22
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI CHUO CHA UALIMU MARANGU DIPLOMA YA KAWAIDA YA ELIMU YA MSINGI SOMO.STADI ZA RAMANI NA JIOMOFIKI MSIMBO:05202 KAZI YA KIKUNDI WASHIRIKI. 1. PAUL MEELA---------------------------------18307 2. SALEHE SEIPH-------------------------------18316 3. MARIJANI SHABANI-----------------------18282 4. YONA MABALA------------------------------18331 5. STEVEN MVUONI---------------------------18323 6. SIKUJUA SARIZA-------------------------- 7. YOHANA MARIUS--------------------------18330 Swali: Chunguza shughuli ya kilimo cha Kahawa katika eneo la Marangu ,kisha onesha :- i. Chimbuko la shughuli husika. ii. Namna inavyofanyika. iii. Umuhimu /mchango wake kwa wahusika. iv. Hali ya shughuli hiyo kwa sasa v. Changamoto zake. vi. Mapendekezo kwa ajili ya maboresho. vii. Mustakabathi wa shughuli husika.

Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

CHUO CHA UALIMU MARANGU

DIPLOMA YA KAWAIDA YA ELIMU YA MSINGI

SOMO.STADI ZA RAMANI NA JIOMOFIKIMSIMBO:05202

KAZI YA KIKUNDIWASHIRIKI.

1. PAUL MEELA---------------------------------183072. SALEHE SEIPH-------------------------------183163. MARIJANI SHABANI-----------------------182824. YONA MABALA------------------------------183315. STEVEN MVUONI---------------------------183236. SIKUJUA SARIZA--------------------------7. YOHANA MARIUS--------------------------18330

Swali:Chunguza shughuli ya kilimo cha Kahawa katika eneo la Marangu ,kisha onesha :-

i. Chimbuko la shughuli husika.ii. Namna inavyofanyika.

iii. Umuhimu /mchango wake kwa wahusika.iv. Hali ya shughuli hiyo kwa sasav. Changamoto zake.

vi. Mapendekezo kwa ajili ya maboresho.vii. Mustakabathi wa shughuli husika.

Page 2: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

Yaliyomo

1. Dibaji…………………………………………………………………………i

2. Shukrani……………………………………………………………………..ii

3. Chimbuko la shughuli ya kilimo cha kahawa……………………………...

4. Namna shughuli ya kahawa inavyofanyika……………………………….

5. Umuhimu wa shughuli wa kahawa kwa wahusika……………………….

6. Hali ya shughuli ya kahawa kwa sasa……………………………………..

7. Changamoto zake…………………………………………………………...

8. Mapendekezo kwa ajili ya maboresho……………………………………

9. Mustakabadhi wa shuhuli ya kahawa……………………………………

10. Rejea……………………………………………………………………….

Page 3: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

Dibaji

Kahawa ni zao ambalo linawaingizia wananchi kipato kikubwa sana na taifa kwa ujumla zao la

pili ni tumbaku ambayi inalimwa zaidi kanda za kati kwa kuona umuhimu wa zao hili tumeona

tulifwatilie kwa kufanya utafiti na kuona maendeleo ya zao hili ambalo ni sehemu kubwa na

mchango mkubwa wa mwananchi yeyote na taifa kwa umjumla.

Zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,kagera ,Rukwa na Kigoma.

Kwa kuzingatia umuhimu wa zao hili tumeweza kutembelea maeneo zao hili linapolimwa

ambapo ni maeneo ya Marangu na maeneo ya Maua ipo katika eneo hili.

Zao hili linaonyesha kukumbwa na changamoto nyingi sana,licha ya kuwa an faida kubwa kwa

taifa na jamii ambayo wanalima zao hilo.

i

Page 4: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

Shukrani

Napenda kuwashukuru wafuatao kwa mawaidha na misaada mbalimbali waliotupa katika

kuafanya swali hili.

Uongozi wa chuo cha Ualimu Marangu kwa kuturuhusu kutoka nje ya chuo na kwendakupata

taarifa toka kwa wakulima wanaojihusisha na zao hili.

Wakufufunzi wa somo la stadi za ramania na Jiomofiki kwa kutupa maelekezo mazuri ya swali

na ufafanuzi nini swali linahitaji.

Mtaalamu wa kilimo cha kahawa mama ………………kwa kutupa maelekezo mazuri kuhusu

shughuli hii.

Ofisi ya chama cha ushirika Ashira kwa kutupokea na kutupa maelekezo mazuri.

Tunawashukuru wanachuo wote kwa ushauri maelekezo na hoja katika kufanya kazi hii.

ii

Page 5: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

1. Chimbuko la zao la kahawa

Baadhi ya vyama maarufu vya wakulima vilivyoanziswa enzi hizo ni Kilimanjaro Native

Planters Assosiation mwaka 1925 chama hiki kilikuwa na malengo yafuatayo:-

i. Kuboresha hali ya wakulima na kupanga bei nzuri ya zao la kahawa.

ii. Kupinga wakoloni kuweka bei ya zao kahawa.

iii. Kuunganisha wakulima wote wa kahawa ili wawe na sauti moja ili kutetea maslai yao.

Baadae wananchi wa kilimanjaro walibadili jina la chama cha Kilimanjaro Native Planters

Assosiation na kukiita Kilimanjaro Native Cooperative Union (KNCU) . Kipango R.(2011)

Kuna aina mbili za kahawa Robusta na Arabika. TET(1995)

Kahawa iliingia tanzania na kizinduliwa mwaka 1830 ililetwa na wamisionari wakatolilki huko

morogoro kwenye milima ya Uluguru.mwaka 1893 ililetwa kilema maeneo ya maua katika

maeneo ya Marangu wanalima kahawa aina ya Arabiaka.

Vilevile kahawa ilimwayo nchini Kenya ilitoka Kilema-Moshi.(TET 1981)

Arabika hulimwa pia mikoa ya Kilimanjaro,Meru,Oldendai,Pare.

2. Namna inavyofanyika

1. Kwanza kabisa ni kuandaa kitalu na kuweka mbolea ya samadi kuweka udongo na kuuchanganya na unapiga mstari wakusia . Katiaka mashimo hayo mkulima huweka mshimo mbolea ya samadi mshimo hayo huachwa wazi kwa muda wa mwezi au miezi miwili ili mbolea ioze na kupoa.Otmar(1964)

Page 6: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

Umbali wa mstari mmoja na mwingine ni sentimeta 15 na mbegu na mbegu sentimeta 15. Mstari

unalala chini mgongo unaangalia juu na kufunika na udongo nusu nchi.

Unaweka matandazo ya majani makafu ya majani yasiyo na mbegu kisha unamwagilia kwa

kutumia kopo lenye matundu maana ukitumia ndoo itachimaba.

Umwagiliaji ni asubuhi na jioni maana mchano joto linaunguza, kuota kwa mbegu ni siku 60

hadi siku 90 ili iote upesi unailoweka kabla ya kusia kwa masaa 12 hadi 24 ili iote haraka.

Inatakiwa iote urefu wa sentimeta 15 hadi 30 kabla yakupelekwa shambani.

SHAMBANI

Unaandaa shamba unachimba mashimo miezi mitatu kabla ya kupanda mche urefu uwe

sentimeta 60 na upana sentimeta 60 shimo hadi shimo ni meta 3 kwa meta 3 .Unapochimba

mashimo baada ya miezi miwili unaweka mbolea na kufukia na kusimamisha miti katikati ya

shimo kama alama mwezi wa tatu unachukuwa sepeto unachimba katikati na unachukuwa mche

na mizizi yake unaupanda katikati na kisha unatandaza majani makafu na kuanza kumwagilia

na muda mzuri wakupanda miche hii inakuwa ni jioni ili mmea ukae katika hali ya kuto kupata

jua ili uweze kuanza kushika vizuri ardhini.

Mmea hukaamiaka mitatu

MAGONJWA

Kahawa ni zao kubwa la biashara linaloliingizia taifa fedha nyingi za kigeni. Ni la pili baada ya

Tumbaku. Lakini zao hili linakabiliwa na changamoto nyingi ambazo ni magonjwa na wadudu

achilia mbali Pembejeo, haya yote yanamuhusisha moja kwa moja mkulima..

1. CHULEBUNI (CBD).

Chulebuni ama kama ujulikanavyo kama Coffee Berry Disease (CBD), ni ugonjwa mbaya sana

na huenea kwa kasi. Mbuni ulioshambuliwa haufi ila mkulima anaweza kupoteza mpaka asilimia

90 ya mavuno kama hatazingatia namna bora ya kuuzuia. CBD huathiri matunda ya kahawa hasa

Page 7: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

kanda za juu na kati. Ushambuliaji ni mkubwa zaidi wakati wa masika kwani CBD hupenda hali

ya unyevu na hali ya baridi.

Dalili na madhara ya CBD:

* CBD hushambulia mibuni katika hatua tatu muhimu ambazo ni:

. Maua yanapochanua.

. Punje zikiwa changa na laini.

. Punje zinazoiva.

* Madhara makubwa hutokea walati punje zikiwa changa na laini amnapo:

. Maua yaliyoshambuliwa hunyauka na kuanguka.

. Vidonda vyeusi na vilivyobonyea huonekana kwenye matunda yaliyoshambuliwa. Mengi huoza

na kudondoka. Yaliyobakia hukaukia kwenye mti na kuwa chanzo cha uambukizaji kwenye

mavuno ya msimu unaofuata.

* Matunda yaliyoiva hukaukia kwenye matawi na huvunwa kama buni.

* Hupunguza zao kwa asilimia kati ya 30 na asilimia 60 wakati mwingine hufikia hadi asilimia

90.

* Kudhibiti CBD hufikia hadi asilimia 35 ya gharama za uzalishaji.

* Hupunguza ubora wa kahawa kwa kiasi kikubwa.

Jinsi ya kuzuia chulebuni (CBD):

- Panda aina mpya ya kahawa inayohimili mahambulizi ya Chulebuni ambayo ni mkombozi

dhidi ya ugonjwa huu hatari.

- Punguza kivuli shambani.

Page 8: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

-Kata matawi kwa wakati na sahihi. Ondoa maotea mara kwa mara.

- Ondoa masalia ya buni zilizoathirika na teketeza kwa moto.

- Kwangua magamba kwenye mashina machafu ya kahawa.

- Anza kunyunyizia vizuia kuvu kukinga matunda machanga ndani ya wiki tatu kabla ya mvua za

msimu kuanza.

- Hamasisha majirani kuzuia chulebuni kwa wakati mmoja.

3. KUTU YA MAJANI (LEAF RUST).

Mtenga, D.J. (2008) Tofauti katika uwezo wa kutoa ukinzani kwa chulebuni (Colletotrichum kahawae)na kutu ya majani (Hemileia vastatrix) katika aina za mkusanyiko wa kahawa zilizopo TaCRI Lyamungu.Utafi ti kwa ajili ya Shahada ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro,

Tanzania.

Kutu ya majani ni ugonjwa unaoathiri majani ya kahawa hasa kanda za chini na kati. Ugonjwa

huu unaathiri kahawa aina zote; Robusta na Arabika. Kutu ya mjani isipodhibitiwa inaweza

kupunguza mavuno kwa asilimia 60.

Dalili za ugonjwa:

Majani yaliyoshambuliwa hutokeza madoa madoa ya manjano chini ya jani

Madhara yake:

. Kutu ya majani hupunguza eneo la jani la kutengeneza chakula. Pia hudababisha kupukutika

kwa majani yanayolisha matunda na kukuza mmea.

. Kwa hali hiyo husababisha madhara ya mmea kutoa punje ndogo zenye ubora hafifu.

. Ugonjwa ukishamiri hukausha matawi, shina zima na hatimaye mti mzima kufa.

Page 9: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

Hali zinazochangia kuenea kwa kutu ya majani:

- Unyevu wa hewani unapokuwa zaidi ya aslimia 80 na unapoambatana na kivuli cha kupita kiasi

kwenye shamba.

- Msongamano wa machipukizi na matawi katika mti wa kahawa.

Jinsi ya kudhibiti ugonjwa wa kutu ya majani:

- Punguza kivuli kuzunguka mti wa kahawa.

- Pogolea machipukizi na matawi katika mti wa kahawa.

Kuzuia kutu ya majani:

i) Panda aina mpya zinazovumilia magonjwa ya kutu ya majani na chulebuni.

ii) Boresha huduma muhimu ikiwa ni pamoja na lishe ili kuongeza uvumilivu wa magonjwa

hususani ugonjwa wa kutu ya majani.

iii) Tumia viua kuvu kwa wakati na vipimo sahihi. Unyunyiziaji wa kwanza ufanywe ndani ya

wiki tatu kabla ya mvua kunyesha, na kuendelea hadi mara tatu mpaka nne kwa msimu.

iv) Shirikisha na majirani kudhibiti kutu ya majani.

MAGONJWA MENGINE YA KAHAWA.

Yapo magonjwa mengine kadhaa ya kahawa ambayo umuhimu wake umemezwa na magonjwa

mawili niliyozungumzia hapo juu. Ningependa kuyataja tu baadhi yake pamoja na mbinu za

kuyazuia au kuyatibu.

3. BAKAJANI (Brown eye spot).

Ugonjwa huu huenezwa na kimelea aitwaye "Cercospora cofficola". Hudhibitiwa kwa utunzaji

bora wa shamba na kutumia morututu.

4. UGONJWA WA PUNJE ( Bean disease).

Huu huambukizwa na kuvu aitwaye "Nematospora coryli" akienezwa na kimatira. Ili kuepukana

na ugonjwa huu, ni lazima kuchukua hatua za kumdhibiti kimatira.

5. UGONJWA WA MASHINA (Scarly bark disease).

Page 10: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

Ugonjwa huu hujulikana kama "Ukungu" kwa wakulima walio wengi, upo wa aina mbili ambao

wakulima huwa wanashindwa kutofautisha na huuita kwa ujumla wake Ukungu. Aina hii ya

kwanza ya ukungu huambukizwa na kuvu aitwaye "Fusarium lateritium". Hakuna udhibiti wa

kitaalam mpaka sasa ila kung'oa mti mzima na kupanda upya. Ukishang'oa choma mti hapohapo

na acha kwa muda angalau hata misimu miwili au mitatu kisha panda upya.

6. UGONJWA WA KUOZA MIZIZI (Root rot disease).

Huu ugonjwa unafanana kabisa na ugonjwa wa mashina, ni ukungu wa aina ya pili kama

unavyojulikana na wakulima wengi. Huambukizwa na kuvu aitwaye "Armillaria mellea".

Hakuna udhibiti ila kung'oa na kupanda upya baada ya muda wa misimu miwili au mitatu hivi.

Ndugu zangu wakulima, wataalam na wadau wote wa kilimo, hakikisheni mnajitahidi kwa kadri

inavyowezekana kudhibiti magonjwa hayo. Kwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato

chake na pato la taifa kwa ujumla.

Ugonjwa wa majani

Ni ugonjwa wa fangasi mbaya sana ambao hushambuli majani,shina na matawi

Ili kilimo hiki kiwe na mafanikio kuna makundi ya watu au hatua za mkulima anazotakiwa kuwa

muangalifu ziko saba ili kuuza zao lake lenye ubora husika nazo ni:-

i. Wakulima-

Wassifanye kitu chochote bila kushauriwa na wataalamu kuanzia dawa ,kupanda miche na hatua

zote za kilimo cha zao la kahawa.

ii. Wasindikaji

Page 11: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

Kusafisha sehemu ya kuhifadhia kahawa ,kuhakikisha kahawa kavu isichanganye na kahawa

mbichi pamoja na kukagua ubora wa maji.

iii. Wakoboaji

Hii ni kudumisha usafi katika maeneo ya kukobolea,vifaa vyote visafishwe kabla ya kuanza

kutumua na baada ya kumaliza kutumia magunia yanayopendekezwa ni ya katani na isichangane

gunia la kahawa kavu na kahawa mbichi.

iv. Watunzaji

Kuhifadhi kahawa katika eneo kavu na liwe limepuliziwa dawa ya kuulia vijidudu(fumigation)

pia usitumie dawa yoyote kuhifadhia bila kukubaliana na mnunuzi na usichanganye stoo ya dawa

na sehemu ya kuhifadhia kahawa.

v. Wasafirishaji

Kusafirisha kahawa safi,iwekwe kwenye magunia ambayo hayajatumika mapya kabisa

usisafirishe kahawa na dawa.

vi. Watafiti

Tuwe tunakagua mabaki ya dawa marakwamara na kuangalia kiwango cha uchanganyaji wa

dawa hizo wakati wakuzitumia pia kuwaelwesha wadau wote hapo juu ili soko la kahawa

liendelee kudumu nakuendelea vizuri.

vii. Seriakali na TCB.

Kuweka na kufwatilia kanuni zilizowekwa hapo juu na kutoa usahuri kwa serikali jinsi ya

kuzitekeleza..

Kahawa hustawi vizuri katika sehemu zenye mwinuko ulio kati meta 1400 na 2000 na kwenye

sehemu za udongo wenye rutuba unaopitisha maji kwa urahisi. Pia wastania wa mvua

inayohitajika kwa mwaka ni kati ya milimeta 900 hadi 1800.

Page 12: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

Amri nane: taratibu bora za utunzaji wa kahawa:

• Kupalilia;

• Udhibiti wa magonjwa na wadudu wasumbufu;

• Kuweka matandazo;

• Urutubishaji wa udongo – kuweka mbolea;

• Kumwagilia pale maji yanapopatikana;

• Kupogolea machipukizi;

• Kupanda miti ya kivuli kwa mpangilio; na,

• Kupangilia matawi.

4. UMUHUMU WA HUGHULI HII

Katika shughuli hii kuna umuhimu mkubwa sana kama ifuatavyo:-

a. Kupeleka watoto shule kwa ajili ya ada na michango mingine ya shule.

b. Uhusaidia katika kupata fedha za kujenga nyumba .

c. Nidhamana ya kupewa mkopo kwa ajili ya kilimo hiki kama utatimiza vigezo ambapo

kikezo kikubwa cha kupata mkopo uwe unalima au unajihusisha na kilimo hiki na

umesajiliwa na chama cha ushirika (KNCU).

d. Shughuli hii hutoa ajira kwa watanzania kwa kuajiri Makarani,wenyeviti wna wahasibu

na bodinzima kwa ajili ya kufwatilia na kusimamia shughuli hii kupitia vyama vya

ushirika.

e. Kupata elimu sahihi juu ya kilimo cha zao hili wataalamu wa kilimo hutembelea

wakulima na kuwashauru namna ya kulima vizuri na kupata mazao bora.

5. Hali ya shughuli hii kwa sasa

Shughuli hii ya kilimo cha kahawa hali yake si nzuri maana wananchi wengi wameng’oa na

kupanda mahindi na migomba ya ndizi kwa sababu bei ya zao hili imeshuka sana licha ya

Page 13: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

pembejeo zake kupanda bei sana na wananchi wengi wakaona hamna haja ya juendelea na

kilimo cha zao hili.

Na wengi wao walibaki kuwa wakulima wadogo wadogo.

6. Changamoto ya zake

Chimilila, C. I., H.M. Temu and F.B. Swai (2008). Mifumo ya ukulima na riziki, na

vikwazo

vya tija, ubora na faida ya kilimo cha kahawa kwa wakulima wadogo. Ripoti ya

kitaalamu

ya utafi ti uliofanyika kwa wakulima wa kahawa wa Kilimanjaro, Arusha na Mbinga.

Taasisi ya

utafi ti wa kahawa Tanzania, Moshi, Tanzania. Kurasa 79.

Kilimo cha zao hili kinakabiliwa na changanoto zifuatazo:-

i. Bei ya madawa ya kulia wadudu kuwa na bai kubwa kiasi cha wakulima wengi

kushindwa kununua.

ii. Ufanyajiwa kazi kubwa malipo nikidogo wakati wa kuuza .

iii. Miche hupatikana kwa shida na bei ya mche mmoja ni shilingi miatano 500.

iv. Wakulima wakitembelewa na wataalamu kukataa kuelimishwa na wataalamu na kufuata

jinsi wanavyofahamu na hawataki kubadilika na kilimo chakisasa maana kinatuma

gharama kubwa sana.mfano kupulizia dawa kila baada ya siku 21.

v. Siasa iliingilia kati na wakulima kugundua halina faida kwao linafaida kwa viongozi

wengi wakaamua kuachana na zao hili.

vi. Vijana wengi kutokupenda kulima zao hili na kukimbilia mjini kwa ajili ya biashara na

shughuli nyingine.

vii. Kutokuwa na uaminifu kwa viongozi swanaoongoza vyama vya kisimamia kililmo hiki

cha kahawa.

viii. Mabadiliko ya hali yahewa mvua hazinnyeshi tena kwa wingi kama miaka ya nyuma .

ix. Ukosefu wa dawa ya kutibu baadhi na magonjwa na kusababisha kung’oa mmea wote

licha ya kuchukua muda mrefu hadi kutoa mazao.

Page 14: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

x. Kilimo cha zao la kahawa huchukuwa muda mrefu tangu kupanda hadi kupata mavuno ukilinganisha na mazao mengine kwa mfano kilimo cha migomba na kilimo cha mahindi.

7. Mapendekezo kwa ajili yamaboresho

Yafuatayo ni mapendekezo juu ya kilimo hiki cha kahawa kama ifuatavyo:-

i. Sherikali ipandishe bei ya zao hili ukilinganisha na soko la dunia.

ii. Pembejeo zipatikane kama mbolea na madawa ya kuulia wadudu.

iii. Miche ya kisasa ipatikane yakutosha na iuzwe kwa bei nzuri ambayo wakulima wengi

wataimudu.

iv. Serikali ifufue ofisi za ushirika ambao zimekufa kwa ngazi ya kijiji na kata kwa sasa

zi,mebaki kwa ngazi ya wilayani tu.

v. Elimu itolewe ilpasavyo kwa wakulima.

vi. Wataalamu waajiriwe wakutosha kwa maendeo zao hili linapolimwa ili kuwashauri

wakulima na kuwasaidia.

vii. Somo la kilimo cha kahawa liwekwe kwenye mtaala wa elimu kwa ngazi zote ili

kuwasaidia swanafunzi na vijana kujifunza kulima zao hili.

viii. Wanasiasa waachae kabisa kutumia zao hili kama njia ya kumba kura ili wachaguliwe

kushika nafasi mbalimbali bila matumaini yoyote wanapopata nafasi hiyo.

ix. Serikali iweke ruzuku kwenye bembejeo za zao hili kama motisha kwa wakuli,na na

kutambua mchango wao.

8. Mustakabali wa shughuli ya kilimo cha kahawa

Kilimo cha zao hili kimeendelea kudorora siku hadi siku na sasa kinaelekea kutoweka kabisa

kwa baadhi ya maeneo. .

Ukiangalia maofisi mengi yaliyokuwa yanashughulikia zao hili yamechakaa na kufungwa kabisa

na mengine yamekuwa magofu kabisa.

Kimsingi, Tanzania huzalisha aina mbili za kahawa: Arabika laini iliyooshwa (kiasi cha

55% ya jumla ya kahawa inayozalishwa), Robusta inayokaushwa kwa jua (kiasi cha

Page 15: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

40% ya kahawa inayozalishwa), pamoja na kiasi kidogo cha Robusta ya asili

inayokaushwa kwa jua (chini ya 5% ya kahawa yote inayozalishwa). Zaidi ya 90% ya

kahawa inayozalishwa husafirishwa na kuuzwa kwenye soko la kimataifa. Kiasi cha

Kahawa inayosafirishwa nje imekuwa ni kati ya magunia 600,000 na 950,000 kwa

miongo miwili iliyopita. Wanunuzi wakubwa katika soko la dunia ni Japan (kiasi cha

30% ya thamani ya mauzo ya nje), ikifuatiliwa na Marekani (kiasi cha 15% ya thamani

ya mauzo ya nje), halafu Ujerumani, Italia na Ubelgiji (takriban 10% ya thamani ya

mauzo ya nje kwa kila nchi). Asilimia 25 iliyosalia inagawanywa miongoni mwa nchi

nyingi tofautitofauti kutoka Finland hadi Swaziland. Jumla ya thamani ya mauzo ya

nje ilifikia kiasi cha Dola za Marekani milioni 145 mwaka 2011 (ITC COMTRADE).

Wakati takwimu za uzalishaji zikionekana kutobadilika sana, mabadiliko makubwa

yametokea kwenye mkusanyiko na chanzo cha uzalishaji wa kahawa ya Tanzania.

‐ Kiasi cha uzalishaji wa kahawa ya Robusta kimeongezeka mara mbili katika kipindi

cha miaka thelathini iliyopita.

‐ Kwa upande waArabika laini, uzalishaji katika eneo la Kaskazini (Kilimanjaro, Arusha,

Manyara na Tanga), umeshuka sana, ambapo maeneo ya Kusini (Mbeya na Mbinga)

kumekuwepo na ongezeko kubwa. Kumekuwepo na mabadiliko machache ya

uzalishaji wa Arabika ngumu ya asili (maeneo ya Tarime).

Kuna mikakati mbalimbali iliyowekwa kama ifuatavyo:-

“Dhumuni kuu la mkakati huu ni:

“Kuongeza uzalishaji na ubora wa kahawa kitaifa ili kuboresha mapato katika mnyororowote wa thamani, hususan wakulima wa kahawa”. (TaCRI 2011)

Malengo ya kimsingi ni kama ifuatavyo:

• Ongezeko la uzalishaji wa kahawa safi kwa mwaka kutoka wastani wa sasa wa tani

50,000 hadi angalau tani 80,000 kufikia mwaka 2016 na tani 100,000 kufikia mwaka

2021.

• Kuongeza ubora wa kahawa utakaodhihirishwa na ongezeko la bei ya ziada kwenye

masoko ya nje kutoka 35% ya jumla ya uzalishaji ya sasa hadi angalau 70% kufikia

mwaka 2021.

Page 16: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania

• Hisa ya bei halisi (FOB) ya mkulima kwenye kahawa inayosafirishwa nje inaboreshwa

kufikia angalau 75% ifikapo mwaka 2021.

Rejea

-Programu ya uendeshaji Tija na Ubora (2011) Tasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania

(TaCRI).

-Tasnia ya Kahawa Tanzania (2012)Mkakati wa maendeleo mwaka 2011 hadi 2021.

-Coffee Authority of Tanzania (1983)commision of the European communities.

-Tasisi ya ustawishaji wa Kahawa Tanzania(2008) Moshi-Lyamungu.

-Taasisi ya Elimu,(1981)Jiografia kwa wanafunzi wa shule za msingi,kitabu cha nne –Dar

es salam.

-Kipango R.(2011) historia kitabu cha mwanafunzi darasa la sita,Ben and Coimpany

Limited –dar es salamu .

-Otarm P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania.

Page 17: Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ... P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania