39
Muongozo kuhusu mazingira na maisha endelevu Muongozo kuhusu mazingira na maisha endelevu Muongozo kuhusu mazingira na maisha endelevu Muongozo kuhusu mazingira na maisha endelevu kwa skuli na jamii ya Zanzibar kwa skuli na jamii ya Zanzibar kwa skuli na jamii ya Zanzibar kwa skuli na jamii ya Zanzibar Zanzibar Nell Hamilton na wengineo Endelevu Nell Hamilton, Jokha Omar, Narriman Jiddawi, Anita Walther, Sophia Masuka, Elizabeth Godfrey na David Tanner. Mhariri: Nell Hamilton Jifunze jinsi sote tunavyoweza kusaidia kuzilinda rasilimali zetu ambazo tunazitegemea kwa maisha endelevu ya Zanzibar Chumbe Island Mazingira kwa

Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

  • Upload
    others

  • View
    15

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

Muongozo kuhusu mazingira na maisha endelevu Muongozo kuhusu mazingira na maisha endelevu Muongozo kuhusu mazingira na maisha endelevu Muongozo kuhusu mazingira na maisha endelevu

kwa skuli na jamii ya Zanzibarkwa skuli na jamii ya Zanzibarkwa skuli na jamii ya Zanzibarkwa skuli na jamii ya Zanzibar

Zanzibar Nell H

amilton na wengineo

Endelevu

Nell Hamilton, Jokha Omar, Narriman Jiddawi, Anita Walther, Sophia

Masuka, Elizabeth Godfrey na David Tanner. Mhariri: Nell Hamilton

Jifunze jinsi sote tunavyoweza kusaidia kuzilinda rasilimali

zetu ambazo tunazitegemea kwa maisha endelevu ya Zanzibar

Chumbe Islan

d

Mazingira kwa

Page 2: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

1

Nenda nje! Mazingira ni kila mahali – sisi sote tunachotakiwa kufanya ni kujifunza yanayotuhusu ni kwenda nje

kuangalia yale yote yaliotuzunguka! Angalia viumbe hai na kuweza kujifunza jinsi ambapo wanaishi, jinsi wanavyokuwa, ambacho wanakula, na jinsi wanavyozaliana. Rasilimali gani ambazo wanatumia? Je wanamahusiano gani na viumbe wengine? Na vipi wanakabiliana na kila mmoja, kwako wewe, na kwa mazingira yao? Ni j insi gani watu wanatumia rasilimali za asili ambazo zimewazunguka na kuwanufaisha. Jifunze jinsi ya kuwapenda, waangalie na kuwaheshimu jirani asilia na yale yote ambayo wanatufanyia sisi.

Mazoezi ya Kimazingira – Environmental Code Of Practice

Tafsiri rasmi ya Kiswahili ya kitabu hiki ilifanywa na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar na mhariri Dr Narriman Jiddawi, Taasisi ya Sayansi ya Baharini, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kitabu hiki kinapatikana ‘online’ kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili na kinaweza kuhamishwa au kunakil iwa bila ya malipo kutoka www.chumbeisland.com au nellhamilton.com, au email [email protected].

© 2011 Nell Hamilton / CHICOP. Kitabu hiki kinaweza kunakiliwa chote au sehemu yake, katika umbo lolote liwalo kwa matumizi y a kitaaluma yasiyokuwa y a kupata f aida, bila y a kupata ruhusa mwanzo, iwapo chanzo kitatajwa. CHICOP

wapelekewe nakla y a kazi ambamo kile kilichotolewa ilitumika. Chapisho hili lisiuzwe wala kutumiwa kwa madhumuni y a kibiashara. Ni maruf uku kutumia taariza zilizomo ndani ya kitabu hiki kwa matangazo. Cover images © Nell Hamilton, Jokha Abdallah, Anne Tarv ainen, Anita Walther na Kyla Graham.

Kimechapwa na Rainbow Printers, Dar es Salaam.

Shukurani Kitabu hiki kinachapishwa na Chumbe Island Coral Park kwa kushirikiana na JAMABECO, kwa msaada wa Mpango wa Eneo kwa Usimamizi Endelevu wa Zoni – Pwani za nchi za Bahari ya Hindi (ReCoMap), mpango wa Kamisheni ya Bahari ya Hindi na kufadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya. Waandishi wanapenda kuwashukuru: • Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa uongozi na ushauri wa mitaala. • Lina Mtwana Nordlund wa Chumbe Island Coral Park, kwa maelezo mengi yenye manufaa na maoni katika

mradi wote. • Wapitiaji Dr. Sadri, wa Taasisi ya Sayansi ya Baharini, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Salum Hamed, wa

WIOMSA, Khamis Khalfan, wa Chumbe Island coral Park, na wajumbe wa JAMABECO kwa maoni yao yaliyosaidia kwenye nakala ya awali.

• Washiriki wa timu ya mipango shirikishi ambao walibuni na kutoa dhana ya kitabu hiki: Salum Hamed, WIOMSA, Said Al-abry, NTRC, Zahor Kassim na Hashim Muumin, Wizara ya Uvuvi na Mifugo, Iddi Hussein, SUZA, Ali Usi Basha, Idara ya Misitu na Mali asili Zisizorejesheka, Juma Khamis, MECA, Haji Hassan na Mahfoudh Hassan, JAMABECO, na Moza Nassor Abdullah, Green Pact.

• Mfasiri Kassim Dadi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. • Baraka Kalanghe na Scola wa ReCoMap kwa msaada na uongozi. • Mameneja wa mradi na wafanyakazi wetu wote wa Chumbe Island Coral Park na waelimishaji rika kwa

ushirikiano wao katika kipindi chote cha mradi.

Kitabu hiki kimetolewa kwa vijana wote ambao wanayalinda mazingira,katika kumbukumbu ya Upendo ya Lara Muller, aliyependa bahari.

Mazoezi ya KimazingiraMazoezi ya KimazingiraMazoezi ya KimazingiraMazoezi ya Kimazingira ECOECOECOECO----PracticePracticePracticePractice

Kuwa na tahadhari:

Jihadhari wewe, na watu ambao utakuwa

nao pamoja, msipotee au Kujiumiza!

Heshima kwa wanyamapori:

Usijaribu kuharibu, kuwasumbua au kuwasumbuwa wanyama!

Heshima kwa watu:

Wahusishe na watu wengine ambao

wanatumia mazingira hayo.

Heshima kwa mali za watu:

Ziwache mali za watu wengine ambazo umezikuta!

Kila w akati sisi hutembelea sehemu za

asili au ya mali ya mtu mwingine, ni lazima kuchukua tahadhari katika ziara

zetu kw a kuhakikisha hakuna madhara

ambay o yataharibu mazingira yetu y a asili au haki anazomiliki binadamu, au

kw a sisi w enyew e. Kw a hiy o siku zote ni lazima tufuate

kanuni hii ya mazoezi katika mazingira

(Mazoezi y a kimazingira) popote

tuendakapo.

Acha hali ya usafi na afya:

Chukua takataka nyumbani, zitupe mbali,

na weka maji safi!

Usichukuwe kitu lakini kumbukumbu * Acha chochote lakini nyayo * Ua chochote lakini wakati

Page 3: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

1

Mazingira EndelevuMazingira EndelevuMazingira EndelevuMazingira Endelevu kwa Zanzibarkwa Zanzibarkwa Zanzibarkwa Zanzibar Environmental sustainability in ZanzibarEnvironmental sustainability in ZanzibarEnvironmental sustainability in ZanzibarEnvironmental sustainability in Zanzibar

Mhariri: Nell Hamilton

Watungaji: Nell Hamilton, Jokha Omar, Narriman Jiddawi, Anita Walther,

Sophia Masuka, Elizabeth Godfrey na David Tanner

Yaliomo

1 Mazingira na uendelevu – Environment & sustanability 2

2 Bioanuwai – Biodiversity 6

3 Mikoko – Mangroves 10

4 Nyasi bahari – Seagrass 14

5 Miamba ya matumbawe – Coral reefs 18

6 Uvuvi - Fisheries 22

7 Uchafuzi wa mazingira – Pollution 26

8 Mabadiliko ya hali ya hewa – Climate change 30

9 Chukua hatua – Take action 34

10 Istilahi – Glossary 36

Page 4: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

2

1 Mazingira na uendelevu Tumeitandaza dunia na kuweka juu yake milima isiyoondoka. Tumetoa kutokana nayo aina zote za mimea ya kufurahisha. Fundisho na onyo kwa wenye kutubia. Tunateremsha maji yenye Baraka kutoka mbinguni

ambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo kuipa uhai mpya ardhi iliyokufa. (Qur’an 50:7-10)

Hapo kale, kulikuwa na Kisiwa Miaka mingi iliyopita, mababu na mabibi zako walipokuwa vijana kulikuwa na kisiwa baina ya Pemba na

bara kilichoitwa Maziwe. Maziwe ilikuwa imefunikwa na mikoko iliyomea sana pamoja na msitu wa mwambao, na ilizungukwa na mwamba mzuri wa matumbawe na kujaa samaki. Kisiwa kilikuwa maarufu kwa kasa. Mamia ya aina kasa kijana na kasa wa kawaida walikuja kutaga katika fukwe zenye mchanga za Maziwe kila mwaka. Kilikuwa kisiwa kizuri sana na kilichojaa wanyama pori hata kufikia kuteuliwa kuwa eneo la hifadhi ya marina mnamo mwaka 1975.

Hakukuwa na watu walioishi huo muda wote, japo kuwa lilikuwa eneo la hifadhi. Lilitumiwa na wavuvi wengi kama kambi. Walikusanya kuni kutoka msituni kupikia chakula chao, na kujenga vibanda kwa kutumia miti ya mikoko na makuti ya mnazi. Jambo hili liliendelea kwa siku nyingi. Lakini pole pole, bila ya mtu yoyote kujua msitu huo ulikuwa unatoweka. Mwanzo kulikuwa na wavuvi wachache lakini baada ya karne nyingi wavuvi wengi zaidi walikuja na kila walipokuja, kila mtu alikata au kuchoma matawi na majiti machache tu. Lakini siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, jambo hili liliongezeka na ilipofikia katika miaka ya sabini hakukuwa na mti hata mmoja kisiwani hapo. Maziwe ilikuwa sio chochote isipokuwa mchanga mtupu.

Kwa miaka michache baadaye, wavuvi waliendelea kukitumia kisiwa cha Maziwe, lakini hawakuweza tena kuoka moto na hakukuwa na kinga yoyote kutokana na hali hewa inaobadilika au hali ya hewa mbaya. Mnamo mwaka 1978, janga lilitokea. Wakati wa upepo wa msimu dhoruba kali ililipiga kisiwani hapo. Kwa kuwa hakikuwa na miti ya kukihifadhi, mawimbi, makali yaliondosha kabisa sehemu ya juu ya kisiwa hicho na kuupeleka mchanga wote baharini, na kwenye myamba ya matumbawe. Sasa kinachoweza kuonekana juu ya kisiwa hicho ni ukingo wa mchanga ambao unaweza kuonekana tu nyakati za maji kame, kasa hawana tena mahali pa kutaga mayai yao na hakuna kitu chochote kilichobaki kwa ajili ya watu. Kisiwa chote cha Maziwe kimeondolewa.

Hili linaweza kutokea kwa visiwa vya Zanzibar? Hii ni hadithi ya kweli juu ya yanayotokea tusipochukua hadhari kwa mazingira. Kila mtu pengine alifikiri

walikuwa wakichukua majiti machache – lakini ikiwa watu wengi kila mmoja ataharibu maisha ya wanyama wa misituni, wanyama mwitu kidogo tu, huchangia katika uharibifu mkubwa. Kama vile tutakapoona mazingira ya kimaumbile yanasaidia maisha yetu na hali zetu za maisha kwa namna nyingi na iwapo tutaendelea kuruhusu yaharibiwe tutapata shida hapo baadaye. Familia yako itafanyaje ikiwa watakosa kula samaki kuni za kupikia au maji ya kunywa?

Tutawezaje kuyahifadhi? Hatupaswi kuruhusu hili litokee. Tunaweza kubadili namna tunavyoingiliana na maumbile. Hatujachelewa

kuhifadhi mazingira yenye thamani ya Zanzibar kutokana na vitendo / shughuli haribifu, na ukanda wetu wa pwani haupaswi kufuata Maziwe baharini. Kwanza ni lazima tujuwe kuhusu mazingira yetu na kugundua jinsi dunia ya kimaumbile inatupatia kila kitu tunachohitaji. Pili lazima tujuwe jinsi shughuli zetu zinaweza kudhuru mazingira, na kutishia hali zetu za maisha na hatima yetu. Wa tatu, lazima tuchukuwe hatua kubadili namna tunavyotumia rasiimali asili/za kimaumbile ili zisiharibiwe na yale tunayofanya.

Kitabu hiki kitakuonesha jinsi tunavyoweza kulifikia hili, kitakutambulisha juu ya mazingira na kukuambia kuhusu njia zote ambazo mazingira yetu yanatupatia vitu tunayohitaji ili kuishi maisha ya afya, furaha na usitawi. Pia kitakujulisha jinsi shughuli zetu zinavyoharibu mazingira yetu. Mwisho, utajifunza kuhusu namna ya kuchukua hatua: kuna vitu vingi rahisi tunavyoweza kufanya ili kuhakikisha mazingira yetu yanaendela kutusaidia kwa siku zijazo. Soma ili ujuwe vipi!

Leo hii Kisiwa cha Maziwe: fungu dogo limefunikwa na maji wakati wa kujaa maji © Luca Belis www.trekearth.com/members/Mistral/

Page 5: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

3

Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?

• Katika tokeo la Sunami la mwaka 2011 la Bahari ya Pacific ufukwe wote uliishia kwenye chumba cha kulia cha hoteli, kwa sababu watu walikata mikoko iliyokuwa inawahifadhi na kuwalinda dhidi ya dhoruba.

• Watu na wanyama pori hujua njia yao nyakati za usiku kwa kutumia nyota!

Mazingira Mazingira ni nini?

Mazingira ni vitu vyote vyenye uhai na visivyoishi ambavyo vinatuzunguka – vitu vya maumbile na vilivyofanywa na binaadamu. Mazingira yanajumuisha vitu vyote visivyoishi kama vile hewa tunayovuta maji tunayokunywa, barabara na nyumba, bahari na fukwe, hata jua, mwezi na vyota. Mazingira pia ni pamoja na vitu vyenye uhai kama mimea: misitu na mashamba makubwa, mibuyu, vichaka na nyasi, mikoko, mwani, nyasi bahari, miamba ya matumbawe na mazao, na wanyama wakiwemo wanyama pori, samaki, vipepeo, ndege, nyuki, wanyama wanaofugwa na watu. Kila kitu kilichopo karibu yako ambacho unaweza kukiona, kukigusa, kukihisi, kukinusa au kukisikia ni sehemu ya mazingira.

Mazingira yanatupatia nini? Chakula na maji – Katika Zanzibar maji yetu safi yote yanapatikana kutoka maji ya mvua ambayo

huzama ndani ya ardhi. Hujichuja kupitia mawe ya chokaa, nasi huchimba visima ili tupate maji ya kunywa, kupikia na kuoshea. Samaki wote tunaokula ni viumbe wanaokamatwa baharini, na mifugo yetu pia inategemea chakula na maji yakunywa, mazao kama mpunga, matunda na mbogamboga yanahitaji udongo mzuri wenye rutuba, mvua nyingi na nyuki ndege na popo ili kurutubisha. Bila ya mazingira wangelikula na kunywa nini?

Afya njema – Mimea hupunguza kasi ya umwagikaji wa maji yanayotiririka juu ya ardhi kwa hiyo

yanazama ardhini ambako yanachujwa na mawe, na hiyo hufanya maji yawe salama zaidi kunywa. Hewa safi (oxijini) iliyomo kwenye hewa tunayovuta ambayo inatupa uhai inatolewa na mimea nayo huchukua na kutumia hewa chafu kutoka kwenye hewa. Pia sisi tunatumia mimea mingi inyoota Zanzibar katika kutibu magonjwa, kuanzia malaria hadi mafua: inasaidia kutuweka katika afya njema.

Mahali pa kuishi – Ukiangalia baharini kwenye ufukwe wa mashariki ya Zanzibar unaweza kuona wapi

mwamba ulipo, kwa sababu ya mawimbi makubwa yanayoonekana wakati yanagonga mwamba huo. Lakini ikiwa mwamba huu hautakuwepo na kupiga kwenye ufukwe inaweza kusababisha mmomonyoko. Miamba ya matumbawe, nyasi bahari na mikoko yote hulinda ufukwe dhidi ya mmomonyoko. Ardhini, miti na nyasi (majani) inafanya hivyo hivyo, inazuia udongo usiondolewe na kupelekwa baharini inaponyesha mvua. Bila ya vitu hivyo ardhi iliyopo chini ya nyumba zetu ingeondolewa na nyumba zetu zingeharibiwa hata kupelekwa baharini. Miti hutupatia kivuli na kuzilinda nyumba zetu dhidi ya upepo mkali. Nyumba zetu zimeezekwa kwa makuti ya minazi, mawe mchanga, saruji na miti ya mikoko: vifaa hivi vyote vinatokana na mazingira.

Maisha na ustawi wa kiuchumi – Kazi nyingi katika Zanzibar

zinategemea mazingira. Asilimia 39 ya watu wameajiriwa katika sekta ya huduma (sana kwenye utalii), na asilimia 37 katika kilimo, Misitu na Uvuvi. Uchumi wote wa Zanzibar unategemea mazingira mazuri.

Mali asili Mazingira yanatupatia kila kitu tunachotaka kwa maisha. Vitu tunavyotumia tunaviita ‘rasilimali’.

Rasilimali zinaweza kuwa vitu halisi, kama hewa safi au maji au rasilimali za nishati kama mwangaza wa jua au upepo. Vitu vyote vinavyofanywa na binadamu vinafanywa kwa kutumia rasilimali ambazo hatimaye vinatokana na mazingira ya kimaumbile yanayojulikana kama ‘mali asili’. Kwa mfano saruji inafanywa kwa kuchoma chokaa, plastiki hufanywa kutokana na mafuta, na vioo vinafanywa kutokana na mchanga.

Lakini mali asili zinatoka wapi? Mara nyingi, watu hufanya mambo kama vile rasilimali zote zitadumu milele, lakini kama idadi ya watu inavyoongezeka, baadhi ya rasilimali zinaadimika sana. Kwa hivyo tunapaswa tufikiri tunapotumia vitu: vimefanywa kutokana na nini? Vitu asili vimetoka wapi? Kiasi gani cha vitu hivyo watu wanatumia? Inaweza kumalizika?

Uendelevu Nini maana ya kuwa endelevu?

Kuwa endelevu maana yake ni uwezo wa kuendelea kuwepo. Tunategemea mali asili, kwa hiyo tunazihitaji ziwepo (siku za usoni) kwa ajili ya watoto wetu. Katika muktadha wa maliasili kuweza kuwa endelevu maana yake ni kutumia rasilimali siyo kwa haraka kuliko inavyoweza kupatikana tena. Tunahitaji kutumia rasilimali kwa uangalifu sasa, au hazitakuwepo tena baadaye.

Page 6: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

4

Rasilimali zenye kurudishwa upya na zisizoweza kurudishwa upya Aina mbali mbali za rasilimali hufanywa kwa mchakato wa kimaumbile

katika kasi ya mwendo tofauti na kwa viwango tofauti. Kwa mfano, mwanga wa jua hufanywa mchana wa kutwa, kila siku, lakini mibuyu mikubwa huchukua mamia ya miaka mpaka ikawa mikubwa kiasi hicho. Tunapotumia rasilimali, tunahitaji kuzingatia muda ambao rasilimali hizo zitachukua kujirudi kuwa kama hali ya mwanzo. Iwapo tutatumia kwa haraka resilimali kuliko ambavyo zinaweza kurejea, basi zinaweza kumalizika. Huku sio kuwa endelevu. Ili kuhakikisha tunazo rasilimali hizo tunazohitaji siku za usoni, ni lazima sote tuishi kwa kuzitumia kwa njia endelevui, tusitumie rasilimali kwa haraka kuliko zinavyoweza kurejeshwa.

Tunazingatia kiwango cha kurejesha rasilimali katika muda wa maisha ya mwanadamu. Iwapo maumbile yanarejesha vitu katika muda wa maisha ya mwanadamu tunaviita vitu hivyo vinarejesheka. Maana yake

ni kuwa maumbile yanaweza kuweka tena rasilimali tunazotumia. Rasilimali hizi ni pamoja na maji safi, ambayo yanarejeshwa na mvua inaponyesha, kuni, zinarejeshwa miti mipya inapoota, samaki wanarejeshwa na samaki wapya wachanga, na nishati ya jua au upepo. Lakini vitu ambavyo huchukua muda mrefu zaidi kuliko uhai wa mwanadamu huitwa visivyorejesheka.

Rasilimali zinaporejesheka – Baadhi ya rasilimali hazina kikomo –

hutengenezwa kwa wingi kiasi ambacho zipo zaidi ya tunazotumia, kwa mfano hata tukitumia kiasi gani cha nishati ya mwangaza wa jua au upepo leo (kwa mfano kwa kuchemsha maji kwenye jua au kuendeshea jahazi au mashua) hazitozima jua kung’ara (kutoka mwangaza) au upepo usivume kesho. Hii ina maana tunaweza kutumia kiasi tunachopenda cha rasilimali hizi, na bado zitakuwa zinaendelea na kupatikana!

Rasilimali nyingine huchukua muda mrefu zaidi kurejeshwa kimaumbile (wenyewe), zinachukua miezi, miaka, au hata miongo kabla hazijarejeshwa kimaumbile. Kundi hili ni pamoja na rasilimali hai nyingi kama samaki na kuni – na maji safi, ambayo yanarejeshwa katika msimu wa mvua. Tunapokata miti kuitumia kwa kuni au mbao lazima tupande mingine mipya. Tunapokwenda kuvua samaki, lazima tuwabakishe wengine ili wazae samaki wengine. Lakini iwapo tutakata miti yote na kuwauwa samaki wote au kuyavuta maji yote kutoka ardhini, hakutakuwa

na kilichobaki kwa siku za usoni.

Rasilimali zisizorejesheka – Rasilimali nyingine tunazotumia zilichukua

maelfu au mamilioni ya miaka kufanyika, mara nyingi katika hali ya mazingira tofauti na hizi ya sasa. Kwa hiyo kwa mtazamo wa kibinaadamu rasilimali hizi hazirejesheki. Tukishatumia kile kilichopo sasa hakitakuwapo tena. Rasilimali zisizorejesheka ni pamoja na kisukuku cha fueli – makaa ya mawe, mafuta, gesi, na vitu vinavyotengenezwa kutokana navyo, pamoja na plastiki. Nyingine ni rasilimali za madini – mawe na mawe ya thamani. Uchimbaji wa rasilimali hizi na gharama nyengine za kimazingira tunahitaji kutafuta rasilimali mbadala, zenye kusarifika na kuendelea ili tusizitumie sana.

Kwa nini kuwa endelevu ni muhimu? Tunategemea mazingira kwa namna nyingi mno kwa ajili ya kujipatia riziki, lakini iwapo haturuhusu

rasilimali kuongezeka kutokana na kutumiwa sana, basi samaki tunaokula watatoweka, hatutakuwa na kuni za kupikia, wala maji ya kunywa. Kama vile tunavyotegemea mazingira nayo yanatutegemea pia kwa sisi kuyaangalia na kuyatumia kwa busara.

Lakini hatutumii rasilimali kiuendelevu. Misitu katika Zanzibar inapungua kwa kasi, idadi ya samaki inapungua. Kiwango cha maji yaliyopo ardhini kinashuka na visima vya pwani vinakuwa na maji chumvi na yasiyonyweka. Rasilimali zinaondoka, na iwapo hatutachukua hatua – sote kuanzia sasa – tutakuwa katika shida kubwa baadaye. Huu ndiyo mustakbali ambao vijana wa Zanzibar wataurithi.

Kwa hivyo tunaweza kufanya nini? Tuko katika kipindi cha historia ambacho bado zipo rasilimali, tunaelewa athari tunayopata, na bado tunao muda wa kuchukua hatua. Ni juu yetu kubadili namna tunavyotumia rasilimali na tuzitumie ili zidumu, kuanzia sasa. Ni vizuri kuvua samaki lakini sio wengi kiasi ambacho hawabaki kwa siku za usoni. Samaki wanahitaji muda kukua, kupata mwenza wa kuzaa kama watu na wanyama wa kufugwa wanavyofanya. Miti pia inahitaji muda kukua – tusikate miti kwa haraka sana kuliko inavyoweza kuota na kurejea.

Mali asili zinazorejesheka ambazo zinatumika Zanzibar

Sasa Mwangaza wa jua

Upepo Hewa

Miezi Mchele Muhogo Maji safi Ndizi

Miaka mingi

Uezekaji wa makuti

Mkarafuu Mikoko

Miongo kadha

Mbao ya mnazi

Chewa Muembe Pomboo Papa Kasa

Karne nyingi

Mbuyu Nyangumi Msitu mkubwa

> Miaka 1000 Mchanga

> Miaka 10,000

Mwamba wa matumbawe

>Miaka 100,000

> Miaka Millioni

Mawe yanchi kavu

> Miaka Milioni 100

Mabaki ya fueli

Yen

ye

ku

rud

ish

wa

up

ya

– �� ��

H

azire

jesh

eki

Page 7: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

5

Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!

• Tembea nje na uandike vitu vyote unavyoweza kuviona au kuvihisi ambavyo ni sehemu ya mazingira. Vipi vinaishi na vipi haviishi? Vinatunufaisha vipi? Fanya hivi katika maeneo mbali mbali – mjini, kondeni, ufukweni au msituni – na ulinganishe.

• Vitu gani vya kimaumbile tunavyotumia? Chagua vitu vitano unavyotumia nyumbani kwenu. Vimefanywa kwa kutumia nini? Vimefanywa kwa vitu vinavyoweza kurejeshwa au visivyoweza kurejeshwa?

• Unaweza kuona aina ngapi tofauti za ndege, wadudu, na mimea inaota katika eneo lako unaloishi?

Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!

• Chagua bidhaa inayotengenezwa kwa vitu vinavyoweza kutumika tena.

• Panda mikoko na miti unapotafuta kuni na miti ya kujengea.

• Shiriki katika kusafisha eneo lako unaloishi.

• Jifunze vitu vipya kuhusu mazingira na waelimishe rafiki na familia yako.

Tutafaidika nini tukiishi kwa njia endelevu? Kuishi kwa nia endelevu – kuhifadhi rasilimali kwa matumizi

ya baadaye kutatusaidia kuhifadhi mila zetu za kijamii na kiutamaduni. Tutaboresha hali za maisha ya familia zetu kwa kuhakikisha wanapata chakula cha kutosha, maji safi, mahali pazuri salama pa kuishi na kipato cha kutegemea.

Ni kitu cha kujivunia katika Zanzibar na katika jamii zetu – Zanzibar ni kisiwa maalum. Ni maarufu duniani kote kwa

fukwe zake nzuri, na watu wake wakarimu na marafiki. Ni mahali pazuri ambapo tumebahatika kupata sehemu tunayoiita nyumbani petu – watalii wanaweza kuja kwa wiki moja au mbii tu! Tunayo mengi ya kujivunia iwapo tutayatunza.

Majirani wa kimaumbile – Dunia ya kimumbile inashangaza

na tumepewa tuiangalie, tuitunze. Aina za maisha (vitu) vinavyotuzunguka zinavutia sana. Kuheshimu maajabu na uzuri wa maumbile peke yake na kushangiria katika kujifunza kuhusu viumbe wanaoshangaza wanaoishi katika misitu na bahari yetu. Yana mengi ya kutufunza na kutajirisha maisha yetu kwa namna nyingi tusiyoiona, lakini tungezikosa kama zingetoweka. Fanya juhudi kuona aina tofauti za mimea, ndege, na wadudu walio karibu yako. Tumia muda kukaa na kuangalia tabia zao na angalia namna wanavyobadilika misimu inapobadilika. Tunakuwa na afya mazingira yetu yanapokuwa mazuri.

Nani anahitaji kuchukuwa hatua? Sote tunaweza kuona sehemu nyingi ambapo mazingira yanaharibiwa, na tunahisi kama vile mtu ‘fulani’

angefanya kitu juu yake. Lakini ni nani huyo fulani? Jibu ni bila shaka, wewe na mimi kila mtu aliye karibu nasi. Iwapo wewe ni waziri wa serikali, mzazi, mwalimu, au mwafunzi tunaweza, na lazima sote tuchukuwe hatua na tushirikiane kuyalinda na kuyahifadhi mazingira yetu kwa matumizi ya baadaye.

Tunawezaje kuishi maisha endelevu? Sasa tunaelewa kwamba mazinghira yanatunufaisha kwa kila tunachofanya. Tunajua jinsi ya kufikiria

namna mbalimbali tunazotegemea bahari, misitu, na rasilimali nyingine. Tunajua jinsi ya kujiuliza iwapo vitu tunavyotumia kila siku vimetengenezwa kwa rasilimali zinazorejesheka au zisizorejesheka. Hatua

inayofuata ni kubadili tabia zetu. Chagua bidhaa zilizotengenezwa kwa rasilimali zinazoweza kutumika tena kama vile mikoba ya ukili badala ya mifuko ya plastiki. Saidia dunia ya kimaumbile kurejesha vitu tunavyotumia kwa kupanda miti na kuchagua samaki wanaozaa haraka. Ili kujifunza zaidi kuhusu masuala haya, na jinsi tunavyoweza sote kuhakikisha tunaendeleza manufaa ya mazingira kwa siku za baadaye: endelea kusoma!

Page 8: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

6

TTTTembea ujionee!embea ujionee!embea ujionee!embea ujionee!

• Hifadhi ya kasa katika mahali pa kufugia samaki za Mnarani na Baraka ya Nungwi.

• Kizimkazi kuangalia pomboo.

• Msitu wa Jozani kuangalia kima punju adimu na wengi mimea.

• Kisiwa cha Chumbe kuangalia matumbawe.

• Pemba kuangalia mbweha anayeruka.

• Ghuba ya Menai, Mnemba, ufukwe wa Muyuni, kisiwa cha Misali na Vumawimbi kuangalia kasa wanaotaga.

2 Bioanuwai Wanyama wote ambao wanaranda duniani na ndege wote wanaoruka juu angani ni jamii kama zenu.

(Qur’an 6:38)

Bioanuwai ni nini? Bio maana yake ni maisha, na anuwai ni aina, kwa hiyo, bioanuwai ina maana ya aina ya maisha.

Inajumuisha vitu vyote vinavyoishi duniani na katika bahari, kuanzia nyangumi wakubwa kabisa mpaka bacteria wadogo kabisa. Mahali ambapo aina nyingi tofauti, au ‘spishi’, au vitu vyenye uhai hukua pamoja, kama vile mwamba wa matumbawe au msitu, panasemekana kuwa na bioanuwai nyingi, na mahali ambapo pana spishi chache, kama shamba lililolimwa, au maeneo ya mjini, pana bioanuwai wachache.

Spishi adimu – Kuwa na spishi nyingi sio jambo la pekee muhimu lakini ni muhimu pia (kujua) kama

spishi hizo zinapatikana mahali pote. Spishi adimu ni maalum sana. Kwenye visiwa, kwa sababu makundi ya mimea na wanyama wametengwa na bahari na makundi mengine ya mimea na wanyama, pole pole wanabadilika kuweza kujirekebisha kwa hali za hapo. Baada ya muda, mimea na wanyama hao huwa tofauti sana na jamaa zao kiasi cha kuwa spishi mpya. Sehemu za visiwa kwa hivyo, ni muhimu sana kwa viumbe anuawai kwa sababu kunaelekea kuwa na spishi adimu zaidi kuliko maeneo ya bara yenye ukubwa kama huo.

Bioanuwai katika Zanzibar: makazi na spishi Makazi ya baharini – Kuna aina nyingi tofauti za makazi ya baharini katika Zanzibar – kuanzia ufukweni

mpaka kwenye bahari iliyo wazi. Kila makazi yanamudu mamia ya spishi, na bioanuwai katika Zanzibar ni maarufu duniani kote. Spishi nyingi huishi sehemu ya maisha yao katika makazi moja na waliobaki huishi mahali pengine, kwa hiyo makazi ya bioanuwai ni muhimu sana.

Makazi ya chini ya maji ni vigumu kuyagundua, lakini kuna mengi ya kugundua kwa kutembea tu ufukweni na sehemu za baharini wakati wa maji kupwa. Kwa mara ya kwanza, fukwe zenye mchanga zimeweza

kuonekana hazina viumbe isipokuwa minazi. Lakini viumbe wamejificha hapa – lazima ujuwe pa kutazama. Chimba chini kidogo tu na unaweza kuona chaza; kaa pepo wanaishi katika mashimo na hutembea kwa haraka sana, kwenye fukwe na unaweza kuwaona kwa shida; kaa watawa wamejificha vile vile – katika makome ya viumbe wengine. Fukwe zenye mchanga ni muhimu kwa makazi ya matagio ya kasa, ambao huja ufukweni usiku na kutaga mayai yao chini ya mchanga. Zanzibar inao spishi za kasa bahari, maarufu wao ni kasa wa kijani (green turtle) na kasa wa kawaida (hawksbill). Fukwe zenye mchanga hutumika pia kwa ndege malapulapu ambao wanakula samaki na kombe: korongo, bua bua, ndoero, na wengine wengi. Fukwe za maweni ni mahali muhimu kwa kuangalia bioanuwai wa baharini. Vidimbwi vyenye mawe

vinaweka anemone, kaa, mwanamizi na samaki wachanga, na wanyama kama kombe wa baharini. Aina ya konokono bahari (littorina) na ‘barnacles’ ambao wanaambatana na miamba na kuganda chini ya vyombo. Sehemu hizi asilia za kujionea samaki na viumbe wengine ‘aquarium’ vinakufanya uone aina nyingi tofauti za viumbe wa kushangaza bila ya kuwasumbua. Ukibahatika sana unaweza kuona hata pweza. Wanyama wengi unaoweza kuwaona ni wa ajabu kuliko unavyoweza kufikiria! Maji yanapokupwa mfumo mwingine wa ekolojia unaonekana – vitalu vya nyasi bahari vinaota katika mchanga na matope. Nyasi bahari zinasaidia

viumbe wengi wa kuvutia sana – majongoo bahari, mwanamizi na aina nyingi za kombe / chaza. Kwenye vitalu vya nyasi vya maji mengi, kasa wanakula majani pia.

Kati ya mifumo yetu ya ekolojia ya baharini inavutia sana ni miamba ya matumbawe. Chini ya mawimbi yamejificha mamia

ya spishi ya matumbawe yenye rangi za kung’ara, sponji, kaa, kamba wakubwa, samaki wa miamba, papa, taa na mara nyingine hata wanyama wakubwa duniani – nyangumi (whale shark)! Mbali na miamba katika bahari kuu kuna viumbe wa

ajabu – sio haba wanyama wa hapa petu tu ni spishi 8 za pomboo, 3 za nyangumi na aina moja ya nguva (dugong). Mfano wa aina za pomboo ni pomboo kikomo, pomboo madoto, pomboo mweusi pia nyangumi mwenye nundu, wote wanapatikana katika Ghuba ya Menai.

Msitu pori – Miti huipa misitu muundo ambao hutoa sehemu

nyingi kwa spishi kupata makazi. Kila spishi za miti zinavyoota msituni ndivyo inavyosaidia bioanuwai wengi zaidi. Misitu ya pwani ya Afrika ya Mashariki inafanya mojawapo ya maeneo ya misitu 25 muhimu ya bioanuwai duniani.

Kuna aina tatu kuu za misitu pori katika Zanzibar. Msitu mnyevunyevu hustawi na ni kijani sana. Miti hukua haraka,

Page 9: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

7

Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?

• Popo wa Pemba anayeruka ni mojawapo wa popo wakubwa duniani! Ana uzito wa nusu kilo na urefu wa ubawa kutoka ncha mpaka ncha ni mita moja!

• Watu wengine (wanaojulikana kama wapenda ndege ‘birders’) wanapenda sana ndege na wanaweka orodha ya ndege wote mbalimbali waliopata kuwaona. “Birders” hutoka kwenda kutembea na hata mapumzikoni kwa makusudi kuona ndege zaidi. Watu wengine wanapendelea kutafuta samaki, orchids, miti, popo, vipepeo au nyoka! Katu hawawadhuru au kuwa na wanyama hao au mimea wanaihusudu tu katika maeneo yao ya kimaumbile. Ni mnyama gani pori unayempenda sana?

mikubwa na mirefu, na majani yao yanapoanguka, huoza na kufanya udongo mnene wenye rutba. Sehemu kubwa ya msitu mnyevunyevu ya Zanzibar ipo Pemba, lakini upo msitu mnyevunyevu Unguja Kaskazini na Jozani. Msitu unaoata pembezoni mwa fukwe kwenye mawe mawe huota katika maeneo yenye mvua kidogo, na miti yake inaweza kuhimili ukame. Huota katika ukanda wa matumbawe chokaa ambayo inapitisha maji kwa urahisi, kwa hiyo maji ya mvua hupotea haraka. Maeneo makubwa kabisa ya msitu wa aina hii inayokuwa juu ya mawe katika Zanzibar yapo kusini mashariki ya Unguja. Mikoko huota ukanda wa

pwani na inavumilia chumvi. Mikoko ni muhimu kwa sababu inazaa sana (miti yake huota haraka) na ukuaji huu hutoa chakula kingi kwa wanyama pori. Visiwa vyote viwili vikuu vinahimili mikoko mikubwa na muhimu ambayo inafanya kazi ya sehemu za malezi kwa samaki wengi wanaoishi baadaye katika miamba ya matumbawe.

Zanzibar ni nyumba ya zaidi ya spishi 50 za wanyama wakiwemo wanyama wa hali ya juu kama nyani, kima punju adimu kima bluu Sykes’ na spishi tatu za komba. Tunazo spishi mbili za paa, akiwemo paa nunga (Ader’s duiker) ambaye yupo hatarini kutoweka: wamebaki chini ya 500 duniani karibu wote wakiwa Zanzibar. Pia tuna spishi 23 za popo pamoja na popowa wa Pemba anayeruka (flying fox). Popo wadogo hula wadudu, na wakubwa hula matunda. Mojawapo ya kivutio kisichoaminika au kinachoshangaza cha Zanzibar ni uhamiaji wa popo wanaokula matunda wakati wa kutua jua wanapotoka visiwa vilivyoko baharini, ambako hulala mchana na kuelekea msituni ambako hula wakati wa usiku.

Zipo spishi 177 za ndege, pamoja na chozi ambaye ana rangi inyong’ara, tai adimu na chiriku ambao ni shida kuwaona lakini sauti zao nzuri ni rahisi kuzisikia, hususan kabla ya jua kuchomoza. Pemba ni maarufu kwa ndege wake adimu: kinengenenge wa Pemba, njiwa manga wa kijani wa Pemba, chozi wa Pemba na bundi wa Pemba.

Zipo spishi kadha za nyoka na mijusi, maarufu sana ni kinyonga, anayewezakubadili rangi yake ioane na mazingira! Wapo baadhi ya wanyama wadogo wadogo maalum pia, wakiwemo kaa mnazi mkubwa adimu (coconut crab), na maelfu ya wadudu: vipepeo vizuri, kerengende wanaocheza, vimetameta na ‘mwindaji’ anayevamia kwa kushambulia, na vunja jungu.

Ardhi ya binaadamu – Sehemu kubwa ya ardhi ya Zanzibar imebadilishwa na wanadamu – ardhi ya

kilimo, vijiji na miji. Lakini wapo bioanuwai hapa. Ardhi ya kilimo ni muhimu kwa ndege, nyuki, na vipepeo na kutoa nafasi ambayo wanyama pori, wanaweza kuitumia katika kwenda katika maeneo ya misitu ya kimaumbile. Hata vijijini kuna wanyama pori, kwa vile spishi nyingi za msituni zinaweza kuishi miongoni mwa binadamu, mradi tunawachia miti na vichaka baina ya nyumba zetu.

Kwa nini bioanuwai ni muhimu? Bioanuwai ni muhimu kwa sababu viumbe hai wanategemeana kwa chakula na mahali pa kuishi na

kuzaa. Viumbe hai kama sisi wenyewe ni sehemu ya mtandao wa maisha, na sisi pia tunategemea vitu mbalimbali vinavyoishi kwa chakula chetu, kwa hewa tunayovuta na kwa njia zetu za kujipatia riziki. Iwapo tutauvuruga uwiano wa maumbile kwa kusababisha spishi kufa, mfumo unakuwa sio sawa na mfumo mzima wa ekolojia unaweza kuharibika. Mara nyingine hali hii huyafanya maeneo yasikalike kwa watu kwa mfano yanaweza kugeuzwa jangwa: iwapo miti yote itakatwa, udongo hupeperushwa na mimea kidogo tu inaweza kuota.

Afya – Mimea inatoa oxijini (hewa safi) tunayoihitaji ili tuishi. Mimea inayoota hufyonza gesi hatari, na

kupunguza athari ya mabadiliko ya hali ya hewa. Dunia ya kimaumbile ni nzuri; watu wanaoishi au wanaotumia muda katika maeneo ya kimaumbile wana afya zaidi kuliko wale wanaoishi katika maeneo ambayo hewa imechafuliwa. Maelfu ya mimea hutumika katika dawa za asili za Zanzibar. Ni muhimu kuhifadhi aina mbalimbali za viumbe wa msituni ili kuilinda mimea hii, na mingine pia, kwa vile wana sayansi wanatafuta tiba mpya na bora.

Maji – Misitu husababisha mvua kwa kupunguza mwendo wa mawingu yanapopita juu kwenye ardhi: miti

na mimea huyachuja maji na kuyafanya maji ya chini ya ardhi salama kwetu kuyanywa. Maeneo yaliyo na miti na mimea mingi hupunguza mwendo wa maji yaliyopo juu ya ardhi, kwa hiyo maji huzama ndani ya ardhi badala ya kutiririka na kuupeleka udongo baharini.

Chakula – bioanuwai hutupatia mamia ya samaki tunaokula na miti au mbao tunazohitaji kutengenezea

mitego na kujenga mashua za kuvulia, na moto wa kupikia. Wadudu, popo na ndege wote wanasaidia

Page 10: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

8

kuchavusha mazao tunayolima. Viumbe waliomo katika udongo vile vile ingawa ni wadogo sana, kiasi cha kutoweza kuonekana, huyavunja majani ya miti iliyokufa, na kuyageuza yawe udongo wenye rutuba kwa kupanda mazao, ndege, nyoka na wadudu wanaokula wengine wanakula wadudu wanaoharibu mazao.

Malazi – Miti hupunguza athari ya upepo katika dhoruba na hutoa kivuli kutokana na jua kwa ajili ya

familia zetu, nyumba, mifugo na mazao. Mali ghafi tunayotumia kujengea nyumba zetu – aina mbalimblai za mbao, miti, mapaa, na chokaa vyote vinatokana na vitu vya maumbile.

Njia za kujipatiamaisha (riziki) – Utajiri wa wanyama pori wa Zanzibar unavutia maelfu ya watalii kila

mwaka – kutembelea msitu wa Jozani, kuogelea na pomboo, kuzamia ndani ya maji na kupiga mbizi chini ya maji. Wafanyakazi wote katika kazi ya uvuvi, kilimo au utalii wanategemea aina nyingi za wanyama na mimea mikubwa na midogo kwa kupata riziki zao.

Kwa nini wanyamapori wa Zanzibar wamo hatarini? Inapokuwa idadi ya spishi iko chini au inapungua, spishi hiyo imo katika hatari ya kutoweka kabisa, au

‘imo hatarini’. Hii inaweza kuwa kwa sababu ya tishio kwa mmea au mnyama mwenyewe, au kwa sababu

makazi yake – mahali anapoishi – panaharibiwa au panatoweka. Binadamu wanashindana na mimea na wanyama katika Zanzibar kwa rasilimali na nafasi ya kuishi, na baadhi ya spishi tayari wameshapotea – bioanuwai inapungua Zanzibar.

Kuuliwa moja kwa moja – Spishi nyengine zinauliwa makusudi. Tunavua idadi kubwa ya samaki kila

siku kwa ajili ya chakula, na watu wengine pia huwinda paa. Tunakata miti kwa ajili ya kuni, mkaa, mbao za kujengea nyumba, mashua na ngalawa, na samani. Spishi nyingine wanavuliwa kwa sababu ya kibiashara – baragume ‘tritoni’, kombe, chaza na magamba ya kasa yanauzwa kama mapambo, na mapezi ya papa yanasafirishwa nje ya nchi. Tunawauwa baadhi ya wanyama – kama nyoka – kwa sababu tunawaogopa. Mara nyingine kuwauwa moja kwa moja sio makusudi; pomboo na nyangumi wa baharini na kasa hukwama katika nyavu. Uuwaji wa moja kwa moja usio dhibitiwa una athari kubwa sana katika idadi yao na wengi wa spishi hizo wamo hatarini – wakiwemo papa, kasa, pomboo, na baragumu. Kuna spishi moja, ambayo ilikuwa ya aina yake kwa Zanzibar lakini tumeshachelewa. Chui wa Zanzibar aliwindwa mpaka akatoweka kabisa katika miaka ya 1990.

Upoteaji wa makazi kutokana na udhalishaji na uharibifu – Tunaharibu miamba ya matumbawe

baharini na vitalu vya nyasi bahari kwa kutumia vifaa vya uvuvi kama nyavu ya kukokota na baruti. Maendeleo ya pwani na mmomonyoko wa ardhi inasababisha kasa wasiweze tena kupata mchanga mkavu ufukweni kwa ajiliya kutaga mayai yao na kulalia waktai wa usiku. Kasa wachanga huchanganyikiwa kutokana na mwanga mkali unaotoka hotelini, kwa hiyo, hupotea na hawawezi kuijua njia ya kwenda baharini! Uchimbaji wa mchanga na mawe ya chokaa ni tatizo kubwa sana katika fukwe na hata ndani kwenye ardhi. Msitu inakatwa Zanzibar, lakini hususan katika ukanda wa pwani ili kupisha kilimo, barabara, nyumba na hoteli: kilimo cha kuhama hama kukata au kuchoma eneo la msitu kwa ajili ya kupanda mazao, halafu kwenda katika eneo jengine baada ya miaka michache – bado kinaendelea, lakini namna kinavyofanywa sasa sio endelevu. Kimila mashamba ya zamani yaliachwa ili misitu iote tena, lakini sasa watu wengi sana wanahitaji ardhi yakulima kiasi cha kuwa msitu hauachwi uote tena.

Spishi haribifu – Mara nyingine, watu wanapokwenda duniani huchukua wanyama na mimea kutoka

mahali pamoja na kuwaanzisha mahali pengine, ambapo si pao. Kwa kawaida hawaishi, lakini iwapo hawana wanyama wanaokula wenzao katika hapo mahali papya, wanaweza kuzaa kwa haraka sana na kuangamiza idadi kubwa ya mimea au wanyama wa hapo, na kuchafua usawa wa kimaumbile wa mfumo wa ekolojia. Meli hupeleka panya visiwani ambapo kwa haraka sana huwamaliza ndege wanaojenga ardhini. Spishi haribifu mbaya kabisa wa Zanzibar ni kunguru wa nyumbani aliyeingizwa kutoka India. Kunguru wapo kila mahali, wanakula uchafu wa chakula na mboga – na ndege wa kienyeji na mayai yao, mijusi, vyura na wanyama wengine wadogo. Idadi ya spishi za kienyeji zinapungua Zanzibar pote, lakini hasa Pemba ambako wawili kati ya spishi nne za ndege adimu wanahofiwa wametoweka sasa. Paka wa kufugwa wanaweza kusababisha matatizo iwapo wataingia porini, wanazaa kwa haraka, hawana wanyama wanaowala, na wanakula vinyama vidogo, ndege na mijusi.

Uchafuzi wa hewa – Usimamiaji wa takataka katika Zanzibar hautoshelezi, na plastiki, kemikali, maji

machafu na vitu vingine vingi vinasababisha matatizo makubwa kwa bioanuwai. Kemikali hususan dawa zakuulia wadudu, sumu ya wanyama pori, vipande vya platiki vinapenya kuingia kwenye mazingira ambako wanyama wengi wanaufananisha na chakula, kwa hiyo matumbo yao hujaa na kwa hiyo hufa kwa njaa. Uchafuzi wa hewa unachangia katika ongezeko la idadi ya kunguru wa majumbani kwa njia isiyo dhahiri, kwa kusababisha athari ya kupungua kwa wanyama pori.

Ilikuwa tayari ni nadra ulipochapishwa huu mhuhuri mnamo 1984, Chui wa Zanzibar tayari ameshatoweka

Page 11: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

9

Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!

• Saidia wanyama pori katika jamii yako kwa kuacha maeneo ya miti na mimea pori na kupanda miti vichaka na maua mazuri kunapunguza mmomonyoko wa ardhi, kunaboresha udongo, kunatoa kivuli na kuvutia wanyama pori.

• Nunua matunda ambayo yamelimwa kioganiki bila ya dawa za kuulia wadudu.

• Kuanzisha klabu ya kuangalia wanyamapori katika skuli au jamii yako na kuuchunguza kwa pamoja mwitu wa Zanzibar.

• Usidondoshe takataka kabisa.

Tunawezaje kulinda bioanuwai? Tusipochukua hatua kuhifadhi, spishi za Zanzibar zilizomo hatarini kutoweka pamoja na makazi yao,

tutapoteza bioanuwai wetu wengi vyenye thamani sana, spishi nyingi zaidi watatoweka kabisa na mengi yanayoifanya Zanzibar iwe maalum yatapotea.

Hifadhi spishi zilizomo katika hatari ya kutoweka – Tunategemea samaki, kwa hiyo ili kuhakikisha

kwamba samaki wetu wataendelea kuwepo hapo baadaye, ni lazima tuepuke kuwavua au kuwala samaki ambao wamo hatarini kutoweka. Na lazima tusitumie njia haribifu kuwavua: papa, vinyama vya baharini na kasa wana faida kwetu wakiwa hai tu. Iwapo utabahatika kukutana na kasa anayetengeneza kiota usimsumbue yeye au mayai yake, ikiwa kiota hicho kipo hatarini, watu wa hifadhi ya kasa wanaweza kuyachukua mayai na kuyaweka salama kwa hutengeneza viota mpaka yaanguwe. Kisha hawa wachanga walioanguliwa wanaweza kuachiwa warudi baharini. Hoteli ambazo kasa hutaga kwenye fukwe zake zisiwe na mwanga mkali ulioelekea ufukweni, ambao utawababaisha kasa wachanga. Badala ya kutumia mbao kutoka msitu pori, chukua spishi ya miti inayokua kwa haraka kama mnazi, na msonobari iliyopandwa katika mashamba endelevu, ambako miti mipya inapandwa badala ya ile iliyokatwa.

Hifadhi makazi – Tunapokata msitu, wanyama na miti pori mingi hupoteza, makazi yao, sababu nyingine

ya kuyahifadhi. Lazima tuheshimu kanuni za kutokukata au kuvuna katika maeneo yanayolindwa. Yako maeneo sita yanayolindwa na kuhifadhiwa (angalia kurasa ya 21). Maeneo ya Bahari ya Taifa yanayolindwa. Matatu yapo Pemba (Hifadhi ya msitu wa kimaumbile ya Ngezi-Vumawimbi, wenye hekari 2,900, Hifadhi ya Msitu wa rasi Kiuyu wenye hekari 270 na Hifadhi ya Msitu Mkuu wenye hekari 180) na tatu Unguja (Mbuga ya Taifa ya Ghuba ya Jozani-Chwaka, wenye hekari 5,000, Hifadhi ya Msitu wa Kiwengwa-Pongwe, wenye hekata 3,325 na Msitu wa mvua wa Masingini wenye hekari 285). Bioanuwai wanaweza kutoa kazi endelevu, kwa mfano kupitia utalii unatunza mazingira, watalii watalipa zaidi kwa kutembelea meneo yenye bioanuwai wengi, pesa za kutosha kwa hifadhi yao. Bustani ya matumbawe ya kisiwa cha Chumbe inaajiri karibu watu 50 inawapatia wafanyakazi hoteli zinazolinda mazingira na wanaulinda msitu na makazi ya mwamba wa matumbawe, wanalipwa kwa kutumia dola zilizolipwa na watalii. Mahali penye bioanuwai wachache bado ni muhimu – ni muhimu kuhifadhi maeneno madogo madogo ya miti katika eneo lote la ardhi ili kushajiisha ndege, nyuki, popo, na wachavushaji.

Hifadhi ya spishi haribifu – Kuangamiza spishi haribifu ni ghali sana na changamoto kubwa, lakini

kunaweza kutimizwa. Bustani ya matumbawe ya kisiwa cha Chumbe kilifanikiwa kuwaangamiza panya na kunguru: panya waliuliwa kwa sumu na kunguru wametegwa na kupigwa risasi. Kuwaangamiza kunguru kutoka Zanzibar itakuwa ni kazi kubwa zaidi, na inahitaji ushirikiano kati ya mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali (NGOs), serikali na wananchi sote tunaweza kusaidia kupunguza wanyama na ndege waharibifu kwa kufunika marundo ya mbolea na madebe ya takataka. Serikali inaandaa mpango wa kuwanasa na kuwapiga risasi kunguru. Kuwaangamiza wote kabisi hakutarajiwi, lakini kazi hiyo itapunguza idadi yao ili ndege wa kienyeji waweze kustawi na kuongezeka tena. Kuna paka wengi wanaoishi porini katika Zanzibar – raia ana jukumu la kuondosha kizazi cha paka wao ili kupunguza idadi ya paka wachanga wasiotakiwa au waliotelekezwa.

Punguza Uchafuzi wa hewa – Epuka kutumia dawa za

kuulia wadudu kwa mazao yako – badala yake panda matunda na mboga za asilia ‘oganiki’. Saidia mipango ya jamii ya kutumia tena vifaa, na tumia vyoo – usijisaidie vichakani au ufukweni.

Page 12: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

10

3 Mikoko Iwapo atapanda mti atalipwa kiasi kile kile cha matunda ambacho kinazaliwa na mti huo. (Imepokewa na

Imam Ahmad)

Mikoko ni nini? Mikoko ni misitu inayopatikana katika nchi za joto sana na la kiasi ambayo inaweza kuota na kumea katika

maeneo ya maji chumvi ambayo yapo katika ukanda unaofikiwa na maji kujaa na kutoka/kupwa. Pia ambapo inaweza kuishi kwa kufunikwa na maji ya bahari kwa kiasi fulani mara mbili kwa siku wakati wa maji kujaa. Mikoko pia huhitaji maji baridi, kwa hivyo husitawi vizuri katika sehemu zinakokaa maji baridi na zinazoingia ndani kutoka baharini ambapo maji baridi na ya chumvi huchanganyika. Katika mazingira mazuri, misitu ya mikoko inaweza kuingia kufikia kilomita kadha ndani, na aina nyengine ya mikoko inaweza kufikia urefu wa mita 40.

Mikoko ina nini pekee? Karibu mimea yote haiwezi kuishi katika ukanda unaofikiwa na maji kujaa na kutoka, lakini mikoko

imejiwekea maumbile maalum inayoiwezesha kusitawi katika mazingira haya inayoishi yenye changamoto. Kwa sababu kiwango cha maji hubadilika mita kadha kulingana na kujaa na kupwa kwake, viwango vya wingi wa chumvi na upatikanaji wa hewa safi (oxijini) hubadilika wakati wote. Zaidi ya hayo, mabadiliko ya maji baridi katika mazingira mazuri ambamo mikoko huishi – sehemu zinazoingia maji kujaa na kupwa, ambayo chumvi yake hupungua inaponyesha mvua kubwa na kuongezeka wakati wa kiangazi – hufanya mimea mingine isiyokuwa maalum isiweze kuishi humo kutokana na mabadiliko ya hali kutokana na kutoweza kujiwekea mazingira ya kuishi humo.

Kiwango kikubwa cha chumvi, kwa kawaida ni sumu kwa mimea lakini mikoko inaweza kumudu kuishi katika udongo na maji kwa namna tatu kuu. Kwanza, mikoko inazo chembe chembe za uhai maalum katika mizizi na mashina yao ambazo zinapunguza uingiaji wa chumvi. Mikoko pia inaweza kutoa chumvi kupitia tundu maalum zilizoko kwenye majani yao. Mwisho, mikoko huhifadhi chumvi ya ziada katika majani maalumu yaliyojitolea muhanga. Miti hii hatimaye huyapukutisha majani haya ya manjano, jambo ambalo huenda umepata kuliona kutokea kwenye mikoko hapa Zanzibar. Majani ya mikoko ni manene na kama yenye nta, na vinywele upande wa chini, na hali hizi zote husaidia mti huu kuhifadhi maji baridi.

Mizizi ya mimea huhitaji hewa. Je ni kwa namna gani mikoko inaweza kuishi katika udongo wenye maji ambamo huota? Ni kwamba, aina nyingi ya mikoko inayo mizizi maalumu inayoota kwenye hewa (inayoitwa mizizi ya hewani), ambayo hufyonza hewa safi, kutoka hewani. Ziko aina tatu za mizizi ya hewani: goti, miundi, na pegi, mizizi hii maalumu pia huisaidia kuuzuia mti huu katika udongo laini usioshikamana.

Aina mbali mbali ya mikoko inajiweka katika hali nzuri kwa namna tofauti, na kwa hiyo, huishi vizuri zaidi katika mazingira tofauti kulingana na wingi wa maji baridi yaliyopo katika mazingira yao. Matokeo yake ni kuwa, iwapo utatembea kupita kwenye mikoko kutoka kwenye ardhi kavu kwenda ukingoni mwa maji ya bahari, utaona mpangilio maalum ambazo aina mbali mbali za mikoko ni mingi zaidi kutegema na sehemu ilioko.

Mikoko inayo aina nyingine ya kumudu mazingira pia. Baadhi ya aina ya mikoko hutoa mbegu, maalumu zinazoitwa mbegu za mikoko. Mbegu hizi kubwa za kijani zina urefu tofauti wa kuanzia sentimita 10 hadi 40. Mbegu hizi huchipua kwa kutoa miche ya mikoko zikiwa bado zinaning’inia juu ya mti, kisha miche hii hudondoka kwenye udongo au bahari chini (ya mti) na kuanza kuota moja kwa moja. Mbegu hizi mbegu za mikoko zinaweza kuishi kwa miezi, mingi na kusafiri masafa marefu baharini kabla ya kufika kwenye udongo na kuanza kuota mizizi. Mbegu za mikoko

© Jonathan Bird

Aina fulani ya mizizi ya mikoko iliyo kwenye hewa © www.shorecrest.org

Page 13: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

11

Mikoko katika Zanzibar Zanzibar inayo karibu hekari 18,000 za msitu wa mikoko

hekari 6,000 zipo katika kisiwa cha Unguja na hekari 12,000 katika kisiwa cha Pemba. Maeneo makubwa kabisa ya mikoko katika kisiwa cha Unguja yapo katika Ghuba ya Chwaka na kisiwa cha kwa Pemba ni Ngezi / Micheweni. Zipo aina kumi za mikoko zinazoota katika Zanzibar lakini maarufu sana ni mikoko myekundu au mkandaa, mkoko magondi, na mikoko aina ya mpira na mchu.

Kwa nini mikoko ni muhimu? Mkoko inayo umuhimu ya kimaumbile katika mifumo ya

pwani katika nchi zote za joto, pamoja na Zanzibar. Kimataifa, mikoko inathaminiwa kwa kiwango cha dola 200 - 900 kwa hekari kutokana na huduma zao za kimaumbile. Wazanzibari, hususan wale waliopo katika jamii za pwani wana uhusiano wa karibu sana na utegemezi juu ya mikoko kwa maisha na chakula.

Kulinda ardhi – Mikoko huunda kizuizi cha kimaumbile

baina ya bahari na ardhi. Mikoko hulinda ufukwe kutokana na uharibifu wa mmomonyoko na dhoruba zinazotokea baharini. Huzuia nguvu zinazotoka kwenye upepo na mawimbi na kupunguza athari za dhoruba, vimbunga, na sunami (wimbi kubwa sana la baharini linalosababisha tetemeko la chini ya ardhi au mwenendo wa ardhi). Kwa mfano, baada ya tokeo la sunami la Bahari ya Hindi la mwaka 2004, kulikuwa na vifo vichache zaidi na uharibifu wa mali katika maeneo yaliyokuwa na mikoko mizuri kuliko katika maeneo ambayo mikoko ilikwisha haribiwa. Maeneo mengine hulindwa na vizuizi vya kibinadamu. Hata hivyo, mkoko hujitengeneza wenyewe na kuwa mizuri, wakati ambapo vizuizi vilivyofanywa na binaadamu ni ghali kuvitengeneza na havifanyi kazi ipasavyo (au si vizuri kuviangalia).

Kulinda bahari – Maji yanayomiminika kutoka kwenye nchi

kavu kwenda baharini hupungua kasi yanapofika kwenye mikoko. Takataka hutuwama, bila ya kuwepo mikoko takataka huelea kwenye maji yanaweza kuyasokota matumbawe na vitalu vya nyasi bahari. Iwapo maji ni machafu sana na mepesi hayawezi kufikia mimea inayoota chini. Pamoja na takataka ambazo mikoko huzikusanya na kuzihifadhi, vitu vyovyote vichafuzi kama vile maji machafu, kutoka nchi kavu pia vitatuwama katika matope ya mikoko badala ya kupita kwenye majani laini ya bahari na

matumbawe. Vichafuzi si vitu vizuri kwa mikoko, lakini mikoko inaweza kustahamilia vizuri zaidi kuliko vitu vingine baharini kama vile ardhi inayoota nyasi bahari na mwamba wa matumbawe.

Bionuwai na uvuvi – Muundo taka wa mizizi, mashina, majani na matawi ya mikoko hutoa mahali pengi

kwa wanyama na mimea kuishi, kwa hivyo husaidia aina mbalimbali za viumbe wa baharini na nchi kavu. Shughuli ya uvuvi kisiwani Zanzibar inategemea mikoko. Huduma mojawapo muhimu ya mikoko ni kutoa mazalio, sehemu ya kulelea na malishio katika mizizi kwa samaki na kaa ambao pia hupata makazi na hifadhi dhidi ya maadui zao (wanyama wanaokula wengine). Hawa ni pamoja na samaki nyengine muhimu kiuchumi. Kamba wa kawaida (prawns), na kaa matope wanaishi maisha yao yote katika mikoko, na samaki wengine mbalimbali huishi miezi michache ya maisha yao katika mikoko kabla ya kuhamia katika nyasi na miamba ya matumbawe ambako huishi mpaka wanapokuwa wakubwa. Miamba na vitalu vya nyasi bahari viliopo karibu na mikoko hutoa samaki wengi zaidi kuliko sehemu ambazo hazina mikoko karibu. Mikoko pia huwapatia makazi wanyama kama kima punju, ambao wameenea mahali pengi, nyoka, mijusi na ndege wengi pamoja na wanyama wadogo wadogo wa baharini, mafunza na wadudu. Wanyama na wadudu hawa huifanya mikoko mahali pa kuvutia sana kwa watu wanaovutiwa na wanyama pori.

Mabadiliko ya hali ya hewa – Kama ilivyo mimea yote, mikoko hufyonza hewa ukaa kwa ajili ya

utengenezaji wa chakula na kuigeuza wanga ambayo huhifadhiwa katika mbao (bila shaka, tukiichoma moto mikoko hewa chafu hiyo, itatoka na kuchanganyika na hewa safi tena). Kwa hiyo upandaji na uhifadhi wa mikoko unasaidia kupunguza utoaji wa gesi zenye sumu – lakini kuikata kunachangia katika mabadiliko ya hali ya hewa. Mikoko yenyewe inaweza kuvumilia mabadiliko ya hali ya hewa, na kwa kuulinda dhidi ya vihatarishi kama mmomonyoko wa ardhi, mikoko mizuri itasaidia Zanzibar kupambana na athari ya hali ya hewa kama vile kupanda kwa kiwango cha bahari na dhoruba za mara kwa mara.

Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?

• Mikoko yote ya Zanizbar ina hadhi ya misitu iliyohifadhiwa.

• Miche ya mikoko myekundu inaweza kuishi ikiwa inaelea baharini kufikia mwaka mmoja mpaka ufike mahali pazuri pa kuota.

• Si watu peke yao wanaopata tabu kupanda juu ya mizizi ya msitu wa mikoko wanyama wanaokula wengine pia wanapata tabu! Kwa hiyo mizizi ya mikoko hutoa hifadhi muhimu kwa samaki, kaa, kamba wadogo na wanyama wengine wa baharini kujificha dhidi ya wanya wa chini ya bahari wanaokula wengine, wakati ndege wengi wanaweka viota vyao pale wanyama wanaokula wa ardhini wengine wasipofika.

Mizizi ya mikoko kutoa kimbilio kwa wanyama wanaokula wenzao wakiwemo samaki wadogo © Wikimedia commons

Page 14: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

12

Matumizi ya moja kwa moja – Sisi hutumia mikoko kwa mambo mengi kama kuni na mkaa kwa kupikia,

nyumba zetu hujengwa kwa nguzo za mikoko na kwa kutumia mkaa kufanyia chokaa. Mbao za mkoko hufanyiwa mashua imara na mitego ya samaki pia hutumia miti ya mikoko. Mikoko pia hutumika kwa kutia rangi ya hudhurungi ngozi na kufanya maboma kuzuia maji yasienee. Shughuli hii ilikuwa mojawapo ya shughuli kubwa, lakini sasa ni watu wachache tu sasa ndio wanaofanya shughuli hii kiwango kidogo. Matunda ya mkoko wa aina ya mzinga au mkomafi hutumika kama dawa asilia kutibu upele na maumivu ya tumbo.

Nini tishio la mikoko Zanzibar? Kuharibu misitu – Kupotea kwa mikoko sana kunasababishwa na

kuharibiwa kwa misitu kutokana na ukataji wa mbao usioweza kusarifika kwa ajiliya ujenzi wa mashua (madau, milingoti, ngalawa, kafi) na ujenzi/majengo (mapau, majiti ya majukwaa fremu za madirisha, milango) mitego ya samaki na vielezo pamoja na kuni na mkaa. Shughuli hizi za kijadi zinatishia kuwepo kwa mikoko kwa sababu wakaazi wa pwani wameongezeka na mahitaji ya mazao ya mbao yameongezeka. Ubora wa mbao zilizopo umepungua kwa kiasi ambacho miti ya kujengea inayopatikana hapa si ya ubora na kwa hiyo watu wengi sasa hununua mbao kutoka bara.

Utengenezaji wa fukwe – Waendelezaji wa hoteli wanataka kuwapatia watalii fukwe zenye mchanga

ambao kwao Zanzibar ni maarufu. Wanajaribu kutengeneza upya hali ya vitalu kwa kutumia mikoko, ambapo huikata mikoko bila ya kujali kama ndiyo inayolinda mali yao dhidi ya mmomonyoko wa ardhi katika jaribio la kuunda ufukwe. Baada ya dhoruba chache, pasipokuwa na hifadhi ya miti, mchanga huondolewa, na kuzisonga nyasi pamoja na matumbawe yaliyo karibu na kuyafanya majengo yakose hifadhi dhidi ya mawimbi.

Uvuvi na utamaduni wa pwani – Miti ya mikoko hutumika katika uvuvi mitego ya samaki ya dema na

ukulima wa mwani. Katika maeneo mengine, watu hukata mikoko ili kupata eneo la kufugia samaki na chaza.

Uchafuzi wa hewa – Umwagikaji wa mafuta ni hatari sana kwa mikoko, kwa sababu mafuta hayo

hufunika mizizi iliyopo hewani na kufanya miti hiyo ife kwa kukosa hewa safi. Uchafuzi mwingine wa hewa si tishio sana kwa mikoko kuliko ilivyo kwa viumbe vingine vya baharini kwa sababu mikoko inaweza kuishi iwapo inakutana na madawa chafuzi na viwango vingine vya maji machafu. Hata hivyo, wanyama mbali mbali wanaoishi ndani yake, wakiwemo samaki na chaza tunaokula, wanaathirika vibaya sana. Zaidi ya hayo, samaki na chaza wanaopatikana kutoka kwenye mikoko iliyochafuliwa bado ni hatari kwetu sisi kula.

Utengenezaji wa chumvi – Utengenezaji wa chumvi unaharibu mikoko kwa namna mbili. Watu wengine

huchemsha maji ya chumvi kwa kutumia moto wa mkaa wa mikokoInakadiriwa hutumika kilo 7 za kuni kwa kila kilo moja ya chumvi. Njia nyingine ni kufanya dimbwi kubwa tambarare katikamikoko ambamo maji chumvi yanaingia na kugeuka kuwa mvuke, kwa kuikata miti hiyo.

Urejeshaji wa ardhi – Katika maeneo mengine, mikoko imejaa udongo, kisha hupandwa tena miti ili

kuigeuza ardhi inayopata maji chumvi kuwa ardhi ya maji baridi kwa kilimo. Hata hivyo ardhi hii huwa ni ya ubora wa chini kadri inapopata chumvi nyingi.

Shindikizo la idadi ya watu – Idadi ya watu Zanzibar inaongezeka kwa kasi, zaidi ilisababishwa na ukuaji

wa shughuli za utalii. Hii ina maana kuwa mahitaji ya rasilimali kama vile mikoko inaongezeka. Utumiaji huo umeongezeka kwa kiwango cha kutoweza kuhimilika, na kwa hiyo misitu ya mikoko inapungua kwa kasi: Zanzibar imepoteza thuluthi ya mikoko yake katika muda wa kipindi cha miaka 50.

Tunawezaje kuilinda na kuihifadhi mikoko? Jamii hutumia mikoko kwa mambo mengi. Baadhi ya matumizi haya yanatokana na mila za miaka mingi

na ni matumizi yanayosarifika ya makazi. Mengine kwa bahati mbaya, ama ni mapya au matumizi yanayoongezeka na yanasababisha matatizo makubwa kwa mfumo huu muhimu wa ekolojia.

Njia mbadla ya kujipatia riziki – Hatuhitaji kuiua mikoko kutokana na faida zake za kiuchumi. Zifuatazo

ni njia mbadala za kujipatia riziki ambazo ni rafiki kwa mikoko.

Utalii usiochafua mazingira – Mikoko pamoja na aina mbalimbali za viumbe viliyomo ndani yake ni

mizuri na inavutia watalii wanaopenda wanyama pori. Kwa mfano, katika eneo la hifadhi ya Jozani-Chwaka, wamejenga njia ya mbao kwa watembeao kwa miguu kwenye mikoko inayowawezesha wageni kutembea katika msitu na kuona miti, ndege, kaa na viumbe wengine wanaoishi humo.

Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!

• Tembelea mikoko iliyo katika eneo lako.

• Tembelea Hifadhi ya Jozani kwenye mikoko na Chwaka Kisiwani Unguja na Mikoko ya Micheweni Kisiwa cha Pemba.

Page 15: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

13

Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!

• Weka taka taka mahali panapofaa, sio baharini kwenye mikoko.

• Epuka kununua chokaa iliyofanywa kwa kuni za mikoko.

• Tumia nishati mbadala kama vile vipande vya miti au magogo yaliyopeperushwa pwani na upepo, kuni za mti uliokufa au kuanguka, mabaki ya mimea au miti na majiko yanayotumia nguvu ya jua badala ya kuni na mkaa wa mikoko.

• Peleka taarifa wakataji haramu wa mikoko kunakohusika.

• Anzisha kitalu cha mikoko katika sehemu unayoishi, au jitolee kwa mpango wa upandaji wa miche ya mikoko.

• Yaombe mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ya nchini na ya kimataifa na idara za serikali zinazohusika walinde zaidi mikoko yenu kupitia usimamizi wa mikoko uliopo katika jamii, kukuza mapato mbadala rafiki kwa mikoko kwa watu wanaotegemea kupata riziki zao kutokana na mikoko, na kuongoza katika utumiaji wa takataka za mimea na miti kuzitengeneza nishati mbadala ambayo ni bora katika jamii yako.

• Wajulishe watu wa familia yako na marafiki katika jamii yako kuhusu umuhimu wa mikoko.

• Fanya kazi pamoja na jamii kuilinda mikoko iliyopo hapo kwa kuacha vitendo vya uharibifu kwa mfano, anzisha au jiunge katika juhudi zinazoongozwa na jamii kulinda mikoko iliyo katika eneo

lako.

Kunenepesha kaa matope – Ikiwa mikoko haikatwi matundu

madogo yanaweza kujengwa kuwalinda kaa matope wadogo dhidi ya wanyama wanaokula wenzao, na kuwawezesha wakuwe kwa haraka ili waweze kuuzwa. Aina nyingi za samaki na kaa pia wanaweza kutoa uchumi endelevu.

Vitalu vya mikoko – Miche ya mikoko inagharimu pesa kidogo

na kwa hiyo tunaweza kuchukua miche iliyozidi kutokana na mikoko mizuri kuipanda tena na kurejesha mikoko katika maeneo mengine.

Ufugaji wa nyuki – Asali inayopatikana kutokana na maua ya

mikoko ina thamani kubwa katika soko la ndani na la watalii. Nyuki ni wacharushaji muhimu, kwa hivyo ufugaji wa nyuki ni muhimu sana kwa bioanuwai pia.

Utumiaji wa nishati mbadala – Hii ni teknolojia ambayo inaweza

kutumiwa kama chanzo mbadala cha nishati kwa kupikia badala ya mkaa au kuni. Teknolojia hii inatumia taka-taka za kilimo zisizokuwa kuni: majani makavu na takataka nyengine za mimea na miti kama vile makumbi (ya nazi). Vitu hivi vinaweza kutumiwa kwa kupikia na jamii inayovitengeneza na pia zinaweza kutumiwa na jamii jirani huku vikitoa pato mbadala ambalo ni endelevu.

Msitu unaoweza kusarifika – Bila shaka utumiaji wa kuni

zinazotokana na mikoko kunaweza kuendelea lakini ili kuihifadhi na kuilinda shughuli hii, ni muhimu kwamba iendeshwe vizuri ili iweze kuendelea. Miti mingine ambayo ina afya nzuri na ambayo ni ya aina nzuri ya kibiashara lazima iwachwe na afya ili iwe kama ‘mama’ na kutoa miche ili kuirejesha katika sehemu ilipovunwa (katwa). Jambo hili tayari linafanyika katika Ghuba ya Chwaka. Hata hivyo, hailekei kuwa mikoko iliyopo Zanzibar inaweza kuendelea kutosheleza mahitaji yote ya mbao ya kisiwa hiki bila kuirejesha mikoko kwa kiasi kikubwa, kwa hiyo vifaa vingine vya ujenzi vinavyoweza kusarifika lazima vitafutwe kutoka misitu iliyotunzwa vyema ambayo inapandwa tena miche mipya kwa kila mti uliokatwa. Mzunguko ni lazima uwe katika mzunguko wa miaka 10. Mkoko aina ya Mkoko magondi (Rhizopora mucronata) ndio

unaopendekezwa kwa kurejesha tena mikoko kwani ni mjenzi mzuri wa makazi na hukua kwa haraka. Maeneo yaliyokatwa mikoko yanahitaji kujirudi hali yao kabla ya kukatwa tena. Utekelezaji wa sheria wenye kulenga kuzuia ukataji haramu wa mikoko pamoja kuhusishwa zaidi kwa jamii katika mipango ya usimamiaji wa mikoko ni mkakati unaofaa sana katika kulinda na kuhifadhi mikoko yetu.

Mbegu za mikoko zimepandwa tena Nyamanzi © Nell Hamilton

Page 16: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

14

4 Nyasi bahari Kwa hakika kuumbwa kwa mbingu na ardhi ni (jambo) kubwa zaidi kuliko kuumbwa kwa binadamu: lakini

watu wengi hawaelewi. (Qur’an 40:57)

Nyasi bahari ni nini? Nyasi bahari ni mimea inayoishi baharini. Hii ni mimea maalumu ya baharini ambayo hutoa maua na

imekaribiana kiuhusiano na miembe iliyo nchi kavu kuliko mwani wa baharini, ambao ni mwani. Nyasi bahari huota katika maji machache, karibu na ufukwe na yana jukumu muhimu sana katika mfumo wa maisha ya baharini / maji chumvi kwa sababu yanafanya eneo zuri kwa kuishi wanyama. Ziko takriban aina 60 za majani bahari duniani, 13 kati ya hizo zinapatikana katika fukwa za Zanzibar.

Nyasi bahari zimekaaje na zinaotaje? Nyasi bahari zimepata jina lake hilo kwa sababu aina nyingi zina majani marefu membamba kama nyasi

zinazoota nchi kavu. Namna nyasi bahari zinavyoota pia zinafanana zikiweka bustani sehemu yenye mchanga, chini ya bahari, kama shamba lenye nyasi. Ziko aina nyingi tofauti za nyasi bahari, lakini si, zote ziliofanana na nyasi. Spishi nyingine zina majani yenye simbola makasia madogo (mviringo), wakati nyengine zina umbo la utepe ‘ferns’ au hata nyembamba kama tambi. Chini ya majani yake, mmea wa nyasi bahari una kigogo na mizizi. Kama zilivyo nyasi halisi, kigogo cha nyasi bahari huota usawa wa ardhi. Kigogo hiki kilichokuwa vya kutosha, kinaitwa rizomu. Rizomu hufanywa kwa vipande, na kwenye viungo baina ya sehemu hizo, au vifundo, huota mizizi kwenda chini na hufyonza maji na virutubishi. Vigogo na majani – ile sehemu tunayoweza kuiona huota kuja juu.

Maisha yote ya mmea huu huwa ndani ya maji. Nyasi bahari nyingi zinaweza kuzaa kwa njia mbili. Zinazaa kwa njia isiyotumia jinsia: rizomu huota na kutoa matawi na kwa hiyo mmea huo hutawanyika, na iwapo vipande / sehemu za rizomu zitavunjika, zinaweza kuota na kuwa mmea mpya. Iwapo hali ya mazingira ni nzuri, nyasi bahari nyingine huzaa kwa njia ya jinsia ambapo mauwa ya kiume hutoa unga wa chavua ambao husafirishwa kwa mikondo ya maji kurutubisha mayai yanayotolewa na maua ya kike kwenye mmea mwingine ili kufanya mbegu. Maua haya kwa kawaida ni madogo sana, kwa hiyo ni lazima uyakaribie sana ili uweze kuyaona. Mbegu hutofautiana kwa umbo na ukubwa kutegemea na spishi, misimu ya utoaji wa maua na msimu ya uchavushaji, unatofautiana baina ya spishi na baina ya mimea katika sehemu mbali mbali.

Nyasi bahari zinaota wapi? Nyasi bahari huota katika maeneo tambarare yenye matope na mchanga ambayo hufikiwa na maji ya

bahari. Vitalu vikubwa vinaweza kuonekana katika nyangwa za fukweni, zikiwa zimelindwa na mawimbi na mikondo mikali. Katika baadhi ya vitalu vya baharini aina nyingi ya nyasi hizi tofauti huota pamoja, wakati sehemu nyengine kuna aina moja tu. Katika maeneo yanayopata maji chumvi, majani huzuia maji wakati maji yanapotoka, jambo ambalo huhifadhi mimea ya nyasi bahari dhidi ya kupata joto kupita kiasi na kukauka.

Thalassodendron ciliatum

Thalassia hemprichii Cymodocea rotundata Halodule sp. Halophila ovalis

Aina maarufu za nyasi bahari Zanzibar zikionesha aina tofauti ya majani © www.seagrasswatch.org

Page 17: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

15

Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?

• Nyasi bahari ni nyasi halisi kwa kweli zimehusiana sana na mmea aina ya yungi yungi na kiungo cha tangawizi Zanzibar.

• Nyasi bahari ni mimea pekee inayotoa maua ambayo inaishi majini kikamilifu!

• Aina mbalimbali huota katika viwango tofauti vya maji kujaa na kupwa na kufanya kanda mbalimbali za ekolojia!

• Majani mengine ya nyasi bahari yanaweza kuwa madogo kama kucha za vidole vyako, lakini mengine yanaweza kuwa hata kufikia urefu wa mita moja au zaidi!

• Kasa wa kijani aliyekomaa hula kama kilo mbili za nyasi bahari kwa siku na nguva aliye komaa mpaka kilo 40 kwa siku!

• Malisho makubwa kabisa ya wanyama ya nyasi bahari ya dunia yanaweza kuonekana kutoka angani!

Kwa ujumla, nyasi bahari huota vyema katika masimbi kama mchanga na matope, kwa sababu, mizizi inaweza kuushikilia mmea kwa urahisi chini ya bahari na kupata virutubisho muhimu. Yapo masharti kadha ya kijumla ya kimazingira ambayo ni muhimu kuhusuI wapi na wapi nyasi bahari zinaota. Sharti moja muhimu ni upatikanaji wa mwanga. Kama ilivyo kwa mimea yote, nyasi bahari zinahitaji mwanga kwa ajili ya utengenezaji wa chakula, kwa hiyo nyasi bahari huota vyema kwenye maji kidogo hadi kufikia mita 25 hapa Zanzibar. Ukuaji wa nyasi bahari pia huathiriwa na joto la maji na wingi wa chumvi; spishi tofauti zina mahitaji tofauti.

Kwa nini nyasi bahari ni muhimu? Kwa jicho la haraka kitalu cha nyasi bahari kinaweza kuonekana

hakisaidii maisha sana, lakini kwa hakika jumuiya za nyasi bahari ni mojawapo ya mifumo ya ekolojia yenye manufaa na hali ya utafauti mkubwa duniani. Pia zina maingiliano ya karibu na mifumo mingine ya ekolojia ya baharini, hususan miamba ya matumbawe na mikoko.

Mojawapo ya majukumu / kazi muhimu ya nyasi bahari ni kutoa sehemu ya malezi na makuzi ya aina mbalimbali ya samaki na chaza kama vile samaki aina ya janja kombe, tasi na makorobwe ambao wana thamani kubwa kwa wavuvi na familia zao. Samaki wachanga hukua katika sehemu zenye vivuli vya nyasi bahari wakiwa wamelindwa kutokana na mikondo mikali na samaki/wanyama wanaokula wengine, na pia hupata chakula kingi. Baadaye, wanapokuwa wakubwa zaidi kujificha katika nyasi. Wakubwa huenda kwenye miamba ya matumbawe yaliyo karibu. Wanyama wengine kama vile kaa mchanga, farasi bahari, na kombe hutumia maisha yao yote katika vitalu vya nyasi bahari. Hata hivyo, si samaki wadogo tu wanaotegemea nyasi bahari, lakini hata samaki wakubwa sana hutegemea nyasi bahari, chanzo kikuu cha wanyama wanaokula majani kama vile nguva na kasa, ambao hula nyasi zenyewe na mwani, unaoota kwenye majani yake.

Vitalu vya nyasi bahari pia huwapatia watu chakula. Wanawake wengi na watoto huokota kombe na chaza za aina mbalimbali katika eneo la malisho

ya mifugo ya nyasi bahari katika Zanzibar. Hii ni njia nzuri ya kuongeza kipato na hamirojo (protini) katika mlo.

Jambo jengine muhimu linalofanywa na nyasi bahari ni kuituliza bahari chini ya bahari kwa mizizi. Mtandao ulioshikamana wa majani ya nyasi bahari hupunguza utembeaji wa maji na huzuia takataka (matope) zinazoelea katika maji na kwa hiyo, hutuama chini. Jambo hili hulinda na kuhifadhi fukwe na mali za pwani dhidi ya mmomonyoko na kuyafanya maji yawe safi zaidi, jambo linalonufaisha matumbawe na viumbe wengine wanaohitaji mwanga. Mchakato, huu wa kutuliza (chini ya bahari) pia hurejesha virutubishi, ambavyo hurudishwa katika mfumo wa ekolojia ya baharini kupitia mimea ya bahari. Usanidi mwanga unaofanywa na nyasi bahari hutoa hewa safi inayohitajiwa na samaki na wanyama wengine baharini na hupunguza kiwango cha hewa chafu. Jambo hili ni muhimu kwa sababu ikiwa kiwango cha hewa chafu kipo juu sana, bahari huwa yenye tindikali (asidi) na inaweza kuyeyusha matumbawe.

Hata hivyo, baada ya kufa, nyasi bahari bado zina manufaa. Majani ya nyasi bahari yaliyosukumwa kwenye fukwe hutuliza / huupoza mchanga na kusaidia kulinda ufukwe dhidi ya mmomonyoko. Pia hutoa virutubisho kwa viumbe wanoishi maeneo yanayopata maji chumvi,

Thalasodendron ciliatum bustani ya Chumbe Island Coral Park © Nell Hamilton

Mtafutaji wa wanyama wasikwe na ngongo akiokota kombe/chaza kwa chakula chake katika kitalu cha nyasi – zanzibar © Lina Mtwana Nordlund

Page 18: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

16

yanapopeperushwa kwenye ufukwe, yanasaidia mimea kukua kule, na hivyo kuituliza zaidi ukanda wa pwani.

Nyasi bahari zinakabiliwa na tishio gani? Malisho ya wanyama ya nyasi bahari yana uwezekano wa kudhuriwa haraka kwa kusumbuliwa pamoja na

mabadiliko ya hali ya hewa, na yanaharibiwa duniani kote kwa kiwango cha juu cha asilimia 7 kwa mwaka! Uharibifu huu moja kwa moja au vinginevyo, husababishwa na shughuli za binaadamu kwa kiwango kikubwa.

Mara nyingi, uharibifu hutokea kwa bahati mbaya. Watu hawajui kama pana nyasi bahari au wanazidhuru kwa namna gani! Mashua, zinazotia nanga juu ya nyasi bahari huwekea kivuli, na wakati wa maji kupwa huyasokota. Nanga huchana nyasi bahari, na boti za mashine zinazosafiri kwa kasi mno katika maji madogo, huyachana chana kwa mapangaboi yao na kuacha makovu yanayochukuwa miaka mingi kurejea hali yake. Athari hii huathiri nyasi bahari mbalimbali kwa sababu matope hukorogeka na masimbi mengi huingia kwenye maji. Jambo hili huzuia mwanga huzifikia nyasi kwa hivyo haziwezi kuota.

Ni hatari zaidi utoaji wa michanga chini ya maji ambao hutolewa kwa kuchimbuliwa michirizi ili kuyafanya maji yawe na kina kirefu zaidi kwa ajili ya kutosheleza meli kubwa. Michanga na matope inayotolewa hurundikwa katika mahali pengine. Kitendo hiki hukoroga kiasi kikubwa cha masimbi na matope ambayo huyafanya maji yawe meusi na kutuwama katika tabaka nene juu ya vitalu vya nyasi bahari, na kuziua nyasi bahari pamoja na matumbawe yoyote yaliyo karibu.

Mara nyengine nyasi bahari huuliwa kwa makusudi. Kwa mfano, baadhi ya hoteli zilizopo ufukweni huzing’oa nyasi ili uonekane mchanga mweupe ambao wanadhani watalii wanautarajia na kuupenda. Kitendo hiki huingilia mzunguko wa kimaumbile wa virutubisho. Baya zaidi ni kuwa vitalu vizima huongolewa mara nyingine. Lakini wenye hoteli hugundua haraka kwamba bila ya kuhifadhi nyasi bahari, ufukwe unaoondolewa na mmomonyoko hunyemelea majengo ya hoteli. Hii ndiyo sababu kwa nini hoteli ambazo mbele zimeelekea ufukweni zina kuta mbaya za kangriti sasa – wameharibu majani ya kimaumbile ambayo yangelinda mali yao. Baya zaidi pia, mchanga uliochimbuliwa unapelekwa baharini na kuyakaba matumbawe yaliyopo juu ya mwamba!

Nyasi bahari mara nyingi huuliwa kutokana na ukulima wa mwani. Nyasi bahari hungolewa ili kupatikana mashamba ya mwani, jambo linalopelekea mchanga usiwa imara na kuongeza mmomonyoko wa ardhi. Hata kama nyasi bahari hazikatwi kwa makusudi, mwani ambao unaota juu ya vitalu huzifunika nyasi kwa hivyo hazipati mwangaza wakutosha ili ziote. Asilimia 3 ya watu wa pwani wa Zanzibar wanajihusisha na kilimo cha mwani hasa wanawake. Nyasi bahari zinachukuwa asilimia 20 ya mapato ya nje ya Zanzibar! Nyasi bahari hutumiwa, hasa katika vijiji vya pwani, kwa kutengenezea magodoro au hutumika kama mbolea au chakula cha ng’ombe. Pia hutumika kwa dawa za asili vitu vya sanaa na utengenezaji wa karatasi.

Mara nyengine uharibifu wa vitalu vya nyasi bahari unatoka kwenye ardhi. Matatizo makubwa hutokea wakati maji machafu yanapotiririka baharini baada ya

mvua. Maji haya, yaliyochafuliwa na mashamba, viwanda au maji machafu yatokayo majumbani, yamejaa matope. Pia yana kiwango kikubwa cha virutubisho na kemikali, ambavyo hupelekea ukuaji mkubwa wa mwani – au mauaji ya mwani. Mambo haya kwa pamoja huyafanya maji yawe na mavumbi kiasi ambacho mwanga wa jua hauwezi kufika kwenye nyasi bahari kwa ajili ya usanidi mwanga au kukua. Vitu vingine vinavyoharibu maji kama vile mafuta yanayotoka nje ya magari, yanalewesha nyasi na viumbe wanaoishi ndani yake. Takataka pia husukumwa baharini iwapo hazikuhifadhiwa vizuri. Mara tu yafikapo majini, zinaweza kudhuru mimea ya nyasi bahari kwa kuyasokota na kuyatia sumu pamoja na wanyama wengine wote na mimiea inayoishi miongoni mwao. Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoishi kweye

Hoteli ambazo wanaondosha nyasi bahari huishia kujenga kuta ili kuzuia mmong’onyoko wa mali zao © Nell Hamilton

Page 19: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

17

Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!

• Anzisha uwelewa kwa kuwafahamisha rafiki na familia yako umuhimu wa nyasi bahari!

• Usidondoshe takataka – zitumie tena!

• Usijisaidie ufukweni!

• Nunua matunda na mboga mboga zinazopandwa kioganiki bila ya kutumia dawa bandia na mbolea za viwandani ambazo zinaweza kuharibu vitalu vya nyasi bahari.

• Kuwa mwangalifu kwa nyasi bahari unapoendesha boti – endesha pole pole, epuka maji machache, na usitie nanga juu ya nyasi bahari!

• Anzisha maeneo tengefu yatakayolinda vitalu vya

majani bahari na viumbe vyengine vya bahari.

pwani za Zanzibar malisho ya thamani ya nyasi bahari yanatoweka zaidi na zaidi. Kwa hivyo kuzidi kwa maendeleo kwenye ukanda wa pwani ni tatizo kubwa kwa mazingira ya baharini na watu wa Zanzibar wanaoyategemea.

Nyasi bahari pia zimo hatarini. Kimataifa na athari ya mabadiliko ya hali ya hewa. Maji yanapokuwa ya moto zaidi magonjwa na ukuwaji wa mwani unaongezeka, na kuweka shindikizo kwa viumbe wa baharini. Pamoja na hivyo, matokeo ya hali mbaya ya hewa ambayo yanaharibu mazingira ya bahari, kama vile vimbunga, dhoruba na wimbi la joto yanatokea mara kwa mara.

Tutawezaje kuyahifadhi na kuyalinda malisho ya nyasi bahari?

Manahodha wa boti, mashua na majahazi wanapaswa wawe na hadhari wanapoendesha vyombo vyao katika maeneo yenye nyasi bahari, wasitie nanga juu ya nyasi: waweke nanga juu ya mchanga, au badala yake waweke nanga isyotikisika. Vilevile epuka kuendesha chombo katika maeneo yenye maji machache ambapo pangaboi linaweza kuzikata nyasi au kukoroga matope.

Wamiliki wa hoteli wakumbuke kwamba nyasi bahari huzuia mmomonyoko wa mchanga wa fukwe ambao watalii wanakuja kuufurahia, na kuchangia mapato ya wenyeji, na kwamba wasing’owe nyasi zilizoko mbele ya hoteli zao.

Wavuvi watumie mbinu ambazo hazitoharibu nyasi bahari. Kwa mfano wavue zaidi kwa miguu badala ya kutumia nyavu. Ni vizuri kuvua viumbei wakubwa tu na kuwaacha wachanga wakuwe na wazae na kuhakikisha kuwa kutakuwa na samaki na chaza kwa siku za usoni.

Wakulima wa mwani wakumbuke kwamba kung’oa nyasi bahari kutapelekea matope zaidi kuchanganyika katika maji kwa hiyo muangaza utapungua kufika kwenye mazao ya mwani na hautaota vyema. Ni bora kuweka mashamba ya mwani katika konde zenye nyasi chache ili kuepuka kuzizuia nyasi kupata mwangaza wa jua.

Jamii zinazoishi ukanda wa pwani wanaweza kulinda malisho yao ya nyasi bahari pamoja na uvuvi ambao unawaendesha kwa kulinda majani ya pwani kama vile mikoko, ili kuepuka mmomonyoko wa ardhi na matope kuvisinga vitalu vya nyasi bahari.

Jamii pia zichukuwe hatua kuvilinda vitalu vya nyasi bahari ambazo wanazitegemea kwa chakula na hifadhi dhidi ya mmomonyoko wa ardhi. Heshimu maeneo yaliyopo yaliyohifadhiwa, na kama inawezekana kuanzisha maeneo yasiyo ruhusiwa kuchukua vitu ili kuhifadhi chaza kuongezeka katika sehemu zakaribu yao zinazovuliwa. Nyasi bahari zinaweza kurejeshwa mahali pake kwa kuzipanda tena pale ambapo zimeharibiwa.

Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!

• Huna haja ya kusafiri ili kuweza kuona nyasi bahar.IBahari yote ya Zanzibar ina nyasi bahari!

Wewe tembea tu katika ufukwe wa mchanga wa karibu yako wakati wa maji kupwa, na utaviona

vitalu vya nyasi bahari hapo.

• unapotembea vitalu vya nyasi bahari jaribu kugundua ni aina ngapi tofauti za nyasi bahari unaweza

kuziona hapo? (zinduka: angalia aina tofauti za majani!)

• kanyaga matope au mchanga ili kuhisi jinsi mizizi inavyokuwa, na jinsi gani nyasi bahari

zinajitawanya. Unaweza kuona maua yoyote au mbegu?

• Aina ngapi tofauti za wanyama unaweza kuziona wanaoishi katika nyasi bahari?

• Watu wangapi unaweza kuwaona wanaokota vinyama vidogo vya pwani ambavyo vinaishi katika

vitalu vya nyasi bahari? Ni watu wangapi wanaofaidika na vinyama hivi? Ingetokea nini kwa watu

hao iwapo nyasi bahari zingetoweka.

Page 20: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

18

5 Miamba ya matumbawe Ameinyanyua mbingu juu na kuweka mizani ya vitu vyote, ili msivunje mizani hiyo. Toweni uzito na vipimo

vya haki. (Qur’an 55:1-9)

Matumbawe ni nini?

Miamba ya matumbawe ni mojawapo ya vitu vya kuvutia katika maumbile ya dunia! Zamani baadhi ya watu walifikiri kuwa matumbawe yalikuwa aina ya mawe, lakini sasa wanaelewa kuwa matumbawe ni mkusanyiko wa wanyama wadogo sana wanoitwa ‘polipu’ (polyps) ambao wana kiunzi cha mfupa mgumu kwa nje mithili ya jiwe. Polipu wamehusiana na jejeta (mdudu wa bahari wa yavuyavu) na anemoni na kama wao wana vikia vyenye kuchoma ambayo wanaitumia kwa kulia ‘plankitoni’ – mimea na wanyama wadogo sana wanaoeleya katika mikondo ya maji. Lakini matumbawe yanakula kwa namna nyingine ya pekee. Ndani ya seli za polipu kuna chembe za uhai (seli) za aina maalumu za mwani mdogo zinazoitwa. Kama ilivyo mimea yote mwani mdogo inatumia mwangaza wa jua, maji na hewa ya ukaa ili kutengeneza chakula (mchakato huu unaitwa usanisi mwanga au kwa kitaalamu (photosynthesis)). Sukari hii baadaye hugawanwa kati ya polipu ambaye ni mwenyeji wao. Faida yake ni kuwa polipu hulinda mwani mdogo dhidi ya wanyama wanaokula wengine na kutoa virutubisho pamoja na hewa ukaa. Rangi ya asili iliyomo ndani ya chembe za uhai za mwani ambazo zinafyonza mwangaza wa jua zina rangi inayong’aa sana.

Aina nyingi kabisa za matumbawe huota vyema mahali ambapo joto la bahari ni kuanzia nyuzi joto 23 - 29 sentigredi na hayawezi kuishi katika maji yaliyo na joto la chini ya nyuzi joto 18 sentigredi. Pia yanahitaji maji safi yasiyochafuka ambayo yanapata mwangaza wa jua mwingi na yenye mkusanyiko wa chumvi asilimia 3 - 4. Mahitaji haya maalum yanamaanisha kuwa aina nyingi sana za matumbawe na miamba hupatikana katika bahari za nchi za joto kwenye kina cha mita 2 - 30.

Mwamba wa matumbawe ni nini?

Ni umbo la jiwe kama kiunzi cha mfupa wa polipu ambayo hufanyika kutokana na kalisiamu kaboneti chokaa inayowekwa na polipu wanapokua. Polipu wanapokufa, mifupa yao hubaki na polipu wengine huota juu ya mifupa mitupu, kwa hiyo tabaka jembamba la juu ya matumbawe linalongara ndilo lililohai. Baada ya muda mkusanyiko wa mifupa hii hukua na kufanya umbo kubwa la jiwe linaloitwa koloni la matumbawe. Makoloni ya matumbawe ya aina mbalimbali hukua katika sura tofauti, yaliyotoa matawi kama miti, kama rafu tambarare au kama maduara. Katika kipindi cha karne nyingi makoloni mbali mbali ya ukubwa tofauti, na maumbo na umri tofauti hukua pamoja, na hili hugeuka kuwa mwamba wa matumbawe. Zanzibar inazo kilomita 90 za mraba za mwamba wa matumbawe wa aina tatu. Miamba iliyopinda (fringing reefs) inayopakana na ufukwe unaotenganishwa na mkondo mdogo baina yao. Miamba vizuizi (barrier reefs) imetenganishwa na ufukwe na wangwa, na miamba mabaka (patch reefs) ni miamba midogo, ya hapa na

pale inayopatikana katika nyanga zenye mchanga.

Kwa nini miamba ya matumbawe ni muhimu? Bioanuai – miamba ya matumbawe ni mojawapo ya

mifumo ekolojia tofauti iliyopo kwenye dunia yetu. Kuna spishi zipatazo 845 za mtumbawe yanayojenga miamba duniani kote, ambazo huwapatia makazi maelfu ya samaki wa miamba, chaza na kombe, kaa, kamba koche, spongi na mwani. Miamba ya Zanzibar ni makazi ya mamia ya spishi za samaki wa miamba ya mawe. Bustani ya matumbawe ya kisiwa cha Chumbe lina eneo lililohifadhiwa la Bahari lenye ukubwa wa 0.4 km², lina zaidi ya matumbawe 200 na hawapungui spishi 432 za samaki.

Chakula – Samaki hutoa asilimia 60 ya protini ya

wanyama inayoliwa Zanzibar, na kwa hiyo samaki ni chanzo muhimu cha chakula cha kisiwa hiki. Wengi wa

Muundo polipu wa matumbawe imechorwa © Patterson Clark / Washington Post

Mwamba wa matumbawe ya Chumbe Island Coral Park © Oskar Hendrikson

Page 21: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

19

samaki hawa wanalazimika kuishi sehemu ya maisha yao katika miamba ya matumbawe.

Kipato – Uvuvi ni shughuli kuu ya kiuchumi katika vijiji vya pwani, vikiwa kwa uchache na wavuvi wapatao

34,000 katika Zanzibar. Wavuvi wa Zanzibar huvua samaki wapatao tani 24,000 kila mwaka.

Uzuri wa kimaumbile – Sura na rangi tofauti zinazopendeza za miamba ya matumbawe na samaki wa

matumbawe ni kivutio kizuri sana kwa watalii kuja Zanzibar kuzamia kwa kutumia gesi na kupiga mbizi. Utalii unatoa ajira si chini ya ya watu laki moja wa Zanzibar na asilimia 20 ya pato la taifa la Zanzibar.

Hifadhi – Miamba ya matumbawe hutoa kizuizi cha kimaumbile baharini ambacho huwahifadhi watu wa

eneo la pwani na fukwe za Zanzibar dhidi ya mmomonyoko na mafuriko kutokana na mawimbi ya dhoruba.

Kupunguza kaboni – Polipu wa matumbawe hufanya mifupa yao ya chokaa kutokana na kalisiamu

(calcium) na kaboni (carbon) iliyoyeyuka katika maji chumvi. Mchakato huu, unaojulikana kama upunguzaji wa kaboni, husaidia kupunguza wingi wa hewa chafu katika hewa na kwa hiyo hupunguza kasi ya mabadiliko ya hewa.

Tishio la miamba ya Zanzibar.

Miamba ya matumbawe imekabiliwa na matishio au hatari mbalimbali, hasa zinazotokana na shughuli za binaadamu.

Uvuvi wa kupindukia na uvuvi mbaya – Mahitaji ya samaki

yanaongezeka kutokana na ongezeko la idadi ya watu na idadi ya watalii. Uvuvi wa kupindukia wa samaki, pweza, kaa na kamba ni jambo linalotia wasi wasi. Katika maeneo mengine ya Zanzibar, idadi ya samaki, kombe na chaza wa biashara wanapungua sana kiasi ambacho wavuvi wanawapata wachache. Jambo hili linaleta matatizo zaidi. Kwa mfano samaki aina ya pono hula matumbawe, ambayo huyasaza menoni mwao na kutoa mchanga katika kinyesi chao ambao huchangia katika kukusanya mchanga. Vile vile njia nyingine za uvuvi zinaharibu matumbawe, kama vile baruti utumiaji wa sumu na uvuvi aina ya ‘kigumi’ njia ambayo wavuvi hutumia majiti kuvunja matumbawe na kuwatoa samaki. Njia hizi ni haramu; zinaharibu maeneo makubwa ya miamba na kuua samaki wote waliopo, na sio samaki waliokusudiwa tu. Nyavu zinazokokotwa juu ya miamba zinaleta uharibifu mkubwa, zinapokokotwa juu ya mwamba, na kuinasa na kuivunja vipande vipande. Nyavu nyingi kubwa zimenasa katika miamba na kuachwa hapo hapo katika Zanzibar.

Matukambe – Aina hii ya kiti cha pweza

wenye mikia mingi wanakula polipu wa matumbawe. Kwa kawaida wanyama wanaokula wengine, kama vile aina ya kombe linaloitwa tritoni, huwala hawa matukambe, na kupunguza idadi yao, lakini makombe ya tritoni hupendwa sana na watalii na kwa hivyo hukusanywa kwa wingi na watu wanokusanya makombe, kwa hivyo wameondolewa katika sehemu nyingi na watu wanaofanya biashara ya mapambo ya makombe. Bila ya kuwepo wanyama wanaokula wengine, husababisha mripuko wa maelfu ya matukambe haya ambayo, hufunika miamba na kusababisha uharibifu mkubwa.

Kuogelea kwa kioo na kupiga mbizi – Polipu wa matumbawe wanahisi upesi wanapoguswa na

utapogusa koloni la matumbawe japo kidogo tu, polipu hizo hufa baada ya siku chache. Watu wanaoogelea majini na wapiga mbizi ambao hawana hadhari hurusha mchanga na kuharibu polipu na uharibifu mbaya zaidi hutokea wanapoyakanyaga matumbawe au kukaa juu yake. Inawezekana pia kukojoa majini na kujipaka kwa waogoleaji aina ya mafuta ya kuzuia jua ‘sunscreen’ kuna athari mbaya kwa miamba ya matumbawe ambayo hutembelewa na watalii wengi.

Mashua – Mashua zinapokwama miambani, huvunjika na kuua matumbawe wakati mashua hizo

zinapochukuliwa na mawimbi. Kutia nanga kwenye matumbawe pia kunaleta madhara makubwa kwa sababu sio tu kwamba nanga huvunja matumbawe, lakini pia mnyororo hufanya hivyo unapoyumba. Wenye mashua wanaua matumbawe vile vile wanapoyakanyaga.

Mpiga mbizi akiondoa nyavu iliyotelekezwa kutoka kwenye mwamba wa matumbawe katika Zanzibar © Anne Tarvainen

Kuenea kwa kiti cha pweza katika mwamba wa kisiwa cha Pemba mwamba © Chris Bartlett

Page 22: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

20

Ulikua unajUlikua unajUlikua unajUlikua unajua…?ua…?ua…?ua…?

• Matumbawe mengi yaliyopo yana umri wa kati ya miaka 6,000 na 9000!

• Matumbawe mengi yanakula plankitoni (mimea na wanyama wadogo sana wanaoishi majini) nyakati za usiku, hujificha vikia vyaonyakati za mchana ili wasiliwe na samaki au kuhifadhi mwani mdogo zisipate mwangaza wa jua ambao wanauhitaji kwa ufanyaji wa chakula!

• Ingawaje miamba ya matumbawe huchukua asilimia moja tu ya dunia inapatia makazi robo (asilimia 25) ya samaki wote duniani!

• Thamani ya miamba ya matumbawe duniani inafikia dola bilioni 30 za Marekani!

• Thuluthi moja ya spishi zote za matumbawe duniani zimeorodheshwa kama zipo hatarini kutoweka katika orodha ya IUCN ya orodha ya spishi zilizomo katika hatari yakutoweka.

Uchimbaji wa matumbawe na utengenezaji chokaa –

Matumbawe yaliyo hai yanachimbwa na kutengenezwa chokaa kwa ajili ya ujenzi katika baadhi ya sehemu. Hiki ni kitendo cha uharibifu mkubwa, uharibifu wa makazi muhimu ya miamba ambayo huchukua miongo kadha kuyarudisha. Tatizo jengine ni kwamba tanuri / tanu zinazotumika kwa kutengeneza chokaa zinatumia mkaa wa mikoko, na kupelekea uharibifu zaidi wa rasilimali asili za pwani ya Zanzibar.

Kukusanyika kwa mchanga – Kila ardhi inapokatwa

miti na mikoko inapokatwa kwa ajili ya kupata makazi (nyumba), na kilimo, ndiyo udongo zaidi unapoondoka kwenye ardhi na kwenda baharini hasa nyakati za mvua nyingi na kuyasonga matumbawe yaliyopo karibu. Kuvua kwa wavu pia kunapelekea kukusanyika kwa mchanga kwa sababu matope laini yanakorogeka wakati wa kuvua.

Uchafuzi wa mazingira – Kila idadi ya watu na watalii

wanaotembelea Zanzibar inapoongezeka na ndivyo wingi wa maji machafu, mafuta, uchafu wa kemikali za takataka yatokayo majumbani zinavyoingia baharini. Haya yote yanaharibu matumbawe na viumbe wengine wa baharini.

Kupauka kwa matumbawe na mabadiliko ya hali ya hewa – Mabadiliko ya hali ya hewa yana athari nyngi kwa

miamba ya matumbawe. Licha ya kuwa maji huwa ya moto zaidi, lakini hali ya hewa mbaya hutokea mara kwa mara. Kwa mfano, hutokea dhoruba kali zaidi – ambazo hukata vipande vya matumbawe, kuvuruga matope na mchanga na kupunguza viwango vya chumvi. Maji yanapokuwa ya moto kupita kiasi, tumbawe wa polipu hutoa mwani mdogo katika seli za uhai. Matumbawe hai hupata rangi zao zinazoonekana kutokana na mwani huu kwa hiyo baada ya kutolewa matumbae huwa na rangi nyeupe inayong’ara. Tokeo hili linaitwa upaukaji. Kupauka kwa matumbawe ni jambo baya kwa sababu polipu hupata asilimia 90 ya chakula chao kutokana na mwani. Mara maji yanapokuwa baridi, yanaweza kula tena ‘mwani’, lakini maji yanapoendelea kuwa ya moto, polipu hufa haraka. Upaukaji wa matumbawe limekuwa jambo linalotokea mara kwa mara, na matokeo haya yanaathiri maeneo makubwa zaidi na miamba ya kina cha maji kikubwa kwa kila mara. Ugonjwa wa miamba pia unaongezeka katika baadhi ya matumbawe yenye hali ya joto zaidi.

Kufanyika kwa tindikali katika bahari – Ongezeko la hewa chafu ya kabondioxidi katika anga

inalopelekea mabadiliko ya hali ya hewa pia hufyonzwa na bahari ambako huchanganyika na chumvi iliyoyeyuka na kuifanya bahari kuwa na asidi / tindikali. Baadaye huiyeyusha chokaa ya mifupa ya matumbawe na kuifanya laini zaidi kwa matumbawe kujenga mifupa yao. Kuvunjika kwa miamba kutokana na tindikali ni jambo linalotia wasiwasi sana.

Tunawezaje kuhifadhi na kulinda miamba yetu ya matumbawe?

Kama tulivyokwisha kuona, miamba ya matumbawe ni sehemu muhimu sana ya mazingira yetu. Tunayatengemea kwa mambo mengi. Matumbawe ni muhimu sana lakini pia ni rahisi kuvunjika na yanaweza kuharibika kwa urahisi kwa hiyo ni lazima tufanye kila tuwezalo na tushirikiane kuyalinda na kuyahifadhi.

Waogeleaji, wapiga mbizi na watumiaji gesi chini ya bahari wawe waangalifu wasiguse matumbawe na katu wasisimame juu ya miamba! Ni muhimu kukaa mbali na matumbawe, na kuwa na tahadhari usiyapige mateke matumbawe au kuvuruga mchanga.

Waendeshaji mashua na ngalawa wakae kwenye maji ya kina kirefu, na sio, kwenye miamba ya maji haba, na watie nanga kwenye mchanga au watumie boya lililotulia kuweka alama ya wapi wafunge au kuweka nanga.

Wavuvi lazima waepuke au waache kutumia njia za uvuvi zinazoharibu miamba ya matumbawe: iwapo itaharibiwa samaki watatoweka. Wavuvi washirikiane na (watu) wengine katika jamii katika kusimamia rasilimali kwa kushirikiana, kwa mfano, kwa kuanzisha eneo linalohifadhiwa na jamii ili kuwalinda samaki.

Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!

• Tembelea maeneo ya hifadhi Zanzibar, mengi yana mipango ya elimu kwa ajili ya skuli, jamii, watalii na mengineyo.

• Tembea kwenye ufukwe wenye mawe wakati wa maji kupwa unaweza kuona vitumbawe vinaota katika vidimbwi vyenye mawe.

• Ongea na wavuvi wa eneo lako kuhusu mahali yalipo miamba ya matumbawe na jinsi uvuvi ulivyobadiilka katika miaka kadha.

Page 23: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

21

Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!

• Kamwe usisimame juu ya miamba ya matumbawe!

• Usitupe taka baharini au ufukweni weka taka vizuri; zipunguze, zitumie tena, zirudishe kutengeneza vitu.

• Usitumie njia za uvuvi zenye kuharibu mazingira wala usinunue samaki waliokamatwa kwa mabomu/baruti au uvuvi wa sumu au njia nyengine za kuharibu mazingira.

• Epuka kununua chokaa iliyotengenezwa kwa kuchoma matumbawe hai – tumia vitu vyengine bora kama vile matofali ya udongo, kuni zinaoweza kusarifika, au chokaa iliyotengenezwa kutoka maeneo ya mabaki ya miyamba ya matumbawe na wafahamishe wenzako jinsi wanavyoweza kuepuka shughuli zinazoharibu miamba ya matumbawe.

• Ripoti shughuli haramu za uvuvi kwa viongozi/vyombo vinavyohusika. Uharibifu wa matumbawe ni kuharibu maisha ya watu wa Zanzibar, sasa na baadaye.

• Washawishi viongozi wa eneo kwa kuhifadhi na kulinda zaidi miamba ya eneo lako.

• Usiokote, kununua wala kuuza makombe hasa makombe aina ya baragumu.

Kitunze kidumu – Maeneo ya Bahari

yanayohifadhiwa (MPAs) ambazo rasilimali asili za bahari ni zoni zinazohifadhiwa dhidi ya shughuli zenye uharibifu. Hatua za kuchukua ili kuhifadhi maeneo hayo zinaweza kujumuisha kupiga marufuku njia za uvuvi zinazoharibu au kupunguza idadi ya watalii wanaoruhusiwa kuzamia kwa kutumia gesi chini ya bahari au kupiga mbizi ili kulinda matumbawe ambayo ni rahisi kuvunjika pamoja na makazi mengine ya baharini. Faida yake ni kuwa samaki watapata mahali pa kukaa ambapo wanaweza kukua kwa haraka na kuzaa. Jambo hili kwa kweli linawanufaisha wavuvi kwa sababu huongeza idadi ya samaki katika sehemu za karibu kufikia mita 500 kutoka eneo la hifadhi zinazovuliwa kutokana na samaki kuhamia kwenye sehemu hizo! Matumbawe na idadi ya samaki inafuatiliwa na kuangaliwa, na matukambe wanaondolewa wakati wa kuzuka (wakiwa wengi). Kwa sasa kunasehemu sita za Hifadhi ya Bahari Katika Zanzibar: Kisiwa cha Chumbe (Kilichoanzia 1994, km² 0.4), Mnemba-Ghuba ya Chwaka (ikiwemo Hifadhi ya Kisiwa cha Mnemba (1997, km² 0.15), Hifadhi ya Ghuba ya Menai (1995, km² 467), Hifadhi ya Kisiwa cha Changuu-Bawe (2010), Hifadhi ya Kisiwa cha Tumbatu (2010) na hifadhi ya Mkondo wa Pemba (Ikiwemo Hifadhi ya Kisiwa cha Misali (1998, km² 23)). Maeneo mazuri ya Hifadhi ya Bahari zinaonesha muamko katika maeneo na jamii ziliomo ambazo zinategemea miamba ya matumbawe, kuhusu umuhimu na faida ya miamba ya matumbawe na jinsi gani tunaweza kuhifadhi vizuri.

Pia tunaweza kuyalinda matumbawe kwa kupitia shughuli za ufukweni. Usinunue au kuuza matumbawe au makombe makubwa kama ukumbusho spishi za makome mengi makubwa tayari ni wanyama waliyomo hatarini ya kutoweka na kombe la aina ya baragumu lina jukumu / kazi muhimukatika kuhifadhi matumbawe dhidi ya matukambe!

Misitu, mikoko na nyasi bahari zote hufanya mchanga, matope na udongo utulie zaidi, kwa hiyo tunapaswa kuyahifadhi makazi haya ili kuzuia takataka zisiingie kwenye matumbawe na kuyasokota. Kwa mfano, tumia njia ya kupanda tena miti iliyokatwa kwa ajili ya kuni na sio kukata mikoko.

Maeneo ya Hifadhi ya Bahari ya Zanzibar © Nell Hamilton

Page 24: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

22

6 Uvuvi Ni Yeye (Mwenyezi Mungu) aliyekudhalilishieni bahari mkala kutokana nayo samaki safi na mkatoa

kutokana nayo mapambo mnayoyavaa na mkaviona vyombo vya baharini vikipita juu yake ili kutafuta fadhila zake ili mpate kushukuru. (Qur’an 16:14)

Uvuvi ni nini? Neno uvuvi hutumika kumaanisha harakati au kitendo cha kuvua samaki katika eneo maalum. Uvuvi

hujumuisha uvuaji wa samaki kutoka maeneo ya bahari, maziwa au mito au katika maeneo maalum yaliyotengwa kwa ufiugaji wa samaki. Ama kwa Zanzibar uvuvi hufanyika kwa maeneo ya baharini zaidi. Uvuvi hugawanywa kulingana na aina ya samaki wanaovuliwa, aina ya njia za uvuvi zinazotumika pamoja na mitego, vyombo na pia maeneo ambayo uvuvi hufanyika. Baadhi ya wavuvi huwatumia samaki kwa ajili ya kujikimu, baadhi kwa ajili ya biashara na baadhi kwa ajili ya kujifurahisha.

Ni aina ngapi za uvuvi zinazofanyika Zanzibar? Ziko njia nyingi za uvuvi zinazofanyika Zanzibar. Wavuvi hutafuta aina

mbali mbali za samaki katika maeneo tofauti kwa kutumia mbinu mbali mbali. Wavuvi wengi wa Zanzibar ni wavuvi wadogo wadogo, ambao ambao huendesha shughuli zao katika maeneo ya matumbawe ambayo yapo katika maeneo ya mwambao ambapo usafiri wa kijadi kama vile ngalawa, dau, mitummbwi, mashua vina uwezo wa kufika. Pia mitego ya aina mbalimbali hutumika kama vile madema, uzio, jarife, mishipi n.k. vile vile kuna utamaduni wa kuokota kombe na chaza na wanyama wadogo wadogo wa baharini katika maeneo ya fukwe yanayotokewa na maji. Hili ni maarufu miongoni mwa wanawake na watoto ambao hutumia mazao wayapatayo kwa kujikimu na hata kwa biashara.

Wakati samaki wengi wanaopatikana hutumika kwa kujikimu (chakula) au kuuzwa katika soko la ndani, mahitaji ya samaki yanaongezeka kwani hoteli na migahawa mingi ya kitalii inahitaji samaki wa aina ya hadhi ya juu kama vile ngisi, pweza, kaa, nduaro na nguru. Hivi sasa wawekezaji kutoka nje wanajaribu kuikuza na kuipa uwezo sekta ya uvuvi. Mashua, ngalawa za mashine zinawawezesha wavuvi kwenda mbali zaidi kutafuta samaki, pia nyavu kubwa zinatumika kukamata samaki zaidi ukilinganisha na mbinu za kizamani. Mbinu hizi zinawawezesha wavuvi wa Zanzibar kuwafikia hata wavuvi wa Tanzania Bara. Matumizi ya njia zisizofaa na zisizokubalika kisheria kama vile makorokoro, mishale, bunduki ya majini, sumu, mripuko / baruti, nyavu za kukokota na beach seines umeongezeka pia.

Uvuvi wa burudani 'game fishing' bado haujaenea kwa kiasi kikubwa katika Zanzibar, lakini unaonekana kupata umaarufu kwa watalii. Uvuvi wa samaki kama burudani kwa kawaida hufanyika kwa kutumia boti maalumu kwa kutumia ujiti na mishipi ambayo hukusudia kukamata samaki wa aina mbali mbali kuu kama vile nduwaro, samsuli papa. Kwa Zanzibar, samaki wa aina hizi hutafutwa na wazamiaji hasa watalii ambao hutumia bunduki ili kuwapata hii ni njia haramu hapa.

Kwa nini uvuvi ni muhimu Zanzibar? Jamii zinazoishi katika maeneo ya mwambao kote Zanzibar wanategemea kwa kiasi kikubwa rasilimali za

bahari kwa maisha yao. Watu wengi huishi maisha ya kimila ikiwa ni pamoja na kujitafutia chakula kwa mujibu wa mahitaji. Samaki huwapatia asilimia 98 ya protini wa wale waishio kwa mlo wa kipato cha chini hapa Zanzibar. Kwa familia nyingi samaki hutumika kama ni njia kuu ya kujipatia kipato pia. Takriban wavuvi wapatao 34,000 wanajiajiri katika sekta hii. Kwa kawaida samaki wanaopatikana huuzwa katika soko la ndani. Karibu tani 24,000 za samaki hupatikana kwa mwaka wenye thamani ya shilingi 36 milioni kwa uchumi wa Zanzibar.

Uvuvi pia una umuhimu katika masuala ya utamaduni kwani familia za wavuvi zimeanza vizazi vingi nyuma. Hivyo ni muhimu sana kwa jamii zinazoishi maeneo ya mwambao. Pia inatoa ajira kwa wauzaji na watengenezaji vyombo vya kuvulia na mitego ya kuvulia pia.

Kiasi kikubwa cha utalii wa Zanzibar unaendeshwa kwa kutumia hadhi yake kimataifa ya viumbe wa baharini, kwani watalii wengi huvutika na vyakula vizuri vitokanavyo na mazao ya baharini, michezo ya baharini (kufuta pumzi baharini) na kuzamia kuangalia samaki wa aina mbali mbali wenye rangi za kupendeza, bustani za miamba na mamalia wanaopatikana baharini. Jambo hili huleta ajira nyingi katika Zanzibar ambazo pia zinategemea kuendelea kuwepo kwa rasilimali hai katika maeneo ya mwambao.

Uvuvi asilia aina ya dema © Nell Hamilton

Page 25: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

23

Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?

• Wavuvi kusini ya Unguja walitumia nyama ya pomboo kama chambo cha kuvulia papa. Hii ni kwa sababu nyama yake ina damu nyingi ambayo huwavutia papa. Lakini sasa wananufaika mno kupitia utalii wa pomboo, sasa hawavui tena pomboo!

• Pono wanaweza kuzalisha mchanga. Wanauchukua kutoka kwenye miamba na kuutoa kupitia tundu za choo kama udongo. Samaki mmoja ana uwezo wa kutengeneza kilo 90 za mchanga kwa mwaka!

• ‘Reef balls’ (vitufe vya matumbawe) ni vitufe vya kutengenezwa ambavyo viliwekwa baharini na kufanya makazi ya matumbawe na yanatumika kuhifadhi matumbawe Pemba kote!

• Bioanuwai vinaopatikana katika kisiwa cha Chumbe ni wengi zaidi kuliko wanaopatikana nje ya kisiwa hicho. Kaika km² 0.4 za hifadhi mna miamba 200 na spishi 400 za samaki.

• Pia samaki wapatikanao ndani ya hifadhi ya kisiwa cha Chumbe ni wakubwa zaidi na wengi kuliko maeneo mengine ya nje ya kisiwa, kiwango cha samaki kwa kilomita za mraba kinakisiwa kuwa mara tatu zaidi ya samaki wanaopatikana maeneo ya nje ya kisiwa!

Nini athari zinazokabili uvuvi? kuvua kupita kiasi – Mvuvi yeyote ukimuuliza anaweza

kukwambia kwamba hakuna samaki wengi sasa kama ilivyokuwa hapo kabla, na wanalazimika kusafiri mbali zaidi kuliko walivyokuwa wanafanya kupata kiwango kile kile cha samaki. Kuna sababu nyingi zinazopelekea hali hii zikiwemo hizi zifuatazo: kuongezeka kwa idadi ya wavuvi, kuongezeka kwa vyombo vya uvuvi ambavyo ni vikubwa na wavuvi wanatumia nyavu kubwa zaidi kama vile jarife nyavu kubwa na ushashi zenye macho madogo zaidi, ukilinganisha na zamani. Maji ya Zanzibar pia yanawavutia wavuvi kutoka maeneo mengine (wavuvi wahamiaji) au kwa jina maarufu kama ujulikanavyo uvuvi wa ‘dago’ kwa sababu samaki wa maeneo yakaribu yameshaharibiwa mno. Baya zaidi hadi sasa ni kutumika kwa jarife ndefu zenye urefu wa karibu mita 900 ambazo hutegwa katika bahari yenye kina kirefu ili kukamata samaki kama vile nguru, nduwaro, tuna na samsuli. Pia kuwepo kwa nyavu zinazotegwa chini zenye urefu wa hadi mita 450 ambazo hutegwa karibu sana na maeneo ya fukwe ili kukamata samaki kama vile papa na vinyenga au taa.

Mwanzoni mwa utumiaji wa mbinu hizi samaki wengi walipatikana hivyo, idadi ikapungua. Aina chache tu za samaki wanazaa haraka, na idadi yao ingeweza kurejea haraka baada ya shindikizo kubwa la Uvuvi linaposita, lakini wengi wao wakiwemo papa na chewa huzaa kwa taratibu sana na yawezekana wasiweze kurejea katika hali yao ua awali. Hivyo basi ni muhimu kufahamu ikolojia ya ya samaki ambao tunawategemea na kufuatilia taathira zinazokana na uvuvi kwa ukaribu zaidi. Wanasayansi wanaofuatilia uwepo wa samaki wamethibitisha kile ambacho wavuvi wanakijua: samaki wapatikanao katika maeneo ya ndani ya mwambao wa

Zanzibar ambao tunakula wanazidi kuwa wadogo na wanazidi kupungua kila mwaka. Kama hili halikuzuiwa basi baadae tutakuwa hatuna samaki watakaobaki kabisa!

Mbinu za uvuvi zisizofaa? – Pamoja na kwamba samaki hupatikana wengi zaidi ukilinganisah na zile

mbinu za kizamani, mbinu mpya za uvuvi zina onekana kuharibu zaidi makazi ya samaki. Nyavu za kukokota huyavunja na kuyaharibu matumbawe, na wavuvi wa makokoro na wavuvi wa baruti huyang’oa matumbawe na kuyaacha vipande vipande hali ambayo hupelekea kuuwa kila kitu, vinavyoliwa na visivyoliwa. Miamba ya matumbawe na vitalu vya nyasi bahari yanayoharibiwa kwa njia hizi za uvuvi huchukua miaka mingi kurejea katika hali yake ya awali. Hivyyo njia zote hizi zimepigwa marufuku katika bahari ya Zanzibar, hata hivyo ni vigumu kufuatilia kufanya doria katika bahari kuu na vitendo hivi bado haramu viaendelea katika baadhi ya maeneo.

Kukamata samaki bila kukusudia – Hii ni njia ambayo samaki

hukamatwa kwa bahati mbaya katika mitego iliyowekwa kukamata samaki wa aina fulani. Kwa kawaida katika baadhi ya nchi, samaki wapatikanao kwa njia hii huwa hawahitajiki hivyo hutupwa wakiwa wafu hivyo hakuna anaenufaika, lakini Zanzibar kila kitu kinaliwa. Baadhi ya mbinu za uvuvi kama vile madema huwakamata samaki wachache wa aina hii, lakini baadhi ya mitego kama vile wavu wa kukokota, jarife na nyavu za kutega chini ya maji hukamata samaki wengi zaidi wasiowataka kuliko wale wawatakao. Walio katika hatari zaidi hususan kwa nyavu kubwa ni viumbe wapatikanao baharini kama vile nyangumi, pomboo, nguva na kasa. Matukio mengi ya kukamatwa kwa viumbe vya baharini hapa Unguja hutokea katika nyavu zinazotegwa katika maeneo ya Kaskazini ya kisiwa cha Unguja na idadi kubwa ya pomboo na aina mbali mbali za kasa zinaendelea kupungua.

Kasa walio hatarini sana kutoweka akiwa amekamatwa na kuuwawa katika nyavu iliyotelekezwa visiwani Zanzibar © Nell Hamilton

Page 26: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

24

Nyavu zilizotelekezwa – Iwapo mvuvi atapoteza madema kwa sababu ya kuharibika au kupotea kwa

boya, basi mtego ambao umetengenezwa kwa nyenzo za kimaumbile, taratibu nyenzo hizo huanza kuteketea. Lakini cha kusikitisha ni kwamba nyavu za kisasa zimetengenezwa kwa kutumia nyenzo ambazo haziwezi kuvunjika au kuoza, hivyo ikiwa zitapotea zitaendelea kukamata na kuua viumbe wa baharini kwa karne nyingi.

Uchafuzi wa mazingira – Athari za uchafuzi wa mazingira katika

uvuvi zinaweza kuwa mbaya sana. Samaki wanaweza kukutana na vipande vya plastiki wakavila. Vipande hivi vya plastiki huziba matumbo yao na hufa kwa njaa. Maji machafu yasiyotiwa dawa yanaweza kuchafua vyakula vya baharini vipatikanavyo katika maeneo ya fukwe ambapo vikitumiwa vinaweza kusambaza maradhi yanayouwa kama vile kipindupindu na homa ya matumbo. Kemikali za sumu zipatikanazo kwenye madebe ya takataka, wakulima wanaotumia mbolea za kemikali na madawa ya kuulia wadudu, zinazoingia baharini ambazo hujijenga katika tishu za viumbe wa baharini wanavyovila, hivi vinaweza kusababisha ugumba, kensa, na maradhi mengine kwa samaki na binaadamu, na pia vinaweza kusababisha vifo. Kiwango cha sumu huongezeka kila mfuatano wa chakula unavyopanda, hivyo kuendelea kuleta madhara kwa watu wanaotumia samaki waliobeba vimelea, watoto ndio hasa walio katika hatari zaidi.

Vipi tunaweza kulinda uvuvi wa Zanzibar? Zanzibar si nchi ya mwanzo kukutwa na changamoto kama hizi, na ziko njia nyingi za utatuzi ambazo

zimetumika kwa mafanikio katika maeneo mengine. Iwapo watoto au watu wazima, mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu, tunaweza kusaidia kulinda Uvuvi wetu na kuhifadhi uwezo wa kuishi kwa vizazi vijavyo.

Maeneo ya hifadhi ya bahari (MPAs) – Kama ilivyo kwa matumbawe, njia moja nzuri zaidi ya kutunza

mazalio ya samaki ni kuanzisha maeneo ya hifadhi ya baharini, maeneo ambayo shughuli za uvuvi zitapigwa marufuku. Maeneo haya huhifadhi matumbawe, mikoko na nyasi bahari ili yasiharibiwe: hii itasaidia kuhifadhi maeneo ambayo samaki watazaliana na itakuwa ni kama vitalu kwa samaki wadogo kuweza kukua. Watatoa chakula kwa aina nyengine za samaki, na itakuwa ni eneo la hifadhi kwa aina nyengine za samaki ambazo ziko hatarini kutoweka. Katika baadhi ya maeneo ya hifadhi, uvuvi hupigwa marufuku, wengine huruhusu ili watu wavue kujikimu tu na sio kwa kutumia njia zisizofaa za uvuvi. Kwa kawaida maeneo haya huwa katikati ya maeneo ambayo uvuvi unaruhusiwa. Uvuvi huzuiliwa kwa baadhi ya nyakati ili kudhibiti aina fulani ya samaki wakati wa kuzaliana kwao lakini watu huruhusiwa kuvua bada ya muda fulani. Kwa hivi sasa hapa Tanzania asasi nyingi za kiraia zimeanzishwa na vikundi vya wavuvi ili kuwawezesha kupata samaki wa kutosha sasa na kuhifadhi mazalio ya samaki kwa ajili ya baadae.

Ingawa uvuvi huzuiliwa katika maeneo ya hifadhi, kwa ujumla wanaonufaika ni wavuvi. Huwapa samaki hifadhi na chakula cha kutosha ambapo hukua kwa ukubwa wa kuridhisha bila ya kuvuliwa. Huzaliana vizuri na hukua kwa haraka, na huzaliana kwa wingi na hukuza hifadhi. Baada ya kukuwa vizuri baadhi ya samaki huhamishiwa katika maeneo ya karibu na hifadhi ambapo uvuvi huruhusiwa. Hivyo samaki wapatikanao maeneo ya karibu na hifadhi huwa ni wakubwa zaidi na ni wengi kuliko wanaopatikana mbali na maeneo hayo. Hali hii hujitokeza karibu mita 500 kutoka eneo la hifadhi na ni eneo maarufu sana kwa wavuvi. Na hii ndio maana wavuvi wengi huvua nje kidogo ya eneo la hifadhi katika kisiwa cha Chumbe. Hii ni kwa sababu wanajua watapata samaki zaidi kuliko watakapovua maeneo mengine na pia watapata pesa zaidi. Bila shaka maeneo ya hifadhi yanahitaji kuchungwa sana ili kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa na jamii zinanufaika kutokana na maeneo ya hufadhi. Hivyo basi hili litafanyika zaidi iwapo kutakuwa na mfumo wa kuishirikisha jamii katika utekelezaji. Mpango wa udhibiti wa maeneo ya pwani lazima uhakikishe kwamba matumbawe, majani ya pwani na mikoko vyote vinahifadhiwa. Kanuni zilizowekwa kulinda bidhaa ya samaki lazima zitumike na kufanyiwa kazi ipasavyo.

Kusaidia mfumo wa uvuvi endelevu – Wavuvi wanaweza

kusaidia uvuvi uwe na faida kwa kutumia mbinu endelevu na pia kusaidia kuwaelimisha wenzao kufanya hivyo. Kwa mfano:

• Acha kukamata makundi adimu ambao hawazaliani kwa haraka, kama vile papa, taa vinyenga, nduwaro na samaki ambao ni muhimu kiikolojia kama vile pono, kikande na tritoni.

• Tumia nyavu zenye macho makubwa ili kuepuka kukamata samaki wachanga.

• Epuka kuharibu matumbawe kwa kutumia nanga, boti, nyavu, na mitego mengine au hata kutembea tembea juu yake.

Watoto hukusanya samaki wa magamba katika pwani ya Zanzibar © Nell Hamilton

Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!

• Tembelea bandari ya samaki kama Malindi au Mkokotoni – au ufukwe ulio karibu.

• Tembelea masoko ya samaki ya Chwaka, Matemwe, Uroa, Darajani, Nungwi au Pwani Mchangani.

• Ongea na wavuvi katika familia yako na jamii kuhusu jinsi mitego na njia za uvuvi zilizobadilika.

Page 27: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

25

Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!

• Saidia katika kuongeza mwamko:waambie marafiki,jamaa na wafanyakazi wenzako kuhusu umuhimu wa Uvuvi endelevu.

• Usidondoshe takataka, zirejeshe zitumike tena.

• Usijisaidie maeneo ya fukwe. Tumia vyoo vilivyo mbali na vyakula.

• Epuka maradhi hatari kama vile kipindupindu au homa yamatumbo kwa kuokota chaza na makorobwe katika fukwe zilizo safi tu, zilizo mbali na yanapotoka maji machafu.

• Ungana na vikundi vya kijamii kuishawishi serikali iongeze bidii katika kushughulikia takataka na kujenga vyoo vya umma ili kuepusha takataka kutupwa baharini.

• Mwandikie Sheha wako au mbunge ili kumfahamisha kwamba Uvuvi endelevu una umuhimu mkubwa.

• Kamwe usivue samaki ambao wako katika hatua ya kuzaliana.

• Tumia mbinu bora za uvuvi ili kuepuka kukamata samaki usiowahitaji hususan mamalia (pomboo, nguva na nyangumi) wa baharini na kasa.

• Hakikisha kwamba mitego yako haipotei kirahisi baharini.

• Heshimu maeneo ya hifadhi yaliyopo na ungana na wavuvi na wanajamii wengine kuanzisha maeneo ya hifadhi au maeneo tengefu ili kulinda mazalio ya samaki kwa ajili ya baadae.

Maisha mbadala – Kwa kadri idadi ya watu inavyoongezeka hapa Zanzibar,

watu wanahitaji njia endelevu ili waishi bila kuharibu mazalio ya samaki yanayoteketea. Katika kulifanikisha hili mambo mengi yanaendelea kujitokeza:

Kwanza, kilimo cha mwani: Kilimo hiki kimeeenea takriban maeneo mengi ya

Zanzibar ambapo asilimia kubwa ya wakulima wa mwani ni wanawake ambao huotesha mwani kwa kutumia kamba na vijiti katika maeneo ambayo maji hupwa na kujaa kwa ajili ya kusafirisha nje. Hii ni njia moja muhimu ya kujitafutia maisha ambayo huzalisha zaidi ya tani 7000 kwa mwaka.

Pili, ufugaji kaa: Baadhi ya jamii huwakusanya kaa wadogowadogo na

kuwaweka katika eneo la mikoko na kuwazunguushia nyavu au vijiti ili kuwalinda na maadui zao. Humo kaa hupewa chakula chenye wanga wa kutosha hivyo hufikia kiwango cha kuuzwa kwa haraka.

Ukulima wa lulu: Wanajamii wengi katika Ghuba ya

Fumba hulima lulu kwa kutumia chaza wanaowapata katika maeneo yao ikiwa ni njia moja ya kujipatia kipato. Soko kwa ajili ya lulu zinazozalishwa Zanzibar linapatikana kupitia maelfu ya watalii wanaotembelea Zanzibar kila mwaka, lakini ni muhimu kuhakikisha ya kuwa chaza wanaendelea kuwepo. Ili kutekeleza hili vijiji vinavyofanya shughuli hii hapa Zanzibar vimeanzisha maneo tengefu.

Utalii endelevu: Njia muhimu sana ambayo maeneo ya

hifadhi huongeza pato la kaya ni kwa kuzalisha ajira mpya. Kwa kupitia watu kama vile; msimamizi wa

maeneo ya hifadhi, manahodha wa boti, wana mgambo, waongozaji katika masuala ya kupiga mbizi, wahudumu wa hoteli na waongozaji katika masuala ya kuvua. Mbali na hayo, watalii hutupatia soko kwa kazi za mikoko zinazotengenezwa kwa kutumia maligahafi za ndani.

Uvuvi wa burudani: Huu uvuvi kwa njia ya michezo

amba baada ya kupigwa picha samaki waliokamatwa huachiwa wakiwa hai na hurejeshwa baharini.

Matendo ya watumiaji – Ili kuunusuru uvuvi lazima

sote tufanye kazi kwa pamoja kuhakikisha kwamba uvuvi unafanyika katika utaratibu endelevu ili watu waweze kujipatia mahitaji yao kutokana na rasilimali za kimaumbile na waweze kusaidia familia zao kwa sasa na pia vizazi vijavyo. Ikiwa kila mmoja ataonesha mwamko katika jamii yake na kuwasaidia wavuvi ambao wanavua samaki kwa njia endelevu, basi makundi ya samaki adimu yangebaki na samaki wa kutosha wangeendelea kuzaliana. Hebu tujenge kawaida ya kuuliza ni vipi samaki wamepatikana, na tuache kununua samaki adimu, wadogo, au samaki waliopatikana kwa kutumia mitego iliyopigwa marufuku mitego ambayo huwafanya watu wa kawaida wakose shughuli ya kufanya na kuhatarisha vizazi vijavyo kukosa kabisa kutumia samaki watokanao na mazingira yao. Hasa katika maeneo ya mikahawa tutoe mwamko kwa wafanyakazi na tubuni mbinu mbadala za kuwafanya samaki waliomo hatarini kutoweka wasiingie katika orodha ya vyakula mahotelini na baharini.

Mkulima wa mwani Zanzibar © Nila Uthayakumar

Lulu za Fumba © Narriman Jiddawi

Page 28: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

26

7 Uchafuzi wa mazingira

Ufisadi (ikiwemo uchafuzi wa mazingira) vimekithiri nchi kavu na baharini vikiwa ni matokeo ya matendo maovu ya binadamu. Ameamuru ili waonje matunda ya yale waliyoyatenda ili wapate kujirekebisha.

(Qur’an 30:41)

Uchafuzi wa mazingira ni nini? Uchafuzi wa mazingira ni uchafu wenye madhara katika mazingira ya kimaumbile. Vitu vinavyochafua

mazingira vinaweza kuwa vitu vigumu, vitu vya maji maji na hata hewa. Vyote hizi vinaweza kuleta madhara kwa sehemu zote za mazingira kama vile ardhi, maji baridi, bahari na hewa; udongo tunaotumia kupanda vitu, maji tunayokunywa na mahali tunapovua, na hewa tunayovuta. Zamani takataka nyingi zilikuwa za kimaumbile na zilikuwa zikioza kwa urahisi na kutoweka kabisa, lakini sasa vitu vingi vinavyotengenezwa na mwanadamu vinaweza kudumu kwa maelfu ya miaka katika mazingira ambayo huleta madhara kwa wanyama na sisi binadamu pia.

Takataka ngumu – Uchafuzi wa mazingira unaotokana na takataka ngumu ndizo huonekana kwa uwazi

zaid. Nyingi ya hizo ni takataka: takataka zitokazo majumbani na maeneo ya biashara ambazo zimetupwa katika sehemu mbali mbali. Maji machafu pia ni aina ya takataka ngumu na yanachafua mazingira kama hayashughulikiwi ipasavyo.

Uchafu wa maji maji na udongo – Vitu vya majimaji kama vile kemikali, mafuta, na uchafu mwengine

unapoachiwa kusambaa katika mazingira, huingia katika udongo, maji yaliyoko chini ya ardhi na pia baharini. Vile vile, takataka zilizooza kutoka katika majaa, na mavumbi ya takataka zilizochomwa huwa na kemikali za sumu ambazo hufyonzwa wakati wa mvua. Vitu hivi vingi ni sumu kwa wanyama na binaadamu. Vitu vya oganiki vinavyooza kutokana na takataka na vitu vinavyotoka kwenye kilimo vina naitreti ambayo huufanya udongo na maji kua haufai kwa jamii muhimu za kimaumbile, hususan misitu, miamba ya matumbawe na nyasi bahari kwa sababu nitreti husaidia ukuaji wa mwani ambao huyafanya maji yawe na ‘mawingu’ na kuzuia mwanga usipite chini ya bahari.

Uchafuzi wa hewa – Asilimia kubwa ya uchafuzi wa hewa unatokana na vitu vinavyochomwa moto.

Moshi una kaboni monokside (hewa mkaa) ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya hali ya hewa. Moshi utolewao na vyombo vya moto una hewa nyingi zenye madhara kama vile, salfa, nitrojini dioksidi na haidrokabon amabayo ni sumu. Uchomaji wa plastiki husambaza gesi za sumu hewani. Njia nyengine za uchafuzi wa hewa ni uozaji wa takataka ambazo huzalisha mitheni ambayo ina madhara zaidi kuliko gesi ya ukaa.

Mkusanyiko wa sumu katika viumbe – Wanyama wanapokula vitu vyenye takataka ambavyo haviwezi

kuvunjika vunjika, haviwezi kusagika baada ya kuliwa, hujikusanya ndani ya mwili wa mnyama huyo. Wakati mnyama yule anapoliwa na mwengine zile takataka za sumu zinazidi kujikusanya. Takataka hizi hukuwa kadiri mfumo wa chakula unavyokuwa, hivyo basi walaji wenzao wakubwa wa mwisho kabisa: samaki, ndege, mamalia wa baharini na binadamu – hasa watoto – wanaweza kuathirika vibaya sana.

Ni vipi uchafuzi wa mazingira unaiathiri Zanzibar na Wazanzibari? Takataka ngumu – Jamii nyingi na wafanyabiashara kadhaa ndani ya Zanzibar, hawana utaratibu mzuri

wa ukusanyaji wa takataka ngumu, hivyo barabara zetu nyingi na maeneo mengi ya jamii zetu huchafuliwa kwa mifuko ya plastiki na chupa, makopo ya mabati, matambara, betri mbovu, mipira na nepi. Hili ni jambo baya sana; ni jambo la mwanzo watalii wanaliona kwa urahisi sana na hurudi makwao wakiwa na dhana kwamba hatuyajali mazingira yetu. Pia linaweza kusababisha madhara makubwa kwa mazingira yetu. Madhara hayo si kwa yale maeneo ambayo takataka hizo huonekana tu, lakini hupeperushwa na upepo, nyengine hukokotwa na maji wakati wa mvua hadi kufikia baharini, nyengine hubaki katika maeneo ya fukwe, nyengine hunasa kwenye matumbawe na nyengine huliwa na viumbe hai wakidhani ni chakula.

Plastiki: Plastiki huchukua maelfu ya miaka kuharibika na zina madhara popote zitakapokuwepo iwe ni

ardhini au baharini. Takatka za plastiki huliwa na ng’ombe, mbuzi, na hata punda. Vipande vya polisterini na vishungi za sigireti huliwa na ndege na samaki na mifuko ya plastiki huliwa na kasa wakidhani ni makonyeza. Plastiki huziba matumbo ya viumbe hawa hivyo, huweza kusababisha vifo vyao. Mifuko na chupa hukokotwa na maji kwenye mitaro hadi baharini. Mifuko ya plastiki huzizonga nyasi bahari na huweza kunasa kwenye matumbawe na kuyavunja. Nyavu za plastiki zilizotelekezwa hukwama katika miamba na huendelea kuua samaki, kasa na viumbe wengine wa baharini.

Mipira ya gari: Mipira ya gari ya zamani huhifadhi maji ambayo ndani yake mbu waenezao malaria

huzaliana. Pia kuchoma mipira ya aina hiyo huzalisha moshi wenye sumu.

Vioo: Vioo vinaweza kuwa chanzo cha moto katika majani makavu, na vioo vilivyovunjika vinaweza kuleta

madhara kwa watu, wanyama na hata kutoboa mipira ya vyombo vya barabarani.

Page 29: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

27

Je UlijuaJe UlijuaJe UlijuaJe Ulijua…?…?…?…?

• Takataka ni moja kati ya mambo matatu makubwa yanayolalamikiwa na watalii?

• Vishungi vya sigara huchukua takriban miaka 65 kuoza.

• Mripuko wa maradhi ya homa ya matumbo katika jamii fulani ulisababishwa na tabia za watu hao kujisaidia katika maeneo ya fukwe.

• Urejeshaji wa makopo vya vinywaji na vyakula huchukua asilimia tano (5%) ya nishati ya kutengeneza vipya.

• Aina mbili za ndege wapatikanao Pemba tu wamekuwa wakitoweka kwa sababu ya kunguru waliovamia visiwa vya Unguja na Pemba.

Mabati: Vipande vya mabati au misumari yenye kutu inaweza kusababisha madhara mengi kama vile

kuwakata watoto au wanyama. Mabati huchukua muda mrefu kuharibika hivyo hutoa madini ambayo ni hatari sana kwa mazingira, madini ambayo huingiza sumu katika ardhi na pia kwenye maji.

Mbao: Mbao ni vitu vya kimaumbile ambavyo huharibika kwa haraka. Hata hivyo bidhaa za mbao

zilizopakwa rangi au zilizotiwa dawa huchukua muda mrefu kuharibika na kemikali zinazopatikana ndani yake huwa ni sumu kwa viumbe hai. Bidhaa za mbao zinazopatikana zikielea baharini pia ni hatari kwa vyombo vya baharini kama vile boti. Mbao hupatikana kutokana na miti hivyo, kununua na kuuza mbao kunasababisha upungufu wa miti hapa kwetu na kwengineko.

Karatasi na kadi: Kama mbao, hatimaye hizi nazo zitaoza, lakini hata zikifikia hatua hiyo huwa tayari

zimeshasambaa maeneo mengi sana na ni mbaya.

Vyombo / vifaa: Vitu vyote vinavyotumika kutengenezea vyombo na vifaa kama vile betri, vioo na plastiki

vina uwezo wa kuleta madhara kwa mazingira yetu. Vyombo na vifaa vinavyotelekezwa navyo ni vibaya sana. Mafriji na mafriza ya zamani yana hewa ambazo zinachafua mazingira na watoto wanapocheza wanaweza kunasa ndani yao.

Betri: Betri zina kemikali za sumu kama vile zebaki, risasi na tindikali. Betri za simu za mkononi zina

nikeli (nickel) na kadimiam ambazo husababisha saratani. Betri zinapotupwa kwenye mashimo gesi zinazochafua hewa hutoka taratibu; iwapo zitachomwa moto hutoka kwa haraka katika moshi na majivu yatokanayo na moto. Metali nzito kama makyuri hujijenga katika samaki wa magamba, na kuwa sumu, ambayo huweza kutufikia sisi tunapowala.

Maji machafu: Zanzibar haina mfumo wa kushughulikia maji machafu ili yawe salama. Katika maeneo ya

Mji Mkongwe na Maruhubi na maeneo mengine mashimo, mabomba ya maji machafu yatokayo majumbani huelekezwa moja kwa moja baharini. Katika maeneo ambayo hakuna mitaro, watu hutumia vyoo vya shimo, lakini wakati wa kuvisafisha maji machafu hayo kwa kawaida humwagwa katika maeneo yasiyokaa watu; vinginevyo watu hawana hiari ila hufanya haja zao katika maeneo ya misitu na fukwe. Pia watu wana tabia ya kutupa nepi chafu katika maeneo ya fukwe, katika Zanzibar yote. Mbali ya kuwa jambo hili halifurahishi lakini pia ni hatari sana. Watu wanaotembea, watoto wanaocheza, wengine huokota kombe na chaza baharini na wengine hulima mwani katika fukwe hizi, au watu wanaokula kombe na chaza zilizookotwa katika fukwe hizi wanakutana na kinyesi kinachoweza kuwasababishia magonjwa kama vile kipindupindu, homa ya matumbo, uvimbe wa ini unaoambukiza vimelea vya maradhi haya vinaweza kupatikana kupitia uchafu wa binaadamu ambao haukushughulikiwa. Vimelea pia huweza kujikita ndani ya maji ya chini kwa chini hivyo kuyafanya maji yetu ya kunywa yasiwe salama.

Kinyesi cha wanyama: Kinyesi cha wanyama hunuka vibaya mno na ni kivutio cha wadudu waharibifu

kama vile inzi. Pia kuna baadhi ya vimelea wabaya ambao hupatikana kutokana na kinyesi kilichoambukizwa.

Uchafu mwengine mgumu: Uchafu mwengine unaotokana na viumbe hai kama, samaki na mboga huoza,

lakini unaweza kusababisha matatizo. Wakati unapotupwa huoza katika marundo ambako huwa hakuna hewa hali ambayo huzalisha gesi ya mitheni ambayo ni hatari sana kimazingira. Ikiwa takataka hizi zitaoza katika maeneo ya wazi huwa kivutio kwa panya ambao huchukua maradhi kunguru ambao huua mamia ya ndege wetu wa asili.

Uchafu wa maji maji na udongoi – Maji huchafuliwa na

kaya na viwandani. Takataka zilizooza katika majaa mbali mbali na moshi unaopatikana baada ya kuchoma takataka yana kemikali za sumu ambayo huyeyuka wakati mvua inaponyesha. Vitu vya usafi vinavyotumika kusafishia vitu vya majumbani, kemikali mbalimbali zinazotumika katika michakato ya viwandani, na dawa za kuulia wadudu zinazotumika mashambani, zote hizi hufyonzwa katika udongo na kuathiri ukuaji wa mimea, na kuingia katika maji ya chini ya ardhi na kuchafua maji tunayokunywa na kufikia baharini ambapo huingia katika viumbe na kusababisha matatizo ya afya kwa wanayama na watu wanaowala.

Mafuta: Kuna aina nyingi za mafuta ambayo husababisha

matatizo maalum. Mafuta hutumika katika mapishi na humwagwa. Aina nyengine za mafuta humwagwa majumbani na pia katika magereji. Iwapo mafuta haya yatamwagwa kwenye mitaro ya kupitishia maji yatafikia katika maji ya chini ya ardhi na hatimaye baharini ambako huingiza sumu viumbe wa baharini wakiwemo samaki na kombe na chaza ambao

Page 30: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

28

tunawala. Mafuta yanayotokana na injini, petroli na dizeli hutolewa kutoka kwenye mashine za vyombo mbali mbali vya usafiri na kutoka melini wanaposafisha matangi yao ya mafuta. Haya huzisonga nyasi bahari, matumbawe, na mwani uliopandwa. Ndege wa baharini hufunikwa na mafuta hayo, kasa na mamalia wa baharini hushindwa kuvuta hewa. Mabaki ya mafuta hayo iwapo yatafikia maeneo ya fukwe kombe na chaza wanaathirika kwa sumu pia, na fukwe haziwezi kutumiwa tena na watalii au hata wenyeji, ni vigumu kuzisafisha. Umwagikaji wa mafuta kutoka melini hutokea kwa nadra lakini unapotokea husababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira.

Uchafuzi wa hewa – Kukosekana kwa utaratibu mzuri wa ukusanyaji takataka, watu wengi hulazimika

kuchoma takataka zipatikanazo majumbani mwao au maeneo ya biashara, wengi kati yetu hupika kwa kutumia kuni au mkaa. Ni kinyume kiafya kuvuta moshi wa aina yoyote kwani unaweza kusababisha ugonjwa wa mapafu na hata saratani. Lakini kubwa hasa ni moshi utokanao na kuchomwa kwa plastiki, mipira au betri na gesi zitolewazo na vyombo vya usafiri. Harufu mbaya, hususan harufu ya makaro, na harufu ya takataka zinazochomwa ni hatari kuishi nazo na hukimbiza watalii.

Nini kasoro ya hatua zinzochukuliwa sasa? Kutupa takataka baharini – Wakati athari za kutupa takataka baharini ni vigumu kuziona, kuna taathira

mbaya sana kwa viumbe waishio baharini ikiwa na maana rasilimali za baharini ambazo tunazitegemea. Mara nyingi ni upotezaji wa wakati pia, kwa sababu nyingi ya takataka hizo husukumwa tena ufukweni inapotokea dhoruba kubwa. Takataka zisizoshughulikiwa hubeba vimelea na kuchafua fukwe na chakula kipatikanacho baharini.

Uchomaji moto – Takataka za baadhi ya bidhaa zinaweza kuchomwa kwa usalama kabisa, hata hivyo,

uchomaji wa plastiki, mabaki ya vitu mbalimbali, mipira na betri huzalisha moshi na majivu yenye sumu. Mioto inayowashwa katika sehemu za wazi, pia huwa ni chanzo cha mioto myengine ambayo huharibu majumba, biashara na kuuwa watu. Hewa ya ukaa inayotolewa pia ina madhara makubwa kimazingira.

Kufukia kwenye mashimo – Takataka ziinazokusanywa Mji Mkongwe hupelekwa kwenye majaa ya

baraza la mji na katika majaa ya jamii kama vile Jumbi kwa Unguja, lakini hakuna utaratibu wa baraza la mji kukusanya takataka kwa baadhi yamaeneo. Vimelea vya magonjwa na kemikali zitokanazo na uchafu (zikiwemo takataka kutoka hospitalini), hupenya ndani ya maji yaliyo chini ya ardhi. Majaa haya hayafunikwi hivyo, huwavutia panya na kunguru matokeo yake mifuko ya plastiki hupeperuka huku na kule. Kutokana na wingi wa mkusanyiko wa takataka, takataka hizo huoza bila ya hewa, kwa hiyo hutoa hewa aina ya mitheni amabayo ina madhara mara nne zaidi kimazingira ukilinganisha na hewa ukaa (dioksidi ya kaboni). Mashimo ya majaa hatimaye hujaa – ili kutoa nafasi kwa takataka nyengine, takataka zilizopo huchoma jambo ambalo ni hatari na haliwafurahishi wanajamii ambao hulazimika kuvuta moshi wenye madhara na unaonuka vibaya.

Tunawezaje kusafisha Zanzibar? Uchafuzi wa mazingira unaendelea kuathiri afya zetu, unaharibu rasilimali ambazo tunazihitaji, unaathiri

shughuli ambavyo tunavitegemea kama vile uvuvi na utalii. Sasa nini tunaweza kufanya kulibadilisha hili?

Punguza – Tunahitaji kupunguza viwango vya takataka tunazozizalisha. Iwapo hatuzizalishi, hatutakuwa

na tatizo la takataka kulitatua. Kwa lugha nyepesi au rahisi tupunguze vitu tunavyonunua. Jiulize, ‘Je kweli mimi nakihitaji kitu hiki?’ unapokwenda dukani. Chagua bidhaa ambazo zinahitaji kufungwa kidogo, kwa sababu vitu vya kufungia vyote hugeuka kuwa takataka.

Tumia tena – Tumia bidhaa unazozihitaji mara nyingi zaidi ya unavyoweza. Kama kitu kimeharibika

kifanyie matengenezo badala ya kununua kipya. Vitowe vitu ambavyo huvihitaji tena. Andaa eneo la mauzo kwa ajili ya wanajamii; watu wawe wanaleta vitu vikongwe kama vile, vitu vya kuchezea watoto, nguo, samani na vitu vyengine ambavyo hawavihitaji tena; majirani wanaweza kununua au kubadilishana baina yao. Pia unaweza kuokoa pesa.

Rejesha upya – Kwa kutumia ubunifu mdogo tu, takataka nyingi

zinazozagaa mitaani mwetu na sehemu za fukwe zinaweza kurejeshwa upya. Hili linaweza kuwa kwa kiwango kidogo ambapo wenyeji wanaweza kutengeneza vitu vizuri vya kuviuza kwa watalii. Vitu vingi vinaweza kurudishwa upya siku hizi kupitia viwandani vikiwemo plastiki na vioo, pia vituo vya ukusanyaji wa bidhaa zinazohitaji kurejeshwa upya vinaendelea kuanzishwa na wananchi wengi Zanzibar kote. Kwanza vitu hupangwa kwa mujibu wa nyenzo zilizotengenezewa, kisha kila kitu hukatwakatwa kwa kutumia mashine. Baadae vitu vilivyokatwakatwa vizuri husafirishwa nje ya nchi ambako hutumika tena kutengenezea bidhaa mpya. Hebu uliza vituo vya urudishaji upya vilivyo karibu yako ni vitu gani wanavyokusanya.

Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!

• Jumbi kwenye jaa la taka

• Mtaa wowote au ufukweni

• Maruhubi

• Wesha na Mtoni

• Micheweni

• Soko la samaki Malindi

• Kituo cha urejeshaji plastiki

Page 31: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

29

Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!

• Usidondoshe takataka!

• Usitumie mifuko ya plastiki – chukua mkoba au mfuko wa kitambaa unapokwenda dukani.

• Jaza tena maji na zitumie tena chupa za maji.

• Tumia nepi za kitambaa ambazo zinaweza kuoshwa na kutumika tena badala ya nepi za plastiki ambazo lazima zitupwe.

• Shiriki katika usafi wa jamii na ufukwe.

• Vifanyie huduma za kiufundi vyombo vyako kwa muda maalum ili kuhakikisha kuwa vinachoma mafuta vizuri, na visiwe vinatoa moshi mwingi mweusi wenye madhara.

• Shawishi Serikali kuboresha ukusanyaji wa takataka na kutumia tena vifaa vilivyotumika zamani.

• Punguza, tumia tena, rejesha vitumike tena! Orodha ifuatayo inakujulisha kitu bora cha kufanya kwa takataka za nyumbani, njia mbadala zinazokubalika na nini unaweza kufanya kama ni jambo la mwisho kama hakuna lingine la kufanya na nini usifanye kabisa, kwa sababu ni hatari kwa afya yako!

Nini la kufanya

kwa uchafu

Pu

ng

uza

Tu

mia

ten

a

Reje

sh

a

mb

ole

a

Ch

aku

la c

ha m

nyam

a

Ch

om

a

Sh

imo

ni

Tu

mb

ukiz

a b

ah

ari

ni

���� Chaguo bora � Inakubalika � Chaguo la misho ���� Hatari

Plastiki ���� ���� ���� ���� ���� ���� � ���� Mpira ���� ���� ���� ���� ���� ���� � ���� Kioo ���� ���� ���� ���� ���� � � ���� Metali ���� ���� ���� ���� ���� � � ���� Mbao ���� ���� ���� � ���� ���� � � Karatasi / kadi ���� ���� ���� � ���� � � � Nguo kongwe ���� ���� ���� � ���� ���� � ���� Vifaa ���� ���� ���� ���� ���� ���� � ���� Betri ���� ���� ���� ���� ���� ���� � ���� Uchafu wa mimea � � ���� ���� ���� � � � Uchafu wa nyama / samaki

� � ���� ���� � � � �

Kinyesi cha wanyama � � � ���� ���� � � ���� Nepi na pedi ���� ���� ���� ���� ���� � ���� ���� Mafuta na petroli ���� � ���� ���� ���� ���� � ����

Hadi Zanzibar itakapokuwa na kituo cha urudishaji vitu vyote, kutakuwa na wakati huwezi kupunguza, kutumia tena, wala kurudisha upya – kama hilo litatokea utafanya nini?

Mbolea / mboji – Takataka zitokanazo na mabaki ya vitu vya

kimaumbile vilivyooza kama vile mabaki ya chakula, takataka za bustani na hata vipande vya karatasi, vitu hivi huweza kufanywa mbolea. Mbolea ni kiboreshaji bora kabisa cha udongo ambacho huipatia mimea inayoota virutubisho na husaidia katika kuzuia maji. Unaweza kufanya mbolea ya chakula kilichopikwa lakini ni lazima vizikwe chini sana ndani ya

rundo ili kuepusha kuwa kivutio kwa wadudu waharibifu kama vile panya na kunguru. Pia unaweza kufanya mbolea ya kinyesi cha ng’ombe, mbuzi na hata punda. Kwa usalama kinyesi cha mbwa, paka na binaadamu kitaoza pia lakini vinaweza kusambaza maradhi hivyo, usiviweke katika marundo yako ya mbolea.

Kuchoma moto – Wakati kuchoma

baadhi ya vitu ni vibaya, kuchoma baadhi ya vitu vya kimaumbile kama vile mbao/magogo, mimea, mifupa, mabaki ya chakula au kinyesi cha wanyama, vinaweza kuchomwa. Unapochoma takataka fanya hivyo katika hali ya usalama kabisa. Uache moto mdogo na usiuache bila ya uangalizi, tafuta eneo ambalo liko mbali na majumba na pia ambalo hakuna miti au eneo ambalo upepo hauwezi kupulizia upande wao, na usiwashe moto katika kipindi cha jua au upepo mkali sana. Katu usichome betri, mipira, viondoa harufu au plastiki kwa kuzingatia moshi na majivu yanayotolewa nayo ni sumu.

Kufukia kwenye mashimo – Baadhi

ya wakati hulazimika kuzipeleka takataka katika mashimo. Tunapofanya hivyo tunatakiwa tuhakikishe kwamba takataka zimefungwa vizuri katika mifuko ambayo haziwezi kupeperushwa na takataka za vitu vya hatari kama vile injini au zimehifadhiwa vizuri. Majaa kwa kawaida huzikusanya takataka zote mahali pamoja na kuna nadharia kwamba, takataka zinaweza kutumika kama chanzo kwa ajili ya kuzalisha umeme hapo baadaye.

Mbolea ambayo hukusanywa katika kisiwa cha Chumbe – asilimia 80 ya taka ambazo zinatoka majumba ya Zanzibar zinawezekana kutengezea mbolea © Nell Hamilton

Page 32: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

30

8 Mabadiliko ya hali ya hewa Kisha tukakufanyeni nyiye ndio wenye kushika mahala pao baada yao katika ardhi ili tuone jinsi mtakavyo

tenda. (Qur’an 10:14)

Hali ya hewa, na miongo: baadhi ya maelezo Hali ya hewa, ni hali ya hewa inayotuzunguka katika wakati wowote. Je, ni ya joto, au baridi, ya jua au ya

mawingu, isiyokuwa na mvua au yenye mvua, yenye upepo au iliyotulia? Miongo ni mabadiliko ya kawaida

katika aina mbalimbali za hali ya hewa (nguvu ya upepo na muelekeo wake, mvua, n.k.) katika nyakati tofauti za mwaka. Climate ni aina moja maalumu (ya kawaida) ya hali ya hewa inayopatikana (inafanyiwa

hesabu kutokana na vipimo vya mvua, hali ya joto, n.k.), inayofanyiwa wastani katika kipindi kirefu, katika miongo tofauti kwa miaka mingi. Hali ya hewa (climate) ya dunia ni wastani wa hali ya hewa katika dunia nzima.

Miongo na hali ya hewa ya Zanzibar – Zanzibar inayo hali ya hewa ya tropiki ya monsuni (pepo za

msimu) kwa kawaida ni ya joto na yenye unyevu. Miongo huletwa na pepo za msimu au za ‘biashara’. Kuanzia mwezi wa Novemba mpaka Machi upepo huvuma kutoka kaskazini na kuleta mvua za muda mfupi (vuli) katika mwezi wa Novemba, zinazofuatiwa na msimu wa joto na kiangazi kuanzia Disemba mpaka Machi. Katika mwezi wa Aprili, pepo za msimu huanza kuvuma kutoka kusini, na kuleta mvua za muda mrefu za masika ambazo huendelea mpaka mwezi wa Mei na kufuatiwa na msimu mrefu wa baridi (kipupwe) ambao unaendelea mpaka Septemba.

Hali ya hewa inaweza kubadilika kila siku lakini aina mbalimbali za miongo zinaweza kutaribika na haibadiliki sana, lakini (hali ya hewa ya) kawaida haibadiliki sana katika kipindi cha maisha ya mwanadamu.

Nini huathiri hali ya hewa ya muda mfupi? Jua – Karibu nishati yote ambayo hudhibiti hali ya hewa yetu ya muda mrefu asili yake inatoka kwenye

jua.

Anga – Karibu nusu ya nishati inayotoka kwenye jua inayofika duniani hufyonzwa na ardhi na bahari na

kuipasha moto, inayobaki hurejeshwa kama joto. Lakini si joto lote linalorejeshwa linaingia kwenye hewa. Tabaka la gesi zinazokuwepo kumaumbile katika mchanganyiko wa gesi katika dunia, hufanya kazi kama paa la blangeti au kiyoo na kuliweka joto ndani yake na kuipasha dunia joto. Mchakato huu wa kuzuia joto unaitwa athari ya mpitisho wa mionzi ya jua kwenye hewa na ni ya lazima kwa maisha ya hapa duniani. Gesi ambazo zinapeleka hali hii zinajulikana kama ‘gesi zinazoathiri hali ya hewa’. Gesi hii ambayo ipo kwa wingi sana ni gesi ya dioksidi ya kaboni ambayo hutolewa katika kuvuta na kutoa pumzi, kuchoma vitu, na wanyama na mimea inapooza katika hewa. Mitheni siyo nyingi sana lakini ni kizuia joto chenye nguvu zaidi, huzuia joto mara 20 zaidi kuliko dioksidi ya kaboni. Gesi ya mitheni hutolewa na mimea inapooza bila ya kuwepo hewa, kwa mfano katika ardhi iliyojaa maji au sehemu zenye (landfill sites). Gesi nyengine inayoathiri hali ya hewa oxidi naitrojini inayotolewa na udongo misitu inapokatwa.

Latitude na Urefu wa Kitu usawa wa bahari – Katika nchi za tropiki (joto), karibu na mstari wa ikweta,

jua huwepo juu usawa wa kichwa na mishale yake hungara moja kwa moja chini mpaka juu ya dunia. Kwa hiyo nishati zaidi hufika aridhini. Hata hivyo, Kaskazini na Kusini ya ncha ya dunia (latitude za juu) nishati ya jua lazima isafiri kupitia kwenye anga kwa hiyo, ardhi huwa ni baridi zaidi na hufunikwa na barafu kwa mwaka mzima. Katika sehemu zilizonyanyuka sana kama vile juu ya milima kuna tabaka chache zaidi za michanganyiko ya gesi kuzuia joto ndani yake, kwa hivyo kila ukienda juu zaidi, ndivyo kunakokuwa baridi zaidi. Hiyo ndiyo maana kwa nini kuna barafu juu ya Mlima Kilimanjaro ingawa upo katika nchi ya tropiki.

Bahari – Bahari inasaidia kudhibiti kiwango cha joto na baridi kupita kiasi kwa kuhifadhi na kuondosha

joto. Hali ya joto na baridi katika sehemu za pwani hazibadiliki kama sehemu za ndani. Kwa mfano katika Zanzibar tofauti baina ya hali ya joto na baridi mchana na usiku ni kama nyuzi sita wakati katika ji wa Dodoma ni nyuzi 12 baridi zaidi usiku kuliko mchana. Mikondo ya baridi hupelekea maji yaliyo na joto zaidi kutoka sehemu za tropiki (joto) kwenda kwenye sehemu za baridi zaidi za dunia, na kuzipatia joto zaidi, na maji baridi yanatiririka nyuma.

Maisha – Mimea na wanyama huathiri hali ya hewa ya muda mrefu. Tishu za mimea hufyonza hewa

chafu inapoota, na huiachia inapooza. Kwa hiyo mimea yote inayoota katika misitu ya duniani na baharini ni ghala za gesiukaa, wanaziweka gesi sinazoathiri hali ya hewa nje ya mchanganyiko wa gesi na kupunguza athari ya joto. Mamilioni ya miaka iliyopita, mingi ya misitu ya dunia ilikuwa imejaa maji, jambo lililopunguza kasi ya uozaji. Kwa hiyo, miti ilipokufa, matawi na majani yaliyokufa yalijenga matabaka katika sehemu zilizotapakaa maji. Baada ya muda, matabaka ya tishu za mimea ziligandamizwa na hatimaye kubadilika na kuwa makaa ya mawe, mafuta na gesi asilia nishati hizi kisukuku, kwa hiyo zimehifadhi hewa chafu na kuizuia nje ya mchanganyiko wa gesi kwa mamilioni ya miaka. Wanyama hutoa gesi ukaa kwa uvutaji na

Page 33: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

31

utoaji wa pumzi, na ng’ombe na mchwa wanaposaga chakula chao (majani) hutoa gesi ya mitheni katika matumbo yao, ambayo hutolewa nje wanapokwenda mbweu au wanapojamba!

Tunakusudia nini tunaposema mabadiliko ya hali ya hewa au tabia nchi? Mabadiliko ya hali ya hewa hutokea kunapokuwa na

mabadiliko katika wastani wa hali ya hewa kwa kipindi kirefu, kama yanavyooneshwa na vipimo vya hali ya hewa, miongo na mahali ya miaka kadhaa.

Tunajuaje kama hali ya hewa imebadilika? – Katika kipindi

cha maisha ya mwanadamu, hali ya hewa inaonekana kama haibadiliki, lakini wanasayansi wamegundua ushahidi mwingi (unaonesha) kwamba katika mamilioni ya miaka iliyopita, dunia imekuwa baridi na joto zaidi kuliko ilivyo leo. Katika sehemu baridi zaidi za dunia, kuna mawe yenye wanyama wa tropiki waliogeuka kisukuku kama vile matumbawe, katika mahali ambapo sasa ni baridi mno kwa mawe kuota, kwa hiyo maeneo hayo lazima yalikuwa na joto hapo zamani. Barafu (kubwa) itelezayo kuelekea chini ya mlima leo huchonga mabonde katika miamba, na tunaona mabonde kama hayo katika maeneo yenye joto mno kwa barafu kubwa, kwa hiyo lazima zilikuwa na joto zaidi hapo zamani.

Tunapimaje mabadiliko ya hali ya hewa? – Wanasayansi

wamekuwa wakiweka kumbukumbu ya hali ya joto na baridi na mvua duniani kote kuanzia mwaka 1850! Vipo vituo 22,000 vinavyoangalia na kufuatilia hali ya hewa yetu duniani kote na baharini. Setilaite hupima mawingu na joto linalotolewa duniani kote, zikitupa vipimo sahihi sana juu ya yaliyotokea kwa hali ya hewa ya dunia kwa miongo mingi. Tunaweza kujifunza zaidi kuhusu hali ilivyokuwa zamani sana kutokana na barafu ya kudumu – katika barafu kubwa za juu ya mlima kama Mlima Kilimanjaro, au katika barafu zilizoko katika ncha ya dunia. Kila mwaka tabaka jipya la barafu kubwa hufanyika tabaka nene katika miaka ya baridi na tabaka jembamba katika miaka ya joto zaidi. Wanasayansi wamehesabu matabaka ya barafu katika miaka ya nyuma na kupima unene wao kujua jinsi hali ya hewa ilivyobadilika, na kwa haraka kiasi gani katika miaka ya 800,000 iliyopita. Pia tunapima ukubwa wa mabamba ya barafu na barafu kubwa, na kufuatilia viwango vya bahari, ambavyo hupanda na kushuka wakati barafu ya ncha ya

dunia inapoyeyuka na kuganda: kipimo cha maji kujaa na kupwa kilichopo nje ya Mji Mkongwe kinapima kiwango cha bahari cha Bahari ya Hindi.

Tumegundua nini? – Taarifa na vipimo vyote vinatujulisha jambo hilo hilo:

dunia yetu inakuwa na joto zaidi. Katika kipindi cha miaka 25 iliyopita dunia imeongezeka joto kwa nyuzi 0.5. Katika Tanzania, wastani wa hali ya joto kwa mwaka umeongezeka kwa nyuzi moja kuanzia mwaka 1960 na inategemewa kuongezeka nyuzi nyingine kufikia mwaka 2060; ongezeko hilo la wastani wa nyuzi 0.02 kwa mwaka katika Tanzania. Ongezeko hili linaweza kuonekana si kubwa – ni dogo mno kulihisi – lakini hali hii inarudiwa duniani kote: hatua ndogo zinaongeza mabadiliko makubwa. Taarifa hizo zinaonesha kwamba barafu ya kudumu inayeyuka – barafu ya ncha ya dunia na barafu kubwa zieleazo milimani zinapotea kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa joto. Viwango vya bahari vinaongezeka wakati barafu inapoyeyuka na kutiririkia baharini. Hali ya joto inaongezeka kwa kasi zaidi na mabadiliko yanatokea kwa haraka zaidi kuliko yalivyotokea kabla. Athari ya ongezeko la joto haidhibitiki.

Nini kinapelekea mabadiliko ya hali ya hewa sasa? – Nguvu za

kimaumbile zitaathiri hali ya hewa daima, lakini hazitoshi kuelezea kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea sasa. Kwa hiyo, nini kilichobadilika?

Uchomaji wa mabaki ya fueli – Tunapochoma mabaki ya fueli (petroli, makaa ya mawe na gesi asilia)

kwa kupikia nishati ya vyombo vya usafiri au kuzalisha umeme kwa matumizi ya nyumbani na biashara, gesi ya ukaa ambayo ilikuwa imehifadhiwa na mimea kwa mamilioni ya miaka, hutolewa. Hali ya joto la dunia ilianza kupanda miaka 150 iliyopita: muda ambao binaadamu alianza kuchoma mabaki ya fueli.

Kilele cha barafu katika Mlima Kilimanjaro mnamo mwaka 1993 na 2000; wanasayansi wanakadiria barafu kutoweka ifikapo mwaka 2015 © NOAA

Takataka ambazo zinaoza hutoa mitheni, gesi chafu © Nell Hamilton

Page 34: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

32

Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?Ulikua unajua…?

• Ng’ombe mmoja hutoa zaidi ya lita 200 za mitheni kila siku!

• Joto la Tanzania linaongezeka kwa nyuzi 0.2 kila miaka 10. Tanzania 1992 - 2005

22.522.6

22.722.822.9

23

23.123.223.3

23.423.5

1991 1996 2001 2006

Year

Av

era

ge

Te

mp

era

ture

Ukataji wa Miti – Kila idadi ya watu inapoongezeka duniani, ndivyo tunavyohitaji gesi ya ukaa,

tunavyohitaji kuni na ardhi zaidi, kwa ajili ya kupanda mazao. Miti inayoishi hufyonza dioksidi ya kaboni wakati wa mchakato wao wa kutengeneza chakula (usanidi mwanga) na huhifadhi kaboni katika tishu zao inapokua. Tunapokata misitu, inaacha kuchukua gesi ya ukaa kutoka kwenye mchanganyiko wa gesi, na tunapochoma kuni tunaiacha gesi ukaa iliyohifadhiwa irudi hewani. Idadi ya watu wa Zanzibar inaongezeka kwa asilimia 3 kwa mwaka na ukataji wa misitu unaongezeka – tunakata zaidi ya hekari 500 za misitu kila

mwaka.

Kilimo – Ukataji wa misitu kwa ajili ya ardhi ya kilimo

huiachia oksidi za naitrojini kwenye mchanganyiko wa gesi ulioko hewani. Watu wanafuga ng’ombe na mbuzi wengi ambao hutoa mitheni, na mimea inapooza katika mashamba ya mpunga na uchafu wa chakula na mimea inapooza katika ardhi, mitheni nyingi hutolewa.

Je, binadamu kweli wanaibadili hali ya hewa ya dunia nzima? – Ndio. Kwa bahati mbaya tunafanya hivyo.

Wanasayansi wana uhakika kwamba dunia inapata joto, na hii sana inatokana na vitendo na shughuli za binadamu, hususan uchomaji wa mabaki ya fueli. Viwango vya gesi ukaa katika mchanganyiko wa gesi vimeongezeka kwa asilimia 40, na viwango vya mitheni vimeongezeka mara mbili tangu mwaka 1750, na vinaweza kuongezeka tena mara mbili hadi kufikia 2050. Uongezaji wa gesi hatari kwenye mchanganyiko wa gesi ni kama kuvaa nguo zaidi – gesi hizo hukamata joto zaidi, dunia hupata joto, na hali ya hewa inabadilika.

Vipi Mabadiliko ya hali ya hewa huathiri mazingira yetu na sisi (wenyewe)?

Hali ya hewa iliyovuka mpaka – Dhoruba, ukame, mafuriko na matokeo mengine ya hai ya hewa

iliyovuka mpaka, kama vile vimbunga katika Bahari ya Hindi, hutokea mara kwa mara. Misitu, miamba, mashamba, miji na vijiji vinazidi kuathirika na matokeo hayo na hayapati muda wa kujirudi katika hali yake ya awali baina ya dhoruba moja na nyengine.

Hali joto za juu na bahari zenye joto zaidi – Kumbukumbu zinaonesha hali joto katika bahari kuu katika

miongo ya karibu zimesababisha upayukaji ulioenea wa matumbawe katika Bahari ya Hindi, ambayo mengi yao hayajajirudi katika hali yake ya awali, ikiwa na athari muhimu zinazoendelea za kiuchumi na kijamii kwa spishi muhimu kwa samaki wa miamba.

Bahari yenye tindikali – Hewa chafu kutoka angani / hewani huyeyuka katika bahari, na kuifanya iwe na

tindikali zaidi, na inaweza kuuwa viumbe wa baharini (hususan mayai ya samaki) huyeyusha mifupa ya matumbawe na hudumaza ukuaji wa kombe na chaza.

Mabadiliko ya mvua – Nyakati za mababu na mabibi zetu, miongo ilikuwa ikitokea kwa kawaida na

ikitabirika. Lakini sasa nyakati za miongo zinabadilika sana, na katika baadhi ya miaka, katika sehemu nyingine za Afrika ya Mashariki, miongo ya mvua haiji kamwe. Hili linapotokea maelfu, hata mamilioni ya watu hukumbwa na njaa. Katika Zanzibar, maji yote tunayokunywa yanatokana na mvua ambayo huzama ardhini. Tabaka la matumbwawe hufanya kazi kama sponji la chini ya ardhi na kuyahifadhi. Tungekuwa na mwaka mmoja bila ya mvua hapa sehemu kubwa ya Zanzibar zingekosa maji safi ya kunywa na badala yake maji chumvi yangeingia katika mawe. Baadhi ya vijiji vya pwani tayari wameshapta tatizo hili. Wale wanaoweza kununua maji wanayanunua sehemu nyengine lakini watu wengi hawawezi – na ingekuwaje kusingekuwa na maji mahali popote?

Kuyeyuka kwa barafu na theluji – Mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha kutoweka kwa asilimia 80

ya kofia ya theluji juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro katika kipindi cha miaka 100, iliyopita. Kwa wastani huu, theluji yote itakuwa imetoweka ifikapo mwaka 2015. Theluji na barafu, kubwa itelezayo kwenye Mlima Kilimanjaro inafanya kazi kama mnara wa maji, unaohifadhi maji ambayo yanaingia kwenye mito kadha inapoyeyuka wakati wa kiangazi. Barafu inapotoweka mito hukauka, na kuziwacha jamii za karibu bila ya maji.

Kupanda kwa viwango vya bahari – Barafu ya ncha ya dunia na inayoteleza milimani inapoingia

baharini, na maji ya bahari yanapopanda yenyewe, yanapokuwa na joto zaidi: kiwango cha bahari kinapanda. Jambo hili litakuwa na athari kubwa kwa maeneo ya pwani yaliyo mabondeni pamoja na visiwa kama Zanzibar. Upandaji wa maji ya bahari, pamoja na dhoruba za mara kwa mara, huongeza mmomonyoko wa ufukwe, kurudi nyuma ukanda wa pwani, na ardhi huwa bahari. Zanzibar bado haijaathirika, lakini visiwa vingine vya Bahari ya Hindi vimeathirika. Viwango vya bahari katika bara la Afrika

Page 35: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

33

Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!Tembea ujionee!

• Waulize babu na bibi yako iwapo miundo ya hali ya hewa imebadilika uhai wao.

• Tembelea hoteli zilizopo kwenye ufukwe – zinayaacha majani, mimea na miti iliyopo ufukweni kuilinda dhidi ya kupanda kwa viwango vya bahari?

Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!Kitunze kidumu!

• Zima taa, mafeni na kiyoyozi ikiwa huvitumii.

• Tumia matungi ya taa yanayookoa nishati.

• Usiwache mfereji wazi unapoosha masufuria, nguo au wewe mwenyewe – tumia ndoo!

vinaweza kuongezeka kwa karibu sentimita 60 kufikia mwaka 2100, jambo ambalo litaadhiri vibaya pwani ya Zanzibar.

Athari kwa bioanuwai – Maisha (viumbe) katika dunia vimestahamili na kuvumilia mabadiliko ya ardhi

yaliyotokea kabla, lakini mabadiliko ya kihistoria yalitokea kwa kasi ndogo, na wanyama pori waliweza kuishi kulingana na hali halisi iliyokuepo, ama na makundi ya watu kwa kila kizazi kutawanyika zaidi kuelekea Kaskazini au Kusini, au kubadilika ili kuishi katika hali mpya. Mabadiliko yanayotokea sasa yanatokea kwa haraka sana kwa makundi ya watu kuweza kuishi kulingana na mazingira kimaumbile, na kama wangeweza, mashamba, barabara na makazi ni vikwazo vinavyozuia uhamiaji baina ya maeneo yenye wanyama pori wengi. Wanyama na mimea iliyopo visiwani haiwezi kuvuka bahari, kwa hiyo iwapo visiwani mabadiliko ya hali ya hewa yanasababisha maji mengi mno au yasiyotosha, au spishi za chakula zinakuwa adimu, spishi nyingi hazitoweza kujirekebisha kuweza kuishi na zitatoweka kutoka Zanzibar, na spishi za wanyama adimu kuna uwezekano wa kutoweka kabisa.

Athari kwa shughuli za kiuchumi – Tunamwaga mbegu, tunapanda

na kuvuna mazao kulingana na msimu. Mawimbi ya joto, ukame au mvua zisizokuwa za miongo zinaweza kuharibu mazao yetu. Mafuriko yanaweza kuangamiza ardhi ya mashama na mali, na ukame ulioenea unaweza kusababisha mateso makubwa. Matumbawe yanapopauka na kufa, idadi ya samaki hupungua, na iwapo Zanzibar itapungukiwa na maji, haitaweza kuhimili watalii wengi. Watu wengi watapoteza au kukosa kazi.

Tunawezaje kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa? Punguza kutolewa kwa gesi zinazoathiri hali ya hewa – Gesi nyingi

zinazoathiri hali ya hewa hutolewa na nchi nyingi zilizoendelea zaidi, lakini lazima tufanye sehemu yetu hapa Zanzibar. Tunaweza kutembea au kupanda baiskeli au daladala badala ya kuendesha gari n.k. na kutumia kivuko badala ya kutumia ndege. Watu wenye magari au pikipiki wahakikishe inatembea vizuri na inaunguza fueli ipasavyo – kusiwe na moshi mweusi unaoruka. Kwa kununua bidhaa zinazolimwa au kufanywa Zanzibar, na zilizofanywa kwa vitu vya hapa hapa, tunapunguza fueli inayotumika kuzisafirisha. Tunaweza kupunguza utolewaji wa gesi ya mitheni kutokana na mabaki ya mimea na chakula (kwa hiyo inaoza hewani) badala ya kuitupa – mbolea hiyo itarutubisha udongo na mazao yetu! Plastiki hufanywa kutokana na mabaki ya fueli, kwa hiyo kuifanya na kuichoma hutoa gesi zinazoathiri hali ya hewa. Lazima tupunguze matumizi ya plastiki, tuanzishe vituo vya matumizi mapya ya plastiki katika jamii zetu, na tuvitumie! Katika siku za usoni, Zanzibar inaweza kutoa umeme unaohitaji kutokana na vyanzo vinavyorejesheka kama jua, upepo na nishati ya maji kupwa na kujaa. Ipo teknolojia hata ya kuzalisha umeme kutoka takataka!

Punguza ukataji wa misitu – Misitu ya Zanzibar ilindwe na

ihifadhiwe. Kila mmoja wetu anaweza kupunguza matumizi ya kuni kwa kutumia majiko yanayotumia fueli kidogo na vizuri badaa ya jiko la mawe matatu na kuchoma vitu vya biokemia badala ya kuni na makaa. Tutumie mbao kutokana na miti inayoota haraka, zilizovunwa kutoka mashamba makubwa na siyo misitu ya upepo, na panda miti mipya badala ya ile iliyokatwa.

Na hatimaye – jifunze kuishi na mabadiliko ya hali ya hewa –

Bila ya shaka lazima sote tufanye sehemu zetu kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa, lakini lazima tukubali kwamba hali ya hewa inabadilika kuwa ya joto zaidi na baridi kali zaidi, na jambo hili litaleta mabadiliko katika mazingira. Kwa hiyo, lazima tujifunze kuishi katika dunia inayobadilika. Miamba ya matumbawe, vitalu vya nyasi bahari, fukwe, mikoko – mimea na miti yote ya pwani –

inasaidia kulinda mali ya pwani dhidi ya athari za dhoruba na kuongezeka kwa kiwango cha bahari, kwa hiyo tunahitaji kuyathamini makazi haya. Maendeleo mapya katika maeneo ya pwani yaanzishwe mbali na ufukwe ili kuruhusu bahari inayosogea, na mchanga usichukuliwe kutoka kwenye fukwe. Mimea na miti ilindwe na kuhifadhiwa, ili maji ya mvua yaweze kufyonzwa ndani ya ardhi, badala ya kupelekwa baharini, huku ikichukua udongo na virutubisho. Lazima tuyakinge maji ya mvua na tusitumie maji kupita kiasi. Wakulima wanaweza kuchagua aina za mazao yanayohimili ukame ambayo hayahitaji maji mengi na shughuli ya utalii ipunguze matumizi yake ya maji. Sote kwa pamoja tunaweza kuvilinda visiwa vyetu vizuri kwa

Mikoko kusaidia kulinda jamii za pwani kutokana na kuongezeka kwa kima cha maji, dhoruba, na mmomonyoko wa udongo © Rachel Hamilton

Page 36: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

35

9 Chukua hatua Hatua na njia za haraka ambazo zitasaidia kuyalinda mazingira, kila siku!

1 Mazingira na uendelevu – Environment & sustainability

� Fuata Mazoezi ya Kimazingira (ECO-Practice) wakiti wote (angalia sehemu ya mbele ndani ya kitabu hiki)

� Kila mara unapofanya maamuzi ambao unaweza kuathiri mazingira, jiulize mwenyewe kama mazingira yatakuwa mazuri au mabaya ikiwa kila mtu atafanya uamuzi, na kuchagua chaguo endelevu

� Zungumza na rafiki zako na familia juu ya mazingira na kwa nini kuhifadhi kuna umuhimu

� Jaribu kununua bidhaa ambazo zimetengenezwa na vikundi vidogo vidogo vya wanawake ili kuwapa moyo

2 Bioanuai – Biodiversity � Usiwaweke wanyama pori wadogo ikiwa ni pamoja na kasuku na kima, au samaki wa kuwindwa

� Epuka na ukataji wa miti, na kununua bidhaa ambazo zimetokana na mbao ambazo zimo hatarini kuisha, chagua mbao ambazo zina matumizi endelevu nazo ni mbao za minazi au za matunda kutoka kwenye mabustani badala yake

� Usinunue bidhaa ambazo zimetengenezwa kwa wanyama hatarini mfano pembe

� paka wako ametolewa uzazi

� Kuhamisisha wanyama pori kwa kuotesha miti asilia

� Punguza kuwepo kwa kunguru: hakikisha unatupa taka hasa taka za vyakula, ambapo hawawezi kufikia

� Siku ambazo za matembezi Zanzibar, saidia biashara za jamii na utembelee sehemu zilizoanzishwa hifadhi

� Ambazo zinapunguza athari za kimazingira na kusaidia kulinda wanyama pori

� Siku ambazo utakuwa kwenye matembezi kisiwa cha Zanzibar, jaribu kuwasaidia kuwahamasisha wafanyabiashara wa ndani ya jamii, na kutembelea hifadhi ambayo inapunguza madhara juu ya mazingira na zinasaidia kulinda wanyamapori

3 Mikoko – Mangroves � Usikate mikoko kwa ajili ya kuni, chagua njia mbadala ambazo zinapatikana na endelevu

� Nunua mbao na karatasi zinazotokana na vyanzo endelevu

� Badilisha karatasi, kadi, kununua bidhaa ambazo zimebadilishwa kutokana na karatasi

� Tumia pande zote mbili za karatasi na rejea kutumia bahasha kwa matumizi mengine

4 Nyasi ya bahari – Seagrass � Usiwachie boti yako au nanga ikaharibu nyasi bahari

� Usiokote changarawe au sheli, au kuchukuwa mawe au mchanga kutoka kwenye fukwe kwa ajili ya kujengea

5 Miyamba ya matumbawe – Coral reefs � Usijaribu kutupa takataka au uchafu, hasa katika au karibu na bahari

� Usichukue au kununua kombe au matumbawe

� Jaribu kuuliza vipi samaki ambao umenunua wamevuliwa kwa njia zipi na usinunue samaki ambao wamevuliwa kwa mabomu / baruti

Page 37: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

36

6 Uvuvi – Fisheries � Angalia nyakati ambazo zimefungwa kwa ajili ya ukusanyaji wa kombe

� Chagua dagaa endelevu: kula madema au mishipi ya jadi ya kuvulia samaki kutoka kwenye hifadhi endelevu, epuka kula aina samaki ambao wapo hatarini kupotea kama vile papa,paa au pono

� Usijaribu kukusanya au kununua viumbe vya baharini kama vile konokono kwa ajili yakumbukumbu ya utalii!

7 Uchafuzi wa mazingira – Pollution � Tupa takataka na uchafu wa majumbani sehemu ambazo zinatambulika, hasa plastiki: kupunguza,

tumia upya, badilisha upya

� Rekebisha gari yako endapo itatoa harufu mbaya au moshi mweusi

� Kupunguza matumizi ya madawa makali na epusha katika uchafuzi wa mitaro ya maji na vianzio vya kusambaza maji safi

� Panda nafaka za chakula kwa mbolea ya samadi na mbolea ya asili jiepushe na madawa makali ya kuulia wadudu

� Tumia choo ambacho ni safi na salama kwa mazingira –sio katika fukwe!

� Epukana na uhifadhi mbaya – chukua mkoba au kikapu wako maalum wa kuhifadhia matunda na mbogamboga utakapoenda sokoni

� Jaribu kutengeneza mbolea ya mboji kwa mabaki ya vyakula ambavyo vinaoza na majani

� Usiache vioo ambavyo vimevunjika-ni hatari vinaweza kumkata mtu na kusababisha hat kuwaka kwa moto

� Tupa betri vizuri ambazo hazitumiki tena

� Usitupe take katika fukwe, bahari au sehemu yeyote

8 Mabadiliko ya hali ya hewa – Climate change � Hifadhi nishati: zima taa na umeme ambao utakuwa hutumii na tumia balbu ambazo hazitumii umeme

mwangi

� Pika chakula haraka haraka, ili utumie nishati ndogo, na tumia chombo ambacho kitapitisha joto haraka kwa ajili ya kupikia

� Jaribu kutumia usafiri wa kawaida, au tembea kuliko kuendesha gari, pendelea kusafiri kwa njia ya majini kuliko angani

� Hifadhi maji: chemsha kadri upendavyo, na usiwache mifereji wazi yakamwaga maji – kosha vyombo na mbogamboga kwenye chombo chenye maji,usikoshe kwenye maji ambayo yanatiririka kwenye mifereji

� Chagua miti ambayo inastahmili hali ya ukame, hii inamaanisha ya kwamba uhitaji kumwagilia maji

Page 38: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

37

10 Istilahi

Anga – Tabaka za gesi katika dunia

Bahari kuu – Maji ya bahari amabyo yapo mbali na nchi kavu na ya kina kirefu

Baruti – Ulipukaji wenye nguvu; au uvuvi haramu wa kulipua

Bustani – Shamba ambalo majani (nyasi) huota

Chombo – Mashine ya umeme ya nyumbani, k.m. mashine ya kufulia, simu za mikononi

Gesi zinazoathiri hali ya hewa – Gesi inayochangia katika kupata joto dunia kutokana na gesi inaokusanya

joto kutoka kwenye jua, kama dioksidi ya kaboni na mitheni

Ghuba – Eneo la bahari lililozungukwa na ardhi / nchi kavu pande tatu

Kitalu cha nyasi bahari – Eneo la mchanga au tope ambapo nyasi bahari zinaota

Kujikimu – Hali ya kuwa na vitu vya kutosha unavyohitaji ili kukuwezesha uishi, lakini huna cha kuweka

Kuogelea kwa kioo – Ni kuogelea kwa kutumia kioo na mrija wa kuvutia hewa

Kupauka kwa matumbawe – Mchakato ambao kwake polipu wa matumbawe hutoa nje kutoka kwenye

chembe chembe zao za maisha (seli) mwani mdogo zenye rangi joto linapozidi

Latitude – Masafa kutoka Kaskazini au Kusini ya Ikweta

Mabadiliko – Mchakato ambao kwake mimea na wanyama hubadilika ili kuweza kukabiliana na mazingira

mapya

Mabaki ya fueli – Mafuta tyaliyofanyika chini ya ardhi kutokana na mabaki ya mimea na wanyama

mamilioni ya miaka iliyopita, mfano gesi, makaa ya mawe na mafuta ya petroli

Maji kujaa na kupwa – Kupanda na kushuka kwa kawaida kwa viwango vya bahari vinavyotokana (mara

mbili kwa siku) na mvuto wa graviti wa mwezi (na jua)

Makazi – Ni eneo ambalo mnyama au mmea unaishi

Mbegu za mikoko – Kipande cha mmea kinachovunjika na kuota mmea mwengine, kama miche ya mkoko

inayochipua juu ya mti huo kabla ya kuanguka

Mbolea – Iliyofanywa kutokana na mimea iliyooza na uchafu wa wanyama – Iliowekwa kwenye chungu cha

mbolea

Mwamba wa matumbawe – Mwamba uliopo chini yamaji uiliofanywa kutokana na mifupa ya maelfu ya

makoloni ya matumbawe hai na sponji

Mwani mdogo – Mimea yenye seli moja ambayo inaishi katika tishu za wanyama kama matumbawe,

ambayo ina kitu chenye rangi kinacho ipatia rangi mimea

Pangaboi – Sehemu ya mota inayozunguka yenye viwembe viwili au zaidi, ambayo inazunguka katika maji

au hewa kuifanya mashua au ndege iende

Polipu – Mnyama mdogo sahili wa majini kama anemone, ambaye amehusiana naye kwa karibu (sana)

Polisterini – Plastiki nyepesi yenye mapovu ya hewa, inayotumika kuhifadhia na kulinda vitu dhaifu, au

huwekea vitu moto au baridi

Rasi – Eneo la bahari ambalo limetenganishwa na bahari kuu kwa mwamba (= mstari wa mawe, mchanga

au matumbawe ambao upo kwenye maji ya kina kidogo)

Rizomu – Kigogo cha baadhi ya mmea vinavyoota kulalo juu au chini ya ardhi na inayotoa mizizi na majani

Shimo – Kuondoa takataka nyingi kwa kuzizika, au mahali ambazo takataka huzikwa

Spishi – Kundi la vitu vinavyoishi (ambavyo vinaweza kuwa aina ya mnyama, mmea, fangasi au bacteria)

ambao wanafanana na wanaweza kuzaliana wenyewe kwa wenyewe lakini si pamoja na wengine wa makundi mengine

Spishi adimu – Spishi inyoishi mahali maalum tu

Sunami – Wimbi kubwa sana la uharibifu linalosababishwa na mtetemeko wa chini ya ardhi au mwendo wa

dunia

Tia nanga – Kuifunga mashua, ngalawa ili ibaki mahali pamoja

Tia rangi ya hudhurungi – Kubadilisha ngozi ya wanyama kuwa ngozi ya kutumiwa kwa kutumia dawa ya

kuhifadhiwa / kupaka rangi ili isiharibike kama vile magome ya mikoko

Toweka kabisa – Mchakato ambapo spishi hufa kabisa na haonekani tena

Uchimbaji – Utoaji wa rasilimali kama mawe na metali kutoka ardhini

Ufukwe – Kishorobo cha nchi kavu kwenye ukingo wa bahari, ziwa, au mto mpana; fukwe zinaweza kuwa

za mchanga, mawe au tope

Usanidi mwanga – Mchakato ambao mmea hutumia nishati inayotoka kwenye mwanga wa jua kuzalisha

chakula chake.

Page 39: Mazingira Endelevu - Chumbe Island Coral Parkambayo kutakana nayo tunazalisha mabustani na nafaka zinazovunwa na mitende mirefu iliyobeba makocha ya tende, riziki ya watu na kwahivyo

Ma

zin

gira

en

dele

vu

kw

a Z

an

zib

ar

Ma

zin

gira

en

dele

vu

kw

a Z

an

zib

ar

Ma

zin

gira

en

dele

vu

kw

a Z

an

zib

ar

Ma

zin

gira

en

dele

vu

kw

a Z

an

zib

ar

Co

ral P

ark

Jifunze kuhusuJifunze kuhusuJifunze kuhusuJifunze kuhusu::::

+ Wanyama na mimea

ya kushangaza

inayoishi karibu nasi

na kwa nini

tunaihitajia!

+ Jinsi mazingira asili

yanasaidia kuhifadhi

nyumba zetu,

yanavyotulisha na

kutuweka katika hali

nzuri ya kiafya.

+ Jinsi ya kufaidika na

maumbile bila ya

kuyaharibu.

+ Kuchagua chakula cha

bahari kwa busara ili

kuhifadhi walobaki na

viumbe vyengine.

+ Namna ya kujipatia

riziki katika maisha

na kulinda mazingira

kwa faida ya baadae.

+ Kugeuza taka taka

kuwa malighafi.

+ Namna

tunavyofaidika

tunaposafisha fukwe

na jamii zetu.

+ Namna tunavyoweza

kulinda mazingira

yetu kwa faida ya

baadae!

Chumbe Island Coral Park ni mradi wa hifadhi ya pwani ambao umejizolea sif a na zawadi ny ingi kimataifa. Mradi huu unajiendesha

weny ewe kupitia loji y ake ya kimazingira iliopo katika kisiwa cha Chumbe. Ada ambayo wanalipa wageni hutumika kwa uf atiliaji na

utaf iti kwa matumbawe na pia hudhamini ziara za wanaf unzi kwenda Chumbe kupata elimu y a mazingira kwa kila mwaka huenda

wanaf unzi wapato 500-600. Kisiwa kina nyumba za kulala wageni ambazo zimejengwa kwa usanifu, ubunif u na ujenzi ambao ni raf iki wa

mazingira ikiwa ni pamoja na vyanzo vya maji ya mv ua, nishati y a mwanga, maji y a moto yakanzway o na jua,vyoo vya kutumia mbolea

na maji machafu yanay ochujwa kwa kutumia mimea.

ISBN 978-9987-9467-2-3