48
GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR (Hupigwa Chapa kwa Amri ya Serikali) Sehemu ya CXXIII Nam. 6511 26 Mei, 2014 Bei Sh Imekubaliwa na Mkuu wa Posta kuwa ni Gazeti Hutolewa k YALIYOMO Ukurasa Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Sheria ya Hati ya Uwakala na Mambo Mengine Yanayohusiana nayo Nam. .................................... 29 SEHEMU YA SHERIA Tangazo la Mswada uliyotajwa hapo chini umetangazwa katika Gazeti Rasmi hili Tangazo la Mswada Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Sheria ya Hatiya Uwakala na Mambo Mengine Yanayohusiana nayo T A N G A Z O Mswada ufuatao utawasilishwa katika Mkutano wa Baraza la Wawakilishi ulioanza tarehe 14 Mei, 2014 kwa kusomwa kwa mara ya kwanza na unachapishwa pamoja na Madhumuni na Sababu zake kwa ajili ya kutoa taarifa kwa wananchi. ZANZIBAR (Dkt. ABDULHAMID Y. MZEE) 26 Mei, 2014 Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi .

GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA · PDF fileKazi za Kamati ya Ushauri wa Mazingira 10. Mikutano na Akidi ya kamati ya ushauri wa Mazingira 11. Uwezo na Majukumu ya Waziri 12

  • Upload
    hadat

  • View
    352

  • Download
    16

Embed Size (px)

Citation preview

GAZETI RASMI LA SERIKALI YAMAPINDUZI YA ZANZIBAR

(Hupigwa Chapa kwa Amri ya Serikali)

Sehemu ya CXXIII Nam. 6511 26 Mei, 2014 Bei ShImekubaliwa na Mkuu wa Posta kuwa ni Gazeti Hutolewa k

YALIYOMO Ukurasa

Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Sheria yaHati ya Uwakala na Mambo MengineYanayohusiana nayo Nam. .................................... 29

SEHEMU YA SHERIA

Tangazo la Mswada uliyotajwa hapo chini umetangazwa katika GazetiRasmi hili

Tangazo la Mswada

Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Sheria ya HatiyaUwakala na Mambo Mengine Yanayohusiana nayo

T A N G A Z O

Mswada ufuatao utawasilishwa katika Mkutano wa Baraza la Wawakilishiulioanza tarehe 14 Mei, 2014 kwa kusomwa kwa mara ya kwanza naunachapishwa pamoja na Madhumuni na Sababu zake kwa ajili ya kutoa taarifakwa wananchi.

ZANZIBAR (Dkt. ABDULHAMID Y. MZEE)26 Mei, 2014 Katibu wa Baraza la Mapinduzi na

Katibu Mkuu Kiongozi.

RASIMU YA SHERIA YA USIMAMIZI WA MAZINGIRAZANZIBAR, 2015

_______________________

YALIYOMO

VIFUNGU JINA

SEHEMU YA KWANZAUTANGULIZI

1. Jina fupi na kuanza kutumika

2. Ufafanuzi

SEHEMU YA PILIMAJUKUMU YA JUMLA YA KIMAZINGIRA

3. Madhumuni ya Sheria4. Usimamizi wa mazingira katika mipango ya maendeleo5. Haki na wajibu wa kuwa na mazingira bora, safi na salama6. Misingi ya Usimamizi wa Mazingira

SEHEMU YA TATUUTAWALA NA MUUNDO WA TAASISI

7. Uanzishaji wa Kamati ya Ushauri wa Mazingira8. Muundo wa Kamati ya Ushauri wa Mazingira9. Kazi za Kamati ya Ushauri wa Mazingira10. Mikutano na Akidi ya kamati ya ushauri wa Mazingira11. Uwezo na Majukumu ya Waziri12. Mkurugenzi wa Mazingira13. Kazi za Mkurugenzi wa Mazingira14. Uanzishaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar15. Muundo wa Mamlaka na Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa

Mamlaka16. Kazi za Mamlaka17. Uwezo na Uendeshaji wa Mamlaka18. Uanzishaji wa Bodi ya Mamlaka19. Muda wa uteuzi na ukomo wa wajumbe wa Bodi20. Kazi za Bodi

TAHADHARI YA KIMAZINGIRA

24. Tahadhari ya kimazingira

SEHEMU YA TANOVITENGO VYA MAZINGIRA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

25. Uanzishaji wa Kitengo cha Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi26. Kazi za Kitengo cha Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi

SEHEMU YA SITAUSIMAMIZI WENYE UWIANO WA UKANDA WA PWANI

27. Eneo la ukanda wa pwani la Zanzibar28. Uanzishaji wa ukanda maalumu wa pwani.

SEHEMU YA SABAUSIMAMIZI WA MALIASILI ZISIZOREJESHEKA

29. Uanzishaji wa kamati ya pamoja ya maliasili zisizorejesheka30. Muundo wa Kamati ya pamoja ya maliasili zisizorejesheka31. Kazi za Kamati ya pamoja ya maliasili zisizorejesheka32. Akidi ya mikutano ya Kamati ya pamoja ya maliasili zisizorejesheka33. Kibali cha maliasili zisizorejesheka.34. Jukumu la kurejesha eneo lililochimbwa35. Kumbukumbu za maliasili zisizorejesheka36. Katazo la mchanga wa ufukwe na fungu

SEHEMU YA NANEELIMU YA MAZINGIRA NA UTAFITI

37. Upatikanaji wa taarifa za kimazingira38. Utafiti wa Kimazingira

SEHEMU YA TISATATHMINI YA ATHARI ZA KIMAZINGIRA NA KIJAMII

39. Mahitaji ya Tathimini ya Athari za Kimazingira40. Vigezo vya kuzingatia kwa shughuli zinazohitaji kufanyiwa tathmini ya

athari za kimazingira41. Utambuzi wa kampuni na wataalamu wa kufanya Tathmini ya Athari za

Kimazingira42. Maoni ya Jamii43. Ufuatiliaji44. Taarifa zinazohitajika

MKAKATI WA TATHMINI ZA KIMAZINGIRA

48. Mkakati wa Tathmini za Kimazingira49. Majukumu ya Mkurugenzi wa Mazingira juu ya utekelezaji wa Mkakati

wa Tathmini za Kimazingira.

SEHEMU YA KUMI NA MOJAUZUIAJI WA UCHAFUZI WA MAZINGIRA NA

USIMAMIZI WA TAKA

50. Viwango vya Kimazingira51. Katazo la uchafuzi52. Katazo la kutupa kwenye eneo la bahari53. Usimamizi wa Taka na Maji Machafu54. Katazo la kuharibu au kutupa bidhaa zisizofaa kwa matumizi55. Ufuatiliaji na ukaguzi56. Taka za hatari57. Vitu vya hatari58. Taka za hospitali59. Utafutaji, Uchimbaji au usafishaji wa mafuta au gesi60. Umwagikaji wa mafuta au uvujaji wa gesi

SEHEMU YA KUMI NA MBILIUHIFADHI WA BIOANUWAI NA USIMAMIZI

WA VYANZO VYA MAJI

61. Kutangazwa maeneo ya hifadhi62. Usimamizi wa maeneo ya hifadhi63. Miongozo ya uhifadhi wa bioanuwai64. Katazo la bioanuwai65. Usimamizi wa vyanzo vya maji

SEHEMU YA KUMI NA TATUUSIMAMIZI WA MABADILIKO YA TABIANCHI

66. Taasisi dhamana ya kusimamia mabadiliko ya tabianchi67. Uanzishaji wa kamati za Mabadiliko ya Tabianchi

SEHEMU YA KUMI NA NNEVIFUNGU VYA FEDHA

68. Uanzishaji wa Mfuko wa Mazingira69. Matumizi ya fedha za Mfuko

72. Makosa yanayohukumiwa nje ya mahakama73. Makosa yanayohusiana na kurudia au kuendelea kutenda kosa74. Makosa yanayohusiana na jaribio la kutenda kosa75. Adhabu za Jumla76. Vifungu vya ujumla vinavyohusiana na adhabu

SEHEMU YA KUMI NA SITAMASHARTI MENGINEYO

77. Uteuzi wa afisa mazingira na afisa mwenye mamlaka78. Kinga79. Mwendesha Mashtaka wa Mazingira80. Uwezo wa Waziri wa kuzuia81. Uwezo wa kutunga Kanuni82. Kufuta na kuhifadhi

MSWADA WA SHERIA YA USIMAMIZI WA MAZINGIRAZANZIBAR, 2015

MSWADA

WA

SHERIA YA KUFUTA SHERIA YA USIMAMIZI WAMAZINGIRA KWA AJILI YA MAENDELEO ENDELEVU

NAMBA 2 YA MWAKA 1996 NA KUWEKA BADALAYAKE MASHARTI BORA YA KUHIFADHI, KULINDA

NA KUSIMAMIA MAZINGIRA ZANZIBAR NA MAMBOMENGINE YANAYOHUSIANA NA HAYO

_____________________________

IMETUNGWA NA BARAZA LA WAWAKILISHI LAZANZIBAR

SEHEMU YA KWANZA UTANGULIZI

1. Sheria hii itajuilikana kama Sheria ya Usimamizi wa MazingiraZanzibar, 2015 na itaanza kutumika mara baada ya kusainiwa na Rais.

2. Katika Sheria hii, isipokuwa kama maelezo yatahitaji vyenginevyo:-

“Afisa mwenye mamlaka” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwakwa mujibu wa kifungu cha 82 cha Sheria hii;

“Bidhaa zisizofaa” maana yake ni bidhaa zilizotajwa kwa mujibu waSheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Zanzibar Namba 2 yamwaka 2006 au sheria nyengine yoyote ambazo zinatakiwakuharibiwa au kuangamizwa;

Jina fupi nakuanzakutumika

Ufafanuzi

“Bioanuwai” maana yake ni viumbe hai vyote ikijumuisha miti,wanyama, ndege na viumbe hai wengine wasionekana kwa machowanaopatikana kwenye mazingira ya nchi kavu na majini;

“Bodi” maana yake ni Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa MazingiraZanzibar iliyoanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 15 cha Sheriahii;

“Eneo la Hifadhi” maana yake ni eneo lolote lililotangazwa kwamujibu wa kifungu cha 61 cha Sheria hii au sheria nyengine yoyoteinayotumika;

“Fungu” maana yake ni chungu au mkusanyiko wa mchanga uliopobaharini ambao hufunikwa wakati wa maji kujaa na huwa waziwakati maji yanapokupwa;

“Kichafuzi” maana yake ni kitu chochote ambacho kikiingia aukuingizwa kwenye mazingira kitasababisha uchafuzi;

“Kumwaga” maana yake ni kutoa, kuvujisha au kutiririsha majimachafu, mafuta, moshi au hewa;

“Maliasili Zisizorejesheka” maana yake ni rasilimali ambazo hazinauhai na haziwezi kujirejesha zinapochukuliwa au kutumika ikiwani pamoja na mchanga, udongo, mawe, kifusi, kokoto, jasi, tofalila jiwe au kitu chengine chochote cha mfano wa hayo;

“Mamlaka ya Serikali za Mitaa” maana ni Jiji, Manispaa, Baraza laMji au Halmashauri ya Wilaya;

“Mamlaka” maana yake ni Mamlaka ya Usimamizi wa MazingiraZanzibar iliyoanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheriahii;

“Mazingira” maana yake ni mambo yote yanayomzunguukabinadamu ikiwa ni pamoja na hewa, ardhi, maji na kila kitukilichomo ndani yake, chenye uhai na kisichokuwa na uhai namaingiliano na mahusiano ya vitu hivyo na mazingira yao pamojana mahusiano na maingiliano ya vitu hivyo na binaadamu;

“Mfumo Ikolojia” maana yake ni eneo lenye mfumo mmoja wakimazingira ambalo ndani yake vimo viumbe vyenye uhai na visivyouhai vinavyotegemeana pamoja na mazingira yao;

“Mkakati wa Tathmini za Kimazingira” maana yake ni utaratibuunaofanywa kwa ajili ya kuwezesha sera, mipango au programuinayoandaliwa kuzingatia masuala ya kimazingira na kijamii katikautayarishaji na utekelezaji;

“Mkurugenzi Mkuu” maana yake ni Afisa wa Serikali aliyeteuliwakwa mujibu wa kifungu cha 21 cha Sheria hii;

“Mkurugenzi wa Mazingira” maana yake ni Afisa wa Serikalialiyeteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha Sheria hii;

“Mtu” inajumuisha mtu mwenyewe, kikundi cha watu, jamii, taasisiya Serikali, taasisi binafsi, shirika, kampuni kiwanda au jumuiya;

“Rais” maana yake ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi;

“Sheria” maana yake ni Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar,2015;

“Shughuli” maana yake ni kazi yoyote inayohusiana na maendeleo,ujenzi, miradi, mipango, viwanda au uwekezaji ambao utafanywakatika sehemu yoyote ya mazingira;

“Taka za hatari” maana yake ni uchafu wa aina yoyote utakaokuwakatika hali ya taka ngumu, maji maji, hewa au tope ambao nisumu, unaweza kuchubua, kuripuka, kuwaka moto, una mionzihatari au ni tishio kwa binaadamu, viumbe hai au mazingira;

“Taka za Hospitali” maana yake ni uchafu unaotokana na shughulizote zinazoambatana na matibabu ikiwa ni pamoja na sindano,chupa za dawa, bendeji, viungo vya binaadamu, damu, mabakiya dawa, au vifaa vya matibabu vyenye mionzi ya hatari;

“Tathmini ya Athari za Kimazingira” maana yake ni utaratibu wakutambua na kuainisha athari za kimazingira na kijamii zinazoweza

kujitokeza katika kuanzisha au kuendesha shughuli na kuelekezahatua zinazofaa kuchukuliwa za kuondoa athari;

“Uchafuzi” maana yake ni kuingia kichafuzi kwenye mazingira kwakiwango mbacho kinaweza kuathiri mfumo wa ikolojia, bioanuwaiau kusababisha mabadiliko mabaya ya mazingira;

“Ufuatiliaji wa Kimazingira” maana yake ni kuangalia hali halisi ilivyoya kimazingira kwenye shughuli inayotekelezwa ili kuona ni kwakiasi gani shughuli hiyo inazingatia uhifadhi wa mazingira;

“Uharibifu wa mazingira” maana yake ni mabadiliko yanayopelekeakuharibika kwa mfumo wa ikolojia kunakopelekea kupotea aukupungua maliasili na bioanuwai;

“Ukaguzi wa Kimazingira” maana yake ni tathmini inayofanywa kwamuda maalum kwa lengo la kuangalia ni kwa kiasi gani programu,miradi au shughuli zinazingatia miongozo ya kimazingira sambambana kuelekeza hatua zinazofaa kuchukuliwa;

“Ukanda maalumu wa pwani” maana yake ni eneo la masafa kati yamita thalatheni hadi mita mia moja kuelekea ardhini linalopimwakuanzia alama ya mwisho inayofikiwa na maji kujaa, masafa yamita thalatheni hadi mita mia moja inategemea na aina ya ukandahusika;

“Uwekezaji” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika sheria yaKulinda na Kuendeleza Uwekezaji Zanzibar Nam. 11 ya mwaka2004;

“Vyanzo vya maji” maana yake ni mtandao wa maji ya asiliunaopatikana kwenye dunia ambao ni muhimu kwa matumizi yabinaadamu ukijumuisha maji ya mto, mkondo wa maji, eneo lamakinga maji, ziwa, pango la maji, au maji yaliopo chini ya ardhi;

“Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya usimamizi wamazingira Zanzibar;

SEHEMU YA PILIMAJUKUMU YA JUMLA YA KIMAZINGIRA

3. Kila mtu ana wajibu wa kulinda mazingira kwa manufaa ya vizazivilivyopo na vijavyo.

4. Kila mtu analazimika kuhakikisha kwamba mipango na shughuli zamaendeleo zinatekelezwa kwa kuzingatia usimamizi endelevu kwa mazingirabora.

5.-(1) Kila mtu ana haki ya kuwa na mazingira bora, safi na salama.

(2) Kila mtu ana wajibu wa kudumisha, kulinda na kuimarishamazingia bora, safi na salama.

(3) Kila mtu ana haki ya kutoa malalamiko kwa taasisi husika aukuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu aliyesababisha au anayetakakusababisha uharibifu au uchafuzi wa mazingira.

(4) Kila mtu ana wajibu wa kutoa taarifa kwa Mamlaka juu yampango au shughuli yoyote ambayo inaweza kusababisha uharibifu auuchafuzi wa mazingira.

(5) Mamlaka itawajibika kuzifanyia kazi taarifa zilizowasilishwa kwamujibu wa kifungu kidogo cha (4) cha kifungu hiki.

(6) Ikiwa Mamlaka itashindwa kuchukua hatua kwa mujibu wakifungu kidogo cha (5) cha kifungu hiki, mtu aliyewasilisha taarifa hizoatapeleka malalamiko yake kwenye Bodi.

6. Ili kufikia lengo la Sheria hii, kila mtu atatekeleza wajibu aliopewaachini ya Sheria hii kwa kuzingatia misingi ifuatayo:

(a) Msingi wa tahadhari za kimazingira;

(b) Msingi wa malipo kwa uchafuzi na uharibifu wa mazingira;

(c) Msingi wa uhifadhi wa mifumo ya ikolojia;

Jukumu lakulindamazingira

Usimamizi waMazingirakatika Mipangoya Maendeleo

Haki na wajibuwa kuwa namazingira bora,safi na salama

Misingi yaUsimamizi waMazingira

(d) Msingi wa ushiriki wa jamii katika utayarishaji wa sera,mipango na shughuli za usimamizi wa mazingira;

(e) Msingi wa mahusiano ya kimataifa kwa ajili ya usimamiziwa mazingira; na

(f) Msingi wa uwajibikaji wa pamoja wenye majukumutofauti.

SEHEMU YA TATUUTAWALA NA MUUNDO WA TAASISI

7. Kunaanzishwa Kamati ya Ushauri wa Mazingira.

8. Wajumbe wa Kamati ya Ushauri wa Mazingira watakuwa ni:

(a) Katibu Mkuu wa taasisi inayohusiana na usimamizi wamazingira ambaye atakuwa mwenyekiti wa Kamati;

(b) Mkurugenzi wa Mazingira ambaye atakuwa ni Katibu waKamati;

(c) Mkurugenzi wa taasisi inayohusiana na maliasilizisizorejesheka;

(d) Mkurugenzi wa taasisi inayohusiana na mamlaka yaserikali za mitaa;

(e) Mkurugenzi wa taasisi inayohusiana Usimamizi wa Maafa;

(f) Mkurugenzi wa taasisi inayohusiana na Afya ya Jamii;

(g) Mwanasheria kutoka Afisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali;

(h) Mjumbe kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara, wenyeViwanda na Wakulima Zanzibar; na

(i) Wajumbe wengine wasiozidi wawili wanaweza kualikwaendapo Waziri ataona inafaa.

Uanzishaji waKamati yaUshauri waMazingira.

Muundo waKamati yaUshauri waMazingira.

9. Kamati ya Ushauri wa Mazingira itakuwa na kazi zifuatazo;

(a) Kumshauri Waziri juu ya utekelezaji wa majukumu nauwezo aliopewa kwa mujibu wa Sheria hii;

(b) Kushauri juu utekelezaji wa sera, mikakati na mipango yausimamizi wa mazingira;

(c) Kusuluhisha na kutatua migogoro baina ya taasisi zaserikali, taasisi binafsi au jamii kwenye masuala yakimazingira; na

(d) Kutekeleza jambo jengine lolote litakaloelekezwa naWaziri.

10.-(1) Kamati ya Ushauri wa Mazingira itakutana mara nne kwamwaka.

(2) Kamati ya ushauri wa mazingira itakuwa na taratibu zake zamikutano.

11.Waziri atakuwa na uwezo na kazi zifuatazo:

(a) Kutoa miongozo muhimu kwa ajili ya ukuzaji, ulinzi nauhifadhi wa mazingira;

(b) kutoa miongozo ya jumla ya kimazingira kwa taasisimbalimbali za serikali, binafsi na jumuiya za hiari au taasisinyingine yoyote kwa ajili ya utekelezaji wa masharti yaSheria hii;

(c) kutoa taarifa juu ya hali ya dharura ya kimazingira kwataasisi inayohusika na Usimamizi wa Maafa Zanzibar; na

(d) kufanya kazi nyengine yoyote kwa ajili ya utekelezaji borawa Sheria hii.

12.-(1) Kutakuwa na Mkurugenzi wa Mazingira ambaye atateuliwana Rais.

(2) Mtu ili aweze kuteuliwa kuwa Mkurugenzi kwa mujibu wakifungu kidogo (1) cha kifungu hiki ni lazima awe na sifa zifuatazo:

Kazi zaKamati yaUshauri waMazingira.

Mikutano naAkidi yakamati yaushauri wamazingira.

Uwezo na kaziza Waziri.

MkurugenziwaMazingira.

(a) kiwango cha elimu kisichopungua shahada ya kwanza auinayolingana nayo kutoka katika Chuo kinachotambulikana Serikali kati ya moja miongoni mwa fani zifuatazo ;

(i) fani ya usimamizi wa mazingira,

(ii) uhandisi mazingira,

(iii) ikolojia,

(iv) sayansi ya bahari,

(v) sheria ya mazingira,

(vi) sayansi ya mazingira,

(vii) mabadiliko ya tabianchi,

(viii) usimamizi wa maliasili,

(ix) maendeleo endelevu, au

(x) fani nyengine yoyote inayohusiana na usimamizi wamazingira; na

(b) Afisa Mwandamizi wa Serikali kutoka miongoni mwa fanizilizotajwa katika kifungu kidogo cha (2)(a) cha kifunguhiki.

(3) Kutakuwa na maofisa wengine kwa madhumuni ya kutekelezakazi za Afisi ya Mkurugenzi wa Mazingira.

13. Kwa madhumuni ya usimamizi wa mazingira, Mkurugenzi waMazingira atakuwa na kazi zifuatazo:

(a) kuendeleza mikakati ya kitaifa na miongozo ya usimamiziwa mazingira;

(b) kuratibu utekelezaji wa mikakati ya kitaifa na miongozoya usimamizi wa mazingira;

Kazi zaMkurugenziwa Mazingira.

(c) kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa miongozo yaMkakati wa Tathminini ya Kimazingira kwa mujibu wakifungu cha 48 cha Sheria hii;

(d) kupendekeza viwango vya kimazingira;

(e) kuratibu utekelezaji wa mikataba ya kimataifa yakimazingira;

(f) Kuandaa na kutoa ripoti ya hali halisi ya kimazingira kwaZanzibar na kuwasilishwa kwa Waziri katika kila kipindicha miaka mitano;

(g) kuratibu utekelezaji wa Sera ya Mazingira;

(h) kuratibu masuala ya mabadiliko ya tabianchi ikiwa nipamoja na shughuli za kuhimili na kukabiliana na athari zamabadiliko hayo;

(i) kuendeleza utoaji wa elimu ya mazingira kwa jamii nawadau wengine kwa mujibu wa majukumu yake;

(j) kuratibu na kushajihisha utafiti wa kimazingira; na

(k) kutekeleza kazi nyengine yoyote katika kufanikishautekelezaji wa Sheria hii.

14.-(1) Inaanzishwa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar.

(2) Jina fupi la Mamlaka litakuwa ni “ZEMA”.

(3) Mamlaka itakuwa ni Wakala wa Serikali ambayo itawajibikakwa Waziri.

15.-(1) Kutakuwa na Bodi ya Mamlaka ambayo itasimamia kazi zaMamlaka kwa mujibu wa Sheria hii.

(2) Bodi itakuwa na wajumbe wafuatao:

(a)Mwenyekiti ambaye atateuliwa na Rais;

Uanzishaji waMamlaka yaUsimamizi waMazingiraZanzibar

Muundo nauteuzi wawajumbe waBodi.

(b) Mkurugenzi Mkuu;

(c) Mkurugenzi wa Mazingira; na

(d) Wajumbe wengine wanne ambao watateuliwa na Waziri,kati ya hao wanne, mmoja wao ni kutoka taasisi binafsina wawili wawe wanawake.

(3) Mtu hatateuliliwa chini ya kifungu kidogo cha 2(a) na 2(d) chakifungu hiki isipokuwa awe na kiwango cha elimu angalau shahada yakwanza na uzoefu usiopungua miaka mitano juu ya masuala ya mazingira,sheria, utawala au maendeleo ya jamii.

16. (1) Mwenyekiti wa Bodi ambaye atakuwa Mwenyekiti kwa kipindicha miaka mine na ataweza kuteuliwa tena kwa kipindi kisichozidi kimoja.

(2) Mjumbe yeyote wa Bodi zaidi ya mjumbe anayeingia kwawadhifa wake atakuwa mjumbe kwa kipindi cha miaka mitatu na anawezakuteuliwa tena kwa kipindi chengine kisichozidi kimoja.

(3) Mjumbe yeyote wa Bodi zaidi ya mjumbe anayeingia kwawadhifa wake atasita kuwa mjumbe ikiwa:

(a) atajiuzulu kwa maandishi kwa kumuandikia Waziri;

(b) atakufa;

(c) atashindwa kutekeleza majukumu yake kutokana naugojwa wa kimwili au akili utakaothibitishwa na daktari;

(d) atapatikana na hatia ya kosa lolote la jinai;

(e) atashindwa kuzingatia majukumu ya Bodi; au

(f) atashindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila ya kutoasababu ya msingi kwa Katibu wa Bodi.

(4) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (3) cha kifungu hiki,mamlaka ya uteuzi, atamteua mjumbe mwingine kujaza nafasi iliyowazi.

17. Bodi itakuwa na kazi zifuatazo:

Muda wakutumikiaAfisi kwawajumbe.

Kazi za Bodi.

(a) Kusimamia utekelezaji wa kazi za Mamlaka ili kuhakikishamalengo ya Mamlaka yanafikiwa;

(b) kuthibitisha mipango na bajeti ya Mamlaka;

(c) kutoa muongozo kwa Mkurugenzi Mkuu juu ya masualayanayohusiana na utawala na usimamizi wa Mamlaka;

(d) kupanga na kuteuwa Wakuu wa Vitengo vya Mamlaka;na

(e) kufanya kazi nyengine yoyote itakayoonekana inafaa kwaajili ya kufikia malengo ya Mamlaka.

18.-(1) Bodi itafanyika vikao vyake angalau mara moja katika kilabaada ya miezi mitatu;

(2) Mwenyekiti anaweza kuitisha kikao maalum wakati wowoteitakapohitajika;

(3) Mwenyekiti ataongoza vikao vya Bodi na ikiwa hayupo,wajumbe wa Bodi watamteua mjumbe mmoja miongoni mwao kuongozakikao hicho;

(4) Akidi ya kikao cha Bodi itakuwa zaidi ya nusu ya wajumbewa Bodi.

19.-(1) Maamuzi yote ya Bodi yataamuliwa kwa makubaliano yapamoja, iwapo hawatakubaliana katika maamuzi hayo, jambo husikalitaamuliwa kwa wingi wa kura za zaidi ya nusu ya wajumbe waliohudhuriakatika kikao.

(2)Endapo kutakuwa na usawa wa kura, Mwenyekiti atakuwa nakura ya maamuzi.

20.-(1) Wakili wa Serikali wa Wizara inayohusika na Mazingiraatakuwa Katibu wa Bodi.

(2) Katibu wa Bodi ataweka kumbukumbu za vikao na maamuziyanayotolewa na Bodi na kufanya kazi nyengine kama itakavyoamuliwana Bodi.

Vikao vyaBodi.

Maamuzi yaBodi.

Katibu waBodi.

21.-(1) Kutakuwa na;

(a) Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ambaye atateuliwa naRais kwa kuzingatia sifa zilizotajwa kwenye kifungu kidogocha (2) cha kifungu hiki na atakuwa ndiye Afisa mtendajimkuu wa Mamlaka;

(b) Wakuu wa vitengo watakaoteuliwa na Bodi kwa mujibuwa masharti Sheria ya Utumishi wa Umma; na

(c) Maafisa na wafanyakazi wengine wa Mamlakawatakaoajiriwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria yaUtumishi wa Umma.

(2) Mtu ili aweze kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu kwa mujibuwa kifungu kidogo (1)(a) cha kifungu hiki ni lazima awe na sifa zifuatazo:

(a) kiwango cha elimu kisichopungua shahada ya kwanza auinayolingana kutoka Chuo kinachotambulika na Serikalikatika moja ya fani zifuatazo.

(i) fani ya usimamizi wa mazingira,

(ii) uhandisi mazingira,

(iii) ikolojia,

(iv) sayansi ya bahari,

(v) sheria ya mazingira,

(vi) sayansi ya mazingira,

(vii) mabadiliko ya tabianchi,

(viii) usimamizi wa maliasili,

(ix) maendeleo endelevu, au

(x) fani nyengine yoyote inayohusiana na usimamizi wamazingira; na

Uteuzi nauajiri.

(b)Afisa Mwanadamizi wa Serikali mwenye moja wapo kati ya fanizilizotajwa kwenye kifungu kidogo cha (2) (a) cha kifungu hiki.

22.-(1) Kazi za Mamlaka zitakuwa ni:

(a) kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Sheria hii;

(b) kuratibu hatua za Tathmini za Athari za Kimazingira kwashughuli au uwekezaji wowote;

(c) kuratibu ukaguzi wa kimazingira kwa shughuli au uwekezajiwowote;

(d) kufanya ufuatiliaji wa kimazingira ambao utasaidiakuendeleza usimamizi bora na uhifadhi wa mazingira;

(e) kutoa vyeti vya kimazingira, ruhusa au uthibitisho;

(f) kupokea na kuyafanyia kazi malalamiko yanayohusiana namazingira;

(g) kuendeleza utoaji wa elimu ya mazingira kwa jamii nawadau wengine kuhusiana na majukumu ya Mamlaka;

(h) kutekeleza kanuni na kuhakikisha uzingatiaji wa viwango,miongozo na amri kuhusiana na mazingira;

(i) kufuatilia bioanuwai, maliasili, mifumo ya ikolojia ya nchikavu na baharini, ukanda wa pwani, na utupaji endelevuwa taka na maji machafu;

(j) kufuatilia utekelezaji wa programu, mipango, miongozo yaulinzi na usimamizi wa mazingira;

(k) kuandaa na kuwasilisha kwa Waziri ripoti ya utekelezajikwa kila mwaka;

(l) kuendeleza usimamizi wa mfumo wa uwekaji wa taarifa zakimazingira kwa njia ya digitali;

(m) kuhamasisha upatikanaji wa fedha, kupokea michango,misaada au mikopo kutoka vyanzo vinavyofahamika; na

(n) kutekeleza kazi nyengine yoyote katika kufanikishautekelezaji wa Sheria hii.

Kazi zaMamlaka

23. Mamlaka itakuwa na uwezo wa:

(a) kutoa maelekezo ya hatua zinazofaa kuchukuliwa kwa ajiliya usimamizi bora wa mazingira;

(b) kutoa amri ya kusitisha shughuli yoyote kwa mtu yeyoteanayekwenda kinyume na masharti ya Sheria hii;

(c) kutoa amri ya kufungwa shughuli yeyote inayofanywa kwakukiuka masharti ya Sheria hii;

(d) kuweka na kutoza ada na malipo kwa utowaji vyeti,vibali au ruhusa za huduma za kimazingira zitakazotolewana Mamlaka;

(e) Kubadilisha, kusimamisha au kufuta cheti, vibali au ruhusaya kimazigira iliyotolewa kwa mujibu wa Sheria hii;

(f) Kuingia katika mikataba na mtu yeyote kwa ajili ya kutimizamajukumu ya Mamlaka;

(g) kutafuta taarifa za kimazingira kwa mtu yeyoteitakapohitajika;

(h) kuzuai mali yoyote iliyonekana inahusika na uvunjwaji washarti lolote la Sheria hii; na

(i) kumkamata mtu yoyote atakaebainika amevunja shartilolote la Sheria hii.

(2) Waziri anaweza kutunga kanuni juu ya mambo yanayohusianana kifungu hiki.

SEHEMU YA NNETAHADHARI YA KIMAZINGIRA

24.-(1) Ikitokea tukio la dharura la kimazingira kwa sababu zakimaumbile au kibinaadamu, Waziri anaweza kutoa taarifa kwa taasisiinasimamia mambo ya Maafa juu ya hali ya dharura ya kimazingira;

Uwezo waMamlaka

Tahadhari yakimazingira.

(2) Endapo itathibitika kwamba dharura ya kimazingiraimesababisha uchafuzi kwa makusudi au kwa ajali, aliyesababisha uchafuzihuo:

(a) atawajibika kwa uharibifu wowote utakaotokea;

(b) atawajibika kulipa fidia kwa watu walioathirika na uchafuzihuo; na

(c) atawajibika kulipa gharama zote za kurejesha eneo.

(3) Mtu yeyote ambaye atakwenda kinyume na masharti ya kifungukidogo cha (2) cha kifungu hiki ametenda kosa na akipatikana na hatiaatatozwa faini isiyopungua Shilingi Milioni kumi na isiyozidi milioni mia mojaau kifungo kwa muda usiopungua miaka mitano na isiyozidi miaka mitanona isiyozidi miaka kumi na tano au adhabu zote mbili kwa pamoja.

(4) Pamoja na adhabu itakayotolewa kwa mujibu wa kifungu hiki,Mahkama itaamuru malipo ya fidia na gharama za kurejesha eneolililoharibiwa zitakazotolewa na Mamlaka ambazo zitalipwa na mtualiyesababisha uchafuzi.

SEHEMU YA TANOKITENGO CHA MAZINGIRA NA MABADILIKO

YA TABIANCHI

25.-(1) Kunaanzishwa Kitengo kitakachohusiana na Mazingira naMabadiliko ya Tabianchi katika kila Wizara na Mamlaka ya Serikali zaMitaa.

(2) Kila kitengo cha Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi;

(a) kitakuwa na wataalamu wasiopungua wawili wenye fanitofauti au uzoefu unaohusiana na mazingira na mabadilikoya tabianchi;

(b) kitakuwa na bajeti ya uendeshaji kutoka Wizara auMamlaka ya Serikali za Mitaa husika; na

(c) kitakuwepo na kitaratibiwa katika Idara inayohusika naMipango ya Wizara au Mamlaka ya Serikali za Mitaahusika.

Uanzishaji waKitengo chaMazingira naMabadilikoya Tabianchi.

26. Kitengo cha Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi kitakuwa nakazi zifuatazo:

(a) kuratibu masuala yote ya mazingira na mabadiliko yatabianchi ndani ya Wizara au Mamlaka ya Serikali zaMitaa husika;

(b) kuzingatia na kuingiza masuala ya mazingira na mabadilikoya tabianchi katika sera, mipango, program, miradi nashughuli za taasisi husika; na

(c) kutayarisha na kuwasilisha ripoti ya nusu mwaka yamazingira na mabadiliko ya tabianchi ya sekta husika kwaIdara ya mipango ya Wizara au Mamlaka ya Serikali zaMitaa husika;

SEHEMU YA SITAUSIMAMIZI WENYE UWIANO WA UKANDA WA PWANI

27.-(1) Eneo lote la mipaka ya Zanzibar kama lilivyoelezwa kwenyeKatiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, litakuwa ni eneo la ukanda wapwani la Zanzibar.

(2) Kamati ya Mabadiliko ya tabianchi ziliyoanzishwa chini yakifungu cha 67 cha Sheria hii zitashughulikia Eneo la Ukanda wa Pwani.

(3)Waziri anaweza kutunga kanuni zinazohusiana na usimamiziwenye uwiyano wa ukanda wa pwani.

28.-(1) Kunaanzishwa Ukanda maalumu wa Pwani wa Zanzibar.

(2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kufanya shughuli yoyote katikaeneo la ukanda maalum wa pwani bila ya ruhusa ya Mamlaka.

(3) Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifungukidogo cha (2) cha kifungu hiki ametenda kosa na akipatikana na hatiaatatozwa faini isiyopungua Shilingi milioni tano na isiyozidi Shilingi milionikumi au kifungo kwa muda usiopungua miaka miwili na usiozidi miakaminne au adhabu zote mbili kwa pamoja.

Kazi zaKitengo chaMazingira naMabadiliko yaTabianchi.

Eneo la Ukandawa Pwani laZanzibar.

Uanzishaji waUkandamaalumu waPwani.

SEHEMU YA SABAUSIMAMIZI WA MALIASILI ZISIZOREJESHEKA

29.-(1) Mkuu wa Wilaya husika ambayo maombi ya uchimbaji wamaliasili zisizorejesheka yamefanywa, ataanzisha kamati ya pamoja yausimamizi wa maliasili zisizorejesheka.

(2) Wajumbe wa Kamati iliyoanzishwa kwa mujibu wa kifungukidogo cha (1) cha kifungu hiki watakutana kila kutakapokuwa na ombi lauchimbaji wa maliasili zisizorejesheka kwa taasisi inayohusika na maliasilizisizorejesheka kwa utaratibu utakaowekwa na taasisi hiyo.

30. Kamati ya pamoja ya usimamizi wa maliasili zisizorejesheka itakuwana wajumbe wafuatao:

(a) Mkuu wa Wilaya ambayo ombi la uchimbaji wa maliasilizisizorejesheka limefanywa ambae atakuwa mwenyekiti;

(b) Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka;

(c) Mkurugenzi anayehusika na masuala ya Ardhi na Usajili;

(d) Mkurugenzi anayehusika na masuala ya Mipango Miji naVijiji;

(e) Mkurugenzi anayehusika na masuala ya Maliasilizisizorejesheka ambaye atakuwa Katibu wa Kamati;

(f) Mkurugenzi anayehusika na masuala ya Nishati;

(g) Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ambako ombi lauchimbaji wa maliasili zisizorejesheka limewasilishwa;na

(h) Mjumbe mwengine yoyote kutoka taasisi nyengine yoyoteatakayeonekana anafaa.

31. Kamati ya pamoja ya usimamizi wa maliasili zisizorejesheka itakuwana kazi zifuatazo:

(a) Kujadili maombi na kufanya ukaguzi wa maeneo ya uchimbaji wa maliasilizisizorejesheka katika Wilaya husika;

Uanzishaji wakamati yapamoja yausimamizi wamaliasilizisizorejesheka.

Muundo waKamati yapamoja yausimamizi wamaliasilizisizorejesheka.

Kazi zaKamati yapamoja yausimamizi wamaliasilizisizorejesheka.

(b) Kuishauri taasisi inayosimamia maliasili zisizorejehseka juuya maombi ya uchimbaji wa maliasili zisizorejesheka;

(c) Kuchunguza na kupendekeza maeneo ya uchimbaji wamaliasili zisizorejesheka;

(d) Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa maeneoyaliyoruhusiwa kuchimbwa maliasili zisizorejesheka; na

(e) Kufanya mapitio ya malipo ya ada kwa ajili ya uchimbajina usafirisahaji wa maliasili zisizorejesheka.

32.-(1) Akidi ya vikao vya kamati ya pamoja ya maliasili zisizorejeshekaitakuwa nusu ya wajumbe wa kamati.

(2) Katibu wa kamati ya pamoja ya maliasili zisizorejeshekaataweka kumbukumbu za vikao vya kamati.

33.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba, kuondosha, kusafirishaau kuuza maliasili zisizorejesheka bila ya kibali kutoka taasisi inayosimamiamaliasili zisizorejesheka.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1) cha kifunguhiki, kibali kwa ajili ya uchimbaji wa maliasili zisizorejesheka kitatolewabaada ya kusainiwa mkataba wa kuendeleza eneo liliochimbwautakaotolewa na taasisi inayosimamia maliasili zisizorejesheka.

(3) Mtu atakayepewa kibali kwa ajili ya uchimbaji wa maliasilizisizorejesheka ataweka dhamana ya kimazingira kwa taasisi inayosimamiamaliasili zisizorejesheka kwa kuzingatia yafuatayo:

(a) ukubwa wa eneo litakalochimbwa;

(b) athari zitakazojitokeza; na

(c) gharama za hatua za uendelezaji.

(4) Waziri anaweza kutunga kanuni kwa ajili ya usimamizi wamaliasili zisizorejesheka.

Akidi yavikao vyakamati yapamoja yausimamizi wamaliasili

zisizorejesheka.

Kibali chaMaliasilizisizorejesheka.

34.-(1) Mtu aliyepewa kibali cha uchimbaji wa maliasili zisizorejeshekaatakuwa na jukumu la kuendeleza eneo lililochimbwa.

(2) Taasisi inayosimamia maliasili zisizorejesheka itakuwa na jukumula kuhakikisha kuwa eneo lililochimbwa linaendelezwa ipasavyo.

(3) Endapo eneo lililochimbwa litaendelezwa ipasavyo, mtu alietoadhamana ya kimazingira atarudishiwa fedha zake alizoweka dhamana kwaajili ya kuliendeleza eneo hilo.

(4) Endapo fedha zilizowekwa dhamana kwa ajili ya kuendelezaeneo lililochimbwa hazikutosha kwa kazi hiyo, mtu aliyepewa kibali chauchimbaji wa maliasili zisizorejesheka atalazimika kulipa ziada ya fedhakatika taasisi inayosimamia maliasili zisizorejesheka kwa ajili yakuendelezwa eneo hilo.

(5) Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifungukidogo cha (1) au (4) cha kifungu hiki ametenda kosa na akipatikana nahatia atatozwa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioniishirini au kifungo kwa muda usiopungua miezi sita na usiozidi miaka mitanoau adhabu zote mbili kwa pamoja.

35. Taasisi inayohusiana na maliasili zisizorejesheka itaweka kumbukumbuzote zinazohusiana na usimamizi wa maliasili hizo pamoja na kuwasilishakumbukumbu hizo kwa Mkurugenzi wa Mazingira kila baada ya mwezimitatu.

36.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba, kukusanya, kuondoa,kusafirisha au kuuza mchanga kutoka kwenye ufukwe au fungu la mchangakwa madhumuni ya kibiazhara au matumizi mengine yanayolingana na hayo.

(2) Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifunguhiki atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa fainiisiyopungua shilingi milioni mbili na isiyozidi shilingi milioni ishirini au kifungokwa muda usiopungua mwaka mmoja na usiozidi miaka mitano au adhabuzote mbili kwa pamoja.

Jukumu lakuendelezaeneolililochimbwa.

Kumbukumbuza maliasilizisizorejesheja.

Katazo lamchanga waufukwe nafungu.

SEHEMU YA NANEELIMU YA MAZINGIRA NA UTAFITI

37.-(1) Kila mtu ana haki ya kupata taarifa za kimazingira.

(2) Haki ya kupata taarifa za kimazingira kwa mujibu wa kifungukidogo cha (1) cha kifungu hiki inaweza kukataliwa ikiwa taarifazinazohitajika:

(a) hazipo katika kumbukumbu rasmi za taasisi;

(b) zipo chini ya usalama wa Taifa au maslahi ya umma; au

(c) zipo chini ya hifadhi ya siri za kibiashara na viwanda.

(3) Mkurugenzi wa Mazingira au Mkurugenzi Mkuu wa Mamlakaatakuwa na haki ya kupata taarifa yoyote ya mazingira kutoka kwa mtuyeyote ambazo zinazohusiana na utekelezaji wa Sheria hii.

38.-(1) Mkurugenzi wa Mazingira ataendeleza utafiti wa kimazingirautakaosaidia usimamizi na uhifadhi bora wa mazingira.

(2) Mkurugenzi wa Mazingira atahifadhi na kutumia matokeo yautafiti wa kimazingira kwa madhumuni ya utekelezaji wa Sheria hii.

SEHEMU YA TISATATHMINI YA ATHARI ZA KIMAZINGIRA NA KIJAMII

39.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kufanya shughuli yoyote ambayoitakuwa na athari kubwa kwa mazingira na jamii bila ya cheti cha Tathminiya Athari za Kimazingira kilichotolewa na Mamlaka kwa mujibu wa Sheriahii.

(2) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki, Tathminiya Athari za Kimazingira itafanywa kwenye hatua za mwanzo za mradikabla haujaanza.

(3)Waziri anaweza kutengeneza Kanuni kwa ajili ya kuwekautaratibu wa Tathmini ya Athari za Kimazingira.

(4)Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifunguhiki ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingimilioni kumi na isiyozidi shilingi milioni ishirini au kifungo kwa muda

Upatikanajiwa taarifa zaKimazingira.

Utafiti waKimazingira.

Mahitaji yaTathmini yaAthari zaKimazingira.

usiopungua miaka mitano na usiozidi miaka kumi au adhabu zote mbilikwa pamoja.

(5) Pamoja na adhabu itakayotolewa kwa mujibu wa kifungu hiki,Mahakama itaamuru mtenda kosa kulipa fidia kwa muathirika na gharamanyengine zinahusiana na uendelezaji wa mazingira yaliyoathirika ambazozitalipwa kwa Mamlaka.

40. Kwa madhumuni ya kifungu hiki, shughuli ambayo inaelekeakuwa na athari kubwa kwa mazingira na itahitaji kufanyiwa tathmini yaathari za kimazingira kama shughuli yenyewe itakuwa auimechanganyika na shughuli nyengine za aina moja au eneo moja:

(a) zinazotumia kiasi kikubwa cha rasilimali zilizo na uhai auzisizo na uhai;

(b) zinazopelekea uzalishaji wa taka ambazo zitakuwa kwakiwango kikubwa au zenye asili ya hatari;

(c) zinazopelekea kubadilisha mazingira kwa kiwangokikubwa;

(d) zinazopelekea watu kuhama katika makaazi yao aukuacha kazi zao za kimaisha;

(e) zinazopelekea kuathiri maeneo muhimu ya kimazingira;au

(f) zitakazo kuwa na sifa nyengine kama zitakavyoainishwachini ya Sheria hii.

41.-(1) Tathmini ya Athari za Kimazingira itafanywa na wataalamu aukampuni ambayo sifa zake zitaelezwa katika Kanuni zitakazotungwa kwamujibu wa Sheria hii.

(2) Mamlaka itaweka kumbukumbu za wataalamu au kampunizilizoruhusika kufanya Tathmini ya Athari za Kimazingira Zanzibar.

(3) Mmiliki wa mradi atachagua wataalamu miongoni mwawataalamu au kampuni zenye sifa zilizoelezwa katika Kanuni kwa ajili yakufanya Tathmini ya Athari za Kimazingira.

Vigezo vyakuzingatiashughulizinazohitajikufanyiwatathmini yaathari zakimazingira.

Utambuzi wakampuni nawataalamu wakufanyaTathmini yaAthari zaKimazingira.

(4) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (1) na (2) chakifungu hiki, Mamlaka itatoa leseni kwa wataalamu au kampuni za kufanyaTathmini ya athari za kimazingira au ukaguzi wa kimazingira ambayo italipiwaada ya kila mwaka kama itakavyoainishwa katika Kanuni zitakazotungwakwa mujibu wa Sheria hii.

42.-(1) Mamlaka inaweza kusikiliza maoni ya jamii yanayohusiana naripoti ya tathmini ya athari za kimazingira.(2) Mamlaka itaweka taratibu zakusikiliza maoni ya jamii.

43.-(1) Mamlaka, kwa kushirikiana na wadau husika, itafanya ufuatiliajiwa mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba masharti yaliyotolewa pamojana Cheti cha Tathmini ya Athari za Kizamingira yanatekelezwa.

(2) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (1) cha kifunguhiki, endapo ufuatiliaji utaonesha ukiukwaji wa sharti lolote lililotolewapamoja na Cheti cha Tathmini ya Athari za Kimazingira, mmiliki wa chetiatachukua hatua zitakazotolewa na Mamlaka.

(3) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1) cha kifunguhiki, Mamlaka itafanya ufuatiliaji wa kimazingira wa mara kwa mara.

(4) Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifungukidogo cha (2) cha kifungu hiki ametenda kosa na akipatikana na hatiaatatozwa faini isiyopungua shilingi milioni tano na isiyozidi shilingi milioniishirini au kifungo kwa muda usiopungua miaka miwili na usiozidi miakakumi au adhabu zote mbili kwa pamoja.

44. Mmiliki wa cheti cha Tathmini ya Athari za Kimazingira atatoataarifa yoyote itakayohitajika na Mamlaka kwa madhumuni ya kuhakikishautekelezaji wa masharti yaliotolewa pamoja na Cheti cha Tathmini ya Athariya Kimazingira.

45.-(1) Mtu yoyote atakayefanya shughuli yoyote ambayo kwa mujibuwa Sheria hii itaonekana haihitaji kufanyiwa Tathmini ya Athari zaKimazingira atatayarisha Ripoti ya Mazingira kama itakavyoelekezwa katikaKanuni itakayotungwa kwa mujibu wa kifungu cha 39(3) cha Sheria hii.

(2) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (1) cha kifunguhiki, Mamlaka endapo itaridhishwa na Ripoti ya Kimazingira, itatoa Cheticha Kimazingira kwa ajili ya shughuli inayohitaji kutekelezwa.

Kusikilizamaoni yaJamii.

Ufuatiliaji.

Taarifazinazohitajika.

Ripoti yaKimazingira.

(3) Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifungukidogo cha (1) cha kifungu hiki ametenda kosa na akipatikana na hatiaatatozwa faini isiyopungua shilingi milioni mbili na isiyozidi shilingi milionitano au kifungo kwa muda usiopungua mwaka mmoja na usiozidi miakatano au adhabu zote mbili kwa pamoja.

46.-(1) Ukaguzi wa Kimazingira utafanywa kwenye shughuli kwakuzingatia vigezo vifuatavyo:

(a) shughuli ambayo inafanyika bila ya kuwa na Cheti chaTathmini ya Athari za Kimazingira na inaelekea kuwa naathari kubwa kwa mazingira na jamii; au

(b) shughuli ambayo itakuwa na Cheti cha Tathmini ya Athariza Kimazingira na utekelezaji wake umefikia miaka mitano.

(2)Bila ya kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1)(b) chakifungu hiki, ukaguzi wa kimazingira unaweza kufanywa kwa shughuli yeyoteitakayoamuliwa na Mamlaka kupitia ufuatiliaji wa mara kwa mara.

(3)Ukaguzi wa Kimazingira utafanywa na mtaalamu au kampuniitakayotambuliwa kwa mujibu wa Sheria hii.

(4)Kwa kuzingatia kifungu cha 39(3) cha Sheria hii, utaratibuutakaotumika kufanya Tathmini ya Athari za Kimazingira pia utatumikakwa ajili ya Ukaguzi wa Kimazingira.

(5)Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifunguhiki ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopunguashilingi milioni kumi na isiyozidi shilingi milioni ishirini au kifungo kwa mudausiopungua miaka mitano na usiozidi miaka kumi au adhabu zote mbilikwa pamoja.

47. Mmiliki wa mradi atahusika na gharama za:-

(a) utaratibu wa kufanya Tathmini ya Athari za Kimazingira;

(b) utaratibu wa kufanya ukaguzi wa kimazingira;

(c) utaratibu wa kuandaa ripoti ya kimazingira;

Ukaguzi waKimazingira.

Mgharamikaji.

(d) utekelezaji wa mpango wa usimamizi wa kimazingira na

kijamii;

(e) ufuatiliaji wa utekelezaji wa mpango wa usimamizi wa

kimazingira na kijamii; na

(f) gharama nyengine zozote zitakazohitajika.

SEHEMU YA KUMIMKAKATI WA TATHMINI ZA KIMAZINGIRA

48. Mkakati wa Tathmini za Kimazingira utatayarishwa kwa ajili yautekelezaji wa sera, mkakati na programu za maendeleo na kiuchumi pamojana utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi kwa ajili ya:-

(a)kuimarisha mazingira;

(b)kulinda afya ya binaadamu;

(c)matumizi bora na endelevu ya maliasili; na

(d)kuimarisha misingi ya tahadhari ya usimamizi wa mazingira.

49.-(1) Wajibu wa Mkurugenzi wa Mazingira katika utayarishaji waMkakati wa Tathmini za Kimazingira utakuwa ni:

(a) kutayarisha miongozo kwa ajili ya kutengeneza Mkakatiwa Tathmini za Kimazingira;

(b) kuainisha na kuhusisha wahusika wakuu wote katikangazi mbalimbali;

(c) kuimarisha mawasiliano yaliopo, utoaji wa taarifa, naelimu ili kukidhi mipango ya sekta zote, sera, mikakati,na programu pamoja na sekta ya mafuta na gesi; na

(d) kukuza ushirikiano wa ndani, kikanda na kimataifapamoja na masuala ya tathmini ya athari za kimazingirakatika sekta zote kama Mkurugenzi wa Mazingiraatakavyoona inafaa.

Mkakati waTathmini zaKimazingira.

Majukumu yaMkurugenziwa Mazingirajuu yaUtekelezajiwa Mkakatiwa Tathminiza

Kimazingira.

(2) Waziri anaweza kutunga Kanuni kwa ajili ya Mkakati wa Tathminiza Kimazingira.

Katazo la kuharibu au kuangamiza bidhaa zisizofaa kwa matumizi.SEHEMU YA KUMI NA MOJA

UZUIAJI WA UCHAFUZI NA USIMAMIZI WA TAKA

50.Mkurugenzi wa Mazingira atapendekeza viwango vya kimazingirakwa Taasisi ya Viwango ya Zanzibar vinavyohusiana na kelele, maji, hewaau maji machafu ili kuimarisha ubora wa mazingira.

51.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchafua au kumruhusu mtumwingine kufanya kitendo kitakachosababisha uchafuzi wa mazingira kwakukiuka viwango vyovyote vya kimazingira vilivyoweka na sheria yoyoteinayotumika.

(2)Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifunguhiki ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopunguashilingi milioni mbili na isiyozidi shilingi milioni kumi au kifungo kwa mudausiopungua miaka miwili na usiozidi miaka mitano au adhabu zote mbilikwa pamoja.

52.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kutupa au kusababisha kutupwakwenye eneo la bahari lililo chini ya mamlaka ya Zanzibar taka za ainayoyote au kitu chengine chochote kutoka kwenye meli, boti, manuwari,ndege, helikopta au chombo chengine chochote cha baharini au cha angani.

(2)Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifunguhiki ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopunguashilingi milioni moja na isiyozidi shilingi bilioni kumi au kifungo kwa mudausiopungua mwaka mmoja na usiozidi miaka hamsini au adhabu zote mbilikwa pamoja.

(3)Itakuwa ni kinga kwa kosa lililofanywa chini ya kifungu kidogocha (1) cha kifungu hiki kama utupaji ulikuwa lazima kufanywa au kutokeakwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wa binaadamu au kwa lengo lakuokoa maisha ya watu.

Viwango vyaKimazingira.

Katazo lauchafuzi

Katazo lakutupakwenye eneola bahari.

53.(1) Kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa au Taasisi nyengine yoyoteitakayoanzishwa kushughulikia taka au maji machafu itasimamia taka aumaji machafu yatakayozalishwa ndani ya maeneo ya mamlaka husika.

(2) Kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa au Taasisi nyengine yoyoteitakayoanzishwa kusimamia taka na maji machafu, kwa mashauriano nawadau husika, itachagua eneo kwa ajili ya uhifadhi, utupaji na uangamizajiwa taka na maji machafu ambalo litaidhinishwa na Mamlaka.

(3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kutupa au kuangamiza aina yoyoteya taka au maji machafu nje ya eneo lililotengwa kwa mujibu wa Sheria hii.

(4)Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifungu hiki ametendakosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingi laki mojana isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo kwa muda usiopungua miezimitatu na usiozidi miaka miwili au adhabu zote mbili kwa pamoja.

(5)Pamoja na adhabu itakayotolewa kwa kosa lililofanyika kwamujibu wa kifungu hiki, Mahakama itaamuru mtenda kosa kulipa gharamaza urejeshaji na fidia kwa muathirika.

54.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuharibu au kuangamiza aukusababisha kuharibiwa au kuangamizwa aina yoyote ya bidhaa zisizofaakwa matumizi bila ya kibali kutoka Mamlaka.

(2) Waziri anaweza kutunga Kanuni kwa ajili ya kuharibu aukuagamiza bidhaa zisizofaa kwa matumizi.

(3)Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifunguhiki ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingimilioni tano na isiyozidi shilingi milioni mia moja au kifungo kwa mudausiopungua miaka mitatu na usiozidi miaka thelasini au adhabu zote mbilikwa pamoja.

(4)Pamoja na adhabu itakayotolewa kwa kosa lililofanyika kwamujibu wa kifungu hiki, Mahakama inaweza kuamuru bidhaa isiyofaa kwamatumizi au iliyomaliza muda kurejeshwa ilikotoka.

Usimamizi wataka na majimachafu.

Katazo lakuharibu aukuangamizabidhaazisizofaa kwamatumizi.

Ufuatiliaji na

ukaguzi55.-(1) Mamlaka itafanya ufuatiliaji na ukaguzi wa mara kwa mara

kwenye eneo lolote la jamii au binafsi wakati wowote inapohitajika kwaajili ya kutekeleza usimamizi wa mazingira.

(2) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (1 ) cha kifunguhiki, Afisa aliyepewa mamlaka atafanya ufuatiliaji na ukaguzi kwa mujibuwa taratibu na maelekezo yaliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu.

56.(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuingiza, kukusanya,kushughulikia, kuhifadhi, kusafirisha au kutupa aina yoyote ya taka za hatari.

(2) Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifunguhiki ametenda kosa na akipatikana na hatia atafungwa kwa mudausiopungua miaka kumi na usiozidi miaka thalathini.

(3)Pamoja na adhabu itakayotolewa kwa mujibu wa kifungu hiki,Mahakama itaamuru mtenda kosa kulipa fidia kwa muathirika na gharamanyengine zinahusiana na ushughulikiaji wa taka hizo au urejeshaji wamazingira yaliyoathirika kwa Mamlaka.

(4) Bila ya kupingana na masharti ya kifungu kidogo cha (1) chakifungu hiki, Mkurugenzi wa Mazingira anaweza kuweka muongozo wakushughulikia taka za hatari zitakazokuwepo Zanzibar.

57.Ni marufuku kwa mtu yeyote kushughulikia au kutupa au kumruhusumtu mwengine kushughulikia au kutupa aina yoyote ya vitu vya hatariisipokuwa kwa mujibu wa Kanuni zilizotungwa chini ya Sheria hii.

(2) waziri anaweza kutunga kanuni zinazohusiana na masharti yakifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki.

(3) Mtu yeyote atakaekwenda kinyume na masharti ya kifunguhiki ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopunguashilingi milioni tano na isiyozidi shilingi milioni thelathini au kifungo kwamuda usiopungua miaka miwili au usiozidi miaka kumi au adhabu zotembili kwa pamoja.

(4) Mkurugenzi wa Mazingira anaweza kutoa miongozo na kuelezahatua za usimamizi wa vitu vya hatari.

Taka zahatari.

Vitu vyahatari.

58. Mamlaka ya Serikali za Mitaa au Taasisi nyengine inayohusika nataka, kwa kushirikiana na Wizara inayohusika na Afya, itahakikishakwamba aina zote za taka za hospitali zinakusanywa, zinahifadhiwa,zinasafirishwa na zinateketezwa kwa utaratibu unaofaa utakaothibitishwana Mamlaka.

59.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kutafuta, kuchimba, kusafisha aukuhifadhi kwa ajili ya biashara, mafuta au gesi bila ya cheti cha tathmini yaathari za kimazingira.

(2) Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifunguhiki atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa fainiisiyopungua shilingi milioni hamsini na isiyozidi shilingi milioni mia moja aukifungo kwa kipindi kisichopungua miaka ishirini na tano na kisichozidimiaka hamsini au adhabu zote mbili kwa pamoja.

(3)Pamoja na adhabu itakayotolewa kwa mujibu wa kifungu hiki,Mahakama itaamuru mtenda kosa kulipa fidia kwa muathirika na gharamanyengine zinahusiana na urejeshaji wa mazingira yaliyoathirika ambazozitalipwa kwa Mamlaka.

60.-(1) Kila mmiliki wa kituo atalazimika:

(a) kuchukua hatua za kuzuia umwagikaji au uvujaji wa mafutaau gesi; na

(b) kuwa na mpango wa dharura wa kuondoa, kurejesha aukupunguza madhara ya umwagikaji mafuta au uvujaji wagesi.

(2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kumwaga au kusababishakumwagwa aina yoyote ya mafuta au mchanganyiko wowote wenye mafutabila ya kibali kutoka kwa Mamlaka.

(3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, neno “kituo” maana yake nikiwanda, sehemu ya kuchimba au kusafishia mafuta au gesi; chombo chabaharini, sehemu ya kushushia na kuhifadhia mafuta, gari la kuchukulia nakusafirishia mafuta, gereji, sehemu ya kuhifadhia na kuuuzia mafuta, ghalala kuhifadhia gesi; duka la kuuzia gesi au sehemu au kifaa chengine chochotekitakachohusika na uhifadhi au kusafirisha mafuta au gesi.

Taka zaHospitali.

Utafutaji,

uchimbaji auusafishaji wamafuta augesi.

Umwagikajiwa Mafuta auUvujaji waGesi.

(4) Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifunguhiki ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingimilioni ishirini na isiyozidi shilingi milioni thelathini au kifungo kwa kipindikisichopungua miaka saba na kisichozidi miaka kumi au adhabu zote mbilikwa pamoja.

(5) Pamoja na adhabu itakayotolewa kwa mujibu wa kifungu hiki,Mahakama itaamuru mtenda kosa kulipa fidia kwa muathirika na gharamanyengine zinahusiana na urejeshaji wa mazingira yaliyoathirika ambazozitalipwa kwa Mamlaka.

SEHEMU YA KUMI NA MBILIUHIFADHI WA BIOANUWAI NA USIMAMIZI

WA VYANZO VYA MAJI

61. Waziri anayehusika na maliasili za nchikavu au baharini, kwamashauriano na Waziri anaweza kutangaza eneo lolote la Zanzibar lenyeumuhimu wa mifumo ya ikolojia kuwa ni eneo la hifadhi.

62. Waziri atakayetangaza eneo lolote la hifadhi kwa mujibu wa kifungucha 61 cha Sheria hii atatayarisha Kanuni, na kuanda na kutekeleza mpangowa usimamizi wa eneo hilo.

63.-(1) Mkurugenzi wa Mazingira atakuwa na jukumu la kuwekamiongozo kwa ajili ya usimamizi na uhifadhi endelevu wa bioanuwai.

(2) Mkurugenzi wa Mazingira, katika kuweka miongozo kwamujibu wa kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki, anaweza:

(a) kuainisha mikakati, mipango na programu za Zanzibar kwaajili ya uhifadhi na matumizi endelevu ya bioanuwai;

(b) kuzingatia misingi ya uhifadhi na matumizi endelevu yabioanuwai;

(c) kuainisha, kutayarisha na kuendeleza ukaguzi wa mara kwamara wa bioanuwai ya Zanzibar; na

Kutangazwaeneo lahifadhi.

Usimamizi

Miongozo yauhifadhi wabioanuwai.

(d)kuainisha aina za bioanuwai ambazo ni adimu au zilizo katikatishio la kutoweka.

64.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuingiza nchini, kuuza, kununua,kumiliki, kupitisha, kupeleka nje ya nchi, kusafirisha, au kuharibu bioanuwaiau mazao yatokanayo na bioanuwai yoyote iliyoorodheshwa kimataifa kuwakatika tishio la kutoweka bila ya kibali kutoka taasisi husika.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu hiki, hairuhusiwi kwa mtuyeyote kuingiza nchini, kupitisha, kuuza, kununua, kumiliki, kupeleka njeya nchi, kusafirisha au kuharibu bioanuwai au mazao yatokanayo nabioanuwai ambazo hazikutajwa kwenye kifungu kidogo cha (1) cha kifunguhiki bila ya kibali kutoka taasisi husika.

(3) Kwa kuzingatia masharti kifungu kidogo cha (2) cha kifunguhiki, taasisi zinazohusika na usimamizi wa bioanuwai zitaweka utaratibu wakuvuna, kuuza, kununua, kumiliki, kupeleka nje ya nchi au kusafirishabioanuwai au mazao ya bioanuwai ziliopo Zanzibar.

(4) Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifunguhiki ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingilaki tano na isiyozidi Shilingi milioni thalathini au kifungo kwa mudausiopungua miezi sita na usiozidi miaka kumi au adhabu zote mbili kwapamoja.

65.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuharibu na kuchafua kwa namnayeyote vyanzo na makinga maji.

(2) Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya kifunguhiki ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingimilioni moja na isiyozidi Shilingi milioni thalathini au kifungo kwa mudausiopungua miezi sita na usiozidi miaka kumi au adhabu zote mbili kwapamoja.

SEHEMU YA KUMI NA TATUUSIMAMIZI WA MABADILIKO YA TABIANCHI

66.Wizara inayohusika na mazingira ndiyo itakuwa taasisi yenyedhamana ya kuratibu masuala yote yanayohusu Mabadiliko ya Tabianchikwa Zanzibar.

Katazo laBioanuwai.

Uhifadhi wavyanzo vyamaji.

Taasisidhamana yakusimamiaMabadilikoya Tabianchi.

67.-(1) Kwa usimamizi bora wa masuala ya Mabadiliko ya TabianchiZanzibar, zinaanzishwa Kamati za Mabadiliko ya Tabianchi zifuatazo:

(a) Kamati ya Uongozi; na

(b) Kamati ya Kitaalamu;

(2) Waziri kwa kushauriana na Mkuu wa Wilaya husika anawezakuanzisha Kamati za Mabadiliko ya Tabianchi za Wilaya na Shehia kamaitakavyoonekana inafaa.

68-(1) Kamati ya Uongozi ya Mabadiliko ya Tabianchi itakuwa nawajumbe wafuatao:

(a) Katibu Mkuu wa Wizara inayohusika na Mazingira naMabadiliko ya Tabianchi ambaye atakuwa Mwenyekiti waKamati;

(b) Katibu Mkuu wa Wizara inayohusika na Fedha;

(c) Katibu Mkuu wa Wizara inayohusika na Usimamizi waMaafa;

(d) Katibu Mkuu wa Wizara inayohusika na Kilimo naMaliasili;

(e) Katibu Mkuu wa Wizara inayohusika na Ardhi;

(f) Katibu Mkuu wa Wizara inayohusika na Uvuvi na Mifugo;

(g) Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango ya Zanzibar;

(h) Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar; na

(i) Mkurugenzi wa Mazingira, ambaye atakuwa ni Katibu waKamati.

(2) Kamati ya Uongozi ya Mabadiliko ya Tabianchi itakuwa nakazi zifuatazo:

(a) kutoa ushauri kwa Waziri wa Taasisi Kitaifa yenye dhamanawa masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi juu ya masualayote yanayohusu Mabadiliko ya Tabianchi Zanzibar;

Uanzishaji waKamati zaMabadiliko yaTabianchi.

Muundo nakazi zaKamati yaUongozi yaMabadiliko yaTabianchi.

(b) kupendekeza na kutoa muongozo wa kisera, mikakati,Mpango wa Utekelezaji wa Kitaifa wa Kujihami naMabadiliko ya Tabiachi na shughuli yoyote inayohusianana mabadiliko ya tabianchi kama itakavyoelekezwa kilabaada ya muda na Mkataba wa Umoja wa Mataifa waMabadiliko ya Tabianchi na Itifaki yake;

(c) kufanya tathmini ya utekelezaji wa sera, mikakati, mipangoya Kitaifa ya kuhimili na mipango mengine ya Mabadilikoya Tabianchi Zanzibar; na

(d) kusimamia shughuli zote zinazohusiana na Usimamizi wenyeUwiano wa Ukanda wa Pwani.

69-(1) Kamati ya Kitaalamu ya Mabadiliko ya Tabianchi itakuwa nawajumbe wafuatao:

(a) Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti wa Wizarainayohusika na Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchiambaye atakuwa ni Mwenyekiti wa Kamati;

(b) Kamishna wa Mipango ya Kitaifa, Mipango ya Kisektana Upunguzaji wa Umasikini;

(c) Mkurugezi wa Usimamizi wa Maafa;

(d) Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uvuvi;

(e) Kamishna wa Fedha za Nje;

(f) Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mifugo;

(g) Mkurugezi wa Misitu na Maliasili Zisizorejesheka;

(h) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania,Kanda ya Zanzibar;

(i) Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Baharini;

(j) Mwakilishi wa Jumuiya Isiyokuwa za Kiserikali inahusianana mazingira; na

(k) Mkurugenzi wa Mazingira ambaye atakuwa ni Katibu waKamati.

Muundo nakazi zaKamati yaKitaalamu yaMabadiliko yaTabianchi.

(2) Kamati ya Kitaalamu ya Mabadiliko ya Tabianchi itakuwa nakazi zifuatazo:

(a) kutoa msaada wa kitaalamu kwa Kamati ya Uongozi yamabadiliko ya Tabianchi juu ya masuala yote yanayohusianana Usimamizi wenye Uwiano wa Ukanda wa Pwani naMabadiliko ya Tabianchi Zanzibar;

(b) kutayarisha Sera na Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchiwa Zanzibar;

(c) kutayarisha Mpango wa Utekelezaji wa Kitaifa waKujihami na Mabadiliko ya Tabiachi na nyaraka nyenginezinazohusiana na Mabadiliko hayo; na

(d) kufuatilia, kufanya tathmini ya mwenendo wa mabadilikoya hali ya hewa na mabadiliko ya Tabianchi na athari zakekwa jamii, uchui na mazingira, na kutoa muongozo kwaajili ya hatua zinazofaa za kujihami na kupunguza athari zamabadiliko ya tabianchi.

(3) Waziri anaweza kutayarisha Kanuni za usimamizi wamabadiliko ya tabianchi pamoja na mambo yanayohusianana kamati zilizoanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 67cha Sheria hii.

SEHEMU YA KUMI NA NNEVIFUNGU VYA FEDHA

70. Mamlaka itakuwa na Voti yake kwa fedha zote zitakapitishwa naBaraza la Wawakilishi na fedha nyengine kutoka vyanzo vyengine vya fedha.

71-(1) Fedha za Mamlaka zitasimamiwa na Mkurugezi Mkuu baadaya kuthibitishwa na Bodi na kupitishwa na Baraza la Wawakilishi.

(2) Fedha na mapato ya Mamlaka yatatokana na:

(a)bajeti itakayopitishwa na Baraza la Wawakilishi;

Fedha zaMamlaka.

Vyanzo vyamfuko.

(b) michango, zawadi na ruzuku kutoka kwa mtu yeyoteatakayethibitishwa na Serikali;

(c) asilimia tano ya faida ya miradi itakaoanzishwa na Mamlakakwa lengo la kuingiza kipato;

(d) ada na malipo yanayokusanywa na Mamlaka kutokana nahuduma zinazotolewa na Mamlaka kwa mujibu wa Sheriahii;

(e) asilimia tano ya faini zitakazotozwa kwa mujibu wa Sheriahii; na

(f) chanzo chengine chochote kitakachothibitishwa naSerikali.Matumizi ya Fedha na Mapato ya Mamlaka.

72. Mamlaka itatumia fedha na mapato yake kwa ajili ya kutekelezakazi zake kama zilivyoelezwa kwenye Sheria na kwa mujibu wa mashartina matakwa ya fedha zilivyopatikana.Kuanzishwa kwa mfuko wa Mazingira

73-(1) Kwa masharti ya Sheria ya Utumishi wa Umma, kutaanzishwaMfuko wa mazingira utakaoratibiwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mazingira.

(2) Fedha za Mfuko zitatokana na:

(a) bajeti itakayopitishwa na Baraza la Wawakilishi;

(b) michango, zawadi na ruzuku kutoka kwa mtu yeyoteatakayethibitishwa na Serikali;

(c) asilimia tano ya faini zitakazotozwa kwa mujibu wa Sheriahii; na

(d) chanzo chengine chochote kitakachothibitishwa naSerikali.Matumizi ya Fedha za Mfuko wa Mazingira.

74 -(1) Fedha za Mfuko zitatumika kwa ajili ya Programu Maalum zaKitaifa za Uhifadhi wa Mazingira ambazo zitathibitishwa na Kamati yaUshauri wa Mazingira na kwa mujibu wa taratibu na sheria za usimamiziwa fedha.

Kuanzishwakwa mfuko waMazingira

Matumizi yaFedha naMapato yaMamlaka

Matumizi yaFedha zaMfuko waMazingira

(2)Wizara ya fedha kwa kushauriana na taasisi inayohusika namazingira itaandaa utaratibu kwa ajili ya usimamizi wa mfuko.

SEHEMU YA KUMI NA TANOMAKOSA NA ADHABU

75. Mtu yeyote ambae:

(a) atamzuaia Afisa mwenye mamlaka kuingia katika jengo;

(b) atamzuia Afisa mwenye mamlaka kutekeleza majukumundani ya jengo kwa mujibu wa Sheria hii;

(c) atatoa taarifa za uongo kwa Afisa mwenye mamlaka;

(d) amefanya au ameacha kufanya kitendo ambacho kinawezakupelekea aina yoyote ya usumbufu kwa Afisa mwenyemamlaka katika utekelezaji wa majukumu katika sheriahii;ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa fainiisiyopungua Shilingi laki tano na isiyozidi Shilingi milioni tanoau kifungo kwa muda usiopungua miezi mitatu na usiozidimwaka mmoja au adhabu zote mbili kwa pamoja.

76. Mtu yeyote ambae atashindwa kutii amri ya kusitisha iliyotolewakwa mujibu wa Sheria hii ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwafaini isiyopungua Shilingi milioni mbili na isiyozidi Shilingi milioni arobaini aukifungo kwa muda usiopungua mwaka mmoja na usiozidi miaka ishirini auadhabu zote mbili kwa pamoja.

77.Waziri, kwa mapendekezo ya Mkurugenzi Mkuu, ikiwa ataridhikakwamba kuna mtu ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria hii na kwambamtu huyo amekiri kuwa ni mkosa na amekubali kwa maandishi kosa lakekushughulikiwa kwa mujibu wa kifungu hiki, anaweza:

(a) kuhukumu kosa kwa kukubali kiwango cha pesa zisizozidikiwango cha juu cha faini ya kosa hilo au kosa lililotendwapesa ambazo zitalipwa kwa Mamlaka; na

(b) kuamuru kuachiwa kitu chochote kilichokamatwakuhusiana na kosa kwa malipo ya pesa yasiyozidi thamaniya kitu hicho.

MakosayanayohusianaAfisamwenyemamlaka.

Makosayanayohusianana kushindwakutii amri yakusitisha.

Makosayanayohukumiwanje yamahakama.

78. Adhabu kwa kosa la kurudia au kuendelea kutenda kosa kwamujibu wa Sheria hii itakuwa ni mara mbili ya adhabu iliyotolewa kwakosa husika.

Makosa yanayohusiana na jaribio la kutenda kosa.

79. Bila ya kuathiri masharti ya vifungu vya 395 na 396 vya Sheria yaAdhabu Namba 6 ya mwaka 2004, kosa lolote litakalotendeka chini yaSheria hii au kanuni zitakazotungwa kwa mujibu wa Sheria hii litajumuishajaribio la kutenda kosa.

80. Mtu yeyote ambae atakwenda kinyume na masharti ya Sheria hii,ambapo hakuna adhabu iliyowekwa kwa kosa alilotenda na akipatikanana hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingi milioni mbili na isiyozidi Shilingimilioni hamsini au kifungo kwa muda usiopungua mwaka mmoja na usiozidimiaka ishirini na tano au adhabu zote mbili kwa pamoja.

81-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria nyengine yoyote ambayoinatumika, Mahakama inaweza, pamoja na adhabu itakayotolewa kwamtu aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria hii:

(a) ikiwa ni taasisi, kuamuru kufutwa kwa kibali au leseniyoyote ya biashara iliyotolewa kwa taasisi hiyo; au

(b) ikiwa ni mtu mwenyewe, kuamuru kufutwa kwa ruhusa yakufanya kazi zinazohusiana na utaalamu wa mtu huyo.

(2) Hakutakuwa na sharti katika Sheria hii litakalomuondolea mtuyeyote wajibu wake katika kesi ya madai iwapo amefanya kosa la madaikatika sheria nyengine yoyote, au ametakiwa na mtu aliyeathirika na madaihayo kusamehe madai yake.

SEHEMU YA KUMI NA SITAMASHARTI MENGINEYO

82-(1) Mkurugenzi Mkuu atateua Afisa kutoka ndani au nje yaMamlaka kuwa Afisa mwenye mamlaka kwa madhumuni ya utekelezajiwa Sheria hii;

Makosayanayohusianana kurudia aukuendeleakutenda kosa.

Adhabu zajumla.

Makosayanayohusianana jaribio la

kutenda kosa

Vifungu vyaujumlavinavyohusianana adhabu.

Uteuzi nauwezo waAfisa mwenyemamlaka.

(2) Uteuzi unaofanywa chini ya kifungu cha (1) cha kifungu hikikutoka nje ya Mamlaka utafanywa kwa kushauriana na taasisi husika.

(3) Afisa yoyote mwenye mamlaka aliyeteuliwa chini ya kifungukidogo cha (1) cha kifungu hiki atatangazwa kwenye Gazeti Rasmi.

(4) Afisa yeyote mwenye mamlaka aliyeteuliwa kwa mujibu wakifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki, bila ya kibali,wakati wowote kwamsaada unaostahiki anaweza:

(a) kuingia katika jengo, chombo cha majini, angani, nchi kavuau sehemu nyengine yoyote itakayotuhumiwa kwamadhumuni ya kutekeleza Sheria hii;

(b) kuzuia kitu chochote ambacho kimehusika na uvunjaji washarti lolote la Sheria hii;

(c) Kumkamata mtu yeyote ambae amehusika na uvunjaji washarti lolote la Sheria hii;

(d) kuchukua sampuli kwa ajili ya majaribio na ushahidi;

(e) kutaka uthibitisho wa nyaraka;

(f) kutaka taarifa za maandishi au mdomo kwa mtu yeyoteanayehusika;

(g) kuamuru kuondolewa kwa taka au kitu chochotekinachosababisha uchafuzi au kitu chengine chochotekilichothibitisha kuwa na madhara kwa mazingira au jamii;na

(h) kufuatilia malalamiko yoyote ya kimazingirayanaliyowasilishwa kwenye Mamlaka kwa ajili yakuchukuliwa hatua.

83. Afisa yeyote kutoka katika Mamlaka au Afisa yeyote mwenyemamlaka aliyepewa uwezo kwa mujibu ya Sheria hii, hatoshitakiwa aukuwa na dhima kwa jambo lolote ambalo amelifanya au analotarajiakulifanya kwa nia njema katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibuwa Sheria hii.

84-(1) Mkurugenzi wa Mashtaka, kwa mapendekezo ya taasisiinayohusiana na mazingira, anaweza kumteua mtumishi wa Serikali awemwendesha mashtaka kwa kesi za kimazingira kwa mujibu wa Sheria hii.

Kinga

MwendeshaMashtaka waMazingira.

(2)Mtu aweze kuteuliwa kuwa mwendesha mashtaka wa mazingirani lazima awe na :

(a) angalau shahada ya kwanza katika fani ya sheria; na

(b) angalau uzoefu wa kazi za kimazingira kwa kipindi chamiaka mitano.

85. Waziri kwa kushauriana na Kamati ya Ushauri au Mamlaka atakuwana uwezo wa kupiga marufuku kitu chochote ambacho kinasababisha aukinaweza kusababisha madhara makubwa kwa mazingira na kwa jamii.

86. Waziri anaweza kutunga kanuni kwa ajili ya utekelezaji mzuri waSheria hii.

87-(1) Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kwa Maendeleo EndelevuNamba 2 ya mwaka 1996 inafutwa.

(2) Bila ya kuathiri ufutaji uliofanywa kwa mujibu wa kifungu kidogocha (1) cha kifungu hiki:

(a) kanuni au amri yoyote iliyotolewa kwa mujibu wa Sheriailiyofutwa kabla ya kuanza utekelezaji wa Sheria hiizitaendelea kutumika isipokuwa kama zitarekebishwa,zitafutwa au kuondolewa na kuwekwa nyenginezitakazotungwa kwa mujibu wa Sheria hii;

(b) leseni, vibali, ruhusa au nyaraka nyengine zote zilizotolewakwa mujibu wa Sheria iliyofutwa zitaendelea kutumikampaka zitakapomaliza muda, kusitishwa au kubadilishwakwa nyengine zitakazotolewa kwa mujibu wa Sheria hii;na

(c) wafanyakazi wa Idara ya Mazingira waliopo hivi sasawataendelea na kazi zao hadi itakapopitishwa Sheria hii.

Uwezo waWaziri wakuzuia.

Uwezo wakutungaKanuni.

Kufuta nakubakiza.

MADHUMUNI NA SABABU

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuweka mfumo bora wakisheria na kitaasisi wa usimamizi wa mazingira Zanzibar. Uwekaji wamfumo huo unatokana na haja iliyopo kwa kuzingatia mambo muhimuyafuatayo:

(i) Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kwa MaendeleoEndelevu ya mwaka 1996 iliyopo hivi sasa inatoamuongozo wa kisheria wa usimamizi wa mazingirakatika Visiwa vya Zanzibar. Hata hivyo, kumekuwana changamoto kadhaa ambazo zinapelekea Sheriahiyo kufutwa na kutengeneza Sheria mpya.Miongoni mwa changamoto hizo ni:

(a) mapungufu katika baadhi ya vifungu vya Sheria hiyo, haliiliyopelekea kushindwa kupatikana ufanisi wa utekelezajiwa Sheria yenyewe. Kwa mfano kifungu cha 95 kinaelezeamakosa ya Tathmini za Athari za Kimazingira (EnvironmentalImpact Assessment – EIA) na kifungu cha 100 kinaelezeamakosa yanayohusiana na kutokutii amri ya kusitisha (Stoporder). Vifungu hivi vinaelezea kuwa mtu yeyoteatakayekiuka masharti ya vifungu hivyo atakuwa ni mkosana ataadhibiwa kwa mujibu wa Jaduweli ya nne ya Sheriahiyo. Kwa bahati mbaya Jaduweli hiyo kimakosahaikuonesha adhabu inayohusika na makosa hayo.

(b) kuwepo kwa vifungu ambavyo utekelezaji wake umekuwamgumu. Kwa mfano kifungu cha tisa cha Sheria hiyokinataka kuanzishwa kwa Kamati Maalum ya Mazingiraya Baraza la Mapinduzi, kuwa ni chombo cha mwisho chamaamuzi kwa masuala ya mazingira (highest decisionmaking body on environmental matters in Zanzibar), jamboambalo utekelezaji wake uko kinyume na utaratibu.

(ii) Mwaka 2013, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarkupitia Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Raisilizindua Sera mpya ya Mazingira kufuatiakubadilishwa kwa Sera ya Mazingira ya mwaka

1992. Sera hiyo inatoa muongozo wa kutayarishwakwa Sheria mpya ya Mazingira na kufutwa Sheriailiyopo ya mwaka 1996 ili kwenda sambamba nahoja za kimazingira zilizoainishwa kwenye Sera hiyompya.

(iii) Hivi sasa Zanzibar inashuhudia uharibifu na uchafuzimkubwa wa mazingira ambao udhibiti wake unahitajimsukumo mkubwa wa kisheria na kitaasisi kwafaida ya kizazi cha sasa na kijacho.

(iv) Mazingatio maalumu ya Dunia juu ya usimamizi wamabadiliko ya tabianchi na uchimbaji wa mafuta nagesi ni mambo muhimu ambayo yanatakiwakuzingatiwa kikamilifu kwenye Sheria ya Mazingira,ambayo hayamo kwenye Sheria iliyopo hivi sasa.

(v) Haja ya kutenganisha shughuli za kiutekelezaji nauzingatiaji wa Sheria (enforcement and compliance)na kiusimamizi (governance) wa shughuli zakimazingira kwa ajili ya kuongeza ufanisi wakupunguza uchafuzi na uharibifu wa mazingira uliopo.

Kwa kuwa suala la mazingira ni suala mtambuka ni wazi kuwamapendekezo ya mswaada huu yatasaidia uhifadhi na usimamizi wamazingira Zanzibar na hivyo kusaidia kupatikana kwa ufanisi katika kufikiamalengo ya sera ya mazingira (2013) na sera nyengine mbambalizinazoambatana na mazingira.

Aidha, kufutwa sheria ya mazingira iliyopo na kuwekwa sheria mpyaya mazingira kutasaidia kuondoa kasoro zilizomo kwenye Sheria hiyo nakuongeza ufanisi wa utekelezaji na uzingatiaji wa Sheria kwa ajili ya kufikiausimamizi endelevu wa mazingira.

Mswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Zanzibar una jumlaya sehemu 16 na vifungu 87 kama ifuatavyo:

Sehemu ya Kwanza: Sehemu hii ya mswaada wa sheria inahusuutangulizi na ina vifungu viwili ambavyo ni jina fupi na kuanza kutumika ;naufafanuzi wa maneno yaliyotumika kwenye Sheria hii.

Sehemu ya Pili: Sehemu hii inahusu Majukumu ya Jumla yaKimazingira yenye vifungu vinne ambavyo ni kifungu cha 3 hadi cha 6ambavyo ni jukumu la kulinda mazingira, usimamizi wa mazingira katikamipango ya maendeleo, haki na wajibu wa kuwa na mazingira bora, safi nasalama; na misingi ya usimamizi wa mazingira.

Sehemu ya Tatu: Sehemu hii inahusu Utawala na Muundo waKitaasisi. Sehemu hii ina vifungu kumi na saba ambavyo vimeanzia kifungucha 7 hadi cha 23 vinavyohusu Uanzishaji wa Kamati ya Ushauri waMazingira; Muundo wa Kamati ya Ushauri wa Mazingira; Kazi za Kamatiya Ushauri wa Mazingira; Mikutano na Akidi ya Kamati ya Ushauri waMazingira; Uwezo na kazi za Waziri; Mkurugenzi wa Mazingira; Kazi zaMkurugenzi wa Mazingira; Uanzishaji wa Mamlaka ya Usimamizi waMazingira; Muundo na uteuzi wa wajumbe wa Bodi; Muda wa kutumikiaAfisi kwa wajumbe; Kazi za Bodi; Vikao vya Bodi; Maamuzi ya Bodi;Katibu wa Bodi; Uteuzi na Uajiri; Kazi za Mamlaka; na Uwezo waMamlaka.

Sehemu ya Nne: Sehemu hii inahusu Tahadhari ya kimazingira ambayoitakuwa na kifungu kimoja cha 24 kinachohusu Tahadhari ya kimazingira.

Sehemu ya Tano: Sehemu hii inahusu Vitengo vya Mazingira namabadiliko ya tabianchi ambayo ina vifungu viwili vya 25 na 26 vinavyohusuUanzishaji wa Vitengo vya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi; na Kaziza Vitengo vya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi.

Sehemu ya Sita: Sehemu hii inahusu Ukanda wa Pwani wa Zanzibarambayo ina vifungu viwili kuanzia kifungu cha 27 hadi cha 28 ambavyovinahusiana na eneo la ukanda wa pwani la Zanzibar; na Uanzishaji waukanda maalumu wa pwani.

Sehemu ya Saba: Sehemu hii inahusu Usimamizi wa MaliasiliZisizorejesheka yenye jumla ya vifungu saba kuanzia kifungu cha 29 hadicha 36. Vifungu vinahusu Uanzishaji wa kamati ya pamoja ya usimamizi

wa maliasili zisizorejesheka; Muundo wa Kamati ya pamoja ya usimamizi;Kazi za Kamati ya pamoja ya usimamizi wa maliasili zisizorejesheka; Akidiya vikao vya Kamati ya pamoja ya usimamizi; Kibali cha maliasilizisizorejesheka; Jukumu la kuendeeza eneo lililochimbwa; kumbukumbuza maliasili zisizorejesheka; na Katazo la mchanga wa ufukwe na fungu.

Sehemu ya Nane: Sehemu hii inahusu Elimu ya Mazingira na Utafitiyenye vifungu viwili kuanzia kifungu cha 37 hadi cha 38 vinavyozungumziaUpatikanaji wa taarifa za kimazingira; na Utafiti wa Kimazingira.

Sehemu ya Tisa: Sehemu ya tisa inahusu Tathmini ya Athari zaKimazingira na Kijamii ambayo ina jumla ya vifungu tisa kuanzia kifungucha 39 hadi cha 47. Vifungu hivi vinaelezea Mahitaji ya Tathmini ya Athariza Kimazingira; Vigezo vya kuzingatia kwa shughuli zinazohitaji kufanyiwatathmini ya athari za kimazingira; Utambuzi wa kampuni na wataalamu wakufanya Tathmini ya Athari za Kimazingira; Kusikiliza maoni ya Jamii;Ufuatiliaji; Taarifa zinazohitajika; Ripoti ya kimazingira; Ukaguzi wakimazingira na nani anapaswa kugharamikia tathmini za kimazingira(Mgharamikaji).

Sehemu ya Kumi: Sehemu hii inahusu Mkakati wa Tathmini zaKimazingira na ina vifungu viwili ambavyo ni kifungu cha 48 na 49vinavyohusu Mkakati wa tathmini za kimazingira pamoja na Majukumu yaMkurugenzi wa Mazingira juu ya utekelezaji wa Mkakati wa Tathmini zakimazingira.

Sehemu ya Kumi na Moja: Sehemu hii inahusu Uzuiaji wa Uchafuziwa Mazingira na Usimamizi wa taka. Sehemu hii ina jumla ya vifungu kumina moja kuanzia kifungu cha 50 hadi cha 60 vinavyohusiana na Viwangovya kimazingira; Katazo la uchafuzi; Katazo la kutupa taka kwenye eneola bahari; Usimamizi wa taka na maji machafu; Katazo la kuharibu aukuangamiza bidhaa zisizofaa kwa matumizi; Ufuatiliaji na ukaguzi; Taka zahatari; Vitu vya hatari; Taka za Hospitali; Utafutaji, Uchimbaji au Usafirishajiwa Mafuta au Gesi; na Umwagikaji wa Mafuta au Uvujaji wa Gesi.

Sehemu ya Kumi na Mbili: Sehemu hii inahusu Uhifadhi waBioanuwai na Usimamizi wa vyanzo vya maji. Sehemu hii ina jumla yavifungu vitano kuanzia kifungu cha 61 hadi cha 65 vinavyohusu Kutangazwa

maeneo ya Hifadhi; Usimamizi wa eneo ya Hifadhi; Miongozo ya uhifadhiwa bioanuwai; Katazo la bioanuwai na Uhifadhi wa vyanzo vya maji.

Sehemu ya Kumi na Tatu: Sehemu hii inahusu Usimamizi wamabadiliko ya tabianchi ambayo ina vifungu vinne vya 66 hadi 69. Vifunguvinataja Taasisi dhamana ya kusimamia mabadiliko ya tabianchi; Uanzishajiwa kamati za mabadiliko ya tabianchi; Muundo na kazi ya Kamati yaUongozi ya Mabadiliko ya Tabianchi, na Muundo na kazi ya Kamati yaKitaalamu ya Mabadiliko ya Tabianchi.

Sehemu ya Kumi na Nne: Sehemu hii inaelezea Vifungu vya fedhana ina jumla ya vifungu vitano vya 70 na 74 ambavyo vinaelezea fedha zaMamlaka; Vyanzo vya fedha za Mamlaka; Matumizi ya fedha na mapatoya Mamlaka; Kuanzishwa kwa mfuko wa Mazingira; na Matumizi ya fedhaza Mfuko wa Mazingira.

Sehemu ya Kumi na Tano: Sehemu hii inahusu makosa na adhabuna ina jumla ya vifungu saba kuanzia kifungu cha 75 hadi cha 81 ambavyovinaelezea Makosa yanayohusiana na afisa mwenye Mamlaka; Makosayanayohusiana na kushindwa kutii amri ya kusitisha; Makosayanayohukumiwa nje ya mahakama; Makosa yanayohusiana na kurudiaau kuendelea kutenda kosa; Makosa yanayohusiana na jaribio la kutendakosa, Adhabu za jumla; na Vifungu vya ujumla vinavyohusiana na adhabu.

Sehemu ya Kumi na Sita: Sehemu hii inahusu Masharti mengineyona ina jumla ya vifungu sita kuanzia kifungu cha 82 hadi cha 87 vinavyoelezeaUteuzi na uwezo wa Afisa mwenye mamlaka; kinga; Mwendesha mashtakawa mazingira, Uwezo wa waziri wa kuzuia; uwezo wa Waziri kutungakanuni; na kufuta na kubakiza.

…………..................…………....FATMA ABDULHABIB FEREJ

WAZIRI WA NCHI,OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS,

ZANZIBAR.