ya kuwa na unyumbufu na mawanda anuai, na unafanywa na wadau mbalimbali chini ya usimamizi wa wizara na sekta mbalimbali. Hali hii husababisha changamoto katika upatikanaji wa takwimu za uhakika na sahihi zinazoweza kusaidia kuboresha sera na kazi za utekelezaji. Mifumo iliyopo ya usimamizi wa takwimu imebuniwa kwa ajili hasa ya kushughulikia takwimu za mfumo rasmi wa elimu. Hivyo, kuna haja ya kuwa na mifumo na mikakati madhubuti ambayo inaweza kuwa na nafasi

ya kubeba pia programu za kisomo na elimu kwa umma.

Mikakati

a) Kufanya upembuzi yakinifu wa hali halisi ya mifumo ya usimamizi wa takwimu za kisomo na elimu kwa umma;

b) Kuimarisha mifumo ya usimamizi wa takwimu za kisomo na elimu kwa umma katika ngazi zote za utekelezaji; na

c) Kujumuisha takwimu za kisomo na elimu kwa umma katika mifumo

ya usimamizi wa takwimu iliyopo.

Shabaha

i. Kubainishwa kwa hali halisi ya mifumo ya usimamizi wa takwimu za kisomo na elimu kwa umma ifikapo mwaka 2021;

ii. Kuingizwa kwa viashiria vya takwimu za kisomo na elimu kwa umma katika mifumo ya BEMIS, EMIS na masijala za vijijini ifikapo mwaka 2022;

iii. Kujengewa uwezo wa kukusanya na kuchakata takwimu kwa mamlaka za serikali za mitaa ifikapo mwaka 2022; na

iv. Kusambazwa kwa takwimu za kisomo na elimu kwa umma kwa

wadau ifikapo mwaka 2023.

Page 31: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

21

Viashiria vya Mafanikio vya Msingi

i. Kuwepo na kutumika kwa ripoti ya hali halisi ya mifumo ya

usimamizi wa takwimu;

ii. Idadi ya zana zinazotumika za kushughulikia takwimu za kisomo

na elimu kwa umma;

iii. Idadi na aina za watekelezaji waliopata mafunzo ya usimamizi

wa takwimu za kisomo na elimu kwa umma;

iv. Kuwepo kwa takwimu za kisomo na elimu kwa umma katika mifumo

ya BEMIS, EMIS, na masjala ya vijijini; na

v. Uwepo wa taarifa ya kila mwaka ya kisomo na elimu kwa umma.

LK 4� Kuweka viwango vya sifa za kitaaluma kwa ajili ya programu

za kisomo na elimu kwa umma

Sababu

Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Elimu unaonesha kwamba wanafunzi

katika ngazi zote za elimu wanapaswa wapate kiwango cha elimu ya

msingi kinachokubalika, inayoweza kuhawilishwa na mafunzo ya ufundi

na stadi kupitia mfumo rasmi wa elimu, ufundi, elimu ya watu wazima

pamoja na elimu katika mfumo usio rasmi. Ni dhahiri kwamba wanafunzi

wengi wanahitaji kutambuliwa, kuhalalishwa na kupewa ithibati kwa

ujifunzaji wao kuonesha thamani ya kile wanachojifunza. Tofauti na elimu

ya mfumo rasmi, programu za kisomo na elimu kwa umma zimekuwa

zikitumia mitaala na nyakati za kujifunza nyumbufu na zenye mawanda

anuwai kukidhi matakwa na mazingira ya walengwa. Muundo wake una

vigezo nyumbufu vya udahili na kuhitimu katika programu, na kudahili

tena na kuhitimu tena. Kwa hiyo, kuna uhitaji wa umakini katika kuweka

vigezo sanifu vya viwango vya sifa ili kushughulika kwa usahihi na hali hii

ya unyumbufu wa maudhui na njia za ufundishaji na ujifunzaji.

Page 32: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

22

Mikakati

a) Kufanya upembuzi yakinifu wa hali halisi ya uendeshaji wa programu za kisomo na elimu kwa umma na waendeshaji;

b) Kuweka viwango vya sifa za kitaaluma na njia za kuendelea na elimu kwa programu za kisomo na elimu kwa umma; na

c) Kuanzisha mfumo rasmi wa upimaji na utoaji tuzo kwa programu

za kisomo na elimu kwa umma.

Shabaha

i. Kubainishwa kwa hali halisi ya uendeshaji na waendeshaji wa programu za kisomo na elimu kwa umma ifikapo mwaka 2021;

ii. Kuanzishwa kwa mfumo rasmi wa upimaji na utoaji tuzo kwa programu za kisomo na elimu kwa umma ifikapo mwaka 2022; na

iii. Kuwekwa kwa viwango vya sifa za kitaaluma na njia za kuendelea na elimu kwa programu za kisomo na elimu kwa umma ifikapo

mwaka 2022.

Viashiria vya Mafanikio vya Msingi

i. Uwepo wa ripoti ya upembuzi yakinifu inayoonesha vithibitisho vya uendeshaji na waendeshaji wa programu za kisomo na elimu kwa umma;

ii. Idadi ya programu za kisomo na elimu kwa umma pamoja na waendeshaji wa programu hizo wanaozingatia viwango vya sifa vilivyowekwa;

iii. Idadi ya wanafunzi wanaoendelea na ngazi nyingine zinazofuata za elimu;

iv. Idadi ya wahitimu wa programu za kisomo na elimu kwa umma wanaotambuliwa na mamlaka kuu za mifumo ya viwango; na

v. Idadi ya programu na waendeshaji wa programu za kisomo

na elimu kwa umma waliohalalishwa na kupewa ithibati kutoa

programu za kisomo na elimu kwa umma.

Page 33: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

23

LK 5� Kuandaa zana na vifaa bora vya kufundishia na kujifunzia

katika program za kisomo na elimu kwa umma

Sababu

Vifaa vya kielimu kama vile vitabu, video, programu za kompyuta, na

vifaa vingine ni muhimu sana katika kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji.

Programu za kisomo na elimu kwa umma zinahitaji vifaa vinavyoendana

na uwezo na matakwa ya walengwa wenye sifa tofauti-tofauti. Hivyo,

utayarishaji wake unatawaliwa na kanuni zinazoendana na mahitaji hayo

na kukidhi haja. Vifaa vya kufundishia na kujifunzia ambavyo vimezoeleka

kutumika katika programu za kisomo vimekuwa vile vilivyochapishwa

katika nakala ngumu, ambazo zimekuwa na gharama kubwa, ngumu

kupatikana na zisizo na mvuto mkubwa kwa wanaojifunza. Maendeleo ya

kiteknolojia ya sasa yanaweza kutoa fursa za kutumia pia vifaa ambavyo

haviko katika machapisho ya nakala ngumu.

Mikakati

a) Kuandaa zana na vifaa vya kufundishia na kujifunzia vilivyo

katika mfumo wa nakala ngumu kwa kufuata miongozo iliyopo na

mazingira halisi;

b) Kuongeza matumizi ya vifaa mbalimbali vya kihabari katika

programu za kisomo na elimu kwa umma; na

c) Kutumia vituo vya walimu kujenga uwezo wa kuandaa zana na

vifaa vya kujifunzia na kufundishia katika kisomo na elimu kwa

umma.

Shabaha

i. Kuandaliwa kwa mwongozo wa kuandaa zana na vifaa vya

kufundishia na kujifunzia kwa ajili ya programu za kisomo na

elimu kwa umma ifikapo mwaka 2022;

Page 34: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

24

ii. Kuzalishwa kwa zana na vifaa vinavyohitajika kufundishia na

kujifunzia katika vituo vya kisomo na elimu kwa umma ifikapo

mwaka 2025;

iii. Kuandaliwa kwa zana na vifaa vya kufundishia na kujifunzia

vinavyozingatia muktadha katika kila wilaya ifikapo 2025;

iv. Kuandaliwa na kutumika kwa mwongozo wa kutumia vifaa

mbalimbali vya kihabari katika programu za kisomo na elimu kwa

umma ifikapo mwaka 2024; na

v. Kutumika kwa vituo vya walimu katika kujenga uwezo wa wadau

kuandaa zana na vifaa vya kisomo katika mazingira yao ifikapo

mwaka 2025.

Viashiria vya Mafanikio vya Msingi

i. Kuwepo na kutumika kwa mwongozo wa kuandaa zana na vifaa

vya ufundishaji na ujifunzaji;

ii. Idadi na aina za zana na vifaa vya kufundishia na kujifunzia vilivyo

bora na vinavyoendana na mahitaji ambavyo vimeandaliwa,

kuzalishwa katika nakala ngumu na kutumika;

iii. Kuwepo na kutumika kwa mwongozo wa kutumia vifaa mbalimbali

vya kihabari kufundishia na kujifunzia; na

iv. Idadi na aina ya zana na vifaa vya kisomo na elimu kwa umma

vilivyoandaliwa na kutumika katika mazingira husika.

LK 6� Kujenga uwezo wa wawezeshaji na waratibu wa kisomo na

elimu kwa umma

Sababu

Nchini Tanzania, wanafunzi walio wengi ambao wamedahiliwa katika

taasisi za mafunzo katika eneo la elimu ya watu wazima ni wale ambao

Page 35: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

25

ni waajiriwa waliopo kazini. Baada ya kuhitimu, wanafunzi hawa hurudi

katika vituo vyao vya kazi vya awali ambavyo, kwa kiasi kikubwa, ni

katika elimu ya mfumo rasmi, huku wakiziacha programu za kisomo na

elimu kwa umma zikihudumiwa na wafanyakazi wasio na sifa stahiki.

Hali halisi iliyopo ya kwamba sekta ndogo ya elimu ya watu wazima

inakosa utambulisho dhahiri katika muundo wa ajira za utumishi wa umma

inaongeza upeo wa tatizo hili. Hivyo basi, kuna haja ya kuimarisha mfumo

wa mafunzo ya kozi za muda mfupi na za muda mrefu katika eneo la

elimu ya watu wazima na kufanya juhudi ya kutafuta kutambulika kwa

wataalamu wa eneo hili katika muundo wa ajira za utumishi wa umma.

Mikakati

a) Kuandaa programu za muda mfupi na muda mrefu za kujenga

uwezo katika maeneo ya ufundishaji, usimamizi na uaandaaji wa

zana na vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika programu za

kisomo na elimu kwa umma;

b) Kuendesha mafunzo ya muda mfupi kwa ajili ya wawezeshaji na

waratibu wa vituo vya kisomo na elimu kwa umma; na

c) Kuweka viwango vya sifa za weledi katika eneo la kisomo na

elimu kwa umma kulingana na matakwa ya utumishi wa umma.

Shabaha

i. Kuanzishwa kwa programu mbili za mafunzo ya muda mfupi

zinazohusiana na uwezeshaji, uendeshaji na uandaaji wa zana

katika kila wilaya ifikapo 2025;

ii. Kuanzishwa kwa programu moja ya muda mrefu inayohusiana

na uwezeshaji, uendeshaji na uandaaji wa zana na vifaa vya

programu za kisomo na elimu kwa umma ifikapo 2025;

Page 36: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

26

iii. Kupatiwa mafunzo kwa walimu watano kutoka katika kila wilaya

kila mwaka kuhusu uratibu wa programu za kisomo na elimu kwa

umma ifikapo mwaka 2025;

iv. Kupatiwa mafunzo wawezeshaji wasaidizi wawili na mwezeshaji

mtaalamu mmoja walio kwenye kila kituo ifikapo 2022; na

v. Kuandaliwa na kutambuliwa kwa viwango vya sifa za weledi kwa

ajili ya wawezeshaji na waratibu wa programu za kisomo na elimu

kwa umma ifikapo mwaka 2025.

Viashiria vya Mafanikio vya Msingi

i. Idadi ya kozi fupi-fupi na kozi za muda mrefu zilizoanzishwa;

ii. Idadi ya wawezeshaji waliohudhuria mafunzo ya muda mfupi

katika kila wilaya;

iii. Idadi ya wawezeshaji, waratibu na wadau wengine waliopatiwa

mafunzo kwa mwaka;

iv. Kutambuliwa kwa viwango vya sifa za weledi kwa wawezeshaji

wa programu za kisomo na elimu kwa umma katika muundo wa

utumishi wa umma;

v. Idadi ya waelimishaji wa kisomo na elimu kwa umma

wanaotambuliwa katika muundo wa utumihi wa umma; na

vi. Kuthibitika kwa uendeshaji wa programu za kisomo na elimu kwa

umma ulioboreshwa.

Page 37: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

27

LK 7. Kukuza kazi za tafiti, uvumbuzi na ubunifu katika masuala ya

kisomo na elimu kwa umma

Sababu

Licha ya kuwepo kwa mabadiliko ya kiteknolojia, kijamii na ya kiuchumi

katika ulimwengu wa sasa, elimu ya watu wazima bado haijawa na

uvumbuzi na ubunifu kwa kiasi cha kutosha. Uhaba wa tafiti, uwekezaji,

maendeleo ya kiteknolojia na maendeleo duni ya ubunifu mahalia ni

miongoni mwa sababu za kuwepo kwa hali hii. Kwa hiyo, lengo hili la

kimkakati linalenga kuendeleza kazi ya utafiti, uvumbuzi na ubunifu kwa

ajili ya maendeleo na uendelevu wa programu za kisomo na elimu kwa

umma. Linahimiza kuhusu uratibu madhubuti wa kazi za utafiti na uvumbuzi

ili kuwezesha uendelezaji wa maarifa, uboreshaji wa utendaji na taarifa

za kisera katika eneo la kisomo na elimu kwa umma.

Mikakati

a) Kuweka miundo ya ushirikiano ya wadau ili kuongoza ubainishaji

wa agenda za utafiti katika kisomo na elimu kwa umma nchini;

b) Kuimarisha uwezo wa wadau mbalimbali wa kisomo na elimu kwa

umma katika kufanya tafiti na kuwasilisha matokeo;

c) Kuanzisha utaratibu wa kukuza ubunifu, uvumbuzi na tafakuri

katika eneo la kisomo na elimu kwa umma; na

d) Kuhimiza utamaduni wa ujifunzaji endelevu miongoni mwa

watendaji wa elimu ya watu wazima.

Shabaha

i. Kubainishwa kwa agenda ya kitaifa ya utafiti katika kisomo na

elimu kwa umma ifikapo mwaka 2025;

ii. Kupatiwa mafunzo ya kufanya utafiti na kuwasilisha matokeo ya

utafiti kwa watekelezaji mia moja na sitini na tisa (169) wa kisomo

na elimu kwa umma ifikapo mwaka 2025;

Page 38: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

28

iii. Kufanyika kwa kazi moja ya utafiti kuhusiana na kisomo na elimu

kwa umma katika kila wilaya ifikapo mwaka 2025;

iv. Kuanzishwa kwa programu moja ya mafunzo elekezi kuhusu utafiti,

ubunifu na uvumbuzi katika kila wilaya ifikapo mwaka 2024;

v. Kuandaliwa na kufanyiwa majaribio programu moja ya mfano

ya kisomo na elimu kwa umma katika kila mkoa ifikapo mwaka

2025;

vi. Kujengewa uwezo wa watekelezaji katika kubuni programu na

mitaala ya kisomo na elimu kwa umma kwa kuzingatia muktadha

husika ifikapo mwaka 2025;

vii. Kuendeshwa kwa mikutano, semina, warsha na matamasha kuhusu

mahitaji mbalimbali ya watendaji wa elimu ya watu wazima

katika ngazi ya taifa, mkoa na wilaya ifikapo mwaka 2025; na

viii. Kufanyika kwa onesho moja la kitaifa kuhusiana na uzoefu wa

kazi na fikira za kiuvumbuzi kuhusu kisomo na elimu kwa umma

kila mwaka.

Viashiria vya Mafanikio vya Msingi

i. Kuwepo kwa agenda ya kitaifa ya utafiti;

ii. Idadi na aina za miongozo iliyopo ya kuboresha kazi za kisomo

na elimu kwa umma;

iii. Idadi ya watendaji waliopata mafunzo ya utafiti, ubunifu na

uvumbuzi;

iv. Idadi na aina za programu za mafunzo yaliyofanywa kuhusu

utafiti, ubunifu na uvumbuzi;

v. Kuongezeka kwa idadi ya ripoti za utafiti na machapisho

yaliyosambazwa katika ngazi mbalimbali za utekelezaji na kwa

jamii;

Page 39: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

29

vi. Ongezeko la idadi ya uzoefu uliowasilishwa na wadau mbalimbali

kuhusu programu za kisomo na elimu kwa umma;

vii. Idadi ya mitaala na programu za kisomo na elimu kwa umma

zenye ubora na zenye kukidhi mahitaji iliyoandaliwa na watendaji

mbalimbali;

viii. Kuongezeka kwa asilimia, idadi na aina za programu za kisomo

na elimu kwa umma zinazotolewa na waendeshaji mbalimbali; na

ix. Kuongezeka kwa vithibitisho vilivyoandikwa kuhusu mchango wa

jamii kusaidia jitihada za kisomo na elimu kwa umma.

Page 40: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

30

SURA YA TANO

MFUMO WA USHIRIKIANO KITAASISI KATIKA KUTEKELEZA MTaKEU

5�1 Wahusika wa MTaKEU

MTaKEU unatambua kwamba kisomo na elimu kwa umma ni masuala yanayohusisha sekta nyingi na yanapaswa kushughulikiwa na wadau wengi katika sekta ndogo ya elimu ya watu wa wazima na elimu nje ya mfumo rasmi. Utekelezaji wake unatakiwa kufanywa na wadau mbalimbali na katika ngazi mbalimbali. Inatakiwa kuratibiwa ikiwa ndani ya mfumo wa kitaasisi uliopo tayari ili kuwezesha mipango na mgawanyo madhubuti wa rasilimali. Utekelezaji wa mkakati huu unahusisha watendaji mbalimbali ambao wanaweza kuwa katika makundi ya watu binafsi, taasisi au

mashirika. Watekelezaji wakuu wa mkakati huu ni hawa wafuatao:

i. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;

ii. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa;

iii. Wizara ya Fedha na Mipango;

iv. Wizara nyingine, Idara na Mashirika ya umma;

v. Taasisi ya Elimu ya Watu wazima;

vi. Vyuo vya maendeleo kwa wananchi;

vii. Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;

viii. Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania;

ix. Vyuo vya elimu ya juu;

x. Asasi za kiraia, mashirika ya kidini na mashirika yasiyokuwa ya

kiserikali;

xi. Washirika wa maendeleo;

xii. Watoaji binafsi wa programu za kisomo na elimu kwa umma;

xiii. Wanajamii mmojammoja; na

xiv. Vikundi vya walengwa na mlengwa mmojammoja.

Page 41: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

31

5�2 Mfumo wa Kitaasisi katika Kutekeleza MTaKEU

Utekelezaji wa shughuli za kisomo na elimu kwa umma, usimamizi, uratibu

na uendeshaji kwa jumla hufanywa kwa kuzingatia taratibu za kitaasisi

katika mgawanyo wa wajibu na majukumu kama ifuatavyo:

a) Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST)

Majukumu na wajibu wa WyEST yatakuwa ni:

i. Kutoa mwongozo wa jumla katika kuandaa na kutekeleza MTaKEU

kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI;

ii. Kuhakikisha utekelezaji wa MTaKEU unaendana na sera

ndogondogo za sekta zinazohusika;

iii. Kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa MTaKEU katika ngazi ya

kitaifa;

iv. Kuweka mfumo wa uratibu na kuwa kiungo kati ya Wizara, Idara

na mashirika, asasi za kiraia, sekta binafsi, vyuo vya elimu ya juu,

na wadau wengine katika kutoa programu za kisomo na elimu

kwa umma; na

v. Kutafuta rasilimali fedha kutoka serikalini, wadau wa maendeleo,

na wadau wengine wa elimu katika kusaidia utekelezaji wa

MTaKEU.

b) Wizara ya Fedha na Mipango

Majukumu na wajibu wa Wizara ya Fedha na Mipango katika

utekelezaji wa MTaKEU yatakuwa ni:

i. Kuhakikisha programu za kisomo na elimu kwa umma zinaingizwa

katika mipango na bajeti ya serikali;

Page 42: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

32

ii. Kuandaa mwongozo wa uwezeshwaji wa kifedha kwa shughuli za

kisomo na elimu kwa umma nchini; na

iii. Kuhakikisha fedha kwa ajili ya utekelezaji wa MTaKEU zinatolewa

kwa kila mkoa kwa wakati mwafaka.

c) Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW)

Majukumu na wajibu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima katika

utekelezaji wa MTaKEU yatakuwa ni:

i. Kuandaa miongozo ya mtaala na zana na vifaa vya kufundishia

na kujifunzia katika kuwezesha utekelezaji wa pragramu za

kisomo na elimu kwa umma katika ngazi ya kitaifa;

ii. Kuanzisha na kufanya majaribio ya programu za mfano za kisomo

na elimu kwa umma;

iii. Kuandaa zana sanifu za kitaifa za kisomo za kupimia na kutahini

katika kisomo na tathmini kwa ujumla;

iv. Kuweka viwango sanifu vya upimaji na viwango vya sifa kwa

programu za kisomo nchini;

v. Kubuni na kuendesha kozi za muda mfupi na muda mrefu kwa ajili

ya waratibu, wawezeshaji, wawezeshaji-wasaidizi na watoaji wa

programu za kisomo na elimu kwa umma nchini;

vi. Kutunga na kuandaa vijitabu na vifaa vya kujifunzia kwa

wanakisomo;

vii. Kuendesha programu za kujenga uwezo kwa watekelezaji wa

MTaKEU nchini;

viii. Kutoa ushauri na huduma za kitaalamu katika masuala yanayohusu

kisomo na elimu kwa umma;

Page 43: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

33

ix. Kufanya tafiti za kitaifa za kisomo na elimu kwa umma na

kuwasilisha matokeo kwa wadau;

x. Kufanya ufuatiliaji na tathimini ya shughuli za kisomo na elimu kwa

umma nchini;

xi. Kutoa msaada wa kitaalamu kwa watendaji na wadau;

xii. Kuratibu taratibu za upimaji na utahini na kusimamia mfumo wa

utoaji tuzo wa programu za kisomo na elimu kwa uma katika

mikoa; na

xiii. Kuanzisha na kusimamia kanzidata za kisomo nchini.

d) Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-

TAMISEMI)

Majukumu na wajibu mahususi wa OR-TAMISEMI kuhusiana na

utekelezaji wa MTaKEU yatakuwa ni:

i. Kuratibu, kufuatilia na kutathimini mipango ya kielimu ya mkoa

ambayo inajumuisha shughuli za kisomo na elimu kwa umma;

ii. Kuingiza mipango na bajeti za mikoa katika mipango ya kitaifa

ambao utakuwa msingi wa kupitisha na kuhamisha fedha kutoka

hazina kwenda katika mamlaka za serikali za mitaa;

iii. Kusimamia shughuli za utoaji wa programu za kisomo na elimu

kwa umma katika mamlaka ya serikali za mitaa;

iv. Kuhakikisha kwamba mamlaka za serikali za mitaa zinaandaa

mpango thabiti wa muda wa kati wa matumizi, mipango ya bajeti

ya kielimu ya mwaka mmoja-mmoja na ya miaka mitatu-mitatu

kwa kuzingatia mpango wa utekelezaji uliotolewa kutoka ngazi

ya kata hadi ngazi ya halmashauri kwa kulingana na malengo ya

kiserikali, sera za kielimu, na vigezo vya uthibiti ubora.

Page 44: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

34

v. Kushirikiana na WyEST ili kusimamia, kufanya mapitio na

kutathmini mafanikio na matokeo ya programu za kisomo na elimu

kwa umma katika mamlaka ya serikali za mtaa;

vi. Kuhakikisha kwamba ripoti za robo mwaka za programu za

kisomo na elimu kwa umma na takwimu kuhusu usajili, uhifadhi na

ushiriki vinakusanywa kutoka mikoani na wilayani na kuwasilishwa

kwa usahihi kwa OR-TAMISEMI; na

vii. Kutoa miongozo na maelekezo kuhusu kutumia fedha kwa usahihi,

rasilimali watu na vifaa vingine vikiwemo kona za usomaji, maktaba

zinazohamishika, maktaba za vijijini, maktaba za kimkoa, vifaa

vya vyombo tofauti vya habari vinavyotumika, raslimali za vituo

na wawezeshaji katika maeneo husika.

e) Ngazi ya Mkoa

Ngazi ya mkoa itahusisha Katibu Tawala wa Mkoa, Afisa Elimu wa

Mkoa, wakuu wote wa idara na wakufunzi wakazi wa TEWW wa

mikoa. Wajibu na majukumu ya ngazi ya mkoa kuhusu utekelezaji

wa MTaKEU yatakuwa ni:

i. Kuratibu na kufuatilia usajili, mahudhurio na maendeleo ya vijana

na watu wazima katika vituo vya mafunzo ya kisomo katika

wilaya zote za mkoa;

ii. Kufanya shughuli za kuratibu na kufuatilia uendeshaji wa programu

za kisomo na elimu kwa umma;

iii. Kufuatilia mgawanyo wa fedha, utoaji wa fedha, malipo ya posho

na marupurupu mengine kwa wawezeshaji wa programu za kisomo

na elimu kwa umma na wasaidizi katika ngazi ya halmashauri ya

wilaya au manispaa;

Page 45: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

35

iv. Kuunganisha mipango na bajeti za kisomo na elimu kwa umma

kimkoa na kuhakikisha kuwa shughuli za kisomo na elimu kwa umma

zinajumuishwa katika bajeti na mipango ya mwaka ya mkoa;

v. Kupanga, kuratibu na kufanya shughuli za kisomo na elimu kwa

umma wakati wa juma la elimu ya watu wazima;

vi. Kuhakikisha kwamba halmashauri za wilaya au manispaa

zinaanzisha rasilimali na kona za kusomea, maktaba

zinazohamishika, maktaba za vijiji na vituo vya vyombo mbalimbali

vya habari vya umma;

vii. Kuratibu na kusimamia kazi ya kutambua makundi yaliyotengwa

kielimu wakiwemo watu wenye ulemavu, wanawake, vijana na watu

wazima wasiojua kusoma na kuandika na kuhakikisha kwamba

wamesajiliwa na kuendelea kuhudhuria katika vituo vya mafunzo

ya programu za kisomo katika wilaya; na;

viii. Kuratibu upimaji na utahini wa wanafunzi wa kisomo na elimu kwa

umma katika mkoa.

f) Ngazi ya Halmashauri

Afisa Elimu Wilaya na wakuu wa idara wote wanaohusika watasimamia utekelezaji wa MTaKEU katika maeneo yote yaliyo katika uangalizi wao kama vile kata, vijiji/mitaa na vituo vya mafunzo ya kisomo. Wajibu na majukumu ya serikali za mitaa hizi

yatakuwa ni;

i. Kuhakikisha ufanyikaji wa usajili, mahudhurio na maendeleo ya

vijana na watu wazima katika vituo vya mafunzo ya kisomo katika

ngazi ya wilaya au manispaa;

ii. Kuandaa mpango kazi wa kisomo, bajeti na kuhakikisha malipo ya

mishahara na posho kwa wataalamu/wawezeshaji na wasaidizi

yanajumuishwa ndani ya bajeti ya mwaka ya wilaya;

Page 46: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

36

iii. Kuhakikisha kwamba masuala ya kisomo na elimu kwa umma

yanajumuishwa kama agenda ya kudumu katika vikao na ripoti

za halmashauri za robo mwaka;

iv. Kuhakikisha kwamba data na ripoti za robo mwaka za kisomo

na elimu kwa umma zinawasilishwa kutoka katika vituo vya vijiji/

mitaa kupitia ofisi za waratibu wa elimu kata;

v. Kuanzisha vituo au kona za usomaji, maktaba zinazohamishika,

maktaba za vijiji na vituo vya habari kwa umma katika ngazi za

wilaya na za chini kwa mfano kata, vijiji/ mtaa;

vi. Kuongoza katika kuboresha utekelezaji wa kisomo na elimu kwa

umma katika wilaya;

vii. Kukusanya na kugawa rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa

programu za kisomo na elimu kwa umma katika halmashauri za

wilaya au manispaa;

viii. Kuhakikisha kwamba posho na marupurupu mengine yanatolewa

kwa wawezeshaji wa kisomo na wataalamu wengine katika

wilaya;

ix. Kuhamasisha na kuhimiza wadau kusaidia na kushiriki katika

utekelezaji wa shughuli za kisomo na elimu kwa umma;

x. Kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara wa shughuli za kisomo na

elimu kwa umma na kutoa msaada wa kiufundi kwa watendaji na

wadau;

xi. Kuwajengea uwezo waratibu elimu kata na waratibu wa vituo

katika programu za kisomo na elimu kwa umma; na

xii. Kusimamia kazi ya upimaji wa wanafunzi wa kisomo na elimu kwa

umma kulingana na miongozo iliyowekwa.

Page 47: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

37

g) Ngazi ya Kata

Afisa Elimu Kata na maafisa wengine wanaohusika katika ngazi ya kata watatakiwa kuwa na wajibu na majukumu yafuatayo katika utekelezaji wa MTaKEU:

i. Kuhakikisha kwamba kila kijiji/mtaa kinabainisha, kusajili na kuhakikisha mahudhurio ya vijana na watu wazima katika vituo vya mafunzo;

ii. Kuratibu shughulli za vituo vya kisomo na elimu kwa umma ndani ya kata;

iii. Kuhamasisha wadau ili kuhakikisha wasaidia juhudi za upatikanaji wa rasilimali za kuwezesha shughuli za kisomo na elimu kwa umma katika ngazi ya kata;

iv. Kuhakikisha kwamba takwimu zinazohusu vijana na watu wazima walio katika programu za kisomo na elimu kwa umma katika kata zinakusanywa, kuhifadhiwa, kuhuishwa na kupelekwa katika ngazi ya wilaya; na

v. Kuanzisha zana na vifaa au kona za kujifunzia, maktaba zinazohamishika, maktaba za vijiji na vituo vya midia kwa umma

katika ngazi ya kata.

h) Ngazi ya Kijiji/ Mtaa

Jamii na uongozi wa kijiji/mtaa watakuwa na wajibu na majukumu

yafuatayo:

i. Kuhakikisha kwamba kazi za usajili, mahudhurio na ushiriki wa

vijana na watu wazima zinafanyika katika vituo vya mafunzo ya

kisomo katika ngazi ya vijiji/mtaa;

ii. Kuhakikisha kwamba rasilimali na vifaa kama vile vyumba vya

madarasa, walimu, vituo vya kisomo na viwanja vinatunzwa kwa

ajili ya kutumika kuwezesha utekelezaji wa kisomo na elimu kwa

umma;

Page 48: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

38

iii. Kuhakikisha vijana na watu wazima wenye mahitaji maalumu au kutoka katika mazingira yaliyosahaulika wanajumuishwa katika shughuli za kisomo na elimu kwa umma;

iv. Kuhamasisha wanajamii kushiriki katika kutekeleza shughuli za kisomo na elimu kwa umma katika vijiji/mtaa;

v. Kuhamasisha vijana na watu wazima kuhusu faida za kujiunga na kushiriki katika kisomo na elimu kwa umma kwa manufaa na maendeleo yao kiuchumi na kijamii; na

vi. Kuhakikisha masuala ya kisomo ya vijana na watu wazima yanajadiliwa katika mikutano ya kijiji/mtaa.

i) Ngazi ya Vituo vya Mafunzo

Mratibu wa kituo cha mafunzo na wawezeshaji watakuwa na majukumu na wajibu ufuatao katika kuhakikisha utekelezaji wa MTaKEU katika ngazi ya vituo vya mafunzo:

i. Kusajili vijana na watu wazima katika vituo vya mafunzo ya kisomo;

ii. Kuweka mazingira bora ya ujifunzaji kwa vijana na watu wazima katika kituo;

iii. Kuhamasisha na kuhakikisha matumizi sahihi ya rasilimali katika kituo;

iv. Kushirikiana na uongozi wa kijiji/mtaa kuingiza shughuli za kituo katika mipango ya maendeleo ya mwaka ya kijiji/mtaa;

v. Kuandaa ripoti ya mara kwa mara ya utekelezaji wa shughuli za kisomo na elimu kwa umma na kuiwasilisha kwa Afisa Elimu Kata;

vi. Kuanzisha na kudumisha mahusiano ya karibu na wadau wote wa

elimu; na

vii. Kuanzisha kamati ya kituo ya kisomo na elimu kwa umma.

Page 49: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

39

5�3 Wajibu na Majukumu ya Taasisi na Washirika Wengine

a) Mamlaka ya Mafunzo na Elimu ya Ufundi

Majukumu na wajibu wa Mamlaka ya Mafunzo na Elimu ya Ufundi

katika kutekeleza MTaKEU yatakuwa ni:

i. Kutoa msaada wa kiufundi kwa wawezeshaji wa kisomo na elimu

kwa umma katika kutoa elimu ya ufundi wa awali; na

ii. Kusaidia kufanyika mafunzo kwa vitendo ya ufundi wa awali ya

programu za kisomo na elimu kwa umma.

b) Vyuo vya Maendeleo ya Jamii

Wajibu na majukumu ya vyuo vya maendeleo ya jamii katika

kutekeleza MTaKEU yatakuwa ni:

i. Kushirikiana na TEWW katika kuhimiza programu za kisomo na

elimu kwa umma nchini;

ii. Kuhimiza kisomo na elimu kwa umma kwa kutoa maarifa na stadi

za ufundi wa awali kwa vijana na watu wazima;

iii. Kuwa vituo maalumu vya kukuza stadi za utafiti, ugunduzi na

uvumbuzi wa programu za kisomo na elimu kwa umma; na

iv. Kutoa msaada wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika

kutekeleza programu za MTaKEU.

c) Taasisi za Elimu ya Juu

Katika kutekeleza MTaKEU, vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu

ya juu za Tanzania zitakuwa na wajibu na majukumu ya:

i. Kubuni na kujaribu programu za mfano za kisomo na elimu kwa

umma;

Page 50: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

40

ii. Kuwajengea uwezo wafanyakazi wa ngazi mbalimbali kuhusu

stadi za kisomo na elimu kwa umma;

iii. Kufanya tafiti kuhusu kisomo na elimu kwa umma na kushirikisha

matokeo kwa wadau; na

iv. Kutoa huduma ya ushauri wa kitaalamu katika eneo la kisomo na

elimu kwa umma.

d) Asasi za Kiraia, Mashirika ya Kidini na Mashirika yasiyokuwa

ya Kiserikali

Katika utekelezaji wa MTaKEU, wajibu na majukumu ya asasi za

kiraia, mashirika ya kidini na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali

yatakuwa ni:

i. Kuhakikisha kwamba kazi za usajili na ushiriki wa vijana na watu

wazima katika programu za kisomo zinafanyika kwa ufasaha

katika vituo vyao vya kisomo.

ii. Kutafuta rasilimali za kuwezesha utekelezaji wa MTaKEU nchini

zikiwemo jamii ambazo ni ngumu kufikiwa;

iii. Kuweka mfumo wa kuratibu kazi na mashirikiano miongoni mwa

asasi za kiraia, mashirika ya kidini na mashirika yasiyokuwa ya

kiserikali yanayoendesha programu za kisomo na elimu kwa umma

nchini;

iv. Kufanya na kusaidia tafiti katika masuala ya kisomo na elimu kwa

umma na kutoa taarifa serikalini; na

v. Kushiriki katika kukuza mtaala.

Page 51: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

41

e) Washirika wa Maendeleo

Wajibu na majukumu ya washirika wa maendeleo katika

kutekeleza MTaKEU yatakuwa ni:

i. Kutoa rasilimali zitakazosaidia utekelezaji wa MTaKEU;

ii. Kushiriki katika kufanya mapitio na tathimini ya mipango ya

kisomo na elimu kwa umma;

iii. Kutoa msaada wa kiufundi katika kufanikisha utekelezaji wa

MTaKEU;

iv. Kuanzisha mawasiliano na mitandao; na

v. Kushirikisha mawazo na uzoefu kuhusu kisomo na elimu kwa umma.

f) Bodi ya huduma za Maktaba Tanzania

Wajibu na majukumu ya bodi ya huduma za maktaba tanzania

katika kutekeleza MTaKEU yatakuwa ni:

i. Kutoa nafasi ya kujisomea kwa vijana na watu wazima walio

katika programu za kisomo na elimu kwa umma;

ii. Kutoa vitabu na vifaa vingine vya kujisomea kwa vijana, watu

wazima na wawezeshaji wa programu za kisomo na elimu kwa

umma; na

iii. Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu huduma za maktaba kuhusiana

na utekelezaji wa MTaKEU.

Page 52: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

42

SURA YA SITA

UFUATILIAJI, TATHMINI NA MFUMO WA UTOAJI TAARIFA

6�1 Maelezo ya Jumla

Mpango wa ufuatiliaji, tathmini na uwasilishaji wa taarifa huonesha

jinsi mfumo wote wa usimamizi, tathmini na utoaji wa taarifa za kazi

za mkakati utakavyokuwa. Mpango huo hujumuisha viashiria, nani ana

wajibu wa kuvikusanya, kwa njia zipi na zana zipi zitakazotumika, na jinsi

gani mtiririko wa data utakavyokuwa katika taasisi. Ufuatiliaji, tathmini

na uwasilishaji wa taarifa unalenga kuwezesha kufuatilia utekelezaji wa

MTaKEU hatua kwa hatua kwa kutoa kwa wakati taarifa sahihi na za

uhakika kwa wadau ili kuwezesha kazi ya kufanya maamuzi.

Mpango mzima wa ufuatiliaji na tathimini umejengwa katika njia ya

mfumo wa kimantiki. Njia hii inatoa fursa ya kupitia malengo mahsusi na

kazi katika mtiririko wa kimantiki. Vilevile njia inatoa fursa ya kuunganisha

malengo, matokeo endelevu, matokeo tarajiwa na shughuli za lazima

zinazopaswa kufanikisha malengo katika namna ya kutegemeana na

katika ngazi tofauti katika mfuatano wa malengo husika.

Njia hiyo inatafsiri vipengele vya msingi vya mfumo wa ufuatiliaji na

tathmini. Inatafsiri viashiria vinavyohitajika kupima kiwango cha mafanikio,

inabainisha vyanzo vya taarifa kwa ajili ya viashiria na kutengeneza kauli

bunifu. Hata hivyo, kauli za kubuni haziwezi kujumuishwa katika ngazi

za matokeo na shughuli kwa sababu hatua hizi zipo katika uangalizi

madhubuti wa utawala wa ndani katika kutekeleza mkakati.

6�2 Ufuatiliaji na Tathmini ya utekelezaji wa MTaKEU

Katika utekelezaji wa MTaKEU ufuatiliaji utahusisha ukusanyaji wa taarifa,

uhakiki wa taarifa, uhifadhi wa taarifa na utoaji wa taarifa. Kutakuwa na

Page 53: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

43

mfululizo wa ripoti kwa ajili ya kufuatilia mafanikio ya mkakati. Kutakuwa

na ripoti za robo mwaka zitakazotokana na zana za ndani za ufuatiliaji

kwa ajili ya kulingalisha na mpango kazi uliothibitishwa kwa kuwa na

mafanikio halisi na kubaini vikwazo na kupendekeza hatua stahiki

zinazohitajika. Pia kutakuwa na ripoti za utekelezaji wa mkakati kwa nusu

mwaka na kwa mwaka mzima. Tathmini itapima matokeo na athari za

mkakati kwa kuzingatia malengo ya kimkakati kupitia tathmini ya muda wa

kati na ya mwisho. Itapima mafanikio ya mkakati kwa kuzingatia ufanisi,

tija, matokeo na uendelevu wake. Matokeo ya ufuatiliaji na viashiria vya

tathmini yataripotiwa kwa hadhira husika kama inavyotakiwa.

Page 54: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

44

SURA YA SABA

UWEZESHWAJI WA KIFEDHA NA UENDELEVU WA MKAKATI

7�1 Uwezeshwaji wa Kifedha wa MTaKEU

Kwa kutambua kwamba utoaji wa elimu ya watu wazima ni ajenda

shirikishi kwa wadau, fedha za utekelezaji wa MTaKEU zitatokana na

vyanzo mbalimbali. Vyanzo vikuu ni:

i. Serikali: Hiki ni chanzo kikuu cha fedha za utekelezaji wa mradi wa

MTaKEU, kupitia bajeti za kila mwaka (MTEF katika ngazi tofauti

za utekelezaji kutoka ngazi ya taifa hadi serikali za mitaa); na

ii. Wadau tofauti kama vile mashirika ya kiraia, washirika wa

maendeleo, sekta binafsi na jamii kwa ujumla.

7�2 Mikakati ya Kupata Fedha

i. Wizara, idara na mashirika ya umma yataanzisha na kuimarisha njia za uchangishaji na ukusanyaji wa fedha kutoka vyanzo mbalimbali;

ii. Wizara ya fedha na mipango itatoa fedha ya kutosha kutekeleza MTaKEU;

iii. Wizara, idara na mashirika ya umma yasisitize kuhusu kutumia mfumo wa serikali uliopo sasa na kuwajibika kwa ufanisi na kutoa ripoti ya fedha za MTaKEU;

iv. Wizara, idara na mashirika ya umma yatahakikisha miongozo iliyopo na sheria za udhibiti wa fedha ikiwemo ugavi vinatolewa katika ngazi zote ili kuongoza utekelezaji wa MTaKEU;

v. Wizara, idara na mashirika ya umma yatatenga fedha kwa

ajili ya upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa

ajili ya MTaKEU, posho kwa wawezeshaji na kuwajengea uwezo

watendaji wa maeneo husika; na

vi. Wizara, idara na mashirika ya umma yatashirikiana na asasi za

kiraia na sekta binafsi katika kuunga mkono MTaKEU.

Page 55: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

45

7�3 Makadirio ya Gharama za MTaKEU kwa kipindi cha 2020/2021-

2024/2025

Makadirio ya gharama za MTaKEU yanazingatia idadi ya vipengele

vinavyoathiriwa na:

i. Idadi ya wanafunzi wa kisomo wanaotarajiwa kusajiliwa chini ya

programu za kisomo (rejea Jedwali 1); na

ii. Idadi ya wawezeshaji watakaoajiriwa, kupewa mafunzo na

kulipwa kulingana na ukubwa wa darasa (rejea Jedwali 2).

Jedwali 1: Idadi ya Wanafunzi kwa Kipindi cha 2020/2021 Hadi

2024/2025

Shughuli Idadi ya Wanafunzi kwa Kipindi cha 2020/2021 Hadi 2024/2025

2020/21 2021/2022 2022/2023 2023/2024 2024/2025 Jumla Kuu

Kisomo chenye manufaa

500,000 470,000 350,000 480,000 400,000 2,200,000

Kisomo cha Kujiendeleza

750,000 620,000 600,000 3,300,000 270,000 2,570,000

Jumla 1,250,000 1,090,000 950,000 810,000 670,000 4,770,000

Jedwali 2: Idadi ya Wawezeshaji kwa Kipindi cha 2020/2021 Hadi

2024/2025

Shughuli Idadi ya Wawezeshaji kwa Kipindi cha 2020/2021 Hadi 2024/2025

2020/21 2021/2022 2022/2023 2023/2024 2024/2025 Jumla Kuu

Kisomo chenye manufaa

5,570 5,000 6,000 4,500 5,070 26,140

Kisomo cha Kujiendeleza

5,200 4,535 3,537 3,535 2,535 19,342

Jumla 10,770 9,535 9,537 8,035 7,605 45,482

Page 56: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

46

Ukubwa wa darasa la vijana na watu wazima linakadiriwa kuwa na

wanafunzi 30 kama ilivyoelekezwa katika miongozo ya usajili wa elimu

ya watu wazima; na linasimamiwa na mwezeshaji mmoja na wawezeshaji-

wasaidizi wawili.

Kwa kila mwanafunzi mtu mzima aliye katika programu ya kisomo na

kisomo cha kujiendeleza, makadirio ya gharama ya TZS. 6,500 (US $ 3)

kwa kila mtu zimetengwa kwa ajili ya vitabu na shajara kwa muda wote

wa mafunzo. Programu za kisomo katika ngazi za vituo zitawezeshwa

na wawezeshaji na wawezeshaji wasaidizi. Wakati wa uwezeshaji,

watapewa posho ili kuwapa motisha.

Wawezeshaji katika madarasa ya kisomo na kisomo cha kujiendeleza

watapewa posho ya TZS. 50,000 kwa mwezi kwa kadirio la juu la miezi

10. Makadirio ya gharama kwa wawezeshaji ni malipo yatakayolipwa

kwa wale ambao tayari wapo katika mfumo wa malipo ya serikali kwa

kazi hii ya kufundisha madarasa haya kama awamu ya pili. Wawezeshaji

ambao ni wasaidizi watalipwa kiwango cha TZS. 50,000 pia kwa kadirio

la juu kwa miezi 10 kwa mwaka.

Jumla ya gharama za MTaKEU itakuwa takribani TZS bilioni 42.6 kwa

kipindi cha miaka mitano. Mgawanyo wa fedha umeoneshwa kwa kifupi

katika Jedwali la 3.

Page 57: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

47

Jedw

ali 3

:

Muh

tasa

ri w

a M

akad

irio

ya G

hara

ma

za S

hugh

uli z

a M

TaKE

U 2

020/

2021

-202

4/20

25

Shug

huli

Muh

tasa

ri w

a G

hara

ma

za M

kaka

ti kw

a K

ipin

di c

ha 2

020/

2021

Had

i 202

4/20

25

2020

/202

120

21/2

022

2022

/202

320

23/2

024

2024

/202

5Ju

mla

Kuu

Kiso

mo

chen

ye

man

ufaa

3,25

0,00

0,00

03,

055,

000,

000

2,27

5,00

0,00

03,

120,

000,

000

2,60

0,00

0,00

014

,300

,000

,000

Kiso

mo

cha

kujie

ndel

eza

4,87

5,00

0,00

04,

030,

000,

000

3,90

0,00

0,00

02,

145,

000,

000

1,75

5,00

0,00

016

,705

,000

,000

Ufu

ndish

aji

538,

500,

0000

476,

750,

000

476,

850,

000

351,

750,

000

380,

250,

000

2,22

4,10

0,00

0

Kuje

nga

uwez

o, ta

thm

ini

ya m

ahita

ji,

usim

amiz

i

wa

data

,

kusim

amia

viw

ango

na

upim

aji

na

tath

min

i

5,73

5,00

0,00

028

0,00

0,00

032

1,10

0,00

011

0,12

1,00

013

0,00

0,00

09,

466,

121,

000

Jum

la k

uu14

,398

,500

,000

7,84

1,75

0,00

09,

862,

850,

000

5,72

6,87

1,00

04,

865,

250,

000

42,6

95,2

21,0

00

47

Page 58: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

48

7�4 Uendelevu katika Utekelezaji wa MTaKEU

Katika kuhakikisha uendelevu wa utekelezaji wa MTaKEU, Serikali itaweka

mazingira mazuri kwa wadau mbalimbali kushiriki katika programu za

kisomo na elimu kwa umma; na kwa upekee:

i. Wizara, Idara na Mashirika ya umma yatatoa msaada wa kiufundi kwa mamlaka za serikali za mitaa katika kupanga na kujumuisha MTaKEU katika mipango yao ya maendeleo;

ii. Wizara, Idara na Mashirika ya umma na mamlaka za serikali za mitaa zitatumia vizuri fursa tofauti zilizopo, ikiwemo Maadhimisho ya Mwaka ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu kwa Wote;

iii. Wizara, Idara na Mashirika ya umma na mamlaka za serikali za mitaa watatafuta fedha za kuwezesha utekelezaji wa shughuli za MTaKEU;

iv. Wizara, Idara na Mashirika ya umma pamoja na vyombo vya habari watafanya kampeni katika vyombo vya habari ili kuhamasisha na kuwaweka pamoja wadau wengine kuchukua jukumu la kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono MTaKEU;

v. Wizara, Idara na Mashirika ya umma na mamlaka za serikali za mitaa watatumia kikamilifu kamati za elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi zilizoundwa katika ngazi zote katika kufuatilia na kutathmini shughuli za MTaKEU;

vi. Wizara, Idara na Mashirika ya umma na mamlaka za serikali za mitaa watahakikisha kunakuwa na uwazi katika kukusanya rasilimali na mgawanyo wake kupitia mifumo ya uwajibikaji iliyopo;

vii. Wizara, Idara na Mashirika ya umma watajenga uwezo kuhusu utendaji thabiti katika utekelezaji wa MTaKEU; na

viii. MTaKEU itafanyiwa mapitio baada ya miaka mitano.

Page 59: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

49

KIA

MBA

TISH

O

Mal

engo

ya

Kim

kaka

ti, V

iash

iria

vya

Maf

anik

io, S

haba

ha, M

zung

uko

wa

Uku

sany

aji w

a D

ata,

Mhu

sika

na M

uda

wa

Ute

kele

zaji

Na�

Leng

o la

K

imka

kati

Via

shiri

a vy

a M

afan

ikio

Shab

aha

Mzu

nguk

o w

a ku

kusa

nya

da

ta

Mhu

sika

Mud

a w

a U

teke

leza

ji

1.Ku

anzi

sha

prog

ram

u za

ki

som

o na

elim

u kw

a um

ma

ziliz

o bo

ra n

a ze

nye

man

ufaa

kw

a ja

mii.

i. Id

adi y

a vi

tuo

vya

kiso

mo

viliv

yoan

zish

wa

katik

a ki

la w

ilaya

.

ii. id

adi y

a wa

leng

wa

walio

nufa

ika

katik

a

prog

ram

u za

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a.

i. Ku

anzi

shwa

kwa

kitu

o ki

moj

a ch

a

kiso

mo

katik

a ki

la

kata

ifika

po m

waka

2025

.

ii. K

uwep

o kw

a

wale

ngwa

mili

oni

mbi

li wa

lionu

faik

a

na p

rogr

amu

za

kiso

mo

ifika

po

mwa

ka 2

025.

Robo

m

wak

a

Mw

aka

Mud

a w

a ka

ti

TEW

W,

WyE

ST, O

R-

TAM

ISEM

I,

Serik

ali z

a

mita

a, A

ZISE

,

VET

A, S

IDO

2021

-202

5

49

Page 60: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

50

Na�

Leng

o la

K

imka

kati

Via

shiri

a vy

a M

afan

ikio

Shab

aha

Mzu

nguk

o w

a ku

kusa

nya

da

ta

Mhu

sika

Mud

a w

a U

teke

leza

ji

2.Ku

imar

isha

mifu

mo

na

prog

ram

u w

ezes

hi z

a ku

ende

leza

ki

som

o na

elim

u kw

a um

ma

i. Id

adi y

a pr

ogra

mu

wez

eshi

za

kiso

mo

zina

zofa

nya

kazi

ka

tika

jam

ii.

ii.

Ong

ezek

o la

asil

imia

ya

jam

ii zi

nazo

fikiw

a na

pro

gram

u bo

ra z

a ki

som

o na

elim

u kw

a um

ma

kupi

tia v

yom

bo

vya

haba

ri

i. Ku

anzi

shwa

kwa

prog

ram

u m

oja

ya k

isom

o kw

a

njia

ya

redi

o

katik

a ki

la m

koa

ifika

po m

waka

2025

.

ii. K

uanz

ishwa

kwa

kitu

o ki

moj

a

cha

kiso

mo

cha

kujie

ndel

eza

katik

a ki

la k

ata

ifika

po m

waka

2025

.

Robo

mw

aka

Mw

aka

Mud

a w

a ka

ti

TEW

W,

WyE

ST, O

R-

TAM

ISEM

I,

Serik

ali z

a

mita

a, A

ZISE

,

Was

hirik

a w

a

mae

ndel

eo,

Vyuo

vik

uu,

Bodi

ya

Mak

taba

,

SID

O

2021

-202

5

50

Page 61: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

51

5150

Na�

Leng

o la

K

imka

kati

Via

shiri

a vy

a M

afan

ikio

Shab

aha

Mzu

nguk

o w

a ku

kusa

nya

da

ta

Mhu

sika

Mud

a w

a U

teke

leza

ji

3.Ku

bore

sha

mifu

mo

ya

usim

amiz

i wa

takw

imu

za

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a

i. Ku

wep

o kw

a ta

kwim

u za

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a ka

tika

mifu

mo

ya B

EMIS

, EM

IS, n

a m

asja

la y

a vi

jijin

i

ii.

Idad

i na

aina

za

wat

ekel

ezaj

i wa

liopa

ta m

afun

zo

usim

amiz

i wa

takw

imu

za k

isom

o na

elim

u kw

a um

ma

i. Ku

ingi

zwa

kwa

vias

hiria

vya

takw

imu

za

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a ka

tika

mifu

mo

ya B

EMIS

,

EMIS

na

mas

ijala

za v

ijijin

i ifik

apo

mwa

ka 2

022

ii. K

ujen

gewa

uw

ezo

wa k

ukus

anya

na k

ucha

kata

takw

imu

kwa

mam

laka

za

serik

ali z

a m

itaa

ifika

po m

waka

2022

Robo

mw

aka

Mw

aka

Mud

a w

a ka

ti

TEW

W,

WyE

ST, O

R-

TAM

ISEM

I,

Serik

ali z

a

mita

a,

2020

-202

5

Page 62: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

52

Na�

Leng

o la

K

imka

kati

Via

shiri

a vy

a M

afan

ikio

Shab

aha

Mzu

nguk

o w

a ku

kusa

nya

da

ta

Mhu

sika

Mud

a w

a U

teke

leza

ji

4.Ku

wek

a vi

wan

go

vya

sifa

za

kita

alum

a kw

a aj

ili y

a pr

ogra

mu

za

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a

i. Id

adi y

a pr

ogra

mu

za k

isom

o na

elim

u

kwa

umm

a pa

moj

a

na w

aend

esha

ji

wa p

rogr

amu

hizo

wana

ozin

gatia

viw

ango

vya

sifa

viliv

yow

ekwa

.

ii.

Idad

i ya

wana

funz

i wa

naoe

ndel

ea

na n

gazi

nyi

ngin

e zi

nazo

fuat

a za

elim

u.

iii.

Idad

i ya

wahi

timu

wa

prog

ram

u za

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a wa

naot

ambu

liwa

na m

amla

ka k

uu z

a m

ifum

o ya

viw

ango

i. Ku

anzi

shwa

kwa

m

fum

o ra

smi

wa u

pim

aji n

a ut

oaji

tuzo

kwa

pr

ogra

mu

za

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a ifi

kapo

mwa

ka

2022

.

ii. K

uwek

wa k

wa

viwa

ngo

vya

sifa

za k

itaal

uma

na

njia

za

kuen

dele

a na

elim

u kw

a pr

ogra

mu

za

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a ifi

kapo

m

waka

202

2

Robo

mw

aka

Mw

aka

TEW

W,

WyE

ST, O

R-

TAM

ISEM

I,

Serik

ali z

a

mita

a

2020

-202

2

52

Page 63: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

53

5352

Na�

Leng

o la

K

imka

kati

Via

shiri

a vy

a M

afan

ikio

Shab

aha

Mzu

nguk

o w

a ku

kusa

nya

da

ta

Mhu

sika

Mud

a w

a U

teke

leza

ji

5.Ku

anda

a za

na

na v

ifaa

bora

vy

a ku

fund

ishia

na

kuj

ifunz

ia

katik

a pr

ogra

mu

za

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a.

i. Id

adi n

a ai

na z

a za

na n

a vi

faa

vya

kufu

ndish

ia n

a ku

jifun

zia

viliv

yo b

ora

na v

inav

yoen

dana

na

mah

itaji

amba

vyo

vim

eand

aliw

a,

kuza

lishw

a ka

tika

naka

la n

gum

u na

ku

tum

ika.

i. Ku

zalis

hwa

kwa

zana

na

vifa

a vi

navy

ohita

jika

kufu

ndish

ia n

a ku

jifun

zia

katik

a vi

tuo

vya

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a ifi

kapo

m

waka

202

5.

ii. K

utum

ika

kwa

vitu

o vy

ote

vya

walim

u vi

livyo

hai

ka

tika

kuje

nga

uwez

o wa

wad

au

kuan

daa

zana

na

vifa

a vy

a ki

som

o ka

tika

maz

ingi

ra

yao

ifika

po

mwa

ka 2

025.

Robo

mw

aka

Mw

aka

Mud

a w

a ka

ti

TEW

W,

WyE

ST, O

R-

TAM

ISEM

I,

Serik

ali z

a

mita

a, A

ZISE

,

Bodi

ya

Mak

taba

,

2020

-202

5

Page 64: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

54

Na�

Leng

o la

K

imka

kati

Via

shiri

a vy

a M

afan

ikio

Shab

aha

Mzu

nguk

o w

a ku

kusa

nya

da

ta

Mhu

sika

Mud

a w

a U

teke

leza

ji

6.Ku

jeng

a uw

ezo

wa

waw

ezes

haji

na w

arat

ibu

wa

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a

i. Id

adi y

a ko

zi fu

pi-

fupi

na

kozi

za

mud

a m

refu

zili

zoan

zish

wa

ii.

Kuta

mbu

liwa

kwa

vi

wang

o vy

a sif

a za

wel

edi k

wa

waw

ezes

haji

wa

prog

ram

u za

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a ka

tika

muu

ndo

wa

utum

ishi w

a um

ma

i. Ku

anzi

shwa

kw

a pr

ogra

mu

2 za

maf

unzo

ya

mud

a m

fupi

zi

nazo

husia

na

na u

wez

esha

ji,

uend

esha

ji na

ua

ndaa

ji wa

za

na k

atik

a ki

la

wila

ya ifi

kapo

20

25ii.

Kua

ndal

iwa

na

kuta

mbu

liwa

kwa

viwa

ngo

vya

sifa

za

wel

edi k

wa a

jili

ya w

awez

esha

ji na

war

atib

u wa

pro

gram

za

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a ifi

kapo

m

waka

202

5

Robo

mw

aka

Mw

aka

Mud

a w

a ka

ti

TEW

W,

WyE

ST, O

R-

TAM

ISEM

I,

Serik

ali z

a

mita

a, A

ZISE

,

Vyuo

vik

uu,

Bodi

ya

Mak

taba

,

SID

O

2021

-202

5

54

Page 65: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

55

54

55

Na�

Leng

o la

K

imka

kati

Via

shiri

a vy

a M

afan

ikio

Shab

aha

Mzu

nguk

o w

a ku

kusa

nya

da

ta

Mhu

sika

Mud

a w

a U

teke

leza

ji

7.Ku

kuza

kaz

i za

tafit

i, uv

umbu

zi

na u

buni

fu

katik

a m

asua

la

ya k

isom

o na

el

imu

kwa

umm

a.

i. Id

adi y

a wa

tend

aji

walio

pata

maf

unzo

ya

uta

fiti,

ubun

ifu n

a uv

umbu

zi.

ii.

Idad

i ya

mita

ala

na

prog

ram

u za

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a ze

nye

ubor

a na

ze

nye

kuki

dhi m

ahita

ji ili

yoan

daliw

a na

wa

tend

aji m

balim

bali.

i. Ku

patiw

a m

afun

zo y

a ku

fany

a ut

afiti

na k

uwas

ilish

a m

atok

eo

ya u

tafit

i wa

teke

leza

ji m

ia

moj

a na

sitin

i na

tisa

(169

) wa

kiso

mo

na

elim

u kw

a um

ma

ifika

po m

waka

20

25.

ii. K

ujen

gewa

uw

ezo

wa w

atek

elez

aji

katik

a ku

buni

pr

ogra

mu

na

mita

ala

ya

kiso

mo

na e

limu

kwa

umm

a kw

a ku

zing

atia

m

ukta

dha

husik

a ifi

kapo

mwa

ka

2025

.

Robo

mw

aka

Mw

aka

Mud

a w

a ka

ti

TEW

W,

WyE

ST, O

R-

TAM

ISEM

I,

Serik

ali z

a

mita

a, A

ZISE

,

Was

hirik

a w

a

mae

ndel

eo,

Vyuo

vik

uu,

Bodi

ya

Mak

taba

,

SID

O, V

ETA

2021

-202

5

Page 66: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

56

Page 67: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi

57