15
MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA UTANGULIZI Mafanikio ya Wilaya ya Kwimba yanapimwa katika awamu mbili kabla ya Muungano na baada ya Muungano. ENEO NA MAENEO YA UTAWALA Wilaya ya Kwimba ina eneo la kilometa za mraba 3903. Kwa ujumla eneo hili lote ni kavu. Wilaya ya Kwimba inazo Tarafa tano (5), Kata 30, Vijiji 115, Vitongoji 802 na Mamlaka ya Mji Mdogo. Wilaya inayo Majimbo mawili (2) ya Uchaguzi wa Bunge na Madiwani ambayo ni Kwimba na Sumve. Makao Makuu ya Wilaya ni Ngudu iliyo umbali wa kilomita 94 toka Jiji la Mwanza. IDADI YA WATU Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Wilaya ilikuwa na jumla wa watu 406,509 kati ya hao wanaume ni 198,096 na wanawake 208,413. Ongezeko la watu lilikuwa ni 12.8% kwa mwaka). Kwa mujibu wa makadirio hayo ya sensa, kuna kaya 61,518 zenye wastani wa watu 6.3 kwa kila kaya. ULINZI NA USALAMA Pamoja na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutokuwa miongoni mwa Wizara za Muungano, lakini baadhi ya watendaji wa vyombo vya ulinzi na Usalama chini ya Wizara za Muungano wapo karibu na wanachi wa Serikali za Mitaa. Kupitia ulinzi shirikishi jamii na Polisi jamii kumekuwa na ulinzi na usalama wa uhakika chini ya Muungano ingawa kumekuwa na changamoto za kiutendaji, mazingira na uwezo ( Weledi,dhana na zana za kutumia katika ulinzi na usalama). Hili kwa sasa ni jukumu la jamii nzima kutoa haki na kusuluhisha kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama. Kutokana na Muungano Kiini cha amani kimetokana na ushirikiano kati ya viongozi na wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar kuongoza, na kulinda watu wake hivyo kuzuia au kudhibiti uvunjifu wa amani. MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili katika nyanja zote zikiwemo huduma za kijamii kama vile ulinzi na usalama, afya, elimu, maji na shughuli za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji, ushirika, biashara, ardhi, maliasli na mazingira. Wilaya imeboresha sekta hizo kwa nia ya kuwawezesha wananchi kupata huduma iliyo bora kwa kuwapa elimu inayohusiana na sekta 1

MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

  • Upload
    others

  • View
    86

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA

UTANGULIZIMafanikio ya Wilaya ya Kwimba yanapimwa katika awamu mbili kabla yaMuungano na baada ya Muungano.

ENEO NA MAENEO YA UTAWALA

Wilaya ya Kwimba ina eneo la kilometa za mraba 3903. Kwa ujumla eneo hili lote

ni kavu. Wilaya ya Kwimba inazo Tarafa tano (5), Kata 30, Vijiji 115, Vitongoji

802 na Mamlaka ya Mji Mdogo. Wilaya inayo Majimbo mawili (2) ya Uchaguzi wa

Bunge na Madiwani ambayo ni Kwimba na Sumve. Makao Makuu ya Wilaya ni

Ngudu iliyo umbali wa kilomita 94 toka Jiji la Mwanza.

IDADI YA WATUKwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Wilaya ilikuwa na

jumla wa watu 406,509 kati ya hao wanaume ni 198,096 na wanawake 208,413.

Ongezeko la watu lilikuwa ni 12.8% kwa mwaka). Kwa mujibu wa makadirio hayo

ya sensa, kuna kaya 61,518 zenye wastani wa watu 6.3 kwa kila kaya.

ULINZI NA USALAMAPamoja na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutokuwa miongoni mwa Wizara zaMuungano, lakini baadhi ya watendaji wa vyombo vya ulinzi na Usalama chini yaWizara za Muungano wapo karibu na wanachi wa Serikali za Mitaa. Kupitia ulinzishirikishi jamii na Polisi jamii kumekuwa na ulinzi na usalama wa uhakika chini yaMuungano ingawa kumekuwa na changamoto za kiutendaji, mazingira na uwezo( Weledi,dhana na zana za kutumia katika ulinzi na usalama). Hili kwa sasa nijukumu la jamii nzima kutoa haki na kusuluhisha kwa kushirikiana na vyombovya ulinzi na usalama. Kutokana na Muungano Kiini cha amani kimetokana naushirikiano kati ya viongozi na wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibarkuongoza, na kulinda watu wake hivyo kuzuia au kudhibiti uvunjifu wa amani.

MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili katikanyanja zote zikiwemo huduma za kijamii kama vile ulinzi na usalama, afya, elimu,maji na shughuli za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji, ushirika, biashara, ardhi,maliasli na mazingira. Wilaya imeboresha sekta hizo kwa nia ya kuwawezeshawananchi kupata huduma iliyo bora kwa kuwapa elimu inayohusiana na sekta

1

Page 2: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

husika kwa lengo la kujipatia kipato na maendeleo kama itakavyo elezwa kwakila sekta hapa chini.

MAFANIKIO YA MIAKA 50 BAADA YA MUUNGANO

Kwa imani ya Muungano kumekuwa na Amani, Utulivu, Mshikamano na umoja.Pamoja na changamoto za Muungano hapa chini ni baadhi tu ya mafanikioyaliyopatikana baada ya miaka 50 ya Muungano.

Ujenzi wa nyumba za walimu na ujenzi wa chuo cha michezo malyakinachohudumia michezo Afrika Mashariki

Jengo la uwanja wa michezo ya ndani –chuo cha michezo Malya

2

Page 3: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

Jengo la hosteli chuo cha michezo Malya

Kutokana na Muungano, wananchi wamekuwa wakishirikishwa katikakubuni, kuchagua, kupanga, kutekeleza, kusimamia na kutathiminiutekelezaji na matokeo ya miradi na utoaji wa huduma mbalimbali za jamiikuanzia ngazi za vijiji, kata, Wilaya hadi Taifa. Kwa kuzingatia Sheria,Kanuni, taratibu, Miongozo, Sera, na Mikakati ya kijamii, kitaifa naKimataifa.

Jumla ya Wakulima 450 Katika vikundi 15 (Vijiji 15) wameweza kupataMatrekta (45) madogo (Power tillers) kwa ajili ya shughuli za kilimo kwakuchangia asilimia 20 ya thamani ya kila trekta, hii imesaidia kuongezauzalishaji wa tija na kuboresha kipato na hali ya maisha kwa ujumla. AidhaWilaya imehamasisha matumizi ya pembejeo na zana za kisasa za kilimokama vile matumizi ya trekta ndogo (Power tiller). Tayari trekta 55zimenunuliwa kati ya hizo 3 ni kwa ajili ya chuo cha mafunzo Malya na 52kwa ajili ya vikundi vya wakulima.

Kwa kuzingatia hali ya hewa ya Wilaya ya Kwimba ya ukame, Miradi yaMalambo, Visima vifupi, imekuwa ikiibuliwa ili kukabiliana na changamotozinazokabili ufugaji, hii imesaidia hupatikanaji wa maji msimu wote kwa

3

Page 4: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

ajili ya Mifugo, Pia Majosho na Vibanio imejengwa na kukarabatiwa karibuna malambo hayo. Zaidi ya wafugaji 35,000 wamenufaika.

Miradi 2 ya Kilimo cha umwagiliaji inaendelea kujengwa katika kata yaMalya na Mwang’halanga. Mradi wa Mahiga katika Kata yaMwang’halanga wenye ukubwa wa Ha 200, utanufaisha kaya 104 zenyewakulima 192 (100 me na 92 ke). Mradi mwingine uko kijiji cha Malya,Kata ya Malya, wenye hekta 94, na kwa sasa ukarabati upo hatua yaukamilishaji.

Wilaya inaendelea kutekeleza mpango wa maendeleo ya kilimo na mifugokwa kuanzisha mashamba darasa 88 ya mazao ya chakula, 49 ya zao lapamba na 43 ya mifugo ili kuwezesha wakulima kulima kilimo chenye tijazaidi ili kuondoa tatizo la upungufu wa chakula na kuongeza kipato kwakaya.

Wilaya imefanikiwa kutoa huduma za usafirishaji wagonjwa wa dharuahasa kwa kutumia ambulance 3 zilizopo wilayani.

Wilaya imekarabati jengo la wodi ya wagonjwa wa nje OPD katikaHospitali ya Wilaya Ngudu na ujenzi wa wodi ya wagonjwa mahututiambao kwa sasa umekamilika bado kuweka vifaa tiba.

Ujenzi wa wodi ya wagonjwa wa nje katika zahanati ya Ndamhi, ujenzi wajengo la OPD zahanati ya Nyang’honge na Mwanekeyi. Pia ukarabati wajengo la OPD zahanati ya Ibindo, Milyungu, Lyoma, Izizimba 'A',Mwakilyambiti, Buyogo, Ngudu na Mwankulwe.

Ujenzi na ukarabati wa zahanati katika vijiji vya Ilula, Manawa, Kiliwi,Maligisu, shushi, Mwangika, Ndamhi, Manayi na VCT zahanati yaMwankulwe.

Zaidi ya watoto wapatao 43,788 wamepewa chanjo mbalimbali.Kumekuwa na idadi kubwa ya watu wanaopata huduma za afya, kwamfano,kumekuwa na ongezeko la idadi ya wanawake waliojifunguliahospitalini.

Ukarabati wa nyumba za watumishi wakiwemo wa afya, elimu, uvuvi,kilimo na umwagiliaji na sekta nyingine.

Ukarabati wa RHC na SUIT FANCE hospitali ya Sumve, na Ngudu. Ukarabati wa jengo la huduma za mama na mtoto kituo cha afya Malya. Upanuzi wa Zahanati kuwa kituo cha afya Nyamilama. Ukarabati wa jengo la ofisi Hospitali ya Wilaya Ngudu na jengo la ofisi ya

Mganga Mkuu.

4

Page 5: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

Ujenzi wa wodi ya kulaza wagonjwa daraja la pili Hospitali ya wilayaNgudu.

Ujenzi wa nyumba 10 za watumishi makao makuu ya Halmashauri. Kwa kipindi cha Miaka Hamsini ya Muungano huduma za kisheria

zimekuwa zikiwafikia wananchi kwa urahisi na kwa gharama nafuu kwakadri huduma zinavyohitajika ikiwepo kupata uwakilishi kwenye vyombovya Sheria kama vile mahakama. Hii ni sambamba na kupata elimu yaSheria ya Katiba na Haki za Bindamu.

Kwa kipindi cha Miaka Hamsini ya Muungano migogoro mingi ya ardhiimepungua kwa kiasi kikubwa na kusababisha uwepo wa amani na utulivumiongoni mwa jamii kwa kupitia mamlaka za utatuzi wa migogoro zilizopokwenye jamii kama vile Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji.

Kwa kipindi cha Miaka Hamsini ya Muungano wananchi wamekuwawakishirikishwa katika kuweka misingi na taratibu za kujiongoza kwakutunga Sheria ndogo ndogo za Halmashauri ambazo kwa mujibu waSheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya Mwaka 1982 maoniya wananchi yanazingatiwa katika mchakato wa kupitisha Sheria ndogokwa manufaa yao.

Mafanikio ya miaka hamsini ya muungano una mafanikio ya jumla ya muungano katika sekta ya elimu kama ifuatavyo:-

Kutokana na Amani na utulivu kama zao mojawapo la muungano miaka hamsini ya muungano , sekta ya elimu imeshuhudia mazingira rafiki ya ufundishaji na ujifunzaji katika taasis za elimu kwa Tanzania Bara na Tanzania visiwani.

Watumishio wa Halmashauri za Wilaya na watu wengine wanaotoka Tanzania Bara na Tanzania Visiwani wamekuwa wamekuwa wakitembelea makumbusho ya Taifa na kujifunza bila masharti wala malipo ya fedha za kigeni ( Dolla).

Kila mtanzania amepata fursa ya kujifunza mila na desturi nzuri na kuachana na mila potofu.

Kutokana na Muungano wapo baadhi ya walimu kutoka Tanzania Bara wanaofundisha Zanzibar na Baadhi ya Walimu kutoka Zanzibar wanaofundisha Tanzania Bara.

Kupitia muungano sekta ya Uchumi, Mipango na uwezeshaji imekuwa

ikiwashirikisha wanachi kutambua, kubaini, kubuni, kupanga, kuchagua na

kutekelza miradi na utoaji huduma kwa kuzingatia vipaumble kulingana na

mahitaji ya jamii na vpaumbele vya kitaifa kwa manufaa makubwa ya nchi

na wananchi. Haya yote yamekuwa yakitekelezwa kwa kuzingatia Sheria,

Kanuni, taratibu, será, miongozo ya serikali kulingana na muda, mazingira

na mahitaji.

CHANGAMOTO MAHSUSI ZA MIAKA 50 ILIYOPITA

5

Page 6: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

a. Kumekuwa na upungufu wa watumishi katika kipindi cha miaka 50kuanzia 1964 hadi 2014. Watumishi wengi wameajiriwa katika kipindicha miaka ya 2009 na 2010, wakati kuanzia mwaka 2011 hadi 2014watumishi walioajiriwa zaidi ni wa sekta za Elimu, Afya, Kilimo naMifugo. Pamoja na ajira katika sekta hizi bado kuna mapungufumakubwa ya watumishi hasa katika sekta za kilimo,umwagiliaji naushirika, mifugo na uvuvi, na Afya. Sekta nyingine za maji, fedha,M/Jamii, ujenzi, Ardhi na maliasili, ushirika zimekuwa na mapungufumakubwa kwani ajira zao hazipo tangu mwaka 2010. Hali kadhalikahali ya kijiografia na mazigira magumu ya kazi yamesababishawatumishi wengi wanaoajiriwa kuhama muda mfupi baada ya kujiriwakwa sababu zifuatazo:

Kukosekana kwa nishati ya Umeme ya kutosha katika baadhi ya maeneona kukatikakatika kwa umeme mara kwa mara kunachangia watumishiwengi kupunguza morali na ufanisi wa utendaji kazi ukizingatia kwambadunia ya leo hii ni kijiji, hivyo kusababisha watu wengi kuondoka aukutoripoti kwenye vituo vyao walivyopangiwa hasa katika maeneo yaHalmashauri, Kata na Vijiji.

Pamoja na huduma ya maji kuboreshwa, kukosekana kwa huduma yamaji ya kutosha katika maeneo ya mjini na vijijini kunasabisha watumishiwengi kushindwa kumudu mazingira yao ya kazi, matokeo yake nikuondoka/ kutoroka na kwenda halmashauri nyingine. Vilevile Wilayakutokuwa na huduma ya ndege na barabara ya lami kati ya Mabuki naNgudu kumepuguza huduma ya dharura kwa watumishi wagonjwawanaohitaji tiba ya haraka.

Pia madaktari maalum(flying doctors) kushindwa kufika na kutoa hudumakwa wakati kutokana na ukosefu wa viwanja vya ndege. Hali hiiinasababisha baadhi ya watumishi kuhamia sehemu yenye huduma nzurikwa ajili ya kuchunguzwa afya zao.

Kuwepo kwa miundo mbinu mibovu na ukosekanaji wa vyombo vya usafirikwa watendaji wa Vijiji, Kata, baadhi ya Vitengo na Idara kama vileMaendeleo ya jamii, Ushirika na Biashara kunasabisha ufanisi wa kazikwa watumishi kuwa mdogo kwani maeneo mengi hayapati huduma kwawakati.

b. Elimu duni kwa wakulimaWakulima wengi kushindwa kuiga mbinu bora za kilimo na mifugo ilikuongeza uzalishaji wa tija.

6

Page 7: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

c. Uhaba wa wataalamuUkosefu wa wataalam huchangia kukosekana Elimu kwa wakulima,ambapo lengo ni kuwa na wataalam 214 katika ngazi ya Wilaya,Kata naVijiji hadi sasa wapo 84.

d. Uhaba wa vitendea kazi na zana bora za kilimoWakulima wanategemea jembe la mkono katika baadhi ya maeneo,hadisasa kuna trekta ndogo 45, trekta kubwa 55.Ukosefu wa usafiri kwa wataalam wa vijijini na uhaba wa vifaa vyawataalam kama vile extension kit, nk.

e. Ufinyu wa bajeti kwa ajili ya mafunzo,semina na tafitiWataalam kukosa mafunzo/semina juu ya mabadiliko ya teknolojia zauzalishaji katika kilimo na mifugo, Mfano uhamilishaji n.k.Ukosefu wa tafiti za kutosha za magonjwa ya mimea, mifugo, udongo n.k ilikukabiliana na mabadiliko ya tabia nchini.

f. MasokoWakulima wengi kuendelea kutegemea masoko ya ndani kwa mazao ya chakula,na masoko ya nje kwa mazao ya biashara. AidhauUkosefu wa viwanda vidogo vodogo vya kusindika mazao ili kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuuza.

g. Ukosefu wa miundombinu ya umwagiliajiKati ya hekta 220,820 zinazofaa kwa kilimo ni hekta takribani 300 tu zitakazokuwa chini ya umwagiliaji hadi kufikia 2012/2013.

CHANGAMOTO NYINGINEZO

Ongezeko kubwa la makazi yasiyo rasmi hasa katika baadhi miji iliyokua kamaHungumalwa, Malya, Sumve, Mwabilanda, na Nyambiti kumesababisha maeneohaya kuwa na msongamano wa makazi na watu. Upimaji wa viwanja umekuwa sisambamba ukilinganisha na idadi kubwa ya watu waingiao mjini na huitaji waviwanja vya makazi katika baadhi ya maeneo. Hii inatokana na kutokuwepo kwavitendea kazi na watalaam wa kutosha hasa katika Kitengo cha mipango miji nauthamini ukilinganisha na sasa ambapo kuna kifaa cha upimaji na baadhi yawatalaam.

Ufugaji wa mifugo mingi isiyo kuwa na tija katika ardhi isiyoongezekakumeleta mgangano kwa wakulima na wafugaji na kusababisha maeneomengi kutumika sambamba kwa mifugo na kilimo.

Kuwepo kwa gharama kubwa za viwanja vya makazi na biasharakumesabisha wananchi wengi kushinda kununua viwanja hivyo na kufanyabaadhi ya maeneo yaliyopima kushindwa kununuliwa na kumilikishwa kwawananchi.

7

Page 8: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

Sekta ya uvuvi inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama ifuatavyo-:Hali ya ukame, hali hii ya ukame imesababisha mabwawa mengi pamojana yale yaliyotumika kwa kufugia samaki kukauka na hivyo kupelekeasamaki wote walinaofugwa kufa kwa ajili ya kukosa maji.

Pia jamii kutopata ufahamu wa kutosha juu ya kutambua samaki waliovuliwa kwa njia haramu ambayo ni sumu au baruti.

Watu kuendelea kukata miti ovyo pasipo kuzingatia kanuni na taratibu zamisitu. Hii imepelekea baadhi ya sehemu kukosa uoto wa asili. Elimu yaMazingira zaidi bado inahitajika kwa wananchi juu ya kuhifadhi mazingirayetu ili yawe bora na endelevu na ukosekanaji wa mvua ya kutosha.

Miongoni mwa matatizo makubwa yanayoikabili Idara ya maji ni pamoja na upungufu wa watumishi wenye sifa na rasilimali fedha kwa ajili ya shughuli za kiofisi.

Kamati za maji kushindwa kujua wajibu wao kwani kumekuwa na kushindwakukarabati vyanzo vya maji pindi mabomba/mitambo inapo haribika.

Mwamko wa ufahamu wa jamii kuhusu gharama za uchangiaji umekuwa ni mdogo sana kupelekea kamati kushindwa kukusanya mapato kutoka Idadi ya wanafunzi kuwa wengi katika darasa moja kufanya walimu kushidwa

kufundisha vizuri na matokeo yake mwanafunzi kushindwa kuelewa vizuri.Hali hii hufanya kuwepo kwa mdodoko wa elimu kwa wanafunzi.

Uhaba wa vifaa vya kufundishia kwa mwalimu, kukosekana kwa vitabu vyakutosha kwa kila mwanafunzi hatima yake ni kuwepo na kundi kubwa lawatoto wasiojua kusoma na kuandika.

Upungufu wa walimu kumepelekea kuwepo kwa matokeo mabovu kwawanafunzi katika mitihani yao

Mimba mashuleni kuna sababisha watoto wengi kuacha shule na utoro wamara kwa mara.

Baadhi ya barabara katika maeneo mbalimbali ya wilaya ni mbovu/duni

japokuwa zimefanyiwa ukarabati. Hali hii inatokana na janga la mvua zamasika ambazo huharibu sehemu kubwa ya barabara.

Ufinyu wa bajeti ambao hauendani na hali halisi ya ubovu wa barabarazilizopo ambazo zina hitaji ukarabati.

Vilevile baadhi ya wakandarasi kutokamilisha ujenzi na ukarabati wabarabara, majengo kwa wakati kipindi wanapoingia mkataba na Halmashauri.

Wazazi kutokujua wajibu wao katika kuwalea watoto wao. Kuwa na wake na watoto wengi inasababisha baba kushindwa kuhudumia

watoto wake. Pia mwanaume wanaoa wake zaidi ya mmoja na wakati kipato chake ni

kidogo. Baadhi ya wanaume wanaendelea na mfume dume katika ndoa zao Usafiri wa kuzifikia SACCOS zote ndani ya Wilaya imekuwa tatizo.

8

Page 9: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

Shule nyingi hazina nyumba za walimu karibu na shule na hata za kupanga

mtaani nazo ni tatizo. Hali hii inafanya mazingira ya kufanyia kazi kwa walimu

kuwa magumu.

Samani za shule hususani meza na viti vya wanafunzi hazitoshelezi mahitaji.

Hali huwa mbaya zaidi unapofika wakati wa kufanya mitihani. Kwa ujumla,

mazingira ya mwanafunzi kujifunza huwa ni magumu sana.

Upungufu wa fedha katika baadhi ya shughuli mbalimbali za Idara. Bohari ya Madawa (Msd) kutokidhi mahitaji ya dawa na vifaa vya tiba katika

Wilaya. Upungufu wa vyombo vya usafiri hasa kwa wagonjwa wa dharura

(AMBULANCE) kwani kila kituo cha afya kinatakiwa kuwa na ambulance Jamii kutohamasika kiasi cha kutosha kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii.

Nyumba nyingi za watumishi zinahitaji ukarabati mkubwa.

Michango ya ujenzi ya wa vituo vya kutolea huduma ya tiba kwa upande wa jamii bado ni tatizo kwani wananchi bado wanamwamko mdogo.

MATARAJIO YA MIAKA 50 IJAYO

Kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Kilimo Kwanza yaliyotolewa na viongozimbalimbali na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji katika maeneo yenye skimukama vile kimiza na shilanona

Kuunda zaidi vikundi vya mashamba darasa ya mazao mbalimbaliikiwemo alizeti, pamba, na mahindi pamoja na mazao mengine.

Kusimamia na kufuatilia maendeleo ya shamba darasa na kuhimizawakulima kununua na kutumia zana mbalimbali zakukotwa nang’ombe na tekta za mikono (power tiller).

Kuhimiza wakulima kupanda mazao yanayoendana na hali ya hewa(yanayostahimili ukame na yale yanayokuwa kwa muda mfupi).

Kuboresha huduma za Ugani kwa wakulima ,kuwa na Afisa uganiangalau 1 kwa kila kijiji.

Kuboresha elimu ya kilimo na mifugo kupitia mashamba darasa. Kuhakikisha asilimia 80 ya wakulima wamepata mafunzo ya kilimo na

mifugo kupitia Elimu ya shamba darasa. Kuwa na vituo vya kupashiana na kutolea Elimu ya Kilimo na Mifugo

katika kila kata (Agric.Resource Centre). Kuwa na Mashamba ya kudumu ya mfano katika kila kata (FFS) kwa

ajili ya kufundishia wakulima na wafugaji. Kuhakikisha kila kikundi cha wakulima 25-30 wanakuwa na Trekta

ndogo za kilimo/Zana za kukokotwa na wanyama kazi. Kuongeza mashine za usindikaji nafaka ili kuongeza thamani ya

mazao hususani mahindi na mpunga

9

Page 10: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

Kuhamasisha vikundi/wawekezaji kuweka mashine za kusindikiamazao mbalimbali ili kuongeza soko na thamani ya mazao kama vileAlizeti- Mashine za kukamua MafutaPamba- Mashine za kuchambua nyuzi na mbeguMihogo- Mashine za kusindika

Kuhimiza ufuatiliaji na uimarishaji wa SACCOS na ushirika nakuimarisha mfumo wa vocha kipindi ununuzi wa viatilifu unapofanyika.

Kuhamasisha na kuwaelimisha wananchi juu ya sera kutokata mitihovyo na ikibidi kwanza upande miti ndipo ukate mti na kuhimizawananchi kuanzisha bustani za miti kwa kushirikiana na asasi binafsi.

Kuzijengea uwezo kamati za misitu na hifadhi ya mazingira kwakuwapa mafunzo na mbinu mbalimbali juu ya kuhifadhi na upandaji wamiti.

Kutoa elimu kwa wananchi juu ya hifadhi ya mazingira na kutumiasheria ndogo za mazingira ili mazingira yawe endelevu pamoja nautumiaji wa majiko banifu.

Kuendelea na zoezi la kupanda miti 1,5000,000 kwa mwaka hii ni

pamoja na Wananchi, Taasisi na vikundi mbalimbali vilivyo wilayanikuhamasishwa uoteshaji na upandaji wa miti 1,500,000 kwa mwaka.

Wilaya inayo mpango kabambe wa kuanzisha kituo cha kuzalishiavifaranga vya samaki, hii ni katika kutekeleza lengo la serikali lakuzalisha viumbe wa majini hasa samaki ilikupunguza mgandamizo wawavuvi katika ziwa victoria na kuwapatia wananchi lishe, kipato pamojana ajira. Katika kutekeleza hili Halmashauri imebaini maeneo yaBungulwa, Malya na Ngudu kwa ajili ya zoezi hilo

Utalii Halmashauri imekuwa ikifanya jithada ya kubaini maeneo ya utalii ili yatambulikekwa jamii ya ndani na nje ya wilaya. Vivutio hivi vya Utalii ijapokuwa havijulikanikwa waliowengi lakini Wilaya inao mpango wa kuvitatangaza katika vyombo vyahabari na katika magazeti, ili tuweze kuvutia watalii wa ndani na nje.

Jedwali Na. 50: Baadhi ya Sehemu Muhimu za Utalii, 2014Na Jina la Mahali Aina ya Utalii Uliopo1 Mwakubilinga Nyayo za mganga wa jadi maarufu kama

Mwanamalundi zinapatikana juu ya mwamba wa jiwe)2 Mhande Hill Pango la Watemi ambapo kiti na kitanda cha mawe

vinapatikana hapo3 Nyambiti Njia

PandaMsumari uliochomekwa kwa mkono juu ya jiwe na Mwanamalundi unapatikana hapo.

4 Malya Kuna nyumba ya msonge ambapo watemi wote wa

10

Page 11: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

KISUKUMA walikutana hapo.5 Jojiro Ni mahali ambapo makaburi ya watemi yanapatikana

hapo na sehemu hiyo imehifadhiwa kama msitu wa asili (ngitiri)

6 Ngudu Ni mahali ambapo visima vya jadi vinapatikana na vinatoa maji mwaka mzima.

7 NgullaChanzo: Idara ya Ardhi,Maliasili na Mazingira , 2014

Kuhakikisha kwamba kuna kuwa walimu wa kutosha katika shule za awali,

msingi na sekondali.

Ujenzi wa nyumba za walimu 447 pamoja na maabara kwa shule za msingi

na nyumba 275 sekondari zinajengwa Mihtasari ya masomo.

kuhamasisha jamii kujenga nyumba za kupangisha za gharama nafuu

maeneo ya karibu na shule ili walimu wapange humo.

Kutekeleza mradi mkubwa wa maji Vijijini mradi wa Mwamashimba

utakaohusisha Vijiji 16 ambavyo ni Mhalo, Bupamwa, Chasalawe, Sanga,

Kawekamo, Chibu, Ndhami, Nyang’honge, Milyungu, Igumangobo,

Dodoma, Shilembo, Mwalujo, Shigangama, Kijida, na Mwalujo. Mchakato

wa kusambaza mabomba ya maji unaendelea.

Kusajili vikundi vya kamati za maji katika vijiji 115 wilayani vilivyopo katika

Bonde la Ziwa Victoria ili waweze kupata hati halali ya maji(Wate right).

Kupunguza au kuondoa rushwa mahali pa kazi na kudumisha utawala

bora.

MIUNDO MBINU NA MAWASILIANO.Kabla ya Muungano hakukuwa na usafiri unaotumia njia za barabara isipokuwareli ambayo ilijengwa na wajerumani mwaka 1918. Barabara zilizokuwepo kipindihicho ni Mabuki- Malya, Runele- Malampaka, Magu-Ngudu, Mantare-Nyambiti-Malya, Ngudu- Magu, Kwimba- Misungwi, Bukwimba( Nkalalo)- Kadashi.

Baada ya Muungano mwaka 1964, Wilaya ya Kwimba ina barabara zenye jumlaya urefu wa kilomita 861.4 kwa mgawanyo ufuatao, Barabara kuu Km 40.3,barabara za mkoa (Regional Roads) Km 234.1, barabara za Wilaya, Vijiji na Mjini(District Feeder and Urban Road) Km 587. Hali ya barabara zinazomilikiwa naHalmashauri ya wilaya ni kama ifuatavyo:-

11

Page 12: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

Wilaya ina barabara za udongo zenye urefu wa Km415.8, Km 355.2 kati ya hizoambayo ni sawa na 82% zinapitika. Pia Halmashauri ina barabara zachangarawe zenye urefu wa Km 171.2 ambazo zinapitika majira yote ya mwaka.

Mtandao wa Barabara za Wilaya umeongezeka kutoka Km 514.46 kwa mwaka2005 mpaka Km 587 kwa mwaka 2011, ongezeko hilo likiwa ni sawa na 14%.Vilevile barabara za Mkoa zimebadilika katika idadi kutoka barabara 17 zenyeKm 198.1 hadi 19 zenye Km 234.1ongezeko hilo ni sawa na 18%. Wakati huobarabara kuu 1 yenye Km 40.3 haijabadilika kama linavyoonesha jedwalilifuatalo:-

Matengenezo ya barabara za Wilaya, Vijiji na Mjini hutumia fedha kutoka mfuko wabarabara (Road Fund), Mpango wa maendeleo wa Wilaya (DDP) na Ruzuku yamaendeleo (LGCDG) Matengenezo yote ya Barabara za Wilaya, Vijiji na Mjinihutumia nguvu kazi katika utekelezaji wa matengenezo hayo.Ili kukabiliana na hali hiyo Halmashauri imekuwa kila mwaka ikipanga kufanyamatengenezo mbalimbali ya barabara za Wilaya, Vijiji na Mjini ili ziweze kupitikamajira yote ya Mwaka.

Lengo kubwa la Halmashauri ni kuhakikisha kwamba barabara zote katika wilayazinaimarishwa na kufanya mwasiliano kati ya kijijji kimoja na kingine hatimayeWIlaya kufikiwa kwa urahisi. Hii ni pamoja na fedha za mfuko wa barabarakusimamiwa vizuri hatimaye katika miaka ijayo barabra zote ziwe kaika kiwangocha changarawe ili zipitike kwa mwaka mzima.

Mbali na barabara Sekta hii ya Ujenzi inajishughulisha vilevile na usimamizi wamajengo ya serikali. Katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2010 kumekuwa namafanikio makubwa katika ujenzi wa Ofisi za Serikali kuu na Halmashauri,Hospitali, Shule, Zahanati pamoja na nyumba za Watumishi katika maeneombalimbali ya wilaya yetu.

Usafiri wa Reli Katika mwaka 1918 hadi 2009 shirika la reli limekuwa likitoa huduma ya usafirikwa abiria na mizigo muda wote lakini mwanzoni mwa mwaka 2010 shirika hilililisitisha huduma yake kutokana na miundo mbinu yake kuwa mibovu, hivyokuleta usumbufu kwa abiria ambao wanategemea sana usafiri huo. Kukosekana kwa usafiri huo kumesababisha baadhi ya vituo kama cha Mantarekufungwa aidha vituo vya Nkalalo na Malya vina watumishi ambao kwa sasahawafanyi kazi zao barabara. Kwa ujumla usafiri huu wa reli unagharama nafuuya nauli ukilinganisha na usafiri wa aina nyingine hapa wilayani na ukizingatiakuwa jamii nyingi zinaishi chini ya dola moja kukosekana kwa usafiri huukumekuwa ni kero kubwa kwa wananchi waishio kandokando ya reli hii.

Mitandao ya Simu

12

Page 13: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

Mpaka kufikia mwaka 1957 kulikuwa na simu moja tu ambayo ilikuwa katikameza ya ofisi ya Mkuu wa wilaya, Aina ya simu hiyo ni “Wireless Telephone”. Piakulikuwa na simu ya upepo katika stesheni za reli na ofisi za Ginneyr,pamoja nahuduma ya ujumbe wa Telegramu kupitia vituo vya stesheni. Vilevile huduma yaposta ilikuwepo katika maeneo machache kama vile Nyambiti na Ngudu. Baada ya Muungano suala la mawasiliano liliboreshwa na hadi mwaka huu 2014Wilaya ya Kwimba inapata zaidi ya 80% mawasiliano ya simu kupitia kampuni zaTTCL, TIGO, VODACOM, ZANTEL na ZAIN, ambazo zimeunganisha MakaoMakuu yq Wilaya na sehemu zingine za wilaya na nchi ukiliganisha na mwaka2005 ambapo ilikuwa asilimia 60.Hali hii ya ukuaji wa mawasiliano umefanywana makampuni ya simu za mkononi katika maeneo mbalimbali ya wilaya.

Moja ya minara ya mawasiliano ya simu wilayani Kwimba.

Uwanja wa Ndege Kabla ya Muungano hapakuwa na uwanja wa ndege na baada ya Muunganokulikuwa na viwanja vidogo vya ndege katika maeneo ya Malya na Sumve.Uwanja huu wa Sumve ulitumiwa na madaktari (flying doctors) kwalengo la kutoahuduma katika Hospitali ya Sumve wakati ule wa Malya ulitumiwa na wazungukwa shughuli zao mbalimbali. Viwanja kwa sasa havipo tena.

MASHIRIKA NA MAKAMPUNI MUHIMU.

13

Page 14: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

Wilaya ina mashirika ya TANESCO, POSTA na Benki ya NMB ambayoyanaendelea kutoa huduma ndani na nje ya wilaya. Mashirika haya yanaowafanyakazi wa kutosha ambao hufanya kazi zao barabara.

Shirika la POSTA limekuwa likifanya shughuli zake kama kawaida hii ni pamojana upokeaji na upelekaji wa mizigo katika sehemu mbalimbali ya wilaya na hatanje ya wilaya.

Benki ya NMB pia inafanya huduma yake vizuri kwani inao watumishi wakutosha. Baadhi ya huduma wazipatazo wananchi ni pamoja na kuweka na kutoafedha zao benki, kufungua akaunti, kupewa elimu ya kibenki na uchukuaji wamikopo.

NISHATIWilaya ya kwimba ni mojawapo ya wilaya ambazo imeunganishwa katika gridi yaTaifa – TANESCO. Huduma hii ya nishati ya umeme inachangia kwa sehemukubwa kusukuma mbele maendeleo katika wilaya yetu. Miji na vijiji vinavyopatahuduma ya umeme ni Mji wa Ngudu, vijiji 7 vya Nyambiti madukani, Mwabilanda,Sumve, Nkalalo Lyoma na Malya. Aidha Viwanda 2 kati ya viwanda 4 vyakati vya kuchambulia pamba vinapatahuduma hii ya umeme ambavyo ni SM Holdings na Nyambiti ginery. Shule 2 zasekondari, shule ya msingi 1na vituo cha kutolea huduma za afya 3 vinapata piaumeme huu.Baadhi ya sehemu za Wilaya zinahudumiwa na umeme wa juu(solar energy) kwenye maeneo ya kutolea huduma za elimu na vituo vya afya,jumla ya vituo 6 vya huduma za afya na shule 4 za sekondari zinatumia umemewa jua (Solar energy). Ili kupunguza tatizo hilo la nishati ya umeme vijijini, Wilayainahamasisha Jamii kuchangia uwekaji wa mfumo wa umeme wa jua (Solarenergy) hasa kwenye maeneo ya kutolea huduma za jamii. Aidha shule zasekondari za Ngudu, Nyamilama na Mwamashimba zipo mbioni kupata nishatikwa kutumia biogas.

HALI YA USTAWI WA JAMIIIli kuhakikisha jamii inakuwa katika hali ya ubora ni muhimu kuona watu wanaishikatika amani na maisha bora. Wilaya imefanya shughuli mbalimbali kamaifuatavyo:- Utambuzi wa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi umefanyikakwa kata 4 ambazo ni Malya, Mantare, Ngulla na Nyamilama. Jumla ya watoto9075 walitambuliwa katika kata hizo, wasichana wakiwa 4312 na wavulana 4763.Aidha wilaya inaendelea na utambuzi huo kwa kata zilizobaki. Wilaya inashughulika na utoaji wa huduma kwa makundi maalum kupitiaprogramu mbalimbali za serikali. Mfano mradi wa TASAF umekuwa ukisaidiamakundi maalum kama ifuatavyo:- Walemavu,Wajane ,Wagane ,Watu waishiona VVU na WatotoYatima. Makundi haya yamekuwa yakipatiwa miradi yakujiongezea kipato kama vile mashine za kusaga na kukoboa, miradi ya ushonajina miradi ya ufugaji.

14

Page 15: MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WILAYA YA KWIMBA ... · MAJUKUMU YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Majukumu ya serikali ni kuhakikisha jamii inapata huduma zinayostahili

Nawasilisha

A.I Ng’waniKAIMU KATIBU TAWALA WILAYA

KWIMBA

15