42
Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Vijijini Dodoma Septemba 2016

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

  • Upload
    others

  • View
    28

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)

Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Vijijini

Dodoma

Septemba 2016

Page 2: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)

Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Vijijini

Dodoma

Imeandaliwa na Timu ya SAM Septemba 2016

Page 3: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”
Page 4: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

i

Kukamilika kwa mchakato mzima ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Vijijini mnamo Septemba 19, 2016 kumetokana na mchango mkubwa wa wadau mbalimbali hapa wilayani. Shukrani zetu za dhati ziende kwa uongozi mzima wa wilaya kwa kuanzia ofisi ya Mkuu wa Wilaya inayoongozwa na Mh. Sezaria V.Makota na Katibu Tawala, Bi. Winnie Kijazi. Vilevile, Baraza la madiwani na uongozi mzima wa Halmashauri chini ya Mwenyekiti Mh. Alhaji Omari Kariati na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Kibasa Falesy Mohamed pamoja na wakuu wa idara. Aidha, tunamshukuru Mganga Mkuu wa Wilaya Dk. Zulkanine Ikaji na timu yake ya CHMT, wote hawa walionyesha ushirikiano mkubwa, uwazi na kujitolea tangu hatua za awali. Ushauri na miongozo yao ilisaidia kufanikisha zoezi hili kwa kiwango kikubwa. Ni imani yetu kuwa timu iliyound-wa kuwawakilisha wananchi wa Kondoa itaendelea kupata ushirikiano wa kutosha kwa muda wote wa kutekeleza majukumu yetu kwa manufaa ya watu wote wa Wilaya ya Kondoa na Taifa kwa ujumla. Pili shukrani za pekee ziende kwa shirika la Sikika pamoja na wafadhili wake wote kwa kuende-lea kuratibisha zoezi hili hapa wilayani. Hakika wawezeshaji wa zoezi hili la UUJ/SAM kutoka shiri-ka la Sikika; Ndg. Fredrick Ngao, Bi. Alice Monyo, na Ndg. Nelson Lema walifanya kazi kubwa ya kuratibu na kufanikisha kutujengea uwezo ambao kwa sasa tunaweza kujivunia kwa vitendo. Tatu ni kwa wananchi wa Kondoa kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa muda wote hususani waka-ti wa kutembelea vituo vya kutolea huduma za afya hapa wilayani kwa lengo la kuona hali halisi.

Mwisho napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wajumbe wote 15 wanaounda timu ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ/SAM) Wilaya ya Kondoa Vijijini-2016 kwa kujitolea kikamilifu kushiriki mafunzo na kufanikisha zoezi zima pamoja maandalizi ya ripoti hii. Kwa kuwatambua, wajumbe hao ni pamoja na; wawakilishi wa wananchi; Ndg. Ally Mustafa Isere, Ndg. Huseni Abdala Gau, Ndg. Isaka Timoth Majuva na Ndg. Omari Mohamedi Saidi; wawakili-shi wa madiwani; Mh. Bashiru Mtoro Ramadhani na Mh. Jamila Juma Gamaha. Mwakil-ishi wa Timu ya Uendeshaji wa Shughuli za Afya ya Halmashauri; Ndg. Deousderatus Y. Namfua; mwakilishi wa viongozi wa dini Ndg. Dominick S. Maloway, mwakilishi wa timu ya wataalamu ya Halmashauri Ndg. Heri Hassan Suba, mwakilishi wa Bodi ya Afya ya Halmashauri Ndg. Mohamed Shaaban Thawa, mwakilishi wa watendaji wa kata; Mwanaisha Ally Maiwa, wawakilishi wa makundi maalumu ya jamii; Ndg Omari I. Kidima- (wale-mavu) na Bi.Shamila Ibrahimu Athuman –(WAVIU), mwakilishi wa Kamati ya Afya ya Kituo; Ndg.

Ramadhan Omari Duru na mwakilishi wa Asasi zisizo za Kiraia Kondoa; Bi. Salama Juma Salum.

Asanteni sana,Ndugu Mohamed Shaaban ThawaMwenyekiti wa Timu ya SAM

Shukrani

Page 5: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

ii

SHUKRANI iORODHA YA VIFUPISHO iiiMUHTASARI iv 1SEHEMU YA KWANZA 11.0 Utangulizi 21.1 Mchakato wa utekelezaji wa zoezi UUJ/SAM 51.2 Muundo wa timu ya UUJ/SAM 51.3 Mafunzo ya nadharia na uchambuzi wa nyaraka 51.3.1 Mpango mkakati na mgawanyo wa rasilimali 51.3.2 Usimamizi wa matumizi 61.3.3 Usimamizi wa utendaji 61.3.4 Usimamizi wa uadilifu 61.4 Maeneo yaliyotembelewa na timu ya SAM 7SEHEMU YA PILI 72.0 Matokeo 72.1 Matokeo ya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali 72.1.1 Mpango mkakati wa Halmashauri 2012-17 na mpango kabambe 2014/15 72.1.2 Usimamizi wa matumizi 82.1.3 Watoa huduma 82.1.4 Gharama za mitungi ya gesi 92.1.5 Gharama za umeme za Hospitali ya Wilaya 102.1.6 Dawa na vifaa tiba 102.1.7 Ukarabati wa wodi - hospitali 122.1.8 Marekebisho ya mfumo wa maji - hospitali 132.1.9 Ukarabati wa choo cha nje - hospitali 132.1.10 Vifaa vya kujifungulia - hospitali 142.1.11 Mafunzo ya watoa huduma 142.1.12 Ununuzi wa vifaa vya kupima uzito na urefu 142.3 Changamoto katika kutekeleza zoezi la SAM 27

SEHEMU YA TATU 293.0 Maazimio 29

SEHEMU YA NNE. 314.0. Hitimisho na mapendekezo 31

Kiambatanisho 1: Vituo vilivyotembelewa na timu ya SAM 32

Yaliyomo

Page 6: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

iii

AZAKI Asasi za Kiraia

BRN Big Result Now/ Matokeo Makubwa Sasa

CHF Community Health Fund/ Mfuko wa Afya ya Jamii

CHMT Council Health Management Team/ Timu ya uendeshaji wa

shughuli za Afya za Halmashauri

CMT Council Management Team/ Timu ya uendeshaji ya Halmashauri

DHSB District Health Service Board/ Bodi ya Huduma za Afya ya Wilaya

HSBF Health Sector Basket Fund/ Mfuko wa Pamoja wa Sekta ya Afya

KE Mwanamke

ME Mwanamume

MSD Medical Store Department /Bohari Kuu ya Dawa

N.K. Na kadhalika

NHIF National Health Insurance Fund /Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya

OC Other Charges (Matumizi mengineyo)

R&R Form Report and request form/fomu za kuombea na kutolea taarifa za

dawa

SAM Social Accountability Monitoring / Ufuatiliaji Uwajibikaji wa Jamii

SH Fedha Taslimu ya Tanzania (Shilingi)

UK Ukurasa

UUJ Ufuatiliaji Uwajibikaji wa Jamii

WAVIU Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi

WEO Ward Executive Officer/ Mtendaji Kata

NDG Ndugu

DKT Daktari

Orodha ya Vifupisho

Page 7: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

iv

Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring” (SAM)

ni zoezi lenye lengo la kuiwezesha jamii kushiriki katika kupanga, kufuatilia na kuchambua utekelezaji

wa mipango kuanzia ngazi ya jamii mpaka halmashauri. Lengo kuu la SAM ni kuhimiza ushirikishwaji,

ufuatiliaji na uwajibikaji wa watendaji/watoa huduma ikiwemo huduma za afya ili kuwapa wananchi

haki zao za msingi kama ilivyoainishwa katika sheria za nchi na mikataba ya kimataifa ambayo

Tanzania imeridhia. Sheria na mikataba hiyo ni pamoja na; Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

(1977) Ibara za (11), (12), (14) – (28), Mkataba wa Banjul (Afrika) na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za

Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni unaofahamika kwa lugha ya Kiingereza kama“International Covenant

for Economical, Social and Cultural Rights (ICESCR, 1976)”, ambayo yote imejikita katika kuhakikisha

uwajibikaji katika kufikia upatikanaji na utoaji wa haki za binadamu na mahitaji ya msingi ya jamii.

Tangu mwaka 2012, Sikika imekuwa ikishirikiana na halmashauri mbalimbali katika kuendesha zoezi la

SAM kwa kuunda timu katika halmashauri hizo. Timu hizi za SAM zinajumuisha wananchi wa makundi

yote, wajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa dini na wa madiwani.

Timu ya SAM hujengewa uwezo wa kushiriki katika kupanga na kufanya uchambuzi wa taarifa mbal-

imbali pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.

SAM pia inalenga kuiwezesha jamii kuhoji uwajibikaji wa wasimamizi na watoa huduma za umma ili

waweze kutoa huduma zinazokidhi mahitaji muhimu na ya msingi kwa jamii kama vile afya, elimu, maji,

chakula na makazi.

Sikika imekuwa likiendesha zoezi katika wilaya zaidi ya 10 zikiwemo Mpwawa, Kilwa, Ilala,

Kibaha, Singida Vijijini, Lindi, Kilolo, Simanjiro, Kiteto, Temeke na Kinondoni. Katika wilaya

ambazo zimewezeshwa kuwa na timu ya SAM, ufutuatiliaji na uwajibikaji katika upatikanaji wa

huduma za afya umeongezeka, ikiwemo uboreshaji wa miundombinu katika vituo vya huduma za

afya na vilevile, katika kupanga bajeti yenye kufuata vipaumbele sambamba na matumizi yenye tija.

SAM katika Wilaya ya Kondoa imefanyika Septemba, 2016, ikiwa ni kwa mara ya tatu baada ya mwaka

2012 na 2014. SAM Kondoa imekuwa na historia kubwa hasa baada ya shirika la Sikika kusimamishwa

kufanya kazi zake mwaka 2014 wakati zoezi la SAM likiendelea. Uhusiano na ushirikiano mkubwa wa

wananchi ulifanikisha kurejesha tena shughuli za shirika mwaka 2016 na kuanza utekelezaji wa zoezi

hilo mwaka huohuo.

Matokeo ya uchambuzi wa nyaraka na ziara vituoni unaonyesha kuwa kuna baadhi ya maeneo

ambayo halmashauri imepiga hatua kubwa katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya. Kwa

mfano, ongezeko la watoa huduma katika vituo; ingawa changamoto bado ipo lakini uhaba wa

watumishi umepungua kutoka asilimia 71 mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 45 mwaka 2015.

Katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kumekuwa na ongezeko la kaya kwa asilimia 18 kwa mwaka

2013/14 na 2014/15. Ongezeko hili la kaya limesababisha ongezeko la mapato yatokanayo na CHF.

Page 8: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

v

Pamoja na kuimarika kwa baadhi ya maeneo, matokeo ya SAM pia yanabainisha maeneo ambayo

mikakati ya makusudi inahitajika ili kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya. Maeneo hayo

ni pamoja na mafunzo kwa kamati za usimamizi wa vituo vya kutolea huduma za afya, kuboresha

miundombinu ya vituo na ukamilishaji wa majengo (nyumba za watumishi, maabara na vituo vya hudu-

ma) kwa wakati. Zoezi hili lilihitimishwa katika mkutano wa wadau wa afya kujadili na kuweka maazimio

yenye lengo la kutoa kipaumbele na mikakati ya kuhakikisha maeneo yenye changamoto yanapatiwa

ufumbuzi. Inategemewa kwamba wadau watashirikiana na Halmashauri katika kutekeleza maazimio

hayo ikiwa ni pamoja na kuishawishi jamii kufanya kazi kwa pamoja na bidii ili kufanikisha uboreshaji

wa huduma za afya kwa manufaa ya wananchi wote wa Wilaya ya Kondoa na Taifa kwa ujumla.

Page 9: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

1

Sehemu ya Kwanza

1.0 Utangulizi

Zoezi la Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (SAM) ni dhana shirikishi kati ya wananchi (wenye wajibu na haki)

na watendaji (wenye wajibu na dhamana) kwa pamoja huhakikisha upatikanaji wa mahitaji muhimu

ya jamii. SAM inasimamia usawa, haki, uwazi, uwajibikaji na uadilifu wa watoa huduma pamoja na

wananchi katika kuhakikisha mahitaji ya jamii yanafikiwa kikamilifu. Pia SAM inalenga kuwawezesha

wananchi kufahamu haki zao na kujua wajibu wao bila ya ubaguzi kutokana na kuboreshwa kwa hudu-

ma za msingi kwa kutumia rasilimali zilizopo ipasavyo. Katika mfumo huu, wananchi wana haki na

wajibu wa kuhoji/kuhojiwa juu ya masuala mbalimbali ambayo kiutaratibu na kisheria wanayo haki na

wajibu wa kuhabarishwa, kwa mfano mwenendo wa mapato na matumizi, ushiriki wa wananchi kwenye

mikutano ya kijamii na kupata taarifa mbalimbali za utekelezaji.

Kwa upande wa watendaji, hawa wana dhamana na wajibu wa kutoa ufafanuzi, uthibitisho, uhalalisho,

na kurekebisha masuala mbalimbali ili kufikia upatikanaji wa huduma bora za afya. Zoezi la SAM kwa

mwaka 2016 linaendelea kutoa taswira endelevu ya uwajibikaji wa jamii katika Wilaya ya Kondoa kwani

hii ni mara ya kufanyika. Kama ilivyokuwa katika programu za SAM zilizotangulia, zoezi hili pia lilizinga-

tia sheria na miongozo mbalimbali katika utekelezaji wake. Uchambuzi uliofanywa na timu uliwezesha

kufanya uhakiki katika vituo vya kutolea huduma za afya vipatavyo 24. Hatua hii ilisaidia kuthibitisha

baadhi ya hoja na hivyo kuwezesha mjadala bora kati ya timu ya SAM kwa niaba ya wananchi na wa-

tendaji wa Halmashauri ambao ni watoa huduma.

1.1. Mchakato wa utekelezaji wa zoezi UUJ/SAMMchakato wa zoezi la SAM katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Vijijini ulianzia kwenye mkutano na Baraza la madiwani tarehe 04/08/2016 ambapo waheshimiwa madiwani walielezwa kwa kina maana na umuhimu. Mkutano huo pia ulicha-gua wawakilishi wawili (mwanamke na mwana-mume) kujumuika na wa-jumbe wengine kuunda timu ya SAM.

Page 10: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

2

Hatua ya pili ilikuwa ni mikutano ya kijamii iliyofanyika tarehe 09-10/08/2016 ambayo mbali na

kueleza umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mambo ya afya,

ilitoa fursa ya uwakilishi wa wananchi wanne waliotoka katika kata za Busi, Mnenia, Soera na Kisese.

Baadhi ya Wazee wa Kata ya Busi wakiwa katika mkutato wa kijamii.

Hatua ya tatu ni mkutano wa kwanza wa wadau wa afya uliofanyika tarehe 11/08/2016, ambapo wadau

mbalimbali wa afya wilayani walialikwa, lengo likiwa kuelewa dhana nzima ya SAM, pia kutoa wawakilishi

walioungana na wawakili-

shi wa wananchi na madi-

wani kuunda timu ya SAM

ya wilaya. Wawakilishi

walitoka katika makundi

mbalimbali kama yalivy-

oelezwa katika UK (iii)

kipengele cha shukrani

hapo juu. Timu ya SAM

yenye wajumbe 15 ilizin-

duliwa rasmi na ofisi ya

mkuu wa wilaya katika

mkutano huo wa wadau. Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota akifungua kikao

cha kwanza cha zoezi la SAM.

Page 11: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

3

Hatua ya tano ni uhakiki kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa lengo la kupata uhalisia wa

utekelezaji wa shughuli za afya kama zilivyoainishwa kwenye nyaraka zilizofanyiwa uchambuzi. Kazi

hii ya kutembelea vituo vya kutolea huduma za afya ilifanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 29/08/2016

hadi 02/09/2016.

Hatua ya sita ilikuwa ni kikao cha ndani baina ya timu ya wataalamu wa Halmashauri, timu ya

uendeshaji wa shughuli za afya

za Halmashauri, timu ya SAM

na wawezeshaji kutoka shiri-

ka la Sikika. Kikao kilifanyika

tarehe 16-17/09/2016 kikiwa

na lengo la kujadili rasimu ya

awali ili kupata ufafanuzi wa

mambo yaliyojitokeza katika

uchambuzi na uhakiki wa vit-

uo vya kutolea huduma za afya.

Baadhi ya wajumbe wa timu ya SAM wakichambua nyaraka mbalimbali za halmashauri.

Mafunzo na uchambuzi ni hatua ya nne iliyowezesha timu kujifunza dhana ya SAM, haki na wajibu

wa mwananchi katika kushiriki uboreshaji na ufuatiliaji wa huduma za afya. Katika hatua hii, timu pia

ilifanya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali za Halmashauri na hatua hii ilidumu kwa takribani wiki mbili

kuanzia tarehe 12/08/2016.

Mjumbe wa timu ya SAM Mh. Jamila Gamaha akichangia hoja wakati wa kikao cha wadau wa afya.

Page 12: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

4

Hatua ya saba ni mkutano wa pili wa wadau wa afya ambao lengo lake ni kutoa mrejesho wa zoezi

zima na ulifanyika tarehe 19/09/2016 na baada ya mrejesho na majadiliano, makubaliano yalifikiwa.

Hatua ya mwisho katika mchakato huu wa SAM ni ufuatiliaji, uwajibikaji na utekelezaji wa makubaliano

yaliyoafikiwa katika kikao cha ndani na mkutano wa mrejesho kwa wadau. Kwa ufupi mchakato wa

zoezi la SAM unaonekana katika jedwali namba moja hapa chini.

Mjumbe wa timu ya SAM Bi. Salma Salum akiwasilisha ripoti ya

SAM kwa wadau wa afya.

Jedwali Na.1 Mchakato wa zoezi la SAM-Kondoa

Chanzo: Sikika 2017

Page 13: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

5

1.2. Muundo wa timu ya UUJ/SAM

Muundo wa timu ya UJJ/SAM kwa kila wilaya kwa shirika la Sikika ni wajumbe 15 tu wanaowakilisha

makundi mbalimbali kama yalivyoonyeshwa kwenye jedwali namba 2.

Jedwali Na 2. Uwakilishi wa wajumbe wa timu ya SAM Kondoa Mwaka 2016

1.3. Mafunzo ya nadharia na uchambuzi wa nyarakaMafunzo ya nadharia yalikwenda sambamba na uchambuzi wa nyaraka muhimu za idara ya afya na

Halmashauri, taarifa zilizochambuliwa zilikuwa ni za mwaka wa fedha 2014/2015. Nyaraka za Hal-

mashauri zilizochambuliwa na timu ni pamoja na mpango mkakati, mpango kabambe wa afya, taarifa

za utekelezaji wa shughuli za afya, taarifa za madiwani katika robo zote nne, mpango wa muda wa kati

na bajeti /MTEF, taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za UKIMWI, taarifa za mkaguzi wa ndani

na taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Katika kipengele hiki, mafunzo

na uchambuzi yalifanyika kwa kuzingatia hatua kuu tano za SAM kama ifuatavyo:

1.3.1. Mpango mkakati na mgawanyo wa rasilimali Katika hatua hii, timu ya SAM ilipata fursa ya kujifunza kwa kuangalia mpango mkakati wa wilaya, maa-

na, lengo na muundo wake, ushiriki wa wananchi na wadau wengine, tathmini ya mahitaji yaliyopita na

mahitaji ya sasa na jinsi mgawanyo wa rasilimali kwa vipaumbele unavyofanyika.

1.3.2. Usimamizi wa matumiziTimu ilifanya ulinganifu wa vipaumbele, mipango na matumizi katika sekta ya afya na kuangalia njia za

usimamizi, mifumo na vyombo mahususi katika usimamizi wa matumizi ya rasilimali. Pia, uchambuzi

ulilenga uzingatiaji wa miongozo, kanuni na sheria za ndani na za kimataifa za matumizi ya fedha za

umma.

Wananchi Madiwani

Watendajikata

Timu ya uende-shaji afya

Timu ya wat-alamu

wa Hal

mashauri

Kamati ya usi-mamizi wa shu-ghuli za

afya

Bodi ya afya

Asa-si za kiraia

JUMLA

Wananchi WAVIU Viongozi wa dini

Walemavu

2 1 1 1 1 1 1

4 1 1 1

7 2 1 1 1 1 1 1 15

Page 14: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

6

1.3.3. Usimamizi wa utendajiTimu ya SAM ilifanikiwa kufanya ulinganifu wa mipango na maazimio yaliyo katika nyaraka

mbalimbali na hali ya utekelezaji wake. Ilitembelea ofisi ya mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya

Kondoa Vijijini, Hospitali ya Wilaya, vituo vya afya na zahanati. Timu iliweza pia kufanya mahojiano

na watendaji/watoa huduma, watumia huduma na hata wananchi waliokuwa maeneo husika. Kwa

ujumla, timu ilifuatilia hali ya utendaji na utoaji huduma. Jedwali na 3 UK.4 linaonyesha mtiririko

wa ongezeko la vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2014/2015.

1.3.4. Usimamizi wa uadilifuTimu ilipata fursa ya kuchambua na kuangalia mifumo iliyowekwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na

miongozo kusimamia uadilifu kwa watoa huduma ili kuwafikishia wananchi wote huduma katika hali

ya usawa na haki. Pia iliangalia taarifa za vikao vya madiwani, mkaguzi wa ndani na Mdhibiti na

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Vyombohivi muhimu vilitoa maoni yao ambayo timu

iliangalia ni kwa namna gani yamezingatiwa na watoa huduma ili kuboresha matumizi ya fedha na

rasilimali za umma kwa ujumla wake. Lakini pia timu iliangalia nafasi ya jamii kushiriki katika kuandaa,

kufuatilia, kutoa taarifa na hata kuwawajibisha wale waliowapa dhamana ya kusimamia rasilimali zao.

1.3.5. Usimamizi wa uwajibikajiTimu ya SAM/UJJ Kondoa ilichambua taarifa za vikao vya madiwani, mkaguzi wa ndani wa

Halmashauri na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kuona jinsi vyombo

hivyo vilivyoshauri juu ya matumizi ya fedha za umma katika kutekeleza shughuli mbalimbali.

1.4. Maeneo yaliyotembelewa na timu ya SAMKwa lengo la kuelewa utekelezaji wa shughuli za afya kama zilivyoainishwa kwenye nyaraka mbalimbali

zilizochambuliwa, timu ya SAM-2016 ilitembelea vituo vya kutolea huduma za afya 24 ikiwemo Hospitali

ya Wilaya ya Kondoa, vituo vya afya vitatu (Kisese, Busi na Mnenia) na zahanati 20 ambazo ni Kikilo,

Bumbuta, Masawi, Kinyasi, Kwadelo, Bolisa, Sakami, Makirinya, Hebi, Haubi, Baura, Humai, Kiteo, Bereko,

Salanka, Thawi, Mongoroma, Kikore, Mkekena, na Masange. Vilevile, timu ilitembelea maeneo ya ujenzi

wa vituo 13 vya kutolea huduma za afya kama inavyoonekana kwenye kiambatanisho namba 1 UK. 27.

Jedwali Na 03: Mtiririko wa vyanzo vya mapato vya Halmashauri ya Kondoa kwa miaka mitatu

Mwaka wa Fedha

Makadirio yaliyo-pitishwa (Sh)

Makusanyo halisi (Sh) Tofauti (Sh) Asilimia

2014/2015 1,291,628,980 1,583,009,234 291,380,254 23 (ongezeko)

2013/2014 977,604,366 893,774,669. (83,829,697) 9 (pungufu)

2012/2013 1,638,834,132 1,116,881,676 (521,952,456) 32 (pungufu)

2011/2012 2,022,367,000 1,350,924,755 (671,422,245) 33 (pungufu)

Chanzo. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (2014/2015)

Page 15: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

7

Sehemu ya Pili 2.0 Matokeo

2.1 Matokeo ya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali2.1.1.Mpango mkakati wa Halmashauri 2012-17 na mpango kabambe 2014/15Katika hatua hii, timu ya SAM iliangalia kwa kina mpango mkakati wa Halmashauri na mpango kabam-

be wa afya kwa lengo la kuelewa vipaumbele vyake Halmashauri na mikakati iliyoko katika kutekeleza.

Uchambuzi wa mipango hii ulibainisha mambo kadhaa yaliyochochea mjadala mpana ulioibua mambo

mbalimbali yakiwemo:

• Ushirikishwaji wa jamii na wadau mbalimbali katika uandaaji wake na orodha ya washiriki iliambat-

anishwa kwenye mpango.

• Ulieleza mafanikio na changamoto za mpango mkakati uliopita.

• Katika uchambuzi huo, ilibainika kuwa katika uandaaji wa vipaumbele, elimu na afya zilipewa na-

fasi kubwa japo suala la kilimo kwanza lilipewa msukumo mkubwa na rasilimali zaidi hivyo kuathiri

elimu na afya.

Pamoja na mkakati huo kuandaliwa vizuri, yapo maeneo machache yaliyokuwa na

changamoto:

• Mpango haukubainisha kwa kina mbinu na mikakati endelevu ya kuzikabili changamoto zilizoain-

ishwa kama vile mdororo wa kilimo kutokana na ukame, upungufu wa rasilimali watu katika kutoa

huduma, miundombinu hafifu, na ukusanyaji mdogo sana wa mapato ya ndani.

• Pia, kulikuwa na baadhi ya taarifa ambazo hazihusiani na Wilaya ya Kondoa. Inawezekana baada

ya kuandaliwa, mpango haukupitiwa vyema kuhakikisha unakuwa na taarifa sahihi. Kwa mfano,

ukurasa (UK.) 11 wa mpango mkakati unaonyesha kuwa maambukizi ya VVU/UKIMWI katika

wilaya ni asilimia 5.8 na yanachangiwa na hali ya biashara hasa kahawa na madini. Wakati katika

kurasa za 28 na 30 zinaonyesha kupunguza kwa maambukizi kutoka asilimia 1.9 hadi asilimia

moja . Vilevile, zao kuu la biashara katika Wilaya ya Kondoa sio kahawa na wala hakuna madini

kwa kiasi hicho.

Maoni ya TimuKwanza, timu ilitoa pongezi kwa ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika kuanda mpango mkakati

wa halmashauri.

• Pili, ilishauri Halmashauri kuwa ni vyema kuainisha bayana namna ya kukabiliana na changamoto

za afya zilizoko hali itakayosaidia kuboresha sekta ya afya na hata nyingine.

• Pia walishauri kwamba wakati mpango mkakati huu unaishia 2016/2017, ni vyema maandalizi ya

mpango mkakati mwingine yaanze mapema ili kuepuka changamoto ya Halmashauri kukaa kwa

muda mrefu bila ya kuwa na mpango mkakati kama iliyotokea katika huu unaoishia.

• Mwisho, ni vyema mkakati au mpango mwingine wowote unapoandaliwa uwe unapitiwa kwa uan-

galifu ili kuepusha taarifa zisizo kuwa sahihi na zinazoweza kupotosha.

Page 16: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

8

Majibu ya Menejimenti• Ushauri umepokewa na utafanyiwa kazi katika kuandaa mipango inayokuja.

2.1.2 Usimamizi wa matumiziTimu ilifanya ulinganifu wa vipaumbele, mipango na matumizi katika sekta ya afya na kuangalia njia za

usimamizi, mifumo na vyombo mahususi katika usimamizi wa matumizi ya rasilimali. Pia, uchambuzi

ulilenga uzingatiaji wa miongozo, kanuni na sheria za ndani na za kimataifa za matumizi ya fedha za

umma. Vilevile, wakati wa uhakiki vituoni, timu ilihitaji kupata ufafanuzi juu ya hili na mambo yafuatayo

yalionekana:

• Pongezi: Kwenye vituo vyote vilivyotembelewa, kulikuwa na kamati za usimamizi wa vituo vya afya

hata hivyo, kulikuwa na changamoto katika kamati za usimamizi wa vituo (zahanati na vituo vya

afya) ya kutokujua kanuni na miongozo ya usimamizi wa mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya

fedha za vituo vya kutolea huduma za afya hivyo kushindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo. Kati-

ka vituo 22 (zahanati na vituo vya afya) vinavyofanyakazi ni kimoja pekee ambacho kamati yake

ilipata mafunzo kuhusu wajibu wao na usimamizi wa vituo ikiwemo rasilimali fedha. Katika vituo

vingine 19, kamati hazijawahi kupata mafunzo na katika vituo viwili hakukuwa na taarifa.

• Changamoto ya mifumo hii ya usimamizi katika ngazi ya Halmashauri imechangia kupotea kwa

fedha au kutoonekana kwa madokezo, vocha zilizoombea fedha na taarifa za utekelezaji wa kazi

husika. Zaidi ya shilingi 180 milioni za Halmashauri zikiwemo fedha za idara ya afya ziliibuliwa na

ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na suala hili lilikuwa mahakamani na kesi

ilikuwa katika hatua za uchunguzi.

Maoni ya timu• Timu Iliishauri Halmashauri kuwa, ni vyema kamati za afya zinapochaguliwa zipate mafunzo ya

wajibu wao na hususani usimamizi wa fedha.

• Timu ilitoa pongezi kwa mganga wa Kituo cha Afya cha Busi ambaye alitoa mafunzo kwa kamati

mara baada ya kuchaguliwa na kushauri vituo vingine kuiga mfano huo. Inapendekezwa kwamba

waganga wafawidhi wa vituo waige mfano wa mganga mfawidhi wa Kituo cha Afya Busi alyetenga

muda wake kuipatia mafunzo timu ya usimamizi kuhusu majukumu yao.

Majibu ya menejimenti• Ushauri wa kamati za afya kupata mafunzo umepokewa na utafanyiwa kazi.

• Suala la upotevu wa fedha za afya liko katika vyombo vya sheria hivyo si utaratibu kulijadili kabla

ya uchunguzi na mahakama kukamilika.

2.1.3 Watoa hudumaTimu ya SAM ilifanikiwa kufanya ulinganifu wa mipango na maazimio yaliyo katika nyaraka mbalimbali

na hali ya utekelezaji wake. Vilevile, ilitembelea ofisi ya mganga mkuu wa wilaya, Hospitali ya Wilaya,

vituo vya afya na zahanati na kufanya mahojiano na watendaji/watoa huduma, watumia huduma na

hata wananchi waliokuwa maeneo husika, kwa ujumla timu ilifuatilia hali ya utendaji na utoaji huduma.

Page 17: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

9

Yaliyojitokeza ni kama ifuatavyo;

• Halmashauri hususani idara ya afya chini ya Mganga Mkuu wa Wilaya Dk. Zulkanine walifanya

jitihada za dhati kuhakikisha changamoto ya uhaba wa watumishi wa afya inapungua kama ina-

vyoonekana katika jedwali namba 5. Wakati wa zoezi la SAM mwaka 2012, uhaba wa watumishi

sekta ya afya ulikuwa karibu asilimia 71 na ulipungua hadi kufikia asilimia 45 Desemba 2015 kama

inavyoonekana katika jedwali namba 6.

Jedwali Na. 4 Mwenendo wa ongezeko la idadi ya watumishi wa afya Halmashauri ya Kondoa Vijijini

Chanzo: Ofisi ya Mganga Mkuu Wilaya ya Kondoa.

Maoni ya timu• Kwanza, timu ilitoa pongezi kwa jitihada za kuhakikisha watumishi wa afya wanapatikana katika

vituo vya afya kulingana na mahitaji.

• Pili, iliishauri Halmashauri kuwa bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa asilimia

45 wa mahitaji, hali inayosababisha vituo vya kutolea huduma kuwa na watumishi wasiotosheleza

mahitaji na kuchangia kuzorotesha huduma za afya hususani maeneo ya vijijini. Hivyo mikakati ya

kuongoza watumishi iendelee.

Majibu ya Menejimenti• Timu ya Uendeshaji wa Shughuli za Afya (CHMT) iliitaarifu timu ya SAM kuwa inao mpango in-

aoutekeleza ili kuhakikisha uhaba huo unaondoka. Kwa mfano, mwaka 2014/15 walipata kibali

cha kuajiri watumishi 177 hata hivyo, kwa mwaka 2015/16 Serikali ilipositisha ajira, mpango huo

ulisimama mpaka kibali cha kuajiri kitakapotolewa tena.

2.1.4 Gharama za mitungi ya gesi• Timu ilibaini taarifa zisizoeleweka juu ya gharama za ununuzi na ujazaji wa mitungi ya gesi kwa ajili

ya huduma za mnyororo baridi. Katika mpango kabambe UK. (19) imeelezwa kuwa mitungi 260

Jedwali Na.5 Hali ya jumla ya watumishi hadi Desemba 2015

Mahitaji (Kada zote) Watumishi waliopo

upungufu

Idadi Asilimia (%) Idadi Asilimia (%)

715 393 55 322 45

Page 18: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

10

ya gesi ilipangwa kujazwa kwa chanzo cha fedha kutoka mfuko wa pamoja (HSBF) kwa gharama

ya TSh. 23,399,997 hata hivyo, taarifa ya utekelezaji wa shughuli za afya UK. (70) 02 (C02S)- in-

aonyesha kuwa ni mitungi 64 tu ndiyo iliyojazwa kwa gharama hiyo, ikiwa na maana kuwa mtungi

mmoja kujazwa kwa shilingi 365,624/= jambo ambalo liliitia shaka timu.

Majibu ya menejimenti• Timu ya Uendeshaji wa Shughuli za Afya (CHMT) ilikiri kuwa taarifa ya utekelezaji ina upungufu

na kutoa uthibitisho/viambatanisho mbalimbali vya ununuzi kutoka kitengo husika. Viambatanisho

hivyo vilionyesha kuwa idadi ya mitungi iliyojazwa gesi (LPG) kwa mwaka huo 2014/15 ni 272 am-

bayo ni wastani wa mitungi 68 kwa kila robo na kusambazwa mitungi miwili kwa kila kituo.

Maoni ya Timu• Ni vyema uhakiki wa ripoti za utekelezaji ukafanyika kwa umakini kabla ya kutolewa ili kuwa na

ripoti sahihi.

• Timu iliridhishwa na majibu ya menejimenti kwa kutoa vielelezo na pia ilipotembelea vituo vya ku-

tolea huduma, vyote vilionekana kuwa na huduma hai ya mnyororo baridi kwa kupata mitungi ya

gesi kwa wakati kila robo mwaka. Timu iliipongeza menejimenti kwa hilo.

2.1.5 Gharama za umeme za Hospitali ya Wilaya• Katika shughuli za kiutawala na huduma za kawaida kama umeme na maji, mpango ulionyesha ku-

panga kutumia chanzo cha fedha za HSBF kiasi cha Sh. 44,284,100 kama ilivyoonekana kwenye

shughuli Na.C04S01CCHP, UK. (49/50). Hata hivyo, kutoka chanzo hicho fedha iliyotolewa 0/=.

Vilevile, katika ripoti ya utekelezaji UK (29) matumizi yanaonekana ni kiasi cha Sh. 12,873,100.

Timu ilihitaji kujua; Je, fedha iliyotumika ilitoka katika chanzo kipi?

Majibu ya menejimenti• Ni jambo lisilopingika kuwa bili za maji, umeme, chakula cha wagonjwa zilikuwa zikilipwa kwa fed-

ha za OC kwa miaka hiyo ambayo OC ilikuwa inakuja. Kiasi kilichopokewa kilipaswa kuandikwa

lakini kwa makosa ya kibinadamu sehemu hiyo ilisahaulika.

Maoni ya timu• Pamoja na majibu ya menejimenti, timu ya SAM haikuridhika na iliiomba menejimenti kutoa uth-

ibitisho ambao haukupatikana kwa wakati. Timu iliishauri menejimenti kuwa ni vyema kuhakiki

taarifa na kuweka vithibitisho vinavyohitajika kwa ajili ya uwazi na uwajibikaji.

2.1.6 Dawa na vifaa tiba• Timu ilihitaji kujiridhisha juu ya ununuzi wa dawa na vifaa kama ilivyoainishwa kwenye mpango ka-

bambe, shughuli Na 01 (CO1S) UK (XIII na 55) na taarifa za utekelezaji UK. 09. Taarifa zilionesha

kuwa, ununuzi wa dawa, vifaa vya maabara hadi kufikia Juni 2015, kilikuwa kutoka chanzo cha

fedha za mfuko wa pamoja (Basket Fund). Fedha zilizopokewa kutoka chanzo hicho ni kiasi cha

Sh 73,573,197/= na kilichotumika 73,322,953/=. Mchanganuo wake ulikuwa; Dawa- 45,832,833/=,

Page 19: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

11

vifaa vya meno (dental) 5,499,940/= Vifaa tiba 9,166,566/= Vifaa vya maabara 7,333,253/= na

Vifaa 5,499,940/=.

• Vilevile, katika mpango kabambe UK. wa 70 na ripoti ya utekelezaji UK. wa 13 zinaonyesha kuwa

fedha zilitengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa kwa zahanati. Fedha zilizopitishwa kutoka Mfuko

wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kiasi cha Sh. 61,415,995/= zilizopokewa ni Sh. 58,357,387/= na

zilizotumika ni Sh. 47,327,179/= na zilizobaki ni Sh. 11,030,208/=

Majibu ya menejimenti• Ofisi ya mfamasia iliwasilisha nyaraka za ununuzi na kuthibitiswa na wajumbe, pamo-

ja na maelezo ya ziada juu ya utaratibu unaofuatwa kuagiza dawa. Dawa hununuliwa bila ku-

jali cost centre (central procurement) kisha zahanati na vituo vya afya na Hospitali ya Wilaya

hugawiwa kulingana na mahitaji yao. Hivyo ukitaka upatiwe ushahidi wa ununuzi wa dawa

kwa hospitali pekee au zahanati hutapata badala yake ushahidi pekee uliopo ni gharama

ya jumla iliyotumika kununulia dawa. Katika mwaka wa fedha 2014/2015, utekelezaji wa un-

unuzi wa dawa ulikuwa asilimia 93.16 na umechangia kuongezeka kwa dawa vituoni. Hii in-

atokana na kuongezeka kwa mapato ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, papo kwa papo na

Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kama inavyoonekana kwenye jedwali Na. 6 na 7. UK. 10.

• Pamoja na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), kuongeza mapato na namba ya kaya zilizoandikishwa,

bado haujawa chanzo cha kutosheleza mahitaji. Kwa mujibu mratibu wa CHF Wilaya ya Kondoa,

kuanzia Julai 2014 hadi Juni 2015, kumekuwa na ongezeko la kaya kwa asilimia 18 kutoka mwa-

ka 2014 mpaka 2015, idadi ya kaya katika Halmashuri kwa mwaka 2014-2015 ni kaya 54,189.

Jedwali na. 6 UK. 10 linaonyesha mwenendo wa ongezeko la kaya na mapato kwa miaka miwili

ambalo limechangia kwa kiasi katika ununuzi wa dawa na vifaa tiba. Ongezeko hili lilitokana na

kuandikishwa kaya zenye hali duni zilizopo kwenye programu ya TASAF III.

Jedwali Na 6: Mwenendo wa mapato ya papo kwa papo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya

Chanzo: Ofisi ya Mganga Mkuu (W) Kondoa, Septemba 2016

Page 20: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

12

Jedwali na. 7 Mwenendo wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)

Maoni ya timu• Timu ilitoa pongezi kwa menejimenti kuhakikisha upatikanaji wa dawa unaongezeka hali ili-

yoonekana kwenye vituo vingi vilivyotembelewa.

• Dawa zikiwa zimehifadhiwa juu ya kitanda katika Zahanati ya Mkekena kutokana na upungufu wa

samani.

• Halmashauri iendelee kuboresha mikakati ya kushawishi kaya kujiunga na CHF ili kuboresha

huduma za afya.

2.1.7 Ukarabati wa wodi - hospitali• Mpango Kabambe UK. wa 61, ulionesha shughuli ya kukarabati wodi moja kwa kutumia fedha za

papo kwa papo na fedha zilizotengwa ni 10,000,000/=. Shughuli hiyo katika ripoti ya utekelezaji

ukurasa wa 39 imeonesha kuwa ukarabati umekamilika kwa asilimia 50 huku kukiwa hakuna fedha

zilizotumika japokuwa kiasi cha 3,000,000/= kimeonekana kupokelewa na kolamu ya bakaa usalia

na 3,000,000/=. Timu ya SAM ilipenda kupata ufafanuzi wa utekelezaji wa ujenzi huo wa wodi hasa

baada ya kutembelea ujenzi na kuona ukarabati umefanyika kwa kiwango kikubwa zaidi.

Majibu ya menejimenti• Idara imetekeleza kazi mbili katika Hospitali ya Wilaya. Ukarabati na upanuzi wa jengo la upasuaji

na pia ukarabati wa wodi namba 6. Gharama za jumla za ukarabati huo ni 49,954,600/= na ume-

kamilika na mkandarasi tayari amelipwa fedha zake zote. Vielelezo vya malipo vilionyeshwa. Kwa

mwaka huo wa 2014/15, hakuna malipo yaliyofanyika kwa kuwa mkandarasi hakuwa ameomba

malipo ndio maana kwenye ripoti ya utekelezaji inaonyesha kukamilika kwa asilimia 50 na hakuna

malipo yaliyofanyika.

Maoni ya timu• Timu ilitoa pongezi kwa menejimenti kukarabati wodi na kufanya upanuzi wa jengo la upasuaji na

Page 21: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

13

kushauri iwapo ripoti ya utekelezaji inaweza kutoa ufafanuzi pale ambapo utekelezaji umefanyika

au kutofanyika na sababu zake ili kuwawezesha watumiaji wa ripoti kuelewa vizuri.

2.1.8 Marekebisho ya mfumo wa maji - hospitali• UK. 59 wa mpango kabambe unaonyesha kuwa 16,000,000/= zilitengwa kutoka fedha za LGDG

kwa ajili ya kurekebisha mfumo wa maji katika Hospitali ya Wilaya. Hata hivyo, ripoti ya utekelezaji

haionyeshi kutekelezwa kwa mpango huo (UK.27). Timu ilipenda kujua iwapo ukarabati ulifanyika

na mfumo wa maji uko katika hali gani kwa sasa?

Majibu ya menejimenti• Ni kweli jumla ya Sh 16,000,000 zilitengwa kutoka chanzo cha LGDG kwa ajili ya ukarabati wa

mfumo wa majisafi katika Hospitali ya Wilaya, lakini fedha hizo hazikupokewa. Hata hivyo, kupitia

ongezeko la makusanyo ya fedha za uchangiaji huduma za afya, marekebisho yalifanyika baa-

daye kwa kujenga kisima cha ardhini chenye ujazo wa lita 70,000 na kuweka simtank za ujazo wa

lita 10,000 na pumpu ya kupandisha maji kwenye simtank ili kuhakikisha maji yanapatikana katika

wodi zote na kwenye mabafu. Gharama za ujenzi wa mfumo huo wa maji ni Sh 14, 451,000 na

ukarabati huo upo hatua za mwisho.

Maoni ya timu• Timu ilitoa pongezi kwa menejimenti kwa ukarabati huo na kama ilivyoshauri katika maeneo

mengine, ni vyema ripoti ziwe na maelezo ya kutosha ili kuepuka na maswali mengi kwa wadau

kila mara wanaposoma ripoti ambayo maswali hayo yapo ndani ya uwezo wao.

2.1.9 Ukarabati wa choo cha nje - hospitali• Timu ilipenda kupata ufafanuzi wa ukarabati wa choo kama ilivyoainishwa kwenye mpango ka-

bambe UK wa 59 na katika ripoti ya utekelezaji UK wa 28. Kwa kutumia 8,000,000/= za LGDG

kazi hiyo inatarajiwa kufanyika lini? Je, choo kiko katika hali gani kwa sasa?

Majibu ya menejimenti• Fedha hazikupokewa na ukarabati huo haujafanyika. Ni mategemo yetu kuwa utafanyika kwa

fedha za uchangiaji katika mwaka huu wa fedha 2016/2017 kwa kuwa tumeongeza makusanyo ya

Papo kwa papo kutoka wastani wa 4,294,042/= kwa mwezi mwaka 2013 hadi 8,285,441/= kwa

mwezi mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilimia 93. Aidha, katika kipindi hicho mapato ya NHIF

pia yameongezeka kwa asilimia 64.5.

Maoni ya timu• Timu iliishauri menejimenti kuupa ukarabati huo kipaumbele kwa kuwa choo hicho ni muhimu na

kinatumiwa na wagonjwa wa nje na wanaowasaidia au kuwatembelea.

Majibu ya menejimenti• Ushauri umepokewa na kuzingatiwa

Page 22: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

14

2.1.10 Vifaa vya kujifungulia - hospitali• Timu ilipenda kupata ufafanuzi wa upatikanaji wa vifaa vya kujifungulia kwa kuwa pamoja kuwa na

bajeti fedha haikutumika na vifaa vilipatikana kama inavyoonekana kwenye mpango kabambe UK.

56 na ripoti ya utekelezaji UK. 16

Majibu ya menejimenti• Vifaa hivyo vilipatikana bila gharama kupitia ufadhili wa mradi wa Harvard School of Public Health

uliokuwa na lengo la kupunguza vifo vya wajawazito na watoto. Hivyo MSD walikuwa wakizipatia

Halmashauri delivery packs na bajeti hiyo iliwekwa kama buffer tu endapo hakutakuwa na ufadhili.

Vielelezo vya kupokea vifaa hivyo ulitolewa kwa timu.

2.1.11 Mafunzo ya watoa huduma• Mpango kabambe UK. 57 unaonyesha kupangwa kwa mafunzo ya watoa huduma 18, wauguzi

15 na tabibu watatu kwa kutumia fedha za CHF kwa kiasi cha Sh. 4,310,000. Wakati ripoti ya

utekelezaji UK. 16 inaonyesha kuwa ni watoa huduma 18 pekee waliopata mafunzo huku mafani-

kio yakiwa asilimia 100. Timu ilipenda kupata ufafanuzi.

Majibu ya menejimenti• Katika kumbukumbu zetu mafunzo haya hayakufanyika. Labda kama yalifanyika kupitia chanzo

kingine cha fedha. Hata katika ripoti ya kitabu hakuna fedha iliyopokewa wala iliyotumika. Uweze-

kano ni kuwa huenda chanzo hiki kimewekwa kutokana na ufinyu wa bajeti ili kitabu kiweze kui-

dhinishwa tu.

Maoni ya timu• Timu inashauri kuwa ni vyema ripoti za utekelezaji zikawa na taarifa sahihi pia kuhaririwa na wa-

husika mbalimbali ili kuhakikisha kuwa ripoti ya mwisho haina makosa mengi ya kiuandishi.

2.1.12 Ununuzi wa vifaa vya kupima uzito na urefu• Timu ilipenda kujua kwa vipi shughuli hii ilikamilika kwa asilimia 100 wakati fedha zlizoidhinishwa

Sh. 5,600,000 kutoka CHF hazikupokewa kama inavyojieleza kwenye mpango kabambe UK 63 na

ripoti ya utekelezaji UK 18.

Majibu ya menejimenti• Ni kweli fedha hazikupokewa kutoka chanzo cha fedha za CHF hata hivyo, vifaa hivyo vilipatikana

kutoka kwa wafadhili walioletwa na TFNC na vilisambazwa kwa vituo husika. Kwa sasa ni ngumu

kuandika kwenye mfumo wa CCHP maelezo ya ziada. Hata hivyo, tutashauri kwa wanaohusika.

Maoni ya timu• Timu inashauri kuwa ni vyema ripoti za utekelezaji zikawa na taarifa ambazo zinakidhi na zisi-

zohitaji maelezo ya ziada nje ya ripoti.

Page 23: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

15

2.1.13 Malipo ya ziada kwa watumishi wa vituo vya afya• Timu ilipenda kupata ufafanuzi wa malipo ya muda wa ziada kwa watumishi kama ilivyoonekana

kwenye mpango kabambe UK 65 na ripoti ya utekelezaji UK wa 31. Taarifa inaonyesha kuwa fedha

zilizoidhinishwa ni Sh. 9,828,000 na zilizopokewa ni Sh. 7.800,000 na zilitumika zote. Timu iliomba

ufafanuzi kwa kuwa baadhi ya vituo viliyotembelewa havikuwa vimepokea malipo hayo.

Majibu ya menejimenti• Fedha hizi ni malipo baada ya saa za kazi (on call allowance) na zimekuwa zikitolewa kwa watumi-

shi wa vituo vyote kulingana na fedha zilivyopokewa na zililipwa kwa watumishi wote wa vituo vya

afya. Nakala za uthibitisho wa malipo zinaweza kuombwa kwa mkurugenzi.

Maoni ya Timu• Timu haikuweza kupata nakala kutokana na muda ila walishauri menejimenti kufuatilia baadhi ya

vituo ambavyo havikuwa vimepokea malipo hayo kama Kisese na Busi.

2.1.14 Jengo la Upasuaji Kituo cha Afya Busi• Timu ilipenda kupata ufafanuzi ni lini ujenzi wa jengo la upasuaji utakamilika kwa kuwa fedha

zilizoidhinishwa mwaka 2014/15 kiasi cha Sh. 46,170,000 (Mpango kabambe UK 67 na ripoti ya

utekelezaji UK 40) hazikutoka na timu ilipotembelea mwaka 2016, ujenzi ulikuwa haujaanza.

2.1.15 Jengo la Utawala Kituo cha Afya Kikilo• Timu ilipenda kujua mipango ya Halmashauri kuhusu ujenzi wa jengo la utawala ambalo fedha

ziliidhinishwa kwa ukamilishaji kiasi cha Sh. 35,000,000 kama inavyoonekana kwenye ripoti ya

utekelezaji UK. 39 na mpango kabambe UK 67, ujenzi bado haujaanza.

Majibu ya menejimenti• Halmashauri imekua na utaratibu wa kuhamasisha jamii kuchangia katika ujenzi wa miradi ya

maendeleo na Halmashauri kumalizia sehemu iliyobaki na kuweka vifaa, watumishi na mahitaji

mengine kupitia wadau mbalimbali. Katika vituo hivi vya afya Busi na Kikilo, wananchi hawajaanza

ujenzi ila uandaaji wa mipango kwa maelezo kutoka kwa wataalamu inaelekezwa miradi inayotaki-

wa kutengewa fedha ni ya ukamilishaji na si miradi mipya kama kuanza ujenzi. Hivyo ndio maana

katika kitabu cha mpango inasomeka ukamilishaji na wakati huo ujenzi haujaanza.

Maoni ya timu• Timu inaishauri menejimenti kushirikiana na viongozi wa wananchi kuhakikisha wanaelewa wajibu

wao katika kuchangia maendeleo ili fedha za ukamilishaji zikipatikana, basi ukamilishaji uweze

kufanyika. Vilevile, kuweka vyanzo mbadala vya kukamilisha ujenzi kwa kuwa kwa miaka karibu

mitatu Halmashauri haijapokea fedha hizo za maendeleo kutoka serikali kuu.

Page 24: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

16

2.1.16 Jengo la kina mama wajawazito (maternal ward) Thawi• Timu ilipenda kujua mipango ya Halmashauri kuhusu Ukamilishaji wa jengo la kina mama

ambalo ujenzi wake umesimama muda mrefu katika hatua ya lenta. Fedha zilizoidhinishwa kwa

ukamilishaji kiasi cha Sh 38,830,000 kama inavyoonekana kwenye ripoti ya utekelezaji UK. 39 na

mpango kabambe UK 67.

2.1.17 Jengo la Maabara Mnenia• Timu ilipenda kujua mipango ya Halmashauri kuhusu ukamilishaji wa jengo la maabara ambalo

ujenzi wake umesimama muda mrefu katika hatua ya madirisha kabla ya kufunga lenta. Fedha

zilizoidhinishwa kwa ukamilishaji kiasi cha Sh. 38,830,000 kama inavyoonekana kwenye ripoti ya

utekelezaji UK. 39 na mpango kabambe UK 67.

Jengo la Zahanati ya Thawi litakalotumika kwa ajili akinamama wajawazito,

ambalo ujenzi wake umesimama kwa mura mrefu.

Jengo la maabara katika Kituo cha Afya Mnenia ambalo ujenzi wake umesimama kwa muda mrefu sasa.

Page 25: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

17

Majibu ya menejimenti• Pamoja na nguvu ya wananchi kujenga mpaka kufikia kwenye hatua ya lenta katika vituo vya

afya vya Mnenia na Thawi, ni kweli kwamba ujenzi huo umesimama muda mrefu kwa kukosa

fedha za kumalizia. Halmashauri haikupokea fedha kipindi hicho na mpaka sasa haijapokea ili

kukamilisha ujenzi huo.

2.1.18 Ujenzi wa mashimo ya kutupia kondo za uzazi (placenta pits) kwa kutumia fedha za CHF• Mpango kabambe UK. wa 73, unaonyesha kuwa kiasi cha Sh. 6,000,000 kilitengwa kutoka CHF

kwa ajili ya ujenzi wa mashimo ya kutupia kondo za uzazi katika zahanati za Kiteo, Bumbuta na

Baura. Ripoti ya utekelezaji UK. wa 23 inaonyesha kuwa kiasi cha Sh. 2,000,000 kilipokewa na

Sh. 914,723 ndizo zilizotumika. Timu ilipenda kupata ufafanuzi wa hoja hii baada ya kukosekana

kwa mashimo katika zahanati hizo. Katika Zahanati ya Kiteo na Bumbuta, mashimo ya vyoo hutu-

mika kutupia na kusababisha harufu kali wakati Zahanati ya Baura hutupa kwenye “septic tanks’

mashimo ya maji machafu.

2.1.19 Ujenzi wa mashimo ya kutupia kondo za uzazi kutumia fedha za Mfuko wa Afya wa Pamoja (HSBF)• Mpango kabambe UK. wa 80, unaonyesha kuwa kiasi cha Sh. 8,732,450 kilitengwa kutoka HSBF

kwa ajili ya ujenzi wa mashimo ya kutupia kondo za uzazi katika zahanati za Bolisa, Baura, Mkek-

ena, Bukulu, Hebi na Bumbuta. Hata hivyo, Ripoti ya utekelezaji UK. wa 23 inaonyesha kuwa

fedha hazikufika hivyo ujenzi haukufanyika. Pia timu ilipotembelea vituo vyote isipokuwa Bukulu,

hakukuwa na mashimo na ilielezwa kuwa watoa huduma hutupa kwenye vyoo, mashimo ya maji

machafu ‘septic tanks’ na wakati mwingine kuwafungia kina mama kwenda kutupa nyumbani, hali

ambayo inaweza kusambabisha maambukizi yanayoweza kuzuilika iwapo kunakuwa na mashimo

maalaumu.

Majibu ya menejimenti• Ujenzi huu ulitakiwa kutekelezwa katika ngazi ya kituo cha huduma kutokana na fedha za papo

kwa papo. Hata hivyo, vituo hivyo havikuwa na makusanyo ya kutosha hivyo kushindwa kutekeleza

shughuli hiyo. Kuhusu fedha zilizotumika, hatuna rekodi hiyo pengine ni katika vocha zenye utata.

• Kwa ujenzi uliohitaji fedha za HSBF ni kwamba hazikutoka na Halmashauri haikuwa na fedha za

ndani kuweza kujenga mashimo katika zahanati hizo.

Maoni ya timu• Ni vyema Halmashauri ikatafuta vyanzo vingine vya fedha kuhakikiksha mashimo ya kutupia

kondo za uzazi yanakuwapo katika kila kituo cha kutolea huduma za afya.

Page 26: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

18

2.1.20 Zoezi la ukaguzi wa dawa na mafunzo ya mfumo mpya wa dawa (ILS)• Fedha zilizopitishwa ni Sh.4,130,000, zilizopokewa ni Sh. 4,372,500, zilizotumika ni Sh. 4,130,000

na zilizobaki ni 242,500. Timu inapenda kujiridhisha utekelezaji wa zoezi hili katika zahanati 32 na

ni kwa nini zahanati nane hazikufanyiwa zoezi hili kama ilivyopangwa? Vilevile, timu ilipotembelea

vituo vya huduma hakukuwa na taarifa kutoka kwa walengwa juu mafunzo yaliyofanyika kwa ajili

ya mfumo wa uagizaji na utoaji wa dawa.

Majibu ya menejimenti• Shughuli hii ilifanyika na taarifa inapatikana. Hata hivyo, kilichofanyika si mafunzo, bali ni kuwajen-

gea uwezo mahala pa kazi (coaching) wakati wa “supervision” na siyo mafunzo kama ilivyoeleweka.

2.1.21 Motisha kwa watoa huduma za afya 60• Timu ilipenda kujua watoa huduma waliopata motisha kama ilivyopangwa kwenye UK wa 71 wa

mpango kabambe na ripoti ya utekelezaji UK wa 19 ambako ilielezwa kuwa kiasi cha Sh. 3,360,000

kilitumika. Hii ilitokana na zahanati zilizotembelewa kuelezwa kwamba hazikuwa zimepokea moti-

sha isipokuwa Zahanati ya Bolisa ni mtu mmoja tu aliyekuwa amepokea.

Majibu ya menejimenti• Sehemu ya fedha hizi zilitumika kuwalipa watumishi sita wakati wa Mei Mosi. Hata huyo wa Boli-

sa alilipwa kutokana na ufanyakazi bora. Pia, watumishi wote wa wodi namba 2 walilipwa malipo

ya motisha kwa kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kutumia fedha hizo.

Maoni ya Timu• Timu inashauri kuwa ni vyema ripoti za utekelezaji zikawa na taarifa ambayo inakidhi, isiyohitaji

maelezo ya ziada nje ya ripoti.

2.1.22 Usimamizi na ufuatiliaji wa huduma za Afya• Mpango kabambe UK. wa 64, unaonyesha kuwa fedha kiasi cha Sh. 2,145,00 zilitengwa kutoka

CHF kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji katika vituo vya huduma. Lakini katika ripoti ya utekelezaji

UK. wa 24, hakuna fedha iliyopokewa ila shughuli imefanyika kwa asilimia 100. Timu ilipenda kujua

shughuli hii ilifanyika kwa kutumia fedha kutoka kifungu gani? Pia kuna marudio ya shughuli hii

kwenye Na. 2,3 na 4 ya mpango kabambe UK wa 64.

Majibu ya menejimenti• Shughuli hii haikupokea fedha kama ilivyoonyeshwa katika ripoti. Hata hivyo, kazi hii iliunganishwa

(integrarted) na kazi za kawaida za usimamizi elekezi (supportive supervision) unaofanyika kila

mwezi ambao ulitengewa fedha katika bajeti ya HSBF.

• Kujirudia kwa kwa shughuli katika maeneo tajwa ni kasoro za kiuandishi ambazo zitazingatiwa

katika taarifa na ripoti za mbeleni.

Page 27: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

19

2.1.23 Ukarabati wa choo Zahanati ya Bolisa• Mpango kabambe UK. wa 75 unaonyesha kuwapo kwa mpango wa kukarabati choo

katika Zahanati ya Bolisa kwa kiasi cha 4,000,000/= kupitia HSBF. Timu ingependa

kujua kwa nini ukarabati huo haukufanyika wakati kulikuwa na bakaa ya kiasi cha Sh. 4,000,000/=?

Ujenzi wa choo kipya cha Zanahati ya Bolisa, pembeni yake ni hali ya choo kinachotumika.

Majibu ya menejimenti• Choo hakikukarabatiwa kwa sababu fedha hazikufika kwa wakati ndio maana kumekuwa na bakaa

kwa kiasi hicho cha fedha.

2.1.23 Vocha za mawasiliano kwa vituo vya huduma 36• Mpango kabambe UK. wa 75 unaonyesha mpango wa kununua vocha kwa ajili ya mawasiliano

kwa zahanati 36 kwa kutumia fedha za HSBF kwa kiasi cha Sh. Sh 3,600,000. Lakini licha ya ripoti

ya utekelezaji UK wa 36 kuonyesha kupokewa kwa kiasi cha Sh. 5,500,885 kwa ajili ya ununuzi

huo, vituo havikupata vocha na kulikuwa na bakaa kiasi cha Sh. 5,500,885. Timu ilipenda kujua

kwa nini vocha hazikununuliwa wakati fedha zilikuwapo tena zaidi ya zilizoidhinishwa?

Majibu ya menejimenti• Vocha hazikununuliwa mwaka huo 2014/15 kwa sababu fedha hazikufika kwa wakati. Ila kila kituo

kimepokea kiasi cha Sh. 60,000 kwa mwaka 2016 na tayari zimetumwa na kupokewa.

Page 28: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

20

2.1.24 Ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi Baura• UK. wa 76 wa CCHP unaonyesha kwamba kiasi cha Sh. 16,000,000 kutoka MMAM kilitengwa ili

kumalizia ujenzi wa nyumba ya mtumishi ulioanza mwaka 2012/13 na kupauliwa mwaka huohuo.

Hata hivyo, katika ripoti ya utekelezaji UK wa 36, inaonyesha kuwa bado jengo halijakamilika. Timu

inapenda kujua nini mipango ya Halmashauri kuhakikisha ujenzi huo unakamilika? Nyumba ya

mtumishi katika Zahanati ya Baura ambayo bado haijamaliza kujengwa.

Majibu ya menejimenti• Ujenzi huo umesimama kwa muda kwa sababu hatukupokea fedha kama ilivyotarajiwa kwa miaka

miwili mfululizo, 2014/15 na 2015/16. Bado Halmashauri inajipanga kuona ujenzi huo na wa ma-

jengo mengine unamalizika.

• 2.1.25 Ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati za Kalamba, Kwamafunchi, Mitati, Kinyasi (jengo jipya) Choka, Masange (jengo jipya), Mulua, Salale, Mwisanga na Berabera

• Timu ya SAM ilipenda kujua sababu za kutenga fedha za kumalizia majengo ya zahanati wakati

ujenzi wa majengo hayo haujaanza. UK wa 76-78 wa CCHP unaonyesha kuwa fedha ziliteng-

wa kwa ajili ya umaliziaji wa majengo tajwa hapo juu kutoka vyanzo mbalimbali kama MMAM

na LGDG. Vilevile, ripoti ya utekelezaji kuanzia UK wa 40-42 inaonyesha kuwa fedha hizi hazi-

kupokewa hivyo timu ya SAM ilipenda kujua mipango ya Halmashauri katika kuhakikisha ujenzi

wa zahanati hizo unakamilika kwa kuwa baadhi ya maeneo yaliyotembelewa wananchi walikuwa

wameandaa vifaa kama vile mabati, mawe na matofali. Pia, katika baadhi ya maeneo kwa mfano,

Mwisanga baadhi ya vifaa kama matofali yalikuwa yameshaharibika.

Wajumbe wa timu ya SAM wakikagua eneo ambalo Zahanati ya Mulua ilitakiwa kuwa imeshaanza kujengwa.

Page 29: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

21

Majibu ya menejimenti• Halmashauri imekua na utaratibu wa kuhamasisha jamii kuchangia katika ujenzi wa miradi ya

maendeleo hadi kufikia hatua ya lenta na yenyewe kumalizia kupitia wadau mbalimbali. Uandaaji

wa mipango kwa maelezo kutoka kwa wataalamu ni kuwa, miradi inayotakiwa kutengewa fedha ni

ya ukamilishaji na si mipya. Hii ndio sababu ya CCHP kutenga fedha za ukamilishaji, kukamilika

kwa ujenzi kutategemea kujitoa kwa wananchi hao.

• Vilevile, fedha za ukamilishaji wa majengo hazijapokewa kwa takribani miaka mitatu hivyo zitaka-

popatikana zitahakikisha ujenzi wa zahanati hizo unatekelezwa.

Maoni ya timu• Timu inashauri kuwa ni vyema Halmashauri ikawawezesha watendaji na viongozi wa kata na vijiji

kuelewa wajibu wao hasa kwenye suala la ujenzi ili nao wawawezeshe wananchi kutekeleza wa-

jibu wao kwa wakati kwa sababu baadhi ya maeneo, ujenzi wa msingi (foundation) ulianza muda

mrefu kiasi kwamba unaweza kuwa umeshachakaa kwa mfano, Mwisange (2007) na Masange

(2003).

2.1.26 Ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati za Gaara, Mafui, Makirinya na Humai • Timu ya SAM ilipenda kujua mipango ya Halmashauri kuhakikisha ujenzi wa zahanati hizo unaka-

milika kwa kuwa fedha za kukamilisha hazikupokewa na wananchi wamejenga hadi ngazi ya lenta.

Taarifa ya CCHP UK 76-78 na ripoti ya utekelezaji UK wa 40-42, zinaonyesha mipango ya ujenzi

kutotekelezeka kutokana na fedha kutopokewa. Vilevile, timu ilipenda kuifahamisha manejimenti

kuwa jengo la nyumba ya mtumishi Makirinya limechakaa kutokana na kukaa muda mrefu bila

kukamilika na ni vigumu kumalizia ujenzi kwa hali lililonayo.

Majibu ya menejimenti• Kama ilivyoelezwa hapo awali kuwa ni utaratibu wa Halmashauri kuhamasisha jamii kuchangia

ujenzi, na katika maeneo hayo wananchi wamechangia hadi majengo yakafika katika hatua ya

ukamilishaji. Hata hivyo, fedha hazikutoka wakati huo.

• Katika mwaka wa fedha 2016/17, Zahanati za Gaara na Mafui zimetengewa tena fedha za

kukamilisha na zitakapopokewa ujenzi wake utakamilika. Aidha, Zahanati ya Mafui imepatiwa

mabati 240 kutoka kwa mbunge na mwaka huu wa 2016, tunaamini ujenzi wake utakamilika.

• Ujenzi wa Makirinya umekamilika kwa ufadhili wa - Shirika la Hifadhi za Taifa - Tanzania National

Parks (TANAPA). Fedha za ujenzi zitakapopatikana ujenzi wa nyumba ya mtumishi utafanyika.

Vilevile, ujenzi wa jengo la Zahanati ya Humai umekamilika na linatumika kwa sasa na tayari wa-

tumishi watatu, muuguzi mmoja na wahudumu wa afya wawili wamepelekwa kituoni.

Page 30: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

22

Maoni ya timu• Timu inashauri Halmashauri kuhakikisha inatafuta fedha kwa wakati ili kukumilisha ujenzi uliofan-

ywa na wananchi na kuzuia kupotea kwa rasilimali kama ambavyo imeonekana kwenye jengo la

nyumba ya mtumishi Makirinya kuchakaa baada ya kukaa muda mrefu bila kumaliziwa ujenzi hivyo

kuhitaji kujengwa upya.

2.1.27 Kukamilisha wa ujenzi wa Zahanati za Potea, Mongolo na Hachwi• Timu ya SAM ilipenda kujua mipango ya Halmashauri katika kuhakikisha ujenzi wa zahanati hizo

ambazo ujenzi wake ulifanywa na wananchi hadi kufikia hadi ngazi ya lenta unakamilika. Ujenzi

huo ulianza muda mrefu kwa kutumia ramani za zamani (Potea- 2002 wakati ni Mongolo -1994).

Wananchi wa Mongolo wameonyesha kuwa hawako tayari kujenga upya jambo ambalo limesa-

babisha mgogoro wa muda mrefu kama timu ilivyoelezwa na viongozi wa kijiji walipotembelea

eneo hilo. Vilevile, timu ilipenda kujua mipango ya Halmashuri katika kukamilisha huduma muhimu

kama vile vyoo, maji na umeme katika Zahanati ya Hachwi ambao ujenzi wake ulianza mwaka

2005 kwa nguvu za wananchi na kumalika 2007 kwa ufadhili wa Mholanzi (mtu binafsi).

Majibu ya menejimenti• Timu ya wataalamu ikishirikiana na mhandisi wa Halmashauri ilitembelea jengo la Zahanati ya

Potea na kutoa ushauri kuhusu maboresho ya jengo hilo ili kuendana na ramani inayotakiwa.

Ukamilishaji wa jengo hilo utategemea marekebisho hayo yatakapofanyika na fedha za kumalizia

zitakapotoka.

• Ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Mongolo unatakiwa kuanza upya kwa kufuata ramani ya sasa

inayokidhi mahitaji. Hivyo Halmashauri itafanya ukamilishaji pale jengo litakapofikia hatua ya lenta

na hii itategemea na upatikanaji wa fedha.

• Tuliwashauri wananchi kutenga eneo la kutosha kwa ajili ya zahanati na tumepewa ramani sahihi

ya zahanati kutokana na jengo la awali kutozingatia ramani inayotakiwa kwa mujibu wa muongozo

wa wizara ya afya.

Maoni ya timu• Timu inashauri kuwa ni vyema Halmashauri ikaangalia suala la Mongolo kwa umakini ili kuondoka-

na na mgogoro uliopo na kufikia muafaka. Kama menejimenti ilivyoahidi katika kikao cha ndani

kuwa itapeleka wataalamu kuingilia kati suala hili upya ni vyema ikatekeleza hilo kwa wakati.

2.1.28 Taarifa za vikao vya madiwani – Kibali cha Ajira• UK. wa 12 na 13, unaonyesha kuwa Halmashauri ilipata kibali cha ajira ya watumishi 177. Kati yao,

walioripoti ni 136 na walioingizwa kwenye orogha ya malipo (pay roll) ni 118 na waliofika kazini ni

watumishi 60 pekee. Hivyo timu ilipenda kupata ufafanuzi juu ya watumishi 136 walioripoti ambao

hawakuingizwa wote kwenye pay roll na pia ilitaka kujua kwa nini ni 60 pekee ndio walioripoti

kazini?

Page 31: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

23

Majibu ya menejimenti• Watumishi wote walioripoti na waliokuwa na sifa ndio walioingizwa katika payroll. Hata hivyo, kupa-

tikana kwa mishahara yao kulitegemea kasi ya uidhinishaji katika ngazi ya menejimenti ya utumi-

shi wa umma (Dar es Salaam). Watumishi wote walioripoti walifika kituoni. Idadi ya watumishi 60

waliofika kazini ni kwa mujibu wa taarifa za kipindi hicho cha mwanzo. Hivyo watumishi wote 136

walioripoti waliingizwa katika payroll na wapo kazini isipokuwa kwa sasa wawili wamefariki.

2.1.29 Taarifa za vikao vya madiwani – Takwimu za UKIMWI na mafunzo kwa kamati za UKIMWI za kata• Timu ya SAM ilitoa rai kwa menejimenti kuwa ni vyema takwimu za upimaji na taarifa za maam-

bukizi ya UKIMWI zikafafanuliwa kuliko kuripotiwa kiujumla. Hii itasaidia kuleta uelewa wa hali ya

Halmashauri katika kudhibiti maambukizi ya UKIMWI. Vilevile, timu iliomba kujua mafunzo yalitole-

wa lini kwa kamati za UKIMWI za kata.

Majibu ya menejimenti• Shughuli za mafunzo kwa kamati za UKIMWI za kata hufanywa na Idara ya Maendeleo ya Jamii

kupitia Mratibu wa UKIMWI (CHAC) na sio Idara ya Afya.

2.1.30 Ripoti ya Mkaguzi wa ndani – ununuzi wa dawa• Ripoti katika UK. wa 10, inaonyesha kuwa Sh. 33,545,600 kwenye vocha ya malipo namba 2/8

na hawala ya fedha namba 000002 zilitumika kununua dawa lakini hazikupitishwa na kamati ya

ununuzi na pia dawa hazikukaguliwa. Timu inapenda kujua kuna mikakati gani kuhakikisha hili

halijirudii tena? Je, kamati ya ukaguzi wa dawa ipo?

Majibu ya menejimenti• Kamati ya ukaguzi wa dawa (HMT) ilikuwepo na ipo na dawa hizo zilikaguliwa kabla ya kuingizwa

kwenye leja. Hata hivyo, wakati wa ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi wa Ndani wa Wilaya (DIA),

nyaraka hizo zilikuwa bado zipo hospitali wakati mkaguzi alikuwa anafanyia kazi Halmashauri.

Mkaguzi alionyeshwa nyaraka husika na kuifuta hoja, lakini inaonekana kwenye ripoti haikufutwa.

2.1.31 Ripoti ya Mkaguzi wa Ndani – Matumizi ya fedha za Mfuko wa Pamoja (HSBF)• Timu inapenda kujiridhisha kuhusu jumla ya Sh. 309,181,435 ambazo hazijaainishwa shughuli

zilizofanyika kama ilivyoripotiwa na Mkaguzi wa Ndani katika UK. wa 24.

Majibu ya menejimentiKwa sasa ni vigumu kuainisha shughuli zilizofanyika inahithaji usuluhishi wa kibenki kupitia malipo

yalivyotolewa.

Maoni ya timuTimu ilipenda kupata mrejesho wa hili baada ya usuluhishi wa kibenki kufanyika. Hata hivyo, baada ya

kikao na menejimenti timu haikupata muda wa kufuatilia jambo hili.

Page 32: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

24

2.2 Matokeo ya vituo vya kutolea huduma za afyaKama ilivyoelezwa kwenye utangulizi (ukurasa wa 4), timu ya SAM ilifanikiwa kutembelea vituo vya ku-

tolea huduma za afya 24 ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Kondoa, vituo vya afya vitatu na zahanati 20.

Baadhi ya vitu vilivyoangaliwa, hivi ni pamoja na miundombinu, uwepo wa kamati za afya, upatikanaji

wa dawa na watoa huduma.

2.2.1 Kamati za afya za vituo vya afya na zahanatiVituo vyote vilivyotembelewa vilikuwa na kamati za afya. Hata hivyo, changamoto ilikuwa kupatiwa

mafunzo. Ni Kituo cha Afya cha Busi waliopata mafunzo juu ya wajibu wa kamati na mafunzo haya

yalifanywa na mganga mfawidhi wa kituo cha afya. Timu ya SAM iliishauri menejimenti kufuatilia na

kuhakikisha kamati hizi zinapata mafunzo pale tu wanapochaguliwa.

Majibu ya menejimentiUshauri umepokewa. Hata hivyo, inaamini kuwa kamati zilizopata mafunzo ni zaidi ya moja. Kuhusu

Busi, menejimenti ilikiri kuwa jitihada binafsi za mfawidhi zimechangia sana maendeleo ya kituo cha

afya.

2.2.2 Vizimba vya kuchomea takaVizimba vya kuchomea taka ni tatizo katika vituo vingi vya kutolea huduma za afya. Katika Kituo cha

Afya cha Busi na Zahanati ya Pahi ndiko kulikokuwa na vizimba bora vya kuchomea taka hatarishi.

Timu ya SAM iliishauri Halmashuri kuona namna inavyoweza kuharakisha ujenzi wa vizimba hasa

kwa kuwa uchomaji wa taka hatarishi usipofanyika unaweza kuleta madhara kwa watoa na watumiaji

huduma jambo mbalo linaweza kuzuilika.

Kizimba cha kuchomea taka

hatarishi katika kituo cha

Mnenia ambacho hakijatumika

kwa zaidi ya miaka 10 kutokana

na kukosa fedha za ukarabati.

Shimo linalotumika kuchomea taka hatarishi

katika kituo cha Mnenia.

Page 33: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

25

2.2.3 Mashimo maalumu ya kutupia kondo za uzaziMashimo haya maalumu yalikuwa katika Kituo cha Afya cha Busi na Zahanati za Bereko, Kwadelo

na Masawi, sehemu zilizobaki hayakuwepo. Katika baadhi ya maeneo wanatumia vyoo (vya shimo)

kutupa na kusababisha harufu kali kiasi cha watu kushindwa kutumia vyoo hivyo. Wengine hutumia

mashimo ya kuhifadhi uchafu (septic tanks) na wengine kuwapa kina mama wakatupe nyumbani jambo

ambalo si jema. Timu ilishauri ni vyema Halmashauri ikatoa kipaumbele kwa ujenzi wa mashimo haya.

Majibu ya menejimentiUshauri umepokewa hata hivyo, changamoto kubwa ni rasilimali fedha kuwa ndogo kulinganisha na

mahitaji katika vituo. Menejimenti itapanga kuona namna ya kutatua changamoto hizi za vizimba na

mashimo kwa njia nyingine kwa kuwa kama ilivyokuwa imeonekana kwenye, CCHP ilitengewa fungu

lakini fedha hazikupokewa.

2.2.4 Miundombinu Maji – Yanapatikana katika vituo vya Afya vya Busi na Kisese hata hivyo, katika Kituo cha afya cha Mne-

nia kuna changamoto ya miundombinu kutoka kwenye chanzo cha maji hadi kufika kituoni yanakoweza

kuhifadhiwa kwenye tenki. Kwa ngazi ya zahanati, maji yalikuwapo katika Zahanati ya Kikilo pekee na

zilizobaki 19 hazikuwa na maji. Ni changamoto hasa kwa watoa huduma ambao inawalazimu kutafuta

maji kabla ya kutoa huduma, ni katika maeneo machache wakazi wanasaidia kupeleka maji katika

zahanati.

Umeme - Nishati ya umeme

wa jua au TANESCO ipo katika

vituo vyote vya afya na zahanati

isipokuwa katika zahanati za Hu-

mai, Makirinya & Kinyasi. Katika

Zahanati ya Kikore kulikuwa na

changamoto ya kuharibika kwa

paneli za umeme wa jua hivyo ku-

kosekana kwa umeme kwa wakati

huo.

Vyoo – Katika vituo vinane vya

kutolea huduma, majengo ya

vyoo yapo katika hali nzuri, navyo ni vituo vya afya vya Kisese na Busi, na Zahanati za Salanka, Hau-

bi, Kwadelo, Kinyasi, Masawi na Humai. Kutokana na mgao wa maji katika Kituo cha afya cha Kisese

wamelazimika kuwa na vyoo vya muda ambavyo hutumiwa na wagonjwa na haviko katika hali nzuri.

Majengo ya vyoo katika zahanati saba yanahitaji ukarabati mdogo ili kuviweka katika hali nzuri hivyo

ni Kikore, Kiteo, Bereko, Baura, Hebi, Bolisa na Kikilo. Vilivyobaki ambavyo ni kituo kimoja cha afya na

zahanati nane zinahitaji ujenzi mpya wa vyoo bora.

Page 34: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

26

Majengo – Majengo mengi ya vituo vya kutolea huduma yako katika hali nzuri hata hivyo, baadhi

yanahitaji ukarabati ili kuyaboresha. Haya ni pamoja na Kikilo, Bumbuta, Kiteo na Kisese. Zahanati

za Masange na Mongoroma, majengo yake yako katika hali duni kama kuwa na nyufa kubwa kwenye

kuta, dari kubomoka na milango iliyoliwa na mchwa jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa watoa na

watumiaji huduma. Vilevile ubovu wa majengo unasababisha kutokuwa na usiri wakati wa matibabu

kwa mfano, katika Zahanati ya Masange chumba cha kujifungulia hakina usiri wowote na ni kibovu.

Vilevile, majengo mengi hayaingiliki kirahisi na watu wenye mahitaji maalumu kama wagonjwa

waliozidiwa, walemavu na wazee. Mfano ni miundombinu ya Kituo cha Afya Kisese. Hata hivyo, baadhi

ya maeneo kama Kituo cha Afya Mnenia na Zahanati za Kikore na Baura kuna miundombinu rafiki kwa

wenye mahitaji maalumu.

Majibu ya menejimentiTutashirikiana na kamati za afya na wananchi kuona namna ya kutatua tatizo la vyoo katika vituo vya

kutolea huduma. Pia baadhi ya zahanati mlizoziona zikiwa na hali mbaya kama Masange, zimepokea

fedha Sh. Milioni 10 bada ya zoezi la ukaguzi (star rating) ili kuboresha majengo yenye hali mbaya.

2.2.5 Tathimini ya Utendaji/Open Performance Review and Appraisal System (OPRAS)Timu ya SAM ilipenda kujua namna utendaji wa watumishi unavyofanyiwa tathmini kwa kutumia mfumo

wa Serikali wa OPRAS. Katika vituo vya kutolea huduma 15 vilivyoulizwa kuhusu OPRAS na nam-

na watumishi wanavyopata mrejesho wa tathmini, hakukuwa na watumishi waliokuwa na uelewa wa

kutosha kuhusu mfumo huo. Baadhi hawajawahi kujaza fomu za OPRAS, wengine wamewahi mara

moja ila hawakupata mrejesho baada ya tathmini na wengine hawaelewi kabisa. Hivyo timu iliishauri

menejimenti kwamba kama inataka kuona OPRAS bado inatumika, ni vyema watumishi vituoni wa-

kaelimishwa umuhimu, ujazaji na pia kupata mrejesho kwa wakati.

Majibu ya menejimentiUshauri umepokewa na kuzingatiwa

2.2.6 Mengineyo• Katika vituo vingi vya kutolea huduma kulikuwa na dawa zinazohitajika na watumishi walikiri kuwa

upatikanaji umeongezeka hasa kwa kuwa na msambazaji binafsi katika Mkoa wa Dodoma. Vile-

vile, vituo vingi vilikuwa na miundombinu mizuri ya uhifadhi wa dawa kama mashelfu, makabati na

huduma ya mnyororo baridi. • Dawa iliyokosekana karibu kwa vituo vyote vinavyotoa huduma za VVU/UKIMWI ni Septrin am-

bayo wakati wa majadiliano na watendaji wa Halmashauri, DMO alikiri kukosekana kwa dawa hiyo

inayosaidia kukinga magonjwa nyemelezi.• Changamoto ipo kwenye vifaa tiba kama vile mashine ya CD4 (Kituo cha Afya Kisese), kitanda cha

kujifungua (Zahanati ya Masange), vitanda vya kupimia wagonjwa na vya kupumzisha wagonjwa

vituoni.

Page 35: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

27

• Sehemu kubwa ya watumishi wa afya bado wana changamoto ya ukosefu wa nyumba za kuishi ndani ya vituo, wengi wamekodisha nyumba mtaani ambako ni mbali na vituo hivyo kuwa vigumu

kutoa huduma wakati wa dharura hususani kina mama wajawazito wanapotaka kujifungua.

• Kituo cha Afya cha Mnenia pamoja na kuwa na gari la wagonjwa, kwa zaidi ya mwezi mmoja gari hilo lilikuwa Halmashauri wakati gari la Kituo cha Afya cha Kisese haliko kituoni tangu mwaka 2014 na hivyo kusababisha usumbufu kwa wagonjwa na watumishi wakati kwa kupeleka wagonjwa wa

dharura Hospitali ya Wilaya.

• Masanduku ya maoni yako katika vituo vingi vya kutolea huduma ila kunakosekana utaratibu mzuri wa kuyafungua na kuyafanyia kazi. Funguo wanazo watumishi jambo ambalo linapunguza uwa-

jibikaji.

2.3 Changamoto katika kutekeleza zoezi la SAM.• Baadhi ya taarifa, ripoti na mipango zina makosa au marudio yanayoweza kupotosha au kuleta

maana nyingine. Mfano, suala la uandishi wa ukamilishaji wa majengo ya zahanati za Mulua, Sal-are, Berabera, Kalamba, Kwamafunchi, Kinyasi –jengo jipya, Mitati, na Choka ambapo kiuhalisia hakukuwa na ukamilishaji wa maeneo hayo kwani timu ilipotembelea, ilikuta maeneo hayo yapo kwenye hatua za awali za ujenzi wa msingi na mengine kwenye hatua ya usafishaji wa maeneo,

hivyo lugha au maneno yanayotumika yamwezeshe mtumia taarifa kupata picha halisi.

• Pia kulikuwa na changamoto ya kukosekana kwa taarifa muhimu hasa za utekelezaji wa shughuli katika vituo vya kutolea huduma kama taarifa za mafunzo yaliyofanyika, gharama za ununuzi wa

dawa na vifaa hasa ununuzi unapofanyika katika ngazi ya Halmashauri.

• Pia, makabrasha kutokuwa na saini za wahusika kwa mfano, CCHP, taarifa za madiwani n.k. Timu inapendekeza suala la saini ni la muhimu na kutokana na muongozo wa uandaaji wa taarifa za afya na kwamba hiki ni kepengele cha lazima, hivyo ni vyema pia hata mkoani wawe makini katika hili kabla ya kupitisha mipango ya afya ya Wilaya na ili kuondokana na changamoto hii, ni vyema rasimu za taarifa za awali ziwe zinawasilishwa katika mfumo wa “soft copy”. Hii itasaidia hata ku-

punguza gharama katika utoaji wa nakala za rasimu na mchanganyo wa rasimu ya mwisho.

• Upatikanaji wa taarifa kwa timu haukuwa wa wakati na pia taarifa hazikuwa zimekamilika jambo lililosababisha kuchelewesha kutekeleza zoezi kama lilivyokuwa limepangwa. Hata hivyo, timu inamshukuru Mkurugenzi mpya Mwl. Kibasa Falesy Mohamedi kwa kuwezesha kupatikana kwa taarifa kwa muda mfupi pindi alipowasili. Hii ilitokana na kujulishwa kuhusu changamoto za upati-kanaji wa taarifa iliyokuwa imejitokeza.

• Vituo vichache vilikuwa vimefungwa muda wa kazi wakati timu ilipotembelea kujionea utoaji wa

huduma na hili hili linachangiwa na uhaba wa watumishi. Kwa mfano, katika Zahanati ya Mkekena

ilikuwa imefungwa muda wa kazi huku wagonjwa wakisubiri na baadhi kuondoka. Kuna watumishi

wawili tu, mmoja alikuwa safarini na mmoja alitoka kwa dharura hivyo kufunga kituo kwa muda.

Page 36: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

28

Jengo la Zahanati ya Mkekena lenye sehemu maalumu ya kupitia watu wenye mahitaji maalumu na picha ya chini yake ni choo cha Zahanati hiyo.

Page 37: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

29

3.0 MaazimioMaazimio kadhaa yalifikiwa katika mkutano wa ndani wa watendaji wa idara ya afya pamoja na wadau

wa afya katika Halmashauri ya Kondoa baada mrejesho wa zoezi la SAM kutolewa na wadau kujadili

ripoti na kutoa mapendekezo.

3.1 Ukamilishaji wa majengoHalmashauri kupitia idara ya afya imeahidi kuupa kipaumbele ukamilishaji wa kazi majengo yote yal-

iyosimama kwa muda mrefu. Ofisi ya Mganga mkuu wa Halmashauri iliahidi kutembelea majengo

hayo ikiwa na watalamu wa ujenzi wa Halmashauri kwa ajili ya ushauri kwani majengo mengi yalikuwa

yamejengwa kwa muda mrefu kwa kutumia ramani za zamani. Vilevile, kwa majengo ambayo hay-

akuendelezwa kama zahanati, wataalamu watashauri namna ujenzi huo unavyoweza kukamilishwa

kwa matumizi mengineyo kama nyumba za watumishi. Pia, wadau walishauri ujenzi wa majengo map-

ya wakati ya zamani hayajakamilika unafifisha matumizi sahihi ya rasilimali chache na kuchelewasha

utoaji wa huduma stahiki.

3.2 Kuongeza Watumishi wa afya - wataalamuOfisi ya mganga mkuu imeahidi kuendelea kufuatilia katika ngazi husika na kushirikiana na wadau

mbalimbali kama ilivyofanya kwa mwaka wa fedha 2014/15 ili kuongeza idadi ya watumishi katika nga-

zi zote. Ongezeko la watumishi litahusisha zaidi wataalamu ambao ndio changamoto kubwa kwa sasa

kwa ngazi za zahanati na vituo vya afya.

3.3. Ushiriki wa wananchiHalmashauri imeahidi kuimarisha utaratibu wa wananchi kushiriki katika kuibua vipaumbele na kupata

nafasi ya ushiriki wakati wa utekelezaji, ufuatiliaji ili kuimarisha umiliki wa shughuli kwa jamii.

3.4 Motisha kwa watumishiHalmashauri kupitia idara ya afya imeahidi kuendelea kutoa motisha kwa watumishi walioko katika

vituo vya kutolea huduma ili kuongeza ufanisi. Kwa mwaka 2014/15 (mwaka wa uchambuzi), hakuku-

wa na motisha kwa vocha za mawasiliano za siku hata hivyo, mwaka 2016/17 vocha za mawasiliano

zimetolewa kwa kila kituo na litakuwa endelevu.

3.5 Upatikanaji wa taarifaHalmashauri kupitia idara ya afya imeahidi kuimarisha mfumo na utaratibu wa upatikanaji wa taarifa za

muhimu kwa wananchi na wadau wa afya katika ngazi zote kuanzia Halmashauri mpaka kwenye vituo

vya utoaji huduma. Vilevile, wajumbe wa timu ya SAM pindi wanapohitaji taarifa kwa ajili ya ufuatiliaji

wa huduma watapata kwa wakati ili kujenga uwajibikaji na ushirikiano kati ya wananchi na watoa hudu-

ma katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya.

Sehemu ya Tatu

Page 38: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

30

3.6 Kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa makundi maalumuHalmashauri kupitia idara ya afya imeazimia kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa makundi maalu-

mu kama vile wazee na walemavu. Hii ni pamoja na kukarabati miundombinu ya kuingilia katika vituo

vya kutolea huduma ili kuwa rafiki na kupitika kwa urahisi kwa watu wenye changamoto katika kutumia

ngazi. Mfano ngazi zilizopo katika Kituo cha Afya Kisese.

3.7 Kamati za afya za vituoHalmashauri kupitia idara ya afya imeazimia kuhakikisha kamati zote za afya za vituo vya huduma za

afya hususani vituo vya afya na zahanati, zinapatiwa mafunzo pindi zinapoundwa ili zijue wajibu wao

na kuutekeleza kikamilifu.

3.8 Uwazi wa taarifa za dawa vituoniHalmashauri kupitia idara ya afya imeazimia kuimarisha upatikanaji wa taarifa za dawa katika vituo vya

kutolea huduma. Kamati za afya za kituo zitashiriki kikamilifu katika kupokea na kuhakiki dawa na vifaa

tiba katika vituo vya kutolea huduma na taarifa zake zitakuwa wazi kwa wananchi na watumia huduma.

3.9 Taarifa za fedha vituoniHalmashauri kupitia idara ya afya imeazimia kuimarisha taarifa za fedha za vituo vya kutolea huduma

na kwa kuwezesha kamati kushiriki kikamilifu kusimamia na kufuatilia ikiwa ni pamoja na kuhakikisha

zinabandikwa kwenye mbao za matangazo kwa ajili ya wananchi ili kuimarisha uwazi, uwajibikaji na

ufuatiliaji.

3.10 Kuimarisha miundombinuHalmashauri kupitia idara ya afya imeazimia kuimarisha miundombinu katika vituo vya kutolea huduma

za afya kama ilivyoripotiwa na timu ya SAM. Miundombinu hii ni pamoja na vyoo, mashimo ya kutupa

kondo za uzazi, vizimba vya kuchomea taka hatarishi na mifumo ya maji.

3.11 Kuboresha mifumo ya usimamizi wa rasilimaliHalmashauri kupitia idara ya afya imeazimia kuboresha wa mifumo ya usimamizi wa rasilimali fedha za

idara katika ngazi zote ili kuepuka changamoto za upotevu wa fedha kama ilivyotokea katika mwaka

wa fedha 2014/15 ambako takribani Sh. milioni 180 zilipotea na kuathiri utekelezaji wa shughuli mbal-

imbali za idara ya afya.

3.11 Uhakiki wa ripoti, mipango na taarifa za idara Halmashauri kupitia idara ya afya imeahidi kuhakikisha taarifa na ripoti zote zinafanyiwa uhakiki wa

kina kabla ya kuziweka wazi kwa matumizi ya umma ili kuepuka makosa ambayo yanaweza kusaba-

bisha upotoshaji. Hii ni pamoja na kuhakikisha ripoti na taarifa zote zinakuwa na sahihi stahiki, makosa

ya kurudia au kuacha taarifa muhimu yanaondoka kama ilivyoonekana kwenye mpango kabambe,

mpango mkakakti na ripoti mbalimbali zilizopitiwa na timu ya SAM.

Page 39: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

31

Sehemu ya Nne4.0. Hitimisho na mapendekezo4.1 HitimishoZoezi la SAM-2016 kwa Halmashauri ya Kondoa Vijijini lilikwenda vizuri na kupata ushirikiano kutoka

kwa viongozi wa Wilaya na Halmashauri na wadau wa afya. Ni matumaini ya timu kwamba changamo-

to na mapendekezo yaliyotolewa na timu ya SAM na wadau yatafanyiwa kazi na Halmashauri kupitia

idara ya afya kwa wakati kama ililivyokubaliwa katika kikao cha ndani na kikao cha mrejesho kwa wa-

dau wa afya. Pamoja na Halmashauri kuongoza utekelezaji wa maazimio hayo, ni vyema kila mdau wa

afya akawajibika na kuishawishi jamii kufanya kazi kwa pamoja na bidii ili kufanikisha uboreshaji wa

huduma za afya kwa manufaa ya wananchi wote wa Wilaya ya Kondoa na Taifa kwa ujumla.

4.2 Mapendekezo Timu ya SAM ina mapendekezo yafuatavyo;

• Kwa kuwa zoezi hili lina lengo la kutoa taswira ya afya na kuwawezesha watoa huduma, wadau na

wananchi kuhimiza masuala ya wajibu na haki katika kufikia lengo la upatikanaji wa huduma bora

za afya kwa wote, ni vyema taarifa mbalimbali za utekelezaji wa zoezi hili zikawa zinatolewa kwa

wakati ili kufanikisha mwendelezo wa ufuatiliaji.

• Taarifa za mipango na bajeti za afya zinapowasilishwa mkoani, ni vyema zikakaguliwa vizuri ili

kuondoa changamoto mbalimbali kama kupitishwa kwa mpango na bajeti ya afya bila kusainiwa

na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya na Mganga Mkuu wa Wilaya kama ilivyotokea kwenye mpango

kabambe wa Wilaya kwa mwaka wa fedha 2014/2015. Pia, katika upelekaji wa taarifa ya mpango

na bajeti mkoani ni vyema rasimu za awali zikawa zinapelekwa kwa “soft copy” na kisha rasimu

ya mwisho ambayo imetiwa saini ndiyo ipelekwe kwa “hard copy”, hii itapunguza mchanganyo wa

kupewa taarifa ambazo hazijasainiwa na pia kupunguza gharama kwa idara husika.

• Mpango mkakati huu wa Halmashauri unaishia mwaka wa fedha 2016/ 2017, timu inapendekeza

kwamba ni vyema maandalizi ya mpango mkakati mpya yakafanyika kwa wakati na kwa ufasaha

ili kuhakikisha kabla ya mwaka wa fedha kuisha kuna mpango mkakati wa miaka mingine mitano

unaoanza mwaka mwingine wa fedha.

• Taarifa za mpango na bajeti wa afya ni vyema pia zikawasilishwa kwa lugha ya Kiswahili ili ku-

wawezesha wananchi kusoma na kuelewa vizuri mipango na bajeti ya idara ya afya, ikilinganishwa

na sasa mipango na bajeti inaandikwa kwa lugha ya kitaalamu.

• Katika ripoti ya utekelezaji na fedha, hakuna maoni wala mapendekezo juu ya kazi zilizofanyika au kutofanyika, timu inashauri ni vizuri wakati wa uandaaji wa taarifa katika robo ya mwisho ya mwa-ka, sehemu ya maoni ijazwe ili kutoa hali halisi ya utekelezaji wa shughuli husika na kuwezesha wadau kuelewa vizuri taarifa za idara.

Page 40: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

32

• Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iweke mikakati madhubuti ya kutatua changa-moto ya vyanzo vya mapato vya ndani na viwe endelevu, hii itasaidia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Halmashauri ikiwa ni pamoja na za idara ya afya kutekelezwa kwa wakati.

Page 41: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

33

Kiambatanisho 1: Vituo vilivyotembelewa na timu ya SAMVituo vya kutolea huduma za afya (24) na maeneo 13 ya ujenzi yaliyotembelewa

na timu ya SAM-2016Na. NGAZI YA WILAYA VITUO VYA

AFYAZAHANATI Maeneo ya ujen-

zi wa zahanati1 Hospitali ya Wilaya Kondoa Mnenia Masange Mitati2 Kisese Mkekena Mwisanga3 Busi Kikore Berabera4 Mongoroma Mafai5 Thawi Hachwi6 Salanka Mulua7 Bereko Potea8 Kiteo Choka9 Humai Changaa10 Baura Salale11 Haubi Kwahengwa12 Hebi Kwamafunchi

13 Makirinya Mongolo14 Sakami15 Bolisa16 Kwadelo17 Kinyasi18 Masawi19 Bumbuta

20 KikiloJUMLA 01 03 20 13

Page 42: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2018-07-04 · iv Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring”

“Sikika inafanya kazi ya kuhimiza uboreshaji wa mifumo ya afya na

usimamizi wa fedha kupitia uwajibikaji jamii na uraghibishi

katika ngazi zote za serikali”

Nyumba Na.69Ada Estate, Kinondoni Barabara ya Tunisia Mtaa wa WaverleyS.L.P 12183Dar es Salaam, Tanzania.Simu: +255 22 26 663 55/57

Nyumba Na. 340 Mtaa wa Kilimani S.L.P 1970 Dodoma, Tanzania. Simu: 0262321307 Nukushi: 0262321316

Ujumbe mfupi: 0688 493 882 Nukushi: +255 22 26 680 15Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.sikika.or.tzBlog: www.sikika-tz.blogspot.com Twitter: @sikika1Facebook: Sikika1Instagram: Sikika Tanzania