22
MWONGOZO WA UFUATILIAJI UWAJIBIKAJI JAMII Kwa Matumizi ya Marafiki wa Elimu Wawezeshaji HakiElimu 2011

MWONGOZO WA UFUATILIAJI UWAJIBIKAJI JAMII Kwa Matumizi …hakielimu.org/files/publications/Mwongozo wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji... · Ibara ya 18 sehemu a mpaka d ya Katiba ya Jamhuri

  • Upload
    others

  • View
    12

  • Download
    2

Embed Size (px)

Citation preview

MWONGOZO WA UFUATILIAJI UWAJIBIKAJI JAMIIKwa Matumizi ya Marafiki wa Elimu Wawezeshaji

HakiElimu 2011

iUwajibikaji wa jamii

Mhariri: Elizabeth Missokia

Waandaji: Pius Makomelelo, Lilian Urassa, Naomi Mwakilembe,

Joyce Mkina, Magreth Paul

Wachangiaji: Robert Mihayo, Vicent Mnyanyika

Sehemu yeyote ya kitabu hiki inaweza kunakiliwa kwa minajili isiyo ya

kibiashara, ilimradi chanzo cha sehemu inayonakiliwa kinaonyeshwa na

nakala kutumwa kwa HakiElimu.

ii Uwajibikaji wa jamii

YALIYOMO

1. Dhana ya kufuatilia uwajibikaji wa kijamii .............................. 1

2. Maana ya uwajibikaji wa jamii ................................................. 2

3. Nafasi ya mwananchi katika ufuatiliaji wa kijamii ................... 3

4. Mfumo rahisi na nyenzo za kufuatilia uwajibikaji wa kijamii ... 4

5. Nyenzo za ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii ............................... 11

6. Hatua za kufanikisha ufuatiliaji jamii kwa kutumia kadi pima 12

1Uwajibikaji wa jamii

UTANGULIZI: DHANA YA KUFUATILIA UWAJIBIKAJI WA KIJAMII

Jitihada za serikali za kuimarisha misingi ya utawala bora nchini zinazidi kupata nguvu kutoka kwa wadau mbalimbali hususani wanaharakati wa kimaendeleo ambao wanajitahidi kufuatilia wajibu wa serikali katika kuleta maendeleo na usawa katika ugawaji wa rasilimali na utekelezaji wa ahadi zake. Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi ni mambo ya msingi sana katika kuimarisha dhana nzima ya Utawala Bora kwa maendeleo ya Taifa letu. Dhana ya ufuatiliaji wa Kijamii inaainisha misingi endelevu juu ya ushiriki wa wananchi katika kufuatilia michakato ya kiutendaji na utoaji huduma ndani ya jamii. Lengo ni kuona huduma itolewayo inaleta tija na inazingatia mahitaji halisi ya wananchi. Dhana hii inatoa nafasi kwa wananchi kuwa na uwezo wa kufuatilia mchakato mzima wa upangaji na ugawaji wa rasilimali, usimamizi na matumizi yake, ufanisi wa watendaji, uzingativu wa maadili, na usimamizi wa kimamlaka.

Huu ni mwendelezo mzuri katika kufanikisha utekelezaji wa programu ya ugatuzi wa madaraka kwenda kwa wananchi. Miradi mingi iliyopo kama ya kuboresha elimu ya msingi na sekondari (MMEM na MMES) imejengwa kwa kuzingatia misingi na umuhimu wa ushiriki wa wananchi kama wawezeshaji wakubwa katika utekelezaji, usimamizi na ufuatiliaji wake. Miradi hii ni pamoja na ile inayotumia fedha zitokanazo na kodi za wananchi au mikopo mfano mfuko wa jimbo, katika ujenzi wa utekelezaji wa miradi kama vile ya ujenzi wa zahanati, barabara, shule, visima vya maji na kadhalika; miradi inayolenga kuboresha huduma kwa wananchi. Hivyo ni vizuri kupima ufanisi wa miradi hii kwa kufanya ufuatiliaji wa tathimini.

Ufuatiliaji wa uwajibikaji wa kijami katika miradi ya jamii kama vile, elimu, maji, miundombinu na kutetea haki za binadamu. Ni msingi na nguzo muhimu katika kuchochea jitihada za wananchi za kujiletea maendeleo endelevu. Ni nyenzo muhimu pia katika kutekeleza na kuimarisha dhana nzima ya uwazi na utawala bora ndani ya jamii.

2 Uwajibikaji wa jamii

Katika hali ya sasa, miradi mingi inaanzishwa lakini michache sana huakisi mahitaji halisi ya wananchi zaidi ya kujaa fikra na mahitaji ya baadhi ya watendaji wasiojali masilahi ya umma. Pia, miradi mingi inatekelezwa bila ya kuzingatia ufanisi, hivyo mwendelezo wake unakuwa mgumu na mara nyingi haina tija kwa wananchi. Jamii inaona watendaji walio wengi (wenye madaraka), hawajali masilahi ya umma katika utoaji wa huduma.

Dhana hii inachagiza vile vile uwepo wa namna bora ya kuwarudisha watendaji kwenye mstali, wazingatie maadili ya uongozi katika utoaji wa huduma kwa jamii katika na usimamizi wa miradi ya umma. Ufutiliaji wa kijamii unatoa nafasi ya sauti ya wananchi kusikika ili kupunguza au kuondoa ukiritimba wa baadhi ya watendaji katika utoaji wa huduma na kwa namna moja au nyingine kusaidia kuongeza uwajibikaji wa viongozi wa wananchi kwa ujumla kwa masilahi ya taifa.

MAANA YA UWAJIBIKAJI WA JAMII

Uwajibikaji jamii ni haki ya kupata uthibitisho/uhalalisho na maelezo au ufafanuzi kutoka kwa viongozi wa umma na wakala watoa huduma kwa utendaji/ufanisi wao katika kusimamia rasilimali za umma. [Ni wajibu wa watoa huduma kuthibitisha/kuhalalisha, kueleza na kuchukua hatua sahihi; Maafisa wanapaswa kuthibitisha/kueleza upangaji wa vipaumbele rasilimali zilizopo na waoneshe jinsi vipaumbele hivyo vitakavyofanikisha kupatikana kwa mahitaji muhimu ya wanajamii kiuchumi na kijamii].

Ili kuwawajibisha watoa huduma kwa matumizi ya rasilimali za umma, ni lazima kujiuliza

• Kuna rasilimali kiasi gani?

• Namna gani rasilimali zitapangiwa au zimepangiwa vipaumbele?

• Serikali lazima ieleze na kuhalalisha upangaji wa vipaumbele kwa rasilimali zilizopo

• Kipi kinahitaji kupewa kipaumbele?

3Uwajibikaji wa jamii

NAFASI YA MWANANCHI KATIKA UFUATILIAJI WA KIJAMII

Miradi yote inayochagiza ushiriki wa mwananchi katika kufuatilia uwajibikaji imejikita katika mchakato mzima wa kutimiza misingi ya haki za msingi za binadamu. Haki za msingi za binadamu zaidi ya kuakisiwa kwenye mikataba mbalimbali ya Umoja wa Mataifa zimeainishwa pia kwenye katiba ya nchi yetu.

Ibara ya 18 sehemu a mpaka d ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasisitiza juu ya haki ya mtanzania kuwa na uhuru wa kutoa mawazo. Kipengele d kinasema “kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii” Kipengele a katika ibara hii kinasema “kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake”

Haki za binadamu kimsingi ni stahili ambazo mwanadamu anazaliwa nazo. Haki haiwezi kutolewa kama zawadi na mtu bali ni kitu anachokirithi moja kwa moja mwanadamu mara anapozaliwa. Hivyo haki ya kupewa au kutoa habari haiji kama zawadi. Uwajibikaji wa kijamii umejikita katika kupata taarifa kuhusiana na huduma za kijamii kwa lengo la kuainisha usahihi katika utekelezaji na kama huduma hiyo inasaidia jamii husika. Kwa mantiki hii, uwajibikaji wa kijamii ni utekelezaji wa katiba ya nchi yetu.

Mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii katika hali ya kawaida una hatua tano zinazotegemeana. Kila hatua ina maswali ambayo wananchi/jamii wanatakiwa kuyaibua kuzingatia hasa wakati wa usaili na ukusanyaji wa taarifa mahususi kwa lengo la kupima kiwango cha uwajibikaji. Maswali yaliyopendekezwa kwenye mwongozo huu ni baadhi tu ambayo Rafiki wa Elimu mwezeshaji anaweza kuyatumia wakati wa ufuatiliaji huu.

4 Uwajibikaji wa jamii

MFUMO WA UFUATILIAJI JAMII: KWA NINI TUNAHITAJI

Uwajibikaji wa kijamii husaidia kufanikisha utekelezaji wa miradi kama ilivyopangwa kwa kuzingatia muda, na kwa viwango. Tukifutilia kwa kuzingatia haya tutakuwa tumefanikiwa kutekeleza majukumu yetu ipasavyo na hivyo kusaidia kuimarisha ubora wa maisha na ustawi wa jamii zetu. Uwazi na uwajibikaji ni nguzo muhimu katika kutufikisha kwenye ustawi tunaohitaji.

Uwajibikaji tunaousema hapa hauwalengi watendaji pekee, bali pia wananchi. Pamoja na kwamba ni haki ya kikatiba kama tulivyosema awali kwa mwananchi kujua nini kinaendelea ndani ya shule na ndani ya jamii kwa ujumla kuhusiana na maisha yake,ni wajibu wa wananchi pia kutimiza wajibu wake kwa jamii.

5Uwajibikaji wa jamii

Upatikanaji wa taarifa sahihi ni moja ya misingi ya kujenga uwajibikaji na dhana nzima ya utawala bora. Inaimarisha mwitikio wa wananchi katika shughuli za maendeleo. Dhana hii inajenga pia misingi ya uadilifu kati ya watendaji, wasimamizi wa miradi ya jamii na watoa huduma.

Mambo mengi yanafanyika lakini wananchi hawana taarifa. Katika mpango wa kuboresha Elimu ya msingi MMEM I na II. Kwa mfano, serikali ilipanga na kudhamiria kuwa kila mwanafunzi mlemavu atapata Tsh 20,000 kila mwaka kama ruzuku. Cha kushangaza ni kwamba shule nyingi hazijawahi kupata wala kusikia habari hii.

Mfano mzuri ni shule ya msingi Mbweera iliyopo wilayani Hai, ina darasa la wanafunzi wenye ulemavu,lakini hawajawahi kupokea ruzuku yeyote tangu kuanza kwa utekelezaji wa MMEM II.

Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani. Watendaji wanashindwa kuwajibika hata kwa yale waliyokubaliana kuyatekeleza.Ufatiliaji wa uwajibikaji jamii utasaidia katika kuanika ni matatizo yaliyopo katika utoaji wa ruzuku hii kama ulivyokuwa umepangwa awali.

Zaidi waananchi wanatakiwa kufuatilia mapato na matumizi ya fedha za miradi kwenye maeneo yao kwani ni jukumu la kila mwananchi, pia ni haki yake kujua mapato na matumizi ya miradi husika,kwa kuzingatia makubaliano ya awali kama makubaliano yaliyopangwa yametekelezwa, kama ilivyo anishwa kwenye mkataba .Tunaweza kufuatilia kwa kuangalia kwa mfano kama mkandarasi amezingatia ujenzi kama iliyoanishwa kwenye mkataba mfano, ameweka idadi kamili ya makaravati kama ilivyokubalika au la.

6 Uwajibikaji wa jamii

MFUMO WA UWAJIBIKAJI KATIKA JAMII

Mfumo wa uwajibikaji katika jamii una hatua tano za msingi kama

zilivyoonyeshwa hapo juu na kufafanuliwa zaidi hapa chini.

. HATUA YA KWANZA: UPANGAJI NA UGAWAJI WA rASILIMALI

Hatua ya kwanza inalenga kupima mambo ya msingi ambayo yanategemewa katika hatua ya mwanzo kabisa ya utekelezaji wa mradi au utoaji wa huduma yoyote ile katika jamii. Maswali ya kuzingatia katika hatua hii ni pamoja na haya:

• Ni rasilimali kiasi gani (fedha, watu, n.k) kipo kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya jamii?

• Ni fedha kiasi gani cha ruzuku kimepatikana kati ya iliyopangwa? (kila mwanafunzi anatakiwa kupata sh. 10,000 kutokana na mpango wa MMEM); fedha ya maendeleo kutoka serikali kuu ni kiasi gani imefi ka?

7Uwajibikaji wa jamii

• Michango ya wazazi iliyopanga/iliyopatikana ni kiasi gani?

• fedha kutoka vyanzo vingine ni kiasi gani?

• Wataalamu waliopo kwa ajili ya kufanikisha shughuli hii, Mahitaji au vipaumbele vya wananchi ni vipi?

• Je vimezingatiwa katika mradi huu?

• Kama havikuzingatiwa ni kwa nini?

• Nani alibadilisha (kama mradi umeshatekelezwa). Kiasi gani cha fedha kimepangwa/kilipangwa kutumika katika utekelezaji wa mradi unaofuatiliwa?

HATUA YA PILI: KUSIMAMIA MATUMIZI

Hatua hii inalenga kufuatilia na kupima kwa kiasi gani watendaji wamesimamia ipasavyo matumizi kama ilivyoainishwa kwenye mradi. Vitu vikubwa vya kuzingatia hapa ni kukusanya taarifa mbalimbali za mradi mfano andiko la mradi, stakabadhi za manunuzi, taarifa mbalimbali za ukaguzi, nk. Maswali makuu katika hatua hii ni pamoja na:

Kiasi gani cha rasilimali fedha kilipangwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu? kiasi gani kilipatikana na kutumiwa katika utekelezaji wa mradi huu? kiasi gani hakikufika katika mradi na kwa nini? fedha zilizotumika zimetumika katika manunuzi yapi? [Rejea za kupitia kuhakikisha matumizi, ni pamoja Na mpango kazi, budget, ripoti za utekelezaji, maoni ya wananchi juu ya mradi husika, stakabadhi za manunuzi, nk Kikubwa ni kuona je, fedha za umma zimetumiwa vizuri na kwa tija?

8 Uwajibikaji wa jamii

HATUA YA TATU: KUSIMAMIA UFANISI

Kusimamia Ufanisi ni haki ya kupata uthibitisho/uhalalisho na maelezo au ufafanuzi kutoka kwa viongozi wa umma na wakala watoa huduma kuhusu utendaji na ufanisi wao katika kusimamia rasilimali za umma. Ni wajibu wa watoa huduma kutoa taarifa zinazohusu utendaji wao.

Maafisa wanapaswa kuthibitisha/kueleza upangaji wa vipaumbele vya rasilimali zilizopo na waonyeshe jinsi watakavyoendelea kufanikisha mahitaji muhimu ya jamii na kiuchumi. Katika hatua hii ufanisi utapimwa kama wasimamizi wa mradi wamefikia malengo yaliyopangwa na zao la kazi yao lina viwango ambavyo wananchi walitegemea. Ufanisi katika miradi ya elimu itapimwa kwa kuangalia kwa mfano, jengo (darasa, nyumba za walimu, maabara, etc kama zimekamilika na zimezingatia viwango vinavyokubalika kitaifa na kama stakabadhi za manunuzi imezingatiwa, vitabu vilivyonunuliwa kama ndivyo vinavyokubalika na serikali, vilevile vifaa vya kufundishia au kujifunzia kadhalika. Ufuatiliaji vilevile unaweza kuangali uondoaji wa msongamano madarasani, ikama inayostahili ya walimu, mazingira mazuri ya kujifunzia. [Vigezo vingine vinavyotumika kupima ufanisi katika elimu ni pamoja na ikama ya walimu kwa wanafunzi ambayo inatakiwa kulingana na sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 1995 kuwa 1:45; darasa moja linatakiwa kuwa na wanafunzi 40/45, kitabu kimoja kinatakiwa kusomwa na mwanafunzi 1; tundu moja la choo linatakiwa kuhudumia watoto wa kike 20 na watoto wa kiume 25, kila shule inatakiwa kuwa na maktaba na maabara kwa shule za sekondari. Kitu cha kujiuliza katika muda wote wa uwepo wa shule je, rasilimali zetu zimefanikisha kupatikana kwa mambo yapi?]

Ili kuwawajibisha watoa huduma kwa matumizi ya rasilimali za umma, ni muhimu ufuatiliaji uweze kujibu maswali hayo hapo juu. Tathimini hii inahusu zaidi wananchi; kuona jinsi gani walengwa / wananchi wanafaidika au kuathirika na utendaji au utekelezaji wa mpango huo na kwa kiwango gani, na ni hatua zipi zichukuliwe kuondokana na athari zinazojitokeza.

9Uwajibikaji wa jamii

HATUA YA NNE: UADILIFU WA WENYE MAMLAKA Tunatakiwa kuwa na viongozi ambao wanajali masilahi ya jamii na rasilimali zetu: Watendaji wetu wanatakiwa kuwa watu wadilifu, watu wanaojituma, watu wanaojali masilahi ya wananchi, watu wanaoelewa na kuvumilia tabia za watu, watu wanaosikiliza shida za watu na watendaji walio waaminifu wasiojihusisha na wizi, udanganyifu, ubadhirifu au rushwa. Wanaoshirikisha wananchi katika maamuzi bila ubaguzi; wakweli na wawazi; wanaojiamini na kuwaamini wengine; walio tayari kujikosoa na kukosolewa; wenye upeo mpana; wanaopenda kujifunza kutoka kwa umma na kukubali mabadiliko.

Katiba ya nchi inaelekeza kwamba ni haki na wajibu wa kila mtu kufanya kazi halali ya uzalishaji mali ili kujipatia riziki. Ni wajibu wa viongozi kuwezesha wananchi kutumia rasilimali zilizopo ili kujipatia riziki.

[Katika hatua hii wafuatiliaji wakifuatilia na kujua uzingativu wa maadili katika utekelezaji wa miradi ya umma na namna wale waliotumia madaraka yao vibaya wamechukuliwa hatua za namna gani? Ni utaratibu gani uliopo wa kuzuia ubadhilifu na hatua zipi zimewekwa au zinachukuliwa kwa ajili ya kurekebisha]

HATUA YA TANO: USIMAMIZI

Mfumo wa uwajibikaji jamii unatakiwa kutumia viongozi wa wananchi na serikali kuhakikisha watendaji wanawajibika kwa nafasi zao ndani ya jamii. Katika hali ya kawaida, madiwani wanatakiwa kuchukua jukumu la kuhakikisha watendaji katika ngazi za halmashauri wanawajibika moja kwa moja katika utoaji wa huduma ngazi ya wilaya bila ubaguzi wa aina yoyote. Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa bajeti ya halmashauri imezingatia kwa uhakika mahitaji na vipaumbele vya msingi vya wananchi. Vilevile wanatakiwa kuhakikisha wanadhibiti matumizi ya bajeti yaendane na mpango uliokubalika. Wabunge na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ni vyombo katika kuhakikisha ufuatiliaji wa kijamii unafanikiwa kwa lengo la kuongeza uwajibikaji ili kiwango cha huduma kwa jamii kiboreke zaidi.

10 Uwajibikaji wa jamii

[Cha msingi hapa ni kwa wafuatiliaji kuangalia namna mamlaka hizi za usimamizi zinavyofanya kazi; kuhakikisha kuwa ripoti mfano ya mkaguzi mkuu wa serikali inatumiwa kama chanzo kingine cha taarifa ili kujiridhisha na uhakika wa taaifa itakayopatikana. Swali kubwa hapa ni je maafi sa au watendaji wakuu wanaoboronga kwenye nafasi zao za utendaji na kuisababishia jamii hasara wanawajibishwaje kutokana na madudu waliyofanya? Wanawajibishwa namna gani? Lengo hapa ni kujenga uaminifu wa wananchi kwa wasimamizi wao].

Wanafunzi wamesongana darasani

Hatua zote hizi tano zinalenga kufanikisha upatikanaji wa haki za binadamu na kukuza uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.

Uwajibikaji na Ufuatiliaji wa rasilimali: Athari za kutofuatilia

11Uwajibikaji wa jamii

NYENZO ZA UFUATILIAJI WA UWAJIBIKAJI JAMII: KADI PIMA

MFANO WA PIMA KADI

Utendaji katika Elimu-A1. Utendaji wa WalimuA1.1 Kwa kiasi gani walimu wanatekeleza wajibu wao wa kufundisha

na kuwapa wanafunzi wao taaluma inayotakikanaMaelezo Nzuri

sanaNzuri Unarid-

hishaSio nzuri

Mahudhuri ya wanafunzi darasani

Upatikanaji wa elimu bora kwa wanafunzi

Utoaji wa mazoezi kwa wana-funzi

Ushirikino na wazazi

B1 Matumizi ya rasilamali za shuleB1.1 Kwa kiasi gani uongozi wa shule umetumia vyema/vibaya rasi-

mali za shuleMatumizi ya fedha za ruzuku

Matumizi ya michango ya wazazi

Kadi pima ni nyenzo inayotumika kupima kiwango cha uwajibikajiwa watendajina watoa huduma katika kufanikisha upimaji kwa kutumia kadi pima.

12 Uwajibikaji wa jamii

Zipo aina au njia nyingi za kuainisha kazi ambazo zinatekelezwa katika mchakato huu. Mara nyingi ni hatua saba na kikundi chaweza kuwa na watu saba hadi tisa.

Kadi pima ni nyenzo inyotumika kuongoza nguvu ya umma na kiwango cha wajibikaji katika ngazi za kata na kijiji.

Katika kupima kiwango cha uwajibikaji, kadi hii inapendekeza hatua tisa ambazo kikundi cha jamii kinaweza kupita. Ni rahisi na imeonesha mafanikio katika maeneo mengi barani Afrika! Wadau wengi wanaiita “PIMA KADI” au “SCORE CARD”

HATUA ZA KUFANIKISHA UFUATILIAJI JAMII KWA KUTUMIA PIMA KADI

1. Maandalizi

2. Katika jamii: Mikutano ya awali

3. Katika Jamii : Vikundi maalumu

4. Katika jamii : Mikutano ya pamoja

5. Warsha za Mirejesho

6. Majukwaa ya wadau – Wilayani

7. Usambazaji wa taarifa na Ushawishi

HATUA YA KWANZA: MAANDALIZI

Kufahamiana ni jambo la msingi kwa kikundi ili kurahisisha ufuatiliaji.

• Jenga uelewa wa (hamasisha) jamii ya eneo husika juu ya mchakato wa pima kadi. Ni vizuri kuwaelewesha wanajamii mipango yenu ili iwe rahisi kufuatilia.

• Toa taarifa juu ya mchakato wa pima kadi kwa wanajamii katika kata au kijiji husika, ikibidi ni vizuri pia kutoa taarifa kwa uongozi wa halmashauri ya wilaya ili kupata baraka zao na ukumbuke kuwa ofisi hizi ni chanzo kizuri cha taarifa nyingi utakazotumia kwenye

13Uwajibikaji wa jamii

mchakato mzima wa ufuatiliaji huu

• Chagua /tengeneza kamati ya wanajamii

• Jenga uwezo wa kuraghibisha kwa wanakamati

HATUA YA PILI: KATIKA JAMII: MIKUTANO YA AWALI

• Saidia wanajamii kuchagua masuala au huduma ambayo wanajamii

wanahitaji kuifuatilia na kuipima mfano elimu, afya, mazingira, miundo mbinu, nk

• Wasaidie wanakamati kukubaliana juu ya viashiria vya mafanikio (zingatia pia viashiria vya sera husika kama vilivyoainishwa kwenye mwongozo huu. unaweza kupata ufahamu zaidi kwa kuwasiliana na wakuu wa idara ngazi ya halmashauri)

• Unaweza kuwagawa wanajamii katika vikundi maalumu

HATUA YA TATU: VIKUNDI MAALUMU (FOCUS GrOUPS) KATIKA JAMII

Kukutana na vikundi maalumu vya wanajamii (wahudumiwaji) pamoja na watoa huduma kama kundi jingine maalumu ili kupata maoni yao juu ya huduma mnayoifuatilia

• Kila kikundi kitoe alama katika viashiria walivyokubaliana

• Rejea taarifa za watoa huduma, kamati moja au zaidi inaendelea kukusanya taarifa

• Wajumbe wa Kamati wanatoa sababu ya alama wanazotoa

• Wasaidie wajumbe wa kamati kujadili mbadala au namna bora za kuboresha

14 Uwajibikaji wa jamii

HATUA YA NNE: MIKUTANO YA PAMOJA KATIKA JAMII

• Kamati itoe alama zake (mraghibishi anatarajiwa kutoa msaada

zaidi)

• Mjadala wa alama unaanza

• Wapewe nafasi watoa huduma kutoa maelezo juu ya alama na maoni ya wajumbe wa kamati

• Wote wanajadili namna za kuboresha

• Fahamisha jamii katika ngazi ya wilaya ambapo wadau wa maendeleo watahudhuria. Wanavikundi wanachagua watu wa kuzunguka katika mdahalo katika halmashauri ya wilaya.

15Uwajibikaji wa jamii

HATUA YA TANO: WArSHA ZA MIrEJESHO

• Timu ya waraghibishi wanatakiwa kukutana ili kujadili

changamoto, kukusanya taarifa, na kupanga mdahalo wa wadau katika ngazi ya wilaya.

• Taarifa ya pamoja ya kamati zote inatengenezwa, mfano: Kwa mujibu wa kamati maalumu wanawake katika jamii wanasema kuwa…. Na wanaume wa eneo wanasema kuwa … (yapange matokeo kutokana na kundi husika. Mfano. wanawake kwenye jamii 16 wamesema x, wanaume kwenye jamii 16 wamesema Y.

HATUA YA SITA: MAJUKWAA YA WADAU – KATIKA HALMASHAUrI ZA WILAYA

• Waraghibishi na wanajamii wanawakilisha majibu ya alama walizotoa (katika pima kadi zao)

• Wasemaji wa jamii watoe dukuduku zao

• Pata maoni ya watoa huduma

• Mjadala wa pamoja

• Watu wachache wafanyie kazi suala moja na waanze kutengeneza mpango kazi wao

• Mrejesho wa kazi za vikundi vya watu wachache

16 Uwajibikaji wa jamii

HATUA YA SABA: USAMBAZAJI WA TAArIFA NA USHAWISHI

• Tengeneza taarifa na kuisambaza kwa wadau wengi

• Taarifa inaweza kufananishwa matokeo na mafanikio au mipango au uzoefu wa kata au halmashauri zingine na sekta zingine

• Sambaza taarifa kwa vyombo vya habari na mbao za matangazo

• Endelea kutafuta maeneo ya kushawishi na michakato mingine inayoweza kubadili hali hiyo kama hali hairidhishi.

!&""

Tsh/= Ujenzi wa madarasa

Tsh/= Urekebishaji/ Ujenzi wa barabara

Mkutano wa wajumbe

Kutengeneza ripoti ya mirejesho

Mkutano wa wananchi wa kujadili sekta ipi wataifanyia ufatiliaji na kuchagua kamati.

Kuchambua taarifa Kutoa mafunzo kwa Kamati kuhusu kukusanya taarifa.

Kutengeneza PIMA KADI

Kuchambua bajeti ya serikali za mtaa kwa kuangalia sekta na rasilimali.

17Uwajibikaji wa jamii

MFANO WA UFUATILIAJI

Kwa kuangalia matokeo mbalimbali ya ufuatiliaji wa ruzuku ambazo zinatolewa na serikali kwa wanafunzi kwa shule za msingi mfano kwenye mwaka 2009/2010 ngazi ya wilaya, ufutialiji wa ruzuku kwa wanafunzi Wilaya ya Njombe, Bunda na Babati, Matokeo yalikuwa hivi; Bunda ilipata kiasi cha Sh. 503,830,500 badala ya 812,830,000 ilizotakiwa ipate kwa idadi ya mwanafunzi 81,283 iliyokuwa nao. Kwa hiyo kila wanafunzi alipata gawio la shilingi Sh.6,198 badala ya 10,000 zinazohitajika kwa mwaka.

Wilaya ya Njombe ilipata kiasi cha Sh. 130,553,600 badala ya 763,660,000 kukiwa na idadi ya mwanafunzi 76,366 sawa na gawio la Sh.1,710 kwa kila mwanafunzi kama ruzuku kwa mwaka. Wakati katika wilaya ya Babati walipokea kiasi cha sh.303,770,000 ikiwa na idadi ya wanafunzi 61,254 ruzuku kwa kila mwanafunzi ni kiasi cha Sh. 4,959 kwa mwaka.

Kwa kuangalia mgawanyo huo hauwezi kabisa kulinganisha maendeleo ya shule moja kwenda nyingine kwa sababu ruzuku zinatofautiana kutokana na kiasi wanachopokea.

Tofauti hii inasikitisha tena inasababisha shule zilizopata ruzuku kidogo kushindwa kutekeleza mipango yao, matokeo yake kushindwa kufaulisha kwa sababu ya kukosa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa kuzingatia uzoefu, usimamizi mbaya wa rasilimali na miradi ya wananchi inaishia kwenye matokeo mabaya, ufujaji wa rasilimali na maisha duni ya wananchi.

Kwa kuwa wananchi ndiyo wamiliki wa miradi yote ya maendeleo, wanayo sababu tosha kufuatilia nini kinaendelea kwenye miradi yao badala ya kukaa kimya ili hali mambo yanaenda vibaya. Miradi mingi inaishia vibaya kutokana na kukosekana kwa ushiriki wa wananchi katika ufuatiliaji na hivyo kuwepo kwa nafasi ya mafisadi kutumia mwanya kuiba au kutumia vibaya rasimali za umma.

18 Uwajibikaji wa jamii

Ni wazi nguvu za wananchi zinaweza kuleta mabadiliko hasa katika kuongeza uwajibikaji wa kila mtu ndani ya jamii. Marafiki wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kufafanua sera na miongozo kwa wananchi wenzao.

Pia Marafiki kama wakitumia mijadala ya wazi na kushirikisha wenzao kutambua sera, hali halisi na kero zilizopo ndani ya jamii basi mabadiliko chaya tunayohitaji kuyaona ndani ya jamii yataonekana. Kama ushiriki wa wananchi na Marafiki kwenye mipango ya maendeleo utakuwa hafifu ni vigumu kwa jamii kufikia malengo ambayo tunayataka kwenye milenia hii.

Juhudi za Marafiki katika kuielimisha jamii ni nyenzo nzuri inayoweza kuleta mabadiliko tunayotegemea. Kutokana na jumuiko hili la Marafiki, sauti za wanyonge zitasikika kwa lengo la kushawishi mabadiliko na vipaumbele vyao kufuatwa.Tuitumie nyenzo hii kuleta mwamko mpya wa uwajibikaji jamii.

Harakati za Marafiki wa Elimu zikiimarishwa kama mkakati wa kuamsha ushiriki wa wananchi katika kuchagiza mabadiliko katika usimamizi, utoaji na ufuatiliaji wa maendeleo ya elimu nchini utaongezeka kwa kasi kubwa ya maendeleo. Ni wajibu wa Marafiki kuelimisha umma na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika maamuzi, utetezi, utekelezaji na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo hususani katika sekta ya elimu. Tunawaomba Marafiki na wadau wengine wa maendeleo pamoja na wananchi kwa ujumla kusisitisa uwajibikaji wa pamoja. Tutafanikiwa, ni wajibu wa kila Mtanzania kufuatilia miradi, mapato, matumizi, na uwajibikaji wa kila mdau katika shughuli za jamii.

Marafiki wa ElimuC/O HakiElimu

739 Mtaa wa Mathuradas, UpangaS.L.P 79401 Dar es Salaam

Simu: (022) 2151852/3, 0754 354 681, 0787 655 000, 0715 723 454Nukushi: (022) 2152449

Barua Pepe: [email protected]: www. hakielimu.org