Upload
phamthu
View
879
Download
8
Embed Size (px)
Citation preview
1
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein
‘Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
TAARIFA YA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA UTEKELEZAJI WA
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM
KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO
(NOVEMBA, 2010 HADI JULAI, 2015)
Imetayarishwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar
2
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
JULAI, 2015
i
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
YALIYOMO
SEHEMU YA KWANZA
1.0 UTANGULIZI .................................................................................................................................. 1
SEHEMU YA PILI
2.0 HALI YA SIASA .................................................................................................................................... 3
2.1 Matukio Makubwa ya Kisiasa Yaliyotokea ............................................................................................ 3
2.1.1 Kufanyika kwa chaguzi ndogo kwa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani ................................. 3
2.1.2 Maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ........................................................................ 4
2.1.3 Matukio ya Uvunjifu wa Amani .......................................................................................................... 5
2.2 Masuala ya Muungano ............................................................................................................................ 6
2.2.1 Vikao vya Pamoja vya Mashirikiano ................................................................................................... 7
2.2.2 Mchakato wa Kuandaa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .................................... 8
SEHEMU YA TATU
3.0 SEKTA YA KIUCHUMI ..................................................................................................................... 10
3.1 Ukuaji wa Uchumi ................................................................................................................................ 10
3.2 Mfumko wa Bei .................................................................................................................................... 11
3.3 Mapato na Matumizi ya Serikali ........................................................................................................... 11
3.3.1 Kushuka kwa Kiwango cha Nakisi ya Bajeti ..................................................................................... 11
3.4 Kuimarisha Maeneo Huru ya Kiuchumi ya Fumba. ............................................................................. 12
3.5 Uwakilishi wa Sekta Binafsi katika Vikao Mbalimbali ........................................................................ 13
3.6 Kuandaa Mazingira Bora ya Kiuchumi ili Kuvishawishi Vyombo vya Fedha Kutoa Mikopo Yenye
Masharti Nafuu. .......................................................................................................................................... 13
3.7 Kuanzisha Maeneo Mapya ya Kiuchumi .............................................................................................. 14
3.8 Miradi Iliyowekezwa kwa Kipindi cha 2010 - 2015 ............................................................................. 14
SEHEMU YA NNE
4.0 SEKTA ZA UZALISHAJI MALI ........................................................................................................ 16
4.1 KILIMO ................................................................................................................................................ 16
4.1.1 Kutekeleza Mkakati wa Uimarishaji wa Zao la Karafuu ................................................................... 16
4.1.2 Kuimarisha Miundombinu ya Umwagiliaji Maji ............................................................................... 18
ii
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
4.1.3 Kuendeleza Programu za Tafiti za Kilimo na Maliasili kwa Kuwashirikisha Wakulima na Washiriki
Wengine ...................................................................................................................................................... 19
4.1.3.1 Utafiti wa Mazao ya Nafaka na Jamii ya Kunde ............................................................................ 19
4.1.3.2 Jaribio la Mbolea Mpya na Mafunzo kwa Wakulima Chini ya Mradi wa NAFAKA .................... 19
4.1.3.3 Ruzuku katika Kilimo ..................................................................................................................... 20
4.1.3.4 Tafiti za Mazao ya Mizizi (Muhogo na Viazi Vitamu)................................................................... 21
4.1.3.5 Uboreshaji wa Miundombinu ya Utafiti ......................................................................................... 21
4.1.4 Kuhimiza na Kushajiisha Matumizi ya Pembejeo na Mbinu Bora za Kilimo ................................... 22
4.1.5 Kuendelea Kuhimiza na Kutilia Mkazo Mafunzo na Matumizi ya Kanuni za Kilimo Bora kwa
Mazao ya Chakula, Biashara na Matunda ................................................................................................... 23
4.1.6. Uimarishaji wa Chuo cha Kilimo Kizimbani .................................................................................... 23
4.1.7 Kutekeleza Mkakati wa Kuanzisha Akiba ya Chakula ya Zanzibar (National Food Reserve) .......... 25
4.2.1 Kuendeleza Kazi za Tafiti kwa Wanyama ......................................................................................... 27
4.3 UVUVI NA MAZAO YA BAHARINI ................................................................................................ 29
4.3.1 Uimarishaji wa Zao la Mwani ............................................................................................................ 30
4.4 MALIASILI .......................................................................................................................................... 33
4.4.1 Kutekeleza Mpango wa Muda Mrefu wa Usimamizi wa Rasilimali za Misitu na Maliasili
Zisizorejesheka ........................................................................................................................................... 33
4.5 MAZINGIRA ........................................................................................................................................ 36
4.5.1 Kusimamia Utekelezaji wa Mpango wa Hifadhi ya Mazingira katika Maeneo ya Ardhi, Bahari na
Ukanda wa Pwani ....................................................................................................................................... 36
4.5.2 Kufanya Mapitio ya Miradi Inayohusiana na Mazingira ................................................................... 38
4.6 UTALII ................................................................................................................................................. 38
4.6.1 Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Mpango Mkuu wa Utalii ................................................ 39
4.6.2 Kuitangaza Zanzibar Kiutalii Nje ya Nchi ili Kuongeza Kipato ....................................................... 39
4.6.3 Kuimarisha Utalii wa Kumbukumbu za Kihistoria ............................................................................ 40
4.6.4 Kuibua Maeneo Mapya ya Vivutio vya Utalii ................................................................................... 40
4.6.5 Kumbukumbu na Mambo ya Kale ..................................................................................................... 42
4.6.5.1 Kuhifadhi Kumbukumbu za Kihistoria na Mambo ya Kale ........................................................... 42
4.6.5.2 Kuendeleza Matengenezo ya Makumbusho ................................................................................... 42
4.6.6 Kufanya Uhakiki wa Hoteli za Kitalii ............................................................................................... 43
4.6.7 Kuimarisha Huduma za Utalii kwa Kuziendeleza Jumuiya za Watoa Huduma ................................ 44
4.6.8 Kupunguza Vituo vya Ukaguzi Katika Maeneo Wanayopita Watalii ............................................... 44
iii
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
4.6.9 Kukiimarisha Chuo cha Maendeleo ya Utalii .................................................................................... 45
4.7 VIWANDA NA BIASHARA ............................................................................................................... 45
4.7.1 Kuimarisha Mtandao wa Usambazaji Habari za Biashara kwa Wafanyabiashara ............................. 48
4.7.2 Kufanya Utafiti wa Usarifu wa Zao la Karafuu ................................................................................. 48
4.8 VYAMA VYA USHIRIKA .................................................................................................................. 49
4.8.1 Kusimamia Utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Ushirika na Program Mbalimbali ....................... 51
4.8.2 Kuendelea Kusajili na Kufanya Ukaguzi wa Vyama Vipya vya Ushirika ........................................ 51
SEHEMU YA TANO
5.0 MIUNDOMBINU YA KIUCHUMI ..................................................................................................... 52
5.1 BARABARA ........................................................................................................................................ 52
5.1.1 Kusimamia Utekelezaji wa Sheria Zinazohusiana na Usalama Barabarani ....................................... 55
5.2 USAFIRI WA BAHARINI ................................................................................................................... 55
5.2.1 Ujenzi wa Bandari ya Mpigaduri ....................................................................................................... 58
5.3 Kuliimarisha Shirika la Meli ................................................................................................................. 58
5.3.1Ununuzi wa Meli Mpya ya Serikali .................................................................................................... 58
5.3.2 Kubadili Mfumo wa Uendeshaji wa Ofisi ya Mrajis wa Meli na kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa
Usafiri wa Baharini ..................................................................................................................................... 59
5.3.3 Kuendeleza Mazingira ya Kuvutia Wawekezaji wa Nje na Ndani ili Kuekeza zaidi katika Usafiri wa
Baharini ....................................................................................................................................................... 59
5.4 USAFIRI WA ANGA ........................................................................................................................... 60
5.4.1 Kuwajengea Uwezo Wafanyakazi ..................................................................................................... 60
5.4.2 Kusimamia Utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Uendeshaji wa Kiwanja cha Kimataifa cha Zanzibar
.................................................................................................................................................................... 60
5.4.2.1 Uendelezaji Ujenzi wa Uzio na Jengo Jipya la Abiria Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid
Amani Karume ............................................................................................................................................ 60
5.4.2.2 Ujenzi wa Maegesho na Njia ya Kupitia Ndege Uwanja wa Ndege wa Kimataifa ........................ 61
5.4.2.3 Kukamilisha Kazi za Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Pemba ......................................................... 62
5.5 UMEME................................................................................................................................................ 62
5.5.1 Kuimarisha Mazingira ya Kuvutia Wawekezaji katika Sekta ya Nishati ya Umeme ........................ 65
5.5.2 Kuwapatia Mafunzo Wafanyakazi katika Fani za Nishati na Madini ................................................ 65
5.5.3 Kuliimarisha Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) ........................................................................... 65
5.5.4 Kusimamia Uendeshaji wa Nishati ya Mafuta na Gesi ...................................................................... 65
5.6 ARDHI .................................................................................................................................................. 66
iv
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
5.6.1 Usajili za Ardhi kwenye Maeneo ya Fukwe na Miji.......................................................................... 67
5.6.1.1 Maeneo ya Fukwe ........................................................................................................................... 67
5.6.1.2 Maeneo ya Miji ............................................................................................................................... 67
SEHEMU YA SITA
6.0 HUDUMA ZA JAMII ........................................................................................................................... 68
6.1 Elimu ..................................................................................................................................................... 68
6.1.1 Elimu ya Maandalizi .......................................................................................................................... 68
6.1.1.1 Utayarishaji wa Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia vya Elimu ya Maandalizi .......................... 69
6.1.1.2 Kuongeza Idadi ya Madarasa ya Elimu ya Maandalizi ................................................................... 69
6.1.1.3 Kukamilisha Sera ya Makuzi na Malezi ya Mtoto .......................................................................... 70
6.1.2. Kuimarisha mazingira ya Skuli za Msingi ........................................................................................ 70
6.1.2.1 Kuimarisha Ufundishaji katika Madarasa ya Awali ya Msingi (Std 1-4) ....................................... 71
6.1.2.2 Kuondoshwa kwa Michango ya Wazee katika ngazi ya Elimu ya Msingi ..................................... 72
6.1.3 Elimu ya Sekondari ............................................................................................................................ 72
6.1.3.1 Kuimarisha Elimu ya Sayansi na Hesabati kwa Kuendeleza Kambi za Sayansi ............................ 74
6.1.3.2 Kutoa Mafunzo kwa Walimu Wakuu na Maafisa wa Elimu wa Wilaya na Mikoa ........................ 75
6.1.4 Elimu Mbadala na Elimu ya Watu Wazima ....................................................................................... 75
6.1.5 Huduma za Maktaba .......................................................................................................................... 76
6.1.5.1 Kuendeleza Mafunzo ya Ukutubi ................................................................................................... 76
6.1.5.2 Kuhamasisha Wananchi Kutumia Maktaba .................................................................................... 77
6.1.6 Elimu ya Juu ...................................................................................................................................... 77
6.1.7 Kuimarisha Mafunzo ya Ualimu ........................................................................................................ 79
6.1.7.1 Mafunzo ya Ualimu ........................................................................................................................ 80
6.1.8 Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Amali ............................................................................................. 80
6.1.8.1 Kuimarisha Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia .............................................................. 80
6.1.8.2 Kuimarisha Skuli ya Ufundi Kengeja ............................................................................................. 81
6.2 Sekta ya Afya ........................................................................................................................................ 81
6.2.1 Huduma za Kinga .............................................................................................................................. 81
6.2.2 Huduma za Tiba ................................................................................................................................. 82
6.2.3 Huduma Bora za Afya kwa Wananchi Wote ..................................................................................... 83
6.2.4 Kuendeleza Huduma za Tiba Asili .................................................................................................... 84
6.2.4.1 Baraza la Tiba Asili ........................................................................................................................ 84
v
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
6.2.5 Kuimarisha Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya .......................................................................... 85
6.2.6 Kuendeleza Mapambano dhidi ya Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu na Ukoma ............................... 87
6.2.6.1 Malaria ............................................................................................................................................ 87
6.2.6.1.1 Usambazaji wa Vyandarua katika Vituo vya Afya. ..................................................................... 87
6.2.6.2 UKIMWI ......................................................................................................................................... 89
6.2.6.3 Kifua Kikuu na Ukoma ................................................................................................................... 90
6.2.6.4 Kuipandisha Daraja Hospitali ya Wete ........................................................................................... 91
6.2.6.5 Kuipandisha Daraja Hospitali ya Abdalla Mzee Pemba ................................................................. 91
6.2.6.6 Kuipandisha Daraja Hospitali ya Micheweni ................................................................................. 92
6.2.6.7 Kuipandisha Daraja Hospitali ya Kivunge...................................................................................... 93
6.2.6.8 Kuimarisha Hospitali ya Makunduchi ........................................................................................ 93
6.2.6.9 Kuendelea Kuimarisha Huduma za Hospitali ya Mnazi Mmoja ili kufikia Hadhi ya Hospitali ya
Rufaa ........................................................................................................................................................... 94
6.3 MAJI ..................................................................................................................................................... 98
6.3.1 Kuzifanyia Mapitio Sera na Sheria ya Maji ....................................................................................... 98
6.4 MAKAAZI .......................................................................................................................................... 101
6.4.1 Kukamilisha Ujenzi wa Nyumba ya Maendeleo Bambi .................................................................. 101
6.4.2 Uendelezaji wa Mamlaka ya Mji Mkongwe .................................................................................... 102
SEHEMU YA SABA
7.0 MAENEO MENGINE YA KIPAUMBELE....................................................................................... 103
7. 1 Utamaduni na Michezo ...................................................................................................................... 103
7.1.1 Kuandaa Sera ya Utamaduni na Michezo ........................................................................................ 103
7.1.2 Kusimamia Utekelezaji wa Sera na Sheria za Michezo na Utamaduni ........................................... 103
7.1.3 Kujenga Kiwanja cha Kisasa cha Michezo ya Ndani ...................................................................... 103
7.1.4 Kukamilisha Ujenzi wa Kituo cha Michezo Dole ........................................................................... 104
7.1.5 Ujenzi wa Uwanja Mpya wa Michezo ............................................................................................. 104
7.1.6 Matengenezo ya Kuboresha Uwanja wa Gombani Pemba .............................................................. 104
7.1.7 Kuendeleza na Kuimarisha Vipaji vya Wanamichezo ..................................................................... 105
7.1.8 Kuendeleza Kudumisha Mila, Silka na Maadili Mema ya Wazanzibari ......................................... 106
7.2 VYOMBO VYA HABARI ................................................................................................................. 107
7.2.1 Kusimamia Utekelezaji wa Sera ya Habari na Kuendeleza Uhuru wa Vyombo vya Habari ........... 107
7.2.2 Kusimamia Utekelezaji wa Muongozo, Kanuni na Sheria ya Vyombo vya Habari ........................ 107
vi
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
7.2.3 Kuendeleza Mafunzo kwa Watendaji wa Vyombo vya Habari na Utangazaji ................................ 108
7.2.4 Kuviimarisha Vyombo vya Habari ikiwemo ZBC TV na ZBC Redio ........................................... 108
7.2.5 Ujenzi wa Studio ya Wasanii ........................................................................................................... 109
7.2.6 Kuendelea Kukiimarisha Chuo cha Uandishi wa Habari ................................................................. 110
7.2.7 Kusimamia na Kudhibiti Uingizaji wa Vifaa vya Utangazaji .......................................................... 111
7.2.8 Mradi wa ‘E-Government’ ............................................................................................................... 112
7.3 MAJANGA NA HUDUMA ZA UOKOZI ......................................................................................... 112
7.3.1 Kuanzisha na Kuimarisha Kamati za Maafa kwa Ngazi ya Taifa, Wilaya na Shehia ..................... 112
7.3.2 Kuimarisha Vikosi vya Uokozi Wakati wa Maafa .......................................................................... 114
7.3.3 Kuimarisha Kikosi cha Zimamoto na Uokozi.................................................................................. 114
7.4. DAWA ZA KULEVYA .................................................................................................................... 115
7.4.1 Kusimamia Utekelezaji wa Sheria ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya ............................................. 115
7.4.2Kushirikiana na Asasi za Kijamii ..................................................................................................... 116
7.4.3 Kuanzisha Vituo Maalumu vya Kurekebisha Vijana Walioathirika na Dawa za Kulevya .............. 116
7.4.4 Taaluma na Ushauri Nasaha kwa Wananchi .................................................................................... 116
7.5 DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA .......................................................................................... 116
7.5.1 Kuzingatia Misingi ya Demokrasia na Utawala Bora ...................................................................... 117
7.5.2 Kusimamia Utekelezaji wa Kazi na Majukumu ya Serikali ............................................................ 118
7.5.3 Kuendeleza Kazi ya Utekelezaji wa Mkakati wa Elimu ya Uraia, Kidemokrasia, Haki za Binaadamu
na Utawala Bora ........................................................................................................................................ 118
7.5.4 Kuimarisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ........................................................... 119
7.5.5 Kuanzisha Mahakama ya Biashara Zanzibar ................................................................................... 119
7.6 OFISI YA MKURUGENZI WA MASHTAKA ................................................................................. 120
7.7 Kuimarisha Kiwanda cha Upigaji Chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ................................... 120
7.8 SERIKALI ZA MITAA ...................................................................................................................... 121
7.8.1 Kusimamia Suala la Usafi ................................................................................................................ 122
7.8.2 Kuhamasisha Wananchi Kuunda Kamati za Maendeleo ................................................................. 123
7.8.3 Kuvijengea Uwezo Vikosi Maalum vya SMZ ................................................................................. 123
7.8.3.1 Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) .......................................................................... 124
7.8.3.2 Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ................................................................................................... 125
7.8.3.3 Kikosi Cha Valantia Zanzibar ....................................................................................................... 126
7.8.3.4 Kikosi Cha Mafunzo ..................................................................................................................... 127
7.9 Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ................................................................................................................ 127
vii
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
SEHEMU YA NANE
8.0 KUYAENDELEZA MAKUNDI MBALIMBALI ............................................................................. 131
8.1 WATOTO .......................................................................................................................................... 131
8.2 VIJANA .............................................................................................................................................. 132
8.2.2 Kukamilisha Uanzishaji wa Baraza la Taifa la Vijana .................................................................... 132
8.3 WANAWAKE .................................................................................................................................... 132
8.4 WAZEE .............................................................................................................................................. 134
8.5 WATU WENYE ULEMAVU ............................................................................................................ 135
8.5.1 Kubaini Watu Wenye Ulemavu Wanaoweza Kufanyakazi za Uzalishaji Mali ............................... 135
8.6 WAFANYAKAZI .............................................................................................................................. 135
8.6.1 Kuandaa Sera ya Hifadhi ya Jamii na Kufanya Mapitio ya Sheria za Kazi ..................................... 135
8.6.2 Kusimamia Utekelezaji wa Sera ya Ajira ........................................................................................ 136
8.6.3 Kuimarisha Mashirikiano kati ya Serikali, Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi na Waajiri
.................................................................................................................................................................. 137
8.6.4 Kuendelea Kuimarisha Mazingira bora na Maslahi ya Wafanyakazi .............................................. 137
SEHEMU YA TISA
9.0 MAENEO MENGINEYO MUHIMU ................................................................................................ 140
9.1 SEKTA YA SHERIA ......................................................................................................................... 140
9.1.1 Kuwaendeleza Wataalamu wa Sheria za Mikataba ......................................................................... 140
9.1.2 Kuyatafutia Ufumbuzi Masuala ya Mrundikano wa Kesi Mahakamani .......................................... 141
9.1.3 Kuwapatia Mafunzo Mahakimu wa Mahakama ya Mwanzo .......................................................... 141
9.1.4 Kukamilisha Mchakato wa Kutenganisha Shughuli za Upelelezi na Uendeshaji Mashtaka ........... 141
9.1.5 Msaada wa Kisheria ......................................................................................................................... 142
9.1.6 Kupeleka Huduma za Mahakama Karibu na Wananchi .................................................................. 142
9.1.7 Mapambano Dhidi ya Rushwa na Uhujumu wa Uchumi ................................................................ 143
SEHEMU YA KUMI
10. Changamoto Zilizojitokeza na Hatua za Kukabiliana Nazo ............................................................... 145
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
11. HITIMISHO ........................................................................................................................................ 147
viii
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
ORODHA YA JADWELI
Jadweli namba1: Takwimu za Ukuwaji Uchumi Zanzibar………………………………………10
Jadweli namba 2: Maeneo yaliyopimwa viwanja Zanzibar……………………………………...66
Jadweli namba 3: Idadi ya Nyumba za walimu zilizojengwa Unguja na Pemba………………..73
Jadweli namba 4: Takwimu za usajili wanachama waajiri 2010 – 2014……………………….128
Jadweli namba 5: Takwimu za usajili wanachama waajiriwa 2010 – 2014……………………128
Jadweli namba 6: Idadi ya Vijana waliosajiliwa kuomba kazi katika kituo cha kutoa taarifa za ajira
2010 – 2015……………………………………………………………………………….137
Jadweli namba 7: Idadi ya Vijana walioajiriwa kwa kuunganishwa na waajiri kupitia Kituo cha
kutoa taarifa za ajira 2010 – 2015………………………………………………………………137
Jadweli namba 8: Taasisi zilizofanyiwa Ukaguzi kazi 2010 – 2015…………………………...139
Jadweli namba 9: Ukaguzi wa Usalama na Afya Kazini 2010 – 2015…………………………139
ix
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
UFAFANUZI WA VIFUPISHO
AGOA - African Growth and Opportunity Act
AMR - Automated Meter Reading
AMREF - African Medical and Research Foundation
ARV - Anti Retroval Viruses
BADEA - Arab Bank for Economic Development in Africa
CATC DSM - Civil Aviation Training Center Dar-es-Salaam
CCM - Chama Cha Mapinduzi
CFP - Community Forests Pemba
CHAVIZA - Chama Cha Viziwi Zanzibar
CHEC - China Habour Engeneering Company
CPI - Consumer Price Index
CUZA - Cooperative Union of Zanzibar
DAMA - Department of Archives, Museum and Antiquities
EAC - East African Community
ECG - EchoCardioGraphy
EIA - Environmental Impact Assessment
EU - European Union
FEASSA - Federation of East Africa Secondary School Associations
GDP - Gross Domestic Product
HIMA - Hifadhi Misitu ya Asili
HIPZ - Health Improvement Project Zanzibar
ICAP - International Center for AIDS Care and Treament Programs
IFAD - International Fund for Agricultural Development
IMF - International Monetary Fund
IMO - International Maritime Organization
IMS - Institute of Marine Science
IRRI - Internationa Rice Reseach Institute
JICA - Japan Internation Cooperation Agency
JMZ - Jumuiya ya Maalbino Zanzibar
x
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
JUWAUZA - Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar
KMKM - Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo
KUC - Kenya Utalii College
MACEMP - Marine and Coastal Environment Management Project
MIMCA - Mnemba Island Marine Conservation Area
MKUZA II - Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar
MCC - Millenium Challenge Cooperation
MCU - Marine Conservation Unit
NACTE - National Council for Technical Education
NEC - National Electoral Commission
NGOs - Non Governmental Organizations
NORAD - Norwegian Agency for Development Co-operation
PECCA - Pemba Channel Conservation Area
PUM - Programma Uitzending Managers (Manager Deployment Program)
SACCOS - Savings and Credit Co-operatives Societies
SADC - Southern African Development Community
SADZ - Sports Association for Disable Physicaliy Zanzibar
SMASSE - Strengthening of Mathematics and Science in Secondary Education
SUMATRA - Surface and Marine Transport Regulatory Authority
TAKUKURU - Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
TAMSA - Tanzanian Medical Students Assossiation
TANESCO - Tanzania Electric Supply Company
TAP - Teachers Advancement Programs
TCRA - Tanzania Communication Regulatory Authority
TRTF - Tax Reform Task Force
TSP - Triple Supper Phosphates
TUKUZA - Tumia Umeme kwa Uangalifu Zanzibar
UKIMWI - Ukosefu wa Kinga Mwilini
UNDP - United Nation Development Programs
UNESCO - United Nation Education Scientific and Cultural Organization
UWZ - Umoja wa Walemavu Zanzibar
xi
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
VAT - Value Added Tax
VEHICLE - Vocational Education for Higher Categories and Levels
VVU - Virusi Vya UKIMWI
ZANAB - Zanzibar National Association of the Blind
ZAPDD - Zanzibar Association for People with Developmental Disabilities
ZAPHA+ - Zanzibar Assossiation for People Living with HIV/AIDS
ZARI - Zanzibar Agricultural Research Institute
ZATI - Zanzibar Association of Tourism Investors
ZATO - Zanzibar Association of Tours Operators
ZATOGA - Zanzibar Tour Guide Association
ZAWA - Zanzibar Water Authority
ZBC - Zanzibar Broadcasting Corporation
ZBS - Zanzibar Board of Standard
ZEC - Zanzibar Electoral Commission
ZFDB - Zanzibar Food and Drugs Board
ZIPA - Zanzibar Investment Promotion Authority
ZMA - Zanzibar Maritime Authority
ZSTC - Zanzibar State Trading Corporation
ZURA - Zanzibar Utility Regulatory Authority
1
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
SEHEMU YA KWANZA
1.0 UTANGULIZI
Awamu ya Saba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatekeleza mipango mbalimbali ya
maendeleo kwa kuzingatia muelekeo na malengo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM) ya mwaka 2010 hadi 2015. Malengo hayo yamewekwa katika Sekta za kiuchumi,
uzalishaji mali, miundombinu na huduma za kiuchumi, uwezeshaji wananchi kiuchumi, huduma
za kijamii na maeneo mengine ya kipaumbele. Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 - 2015
imetoa mazingatio maalum kwa Zanzibar kwa kuzingatia maeneo maalumu ya kisekta.
Katika kipindi cha miaka mitano (2010 - 2015), Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetekeleza
Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa mafanikio makubwa (wastani wa asilimia 90). Mafanikio hayo
yamepatikana chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein.
Mafanikio hayo ni pamoja na kuendelea kwa hali ya amani na utulivu hapa nchini, kuongezeka
kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka vianzio mbalimbali kufuatia kuziba mianya ya uvujaji
wa mapato hayo. Vilevile, mafanikio hayo yalitokana na kuimarika kwa utawala bora unaotilia
Rais wa Zanzibar wa Awamu ya Saba, Dkt. Ali Mohamed Shein akiapa kuwa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi tarehe 03 Novemba, 2010
2
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
mkazo suala la uwajibikaji ndani ya sekta ya umma, kuongezeka kwa mshikamano wa wananchi,
na kukua kwa sekta za kijamii na kiuchumi. Pia, mashirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi
yameimarika kwa kiwango kikubwa.
Sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 hadi 2015, Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar iliendelea kutekeleza Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza
Umasikini Zanzibar (MKUZA II) ambao unatekelezwa kupitia miradi mbalimbali ya kisekta kwa
lengo la kuimarisha hali za maisha ya wananchi wa Zanzibar. Aidha, katika kipindi cha miaka
mitano iliyopita miradi ya maendeleo imetekelezwa kwa mafanikio makubwa kwa kushirikiana na
jamii pamoja na washirika wengine wa maendeleo. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa madarasa
ya skuli, usambazaji wa maji, ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa jengo jipya la abiria katika
Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume na ujenzi wa njia ya maegesho katika uwanja huo
pamoja na ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba.
Taarifa hii ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawasilisha maeneo mbalimbali ya utekelezaji
wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano (2010 - 2015). Pia, inafafanua
changamoto zilizojitokeza katika kipindi hicho cha utekelezaji wa malengo ya Ilani yaliyowekwa.
SEHEMU YA PILI
3
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
2.0 HALI YA SIASA
Hali ya kisiasa Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015) imeendelea kuwa ya
amani na utulivu. Hali hii imetokana na Sera ya Msingi ya Chama cha Mapinduzi ya kuenzi Umoja
wa Kitaifa, Amani na Utulivu pamoja na wananchi kuzidi kuelewa umuhimu wa masuala haya.
Aidha, hali ya sasa imewezesha kuondokana na siasa za chuki na uhasama na wananchi
kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi na maendeleo katika maeneo yao.
2.1 Matukio Makubwa ya Kisiasa Yaliyotokea
2.1.1 Kufanyika kwa chaguzi ndogo kwa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliendesha uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la
Chambani Pemba. Aidha, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) iliendesha chaguzi ndogo za
Uwakilishi katika Majimbo matatu (3) ya Uzini, Bububu na Kiembe Samaki ambapo Wawakilishi
wa CCM walishinda kwa kishindo katika chaguzi hizo. Pia, chaguzi ndogo mbili (2) za udiwani
ziliendeshwa katika Wadi za Kiboje na Ng’ombeni ambapo kwa Wadi ya Kiboje mgombea wa
CCM alishinda.
2.1.2 Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo kulia na Mheshimiwa Hussein Ibrahim Makungu kushoto
wakila kiapo mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi baada ya kushinda chaguzi za Majimbo yao
ya Kiembe Samaki na Bububu
4
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
2.1.2 Maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilifanya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu
ambayo yalizinduliwa rasmi tarehe 15 Agosti, 2013 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein na kufikia kilele chake tarehe 12 Januari, 2014 katika
Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Madhumuni ya maadhimisho hayo ni kukumbuka Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari, 1964 yaliyoleta maisha bora kwa kila Mzanzibari na
kuondoa ubaguzi wa aina zote na kuleta umoja na maendelo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na
kiutamaduni kwa makundi yote katika jamii.
Katika maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zilifanyika ikiwemo usafi wa mazingira, michezo
na burudani, uwekaji wa mawe ya msingi pamoja na uzinduzi wa miradi. Jumla ya miradi 41
imewekewa jiwe la msingi na miradi 73 imezinduliwa wakati wa maadhimisho hayo.
Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Januari, 2014
5
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
2.1.3 Matukio ya Uvunjifu wa Amani
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kulijitokeza matukio mbalimbali yaliyoashiria uvunjifu
wa amani ambayo yalikuwa na nia ya kuifanya nchi isitawalike. Matukio hayo ni pamoja na
kuuawa kwa kiongozi wa dini, kumwagiwa tindikali kwa wageni, viongozi wa dini na Serikali
pamoja na mripuko wa bomu la kutupwa katika eneo la biashara la Darajani mjini Unguja. Aidha,
vilijitokeza baadhi ya vikundi vya wananchi kufanya vurugu kwa kuandaa mihadhara iliyodaiwa
kuwa ni ya kidini. Vikundi hivyo pia, vilifanya maandamano bila ya kupata kibali na kusababisha
uharibifu mkubwa wa mali za Serikali, Chama cha Mapinduzi na za wananchi pamoja na nyumba
za ibada. Vilevile, Maskani kadhaa na matawi ya Chama cha Mapinduzi yalichomwa moto na
askari mmoja wa Jeshi la Polisi kuuawa kikatili katika eneo la Bububu. Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar chini ya uongozi mahiri wenye hekima na busara wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mpinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein ilifanikiwa kudhibiti vurugu hizo
kwa kuwakamata waliohusika na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Mnara wa Kumbukumbu za Miaka 5O ya Mapinduzi ya Zanzibar Ukiwa hatua za
mwisho za Ujenzi katika Eneo la Michezani, Zanzibar
6
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
2.2 Masuala ya Muungano
Katika kipindi cha miaka mitano ya (2010-2015) nchi yetu iliadhimisha miaka 50 ya Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar. Kipindi hicho ni kirefu na nchi yetu ina kila sababu ya kujivunia
kutokana na kuudumisha Muungano wetu kwa muda wote huo. Mafanikio makubwa
yamepatikana kupitia Muungano wetu huu ikiwa ni pamoja na kuendelea kubaki katika hali ya
amani na utulivu katika nchi yetu na kuwepo kwa fursa ya kuendeleza na kuimarisha mahusiano
ya kidugu yaliyopo kati ya wananchi wa Tanzania bara na Zanzibar pamoja na kuimarisha
maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Maskani ya CCM ya Mwembe Kisonge iliyopo Michenzani iliyotiwa Moto na
wafuasi wa Kundi la Muamsho mwaka 2012
7
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
2.2.1 Vikao vya Pamoja vya Mashirikiano
Katika kuuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuzipatia ufumbuzi hoja za
Muungano wetu, Vikao mbalimbali vya Kamati ya Pamoja, Sektretariat na Vikao vya
Mashirikiano vya Kisekta vimefanyika ili kujadili na kutatua hoja zilizowasilishwa. Vikao vya
Pamoja viliwashirikisha Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar chini ya Uenyekiti wa Mheshimiwa Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jumla ya hoja 15 zimewasilishwa kwa kipindi
cha mwaka 2010 hadi 2015 ambapo hoja 10 tayari Serikali zetu mbili zimefikia makubaliano
muafaka na hoja tano (5) zilizobakia ziko katika hatua ya kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu. Hoja
zilizopatiwa ufumbuzi ni:-
i. Utekelezaji wa Sheria ya Haki za Binaadamu Zanzibar.
ii. Uvuvi kwenye ukanda wa Bahari Kuu.
iii. Utekelezaji wa “Merchant Shipping Act” katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Uwezo wa Zanzibar Kujiunga na IMO.
iv. Mgawanyo wa Mapato. Hoja hii imegusa vipengele viwili.
Mgawanyo wa Mapato yatokanayo na Misaada kutoka nje.
Misaada ya mikopo ya fedha kutoka IMF.
Kushoto Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi la
maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kulia tamasha la halaiki siku ya Kilele
cha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
8
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
v. Uwezo wa Zanzibar kukopa ndani na nje ya nchi.
vi. Malalamiko ya Wafanyabiashara wa Zanzibar kutozwa kodi mara mbili.
vii. Ongezeko la gharama za Umeme kutoka TANESCO kwenda ZECO.
viii. Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
ix. Ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
x. Ajira kwa Watumishi wa Zanzibar katika Taasisi za Muungano.
Hoja ambazo ziko katika hatua za kutafutiwa ufumbuzi ni:-
i. Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia.
ii. Usajili wa vyombo vya moto.
iii. Tume ya Pamoja ya Fedha.
iv. Kodi nyenginezo (PAYEE).
v. Ushirikiano wa Zanizibar na Taasisi za Nje.
2.2.2 Mchakato wa Kuandaa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zilianzisha
mchakato wa kutayarisha Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mchakato huo
ulipitia katika hatua mbalimbali ikiwemo utungwaji wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 2013,
kuundwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ukusanyaji wa maoni ya wananchi, kuandaa na
kujadiliwa Rasimu ya Awali ya Katiba katika Mabaraza ya Katiba na hatimae Bunge Maalumu la
Moja ya Kikao cha Kamati ya Pamoja cha SMT na SMZ chini ya Uenyekiti wa Makamu wa Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa na Waziri Mkuu
Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi
9
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Katiba na kupatikana kwa Katiba Inayopendekezwa ambayo inasubiri hatua ya kupigiwa kura na
wananchi. Katiba hiyo inayopendekezwa inagusa makundi yote ya jamii wakiwemo watu wenye
ulemavu, wanawake na watoto, vijana na wazee, wafanyakazi, wakulima, wavuvi, wafugaji na
wafanyabiasha. Pia, Katiba hiyo inayopendekezwa imelenga kuimarisha zaidi Muungano wa
Tanzania kwa kuyapatia ufumbuzi masuala yote yaliyotajwa kama ni changamoto za Muungano.
SEHEMU YA TATU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
Wakizionyesha Nakala za Katiba Inayopendekezwa katika Uwanja wa Jamhuri -Dodoma
10
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
3.0 SEKTA YA KIUCHUMI
Katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2010 hadi 2015, Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imeendeleza mafanikio yote ya kiuchumi yaliyopatikana nchini ikiwemo
kutekeleza Sera na Sheria za Uwekezaji pamoja na ujenzi wa msingi wa uchumi endelevu
unaoendeshwa kwa nguvu za soko.
3.1 Ukuaji wa Uchumi
Uchumi wa Zanzibar umeendelea kuonyesha mwenendo mzuri wa ukuaji mwaka hadi mwaka.
Katika kipindi cha miaka mitano, uchumi wa Zanzibar umekuwa kutoka asilimia 6.4 mwaka 2010
hadi asilimia 7.4 mwaka 2014. Aidha, mfumko wa bei ulikuwa ukipanda na kushuka katika kipindi
cha miaka mitano (5). Mwaka 2010/2011 mfumko wa bei ulikuwa wa wastani wa asilimia 6.1 na
ulipanda kufikia asilimia 14.7 mwaka 2011/2012 na mwaka 2013/14 ulishuka na kufikia kiwango
cha asilimia 5. Takwimu za ukuaji huo zinaonekana katika jedwali namba 1.
Jadweli namba 1. Takwimu za ukuaji wa uchumi Zanzibar (2010-2014)
KIASHIRIA 2010/11 2011/12 2012/13 2013/14
Ukuaji wa Pato la Taifa % 6.4 6.6 7.1 7.4
Mfumko wa bei % 6.1 14.7 9.4 5
Ukuaji huo wa uchumi wa mwaka hadi mwaka umechangiwa kwa kiasi kikubwa na mambo
yafuatayo:
Kuimarika kwa Sekta ya Kilimo, Misitu na Uvuvi;
Kuimarika kwa Sekta ndogo ya Uzalishaji wa Viwanda;
Kuimarika kwa Sekta ya Huduma kulikochangiwa na ongezeko la ukuaji wa Sekta
ndogo ya Hoteli na Mikahawa;
Kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaoingia nchini mwaka hadi mwaka;
Kuwepo kwa hali ya utulivu, amani na mshikamano wa wananchi ambayo imejenga
mazingira mazuri ya kuwekeza na kufanyakazi kunakoleta tija kwa nchi yetu.
Chanzo: Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, 2014
11
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
3.2 Mfumko wa Bei
Kwa ujumla kasi ya mfumko wa bei imeshuka kutoka asilimia 6.1 mwaka 2010 hadi asilimia 5.0
mwaka 2013. Hata hivyo, kwa kipindi cha mwaka 2011 hali ya mfumko wa bei ilipanda zaidi hadi
kufikia asilimia 14.7 kutokana na sababu za kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la Dunia na
kushuka kwa thamani ya Sarafu ya Tanzania. Kushuka kwa mfumko wa bei mwaka 2013
kulitokana na juhudi za Serikali katika kudhibiti mfumko wa bei ikiwemo kutoa ruzuku za
pembejeo za kilimo kwa wakulima ambako kulipelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya
chakula nchini. Aidha, mfumko wa bei uliendelea kushuka kutokana na Serikali kuendelea kutoa
misamaha ya kodi kwa bidhaa muhimu za chakula kama vile Unga, Sukari na Mchele na kushuka
kwa bei za bidhaa za mafuta na chakula katika Soko la Dunia.
3.3 Mapato na Matumizi ya Serikali
Miongoni mwa mafaniko ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka
mitano ni ongezeko la ukusanyaji wa mapato kutoka vianzio mbalimbali vilivyopo nchini. Kwa
ujumla mapato ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yameonyesha kuongezeka kutoka Shilingi
bilioni 181 kwa mwaka 2010/11 hadi kufikia Shilingi bilioni 330 mwaka 2013/2014. Makusanyo
hayo ya Shilingi bilioni 330.0 zilizokusanywa ni sawa na asilimia 94 ya makadirio ya Shilingi
bilioni 338.45. Ongezeko hilo la mapato ya ndani limetokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa
na Serikali zikiwemo kuziba mianya ya uvujaji wa mapato ya nchi kwa kuyafanyia kazi
mapendekezo yaliyotolewa kupitia maabara ya upatikanaji wa rasilimali fedha “resource
mobilization” na mapitio ya Sekta ya Fedha.
3.3.1 Kushuka kwa Kiwango cha Nakisi ya Bajeti
Katika kukabiliana na ukuaji mkubwa wa mahitaji ya nchi, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali fedha ambao utaendana na
mahitaji ya nchi yetu ili kushusha nakisi ya bajeti kutoka uwiano wa asilimia 9.2 ya Pato la Taifa
la mwaka 2007/2008 na kufikia asilimia 8.0 katika mwaka 2014/2015. Miongoni mwa jitihada
zilizofanikisha ushushaji wa nakisi ya bajeti ni pamoja na kuimarika kwa usimamizi wa ukusanyaji
mapato pamoja na kutumika kwa hatua kadhaa za mikakati ya kuimarisha mapato katika kipindi
hicho. Mikakati hiyo ni pamoja na kufanya marekebisho ya sheria na viwango vya kodi na ada
mbalimbali zikiwemo marekebisho ya Sheria ya Ongezeko la Thamani (VAT), Sheria ya Kodi za
Hoteli, Sheria ya Ada za Bandari, Ushuru wa Stempu, Sheria ya Kodi ya Mafuta pamoja na Sheria
12
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
ya Usafiri wa Barabarani. Pamoja na jitihada zilizofanywa, Serikali ilichukua hatua kadhaa za
kiutawala na utendaji ambazo zimesaidia sana kuongeza ukusanyaji wa Mapato ya Serikali.
3.4 Kuimarisha Maeneo Huru ya Kiuchumi ya Fumba.
Serikali imeanza kutekeleza ahadi ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015 ya
kuendeleza Maeneo Huru ya Kiuchumi ya Fumba. Katika utekelezaji wa ahadi hii, Serikali
imechukuwa hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutayarisha Mpango Mkuu wa Matumizi ya
Ardhi Fumba, upimaji na utayarishaji wa mchoro wa ramani ya eneo hilo. Jumla ya hekta 3,000
zimepimwa na kugaiwa kwa matumizi tofauti ambapo hekta 743 zimetengwa kwa ajili ya
uwekezaji wa shughuli za kibiashara, hekta 1,310 kwa ajili ya vijiji vya asili na makaazi na hekta
946 kwa ajili ya eneo la akiba. Pia, Serikali imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa njia kuu ndani ya
eneo la uwekezaji Fumba yenye urefu wa kilomita 10 kwa kiwango cha lami. Hatua ya
kutengeneza njia ndogondogo tatu za ndani ambapo njia moja yenye urefu wa kilomita mbili
kuanzia skuli ya Bwefum-Kororo imekamilika na kazi ya kushughulikia njia nyengine mbili za
Bweleo – Pwani na Dimani – Fumba inaendelea.
Vilevile, katika uendelezaji wa utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Eneo Huru la Kiuchumi Fumba,
Serikali imekamilisha mazungumzo na Muwekezaji wa Kampuni mama ya Bakheressa Group juu
ya kushirikiana katika uwekezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Kisasa wa Fumba (Fumba Bay
Satillite City). Kwa sasa kiwanda kikubwa cha usarifu maziwa cha Azam Dairy Milk na Zanzibar
Fiber Glass tayari vimeanzishwa na vinaendelea na kazi na miradi mengine ya huduma na nyumba
za makaazi imo katika hatua za awali. Kutekelezwa kwa miradi ya aina hii katika eneo hilo la
Fumba kunatarajiwa kuzalisha ajira zaidi kwa wananchi pamoja na kukuza Pato la Taifa. Aidha,
Serikali imeanza hatua za utekelezaji wa miradi mikubwa ikiwemo mradi wa ujenzi wa mji
mdogo wa kisasa, mradi wa uanzishaji wa Eneo la Viwanda (Industrial Park) na mradi wa
kujenga Kituo kikubwa cha Mikutano cha Kimataifa (Zanzibar International Convention Centre).
13
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
3.5 Uwakilishi wa Sekta Binafsi katika Vikao Mbalimbali
Serikali kupitia Wizara ya Fedha imeendelea kushirikiana na Sekta Binafsi katika vikao
mbalimbali ambavyo vinaimarisha utendaji kazi wa Serikali. Kwa sasa Sekta Binafsi
zinauwakilishi katika vikao vya kuimarisha mapato “Tax Reform Task Force (TRTF)”, vikao vya
kujadili Pato la Taifa (GDP), Faharisi ya Bei ya Mlaji “Consumer Price Index (CPI)” na vikao vya
kuratibu misaada kwa taasisi zisizo za kiserikali (“Aid Cordination Meeting for NGOs”). Lengo
kuu la uwakilishi huo ni kuendelea kuwavutia wawekezaji wa ndani ili wawekeze katika sekta
mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
3.6 Kuandaa Mazingira Bora ya Kiuchumi ili Kuvishawishi Vyombo vya Fedha Kutoa
Mikopo Yenye Masharti Nafuu.
Katika kuandaa mazingira bora ya kiuchumi, Serikali imeifanyia marekebisho Sheria ya Fedha ili
kuweza kuendana na mazingira halisi ya kiuchumi. Aidha, Serikali imefanya mapitio ya Sekta ya
Fedha na kuweza kuziona kasoro zilizopo na kuzifanyia kazi. Vilevile, Sera ya Sekta ndogo ndogo
za Fedha imeandaliwa na kuanza kutumika. Sera hiyo inatoa muongozo wa kuwawezesha
wajasiriamali wadogo kujipatia mitaji kwa urahisi.
Jengo na Mitando ya Kiwanda cha Fiber Glass katika Maeneo Huru ya Kiuchumi - Fumba
14
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Pia, Serikali imeimarisha huduma za mikopo kwa wajasiriamali wadogo wadogo kwa kuunganisha
mifuko iliyokuwepo na kuanzisha Mfuko mmoja unaojulikana kama Mfuko wa Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi. Madhumuni ya kuanzishwa kwa Mfuko huo ni kutanua fursa za mikopo
nafuu kwa wajasiriamali, hususan wanawake, vijana na watu wenye kipato cha chini, ili waweze
kuanzisha na kuimarisha shughuli za kiuchumi zitakazowasaidia kujiajiri na kunyanyua kipato
chao. Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi una mtaji wa mikopo (Revolving Loan Fund)
wenye thamani ya Shilingi bilioni 2.3. Sambamba na hayo, Serikali katika kipindi cha miaka
mitano iliyopita imetoa mikopo 1,603 yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.45 katika Shehia 305 za
Unguja na Pemba, ambayo imetoa jumla ya ajira za moja kwa moja 20,614 kwa makundi
mbalimbali. Kati ya waliofaidika na ajira na kujihakikishia kipato ni wanaume 8,741 na wanawake
11,873. Aidha, Serikali imeweka fedha za dhamana (Shilingi 100,000,000) katika Benki ya CRDB
ili kuviwezesha vikundi vya vijana kujipatia mikopo kutokana na dhamana hiyo.
3.7 Kuanzisha Maeneo Mapya ya Kiuchumi
Serikali imeendelea kuzitangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini kwa kupitia njia mbalimbali,
ikiwemo kuimarisha tovuti yake (www.zanzibarinvest.org) na kuitafsiri katika lugha za kigeni
(Kichina, Kituruki na Kirusi) ili kufikia Soko la Kimataifa. Hatua hii itasaidia kutangaza fursa
zilizopo za uwekezaji kwa kuwavutia wawekezaji kutoka nchi hizo kuja kuwekeza nchini. Kupitia
juhudi hizo wawekezaji kutoka Poland wamewekeza miradi minne (4) yenye mtaji wa Dola za
Kimarekani 29,471,549. Aidha, Serikali katika kipindi hiki imepokea ujumbe wa wawekezaji
kutoka Marekani, Uholanzi, Urusi, Croatia, Uturuki na China kwa lengo la kuona fursa zaidi za
uwekezaji nchini. Pia, Serikali ilipokea ugeni kutoka Ubalozi wa Thailand ulioko Nairobi na
kukubaliana kushirikiana katika uwekezaji. Serikali kupitia Mamlaka ya Uwekezaji imefanya ziara
za kujitangaza katika nchi mbalimbali ikiwemo Marekani, China, Uturuki na Uholanzi.
3.8 Miradi Iliyowekezwa kwa Kipindi cha 2010 - 2015
Katika kipindi cha 2010 - 2015 Serikali imeweza kuidhinisha jumla ya miradi 153 ya uwekezaji
yenye mtaji wa Dola za Kimarekani 1,493,139,968. Kati ya miradi hiyo, miradi 63 inamilikiwa
na wawekezaji wazalendo. Miradi hiyo inatarajiwa kutoa ajira zipatazo 6,658 kwa wananchi, hali
hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira nchini. Sekta ya Utalii inaongoza kwa kuwa na asilimia 52
ya miradi iliyoidhinishwa kwa kipindi hiki. Aidha, Serikali imefanya tafiti mbalimbali ikiwemo
15
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
utafiti wa kuibua maeneo mapya ya kuwekeza na kufanya utafiti wa mwenendo wa Mitaji Binafsi
ili kuona namna gani mitaji hiyo inatoa mchango katika uchumi wa nchi.
SEHEMU YA NNE
16
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
4.0 SEKTA ZA UZALISHAJI MALI
4.1 KILIMO
Sekta ya Kilimo bado inaendelea kuwa ni mhimili mkuu wa uchumi wa Zanzibar na inatoa
mchango wa moja kwa moja kwa wananchi katika kujikimu kimaisha. Sekta hii pia ni muhimu
kwa kukuza hali ya uhakika wa chakula na kuimarisha lishe na afya za wananchi walio wengi
vijijini na mijini. Kwa wastani Sekta hii inachangia asilimia 30 ya Pato la Taifa na inakadiriwa
kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wanategemea Sekta ya Kilimo kwa kuwapatia ajira na
kipato. Kwa kipindi cha miaka mitano, Serikali imetekeleza mambo mbalimbali katika kuimarisha
na kuendeleza Sekta ya Kilimo.
4.1.1 Kutekeleza Mkakati wa Uimarishaji wa Zao la Karafuu
Serikali imetekeleza mkakati wa kuliimarisha zao la karafuu ambao umeanza kutoa mafanikio kwa
kuongezeka kwa kiwango cha uoteshaji wa miche na uzalishaji wa zao la karafuu kwa ujumla.
Jumla ya miche 2,216,328 katika vitalu mbalimbali vya Unguja na Pemba imezalishwa katika
kipindi cha 2010 - 2015. Kati ya miche hiyo, miche 1,339,192 imetolewa na kusambazwa kwa
wakulima bila malipo kwa ajili ya kupandwa mashambani ambapo wastani wa asilimia 44 ya
miche hiyo imeota. Vilevile, Serikali imeongeza bei ya zao la karafuu kwa wakulima kutoka
Shilingi 4,500 (2010) hadi kufikia Shilingi 14,000 (2014) kwa kilo moja. Hali hii imewahamasisha
zaidi wakulima kulishughulikia na kuongeza uzalishaji wa zao hilo kutoka tani 2,673 mwaka 2010
na kufikia tani 5,340 mwaka 2014.
17
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Pia, Serikali imefanya tathmini ya Sensa ya Miti (Woody Biomass Survey) mwaka 2013 ambayo
imeonesha kwamba, Zanzibar kwa sasa ina idadi ya mikarafuu 4,131,783 (Unguja 277,196 na
Pemba 3,854,587). Tathmini hiyo pia inaonyesha kuwa asilimia 60 ya Mikarafuu ni midogo yenye
umri kati ya mwaka mmoja hadi sita. Hivyo, Zanzibar bado inayo nafasi ya kuongeza uzalishaji
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akikagua miche ya mikarafuu katika vitalu - Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akiangalia zao la karafuu alipotembelea katika shamba la Bw.Said Sinani
Shumbageni Kusini Pemba
18
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
wa karafuu kwa wingi zaidi kwa siku zijazo. Aidha, Serikali katika kuendeleza zao la karafuu,
mwaka 2013 ilianzisha mashamba darasa 20 ya mikarafuu (Pemba 12 na Unguja 8) kwa ajili ya
kuotesha miche bora na kutoa taaluma ya uzalishaji wa mikarafuu kwa wakulima.
4.1.2 Kuimarisha Miundombinu ya Umwagiliaji Maji
Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji maji ili kukabiliana na mabadililiko
ya hali ya hewa pamoja na kuongeza uzalishaji na kipato kwa wakulima. Katika kipindi cha miaka
mitano, jumla ya hekta 800 (2014) kutoka hekta 600 (2010) zimeimarishwa miundombinu ya
umwagiliaji maji. Pia, mita 170 za misingi zimejengwa kwa saruji na mita 200 kwa udongo, mita
670 zimefanyiwa matengenezo na vigingi 50 vimejengwa kwa Unguja na Pemba. Aidha, matuta
kwa ajili ya misingi ya kumwagilia maji mita 2,000 yamejengwa pamoja na kazi ya kupima na
kusanifu misingi ya kutolea maji machafu (Drainage) mita 4,000 imefanyika. Aidha, maeneo 40
ya uvunaji wa maji ya mvua yameanzishwa na wakulima 2,000 wamefaidika Unguja na Pemba.
Pia, kazi ya ujenzi wa bwawa la kukusanyia maji imeanza katika bonde la Mtwango. Jumla ya
wakulima 8,000 kati ya wakulima 28,000 wanaolima zao la mpunga wameongeza uzalishaji
kutoka tani 1.3 na kufikia tani 3.8. Aidha, Serikali inaendelea na kazi ya kupima, kuchora ramani
na kusanifu miundombinu ya umwagiliaji maji katika vituo vya Cheju, Kilombero, Chaani,
Mlemele na Makwararani maeneo ambayo yanajumuisha hekta 2,105.
Kushoto Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata
maelezo wakati alipotembelea na kukagua miundombinu na maendeleo ya Kilimo cha Umwagiliaji wa
Mpunga katika Bonde la Bumbwisudi Zanzibar
19
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
4.1.3 Kuendeleza Programu za Tafiti za Kilimo na Maliasili kwa Kuwashirikisha Wakulima
na Washiriki Wengine
Serikali imeendelea na jitihada zake katika kuendeleza tafiti tofauti za kilimo na maliasili pamoja
na kusambaza matokeo ya tafiti hizo kwa wakulima na wadau wengine wa kilimo kupitia Taasisi
ya Utafiti wa Kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija.
4.1.3.1 Utafiti wa Mazao ya Nafaka na Jamii ya Kunde
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Zanzibar (ZARI), imefanya na kuendeleza tafiti mbalimbali katika
mazao ya nafaka na jamii ya kunde kwa mashirikiano na taasisi za utafiti za Kanda ya Afrika
Mashariki na Kati chini ya uratibu wa Kanda ya IRRI. Katika tafiti za zao la mpunga, ZARI
ilifanya uchunguzi wa awali wa mbegu 28 za mpunga kutoka IRRI katika bonde la umwagiliaji
maji la Mtwango, aina 15 ya mbegu za mpunga kutoka IRRI zilijaribiwa katika bonde la utafiti wa
mpunga Mwera-Barabarani. Uchunguzi wa awali wa aina 7 za mbegu za mpunga kutoka Vietnam
katika kituo cha utafiti wa mpunga Mwera (Unguja) na Tungamaa (Pemba) umeonesha kuwa
mbegu zote zinafaa kuendelezwa na hatua nyengine za jaribio zinaendelea. Katika tafiti shirikishi
ya uchunguzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, kila nchi ilitakiwa itoe mbegu mbili kwa
ajili ya jaribio hilo ambapo mbegu ya SUPA BC ilijitokeza kuwa ni miongoni mwa mbegu
zilizofanya vizuri.
4.1.3.2 Jaribio la Mbolea Mpya na Mafunzo kwa Wakulima Chini ya Mradi wa NAFAKA
Katika kipindi cha miaka mitano, Serikali imeendelea na majaribio ya mbolea mpya za kilimo
zikiwemo za YaraMilla na UDP. Majaribio hayo yalifanyika katika vituo vya kilimo Kizimbani,
Ole na Bumbwisudi. Matokeo ya awali ya tafiti hizo yamepatikana na kuonyesha kuwa YaraMilla
Shamba la majaribio la mpunga la Cheju juu ya Utafiti wa matumizi ya mbolea aina ya
YARAMILLA
20
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
na UDP zimefanya vizuri kwa asiliamia 60 katika mpunga wa kutegemea mvua na asilimia 49
katika mpunga wa umwagiliaji maji ukilinganisha na TSP na Urea ambazo zimezoeleka. Serikali
imetoa mafunzo ya nadharia na vitendo kwa wakulima 400 juu ya mbinu bora za kilimo cha
mpunga cha umwagiliaji maji. Aidha, wakulima 2,000 (700 Pemba na 1,300 Unguja) walipatiwa
mafunzo ya mbinu bora za uzalishaji mpunga katika mashamba darasa 40 ambapo kila shamba
walifundishwa wakulima 50.
4.1.3.3 Ruzuku katika Kilimo
Serikali inaendelea kutoa ruzuku za pembejeo na huduma za matrekta kwa lengo la kuimarisha
uzalishaji wa mazao mbali mbali, hasa zao la mpunga. Katika kipindi cha miaka mitano (2010 –
2015), Serikali imetoa ruzuku ya jumla ya shilingi 7,129,591,148 za kuendeleza kilimo, kwa ajili
ya ununuzi wa mbolea, madawa, mbegu na kutoa huduma za matrekta kwa wakulima. Katika
kufanikisha suala hili la ruzuku, Serikali imepunguza bei ya mbolea kutoka bei halisi ya soko ya
shilingi 80,000 hadi shilingi 10,000 kwa mfuko wa kilo 50 (sawa na ruzuku ya asilimia 88). Pia,
imepunguza bei ya madawa kutoka shilingi 25,000 hadi shilingi 10,000 kwa lita (ambayo ni ruzuku
ya asilimia 60), na bei ya mbegu ya mpunga kutoka shilingi 2,500 hadi shilingi 200 kwa kilo (ikiwa
ni ruzuku ya asilimia 92). Vile vile, wakulima wanalipia shilingi 16,000 tu kwa ekari moja kwa
ajili ya kupatiwa huduma za matrekta (kuchimba na kuburuga) kutoka bei halisi ya shilingi 30,000
(hii ni ruzuku ya asilimia 57). Zaidi ya kaya 60,000 (wastani wa wakulima 360,000) zinafaidika
na ruzuku zinazotolewa na Serikali katika Kilimo kwa Unguja na Pemba.
Picha ya Shamba darasa la Mpunga huko Bumbisudi
21
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
4.1.3.4 Tafiti za Mazao ya Mizizi (Muhogo na Viazi Vitamu)
Katika jitihada za kutafuta mbegu bora za mazao ya mizizi, Serikali imefanya majaribio ya mbegu
bora aina saba (7) za muhogo katika maeneo matano (5) ya mashamba ya wananchi Unguja na
Pemba. Maenoeo hayo yapo katika vijiji vya Kizimbani, Bungi na Chaani kwa Unguja na
Matangatuani na Pembeni kwa Pemba. Tafiti hizo zinaonyesha kwamba asilimia 50 ya mbegu
zinafaa kutokana na kuvumilia maradhi na wadudu. Aidha, Serikali imefanya majaribio ya viazi
vitamu yalioyojumuisha aina 34 za mbegu katika maeneo sita (6) ambayo ni Bambi, Kizimbani na
Kilombero kwa Unguja na Makangale, Mjimbini na Matangatuani kwa Pemba. Sambamba na kazi
hizo, Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar imeendelea kuhifadhi
mbegu 36 za kienyeji na za kigeni kwa ajili ya kutunza viini vya kijenitiki (Genetic Resources
Conservation).
4.1.3.5 Uboreshaji wa Miundombinu ya Utafiti
Serikali kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar kwa kushirikiana na wadau wengine wa
maendeleo imekamilisha ujenzi wa maabara mpya ya utafiti wa mpunga pamoja na ukarabati wa
maabara ya udongo na maabara ya usarifu wa mazao. Maabara hizo zimechangia katika kuongeza
juhudi za utafiti wa mazao ya chakula na biashara.
Muhogo uliolimwa kutokana na Mbegu Bora iliyofanyiwa Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu katika
Shamba la Kizimbani
22
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
4.1.4 Kuhimiza na Kushajiisha Matumizi ya Pembejeo na Mbinu Bora za Kilimo
Serikali imenunua Matrekta mapya 45 kutoka SUMA JKT – Tanzania Bara (18 Pemba na 27
Unguja) na imepokea matrekta 20 kutoka SUMA JKT Bara, Matrekta 10 yamepelekwa Pemba.
Vile vile, Serikali imenunua mashine za kuvunia mpunga 14 (Combine harvester) na kuyafanyia
matengenezo matrekta 37 (Pemba 13 na Unguja 24). Aidha, Serikali imenunua jumla ya Tani
5,870.5 za mbolea ya TSP na Urea na kusambazwa kwa wakulima Unguja na Pemba pamoja na
lita 68,000 za dawa ya kuulia magugu. Aidha, Jumla ya tani 2,145.6 za mbegu ya mpunga, tani 20
za mbegu ya kunde zimenunuliwa na kusambazwa kwa wakulima na tani 623 ya mbegu ya mpunga
aina ya BKN Supa imezalishwa kupitia wakulima wa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia tafiti mbalimbali
katika maabara ya utafiti katika Chuo cha Kilimo Kizimbani
Matrekta kutoka SUMA JKT yakifanya kazi za kutayarisha mashamba katika Bonde la
Kilombero
23
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Jitihada hizi zimewezesha kuongeza eneo la uzalishaji kutoka ekari 10,000 mwaka 2010 hadi
kufikia ekari 34,000 mwaka 2014. Aidha, kumekuwepo na ongezeko la idadi ya kaya
zinazojihusisha na kilimo cha mpunga kutoka kaya 10,000 mwaka 2010 hadi kufikia kaya 70,000
mwaka 2014. Vilevile kumekuwepo ongezeko la uzalishaji wa mpunga kutoka tani 20,000 mwaka
2010 hadi kufikia tani 33,655 mwaka 2014.
4.1.5 Kuendelea Kuhimiza na Kutilia Mkazo Mafunzo na Matumizi ya Kanuni za Kilimo
Bora kwa Mazao ya Chakula, Biashara na Matunda
Serikali imeendelea kutoa mafunzo kwa wakulima kupitia njia ya kuwatembelea wakulima
mashambani, mashamba darasa na skuli za wakulima. Aidha, mafunzo kwa wakulima pia
yamekuwa yakitolewa kupitia Chuo cha Kilimo cha Kizimbani. Katika kuendeleza utoaji wa
huduma za elimu kwa wakulima, Serikali imeongeza idadi ya mabwanashamba/mabibishamba
kutoka 172 mwaka 2010 hadi kufikia 212 mwaka 2015. Pia, mitego 85,000 ya kunasia nzi
waharibifu wa matunda imesambazwa kwa wakulima, Unguja na Pemba.
4.1.6. Uimarishaji wa Chuo cha Kilimo Kizimbani
Katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 - 2015 Serikali imekiimarisha Chuo cha
Kilimo Kizimbani katika utoaji wa mafunzo na ujenzi wa miundombinu. Kwa upande wa mafunzo,
jumla ya vijana 48 wamemaliza mafunzo ya kilimo na mifugo katika ngazi ya Diploma na Vijana
300 katika ngazi ya Cheti. Aidha, Chuo kinaendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi 140 wa ngazi
ya cheti na 50 kwa ngazi ya Diploma. Pia, walimu 10 wa chuo hicho wanaendelea na masomo
ngazi ya Shahada ya Pili (Masters) na mwalimu mmoja (1) anaendelea na masomo ya Shahada ya
Tatu (PhD). Kwa upande wa miundombinu, Serikali imejenga Dakhalia ya wanafunzi wa kike
yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 28 kupitia msaada kutoka IFAD pamoja na michoro ya
Ujenzi wa Dakhalia yenye ghorofa 4 na uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 umekamilika. Aidha,
ukarabati wa mabweni mawili (2), madarasa manne (4) na majengo mawili (2) ya ofisi umefanyika
pamoja na matengenezo na ununuzi wa vifaa vya maabara ya mifugo, maktaba, samani na vifaa
mbalimbali. Vilevile, katika kuimarisha elimu inayotolewa, ununuzi wa vifaa vya kufundishia na
vitendea kazi ikiwemo vitabu 860 vya kiada na ziada na kompyuta 50 zimenunuliwa na kuanza
kutumika.
24
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi akifungua na kukagua Jengo la Dakhalia
ya Chuo cha Kilimo Kizimbani
25
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
4.1.7 Kutekeleza Mkakati wa Kuanzisha Akiba ya Chakula ya Zanzibar (National Food
Reserve)
Katika utekelezaji wa Mkakati wa Kuanzisha Akiba ya Chakula Zanzibar kwa lengo la
kuhakikisha upatikanaji wa kuaminika wa chakula pamoja na kuwa na chakula cha akiba kwa ajili
ya kukabiliana na dharura ya ukosefu na upungufu wa chakula nchini unaoweza kusababishwa na
hali ya ukame, mafuriko na majanga mengine ya asili, Serikali inaendelea kutekeleza mpango
wake wa kuanzisha Hifadhi ya Chakula kwa kuanza kuyafanyia ukarabati maghala mawili
makubwa yaliyopo Tibirinzi - Pemba na Malindi - Unguja. Vilevile, Serikali imetayarisha
miongozo ya kisheria na taratibu juu ya uendeshaji na usimamiaji wa hifadhi hiyo ikiwemo;
Muongozo wa Kazi na Taratibu za Uendeshaji na Kanuni za Kusimamia hifadhi kwa lengo la
kuweka utaratibu na mfumo wa kisheria katika uendeshaji na usimamiaji wa hifadhi ya chakula
nchini. Aidha, Serikali imeanza utayarishaji wa Programu maalumu ya kuongeza uzalishaji wa
mpunga kwa ajili ya Hifadhi ya Chakula. Mikakati ya Serikali ni kuongeza ufanisi katika
uzalishaji wa mpunga na hatimae Hifadhi ya Chakula iendeshwe kwa kutegemea mpunga
unaozalishwa nchini na kupunguza utegemezi wa mchele kutoka nje ya nchi.
Wanafunzi wa Chuo cha Kilimo Kizimbani wakiwa katika masomo kwa vitendo
26
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
4.2 UFUGAJI
Ili kuleta mapinduzi ya ufugaji nchini, Chama cha Mapinduzi kupitia Ilani ya Uchaguzi ya mwaka
2010-2015 iliagiza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushughulikia utekelezaji wa sera na sheria ya
mifugo pamoja na programu na miradi mbalimbali zitakazowezesha wafugaji wadogo wadogo
kuendeleza ufugaji wa kisasa. Aidha, Ilani hiyo iliagiza kuimarishwa kwa kazi za utafiti na huduma
za kinga na tiba ya mifugo na kuendeleza vituo vya huduma za ufugaji na huduma za kinga na tiba
ya mifugo.
Katika kusimamia utekelezaji wa Ilani, Serikali imesimamia matibabu ya wanyama ambapo jumla
ya wanyama 240,108 walitibiwa, wanyama 258,350 walichanjwa na wanyama 103,688
walikogeshwa. Pia, katika kuikinga Zanzibar na magonjwa yasiyo na mipaka, jumla ya sampuli
3,658 za maziwa na 2,505 za damu zimefanyiwa uchunguzi wa ‘bacteria na fungus’, sampuli
4,034 za kinyesi kwa ajili ya uchunguzi wa minyoo, na sampuli tofauti 3,000 (2,922 za maziwa,
30 za kuku na 48 za maji) zimeoteshwa katika maabara za Wizara.
Aidha, wanyama 14,626 walikaguliwa katika Kituo cha Karantini cha Kisakasaka, wanyama hao
ni pamoja na ng'ombe, mbuzi, kondoo, jamii ya ndege na wanyama wengineo. Katika kituo cha
bandarini jumla ya wanyama na jamii za ndege 5,105,352 walikaguliwa na katika kituo cha
Uwanja wa Ndege wanyama na ndege 731,802 pia walikaguliwa. Vilevile, katika ukaguzi wa
wanyama waliochinjwa, Ng’ombe 41,180, Mbuzi 5,538 na Kondoo 3,310 walikaguliwa.
Ghala za Akiba ya Chakula kwa Unguja na Pemba
27
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Aidha, kupitia mradi wa kichaa cha mbwa, jumla ya mbwa 19,822 na paka 5,577 walipatiwa
chanjo dhidi ya maradhi hayo. Vilevile, jumla ya mbwa 3,507 na paka 1,693 walifungwa uzazi.
Mbwa 3,595 na paka 1,319 walipatiwa matibabu ya maradhi mbalimbali, kati yao mbwa 9,945 na
paka 2,142 walipatiwa dawa za minyoo, na mbwa 4,702 na paka 1,258 waliogeshwa ili kuwakinga
na kupe. Serikali imetoa mafunzo kwa watoa huduma za msingi (CAHWs) 42, na madaktari
wasaidizi 90 kwa Unguja na Pemba. Pia, mafunzo juu ya kujikinga na ugonjwa wa kichaa cha
mbwa yalitolewa kwa skuli mbalimbali za Unguja na Pemba na vipindi mbalimbali vya
kuhamasisha jamii juu ya athari za kichaa cha mbwa vimerushwa kupitia vipindi vya redio na
televisheni.
4.2.1 Kuendeleza Kazi za Tafiti kwa Wanyama
Katika kipindi cha miaka mitano 2010 - 2015, Serikali imendeleza kazi ya utafiti wa upandishaji
wa wanyama wakiwemo ng’ombe, mbuzi na kuku. Upandishaji wa ngombe kwa njia ya sindano
ulifanyika ili kupata mbegu bora ya ng’ombe wa maziwa na nyama. Jumla ya ng'ombe 5,500
wamepandishwa Unguja na Pemba. Ng'ombe 1,874 waliangaliwa ushikaji wa mimba na ndama
547 wamewekewa kumbukumbu. Aidha, jumla ya wafugaji 21,793 wa ng'ombe, mbuzi, kuku na
vikundi vya ushirika wametembelewa na kupewa ushauri juu ya ufugaji wa kisasa. Wafugaji 40
wamepewa mafunzo ya usindikaji wa mazao ya maziwa (jibini, siagi, samli na mtindi). Vilevile,
Wanyama wakifanyiwa Ukaguzi na Matibabu
28
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
uzalishaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita 24,343,351 (2010) hadi lita 27,243,351 (2015)
ikiwa ni sawa na asilimia 12, na uzalishaji wa mayai umeongezeka kutoka mayai 164,270,132
(2010) hadi mayai 186,870,292 (2015) sawa na asilimia 14.
Pia, Serikali inaendeleza utafiti wa kuchanganya damu za kuku wetu wa asili na kuku wa kigeni
kwa kutumia kuku asili wa kabila la kishingo na kuku wa kigeni aina ya White Leghorns/Rhode
Island Red/Australop. Matokeo ya utafiti huu umeonyesha kuwa kuku chotara anayezalishwa
anataga mayai maradufu ya kuku wetu wa asili. Kuku hawa hutaga wastani wa mayai 200 kwa
mwaka badala ya mayai 60 yanayozalishwa na kuku wetu wa asili.
Katika suala la kushajiisha utunzaji wa mazingira na matumizi ya samadi katika jamii ya wafugaji,
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeweza kushajiisha wafugaji juu ya utumiaji wa samadi kama
nishati mbadala kwa ujenzi wa mitambo ya Biogesi. Hadi sasa jumla ya mitambo 32 imejengwa
Unguja na Pemba.
Mashamba ya Wafugaji Waliopatiwa Taaluma ya Ufugaji Bora wa Kuku na Ng’ombe
29
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Serikali imeendelea kushajiisha Sekta binafsi kuwekeza katika Sekta ya mifugo na hadi hivi sasa
wawekezaji wawili (2) wamejitokeza kuwekeza katika sekta hii. Mwekezaji mmoja (mzalendo)
ameanzisha kiwanda cha maziwa Fumba na mwengine (mgeni) ameanzisha kiwanda cha kusarifu
kuku Maruhubi Zanzibar. Viwanda hivi vinatoa fursa ya soko la bidhaa za maziwa na nyama ya
kuku kwa wafugaji.
4.3 UVUVI NA MAZAO YA BAHARINI
Sekta ya Uvuvi ni moja ya sekta inayochangia katika Pato la Taifa na kipato cha mtu mmoja mmoja
kutokana na mazingira yetu kuwa ni visiwa na kuzungukwa na bahari pande zote. Kutokana na
umuhimu huo, Serikali inaendeleza mikakati mbalimbali ya kusaidia wavuvi wadogo wadogo ili
kuwawezesha kuwa na uvuvi wenye tija na kuhifadhi mazingira. Kwa kipindi cha miaka mitano
iliyopita, Sekta ya Uvuvi imechangia katika Pato la Taifa kwa wastani wa asilimia 7.2. Jumla ya
tani 148,535 za samaki zenye thamani ya Shilingi bilioni 527.5 zilivuliwa kufikia mwaka 2914.
Aidha, katika kipindi hicho, Serikali imewezesha kuundwa kwa vikundi vya uvuvi 167 na
kupatiwa misaada ya boti, mashine pamoja na vifaa vyengine vya uvuvi. Vilevile, Serikali kupitia
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea kutoa elimu kwa wavuvi wadogo wadogo na wananchi
kwa ujumla juu ya uvuvi bora na utunzaji wa mazingira.
Ujenzi wa Mtambo wa Biogesi na Matumizi ya Nishati hiyo
30
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Serikali imesimamia Mpango Shirikishi wa Maeneo ya Hifadhi ya Baharini ikiwemo eneo la
Menai, MIMCA na PECCA na imetoa mafunzo ya uvuvi wa Zanzibar na changamoto zake,
usimamizi wa shughuli za doria, majukumu ya Kamati za Uvuvi za vijiji na utatuzi wa migogoro.
Aidha, katika kuwajengea mazingira mazuri wananchi wetu ili waweze kushiriki katika uwekezaji
wa uvuvi wa bahari kuu, Serikali imewasomesha wavuvi vijana 55 juu ya uvuvi wa bahari kuu
katika Chuo cha Uvuvi cha Mbegani Tanzania Bara. Pia, Serikali inaendelea na kupambana na
Uvuvi haramu na uharibifu wa mazao ya baharini kwa kufanya doria, ambapo jumla ya doria 127
zimefanywa. Katika mwaka 2010 - 2015 jumla ya leseni 32,900 za wavuvi zimetolewa na vyombo
10,210 vimesajiliwa. Vilevile, shughuli za usimamizi shirikishi zimeanzishwa kwa kuanzisha
Kitengo cha Kusimamia Maeneo yote ya Hifadhi za Baharini (MCU), ambapo pia vikundi 48 vya
uhifadhi wa mazingira vimeanzishwa.
4.3.1 Uimarishaji wa Zao la Mwani
Katika juhudi za kuimarisha zao la mwani, Serikali kwa kushirikiana na Taasisi za Sayansi ya
Bahari (IMS) na Kampuni ya ununuzi wa mwani ya Birr imefanya utafiti juu ya mwani mnene wa
“cottonii” utafiti ambao umetoa mafanikio mazuri kwa kuzalisha zaidi ya tani 64,988.6. Aidha,
tani 60,433 zenye thamani ya Shilingi bilioni 24.7 zimesafirishwa na kuuzwa nje ya nchi kwa
kipindi cha miaka mitano. Vilevile, jumla ya vikundi vya wakulima wa mwani 85 na wakulima
binafsi 15 wamefaidika na Mpango wa Ugawaji wa Vihori vya kubebea mwani kwa Unguja na
Pemba. Vihori hivyo vinaweza kubeba kilo 400 za mwani mbichi kwa mara moja. Mpango huu
Samaki wa aina ya Nduwari aliyevuliwa katika Bahari ya Nungwi akishushwa
katika Soko la Darajani
31
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
ulitekelezwa na Serikali kwa mashirikiano na Shirika la Kujitolea la Canada baada ya utafiti
mdogo uliofanywa kwa wakulima wa mwani na kugundua kuwa wakulima wa zao hilo
wanatembea masafa marefu hadi kwenye mashamba yao na wanamudu kubebe kilo 50 hadi 100
za mwani mbichi kupeleka fukweni. Aidha, utafiti huo umeonyesha kuwa wakulima hawana
uwezo wa kulima zao hilo katika maji ya kina kirefu ambapo maeneo hayo mwani humea vizuri
zaidi kulinganisha na maji ya kina kifupi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali
Mohamed Shein akikagua Vihori vya Kubebea Mwani Baada ya Kukabidhiwa na
Shirika la Kujitolea la Canada katika Hoteli ya Bwawani Zanzibar
32
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Katika kuimarisha ufugaji wa viumbe wa baharini (samaki, kaa, chaza, lulu na majongoo) vikundi
144 vya ufugaji wa viumbe vya baharini vimeanzishwa na jumla ya wavuvi 2,320 wamepatiwa
taaluma, vifaa na mbinu bora za uvuvi na ufugaji wa samaki unaozingatia hifadhi ya mazingira ya
bahari. Pia, Serikali imeanzisha mabwawa matano (5) ya mfano ya kufugia samaki ambayo ni
mashamba darasa Unguja na Pemba pamoja na kusaidia vifaa kama vile mashine za kuvutia maji
katika mabwawa hayo. Vilevile, jumla ya vifaranga vya samaki 33,081 vimetolewa kwa wafugaji
wa samaki Unguja na Pemba, kwa lengo la kuwasaidia kuinua uzalishaji wa samaki na
kuwaongezea kipato wafugaji hao. Aidha, jumla ya wajasiriamali 59 wa mazao ya baharini
walipelekwa nchini China kwa lengo la kujifunza teknolojia bora za ufugaji wa mazao ya baharini
itakayowasaidia kuimarisha kazi zao za ufugaji wa samaki na mazao mengine ya baharini hapa
nchini.
Wakulima wa Mwani Wakipanda, Wakivuna na Kuonyesha Njia Bora za Uanikaji wa Zao hilo
33
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Katika kuendeleza uhifadhi wa viumbe hai na adimu vya baharini mfano pomboo, kasa na
nyangumi na kuvitumia kama vivutio vya utalii, Serikali imetoa mafunzo kwa wavuvi yanayohusu
utengenezaji wa mitego ya jarife yenye uwezo wa kuwaachia viumbe hao pindipo wanaponasa.
Aidha, utafiti wa majaribio umefanywa wa kuiwekea mitego ya jarife vifaa vyenye kutoa sauti
(pingers) ili kuwatahadharisha pomboo wasinase katika mitego hiyo. Vilevile, Serikali imeendelea
na kufuatilia uhifadhi wa wanyama adimu hasa kasa katika maeneo ya bahari yetu ya Zanzibar
pamoja na maeneo yote ya hifadhi. Vikundi vipya viwili (2) vimeanzishwa na vinajihusisha na
ufugaji wa kasa kwa ajili ya kuwahifadhi na kuwatumia kama kivutio cha utalii. Aidha, jumla ya
kasa 130 waliohifadhiwa katika mabwawa huko Nungwi wameweza kuachiliwa kwa kurejeshwa
baharini kwa lengo la kuongeza idadi na kuhifadhi aina ya viumbe hivi visipotee.
4.4 MALIASILI
4.4.1 Kutekeleza Mpango wa Muda Mrefu wa Usimamizi wa Rasilimali za Misitu na
Maliasili Zisizorejesheka
Serikali kupitia Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka imeendelea na udhibiti wa maliasili
zikiwemo rasilimali za misitu na maliasili zisizorejesheka pamoja na kulinda na kuhifadhi
wanyama pori na bayoanuai zilizomo. Jumla ya miche 6,020,861 ikiwemo miti ya mikarafuu,
misitu, matunda na viungo imesambazwa kwa ajili ya upandaji katika mashamba ya Serikali,
barabarani, maeneo yaliyoathirika kwa uchimbaji wa mchanga na kwa wanajamii ambapo miche
Shamba Darasa la Ufugaji Samaki Linalotumika Kuwafundishia Wakulima lililopo Pujini - Pemba
34
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
358,263 imepandwa katika hekta 600 za mashamba ya Serikali. Aidha, miche 5,662,598 ya misitu
imepandwa katika mashamba ya wakulima, pembezoni mwa barabara na maeneo yalimochimbwa
mchanga. Vilevile, vikosi na maafisa misitu na maliasili wamekuwa wakifanya doria katika
maeneo mbalimbali ya misitu aina ya mikoko Unguja na Pemba ambapo matukio ya ukataji wa
mikoko yaliyowahi kugunduliwa ni pamoja na maeneo ya Pujini na Sizini na hatua za kisheria
zimechukuliwa dhidi ya wahusika.
Katika juhudi za kuhifadhi misitu, Serikali inaendelea na uandaaji wa Sera na Sheria za uhifadhi
Misitu. Aidha, Serikali imeipandisha hadhi misitu ya Jambiani-Muyuni na Ufufuma-Pongwe
yenye ukubwa wa hekta 405. Vilevile, Maeneo 12 ya uhifadhi wa Misitu ya Jamii yametayarishiwa
mipango ya uhifadhi na kufanya idadi ya maeneo yote ya uhifadhi ya wanajamii kuongezeka
kutoka 45 hadi 57 (Unguja 33 na Pemba 24). Pia, Serikali imeendelea kushirikiana na wananchi
katika usimamizi na uhifadhi wa Maeneo Tengefu ya Jozani na Ngezi pamoja na Misitu ya asili
ya Masingini na Msitu Mkuu wa Kiwengwa. Kazi hizi zinajumuisha kufanya doria za pamoja na
wananchi, kuelimisha jamii/watendaji pamoja na kuanzisha miradi yenye faida za Kiuchumi na
Mazingira.
Mafanikio ya utekelezaji wa misitu ya jamii umetokana na kukamilika kwa Mradi wa Uhifadhi wa
Misitu ya Asili (HIMA), Wananchi wengi wameelimishwa na kuhamasishwa katika matumizi
endelevu ya maliasili. Aidha, Mipango 50 ya Usimamizi wa Misitu ya Jamii kwa Unguja na Pemba
Eneo Tengefu la Msitu wa Hifadhi ya Jozani
35
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
imetayarishwa na kuanza kutumika. Katika juhudi za kupunguza matumizi ya kuni na mkaa,
Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo imewezesha Mpango wa kuzipatia kaya
4,500 gesi bila ya malipo. Pia, jumuiya 40 (15 Pemba na 25 Unguja) zimepatiwa jumla ya Shilingi
430,400,000 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maendeleo inayohusiana na utunzaji wa rasilimali
zetu. Matokeo ya uwezeshaji huo yamepelekea kupunguza matumizi ya rasilimali misitu ambapo
hivi sasa maeneo mbalimbali nchini ikiwemo watu binafsi na maeneo ya biashara wameanza
kutumia gesi kwa matumizi ya nishati.
Serikali imeandaa Kanuni ya Udhibiti wa Matumizi ya Misumeno ya Moto kudhibiti uingizaji na
matumizi yake kwa lengo la kupunguza uharibifu wa misitu unaotokana na misumeno hiyo. Jumla
ya wafanyakazi 21 wa Hifadhi ya Taifa ya Jozani na Ghuba ya Chwaka wamepatiwa mafunzo ya
Zimamoto na Uokozi. Aidha, vifaa vya kuzimia moto vimenunuliwa na jumla ya visima 10
vimechimbwa katika maeneo tofauti ya Hifadhi ya Jozani ambavyo vinatarajiwa kutoa maji kwa
ajili ya kazi ya uzimaji moto pale utakapotokea. Vilevile, kazi ya uwekaji wa mipaka ya kudumu
na uchoraji wa ramani katika Msitu wa Jozani imekamilika.
Katika juhudi za kuwahamasisha shughuli za ufugaji wa nyuki, Serikali imetoa jumla ya mizinga
3,000 kwa vikundi mbali mbali vya wafugaji wa nyuki. Hatua hii imepelekea ongezeko la
uzalishaji wa asali na kufikia wastani wa tani tano za asali kila mwaka kuanzia 2013.
Pia, Serikali katika utekelezaji wa mkakati wa kuwaangamiza ndege aina ya Kunguru,
imewaelimisha wanajamii 1,500 na wafanyakazi 27 wa Baraza la Manispaa na kuhamasishwa
Ufugaji wa Nyuki kisiwani Pemba chini ya Mradi wa CFP
36
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
kushiriki katika kazi ya kuangamiza ndege hao. Kutokana na juhudi hizo, jumla ya kunguru
200,736 wameuliwa kwa kutumia sumu na mitego Unguja na Pemba.
Katika kuendeleza utunzaji na hifadhi ya wanyama pori walio katika hatari ya kutoweka hasa
Kimapunju, Popo wa Pemba na Paa Nunga na kuwatumia kama vivutio vya utalii, Serikali
imewezesha kuongezeka idadi ya wanyamapori hao adimu wakiwemo Popo wa Pemba kutoka
4,000 hadi 37,000 na Kima Punju kutoka 2,500 hadi 3,000. Juhudi hizi zimetokana na uanzishwaji
wa maeneo ya uhifadhi na mazalio kwa wanyama hao.
4.5 MAZINGIRA
4.5.1 Kusimamia Utekelezaji wa Mpango wa Hifadhi ya Mazingira katika Maeneo ya Ardhi,
Bahari na Ukanda wa Pwani
Katika kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Hifadhi ya Mazingira, Serikali imeandaa Sera ya
Mazingira ya mwaka 2013 na Sheria ya Mazingira ya mwaka 2015 ambazo zinatoa muongozo na
kuweka mfumo bora wa kisheria na kitaasisi juu ya usimamizi wa mazingira Zanzibar. Aidha,
Wanyama adimu na kivutio kikubwa cha watalii ambao ni Kimapunju, Popo wa Pemba na
Paa Nunga wanaopatikana katika Misitu ya Zanzibar
37
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Serikali imepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kuandaa Kanuni ambayo inakataza
kuingiza, kutumia, kusafirisha na kuhifadhi mifuko ya aina zote ya plastiki hapa Zanzibar. Kanuni
hii imetayarishwa kwa ajili ya kupunguza uchafuzi wa mazingira unaotokana na mifuko hiyo.
Vilevile, Serikali imeandaa Kanuni ya usimamizi wa maliasili zisizorejesheka ili kupunguza
wimbi la uchimbaji kiholela wa maliasili hizo. Serikali pia imeandaa Mpango wa Utekelezaji wa
Usimamizi wa Mazingira wa Zanzibar ambao umeshaanza kutekelezwa. Aidha, vikosi kazi
vimeundwa vya kufanya operesheni za kudhibiti uchimbaji kiholela wa maliasili zisizorejesheka
na matumizi ya mifuko ya plastiki. Tokea kuanzishwa kwa vikosi kazi hivyo, mafanikio makubwa
yamepatikana katika kudhibiti uchimbaji kiholela wa maliasili zisizorejesheka na uingizaji na
utumiaji wa mifuko ya plastiki.
Aidha, Serikali imefanya utafiti wa kuangalia athari za mabadiliko ya tabianchi kwa uchumi wa
Zanzibar. Utafiti huo umebaini kuwa karibu sekta zote kuu za Uchumi wa Zanzibar kwa njia moja
ama nyengine zinaathiriwa na mabadiliko ya tabianchi. Pia, utafiti umeorodhesha maeneo 148
yanayoingia maji ya Chumvi kwa Unguja na Pemba kutokana na kupanda kwa kina cha baharí
kunakosababishwa na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kutokana na hali hii, Serikali imeandaa
taratibu maalum ili maeneo hayo yaendelee kutumika kwa shughuli mbalimbali za kilimo na
nyenginezo. Vilevile, wananchi wa kijiji cha Nungwi wapatao 8,000 wamepatiwa maji safi na
salama kupitia mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abrahman Kinana akijumuika na wananchi wa kikundi cha
kuhifadhi Mazingira Fuoni Kibondeni katika Upandaji wa Miti ya Mikoko
38
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
4.5.2 Kufanya Mapitio ya Miradi Inayohusiana na Mazingira
Jumla ya Miradi 221 imefanyiwa ukaguzi kupitia Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi
Zanzibar (ZIPA). Pia, Miradi 71 ya uwekezaji imefanyiwa Tathmini ya Athari ya Kimazingira
(EIA) na kutolewa vyeti vya Mazingira. Vilevile, ripoti 66 za maelezo yakinifu (Feasibility Study)
za miradi mbalimbali zimewasilishwa Idara ya Mazingira kwa ajili ya kupatiwa ushauri wa
kimazingira.
4.5.3 Kuwaelimisha Wananchi Juu ya Umuhimu wa Utunzaji na Hifadhi ya Mazingira.
Katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji na hifadhi ya mazingira vipindi mbalimbali
vya Radio na TV vinavyohusiana na usimamizi wa mazingira vimetayarishwa na kurushwa
hewani. Aidha, Semina, Mikutano na Makongamano juu ya athari za mifuko ya plastiki na
uchafuzi wa mazingira zimefanywa kwa Skuli za Msingi na Sekondari, Kamati za Shehia, Polisi
Jamii, Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya
na Madiwani nchini.
4.6 UTALII
Kwa kutilia maanani kwamba Zanzibar ni visiwa vyenye vivutio vingi vya utalii kama vile fukwe
zinazovutia, wanyama adimu kama popo, kima punju, paa nunga pamoja na urithi wa kimataifa
wa mji mkongwe, Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 - 2015 imetilia mkazo suala la utalii
nchini. Katika kulitekeleza hili, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuimarisha sekta hii ili
Makamu wa Kwanza wa Rais Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad akiangalia Baadhi ya Maeneo
yaliyoathirika na Matokeo ya Mabadiliko ya Tabianchi (Kilimani na Kinazini-Unguja)
39
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa na kuinua maisha ya wananchi. Miongoni mwa hatua
zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ni kama zifuatazo
4.6.1 Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Mpango Mkuu wa Utalii
Serikali imeweza kuimarisha shughuli za utalii kwa kufanya marekebisho ya Sheria ya Utalii
yanayolenga kwa kiasi kikubwa kutekeleza Sera ya Utalii kwa Wote na kuanzisha awamu mpya
ya uendeshaji wa utalii nchini. Aidha, Serikali imechukua hatua mahsusi kwa kuzishirikisha taasisi
nyingine muhimu za kiuchumi ikiwemo Sekta Binafsi na taasisi mbalimbali za Serikali katika
kuendeleza utalii. Vilevile, Serikali imeanzisha Programu ya Uendelezaji wa Sekta ya Utalii kwa
kupitia Mpango wa Matokeo kwa Ustawi (Result for Prosperity) unaotokana na matokeo ya
Maabara ya Utalii (Tourism Lab). Mpango huo unakisiwa kugharimu jumla ya Shilingi bilioni
5,595,375,000 na umeandaliwa kwa kuzihusisha taasisi mbalimbali za Serikali na Sekta Binafsi.
4.6.2 Kuitangaza Zanzibar Kiutalii Nje ya Nchi ili Kuongeza Kipato
Serikali kupitia Kamisheni ya Utalii imeendelea kushiriki katika maonesho mbalimbali ya Kitaifa
na Kimataifa kwa lengo la kuitangaza Zanzibar ili kuwavutia watalii wengi zaidi kutembelea nchi
yetu. Katika jitihada za Serikali juu ya kuitangaza Zanzibar kiutalii, vyombo vya habari tofauti
vya kitaifa na kimataifa vimeshirikishwa kwa lengo la kutoa taarifa za vivutio vya kiutalii
vilivyopo Zanzibar. Taarifa hizo zimetolewa katika vyombo vya habari ikiwemo Magazeti na
Majarida ya Masoko na mafanikio makubwa yamepatikana kwa kuongozeka kwa idadi ya watalii
wanaotembelea Zanzibar kutoka 132,836 mwaka 2010 na kufikia watalii 310,500 mwaka 2014,
hii ni sawa na ongezeko la asilimia 107.
40
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Katika kuendeleza utekelezaji wa mikakati ya kuitangaza Zanzibar kiutalii, Zanzibar imekuwa
ikishiriki katika maonesho 10 ya kimataifa kila mwaka katika masoko ya zamani na mapya
yakiwemo China na Urusi kwa lengo la kuwavutia watalii wengi zaidi kutembelea Zanzibar.
Vilevile, Zanzibar imejiunga na Jumuiya ya Utalii wa Visiwa vya Vanila (Vanila Islands Tourism
Association) ili kufaidika na fursa za kiutalii zilizopo katika jumuiya hiyo.
4.6.3 Kuimarisha Utalii wa Kumbukumbu za Kihistoria
Serikali imejikita zaidi katika kuyatangaza maeneo ya kihistoria yaliyopo Zanzibar na kutoa nafasi
maalumu kwa kuyaimarisha makumbusho ikiwa ni pamoja na kuyapatia vifaa mbalimbali vya
kihistoria na mambo ya kale ambavyo ni vivutio vya msingi kwa watalii. Aidha, katika
kuendeleza utalii wa ndani, Serikali imeshajiisha ziara za wanafunzi na wananchi kutembelea
maeneo ya kihistoria na pia wananchi wameshajiishwa kuanzisha matamasha ya kiutamaduni
katika maeneo yao ili kuvutia watalii zaidi.
4.6.4 Kuibua Maeneo Mapya ya Vivutio vya Utalii
Katika kuongeza vivutio vya utalii nchini, Serikali inaendelea kutafuta na kuibua maeneo mapya
na kuyafanyia matengenezo maeneo ya kihistoria, Unguja na Pemba. Miongoni mwa maeneo
mapya yaliyoibuliwa ni pamoja na Kuumbi, Kiwengwa, Muyuni, Dimani, Mwanampambe,
Watendaji wa Kamisheni ya Utalii wakishiriki katika maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ili kuitangaza
Zanzibar
41
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Mwana wa Mwana, Tazari na kijiji kilichozama Mkumbuu pamoja na maeneo ya uhifadhi wa
wanyama.
Aidha, katika kuyafanyia matengenezo maeneo ya kihistoria, Serikali imetekeleza Mradi wa
Ukarabati wa Uhifadhi wa Maeneo ya Kihistoria wenye thamani ya Shilingi milioni 230. Mradi
huu unajumuisha ukarabati, upimaji wa maeneo, ulipaji wa hati miliki, utangazaji, uwekaji
mabango ya matangazo na kuonesha njia. Maeneo yanayohusika na mradi huo ni Mkama Ndume,
Mkumbuu, Chwaka, Unguja Ukuu, Kizimkazi na Bikhole.
Serikali imeendelea kuchukua juhudi za kuyafufua mashindano ya Trithlon kwa kushirikiana na
Jumuiya ya Mashirika ya Ndege Duniani na wataalamu wa Trithlon kutoka Afrika ya Kusini na
Ethiopia. Aidha, Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya DISALVAMENTO kutoka Italia
inaendelea na utaratibu wa kufufua mbio za Marathon. Pia, katika kuongeza kuwavutia watalii
wengi wa hadhi ya juu kuja kutembelea Zanzibar na kuongeza Pato la Taifa, Serikali kwa
kushirikiana na Hotel ya Manta Reef iliopo Makangale Pemba walizindua Chumba cha chini ya
bahari ambapo watalii wengi wa hadhi ya juu wanategemewa kutembelea chumba hicho.
Msikiti wa kihistoria wa Kizimkazi ambao ni kivutio kwa watalii
42
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
4.6.5 Kumbukumbu na Mambo ya Kale
Kwa azma ya kuendeleza kumbukumbu na mambo ya kale, Serikali imetekeleza mambo muhimu
yafuatayo.
4.6.5.1 Kuhifadhi Kumbukumbu za Kihistoria na Mambo ya Kale
Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuimarisha uhifadhi wa kumbukumbu na
mambo ya kale, Serikali imefanya utafiti wa uchimbaji wa Ngome ya Mazrui, Chwaka na Tumbe
uliofanyika kwa ufadhili wa MACEMP/DAMA pamoja na utafiti wa kiaikolojia katika eneo la
Ngome Kongwe, Forodhani Unguja chini ya Udhamini wa “African Archaelogy Network” na
DAMA. Katika uchimbaji huo kulingunduliwa vigae vya vyungu, ‘Kwale pottery’ vya karne ya
kwanza.
4.6.5.2 Kuendeleza Matengenezo ya Makumbusho
Serikali imeyafanyia matengenezo majengo ya Mangapwani kwenye Mahandaki ya Vita Vikuu
vya Pili vya Dunia, Magofu ya Kizimbani, Mahodhi ya Hamamni (Hamam Baths) pamoja na
kusafisha kisima cha maji na mnara katika Chemba ya Watumwa Mangapwani ili kuyarejeshea
hadhi yake ya awali kwa ajili ya kuwavutia wageni wengi zaidi kuitembelea Zanzibar. Aidha,
Serikali imejenga jengo la Makumbusho ya Kuumbi Jambiani, Mkoa wa Kusini Unguja kwa lengo
la kuhifadhi na kutunza kumbukumbu za mambo ya kale.
Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi akikagua chumba cha chini ya baharí mara
baada ya kukizindua rasmi, novemba 2014
43
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
4.6.6 Kufanya Uhakiki wa Hoteli za Kitalii
Serikali imefanya uhakiki wa hoteli za kitalii ili kuziwekea daraja zinazostahiki hoteli hizo.
Matokeo ya uhakiki huo yameonesha kuwa hoteli 74 zilifikia vigezo vilivyowekwa na Jumuiya ya
Afrika Mashariki. Kati ya hizo, hoteli za nyota tano ni 16, nyota nne tisa (9), nyota tatu 43 na nyota
mbili sita (6).
Makumbusho ya Kuumbi yaliopo Jambiani pamoja na baadhi ya vifaa vya kihistoria vilivyomo Unguja
44
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
4.6.7 Kuimarisha Huduma za Utalii kwa Kuziendeleza Jumuiya za Watoa Huduma
Katika hatua za kuimarisha huduma za utalii na kuziendeleza Jumuiya za Watoa Huduma, Serikali
imeendelea kushajiisha Kampuni za Watembezaji na Wasafirishaji Watalii kuwa na wahudumu
wenye taaluma na wenye kuithamini Sekta ya Utalii. Aidha, Wanajumuiya wamehamasishwa
kushiriki katika Maonesho mbalimbali ya Kitalii ya Kitaifa na Kimataifa ili wawe na muamko
mkubwa zaidi wa namna Sekta ya Utalii inavyokua na jinsi ya kuhudumia wageni ipasavyo.
Vilevile, Serikali imeiongezea uwezo Jumuiya ya Watoa Huduma ili iweze kukabiliana na
ushindani wa Jumuiya na Mashirika mbalimbali ya kimataifa. Pia, wadau wote wanaoshughulikia
mambo ya utalii wamekutanishwa katika kutathmini hali halisi ya mwenendo na changamoto
zinazoikabili Sekta ya Utalii ikiwemo masuala ya ulinzi na usalama wa watalii na mali zao na jinsi
ya kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.
4.6.8 Kupunguza Vituo vya Ukaguzi Katika Maeneo Wanayopita Watalii
Serikali imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora kwa watalii kwa kushirikiana na
wadau wa Sekta hiyo wakiwemo Jumuiya za ZATI, ZATO, ZATOGA, pamoja na taasisi
Hoteli mbalimbali za Kitalii Zanzibar
45
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
zinazosimamia Sekta ya Utalii ikiwemo Jeshi la Polisi. Wadau hao wanakutana kila baada ya miezi
mitatu kwa lengo la kuimarisha huduma za utalii nchini bila kuathiri taratibu za kiusalama.
4.6.9 Kukiimarisha Chuo cha Maendeleo ya Utalii
Serikali imekiimarisha Chuo cha Maendeleo ya Utalii kwa ujenzi wa jengo la madarasa na ofisi
za Chuo uliogharimu jumla ya Shilingi 800,000,000. Aidha, Serikali imewapatia mafunzo
wakufunzi sita (6) wa Chuo hicho katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Vilevile, Chuo
kimefanya makubaliano ya mashirikiano baina yake na Chuo cha Utalii Kenya (KUC) kwa ajili
ya kubadilishana uzoefu na utaalamu. Pia, mitaala ya Chuo imefanyiwa mapitio kwa mashirikiano
na taasisi ya “Programma Uitzending Managers” ya Netherland. Chuo kinatekeleza Mradi wa
“Vocational Education for Higher Categories and Level” (VEHICLE) ambao umesaidia Chuo
kujitangaza kibiashara na kujenga mahusiano mazuri na wadau wengine wa utalii.
4.7 VIWANDA NA BIASHARA
Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2010 - 2015 imeiagiza SMZ kusimamia utekelezaji
wa Sera ya Uendelezaji wa Viwanda Vidogo vidogo na vya Kati na kuifanyia mapitio Sera ya
Biashara ya Mwaka 2006 ili kubaini mapungufu na kuchukua hatua zinazopaswa pamoja na
kuweka mfumo bora zaidi katika utoaji wa leseni. Katika kulitekeleza hilo, Serikali inasimamia
kikamilifu utekelezaji wa Sera ya Uendelezaji wa Viwanda Vidogo Vidogo na vya Kati. Pia,
Serikali imeunda Kamati ya Ushauri yenye wajumbe 12 (wajumbe 6 kutoka Sekta ya Umma na
Jengo jipya la Chuo cha Maendeleo ya Utalii – Zanzibar kilichopo Maruhubi
46
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
wajumbe 6 kutoka Sekta Binafsi) ili kuishauri juu ya utambuzi na utatuzi wa changamoto
zinazoikabili Sekta ya Viwanda.
Kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na Serikali, Kampuni ya Azam
imeweza kuanzisha Kiwanda cha Maziwa (Azam Diary Factory) katika eneo la Fumba na
kinatarajiwa kuajiri zaidi ya watu 200. Hivi sasa Kiwanda kimeshaanza rasmi uzalishaji na
usambazaji wa maziwa.
Vilevile, ukarabati mkubwa umefanyika katika Kiwanda cha Sukari Mahonda kwa kuweka
mashine mpya na kuimarisha mashamba ya miwa. Kiwanda kimeajiri wafanyakazi 350 na kazi
ya uzalishaji inaendelea na tayari sukari inayozalishwa katika Kiwanda hicho iko sokoni.
Kiwanda cha Maziwa cha Azam kilichopo katika Maeneo Huru ya Uwekezaji - Fumba
Kiwanda cha Sukari Mahonda na bidhaa ya sukari iliyozalishwa kiwandani hapo
47
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Kwa upande wa biashara, Serikali inaendelea na hatua za kuifanyia mapitio Sera ya Biashara ya
Mwaka 2006 kwa lengo la kubaini mapungufu na kuchukua hatua zinazofaa zitakazoimarisha
shughuli za biashara nchini. Pia, Serikali imetunga Sheria ya Utoaji Leseni za Biashara na Usajili
Nam.13 ya mwaka 2013 ambayo tayari inatumika. Sheria hii inaweka mfumo bora zaidi wa utoaji
wa leseni za biashara nchini. Aidha, Serikali imezifanyia mapitio Sheria Namba.2 ya Kusimamia
Mwenendo wa Biashara na Kumlinda Mlaji ya mwaka 1995, Sheria Nam.4 ya Mizani na Vipimo
ya mwaka 1983 na Sheria Nam.4 ya Biashara ya mwaka 1989 na kutunga Sheria mpya Nam.14 ya
Biashara ya Zanzibar ya 2013. Sheria hizi zimetungwa kwa lengo la kukidhi mazingira ya sasa
ya biashara ikiwemo uendeshaji uchumi na biashara kwa kuzingatia misingi ya nguvu za soko,
maendeleo ya teknolojia na kuzigeuza sheria kuwa rafiki wa kukuza uchumi na ustawi wa biashara.
Serikali pia imeanzisha Taasisi ya Viwango ya Zanzibar (ZBS) kwa mujibu wa Sheria ya Viwango
Namba. 1 ya 2011 kwa lengo la kusimamia biashara nchini kwa kuzingatia viwango vya bidhaa
vinavyohitajika. Aidha, Kamati 10 za kitaalamu zimeundwa kwa ajili ya kuzingatia mapendekezo
ya viwango vya bidhaa. Kamati hizo zina jukumu la kuainisha viwango vya kipaumbele katika
bidhaa za vyakula na vinywaji, mafuta ya mimea na viungo, umeme na eletroniki, nishati na gesi,
sabuni, vifaa vya ujenzi na mazingira.
Vilevile, Serikali imezingatia na kupitisha jumla ya viwango 25 vya bidhaa mbalimbali na kutoa
taaluma ya viwango na ubora wa bidhaa kupitia maonesho ya biashara, vipindi vya redio na TV,
ziara kwa wajasiramali na wazalishaji pamoja na kuandaa taratibu za upimaji na udhibiti wa ubora
wa bidhaa. Serikali kupitia ZBS imetengeneza alama ya utambulisho (logo) na alama ya ubora wa
bidhaa (Standard Mark) ambayo itaonesha ubora wa bidhaa hizo.
Katika kuwajengea uwezo wazalishaji na wajasiriamali ili waweze kuzalisha bidhaa bora zaidi na
kwa kiwango cha juu, Serikali imetoa mafunzo kwa wazalishaji wadogo wadogo 285 Unguja na
Pemba juu ya usindikaji mazao, ujasiriamali, kuongeza thamani ya mazao na mbinu bora za
kuendesha biashara.
Kwa upande wa masoko, Serikali imefanya jitihada za kuitangaza Zanzibar na kuwatafutia
masoko wafanyabiashara, wajasiriamali na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili waweze kutumia
fursa za masoko ya EAC, SADC, AGOA na EU. Aidha, Serikali inaendelea na kutayarisha
michoro ya ujenzi wa Uwanja wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa unaotarajiwa kujengwa
48
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
katika eneo la Dimani. Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko imeratibu
ushiriki wa wajasiriamali na wafanyabiashara 500 kushiriki katika maonesho ya biashara
mbalimbali ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa ili kutangaza na kuuza bidhaa zao.
4.7.1 Kuimarisha Mtandao wa Usambazaji Habari za Biashara kwa Wafanyabiashara
Serikali imeunda Kitengo cha Habari na Mawasiliano ili kiweze kusambaza taarifa mbalimbali za
biashara kwa wafanyabiashara na wadau wengine. Kitengo hicho kinakusanya taarifa na
kumbukumbu mbalimbali zinazohusiana na biashara, uendelezaji wa viwanda na masoko
zikiwemo tafiti, sera, hotuba za bajeti na picha za matukio kwa ajili ya Maktaba ya Wizara ili
wadau wanaozihitaji waweze kuzipata. Aidha, Serikali imetayarisha taarifa za maendeleo ya
biashara kwa kipindi cha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar na kusambaza kwa wadau. Vilevile,
Serikali imezindua Mpango wa Elimu kwa wananchi kuhusu Sheria Mpya ya Biashara Nam.14 ya
2013.
4.7.2 Kufanya Utafiti wa Usarifu wa Zao la Karafuu
Serikali kupitia Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC) imeanza kuchukua hatua za kuilinda na kuipa
hadhi zaidi karafuu ya Zanzibar pamoja na kuitangaza Zanzibar ulimwenguni kupitia bidhaa
nyengine za viungo zikiwemo Mdalasini, Pilipili Hoho na Pilipili Manga. Kazi hii inatekelezwa
kupitia mradi wa Tasnia Malibunifu (Branding). Aidha, Serikali kupitia Shirika la ZSTC
imeanzisha Kituo Maalum (Eneo Tengefu) katika eneo la Saateni kwa ajili ya utekelezaji wa
Mradi huu pamoja na kutoa mafunzo maalum kwa wakulima 50 Unguja na Pemba wa mazao hayo
ili kuwatayarisha na kuwajengea uwezo. Serikali kupitia Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko
imesajili Jina la Biashara (Trade Mark) ambalo litatumika kwa ajili ya Mradi huu ambalo ni
“Zanzibar Exotic Original”. Aidha, Serikali imetayarisha kitabu maalum kwa lengo la kuelezea
historia ya zao la karafuu, jinsi ilivyoingia Zanzibar na utamaduni wa Zanzibar katika matumizi
ya zao hilo.
49
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Pia, Serikali imeingia makubaliano ya kibiashara na Kampuni ya Land Co. ya Japan ambapo
Kampuni hiyo inasaidia uimarishaji wa bidhaa za mafuta ya mimea ikiwemo karafuu ili yaweze
kuuzwa katika soko la Japan.
4.8 VYAMA VYA USHIRIKA
Serikali imetathmini na kuziwekea madaraja ya ubora SACCOS 203 zilizopo nchini. Aidha,
matokeo ya tathmini hiyo yameonesha kuwa mitaji ya Shilingi bilioni 3.5 imechangwa na
wananchi na mikopo ya Shilingi bilioni 7 imetolewa na SACCOS hizo. Aidha, Serikali
imeziunganisha SACCOS 17 na Taasisi za kifedha na kupata mikopo ya thamani ya Shilingi
bilioni 3. Hatua hii imesaidia kuongeza utoaji wa mikopo kwa wanachama na kuimarisha biashara
zao.
Bidhaa mbalimbali zitokanazo na zao la karafuu zinazouzwa ndani na nje ya nchi
50
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Katika kuendeleza Vyama vya Ushirika, Serikali imetoa mafunzo juu ya ushindani, ubunifu na
ujasiriamali kwa washiriki 73 kutoka vyama vikuu vya mikoa mitano ya Zanzibar na Muungano
wa Vyama vya Ushirika Zanzibar (CUZA). Aidha, Serikali imetoa mafunzo ya ubunifu, haki na
wajibu kwa Vyama vya Ushirika 79 vilivowashirikisha wanachama 697 (wanawake 459 na
wanaume 238) wa Vyama vya Ushirika kutoka Wilaya zote za Unguja na Pemba. Kati ya vyama
hivyo, SACCOS ni 28 na vyama vya uzalishaji 51.
Kikwajuni SACCOS Benki iliyopo katika Jimbo la Kikwajuni
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed
Shein akikagua Kazi na Bidhaa za Wajasiriamali na SACCOS Vilivyoshiriki Maonesho
Mbalimbali ya Biashara
51
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Katika hatua za utunzaji wa rasilimali na hesabu za ushirika, Serikali imefanya ukaguzi wa hesabu
za Vyama vya Ushirika 200 (Unguja 139 na Pemba 61) zikiwemo SACCOS 49 na vyama vya
ushirika vya uzalishaji mali na utoaji huduma 151. Pia, Serikali imefanya upekuzi na kutoa
mafunzo ya vitendo kwa Vyama vya Ushirika 1,222 ili kuimarisha utendaji wao.
4.8.1 Kusimamia Utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Ushirika na Program Mbalimbali
Katika kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Ushirika na Programu mbalimbali, Serikali
imevifanyia ukaguzi wa kawaida vyama 2,243 ili kutathmini hali ya uendeshaji, utekelezaji wa
sheria, uandishi na utunzaji wa vitabu vya hesabu. Pia, Vyama vya Ushirika 485 vimefanyiwa
ukaguzi wa hesabu na ripoti kuwasilishwa kwenye Mikutano Mikuu ya vyama hivyo kwa kutolewa
maamuzi. Matokeo ya kaguzi hizo yameonesha Vyama vya Ushirika vinaimarika na vinaendeshwa
kwa kuzingatia Sera na Sheria ya Vyama vya Ushirika Namba. 4 ya mwaka 1986. Serikali pia,
imekamilisha Sera ya Maendeleo ya Ushirika Zanzibar na inaendelea kufanya mapitio ya Sheria
ya Ushirika, ili iendane na malengo ya Sera na mahitaji yaliyopo sasa.
4.8.2 Kuendelea Kusajili na Kufanya Ukaguzi wa Vyama Vipya vya Ushirika
Serikali imesimamia usajili wa Vyama vya Ushirika 826 vya aina mbalimbali. Kati ya hivyo
Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS) 16 na Vyama vya Uzalishaji Mali na Utoaji Huduma
ni 770. Idadi ya Vyama vya Ushirika imeongezeka na kufikia vyama 2,493 vilivyo hai na ambavyo
vimeweza kuwajumuisha wananchi 39,664 katika harakati za kiuchumi.
SEHEMU YA TANO
52
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
5.0 MIUNDOMBINU YA KIUCHUMI
Miundombinu ya kiuchumi inajumuisha barabara, viwanja vya ndege, usafiri wa baharini, umeme
na bandari. Chama cha Mapinduzi kupitia Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2010 - 2015
imeelekeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa kipaumbele katika kuendeleza sekta hii
muhimu.
5.1 BARABARA
Serikali inaendelea na ujenzi wa Barabara za Unguja na Pemba ili ziendelee kupitika kwa wakati
wote na kuwarahisishia wananchi usafiri. Katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi (2010 - 2015),
Serikali imejenga na kuzifanyia matengenezo barabara mbalimbali zenye jumla ya Kilomita 181.7
kwa Unguja na Pemba kwa kiwango cha lami. Kwa Unguja barabara hizo ni:-
i. Mfenesini - Bumbwini (Km. 13)
ii. Welezo - Dunga (Km. 12.75)
iii. Amani - Mtoni (Km. 4)
iv. Mahonda - Donge (Km. 14)
v. Njia nne Umbuji (Km. 5)
Aidha, Serikali kupitia msaada wa Watu wa Marekani (MCC) imejenga barabara tano (5) za vijijini
katika Mkoa wa Kaskazini Pemba zenye urefu wa kilomita 35.5. Barabara hizo ni:-
i. Bahanasa – Daya – Mtambwe (Km. 13.6)
ii. Mzambarau Takao – Pandani – Finya (Km. 8)
iii. Mzambarau Karim – Mapofu (Km. 8.9)
iv. Chwale – Kojani (Km. 2)
v. Kipangani – Kangagani(Km. 3)
53
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Pia, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Africa (BADEA) na Mfuko
wa Maendeleo wa Saudi Arabia (Saud Fund) imekamilisha ujenzi wa barabara tatu (3) Pemba
zenye urefu wa kilomita 54. Barabara hizo ni:-
i. Wete – Konde (Km. 15).
ii. Wete – Gando (Km. 15).
iii. Chake chake – Wete (Km 24).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
akiwa pamoja na Balozi Mdogo wa Marekani wakati wa ufunguzi wa Barabara tano za
vijijini zilizojengwa kwa Msaada wa MCC Mkoa wa Kaskazini-Pemba.
Baadhi ya Barabara zilizokamilika kujengwa, Pemba
54
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Aidha, Serikali imekamilisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 43.4 Pemba kwa
kiwango cha lami. :-Barabara hizo ni:-
iv. Mtambile – Kengeja – Mwambe (Km. 9)
v. Kenya – Chambani (Km. 3.2)
vi. Mizingani – Wambaa (Km. 10)
vii. Chanjamjawiri – Tundaua (Km. 10)
viii. Chanjaani – Pujini (Km. 5)
ix. Mtambile – Kangani (Km. 6.2)
Pia, barabara saba (7) zenye ukubwa wa kilomita 36.5 zimejengwa kwa kiwango cha kifusi kwa
Unguja na Pemba. Barabara hizo ni:-
i. Fukuchani – Kigongoni (Km. 8)
ii. Utambi - Tazari(Km. 0.8)
iii. Boshoa – Kilimani (Km. 4)
iv. Donge – Mtambile – Mwanda (Km. 3.8)
v. Mgagadu – Kiwani (Km. 7.5)
vi. Shumba Viamboni – Tumbe (Km. 5)
Baadhi ya Barabara zilizojengwa na Kufanyiwa Matengenezo kwa Unguja na Pemba
55
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
vii. Kiyuni – Ngomeni (Km. 4)
Aidha, Serikali inaendelea na hatua za ujenzi wa barabara tatu (3) za Unguja zenye jumla ya
kilomita 45.5. Barabara hizo ni:-
i. Mkwajuni – Kijini (Km. 9.5).
ii. Jendele – Cheju – Kaibona (Km. 11.6).
iii. Jumbi – Koani (Km. 6.4).
Vilevile, Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya Ole-Kengeja Pemba yenye urefu wa
kilomita 35 kwa Mkopo wa riba nafuu wa Dola za Kimarekani 11,000,000 kutoka Benki ya OFID.
5.1.1 Kusimamia Utekelezaji wa Sheria Zinazohusiana na Usalama Barabarani
Serikali imeendelea kuimarisha usalama barabarani kwa kuwapatia elimu watumiaji wa barabara
na kutunga Sheria ya Barabara “Road Act” pamoja na kuweka kanuni zake ili kupunguza ajali.
Pia, Kanuni ya adhabu za papo kwa papo imetengenezwa na kuanza kutumika. Aidha, Serikali
imeandaa Sheria ya Vyombo vya Usafiri ya mwaka 2014 pamoja na miongozo ya kusimamia
matumizi ya vyombo vya usafiri.
5.2 USAFIRI WA BAHARINI
Katika kuimarisha Shirika la Bandari, Serikali kwa kushirikiana na Kampuni binafsi ya AZAM
MARINE imeiimarisha Bandari ya Malindi kwa kujenga majengo ya kuhudumia abiria ikiwemo
jengo la Watu Mashuhuri (VIP), Ofisi ya Uhamiaji, Ofisi ya afya na Ofisi ya ushuru wa bandari
pamoja na kuimarisha huduma nyengine za abiria.
56
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Serikali imelifanyia matengenezo eneo la kuhifadhia makontena bandarini lenye ukubwa wa mita
za mraba 6,000. Pia, Serikali imenunua vifaa vitatu vipya vya kunyanyulia mizigo bandarini
ambavyo ni “Reach Staker” moja yenye uzito wa tani 45, “Fort lift Compty Handle” yenye uzito
wa tani saba (7) na “Fork lift” yenye uzito wa tani tano (5) ili kuongeza ufanisi katika huduma za
bandari.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi akikagua utendaji kazi
Bandarini-Zanzibar
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akifungua na kukagua jengo jipya la abiria katika bandari ya
Malindi -Zanzibar
57
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Vilevile, Serikali imekamilisha matengenezo makubwa ya gati ya Mkoani Pemba na kuondoa
tatizo la kutuama kwa maji juu ya gati, pamoja na kukamilisha matengenezo ya kiungo cha gati
hiyo ambacho kiliathirika kutokana na nguvu za mawimbi ya bahari.
Miongoni mwa vifaa vya kuinulia mizigo kikitoa huduma hiyo katika bandari ya Malindi
Gati ya Mkoani Pemba inayoendelea kufanyiwa matengenezo
58
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
5.2.1 Ujenzi wa Bandari ya Mpigaduri
Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2010 – 2015 imeiagiza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea
na mkakati wa ujenzi wa Bandari mpya ya Mpigaduri. Katika kulitekeleza agizo hili, Serikali tayari
imeshatiliana saini Hati ya Makubalinao (MoU) na Kampuni ya China Habour Engineering
(CHEC) ya China kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na uchunguzi wa kimazingira kwa
Mradi wa Ujenzi wa Bandari hiyo kwa Awamu ya Kwanza. Mapendekezo ya upembuzi yakinifu
huo ni kujenga bandari yenye urefu wa mita 300 na upana wa mita 490 itakayo hudumia meli
zenye uzito wa 50,000DWT na makontena yenye uzito wa 200,000 TEU na mizigo ya
mchanganyiko yenye uzito wa tani 300,000 kwa mwaka. Aidha, Serikali tayari imetiliana saini
mikaba ya ujenzi wa Bandari ya Mpigaduri baina yake na Kampuni hiyo ya Kichina na maombi
ya mkopo kwa ajili ya ujenzi wa bandari hiyo tayari yamewasilishwa Benki ya Exim ya China.
Kukamilika kwa ujenzi wa Bandari hiyo kutaongeza uwezo wa bandari yetu kuhudumia mizigo
mingi na meli kubwa zaidi na kwa kiasi kikubwa itaondosha tatizo lilopo sasa la msongamano wa
mizigo katika bandari ya Malindi pamoja na kuongeza Pato la Taifa.
5.3 Kuliimarisha Shirika la Meli
Katika kuliimarisha Shirika la Meli na kuwapatia wananchi usafiri wa uhakika, Serikali imetunga
Sheria Namba. 3 ya mwaka 2013 kwa madhumuni ya kulianzisha upya Shirika hilo. Mpango wa
Mageuzi wa Kimuundo na Uendeshaji wa Shirika umeandaliwa ambao pia umehusisha Mpango
Mkakati wa Shirika tayari umeridhiwa na Serikali. Aidha, Serikali kupitia Shirika la Meli
imezifanyia matengenezo makubwa meli zake mbili (2) MV. Maendeleo na MV. Ukombozi ili
kuendelea kutoa huduma bora zaidi za usafiri baharini.
5.3.1Ununuzi wa Meli Mpya ya Serikali
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kununua meli mpya ili kupunguza tatizo la usafiri wa
baharini kati ya visiwa vya Unguja na Pemba na maeneo mengine ya mwambao wa Afrika
Mashariki jambo ambalo limeleta usumbufu kwa wananchi wetu kwa muda mrefu. Katika
utekelezaji wa maamuzi haya mwezi wa Julai 2013, Serikali ilitiliana saini Mkataba na Kampuni
59
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
ya DAEWOO International ya Korea Kusini kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya ya abiria na mizigo.
Meli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mizigo yenye uzito wa tani 200.
Ujenzi wa meli hiyo tayari umekamilika na mwezi Machi 2015 ilishushwa rasmi baharini kwa
majaribio (sea trials) ambayo yameanza kufanyika mwishoni mwa mwezi Juni 2015 na meli hiyo
tayari iko safarini kuja Zanzibar na inatarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi wa Julai 2015.
5.3.2 Kubadili Mfumo wa Uendeshaji wa Ofisi ya Mrajis wa Meli na kuwa Mamlaka ya
Usimamizi wa Usafiri wa Baharini
Serikali imebadilisha mfumo wa uendeshaji wa Ofisi ya Mrajis wa Meli kwa kuanzisha Mamlaka
ya Usafiri wa Baharini ijulikanayo kama “Zanzibar Maritime Authority” (ZMA). Mamlaka hii
imeimarisha ukaguzi wa vyombo vya baharini kwa kushirikiana na SUMATRA, hatua ambayo
imepelekea kupungua kwa ajali za vyombo vya baharini kwa kiasi kikubwa.
5.3.3 Kuendeleza Mazingira ya Kuvutia Wawekezaji wa Nje na Ndani ili Kuekeza zaidi
katika Usafiri wa Baharini
Serikali kupitia Shirika la Meli imezidi kutoa ushirikiano na kushajiisha wawekezaji wa ndani na
nje kuendelea kuwekeza katika Sekta ya Usafari wa Baharini ambapo jumla ya Kampuni 23
zimewekeza katika usafiri wa baharini. Aidha, kazi za uimarishaji wa miundombinu na huduma
mbalimbali za bandari pamoja na kuandaa taratibu za matumizi bora ya bandari zinaendelea.
Boti ya Kilimanjaro III inayomilikiwa na Kampuni ya Azam Marine
60
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
5.4 USAFIRI WA ANGA
5.4.1 Kuwajengea Uwezo Wafanyakazi
Serikali imewapatia mafunzo wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege katika fani za
“Basic Airport Operation Course” katika chuo cha CATC DSM, mafunzo ya kutangaza kwa
kutumia mtambo wa kutolea matangazo na mafunzo ya “customer care training” katika chuo cha
Diplomasia Dar-es-Salaam.
5.4.2 Kusimamia Utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Uendeshaji wa Kiwanja cha Kimataifa
cha Zanzibar
Katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015 kuhusu kusimamia
Mpango Mkuu wa Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume
na ujenzi wa jengo jipya la abira, Serikali imekamilisha uundaji wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Zanzibar na kuipa jukumu la kusimamia na kuendesha viwanja vya ndege vilivyopo
Zanzibar. Aidha, Serikali imekamilisha ujenzi wa eneo la kuegesha magari na njia za kuingilia
zenye ukubwa wa mita za mraba 15,000.
5.4.2.1 Uendelezaji Ujenzi wa Uzio na Jengo Jipya la Abiria Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Abeid Amani Karume
Katika kuimarisha huduma za Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume,
Serikali imeendelea na kazi ya kujenga uzio wenye urefu wa kilomita 11.9 katika kiwanja hicho.
Aidha, Serikali inaendelea na ujenzi wa jengo jipya la abiria lenye ukubwa wa mita za mraba
25,000. Jengo hilo litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 1,600,000 kwa mwaka. Serikali
inaendelea kufanya marekebisho na kuongeza eneo la kuegeshea ndege lenye ukubwa wa mita za
mraba 37,000. Marekebisho hayo yatabadilisha mfumo wa uegeshaji wa ndege kubwa kutoka
mbele ya jengo (airside) na badala yake kuegesha upande wa kusini ya jengo.
61
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
5.4.2.2 Ujenzi wa Maegesho na Njia ya Kupitia Ndege Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
Serikali imefanya marekebisho makubwa ya sehemu ya maegesho ya ndege (apron) kwa kujenga
eneo jipya la maegesho (apron) lenye ukubwa wa mita za mraba 48,000 pamoja na kuzitanua njia
za kupitia ndege (taxiways) kutoka mita 1,800 hadi kufikia mita 3,400 katika Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume. Matengenezo yaliyofanyika yamepelekea kiwanja hicho
kuwa na uwezo wa kuchukua aina zote za ndege. Aidha, eneo la maegesho ya ndege lina uwezo
wa kuchukua ndege kubwa mbili (2) na ndogo moja (1) kwa wakati mmoja na uimara wa “run
way” umefikia PCN 61 kutoka PCN 42.
Ujenzi unaoendelea wa jengo la abiria la”Terminal II”na mchoro wa hali ya jengo hilo litakavyoonekana baada
ya ujenzi kukamilika
Ndege mbalimbali zikiwa katika eneo la Maegesho ya Ndege katika Uwanja wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume -Zanzibar
62
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
5.4.2.3 Kukamilisha Kazi za Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Pemba
Serikali imeimarisha Uwanja wa Ndege wa Pemba kwa kufanya ukarabati wa jengo la abiria,
kuongeza urefu wa njia ya kutulia na kurukia ndege kutoka mita 1,500 hadi 2,300, uwekaji wa taa,
uzio katika barabara ya kurukia na kutulia ndege na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa
huduma mbalimbali katika kiwanja hicho. Rasimu ya Upembuzi yakinifu wa kifedha na
kimazingira imekamilika na sasa Serikali ipo katika hatua za manunuzi ili Wakandarasi waweze
kukamilisha kazi hiyo.
5.5 UMEME
Nishati ya Umeme ni muhimu katika kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa Taifa
linalojitegemea. Lengo kuu la Serikali ni kuendeleza mpango wa upatikanaji wa umeme mbadala
ambapo hatua ya matayarisho kwa uchambuzi yakinifu wa kuzalisha umeme mbadala tayari
yameanza. Serikali imesimamia kikamilifu utekelezaji wa Mradi wa Kujenga Njia ya Pili ya
Umeme inayopita chini ya bahari kutoka Ras Kiromoni Tanzania Bara hadi Fumba Unguja kupitia
mradi wa MCC. Kukamilika kwa mradi huu kumeiwezesha Serikali kupata mafanikio makubwa
kwa kuongezeka kwa kiwango cha umeme hadi kufikia Megawatt 100 kwa Unguja. Kwa upande
wa Pemba, Serikali imejenga njia ya umeme ya Megawati 20 inayopita chini ya bahari kutoka
Tanga hadi kisiwani Pemba kupitia mradi wa NORAD na kukiwezesha kisiwa cha Pemba kupata
umeme wa uhakika kutoka katika gridi ya Taifa.
Uwanja wa Ndege wa Karume - Pemba
63
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein akikagua Kituo cha Umeme – Mtoni
Kazi ya Kulaza Nyaya za Umeme kutoka Tanga kwenda Pemba
64
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Katika kuimarisha na kuendeleza mipango ya usambazaji wa huduma ya umeme kwa wananchi
wa mijini na vijijini, Serikali imeimarisha njia na miundombinu ya umeme kwa ujenzi wa njia za
kusambaza umeme kuanzia Mtoni-Tunguu, Mtoni-Fumba na Mtoni-Mahonda kwa lengo la
kuimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo hayo. Aidha, Serikali imejenga vituo vya
kusambaza umeme katika maeneo ya Mtoni, Welezo na Mwanyanya ili kurahisisha upatikanaji
wa umeme kwa wananchi. Mradi huu umefadhiliwa na Serikali ya Japan kwa kushirikiana na SMZ
na umegharimu Shilingi Bilioni 55.
Pia, Serikali imejenga laini kubwa ya Umeme (H/T) yenye urefu wa kilomita 5.2 katika vijiji vya
Kibonde Maji na Pongwe kwa Unguja na vijiji vya Kivugo na Kichuwani kwa Pemba. Aidha, vijiji
129 badala ya 123 vilivyokusudiwa awali vimefikishiwa huduma za umeme Unguja na Pemba.
Sambamba na hayo Serikali inaendelea na jitihada zake za kuyapatia nishati ya umeme maeneo ya
Kisiwa cha Makongwe, Kisiwa Panza na Kisiwa cha Shamiani Pemba.
Katika kuendeleza juhudi za utafiti wa vyanzo vya nishati ya umeme mbadala ukiwemo umeme
wa jua, mawimbi ya bahari, upepo na gesi asilia, Serikali imeyakagua upya na kuyafanyia uhakiki
maeneo yote ambayo yalifanyiwa utafiti wa awali na kupendekezwa na wataalamu kutoka EU ili
kutumika kwa ajili ya nishati mbadala kabla ya kuanza hatua ya utekelezaji.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika Picha ya
Pamoja baada ya Ufunguzi wa Umeme katika Kijiji cha Ukunjwi
65
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
5.5.1 Kuimarisha Mazingira ya Kuvutia Wawekezaji katika Sekta ya Nishati ya Umeme
Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji kwa kufanya utafiti yakinifu
katika nyanja za umeme mbadala wa upepo, jua na takataka ili kuwapa wepesi wawekezaji kuja
kuekeza. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana saini na Kampuni ya Italia ambayo itafunga
minara itakayotumika kufanyia tafiti hizo kwa kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU). Vilevile,
Serikali kupitia Shirika la Umeme imetayarisha “Customer charter” ambayo inatarajiwa
kuwasilishwa kwa wananchi na wawekezaji wote.
5.5.2 Kuwapatia Mafunzo Wafanyakazi katika Fani za Nishati na Madini
Serikali imeendelea na juhudi za kuwapata wataalamu wa mafuta na gesi. Jumla ya vijana 30
wanaendelea na mafunzo ya fani hizo kupitia vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi. Vilevile,
Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya RAKGAS imedhamini mafunzo kwa vijana wawili (2)
katika fani ya uhandisi wa mafuta na gesi, kati ya hao mmoja (1) ameshamaliza masomo yake
katika Shahada ya Pili na mmoja (1) anaendelea na Shahada ya Kwanza.
5.5.3 Kuliimarisha Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO)
Serikali inaendelea kulisaidia Shirika la Umeme ili kuweza kujiendesha kibiashara kwa
kutekeleza miradi ambayo ni muhimu sana kwa Shirika hilo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
na Serikali ya Sweden wametiliana saini kuhusu ZECO kupatiwa msaada wa kubadilisha mita
zote za kawaida “Post paid” na kufungwa mita za TUKUZA “Pre-paid” kwa Unguja na Pemba.
Pia, Serikali imepanga kufunga mita maalum kwa matumizi ya wateja wakubwa “AMR” ambazo
zitarahisisha kupata mapato na kugundua udanganyifu wowote utakaofanywa na mteja. Aidha,
Serikali kupitia Shirika la Umeme inawaungia wananchi huduma ya umeme kwa njia ya mkopo
kwa wananchi ambao kipato chao ni cha chini ili kuwawezesha kupata huduma hiyo na
kuliongezea Shirika mapato.
5.5.4 Kusimamia Uendeshaji wa Nishati ya Mafuta na Gesi
Katika kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nishati, Serikali imeandaa Mpango Mkakati wa
Utekelezaji wa Sera ya Nishati. Vilevile, Serikali imekamilisha utayarishaji wa Sheria ya Udhibiti
wa Huduma ya Maji na Nishati na Sheria ya Uanzishwaji wa Mamlaka ya Kusimamia Nishati ya
2013 (ZURA). Aidha, suala la Mafuta na Gesi lilijadiliwa katika Baraza la Nane la Wawakilishi
ambapo Serikali imeshauriwa kwa namna mbalimbali kuhusiana na suala hili. Katika kuufanyia
66
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
kazi ushauri huo, Serikali imelifuatilia kwa karibu zaidi suala hili, na kwa kuanzia imefanya
mazungumzo na kusaini makubaliano ya awali na Kampuni zinazojishughulisha na Uchimbaji wa
Mafuta na Gesi Asilia ikiwemo Kampuni ya RAK GAS ya Ras Al khaima na Kampuni ya Shell
ya Uholanzi. Dhamira ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kuona kuwa katika kipindi kifupi
kijacho Mafuta na Gesi yanachimbwa Zanzibar baada ya kufanyiwa kazi masuala ya Kisheria.
5.6 ARDHI
Kwa kujua umuhimu wa ardhi kwa maendeleo ya kisasa ya uchumi na ya kijamii, Ilani ya CCM
ya mwaka 2010 - 2015 imeiagiza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kukamilisha Sera ya Ardhi
ya Zanzibar na kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Matumizi Bora ya Ardhi.
Serikali katika kulitekeleza agizo hili imeendaa Sera ya Ardhi ambayo itasimamia matumizi bora
ya ardhi kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo. Aidha, kazi za kupitia na kutayarisha upya Mpango
Mkuu wa Kitaifa wa Matumizi Bora ya Ardhi wa Zanzibar (National Land Use Plan) umefikia
asilimia 80. Vilevile, utayarishaji wa mipango ya kina ya vijiji vya ukanda wa pwani kwa ajili ya
maendeleo ya utalii kwa kijiji cha Nungwi imefikia asilimia 85. Kazi inayoendelea ni utayarishaji
wa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Maendeleo ya Miji (National Spatial Development Strategy)
unaokusudiwa kutoa muongozo maalum wa uendelezaji wa miji yetu ya Unguja na Pemba ili
kuwezesha ukuaji endelevu wa miji hiyo. Mpango huu unakwenda sambamba na Mpango Mkuu
wa Matumizi Bora ya Ardhi nchini. Vilevile, ripoti za hali halisi ya Mji wa Zanzibar, na uchambuzi
wa taarifa kwa ajili ya utayarishaji wa Mpango Mkuu wa Matumizi ya Ardhi ya Mji wa Zanzibar
zimetayarishwa. Pia, Serikali imeongeza kazi ya upimaji wa viwanja ambapo jumla ya viwanja
1,185 vimepimwa kama inavyoonekana katika jedwali Namba 2.
Jedwali Namba 2: Maeneo yaliyopimwa viwanja Zanzibar
Na. MAENEO IDADI
1. MAKAAZI 459
2. HUDUMA 162
3. VITEGA UCHUMI 101
4. TAASISI 92
5. MASHAMBA 371
67
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
JUMLA 1,185
Serikali imeendeleza kazi ya usajili wa ardhi katika maeneo mbalimbali hasa maeneo ambayo
hayajapimwa ili kuyapima na kuwapatia wahusika hati za umiliki wa ardhi kwa mujibu wa Sheria.
Katika juhudi za kupunguza migogoro ya ardhi na kupunguza kesi za malalamiko ya ardhi, Serikali
imeziimarisha Mahakama za Ardhi na kuanzisha Mahakama nyengine za ardhi katika Mikoa yote
ya Unguja na Pemba na kuongeza idadi ya Mahakimu katika Mahakama hizo. Pia, Serikali
imezifanyia mapitio na marekebisho ramani zote kwa mujibu wa mabadiliko yanayojitokeza,
pamoja na kuzihuisha ramani za miji ya Zanzibar (Unguja Mjini, Chake Chake, Wete na Mkoani)
vikiwemo visiwa vidogo vidogo. Katika hatua hii Serikali imechapisha ramani mpya ya visiwa
vya Unguja na Pemba ambazo zimeanza kutumika. Aidha, Serikali imefanya matayarisho ya
mipaka ya kiutawala ya Mikoa na Wilaya za Unguja na Pemba, ambapo kwa upande wa Unguja,
upimaji wa maeneo tayari umefanyika:-
• Wilaya ya Kaskazini A na Kaskazini B,
• Wilaya ya Kaskazini B na Wilaya Magharibi A na Wilaya ya Kati,
• Wilaya ya Magharibi A na Wilaya Magharibi B na Wilaya ya Kati
• Wilaya ya Mjini na Wilaya ya Magharibi A na Wilaya ya Magharibi B
Na kwa upande wa Pemba pia upimaji huo unaendelea ambapo maeneo yafuatayo yamepimwa:-
• Wilaya ya Micheweni na Wilaya ya Wete,
• Wilaya ya Wete na Wilaya ya Chake Chake.
5.6.1 Usajili za Ardhi kwenye Maeneo ya Fukwe na Miji
5.6.1.1 Maeneo ya Fukwe
Serikali imefanya kazi ya utambuzi wa umiliki wa ardhi katika maeneo ya fukwe za Nungwi, Paje
na Chwaka kwa Unguja na maeneo ya Michenzani kwa Pemba. Jumla ya wamiliki 1,600
wametambuliwa kwa upande wa Nungwi na wamiliki 1,000 kwa upande wa Paje.
5.6.1.2 Maeneo ya Miji
Katika maeneo ya miji, kazi ya utambuzi wa umiliki wa ardhi ilifanyika kwa kipindi cha majaribio
(Pilot) ambapo jumla ya wamiliki 6,000 walitambuliwa na tayari wameshasajiliwa. Maeneo ya
68
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
miji ambayo yameshasajiliwa ni Shehia zote za Mji Mkongwe, Mchangani, Vikokotoni,
Mwembetanga, Mlandege, Kikwajuni bondeni, Mwembeladu, Mwembeshauri, Miembeni,
Rahaleo, Gulioni, Kwahani, Kwalinatu, Chukwani na Kidongochekundu.
SEHEMU YA SITA
6.0 HUDUMA ZA JAMII
6.1 Elimu
Serikali imetoa kipaumbele kwa Sekta ya Elimu kwa sababu ndio msingi wa maendeleo ya jamii
na Taifa kwa jumla. Katika kulitilia uzito suala hilo Serikali imechukua hatua mbalimbali katika
kuboresha elimu.
6.1.1 Elimu ya Maandalizi
Katika kuendeleza juhudi za kuongeza ushiriki wa wanafunzi katika ngazi ya maandalizi, Serikali
imendelea kutekeleza Sera ya Elimu ya mwaka 2006, ambayo imeelekeza kuwa elimu ya
maandalizi ni sehemu ya elimu ya lazima. Madarasa ya elimu ya awali yamefunguliwa katika skuli
73 za msingi Unguja na Pemba. Aidha, idadi ya wanafunzi wa skuli za maandalizi imeongezeka
kutoka 29,732 (15,216 wanawake na 14,516 wanaune) mwaka 2010 hadi kufikia wanafunzi
38,808 (19,654 wanawake na 19,154 wanaume) mwaka 2015.
69
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
6.1.1.1 Utayarishaji wa Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia vya Elimu ya Maandalizi
Skuli za Maandalizi zimepatiwa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kupunguza mzigo kwa
wazazi wa kuchangia ununuzi wa vifaa vya skuli. Serikali imewapatia mafunzo watendaji 48
wanaohudumia watoto katika skuli za maandalizi juu ya elimu ya afya, maji na usafi wa mazingira
ili waweze kuwatunza vyema watoto hao.
Aidha, Serikali imekamilisha uchapishaji wa moduli ya nne (4) na ya tano (5) kwa ajili ya kutolea
mafunzo kwa wakufunzi wa walimu kwa njia ya TEHAMA. Vilevile, vifaa vya kujifunzia
wanafunzi wa elimu ya maandalizi vimenunuliwa vikiwemo vibao vya kuandikia (slates), kadi za
nambari na za maneno. Pembea kwa ajili ya michezo ya wanafunzi wa maandalizi zimejengwa
katika skuli 30. Mafunzo ya Mtaala wa masomo ya Kiingereza na Kiarabu yametolewa kwa
walimu wa skuli za maandalizi za Serikali za Unguja na Pemba.
Serikali imewapatia mafunzo walimu wapatao 201 ya kuinua uwezo wa kufundisha watoto
wadogo, walimu 280 walipatiwa mafunzo juu ya mtaala mpya wa elimu ya maandalizi. Aidha,
wakufunzi 63 watasomesha walimu wa maandalizi kwa njia ya redio Unguja na Pemba.
6.1.1.2 Kuongeza Idadi ya Madarasa ya Elimu ya Maandalizi
Idadi ya skuli za maandalizi imeongezeka kutoka skuli 238 mwaka 2010 hadi 279 mwaka 2015,
ongezeko hili ni sawa na asilimia 17. Aidha, Serikali imekamilisha ujenzi wa skuli za maandalizi
za Kama, Potoa, Tunduni, Jongowe na Konde na kuzipatia samani za madarasani na ofisini. Aidha,
ukarabati wa skuli ya maandalizi ya Machomane umefanyika. Vilevile, jumla ya madawati (meza
na viti) 545 yamesambazwa katika skuli mbalimbali katika kipindi cha miaka mitano.
70
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Pia, Sekta Binafsi imeitikia wito wa Serikali wa kuanzisha skuli za maandalizi. Hadi kufikia
mwaka 2014/2015, jumla ya skuli za maandalizi za Watu Binafsi zimefikia 244 zikiwa na idadi ya
wanafunzi 30,256 na Skuli za maandalizi za Serikali ni 35 zenye jumla ya wanafunzi 16,624.
6.1.1.3 Kukamilisha Sera ya Makuzi na Malezi ya Mtoto
Serikali inaendelea na mchakato wa kutengeneza sera mpya ya watoto itakayojulikana kama Sera
ya Watoto Zanzibar (Zanzibar Children Policy). Sera hiyo itachukua nafasi ya Sera ya mwanzo
iliyojulikana kama Sera ya Hifadhi na Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2001. Sera hiyo mpya
pamoja na mambo mengine itazingatia mambo makuu yaliyozuka mfano Sheria ya Mtoto Namba
6 ya 2011, Mahakama ya Mtoto, MKUZA II na Vision 2020. Sera hiyo pia, itazingatia masuala
ya Makuzi na Malezi ya Mtoto.
6.1.2. Kuimarisha mazingira ya Skuli za Msingi
Serikali inaendelea kuhamasisha wananchi na wadau wengine wa maendeleo kujenga skuli mpya
za msingi. Kutokana na uhamasishaji huo, idadi ya skuli za msingi imeongezeka kutoka 299
mwaka 2010 hadi kufikia 359 mwaka 2015, ongezeko hilo ni sawa na asilimia 20. Vilevile, katika
kipindi hichi cha miaka mitano, Serikali imekamilisha ujenzi wa madarasa 326 (180 Unguja na
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akifungua Skuli Mpya ya Maandalizi ya Saemaul Cheju
Zanzibar
71
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
146 Pemba). Pia, jumla ya madawati 7,955, seti za viti vipatavyo 2,371 na meza za walimu 2,329
zimechongwa na kusambazwa katika madarasa yaliyokamilishwa kujengwa Unguja na Pemba.
Aidha, Serikali imeboresha mazingira ya skuli nyingi mpya na kongwe Unguja na Pemba kwa
kujenga “ramp” ambazo watoto wenye ulemavu wanaweza kuingia madarasani kwa urahisi.
Aidha, ujenzi wa vyoo unaendelea katika skuli mbalimbali Unguja na Pemba, Serikali imetenga
vyoo maalumu kwa matumizi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum. Jumla ya wanafunzi 203
wenye aina mbalimbali za ulemavu wameandikishwa skuli katika ngazi ya elimu ya msingi kupitia
elimu mjumuisho.
6.1.2.1 Kuimarisha Ufundishaji katika Madarasa ya Awali ya Msingi (Std 1-4)
Serikali imeajiri walimu 975 wa ngazi ya cheti na kupangiwa kazi katika skuli za mikoa mitano
ya Unguja na Pemba. Aidha, walimu 1,823 wanaofundisha katika ngazi ya elimu ya msingi
wamepatiwa mafunzo ya ngazi ya Stashahada ya Elimu ya Msingi katika chuo cha Kiislamu
Mazizini Unguja, Chuo cha Kiislamu Micheweni Pemba na Chuo cha Ualimu cha Benjamin
William Mkapa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita. Vilevile, jumla ya vitabu vya kiada
711,054 vya elimu ya msingi (Std 1-4) vimechapishwa na kusambazwa katika skuli za Unguja na
Pemba. Vitabu husika ni vya masomo ya Kiswahili, Hesabati, Sayansi, Sayansi Jamii na
Kiingereza. Idadi ya wanafunzi walioandikishwa katika darasa la kwanza imeongezeka kutoka
38,743 (19,163 wanawake na 19,580 wanaume) mwaka 2010 hadi kufikia 43,062 (21,129
Mabanda sita mapya ya skuli ya Msingi Jojo Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba
72
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
wanawake na 21,933 wanaume) mwaka 2015. Pia, uandishi wa vitabu vya masomo 10 (kati ya 12)
ya madarasa ya tano (5) na sita (6) unaendelea.
6.1.2.2 Kuondoshwa kwa Michango ya Wazee katika ngazi ya Elimu ya Msingi
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeondosha michango ya wazee wa wanafunzi wa ngazi ya
msingi ili kuhakikisha fursa sawa ya elimu inapatikana kwa watoto wote wa Unguja na Pemba bila
kujali kipato cha wazee wao. Katika kulitekeleza hili, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, itazipatia skuli zote, za msingi za serikali, vifaa vya
kujifunzia na kusomeshea kwa ajili ya wanafunzi wao. Vifaa hivyo ni Mabuku, Chaki, Daftari la
Mhudhurio, Manilla, Karatasi za A4, Gundi, Mkasi, Marker Pen, Vifaa vya Maabara na Vitabu.
Dhamira hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza au kuondosha kabisa tatizo la watoto
kutopelekwa skuli kwa sababu ya umasikini wa wazee wao katika kuwahudumia watoto wao
mahitaji yao ya skuli.
6.1.3 Elimu ya Sekondari
Katika kuendeleza juhudi za ujenzi wa skuli mpya za sekondari, Serikali imekamilisha ujenzi wa
skuli 19 Unguja na Pemba. Ujenzi huo umefanya idadi ya skuli za Sekondari kuongezeka na
kufikia jumla ya skuli 263 mwaka 2015 kutoka skuli 194 mwaka 2010. Skuli zenyewe ni Mlimani
(Matemwe), Mwanda, Mapinduzi (Chaani), Umoja Uzini, Mikindani (Dole), Jumbi, Kombeni,
Mtule, Kiembesamaki, Faraja (Kwa Mtipura) na Mpendae kwa upande wa Unguja na Shamiani,
Wawi, Ngwachani, Kiwani Mauani, Utaani, Pandani, Konde na Chwaka Tumbe kwa upande wa
Pemba. Aidha, ujenzi wa skuli ya Sekondari za Kibuteni, Donge na Mkanyageni unaendelea.
Vilevile, katika kipindi cha miaka mitano, Serikali imekamilisha ukarabati wa madarasa 263 ya
skuli za sekondari Unguja na Pemba.
73
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Kukamilika kwa skuli hizo kumesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kwa baadhi ya
skuli za sekondari. Kutokana na juhudi hizi, idadi ya wanafunzi katika ngazi ya sekondari kidato
cha kwanza hadi cha nne imeongezeka kutoka 78,165 (41,804 wanawake na 36,361 wanaume)
mwaka 2012 na kufikia 79,662 (43,544 wanawake na 36,118 wanaume) mwaka 2014. Vilevile,
Serikali imechonga na kusambaza jumla ya madawati 80,806, viti 4,934 na meza 5,800 kwa Skuli
Jengo la Skuli ya Sekondari ya Faraja lililofunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Kwamtipura Mjini Zanzibar
Jengo la Skuli ya Madungu Sekondari lililojengwa hivi karibuni
74
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
za Sekondari mpya zilizojengwa kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia pamoja na zile za wananchi
Unguja na Pemba.
Katika kuhakikisha upatikanaji wa vitabu kwa Skuli za Sekondari, Serikali imesambaza jumla ya
vitabu 201,162 katika skuli za Unguja na Pemba. Jumla ya vitabu vya kiada vipatavyo 748,316 na
vya maktaba 30,260 kwa skuli za sekondari vimenunuliwa na kusambazwa. Vitabu hivyo ni vya
masomo ya Kiswahili, Kiingereza, Jiografia, Civics, Historia, Kompyuta na masomo ya Ualimu.
Pia, vifaa vya maabara vya skuli za sekondari kwa kidato cha nne (4) na sita (6) vimenunuliwa na
kusambazwa katika skuli 100 za Unguja na Pemba.Vilevile, Serikali imekamilisha ujenzi wa
nyumba 27 za walimu katika skuli za Unguja na Pemba kama zinavyoonekana katika jedwali
namba 3.
Jadweli namba 3: Idadi ya nyumba za walimu zilizojengwa Unguja na Pemba
Na. SKULI IDADI YA
NYUMBA
1 Mwanda 3
2 Uzini 3
3 Paje (Mtule) 3
4 Pandani 3
5 Chwaka Tumbe 3
6 Kiwani 3
7 Wawi 3
8 Utaani 3
9 Matemwe 3
Jumla 27
6.1.3.1 Kuimarisha Elimu ya Sayansi na Hesabati kwa Kuendeleza Kambi za Sayansi
Katika juhudi za kuimarisha ufundishaji wa masomo ya sayansi, jumla ya walimu 10 wamepatiwa
mafunzo nje ya nchi na walimu 450 wa Sekondari wamepatiwa mafunzo ya kuinua uwezo wao wa
kufundisha masomo ya hesabati na sayansi ikiwemo utumiaji wa vifaa vya maabara kikamilifu.
Aidha, Kambi za sayansi zimeendeshwa kwa washiriki 560 katika Vituo vya Walimu viliopo
75
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Unguja na Pemba ili kuwavutia wanafunzi wapende masomo ya sayansi na hesabati. Pia, Serikali
imeziteuwa Skuli za Benbella kwa Unguja na Utaani kwa Pemba kuwa skuli maalum za sayansi
kwa wanawake.
6.1.3.2 Kutoa Mafunzo kwa Walimu Wakuu na Maafisa wa Elimu wa Wilaya na Mikoa
Serikali imewapatia mafunzo Walimu Wakuu 350 juu ya miiko na maadili ya kazi ya ualimu.
Vilevile, mafunzo ya uongozi kwa walimu wakuu na wasaidizi walimu wakuu wapya wa skuli 32
za Unguja yametolewa. Pia, mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi pamoja na walimu wakuu
92 yametolewa ili kuimarisha kazi ya ukaguzi wa skuli.
6.1.4 Elimu Mbadala na Elimu ya Watu Wazima
Juhudi za kufuta ujinga wa kutojua kusoma na kuandika zimendelezwa. Hivi sasa kuna madarasa
431 yenye wanakisomo 6,963 (5848 wanawake na 1,115 wanaume). Aidha, uandaaji wa mitaala
kwa ajili ya mafunzo ya wakufunzi wa Mafunzo ya Amali umekamilika. Kazi ya kuandika
mihutasari mipya ya masomo imekamilika na kazi ya kuandika vitabu vya wanafunzi vya masomo
11 pia imekamilika. Serikali inaendelea kutoa elimu mbadala kwa lengo la kuwapatia masomo
vijana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 15 walioko nje ya skuli, wakiwemo walioacha masomo
njiani kwa sababu mbalimbali na waliokosa fursa ya kuanza masomo wakiwa na umri mdogo.
Maabara Mpya katika Skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki
76
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Kituo cha Elimu Mbadala Rahaleo kinatoa fani mbalimbali zikiwemo ushoni, upishi, umeme,
uchongaji na utunzaji nyumba. Idadi ya wanafunzi katika kituo hicho imeongezeka kutoka 256
mwaka 2011 (wanawake 67 na wanaume 179) hadi kufikia wanafunzi 305 (wanawake 73 na
wanaume 232) mwaka 2015.
6.1.5 Huduma za Maktaba
Katika kuimarisha huduma za maktaba, Serikali imekamilisha Ujenzi wa Maktaba Kuu ya
Zanzibar na ujenzi wa Maktaba Kuu Pemba unaendelea. Aidha, jumla ya vitabu 7,116 mwaka
2011 vya masomo mbalimbali vikiwemo vitabu vya watoto, vitabu vya kiada vya msingi,
sekondari, elimu ya juu pamoja na masomo ya ualimu vimenunuliwa. Kwa mwaka huu 2015,
jumla ya vitabu 5,467 vimenuuliwa kwa ajili ya matumizi kwa Maktaba Kuu Unguja na Maktaba
Kuu Pemba.
6.1.5.1 Kuendeleza Mafunzo ya Ukutubi
Serikali imeanzisha mafunzo ya ukutubi ya awali ambapo jumla ya wakutubi 151 wamehitimu
mafunzo ya ukutubi ngazi ya awali. Aidha, wafanyakazi saba (8) wameendelezwa katika ngazi ya
Stashahada ya Ukutubi na utunzaji kumbukumbu. Vilevile, mafunzo ya ukutubi yametolea kwa
walimu wa skuli 44 za Unguja na skuli 40 za Pemba ili wapate taaluma sahihi juu ya namna bora
ya kutoa huduma za maktaba na kukuza maendeleo ya elimu nchini. Pia, jumla ya walimu 560
Maktaba Kuu ya Zanzibar iliyopo eneo la Maisara Mpirani
77
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
kutoka skuli za Wilaya ya Kaskazini ‘A’, Kusini Unguja, Chake Chake na Mkoani walipatiwa
mafunzo juu ya usimamizi wa maktaba.
6.1.5.2 Kuhamasisha Wananchi Kutumia Maktaba
Serikali imeendelea kushajiisha na kutoa ushauri kwa wananchi juu ya kuanzisha maktaba katika
maeneo mbalimbali yakiwemo skuli na maeneo ambayo jamii zinaishi. Aidha, Shirika la Maktaba
kwa kushirikiana na Jumuiya isiyo ya kiserikali MJUKIZA limeanzisha utaratibu wa kuwa na
maktaba za jamii ili ziweze kutoa huduma kwa jamii kwa ukaribu zaidi. Hadi sasa jumla ya
maktaba nane (8) za jamii katika maeneo ya Chumbuni, Welezo, Kiembesamaki, Mpapa, Uzini,
Fumba, Bweleo na Tumbatu zinatoa huduma. Pia, Programu 182 za watoto zimeendeshwa katika
Maktaba Kuu za Unguja na Pemba.
6.1.6 Elimu ya Juu Serikali inatilia mkazo katika kuendeleza elimu ya juu kwa kushirikiana na Sekta Binafsi. Kwa
kuzingatia hili, Serikali inashirikiana na Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi Afrika
(BADEA) katika ujenzi wa Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Tunguu. Ujenzi huo umekamilika kwa
majengo manne (4) pamoja na kuwekwa samani, kompyuta na vifaa vya maabara na majengo hayo
tayari yameanza kutumika. Pia, Chuo kimewapeleka masomoni ndani na nje ya nchi wafanyakazi
51 (31 ngazi ya shahada ya uzamivu, 14 ngazi ya shahada ya uzamili, 3 shahada ya kwanza na 3
stashahada) ili kuwaendeleza wakufunzi wake na kuimarisha ufanisi katika Chuo hicho. Vilevile,
Chuo kimeanzisha Diploma ya Sayansi ya Ualimu yenye jumla ya wanafunzi 102 na Diploma ya
Uongozi yenye jumla ya wanafunzi 100.
Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA) imeanzisha Skuli ya Afya na Sayansi
za Tiba katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Skuli hii imeanza na fani ya udaktari
(Medical Doctor – MD) kwa msaada wa madaktari kutoka Cuba na inaendesha shughuli zake
katika majengo ya Wizara ya Afya yaliyopo katika hospitali ya Mnazimmoja. Hadi sasa skuli
imeshaandikisha jumla ya wanafunzi 81 kati ya hao 31 wapo mwaka wa pili na 51 wapo mwaka
wa kwanza. Chuo kwa upande wake kinafanya jitihada za kufundisha vijana wa Kizanzibar ambao
watakuja kufundisha katika skuli hiyo. Hivi sasa tayari yupo mwalim Mzanzibar mmoja na
wengine wako masomoni kupitia ufadhili wa mradi wa Oman (OAF).
78
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Udahili wa wanafunzi katika Chuo hicho umeongezeka kutoka wanafunzi 1,972 mwaka 2010
(wanawake 853 na wanaume 1,119) na kufikia wanafunzi 2,078 (wanawake 1,244 na wanaume
834) mwaka 2015. Aidha, Chuo kimeongeza kutoa wahitimu wa fani mbalimbali kutoka 524
mwaka 2010 (wanawake 347 na wanaume 177) na kufikia 749 (418 wanawake na wanaume 331)
mwaka 2015.
Aidha, katika kuimarisha elimu ya sayansi na teknolojia ya kisasa, Vyuo Vikuu viliopo nchini
vimeanzisha programu za sayansi na IT kwa ngazi ya Shahada na Stashahada.
Katika kuongeza wigo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ndani na nje ya nchi,
idadi ya wanafunzi wanaodhaminiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imeongezeka kutoka
1,022 mwaka 2010 (wanawake 534 na wanaume 488) na kufikia 2,658 (wanawake 1,372 na
wanaume 1,286) mwaka 2015. Kwa mwaka 2015, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imewadhamini
wanafunzi wapya 1,410. Kati ya hao 1,028 wamejiunga na masomo katika vyuo vya ndani ya
Zanzibar, 370 vyuo vya Tanzania bara na 12 vyuo vya nje ya nchi. Jumla ya wanafunzi 2,823
ambao wanadhaminiwa na Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu, wanaendelea na masomo kwa vyuo
mbalimbali ndani na nje ya nchi. Kiwango cha kukusanya madeni kwa wanafunzi waliokopeshwa
Majengo ya Vitivo vya Sayansi na Kompyuta katika Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA)
79
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imeongezeka kutoa Shilingi 8,200,000 mwaka 2011 hadi
kufikia Shilingi 99,941,218 mwaka 2015.
Vilevile, Serikali imeboresha mazingira ya wawekezaji wa Sekta Binafsi kuendelea kuekeza katika
elimu ya juu. Chuo Kikuu cha Zanzibar (Zanzibar University) kinaendelea kutoa mafunzo
mbalimbali katika Shahada ya Kwanza na Shahada ya Pili. Chuo cha elimu Chukwani
kimepandishwa hadhi na kuwa Chuo Kikuu kamili (Al-ssumait University) na hivyo kukiwezesha
kutoa shahada za juu.
6.1.7 Kuimarisha Mafunzo ya Ualimu
Serikali imeandaa Rasimu ya Sera ya Mafunzo ya Ualimu Kazini na imefanya mapitio ya Mtaala
wa Diploma ya Msingi. Mtaala huo umeingiza masomo mapya yakiwemo ya Habari na
Mawasiliano, Mafunzo ya Amali, Uongozi na Michezo. Kazi ya kutayarisha mtaala wa stashahada
kwa walimu wa maandalizi inaendelea katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
Vilevile, mafunzo kwa wakufunzi wa vyuo juu ya matumizi ya mtaala mpya yalitolewa na
mafunzo kazini ya masomo mbalimbali kwa walimu wa skuli za msingi na sekondari yametolewa.
Jumla ya walimu wa skuli za msingi 1,539 walishiriki mafunzo ya sayansi na walimu 2,000
walishiriki mafunzo ya lugha ya kiingereza. Kwa upande wa skuli za sekondari walimu 150
walishiriki mafuzo ya sayansi na hesabati. Serikali imeendelea kutoa mafunzo maalum kwa
wakufunzi wa TAP wapatao 19 (Unguja 12 na Pemba 7). Pia, mafunzo ya kompyuta yametolewa
kwa walimu 120 Unguja na Pemba. Vilevile, vituo viwili vya ualimu vya Dunga na Kiembesamaki
vimepatiwa kompyuta na vifaa vyake kwa ajili ya matumizi ya vituo, ukuzaji wa matumizi ya
TEHAMA na kurahisisha uwekaji wa kumbukumbu.
Aidha, walimu 16 walipatiwa mafunzo ya lugha ya kiingereza na mbinu za kufundishia kwa njia
ya mtandao, Walimu saba (7) na Mkaguzi mmoja (1) walishiriki mafunzo hayo ya ufundishaji wa
masomo ya sayansi yaliyotolewa kupitia Mradi wa SMASSE huko Nairobi. Serikali pia,
imeendelea kutoa mafunzo ya ualimu kwa njia ya elimu masafa kwa walimu wa msingi
wasiosomea ili kuweza kupunguza idadi ya walimu wasiosomea mafunzo hayo. Idadi ya walimu
wasiosomea imepungua kutoka walimu 630 mwaka 2010 (wanawake 515 na 115 wanaume) hadi
kufikia walimu 501 (445 wanawake na 56 wanaume) mwaka 2015. Jumla ya wafanyakazi 2,867
80
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
wameendelezwa katika vyuo vya ndani na nje ya nchi katika ngazi za Cheti, Stashahada, Shahada
ya Uzamivu na Uzamili.
6.1.7.1 Mafunzo ya Ualimu
Mafunzo ya ualimu hutolewa katika vyuo vitatu ambavyo ni Chuo cha Kiislamu Mazizini, Chuo
cha Kiislamu Kiuyu na Chuo cha Benjamin William Mkapa Pemba. Vyuo hivi vinatoa mafunzo
ya ualimu katika ngazi ya Stashahada ya Sanaa Sekondari, Stashahada ya Sayansi Sekondari,
Stashahada Ualimu Msingi, Stashahada ya somo la Dini na Kiarabu na Cheti cha Ualimu wa Elimu
Mjumuisho. Kwa kipindi cha miaka mitano, vyuo hivyo vimesomesha jumla ya wanafunzi 5,009
(3,740 wanawake na 1,269 wanaume). Kati ya wanafunzi hao, wanafunzi 71 (66 wanawake na 5
wanaume) ni wa mafunzo ya Cheti cha Ualimu wa Elimu Mjumuisho.
6.1.8 Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Amali
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imeendelea kutoa elimu ya amali kwa
wanafunzi 3,130 (936 wanawake na 2,194 wanaume) katika vituo vitatu vya Mafunzo ya Amali
vya Mkokotoni, Mwanakwerekwe na Vitongoji. Vituo hivyo vinatoa mafunzo ya fani mbalimbali
za ufundi zikiwemo Useremala, Ushoni, Uhunzi, Upishi, Uchoraji na Uandishi wa alama, Uashi,
Ufundi Bomba, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Huduma za Chakula na Vinywaji, Ufundi
magari, Umeme na Ufundi mafriji na Viyoyozi. Aidha, elimu ya ufundi inaendelea kutolewa katika
Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia. Idadi ya wanafunzi imeongezeka katika Taasisi hii
kutoka 237 mwaka 2010 (wanawake 55 na wanaume 182) hadi kufikia wanafunzi 1,308
(wanawake 250 na wanaume 1,058) mwaka 2015. Aidha, Taasisi ilikuwa na jumla ya wanafunzi
185 kwa mwaka 2011 (wanawake 36 na wanaume 149) na kuongezeka hadi wanafunzi 277 (64
wanawake na 213 wananume) wa ngazi ya stashahada (NTA 4 – NTA 6) ambao wanaendelea na
masomo katika fani za uhandisi ujenzi na usafirishaji, uhandisi mitambo, uhandisi magari, uhandisi
mawasiliano ya anga, elektroniki na kompyuta na uhandisi umeme.
6.1.8.1 Kuimarisha Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia
Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia imeimarishwa kwa ukarabati wa mfumo wa maji na
umeme na ukarabati wa vyoo vya jengo la ICT pamoja na dahalia za wasichana na wavulana
umefanyika. Pia, majengo ya taasisi hiyo yameunganishwa na nishati ya umeme wa jua ili
81
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
kupunguza gharama za umeme. Vilevile, vifaa mbalimbali vya kufundishia vikiwemo vitabu 150
vya masomo mbalimbali vimenunuliwa.
6.1.8.2 Kuimarisha Skuli ya Ufundi Kengeja
Katika kuimarisha Skuli ya Ufundi Kengeja, Serikali imenunua vifaa vya karakana ya umeme,
vifaa vya “workshop” za uhunzi na kompyuta. Aidha, ujenzi wa madarasa manne (4) na ukarabati
wa majengo na miundombinu ya maji umefanyika.
6.2 Sekta ya Afya
Kama inavyofahamika kuwa afya ni suala la msingi kwa binadamu katika kujiletea maendeleo yao
na taifa kwa ujumla. Kwa kuzingatia Ilani ya CCM mwaka 2010 – 2015, Serikali imejikita katika
kusimamia utekelezaji wa sera na programu mbalimbali zinazohusiana na Sekta ya Afya. Aidha,
Huduma za Kinga na Tiba zimeimarishwa katika hospitali na vituo vya afya pamoja na kutolewa
elimu ya afya kwa wananchi ili kujikinga na maradhi ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.
6.2.1 Huduma za Kinga
Serikali imefanya utafiti wa kuangalia kiwango na sababu hatarishi zinazopelekea kupata maradhi
yasioambukiza (National Non Communicable Disease Risk Factors Survey). Matokeo ya utafiti
huo yanaonesha kuwa asilimia 14.3 ya watu wana uzito mkubwa (obesity), asilimia 33 ya watu
walio katika umri wa miaka 45 - 64 wana shindikizo la damu. Serikali inaendelea kuchukua juhudi
Wanafundi wa Chuo cha Ufundi Karume wakiwa katika mafunzo ya vitendo
82
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
mbalimbali za kukuza uelewa wa jamii juu ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza yakiwemo
kula vyakula vyenye chumvi nyingi, kuvuta sigara, kutokufanya mazoezi ya viungo na matumizi
ya sukari kwa kiwango kikubwa. Uelewa huo umetolewa kupitia maonyesho maalum ya filamu
na vipindi mbalimbali vya redio na televisheni.
Serikali kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Kisukari, imeshajiisha jamii
kuanzisha vikundi vya mazoezi katika Wilaya zote za Unguja na Pemba kwa nia ya kujikinga na
maradhi hayo. Hadi sasa jumla ya vikundi 10 vimeanzishwa katika maeneo mbalimbali Unguja na
Pemba. Vikundi hivi vimekuwa vikitembelewa mara kwa mara na kupewa maelekezo na pia
kualikwa katika Matamasha tofauti yanayohusiana na mazoezi. Katika kuendeleza utoaji wa elimu
ya afya ya jamii, Serikali imeanzisha redio ijulikanayo kwa jina la Afya FM Redio ambayo inatoa
elimu ya masuala ya afya kwa jamii.
6.2.2 Huduma za Tiba
Serikali imeandaa muongozo wa matibabu ya maradhi yasiyoambukiza kama vile Shindikizo la
damu, kansa na kisukari. Muongozo huu umezingatia matibabu ya maradhi yasiyoambukiza kwa
upana wake. Aidha, Serikali imeweza kutoa huduma za maradhi ya moyo na shindikizo la damu
katika hospitali za Wilaya za Chake Chake, Wete na Abdalla Mzee kwa kushirikiana na madaktari
kutoka Hospitali ya Mnazimmoja. Pia, Serikali kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanafunzi wa
Udaktari – ‘Tanzania Medical Students Association (TAMSA), imefanya uchunguzi wa maradhi
ya Kisukari na Shindikizo la Moyo katika Wilaya za Mjini, Magharibi, Kati, Kusini, Kaskazini A
na Kaskazini B. Jumla ya watu 1,800 walifanyiwa uchunguzi wa Kisukari na matibabu yalitolewa
kwa waliogunduliwa na matatizo hayo.
Vilevile, jumla ya watu 2,585 wamepatiwa huduma za uchunguzi wa macho kwa mashirikiano na
uongozi wa Shirika la Al-nour Charitable Agency la Zanzibar na Shirika la Bilal Muslim Agency
kutoka Arusha Tanzania Bara. Watu 220 walifanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho.
Katika jitihada za kuondoa maradhi ya kichocho, Serikali imeandaa Mpango wa ufuatiliaji wa
makonokono katika mito na mabwawa; mabadiliko ya tabia kwa wananchi dhidi ya maradhi ya
Kichocho na ulishaji wa dawa za Kichocho. Aidha, ulishaji wa dawa za Kichocho, Minyoo na
83
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Matende umeendelea kutolewa kwa lengo la kutibu na kupunguza maambukizo mapya ya maradhi
hayo. Dawa hizi zilitolewa na zinaendelea kwa wale wote wanaostahiki ambapo jumla ya watu
915,954 kwa Unguja na Pemba walipatiwa dawa hizo, idadi hii ni sawa na asilimia 83 ya
waliostahiki kutumia dawa hizo.
6.2.3 Huduma Bora za Afya kwa Wananchi Wote
Ili kuhakikisha kuwa huduma bora zinatolewa kwa wananchi wote nchini, Serikali imeendelea
kuviendeleza vituo vya afya 84 vikiwemo vya Daraja la Kwanza na Daraja la Pili ambavyo vinatoa
huduma za ziada kama vile huduma za uzazi, maabara na huduma za meno. Aidha, Serikali
imeifanyia mapitio Sera ya Afya ya mwaka 1999 na kuwa na Sera mpya ya mwaka 2011 pamoja
na Sheria ya Afya ya Jamii ambazo zinakwenda sambamba na mahitaji pamoja na mikataba ya
kitaifa, kikanda na kimatifa katika utoaji wa huduma za afya nchini. Vilevile, Sheria ya Mkemia
Mkuu wa Serikali (Chief Government Laboratory Act No. 10 2011) imeandaliwa ambayo
inaifanya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufanya kazi zake kisheria. Tayari Mwenyekiti
na wajumbe wa bodi itakayosimamia utekelezaji wa sheria hii wameshateuliwa na wameshaanza
kazi rasmi.
Ili kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu katika vituo vya afya unakuwa wa kuridhisha kwa
wananchi wake, Serikali inaendelea kutoa huduma hizo bila ya malipo katika hospitali zote na
vituo vya Afya vikiwemo Chukwani, Fuoni, Mahonda, Donge Vijibweni, Uroa, Jambiani,
Nungwi, Matemwe, Pwani Mchangani, Tumbatu Gomani na Bumbwini Misufini kwa Unguja na
kwa upande wa Pemba ni Makangale, Konde, Wingwi, Mizingani, Kojani Ukutini, Fundo na
Bogoa. Vituo vyote hivi vinafaidika na upatikanaji wa dawa chini ya mpango maalum ujulikanao
kama “Zanzibar Integrated Logistic System”. Vilevile, Serikali imejenga Bohari Kuu ya Dawa
iliyopo Maruhubi ambayo itarahisisha kupata na kutoa taarifa za hali ya upatikanaji wa dawa
kutoka hospitali na vituo vya afya mbalimbali nchini.
84
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Aidha, Serikali imewasomesha wanafunzi 38 madaktari kwa kushirikiana na Serikali ya Cuba
wakiwemo wanawake 19 na wanaume 19 ambao tayari wamemaliza masomo yao na hivyo kupata
madaktari wengine wazalendo 38. Idadi hiyo imewezesha madaktari wote wanaotoa huduma
Zanzibar kufikia 142, kati ya hawa madaktari 40 ni madaktari wa kigeni kutoka Cuba na China
hali ambayo imepelekea kwa sasa kuwa na uwiano wa daktari mmoja kuhudumia wastani wa
wagonjwa 9,708. Vilevile, Jumla ya wafanyakazi 142 wa kada mbalimbali wamepelekwa
masomoni ndani na nje ya nchi wakiwemo Madaktari 9, Wasaidizi madaktari 12, Wauguzi 96 na
wengine kada nyenginezo za afya na zisizo za Afya. Hivyo, kufanya idadi ya wafanyakazi wote
wanaoendelea na masomo kufikia 246 (wanaume 110 na wanawake 136). Aidha, jumla ya
wafanyakazi 44 wamerudi masomoni na kupangiwa kazi kwa mujibu wa taaluma zao.
6.2.4 Kuendeleza Huduma za Tiba Asili
6.2.4.1 Baraza la Tiba Asili
Serikali kupitia Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala imeelimisha jamii kupitia vyombo
mbalimbali vya habari, kutumia vipeperushi pamoja na kufanya mikutano na waganga wa tiba
asilia kupitia Masheha, Madiwani na Wakuu wa Wilaya. Pia, Baraza limefanikiwa kutengeneza
Kanuni (regulations) za Tiba Asili na kutoa elimu kwa waganga. Sambamba na hayo, Baraza
limeweza kusajili jumla ya Waganga 193 na Waganga Wasaidizi 58, baada ya kutimiza masharti
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali
Mohamed Shein akikagua Bohari Kuu ya Dawa - Maruhubi
85
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
yaliyowekwa ikiwa ni pamoja na kutenga sehemu maalumu ya kutoa huduma kwa wagonjwa.
Aidha, jumla ya kliniki 18 za tiba asili na tiba mbadala, viringe au sehemu wanazofanyia kazi 125
na maduka ya dawa za asili 39 yamesajiliwa baada ya kutimiza masharti ya sheria za Baraza. Pia,
sampuli 23 za dawa asilia zimechunguzwa na Maabara ya Bodi ya Chakula na Madawa (ZFDB).
Katika kuhakikisha Baraza la Tiba Asili linafanya kazi zake vizuri na ipasavyo limejenga uhusiano
mzuri kati ya madaktari wakisasa (Biomedical Practitioners) na waganga wa asili (Traditional
Healers).
6.2.5 Kuimarisha Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya
Chuo cha Taaluma cha Sayansi ya Afya kinaendelea kutoa taaluma za afya kwa kiwango cha
Stashahada katika fani mbalimbali. Katika kipindi cha miaka mitano (2010 - 2015) chuo
kimezalisha wahitimu 1,629 wakiwemo Wauguzi 612, Wasaidizi Madaktari 198, Maafisa afya ya
Mazingira 136, Ufundi Sanifu wa Maabara 122, Wasaidizi Madaktari wa Afya ya Kinywa na
Meno 201, Wafamasia 127, Ufundi Sanifu wa Vifaa Tiba (Biomedical Engineers) 55, Afisa
Maabara 74, Wasaidizi Tabibu 50 na Wakunga 54.
Ili kuweka mazingira mazuri kiutendaji na hatimae kuongezeka kwa motisha kwa wafanyakazi wa
Chuo, muundo wa Utumishi kwa wafanyakazi wa Chuo umetayarishwa na tayari
umeshawasilishwa Serikalini kwa hatua za utekelezaji.
Wanafunzi wa Chuo cha Taaluma ya Sayansi ya Afya Mbweni wakiwa darasani
86
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Serikali imeendelea kukiimarisha Chuo cha Sayansi ya Afya kwa kujenga jengo litakalotumika na
wanafunzi wa shahada ya kwanza pamoja na majengo mawili ya dakhalia kwa msaada wa Serikali
ya Oman. Pia, chuo kimeandaa Mpango wa Kujiendesha Kibiashara (Bussiness Plan) ili kiweze
kukidhi mahitaji yake. Vilevile, chuo kimeanzisha masomo ya kujiendeleza kwa wafanyakazi
wenye cheti kwa muda mrefu ambao hawakupata bahati ya kujiendeleza kielimu katika fani za
Afya ambapo jumla ya wafanyakazi wanafunzi 183 wanaendelea na mafunzo chuoni hapo.
Wanafunzi 11 wanaendelea na mafunzo ya elimu masafa kupitia Shirika la AMREF. Serikali
kupitia Chuo cha Sayansi ya Afya inaendelea kuufanyia mapitio Mtaala wa Kada ya Dawa
(Pharmaceutical science). Pia, imetengeneza Mtaala wa Kada ya Maradhi ya Viungo
(Physiotherapy) kwa lengo la kuanzisha masomo hayo katika muhula wa masomo 2014/15 ili
kuimarisha huduma za afya kwa wananchi.
Jengo jipya la Chuo cha Taaluma ya Sayansi ya Afya - Mbweni
87
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
6.2.6 Kuendeleza Mapambano dhidi ya Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu na Ukoma
6.2.6.1 Malaria
Serikali imeweza kupunguza ugonjwa wa Malaria katika jamii kutoka asilimia 0.9 mwaka 2010
hadi kufikia asilimia 0.03 mwaka 2015. Katika jitihada za kutokomeza kabisa ugonjwa wa malaria,
Serikali kupitia Wizara ya Afya imefanikiwa kuchunguza watu 8,126 katika shehia tisa (9)
zilizokuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa Malaria, watu 97 sawa na asilimia 1.2
waligundulika kuwa na vimelea vya Malaria. Uchunguzi huo ulihusisha shehia za Cheju,
Ng’ambwa, Uzi, Ukongoroni, Shakani, Bweleo, Donge Mchangani, Mtende na Kibuteni. Vilevile,
katika kudhibiti kasi ya kuenea maradhi ya Malaria, Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea
kuwafuatilia wagonjwa wanaoripotiwa kuwa na dalili za Malaria majumbani ambapo watu 1,282
walifanyiwa uchunguzi na watu 282 wamegundulika kuwa na malaria na kupatiwa matibabu.
6.2.6.1.1 Usambazaji wa Vyandarua katika Vituo vya Afya.
Serikali kupitia Wizara ya Afya chini ya Mradi wa Kumaliza Malaria kwa kushirikiana na wahisani
mbalimbali imeweza kugawa vyandarua vilivyotiwa dawa ili kupunguza maambukizo. Katika
mwaka 2010 -2014 jumla ya vyandarua 717,000 viligaiwa kwa wananchi Unguja na Pemba kwa
wastani wa vyandarua vitatu (3) kwa kaya.
Mahafali ya 21 ya Wanafunzi wa Chuo cha Taaluma ya Sayansi ya Afya - Mbweni
88
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Aidha, Kitengo hiki kimebadilisha utaratibu wa kugawa vyandarua kutoka kwenye mgao wa
pamoja na kuingia kwenye ugawaji endelevu wa vyandarua. Utaratibu huu unahusisha mama
wajawazito, watoto wenye chanjo ya miezi tisa, wanaogunduliwa na malaria wakati wa ufuatiliaji
pamoja na makundi yenye mahitaji maalum. Jumla ya Vyandarua 30,474 vimesambazwa katika
Vituo vya Afya Unguja na Pemba.
6.2.6.1.2 Upigaji Dawa Majumbani
Serikali inaendelea na upigaji dawa majumbani ambapo jumla ya nyumba 57,385 zilipigwa dawa
sawa na asilimia 96 ya lengo. Zoezi hili limefanyika katika Wilaya tisa (9) za Unguja na Pemba
ambapo limelenga kuzifikia Shehia 38 ambazo zimeonekana kuwa na wagonjwa wa Malaria mara
kwa mara na nyumba 59,462 zilizohusika katika zoezi hili.
Watoto wakirudi kuchukuwa Vyandarua vilivyotiwa dawa kufuatia mgao wa vyandarua hivyo
89
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
6.2.6.2 UKIMWI
Kiwango cha mambukizi ya UKIMWI kimeendelea kubakia kuwa asilimia 0.6 na idadi ya watu
walioambukizwa virusi vinavyosababisha UKIMWI (VVU) waliosajiliwa ni 7,820 kati ya hao
watu 5,375 wanapata huduma ya ARV. Katika kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI,
Serikali imeimarisha huduma za tiba, huduma za kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto,
vituo vya ushauri nasaha na upimaji wa VVU. Uimarishaji huo umefanywa kwa kuhakikisha
nyenzo za kufanyia uchunguzi zinapatikana kwa wakati, kufuatilia maambukizi ya VVU miongoni
mwa makundi yaliyo katika hatari ya maambukizo pamoja na makundi maalum na kuendeleza
kutoa elimu kwa jamii juu ya kupunguza unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU.
Pia, Serikali imesambaza mashine tatu mpya za CD4 ambazo zimepelekwa katika Hospitali ya
Mnazi Mmoja, Mwembeladu, na Kivunge. Aidha, mashine aina mbili za “Haematology” na
“Chemistry” zimesambazwa katika Hospitali za Micheweni, Makunduchi, na Mwembeladu.
Vilevile, Serikali inaendelea kuwahamasisha wananchi kuwa na tabia ya kupima afya zao na
kujiepusha na maambukizi mapya ya UKIMWI. Serikali kupitia Tume ya UKIMWI imeipatia
Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (ZAPHA+) jumla ya Shilingi 551,471,765
ili kuendelea na shughuli zao za kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya UKIMWI. Pia, vituo
Wapiga Dawa ya kuuwa Mbu wanaosababisha Malaria Majumbani
90
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
vinavyotoa huduma ya ushauri nasaha na upimaji wa VVU vimeongezeka kutoka vituo 87 mwaka
2012 hadi kufikia vituo 91 mwaka 2015, kati ya hivyo Unguja 58 na Pemba 33.
6.2.6.3 Kifua Kikuu na Ukoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kutoa matibabu ya Magonjwa ya Kifua Kikuu na
Ukoma kwa wananchi, ambapo Mpango wa Ulishaji Dawa kwa Jamii (Community TB Care)
umeendelea. Takwimu zinaonesha kwamba wagonjwa 2,865 wamegundulika na maambukizi
katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Kwa upande wa maradhi ya ukoma jumla ya watu 598
waligundulika na maradhi haya, kati yao wagonjwa sita (6) walikua na ulemavu Daraja la Pili.
Aidha, ununuzi wa vifaa vya kutengenezea miguu bandia na kiatu chake ulifanyika kwa
walioathirika na Ukoma. Pia, Serikali imeendesha mafunzo kwa vijiji 24 vya Unguja na Pemba
juu ya Elimu ya Ukoma ambapo jumla ya watu 1,280 (Unguja 805, Pemba 475) walihudhuria
mafunzo hayo na watu saba (7) waligundulika na Ukoma. Vilevile, Serikali imeendesha mafunzo
juu ya ugonjwa wa ukoma kwa watu 169 ambao ni jamaa za wagonjwa wa maradhi hayo. Elimu
ya afya juu ya maradhi ya ukoma inaendelea kutolewa kwa wananchi Unguja na Pemba kupitia
vyombo vya habari.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi katika Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani
akikagua huduma ya kuchangia damu salama
91
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Katika hatua nyengine, vituo vitatu vya kutoa huduma za kujitunza vimeanzishwa ili wagonjwa
wasiweze kupata ulevamu zaidi. Madhumuni ni kuwafundisha wagonjwa namna ya kujitunza na
kujilinda na ulemavu na baadae waweze kujihudumia katika vikundi vyao.
6.2.6.4 Kuipandisha Daraja Hospitali ya Wete
Katika jitihada za kuipandisha hadhi Hospitali ya Wete, Serikali imeiongezea majengo hospitali
hiyo ikiwemo wodi mpya ya akina mama pamoja na jengo la huduma ya afya ya akili (Mental
health Wing) na sehemu ya kuhifadhia maiti. Sambamba na hili, Serikali imefanya matengenezo
ya wodi ya wanaume na kuiwekea samani. Vilevile, chumba cha kuhifadhia dawa na Kliniki ya
watoto zimefanyiwa matengenezo. Aidha, hospitali imepatiwa mashine ya “Ultrasound” na
mashine ya kupimia moyo (ECG). Kupatikana kwa mashine hizi pamoja na kupatikana kwa
madaktari wawili (2) wa upasuaji kumeimarisha utoaji wa huduma katika hospitali hiyo.
6.2.6.5 Kuipandisha Daraja Hospitali ya Abdalla Mzee Pemba
Katika azma ya kuipandisha daraja Hospitali ya Abdalla Mzee, Serikali imeendelea na mpango
wake wa kuijenga upya hospitali hii ili iweze kutoa huduma bora na kuweza kufikia hadhi ya kuwa
Hospitali ya Mkoa. Hatua iliyofikia kwa sasa ni kulipwa fidia kwa wote waliobomolewa nyumba
zao ili kuwezesha kufanya upanuzi wa majengo. Jumla ya Shilingi Bilioni 1.2 zimelipwa kwa ajili
ya fidia hizo. Wakandarasi wa Kampuni kutoka China tayari wameshawasili kuanza kazi ya ujenzi
wa hospitali hiyo. Gharama za ujenzi huo zinatarajiwa kuwa ni Shilingi Bilioni 18.6.
92
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
6.2.6.6 Kuipandisha Daraja Hospitali ya Micheweni
Serikali imeendelea na uimarishaji wa Hospitali ya Micheweni kwa lengo la kuifanya ifikie kuwa
na hadhi ya Hospitali ya Wilaya. Hatua za awali za kujua mahitaji halisi ya majengo, wafanyakazi
pamoja na vitendea kazi tayari zimefanyika. Kwa sasa Serikali imeweza kufanya upanuzi wa
majengo ili kuboresha huduma katika hospitali hiyo ikiwemo wodi ya wazazi, chumba cha
upasuaji na ujenzi wa maabara mpya na ya kisasa.
Michoro ya Jengo la hospitali ya Abdalla Mzee itakavyokuwa baada ya kumalizika kwa
ujenzi wake
Hospitali ya Abdallah Mzee ikiendelea na ujenzi
93
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
6.2.6.7 Kuipandisha Daraja Hospitali ya Kivunge
Katika kuimarisha Hospitali ya Kivunge, Serikali imefanya matengenezo ya nyumba 12 za
wafanyakazi, pamoja na chumba cha upasuaji na wodi mbili (2) za watoto. Vilevile, jengo jipya la
wagonjwa wa nje (Out Patient Department) limejengwa ili kusaidia kupunguza msongamano ndani
ya hospitali. Aidha, mashine za operesheni na “ultrasound” zimewekwa katika hospitali hiyo.
Serikali kupitia Mradi wa HIPZ, imefanikiwa kuanzisha Kitengo cha Huduma za Dharura
(Emergency Unit) kitakachotoa huduma za haraka kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura
hospitalini hapo. Aidha, Serikali imeipatia hospitali hiyo “incinerator” kwa ajili ya kuchomea taka.
6.2.6.8 Kuimarisha Hospitali ya Makunduchi
Katika jitihada za kuimarisha Hospitali ya Makunduchi, Serikali imejenga jengo jipya la kupokelea
wagonjwa wa nje (outpatient department) pamoja na kukifanyia matengenezo chumba cha
kuzalishia, wodi ya kina mama wajawazito, chumba cha matibabu ya meno pamoja na ununuzi wa
vifaa vipya kwa ajili ya matibabu ya meno.
Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi akishuhudia utiaji saini na
kukagua ujenzi wa hospitali ya Micheweni - Pemba
94
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
6.2.6.9 Kuendelea Kuimarisha Huduma za Hospitali ya Mnazi Mmoja ili kufikia Hadhi ya
Hospitali ya Rufaa
Serikali kwa kushirikiana na Shirika la ICAP imefanya matengenezo makubwa katika maabara ya
Hospitali ya Mnazimmoja. Matengenezo hayo yamehusisha idara zote muhimu ambazo ni
“microbiology, parasitology, haematology, biochemistry na blood transfusion”. Matengenezo
hayo yameifanya maabara hiyo kuwa katika kiwango kizuri cha utendaji ambacho kinalingana na
maabara nyengine zilizo ndani ya nchi za Afrika mashariki. Jumla ya Shilingi milioni 300
zimetumika kwa ujenzi huo. Kutokana na matengenezo hayo hospitali inaweza kufanya vipimo 67
ukilinganisha na vipimo 30 ambavyo vilikuwa vikifanywa katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita na kuwezesha tiba ya maradhi kufanywa kwa ufanisi na usahihi. Aidha, huduma za
“histopathology” kwa uchunguzi wa saratani zimeanza kutolewa na hivyo imewarahisishia
wananchi wetu kupata huduma hizo hapa Zanzibar badala ya kuzifuata nje ya nchi. Vilevile,
Maabara hiyo imeanza kutoa huduma ya uchunguzi wa maradhi ya kifua kikuu kwa kutumia
mashine mpya ya kisasa (Gene expert) yenye uwezo mkubwa wa kugundua vimelea vya maradhi
hayo kwa haraka na kubainika hata kama vimelea vya maradhi ni kidogo, hii imewezesha
wagonjwa wa maradhi hayo kugundulika mapema na kupata tiba sahihi.
Vilevile, hospitali imeanza kutoa huduma za uchunguzi wa maradhi na tiba za mfumo wa chakula
(Gastro-enterology Endoscopic Services). Kitengo hiki kinaweza kuchunguza maradhi yote
Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kulifungua
jengo jipya la Wagonjwa wa nje katika hospitali ya Makunduchi
95
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
yatokanayo na mfumo wa chakula na kupatiwa tiba sahihi kwa mujibu wa maradhi hayo. Pia,
Serikali imeweza kuweka vifaa vya huduma nyengine za uchunguzi ikiwa ni pamoja na
“Laparascopy, CT scan, Fluoroscopy na Ultrasound” kwa ajili ya uchunguzi wa maradhi
mbalimbali. Aidha, huduma za macho zimeimarika kwa kuwekewa na kutumia vifaa vya kisasa
vya uchunguzi kama vile “slitlamp”, “A-P Scanner”, darubini ya kuchunguza matatizo ya macho,
kifaa cha kupima pressure ya macho pamoja na vifaa vya upasuaji wa macho. Sambamba na hayo,
katika kuimarisha huduma za uchunguzi na matibabu ya maradhi ya moyo Serikali imeweza
kununua mashine ya “Echocardiography” (ECG) na pia kupata daktari bingwa mzalendo wa
maradhi ya moyo.
Serikali imefanya matengenezo ya jengo la Kiwanda cha Dawa cha zamani ili kiweze kutoa
huduma bora za mama na mtoto. Matengenezo hayo yamegharimu jumla ya Shilingi bilioni
18,643,200,000. Gharama hizi zinahusisha ujenzi, vifaa na mafunzo ya utumiaji wa vifaa. Aidha,
Serikali imefanya matengenezo ya Vituo 19 vya Afya ya Msingi kwa Unguja na Pemba. Vilevile,
Serikali imefanya ujenzi na uwekaji wa vifaa katika Kitengo cha Upasuaji wa Uti wa Mgongo
(neorosurgical unit), jengo hilo tayari limeshaanza kutoa huduma. Ujenzi huo umefanywa kwa
mashirikianao na Taasisi ya “Neurosurgical Education and Development” ya Hispania. Pia,
Serikali inaendelea na ujenzi wa jengo jipya lenye wodi ya watoto ambayo inatarajiwa kuwa na
vitanda 100 vya kulaza wagonjwa, kitengo kwa ajili ya wagonjwa mahututi pamoja na wagonjwa
wenye matatizo ya figo.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akifungua Kitengo cha matibabu ya Uti wa
Mgongo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja
96
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Serikali imekifanyia ukarabati mkubwa Kitengo cha Wagonjwa Mahututi kwa kuwekewa vifaa
vya kisasa vikiwemo mtambo wa kusambaza “oxygen”, uwekaji wa vipoza hewa, “mechanical
ventilater”, “Arterial blood gas analyser” na “electronic machines”. Aidha, “air vaccum”
imewekwa kwa wodi ya ICU, wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akikagua
mashine za upasuaji katika Jengo jipya la Upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo
(Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja
Kitengo cha Wagonjwa Mahututi Kilichofanyiwa Matengenezo Makubwa katika
Hospitali ya Mnazi Mmoja
97
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Kwa upande wa Kitengo cha Meno (Dental Unit) cha Mnazi Mmoja Serikali imekifanyia
matengenezo makubwa pamoja na uwekaji wa vifaa vipya vya kisasa.
Vilevile, juhudi za uanzishwaji wa tiba kwa njia ya mawasiliano ya simu (Telemedicine) katika
Hospitali ya Mnazi Mmoja tayari zimeanza kwa maradhi ya kawaida na ya upasuaji na uti wa
mgongo. Hospitali pia, inatoa huduma za matatizo ya figo kwa wagonjwa.
Katika kuhakikisha kuwa Hospitali ya Mnazi Mmoja inafikia hadhi ya kuwa hospitali ya rufaa,
Serikali imefanikiwa kuongeza idadi ya madaktari wa kawaida (MD general) na kufikia 46 kati
yao wazalendo 44 na wageni 2 kutoka Norway. Aidha, Serikali imeongeza idadi ya madaktari
bingwa 44 kati yao 13 ni madaktari wazalendo na 31 ni wageni kutoka China, Cuba, Norway na
Denmark. Vilevile, Serikali inawaendeleza madaktari 14 waliopo kuwa madaktari bingwa kwa
maradhi ya saratani, maradhi ya watoto, maradhi ya kina mama, maradhi ya kawaida, daktari
bingwa wa radiolojia, daktari bingwa wa maradhi ya mifupa (OT), upasuaji wa uti wa mgongo na
maradhi ya macho.
Makamu wa Kwanza wa Rais Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad akikagua chumba
cha Wagonjwa Mahtuti katika Hospital ya Mnazi Mmoja baada ya Kukifunguwa ikiwa ni
miongoni mwa Shamrashamra za Miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
98
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Kwa sasa Hospitali ya Mnazi Mmoja inautaratibu wa kupokea madaktari bingwa kutoka Hispania
na Uholanzi ili kutoa huduma za upasuaji wa mgongo na vichwa maji na upasuaji wa “plastic
surgery”. Vilevile, Serikali ina makubaliano na Chuo Kikuu cha Hauckland cha Norway ya kuleta
madaktari bingwa kufanya kazi na madaktari wazalendo. Sambamba na hayo, madaktari wa
Zanzibar kutoka Hospitali ya Mnazi Mmoja nao hupata fursa ya kwenda Norway ili kufanya kazi
katika hospitali ya chuo hicho.
6.3 MAJI
Katika hatua za kuendeleza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi, Serikali
inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya kuwapatia wananchi maji safi na salama katika
maeneo yote ya mijini na vijijini. Suala hili limepewa kipaumbele katika Ilani ya Uchaguzi ya
CCM sambamba na mikakati ya Serikali ya kukuza uchumi na kupunguza umasikini.
6.3.1 Kuzifanyia Mapitio Sera na Sheria ya Maji
Serikali inaendelea kuzifanya mapitio Sera na Sheria ya Maji ili kuondoa mapungufu yaliyomo na
kuzifanya Sera na Sheria hizo kuendana na wakati na kwa mujibu wa mahitaji ya sasa na baadae.
Kukamilika kwa Sheria na Sera ya maji kutaimarisha utoaji na upatikanaji wa huduma ya maji safi
na salama mijini na vijijini.
6.3.2 Kuendeleza Usambazaji wa Maji Safi na Salama Unguja na Pemba
Usambazaji wa huduma ya maji safi na salama umeendelea kukua kutoka asilimia 75 mwaka 2010
hadi kufikia asilimia 87 mwaka 2015 kwa maeneo ya Mijini na kutoka asilimia 60 mwaka 2010
hadi kufikia asilimia 70 mwaka 2015 kwa upande wa vijijini. Jitihada hizo zimefanywa kupitia
Serikali kuu, Wadau wa Maendeleo pamoja na nguvu za Wananchi.
Aidha, Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo imetekeleza mradi mkubwa wa
Usambazaji Maji Safi na Usafi wa Mazingira ambao upo katika hatua ya majaribio. Kukamilika
kwa mradi huu kutaongeza uzalishaji wa maji kwa lita milioni 17.6 kwa siku. Mradi umechimba
visima 41, umejenga matangi 17 yenye ujazo wa viwango tofauti na ulazaji wa mabomba yenye
urefu wa kilomita 255.5 katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-
Ujenzi wa matangi nne (4) ya Matemwe (Lita 3, 000,000), Nungwi (Lita 3, 000,000),
Machui (Lita 1, 500,000) na Tunguu (Lita 1, 200,000).
99
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Uchimbaji na ujenzi wa visima tisa (9) vya uzalishaji pamoja na kujenga vibanda vya
kuendeshea mitambo na kufunga pampu.
Uchimbaji na ulazaji wa mabomba kwa maeneo yote yaliokubaliwa ya Machui (kilomita
13.1), Dunga/Tunguu (kilomita 7.8) na Matemwe (kilomita 13.9) na Nungwi kilomita
(5.8).
Ujenzi wa Matangi saba (7) ambayo ni Ndagoni (Lita 1,000,000), Vikunguni (Lita
300,000), Vitongoji Ali Khamis Camp (Lita 300,000), Kambini (Bahanasa) (Lita
1,000,000 na Lita 300,000) Wambaa (Lita 500,000) na Mizingani (Lita 300,000).
Uchimbaji wa visima 14 vya uzalishaji pamoja na kujenga vibanda vya kuendeshea
mitambo na kufunga pampu.
Ulazaji wa mabomba kwa maeneo yote yaliopangwa ya Wambaa (kilomita 10.2),
Mizingani (kilomita 25.8), Ndagoni (kilomita 27.3), Vitongoji (kilomita 29.5) na Kambini
(kilomita 41.3).
Ujenzi wa matangi ya chini (ground tanks) ya Wete Taifu (Lita 2,500,000), Wete Mtemani
(Lita 800,000), Chake-Chake (Lita 3,000,000) na Mkoani (Lita 800,000) pamoja na ujenzi
wa chemba za matangi haya zimo katika hatua za mwishoni.
Ujenzi wa matangi ya juu (elevated tanks) ya Chake-Chake (Lita 250,000) na Mkoani (Lita
250,000) unaendelea.
Uchimbaji wa visima 18 vya uzalishaji tayari umekamilika.
Ulazaji wa mabomba kwa maeneo yote yaliokubaliwa ya Chake-Chake (kilomita 31.2),
Wete (kilomita 31.9) na Mkoani (kilomita 17.6) umekamilika.
100
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
6.3.3 Kupunguza kiwango cha Upotevu wa Maji
Serikali inaendelea kuhamasisha wananchi kuwa na mwamko katika kuchangia huduma za maji
ili ziwe endelevu na kutoa kipaumbele katika kulinda, kuhifadhi na kutunza rasilimali maji. Pia,
Serikali inaendelea kufunga mita za maji katika makaazi ya wananchi wake ambapo jumla ya mita
2,581 zimefungwa. Kati ya mita hizo, mita 1,188 zimefungwa kwa wateja wa majumbani na mita
1,393 zimefungwa kwa wateja wa biashara. Ufungaji huo unalenga kupunguza kiwango cha
upotevu wa maji na kuchangia huduma ya maji kwa mujibu wa matumizi. Vilevile, Serikali
imeendelea kutoa elimu kwa umma mijini na vijijini kupitia vyombo vya habari pamoja na kufanya
makongamano ili kushajiisha wananchi katika suala la uchangiaji wa huduma ya maji. Sambamba
na hayo, zoezi la utambuzi wa mabomba yanayovuja (Leakage survey) umefanyika katika Mkoa
wa Mjini Magharibi na maeneo yote yaliyobainika yameweza kufanyiwa matengenezo. Kazi hizo
zimefanyika kupitia mafunzo ya vitendo kazini kupitia wataalamu wa JICA katika Mradi wa
kuijengea uwezo ZAWA.
Serikali ililazimika kuchukua maamuzi magumu ya kuendesha operesheni ya kuwahamisha
waliojenga katika eneo la chemchem ya Mwanyanya na kuwatahadharisha wengine waliotaka
Kazi ya Ulazaji wa Mabomba na Ujengaji wa Matangi ya Kuhifadhia Maji katika Maeno
mbalimbali nchini
101
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
kuvamia katika eneo hilo na maeneo mengine ambayo yanakabiliwa na uharibifu mkubwa wa
kimazingira ikiwemo ujenzi wa nyumba, ukataji wa miti na uchimbaji wa mchanga.
6.3.4 Kukamilisha Awamu ya Pili ya Mradi wa Usambazaji Maji Safi na Salama katika
Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
Utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Mkoa wa Mjini Magharibi Awamu ya Pili umekamilika kwa
ujenzi wa matangi makubwa mawili maeneo ya Kinuni na Dole. Aidha, visima vitano (5)
vimechimbwa katika maeneo ya Kizimbani na Msikiti Mzuri. Shughuli za ulazaji wa mabomba
yenye urefu wa kilomita 21 zimefanyika katika maeneo ya Kinu Moshi hadi Tangi la Dole kutoka
Dole kuelekea Bububu na kutoka Chunga kuelekea Kinuni, Magomeni hadi Kiembe Samaki.
6.4 MAKAAZI
Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi imeiagiza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Nyumba na kuandaa Sheria ya “Condominium” ili
kuwezesha wananchi waliopangishwa katika nyumba za maendeleo mijini na vijijini kuuziwa
sehemu ya majengo hayo.
Serikali imekamilisha uandaaji wa Sheria ya “Condominium” na kuunda Bodi ya kusimamia
utekelezaji wa Sheria hiyo. Aidha, Serikali kwa kuzingatia agizo hilo imeendelea kusimamia
utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Nyumba na kupitisha Sheria ya Shirika la Nyumba la Zanzibar ya
mwaka 2014. Pia, Serikali inaendelea na zoezi la kuwashajiisha Wawekezaji kuwekeza katika
Sekta ya Nyumba. Vilevile, Serikali inaendelea kuufanyia mapitio Mpango Mkuu wa Mji wa
Zanzibar (Master Plan) ili kutenga maeneo maalum ya ujenzi wa nyumba za ghorofa na kupunguza
tatizo la uhaba wa ardhi.
6.4.1 Kukamilisha Ujenzi wa Nyumba ya Maendeleo Bambi
Serikali imekamilisha ujenzi wa jengo moja la Nyumba za Maendeleo Bambi (Mpapa) ambapo
nyumba 24 zimekabidhiwa kwa wananchi wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
102
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
6.4.2 Uendelezaji wa Mamlaka ya Mji Mkongwe
Mji Mkongwe wa Zanzibar ni hazina kubwa na kivutio cha historia ya Zanzibar. Kwa kutambua
hilo, Serikali kwa kushirikiana na watu binafsi na Mashirika ya Kimataifa inaendelea kuulinda,
kuihifadhi na kutumika kama kivutio cha utalii na kubakisha dhana ya urithi wa dunia kwa
kukarabati majengo yaliyomo bila kubadilisha uhalisia wake. Mamlaka ya Mji Mkongwe
imefanya ukaguzi wa nyumba zilizo katika hali mbaya ya uchakavu na kuziingiza katika Mfumo
wa Kuhifadhia Taarifa (database system) sambamba na kuwashajiisha wapangaji na wenye
nyumba binafsi kufanya matengenezo mara tu athari zinapoanza kujitokeza. Ukaguzi huo
umegundua kwamba majengo 42 yapo katika hali mbaya na majengo 267 yamefanyiwa
matengenezo. Aidha, Mpango wa Matumizi Endelevu wa Eneo la Mji Mkongwe wa 1994
unaendelea kufuatwa kwa azma ya kuendeleza uhifadhi wa mji huu. Wakati huo huo, Mamlaka
inaendelea kushirikiana na Jumuiya ya Miji ya Urithi wa Dunia (Organization of World Heritage
City).
Katika kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Matumizi ya Magari na Vyombo vya Moto (Traffic
plan) ndani ya Eneo la Mji Mkongwe, Serikali imetangaza utaratibu wa utumiaji barabara kwa
njia zitakazotumika upande mmoja (one way road), njia zitakazotumika pande mbili (two way
roads), njia zitakazofungwa, maegesho ya magari, pamoja na sehemu zisizoruhusiwa kupitwa (No
entry) na mikokoteni na vyombo vya moto.
Jengo la nyumba ya Maendeleo Bambi
103
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
SEHEMU YA SABA
7.0 MAENEO MENGINE YA KIPAUMBELE
7. 1 Utamaduni na Michezo
Kama inavyofahamika kuwa Utamaduni ni moja katika mambo muhimu katika Taifa lolote
Duniani, Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2010-2015 imeielekeza Serikali kudumisha na kuendeleza
mila na silka za jamii ya Zanzibar.
7.1.1 Kuandaa Sera ya Utamaduni na Michezo
Serikali imeifanyia mapitio Sera ya Utamaduni ikiwa ni muongozo kwa taasisi zinazosimamia
utamaduni ili kwenda na wakati kwa kuihusisha Sekta ya Utalii na Utamaduni. Aidha, katika
kuufanya utamaduni uwe na tija zaidi, Serikali imekamilisha mchoro wa ramani ya utamaduni
katika shehia za Unguja na Pemba. Pia, utafiti wa Urithi wa Utamaduni Usioshikika umekamilika
katika mikoa yote ya Zanzibar na hatimaye kuhifadhiwa na kutangazwa kimataifa kwa kuingizwa
katika orodha ya “UNESCO” ya Utamaduni zilizohifadhiwa. Urithi wa utamaduni usioshikika
ni Kumbukumbu za Utamaduni zisizo na umbo linalogusika wala kushikika kama ufundi na
ustadi wa utengenezaji wa vifaa vya kiasili, uhunzi, ubunifu wa sanaa, elimu ya tiba asilia, lugha,
maigizo, matamasha, sherehe za kimila, nyimbo, imani, matambiko, mila, simulizi na itikadi.
7.1.2 Kusimamia Utekelezaji wa Sera na Sheria za Michezo na Utamaduni
Serikali imezifanyia mapitio Sera ya Utamaduni na Sera ya Michezo kwa lengo la kuzifanyia
marekebisho. Pia, Serikali imetoa mafunzo kwa wasanii wa kazi za mikono ili kuweza
kuwahamasisha wasanii hao kuzalisha kazi zilizo bora zaidi. Vilevile, Mabaraza ya Michezo ya
Wilaya zote za Zanzibar yameimarishwa kwa kupatiwa mafunzo juu ya namna ya kuendesha na
kusimamia shughuli za michezo katika ngazi za Wilaya. Aidha, Serikali imekamilisha uandaaji wa
Sheria ya Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni, 2015 ambayo imeunganisha Bodi
ya Sensa na Baraza la Sanaa ili kuleta ufanisi zaidi katika uimarishaji wa utamaduni nchini.
7.1.3 Kujenga Kiwanja cha Kisasa cha Michezo ya Ndani
Serikali imefanya matayarisho ya ujenzi wa kiwanja cha kisasa cha michezo ya ndani katika
Uwanja wa Amaan kwa kuandaa mchoro wa ujenzi wa kiwanja hicho kitakachotoa fursa zaidi kwa
vijana kushiriki katika michezo hiyo ikiwemo kuogelea, mpira wa vinyoya na mpira wa meza.
104
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Vilevile, ukumbi wa Zanzibar Budocan uliojengwa ndani ya Uwanja wa Amaan kwa kushirikiana
na Serikali ya Japan umeanza kutumika kwa michezo ya Judo, Karati na michezo mingine ya ndani
inayolingana na hiyo.
7.1.4 Kukamilisha Ujenzi wa Kituo cha Michezo Dole
Serikali imejenga Kituo cha Michezo Dole ambacho kinatumika ili kukuza vipaji vya michezo
kwa vijana wa Zanzibar. Vilevile, viwanja viwili (2) vya michezo vimeanzishwa katika kituo hicho
ambapo zaidi ya vijana 3,000 wamepata mafunzo ya michezo na kupata fursa za kushiriki
mashindano ya ndani na nje ya nchi kama vile “SAMSUNG Youth Games”.
7.1.5 Ujenzi wa Uwanja Mpya wa Michezo
Serikali imeamua kuujenga upya Uwanja wa Mao Tse Tung uliopo mjini Unguja ili uweze
kutumika kwa shughuli za michezo na sherehe za kitaifa. Aidha, michoro ya awali ya ujenzi huo
imekamilika na kazi za ujenzi zimeanza. Serikali ya Watu wa China ndio inayosaidia ujenzi wa
Uwanja huo.
7.1.6 Matengenezo ya Kuboresha Uwanja wa Gombani Pemba
Serikali imeufanyia marekebisho uwanja wa Gomabani Pemba ili kuuwezesha uwanja huo
kukidhi haja ya mashindano ya kimataifa ya mpira wa miguu. Aidha, matengenezo ya taa za
uwanja huo yamekamilika ambayo yanauwezesha uwanja kutumika hata wakati wa usiku.
Vilevile, Serikali imekamilisha ujenzi wa njia ya kukimbilia “running track” maarufu kama “tatan”
ili kutoa fursa ya michezo ya riadha kufanyika kwa ufanisi mkubwa. Pia, kwa kushirikiana na
Serikali ya Japan, Serikali imejenga kiwanja cha michezo ya ndani katika Uwanja wa Gombani
Pemba ambacho kinatumika kwa michezo ya mpira wa meza, mpira wa wavu, mpira wa vinyoya,
judo, karati na michezo mengine ya ndani.
105
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
7.1.7 Kuendeleza na Kuimarisha Vipaji vya Wanamichezo
Serikali imeviwezesha vyama vya michezo kuandaa mashindano ya ndani kwa vilabu vyao pamoja
na kushiriki katika mashindano ya kitaifa na kimataifa kwa michezo ya mpira wa miguu, riadha,
judo, karati, mpira wa mikono, kunyanyua vitu vizito, mpira wa wavu na michezo mengine. Pia,
hatua mbalimbali zimechukuliwa za kuendeleza na kuimarisha vipaji vya wanamichezo wetu kwa
kuwapatia mafunzo ya utawala na uendeshaji kwa viongozi 20 na walimu wa michezo 150.
Vilevile, Serikali imeendesha semina za mafunzo kwa Makatibu, Wenyeviti na Makocha kutoka
Wilaya zote ili kuinua viwango vya michezo nchini.
Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imeshiriki katika michezo ya “VIVA WORLD
CUP” nchini Kurdistan na katika mashindano ya “Senior Challenge Cup” yanayofanyika kila
mwaka ambapo kwa mwaka 2012 timu ilishika nafasi ya tatu katika mashindano hayo. Pia, Timu
za vijana chini ya umri wa miaka 13 na ile ya baina ya miaka 14 - 15 za Mpira wa Miguu
zimeshiriki katika mashindano ya Vituo vya Academia ya Michezo (Olympafrica Centres) vya
Afrika Mashariki na Kati yaliyofanyika nchini Burundi na kufanikiwa kuwa Bingwa na
kutunukiwa kombe lijulikanalo kwa jina la “Daimler Cup” 2010/2011.
Kwa upande wa mchezo wa riadha, Serikali imewawezesha wanaridha 20 kushiriki katika
mashindano ya vijana ya kitaifa na kimataifa yaliyofanyika Tanzania Bara na Botswana. Aidha,
Uwanja wa Gombani - Pemba Uliowekewa Nyasi Bandia
106
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Serikali imewawezesha wanamichezo mbalimbali kushiriki katika mashindano ya “All Africa
Games” yaliyofanyika Maputo Msumbiji. Pia, timu ya Watu Wenye Ulemavu wa akili ilishiriki
katika mashindano ya “Special Olympic” nchini Ugiriki na Kibaha Tanzania Bara.
Kwa upande mwengine, Serikali imeziwezesha timu za Taifa za Judo na Riadha kushiriki
Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati yanayofanyika kila mwaka ikiwemo ya
Zanzibar. Vilevile, timu za mpira wa mikono zimeshiriki katika Mashindano ya Kombe la
Challenge, Nairobi na Mashindano ya Shirikisho la Michezo kwa Skuli za Sekondari, Afrika ya
Mashariki (FEASSA) yaliyofanyika nchini Uganda.
7.1.8 Kuendeleza Kudumisha Mila, Silka na Maadili Mema ya Wazanzibari
Serikali imechukua hatua za kuzikagua kazi za sanaa kwa lengo la kulinda na kuhifadhi mila na
silka za Wazanzibari. Vilevile, imeandaa Kamusi ya Kipemba, Kimakunduchi na Kitumbatu kwa
lengo la kupelekea wananchi kuzitumia Kamusi hizo ili kulinda na kuhifadhi utamaduni wa
Kizanzibari. Pia, Bodi ya Sensa ya Filamu imefanya utafiti juu ya suala zima la maadili
katika Wilaya za Zanzibar kwa lengo la kuweka mikakati ya kuendeleza juhudi za kulinda,
kuhifadhi na kudumisha mila, silka, na maadili mema ya Wazanzibari. Matokeo ya utafiti huo
yamechapishwa katika kitabu kiitwacho Hazina Inayopotea, 2012.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein
akiwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi
wakiangalia watoto wakicheza ngoma za utamaduni – Mangapwani Unguja
107
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Aidha, Serikali kupitia Bodi ya Sensa ya Filamu imefanya uhakiki wa Matamasha, Matangazo ya
Kibiashara, Video za Nyimbo, tenzi zenye maudhui mbali mbali na filamu tofauti katika
maduka ya kukodishia kanda Unguja na Pemba. Bodi pia, imekagua vikundi vya ngoma,
michezo ya kuigiza jukwaani, tenzi na mashairi ya kughani ili kuhakikisha mila, silka na
utamaduni wa Kizanzibari hauathiriwi. Aidha, Serikali imejenga Studio ya kisasa ya kurekodia
filamu na muziki kwa lengo la kuwapunguzia gharama za kurekodia kazi za wasanii wa Zanzibar.
7.2 VYOMBO VYA HABARI
Vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kuhabarisha, kuelimisha, kuhamasisha na kuburudisha
jamii juu ya masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Serikali imeweka mikakati na
kutekeleza hatua mbalimbali za kukuza na kuendeleza uhuru wa vyombo vya habari nchini.
7.2.1 Kusimamia Utekelezaji wa Sera ya Habari na Kuendeleza Uhuru wa Vyombo vya
Habari
Serikali imeweza kufanya mageuzi makubwa katika kusimamia na kuendeleza vyombo vya habari
kwa kuvipa uhuru na haki ya kuhoji, kutafuta, kupokea na kuchapisha habari na maoni kwa
kuzingatia taratibu na sheria zilizopo. Kwa kutekeleza lengo hilo na kuzingatia demokrasia ya
ushirikishwaji wa umma, Serikali imetoa fursa ya kuanzishwa kwa vyombo vya habari nchini na
kutoa fursa kwa wananchi kuvitumia vyombo hivyo kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla. Hivi
sasa jumla ya Redio tisa (9) za FM na Televisheni sita (6) zimeanzishwa katika kipindi cha 2010
hadi 2015. Vyombo hivyo ni pamoja na Mtegani FM, Voice of Istiqama FM, Tumbatu FM,
Mkanyageni FM, Marhaba FM, Bahari FM, Mkoani FM, Assalam FM, ABM FM, ZUKU Satallite
TV, Star Times, Zenj TV, CCTV, Coconut TV na Azam TV. Aidha, idadi ya Magazeti na
Majarida yaliyosajiliwa na kufanyakazi Zanzibar imeongezeka kutoka matano (5) mwaka 2010
hadi 50 mwaka 2015. Pia, usambazaji wa Magazeti ya Serikali umeongezeka kwa kuwafikia
wasomaji wengi zaidi katika mikoa yote ya Zanzibar na mikoa 14 ya Tanzania Bara.
7.2.2 Kusimamia Utekelezaji wa Muongozo, Kanuni na Sheria ya Vyombo vya Habari
Serikali imeandaa na kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyombo vya Habari, Kanuni na
Miongozo kwa lengo la kuleta ufanisi katika mageuzi ya mfumo wa utangazaji kutoka Analogi
kwenda Dijitali. Aidha, miongozo imetolewa kwa vyombo vya habari kuzingatia maadili ya
uandishi wa habari na kuwajibika kwa jamii pamoja na kuheshimu haki za faragha kupitia semina
108
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
na mikutano. Vilevile, mafunzo ya umuhimu wa kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari
yametolewa kwa kutumia vyombo vya habari vya Serikali na watu binafsi. Pia, utaratibu wa
ufuatiliaji wa matangazo na vipindi vya vituo vya redio na TV (Monitoring System) umeanzishwa
na unafanyakazi kwa ufanisi ambapo hivi sasa vipindi vyote vinarikodiwa, kuhifadhiwa na
kufuatiliwa. Sambamba na hayo, Sheria Namb. 4 ya mwaka 2013 ya kuunda Shirika la Utangazaji
la Zanzibar (ZBC) imepitishwa na imeanza kufanyakazi.
7.2.3 Kuendeleza Mafunzo kwa Watendaji wa Vyombo vya Habari na Utangazaji
Serikali imetoa mafunzo ya kuwaendeleza wanahabari mbali mbali ili waweze kutekeleza
majukumu yao kwa ufanisi mkubwa. Katika kulifanikisha hilo, waandishi 114 (wanawake 78 na
wanaume 36) wameweza kupatiwa mafunzo katika ngazi tafauti zikiwemo PhD 4, Shahada ya Pili
13, Shahada ya Kwanza 20, stashahada 51 na Cheti 26. Vilevile, taaluma mpya ya teknolojia ya
dijitali imetolewa kwa mafundi, watayarishaji vipindi, wapiga picha na viongozi wa vituo vya
utangazaji vya Serikali na Binafsi vilivyopo Zanzibar.
7.2.4 Kuviimarisha Vyombo vya Habari ikiwemo ZBC TV na ZBC Redio
Serikali imeviimarisha Vyombo vya Habari vya Zanzibar kwa kuvinunulia vifaa mbalimbali vya
kisasa vinavyotumia teknolojia ya digitali. Studio za Televesheni Unguja na Pemba zimefungwa
vifaa vipya vya kukusanyia na kurushia matangazo vyenye uwezo wa kuonekana na kusikika ndani
na nje ya Zanzibar. Vifaa hivyo vya digitali vina thamani ya Shilingi Bilioni 1.85. Aidha, mitambo
ya digitali imefungwa katika vituo vya kurushia matangazo vilivyoko Rahaleo, Masingini,
Muyuni, Nungwi, Mizemiumbi, Mkanjuni na Bungala kwa lengo la kuwawezesha wananchi
kupata huduma mpya za matangazo hayo. Mitambo hiyo imegharimu jumla ya Shilingi Bilioni
8.14.
109
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Matangazo ya Redio ya ZBC yameimarishwa kwa kuhamisha Mnara wa Masafa ya Kati (Medium
Wave) kutoka Chumbuni kwenda Bungi ambayo imegharimu Shilingi 1, 496,600, 000.
Uhamishwaji wa mnara huo pia unarahisisha utuaji wa ndege zinazoingia na kutoka nchini kwa
usalama zaidi. Aidha, Ofisi, Studio na nyumba mbili (2) za kisasa za wafanyakazi wa familia nne
(4) zimejengwa katika eneo hilo la Bungi ili kuimarisha utendaji mzuri wa kazi. Vilevile, kazi ya
ukarabati wa mnara wa mawimbi mafupi (Short Wave) umefanyika kwa ushirikiano na Serikali
ya Jamhuri ya Watu wa China, ambapo Shilingi Bilioni 2,440,000,000 zimetumika. Ukarabati huo
umeongeza nguvu za kusikika matangazo ya ZBC hadi nje ya Bara la Afrika.
7.2.5 Ujenzi wa Studio ya Wasanii
Serikali imekamilisha mradi wa ujenzi wa studio ya kisasa ya kurikodia nyimbo na michezo ya
kuigiza kwenye jengo la zamani la Utangazaji la Sauti ya Tanzania Zanzibar baada ya jengo hilo
kufanyiwa matengezo makubwa. Tayari Serikali imenunua na kufunga vifaa vipya kwa ajili ya
studio hiyo ambavyo vimegharimu jumla ya shilingi 291,534,000. Vifaa hivyo ni pamoja na Sony
xdcamex, Camera tripods na Track dolly, Camera cran, Lens fish eye, Digital video mixer, Digital
audio mixer na Power amplifier.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed
Shein akifungua Kituo cha kurushia matangazo ya Televisheni kwa mfumo wa Digitali
kilichopo Rahaleo
110
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
7.2.6 Kuendelea Kukiimarisha Chuo cha Uandishi wa Habari
Serikali imekiimarisha Chuo cha Uandishi wa Habari kwa kuweka vifaa pamoja na kuajiri walimu
wenye ujuzi ili kuweza kutoa wahitimu wenye uwezo wa kuzungumza na kuandika lugha fasaha
katika vyombo wanavyovifanyia kazi. Idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka 75 mwaka 2010
hadi kufikia 180 kwa mwaka 2015 kwa ngazi ya cheti na stashahada. Vilevile, Chuo kimeweza
kutengeneza nyaraka mbalimbali za kitaalamu ikiwemo Kitabu cha Miongozo wa Shughuli za
Chuo (Prospectus), Mpango Mkakati (Strategic Plan) na Vipeperushi. Pia, Chuo kimeweza
kuanzisha mafunzo ya lugha ya kichina kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa
China. Sambamba na hayo, Chuo kimekuwa na ushirikiano wa karibu na Redio ya Kimataifa ya
Deutsche Welle (DW) ya Ujerumani ambayo imekuwa ikisaidia kuwajengea uwezo walimu na
wanafunzi kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali. Aidha, Chuo kimeimarishwa kwa kupatiwa eneo
kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la chuo katika eneo la Kilimani, mjini Unguja.
Kituo cha Kurushia Matangazo ya Redio pamoja na Mnara wa Masafa ya Kati viliopo Bungi -
Zanzibar
111
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
7.2.7 Kusimamia na Kudhibiti Uingizaji wa Vifaa vya Utangazaji
Serikali imeendelea kuchukua juhudi za kukabiliana na hali ya ongezeko la uingizwaji wa vifaa
vya utangazaji vya teknolojia ya analogia ambavyo havitumiki tena katika nchi nyingi. Ili kudhibiti
Zanzibar isigeuzwe jaa la kutupia vifaa hivyo, mikakati imeandaliwa ya kuzuia uingiaji wa vifaa
hivyo sambamba na mkakati wa mageuzi ya teknolojia ya Utangazaji kutoka analogia kwenda
digitali. Aidha, semina, makongamano na warsha zimetolewa kwa wafanyabiashara ili kuwapa
uelewa wa hasara ya kuendelea kuagiza vifaa vya utangazaji vya analogia kwa ajili ya kutunza
mazingira na matumizi ya wananchi. Serikali pia imekuwa ikirusha vipindi maalumu kupitia
vyombo vya habari vya kuwafahamisha wananchi athari za mageuzi ya teknolojia ya utangazaji
wa digitali na matumizi makubwa ya nishati ya umeme kwa kutumia televisheni za analogia.
Vilevile, Serikali imetoa miongozo ya utumiaji wa vifaa vya kupokea matangazo ya digitali ikiwa
ni pamoja na kufanya semina elekezi kwa Watendaji Wakuu na Wamiliki wa Vituo vya Utangazaji
nchini juu ya changamoto za digitali kupitia Mkakati wa Mawasiliano (Communication Strategy
for Analogy to Digital Migration) sambamba na Mkakati wa Mageuzi ya Teknologia ya Utangazaji
kutoka analogia kwenda digitali (Analogy to Digital Migration Strategy, 2011-2015). Pia, vikao
Moja ya Majengo Manne ya Chuo cha Uandishi wa Habari yaliyoanza kujengwa
katika Eneo la Kilimani Mjini Zanzibar.
112
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
vya mashirikiano kati ya TCRA na Tume ya Utangazaji Zanzibar vimefanyika kwa lengo la
kuzungumzia mikakati ya kudhibiti uingizaji wa vifaa vikongwe vya analogia.
7.2.8 Mradi wa ‘E-Government’
Kwa lengo la kuimarisha huduma za mawasiliano Serikalini, Serikali imeanzisha mradi wa e-
government mwezi Januari 2013. Hadi hivi sasa, jumla ya majengo 86 ya Serikali
yameunganishwa katika mtandao huo na tayari yameanza kupata huduma ya ‘internet’ bila ya
malipo. Aidha, Serikali imo katika maandalizi ya kuiunganisha Zanzibar na Tanzania Bara kupitia
Mkonga wa Taifa na ule wa Kimataifa.
7.3 MAJANGA NA HUDUMA ZA UOKOZI
Katika jitihada za kukabiliana na maafa, Serikali imekamilisha utungaji wa Sera ya Kukabiliana
na Maafa ya mwaka 2011 pamoja na Sheria ya Kukabiliana na Maafa ya mwaka 2015 ambazo
zinatoa miongozo katika shughuli za kukabiliana na maafa na majanga pamoja na kutoa huduma
za kibinadamu kwa waathirika. Aidha, Serikali imeandaa nyaraka za Muongozo wa Ufuatiliaji na
Tathmini ya Sera, Muongozo wa Taifa wa Uendeshaji wa Sera ya Kukabiliana na Maafa, pamoja
na Mpango wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa Zanzibar na Utafutaji wa Rasilimali za
Kukabiliana na Maafa. Vilevile, Serikali imeandaa mipango ya kukabiliana na maafa ya Wilaya
tano ambazo ni Mjini, Magharibi, Kaskazini A, Micheweni na Wete. Pia, elimu ya kukabiliana na
maafa kwa ajili ya kujenga uelewa juu ya majanga na maafa imetolewa kwa makundi mbalimbali
Unguja na Pemba ikiwa ni pamoja na Waandishi wa Habari, Wanafunzi , Watu wenye Ulemavu
na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Serikali kupitia Idara ya Kukabiliana na Maafa inaendelea
kutoa elimu kupitia kipindi kinachorushwa na ZBC redio kila siku ya Jumatatu na kuanzisha
Tovuti na Jarida la ‘TUKABILIANE NA MAAFA’ linalotoka kila baada ya miezi mitatu.
7.3.1 Kuanzisha na Kuimarisha Kamati za Maafa kwa Ngazi ya Taifa, Wilaya na Shehia
Serikali imeanzisha Kamati 277 za Kukabiliana na Maafa katika ngazi ya Shehia Unguja na Pemba
pamoja na kuzipatia mafunzo ya msingi ya kukabiliana na maafa. Kamati hizo ni sawa na asilimia
82 ya Shehia zote zilizopo Zanzibar. Aidha, Kamati za Maafa za Wilaya na Shehia Unguja na
Pemba zimefanyiwa Makongamano, Warsha na Semina ili kuzijengea uwezo wa kujikinga na
kukabiliana na maafa katika maeneo yao. Vilevile, Serikali inaendelea na kutoa huduma za
113
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
kibinaadamu kwa wahanga waliofikwa na maafa katika maeneo mbalimbali nchini kupitia Kamati
zao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein
akikagua Maeneo yaliyoathrika Kutokana na Maafa ya Mvua zilizonyesha Mwezi Mei, 2015.
Baadhi ya Wajumbe wa Sekreatrieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM,
walipotembelea maeneno yaliyofikwa na mafuriko kwa lengo la kuwafariji wananchi walioathirika
na maafa hayo.
114
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
7.3.2 Kuimarisha Vikosi vya Uokozi Wakati wa Maafa
Serikali imeendelea kushajiisha wananchi kuanzisha vikosi vya uokozi katika maeneo yao ili
viweze kukabiliana na maafa. Aidha, Serikali inaendelea kuiwezesha Jumuiya ya Uzamiaji na
Uokozi ya Zanzibar kwa kuipatia elimu ya kukabiliana na maafa na vifaa wakati wa matukio.
Jumuiya hiyo inajumuisha vikosi vya kijamii vya uzamiaji na uokozi.
7.3.3 Kuimarisha Kikosi cha Zimamoto na Uokozi
Serikali imeendelea kukiimarisha Kikosi cha Zimamoto na Uokozi kwa kununua gari nne (4), kati
ya hizo gari mbili (2) za kuzimia moto na mbili (2) kwa ajili ya shughuli za utawala. Aidha, Kikosi
kimepatiwa zana na vifaa vya kisasa vya uokozi na kuzimia moto na kuvisambaza katika vituo
vyake vyote Unguja na Pemba. Hali ambayo imekiwezesha Kikosi kutoa huduma zake kwa
ufanisi. Vilevile, Serikali imeendelea kuwajengea uwezo watendaji wake kwa kuwasomesha
katika fani ya zimamoto na fani tofauti katika ngazi mabalimbali ndani na nje ya nchi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ambaye pia ni Katibu wa
Kamati ya Maafa Kitaifa akipokea misaada baada ya Maafa yaliyosababishwa
na Mvua zilizonyesha Mwezi Mei, 2015.
115
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Serikali pia imeweza kusogeza huduma za zimamoto kwa wananchi kwa kila Wilaya za
Unguja na Wilaya tatu (3) za Pemba (Mkoani, Wete na Chakechake) na kuanza kutoa huduma
katika Bandari ya Malindi kwa Unguja na Mkoani kwa Pemba. Aidha, Kikosi kimefanikiwa
kukuza uhusiano na mashirikiano ya namna ya kukabiliana na majanga
mbalimbali kwa kushiriki katika vikao mbali mbali vya Afrika
Mashariki.
7.4. DAWA ZA KULEVYA
7.4.1 Kusimamia Utekelezaji wa Sheria ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya
Katika kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya, Serikali kupitia Tume
ya Kitaifa ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya imeweza kuandaa Mpango Maalum (Road
Map) wa utekelezaji wa Sheria ya Dawa za Kulevya ambapo uliwashirikisha wadau kutoka taasisi
mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali ili kuhakikisha kwamba michango mbalimbali
inatolewa kudhibiti uingizaji, usafirishaji, usambazaji na matumizi ya Dawa za Kulevya.
Serikali imefanya vikao vya Kamati ya Kitaaluma ya Kupambana na Dawa za Kulevya na wadau
wengine kwa lengo la kujadili njia mbalimbali za kuendeleza mbele mapambano juu ya udhibiti
wa Dawa za Kulevya. Vilevile, Serikali imeandaa Sera ya Dawa za Kulevya na kufanya mikutano
Gari ya Kikosi cha Uokozi na Zimamoto katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar
116
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
na vyombo vya kusimamia sheria (Law Enforcement Agency- LEA) ili kukuza mashirikiano na
vyombo hivyo katika kudhibiti mapambano ya Dawa za Kulevya.
7.4.2Kushirikiana na Asasi za Kijamii
Serikali imeweza kutoa taaluma kupitia taasisi mbalimbali kama vile sehemu za kazi, Skuli na
Shehia mbalimbali za Unguja na Pemba kuhusu athari za matumizi ya dawa ya kulevya. Aidha,
vipindi mbalimbali vya kuelimisha jamii juu ya athari za dawa za kulevya vimerushwa kupitia
vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi. Vilevile, Serikali imeanzisha Mpango
Maalum wa Taaluma juu ya Athari ya Dawa za Kulevya unaoshirikisha viongozi wa ngazi
mbalimbali nchini.
7.4.3 Kuanzisha Vituo Maalumu vya Kurekebisha Vijana Walioathirika na Dawa za
Kulevya
Serikali inaendelea na ujenzi wa Kituo maalumu cha kurekebisha Vijana walioathirika na Dawa
za Kulevya katika eneo la Kidimni Wilaya ya Kati. Aidha, Nyumba za Marekebisho ya tabia
(Sober Houses) 13 zimeanzishwa ambazo zimetoa huduma kwa vijana 1,020 kwa Unguja na
Pemba. Serikali imechukua jitihada kubwa ya kuziendeleza nyumba hizo ili ziweze kutoa huduma
zinazostahiki.
7.4.4 Taaluma na Ushauri Nasaha kwa Wananchi
Serikali kupitia Vituo vya Ushauri Nasaha imeendelea kutoa ushauri nasaha kwa waathirika wa
dawa za kulevya. Taaluma juu ya athari ya dawa za kulevya imetolewa katika Shehia mbalimbali
za Unguja na Pemba, Vikosi vya SMZ pamoja na Skuli kupitia Mikutano, Makongamano, Semina
pamoja na utoaji wa Kalenda na Vipeperushi. Aidha, jumla ya watu wapatao 3,673 (wanawake
1,956 na wanaume 1,717) wamehamasishwa na kupima VVU.
7.5 DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 – 2015 imeiagiza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kufuata misingi ya Demokrasia na Utawala Bora katika kuhudumia wananchi. Utekelezaji wa
agizo hili umelenga katika masuala yafuatayo:
117
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
7.5.1 Kuzingatia Misingi ya Demokrasia na Utawala Bora
Serikali imeendelea kudumisha muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kama ilivyoelekezwa na
Katiba ya Zanzibar ya 1984, mabadiliko ya 10, Toleo la 2010. Aidha, Serikali imeendelea
kuzingatia na kudumisha misingi ya kidemokrasia na utawala bora kwa kuunda na kuhakikisha
kuwa mihimili mikuu mitatu (Mahakama, Serikali, na Baraza la Wawakilishi) ya demokrasia na
utawala bora inafanya kazi zake kwa uhuru bila ya kuingiliana na chombo chengine. Vilevile,
Serikali imetoa elimu juu ya Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa Wajumbe wa Baraza
la Wawakilishi, Maafisa wa SMZ, Maafisa Wadhamini, Maafisa Tawala wa Mikoa na Wilaya
pamoja na Wawakilishi wa Jumuiya za Kiraia Unguja na Pemba. Aidha, Serikali imetoa
vipeperushi juu ya mfumo huo kwa ajili ya kutumika katika kutoa elimu hiyo kwa makundi
mbalimbali ya kijamii. Pia, Viashiria vya Kitaifa vya Utawala Bora vimeandaliwa na kutumika
kwa ajili ya kusimamia uwajibikaji na ufanisi katika utendaji wa Shughuli za Serikali.
Aidha, Serikali kupitia Baraza la Wawakilishi imepitisha jumla ya Miswada 63 ya Sheria ambayo
yote imesainiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed
Shein na tayari zimekuwa Sheria kamili. Pia, jumla ya maswali ya msingi 1,558 na maswala ya
nyongeza 3,103 yameulizwa kwa Serikali na yamepatiwa majibu sahihi.
Vilevile, Serikali imefanya vikao vyote vya kawaida na vya kisheria kwa lengo la kujadili Nyaraka
kadhaa zikiwemo za Sheria, Sera pamoja na kupokea na kujadili taarifa mbali mbali. Aidha,
Mikutano kati ya Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Viongozi wa Wizara za SMZ kujadili
utekelezaji wa malengo ya Bajeti imefanyika.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza na viongozi wa
Mawizara kujadili utekelezaji wa Malengo ya Bajeti
118
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
7.5.2 Kusimamia Utekelezaji wa Kazi na Majukumu ya Serikali
Serikali imeandaa na kupitisha Sera ya Utawala Bora pamoja na Sheria Nambari 4 ya Mwaka 2015
ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa lengo la kuhakikisha kwamba Viongozi wa Umma
wanafuata maadili ya kazi zao. Pamoja na mambo mengine Sheria imefafanua maswala
mbalimbali ikiwemo jinsi ya kuondoa mgongano wa kimaslahi kwa jambo ambalo Kiongozi wa
Umma ana maamuzi nalo.
Vilevile, Serikali imetoa elimu ya Uraia kwa wananchi juu ya Sera ya Utawala Bora, Rushwa na
Haki za Binaadamu kupitia vyombo vya habari, ziara za vijijini pamoja na kutumia vikundi vya
sanaa za maonesho. Pia, Sheria na Kanuni za kuzuia rushwa na uhujumu uchumi zimetayarishwa
na kuanza kutumika. Vilevile, Serikali imeiimarisha Mamlaka ya Kuzuia Rushwa kwa
kuwasomesha watendaji wake na kuwapatia watumishi wake mafunzo kwa vitendo katika
Mamlaka ya Kuzuia Rushwa Tanzania Bara (TAKUKURU) pamoja na kununua vifaa
vinavyohitajika katika kufanya uchunguzi na uendeshaji wa ofisi.
7.5.3 Kuendeleza Kazi ya Utekelezaji wa Mkakati wa Elimu ya Uraia, Kidemokrasia, Haki
za Binaadamu na Utawala Bora
Serikali imeandaa Programu za Kujenga Uelewa kwa Wananchi juu ya Elimu ya Uraia, ikiwemo
elimu ya kidemokrasia, haki za binaadamu na utawala bora. Vipindi mbalimbali vya redio na TV
vimetayarishwa na kurushwa hewani kupitia Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kuhusiana na
programu hizo. Pia, elimu ya rushwa na uhujumu wa Uchumi imetolewa kwa shehia za Unguja na
Pemba pamoja na kusambaza Vijarida juu ya mapambano dhidi ya rushwa na uhujumu wa uchumi.
Aidha, vipindi mbalimbali kuhusu utawala bora vimerushwa hewani na Shirika la Utangazaji
Zanzibar pamoja na redio binafsi za Zanzibar. Vilevile, Shehia za Zanzibar zimepatiwa elimu ya
uraia juu ya Utawala Bora na Haki za Binaadaam kupitia ziara za vijijini. Pia, Elimu ya Haki za
Binaadamu na Utawala Bora imetolewa kwa watu weye Ulemavu na Waandishi wa Habari.
Serikali inasimamia utoaji wa taarifa za Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kwa wakati muafaka. Idadi ya vyombo vinavyotoa
taarifa hizo vimeongezeka kutoka vyombo vinne (4) mwaka 2010 hadi 11 mwaka 2015. Aidha,
119
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Jarida la Ikulu matoleo 16 yamechapishwa na kusambazwa katika taasisi zote za Serikali na Binafsi
na Tovuti (Website) ijulikanayo kwa jina la www.ikuluzanzibar.go.tz inatumika kutoa taarifa hizo.
7.5.4 Kuimarisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
Serikali imeimarisha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili iweze
kuimarisha kazi za ukaguzi, kutoa ripoti za ukaguzi zilizokuwa na viwango vinavyokubalika
Kimataifa na kwa wakati muafaka. Aidha, Serikali imejenga majengo ya kisasa ya Ofisi Unguja
na Pemba pamoja na kuziwekea vifaa vya kisasa vikiwemo komputa, kamera na “server” kwa ajili
ya kuwekea kumbukumbu za kazi za ukaguzi. Vilevile, Serikali inaendelea kuwapatia mafunzo ya
muda mfupi na mrefu wafanyakazi wake katika fani za Ukaguzi wa Thamani (Value for Money
Auditing), Ukaguzi wa Komputa (Computerized Auditing) na Ukaguzi wa Mazingira
(Environmental Auditing). Sambamba na hayo, Muundo wa Utumishi (Scheme of Service) kwa
ajili ya wakaguzi umeandaliwa ili kuwapatia maslahi yanayolingana na kazi zao.
7.5.5 Kuanzisha Mahakama ya Biashara Zanzibar
Katika kufanikisha juhudi za kuanzisha Mahakama ya Biashara Zanzibar, Serikali imekamilisha
uandaaji wa Sheria ya Kuanzisha Mahakama hiyo na imelifanyia matengenezo jengo linalotumika
kwa Mahakama ya Biashara.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe
kulifungua Jengo la Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Wete Pemba
120
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
7.6 OFISI YA MKURUGENZI WA MASHTAKA
Serikali imeanzisha Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar kwa mujibu wa Sheria Nam. 2 ya
2010. Aidha, Kitabu cha Muongozo wa Uendeshaji Mashtaka kimetayarishwa na kuanza
kutumika. Pia, Serikali imejenga jengo jipya lenye Maktaba ya Sheria iliyopo Unguja. Maktaba
hiyo inatoa huduma kwa wafanyakazi na wanasheria wa Serikali kutoka taasisi mbalimbali pamoja
na wanafunzi wa Sheria. Vilevile, Kituo cha Mafunzo na Utafiti wa Sheria kimeanzishwa rasmi
mwaka 2012 ambacho kinasomesha masomo ya sheria ngazi ya Cheti na Diploma. Sambamba na
hayo, Jarida la SHAHIDI limeanza kuchapishwa kuanzia 2010 ambapo Matoleo 11
yamechapishwa na kusambazwa kwenye Wizara, Idara, Taasisi za elimu na wananchi kwa lengo
la kuelimisha umma juu ya masuala ya makosa ya jinai.
Serikali inaendelea kujenga nyumba za Waendesha Mashtaka katika Wilaya za Kusini, Kaskazini
“A” na Magharibi. Aidha, Serikali imelifanyia matengenezo jengo la Kitengo cha Uendeshaji wa
Mashtaka katika Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe, imejenga Kituo cha Mafunzo ya Sheria
Miembeni na kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Makunduchi. Vilevile,
Serikali pia imeajiri Wanasheria wapya 28 na Makarani wa sheria wanne (4) pamoja na kusomesha
Wanasheria 33. Kati ya hao, wanane (8) Shahada ya Uzamili ya Sheria, wanne (4) Shahada ya
Kwanza ya Sheria, wanne (4) ngazi ya Cheti na Wanasheria 17 wamepatiwa mafunzo ya muda
mfupi.
Serikali kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka imefungua na kusimamia kesi za jinai 5,276
katika Mahakama za Zanzibar katika ngazi tofauti. Serikali pia, imeanzisha utaratibu wa wahalifu
kutumikia Jamii badala ya kutumikia katika Chuo cha Mafunzo. Mpango huo tayari umeanza
kutumika ambapo hukumu za aina hiyo tayari zimeanza kutolewa katika Mahakama mbalimbali.
Watuhumiwa 15 (10 Unguja na 5 Pemba) waliotiwa hatiani wamepewa hukumu za kuitumikia
jamii.
7.7 Kuimarisha Kiwanda cha Upigaji Chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali
Kwa lengo la kutekeleza azma ya Serikali ya kukiimarisha Kiwanda cha Upigaji Chapa na Mpiga
Chapa Mkuu wa Serikali kwa kurudisha hadhi yake na kuinua kiwango cha uzalishaji, Serikali
imelifanyia matengenezo makubwa jengo lililokuwa Kiwanda cha Sigara Maruhubi ili kutumika
121
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
kwa shughuli za Kiwanda cha Upigaji Chapa na Mpigaji Chapa Mkuu wa Serikali. Aidha, Serikali
imekipatia Kiwanda mitambo mipya ya kisasa ya Uchapaji (Digital Printing Machines) kwa
Awamu ya Kwanza. Kwa sasa kiwanda kinatekeleza majukumu yake ya kuchapisha nyaraka zote
za Serikali kwa ubora na ufanisi wa hali ya juu.
7.8 SERIKALI ZA MITAA
Kwa lengo la kuziendeleza na kuziimarisha Serikali za Mitaa, Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2010-
2015) inaelekeza Serikali kuzifanyia mapitio sera na sheria ili kuimarisha uwajibikaji na kuongeza
ufanisi wa kazi. Katika kuitekeleza azma hiyo, Serikali imefanikiwa kuandaa Sera ya Serikali za
Mitaa na kufanikisha kufanya mapitio ya Sheria mbili (Sheria Nam.1 ya 1998 ya Tawala za Mikoa
na Sheria Nam. 3 na 4 ya Baraza la Manispaa) na kuwa na Sheria Nam. 8 ya mwaka 2014 ya
Tawala za Mikoa na Sheria Nam 7 ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa ya mwaka 2015. Aidha,
Serikali imewajengea uwezo wafanyakazi wa Serikali za Mitaa kwa kuwapa mafunzo ya muda
Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein akikagua maeneo mbalimbali
katika Kiwanda cha Uchapaji na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali
122
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
mrefu na mfupi pamoja na ziara za kimasomo ndani na nje ya nchi kwa azma ya kuimarisha Taasisi
za Serikali za Mitaa ili kuendana na Mfumo mpya wa Mageuzi ya Serikali za Mitaa. Pia, elimu
juu ya kuanzisha mfumo madhubuti wa ukusanyaji na utunzaji wa mapato ya Serikali za Mitaa
(Data base System) katika Taasisi za Halmashauri zote za Unguja na Pemba imetolewa.
Aidha, Serikali imeendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii katika miji ya Zanzibar na
kuhifadhi eneo la Urithi wa Mji Mkongwe kupitia Mradi wa Huduma za Jamii Mjini (Zanzibar
Urban Service Project). Kupitia mradi huu uwezo wa kitaasisi wa Baraza la Manispaa Zanzibar na
Mabaraza ya Miji ya Pemba umeimarishwa kwa kufanya ukarabati wa majengo, kutoa mafunzo
kwa wafanyakazi na ununuzi wa vifaa vya ofisi, gari na vifaa vya usafi. Ukarabati mkubwa wa
Ofisi ya Baraza la Manispaa iliopo Darajani na Karakana kuu iliopo Saateni unaendelea. Aidha,
kazi ya ujenzi wa vibaraza vya kuwekea makontena ya kutupia taka unaendelea. Vilevile, vifaa
mbalimbali ikiwemo gari 10, vespa 25 na pikipiki 7 zimenunuliwa kwa matumizi ya ofisi na gari
8 za kuzolea taka, gari 3 za kubebea makontena, gari 3 za kunyonyea maji taka, na gari moja (1)
ya kubebea magari yaliyoharibika zimepatikana. Aidha, Serikali imelipatia Baraza la Manispaa
makontena ya taka 192, marikwama 70 pamoja vikapu 1,000 vya kutilia taka. Vifaa hivyo ni kwa
ajili ya matumizi ya Baraza la Manispaa Zanzibar na Mabaraza ya Miji ya Pemba.
7.8.1 Kusimamia Suala la Usafi
Serikali imeendelea kutoa huduma endelevu za usafishaji wa mji kwa kushirikisha jamii ili kuweka
mazingira bora. Vilevile, Serikali kupitia Baraza la Manispaa na Halmashauri za Wilaya imeingia
mikataba na vikundi vya kijamii kwa ajili ya kufanya usafi katika masoko, bustani, mitaro,
barabara na kuondoa taka katika maeneo ya Zanzibar. Aidha, Serikali imeweza kuimarisha kikundi
kazi cha kusimamia zoezi la uondoaji mifugo inayozurura ovyo maeneo ya Manispaa na vitongoji
vyake. Sambamba na hilo, katika kuimarisha mandhari ya mji wa Zanzibar, Serikali imeziimarisha
bustani za njia kuu za Mji. Serikali pia, imeweza kuweka taa za barabarani na taa za kuongozea
magari zinazotumia umeme wa jua katika maeneo ya Darajani, Mkunazini na Kwamchina.
123
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
7.8.2 Kuhamasisha Wananchi Kuunda Kamati za Maendeleo
Serikali imewahamasisha wananchi kuunda Kamati za Maendeleo za Shehia na Majimbo ambapo
Shehia zote 336 katika majimbo 50 ya Unguja na Pemba zimeunda kamati hizo. Jukumu kubwa la
kamati hizo ni kusimamia miradi ya maendeleo ya wananchi katika majimbo yao. Aidha,
Wenyeviti, Makatibu na Washika fedha wa kamati zote wamepatiwa mafunzo juu ya uibuaji wa
miradi, utunzaji wa kumbukumbu na udhibiti wa fedha.
7.8.3 Kuvijengea Uwezo Vikosi Maalum vya SMZ
Ilani ya CCM (2010-2015) imeagiza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuvijengea uwezo na
mazingira mazuri ya kazi Vikosi vya SMZ ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi. Katika
kulitekeleza hilo, Serikali imefanya ununuzi wa vifaa mbalimbali vya maofisa na wapiganaji wa
Vikosi vya SMZ ikiwemo sare za wapiganaji, huduma ya chakula na ununuzi wa vifaa vya
kambini. Aidha, Serikali imeendelea na ujenzi na kuyafanyia ukarabati majengo mbalimbali ya
vikosi Unguja na Pemba. Pia, maafisa na askari wamejengewa uwezo wa kitaaluma katika fani
mbalimbali na viwango tofauti ikiwemo fani za Afya, Sheria, Uzamiaji, Utawala, Manunuzi na
Ugavi, Usimamizi wa Fedha, Rasilimali watu, Ubaharia pamoja na masomo mbalimbali ya ufundi.
Taa za barabarani zinazotumia nishati ya jua katika mji wa Zanzibar
124
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
7.8.3.1 Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM)
Katika hatua za kukiimarisha Kikosi cha KMKM, Serikali imetoa mafunzo ndani na nje ya nchi
kwa wapiganaji wake katika fani mbalimbali kuendana na kada zao. Pia, Serikali imefanya
matengenezo ya majengo mbalimbali ya Kikosi cha KMKM kwa Unguja na Pemba, Aidha,
Serikali imekipatia Kikosi hicho vifaa vya mawasiliano na huduma nyengine muhimu. Vilevile,
Serikali imekiimarisha Kitengo cha Uzamiaji kwa ununuzi wa vifaa vya kisasa kwa ajili ya
mafunzo ikiwemo “troller” kwa shughuli za uzamiaji. Sambamba na hayo, Serikali imefanya
ukarabati wa vyombo vikubwa ikiwemo KM Miwi na KM Bawe pamoja na ukarabati wa magari
yote ya KMKM. Serikali inaendelea kukiimarisha Kikosi cha KMKM ili kiendelee kufanya
shughuli zake za doria za ulinzi na usalama baharini na nchi kavu pamoja na uokozi wakati wa
majanga ya baharini.
Vilevile, Serikali imeendelea kuimarisha utoaji wa matibabu kwa wapiganaji na raia kwa kujenga
Hospitali kubwa ya kisasa katika eneo la Kibweni pamoja na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya
matibabu na maabara.
Boti za Kikosi cha KMKM zikiwa katika doria zake za kawaida
125
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
7.8.3.2 Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU)
Ilani ya CCM imeitaka SMZ kuendeleza juhudi za kuliimarisha Jeshi la Kujenga Uchumi na
kuimarisha miundombinu ya kambi zake ili kuwavutia vijana wengi zaidi kujiunga kupata
mafunzo ya ukakamavu, uzalendo na stadi mbalimbali za maisha ili waweze kujitegemea. Katika
kulitekeleza hilo, Serikali imeanzisha mafunzo ya stadi mbalimbali za maisha ikiwemo ufundi wa
ushoni, ufundi bomba na useremala katika Chuo cha JKU Mtoni. Serikali pia, imekamilisha ujenzi
wa miundombinu ya Kambi za JKU ikiwemo jengo la ghorofa 3 la Skuli ya Sekondari ya JKU,
mabweni ya kulala wanafunzi, vyoo na nyumba za familia za askari.
Katika kipindi cha miaka mitano (5) iliyopita, jumla ya vijana 8,000 wamepata nafasi ya kujifunza
katika Chuo cha Amali cha JKU na katika kambi zake Unguja na Pemba. Vilevile, jumla ya
Wapiganaji 86 wamekamilisha mafunzo ya uongozi mdogo na Wapiganaji 57 wanaendelea na
masomo katika fani mbalimbali ikiwemo Afya, Sheria, Habari na Kilimo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akikagua Hospital ya KMKM baada ya kuifungua – Kibweni,Zanzibar.
126
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
7.8.3.3 Kikosi Cha Valantia Zanzibar
Katika kukiimarisha Kikosi cha Valantia Zanzibar, Serikali imekamilisha ujenzi wa jengo la
Makao Makuu ya Kikosi pamoja na kujenga makaazi ya wapiganaji na Maofisa wa Kikosi hicho.
Aidha, Serikali imewajengea uwezo kwa kuwapa mafunzo ya muda mrefu na mfupi wafanyakazi
wake katika fani mbalimbali.
Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein akizindua rasmi na kukagua Mradi
wa Kilimo cha Mboga mboga katika Shamba la JKU - Bambi
127
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
7.8.3.4 Kikosi Cha Mafunzo
Serikali imeendelea kukiimarisha kikosi cha Vyuo vya Mafunzo kwa kufanya ukarabati wa
majengo katika kambi zake za Unguja na Pemba. Aidha, Serikali tayari imeshafanya upimaji wa
maeneo ya Langoni, Kinumoshi, Ubago na Eneo la Ofisi Pemba ili kuyakinga maeneo hayo na
uvamizi. Vilevile, maafisa na wapiganaji mbalimbali wa Kikosi cha Mafunzo wamejengewa
uwezo katika fani na ngazi mbalimbali.
7.9 Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
Serikali imekamilisha uandaaji wa Sera ya Hifadhi ya Jamii na kuanza utekelezaji wake. Lengo la
sera hiyo ni kujenga mfumo wa hifadhi ya jamii unaolenga kutoa huduma bora za hifadhi kwa
watu wote, hasa maskini na wanaoishi katika mazingira magumu zaidi, pamoja na kuimarisha
mfumo wa uratibu wa huduma za hifadhi ya jamii. Kwa kutambua umuhimu wa Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii, Serikali imeimarisha ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sheria ya mfuko huo. Katika kipindi
cha 2010 - 2014 Mfuko wa Hifadhi ya Jamii umesajili waajiri kutoka Serikali Kuu 295, Mashirika
ya Serikali 80 na Taasisi Binafsi 3,472 pamoja na wanachama 66,111 kutoka Serikali Kuu,
Mashirika ya Serikali na Taasisi Binafsi. Aidha, kwa kutambua umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa
wananchi, Mfuko umeanzisha Mfumo wa Uchangiaji wa Hiari (Zanzibar Voluntary Social
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,
alipotembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Valantia Mtoni
128
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Security Scheme) ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanafikiwa na kunufaika na matunda ya
hifadhi ya jamii yanayotolewa na Mfuko huo. Tokea kuanzisha kwa mfumo huo mwaka 2012,
Mfuko umeshasajili wanachama 4,970 kutoka vikundi mbalimbali vya uzalishaji, wajasiriamali,
watu binafsi pamoja na Wazanzibari wanaofanya kazi nje ya nchi na kukusanya Shilingi milioni
122 hadi kufikia mwezi Juni 2014. Angalia Jadweli Namba 4 na 5.
Jadweli namba 4: Takwimu za usajili wa wanachama waajiri (2010-2014)
Jadweli namba 5: Takwimu za usajili wa wanachama waajiriwa (2010-2014)
Katika kuhakikisha watoto wetu wanapata maeneo ya kucheza na kufurahi, Serikali kwa
kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii imekijenga upya Kiwanja cha Kufurahishia Watoto
cha Uhuru kiliopo kariakoo kwa gharama za shilingi bilioni 15. Kiwanja hicho kimefunguliwa
rasmi tarehe 8 January 2015 wakati wa shamrashamra za Miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Aidha, Serikali inaendelea na matengezo ya Kiwanja cha Kufurahishia Watoto cha Tibirizi Pemba
ambapo matengenezo hayo yako katika hatua za mwisho. Pia, Serikali kwa kushirikiana na Mfuko
huo imeweza kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo. Miongoni mwa miradi hiyo ni
ujenzi wa Mnara wa Kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar na ujenzi wa nyumba
kumi (10) za makaazi Mbweni.
Mwaka Serikali kuu Mashirika ya Serikali Taasisi Binafsi
2009/2010 71 20 756
2010/2011 74 20 833
2011/2012 74 20 909
2012/2013 76 20 974
Mwaka Serikali kuu Mashirika ya Serikali Taasisi Binafsi
2009/2010 32,674 2,631 23,187
2010/2011 33,410 2,603 25,383
2011/2012 33,953 2,735 28,313
2012/2013 33,300 2,644 30,167
129
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Aidha, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii umekuwa ukitoa mikopo kwa Serikali, Taasisi za Serikali na
Taasisi Binafsi ikiwa ni moja ya njia ya kuwekeza fedha zinazotokana na michango ya wanachama
wa Mfuko kama inavyoelezwa katika Sheria ya Mfuko ikiongozwa na Sera ya Uwekezaji ya
Mfuko huo. Fedha hizo huwekezwa kwa kuzingatia usalama, faida, urahisi wa upatikanaji fedha,
Wananchi wakifurahika katika Kiwanja cha ZSSF-Uhuru
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
akifungua Kiwanja cha Kufurahishia Watoto cha Uhuru - Kariakoo Mjini Zanzibar
130
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
mgawanyo na faida ya kiuchumi na kijamii. Katika kipindi cha 2010 hadi 2015 Mfuko
umezikopesha taasisi mbalimbali jumla ya Shilingi bilioni 14.7 kama ifuatavyo;
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (ZIFA), TZS 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa Hostel.
Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), TZS 5.0 bilioni kwa ujenzi wa ofisi Mazizini.
Coastal Fast Ferries, USD 4,000,000 kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za usafiri wa
baharini.
Zanzibar cable Television (ZCTV), TZS 329 milioni kwa uboreshaji wa huduma za
matangazo ya televisheni.
Halmashauri ya Kaskazini ‘B’, TZS 111.8 milioni kwa ajili kuanzisha biashara ya uuzaji
na usambazaji wa vifaa vya ujenzi kwa wananchi kwa gharama nafuu.
131
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
SEHEMU YA NANE
8.0 KUYAENDELEZA MAKUNDI MBALIMBALI
8.1 WATOTO
Katika juhudi za Serikali za kuimarisha haki na maendeleo ya watoto, imeandaa Sheria ya Mtoto
ya 2011 na kutengeneza Kanuni za kusimamia utekelezaji wa Sheria hiyo. Kanuni hizo zinahusu
Masuala ya Hifadhi ya Mtoto, Usajili wa Vituo na Makaazi ya Kulelea Watoto, Ukaazi na Ulezi
wa Kambo pamoja na Kinga Maalum Kuhusu Hifadhi, Ridhaa ya Kupima UKIMWI na Matibabu.
Aidha, Serikali imeandaa Mkakati wa Masuala ya Sheria kwa Watoto (2013-2018) kwa lengo la
kuifanyia kazi Sheria ya Mtoto ili kuhakikisha kunakuwepo mfumo mzuri wa haki na ustawi wa
watoto wa Zanzibar. Vilevile, Serikali imeendelea kuimarisha Mfumo wa Hifadhi ya Mtoto
ikiwemo uanzishwaji wa Mahakama za Watoto. Pia, Serikali imo katika hatua za mwisho za
kuifanyia marekebisho Sera ya Uhai, Hifadhi na Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2001 ili iende
sambamba na mahitaji mapya yanayojitokeza kulingana na mabadiliko ya maendeleo na mahitaji
ya mtoto.
Serikali imesimamia uundwaji wa Mabaraza ya Watoto nchini ambapo jumla ya Mabaraza 239
yameundwa katika shehia mbalimbali za Unguja na Pemba. Mabaraza hayo yameundwa kwa lengo
la kuwakutanisha watoto kuzungumza masuala yanayowahusu pamoja na changamoto
zinazowakabili. Aidha, kupitia Mabaraza haya, ushiriki wa watoto katika kutoa maoni yao juu ya
mambo yanayowahusu umeongezeka, watoto wamepata uelewa zaidi juu ya haki na wajibu wao
na wanaweza kuelimishana. Pia, katika kukusanya maoni ya uanzishwaji wa Katiba Mpya ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jumla ya watoto 150 kutoka katika mabaraza 131 ya Unguja
na Watoto 105 kutoka katika mabaraza 22 ya Pemba walishiriki katika utoaji wa maoni.
Vilevile, Serikali imekamilisha ujenzi wa Nyumba ya Kulelea Watoto iliyopo Mazizini na tayari
watoto wanalelewa katika nyumba hiyo. Serikali pia, imeandaa na kuisambaza Miongozo ya
Uanzishaji na Uendeshaji wa Nyumba za Kulelea Watoto kwa taasisi binafsi pamoja na kuandaa
kitini cha kufundishia watendaji wa vituo hivyo kwa lengo la kuimarisha malezi ya watoto katika
vituo hivyo. Aidha, Serikali imefanya zoezi la kuvitambua vituo 13 vya kulelea watoto na
kusimamia utekelezaji wake. Vilevile, Serikali inaendelea na usajili wa kuwatambua watoto walio
katika mazingira magumu ambapo jumla ya watoto 12,453 wamesajiliwa na kutambuliwa mahitaji
132
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
yao kutoka Unguja na Pemba. Serikali inaendelea kutoa misaada ya kibinaadamu ikiwemo vyakula
na mavazi kwa familia mbalimbali zinazoishi na watoto walio katika mazingira magumu.
8.2 VIJANA
8.2.1 Kusimamia Utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Vijana
Kwa lengo la kuwaendeleza na kuzipatia ufumbuzi changamoto za Vijana, Serikali imesimamia
na kuratibu utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Vijana pamoja na kuzijengea uwezo taasisi za
Vijana zipatazo 158 katika nyanja mbalimbali, ikiwemo kuwapatia mafunzo na semina za
ujasiriamali, stadi za maisha na kusaidia upatikanaji wa ruzuku ili kusaidia utekelezaji wa Sera
hiyo. Aidha, Serikali kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia imekuwa ikiendelea kutoa elimu zaidi
juu ya Sera hiyo kwa Vijana na wahusika wengine wa masuala ya maendeleo ya vijana Unguja na
Pemba. Pia, kutokana na utekelezaji wa Sera hiyo, vikundi 258 vya Vijana vimeanzishwa kupitia
SACCOS mbili (2) kubwa za vijana Unguja na Pemba. Vilevile, Serikali imeweza kuanzisha
mashamba mawili (2) ya mfano Unguja na Pemba ili kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia shughuli
za kilimo.
Vilevile, Serikali kwa kushirikiana na Taasisi zisizo za kiserikali zimeweza kuwapatia vijana
mafunzo ya ujasiriamali, vifaa pamoja na kuwawezesha kujiajiri wenyewe. Aidha, Serikali
imeanzisha Mfuko Maalum wa Vijana ambao unatoa mikopo nafuu kwa kupitia vikundi vyao
walivyoanzisha. Mfuko huu tayari umeshawapatia vijana mikopo yenye thamani ya jumla ya
Shilingi milioni 813,800,000 kwa vijana 2,285 kupitia vikundi 258 Unguja na Pemba.
8.2.2 Kukamilisha Uanzishaji wa Baraza la Taifa la Vijana
Serikali imekamilisha uandaaji wa Sheria na Kanuni ya kuanzisha Baraza la Vijana Zanzibar lenye
lengo la kuwashirikisha vijana katika ngazi mbalimbali za maamuzi. Aidha, Baraza hilo tayari
limeshaundwa na Katibu wa Baraza la Vijana tayari ameshateuliwa na Mheshimiwa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
8.3 WANAWAKE
Katika utekelezaji wa Sera ya Hifadhi na Maendeleo ya Wanawake ya mwaka 2001, Serikali
imeweza kuwajengea uwezo na uthubutu wanawake wa kutumia fursa za kujiendeleza kiuchumi,
133
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
kijamii na kisiasa. Wanawake wengi hivi sasa wameweza kumiliki mitaji na kufanya biashara
kubwa na ndogo zinazoendesha maisha yao, familia zao na kuchangia uchumi wa Taifa. Aidha,
kutokana na utekelezaji mzuri wa sera hiyo, wanawake wameweza kuhamasika na kujitokeza
kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi zote za maamuzi. Idadi ya wanawake katika
vyombo vya utoaji maamuzi na ngazi mbalimbali za uongozi ni kama ifuatavyo: Baraza la
Wawakilishi asilimia 40, Madiwani asilimia 14, Mawaziri asilimia 25, Makatibu Wakuu asilimia
25, Wakurugenzi asilimia 42, Wakuu wa Mikoa asilimia 20, Wakuu wa Wilaya asilimia 20,
Makatibu Tawala asilimia 20, Majaji asilimia 33 Mahakimu asilimia 21 na Masheha asilimia 8.
Aidha, Serikali imewashajiisha na kuwawezesha wanawake na makundi mengine ya wanaharakati
kutathmini juhudi wanazozichukua katika kupambana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa
kijinsia, kubaini changamoto na kupanga mipango ya baadae. Pia, Kwa kushirikiana na Shirika la
Action AID, Serikali imeanzisha Nyumba Salama kwa ajili ya kuwahifadhi na kuwahudumia
waathirika wa vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto, pamoja na kufuatilia kesi zao
Mahakamani ambapo hadi sasa jumla ya waathirika 26 wamepatiwa huduma ya hifadhi katika
nyumba hiyo. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita malalamiko mbalimbali yanayohusu haki
za wanawake (udhalilishaji, kutelekezwa na kukosa matunzo) yameripotiwa na kushughulikiwa
katika vyombo vya kisheria. Sambamba na hayo, Serikali imeanzisha na kuzijengea uwezo
Kamati za Kupambana na Ukatili na Udhalilishaji wa Kijinsia kutoka ngazi ya Taifa hadi Shehia,
imeunda Mtandao wa Wanaume wa kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia,
imetayarisha miongozo ya kufundishia na kushirikiana na viongozi wa dini katika mapambano
hayo. Aidha, Serikali imefanya uchambuzi wa sheria na kanuni zinazohusiana na udhibiti wa
vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, na kuweza kubaini mapungufu mbalimbali ambayo tayari
yameanza kufanyiwa kazi.
Serikali inaendelea na juhudi zake za kuvipatia mafunzo, kuvihamasisha, kuvishauri na
kuvitembelea vikundi vya wanawake vya uzalishaji mali, wajasiriamali na SACCOS kwa lengo la
kuviimarisha na kuvifanya vijitegemee ili vichangie katika kupiga vita umasikini na kukuza hali
zao kiuchumi. Jumla ya vikundi vya wanawake 551 (Unguja 209 na Pemba 362) na SACCOS 53
(Unguja 24 na Pemba 29) zimetembelewa na kuhamasishwa. Wanawake wengi wamehamasika
134
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
kujiunga katika vikundi vya uzalishaji pamoja na SACCOS Unguja na Pemba na kuweza
kujikwamua na hali ngumu ya kiuchumi.
8.4 WAZEE
Katika juhudi za kuwapatia hifadhi ya makaazi, huduma za afya na misaada ya kijamii wazee
wasiojiweza na wasio na jamaa, Serikali inaendelea kuwatunza na kuwahudumia wazee 91 katika
Nyumba za Wazee za Serikali zilizopo Unguja na Pemba na kupatiwa chakula, mavazi na huduma
za afya. Aidha, wazee 149 wanapatiwa fedha za posho ya kujikimu kimaisha kila mwezi. Vilevile,
Serikali imeiyafanyia matengenezo makubwa majengo ya Nyumba za Wazee Sebleni. Ukumbi wa
Mikutano na Msikiti pamoja na kuzungushiwa ukuta katika makazi hayo. Pia, vifaa vyote muhimu
vimenunuliwa na kuimarisha miundo mbinu ya maji na umeme katika makaazi hayo. Hatua hizo
zimeimarisha hali ya wazee pamoja na utulivu na usalama wao.
Aidha, katika juhudi za kuimarisha maslahi ya wazee, Serikali imeamua kuanzisha Mpango wa
Malipo ya Pencheni Jamii kwa Wazee Wote (Universal Pension). Mpango huu utawahusisha
wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea ambapo kila mzee atapewa 20,000 kwa mwezi.
Mpango huu utatekelezwa na Serikali kupitia Sekta ya Uwezeshaji na Ustawi wa Jamii.
8.4.1Kuhamasisha Jamii Kuendeleza Utamaduni wa Kuwaheshimu, Kuwaenzi na
Kuwatunza Wazee wetu
Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi akifungua Majengo ya Nyumba
za Wazee Sebleni zilizofanyiwa Ukarabati mkubwa.
135
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Serikali inaendelea na kuihamasisha jamii kuendeleza utamaduni wa kuwaheshimu, kuwaenzi na
kuwatunza wazee wetu. Kila ifikapo siku ya tarehe 01 Oktoba ya kila mwaka Serikali inasimamia
maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani kwa lengo la kutathmini mafanikio na changamoto
zilijitokeza katika jitihada za kuwatunza, kuwaheshimu na kuwaenzi wazee ikiwa ni pamoja na
kuihamasisha jamii na wadau wengine kuongeza juhudi za kuendeleza kuwaheshimu, kuwaenzi
na kuwatunza wazee. Aidha, Serikali inakamilisha matayarisho ya kuwapatia pencheni Jamii kwa
wazee wote wenye umri wa kuanzia miaka 70 na kuendelea.
8.5 WATU WENYE ULEMAVU
8.5.1 Kubaini Watu Wenye Ulemavu Wanaoweza Kufanyakazi za Uzalishaji Mali
Ili kuwa na takwimu sahihi za Watu wenye Ulemavu na aina ya Ulemavu walionao pamoja na
kurahisisha upangaji wa Sera, Mikakati ya Mipango mbalimbali hapa nchini, Serikali imefanya
usajili katika Wilaya zote za Unguja na Pemba na jumla ya watu wenye ulemavu 542 (321 Unguja
na 259 Pemba) wamesajiliwa. Watu hao wanajishughulisha na kazi mbalimbali zikiwemo ufundi
magari, useremala, ufinyanzi, ufundi wa TV, uashi, ufundi umeme na ushoni. Aidha, Serikali
imetayarisha Sera ya Watu wenye Ulemavu pamoja na Mpango wa Utekelezaji wa Sera. Pia,
muongozo wa kuombea ruzuku kwa Jumuiya za Watu wenye Ulemavu umeandaliwa. Vilevile,
vikao mbalimbali vya kawaida vya Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu na vikao vya maafisa
waratibu vimefanyika. Usajili wa Watu wenye Ulemavu unaendelea kufanyika pamoja na
kuwapatia Watu wenye Ulemavu visaidizi na Dawa kwa Unguja na Pemba. Serikali imeendelea
kutoa elimu inayohusu mikataba, haki, fursa na wajibu wa Watu wenye Ulemavu katika Shehia
zote za Unguja na Pemba. Pia, Serikali inaendelea kutoa ruzuku kwa Jumuiya za Watu wenye
Ulemavu Unguja na Pemba ili ziweze kutimiza malengo yao. Jumuiya hizo ni CHAVIZA,
ZANAB, UWZ, JMZ, SADZ, JUWAUZA, ZAPDD, na SOZ. Serikali imeendelea Kuratibu Mfuko
wa Maendeleo ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar. Hadi kufika Septemba 2013 mfuko
umekusanya jumla ya Shilingi milioni. 167.6.
8.6 WAFANYAKAZI
8.6.1 Kuandaa Sera ya Hifadhi ya Jamii na Kufanya Mapitio ya Sheria za Kazi
Serikali ina jukumu la kuzifanyia mapitio Sheria za Kazi ambapo Kanuni kumi (10) za Sheria ya
Ajira Nambari 11 ya mwaka 2005 zimetayarishwa na kuanza kutumika. Kanuni hizo zinahusu
136
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
mambo mbalimbali yakiwemo Maslahi ya Wafanyakazi katika Sekta Binafsi, Usajili na Utendaji
kazi wa Vyama vya Wafanyakazi, Mikataba, Likizo Bila ya Malipo na Makundi Maalum ya
Wafanyakazi. Kukamilika kwa kanuni hizi kutarahisisha utekelezaji wa Sheria za Kazi katika
maeneo yaliyotajwa. Pia, Kanuni za Utumishi wa Umma zimeshatayarishwa na zimeshasambazwa
kwa wahusika wote.
Vilevile, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani imezinduwa rasmi Toleo Maalumu
la Sheria za Kazi katika lugha nyepesi. Toleo hilo limefafanuwa vipengele muhimu vya Sheria
tano (5) za kazi zikiwemo Sheria ya Ajira, Sheria ya Uhusiano Kazini, Sheria ya Usalama na Afya
Kazini, Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, Sheria ya Fidia pamoja na Sheria moja ya Usafiri
Baharini.
8.6.2 Kusimamia Utekelezaji wa Sera ya Ajira
Serikali imeufanyia mapitio ya Mpango wa Ajira kwa Vijana wa mwaka 2009 – 2015 na kuandaa
Mpango mpya wa mwaka 2014 – 2018. Mpango huo tayari umesambazwa katika Taasisi za
Umma na Taasisi Binafsi. Mpango huo ni Dira katika suala zima la ajira na kuwawezesha vijana
kujiajiri. Katika hatua za msingi za utekelezaji wa Mpango huo, Serikali imeandaa Makongamano
na Semina mbalimbali za kujadili Mpango wa Ajira kwa Vijana wa miaka minne kuanzia mwaka
2014-2018 kwa vijana kutoka Unguja na Pemba. Aidha, Serikali imezindua mfuko wa uwezeshaji
wananchi kiuchumi kwa kuunganisha Mfuko wa Kujitegemea, Mfuko wa AK/JK na Mfuko wa
Vijana ili kuweza kukabiliana na tatizo la ajira na kuinua uchumi wa Zanzibar. Vilevile, kwa
mashirikiano na taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi, Serikali imeendelea kuishughulikia
changamoto ya upatikanaji wa ajira hasa kwa vijana nchini kwa kuwaorodhesha watafuta kazi
kupitia Kituo cha Kutoa Taarifa za Soko la Ajira ili kuweza kuwaunganisha na waajiri. Jumla ya
vijana 2,473 wameorodheshwa, ambapo vijana 1,978 wamefanikiwa kuajiriwa ndani na nje ya
nchi kupitia Kituo hicho.
Jadweli namba 6: Idadi ya Vijana Waliosajiliwa Kuomba Kazi Katika Kituo cha Kutoa
Taarifa za Ajira 2010 hadi 2015
Mwaka Wanawake Wanaume Jumla
2010 – 2011 145 162 307
137
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
2011 – 2012 122 134 256
2012 – 2013 105 109 214
2013 – 2014 172 292 464
2014 – 2015 487 745 1,232
Jumla 1,031 1,442 2,473
Jadweli namba 7: Idadi ya Vijana Walioajiriwa kwa Kuunganishwa na Waajiri Kupitia
Kituo cha Kutoa Taarifa za Ajira 2010 hadi 2015
Mwaka Wanawake Wanaume Jumla
2010 – 2011 120 102 222
2011 – 2012 86 150 236
2012 – 2013 74 96 170
2013 – 2014 80 270 350
2014 – 2015 642 358 1,000
Jumla 1,002 976 1,978
8.6.3 Kuimarisha Mashirikiano kati ya Serikali, Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi
na Waajiri
Serikali imeendelea kuimarisha mashirikiano ya UTATU kati ya Shirikisho la Vyama Huru vya
Wafanyakazi, Jumuiya ya Waajiri na Serikali. Mashirikiano hayo yamewezesha kufanyika kwa
majadiliano ya pamoja katika mambo ya maslahi ya wafanyakazi, kuweko kwa utulivu na amani
katika maeneo ya kazi na pia utatu huo umeiwezesha Zanzibar kutekeleza mikataba na maazimio
yanayohusiana na masuala ya ajira ambayo Tanzania imetia saini na kuyaridhia.
8.6.4 Kuendelea Kuimarisha Mazingira bora na Maslahi ya Wafanyakazi
Serikali imefanya tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Muundo wa Utumishi kwa Wizara,
Mashirika ya Serikali na Taasisi za Umma. Wizara 13 zimeweza kufavyiwa tathmini Unguja na
Pemba. Pia, Serikali imeandaa muongozo unaolenga kupima uzito na kufanya tathmini ya kazi
(Job evaluation and grading) ili kuondoa malalamiko katika malipo ya mishahara kwa watumishi
138
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
wa Umma. Vilevile, katika kuimarisha mazingira bora na maslahi ya wafanyakazi, Serikali
inaendelea na uandaaji wa Sera ya Malipo kwa Watumishi wa Umma kwa lengo la kuimarisha
mfumo mzima wa malipo ya mishahara na stahiki nyengine za Watumishi. Aidha, Serikali
inaendelea na uandaaji wa upangaji wa taarifa za wafanyakazi kupitia malipo ya mishahara kwa
ajili ya kutoa muongozo na kutatua changamoto zinazojitokeza katika Utumishi wa Umma.
Vilevile, Serikali imefanya mapitio ya mishahara na malipo mengine ya Watumishi wa Umma
Unguja na Pemba, pamoja na kufanya marekebisho ya nyongeza za mishahara kwa watumishi
wenye uzoefu usiopungua miaka 15 ya utumishi kwa kada zote. Serikali imepandisha kima cha
chini cha mshahara kutoka TZS. 125,000/= hadi TZS. 150,000/= hii ni sawa na ongezeko la
asilimia 20. Kwa upande wa Sekta Binafsi, Serikali imeweka kima cha chini cha mshahara kuwa
TZS.145,000/= kutoka TZS. 70,000/= cha mwaka 2010 ikiwa ni ongezeko la asilimia 107. Aidha,
Serikali imeendelea na kazi ya kutoa taaluma ya utayarishaji wa Mkataba wa Utoaji Huduma kwa
Mteja kwa Wizara 16.
Katika kusimamia utekelezaji wa Sheria Nambari 8 ya mwaka 2005 ya Usalama na Afya Kazini,
Serikali imefanya Ukaguzi Kazi na ukaguzi wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi kwa taasisi zote
za watu binafsi katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba. Miongozo imetolewa juu ya mapungufu
yaliyobainika na kuagiza kurekebishwa kasoro hizo. Vilevile, hatua mbalimbali za kisheria
zimechukuliwa dhidi ya waajiri walioonekana kukiuka Sheria za Kazi kwa makusudi, licha ya
ushauri uliotolewa awali wa kurekebisha kasoro hizo. Aidha, sehemu za kazi 351 zimesajiliwa
ili kuzitambua na kuweka taarifa zao kwenye Daftari la Usajili wa Sehemu za Kazi. Utambuzi huu
unarahisisha shughuli za ukaguzi kwa kutambua mapema mazingira ya kazi zao, hatari
zinazoweza kutokea katika sehemu hizo na hivyo kutoa ushauri na maelekezo yanayofaa, kabla ya
kutokea tatizo au ajali. Jadweli Namba 8 na 9 linachanganua hali ya Ukaguzi Kazi na Ukaguzi
Afya na Usalama kazini.
Jadweli namba 8: Taasisi Zilizofanyiwa Ukaguzi Kazi 2010 hadi 2015
Mwaka Mjini
Magharibi
Kusini
Unguja
Kaskazini
Unguja
Kusini
Pemba
Kaskazini
Pemba
Jumla
2010 – 2011 59 41 58 18 15 191
139
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
2011 – 2012 60 45 59 21 18 203
2012 – 2013 57 37 54 19 17 184
2013 – 2014 75 41 67 30 35 248
2014 – 2015 74 58 62 24 23 241
Jumla 325 222 300 112 108 1,067
Jadweli namba 9: Ukaguzi wa Usalama na Afya Kazini
Mwaka Mjini
Magharibi
Kusini
Unguja
Kaskazini
Unguja
Kusini
Pemba
Kaskazini
Pemba
Jumla
2010 – 2011 71 12 15 22 10 130
2011 – 2012 17 14 16 14 13 74
2012 – 2013 75 45 64 25 22 231
2013 – 2014 62 35 59 20 18 194
2014 – 2015 52 45 61 12 15 185
Jumla 277 151 215 93 78 814
SEHEMU YA TISA
140
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
9.0 MAENEO MENGINEYO MUHIMU
9.1 SEKTA YA SHERIA
Katika kuimarisha Sekta ya Sheria, Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 imeagiza Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kuimarisha Mahakama kwa kujenga majengo mapya na kuzipatia vifaa
vya kisasa, kujenga nyumba za Mahakimu Unguja na Pemba na kufanya marekebisho ya Sheria
na Kanuni za Utendaji kazi wa Mahakama.
Katika kutekeleza maagizo hayo, Serikali imefanya matengenezo makubwa ya jengo la Mahakama
Kuu Vuga, Mahakama ya Makunduchi, Mahakama ya Kadhi wa Wilaya Mwanakwerekwe,
majengo ya Mahakama Chwaka na matengenezo ya jengo la Mahakama Kuu Chake chake Pemba.
Aidha, Serikali imenunua vitendea kazi na kusomesha wafanyakazi 78 katika kada na ngazi
mbalimbali ili kuimarisha utendaji kazi wa Mahakama. Vilevile, katika juhudi za kuondoa
matatizo ya ushughulikiaji wa kesi za watoto, Serikali imeanzisha Mahakama ya Watoto ambayo
tayari inaendelea kufanya kazi zake.
Kwa upande wa Majaji Serikali imefanikiwa kuongeza idadi yao kutoka wawili (2) mwaka 2011
hadi sita (6) (wakiwemo wanawake wawili (2)) mwaka 2014. Vilevile, kwa upande wa Mahakimu
wa ngazi mbalimbali Serikali imefanikiwa kuongeza idadi yao kutoka 43 mwaka 2010 hadi kufikia
85 mwaka 2015 hii ni sawa na ongezeko la asilimia 97.7.
9.1.1 Kuwaendeleza Wataalamu wa Sheria za Mikataba
Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imeanzisha Kitengo kinachohusiana na masuala ya
Mikataba, ambacho kina wataalamu wanaoshughulikia masuala yote ya mikataba ya Serikali.
Aidha, Serikali imewapatia mafunzo maafisa wa Sheria kutoka Taasisi mbalimbali juu ya uandishi
wa sheria, utatuzi wa migogoro, ufungaji na uingiaji wa mikataba ya kitaifa na kimataifa. Mafunzo
hayo yamedhaminiwa na Serikali kwa mashirikiano na UNDP kupitia Mradi wa Mageuzi katika
Sekta ya Sheria (Zanzibar Legal Sector Reform Program).
141
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
9.1.2 Kuyatafutia Ufumbuzi Masuala ya Mrundikano wa Kesi Mahakamani
Serikali imeajiri mahakimu wapya na kufanya matengenezo ya majengo yake ili kupunguza
changamoto ya mrundikano wa kesi katika Mahakama zake. Serikali kupitia Mahakama
imeanzisha Kamati ya Kusukuma Kesi kwa kuwashirikisha wadau wote wa masuala ya kesi.
Kamati hiyo inakutana kila baada ya miezi mitatu kujadili namna ya kuendesha na kuharakisha
kesi hizo. Vilevile, Mahakama kupitia Mradi wa Mageuzi ya Sekta ya Sheria inaendelea na
utaratibu wa kuanzisha Mfumo wa Kisasa wa Usimamizi wa Uendeshaji Kesi (Case Management
System). Aidha, Serikali imezipatia Mahakama zote vifaa ili kusadia kupunguza mrundikano wa
kesi.
9.1.3 Kuwapatia Mafunzo Mahakimu wa Mahakama ya Mwanzo
Katika azma ya kuwaendeleza Mahakimu, Serikali kupitia Programu ya Mabadiliko katika Sekta
ya Sheria, imewapatia mafunzo Majaji, Mahakimu na Waendesha Mashtaka ili kuwazidishia ujuzi
katika utendaji wa kazi zao za kila siku. Miongoni mwa mafunzo yaliyotolewa ni pamoja na
teknolojia ya habari na sheria, uendeshaji wa kesi na utoaji wa haki, usimamizi wa kesi, na uandishi
wa sheria.
9.1.4 Kukamilisha Mchakato wa Kutenganisha Shughuli za Upelelezi na Uendeshaji
Mashtaka
Katika kukamilisha utaratibu wa kutenganisha shughuli za upelelezi na uendeshaji wa mashtaka,
Serikali imeajiri Waendesha Mashtaka katika Mahakama za Wilaya. Hivi sasa Waendesha
Jengo la Mahakama Kuu baada ya kufanyiwa Matengenezo – Vuga Mjiji
Zanzibar
142
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
Mashtaka wapo katika Mahakama Kuu, Mahakama zote za Mkoa na Mahakama sita (6) za Wilaya
ambazo ni Mjini, Magharibi, Chake Chake, Mkoani, Micheweni na Wete. Hatua za kupeleka
Waendesha Mashtaka katika Mahakama nne (4) za Wilaya zilizobaki zinaendelea, ambazo ni
Mkokotoni, Mfenesini, Mwera na Makunduchi.
9.1.5 Msaada wa Kisheria
Serikali inaendelea na utayarishaji wa Sera ya Msaada wa Kisheria (Zanzibar Legal Aid Policy).
Sera hiyo itakapopitishwa itatoa fursa kwa makundi maalum ikiwemo watoto, wanawake, watu
Wenye Ulemavu na masikini kupata haki zao.
9.1.6 Kupeleka Huduma za Mahakama Karibu na Wananchi
Serikali imepeleka huduma za Mahakama karibu na wananchi kwa kuendesha vipindi vya redio
na televisheni, mikutano ya hadhara katika shehia na maskuli na kutoa na kusambaza kwa
wananchi Matoleo mbalimbali ya Jarida la Mahakama la Shahidi kwa ajili ya kuelimisha wananchi
kuhusu huduma na masuala ya Mahakama na jinai. Katika kipindi cha 2010 hadi 2015, jumla ya
kesi 28,870 zilisajiliwa katika Mahakama mbalimbali Unguja na Pemba, ambapo kesi 14,267 sawa
na asilimia 49 zilitolewa uamuzi. Aidha, Serikali imekamilisha uchapishaji wa seti 890 za Sheria
za Zanzibar kuanzia mwaka 1980 hadi 2009. Kwa kawaida seti moja inachukua ‘Volume’ 14.
Sheria hizo tayari zimesambazwa kwa wadau. Vilevile, Serikali imefanya kazi ya kuziweka
pamoja Sheria za Zanzibar (consolidation) kuanzia mwaka 1959 hadi 2010, Rasimu ya Mwanzo
kwa mwaka 1980 hadi 2010 imekamilika. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imeweza kuandaa
Miswada ya Sheria 69, Kanuni 8, Matangazo na Machapisho 650 ya kisheria, Ofisi pia imeweza
kusimamia kesi 53 dhidi ya Serikali na kutoa ushauri kwa Taasisi za Serikali.
143
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
9.1.7 Mapambano Dhidi ya Rushwa na Uhujumu wa Uchumi
Kutokana na umuhimu wa kupambana na rushwa na uhujumu uchumi, Serikali imetunga Sheria
na. 1 ya mwaka 2012 ambayo imetoa mamlaka ya kuanzishwa kwa Kitengo cha Kupambana na
rushwa na uhujumu Uchumi Zanzibar. Aidha, Serikali imeandaa Kanuni za utekelezaji wa Sheria
pamoja na kutoa elimu juu ya mapambano dhidi ya rushwa na uhujumu uchumi kwa kutumia njia
mbalimbali zikiwemo vipindi maalum vya redio na televisheni, majarida, vipeperushi, stika,
Jengo Jipya la Wizara ya Katiba na Sheria lilopo Mazizini Mjini Zanzibar
Jengo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lilopo
Mazizizni Mjini Zanzibar
144
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
semina pamoja na mikutano ya hadhara. Vilevile, Serikali imewapatia mafunzo watendaji wake
wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa na kujifunza kwa njia za ziara za kubadilishana uzoefu baina
ya wafanyakazi wa Kitengo cha Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar na wenzao
wa Tanzania Bara.
145
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
SEHEMU YA KUMI
10. Changamoto Zilizojitokeza na Hatua za Kukabiliana Nazo
Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM
ya mwaka 2010 hadi 2015, kulijitokeza baadhi ya changamoto ambazo Serikali ililazimika
kutumia rasilimali zake ili kukabiliana nazo. Changamoto hizo ni kama zifuatazo:-
Kutokea kwa vitendo au matukio yaliyoashiria uvunjifu wa amani na utulivu tulionao hapa
nchini. Vitendo hivyo ni pamoja na baadhi ya watu na viongozi wa dini kumwagiwa tindi kali;
mlipuko wa bomu la kutupwa, na watu wawili kuuawa katika mazingira ya kutatanisha.
Vitendo hivyo viliathiri Sekta ya Utalii kwa watalii wanaotembelea Zanzibar pamoja na
kuathiri uchumi kwa ujumla.
Kutokea kwa maafa mbalimbali, ikiwemo kuzama kwa Meli ya Spice Islander huko eneo la
bahari ya Nugwi na Meli ya MV Skaqit katika maeneo ya Chumbe ambapo zaidi ya watu 1,600
walipoteza maisha; kutokea kwa upepo mkali katika maeneo mbalimbali ya visiwa vya Unguja
na Pemba na kuleta uharibifu wa makaazi ya watu na mazao. Majanga haya yalipelekea
kupoteza kwa nguvu kazi pamoja na matumizi makubwa kwa Serikali ambayo hayakutarajiwa.
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walikabiliana na majanga hayo kwa pamoja,
ikiwemo huduma za uokozi na huduma za kibinaadamu na kutoa pole kwa waathirika.
Mfumko wa bei za vyakula uliotokana na tatizo la kupanda bei za mafuta na chakula katika
soko la dunia, hasa katika miaka ya 2010 na 2011.Wananchi wengi hasa wenye kipato cha
chini waliathirika na tatizo hilo kwa kushindwa kununua chakula na mahitaji yao mengine ya
msingi. Serikali ilihamasisha wananchi hasa wakulima kuongeza bidii katika shughuli za
kilimo na uzalishaji mali ili kuweza kupata chakula cha uhakika na kujiongezea kipato. Aidha,
Serikali ililazimika kutoa ruzuku kwa ushuru wa bidhaa za chakula zinazoingizwa nchini ili
kudhibiti mfumko wa bei. Vilevile, kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya
Dola ya Kimarekani kumeongeza bei kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi na
kuwaongezea wananchi gharama za maisha. Serikali kupitia Benki kuu inaendelea kuchukuwa
hatua madhubuti ya kupunguza kasi ya kushuka thamani ya Shilingi na kupunguza athari katika
uchumi wa nchi.
146
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
147
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi – 2010-
2015
11. HITIMISHO
Kwa ujumla katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 - 2015), Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar ilitekeleza maagizo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa mafanikio makubwa. Mafanikio
haya kwa kiasi kikubwa yametokana na mashirikiano na mshikamano kati ya wananchi na
viongozi katika ngazi mbalimbali katika jamii yetu kuanzia ngazi ya Shehia, Wilaya, Mkoa hadi
Taifa. Hali hii inadhihirisha wazi kwamba, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia sera na
mipango yake thabiti imeweza kuwashirikisha wananchi wake wote bila ya kujali tofauti zao za
kisiasa, kidini na kijamii chini ya uongozi imara wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein.
Kutokana na mafanikio yaliyopatikana ni dhahiri kwamba wananchi wameongeza imani ya Chama
cha Mapinduzi na watakichagua tena kuongoza Serikali zote mbili (2) kwa kishindo kikubwa
katika Uchaguzi utakaofanyika mwezi Oktoba, 2015. Ni imani ya Serikali kwamba katika kipindi
cha miaka mitano ijayo (2015 – 2020) wananchi na viongozi watazidisha mashirikiano yao katika
utekelezaji wa mipango na sera zitakazoletwa na Chama Chetu kwa lengo la kuiwezesha nchi yetu
kupiga hatua zaidi za maendeleo katika Sekta za kiuchumi, uzalishaji mali, huduma za jamii na
Sekta nyengine muhimu.
Kufanikiwa kwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2010 – 2015) kumetokana na juhudi
za viongozi, taasisi mbalimbali na wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla. Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inatoa shukurani za dhati kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wote wa Chama cha Mapinduzi wa
Tanzania Bara na Zanzibar, wananchi wote wa Tanzania kwa mashirikiano makubwa
yaliyopelekewa kufanikiwa utekelezaji wa Ilani ya Chama chetu.
Aidha, tunashukuru na kupongeza Sekta binafsi, Asasi za Kiraia, Washirika wa Maendeleo na nchi
marafiki kwa ushirikiano na mahusiano yao yaliyoiwezesha Serikali kutekeleza majukumu yake
kwa ufanisi mkubwa sana. Tunaomba mashirikiano hayo yaendelee ili kuleta maendeleo ya
kudumu katika nchi yetu na kuwaondoshea wananchi wetu umasikini.
“KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI”