12
Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania Warsha ya Kitaifa juu ya Ubia ka ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kaka Uendeshaji wa Masoko ya Mazao Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo cha Wanawake, CCT, Morogoro 24 Oktoba 2011

Warsha ya Kitaifa juu ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na ... · Nafasi ya Wazalishaji Wadogo katika Mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano waTanzania ambayo ... Malengo makuu

  • Upload
    others

  • View
    15

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania

Warsha ya Kitaifa juu ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Uendeshaji wa

Masoko ya Mazao

Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo cha Wanawake, CCT, Morogoro

24 Oktoba 2011

2

Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Masoko

1. Utangulizi

Warsha ya kitaifa yenye kauli mbiu Soko la Uhakika, Kichocheo cha Uzalishaji na mada kuu Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Uendeshaji wa Masoko ya Mazao iliandaliwa na MVIWATA na kujadiliwa sambamba na Mkutano Mkuu wa 16 wa MVIWATA.

Warsha hii ilifanyika kwa siku moja tarehe 24 Octoba 2011 katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo cha Wanawake (CCT) Morogoro. Jumla ya washiriki 257 (wanawake 166 na wanaume 91) walihudhuria warsha hiyo. Washiriki wa warsha walikuwa ni wakulima wanachama wa MVIWATA, wawakilishi kutoka wizara na asasi za serikali, mashirika wenza, watumishi na viongozi wa MVIWATA na waandishi wa habari.

Malengo ya warsha hii yalikuwa yafuatayo;i. Kuwapa uelewa wanachama na washiriki wengine juu ya dhana ya ubia

kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika uendelezaji wa masoko ya mazao ya kilimo.

ii. Kutathmini na kujadili mapungufu ya sera na maeneo ya katiba yanayogusa mfumo mzima wa uzalishaji na soko la mazao ya mkulima mdogo.

Washiriki wa warsha wakilisikiliza mawasilisho ya mada

Mada za WarshaMada zifuatazo ziliwasilishwa katika warsha hii:1. Sera ya Masoko na Ushiriki wa Wadau Mbalimbali ambayo

3

Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Masoko

iliwasilishwa na Bw. Alfred Mapunda, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Masoko, Wizara ya Viwanda na Biashara.

2. Ubia wa Vyama vya Wakulima na Halmashauri za Wilaya katika Uendeshaji Masoko: Uzoefu wa MVIWATA ambayo iliwasilishwana Ndugu Nickson Elly, Mratibu wa Kitengo cha Masoko MVIWATA.

3. Fursa na Vikwazo katika Biashara ya Mazao ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo iliwasilishwa na Dr.Abdala Makame, Mkurugenzi Msaidizi, Wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

4. Nafasi ya Wazalishaji Wadogo katika Mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano waTanzania ambayo iliwasilishwa na Ndugu Bashiru Ally, Mhadhiri Chuo Kikuu Dar es salaam.

5. Haki na Upatikanaji wa Habari kwa Watu wa Vijijini ambayo iliwasilishwa na Bw. Rashid Kejo.

Mchakato wa WarshaWarsha ilianza kwa utangulizi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MVIWATA Ndugu Stephen A. Ruvuga ambaye aliwakaribisha wajumbe na wageni wote na kufanya utambulisho kwa washiriki wote wa warsha. Baada ya utambulisho alielezea malengo ya warsha hii na baadaye kumkaribisha Mwenyekiti wa MVIWATA Ndugu Yazid Makame Ame ambaye naye alimkaribisha Mgeni Rasmi Ndugu Steven Mashishanga kwa ajili ya Ufunguzi rasmi.

Mkurugenzi Mtendaji wa MVIWATA akielezea malengo ya warsha na kulia Mwenyekiti wa MVIWATA akimkaribisha Mgeni Rasmi

4

Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Masoko

Baada ya ufunguzi, warsha iliendeshwa kwa njia ya mawasilisho kutoka kwa wawezeshaji na kufuatiwa na mijadala, maswali na majibu kutoka kwa washiriki wa warsha. Baada ya majadiliano washiriki waliweka maazimio.

Wajumbe wa warsha wakichangia mawazo baada ya mawasilisho

Hotuba ya Mgeni Rasmi Ndugu Steven MashishangaKatika hotuba yake Mgeni Rasmi Ndugu Stephen Mashishanga aligusia juu ya Sera ya Masoko, ubia wa vyama vya wakulima na Halmashauri za Wilaya, fursa na vikwazo katika biashara ya mazao, nafasi ya wazalishaji wadogo katika na mchakato wa katiba mpya na haki ya upatikanaji habari vijijini.

A k i o n g e l e a j u u y a sera za masoko alitaja kuwa MVIWATA ndiyo mwakilishi sahihi wa mkulima mdogo na kama mkulima hatashirikishwa ipasavyo katika uundwaji wa sera, mafanikio katika utekelezaji wa sera yatakuwa madogo sana kwani mkulima mdogo ndiye mlengwa haswa wa sera yenyewe.

Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mh. Stephen Mashishanga akifungua warsha

5

Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Masoko

Katika kusimamia utekelezaji wa sera na kuboresha soko la mazao ya kilimo, mgeni rasmi alihimiza kuwepo wa ubia kati ya vyama vya wakulima na halmashauri za wilaya katika uendeshaji wa masoko ya mazao ya kilimo hasa katika kujenga uwezo wa watumiaji masoko, kukusanya na kusambaza taarifa za masoko na utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi ghalani. Aliishauri serikali iondoe vikwazo visivyo vya kisera vya kuzuia upatikanaji wa fursa za soko la pamoja la Afrika Mashariki zikiwemo amri za kutouza mazao nje pamoja na kujenga uelewa kwa wadau kuhusu maendeleo na fursa za masoko zilizoko ndani na nje ya nchi yetu.

Ili kukifanya kilimo kiwe chenye tija, alipendekeza mchakato wa kuunda katiba mpya ulenge kuwafikishia wakulima maarifa na teknolojia, kuendesha kilimo cha umwagiliaji, kuboresha huduma za utafiti na ugani, kuhakikisha mazao ya mkulima yanazalishwa, yanaongezwa thamani, kufungashwa na kuuzwa katika masoko ya ndani na nje, kuboresha miundombinu ya masoko na upatikanaji wa mitaji kwa masharti nafuu.

6

Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Masoko

2. Mawasilisho ya Mada

2.1 Sera ya Masoko ya mazao na bidhaa za kilimo na ushiriki wa sekta binafsi

Mada juu ya Sera ya Masoko ya Mazao na Bidhaa za Kilimo (2008) iliwasilishwa na Bw. Alfred Mapunda, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Masoko, Wizara ya Viwannda na Biashara.

Akielezea uundwaji wa sera hii alitaja kuwa mchakato wake ulianza mwezi novemba, 2003 na utekelezaji wa mikakati yake umeanza mwaka 2009. Wadau waliohusishwa ni wizara za serikali, bodi za mazao, taasisi za utafiti, vyuo vya elimu ya juu, vyama vya ushirika vya wakulima, wasindikaji wa mazao ya kilimo na wadau wa maendeleo kupitia warsha, semina, saili na mikutano. Alitaja kuwa sera hii ina malengo ya aina mbili yaani: Malengo makuu na Malengo maalum.Malengo makuu yanalenga mabadiliko ya soko la ndani na la kimataifa na malengo maalum yamelenga utatuzi wa maeneo ya changamoto.

Aliyataja maeneo makuu ya sera kuwa ni: Kuongeza thamani kwa mazao ya kilimo, Ubora na Viwango vya mazao na bidhaa za kilimo, Mfumo wa sheria na urekebishaji, Mfumo wa kitaasisi, Ujuzi wa masoko na ujasiriamali, Miundombinu ya Masoko, Taarifa za Masoko, Utafiti na intelijensia/ushushushu wa masoko, Udhibiti wa mifumo hatarishi katika kilimo, Upatikananji wa mikopo ya kilimo, Biashara ya mazao ya kilimo katika masoko ya kikanda na kimataifa na masuala mtambuka.

7

Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Masoko

Hata hivyo baada ya mawasilisho ilionekana wazi kwamba wakulima hawana uelewa wa sera yenyewe kwa sababau ya kutoshiriki na kutopewa habari juu ya sera na hivyo washiriki walishauri kuwa serikali iwashirikishe wakulima katika hatua zote za uundwaji na utekelezaji wa sera kwani malengo ya sera ni mazuri lakini utekelezaji wake umekuwa siyo mzuri na hivyo kushindwa kufikia malengo yake.

2.2 Ubia wa Vyama vya Wakulima na Halmashauri za Wilaya katika Uendeshaji Masoko

Mada hii iliwasilishwa na Bw. Nickson Elly, Mratibu wa Kitengo cha Masoko cha MVIWATA. Katika kuwasilisha mada hii, alibainisha kwamba changamoto za soko kwa wakulima wadogo ziliibuka baada ya serikali kufungua m i l a n g o y a s o k o huria. Katika kutatua changamoto za soko la mazao ya wakulima, MVIWATA ilibuni mkakati uliowezesha kujengwa kwa masoko ya mazao ya kilimo ya nusu jumla na mpaka sasa MVIWATA tayari imejenga masoko tisa yanayosimamiwa kwa ubia kati ya MVIWATA na halmashauri za wilaya. Masoko yote haya yanasimamiwa na bodi zilizosajiliwa kama kampuni binafsi zenye wawakilishi kutoka MVIWATA na halmashauri za wilaya. Mafanikio: Mafanikio yanayotokana na ubia katika kusimamia masoko. Wadau kuyaona masoko kama mali yao ambayo imepelekea kuwepo ushirkiano wa karibu wa wadau katika kuhakikisha kwamba masoko yanaendeshwa vizuri. Mafanikio mengine ni wanunuzi wa mazao kuongezeka kutokana na kuwepo kwa miundombinu ya soko inayoendeshwa na wadau

8

Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Masoko

wenyewe, kukua kwa shughuli za kiuchumi na kipato cha watu kuongezeka maeneo yenye masoko, kuongezeka kwa mapato ya halmashauri, kuwepo uwazi kwa shughuli zinazoendelea sokoni kwa MVIWATA na halmashauri na taarifa za changamoto zilizopo sokoni kufika kwa urahisi halmashauri kwa kupitia kwa wawakilishi wake.

Changamoto: Changamoto nyingi zitatokana na kutokuwepo kwa vikao vya pamoja vya mara kwa mara kati ya MVIWATA, halmashauri za wilaya na bodi za masoko ili kuangalia maendeleo ya masoko. Changamoto nyingine ni mitazamo tofauti juu ya soko kama nyenzo ya huduma na soko kama chanzo cha mapato kwa halmashauri zetu. Hali imepelekea migongano hasa halmashauri inapoongeza kiwango cha makusanyo ya ushuru bila mapitio ya kina katika mipango kazi na bajeti za soko. Hata hivyo, fundisho tulilolipata katika changamoto hii ni kuwa na vikao vya mara kwa mara ili kuwa na mtazamo mmoja.

2.3 Fursa na vikwazo katika biashara ya mazao ndani ya Jumuiya ya Afrika mashariki

Mada hii iliwasilishwa na Dr.Abdalla Makame, Mkurugenzi Msaidizi, Wizara ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki. Katika mawasilisho yake, alitaja maeneo makuu manne ya soko la pamoja la Afrika Mashariki ambayo ni soko la bidhaa, soko la huduma, soko la ajira na soko la mitaji.

Akiwasilisha mada yake alitoa taarifa kuwa nchi wanachama zimeunda umoja wa forodha ambao hutoa fursa kwa biashara ya bidhaa ikiwemo bidhaa za ki l imo, kubwa kati ya hizo fursa ni kutanuka kwa wigo wa soko la bidhaa

9

Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Masoko

ambapo mfanyabiashara ana fursa ya kuuza katika nchi tano wanachama wa umoja wa Afrika mashariki ambazo zinakadiriwa kuwa na idadi ya walaji wapatao 130 milioni. Alibainisha kwamba fursa nyingine ni umoja wa forodha kufuta ushuru wa mipakani kwa bidhaa zilizozalishwa ndani ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mtoa mada alitaja kuwa katika mchakato wa soko hili la pamoja sera na sheria za ardhi zitabaki kwa kila nchi mwanachama.

Alizitaja changamoto zinazolikabili soko la pamoja kuwa ni pamoja na ukosefu wa miundombinu bora ya masoko, mgongano wa sera za nchi wanachama na usimamizi hafifu wa makubaliano.

Wakichangia mjadala washiriki wa warsha walisema kuwa licha ya kuwepo kwa fursa ya kuuza mazao ya wakulima nje ya nchi katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, serikali imeendelea kuwazuia wakulima kutumia fursa hii kwa kuweka maagizo ya mara kwa mara ya kuzuia uuzaji wa mazao nchi katika nchi jirani na hivyo kufisha juhudi za kuzalisha zaidi na pia kuwakatisha tamaa wakulima.

2.4 Nafasi ya wazalishaji wadogo katika mchakato wa katiba mpyaAkitoa mada hii Ndugu Bashiru Ally alisema kuwa wakulima ni kundi kubwa na ndiyo wanaolisha taifa, hivyo wakijipanga na kuamua nini kiwekwe katika katiba mpya inawezekana. Alipendekeza kuwa mambo muhimu yanayopaswa kuwa katika katiba mpya ni:I. Katiba mpya lazima iainishe mamlaka za kujitawala na kutoa nguvu

zaidi kwa wananchi.II. Umiliki wa ardhi uwe kwa wazalishaji wadogo na wawe na mamlaka

juu ya matumizi ya ardhi yao.

Katika kuhitimisha mawasilisho yake alisema kuwa ni lazima tuwe na katiba itakayotambua na kuhakikisha usalama wa mkulima mdogo.

10

Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Masoko

Wa k i t o a m a o n i ya o , washiriki wa warsha walichangia kuwa kuna tatizo la kujilimbikizia ardhi kwa watu wachache wanaojiita wawekezaji ambao kimsingi mitaji ya kuendeshea shughuli zao wanaipata kutoka katika vyombo vya kifedha vya ndani. Wakati wazalishaji wadogo wakihangaika kupata mitaji imedhihirika kwamba kipaumbele kipo kwa wawekezaji kutoka nje. Ili kupunguza changamoto hii wakulima walishauriwa wasimame na kuwa na sauti moja, kwa kupitia chombo chao yaani MVIWATA wanatakiwa wadai suala la usimamizi wa ardhi kwa nguvu zao zote hasa katika mchakato wa kutunga katiba mpya.

2.5 Haki na upatikanaji wa habari kwa watu wa vijijiniAkiwasilisha mada hii Ndugu Rashid Kejo alitaja kuwa wakulima wa vijijini kama walivyo wananchi wengine wana haki ya kupokea taarifa mbali mbali zinazohusiana na kilimo. Hata hivyo alielezea kuwa wakulima wengi vijijini bado hawapati taarifa za kilimo kutokana na changamoto mbali mbali zikijumuisha jiografia ya nchi yetu na hivyo baadhi ya maeneo kutofikika kiurahisi, uchache wa rasilimali hivyo waandishi kushindwa kufika katika baadhi ya vijiji.

Baada ya majadiliano ilionekana kuwa ni jukumu la kila mwananchi kutafuta habari ili kujua kitu gani kinaendelea katika nchi yake.

11

Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Masoko

3. Maazimio ya Warsha

1. Kwa kuwa kuna masoko katika wilaya mbalimbali ambayo hayafanyi kazi, Halmashauri za Wilaya katika wilaya hizo zijifunze na kutumia mfumo wa ubia kati ya Halmashauri na wadau wanaotumia soko katika kuyaendesha masoko hayo kama njia ya kuweka mfumo endelevu wa uendeshaji.

2. Wizara zinazohusika na masoko ziratibu sera na taratibu zake ili kuepusha vikwazo mbalimbali vya masoko ikiwemo vizuizi na ushuru usiokuwa na uhalali.

3. Sera ya masoko ilenge kuondoa vikwazo vya kibiashara (kutouza nje). MVIWATA ihakikishe inaleta msukukumo ili Wizara husika ichukue hatua madhubuti kwa ajili ya kuondoa kasoro hiyo

4. Wizara zihakikishe ushiriki wa vyombo halisi vya wakulima wadogo katika kamati zinazoundwa badala ya kuwakilishwa na vyombo ambavyo si vya wakulima. Uongozi wa MVIWATA ukutane na Wizara husika kwa ajili ya kuwasilisha azimio hili.

5. MVIWATA iweke mikakati ya kushiriki katika mchakato wa uundaji wa katiba mpya kwa kujipanga vema na kuwa na mikakati thabiti kuhakikisha hoja na kero zinazohusu maslahi ya wakulima wadogo zinazingatiwa, mfano, suala la ugawaji na umilikikaji ardhi.

P.O. Box 3220, Morogoro, Tanzania

Tel/fax: +255 23 261 4184. Email: [email protected]

www.mviwata.org